109
1 BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Kumi na Sita Tarehe 30 Juni, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. George B. Simbachawene) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Mwenyekiti! MWENYEKITI: Hakuna Mwongozo wakati wa maswali. Tundelee, swali letu la kwanza leo litakwenda Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mheshimiwa Kidawa Hamid Saleh, atauliza swali hilo. Na. 150 Dawa za Kutibu Ugonjwa wa Kisukari MHE. FATMA A. MIKIDADI (K.n.y. MHE. KIDAWA HAMID SALEH aliuliza:- Ugonjwa wa Kisukari umekuwa ni tatizo na unawapata watu wa rika zote; kumejitokeza wimbi kubwa la Waganga Asilia wanaojitangaza kuwa wanazo dawa zinazotibu ugonjwa huo:- Je, Serikali inawaeleza nini wananchi juu ya dawa hizo? NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kidawa Hamid Saleh, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mfumo wa tiba asili, kuna dawa nyingi zinazotumika kudhibiti ugonjwa wa Kisukari mwilini kama ilivyo katika mfumo wa tiba Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

  • Upload
    others

  • View
    0

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

1

BUNGE LA TANZANIA ______________

MAJADILIANO YA BUNGE _____________

MKUTANO WA NNE

Kikao cha Kumi na Sita – Tarehe 30 Juni, 2011

(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Mwenyekiti (Mhe. George B. Simbachawene) Alisoma Dua

MASWALI NA MAJIBU

MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Mwenyekiti!

MWENYEKITI: Hakuna Mwongozo wakati wa maswali. Tundelee, swali letu la kwanza leo litakwenda Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mheshimiwa Kidawa Hamid Saleh, atauliza swali hilo.

Na. 150

Dawa za Kutibu Ugonjwa wa Kisukari

MHE. FATMA A. MIKIDADI (K.n.y. MHE. KIDAWA HAMID SALEH aliuliza:-

Ugonjwa wa Kisukari umekuwa ni tatizo na unawapata watu wa rika zote; kumejitokeza wimbi kubwa la Waganga Asilia wanaojitangaza kuwa wanazo dawa zinazotibu ugonjwa huo:-

Je, Serikali inawaeleza nini wananchi juu ya dawa hizo?

NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kidawa Hamid Saleh, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mfumo wa tiba asili, kuna dawa nyingi zinazotumika kudhibiti ugonjwa wa Kisukari mwilini kama ilivyo katika mfumo wa tiba

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

2

ya kisasa. Wizara kupitia Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Taasisi ya Tiba Asili iliyo chini ya Chuo Kikuu cha Tiba ya Sayansi na Afya za Jamii Muhimbili hufanya utafiti wa kubaini aina mbalimbali za dawa za asili zinazosadikiwa kutibu magonjwa mbalimbali ukiwemo ugonjwa wa kisukari. Matokeo ya tafiti zilizofanyika hayajaonesha kuwa kuna dawa yoyote ya asili yenye uwezo wa kutibu ugonjwa wa kisukari isipokuwa kudhibiti ugonjwa huo kama ilivyo dawa za kisasa.

Hivyo, wananchi wanashauriwa kuwa na tabia ya kwenda hospitali kupimwa afya

zao ili kufahamu hali (status) ya afya zao. Kisukari ni ugonjwa hatari sana usipodhibitiwa, hivyo mara wanapohisi kuwa na dalili za kisukari wanashauriwa kwenda kupima kabla ya kuanza matibabu ya kisukari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waganga wa Tiba Asili wanashauriwa kuwasiliana na

Taasisi za Utafiti, ili kupata maelekezo yanayohusu ufanisi na usalama wa dawa wanazozitumia kudhibiti ugonjwa wa kisukari na dawa za magonjwa mengine. Dawa inapotangazwa kwenye vyombo vya habari, inatakiwa iwe imefanyiwa utafiti na kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika na ni salama kwa mtumiaji.

Kwa Waganga walio katika maeneo ya vijijini, wanashauriwa kuwasiliana na

Waratibu wa Tiba ya Asili, waliopo katika Ofisi za Waganga Wakuu wa Wilaya, katika kila Halmashauri. Waratibu hao wataweza kuwashauri namna ya kufanya mawasiliano na Taasisi za Utafiti kwa lengo la kufanyiwa utafiti dawa zao ili kuona kama zina uwezo wa kutibu na ni salama kwa mtumiaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kuchukua nafasi hii kusisitiza kuwa

Waganja wa Tiba Asili nchini kote watoe huduma hiyo kwa kuzingatia Sheria ya Tiba Mbadala, Na. 23 ya mwaka 2002 na Kanuni zake. Waganga wa Tiba Asili wawe na mawasiliano na Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, kupitia Waratibu waliopo ili kurahisisha uelewa wa mambo yanayohitaji ufafanuzi.

MHE. FATMA A. MIKIDADI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa

nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeishaona kwamba ugonjwa wa kisukari hauna

dawa, unaua, unakuja ghafla tu mwilini wewe mwenyewe huna habari na hivyo ulivyotushauri kwamba tuweze kupima ni vizuri zaidi.

Lakini sasa naona ni wakati mwafaka wa kupata takwimu za wagonjwa wa

kisukari ili watu wawe na tahadhari ya suala hili, wakiona watu wengi wanakufa au kuathirika, watu watakuwa na ule moyo wa kwenda kupima afya zao.

Je, Serikali inalionaje suala hilo?

NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII: Mheshimiwa

Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, naomba kujibu swali la

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

3

nyongeza la Mheshimiwa Fatma A. Mikidadi, Mbunge wa Viti Maalum, Lindi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli wakati tunapokuwa na matatizo ya kiafya na

tunapoona kwamba kuna matatizo basi ni vyema tukawa na takwimu ambazo ni sahihi. Mimi naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba sasa hivi ugonjwa wa kisukari unaonekana ni tatizo na sisi kama Wizara tumeishatoa maelekezo kwa Taasisi yetu ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), watufanyie utafiti na nafikiri baada ya muda si mrefu tutaweza kupata jibu na tunaweza tukaleta hizo takwimu kupitia maswali au kupitia kwenye Bajeti yetu ya mwaka ujao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Mbunge awe tu na subira, ila

naomba kutoa wito kwa Watanzania wale ambao wanaona matangazo kwenye notice board, magazeti au kwenye nini, kwamba kuna mganga anayetibu kisukari.

Mimi naomba kusema kwamba kisukari ni ugonjwa hatari, mgonjwa aendelee na

dawa zake ambazo amepewa na daktari, aendelee kupima afya yake ajue kwamba ugonjwa unakwendaje kwa sababu tukiuchezea utaua figo pamoja na kutusababishia magonjwa mengine tukapoteza uhai mapema.

MHE. DKT. MAUA ABEID DAFTARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, asante.

Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba niulize swali moja dogo la nyongeza.

Kwa kuwa tumesikia kwamba Babu wa kule Loliondo dawa yake inatibu sana

masuala ya sukari, lakini pia tunasikia kwamba Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii nayo ilikuwa inafanya tafiti juu ya dawa hii.

Je, anaweza kutueleza nini kwamba kweli dawa ile inatibu kisukari au ni nini?

(Makofi) NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII: Mheshimiwa

Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Maua Abeid Daftari, Mbunge wa Viti Maalum, kutoka Pemba kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Babu wa Loliondo amejitokeza na

kwa sababu watu wanachoka kutumia dawa kila siku, wanaochomwa sindano, wanaomeza vidonge wamejitokeza kwa wingi kwenda kwake. Hilo halijawa tatizo kwetu kwa sababu hatuwezi kumuingilia anafanya kazi yake kufuatana na itikadi na imani ya dini yake.

Ninachotaka kusema ni kwamba ile dawa ya Babu wa Loliondo ambaye anaishi

katika Kijiji cha Samunge, Taasisi yetu ya Utafiti wa Dawa za Binadamu imefanya utafiti pamoja na Mkemia Mkuu wa Serikali, kuangalia tu usalama wake kwanza kwa

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

4

watumiaji, tukaona kwamba ile dawa ni salama kwa kiwango anachotumia na jinsi anavyotayarisha, haina madhara kwenye mwili wa binadamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini sasa uwezo wa dawa hiyo kutibu haya maradhi

yote ambayo tunaambiwa kwamba yanatibika, ni lazima tufanye utafiti wa kisayansi na ndiyo sababu tumewaagiza NIMR wakishirikiana na Taasisi nyingine ambazo zinafanya utafiti wa maradhi hayo, hususani ugonjwa wa Kisukari, maradhi ya moyo pamoja na ugonjwa wa HIV, wafanye utafiti. Kwa hiyo, utafiti umeanza naomba tu tuvute subira tutaangalia kwamba matokeo yake yatakuwa ni nini, kama yatakuwa siyo mazuri tutayatangaza, kama yatakuwa ni mazuri tutayatangaza pia. Lakini kwa sasa hivi naomba kusema kwamba tiba ya ile dawa inategemeana na imani ya anayeitumia.

Na. 151

Ugonjwa wa Saratani

MHE. SILVESTRY F. KOKA (K.n.y. MHE. SHAFFIN A. SUMAR)

aliuliza:-

Watanzania wengi wameathirika na maradhi ya Saratani, ugonjwa unaoweza kutibika kama ukibainika mapema ukiwa katika hatua za mwanzo na kwa gharama nafuu.

Je, Serikali imejipanga vipi kuwasaidia wanannchi hasa walioko vijijini waweze

kupata huduma za msingi ikiwemo jinsi ya kutambua dalili za ugonjwa huo kabla haujafikia hatua za juu zaidi na kupata matibabu mapema.

NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,

naomba kujibu swali la Mheshimiwa Shaffin A. Sumar, Mbunge wa jimbo la Tabora Kaskazini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, huduma kwa wagonjwa wenye Saratani zinatolewa

katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dar es Salaam. Baada ya mwaka 2007 Sera Mpya ya Taifa ya Afya, Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya wa III na Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM), huduma za magonjwa yasiyoambukiza zinatakiwa kutolewa kuanzia ngazi ya kijiji hadi juu (Taifa).

Katika azma hiyo hiyo Serikali inaimarisha uchambuzi (Screening) wa Saratani

ya Matiti, Shingo ya Kizazi, Tezi ya Kibofu cha mkojo (prostate kwa wanaume) kwa kuweka mfumo wa uchambuzi wa kuwafikia wananchi wote kwenye ngazi zao. Kwa kuanzia, Serikali itashirikiana na mashirika yafuatayo; QAUGEN la Uingereza, MERCK la Marekani na UCC la Uswisi katika kutoa huduma ya uchambuzi na kinga.

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

5

Mpango huu utalenga katika kutoa chanjo ya Shingo ya Kizazi, kwa watoto wa shule wasichana, uchambuzi wa Saratani ya Matiti na Tezi ya Kibofu kwa watu wazima. Ili kufanikisha huduma hizi, ni muhimu kuongeza wataalam wa afya.

Mpango wa kusomesha wataalam hao unaendelea kwa kutumia Mpango Mkakati

wa Kuboresha Uendeshaji wa Watumishi wa Afya na Ustawi wa Jamii. (Makofi) MHE. SILVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa kuwa ugonjwa wa Saratani umeua takribani watu mlioni 9.9 kwa mwaka

2010 Duniani na kwa kuwa 75% ya watu hao wanatoka katika nchi zinazoendelea ikiwa ni pamoja na Tanzania, na kwa kuwa sasa katika Tanzania kumekuwa na mpango madhubuti kupitia Chama cha Madaktari Wanawake (MEWATA) kuchunguza na kubaini mapema Saratani ya Matiti kwa ajili ya akina mama.

Je, Serikali ina mpango gani madhubuti wa kuhakikisha kuwa wanaume nao

wanafanyiwa uchunguzi mapema kwa ajili ya Saratani ambayo kwa jina la kitaalam ni Prostate Cancer ambayo vilevile inashambulia na kudhuru viungo vya uzazi kwa upande wa wanaume? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu. Lakini naamini huyo siyo Shafii,

ni Mheshimiwa Koka eeh? MHE. SILVESTRY F. KOKA: Ndiyo! MWENYEKITI: Basi ukiuliza swali la msingi kwa niaba ya mtu, nadhani

aliuliza huyo huyo? MHE. SILVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, niliuliza kwa niaba

yake. MWENYEKITI: Basi ulitakiwa useme kwa niaba yake ili na mimi nijue.

Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Silvestry F. Koka, kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Shirika la Madaktari Wanawake

ambako na mimi ni mwanachama, wanafanya juhudi kubwa sana katika kufanya screening ya Saratani ambazo zinawagusa Wanawake (Saratani ya Matiti na Saratani ya Mlango wa Kizazi) pamoja na kutoa elimu.

Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, kwenye jibu langu la

msingi nimesema kwamba tutashirikiana na Taasisi tatu (3) moja kutoka Marekani, nyingine kutoka Uingereza na moja kutoka Uswisi, na moja wapo ya aina za cancers

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

6

ambazo tutazifanyia screening ni hiyo cancer ya prostate, ili tuweze kuigundua mapema, ni cancer inayotibika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu ambacho ningependa kusema tu ni kwamba

pamoja na juhudi hizo zote kama Wanaume hawatajitokeza na kujenga utamaduni wa kutaka ku-check afya zao hatutafanikiwa. Naomba kusema kwamba, Wanawake wanajitokeza, wanaulizia, wengi wanajipeleka wenyewe Ocean Road kwenda kufanyiwa screening kwa gharama zao za Shilingi 50,000/=. Lakini tunapokuwa sasa tunatoa uchunguzi wa kiafya kwa Wanaume inakuwa ni ngumu. Ninaomba basi tutakapojitayarisha Bunge hili liwe mstari wa mbele katika kwenda kufanyiwa hiyo screening kwa sababu tunataka muwe na afya njema. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa Naibu Waziri, wanaume

tujitokeze tuka-check afya zetu. (Makofi)

Na. 152

Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria MHE. AZZA H. HAMAD aliuliza:-

Awamu ya Pili ya Mradi wa Ziwa Victoria inalenga kupeleka maji Nzega Mkoani

Tabora:- (a) Je, kwa nini Serikali isipitishe Mradi huo Kata za Isaka Wilaya ya Kahama na

Tinde Wilaya ya Shinyanga? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka maji ya Ziwa Victoria Mhunze

(Makao Makuu ya Wilaya ya Kishapu) ambayo kwa hivi sasa yamefika Manispaa ya Shinyanga?

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji, naomba

kujibu swali la Mheshimiwa Azza H. Hamad, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, mwezi Juni, 2010 Serikali ilifanya upembuzi

yakinifu kwa ajili ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mradi wa Maji wa Ziwa Victroria, utakaohudumia miji midogo ya Nzega, Igunga pamoja na Manispaa ya Tabora.

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

7

Hadidu za rejea kwa ajili ya kumWajiri Mhandisi Mshauri atakayesanifu mradi. Zimeandaliwa na kuwasilishwa Benki ya Dunia ili kupata kibali cha kutangaza.

Vile vile, usanifu kwa ajili ya Mradi wa Maji utakaohudumia miji midogo ya

Kagongwa, Isaka na Tinde utafanyika katika mwaka wa fedha 2011/2012. Kazi hiyo itatekelezwa chini ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP). Mhandisi Mshauri ataajiriwa mwezi Oktoba, 2011 na usanifu utaanza Novemba, 2011.

(b)Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa

kupeleka maji ya Ziwa Victoria hadi Mhunze, Makao Makuu ya Wilaya ya Kishapu. Tayari usanifu umekamilika mwaka 2010 na tangazo la kuwataka Wakandarasi

kuleta maombi kwa ajili ya ujenzi imeandaliwa na kuwasilishwa Benki ya Dunia ili kupata kibali cha kutangaza. Mkandarasi ataajiriwa mwezi Januari, 2012 na ujenzi utaanza Machi, 2011.

MHE. AZZA H. HAMAD: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba kumwuliza maswali mawili ya nyongeza.

(i) Serikali inawaambia nini wananchi wa mji mdogo wa Tinde ambao una

takribani wakazi 5340 lakini mpaka sasa hivi unatumia kisima kimoja tu cha maji, na maji yale ukiyatazama yana rangi kama ya Chai ya Maziwa?

(ii) Serikali inasema nini kuhusu tamko la Mheshimiwa Rais, mara tatu tofauti

katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga la kuvipatia maji vijiji vyote ambavyo viko kilomita 15 kutoka katika Bomba Kuu la Maji ya Ziwa Victoria?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya

Mheshimiwa Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Azza H. Hamad, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa naomba nikuhakikishie kwamba mji wa

Tinde upo katika programu ambayo tunaiandaa ya awamu ya pili ya kupeleka maji Nzega, Manispaa ya Tabora pamoja na Igunga.

Katika sehemu ya pili ya swali lake, anasema kwamba Rais alitoa tamko. Rais

akiishasema maana yake ndiyo agizo na sisi tunatekeleza agizo la Rais kwamba vijiji vyote ambavyo viko ndani ya kilomita 12 kila upande, kuanzia kwenye hilo bomba kubwa vitapata huduma ya maji ya kutoka Ziwa Victoria.

MHE. STEPHEN J. MASELE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa

kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa Wananchi wa Shinyanga tayari

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

8

wameishakata rufaa EWURA kupinga upandaji wa bei ya maji kwa asilimia 85 kwa mkupuo mmoja.

Je, Serikali inatoa tamko gani na inawasaidiaje wananchi wa Shinyanga

kupunguza bei ya maji ambayo imepandishwa kwa mara moja kwa asilimia 85?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kuhusu suala la bei za maji. Katika sera yetu ya maji tunasema kwamba wananchi lazima wachangie gharama za kuendesha miradi hii ya maji, miradi hii ya maji ni gharama kubwa sana hasa zinatumia umeme mwingi sana na ni gharama kubwa. Mradi wa Kahama Shinyanga umetoa maji kutoka kijiji cha Hihelele kilomita 150, sasa mtu akikuletea maji kilomita 150 kuna gharama. Tulivyoanza na huu mradi bei ya maji ilikuwa ndogo sana walikuwa wanalipa kama shilingi 8/= kwa dumu moja. Katika vijiji vya Shinyanga sasa hivi maji wanauziwa dumu moja shilingi 20/=. Watu wa Mjini Shinyanga wameongezewa maji kufikia dumu shilingi 10/= na hivyo wanalalamika. Lakini nasema ukiangalia kwa kweli bei ya maji bado ni nzuri ni ya wastani na ukilinganisha na gharama ambayo inatumika, sawa wamekata rufaa lakini rufaa ile itaangaliwa watumiaji wa maji pamoja na gharama ambazo Serikali inatumia kupeleka maji Shinyanga. MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa kuwa upembuzi yakinifu pamoja na hatua ya kutangaza mkandarasi ya mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria katika Wilaya ya Kishapu na Maswa sasa umekamilika. Serikali itakubaliana na mimi kwamba sasa umefika wakati wa upembuzi yakinifu kutoka pale Maswa kwenda katika kijiji cha Mwabuswalu, Mwandoya, Lubiga na kisha Wilayani Meatu? NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba niseme kuwa suala lake ni jipya nitakuwa natoa majibu ya kubabaisha. Naomba tuwasiliane ili nimweleze hali halisi ya kuweza kupeleka maji katika Wilaya ya Meatu.

Na. 153

Mradi wa Maji wa Benki ya Dunia

MHE. MWIGULU L. N. MADELU (K.n.y. MHE. GOSBERT B. BLANDES) aliuliza:- Ni zaidi ya miaka minne sasa tangu Serikali iahidi kuwafikishia maji wananchi vijijini kupitia Mradi wa Benki ya Dunia, na mwaka 2009 Serikali ilitoa kauli Bungeni kuwa Wahandisi Washauri tayari wamepatikana na kwamba ujenzi ungeanza wakati wowote kuanzia mwaka 2010 lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika:-

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

9

Je, ni lini miradi hiyo ya maji itaanza na kukamilika ili wananchi wa vijiji vya Jimbo la Karagwe wapate maji safi na salama?

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Gosbert Begumusa Blandes, Mbunge wa Karagwe, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti tarehe 13 Julai, 2009, Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe ilisaini Mkataba na Mtaalam Mshauri (M/S Tanzania Association of Enviromental Engineers) kwa ajili ya kutafiti na kupima vyanzo vya maji; kuhamasisha jamii kuhusu usafi wa mazingira; kuhamasisha kuhusu uundaji na usajili wa vyombo vya watumiaji maji, usanifu wa miradi; na kuandaa zabuni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji. Mheshimiwa Mwenyekiti hadi kufikia mwezi Juni, 2010 Mtaalam Mshauri alikuwa ameandaa zabuni kwa ajili ya kumwajiri Mkandarasi wa kuchimba visima vya maji kwenye vijiji saba vya Nyaishozi, Kayungu, Chabuhora, Nyakakika, Chamuchuzi, Kigorogoro na Iteera, ambapo kati ya hivyo vijiji sita vya Nyaishozi, Kayungu, Chabuhora, Nyakakika, Chanika na Chamuchuzi vipo kwenye Jimbo la Karagwe. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika zabuni iliyotangazwa mwezi Agosti, 2010 ya kumwajiri Mkandarasi wa kuchimba visima, ni Kampuni moja tu iliyojitokeza kufanya kazi hiyo. Halmashauri haikupata kibali cha kuajiri Kampuni hiyo kwa sababu gharama zake zilikuwa kubwa kuliko gharama zinazokubalika, hivyo kusababisha zoezi kuanza upya. Zabuni ilitangazwa tena mwezi Desemba, 2010, tarehe 8 Machi, 2011, Halmashauri ilipata kibali cha kuajiri Mkandarasi wa kuchimba visima ambapo tarehe 14 Aprili, 2011 ilisaini Mkataba na Mkandarasi (M/S Ardhi Water Wells Ltd.) na kazi ya kuchimba visima itaanza baada ya mvua zinazoendelea kwisha. Matarajio ni kwamba uchimbaji wa visima, usanifu wa miradi na uandaaji wa zabuni za ujenzi wa miundombinu ya maji utakamilika ifikapo mwezi Septemba 2011, ikifuatiwa na kuanza kwa ujenzi wa miundombinu katika robo ya kwanza ya mwaka 2011/2012. MHE. MWIGULU L. N. MADELU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa ahadi hii imechukua muda mrefu sana takriban miaka 4 sasa na wananchi wamechoka kusubiri maji hayo na hawajui ni lini yatawafikia maji hayo. Je, Serikali inaweza kuwaeleza wananchi wa Jimbo la Karagwe la Mheshimiwa Blandes ni lini hasa maji hayo yataanza kutoka kwenye mabomba katika vijiji hivyo? Na kwa kuwa vijiji vya Nguvumali, Mgungia, Mlandala vya Tarafa ya Ndago, Ujungu, Mseko na Kizonzo vya Tarafa ya Shelui na Mingela pamoja na Nganguli Tarafa ya Kinampanda navyo viko kwenye mpango huu. Je, ni lini Serikali itafikisha maji

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

10

katika vijiji hivyo na vijiji vingine vyenye shida ili kuondoa adha hiyo ambayo ni tishio pamoja na mifugo ya wananchi wa Jimbo la Iramba Magharibi?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye jibu langu la msingi nimesema kwamba tayari Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe imeshamwajiri mkandarasi atakayechimba visima. Sasa baada ya kuchimba visima wakishapata maji tunatengeneza miundombinu ili wananchi waweze kupata maji. Siwezi kusema lini, ina maana tarehe. Kwa sababu hii ni process ni kazi ambayo inachukua muda ikimalizika watapata maji. Kwa hiyo, nina uhakika fedha zipo wananchi wa Karagwe watapata maji kama tulivyoeleza kwenye jibu la msingi.

Kuhusu Tarafa ya Shelui tunatekeleza mradi wa vijiji 10 katika Halmashauri zote katika nchi hii. Kila Halmashauri imefikia hatua fulani. Niwahakikishie tu kwamba vile vijiji 10 ambavyo tumewaahidi na ambavyo viko ndani ya programu, vijiji vyote vitapata maji. Aidha, katika awamu hii ya kwanza vile vijiji ambavyo havitapata maji tutaendelea katika awamu ya pili. MHE. DEOGRATIAS A. NTUKAMAZINA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwa kuwa tatizo la upatikanaji wa maji chini ya Mradi wa World Bank iliyoko Karagwe ni sawa sawa na lililoko Ngara ambako vijiji 13 kati ya 72 viliahidiwa kupata maji chini ya mradi wa World Bank. Jana nimepigiwa simu na wananchi wamepata wasiwasi wameambiwa kwamba kati ya vijiji 13 ni 2 tu vitapatiwa maji chini ya Mradi wa World Bank. Naomba Mheshimiwa Waziri atoe kauli ambayo wananchi wa Ngara wataisikia kuhusu vijiji hivyo vingine? Ahsante sana Mwenyekiti. NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli wameelekezwa kwamba waanze na vijiji viwili (2) na hii inatokana kwamba baada ya kufanya usanifu imeonekana kwamba gharama ya kuweza kujenga miundombinu ile itakuwa ni kubwa kuliko fedha ambazo zilikuwa zimepangwa. Lakini haina maana kwamba vijiji vile vingine havitapata huduma ya maji, ni ahadi ya Serikali kwamba vijiji vyote vitapata huduma ya maji. Tunaanza na hivyo (2) viwili tutaendelea na vingine. MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa wafadhili wengi wamekuwa wakisaidia katika kupunguza tatizo hilo la maji vijijini kwa mfano Mpango wa Maji Mango/Liuli na kwa muda mrefu mpango huu ulikuwa chini ya Wizara ya Maji. Lakini hawakuweza kuufanyia matengenezo kwa muda kiasi kwamba kuna tatizo kubwa sana la maji katika Kata ya Liuli kutokana na mpango huu wakati chanzo chake cha maji ni kizuri sana na kuna tanki kubwa zuri sana. Je, kwa kuwa Wizara ilikaa na Mpango huu kwa miaka 10 bila ya kuushughulikia na barua imeshaandikwa kwao bado haijaleta majibu, ni lini itachukua hatua ya kusaidia eneo hili? NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa suala hili kwa kweli kwangu ni jipya, naomba Mheshimiwa Stella Manyanya tuwasiliane ili tuweze kuona namna gani tutaweza kushughulikia na kutoa majibu yanayofaa kwa wananchi.

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

11

Na. 154

Fursa za Ajira kwa Vijana Nchini

MHE. CATHERINE V. MAGIGE aliuliza:- Kwa mujibu wa takwimu za Sensa hapa nchini zaidi ya nusu ya Watanzania wapo kwenye umri wa miaka 17 na kuendelea:-

(a) Je, Serikali inaliandaaje Taifa kwa kuweka fursa za ajira kwa vijana hao? (b) Je, Serikali inatambua kuwa tatizo la ajira hasa kwa vijana ni hatari sana

kwa usalama wa Taifa kama halitapatiwa uzito unaostahili?

NAIBU WAZIRI WA KAZI NA AJIRA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Kazi na Ajira, naomba kujibu

swali la Mheshimiwa Catherine Valentine Magige, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti ili kuwezesha fursa za ajira kwa vijana Serikali

imefanya yafuatayo:- (i) Bajeti ya mwaka 2011/2012 na hata Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano

(2011-2015/16) umeweka suala la kukuza ajira kama moja ya vipaumbele vitano vya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano. Aidha, vipaumbele vingine kama kilimo, nishati, viwanda na miundombinu vinatoa pia fursa kwa vijana kuajiriwa na kujiajiri.

(ii) Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya kisera na kisheria ili kuvutia

wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika sekta zenye uwezo wa kuongeza fursa za ajira kama vile ujenzi, kilimo na ufugaji, madini, biashara, uvuvi, mawasiliano na kadhalika.

(iii) Serikali pia inaendelea kuboresha sekta ya elimu na mafunzo ili kuwezesha

nguvu kazi inayoingia katika soko la ajira ambayo sehemu kubwa ni vijana kuwa na ujuzi unaotakikana katika soko la ajira.

(iv) Wizara yangu na Wizara zingine zinatekeleza programu mbalimbali za

kuwezesha kuongeza ajira hasa zile za kujiajiri na kuwa wajasiriamali ikiwemo Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Wanawake, Wajasiriamali, Mpango wa Kazi unaotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Serikali ya Denmark na programu nyingine za kisekta.

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

12

(v) Serikali imeanzisha Wakala wa Huduma za Ajira (Tanzania Employment Services Agency (TAESA) kwa lengo la kuwaunganisha Waajiri na watafuta kazi ndani na nje ya nchi.

(vi) Serikali imeanzisha Sekretariet ya Ajira chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti

ya Utumishi wa Umma ili kuratibu ajira katika sekta ya Umma. (vii) Pia Wizara yangu imeandaa Programu maalum ya kukuza ajira ambayo

itawezesha vijana kupata fursa za kuajiriwa na kujiajiri wao wenyewe. (b) Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua kabisa kuwa tatizo la ajira kwa

vijana ni hatari kwa Usalama wa Taifa kama halitapewa uzito unaostahili, ndio maana Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana. Aidha, naomba kumtaarifu Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Wadau wa Sekta Binafsi, Vyama vya Kiraia, Washirika wa Maendeleo na Jamii yote katika kukabiliana na changamoto hii ili amani na utulivu wa nchi yetu viendelee kudumishwa. (Makofi)

MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri, napenda kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Kwa kuwa kumekuwa na malalamiko mengi ya Watanzania kukosa ajira na

wageni wakipewa kipaumbele. Je, Serikali inatoa tamko gani kuhusiana na hili? (Makofi) Kwa kuwa jana hapa Bungeni tulitangaziwa kuwepo kwa Waziri wa Ujenzi wa

Uganda ambaye alikuja kusaini mkataba wa upanuzi wa bandari ya Tanga na ujenzi wa barabara. Je, Serikali inategemea kutengeneza ajira ngapi za vijana kuhusiana na mradi huo?

NAIBU WAZIRI WA KAZI NA AJIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza

nichukue nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Magige kwa kazi kubwa anayoifanya ya kutetea vijana ndani ya Bunge hili na nje hasa kule mkoani kwake Arusha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu maswali yake mawili nieleze tu kwamba

Serikali iko makini sana kuhakikisha kwamba zile kazi ambazo zinaweza kufanywa na Watanzania zisipewe watu kutoka nje.

Wizara yangu ikishirikiana na Wizara zingine za Kisekta kama Wizara ya

Biashara na Viwanda tunafanya kila aina ya mbinu na mikakati ya kuangalia kwamba wageni wanaoingia kupata vibali vya kazi ni wale tu ambao kazi zile haziwezi kufanywa na Watanzania. Pale ambapo kuna ukiukwaji wa hali hii basi tunafanya kaguzi na kuhakikisha kwamba Watanzania wanapata kazi zile ambazo zinaweza kufanyika. (Makofi)

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

13

Lakini nitoe wito kwamba Watanzania na sisi wenyewe tunapopewa kazi hizi basi tuweze kujiamini tuzifanye kwa ufanisi kwa maadili ili tuonekane kwamba kweli tunaweza kuzifanya kuliko wale wageni. Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu miradi ambayo itatekelezwa baada ya Waziri kutoka Uganda kuja, kwa vyovyote miradi ile ya miundombinu na bandari ya reli itaongeza ajira kwa wingi. (Makofi) Lakini ni mapema mno kwa sasa kusema ni ajira ngapi zitatokana na miradi hiyo. Lakini kwa vyovyote kwa sababu miradi kama hiyo ya uwekezaji ndiyo njia mojawapo ya kuongeza ajira kwa vijana na watu wengine ambao wanatafuta kazi kwa sababu kwa vyovyote bila nguvu kazi miradi hiyo haiwezi kufanyika. MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona. Kwa kuwa Serikali imekiri wazi kwamba suala la ajira kwa vijana ni tatizo katika Taifa letu. Na kwa kuwa Taifa bila vijana ni sawasawa na Jeshi bila silaha. Je, sasa Serikali inaweza kuwaeleza Watanzania vijana wetu wanafanya kazi sekta binafsi zaidi hasa ni ajira gani na ni kwa nini wanafanya hizo ajira tofauti na zile ambazo ni za ki-official zaidi Kiserikali? Ahsante sana. NAIBU WAZIRI WA KAZI NA AJIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, tafiti ambazo zimefanywa kazi ambazo zinafanywa na vijana. Kwanza niseme kwamba nguvukazi kubwa asilimia zaidi karibu 68 ya nguvukazi ni vijana. Kwa sababu kazi kubwa ambayo inavutia ajira katika nchi yetu ni kilimo, ingawaje sasa ile nguvukazi kwenye kilimo inazidi kupungua mwaka hadi mwaka kwa sababu ya kupanuka kwa sekta zingine binafsi za biashara, mawasiliano, ujenzi, madini na vile vile ujasiriamali na hasa kukua kwa miji yetu. Kwa hiyo vijana wengi wako kwenye kilimo, sasa hivi ni asilimia 40 tu wanaokwenda kwenye kilimo. Hii asilimia 60 inavyoonekana inakwenda sasa kwenye sekta binafsi ambayo sio kilimo na sekta isiyo rasmi. Kwa hiyo niseme tu kwamba ukiacha wale vijana wanaotoka Vyuo Vikuu ambao wanaopata ajira moja kwa moja kutokana na kupata taaluma mbalimbali, vijana walio wengi kweli wanaingia kwenye sekta isiyo rasmi na sekta binafsi ambayo inaajiri vijana kwa wingi. MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona. Kwa kuwa tatizo hili la ajira ni kubwa sana hasa kwa mkoa wetu wa Iringa, vijana wetu wengi huajiriwa kufanya kazi za ndani. Na kwa kuwa ajira hii haina mkataba kati ya mwajiri na mwajiriwa. Je, Serikali inawaambia nini vijana wanaofanya kazi za ndani kujua haki zao zikiwemo kima cha chini cha mshahara wao? (Makofi)

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

14

NAIBU WAZIRI WA KAZI NA AJIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ajira

isiyokuwa na mkataba sisi kama Serikali tunaipiga vita. Pale inapowezekana kwa kweli kazi zote zikiwemo za ndani zinatakiwa ziwe na mikataba ili wafanyakazi waelewe kwamba wana mikataba na wanayo masharti gani ya kazi wanazozifanya.

Ni kweli kwamba hasa wafanyakazi wa ndani kumekuwepo na hali hiyo ya

kutokuwa na mikataba, lakini kwa kadri iwezekanavyo kwa kweli hili linatakiwa lirekebishwe. Sasa Bodi za Mishahara kima cha chini tumeziunda na hivi karibuni zitaanza kukaa ikiwemo na Bodi ambayo inahusika na kima cha chini cha watumishi wa aina hii ambao wanafanya kazi za ndani. Mimi nina hakika baada ya hizi Bodi kuanza kufanya kazi tunaweza tukajua kwa undani na wataweza kuwa na mahali maalum pa kupeleka malalamiko yao na sisi kama Wizara husika tutakuwa tunafuatilia haki zao. MHE. FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi hii. Kwa kuwa vijana wengi wa Tanzania sio wavivu na wana vipaji vya kujiajiri wenyewe. Je, Serikali haioni umuhimu wa kukuza vipaji kwa vijana hawa?

NAIBU WAZIRI WA KAZI NA AJIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kwa kweli iko makini sana kutaka kusaidia vijana kukuza vipaji vyao, kitu ambacho ningetoa wito kwa kweli vijana kujitokeza katika fani mbalimbali wanazoweza kuzifanya ili Serikali iweze kuwasaidia na iko mifano mingi ambayo inaonesha kwamba Serikali imekuwa ikikuza vijana kwenye mambo ya sanaa, kwenye michezo na hata kwenye ujasiriamali kwa maana ya miradi ya kiuchumi ya kuendeleza vijana. (Makofi)

Kwa hiyo, mimi natoa wito kwa vijana wajitokeze wawe wabunifu. Kwa kweli

bila vijana kujitokeza Serikali haiwezi kuwasaidia, hatuwezi kujua wako wapi. Kwa hiyo, wakijitokeza mimi ninahakika Serikali kupitia Wizara yangu na

Wizara zingine za Kisekta zinaweza kuwasaidia sana vijana hao. (Makofi) MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa

fursa ya kuuliza swali moja ya nyongeza. Mwaka jana tumeshuhudia matokeo ya kidato cha nne ambapo wanafunzi wengi sana walifeli na mfumo wetu wa elimu hivi sasa hauna ngazi ambayo inaweza ikawabeba wanafunzi ambao wamefanya vibaya kidato cha nne kuingia katika vyuo vya ufundi na kadhalika na kumekuwa na mpango wa kujenga VETA kila Wilaya.

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

15

Serikali imeweka utaratibu gani wa kuhakikisha kwamba VETA zinajengwa ndani ya miaka mitano ili kuhakikisha kwamba Jeshi hili la vijana ambao wanamaliza kidato cha nne na hawawezi kuendelea na elimu wanakuwa absorbed kwenye vyuo vya ufundi na kuweza kusaidia uchumi wa nchi yetu?

NAIBU WAZIRI WA KAZI NA AJIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti,

nikubaliane na Mheshimiwa Zitto kwa asilimia mia kwamba kwa kweli ili ku-absorb hawa vijana ambao wanamaliza shule za sekondari ambao bila kupata nafasi za kuendelea na elimu ya juu waweze kuingia kwenye vyuo vya ufundi.

Kwa hiyo ni nia ya Serikali kama ambavyo tulikuwa tumeeleza na kupitia Wizara

ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuanzisha vyuo hivi vya VETA. Lakini sio vyuo vya VETA tu, Wizara yangu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na wenyewe wanavyo vyuo ambavyo vinaweza vikawaendeleza vijana wa ngazi hii wanaomaliza kidato cha nne.

Kwa hiyo Serikali katika programu zake kama ambavyo mtakuwa mmeona

kwenye bajeti na hata kwenye Mpango wetu wa Maendeleo ya Miaka Mitano ni kuendeleza nguvu kazi hii kwa kuanzisha vyuo vya ufundi kwa wingi iwezekanavyo. Mimi nataka nitoe wito kwa Waheshimiwa Wabunge, hata kwenye Majimbo yetu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tuanzishe vyuo vya ufundi na sio lazima viwe vya ngazi ya VETA hivi vinavyoanzishwa na Wizara. Lakini katika ngazi ya ufundi wa kawaida katika Majimbo yetu tutakuwa tumewasaidia sana hawa vijana.

MHE. MOHAMMED HABIB JUMA MNYAA: Mheshimiwa Mwenyekiti,

nashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza. Kwa kuwa tatizo la ajira, za vijana liko katika njia pana pamoja na watu wanatoka nchi za nje kuja kujipenyeza kuchukua kazi nchini Tanzania na kwa kuwa hivi karibuni nilipokuwa nachangia Bajeti ya Serikali nilionesha mpaka ushahidi ambao watu wanafanyakazi bila ya vibali na ambao Wizara yako Mheshimiwa Waziri ni moja ya Wizara inayohusika. Utafanya nini sasa watu hawa wanaojipenyeza wanaofanya kazi nchini kinyume cha Sheria na kuchukua nafasi za vijana wetu na wewe Wizara yako inaona pamoja na wahamiaji?

NAIBU WAZIRI WA KAZI NA AJIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati

tukiendeleza hizi za integration ambazo tunazo hatuwezi kuzuia watu kutoka nje na hasa East African Community kuingia Tanzania na kupata ajira. Lakini yatakuwa ni kwenye maeneo yale mahusisi ambayo tumekubaliana katika Mkataba wetu na hawataingia kwa kinyemela.

Sasa hawa ambao wanasema wanaingia kinyemela kama kuna mifano kama

walivyosema sisi tuko tayari kufuatilia. Ni kweli kwamba kumekuwepo na tatizo la Ofisi nyingi kushughulikia masuala haya ya wageni. Ofisi ya Uhamiaji, TIC na Wizara yetu.

Hivi karibuni tumeanzisha dialogue ambayo tutakuwa tunakutana kati ya pande

zote hizi mbili ikiwepo pamoja na Wizara ya Biashara kuangalia kwamba sehemu moja ya Serikali hairuhusu wafanyakazi kutoka nje kuingia bila kibali hasa Wizara yetu

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

16

ambayo ndiyo inatoa kibali cha ajira. Kwa sababu kuna vibali vya kuishi nchini na vibali vya kufanya kazi nchini. Vile vya kufanya kazi lazima Wizara ya Kazi na Ajira ihusike na tumeelewana vizuri. Mimi nadhani tutakuwa na ufuatiliaji mzuri sana kuanzia sasa. Lakini kama ni mfano hiyo aliyosema basi atupatie tufuatilie tuone tunachukua hatua gani. (Makofi)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, maswali ya leo yamekwisha

hayakuwa mengi sana kwa hiyo kipindi chetu cha maswali kimekwisha. Sasa ni matangazo.

Wageni waliopo, Tunao wanafunzi 78 wa Shule ya Sekondari Edmund Rice

Cinon Arusha msimame, karibuni sana. Ongezeni bidii katika masomo na sisi tunafanya mambo yetu hapa kwa ajili yenu. Matangazo ya kazi, Mheshimiwa Dr. Abdallah Omar Kigoda, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha na Uchumi anaomba niwatangazie, kwamba leo tarehe 30 Juni, 2011, mara baada ya kuahirisha Kikao cha Bunge Saa saba mchana kutakuwa na Kikao cha Kamati kwenye Ukumbi namba 219 ghorofa ya pili, Jengo la Utawala.

Mheshimiwa Magdalena Sakaya, Katibu wa Wabunge wa CUF anaomba

niwatangazie Wabunge wote wa CUF kuwa wanatakiwa kuhudhuria kikao kitakachofanyika leo saa saba mchana baada ya kuahirishwa shughuli za Bunge, Ukumbi namba 231 na Mheshimiwa Hussein Mzee, Katibu wa Kamati ya Waheshimiwa wote wa CCM anaomba niwatangazie Wajumbe wa Kamati ya Wabunge wote wa CCM kuwa kutakuwa na Kikao cha Kamati leo saa saba mchana baada ya Kikao cha Bunge katika Ukumbi wa Pius Msekwa. Hivyo Wabunge wote wa Kamati hiyo mnaombwa mhudhurie bila kukosa.

Mheshimiwa Pindi Chana, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya

Katiba, Sheria na Utawala, anaomba niwatangazie Wajumbe wa Kamati hiyo kuwa leo tarehe 30 Juni,2011 mara baada ya kuahirisha Kikao cha Bunge saa saba mchana kutakuwa na kikao cha Kamati hiyo katika Ukumbi Namba 227 ghorofa ya pili jengo la utawala.

Mheshimiwa Said Nkumba, Mwenyekiti wa Club ya Kulenga Shabaha, anaomba

niwatangazie Waheshimiwa Wabunge wanaotaka kwenye kwenye zoezi la kulenga shabaha JKT Makutupola tarehe 23/7/2011 wajiorodheshe ili waweze kwenda kushiriki katika mambo haya ya shabaha na Mheshimiwa Godfrey Zambi anaomba niwatangazie Wabunge wote wa Mikoa ya Rukwa, Katavi, Mbeya, Iringa, Njombe wakutane Ukumbi wa Msekwa Saa saba mchana. Kama kutakuwa na Kikao cha Kamati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) basi watakutana baada ya Mkutano huo.

Waheshimiwa Wabunge, tangazo letu la mwisho na hili ndilo natoa mimi

mwenyewe, mimi ndiyo Kapteni wa Timu ya Pool Table ya Bunge. Kwa hiyo, nawaomba sana wale wote Waheshimiwa Wabunge wa chama cha Pool Table, Tanzania (TAPA) kinategemea mashindano ya mchezo wa Pool Table kwa

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

17

Waheshimiwa Wabunge tarehe 23/7/2011, mashindano hayo yatafanyika hapa Mkoani Dodoma, hivyo Waheshimiwa Wabunge wanaocheza mchezo huu wanaombwa wajiorodheshe kwenye mlango mkuu wa kuingilia ukumbi huu.

Mimi ndiye mchezaji namba moja, kwa hiyo wengine njooni tutengeneze timu

nzuri ili tucheze na hawa viongozi wa Pool Table wa chama cha Pool Table Taifa. (Makofi)

Hayo ndiyo yalikuwa matangazo yetu. Katibu tuendelee na Order Paper.

(Makofi)

MWONGOZO WA MWENYEKITI

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mwongozo wa Mwenyekiti. MWENYEKITI: Mwongozo wa Mwenyekiti. MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba mwongozo wako

kwa mujibu wa Kanuni ya 68(7) kuhusu jambo ambalo limetokea Bungeni mapema jana na mapema leo kuhusiana na suala la Maswali kwa Waziri Mkuu.

Katika siku hizi za karibuni kumekuwepo na mambo ambayo yamezua utata na

utata huu unahitaji kauli ya Serikali, kauli ambayo kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu ingekuwa ni wasaa muafaka. (Makofi)

Mathalani kauli aliyonukuliwa Mheshimiwa Waziri Mkuu kwenye vyombo vya habari kuhusiana na mchakato wa Katiba kutoa maelekezo kwa Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa na baadaye kuondolewa kwa ule Muswada ambao ulikuwa uingie Bunge hili kuhusu Katiba.

