15
Bulletin News Ofi si ya Mawasiliano Serik alini inapoke a ha bari z a matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bul lettin hii na Jarida la Wizar a ya Nishati na Madini Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Osi y a Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected] http://www.mem.go.tz HABARI ZA NISHATI &MADINI  To le o No. 34 Limesambazwa kw a Taas is i na Id ar a zo te MEM  Ta rehe - Se pt emba 19-25, 20 14 Mtambo wa mfano wa kuchakata dhahabu wazinduliwa Geita - Uk 4  S o ma  U k .  2 n Wadau waridhishwa Mradi wa Umeme nWashirika wa Maendeleo wapongeza hatua iliyofikiwa nMwenyekiti CCM Dar: Watanzania tunaweza tukiamua nMeck Sadik: miundombinu itunzwe Mtambo wa kuzalisha umem e ambao ni miongoni mwa mitambo itakayotum iwa katika kuzalisha ki asi cha megawati 150 katika Mradi wa Kinyerezi I jijini Dar es Salaam. Kinyerezi I

34a

Embed Size (px)

Citation preview

  • BulletinNews

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

    Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    http://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI &MADINI

    Toleo No. 34 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - Septemba 19-25, 2014

    Mtambo wa mfano wa kuchakata dhahabu wazinduliwa Geita -Uk4

    Soma Uk. 2n Wadau waridhishwa Mradi wa Umeme nWashirika wa Maendeleo wapongeza hatua iliyofikiwanMwenyekiti CCM Dar: Watanzania tunaweza tukiamua nMeck Sadik: miundombinu itunzwe

    Mtambo wa kuzalisha umeme ambao ni miongoni mwa mitambo itakayotumiwa katika kuzalisha kiasi cha megawati 150 katika Mradi wa Kinyerezi I jijini Dar es Salaam.

    Kinyerezi I

  • 2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (wa kwanza kulia) akiwaongoza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik (katikati), Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida (kulia kwa Katibu Mkuu) na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa, wakati wakitembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi I na Kituo cha kupokea gesi.

    Makundi mbalimbali ya wadau wa maen-deleo hapa nchini wakiwemo Wa-shirika wa Maendeleo, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mkoa wa Dar es Salaam na Uongozi wa Serikali ya Mkoa huo, wali-otembelea Mradi wa kuzalisha Umeme wa Kinyerezi I na kituo cha kupokea Gesi, wameeleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo.

    Wadau hao waliotembelea Miradi husika kwa nyakati tofauti hivi karibuni, walisema wamefari-jika kuona Miradi inatekelezwa kwa kasi na viwango vya hali ya juu.

    Mkurugenzi Mkaazi wa Ben-ki ya Dunia anayesimamia nchi za Tanzania, Uganda na Burundi, Philippe Dongier, akizungumza kwa niaba ya washirika wa maen-deleo alieleza kuwa, wameri-dhishwa na hatua ambazo miradi hiyo imefikia na kupongeza jitiha-da za Serikali kuhakikisha kwam-ba inafanyia kazi changamoto ya upatikanaji umeme wa uhakika Tanzania.

    Aidha, Dongier aliitaka Seri-kali kushirikiana na wadau katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya umeme ili iweze kufikia lengo lake la kuhakikisha Tanzania inazalisha umeme wa kiasi cha megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025.

    Kwa upande wake Mwenyeki-ti wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida alisema ni jambo la kutia moyo kwamba wataalamu wazalendo ndiyo wanaosimamia miradi hiyo inayokwenda kwa kasi na yenye ubora wa viwango vya kimataifa.

    Hakika Watanzania tunaweza tukiamua, alisema Madabida na kuongeza kuwa uw-ezo huo wanaouonesha Wataal-amu wazalendo ni matunda ya elimu nzuri waliyopatiwa na Wiz-ara ya Nishati na Madini.

    Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik alitumia fursa hiyo kuwaasa wa-nanchi wote kuachana na tabia ya kutokujali miundombinu mbal-imbali inayojengwa kwa gharama kubwa na matokeo yake inaha-ribika mapema na kusababisha hasara kubwa.

    Alitoa rai kwa kila mwananchi kwa nafasi yake kuhakikisha ana-linda na kutunza miundombinu ya bomba la gesi linalojengwa na Serikali ili linufaishe nchi kama Serikali ilivyokusudia.

    Ninatoa wito wa kulinda bomba hili kwa gharama yoyote

    vinginevyo kazi yote iliyofanyika itakuwa ni bure, alisisitiza Mkuu wa Mkoa.

    Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati makundi hayo ya wadau yalipotembelea kituo cha kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 150 na kituo cha kupokea gesi katika eneo la Kiny-erezi jijini Dar es Salaam, Ka-tibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi alieleza kuwa, Wizara imeona ni jambo la msingi kwa wadau hao kutembe-lea miradi hiyo ili kujionea hatua mbalimbali ambayo miradi hiyo imefikia.

    Aidha, Maswi aliongeza kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, imedhamiria kuleta mabadiliko ya kiuchumi kupitia sekta ya nishati hususani kupitia gesi asilia na kuongeza kuwa, hakuna kinachoshindikana hivyo, miradi hiyo inatarajiwa kukamilishwa kwa wakati kama ilivyopangwa.

    Akizungumzia kuhusu fedha za ujenzi wa kituo cha kinyerezi I na ujenzi wa vituo vingine vya kinyerezi II, III na IV, Katibu Mkuu Maswi alieleza kuwa, fed-ha za ujenzi wa Mradi wa Kiny-erezi I zimetolewa na Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanza-nia (TANESCO).

    Kuhusu ujenzi wa Kinyerezi II alieleza kuwa, fedha itatokana na ubia kati ya Serikali ya Tan-zania na Japani wakati ujenzi wa Kinyerezi III na IV fedha zitato-kana na ubia kati ya Serikali na kampuni ya Kichina.

    Kwa mujibu wa Meneja Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Gesi kutoka Shirika la maende-leo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mhandisi Kapuulya Musomba, ameeleza kuwa, ujenzi wa kituo cha kupokea gesi cha Dar es Salaam umekamilika kwa asil-imia 60. Naye Meneja Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha kuzalisha Umeme cha Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Saimoni Jilima ameeleza kuwa, ujenzi wa kituo hicho umekamilika kwa asilimia 70.

    Washirika wa Maendeleo wal-iotembelea miradi hiyo ni pamoja na Benki ya Dunia, GIZ, US-AID, MCC, JICA, UNDP, Korea Exim Bank, Benki ya Maende-leo ya Afrika(ADB), DFID na Umoja wa Ulaya. Vilevile Balozi mbalimbali ziliwakilishwa katika ujumbe huo zikiwemo Ubalozi wa Sweden, Ubalozi wa Norway, Ubalozi wa Ujerumani na Uba-lozi wa Ufaransa.

    Umeme Kinyerezi Asteria Muhozya na Veronica Simba, Dar es Salaam

    Meneja wa Ujenzi wa Miradi ya Uzalishaji ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Simon Jilima akitoa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi I kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik (katikati), Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida (kushoto kwa Mkuu wa Mkoa) na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mkoa huo. Pamoja nao ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (Kulia kwa Madabida).

  • 3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    TahaririMEM

    Na Badra Masoud

    FIVE PILLARS OF REFORMS

    KWA HABARI PIGA SIMU KITENGO CHA MAWASILIANO

    BODI YA UHARIRI MHARIRI MKUU: Badra Masoud

    MSANIFU: Essy OgundeWAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson Mwase

    Teresia Mhagama, Nuru Mwasampeta

    INCREASE EFFICIENCYQUALITY DELIVERY

    OF GOODS/SERVICESATISFACTION OF

    THE CLIENTSATISFACTION OF

    BUSINESS PARTNERS

    SATISFACTION OF SHAREHOLDERS

    TEL-2110490FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Nishati na Madini ni kazi kwenda mbele!!!!

    TEL-2110490FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Teresia Mhagama

    Imeelezwa kuwa Tanzania imeshika nafasi ya kwanza katika nchi zinazo-vutia uwekezaji katika nchi za Afrika Mashariki na kushika nafasi ya tisa barani Afrika.

    Hayo yamesemwa na Balozi wa Australia kwa nchi za Afrika Mashariki, Geoff Tooth wakati akihitimisha Maone-sho ya Kimataifa ya Madini yaliyofanyi-ka Perth, Australia yajulikanayo kama Africa Down Under (ADUC) ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kutoa fursa kwa nchi za kiafrika zenye utajiri wa madini ikiwemo Tanzania kutangaza fursa za uwekezaji katika sekta ya madini ili ku-vutia wawekezaji kutoka sehemu mbal-imbali duniani.

    Balozi Tooth alitumia fursa hiyo kuiasa Tanzania kuendeleza juhudi za kuvutia uwekezaji nchini kwa kuweka mazingira wezeshi ikiwemo kuwa na mundombinu madhubuti ya barabara, bandari, reli, kuboresha upatikanaji wa umeme na kuwa na sera na sheria zi-sizobadilika mara kwa mara.

    Akizungumzia kuhusu mafanikio ya ushiriki wa Tanzania Katika maone-sho hayo ya siku tatu yaliyoshirikisha nchi mbalimbali duniani, Kamishna wa Madini, Wizara ya Nishati na Madini, Eng. Paul Masanja ameeleza kuwa Tan-

    zania ilipata upendeleo wa kipekee katika maonesho hayo kwani mnamo tarehe 4 Septemba mwaka huu, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Eng Ngosi Mwihava alipata nafasi ya kutoa mada mahsusi kuhusu fursa za uwekezaji katika sekta ya madini hapa nchini.

    Aliongeza kuwa, tarehe 5 Septemba mwaka huu, Tanzania ilipangiwa muda maalum wa kueleza kwa undani kuhusu fursa zilizopo katika sekta ya madini nchini (Tanzania Investment Forum), pamoja na kukutana ana kwa ana na wawekezaji wenye nia ya kuja kuwekeza nchini.

    Kupitia fursa hiyo, Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava, ulipata fursa ya kueleza masuala mbalimbali ikiwemo historia ya Tanzania, maendeleo ya sekta ya madini, vivutio mbalimbali vya uwekezaji, pamoja na miradi ambayo inaweza kuendelezwa kwa ubia kati ya wawekezaji hao na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO). Alieleza Kamishna.

