45
MAOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA? J. C. Ryle (1816-1900) “Kisha Yesu akawapa wanafunzi wake mfano ili kuwaonyesha kuwa yawapasa kuomba pasipo kukata tamaa” (Luka 18:1). Maombi la jambo la muhimu sana katika maisha ya ukristo. Mambo mengine yote kama, kusoma Biblia, kuiheshimu Siku ya Jumapili, kusikiliza mahubiri, kuenda kanisani na hata kula meza ya Bwana, ni mambo ambayo yanakuja baada ya maombi. Haya mambo yote ni ya muhimu sana, lakini maombi ni ya muhimu Zaidi. Kwanza, mtu lazima aombe ikiwa ataokoka. Mtu yeyote asitarajie kuokoka bila kuomba. Ni ukweli kwamba wokovu unapatikana kwa neema pekee na wala si kwa kuomba. Lakini ili mtu apate kuokoka lazima aombe. Katika Biblia hatusomi mahali popote ambapo mtu alipata kuokoka bila kuomba. Hakuna mtu ambaye ataokoka bila kumwomba Yesu Kristo amuokoe. Ni ukweli kwamba hakuna mtu ambaye ataokolewa kwa sababu ya maombi yake, lakini hata hivyo hakuna yeyote ambaye ataokoka bila kuomba. Siku ya mwisho wakristo wote watakusanywa kutoka pembe zote za ulimwengu nao watakuwa kusanyiko moja kubwa sana ambalo hakuna mtu awezaye kuhesabu (Ufunuo 7:9). Kusanyiko hili la watakatifu litaimba nyimbo za kumsifu mwokozi. Nao watapaza sauti zao juu sana zaidi ya sauti za maji mengi.Watakuwa wanaimba kwa sauti moja na kwa moyo mmoja. Nao watakuwa wale ambao walimwamini Yesu Kristo na kuoshwa katika damu Yake. Hao wote watakuwa wamezaliwa mara ya pili na wote watakuwa watu ambao waliomba. Ikiwa tunataka kuimba huko mbinguni pamoja na watakatifu wengine, lazima tuombe wakati tuko hapa ulimwenguni. Ni lazima tujifunze kuomba la sivyo, hatutawahi kuwa miongoni mwa wale ambao watakuwa wakimsifu Mungu huku mbinguni. Kwa ufupi, ni kwamba kukosa kuomba, ni kuwa bila Mungu, bila Kristo,bila neema,bila tumaini na kuikosa mbingu. Inadhihirisha kwamba uko njiani ukielekea Jehanamu.

AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

  • Upload
    others

  • View
    2

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

MAOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA? J. C. Ryle (1816-1900)

“Kisha Yesu akawapa wanafunzi wake mfano ili kuwaonyesha kuwa yawapasa kuomba pasipo kukata tamaa” (Luka 18:1).

Maombi la jambo la muhimu sana katika maisha ya ukristo. Mambo mengine yote kama, kusoma Biblia, kuiheshimu Siku ya Jumapili, kusikiliza mahubiri, kuenda kanisani na hata kula meza ya Bwana, ni mambo ambayo yanakuja baada ya maombi. Haya mambo yote ni ya muhimu sana, lakini maombi ni ya muhimu Zaidi.

Kwanza, mtu lazima aombe ikiwa ataokoka. Mtu yeyote asitarajie kuokoka bila kuomba. Ni ukweli kwamba

wokovu unapatikana kwa neema pekee na wala si kwa kuomba. Lakini ili mtu apate kuokoka lazima aombe. Katika Biblia hatusomi mahali popote ambapo mtu alipata kuokoka bila kuomba. Hakuna mtu ambaye ataokoka bila kumwomba Yesu Kristo amuokoe. Ni ukweli kwamba hakuna mtu ambaye ataokolewa kwa sababu ya maombi yake, lakini hata hivyo hakuna yeyote ambaye ataokoka bila kuomba.

Siku ya mwisho wakristo wote watakusanywa kutoka pembe zote za ulimwengu nao watakuwa kusanyiko moja kubwa sana ambalo hakuna mtu awezaye kuhesabu (Ufunuo 7:9). Kusanyiko hili la watakatifu litaimba nyimbo za kumsifu mwokozi. Nao watapaza sauti zao juu sana zaidi ya sauti za maji mengi.Watakuwa wanaimba kwa sauti moja na kwa moyo mmoja. Nao watakuwa wale ambao walimwamini Yesu Kristo na kuoshwa katika damu Yake. Hao wote watakuwa wamezaliwa mara ya pili na wote watakuwa watu ambao waliomba.

Ikiwa tunataka kuimba huko mbinguni pamoja na watakatifu wengine, lazima tuombe wakati tuko hapa ulimwenguni. Ni lazima tujifunze kuomba la sivyo, hatutawahi kuwa miongoni mwa wale ambao watakuwa wakimsifu Mungu huku mbinguni. Kwa ufupi, ni kwamba kukosa kuomba, ni kuwa bila Mungu, bila Kristo,bila neema,bila tumaini na kuikosa mbingu. Inadhihirisha kwamba uko njiani ukielekea Jehanamu.

Page 2: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

2

Tabia ya maombi ni ishara kuu ya mtu ambaye ameokoka. Watoto wa Mungu wote katika ulimwengu huu, wanafanana, kwa

sababu wao ni watu wa maombi. Wakati wao wanapata uhai wa kiroho, wao huanza kuomba. Kama tu vile mtoto anapozaliwa katika ulimwengu huu, ishara ya kuonyesha kwamba yuko hai, yeye hulia. Vivyo hivyo mtoto wa Mungu ishara kuu katika maisha yake kwamba yeye ni wa Mungu, ni kwamba yeye huomba.

Hii ni mojawapo wa ishara ya wale wote ambao wameokoka, wanaomba mchana na usiku (Luka 18:7). Roho Mtakatifu ambaye anatufanya kuwa viumbe vipya, hutudhihirishia kwamba sisi ni watoto wa Mungu, na anatuwezesha kulia, “Abba, yaani Baba” (Warumi 8:15). Wakati Bwana Yesu Kristo anatuokoa, yeye hutuambia kwamba, “msiwe mabubu tena.” Watoto wa Mungu si mabubu. Maombi ni asili yao mpya kama tu vile mtoto mdogo aliavyo. Wao huona haja yao ya neema na huruma. Wao huhisi uovu wao na dhambi na kwa hivyo wao wanaomba.

Nimesoma katika Biblia kuhusu watu wa Mungu wote, na sijaona mtu ambaye hakuwa mtu wa maombi. Ilikuwa tabia yao kila wakati kumwita Baba yao ambaye ni Mungu, na pia kwamba wao waliliita jina la Kristo Yesu. Biblia inasema kwamba ni tabia ya wale ambao hawajaokoka, kukosa kuomba (1 Petro 1:17; 1 wakorintho 1:2; Zaburi 14:4).

Nimesoma sana kuhusu maisha ya wakristo wengi ambao walikuwa matajiri na wengine walikuwa maskini; wengine walikuwa watu ambao wamesoma sana na wengine walikuwa hawajasoma; wao walitoka katika madhehebu tofauti tofauti na walikuwa na jambo moja ambalo lilifahamika miongoni mwao na hilo ni, wao walikuwa watu wa maombi.

Pia tunapaswa kujua kwamba kuna wengi ambao wanaomba, lakini maombi yao haitoki katika mioyo yao. Pia tunapaswa kujua kwamba maombi hayamaanishi kwamba mtu huyu ni mtakatifu kwa sababu kuna wengi ambao wanaomba lakini hawajaokoka, maombi yao ni maneno matupu maskioni mwa Mungu.

Kukosa kuomba ni ishara kwamba mtu hajaokoka. Huyu ni mtu ambaye hahisi dhambi zake na yeye hampendi Mungu. Yeye hawezi kutamani utakatifu na yeye hana tamaa ya mbinguni, na yeye hajazaliwa mara ya pili. Hata kama mtu huyu anaweza kudai kuelewa mafundisho ya kweli ya Biblia. Kwa mfano, anaweza kuamini kwamba Mungu ndiye aliwachagua wote ambao wanaokoka, wokovu ni kwa

Page 3: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

Maombi ya wale ambao wameokoka 3

neema, ni kwa imani tu ndani ya Kristo mtu anaokolewa na anapata tumaini la kweli la mbinguni. Ukweli ni kwamba ikiwa mtu huyu haombi, haya yote anaamini hayamsaidii.

Ishara ya kazi ya Roho mtakatifu katika maisha ya mtu ni kwamba mtu huyo anaomba. Mtu anaweza kufanya mambo mengi sana. Kwa mfano mtu anaweza kuwa anajua kuzungumza vizuri sana, na pia anaweza kuandika vitabu vizuri sana, lakini awe kama Yuda Iskariote ambaye hakuwa ameokoka. Mtu hawezi kuomba kwa kweli ikiwa yeye hajaokoka. Mojawapo wa ishara ambazo Mungu ameweka katika maisha ya yule ambaye ameokoka ni kwamba mtu huyo, ni mtu wa maombi. Wakati Mungu alipomtuma Anania kwa Sauli alimwambia, “..kwa maana wakati huu anaomba” (Matendo 9:11). Ninajua kwamba wale ambao wameokoka, ni wale ambao Mungu aliwachagua kabla ya kuiweka misingi ya ulimwengu. Pia ninajua kwamba ni Roho Mtakatifu ambaye anawaongoza kuja kwa Kristo Yesu. Hakuna mtu ambaye anaweza kumfanya mwingine afanywe mwenye haki mbele za Mungu ikiwa mtu huyu hataamini. Hakuna mtu ambaye anaamini, na awe haombi. Ishara ya kwanza ya imani ni kuomba Mungu. Imani ndio maisha ya nafsi. Maombi ni kudhihirishi imani kama tu vile pumzi inadhihirisha uhai ndani ya mtu. Haiwezekani kwamba mtu ambaye ameokoka, ni mtu ambaye haombi. Ikiwa umeokoka, lazima wewe utakuwa mtu wa maombi, unapenda kuzungumza na Mungu, ambaye ni Baba wako.

JE, MAOMBI YA KWELI NI MAOMBI YA

AINA GANI? John Bunyan (1628-1688)

Maombi ni kuzungumza maneno ambayo yanaeleweka kwa Mungu kutoka ndani ya mioyo yetu, tukikiri kwa imani ahadi zake ambazo zinapatikana katika Neno Lake, kupitia kwa Yesu Kristo, tukiwa tunaongozwa na Roho Mtakatifu. Maombi yanaombwa tu, kwa uzuri wa kanisa la Mungu kwa unyenyekevu katika imani na kwa mapenzi ya Mungu.

Katika ufafanuzi huu kuhusu maombi, kuna mambo saba.

Page 4: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

4

a). Maombi ni jambo ambalo linatoka moyoni mwa mtu. b). Maombi ni kuzungumza Kutoka ndani ya moyo wako c). Maombi ni Kuzungumza na Mungu maneno ambayo yanaeleweka

kutoka ndani ya moyo wako. d). Maombi ni kuzungumza na Mungu kutoka ndani ya moyo wako

kupitia kwa Kristo tukisaidiwa na Roho Mtakatifu. e). Maombi ni kuzungumza na Mungu kulingana na neno Lake. f). Maombi yanapaswa kuombwa kwa uzuri wa kanisa g). Maombi yanaombwa kwa unyenyekevu kwa imani na kwa

mapenzi ya Mungu.

a). Maombi ni jambo ambalo linatoka moyoni mwa mtu. Kufanya mambo kutoka katika moyo ni jambo ambalo

linamfurahisha Mungu sana. Ikiwa hatutafanya mambo ya Mungu kwa mioyo yetu yote, basi ni wazi kwamba hatutamfurahisha Mungu kamwe. Daudi anazungumza kuhusu jambo hili na kusema, “Ninamlilia kwa kinywa changu, sifa zake zilikuwa katika ulimi wangu” (Zaburi 66:17). Maombi ambayo yanaombwa na hayatoki katika moyo wa mtu, Mungu hayakubali kamwe. Biblia inasema, “Ee Mungu, uniweke salama kwa maana kwako nimekimbilia. Nilimwambia BWANA, “Wewe ndiwe Bwana wangu; pasipo wewe sina jambo jema.” Kwa habari ya watakatifu walioko duniani, ndio walio wa fahari ambao ninapendezwa nao. Huzuni zitaongezeka kwa wale wanaokimbilia miungu mingine. Sitazimimina sadaka zao za damu au kutaja majina yao midomoni mwangu” (Zaburi 16:1-4). Mungu anaendelea kusema katika neno lake kwamba, “Kisha mtaniita na mtakuja na kuniomba, nami nitawasikiliza. Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote” (Yeremia 29:12-13). Kwa sababu ya kutoomba kutoka kwa mioyo yao, Mungu alikataa maombi ya wengi: “Hawanililii mimi kutoka mioyoni mwao, bali wanaomboleza vitandani mwao. Hukusanyika pamoja kwa ajili ya nafaka na divai mpya, lakini hugeukia mbali nami” (Hosea 7:14). Ni unafiki kuonekana kwamba mtu anaomba ilhali katika moyo wake haombi kabisa. Jambo la kuzungumza kutoka katika mioyo yetu ni jambo ambalo Kristo aliliona katika Nathanieli wakati alipokuwa chini ya mti: “Tazama ni mwisraeli kweli kweli, hana hila ndani yake” (Yohana 1:47). Wale wote ambao wanaomba kutoka katika mioyo yao, wao humpendeza Mungu sana: “Bwana huchukia sana dhabihu za waovu, bali maombi ya wanyofu humfurahisha Mungu” (Mithali 15:8).

Page 5: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

Maombi ya wale ambao wameokoka 5

Je, ni kwa nini tunapaswa kuomba kutoka katika mioyo yetu? Ni kwa sababu hali hii inawezesha moyo kumlilia Mungu bila unafiki wowote na bila uoga wowote: “Hakika nimeyasikia maombolezo ya Efraimu: Ulinirudi kama ndama mkaidi, nami nimekubali kutii” (Yeremia 31:18). Maombi ambayo yanatoka katika moyo, ni maombi ambayo hayabadiliki katika hali yoyote. Mtu akiwa peke yake ataomba na hata akiwa mbele za wengine pia ataomba. Mtu kama huyu haombi kwa sababu ya kuwafurahisha watu au kwa sababu aonekane yeye ni mtu wa maombi. Yeye huomba kwa sababu anapenda na anajua kwamba Mungu wake anamsikia na atajibu. Mungu huwa anatazama ndani ya moyo, na humo ndimo maombi ya kweli yanafaa kutoka.

b). Maombi ni kuzungumza na Mungu maneno ambayo yanaeleweka kutoka ndani ya moyo wako.

Maombi si kuzungumza-zungumza tu maneno matupu kama wengi wanavyowaza na kufanya. Maomba yanapaswa kueleweka kwa sababu yule ambaye anaomba anajua ni mambo gani ambayo anayaombea. Maombi ya aina hii, yanatambua dhambi, hushukuru kwa sababu ya neema ya Mungu na kuomba msamaha kutoka kwa Mungu.

i). Mtu ambaye anaomba, yeye huomba ahurumiwe kwa sababu anajua hatari ya dhambi zake.

Nafsi yake inahisi dhambi na kwa sababu hiyo, yeye anamlilia Mungu kwa ajili ya huruma wake na msamaha wa dhambi zake. Mtu anaomba kwa sababu anajua uzito na huzuni ambao umeletwa na dhambi (Isaya 1:10 Zaburi 69:3). Daudi aliomba na akamlilia Mungu, akadhofika na kupondwa kabisa, alisononeka kwa maumivu makuu moyoni na moyo wake ulipigapiga (Zaburi 38:8-10). Hezekia alilia kama korongo (Isaya 38:14). Efraimu aliomboleza (Yeremia 31:18). Petro alilia sana (Mathayo 26:75). Yesu Kristo alilia kwa machozi (Waebrania 5:7).

Hii yote inatokana na kujua kwamba Mungu ni mwenye haki, sisi ni wenye hatia mbele za Mungu na tunastahili jahanum ni mahali pa mateso na uangamizi. Daudi aliomba akisema, “Kamba za mauti zilinizunguka, maumivu makuu ya kuzimu yalinipata, nikalemewa na taabu na huzuni. Ndipo nikaliita jina la BWANA: “Ee BWANA, niokoe”( Zaburi 116:3-4). Pia aliomba, “Nilipokuwa katika taabu, nilimtafuta BWANA, usiku nilinyosha mikono bila kuchoka na nafsi yangu ilikataa kufarijiwa” (Zaburi 77:2). Tena aliomba akisema, “Nimeinamishwa chini na kushushwa sana, mchana kutwa nazunguka

Page 6: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

6

nikiomboleza” (Zaburi 38:6). Katika hali hizi zote, unaona kwamba maombi yanaombwa kwa njia ambayo inaeleweka. Yaani wanaomba wakielewa kile wanaomba na hali ambayo wako ndani wakati wanakuja katika maombi.

ii. Wale wanaomba wanahurumiwa, hufarijiwa, hupewa nguvu na kuhimizwa.

