Bulletin 38

Embed Size (px)

DESCRIPTION

JARIDA LA WIKI LA NISHATI NA MADINI TOLEO LA 38

Citation preview

  • BulletinNews

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

    Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    http://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI &MADINI

    Toleo No. 38 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - Oktoba 17-23, 2014

    STAMICO yauza dhahabu za bilioni 5.19

    Soma habari Uk. 2Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimkaribisha Balozi wa Finland nchini Bi. Sinikka Antila kabla ya kuanza kwa kikao kilichojadili utekelezaji wa mradi mkubwa wa kuboresha umeme katikati ya jiji la Dar es Salaam. Pia kikao hicho kilihusisha ujumbe wa Balozi wa Finland na wataalamu kutoka wizara ya Nishati na Madini.

    Bilioni 56 kuboresha umeme Dar es Salaam Bilioni 56 kuboresha umeme Dar es Salaam

    -Uk8

  • 2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzNISHATI/MADINI

    Bilioni 56 kuboresha umeme Dar ifikapo Agosti 2015

    Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

    Mradi mkubwa wa megawati 80 kwa ajili ya kuboresha umeme katikati ya jiji la Dar es salaam unata-rajia kukamilika mwezi Agosti mwakani.

    Hayo yamesemwa na Kam-ishna Msaidizi wa Umeme Mhandisi Innocent Luoga kwenye kikao kilichokutanisha

    Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Balozi wa Finland Nchini Bi. Sinikka Antila na ujumbe wake pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini na taasisi zake.

    Mhandisi Luoga alisema kuwa mradi huo wenye tham-ani ya shilingi bilioni 56 utaun-ganisha vituo vya kusambaza umeme katikati ya jiji la Dar es Salaam ili kuhakikisha kuwa umeme haukatiki kabisa.

    Alitaja vituo hivyo kuwa

    ni pamoja na Ilala, Kariakoo, kituo cha reli, Sokoine na Ma-kumbusho na kuongeza kuwa mradi huo upo katika hatua ya utekelezwaji ambapo vifaa vya mradi vimeshapatikana pamo-ja na wataalamu kutoka Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kupatiwa mafunzo ndani ya nchi na nchini Finland.

    Mafunzo ya jinsi ya kuongoza vituo vya kusamba-za umeme kwa kutumia vifaa vya kisasa yameshatolewa kwa asilimia 80 kwa wataalamu

    wa TANESCO lengo likiwa ni kuwajengea uwezo kwani ndio watakaokuwa watekelezaji wakuu wa mradi huo. Ali-sisitiza Mhandisi Luoga.

    Aliongeza kuwa mkandara-si ambaye ni kampuni ya Eltel Oy kutoka Finland ameshaka-bidhiwa eneo la ujenzi na ku-choronga barabara kwa ajili ya kupitisha nyaya.

    Mhandisi Luoga alisema kuwa mradi huo ulioanza mapema Februari mwaka jana ulikuwa ukamilike Desemba

    Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akisisitiza jambo katika kikao kati ya masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na ushirikiano baina ya nchi ya Tanzania na Finland katika masuala ya teknolojia, uendelezaji wa rasilimali watu na usimamizi wa fedha. Balozi wa Finland Nchini Sinikka Antila (kulia) alizungumzia jinsi nchi ya Finland ilivyopiga hatua kimaendeleo hususani katika sekta ya nishati pamoja na utayari wa nchi hiyo kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha sekta za Nishati na Madini.

    mwaka huu lakini ulishindwa kukamilika kwa wakati kuto-kana na changamoto mbal-imbali zilizojitokeza. Hata hivyo alisisitiza kuwa tayari wameshaanza kuzifanyia kazi changamoto hizo ikiwa ni pamoja na kuwakutanisha wa-dau wote wa mradi hususan TANESCO na Wakala wa Ujenzi wa Barabara Nchini (TANROADS)

    Alisema lengo la kikao kati ya Profesa Muhongo na Ba-lozi wa Finland nchini liliku-wa ni kujadili hatua iliyofiki-wa ya utekelezaji wa mradi huo pamoja na changamoto zake na kuzipatia ufumbuzi, na mradi huo kuanza kwa kasi mpya.

    Kwa upande wake Balozi wa Finland Nchini Bi. Sinik-ka Antila alimshukuru Profe-sa Muhongo na kueleza kuwa nchi ya Finland ipo tayari kushirikiana na Tanzania ka-tika kuhakikisha kuwa mradi huu unakamilika kwa wakati ili jiji la Dar es Salaam lipate nishati ya umeme wa uhakika.

    Balozi Antila aliahidi kue-ndelea kushirikiana bega kwa bega na Profesa Muhongo kwa kila hatua ya utekelezaji wa miradi yake na kuhakiki-sha kuwa nishati ya umeme inachangia ukuaji wa uchumi.

    Naye mtaalamu wa masu-ala ya Ukuaji wa Uchumi katika Ubalozi wa Finland nchini Bw. Oskar Kass alishukuru Wizara ya Nisha-ti na Madini kwa kushirikiana na mkandarasi wa ujenzi ka-tika hatua za awali za usajili na vibali mbalimbali kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo. Aliongeza kuwa kuwa Ubalozi wa Finland utaendelea kushirikiana na Tanzania katika fursa ny-ingine za uwekezaji hususani ili kuchangia ukuaji wa uchu-mi wa nchi.

    TANESCO yajifunza kwa WamarekaniNa NeemaMbuja

    Inakadiriwa kuwa upotevu wa umeme unaigharimu dunia kiasi cha dola bilioni 200 hasa wakati unaposafirishwa na hivyo ku-sababisha hasara kubwa kwa kam-puni zinazozalisha na kusambaza umeme duniani

    Mtaalamu Mwandamizi wa Usi-mamiaji wa Miradi ya Umeme kutoka Marekani Bw. Nicolas Colombo ame-bainisha hayo mbele ya mkutano wa wadau wa sekta ya umeme uliofanyi-ka wiki hii, ulioandaliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) na kuwashirikisha wataalamu wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO).

    Bw. Colombo alisema licha ya

    nchi za Afrika ikiwemo Tanzania kukumbwa na tatizo hilo, hata nchi kama Marekani inapoteza pia kiasi cha Dola bilioni 6 kwa mwaka kwa umeme unaopotea licha ya kuwa na teknolojia za kisasa za ufuaji na usa-firishaji wa umeme duniani.

    Marekani inapoteza dola bilioni sita kati ya dola bilioni 200 ambazo Dunia inapoteza kutokana na nishati ya umeme inayopotea bila kutumika, lakini tumejifunza na tunajitahidi kukabiliana na tatizo hilo na ndio maana tunaisaidia Afrika kukabiliana na changamoto hii alisema Bw. Co-lombo.

