6
46 Y enye kuwajibisha kuoga 1- Kutokwa na manii Na manii ni maji meupe, mazito yanatoka kwa kasi wakati wa matamanio, na yana harufu inayofanana na yai lililoharibika, kwa neno lake Mwenyezi Mungu : {Na mkiwa na janaba jitwahirisheni} [5: 6] na neno lake Mtume kumwambia Ali (RA). (Ukimwaga maji oga) (1) . Fadhh almaa: kutoka maji kwa kasi, na makusudio yake ni manii (1) Imepokewa na Abu Daud. Kuoga Kuoga Kuoga kilugha Kueneza maji juu kitu Kuoga kisheria Kueneza maji mwilini kwa namna maalumu kwa kusudia kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu 9 Yaliyomo Maana ya kuoga Yenye kupasisha kuoga 1- Kutokwa na manii 2- Kujamiana 3- Kusilimu kwa kari 4- Kukatika damu ya hedhi 5- kufa Namna ya kuoga Yanayoharamishwa kwa mwenye janaba Kuoga kunakopendekezwa www.fiqhiswahili.com www.fiqhiswahili.com

9 Kuoga  · kumwambia Ali (RA). ... 5- Akiwa na janaba akaoga, kisha akatokwa na manii baada ya kuoga, haimlazimu kuoga tena, kwa kuwa hayo kwa kawaida hutoka bila matamanio

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: 9 Kuoga  · kumwambia Ali (RA). ... 5- Akiwa na janaba akaoga, kisha akatokwa na manii baada ya kuoga, haimlazimu kuoga tena, kwa kuwa hayo kwa kawaida hutoka bila matamanio

46

Yenye kuwajibisha kuoga1- Kutokwa na manii Na manii ni maji meupe, mazito yanatoka kwa kasi wakati wa matamanio, na yana harufu inayofanana na yai lililoharibika, kwa neno lake Mwenyezi Mungu : {Na mkiwa na janaba jitwahirisheni} [5: 6] na neno lake Mtume ملسو هيلع هللا ىلصkumwambia Ali (RA). (Ukimwaga maji oga) (1).

Fadh’h almaa’: kutoka maji kwa kasi, na makusudio yake ni manii

(1) Imepokewa na Abu Daud.

Kuoga

Kuoga

Kuoga kilugha Kueneza maji juu kitu

Kuoga kisheria Kueneza maji mwilini kwa namna maalumu kwa kusudia kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu

9

Yaliyomo

Maana ya kuogaYenye kupasisha kuoga1- Kutokwa na manii2- Kujamiana3- Kusilimu kwa kafiri4- Kukatika damu ya hedhi5- kufaNamna ya kuogaYanayoharamishwa kwa mwenye janabaKuoga kunakopendekezwa

www.fiqh

iswah

ili.co

m

www.fiqhiswahili.com

Page 2: 9 Kuoga  · kumwambia Ali (RA). ... 5- Akiwa na janaba akaoga, kisha akatokwa na manii baada ya kuoga, haimlazimu kuoga tena, kwa kuwa hayo kwa kawaida hutoka bila matamanio

Mlango wa Tohara 47

Maelezo1- Lau mtu aota na asitokwe na manii, basi haimpasi

kuoga. Na yanapotoka baada ya kuamka itamlazimu kuoga.

2- Akikuta manii na asikumbuke kuwa ameota itamlazimu aoge kwa ajili ya kutokwa na manii. Mtume ملسو هيلع هللا ىلص amesema: (Hakika Ulazimu wa kutumia maji unasababishwa na kutokwa na maji) (1), yaani: Kuoga kunalazimu kwa kutokwa na manii.

3- Lau ahisi kuwa manii yanataka kutoka kisha yasitoke, basi haimlazimu kuoga.

4- Lau atokwa na manii kwa hitilafu fulani mwilini mwake au ugonjwa bila ya matamanio, basi hana ulazima wa kuoga.

5- Akiwa na janaba akaoga, kisha akatokwa na manii baada ya kuoga, haimlazimu kuoga tena, kwa kuwa hayo kwa kawaida hutoka bila matamanio. Na kutoka shakani ni kutawadha.

6- Aamkapo usingizini mwenye kulala akapata urutuba(maji maji ya manii) ambao hajui sababu yake, huwa ni moja kati ya hali tatu:

a. Akate kuwa ni manii, na hapo itampasa kuoga, awe akumbuka kuwa ameota au hakumbuki.

b. Akate kuwa si manii, hapo haimpasi kuoga, na hukumu yake ni hukumu ya mkojo.

c. Awe na shaka baina ya kuwa ni manii au si manii. Hapo ni juu yake ajitahidi, akikumbuka chenye kutilia nguvu kuwa ni manii, basi ni manii. Na akikumba chenye kutilia nguvu kuwa ni madhii, basi ni madhii. Na akitokumbuka chochote itamlazimu kuoga kwa kuondoa shaka.

