12
SHERIA (TORATI) YA AGANO LA KALE 1 Masharti ya agano kwa Israeli VItabu vya sheria vinaeleweka kwa jina ya jumla ”Pentateuch” Penta = Tano, Teuch = kifaa / kitabu Mwanzo [Genesis], Kutoka [Exodus], Walawi [Leviticus], Hesabu [Numbers / Numerus], Kumbukumbu la torati [Deuteronomy] Sheria hasa imeandikwa kuanzia Kutoka 20 hadi mwisho wa Kumbu kumbu. Mwanzo na Kutoka 1-19 si maandiko ya kisheria lakini inahesabika katika vitabu vya sheria Katika Agano Jipya A.K. lote linatumika kama rejea ya Sheria kwa sababu inahesabika kuwa ufafanuz wa utendaji wa sheria.

7. Sheria za Agano la Kale · Baadhi ya maagizo ya A.K. haiku rudiwa katika A.J. • Tunaweza kuzigawa katika sehemu mbili: • Ya kwanza ni sheria ya usalama na mazingira (Adhabu

  • Upload
    others

  • View
    13

  • Download
    3

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: 7. Sheria za Agano la Kale · Baadhi ya maagizo ya A.K. haiku rudiwa katika A.J. • Tunaweza kuzigawa katika sehemu mbili: • Ya kwanza ni sheria ya usalama na mazingira (Adhabu

SHERIA (TORATI) YA AGANO LA KALE 1

• Masharti ya agano kwa Israeli • VItabu vya sheria vinaeleweka kwa jina ya jumla ”Pentateuch”

• Penta = Tano, Teuch = kifaa / kitabu • Mwanzo [Genesis], Kutoka [Exodus], Walawi [Leviticus],

Hesabu [Numbers / Numerus], Kumbukumbu la torati [Deuteronomy]

• Sheria hasa imeandikwa kuanzia Kutoka 20 hadi mwisho wa Kumbu kumbu.

• Mwanzo na Kutoka 1-19 si maandiko ya kisheria lakini inahesabika katika vitabu vya sheria

• Katika Agano Jipya A.K. lote linatumika kama rejea ya Sheria kwa sababu inahesabika kuwa ufafanuz wa utendaji wa sheria.

Page 2: 7. Sheria za Agano la Kale · Baadhi ya maagizo ya A.K. haiku rudiwa katika A.J. • Tunaweza kuzigawa katika sehemu mbili: • Ya kwanza ni sheria ya usalama na mazingira (Adhabu

SHERIA (TORATI) YA AGANO LA KALE 2

• Wakristo na sheria ya Agano la Kale • Tutafahamuje tamko la Yesu katika Matt 5:18? ”..yodi moja wala

nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie..” Je, tunapaswa kutii na kufuata sheria zote au baadhi ya sheria ambazo zimo katika Kutoka 20 hadi Kumbukumbu 33? Hapa kuna taratibu sita za kufuata wakati tunapojibu swala hilo la muhimu sana.

Page 3: 7. Sheria za Agano la Kale · Baadhi ya maagizo ya A.K. haiku rudiwa katika A.J. • Tunaweza kuzigawa katika sehemu mbili: • Ya kwanza ni sheria ya usalama na mazingira (Adhabu

SHERIA (TORATI) YA AGANO LA KALE 3

• 1. Torati, sheria, ya Agano la Kale ni mkataba. Ni mkataba kati ya watu wawili. Ilikuwa kawaida kwa wakati huokwamba watawala wawili waliingia katika mkataba fulani, mara nyingi ilikua mkubwa anaingia mkataba na mdogo. Yule mkubwa aliahidi usalama na ulinzi na kwa msada huo yule mwingine alimwahidi kua atakua mwaminifu kwake. Kama mkataba wa namna hii ulivunjwa kulikuwepo adhabu ambayo yule mdogo aliyovunja aliipata. (Siyo rahisi kwa yule mdogo kumweza yule mkubwa)

• Mkataba wa jinsi hii ulifanyika katikati ya Mungu na Israeli, na ilifanana sana na mikataba iliyoandikwa na watawala wengine wakati huo.

• Mkataba huo ulikua na vipengele sita: Utambulisho - ambao uliwatambulisha walioingia katikamkataba huo. Utangulizi - ulitoa historia fupi ambayo ilieleza sababu za kuandikiana mkataba. Mashariti - Sheria au kanuni ambazo zilikuwepo katika mkataba huo. Matokeo - Matokeo ya kufuata na kuvunja huo mkataba. Hitimizo - Inasisitiza umuhimu wa kufuata huo mkataba na kushika katika mawazo ya kila siku.

