30
SERIKALI YAWATAKA WATANZANIA WOTE KUSHIRIKI KATIKA KUIMARISHA UTAWALA BORA ILI KUTOA MCHANGO KATIKA MAENDELEO YA TAIFA uk.1 Mhe.Dkt. Mwanjelwa aelekeza kusimamisha mishahara ya waajiri na maafisa utumishi watakaowasilisha taarifa zisizo sahihi kwenye mfumo wa malipo ya mishahara (HCMIS)uk.10 Serikali yawataka wakuu wa idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu serikalini kusimamia vizuri rasilimaliwatu uk.5 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro Hutolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini , Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Barabara ya Mkalama, S.L.P 670, 40404,Dodoma, Barua Pepe:[email protected] Tovuti:www.utumishi.go.tz Toleo Na.9 Januari-Juni, 2019

UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

  • Upload
    others

  • View
    3

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

SERIKALI YAWATAKA WATANZANIA WOTE KUSHIRIKI KATIKA KUIMARISHA UTAWALA BORA ILI KUTOA MCHANGO KATIKA

MAENDELEO YA TAIFA uk.1

Mhe.Dkt. Mwanjelwa aelekeza kusimamisha mishahara ya waajiri na maafisa utumishi watakaowasilisha taarifa zisizo sahihi kwenye mfumo wa malipo ya mishahara (HCMIS)uk.10

Serikali yawataka wakuu wa idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu serikalini kusimamia vizuri rasilimaliwatu uk.5

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb)

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro

Hutolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ,Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,

Barabara ya Mkalama, S.L.P 670, 40404,Dodoma,Barua Pepe:[email protected]

Tovuti:www.utumishi.go.tz

Toleo Na.9 Januari-Juni, 2019

UTUMISHI News

Page 2: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

1.Serikali yawataka watanzania kuimarisha utawala bora..........................................................................1-2

2. Watendaji katika sekta ya umma watakiwa kujiepusha na mgongano wa maslahi ili kujenga uchumi imara wa taifa........3-4

3. Serikali yawataka Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini kusimamia Vizuri rasilimaliwatu.............................................................5

4. Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu serikalini watakiwa kuwatumikia watumishi wa umma wanaowasimamia ili kuwajengea ari ya utendaji kazi..6-7

5. TAKUKURU yaelekezwa kuweka mkakati madhubuti kupambana na rushwa kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa...............8

6.Ofisi ya Rais-Utumishi yakabidhi Kiwanja kwa TBA ili kuanza ujenzi wa ofisi................................................................9

7.Dkt. Mwanjelwa aelekeza kusimamisha mishahara ya waajiri na maafisa utumishi watakaowasilisha taarifa zisizo sahihi kwenye mfumo wa malipo ya mishahara (HCMIS) .............10-11

8. Serikali yawapongeza wanufaika wa miradi ya maendeleo mkoani iringa kwa kutumia vizuri fedha za miradi ya maendeleo kujikwamua kiuchumi..............12-13

9. Wakala wa Majengo Tanzania yatakiwa kumaliza kwa wakati ujenzi wa kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa cha kanda ya ziwa kinachojengwa Jijini Mwanza......13-14

10. Serikali yawapatia huduma ya usafiri wajane wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Tanzania, Hayati Alhaji Aboud Mwinyi Jumbe..........................15

11. Utumishi yaunga mkono kwa Vitendo kampeni ya Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa kijani kwa kupanda miti.............16

12. Serikali yawapandisha madaraja watumishi wa umma 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012........uk.17

13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Kilimanjaro watakiwa kutumia Vizuri fedha za ruzuku ili Kuboresha maisha yao.........18-19

14. Uzingatiaji wa maadili na nidhamu ya kazi ndio msingi na nyenzo ya utendaji kazi kwa watumishi wa umma nchini.20-21

15. Serikali yawataka watumishi wa umma wilayani Kilolo kuishi maeneo wanayofanyia kazi ili kutekeleza Majukumu yao ipasavyo..22

16. Watumishi wa Umma watakiwa kuwa tayari kufanya kazi mahali popote nchini ili kuwahudumia wananchi........... 23-24

17. Naibu Katibu Mkuu-UTUMISHI aomba ushirikiano kutoka kwa watumishi wa ofisi yake ili kufikia malengo ya Mhe.Rais ya kutoa huduma bora kwa wananchi..............25

18. Matukio katika picha..............................................26-27

Bodi ya Uhariri:

Dira

Dhamira

Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora (OR-MUUUB) kuwa Taasisi itakayowezesha kuwa na Utumishi wa Umma uliotukuka kwa kutoa huduma

bora kwa Umma na hivyo kuchangia katika kukuza uchumi, kupunguza umaskini na kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania

ifikapo mwaka 2025.

Kuhakikisha kuwa utumishi wa umma nchini unasimamiwa vizuri na kwa ufanisi kupitia usimamizi wa rasilimaliwatu, mifumo na

miundo ya kiutumishi

Dkt. Laurean NdumbaroDkt. Francis MichaelBi. Mary MwakapendaBw. James KatubukaBi.Happiness Shayo

YALIYOMO

CHUMBA CHA HABARI

uk.

Page 3: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

Serikali yawataka watanzania wote kushiriki katika kuimarisha utawala bora ili kutoa mchango katika maendeleo

ya taifa

Serikali imewataka watanzania wote kushiriki katika kuimarisha utawala bora nchini ili kutoa mchango wenye tija kwa maendeleo

ya taifa badala ya kuviachia jukumu hilo vyombo vinavyosimamia masuala ya utawala bora.

Wito huo ulitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika wakati akizindua maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa, jijini Dodoma.

Mhe. Mkuchika alisema, ili kuwa na utawala bora katika nchi yetu, watanzania wote wanahusika kwa maana ya wale waliopewa dhamana ya kusimamia utawala bora na wananchi wa kawaida, kwani wenye dhamana ya kusimamia utawala bora wanahitaji ushirikiano kutoka kwa wananchi ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Mhe. Mkuchika aliongeza kuwa, mtanzania wa kawaida anatakiwa abadilike kimtazamo

na kifikra kuhusu uzingatiaji wa maadili, nidhamu ya kazi, vita dhidi ya rushwa, haki za binadamu, uwazi na uwajibikaji, na kusisitiza kuwa mabadiliko haya yawe ndio utamaduni wa mtanzania wa kila siku.

Mhe. Mkuchika alifafanua kuwa, duniani kote, suala la utawala bora linapewa kipaumbele, kwasababu bila nchi kuwa na mfumo madhubuti wa maadili kuanzia ngazi ya familia haiwezi kufanikisha vita dhidi ya mmomonyoko wa maadili. Aidha, alitoa wito kwa watanzania wote nchini kuwa waadilifu ili kuwa mfano wa kuigwa na vizazi vijavyo.

Naye, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) aliwataka watanzania kuwa wazalendo kwa kutanguliza masilahi ya umma kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa alisema, kupitia kauli

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akisoma Kauli Mbiu ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa mara baada ya kuzindua rasmi siku hiyo jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).

1

Page 4: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu ya mwaka huu inayosema “Udhibiti wa Mgongano wa Masilahi-Nguzo Muhimu Kujenga Utawala Bora” ni vema kwa kila mtanzania kutanguliza masilahi ya umma mbele badala ya masilahi binafsi ili kufikia lengo la uchumi wa kati wa viwanda kama inavyohimizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa aliongeza kuwa, utekelezaji wa kauli mbiu hii ni muafaka kwasasa kwani taifa liko katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo ambapo uzalendo na uadilifu ni nguzo kuu itakayowezesha utekelezaji wa miradi hiyo.