Mfano mwingine ni kuhusu suala la mgao wa umeme ambao sasa limezua

tahariku na taarifa tulizonazo ni kwamba wananchi wametaka kuandama na Serikali inapaswa kutoa kauli. Lakini lingine ambalo limetolewa leo ambapo limetokana na kauli vilevile za Serikali magazetini za Wakuu wa Wilaya, wanafunzi wa vyuo warudishwe kwa kuangalia vyama vyao na baadaye ukatolewa Waraka wa Serikali wenye kuekeleza Chuo kufanya baadhi ya mambo na leo kuna taarifa kwamba wanafunzi wameanza kurudishwa kiitikadi. Sasa tulitarajia kwamba kutakuwa na fursa wanafunzi wa UDOM kungetolewa Kauli na Serikali kupitia Maswali kwa Waziri Mkuu.

Lakini kinyume kilivyotokea, jana Kanuni ya 150(1) na (4) zinazohusu kutengua

Kanuni zilikiukwa na kukatolewa tu tangazo kwamba leo hakutakuwa na na Maswali kwa Waziri Mkuu bila Utaratibu wa hoja ya kutengua Kanuni kutolewa. Kwa mujibu vilevile wa Kanuni ya Bunge ya 38 ambayo ndiyo inaongoza masuala yanayohusiana na maswali yanayohusiana na Maswali kwa Waziri Mkuu, imeeleza ni mazingira gani ambayo kipindi hiki cha maswali kwa Waziri Mkuu kinaweza kisiwepo.

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

18

Kanuni hii ya 38 imesema bayana kwamba Waziri Mkuu anapokuwa hayupo ndiyo sababu ya kutokuwepo na Maswali kwa Waziri Mkuu na tunaelewa kwamba Waziri Mkuu leo yupo na sababu ambayo ilifanya kusiwe na Maswali kwa Waziri Mkuu wiki iliyopita ni kwa sababu siku ile Waziri Mkuu alikuwa anasoma Hotuba yake. Kwa hiyo, ikabidi kipindi kile kiondolewe ili kumpa fursa ya kujiandaa. Leo Waziri Mkuu hasomi hotuba, atafanya majumuisho kesho. Kwa hiyo, leo kuna fursa ya Waziri Mkuu kuweza kutumia hiyo fursa ya maswali kutoa kauli za msingi za kuhusiana na taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie tu, Kanuni ya 150(4) inayohusu kutengua

Kanuni inasema bayana kwamba Kanuni huwa zinatenguliwa kwa dhumuni maalum, kwa sababu maalum inayoelezwa wakati wa kutengeliwa kwa Kanuni husika.

Imani yangu ni kwamba Kanuni ilipotenguliwa wiki iliyopita sababu zake

zilikuwa za wakati ule na zili-save wakati ambazo hazihusiani na sasa. Kwa hiyo, naomba mwongozo wako kwa kutumia Kanuni ya 30(6) ambayo inatoa mwanya kwako kama meza pamoja na shughuli kutokuwepo kwenye orodha ya Serikali, shughuli kuweza kuendelewa kujadiliwa ili Kanuni hiyo itumike sasa kwa Waziri Mkuu aweze kupata fursa ya kuulizwa maswali sasa hivi kuhusu masuala yanayoikabili taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba mwongozo wako. (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge, ni kweli kwamba tulitengua Kanuni ili

kumpa fursa Mheshimiwa Waziri Mkuu aweze kujiandaa vizuri wakati anaposhughulika na Bajeti yake na kwa madhumuni yale yale jana tuliona sababu zile zile bado zipo. Mheshimiwa Waziri Mkuu anahitaji kusikiliza sana hoja za Waheshimiwa Wabunge ili ajiandaye kuweza kutoa majibu mazuri na ya uhakika ya Serikali. Sasa inawezekana pengine inaonekana si busara kwa mtu mwingine lakini Bunge lina utaratibu mwingi sana wa namna ya Wabunge kutoa hoja zao.

Zipo Kanuni hapa ambazo zinaruhusu Mbunge kuja na hoja maalum ya dharura

ambapo ungeweza kufanya hivyo kupitia mlango huo wa kutoa hoja. Kusema kwamba kutokuwepo kwa Maswali kwa Waziri Mkuu hakuna namna yoyote ile ya Bunge kuwasiliana na Serikali hususani yeye mwenyewe Waziri Mkuu nadhani si kweli sana.

Nikuombe tu, kama unadhani kuna jambo mahususi la dharura linalohitaji majibu

ya haraka ya Serikali kwa maana ya Waziri Mkuu unaweza ukatumia njia nyingine na hili kwa kuwa limepita sasa mjadala wake utakuwa ni kama unatupotezea fursa ya kufanya mambo mengine ambayo yanafuata siku ya leo. Ninashauri unayo fursa ya kufanya hivyo kwa kutumia milango mingine ya kutoa hoja Bungeni. Kwa hiyo, hili kwa kuwa limeshapita lisituchukulie muda mwingi. (Makofi)

Mwongozo wangu ni kwamba tumia nafasi hiyo na hii imeshapita ili uweze

kuweka hoja yako kama unadhani bado unahitaji kufanya hivyo. Huo ndiyo mwongozo wangu.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mwongozo wa Mwenyekiti.

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

19

MWENYEKITI: Kiti kikisha tolea uamuzi jambo huwezi uka-rewind tena

nitaamua nini. Niliyeamua ni mimi na ndiye niko hapa sasa maana yake nipinge uamuzi wangu. Siwezi kufanya hivyo lakini hata hivyo kama hujaridhika na uamuzi wangu unao mlango mwingine tena wa kuona kwamba unaweza ukanipinga mimi au kiti kwamba nimekosea kutoa uamuzi wangu na hivyo unadhani nilipaswa kufanya nini kwa njia nyingine sio ya kuniomba mimi tena mwongozo juu ya mwongozo. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tuendelee. Katibu tuendelee na Order Paper. (Makofi) HOJA ZA SERIKALI Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2011/12012 - Ofisi ya Waziri

Mkuu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

(Majadiliano yanaendelea)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na Wachangiaji, kwenye

Hoja ya Mheshimiwa Waziri Mkuu na mchangiaji wetu wa kwanza ni Mheshimiwa Profesa David Homeli Mwakyusa, Mbunge wa Rungwe Magharibi.

MHE. DAVID H. MWAKYUSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa

kunipa nafasi hii ya kwanza kuchangia leo asubuhi Hoja ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Nianze kwa kusema kwamba mwezi uliopita Wilaya ya Rungwe ilimpoteza Mwenyekiti wake wa Halmashauri ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa John Mwankenja.

Napenda kutumia fursa hii kutoa rambirambi zangu kwa mjane na familia lakini

pamoja na wananchi wote wa Wilaya ya Rungwe kwa kupotelewa na mtu wa maana sana kwetu, nawapa pole nyingi sana.

Vilevile napenda kuwashukuru wananchi wangu wa Jimbo la Rungwe Magharibi

kwa kunirudisha katika Ukumbi huu kwa mara ya tatu. Safari hii waliona hakuna haja ya kuwa na mpinzani waliniambia unatosha, umejaa kwa hiyo nenda katutumikie. Kwa hiyo, nipo hapa kwa niaba yao na ninawashukuru na kuwaahidi kwamba tutashirikiana kama ilivyokuwa huko nyuma sasa hivi twende haraka zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kumpongeza Waziri Mkuu, nilimsikiliza

alipokuwa anatoa Hotuba yake na nimeisoma kwa makini, niseme tu kwamba, nimeshiba na ninaiunga mkono kwa asilimia mia moja.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wananchi wangu wa Rungwe Magharibi, wana

changamoto nyingi sana za maendeleo, ambazo wamenituma niziwasilishe kwa Serikali, lakini leo nitajikita katika mambo ya Kitaifa na mambo yanayohusu Rungwe nitayaongea kwenye Wizara kama nitapewa nafasi wakati watakapoleta bajeti zao.

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

20

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka nijadili kidogo kuhusu huu mgomo wa

wanafunzi wetu hapo Chuo Kikuu cha Dodoma unaoendelea. Tupo humu ndani, vijana wetu zaidi ya 400 wako majumbani hawapo madarasani. Tumeelezwa sababu kwamba, walikuwa na madai wakagoma, wakaandamana na kwa hiyo wakatimuliwa. Tukio hili tumelijadili sana hapa ndani, lakini hata nje ya Bunge, kwenye mabasi, kwenye taksii, kwa vinyozi, yote hii ikiwa ni ishara kwamba, imewagusa Watanzania wote kwa ujumla wake. Kwa jinsi watu wanavyojadili, imechukua sura ya lawama, watu wanawalaumu wanafunzi, wengine wanaulaumu Uongozi wa Chuo, wengine Serikali, lakini vilevile tulimwona Makamu Mkuu wa Chuo, akisema kwamba, wanasiasa wengine waliingia pale Chuoni na kutia sumu na walichangia hali tunayoiona hivi sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Wananchi wananyosheana vidole na kutafuta

mchawi, tukumbuke kwamba, vijana wetu hawako madarasani, wengine wapo hapa mjini walikosa hata nauli ya kurudi nyumbani. Ninasema kwamba, malumbano ambayo yanaendelea hivi sasa kuhusu hili suala, hayana tija kama hutoi pendekezo lolote. Vijana wetu wanaendelea kusota nyumbani, wanaendelea kukosa masomo, taaluma zao binafsi zinaathirika, lakini vilevile taaluma ya Taifa inakuwa hafifu kwa vizazi vijavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mipango madhubuti ya kupata academic

intellectual self sufficiency, kwa mtindo huu hatutafika mbali. Ninadiriki kusema kwamba, katika pande zote hizi zinazovutana katika mzozo huu, hakuna aliyeshinda; siyo Wanafunzi, Uongozi wala Serikali. Wote tumewahi kupita kwenye Vyuo Vikuu kwamba, kunapotokea matatizo kama haya wengine wanaingia kwa mkumbo, wengine mob psychology inawafikisha hapo, lakini tujue kwamba, kuna vitisho vingi sana. Kwa hiyo, asilimia kubwa ya vijana ambao wanakosa masomo sasa hivi kusema kweli imekuwa siyo kwa ridhaa yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, rai yangu ni kwamba, Serikali ijitahidi kupata suluhu

ya suala hili mapema iwezekanavyo, tuone vijana wetu wanarudi madarasani. Ninamfahamu Profesa Kikula, ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo, nimefanya naye kazi; ni mtu msikivu, nina imani yeye pamoja na Baraza lake, wanaweza wakatupa suluhu. Tunachopenda ni kwamba, watoto wetu waendelee na masomo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini baada ya wanafunzi hawa kurudi, ningependa

kuona migomo hii inakoma kabisa Vyuoni. Ipo haja ya kutafuta visababisho, tujue ni nini kinatufikisha hapo. Katika tiba tunasema a correct diagnosis leads to a correct treatment and cure; sasa matatizo kama haya yametokea leo, yatatokea na kesho na tunatumia mtindo wa zimamoto, tuna-interrupt masomo ya vijana na sidhani kama tutapata vijana ambao ni mahiri huko mbele ya safari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwanzoni mwa miaka ya 2000 kulikuwa na migomo

mingi katika Sekta ya Afya, Watumishi wa Sekta ya Afya walikuwa wanagoma sana, kilele ilikuwa mwezi Novemba mwaka 2005 ambapo watumishi across the board kuanzia Madaktari, Wauguzi, wa X-Ray 253 walifukuzwa kazi. Serikali ya Awamu ya

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

21

Nne ilipoingia mwezi Januari 2006, iliwarejesha kazini, lakini tukaunda Tume chini ya Uenyekitiki wa Dokta Msengi, ambaye sasa hivi ni DC wa Tanga ili wajaribu kubaini kiini cha matatizo na watoe mapendekezo. Walifanya kazi nzuri wakatoa Ripoti, ikafanyiwa kazi na mpaka sasa sijasikia kama kumekuwa na migomo katika Sekta ya Afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nitoe pongezi kwa Dokta Msengi, lakini

vilevile kwa Wafanyakazi wote, kwa uvumilivu wao; sidhani kama matatizo yamekwisha, lakini ina maana kwamba, katika uvumilivu wao wana namna ya kuyapeleka matatizo yakapata suluhu ile inayowezekana kwa wakati ule na migomo imeondoka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeambiwa kwamba, UDOM inaongoza kwa migomo

katika Vyuo vyetu vya Elimu. Tunavyo Vyuo zaidi ya kumi, SUA wanagoma, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, MUHAS na Vyuo vyote kunakuwa na migomo, lakini sijawahi kusikia kwamba, Chuo Kikuu cha Mzumbe kumekuwa na mgomo; tujiulize kulikoni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda ni-declare interest; wakati Chuo kinaanza

nilikuwa na uhusiano wa karibu na Chuo hiki na tulipokuwa pale tulibaini kwamba, kuna makundi matatu ya jamii iliyopo pale Mzumbe; kulikuwa na Wanataaluma, Wafanyakazi Waendeshaji na Wanafunzi. Tulifanya uamuzi wa makusudi kwamba, Viongozi wakutane na haya makundi regularly, kama ni kila mwezi au kila baada ya miezi miwili na tukawa tunazungumza masuala yanayohusu section ile na tuliweza kuepusha matatizo mengi sana. Tusingojee wakati wa matatizo ndiyo tuanze kutafuta zimamoto, tuelewe kwamba, taarifa zikiwafikia wanafunzi mapema na zikiwa sahihi, tunaweza tukaepusha mambo mengi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi ya Dean of Students ni muhimu sana, anatikwa

awe mtu muelewa, mwenye huruma, awe na open door policy, vijana wawe na mahali pa kwenda kupumulia. Tuepuke ile ya kusema kwamba, inafika taarifa halafu inawafikia wanafunzi kwamba eti wamesema hivi, ninadhani mimi kama Kiongozi, nina wajibu wa kuweza kuwaambia, kama ni Kiongozi usiogope watu unaowaongoza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niishie na mapendekezo kidogo kwamba,

kwanza, Tume iundwe, ijaribu kubaini matatizo na taarifa sahihi ziwe zinawafikia na kama kuna mkono wa siasa, tuone kwamba ndugu zangu hapa ninafananisha na mimba ya utotoni; wale ni watoto tusiwape sumu ya siasa wakati kama huu. Kweli ni mtaji lakini acha wakue kidogo, ndiyo hao hao tutawahitaji, tukiharibu taaluma yao sasa hivi hata tukishika madaraka ndiyo hao tutakaowahitaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimefarijika kuona kwamba, elimu ni mojawapo ya

vipaumbele vitano katika Mpango mzima wa Maendeleo ya Miaka Mitano. Huu ni uamuzi sahihi, tukizingatia kwamba, Mataifa yote yaliyoendelea kilichowafikisha hapo ni elimu. Waliwekeza katika elimu na sasa wanavuna maendeleo.

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

22

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuanzia ukurasa wa 41 mpaka 44 wa Hotuba ya Waziri Mkuu, zimeonesha mafanikio katika Sekta ya Elimu ni muhtasari tu, kuna mengi sana ambayo yamefanyika. Katika Jimbo langu tulikuwa na shule mbili tu za sekondari za Serikali, sasa hivi Wananchi wameweza kujenga shule 27, changamoto ni uhaba wa Walimu. Hili limezungumzwa sana kwenye maswali, katika michango, lakini sote tutambue juhudi za Serikali katika ku-address issue hii kutafuta jawabu la upungufu wa Walimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mikakati ambayo tumeiona zaidi imelenga kuzalisha

Walimu wengi, tulikuwa na UPE, Voda Fasta, lakini hoja ninayotaka kuijenga ni kwamba, sasa ni wakati wa kubuni mikakati ya kujihakikishia Walimu bora. Imani ya Wananchi ni kwamba, watu wanaojiunga na Vyuo vya Ualimu ni wale ambao wameshindwa kujiunga katika taaluma zingine. Mara ngapi tunasikia kwamba, mtoto wa fulani hajapata kazi, halafu mtu anauliza hata ualimu!

Mheshimiwa Mwenyekiti, busara inaelekeza kwamba, kwa anayestahili kuitwa

mWalimu yeye mwenyewe awe muelewa, awe mtu anayefundishika na pia mtu ambaye akili zake zinachemka. Kwa hiyo, tubuni mikakati ya kuwanasa hawa vijana ambao wameonesha uwezo wa kitaaluma, washawishiwe kujiunga na vyuo vya ualimu, tupate ile cream.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hili wazo litakubalika siyo lazima iwe leo, lakini

huko mbele ya safari tunakokwenda ni lazima mageuzi makubwa yafanyike katika sera zetu za kufundishia, mazingira yabadilishwe kuanzia tunapozalisha Walimu. Vilevile tuangalie maslahi; kuwe na vivutio na vijana wapende kuwa Walimu kwa sababu tumeweka vivutio, tukiwanasa hawa ioneshe kwamba, kuna upendeleo ulio wa wazi, iwe taaluma ambayo ni competitive.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huwa ninaona aibu kupigiwa kengele ya pili, lakini

nilikuwa na mengi ya kusema, ninaomba niishie hapa kwa kukushukuru na kumshukuru Waziri Mkuu na kusema kwamba, ninaunga mkono hoja hii. Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Profesa. Ninajua Profesa hawezi kukubali

kupigiwa kengele. Mchangiaji wetu anayefuata ni Mheshimiwa Raya Ibrahim, atafuatiwa na Mheshimiwa Conchesta Rwamlaza na baadaye Mheshimiwa Naomi Mwakyoma Kaihula, ajiandaye.

MHE. RAYA IBRAHIM KHAMIS: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru

kwa kunipa nafasi ya kuchangia Hotuba ya Waziri Mkuu. Kwanza kabisa, ninapenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, ambaye amenijalia uhai na afya mpaka leo hii nipo hapa ninasimama na kutaka kuongea niliyoyakusudia. Pili, ninapenda kuwashukuru Wazazi wangu na tatu, ninapenda kukishukuru Chama changu na Viongozi wote wa Chama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiingia katika Hotuba yetu ya Waziri Mkuu,

ningependa kusema kwamba, Waziri Mkuu ni Waziri ambaye ameteuliwa na Rais, na

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

23

Rais ambaye amechaguliwa na Wananchi wa Tanzania, miongoni mwa Watanzania ikiwemo Zanzibar na Tanganyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna msemo wenzetu wanasema; usijaji kitabu kwa

cover yake. Ningependa niseme kitabu hiki ambacho ni Hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kimeongelea masuala ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo ni Serikali ya Muungano wa Tanzania. Kwa haraka haraka utasema kina mambo ambayo na Muungano umehusishwa, lakini kwa bahati mbaya kwa kuangalia tu, hazizidi page mbili ambapo masuala ya Muungano ama masuala ya Zanzibar yamezungumziwa. Kwa hiyo, tunaweza kusema kwamba, some how Serikali inatusahau Wazanzibari, inatutenga na siyo kusudio ambalo tumeingia nalo katika Muungano wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Muungano umeingiwa ukiwa na mambo mengi, lakini

tunaona kwamba, Muungano humu ndani ni wa nchi mbili; ulikuwa wa Nchi ya Zanzibar na Tanganyika, lakini tunaweza kusema kwamba, tumemezwa. Ukiona hiki kitabu ndiyo maana tunasema usijaji kitabu kwa cover yake, kinaonesha Muungano kwa Zanzibar, unaweza ukahisi kwamba ndani ya hiki kitabu utakuta angalau robo tatu kimezungumzia Zanzbar, kimezungumzia kitu gani ambacho Wazanzibari wanakitarajia kutoka katika Hotuba ya Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bila kupoteza muda, ningependa niende katika masuala

ya Muungano. Suala la kwanza tunaweza kusema kwamba, ni mfumo wa Serikali mbili ambao ndiyo tupo nao; Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Muungano. Tunaona kwamba, suala zima la Zanzibar lipo chini ya SMZ, kwa hiyo, mambo ya Zanzibar ni ya Zanzibar yanashughulikiwa chini ya SMZ. Mfano mzuri ni suala zima la mafuta; mafuta ni ya Zanzibar na kutaka yaendelee kuwa ya Zanzibar chini ya SMZ. Tukirudi upande wa pili, tunasema kwamba, kuna Serikali ya Muungano, ambapo ndani ya Serikali ya Muungano Wazanzibari tunahusika, tunatakiwa tushirikishwe tuwemo tujue what is going on. Tunakuja kuangalia kwamba katika suala zima la Sekta za Muungano; Wizara zake zote Makao Makuu yapo Tanganyika, yaani Tanzania Bara. Kwa hiyo, kwa Zanzibar tunaweza kusema hatujapewa nafasi hiyo ya kupewa angalau Sekta mbili za Muungano ziwe na Makao Makuu Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninasema huu mwendo ambao tunakwenda nao siyo

Muungano ambao Wazanzibari tunautaka. Ukija katika suala la ajira katika Muungano huo, Sekta za Muungano, mfano mzuri ni Jeshi na Polisi, katika ajira tunatakiwa kuwe na uwiano katika kutoa waajiriwa au watumishi katika sekta hizo; lakini kwa bahati mbaya ninaweza kusema, list yote ya IGPs waliopo, hakuna ambaye ni miongoni mwa Wazanzibari waliowahi kukamata nafasi ya kuwa IGP. Tunasikitika kwa hilo na siyo tegemeo letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikienda katika point nyingine, ambayo ni Muungano;

unakuta Mashirika ya Nchi za Maendeleo, mfano, Norway, Canada na Sweden, ambazo zinaitwa SIDA, JICA na zingine zina majina mengine; kwa kuangalia haraka haraka kuna post ambazo zinakuja Tanzania, Tanzania ambayo ina Tanganyika na Zanzibar, lakini

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

24

jambo la kusikitisha ni kwamba; tunakuta before ilikuwa zikija post 20, tano ziende Zanzibar na 15 zije upande wa pili wa Muungano; lakini tukiangalia katika Ripoti za juzi juzi na maelezo ambayo tunayaona, nafasi hizi zikija mfano zimekuja nafasi 30, basi ukila na kipofu ujue kula naye usile ukajisahau ukamkamata mkono; kwa sababu ndani ya post 30 unakuta Mzanzibari mmoja; huu ni Muungano wa nchi mbili ama Muungano wa Wilaya na Mkoa Kwa hiyo, hilo nalo tunataka lirekebishwe na litazamwe kwa macho yetu, zikiwepo post Wazanzibari nao wahusishwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda niingie katika suala zima la Bunge. Tuna

Makao Makuu ya Bunge ambayo ni Dodoma, kuna Ofisi za Bunge Dar es Salaam na tunazo Ofisi za Bunge Zanzibar. Ofisi za Bunge Dar es Salaam unapokwenda ukiwa na shida yoyote, unakuta watendaji na shida yako inatekelezeka. Ofisi ya Bunge ya Zanzibar, unakwenda unawakuta watendaji lakini siyo kama waliopo Ofisi za Bunge za Dar es Salaam. Vilevile matumizi ya Ofisi ambayo ipo Dar es Salaam na Zanzibar, tunaona kwamba, kabla ya kuja Bungeni huwa tuna wiki mbili za kukutana kwa ajili ya Kamati, lakini tangu Ofisi ya Zanzibar imejengwa, hakuna Kamati ambayo imeelekezwa ikutane Zanzibar na majengo ya Ofisi ya Zanzibar yatumike ipasavyo. Hatimaye, utakuta tunatumia pesa kukodisha kumbi kwa ajili ya Wabunge wa Kamati fulani wakae wajadiliane katika kumbi hizo na kusahau kwamba, kuna Ofisi Zanzibar ambazo hazitumiki na hakuna Kamati inayokaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaitaka Serikali, siyo kwamba tunaomba, kwa sababu ofisi ipo inatakiwa ifanyiwe kazi, majengo yatumike kama ipasavyo na ikiwezekana safari ijayo tunategemea tuone Kamati zinakaa Zanzibar kama zinavyokaa Dar es Salaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda niongelee suala zima la Jumuiya ya Afrika

Mashariki. Muungano tunaupenda, lakini wenzetu mnatutupa mkono; hakuna Mwakilishi ambaye anaiwakilisha Zanzibar katika Afrika Mashariki, tunaitaka Serikali iliangalie suala hili na kutoa Mwakilishi wa Afrika Mashariki kutoka Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkataba wa Muungano ulipoingiwa, ulikuwa na

mambo 11, kila siku zinapokwenda mambo ya Muungano yanaongezeka na hatujui yanatokea wapi, kimizengwe mizengwe tu mambo yanaongezeka. Ninaomba nikumbushe ya kwamba, katika Bunge hili Tukufu, tarehe 10 Juni mwaka 1965, kulipitishwa Certificate of Urgency ndani ya Bunge ambapo ndani ya Order haikuwepo, ikaingiza suala la fedha kuwa la Muungano wakati hili suala zima la fedha halikuwa suala la Muungano ndani ya Bunge. SMZ kama Serikali ya Zanzibar, haikushirikishwa, lilipitishwa hili jambo na ninanukuu yaliyosemwa. Kwa kuwa haikuwa katika Order Paper. Nilichosema ni kwamba, ninataka nizungumze jambo lisilo katika Order Paper kwa sababu ni jambo la siri. Jambo hilo ambalo wamelifanya siri ni Muungano, ambao haukuwa wa siri. Wazanzibari hawakutegemea yaingizwe mambo ndani ya Muungano kisirisiri kama ambavyo wamekusudia wao. Wao walikusudia mambo yatakayoingizwa watashirikishwa na mfano wa hayo ni mengine mengi ambayo yapo yameingizwa, mfano wake ndiyo huo nimeutoa wa suala zima la fedha.

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

25

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nichangie katika suala la Loan Board kwa wanafunzi kutoka Zanzibar. Loan Board inatoa mikopo kwa wanafunzi hawa, wanatakiwa walipe mikopo ndani ya miaka kumi. Mwanafunzi ambaye amemaliza Chuo Kikuu ameajiriwa Zanzibar na mwanafunzi ambaye amemaliza Chuo Kikuu ameajiriwa upande wa pili wa Muungano, tunaona kwamba, kuna tofauti kubwa ya kiwango cha mishahara ambacho anakipata. Ninapendekeza kwamba, muda wa kulipa mikopo wanafunzi wa kutoka Zanzibar uongezwe, kwa sababu ukiangalia kiwango ambacho kinakatwa ni sawa na kiwango ambacho wanakatwa waliopo Tanzania Bara. Hali hii inasababisha mshahara wake anaoupata unakuwa kidogo sana, kiasi ambacho hakiwezi kumtosheleza katika mahitaji yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine, ningependa nichangie suala zima la ulinzi na

Jeshi la Taifa. Kwa upande wa Zanzibar, kuna Kambi ya Jeshi ipo Nyuki, karibu na Shule ya SOS pale Zanzibar. Katika Kambi ya Matrector iliyopo Wawi, Pemba, kuna Meccy ambayo watu wa Jeshi wanaitumia kufanya starehe; wanapiga miziki mpaka muda wanaoutaka wao; kitu ambacho ni kinyume na tamaduni za Kizanzibari. Eneo hilo lipo katikati ya maeneo ya watu, tunachoomba sisi na tunachokita ni kwamba, hayo maeneo yasitumike vibaya.

Kama wanataka kuweka vilabu kwa ajili ya vileo, sisi tunasema kwamba,

wanatubugudhi hasa katika eneo la SOS. Kuna shule pale kuna wanafunzi ambao wana hosteli, pale ambapo wanaishi inawa-disturb sana katika masomo yao, yaani kwa kifupi inawa-discourage katika kuendeleza shughuli zao za kimasomo.

Kwa haraka haraka nikimbizie muda, ningependa niingie upande wa pili wa

Muungano. Ninaanza na Law School, tunaona kwamba, Serikali yetu ya Muungano ina tatizo na ina uhaba wa Majaji ama Wanasheria; hakuna support yoyote ambayo Serikali inaitoa kwa wanafunzi hawa katika kuwawezesha waende Law School ili wawe Wanasheria wazuri, ambao watasimama ndani ya nchi yao na kupunguza tatizo hilo la uhaba. Tunaitaka Serikali iwafikirie na iwawezeshe katika masomo yao ya Law School.

Upande wa pili, ninapenda kumnukuu Baba wa Taifa, alisema; “Tunataka tuwe na Vyama vya Ukombozi na si Vyama vya Uongozi kama ambavyo vyama vyetu vipo.” Ninasema hivi kwa kuwa ndani ya nchi yetu ya Tanzania, Katiba ambayo imetengenezwa na imeundwa na watu ambao kwa kifupi ni wasomi, watu ambao wanaona mbali, ndani ya Katiba kumewekwa neno maandamano. Maandamano ni haki ya Mtanzania, lakini cha kushangaza, ninaomba ninukuu kabla sijasema ninachotaka kusema; Kitabu cha Baba wa Taifa, Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania kinasema; ninanukuu: “Viongozi wetu hivi sasa wanaogopa kutumia nguvu za hoja ili kufikia maamuzi muhimu. Kwa sasa wanatumia hila zaidi kuliko hoja. Vitisho kwao ni mbinu rahisi zaidi kuliko adha ya kutumia akili kwa kupata hoja safi ya kumjibu Mpinzani katika mjadala. Viongozi hawa wakipewa nafasi watatumia hoja ya nguvu tu, hawatakuwa na haja ya kutumia akili. Kichini chini, baadhi yao tayari wameanza kutumia hoja za vitisho. Kama tukiacha utamaduni wa woga ukazagaa, tutakuwa tunakaribisha udikteta.” (Makofi)

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

26

Ninapenda kusema kwamba, Viongozi wetu wanawatisha Watanzania kusema kwamba, maandamano ni fujo, maandamano ni kuvunja amani ...

(Hapa kengele ililia kuashiria muda wa mzungumzaji kwisha)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge, muda wako umekwisha. MHE. RAYA IBRAHIM KHAMIS: Ninasema kwamba, ni haki ya Katiba na

Viongozi wazuri wanatakiwa wawe na hoja katika kutetea. (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge, ili uje uwe Mbunge mzuri baadaye,

inabidi uheshimu muda. Mimi ninaamini wewe ni msomi na ni mwanasheria, mchango wako ulikuwa mzuri, lakini usilazimishe. Muda umekwisha, mimi nimekupa kama sekunde kadhaa, niheshimu na mimi unisaidie niweze kuongoza hiki Kiti. (Makofi)

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante

sana kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia Hoja ya Waziri Mkuu. Kwanza; na mimi ninapenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kutuwezesha kuwepo wote hapa ndani ya Bunge siku ya leo. Ninapenda pia kutoa pongezi kwa Kiongozi Rasmi wa Kambi ya Upinzani, Mheshimiwa Freeman Mbowe, kwa Hotuba yake aliyoitoa. Nina uhakika, Serikali itaweza kuona mwangaza wa kuweza kutumia maoni haya ili tuweze kuiendesha nchi yetu vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni napenda niende moja kwa moja kwenye suala la

uwezo wa Madiwani katika kuendesha mambo ya Halmashauri. Halmashauri ni Mamlaka ambazo zimeundwa ili ziweze kusogeza huduma kwa Wananchi. Zimeundwa ili ziweze kulinda rasilimali za nchi mahali zilipo, usalama wa watu na well being yao kwa ujumla.

Madiwani wetu ambao ndiyo Wasimamizi Wakuu wa Mamlaka hizi, tuangalie

uwezo wao, kwa sababu ukiangalia katika Halmashauri inaongozwa na watu wawili; Watendaji ambao ni Executive, pamoja na Madiwani ambao ni Wanasiasa. Ukifika katika Halmashauri, unakuta Wakurugenzi wana degree, Mipango wana degree, Maafisa Elimu ni Wasomi na Idara nyingine. Kwa kuwa masharti ya uwakilishi katika nchi katika vyombo hivi yanasema ujue kusoma na kuandika Kingereza au Kiswahili, hakuna msimamo wa elimu na ndivyo tulivyo na ndivyo tunavyokwenda. Kwa hiyo, Madiwani wetu waliopo ndiyo hao na lazima tuwaheshimu.

Ninachosema ni kwamba, ninaishauri Serikali waandae mafunzo kwa Madiwani.

Waziri wa TAMISEMI, katika Hotuba yake amesema, ameandaa mafunzo ya siku saba. Mimi sikubaliani na mafunzo ya siku saba; ninapenda nimrejeshe kati ya mwaka 2000/2003, yalikuwepo mafunzo yalitolewa kadiri ya Madiwani, ninakumbuka kipindi kile Waziri Mkuu ndiye aliyekuwa Waziri wa TAMISEMI, mafunzo haya anayaelewa vizuri. Mafunzo hayo yalikuwa na hatua ya kwanza mpaka hatua ya tano, yalikuwa yanamuwezesha Diwani kwa sababu hata mimi mwenyewe nilikuwa Diwani nilishiriki mafunzo hayo. Mafunzo hayo yaliwezesha Madiwani kusoma, yalikuwa na hatua mbalimbali. Isitoshe, kukikuwa na hatua ambayo ilikuwa inawakutanisha Wakurugenzi

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

27

na Wakuu wa Idara. Yaliwawezesha Madiwani, Wakuu wa Idara na Wakurugenzi ambao ni Executive yote kusimama na Madiwani kuona namna ya kuendesha Halmashauri na yaliweza kuondoa migogoro kati ya Wakurugenzi au tuseme Executive kwa ujumla kwa Madiwani. (Makofi)

Mafunzo hayo yaliwaondolea uwoga Madiwani, yaliwajengea skills, yaliwapa

ujasiri kabisa wa kuweza kutetea Halmashauri zao. Ninasema hivyo kwa sababu nimewahi kuwa Diwani, ninajua kwamba, wapo Wakurugenzi wababe; wanatumia uwezo mdogo wa kielimu wa Madiwani kuweza kuwanyanyasa kwa kuwaambia lugha ya kwamba, mimi ninasikiliza watalaam. Hali hiyo imefanya Madiwani wanyong’onyee. Wabunge wengi wamesema hapa juu ya mishahara yao.

Ukiweka elimu yao na uwezo mdogo wa kimapato, basi Madiwani wanabaki

kuwapigia makofi Wakugurenzi na wakati mwingine kushindwa. Hata ukiangalia katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Madiwani ambao wana uwezo wa kusimamia hakuna wizi. Kwa hiyo, ninaweka msisitizo kwamba, TAMISEMI iangalie namna ya kuwafundisha Madiwani, siyo kuwapa semina za siku saba. Zile ni za kugawana, wawafundishe katika hatua kama zile warudie mafunzo yale. Serikali isione adha kutenga bajeti, heri uweke fedha ulinde fedha. Wasomi hatua kwa hatua wajenge ujasiri na wao wajione kwamba, kweli wamepelekwa kwenye training. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hapo, ninaomba sasa nirudi katika Mkoa

wangu wa Kagera. Nitaongelea hali ya matibabu na utabibu katika Hospitali yetu ya Mkoa. Hospitali za Mikoa, nchi yetu yote zinaeleweka kama ni Hospitali za Rufaa katika Mikoa. Hospitali yetu ya Mkoa haina specialists kwa sababu waliopo ni wawili. Wale wote wana kazi za kufanya, ambazo zinawafanya wasiweze kabisa kutimiza azma yao ya matibabu na utabibu. Katika Hospitali yetu ya Mkoa tunao specialists wawili tu; mmoja ni mtaalam wa wanawake, lakini huyu ni Mkurugenzi wa Hospitali.

Tunaye mwingine ambaye ni wa magonjwa ya jumla, lakini yeye huyu ndiye

anayeongoza mambo yote yanayohusu general na mambo ambayo ni nje ya hospitali; kwa mfano, ni Mkuu wa Vitengo vyote vya CTC; ni Regional Aids Coordinator; ni Mkuu wa Research ya Mambo ya Ukoma na Polio na mambo mengine. Kwa hiyo, unakuta hana muda wa kuweza kuangalia magonjwa ndani ya Hospitali yetu ya Mkoa; inaongozwa na Assistant Medical Officers. Kuna kipindi kabla sijawa Mbunge, nilikuwa ninasikia mlitaka kukifuta cheo hicho. Sisi katika Hospitali yetu ya Mkoa ndiyo hawa hawa wanaoendesha matibabu. Kwa hiyo, mnaweza kuona adha iliyopo kwamba, wakati mwingine wanazidiwa. Kupitia Bunge hili, ninapenda kuwapa pongezi Assistant Medical Officers waliopo katika Hospitali ya Mkoa kwamba, hawa ndiyo wanaendesha na ndiyo wanaotoa referral. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu niongee kuhusu referral. Zamani mgonjwa

alikuwa akiandikiwa kwenda kwa Hospitali ya Rufaa, nesi anapewa fedha. Sasa hivi wakishamwandikia hiyo karatasi kwamba, unakwenda Bugando au unakwenda Muhimbili, wanamwambia sasa uende ukatafute fedha. Mgonjwa atakwambia ngoja nirudi nyumbani niangalie familia yangu, kumbe ndiyo anakwenda kufanya hivyo.

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

28

Tunaomba Serikali irudishe ule utaratibu wa kuwasaidia manesi na kuwawezesha kwenda katika Hospitali za Rufaa ili watu waweze kupata matibabu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa sababu tuna tatizo la kuiomba Serikali, ninaitaka

Serikali, tuna tatizo la kuomba Serikali na Serikali tunaiambia kwamba, ituonee huruma. Serikali haipaswi kuona huruma, it is obliged, inapaswa kutimiza wajibu wake; hayo mambo ya kusema ituonee huruma ndiyo tunawafanya muwe na viburi. (Makofi/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende sasa kwenye adha ya Watu wa Mkoa wa

Kagera na gharama za maisha. Watu wa Mkoa wa Kagera sijui tunaishi wapi, mtatutafutia nchi leo kupitia kwako na Waziri Mkuu na Serikali kwa ujumla. Serikali iliiua reli, Serikali ilituondolea meli yetu inayoitwa MV Umoja na kweli tukifika katika Bajeti ya Waziri wa Uchukuzi, atuambie meli yetu ya MV Umoja aliiweka wapi? Kichaka gani? Kwa sababu reli imekufa kutokana na mikataba mibovu ya Serikali hii. Mmetuondolea meli yetu ya MV Umoja mkaipeleka sijui kichaka gani; Watu wa Kagera wana adha kubwa sana ya bei za bidhaa na hasa za ujenzi. Hii ni kwa sababu bidhaa zote zinasafirishwa kutoka Dar es Salaam kwa kutumia ma-truck.

Hebu nijaribu kuwaambia bei za Mkoa wa Kagera; tunanunua mfuko wa saruji

kwa shilingi 22,000; bundle la bati kwa shilingi 300,000; hebu jaribuni kuangalia bei zilizoko Dar es Salaam na tofauti iliyopo Mkoa wa Kagera. Watu wa Mkoa wa Kagera wanaumia. Turudisheni reli na meli yetu ya MV Umoja, iliyokuwa inasafirisha mizigo. Tunasikia tetesi watu ambao wanaua reli hiyo na kutuwekea ma-truck wengine ni vigogo. Mnatuumiza Watu wa Kagera na wananisikia wanajua. Ukitaka kujenga nyumba Mkoa wa Kagera, ufunge mkanda wa chuma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nirudi kwenye kilimo; Hotuba imeongelea Kilimo

Kwanza, lakini mimi labda nijadili bei za mazao nikiangalia bei ya kahawa katika Mkoa wetu wa Kagera, kwa sababu Mkoa wa Kagera uchumi wake mkubwa ulikuwa unahusu Zao la Kahawa. Bei ya kahawa inazidi kudidimia, lakini kuna tozo; wakati mnasemea tozo za mafuta angalieni tozo za bei ya kahawa katika Mkoa wetu. Mkulima wa Kahawa katika kilo yake moja, analipa tozo mbalimbali. Kwanza, anakatwa kwa ajili ya Chama cha Msingi; anakatwa kwa ajili ya Ushirika Chama Kikuu; anakatwa VAT; anakatwa Mfuko wa Elimu; anakatwa TACRI, yaani research; anakatwa hata ule mfuko wa kilo 50 unaoweka anakatwa kilo mbili, mfuko ambao haufikii nusu kilo. Ninaomba Serikali iangalie tozo hizo katika bei za mazao. TACRI wanaofanya research, ninashangaa mkulima anayelipia research. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakulima wa Kahawa wanaumia sana katika Mkoa

wetu. Tunaomba tozo hizi zisiangaliwe kwenye mafuta, ziangaliwe hata katika mazao mengine ya kibiashara. Mkoa wetu tunazuiwa kuuza kahawa kwenye soko huria. Wakulima wanalazimishwa kupangiwa bei. Wanakatwa yote haya halafu wanatupiwa mabaki kwamba, ndiyo bei ya kahawa; kwa kweli wakulima na uchumi wetu tuangalie jinsi tunavyoumia na bei nilizozisema, halafu mnatutoza kwenye kahawa watu wanaumia, maisha yanakuwa duni.

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

29

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumalizia, ninaomba sasa niongelee kuhusu maandamano ya CHADEMA. Wabunge wengi wamekuwa na woga; kila chama kina mkakati wake wa uenezi; hakuna mahali ambapo CHADEMA tumeandamana tukiwa na nyembe mfukoni na hakuna mahali ambapo tumeandamana hata sanduku la mwuza karanga likapigwa teke.

Tukifanya hivyo kueneza chama chetu na kuondoa watu kwenye chupa kwa

sababu tunawa-mobilize, tunataka kuwaelimisha Watanzania wajue Serikali yao inataka kuwafanyia nini. Ninashangaa wakati ninyi mnatubeza hapa na ninyi mna uenezi wenu mnaofanya kwa kuvua magamba; mbona sisi hatuwasemi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nisigongewe kengele ya mwisho; ninasema hivi; mimi

ni mwanamke, ukiona bahati umegombana na mwanaume akarusha konde, ukarusha konde, halafu akachukua kona akakukwaruza ili kuua reception, halafu akakuuma matiti; ni dalili ya woga. Hii ni CHADEMA. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante sana. Sasa nitamwita Mheshimiwa Naomi Kaihula na

Mheshimiwa Agripina Buyogera, ajiandae. Hiyo ndiyo Siasa ya Vyama Vingi. MHE. NAOMI A. M. KAIHULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa

kunipatia wasaa huu ili niweze kuchangia katika Hotuba ya Waziri Mkuu wetu. Awali ya yote, ninapenda nimshukuru Mwenyezi Mungu, ambaye ameniwezesha kufika hapa katika chombo hiki kitukufu. Ninamrudishia sifa na utukufu. Pili, ninapenda nikishukuru Chama changu cha CHADEMA, kwa kuniteua kuwa Mwakilishi wa Wananchi wa Tanzania katika Bunge hili Tukufu. Zaidi ya yote, ninapenda pia niwatambue Viongozi wetu wa CHADEMA, kuanzia Taifa mpaka chini, ambao walitutayarisha kuja kuwa wawikilishi wazuri katika Bunge na hususan ninapenda nimtambue Dkt. Willibrod Slaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA, kwa ujasiri wake kwa kuweza kuthubutu kuvunja tunaita myth ya kwamba, Chama cha Mapinduzi hakiwezi kikapata mtu ambaye anaweza kingamana naye sawa sawa. Ninampongeza na ninampa hongera aendelee.

Ninapenda nimpongeze Kamanda wetu, Mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe, kwa kuweza kutuongoza vizuri na kutufikisha humu Bungeni na yeye pia kuwa Bungeni; na pia humu Bungeni nampongeza sana kwa kuwa Kiongozi mahiri katika Upinzani na asiyeogopa. Ninapenda nimpe pia pongezi za wanaharakati na Wananchi wengi kwa jinsi ambavyo ametuinua wanawake katika Baraza lake la Mawaziri na mimi ni mmojawapo, ameniteuwa kuwa Waziri Kivuli katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto; tunakupongeza na kukuheshimu, tunakuahidi hatutakuangusha, endelea kusonga mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda pia niwashukuru watoto wangu kwa kuni-support wakati nikigombea Ilala na pia kuonesha kwamba, tunaweza tukagombea na kiti cha wale wa enzi, ambao ninasema miaka mia moja tunaweza, tuligombea. Mwisho wa

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

30

yote, ninawashukuru waombaji wote wanaoiombea amani nchi yetu; ahsanteni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hapo ninaomba nizungumzie sasa Bajeti.