    Mbali na kupata muda maalum wa kutoa mada katika mikutano iliyokuwa ikienda sambamba na maonesho hayo, Kamishna wa Madini ameeleza kuwa, wataalam katika banda la Tanzania, walikuwa wakitoa elimu na taarifa

    mbalimbali ikiwemo sera ya madini ya mwaka 2009, sheria na kanuni zinazosi-mamia sekta hiyo, madini yapatikanayo Tanzania, tafiti za kijiolojia na mashapo yaliyopo Tanzania, pamoja na huduma za kijiolojia zinazotolewa na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST).

    Watalaam wetu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, GST, STAMICO, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanza-nia (TMAA) pia walikuwa wakitangaza miradi ambayo STAMICO inahitaji wawekezaji wenza, walitangaza shughuli za maabara ya kisasa ya TMAA, taar-ifa mpya za kijiolojia zilizokusanywa na GST, walikutana ana kwa ana na wawekezaji kwa maana ya kupata ufa-hamu zaidi kuhusu masoko na mitaji na vilevile walipata fursa ya kujifunza jinsi nchi nyingine za kiafrika zinavyosimam-ia sekta ya madini. Alisisitiza Mhandisi Masanja.

    Maonesho hayo ya Kimataifa ya ADUC yaliyoanzishwa rasmi mwaka 2003, yalikutanisha zaidi ya washiriki 2000 kutoka sehemu mbalimbali duniani na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri wa Madini kutoka baadhi ya nchi za Kiafrika na Australia, maafisa waandamizi wa madini wa nchi hizo, wataalam kutoka taasisi za fedha duniani, wawekezaji, na watoa huduma kwenye sekta ya madini.

    Tanzania Kidedea kuvutia uwekezaji

    Wiki hii Washirika wa Maendeleo walitembelea Ujenzi unaoendelea wa mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia wa Kinyerezi I, halikadhalika kituo cha kupokea gesi hiyo ili kuona maendeleo ya ujenzi wa vituo vyote vi-

    wili.Kama msemo usemao kwa kimombo to see is to believe,

    kuona ndiyo kuamini, basi kwa washirika wetu wa maendeleo ndivyo ilivyokuwa kwani hawakuamini macho yao kwa kuona kasi ya ujenzi unaoendelea si ya kawaida.

    Kwa mtu ambaye amezoea kufanya kazi kwa mazoea akija Wizara ya Nishati na Madini atapata taabu na atashindwa kue-ndana na kasi inayoendelea ya utendaji kwani ni lazima kila mtumishi kwa nafasi yake atekeleze majukumu yake kwa vi-tendo na awe na kasi kubwa.

    Kasi ya utendaji huu umejengwa na viongozi wa Wizara waliopo wakiongozwa na Kiranja Mkuu ambaye si mwingine Mhe. Prof. Sospeter Muhongo Waziri wa Nishati na Madini ambaye kila kukicha anataka kuona mabadiliko na maendeleo makubwa katika sekta ya Nishati na Madini.

    Kwa hakika kazi kubwa inafanyika katika sekta hizi mbili kwani hata washirika wetu wa Maendeleo kama nilivyoeleza waliridhika na kasi hiyo na kusema utendaji wa Wizara unawa-pa moyo na kwamba wataendelea kushirikiana na Serikali na wataendelea kusaidia sekta hizi mbili.

    Lakini kikubwa ni kupata ushirikiano kwa kila Mtanzania ili tuweze kuendeleza sekta hizi mbili ambazo ndiyo zimebeba uchumi wa taifa letu kwa namna moja ama nyingine kwani un-apozungumzia umeme ninaamini unagusa maisha ya kila mmo-ja wetu halikadhalika, madini hakuna asiyeelewa thamani yake na kwamba ikisimamiwa vizuri itakuza pato letu kitaifa.

    Ni ukweli usiopingika na mwenye macho haambiwi tazama vilevile na mpenda maendeleo yeyote atakuwa ameona mabadi-liko makubwa yanayoendelea kufanyika katika Wizara ya Ni-shati na Madini pamoja na taasisi zake.

    Mabadiliko hayo ya kiutendaji yanayoendelea yameanza kuipa heshima kubwa Wizara ya Nishati na Madini na kuwa Wizara ya kuigwa au ya mfano kwani kila mmoja wetu lazima atimize wajibu wake kwa vitendo na kazi lazima ionekane na ikamilike kwa wakati jambo linalofanya hata wadau wetu mbal-imbali nao kufuata nyayo hizo.

    Mathalan katika sekta ya madini anayeomba leseni kwa sasa anapewa leseni kabla ya siku mbili kupita na vilevile kuanzia sasa kila anayeomba leseni ya utafutaji na uchimbaji madini ataomba kwa njia ya mtandao na wale wote waliokwisha ku-pewa leseni siku za nyuma wataonekana kwenye mtandao iwe mchimbaji mdogo, wa kati ama mkubwa.

    Hali kadhalika na kwenye sekta ya nishati mambo ni hivyo hivyo, kila anayeomba umeme ataunganishwa ndani ya siku 30 ama chini ya hapo na marufuku kutoa rushwa kwani atakaye-bainika kuomba au kupokea rushwa kwa ajili ya kuunganisha umeme hataachwa. Bila kusahau kuwa, mgawo wa umeme ul-iokuwa kilio cha Watanzania, sasa hakuna.!!!

    Kama hiyo haitoshi, wawekezaji wote wawe wa madini au nishati, wote lazima wafuate sheria, taratibu na kanuni za nchi na kamwe Wizara haiwavumilii hata kidogo wawekezaji waba-baishaji ambao wanakuja nchini mwetu kutaka kuwekeza huku wakiwa hawana uzoefu, mitaji, teknolojia.

    Msimamo na utendaji huu wa sasa wa Wizara ya Nishati na Madini umejenga heshima kubwa miongoni mwa jamii na Wa-tanzania wengi wanaridhishwa na utendaji huu wa kasi ambao matokeo yake yanaonekana na si maneno au porojo.

    Nishati na Madini ni vitendo na si maneno Watanzania tu-ungeni mkono tujenge nchi yetu.

    Asteria Muhozya na Veronica Simba, Dar es Salaam

    Ujumbe wa Tanzania uliohudhuria Maonesho ya Kimataifa ya Madini, katika mji wa Perth nchini Australia, ukiwa mbele ya banda la Tanzania lililokuwa linatumiwa na wataalam wa Tanania katika kutoa elimu kwa wageni zaidi ya 2000 waliohudhuria maonesho hayo. Ujumbe huo uliongozwa na Naibu Katibu mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eng. Ngosi Mwihava,(wa saba kutoka kulia). Wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo (wa nne kutoka kushoto mstari wa mbele), Kamishna wa Madini Eng.Paul Masanja (wa sita kulia), Mtendaji Mkuu wa TMAA, Eng.Dominic Rwekaza (wa pili kulia), Kamishna Msaidizi Madini-Uchumi na Biashara, Salim Salim (wa tatu kulia), Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Prof. Abdulkarim Mruma (wa tano kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Kazidata (Database) (GST), Bi Yorkbeth Myumbilwa (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Utawala wa Fedha na Utawala (TMAA), Bruno Mteta (wa tatu kushoto mstari wa mbele), Meneja Masoko na Mahusiano kwa Umma , STAMICO , Koleta Njelekela (wa kwanza kulia) na wataalam wengine kutoka Wizara na Taasisi zake.

  • 4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Na Nuru Mwasampeta

    Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na wachimbaji wakubwa wa madini nchini im-ezindua mradi wa kwanza Afrika wa mfano wa kuchakata dhahabu kwa wachimbaji wadogo wa madini katika kijiji cha LWAMGASA wilayani Geita.

    Mradi huo umezinduliwa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini) Mhe. Stephen Masele aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa mradi huo ulioanza kujadili-wa mwishoni mwa mwaka jana.

    Wizara ya Nishati na Madini kwa kugundua umuhimu na mchango wa wachimbaji wadogo wa madini katika uchumi wa nchi ulibuni mradi huu na kuwashirikisha wadau wengine wa maen-deleo wakiwemo Benki ya Dunia, Migodi mikubwa ya dhahabu na Chama cha wachimbaji wadogo na kusaini mkataba wa makubaliano mnamo mwaka 2009.

    Kwa upande wake mwakilishi toka Benki ya Dunia Mamadou Barry alizun-gumzia utekelezaji wa mradi huo kuwa ni matokeo ya utendaji mzuri wa Serikali ya Tanzania hususan Wizara ya Nishati na Madini katika kutekeleza miradi inayofa-dhiliwa na benki hiyo hivyo kuifanya benki hiyo kuwa na imani na watendaji wake.

    Aidha Mamadou ameeleza kuwa kwa kutambua mchango wa sekta ya madini kwa maendeleo ya Tanzania na kuwa na nafasi kubwa ya kutoa ajira kwa takribani watanzania milioni moja, ikiwa ni ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, Benki ya Dunia imeona ni vema ku-waendeleza wachimbaji wadogo ili kuwa-saidia katika kukuza uchumi wao binafsi na kuinua kipato cha taifa kwa ujumla.

    Kwa upande wake Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo mjini Geita Mr. Christopher Tadeo alizungumzia kuwa uchimbaj mdogo wa madini wilayani Geita ulianza kushamiri mwaka 1986. Aidha amebainisha changamoto zina-zowakabili wachimbaji wadogo katika uzalishaji wa madini kuwa ni pamoja na uhaba wa mtaji, tekinolojia duni, elimu duni, kutokuwa na maeneo ya kutosha kukidhi haja.

    Aidha Bw. Tadeo ameiomba serikali kutekeleza kwa haraka ahadi walizozitoa kwa wachimbaji wadogo wa madini ikiwa ni pamoja na kuwanunulia vifaa kwa ajili ya wachimbaji wadogo, kuwagawia maeneo yanayorudishwa na wachimbaji wakubwa wa madini na kuwafikishia hu-duma ya nishati ya umeme katika maeneo ya machimbo.

    Hata hivyo Bw. Tadeo amethibitisha kuwa mradi uliozinduliwa ni kielelezo tosha cha kutambua mchango wa serikali hususani uongozi wa wizara kw kutambua uhitaji wa wachimbaji wadogo wa madini.