    Akitoa tathmini juu ya hali ya upotevu wa umeme kwa nchi za Af-rika, Bw. Colombo alisema Tanza-

    nia, kupitia TANESCO imefanikiwa kupunguza ukubwa wa tatizo hilo kwa kuhakikisha kuwa wanadhibiti vyanzo vya upotevu wa umeme kuan-zia unapozalishwa, unaposafirishwa hadi unaposambazwa kwa wateja wadogo wadogo na kwenye viwanda vikubwa.

    Naye Meneja Mwandamizi Masoko na Mauzo wa TANESCO, Mhandisi Nicholaus Kamoleka alisema awali TANESCO ilikuwa inapoteza umeme kwa asilimia 28.7 mwaka 2002 na kufanikiwa kupungu-za ukubwa wa tatizo hadi kufikia asil-imia 21.85 kwa mwaka 2010, lengo likiwa ni kupunguza tatizo la upotevu wa umeme hadi kufikia asilimia 19 ifi-kapo mwaka 2015.

    Mafanikio yaliyofikiwa ni ku-tokana na juhudi za Shirika kufunga mita mpya na za kisasa ambazo hazi-hitaji msoma mita (Automatic Meter Reading) maarufu kama AMR kwa ajili yakudhibiti wizi na upotevu wa umeme, pamoja na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa matumizi ya umeme hasa kwa wateja wakubwa, aliongeza.

    Akitoa uzoefu wake kwa nchi ya Ghana, Mtaalamu wa Ukaguzi wa Umeme kutoka Shirika la Umeme la Ghana Mhandisi Michael Kwasi Okai alisema Ghana ilikuwa inakabiliwa na tatizo la upotevu wa umeme kwa kiasi kikubwa ambapo inakadiriwa kuwa karibu asilimia 27 ya umeme unao-zalishwa ulikuwa unapotea na hivyo

    kusababisha hasara kubwa.Mhandisi Okai alisema kwa sasa wamejipanga kuhakikisha ifikapo 2015 wanapungu-za tatizo hilo hadi kufikia asilimia 15.

    Ghana tulikuwa na tatizo kubwa la upotevu wa umeme kutokana na wateja wasio waaminifu kuchezea mita lakini kwa sasa mita za kisasa zimesaidia sana kukabiliana na changamoto hii ambayo ilikuwa ina-tusababishia hasara kubwa alisema Mhandisi Okai.

    Mkutano huo umeandaliwa na wataalamu kutoka mradi wa umeme Afrika (Power Africa Initiative) un-aofadhiliwa na Marekani kwa ajili ya kusaidia nchi za Afrika kuondokana na changamoto ya nishati ya umeme inayozikabili nchi nyingi zaAfrika.

    n Ni kuhusu kukabili upotevu wa umeme

  • 3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz MAONI

    Na Samwel Mtuwa

    Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) , umefanikiwa kupun-guza gharama za upimaji wa sampuli za dhahabu katika maabara yake baada ya ku-fanikiwa kwa asilimia mia moja kuweza kutengeneza vikombe vya kupimia sampuli hizo (Crusible) ndani ya maabara hiyo iliyoko mkoani Dodoma.

    Mtaalam wa Jiolojia katika Maabara ya GST, Bw. Philipo Momburi alieleza kuwa, hapo awali, maabara ilikuwa inaagiza vikombe vya kupimia dhahabu kutoka nje ya nchi , jambo ambalo lilikuwa likiingiza taasisi katika gharama kubwa , lakini baada ya utafiti kufanyika gharama hizo zimepungua kwa asilimia 50.

    Momburi aliongeza kuwa utafiti ulianza mwaka 1994 am-bapo ulidumu kwa miaka ishirini kabla ya kukamilika kwake.

    Baada ya kukamilika kwa utafiti wa vikombe hivyo, utekelezaji wake ulianza rasmi

    mwaka 2013, na sasa licha ya ku-punguza gharama za upimaji sam-puli kwa asilimia 50, tumeweza kuongeza huduma za kibiashara kwa kuongeza idadi ya upimaji wa sampuli kutoka vikombe 20 mpaka 40 kwa siku, aliongeza Momburi.

    Kwa upande wake Mkuru-genzi wa Maabara ya Jioloji ,GST, Augustine Rutaihwa, alisema kuwa baada ya kuanza kuten-geneza vikombe hivyo , Wakala

    umeweza kupata ubora katika upimaji wa sampuli , kuongeza ujuzi kwa wataalamu , kutoa hu-duma kwa wakati , na kuweza ku-tumia malighafi za ndani badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi.

    Maabara ya upimaji wa sam-puli za madini ilianzishwa mwaka 1929 kwa ajili ya kuboresha shu-ghuli za Wakala hasa kwa upande wa uchambuzi wa kimaabara wa sampuli za miamba , madini na maji.

    TahaririMEM

    Na Badra Masoud

    FIVE PILLARS OF REFORMS

    KWA HABARI PIGA SIMU KITENGO CHA MAWASILIANO

    BODI YA UHARIRI MHARIRI MKUU: Badra Masoud

    MSANIFU: Essy OgundeWAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson Mwase

    Teresia Mhagama, Nuru Mwasampeta

    INCREASE EFFICIENCYQUALITY DELIVERY

    OF GOODS/SERVICESATISFACTION OF

    THE CLIENTSATISFACTION OF

    BUSINESS PARTNERS

    SATISFACTION OF SHAREHOLDERS

    TEL-2110490FAX-2110389

    MOB-0732999263

    TUMEJIPANGA KUSHIKA NAFASI YA KWANZA

    Kati ya Juni 16 na Julai 7, mwaka 2014, Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA), Tawi la Tanzania (MISA-TAN) liliendesha Utafiti wa Upatikanaji Taarifa kutoka taasisi za serikali. Mwaka huu, utafiti ulihusisha taasisi nane za serikali.

    Kati ya hizo, 2 ambazo ni Wizara ya Nishati na Madini na Wizara ya Afya na Ustawi, zilitokana na utafiti uliofanyika mwaka jana.

    Taasisi hizo zilichaguliwa kwa kuwa Wizara ya Nishati na Madini ilikuwa ya kwanza kwenye utafiti wa 2013 na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilikuwa ya mwisho.

    Taasisi nyingine zilizoshindanishwa mwaka huu ni Wiz-ara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wiz-ara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mamlaka ya Vitambu-lisho vya Taifa (NIDA), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Idara ya Mahakama na Bunge.