7- Aonapo manii na asikumbuke aliota lini, basi itamlazimu kuoga na kuzirudia Swala usingizi wa mwisho aliyoulala.

(1) Imepokewa na Bukhari na Muslim.

2-Kuundama Nako ni kukutana tupu ya mwanamume na tupu ya mwanamke, kwa kuingia sehemu ya mbele yote ya dhakari kwenye tupu, hata bila ya kushusha manii, kwa kauli ya Mtume ملسو هيلع هللا ىلص: (Tupu ikishapita kwenye tupu, basi kuoga huwa kumeshalazimu)(2).

3- Kafiri kusilimu Kwa kuwa Mtume ملسو هيلع هللا ىلص alimuamuru Qais bin ‘Aswim aliposilimu kuoga (3).

4- Kukatika damu ya hedhi na nifasi Kwa hadithi ya ‹Aishah kwamba Mtume alimwambia Fatimah binti Abi Hubaish ملسو هيلع هللا ىلص(Hedhi ikija acha kuswali, na ikiondoka oga na uswali) (4). Na nifasi ni kama hedhi kulingana na maoni ya wanavyuoni kwa umoja wao.

(2) Imepokewa na Tirmidhi(3) Imepokewa na Abu Daud.(4) Imepokewa na Bukhari na Muslim.

Kuogawww.fi

qhisw

ahili.

com

www.fiqhiswahili.com

Page 3: 9 Kuoga  · kumwambia Ali (RA). ... 5- Akiwa na janaba akaoga, kisha akatokwa na manii baada ya kuoga, haimlazimu kuoga tena, kwa kuwa hayo kwa kawaida hutoka bila matamanio

Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa48 Mlango wa

Tohara

5- Kifo Kwa kauli yake Mtume ملسو هيلع هللا ىلص katika hadithi ya kumuosha binti yake zainab alipokufa: (Muosheni mara tatu, au tano, au zaidi ya hapo mkiona hivyo) (1).

Namna ya kuoga Linalolazimu katika kuoga ni kueneza maji kwenye mwili kwa namna yoyote ile. Lakini inapendekezwa afuate vile Mtume ملسو هيلع هللا ىلص alivyooga, nayo ni kama ilivyoelezwa na Maimunah, Mama wa Waumini aliposema (Mtume aliweka chombo cha maji ya kujitwahirishia na janaba, akajimiminia maji kwenye kitanga cha mkono wa kushoto akitumia kitanga cha mkono wake wa kulia mara mbili au tatu, kisha akaosha tupu yake, kisha akapiga mkono wake kwenye ardhi au ukuta mara mbili au tatu, kisha akasukutua na akapaliza puani, akaosha uso wake na mikono yake, kisha akajimiminia maji kichwani mwake, kisha akaosha mwili wake, kisha akajiweka kando akaosha miguu yake)(2). Asema Maimunah: (Nikamletea kitambaa, hakukitaka, akawa ajifukuta kwa mkono wake). Hivyo basi namna ya kuoga ni:

1- Aoshe vitanga vyake vya mikono, mara mbili au tatu.

2- Aoshe tupu yake.

3- Apige mkono wake kwenye ardhi au ukutani, mara mbili au tatu.

4- Atawadhe kama vile anavyotawadha kuswali, bila ya kupukusa kichwa chake na kuosha miguu yake.

5- ajimiminie maji kichwani.

6- Aoshe mwili wake wote.

7- Ajiweke kando na aoshe miguu yake.

(1) Imepokewa na Bukhari na Muslim.(2) Imepokewa na Bukhari

1

2

3

4

5

www.fiqh

iswah

ili.co

m

www.fiqhiswahili.com

Page 4: 9 Kuoga  · kumwambia Ali (RA). ... 5- Akiwa na janaba akaoga, kisha akatokwa na manii baada ya kuoga, haimlazimu kuoga tena, kwa kuwa hayo kwa kawaida hutoka bila matamanio

49 Mlango wa

Tohara

Kuoga kunakopendekezwa1- Kuoga kwa Ijumaa Kwa kauli ya Mtume ملسو هيلع هللا ىلص: (Mwenye kutawadha kwa ajili ya kwenda Ijumaa, hilo ni jambo zuri, na mwenye kuoga, basi kuoga ni bora) (4)

2- Kuoga wakati wa kuhirimia kwa Umra au Hija: Imepokewa kutoka kwa Zaid bin Thabit kwamba yeye alimuona Mtume ملسو هيلع هللا ىلص akijiondoa na nguo za kawaida kwa ibada ya Hija na akaoga (5)

3 Kuoga baada ya kuosha maiti: Kwa neno la Mtume ملسو هيلع هللا ىلص: (Mwenye kuosha maiti aoge)(6)

4-Kuoga baada ya kila tendo la ndoa imepokewa na Abu Rafi› kwamba Mtume (SAW.) siku moja aliwapitia wake zake, na alikuwa akioga baada ya kumaliza kwa huyu na kwa yule. Mpokeaji asema: (Nikamwambia”Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! usiuoge mara moja? Akasema (SAW “ Hili ni safi zaidi, bora zaidi na twahara zaidi) (7).(4) Imepokewa na Abu Daud.(5) Imepokewa na Tirmidhi(6) Imepokewa na Ibn Majah.(7) Imepokewa na Abu Daud.