    Kwa upande wao wachimbaji wadogo mkoani Geita waliohojiwa na mwandi-shi wa habari hizi kwa pamoja walikiri kuupokea mradi huo kwa mikono miwili na kuishukuru serikali kwa kuwakumbuka na kutafuta njia za kuwasaidia, aidha wali-sisitiza umuhimu wa wao kupatiwa elimu juu ya kuvitumia mitambo hiyo kutokana na ukweli kwamba walizoea njia duni na kwamba hawana elimu na ujuzi wa kuweza kutumia vifaa hivyo vya kisasa.

    Sisi hatujasoma sasa wanasema hiyo mitambo inaendeshwa na wasomi inamaana sisi tutazidi kuwa masikiniBi Jenipher Hagai alizungumza kwa huzuni na kuongeza kuwa wanaiomba serikali ifikilie kuwapa elimu juu ya uendeshaji wa mitambo hiyo jambo ambalo limek-wishakufanyiwa kazi na tayari mpango wa kuwaelimisha wachimbaji hao upo na kwamba hawatakabidhiwa mitambo hiyo kuiendesha wenyewe mpaka pale wataka-popata mafunzo na kufaulu kutumia vifaa hivyo. Hayo yalibainishwa na mshauri mwelekezi Bw.John-Bosco Tindebwa

    Naibu waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele (katikati) akijiandaa kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Mtambo huo. Wengine kutoka kushoto ni mwenyekiti wa kijiji cha Nyamgusu, Mtendaji Mkuu wa Mgodi wa madini wa Geita Bw.Michael Vananen kushoto kwa Masele ni Mkuu wa Wilaya ya Geita Bw. Omary mazie Magochie

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele akiweka mchanga katika mtambo wa kuchakata dhahabu uliozinduliwa mkoani Geita ikiwa ni ishara ya kuanza kazi kwa mtambo huo.

    Mtambo wazinduliwa Geitan Ni mtambo wa mfano wa kuchakata dhahabu n Ni wa kwanza kutumiwa na wachimbaji wadogo wa madini Afrika nSerikali, Benki ya Dunia na migodi Geita na Barrick washirikiana

    Mtambo wazinduliwa Geita

  • 5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    katika usimamizi wa sekta ya madini kupi-tia wawekezaji.

    Alisema kuwa ofisi za madini zinapas-wa kuongeza kasi ya ushirikishaji wa taarifa zake za kijiolojia pamoja na kuwatam-bulisha wawekezaji kwa ofisi za mikoa na wilaya kabla ya kuanza kwa shughuli za utafiti na uchimbaji wa madini katika maeneo husika.

    Alisisitiza kuwa kupatikana kwa taarifa sahihi na kwa wakati, kunarahisisha katika usuluhishi wa migogoro kati ya wawekezaji na jamii inayozunguka migodi inayoweza kujitokeza.

    Tunaamini kuwa kupitia makanmish-na wasaidizi wa madini, tunaweza kuwa na taarifa zote za kijiolojia, aina na idadi ya wawekezaji walioko katika maeneo yetu, na hii inaturahisishia katika usuluhishi wa migogoro kati ya wawekezaji na jamii inayowazunguka inayoweza kujitokeza, Alisema Bw. Mwamlima.

    Naye mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Jones Mushi alisema kuwa katika Sheria ya Madini kuna kifungu kinamtaka mwekezaji kujitambuli-sha katika ofisi ya mkoa na wilaya kabla ya kuanza kwa shughuli za utafiti na uchimbaji wa madini katika eneo husika.

    Mhandisi Mushi alisema kuwa Wizara imekuwa ikihimiza makamishna wasaidizi wa madini wa kanda kushirikiana kwa karibu zaidi na ofisi za mikoa na wilaya ili kuboresha sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza.

    Wakati huo huo timu ya majaji ilitem-belea mgodi wa utafiti wa madini aina ya dhahabu wa GBN ambapo uongozi wa kampuni hiyo umesema kuwa unata-rajia kuanza uzalishaji wa madini mwezi

    Oktoba.Akizungumza na timu hiyo kwa niaba

    ya mgodi huo, msimamizi wa mgodi huo Bw. Edson Steven amesema kuwa mgodi huo unatarajia kuanza uzalishaji wa dha-habu baada ya utafiti wake kukamilika.

    Alisema kuwa mgodi huo ulianza rasmi mwaka 2013 kwa kufanya utafiti wa madini ya dhahabu na hadi kufikia Juni mwaka huu ulikuwa umejiridhisha na kiasi cha madini ya dhahabu kilichopo katika mgodi huo.

    Akielezea mafanikio ya mgodi huo kwa kipindi cha mwaka 2013 Bw. Steven alisema kuwa mgodi ulichangia katika ujenzi wa shule ya sekondari ya Machim-boni, kompyuta kwa ajili ya ofisi ya mkuu wa polisi ya mkoa

    Naye Afisa Utawala na Fedha wa ki-wanda cha kuyeyusha madini ya shaba cha TPM ambacho pia kilitembelewa na timu ya majaji kwa ajili ya tathmini Bw. Philip Muna, akielezea mafanikio ya kiwanda hicho alisema kuwa, katika kipindi cha mwaka 2014 kiwanda kilinunua mashine ndogo ya kusaga mawe yenye dhahabu kwa ajili ya kikundi cha wachimbaji wadogo saba kama moja ya utekelezaji wa shughuli za jamii.

    Bw. Muna alisema kuwa kiwanda kil-ianza na uhamasishaji kwa wachimbaji wa-dogo wa madini ya dhahabu waozunguka maeneo ya kiwanda hicho kuunda umoja ili waweze kuwapatia mashine ndogo kwa ajili ya kusaga mawe yenye dhahabu na kuchenjua ili kujipatia kipato.

    Alisema kuwa mara baada ya vijana hao kuunda kikundi chao chenye jumla ya wajumbe saba, uongozi wa kiwanda hicho uliwapatia mashine hiyo ambayo imekuwa msaada mkubwa kwao.

    Makamishna wasaidizi wa madini watakiwa kushirikiana na Wilaya

    Mkuu wa wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima akizungumza na timu ya majaji na sekretarieti iliyomtembelea ofisini kwake kabla ya kufanya ziara katika kiwanda cha kuyeyusha madini ya shaba cha TPM kilichopo katika wilaya ya Mpanda mkoani Katavi

    u

    Bomba la gesi kuokoa Sh. trilioni 1.6

    Bomba la gesi

    Na Greyson Mwase, Katavi

    Makamishna wasaidizi wa ma-dini wa kanda wametakiwa kuongeza ushirikiano wa ka-ribu na viongozi waandam-izi wa mikoa na wilaya ili kukuza sekta ya madini ili iwe na mchango mkubwa katika uchumi wa taifa.

    Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bw. Paza Mwam-lima alipokutana na timu ya majaji na sekretarieti iliyomtembelea ofisini kwake kabla ya kuendelea na zoezi lake la kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais

    ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji katika wilaya ya Mpanda. Timu hiyo inafanya tathmini katika makampuni ya madini katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya jamii ili kumpata mshindi atakayekabidhiwa tuzo na Rais mapema mwezi Novemba. Maeneo yanayoan-galiwa ni pamoja na miundombinu, maji, afya, elimu, manunuzi ya ndani, ajira pamoja na uwezeshaji wa vikundi vidogo vidogo katika jamii husika.

    Bw. Mwamlima alisema kuwa ili ku-hakikisha kuwa sekta ya madini inakuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa wilaya na mkoa, ni vyema ofisi za madini zikafanya kazi kwa karibu kwa kushirikiana na ofisi za mikoa na wilaya

    nSerikali kuanza kurudisha mitambo ya kukodi

    Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam

    Kiasi sha Shilingi trilioni 1.6 za Kitanzania kitaokolewa baada ya kukamilika kwa Mradi wa ujenzi wa bomba la gesi fedha ambazo zitato-kana baada ya serikali kuachana na matumizi ya mafuta kutumika kuzalisha umeme.

    Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Ma-dini, Eliakim Maswi, aliyaeleza hayo wakati Washirika wa Maendelo na wawakilishi wa balozi mbalimbali nchini walipotembelea Mradi wa kuzalisha Umeme wa Kinyerezi I na kituo cha kupokea Gesi cha Dar es Salaam.

    Fedha inayopotea kwenye mafuta ni nyingi, tunataka kuokoa kiasi hicho cha fedha, lakini pia bomba la gesi litawasaidia Tanesco kuonesha uwezo wao wa kiuchumi,aliongeza Maswi.

    Aidha, aliongeza kuwa, endapo seri-kali itaachana na matumizi ya mafuta katika kuzalisha umeme, hali hiyo inatarajia kuwapunguzia gharama za nishati ya umeme watanzania kutokana na kwamba, umeme utakaozalishwa kutokana na gesi utakuwa wa

    gharama nafuu.Aliongeza kuwa, Serikali itaanza kurudi-

    sha mitambo ya kukodi inayotumia mafuta kuzalisha umeme ifikapo mwezi Novemba mwaka huu na badala yake kuanza kutumia mitambo ya Serikali ambayo haitumiki kwa sasa.

    Mtambo wa Symbion wenye uwezo wa kuzalisha megawati 112 kwa sasa unatumia mafuta ya ndege lakini baada ya bomba kukamilika tutatumia gesi. Lakini pia tuna mtambo wetu wa Ubungo I wenye uwezo wa kuzalisha megawati 100 upo na utatumika pia, aliongeza Maswi.

    Aliongeza kuwa, serikali inatarajiwa kuka-bidhiwa na wakandarasi mradi wa Kinyerezi I ifikapo mwezi Machi, mwakani ambapo kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati za umeme 150 ambazo zitaingizwa katika Gridi ya Taifa, na kuongeza kuwa uzalishaji wa majaribio unatarajiwa kufanyika mwezi Januari ambapo umeme utakaozalish-wa utauzwa moja kwa moja kwa wananchi.

    Washirika wa maendeleo wameona tuna-chokifanya. Wameona maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kupokea gesi na mradi wa kufua umeme. Tunataka kuachana na matumizi ya

    mitambo ya kukodi,alisisitiza Maswi.Kwa upande wake Meneja Mradi wa

    Ujenzi wa Bomba la Gesi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), alieleza kuwa, gharama za ujenzi wa kituo cha kupokea gesi zimegharamu kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.23 kati ya hizo, zaidi ya dola za marekani milioni 100 zimetolewa na Serikali ya Tanzania.