Kero yangu ya kwanza katika hii Bajeti ambayo itanifanya niwe na mashaka hata kuiunga mkono ni kwamba; bajeti hii inaelekea kutokwenda kwenye kutatua mizizi, inakwenda kwenye kukata matawi. Ninasema hivi kwa sababu katika hii Bajeti, sijaona inajikita kutatua mahitaji ya Wananchi, yaani kuleta maendeleo ya Wananchi hasa ukianzia kwa watoto. Kwa mfano, shida zote hizi tunazozipata; mikopo ya wanafunzi; mitahani; watoto sijui wanauzwa; ni kwa sababu Bajeti yenyewe hii ambayo tunaishughulikia hivi sasa imejengwa kwenye Mpango ambao pia haujaelekeza vizuri; ndiyo matatizo yenyewe yanatokea hivi. Ninasema hivi kwa sababu ukichukua suala la watoto ni nchi ya ajabu sana hii Tanzania, ambayo ina-claim, inajivunia kwamba, ina watoto, lakini haina watoto. Mtu ukiwa na mtoto ni lazima yule mtoto umpangilie, umtayarishe kwa ajili ya leo, kesho na kesho kutwa; Tanzania hatuna hivyo. Sisemi hivi kwa ajili ya ushabiki, ninasema kama Mtanzania na mimi ni Mbunge wa Viti Maalum, ninasema kwa ajili ya nchi yangu. Watoto wa Tanzania hawana mahali popote ambapo baba yao kawawekea pesa ili katika maisha yao waweze kuendelea, wanapopigwa huko, warudi waseme baba nimepigwa akwambie chukua hiki.

Katika nchi zozote ambazo zinataka Mataifa yao yaendelee kuwepo Duniani,

zinawawekea watoto wao chochote katika ghala kusudi mtoto akiteswa huko nyumbani kwa wazazi wake waliomzaa anakwenda kwenye Serikali yake, anawaambia Serikali mimi sina fees, hela yake ipo iliwekwa, siyo inaanza kutafutwa, iliwekwa. Mtoto akinyanyaswa huko kwenye mitaa, atakwenda kwenye Serikali yake, hela yake ipo siyo kwamba Serikali unakwenda kuomba kwenye Mission, kwenye Vituo vya Wawekezaji au NGOs. Mtoto anapopata tabu kama hii ya mkopo, kwanza, kusingekuwa na sababu ya mikopo hata kidogo, kwa sababu kila mtoto angekuwa na fungu lake ambalo anawekewa mpaka anapofikia umri wa miaka kumi na nane, anapoweza kujitegemea, ndipo anapoacha kurudi kwenye Serikali yake kuchukua pesa yake; lakini Tanzania hili hatuna na sababu ya kutokuwa nalo haieleweki jamani Tanzania sisi tumerogwa na nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, humu tumekaa wasomi wengi, watu wenye hekima, wenye elimu; yaani tukichukua katika maana ya elimu, mtu mwenye elimu ambaye anajua kwamba, kitu hiki kikifanywa kitatokea hivi na hiki tukifanya hivi kitatokea hivi, tumo humu na kila wakati tunaongezeka, lakini hili jambo hatulioni kwamba; watoto wetu wawekewe pesa yao katika Serikali, sijui ni mifuko, sijui ni nini, lakini wawe na pesa. Kwa nini tunashindwa kutumia maliasili ambazo zinaporwa, ambazo zinatolewa ovyo? Kwa nini tunashindwa kwenye madini kuhakikisha kwamba katika madini, Mtoto wa Tanzania kuanzia umri sifuri, yaani anapokuwa tumboni anawekewa fungu lake hata asilimia point 0.01 katika mfuko wake wa kumwendeleza ili atakapozaliwa atapata clinic bila matatizo, atapata dawa bila matatizo, atakapokwenda shule atapata daftari, atapata kalamu na chakula.

Jamani nani asiyejua ninachosema? Mtu yeyote mwenye elimu, mtu mwenye

kufikiri, anahitaji chakula bora siyo tunachofanya kwamba, pengine sijui wakusanye

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

31

nendeni mkawape uji tu na maharage; kwa nini? Nchi hii ambayo inasema inataka kuendelea kuwepo katika sura ya Dunia na iweze kupambana na nchi zinazoendelea, haiwezekani hata kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninasema sijaona mahali popote ambapo hii

Bajeti inarudi kwenye tatizo la msingi, kwenye kuchimba mizizi na kuiondoa ili kwamba, matatizo yale ambayo tunapambana mpaka humu tunaanza kutupiana mipira kama alivyosema kaka yangu; kwa kweli hili suala ni lazima lifikiriwe. Kwa hiyo, maliasili na rasilimali za nchi ni kwa ajili ya Watanzania na Watanzania wanaanza kutoka wakiwa watoto wadogo, wawekewe kwenye misitu inayoporwa kupelekwa China, Malaysia na kwingine, pale kuwe na percent inayopelekwa kwa ajili ya kila motto. Nikisema hilo ninaamini kwamba, hizo bajeti kama siyo leo basi baadae ni lazima hili suala lifikiriwe kwa haraka ili kutatua matatizo ambayo ni makubwa, ambayo hayahitajiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hilo, ninapenda pia nizungumzie suala lingine

ambalo ni la elimu, ambalo pia limenigusa kwa sababu hata mimi nimekuwa mWalimu wa muda mrefu katika ngazi mbalimbali. Unapozungumzia elimu, unazungumzia kuanzia wale watoaji elimu, unawalenga wale watoaji elimu, kwa sababu ndiyo ambao wanakujengea yule anayepata elimu, lakini katika Taifa hili wamekwisharudia hayo. Mimi nitasema kwamba, kama kweli tuna nia ya kuondoa mzizi wa fitina na elimu, basi Walimu wale wapewe motisha. Sisi tulipokuwa tunasoma tulikuwa tunaweza kufanya kazi kwa bidii sana na kuipenda, kwa sababu tulikuwa na nyumba nzuri tena tulikuwa hatulipii kodi, tulikuwa na matibabu, tulikuwa tunaheshimika na tulikuwa na motisha. Jamani Walimu walikuwa wanapewa posho kwa ajili ya kazi kubwa ya kusahihisha. (Makofi)

Siku hizi Walimu wanasahihisha madaftari mia moja hawapati hata kitu chochote

na mishahara yao inazidi kwenda chini; kwa nini tusiwape mishahara mikubwa kama tulivyowapa Wafanyakati wa TRA kusudi wafanye kazi nzuri ya kukusanya mapato? Kwa nini tunashindwa kuwapa Walimu ili waweze kuleta Taifa maana wao ndiyo wanaojenga, kwa sababu mWalimu wa kindergarten ni daktari, mama, nesi, yeye ni kila kitu, lakini tunashindwa kumpa kiasi kinachostahili; kwa nini wakati tunaweza kuwapa watu wengine kama hawa wa TRA na watu wengine wa huko juu?

Katika hili, nilikuwa nimesafiri kwenye Programu za Exchange, Finland, Sweden,

Ujerumani, Marekani na Uingereza, tuliona kwamba, wenzetu kule Walimu wanawatambua kwa kazi yao; ni miongoni mwa wanaolipwa mishahara mikubwa na wanalindwa sana, lakini kinyume chake hapa Tanzania unataka uje upate watoto wazuri, huwezi kupata watoto wazuri, ni lazima na wewe uwajenge wale. Katika mipango yetu vipaumbele havifanyi kazi hapa, huwezi ukaanza kuleta shule nyingi kabla hujaweka facilities za kusomea, hapo unajenga kwenye wingi na siyo ubora, you aim at quantities instead of quality.

Tunachotaka hasa ni quality, tunataka washindane, tunataka wawe wavumbuzi,

wagunduzi, tunataka wawe na uwezo siyo tu tuna watu wa maonesho kwamba, tumesomesha watu wengi. Ngoja niwaambie, mimi nimesoma zamani, kulikuwa kuna

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

32

shule zilikuwa zinaitwa shule za tapa, watu walizichukia; mtoto ukimwambia umekwenda sekondari ya tapa anachukia na sisi ndiyo tunataka kuzifikisha hizi shule za kata kwa sababu hatujazitayarisha. Tungekuwa tuna nia hiyo, tungezitayarisha kwanza kwa vifaa, elimu ni vifaa; madeski, kalamu na vitabu. Vitabu vyenyewe ukienda kule vinavyotolewa si vitabu si chochote, ninawaambieni. Kwa hiyo, nilikuwa ninaomba kwamba, katika hiyo Bajeti haijazingatia vizuri, izingatie vizuri ndiyo ambapo itakuwa Bajeti inayolenga maendeleo ya watu badala ya kulenga maendeleo ya vitu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, ninaona muda unakwenda haraka, ninaomba

nizungumzie pia suala la elimu katika elimu ya uraia. Elimu ya uraia ninafikiri imekosekana, ndiyo maana hapa tunaanza kugombana sijui nini. Elimu ya uraia inapaswa itolewe, fungu liwepo kwenye Bajeti, ambapo mtu anaelewa kazi ya Chama cha Upinzani, kazi ya Chama cha Upinzani kama CHADEMA ndiyo hii tunayofanya sisi. Ninawaambieni ukweli kama Mtanzania, Vyama vya Upinzani vilianzishwa ili kukisimamia chama kimoja kinachokuwa madarakani; ambapo kinakuwa kama ni nyenzo ya kukisukuma kwenda kufanya kazi. Maandamano yamefanya kazi hii, Wabunge wengi tu waliposikia CHADEMA wamekwenda kule mbona walikuja. Ahsanteni sana. Ninaomba tusichukiane. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa kwa mchango wako. Sasa

nitamwita Mheshimiwa Agripina Buyogera na Mheshimiwa Dunstan Mkapa ajiandae na baadae Mheshimiwa Hemed Salum ajiandae; hayupo ana udhuru. Sasa nitamwita Mheshimiwa Dunstan Mkapa.

MHE. DUSTAN D. MKAPA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana

kwa kunipa fursa hii na mimi niweze kuchangia katika Hotuba hii ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Awali ya yote, ninapenda kukishukuru Chama changu cha Mapinduzi na kukipongeza kwa kupata ushindani mnono katika Uchaguzi Mkuu uliopita. (Makofi)

Pili, ninaomba nitumie fursa hii, kuwashukuru Wapiga Kura wangu wa Wilaya ya

Nanyumbu, kwa kunirudisha tena Bungeni. Hii ni pamoja na Wapiga Kura wa Kata ya Sengenya; ninawapa shukrani nyingi sana. Ninaomba tuendelee kushikamana, yaliyopita si ndwele. Pia ninapenda kutoa shukrani za pekee kwa mke wangu Yolanda na watoto wangu wote, kwa kunipa moyo wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu uliopita. Vilevile ninaomba niwashukuru Wabunge wenzangu, kwa ushirikiano mnaoonesha ndani ya Bunge hili, tuache malumbano, tuache tofauti zetu, tulitumikie Taifa na wapiga kura wetu. Ninaomba niipongeze Hotuba ya Waziri Mkuu, kwani imelenga katika kutatua matatizo mengi yaliyopo huko tunakotoka, lakini tukubali kwamba, uwezo ungekuwepo, matatizo mengi yangeweza kutatuliwa. Kwa hiyo, ninadhani Hotuba ya Waziri Mkuu, imelenga katika kufanikisha mambo mengi ndani ya Nchi yetu ya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninawashukuru pia Wasaidizi wake, ninajua ni watu

mahiri; Mheshimiwa Mkuchika, Mheshimiwa Mwanri, Mheshimiwa Majaliwa, Mheshimiwa Nagu na wengine wote waliopo katika Wizara hii. Ninadhani mtamsaidia vizuri sana Waziri Mkuu katika kutekeleza majukumu yake. La kwanza, ninalotaka kuchangia ni kuhusu kilimo.

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

33

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilimo ni uti wa mgongo katika Wilaya yangu ya

Nanyumbu. Wananchi wake wengi, karibu asilimia tisini na nane, wanafanya shughuli za kilimo na hivyo kuweza kujipatia riziki zao za kila siku. Kilimo hiki kina matatizo ndani ya Wilaya yangu ya Nanyumbu, kwanza ni kutokana na zana duni, bado wanatumia jembe la mkono; hivyo, upatikanaji wa mazao na uzalishaji unakua mdogo.

Ninaomba sana Serikali badala ya kutuletea matrekta madogo madogo, ituletee

matrekta makubwa ili tuweze kupanua kilimo chetu ndani ya Wilaya ya Nanyumbu. Nikija kwenye Zao la Korosho, Waheshimiwa Wabunge, wenzangu ninaomba nitumie fursa hii kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, kwa kazi kubwa aliyoifanya kufanikisha na kuweka katika hali ya ufanisi, mtindo wa stakabadhi ghalani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ameweza kuokoa pesa nyingi ambazo zilikuwa

zinakwenda mifukoni mwa wajanja na sasa hivi pesa zile kwa mabilioni zinakwenda kwa Wakulima wa Zao la Korosho Mkoani Mtwara. Amesimamia vizuri stakabadhi ghalani na sasa hivi imeleta ufanisi mkubwa, kwa hiyo, shukrani zangu za pekee kwa Kanali Mstaafu Anatory Tarimo, ninamwomba aendeleze wembe huo huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wananchi wa Wilaya wa Nanyumbu, walihamasishwa

sana tena sana kulima Zao la Choroko. Mwaka jana bei ilikuwa nzuri, shilingi elfu moja mia tano, lakini mwaka huu wamelanguliwa kiasi ambacho ninawaonea huruma. Bei ya choroko ilianza kwa shilingi elfu moja mia mbili, ikateremka hadi shilingi mia saba; hii yote ni kutokana na wanyonyaji wachache ambao walijitokeza kununua zao hili hatimaye kuwanyonya Wananchi hawa wa Wilaya ya Nanyumbu. Mimi binafsi nimesikitishwa sana, kwa sababu bei iliyokuwa imekubalika ilikuwa ni ya shilingi elfu moja mia mbili, sasa iweje imeporomoka mpaka kufikia shilingi mia tano au mia saba?

Ninaomba Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizara ya Kilimo, ziwasaidie

wakulima hawa wa Wilaya ya Nanyumbu ili wasiweze kupunjwa tena, wapate bei nzuri na waweze kuendesha maisha yao ya kila siku na kujikwamua katika wimbi kubwa la umaskini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na Zao la Korosho, kuna pembejeo inaitwa

sulphur. Wananchi hawa wa Wilaya ya Nanyumbu wamezoea ile sulphur ya unga, lakini nimeambiwa nikiwa hapa hapa Bungeni kwamba, wamepelekewa sulphur ya maji, kitu ambacho wananchi hawa hawaitaki; hivi ni nani huyu anayewalazimisha kutumia sulphur ya maji? Nani huyo aliyeagiza hizo sulphur za maji?

Mimi ninaomba nichukue fursa hii, Mheshimiwa Waziri Mkuu na Wasaidizi

wako, basi angalau tuwafahamu hawa walioleta hii sulphur ya maji na ikiwezekana wawajibishwe kwa sababu ni kero kubwa. Kwanza, maji yenyewe ya kutumia katika hii sulphur ya maji ni ya shida, sehemu zingine hawana maji ya kunywa, leo utatumia maji kuweka ndani ya sulphur kwa kweli ni kuwanyanyasa.

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

34

Vilevile mabomba ya kupulizia hiyo sulphur ya maji hawana, sasa sijui watafanyeje maskini hawa, lakini ninaomba tu Serikali ilione hilo kwamba, Watu wa Nanyumbu hawataki sulphur ya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu elimu, kama walivyosema wachangiaji wengi

hapa, Wilaya yangu ya Nanyumbu, ina uhaba mkubwa wa Walimu, madarasa, maabara, madawati, nyumba za Walimu ni chache, tunahitaji nyumba 395, vyumba vya madarasa 263; hivyo, ninaomba Ofisi yako Mheshimiwa Waziri Mkuu, ipeleke pesa nyingi Wilayani Nanyumbu ili tuweze kukidhi mahitaji haya ambayo tumeyaomba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu afya; Wilaya ya Nanyumbu haina Hospitali ya

Wilaya, tuna Vituo vitatu vya afya na zahanati kumi na nne; sasa unaweza kuona tuna matatizo gani ya Sekta ya Afya katika Wilaya ya Nanyumbu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile kuna matatizo ya magari ya wagonjwa katika

Vituo vya Afya vya Michiga na Nanyumbu. Watu wanapakiwa kwenye baiskeli, kwenye matenga mtu anapelekwa hospitali. Kwa kweli ni tatizo kubwa ambalo naomba Ofisi hii ya Waziri Mkuu ilione hili na itusaidie kwa kadri inavyoweza. Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile UKIMWI nao Nanyumbu upo. Tatizo letu kubwa ni upungufu mkubwa wa watumishi wenye sifa za kuweza kuwahudumia na kuratibu magonjwa haya ya UKIMWI. Lakini vile vile kuna tatizo la wafanyakazi kwenye Zahanati zetu na Vituo vya Afya. Tunaomba Serikali itusaidie sana kutatua kero hii.

Kuhusu barabara, hapa naomba nitoe shukrani kwa Serikali kwa kutujengea barabara katika kiwango cha lami kutoka Masasi hadi Mangaka. Tunashukuru sana barabara ile karibu inakamilika. Lakini katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi imeahidi kujenga barabara kutoka Mangaka kwenda Mtambaswala. Vile vile Mheshimiwa Rais alipokuja alitoa ahadi ya kujenga barabara kwa kiwango cha lami kutoka Nangomba kwenda Nanyumbu. Naomba sana Serikali itimize azma hii pamoja na hiyo ahadi ya Mheshimiwa Rais. Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu barabara, ningependa nizungumzie suala la barabara kutoka Nyamwage mpaka Somanga. Barabara hii kwa kweli imekuwa ni kero kubwa, haiishi, sijui itakwisha lini! Kila mara itakwisha, itakwisha, mpaka leo hii barabara haijaweza kwisha. Tunaomba mkandarasi aliyepo abanwe zaidi ili barabara hii iweze kwisha haraka. Pia naomba lile daraja la Mto Lukwamba katika Kata ya Napacho ijengwe. Wananchi wale wa Mpombe na Mburusa wanapata taabu sana wakati wa masika. Naomba sana Serikali katika bajeti ya mwaka huu ione uwezekano wa kumaliza kero hii. Mheshimiwa Mwenyekiti, naishukuru sana Serikali kwa kutujengea benki pale Mangaka. Nilikuwa nimeomba hapa Bungeni tujengewe benki pale Mangaka na vile vile alipokuja Mheshimiwa Rais wakati wa kampeni nikamwomba. Kilio changu kimesikika

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

35

na benki imejengwa karibu tutaanza kuitumia. Nashukuru sana Serikali kwa jambo hili. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna Tarafa nne katika Wilaya ya Nanyumbu. Tarafa tatu hazina Maafisa Tarafa. Ni mmoja tu na yule aliyepo ni Afisa Tawala. Kwa hiyo, tunaomba ajira za kujaza Maafisa hawa ifanywe haraka ili shughuli ziende kama kawaida.

Kuhusu Wizara ya Mambo ya Ndani, Mangaka hakuna Kituo cha Polisi rasmi. Kwa hiyo, hakuna mahususi cha mahabusu. Kila mahabusu wanapelekwa Masasi na kurudi kwenda kuchukuliwa na kurudi kiasi cha kilomita 60. Naomba Wizara husika wa Mambo ya Ndani alione hilo atusaidie kujenga Kituo kizuri cha Polisi, nyumba za Maaskari na vitendea kazi, kwani wana shida sana kule mpakani. Kuna mambo mengi yanafanyika, gari zipo mbili lakini moja liko taabani kidogo. Kuhusu nishati, Wilaya nzima haina umeme. Tupo gizani kila siku. Wakati wengine wanalalamikia mgao wa umeme, sisi tunalalamikia mgao wa mbalamwezi kwamba leo sijui tutapata mbalamwezi au vipi. Naibu Waziri wa Nishati na Madini aliahidi kwamba mwaka ujao wa fedha tutapatiwa umeme katika Wilaya yetu ya Nanyumbu. Naomba ahadi hiyo itimie. Mheshimiwa Mwenyekiti, maji ni kero kubwa namba moja Wilayani Nanyumbu. Kwa kweli pale Mangaka wananchi wanakunywa maji ya chumvi. Naomba sana Wizara husika itusaidie kutatua kero hii. Kuna maeneo mengi tu yana shida ya maji kama Kamundi, Nawaje, Lumesule, Likokona, Chivirikiti, Mikuva, Chitowe, Chikunja, Cheleweni, Namasogo, Mhinawe, Maneme, Nemeka, Namalombe, Chinyanyira, Rokumbi, Mkumbaru, Nahawara na maeneo karibu mengi ndani ya Wilaya ya Nanyumbu yana shida ya maji. Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee kuhusu suala la vijana. Vijana wa Wilayani Nanyumbu wamesahaulika sana. Hawana pa kwenda, hawapati mikopo na hawapati elimu ya ujasiriamali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi) MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia bajeti hii ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Moja katika tatizo kubwa sana la Mkoa wa Shinyanga ni tatizo la njaa. Tumepata matatizo haya kwa muda mrefu, sasa nikifikiria namna gani tuweze kutatua tatizo hili kwa kweli nakosa majibu kama hatupati nguvu ya Serikali Kuu. Nimepata taarifa kwamba kuna chakula kinakwenda kwa ajili ya kuondoa tatizo hili. Sijui ni tani ngapi! Lakini napenda kusema tu kwamba adha na tatizo la njaa katika Jimbo la Solwa ni kubwa mno. Mwezi wa nne tulipata tani 864 kwa ujumla wake. Nilipokwenda kwenye ziara wananchi hawakuweza kunisikiliza kabisa, kwa maana kwamba miradi ama maendeleo gani tunafanya? Ama tutarajie nini kwa mwaka huu wa fedha ujao? Walisema

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

36

kwa yote tunakuamini sana Mheshimiwa Mbunge, utuondelee kwanza tatizo la njaa. Sasa naiomba Serikali na ninajua kabisa ni makini na inafuatilia kuondoa tatizo hili. Kubwa zaidi ni kwamba tani za mahindi kwa ajili ya kuondoa njaa, jamani ziwe za kutosha ili tusipate adha nyingine kwa wananchi wa Jimbo la Solwa. Maeneo mengi sana nilipokuwa nikienda wanawake walikuwa wakiniambia Mheshimiwa ukichelewa zaidi ya miezi mitatu kupata msaada wa chakula, wanaume wetu watatukimbia, tutaachwa na watoto. Pale kwenye kijiji cha Mhangu kuna wanawake wawili walisema hivyo na mengine mengi tu. Kata ya Mwamala na maeneo mengi tu walilalamikia sana tatizo la njaa. Sasa naomba sana Serikali kwa sababu tathmini iliyofanywa sasa hivi nadhani wamekosea, imekwenda chakula kana kwamba hakuna chochote kwa wale ambao hawajiwezi na sasa hivi wakikosea tena tatizo litabaki, ni pale pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali ifuate tathmini iliyofanywa mwaka 2006. Tulipata tani 5,200 tatizo likaisha kabisa. Sasa hivi kibaya zaidi ni kwamba mazao waliyolima hawajavuna kabisa. Naiomba sana Serikali tatizo la njaa katika Jimbo la Solwa ni la kimsingi na kwa sababu hiyo, tuondoe tatizo hili. Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri kwamba nguvu kubwa tuweke suala zima la umwagiliaji. Jimbo la Solwa tupate umwagiliaji wa kutosha. Maeneo mengine kwenye Mkoa wa Shinyanga inapotokea tu tatizo la msimu mbaya wa mvua sisi ndiyo wa kwanza kabisa kuathirika. Fedha kubwa za kutosha ziweze kuwekezwa kuhusu suala zima la umwagiliaji. Tunayo maeneo mengi tu pale kwenye Kata ya Mwakitolyo, Yabukande na Usule. Usule sasa hivi kuna mradi mmoja pale Ishololo wa umwagiliaji tunafanya kwa shilingi milioni 200. Tuwekeze zaidi kwenye umwagiliaji na maeneo ambayo yataweza kuhifadhi maji. Tukikosa mvua tunatumia umwagiliaji kuondoa tatizo hili. Mheshimiwa Mwenyekiti, naishukuru Serikali imeweka hela nyingi sana pale TIB. Lakini nina wasiwasi sana kwamba masharti yaliyokuwepo pale kwa ajili ya kuwasaidia wakulima ni mazito ambayo yanahitaji nguvu yangu kubwa mno kwa ajili kusaidiana na wananchi wa Jimbo la Solwa. Naishauri sana TIB ama naishauri sana Serikali kwa kuwa hizi fedha ni zetu, ibadili masharti haya ili tuweze kuwasaidia wananchi wengi kupitia vikundi vyao vya wakulima na SACCOS. Lakini tukienda kwa mfumo wa kibenki bado nina wasiwasi mkubwa sana. Mimi nitajitahidi tu kwa namna yoyote ile angalau kwa hatua ya kwanza tuweze kupata fedha hizi. Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini bado naishauri Serikali kwamba uwekwe mfumo au masharti nafuu mno kwa maana ya wakulima wetu wa Jimbo la Solwa na maeneo mengine waweze kupata mikopo hii ya kilimo na Benki ya Kilimo iharakishe sasa na inapofanya hivi angalau kufungua kuwa na Benki ya Kilimo kwenye Kanda. Kanda ya Ziwa tupate pale Mwanza au Shinyanga ili kuweze kuwa na urahisi kwa wakulima wetu kwenda kupata hii mikopo ya kilimo. Mheshimiwa Mwenyekiti, Madiwani pamoja na Wenyeviti wa Serikali ya Vijiji, wanafanya kazi kubwa sana. Hili hatutakubaliana nalo mpaka kieleweke. Haiwezekani Wenyekiti wa Vijiji wafanye kazi kubwa yote ya utekelezaji wa Ilani yetu ya Chama cha

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

37

Mapinduzi, halafu kuanzia asubuhi mpaka jioni wasipate hela. Tupunguze tu kwenye bajeti hizi, kwenye fedha za matumizi mengineyo ambayo siyo ya maendeleo asilimia 10, 13 na 14 tunapata fedha za kuwalipa hawa. Kama tunakwenda safari mara moja, mara mbili, mara tatu, twende mara moja. Kama unakunywa chai vikombe viwili, leo vitumbua vinne, tukate nusu nyingine kwenye vijiji vyetu kule. Kwa hiyo, suala siyo tatizo, hapa ni kupunguza bajeti hii ya recurrent ili kuweza kupata fedha za kutosha kwa ajili ya Wenyeviti wetu. Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba sana Serikali kwamba kwa kuwa bajeti yetu tumepitisha, basi kwa mwaka wa fedha ujao tunapenda kuona Wenyeviti wa Serikali ya Vijiji pamoja na Madiwani wanapata mishahara na kama ni suala la Sheria ama ni Katiba leteni hapa tuirekebishe na wao waweze kufanya kazi. Bila Madiwani na bila Wenyeviti kwa kweli hata sisi Wabunge hatuwezi kufanya kazi vizuri kwenye majimbo yetu. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda sasa kuzungumzi maji. Katika kipindi cha maswali hapa niliposikia asubuhi, Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji alipokuwa akijibu swali la Mheshimiwa Azza ilionekana sasa mradi mkubwa wa Ziwa Victoria utatokea Kahama kupitia Timbe. Suala hilo ni zuri. Naamini kabisa hata sasa Kata ya Didia na Itwangi kwa maana kwamba lile bomba likipita pale na wenyewe watapata maji. Sasa ni suala ambalo litachukua miaka miwili, mitatu, naamini kabisa hii ni sherehe kubwa sana kwa wananchi wa Kata ya Didia. Lakini kuna mradi wa World Bank ambao sisi tulichimba zaidi ya visima 15, inachukua muda mrefu sana. Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tunawashukuru, hizi fedha zinatusaidia. Lakini naiomba Serikali ijaribu kuongea na hawa watu wa World Bank waweze kutuletea fedha hizi tukamilishe miradi hii haraka iwezekanavyo, ambayo ni Miradi ya Ziwa Victoria ili vijiji vilivyo ndani ya kilomita 12, kwa awamu ya pili viweze kupata fedha. Hizi ni kwa ajili ya fedha zetu za ndani. Naiomba Serikali itenge fedha kwa mara moja tuondokane na matatizo haya, Serikali inaweza. Tuthubutu kuchukua maamuzi. Serikali inaweza, wala haiwezi kushindwa. Mimi naamini kabisa mwaka mmoja au miwili tatizo la maji litabaki ni historia katika Jimbo la Solwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Solwa, Kahama, sasa imepanda imekuwa ya Tanroad. Solwa, Mwakitolyo, Kahama na kuna kampuni ya migodi pale ya Barrick ambayo itakuja kuwekeza. Sasa naomba mambo mawili. Kwanza, ifanye maongezi na kampuni hii, Barrick yenyewe waitengeneze, wana magari makubwa mno ambayo tukitengeneza sisi kwa fedha zetu tutakuwa kama tunapoteza hela. Magari yao yakipita pale yatavuruga ile barabara. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba sana Serikali iongee na kampuni hii kwa ajili ya utengenezaji wa barabara ile. Pili, kabla ya uwekezaji, Serikali kwa maana Wizara ya Nishati na Madini inakuwa hamtushirikishi sisi Halmashauri. Wameshapewa leseni, wanakuja pale kuchimba, wanakuwa na mradi wao sasa. Sisi Halmashauri tunafanya kuelezwa tu.

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

38

Nashauri kwamba kabla ya uwekezaji wa aina yoyote ile, lazima tufanye maongezi na kampuni ya Barrick pamoja na wananchi wenyewe watakaolipwa fidia pale ili haki itendeke vizuri na wananchi waweze kuridhika vizuri. Kinyume na hapo, tunasema hakuna mradi utaofanyika kwenye Kata ya Makitorio bila ridhaa, bila sisi kushirikishwa. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee kuhusu ahadi za Mheshimiwa Rais. Mheshimiwa Rais alipokuja kwenye kampeni mwaka 2010 pale Lyabukande aliahidi kwamba atatusaidia ujenzi wa hospitali yetu ya Wilaya na tumeshaandika maombi rasmi Hazina, maombi maalum. Naomba tujue tu maombi hayo tumepata ama hatujapata ama lini tunapata? Maana kwa Hospitali ya Wilaya, kwa sisi kama Halmashauri zetu hizi fedha ni ndogo mno, hazitoshi. Tukikaa kutenga shilingi milioni 300 au shilingi milioni 200 kila mwaka itachukua zaidi ya miaka mitano. Kwa hiyo, naomba sana Serikali iweze kutusaidia angalau hizi fedha tulizoomba tukamilishe hii ahadi ya Rais na tuwe na hospitali ya Wilaya nzuri mno kwenye Wilaya yetu. Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais pia wakati anakwenda Kahama, alisimama pale akasalimia wananchi wake, akawaahidi kwamba Nyashimbi na Puni tunawaletea umeme. Bado tumeandika barua, iko Ofisi ya Rais. Sasa nataka kujua, ahadi hii itatekelezeka lini? Tumeandika kwa mtiririko mzuri kupitia Rais, iko pale Ikulu na vile vile tumepeleka Hazina. Napenda kujua, wakati Mheshimiwa Waziri Mkuu ana-wind up hii Nyashimbi na Puni umeme watapata mwaka huu ama mwaka ujao? Ili sasa ninapokwenda kufanya ziara Jimboni, tuweze kuwaeleza kwamba umeme unakuja lini. Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais alituahidi mwenyewe mnara wa simu na vile vile nimemwandikia Mheshimiwa Waziri wa Mawasiliano kuhusiana na suala hili la ahadi ya Rais. Naomba kupata majibu kwamba amekwishawasiliana na Makampuni mangapi? Lakini tunashauri sana Airtel kwa sababu mtandao mkubwa kule ni Airtel ili na wananchi waliopo Lyabukande na Mwakitolyo nao waweze kupata mawasiliano mazuri. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Jimbo la Solwa walikuwa hawalimi sana. Nimehamasisha sasa hivi wamehamasika kwa sababu ya bei sasa ni nzuri sana. Lakini kuna hili tatizo la CDTF kukata Sh. 200/= kwa maana Sh. 100/= kutoka kwa mkulima na Sh.100/= kutoka kwa mnunuzi. Halafu bei sasa inabaki Sh. 1,100/= kwa mkulima. Mimi nashauri imekuwaje sasa hizi Sh. 200/= zimepanda? Mwaka jana tulikuwa tunalipa Sh.14/=. Sasa hivi wameipandisha mpaka Sh. 200/=. Mimi nashauri kwamba hii ifutwe, mwananchi apate hela kamili, sh.1,200/= kama ni suala la kununua pembejeo si wakulima wenyewe watanunua kupitia ruzuku ya Serikali. Lakini wakikata hapa CDTF itabaki historia wala hakuna ruzuku, wala hakuna pembejeo tutaendelea tu kulaumiana tu. Sasa hivi wanunuzi wamesitisha kwa sababu kuna mgogoro mkubwa mno. Mimi naiomba Serikali iingilie suala hili. Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na makaimu wengi sana sasa hivi Tanzania. Maamuzi hayachukuliwi. Kuna baadhi ya Wakuu wa Idara maeneo mengi tu wanakaimu.

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

39

Ukiingia sehemu unakuta Kaimu. Hata hospitali ya Muhimbili, Mkurugenzi naye ni Kaimu zaidi ya miezi sita au saba. Naishauri tu Serikali iwathibitishe haraka ili sasa maamuzi haya yaweze kwenda vizuri kwenye Idara zetu za Serikali. Mheshimiwa Mwenyekiti, nyumba za walimu. Tatizo hili tunaliongea kila siku, nafahamu kabisa ni kubwa na Serikali inalifanyia kazi. Hebu tupange sasa. Kupanga ni kuchagua. Kwa mwaka wa fedha ujao nyumba za walimu kwenye shule zetu za Sekondari liishe kabisa, angalau miaka miwili, mitatu tuondoe tatizo hili la nyumba za walimu. Mimi katika Jimbo la Solwa tuko vijijini mno, wanapokuja walimu kule, mwalimu kama amezoea madisko, amezoea kujirusha roho, akiingia Mwakitolyo siku ya pili mkuku, anaondoka. Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo rahisi kabisa. Sasa kama hakuna vivutio namna hii inakuwa ni taabu mno kuvutia walimu waweze kufundisha katika maeneo yetu. Nashauri sana Serikali tatizo hili tuliondoe haraka. Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nizungumzie zahanati. Mimi nina zahanati mbili ambazo ziko tayari na nyingine tano ziko kwenye lenta. Vituo vya Afya karibu vitatu au vinne viko tayari. Tuna Zahanati pale Butini iko kwenye lenta. Tuna zahanati Bukumbi ipo kwenye lenta. Tuna Kituo cha Afya Didia pale. Sasa nashauri sana Zahanati zetu zinapokuwa zimefika kwenye lenta, tunavyoomba fedha za kutosha zije tukamilishe, tusijenge magofu, mengi sana yakawa hayana impact kwa maana ya wenye kutoa huduma kwa wananchi. Tuwe na zahanati hata ambazo zitafika kwenye lenta, tuzikamilishe ziishe kabisa na waganga waje watoe huduma kwa wananchi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna swali katika ziara yangu niliyokuwa nikifanya pale. Naambiwa sasa Mheshimiwa Mbunge zahanati tunajenga, tulishajenga Shule za Msingi nyingi, tatizo likaja la upungufu wa walimu, hizi zahanati nazo hazitakuwa na tatizo la upungufu wa waganga?

Kwa hiyo, naiomba Serikali, hili nalo ilichukue kuona kwamba pale ambapo tumefungua Zahanati mpya tupate waganga pale pale waje kutoa huduma na kuwasaidia wananchi wetu kwenye maeneo ya Jimbo la Solwa. Baada ya kusema hayo, nasema ahsante sana kwa kunipa nafasi. Nashukuru sana, naunga mkono hoja. Asante sana. (Makofi)

MHE. SUSAN L. A. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii. Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu. Pia naunga mkono Hotuba ya Kambi ya Upinzani iliyowasilishwa hapa na Mheshimiwa Freeman Elikaeli Mwana wa Mbowe, Mbunge machachari kule Hai na Mkuu wa Kambi ya Upinzani na Mwenyekiti wa Chama. Nina sababu nyingi na nina sababu za muhimu za kuunga mkono hotuba ya Mwenyekiti au Mheshimiwa Freeman Elikaeli Mbowe, kwa kuwa inawasilisha kwa upana zaidi mawazo ya Watanzania ambapo ninaamini, kwa kuwa nilikuwa Mratibu wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania na mwitiko wa wananchi tulipokuwa tunakwenda katika vijiji mbalimbali, ninaamini kabisa Watanzania wengi wana imani

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

40

kubwa na CHADEMA. Hivyo ni vyema mawazo yao tukayawasilisha Bungeni, wawe sehemu ya maamuzi ndani ya Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli nilivyomaliza ule uchaguzi, roho yangu

ilikuwa inadunda sana. Lakini kwa hekima za Dokta wa ukweli, Dkt. Wilbroad Peter Slaa, aliyekaa kimya akatulia, pamoja na kuwa matokeo ya uchaguzi yalikuwa na matatizo makubwa, lakini alitulia na Viongozi wa Chama na wananchi walikuwa wanapiga simu kila kona, walikuwa wanataka kuingia barabarani ili kupinga matokeo hayo. Lakini aliwatuliza na sasa hali ya nchi iko shwari. (Makofi)

TAARIFA

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa. MWENYEKITI: Taarifa. MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kumpa

taarifa mchangiaji hapo kwamba, chama chake kwenye kampeni, amesema kimeweza ku-present mawazo ya wananchi kwa kupata watu wengi. Lakini pia napenda kumpa taarifa hivyo hivyo na mimi nilikuwa miongoni mwa vijana waliozunguka kwenye kampeni na mgombea urais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, tuliona mwitikio wa watu na ndio waliodhihirisha kukipa kura Chama cha Mapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia nimpe taarifa, kwa kuwa amesema Katibu

Mkuu wake ambaye alikuwa Mgombea Urais, alitulia baada ya matokeo kutanganzwa. Inawezekana ana matatizo ya kumbukumbu kwamba, Dkt. Slaa, ali-complain na watu wanajua…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge, unajua kuna mambo mengine hayana

sababu. Yeye alivyoona, aliona ni wengi ingawa hawakushinda. Wao waliona ni wengi. Sasa wewe kama uliona wale wachache ni jambo la kwako, na kwa kuwa mgombea wako uliyekuwanaye alishinda, wewe una sababu gani? Yeye aliona wengi, acha aendelee kuona ni wengi. Kwa hiyo, usimvurugie hotuba yake, mwache azungumze. Mbunge ana muda wake wa kuzungumza hapa.

Mheshimiwa Mbunge, endelea wala hiyo sio taarifa. (Makofi) MHE. SUSAN L. A. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa

kunilinda. Mheshimiwa Mwenyekiti, demokrasia ndani ya nchi yetu ni kitu muhimu sana.

Nimejifunza demokrasia katika mfumo huu wa Vyama Vingi tangu uanze ni habari ya uhakika kabisa isiyokuwa na mashaka kwamba, kuna vyama viko ndani ya nchi yetu, kikiwemo tawala na vile ambavyo haviko katika madaraka. Lakini inaonesha kabisa kitakwimu vile vilivyoko katika madaraka na vyama vingine vinaporomoka, lakini Chama kinachokuwa pekee ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA,

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

41

hakuna ubishi. Kwa hiyo, ni matumaini kwa Watanzania kwamba CHADEMA inakua na ipo siku tutashika madaraka ya nchi, sasa tumechukua reja reja ndio maana tumekamata Halmashauri na ni malengo ya Chama cha siasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kuzungumzia katika Hotuba ya Waziri

Mkuu, hususan katika eneo zima la Ofisi ya Rais kwamba katika bajeti hiyo, pamoja na kuangalia mambo mengi, lakini nimeona katika kifungu cha chai, mwaka 2010/2011 walitengewa Sh. 374,190,000/=, lakini cha kushangaza, mwaka huu wametengewa Sh. 1,945,735,500/=. Sasa najiuliza: Je, katika kifungu hicho kama mwaka jana walitengewa shilingi milioni 300 na mwaka huu wametengewa shilingi bilioni:- Je, kuna watu walikosa huduma? Mbona hatuna taarifa hizo? Kimetokea nini? Kwa nini, bajeti zinakuwa namna hii, wakati uchumi unakuwa taratibu, lakini matumizi yanaongezeka kwa haraka? Hapa ndipo inapoonekana kwamba umasikini utaendelea kuwepo ndani ya nchi yetu kwa sababu ya matumizi ambayo siyo ridhaa ya Watanzania. Hivyo, naishauri Serikali, ni vyema sasa ikabadilisha mtindo wa mazoea ya chai chai na nini, makaribisho mengi, basi waone, wafunge mkanda, waone sasa tunafunga mkanda, uchumi wetu, fedha zetu tunazokusanya tuelekeze kwa maendeleo ya Watanzania ambao 74% wako vijijini. Tuna haja ya kupunguza starehe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kitabu cha hali ya uchumi, nimeangalia,

nimeperuzi katika ukurasa wa 200 mpaka 202, nikaona mtiririko mzima namna madini yetu yanavyouzwa nje ya nchi kwa dola kadhaa. Lakini ninajiuliza, hizi dola zinarudi Tanzania au zinakwenda nchi za nje? Kumbe ni hawa wawekezaji wamewekeza ndani ya nchi yetu, wakipata hizo hela sasa wanatumbia kwamba wameuza madola na madola, wameuza dhahabu mizigo na mizigo na madini mengine nje ya nchi na wao wamepata dola nyingi, lakini sisi tunapata 3%. Hayo ni matatizo, lazima tujiangalie, tuna matatizo gani ndani ya nchi yetu? Ni kwa nini wewe kama nchi yako, una ardhi una kila kitu, mwekezaji anakuja anawekeza, yeye anachukua kila kitu anawaachia ninyi 3%. Haya ni matatizo makubwa ndani ya nchi yetu. Kwa mtindo huu hatuwezi kuendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndio maana tunasema miaka 50 ya uhuru, maendeleo

hayalingani na uchumi wa nchi yetu jinsi unavyoibiwa ndani ya nchi yetu unavyobebwa. Madini yanabebwa, tunabaki na mashimo, wanyama wazima wazima kama twiga tumeona kwenye vyombo vya habari wamebebwa. Sijui ndege ya aina gani imembeba twiga kumpeleka nchi za nje! Watanzania tupo, Serikali ipo, wamepita katika viwanja gani? Haya ni matatizo makubwa. Hivyo basi, hatuwezi kukaa hapa Bungeni tukiwa kama Wabunge, wawakilishi wa Watanzania, leo hii tukaangalia badala ya kuielekeza Serikali, sisi kazi yetu kuipongeza, haiwezekani na wala Katiba haijatwambia hivyo. Hatujaja Bungeni kwa kupongeza, tumekuja Bungeni kwa kuielekeza Serikali na kuisimamia ili ifanye kazi vizuri wananchi wetu wapate huduma zinazostahili. (Makofi

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na uchumi mwingi unaoondoka ndani ya nchi

yetu na sisi tunabaki na baridi na vumbi na mashimo, hawa watu wa mazingira wako wapi? Ukiangalia kule Nyamongo, kwenye ule mgodi wa Barrick wa Nyamongo, utakuta milima imeoteshwa, sio milima asilia, ni milima artificial ambayo wachimbaji wa madini wanachimba, milima inaota, wananchi wanabaki wanaangalia macho kodoo! Wanaokota

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

42

okota pembeni yale mawe na wakifanya mchezo wanapigwa risasi, wanauwawa. Tunakwenda wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni nchi yetu, eti baba na mama wanasonga ugali, ugali

wote tunawapa wageni, watoto wanakwangua ukoko. Haiwezekani. Ni lazima tujiulize, tumekosea wapi? Kama haiwezekani kuondoa haya madini, tuache, tuseme sisi haya madini tunayaacha, tunajikita kwenye kilimo. Bahati nzuri nchi yetu ni nchi ambayo ina hali ya hewa zote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna nchi Mungu ameipendelea katika dunia hii,

basi ni Tanzania. Ina hali zote za hewa katika dunia, ndio maana Wazungu wakizidiwa na baridi kule kwao wanakuja kwetu kubadilisha hali ya hewa. Kuna kila aina ya hali ya hewa, kuna kipupwe, kuna joto, kuna baridi, kuna kila aina na mazao yote yanaota ndani ya nchi yetu. Sasa ni vyema Serikali ikajielekeza katika eneo moja ili tuone sasa kama tunajikita kwenye kilimo, basi tujikite kwenye kilimo na tunaweza tukainua uchumi wetu bila hata kugusa zana nyingine. Lakini ile kushika hapa, kushika hapa, kushika hapa, ndio maana, kuna usemi usemao, Mtaka mengi kwa pupa, hukosa yote. Madini yanabebwa, misitu, wanyama wanabebwa, mara tunasikia kuna uranium Namtumbo, madini ya dhahabu, almasi na tanzanite, hatujui yametufaidisha vipi! Sasa kuna uranium Namtumbo!

