98
Coast Development Authority Bonde la Pangani: Uchambuzi wa Hali Halisi (Toleo la pili)

Bonde la Pangani - portals.iucn.orgbila ya kuomba kibali kutoka kwa mmiliki, ilimradi rejeo litajwe. IUCN ingependelea kupata nakala ya makala yoyote ambayo itatumia kitabu hiki kama

  • Upload
    others

  • View
    0

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

  • Coast Development Authority

    Bonde la Pangani:Uchambuzi wa Hali Halisi (Toleo la pili)

  • Bonde la Pangani:Uchambuzi wa Hali Halisi (Toleo la pili)

    Programu ya IUCN Afrika Mashariki na Kusini

    2009

    i

  • Mchapishaji:

    Hatimiliki: © 2009 Shirika la Kimataifa la Uhifadhi ya Uasili na Maliasili.

    Kitabu hiki kinaweza kutolewa chote au sehemu yake kwa njia yoyote kwa matumizi ya maendeleo ya elimu au matumizi mengine yasiyo ya biashara bila ya kuomba kibali kutoka kwa mmiliki, ilimradi rejeo litajwe. IUCN ingependelea kupata nakala ya makala yoyote ambayo itatumia kitabu hiki kama rejea.

    Hairuhusiwi kuuza kitabu hiki, au kukitumia kwa madhumuni mengine ya kibiashara bila ya idhini ya maandishi ya IUCN.

    Jina kamili: Programu ya IUCN Afrika ya Mashariki, 2009. Uchambuzi wa Hali Halisi Bonde la Mto Pangani. Toleo la pili, xii + uk.83.

    ISBN: 978-2-8317-1191-1

    Usanifu na Mpangilio: Gordon O. Arara

    Mpiga chapa: Kulgraphics Ltd.

    Picha ya 1: Kilele cha Mlima Kilimanjaro; Picha ya 2: Sehemu ya msitu wa Shiri Njoro; Picha ya 3: Banio la kudhibiti maji yanayoingia katika mfereji wa umwagiliaji; Picha ya 4: Watoto wakiogelea kwenye hodhi ya maji ya umwagiliaji; Picha ya 5: Shamba la mkonge; Picha ya 6: Mradi wa umwagiliaji wa mpunga ; Picha ya 7: Kituo cha kupimia usawa wa maji- Chemchemi ya Chemka; Picha ya 8: Banio la mfereji wa umwagiliaji lililoharibiwa; Picha ya 9: Ukuta wa Bwawa la Nyumba ya Mungu (mabadiliko ya rangi yanaonesha upunguaji wa kina cha maji); Picha ya 10: Mchuuzi akiuza maji kutoka kwenye kisima.

    Picha namba 1, 3, 5, 6, 8, 9 hatimiliki ya 2003 ya Kelly West; Picha namba 2 na 7 hatimiliki ya 2002 ya Kim Geheb; Picha namba 4 na 10 hatimiliki ya 2003 ya Ger Bergkamp.

    Kitabu hiki kinapatikana: Kitengo cha Huduma za Uchapishaji cha IUCN-ESARO, S.L.P. 68200–00200, Nairobi, Kenya; Simu ++254 20 890605-12 Faksi ++254 20 890615; Barua pepe; [email protected]

    Uteuzi wa Maumbo ya kijiografia na nyenzo zilizotumika kuwasilisha ujumbe katika kitabu hiki, hayawakilishi kwa namna yoyote ile maoni ya asasi zinazoshiriki kuhusiana na sheria ya nchi yoyote, au eneo lake, au mamlaka zake, au kuhusu makazi na uwekaji wa mipaka yake.

    Maoni yaliyotolewa na waandishi katika kitabu hiki sio lazima kwamba yanawakilisha maoni ya PBWO, CDA, WANI au IUCN.

    1

    2 3 4

    5

    6

    7 89 10

    ii

  • Yaliyomo Tafsiri ya vifupisho ............................................................................................................................vDibaji ................................................................................................................................................viiMuhtasari .......................................................................................................................................viii

    A Utangulizi wa Uchambuzi wa Hali Halisi wa Bonde la Mto Pangani ...................................1 A.1 Maelezo ya jumla ya Bonde la Mto Pangani ...................................................................1A.2 Usimamizi wa Pamoja wa Mabonde ya Mito (wa) ............................................................5 A.3 Programu ya Hifadhi ya Maji na Uasili (WANI) .................................................................6 A.4 Uchambuzi wa Hali Halisi: madhumuni na matokeo ........................................................7 A.5 Vyanzo vya data ..............................................................................................................7 A.6 Muundo wa Uchambuzi wa Hali Halisi .............................................................................8

    B Rasilimali za asili zilizopo katika Bonde la Mto Pangani .....................................................9B.1 Utangulizi .............................................................................................................................9B.2 Misitu iliyopo katika Bonde ..................................................................................................9B.3 Maji na ardhioevu ..............................................................................................................15B.4 Maeneo yaliyohifadhiwa ....................................................................................................19B.5 Bayoanuwai na Hifadhi ......................................................................................................20B.6 Uvuvi .................................................................................................................................22B.7 Udongo ..............................................................................................................................23B.8 Majumuisho ya hoja...........................................................................................................23

    C Uchumi wa kijamii katika Bonde la Mto Pangani ................................................................25C.1 Maelezo ya jumla ..............................................................................................................25C.2 Shughuli za Viwanda .........................................................................................................27C.3 Shughuli za Kilimo .............................................................................................................27C.4 Shughuli za Wafugaji .........................................................................................................31C.5 Shughuli za Mijini ..............................................................................................................32C.6 Shughuli za Asasi Zisizo za Kiserikali na Mashirika ya Kimataifa ....................................32C.7 Migogoro ...........................................................................................................................40C.8 Majumuisho ya hoja .........................................................................................................46

    D Usimamizi wa Maliasili katika Bonde la Mto Pangani .......................................................47D.1 Utangulizi ........................................................................................................................47D.2 Usimamizi wa Serikali, Sheria na Sera............................................................................ 47D.3 Usimamizi katika ngazi ya jamii ........................................................................................52D.4 Usimamizi wa bonde kimataifa .........................................................................................55D.5 Ukusanyaji na ufuatiliaji wa data ......................................................................................55D.6 Majumuisho ya hoja..........................................................................................................57

    E Matatizo na masuala mbalimbali katika Bonde la Mto Pangani......................................58E.1 Utangulizi ..........................................................................................................................58E.2 Masuala na matatizo ya Bonde la Mto Pangani ................................................................58E.3 Maeneo ya kipaumbele kwa Utendaji ...............................................................................62

    F Hitimisho ................................................................................................................................64F.1 Majumuisho ya Matokeo ...................................................................................................64

    G Rejea ....................................................................................................................................68 H Kiambatanisho cha 1: Mabonde madogo yaliyojumuishwa kiutawala

    katika Bonde la Pangani ..................................................................................................... 75H.1 Utangulizi .........................................................................................................................75

    iii

  • H.2 Bonde la Mto Umba .........................................................................................................75H.3 Bonde la Mto Msangazi....................................................................................................77H.4 Bonde la Mto Zigi .............................................................................................................78H.5 Bonde la Mto Mkulumuzi ..................................................................................................82

    Orodha ya MajedwaliJedwali la 1: Aina, matumizi na hadhi ya kisheria ya misitu ya Tanzania ...........................................9Jedwali la 2: Upotevu wa utando wa msitu wa Milima ya Tao la Mashariki katika

    Bonde la Mto Pangani .................................................................................................13Jedwali la 3: Makadirio ya mahitaji ya maji kwa mwaka 1995 na matarajio ya

    mahitaji ya maji mwaka 2015 ......................................................................................18Jedwali la 4: Misingi ya Uchumi wa kijamii wa Tanzania na Kenya mwaka 2001 ............................26Jedwali la 5 Idadi ya Mifugo katika baadhi ya maeneo ya Bonde la Mto Pangani (2002) ............ 31Jedwali la 6: Hati za kutumia maji katika Bonde la Mto Pangani (Tanzania), Mei, 2003 ..................50Jedwali la 7: Eneo la misitu chini ya Usimamizi wa Misitu wa Pamoja kwa mikoa ..........................54

    Orodha ya Michoro Mchoro Na.1: Bonde la mto Pangani lilivyoenea Tanzania na Kenya .................................................2 Mchoro Na 2: Bonde la Mto Pangani ..................................................................................................3Mchoro Na 3: Utawala wa Misitu Tanzania .......................................................................................51Mchoro Na 4: Ramani ya Bonde la Pangani- Utawala .....................................................................83

    Orodha ya PichaPicha ya 1: Ramani ya Bonde la Mto Pangani .................................................................................33Picha ya 2: Ramani ya Bonde la Pangani kiutawala ........................................................................34Picha ya 3: Kilele maarufu chenye barafu cha Mlima Kilimanjaro mwaka 1993 na 2000 ................................................................................................................35Picha ya 4: Mto Karanga - Moshi ......................................................................................................36Picha ya 5: Mlima Kilimanjaro ..........................................................................................................36Picha ya 6: Mfereji wa umwagiliaji Wilayani Moshi ...........................................................................37Picha ya 7: Chemchemi iliyofunikwa ya Shiri-Njoro ..........................................................................38Picha ya 8: Miteremko kwenye misitu ya Mlima Meru ......................................................................38

    Orodha ya VisandukuKisanduku cha 1: Usimamizi wa Mahitaji ya maji ................................................................................6Kisanduku cha 2: Taarifa za msingi za misitu ya Bonde la Mto Pangani ...........................................10Kisanduku cha 3: Milima ya Taita ......................................................................................................11Kisanduku cha 4: Tishio kwa misitu ya Bonde la Mto Pangani..........................................................14Kisanduku cha 5: Taarifa za msingi za maji na ardhioevu katika Bonde la Mto Pangani .............15Kisanduku cha 6: Tishio kwa rasilimali za maji na ardhioevu ya Bonde la Mto Pangani ..................16Kisanduku cha 7: Tishio kwa maeneo yaliyohifadhiwa ya Bonde la Mto Pangani ............................20Kisanduku cha 8: Maeneo muhimu sana kwa bayoanuwai ..............................................................21Kisanduku cha 9: Kundi la kwanza la spishi ya ndege wa Milima ya Usambara

    walio hatarini ........................................................................................................22Kisanduku cha 10: Kasoro za usanifu wa miundombinu ya mifereji ya asili .....................................28Kisanduku cha 11: Magadi na chumvichumvi ....................................................................................30Kisanduku cha 12: Utawala wa Maji nchini Kenya ............................................................................51Kisanduku cha 13: Uanzishwaji wa usimamizi wa kijamii katika msitu wa Duru-Haitemba,

    Mkoani Manyara ............................................................................................53Kisanduku cha 14: Mfano wa Chama Cha Watumia Maji .................................................................56

    iv

  • Tafsiri ya VifupishoANR ...................... Hifadhi ya Asili ya AmaniASL ....................... Juu ya Usawa wa BahariAUWSA................. Mamlaka ya Maji safi na na Maji taka ArushaBWB ..................... Bodi ya Maji ya BondeBWO ..................... Afisa wa Maji wa BondeCBNRM ................ Usimamizi wa Maliasili KijamiiCCM ..................... Chama Cha MapinduziCDA ...................... Mamlaka ya Maendeleo Pwani (Kenya)CFR ...................... Hifadhi ya Misitu ya JamiiCFP ...................... Mradi wa Misitu Eneo la Chanzo cha MtoCPRs .................... Rasilimali za JamiiDFO ...................... Afisa Misitu wa WilayaDGIS ..................... Wizara ya Mambo ya Nje ya UholanziEACBP ................. Mradi wa Bayoanuwai za kimataifa za Afrika MasharikiEU......................... Umoja wa Nchi za UlayaEU-ACP ................ Umoja wa Ulaya – Afrika, Caribbean na PasifikiFAO ...................... Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa MataifaFBD ...................... Idara ya Misitu na NyukiGEF ...................... Mfuko wa huduma ya Mazingira DunianiGIS ....................... Mifumo ya Habari wa KijiografiaGOK...................... Serikali ya KenyaHa ......................... HektaIRBM ..................... Usimamizi wa Pamoja wa Mabonde ya MitoIDA ........................ Chama cha Maendeleo cha KimataifaIUCN ..................... Shirika la Kimataifa la Hifadhi ya Uasili JFM ....................... Usimamizi wa Pamoja wa MisituKWH ..................... Kilowati kwa saaLGA....................... Serikali za MitaaLMIS ..................... Skimu ya Umwagiliaji ya “Lower Moshi”MAFS .................... Wizara ya Kilimo na ChakulaMCM ..................... Mita za ujazo Milioni MGR ..................... Hifadhi ya Wanyamapori ya MkomaziMMP ..................... Mradi wa Usimamizi wa MikokoMoU ...................... Mkataba wa MakubalianoMoWLD ................. Wizara ya Maji na Maendeleo ya Mifugo MTESM ................. Mkakati wa Taifa Kuendeleza Sekta ya MajiMW ....................... MegawatiNAWAPO .............. Sera ya maji ya Taifan.d......................... Hakuna TareheNEMC ................... Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira

    v

  • NGO ..................... Shirika Lisilo la KiserikaliNPF ...................... Mradi Mpya wa Maporomoko ya Mto PanganiNORAD ................. Shirika la Kimataifa la Misaada la NorwayNRM ..................... Usimamizi wa MaliasiliNWP ..................... Sera ya MajiNyM ...................... Bwawa la Nyumba ya MunguPA ......................... Maeneo Yaliyohifadhiwa PBWB ................... Bodi ya Maji ya Bonde la PanganiPBWO ................... Ofisi ya Maji ya Bonde la PanganiPRB ...................... Bonde la Mto PanganiPRBMP ................. Mradi wa Usimamizi wa Bonde la Mto PanganiRBM ...................... Mradi wa Usimamizi wa Matumizi Bora ya MajiRBMSIIP ............... Mradi wa Usimamizi wa Matumizi Bora ya Maji na Uboreshaji wa Kilimo cha

