16
1

BIASHARA NDANI YA AJIRA. - JamiiForums · ambacho wanakuwa hawajakijua ni kwamba hii ni hatari kubwa zaidi. Kwa sababu ukichukua muda na kuwafuatilia wengi wa wanaostaafu, huishia

  • Upload
    others

  • View
    160

  • Download
    34

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: BIASHARA NDANI YA AJIRA. - JamiiForums · ambacho wanakuwa hawajakijua ni kwamba hii ni hatari kubwa zaidi. Kwa sababu ukichukua muda na kuwafuatilia wengi wa wanaostaafu, huishia

1

Page 2: BIASHARA NDANI YA AJIRA. - JamiiForums · ambacho wanakuwa hawajakijua ni kwamba hii ni hatari kubwa zaidi. Kwa sababu ukichukua muda na kuwafuatilia wengi wa wanaostaafu, huishia

2

BIASHARA NDANI YA AJIRA. Anzisha Na Kuza Biashara Yako Ukiwa Bado Umeajiriwa.

MAKIRITA AMANI

+255 717 396 253

[email protected]

www.amkamtanzania.com

MAY 2016

Page 3: BIASHARA NDANI YA AJIRA. - JamiiForums · ambacho wanakuwa hawajakijua ni kwamba hii ni hatari kubwa zaidi. Kwa sababu ukichukua muda na kuwafuatilia wengi wa wanaostaafu, huishia

3

Kitabu hiki kimeandikwa na;

Makirita Amani,

Simu; +255 717396253/ +255 755953887

Barua pepe; [email protected] au [email protected]

Blogu; www.kisimachamaarifa.co.tz

www.amkamtanzania.com

Toleo la kwanza May 2016.

Hatimiliki

Haki zote za kitaaluma zimehifadhiwa haipendezi na ni kinyume na sheria

kunakili au kuchukua chochote kilichoandikwa katika kitabu hiki bila idhini

kutoka kwa Mwandishi wa kitabu hiki; Lakini kinaruhusiwa kutumiwa popote

palipo na mafundisho yanayohusiana na yaliyoandikwa humu kwa ruhusa ya

mwandishi.

Kwa matumizi ya kitabu hiki katika mafundisho tafadhali wasiliana na

mwandishi kwa mawasiliano yaliyopo hapo juu.

OMBI MAALUMU;

HONGERA KWA KUPATA KITABU HIKI KIZURI CHA BIASHARA NDANI YA

AJIRA. KISOME NA TUMIA MAFUNDISHO HAYA KWENYE SAFARI YAKO YA

MAFANIKIO.

KAMA UMEPOKEA KITABU HIKI KAMA NAKALA TETE (SOFTCOPY) TAFADHALI

USIMTUMIE MTU YEYOTE KITABU HIKI HATA KAMA NI WA KARIBU SANA

KWAKO. KAMA KUNA YEYOTE ATAKAYEKIHITAJI TAFADHALI MWELEKEZE

JINSI ULIVYOKIPATA WEWE, ITAMSAIDIA SANA KUPATA MAFUNZO HAYA

TOFAUTI NA WEWE UKIMTUMIA TU.

KILA LA KHERI NA TUPO PAMOJA KATIKA SAFARI HII YA KUHAKIKISHA

MAISHA YETU YANAKUWA BORA ZAIDI.

ASANTE SANA.

Page 4: BIASHARA NDANI YA AJIRA. - JamiiForums · ambacho wanakuwa hawajakijua ni kwamba hii ni hatari kubwa zaidi. Kwa sababu ukichukua muda na kuwafuatilia wengi wa wanaostaafu, huishia

4

YALIYOMO UTANGULIZI. ...................................................................................................... 6

AJIRA NI SEHEMU NZURI YA KUANZIA BIASHARA............................................... 7

HATARI YA KUCHOMA MELI MOTO. ................................................................. 11

UNA MUDA WA KUTOSHA. .............................................................................. 17

CHANZO KIMOJA CHA KIPATO NI UTUMWA. ................................................... 22

BIASHARA INAHITAJI MUDA KUKUA. ............................................................... 26

TENGENEZA MPANGO BORA KWAKO. ............................................................. 29

KUBALI KUPOTEZA. .......................................................................................... 33

BIASHARA UNAZOWEZA KUFANYA UKIWA BADO UMEAJIRIWA. ..................... 36

KIPAJI ULICHONACHO .................................................................................. 36

UTAALAMU NA UZOEFU WAKO ................................................................... 39

BIASHARA ZA KAWAIDA ............................................................................... 41

BIASHARA YA MTANDAO ............................................................................. 42

KILIMO CHA KIBIASHARA ............................................................................. 43

UWEKEZAJI UNAOWEZA KUFANYA UKIWA BADO UMEAJIRIWA ...................... 45

UWEKEZAJI KWENYE MFUKO WA UMOJA .................................................... 45

UWEKEZAJI KWEYE SOKO LA HISA ................................................................ 47

UWEKEZAJI KWENYE MALI ........................................................................... 47

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOANZA BIASHARA UKIWA KWENYE AJIRA. ..... 50