Daudi anaomba akimbariki, kumsifu na kumtamani Mungu kwa ajili ya rehema zake kwa wenye dhambi: “Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, vyote vilivyomo ndani yangu vilihimidi jina lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, wala usisahau wema wake wote, akusamehe dhambi zako zote, akuponya magonjwa yako yote, aukomboa uhai wako na kaburi, akuvika taji ya upendo na huruma, atosheleza mahitaji yako kwa vitu vyema, ili ujana wako uhuishwe kama wa tai” (Zaburi 103:1-5). Haya ni maombi ya watu wa Mungu ambayo kwa wakati mwingine huwa yanageuka na kuwa wimbo wa sifa kwa Mungu. Biblia inasema kwamba, “Msijisumbue kwa jambo lolote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu” (Wafilipi 4:6). Kumshukuru Mungu kwa ajili ya huruma wake ni maombi ambayo yanamfurahisha Mungu sana na yanafaa.

iii. Wale wanaomba, wao huomba wakitarajia kuhurumiwa. Biblia inasema, “Ee BWANA mwenye nguvu zote, Mungu wa Israeli,

umelifunua hili kwa mtumishi wako, ukisema, ‘Nitakujengea nyumba’ Hivyo mtumishi wako amepata ujasiri kukuletea dua hii” (2 Samweli 7:27). Hili liliwafanya, Yakobo, Daudi, Danieli na wengine kumlilia Mungu kwa sababu walijua Mungu alikuwa tayari kuwapa mahitaji yao. Pia Mungu alikuwa tayari kuwasamehe dhambi (Mwanzo 32:10-11; Danieli 9:3-4).

c). Maombi ni Kuzungumza na Mungu kutoka ndani ya moyo wako. Katika maombi ya kweli, kuna nguvu, uzima na upendo: “Kama vile

paa aoneavyo shauku vijito vya maji, ndivyo nafsi yangu ikuoneavyo shauku, Ee Mungu” (Zaburi 42:1); “Tazama jinsi ninavyoonea shauku mausia yako! Hifadhi maisha yangu katika haki yako” (Zaburi 119:40); “Ee BWANA, ninatamani wokovu wako, na sharia yako ni furaha yangu” (Zaburi 119:174); ‘Nafsi yangu inatamani sana, naam, hata kuona shauku, kwa ajili ya nyua za BWANA; moyo wangu na mwili wangu vinamlilia Mungu Aliye Hai” (Zaburi 84:2); ‘Nafsi yangu inataabika kwa shauku kubwa juu ya sharia zako wakati wote” (Zaburi

Page 7: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

Maombi ya wale ambao wameokoka 7

119:20). Katika kitabu cha Danieli tunasoma, “Ee BWANA, sikiliza! Ee, BWANA samehe! Ee, BWANA sikia na ukatende! Kwa ajili yako, Ee Mungu wangu, usikawie, kwa sababu mji wako na watu wako wanaitwa kwa Jina lako” (Danieli 9:19). Yakobo anaita maombi haya kuwa, maombi yenye nguvu na yanafaa sana. Tunasoma katika Luka kwamba, “Naye akiwa katika maumivu makuu, akaomba kwa bidii” (Luka 22:44). Yesu Kristo alijua kwamba ni Mungu pekee ambaye angempa nguvu na uwezo wa kuvumilia msalaba. Wamebarikiwa sana na wanabarikiwa sana wale wote ambao wanaomba maombi ya aina hii.

Lakini jambo la huzuni ni kwamba kuna wengi leo ambao wanaomba, lakini maombi yao si yenye nguvu na kwamba pia hayafai. Wengine wao wengi maombi yao hayatoki katika mioyo yao na hayazingatii ukuu wa Mungu na huruma zake kwetu wenye dhambi. Watu kama hawa wanatosheka tu na maneno machache ambayo wanayarudia mara kwa mara. Ni wakati ambapo tunaomba kutoka kwa mioyo yetu na kukizingatia ukuu wa Mungu na huruma zake kwetu, ndipo nafsi zetu zitajengwa na Kristo kutukuzwa. Ni katika maombi watakatifu wamemaliza muda wao mwingi wakihakikishwa kwamba wanabarikiwa na Mungu (Zaburi 69:3; 38:10; Mwanzo 32:24,26).

Wengi hawaombi jinsi inanwapasa kwa sababu ya kupuuza na kukosa tamaa ya utakatifu katika maisha yao. Wengi wao wako na tamaa ya kufuata dini lakini si tamaa ya kuomba jinsi wanapaswa. Wengi wao pia hawajui mtu ameokoka ni mtu wa aina gani. Pia hawajui kuwa na ushirika na Mungu baba kupitia kwa Kristo Yesu na kuwa na nguvu za utakaso katika moyo wa mtu inamaanisha nini. Hata kama wao wanaomba, wao bado wanaishi maisha ambayo yamelaaniwa, maisha ya ulevi, ya zinaa ambayo ni chukizo kwa Mungu. Maisha yao yamejawa na chuki, wivu, masengenyo na kuwatesa watoto wa Mungu. Wao hawajui hatari ambayo wako ndani yake. Hukumu ya Mungu inakuja juu yao. Maombi yao yote ambayo wanaomba hayatawasadia wakati wa hukumu ya Mungu.

Maombi ni kumsifu Mungu, kumlilia Mungu kwa ajili ya dhambi zetu na kuleta mahitaji yetu yote mbele zake, kutoka kwa mioyo yetu. Daudi anasema kwamba, “Ee BWANA, yote ninayoyaonea shauku yako wazi mbele zako, kutamani kwangu sana hakufichiki mbele zako” (Zaburi 38:9). Pia Daudi anaomba akisema kwamba, “Nafsi yangu inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye Hai. Ni lini nitaweza kwenda kukutana na Mungu?..Vitu hivi ninavikumbuka ninapoimimina nafsi yangu: Jinsi nilivyokuwa nikienda na umati wa watu..” (Zaburi 42:2,4). Daudi anasema, anaimimina nafsi yake. Hili ni dhihirisho kwamba,

Page 8: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

8

kupitia kwa maombi, tunaunganishwa na nguvu za Mungu. Biblia inasema kwamba, “Enyi watu, mtumainini yeye, wakati wote, mmiminieni yeye mioyo yenu, kwa kuwa Mungu ni kimbilio letu’ (Zaburi 62:8). Hili ndilo ombi ambalo Mungu ameahidi kwamba atamwokoa yule ambaye amefanywa kuwa mtumwa na dhambi na shetani: “Lakini kama mtamtafuta BWANA Mungu wenu, mtampata kama mtamtafuta kwa moyo wenu wote na kwa roho yote” (Kumbukumbu la Torati 4:29).

Tena tunaona kwamba maombi ni kuumimina moyo wako wote mbele ya Mungu. Hii pia inatuonyesha umuhimu wa maombi. Maombi ni kwa Mungu pekee. Biblia inasema kwamba, “Nafsi yangu inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye hai. Ni lini nitaweza kwenda kukutana na Mungu? (Zaburi 42:2). Ni ukweli kwamba mtu ambaye anaomba kwa kweli kwa moyo wake wote, yeye huona vitu vya hapa ulimwenguni vikiwa ni bure na ni katika Mungu pekee nafsi yake inapata pumzisho la kweli na kutosheka. Biblia inasema, “Mwanamke ambaye ni mjane kweli kweli, yaani, yeye aliyebaki peke yake, huweka tumaini lake kwa Mungu naye hudumu katika maombi usiku na mchana, akimwomba Mungu ili amsaidie” (1 Timotheo 5:5). Daudi anasema naye, ‘Ee BWANA, nimekukimbilia Wewe, Usiniache nikaaibika kamwe. Kwa haki uniponye na kuniokoa, unitegee sikio lako uniokoe. Uwe mwamba wa kimbilio, mahali nitakapokimbilia kila wakati; toa amri ya kuniokoa, kwa kuwa wewe, ni mwamba wangu na ngome yangu. Ee Mungu wangu niokoe kutoka kwenye mkono wa mwovu, kutoka kwenye makucha ya watu wabaya na wakatili. Ee BWANA mwenyezi, kwa kuwa umekuwa tumaini langu, tegemeo langu tangu ujana wangu” (Zaburi 71:1-5). Wengi huzungumza kumhusu Mungu, lakini maombi ya kweli humfanya Mungu awe ndiye tumaini, ngome na kila kitu katika kila hali. Maombi ya kweli huwa haizingatii jambo jingine lolote isipokuwa utukufu wa Mungu. Hili ndilo ombi la kweli ambalo lafaa.

Ikiwa maombi hayaombwi kupitia kwa Kristo Yesu, basi hayo si maombi kwa Mungu. Kristo ndiye njia ambapo tunapata kuwa na kibali mbele za Mungu. “nanyi mkiomba lo lote kwa jina Langu, hilo nitalifanya, ili Baba apate kutukuzwa katika Mwana. Kama mkiomba lo lote, kwa Jina Langu, nitalifanya” (Yohana 14:13-14). Hii ndio njia ambayo Danieli alitumia wakati alikuwa anawaombea watu wa Mungu. Yeye aliwaombea katika Jina la Kristo: “Basi Mungu wetu, sasa sikia maombi na dua ya mtumishi wako. Ee Bwana, kwa ajili yako tuangalie kwa huruma ukiwa ma mahali pako patakatifu” (Danieli 9:17). Daudi

Page 9: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

Maombi ya wale ambao wameokoka 9

naye aliomba, “Ee BWANA,kwa ajili ya jina lako, unisamehe uovu wangu, ijapokuwa ni mwingi” (Zaburi 25:11). Hii sasa haimaanishi kwamba kila mtu ambaye analitaja jina la Kristo, anaomba kwa Mungu. Kuja mbele za Mungu kupitia kwa Kristo ndilo jambo ambalo si rahisi kwa kila mtu. Mtu anaweza kweli kuwa anaomba kwa moyo wake wote, lakini awe haombi kupitia kwa jina la Kristo. Mtu ambaye anakuja kwa Mungu kupitia kwa Kristo, lazima amtambue Kristo: “..kwa ye yote anayemjia Mungu lazima aamini kwamba yeye yupo na kuwa huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii” (Waebrania 11:6). Kwa hivyo yule ambaye anakuja kwa Mungu kupitia kwa Kristo ni lazima awe amewezeshwa kumjua Kristo: “Ikiwa umependezwa nami, nifundishe njia zako ili nipate kukujua, nami nizidi kupata kibali mbele zako” (Kutoka 33:13).

Hakuna mtu ambaye anaweza kumjua Kristo asipofahamishwa na Mungu Baba (Mathayo 11:27). Kuja kwa Mungu kupitia kwa Kristo ni kuwezeshwa na Mungu Baba kuwa ndani ya Kristo (Mathayo 16:16). Kwa sababu hiii, Daudi anamwita Kristo kuwa ngao yake, mwamba wake imara na mnara wake (Zaburi 18:2; 27:1; 28:1). Daudi hasemi hivyo kwa sababu ni kupitia kwa Kristo yeye aliwashinda adui wake, bali pia ni kwa sababu kupitia kwa Kristo Yesu, yeye alipata kukubalika na Mungu Baba. Mungu alimwambia Abraham, “Usiogope Abramu. Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana” (Mwanzo 15:1). Kwa hivyo mtu ambaye anakuja kwa Mungu kupitia kwa Kristo, lazima awe amemwamini Kristo kwa ajili ya wokovu wake. Yule ambaye yuko na Imani ndani ya Kristo, Biblia inasema kwamba yeye amezaliwa na Mungu na sasa yeye ameunganishwa kwa Kristo na yuko ndani ya Kristo (Yohana 3:5,7; 1:12). Kwa hivyo kwa sababu sasa yeye yuko ndani ya Kristo, sasa anaweza kuja kwa Mungu, kwa sababu sasa Mungu anamtazama mtu huyu akiwa na Kristo na katika Kristo. Yeye sasa ni mmoja wa mwili wa Kristo, ambaye ameunganishwa kwa Kristo kwa sababu Mungu alimchagua, akamwokoa na sasa yuko na Roho Mtakatifu katika moyo wake ambaye Mungu amempa (Waefeso 5:30). Wakati mtu huyu anakuja kwa Mungu, haji kwa nguvu zake, bali kwa nguvu za Kristo, kazi ya Kristo ikiwa ndio msingi wa kukubalika kwake mbele za Mungu (Waefeso 1:6). Anapokuja kwa Mungu katika maombi, yeye husaidiwa na Roho Mtakatifu kuomba.

d). Maombi ni kuzungumza na Mungu kutoka ndani ya moyo wako kupitia kwa Kristo tukisaidiwa na Roho Mtakatifu.

Page 10: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

10

Mambo ambayo tunayataja hapa ni mambo ambayo yote lazima yawe pamoja ikiwa maombi ambayo tutaomba yatakubalika na Mungu. Haijalishi mtu anazungumza maneno ya aina gani na ni mangapi, ikiwa maombi yake, si kupitia kwa Kristo na haongozwi na Roho Mtakatifu, basi maombi yake hayatasikilizwa na Mungu. Wao watakuwa kama watoto wa Haruni ambao walitumiwa moto mbaya na waliuawa na Mungu (Walawi 10:1-2).

Maombi ambayo hayaongozwi na Roho Mtakatifu, hayo hayaombwi kulingana na neno la Mungu (Warumi 8:26-27). Hakuna mtu au kanisa ambalo linaweza kuja kwa Mungu kwa maombi bila usaidizi wa Roho Mtakatifu. Biblia inasema kwamba, “Kwa maana kwa kupitia Kwake, sisi sote tunaweza kumkaribia Baba katika Roho mmoja” (Waefeso 2:18). Pia Biblia inaendelea kusema kwamba, “Vivyo hivyo, Roho hutusaidia katika udhaifu wetu, kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo. Lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu usioweza kutamkwa. Naye Mungu aichunguzaye mioyo, anaijua nia ya Roho, kwa sababu Roho huwaombea watakatifu sawasawa na mapenzi ya Mungu” (Warumi 8:26-27). Biblia inatuonyesha kwamba mwanadamu hawezi akajileta peke yake mbele za Mungu. Lazima amtegemee Roho Mtakatifu.

Mungu aliwatumia mitume kueneza ujumbe wa injili kwa watu wote lakini hata katika maandishi ya Biblia, Paulo anaandika akisema kwamba, hatujui kuomba ipasavyo, Paulo pia akiwa mmoja wa wale ambao anasema kwamba hawajui kuomba. Mitume hawa pia walikuwa wanadamu kama tu wanadamu wengine, na kwa hivyo walipungukiwa katika mambo mengi kama tu wanadamu wengine. Njia za neema ya Mungu katika maisha ya watu wake, ndizo njia ambazo Paulo na mitume wengine walitumia. Wao walikuwa wamepewa karama za kumtumikia kama tu Mungu amewapatia karamu wengine. Lakini hata hivyo, wao pia walisaidiwa kuomba na Roho Mtakatifu.

Hatujui jinsi ya kuomba, mambo ambayo tunapaswa kuyaombea au njia ambayo tunapaswa kutumia wakati tunaenda mbele za Mungu. Wakati mwingi tunachanganyikiwa kama tuombe juu ya Imani au neema au utakatifu. Huwa hatujui ni lipi tunafaa kuliombea. Lakini kwa nguvu na uwezo Roho Mtakatifu, tunawezeshwa kuomba jinsi tupasavyo. Biblia inasema kwamba, “Kwa maana ni nani anayejua mawazo ya mtu isipokuwa roho iliyo ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo hakuna mtu ajuaye mawazo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu” (1 Wakorintho 2:11). Mstari huu unazungumza juu ya mambo ya kiroho ambayo ulimwengu hautambui kamwe (Isaya 29:11).

Page 11: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

Maombi ya wale ambao wameokoka 11

Hatuwezi kuomba bila kusaidiwa na Roho Mtakatifu kwa sababu hatujui hata jinsi tunapaswa kuomba. Biblia inasema, “hatujui kuomba ipasavyo. Lakini Roho mwenywe hutuombea kwa uchungu usioweza kutamkwa.” Mitume pia wao hawakuweza kutekeleza jukumu hili kama tu vile leo pia hatuwezi kulitekeleza bila kusaidiwa na Roho Mtakatifu. Wakati Roho Mtakatifu aliwasaidia mitume kuomba, wao walitamka maneno kwa uchungu usioweza kutamkwa.