    Umwagiliaji cha Wakulima Wadogo wadogoRCE ...................... Kituo cha Kanda cha viumbe vipatikanavyo kipekeeRHO ...................... Afisa Haidrolojia wa MkoaRNRO ................... Afisa Maliasili wa MkoaSA ......................... Uchambuzi wa Hali Halisi SNV ...................... Shirika la Maendeleo la UholanziTANAPA ................ Mamlaka ya Hifadhi za TaifaTANESCO ............ Shirika la Ugavi wa Umeme TanzaniaTCMP ................... Ubia wa Usimamizi wa Pwani TanzaniaICZCDP ................ Programu ya Hifadhi na Maendeleo ya Ukanda wa Pwani TangaTFAP ..................... Mpango wa Utekelezaji wa Misitu TanzaniaTFCG .................... Kikundi cha Hifadhi ya Misitu TanzaniaTIP ........................ Shirika la Umwagiliaji Kiasili na Maendeleo ya MazingiraTPC ...................... Kampuni ya Kiwanda cha Sukari Moshi (Tanzania)UNICEF ................ Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Dharura kwa WatotoUNDP ................... Shirika la Maendeleo la Umoja wa MataifaUSAID................... Wakala wa Marekani kwa Maendeleo ya KimataifaVNRC ................... Kamati ya Maliasili za KijijiVWN ..................... Dira ya Maji na UasiliWANI .................... Programu ya Hifadhi ya Maji na Uasili ya IUCNWDM ..................... Usimamizi wa Mahitaji ya MajiWHO ..................... Shirika la Afya la Umoja wa MataifaWRMA .................. Mamlaka ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji (Kenya)WRM Act ............... Sheria ya Usimamizi wa Rasilimalui za Maji ya mwaka 2009WUA ..................... Chama Cha Watumiaji Maji

    vi

  • Dibaji

    Madhumuni ya toleo la kwanza la Uchambuzi ya Hali ya Bonde la Mto Pangani yalikuwa kuainisha rasilimali za asili zilizomo katika Bonde hilo, matukio yanayoziathiri na kutambua maeneo ya kufanyia kazi. Madhumuni mengine yalikuwa kutambua mashirika, asasi na wadau wengine ambao IUCN ingeweza kushirikiana nao.

    Lengo la WANI ni kuhakikisha kwamba suala zima la ikolojia linazingatiwa katika sera, mipango, na usimamizi wa mabonde ya mito. Katika maeneo ya mabonde ya kufanyia maonyesho yaliyoteuliwa duniani, WANI imepania: kuonyesha namna ya kusimamia mfumo ikolojia, kuwawezesha wananchi kushiriki katika usimamizi endelevu wa rasilimali za maji, kuendeleza usimamizi bora wa vyanzo vya maji na ardhioevu, kuanzisha na kutumia nyenzo za kiuchumi na vivutio, kuongeza maarifa ya kusaidia kufikia maamuzi na kutoa mafunzo yatakayoleta mwamko wa matumizi bora ya maji.

    Kufuatia mashauriano na wadau katika Bonde na kwa kuzingatia maazimio ya warsha iliyoendeshwa na Ofisi ya Maji ya Bonde la Pangani (PBWO) kwa ushirikiano na IUCN - Shirika la Kimataifa la Kuhifadhi Uasili iliyofanyika Moshi, Tanzania, kuanzia tarehe 8 hadi 10 Mei, 2002, Bonde la Mto Pangani nchini Tanzania na Kenya lilichaguliwa kuwa eneo la maonyesho la WANI.

    Ikiwa ni sehemu ya shughuli zake za mradi wa maendeleo katika Bonde la Mto Pangani, IUCN ilimwajiri Mshauri Mtaalamu Dk. Kim Geheb, kufanya Uchambuzi wa Hali halisi ya bonde hili. Kazi za ugani kwa ajili ya uchambuzi wa hali halisi zilifanyika mwezi Novemba, mwaka 2002, na ilihusisha mahojiano na wadau mbalimbali katika bonde. Vyanzo vya ziada vya taarifa vilikuwa ni marejeo ya machapisho pamoja na mjadala wa warsha iliyotajwa hapo juu, iliyojulikana kwa jina la “Bonde la Mto Pangani: Usimamizi Shirikishi”

    Madhumuni ya Uchambuzi wa Hali halisi ni kama yafuatayo:-• Kuainisha rasilimali mbalimbali zilizomo katika Bonde la Mto Pangani , na kufahamu michakato na

    matukio yanayoziathiri.• Kutambua kwa mapana maeneo ya kiutendaji ambayo yanaweza kushughulikiwa kwa manufaa ya

    kimaendeleo.• Kutambua taasisi na asasi mbalimbali zilizopo, na zenye nia ya kujishughulisha na rasilimali za

    maji, ambazo IUCN inaweza kuingia nazo ubia kwa lengo la kuendeleza juhudi za WANI katika Bonde la Mto Pangani.

    Kitabu hiki “Uchambuzi wa Hali Halisi ya Bonde la Mto Pangani“ awali kilitafsiriwa na Ofisi ya Maji Bonde la Pangani. Bw. Ipyana E. Mwakalinga alikamilisha kwa kuboresha baadhi ya sehemu na kuhariri toleo hili la pili kwa lugha ya Kiswahili.

    Rasimu ya kwanza ya Uchambuzi wa Hali Halisi katika Bonde la Mto Pangani ilikamilika mwishoni mwa mwaka 2002 na kusambazwa kwa wadau kwa ajili ya mapitio na maoni. Katika warsha iliyoandaliwa na PBWO na IUCN mjini Moshi mwezi Machi 2003, wadau walitoa maoni na kupendekeza marekebisho kadhaa. Maoni na mapendekezo ya ziada yalipokelewa kutoka PBWO na Mamlaka ya Maendeleo ya Pwani (CDA - Kenya) kwenye mkutano wa IUCN, PBWO na CDA uliofanyika Nairobi mwezi Mei, mwaka 2003. Mwaka 2009 uchapishaji upya wa Uchambuzi ya Hali ya Bonde ulihitajika na ikaamuliwa kutumia nafasi hii kufanyia mapitio ya taarifa chache ikizingatiwa kuwa sheria mpya ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji iliyopitishwa July 2009 na inafanya kazi. Ieleweke kuwa taaarifa zilizofanyiwa mapitio ni zile tu zinazohusu miuondo ya utawala, mifumo ya kitaasisi, sheria na sera za maji, vilevile taarifa mpya kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa Mradi wa Usimamizi wa Bonde la Pangani zimeongezewa, lakini maeneo mengine yote ya uchambuzi yameachwa kama yalivyo. Kazi hii yakufanyia mapitio Uchambuzi ya Hali ya Bonde la Pangani imegharamiwa na Global Water initiative (mpango wa maji wa dunia) unaofadhiliwa na mfuko wa Howard G. Buffett (Howard G. Buffett Foundation).

    Felix Peter, Helen Lema, Fatuma Omar na Renalda Mukaja kutoka Mradi wa Usimamizi wa Matumizi Bora ya Rasilimali za Maji uliopo chini ya Wizara ya Maji na Maendeleo ya Mifugo ya Tanzania walijitolea kutayarisha na kufanya makadirio ya maeneo katika ramani zilizopo katika kitabu hiki.

    vii

  • Muhtasari

    Bonde la Mto Pangani lina eneo la takriban kilomita za mraba 43,650, sehemu kubwa ikiwa nchini Tanzania na karibu asilimia 5 iko katika Jamhuri ya Kenya. Nchini Tanzania, bonde hili limeenea katika mikoa minne: Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga. Katika Jamhuri ya Kenya eneo la bonde liko katika Wilaya ya Taita-Taveta. Mto Pangani unaundwa na matawi makubwa mawili , Mto Kikuletwa na Ruvu ambayo huunganika katika bwawa la Nyumba ya Mungu lenye eneo la kilomita za mraba 140. Mto unapotoka katika bwawa hili unajulikana kwa jina la Mto Pangani, ambao hutiririka kwa umbali wa kilomita 432 kabla ya kuingia Bahari ya Hindi.

    Bonde hili lina rasilimali nyingi. Bila shaka maji na ardhi inayofaa kwa kilimo ndizo rasilimali muhimu zaidi kwa wakazi wapatao milioni 3.7 wa bonde hili waishio upande wa Tanzania. Nyanda za juu za bonde hupata mvua nyingi zaidi ukilinganisha na uwanda wa chini. Hata hivyo kutokana na msongamano na ushindani wa kupata ardhi ulioko katika nyanda za juu, wakulima wamelazimika kuanza kumwagilia maji mashamba yao ili kuinua uzalishaji. Wale walioshindwa kupata ardhi katika nyanda za juu wamelazimika kutafuta maeneo katika uwanda wa chini wenye mvua haba, ambako kilimo cha umwagiliaji ni wa muhimu sana. Ugumu wa hali unazidishwa zaidi na mwenendo wa upungufu wa mvua katika bonde.

    Ushindani wa kupata ardhi umesababisha rasilimali nyingine katika bonde kama vile misitu, kuingia katika ushindani wa moja kwa moja na kilimo. Sehemu ya misitu inalindwa kutokana na hadhi yake ya hifadhi, kama vile Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) ambayo ipo chini ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA). Misitu mingine inalindwa na idara za misitu za Kenya na Tanzania. Kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo uhaba wa wafanyakazi na ukosefu wa fedha, misitu hii haifaidi viwango sawa vya hifadhi ikilinganishwa na ile iliyopo chini ya TANAPA. Kuwepo shinikizo kwenye misitu ya pwani na Milima ya Tao la Mashariki katika bonde la mto Pangani kunatia wasiwasi mkubwa sana, hasa ikizingatiwa kuwa maeneo hayo yana kiwango cha juu cha mimea na viumbe adimu ndani yake.

    Rasilimali nyingine katika bonde ni madini, ambayo ni pamoja na tanzanite, bati na vito. Nyingine ni uvuvi, maeneo ardhioevu na vivutio vingi vya utalii.

    Rasilimali hizi hutumika kwa namna mbali mbali. Uchambuzi huu wa hali halisi unaweka matumizi hayo katika makundi yafuatayo:

    • Shughuli za viwanda, ambazo ni pamoja na mchango mkubwa wa nishati ya umeme wa nguvu ya maji katika gridi ya taifa, uchimbaji wa madini na viwanda vya kilimo kama vile kiwanda cha sukari na vya usindikaji wa katani.

    • Shughuli za kilimo: Kwa sehemu kubwa kilimo katika bonde hili ni cha asili na hutegemea umwagiliaji. Mifereji ya umwagiliaji ina ufanisi mdogo sana, inaweza kupoteza kiasi cha asilimia 85 ya maji kati ya mahali yanapochukuliwa hadi yanapopelekwa. Kadhalika kuna kilimo cha umwagiliaji cha viwango vikubwa katika bonde, yakiwemo mashamba ya miwa, mkonge na maua. Kadiri ya hekta kati ya 29,000 na 40,000 humwagiliwa katika bonde la Pangani upande wa Tanzania. Kiasi cha maji kinachotumiwa kinakadiriwa kuwa kati ya mita za ujazo milioni 400 na 480 kwa mwaka.

    • Shughuli za ufugaji: Idadi kamili ya mifugo iliyopo katika bonde kwa sasa haifahamiki. Inadhaniwa kuwa, ifikapo mwaka 2015, ufugaji utatumia mita za ujazo 36,400 za maji kwa siku.

    • Shughuli za mijini: Bonde lina miji miwili mikubwa, yaani Arusha na Moshi. Kadri miji hii inavyokua, mahitaji ya maji yameongezeka katika nyanja mbili: kwa matumizi ya viwandani na nyumbani, na kama njia ya kuondolea maji taka. Inatarajiwa kuwa, ifikapo mwaka 2015, mahitaji ya maji mijini katika bonde yatafikia mita za ujazo 163,600 kwa siku.

    viii

  • Kutokana na hali hiyo kuna asasi na mashirika mbalimbali katika bonde, ambayo yanaweza kutumia madaraka ya viwango tofauti katika kumiliki rasilimali zilizoko katika bonde. Tofauti hii ya viwango vya madaraka ni msingi wa migogoro mingi ya matumizi ya rasilimali hizo. Uchambuzi huu wa hali halisi unainisha migogoro hiyo kama ifuatavyo:

    • Migogoro itokanayo na viwango: Uhusiano kati ya watumiaji wa maji wa ukubwa na uwezo tofauti katika bonde la Mto Pangani mara nyingi huelezewa katika hali mbili kinzani. Hivyo mashamba makubwa yatumiayo mamia ya lita za maji kwa sekunde na kutumia mifumo ya umwagiliaji maji yenye ufanisi wa hali ya juu, hutofautiana sana na watumiaji wadogo ambao hutumia maji kidogo na mifumo duni ya umwagiliaji yenye ufanisi mdogo. Tofauti hizi kubwa za matumizi ndiyo vyanzo halisi vya migogoro. Uchambuzi huu wa hali halisi unatoa mifano ya migogoro ya aina hii kuwa ni maslahi kati ya watumiaji wa mijini na vijijini; na kati ya wachimbaji madini wa viwango vikubwa na vidogo.

