15

1. - ushirikiano.or.tz WA UG WA MWAKA 2015-2016.pdf · 8.0 Mpango kazi wa Ushirikiano Group kwa mwaka wa fedha 2015/2016 Lengo Kazi Kipimo cha utekelezaji Muda wa utekelezaji J A

  • Upload
    others

  • View
    35

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

1

1. Utangulizi

Mpango ni utaratibu ambao mtu binafsi au kikundi cha watu

hujiwekea katika kutimiza malengo waliojiwekea kwa muda

waliokubaliana, mpango huwezesha kufikia malengo kwa kupita

njia sahihi. Sababu ya kuwa na Mpango kwa ufupi ni hizi

zifuatazo:-

a) Kuuweka umoja wetu (Ushirikiano) kuwa na dira na

mwelekeo.

b) Kuwawezesha wanachama kuupima utendaji wa viongozi

waliowaweka madarakani, hivyo kuongeza uwajibikaji.

c) Kuwawezesha wanaushirikiano kujua matarajio na jinsi ya

kufikia matarajio hayo.

d) Kuongeza ushirikishwaji wa wanaushirikiano katika

kupanga maendeleo yao.

Mpango huu umeandaliwa kwa kurejea mpango wa mwaka wa

fedha 2014/2015.

2. Dira na dhima (Vision and Mission statement)

a) Dira (Vision) yetu ni kuwa kikundi imara cha kijamii na

kiuchumi nchini Tanzania

b) Dhima (Mission) yetu ni kukuza ushirikiano katika mambo

ya Kijamii na Kiuchumi kwa kuunganisha nguvu zetu kwa

faida ya wanaushirikiano wote

2

3. Madhumuni ya Ushirikiano Group DSM Madhumuni ya umoja huu ni kusaidiana katika masuala ya kijamii na

kiuchumi.

4 Uchambuzi yakinifu wa Ushirikiano Group (swoc), yaani

Uimara, udhaifu,fursa na changamoto

4.1 Uimara

a) Kikundi kina wataalam wa fani mbalimbali, yaani

Wahandisi, Wahasibu, Wanasheria, Wajasiliamali na

Wafanyabiashara, WanaTEHAMA, Waalimu, Madaktari n.k.

b) Hakuna ubaguzi, upendeleo, ukabila au udini.

c) Wanachama wana malengo yanayofanana na ni marafiki

tayari.

d) Kuna uongozi imara na wenye lengo la kusonga mbele.

e) Kikundi kina mfuko wake.

f) Kikundi kina katiba na kanuni za uendeshaji.

4.2 Udhaifu

a) Tumekuwa na tabia ya kutotekeleza tunachokubaliana.

b) Tumekuwa hatuchukulii hatua wanaoturudisha nyuma.

c) Tumekuwa hatutunzi kumbukumbu za vikao na mikutano.

d) Tumekuwa wazito kuchukua maamuzi.

e) Tumekuwa tunavunjika moyo pale tunapoona mambo

hayaendi vizuri.

3

f) Tumekuwa na mahudhurio yasiyoridhisha kwenye

mikutano yetu na pengine tunachelewa sana bila sababu za

kueleweka.

g) Hatuna ofisi ya kikundi.

4.3 Fursa

a) Kuna fursa nyingi nchini zinazosaidia vikundi kama vya

kwetu.

b) Tunaweza kupata mikopo kama kikundi.

c) Kuna teknolojia ya habari na mawasiliano.

d) Kukutana (networking) na kuwa karibu zaidi miongoni mwa

wanachama.

e) Kufanya kazi kwa ubia (joint venture) miongoni mwa

wanachama.

f) Kuweza kupata bima ya afya.

g) Kuwa na uwekezaji.

4.4 Changamoto

a) Upungufu wa ajira

b) Wanaushirikiano kuwa na majukumu mengi katika kazi zao

na wengine katika masomo, kwa hiyo kukosa muda wa

kuhudhuria vikao.

c) HIV/AIDS bado ni tishio kwenye jamii pamoja na familia

zetu.

4

5 Tabia ya Kikundi (Core Values)

Hii itatutofautisha vikundi vingine na ushirikiano Group DSM.

a) Ushirikiano (Teamwork) – Kuwa na wanachama

wanaopenda ushirikiano, kuaminiana, maelewano na

kuheshimiana.

b) Uaminifu (Integrity)- kuwa na wanachama wakweli,

waminifu, watii wa sheria kanuni na taratibu.

c) Kutopendelea (Impartiality)- kuwa na wanachama wasio

wabaguzi wa aina yoyote.

d) Uwajibikaji (Accountability)- Kuwa na wanachama

wawajibikaji na wachapa kazi.