Awali, akitoa neno la utangulizi, Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela alisema, maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa ni muhimu kwani yanahimiza na kutukumbusha kuzingatia misingi ya maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, mapambano dhidi ya rushwa hasa kwa watumishi wa umma ambao jukumu lao kubwa ni kutoa huduma kwa wananchi.

Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa huratibiwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sekretarieti

ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali, Tume ya Utumishi wa Umma, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, lengo likiwa ni kuhamasisha uadilifu, uwazi, uwajibikaji na utawala bora nchini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya

Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akizungumza na

wadau wa maadili na haki za binadamu wakati wa

uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa, jijini

Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakimkabidhi zawadi Mlezi wa Klabu ya Maadili wa shule ya Sekondari Dodoma, Mwalimu Marco Benedict Magwa, mara baada ya kuzindua maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa, jijini Dodoma. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Patrobas Katambi

2

Page 5: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

Viongozi, watumishi na wataalam mbalimbali nchini, wametakiwa

kujiepusha na mgongano wa maslahi kwa kutotumia nyadhifa zao au ofisi zao kujinufaisha wao wenyewe, kuwanufaisha ndugu zao au jamaa zao na watu wengine ili waweze kutekeleza wajibu wao ipasavyo katika ujenzi wa uchumi imara wa taifa.

Wito huo ulitolewa na Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman wakati akifungua mjadala kwenye maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa, jijini Dodoma.

Mhe. Othman alisema, mgongano ya maslahi ni lazima udhibitiwe kwa nguvu zote

kwani unailetea sifa mbaya serikali, taasisi, idara na sekta binafsi ambazo mgongano wa maslahi unajitokeza, na kuongeza kuwa unamletea pia sifa mbaya ya kiutendaji kiongozi au mtumishi kwenye fani au taaluma aliyobobea.

Mhe. Othman aliainisha njia za kuweza kuepukana na mgongano wa maslahi, njia hizo ni kujiuzulu au kujitoa endapo kiongozi anaona kuna maslahi binafsi kwenye jambo atakalolitolea maamuzi kwa ajili ya kulinda maslahi ya umma.

Mhe. Othman alisisitiza kuwa, ni jukumu la mtendaji mwenyewe kutamka mapema, kukiri kwa hiari na kwa uwazi kwamba ana mgongano wa maslahi kwenye suala

atakaloenda kulitolea maamuzi badala ya kungoja kuambiwa ajiuzulu na kushutumiwa kuwa na mgongano wa maslahi kwenye suala aliloshiriki kutoa maamuzi. Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika alisema, moja kati ya mambo ambayo ofisi yake inapambana nayo ni kuhakikisha inaondoa uwezekano wa kuwepo kwa mgongano wa maslahi katika taasisi za umma.

Mhe. Mkuchika alifafanua kuwa, kiongozi au mtumishi yeyote katika sekta ya umma hatakiwi kufanya biashara na taasisi yake kwasababu kuna uwezekano mkubwa

Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,

Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakifuatilia mada wakati wa mjadala kwenye maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa, uliofanyika jijini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela.

Watendaji katika sekta ya umma watakiwa kujiepusha na mgongano wa maslahi ili kujenga uchumi imara wa taifa

3

Page 6: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

wa kupendelea kampuni yake kuipatia zabuni na kuiongezea malipo ili aweze kujinufaisha na hatimaye kuitia hasara serikali.

Aidha, Mhe. Mkuchika alitoa wito kwa washiriki wa mjadala kuhakikisha wanatoa maoni na mapendekezo ambayo yataondoa changamoto ya mgongano wa maslahi katika sekta ya umma.

Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alisema, viongozi na watumishi ambao wanasimamia maadili wanapaswa kuyaisha yale wanayoyasema, na ni muhimu pia ni wajibu wao kuonyesha njia katika uzingatiaji wa maadili ili wanapohubiri maadili mema wawe na ushawishi kwa umma.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa aliongeza kuwa, vitendo vya mmomonyoko wa maadili vinatakiwa kukemewa bila kusita wala kuonewa haya kuanzia kwenye ngazi ya familia ili kujenga taifa lenye uadilifu.

Mada zilizojadiliwa katika mjadala huo ni pamoja na, Mgongano wa masilahi katika utumishi wa umma, Ulinzi wa haki za binadamu na mgongano wa maslahi na matumizi mabaya ya madaraka yanayopelekea mgongano wa maslahi na uwepo wa rushwa nchini.

Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akifungua mjadala kwenye maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za

Binadamu Kitaifa, jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi ya

Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma

na Utawala Bora, Bw. Fabian Pokela akitoa

mchango wa Idara yake katika

ukuzaji wa maadili kwenye sekta ya

umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akizungumza na

washiriki wa mjadala kwenye maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa, kabla ya kumkaribisha Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania,

Mhe. Mohamed Chande Othman kufungua rasmi mjadala huo jijini Dodoma.

4

Page 7: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

Serikali imewataka Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika

Taasisi za Umma nchini kuhakikisha rasilimaliwatu inasimamiwa vizuri ili kuwezesha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Wito huo ulitolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) kinachofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.

Dkt.Ndumbaro alisema kuwa, rasilimaliwatu ikisimamiwa vibaya matokeo yake ni

kushuka kwa utendaji kazi, na utendaji kazi ukishuka unasababisha uchumi wa nchi kutokukua inavyotakiwa, hivyo Taifa kushindwa kufikia lengo lake la kutoa huduma bora kwa wananchi.

Dkt.Ndumbaro aliwasisitiza Wakurugenzi wanaosimamia rasilimaliwatu katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala na Mashirika ya Umma kuwa taasisi zote za Umma zifanye kazi kwa pamoja ili kutekeleza vipaumbele vya Taifa.

Aidha, Dkt.Ndumbaro aliwakumbusha Wakuu hao

wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu kuzingatia maadili katika utendaji kazi ili wawe mfano wa kuigwa na watumishi wengine.

Naye aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Dorothy Mwaluko aliwaasa watendaji hao kuwa washauri wazuri, walezi bora, walimu wazuri na watatuzi wa changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wanaowasimamia ili wawe na tija katika maendeleo ya Taifa.

Bi. Mwaluko aliwataka Watendaji hao kuhakikisha wanasimamia vema nidhamu ya watumishi wa umma ili kujenga taswira nzuri ya utumishi wa umma.

Mkutano kazi huo wa Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma ulilenga kuwakumbusha na kuwahimiza watendaji hao utekelezaji wa masuala mbalimbali ya kiutendaji, uendeshaji na usimamizi wa rasilimaliwatu kwa kuzingatia malengo,shabaha na vipaumbele vya kitaifa.

Serikali yawataka Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu serikalini kusimamia vizuri rasilimaliwatu

Baadhi ya Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu wakimsikiliza aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Dorothy Mwaluko (hayupo pichani) wakati akiwasilisha mada kuhusu Wajibu na Majukumu ya Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika kikao kazi cha watendaji hao kinachofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akiongoza kikao kazi cha Wakuu wa Idara za

Utawala na Rasilimaliwatu kinachofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma. Kushoto ni

aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Dorothy Mwaluko.

5

Page 8: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

6

Wakuu wa Idara za Utawala na R a s i l i m a l i w a t u

kutoka katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma wametakiwa kuhakikisha wanawahudumia vema watumishi wanaowasimamia ili kuwajengea ari ya utendaji kazi kwa watumishi hao.