Yanayoharamishwa kwa mwenye janaba

1- Kuswali: Kwa neno lake Aliyetukuka: {Enyi mlioamini! Msikaribie Swala hali mmelewa, mpaka myajue mnayo sema, wala hali mna janaba isipo kuwa mmo safarini mpaka muoge}.[ Al-Nisaa 43]

2- Kuitufu Nyumba Tukufu (Alkaba): Kwa neno lake Mtume ملسو هيلع هللا ىلص:

(Kutufu Alkaba ni kama kuswali) (1).

3- Kugusa Msahafu: Kwa neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Hawaigusi isipokuwa waliotwahirishwa} [56: 9]. Na neno la Mtume ملسو هيلع هللا ىلص (Haugusi Msahafu isipokuwa aliye twahara) (2).

4- Kusoma Qur›ani: Imepokelewa kutoka kwa Sayyidna Ali(RA) akisema (alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu akitoka chooni na akitusomea ملسو هيلع هللا ىلصQur’ani, na akila nyama pamoja na sisi. Na hakuwa akizuiliwa na kitu chochote kusoma Qur’ani isipokuwa janaba) (3).

5- Kukaa msikitini isipokuwa kwa mpita njia: Kwa neno lake Aliyetukuka: {Enyi mlioamini! Msikaribie Swala hali mmelewa, mpaka myajue mnayo sema, wala hali mna janaba isipo kuwa mmo safarini mpaka muoge}.[ Al-Nisaa 43](1) Imepokewa na Nasai.(2) Imeipokewa na Malik katika Muwatta’.(3) Imepokewa na Tirmidhi

Kushika Msahafu

Kukaa msikitini

Kutufu Alkaba

Kusoma Qur›ani

Kuswali

(5) Imepokewa na Tirmidhi(6) Imepokewa na Ibn n MaMajMajjahah.ah.(7) Imepokewa na Aa AAbbubu u DDauDauaudd.d.

Kuogawww.fi

qhisw

ahili.

com

www.fiqhiswahili.com

Page 5: 9 Kuoga  · kumwambia Ali (RA). ... 5- Akiwa na janaba akaoga, kisha akatokwa na manii baada ya kuoga, haimlazimu kuoga tena, kwa kuwa hayo kwa kawaida hutoka bila matamanio

Fiqhi ya ‘Ibada yenye picha zilizochorwa50 Mlango wa

Tohara

FAIDA• Si lazima kwa mwanamke kufunguwa nywele zake anapo taka kuoga janaba au hedhi,

Itamtosheleza kujimiminia maji na kuhakikisha kuwa maji yamefika kwenye ngozi ya kichwa.

• inapendekezwa kwa mwanamke anapo oga hedhi au nifasi achukuwe pamba au mfano wake na aiweke misk kisha ajiondoshe athari ya damu.

• Mtu anapo oga janaba inasihi kwake kuswali kwa josho hilo, sawa alitia nia ya kutawadha ama hakutia

www.fiqh

iswah

ili.co

m

www.fiqhiswahili.com

Page 6: 9 Kuoga  · kumwambia Ali (RA). ... 5- Akiwa na janaba akaoga, kisha akatokwa na manii baada ya kuoga, haimlazimu kuoga tena, kwa kuwa hayo kwa kawaida hutoka bila matamanio

51 Mlango wa

Tohara

Makatazo1-kuchelewesha kuoga janaba mpaka utoke wakati wa Swala.

2-kwa mwanamke aliyetwahirika na hedhi kuacha Swala ya wajibu. Na lau atwahirika kabla ya kutoka wakati wa adhuhuri kwa kadiri ya rakaa moja, basi itampasa aoge na aswali adhuhuri. Mtume ملسو هيلع هللا ىلص amesema (Mwenye kuwahi rakaa moja ya asubuhu kabla ya kuchomoza jua, basi amewahi Swala ya asubuhi. Na mwenye kuwahi rakaa moja ya alasiri kabla ya jua kuzama, basi amewahi Swala ya alasiri) (1).

(1) Imepokewa na Bukhari na Muslim.

Kuogawww.fi

qhisw

ahili.

com

www.fiqhiswahili.com