Anzisha Brief

Embed Size (px)

DESCRIPTION

anzisha brief

Citation preview

TAASISI YA SEKTA BINAFSI TANZANIA (TPSF).

MAELEZO KUHUSU TUZO YA ANZISHA. (ANZISHA PRIZE).Tuzo hii ilianzishwa na Chuo cha Uongozi Afrika (African Leadership Academy) cha Afrika kusini kwa lengo la kuwawezesha wajasiriamali vijana barani Afrika kupanua biashara zao ili kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi barani Afrika.Kwa hapa nchini tuzo hii inasimamiwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) ambayo ina jukumu la kuitangaza na kuwahamasisha vijana wajasiriamali wenye umri wa miaka 15-22 kuomba kushiriki katika tuzo hii.Kila mwaka, washindi 12 kutoka nchi mbalimbali barani Afrika hupata nafasi ya kushiriki mafunzo ya wiki mbili ya ujasiriamali katika Chuo cha Uongozi Afrika (ALA) ambapo pia hupatiwa tuzo ya fedha taslim kiasi cha dola za kimarekani 75,000 ambapo kati ya hizo mshindi wa kwanza atajinyakulia dola 25,000 ili kukuza biashara yake ambapo dola 50,000 zinazobaki watagawana washindi wengine 11 waliobaki.Tayari vijana 12 wameingia fainali kuwania tuzo kuu (Grand Award) kwa mwaka 2015 ambao wamepatikana baada ya mchujo wa zaidi ya maombi 500 yaliyoshindanishwa, kati ya hao 12 watanzania wawili Sirjeff Dennis ambaye anafanya biashara ya ufugaji wa kuku na George Mtemahanji anayefanya biashara ya umeme-jua wamefanikiwa kuingia fainali.Tuzo za Anzisha zimelenga kuongeza kasi ya vijana wengi zaidi barani Afrika kupata mwamko wa kuingia katika ujasiriamali ili kuchochea mabadiliko ya kiuchumi barani Afrika.Fomu za maombi ya kushiriki tuzo hii hupatikana kwa lugha za Kiingereza, Kifaransa, Kireno na Kiarabu.Katika kufanikisha zoezi hili timu ya Anzisha itafanya ziara katika nchi rafiki ili kushiriki uhamasishaji kupitia vyombo vya habari.TPSF ni miongoni mwa Taasisi washirika zaidi ya 25 barani Afrika ambazo zinasimamia na kuratibu zoezi la kuhamasisha ushiriki wa vijana katika tuzo hii ya Anzisha.Maombi ya mwaka kesho yataanza kupokelewa Machi 15 - Aprili 15, 2016.Tunawakaribisha vijana wote wenye sifa watume maombi yao.Maombi yatapokelewa kwa njia ya barua za kawaida na barua pepe kupitia anuani zifuatazo:-Senior Programs Manager, Mkurugenzi Mtendaji,African Leadership Academy Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania.Postnet Suite 413,Private Bag X1 NorthCliff 2115S.L.P 11313 Dar Es Salaam.South Africa Email:[email protected]: [email protected]