HATARI ZA KUEPUKA ILI BIASHARA YAKO IFANIKIWE. ...................................... 56

KUWA NA MSHIRIKA. ....................................................................................... 60

USIFANYE KILA KITU PEKE YAKO. ...................................................................... 63

FAIDA NYINGINE ZA KUENDELEA KUBAKI KWENYE AJIRA. ............................... 65

NIDHAMU .................................................................................................... 65

MTANDAO ................................................................................................... 66

RASILIMALI ................................................................................................... 67

MIFEREJI NANE YA KIPATO UNAYOHITAJI KUWA NAYO. .................................. 69

TENGENEZA MFUMO. ...................................................................................... 74

LINDA KAZI YAKO. ............................................................................................ 77

Page 5: BIASHARA NDANI YA AJIRA. - JamiiForums · ambacho wanakuwa hawajakijua ni kwamba hii ni hatari kubwa zaidi. Kwa sababu ukichukua muda na kuwafuatilia wengi wa wanaostaafu, huishia

5

WAKATI SAHIHI WA KUONDOKA KWENYE AJIRA. ............................................ 81

KITU MUHIMU KUFANYA MUDA WOTE. .......................................................... 87

ANZA SASA, NUNUA UHURU WAKO. ................................................................ 90

Page 6: BIASHARA NDANI YA AJIRA. - JamiiForums · ambacho wanakuwa hawajakijua ni kwamba hii ni hatari kubwa zaidi. Kwa sababu ukichukua muda na kuwafuatilia wengi wa wanaostaafu, huishia

6

UTANGULIZI. BIASHARA NDANI YA AJIRA ni kitabu ambacho kinakupa mbinu za kuanzisha na

kukuza biashara yako ukiwa bado umeajiriwa. Ni kitabu ambacho kila

mwajiriwa anapaswa kukisoma kwa sababu kina maarifa muhimu ya

kumwezesha mwajiriwa kujikomboa kiuchumi.

Wote ni mashahidi kwamba hali ya ajira kwa sasa imebadilika sana. Na kipato

cha ajira kimekuwa hakitoshelezi. Na hata zile njia ambazo watu walikuwa

wanatumia kujipatia kipato cha ziada kama posho, marupurupu na hata

rushwa kwa sasa vimedhibitiwa kwa kiasi kikubwa.

Hivyo njia pekee kwa waajiriwa kuweza kujitengenezea uhuru wa kipato ni

kuwa na vyanzo mbadala vya mapato. Kupitia kitabu hiki itajifunza mbinu za

kuanzisha biashara na kuikuza. Pia itajifunza aina za biashara unazoweza

kufanya ukiwa bado kwenye ajira. Utajifunza uwekezaji unaoweza kuanza

kufanya ukiwa hapo kwenye ajira yako.

Kikubwa na muhimu zaidi utajifunza mifereji nane ya kipato unayotakiwa

kujijengea ili kuweza kufikia uhuru wa kifedha. Utajifunza changamoto na

hatari za kuepuka na pia kuweza kuilinda kazi yako pale unapofanya biashara.

Kitabu hiki ni mwongozo muhimu kwako kufikia uhuru wa kifedha kwa kuwa na

biashara ya pembeni wakati umeajiriwa.

Soma kitabu hiki na yatumie yale ambayo umejifunza kwenye kitabu hiki katika

kuboresha kazi yako na biashara yako pia. Na mwishowe utafikia uhuru wa

maisha yako na mafanikio makubwa.