    • Migogoro itokanayo na umiliki: Kitabu hiki kinafafanua umiliki kama haki ya kusimamia rasilimali. Nchini Tanzania, Usimamizi wa Maliasili Kijamii (CBNRM) umeonekana kama njia ya kuvutia ya kuongeza ufanisi wa Usimamizi wa Maliasili za Taifa (NRM). Mwenendo huu haufuatwi sana nchini Kenya. Ukinzani katika mifumo hii unahusiana na matumizi na usanifu wake. Hapa, jamii zinaweza zisishirikishwe katika kubuni mkakati wa usimamizi, utekelezaji wake au hata mifumo yake ya kisheria. Hali hii inaweza kudhihirisha kuwa taasisi hizi hazitimizi wajibu wa usimamizi ulioundwa ili ziufanyie kazi. Mifano ni migogoro ya usimamizi wa misitu kati ya ngazi ya jamii na serikali; baina ya watumiaji rasilimali wa aina mbalimbali; na migogoro kuhusu nyanja mbali mbali za usimamizi.

    • Migogoro itokanayo na mahali: Watumiaji walioko maeneo ya juu ya mito wana nafasi nzuri ya kutumia maji kuliko walioko sehemu za chini. Kwa kiwango kikubwa matatizo haya yanaweza kuonekana kwenye mifereji ya umwagiliaji ambako watumiaji walio karibu na chanzo cha maji wanaweza kuotesha mazao yanayohitaji kiasi kikubwa cha maji (kama vile mpunga) na wale walioko mwishoni mwa mifereji wakilazimika kupanda mazao yanayohitaji maji kidogo. Matatizo makubwa yanayoikabili mitambo ya umeme wa maji iliyoko upande wa chini wa mito ni mfano mwingine. Mifano ya migogoro ya aina hii ni ile iliyopo kati ya watumiaji wa maji wa maeneo ya juu ya mto na wa maeneo ya chini ya mto, na migogoro kati ya wazalishaji wa umeme wa maji na wamwagiliaji wadogo wadogo.

    Migogoro juu ya rasilimali ni moja ya ushahidi wa ushindani mkubwa uliopo baina ya watumiaji wa rasilimali zilizoko katika bonde. Athari ya ongezeko la watu, tofauti ya mgawanyo wa rasilimali na hali ya kuwa na ukomo husababisha mbinu za matumizi yake mara nyingi kuwa mbaya. Mifano ya uharibifu wa rasilimali ni kama ifuatayo:

    • Misitu iliyopo katika bonde inakabiliwa na hatari ya ukataji hovyo wa miti, kuingiliwa ndani ya mipaka yake kwa mahitaji ya matumizi ya ardhi, uchomaji wa mkaa na ukusanyaji kuni. Inakisiwa kuwa karibu asilimia 77 ya misitu ya Milima ya Tao la Mashariki imepotea katika kipindi cha miaka 2,000 iliyopita kutokana na shughuli za binadamu, wakati kilomita za mraba 41 za misitu asilia ya Kilimanjaro zimetoweka kati ya mwaka 1952 na 1982.

    • Ugawaji wa maji katika bonde unakabiliwa na tatizo la mahitaji makubwaambapo imedhihirika kuwa mahitaji ya rasilimali hiyo yanazidi upatikanaji wake. Sababu kuu ya ongezeko la mahitaji ni mifumo duni ya umwagiliaji kwa njia ya mifereji yenye ufanisi mdogo. Maeneo ya ardhioevu katika bonde yapo hatarini kutoweka kutokana na ujenzi wa mabwawa.

    • Maeneo yaliyohifadhiwa ya bonde yanakabiliwa na ujangili, na matatizo mengine kama yale yanayoikabili rasilimali ya misitu.

    • Sehemu kubwa ya viumbehai katika bonde inatokana na mazingira ya kipekee ya misitu iliyopo. Tishio la maisha ya viumbehai hutokea kutokana na hatari inayokabili mazingira.

    ix

  • • Uvuvi katika bonde la Mto Pangani unakabiliwa na shinikizo la uvuvi uliokithiri, na ukuaji wa magugumaji unaosababishwa na shehena kubwa ya virutubisho. Takriban tani 24 za udongo kwa hekta kutoka eneo la vyanzo vya mito huingia katika bwawa la Nyumba ya Mungu kila mwaka. Mwaka 1970, tani 28,509 za samaki zilivuliwa kutoka bwawa la Nyumba ya Mungu. Upatikanaji wa samaki umekuwa ukipungua kwa kiasi kikubwa tokea hapo, na katika mwaka 1983, tani 2,430 za samaki zilipatikana.

    Kuna idadi kubwa ya mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali katika bonde hili yanayotaka kudhibiti uharibifu uliotajwa na kujaribu kuboresha maisha ya watumiaji wa rasilimali. Katika miaka ya karibuni, shughuli muhimu za kiwango kikubwa ni zile zilizogharamiwa na Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Usimamizi wa Matumizi ya Rasilimali za Maji na Uboreshaji wa Kilimo cha Wamwagiliaji Wadogo Wadogo (RBMSIIP), na Mradi wa UNDP-GEF wa Viumbe anuwai wa Afrika Mashariki. Mradi wa kwanza ulikuwa maalum katika kuimarisha Ofisi ya Maji ya bBonde la Pangani (PBWO) na vilevile kuimarisha uwezo wa usimamizi wa matumizi ya maji katika bonde.

    Juhudi za mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) katika bonde hili ni pamoja na kujihusisha na Usimamizi Shirikishi wa ukanda wa pwani ya Tanzania na misitu yake ya mikoko, na Kaskazini mwa bonde ni uboreshaji wa umwagiliaji wa kiasili, na uwezeshaji wa njia za mawasiliano baina ya watumiaji wa ngazi ya chini wa rasilimali na uongozi wa bonde. Juhudi za ziada zinatilia mkazo hifadhi ya rasilimali za misitu na wanyamapori katika bonde.

    Mfumo wa Utawala wa bonde ni changamano. Nchini Tanzania, ni kawaida kutokea vyombo viwili kutawala rasilimali moja: Utawala unaotokana na serikali kuu na ule wa serikali za mitaa. Wakati huo huo, Bodi ya Maji ya Bonde la Pangani (BMBP) imeanzishwa katika bonde kwa lengo la kusimamia rasilimali ya maji katika bonde zima. Hii maana yake ni kuwa, mara nyingi, mipaka ya mamlaka baina ya watawala wa rasilimali na wasimamizi inaweza kuwa haieleweki na/ au yenye utata. Aina hii ya utata inajirudia katika ngazi za chini. Kama ilivyoelezwa awali, Tanzania imegeukia kwa kiasi kikubwa kwenye Usimamizi wa Maliasili Kijamii (CBNRM) kama njia ya kuboresha usimamizi wa rasilimali zake za asili. Hata hivyo, hali hii inamanisha kuwa kamati au mashirika mengine ya ngazi ya jamiii yameundwa kushughulikia rasilimali maalum, na sio maliasili kwa ujumla. Hivyo, kuna Kamati za Maliasili za Vijiji (VNRCs), Vyama vya Watumiaji Maji (WUAs), Serikali za Vijiji n.k, hali inayozidisha utata katika usimamizi na kuongeza gharama za uendeshaji kwa kiasi kikubwa.

    Nchini Kenya, hivi karibuni rasilimali za maji zimewekwa chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji (WRMA) inayotumia mabonde ya mito kama maeneo ya msingi ya usimamizi, na ambayo imekabidhiwa jukumu la kuratibu usimamizi shirikishi wa mabonde hayo na kuhusisha vikundi vya wadau katika muundo wa usimamizi. Huu ni utaratibu mpya kiasi, unaoweza kukabiliana na vikwazo kuhusiana na uhusishaji wa wadau katika muundo wa usimamizi, na ugumu wa kushirikisha sekta mbali mbali za utawala wa mabonde.

    Njia hii ya usimamizi kisekta ipo pande zote za mpaka na inajionesha katika hali ambapo idara zinahusika na usimamizi wa misitu, maji, umwagiliaji, wanyamapori na rasilimali nyingine. Hali hii inaweza kusababisha malengo ya usimamizi na njia za kuyafikia kwenda sambamba, na hivyo kuleta utata katika uwezekano wa kuweka usimamizi shirikishi wa bonde. Hata hivyo PBWO imeamua kuhakikisha angalau idara mbalimbali zinakuwa na mawasiliano baina yao kwa kutuma wawakilishi katika Bodi ya Maji ya Bonde la Pangani (PBWB). Hata hivyo Bodi ya Maji ya Bonde la Pangani ina wawakilishi kutoka idara mbalimbali za serikali ili kuhakikisha kuwa angalau idara hizi zinawasiliana. Kwa mujibu wa sheria mpya ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji, bodi ina mamlaka ya kuandaa mipango ya usimamizi wa rasilimali za maji katika bonde, kwa kuwahamasisha na kuwahusisha wahusika wote, wakiwemo wasimamizi na watumia rasilimali za bonde.

    Uchambuzi huu wa Hali Halisi unaeleza kwa ufupi ugumu wa hali na matatizo yaliyotajwa juu kwa kuainisha masuala mbalimbali ambayo yanahitaji umakini mkubwa katika usimamizi wake. Kimsingi, matatizo ya mazingira ni matatizo ya kijamii. Kwa urahisi na kwa ajili ya kuonesha hali ya mazingira ya bonde la Mto Pangani, matatizo haya yanagawanywa kati ya masuala ya mazingira na ya kijamii kama ifuatavyo:

    x

  • Masuala ya mazingira:• Ukataji miti - husababisha matatizo katika uviaji wa maji ardhini, ongezeko la kasi ya mitiririko

    ya maji na hivyo kusababisha mmomonyoko wa udongo, mafuriko na ongezeko la usafirishaji wa mchangatope.

    • Mahitaji ya Ardhi – misitu mingi iko kwenye maeneo muhimu ya kilimo ambayo hupata kiasi kikubwa cha mvua. Jambo hili ni tishio kubwa kwa hifadhi ya misitu ya bonde hili.

    • Shughuli za kilimo: mbinu mbalimbali za kilimo katika bonde hili zilianzishwa wakati idadi ya watu ilikuwa ndogo sana, na upatikanaji wa rasilimali ulikuwa ni wa kutosha. Kwa kuwa idadi ya watu imeongezeka mbinu hizo sasa zinaweza kutishia uhai wa mazingira ya bonde hili. Mifumo iliyopo haina ufanisi wa matumizi ya maji na umwagiliaji wa mfululizo unaweza kusababisha hali ya chumvi chumvi na/au magadi ardhini.

    • Ongezeko la mifugo: suala hili halijulikani sana lakini linadhaniwa kuwa ni tatizo kubwa. Kutokana na kuongezeka kwa kilimo katika maeneo tambarare ya bonde, ardhi kwa ajili ya ufugaji imechukuliwa na wakulima, na hivyo kukuza zaidi ukubwa wa tatizo la wingi wa mifugo.

    • Maendeleo: maendeleo yasiyosimamiwa katika bonde hili ni chanzo cha uchafuzi wa mazingira kutokana na njia zisizotosheleza za uondoaji taka.

    • Ubora wa maji: ubora wa maji unaathiriwa na uchafuzi, lakini pia maji yanachafuliwa kutokana na hali ya kijiolojia inayosababisha ongezeko la madini ya floraidi majini.

    • Uvuvi unaokithiri: shughuli za uvuvi katika bwawa la Nyumba ya Mungu zinaonekana kukithiri. Uvuvi pia unatishiwa na ukuaji wa magugumaji kwenye mito na maziwa unaosababishwa na ongezeko la virutubisho katika bonde.

    • Uchimbaji madini: shughuli za uchimbaji madini zisizodhibitiwa katika bonde ni tishio kwa mandhari yake na manufaa ya ardhi katika siku zijazo. Aidha, hali hiyo ni tishio la uchafuzi wa mazingira. Uchimbaji wa mchanga mitoni hudhoofisha kingo za mito hiyo.

    • Ukosefu wa mwamko wa mazingira baina ya wakazi wa bonde.

    .

    Masuala ya kijamii, kiuchumi na kisiasa• Umasikini: Kutokuwepo kwa shughuli za ngazi ya pili na ya tatu katika bonde ambazo ni ajira

    katika sekta za biashara na viwanda, wakazi wake wengi hujitafutia maisha katika shughuli za msingi kama vile kilimo, uvunaji wa mazao ya misitu, uvuvi n.k.

    • Migogoro: kwa vile watu wengi hujihusisha na shughuli za msingi, hali ya migogoro huibuka baina ya watumiaji wadogo, na kati ya watumiaji wadogo na wakubwa.

    • Manufaa ya kisiasa: wanasiasa wenye shauku ya kupata kura kutoka kwenye majimbo yao ya uchaguzi, wakati mwingine huchochea matumizi yasiyo endelevu ya rasilimali.

    Masuala ya usimamizi na utawala• Sera zisizotosheleza: sera zinazoonekana kuwa sahihi na zilizotungwa vizuri zinaweza zisifae

    kwa sababu utekelezaji wake hauwezi kufuatiliwa, na wahalifu hawaadhibiwi.• Matatizo ya kifedha: Haya hujitokeza karibu katika kila sehemu ya utawala wa bonde, kuanzia

    kwenye ugumu wa kutoa malipo ya kutosha hadi kwenye ununuzi wa teknolojia itakayosaidia ufuatiliaji katika bonde.

    xi

  • • Ukosefu wa Usimamizi Shirikishi: mgawanyo wa kiutawala kati ya ngazi ya mkoa na ya taifa ukiunganishwa na njia za usimamizi za kisekta unadhihirisha kuwa sehemu kubwa ya usimamizi wa rasilimali za asili (NRM) katika bonde siyo shirikishi, kwa kuwa sekta au ngazi moja ya utawala hutumia mbinu ya usimamizi iliyo tofauti na ngazi au sekta nyingine katika bonde. Tatizo hili vile vile linajitokeza katika ngazi ya kimataifa: hakuna utaratibu uliowekwa kati ya Kenya na Tanzania wa kuratibu usimamizi wao katika Bonde la Mto Pangani.