Page 4: 7. Sheria za Agano la Kale · Baadhi ya maagizo ya A.K. haiku rudiwa katika A.J. • Tunaweza kuzigawa katika sehemu mbili: • Ya kwanza ni sheria ya usalama na mazingira (Adhabu

SHERIA (TORATI) YA AGANO LA KALE 4

2. Agano la Kale siyo Agano letu. • A.K. ni agano la zamani ”zilipendwa”, ambalo hatulazimiki

kulishika leo. Kwa hiyo hatuwezi kusema kwamba A.K. inatuhusu sisi.

• Sisi tuko katika msimamo mwingine unaosema; ”Hakuna agizo katika A.K. ambao inatuhusu isipokua zile zilizorudiwa kutamkwa katika A.J.” (Warumi 6:14-15) Kwa sababu kuna mabadiliko makubwa wakati tulipopata A.J.

• Kitu ambayo Mungu anategemea kwetu ni uaminifu wa namna nyingine tofauti na ya wakati ule. Uaminifu bado ni muhimu, lakini jinsi ya kuonyesha huo uaminifu ni tofauti.

Page 5: 7. Sheria za Agano la Kale · Baadhi ya maagizo ya A.K. haiku rudiwa katika A.J. • Tunaweza kuzigawa katika sehemu mbili: • Ya kwanza ni sheria ya usalama na mazingira (Adhabu

SHERIA (TORATI) YA AGANO LA KALE 53. Baadhi ya maagizo ya A.K. haiku rudiwa katika A.J. • Tunaweza kuzigawa katika sehemu mbili:

• Ya kwanza ni sheria ya usalama na mazingira (Adhabu iliyofuatana na makosa ya ”kiserekali”) sheria hizo zilikua na nguvu tu wakati ule katika mazingira yale. Hakuna mtu ambaye inamuhusu leo maana hakuna mtu leo ambaye aliishi wakati ule.

• Sehemu ya pili ni sheria ya jinsi ya kuabudu na matoleo. Inahusika na utoaji wa wanyama, kuchomwa. Kama tungeendelea na mambo haya leo katika nchi zingine tungefungwa kwa ajili ya kutesa wanyama. Tumepewa dhabihu tofauti na mpya, tena ambayo hatukuweza kutoa sisi bali alijitoa, ni Yesu na alijitoa mara moja nayo inatosha sana. (Ebr 9:24-28) Sadaka yake ilifanya sadaka zote zingine ziishiwe nguvu na maana.

• Lakini je lile tamko ya kwamba hakuna litakalo toweka...? Hapana, aliyosema ilikua kwamba torati haiwezi kubadilika. Torati na manabii kazi yao imekwisha na iliisha wakati Yohana mbatizaji alianza kutangaza na kuhubiri Agano Jipya litakalokuja.., ndiyo maana hata Yesu alijitahidi kuwaingiza watu katika agano hili jipya waiingie katika ”Ufalme wa Mungu” bila hivyo wangebaki chini ya ”utawala wa agano la kale”, maana haiwezi kufutika.

• Agano Jipya ilikua na msingi mpya kabisa, msingi wa upendo... nayo inazidi agano la sheria...

• Taratibu zinazotumika katika kurudia (renew) mkataba pia hapa zinatumika. Kwa maana hiyo mengine yanafuata ndani ya mkataba mpya, mengine yana ”chujwa” na kupotea maana havihitajiki. Lakini pia kuna mengine mapya yanaongezeka.

Page 6: 7. Sheria za Agano la Kale · Baadhi ya maagizo ya A.K. haiku rudiwa katika A.J. • Tunaweza kuzigawa katika sehemu mbili: • Ya kwanza ni sheria ya usalama na mazingira (Adhabu

SHERIA (TORATI) YA AGANO LA KALE 64. Baadhi ya mambo ya A.K. yanatufuata katika kuingia A.J. • Basi kitu gani inayofuata? Kuna kanuni za kimaadili ambao tunazikuta katika A.K. na A.J.

Mungu mwenyewe alipendekeza ziwemo. Zinauzito kwa sababu ndiyo mising miwili ambayo ni misingi pia katika A.K. (Mt 22:37-40). Katika Torati pia tunaikuta (Kum 6:5; Law 18:18) Yesu anachukua Sheia, kanuni , mbili na anaziweka katika Agano ambalo anaileta mpya. (Mt 5:21-48) Lakini analolifanya ni kwamba kanuni zinazohusika na upendo zinafuata na dizo tunatakiwa kufuata.