Wito huo ulitolewa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko wakati akifunga kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu serikalini kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro kilichofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.

Bi. Mwaluko aliwasisitiza Watendaji hao, kutojifanya miungu watu na badala yake wawahudumie watumishi wote

kwa kuzingatia weledi, kauli nzuri na bila chuki ya aina yoyote.

Bi. Mwaluko aliwaelekeza watendaji hao, kuwahudumia vizuri Watanzania hususani wanyonge kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anavyosisitiza mara kwa mara.

Naye, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,

Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari, alisema mkutano huo ulikuwa na lengo la kuwaelimisha watendaji hao masuala ya kiutawala na usimamizi wa rasilimaliwatu ili waweze kutimiza majukumu yao kikamilifu kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya kiutumishi.

Dkt.Ndumbaro aliongeza kuwa, kupitia mkutano huo serikali imewasisitiza viongozi hao kuwajibika ipasavyo kwa umma na kwa watumishi walio chini yao.

Aidha, Dkt.Ndumbaro aliwataka viongozi hao kuwaelimisha watumishi wa umma walio chini yao kuhusu umuhimu wa kudai risiti pindi wanapofanya manunuzi ili kuiongezea serikali mapato yatakayoiwezesha kuongeza mishahara na kuboresha

Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu serikalini watakiwa kuwatumikia watumishi wa umma wanaowasimamia ili kuwajengea ari ya utendaji kazi

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi.Dorothy Mwaluko akizungumza na Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu waliohudhuria kikao kazi kilichofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.

Page 9: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

7

maslahi ya watumishi wa umma.

Sanjari na hayo, Dkt. Ndumbaro aliwashauri watumishi wa umma nchini kujiendeleza katika kada walizoingilia katika utumishi wa umma ili elimu watakayoipata iwe na manufaa kwao na tija katika utumishi wa umma.

Mkutano kazi huo ulihusisha jumla ya washiriki 456 kutoka katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma ambao walipata fursa ya kujifunza masuala mbalimbali ya kiutendaji, uendeshaji na usimamizi wa rasilimaliwatu kwa kuzingatia malengo,shabaha na vipaumbele vya kitaifa.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati mstari wa mbele), akifuatilia moja ya mada zilizowasilishwa katika kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu kilichofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.Kushoto kwake ni aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Dorothy Mwaluko na kuli kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma Bw.Mathew Kirama.

Baadhi ya Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu serikalini wakimsikiliza aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Dorothy Mwaluko (hayupo pichani) wakati akifunga kikao kazi cha watendaji hao kilichofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.

Page 10: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

8

Serikali imeiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)

kuweka mkakati na mbinu mpya za kisasa za kuhakikisha kuwa wanadhibiti vitendo vya rushwa katika kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa ili kupata viongozi waliochaguliwa kwa haki bila rushwa.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa watumishi wa TAKUKURU nchini uliofanyika katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa, jijini Dodoma.

Mhe. Mkuchika alisema wakati wa kipindi cha uchaguzi kunakuwa na malalamiko yanayotolewa na baadhi ya wagombea na wananchi kuhusu uwepo wa vitendo vya rushwa hivyo ni jukumu la TAKUKURU kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unakuwa huru na wa haki.

Aidha, Mhe. Mkuchika aliipongeza TAKUKURU kwa kushinda kesi kwa kiwango kikubwa, na kuokoa fedha za umma katika kipindi cha mwaka 2017/2018.

Mhe. Mkuchika aliainisha kuwa katika kipindi cha mwaka 2017/2018 TAKUKURU

imeshinda kesi 178 kati ya kesi 296 zilizoamuliwa mahakamani na kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 70.3 zilizokuwa ziingine kwenye mifuko ya mafisadi wanaolihujumu taifa letu.

Mhe. Mkuchika alifafanua kuwa, mara baada ya

TAKUKURU kupata taarifa za ubadhirifu wa fedha za umma,

ilifuatilia na kubaini taratibu za malipo zikiendelea, hivyo

iliingilia kati kuzuia malipo hayo batili yasifanyike.

Mhe. Mkuchika alisema, serikali inazitumia fedha hizo zilizookolewa kuboresha huduma za kijamii hususan za afya kwani zimewezesha kununua vifaa tiba na

dawa katika hospitali zetu.

TAKUKURU yaelekezwa kuweka mkakati madhubuti utakaodhibiti vitendo vya rushwa katika kipindi cha

uchaguzi wa serikali za mitaa

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU uliofanyika katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa, jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakiwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU uliofanyika katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa, jijini Dodoma.

Page 11: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

9

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

imekabidhi kiwanja kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ili wakala hiyo ianze ujenzi wa Ofisi katika Mji wa Serikali jijini Dodoma.

Akikabidhi kiwanja hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Musa Joseph alisema ujenzi wa Ofisi hiyo ni muendelezo wa utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais, Dkt John Pombe Magufuli ya kuhamishia shughuli za Serikali Makao Makuu ya nchi Dodoma.

Bw. Joseph alifafanua kuwa, kiwanja kilichokabidhiwa kina ukubwa wa ekari 5.7 na kuwataka TBA kuanza ujenzi mara moja ili kuwawezesha watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuwahudumia wananchi wakiwa katika mji wa Serikali.

Bw. Joseph aliongeza kuwa, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora tayari imeshaingiza fedha kwenye Akaunti ya Wakala wa Majengo Tanzania kiasi cha shilingi 700, 000,000/= ili kuiwezesha TBA kuanza ujenzi na kuongeza kuwa nia ya kufanya malipo mapema ni kuwezesha ukamilishaji wa ujenzi kwa wakati.

Akipokea kiwanja hicho, Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania mkoani Dodoma, Mhandisi David H. Shunu a l i i s h u k u r u Ofisi ya Rais, Menej iment i ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kuiamini TBA na kuahidi kukam i l i s h a ujenzi wa ofisi hizo kwa wakati na kwa kiwango bora.

Naye, Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Peter Mabale aliitaka TBA kufanya mawasiliano haraka iwezekanavyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pindi kunapotokea changamoto yoyote itakayokwamisha shughuli ya ujenzi badala ya kusubiri vikao ili kutatua changamoto hizo.

Makabidhiano ya Kiwanja hicho yalifanyika baada ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro na aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania, Arch. Elius Mwakalinga kusaini mkataba wa ujenzi wa Ofisi hizo Novemba 22, 2018 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli la kuhamishia Shughuli za Serikali makao makuu ya nchi Dodoma.

Ofisi ya Rais-Utumishi yakabidhi kiwanja kwa TBA ili kuanza ujenzi wa ofisi katika mji wa serikali jijini Dodoma

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph akiwasisitiza Wataalam wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kukamilisha ujenzi wa ofisi kwa wakati katika Mji wa Serikali ili iweze kutumika kuwahudumia wananchi.

Kaimu Mkurugezi wa Huduma za Ushauri wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Dodoma, akiahidi kutimiza jukumu lake ili kuhakikisha ujenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora unakamilika kwa wakati katika Mji wa Serikali uliopo Ihumwa jijini Dodoma.

Page 12: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

10

Mishahara ya Waajiri na Maafisa Utumishi w a t a k a o b a i n i k a

kuwasilisha taarifa za kiutumishi zisizo sahihi kupitia Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara Serikalini (HCMIS) itasimamishwa mara moja na Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, Ofisi Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kuwakumbusha waajiri na maafisa hao kuhakikisha wanawasilisha taarifa sahihi na kwa wakati.