    • Matatizo na utawala wa jamii: hii huhusiana, kwanza na mchango hafifu unaotolewa na jamii katika ubunifu, utekelezaji na utiliaji mkazo wa mfumo wa usimamizi wa rasilimali za asili (NRM) ambao unawaelemea. Pili, nyingi ya njia hizi zinazoshinikizwa kutoka nje ya jamii, zinataka kuanzishwa kwa kamati za NRM za aina mbali mbali, hali ambayo matokeo yake ni mkanganyiko mwingi kupita kiasi katika ngazi ya jamii na hivyo kuchochea matatizo ya kisekta yaliyoelezwa hapo juu, migogoro ya mamlaka na mafanikio duni ya usimamizi.

    Kwa kuzingatia masuala yaliyoelezwa hapo juu, Uchambuzi wa Hali Halisi unabainisha maeneo mbalimbali ya kipaumbele katika utekelezaji kama ifuatavyo:

    Kuwepo kwa mikakati ya usimamizi inayounganisha sekta husika kwa ajili ya bonde la Mto Pangani ikishirikisha majukwaa mbalimbali. Hapana shaka hata kidogo kuwa bonde la Mto Pangani linahitaji haraka mikakati hiyo ambayo inaweza kukidhi upana na ugumu wa maswaala hayo. Mapendekezo yanayoweza kufikiriwa ni pamoja na kutengeneza mikakati ya kutambua mahitaji ya maji, kutathmini mahitaji ya maji ukanda wa chini wa mto kwa ajili ya watu na mazingira, kupanua wigo wa usimamizi wa maji na kuiongezea jamii wajibu wa kubuni na kutekeleza masuala ya usimamizi shirikishi wa rasilimali za asili (NRM).

    Kuwepo kwa mikakati madhubuti ya kuwezesha mazungumzo miongoni na kati ya watumiaji rasilimali na wasimamizi wa aina mbalimbali na waliohusishwa katika sekta mbalimbali kwa lengo la kuongeza uelewa katika ngazi zote za usimamizi. Taratibu zinahitajika ili kuhakikisha kuwa fursa za maongezi kati na miongoni mwa wadau na wasimamizi zinaongezeka kwa kiasi kikubwa, ili kuhakikisha kuwa ubadilishanaji wa habari kwa pande zote unakuwepo, usambazaji unaboreshwa na elimu ya jinsi wadau wote watakavyoshiriki katika ustawi wa bonde inatolewa. Ni muhimu uhamasishaji ufanyike kuhusu vipengele vyote na hali ya usimamizi wa bonde na wadau wake katika ngazi zote za usimamizi na uratibu wake. Sehemu ya ziada ya eneo hili la kipaumbele ni uanzishaji wa mabaraza yenye uwezo wa kuifanya kazi hii, na kutumika kama vyombo vya kutatua migogoro, na viungo kati ya ngazi mbalimbali za utawala.

    Kuainisha na kuanzisha mfumo sahihi wa ukusanyaji na ufuatiliaji wa data. Eneo hili la utendaji haliishii katika mifumo ya uendelezaji na ukusanyaji wa data za kihaidrolojia. Tathmini ya Setilaiti na GIS ya matumizi ya ardhi, viwango vya matumizi na mabadiliko ya kijiografia ni mahitaji ya msingi katika kupanga mipango na ufuatiliaji wa matumizi ya ardhi. Uundaji wa mbinu za kutathmini na kupima sababu za msingi za kijamii na za kiuchumi zinazosababisha uharibifu wa mazingira na utumiaji wa rasilimali uliokithiri pia zinahitaji kutambuliwa. Mifumo kama hii inabidi pia iwe na uwezo wa kutambua mahitaji ya maji katika Bonde. Mifumo ya data na ufuatiliaji iliyopendekezwa lazima iendane na uwezo wa ndani wa kifedha na matengenezo.

    xii

  • A Utangulizi wa Uchambuzi wa Hali Halisi Bonde la Mto Pangani

    A.1 Maelezo ya jumla ya Bonde la Mto Pangani

    Bonde la Pangani ni moja kati ya mabonde 9 yaliyoanzishwa na kuchapishwa katika gazeti la serikali kwa mujibu wa Sheria ya Maji ya 1074 (Usimamizi na Udhibiti) Na. 42 na marekebisho yake Na. 10 ya 1981 (sheria hii ilifutwa na sheria mpya ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji ya mwaka 2009) kwa madhumuni ya kuhamisha madaraka ya usimamizi wa maji kutoka ngazi ya Taifa na kupeleka ngazi ya mabonde. Bonde la Pangani lina eneo kadiri ya kilomita za mraba 58,8001 kiutawala na linajumuisha Bonde la Mto Pangani na mabonde ya mito midogo ya Umba, Msangazi, Zigi2 na mito midogo ya pwani, ukiwemo Mkulumuzi. Uchambuzi huu wa hali halisi unahusu zaidi Bonde la Mto Pangani. Maelezo ya mabonde ya mito midogo yanayosimamiwa kiutawala na Ofisi ya Maji ya Bonde la Pangani yanatolewa katika Kiambatanisho Na.1.

    Bonde la Mto Pangani lina eneo la kilomita za mraba 43,6501, kati ya hizo, kilomita za mraba 3,9141 ziko Kenya (Mchoro wa 1). Nchini Tanzania, bonde hili lipo katika mikoa ya Kilimanjaro, Manyara, Arusha na Tanga. Sehemu ya bonde iliyopo Kenya karibu yote ipo katika wilaya ya Taita- Taveta.

    Mto Pangani unaundwa na matawi makubwa mawili, ambayo yanatokea katika sehemu ya Kaskazini ya bonde. Tawi la kwanza ni Mto Kikuletwa unaonzia katika miteremko ya Mlima Meru na miteremko ya Kusini ya Mlima Kilimanjaro, na la pili ni Mto Ruvu, unaoanzia katika miteremko ya Mashariki ya Mlima Kilimanjaro na Ziwa Jipe. Mito hii inaungana katika bwawa la Nyumba ya Mungu, lenye eneo la kilomita za mraba 140 (Rohr na Killingtveit, 2002). Mto Pangani3 hutoka katika bwawa hili, ukitiririka kwa umbali wa kilomita 432 kabla ya kuingia katika Bahari ya Hindi..

    Kwa ujumla, bonde hili lina mwinuko mdogo unaoteremka kuelekea upande wa Kusini na Kusini Mashariki hadi Bahari ya Hindi. Kwa wastani, sura hii ya nchi ijulikanayo kama Nyika za Masai ziko kwenye usawa wa mwinuko wa mita 800, na sehemu yake kubwa hupata mvua inayozidi kidogo milimita 500 kwa mwaka. Mkabala nayo ni safu ya milima inayoinuka kutoka uwanda huu ambayo mwinuko wake unafidia kwa kiwango kikubwa matatizo ya hali ngumu ya uwanda wa nyika. Katika sehemu hii ya juu, kiasi cha mvua kwa mwaka kinafikia milimita 2,000. Jinsi ilivyo, milima hii ni kama visiwa, wakati ambapo nyanda zinazoizunguka zinaonesha bayoanuwai duni, na hali ngumu ya kujitafutia riziki, milima hii ni visiwa vya bayoanuwai ya kuvutia na viumbe hai wengi. Binadamu hawakushindwa kuona ubora wa milima hii, na hata kabla ya ujio wa utawala wa kikoloni nchini Tanzania, milima iliyopo katika Bonde la Mto Pangani ilikuwa eneo linalokaliwa na idadi kubwa zaidi ya watu katika bonde hili.

    1

    1Tafiti nyingi za awali zinalielezea eneo la chanzo cha mto lililoko kwenye utawala wa Bonde la Pangani nchini Tanzania kuwa ni kilomita za mraba 56,300, na eneo la Bonde la Mto Pangani katika Tanzania na Kenya kuwa ni kilomita za mraba 42,000 kulingana na makisio ya planimita yaliyofanywa na S. Kamugisha (1992). Hatimaye taasisi mbili tofauti (TANRIC ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mradi wa Usimamizi wa Matumizi Bora ya Rasilimali ya Maji katika Wizara ya Maji na Maendeleo ya Mifugo) zimekadiria maeneo haya kwa kutumia GIS. Makadirio haya ya hivi karibuni ni makubwa zaidi kuliko yale ya awali ya makisio ya planimita. Tofauti hizi huenda ni matokeo ya tafsiri mbalimbali za mipaka ya bonde, hasa upande wa magharibi na tofauti kati ya njia za planimeta na zile za GIS (Kamugisha na Mwakalinga pers. Wahojiwa, 2003).2Baadhi ya Waandishi hutumia tahajia za “Sigi”, “Zigi” ndiyo tahajia inayopendelewa na wakazi wa eneo la chanzo cha mto huu (Wahojiwa, 2003).3Baadhi ya tafiti na ramani zinataja Mto utokao katika Bwawa la Nyumba ya Mungu kuwa ni Ruvu mpaka unapoungana na Mto Mkomazi, mahali ambapo unakuwa Mto Pangani. Utafiti huu unataja Mto huu kutoka unapotoka Nyumba ya Mungu hadi unapoingia baharini kuwa ni Mto Pangani.

  • Jinsi Mto Pangani unavyoambaa kuelekea Mashariki, na kushukia uwanda wa pwani ya Tanzania, ndivyo unavyozidi kukabiliana na hali ya hewa na mazingira ya kutatanisha. Kinyume na hali ya hewa ya Kaskazini, ambayo imebadilika kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka elfu moja kutoka kipindi kimoja cha barafu hadi kingine, hali ya hewa inayotokana na Bahari ya Hindi imebakia bila mabadiliko makubwa. Mwambao wote wa pwani ya Afrika Mashariki unaonesha viunga vya misitu ya kale, na hali yake ya hewa imewezesha misitu hii kuhifadhiwa kutokana na uthabiti wake.

    Mabadiliko ya tabianchi katika maeneo mengine barani Afrika yamebadili kabisa hali ya mazingira, na kusababisha kwa kiwango kikubwa kutoweka kwa viumbe hai na kuanza upya mchakato wa hatua za mabadiliko, kiasi cha kufanya misitu ya mwambao mwa Tanzania ifanane kidogo na misitu ya sehemu nyingine barani. Katika milima iliyopo bonde la Mto Pangani, mistiu hii inaonesha kutetereka kwa bayoanuwai na upatikanaji wake katika maeneo haya.

    Leo hii idadi ya watu wanaokadiriwa kufikia milioni 3.7 huishi katika sehemu ya bonde iliyoko Tanzania, wakati ambapo nchini Kenya idadi ya watu wa Taita -Taveta inakaribia 40,900. Mtindo wa makazi katika bonde ni taswira ya kutowiana kwa hali ya mazingira ya bonde hili. Nchini Tanzania asilimia 90 ya watu wanaoishi katika bonde hili huishi katika nyanda za juu, asilimia 80 ya hao kwa njia moja au nyingine hutegemea kilimo kwa ajili ya mahitaji yao (Mwamfupe, 2002). Mkusanyiko huu wa makazi huleta msongamano wa watu unaofikia hadi watu 300 kwa kilometa ya mraba. Mwaka 1988, mikoa ya pwani ya Tanzania ilikuwa na idadi ya watu 28.4 kwa kilometa ya mraba (ukiacha Dar es Salaam), ongezeko la kutoka watu 18 tu kwa kilometa ya mraba mwaka 1967. Katika Milima ya Usambara Magharibi, idadi ya watu imekua kwa mara 23 tangu mwaka 1900, wakati katika maeneo ya nyanda za juu za Mlima Kilimanjaro, msongamano wa watu ni mkubwa kiasi cha watu 900 kwa kilomita ya mraba (Gillingham, 1999). Kinyume chake, maeneo ya nyanda za chini yameonesha kuwa na msongamano mdogo wa kiasi cha watu 65 kwa kilomita ya mraba.

    Kihistoria, wakazi wa bonde hili wamekuwa na shughuli za kiuchumi ambazo ni kielelezo cha hali zilizotofauti za mazingira katika bonde. Nyanda za chini zilikimu wafugaji, wakati nyanda za juu zilikimu wakulima. Kutokana na ujio wa wakoloni kutoka Ulaya, maeneo makubwa ya ardhi ya kilimo yalitengwa kwa kilimo cha mashamba makubwa. Katika wilaya ya Taita – Taveta ya Kenya, karibu ardhi yote ilitengwa kwa ajili ya kilimo cha mkonge. Hali hii ilisababisha kukua kwa kiwango cha kilimo. Johnston (1946) anasema kuwa, mwaka 1943, umilikaji ardhi katika nyanda za juu za Kilimanjaro kwa wastani ulikuwa hekta 1.2 kwa mtu mmoja. Katika mwaka 1946, ulikuwa mita za mraba 2.5 tu.

    Wastani wa kiwango cha umilikaji wa ardhi katika nyanda za juu za Kilimanjaro umeongezeka tokea hapo, na Lein (2002) anasema kiwango cha umilikaji ardhi kuwa ni wastani wa hekta 0.6 kwa kaya. Kaya za nyanda za chini hulima mashamba ya wastani wa eneo la hekta 10.4.