    Mwaka huu, 2014, Wizara ya Nishati na Madini ime-shika nafasi ya pili ya taasisi ya Serikali inayofanya vizuri zaidi katika utoaji taarifa kwa umma.

    Ofisi ya Takwimu ya Taifa imeshika nafasi ya kwanza kwa taasisi iliyofanya vizuri zaidi katika utoaji taarifa kwa umma kwa mwaka huku Idara ya Mahakama imekuwa taasisi iliyofanya vibaya zaidi katika utoaji taarifa kwa umma.

    Kushika nafasi ya pili ni changamoto ambayo Wizara ya Nishati na Madini inaweza kuikabili. Wizara ina kila uw-ezo, sababu na nia ya kushika nafasi ya kwanza tena.

    Wizara imeimarisha kitengo cha mawasiliano ya seri-kali kwa kukijengea uwezo wa vifaa na rasilimali watu na imeweza kuongeza vipindi vyake kwa umma kupitia vituo mbalimbali vya redio na televisheni.

    Maboresho makubwa yamefanywa katika tovuti ya wiz-ara kwa kuongezwa links nyingine zenye taarifa muhimu kwa umma. Kwa mfano, hivi sasa mtu yeyote anaweza kuomba leseni ya kumiliki kitalu cha madini kwa kujaza fomu kupitia tovuti ya wizara.

    Pia kupitia tovuti ya wizara, mtu yeyote anaweza kupata orodha na mawasiliano ya wafanyabiashara wa madini we-nye leseni halali.

    Kitengo cha mawasiliano ya Serikali kimeongeza idadi ya machapisho yake lengo likiwa kuwapatia umma taarifa zote zinazohusu wizara na taasisi zake.Ukiacha jarida la wizara la kila wiki, wizara itaanzisha magazine itakayoku-wa ikitoka mara nne kwa mwaka kwa lugha ya Kiswahili na Kingereza.

    Aidha viongozi wa ngazi za juu wa wizara wameweka utaratibu wa kukutana mara kwa mara na wahariri wa vy-ombo vya habari kupitia Jukwaa la Wahariri (TEF), lengo likiwa ni kubadilishana mawazo na taarifa kwa manufaa ya umma.

    Vilevile taarifa za wizara zinarushwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kama blogs, twitters na facebook ili kuhakikisha taarifa za wizara zinasambaa kwa haraka duni-ani kote na kwa watu wa rika zote.

    Mipango na mikakati iliyopo, na juhudi zinazofanyika, zinatoa matumaini makubwa kuwa Wizara ya Nishati na Madini itashika tena nafasi ya kwanza ya taasisi ya serikali inayofanya vizuri zaidi katika utoaji taarifa kwa umma.

    TEL-2110490FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Gharama za upimaji sampuli za dhahabu zapungua kwa 50%

    44 waula GSTNa Samwel Mtuwa DodomaTaasisi ya Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) iliyo chini ya Wiz-ara ya Nishati na Madini(MEM) imetoa nafasi arobaini na nne (44) za ajira kwa watanzania kupitia Ofisi ya Rais, Sekreterieti ya Ajira utumishi wa umma.

    Kwa mujibu wa Meneja Rasili-mali Watu na Maendeleo wa GST, Bw.Gabriel Kasase alimweleza

    mwandishi wa habari hii kuwa ajira hizo 44 zinahusu Idara mbal-imbali ndani ya Wakala huo.

    Alizitaja Idara hizo na idadi ya nafasi kuwa ni; Idara ya utawala nafasi kumi na sita (16) , Idara ya Jiolojia nafasi kumi na moja(11) , Idara ya Maabara nafasi nne (4) , idara ya KanziData nafasi nne (4) na kwa upande wa vyeo ni nafasi ya Mkurugenzi nafasi tatu (3) , na nafasi ya Meneja saba (7).

    Bw.Kasase alisema kuwa nafasi hizi zimetangazwa kwa

    kufuata mpango mkakati wa GST wa mwaka 2010- 2015 ambapo kulingana na muundo wa taasisi nafasi hizo endapo zitafanikiwa kujazwa kulingana na idadi iliyota-jwa, zitakuwa zimekidhi mpango mkakati huo.

    Kasase aliongeza kuwa matarajio makubwa baada ya ya mchakato kukamilika ni kwamba Wakala utaweza kutekeleza dira na dhima yake kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na hapo awali kabla ya muundo kukamilika.

    Meneja Utawala huyo alitoa wito kwa watumishi wa GST ku-fuata utaratibu , sheria na kanuni za utumishi wa umma kwa sababu ndiyo njia pekee ya kufanikisha Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

    Mtaalam wa Jiolojia kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Bw. Philipo Momburi akionesha vikombe vya kupimia dhahabu katika maabara ya GST ambavyo vimetengenezwa na wataalam kutoka Wakala huo.

  • 4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Kampuni kutoka Norway yaomba ushirikiano

    Ofisi ya Madini Kanda ya Ziwa Nyasa yaanzisha msako wa wachimbaji haramu

    GST yanyakua medali, kombe SHIMIWI

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Mhe. Charles Kitwanga (kulia) akifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Studentweb ya Norway, Bw. Ari Mathias (kushoto).

    Mohamed Saif

    Kampuni ya Studentweb ya Norway imeomba kushiriki-ana na Wizara ya Nishati na Madini katika mpango maalumu wa kuwajengea uwezo Watanzania (capacity building) katika sekta ya Nishati na Petroli.

    Ombi hilo lilitolewa na Mkuru-genzi wa Kampuni hiyo, Ari Mathi-as kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Mhe. Charles Kitwanga

    hivi karibuni wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea wizarani hapo kwa lengo la kutambulisha mpango huo.

    Alisema kuwa kampuni yake im-eandaa mpango ambao unashiriki-sha vyuo vikuu mbalimbali duniani ambavyo vitashirikiana kwa pamoja kwa ajili ya kutoa mafunzo hususan yanayohusu masuala ya Nishati na Petroli kwa njia ya mtandao.

    Kwa mujibu wa Bw. Mathias, kozi zinazotarajiwa kutolewa kupi-tia mpango huo ni pamoja na sha-

    hada ya uzamivu katika Nishati na Petroli, Computer Science, Nano, Subsea na Biotechnology.

    Mpango huu utawawezesha wale wasiokuwa na fedha za ku-soma nje ya Tanzania, kupata elimu kwa njia ya mtandao kutoka katika vyuo vikubwa duniani na pia uta-wawezesha kusoma kozi ambazo hazipo hapa nchini lakini zinatole-wa na vyuo vingine nje ya nchi alisema Bw. Mathias.

    Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa kampuni yake imeanza ma-

    zungumzo na vyuo vikuu mbalim-bali nchini humu kuhusu namna vyuo hivyo vinavyoweza kujiunga katika mpango huo. Alivitaja vyuo ambavyo tayari vipo katika mpango huo kuwa ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Bergen, Chuo Kikuu Kishiriki cha Alesund, Chuo Kikuu cha Sta-vanger, Chuo Kikuu cha Agder, Chuo Kikuu cha Texas, Chuo Ki-kuu cha Aberdeen, Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Curtin, Chuo Kikuu cha Taifa cha Singapore, na Chuo Kikuu cha Houston.

    Samwel Mtuwa, Morogoro

    Timu ya michezo ya Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), imefanya vizuri katika mashindano ya Shirikisho la Mich-ezo ya Wizara na Taasisi za serikali (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Morogoro kwa mwaka 2014 na kufanikiwa kupata medali mbili za shaba na kombe.

    GST ilifanikiwa kuchukua me-dali za shaba katika mchezo wa riadha wa mbio za mita 100 na im-echukua kombe katika mchezo wa draft.

    Katika mashindano hayo timu ya GST iliweza kushiriki katika michezo ya, mpira wa pete , kuvuta kamba, riadha , mbio za baiskeli , draft , dasti na mchezo wa bao.

    Akizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa GST katika makabidhiano ya kombe hilo yali-yofanyika katika viwanja vya GST mjini Dodoma, Kaimu Mtendaji Mkuu wa GST, Augustine Ru-taihwa, aliwahimiza wanamichezo kushiriki michezo na kufanya ma-zoezi pale wanapopata muda kwa manufaa ya afya ya akili na mwili .

    Kwa upande wake katibu mkuu wa klabu ya michezo ya GST , Bw Heri Issa Gombera , alimwomba Mtendaji Mkuu ambaye ndiye md-hamini wa klabu juu ya kuimarisha ushiriki wa michezo ya bonanza kwa watumishi kwa lengo la kuima-risha mahusianao baina ya watumi-shi.

    Mohamed Saif

    Ofisi ya Madini, Kanda ya Ziwa Nyasa imeandaa mkakati maalumu wa kufanya msako ili kubaini wachimbaji na wafanyabi-ashara wanaofanya shughuli za ma-dini kinyume na sheria.

    Mkakati huo ulipendekezwa hivi karibuni katika kikao cha watumishi wa ofisi ya Kanda ya Ziwa Nyasa walipokutana kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uchimbaji na biashara ya madini ka-tika kanda hiyo.

    Katika taarifa iliyoandaliwa baada ya kikao hicho na kusainiwa

    na Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Ziwa Nyasa, Julius Sarota ilibainisha kuwa kumekuwepo na wa-nanchi ambao wanajihusisha na bi-ashara ya madini kinyume na sheria.

    Aidha, katika taarifa hiyo, iliele-zwa kuwa wale watakaobainika ku-fanya biashara ya madini kinyume na sheria, hatua kali za kisheria zita-chukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kuhakikisha madini watakayokut-wa nayo yanataifishwa na kuwa mali ya Serikali.

    Mbali na mkakati huo, taarifa ya kikao hicho inabainisha kuwa ofisi hiyo imejipanga kuandaa semina kwa viongozi na watendaji wa Hal-

    mashauri za Mkoa wa Njombe ili kutoa elimu ya sheria na taratibu za utafutaji, uchimbaji na biashara ya madini.

    Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kanda ya Ziwa Nyasa imedhamiria kuongeza makusanyo kwa asilimia zaidi ya 20 katika robo ya pili ya mwaka kupitia madini ya ujenzi ku-toka Sh 319, 179, 501 zilizokusanywa katika robo ya kwanza ya mwaka ili-yoishia mwezi Septemba.

    Ofisi ya Madini Kanda ya Ziwa Nyasa ina jumla ya ofisi tatu ambazo ni Njombe, Tunduru na Songea na huku ofisi ya Songea ikiwa ndiyo makao makuu ya kanda.

    Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Nyasa, Julius Sarota akizungumza na wachimbaji wadogo.

  • 5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Kitwanga: Symbion tekelezeni wajibu wenu

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga akisisitiza jambo wakati wa kikao baina yake na Kampuni ya kuzalisha Umeme ya Symbion, wengine ni watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania TANESCO.

    Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwan-ga, ameitaka Kampuni ya kuzali-sha Umeme ya Symbion kuka-milisha kwa wakati, utekelezaji wa kuiunganishia umeme mikoa ambayo iko chini ya mradi un-aotekelezwa na kampuni hiyo kupitia mradi unaosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini ( REA) awamu ya kwanza, ifikapo

    Disemba,2014.Kauli hiyo ya Kitwanga in-

    afuatia ucheleweshaji wa mradi huo ambao awali ulipangwa kukamilika tangu mwaka 2012 kwa mujibu wa mkataba na makubaliano yake na Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

    Niambieni ugumu uko wapi? Haiwezekani tangu mwaka 2012 hadi sasa mradi huu haujakamil-ishwa. Hatuwezi kuwachelew-esha namna hii wananchi na

    huduma muhimu ya umeme. Hili haliwezekani, alisisitiza Kit-wanga.

    Aidha, Naibu Waziri Kitwan-ga alizikataa sababu zilizotolewa na kampuni hiyo ikiwemo wizi kuwa zimesababisha kuchelewa kukamilika kwa mradi huo.

    Msisingizie kwamba jambo hili limecheleweshwa kutokana na wizi. Hili halikubaliki. Tuna-chotaka mtekeleze mradi kama tulivyokubaliana. REA wame-saini mikataba mwezi Februari, 2014 na hadi sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 66 lakini

    ninyi tangu 2012 hamjakamilisha mradi wenu, alibainisha Kit-wanga. Pia katika kikao hicho, Naibu Waziri Kitwanga amei-taka kampuni hiyo kuwasilisha kila baada ya wiki mbili taarifa ya utekelezaji wa mradi huo. Tuko hapa kufanya biashara, na tuna-taka kufanya biashara na ninyi la-kini kama mtashindwa kuendana na kasi yetu, hatutakubali jambo hili, aliongeza Kitwanga.

    Kampuni ya Symbion ina-takiwa kutekeleza mradi huo ka-tika Mikoa ya Mwanza, Pwani na Morogoro.

    NISHATI NA MADINI YANGARA KIUTENDAJINa Veronica Simba

    Wizara ya Nishati na Madini ime-shika nafasi ya pili kwa taasisi za Serikali zinazofanya vizuri zaidi katika utoaji taarifa kwa umma.