Nakutakia kila la kheri kwenye usomaji wa kitabu hiki, nina imani utajifunza

mengi na utayatumia kwenye kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa

ujumla.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

[email protected]

www.amkamtanzania.com

www.kisimachamaarifa.co.tz

Page 7: BIASHARA NDANI YA AJIRA. - JamiiForums · ambacho wanakuwa hawajakijua ni kwamba hii ni hatari kubwa zaidi. Kwa sababu ukichukua muda na kuwafuatilia wengi wa wanaostaafu, huishia

7

AJIRA NI SEHEMU NZURI YA KUANZIA BIASHARA. Tunaishi kwenye zama ambazo mabadiliko yanaendelea kutokea kwa kasi

kubwa sana. Hizi ni zama ambazo tunatoka kwenye ajira kuwa chanzo cha

uhakika cha kipato na tunaelekea kwenye biashara na ujasiriamali kama

chanzo cha uhakika cha kipato.

Miaka ya nyuma, hasa baada ya mapinduzi ya viwanda, kupata kazi ilikuwa

ndiyo ndoto kubwa ya kila mtu. Watu walisisitizwa kwenda shuleni, kusoma

kwa bidii sana ili wafaulu na kuweza kupata kazi nzuri. Kazi zilikuwa za uhakika

na wale waliokuwa wamesoma na kufaulu vizuri walikuwa na uhakika wa kazi.

Lakini kama ilivyo asili ya dunia kila kitu kinabadilika, na kila zama zina mambo

yake. Sasa hivi zama zile za kusoma ili upate kazi na uwe na uhakika wa maisha

mazuri hazipo tena. Ujio wa mapinduzi ya kiteknolojia umerahisisha sana

ufanyaji wa kazi. Mahali ambapo wangefanya kazi watu watano, anaweza

kufanya kazi mtu mmoja na kompyuta. Na pia zama hizi watu wengi sana

wameweza kupata elimu ya juu, wamesoma na kufaulu vizuri.

Kwa hali hii, ya nafasi za kazi kuwa chache, na wanaozitafuta nafasi hizo kuwa

wengi, thamani ya kazi imeshuka. Ule uhakika wa kwamba ukipata kazi nzuri

ndiyo uhakika wa kuwa na maisha mazuri haupo tena. Mtu anaweza kuwa

kwenye kazi leo na mwezi ujao kazi hiyo akawa hana tena.

Zamani ilikuwa kawaida kwa mtu kufanya kazi kwenye kampuni au taasisi moja

kuanzia ujana mpaka anazeeka, ila kwa sasa mpaka mtu anazeeka anakuwa

amefanya kazi sehemu tofauti zisizopungua tano. Hali hii inafanya kutegemea

ajira kama sehemu kuu ya kipato kushindikana na hivyo kila mtu anahitaji njia

mbadala ya kujiongezea kipato.

Na kwa hali ilivyo sasa, njia pekee ya uhakika ya kujitengenezea kipato ni

kupitia biashara na ujasiriamali. Kwa sababu kumekuwa na fursa nyingi za

kibiashara, sasa hivi karibu kila mtu anaweza kuingia kwenye biashara.

Mahitaji ya kuanza biashara kwa sasa ni rahisi kuliko kipindi cha nyuma. Fursa

za kibiashara ni nyingi na uzuri zaidi kuna biashara ambazo mtu anaweza

kuanza na mtaji kidogo sana na akaweza kuikuza. Pia mapinduzi ya kiteknolojia

pamoja na uwepo wa mtandao wa intaneti umerahisisha sana ufanyaji wa

biashara.

Page 8: BIASHARA NDANI YA AJIRA. - JamiiForums · ambacho wanakuwa hawajakijua ni kwamba hii ni hatari kubwa zaidi. Kwa sababu ukichukua muda na kuwafuatilia wengi wa wanaostaafu, huishia

8

Changamoto kwa waajiriwa.

Pamoja na uhakika huu wa kuweza kutengeneza kipato kupitia biashara na

pamoja na fursa nyingi zilizopo kwa wanaotaka kuanza biashara, waajiriwa

bado wamekuwa na changamoto moja kubwa. Na changamoto hii inaanzia

kwenye swali hili;

Je niache kazi na kuingia kwenye biashara au nikae kwenye kazi na biashara

nifanye baadaye nikishapata mtaji?

Hili ni swali zito ambalo limewafanya wengi kuwa njia panda na kushindwa

kufanya maamuzi sahihi. Na pia wapo ambao wamefanya maamuzi ambayo

siyo sahihi na kujikuta kwenye wakati mgumu kuliko walivyokuwa wanafikiri

awali.

Maamuzi mabovu.