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi katika gazeti wamesema yule anayetafiti pale ile

uranium, kama sio gazeti la Mwananchi ni Nipashe. Wameripoti, kuna yule mwekezaji amemchukua mtoto wa kike, ashakum siyo matusi, amembaka na amempa ujauzito, yule mtoto alipopimwa ameonekana ana UKIMWI. Wawekezaji hao! Tunawalinda vipi wananchi wetu? Wanaoathirika ni akina mama. Tusishike huku na huku, hebu tuangalie eneo moja tuone tutakuza vipi uchumi wetu. Wananchi watafaidika vipi na uchumi wao?

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye eneo la Serikali za Mitaa, huko ndiyo

shughuli ilipo. Serikali za Mitaa kuna matatizo mengi ambayo Ofisi ya Waziri Mkuu na TAMISEMI, pamoja na kuwa Viongozi wengi katika Halmashauri ni wa Kukaimu, lakini utaratibu wa kukaimisha viongozi hao, ndipo Halmashauri zetu zinakosa maendeleo kwa sababu watu hawajiamini. Lakini mtu anakaimu miaka saba, ni muhimu sasa Serikali ikaangalia upya ili Kiongozi athibitishwe katika Idara mbalimbali kwa upande wa Serikali za Mitaa na Wakurugenzi. Muda wa kukaimu urudishwe nyuma, iwe hata miaka miwili ndugu zangu. Huu uzoefu wa miaka saba anakaa tu kukaimu, ndio maana hela nyingi zinakwenda huko, watu wamekaimu. Lakini kibaya zaidi, hawa wanaokaimu ni kwa sababu wanafanya vibaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, katika Halmashauri, mtu ametoka katika

Halmashauri ya Mvomero, Afisa Ardhi, ameharibu pale wamemfukuza, Serikali za Mitaa wamempeleka Kilombero. Kilombero leo kuna matatizo makubwa ya ardhi. Ukiangalia, kuna migogoro katika vijiji mbalimbali katika Wilaya ya Kilombero, Namwawala, Kisegese, Mbingu, Miyomboni, Mofu, Miwangani, Chiwachiwa, kote kuna migogoro ya ardhi, lakini haishughulikiwi.

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

43

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo basi, naomba Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, aangalie kwa jicho la karibu Wilaya ya Kilombero na migogoro ya ardhi. Leo kuna watu wanadanganya, ndani ya Wilaya ya Kilombero kuhusu kuchukua ardhi ya Wilaya ya Kilombero katika Kijiji cha Namwawala. Barua zimekwenda mpaka kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu wakilalamika, lakini watu hawa wakionekana wanafuatilia kuporwa kwa ardhi yao, viongozi wa Kiserikali ngazi ya Wilaya wanawabambikia kesi na hivi kesi zote ziko Mahakamani. Wananchi wanapata shida, Kilimo Kwanza kitafanikiwa vipi wakati ardhi ina migogoro kibao? Kwa hiyo, ni vyema tukatatua kwanza migogoro ya ardhi ambako ndiko tunasema Kilimo Kwanza, wananchi walime. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakumbuka wakati wa Nyerere, kulikuwa na kilimo

cha pamba. Wanasema kila mwananchi alime ekari moja ya pamba na ekari nyingine za mazao. Lakini hiki Kilimo Kwanza kinawaelekeza nini wananchi wakati kila mahali kuna migogoro? Kilimo kwanza bila kuwaambia wananchi watapataje ardhi? Wilaya ya Kilombero yenye vijiji 81, eti mpaka mwaka 2010 wamepima vijiji viwili tu! Kilimo Kwanza kitakwenda wapi? Ni muhimu ardhi zikapimwa, watu wakakabidhiwa wapate kulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo la Madiwani, Madiwani na Wenyeviti wa

Serikali za Vijiji na Mitaa na Vitongoji wanafanya kazi kubwa sana kwa sababu Serikali ndiyo inapeleka hela nyingi kule. Wasimamiaji wa maendeleo hayo, tunajisifu hapa ujenzi wa Shule za Kata, waliofanya hizi kazi ni Madiwani, Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji. Wanakaba watu, wanakusanya michango, wanasimamia haya majengo, lakini watu hawa wamesahaulika kana kwamba hawako Tanzania. Ni vyema sasa Ofisi ya Waziri Mkuu ikaangalia ni namna gani watapewa uwezo hawa watu kwa kuwapa vitendea kazi na kuwapa mishahara ili waendelee kufanya kazi ya kulijenga Taifa hili, ni muhimu katika Utawala Bora. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo la Serikali za Mitaa, kuna tatizo kubwa la

kuhamisha Wakurugenzi walioharibu katika Wilaya fulani kuwapeleka Wilaya nyingine. Nasisitiza kwa sababu nimezunguka, huo mtindo katika Ofisi ya Serikali za Mitaa, achana nao!

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi) MHE. JAMES D. LEMBELI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa

kunipa nafasi hii kuchangia hotuba ya Waziri Mkuu. Nimeipitia vizuri kabisa hotuba ya Waziri Mkuu, haina shaka na mimi ninapenda nianze kwa kusema ninaiunga mkono kwa asilimia mia moja.

Mheshimiwa mwenyekiti, nitaanza mchango wangu siku ya leo kwa kupongeza

na kushukuru kwa mema yote ambayo yamefanyika tangu Uchaguzi Mkuu. Napenda niwashukuru wananchi wa Jimbo la Kahama kwa imani yao kwangu, kwa imani kwa Chama cha Mapinduzi, kwa kunirejesha tena Bungeni awamu ya pili. Napenda tu niwahakikishie wananchi wa Jimbo la Kahama na Wilaya ya Kahama kwamba

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

44

nitaendelea kuwatumikia kama ilivyokuwa katika kipindi cha 2005/2010. Lembeli ni huyo huyo, hatabadilika na msimamo wake katika baadhi ya mambo ni ule ule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda niipongeze Serikali kwanza kwa kutekeleza

kwa vitendo ahadi ya Rais kwa wananchi wa mji wa Kahama, ambapo aliahidi atawajengea barabara ya lami ya kilometa tano katika mji ule. Utekelezaji wa ahadi hiyo umeshaanza, awamu ya kwanza imekamilika, barabara ya lami imejengwa kutoka Phantom mpaka CRDB na nina hakika awamu inayobaki itakamilika katika bajeti ijayo. Hapa napenda nimshukuru na nimpongeze kwa dhati kabisa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Brigedia Jenerali Mstaafu Balele, kwa kufuatilia utekelezaji wa ahadi hii, hasa pale ambapo mizengwe iliingia. Ninampongeza na ninamshukuru kwa mambo mema na mazuri ambayo ameyafanya katika Mkoa wa Shinyanga na Wilaya yetu ya Kahama.

Hapohapo nampongeze Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Meja Mstaafu Bahati

Matala na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama, wote wanafanya kazi kwa uadilifu, na ni watendaji wazuri. Nawasihi wananchi tushirikiane nao kwa maendeleo ya Kahama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pongezi nyingine kwa Serikali na hususan Waziri

Mkuu, kwa kuanzisha Halmashauri mpya tatu katika Wilaya ya Kahama. Kwa maana, Halmashauri ya Mji wa Kahama, Halmashauri ya Ushetu na Halmashauri ya Msalala, haijawahi kutokea. Lakini naiomba Serikali kabla ya mambo hayajaharibika, ifafanue ni kwa nini Serikali imebatilisha uamuzi wake wa kuanzisha Wilaya mpya ya Ushetu? Pia ifafanue wananchi waelewe katika Wilaya moja, utaratibu wa kiutawala kwa Halmashauri hizi utakuwaje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nayasema haya kwa sababu iliwahi kutokea

mkanganyiko. Baada ya Serikali kutangaza kuanzisha Wilaya ya Ushetu, baadaye ilitangazwa sijui ilitokea wapi, Jimbo la Ushetu na Lembeli akaingia Mkenge. Hilo Jimbo halikuwepo. Sasa kwa utaratibu huu huu, ili wananchi waelewe kwamba tangazo hili la Waziri Mkuu ni la kweli, ufafanuzi wa kina naomba utolewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, katika pongezi ni kuipongeza Serikali kwa

uamuzi wake wa hivi majuzi wa kusitisha ujenzi wa barabara ya lami ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Mimi ni mdau na nilikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanapinga kwa nguvu zote ujenzi wa barabara ya lami katikati ya Serengeti. Uamuzi huu umepokelewa na wapenda uhifadhi wengi duniani. Hii imeiongezea sifa Tanzania, kama Tanzania ni mhifadhi namba one duniani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya pongezi hizo, sasa nataka nizungumzie

Kilimo Kwanza. Pamoja na nia njema ya Serikali kuhusu Kilimo Kwanza, zipo changamoto nyingi. Ili kilimo kwanza kiweze kufaulu, lazima iwepo mvua ya kutosha na hapa ndiyo kwenye tatizo watu wanahamasishwa lima, wanalima, lakini mvua zitoke wapi wakati misitu inateketea? Maji yatokee wapi kwa kilimo cha umwagiliaji wakati vyanzo vya maji vimevamiwa na sehemu nyingi zenye vyanzo vya maji wanaovamia siyo

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

45

watu maskini, siyo watu hohe hahe, ni watu wakubwa, ndiyo wanaopeleka kule mifugo yao. Sasa ombi langu kwa Serikali ni kwamba programu ya Kilimo Kwanza iende sambamba na kuhakikisha kwamba utunzaji wa mazingira unatekelezwa. Misitu inachomwa moto, hifadhi za Taifa zinavamiwa, hatua hazichukuliwi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kilimo Kwanza itakuwa ni wimbo, bila kuhakikisha

kwamba mazingira ya nchi yetu yanaendelea kuwa intact kama ilivyokuwa miaka ya 1960, miaka ya 1970 wote tunaona tukipita Morogoro pale. Mimi nikisoma Shule hata wakati wa kiangazi maji yalikuwa yanatiririka juu ya milima ya Uluguru, leo haipo na mtu akisema sasa tuhifadhi milima ya Uluguru, huyo atapigwa vita mpaka atatokomea kizani. Sasa Kilimo Kwanza Morogoro kitafanikiwa vipi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala hili la Kilimo Kwanza, yako mafanikio

makubwa yamefanyika katika Wilaya ya Kahama na hususan Jimbo la Kahama wananchi wameitikia vizuri sana programu ya Kilimo Kwanza hasa katika zao la tumbaku. Mwaka jana wakulima wa Tumbaku katika Wilaya ya Kahama, wengi wako kwenye Jimbo la Kahama, walilima vizuri sana tumbaku. Mwaka huu tatizo ni kubwa, kwanza bei imeteremka kutoka dola 2.5 hadi dola 1.60 za Marekani. Wananchi hawaelewi. Naiomba Serikali itengeneze utaratibu wa kulinda bei ya mkulima isiteremke pale ambapo imefika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo lingine kwa wakulima wa tumbaku ni hawa

wanunuzi. Sielewi wanatoa wapi nguvu za kuweza ku-dictate mambo jinsi wanavyotaka. Miaka yote kuna watu wanaitwa leaf man, hawa ni wale wanaoteuliwa na wanunuzi. Miaka yote haijawahi kujitokeza tatizo ambalo katika Wilaya ya Kahama mwaka huu limejitokeza. Baada ya wakulima kuzalisha tumbaku kwa wingi sana, bei imeteremka, safari hii leaf man wamekuja na utaratibu usio wa kawaida. Wakifika kwenye soko, kati ya mabeli 1,000 wanachukua 20, 30 mengi wanasema haya yamefungwa vibaya, yana grade mbovu, sasa utaratibu huu umeanza lini? Yote hii ni kuikomoa Serikali. Nami nafikiri Serikali lazima iwe makini sana na hawa watu.

Katika Kilimo Kwanza changamoto nyingine ni pembejeo. Vocha zimetolewa,

lakini usambazaji unakuwa wa matatizo makubwa sana, kijiji kimegawiwa vocha 200, pembejeo zinaletwa hazifiki kwa watu wasiozidi 80, sasa hiki ni kitu gani? Nilitaka niseme mambo hayo. Naona muda unakwenda kwa haraka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, nizungumze la migomo, maandamano.

Naomba sana suala hili tusiendelee kulizungumza huku ndani ya Bunge, linaumiza. Tanzania siyo kisiwa, duniani kote leo unaona watu wanaandamana watu wazima na akili zao, watu wanagoma.

Mimi cha msingi hapa, badala ya kunyosheana vidole, sisi humu ndani, tuiambie

Serikali kinachowafanya watu hawa wateremke kutoka huku juu kuja chini ni kitu gani? Serikali hebu iangalie, vingenevyo tutaendelea humu kusema kila siku na hawa watu wataendelea. Leo nilikuwa naangalia televisheni, watu wa Ugiriki wana matatizo makubwa sana, wananchi wako mitaani. Kazi iliyofanywa na Bunge la Ugiriki ni kuamua

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

46

kwa uchungu kwamba Serikali lazima ifanye moja, mbili, tatu, nne. Sasa sisi hapa tunaendelea kuwalaumu, ndugu zangu ukiona watu wanalandalanda mitaani kama mbuzi ambao hawana mwenyewe, ni tatizo kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuache kunyoosheana vidole. Sote ni Watanzania, hapa

kazi yetu ni moja kuhakikisha kwamba maandamano, migomo, haipo tena na mimi naamini Serikali ya Chama cha Mapinduzi inaweza. Tuzungumze mambo ya msingi ya kuondoa migomo hiyo. Kama mtoto hajapata mkopo, apewe mkopo na kwa wakati. Wote tunaona hapa Dodoma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi sihitaji hayo makofi, niacheni nizungumze.

Ukienda CRDB pale utaona jinsi ambavyo watoto wa kike wanapanga foleni kuanzia saa moja mpaka saa tatu hawaja-access benki na wakiingia mle ndani wanaambiwa pesa hazijaingizwa. Hata ningekuwa mimi, kwa nini usilalamike? Ukae tu! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu ni kwamba Serikali isome yale mabango

yanasema nini, iyafanyie kazi yale mambo, basi. Prof. Mwakyusa amesema hapa migomo imekuwepo tangu enzi za Mwalimu, wapo watu waliochapwa viboko, wengi wamo humu humu, lakini si yalikwisha na leo ni viongozi! Sasa sisi tukianza humu ndani kila mmoja anafanya hivyo! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, muda umekwenda, nilikuwa na mengi ya kuzungumza,

madini, Wilaya ya Kahama yote, yote imegawiwa kwa Barrick, hata ukitaka kuchimba mawe kwa ajili ya kuuza Barrick, watu wa madini watakukamata. Niliwahi kusema ndani ya Bunge hili kwamba kimsingi Wanyamwezi, Wasukuma, Wazinza ni watu wasitaarabu sana, hawataki ugomvi, lakini kwa yale yanayoendelea kule Kahama na sehemu nyingine, ni hatari sana. Bahati mbaya sana Mheshimiwa Maige hapa hayupo, ni Waziri hawezi kusema tu, ana matatizo makubwa sana kwenye Jimbo lake. Wachimbaji wadogo wadogo wa Kahama ambao wamechimba dhahabu miaka yote leo hawana pa kwenda, Barrick kapewa maeneo yote. Huyu Barrick ni nani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Ngeleja wewe ni msukuma, ukitoka huko

front bench utakwenda wapi? Ndugu zako kule wanasumbuka wanatoka Geita, wanakwenda Kahama, wanakwenda wapi na kwanini Barrick apewe maeneo yote? Ni jambo ambalo linasikitisha! Kwa Mbunge ambaye anatoka eneo ambako madini yapo na hususan dhahabu, ni bomu! Mheshimiwa Nyangwine simwoni hapa, sijui alikimbiaje! Sasa nimemsikia ndugu yangu Ahmed hapa, Mwakitolyo wanaanza mradi hao hao Barrick, ni hatari sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi) MHE. KABWE Z. ZUBERI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kukushukuru

kwa kunipa nafasi ya kuchangia hotuba ya Waziri Mkuu kama jinsi ambavyo iliwasilishwa hapa na Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni hotuba ya hali ya nchi kwa sababu yeye ndiye anaratibu shughuli nzima za Serikali, Wizara zote na vilevile kuangalia masuala ya siasa, uchaguzi, Bunge na kadhalika.

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

47

Kwanza kabisa, napenda niwapongeze Watanzania wote walioshiriki kwenye

Uchaguzi Mkuu mwaka 2005, lakini napenda niwapongeze sana Watanzania ambao walikipatia CHADEMA kura nyingi na kuongeza idadi ya Madiwani kutoka Madiwani 101 mpaka Madiwani 455, kwa mujibu wa taarifa ambayo Waziri Mkuu ameitoa kutoka Wabunge 11 mpaka Wabunge 48. Tunawashukuru sana kwa heshima hiyo ambayo mmetupa na tutawatumikia jinsi ambavyo Mwenyezi Mungu atakavyotuwezesha. Inshallah. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nitoe shukrani zangu za dhati kwa Mkuu wa

Mkoa wa Kigoma na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma ambalo Jimbo langu lipo kwa ushirikiano wao mkubwa. Nami katika kazi za maendeleo ya Jimbo la Kigoma Kaskazini, Wilaya yetu na Mkoa wetu wa Kigoma, wiki ijayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anakwenda Kigoma, kuzindua barabara ya Mwandiga Manyovu ambayo ipo ndani ya Jimbo la Kigoma Kaskazini ambayo ni barabara ya kwanza ya lami ya zaidi ya kilomita 60 ambayo imejengwa Kigoma toka tupate uhuru. Inawezekana kabisa Serikali yenu Mheshimiwa Waziri Mkuu labda isionekane na legacy, lakini kwa sisi watu wa Kigoma tunaiona legacy, kwa sababu toka nchi yetu ipate uhuru, toka utawala wa Mwalimu, Rais Mwinyi na Rais Mkapa, Kigoma haijawahi kupata maendeleo kwa kiwango ambacho tunakipata hivi sasa. Tutakuwa ni watovu wa fadhila tusiposhukuru katika jambo hili. (Makofi)

Nimetoka kuzungumza na Waziri wa Nishati na Madini - Mheshimiwa William

Ngeleja kuhusiana na suala la umeme kwa sababu suala la barabara tumemaliza. Tumekubaliana kwamba sasa hivi tunaingia kwenye suala la umeme na vijiji vya Kigoma Kaskazini tunaamini kabisa kwamba ndani ya hii miaka mitano vyote vitaweza kupata umeme.

Nilizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii - Mheshimiwa Maige, tuna mradi

mkubwa sana wa utalii katika kijiji cha Mwamgongo ambao shirika la TANAPA linashiriki na Chuo Kikuu cha Berlin (Technical University of Berlin), itakuwa ni pilot project kwa ajili ya masuala ya community based tourism. Napenda kushukuru sana. Lakini nawashukuru zaidi kwa sababu hawa ni Mawaziri vijana wenzangu na tunapokuja kwenye maendeleo tunaweka tofauti zetu za itikadi pembeni na tunakwenda kwenye shughuli za kuweza kuwasaidia wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Mkuu, tuna tatizo Kigoma la

Makampuni ya tumbaku. Nimefahamishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri kwamba sisi tulipitisha sheria ndogo ya kutoza asilimia tano kama tozo, wao walilipa asilimia tatu na sasa hivi tunawadai asilimia mbili na bado hawajalipa. Tulikuwa tunaomba Wizara yako na hasa Waziri wa TAMISEMI au ndugu Mwanri, ananisaidia tuweze kufuatilia tuweze kupata fedha hizi, ni zaidi ya shilingi milioni 280.

Lakini pili, kuna ahadi ambazo Rais alizitoa wakati alitembelea Kigoma mwezi

Juni, 2010 kabla ya uchaguzi. Kwa hiyo, alizitoa ahadi, siyo kama Mgombea, alizitoa ahadi kama Rais wa nchi, ya Vituo vya Afya viwili katika Kata ya Mkigo na Kata ya

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

48

Mahembe na tumepeleka maombi maalum kwa Kamishna wa Bajeti, lakini mpaka sasa hatujaweza kupata jibu hilo. Nilikuwa naomba tufuatilie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kwa ajili ya barabara ya Chankele - Mwamgongo ambayo Mheshimiwa Waziri Mkuu uliifungua na tuliomba maombi maalum ili barabara hii iweze kukamilika. Tunakuomba sana Mheshimiwa Waziri Mkuu uweze kulifuatilia hili ili kuweza kuhakikisha kwamba Mkoa wa Kigoma, Jimbo la Kigoma Kaskazini linakua kweli, ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikuwa nyuma kwa muda mrefu sana toka wakati wa

ukoloni. Sisi ilikuwa ni eneo la manamba, eneo la kutoa wafanyakazi. Lakini sasa kwa juhudi ambazo tumezifanya Wabunge wote wa Kigoma na viongozi wa kiserikali tunaona sasa mwelekeo unakuwa ni mkubwa sana, kwa hiyo, tulikuwa tunaomba utusaidie jambo hili tuweze kulikamilisha jinsi ambavyo inapaswa kuwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ukurasa

wa 13, umezungumzia uendelezaji wa sekta binafsi na uwekezaji nchini, hili ni eneo ambalo tunapaswa kuliangalia kwa makini sana na ningeomba ni-quote maneno ambayo umeyatumia katika hotuba yako:

“Kwa kuwa kiwango cha uwekezaji, uwekaji akiba kwa wananchi ni kidogo

kukidhi uwekezaji unaotakiwa kukuza pato la Taifa, Serikali inahimiza uwekezaji kutoka nje ili kufidia pengo la ndani. Tumekuwa tukipata wawekezaji kwa muda mrefu toka tumefungua milango ya biashara”. Wakati wa bajeti kulikuwa na malalamiko mengi kuhusiana na misamaha ya kodi, lakini Serikali iliweka msimamo wake kwamba ni lazima ile misamaha iweze kuendelea. Lakini kuna msamaha ambao kwa kweli tumeutoa, nadhani hatukufikiria vizuri na nililijadili jambo hili kwenye Kamati ya Fedha na Uchumi tukatarajia kwamba tungekuja kulibadilisha kwenye Bunge lilipokaa kama Kamati ya Matumizi lakini halikuweza kufanywa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Mkuu alikutana na Makampuni ya

kutafuta mafuta nchini wakawa wamemwomba na hapo ndiyo maana ya lobbying, wakawa wamemwomba kwamba waondolewe kodi katika mafuta wanayotumia kutafuta mafuta. Kulikuwa na hoja ya kwamba jambo hili litasadia uwekezaji zaidi. Napenda Mheshimiwa Waziri Mkuu afahamu na Watanzania wote wajue kwamba kwa sasa hivi Tanzania kwenye eneo la kutafuta mafuta na gesi hakuna wa kushindana na sisi wala hatuwezi kutoa vivutio kama ambavyo Kenya wanatoa. Kenya wana makampuni manne tu yanatafuta mafuta, sisi tuna zaidi ya makampuni 22. Hatuwezi kutoa vivutio kama Mozambique wanavyotoa, Mozambique, advantage pekee waliyonayo ni gesi ambayo Anadarko wameigundua ambayo iko Kusini ya Mtwara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu ambacho sisi tunatakiwa kufanya ni kuhakikisha

tuna-move haraka, kuhakikisha LNG plant inajengwa Mtwara haraka iwezekanavyo kabla ya wenzetu wa Msumbiji hawajafanya.

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

49

Sisi hatutakuwa na advantage kutoa vivutio kwa mafuta ya makampuni ambayo yanatafuta madini, tutapoteza pesa bila sababu ya msingi na jambo hili hasa la kuangalia kwa sababu kwenye mikataba yetu ya mafuta tuna vitu viwili, kuna kitu kinatiwa profit oil na cost oil. Cost oil maana yake ni kwamba kampuni ya mafuta ukishapata mafuta inatoa gharama zake zote wanajilipa, wakishajilipa zile gharama, yale mafuta yaliyobakia ya ziada profit oil ndiyo tunayogawana.

Sasa Serikali mmeenda kukubaliana na makampuni ya mafuta kuwapa msamaha

huu, hakuna udhibiti ambao tutakaoweza kuufanya na hili ndiyo tatizo kubwa ambalo tunalo. Nimewaambia viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, Mheshimiwa Ngeleja na Mheshimiwa Malima kwamba kampuni inakuja inatafuta mafuta, inasema tumechimba visima, gharama yake ni dola milioni 200, hakuna mtu ambaye amekwenda ku-verify kama ile gharama kweli ni dola milioni 200. Madhara yake ni kwamba mafuta au gesi itakapoanza kuchimbwa anarejesha kwanza zile dola milioni 200 zake mtakaa muda mrefu sana hamjapata kodi ambayo inayotakiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kosa ambalo tumelifanya, naomba tulirekebishe na

ndiyo madhara ya lobbying na itafikia wakati tutunge sheria ya ku-regulate lobbying kwa sababu siyo vizuri kumchukua Waziri Mkuu kwenda kufungua Mkutano wa wawekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wawekezaji wanaomba concessions, hatukai

tukaziangalia vizuri, tuna-offer zile concessions, tutaingia kwenye matatizo makubwa sana. Nilikuwa naomba jambo hili tuweze kuliangalia kwa karibu kwenye mafuta na gesi.

Waheshimiwa Wabunge, sisi sasa hivi ni giant kwenye eneo la East and Central

Africa. Tuna uhakika very soon tutakuwa ni wachimbaji wakubwa wa mafuta, tutakuwa ni wachimbaji wakubwa wa gesi, hatuna sababu ya kutoa hizo concessions kwa sababu ile risk ambayo makampuni yanaingia kwa ajili ya kutafuta yale mafuta watakuja kurejeshewa zile pesa zao na kama hawatayapata hayo mafuta, ndiyo risk ya uwekezaji. Kwa hiyo, nilikuwa naomba jambo hili Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa sababu wewe ulihusika moja kwa moja, uliangalie, watu wa Wizara ya Fedha walipitie upya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Kamati ya Fedha na Uchumi tuliwakatalia

watu wa Wizara ya Fedha tukawaambia hapana, msitoe kwanza, nendeni mkafanye tathmini, wamerudi hapa Bungeni wameleta kama jinsi ambavyo tumelikataa kwenye Kamati ya Fedha na haya ndiyo matatizo ambayo tunayo. Tukisema kwamba hawa watu wa Wizara ya Fedha wamehongwa, watakataa vipi? Kwenye Kamati, Kamati imesema hapana. Wao wamekuja hapa Bungeni na bahati nzuri guillotine ikawasaidia suala hili limepita, tutapata hasara kubwa sana. Nilikuwa naomba jambo hili liende likaangaliwe.

La pili, Mheshimiwa Waziri Mkuu amezungumzia madini page 38 na page 39,

baada ya kupitisha sheria ya madini (the Mining Act 2010), tuliruhusu na nchi yetu ikaomba kuwa mwanachama wa Extractive Industry Transparent Initiative (EITI), wamefanya audit.

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

50

Mheshimiwa Mwenyekiti, audit inayofanywa ni kwamba wanakwenda kwenye makampuni ya madini wanasema ninyi mmelipa kiasi gani Serikalini? Wanaonyesha receipt zao, wanakuja, Serikali ninyi mmepokea kiasi gani kutoka kwenye makampuni ya madini? Wanaonyesha receipts zao. Katika mwaka wa fedha 2008/2009 wale auditors wamekuta kati ya kiwango ambacho makampuni ya madini wameilipa Serikali na kiasi ambacho Serikali imepokea kutoka kwa makampuni ya madini kuna discrepancy ya 20 billions Tanzanian Shillings. 20 billions!

Mheshimiwa Rais alikwenda Paris kwenye mkutano wa EITI, akaiahidi Dunia

kwamba atamwomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali afanye ukaguzi kuona shilingi 20 bilioni zimekwenda wapi kwa sababu ni discrepancy. Makampuni ya Madini yanasema yamelipa kiasi fulani na Serikali inasema tumepokea kiasi fulani, kuna discrepancy ya shilingi 20 bilioni kwa upande wa Serikali. Naomba hili Mheshimiwa Waziri Mkuu haraka iwezekanavyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali afanye ukaguzi na asifanye kwa mwaka huo mmoja aangalie miaka 10 ya nyuma kwa sababu kuna uwezekano kabisa tukawa tumeingia kwenye ugonjwa wa Nigeria kwamba royalty zinalipwa lakini kuna mfuko fulani ambapo zinapita kwa ajili ya watu wachache. Kwa hiyo, naomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali atekeleze agizo hilo la Mheshimiwa Rais, afanye hiyo audit kwa miaka 10 iliyopita ili kuweza kufahamu hizi discrepancy zimetokea wapi maana watu wa Wizara ya Nishati na Madini walipoulizwa kwa nini hii discrepancy wakasema kwamba nyaraka tumezichoma, ndani ya mwaka mmoja huwezi kuchoma nyaraka ya Serikali. Nyaraka za Serikali zinakwenda kwenye Archive ya Serikali. Ndiyo majibu ambayo waliwapa wale Auditors. Kwa hiyo, naomba jambo hili liangaliwe vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, ni mafuta ya taa. Tumekubaliana kama

Bunge kwamba tunadhibiti uchakachuaji na hii tabia ya Viongozi wa Kisiasa kuogopa kueleza mambo ambayo wananchi hawayataki, haifai. Kwa sababu sasa hivi hakuna Mwanasiasa anayezungumzia mafuta ya taa kwa sababu wanajua wananchi wanalalamika kwamba mafuta ya taa yamepanda bei. Tuepuke uongozi wa kusimama asubuhi unanyoosha mkono, upepo unaelekea wapi na wewe unaelekea hukohuko. Tumepandisha bei ya mafuta ya taa kwa sababu ya kuzuia uchakachuaji, lakini huu ushuru tunaupeleka wapi? Lazima huu ushuru urudi kwa wananchi ambao wanaumia. Ndiyo maana tumependekeza kwamba ushuru wote ulioongezeka kati ya shilingi 52/= na shilingi 400/= kwenye mafuta ya taa uende Rural Energy Agency (REA) upeleke umeme vijijini, ndiyo njia pekee ya kuweza kuwasaidia wananchi vinginevyo sisi Bunge zima hapa tutaonekana ni traitors, tutaonekana tunalinda maslahi ya matajiri ambao mafuta yao yanachakachuliwa na hatuwalindi wananchi maskini ambao ndiyo wametuchagua na kutuleta Bungeni. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri Mkuu, litoke agizo la Serikali kwamba ushuru wote unaokusanywa katika ile ziada ambayo tumepandisha kwenye ushuru wa mafuta ya taa kati ya shilingi 52/= mpaka shilingi 400/= wote uende REA tufanye Rural Electrification, wananchi wapate umeme, tuwapunguzie gharama. Hii ndiyo njia pekee ya kuweza kuendesha nchi.

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

51

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho kabisa, ni Shirika la Masoko Kariakoo. Mheshimiwa Waziri Mkuu na TAMISEMI, Kamati ya Mashirika ya Umma imekagua Shirika la Masoko Kariakoo, Shirika hili …

(Hapa kengele ililia kuashiria muda wa mzungumzaji kwisha)

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Zitto kwa mchango mzuri na sasa

nitamwita Mheshimiwa Said Omar Nkumba na baadaye Dkt. Kabwe S. Kebwe ajiandae.

MHE. SAID O. NKUMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote, naomba nichukue fursa hii kwa sababu nazungumza kwa mara ya kwanza, niwashukuru sana wananchi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi wa Jimbo langu la Sikonge kwa kunichagua kwa awamu ya tatu kuwa Mbunge wao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya shukrani, naomba nichukue fursa hii kupitia

kwako, nimpongeze sana mdogo wangu aliyemaliza kuzungumza sasa hivi, Mheshimiwa Zitto Kabwe. Amezungumza vizuri na katika maelezo aliyoyatoa mimi nafikiri sasa tunaanza kufungua ukurasa mpya. Wabunge wengine wa Upinzani wangeanza kuiga kwamba mambo mema yanayofanywa na Chama cha Mapinduzi hata kama si chama chako yanafanywa na Serikali basi ni vizuri kupongeza, siyo dhambi! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nitajielekeza sana kwa mambo makubwa ambayo

yanafanywa katika Jimbo langu. Kwanza, naomba niipongeze sana Serikali ya Chama cha Mapinduzi kama alivyosema Mheshimiwa Zitto Kabwe, Kigoma hatuna tofauti sana na Tabora, lakini Serikali ya Chama cha Mapinduzi ni Serikali sikivu, Wabunge tumesema katika Awamu mbili au tatu zilizopita leo utekelezaji mzuri umeanza kujitokeza. Hapa ninapozungumza zipo barabara za Mkoa wa Tabora zimeanza kujengwa kwa kiwango cha lami. Naishukuru sana Serikali ya Chama cha Mapinduzi. Ombi langu ni kwamba barabara hizi zijengwe kwa kuzingatia muda uliopangwa katika mkataba lakini vilevile zijengwe kwa kiwango kizuri zaidi kwa maana ya ubora. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijielekeze katika suala la kilimo. Wakulima

hawaaminiwi sana na benki ili wakope na kuendeleza shughuli zao za kilimo. Niishukuru sana Serikali ya Chama cha Mapinduzi kwa kuanzisha utaratibu wa benki ya TIB kuwakopesha kupitia dirisha ambalo baadaye tutaweza kuwa na Benki ya Kilimo. Nataka kutoa angalizo, Benki ya TIB iko katika maeneo machache sana nchini, sasa mikopo hii isije ikawa inachukuliwa na watu wachache tu. Naomba sana kwamba uwepo uhusiano na benki ambazo zipo karibu sana na wananchi ambazo zitafungua madirisha ya kuwasaidia wakulima wadogowadogo ili waweze kukopa na kufaidika na mikopo hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tumeshuhudia katika mikopo ya fedha za

Mfuko wa Pembejeo, watu wachache ambao wengine si wakulima walikuwa wanafaidika

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

52

nayo. Sasa katika kipindi hiki, naomba sana wakulima ndiyo waelekezwe kukopa na kufaidika na mikopo hii, wasitumike watu wengine kukopa na kufaidika na fedha ambazo hazikuandaliwa kwa ajili yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nizungumzie kuhusu suala la tumbaku

ambalo kwa kweli nitalizungumza kwa muda kidogo. Naomba kwanza ku-declare interest kwamba mimi natoka katika maeneo ya kilimo cha tumbaku, lakini vilevile ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku Tanzania. Kwa hiyo, haya nitakayoyasema basi mengine yatakuwa ya Serikali na mengine yatakuwa ya wapigakura wangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, niwapongeze wakulima wa tumbaku wote

nchini kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kujiongezea kipato, lakini pia kuiongezea kipato Serikali ya Chama cha Mapinduzi. Wakulima katika mtiririko wa kuanzia mwaka 2006 wamekuwa na uzalishaji mkubwa sana wa zao hili, kwa kweli ni zao ambalo linategemewa kuingiza fedha nyingi sana nchini kwa maana ya wakulima wenyewe, lakini fedha za kigeni vilevile zinaingizwa kwa kiwango kikubwa zaidi. Mwaka 2006 wakulima wa tumbaku walijipatia shilingi bilioni 60 na milioni 976, lakini tuliuza mauzo ya nje dola 65 milioni. Mwaka 2007 dola bilioni 75 zilikwenda kwa wakulima na dola 87 ziliuzwa kwa mauzo ya nje. Mwaka 2008 dola bilioni 170.393 ziliuzwa na zikawapatia wakulima mauzo ya nje dola milioni 176 lakini mwaka 2009/2010 wakulima walipata shilingi bilioni 317 lakini mauzo ya nje yalifikia dola milioni 232. Mazao tuliyoyauza mwaka 2009/2010 yote ya biashara nchini yalifikia kiwango cha dola milioni 500. Kwa hiyo, utaona kwamba kwa zao la tumbaku tu tulifikia dola milioni 232, tulikuwa tunakaribia nusu ya mazao yote ambayo tumeyauza nchini. Kwa hiyo, nawashukuru na kuwapongeza sana wakulima wa tumbaku kwa kuongeza kipato chao, lakini pia kuongeza kipato cha Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama alivyosema ndugu yangu Mheshimiwa James

Lembeli, masoko yanayoendelea nayo yana matatizo kwa sababu utaratibu uliopo sasa hivi unawanyanyasa sana wakulima. Wakulima wanapeleka mitumba yao sokoni, lakini ikishafika sokoni wanunuzi wananunua mtumba wa kwanza na wa pili, wakiona kuna tatizo lolote wanasema mitumba yote hii haifai na soko linaahirishwa, huku ni kuwanyanyasa wakulima wa tumbaku. Walikuma ambao kwa kweli watapatikana na tatizo wahukumiwe wao lakini wakulima wengine mitumba yao ni vizuri ikauzwa ili waweze kupata fedha zao kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la bei kama walivyosema Waheshimiwa

Wabunge wenzangu kwa mwaka huu 2011 imeteremka lakini utakuwa umeteremka kutokana na mambo mengi. Kwanza, inawezekana soko lenyewe kidunia likawa na tatizo lakini kwa namna moja ama nyingine yapo mambo mengine ya kwetu humu ndani tukiyarekebisha basi wakulima wataendelea kuuza mazao yao vizuri na kupata fedha vizuri. Niishukuru sana Serikali ya Chama cha Mapinduzi kwa kuondoa makato ambayo yalikuwa yanakatwa na Bodi zote za mazao nchini. Bodi ya Tumbaku kama Bodi nyingine zimeondolewa kuchukua fedha kutoka kwa wakulima. Kwa hiyo, Bodi nyingine zote za mazao zinajiendesha zenyewe kupitia mfuko wa Serikali ambao unazigawia fedha kujiendesha zenyewe. Kwa utaratibu wa kiushirika vilevile naomba yale makato ambayo

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

53

yanawekwa kwa ajili ya kuwakata wakulima nayo yaangaliwe na Serikali isikae tu ikasema ushirika unajiendesha wenyewe, ukae hivyohivyo! Yapo makato mengi sana ambayo wakulima wa tumbaku wanakatwa, mengine hayana sababu za msingi na vyombo vingine haviwasaidii sana wakulima, watu wamekaa hawalimi, wanakula mishahara na kupata posho lakini wakulima wananyanyasika. Naomba sana Serikali iingilie kati kuangalia wakulima wa tumbaku, yale makato wanayokatwa kwa mtitiriko wa kiushirika yawe ni makato ambayo yanawasaidia vilevile wakulima katika kuendesha shughuli zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanunuzi wa tumbaku walianzisha chombo chao

kinachoitwa ATTT, ni muungano wao, wakulima wanasema Serikali ni vizuri mambo mengine haya iyaangalie na iingilie kati. Ni muungano wao na siyo muungano wa wakulima, wameanzisha wao wenyewe lakini ukienda katika makato ambayo wanakatwa wakulima unakuta ipo shilingi 120/= inaondolewa kwa kila mkulima anayelima tumbaku kwa kilo ili kuendesha chombo ambacho si cha kwao, hiyo siyo haki. Serikali naomba sana iingilie kati kuhakikisha kwamba jambo hili linaondolewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naomba nizungumzie suala la vita dhidi ya

tumbaku. Mimi nikimsikia Waziri wa Afya au Mtendaji yeyote wa Sekta ya Afya anazungumzia vita dhidi ya tumbaku, namuelewa na ninaomba muendelee maana hiyo ndiyo kazi yenu. Waziri wa Afya umeajiriwa kwa nafasi ya Uwaziri kwa sababu ya kazi hiyo, nikikusikia Waziri wa Afya unasema, tumbaku safi, nitakushangaa, hiyo ndiyo kazi yako endelea lakini sisi wakulima wa tumbaku kwa hizi takwimu nilizozisema tunavyoingiza kipato kikubwa cha tumbaku lakini tunaingiza fedha nyingi sana kwa wakulima na fedha nyingi sana kwa pato la Taifa, tutaendelea kulima tumbaku kwa sababu soko bado lipo, tutaendelea kulima tumbaku na kasi yetu inaendelea kukua mwaka hadi mwaka. Tutaendelea hivyo maana tunapoendelea kulima tumbaku nyingi zaidi ndiyo sababu vilevile inayoifanya Serikali iendelee vizuri, vilevile na Wizara ya Afya ifanye kazi yake vizuri zaidi. Kwa hiyo, utaendelea kwa upande wako kusema lakini na sisi tutaendelea ili kuwawezesha Serikali iweze kutekeleza wajibu wake vizuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme kwamba yamekuwepo maneno mengi

dhidi ya tumbaku na maneno mengine yanasemwa na watu wengine ambao wala hawaijui tumbaku. Mtu anatoka Moshi au Arusha anakuja Sikonge, anakwenda Namtumbo mpaka Mpanda, anakwenda kuzungumzia suala la tumbaku, anakwenda Sikonge mpaka Songea, jamani!

MBUNGE FULANI: Na Kaliua! MHE. SAID O. NKUMBA: Na Kaliua! Jamani tumbaku ina wenyewe na

wenyewe ndiyo sisi tunaifahamu tumbaku. MBUNGE FULANI: Imetulea sisi!

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

54

MHE. SAID O. NKUMBA: Watu wamelelewa hapa na tumbaku, akina Mheshimiwa Kapuya!

MBUNGE FULANI: Na tumesomeshwa na tumbaku! MHE. SAID O. NKUMBA: Akina Mheshimiwa Kapuya hapa wamesoma kwa

tunmbaku, wako hapa. (Makofi) Sasa unapokuja hapa unadharau tumbaku hujulikani ulikotoka wapi utaleta

matatizo. Kwa hiyo, nawaomba sana wale wanaokuja katika maeneo yetu wanapiga vita zao la tumbaku waache tabia hiyo. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Wametoka Moshi hao! MHE. SAID O. NKUMBA: Watu wanaanza kuhusisha suala la tumbaku na

uvutaji wa sigara, nataka niwape takwimu. Siyo wote wanaolima tumbaku wanavuta sigara na siyo Watanzania wote wanavuta sigara na hakuna uhusiano wowote kati ya wavuta sigara na maisha ya binadamu. Mtanzania mmoja anavuta sigara 177 kwa mwaka na wastani wake wa maisha wa kuishi ni miaka 56 lakini ukienda Japan, Mjapani mmoja anavuta sigara 3,023 kwa mwaka lakini wastani wa maisha ya wananchi wa Japan ni miaka 83, muangalie uwiano huo. Sisi tunaovuta sigara kwa kiwango cha chini tuna umri wa kuishi wa kiwango cha chini, wanaovuta sigara kwa wingi wana wastani mkubwa wa kuishi ambao ni miaka 83. (Kicheko/Makofi)

Sasa unakaa hapa unapiga kelele kwamba tumbaku mbaya, tumbaku mbaya,

inawezekana huli lishe nzuri, uko kama Nkumba hapa umekondakonda... MBUNGE FULANI: Shauri yake! MHE. SAID O. NKUMBA: Tengeneza lishe yako! MBUNGE FULANI: Ndiyo! MHE. SAID O. NKUMBA: Hispania kila anayevuta sigara, mmoja anavuta

sigara 2,779 na wastani wake wa kuishi ni miaka 81, Tanzania hapa ni miaka 56. Ugiriki mvuta sigara mmoja anavuta wastani wa sigara 4,313 kwa mwaka na wastani wake wa kuishi ni miaka 80...

(Hapa kengele ililia kuashiria muda wa mzungumzaji kwisha)

MHE. SAID O. NKUMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja na

ahsante sana. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Nkumba, kwa kweli leo hata mimi

nimechanganyikiwa sasa sielewi kipi kibaya. Anayefuatia sasa ni Mheshimiwa Dkt.

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

55

Kebwe S. Kebwe atafuatiwa na Mheshimiwa Silverstry Koka, tumsikilize na Daktari atasema nini.