    Matokeo hayo ni kutokana na Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanza-nia (MISA-TAN) mwaka huu, 2014 kuhusu upatikanaji wa taarifa kutoka Taasisi za Seri-kali.

    Akizungumza mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam katika warsha maalumu kwa Maafisa wa Serikali hususan wanaohusika na utoaji habari kwa jamii, Afisa Habari wa

    MISA-TAN, Gasirigwa Sengi-yumva alisema Wizara ya Ni-shati na Madini ni miongoni mwa taasisi za serikali zinazo-fanya vizuri sana katika utoaji habari kwa jamii kupitia tovuti yake na pia kwa kujibu maswali yanayowasilishwa na wananchi wa kada mbalimbali.

    Utafiti wa mwaka huu uli-husisha taasisi nane za serikali ambapo Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) imeshika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Wizara ya Nishati na Madini wakati Idara ya Mahakama ikishika nafasi ya mwisho, alisema Sengiyumva.

    Alisema lengo kuu la utafiti husika ni kubainisha jinsi gani wananchi wa kawaida wa-naweza kupata taarifa muhimu ili ziwasaidie katika kufanya

    maamuzi sahihi yanayohusu maisha yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

    Vilevile, alisema utafiti huo hutumika kuwakumbusha walio madarakani hususan ka-tika ofisi mbalimbali za umma kutimiza wajibu wa kutumikia umma kwa uwazi na ukweli ili kuleta maendeleo stahiki nchi-ni.

    Akizungumzia vigezo vili-vyotumika kuchagua taasisi zilizofanyiwa utafiti mwaka huu, Sengiyumva alitaja sifa mojawapo kuwa ni matokeo ya utafiti wa mwaka 2013 am-bapo taasisi iliyoshika nafasi ya kwanza ambayo ni Wizara ya Nishati na Madini na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii il-iyoshika nafasi ya mwisho zil-

    ipewa nafasi tena mwaka huu ili kufuatilia maendeleo yake.

    Wizara ya Nishati na Ma-dini imeshika nafasi ya pili mwaka huu kutoka mshindi wa kwanza mwaka jana hivyo ni changamoto kwao kujitafiti ni wapi wameanguka na kufanya maboresho, alisema Sengi-yumva.

    Akifafanua zaidi kuhusu zoezi la utafiti lilivyoendesh-wa, Sengiyumva alisema njia kuu mbili zilitumika, zikiwa ni kutafiti tovuti za taasisi husika kuona ni aina gani ya taarifa zinapatikana humo pamoja na kutafiti endapo maswali yanay-owasilishwa na wananchi mbal-imbali yanajibiwa kwa wakati.

    Alisema maswali yaliwasil-ishwa kwa wahusika kwa njia

    ya maandishi na kuweka muda wa siku 21 kama kigezo cha ku-toa alama (marks) kwa taasisi husika. Kadri muhusika al-ivyotoa majibu mapema ndivyo alivyopata alama nyingi, ali-fafanua Sengiyumva.

    Vilevile, Sengiyumva alise-ma kwa upande wa tovuti, utafiti ulihusisha kubainisha en-dapo kuna taarifa za kutosha na zinazolenga kuhabarisha umma katika mambo mbalimbali ya msingi yanayofanywa na taasisi husika pamoja na uwekaji taari-fa mpya mara kwa mara.

    Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa MISA-TAN Andrew Marawiti alisema ri-poti ya utafiti wa mwaka 2014 imeonesha kuwa kwa zaidi ya miaka mitano (5) ambayo utafiti huu umekuwa ukifanyi-ka, kumekuwa na mabadiliko makubwa kwenye taasisi husika kwa namna ya utendaji kazi hususan katika kuupatia umma taarifa muhimu.

    Naye Mwanasheria kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, James Marenga, akiwasilisha mada kuhusu haki ya kupata habari kutoka taasisi za Serikali, alisema Watumishi wa Serikali hususan wanaowajibika kutoa habari kwa wananchi wana-paswa kutimiza wajibu wao wa kuwapatia wananchi taarifa na habari kuhusu taasisi zao pa-sipo kusubiri kusukumwa au kulalamikiwa.

    Marenga alisema ni wajibu wa watumishi hao kuwakumbu-sha na kuwahamasisha Maafisa wengine hususan viongozi ma-hala pa kazi, kuona na kutam-bua umuhimu wa kutimiza haki hiyo ya msingi kwa wananchi.

    Katika taarifa ya utafiti wa mwaka 2014 wa MISA-TAN, imependekeza mafunzo ya mara kwa mara kwa watumishi, hasa wale ambao wanahusika moja kwa moja na utoaji taarifa kwa umma ili kujenga imani kwa jamii. Watumishi wanao-pendekezwa ni Maafisa Habari, watumishi wa mapokezi na Masjala.

    Moja ya malengo ya MISA ni kuhakikisha uhuru wa habari unatambulika na Katiba mbalimbali za nchi kama haki ya msingi, pia kuhamasisha umuhimu wa uwazi na uwajibi-kaji serikalini.

    Taasisi zilizohusika ka-tika utafiti wa mwaka huu wa MISA ni Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mam-laka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Ofisi ya Taifa ya Tak-wimu (NBS), pamoja na Idara ya Mahakama na Bunge.

  • 6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    MATUKIO KATIKA PICHAWaziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (wa tatu kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na Viongozi Waandamizi wa Kampuni za Tecnimont, Stamicarbon na Kinetics Technology zinazojishughulisha na masuala ya mafuta na gesi nchini Italia. Waziri Muhongo amezialika kampuni hizo kuja nchini ifikapo tarehe 1 Disemba, 2014, ili kukutana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kujadili masuala ya uwekezaji Kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Italia James Msekela, Afisa anayeshughulikia masuala ya kijamii wa Kampuni ya Maire Tecnimont Francesca Renaldo, Mkuu wa Masuala ya Mawasiliano wa kampuni ya Maire Tecnimont, Carlos Nicolais, Mratibu wa Miradi na Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Kinetics Techonology Alessia Mangiapane (wa pili kulia), na Meneja Masoko wa Kampuni ya Stamicarbon Rutger Bonsel (wa kwanza kulia)

    Wanamichezo kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), wakiwa kwenye maandamano kwenda kukabidhi kombe kwa uongozi wa Wakala huo mara baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya SHIMIWI 2014 yaliyofanyika Morogoro na kuibuka na kombe na medali mbili za shaba. Kutoka kushoto ni Paulo Watowa, Idrisa Lukindo, na Domitila Jumla.

    u

    u

    uWaziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Finland nchini Bi. Sinikka Antila mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati yao.