Pia tunasoma kwamba, “hatujui kuomba ipasavyo.” Wengi hawajaelewa maana ya maneno haya na kwa sababu hii wametunga mbinu tofauti tofauti za kuomba kama vile Yeroboamu alivyofanya (1 Wafalme 12:26-33). Ili tuweze kuomba jinsi inavyotupasa, hatuwezi kubuni mbinu fulani fulani za wanadamu au za malaika jinsi wengi wanavyodai. Bali tunapaswa kumtegemea tu Roho Mtakatifu. Kile mwanadamu anaweza kubuni ni mawazo yake na wala si kile ambacho ameambiwa afanye katika neno la Mungu.

Yakobo anasema, “Mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya, ili mpate kuvitumia hivyo mtakavyopata kwa tamaa zenu” (Yakobo 4:3). Si maneno mengi ambayo yatamfanya Mungu ajibu ombi la mtu. Wakati tunapoomba, Mungu huchunguza nia ya maombi yetu ambayo tunaleta mbele zake (1 Yohana 5:14). Biblia inasema kwamba, “Naye Mungu aichunguzaye mioyo, anaijua nia ya Roho, kwa sababu Roho huwaombea watakatifu sawasawa na mapenzi ya Mungu” (Warumi 8:27). Mungu anasikiliza tu maombi ambayo yanaombwa kulingana na mapenzi yake pekee. Ni Roho Mtakatifu pekee ambaye anaweza kutusaidia kuomba kulingana na mapenzi ya Mungu. Haijalishi tumejifundishwa kuomba kwa njia gani, au ni vitabu gani ambavyo tumesoma kuhusu maombi, ikiwa hatutaomba tukiongozwa na Roho Mtakatifu, basi ni wazi kwamba hatutaomba kulingana na mapenzi ya Mungu. Kwa hivyo Mungu hatayasikia maombi yetu.

e). Maombi ni kuzungumza na Mungu kulingana na neno Lake. Maombi yanakuwa ya kweli na ya hakika wakati mtu anapoomba

kulingana na neno la Mungu. Ikiwa mtu haombi kulingana na neno la Mungu, basi yeye anapiga tu kelele. Daudi katika maombi yake kila wakati alilikumbuka neno la Mungu: “Nimelazwa chini mavumbini, yahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako” (Zaburi 119:25). Pia unaweza soma mistari hii, 41-42,58,65,74,81-82, 107,147,154,169,170). Pia Daudi aliomba kwamba, “Kumbuka neno lako kwa mtumishi wako, kwa sababu umenipa tumaini” (Zaburi 119:49). Roho Mtakatifu hafanyi kazi yake bila neno la Mungu. Yeye hutumia neno la Mungu

Page 12: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

12

kumshawishi mkristo aende mbele za Mungu na kumlilia katika maombi. Ni Roho Mtakatifu ambaye alimwezesha Danieli kukumbuka kwamba siku za utumwa za Waisraeli zilikuwa zimefika mwisho na kwa hivyo, aliomba, “..mimi Danieli, nilielewa kutokana na Maandiko, kulingana na neno la BWANA alilopewa nabii Yeremia, kwamba ukiwa wa Yerusalemu ungetimizwa kwa miaka sabini. Kwa hivyo nikamgeukia BWANA Mungu na kumsihi katika maombi na dua, katika kufunga, kuvaa nguo ya gunia na kujipaka majivu” (Danieli 9:2-3).

Roho Mtakatifu anapotuongoza katika maombi yetu, huwa anatuwezesha kuomba kulingana na neno la Mungu na ahadi za Mungu. Bwana Yesu Kristo aliomba kulingana na neno la Mungu na ahadi za Mungu: “Je, unadhani siwezi kumwomba Baba yangu naye mara moja akaniletea Zaidi ya majeshi kumi na wawili ya malaika? Lakini je, Maandiko yatatimiaje yale yasemayo kwamba ni lazima itokee hivi?” (Mathayo 26:53-54). Ni ukweli kwamba yale Kristo alisema mbeleni yalikuwa katika maandiko, lakini pia alizingatia kukamilika kwa maandiko.

Roho Mtakatifu lazima atuongoza kulingana na neno la Mungu jinsi tunapasavyo kuomba. Biblia inasema, “Nifanyeje basi? Nitaomba kwa Roho lakini nitaomba kwa akili ya pia” (1 Wakorintho 14:15). Lakini tufahamu kwamba hakuna kuelewa bila neno la Mungu. Kwa kuwa neno la Mungu likikataliwa, basi hiyo hekima uliyo nayo itakuwa na namna gani? (Yeremia 8:9).

f). Maombi yanapaswa kuombwa kwa uzuri wa kanisa. Hii inadhihirisha kwamba maombi yanapaswa kuomba kwa utukufu

wa Mungu. Mungu, Kristo na watu wake wako pamoja. Kama tu vile Kristo na Mungu Baba ni kitu kimoja, vivyo hivyo wale ambao wameokoka wako ndani ya Kristo na yeyote ambaye anawatesa watu wa Mungu, huwa anamtesa Kristo mwenyewe (Matendo 9:5). Kwa hivyo Biblia inatuhimiza kwamba tuombee amani ya mji wa Yerusalemu, yaani kanisa la Kristo wakati tunapokuwa unaombea chochote ambacho unakihitaji. Kanisa halitawahi kuwa na amani kamili hadi lifike mbinguni mahali ambapo Kristo anataka liwe. Mbinguni ndipo mahali Mungu amekusudia kanisa lake liwe. Kwa hivyo ni lazima tuombe kwamba kanisa litakuwa na amani na kwamba litaendelea kwa uzuri. Wale wote ambao wanaliombea kanisa, wanaombea watu wake Kristo. Yeyote ambaye anaombea kanisa, anapaswa kuomba kwamba neema ya Mungu itaongezeka katika kanisa na kwamba kanisa litakua katika

Page 13: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

Maombi ya wale ambao wameokoka 13

neema. Pia tunapaswa kuomba kwamba kanisa litashinda majaribu yake yote na kwamba Mungu atalisaidia kanisa katika majukumu yake hapa ulimwenguni. Pia tuombe kwamba kila kitu katika kanisa kitafanyika kwa uzuri wa kanisa na watu wake. Tuombe kwamba Mungu atatulinda katika utakatifu tunapoendelea kuishi miongoni mwa watu waovu (Wafilipi 2:15). Hivi ndivyo Kristo alivyoomba katika Yohana 17. Paulo pia aliomba hivi: “Haya ndio maombi yangu kwamba upendo wenu uongezeke zaidi na zaidi katika maarifa na ufahamu wote, ili mpate kutambua yale yaliyo mema, mkawe safi, wasio na hatia hadi siku ya Kristo, mkiwa mmejawa na matunda ya haki yapatikanayo kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa za Mungu” (Wafilipi 1:9-11). Hili ni ombi fupi sana. Lakini unapolisoma unaona kwamba limejawa na shauku ya kuona kwamba kanisa linaendelea vyema kiroho hadi kuja kwa Kristo Yesu (Waefeso 1:16-21; 3:14-19; Wakolosai 1:13).

g). Maombi yanapaswa kuombwa kwa unyenyekevu chini mapenzi ya Mungu.

Maombi haya yanaombwa kwamba mapenzi ya Mungu yafanyike jinsi Kristo ametufundisha katika Mathayo 6:10. Watu wote wa Mungu tunapaswa kunyenyekea na kuomba kulingana na mapenzi ya Mungu. Tunapaswa kila wakati kuwa tayari kufahamu na kukubali kwamba Mungu atende jinsi inavyomfurahisha na kwa hekima yake. Hata wakati tunanyenyekea hivyo, hatufai kuwa na shaka kwamba Mungu hatayajibu maombi yetu. Bali tunapaswa kujua kwamba Mungu atajibu kwa utukufu wake na kwa uzuri wetu. Kwa hivyo tusiwe na shaka juu ya upendo na ukarimu wa Mungu kwetu. Tuwe waangalifu tusije tukajaribiwa na shetani kuomba maombi ambayo hayamletei Mungu utukufu wala kwa sababu ya uzuri wa kanisa lake. Biblia inasema kwamba, “Huu ndio ujasiri tulio nao tunapomkaribia Mungu, kwamba kama tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atatusikia. Na kama tunajua ya kuwa atatusikia, lo lote tuombalo, tunajua ya kwamba tumekwisha kupata zile haja tulizomwomba” (1 Yohana 5:14-15). Hivi ikiwa tutaomba tukiongozwa na Roho Mtakatifu. Tunapaswa kukumbuka kila wakati kwamba, chochote tunachokiomba, ikiwa hatuongozwi na Roho Mtakatifu, basi tujue kwamba Mungu hatasikia maombi yetu. Kwa sababu ni Roho Mtakatifu ambaye anatuongoza kuomba kulingana na mapenzi ya Mungu. Biblia inasema kwamba, “Kwa maana ni nani anayejua mawazo ya mtu isipokuwa roho iliyo ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo hakuna mtu ajuaye mawazo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu” (1 Wakorintho 2:11).

Page 14: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

14

MAOMBI NI NGUVU ZA MAOMBI KWA

WATU WAKE Eugene Bradford (1915-2010)

“Siku zote tunamshukuru Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, tunapowaombea ninyi, kwa sababu tumesikia juu ya Imani yenu katika Kristo

Yesu na juu ya upendo wenu mlio nao kwa watakatifu wote, Imani na upendo ule utokao katika tumaini mlilowekewa akiba mbinguni na ambalo mmesikia habari

zake katika neno la kweli” (Wakolosai 1:3-5).

Ni kwa sababu ya kazi ya Yesu Kristo ya wokovu ambapo Paulo anaomba kwa ajili ya kanisa. Wakristo katika kanisa la Kolose walikuwa wamemwamini Kristo na Imani yao ilidhihirika kwa jinsi walivyopendana. Kwa sababu hii Paulo anamshukuru Mungu na anaendelea kuwaombea wakristo katika kanisa la Kolose. Kwa sababu ya yale ambayo ameyasikia kwamba walikuwa wakiyafanya kwa ajili ya Kristo, yeye anawaombea na anashukuru kwa sababu ya tumaini walilowekewa akiba mbinguni. Tumaini hilo ni lao kwa sababu walilisikia katika habari ambayo ni neno la Mungu la kweli. Paulo hakuwa na sababu nyingine ambayo ilimfanya aombee wakristo wa kanisa la Kolose. Ombi la Paulo kwa ajili ya kanisa hili la kolose msingi wake ni kazi ya Kristo Yesu. Baada ya Paulo kuwaombea kwamba, wao wawe na hekima, wakue katika utakatifu, waendelee kukua katika kumfahamu Mungu, na pia wawe na uvumilivu, kiasi na furaha, Paulo anamalizia maombi yake, “mkimshukuru Baba, ambaye amewastahilisha kushiriki katika urithi wa watakatifu katika ufalme wa nuru. Kwa maana ametuokoa kutoka katika ufalme wa giza na kutuingiza katika ufalme wa Mwana Wake mpendwa, ambaye katika Yeye tunao ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi kwa njia ya damu yake” (Wakolosai 1:12-14). Kutokana na kifungu hiki, maombi ya Paulo kwa kanisa hili ni kwamba, anatoa shukurani kwa ajili yao kwa sababu wao walimwamini Kristo na kwa sababu ya kuamini kwao, wao walisamehewa dhambi zao na kupewa ahadi ya kuurith Ufalme wa mbinguni. Kwa sababu ya jambo hili, yeye aliomba Mungu kwamba, wakristo wa kanisa la kolose wataendelea kukua na kufurahia neema ya Bwana katika maisha yao.

Katika waraka kwa kanisa la Waefeso, Paulo alifundisha pia juu ya umihimu wa kuombea kanisa. Katika maombi yake anasema kwamba

Page 15: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

Maombi ya wale ambao wameokoka 15

yeye amesikia juu ya imani yao katika Kristo na upendo wao juu ya watu wote amabo wameokoka. Yeye anaambia kanisa kwamba, hakomi kuendelea kumshukuru Mungu kwa ajili yao na kwamba kila wakati anawataja katika maombi yake kwa Mungu. Katika Waefeso 1:18-19, anaandika akisema kwamba, “Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yatiwe nuru ili mpate kujua tumaini mliloitiwa, utajiri wa urithi wa utukufu wake kwa watakatifu na uweza wake mkuu usiolinganishwa kwa ajili yetu sisi tuaminio. Uweza huo unaofanya kazi ndani yetu, ni sawa na ile nguvu kuu mno.” Tazama jinsi anavyozungumza kuhusu nguvu hizo na jinsi zilifanya kazi katika kumfufua Kristo na kumketisha kwa mkono wa kuume wa Mungu Baba. Anaomba, “..na uweza wake mkuu usiolinganishwa kwa ajili yetu sisi tuaminio. Uweza huo unaofanya kazi ndani yetu, ni sawa na ile nguvu kuu mno ambayo aliitumia alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, akamketisha mkono wake wa kuume katika mbingu, juu sana kuliko falme zote na mamlaka, enzi na milki na juu ya kila jina litajwalo, si katika ulimwengu huu tu, bali na katika ule ujao pia. Naye Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguu yake na amemfanya yeye awe kichwa cha vitu vyote kwa ajili ya Kanisa, ambalo ndilo mwili Wake, ukamilifu wake yeye aliye yote katika yote” (Waefeso 1:19-23). Kwa ufupi anawaambia kwamba, ninaomba kwamba nguvu zile ambazo zilimfufua Kristo kutoka kwa wafu, zifanye kazi katika maisha yenu na kwamba Kristo ambaye ameinuliwa juu sana kuliko majina mengine, na ambaye ndiye kichwa cha kanisa, atawala kanisa lake. Kwa sababu Kristo ameshinda nguvu za giza ili aletee kanisa lake uzuri, ambalo ni mwili wake. Paulo anaomba kwamba kila mshirika wa kanisa apate kutawaliwa na nguvu ambazo zilimfufua Kristo kutoka kwa wafu. Kristo ambaye ndiye kichwa cha kanisa hawezi kamwe kutenganishwa na mwili wake ambao ndilo kanisa lake. Muungano huu wa Kristo na kanisa lake umewezeshwa kwa nguvu za Mungu na ni kwa imani pekee wakristo wote wanaamini. Kwa sababu ni nguvu za Mungu ambazo zimemfufua Kristo na kumwinua juu sana kuliko viumbe vyote, pia washirika wa kanisa wataishi kwa nguvu hizi za Mungu.

Page 16: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

16

MAMBO AMBAYO YANAWEZA KUMZUIA

MAOMBI YA MKRISTO Charles H. Spurgeon (1834-1892)

“Vivyo hivyo ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili, nanyi wapeni heshima makitambua ya kuwa wao ni wenzi walio dhaifu na kama warithi pamoja nanyi wa kipawa cha thamani cha uzima, ili kusiwepo na chochote cha kuzuia maombi

yenu” ( 1 Petero 3:7).

Kwa wale ambao huwa hawaombi, mafundisho hayatakuwa na umuhimu wowote kwao. Pia kuna wale ambao huwa wanadai kuomba, lakini maombi yao hayafai hata kidogo. Kwa sababu mtu anapiga magoti au anazungumza maneno fulani fulani akidai kuomba, hiyo haimaanishi kwamba mtu huyu anaomba. Kwa kufanya hivi, ni kumkejeli Mungu. Kuna pia wengi ambao wanapoomba, wanarudia-rudia maneno fulani wakiwaza kwamba wao watasikika zaidi na Mungu.

Kwa wale ambao huwa hawaombi au kwamba wanaomba kwa njia isiofaa, wanapaswa kujua kwamba Mungu hawafurahii hata kidogo na gadhabu yake iko juu yao. Yeyote ambaye haombi kuhurumiwa, yeye hatapata huruma. Wale wote ambao hawaombi, Mungu hatawapatia chochote. Kumwomba Mungu lolote ni jukumu letu na ikiwa hatumwombi, basi tusitarajie kupata kutoka kwake.

Maombi si jambo gumu kufanya, kwa sababu ni jukumu la mwanadamu kutoka kwa muumba wake. Kwa hivyo hili ndilo jambo rahisi ambalo kila mtu anaweza kulifanya na kumuomba Mungu ambaye ameumba. Wale wote ambao hawaombi, siku moja watasikia sauti ya Mungu kwao akisema, “Lakini kwa kuwa mlinikata nilipowaita na hakuna yeyote aliyekubali niliponyosha mkono wangu” (Mithali 1:24). Ikiwa mwenye dhambi hataomba katika jina la Kristo Yesu ambalo ndani mwake Mungu ameahidi msamaha wa dhambi, halitakuwa jambo la kushangaza ikiwa yeye ataangamia katika jahanum. Hakuna mtu ambaye atamlalamikia Mungu ikiwa yeye atatupwa jahanum. Wewe ambaye hutaki kumwomba Mungu, siku moja utasimama mbele yake na kutetemeka sana kwa sababu alikupatia na nafasi ya kuomba, lakini ulikataa.