Kwa wale wanaochagua kuacha kazi na kuingia kwenye biashara moja kwa

moja, wengi wamekuwa wakikutana na changamoto kubwa sana. Hasa pale

ambapo mtu anakuwa na wategemezi wengi, anajikuta akishindwa kukuza

biashara na wakati huo akiwa hana kipato. Tutaona kwenye sura za mbele

hatari ya kuchoma meli moto na pia biashara inahitaji kukua.

Ni wachache wanaochagua njia hii na wakafanikiwa kwenye biashara, tena

hawa ni wale ambao wanafanya maamuzi haya wakiwa bado ni vijana na

hawana wategemezi wengi. Kwa wale ambao wameshakaa kwenye ajira kwa

muda mrefu na wana watu wengi wanaowategemea, maamuzi ya kuacha kazi

na kuingia kwenye biashara ni hatari sana na yanakutana na vikwazo vingi

mno, kuanzia kwa mtu mwenyewe mpaka kwa wale wanaowazunguka.

Kwa upande wa pili kuna wale ambao wanasema hawawezi kuacha kazi na

kuingia kwenye biashara. Wanasema ni bora waendelee kubaki kwenye kazi

huku wakikusanya mtaji na wakishapata mtaji wa kutosha basi wataondoka

kwenye kazi na kuingia kwenye biashara.

Hawa nao wanakuwa wamefanya maamuzi mabovu sana kwa sababu hii moja;

hakuna siku inafika wakaweza kusema sasa nimekusanya mtaji wa kutosha na

nipo tayari kuacha kazi na niingie kwenye biashara. Kila wanapokusanya mtaji

ukafika kiasi fulani inatokea jambo linahitaji fedha na wanajikuta

wameshatumia, wanaanza tena. Na kadiri muda unavyokwenda wakiwa bado

wapo kwenye ajira ndivyo zoezi la kukusanya mtaji linakuwa gumu kwa sababu

majukumu yanaongezeka na kipato hakiwatoshi.

Page 9: BIASHARA NDANI YA AJIRA. - JamiiForums · ambacho wanakuwa hawajakijua ni kwamba hii ni hatari kubwa zaidi. Kwa sababu ukichukua muda na kuwafuatilia wengi wa wanaostaafu, huishia

9

Mwishowe wanaona kwa kuwa imeshindikana kupata mtaji wakiwa kazini, basi

ni heri wasubiri mpaka watakapostaafu ndipo watumie fedha yao ya kustaafu

kuanzisha biashara. Kwa sababu hapo watakuwa na fedha za kutosha. Kitu

ambacho wanakuwa hawajakijua ni kwamba hii ni hatari kubwa zaidi. Kwa

sababu ukichukua muda na kuwafuatilia wengi wa wanaostaafu, huishia

kufanya maamuzi mabovu sana ya kibiashara. Hujikuta wanawekeza kwenye

maeneo ambayo hawayajui vizuri na mwishowe kupata hasara.

Na kinachoumiza zaidi katika wakati huo ni kwamba nguvu zinakuwa

zimepungua na hivyo ile mikiki mikiki ya biashara wanakuwa hawaiwezi. Na hii

inazidi kuwaweka kwenye hali mbaya kiuchumi na kujikuta hawana popote pa

kusimamia.

Maamuzi sahihi kuchukua.

Katika swali ambalo tumeona waajiriwa wengi hujiuliza, iwapo waache kazi na

kuingia kwenye biashara au waendelee na kazi kukusanya mtaji, yote ni

maamuzi mabovu, yaani kuacha kazi ni maamuzi mabovu na kuendelea na kazi

na kuacha biashara ni maamuzi mabovu. Hapa unaweza kubaki na mawazo

mengi, je ni kipi sahihi?

Maamuzi sahihi kwa mwajiriwa kuchukua ni kufanya vyote kwa

pamoja. Yaani kubaki kwenye ajira yake huku akianzisha

biashara yake kwa pembeni.

Ndiyo, haya ni maamuzi bora sana ambayo mwajiriwa yeyote anayetaka

kujiboresha kiuchumi anatakiwa awe ameshayafanya. Na kama mpaka sasa

hujayafanya basi unapomaliza kusoma kitabu hiki fanya maamuzi haya na anza

kuyafanyia kazi

Najua utaanza kupata mawazo kwamba lakini haiwezekani, kazi yangu

inanibana, sina muda, sina mtaji na sababu nyingine nyingi. Sasa sababu zote

hizi ndio zimenifanya nikuandikie kitabu hiki, hivyo endelea kusoma na utapata

majibu ya changamoto zote zinazokuzuia usifanye kazi na biashara kwa

pamoja.