Hayo yalisemwa jijini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipokutana na watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji na kufahamu vema majukumu ya idara hiyo.

Ili kuimarisha nidhamu ya utendaji kazi, Mhe. Dkt. Mwanjelwa aliwataka watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini kutosita hata mara moja kusimamisha mshahara wa mwajiri au afisa utumishi yeyote atakaebainika kuwasilisha taarifa zenye udanganyifu na kuwataka kutozifanyia kazi na kuzirejesha mara moja kwa waajiri na maafisa hao.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa aliainisha kuwa, lawama nyingi zimekuwa

zikielekezwa Ofisi ya Rais-Utumishi hata kosa linapokuwa kwa waajiri, hivyo aliwataka waajiri wote nchini kuhakikisha wanatenda haki kwa kuwasilisha taarifa sahihi na kwa wakati ili ziweze kufanyiwa kazi.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa alihoji kuwa, inawezekanaje mtumishi wa umma kukatwa mshahara wake kwa madai ya kukopa kwenye taasisi ya kifedha wakati hajakopa? na ni kwanini mtumishi husika asiarifiwe na mwajiri au afisa utumishi juu ya makato hayo?

Mhe. Dkt. Mwanjelwa alieleza kuwa, kuna uwezekano wa baadhi ya waajiri na maafisa utumishi kushiriki katika mchezo mchafu wa kutumia mishahara ya watumishi kujinufaisha, hivyo alisisitiza watakaobainika wachukuliwe hatua za kinidhamu, kisheria na kusimamishiwa mishahara

yao pale inapobidi, lengo likiwa ni kurejesha nidhamu ya kazi na kuimarisha uwajibikaji katika Utumishi wa Umma.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa alihuzunishwa na kitendo cha watumishi wa umma kudai malimbikizo ya mishahara ya muda mrefu wakati maafisa utumishi wanaowahudumia wapo, na amehoji uhalali wa uwepo wao wakati malalamiko mengi kuhusu malimbikizo ya mshahara (arreas) yamekuwa yakiendelea kuwasilishwa kwa wingi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kuchelewa, hivyo aliwataka kuwajibika ipasavyo ili kupunguza malalamiko hayo.

Naye, Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, Ofisi Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kamishna Msaidizi wa Polisi

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasimaliwatu katika Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora alipoitembelea idara hiyo jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.

Dkt. Mwanjelwa aelekeza kusimamisha mishahara ya waajiri na maafisa utumishi watakaowasilisha taarifa zisizo sahihi kwenye

mfumo wa malipo ya mishahara (HCMIS)

Page 13: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

11

(ACP) Ibrahim B. Mahumi alisema kuwa, majukumu ya msingi ya Idara hiyo ni kuimarisha uwajibikaji na ufanisi katika usimamizi wa rasilimaliwatu, kuratibu malipo ya mishahara ya watumishi wa umma kupitia Mfumo wa Malipo ya Mshahara (HCMIS) na kuhakikisha utumishi wa umma nchini unakuwa na watumishi wenye sifa stahiki.

ACP Mahumi aliainisha kuwa, Idara ina sehemu kuu tatu zinazotekeleza majukumu, ambazo ni eneo la usimamizi wa rasilimaliwatu, eneo la Usimamizi wa Orodha ya Malipo ya Mishahara (Payroll) na eneo la Uhakiki wa Rasilimaliwatu na Malipo ya Mshahara na kuongeza kuwa, kazi kubwa ya eneo la Usimamizi wa Rasilimaliwatu

ni kuandaa Ikama na Bajeti ya Mishahara ya Serikali.

ACP Mahumi alifafanua kuwa, pia Idara yake ina jukumu la kutoa vibali vya ajira mpya na mbadala Serikalini, kuhakiki uhalali wa sifa za watumishi wa umma wanaoajiriwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma na kuidhinisha taarifa hizo pamoja na nyingine za kiutumishi na mishahara zinazowasilishwa na waajiri kwa usahihi kupitia Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara Serikalini (HCMIS).

Kuhusu utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Mhe. Dkt. Mwanjelwa, (ACP) Mahumi alithibitisha kuwa, Idara yake itatekeleza na tayari imeshaanza kuchukua

hatua kwa kuwasimamishia mishahara maafisa utumishi zaidi ya 56 walioshindwa kutekeleza wajibu wao, na watumishi wengine zaidi ya 500 wenye dhamana ya kufanya kazi kwenye Mfumo wamefikishwa kwenye vyombo vya kisheria kwa makosa mbalimbali yanayohusu kuchezea mfumo ikiwa ni pamoja na baadhi ya waajiri waliohusika.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) aliitembelea Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Utawala Bora ili kuhimiza uwajibikaji.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasimaliwatu katika Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (hawapo pichani) alipoitembelea idara hiyo jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.

Page 14: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

12

Serikali imewapongeza wanufaika wa miradi ya maendeleo mkoani Iringa

hususani akina mama kwa kutumia vizuri fedha za miradi ya maendeleo wanazozipata kwa kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa sera ya uchumi wa viwanda.

Pongezi hizo zilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) wakati akikagua miradi ya maendeleo ya Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF), Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) katika kata za Gangilonga, Kihesa

na Igumbilo mkoani Iringa.

Mhe. Mkuchika alisema, fedha za miradi zimekuwa zikitolewa

kwa akina mama na vijana lakini akina mama wamekuwa wakijiongeza zaidi kwa kidogo wanachokipata na kufanya mambo ya maendeleo kama vile ufugaji, ushonaji, usindikaji wa vyakula, ujenzi wa nyumba,

kununua sare za shule za watoto, shajala na kufanya mambo mengine ya maendeleo yanayowawezesha kujikwamua kiuchumi.

“Nawapongeza sana akina mama kwani pamoja na fedha kidogo za miradi mnazozipata lakini mmekuwa mkifanya shughuli mbalimbali za ujasiliamali na kuongeza thamani ya bidhaa mnazozalisha ambazo z i n a w a o n g e z e a kipato mambo.” Mhe. Mkuchika ameongeza.

Aidha, Mhe. Mkuchika aliwataka vijana

nchini kuiga mfano wa akina mama wanavyojishughulisha na masuala ya ujasiliamali ili waweze kubadilisha maisha yao na kuwa na tija kwa maendeleo ya taifa.

Katika hatua nyingine, Mhe. Mkuchika alikabidhi hati tatu (3) za umiliki wa ardhi kwa wananchi wa Kata ya Igumbilo, hati hizo ni miongoni mwa hati 59 zilizo tayari kukabidhiwa kwa wananchi wa kata hiyo ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa Urasimishaji Ardhi Manispaa ya Iringa.

Aliongeza kuwa Serikali imerahisisha utoaji wa hati hizo za umiliki wa ardhi kupitia MKURABITA ili wananchi waweze kupata fursa ya kukopa katika taasisi za kifedha kwani hati

Serikali yawapongeza wanufaika wa miradi ya maendeleo mkoani Iringa kwa kutumia vizuri fedha za miradi ya

maendeleo kujikwamua kiuchumi

“Nawapongeza sana akina mama kwani

pamoja na fedha kidogo za miradi mnazozipata

lakini mmekuwa mkifanya shughuli mbalimbali za

ujasiliamali na kuongeza thamani ya bidhaa

mnazozalisha ambazo zinawaongezea kipato.”

