View
226
Download
7
Category
Preview:
Citation preview
UHIFADHI WA KAZI ZA FASIHI
SIMULIZI(KIDATO CHA PILI)
Mussa Shekinyashi+255 743 98 98
MALENGO YA SOMO
• Kufikia mwisho wa somo:
• Tujikumbushe maana ya Fasihi Simulizi
• Tufahamu sifa bainifu za Fasihi Simulizi
• Tufahamu Njia za uhifadhi wa Fasihi Simulizi
tukizingatia: Ubora na athari (udhaifu) zake kwa
fasihi simulizi.
MAANA YA FASIHI SIMULIZI
• Fasihi simulizi ni aina ya fasihi inayowasilishwa
kwa njia ya mazungumzo ya mdomo.
• Aina hii ya fasihi imekuwepo tangu enzi na
enzi.
• Imekuwa ikirithishwa kutoka kizazi kimoja
hadi kingine kwa njia ya mazungumzo ya
mdomo.
• Mfano wa fasihi simulizi ni hadithi
tunazosimuliwa na wazazi wetu, nyimbo
tunazoimba, maigizo yanayoigizwa.
SIFA BAINIFU ZA FASIHISIMULIZI
• Huwasilishwa kwa njia ya mzungumzo ya mdomo.
• Huifadhiwa kichwani
• Humpa uhuru msanii wa kufanya mabadiliko kwa
kuzingatia mazingira na uhitaji.
• Huwa ni mali ya jamii nzima.
• Huwa na wakati maalum na pahala maalum pa
kuiwasilisha.
• Huwa inaruhusu fanani na hadhira kukutana ana
kwa ana.
• Huruhusu viungo vingine vya mwili kutumika
katika uwasilishaji.
• Huwa inaruhusu hadhira kushiriki katika
UHIFADHI
• Fasihi inaweza kukusanywa na kuhifadhiwa
kwa njia zifuatazo :
• Kichwa
• Maandishi
• Kanda za kunasia sauti
• Kanda za video, televisheni na filamu za
sinema (CD,DVD na kompyuta)
KICHWA
• Kwa asili uhifadhi wa fasihisimulizi hufanywa kwa vichwavya watu kutoka kizazi hadikizazi.
• Njia hii imetumika kwa kipindikirefu sana.
• Kutokana na njia hii fasihiimeweza kuwepo kutokavizazi vya kale hadi hiki cha sasa.
UHIFADHI WA KICHWA
UDHAIFU/ ATHARI ZA UHIFADHIWA KICHWA
• Kupungua kwa kumbukumbu za mhifadhi/fanani
• Kufa kwa fanani
• Fanani anaweza kubadilisha mambo muhimu katikasimulizi na hivyo kubadili kiini cha masimulizi hayo.
• Ukosekananji wa wahifadhi wa fasihi kwa kichwa. Ni vigumu kupata watu wanaopenda na wanaoweza kuhifadhifasihi simulizi
MAANDISHI
• Njia hii imeimeza fasihi simulizi kwa manufaa ya
baadae.
• Ugunduzi wa alama za uandishi ndio uliopelekea
fasihi simulizi kuhifadhiwa katika maandishi.
• Leo hii ni vigumu kuifahamu kazi ya fasihi simulizi
iliyowekwa kwenye maandishi.
• Njia pekee ya kuipambanua ni kuangalia tabia za
fasihi simulizi ambazo ni: “paukwa…pakawa”au
“hadithi….hadithi njoo”
MAANDISHI
UDHAIFU/ATHARI YA UHIFADHIWA MAANDISHI
• Uhifadhi kwa maandishi huwa na matatizo yafuatayo:
• Kukosekana kwa utendaji,sauti,kuimba vitabia.
• Kukosekana kwa uhusiano wa moja kwa moja kati ya
hadhira na fanani
• Kukosekana kwa mabadiliko ya mara kwa mara.
• Ufinyu wa hadhira, itakuwa na watu wachache tu, wale
wanaojua kusoma na kuandika.
• Inakuwa ni nyenzo ya kibiashara ambapo inahitaji
kugharamiwa.
KANDA ZA KUNASIA SAUTI
• Njia hii pia hutumika kuhifadhi fasihi simulizi.
• Hii ni teknolojia iliyochipukia baada ya maandishi.
• Ilikuwa na uwezo zaidi wa kuhifadhi uhalisia wafasihi simulizi ukilinganisha na njia ya uhifadhi kwamaandishi.
• Katika njia hii kanda hutumika, kanda hizo hushikasauti pamoja na vichombezo vyake.
KANDA ZA KUNASIA SAUTI NAREDIO
UDHAIFU/ATHARI ZA KANDA ZAKUNASIA SAUTI
• Sauti husikika, lakini…
• Ni vigumu kuona matendo ya fanani .
• Hadhira haishirikishwi
• Ni gharama kuipata
• Uhifadhi unahitajika uwe wa hali ya juu
• Kudumaa kwa kazi ilihifadhiwa, haitapata
mabadiliko kamwe.
KANDA ZAVIDEO,TELEVISHENI,FILAMU ZASINEMA, KOMPYUTA, MTANDAO, SIMU ZA MIKONONI, CD NA DVD• Uhifadhi wa namna hii hujumuisha sura na sauti
zinazoonekana kwenye skirini ya video.
• Vifaa maalumu hutumika kutengeneza picha za
namna hiyo.
• Fasihi simulizi imeweza kuhifadhiwa katika vifaa
hivi.
• Hapa uhalisia wa fasihi simulizi hujitokeza zaidi
ukilinganisha na njia zile za mwanzo.
• Hapa matendo na sauti vinaonekana wazi.
CD/DVDHutumika kuhifadhi fasihi simulizi
KANDA ZA VIDEOHizi hutumika pia kurekodi matukio
ya fasihi simulizi.
MTANDAOKwa njia hii fasihi simulizi
huifadhiwa kisha kusambazwa
katika jamii zote duniani .
KOMPYUTAKifaa hiki hutumika kuhifadhi na
kuonesha kazi za fasihi simulizi.
SIMU YA MKONONIHii ni njia rahisi ya kurekodi na
kusambaza kazi za fasihi simulizi
kupitia mitandao ya kijamii kama
facebook, whatsApp na mingineyo
UDHAIFU/ ATHARI YA NJIA HIIYA UHIFADHI
• Upungufu wa ushirikishwaji wa hadhira
• Njia hii ni ya gharama sana
• Haitabadilika kulingana na mahitaji ya hadhira
• Uhifadhi wa vifaa hivi ni wa gharama sana.
UMUHIMU WA KUHIFADHI KAZIZA FASIHI SIMULIZI
• Hukuza na kuendeleza utamaduni wa jamii.
• Zinasaidia katika kuvutia watalii
• Ni sehemu ya ajira.
• Kazi ya fasihi inapohifadhiwa huwa ni chachu
ya umoja wa kitaifa.
ASANTENI SANA!
Recommended