MHE. DKT. KEBWE S. KEBWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa

nafasi hii pamoja na kwamba unanipa nafasi ya pekee kama Daktari kujibu hawa jamaa wenzetu lakini nadhani niende moja kwa moja katika hoja yangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze na usemi usemao kwamba chanda

chema huvikwa pete. Kazi nzuri ambayo inafanywa na Chama cha mapinduzi na Serikali yake na uvumilivu wake mkubwa, ni jambo la kujivunia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wana Serengeti wamenituma kusema hivi, ole wao

wanaotaka kuchafua hali ya amani, utulivu, upendo na mshikamano wa nchi yetu, wakome. Wana Serengeti haohao wanaojiita Jimbo lenye msimamo maana tangu historia ya Vyama Vingi vya kisiasa kukomaa ndani ya nchi yetu, hawajawahi kuchagua chaguo lingine mbali na Chama cha Mapinduzi, Chama mahiri, Chama imara na Chama makini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la migomo limeshazungumziwa sana lakini haya

ninayozungumza ni kukazia na ndiyo sababu mimi kama Mroma na Mkristo, amri ya sita ya kuzuia kuzini, hivi hawa Maaskofu, Mapadri na Makatekista wangeacha kuizungumzia ingekuwa vipi? Suala la migomo ni lazima liendelee kuzunguzwa kwa nguvu zote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika migomo kuna athari katika nyanja mbili, kuna

zile ambazo unaweza ukaziona kwa muda mfupi lakini kuna nyingine ni za muda mrefu mfano rahisi hapa Chuo Kikuu cha Dodoma katika mgomo ambao umejitokeza mara kadhaa athari zake zimeanza kuonekana hata mgomo huu uliotokea juzi na matokeo ambayo yametoka semister iliyopita kiwango kimeshuka. Yote hii ni kutokana na migomo ambayo imeonekana kutokuwa na kikomo, chuo kikubwa katika nchi yetu lakini chuo ambacho migomo yake imekithiri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachoiomba Serikali ijaribu kuangalia kwa umakini

uongozi na hata saikolojia ndivyo inavyotueleza kwamba ukiona kuna mgomo, hiyo ni trigger effect, mgomo hauwezi ukaanza leo na ukafanyika, kunakuwa na mtiririko wa matukio kadhaa. Kwa hiyo, hizi cumulative effects ambazo tunaziona katika migomo ikija sasa ikapata trigger effects tayari mgomo unakuwepo lakini migomo hii ukweli nao uko wazi. Jamani katika vyuo isiwe ni sehemu ya kujifunzia siasa, nasema hivi kwa sababu wako wenzetu wengine wamekwenda wanasema ‘nyie gomeni bwana, sisi tuko na nyie tutawa-support’ mbona Chuo kimefungwa juzi hawakuwa-support? Hawa wanasaidia kuua Taifa letu, wanaleta academic assassination katika Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivi kwa sababu wako vijana wengine watoto wa wakulima, watoto wa maskini wamesukumwasukumwa tu na wimbi la migomo, hawa hata nauli hawana, wamejificha kwa wenzao katika mabweni pale Chuo Kikuu cha Dodoma lakini siku ileile Chuo kinafungwa wachochezi haohao wamepeleka ma-VXs

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

56

wakawachukua watoto wao, wakawaacha watoto hawa wa wakulima wanahangaika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nachoomba vijana wetu na ndugu zetu wengine mlio Vyuo Vikuu, hawa wanapokuja kuleta lugha za uchochezi, ni suala la kuwa na msimamo. Wakati Vyama Vingi vya SIASA vinaanza katika nchi hii mwaka wa 1995 katika uchaguzi ule, maana sera ilipita mwaka 1992, wengi wetu tulikuwa Vyuo Vikuu, mimi nilitarajia kama ni hivyo wakati huo ndiyo kungekuwa na migomo kwelikweli. Leo mazingira haya ya utulivu tunafurahia maisha mazuri, uhuru, iweje kuwe na migomo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, suala hili mimi naiomba Serikali isimame

imara kabisa iwe makini kusimamia suala la migomo. Mbona wakati ule Baba wa Taifa, mgomo ulikuwa unatokea katika Chuo katika historia kulikuwa na Chuo Kikuu kimoja cha Dar es Salaam katika nchi yetu na kwa Sheria ya kuanzisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliyetakiwa kuwa Mkuu wa Chuo ni Mkuu wa Nchi, Rais, alikuwa anakwenda anasema maneno, anafunga chuo palepale ameshawapa vipande vyao. Mimi nashauri badala ya suala hili kuachiwa Makamu Wakuu wa Vyuo, Wakuu wa Vyuo waende katika vyuo, wazungumze, waseme maneno halafu wafunge chuo. Hii itasaidia kujifunza hali halisi ya mazingira ikoje pale, lakini pia itasaidia kujua undani wa matatizo haya ambayo yapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie katika sehemu hiyo ya kuasa, Mheshimiwa

Waziri Mkuu suala la parliamentary language ni lazima lifanyiwe kazi. Bunge ni chombo cha kushauri, ni chombo cha kusimamia, siyo chombo cha kutunishiana misuli. Kwa hiyo, mimi naomba katika kufunda, Mheshimiwa Waziri Mkuu hili liangaliwe upya, suala la parliamentary language, iwe language ambayo kila mwananchi anaielewa na anaweza kuifuatilia vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la njaa. Njaa imezidi nchini kwa sababu ya

unequal distribution ya transport. Haiwezekani leo hii the big five kuna mahindi mpaka yanaharibika, lakini kona nyingine za nchi ni njaa, kuna upungufu mkali kabisa wa chakula. Hivi inakuwaje leo Mwanaserengeti yule ambaye yuko Machochwe, Masinki, Nata, Isenye, Motikeri, Muongezeko, njaa inamuuma, njaa kali kabisa wakati mahindi yanaoza kule Sumbawanga? Suala hili liangaliwe upya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la maslahi kwa Madiwani. Madiwani ndiyo

Wenyeviti wa Kamati za Maendeleo, hivi huyu Diwani atakwenda kusimamia maendeleo yeye mwenyewe katoka nyumbani kwake njaa? Haiwezekani! Posho wanayopata ya shilingi 120,000/= maisha haya ya siku hizi kweli mtu anaweza kuhimili maisha? Suala hili kama ni sheria itazamwe upya, kama ni mshahara wapewe mshahara. Takwimu ambazo zilitolewa kwa harakaharaka ukichukua pamoja na wale Wenyeviti wa Vijiji, shilingi hizi bilioni 27 haziwezi kukosekana kuwapa Waheshimiwa Madiwani mshahara pamoja na Wenyeviti wa Vijiji. Wanafanya kazi katika mazingira magumu, nina mfano, nahisi Wenyeviti wawili wa Vijiji wameuawa wakiwa katika kusimamia juhudi za maendeleo ambazo nchi yetu inazionesha. Mwenyekiti wa Kijiji cha Borenga, ameuawa mwezi wa nne kwa sababu alikuwa ni imara kupambana na hawa wafedhuli wezi wa

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

57

mifugo. Mwenyekiti wa Kijiji cha Musongo, aliuawa kwa sababu ya kusimamia suala zima la wizi wa mifugo. Naomba kuishauri Serikali suala hili la msingi la malipo kwa Wenyeviti wa Vijiji pamoja na Madiwani, ilisimamie kikamilifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia haiwezekani Wakuu wetu wa Wilaya waendelee

kuwa ombaomba. Najua ni matatizo ya kibajeti, lakini Mkuu wa Wilaya anapopewa bajeti ndogo hivi anasimamiaje maendeleo? Naona kama Mkuu wa Wilaya yangu pale Serengeti, anahangaika kwelikweli. Anakwenda kukagua mashamba na wakati huohuo hana uwezo wa kwenda kuzunguka Wilaya nzima. Wilaya ya Serengeti ni Wilaya kubwa kwelikweli katika Mkoa wa Mara, ina coverage ya 52% ya Mkoa. Hivi huyu DC ambaye hana mafuta, hiyo 52% ya Mkoa wa Mara atai-cover namna gani akifuatilia masuala ya maendeleo, uhalifu na vitu vingine mbalimbali katika suala zima la utawala wa kisheria? Suala hili litazamwe upya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Mara, samahani kutumia lugha hii,

umewekwa katika gunia la maendeleo. Ukijaribu kuangalia historia, Mkoa wa Mara katika Awamu ya Kwanza ya utawala wa nchi, ilikubalika kuwa ijengwe reli kutoka Tanga kupitia Arusha kwenda Bandari ya Musoma, katika Mkoa wa Mara lakini suala hilo mimi jana nilipata faraja kwa Waziri wa Ujenzi kutoka Uganda kuja kwa ajili ya kuweka saini ya ujenzi wa reli hiyo. Hilo ni jambo la busara, lakini ukijaribu kuangalia suala la maendeleo ndani ya Mkoa wa Mara, imekuwa ni kisiwa ndiyo sababu vijana hawa hawafanyi kazi, kwa kweli watumie nguvu zao vizuri. Nilishangaa msemaji mmoja kutoka Kambi ya Upinzani anasema suala la bajeti atapunguza semina za Ukimwi, Malaria, hivi hawa vijana ambao tunataka tuwaachie wafe, mchango wao mkubwa wa maendeleo tutaupataje? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, asilimia karibia arobaini (40%) ni hawa akina mama

walio katika umri wa kuzaa pamoja na watoto wadogo walio katika umri wa chini ya miaka mitano (5). Asilimia arobaini (40%) ni sehemu kubwa kweli ya Taifa, tuwaache wafe? Ukienda katika health economics utakuta kwamba karibu asilimia ishirini na tano (25%) katika kaya zetu wanapotea kwa ajili ya magonjwa haya ya kuambukiza ikiwemo malaria na UKIMWI na hata GDP ndivyo zinavyoonesha kwamba katika nchi hizi ambazo zinaendelea ikiwemo Tanzania, 40% ya GDP inapotea katika magonjwa ya kuambukiza ikiwemo malaria. Kwa hiyo, hawa tuwaache waangamie kwa ajili ya manufaa ya watu binafsi kisiasa? Mimi nawashauri ndugu zangu waliotoa usemi ule warejee upya ili kama watapata madaraka leo hii wakaingia madarakani wajiulize hii GDP ambayo inapotea wata–cover namna gani? (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, nikijaribu kuangalia Hospitali ya Mkoa wa Mara, ina vigezo vikuu vitano (5). Ile hospitali ndiyo kituo cha kwanza cha tiba, ndiyo Zahanati, ndiyo Kituo cha Afya, ndiyo Hospitali ya Wilaya na ndiyo Hospitali ya Mkoa ambayo kwa lugha ya siku hizi tunaita ni Hospitali ya Rufaa ya Mkoa. Hospitali ile imechoka kwa sababu imejengwa mwaka 1930. Leo hii ina hali gani na kwa bahati mbaya iko jirani sana na Ziwa ni eneo chepechepe imeanza kuchoka, hakuna eneo la kutanuka. Ombi hili lilipokuja kwako kimaandishi, mimi nilitarajia kwamba kungekuwa na fedha ambayo

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

58

imetengwa kwa ajili ya hospitali hii. Hospitali ambayo kidogo wananchi walianza kujikongoja mwaka 1985 ya Kwangwa, kwa sababu sasa fursa na sera zinaruhusu kujenga Hospitali za Rufaa za Mikoa, hospitali ile ichukuliwe na Serikali ili kusudi kuendeleza Rufaa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumalizia suala la barabara, barabara ambayo vyombo vya habari vimetangaza, gazeti la Mtanzania Jumapili limetengaza kwamba ile barabara ya Serengeti haitajengwa. Mimi nafikiri kuna tatizo la kutafsiri, nasema hivyo kwa sababu ukiangalia vitabu vyetu vya Mpango na Kitabu cha Maendeleo, utaona zimetengwa shilingi bilioni 1.6, hizi hela ambazo zimetengwa ni kwa ajili ya nini? Kulipa fidia kwa wale ambao watatakiwa wapishe ujenzi au kwa ajili ya kuendelea kufanya utafiti wa kina. Mimi nashauri na natoa rai, Waziri wa Ujenzi tukifika sehemu ya Wizara hiyo basi nitatoa shilingi, aelewe kwamba mimi nitatoa shilingi kwa sababu hii barabara katika suala zima la mipango, lazima kuwe na kitu kinaitwa a locative efficiency, mipango ile unapoipanga ni lazima itegemeane na bahati nzuri katika vipaumbele miundombinu ni kipaumbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii ambayo inakadiriwa kuwa na kilomita 452

kutoka Nata – Mugumu – Tabora B – Cranes – Loliondo – Mto wa Mbu, kwa Wilaya ya Serengeti peke yake itaweza kuokoa ajira kwa makadirio ya watu 100,000. Hiyo ni kwa Serengeti peke yake, katika wadau wote ambao ni Wilaya nane (8) watafaidika na barabara hii itakuwa na manufaa makubwa kwelikweli. Pia tuelewe ndiyo njia pekee ya hawa vijana kupata kazi, tunafungua ajira kwa sababu hali ya Wilaya ya Serengeti na utalii, kuna ujangili. Ujangili ambao upo siku hizi ni wa kibiashara, siyo ujangili wa mbogamboga kama vile ambavyo tulikuwa tunafanya zamani kwa sababu tunaishi jirani na hifadhi na hawa wazee wetu wamelinda kweli kweli suala zima la hifadhi. Nashauri Waziri Mkuu atoe somo maalum juu ya barabara hii ili kuondoa uoga, ili kusudi kujenga uelewa mzuri ili wote kama Watanzania tuweze kusimamia barabara hii itatusaidia sana kuleta uchumi na kupanua miundombinu na pia kuleta ajira kwa vijana wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije katika suala zima la Hospitali ya Halmashauri.

Nashukuru Naibu Katibu Mkuu – TAMISEMI, Bwana Maswi ametembelea Hospitali ile. Mimi nimeshangaa napitia kitabu sioni hata senti tano kwenye hospitali hii. Hospitali hii tayari Serikali iliishaweka mkono, mwaka juzi ilitenga shilingi milioni 200 kwa sababu hata mwongozo wenyewe wa kutengeneza mpango mwaka huu ni kwamba, kusiwe na miradi mipya. Huu siyo mradi mpya, ni sawa na ilivyo Hospitali ya Kwangwa, siyo mradi mpya, sasa inakuwa vipi miongozo inatolewa utekelezaji hakuna? Kwa hili mimi naomba wakati wa majumuisho ya Hotuba ya Waziri Mkuu, anipe maelezo ya kina. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru, naunga mkono hoja kwa maelekezo ya

kushika mshahara wa Waziri Mkuu. (Makofi) MHE. SILVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwa

kuwa hii ni mara yangu ya kwanza kusimama kuchangia bajeti, nichukue fursa hii

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

59

kuwashukuru sana wananchi wa Jimbo la Kibaha Mjini, kwa heshima na kazi kubwa waliyoifanya na hadi leo niko Bungeni nikiwawakilisha na nataka niwahakikishie nitawawakilisha kwa nguvu zangu zote kwa ajili ya mafanikio na maendeleo ya Jimbo letu la Kibaha Mjini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue vilevile fursa hii kwa harakaharaka

kushukuru sana familia yangu, mke wangu Celina na watoto, kwa kazi waliyoifanya hadi nikafanikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hii kumpongeza Waziri Mkuu kwa

hotuba yake nzuri. Nimeipitia na bila shaka ni bajeti ambayo italeta tija katika maendeleo ya nchi yetu. Napenda nitamke awali kwa kusema ninaiunga mkono asilimia mia moja (100%). (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ofisi ya Waziri Mkuu na TAMISEMI ndicho

kichocheo kikubwa cha maendeleo kwa Mtanzania ambaye yuko kule chini kabisa ambaye kila siku tunapiga kelele kwamba hata ukuaji wa uchumi haumfikii. Utaratibu na utawala mzima umewekwa mpaka katika Serikali za Mitaa yetu pamoja na Vijiji vyetu, lakini tatizo kubwa lililopo ni namna ya utekelezaji wa mambo na mikakati mbalimbali ya Serikali kumfikia Mtanzania wa kawaida na yeye akanufaika na utaratibu huu. Nasema hivyo kwa sababu tunalo tatizo kubwa la Watendaji katika mitaa na katika vijiji. Wengi wanaokwenda kule kwanza kabisa hawakai, lakini pili mitaa na vijiji vingine havina Watendaji na huyu ndiye anayemwakilisha Mkurugenzi katika mtaa ule na tunajua mipango yote ya maendeleo ili iweze kumfikia Mtanzania wa kawaida aliye maskini ni kupitia katika Serikali zetu za Mitaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba suala hili litupiwe

macho kuhakikisha kwamba uwakilishi wa Serikali katika mitaa yetu uko pale kwa muda wote kwa ajili ya utekelezaji wa hii mipango mizuri tunayoipanga kwa ajili ya wananchi wetu. Huu ni ukweli usiopingika, tumekuwa na mipango mizuri kwa mfano MKURABITA na MKUKUTA, leo hii ukienda katika Kata ukiwauliza wananchi MKURABITA na MKUKUTA ni nini, ni wachache kabisa ambao wanaweza wakakwambia ni nini na mpango huu umewalenga wao, lakini hawaujui na wala hawafaidiki nao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutaendelea kupanga mipango mizuri ya maendeleo

lakini kama hatuangalii namna gani ya kumfikia Mtanzania aliyeko kule chini, bado majawabu ya kukua kwa uchumi wetu kumfikia Mtanzania wa kawaida yatakuwa hayapatikani. Nakuomba sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, ulitilie maanani suala hili ili tuweze kuendelea kwa pamoja. Mheshimiwa Mwenyekiti, nitajikita katika Mkoa wangu wa Pwani, bajeti hii imeutengea Mkoa wa Pwani takribani shilingi bilioni 20, ni bajeti ndogo kabisa, kutoka Mkoa wa mwisho kibajeti, tunafuatia Mkoa wa Pwani. Sasa tunajiuliza ni vigezo gani vimetumika, Mkoa wa Pwani ni ukubwa, ni utajiri au umaskini ulioko Mkoa wa Pwani ulioufanya ukapata bajeti ndogo kiasi hiki? Hilo nakuachia Mheshimiwa Waziri Mkuu

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

60

ulitupie macho, uone ni namna gani unaweza ukaongeza bajeti ya Mkoa wa Pwani kwa sababu Dar es Salaam imezaliwa na Mkoa wa Pwani na tunajua wote Pwani na hususani Kibaha sasa ndiyo next destination ya Dar es Salaam. Sasa kama hatutasukuma maendeleo kwa wingi bado msongamano ulioko Dar es Salaam wa kila namna utaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Pwani na hususani Mji wa Kibaha ni Makao Makuu ya Mkoa wa Pwani toka mwaka 1979 na hadi ninapozungumza leo hii mji huu wala haujaonja barabara ya lami na wala ukipita barabara kuu inayoenda Morogoro ukiambiwa utafute Makao Makuu ya Mkoa wa Pwani, waalah utapata shida na utahangaika. Tumekuwa na ahadi kuanzia kwa Mheshimiwa Rais, tulikuwa na ahadi ya kilomita 10 za mji baadaye ni kilomita tano lakini katika kikao cha Mkoa sasa ni kilomita nne. Wananchi wa Jimbo la Kibaha Mjini na hususan Pwani wanaomba sasa ahadi hii itekelezeke angalau hizo zilizopangwa sasa tuzipate katika Mkoa huu wa Pwani, Makao Makuu yaheshimike. Pwani ndio mama wa Dar es Salaam. Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo bado miundombinu ni hafifu. TANROAD inayo barabara moja tu tunayoitegemea ambayo sasa hivi iko katika upembuzi yakinifu. Barabara ya kutoka TAMCO kwenda Mapinga kuelekea Bagamoyo lakini bado tunazo barabara nyingi. Barabara ya Kongowe kupitia Forest kwenda Bagamoyo. Tunazo barabara zinazotokea Kongowe nyingine zinatokea Kibaha kuelekea Viziwaziwa waliko wananchi wengi wanaofanya uzalishaji wa aina mbalimbali, nazo hizi ziko bado ndani ya mikono ya Halmashauri na uwezo wa Halmashauri wa Mji wa Kibaha ni mdogo. Tunaomba Ofisi ya Waziri Mkuu itutupie macho ili barabara hizi zikabidhiwe TANROAD na ziweze kupata msukumo mkubwa wa kimaendeleo kwa maana ya ujenzi. Mheshimwa Mwenyekiti, tunalo tatizo kubwa la maji hususan katika Jimbo letu la Kibaha Mjini. Wananchi wa Kibaha Mjini wanasikitika kuona kwamba mabomba makubwa yanayopeleka maji Dar es Salaam yanapita pale lakini hawana nafasi ya kupata yale maji. Ni chini ya asilimia 40 ya wananchi wa Kibaha Mjini ambao wanaweza wakapata maji yaliyo safi. Pamoja na Mpango wa Maji ambao tunauita ni Mradi wa Wachina, lakini bado jibu la kuwapatia wananchi wa Kibaha maji halijaonekana. Mji wa Kibaha uko katika maeneo ya miamba ambayo hatuwezi kupata visima. Kwa hiyo, mipango mizuri ya visima katika maeneo mbalimbali sisi hatufaidiki nayo. Naomba utaratibu wa kutupatia maji na bomba letu kama ahadi ilivyokuwa imeshatolewa mwaka kesho utiliwe mkazo ili tuweze kupata bomba letu na tayari tumeshajipanga kupata mamlaka yetu ili kuhakikisha wananchi wa Kibaha wanapata maji na maisha bora kwa kila Mtanzania. Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la afya. Mji wa Kibaha umebahatika kuwa na Hospitali ya Tumbi. Hospitali hii imeteuliwa sasa kuwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa toka mwaka 2008 na upanuzi umeanza. Mradi wa kwanza wa jengo kubwa umekamilika, lakini mradi wa pili wa jengo lingine linalofuatia bado haujakamilika. Naona zimetengwa karibu takriban shilingi bilioni 1.3 lakini hizi pesa ni ndogo sana, hazitoshi na lililo baya kabisa mradi wa awamu ya kwanza kwa maana ya jengo la kwanza

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

61

haliwezi kutumika mpaka jengo la pili likamilike kwa maana miundombinu inayoingiliana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo kubwa tulilonalo sasa kilichokuwa Kituo cha Afya pale Mjini Kibaha ambacho sasa ndicho tunategemea kuwa Hospitali ya Wilaya, Wilaya imejitahidi, imetengeneza michoro na nashukuru sana Chama cha Mapinduzi Wilaya chini ya Kamati ya Siasa baada ya mwaka 2008 ambapo Mheshimiwa Rais alikuja akazindua kituo kile tulikubaliana kimsingi kwamba itakuwa ni Hospitali ya Wilaya na hata Chama cha Mapinduzi kilitoa kiwanja chake kilichokuwa sambamba na hiki, kiwanja cha eka moja ili kuruhusu upanuzi wa hospitali hii. Cha kusikitisha mpaka napozungumza na wewe hapa bado utaratibu wa kujenga hospitali hii haujakamilika. Halmashauri wamejitahidi kuipanua angalau akinamama wapate mahali pa kujifungulia lakini sasa Tumbi inakuwa ni Hospitali ya Rufaa bado Hospitali ya Wilaya haijakamilika wananchi watakwenda wapi kupata matibabu ya kawaida? Namwomba Waziri Mkuu atupie macho suala hili afya ziweze kwenda vizuri. Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile napenda nizungumzie matumizi bora ya fedha za Serikali. Pamoja na mipango mizuri ya Serikali tulionayo, napenda kuona kunakuwa na standards contract hasa katika Halmashauri zetu ili kuweza kuona kwamba fedha zinazotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo zinakwenda kukidhi na kufaidisha wananchi walio wengi badala ya wachache wanaopewa kazi hizi kutumia mikataba hii kujinufaisha zaidi. Nimpongeze Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa sababu ameliona hili na hakika ana mipango mbalimbali ya kuhakikisha anaboresha matumizi mazuri ya fedha za Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu kwamba hoja nyingi watu wanaparamia. Nakumbuka wakati Mheshimiwa Waziri Mkuu anazindua Mpango wa Kilimo Kwanza, ni yeye wa kwanza kusema Serikali itaangalia upya ununuzi na matumizi yake kama ya magari ili kuhakikisha fedha hizi zinapelekwa katika kilimo. Sasa leo hii tayari watu wameshadakia hoja hiyo wanasema kwamba ni ya kwao. Mheshimiwa Waziri Mkuu endelea na mipango mizuri ya Serikali. Tunajua mipango ipo ya kuhakikisha matumizi bora ya Serikali yanapewa kipaumbele chini ya Ofisi yako na sisi Waheshimiwa Wabunge tunakuunga mkono. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kwa harakaharaka hali ya uchumi. Tunataka kusukuma uchumi uende chini, uwafikie wale wananchi ambao wanalalamika, wanapiga kelele ili kuwapa majibu ya ukuaji wa uchumi wetu. Naiomba Serikali ipeleke msukumo katika micro-economy, ihakikishe inazalisha matajiri wazalendo watakaoweka biashara kubwa ambazo sasa wafanyabiashara wadogowadogo watapata biashara za kudumu. Kwa kufanya hivyo, wale wafanyabiashara wadogo hawatatangatanga, watu binafsi watapata kazi, vijana tunao wengi, pale kwangu Kibaha vijana hawana kazi. Nikuombe Mheshimiwa Waziri Mkuu utuletee miradi mbalimbali, viwanda kwa wingi, eneo lipo, Halmashauri ya Mji wa Kibaha imetenga eneo la viwanda kule Zegeleni Misugusugu linasubiri wawekezaji. Maeneo ya makazi ya kuishi tunasubiri wawekezaji, tuangalie kwa jicho la upendeleo Mheshimiwa Waziri Mkuu ili tuweze kusukuma gurudumu la maendeleo.

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

62

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tutakuza uchumi huu wa kati na wa juu nataka

nikuambie ndipo tutakapopata jawabu la uchumi unaozidi kudidimia kwa wale walio wanyonge. Hata kama tutapeleka pesa kiasi gani kwa wananchi kule chini hatutapata majibu zitaishia kwenda kusomesha watoto, zitaishia kulima mashamba madogomadogo hatimaye hata wigo wa kodi hauwezi kupanuka. Tukizalisha matajiri wazalendo hata wale wafanyabiashara wadogowadogo watashiriki katika kodi kwa maana watakuwa wanatoa huduma katika zile biashara kubwa. Haya ni mambo ya kiuchumi nina imani Wachumi na wafanyabiashara wenzangu wananielewa vizuri zaidi. Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kwa harakaharaka mabilioni ya JK. Nimshukuru Rais alikuwa na mawazo mazuri ingawa utekelezaji ulichakachua nia na madhumuni yake. Sasa niseme tufike mahali tutenge fedha kama zilivyotengwa hizi na tuwashindanishe wajasiriamali wazalendo. Najua kabisa kwamba Tanzania Private Foundation wanafanya, lakini kwa kiasi gani? Tuliangalie BBC kwa dola 5,000 wanashindanisha na leo hii wameshazalisha matajiri wangapi na inazungumzwa na inasikika kila mahali, kwa nini hii isizungumzwe, wajasiriamali wa Tanzania walio na shida ya mtaji wakasikia, wakatekeleza, nchi hii tukasonga mbele? Malaysia wametengeneza matajiri wakubwa na ndio maana wamefanikiwa, matajiri wazalendo. Kwa hiyo, Serikali isione haya kutenga fedha na kusaidia. Wako watu wenye rekodi nzuri ya kibiashara, wachaguliwe kwa utaratibu utakaowekwa ili kusukuma mbele uchumi wa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie nishati na madini. Kwa kifupi ...

(Hapa kengele ililia kuashiria muda wa mzungumzaji kwisha)

MHE. SILVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana, ninapata dakika za kumtosha sana Mheshimiwa Faith Mitambo. MHE. FAITH M. MITAMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuweza kunipa nafasi hii na mimi leo niweze kutoa mchango wangu kuhusu hotuba hii ya Waziri Mkuu.

Kwanza kabisa, naomba kuunga mkono hoja kabla sijagongewa kengele na kwamba nampongeza sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa hotuba yake nzuri na yenye kuleta matumaini makubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitachangia kwenye sekta ya kilimo, afya na muda ukitosha pia nitachangia kwenye sekta ya madini. Sekta ya kilimo imetajwa mara nyingi sana kwa kutoa misisitizo mingi, Kilimo Kwanza, Kilimo ni Uti wa Mgongo na kadhalika. Sekta ya kilimo ndiyo inayoajiri Watanzania wengi na tafiti zimeonyesha

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

63

kwamba ukuaji wa uchumi kutokana na ukuaji wa sekta ya kilimo unaweza kupunguza umaskini kwa zaidi ya mara mbili kuliko ukuaji unatokana na sekta nyingine. Sekta ya kilimo ni muhimu sana na itatekelezwa tu iwapo nyenzo kwa maana ya pembejeo zinazokamilisha kilimo hicho zinapatikana kwa wingi na kwa bei nafuu na kwa wakati muafaka. Kumekuwa na tatizo kubwa sana la pembejeo, Wabunge waliopita wengi wameongelea hili na mimi ningeomba niongelee hili kwa ufupi. Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea kuiomba Serikali sana iendelee kuangalia upya na kwa kutilia mkazo suala hili la pembejeo. Wananchi wanaumia sana. Wilaya ya Liwale ambako ninatoka, ni moja ya Wilaya ambazo zinalima zao la korosho kwa wingi sana. Mbunge mwenzangu wa Jimbo la Lulindi, Masasi, Mheshimiwa Mkapa ameliongelea hili. Wilaya ya Liwale mpaka sasa imekosa pembejeo aina ya sulphur. Wananchi hawana kabisa, wanahangaika na sasa wametokea walanguzi wanapeleka sulphur kule na wananchi wale badala ya kuuziwa sulphur mfuko mmoja wa kilo 25 kwa shilingi 18,000/= wanauziwa sasa kwa bei ya shilingi 30,000/=. Hii ni kwa sababu pembejeo hii haipatikani. Kwa masikitiko na ninamwomba Mheshimiwa Waziri Mkuu alichukue suala hili kwamba wananchi wa Wilaya ya Liwale wamekosa sulphur. Kama hali itaendelea hivyo tutegemee kabisa mwaka huu wa 2011 Wilaya ile haitapata mazao kwa maana ya zao hili la korosho kwa kiasi cha kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hii kumwomba yule Wakala wa sulphur kule Mtwara aharakishe kupeleka sulphur kwa wakulima wa Liwale kabla wakulima hawa hawajaathirika kwa kiasi kikubwa. Vile ile namwomba Mheshimiwa Waziri wa Kilimo na Chakula anisaidie kufuatilia suala hili, ili wakulima hao waweze kupata pembejeo hiyo muhimu sana kwa zao hili la korosho. Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa niongelee kidogo kuhusu sekta ya afya. Mimi naishukuru sana Serikali yetu kwa kutusogezea huduma za afya vijijini na kwa kweli Wizara ya Afya imejitahidi, lakini Wizara ya Afya inaangushwa na Medical Stores Department (MSD). MSD imepigiwa kelele mara nyingi sana ama kwa kuagiza vifaa mbalimbali visivyo na ubora, ama kwa kuagiza dawa zisizo na ubora na zenye short expiring date na kadhalika. Nashindwa kuelewa ni kwa nini Wizara ya Afya na Serikali inashindwa kufanya maamuzi magumu kuhusu Medical Stores. Hospitali ya Wilaya ya Liwale ilinunua mashine moja ya kufulia nguo za wagonjwa kutoka Medical Stores kwa mamilioni ya fedha. Mashine ile haijawahi kufanya kazi hata siku moja na hata sasa mashine ile iko pale hospitali. Mhudumu wa hospitali hii anaendelea kufua nguo kwa kutumia mikono yake wakati mashine iliyonunuliwa Medical Stores iko pale na imeshindwa kufanya kazi. Nilipofuatilia kuhusu tatizo lile ikaonekana mashine ile imekuwa imported ikiwa mbovu kama ilivyo na imenunuliwa Medical Stores. Naomba nichukue nafasi hii nimwombe Waziri wa Afya, aturuhusu turudishe ile mashine na tubadilishiwe nyingine kwa pesa zilezile na kwa gharama ileile hata kama ikiwa kubwa zaidi ya ile. Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi juzi nilikuwa Jimboni, nikafanya suprise ya kukagua jengo la Wodi ya Wazazi yaani Maternity Ward na niliyoyakuta kule yalinisikitisha sana. Kule Labour Ward kuna delivery kits ambazo ndani yake kuna vifaa

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

64

mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia akinamama kujifungua kama vile gallipots, kidney dishes, forceps, scissors na vitu vingine. Vifaa vile ambavyo vimeagizwa Medical Stores vyote vina kutu na vifaa hivi ndivyo tunavyotumia kuwasaidia akinamama kujifungua. Inasikitisha sana, Medical Stores badala ya kutusaidia sasa kupata afya njema inatuongezea magonjwa. Namwomba Waziri wa Afya na naiomba Serikali ifanye maamuzi magumu sasa kuhusu Medical Stores ili wasiendelee kupeleka vifaa ambavyo ni vibovu. Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee sekta ya madini. Wilaya ya Liwale kuna fursa hiyo ya madini. Kuna machimbo ya madini kule kwenye kijiji kimoja kinaitwa Lilombe, kuna machimbo ya Kitowelo, Wazungu wanakwenda kule, Wachina wanakwenda kule, Wathailand wanakwenda kule, wachimbaji wadogowadogo kwenye eneo hili sasa wanaonewa. Juzijuzi kumetokea fujo wanavijiji wamepigwa na Polisi na Polisi wale walipelekwa na wachimbaji wakubwa ambao wameambatana na wale Wachina na Wathailand. Naiomba Serikali tusisubiri yatokee maafa kama ya Nyamongo na sehemu nyingine, naomba Serikali na Waziri wa Madini sasa hivi wachukue hatua ya kuanza kutembelea machimbo yale ambayo yapo katika Wilaya ile na kuweza kusuluhisha migogoro ambayo iko pale. Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali kama ikiwezekana tupatiwe Ofisi za Madini katika Wilaya yetu kwa sababu wachimbaji wa madini kutoka ndani na nje ya nchi wanaongezeka siku hadi siku. Itakuwa ni vyema zaidi kama shughuli zote zinazohusu mambo ya madini na sekta ya madini kama kulipia maeneo, kuuza madini na shughuli nyingine ziweze kuendelea katika maeneo yale. Nakuomba sana kwa sababu kinachoonekana pale wachimbaji wakubwa wakishajua machimbo ya wachimbaji wadogowadogo kuna madini, wanakwenda wanalipia harakaharaka katika ofisi za madini halafu wanawanyang’anya, wanawapiga, wanawafanyia fujo na juzijuzi wamewachania hata nguo. Kumekuwa na mgogoro mkubwa kule, naomba sana Serikali iende kule kusije kukatokea tena madhara kama haya yanayotokea maeneo mengine. Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee suala la mwisho kuhusu bima. Nafikiri Shirika la Bima limeshindwa kufanya kazi.

(Hapa kengele ililia kuashiria muda wa mzungumzaji kwisha) MHE. FAITH M. MITAMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na naunga mkono hoja. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Mbunge kwa mchango wako.

Waheshimiwa Wabunge, wachangiaji wetu kwa asubuhi hii ndio hao waliochangia. Napenda niwapongeze kwa michango mizuri na niwakumbushe tu kwamba jioni wachangiaji wetu wa kwanza atakuwa ni Mheshimiwa Yusuph Nassir, atafuatiwa na Mheshimiwa Rachel Mashishanga, Mheshimiwa Ally Mohamed, Mheshimiwa Rashid Ali Omar na wengine nitawataja wakati huo.

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

65

Ninalo tangazo moja kwa kikundi kile cha Wanaharakati wa Jinsia (Champion Against Gender Based Violence) na mimi ni mmojawapo, kwa hiyo, tukutane kwenye ukumbi mdogo pale nje ya mlango huu wa kuingia Bungeni kwa muda mfupi ili tuweze kuweka mambo yetu haya ya kupambana dhidi ya masuala ya ukatili kwa akinamama na watoto. Basi kwa kuwa ndio tumemaliza wachangiaji hawa, nichukue nafasi hii kusitisha Bunge hadi saa 11.00 jioni.

(Saa 7.00 mchana Bunge lilisitishwa mpaka Saa 11.00 jioni)

(Saa 11.00 jioni Bunge lilirudia)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, jioni hii mchangiaji wetu wa kwanza ni Mheshimiwa Yusuph Abdallah Nassir atafuatiwa na Mheshimiwa Mchungaji Msigwa na baadaye Ally Keissy Mohamed. Sasa namwita Mheshimiwa Yusuph Abdallah Nassir.

MHE. YUSUPH A. NASSIR: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwepo mahala hapa. Lakini kadhalika pia kwa heshima na taadhima nimshukuru Mwenyekiti wangu wa Chama cha Mapinduzi, Mzee Athuman Magogo, aliyekuwa Katibu wetu Mama Daina Mbwayu, wana Korogwe katika kila Kata, wapenzi wa CCM na washabiki wa maendeleo bila kujali vyama vyao. Tuliitaka ridhaa na hatmaye tumeipata na sasa ni wajibu wetu kuwatumikia wananchi hao. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo machache, nichukue fursa hii kuliambia Bunge letu Tukufu kwamba, naiunga mkono hoja ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Baada ya kusema hayo machache nijikite kabisa katika kuzungumzia suala la ardhi Korogwe Mjini. Ni ukweli usiopingika tangu wakati wa ukoloni wananchi wa Korogwe Mjini walibanwa, wakapewa sehemu ndogo tu kwa ajili ya matumizi yao. Lakini sehemu kubwa ya eneo lile ikawa imezungukwa na mashamba ya mkonge na hatimaye tukapata ndugu kutoka Uyao, Kigoma na maeneo mengine. Wenyeji wa asili wa eneo lile walikuwa ni Waruvu na hatimaye tukashuka na Wasambaa kutoka maeneo ya Bungu na maeneo ya Usambara. Lakini sasa tuna ndugu wengi, tuna ndugu kutoka Lindi, Mtwara, tuna ndugu pia kutoka Kigoma na hata na Wanyamwezi. Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuzungumza hayo, ni ukweli pia usiopingika kabisa, tija katika mashamba yale ya mkonge sasa imekufa na hatimaye tumeongezewa ndugu wengine, wafugaji kutoka maeneo ya jirani ya Manyara, baada ya kuona kwamba tija kwenye mashamba ya mkonge imekufa wamefanya maeneo yale kama sehemu za malisho. Huku ikiwaacha wakazi wa eneo la Korogwe Mjini bila ya mahali popote. Nilete kwako na hatimaye Mheshimiwa Waziri Mkuu asikie, kumekwishafanyika vikao vingi vinavyohusisha suala la ardhi eneo la Korogwe Mjini na hata ahadi ya Mheshimiwa Rais ya kusema wakati umefika sasa wa kukaa na wale tuliowapa dhamana kama wawekezaji kwenye maeneo hayo tujaribu kuwaangalia kufanya tathmini ili angalau basi

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

66

waweze kurejesha sehemu ya mashamba yale tuwagawie wananchi hata kama ni kwa kuwapa fidia kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kadhalika tuwapime na uwezo wao, kwa sasa uwezo waliokuwanao pia ni mdogo. Kwa bahati mbaya zaidi wengi wa hao wamekuwa sasa ni washauri wetu wa karibu. Wakisema wao ni washauri wa kilimo. Tunawaacha watu kwenye maeneo yetu katika unyonge mkubwa, watu wamekosa mishahara, watu wamekosa maeneo ya kulima na tija hakuna, mashamba yale sasa ni machaka ya nguruwe, tunafanya nini na tunakwenda wapi? Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pamoja na kuunga mkono tuyachukue haya kama ni ushauri, tukatekeleze ahadi ile ya Rais aliyowaahidi wana Korogwe kwamba, tutapewa sehemu ya ardhi ya mashamba yale ya mkonge lakini kadhalika tuitumie fursa hii ya kutaka wale ambao wanahusika walipe haki za waliokuwa wafanyakazi katika mashamba ya mkonge. Watu wameachwa katika unyonge mkubwa na inashangaza kuona hata mtu anayedai 285,000/= mpaka leo ni mwaka wa kumi hajaweza kuzipata. Hii ni fedheha kubwa katika kuangalia mustakabali mzima wa wananchi wetu na ukitilia maanani kwamba hawa ndiyo wenye mji wao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nirukie kwenye kadhia ya maji. Tuna matatizo pale, juzi tu wakati Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI alipokuwa akijibu swali lililohusiana na maji na likahusisha maeneo ya Mgwashi na hata Milima ile ya Usambara, pamoja na maeneo ya Korogwe na kadhalika pia. Kukawa kuna taarifa ya Serikali, inayozungumzia shilingi milioni 740 ambazo zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya Korogwe Mjini tukaambiwa pia kuna mradi wa GIZ, lakini ni juzi tu siku ya Alhamis wiki iliyopita nimekuwa Korogwe Mjini tukishuhudia tena kwa draft ya mwanzo ya mradi wa HTM ambao sasa kuna cluster itakayoingia eneo la Korogwe. Lakini si hivyo tu, wananchi wa Korogwe Mjini tumekuja kupigwa na confusion nyingine inayozungumzia kuwa, sasa tunaingia kwenye Tanga cluster kwa maji ya ZIG Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nimetumwa na wana Korogwe Mjini, tuulize mradi ambao unakwenda pale Korogwe ni upi? Sasa kwa kuwa kuna draft na kwa kuwa kumetangazwa miradi mingi ya maji pia tumekuwa wastahimilivu sana kwa kipindi cha miaka kumi na tano iliyopita tukiambiwa suala la mradi wa maji wa World Bank tufikie mahali sasa tuambiwe ukweli. Sio kila siku tuna-concept ya miradi mipya na hatimaye tunaachwa kwenye giza. Kiangazi kimekwishapiga hodi, tumesimama mahali ambapo si sawa, haitafika mwezi wa Nane akinamama na watoto wataanza kuhangaika kwenye Mto Ruvu ambao nao sasa pia unaanza kupungua ukubwa wake na uwezo wake. Tunawaambia nini wana-Korogwe. Sasa hata kama kuna hiyo miradi mikubwa, nafikiri kila pale panapofanyika miradi mikubwa au palipokuwa na ugonjwa mkubwa huwa panatolewa dawa ya kutuliza. Sasa tumwombe Mheshimiwa Waziri Mkuu kwamba, wawape dawa ya kutuliza matatizo ya maji wana Korogwe Mjini. Hali haieleweki. Miradi inayokuja ni confusion kwao, tunawatia watu kwenye kizungu mkuti. Ni tatizo kubwa kwao.