-Mhe.Mkuchika.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akiangalia moja ya bidhaa iliyotengenezwa na mnufaika wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) wa kikundi cha Pamoja, kata ya Gangilonga mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo yenye lengo la kuzungumza na watumishi wa umma na kutembelea miradi inayotekelezwa na taasisi zilizo chini ya ofisi yake.

Page 15: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

13hizo zinatambulika kisheria.

Mhe. Mkuchika aliwasifu wakazi wa kata hiyo kwa hatua nzuri ya urasimishaji wa ardhi kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia mali zao kutambuliwa na kuwawezesha kupata mitaji kupitia mikopo hiyo.

Jumla ya viwanja 1,287 vimepimwa katika kata ya Igumbilo mitaa ya Mlangali na Igumbilo kupitia utekelezaji wa mradi wa MKURABITA.

Mhe. Mkuchika alifanya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Iringa kwa lengo la kuzungumza na Watumishi wa Umma na kutembelea utekelezaji wa miradi ya Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF), Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania

(MKURABITA) ambapo aliweza kujionea shughuli mbalimbali

za maendeleo zinazotekelezwa na wanufaika wa miradi hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akikabidhi hati ya umiliki wa ardhi kwa mmoja wa wanufaika wa mradi wa MKURABITA, kata ya Igumbilo mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo yenye lengo la kuzungumza na watumishi wa umma na kutembelea miradi inayotekelezwa na taasisi zilizo chini ya ofisi yake.

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imetakiwa kukamilisha

kwa wakati mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa cha Kanda ya Ziwa uliopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.

Wito huo, ulitolewa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko wakati wa ziara ya kikazi kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.

Bi. Mwaluko aliitaka Wakala hiyo kuhakikisha inakamilisha ujenzi kwa wakati ili kuiwezesha Serikali kukusanya, kuchambua, kutunza na kuhifadhi kumbukumbu mbalimbali kutoka katika Taasisi za Umma zilizopo kanda ya Ziwa kwa lengo la kulinda urithi andishi na historia ya Taifa letu.

Bi. Mwaluko aliielekeza Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa kuzungumza na Wakala wa Majengo Tanzania na kukubaliana tarehe rasmi ambayo jengo litakuwa limekamilika ili taarifa hiyo

itolewe kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa iliyopanga kutembelea kituo hicho hivi karibuni kwa lengo la kujiridhisha na ujenzi uliofanyika.

Naye, Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin M. Msiangi alisema, kituo hicho kitakapokamilika kitakuwa ni kitovu cha mafunzo ya namna bora ya utunzaji wa Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa katika kanda ya Ziwa kwa watumishi wa umma na wanafunzi wa vyuo wanaosoma masuala ya utunzaji wa

Wakala wa Majengo Tanzania yatakiwa kumaliza kwa wakati ujenzi wa kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa cha

Kanda ya Ziwa kinachojengwa Jijini Mwanza

Page 16: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

14kumbukumbu na nyaraka.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mkoani Mwanza, Bi. Doreen Swai alisema ili kukamilisha ujenzi kwa ubora unaotakiwa, TBA inategemea kukabidhi kituo hicho mwakani mwezi Februari, 2019.

Serikali katika bajeti ya fedha mwaka 2018/19, iliiidhinishia Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jumla ya shilingi 2,000,000,000/= za kitanzania ili kukamilisha ujenzi wa kituo kitakachokuwa na uwezo wa kuhifadhi makasha (archival boxes) 15,000 ya kumbukumbu

tuli yenye uwezo wa kubeba jumla ya majalada 150, 000 kwa wakati mmoja. Aidha, kituo kitatumika kama kituo mbadala cha Mifumo ya TEHAMA ya kuhifadhi kumbukumbu iliyopo katika Kituo cha Taifa cha Kumbukumbu Dodoma.

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko akitazama ramani ya mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza wakati wa ziara ya kikazi kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko akitoa maelekezo ya kuboresha ujenzi wa Kituo cha kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakati wa ziara ya kikazi kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza na Wataalam wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mara baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Kanda ya Ziwa wakati wa ziara ya kikazi kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.

Page 17: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

15

Serikali imewapatia huduma ya usafiri wa gari wajane wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Hayati Alhaji Aboud Mwinyi Jumbe ikiwa ni sehemu ya kutekeleza Sheria ya Mafao ya Hitimisho la Kazi kwa Viongozi wa Kisiasa Na. 3 ya mwaka 1999 na Marekebisho yake ya mwaka 2005 inayoelekeza utoaji wa stahili kwa wajane wa viongozi wa Kitaifa Wastaafu.

Akikabidhi gari hilo kwa wajane hao jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) alisema licha ya kuwa ni utekelezaji wa sheria lakini pia ni sehemu ya kuuenzi mchango wa wastaafu katika ujenzi wa taifa letu.

Mhe. Mkuchika alifafanua kuwa, kwa mujibu wa sheria hiyo, stahili za wajane kwa viongozi wa

Kitaifa Wastaafu ni pamoja na malipo ya

pensheni, malipo ya posho ya matunzo ya kila mwezi, gharama za matibabu katika hospitali zilizomo nchini na kupatiwa huduma ya usafiri.

A k i z u n g u m z i a mchango wa Hayati Alhaji Aboud Mwinyi Jumbe, Mhe. Mkuchika alisema, alikuwa ni kiongozi mahiri, jasiri na mchapakazi aliyeweza kutuliza m a c h a f u k o yaliyowahi kutokea Zanzibar na amefanya kazi

ya kuwaunganisha watanzania.

Kwa upande wake, mmoja wa mke wa Hayati Alhaji Aboud Mwinyi Jumbe, Bi. Zeyana Rashid aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuihudumia familia hiyo kwa kuipatia mahitaji yote muhimu.

Ziara za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt. (Mst) George H. Mkuchika (Mb) kuwatembelea wastaafu ilikuwa ni mwendelezo wa kuwajulia hali viongozi wa Kitaifa Wastaafu kwa lengo la kuboresha huduma wanazopatiwa na Serikali.

Serikali yawapatia huduma ya usafiri wajane wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Tanzania, Hayati Alhaji Aboud Mwinyi

Jumbe

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akikabidhi funguo ya gari kwa wajane wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Alhaji Aboud Mwinyi Jumbe, Bi.Zeyana Rashid (kushoto) na Bi. Fatma Mohammed Hassan (kulia) jijini Dar es Salaam.

Page 18: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

16

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeunga mkono kwa vitendo kampeni iliyozinduliwa na

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa kijani kwa kupanda miti katika ofisi yake inayojengwa Ihumwa jijini Dodoma kwenye mji wa serikali.

Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro mara baada ya watumishi wa ofisi yake kukamilisha zoezi la upandaji wa miti katika mji wa serikali Ihumwa, eneo ambalo Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inajengwa ili kutoa huduma kwa umma.

Dkt. Ndumbaro alisema kuwa, zoezi la upandaji wa miti katika eneo hilo ni endelevu na kuongeza kuwa, Ofisi yake itahakikisha miti hiyo inatunzwa kwa kuimwagilia maji ili hatimaye kuwe na mandhari ya kijani pindi ofisi yake itakapokamilisha ujenzi wa jengo kubwa.

Naye, mmoja wa watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Menyeaichi Koka

aliongeza kuwa, watumishi wa Ofisi ya Rais - Utumishi wameitikia wito wa Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan wa kupanda miti ili kulifanya jiji la Dodoma kuwa kijani na kuishukuru menejimenti ya ofisi kwa kusimamia vema zoezi hilo ambalo kila mtumishi amelifanya kwa hiyari na kwa moyo mkunjufu.