    Naye Meneja Mradi wa Kituo cha kuzalisha Umeme Kinyerezi I Saimoni Jilima

    alieleza kuwa, mradi huo unakwenda vizuri na kuongeza kuwa, umekamilika kwa asilimia 70, ambapo tayari transfoma zote zimekwisha fungwa ikiwemo ujenzi wa line za Msongo wa kv 220, kv 132 ambao ujenzi wake uko katika hatua nzuri na unaendelea, ikiwemo mitambo miwili ya mwisho ambayo tayari imewasili bandarini.

    Aidha aliongeza kuwa, majengo mengine yanayojengwa ni pamoja na jengo la kuende-sha mitambo na jengo la utawala.

  • 6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    KAMERA YETU

    Meneja Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha kuzalisha Umeme cha Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TA-NESCO), Mhandisi, Saimoni akiuleza jambo ujumbe wa Washirika wa Maendeleo wakati walipotembelea kuona maendeleo wa ujenzi wa mradi huo.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo,(wa kwanza kushoto) katika picha ya pamoja na Mawaziri wa Nishati kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki mara baada ya kikao kilichojadili maendeleo ya Mradi wa Rusumo.

    THAILAND

    Wateja mbalimbali wakihudumiwa katika Banda la Tanzania kwenye maonesho ya vito na usonara ya Bangkok yaliyo-fanyika hivi karibuni nchini Thailand.

    Baadhi ya Watanzania walioshiriki maonesho ya vito na usonara ya Bangkok, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungwa rasmi kwa maonesho hayo.

    Ujumbe wa Tanzania ulioshiriki katika maonesho ya vito na usonara ya Bangkok pia walitumia fursa ya maonesho hayo kutangaza maonesho ya vito ya Arusha yanayotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu jijiji Arusha. Pichani ni Eva Mowo (kushoto) Afisa kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Lightness Makundi, Afisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini, wakiwa wamepozi katika bango lenye ujumbe wa kutangaza maonesho ya Arusha. Maafisa hao walivalia mavazi ya asili (vitenge) na mikufu yenye vito vya Tanzanite kutangaza utamaduni wa Kitanzania na madini hayo maarufu ya vito yapatikanayo Tanzania pekee.

    u

    Maonesho

  • 7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    KAMERA YETU Wataalam kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) washiriki Maonesho ya Saba ya Kimataifa katika masuala ya Gesi na Mafuta -Dongying China .

    Wadau wa Mafuta na Gesi kutoka wakisikiliza kwa makini maelezo ya teknolo-jia mpya za utafiti wa mafuta na gesi duniani huko nchini China. Wadau hawa walihudhuria maonesho ya 7 ya kimataifa ya mafuta, gesi na bidhaa zitokanazo na rasilimali hizo yaliyofanyika katika jiji la Dongying nchini China. Maonesho kama haya hufanyika kila mwaka yakilenga kujenga uhusiano baina ya nchi na nchi pia kubadil-ishana uzoefu katika sekta ya mafuta na gesi duniani.

    Meneja Mkuu wa mgodi wa Williamson Diamond Limited Bw. Arlen Loehmer ( wa pili kutoka kushoto) akisalimiana na mwenyekiti wa jopo la majaji kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji Prof. Samwel Wangwe, mara baada ya jopo hilo kuwasili katika mgodi huo.

    Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (wan ne kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni inayochimba gesi katika eneo la Mnazi Bay, Mtwara, Michael Hochard (wa tano kulia) wakipeana mikono mara baada ya Kampuni hiyo na TPDC kusaini Mkataba wa Makubaliano wa kuuziana gesi kwa ajili ya Mradi wa Bomba la gesi. Wengine katika picha ni baadhi wa Watendaji Wakuu wa Wizara ya Ni-shati na Madini, Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC na wawakilishi wa kampuni za WENTWORTH na MAUREL & PROM.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele akifunua kitambaa ili kuweka wazi maelezo ya mradi wa kusaidia wachimbaji wadogo uliozinduliwa katika eneo la kazi kijijini lwamgasa nyuma yake ni Mkuu wa wilaya ya Geita

    Mtaalamu katika kiwanda cha kuyeyusha madini ya shaba cha TPM Mhandisi Innocent Mushi (kulia) akielezea jinsi mashine ya kuponda mawe yenye dhahabu (pichani) inavyofanya kazi kwa majaji na sekretarieti iliyofanya ziara katika kiwanda hicho ili kufanya tathmini ya kiwanda hicho katika utekelezaji wa miradi ya jamii kwa kipindi cha mwaka 2013

    Bw. Ibrahim Rutta, mtaalamu kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wa pili kulia akipata maelezo juu ya mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia kutoka kwa mmoja wa wanamaonesho huko nchini China. Chini inaonesha mfano wa kiwanda cha kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia kama kinacho-jegwa jijini Dar es Salaam.

    Tenki hili la kuhifadhia maji au aina yoyote ya vimiminika imetengenezwa na masalia ya gesi asilia na ina uwezo wa kuhimili mkandamizo wa 25 MPA.

    u

    Maonesho Maonesho China

  • 8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Kaimu Mkurugenzi Mtendaji STAMICO Eng. Edwin Ngonyani (mwenye suti nyeusi) akiwa na baadhi ya Wakuu wa Idara pamoja na wafanyakazi wa Idara za Uchimbaji, Ulinzi pamoja na Usalama katika eneo la uchimbaji West Zone wakati wa ziara yake katika mgodi wa STAMIGOLD BIHARAMULO mwishoni mwa wiki alipofanya ziara ya kikazi katika mgodi huo.

    Meneja Uchenjuaji Bwana Christopher Mwinuka (wa tano kutoka kulia) akifafanua jambo kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Eng. Edwin Ngonyani alipotembelea eneo la mtambo wa uchenjuaji dhahabu wakati wa ziara yake katika mgodi wa STAMIGOLD BIHARAMULO mwishoni mwa wiki iliyopita.

    STAMICO YAHIMIZA UBUNIFU STAMIGOLD Jacqueline Mat-

    towo na Godfrey Francis, STAMIGOLD BIHARAMULO.

    Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la madini la Taifa STAMICO Eng. Edwin Ngonyani amehimiza Kam-puni ya STAMIGOLD BIHARAMULO kuwa wabunifu katika mifumo na miun-do ya utendaji kazi wake ili kuleta tija kwa Kampuni, Shirika na Taifa kwa ujumla.

    Eng. Ngonyani ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika Mgodi wa Biharamulo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwa na lengo la kukagua maendeleo ya shughuli za uzalishaji dhahabu zinazofanywa na mgodi huo, pamoja na kuzungumza na wafanyakazi ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu ku-shika wadhifa huo mnamo mwezi Juni 2014

    Nataka kuona STAMIGOLD ikiwa na muundo na mfumo wake wa utendaji kazi na sio kuiga mambo yote yaliyoachwa na kampuni iliyopita. Kampuni iliyopita ilikuwa na mfumo na mitazamo yake na nyie mnatakiwa kubuni ya kwenu. Muige yaliyo mazuri na kuachana na yale yasiyohitajika kwa kampuni. Nawataka wataalamu wetu wakae pamoja na kutumia vizuri elimu na uzoefu wao katika kuibua mawazo mapya yatakayoleta tija kwa Kampuni, Shirika na Taifa kwa ujumla . Alifafanua Eng. Ngonyani.

    Aliongeza kuwa, mtu atakayeonesha dalili zozote za kutaka kurudisha nyuma au kuangusha maendeleo ya mgodi atafukuzwa kazi mara moja bila ku-subiri uamuzi wa Bodi ya Wakurugenzi, na kuongeza kuwa Wizara ya Nishati na Madini ipo pamoja na kampuni hiyo ku-hakikisha STAMIGOLD inasonga mbele na kufikia malengo yake.

    Kwa upande mwingine, Kaimu Mkurugenzi Eng. Ngonyani alitangaza katika mkutano huo uteuzi wa Eng. Den-nis Sebugwao kuwa Meneja Mkuu wa Mgodi; ambao ulioanza rasmi tarehe 1 Septemba mwaka huu, baada ya Bodi ya Wakurugenzi ya STAMIGOLD ku-ridhia mapendekezo yaliyotolewa na Me-nejimenti ya STAMICO kufanya uteuzi huo uliolenga kuiwezesha kampuni ya STAMIGOLD kujiendesha kikamilifu hivyo kufanikisha kufikia malengo yake.

    Eng. Sebugwao anakuwa Meneja Mkuu wa Kwanza wa Mgodi wa STA-MIGOLD BIHARAMULO uliojulikana zamani kama Tulawaka, chini ya umiliki wa Kampuni ya African Barrick Gold (ABG) kabla Serikali haijauchukua rasmi mgodi huo na kuukabidhi kwa STA-MICO, mwishoni wa mwezi Novemba 2013. Ana Shahada ya Uzamili ya Sayan-si katika Uhandisi wa Uchenjuaji Madini kutoka Chuo Kikuu cha LENINGRAD MINING INSTITUTE, USSR mwaka 1984

    Wakati huo huo Eng. Ngonyani pia alihimiza wafanyakazi kuimarisha ma-wasiliano mazuri na viongozi wa juu wa Serikali kwa kutoa taarifa sahihi na ze-nye manufaa ili kusaidia kufikia maamuzi yenye tija na kuboresha utendaji katika Kampuni na Shirika kwa ujumla.

    Akizungumza katika mkutano huo Meneja Mkuu wa Mgodi wa STAMI-GOLD BIHARAMULO Eng. Dennis Sebugwao aliwashukuru wafanyakazi kwa ushirikiano wao wanaouendeleza tangu kuanza kwa mgodi huo na kuwa-taka waendelee kufanya kazi kwa bidii na kutumia taratibu rasmi sehemu ya kazi ikiwemo kutumia vikao vya wafanyakazi kutoa taarifa au changamoto zinazowaka-bili utendaji kazi ili kuruhusu menejimen-ti kufanya maboresho kwa wakati.