    Wastani huo unaelekea kupungua. Kadiri ukubwa wa mashamba katika nyanda za juu unavyokuwa mdogo zaidi na zaidi, uwezo wake wa kukidhi mahitaji ya maisha ya watu unapungua, na udongo umechoshwa kutokana na kupanda mazao mfululizo pamoja na umwagiliaji uliokithiri, watu wamelazimika kutafuta ardhi katika maeneo ya nyanda za chini. Kwa sababu hiyo, idadi ya watu imekuwa kubwa kando ya mito ya bonde la mto Pangani na umwagiliaji umeenea kwa kiasi kikubwa sana. Matokeo yake, maeneo ya bayoanuwai yaliyopo hapa na pale katika uwanda wa bonde yako katika shinikizo la kutoweka.

    2

    Mchoro wa 1: Bonde la Mto Pangani lilivyoenea Tanzania na Kenya (Rejea:Mradi wa Usimamizi wa Matumizi Bora ya Rasilimali za Maji)

  • 3

    Mch

    oro

    wa

    2: B

    onde

    la M

    to P

    anga

    ni

    Ang

    alia

    pia

    Pic

    ha y

    a 1,

    uku

    rasa

    wa

    33

    (Rej

    ea: M

    radi

    wa

    Usi

    mam

    izi w

    a M

    atum

    izi

    Bor

    a ya

    Ras

    ilim

    ali z

    a M

    aji)

  • Kwa hiyo, kiini cha matatizo ya Bonde la Mto Pangani kinahusiana na msogamano wa watu na mahitaji yao mawili makuu na muhimu kwa kilimo na ufugaji: ardhi na maji. Mwingiliano wa mambo haya, na mahitaji waliyo nayo watu katika rasilimali za bonde, yamesababisha migogoro ya aina mbalimbali:

    Migogoro itokanayo na viwangoUhusiano baina ya watumiaji maji wa ukubwa tofauti katika Bonde la Mto Pangani mara nyingi unajieleza katika namma mbili, yaani mashamba makubwa yanayotumia mamia ya lita za maji kwa sekunde na kutumia mifumo ya umwagiliaji yenye ufanisi mkubwa, tofauti kabisa na watumiaji wadogo wanaotumia maji kidogo na mifumo duni ya umwagiliaji. Tofauti hizi za viwango vya matumizi haziishii kwenye teknolojia pekee, bali hata ardhi. Watumiaji wakubwa karibu wakati wote hutumia ardhi kubwa zaidi kuliko watumiaji wadogo. Jambo jingine tofauti na la pekee ni kuwepo kwa mitambo ya uzalishaji umeme katika bonde. Ardhi inayokaliwa na mitambo hii siyo kubwa sana, lakini mahitaji yake ya maji ni makubwa sana. Ni dhahiri maji haya hurudishwa mtoni, hii ikiwa na maana uzalishaji umeme huyaacha maji katika hali na kiasi kile kile kilichochukuliwa. Pamoja na hayo matumizi hayo ni kwa maslahi ya taifa. Bonde la Mto Pangani huzalisha kiasi kinachofikia asilimia 17 ya umeme wa Tanzania, na vinu vyake vingi vimesanifiwa maalum kwa kutilia maanani mtiririko wa maji. Iwapo matumizi ya maji kati ya vyanzo vya maji na mitambo ya umeme yatazidi, inabidi mitambo izalishe kwa kiwango chini ya uwezo wake. Mgogoro uliopo hapa ni kulinda maslahi ya kitaifa dhidi ya watumiaji wadogo.

    Migogoro itokanayo na umilikiKitabu hiki kinatumia neno umiliki kama haki ya kusimamia rasilimali. Kama ilivyo kwenye sehemu nyingi ulimwenguni, dhana ya usimamizi kwa misingi ya kijamii katika Tanzania na Kenya ni mpya. Katika nchi ambazo mifumo ya usimamizi inayotegemea serikali, imedumu kwa zaidi ya nusu karne, bila mafanikio mazuri na kusababisha ongezeko la matatizo ya mazingira, usimamizi wa maliasili kwa misingi ya kijamii (CBNRM) unaonekana kuwa chaguo la kuvutia. Kwa hali hiyo nchini Tanzania kuna asasi nyingi mno za usimamizi wa kijamii. Dhana ya usimamizi wa maliasili kijamii inabakia kuwa mpya sana nchini Kenya. Ukinzani wa mifumo hii unahusiana na mwenendo wa matumizi na miundo yao. Hapa, jamii zinaweza zisihusishwe katika uundaji wa mfumo wa usimamizi, utekelezaji wake au hata mifumo yake ya kisheria.

    Migogoro itokanayo na mahaliMaeneo ya watumiaji maji yaliyoko juu hutoa nafasi nzuri zaidi ya matumizi ya rasilimali kuliko ilivyo kwa watumiaji wa maeneo ya chini. Kimsingi, matatizo haya yanaweza kuonekana katika mifereji ya umwagiliaji ambapo watumiaji walio karibu na chanzo cha maji wanaweza kuotesha mazao yanayohitaji maji mengi sana (kama vile mpunga) na wale wanaoishi mwishoni mwa mfereji hulazimika kupanda mazao yenye mahitaji madogo ya maji. Matatizo makubwa yanayoikabili mitambo ya umeme wa maji iliyopo upande wa chini ni mfano mwingine.

    Taasisi kuu mbili zinatawala rasilimali ya maji ya Bonde la Mto Pangani. Nchini Tanzania ni Ofisi ya Maji ya Bonde la Pangani (PBWO), wakati katika Kenya ni Mamlaka ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji (WRMA). Chini ya sheria ya hivi karibuni ya Tanzania, mabonde yote yamewekwa (au yatawekwa) chini ya ofisi kama hizo. Hata hivyo, mabonde mengine ni madogo mno kustahili kuanzishiwa ofisi zitakazojitegemea kiusimamizi. Bonde la Pangani limezungukwa na mabonde manne ya aina hiyo (mito ya Umba, Zigi, Msangazi, na mabonde madogo ya mito ya pwani). Haya kiutawala yanawekwa chini ya PBWO, na hayakujumuishwa katika uchambuzi wa hali halisi katika kitabu hiki. Hata hivyo, muhtasari wa taarifa kuhusu mabonde hayo unaambatanishwa(Kiambatanisho Na 1).

    Bonde la Mto Pangani linakabiliana na matatizo kadhaa makubwa ya kiusimamizi. Kwa kuzingatia tofauti kubwa za aina za maliasili za bonde, pamoja na mahitaji na matarajio mbalimbali ya matumizi, haja ya kuwa na usimamizi shirikishi haiwezi kupuuzwa. Hapo nyuma, njia ile ile ya usimamizi wa ‘kisekta’ kwa bonde hili ilimaanisha kuwa rasilimali ya wanyamapori ilisimamiwa kipekee tofauti na shughuli za misitu, bila kujua, kwa upande mwingine kipaumbele cha usimamizi wa maji. Tatizo pia linajitokeza katika utoaji kipaumbele, sekta ya maji ikidai kuwa maji ni kiungo kinachounganisha rasilimali zote za bonde, lakini watu wa misitu wakilalamika kuwa sehemu kubwa ya maji ya bonde yanatoka katika misitu iliyo kwenye mamlaka yao kisheria.

    4

  • 5

    A.2 Usimamizi wa Pamoja wa Mabonde ya Mito (IRBM)Kwa vyovyote vile, mfumo wa usimamizi wa maliasili kimabonde ndio unaofaa. Mabonde ya mito yanahusisha vyanzo na michakato yote ambayo hatimaye itahakikisha kuwa maji yanafika hadi mwisho wa mto. Hivyo, bonde la mto linahusisha vijito vya awali vya mto, mito midogo na mabonde yake. Pia ni pamoja na delta iliyohusiana na mto, na maji ya ardhini, ardhioevu na mabwawa yoyote yaliyomo.

    Mchanganyiko wa michakato inayohakikisha kuwa maji yanasafiri kutoka kwenye chanzo cha mto hadi mwisho wake ni mgumu na una mambo mengi. Rasilimali za ziada, kama vile misitu na ardhioevu, zinachangia mchakato huu. Kiasi cha maji ambacho hatimaye hufika mwishoni mwa mto pia kitategemea kiasi cha maji yanayochukuliwa kwa matumizi yanapopita katika mkondo wake pamoja na kiwango cha uvukizaji katika maeneo ardhioevu na mimea ya majini na ya kandokando ya mto. Mwisho, ubora wa maji yatakayofika mwishoni mwa mto pia utaonesha michakato iliyopo katika bonde kama vile mbinu za kilimo ambazo huongeza au kupunguza mmomonyoko, maendeleo ya miji au viwanda n.k.

    Usimamizi wa Mabonde ya Mito (RBM) unatambua kuwa usimamiaji wa mto hauwezi kutekelezwa kwa kutenganisha michakato na hali nyingi mbalimbali zinazoathiri mtiririko wa mto na ubora wa maji yake. RBM hulichukulia bonde la mto kama kitengo cha usimamizi kinachohusisha matumizi na uhifadhi wa (a) mifumo midogo ya ikolojia (mabonde madogo ya mito, misitu, ardhioevu, maeneo ya milima, ardhi kame, n.k); na (b) mifumo ya matumizi ya binadamu iliyomo ndani ya eneo la maji (kilimo, umwagiliaji, uvuvi, usafirishaji, uchimbaji madini, viwanda, n.k). RBM kwa kawaida hufuata kanuni ya kuwa maji huunganisha mifumo ikolojia iliyomo ndani ya bonde la mto (Howard, 2002).

    Usimamizi wa Pamoja wa Bonde wa Mto hujaribu kuleta uwiano wa masilahi ya watumiaji wote waliopo katika bonde, na wakati huo huo kukuza ufanisi wa matumizi ya rasilimali na kuhakikisha kunaendelea kuwepo maji ambayo kwayo mifumo hii inategemea (Howard, 2002). IRBM inaweza kufafanuliwa kama ifuatavyo:

    ”… ni mchakato unaokuza uratibu wa maendeleo na usimamizi wa maji, ardhi na rasilimali zinazohusiana nazo ili kuzidisha ustawi wa kiuchumi na kijamii kwa njia ya usawa bila ya kuathiri uendelevu wa mifumo muhimu ya ikolojia (GWP, 2002:1).

    IRBM hushughulika na rasilimali kwa mapana zaidi iwezekanavyo. Inabidi kuziangalia rasilimali za maji kwa mtazamo mzima wa mifumo ya kijamii, kiuchumi na kiikolojia ya mkoa au nchi. Kiutendaji, hii ina maana ya kuwa sera na programu katika maeneo mengine ya rasilimali hazina budi kuchambuliwa kwa makini ili kuona jinsi zinavyoathiri mahitaji yanayoshughulikiwa na sekta ya maji (GWP, 2002) IRBM inayapa mazingira umuhimu sawa na watu katika mahitaji ya rasilimali za maji. IRBM lazima ifanye kazi kulingana na malengo yaliyokubaliwa na wadau wa bonde walio wengi na kufuata kanuni za usimamizi wa rasilimali za maji, usimamizi wa mfumo ikolojia, uhifadhi wa bayoanuwai, usimamizi endelevu wa maliasili na ufufuaji wa mfumo ikolojia. (Howard, 2002).

    Sehemu muhimu ya Usimamizi wa Pamoja wa Bonde wa Mto ni mpango wa matumizi ya ardhi. Kwa kuwa mambo mengi sana yanayotokea kuhusu maji yanahusu maendeleo ya ardhi, ni muhimu matumizi ya ardhi yasimamiwe kwa njia ambayo itahakikisha upatikanaji wa maji na kwamba michakato ya kihaidrolojia haiingiliwi. Kwa mfano, ukuaji wa miji mara nyingi umekuwa na athari kubwa kwa rasilimali ya maji kutokana na ongezeko kubwa la majitaka. Kwa njia hiyo hiyo, misitu na kilimo vinaweza kuwa na athari kwa wingi na ubora wa maji.

    Mifano ya mapendekezo ya usimamizi wa matumizi ya ardhi ni pamoja na (a) kugawa kanda-hapa maeneo maalum hubainishwa ambamo aina fulani za matumizi ya ardhi hukatazwa. Kwa mfano kanda za maji ya kunywa, au maeneo ambayo ujenzi hupigwa marufuku kutokana na hofu ya mafuriko. (b) hatua za kulinda udongo na kudhibiti mmomonyoko, kama vile kilimo cha kontua, au ushauri wa upandaji wa miti (c) kanuni za uondoaji taka, kama vile kuweka maeneo ya kutupa taka (GWP,2002).

  • A.3 Programu ya Maji na Uasili (WANI)IUCN (shirika la kimataifa la kuhifadhi uasili) inasaidia kupata utatuzi wa busara wa changamoto zinazotukabili duniani katika maendeleo ya jamii na utunzaji wa mazingia. IUCN inafadhili tafiti za kisayansi, na inasimamia miradi na huunganisha serikali za kimataifa, asasi zisizo za kiserikali, mashirika ya Umoja wa Mataifa, makampuni na jamii katika kutunga na kutekeleza sera, sheria na utendaji bora.

    IUCN ni mtandao wa masuala ya mazingira ulio mkubwa kuliko yote duniani. Ni umoja wa kidemokrasia wenye wanachama 1,000 kutoka serikali na asasi zisizo za kiserikali, mashirika na wanasayansi 10,000 wa kujitolea katika nchi zaidi ya 160. Ina waajiriwa wataalamu 1,100 katika ofisi zake 62 na mamia ya washiriki kutoka jamii, asasi na sekta isiyo rasmi ulimwenguni kote. Makao makuu yake yapo Gland, karibu na Geneva, Uswisi.

    IUCN ilizindua mpango wa maji na uasili (Water and Nature Initiative (WANI)) mwaka wa 2001. WANI ni mpango wa utendaji unaofanya kazi na washiriki 80 katika nchi 30 katika kuhusisha kwa kiasi kikubwa mambo ya mazingira na jamii wakati wa utayarishaji wa mipangao ya usimamizi wa rasilimali za maji. Mpango wa WANI hutumia menejimenti ya mfumo wa ikologia kama mkakati wa usimamizi uwiano na wa pamoja wa ardhi maji, bayoanuai na jamii. WANI husaidia katika utatuzi wa kuchagua katika mtanziko wa maendeleo ya jamii na hifadhi ya rasilimali zilizo majini kwa kutanzua migogoro ya matumizi ya maji, na kufufua mito na kuchochea maendeleo ya jamii.

    WANI huandaa na kuonyesha njia sahihi ya utendaji katika kutekeleza usimamizi wa rasilimali za maji wa uwiano. Husaidia katika kufanyia mageuzo ya kudumu na kujenga uwezo wa jamii unaohitajika katika kutekeleza mageuzi hayo. Katika awamu ya kwanza, kuanzia mwaka wa 2001 hadi mwaka wa 2008 WANI ilifanya kazi katika mabonde ya maji 12 katika nchi zaidi ya 30 ulimwenguni kote, kazi iliyogharimu dola za Marekani 40m. Sehemu kubwa ya fedha hizi zilitolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uholanzi. Miradi ya majaribio ya WANI ilionyesha nama hali ya watu na mifumo ya ikolojia inavyoweza kunufaika kwa kutumia usimamizi endelevu wa mabonde ya maji. Miradi ya WANI ni washiriki wa jumuia, wanachama wa IUCN, jamii za kiraia na serikali.

    6

    Kisanduku cha 1: Usimamizi wa Mahitaji ya Maji

    Usimamizi wa Mahitaji ya Maji (WDM) umetokana na kutambua kuwa (a) mahitaji ya maji yana-ongezeka bila ya kuambatana na ongezeko la upatikanaji wa maji; (b) matokeo yake, gharama ya kuongeza usambazaji wa maji hupanda kwa sababu uchukuaji maji kutoka katika vyanzo vipya unakuwa mgumu zaidi. Gharama zinazoambatana na uanzishaji wa teknolojia au mbinu mpya ya uchukuaji maji inawezekana zisikubalike. WDM, basi, inajaribu kuokoa maji yachukuliwayo kutoka vyanzo vilivyopo vya maji, yalete manufaa kwa vyote viwili, uchumi na mazingira. WDM inaweza kufafanuliwa kama mkakati wa kuboresha matumizi fanisi na endelevu ya rasilimali za maji kwa kuzingatia masuala ya kiuchumi, kijamii na kimazingira (Wegelin-Schuringa, 1998). Lengo kuu la WDM ni kuchangia katika utoaji huduma za maji na uondoaji majitaka kwa ufanisi na usawa. IUCN inaamini kuwa hili linaweza kufikiwa kupitia utumiaji wa vivutio mbalimbali vya kiuchumi, kukuza ufanisi na usawa wa matumizi ya maji na vile vile hatua kadhaa za kuhifadhi maji zitakazolenga katika kukuza uelewa juu ya uhaba na tabia ya asili ya kumalizika kwa rasilimali hii. WDM huchu-kua hatua mbalimbali zinazolenga kuleta usimamizi endelevu. Nazo ni pamoja na:

    • kulinda ubora wa maji• kupunguza upotevu wa maji• kuboresha ugawaji wa maji baina ya watumiaji • kuweka mfumo sahihi wa upangaji bei• hatua za kuhifadhi maji

  • WANI inasaidia kufanya mabadiliko kwa kuunganisha vipaumbele vya maendeleo, huduma zitolewazo na mifumo ya ikolojia, utawala bora wa rasilimali za maji, ushiriki wa wadau, mapato endelevu ya fedha, kujifunza na uongozi.katika utendaji.

    Toleo la kwanza la Uchambuzi ya Hali ya Bonde llikuwa tokeo la kazi ya awali katika bonde la Pangani na liliweka msingi wa miradi iliyofuata awamu ya kwanza ya WANI ilianza kufanya kazi katika bonde lote la Pangani na kufuatana na matokeo ya kazi hii Ofisi ya Maji Bonde la Pangani iliweza kupata ufadhili wa nyongeza kutoka Kamisheni ya Ulaya kupia msaada wa mfuko wa maji wa Umoja wa Ulaya, Mfuko wa Mazingira wa Ulimwengu (Global Environment Facility) kupitia Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

    A.4 Uchambuzi wa Hali halisi: madhumuni na matokeoUchambuzi wa Hali halisi ni hatua muhimu ya mradi wa IUCN. Ni uchambuzi wa hadhi, hali, mienendo na masuala muhimu yanayoathiri mifumo ikolojia, watu na taasisi katika hali ya kijiografia ya ngazi yoyote (jamii, taifa, kanda, kimataifa)’ (IUCN, 1999:1). Madhumuni ya Uchambuzi wa Hali halisi ni kutoa tathmini inayotosheleza dhamira ya kipaumbele au maeneo ya utendaji yatakayoendelezwa.

    Kwa mantiki hii madhumuni ya Uchambuzi huu ni kama yafuatayo:

    • Kutambua rasilimali zilizomo katika Bonde la Mto Pangani na michakato na matukio yanayoziathiri. Uchambuzi utayaonesha maeneo hayo maalum ambayo yanahitaji kushughulikiwa ili kuyanusuru, kwa kuzingatia ushahidi unaoonesha kuwa uwiano kati ya upatikanaji wa riziki ya kutosha kwa wakazi wa Bonde hili na uendelevu wa rasilimali za Bonde umeharibiwa.

    • Kutambua maeneo ya utendaji kwa mapana ambamo hatua zinaweza kuchukuliwa kwa manufaa. Uchambuzi unatambua kuwa nyingi ya hatua hizo zinaweza zisiwe ndani ya utaalam wa IUCN. Hivyo utataka kuainisha mashirika, vikundi au taasisi nyingine ambazo IUCN inaweza kuingia nazo ubia kadri inavyotaka kuendeleza juhudi za WANI katika Bonde la Mto Pangani.

    A.5. Vyanzo vya data Uchambuzi huu wa Hali halisi umefanyika kwa kutumia data zilizopatikana kutokana na vyanzo vikuu viwili:

    • Taarifa iliyochapishwa. Umuhimu wa kipekee upo katika matokeo ya tafiti juu ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji zilizofanyika katika Bonde la Mto Pangani, ambazo ni juhudi za pamoja kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Teknolojia na Sayansi cha Norway. Kwa nyongeza, Uchambuzi wa Hali halisi pia umetumia taarifa ya warsha iliyoitwa “Bonde la Mto Pangani: Mapendekezo ya Usimamizi Shirikishi”, iliyofanyika hoteli ya “Kilimanjaro Crane” , Moshi, Tanzania, tarehe 8 –10 Mei, 2002.

    • Mahojiano yasiyoandaliwa kikamilifu baina ya mwandishi na wadau wa Bonde la Mto Pangani. Waliohusika ni pamoja na watawala wa maji, watu wa misitu, jamii za wakulima, wahifadhi wa wanyamapori na watumiaji binafsi wa maji. Mahojiano yalifanyika Arusha, Moshi, Hale, Tanga na Dar es Salaam kati ya Novemba 12 na 22, 2002. Mahojiano, wahojiwa na ushirikishwaji wa taasisi zao vimetolewa kama sehemu ya rejea za waraka huu.

    Uchambuzi huu wa hali halisi umefanyiwa mapitio na idadi kubwa ya wadau wa Bonde la Mto Pangani. Wakati wa warsha iliyofanyika Moshi-Tanzania, kati ya tarehe 10 na 12 Machi, 2003, Uchambuzi wa Hali halisi uliwasilishwa kwa wadau kwa ajili ya mapitio na maoni. Mwezi Mei, 2003, maoni ya nyongeza yalipokelewa kutoka Ofisi ya Maji ya Bonde la Pangani na Mamlaka ya Maendeleo ya Pwani (CDA Kenya). Marekebisho yaliyopendekezwa hatimaye yalizingatiwa na yamejumuishwa.

    7

  • A.6 Muundo wa Uchambuzi wa Hali halisiUchambuzi huu wa hali halisi unaanza kwa maoni ya jumla ya rasilimali za bonde hili na matatizo yanayozikabili. Kisha unaangalia shughuli za rasilimali watu katika bonde, uchumi wao, matatizo na vikwazo vya upatikanaji wa rasilimali. Kisha uchambuzi unaendelea kuangalia matatizo na masuala ambayo wadau mbalimbali wanaona kuwa yapo katika bonde kama msingi wa kujadili muundo wa Usimamizi wa Maliasili za bonde. Katika sura nyingi, uchambuzi umefupisha dondoo muhimu ambazo msomaji anatakiwa kuzifahamu na kuzizingatia kadiri anavyoendelea na sehemu za uchambuzi zinazofuata. Mihutasari hii imewekwa pamoja katika hitimisho la kitabu hiki, ambapo majadiliano yatarudi kwenye madhumuni yake, na kuangalia jinsi matatizo yaliyotambuliwa, juhudi za usimamizi ambazo zimechukuliwa na mapendekezo ambayo yamefikiriwa kwenye kitabu hiki kwa pamoja yanaweza kuwa kichocheo na msingi wa uchukuaji wa hatua muafaka na ushirikiano wa WANI.

    8

  • B Maliasili za Bonde la Mto Pangani

    B.1 UtanguliziUtangulizi wa Uchambuzi huu wa Hali halisi umetoa mwanga kuhusu rasilimali anuwai zilizomo katika Bonde la Mto Pangani. Katika sura hii, tunaanza kwa kuangalia misitu iliyopo katika bonde, mchango wake na tishio la hifadhi ambalo linatoa changamoto kwa misitu hiyo. Mfumo kama huo huo utatumika kuangalia rasilimali za ziada katika bonde, zikiwemo maji na maeneo ardhioevu, maeneo yaliyohifadhiwa na bayoanuwai. Sura hii itahitimishwa kwa muhtasari wa dondoo muhimu. Sura hii kimsingi inahusika na rasilimali za maji na viumbe hai. Mashapo ya madini yaliyopo katika bonde hayakuzingatiwa sana kutokana na ukosefu wa data.

    B.2 Misitu ya BondeMgawanyo wa misitu, aina na hadhi yake kisheria nchini Tanzania iko kama ifuatavyo:

    Jedwali la 1: Aina, matumizi na hadhi ya kisheria ya misitu nchini Tanzania.

    Hekta 1,000 %

    Aina ya Msitu

    Misitu (mingine mbali ya misitu ya mikoko) 1,141 3.4

    Misitu ya Mikoko 115 0.3

    Misitu ya Mbao 32,299 96.3

    Jumla 33,555 100.0

    Matumizi ya Ardhi ya Misitu

    Eneo la misitu ya uzalishaji 23,810 71.0

    Eneo la misitu inayohifadhiwa (hasa maeneo ya vyanzo vya mito) 9,745 29.0

    Jumla 33,555 100.0

    Hadhi ya Kisheria

    Hifadhi ya Misitu 12,517 37.3

    Misitu/misitu ya mbao katika mbuga za taifa, n.k. 2,000 6.0

    Ardhi ya misitu isiyohifadhiwa 19,038 56.7

    Jumla 33,555 100.0(Rejea: Lambrechts et al., 2002).

    Misitu ya Bonde la Mto Pangani huwakilishwa na aina kuu tano: (a) Misitu ya milima ya Afrika (b) Misitu ya Mikoko (c) Misitu ya Mwambao (d) Misitu ya Miombo (e) Misitu ya kandokando ya mito. Misitu hii inaweza kuwa ya hifadhi, uzalishaji au misitu isiyokuwa na hadhi maalum. Misitu ya Pwani na ya milima ya Afrika, kutokana na upekee wake wa bayoanuwai, hupata nafasi ya kufikiriwa zaidi. Shughuli za kimataifa za bayoanuwai katika misitu hii pia zinasaidia upatikanaji zaidi wa data kuliko ilivyo kwenye aina nyingine za misitu. Hili linajionesha katika kitabu hiki.

    Sehemu kubwa ya uwezo wa Bonde la Mto Pangani katika upatikanaji wa maji inachangiwa na misitu yake. Kwa mfano kwenye Mlima Kilimanjaro, kiasi cha asilimia 96 ya maji yanayotiririka kutoka mlimani chanzo chake ni kwenye ukanda wa msitu pekee (Lambrechts et al., 1992), na Mlima Kilimanjaro unakadiriwa kutoa asilimia 60 ya maji yanayoingia Bwawa la Nyumba ya Mungu, na asilimia 55 ya maji yatiririkayo juu ya ardhi katika bonde (Rohr na Killingtveit, 2002).

    9

  • Misitu ya vyanzo vya maji inafanya kazi tatu muhimu (Akitanda, 2002):

    • Misitu huchangia kwenye hifadhi ya maji kwa kurekebisha kasi ya maji, kuzuia mmomonyoko wa udongo, kuweka akiba ya maji na kuboresha ubora wa maji.

    • Huhifadhi mkusanyiko wa jeni: Misitu kama ile ya unyevunyevu ya kitropiki huonesha viwango vya juu sana vya bayoanuwai, na huchangia udumishaji wa mkusanyiko wa jeni wa dunia.

    • Misitu hutoa mazao kwa ajili ya matumizi ya jamii, kama vile mbao na mimea ya madawa.

    Misitu ya MikokoMisitu ya mikoko hutoa mchango mkubwa katika kuhifadhi ukanda wa pwani. Huhifadhi mashapo laini yaliyoko kando ya bahari kutokana na mmomonyoko, huzuia masimbi na kutumika kama virutubisho. Miti yenyewe na matope kuzunguka mizizi yake ni makazi muhimu kwa viumbe mbalimbali wa majini na wale wajifichao. Wakati wa mawimbi makubwa, mamia ya aina za samaki huhamia katika misitu ya mikoko ili kujipatia chakula au mazalio. Samaki wengi na kamba hutegemea mikoko kama sehemu za kulelea vifaranga vyao. Miti ya mikoko ni migumu sana na hivyo inastahimili mchwa na kuvu. Inatumika kwa shughuli mbalimbali. Matawi ya Rhizophora, Ceriops na Bruguiera ni marefu na yamenyooka, kwa hiyo hutumika maalum kama miti ya kujengea ingawa hutumika pia kama nguzo, na katika utengenezaji wa mitego ya samaki na samani. Katika miaka ya karibuni, mikoko pia imetumika kutengeneza mkaa na pia

    10

    Kisanduku cha 2: Taarifa za Msingi za Misitu iliyomo katika Bonde la Mto Pangani

    Misitu ya Bonde la Mto Pangani ni muhimu kwa haidrolojia yake kwa sababu:• hurekebisha kasi ya maji, huzuia mmomonyoko wa udongo, huhifadhi maji na kuboresha

    ubora wa maji;• huchangia katika matengenezo na hifadhi ya mkusanyiko wa jeni;• hutoa mbao na madawa kwa matumizi ya jamii .

    Kuna aina kuu tano za misitu katika Bonde:• Misitu ya mikoko: Hutoa mchango mkubwa katika kuhifadhi ukanda wa pwani. Huhifadhi

    mashapo laini yaliyoko kando ya bahari kutokana na mmomonyoko, huzuia masimbi na hutumika kama virutubisho. Miti yenyewe na matope kuzunguka mizizi yake ni makazi muhimu kwa viumbe mbalimbali vya majini na maficho yao.

    • Misitu ya pwani ya Afrika Mashariki: Hii ni misitu ya kipekee iliyoko Afrika Mashariki na ina bayoanuwai na viumbe wengi. Iko katika uwanda wa pwani kati ya misitu ya mikoko na Milima ya Tao la Mashariki.

    • Misitu ya milima ya Afrika (Afromontane): Misitu ya Milima ya Tao la Mashariki ina kiwango cha juu cha bayoanuwai na viumbe wengi kama ilivyo katika misitu ya pwani. Katika Milima ya Kilimanjaro na Meru, misitu hii haionyeshi anuwai inayofanana, lakini inatoa mchango muhimu kihaidrolojia.

    • Misitu ya kandokando ya mito: hii huimarisha kingo za mito, na mto Pangani unapotiririka kupitia nyanda za chini zilizo kavu na kame, huwa maeneo ya kipekee ya miti na vichemchemi kwa matumizi ya binadamu na wanyama pori.

    • Msitu wa miombo: hii inajumuisha kundi kubwa la miti ya jamii ya mnondondo (Brachystegia, Isoberlinia na Julbernadia). Tofauti na misitu ya mvua, misitu ya miombo haisongamani sana kiasi cha kuzuia mwanga usifike ardhini. Matokeo yake ni kuwa, nyasi hufunika eneo kubwa la ardhi chini ya msitu, na wakati wa msimu wa mvua, nyasi hukua hadi kufikia kimo cha mita moja.

  • hukusanywa kama kuni. Misitu ya mikoko iliyoko karibu na miji hutumika kwa wingi kwa madhumuni haya. Mikoko inaweza kupunguzwa matawi ili kuongeza ukuaji wake na upandikizaji upya pia ni rahisi. Hata hivyo hakuna shughuli yoyote kati ya hizi inayofanyika katika mwambao wa Tanzania (Richmond, 1997).

    Karibu mwambao wote wa pwani ya Tanzania umepambwa na misitu ya mikoko. Katika eneo la Bonde la Mto Pangani, inapatikana katika mkoa wa Tanga pekee, ambako karibu asilimia 11 ya mikoko ya Tanzania hupatikana. (Bwathondi na Mwamsojo, 1993) Hii ni pamoja na hekta 753 za misitu ya mikoko iliyosongamana kuzunguka mdomo wa mto Pangani (Kijazi, 2002).

    Misitu ya Pwani ya Afrika MasharikiMisitu ya pwani ya Afrika Mashariki iko katika uwanda wa pwani, kati ya Milima ya Tao la Mashariki na mikoko ya pwani. Misitu hii imetawanyika sana, na viunga vya misitu vimetenganishwa na maeneo ya mifumo ikolojia nusu kame. Imeenea kati ya mwinuko wa mita 500 na 1,000 juu ya usawa wa bahari. Tabia muhimu ya misitu ya pwani (ambayo ipo pia katika misitu ya Milima ya Tao la Mashariki) ni ile ya kuitegemea hali ya hewa ya Bahari ya Hindi na uthabiti wa kihistoria iliyoipatia. Kwa kuwa pekee katika uwanda wa pwani ya Afrika Mashariki, kujitenga kwa misitu hii kutoka mifumo mingine ya misitu ya Afrika kumesababisha viwango vya juu vya upatikanaji wa spishi (tazama hapa chini) (Burgess et al.,1996). Inasadikiwa kuwa kuna misitu 76 ya pwani nchini Tanzania (Burgess et al.,1996). Mingi ipo katika uwanda wa nyasi wa pwani kati ya mdomo wa mto Pangani hadi chini ya milima ya Usambara (tazama Baker na Baker, 2001).

    Misitu ya milima ya Afrika (Afromontane)Milima ya Tao la Mashariki inaambaa kutoka mpaka wa Tanzania na Zambia hadi milima ya Taita nchini Kenya. Inahusisha milima ya kale ya fuwele iliyopo Mashariki ya Tanzania na Kusini Mashariki ya Kenya ambako inakabiliana moja kwa moja ya hali ya hewa ya Bahari ya Hindi. Katika Bonde la Mto Pangani inahusisha milima ya Pare ya Kaskazini na Kusini, milima ya Usambara ya Mashariki na Magharibi na Milima ya Taita. Milima hii ni ya zamani sana, na kipindi cha karibuni zaidi cha uharibifu wa miamba iliyoiathiri kilitokea miaka milioni 7 iliyopita. Kwa kulinganisha, lava ya zamani zaidi katika Mlima Kilimanjaro ina umri wa miaka milioni 1 tu. (Burgess et al., 1996).

    Ukaribu wa milima hii na bahari pia umefanya hali yake ya hewa kubaki kuwa thabiti kabisa. Wakati wa zama za mwisho za barafu, hali ya joto la uso wa bahari ya Hindi haikubadilika. Hivyo, ingawa zama za barafu zinaweza kuwa zimebadili hali ya hewa katika sehemu nyingine za Afrika, haikufanya hivyo kwa milima ya Tao la Mashariki. Kwa hiyo milima hii imefaidi kipindi kirefu sana cha uthabiti wa mazingira, na pia imetengwa na misitu mingine na kwa hakika, kati ya msitu mmoja na mwingine (Burgess et al.,1996).

    Matokeo ya mabadiliko haya ni kuwa tabia za viumbe hai vya milima hii ni za namna mbalimbali na zinaainishwa na viwango vya juu vya upatikanaji kwa wingi au unaokaribia kuwa kwa wingi (tazama chini). Inawezekana kuwa kwa kiasi fulani kiwango cha chini cha spishi anuwai na upatikanaji wake katika Mlima Kilimanjaro ni matokeo ya uchanga wake.

    11

    Kisanduku cha 3: Milima ya Taita

    Milima ya Taita ni Milima pekee ya Tao la Mashariki katika Kenya. Milima hii na misitu yake inachukua spishi zaidi ya 2,000 za mimea yote (flora) na wanyama wote (fauna), ambapo aina 13 kati ya hizo zinapatikana kwa wingi. Mimea 67 ya asili inayojulikana, ikiwemo kahawa mwitu (Coffee fademi), husitawi milimani. Milima ya Taita ni Eneo Muhimu la Ndege (IBA), na ina spishi tatu zinazopatikana kwa wingi: Taita Apalis, Taita Thrush na Taita White – eye. Misitu ya milima hii pia ina utajiri wa amfibia (wanyama waishio majini na nchi kavu), wadudu na viumbe vingine. Ni kilomita za mraba 6 tu ndizo zinazobaki katika Milima ya Taita, zikiwa zimegawanyika katika viunga 13 vya misitu. Newmark (1998) anakadiria kuwa mabaki haya ya milima huwakilisha asilimia 2 tu ya mtandao wa misitu hii miaka 2,000 iliyopita. Milima ya Taita imepoteza misitu zaidi kuliko mlima wowote wa Tao la Mashariki.

  • Msitu wa Mlima Kilimanjaro umegawanyika katika aina mbalimbali za uoto: kanda ya savana, eneo la kilimo na misitu lililo na watu wengi, ukanda wa misitu, ukanda wa mimea (alpine) mirefu kiasi na mirefu. Kwa mifumo ikolojia na bayoanuwai, ukanda wa misitu ni muhimu zaidi katika mlima huu, na una karibu nusu ya spishi zote za mimea ya milima huu (Lambrechts et al., 2002).

    Misitu ya kandokando ya mito (Riverine)Misitu ya kandokando ya mto kuzunguka sehemu ya Kinamasi ya Kirua inaweza kugawanywa katika makundi saba kama ifuatavyo (IVO-NORPLAN, 1997):

    • Uoto wa kando ya mto: huu ni pamoja na uoto unaokwenda hadi mita 50 kila upande wa kingo za mto. Kwa upande wa mashariki, spishi kuu ni Cyperaceae (mf. Cyperus alticulatus C. laevigatus) Gramineae (mf. Phragmites mauritianus, Echnochloa Colonum) na Typhaceae (eg. Typha domingensis). Pale ambapo kina cha ukingo wa mto ni kirefu Ficus Sur na Acacia Zanzibarica ndizo maarufu. Ukingo wa magharibi umetawaliwa na Ficus sur, Trichilia emetica, Elaeis guineense, jamii ya Mchenje/Msesewe (Albizia graberrima, Antidesma Venosum na A. Zanzibarica). Tabaka la vichaka vya kando ya mto linatawaliwa na spishi kama vile Sesbania Sesbans na Phyllanthus muellerianus.

    • Ardhi ya kinamasi cha Cyperus na Sesbania: katika maeneo ambayo maji hutuwama wakati wote, spishi kama Cyperus axaltatus na Typha domingensis ndizo zinazotawala. Katika maeneo yale ambayo hupata mafuriko kwa vipindi, Sesbania sesbands, Cyperus Laevigatus na Mkongoe (Acacia Xanthophloea) ndio aina za pekee za miti zinazohusishwa na aina hii ya uoto. Hii ni aina ya uoto iliyo maarufu sana kwenye eneo la kinamasi la Kirua, ingawa ni maarufu zaidi katika ukingo wa mashariki wa mto kuliko ukingo wa magharibi. Kwa upande wa mashariki, inaweza kutanda hadi kilomita 3 kutoka mtoni, wakati ambapo umbali mrefu zaidi ni kiasi cha mita 700 tu kutoka mtoni kwa upande wa magharibi wa mto.

    • Nyanda za nyasi za Sporobolus pyramidalis na Cynodon dactylon: Jamii ya Poaceae ndio inayotawala hapa, ikiambatana na miti michache iliyotawanyika na vichaka. Katika eneo la Kinamasi la Kirua, aina hii ya uoto inaenea katika eneo kubwa zaidi. Inaweza kutokea kama viunga au maeneo makubwa ya nyasi.

    • Misitu ya mbao ya Mkongoe (Acacia Xanthophloea): Aina hii ya uoto hutawaliwa na spishi ya Acacia, ambayo hufikia urefu wa hadi mita 18, na ikiwa na utando ulioziba eneo la kiasi cha asilimia 20 ya eneo la ardhi. Aina hii ya uoto ina thamani kubwa kijamii na kiuchumi kwa wakazi wa eneo hili oevu.

    • Jangwa lenye vifungu vya Suaeda monoica: Aina ya uoto inayojieleza, ambayo kwa kawaida hupatikana mbali kidogo na mto baada ya sehemu za uoto wa nyasi.

    • Eneo la vichaka vya mpoma wa Afrika (Commiphora africana): Mwendelezo wa ukanda wa eneo la vichaka linalotawaliwa na C. Africana ambao hupatikana chini ya Mwinuko wa Martin. Kwa kawaida, kila kichaka kina urefu pungufu ya mita 6, na utando wake unaziba zaidi ya asilimia 20 ya eneo la ardhi.

    • Ardhi ya kilimo: Mnamo mwaka 1997, kilimo katika eneo la Kinamasi cha Kirua kilikomea kuwa cha maeneo madogo, na kutawaliwa na mazao yanayohitaji maji mengi kama migomba na miwa, pamoja na mahindi.