Bi. Koka aliahidi kuwa, atahakikisha mti alioupanda anauhudumia vizuri kwa kuumwagilia maji ya kutosha ili uweze kustawi vizuri na kuwa ni miongoni mwa miti iliyopandwa na kufanikiwa kukua vizuri na hatimaye kuchangia jiji la Dodoma kuwa kijani.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alizindua kampeni za kulifanya jiji la Dodoma kuwa kijani Julai 21, 2017 kwa kuongoza

zoezi la upandaji wa miti ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kwa vitendo uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wa kuhamishia shughuli za serikali makao makuu ya nchi jijini Dodoma.

Utumishi yaunga mkono kwa vitendo kampeni ya Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kulifanya Jiji la Dodoma

kuwa kijani kwa kupanda miti

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza kuhusu ofisi yake kuunga mkono kwa vitendo kampeni ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa la kijani iliyozinduliwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan mara baada ya watumishi wa ofisi yake (hawapo pichani) kukamilisha zoezi la upandaji miti katika ofisi inayojengwa Ihumwa kwenye mji wa serikali jijini Dodoma.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakiwa tayari kupanda miti katika ofisi inayojengwa Ihumwa kwenye mji wa serikali jijini Dodoma ili kuunga mkono kwa vitendo kampeni ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa la kijani, iliyozinduliwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan Julai 21,2017.

Page 19: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

17

Serikali imewapandisha madaraja watumishi wa umma 113,520

walioajiriwa mwaka 2012 katika awamu tatu, ambapo ya kwanza walipandishwa vyeo Watumishi 28,049 waliokuwa wameidhinishiwa vyeo kabla ya zoezi la uhakiki wa watumishi hewa na uhakiki wa vyeti kuanzia mwezi Juni, 2016, awamu ya pili ilianza mwezi Novemba, 2017 na ilihusisha watumishi 59,967 ambao taarifa zao zilikuwa kwenye Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) kabla ya zuio na awamu ya tatu ilianza mwezi Aprili, 2018 na ilihusisha Watumishi 25,504 ambao barua zao zilikuwa hazijaingizwa kwenye Mfumo.

Ufafanuzi huo, ulitolewa Bungeni na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) wakati akijibu swali la Mhe. Joram Hongoli (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililohusu watumishi wa umma walioajiriwa 2012 kutopandishwa madaraja mpaka hivi sasa.

Dkt. Mwanjelwa alisema, watumishi walioajiriwa Mwaka 2012 walistahili kupandishwa madaraja kuanzia mwaka 2016/2017 kipindi ambacho Serikali ilikuwa ikifanya zoezi la uhakiki wa watumishi

hewa na uhakiki wa vyeti, hivyo mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Serikali ilianza kuwapandisha watumishi hao kwa awamu

hizo tatu kwa kuzingatia vigezo stahiki na kuongeza kuwa watumishi wengine ambao wamekidhi vigezo wataendelea kukasimiwa katika bajeti ya mishahara ili waweze kupandishwa vyeo katika mwaka huu wa fedha 2018/2019.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa aliainisha kuwa, watumishi 31,188 walioajiriwa na TAMISEMI mwaka 2012, kati ya hao watumishi 15,320 wamepandishwa vyeo na kubadilishiwa mishahara, na watumishi 3,349 waajiri wao wamewapandisha vyeo lakini

majina yao yapo UTUMISHI kwa ajili ya kupitia taarifa zao kabla ya kuwabadilishia mishahara na watumishi 1,064 waliopandishwa vyeo

wamebainika kuwa na hoja mbalimbali ambazo waajiri wanapaswa kuzikamilisha na kurejesha majina yao UTUMISHI kwa ajili ya kuwaidhinishia mishahara, watumishi 4,552 hawapo tena katika Utumishi wa Umma na watumishi 6,903 bado hawajapandishwa vyeo ambapo Serikali inatarajia kuwapandishwa vyeo wakati wowote katika mwaka huu wa fedha 2018/19.

Suala la upandishwaji vyeo kwa Watumishi wa Umma linazingatia vigezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na utendaji kazi mzuri, kukidhi sifa zilizoainishwa katika Miundo ya Maendeleo ya Utumishi, uwepo wa nafasi wazi na bajeti iliyotegwa.

Kwa mujibu wa Miundo ya Maendeleo ya Utumishi, mtumishi anapaswa kutumikia cheo kimoja si chini ya miaka mitatu kabla hajafikiriwa kupandishwa cheo. Aidha, iwapo mtumishi ameajiriwa kwa mara ya kwanza atapaswa kumaliza mwaka mmoja wa kuthibitishwa kazini kisha ndipo atumikie cheo hicho si chini ya miaka mitatu, hivyo kwa kuzingatia sifa mtumishi anaweza kupandishwa cheo baada ya miaka 3, 4, 5 au hata saba kutegemea na kukidhi vigezo stahiki.

Serikali yawapandisha madaraja watumishi wa umma 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akijibu swali la Mhe. Joram Hongoli (Mb) Bungeni , kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililohusu upandishwaji wa madaraja kwa watumishi wa umma walioajiriwa mwaka 2012.

Page 20: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

18

Serikali imewataka wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya

maskini mkoani Kilimanjaro kutumia vizuri fedha za ruzuku zinazotolewa na Serikali ili kuondokana na umaskini na hatimaye kuboresha maisha yao.

Wito huo ulitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) alipowatembelea wanufaika wa Mpango wa

Kunusuru Kaya Maskini katika Halmashauri za Wilaya ya Same na Mwanga mkoani Kilimanjaro ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Mhe. Mkuchika alifurahi kuona wanufaika wametumia

vizuri fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Njoro wilayani Same na kijiji cha Kileo wilayani mwanga kwa kujenga nyumba bora za kuishi, kuwanunulia watoto mahitaji muhimu ya shule ikiwa ni pamoja na kujishughulisha na ufugaji wa mbuzi, kondoo, kuku na bata.

Mhe. Mkuchika aliguswa na jitihada za wanufaika wawili katika kijiji cha Njoro Bi. Salome Athumani na Bw. Jumanne Muhamed Idafu na kuwapatia msaada wa

fedha taslimu za kitanzania shilingi 300,000/= ili waweze kukamilisha ununuzi wa bati za kuezekea nyumba zao walizozijenga kupitia fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, sanjali na hao, Mhe. Mkuchika alimpatia msaada

wa fedha taslimu za kitanzania shilingi 200,000/= Bi. Safiyuna Hasani wa kijiji cha Kileo ili aweze kumsomesha vema mwanae mwenye ulemavu wa ngozi (albino) na kumnunulia mahitaji muhimu.

Mhe. Muchika alisisitiza kuwa, Serikali ina lengo la kuhakikisha inawasajili wananchi wote wenye sifa ya kunufaika na fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika vijiji vyote nchini, na kuongeza kuwa mpaka sasa Serikali imefanikiwa

kuwafikia wanufaika wa mpango kwa asilimia sabini tu.

Kwa upande wa wanufaika, Bi. Salome Athumani mkazi wa kijiji cha Njoro, alimshukuru Mhe. Mkuchika kwa msaada wa kifedha aliompatia na

Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Kilimanjaro watakiwa kutumia vizuri fedha za ruzuku ili

kuboresha maisha yao

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na wananchi na wanufaika wa fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Njoro wilayani Same (hawapo pichani) katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi mkoani Kilimanjaro, yenye lengo la kufanya ufuatiliaji wa maendeleo ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini.

Page 21: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

19

Serikali kwa ujumla kupitia Mpango wake wa Kunusuru Kaya Maskini uliomuwezesha kutimiza ndoto yake ya ujenzi wa nyumba na kujishughulisha na ufugaji wa mbuzi na kuku.

Naye, Bi. Salima Abdallah Mzirai mkazi wa kijiji cha Kileo, alishukuru uwepo wa fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini zilizomuwezesha kupata matibabu ya kiafya, kukarabati nyumba yake, kujenga choo, kufuga kuku na kulima bustani.

Aidha, mkazi mwingine wa kijiji hicho, Bw. Daudi Hassan Kalili aliishukuru Serikali kumnufaisha na fedha za mpango z i l i z o m u w e z e s h a kuachana na maisha ya kuishi kwenye nyumba ya nyasi na kuanza shughuli ya ufugaji wa kuku.

Jumla ya kaya maskini 144 katika kijiji cha Njoro wilayani Same zimenufaika na fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kiasi

cha shilingi 91,280,000/= ikiwa ni pamoja na shilingi 1,705,843/= za usimamizi wa mpango,na kaya maskini 197 katika kijiji cha Kileo wilayani Mwanga zimenufaika na shilingi 132,719,000/= pamoja na shilingi 2,287,386/= za usimamizi wa mpango.

Lengo la ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,

Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) mkoani Kilimanjaro, ni kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama tawala ya mwaka 2015 katika eneo la kupambana na umaskini nchini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na mmoja wa wanufaika wa fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, Bi. Salome Athumani wa kijiji cha Njoro wilayani Same mara baada ya kutoa msaada wa fedha kwa mnufaika huyo katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi mkoani Kilimanjaro, yenye lengo la kufanya ufuatiliaji wa maendeleo ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini.

Baadhi ya wananchi na wanufaika wa fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Kileo wilayani Mwanga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya waziri huyo mkoani Kilimanjaro, yenye lengo la kufanya ufuatiliaji wa maendeleo ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini

Page 22: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

20

Watumishi wa umma nchini wametakiwa kuzingatia maadili na nidhamu ya kazi kwani ndio

msingi na nyenzo kuu itakayowawezesha kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipokutana na watumishi wa Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais, M e n e j i m e n t i ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa lengo la kufahamu m a j u k u m u ya idara hiyo na kuhimiza u w a j i b i k a j i .

Mhe. Dkt. M w a n j e l w a alisema, maadili mema kwa watumishi wa umma ndio kitovu cha utumishi wa umma hivyo ameitaka Idara ya Ukuzaji Maadili kuhakikisha watumishi wa umma wanazingatia misingi ya maadili mema na nidhamu katika utendaji ili waweze kutoa huduma bora na kwa wakati kwa wananchi.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa alifafanua kuwa mtumishi wa umma akiwa na maadili mema, utendaji kazi wake utaimarika pia utii, heshima na adabu vitaongezeka hivyo atakuwa mchapakazi hodari na anayezingatia weledi.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa aliongeza kuwa, mtumishi wa umma anatakiwa ajitambue katika mwenendo wake, azingatie mavazi ya heshima mahala pa kazi, awe na lugha nzuri yenye staha kwa wateja ili awe kioo na mfano mzuri wa kuigwa katika jamii.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa aliisisitiza Idara ya Ukuzaji Maadili kutengeneza mkakati madhubuti wenye ubunifu utakaowezesha kutoa elimu ya maadili kwa umma ili jamii itambue umuhimu wa maadili mema mahala pa kazi, na ameongeza kuwa Idara hiyo iweke utaratibu wa kuzitambua Taasisi na watumishi wa umma wanaozingatia maadili ya kazi kwa kuwapa tuzo lengo likiwa ni kuwapa motisha ya utendaji kazi.

Mhe. Dkt. M w a n j e l w a aliainisha kuwa, watumishi wa umma wakiwa waadilifu na w a z a l e n d o , wa taweze sha k u p u n g u z a malalamiko ya wananchi dhidi ya huduma zinazotolewa na Taasisi za Umma.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa aliitaka Idara hiyo kuunga mkono jitihada za Rais wa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa vitendo katika kuhimiza uadilifu na uwajibikaji kwa watumishi wa umma nchini ili utumishi wao uwe na tija katika maendeleo ya Taifa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Maadili, Bw. Fabian Pokela alisema kuwa, majukumu ya Idara hiyo yamegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni Ukuzaji Maadili katika utumishi wa umma na Ufuatiliaji wa Uzingatiaji wa Maadili katika utumishi wa umma sanjari na ushughulikiaji wa malalamiko ya wananchi yanayohusu ukiukwaji wa maadili katika Utumishi wa Umma.

Bw. Pokela alifafanua kuwa, jukumu la sehemu ya Ukuzaji Maadili ni kuhakikisha kuwa watumishi wa umma na wananchi kwa

Uzingatiaji wa maadili na nidhamu ya kazi ndio msingi na nyenzo ya utendaji kazi kwa watumishi wa umma nchini

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora alipoitembelea idara hiyo kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.

Page 23: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

21

ujumla wanapata uelewa kuhusu maadili ya utumishi wa umma kupitia kampeni za uhamasishaji, maonesho mbalimbali, vipeperushi, majarida mbalimbali, semina, warsha, mikutano na mafunzo ya muda mfupi.

Bw. Pokela alisema Idara yake pia imeandaa vipindi vya redio na televisheni vitakavyotoa elimu kwa umma juu ya maadili mema mahala pa kazi na kuhimiza uadilifu kwa Watendaji Wakuu wa Taasisi na mtumishi wa umma mmoja mmoja.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) aliitembelea Idara ya Ukuzaji

Maadili ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika Idara na Vitengo vya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kuhimiza uwajibikaji.

Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Fabian Pokela (kulia) akifafanua majukumu ya Idara yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) alipoitembelea idara hiyo kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.

Baadhi ya watumishi wa Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakipokea maelekezo kutoka kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) alipoitembelea idara hiyo kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.

Page 24: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

22

Serikali imewataka Watumishi wa Umma katika Halmashauri ya

Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kuishi maeneo wanayofanyia kazi yaani katika wilaya hiyo kwa lengo la kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi katika mkoa wa Iringa.

Mhe. Mkuchika alisema kuna baadhi ya watumishi wameajiriwa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo lakini wanaishi Iringa mjini jambo ambalo ni kinyume na taratibu za kiutumishi na pia linasababisha watumishi hao kutokuwa makini katika utendaji kazi wao.

Mhe. Mkuchika alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kilolo kuhakikisha ifikapo Januari, 2019 wote wawe wameshahamishia makazi yao katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo na asiyefanya hivyo atakuwa amejifukuzisha kazi.

“Ninatoa muda wa miezi miwili kwa watumishi hao kuweka makazi yao Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo haraka iwezekanavyo na asiyetaka aandike barua ya kuacha kazi,” Mhe. Mkuchika alisisitiza.

Mhe. Mkuchika aliongeza kuwa lengo la Serikali la kutaka Kilolo kuwa Makao Makuu ya Halmashauri ni kuwawezesha wananchi kupata huduma bora na kwa wakati.

Mhe. Mkuchika alihitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Iringa ambayo ililenga kuzungumza na watumishi wa umma, kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi, pamoja na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na taasisi zilizo chini ya ofisi yake.