Ajira ni sehemu sahihi kwako kuanzia biashara kwa sababu nyingi sana

utakazojifunza kwenye kitabu hiki. Lakini hapa nitakushirikisha chache za

kuanza kuzifikiria wakati unaendelea kusoma kitabu hiki.

Page 10: BIASHARA NDANI YA AJIRA. - JamiiForums · ambacho wanakuwa hawajakijua ni kwamba hii ni hatari kubwa zaidi. Kwa sababu ukichukua muda na kuwafuatilia wengi wa wanaostaafu, huishia

10

1. Una uhakika wa kipato.

Japo ajira siyo za uhakika sana, na japo kipato cha ajira huwa hakitoshi, lakini

kuendelea kuwa na ajira wakati unaanza biashara yako ni nafasi nzuri sana

kwako. Hii ni kwa sababu unakuwa na uhakika wa kipato, kila mwezi unapata

mshahara. Biashara mwanzoni haina uhakika wa kipato, hivyo kuwa nacho

kutoka kwenye ajira, hata kama ni kidogo kinatosha kufanya mkono uende

kinywani, huku ukipambana kukuza biashara yako.

Hakuna kitu kibaya na kinachoweza kukurudisha nyuma kama kuendesha

biashara huku huna uhakika wa mkono kwenda kinywani, na hasa kama una

familia. Kuwa na kipato cha uhakika kunaifanya akili yako itulie na uweze

kufanya maamuzi bora.

2. Unaipa biashara nafasi ya kukua.

Kwa kuwa na kipato kutokana na mshahara wako, kunakufanya usiitegemee

biashara yako wakati wa mwanzoni. Na hii ni muhimu sana kwa sababu wakati

wa mwanzo biashara inakuwa haizalishi, na mbaya zaidi inakuwa inakuhitaji

wewe uweke fedha zaidi kwenye biashara hiyo. Hivyo unapokuwa na mshahara

unaipa biashara nafasi ya kukua bila ya wewe kuiingilia.

3. Una fursa kubwa ya kupata na kuongeza mtaji.

Unapokuwa kwenye ajira, nafasi yako ya kupata msaada wa kifedha hasa kwa

njia ya mkopo ni kubwa kuliko ambaye hayupo kwenye ajira. Kwa kuwa

kwenye ajira pekee ni dhamana ya wewe kupata mkopo hata kama huna

nyumba wala gari. Wakati ambaye hana ajira atahitaji kutafuta dhamani ndiyo

aweze kupata mkopo, kitu ambacho kinaweza kuwa kigumu sana kwake.

Kama upo kwenye ajira na bado hujaanza biashara unajipunja. Unajiweka

kwenye hali ya hatari sana kiuchumi, kama ambavyo tutaona kwenye sura

zijazo, kuwa na chanzo kimoja cha kipato ni hatari kubwa sana. Na kuna faida

nyingi sana za kuanza biashara ukiwa bado umeajiriwa kama tulivyoona hizi

tatu, tutaziangalia nyingine kwa undani kwenye sura za mbele.

Page 11: BIASHARA NDANI YA AJIRA. - JamiiForums · ambacho wanakuwa hawajakijua ni kwamba hii ni hatari kubwa zaidi. Kwa sababu ukichukua muda na kuwafuatilia wengi wa wanaostaafu, huishia

11

HATARI YA KUCHOMA MELI MOTO. “Choma meli moto ili usipate nafasi ya kurudi nyuma”. Huu ni usemi uliokuwa

maarufu sana siku za nyuma ambapo vuguvugu la watu kutoka kwenye ajira na

kuingia kwenye biashara lilipoanza kupamba moto.

Chanzo cha usemi wa kuchoma meli moto.

Usemi huu ulitokana na hadithi moja ya kivita. Ambapo kulikuwa na mapigano

baina ya pande mbili, na kiongozi wa upande mmoja akawachukua wapiganaji

wake kuelekea eneo la mapambano. Ili kufika walitakiwa kupanda meli maana

walitenganishwa na maji na usafiri pekee ulikuwa meli. Walipofika upande wa

pili na kutoa mizigo yao yote kwenye meli, kiongozi aliamuru meli zile

zichomwe moto.