  • 7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    MATUKIO KATIKA PICHA

    Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Nyasa, Julius Sarota akizungumza na wachimbaji wadogo ili kuwafahamisha masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya madini.

    Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi Edwin Ngonyani (wa kwanza kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na Myeyushaji wa dhahabu wa Kampuni ya Argor-Heraeus SA ya Via Moree Mendrisio-Lugano inayonunua mgodi wa dhahabu ya STAMIGOLD. Wa kwanza kushoto ni Meneja Mkuu wa STAMIGOLD Mhandisi Dennis Sebugwao.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga(katikati) akisisitiza jambo wakati wa kikao baina yake na Kampuni ya kuzalisha Umeme ya Symbion, wengine katika picha ni watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania TANESCO.

    u

    u

    u

  • 8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Na Koleta Njelekela

    Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limefanikiwa kupata soko la kudumu la dhahabu nchini Switzer-land na kufanikisha kuuza kilo 103 za dhahabu zenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 3.1 sawa na Shilingi bilioni 5.19.

    Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi Edwin Ngonyani amesema mauzo hayo ya dhahabu ni matokeo ya uzal-ishaji bora uliofanywa na Kam-puni tanzu ya STAMIGOLD kati ya Julai na Septemba 2014, jambo ambalo limeiwezesha Kampuni hiyo tanzu ya STAMICO kulipa Mrabaha wa awali (provisional royalty) wa shilingi milioni 196 kwa Serikali.

    Kuanzia sasa STAMICO ina uwezo wa kuuza dhahabu yake katika soko la kimataifa kila mwe-

    zi baada ya kupata soko la uhakika nchini Switzerland. Fedha zitaka-zopatikana zitasaidia kugharimia uendeshaji wa mgodi, kurudisha mtaji na kulipa madeni Alisisitiza Mhandisi Ngonyani.

    Kaimu Mkurugenzi Mtandaji huyo wa STAMICO pia amesema Kampuni ya STAMIGOLD ikiwa kama Muuzaji (Supplier) ime-tia saini Mkataba wa Mauzo na Kampuni ya Argor-Heraeus SA ya Via Moree Mendrisio-Lugano mnamo tarehe 6 Oktoba, 2014 hatua ambayo imehusisha ufun-guaji wa akaunti ya Madini (Metal Account) ya STAMIGOLD ita-kayotumika kufanya ufuatiliaji wa maendeleo ya kibiashara.

    Amesema STAMICO ime-fuata taratibu zinazotakiwa katika kufanya biashara ya madini nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kupata kibali cha mauzo (Export Per-mit), upimaji wa sampuli kubaini kiwango cha ubora na uzito halisi

    wa mzigo, ufungaji (sealing), usa-firishaji wa mzigo na upokeaji; pamoja na kukamilisha hatua ya muuzaji kumtambua mnunuzi wa bidhaa husika (know your cus-tomer principle)

    Shirika la Ushirikiano wa Ki-uchumi na Maendeleo yaani Or-ganization of Economic Coopera-tion and Development (OECD) linazitaka nchi zinazoshiriki ka-tika soko la dunia la madini hu-susani nchi za maziwa makuu, kutekeleza kanuni ya kumtam-bua mteja; ambapo muuzaji na mnunuzi wanatakiwa kutem-beleana katika kipindi cha miezi sita tangu kuanza kwa hatua za mauziano. Alifafanua kwa kina Mhandisi Ngonyani.

    Kanuni hiyo ya kumtam-bua mteja inahusu zaidi nchi za maziwa makuu na inalenga kuziwezesha pande zote muuzaji na mnunuaji) kufahamiana kibi-ashara, kubaini uwezo wa uzal-

    ishaji wa mgodi husika, ubora wa mitambo na hatua ya uchakataji (refining) wa dhahabu ili kuziwez-esha pande zote kufanya biashara halali na kujiletea maendeleo ya kiuchumi.

    Hii ni pamoja na kudhibiti matumizi ya mapato yasiyo halali ya rasilimali madini kusababisha kuendeleza milipuko ya vita vya wenyewe kwa wenyewe katika za maziwa makuu. Aliongeza Mhandisi Nginyani

    Hivyo Mhandisi Ngonyani amebainisha kuwa STAMICO na Kampuni yake tanzu ya STA-MIGOLD kama muuzaji kwa upande wake imekamilisha kanu-ni hiyo ya Kumfahamu Mteja kwa mujibu wa OECD, na kwamba hatua itakayofuata ni ya Mnunuzi ambaye ni Kampuni ya Argor-Heraeus SA ya Mendrisio ya kuja nchini Tanzania katika kip-indi cha miezi mitatu mpaka sita ijayo kuanzia sasa ili kutembelea

    Mgodi wa uzalishaji Dhahabu wa Biaharamulo unaoendeshwa na STAMIGOLD.

    Akizungumzia kuhusu suala la uwajibikaji sehemu ya kazi kufua-tia mafanikio ya STAMIGOLD, Mhandisi Ngonyani amesema mafanikio hayo yametokana na juhudi kubwa iliyofanywa na Me-nejimenti ya kuzuia wizi, ufujaji na matumizi mabaya ya vitendea kazi vya Shirika na Kampuni. Alisema Shirika halitavumilia vitendo vya aina hiyo (zero tolerance).

    Amesema hatua zinazochuku-liwa na zitakazochukuliwa na Menejimenti ya STAMIGOLD za kudhibiti wizi hasa wa mafuta (diesel) na mawe ya dhahabu zina baraka zote za STAMICO na Seri-kali kwa ujumla.

    Aidha amesisitiza kuwa STA-MICO itamfukuza kazi mara moja mfanyakazi yeyote wa Shiri-ka au Kampuni Tanzu atakaye-husika na wizi wa aina yeyote ile.

    STAMICO yauza dhahabu za bilioni 5.19

    Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi Edwin Ngonyani (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wayeyushaji wa dhahabu. Kampuni ya Argor-Heraeus SA ya Via Moree Mendrisio-Lugano inayonunua dhahabu ya STAMIGOLD. Wa kwanza kushoto ni Meneja Mkuu wa STAMIGOLD Mhandisi Dennis Sebugwao.

