Upload
dinhquynh
View
329
Download
4
Embed Size (px)
Citation preview
HISTORIA YANGU
Naitwa Jumanne Gideon nilizaliwa katika kijiji cha kulimi kilichoko katika kata ya kulimi
kielelezo no 1 JUMANNE GIDEON
Wilaya ya maswa mkoani shinyaga .Nilizaliwa mtoto wa kwanza katika familia ya mzee
Gideon yenye watoto watano, wadogo zangu wakiwa wakiume wawili na wa kike wawili
Baba yangu na mama wote ni wakazi wa mkoa wa Shinyanga ninamaana ya kwamba ni
Wasukuma
Baada ya kufikisha miaka kumi na moja nilianza shule ya msingi Dodoma iliyoko kata ya Buchambi wilaya ya
maswa na baaba ya kufika darasa la tano mwaka 2002 wazazi wangu waliamua kuhamia katika kijiji cha kulimi
kilichoko katika kata ya kulimi iliyoko katika wilaya ya maswa kutokana na shughuki za uzalishaji mali kama
kilimo na ufugaji
Baada ya kuhitimu Elimu ya msingi mwaka 2004, nilichaguliwa na kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2005
katika shule ya sekondari Malampaka ambapo mwaka 2008 ilihitimu mafunzo yangu ya kidato cha nne na
Mwaka2009 nilichaguliwa kujiunga na mafunzo ya Ualimu ngazi ya cheti katika chuo cha Ualimu Tarime
kilichoko Mkoa wa Mara ambapo mwaka 2011 nilihitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya cheti
Mwaka 2012 nilipangiwa Halmashauri ya Wilaya Bukombe ya iliyoko mkoa wa Geita katika shule ya msingi
Bulumbanga iliyoko kata ya Runzewe Magharibi ambapo mpaka sasa nipo nafanya kazi katika Halmashauri
hiyo
Mwaka 2014 nilichaguliwa na kujiunga na stashahanda ya elimu ya msingi katika chuo cha Ualimu
Marangu,Kilichopo wilaya ya Moshi vijijini Mkoani Kilimanjaro .Baada ya hapo nilianza kutafuta uwezekano wa
kupata fomu ya maelezo ya kujiunga na mafunzo hayo ambapo taarfa hizo zilinishikiza na nilianza michakato
ya kupata pesa na hatimaye nilifanikiwa kupata kiasi kidogo baada ya kukusanya nguvu kwa muda mrefu na
hatimaye niliweza kupata nwezekano wa kulipoti katika chuo cha ualimu marangu
Baada ya kumaliza mafunzo ya ualimu mwaka 2011 nilirudi nyumbani kwetu wilaya maswa nilimkuta baba
yangu anaumwa sana kitu kilichonifanya niendelee kuungusa kwa muda mrefu kuanzia mwezi wa sita mwaka
2011 mpaka mwaka mwezi wa kumi na moja 2011,ambapo baba yangu kipenzi mungu alimpenda sana,kitu
kilichoniumwa sana baba yangu amnisomesha hata hajaonja mafanikio ya mwanae mpaka sasa nina mzazi
mmoja ambaye ni mama yangu anaishi katika kijiji cha kulimi kilichopo kata ya kulimi.
HALI YA NDOA
Mnamo mwaka 2008 baada kuhitimu mafunzo ya elimu ya sekondari baba mzazi alishauri nifanya maamuzi ya
busara kwani watumishi walio wengi wamekuwa na tabia ya kukaa muda mrefu .Nami nikaamua kutafuta
mchumba na nilipata mchumba wilaya ya shinyanga vijijini na mwaka 2011 nilifunga ndoa baada ya kuhitimu
Kama kielezo namba 2 na kwa sasa tuna watoto wawili wa kiume Godwin na Greyson
Mwaka 2014 mwezi wa tano niliomba kujiendeleza baada ya baraza la ufundi kutangaza nafasi za ualimu kwa
ngazi ya stahashahada ya elimu ya juu na nilifanya maombi hayo na baada ya hapo nilichanguiliwa na
stashahada ya elimu ya kawaida ya shule ya msingi katika chuo cha ualimu marangu kilichopo wilaya ya moshi
vijijini Mkoa wa Kilimanjaro kama kielelezo no 3 ni maeneo ya chuo cha Ualimu Marangu