6.0 Utekelezaji wa malengo ya mwaka wa fedha 2014/2015

Kwa mwaka wa fedha 2014/2015, Ushirikiano Group DSM

ilitekeleza malengo iliyojiwekea kama ifuatavyo:

6.1 Kuwa na kikundi imara chenye mshikamano na

uwajibikaji

a) Wanachama kushiriki kwenye masuala ya kijamii

yanayomhusu mwanachama kwa mujibu wa katiba na

kanuni za UG.

Kipimo ni idadi ya wanaushirikiano wanaoshiriki kwenye

maswala ya kijamii. Kazi hii ilitekelezeka kwa 60%, watu

wamekuwa wakijitokeza kwenye masuala mbalimbali ya

5

kijamii yanayomhusu mwanachama, mfano misiba,

harusi/send off.

b) Wanachama kuhudhuria vikao vya kila mwezi.

Kipimo ni idadi ya wanaushirikiano kwenye mikutano ya

kila mwezi. Kazi hii imetekelezwa, wanachama

walihudhuria kwenye vikao vya kila mwezi kwa 50%.

c) Kuwa na wanachama wasiozidi familia 30.

Kipimo ni idadi ya wanaushirikiano kuongezeka. Kazi hii

imetekelezwa kwani wanachama wameongezeka kutoka

27 mwezi Juni, 2014 hadi wanachama 31 kwa sasa.

Wanachama waliridhia kuongeza mwanachama mmoja

zaidi.

d) Kufanya vikao vya kila mwezi majumbani kwa

wanachama.

Kipimo ni vikao vya kila mwezi kufanyikia majumbani

mwetu. Kazi imetekelezwa kwa 100%, vikao vinafanyika

majumbani mwa wanachama.

e) Kufanya sherehe ya Ushirikiano day.

Kipimo ni sherehe ya Ushikiano day kufanyika. Kazi

imetekelezwa kwa 100%, ushirikiano day ilifanyika.

f) Kutunga kanuni za Maadili na kurekebisha kanuni za

TEHAMA na Jamii.

Kipimo ni kikundi kuwa na kanuni za Maadili na kanuni

za TEHAMA na Jamii zilizorekebishwa. Kazi hii

imetekelezwa kwa 67%. Kanuni za Maadili zilitungwa,

6

kanuni za Jamii zilirekebishwa, bado kurekebisha kanuni

za TEHAMA.

g) Kuandaa ofisi ya kikundi.

Kipimo ni kikundi kuwa na ofisi. Kazi hii bado

haijatekelezwa.

6.2 Kuwa na uchumi imara na uwekezaji

a) Wanachama kulipa ada za kila mwezi za

uanachama.

Kipimo ni wanaushirikiano kulipa michango yao ya kila

mwezi kwa wakati. Kazi hii imetekelezwa kwa 32%,

wanachama bado wanadaiwa.

b) Kuimarisha mfuko wa uwekezaji.

Kipimo ni kila mwanaushirikiano kuchanga shilingi

1,500,000/=.

Kazi hii imetekelezwa kwa 20% tu, mpaka sasa ni

wanachama 7 tu ndiyo wamechangia. Kati ya hao, ni

watatu tu waliomaliza.

c) Kuanzisha shule ya awali.

Kipimo ni kununua kiwanja na kuanzisha shule ya awali.

Kazi hii bado haijatekelezwa kwa sababu wanaushirikiano

wengi hawajachanga michango ya mfuko wa uwekezaji.

d) Kukopesha wanachama.

Kipimo ni uwezo wa mwanachama kukopa na kulipa

mkopo pamoja na riba. Kazi hii imetekelezwa kwa 80%,

wanachama wamekopa na kurudisha mikopo na riba.

7

Tukijipima utekelezaji wa malengo hayo, lengo la “Kuwa na kikundi

imara chenye mshikamano na uwajibikaji” ndiyo

lililotekelezwa kwa ukamilifu na kuonyesha muelekeo mzuri

wa kikundi chetu. Ndiyo kusema kuwa kikundi chetu

kimefanikiwa zaidi upande wa “Kijamii”. Lakini lengo la “kuwa

na uchumi imara na uwekezaji” halijatekelezwa kwa kiwango

kikubwa, kwani kuna majukumu tuliyotakiwa kuyafanya ili

kutimiza lengo hilo hatukuyafanya. Kumbukeni kuwa na

uchumi imara ndiyo mhimili wa kusitawi kwa kikundi chetu.