  • 9BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    WIZARA YA NISHATI NA MADINI INAPENDA KUWATAARIFU WANANCHI WOTE KUWA:TANZANIA ITAKUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA TANO WA KIMATAIFA WA JOTOARDHI UTAKAOFANYIKA KUANZIA TAREHE 27 OKTOBA HADI TAREHE 2 NOVEMBA, 2014 KATIKA KITUO CHA MIKUTANO CHA KIMATAIFA CHA ARUSHA (AICC).WASHIRIKI WA MKUTANO HUO NI WANACHAMA WA NCHI ZILIZO KATIKA BONDE LA UFA (RIFT VALLEY) YAANI ERITREA, ETHIOPIA, KENYA, RWANDA, TANZANIA NA UGANDA. VILEVILE, NCHI KADHAA ZA AFRIKA, ULAYA, MAREKANI NA ASIA, ZIKIWEMO: BURUNDI, COMORO, JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO, MSUMBIJI, DJIBOUTI, ZAMBIA, MALAWI, ICELAND, NEW ZEALAND, MAREKANI, CANADA, ITALIA, INDIA, JAPANI, UJERUMANI NA INDONESIA ZITASHIRIKI.MKUTANO HUO UTAONGOZWA NA KAULI MBIU ISEMAYO JOTOARDHI NI SULUHISHO LA MAHITAJI YA NISHATI KATIKA AFRIKA (Geothermal: Solution to African Energy Needs).

    JOTOARDHI NI MOJAWAPO YA VYANZO VYA NISHATI ITOKANAYO NA MVUKE UNAOTOKA ARDHINI, HUSUSAN KATIKA MAENEO YALIYO KATIKA BONDE LA UFA (RIFT VALLEY).

    MGENI RASMI KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO

    HUU ANATARAJIWA KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE. AIDHA, MKUTANO HUO UTAFUNGWA NA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. MIZENGO PETER PINDA.MKUTANO HUO UMEANDALIWA NA SERIKALI YA TANZANIA KUPITIA WIZARA YA NISHATI NA MADINI KWA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LINALOSHUGHULIKIA MASUALA YA MAZINGIRA (UNEP) PAMOJA NA WADAU WENGINE WAKIWEMO; UMOJA WA NCHI ZILIZO KATIKA BONDE LA UFA (ARGeo), GEF, SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA (TPDC), SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO), SHIRIKA LA MAENDELEO LA KIMATAIFA LA ICELAND (ICEIDA), NDF, KAMPUNI TANZU YA JOTOARDHI (GDC), FEDERAL INSTITUTE FOR GEOSCIENCES AND NATURAL RESOURCES (BGR), POWER AFRICA, KAMISHENI YA UMOJA WA AFRIKA (AUC), BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AfDB), EAST AFRICAN REGIONAL BRANCH (EARB) OF INTERNATIONAL GEOTHERMAL ASSOCIATION (IGA) NA CHUO KIKUU KINACHOTOA MAFUNZO YA KUENDELEZA JOTOARDHI (UNU-GTP). KWA TAARIFA ZAIDI NA USAJILI TEMBELEA TOVUTI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI (www.mem.go.tz) NA TOVUTI YA KONGAMANO LINALOANDALIWA (c5.theargeo.org).

    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA NISHATI NA MADINI

    MKUTANO WA TANO WA KIMATAIFA WA JOTOARDHI

  • 10 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wasiliana nasi kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    WIZARA YA NISHATI NA MADINI

    Wadaiwa sugu TANESCO watakiwa kulipa madeni Na Leila Muhaji,

    Arusha

    Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa TANESCO Jener-ali Mstaafu Robert Mboma amewataka wadaiwa wote wa umeme kulipa madeni yao ili kuwezesha shirika hilo kufikia malengo yaliyokusudiwa ya utoaji wa huduma ya nishati ya umeme hapa nchini.

    Mwenyekiti Mboma alitoa wito huo alipokuwa akizungumza na kipindi cha TANESCO na Maen-deleo mkoani Arusha hivi karibuni ili kuhamasisha ulipaji wa mad-eni na utoaji wa huduma bora za umeme kwa wateja wake kama njia ya kusukuma mbele maende-

    leo.Alisema iwapo TANESCO

    wangelipwa hata nusu ya madeni inayodai kwa wateja wake shirika lingefika mbali zaidi katika utoaji wa huduma zake kulingana na mpango mkakati wake.

    Pia alitumia nafasi hiyo kusifu juhudi za uongozi wa TANESCO katika kulipa madeni yake kwa wadai wake ambapo hadi sasa zaidi ya nusu ya madeni yote ya-meshalipwa, hali inayotia faraja na kuonesha mwanga mzuri kwa Shirika kutengeneza faida katika kipindi kifupi kijacho.

    Aidha aliusifu uongozi wa Shirika kwa juhudi zake katika su-ala la manunuzi ambapo kwa sasa manunuzi hayo yanafanyika vizuri kwa kufuata taratibu na kanuni za ya umma.

    Jenerali mstaafu Mboma, al-ipongeza pia taratibu zinazofany-wa na viongozi wa shirika za ku-hakikisha taarifa za kila mwezi za utendaji wa Shirika zinaifikia bodi ya wakurugenzi mapema ili kutoa nafasi ya kushauri na kuelekeza mambo mbali mbali ya kiufanisi.

    Mwenyekiti huyo wa Bodi, alisema iwapo shirika litatetereka katika utendaji kazi, hata sekta zingine za uzalishaji na mwananchi mmoja mmoja nchini watatetereka kwa kuwa uzalishaji mzuri wa mali na ukuaji wa uchumi unahitaji hu-duma bora ya nishati ya umeme.

    Pia alitumia nafasi hiyo ku-toa wito kwa sekta hizo nyingine pamoja na wananchi kwa ujumla kukataa na kupingana vitendo vio-vu vya kulihujumu Shirika kwani kuendelea kuachia uhujumu huo

    kutalifanya shirika kushindwa kutimiza malengo yake ya kuwa-hudumia watanzania.

    Katika mahojiano hayo, Mwe-nyekiti Mboma alisema TANE-SCO imeanza kutengeneza faida kubwa kutokana na makusanyo in-ayoyafanya na kulitaka shirika hilo kuanzisha vyanzo zaidi vya ufuaji umeme ili ikiwezekana iachane na ununuzi wa nishati hiyo kutoka kwa wazalishaji wengine ambapo imekuwa ikiligharimu shirika kiasi kikubwa cha fedha.

    Wito mwingine alioutoa kwa shirika ni kutunza vifaa, miundom-binu ya kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme, kukamilisha miradi yake mipya inayoendelea kote nchini na kupambana na tatizo kukatika umeme marakwa mara.

    Na Leila Muhaji, Arusha

    Afisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha kutengeneza vyandarua cha A to Z cha jijini Arusha Bw. Binesh Haria amesifu utendaji kazi mzuri wa Shirika la Umeme nchini TANESCO ambao umewezesha maeneo mengi kupata umeme wa uhakika wakati wote tofauti na miaka ya nyuma.