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

67

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa heshima na taadhima nimesema naiunga mkono Hotuba hii na sehemu ya maswali haya ni katika kujenga tafakari na kuongeza majibu wakati patakapofanyika summation ya hotuba pale Mheshimiwa Waziri Mkuu atakapoifanya pale kesho. Tuna mambo mengi ya kuzungumza mle ndani, wakati wa kuchangia hotuba ya Bajeti tulizungumzia suala la failure zilizotokea kwenye shule zetu za Kata. Sasa nitoe kama ushauri leo kwa Ofisi ya Waziri Mkuu hasa kupitia TAMISEMI kwamba, kutengwe fungu maalum ambalo litafanya madarasa yasiyopungua manne katika kila Halmashauri madarasa haya yakatoe stadi za maisha kwa vijana wetu, aidha, iwe ujasiriamali au iwe ni ufundi mchundo, au iwe elimu yoyote itakayowasaidia kuingia mjini, itakayowasaidia kuwatoa kwenye magenge na kwenye miembe na stendi ya pale Mjini Korogwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa heshima na taadhima, hakuna mtu ambaye angependa kuona mtoto wake anachakachuka na maisha, uwe mkulima, uwe mfanyakazi au uwe mfanyabiashara. Tumesimama kidete kuwashawishi hawa watuchague, tumesimama kidete miaka hii 50 na labda niwakumbushe kwa sisi ambao tupo hapa nchi hii sasa inatimiza miaka 50, sisi tulio na umri wa miaka 50 tuna watoto na wengine tuna wajukuu. Ina maana ndani ya sisi tuna generation tatu, sikwambii wale ambao waliikuta pre-colonial au pre-independence na wana vitukuu pia. Sasa tuangalie basi suffering ambazo zinatokea kwa wananchi wetu, ina maana wanaoumia ni generation tatu. Sasa basi tusimame leo kama viongozi ambao tumepokea uongozi huu kwa mapokeo na kupigania kwa dhati kabisa maslahi ya wananchi wetu. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kuipongeza TAKUKURU, kwa kazi nzuri wanayoifanya, pamoja na upungufu mchache, niipongeze kwa sababu nimeanza kuona harakati zao pale tulipokuwa na harakati za uchaguzi mkuu. Nawapongeza sana kama kuna mahali pa kuboresha basi ndugu zangu mboreshe. Mheshimiwa Mwenyekiti, nijikite kwenye suala zima la kilimo. Nimezungumzia pale mwanzo tuwagawie mashamba wana Korogwe, lakini kadhalika kwenye kitabu cha Hotuba ya Waziri Mkuu, nampongeza sana pale alipoiingiza Tanga hasa ukurasa wa 17, 19, 27 na hata 28 na 29 na kuingiza Tanga katika mpango mzima wa kilimo, uwekezaji na hata ukuzaji. Lakini pia niseme kuna upungufu kidogo. Bajeti ambazo Halmashauri zetu inazileta, baada ya kile kipindi cha mapitio ya Bajeti huwa tunaambiwa turudi nyuma tena, tukapunguze hiki na kile. Nasema ingekuwa vema TAMISEMI wakishapokea ile first draft ya bajeti zetu kabla ya kuturudisha tukapunguze hiki na kile wapokee ile copy ya kwanza, kuna mtindo ambao ni wa Kiserikali wa kusema kuna special request mtindo huu unatuletea adha kidogo. Inakuwa kila wakati kama si Mbunge Mwenyekiti wa Halmashauri au Mkurugenzi waende wakapige magoti, miaka 50 sasa ya uhuru suala, la kupiga magoti kuomba special fund liwe ni jambo la dhiki, lakini sio kwa kitu ambacho tumekiandika kwenye bajeti na hatimaye hatukukipata. Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambo mengi ambayo tumeandika mle ndani yakiwemo gari za taka, magari ya maji machafu na mambo mengine mengi, nyumba za walimu. Ile draft ambayo tunaikabidhi kwanza Halmashauri inapoileta TAMISEMI na hata kule Wizara ya Fedha basi ipokelewe halafu waambiwe warudi watengeneze option

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

68

(b) ambayo sisi tutaitumia vizuri. Suala la special request kwa mantiki nyingine inajenga uhalali wa kujenga urafiki mkubwa kabisa. Ina maana kama sina urafiki na kaka yangu Mheshimiwa Mustafa Mkulo, Wilaya ya Korogwe Mjini haiwezi kupata special request au tutatumia muda mrefu kuipata. Inajenga fasta, fasta ambayo si rahisi kila Mtanzania, Halmashauri au kila Mbunge kuwa na access nayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuchukue hayo kama ni ushauri, lakini kadhalika nijikite kwenye sekta ya nishati. Hapa sijui nianze wapi. Lakini kuna mahali hapajakaa sawa, PSA ambazo tunazisaini sasa baina ya Serikali ya Tanzania na Wawekezaji. Kuna mahali pana upungufu, tunahitaji kabisa kuziangalia upya, tuiangalie existing Pan-Africa, tumepewa taarifa hapa, labda nimesahau kumpongeza Mheshimiwa Zitto kwa testimony aliyoitoa leo ya kuishukuru Serikali ya Chama cha Mapinduzi, pamoja na nia thabiti ya Serikali hii kuangalia Mkoa wa Kigoma kama eneo mahususi. Pan-African Energy wamekuwa na mkataba na Shirika la Maendeleo ya Petroli, lakini kumekuwa na tuzo zilizopita kiasi na hata pale basi tunapofanya mazungumzo kwamba, warejeshe kasma waliyojiongezea, mashirikiano hayapo. Sasa tuiombe Serikali, tumwombe Mheshimiwa Waziri Mkuu asimamie Wizara hii ili zile tozo ziweze kurejeshwa. Pesa za Serikali hazikopeshwi. Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi) MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi hii ili na mimi niweze kutoa mchango wangu, katika Hotuba hii ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Kwanza kabisa napenda kumshukuru Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Mheshimiwa FreemaN Mbowe kwa Hotuba yake mahiri na makini ambayo inatoa mWongozo na dira kwa Taifa letu. Nanukuu sehemu ya hotuba yake alisema: “A politician thinks for next generation, a statesman thinks for coming election.” Ni usemi madhubuti, ni usemi wenye nguvu ambao wakati mwingine kama wanasiasa huwa tunawaza uchaguzi unaokuja badala ya kufikiria kizazi kinachokuja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa bahati nzuri Baba wa Taifa alikuwa analikumbuka Taifa hili, alitujali sisi tuliokuwa watoto wakati wake, alikuwa anaangalia future. Kwa hiyo, ni wakati muafaka na sisi kama Wabunge ambao tumepewa dhamana ya kuwa viongozi katika Taifa hili, kufikiri ni namna gani vizazi vinavyokuja tunaviandaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania si mali ya wanasiasa, Tanzania si mali ya

Serikali hii, Tanzania si mali hata ya Bunge hili. Kwa hiyo nakuwa na unyenyekevu mkubwa kwamba wananchi wametupa dhamana kubwa ya kuwa sehemu ya Bunge la Kumi na tunawajibika kwa sehemu kubwa kuiacha historia kubwa kwa ajili ya vizazi vinavyokuja. Kwa sababu wakati mwingine kama wanasiasa tunajisahau tukipata dhamana hii tunadhani labda nchi hii ni mali yetu. This country is even more than Julius Kambarage Nyerere, is more than CHADEMA, is more than anybody, this country belongs to all of us. Kwa hiyo, tunapotoa maamuzi makubwa katika nyumba hii ni lazima tukumbuke Watanzania wote. Wengine wanaitwa wahuni, wengine wanaitwa wauza madawa ya kulevya, wengine wamelemewa na wakati mwingine kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo kinaitwa chama cha wahuni lakini hata hawa wahuni nchi hii

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

69

inawahusu, kwa hiyo, maamuzi tunayoyatoa katika nyumba hii ni lazima ya-accommodate kila mtu katika Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, najaribu kumnukuu Abraham Lincoln, aliwahi kusema; “If

you want to test man’s character give him power.” Anasema history inatwambia kwamba power leads to abuse of power and abuse of power leads to loose of power na George Bush mkubwa, alipokuwa anaapishwa 1989 alisema: “Hatujapewa mamlaka, ila tumepewa tu hayo mamlaka kwa jambo moja, hatujapewa mamlaka ili tutengeneze majina yetu, ili tuonyeshe show katika ulimwengu, tumepewa Mamlaka ili kuwatumikia watu”. Kwa hiyo, sisi kama viongozi tuna wajibu mkubwa wa kuwatumikia wananchi wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nijikite kwanza kwenye Ripoti ya CAG inaonyesha

kwamba kumekuwa na matumizi mabaya ya fedha katika Halmashauri zetu ambazo ni jumla ya shilingi bilioni 233 na mara nyingi CAG amekuwa akitoa ushauri ambao umekuwa haufuatwi au hautekelezwi. Tunatumia pesa nyingi sana kwenye Ofisi ya CAG na CAG amekuwa kama ni kioo, ni sawa na gari unavyoliendesha kioo kinakuonyesha njia na kwa bahati mbaya kama nilivyosema mara nyingi madaraka huwa yanawapumbaza watu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mara nyingi viongozi tunapokuwa madarakani tunapendwa kuzungukwa na wanaotusifu halafu tukaanguka badala ya kupata watu wanaotu-criticise wakatuonyesha njia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, CAG amekuwa akionyesha njia namna gani kama

Taifa twende mbele na kwa bahati mbaya kama Taifa letu ni kama spaceship ambayo imetoza flight direction haijui ikatue wapi. Kama Taifa hatuna common vision, kama Taifa hatupigani kwa pamoja na ndiyo maana tunapokuwa katika nyumba hii badala ya kujadili mambo ya maana ya kimaendeleo kwa Taifa letu tunapigana vijembe vya kisiasa ambavyo havitusaidii kwa sababu tunasahau kwamba tunatakiwa tuwe na common vision.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba ofisi ya Waziri Mkuu na Serikali kwa ujumla

kwa pamoja kama Taifa, tuwe na common vision, vitu vinavyotuunganisha kama Watanzania regardless our differences katika itikadi zetu, vituunganishe pamoja kwamba, we will speak the same language katika mambo muhimu. Tunapozungumza energy, we should speak the same language, tunapozungumza haki za raia, we should speak the same language, haya siyo mambo ya itikadi, lakini matokeo yake tunapigana vijembe hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, matumizi mabaya ambayo ripoti ya CAG

imeyazungumza, ameeleza kabisa kwamba mfumo wa accounting ni mfumo maalum unaotakiwa kutumika katika idara zote za Serikali ikiwa ni pamoja na Manispaa. Lakini mfumo huu ujulikanao kama IFMS (Integrated Financial Management System) ulikuwa deployed ili kuhakikisha integrity, usiri, availability kwa taarifa zinazotakiwa zipatikane. Vile vile mfumo huu unatakiwa ufanye kazi kwa mategemeo ya efficiency, effectiveness

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

70

na kipimo against accepted standard benchmark. Lakini kwa bahati mbaya mfumo huu katika Halmashauri zetu zote haufanyi kama ulivyotegemewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfumo huu uzuri wake ni kwamba utasababisha

matunzo mazuri ya fedha, hili siyo suala la kiitikadi. Tumeona kuna matatizo mengi katika Halmashauri zetu, iwe ni Halmashauri ya CHADEMA au ya CCM. Huu mfumo Serikali ilikuwa na mawazo mazuri, unatakiwa uungwe mkono lakini hakuna juhudi za makusudi ambazo zinalazimisha mfumo huu ufanye kazi ili kusudi pesa ambazo Mkaguzi amesema kwamba zinapotea zisipotee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna matatizo pande zote mbili, upande wa

Halmashauri zetu hawataki ku-implement mfumo huu kwa sababu unawapa loophole ya kuchota tulichonacho hiki kidogo ambacho tunataka kifanye maendeleo. Upande wa Serikali hakuna juhudi za makusudi kabisa kuhakikisha mfumo huu watu wanakuwa-trained. CAG ameshauri kwamba watu wawe trained lakini bado hawajawa trained, ningependa nijue Waziri Mkuu kwamba ni nani anawajibika kuwa-train hawa watu, ni Halmashauri zenyewe au ni Serikali Kuu. Kama wanatakiwa kuwa trained na huu mfumo utatusaidia kutunza pesa zetu nani anawajibika na mfumo huu ili uweze kufanya kazi katika maeneo yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema haya kwa uchungu mkubwa katika Manispaa

yetu ya Iringa, kuna Kata moja inaitwa Ruaha, wananchi wa Kata hii wamekuwa wakijitolea kuchangia pesa zao kwa ajili ya maendeleo lakini juzi nilifanya ziara kutembelea shule moja ya Sekondari inaitwa Tegamenda, nimekwenda katika shule ile unafika unakwangua kuta zinakwanguka tu, kuna ubadhirifu wa hali ya juu. Ukitembea na kiatu sakafu inaondoka, Milango inaanguka, wananchi hawa waliamua kupiga kelele baadaye, wakaandamana hatimaye mlisikia kwenye vyombo vya habari Mtendaji Kata aliamua kujiua baada ya wananchi kupiga kelele zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna watu ambao wanahusika na ubadhirifu huu

ambao hawajachukuliwa hatua, hakuna hatua za makusudi zinazochukuliwa ili watu wengine wasirudie. Wananchi wale wanavunjika mioyo wanapotaka kuchangia maendeleo yao wenyewe, naomba maeneo haya yazingatiwe na yatiliwe maanani. Wananchi wanapotaka kujua nani anawajibika wanalaumiwa, wanazongwa na wanaonekana wanaleta fujo katika pesa ambazo wao wenyewe wanazichangia. Huo ni mfano mojawapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Naibu Waziri, Mheshimiwa Mwanry

amekwenda sehemu zingine amekataa hizo shule zisipokelewe, naomba ukifika Iringa ukaone mambo kama haya si hadithi yapo kwenye video unaweza ukayaona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo la pili na la mwisho ningependa

nizungumzie kuhusiana na utawala bora. Ndugu zangu utawala bora tunaouzungumza ambao kwa kipindi cha hivi karibuni katika Taifa letu na mambo haya ya udini yanapandikizwa na watu ambao wana sababu zao kwa malengo yao tofauti. Wamekuwa

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

71

wakituhumu CHADEMA kwamba ni Chama cha udini, mwanzo walianza kutuhumu CUF kwamba ni chama cha udini, lakini hoja hiyo ikawashinda, watu wamekuwa wakituhumu CHADEMA kwamba ni chama cha udini hoja hiyo imeshindwa. Wito wangu, kwa heshima na taadhima, nawaomba viongozi wa kisiasa waache kuwatumia viongozi wa kidini na wasitumie dini kwa interest zao. Inapofika wakati wa chaguzi, viongozi wa kidini wakimtabiria mmoja kwamba ni chaguo la Mungu anapigiwa makofi na kushangiliwa, lakini viongozi hawa wa dini wakisema dhahabu yetu inaporwa, twiga zetu zinaporwa, wanyama wetu wanaporwa, wanasema msijiingize kwenye siasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni double standard, tuna-take advantage kuwatumia

viongozi wa dini kwa sababu ya position yao waliyonayo, tuwaache viongozi wa dini wahubiri amani, lakini wanapohubiri amani ni pamoja na kukemea maovu na naomba viongozi wa dini wawe bold, kuongea ukweli, kusimamia haki na misingi ya Taifa hili bila kuoneana aibu. Kama nilivyosema this country belongs to all of us. Hii nchi siyo mali ya chama kimoja, kwa hiyo kuliokoa Taifa hili, wanasiasa wengi wanapotaka Ubunge wanakimbilia kwenye Misikiti au Makanisa, wanasiasa wengi wanapotaka Urais wanakimbilia kwenye Makanisa au Misikiti, wanataka ku-take advantage, wanakwenda wanapeleka na michango ili ku-take advantage. Tuache Makanisa yahubiri neno la Mungu, tuache Misikiti ihubiri neno la Mungu, wanasiasa tusimamie haki na nawaomba viongozi wa dini wasimamie haki bila kumjali mtu waseme ukweli bila kumwonea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho, kuna tabia hii ya kuiomba Serikali,

kama Mbunge I am not coming here to beg, Serikali inapojenga barabara Mkoani Iringa it is not doing me a favour, this is your responsibility. Wabunge wengine wanapiga na magoti, why should I, nimekuja hapa nimetumwa na wananchi wa Iringa kuishauri Serikali na kuielekeza kwamba Iringa tunahitaji barabara, Serikali inatakiwa ifanye kazi, sihitaji kuwa na urafiki na Mheshimiwa Lukuvi ili maji yawe Iringa au na Mheshimiwa Wassira kwa sababu Serikali inatakiwa itimize wajibu wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaposimama hapa Mawaziri mtimize

wajibu wenu na sisi kama Wabunge tubweke, tuwaambie hamjaleta maji, tuwaambie hamjajenga barabara, tuwaambie madawati hayapo, huu ndiyo wajibu wetu siyo kuja kuwapigia magoti ninyi. Wabunge wengine wanafika mahali hapa wanaijibia hoja Serikali, hii ni hoja ya Waziri Mkuu, tunategemea Waziri Mkuu atatujibu yeye. Kama Mbunge anajibu angekuwa Waziri Mkuu lakini tunaye Waziri Mkuu mmoja nchi hii, ambaye ni Mheshimiwa Pinda na ndiye tunategemea atatujibu hoja hizi. Kwa hiyo, naomba Wabunge tushikamane kwenye hoja za msingi, ni wajibu wetu kama Bunge kuisimamia Serikali, kuikemea, kuishauri, siyo kuipongeza hata mahali ambapo haijafanya. Serikali inapaswa itimize wajibu wake ili kuleta maendeleo kwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu ndiyo wajibu wa Mbunge, hatujaja hapa kuisifu

Serikali, tairi langu kwenye gari linapozunguka sina sababu ya kulisifu kwa sababu liliwekwa kwa kazi hiyo, sina sababu ya kusema Serikali naiomba ilete maji wakati ni wajibu wake. Serikali mnakusanya kodi, mnachukua kodi kwa wananchi, mnatakiwa mpeleke maji, mpeleke barabara siyo lazima ni bend kwa Waziri ndiyo maji yaje, wajibu

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

72

wangu ni kupiga kelele hapa kwamba, Mheshimiwa Shukuru Kawambwa madaftari hakuna kule Iringa, vitabu havijafika, Mheshimiwa Ngeleja umeme hakuna huu ndiyo wajibu wangu. Kupiga kelele kwamba umeme haupo ndiyo wajibu wangu, siyo kuja hapa kusema naiomba Serikali ni kutokutimiza wajibu wako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwanafalsafa mmoja anaitwa Dkt. Mazman Raw

anasema: “Whenever purpose is not known or discovered existence has got no meaning”, kama hatujui wajibu wetu kama Wabunge, kama hatujui Bunge lina kazi gani, kuwepo kwa Bunge kutakuwa hakuna maana, hebu tulifanye Bunge letu liwe live mpaka wananchi huko saa zingine wasitupe lawama bila sababu, kwa sababu wajibu wetu ni kuisimamia Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mbunge sitakiwi kuwa rafiki wa Serikali kwa sababu

Serikali haitafanya kazi vizuri, kama una biashara ya mabasi ukitaka upate mavuno mchonganishe kondakta na dereva, hela itakuja, kwa hiyo, ninaomba tushikamane.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante sana Mchungaji Msigwa, sasa nitamwita Mheshimiwa

Ally Keissy Mohamed na baadaye Mheshimiwa Rashid Ali Omar ajiandae. MHE. ALLY KEISSY MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti ahsante sana.

Awali ya yote namshukuru Spika kwa kuongeza muda wa kuchangia hotuba ya Waziri Mkuu kwa sababu bila kuongeza muda nilikuwa kwenye list ambayo nisingeweza kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti awali ya yote nazungumzia suala la maji Namanyere,

Namanyere maji yamekuwa ni mazungumzo ya siku nenda, rudi. Ahadi ya Rais Mkapa ya kupatiwa maji ilikuwepo, pia Rais Kikwete naye ameahidi maji lakini katika bajeti safari hii Namanyere hakuna maji. Mtandao wa maji ulikuwepo tangu enzi ya Namanyere ni kijiji enzi ya Mwalimu, tulikuwa tunapata maji ya bomba lakini tangu Mwalimu alipoondoka na maji ya bomba Namanyere hakuna. Wananchi wa Namanyere wanapata maji asilimia kumi na sita, mimi mwenyewe kama Mbunge hapa nimekaa siku tatu bila kuoga Namanyere, cha ajabu Serikali hii inajenga bwawa la mtu binafsi kwa gharama ya bilioni moja tisini na mbili milioni kwa ajili ya mifugo yake, leo unasema watu hawapati maji Namanyere wakati pesa zipo, wamejenga bwawa kubwa kabisa pale Kawa, Kijiji cha Nkundi bila ya Serikali ya Mkoa kufahamu, bila Serikali ya Wilaya kufahamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Maji hili suala nitalipeleka kwa Okampo,

achunguze hawa waliokwenda kujenga bwawa Namanyere walitoa wapi pesa, bajeti gani ilihusika, kusema kweli napata uchungu sana kwa Serikali yetu, wananchi hawana maji lakini mifugo ya baadhi ya watu inapata maji, sasa kujenga kwenye ranchi ya mtu binafsi bwawa la bilioni moja tisini na mbili milioni, wakati Namanyere hakuna maji hata ya kunawa, kusema kweli Serikali itasema inawatendea haki wananchi hawa?

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

73

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nawapa pole sana wananchi wa Namanyere wana shida kubwa, hatupati maji, mimi kama Mbunge huwa nakwepa kupita sehemu za visima, naona aibu akinamama wanavyopigania maji. Sasa Serikali inajali wananchi, ina masikio inasikia, ina macho inaona kilio cha wananchi? Hatuji hapa ndugu zangu kupiga makofi, hatuji hapa kuja kula posho za bure, tumeletwa kwa nguvu za wananchi. Nimekuwa nikigombania Ubunge miaka mingi kwa ajili ya kutatua matatizo ya Wilaya ya Nkansi, lakini hili limekuwa gumu, ni lazima lipate ufumbuzi, hili ni tatizo. Kama kuna uwezekano tupunguze idadi ya Wabunge, tupunguze idadi ya Viti Maalum, ili wananchi wapate manufaa. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati wa Mwingereza na wakati wa Mkoloni

kulikuwa na Majimbo nane na Serikali ilifanya kazi wakati barabara zilikuwa mbaya, lakini Serikali ilikwenda. Leo tunasema nyota ya kijani, punguzeni uzazi, lakini Serikali haisikii, yenyewe ndiyo inazusha Majimbo, inazusha Wilaya, inazusha Mikoa, sasa tutakwenda wapi, wakati huo Serikali haina pesa? Bila kupata ufafanuzi kutoka kwa Waziri wa Maji kuhusu tatizo la maji sitakubali, nitaondoa mshahara wake, sitakubali kushawishika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimezungumza kikao cha kwanza hapa kuhusu pesa za

Rada, nikaomba pesa za rada angalau zitatue kidogo matatizo ya maji Namanyere, lakini zinapangwa zote katika elimu. Kwanza zile pesa tumepewa bure, tulikuwa tumeibiwa, siyo zetu. Dola milioni 30 zimeibiwa na wale walioiba humu Watanzania wapo wangapi, walioandika huo mkataba tuwajue, tunyang’anye hata mali zao, majumba yao yauzwe na kila ktu ili tupate maji Namanyere. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie habari ya kilimo. Sisi tumekuwa

wakulima wazuri sana, lakini kila mtu akisimama hapa kwenye Wilaya yake anasema kuna njaa, apelekewe mahindi ya bure na mengine auziwe shilingi elfu tano. Lakini watu wa Nkansi walikuwa vibarua wanadhalilishwa, wakisema wanaambiwa wewe umepewa barabara ya lami. Hii barabara japo tumepewa lakini tumecheleweshewa. Hata hivyo, ni haki yetu tupewe barabara ya lami, kwani hatuna haki ya kupata barabara ya lami? Ni Wilaya ngapi zina barabara ya lami hapa, kigezo mmepewa barabara ya lami, hicho siyo kigezo ni haki yetu tupate barabara ya lami kama wengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkulima analima, jana nimesikia kwenye TV, kidogo

nivunje TV, nilitaka kumvamia DC yupo kwenye TV, nikafikiri yupo karibu yangu, DC wa Mkoa karibu na Dodoma hapa, anazuia wananchi wasiuze mahindi shilingi elfu kumi na tano debe, anagawa pikipiki anazuia wakulima wasiuze elfu kumi na tano kwa debe, anataka wakulima wauze debe shilingi elfu mbili, hawaonei huruma wakulima, tena DC mwenyewe ni mwanamke, Kondoa hapo. Nilitaka kuvamia TV baadaye nikashtuka hii ni TV. Anaona uchungu wakulima wapate shilingi elfu kumi na tano kwa debe, yeye hajui tabu ya kilimo. Mnachelewa kupeleka hata mbolea za pembejeo kwa Mkoa wa Rukwa mnapeleka wakati mvua zimeshaanza kunyesha, sasa huyo Mkulima ndugu zangu atawekaje reserve ya pesa?

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

74

Mheshimiwa Mwenyekiti, mnashindwa hata kuwajengea ma-godown, mahindi yanalowana ovyo, sasa tunakuja kupongezana hapa! Sisi ndugu zangu! Hatujaja kupongezana hapa. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunahitaji mtufanyie maendeleo katika Wilaya yetu ya

Nkasi, pelekeni mbolea kwa wakati, wasaidieni wakulima kwa kuwapa bei nzuri ya mazao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa waliofanya utafiti wa power tiller tunataka

tuwajue, leo power tiller imekuwa kama scape tupu katika nchi nzima, hela ya Serikali ya kigeni imepotea na hizi trekta mlizoleta zimelima wapi na nani kazifanyia uchunguzi? Tunataka tufahamu hizi trekta zilizoingizwa nchini kwa mamia ya trekta tujue zimefanyiwa uchunguzi nchi gani, tusiwatwishe wakulima wetu bidhaa ambazo hazijafanywa uchunguzi na hatujui zina ubora gani. Tunataka tujue zimelima nchi gani, tunaleta matrekta hatujui hata aina yake. Siku mbili inakuwa mambo ya kutafuta spare parts ambazo hata hazipatikani, wakulima wanapata shida katika nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nichangie kuhusu suala la afya. Namanyere

Wamishionari wamejenga Kituo cha Afya kizuri sana cha Masista kinaitwa BAKHITA lakini hakina msaada wa Serikali, Chuo cha Manesi, manesi wanapohitimu pale wanasambaa nchi nzima, lakini Serikali haiwasaidii, wameelemewa, wanapata wanafunzi wengi lakini hakuna msaada wowote wa Serikali. Wamejenga majengo mazuri ya ghorofa, hatukuwahi kuona maghorofa Namanyere kwa mara ya kwanza tumeona pale, lakini Serikali haichangii, naiomba Serikali iwasaidie wale wamisionari kwenye kile Chuo cha BAKHITA, Namanyere.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la UKIMWI, ndugu zangu UKIMWI

umetengewa pesa nyingi sana, imetengewa bilioni tisini mia tatu hamsini na sita milioni mita tano hamsini na saba elfu na mia sita tisini na tano. Ndugu zangu UKIMWI ni ugonjwa wa kujitakia sisi wenyewe, ni nani asiyejua UKIMWI nchi hii, unaufuata mwenyewe, hizi pesa zote za nini unazitenga kwenye UKIMWI, wakati Kansa imetengewa bilioni mbili na mia tano milioni, gonjwa ambalo linaingia kwa mtu yeyote tu, lakini UKIMWI unautafuta mwenyewe na nani asiyejua madhara ya UKIMWI katika nchi hii. Achieni wenyewe wenye UKIMWI wakitaka kufa wajifie wenyewe, wanautafuta wenyewe, hizi pesa pelekeni kwenye maendeleo ya wananchi, pelekeni kwenye maji, pelekeni Namanyere hizi pesa. Serikali inachangia kuendeleza UKIMWI, Ali Keissy amekufa kwa UKIMWI siku ya mazishi mnasema amekufa kwa ugonjwa wa moyo au kafa kwa kisukari. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi pesa zote zinaishia kwenye posho, wanachezea tu

pikipiki sisi tunawaona, watu wanaohusika kwenye miradi hii, wamejenga majumba, nina ushahidi, siji hapa Bungeni kusema kitu ambacho sina uhakika nacho, Waratibu wa UKIMWI wote wana majumba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niende katika suala la Bima ya Afya. Hili ni bomu

lingine, tusidanganyane, wenye maduka ya madawa wanauza mara tatu ya bei kwa Bima

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

75

ya Afya na mtu mmoja anakwenda asubuhi na jioni kama anaumwa anaandika bili tu kwamba Bima ya Afya italipa, hii Bima ya Afya ichunguzwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee kuhusu vitambulisho vya Taifa.

Nimezungumza mara ya kwanza kuhusu vitambulisho vya Taifa, hili ni janga la EPA lingine linaingia katika hii, nashauri ipewe Wizara ya Mambo ya Ndani moja kwa moja suala la vitambulisho. Serikali inunue mashine na wawape Wizara ya Mambo ya Ndani moja kwa moja, au Shirika la Posta, kumpa mtu binafsi au kutoa kwa shirika la mtu binafsi hii ni hatari na ni bomu lingine. Hii ni nchi ya fununu hii, pana fununu fununu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile nichangie katika suala la uvuvi. Hakuna kazi

ngumu duniani kama uvuvi, wavuvi wa Ziwa Tanganyika wana kazi ngumu lakini unakuta mvuvi anatakiwa awe na license, nyavu ilipiwe license, mtumbwi ulipiwe na kuna samaki wengine hawakui kwa ukubwa, lakini unakuta maliasili hawana habari. Wanawanyanyasa wavuvi, wanawadhalilisha wavuvi, naomba hizi license za wavuvi ndugu zangu ziondolewe. Mbona mkulima hana license, kondakta hana license, utingo hana license, huyo mvuvi akiingia tu watatu wanne wote wanakuwa na license wamekosa nini kwa Mungu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie sasa kuhusu suala la barabara. Jana

nilimwuliza Waziri kuhusu barabara haijafika bandari ya Kipira amenijibu, mimi nauliza mbili na mbili unatakiwa unijibu nne, mbili na mbili ukiniambia tano nitakubali wapi? Nina ushahidi na mimi ndiyo Mbunge wa kule, Serikali inapoteza bilioni 1.2 kutengeneza bandari lakini barabara inaishia kilomita saba haifiki bandarini. Sasa hii Serikali inakuwa ya kudanganyana, tunakuja kusifiana tu hapa, hamna kusifiana, tunahitaji barabara ifike kwenye bandari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna vijiji vya mwambao wa Ziwa nimelalamika hapa,

havijaona gari tangu uhuru. Lakini hakuna hata utafiti kumtuma mtu kustuka kweli watu kule hawajaona barabara, hata radio hawasikii wanasikia Radio za Congo. Hawana habari hata Radio Tanzania inatangaza nini. Mimi mwenyewe napita kule kwa mguu nasikia radio, radio gani, Radio Moba. Sasa inakuwa Tanzania au Congo. Hawana barabara hata radio hawasikilizi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii barabara ya Itindi-Kibaoni ni ahadi ya Waziri Mkuu mwenyewe na yuko hapa hapa, aliahidi watu wa Itindi kwamba atajitahidi ijengwe, namwomba hii barabara aisimamie mwenyewe Waziri Mkuu. Liazumbwi, Kabwe barabara inatengenezwa wakati wa mvua, nina maana hawa watu TANROAD, wakiona mvua ndio wanatengeneza barabara kuiba hela za Serikali tu na wanaifinya barabara. Sehemu mbaya hawatengenezi, wanatengeneza sehemu zile nzuri nzuri tu. Sasa hapa hii nchi tunakwenda wapi? Ukiuliza tatizo, unaambiwa tumepewa barabara ya Tunduma, Sumbawanga, ukisema, unaambiwa nyie mmeshapewa barabara ya lami, ile haki yetu tupewe. (Makofi/Kicheko)

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

76

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee suala la mafuta. Wabunge wengi walishangilia hapa tuagize kwa pamoja mafuta. Sijui wamezungumza na wale Maharamia wa Kisomari. Wakiteka meli nchi hii itakuwa na mafuta hii? Muwe mnafikiri, mnaona mbele. Tuagize kwa pamoja, watu ehee, tuagize kwa pamoja, Maharamia wakiteka ile meli tutakuwa na mafuta Tanzania? Acheni kurukia mambo, kama mmezungumza na Maharamia tujue. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kampuni moja inayoweka mark, inachukua kwa

mwezi dola milioni 500 lita moja shilingi 6.5. Nchi hii tunakwenda wapi? Inatia mark kwenye mafuta tu. Sasa mafuta ya taa, diesel bei moja mark ya nini? Inachukua 500,000 kwa mwezi, hiyo kampuni ilikuwa inatia mark Kenya, Kenya wajanja wakawa wanailipa mita moja dola 0.49, sisi tunailipa dola 3.6, angalia sisi tunavyoibiwa mchana kweupe ingekuwa usiku tungeibiwa zaidi ya hii. Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mizani na kila lita ya mafuta shilingi mbili. Sasa ndugu zangu tuangalie tunakwenda wapi? (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu posho, naona hii itaondoa udhia sana, nataka

ndugu yangu kwa heshima na taadhima waliochukua posho Jumamosi na Jumapili majina yao yaandikwe kwenye vyombo vya habari, hapa udhia utakuwa umekwisha. Kelele zitakuwa zimekwisha, watajulikana kwa kila mtu. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu ndio huo, naomba Serikali itufikirie

sana, wana Nkasi itusaidie kote nilikosema.

(Hapa kengele ililia kuashiria muda wa mzungumzaji kwisha) MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Mbunge, muda wako umekwisha. MHE. ALLY KEISSY MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono

hoja. (Makofi/Kicheko) MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Ally Keissy Mohamed, Mbunge wa

Nkasi Kaskazini.

TAARIFA MHE. JUMA SELEMANI NKAMIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka

kumsahihisha kidogo mzungumzaji aliyemaliza sasa hivi rafiki yangu Mheshimiwa Keissy kwamba, Wilaya ya Kondoa haina Mkuu wa Wilaya, anayekaimu ni Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bwana Gembe huyo siyo mwanamke. Kwa hiyo, alitaka kuvunja TV kwa sababu ya mwanamke huyo aliyemsema Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, inawezekana aliangalia vibaya. Ahsante.

MWENYEKITI: Kwa kuwa na TV yenyewe hakuvunja taarifa ameshaipata.

Tunaendelea. Mheshimiwa Rashid Omar.

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

77

MHE. RASHID ALI OMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napenda nitoe shukrani zangu za dhati kwa nafasi hii adhimu kabisa niliyoipata siku ya leo ili niweze kuchangia hotuba ya bajeti ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Awali ya yote, kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa dhati kwa kunijalia leo hii katika ndoto zangu za muda mrefu nilizokuwa nazo za kutaka na mimi niwe mmoja katika Chama changu kushiriki katika masuala ya kuitetea nchi yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, narudia kwanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu,

kwa kuweza kuipata nafasi hii adhimu ambayo ilikuwa imo katika ndoto yangu ya muda mrefu ili na mimi nishiriki kikamilifu kuwatetea Watanzania wenzangu popote walipo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, shukrani zangu za dhati ziende kwa majemedali

wangu Wakuu wa Chama cha Wananchi CUF (The Civic United Front) kwa umahiri na ujasiri mkubwa wa kuweza kusimamia shughuli za kisiasa katika hali ya kukamata usukani wa ujemedari wa kuweza kudumisha hali ya amani na utulivu katika nchi hii ya Tanzania. Ni majasiri wakubwa wa kusimamia shughuli nzima au sera nzima ya amani na utulivu ukitoa vyama vingine vyote vya kisiasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitakuwa mwizi wa fadhila kama sikutoa shukrani

zangu za dhati kuwashukuru wananchi wa Jimbo la Kojani kwa kusimama kikamilifu kuitetea hadhi hii ya kisiasa ndani ya mfumo wa Vyama Vingi na nafasi ikapatikana katika upande wetu, upande wa Chama cha Wananchi, CUF kutokana na ujasiri wake mkubwa katika eneo lote la Zanzibar. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kutoa shukrani zangu za dhati hizi vile vile,

napenda niwashukuru watoto wangu walioungana nami katika kuwa na subira kubwa ya shughuli hii nzito ya kisiasa hadi kufikia kuikabidhi nafasi hii ndani ya mikono yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka nielekeze suala hili la uchangiaji wa Bajeti

ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, katika vifungu vifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa, nataka nijikite juu ya suala la amani na

utulivu. Suala la amani na utulivu hatuwezi kuvunja shukrani au hatuwezi kuacha kukishukuru Chama cha Mapinduzi na Serikali yake kuongoza kwa amani na utulivu. Lakini kwa upande wangu nataka kidogo niilaumu Serikali hii mnayoitambia na kusema kuwa ni Serikali ya Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, suala hili naomba Bunge hili Tukufu

lishuhudie usemi wangu huu kwa fikra zangu ilivyo sasa, ningeomba usemi huu wa kuwa hii ni Serikali ya Chama cha Mapinduzi, kidogo mtulize na kidogo muweke upande. Hii napenda niwaeleweshe rasmi wenzangu watani wetu wa Chama cha Mapinduzi, ni kuwa Serikali hii ni Serikali ya Wananchi wa Tanzania kwa ujumla ingawaje uongozi wa madaraka haya uko kwenu lakini tulivyoapa hapa tulipokuja tukaanza kuapa, tuliapa sote tuliomo humu katika Bunge hili kuwa tunaiapia Serikali ya Jamhuri ya Muungano, japo

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

78

kama inaongozwa na Chama cha Mapinduzi, lakini mkileta sura hii ndio sura ambayo mara nyingi sana inaleta ubabaifu ndani ya Bunge letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maana hiyo, ningeomba Serikali yetu hii ya

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, iache kujigamba sana, iache kufanya majigambo makubwa suala hili ndilo linaloletea kuleta mtafaruku humu Bungeni. Kwa sababu nimechunguza kwa muda mrefu kabisa, katika kujifunza kwangu nimeona kwamba utatanishi wote huu unaotokea wa mabishano ya kisiasa humu, unaanzia katika Chama cha Mapinduzi kwa sababu kujitapa kuwa ni Serikali yao peke yao hili wanasiasa wenzetu hawa humu waliomo hawataweza kustahimili. Kwa hiyo, naishauri Serikali, kupitia Wizara yako hii majigambo haya kidogo yapungue ili tupate uwiano wa pamoja tufanye kazi na Bunge letu hili liwe Bunge moja, liwe Bunge la uamuzi mmoja, bila kuingiza masuala ya ukiritimba wa kisiasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa suala hili ninalolizungumzia hivi sasa, naomba

niendelee na mada yangu ya amani na utulivu. Kwanza nataka nielekeze hoja yangu kuhusiana na masuala ya maandamano. Maandamano naona hiki ni kitu halali ila tu yamegawika katika sehemu mbili, kuna maandamano yanayoruhusiwa ambayo ni ya amani na kuna maandamano yale yasiyoruhusiwa ambayo yanaweza kusababisha machafuko ndani ya Taifa letu hili. Ninachokiona hapa kwa fikra zangu watu wa CHADEMA au watu wa CUF au chama kingine chochote cha upinzani hakina imani rasmi ya kufanya maandamano yao katika hali ya utulivu na amani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo linalosababisha, tusifichane na

tusidanganyane, tukawababaisha Watanzania, wenzetu, Serikali hii inasimamia mambo kinyume na haki. Maandamano ni haki yetu. Lakini kinachosikitisha Chama chochote cha Upinzani kama kina maandamano hayo yanabidi yalindwe na vyombo vya ulinzi na usalama. Lakini la kushangaza wenzetu wa Chama kinachotawala na kusema kuwa ni Serikali inayoongoza wanapotaka kufanya maandamano hawana haja hata ya kupitia katika hivyo vyombo vya ulinzi, wenzetu wanafanya tu, hiyo ni uhakika kabisa. Kama taarifa watatoa tu kwa maana kuwa wanatekeleza sheria. Lakini si kweli hawawezi kusimama wakafanya maandamano hayo kwa kupitia haki ile inayopatikana. Kwa sababu Wapinzani na wao wanapotaka kufanya maandamano hawakusudii kufanya maandamano ya kuleta fujo. Kwa sababu nina imani vyombo vyetu vya ulinzi vilivyopo vinaweza kusimamia maandamano wakati wowote isipokuwa kwa vile ni Vyama vya Upinzani vinanyimwa fursa ya kufanya maandamano hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hapa, kupitia Wizara ya Mheshimiwa Waziri Mkuu,

namwomba kwa unyenyekevu kabisa suala la amani na utulivu liwe linatuhusu Watanzania au liwe linahusu vyama vyote. Mara nyingi sana tunapotaka kufanya maandamano Vyama vya Upinzani tunaiomba Serikali kwa heshima zote, lakini ukiangalia sehemu kubwa ya sisi Wapinzani tunapoomba ruhusa ya kufanya maandamano kwa heshima na taadhima lazima kutakuwa na kutolewa na dharura hizi na ili kupinga hatua hizo za kufanya maandamano kwa Vyama vya Upinzani.

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

79

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa namwomba Mheshimiwa Waziri Mkuu, kupitia Hotuba hii ya Bajeti, suala hili liangaliwe vizuri sana. Uvunjifu wa amani unasababishwa na mambo haya yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupoteza haki za kila mtu, haki za kila mtu zikipotezwa

amani lazima ipotee. Kama Serikali itasimama kikamilifu kutekeleza haki kwa pande zote nina imani hakutakuwa na machafuko yoyote. Si CHADEMA, si CUF, si NCCR Mageuzi, sote tumo ndani ya kusimamia ulinzi wa Taifa letu kwa pamoja. Nina imani hatutavunja sheria yoyote isipokuwa wenzetu hamturuhusu kuitumia haki hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nisipoteza muda, wenzangu wengi

wameshayazungumzia masuala haya. Sasa naelekeza kuhusu masuala ya maendeleo. Maendeleo ya nchi yetu kweli yapo na Serikali kweli inatekeleza shughuli hizi za maendeleo ya Chama cha Mapinduzi. Lakini kinachotusikitisha, wananchi hawapewi nafasi au hawana uhuru wa kuzitumia rasilimali zao za nchi hii. Ukizingatia Tanzania ni nchi iliyo na rasilimali nyingi za kuweza kukuza maendeleo ya watu lakini ukiangalia siku hadi siku maendeleo ya watu yanashuka. Isipokuwa tunajitapa kwa maendeleo ya vitu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nieleweshwe katika Bunge lako hili Tukufu,

kwamba maendeleo ya kweli hata Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, nakumbuka alizungumza kauli hii, akasema, maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu na siyo maendeleo ya vitu. Kupatikana kwa ujasiri mkubwa wa kuwa tuna maendeleo ya watu hayaonekani kama tukiwana maendeleo ya vitu na haiwezi kuonekana juhudi yoyote kama hatujapata maendeleo ya watu. Asilimia kubwa ya wananchi wa Tanzania ni wakazi walioko vijijini. Hawa ni watu wanaotegemea kilimo kwa kuendesha maisha yote kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa. Ninavyoamini kama tutajielekeza kwa wananchi ambao ni asilimia kubwa walioko vijijini kama watapewa fursa ya kutumia haki zao za rasilimali walizonazo, wataweza kuendesha maisha yao bila tatizo lolote na Serikali badala yake itashughulikia masuala mengine yanayohusika. Lakini kutokana na kunyimwa haki ya wananchi kuweza kutumia rasilimali zao kutokana na mwenendo mbaya wa uchumi, hili linasababishwa kuwarudisha nyuma wananchi wetu vijijini na hata mijini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninavyokumbuka kilimo kinachukua sehemu kubwa

katika nchi yetu hii ya Tanzania, kama ndio uti wa mgongo wa uchumi wetu. Sasa ukiangalia kila mtu anayesimama katika microphone hizi hapa Bungeni anasikitika na njaa. Njaa, njaa hiki kinasababisha ukosefu wa mipango bora. Kama tutaweza kupewa ruhusa ya kutumia rasilimali zetu tulizonazo, ardhi pamoja na misitu tuliyonayo hii ya hifadhi zetu, basi naamini Tanzania itakuwa ya mwanzo duniani itakayoondokana na matatizo ya janga hili la njaa. Ila hili linasababishwa na ukiritimba wa Serikali uliopo wa kutowapa fursa ya kuzitumia rasilimali hizi wananchi walioko vijijini na badala yake kunyimwa haki ya msingi. Wananchi walio vijijini mara nyingi sana wanataka watumie maeneo yao kwa njia ya kujipatia maslahi lakini utaona kwamba Serikali inawaingilia kati kwa mambo mbalimbali. Mara wanaambiwa wanazitumia rasilimali hizo vibaya, mara mgawanyo wa ardhi haueleweki, wanaingiliwa kati. Sasa kuhusiana na suala hili ni

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

80

suala moja ambalo linarudi pale pale kwenye kutokea uvunjifu wa amani katika nchi yetu. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria muda wa mzungumzaji kwisha) MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge, kengele ya pili hiyo. MHE. RASHID ALI OMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Mbunge, sasa nitamwita

Mheshimiwa Mpina. MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa

kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia Bajeti ya Waziri Mkuu. Nasimama kwa majonzi kutokana na kifo cha Katibu wa Wazazi wa Wilaya ya Meatu ambacho kimetokea jana. Nawatakia wanachama wote wa Chama cha Mapinduzi, wana Meatu wote pamoja na familia ya ndugu Likebuka aliyekuwa Katibu wa Wazazi Wilayani Meatu, wawe na moyo wa subira. Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya marehemu. Amina.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa wananchi wangu wa Jimbo la Kisesa

najua mnani-miss lakini kwa sababu ya majukumu makubwa mliyonikabidhi, haisikiki? Lakini ni kwa sababu ya majukumu makubwa mliyonikabidhi ambayo niko hapa nayatekeleza na kama nilivyowaahidi kuwa sitapumzika hadi maendeleo ya kweli yapatikane katika Jimbo la Kisesa na hapa naendelea kusema Mawaziri nao hawatapumzika hadi maendeleo ya kweli yapatikane katika Jimbo la Kisesa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekuwa tukiendelea na harakati za maendeleo katika Jimbo letu na wananchi wangu niendelee kusisitiza kwamba sera yetu ile gosha sheri gosha ntugi, gosha goru gocha nchezi bado tunaiendeleza hapa Bungeni, lakini mwisho maendeleo Kisesa lazima yapatikane. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee pamba. Napenda kumjulisha Mheshimiwa

Waziri Mkuu kwamba mpaka sasa hizi kuna mgomo wa wanunuzi wa pamba kununua pamba katika Mkoa wa Shinyanga na hii ni kutokana na gharama kubwa zilizopandishwa za makato ya Cotton Development Trust Fund kutoka shilingi kumi na tano mpaka mia mbili kama alivyokuwa amechangia Mheshimiwa Ahmed asubuhi. Kwa hiyo, hii imepelekea gharama kubwa sana kwa wanunuzi, kununua pamba. Lakini vile vile imepelekea kupunguza fedha za mkulima kwa shilingi mia moja. Mnunuzi analazimika kuchangia shilingi mia moja, mkulima naye katika bei ile anatakiwa kuchangia shilingi mia moja. Kwa hiyo, kwa jumla inakuwa shilingi mia mbili kutoka shilingi kumi na tano za mwanzo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi na-appeal kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu,

naomba atoe tamko la kwamba shilingi kumi na tano zilizokuwa zinachangiwa katika mfuko huo, ziendelee kuchangiwa hizo shilingi kumi na tano. Shilingi mia moja zile alizokatwa mkulima arudishiwe badala ya bei kuwa shilingi elfu moja mia moja kama ilivyo sasa, basi iwe shilingi elfu moja mia mbili kama ilivyokuwa. (Makofi)

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

81

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee pia vijiji vya kandokando ya hifadhi.