    Tunataka STAMIGOLD iwe Ki-tovu cha uzalishaji dhahabu kwa Shirika na mfano wa kuigwa kwa migodi min-gine yote itakayoanzishwa chini ya STA-MICO ili migodi hiyo ianzie hapa kwani tunao wataalamu wenye uzoefu na tut-akuwa tayari kuwatoa kwenda kusaidia kuanzisha miradi mingine ya Shirika. Ameongeza kuwa Kampuni itaende-lea kudhibiti gharama za uzalishaji na uendeshaji ili kuleta faida yenye tija kwa Kampuni na Taifa zima. Alisisitiza Eng. Sebugwao.

    Mbali na uteuzi wa Meneja Mkuu wa Mgodi, Bodi ya Wakurugenzi ya STA-MIGOLD pia imewathibitisha kazini Mameneja wawili waliokuwa wakikaimu nafasi zilizokuwa wazi. Mameneja hao ni Meneja Uchimbaji Bwana Abdallah Kwassa na Meneja wa Uchenjuaji Bwa-na Christopher Mwinuka. Uteuzi huo umeanza mara moja.

    Bwana Kwassa ana uzoefu wa miaka 8 katika fani ya uchimbaji wa madini na ameshafanya kazi katika kampuni mbal-imbali hapa nchini ikiwepo kampuni ya African Barrick Gold-Tulawaka na Kam-puni ya Saruji ya Lafarge iliyopo mkoani Mbeya. Bw. Kwassa ana Shahada ya Say-ansi ya Uhandisi wa Uchimbaji wa Ma-dini aliyotunukiwa mwaka 2005 kutoka katika Chuo Kikuu cha Middle East Tech-nical University (METU), TURKEY.

    Kwa upande mwingine, Bwana Mwinuka ana uzoefu wa zaidi ya miaka 6 katika fani ya ya Uchenjuaji Madini, uzoefu alioupata katika kampuni ya Af-rican Barrick Gold-Tulawaka. Bw. Mwi-nuka ana Shahada ya Sayansi ya Uhandisi wa Uchenjuaji wa Madini kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na pia ame-hudhuria mafunzo mbalimbali yanayohu-su uchenjuaji madini ndani na nje ya nchi.

    Kampuni ya STAMIGOLD ina mpango wa kupitia upya muundo wake wa kiutawala ili kuhakikisha mahitaji halisi ya rasilimali watu yanazingatiwa na hivyo kusaidia uwajibikaji baina ya wafanyakazi ili kupunguza gharama za uendeshaji na kuleta faida yenye tija kwa Kampuni.

    CHUO CHA MADINI-DODOMAMINERAL RESOURCES INSTITUTE

    MAHAFALI YA KWANZA CHUO CHA MADINI, 2014Chuo cha Madini Dodoma, kinapenda kuwatangazia wahitimu wote wa Chuo cha Madini kuwa sherehe za mahafali ya kwanza ya Chuo itafanyika tarehe 21 Novemba 2014.MAHALI NA MUDASherehe za mahafali zitafanyika chuoni hapo kuanzia saa nne 4:00 asubuhi, na zinawa-husu wanafunzi wote waliohitimu astashahada kuanzia mwaka 2008 hadi 2014.-Ili kuweza kushiriki katika mahafali haya,wahitimu wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kuanzia tarehe 04 Septemba hadi 04 Novemba, kwa kulipia Tsh.30,000/= kama gharama za majoho katika Akaunti ya CRDB: 01j10882316900, Jina la akaunti: Mineral Resourc-es Institute.Wahitimu wanatakiwa kujisajili kwa kutuma stakabadhi ya malipo, kupitia tovuti ya chuo www.mri.ac.tz au kwa Msajili wa wanafunzi Chuoni. Majoho yataanza kutolewa Chuoni kuanzia tarehe 17 Novemba hadi 20 Novemba 2014. Majoho yanatakiwa kurudishwa chuoni kabla ya siku kumi (10) baada ya sherehe za mahafali. Kila siku moja ikizidi utali-pia Tsh15,000/=MAJARIBIO (REHEARSAL)Wahitimu wote wanaotarajia kuhudhuria mahafali lazima wafike saa 2:00 asubuhi kwenye mafunzo ya majaribio kabla ya sherehe za mahafali kuanza. Watakaoshindwa kufanya mafunzo ya majaribio hawataruhusiwa kuhudhuria kwenye sherehe za mahafali.ANGALIZOWahitimu wote wanaotarajia kuhudhuria sherehe za mahafali, wanatakiwa kuzingatia muda na kukaa kwenye viti watakavyopangiwa kabla ya saa 3:45asubuhi, watakaoche-lewa kufika hawataruhusiwa kuingia kwenye uwanja wa mahafali.

    Imetolewa naKaimu Mkuu wa Chuo - Taaluma

  • 9BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Na Veronica Simba

    Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Makam-puni ya Madini nchini, wame-kubaliana kuendesha programu za mafunzo kwa wananchi kwa ajili ya kujenga uelewa kuhusu fursa zilizopo katika sekta ya madini ili waweze kuzi-tumia ipasavyo kuinua vipato vyao na Taifa kwa ujumla.

    Makubaliano hayo yalifikiwa na pande hizo mbili hivi karibuni jijini Mwanza wakati wa mkutano ulioan-daliwa na Idara ya Madini ya Wizara husika kwa lengo la kuweka mikakati ya pamoja baina yake na Makampuni ya Madini katika kutekeleza Sera ya Ma-dini ya mwaka 2009 inayotoa tamko la sekta hiyo kuwashirikisha Watanzania (local content) na pia kuifungamanisha na sekta nyingine.

    Wajumbe wa mkutano huo kwa pamoja walipitisha maazimio kadhaa yaliyolenga kuhakikisha Watanzania wanashirikishwa ipasavyo katika sekta ya madini ambapo mojawapo ya maa-

    zimio hayo ilikuwa ni kujenga uelewa kwa wananchi waweze kuzitambua fursa zilizopo na kuzitumia.

    Pia, Wajumbe walikubaliana kuwa kufanyike utafiti utakaoainisha mianya iliyopo katika utoaji huduma hususan maeneo ambayo wananchi wanaweza kutoa huduma kwa makampuni ya ma-dini ili huduma zinazoweza kutolewa na wananchi zisitolewe na wageni kutoka nje ya nchi.

    Akifafanua kuhusu wananchi kupewa fursa za kutoa huduma kwa makampuni ya madini, Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje alisema wananchi wana haki ya kutoa huduma zilizo ndani ya uwezo wao hivyo Serikali itahakikisha haki hiyo inatekelezwa kama inavyostahili.

    Sisi kama Serikali tunataka kuboresha ushirikishwaji wazawa katika sekta ya madini na ni lazima makam-puni ya madini yahakikishe wazawa wanashirikishwa ipasavyo, alisisitiza.

    Aidha, maazimio mengine yaliyofikiwa katika mkutano huo ni pamoja na Serikali kwa kushirikiana na makampuni ya madini kuwajengea

    uwezo wazawa (kifedha na utaalamu) kwa kutilia mkazo sekta ya kilimo na uzalishaji.

    Vilevile, pande hizo mbili zilikubali-ana kwamba, kwa kuwa ushirikishwaji wazawa ni suala la kisera, iko haja ya kufanyia marekebisho sheria na kanuni za madini kuhusu ushirikishwaji wa wa-zawa ili kuhakikisha wazawa wanapata haki stahiki.

    Pia, iliafikiwa kuwa kuanzishwe kamati maalumu itakayoshughulikia masuala ya ushirikishwaji wazawa ka-tika sekta ya madini ambayo pamoja na mambo mengine itaainisha mahitaji na viwango katika eneo husika katika hali ambayo ni shirikishi, na pia kusaidia kuainisha fursa zilizopo katika sekta.

    Wajumbe wa mkutano huo pia wa-likubaliana kuwa Wizara ya Nishati na Madini iandae mkutano wa kila mwaka kujadili suala la ushirikishwaji wazawa ambao utashirikisha makampuni yote ya madini, wafanyabiashara na wazal-ishaji wazawa, jamii zinazozunguka migodi pamoja na wizara na taasisi nyingine za serikali zinazohusika.

    Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje akiwakaribisha wajumbe wa mkutano wa kujadili ushirikishwaji wazawa (local content) katika sekta ya madini uliofanyika jijini Mwanza hivi karibuni. Waliokaa meza kuu kutoka kushoto ni Kamishna Msaidizi Kitengo cha Uchumi na Biashara, Salim Salim, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Ndalo Kulwijila na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John Henjewele.

    SERIKALI, MAKAMPUNI YA MADINI KUWANOA WAZAWA

    u

    Mwanasheria wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Rose Mponguliana akiwasilisha mada kuhusu uwajibikaji wa Shirika hilo katika suala la ush-irikishwaji wazawa wakati wa mkutano baina ya Serikali na Makampuni ya Madini uliofanyika hivi karibuni jijini Mwanza.

    Na Nuru Mwasampeta

    Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Ahadi Msangi amewataka waajiriwa wapya ndani ya wizara hiyo kufuata taratibu na kanuni za utumishi wa Umma katika kutekeleza majukumu yao baada ya kupata nafasi ya kuutumikia umma kupitia wizara hiyo.

    Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo yaliyotolewa kwa waajiriwa hao Msangi aliwaasa watumishi hao kutoa mchango wao katika changamoto zinazozikabili sekta za nishati na madini hususan suala la Nishati ya Umeme.

    Aidha aliwakumbusha kuwa

    mada walizojifunza kwa muda wa wiki moja zitawafaa sana na kuboresha utendaji wao hivyo hawanabudi kuzingatia mada zote walizojifunza.

    Akizungumzia mada zilizo-wasilishwa wakati wa mafunzo hayo alisema ni pamoja na maadili, muundo wa serikali na utendaji wake wa kazi, utunzaji wa kum-bukumbu, sheria ya utumishi wa Umma ya mwaka 2002, kanuni za kudumu za utumishi wa umma, masuala ya UKIMWI na utunzaji siri.

    Kwa upande wake mmoja wa waajiriwa hao Injinia Yusuph Msembele alisema kuwa mafunzo waliyoyapata yatawasaidia katika kufanya kazi kwa ufanisi, kujiamini na kwa uhakika kwani tayari tara-tibu zote za utendaji katika utumishi wa umma zimewekwa wazi.