Wapiganaji wake walishangaa sana kitendo kile, wakati meli zinaungua

akawageukia na kuwaambia, wote mnaona meli tulizokuja nazo zinatekelea

kwa moto. Hii ina maana kwamba kwenye hii vita tunatakiwa kuchagua moja

kati ya haya mawili, tushinde vita hii na kuishi, au tushindwe vita hii na

tuuwawe wote, hakuna njia ya kurudi nyuma.

Hii ni hadithi yenye hamasa kubwa sana, yenye kuweza kukusukuma uchukue

hatua, na uweze kufikia mafanikio? Si ndiyo? Ni kweli kwa upande mmoja,

lakini kwenye uhalisia wa maisha, kuna mambo mengi sana unahitaji

kuyafikiria kwa kina kabla hujachoma meli moto.

Kwenye hili la ajira au biashara, kuchoma meli moto itakuwa kuacha kazi mara

moja na kuingia kwenye ajira. Kwa kuwa umeshaacha kazi na huna tena kipato

kingine, basi utapambana kufa na kupona ili uweze kufanikiwa kwenye

biashara unayokwenda kuanzisha, hii ni kweli kwa upande mmoja, lakini kwa

hali ilivyo sasa, ni hatari kubwa sana kuchukua, hasa kama umeshakaa kwenye

ajira yako kwa muda mrefu.

Ni hatari sana kuchoma meli moto kwenye zama hizi kwa

sababu hali ya uchumi imekuwa haitabiriki, biashara zimekuwa

na changamoto kubwa na pia ushindani wa kibiashara

umekuwa mkubwa sana.

Uchumi wa sasa umekuwa hautabiriki, hata mambo yaonekane mazuri kiasi

gani, hakuna mwenye kuweza kujua kwa uhakika hali hiyo itakwenda mpaka

Page 12: BIASHARA NDANI YA AJIRA. - JamiiForums · ambacho wanakuwa hawajakijua ni kwamba hii ni hatari kubwa zaidi. Kwa sababu ukichukua muda na kuwafuatilia wengi wa wanaostaafu, huishia

12

lini. Tumekuwa tunaona mtikisiko wa kiuchumi unavyoleta changamoto

kwenye biashara nyingi duniani. Unaweza kuweka juhudi zako kubwa kwenye

biashara yako, ukawa na wazo zuri la biashara ila sababu za kiuchumi ambazo

wewe huwezi kuziathiri zikazuia biashara yako kukua. Hivyo kwenye hali kama

hii kuchoma meli moto ni kujiweka kwenye hatari kubwa. Wote tunajua ya

kwamba bila ya hatari huwezi kupata faida kubwa, lakini pia ni lazima tupime

vizuri hatari tunazochukua, kama una njia mbili ambazo zote zinakufikisha

sehemu moja, ila moja ina simba na nyingine ina tembo, wote ni hatari, lakini

ni bora kupita kwenye tembo kuliko kupita kwenye simba. Kwa kuwa

inawezekana kuanza biashara yoyote ukiwa bado umeajiriwa, kwa nini ujiingize

kwenye hatari kubwa kwa kuacha kazi ndipo uingie kwenye biashara?

Kuchoma meli moto pia ni hatari sana kwa sababu wazo lako la biashara siyo

biashara yako. yaani wazo unalianza nalo, ambalo linakusukuma kuingia

kwenye biashara, siyo biashara utakayokuja kuifanya huko mbeleni. Kadiri

unavyofanyia kazi wazo lako, ndivyo utakavyozidi kuona ni vitu gani

hukuzingatia au hukujua na hivyo unahitaji kufanya mabadiliko. Sasa

mabadiliko kama haya ni vizuri kuyafanya ukiwa huna msukumo wa kupata

kipato, hivyo kuwa kwenye ajira kunakupa nafasi ya kukuza wazo lako la

biashara na kulijua vizuri. Unapokuwa unategemea biashara unayoanzisha

kama ndiyo njia kuu ya kipato, utashindwa kufanya mabadiliko kwa sababu

hutakuwa na uhakika kama mabadiliko hayo yataleta faida unayotegemea.

Haya ni maamuzi unayoweza kuyafanya kwa uhakika unapokuwa na chanzo

kingine cha kipato tofauti na biashara uliyoanzisha.