Naomba kulisema hili na naiomba sana Serikali yangu isikie, wananchi wanaoishi kandokando ya hifadhi wanapata matatizo makubwa sana na hii ni kwa sababu mipaka hii iliwekwa zamani, watu wameongezeka lakini na mahitaji mengine kama ya kilimo nayo yameongezeka. Wananchi wanateseka, wananchi wangu wa vijiji vya Semu, Bugalabanya, Mwamashimba, Butuli, Matale, Mwasengera, Mwamwongo kila siku ni kukamatwa na game, kila siku ni kulipa faini game, wengine mpaka sasa hivi wamefilisika na hawana alternative, mito yote iliyoko katika Jimbo la Kisesa ambao wao wangekwenda kunyweshea mifugo iko ndani ya hifadhi, hawana alternative wapate wapi maji yakunyweshea mifugo yao, lakini katika vijiji hivyo Serikali haijachimba lambo hata katika kijiji kimoja. Kata za Jimbo la Kisesa ziko nane na Kata nne zote ziko kwenye mtandao wa hifadhi, kwa hiyo, hawana alternative, hawana sehemu za kupata malisho ya mifugo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa wananchi ndiyo waliotupa kura, hawa wananchi

ndiyo waliompa Mheshimiwa Rais kura, Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wa Chama cha Mapinduzi, hivi inatosha tu leo wanakamatwa, wanafungwa, wanawekwa lock up, wanafilisiwa ng’ombe zao kwa sababu kwa bahati mbaya au nyingine wameingia mle kwa ajili ya kunywa maji? Lakini Serikali yao inashindwa kuchukua hatua za binafsi, inashindwa kuchukua hatua za makusudi, hali inayosababisha wananchi hawa wapate maeneo ya malisho ya mifugo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali yetu lazima ijue kuwa hata hawa ng’ombe ni

rasilimali muhimu sana. Wale watu ambao hawana mifugo katika nchi ambazo hazina mifugo wanasali kwa Mwenyezi Mungu kila kukicha wapate mifugo, tumejaliwa na Mwenyezi Mungu rasilimali hii, lazima nayo pia tuithamini. Namwomba Mheshimiwa Waziri Mkuu, kuna mtu amekaa karibu na Kiongozi anamsimulia mambo mengine, lakini naomba Waziri Mkuu asikie hili ninalolisema, ni kilio kikubwa sana kwa wananchi wa Jimbo la Kisesa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge, Waziri Mkuu ana masikio mengi sana.

Kwa hiyo, wewe ukisema yeye anakusikia tu. MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Mwenyekiti, limezungumzwa vizuri

suala la Madiwani, suala la Wenyekiti, nililizungumza wakati nachangia hotuba ya Waziri wa Fedha, nawashukuru Waheshimiwa Wabunge wameliunga mkono vizuri sana, wamelisikia vizuri sana na nimeshamwambia Waziri Mkuu kupitia hotuba ya Waziri wa Fedha lakini mpaka hata kwa kumfuata, kumsisitiza kwamba, tatizo kubwa ambalo linaninyima usingizi ni hawa viongozi muhimu kutokupatiwa maslahi yanayolingana na majukumu yao, Wenyeviti wa vijiji, Madiwani, nikasema Waziri Mkuu wetu anafanya mambo mangapi makubwa ya nchi hii, atashindwa wapi kulipa Madiwani 4,451 ambao kwa mwezi ni bilioni 2.2 tu, Wenyeviti wa Vijiji 11,817 ambapo malipo yao kwa mwezi mzima ni bilioni 3.6, mara kumi na mbili ni bilioni 43.6 kwa mwaka mzima, anaweza. Sasa tumeshaongea, tumeongea kiurafiki, nimechangia na hapa Bungeni kilichobaki ni

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

82

kukamata tu mshahara wake pale itakapofikia sasa Serikali imeshindwa kuzingatia maslahi ya viongozi hawa muhimu kabisa kwa Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile nizungumzie suala la nishati na madini.

Serikali yetu imefanya makubwa, nishati na madini, miradi mikubwa ya Mikoa sita MCC imetekelezwa, lakini Kisesa, kaka yangu Ngeleja hapa tulishikana mashati katika bajeti ya mwaka 2008 ambapo kila siku Serikali ilikuwa ikiahidi kupeleka umeme kwa wananchi wa Jimbo la Kisesa, leo niishukuru sana Serikali, nimshukuru sana Mheshimiwa Ngeleja kwa hatua za makusudi alizozichua, leo hii ninavyozungumza nguzo zimeshafika Kisesa, vifaa vyote vimeshafika Kisesa, mradi wa zaidi ya bilioni 1.5 na hapo ni Jimboni, watu walikuwa wanazungumza kule nyuma umeme kupeleka Mikoani, Wilayani, leo tunazungumza umeme umekwenda kwenye Jimbo la Kisesa, Jimbo tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Solwa, zaidi ya bilioni nne zimekwenda na yeye vifaa

vyote viko site na sehemu zingine zote na bahati nzuri tulisimama na Mheshimiwa Ahmed hapa kwa kweli hatukujali Ngeleja ni nani, hakuna cha kaka, hakuna cha mdogo, lakini umeme uende Solwa, umeme uende Kisesa, namshukuru ametekeleza hilo, hongera sana kaka yangu na shukurani sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijatoka kwenye suala la nishati na madini

niombe sasa umeme huu vijijini, umeme unaotokana na solar, tusambaze kwenye shule zetu ambazo kwa sasa haziwezi kufikiwa na umeme wa grid ya Taifa. Pale Kisesa kuna shirika linaitwa ICS, limesambaza umeme vijijini, limepelekea wananchi umeme bure, sasa wanapata umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilipongeze shirika hili na niiombe Serikali ili-support,

kwanza, lisambaze umeme Kisesa kuhakikisha kwamba kila mji mpaka hata zile nyumba za matende nazo ziwake umeme, halafu baadaye sasa shirika hili liweze kutoa misaada hata kwenye Wilaya zingine mpaka Solwa huko kwa Mheshimiwa Ahmed unahitajika umeme kama huu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niongelee barabara hasa barabara za vijijini.

Tunasema kila siku kwamba tunapeleka umeme vijijini, lakini bajeti yetu imebaki ile ile ya kutoka kwenye Road Fund ambayo haitengenezi barabara, inakarabati barabara zilizopo, sasa tutajenga lini hizi barabara za vijijini? Wananchi wangu wana mateso makubwa, nilisema jana asilimia 70 ya wananchi wa Jimbo la Kisesa hawajawahi kutumia barabara toka Mungu aumbe dunia. Kwa hiyo, sasa leo bilioni 94 zilizotengwa nchi nzima, bilioni 94 kuchonga barabara za vijijini, tutajenga lini hizi barabara za vijijini? Tuamue kwa makusudi, tutafute fedha za kutosha, tukachonge barabara tumalize tatizo la barabara vijijini, wananchi wangu wa Lingeka, Mwaburutagu, Mwamwongo, Mwasengera, Mwanga wana mateso makubwa, pia wa Mwakisandu, Mwanindwa, Mwamashimba, Nyanza, Nambugalamanya, Nasebu wote hawajawahi kuona barabara toka Mungu aumbe dunia. Sasa kufikia mwaka 2015, naomba Jimbo la Kisesa lipitike kila mahali na nchi nzima Tanzania tuchonge barabara za kwenda katika kila kijiji. (Makofi)

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

83

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hayo, sasa niongelee barabara ile ya Mugumu

inayopita kwenye Mbuga ya Serengeti imekubalika kwamba ile mbuga haitajengewa tena lami kwa sababu zile kilomita 53 hazitajengewa lami, sasa kwa sababu tuna barabara ambayo ni alternative na ipo siku zote na wataalam wameipendekeza muda mrefu, ile barabara ya kutoka Lamadi kuja Bariadi na bahati nzuri kutoka Lamadi kuja Bariadi sasa hivi ni lami, sasa kutoka Bariadi uje Kisesa, upitie Mwandoya unyoke uende mpaka Meatu, utoke Meatu uende Mangola uende Karatu. Tutengeneze barabara hiyo sasa ili iwe alternative na ile barabara ambayo hatuwezi kuiimarisha ikawa highway kama ilivyokuwa imependekezwa, ijengwe ya lami wataalam wetu wataunganisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichangie sasa katika suala la maji. Kama nilivyosema

katika maji naomba suala moja tu, sasa hivi upembuzi yakinifu pamoja na ujenzi wa mradi wa maji umefika Maswa kama nilivyouliza swali la nyongeza asubuhi. Maswa kwenda Kisesa ni kilomita kama 35 tu. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri wa Maji, naomba sana sasa upembuzi yakinifu uanze wa kutoka Maswa kwenda katika vijiji nilivyovitaja vya Mwabusaru pamoja na Makao Makuu ya Jimbo la Kisesa pale Mwandoya ili waweze kupata maji safi ya kutoka Ziwa Victoria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, kuna swali ambalo nimekuwa nikiliuliza kila siku na halijapatiwa majibu kwamba, katika taarifa ya global financial integrity yenye topic inayosema a least financial out flow from Africa. Inasema hivi: “Tanzania imepoteza trilioni 11.6 kwa kipindi cha miaka 39, sasa taarifa ile ilifikiwa baada ya kupitia account za wahusika walizopeleka fedha kule nje ya nchi. Serikali imeifanyia kazi vipi taarifa hiyo na ni taarifa muhimu kwa sababu hata kwenye mpango wa maendeleo wamei-site. Sasa trilioni zile 11.6 zinapatikana kwa account number na zinapatikana kwa majina ya wahusika, Serikali imeifanyia kazi vipi taarifa hiyo ya global financial intergrity ya 2008.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naunga mkono hoja. (Makofi) MWENYEKITI: Nakushukuru Mheshimiwa Mpina kwa mchango wako mzuri,

sasa nitamwita Mheshimiwa Rosweeter Faustin Kasikila na Mheshimiwa Ritta Kabati ajiandae.

MHE. ROSWEETER F. KASIKILA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami pia natoa

shukurani zangu nyingi kwa kupata hii nafasi ya kuzungumza maana ni adimu kwelikweli. Lakini pia niwashukuru watoto Evelyn na Joyce ambao muda wote wamekuwa peke yao nyumbani wakati nikiwa nje kwenye shughuli za kikazi ila nawashukuru kwa sababu wana moyo wa uvumilivu na wananielewa kwamba niko kazini. Pia niwashukuru wanawake wa Mkoa wa Rukwa, mimi ni viti Maalum Rukwa kwa kuwa walinichagua kwa kura nyingi sana hata kuniwezesha kufika mahali hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe pongezi nyingi sana kwa Waziri Mkuu na timu

yake yote kwa hotuba hii nzuri waliyoiandaa, hotuba ambayo ina mwelekeo, lakini

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

84

imegusia sekta zote na inaleta matumaini kwa kweli kwa wananchi wa Tanzania wote walio mijini na hata vijijini. Hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ina vipengele vingi sana, lakini nitagusia vichache nikianzia na kipengele hiki cha 86 ambacho kiko chini ya Katiba na Sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipengele cha 86 katika hotuba ya Waziri Mkuu

kinazungumzia kwamba katika 2010/2011, Bunge lako Tukufu lilipitisha Sheria ya Kuanzisha Mfuko wa Mahakama, kuanzishqa kwa Mfuko huo kutaongeza uwezo wa kiutendaji na kuleta ufanisi katika Mahakama zetu nchini. Lakini anaendelea kusema ni imani yangu kuwa kutokana na juhudi hizi za Serikali, Mahakama itaboresha utendaji wake na kutoa huduma bora kwa wananchi hasa kupunguza mlundikano wa kesi zilizoko Mahakamani. Kwa kweli nasifu, nashukuru na napongeza hili wazo la kuwa na Mfuko wa Mahakama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni taratibu katika nchi kwamba kila Wilaya iwe na

Mahakama ya Wilaya, lakini kuwepo na Mahakimu wanaohudumia hizi Mahakama za Wilaya na idadi inakuwepo kulingana na idadi ya watu wanaozunguka Mahakama hii, lakini pia umekuwa ni utaratibu kwamba kila Kata iweze kuwa na Mahakama ya Mwanzo na Mahakimu wake wa Mahakama ya Mwanzo, lakini taratibu hii imekuwa kidogo inasuasua kwa sababu Mahakama za Wilaya ni chache lakini Mahakama za Mwanzo ndiyo zimekuwa chache sana. lakini majengo hayo yaliyopo kwa kweli ni machakavu sana na ni mabovu kwa kiwango kwamba hata kama Hakimu anaendesha kesi na mvua imeanza kunyesha, inabidi asitishe hiyo kesi ili waweze kukimbia kwa sababu watalowana. Kwa hiyo, nina imani kabisa kwamba, Mfuko huu wa Mahakama unakwenda kutengeneza au unakwenda kufanya ukarabati kwenye majengo yaliyo mabovu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Mkoa wetu wa Rukwa, Mkoa mzima una Kata

sitini na nne, kwa hiyo tunataka tuwe na Mahakama za Mwanzo 64, lakini Mahakama za Mwanzo tulizonazo ni saba tu, kwa hiyo tuna upungufu wa Mahakama za Mwanzo 57 na tuna Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo 12 na hivyo pungufu ni 52. Lakini tuna Mahakama moja tu ya Wilaya, Wilaya ya Nkansi hawana Mahakama ya Wilaya. Kwa takwimu chache hizi unaweza ukaona ni jinsi gani wananchi wa Rukwa wanavyopata shida. Mahakimu wa Mwanzo inawabidi watembee kilomita nyingi sana kwenda kutatua kesi ambazo hazina Mahakimu wa Mwanzo, lakini pia hazina Mahakama za Mwanzo. Watatembea au wanakodisha pikipiki au baiskeli kwenda kilomita 80 au 90 kwenda na kurudi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati mwingine mshtakiwa huyu ambaye pengine

Baraza la Kata limeona kwamba kesi yake ni ya kwenda Mahakama ya Mwanzo, mshtakiwa au mlalamikiwa wanafika kiasi cha kukata tamaa kwa sababu hawawezi wakaenda kote huko na hawana hata pesa za kukodisha pikipiki au baisikeli. Kwa hiyo, ni imani yangu kabisa kwamba, Serikali itaujali Mkoa wa Rukwa ili wananchi wa Rukwa wasiwe ni wa kutembea kilomita nyingi kuhangaika kwenda kutatuliwa kesi zao, au mara nyingine inafika kwamba wanakata tamaa, wana-surrender wanasema basi siwezi, tukizingatia kwamba mwananchi wa Rukwa ni mchapakazi, ni mkulima, ebu tuwasaidie

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

85

tuwafikishie huduma hizi hapo walipo, maana nia ya Serikali kusema kwamba kila Kata iwe na Mahakama ya Mwanzo ilikuwa ni kuwapunguzia wananchi misafara mirefu ya kutembea, lakini pia ni kuwasogezea huduma za Mahakama pale walipo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mahakimu kwa kweli hawana mishahara ya kutosha,

mishahara yao ni midogo sana, ni vizuri kuwaongezea mishahara, lakini hata posho wanazodai zilizolimbikizwa ni vizuri wakapewa. Wapewe mishahara mizuri ili angalau waweze hata kukopa kidogo kujenga nyumba, Hakimu kupanga nyumba kwa kweli ni hatari tupu hasa pale ambapo hakimu yuko peke yake. Utakuta labda mwenye nyumba ndiyo mhalifu au ndiyo ana kesi, lakini Hakimu anayesikiliza hiyo kesi ndiyo mpangaji wa huyu baba mwenye nyumba, kwa hiyo inapofika wako Mahakamani sasa inabidi Hakimu na mwenyewe nyumba waangalie kwanza dakika kumi, mambo yatakuaje. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Hakimu atafanyaje, hawezi kuanza kusikiliza

kesi ya baba mwenye nyumba wake, lakini ni hatari na hapo haki inaweza isitendeke, hamna justice hapo kutakuwa na biasness, lakini watu hao wangekuwa na mishahara mizuri kidogo wangeweza kukopa wakawa wanakusanya tofali kidogokidogo wakajenga na hela nyingine, home taking ikawa nzuri wakaendelea kula. Lakini pia tunaona kwamba wangeweza kukopa wakanunua hata vyombo vya usafiri, kwa Hakimu kuingia kwenye gari, public transport na mtuhumiwa ni hatari. Mtu anaweza akachomwa hata kisu cha kichinichini bila kujijua. Kwa hiyo, hebu tuwafikirie Mahakimu wote waongezwe mishahara, nina imani kwamba Mfuko huu utakwenda kuwasaidia. Lakini Mfuko huu utakapokuwa umefanya kazi, utapunguza milundikano ya kesi, lakini sio kesi tu, hata wafungwa Gerezani itapunguza, kwa sababu itabidi watu waelimishwe. Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa tumeona kwamba Wizara ya Afya wamejitahidi kuelimisha wananchi, na wananchi hao wanaelimishwa kwenye ngazi ya vijiji mpaka kitongojini mpaka kwenye kaya. Watoto lazima wapelekwe clinic kwenye chanjo. Wajawazito waelimishwe umuhimu wa kwenda kujifungulia hospitali na ndiyo maana hapa tunaona vifo vinavyotokana na vizazi vimepungua, lakini vifo vya watoto wachanga vimepungua. Sasa basi Wizara ya Katiba na Sheria wana mpango gani kuwa na Maafisa Ugani kwenye Kata? Kwa sababu ukienda kwenye Kata utawakuta Extension Officers wa Kilimo, community development (watu wa afya) wanaelimisha mpaka ngazi ya kijiji, wanaitisha wananchi kwenye mikutano ya hadhara na mtendaji anawaitisha wananchi na mambo mbalimbali yanafundishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Katiba na Sheria wangeweza na wao kuwa na utaratibu huu wa kuwa na Extension Officers wao (wanasheria) kwenye Kata ili hawa Extension Officers wafundishe sheria mbalimbali. Wananchi wanahitaji kujua mambo mengi sana. Kuna Sheria nyingi sana zinazowazunguka, haki za binadamu, lakini hawazijui. Hapa tunakuwa na utaratibu wa ku-amend sheria, ku-amend sijui sera sijui kitu gani. Lakini hata hizo za mwanzo kabla ya kuwa amended wanazifahamu wananchi? Zipo sheria mbalimbali, Sheria ya Ardhi, Sheria ya Ardhi ya Vijiji, Sheria ya Ndoa na Sheria ya Mirathi. (Makofi)

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

86

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi hapa Mheshimiwa Samuel Sitta alikuwa anajibu masuala ya mirathi. Lakini mirathi inapokuwa imeandikiwa wosia haina tatizo. Haichukui muda, mwezi mmoja, miezi miwili mahakamani mambo yameshakuwa tayari, hamna tena mlolongo. Kwa hivyo tungekuwa na extension officers wa Idara ya Sheria au watakaoweza kutoa hizi huduma au watakaoelimisha wananchi huko vijijini wakajua Sheria. Sheria zikijulikana na wananchi hata kesi mahakamani zitakuwa chache. Hata magerezani wafungwa watakuwa wachache. (Makofi) Kuna Mheshimiwa mmoja hapa juzi alisema alikutana na mfungwa akamuuliza kulikoni wewe upo hapa? Akasema nilikuwa napita mahakamani nikapiga kelele. Haa! Sikujua kuwa ni kosa, lakini yumo gerezani. Ni vitu ambavyo wananchi wangefundishwa tusibaki na sheria hizi, tukawa tunazijua sisi wenyewe tumezikariri, unazungumza kitabu kizima chenye kurasa 40, sijui kurasa 400 Sheria iko kichwani, lakini wananchi hawajui chochote, tunakuwa hatuwasaidii. Mimi nilikuwa naomba kuwe na utaratibu wa extension officers wanasheria waende huko. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu nizungumzie suala la afya kidogo. Upungufu wa dawa na vitendea kazi au vifaa tiba hospitalini, hapa tunazungumzia masuala ya MSD. MSD kwanza mimi nawapongeza. Lakini nawapa pole kwa sababu wana kazi kubwa sana. Wametwishwa hiyo kazi lakini kukataa hawataki. MSD ndiyo wanaohudumia nchi nzima how can it be? Ndiyo maana MSD dawa nyingi zinazoagizwa na MSD ni out of stock. Hapa tumesikia watu wanasema hamna drip stand kwao, delivery beds na nini. Dawa zikienda kwenye zanahati na vituo vya afya katika wiki mbili zimekwisha isha. Lakini huwezi ukaagiza items 100 MSD unaletewa items 12 tu, the rest ni out of stock ni kwa sababu wako peke yao. Nilikuwa naona solution wangetafutiwa na counterpart mwingine wakawa wawili ili waweze kusaidiana. MSD peke yao hawawezi. Mheshimiwa Mwenyekiti, mwanzo walikuwa wana-push system ikashindikana. Wakaanzisha pull system kwamba sasa watumishi wawe wanaagiza dawa kulingana na mahitaji yao. Kulingana aina ya dawa zinazotumika kwenye sehemu zao za kazi, lakini hata hiyo imefeli. Mnaweza mkaagiza unaletewa dawa ambazo hukuagiza. Kama umeletewa ulizoagiza ni chache sana au ni nyingi sana. Zingine tulikuta kondomu zimejaa huko Kasanga wakati hawakuziagiza. Lakini mimi niliwauliza mlicheki expiring date? Inawezekana ilikuwa ni dumping place kule, ili kule kuonekane kusafi. (Makofi) Mimi nilikuwa naiomba Serikali ilitilie maanani hilo, suala la MSD limezungumzwa miaka na miaka na miaka. Vikao mbalimbali, mikutano ya wakubwa mbalimbali yamezungumzia suala la MSD. Waendelee kuwepo, lakini wasaidiwe na hii ndiyo inasababisha hata wajawazito, wazee waliopata msamaha, sijui wenye magonjwa sugu waendelee kununua dawa kwenye maduka ya dawa kwa sababu ya out of stock kila siku na hizo out of stock tunapokuja tuagize sasa kwenye maduka ya watu binafsi ni

Page 87: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

87

sheria na taratibu za manunuzi ya umma haziruhusu, wakati mzazi amekuja na high patension inamuua huyu. Lakini dawa tuliyoagiza MSD ni out stock, tunakimbilia kwenye dawa binafsi tusubiri sheria na taratibu za manunuzi ya umma. Tunaomba liangaliwe hilo, watu wanakufa sana. Ndiyo maana sasa mtu akiambiwa dawa hii umeandikiwa nenda kanunue. Hawezi kununua mwananchi dawa za siku tano, ananunua za siku mbili tu na ndiyo usugu unavyoendelea, hatimaye tunakimbilia kwa Babu kwa sababu ya usugu tu. Naomba hili Wizara iliangalie suala hilo. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee kuhusu barabara. Rukwa tunashukuru barabara tumepata, Tunduma – Sumbawanga, Sumbawanga – Mpanda na Sumbawanga – Kasanga barabara inajengwa sasa. Mimi na umri huu tulikuwa tuhangaika porini, inafika mahali tunaacha basi tunatembea kwa mguu. Lakini sasa hivi magari, barabara inachimbwa tena kwa upana mzuri tu, very soon tutakuwa tuna-slide na sisi kwenye lami. Isipokuwa nilikuwa naomba zile barabara ambazo Wabunge wangu wamezungumzia za Nkasi, naomba zitiliwe maanani kwa sababu mimi kama Mbunge wa Viti Maalum zinanipa shida sana, ninapokwenda kutembelea akina huko. Kuna barabara ya Nkana - Kate, Kitosi – Wampembe, Namanyere – Ninde, lakini kuna ya Kalambanzite - Ilemba. Tulikuwa tunaomba chonde pamoja na kwamba tunatengenezewa hizi barabara ndefu ambayo itapita mabasi huko wanakopitisha machela kubeba wajawazito tunaomba na huko watengeneze. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu mimi mara nyingi nikienda kutembelea akinamama, imebidi nisitishe safari, nimemkuta mzazi anazaa hapo, inabidi nikae nigeuze, nisiendelee. Nianze kumhudumia huyu mama mzazi. Ni muhimu sana barabara hizo, tunaona ni ndogo sana, lakini zitiliwe maanani ziweze kutengenezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mawasiliano. Tunawashukuru watu wa Vodacom, Tigo na Airtel kwa minara waliyoleta kwetu. Lakini mawasiliano (network) kule Lake Tanganyika haiwezekani kwa sababu huwezi kuwasiliana na mtu aliyepo Wampembe au Ninde saa hizi, yeye aamue kuwasiliana na wewe. Lakini atakapoamua kuna vichuguu huwa wanakwenda kupanda, akapande kichuguu ndiyo aweze kupata network au akapande juu ya mti, mwanamke anaenda kuparamia mti, anatafuta network ili aweze kuwasiliana na wewe. Tunawashukuru watu wa Vodacom, lakini tunawaomba, ukisema unaomba ni lugha ya kistaarabu tu, huwezi kulazimisha lazimisha, wakikataa utawafanya nini? (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, tunawaomba waende wakaturekebishie network. Naunga mkono hoja kwa asilimia mia kwa mia. (Makofi)

Page 88: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

88

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kukushukuru wewe mwenyewe Mwenyekiti, kwa kunipa nafasi hii. Nichukue nafasi hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu ambaye ameweza kuniwezesha kufika katika Bunge hili. Vile vile niwashukuru sana wananchi wa Iringa na hasa akinamama kwa kura zao nyingi walizonipatia ambazo zimeweza kunifikisha hapa nilipo. Naomba niwaahidi kwamba sitawaangusha na kura walizonipatia hawatazijutia. Nimpongeze pia Mheshimiwa Rais na Wabunge wote wa Chama cha Mapinduzi. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia nichukue nafasi hii kumpongeza Waziri Mkuu kwa hotuba yake nzuri ambayo amewasilisha hapa Bungeni. Kabla sijaanza kuchangia hotuba yangu kwanza nichukue nafasi hii kumshukuru sana Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Madiwani wote wa Manispaa ya Iringa kwa ushirikiano wao ambao wamekuwa wakinipatia kila siku na vilevile kwa kazi nzuri wanayoifanya. Nilikwenda Iringa kwa kushtukiza nikajaribu kupita katika barabara, nikakagua na nikakuta kwamba barabara zipo safi na mji upo safi. Mji wa Iringa ni wa pili kwa usafi. Kwa hiyo, naomba niwapongeze sana Madiwani wote bila kujali itikadi ya vyama. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijaanza kuchangia hotuba hii, naomba kwanza niwaambie wananchi wa Iringa leo hii tupo hapa kwa ajili ya kuwasilisha matatizo yao. Kwa hiyo, naomba wawe tayari kusikia nini tunamwambia Waziri Mkuu na nini tunaomba Serikali hii itufanyie katika Mkoa wetu wa Iringa. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze hotuba hii kwa kuchangia kuhusu daraja la Igumbilo lililopo katika Kata ya Ruaha. Tarehe 9 Juni, 2011 nilileta swali hapa Bungeni linalohusiana na daraja hili. Kwa kweli daraja hili ni kero, ni kero kubwa sana kwa wananchi wa Kata ya Ruaha. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri mwenye dhamana alijibu kwamba daraja lile upembuzi yakinifu inatakiwa kama bilioni 1.09 na uwezo wa Halmashauri wa kujenga daraja hilo ni mdogo sana. Kwa kweli naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu atambue kwamba wananchi wa Kata ya Ruaha wapo takribani 4002 wakiwemo wanafunzi wa shule ya Ugumbilo kama 955. Kuna Chuo pia cha Maendeleo chenye wanachuo kama 2,200 na daraja lile tayari limeshaleta maafa kwani kuna wanafunzi watatu wameshafariki. Kwa hiyo, naomba jambo hili lizingatiwe. (Makofi) Nilipojaribu kumwomba Mheshimiwa Waziri, kwa sababu niliona kama majibu yake anasema kwamba kuna maombi mengi sana zaidi ya mia moja, nikamwomba kama ana uwezo wa kumwomba Waziri wa Ulinzi tupewe daraja la dharura. Kwa hiyo, bado naomba aidha, tupatiwe daraja la dharura. Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi yeye ameolea Iringa, kwa hiyo najua kwamba atalichukua na ataliangalia kwa jicho la huruma. Naomba pia alichukue hilo na alizingatie kwamba pale kuna ndugu zake. (Kicheko/Makofi)

Page 89: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

89

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naomba kama hili halitazingatiwa niko tayari hata kushikilia hata vifungu katika mshahara wa Waziri Mkuu siku itakapopitishwa ili nijue kwamba suluhisho ni nini katika hili daraja. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo napenda kuwasilisha hapa Bungeni ni kuhusiana na mradi wa umwagiliaji wa Mkoga. Huu mradi uko katika Kata ya Isakalilo. Kata hii kabla haijahamia katika Kata ya Manispaa ilikuwa katika Halmashauri ya Iringa. Mradi huu umeshatumia nguvu za wananchi nyingi sana. Mradi huu umeshatumia pesa ya Serikali na sasa hivi mradi huu unasuasua. Zinahitajika kama shilingi milioni 380 ili mradi huu uweze kwenda. (Makofi) Kwa hiyo, naiomba Serikali iangalie kwa uzito ili mradi huu uweze kuendelea. Kwa sababu sasa hivi umesimama. Pia tuna mradi kama huu katika Kata ya Kitwilu (Kitwilu Irrigation Scheme). Huu mradi pia bado unasuasua, nguvu ya wananchi imetumika nyingi sana na fedha za Halmashauri zimeshatumika nyingi sana. Kwa hiyo, mradi huu unahitajika kama shilingi milioni 335 ili uweze kuwasaidia wananchi. Kwa hiyo, naomba hii miradi yote miwili ya umwagiliaji iangaliwe ili wananchi wale waweze kupata maisha bora. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, wanasema kwamba moyo usiokuwa na shukrani hukausha mema yote. Naomba leo hii niishukuru sana Ofisi ya Waziri Mkuu, nimshukuru Mheshimiwa William Lukuvi, Mbunge wa Jimbo la Ismani. Kulikuwa kuna Kata ya Nduli ambayo imetoka katika Jimbo lake, ilikuwa ina matatizo ya njaa, lakini nilipokuja hapa nikamwomba Waziri Lukuvi, nikamwomba Waziri wa Kilimo, hawakusita, walitupatia chakula kile cha msaada na wananchi wale wa Nduli wanakushukuruni sana. Lakini naomba wajue kwamba chakula kile ni kidogo, kwa hiyo, nitakapokuja tena kuwaombea naomba wasisite kuwapatia kwa sababu tatizo bado liko pale pale. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa hilo nalo uliangalie kwa uzito wake. Pia naomba nitoe pongezi kwa ujenzi wa majengo ya polisi pale Kilwa Road. Yale majengo kweli yana hadhi ya askari wetu. Lakini sasa hebu njooni Iringa, majengo ya polisi ni matatizo makubwa sana. Mimi toka nazaliwa nayakuta yale majengo yako vilevile, hayajabadilika, familia ya watu wengi inakaa kwenye chumba kimoja. Hawapati hadhi kama inavyotakiwa. Ninaomba Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani aje Iringa aone jinsi wananchi wale wanavyoishi kwa shida. Mimi naomba tu nimuahidi kwamba naweza hata nikatoa posho zangu zote tukaweka katika helikopta mimi na yeye tukaenda na tukazunguka, tuzunguke tuone jinsi wananchi wale wanavyopata shida. (Makofi) Vile vile Wilaya ya Kilolo ni Wilaya mpya lakini haina majengo ya ofisi za polisi, haina majengo ya kuishi askari. Kwa hiyo, pia hilo liangaliwe ili yaweze kujengwa hayo

Page 90: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

90

majengo. Naomba pia nimpongeze Waziri na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu kwa kutatua tatizo la shule ya Efata. Shule ile ilikuwa na matatizo makubwa sana kiasi kwamba wanafunzi wa pale walikuwa wameshakata tamaa na shule ile ilitaka kufungwa. Shule ile watoto walifanya vurugu kubwa sana. Lakini mimi nilipokwenda pale nikaongea nao, nikapeleka matatizo haya kwa Waziri wa Elimu na Naibu Waziri, baada ya siku tatu namshukuru Mungu Tume ilitumwa ikaenda katika shule ile tatizo lile likatatuliwa na sasa hivi shule ile kuna amani na nakumbuka walikuwa wamenipigia simu kwamba nitakapokwenda Iringa basi wanipokee kwa maandamano, nikasema hapana. Kaeni, someni, hiyo ndiyo furaha yangu. Kwa hiyo, niwashukuru sana Wizara ya Elimu kwa kazi kubwa walioifanya. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo la vijana. Tumekuwa tunawatumia sana vijana katika mambo mengi. Katika maandamano tunawatumia vijana, tunawatumia vijana katika kampeni zetu. Naomba Wabunge wote wanaofanya kazi ya kuwatumia vijana hawa hawasaidii, naomba iwe mwisho sasa hivi. Vijana wale tunapowatumia basi tukumbuke na kuwasaidia. Lakini naomba Halmashauri zetu sasa nchini zitenge maeneo ya biashara kwa ajili ya vijana wetu ili vijana hawa waweze kuwasaidia na tujenge majengo kama yale ya Dar es Salaam Machinga Complex. Vijana wengi sasa hivi wamekuwa wakikimbilia mijini, miji mikubwa wanajua kwamba ndiyo suluhisho la matatizo yao. (Makofi) Lakini tuwatengenezee maeneo ili vijana wetu waweze kufanya kazi pale walipo. Kila sehemu kuna maisha bora, kwa hiyo, naomba Halmashauri zote ikiwemo ya Iringa basi itenge maeneo kwa ajili ya kuwasaidia vijana wetu. Vilevile itenge maeneo kwa ajili ya vituo vya teksi. Naona kuna kero kubwa sana, ushuru wanatozwa lakini maeneo ya teksi hayajatengwa. Kwa hiyo, naomba Halmashauri zote ziweze kutenga maeneo haya. Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia mchango wangu ujikite kuhusu maswali ya Waziri Mkuu siku Alhamisi. Nilijiuliza sana walio-frame Kanuni hii waliipata wapi. Lakini nikagundua kuwa famous ya Kanuni hii waliiga kutoka Bunge la Uingereza ambapo Waziri Mkuu huulizwa maswali. Lakini kwa uelewa wangu mdogo, niligundua pia kuwa Waziri Mkuu huyo wa Uingereza ana executive powers na anaulizwa maswali ya sera tu na si maswali ya Kiwizara. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri wa hapa kwetu hana executive powers mwenye executive powers ni Rais ambaye si Mbunge. Maswali anayoulizwa Waziri Mkuu wetu mengi yao si ya kisera, mengi yao yanaulizwa ni ya Kiwizara. Mifano mingi ninayo, kutokana na muda nitawasilisha kwa maandishi. Najiandaa kuleta hoja ya binafsi ya kuondoa Kanuni hii ya Waziri Mkuu kuulizwa maswali ya papo hapo. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna baadhi ya maswali yanamdhalilisha sana Waziri Mkuu. Ninao mfano, mfano mmojawapo ulijitokeza katika Mkutano wa Pili, Kikao cha Tatu tarehe 10 Februari, 2011. Kwenye Kikao hicho Mheshimiwa Godbless Lema

Page 91: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

91

alinukuliwa akisema hivi, naomba kunukuu; “Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 68(7) naomba kupata ufafanuzi kwamba Mbunge anaweza akachukua hatua gani kama anaona mtu mwenye nafasi kubwa katika nchi hii kama Waziri Mkuu anadanganya Taifa na kumdanganya Mbunge? Ahsante sana.” Mwisho wa kunukuu. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, inaonyesha wazi kuwa swali hilo Mheshimiwa Mbunge alilenga kumdhalilisha Waziri Mkuu na ndivyo ilivyokuwa, najiandaa kuleta hoja ya binafsi. Lakini kabla sijaleta hoja binafsi naomba siku ya maswali atakayekuwa anaongoza kiti basi ajaribu kupima yale maswali. Kama hayo maswali siyo ya kisera wapelekewe Mawaziri ili wale Mawaziri wajibu kwa undani zaidi. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo linanikera ni kuhusu upotoshwaji wa baadhi ya wanasiasa wenzetu. Kumekuwepo na upotoshwaji mkubwa sana ambao yaani naomba wale Mawaziri au Rais nani wawe wanayajibia mapema ili ule upotoshwaji usionekane kama ni ukweli. Na upotoshwaji huu sasa hivi upo hata hapa katika Bunge, kuna watu wanaleta maneno ya kupotosha ambayo sio ya ukweli, unakuwa kama ni uongo mtakatifu. Kwa hiyo, naomba Katibu wa Bunge hili awe anajaribu kutoa ufafanuzi mapema zaidi ili mambo yale yasionekane kama ni ya kweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile kwa sababu mimi nilikuwa Diwani wa Ukonga, naomba nitoe pole nyingi sana kwa wananchi wa Ukonga kwa ajali ile ya mabomu. Kwa kweli nimesikitishwa sana na kitendo cha yale mabomu kulipuka, lakini naomba Serikali hii iangalie, nilipokwenda pale Ukonga nimekuta wananchi wanakaa kwenye ma-tent, akinamama na watoto, bado hawajajua kama vile viwanja au nyumba zitajengwa lini. Kwa hiyo, naomba Serikali hii itoe suluhisho kwa watu wananchi wa Ukonga na Gongo la Mboto, ni lini sasa yale mambo ambayo waliambiwa watafanyiwa, watafanyiwa? Kwa sababu inasikitisha, inatia huruma, yale ma-tent yametoboka, kule ndani kukiwa kuna mvua basi ndio matatizo makubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sitaki kuongea mengi sana, naomba kuunga hoja.

(Makofi) MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa

kunipa fursa hii walau na mimi kuweza kutoa mchango wangu wa mawazo. Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya njema na kuniwezesha leo hii kusimama hapa mbele ya Bunge lako Tukufu ili kuweza kuchangia hotuba hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwapongeze vilevile Baraza la Mawaziri walioteuliwa.

Wazungu wanasema huwezi ku-judge kitabu kwa cover, lakini walau unaweza uka-judge ukifungua tu ukurasa wa kwanza. Mawaziri hawa wameonesha kwamba wanaweza na hasa niwasifie Mawaziri vijana. (Makofi)

Page 92: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

92

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwapongeze vilevile Wabunge wa Bunge lako Tukufu, hasa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao wanatokana na Chama cha Mapinduzi. Kazi iliyokuwepo sio ndogo, ilikuwa ni kazi kubwa, lakini wamepambana, hawakujali fitina, hawakujali uongo, hawakujali, uzushi wa aina yoyote na hatimaye wameingia humu ndani. Nimpongeze Waziri Mkuu sana kwa hotuba nzuri, pamoja na mipango ya Serikali katika kuhakikisha kwamba Tanzania inapiga hatua kutoka hapa tulipo kwenda mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchumi wa Tanzania. Tanzania ni nchi maskini, ni

ukweli ambao haupingiki, ina rasilimali lakini still ni nchi maskini kwa sababu nchi kuwa maskini haina maana kwamba labda tukiwa na rasilimali hizi basi ndio maana yake kwamba sisi Tanzania ni nchi tajiri. Uhalisia wa uchumi ni kwamba Tanzania ni nchi maskini. Lakini tukiangalia licha ya hali hii tuliyokuwa nayo michango mingi sana ya Wabunge katika Bunge hili imekuwa ikilenga sana kuleta mawazo katika kuhakikisha kwamba Serikali inayafanyia kazi ili nchi yetu iweze kupiga hatua moja kwenda hatua nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Vision 2025 (Dira ya Maendeleo 2025), Tanzania

imejiwekea malengo kwamba ifikapo mwaka 2025 iwe ni nchi ya middle income, lakini mpaka sasa uchumi wetu unakuwa kwa kiwango cha 7%! Naipongeza Serikali kwa sababu ni kiwango kizuri na nchi yetu mpaka sasa hivi iko stable licha ya mtikisiko wa kiuchumi. Lakini kiwango hiki hakiwezi kutufikisha kule tunakotaka kwenda by 2025, kwa sababu dira hii by 2025 ilikuwa middle income country, vigezo vyake ni lazima tuwe na per capita income ya dola 3000 mpaka dola 6000. Sasa hivi Tanzania tuko katika dola 700, kwa hiyo, inabidi tukimbie wakati wenzetu wanatembea. Inabidi tukimbie kwa sababu ili tufikie malengo inatakiwa uchumi wetu ukue kwa kiwango cha 15% kwa muda wa miaka 15 mfululizo. Sasa tukiangalia hapa tulipo, kwa hali tuliyokuwanayo, kwa changamoto tulizokuwanazo, je, tutafika? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nchi yetu na Serikali yetu inajitahidi sana

kuhakikisha kwamba walau tunasonga mbele. Licha ya changamoto nyingi tulizokuwanazo, zipo nyingine ambazo zipo ndani ya uwezo wetu lakini kuna nyingine ambazo zipo nje ya uwezo wetu; changamoto kama za hali ya hewa zipo nje ya uwezo wetu, changamoto kama za masuala ya kupanda kwa mafuta zipo nje ya uwezo wetu, changamoto kama za masuala mengine ya pengine utofauti wa manunuzi ya bidhaa zetu za biashara, pia hilo lipo nje ya uwezo wetu! Lakini yapo mengine ambayo yapo ndani ya uwezo wetu, kwa mfano changamoto ya idadi ya watu ambayo hailingani na ukuaji wetu wa uchumi, hiyo ipo ndani ya uwezo wetu. Changamoto mbalimbali za kijamii zipo ndani ya uwezo wetu, lakini kubwa zaidi changamoto za kiutendaji, hizo vilevile zipo ndani ya uwezo wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania imeamua kuja na Sera ya Kilimo Kwanza

katika kuhakikisha kwamba inasaidia uchumi wetu. Tuna makundi mbalimbali ambayo ni makundi sensitive ili kuhakikisha kwamba uchumi wetu unasogea. Kundi la vijana,

Page 93: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

93

Serikali imejitahidi sana kuwa na mpango kama huu ambao Serikali inapanga kuutekeleza kuwa na Vyuo vya VETA kila Wilaya ni mpango mzuri, naipongeza Serikali. Lakini vyuo hivi vinachukua vijana ambao wamemaliza kidato cha nne, lakini vile vile vijana ambao wamefaulu. Je, vijana hawa ambao wamemaliza darasa la saba, ambao hawakufanikiwa kuingia form one, darasa la tisa, tunawafanyia kitu gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa ripoti ya BEST katika kipindi cha

mwaka 2010/2011 vijana takribani 2,498 wamemaliza darasa la saba lakini hawakuweza kujiunga na kidato cha kwanza. Ni tatizo kubwa kwa sababu ukiangalia kama hivi ndivyo, kwa kipindi kifupi cha miaka minne kuanzia mwaka 2006 mpaka 2010 baada ya ripoti hiyo, kama hali ndio hivi, uchumi huu tunataka ukue, tukue nao wote kwa pamoja. Kwa maana ya kwamba kuanzia rika la chini mpaka rika la juu, kwa maana ya kuanzia tabaka la chini mpaka tabaka la juu. Lakini kwa ukuaji huu na kwa hali hii, hatuwezi kukua kwa pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nilikuwa nina ushauri, ninaomba Vyuo vya FDC,

Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, Serikali iweke nguvu ya ziada, iweke upendeleo maalum ili hivi vyuo viweze kuwasaidia hawa vijana. Lakini vile vile katika makundi mengine lipo kundi la wafanyakazi; Serikali inajitahidi kuboresha maisha yao kwa maana ya kuwajengea nyumba kama polisi, wanajeshi na kadhalika na kujaribu kuboresha maisha yao. Lakini vilevile kuangalia stahili zao kama za mishahara kuzifanyia kazi ili mishahara iweze kuongezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lipo kundi moja ambalo mimi ndio nina matatizo

nalo makubwa sana, nalo ni kundi la wakulima. Sera hii ya Kilimo Kwanza, hivi kweli, moyo aliokuwanao Mheshimiwa Rais wetu, tena mimi ninampongeza sana Mheshimiwa Rais, ninaungana nae mkono na kauli aliyoisema Mheshimiwa Ibrahim Sanya, Mbunge wa CUF, alisema kwamba hatutauona uzuri wa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mpaka akiondoka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais huyu ni mvumilivu, Rais huyu ni mwema, Rais

huyu ni mtu ambaye kwa kweli moyo wake hatuwezi kuulinganisha wa watu yaani kama wapo ni wachache sana. Hana kinyongo na mtu yeyote, yupo, ana roho nyeupe na roho safi. Ipo siku tutakuja kujuta tutakapopata mtu ambaye…, mimi nakumbuka yupo Waziri mmoja sitaki kumtaja jina, aliwahi kuniambia hivi, mimi siku moja kama ikija kutokea nikaambiwa kwamba nakaimishwa Urais, hata kama ni kwa wiki mbili yaani huyo Rais akirudi atakuta kila mtu nimemweka ndani! Mimi nikamwambia sababu ni nini? Akasema sababu ni kwamba katika hii nchi kuna watu wana mambo ya ajabu vibaya sana yaani kuna watu wana maudhi vibaya sana, kuna watu wana kauli mbaya vibaya sana, sasa ukinipa nchi kwa wiki mbili ni lazima utakuta mimi nimeshawaweka ndani. Kwa hiyo, ni lazima tutambue kwamba moyo huu aliokuwa nao Mheshimiwa Rais, ni lazima tuuenzi walau basi na sisi kwa kumpa heshima anayostahili. (Makofi)

Page 94: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

94

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika suala hili sasa la kuinua uchumi, Mheshimiwa Rais wetu, Mheshimiwa Waziri Mkuu, kila siku wana nia wanaonekana kabisa hata ukiwaangalia hivi, unaona kabisa kwamba wana nia ya kutunyanyua kutoka hapa tulipo. Lakini kilio changu kikubwa na ugomvi wangu mkubwa, hivi kweli watendaji hawa huku chini, hivi wako pamoja nao? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninasema hivyo kwa sababu gani? Nikizungumzia

suala la kilimo kwa mfano mwaka 2008 Mheshimiwa Kikwete, alikuwa tarehe 31/12/2008 katika salamu zake za mwaka mpya kwa wananchi, alisema Serikali itawawezesha wakulima kupata mbegu bora. Namnukuu, “Kuhusu upatikanaji wa mbegu, tumepanga kuimarisha vituo vyetu vya utafiti wa mbegu na kuongeza uwezo wetu wa kuzalisha mbegu hapa nchini. Kwa ajili, hiyo nimewaagiza Jeshi la Kujenga Taifa na Jeshi la Magereza, watumie sehemu ya mashamba yao kuzalisha mbegu. Nafurahi kwamba viongozi wa Idara zetu hizo, tayari wameshaelewana na wenzao Wakala wa mbegu nchini, kufanikisha mpango huo muhumu.” (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais akishasema ninyi kama mmekaa ni watendaji ni

viongozi, hata mkiangalia TV hivi Rais anahutubia, mnatakiwa mchukue kalamu na karatasi m-note anayoyasema ni maagizo. Lakini mpaka sasa leo hii ninavyozungumza, wakala wa mbegu hajawahi kukaa hata kikao kimoja na JKT kuzungumzia ni jinsi gani wataweza kusaidia JKT kuzalisha mbegu. Lakini tuwapongeze JKT kwa sababu wao walau wameona kwamba agizo la Rais, ni Amiri Jeshi Mkuu, ni Rais wa nchi, akisema kitu ni amri, tutatafuta pesa popote zilipo ili tuweze kutekeleza agizo la Rais. Hawa wakala wa mbegu wanafanya kazi gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hali kama hii, Waziri aliyetoa ule mfano wa

akipewa wiki mbili atafunga watu, huwezi kuwafunga watu katika utaratibu kama huu? Lakini vilevile hawa watendaji wetu katika kipindi cha uchaguzi kilichopita tumeshuhudia mambo mengi sana, Serikali imejitahidi, ime-decentralise, imetoa pesa katika Serikali Kuu imepeleka huku chini, lakini hawa watendaji wana mambo ya ajabu, baadhi ya watendaji sio waminifu! Ili Serikali iweze kufanikiwa, haina budi kuchukua kwa kweli hatua za haraka na muhimu kuhakikisha kwamba hawa watendaji, iwachukulie hatua! (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna vijana wengi wanatafuta kazi, hawana kazi. Hawa

watu ambao wanafanya mambo ya ajabu ajabu sijui migomo na nini, watu wanamaliza shule wanazunguka na vyeti wakati kuna watu wamekaa, wao wanafanya mambo ya ajabu, wanafanya ubadhirifu! Katika ukurasa wa 21 wa hotuba ya Waziri Mkuu, amezungumzia kwamba kuna watu wamefanya ubadhirifu, wamekula pesa za pembejeo na vitu gani, tunawaachia nini hawa watu? Hawa watu watupishe, wakae pembeni, tuendeleze Taifa letu, kuna vijana wana elimu nzuri na wana uwezo na wataweza hizi kazi. (Makofi)

Page 95: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

95

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa ninaomba Serikali ichukue hatua za makusudi katika masuala kama matano au sita yafuatayo; naona muda wangu haunitoshi. Suala la akinamama pamoja na riba; akinamama wanateseka sana hapa nchini kwa sababu ya riba kubwa katika mabenki; Serikali ichukue hatua, iseme hapana, hili suala lazima liishe. Masuala ya bomoa bomoa wakati watendaji wapo kule chini kwenye Halmashauri, Mkurugenzi amekaa anashuhudia watu wanaanza kujenga kuanzia nyumba ya kwanza, Serikali iseme hapana, tuchukue hatua. Suala la mgawanyo wa rasilimali, yale maeneo ambayo hayana kitu hebu tuwape kidogo kaupendeleo kidogo kulinganisha na haya maeneo mengine ambayo yana vitu, tuseme hapana Serikali ichukue hatua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali iweke sababu za makusudi kuhakikisha

kwamba tunatumia jiografia ya nchi yetu vizuri; tuna maziwa, hapa tulipo nchi nyingi zinatutegemea, bandari zetu, tuna maji tumezungukwa na maji, maana wakati mwingine unaweza kujiuliza ukakosa sababu! Haiwezekani Zanzibar imezungukwa na maji, hakuna kiwanda cha samaki! Hayo lakini ni mengine. Serikali ichukue hatua kuhakikisha kwamba masoko ya bidhaa zetu basi walau kama ikiwezekana, waongeze nguvu ili tuweze kuyaboresha na bidhaa zetu ziweze kuuzwa nje, masoko yapatikane. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho kabisa, ninawapongeza sana viongozi wa

vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuendelea kuiweka nchi yetu katika hali ya usalama. Licha ya fujo zote zinazotokea, leo hii unaangalia kwenye gazeti, unasoma Bill Gates yupo Tanzania, yule ni mtu ambaye kabla ya kwenda sehemu ana watu wanamwambia kwamba huko bwana usiende unaweza hata ukapigwa, yaani kuna fujo zinaweza zikatokea! Lakini amehakikisha yupo hapa nchini kwa ajili ya amani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi) MHE. JOHN P. LWANJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Awali ya yote

nichukue nafasi hii kuwashukuru sana wananchi wa Jimbo la Manyoni Magharibi, kwa kuniamini tena kunirudisha humu ndani, hawakukosea, wamelamba dume. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni dialogue sio ugomvi, ni dialogue. Kwa hiyo,

kama ni dialogue basi tuvumiliane na tusikilizane na kuchambua pumba ni ipi na mali safi ni ipi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii inashughulikia sherehe za miaka 50 ya

Uhuru, mimi ni shahidi. Mimi nilipokuwa primary school nilishuhudia kushushwa kwa yule Mjeki na kupandishwa kwa bendera ya Tanganyika, kwa hiyo, mimi ni kielelezo. Nilikuwa Kilimatinde pale, basi ilikuja wheelbase, zile bed ford tukachukuliwa tukapelekwa Mjini Manyoni kwa DC Bwana Haga, baada ya kuondoka Sir Richard Turnbul, basi siku ile tulisherehekea, tulikula sana na ndio siku ile nilifahamu pilau! Sikuwa naijua mimi. (Makofi)

Page 96: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

96

Sasa siku narudi nyumbani baada ya shule kufungwa maana shule zote

hazikufungwa, tulisherehekea shule zote, sasa siku ile narudi nyumbani Mgugani baada ya kufunga shule, mimi nilidhani Uhuru ni pilau! Kwa hiyo, nikamdai baba na mama kwamba jamani, tumepata Uhuru pilau iko wapi eeh? Nikakataa kula ugali, sasa mzee akasema ngoja nikakuletee pilau, basi alikwenda kukata fimbo, nilipigwa vibaya sana. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatoa mfano huu maana wengine wanadhani Uhuru

ni pilau. Akaniambia Uhuru ni kusoma. Nakwambia nilizingatia kitabu na baada ya miaka kumi mwaka 1971 wakoloni walipoitwa kuja kushuhudia ni nini kimefanyika Baba wa Taifa aliwaita wakoloni baada ya miaka kumi kwa wale mnaokumbuka, walirudi kuja kushuhudia. Mimi nilikuwa IDM na Spika huyu, Mama Anna Makinda. Mimi nachukua Public Administration, mama anachukua mambo ya uhasibu na ukaguzi, nafikiri hata na u-CAG. Sasa ningekumbuka pilau ndugu zangu ningefika hapa? Nikasema hivi basi na miaka kumi baadaye nikawa Mkurugenzi wa Utawala kwenye Shirika la Umma katika miaka ya 1980. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini sasa baada ya hapo kukawa na set backs, hili

halielezwi na wenzetu waliozaliwa kabla ya kuzaliwa kwa Taifa hili, hawaelezi vizuri kwamba nchi hii tulipigana vita, tena vita mbaya! Tulivamiwa na Nduli Idd Amin, hili halielezwi kwa ufasaha, tunaeleza habari za liberation struggle na ni kweli tulishiriki kwenye liberation struggle kuliko nchi nyingine yoyote. Sasa hiyo, ilikuwa ni set back kubwa, na hatukupigana na Idd Amin tu, tulipigana na Libya, uongo au kweli ndugu zangu? (Makofi)

WABUNGE FULANI: Kweli. MHE. JOHN P. LWANJI: Mheshimiwa Mwnyekiti, Libya ilitoa saa 48 kwa

Baba wa Taifa kwamba uondoe majeshi yako Uganda vinginevyo Libya tutapigana pamoja na Uganda dhidi ya Tanzania, Mwalimu alikataa na kweli walikuja. Tulipigana na Taifa kubwa tajiri na tuliling’oa. Leo hii NATO inashindwa kumng’oa Gaddafi kutoka Libya! Kwa hiyo, mnaweza kuelewa ukubwa wa jambo lenyewe, tulitumia silaha za kisasa. The first electronic hijacking ya ndege, ndege za adui badala ya kutua Entebbe zinatua Mwanza au zinatua KIA, hawaelewi! Kwa sababu ya ule utaalamu, tulitumia vifaa na tulitumia pesa nyingi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimeshuhudia jinsi uchumi wetu ulivyokuwa

mzuri, hela yetu ilivyokuwa sawasawa kabisa na hela ya Uganda na ya Kenya, lakini watu hawaelewi hili! It takes a lot of time kuja ku-rehabilitate na kufikia tena hapo. (Makofi)

Page 97: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

97

Kwa hiyo basi, miaka yote hii ambayo imepita ndugu zangu imekuwa ni ngumu, Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi alichukua nchi hii ikiwa bankrupt tukaanzia hapo, tukaja kuwa ahueni wakati wa Mheshimiwa Benjamin Mkapa na sasa ndiyo tunaendelea. Lakini vijana ndiyo hawaelewi kabisa, wanadhani ni pilau kuamka asubuhi basi ni kunywa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tafadhali sana tarehe 9 Desemba, 2011 ndugu

zangu kupitia Bunge hili ninaomba shule zote siku ile zisifungwe tena tuna wanyama wengi wapewe kila mmoja nyumbu mmoja kila shule basi watoto wafurahi, wafurahi kabisa kabisa kwanza tuna shule ngapi, shule si nyingi vijiji 11,000, shule 15,000, shule za sekondari 4000, nyumbu peke yake wapo milioni 1.2, tembo ndiyo idadi yake hata hatujui, sasa kila shule na kila kijiji ikipata tukasherekea halafu baada ya hapo…

MBUNGE FULANI: Swala. MHE. JOHN P. LWANJI: Swala, ndugu zangu ninawaomba sana tusherekee

kwa kishindo kwa sababu we are surviving as a nation tuko Taifa moja, Mataifa mangapi yamesambaratika ndugu zangu? Sasa hao wanaozungumza bahati mbaya hatutozi ushuru kwa midomo mibovu midomo hii yetu hakuna ushuru ingekuwa tumeweka utaratibu basi tukaweka Sheria TRA wanatoza ushuru watu wanaozungumza hovyo tungetajirika vibaya sana nawaeleza kabisa, tungekuwa na pesa za bure, maana watu wanajizungumzia hovyo tu, tena wengine wanabeba majina makubwa wanasema hakuna Uhuru, ndugu zangu ni kweli huu ni uungwana kweli? Siyo uungwana hata kidogo. Kwa hiyo, hii mimi nadhani nitakuja na hoja binafsi ili tuwe na sheria ya kutoza midomo ushuru, ukizungumza vibaya kupoteza muda basi posho yako mwaaa! Ukute hakuna kitu, msitupotezee muda hapa. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikirudi kwenye mada ni hivi kwamba ugomvi wetu ni

jinsi ya kugawana kasungura kako, aka kasungura kanatupa shida, trilioni 13 lakini ukiangalia mgawanyo wenyewe mkoa wa Singida ni kama tunaambulia kwato tu, ni kama nyayo, kuna sehemu moja niliona gari moja limeandikwa ukiona manyoya ujue ameliwa. (Makofi/Kicheko)

Ndugu zangu nchi hii ni kubwa, Mheshimiwa Mwenyekiti nikukumbushe

Tanzania ina kilomita za mraba 945,000 yaani Tanzania peke yake, hii nchi ukijumlisha zile nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi ukijumlisha zote zile zina kilomita 877,000 tofauti yake tunawazidi kwa kilomita 67,000 yaani zile nchi zote hizi watu hawajui kwamba Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi wakijumlisha wote bado hawaifikii nchi hii, lakini tuna wilaya ngapi, Burundi tu yenyewe ambayo ina kilomita za mraba 27,000 ina wilaya 116 sasa sisi tunashindwa ku-manage resources zetu kwa sababu tuko mbali na resources.

Page 98: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

98

Mimi jimbo langu kilomita za mraba 18,000; mbuga za akiba tatu, yamekuwa ni mapori ni mashamba ya bibi, watu wanaingia na kuvuna na kuondoka hata wageni kutoka Rwanda na Burundi, watu wa Burundi wapo wanakuja wanavuna wanaondoka. Mimi naomba tungekuwa serious kuhusu hili suala na ndiyo maana mikoa mingine toka ukoloni inaendelea kuwa hivyo hivyo nyuma, Vote 84, Vote 76 zote mimi nimefanya kazi Serikalini na nimeshughulikia masuala hayo nikiwa Administrative Officer nakuta Lindi, Singida ndiyo mikoa hiyo ilivyokuwa ya mwisho na leo basi Singida ndiyo imebaki hivyo na manyoya, huu ni uungwana kweli? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi kwa hiyo ningeliomba sana hili suala liangaliwe,

linasema hivi ripoti ya Serikali inasema kwamba hakuna uonevu katika mgawanyo wa rasilimali Kitaifa na kila mkoa unapata fedha za Matumizi ya Kawaida na Maendeleo kwa kutumia vigezo na vipaumbele vya Kitaifa kama vile ujenzi wa miundombinu katika baadhi ya miundombinu katika baadhi ya maeneo kulingana na mahitaji.

Hata hivyo, Serikali inaendelea kuboresha utaratibu wa kugawa rasilimali kwa

kuangalia maeneo yenye mazingira magumu, lakini ukweli vipaumbele vyenyewe vimeainishwa, idadi ya watu ndiyo kigezo kikubwa 70 percent, ukubwa wa eneo la utawala ten percent, kiwango cha umaskini asilimia 20. Vitu vingine vinavyochangia mgao wa Bajeti ni idadi ya watumishi wa Serikali na idadi ya Halmashauri, Singida Halmashauri nne from time immemorial na tumeongezewa sijui mbili lakini tupo pale pale na wengine wameongezewa kwa hiyo, sisi bado pale pale tumebaki.

Waheshimiwa Wabunge, mimi ningeomba tuwe serious, mkoa wa Singida ni eneo

mojawapo lenye mazingira magumu, Mkoa wa Singida watu hawaufahamu, mkoa huu umekwenda mpaka Chunya mimi nimeelemewa, nikisafiri nashindwa kuhimili eneo hilo kutoka Itigi, mpaka Lupa nakwenda kwa Mheshimiwa Mwambalaswa kule na hard top ningeomba jamani shangingi la Mbowe mnipe basi yeye amelikataa mnipe mimi linisaidie kazi. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vinginevyo hamjui kabisa, juzi wilaya zimegawiwa

hapa wilaya sijui 21, mbili zimerudishwa sijui hawaelewani sikupewa hata moja, zimerudishwa tu moja kwa moja. Ukiuliza unaambiwa bwana hiyo ni shughuli ya Rais ameamua, Rais wapi, Rais ananichukia mimi, anawachukia watu wa Manyoni? Sisi tunajua kinachofanyika, kinachopendekezwa, kinachochakachuliwa, Mkurugenzi unakuta anatoka ni yeye wa kwanza kujikausha. (Makofi)

Sasa mimi ningeomba sana muangalie hiki kilio, nimeahidiwa juzi juzi kwamba

itakuwa Halmashauri, kuna mchakato wa kuifanya Itigi kuwa Halmashauri ya mji mdogo, ripoti ya Waziri hapa imesema hamna kitu cha namna hiyo, hakuja ametaja Nanyamba. Nanyamba ni mkoa wa Mtwara sasa wanajimegea mapema mapema, ni lazima tuzungumze ukweli na kama mchakato upo unakuja basi tuelezwe waziwazi kwa

Page 99: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

99

sababu Waziri Mkuu anania nzuri ya kunisaidia lakini inapokwenda kwa watendaji inachakachuliwa kila mmoja anakimbiza kwake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama watu wa Singida pia hawatanisaidia kwenye

suala hili la wilaya pamoja na kuangalia eneo langu, mimi nitaomba Waziri Mkuu, nitazungumza na wananchi wangu tuhamie mkoa wa Katavi labda tutapata kabisa, hatuwezi labda kwa sababu ya unyonge wangu tu mimi labda naambiwa kwanza mkoa wa Katavi unasua sua kwa idadi ya watu na wilaya, sisi tupo tayari kama hivi nakwenda kuwauliza watu wangu. Kwa sababu nawaona watu wa mkoa wa Singida wamepata wilaya ya Nkungi na Mkalamba basi wamenyamaza, wameridhika, lakini upande wangu kule ambako ndiyo pori kubwa na ndiyo rasilimali kubwa asilimia 58 ya mkoa wa Singida ni kwangu, lakini wamenyamaza sasa nifanye nini. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ningeliomba hili suala liangaliwe critically na

naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu aliangalie, kama sitapata jibu kesho wakati wa majumuisho mimi siondoki hapa nitalala hapa kwenye kiti, mtaniondoa kwa Tanganyika jeki, kweli na nimeona kuna wapambe wawili sasa waje wanikabili hapa, wengine wanapo-protest wanatoka, mimi sitoki nitakaa hapa hapa kieleweke nijue habari za Mji Mdogo wa Itigi walau hilo hapo ndiyo tutaelewana nitakaa hapa na nitafunga, sili wala sinywi maji, ahsante sana, naunga mkono hoja. (Makofi/Kicheko)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Lwanji, najua wananchi wako

wamekusikia na Serikali imekusikia, sasa nitamuita Mheshimiwa Hussein Nassoro Amar na Mheshimiwa Aliko Kibona ajiandae.

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kupata

nafasi hii ya kuweza kuchangia hotuba ya Bajeti ya Waziri Mkuu, pia napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia leo kunipa afya njema na kuweza kufika mahali hapa na kuchangia ambayo nimekusudia kuyachangia. Napenda kumshukuru Waziri Mkuu kwa hotuba yake nzuri ambayo imesheheni ahadi ambazo zikitekelezeka basi Tanzania itakuwa ni nchi ambayo ni ya kupigiwa mfano. (Makofi)

Pia napenda kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kwa kuitangaza rasmi Wilaya mpya ya Jimbo la Nyang’wale. Jimbo la Nyang’wale hivi sasa ni wilaya mpya katika wilaya kumi na tisa, sisi Wananyang’wale tunampongeza sana kwa kutupatia wilaya kwa ajili ya kutusogezea huduma. (Makofi)

Sasa ninaanza kuwasilisha matatizo machache ambayo yanatusibu sisi

Wananyang’wale, tatizo kubwa kabisa ambalo tunalo hivi sasa ni njaa, ukweli njaa tunayo kali sana hivi ninavyozungumza leo hii nimepigiwa simu kuambiwa kwamba debe moja la mahindi ni shilingi 13,000 kwa hiyo tishio kubwa la wananchi wa Jimbo la

Page 100: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

100

Nyang’wale kufa na njaa, uwezekano huo upo kama Serikali haitafanya juhudi za ziada kutupelekea chakula na kuweza kupunguza bei. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaanza pia kuzungumzia tatizo la maji, jimboni

kwangu kuna tatizo kubwa sana la maji, nashukuru jana nimeweza kujibiwa na kuambiwa kwamba zimetengwa pesa kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya kuyatoa maji katika mradi ambao uliokuwepo tangu mwaka 1974 kutoka Nyamtukuza kupita Kakola, Kalumwa, Izunya na Bukwimba, takribani vijiji tisa ambavyo vitanufaika na mradi huo baada ya kuwa umefufuliwa. Lakini nina kata 12, huu mradi unapita kwenye kata nne, ina maana zile kata zingine Serikali ina mpango gani wa kuweza kuwafikishia maji ya kutoka Ziwa Victoria wana jimbo la Nyang’wale? Kwa sababu tatizo la maji katika Jimbo la Nyang’wale ni sehemu zote hakuna ambako kuna nafuu. Sehemu ambazo zina kero kubwa ya maji, ni pamoja na kata ya Shabaka, Busolwa, Nyang’wale, Nyiyundu, Kafita, Nyashilanga, Nyaburanda na Nyugwa. Naiomba Serikali itafakari sana kwa haraka ili iweze kutusaidia kufikisha maji katika kata hizo ambazo nimezitaja. Kwa kweli naipongeza Serikali kwa kutenga fungu kwa ajili ya kutuvutia maji ama kufanya upembuzi yakinifu katika mradi huo. (Makofi)

Pia napenda nizungumzie kwa uchache matatizo yaliyopo katika upande wa

elimu, jimbo langu lina matatizo mengi katika upande wa elimu, lina upungufu mwingi wa madawati, upungufu wa walimu, nyumba za walimu, maabara na madarasa. Naiomba Serikali ijaribu kutuangalia kwa jicho la huruma ili kuweza kutuondolea upungufu huo ili tuweze kuboresha elimu.

Nitazungumzia suala la afya, upande wa afya tuna upungufu mwingi, Jimbo la

Nyang’wale lina vituo vya afya viwili na zahanati saba, lakini upungufu ni mwingi sana, wakiwemo madaktari, wauguzi na dawa. Hivi ninavyozungumza hata darubini za kuweza kupimia yale magonjwa madogo madogo baadhi ya zahanati hazina, naiomba Serikali ituangalie sana katika upande wa afya kwa upungufu ambao nimesema. (Makofi)

Nizungumzie upande wa elimu, walimu wana matatizo, wana malalamiko yao

makubwa kuhusu Bima ya Afya, walimu wa Jimbo la Nyang’wale nimekaa nao na wamenituma wanasema sasa wao hawataki kujiunga na Bima ya Afya kwa sababu hawaoni faida ya Bima ya Afya, wanakatwa pesa zao na inapotokea wameugua wakienda hospitali hawapati matibabu. Wamesema haina haja ya kuendelea kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya. (Makofi)

Pia wakapendekeza kwamba mpango wa Bima ya Afya, zitolewe fomu maalum

za hiyari, mtu ajiunge kwa hiyari na siyo lazima. Kwa hiyo, walimu wa Jimbo la Nyang’wale wamenituma kwamba wao sasa Mfuko wa Bima ya Afya hawautaki tena kwa sababu hawaoni faida. Pia walimu wa jimbo langu kutokana na jiografia ya jimbo langu ukweli wana matatizo mengi, masuala ya usafiri hususan inapofika kipindi cha kwenda kuchukua mishahara yao, wanatumia zaidi ya shilingi 50,000/= kwenda

Page 101: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

101

kufuatilia mshahara, hebu piga hesabu, akatwe bima ya afya na shilingi 50,000/= kwa ajili ya nauli, anabakiza kiasi gani? Na wanaishi katika mazingira magumu sana na mimi naiomba Serikali iwaangalie walimu hawa jimboni kwangu kama kuna uwezakano wakopeshwe hata vipando kama vile pikipiki ili wawe wanakatwa katika mishahara yao na wao wamesema hilo wako tayari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nazungumzia suala la umeme, niliwahi kuuliza hapa

bahati nzuri Waziri Mheshimiwa Ngeleja kanijibu vizuri, naipongeza Serikali kupitia mradi wa MCC kwamba upembuzi yakinifu tayari na sasa hivi wameshapita kule kwa ajili ya kutathimini na nasikia wameshaanza kutoa pesa ama cheque kwa ajili ya malipo ili waweze kupitisha nguzo zao. Kwa kweli naipongeza Serikali na bado naiomba Serikali iongeze speed ili tuweze kupata umeme ili kuweza kunyanyua uchumi wa Jimbo la Nyang’wale. Mheshimiwa Ngeleja, aliniahidi kwamba ni mwezi wa tano pamoja na kwamba umeme haujawaka kanijibu tayari hatua za mwanzo zimeshaanza, nampongeza sana Waziri. (Makofi)

Napenda kuzungumzia suala la mawasiliano ya simu, kwa kweli jimbo langu lina

matatizo makubwa sana ya mawasiliano ya simu. Katika kata 12 ni kata moja tu ambayo ina mawasiliano, nampongeza Naibu Waziri ya Mawasiliano jana niliongea naye na akanipa matumaini kwamba atakuja kututembelea na ifikapo mwezi wa 12 basi tutarajie kata zote zitakuwa na simu. (Makofi)

Pia nizungumzie kuhusu barabara, hilo lilikuwa ndani ya ahadi ya Rais na

nimeliona limo katika mpango, barabara ile naomba ianzishwe tu baada ya mwaka wa fedha zikitoka ili tuweze kuunganisha kati ya Busisi, Kalumwa, Bukwimba na Kahama ili kuchochea maendeleo katika wilaya yetu mpya. Pia barabara ya kutoka Geita, Nyang’wale, Nanyijundu iuganishwe hizo zote zilikuwa ni ahadi za Mheshimiwa Rais. (Makofi)

(Hapa kengele ya kwanza ililia)

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Kutoka na kengele hiyo ya kwanza, nizungumze

haraka haraka kuhusu wafugaji, wafugaji wa Jimbo la Nyang’wale karibu wanakata tamaa na ufugaji kwa sababu hawana soko la mazao yanayotokana na mifugo, ngozi, samli na ng’ombe wenyewe. Pia wanataka kukata tamaa kuwa wafugaji kwa sababu ya matatizo ya maji, mifugo hawapati maji, hawapati majosho ya kuoshea pia na dawa, kwa hiyo, wamenituma kwamba karibu wanakata tamaa sasa na ufugaji. Kwa hiyo, naiomba Serikali ielekeze kule kuwasaidia wananchi wa Jimbo la Nyang’wale kuwachimbia mabwawa na kuongeza majosho na dawa ili wasikate tamaa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo nazungumzia maslahi ya

Madiwani wetu na Wenyeviti, nashukuru kwamba Wabunge wengi mmelipigia kelele na

Page 102: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

102

mimi nikiwa mmojawapo na nina imani kwa sababu Serikali yetu ni sikivu itakuwa imesikia na mimi naomba kabisa kwamba Madiwani na Wenyeviti wapewe mishahara. Suala la posho za Wabunge na mimi kwa kweli nasema kwamba posho za Wabunge pamoja na kwamba imebadilisha ile lugha inaitwa…

MBUNGE FULANI: Mwia! MHE. HUSSEIN N. AMAR: Unaitwa mwia, hautoshi kabisa! Shilingi

150,000/= inatusaidia kitu gani? Tuangalie hapa Dodoma na Majimboni kwetu tunatumia shilingi ngapi, tuangalie kuna matatizo kiasi gani. Kwa hiyo, posho pamoja na mshahara naomba Serikali ituangalie, havitoshi kabisa. Wanaosema vinatosha basi naomba posho zao wazielekeze kwenye Jimbo la Nyang’wale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nizungumzie suala la maandamano. Maandamano

sasa imekuwa ni sera ya chama fulani, kila mara maandamano! Hivi ndiyo mmetumwa kuja kusema haya? Maandamano na migomo kwenye Katiba yapo, yaani hayazuiliwi lakini tuangalie. Mimi leo mmenitia hasara kubwa sana, kuna wadogo zangu wawili wamefukuzwa UDOM, wamepata faida gani? Tujaribu kuangalia haya maandamano, lazima hapa kuna agenda ya siri. Kwani sisi hatuwezi kuandamana? CUF na UDP hawawezi kuandamana? Tunaweza! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chama cha Mapinduzi kimepata ushindi wa 61%, leo

umepata 28% unasema kwamba tuna wasiwasi, hata nusu hukufikia! Tukisema wanachana wa CCM, CUF, UDP, TLP tokeni, patakalika? Agenda yenu ya siri ya kusema kwamba nchi hii haitatawalika tuna wasiwasi, inawezekana! Mimi namuomba Mheshimiwa Waziri Mkuu katika majumuisho yake atuambie katika nchi ya Tanzania kuna Serikali ngapi? Kwa nini Serikali ya Chama cha Mapinduzi imekuwa kimya kiasi hicho? Serikali ya Chama cha Mapinduzi ndiyo yenyewe. Wadogo zangu juzi imebidi niwakatie tiketi waondoke, kwa hiyo, ninaomba katika majumuisho tuambiwe kwamba sasa sera zetu, tuzungumzie maandamano. Maandamano yapo ndani ya Katiba lakini tuangalie sababu za kuwaandamanisha watu. Maendeleo yatakujaje? Kila siku maandamano, wanafunzi wanafukuzwa, watasoma vipi? Ninyi mmeandamana mara ngapi wakati mko vyuoni? Kwa hiyo, tunaomba...

(Hapa kengele ililia kuashiria muda wa mzungumzaji kwisha)

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja ya

Mheshimiwa Waziri Mkuu. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Hussein Nassor Amar. Jamani

ndiyo Bunge la Vyama Vingi ni lazima kidogo tuvumiliane. (Makofi)

Page 103: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

103

Sasa nitamuita Mheshimiwa Aliko Kibona. MHE. ALIKO N. KIBONA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue nafasi

hii kukushukuru sana kwa ajili ya kunipa nafasi hii, nadhani ndiyo ya mwisho kwa siku hii ya leo ili niweze kuchangia katika hotuba ya Bajeti ya Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mahali ninaposali nafundishwa katika maandiko

matakatifu kwamba ombeni nanyi mtapewa, tafuteni mtapata, bisheni mtafunguliwa. Kwa vyovyote mbele ya safari ya mjadala au hotuba yangu au mchango wangu yatakuwepo mambo ya kuomba. Pia nimefundishwa kwamba tiini mamlaka iliyopo maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu. Lakini pia katika Mithali 34:14 inasema kwamba; haki huinua Taifa...

MWENYEKITI: Mstari wa nini? MHE. ALIKO N. KIBONA: Katika Biblia takatifu inasema; haki huinua Taifa

bali dhambi ni aibu kwao wote. Watu wamekuja kuomba hapa vitu mbalimbali kwa ajili ya majimbo yao,

ninashauri kwamba haki itendeke katika mgawanyo wa keki ya Taifa. Tusipokuwa na haki Taifa haliwezi kuinuka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitazungumza katika vipengele vitatu, Kitaifa, Kimkoa

yaani Mkoa wangu wa Mbeya na baadaye Wilaya au Jimbo langu. Baba wa Taifa aliwahi kusema Serikali isiyokusanya kodi ni Serikali corrupt. Nilipokuwa nakuja watu wengi waliniuliza maswali na wengi wameongea yaani upande wa Upinzani na upande wa Chama Tawala ya kwamba hawa wawekezaji kwa mfano kwenye hoteli, mimi nikiwa mgeni nataka kujenga, nakuja kuomba sehemu kisha najenga hoteli, napewa muda wa miaka mitano nisilipe kodi. Baadaye ninaondoka ninamuachia ndugu yangu ambaye Serikali haijui kama ni mtoto wangu au binamu yangu au shemeji yangu. Wapiga kura wa Ileje wanaomba nirudi na maelezo. (Makofi)

Mimi naamini kwa jinsi Serikali ya Chama cha Mapinduzi ilivyo sikivu wakati wa

majumuisho ya Waziri wa Viwanda na Biashara au uwekezaji, vyovyote itakavyokuwa nitakuwa nimeshasheheni kichwani kwangu maelezo sahihi kuhusu misamaha ya kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kodi ni haki, ni kitu muhimu na cha lazima. Mtoto

analipa kodi tangu akiwa tumboni mpaka anazaliwa, mtu anakufa anakwenda kaburini

Page 104: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

104

jeneza analozikwa nalo limelipiwa kodi, blangeti, sanda na manukato zinalipiwa kodi, wanakuja watu matajiri na mandege makubwa hawalipi kodi. Mimi kwa kweli bado sijapata maelezo, nimekuwa nikisikiliza mjadala toka mwanzo hata hainiingii akilini, baadaye nilianza kusema sijui sina akili kuliko Wabunge wote? Hiki kitu gani kinaongelewa kuhusu misamaha ya kodi? Somo hili itabidi lilirudiwe kwani mimi sijaelewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mama akiwa mjamzito anajiandaa, anakwenda dukani

kununua vifaa iwe ni nepi, shuka na kadhalika lakini ukimuona ni mjamzito kama wewe unauza vile vifaa huwezi kusema mama kwa vile ni mjamzito hivi vitu napunguza kodi, haiwezekani! Hali kadhalika mtu anapokuja kununua maua ambayo tunayaita mashada kwenda kwenye sherehe ya makaburini hakuna msamaha wa kodi, marehemu ni lazima alipiwe kodi. Maelezo ya kina yanatakiwa kuhusu misamaha ya kodi. Mimi sikubaliani na sijaelewa, naomba maelezo ya kina. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu tumeanza nimewasikia Wabunge wengi wakilia

na tatizo la njaa katika Mikoa na Wilaya zao, chakula kiko kingi Mbeya. Maghala ya Vwawa yana mahindi na mengine yanakuja Makambako. Nawashukuru watu wa Hifadhi ya Chakula ya Taifa, nimeongea nao na nimewaomba na wamefika Jimboni kwangu tayari kununua mahindi kwa ajili ya Hifadhi ya Taifa. Naamini itakuwa sehemu ya ukombozi kwa bei nzuri ya wakulima wa Wilaya ya Ileje. Naamini chakula hiki cha kutoka Ileje, Mbozi, Chunya na sehemu nyingine kitawasaidia Watanzania wenzetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini naomba niseme kwamba sifa ambayo tunasikia ya Mkoa wa Mbeya inahitaji sasa kuangaliwa upya. Tangu nimezaliwa sijawahi kusikia Rais wa nchi anakuja kufungua barabara ya lami iliyojengwa katika Mkoa wa Mbeya. Hongera Wabunge wa Tabora kwa kusimama kidete, leo tunazungumza barabara ya kutoka Tabora kwenda Urambo, Kaliua mpaka Kigoma, barabara inatoka Tabora inakuja Itigi, nyingine inatoka Tabora inakwenda Sikonge na kadhalika. Hongereni sana Wabunge wa Tabora na maeneo ya Kigoma nasikia wiki ijayo Mheshimiwa Rais atakuja Kigoma kuzindua barabara ya lami lakini Mbeya hatuna barabara ya lami hata moja. Ninayoifahamu ni barabara imetoka Dar es Salaam inakwenda Zambia, Zimbabwe mpaka South Africa, Mbeya hakuna barabara nyingine. Sisi ambao tunawalisha, mwananchi anatoka Kamsamba wakati wa masika kuja Vwawa – Mloo kwa nauli ya shilingi 30,000/=, lakini wewe Mbunge mwenzangu unayeniangalia ukiwa na mtoto wako amepangiwa kufanyia kazi Kamsamba, nauli shilingi 30,000/= kuja kuchukua mshahara na kurudi tena kwa nauli ya shilingi 30,000/= utakubali?

Naomba na nimesema aombaye hupewa, tafuteni mtaoana na bisheni mtafunguliwa. Kwa hiyo, sasa naanza wimbo mpaka nitakapotoka katika Bunge hili, hapa nimetengeneza manoti wimbo huu mpaka ueleweke. Tutaimba Wabunge wa Mbeya barabara ya lami itoke Mbalizi mpaka Mwambani, itoke Mbalizi iende Santilia, Ilembo mpaka Ileje. Nyingine itoke Mlowo iende Kamsamba Msangani, itoke Mpemba, Isongole

Page 105: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

105

mpaka border kule Kyela, itoke KK ije Katengele, Kalembo mpaka Ibungu. Itoke pia Katumba Mwakaleli, Ruangwa, Mbwambo mpaka Kyela na kuja Masoko Tukuyu. Hapo mwimbo wangu utakuwa umeeleweka. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nafanya tathmini Wilaya ya Ileje

inawezekana dunia nzima hakuna mahali kakipande ka nchi kanakolima mazao mengi kama Ileje. Ileje tunalima mazao mengi kama kokoa, mpunga, kahawa, ndizi, magimbi, viazi mbatata, viazi mviringo, ngano, maharage, mahindi, vitunguu, pareto, alizeti, mihogo, ulezi, maparachichi, miti ya mbao na kadhalika. Huu tunaouita Mgodi wa Makaa ya Mawe inawezekana hata Mheshimiwa Waziri Mkuu hajui upo Ileje, Ileje ni kipande nani kwao kuna mazao hayo niliyoyasema?

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini siku moja nilisema makaa ya mawe yaliyopo

Ileje, Waheshimiwa Wabunge wakageuka huku wananishangaa kwa sababu Ileje imedharauliwa. Naomba tuwahurumie wananchi wa Ileje. Barabara katika Wilaya ya Ileje ninasihi barabara ya kutoka Luswisi kwenda Ngulilo - Sapanda kuunganisha Ilembo na Mbalizi zichukuliwe na TANROARDS. Barabara ya kutoka Isoko hospitali kupandisha Mlima Katengera ambapo Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete alipotembelea kule gari yake ilikwama. Huwezi kuamini siku moja nilikuwa nakwenda Nzega nikaambiwa kuna mlima mrefu sana, eti huu Mlima Saranda. Nilipofika Itigi nikauliza mbona siupati mlima? Wakasema, umeshapita! (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, milima ipo Ileje, barabara zinaharibika kwa sababu ya

jiografia ilivyo. Naomba barabara ambayo iliahidiwa na Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa ziara yake Ileje kutoka Mpemba mpaka Mbalizi kwenye majumuisho ya ujenzi wananchi wanasubiri kwa hamu kubwa waweze kujua ni nini kinaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu umeme nashukuru, nimemshirikisha ndugu

yangu Waziri Mheshimiwa Ngeleja. Tuna mpango wa kujenga mitambo ya umeme katika Mto Luswisi kwa ajili ya Kata za Luswisi, Ngulilo, Ibaba, Lubanda, Sange, Kalembo, Isoko, Kafule, Kapelekesi, Malangali, Ndembo na Ikinga. Ameniahidi tutashirikiana na naomba Mungu akukumbushe usije ukasahau maana shetani husahaulisha.

Ndugu yangu Mheshimiwa Ngeleja umeniahidi, nashukuru kwa ajili ya ahadi

hiyo na mimi nitakuwa bega kwa bega na wewe tuhakikishe wananchi wa maeneo haya wanapata umeme kwa njia ya umeme vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu maji katika Wilaya ya Ileje ni kwamba kuna

matatizo ya maji hasa hasa katika maeneo ya Miji Mdogo ya Isongole, Itumba, Itale, Ibaba na maeneo mengine. Naomba muhusika wa Wizara hiyo, nimeleta maombi

Page 106: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

106

maalum nakushukuru kwamba umeniahidi utashughulikia, naomba Mungu akukumbushe, shetani asije akaweka tena vizuizi eneo hilo lisipate maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kilimo katika Wilaya ya Ileje nimesema tuna

mazao mengi lakini kwa Bajeti niliyoiona...

(Hapa kengele ililia kuashiria muda wa mzungumzaji kwisha) MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge muda wako umekwisha. MHE. ALIKO N. KIBONA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru na ninaunga

hoja mkono lakini Mawaziri waangalie maeneo niliyoomba. Ahsante sana. (Makofi) MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, huyu ndiye mchangiaji wetu wa

mwisho kwa siku hii ya leo, lakini kesho tarehe 1 Julai, 2011 mara baada ya kipindi cha maswali kutakuwepo na tukio la kuwatambua, kuwapaongeza na kuwaenzi wanafunzi ambao wamefanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita ngazi ya Kitaifa mwaka 2011. (Makofi)

Hivyo basi, nitamuomba Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,

Sera, Uratibu na Bunge aweze kutoa hoja ya kutengua Kanuni inayohusika ili kuwawezesha vijana hao waweze kingia ukumbini hapo kesho. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge,

karibu!

HOJA YA KUTENGUA KAUNI ZA BUNGE

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBU NA BUNGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa maelezo ya hoja ya kutengua Kanuni za Bunge chini ya Kanuni ya 150(1) cha Kanuni za Kudumu za mwaka 2007. (Makofi)

Kwa kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Kanuni ya 139

imejiwekea utaratibu wa kuwatambua, kuwapongeza na kuwaenzi wananchi mbalimbali kutokana na mambo mazuri wanayofanya; na kwa kuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu ameamua kuwapongeza hapa Bungeni, wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha sita ya mwaka 2011. Na kwa kuwa Kanuni ya 136(1) inaruhusu wageni mbalimbali kuingia ndani ya Ukumbi wa Bunge na kukaa katika maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajili ya wageni; na kwa kuwa wakati wa kutoa pongezi hizo italazimu wanafunzi hao 20 waruhusiwe kuingia ndani ya Ukumbi wa Bunge na kupeana mkono na Mheshimiwa Waziri Mkuu na Mheshimiwa Spika; hivyo basi, Bunge linaazimia

Page 107: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

107

kwamba Kanuni ya 136(1) itenguliwe ili kuruhusu wanafunzi hao 20 watoke kwenye eneo maalum la wageni walilotengewa na waweze kuingia kwenye Ukumbi wanapokaa Waheshimiwa Wabunge kwa ajili ya kupongezwa na viongozi hao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja. (Makofi) WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.

(Makofi)

MWONGOZO WA SPIKA

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwongozo wa Mwenyekiti, tafadhali kabla ya maamuzi. Kwa mujibu wa…

MWENYEKITI: Sijakuruhusu. MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, samahani sana. MWENYEKITI: Mwongozo, Mheshimiwa Zitto! MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Kanuni

za Bunge, Uongozi wa Bunge ni watu watatu ambao ni Spika, Waziri Mkuu na Kiongozi wa Upinzani Bungeni. Katika maelezo ambayo Mratibu wa Shughuli za Chama Tawala (Chief Whip), Mheshimiwa William Lukuvi aliyoyasoma inaonesha kwamba wanafunzi hao watampa mkono Spika na Waziri Mkuu. Nilikuwa naomba arekebishe ili wampe mkono Spika, Waziri Mkuu na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, ndiyo tuweze kupitisha suala hilo. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Nchi, unaweza kurekebisha au kama

huwezi mimi nitoe Mwongozo wangu. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBU NA

BUNGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema kwamba kesho kutakuwa na ratiba ya shughuli hii, kwa hiyo, ratiba ya shughuli ya kesho ndiyo ita-determine matukio mengine yatakayofanyika humu ndani. Nilichokuwa naainisha ni kuwaombea kibali cha kukanyaga carpet hii hapa ndani. Kwa hiyo, kesho kutakuwa na ratiba na Mheshimiwa Mbunge naomba tu asiwahishe ratiba ya kesho, ratiba ya kesho itajitambulisha yenyewe. (Makofi)

Page 108: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

108

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kabwe Zitto, uliomba Mwongozo. Mimi naamini hatujapoteza muda, kwa kuwa kilichokuwa kinatolewa hapa na hoja iliyopo mbele yetu ni kuwafanya wale vijana waweze kuingia tu ndani ya Ukumbi, sasa yatakayotokea hapo kesho nadhani utaratibu wake utafuatwa kwa wakati huo. Kwa hiyo, ama Mwongozo huo utaombwa kabla ya shughuli ile iweze kusemwa pale au Spika anaweza akafanya hivyo kwa wakati ule. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, hoja imetolewa na imeungwa mkono.

(Hoja ilitolewa iamuliwe) (Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Bunge liliafiki kutengua Kanuni za Bunge zilizotajwa)

MWENYEKITI: Kwa hiyo, kesho vijana hawa waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita katika mtihani wa Kitaifa wa mwaka 2011 wataingia ukumbini kwa ajili ya shughuli hiyo. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, baada ya shughuli hii sina tangazo lingine na kwa hivyo

ninaliahirisha Bunge hadi kesho saa tatu asubuhi.

(Saa 1.45 usiku Bunge liliahirishwa mpaka siku ya Ijumaa, Tarehe 1 Julai, 2011 saa tatu asubuhi)

Page 109: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1458797824-HS-4-16-2011.pdf · kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu ugonjwa husika

109