    Waajiriwa wapya wanolewa kujua kanuni za utumishi wa umma

    Mgeni rasmi wakati wa Kufunga mafunzo kwa waajiriwa wapya Bw. Ahadi Msangi, Mhasibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, (mwenye miwani) akiwa katika picha ya pamoja na waajiriwa watakaotumika chini ya Wizara ya Nishati na Madini wakati wa kufunga mafunzo yaliyoandaliwa ili kuwapa mwongozo wa kiutendaji katika utumishi wa Umma. Kushoto kwake ni Bw. Lusius Mwenda Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Rasilimali watu Wizara ya Nishati na Madini na kulia kwake ni Bi. Dorah N. Chenyambunga, Mkufunzi na Mkuu wa Kitengo cha masoko TPSC

    Waajiriwa wapya wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi wakati wa kufunga mafunzo yaliyofanyika katika chuo cha uongozi mwishoni mwa mwezi wa Nane mwaka huu. (Hayupo Pichani)

    nNi kuhusu ushirikishwaji wazawa sekta ya madini

  • 10 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    RC Kilimanjaro aipongeza TANESCO Tanzania, Thailand kushirikiana

    katika madini vito

    Na Leila Muhaji, KILIMANJARO

    Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw. Leonidas Gama amesifu juhudi za Shirika la Umeme nchini (TANESCO) za kufanya upanuzi wa miradi mbalimbali ya umeme ambayo imewez-esha wananchi wa mkoa huo kupata huduma ya uhakika ya umeme.

    Gama alitoa pongezi hizo hivi karibuni katika mahojiano maalumu na muandaaji wa kipindi cha TANESCO na Maendeleo Bi. Leila Muhaji ali-yemtembelea ofisini kwake mjini Moshi ili kufuatilia miradi mbalimbali ya umeme inayotekelezwa na Shirika ndani ya mkoa huo.

    Bw. Gama alitaja miradi mikubwa iliyotekelezwa na TANESCO na ili-yofanikisha kupatikana kwa umeme wa uhakika na kufikia watumiaji wakub-wa na wadodgo kuwa ni Kiyungi,YMCA, KCMC, Makuyuni na kituo cha kusambaza umeme cha KIA.

    TANESCO mmeweza kufikisha huduma ya umeme kwa watumiaji wengi wakiwemo wakubwa na wadogo ambao awali walikuwa wanakosa hu-duma ya umeme wa uhakika na hivyo kudidimiza uchumi wawatumiaji wa nishati hiyo, kwa sasa wateja wenu wanafurahi, nawapongeza sana alisema Bw. Gama.

    Aliongeza kuwa upatikanaji huo wa umeme wa uhakika umewezesha kuongeza kiwango cha uzalishaji mali hususani katika maeneo ya viwandani akitolea mfano wa kiwanda cha Sukari cha TPC na maeneo ya huduma za kijamii kama hospitali, mashule na biashara ndogo ndogo.

    Aidha Bw. Gama alitoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro kuka-biliana na matukio ya wizi wa umeme pamoja na uhujumu wa miundombinu yake kwani vitendo hivyo vimekuwa vikiligharimu Shirika fedha nyingi ya ku-rudishia miundombinu inayoibiwa ambazo zingeweza kutumika kuwapele-kea umeme wananchi wengine ambao bado hawafikiwa na huduma hiyo.

    Alisema Shirika linatumia fedha nyingi kubadilisha nyaya za shaba kwen-da nyaya za aluminum kutokana na kukithiri kwa wizi wa nyaya za shaba katika baadhi ya maeneo mkoani humo.

    Bw. Gama aliwataka wananchi wasio waaminifu kuacha mara moja wizi wa umeme kwa mtindo maarufu wa drip wa kuunga waya kwenye njia ya umeme na kuuchimbia ardhini kwa kuwa ni hatari kwa maisha yao na mara nyingine kuunguza nyumba zao na hivyo kuwataka kufuata njia sahihi za ku-unganishiwa hudumahiyo.

    Mradi wa ujenzi wa kituo cha kusambaza umeme Kiyungi ambacho awa-li kilikuwa na uwezo wa 40MVA sasa kimeboreshwa na kufikia uwezo wa 60MVA na jitihada zinaendelea ili kituo hicho kiwe na uwezo wa 100 MVA.

    Ujenzi wa kituo kipya cha kusambaza umeme cha KIA kipo katika hatua za mwisho na kitakuwa na uwezo wa 40MVA. Kituo hicho kitaboresha upa-tikanaji wahuduma ya umeme katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA pamoja na eneo lote la Mererani ambapo shughuli za uchimbaji wa madini ya Tanzanite unaendelea.

    Kituo kingine cha Makuyuni kilichozinduliwa mwaka jana na Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal na kilichojengwa kwa ufadhili wa Shirika la kimataifa la Japan (JICA) kina uwezo wa 20MVA wakati kile cha YMCA kilichokuwa na uwezo wa 5MVA kimeboreshwa hadi kufikia 17MVA. Kituo cha KCMC ambacho ni maalumu kwa ajili ya kusambaza umeme wa uhaki-ka hospitali ya KCMC na maeneo ya Shanti Town kilichokuwa na uwezo wa 5MVA nacho kimeboreshwa hadi kufikia 10 MVA

    Na Veronica Simba Aliyekuwa Bangkok

    Wafanyabiashara wa madini ya vito na usonara wa Thailand wameonyesha nia ya kushirikiana na Tanzania katika sekta hiyo kwa lengo la kukuza uhusiano na kuzinu-faisha pande zote mbili.

    Hayo yalibainika hivi karibuni katika kikao kilichoku-tanisha Ujumbe wa Tanzania ulioshiriki Maonesho ya Vito na Usonara yaliyofanyika Bangkok nchini Thailand na Uongozi wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa madini hayo kutoka nchini humo.

    Akiwasilisha maoni na mapendekezo kutoka upande wa Tanzania katika kikao hicho, Kiongozi wa Ujumbe kutoka Tanzania, Archard Kalugendo ambaye ni Mkuru-genzi wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), alisema Tanzania inapenda kushirikiana na Wa-Thailand katika sekta hiyo ili pamoja na mambo mengine kuiga na kujifunza kutoka kwao.

    Ninyi wenzetu mmeendelea sana katika sekta hii ya madini ya vito na usonara. Tunapenda kujifunza na kuiga kutoka kwenu ili nasi tufike hapo mlipofikia na hata zaidi ya hapo, alisema Kalugendo.

    Aliongeza kwamba, lengo la Serikali ya Tanzania ni kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha inawawezesha wananchi wake hususan wanaojishughulisha na biashara ya madini ya vito na usonara ili wanufaike ipasavyo kupitia kazi hiyo na pia kulinufaisha Taifa kwa ujumla kwa kukuza uchumi wa nchi.

    Alisema, Serikali inayo nia na imejipanga kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha biashara ya madini ya vito na usonara katika Bara la Afrika na kwamba inatumia njia mbalimbali kufanikisha hilo ikiwemo kuendelea kuboresha Maonesho ya Vito na Usonara ya Arusha (Arusha Gem Fair AGF) yanayofanyika kila mwaka.

    Kalugendo alitumia fursa hiyo kuwakaribisha Wafan-yabiashara wa Thailand katika Maonesho ya Vito ya Aru-sha yanayotarajiwa kufanyika mapema mwezi Novemba mwaka huu jijini Arusha.

    Tanzania inayo mazingira mazuri sana ya uwekezaji na ninawahakikishia kuwa ushiriki wenu katika maonesho hayo utakuwa wenye tija kwenu na kwetu pia, alisema.

    Aidha, Kalugendo alitoa maombi ya Tanzania ku-

    patiwa nafasi kubwa zaidi katika Maonesho ya Vito na Usonara ya Thailand ili washiriki wengi zaidi wakiwemo wachimbaji na wafanyabiashara wa madini hayo waweze kushiriki na kujipatia uzoefu utakaowasaidia kuboresha utendaji wao na hivyo kumudu ushindani katika soko na viwango vya kimataifa.

    Kwa upande wake Mwenyekiti wa Maonesho ya Vito na Usonara ya Arusha, Peter Pereira alisisitiza umuhimu wa Thailand kushiriki katika maonesho ya Arusha na kuwahakikishia kuwa mazingira mazuri yameandaliwa kwa ushiriki wenye tija ikiwemo kuondoa gharama za kodi ya thamani katika bidhaa (VAT) kwa kipindi chote cha maonesho.

    Akijibu hoja na mapendekezo kutoka upande wa Tan-zania, Makamu wa Rais wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito Thailand, ambao ndiyo waandaaji wa Maonesho ya Vito ya Bangkok, Tony Brooke alisema Thai-land inapenda kushirikiana kwa ukaribu zaidi na Tanzania katika sekta hiyo.

    Alisema Wafanyabiashara wa Thailand watashiriki katika maonesho ya vito ya Arusha na kuahidi kuboresha ushiriki wa Tanzania katika maonesho ya vito ya Bangkok.

    Brooke alitoa changamoto kwa Tanzania kujiandaa vema zaidi katika ushiriki wa maonesho kama hayo kwa kuhakikisha inapeleka madini na bidhaa kwa wingi kulin-gana na uhitaji wa wateja.

    Wateja wengi wanatembelea banda la Tanzania ku-liko madini na bidhaa zilizopo. Ongezeni wingi wa bidhaa maana uhitaji ni mkubwa, alisisitiza Brooke.

    Alikubaliana na wazo la kuifanya Tanzania kuwa ki-tovu cha madini ya vito na usonara katika bara la Afrika na kusisitiza kufanya kazi kwa bidii, weledi na kujituma kwa hali juu ili kuhakikisha lengo hilo linatimia.

    Hatua mnayoona tumefikia katika sekta hii ya madini ya vito na usonara imekuja kwa kufanya kazi kwa bidii, weledi na kujituma, hivyo nanyi ili mfanikiwe mnapaswa kufanya hivyo, alisema.

    Nchi ya Thailand ina uzoefu wa miaka 40 katika bi-ashara ya madini ya vito na usonara na imekuwa ikiandaa maonesho makubwa kila mwaka katika kipindi hicho chote ili kuuza bidhaa zitokanazo na madini ya vito na kujitan-gaza zaidi kimataifa.

    Maonyesho ya Vito na Usonara ya Bangkok kwa mwa-ka huu yalifanyika kuanzia Septemba 9 hadi 13 na kush-irikisha mataifa mbalimbali duniani.