7.0 Malengo ya mwaka wa fedha 2015/2016

Katika mwaka wa fedha 2015/2016 Ushirikiano Group DSM

inatarajia kutimiza malengo manne kama ifuatavyo:-

7.1 Kuwa na kikundi imara chenye uwajibikaji na

mshikamano (KAMATI YA JAMII)

a) Wanachama kushiriki kwenye masuala ya kijamii

yanayomhusu mwanachama kwa mujibu wa katiba na

kanuni za UG.

Kipimo ni idadi ya wanaushirikiano wanaoshiriki kwenye

maswala ya kijamii.

b) Wanachama kuhudhuria vikao vya kila mwezi.

Kipimo ni idadi ya wanaushirikiano kwenye mikutano ya

kila mwezi.

c) Kufanya sherehe ya Ushirikiano day.

8

Kipimo ni sherehe ya Ushikiano day kufanyika.

d) Kuandaa ofisi ya kikundi.

Kipimo ni kikundi kuwa na ofisi.

e) Kuwezesha wanachama kujiunga na Mfuko wa Bima ya

Afya (NHIF).

Kipimo ni idadi ya wanachama waliojiunga na Mfuko wa

Bima ya Afya.

7.2 Kuwa na uchumi imara na uwekezaji (KAMATI YA FEDHA

NA UCHUMI)

a) Wanachama kulipa ada za uanachama kiasi cha

shilingi 30,000/= kila mwezi.

Kipimo ni wanaushirikiano kulipa ada ya 30,000/= kila

mwezi kwa wakati.

b) Kuimarisha mfuko wa uwekezaji.

Kipimo ni kila mwanaushirikiano kuchanga shilingi

1,500,000/= ndani ya muda wa miezi kumi. Kila mwezi

shilingi 150,000/=.

c) Kununua kiwanja/eneo.

Kipimo ni kiwanja/eneo kununuliwa.

d) Kukopesha wanachama.

Kipimo ni uwezo wa mwanachama kukopa na kulipa

mkopo pamoja na riba kwa wakati.

Pamoja na kiwango cha kawaida cha mikopo, wanachama

waliowekeza kwenye “Uwekezaji Fund” watapewa

motisha ya nyongeza ya uwezo wa kukopa kwa 50% ya

kiwango walichochangia kwenye mfuko wa uwekezaji.

9

e) Kufanya semina ya ujasiriamali kwa wanachama.

Kipimo ni semina ya ujasiramali kwa wanachama kufanyika.

7.3 Kuwa na kikundi chenye mawasiliano imara na ya kisasa (KAMATI YA TEHAMA)

a) Kurekebisha kanuni za TEHAMA.

Kipimo ni kuwa na kanuni za TEHAMA zilizorekebishwa.

b) Kuhuisha tovuti ya UG kwa wakati.

Kipimo ni kuwa na tovuti iliyo hai kila wakati

C) Kuwaunganisha wanaushirikiano wote na mtandao wa mawasiliano.

Kipimo ni wanaushirikiano wote kuunganishwa kwenye mtandao wa mawasiliano.

7.4 Kuwa na wanachama wenye maadili mema (KAMATI YA MAADILI)

a) Kusimamia katiba na kanuni za UG.

Kipimo ni wanachama wote kutii katiba na kanuni za UG.

b) Kupokea na kujadili mashauri ya ukiukwaji wa maadili ndani ya UG.

Kipimo ni idadi ya mashauri yaliyojadiliwa.

c) Kupendekeza adhabu dhidi ya mwanaumoja anayekiuka katiba na kanuni za UG.

Kipimo ni idadi ya mapendekezo yaliyowasilishwa kwenye mamlaka za juu.

10

8.0 Mpango kazi wa Ushirikiano Group kwa mwaka wa fedha 2015/2016

Lengo Kazi Kipimo cha utekelezaji

Muda wa utekelezaji

J A S O N D J F M A M J

1 Kuwa na kiundi

imara chenye

mshikamano na

uwajibikaji

1.Wanachama kushiriki

kwenye masuala ya

kijamii yanayomhusu

mwanachama kwa

mujibu wa katiba.

Idadi ya

wanaushirikiano

wanoshirikia katika

masuala ya kijamii.

2. Wanachama kuhudhuria vikao vya kila mwezi

Idadi ya wanaushirikiano kwenye vikao vya kila mwezi.

3. Kufanya sherehe ya Ushirikiano day

Sherehe ya Ushirikiano day kufanyika

4. Kuandaa ofisi ya

kikundi.