Page 17: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

Maombi ya wale ambao wameokoka 17

Kwa wale wote ambao wanaomba, maombi ni jambo bora sana na lafaa sana.Tukiomba, Mungu huwa anaachilia baraka zake kwetu. Kwa njia ya maombi Mungu huwa anatosheleza mahitaji yetu. Kwa wale wote ambao wameokoka, maombi ni njia ambayo tunapata nafsi zetu zikihuishwa. Maombi kwa wale ambao tumeokoka, ni chombo ambacho tunatumia kuwasiliana na nyumbani kwetu ambamo ni mbinguni. Maombi ni jambo ambalo lafaa sana na kwa sababu hii, Petero anaandika akisema kwamba ndoa na maisha ya nyumbani, furaha yake; yatokana na jinsi wakristo tunavyoomba. Anawahimiza waume kwamba wanapaswa kuwaheshimu wake wao ili maombi yao yasizuiliwe. Chochote ambacho kinazuia maombi ni kitu kibaya sana. Ikiwa kuna jambo lolote ambalo linafanya tukose kuomba, basi tunafaa kuliacha. Mume na mke wanapaswa kuomba kwa pamoja kwa sababu ni warithi wa ufalme moja na chochote ambacho kinazuia jambo hili, kinapaswa kuachwa kabisa.

Kuna baadhi ya mambo ambayo yanafanya maombi yazuiliwe.

a). Maombi yazuiliwa ikiwa tutakuwa vuguvugu juu ya vitu vya Mungu.

Mkristo ambaye maisha yake ni vuguvugu juu ya vitu vya Mungu, utaona kwamba yeye hatajali maombi. Kwa kawaida mtu anapokuwa mgonjwa sana, utaona kwamba sauti yake haitasikika sana kwa sababu mapafu yake yameugua sana. Hivyo ndivyo ilivyo na mkristo ambaye maisha yake ya kiroho ni mabaya, yeye huacha kuomba na hata kama anaomba, maombi yake yanakuwa dhaifu sana. Maombi katika maisha ya mkristo, yanadhihirisha maisha yake ya kiroho jinsi yanavyoendelea. Kuacha kuomba ni jambo hatari sana katika maisha ya mkristo na kutoomba kabisa ni hatari zaidi katika maisha ya yule ambaye hajaokoka. Mkristo ambaye anachukua jambo la maombi kuwa jambo la muhimu sana katika maisha yake na kwamba yeye analizingatia si kwa sababu ya dini au unafiki bali kwa sababu ya kumtukuza Mungu, mkristo huyu maisha yake ya kiroho yanaendelea vyema kabisa. Lakini ikiwa kwamba maombi yako yanazuiliwa, basi ni kwamba kuna jambo katika maisha yako ambalo unalipasa kulirekebisha kabisa. Maisha yako ya kiroho hayako sawa.

b). Maombi yanazuiliwa kwa sababu ya kukosa wakati wa kuomba.

Page 18: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

18

Hili ni jambo la kawaida kwa wengi. Unapotazama wengi utaona kwamba wana kazi nyingi za kila siku za kufanya. Kwa sababu ya majukumu ambayo kila jamii iko nayo, wengi wamejikuta kwamba wakati wao wa kuomba ni mdogo mno. Kuna wachungaji wengi ambao ni wazuri sana, lakini kwa sababu ya kujihusisha na biashara, wao sasa ni watu ambao hawana hata muda wa kuomba na jambo hili limedhuru sana maisha yao ya kiroho na huduma wao. Tunapaswa kuhakikisha kwamba tunaweka muda katika maisha yetu wa kuomba. Wengi badala ya kutumia muda kwa kumtukuza Mungu, wao wametumia muda wao mwingi wakitafuta mali ya ulimwengu huu. Wengi wameingiwa na tamaa ya ulimwengu na vitu vyake vyote.

Unaposoma kifungu cha Luka 12:20 kuendelea utaona kwamba yule tajiri hakuwa na muda wa kuomba kwa sababu alimaliza muda wake mwingi kwa kushughulika tu na biashara zake. “Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe! Usiku huu uhai wako unatakiwa. Sasa hivyo vitu ulivyojiwekea akiba vitakuwa vya nani” (Luka 12:20) na pia tunasoma kwamba, “lakini masumbufu ya maisha haya, udanganyifu wa mali na tamaa ya mambo mengine huja na kulisonga lile neno na kulifanya lisizae” (Marko 4:19). Ni tamaa ya mali ya ulimwengu na kutotosheka na vile ambavyo wako navyo, ndio sababu ya wao kunaswa na shetani. Hakikisha kwamba maombi yako hayazuiliwi.

Pia tunaweza kuwa na mengi ya kufanya katika kazi ya Mungu na pia tukose muda wa kuomba, na hii itazuia maombi yetu kama vile Matha alivyokuwa na muda mwingi wa kutumika. Si wengi ambao wanaomba jinsi wanavyotumika. Tunapaswa kuahakikisha kwamba tunaomba sana na pia tunamtumikia Mungu sana. Ni vyema kwamba tuhakikishe kwamba tunaomba sana kuliko jinsi tunavyofanya kazi sana. Ninajua kwamba kuna wengi ambao, wanahubiri sana, wanafundisha sana, wanasoma Biblia sana, wanahudhuria mikutano mingi ya kanisa lakini wao hawana muda wa kumaliza katika maombi. Haya mambo yote ni mazuri, lakini tusipokuwa waangalifu, tutakuwa tunaumiza nafsi zetu kwa kukosa kuwa na wakati mwafaka na Mungu wetu. Ni lazima tuombe ikiwa kweli tutahubiri kwa utukufu wa Mungu. Ni jambo la hatari ikiwa tutakosa kuomba kwa sababu tunahubiri.

c). Maombi pia yanazuiliwa kwa sabau ya kuwa wavivu au wazembe katika majuku yetu.

Kuna uwekano mkubwa sana tufanye mengi ambayo yanatuzuia kuomba lakini pia ni ukweli kwamba kuna wakristo wengi ambao wamezembea katika majukumu yao mengi. Mungu amewapatia mali nyingi na hawahitaji kujihusisha na mambo mengine mengi. Mara

Page 19: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

Maombi ya wale ambao wameokoka 19

mingi hawa wako na muda, na mara mingi wanamaliza muda huu kwa njia ambazo ni za kujifurahisha lakini hawajali mambo ya Mungu kamwe. Wanasahau kwamba kuna wengi ambao wanahitaji kufundishwa neno la Mungu, kuna wagonjwa ambao wanahitaji kutembelewa na maskini ambao wanahitaji kusaidiwa. Watu hawa kwa nini wanamaliza muda wao katika anasa na wala si katika kazi ya Mungu. Kwa nini wao hawatumii muda wao katika kuomba? Ukweli ni kwamba wengi wao wamezembea katika kazi ya Mungu na haswa katika maombi. Ninatamani kwamba wao wangefanya maombi kuwa jambo la muhimu sana katika maisha yao na kujitolea katika kumtumikia Mungu.

d). Maombi pia yanazuiliwa kwa sababu ya kukosa mpangilio katika maisha ya wengi.

Wengi huwa wanaamka wakiwa wamechelewa na wanaharakisha sana kuenda kazini kwa sababu wamechelewa. Wengine wanapata kwamba kwa sababu ya kukosa mpangilio, mambo ambayo hawajayapanga yanajitokeza mara kwa mara na wanayashughulikia kwa haraka. Wao hawana nafasi ya kuomba kwa sababu ya shughuli nyingi. Kila mara mambo yanajitokeza na wanajipata kwamba hawezi kuomba iwapasavyo. Na kama hata wataomba, utapata kwamba maombi yao yatakuwa ya haraka-haraka, na maombi kama hayo Mungu hayasikii.

Ni jambo jema kwamba kila mkristo awe na mahali ambapo ameandika majukumu yake ambayo anayapasa kufanya kila wakati. Maombi linafaa kuwa jambo la kwanza katika mipangilio yake yote. Ikiwa utafanya hivi, utapata kuona ni muda gani ambao unamaliza katika maombi. Utapata kwamba muda wako mwingi uko katika shughuli zako mwenyewe, unaumaliza na marafiki zako au katika burudani na wala si na Mungu. Ikiwa utaona hivi, basi huenda itakusaidia kujichunguza ili ujipatia muda wa kutosha katika maombi . Hakikisha kwamba muda mwingi uwe ni ushirika na Mungu.

Tuwe waangalifu kwamba hatuzuiliwe katika maombi. Ni kweli kwamba maombi yetu yanaweza kuzuiliwa kabisa. Kuna

mambo matatu ambayo ninataka tutazame ambayo yanaweza kufanya maombi yetu yazuiliwe kabisa.

a). Maombi yetu yanaweza kuzuiliwa ikiwa tutakosa kumheshimu Mungu Baba.

Tunaweza kukosa kumheshimu Mungu Baba kwa kukosa kutii neno lake. Ikiwa tunakataa mapenzi ya Mungu Baba jinsi neno lake

Page 20: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

20

linafundisha, basi tusishangae wakati tunapata kwamba ni vigumu sana kwetu kuomba. Ikiwa hatutii neno la Mungu, tutapata kwamba hata kutamka maneno ni jambo gumu sana. Litakuwa jambo gumu sana kuomba kikamilifu ikiwa hatumwamini Mungu Baba. Ikiwa moyo wako ni mugumu dhidi ya Mungu, ikiwa wewe huheshimu jina la Mungu, ikiwa huamini kwamba Yeye ndiye huwabariki watu wake, ikiwa huna upendo Kwake, na humwamini, kwa sababu ya mambo haya, wewe maombi yako yatazuiliwa kabisa.

Wakati mkristo moyo wake unampenda Mungu, wakati yeye anamwita Baba kutoka katika moyo wake, na nafsi yake kufurahia katika mapenzi ya Mungu Baba, Mungu atasikia maombi yake. Mungu hatasikia tu, bali pia atatimiza mapenzi yake katika maisha ya mtoto wake.

b). Maombi yatazuiliwa ikiwa tutakosa kumheshimu Kristo ambaye kupitia Yeye, si tunapaswa kuomba Mungu.

Ikiwa tunajiamini wenyewe badala ya kumwamini kristo, ikiwa tunawaza kwamba tunaweza kuishi bila Kristo, na tuombe kama jinsi Mfarisayo aliomba katika Luka 18, basi tujue kwamba maombi yetu yatazuiliwa na Mungu. Ikiwa Kristo si mfano wetu na ikiwa tunaendelea katika dhambi na kumwaibisha na pia ikiwa sisi hatuna shukurani kwa yale ambayo anatufanyia katika maisha yetu, basi tujue kwamba maombi yetu yatazuiliwa kabisa.

c). Maombi yetu yatazuiliwa ikiwa tutakosa kumheshimu Roho Mtakatifu.

Maombi ambayo hayaongozwi na Roho Mtakatifu, si maombi ambayo yanakubalika na Mungu. Maombi ya kweli, ni yale ambayo Roho Mtakatifu anatuongoza kuomba wala si maneno matupu ambayo tunayazungumza. Kwa hivyo ikiwa tutamhuzunisha Roho Mtakatifu, basi ni wazi kwamba hatatusaidia kuomba. Ikiwa tutaomba kinyume na mapenzi ya Roho Mtakatifu, basi hatatusaidia kuomba kulingana na mapenzi ya Mungu. Kwa hivyo tuhakikishe kwamba hatumhuzunishi Roho Mtakatifu haswa kwa kukosa kumtii wakati anatuonya, anatuita na wakati anatuongoza. Ikiwa wewe hutamtii Roho Mtakatifu, basi jua kwamba hatakuongoza katika maombi yako.

Mungu atayasikia maombi ya wale wote ambao wanataka kuhurumiwa ikiwa wataomba kupitia kwa Bwana Yesu Kristo. Yeye Mungu huwa hayakatai maombi ya wale ambao wananyenyekea. Yeye ni Mungu ambaye yuko tayari kuyasikia maombi ya wale wote ambao wanataka kusamehewa, ikiwa wao wataomba na kutubu kupitia kwa

Page 21: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

Maombi ya wale ambao wameokoka 21

Kristo Yesu. Yeye hatasikia tu, bali atawasamehe wao dhambi zao zote. Kwa wale ambao hawajaokoka, maombi yao yote ni makelele masikioni mwa Mungu. Biblia inasema, “Tunajua ya kwamba Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini huwasikiliza wote wanaomcha na kumtii” (Yohana 9:31). Mungu atasikia maombi ya watoto wake pekee na wala si ya wale ambao si wake, yaani hawajaokoka. Pia ni vyema kufahamu kwamba Mungu husikia maombi ya watoto wake wote, lakini kunao miongoni mwa watoto wake ambao maombi yao ni dhaifu, yaani hawatilii manani jambo la maombi. Wao wanaomba, lakini hawaombi sana, hawamalizi muda wao mwingi katika maombi. Ikiwa mtoto wa Mungu anapata kwamba maombi yake hayajibiwi, jambo zuri kufanya ni kujichunguza jinsi anavyoomba na hali ya maisha yao. Ikiwa tutajichunguza, tutapata jibu sahihi kwa nini maombi yetu hayajibiwi.

Maombi ambayo Mungu anayasikia na kuyajibu ni maombi ya aina gani?

a). Mungu anayasikia na kujibu maombi ambayo ni ya wale wakristo ambao wanaishi maisha matakatifu.

Yakobo anaandika akisema, “Kwa hiyo, ndugu zangu, vumilieni hadi kuja kwake Bwana. Angalieni jinsi mkulima angojavyo ardhi itoe mavuno yake yaliyo ya thamani na jinsi anavyovumilia kwa ajili ya kupata mvua za kwanza na za mwisho…maombi ya mwenye haki yana nguvu tena yanafaa sana” (Yakobo 5:7,16). Bwana Yesu Kristo anasema kwamba, “Kaeni ndani yangu, name nikae ndani yenu” (Yohana 15:4) Kristo anasema “kaeni.” Kristo hapa anamaanisha kwamba ikiwa hatutafanya mapenzi yake, naye hatatufanyia yale ambayo tunamwomba atufanyie. Kristo anasema kwamba kulitii neno lake huleta Baraka. Mungu hawezi kamwe kumjibu yule ambaye anajitegemea na hamtegemei Yeye mwenyewe. Yesu alipomponya yule kipofu, kipofu alisema, “Tunajua ya kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini huwasikiliza wote wanaomcha na kumtii” (Nukuu Yohana 9:31).

b). Mungu anayasikia na kuyajibu maombi ambayo yanaombwa kwa Imani.

Biblia inasema kwamba, “lakini pasipo Imani haiwekezekani kumpendeza Mungu” (Waebrania 11:6). “lakini anapoomba lazima aamini wala asiwe na shaka” (Yakobo 1:6). Biblia inasema kwamba bila imani, hakuna mtu ambaye anaweza kumfurahisha Mungu, hata katika maombi. Imani ndio chombo ambacho kinatuleta kwa Mungu katika

Page 22: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

22

maombi na kwa imani sisi huamini kwamba kile ambacho tunaomba kulingana na neno la Mungu, Mungu atakifanya kwa utukufu wake pekee.

c). Mungu anayasikia na kuyajibu maombi ambayo yamejawa na hitaji takatifu.

Ikiwa mambo ambayo tunayahitaji au kuyaombea katika maombi yetu ni mabaya, basi Mungu hatayajibu maombi yetu. Mahitaji yetu lazima yawe yanaambatana na ahadi za Mungu katika neno lake kwetu. Maombi kama haya ni yale ambao yanatuleta kwa Mungu tukifahamu kwamba Yeye anafurahia na atajibu. Maombi haya, hayawezi kamwe kukosa kufaulu, kwa sababu yanatoka mbinguni na yanarudi mbinguni.

d). Mungu anayasikia na kuyajibu maombi ambayo yanaombwa bila kukata tamaa na yanatarajia kile ambacho kinaombwa.

Biblia inasema kwamba, “maombi ya mwenye haki yana nguvu tena yanafaa sana” (Yakobo 5:17). Siyo maombi ya ambayo ni maneno matupu tu. Si maombi ya wale ambao wanaomba bila kuratajia chochote. Katika maombi yetu, lazima kuwa na kutarajia, kumtafuta Mungu kwa ukweli na bila kukata tamaa. Ni lazima yawe maombi ambayo yanatoka mioyoni mwetu kabisa na si maneno tu ambayo hayajali kama Mungu atafanya au hapana. Ni maombi ambayo yanasema, ‘mapenzi ya Mungu na yafanyike.’

e). Mungu anayajibu na kuyasikia maombi ambayo tamaa yake ni utukufu wa Mungu.