    THAILAND

    Makamu wa kwanza wa Rais wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito na Usonara wa Thailand, Bw. Sutipong Dumrong-sakul, akimkabidhi zawadi maalumu Mkuu wa Ujumbe kutoka Tanzania ulioshiriki maonesho ya vito ya Bangkok, Archard Kalu-gendo, mara baada ya kikao kati ya Ujumbe huo na Viongozi wa Taasisi hiyo ya Wafanyabiashara wa Thailand.

    Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw. Leonidas Gama.

    nAisifu kwa miradi kabambe

  • 11BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA NISHATI NA MADINI

    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA NISHATI NA MADINI

    Eng. DOMINIC RWEKAZA

    TAARIFA YA UTEUZI WA MTENDAJI MKUU TMAA SALAM ZA PONGEZI

    Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (Mb.), amemteua Mhandisi Dominic Rwekaza kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).Uteuzi huo umeanza tarehe 1 Septemba 2014.Awali Mhandisi Dominic Rwekaza alikuwa akikaimu nafasi hiyo, iliyoachwa wazi na Mhandisi Paul Masanja aliyeteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Kamishna wa Madini nchini.Mhandisi Rwekaza ana uzoefu katika uendeshaji wa Sekta ya Madini Tanzania baada ya kupata mafunzo kutoka vyuo mbalimbali duniani na pia kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi katika Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania na Wizara ya Nishati na Madini.

    Imetolewa na;KATIBU MKUU

    WIZARA YA NISHATI MADINI

    Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (Mb.) kwa niaba ya uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini na watumishi wote, anampongeza Mhandisi Joackim Joseph kwa kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji katika kampuni ya Umeme ya Rusumo itakayosimamia mradi wa kikanda wa kuzalisha umeme kutoka Bwa-wa la Rusumo utakaonufaisha nchi za Tanzania, Burundi na Rwanda.Mhandisi Joackim amekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kwanza ku-ongoza mradi huo ambao makao makuu yake yapo Kigali nchini Rwanda.Mhandisi Joseph ana uzoefu wa kutosha katika sekta ya umeme kutokana na kuwa na shahada ya kwanza na ya uzamili katika say-ansi ya uhandisi aliyopata kutoka vyuo vikuu ndani na nje ya nchi na kuongoza miradi mbalimbali ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).Wizara inamtakia kila la kheri katika kutimiza wajibu wake huo ili kutimiza lengo la serikali la kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika na wa bei nafuu kutoka vyanzo mbalimbali.

    Imetolewa na;KATIBU MKUU

    WIZARA YA NISHATI MADINI

    WASHIRIKA WA MAENDELEO KATIKA MRADI WA UMEME KINYEREZI

    Baadhi ya Washirika wa Maendeleo wakipita jirani na unapojengwa mmoja wa mitambo wa kupokea gesi katika eneo la Kinyerezi, Jijini Dar es Salaam, walipotembelea maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kupokea gesi.

    Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi (katikati) akiwaongoza Washirika wa Maendelo kuangalia namna utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme na kituo cha kupokea Gesi unavyoendelea katika eneo la Kinyerezi Jijini Dar es Salaam. Pembeni ni mojawapo ya mapipa yatakayotumika kuhifadhi mafuta ambayo yatatumika wakati wa dharura.

  • 12 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Saba kusomea mafuta na Gesi Brazili Mwakani

    Na Asteria Muhozya

    Naibu Katibu Mkuu Wiz-ara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava ameeleza kuwa, Tanzania bado inauhitaji mkubwa

    wa wataalamu waliobobea katika sekta ndo-go ya mafuta na gesi kutokana na kuingia ka-tika uchumi huo, hivyo kuwataka wanafunzi wanaopata bahati ya kusomea fani hizo kuichukua elimu hiyo kwa uzito wa kipekee kwa kuhakikisha wanafanya vizuri katika masomo ya nadharia na vitendo.

    Naibu Katibu Mkuu ameyabainisha hayo wakati akifunga mafunzo ya lugha ya kireno kwa wanafunzi waliopata ufadhili wa kusoma masuala ya gesi na mafuta nchini Brazil na kuongeza kuwa, lugha hiyo ya Kireno itakuwa nyenzo kwa wanafunzi hao kuweza kujifunza masomo ya mafuta na gesi na kuongeza kuwa, Serikali inawahitaji watalaamu hao waweze kuishauri kisera juu ya namna bora ya kuiendeleza sekta hiyo.

    Aidha, aliongeza kuwa, serikali imed-hamiria kuwajengea uwezo wa kitaalamu watanzania ili waweze kushiriki katika sekta ya gesi ikiwemo kuwezesha ushiriki wao ka-tika uchumi huo na kusisitiza kuwa, bado Tanzania inahitaji wataalamu waliobobea kutoka fani mbalimbali ambazo zitawezesha usimamizi mzuri wa rasilimali hiyo.

    Tuna njaa ya elimu ya utaalamu wa gesi, tunawahitaji wataalamu wa gesi kui-wezesha Tanzania kushiriki vema katika uchumi huu. Hivyo, tunahitaji wataalamu katika fani mbalimbali zikiwemo za sheria, uandishi wa habari, lengo letu ni kufanya kazi kwa pamoja kwa masilahi ya Taifa, alisisitiza Mwihava.

    Vilevile, Mwihava alitumia fursa hiyo, kuupongeza Ubalozi wa Brazili nchini, kam-puni ya kuchimba gesi ya PETRO Bras na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), kwa kuwezesha fursa kwa watan-zania kusomea masuala ya mafuta na gesi nchini Brazil.

    Kwa upande wake Balozi wa Brazil Nchini Fransisco Carlos Luiz, amepongeza jitihada za Wizara kuhakikisha inakuwa na wataalamu wake katika fani za mafuta na gesi na kutoa wito kwa vijana kuitumia fursa hiyo na kuongeza kuwa, kipindi hiki ni muafaka kwa wataalamu wa gesi kujifunza fani hizo kabla ya muda wa uzalishaji wa rasilimali hizo kuanza.

    Tulipenda Tanzania ijiandae vema kati-

    ka fani hizi iweze kushiriki kikamilifu katika uchumi huu. Ninafurahi kuona jitihada za Wizara, TPDC na Kampuni ya Petro Bras kulisimamia jambo hili, kwa kuwa uzalishaji unachukua kipindi kirefu lakini kuandaa wataalam ni muhimu zaidi, aliongeza Ba-lozi Luiz.

    Akiongea kwa niaba ya Wanafunzi wali-ohitimu mafunzo hayo, Zahoro Athumani alishukuru jitihada za Serikali na kueleza kuwa ni njia nzuri ambayo serikali inaitu-mia wakati inaingia katika uchumi wa gesi

    na kuongeza kuwa, watahakikisha kwamba wanakuwa wataalamu waliobobea katika masuala ya utafiti na uchimbaji mafuta na gesi na hivyo kuitaka serikali kuweka maz-ingira bora yatakayowawezesha wataalamu mbalimbali wanaohitimu katika fani hizo kutumika kikamilifu.

    Tunashukuru sana Serikali kwa nafasi hii, tunaahidi kuwa wataalamu waliobobea katika fani hizi, lakini niiombe serikali, iwa-tumie wataalamu wake wanapohitimu fani hizo ili waweze kuchangia katika uchumi

    huu, alisisitiza Athumani.Jumla ya wanafunzi 15 wamehitimu

    mafunzo ya lugha ya Kireno ambayo wameisoma kwa kipindi cha miezi 6 ikiwa ni maandalizi ya kuwawezesha kusoma masu-ala ya mafuta na gesi nchini Brazili. Aidha, wanafunzi (7) kati yao tayari wamepata na-fasi ya kujiunga na vyuo vya mafuta na gesi nchini Brazili katika ngazi za Shahada za Uzamili na Uzamivu ifikapo mwezi Machi mwakani wakati 8 kati yao wanasubiri fursa ya kujiunga.

    MwihavaasemabadokunanjaayaWataalam BaloziBraziliasifujitihadazaWizarakuandaawataalamu

    Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (wa kwanza kulia), akiongea na wnafunzi waliopata waliohitimu mafunzo katika lugha ya Kireno ambapo saba kati ya 15 tayari wamepata ufadhili wa kujiunga na vyuo vya mafuta na gesi nchini Brazili, Kushoto ni balozi wa Brazili nchini Fransisco Carlos Luiz, wengine katika picha ni baadhi ya watumishi kutoka Kampuni ya mafuta ya PETRO Bras, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na Wizara ya Nishati na Madini.

    Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (wa nne kulia) na Balozi wa Brazili nchini

    Fransisco Carlos Luiz (wa tatu kulia) katika picha ya pamoja na Wanafunzi 15 walihitimu mafunzo ya lugha ya Kireno.

    Wanafunzi 7 kati yao tayari wamepata ufadhili wa kusoma masuala ya mafuta na gesi katika ngazi za Shahada ya Uzamili

    na Uzamivu nchini Brazili mwezi Machi mwakani.

  • 13BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Ziara ya Masele

    Nyumba 18 za waliopisha mwekezaji mkubwa wa madini Geita mbioni kukamilika

    Na Nuru Mwasampeta

    Nyumba za wananchi wa-nanchi waliopisha mradi mkubwa wa uchimbaji wa madini ya dhahabu chini ya Mgodi wa Madini wa Geita ziko katika hat-ua ya mwisho ya ukamilishaji ili wananchi

    hao wakabidhiwe rasmi.Hayo yamebainika mara baada ya Nai-

    bu Waziri wa Nishati na Madini (Madini) Stephen Masele kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba hizo 18 za wahanga hao ili kuweza kupanga siku ya kuja kukabidhi nyumba hizo kwa wananchi.

    Masele amesema serikali inatambua taabu wanazokutana nazo wananchi wa-

    naopisha miradi mbalimbali ya maendeleo nchini na hivyo kutafuta namna mbalimbali za kuweza kuwasaidia katika kuwapunguzia ugumu wa maisha kama ilivyofanya kwa wananchi waliopisha mradi wa uchimbaji mkubwa wa madini Mkoani Geita.

    Si kweli kuwa serikali imewasahau wananchi na kuwajali wawekezaji.Alisisiti-zaMasele. Baada ya kuona ugumu wa mai-sha ya wananchi waliopisha mradi huo wa uchimbaji serikali iliingilia kati na kuuagiza uongozi wa mgodi kujenga nyumba 19 kwa familia zilizoathiriwa na mradi huo ambapo ujenzi wa nyumba hizo umekamilika kwa asilimia kubwa na sasa tunapanga siku ya kuwakabidhi.

    Amebainisha kuwa nyumba zilizojeng-wa mpaka sasa zipo kumi na nane baada ya mhanga mmoja kugoma kujengewa nyum-ba katika eneo lililoteuliwa na kutaka apewe pesa yake ili ajenge yeye mwenyewe jambo ambalo halikuafikiwa na serikali pamoja na mgodi na hivyo nyumba hiyo kutojegwa.

    Imeelezwa kuwa awali wananchi hao walikuwa wakiishi katika eneo la mtakuja ambapo walihamishiwa kijiji cha kalangala-la maarufu kama Darful wakisubiri kuham-ishiwa katika makazi yao ya kudumu kijiji cha Buhalahala.

    Aidha wananchi hao walionesha furaha

    kubwa mara baada ya kuoneshwa picha za nyumba watakazokabidhiwa na serikali na mgodi pindi zitakapokamilika katika makazi yao ya muda mara baada ya kutembelewa na waandishi wa habari.

    Kwa upande wake Bi Betti Petro mmoja kati ya wahanga hao alitoa shukrani kwa serikali kuwasaidia waweze kujengewa ny-umba hizo na kuiomba serikali kuwaon-doa mapema katika eneo hilo kutokana na ugumu wa maisha waliyonayo na kwenda katika makazi mapya ili waweze kujihusisha na shughuli za kilimo.

    Hamis Charles naye pia alipohojiwa na waandishi wa habari hizi alioneshwa kuri-dhika na juhudi zinazofanywa na serikali katika kuwatetea wanyonge na kuwaasa wa-nanchi wengine kufuata maelekezo yanayo-tolewa na serikali kwani serikali ndiyo yenye kauli ya mwisho.

    Mradi wa ujenzi wa nyumba hizo uta-gharimu kiasi cha Shilingi za kitanzania Bilioni moja na na nusu mpaka kukamilika kwake ambapo suala la kuingiza umeme li-nashughulikiwa na Shirika la Umeme Tan-zania (TANESCO) huku mgodi ukiendelea na uchimbaji wa kisima cha maji ili kuka-milisha mradi mzima na kuweza kuukabidhi kwa wahanga hao.

    Maseleasemawanapangasikuyakukabidhi

    By Blandina Munghezi

    Two Independent Non-Executive Directors, Am-bassador Juma Mwapachu and Ms. Rachel English visited Buzwagi Mine site on 11th Sept 2014 to get a feel of how the site is faring around Community Rela-tions, Health, Safety and Security popularly termed as CHESS. They also wanted to know the priorities, respond and contribute to the fulfill-ment of the priorities of the site.

    The two directors were accom-panied by ABGs Executive General Manager Organizational Effective-ness, Peter Geleta, General Manager Sustainability Asa Mwaipopo, Chief Environmental Advisor Rebecca Stephen and the Chief Community Relations Advisor Stephen Kisakye.

    Upon arrival the dignitaries were taken through a presentation conducted by Safety, Health, Secu-rity, Environmentand Community Relations leads, showing each de-partments organogram, key perfor-mance areas and statistics, focus ar-eas and challenges, plus the previous audit findings and status.

    During a tour of the Process Plant the team was able to see the

    sites initiatives in ensuring proper storage and good housekeeping. We now isolate, arrange, classify and put in newly built warehouses stuff that was once left in the open. Said Buzwagi Mine General Man-ager, Philbert Rweyemamu, who was leading the tour accompanied by the Process Plant Manager Karel Schultz. He said properly arranged items can now be easily located and take stock and those that are no long-er usable can now be sold.

    A visit to the community started off by paying a courtesy call to the Kahama District Commissioners of-fice where the Hon Benson Mpesya said Kahama members of the com-munity are now visibly showing their appreciation to Buzwagi thanks to the visionary CEO, Brad Gordon and the sites General Manager Phil-bert Rweyemamu. Thecommunity feels that Buzwagi is also their mine he said. He praised Buzwagi for in-creasing local procurement of goods saying this has a multiplier effect and improves livelihoods since not every-one can be employed by the mine.

    The team was then taken on a tour of the Kahama town to see a five kilometer network of roads worth 3 Billion Tshs constructed by

    ABG. At the Mwendakulima ward on the outskirts of the town, they met with youth engaged in an inter-locking brick- making project. Also at Mwendakulima they visited the office of a Bee-keeping project. Both the two projects are among several other projects facilitated and spon-

    sored by ABG to improve the liveli-hoods of the community.

    To round up their visit the team met with the rest of the management team and later with staff where in his speech Ambassador Mwapachu said The site has made significant improvement around Safety, Envi-

    ronment, and Community Relations and overall you are on the right track and have assisted in creating the ABG brand that we want to see. He praised the existing strong leader-ship at Buzwagi, the organizational turnaround across all the ABG sites and cost cutting initiatives currently underway.

    On his part the Buzwagi Mine General Manager thanked the ABG SLT for support rendered to Buzw-agi that has enabled the site to pull through. We still have challenges but the team has been performing well he said. When the employees were given a chance to speak,Lloyd Paul, First Line Leader Emergen-cyResponse said on behalf of my colleagues I would like to thank the board and the SLT for believing in us or else this mine would have been closed due to poor performance and the low gold price. He also pointed out the good leadership, encourage-ment and support that stuff has re-ceived from Philbert Rweyemamu the Mine General Manager as one of the causes of success. He said Buzw-agi is now performing with renewed strength and vigor and on behalf of the rest of the staff promised to do even better.

    We promise to do better!-Buzwagi staff promises board CHESS members

    Rehema Bujiku whois in charge of honey marketing showing visitors how she uses a honey extraction hand tool.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini) Mhe. Stephen Masele

  • 14 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

    5TH AFRICAN RIFT GEOTHERMAL CONFERENCE (ARGeo - C5)Geothermal: Solution to Africas Energy Needs

    29th-31st October, 2014 AICC Arusha, TanzaniaHosted and organized by the Government of the Republic of Tanzania in collaboration with UNEP, GOC and other partners, Endorsed by the international Geothermal Association.

    UJUMBE WA WAZIRI WIKI HIIWATENDAJI WOTE WA WIZARA NA TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA

    WAZINGATIE 4Us KATIKA UTENDAJI WAO.UADILIFU, UWAJIBIKAJI, UWAZI NA UBUNIFU

    UJUMBE WA WAZIRI WIKI HII

    Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wasiliana nasi kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    WIZARA YA NISHATI NA MADINI

    KAMPUNI ZA GESI, TPDC WASAINI MKATABA KUUZIANA GESINa Asteria Muhozya, na

    Teresia Mhagama, Dar es Salaam

    Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Kam-puni zinazochimba gesi kati-ka eneo la Mnazi Bay Mkoa-ni Mtwara za WENTWORTH Resources Limited na MAUREL & PROM zimesaini Mkataba wa Makubaliano wa kuuziana Gesi, ambapo kampuni hizo zitaingiza gesi hiyo katika visima vilivyopo Mnazi Bay Mtwara kwa ajili ya Mradi wa Bomba la Gesi.

    Akizungumza katika kikao cha kusaini Makubaliano hayo, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sos-peter Muhongo alisisitiza umuhimu wa kusaini Mkataba huo na kueleza kuwa, ni fursa nyingine kwa Tanza-nia kiuchumi na kuongeza kwamba,

    Serikali imedhamiria kuingia katika biashara ya gesi na hivyo biashara itakayofanyika kati ya Serikali na makampuni hayo inatarajiwa kuwa yenye maslahi kwa taifa kutokana na kwamba serikali imejipanga katika usimamizi na utekelezaji wa biashara ya gesi.

    Lazima tufanikiwe katika hili, watanzania wengi wanafuatilia jam-bo hili kwa karibu, hata kwa upande wetu kila mmoja alikuwa akisubiri jambo hili. Kwa upande wa Tane-sco wanafanya vizuri na kila mmoja yuko tayari kwa biashara yenye ma-slahi, alisisItiza Muhongo.

    Naye Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tan-zania, James Andilile alieleza kuwa, kikao hicho kimetumika kama njia ya kukamilisha michakato ya ku-fikia lengo la makubaliano hayo ikiwemo namna ya kuuziana gesi hiyo ikiwemo bei itakayotumika.

    Wajumbe waliohudhuria kikao cha Kusaini Mkataba wa Kuuziana Gesi kati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na Kampuni zinazochimba gesi katika eneo la Mnazi Bay Mkoani Mtwara za WENTWORTH Resources Limited na MAUREL & PROM wakisaini MKataba huo. Anayeshuhudia mbele ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo pamoja na wawakilishi wengine kutoka kampuni hizo, TPDC, Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

    Madini Ziwa Nyasa yatoa gari kwa Tanesco Ruvuma

    Na Teresia Mhagama

    Tarehe 12 Septemba 2014, Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Ziwa Nyasa, Julius Sarota amekabi-dhi gari namba STK 2622 kwa Ofisi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Ruvuma ambayo ilipokewa na Kaimu Meneja wa TANESCO katika mkoa huo, Eng. Timoth Ramadhani.

    Kutolewa kwa gari hiyo ni matokeo ya ziara kikazi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya

    Nishati na Madini, Eliakim Maswi, aliyoi-fanya mkoani hapo tarehe 23 Agosti 2014 ambapo wafanyakazi wa Tanesco mkoa wa Ruvuma walimweleza kuhusu uhaba wa vi-tendea kazi ikiwemo kuwa na gari itakayosa-idia shughuli za dharura mkoani humo.

    Baada ya kilio hicho, Katibu Mkuu al-imua kuwapa gari mojawapo kati ya tatu zi-lizokuwa zikitumika katika Ofisi ya Madini kanda ya Ziwa Nyasa ili liweze kusaidia ka-tika shughuli za Tanesco mkoani humo.

    Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Nyasa, Julius Sarota, (kulia) akikabidhi nyaraka za gari kwa Kaimu Meneja wa TANESCO katika mkoa wa Ruvuma, Eng. Timoth Ramadhani.