Changamoto pia zinaweza kukuondoa kabisa kwenye biashara kama

umechoma meli moto. Iko hivi, hata ujiandae vyema kiasi gani, hata ufanye

utafiti mkubwa kiasi gani, hata uandaliwe mchanganuo wa biashara na

mtaalamu wa biashara aliyebobea, bado utakutana na changamoto kwenye

biashara, pale unapoingia kufanya. Kwenye makaratasi biashara ni rahisi sana

kuipanga, ila unapoingia kuifanya biashara yenyewe, ndipo unapoona vitu

ambavyo hukutegemea kabisa. Na hata kama ulivipangilia bado kutakuwa na

mambo ambayo hukuzingatia. Sehemu ambayo unaweza kujifunza biashara

kwa uhakika ni kwa kufanya, je ungependa kujifunza biashara kwa akiba yako

pekee huku huna uhakika wa kupata faida, au ungependa kujifunza biashara

huku bado una kipato? Kwa hakika kujifunza biashara huku una kipato ni

chaguo sahihi, ndiyo maana nakushauri usichome meli moto kabla hujaisoma

biashara vizuri.

Page 13: BIASHARA NDANI YA AJIRA. - JamiiForums · ambacho wanakuwa hawajakijua ni kwamba hii ni hatari kubwa zaidi. Kwa sababu ukichukua muda na kuwafuatilia wengi wa wanaostaafu, huishia

13

Kumekuwa na ushindani mkubwa sana wa kibiashara kwa sasa. Biashara

yoyote unayofanya kila mtu anaweza kuifanya. Na mara nyingi utaanza na

biashara ambayo tayari inafanyika. Au hata ukianza na biashara ya kipekee

kwako, kama itaonekana ni nzuri, kwa haraka sana wengi watakuiga. Hivyo kwa

vyovyote vile utajikuta kwenye ushindani mkali. Na njia pekee ya kushinda

kwenye ushindani huu ni kuboresha biashara yako na kutengeneza wateja

ambao wanaiamini biashara yako. zoezi hili linachukua muda, siyo kitu cha

muda mfupi. Kuna wakati utajikuta unaendesha biashara bila ya faida, ili tu

kujenga misingi ya biashara yako. Unaweza kufanya hili vizuri ukiwa bado una

ajira. Unapokuwa umetoka kwenye ajira na unaitegemea biashara kama

sehemu ya kipato, utalazimika kuingia kwenye ushindani wa moja kwa moja,

kitu ambacho kitazidi kuharibu biashara yako. Kuchoma meli moto ukiwa bado

hujajijengea uwezo wa kuzishinda biashara nyingine ni hatari kubwa sana

kwako.

Kazi unayofanya sasa inaweza kuwa sehemu sahihi kwako kukutana na wateja

wa biashara yako mpya. Au kuwepo kwenye kazi hiyo kunakukutanisha na

watu muhimu ambao wanaweza kuisaidia biashara yako kukua. Kuwepo

kwenye ajira pia kunaweza kukupa wewe upendeleo fulani ambao

wafanyabiashara wengine hawawezi kuupata. Kwa wewe kuwa kwenye ajira na

kuziona hizo nafasi vizuri kutakuwezesha kuikuza biashara yako vizuri. Kwa

kuchoma meli moto kunakuzuia wewe kupata fursa hizi nzuri ambazo

zingeiwezesha biashara yako kukua.

Kumekuwa na ushauri kwamba unaweza kuacha kazi kama umeshajiwekea

akiba ya angalau miezi sita ya kuishi bila ya kuitegemea biashara yako. huu nao

ni ushauri mzuri sana, lakini bado changamoto ni kubwa sana. Kama ambavyo

tumeshaona, hali ya uchumi haitabiriki. Unaweza kupanga kwamba kwa miezi

sita unahitaji kiasi fulani cha fedha kuishi, lakini unapokuwa tayari

umeshaondoka kwenye ajira mambo yakabadilika. Na pia bado kuna dharura

ambazo huwezi kujua zitakuja kwa kiasi gani na hivyo chochote unachopanga

kinaweza kisikutoshe kwa muda uliopanga. Hapo bado hujaangalia mwenendo

wa biashara yako kwa miezi hiyo sita, ni mara chache sana biashara inaweza

kuwa imeshaweza kujiendesha yenyewe ndani ya miezi sita. Biashara nyingi

zinahitaji muda mrefu zaidi ya hapo ili ziweze kujiendesha mwenyewe. Hivyo

hata kama unaweza kuweka pembeni kipato cha kukutosha kwa miezi sita,

usichome meli moto.