5. Agano la Kale lote ni maneno ya Mungu, hata kama siyo maneno ya Mungu kama agizo kwetu. • Biblia inayo mengi sana ambayo Mungu anapenda tuelewe, ambayo siyo kanuni ambazo

tumepewa sisi leo. Kwa mfano Mt 11:4 waliyosikia maneno haya walikua wafuasi wa Yohanna. Tunasoma agizo waliopewa lakini haiwezi kutuhusu sisi. Ndivyo ilivyo na Torati walipewa watu wa Israeli waliyoishi katika siku zile na ilikua sheria yao mpaka Agano lingine lilipoanza kufanya kazi.

6. Agizo zile ambazo zilitamkwa kwamba zinafuata, na kuingia katika A.J. ndizo tunazopaswa kuzifuata. • Gal 6:2 Katika sehemu hiyo pia tunaikuta amri kumi na pia zile mbili zilizotajwa hapo juu. Hizo

ni ”sheria” za wakristo wote. Mengine yanaweza kutusaidia katika maisha yetu lakini hatuwezi kuzifanya kua sheria zetu.

Page 7: 7. Sheria za Agano la Kale · Baadhi ya maagizo ya A.K. haiku rudiwa katika A.J. • Tunaweza kuzigawa katika sehemu mbili: • Ya kwanza ni sheria ya usalama na mazingira (Adhabu

SHERIA (TORATI) YA AGANO LA KALE 7• Kazi ya Torati katika Israeli na Bibilia

• Kutokana na mafundisho hapo juu tusione kua torati haina maana sana, au kwamba A.K. hailna uzito.

• Ina maana sana kwetu kama tunataka kuelewa ”historia ya wokovu”.

• Inatuonyesha wazi madai ya Mungu juu ya utakatifu ya watu wake, kwamba haiwezekani kufikia hali hi kama binadamu, ni Mungu tu mwenyewe ambaye anaweza kutupatia utakatifu wa namna hiyo. Hakuna sehemu inayosema kwamba ”torati inaokoa” - Ni Mungu anayeokoa: Kutoka utumwa wa pale Misri, na kadhalika.

• Torati inasimamia mkataba ambao ulifanywa katikati ya Mungu na Israeli.

• Torati inatuonyesha mfano wa uaminifu.

Page 8: 7. Sheria za Agano la Kale · Baadhi ya maagizo ya A.K. haiku rudiwa katika A.J. • Tunaweza kuzigawa katika sehemu mbili: • Ya kwanza ni sheria ya usalama na mazingira (Adhabu

SHERIA (TORATI) YA AGANO LA KALE 8• Sheria za amri • Soma Law 19:9-14, Tukisoma mistari kama hi tunaona kwamba inatupatia mafundisho ya jinsi

Mungu anavyotutakia kuishi. Haitupatii maelezo ya kila swali lakini inaleta mfano wa wastani. Haisemi juu ya kila aina ya mazao na taratibu zake mst 9,10. Pia haisemi juu ya kila aina ya ulemavu wanaotajwa ni vipofu tu.

• Kuachia yaliyo kando kando ya shamba kwa wenye mahitaji, kuacha kuvuna yaliyo chelewa kuiva hata hiyo kwa manufaa ya wanaokosa chakula. Pia kufuta madeni yote, na kumrudishia mtu mali yake kila baada ya miaka hamsini na kila mtu arejee kwake... Kama sheria zote za A.K. yangetuhusu ingebidi hata sheria za namna hii tuzifuate.

• Hivyo tunaona kwamba yapo mengi ambayo hatuyafuati leo, sasa swali ni kwamba tutawezaje kuchagua la kufuata na lakuacha? Kama tulivyoshauri hapo juu ni vema: Sheria ambayo Yesu alizileta kutoka A.K. na kuziingiza katika A.J. zinatosha, zingine hazinauzito kama sheria.

• Torati (sheria) ya A.K. inakua kama sheria ya nchi, inahitaji watalaamu kwa kulielewa na kutekeleza na kuamua. Pia sheria ya nchi inaweza ikapitwa na wakati, wajanja wanaweza kupenya penya... kwa hiyo haileti uhakika wa maisha. Isipokua inaleta muongozo kwa yule anayependa kufuata sheria ya nchi yake. Hakuna anayeweza kufuata sheria ya A.K. hata akashinda . (Rum 8:1-11)

• Torati inatuelimisha juu ya hali yetu jinsi tusivyo watakatifu, hatustahili utakatifu tunaopewa na Mungu na sisi wenyewe tusingeweza kuufanyia kazihuo utakatifu.