    Bw. Haria aliyewakilisha watuami-aji wakubwa wa umeme wa mkoa wa Arusha, alitoa pongezi wakati akizun-gumza na mwandishi wa habari hii na mwandaaji wa kipindi cha TANESCO na Maendeleo ili kupata maoni yake kuhusu utendaji kazi wa Shirika hilo katika utoaji wa huduma zake kwa wateja wakubwa mkoani humo.

    Alilisifu Shirika kwa kusiki-liza maombi ya wateja wakubwa la kuomba wawekewe njia ya umeme inayojitegemea (dedicated line) kwani utekelezaji wake umesaidia kuondoa tatizo la umeme mdogo walilokuwa wakilipata kwa kuchangia njia moja

    na wateja wengine. Bw. Haria alisifu pia uhusiano mzuri uliopo baina ya TANESCO na watumiaji wakubwa wa umeme ambao umesaidia upa-tikanaji wa taarifa mbalimbali kwa wakati na ushughulikiwaji wa mata-tizo ya umeme pindi yanapotokea.

    Afisa Mtendaji Mkuu huyo alise-ma hapo awali kiwanda chake kili-kuwa kikipata huduma hiyo kupitia njia moja kutoka Monduli iliyokuwa

    na watumiaji wengi, kitu ambacho kilisababisha kuzidiwa kwa njia hiyo na hivyo umeme kukatika mara kwa mara na kuwalazimisha kutumia je-nereta ambayo uendeshaji wake ni wa gharama kubwa.

    Alisema kupatikana kwa njia hiyo inayojitegemea kumeboresha utend-aji wa kiwanda na kuweza kutimiza malengo mbalimbali waliyojiwekea kutokana na ukweli kwamba kila

    mtambo unaotumika kiwandani hapo unahitaji nishati ya umeme wa uhaki-ka.

    Bw. Haria alitoa wito kwa uon-gozi wa TANESCO kuhakikisha wa-naboresha zaidi huduma zao kama njia ya kuwavutia zaidi wawekezaji ka-tika sekta mbalimbali hapa nchini ku-tokana na ukweli kwamba uwekezaji mkubwa siku zote unategemea umeme wa uhakika.

    UJUMBE WA WAZIRI WIKI HII UJUMBE WA WAZIRI WIKI HIIWAFANYAKAZI WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI, KAMPUNI NA

    TAASISI ZETU TUENDELEE KUCHAPA KAZI KWA UMAKINI, UADILIFU NA UBUNIFU MKUBWA SANA KWA KUSUDIO LA KUFUTA UMASIKINI NCHINI

    MWETU. TUTASHINDA, TUSIKATISHWE TAMAA.

    Watumiaji umeme wakubwa waisifu TANESCO

    Wafanyakazi wa kiwanda cha A to Z wakiwa kazini

  • 11BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Na Mwandishi Wetu

    Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) umeibuka kid-edea Katika mashinda-no ya Shirikisho la Michezo ya Wiz-ara na Idara za Serikali (SHIMIWI) ya mwaka huu (2014) yaliyofanyika ki-taifa Mkoani Morogoro, ambapo timu ya Wakala huo imefanikiwa kupata kombe la nidhamu kwa upande wa Wakala zilizoshiriki mashindano hayo.

    Kombe hilo la nidhamu lilikabidhi-wa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera kwa Kiongozi wa timu ya TMAA, Robert B. Mujuni lilikuwa ni matokeo ya kujituma katika michezo waliyoshiriki kwa nidhamu na hivyo kufanikiwa kuibuka na kikombe hicho kati ya vilabu wanachama 60 vilivy-oshiriki mwaka huu.

    Wakala huo pia ulifanikiwa kuin-gia katika hatua ya fainali katika mich-ezo ya riadha mita 200 na mita 800 na kufanikiwa kuingia katika hatua za 10 bora katika michezo yote iliyoshiriki pamoja na kupata cheti cha ushiriki wa mashindano hayo.

    TMAA ambaye ni mwanachama SHIMIWI, mwaka huu ulishiriki ka-tika michezo ya riadha wanaume mita 100, mita 200, na kupokezana vijiti,

    mita 100 na mita 800. Vile vile Wakala umeshiriki mbio za baiskeli za kilomita 50, drafti, karata pamoja na kurusha tufe kwa wanaume.

    SHIMIWI huandaa mashindano yanayowakutanisha Watumishi wa Serikali kila mwaka lengo kuu ikiwa ni kuendeleza ushirikiano, upendo, un-dugu na kuimarisha afya ya mwili na akili.

    Mashindano hayo ya SHIMIWI 2014, yalifunguliwa na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani, ambaye aliwataka waajiri katika Wiz-ara, Idara zinazojitegemea, Wakala na Taasisi za Serikali kuhakikisha kuwa wanaweka bajeti ya kutosha na utara-tibu mzuri wa michezo kwa watumishi wao ili kujenga ukakamavu,afya na pia kufahamiana.

    Alieleza kuwa pamoja na changa-moto za ufinyu wa bajeti na kuwa na kazi nyingi,waajiri wanatakiwa wad-umishe michezo sehemu za kazi.

    SHIMIWI ilisajiliwa rasmi na Msajili wa Vilabu na Vyama vya Mich-ezo tarehe 21 Novemba 1984, kwa jina la Inter-Ministerial Sports Organiza-tion (ISO). Tarehe 18, Agosti, 2010, Shirikisho likajisajili kwa jina la Kiswa-hili la Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI).

    TMAA YANGARA SHIMIWI 2014Kiongozi wa Klabu ya michezo ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Robert B. Mujuni (kulia) akipokea kombe kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera, mara baada ya Timu ya Wakala huo kuibuka kidedea katika nidhamu michezoni.

    u

    u

    u

    uMwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Wakala wa Ugaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Mhandisi Oscar Cosmas (kushoto) akimkabidhi Mtendaji Mkuu wa Wakala huo, Mhandisi Dominic Rwekaza, kombe la nidhamu ambalo timu ya Wakala huo ilitunukiwa katika Michezo ya SHIMIWI 2014 yaliyomalizika mjini Morogoro wiki iliyopita.

    Wawakilishi wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) katika Michezo ya SHIMIWI 2014 wakiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala, Mhandisi Dominic Rwekaza (katikati), mara baada ya kumkabidhi kombe la nidhamu walilotunukiwa kwa timu hiyo katika mashindano ya SHIMIWI 2014. Kutoka kushoto ni Omari Rwakyaya, Seif Mwache, Dennis Winston, Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo Oscar Cosmos, Gimonge Chacha na Robert Mujuni.