Kikundi kuwa na ofisi.

5.Kuwezesha

wanachama

kujiunga na

Mfuko wa Bima

ya Afya (NHIF).

Idadi ya wanachama waliojiunga na Mfuko wa Bima ya Afya.

2 Kuwa na uchumi

imara na

uwekezaji.

1. Wanachama kulipa ada za kila mwezi za uanachama shilingi 30,000/=.

Ada za kila mwezi shilingi 30,000/= kulipwa kwa wakati.

2. Kuimarisha mfuko wa uwekezaji

Kila mwanachama kuchanga shilingi 1,500,000/=. Kila mwezi shilingi 150,000/= kwa miezi kumi.

3. Kununua kiwanja/eneo.

Kiwanja/eneo kununuliwa.

11

4. Kukopesha wanachama

Wanachama kukopa na kulipa mikopo pamoja na riba kwa wakati.

5.Kufanya semina ya ujasiriamali kwa wanachama.

Semina ya ujasiriamali kwa wanachama kufanyika.

3 Kuwa na kikundi

chenye

mawasiliano

imara na ya

kisasa.

1. Kurekebisha kanuni za TEHAMA.

Kuwa na kanuni za TEHAMA

zilizorekebishwa.

2. Kuhuisha tovuti ya UG kwa wakati.

Kuwa na tovuti iliyo hai kila wakati.

3. Kuwaunganisha wanaushirikiano wote na mtandao wa mawasiliano.

wanaushirikiano wote kuunganishwa kwenye mtandao

wa mawasiliano.

4. Kuwa na wanachama wenye maadili mema.

1. Kusimamia katiba na kanuni za UG

wanachama wote kutii katiba na kanuni za UG.

2. Kupokea na kujadili mashauri ya ukiukwaji wa maadili ndani ya UG.

Idadi ya mashauri yaliyojadiliwa.

3. Kupendekeza adhabu dhidi ya mwanaumoja anayekiuka katiba na kanuni za UG.

Idadi ya mapendekezo yaliyowasilishwa kwenye mamlaka za juu.

8 Hitimisho

Mwisho wa mwaka wa fedha, kikundi kitatathimini

utekelezaji wa mpango wake ili kuangalia mafanikio na

mapungufu yaliyojitokeza kwenye utekelezaji wake. Ni

12

matumaini yangu kwamba baada ya kupitisha mpango huu,

wanachama watashiriki kikamilifu kwenye utekelezaji wake ili

hatimaye kikundi chetu kiweze kufikia malengo tuliyojiwekea.

Kiambatanisho

Makadirio ya mapato na matumizi ya UG kwa mwaka wa fedha

2015/2016

13

1 MAPATO

Kiasi(Tsh)

A) Mfuko wa Ushirikiano (ushirikiano fund)

i) Fedha iliyopo (balance)

17,506,561.00

ii) Ada

10,979,000.00

iii) Malimbikizo ya ada

1,140,000.00

iv) Marejesho ya mikopo ya 2014/2015

5,132,500.00

Jumla ndogo

34,758,061.00

B) Mfuko wa uwekezaji (Uwekezaji Fund)

i) Fedha iliyopo

6,300,000.00

ii) Michango ya uwekezaji

40,200,000.00

iii) Faini

650,000.00

iv) Malimbikizo ya faini

478,000.00

iv) Riba

1,400,000.00

Jumla ndogo

49,028,000.00

Jumla kuu (A +B)

83,786,061.00

2 MATUMIZI A) Mfuko wa Ushirikiano (Ushirikiano Fund)

i) Matukio ya furaha

1,000,000.00

ii) Matukio ya huzuni

3,000,000.00

iii) Ada (mtandao)

350,000.00

iv) Mikopo

20,000,000.00

v) Vikao

600,000.00

vi) Steshenari /dharura/nauli

600,000.00

vii) Ushirikiano day

3,000,000.00

viii) Ada ya usajili

50,000.00

ix) Gharama pango la ofisi

3,600,000.00

x) Gharama za benki (bank charges)

100,000.00

xi) Semina

400,000.00

Jumla ndogo

32,700,000.00

B) Mfuko wa uwekezaji (Uwekezaji Fund)

i) Kiwanja/eneo

48,000,000.00

ii) Kupigika (Kusaidiana)

360,000.00

Jumla ndogo

48,360,000.00

14

Jumla kuu (A+B)

81,060,000.00

Bakaa (1-2)

2,726,061.00

Marejesho ya mikopo ya 2015/2016

15,000,000.00

Bakaa kuu Juni, 2016

17,726,061.00