    Misitu ya miomboMisitu ya Miombo imeenea katika eneo la asilimia 50 ya Tanzania na ni uoto wa aina moja ulio mkubwa zaidi katika Afrika ya Mashariki. Misitu ya miombo ya Afrika Mashariki ni mfumo uliodhoofishwa wa spishi ya miombo iliyoenea sana katika Afrika ya Kati (Rogers, 1997).Inaweza kuelezewa kama ifuatavyo; ‘miti inayopukutisha majani isiyokuwa na miiba (yenye spishi chache zenye miiba) inayojitokeza katika maeneo ya mvua za msimu mmoja katika ardhi chakavu kijiolojia, yenye asidi, na ya mchanga. Inajulikana kwa miti ya jamii ndogo ya Caesalpinoideae, hususan spishi za jamii ya myombo (Brachystegia na Julbernadia).

    12

  • 13

    Tabaka la vichaka linatofautiana kwa unene, asilimia ya ueneaji na spishi zilizomo. Mara nyingi hutawaliwa na Mgoto/Mtobwe (Diplorhynchus na Combretum spp). Utando wa ardhi hutofautiana kutoka kwenye nyasi nyingi hadi kwenye vichaka haba na nyasi ndogo ndogo. Muundo na spishi zilizomo kwa kiwango kikubwa unadumishwa na mioto ya vipindi vya msimu (Rogers, 1996:301). Kiasi cha kilomita za mraba millioni 3 za Afrika zimefunikwa na misitu ya miombo. Katika Bonde la Mto Pangani imeenea zaidi katika maeneo ya mwambao, pande zote mbili za Kaskazini na Kusini mwa mdomo wa Mto Pangani.

    Tishio na Hadhi ya HifadhiKwenye Mlima Kilimanjaro, misitu inaendelea kutishiwa kuingiliwa zaidi na zaidi kutokana na uvamizi wa kilimo, ambacho kinatokana na ongezeko la idadi ya watu. Vitisho vingine vya ziada ni ukataji wa miti kwa ajili ya mbao, uanzishwaji wa mashamba ya miti ya mbao laini, moto, uvunaji haramu uliokithiri wa miti ya mbao, ujangili na urinaji haramu wa asali (Yanda na Shishira, 2001). Katika sehemu zote isipokuwa katika mitelemko ya Kaskazini, ukataji haramu wa magogo hufanyika kwa wingi katika maeneo ya msitu yaliyo chini ya mita 2,500, ilikoenea zaidi miti ya kafuri, seda na miti mingine ya asili (Lambrechts et al., 2002). Tishio la ziada ni pamoja na uanzishaji wa ‘vijiji vya misituni’ (ambako viko 18 kwenye eneo la hekta 215) ndani ya hifadhi ya msitu. Mashamba pia yanazidi kuwa ya kawaida katika hifadhi. Mwezi Agosti, mwaka 2001, kulikuwa na matanuru 125 ya mkaa yaliyoonekana katika mitelemko ya Kusini Mashariki ya mlima (Lambrechts et al., 2002). Uchungaji wa mifugo hufanyika kufikia kilomita 8 ndani ya msitu, na katika mwezi Agosti, mwaka 2001 wanyama wafugwao 814 walihesabiwa, wengi wao wakiwa kwenye mitelemko ya Kaskazini ya mlima (Lambrechts et al., 2002).

    Kati ya mwaka 1952 na 1982, eneo la misitu ya asili ya Kilimanjaro ilipungua kwa kilomita za mraba 41. Maeneo ambapo awali misitu ya asili ilikuwepo sasa nafasi yake imechukuliwa na kilimo au uoto ulioharibiwa. Kingo za misitu ya hifadhi ndizo zilizoharibiwa vibaya zaidi, (Yanda na Shishira, 2001) hususan kwenye sehemu zijulikanazo kama ‘ukanda wa nusu maili’. Mnamo mwaka 1941, serikali ya kikoloni ilitenga eneo la hifadhi ya msitu wa Kilimanjaro kama eneo la msitu wa kilimo. Ukanda huu umeenea kati ya Mito Kikuletwa na Sanya, na mwendo wa nusu maili kwenda juu ya mlima kutoka kwenye ukingo wa hifadhi. Huu ‘ukanda wa nusu maili’ ulikusudiwa kupandwa miti ikuayo haraka kwa ajili ya matumizi ya jamii za Wachaga waishio chini ya hifadhi, ambako uhaba wa ardhi ulizuia upandaji wa miti (Baldwin, 1946). Leo, kadiri ya asilimia 66 ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya mashamba ya misitu yamekuwa ya kilimo au yamesafishwa, (Lambrechts et al., 2002).

    Jedwali la 2: Upotevu wa utando wa msitu wa Milima ya Tao la Mashariki katika Bonde la Mto Pangani

    Msitu Msitu wa asili Idadi ya Viunga Msitu Upotevu wa tando (km2) vya misitu uliofungwa wa asili wa (km2) msitu (%)

    Pare ya Kaskasini 151 2 28 50

    Pare ya Kusini 333 5 120 73

    Usambara Magharibi 328 17 245 84

    Usambara Mashariki 413 8 221 57

    Taita 6 13 4 98

    Rejea: Newmark, 1998:4) Katika Bonde la Mto Pangani, Milima ya Tao la Mashariki ipo kwenye maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu. Katika Milima ya Usambara Magharibi kwa mfano, idadi ya watu imeongezeka kwa mara 23 tangu 1900 (Newmark, 1998). Katika mazingira ya kijamii yenye sifa ya umaskini, umuhimu wa ardhi ya kilimo hauwiani kwa kiasi kikubwa. Shinikizo linalowakilishwa na tatizo hili kwenye hifadhi zilizobaki za misitu katika bonde linatisha. Ikidhaniwa kuwa Milima ya Tao la Mashariki, kihistoria ilikuwa karibu muda wote imejaa misitu, asilimia yake 77 itakuwa imepotea kutokana na shughuli za binadamu na/au moto katika miaka 2,000 iliyopita (Newmark, 1998). Tatizo la ziada ni kuwa mingi ya michakato hii imesababisha kutokea kwa viunga vya misitu, na spishi za wanyama

  • mara nyingi haziko tayari kuvuka nafasi wazi kati ya viunga vya misitu. Hii ina maana kuwa katika viunga kimoja kimoja, mkusanyiko wa jeni hupungua na uhai wa spishi huhatarishwa kutokana na kuzaliana wenyewe kwa wenyewe. Katika Bonde la Mto Pangani upotevu huu ni kama inavyoonyeshwa katika jedwali la 2.

    Hadhi ya msitu kuwa “msitu wa hifadhi” inaonekana kushindwa kupunguza viwango vya ukataji miti. Katika Hifadhi ya Msitu ya Nilo (hekta 5872.1), katika Milima ya Usambara, kuna hekta 33.8 za ‘kilimo chini ya msitu’, hekta 372.3 za kilimo cha ‘wakulima wadogo wadogo’, hekta 37.2 za ardhi tupu na hekta 1.9 za makazi ya binadamu (Cordeiro, 1998). Misitu ya Pwani ya Tongwe-Muheza ilikuwa na eneo la hekta 1,202, lakini ni hekta 300 tu za msitu zilizobaki, wakati ambapo Hifadhi ya Msitu wa Gombero imefyekwa kabisa kwa ajili ya kilimo (Baker na Baker, 2002).

    Kwenye Mlima Meru, matatizo yanayoikabili misitu yanafanana na yale yanayoutishia Mlima Kilimanjaro, nayo ni kama yafuatavyo (Bwoyo, mhojiwa):

    • Ukataji haramu wa miti – Misitu ya milimani huvunwa miti inayovutia kibiashara ya mireteni (Juniper) na Mshio (Olea Capensis).

    • Malisho – Wakati wa msimu wa kiangazi, jamii za jirani hulisha mifugo yao ndani ya msitu.

    • Uhaba wa ardhi – upande wa Mashariki wa mlima, uvamizi wa ardhi ni tatizo kubwa linaloongezeka.

    • Kutokuungwa mkono - katika baadhi ya vijiji, mradi wa msitu wa maeneo ya vyanzo vya maji (CFP – utakaoelezwa chini) huungwa mkono kwa kiwango kidogo na viongozi wa vijiji, ambao baadhi yao wanahusika binafsi na uvunaji wa msitu.

    • Moto – hili lilikuwa tatizo kubwa kati ya miaka ya 1998 na 1999.

    14

    Kisanduku cha 4: Tishio kwa Misitu ya Bonde la Mto Pangani

    • Mahitaji ya ardhi: kadri msongamano wa watu unavyoongezeka na uchumi unavyobaki kuwa duni, mahitaji ya ardhi ya kilimo huongezeka, na hivyo, misitu hukatwa kutoa nafasi ya kilimo.

    • Mahitaji ya mbao: misitu mingi iliyobaki katika PRB ina spishi za mbao zenye thamani ya kiuchumi, ambayo, jinsi inavyoadimika, ndivyo inavyopata bei kubwa. Miti pia hukatwa kwa ajili ya kuni na utengenezaji wa mkaa.

    • Mahitaji ya malisho: idadi ya mifugo katika bonde inaonekana kuongezeka. Jinsi ardhi ya kilimo inavyoongezeka, ardhi ya malisho hupungua, na wafugaji hupanda milima kutafuta malisho.

    • Makazi ya msituni: kadri watu wanavyojitahidi kutafuta kuongeza ardhi ya kilimo na malisho, hivyo pia hufanya makazi ndani ya mipaka ya misitu.

    • Udhaifu wa Sheria: licha ya hadhi ya uhifadhi wa misitu mingi ya bonde, mamlaka haziwezi kutekeleza sheria zinazotakikana kwa sababu ya uchache wa wafanyakazi, mishahara duni na rushwa. Kwa nyongeza, Idara ya Misitu na Nyuki na Mradi wa Misitu ya vyanzo vya maji inapatiwa fedha karibu zote na wahisani pekee, hali inayoibua maswali kuhusu uendelevu wake. Mwisho, ushirikishwaji wa jamii katika usimamizi wa misitu ya bonde ni dhana ngeni na kwa sasa haijawa na ufanisi mkubwa.

    • Uendelezaji wa misitu: uendelezaji wa misitu ya mashamba badala ya misitu ya asili huongeza matatizo ya uhifadhi.

    • Kugawanyika kwa misitu: Jinsi shinikizo linavyozidi kwenye misitu ya bonde mara nyingi hugawanyika vipande vipande. Spishi nyingi za msituni haziwezi kuvuka nafasi wazi kati ya msitu, na hivyo kusababisha matatizo ya uhifadhi wa bayoanuwai.

    • Moto: Kwa kawaida huanzishwa na binadamu ama makusudi (ili kuharibu misitu inayodhaniwa kuhifadhiwa isivyostahili na iliyozuiliwa) au kwa kawaida zaidi, ajali (kwa mfano, kutokana na ajali wakati wa kuchoma mkaa au kurina asali kutoka kwenye mizinga).

  • • Fedha – CFP haipati fedha zozote kwa ajili ya kuendeshea shughuli zake kutoka serikalini. Bwoyo (mhojiwa) anadai kuwa kwa sababu ya mchango muhimu wa misitu katika Bonde la Mto Pangani, kiasi cha fedha lazima kitengwe kwa ajili ya CFP kutoka kwa makampuni yazalishayo umeme wa maji au Ofisi ya Maji ya Bonde la Pangani (angalia pia Evans, 1997).

    B.3 Maji na ardhioevuMto Pangani unaundwa na matawi ya mito mikubwa miwili: Mto Ruvu, ambao hutokea kwenye miteremko ya Mashariki ya Mlima Kilimanjaro; na Kikuletwa, ambao hutokea kwenye Mlima Meru na mitelemko ya Kusini ya Mlima Kilimanjaro. Mito ya Ruvu na Kikuletwa huungana katika Bwawa la Nyumba ya Mungu, lenye eneo la kadiri ya kilomita za mraba 140 (Rohr na Killingtveit, 2002). Maji yanayoingia katika bwawa yanakaribia kuwa mita za ujazo 43.37 kwa sekunde (TANESCO, 1994). Mto unapotoka kwenye bwawa, huitwa Mto Pangani, na hutiririka kwa kilomita 432 kabla ya kuingia katika Bahari ya Hindi, ambako humwaga maji ya kiasi cha kilomita za ujazo 0.85 kwa mwaka (Vanden Bossche na Beracsek, 1990).

    Ndani ya Bonde la Mto Pangani, Mlima Kilimanjaro ndio sehemu yenye umuhimu wa pekee kihaidrolojia(Lambrechts et al., 2002). Kama ilivyoelezwa awali, mvua kwenye mlima huu zinakadiriwa kutoa asilimia 60 ya maji yanayoingia katika Bwawa la Nyumba ya Mungu, na asilimia 55 ya maji ya juu ya ardhi katika Bonde (Rohr na Killingtveit, 2002). Pia, cha muhimu – ingawa kiasi hakijulikani, ni maji yatokanayo na kuyeyuka kwa barafu kutoka milimani. Barafu inayoyeyuka kutoka mlimani huipa nguvu chemchemi kuu katika hifadhi maarufu ya Taifa ya Amboseli nchini Kenya. Myeyuko pia huzipa nguvu chemchemi ambazo mradi wa Ugavi wa Maji wa Nol Turesh ya Kenya hutegemea, unasambaza maji kwenye miji kadhaa mashuhuri ya Kenya, ikiwa ni pamoja na Machakos na Kajiado.

    Maji katika Bonde la Mto Pangani kwa kiasi kikubwa hutokana na mvua, ambayo mgawanyo wake hauko sawa ndani ya bonde. Kwa wastani, bonde hili hupata mita za ujazo 34, 773.4 kwa mwaka na kiasi cha wastani cha upoteaji maji kwa uchavushaji ni milimita 1,410 kwa mwaka. Kwa kuzingatia tofauti za mvua, bonde hili, linaweza kugawanywa katika mifumo miwili ya kihaidr