Hili ndilo linafaa kuwa kusudi la kila ombi, na ikiwa hili si kusudi la maombi yetu, basi tutakuwa hatuombi kamwe. Ni lazima tuombe chochote na tuwe na imani kwamba Mungu atakileta ili atukuzwe katika hicho. Ni lazima tufahamu kweli kwamba Mungu atatukuzwa wakati anajibu maombi yetu. Ikiwa tunaishi maisha matakatifu ambayo yanamletea Mungu utukufu, maombi yetu kila wakati yatakuwa yanaambatana na mapenzi yake Mungu, na kwa hivyo Mungu atayasikia kabisa na kuyajibu. “Jifurahishe katika Bwana naye atakupa haja za moyo wako” (Zaburi 37:4).

f). Mungu anayasikia na kuyajibu maombi ambayo tarajio lake ni takatifu.

Mtu ambaye anaomba, ni lazima atazame na kuona ni wapi ambapo maombi yake yanaelekea. Ni lazima maombi yetu yawe ni kwa Mungu pekee na tarajio letu liwe kwake tu. Ni lazima tutarajie Mungu kujibu maombi yetu kutokana na kazi ya Kristo Yesu msalabani na wala si kwa yale ambayo tumefanya sisi wenyewe. Ikiwa tunaamini kwamba

Page 23: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

Maombi ya wale ambao wameokoka 23

anatusikia, tutaamini kwamba ataleta yale ambayo tumeweka mbele zake.

Mungu hutupatia neema sisi wakristo ili tuweze kuenenda katika nguvu za Roho Mtakatifu, tukimtumainia Kristo pekee. Ni Yeye Mungu ambaye tunafaa kumtegemea ili atuwezeshe kuomba itupasavyo. Mtu ambaye Mungu amemfundisha kuomba impasavyo, yeye anaomba kulingana na mampenzi ya Mungu na mkono wa Mungu uko pamoja naye popote anapokuwa. Yeye anapofanya jambo, Mungu ndiye analifanya jambo hilo ndani mwake.

JUKUMU LA MCHUNGAJI KUWAOMBEA

WATU WAKE Eugene Bradford (1915-2010)

Maombi ni jambo la muhimu sana katika maisha ya mchungaji. Ni jukumu la mchungaji kwamba kila siku anamaliza muda katika maombi kwa ajili ya nafsi yake na kwa ajili ya wale ambao anawachungaji. Kwa sababu ya mambo mengi ambayo wachungaji wanahusika nayo, ni rahisi kujipata kwamba mchungaji anakosa muda wa kuomba. Wale wachungaji ambao wanapuuza jukumu hili, ni wale ambao watajipata katika shida kubwa sana.

Wachungaji na wale wote wanataka kufanya kazi ya uchungaji wanapaswa kuwa watu ambao wanaomba kwa ajili ya nafsi zao na kwa ajili ya nafsi za wale ambao wanawachunga.

Maombi ndio uhai wa nafsi na bila maombi hatutafanikiwa katika kazi ya huduma. Bila maombi, kazi zote ambazo tunazifanya ni bure. Kabla hatujaanza kazi ya kuhudumu, lazima tuwe kama Musa ambaye aliomba kwanza. Maombi hata ya yule ambaye anaonekana kwamba anafanya kidogo ni ya nguvu sana kuliko ya yule ambaaye anaonekana kufanya mengi lakini haombi. Ikiwa mchungaji si mtu wa maombi, hata kama yeye anajulikana kuwa mhubiri mzuri, ukweli ni kwamba yeye si mtumishi wa Mungu. Yeye ni mtumishi wa shetani ambaye alichaguliwa na shetani kama tu yule nyoka aliye mwongoza Hawa katika dhambi. Mchungaji wa aina hii ni adui mkubwa sana wa watu wa Mungu.

Page 24: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

24

Kwa sababu wachungaji wanamtumikia Mungu kuwapatanisha watu na Naye, maombi ni jukumu letu kufanya. Kupitia kwa maombi ya wachungaji Mungu huwa analeta baraka katika maisha ya kanisa. Kwa hivyo mchungaji huwa tu hawaelezi watu maneno ya Mungu, bali huwa anamweleza Mungu yale ambayo yanawahusu watu wake. Ni jukumu letu wachungaji kwamba kila siku tunapaswa kuleta mahitaji yetu mbele za Mungu kwa maombi na wakati huo huo kuleta ya wale ambao tunawachunga pia. Ni jukumu kuomba kwamba Mungu atawasamehe dhambi zao. Ni jukumu letu kuwaombea wale ambao hawajaokoka kwamba wamwamini Kristo. Pia ni jukumu letu kuhakikisha kwamba tunawahimiza wale ambao wameokoka na kuwaonya. Dhambi na mahitaji ya wale ambao tunawaongoza zinapozidi, ndipo pia tunafaa kuzidishi maombi yetu kwa ajili yao.

Kazi ya mchungaji itaendelea na kuwafaidi wengi ambao anawahudumia ikiwa yeye mwenyewe anamtii Mungu katika majukumu yake yote. Mchungaji wa kanisa ni mtumishi wa Mungu na kwa hivyo anapaswa kumtii Mungu ambaye amemwita kumtumikia miongoni mwa watu wake. Paulo katika Waraka wake kwa Warumi anandika akisema, “Paulo mtumishi wa kristo Yesu, aliyeitwa kuwa mtume na kutengwa kwa ajili ya Injili ya Mungu” (Warumi 1:1). Yeye Paulo ni mtumwa wa Kristo na wala hajitumikii yeye mwenyewe. Yeye alikuwa ameitwa na kutengwa kwa sababu ya injili. Ni kwa kazi hii ambayo ameitwa kufanya ambapo anapaswa kujitolea kabisa kwa kuifanya. Yeye si mfanya kazi wa mtu mwingine au mwanabishara, yeye ni mtumwa na ni balozi wa Kristo. Baada ya Paulo kujitambulisha kwa Warumi yeye ni nani, anaendelea kuwaeleza kwamba haja yake na kusudi ni watu ambao Mungu amemtuma kwao: “Kwanza kabisa namshukuru Mungu wangu kwa nji ya Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa sababu Imani yenu inatangazwa duniani kote. Kwa maana Mungu ninayemtumikia kwa moyo wangu wote katika kuhubiri injili ya Mwanawe, ni shahidi wangu jinsi ninavyowakumbuka” (Warumi 1:8-9). Yeye anasema kwamba hawezi kamwe kuwatumikia warumi ikiwa haombi kwa Mungu. Paulo alionyesha uaminifu wake kwa Mungu kwamba hata katika maombi yake, yeye anamwomba Mungu awe shahidi. Yeye alijua kwamba kazi yake yote ya injili ilikuwa ni kazi ya Mungu na kazi hii ilijumlisha kuwaombea watu wa Mungu. Yeye pia anasema kwamba “Anamtumikia Mungu katika roho, yaani akimaanisha uaminifu wake kwa Mungu. Yeye anaonyesha kwamba anatekeleza majukumu yake, bali anahakikisha kwamba anamtii Mungu ambaye amemwitia kufanya kazi hiyo. Lingekuwa jambo baya sana ikiwa Paulo angesema maneno haya lakini awe hayafanyi.

Page 25: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

Maombi ya wale ambao wameokoka 25

Unaposoma Maandishi ya Paulo utapata kwamba yeye alikuwa mtu ambaye alijitolea kabisa katika kazi ambayo Mungu alikuwa amemwita aifanye. Kwa ufupi ni kwamba, Kwa sababu Paulo alikuwa mtumishi wa Mungu ambaye alikuwa ameitwa na Mungu kuihubiri injili ya Kristo, kwa sababu hii, yeye aliomba kwa ajili ya kanisa la Kristo. Yeye alihakikishia kanisa kwamba aliwaombea kila wakati. Lilikuwa jukumu kubwa sana kwa Paulo kuwaombea wakristo . Yeye aliona kwamba kazi ya mtume alijumlisha kuombea watu wa Mungu. Yeye aliona kwamba maombi ni kuwa mwaminifu kwa yule ambaye alikuwa amemwita kumtumikia, yaani Kristo Yesu.

Je, leo tuko kama Paulo ambaye alijitoa kila wakati kuomba kwa sababu hili likuwa jukumu lake kama mtume wa Mungu? Ni ombi langu kwamba tusije tuione kazi ya mchungaji kuwa kama kazi zingine na kutazama ufanisi wake katika mambo ya nje tu na wala si katika mambo ya kiroho. Tusije tukajaribiwa kuwaza kwamba tunaweza kufanya kazi ya uchungaji kama tunavyofanya kazi nyingine nyingi. Paulo anasema kwamba ni jukumu letu. Anasema, “Kwa maana hatujihubiri sisi wenyewe ila tunamhubiri Kristo kuwa ni Bwana na sisi ni watumishi kwa ajili ya Yesu” (2 Wakorintho 4:5). Katika kuwahudumia wanadamu, tunajukumika kwa Mungu ambaye ametuita katika Kristo kufanya kazi ya uchungaji. Paulo anaandika akisema kwamba, “..tulinena kama watu tuliokubaliwa na Mungu tukakabidhiwa Injili. Sisi hatujaribu kuwapendeza wanadamu bali kumpendeza Mungu, Yeye ayachunguzaye mawazo ya ndani sana ya mioyo yetu” (1 Wathesalonike 2:4). Ikiwa mchungaji katika mahubiri yake hawalengi wasikilizaji wake, basi yeye pia hataweza kuwaombea hawa wasikilizaji wake. Wengi wanaweza kumsifu mchungaji kwamba mahubiri yake ni mazuri sana, Wengi wanaweza kuchukia mahubiri yake na wengine kumsifu kwa jinsi anavyoonekana kuwa mtu ambaye amesoma na anaelewa sana maandiko. Lakini ikiwa mchungaji huyu haombi kwa ajili ya wale ambao anawachunga, yeye si mwaminifu kwa Mungu ambaye amemwita katika kazi hiyo.

Page 26: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

26

UMUHIMU WA MIKUTANO YA MAOMBI Erroll Hulse (1931-2017)

Mikutano ya maombi ya kanisa ni ishara ya kuonyesha jinsi kanisa linavyoendelea kiroho. Unaweza kujua jinsi kanisa linavyoendelea kwa kuona jinsi kanisa linavyomba wakati limekutana pamoja. Je, kanisa liko na lengo la kuwafikia wengi na ujumbe wa injili? Ikiwa lengo hili lipo, utalisikia katika maombi ya kanisa hilo. Je, kuna tamaa ya kuwaona wengi wakija kwa kristo? Pia ikiwa hili la kweli katika kanisa hilo, utalisikia likiombwa. Je, kuna tamaa ya kuona ulimwengu ukikuja kwa Kristo na kujihusisha katika kazi ya Mungu ulimwenguni kote? Ikiwa kanisa liko na mzigo huu, pia utalisikia likiomba juu ya jambo hili. Je, kuna tamaa ya kuona kwamba kuna amani katika ulimwengu ili wale ambao vita na njaa vimewakumba wafikiwa na ujumbe wa Injili? Katika mikutano ya maombi ya kanisa, hili utalisikia likiombwa. Jinsi kanisa linavyoomba itadhihirisha upendo na kujali kwa kanisa juu ya wale wote ambao wanateswa na dhambi na majaribu katika maisha yao. Wale wote ambao wanapitia katika hali ngumu za maisha watapata kwamba watafarijiwa katika mikutano ya maombi kwa sababu Roho Mtakatifu atafanya kazi katika maisha na mioyo yao.

Mikutano ya kila siku ya maombi ya kanisa. Katika nchi ya Korea kulitokea uvuvio kwa sababu ya mikutano ya

kila siku ya maombi. Huko, nilipouliza niliambiwa kwamba kila watu wanakutana kwa kuomba saa kumi na moja ya asubuhi na wakati mwingine saa kumi na mbili za asubuhi. Haya ndio maisha ya baadhi ya wakristo huko.

Rafiki wangu mwingine, alinieleza kwamba baba yake alikuwa mtu ambaye alijitolea kuomba kila siku na alikuwa akifanya kazi kuanzia saa moja asubuhi hadi saa moja jioni. Lakini hata hivyo, yeye alitenga muda wa kuomba kila siku saa kumi na mbili ya asubuhi.

Katika mwaka wa 1866, Mchungaji Spurgeon alianzisha mkutano wa maombi kila siku saa moja asubuhi na saa moja na unusu jioni. Mkutano mmoja wa kanisa lote ulifanyika siku ya Jumatatu kanisani mwao na watu Zaidi ya 3000 walikuwa wakihudhuria.

Page 27: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

Maombi ya wale ambao wameokoka 27

Mafundisho ya Biblia kuhusu maombi. Maombi ni kuleta mahitaji yetu mbele za Mungu kulingana na neno

lake kupitia kwa Kristo Yesu tukisaidiwa na Roho Mtakatifu, pia tukikiri dhambi zetu na kwa kumshukuru Mungu kwa huruma zake.

Tunafaa kukumbuka kwamba hatuwezi kamwe kuomba kulingana na mapenzi ya Mungu ikiwa Roho Mtakatifu hatuongozi. Wakati Roho Mtakatifu anatuongoza, basi ndipo tunaweza kuomba kulingana na neno la Mungu na kumfurahisha Mungu katika maombi yetu. Bila kusaidiwa na Roho Mtakatifu, basi hatuwezi kamwe kuomba na hata kama tutaonekana kuomba, tutakuwa tunasema maneno matupu tu. Ni katika maombi ambapo tunaweza kueleza yale ambayo Roho Mtakatifu anatuongoza ndani. Ni Roho Mtakatifu ambaye huwa anatusaidia katika udhaifu wetu. Biblia inasema, “Vivyo hivyo, Roho hutusaidia katika udhaifu wetu, kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo. Lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu usiyoweza kutamkwa” (Warumi 8:26).

Toba la kweli linatokana na Roho Mtakatifu. Daudi hangeweza kamwe kutubu juu ya ile dhambi yake ya kumuua Uraya na ya kuzini na Bethsheba ikiwa Roho Mtakatifu hangemdhibitishia dhambi yake. Daudi aliandika Zaburi 51, kama matokeo ya toba lake. Kuomba kwa ajili ya utukufu wa Kristo na kwa ajili ya ufalme wa Mungu uendelee kupanuka, ni Roho Mtakatifu ambaye anatuwezesha tuombe hivyo. Wakati huo huo lazima pia tujue kwamba huu ndio unafaa kuwa upendo wetu katika mioyo yetu, yaani utukufu wa Kristo na ufanisi wa Ufalme wake. Si kweli hata kidogo ikiwa tutasema kwamba, hatutaomba hadi Roho aje atuongoze. Biblia inatuhimiza kwamba tunafaa kuomba, wakati huo huo tukimtegemea Roho Mtakatifu atuongoze katika maombi yetu.

Je, tunaweza pia kuwaza kwamba, ikiwa Mungu ameamua kufanya jambo fulani, je, kuna haja ya sisi kuomba? Tunapaswa kujua kwamba Mungu anatawala katika kila jambo na wakati huo huo, tunapawa kujua kwamba Mungu ameweka mbele zetu majukumu ambayo tunafaa kuyatekeleza kikamilifu. Ni lazima mambo haya mawili tuyafahamu vyema kila wakati. Tunawajibika mbele za Mungu kwa kumtegemea Yeye pekee kwa njia ya neno lake na kwa kuomba Kwake. Hivi ndivyo tunavyoishi maisha yetu hapa ulimwenguni. Kufuata mapenzi ya Mungu katika maisha yetu ndio njia ya amani, furaha na uaminifu.

Bwana Yesu alimtegemea Mungu Baba, na kwa hivyo Yeye aliomba Kwake. Hata kama Kristo alikuwa Mungu kamili, Yeye aliomba. Biblia inasema kwamba wakati wa ubatizo wake, Yeye alikuwa anaomba (Luka

Page 28: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

28

3:21). Yeye aliamka mapema sana ili aombe (Marko 1:35). Yeye aliomba usiku kucha kabla ya kuwachagua wanafunzi wake kumi na wawili (Luka 6:12). Yeye alikuwa katika maombi wakati sura yake ilipobadilishwa (Luka 9:29). Maombi ndio ilikuwa njia yake ya kushinda alipokuwa katika bustani ya Gethsemane (Luka 22:44).

Tutumie muda wetu wa maombi katika mikutano ya maombi kuombe mambo mbali mbali. Tukumbuke kuombea jamii, kanisa, kazi ya uinjilisti, makanisa mengine na wachungaji wa makanisa hayo. Tukumbuke pia kuyaombea mataifa yetu, kazi ya Mungu kote duniani, Amani katika mataifa ambayo hayana Amani, maskini, na uaminifu katika uongozi: “Awali ya yote, naishi, kwanza kabisa, naagiza kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili watu wote: kwa ajili ya wafalme na wale wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi kwa Amani na utulivu, katika uchaji wote wa Mungu na utakatifu. Jambo hili ni jema tena linapendeza machoni pa Mungu Mwokozi wetu anayetaka watu wote waokolewa na wafikie kuijua kweli” (1 Timotheo 2:1-4).

Ikiwa siku moja katika juma haitoshi, basi kanisa linafaa kutenga wakati mwingine wa kuomba pamoja. Muda huu unaweza kuwa hata mapema siku ya jumapili kabla ibada zianze. Hii ni njia moja sana nzuri ya kujitayarisha kwa ajili ya ibada za siku hiyo.

Je, katika makanisa ambamo kuna wengi ambao hawahudhurii siku ya maombi nini inapaswa kufanyika? Ukweli ni kwamba hatuwezi kamwe kuwalazimisha watu kukua, lakini tunaweza kuwaongoza kwa njia nzuri kwa upole na ukarimu. Biblia inasema kwamba, “Mwanzi uliopondeka hatauvunja na utambi ufukao moshi hatauzima” (Isaya 42:3).

Katika makanisa yetu, kuna wale ambao Mungu amewapa karama ya kuhimiza wengine (Warumi 12:8). Ikiwa wao watatumia karama hii vyema, watawasaidia wengi kuwa waaminifu katika kuhudhuria mikutano ya maombi ya kanisa.

Katika mikutano ya maombi ya kanisa, kunahitajika kiongozi ambaye anapaswa kuongoza na kuhimiza kutoka katika Biblia. Yeye anastahili kuwahimiza wengine kuomba. Anapaswa kuwaeleza wengine kwamba hafai kutumia muda mrefu sana kwa sababu hiyo pia inaweza kuwazuia wengine wasiombe. Kunahitajika maelezo kabla ya kuomba ili kuwa na mwelekezo mwema. Pia huenda kuwe na haja ya kuyagawana mambo ambayo yanaombewa. Njia hii itawahimiza wengine kuomba pia. Yule ambaye anaongoza anapaswa kuacha kuwe na uhuru wa kuomba kwa wote.

Page 29: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

Maombi ya wale ambao wameokoka 29

Umuhimu wa mkutano wa maombi wa kanisa kulingana na mafundisho ya kitabu cha matendo ya mitume.

Katika sura za kwanza za kitabu cha Matendo ya Mitume, tunasoma kuhusu mikutano ya maombi. Siku ya Pentekoste, tunasoma kwamba wanafunzi wa Kristo Yesu walikuwa wakiomba kabla ya Roho Mtakatifu kuja juu yao. Walikuwa wakiomba wakisubiri ahadi ya Bwana Yesu Kristo kwao, yaanii Roho Mtakatifu. Je, ni wangapi leo ambao wanaomba kwamba Mungu alete uvivio. Baada ya Pentekoste, tunasoma kwamba kulitokea mateso makali sana kwa kanisa na mitume walikatazwa kwamba wasihubiri tena katika jina la Kristo Yesu. Je, katika hali hii, wao wangefanya nini? Jibu ni moja, wao walikutana na kuomba kama kanisa. Walikutana na kumweleza Mungu juu yay ale yote ambayo walikuwa wanapitia kama kanisa. Bwana aliwaongoza na kuwahimiza katika mateso yao. Baada ya muda mfupi tena, Yakobo alichinjwa. Petro naye alikamatwa na kuwekwa kwa jela. Je, wale wanafunzi waliobaki walifanya nini? Wao walikusanyika na wakaomba. Wao waliendelea kuomba kwa siku nane, hadi siku ile Petro alikuwa auliwe. Mungu aliyajibhu maombi yao na akamtuma malaika ambaye alimfungua nyororo Petro na kumwongoza nje ya jela.

Je, Petro alienda wapi wakati alipofunguliwa? Yeye alienda mahali ambapo kanisa lilikuwa likiomba. Je, alijua aje kwamba walikuwa huko? Ni kwa sababu yeye alijua maisha ya kanisa na kwa hivyo alifahamu vyema kwamba walikuwa wakiomba, kwa sababu hii ilikuwa tabia yao kila wakati. Wakati alipoingia, hata mitume walishangaa sana kumwona kwa sababu kama sisi leo, waliomba lakini walikuwa na shauku katika maombi yao.

Baadaye katika kitabu hiki cha matendo ya Mitume, tunasoma kwamba kanisa lingine lilianzishwa katika mkutano wa maombi (Matendo ya Mitume 16:13).

Uvivio na mabadiliko ambayo yanatokana na mikuna ya kanisa ya maombi.

Katika maombi ya kanisa, ni lazima tuombe kwamba Mungu alete uvuvio katika maisha yetu, katika kanisa letu, katika nchi yetu na katika mataifa mengine ulimwenguni. Ndipo Mungu alete uvuvio, Roho Mtakatifu atatupatia uwezo wa kuomba juu ya jambo hili

Mara kwa mara uvuvio hutokana na mikutano ya maombi ya makanisa. Nikimalizia, ninakusihi ukitafute kitabu ambacho kinaitwa nguvu za maombi (Power of Prayer) ambacho kimeandikwa na Samuel

Page 30: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

30

Prime. Kitabu hiki kinafundisha jinsi kulikuwa na uvuvio mkubwa ambao ulianza kwa mkutani mmoja wa maombi. Mkutano wa kila wiki wa maombi ndio mahali pazuri sana pa kumwomba Mungu alete uvuvio katika kazi yake na katika maisha ya watu wake na katika kanisa. Biblia inasema, “Basi kwa Yeye awezaye kutenda mambo ya ajabu yasiopimika kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo kwa kadiri ya uweza wake ule utendao kazi ndani yetu” (Waefeso 3:20).

MCHUNGAJI AMBAYE HAOMBI Andrew Murray (1828-1917)

Wachungaji wengi tuko na hatia ya kuwa watu ambao hatuombi. Hii ni dhambi kubwa sana katika maisha ya mchungaji.

Je, kwa nini kukosa kuomba na mchungaji ni dhambi kubwa sana? Kwanza ninajua kuna wengi ambao huwa wanasingizia kwa kusema kwamba huu ni udhaifu tu. Kuna wengi pia ambao wanasema kwamba hakuna wakati wa kuomba. Lakini hata kama tunavisababu hivi vyote, ukweli ni kwamba kukosa kuomba na mchungaji ni dhambi kubwa sana machoni pa Mungu.

Je, kwa nini hii ni dhambi kubwa sana?

Hii ni kwa sababu kukosa kuomba ni kinyume na mapenzi ya Mungu. Mungu anakualika uje kwake ili uzungumze naye na umwombe vile

vitu ambavyo unavihitaji na upate baraka nyingi kutoka kwake, lakini unakataa. Yeye anakuita ili uwe na ushirika naye lakini wewe bado unakataa. Mungu ametuumba katika umbo lake na kutukomboa kwa njia ya Mwanawe Yesu Kristo, ili katika kumwomba Yeye tuweze kushiriki katika utukufu na wokovu wake.

Je, tunatumiaje hizi baraka zake kwetu? Wengi wanaomba kwa muda mfupi na wansema kwamba wao hawana muda mwingi wa kuomba na mioyo yao haina tamaa ya kuomba. Wao hawaelewi jinsi mtu anaweza kumaliza hata nusu saa katika maombi. Shida si kwamba hawaombi, bali wanapoomba kila siku wao hawana furaha ya kuomba. Wao hawazungumzi na Mungu na kwa hivyo wanadhihirisha katika maisha yao kwamba hawamtegemei Mungu kabisa.

Page 31: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

Maombi ya wale ambao wameokoka 31

Wachungaji hawa, ikiwa rafiki yao anakuja kuwatembelea, wao wanatenga muda mwingi hata kama inamaanisha kuacha kufanya mambo fulani fulani ya muhimu katika maisha yao. Ukweli ni kwamba wako na wakati wakufanya mambo ambayo wanayapenda sana lakini hawana wakati kuwa na ushirika na Mungu na kumfurahia Mungu. Wao wanapata muda wa kumalizana na viumbe lakini hawana muda wa kumalizana na muumbaji wao.

Hii ni kutomheshimu Mungu na kumchukia Mungu ikiwa kweli hatupati wakati wa kumaliza katika maombi tukiwa naye. Hii ni dhambi ambayo tunapaswa kulia juu yake na kumlilia Mungu.

Hiki ndicho chanzo cha ugonjwa hatari wa kiroho. Ni ukweli kwamba hata baada ya kuokoka, hali ya dhambi bado imo

ndani mwetu. Maombi ni uhai wa maisha, kupitia kwa maombi tunaweza kujua hali ya moyo. Dhambi ya kutoomba ni ishara katika maisha ya mkristo au ya mchungaji kwamba maisha ya Mungu katika nafsi yamedhofika sana.

Mambo mengi yamesemwa juu ya udhaifu wa kanisa katika kutekeleza majukumu yake, kushawishi washirika wake katika mema na kuwakomboa kutoka katika nguvu za ulimwengu na vitu vyake na kuwaleta katika maisha ya utakatifu ambayo inamletea Mungu utukufu. Pia mengi yamesemwa juu ya ushawishi wa kanisa katika maisha ya wale ambao hawajaokoka, ambao Kristo alilituma kwao wakahubiri injili ya wokovu kwao. Je, ni kwa nini wengi wa wale ambao wameokoka hawana ushawishi wowote katika maisha ya wale ambao hawajaokoka? Jibu ni moja tu, wao si watu wa maombi. Kanisa haliombi na wachungaji hawaombi iwapasavyo. Katika kazi zao zote kwa Mungu, kanisa limepungukiwa na nguvu za Mungu kwa sababu haliombi jinsi linapaswa kuomba. Ni dhambi ya kutoomba ambayo imesababisha ukose wa nguvu za Mungu katika maisha ya kanisa.

Hatari kubwa sana ambayo kanisa limo kwa sababu ya dhambi ya kukosa kuomba kwa mchungaji wake.

Ni kazi ya mchungaji kuhakikisha kwamba anawafundisha washirika wake kuomba. Je, ikiwa yeye haombi, atawezaje kuwafundisha wengine? Mchungaji hawezi kuelekeza kanisa zaidi ya jinsi yeye anavyofanya. Hawezi kuwafundisha au kuwahubiria kwa hakika jambo ambalo yeye mwenyewe hafanyi kwa sababu huo utakuwa unafiki.

Page 32: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

32

Je, ni wakristo wangapi ambao wanafahamu vyema baraka ambazo zinapatikana katika ushirika na Mungu kupitia kwa maombi? Kuna wengi ambao wanapenda sana kuhimizwa katika jambo hili la maombi lakini katika mahubiri ya mchungaji hawahimizwi kuvumilia na kuendelea hadi wapokea baraka ya Mungu. Sababu ya hii ni kwamba mchungaji mwenyewe hafahamu vyema inamaanisha nini kudumu katika maombi kwa sababu yeye si mtu wa maombi na hajafahamu baraka za Mungu ambazo zinaambatana kwa maombi. Ni ombi langu kwamba wachungaji watafahamu hatari ya kutoomba na kwamba watatubu dhambi hii na kuanza kuomba jinsi iwapasavyo.

Dhambi ya kutoomba husababisha ukosefu wa uwezo wa kuwafikia wengi na ujumbe wa injili.

Hatutaweza kutekeleza majukumu yetu jinsi Kristo amesema ikiwa tutaendelea katika dhambi hii ya kutoomba. Leo hitaji kubwa sana katika huduma zetu, ni roho ya kuomba. Tunahitaji watu ambao wanaomba na wanaomba iwapasavyo kwa Mungu, haswa kwamba wengi wapate kuokoka. Wengi wamesema kwamba Mungu yuko tayari kuwaokoa wengi leo ikiwa watu watamwomba na kumlilia kwa ajili ya nafsi za waliopotea. Lakini swali ni je, hili litawezekanaje ikiwa tuna wachungaji ambao hawaombi jinsi iwapasavyo. Ni lazima kwanza hawa wachungaji watubu na wafanye jinsi Mungu amewaamuru, yaani waombe jinsi wanapaswa kuomba kwa ajili yao na kanisa. Haitoshi tu kuhubiri, au kuwatembelea wengi katika nyumba zao, au kufanya zingine za kanisa, bali jambo la muhimu la kwanza katika maisha ya mchungaji ni, ni kuwa na ushirika na Mungu kwa njia ya maombi ili Mungu na kwa njia hii watapata nguvu za kufanya kazi yake.

Tunafaa kufahamu jambo hili la kutoomba kwamba ni dhambi kubwa sana. Tuombe Mungu atusaidie na atuondoe katika dhambi hii. Tuombe kwamba Mungu atatukomboa kutoka katika dhambi hii kwa damu Kristo Yesu. Bwana nakuomba kwamba utatuondoa katika dhambi ya kutoomba ili tuwe wachungaji ambao ni watu wa maombi kabla tutekeleze lolote katika ufalme wako. Bwana tusaidie ili tupate himizo, furaha, imani na uvumilivu mkubwa, tuwe watu wa kukuomba. Tupe tamaa ya kuomba kila wakati.

Dhambi hii ya kutoomba ni mzigo mkubwa sana katika maisha ya mchungaji na hatutapumzika hadi iondolewe kwa nguvu za Kristo Yesu. Bwana tumwombe na atafanya na kutusamehe na kutupatia nguvu za kuomba kila wakati.

Page 33: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

Maombi ya wale ambao wameokoka 33

KUOMBA AU KUTOOMBA J. C. Ryle (1816-1900)

“Nataka kila mahali wanaume wasali wakiinua mikono mitakatifu pasipo hasira wala kugombana” (1 Timotheo 2:8).

Wacha nizungumze na wale wote ambao huwa hawaombi. Ikiwa wewe huwa huombi, ninataka kuzungumza nawe sasa maneno

ya Mungu. Ninakuonya kwamba wewe uko katika hali ya hatari sana. Ikiwa wewe utakufa sasa, nafsi yako itaelekea jahanum. Hata wakati Kristo atarudi na kukufufua wewe, utafufuliwa ili uingie katika jahanum milele. Ninakuonya kwamba wewe huna sababu yoyote ya kusingizia ni kwa nini wewe huombi. Ninajua kwamba wewe unavijisababu vingi sana ambavyo unavitoa kwa sababu ya ukosefu wako wa kuomba. Ninakuambia kwamba vijisababu hivyo vyote ni bure machoni pa Mungu.

Ninakuonya kwamba: a). Haina maana yoyote ya kusema kwamba wewe hujui kuomba. Kuomba ndilo jambo rahisi sana kufanya katika dini yoyote. Kuomba

ni kuzungumza na Mungu. Ili uombe, huhitaji kitabu cha kujifunza au kuwa na hekima ya juu, unahitaji tu kuwa na moyo ambao unataka kuomba. Mtoto mdogo ambaye anahisi njaa, yeye anahitaji tu kulia. Maskini ambaye huomba-omba anahitaji tu kuweka mkono wake na kuomba watu wamsaidie. Mtu yeyote anaweza kuzungumza na Mungu ikiwa yeye ana akili.

b). Haina maana yoyote ya kusema kwamba huna mahali pazuri pa kuombea.

Mtu yeyote anaweza kupata nafasi mahali popote na aombe. Bwana Yesu Kristo aliomba akiwa mlimani, Petero aliomba akiwa juu ya nyumba, Isaki aliomba akiwa shambani; Nathanieli aliomba akiwa chini ya mti, Yona aliomba akiwa ndani ya samaki mkubwa. Mahali popote ni mahali pazuri pa kumwomba Mungu.

c). Haina maana yoyote kusema kwamba huna wakati wa kuomba. Kuna wakati mwingi sana wa kuomba ikiwa utatengwa wakati huo.

Wakati unaweza kuwa ni mfupi, lakini ukweli ni kwamba kila wakati kuna wakati tosha wa kuomba. Danieli alikuwa na kazi nyingi ya ufalme ya kufanya, lakini tusoma kwamba yeye aliomba mara tatu kila

Page 34: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

34

siku. Daudi alikuwa mfalme wa Israeli, lakini tunasoma akisema, “Jioni, asubuhi na adhuhuri ninalia kwa huzuni, naye husikia sauti yangu” (Zaburi 55:17). Ikiwa kweli tunataka kuomba, wakati utapatikana wa kuomba.

d). Haina maana yeyote kusema kwamba huwezi kuomba hadi wewe uwe na Imani na moyo mpya.

Huwezi kusema kwamba wewe utakaa tu hadi wakati utapata imani ndipo uweze kuomba. Ukifanya hivi, utakuwa unaongeza dhambi juu ya dhambi. Ni jambo la hatari sana mtu akiwa hajaokoka, lakini ni hatari sana kusema kwamba ninajua sijaokoka lakini sitaomba msamaha wa dhambi zangu. Biblia inasema kwamba, “Mtafuteni Bwana maadamu anapatikana; muiteni maadamu yu karibu” (Isaya 55:6); “Chukueni maneno pamoja nanyi, na mumrudie Bwana. Mwambieni: Samehe dhambi zetu zote na utupokee kwa neema, ili tuweze kutoa matunda yetu kama sadaka za mafahali” (Hosea 14:2); “Kwa hiyo tubia huo uovu wako na umwombe Mungu, ili yamkini, aweze kusamehe mawazo uliyo nayo moyoni mwako” (Matendo 8:22). Ikiwa kweli unataka imani na moyo mpya, basi unapaswa kumwomba Mungu akupatie haya mambo mawili.

Wewe ambaye huombi, je, kwa nini humwombi Mungu chochote? Je, wewe uko tayari kuingia jahanum? Je, wewe huombi kwa sababu huna dhambi za kusamehewa? Je, huogopi jahanum? Je, hutamani mbinguni? Ninakusihi kwamba uanze kumwomba Mungu kwa sababu kuna siku ambapo utatamani kuomba lakini litakuwa jambo gumu sana kwako. Wengi siku moja wataomba, “Bwana, Bwana! Tufungulie mlango” (Mathayo 25:11) lakini watakuwa wamechelewa sana. Wengi watalilia milima iwangukie na vilima viwafunike kwa sababu wao walikataa kuomba Mungu. Kwa hivyo ninakuonya kwamba huu usije ukawa ndio mwisho wa nafsi yako. Wokovu uko karibu sana na usije ukakosa mbinguni kwa sababu ulikataa kuomba.

Wacha nizungumze sasa na wale ambao wao huomba. Kuna wale ambao wao wanajua umuhimu wa kuomba na wao

huomba kwa sababu wao ni wana wa Mungu. Kwa hawa wote, niko na maneno ya kuwahimiza kama ndugu zangu. Mara nyingi ninajua kwamba maombi yetu huwa ni madhaifu sana. Biblia inasema, “Hivyo ninaona sharia ikitenda kazi. Ninapotaka kutenda jema, jambo baya liko papo hapo” (Warumi 7:21). Wewe unafahamu vyema maneno ya Daudi, “Ninachukia watu wa nia mbili, lakini ninapenda sheria yako”

Page 35: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

Maombi ya wale ambao wameokoka 35

(Zaburi 119:113). Kila wakati unapoomba kwamba Mungu akuokoe kutoka kwa maadui wako, pia unamwomba kwamba akuokoe kutoka kwa hali yako ya dhambi ya kale. Kuna wakristo wachache sana ambao huwa hawahuzuniki katika maombi yao. Shetani huwa anakasirika sana wakati anatuona tukiomba. Ikiwa maombi yetu hayatugharimu, basi huwa hatujayadhamini hata kidogo. Mara kwa mara utaona kwamba yale maombi ambayo huwa tunayaona kwamba si kitu, hayo ndio huwa yanamfurahisha Mungu.

Maneno machache ya kukuhimiza. a). Ninataka kukuhimiza juu ya umuhimu wa heshima na

unyenyekevu kwa Mungu katika maombi. Tukumbuke kila wakati kwamba sisi ni wanadamu na kwamba

tunapaswa kumheshimu Mungu wakati tunakuja kuzungumza naye katika maombi. Tuhakikishe kwamba hatuji kwa Mungu kwa njia ya haraka-haraka na kutojali. Tunapaswa kujua kwamba kila neno ambalo tunalizungumza lazima liwe ni la kweli. Tukumbuke maneno ya Suleimani: “Usiwe mwepesi kuzungumza, usiwe na haraka katika moyo wako kuzungumza lolote mbele za Mungu. Mungu yuko mbinguni nawe uko duniani, kwa hiyo maneno yako yawe machache” (Mhubiri 5:2). Wakati Abrahamu alizungumza na Mungu alisema, “Kwa kuwa nimekuwa na ujasiri wa kuzungumza na Bwana, ingawa mimi si kitu bali ni mavumbi na majivu” (Mwanzo 18:27; Ayubu 40:4). Hata sisi tuwe kama hawa.

b). Ninataka kukuhimiza juu ya umuhimu wa Kuomba ukiongozwa na Roho Mtakatifu.

Kile ninamaanisha hapa ni kwamba, tunafaa kuhakikisha kwamba Roho Mtakatifu anatauongoza katika maombi yetu na wala hatuongozwi na mambo mengine. Tuhakikishe kwamba tusije tukaanguka katika dhambi ya kutamka tu maneno ambayo hatuyamanishi. Ni rahisi kutumia maneno mazuri sana na hata kunukuu maandiko lakini tuwe kweli hatuombi Mungu, kwa sababu maneno hayo hayatoki mioyoni mwetu. Ninajua kwamba kuna mambo ambayo kila siku tunayahitaji, na kuna njia ambayo tunaweza kuyaomba mambo haya lakini jinsi tunavyoyaomba, iwe si kwa njia ya kweli na hatuongozwi na Roho Mtakatifu. Ulimwengu, shetani na mioyo yetu ni vitu vidanganyifu sana. Kwa hivyo tuhakikishe kwamba maombi yetu si maneno mazuri matupu, bali kwamba tunaongozwa na Roho Mtakatifu.

Page 36: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

36

c). Ninataka kukuhimiza kwamba hakikisha maombi ni jambo la maisha yako ya kila siku.

Tukumbuke kwamba Mungu wetu ni Mungu wa mipangilio. Masaa ya asubuhi na jioni ya kuomba katika hekalu huko Yerusalemu, yaliwekwa kwa mpangilio ambao Mungu alidhibitisha. Kukosa mpangilio katika maisha ya mtu, ni tunda la dhambi. Ni jambo la muhimu sana kuhakikisha kwamba unatenga muda kila siku katika maisha yako kuomba. Kama tu vile unavyoweka muda wa kula, kulala, na kufanya mambo mengine, hakikisha pia unaweka muda wa kuomba. Wewe mwenyewe chagua muda ambao unajua ni mzuri kwako na kwamba wakati huo hutasumbuliwa na mtu. Omba asubuhi kabla hujaanza kufanya lolote na omba usiku baada ya kumaliza shughuli zako zote. Katika haya yoyote kumbuka kwamba maombi ni jambo la muhimu kufanywa kila siku. Hakikisha kwamba unaomba.

d). Ninataka kukuhimiza umuhimu wa kuvumilia katika maombi. Kumbuka kwamba usiwahi acha tabia ya kuomba. Kuna wakati

ambapo moyo wako utakuambia kwamba, “nimeomba na familia pamoja, je hakuna haja ya kuomba pekee yangu.” Wakati mwingine, mwili wako utakuambia, “wewe umechoka sana na unafaa kupumzika.” Pia mawazo yako, yatakuambia, “Una mambo mengi muhimu ya kushughulika nayo, fupisha maombi yako.” Kumbuka kwamba haya mambo yote yanatoka kwa shetani. Kile shetani anataka kutoka kwao, ni uache kuomba kabisa. Ni ukweli kwamba mara kwa mara hatuombi kwa muda sawa, lakini tuhakikishe kwamba huachi tabia ya kuomba. Biblia inasema, “Dumuni katika maombi…ombeni pasipo kukoma” (Wakolosai 4:2; 1 Wathesalonike 5:17). Hii haimanisha sasa kwamba tunafaa kila wakati kuwa tunapiga magoti na kuomba kama jinsi wengi wanafanya. Ikiwa tutafanya hivyo, basi ni wazi kwamba hatutawezi kutekeleza majukumu mengine kama kufanya kazi ili tule na mambo mengine ambayo pia Mungu ametuamuru tuyafanya. Kile Biblia inamaanisha ni kwamba hatufai kuacha tabia ya kuomba kila wakati na kila siku. Mioyo yetu inafaa kuwa mioyo ambayo kila wakati iko katika hali ya mazungumzo na Mungu na kuwa na tamaa ya wakati ambapo tunakuwa na Mungu pekee katika maombi. Pia hata wakati tunafanya kazi, tunaweza kuwa tunaomba katika mioyo yetu. Usiwahi kuwaza kwamba kuomba ni kumaliza muda wako bure. Hakuna hasara katika kuvumilia katika maombi. Bali ni faida na baraka tele ambazo zinapatikana katika jambo hili.

e). Ninataka kukuhimiza uwe mtu wa kuomba kutoka kwa moyo wako.

Page 37: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

Maombi ya wale ambao wameokoka 37

Kwa sababu mtu anaomba kwa sauti kubwa, hiyo haimanisha kwamba kweli yeye anaomba kutoka kwa moyo. Ni vyema kama tutaomba kwa moyo ambao ni mnnyenyekevu tukijua kwamba kile ambacho tunakiomba tutakipata kweli. Biblia inasema kwamba maombi ya mwenye haki yanafaa sana na wala si maombi ya yule ambaye anapiga kelele sana. Biblia inafundisha kwamba maombi ni kulia, ni kutafuta, ni kufanya kazi, kubisha na kujitahidi. Yakobo alimwambia malaika, “Sitakuacha usende usiponibariki” (Mwanzo 32:26). “Ee bwana, sikiliza! Ee Bwana, samehe! Ee Bwana, sikia na ukatende! (Danieli 9:19). Biblia inafundisha kwamba Bwana Yesu Kristo, “alimtolea maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, yeye awezaye kumwokoa na mauti, naye Mungu akamsikia kwa sababu ya kutii kwake kwa unyenyekevu” (Waebrania 5:7). Unaposoma maombi haya yote, utapata kwamba, wengi leo wanaomba kinyume kabisa. Wengi wanaomba wakipiga kelele sana na wengine ni vugu-vugu katika maombi yao. Kulingana na jinsi wengi wanavyoomba, ni ukweli kwamba wao hawataki kile ambacho wanachokiomba. Kwa hivyo tuhakikishe kwamba maombi yetu tuyaomba kwa unyenyekevu na kwa bidii tukijua kwamba kile ambacho tunachokiomba kweli tutakipata. Tuombe bila kukoma. Pia tuombe tukijua kwamba ikiwa yale ambayo tunayaombea hayatafanyika, basi maisha yetu yako hatarini. Tufahamu kwamba maombi yetu ambayo ni vugu-vugu ni kama sadaka bila moto mbele za Mungu.

f). Ninataka kukuhimiza kwamba unapaswa kuomba kwa Imani. Tunafaa kuamini kwamba maombi yetu huwa Mungu anayasikia

ikiwa tutaomba kulingana na mapenzi yake na kwamba Yeye atatupatia kile ambacho tumwomba Yeye. Hii ndio amri ambayo Kristo Yesu alipeana: “Yoyote myaombayo mkisali, amini ya kwamba mmeyapokea nayo yatakuwa yenu” (Marko 11:24). Kuomba bila imani, ni maombi bure na hayafaulu katika lolote. Tujifundishe kuomba kulingana na ahadi za Mungu katika maombi yetu. Tunafaa kuomba kama Samweli: “Basi sasa Mungu ukaitimize ahadi uliyosema kuhusu mtumishi wako na nyumba yake milele” (2 Samweli 7:25). Hivi ndivyo Yakobo, Musa na Daudi walivyoomba. Ukisoma Zaburi 119, utaona jinsi Daudi alivyoomba akinukuu ahadi za Mungu. Pia tujifundishe kutarajia jibu kwa maombi yetu.

Tusitosheke hadi tumeona kwamba maombi yetu yamejibiwa. Tukumbuke kwamba kanisa la Yerusalemu lilimwombea sana Petro alipokuwa gerezani na wakati maombi yao yalijibiwa, wao walishangaa

Page 38: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

38

sana (Matendo 12:15). Ni hatari sana kuomba bila kutarajia, kwa sababu ukweli ni kwamba hutapata lolote.

g). Ninataka kukuhimiza kwamba lazima uwe na ujasiri katika maombi yako.

Kuna wengi ambao huomba kwa bidii na uajasiri lakini ujasiri wao hautokani na utakatifu. Ukweli ni kwamba kuna ujasiri ambao unatokana na utakatifu, na huu ndio kila mtu anapaswa kuwa nao wakati anaomba. Ninazungumza juu ya ujasiri kama ule wa Musa wakati alipowaombea Waisraeli walipoanguka katika dhambi ya kuabudu sanamu. Yeye aliomba na kusema, “Kwa nini wamisri waseme, Ni kwa nia mbaya aliwatoa Misri, ili awaue milimani na kuwafuta usoni mwa dunia” (Kutoka 32:12). Ujasiri kama ule wa Yoshua wakati Waisreali waliposhindwa kule Ai: “Wakanani na watu wengine wa nchi watasikia habari hii, nao watatuzunguka na kutufutilia jina letu duniani. Utafanya nini basi kwa ajili ya jina lako mwenywe lililo kuu” (Yoshua 7:9). Ujasiri kama wa Luther. Wale waliomsikia akiomba, walisema, yeye alikuwa na ujasiri wa juu sana. Yeye aliomba Mungu kwa unyenyekevu lakini wakati huo huo na tumaini na hakika kwa yale alikuwa akiombea. Mara kwa mara, sisi huwa hatuombi hivi kwa sababu huwa hatufahamu kabisa baraka ambazo sisi ambao tumeokoka tuko nazo. Huwa hatuombi jinsi itupasavyo.

h). Ninataka kukuhimiza kwamba unapaswa kuleta haja zako zote mbele ya Mungu.

Bwana Yesu Kristo alituonya juu ya kuwa kama Mafarisayo ambao waliomba maombi marefu sana. Wao walikuwa wanafiki. Yeye anatuonya kwamba tusiwe watu wa kurudia-rudia maombi. Biblia inatuambia kwamba Yesu Kristo mwenyewe aliomba kwa Mungu Baba kwa muda mrefu sana. Hii inatuonyesha umuhimu wa kuwa na muda wa kutosha katika maombi. Hatufai kuomba tu maneno machache machache na kuondoka. Tunapaswa kuwa na muda, lakini tuhakikishe kwamba tusimalize tu muda kwa kurudia-rudia tu maneno fulani fulani. Ikiwa hatumalizi muda katika maombi kwa kuleta mahitaji yetu yote kwa Mungu, basi ni wazi kwamba tuko na machache tu ambayo tunataka Mungu atufanyie. Kuna wengi leo ambao wanalalamika kwamba wao hawasikilizani na wengine au kwamba wao wako na neema kidogo. Haya malalamishi yao ni kwa sababu ya wao kutoomba jinsi inawapasa. Wale ambao wanaomba mengi, Mungu huwapa mengi. Wale wanaomba machache, Mungu huwapa machache. Yakobo anasema kwamba, hamna kwa sababu hamwombi. Msomaji wangu, shida ambayo uko nayo ni yako mwenyewe. Kristo anataka kukupatia mengi

Page 39: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

Maombi ya wale ambao wameokoka 39

lakini wewe unaomba machache. Bwana Yesu anasema, “Kisha akasema, Chukua mishale, naye mfalme akaichukua. Elisha akamwambia, piga ardhi kwa hiyo mishale. Akapiga mara tatu, halafu akaacha. Mtu wa Mungu akamkasirikia na kusema, ungepiga chini mara tano au sita, ndipo ungeishinda Aramu na kuiangamiza kabisa. Lakini sasa utaishinda mara tatu tu” (2 Wafalme 13:18-19).

i). Ninataka kukumihiza kwamba unafaa kutaja yale ambayo unataka Mungu akufanyie katika maombi yako.