Serikali yawataka watumishi wa umma wilayani Kilolo kuishi maeneo wanayofanyia kazi ili kutekeleza majukumu yao

ipasavyo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na watumishi wa umma wilayani Kilolo wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Iringa yenye lengo la kuwasikiliza, kupokea changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi ili kuboresha utumishi wa umma na kuongeza tija katika kuwahudumia wananchi

Baadhi ya watumishi wa umma wilayani Kilolo wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kwa lengo la kuwasikiliza, kupokea changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi ili kuboresha utumishi wa umma na kuongeza tija katika kuwahudumia wananchi.

Page 25: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

23

Watumishi wa umma wametakiwa kuwa tayari kufanya kazi mahali popote na katika mazingira

yoyote nchini ili waweze kuwahudumia wananchi ambao ndio walengwa wakuu wa huduma zinazotolewa na Taasisi za Umma.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipokutana na watumishi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa lengo la kufahamu majukumu ya Idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa alisema, kitendo cha watumishi wa umma kuwa tayari kufanya kazi mahali popote na katika mazingira yoyote bila kujali maslahi binafsi kinaashiria uzalendo kwa Taifa na kinatoa haki kwa wananchi katika maeneo yote hususan ya pembezoni kupata huduma bora wanayostahili.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa aliitaka Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma kutorubuniwa na baadhi ya watumishi na waajiri wanaoomba vibali vya uhamisho kwa maslahi binafsi hivyo kuathiri utoaji huduma kwa umma.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa aliongeza kuwa, Idara hiyo

inatakiwa kujiridhisha na hoja zinazowasilishwa kuombea vibali vya uhamisho kama hoja hizo zina tija na manufaa katika maendeleo ya Taifa.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa alisisitiza kuwa, watanzania wote wana haki sawa ya kupata huduma bora bila kujali mazingira waliyopo hivyo, ni wajibu wa Idara hiyo kuhakikisha kuwa uhamisho wa watumishi hauathiri mahitaji ya huduma kwa wananchi.

Awali, akielezea majukumu ya idara yake, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Bw. Mathew Kirama alisema, Idara hiyo ina Sehemu ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Sehemu ya Watumishi Waandamizi na Sehemu ya Huduma na Ushauri wa Kisheria ambazo kwa pamoja zinalenga kufanikisha uendeshaji wa utumishi wa umma kwa kuwezesha Taasisi za Serikali kupata watumishi wenye sifa na weledi unaohitajika kulingana na malengo yanayotekelezwa na Taasisi hizo.

Bw. Kirama alifafanua kuwa, idara hiyo ina jukumu la kutoa ushauri wa kitaalamu kwa waajiri na watumishi kuhusu sera, sheria, kanuni na nyaraka mbalimbali za masuala ya ajira katika Utumishi wa Umma, kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala ya sheria ikiwa ni pamoja na kusimamia taratibu mbalimbali zinazotawala utumishi wa umma.

Watumishi wa umma watakiwa kuwa tayari kufanya kazi mahali popote nchini ili kuwahudumia wananchi

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisisitiza uwajibikaji kwa watumishi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (hawapo pichani) alipoitembelea idara hiyo kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.

Page 26: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

24

Akizungumzia suala la uhamisho, Bw. Kirama alisema, katika kuleta tija na ufanisi kwenye utumishi wa umma, watumishi wa umma wanaruhusiwa kuhama ikiwa wamezingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo likiwemo sharti la kukaa kwenye kituo kimoja cha kazi si chini ya miaka mitatu na uwepo wa nafasi iliyotengewa fedha kwenye kituo husika.

Aidha, Bw. Kirama alieleza kuwa, Serikali inaweza kumhamisha mtumishi kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma katika maeneo

yenye upungufu wa watumishi.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) aliitembelea Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika Idara na Vitengo vya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kuhimiza uwajibikaji.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora alipoitembelea idara hiyo kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza

uwajibikaji.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Mathew Kirama (wa pili kutoka kulia) akifafanua majukumu ya Idara yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (kulia) alipoitembelea idara hiyo kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.

Page 27: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

25

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael

ameomba kupewa ushirikiano na watumishi wa ofisi yake ili kuhakikisha huduma bora inatolewa kwa wadau na wananchi.

Dkt. Michael alisema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya kuripoti ofisini kwake jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.

Dkt. Michael alisema, watumishi wa ofisi yake wana uelewa mkubwa kuhusiana na masuala ya kiutumishi hivyo, ushirikiano atakaoupata utamsaidia kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kutimiza malengo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwahudumia wananchi.

Aidha, Dkt. Michael aliipongeza menejimenti ya Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuwahudumia

watumishi wa umma nchini.

Dkt. Michael aliongeza kuwa, kazi ya kuwahudumia watumishi ni ngumu sana lakini Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekuwa ikifanya vizuri sana na hii imejidhihirisha pale alipopata huduma inayostahili kupitia wawakilishi aliokuwa akiwaagiza mara kwa mara.

Dkt. Michael aliitaka menejimenti ya ofisi hiyo kuendelea kutoa ushirikiano kwake kama ilivyokuwa ikifanya kwa

Naibu Katibu Mkuu aliyepita ili kufikia malengo ya Mheshimiwa Rais.

Naye, Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Bw. Priscus Kiwango akitoa neno la shukrani kwa niaba ya menejimenti ya Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, aliahidi kutoa ushirikiano mzuri na kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kuwahudumia wananchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alimteua Dkt. Francis K. Michael kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, tarehe 08 Januari, 2019 na kumuapisha tarehe 09 Januari, 2019. Dkt. Michael amechukua nafasi ya Bi. Dorothy Mwaluko ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji).

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael akisalimiana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na

Ugavi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Peter Mabale mara baada ya kuripoti ofisini kwake jijini Dodoma leo kwa ajili ya kuanza

kazi rasmi.

Naibu Katibu Mkuu-UTUMISHI aomba ushirikiano kutoka kwa watumishi wa ofisi yake ili kufikia malengo ya Mhe. Rais ya

kutoa huduma bora kwa wananchi

Page 28: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

MATUKIO KATIKA PICHA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakionyeshwa mipaka ya kiwanja na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro ya eneo linalojengwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akifafanua jambo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Cleopa D. Msuya alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akimtunuku cheti Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James baada ya kuhitimu kozi fupi ya tano ya Viongozi iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na familia ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marehemu Dkt. Omar Ali Juma alipowatembelea nyumbani kwao, jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam kumjulia hali.

26

Page 29: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

MATUKIO KATIKA PICHA

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akimtunuku cheti mmoja wa wahitimu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) wakati wa mahafali ya 29 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri , Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akihimiza usimamizi mzuri wa Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) kwa Mkurugenzi wa Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini, Bw. Hassan Kitenge, alipoitembelea Idara hiyo kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Mathias Kabunduguru, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi akimkabidhi nyaraka za kiutendaji Mkurugenzi wa Sera, Bi Agnes Meena wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Utumishi.

Baadhi ya watumishi wa umma mkoani Iringa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kwa lengo la kuwasikiliza, kupokea changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi ili kuboresha utumishi wa umma na kuongeza tija katika kuwahudumia wananchi.

Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Mathias Kabunduguru, (hayupo pichani) ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Utumishi.

27

Page 30: UTUMISHINewsbahidc.go.tz/storage/app/uploads/public/5c6/d03/acd/5c6d03acd8e... · 113,520 walioajiriwa tangu mwaka 2012.....uk.17 13. Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

utumishiweek Ofisi ya Rais UtumishiOfisi ya Rais Utumishiutumishiweek

Tovuti:www.utumishi.go.tz