Page 9: 7. Sheria za Agano la Kale · Baadhi ya maagizo ya A.K. haiku rudiwa katika A.J. • Tunaweza kuzigawa katika sehemu mbili: • Ya kwanza ni sheria ya usalama na mazingira (Adhabu

SHERIA (TORATI) YA AGANO LA KALE 9• Sheria za dharura • Ni sheria ambazo zinahitaji tukio fulani. Soma Kum 15:12-17. sheria hii inanguvu kama 1. wewe ni muisraeli na

unayo mtumwa mmoja au zaidi au 2. wewe ni muisraeli na unaye mtumwa ambaye wakati wake wautumwa umekwisha na anapenda au hapendi kuendelea katika utumwa.

• Kama wewe siyo muisraeli hiyo sheria haikuhusu. Kuna sehemu nyingi katika Torati ambayo inawahusu watu fulani tu, nayo hazikurudiwa (hazikupewa nguvu mpya) katika A.J. kwa sababu zinahusika na ”sheria za taifa za Israeli, sheria za maadili ya mazingira na sheria za imani na kuabudu” kwa ajili ya maisha ya wana wa Israeli. Kwa hiyo kwa mkristo siyo rahisi kufuata kutokana na mazingira tuliyonayo. (kila mtu mazingira yake) Sasa maandiko ya namna hii inatusaidia nini basi?

• 1. Tunaweza kuona kwamba sheria za Mungu juu ya utumwa (kukaa na watumwa) ilikua ya huruma siyo kama katika mazingira ya watu wengine, wala siyo kama tulivyozoea katika historia yetu.

• 2. Mungu aliwajali watumwa, maana aliwapa sheria ya kuwalinda.

• 3. Pia tunaona kua watumwa waliweza kuishi maisha mazuri katika utumwa wao. Walipewa chakula, nguo na mahali pakukaa. Wengine bilashaka wangepata shida zaidi katika uhuru kuliko katika utumwa ”mwema”.

• 4. Mtumwa hakua mali ya mwenye mtumwa. Baada ya miaka sita ilitakiwa aachiwe. Watu wote mtumwa na tajiri walikua mali ya Mungu.

• Kitu muhimu na maandiko hayo ni kwamba tunajifunza juu ya Mungu. Katika sehemu hii tunaweza kujifunza.

• 1. Tunaweza kufahamu msingi wa mafundisho ya ukombozi wetu

• 2. Tunaelewa kwamba utumwa katika A.K. ni tofauti sana na utumwa tunayouelewa sisi.

• 3. Tunaweza kupata ufahamu wa upendo wa Mungu ambayo tusingepata bila kupata maandiko ya namna hii.

• Kwa hiyo tunaona kwamba maneno haya ni ya maana sana kwetu hata kama sio amri kwetu. Ingawa hatupate kufahamu yote yanayohusika na utumwa katika mazigira ya A.K. Lakini inatuelekeza katika jinsiya kuishi maisha yetu ya kikristo.

Page 10: 7. Sheria za Agano la Kale · Baadhi ya maagizo ya A.K. haiku rudiwa katika A.J. • Tunaweza kuzigawa katika sehemu mbili: • Ya kwanza ni sheria ya usalama na mazingira (Adhabu

SHERIA (TORATI) YA AGANO LA KALE 10• Sheria za Agano la kale na sheria za mataifa mengine wakati ule

• Sheria ya A.K. ilikua ya huruma zaidi kuliko sheria za mataifa mengine, na ilikua ya mapinduzi kweli.

• Sheria za Agano la kale ilikua kama neema kwa Israelli • ”Sheria haikutungwa kwa ajili ya kufuatwa” maana isingewezekana.

• Haikuwezekana kuamini kwamba mtu aneweza kushika kila sheria bila kuanguka. (Rum 2:17-27; 3:20)

• Tatizo ni kwamba ukivunja sheria moja unavuja zote (Yak 2:10) Tukielewa hiyo, na pia tukielewa maana yakuweka sheria, (Iliwekwa kua muongozo wa maisha) na tukikumbuka kwamba masamaha yalipatikana, tunaona neema na ukubwa wa Mungu katika upungufu wa binadamu.

• Sheria inayohusu vyakula • Law11:7, Sheria zilizohusu vyakula ilikua na kusud ya kuwalinda watu wasiugue.

Labda chakula fulani ilikua inauwepesi wa ”kubeba” ugonjwa fulani, labda ilikua gali katika kufuga au kulima. Na pia sababu moja iliweza kua kwamba ilitumika katika dini za kienyeji kwa ajili ya matoleo madhabahuni. Pia inawezekana kwama chakula kilichoruhusiwa iliwasaidia watu wale wasipate ”allergy” (mzio).

Page 11: 7. Sheria za Agano la Kale · Baadhi ya maagizo ya A.K. haiku rudiwa katika A.J. • Tunaweza kuzigawa katika sehemu mbili: • Ya kwanza ni sheria ya usalama na mazingira (Adhabu

SHERIA (TORATI) YA AGANO LA KALE 11• Sheria za utoaji wa damu

• Kut 29:10-12; Mungu alidai sadaka kama ulikosea (kufidia ile kosa) lakini pia alikubali mtu kutumia mnyama kama badala yake. Hapo anaweka msingi wa ukombozi wetu kwamba Yesu aliweza kufa kwa ajili yetu (badala yetu) (Ebr) Pia ni wazi kwamba kama kila mtu angedaiwa alipe mwenyewe kwa kusa lake, wana waisraeli wangefutika wala wasinge baki hata mmoja.

• Sheria za kiajabu (ngeni) • Kum 14:21; Law 19:19: ....usi pande mazao aina mbili kwa pamoja, Usichanganye

wanyama.... Kufanya hivyo ilikua kawaida kwa Wakanaani walifanya hivyo kama kaida ya dini (rite) kusudi mazao yawe mengi. Ilikua kaida ambazo Mungu hakupenda watu wake washiriki. kwa sababu isinge wapa baraka sawa sawa na baraka ambazo Mungu angeweza kuwapa. Kwa wakati wake sheria hizozilikua na maana sana.

• Sheria ambazo ziliwapa watekelezaji baraka • Kum 14:28-29: Sheia iliyosema kwamba utie kikumi kila baada ya miaka mitatu,

ukifanya hivyo utapata baraka. Kusudi ya utoaji huo ilikua ipatikane fedha ya kuwasaidia wasiyojiweza. Kama hutoi pia ile baraka huwezi kupata. Kikumi ni yake naye aliamua jinsi itakavyofanya kazi usipoitoa anasema wewe ni mwizi. Sheria ya namna hii iliwatetea watu fulani na ilitoa muongozo kwa watu wapate nja ya kuweza kuwasaidia watu fulani. Siyo sheria inayohukumu, kikumi leo haitumiki kwakazi kama hiyo leo, lakini kikumi inaweza kutusaidia kuwasaidia wanaohitaji.

• Inakua mfano ambayo tunaweza kufuata katika maisha yetu.

Page 12: 7. Sheria za Agano la Kale · Baadhi ya maagizo ya A.K. haiku rudiwa katika A.J. • Tunaweza kuzigawa katika sehemu mbili: • Ya kwanza ni sheria ya usalama na mazingira (Adhabu

SHERIA (TORATI) YA AGANO LA KALE 12Hitimisho, ”Usifanye na ufanye” chache… • Kumbukumbu sita ambazo zitakusaidia katika utekelezaji wako wa sheria......

• 1.Unaposoma torati uione kama maneno ya Mungu kwa ajili yako. Lakini usiione kama amri ya kutoka kwa Mugu kwako.

• 2.Uione kama msingi wa A.K. na pia kama msingi wa historia ya Israeli. Lakini usiione kama sheria ambayo inamlazimisha mkristo kufuata wakati anaishi na kufaidi A.J. na sheria zake.

• 3.Angalia jinsi Mungu ni mkweli, mwaminifu na wa upendo lakini pia jinsi anavyodai mwanadamu awe. Lakini usisahau kwamba neema ya Mungu ni kubwa sawa sawa na madai yake.

• 4.Usidhani kwamba sheria za A.K. zinatosheleza katika kila hali, sivyo ilivyo. Lakini uione kama mfano mzuri wakuangalia na jinsi watu walivyotakiwa kua katika enzi zile.

• 5.Usitegemee kwamba Manabii na A.J. wana dondoa (quote) torati. Lakini amri kumi pamoja na zile mbili zingine zimewekwa kama msingi wetu na zinaonekana katika manabii na pia katika A.J.

• 6.Uione sheria ya A.K. kama zawadi kwa Israeli, ambayo walipoifuata iliwapatia baraka kubwa sana. Usiione kama sheria za kusumbua watu na kuwaondolea uhuru wao katika maisha yao.