Hatufai tu kutosheka na kusema maneno mengi tu, lakini pia tunafaa kuhakikisha kwamba tunayataja mahitaji yetu mbele za Mungu. Ni vyema kukiri na kutubu dhambi zetu, lakini ni vyema pia kutaja dhambi hizo ambazo tumezitenda na tunajua kwamba tuko na hatia mbele za Mungu. Ni vyema kuomba Mungu ataongoze katika utakatifu, lakini pia ni vyema zaidi kutaja hali ambazo katika maisha yetu tunaona kwamba tunapungukiwa na neema. Pia haitoshi kumwambia Mungu kwamba tuko katika hali hatari, bali pia tunafaa kutaja hatari ambayo tuko ndani mwake. Hivi ndivyo Yakobo aliomba alipokuwa anaenda kukutana na ndugu yake Esau. Alimwambia Mungu kile ambacho haswa alikuwa anakiogopa (Mwanzo 32:11). Hivi ndivyo Eliyaza alifanya wakati alitumwa na Abrahamu kumtafutia Isaka mke (Mwanzo 24:12). Hivi ndivyo Paulo alifanya wakati alikuwa na mwiba katika maisha yake (Wakorintho 12:8). Hii ndio imani ya kweli na ujasiri katika yale ambayo tunayaomba mbele za Mungu. Hakuna kitu kidogo ambacho hatufai kutaja mbele za Mungu. Tunapaswa kukumbuka kwamba Kristo ndiye tabibu mkuu na Baba wa watu wake wote. Tuonyeshe jambo hili kwa njia ya kumweleza kila kitu, kikubwa na hata kile kidogo. Tusifiche siri yoyote kutoka kwake, bali tumweleze yale yote yaliomo katika mioyo yetu.

j). Ninataka kukuhimiza juu ya umuhimu wa kuwaombea wengine. Kawaida sisi sote ni wachoyo na hata baada ya kuokoka, tusipokuwa

waangalifu, choyo hii hubaki nasi. Kuna tabia katika maisha yetu, kuwaza juu maisha yetu pekee na wala si ya wengine. Kwa sababu ya hii, tunafaa sisi sote kuwa waangalifu sana kwa kuomba. Tumwombe Mungu atupatie moyo wa kuwapenda wengine na kuwaza juu yao. Tunafaa kujifundisha pia kuwaombea wengine katika maombi yetu. Tunafaa kuwaombea wale wote ambao hawajaokoka, na wale ambao wameokoka. Tunafaa kuwaombea washirika wenzetu katika kanisa, nchi yetu, viongozi wetu na nyumbani mwetu na marafiki zetu. Kufanya hivi ni kuonyesha ukarimu mkubwa sana katika maisha ya wengine. Tunaonyesha upendo wetu kwa wengine ikiwa tutawaombea

Page 40: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

40

wakati tunaomba. Jambo hili hutufanya tukue katika huruma na mioyo yetu inajawa na upendo kwa wengine kila wakati. Ikiwa tutawaombea wengine katika kanisa, kanisa litafaidika sana. Jambo ambalo linasaidia sana katika kueneza injili ya Kristo, ni kwamba tunaomba kwa ajili ya kazi hii. Bila maombi hatuwezi kamwe kuifanya. Kuombeana ni kuwa katika Kristo Yesu ambaye kila wakati Yeye huwaombea watu wake akiwa Kuhani Mkuu mbele za Mungu Baba. Kuombea wengine, ni kuwa wa msaada mkubwa sana kwa watumishi wa Kristo. Wale ambao wanaomba na kuombeana, hilo ndilo kanisa bora.

k). Ninataka kukuhimiza juu ya kuwa wenye kushukuru katika maombi yako.

Ni jambo moja kuleta mahitaji yako mbele za Mungu na pia ni jingine kuwa mtu mwenye kushukuru Mungu. Unaposoma Biblia, utapata kwamba, kuombea mahitaji na kushukuru ni mambo mawili ambayo huwa yanaambata katika maombi. Kwa hivyo ombi ambalo halina shukurani, hilo si ombi kwa Mungu. Biblia inasema, “Msijusumbue kwa jambo lolote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu” (Wafilipi 4:6). Ni kwa neema ya Mungu kwamba hatuko jahanum. Ni kwa huruma ya Mungu kwamba tuko na tumaini la kuingia mbinguni. Ni kwa neema ya Mungu kwamba tunaishi katika nchi ambamo tunakubalika kuhubiri injili bila kutatizwa. Ni kwa neema ya Mungu kwamba Roho Mtakatifu anatuongoza leo ili tufanye mapenzi ya Mungu. Ni kwa neema ya Mungu kwamba tunaishi leo na kwamba tuko na fursa za kuendelea kumletea Mungu utukufu kwa matendo yetu kwa wengine na katika maisha yetu. Mambo haya yanapaswa kuwa katika mioyo yetu wakati tunaomba. Kweli hatufai kukosa kumsifu na kumshukuru Mungu kwa yale ambayo ametufanyia. Tumshukuru kwa ajili ya neema ambayo ametupatia na ni ya milele. Wale watakatifu wote ambao wameishi siku zote, wamekuwa watu wa shukurani kwa Mungu. Katika nyaraka zote za Paulo, yeye hakosi kumshukuru Mungu.

Ni lazima tuwe na moyo wa kushukuru Mungu katika kila jambo. Wacha maombi yetu yawe ni maombi ya kushukuru.

l). Ninataka kukuhimiza kwamba unafaa kuwa mwangalifu sana juu yay ale ambayo unayaomba.

Ni kupitia kwa maombi tunaanza ukristo wa kweli na ni kupitia kwa maombi tunaendelea katika ukristo wa kweli. Ukristo wa kweli unadhihirika kupitia kwa jinsi mtu anavyoomba. Kupitia kwa maombi, tunajua jinsi tunavyoenedelea kiroho. Kwa hivyo ni lazima kila wakati

Page 41: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

Maombi ya wale ambao wameokoka 41

tuwe waangalifu jinsi tunavyoomba. Hapa ndipo ukristo unadhihirika katika maisha ya mtu. Mahubiri mazuri, vitabu, vijitabu vya kikristo, marafiki ambao wameokoka, mikutano ya mafundisho ya Biblia, haya yote ni mambo mazuri, lakini haiwezi kuchukua nafasi ya maombi. Hakikisha kwamba hakuna kitu ambacho kinakuzuia ili ukose kuomba. Jichunge sana kwamba usije ukapuuza jambo la kuomba. Ikiwa hutapuuza maombi, nafsi yako intakuwa katika hali mzuri kiroho.

Nimetaja mambo haya yote kwa unyenyekevu sana kwa ajili kujichunguza. Ninajua kwamba mimi ndiye mmoja ambaye ninapaswa kukumbuka mambo haya sana. Lakini pia ninaamini kwamba huu ni ukweli kutoka kwa Mungu na ni ombi langu kwamba tutasaidika wote.

Ninaomba kwamba siku ambazo tunaishi, zitakuwa siku za maombi. Ninaomba kwamba wakristo wa sasa wawe wakristo wa kuomba. Ninaomba kwamba kanisa letu la sasa liwe kanisa la kuomba. Nia yangu ya maandishi haya ni kwamba niwasaidie wengi kuwa na moyo wa kuomba katika maisha yao ya ukristo. Ninaomba kwamba wale ambao hawajawahi kuomba, waanze kwa kuliita jina la Mungu; ninaomba kwamba wale ambao wanaomba, waendelee kukua katika maombi kila mwaka na kwamba wa hakikishe kwamba hawaombi bure.

KUDUMU KATIKA MAOMBI Charles H. Spurgeon (1834-1892)

Katika kitabu cha Mwanzo tunasoma kwamba, na watu wakaanza kuliitia Jina la Mungu (Mwanzo 4:26). Katika kitabu cha Ufunuo tunasoma neno hili “Amen” (Ufunuo 22:21). Tuna mifano mingi katika Biblia kuhusu watu wakiomba. Kwa mfano tunasoma kuhusu Yakobo ambaye hakumwachilia malaika, hadi alipombariki, Danieli ambaye aliomba mara tatu kwa siku, Daudi ambaye kwa moyo wake wote alimwomba Mungu. Pia tunasoma kuhusu Paulo na Sila wakiwa gerezani wakiomba. Kuna amri nyingi na ahadi nyingi ambazo zinaambatana na maombi. Je, hizi zinatufundisha nini kuhusu umuhimu wa maombi?

Chochote Mungu amesema katika neno lake, kinahusu maisha yetu. Mungu amesema mengi katika neno lake kuhusu maombi. Hii inamaanisha kwamba Yeye anajua kwamba tunahitaji mengi. Kwa

Page 42: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

42

sababu hii hatufai kupuuza maombi. Je, wewe unawaza kwamba huhitaji chochote? Ukweli ni kwamba ikiwa unawaza hivi, basi wewe hujui kwamba wewe ni maskini wa kiroho sana. Je, wewe kwa nini usimwombe Mungu akuhurumie? Ukweli ni kwamba ikiwa humwombi Mungu akuhurumie, basi ni wazi kwamba wewe hujatambua huruma za Mungu katika maisha yako. Nafsi ambayo haiombi, ni nafsi ambayo Kristo hayumo ndani mwake. Maombi ndio maneno ya moyo ambao unamwamini Mungu, kelele ya mkristo ambaye anaendelea kupigana na dhambi na wimbo wa mkristo ambaye anakufa akiwa katika Kristo Yesu. Maombi ni, pumzi, neno la kutulinda, faraja, nguvu na heshima ya mkristo.

Ikiwa wewe ni mtoto wa Mungu, wewe utakuwa unaomba Mungu na utaishi katika upendo wa Baba wako, ambaye ni Mungu.Omba kwamba mwaka huu wewe utakua katika utakatifu, unyenyekevu, tamaa juu ya vitu vya Mungu na utakua katika uvumilivu ndani ya Kristo. Hakikisha kwamba kila siku unaishi maisha yako karibu sana na Kristo na kwamba kila wakati unadumu katika upendo wake. Omba Mungu kwamba atakusaidia uwe wa Baraka katika maisha ya wengine na kwamba maisha yako utayaishi kwa utukufu wa Mungu pekee. Ombi lako mwaka huu linafaa kuwa, “Kudumu katika maombi” (Wakolosai 4:2).

MAOMBI YA WALE AMBAO

WAMEOKOKA Octavius Winslow (1808-1878)

“ Alipokwisha kukitwaa kile kitabu, wale viumbe wenye uhai wane pamoja na wale wazee ishirini na wane wakaanguka mbele ya yule Mwana-Kondoo. Kila

mmoja wao alikuwa na kinubi, nao walikuwa wameshika mabakuli ya dhahabu yaliyojaa uvumba, ambayo ni maombi ya watakatifu” (Ufunuo 5:8).

Wale ambao wameokoka ni watu ambao wanaomba, ni ishara katika maisha yao kwamba wamemwamini Kristo. Wale ambao hawajaokoka, huwa hawaombi kwa sababu wao wamekufa kiroho. Maombi ni ishara kwamba Roho Mtakatifu anaisha ndani mwa mtu, kwa sababu ni Yeye ambaye anamwezesha mtu huyu kuomba. Maombi ni maisha ya Kiroho

Page 43: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

Maombi ya wale ambao wameokoka 43

ya wale ambao wameokoka. Mtu anaweza kuwa haonekani kufanya mambo mengi ya huduma,

awe hajui mengi katika ukristo lakini ukweli ni kwamba ikiwa yeye ameokoka, yeye atakuwa mtu wa maombi. Yeye huzungumza na Mungu kwa sababu yeye ana maisha ya Mungu ndani mwake na maisha haya ni ya milele. Ndani mwake kuna maisha ya kiroho ambayo inaendelea kukua. Hata katika majaribu mengi na huzuni nyingi, yeye ni mtu ambaye anaomba. Maombi ni jambo zuri ambalo Mungu anatuwezesha kufanya kama watu.

Katika mstari ambao ni kichwa cha sura hii, tunasoma kuhusu maombi ya wale ambao walikuwa wameokoka. Wao walikuwa wamekombolewa na damu ya Kristo Yesu. Wao walikuwa miongoni mwa wale ambao walijumwishwa kwenye kanisa lote la Kristo. Maono haya ya Yohana yamekusdiwa kutufundisha kwamba kanisa la Kristo, ni kanisa ambalo linaomba na kwamba maombi ya watu wa Mungu humfikia Mungu kama uvumba mzuri. Maombi yao yanamfikia Mungu kupitia kwa kazi ya Kristo Yesu.

Je, haya maombi ni ya kina nani? a). Biblia inasema kwamba, haya maombi ni ya watakatifu. Watakatifu ni kina nani? Hawa si watakatifu ambao wako mbinguni

kwa sababu wale ambao wako mbinguni tayari hawaombi. Wao walipokuwa hapa ulimwenguni waliomba, na sasa wako mbinguni, na kwa hivyo huko hawaombi. Sasa wao wako katika utukufu kamili. Sasa wao wako mbinguni wakimsifu Mungu. Hapa ulimwenguni, tunaomba Mungu na kumtumainia katika kila jambo kwa sababu bado hatujafika katika utukufu kamili huko mbinguni.

Ukweli ni kwamba huko mbinguni hakuna kuomba. Biblia inatuelezea kwamba Kuhani wetu mkuu ambaye ni Kristo Yeye anaomba huko mbinguni. Kristo Yesu pekee ndiye mwombaji huko mbinguni. Biblia inasema kwamba Yesu, “hakuingia kwa njia ya damu ya mbuzi na ya ndama, lakini alingia Patakatifu pa Patakatifu mara moja tu kwa damu yake mwenyewe, akiisha kupata ukombozi wa milele” (Waebrania 9:12) na “kwa hivyo anaweza kuwaokoa kabisa wale wanaomjia Mungu kupitia kwake, kwa sababu Yeye adumu daima kuomba kwa ajili yao” (Waebrania 7:25). Bwana Yesu Kristo ndiye mpatanishaji ambaye Mungu anayemsikia pekee huko mbinguni. Yesu ndiye mwombezi wetu huko mbinguni, si malaika au watakatifu

Page 44: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

44

walioko mbinguni. Maombi ya Kristo, Mungu atayasikia na kuyajibu kila wakati.

Kristo huombea kanisa lake na kanisa lake huomba katika jina lake, kwa sababu hakuna jina lingine ambalo limepatiwa kanisa kuomba kwalo. Hii ni baraka kubwa sana kwa kanisa kwamba Kristo anatuombea na kupitia Yeye Mungu anakubali maombi yetu. Hakuna jambo la faraja kwa kanisa kama kufahamu kwamba Kristo anatuombea kila siku na kwamba maombi yake yanakubalika na Mungu wakati wowote.

b). Wale ambao wameokoka, ndio watu ambao wanaomba kwa kweli. Kwa wale ambao wameokoka, maombi ni jambo la muhimu sana kwao.

Wao wanamaliza muda wao mwingi katika maombi na wao wanafuarahia kuomba na pia wanabarikiwa wanapoomba. Maombi huwaleta pamoja kama watu wa Mungu.

Ni Baraka kubwa sana kwa wale ambao tumeokoka kwa sababu sisi ndio Mungu anatuita watakatifu wake. Ni baraka kubwa sana kwa sababu hata kama tumezaliwa tukiwa wenye dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, kwa neema Mungu ametuinua katika Kristo. Kwa sababu ya wokovu ambao Kristo alitununulia, wale wote ambao wamemwaini Kristo wao wamependwa sana na Mungu kuliko viumbe vyote ambavyo ameviumba, hata malaika. Kuvishwa haki ya Mungu (Warumi 3:21-22), ni kupewa nafasi ya heshima na utukufu mkubwa sana ambao hakuna kiumbe kitafikia, isipokuwa Mungu mwenyewe. Tumebarikiwa sana sisi ambao tuna ushirika na Mungu na tuko karibu sana Naye, Yeye mwenye utukufu wote, heshima yote na Yeye ambaye ni wa milele.

c). Je, Uvumba ni nini? “..maombi ya watakatifu.” Maombi ni jambo takatifu. Daudi anasema kwamba, “Maombi yangu

na yafike mbele zako kama uvumba; kuinua mikono yangu juu na kuwe kama dhabihu ya jioni” (Zaburi 142:2).

Tumeona ukweli kwamba watakatifu wa Mungu ni watu ambao wanaomba, na kwamba kuzungumza na Mungu wa Utatu ni jambo ambalo kila mkristo anapaswa kufanya. Hakuna mtakatifu ambaye haombi, na wakatifu wote wa Mungu ni watu wa maombi. Wao wanaombea katika sehemu tofauti tofauti na kuomba kwa njia tofauti tofauti, lakini wao ni watu wa maombi. Wao wanaomba katika jengo ambamo kanisa hukutana, majumbani mwao na popote pale wapatapo nafasi ya kuomba, wao huomba. Watakatifu wa Mungu huja kwa Mungu katika jina la Yesu na kuwa na ushirika na Mungu ambaye

Page 45: AOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA - chapellibrary.org:8443

Maombi ya wale ambao wameokoka 45

haonekani kwa macho ya kiasili. Maombi situ jambo muhimu katika maisha ya wale ambao wameokoka, bali maisha yake yote mkristo ni ya maombi.

Msomaji wangu, ikiwa wewe umeokoka, unahitaji kuwa mtu wa maombi. Maombi ni njia ambayo inatambua utawala wa Mungu katika kila jambo, upendo wake kwetu, jinsi anavyotujali yeye, na jinsi anavyotuongoza katika maisha yetu ya kila siku. Ni kutambua kwamba Mungu ni Baba wetu na ni rafiki wetu wa dhati. Mkristo anapaswa kuomba kwa sababu kila siku yeye anapitia mambo mengi sana magumu. Yeye hupigana na dhambi katika maisha yake, yeye huona kila wakati jinsi amepungukiwa na utukufu wa Mungu, dunia kila wakati inamjaribu kumnasa katika dhambi na tamaa zake,; Yeye pia kila wakati anahuzunika na kuhuzunishwa na wakati mwingine anashushwa moyo. Haya yote hawezi kuyadhibiti bila kuwa mtu wa maombi. Ni kupitia kwa maombi, Mungu atampa nguvu, faraja, tumaini na uwezo wa kukumbana, kuvumilia na nguvu za kushinda mambo haya yote.