Page 14: BIASHARA NDANI YA AJIRA. - JamiiForums · ambacho wanakuwa hawajakijua ni kwamba hii ni hatari kubwa zaidi. Kwa sababu ukichukua muda na kuwafuatilia wengi wa wanaostaafu, huishia

14

Unapokuwa kwenye njia panda ya kuacha kazi na kuingia kwenye biashara au

kuendelea na ajira na kuacha biashara, mimi nakushauri usichome meli moto.

Fanya vyote kwa pamoja na kazana sana kuhakikisha unaifanya biashara yako

kusimama kama kweli unachotaka ni kupata uhuru wa kipato. Kwa haya

tuliyojadili hapa kuhusu kutokuchoma meli moto unaweza kuona kama nakupa

woga wa kutokuondoka kwenye biashara, lakini ninachofanya hapa ni

kukuonesha ukweli halisi ni upi. Kwa sababu watu wengi wamekuwa wakifanya

maamuzi kwa mihemko au wakiwa na hisia kali na hivyo wanashindwa kufikiri

kwa kina. Baadaye wanapojikuta kwenye wakati mgumu ndiyo wanagundua ya

kwamba walifanya makosa makubwa. Usichome meli yako moto, badala yake

kaa kwenye meli hiyo na pambana ukiwa ndani ya meli mpaka uhakikishe

umeshinda vita ya kujijengea uchumi imara.

Page 15: BIASHARA NDANI YA AJIRA. - JamiiForums · ambacho wanakuwa hawajakijua ni kwamba hii ni hatari kubwa zaidi. Kwa sababu ukichukua muda na kuwafuatilia wengi wa wanaostaafu, huishia

15

JIPATIE KITABU UENDELEE KUSOMA. Kama umependezwa na hizi sura mbili za kitabu ulizosoma, jipatie kitabu kamili

ili uweze kujifunza kwa undani zaidi na uweze kuchukua hatua.

Kwenye sura za mbele kuna biashara unazoweza kuanza kufanya ukiwa bado

umeajiriwa, uwekezaji unaotakiwa kufanya na pia kuna mifereji nane ya kipato

unayotakiwa kuanza kuitengeneza. Na katika kila mfereji kuna uzuri wake na

changamoto zake.

Pia kuna mbinu za kuilinda kazi yako dhidi ya mkataba wako wa ajira na hata

majungu ya wafanyakazi wenzako hasa pale biashara yako itakapoanza

kuonesha mafanikio.

JINSI YA KUPATA KITABU HIKI;

Kitabu kinatumwa kama nakala tete yaani softcopy kwenye mfumo wa pdf.

Kwa mfumo huu unaweza kusoma kitabu hiki kwenye simu yako kama ina

uwezo wa kusoma vitabu na pia unaweza kusoma kwa kutumia kompyuta.

Unatumiwa kitabu hiki kwa njia tatu, utachagua ile unayotaka wewe;

1. Kwa njia ya wasap, unaweza kutumiwa kwenye namba yako ya wasap na

ukapakua kusoma.

2. Kwa njia ya telegram, pia unaweza kutumiwa kwenye namba yako ya

telegram na ukapakua kusoma.

3. Kwa njia ya email, unaweza kutumiwa kitabu hiki moja kwa moja kwenye

email yako.

Gharama ya kitabu hiki ni shilingi za Kitanzania elfu kumi tu (tsh 10,000/=). Ili

kupata kitabu hiki tuma fedha kwenye namba zifuatazo;

1. Kama unatumia M- PESA tuma kwenda namba 0755 953 887 (jina AMANI

MAKIRITA)

2. Kama unatumia TIGO PESA au AIRTEL MONEY tuma kwenda namba 0717

396 253 (jina AMANI MAKIRITA)

3. Kama upo nje ya Tanzania tuwasiliane kwa wasap 0717 396 253 au email na

nitakupa utaratibu mzuri wa kulipia kulingana na ulipo.

Page 16: BIASHARA NDANI YA AJIRA. - JamiiForums · ambacho wanakuwa hawajakijua ni kwamba hii ni hatari kubwa zaidi. Kwa sababu ukichukua muda na kuwafuatilia wengi wa wanaostaafu, huishia

16

Ukishatuma malipo ya kitabu, tuma ujumbe wa kawaida au wasap kwenda

namba 0717 396 253 wenye jina la kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA na

utatumiwa kitabu hiki kizuri.

Karibu sana rafiki yangu, ujipatie kitabu hiki ambacho kitakuwezesha kuanzisha

na kukuza biashara yako ukiwa bado umeajiriwa.

TUPO PAMOJA,

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani.