8
1 Shule za umma za kata ya Fayette Darasa 1 Mwongozo wa Familia wa Kujifunza Muhtasari wa yale watoto wanastahili kufahamu na kuweza kufanya na njia za familia kuongeza masomo nyumbani. “Tunaamini familia ni wenzetu. Niwa kwanza na waelimishaji wa watoto wenye nguvu zaidi . Pamoja tutahakikisha mafanikio ya wanafunzi wote.” -Mrakibu Emmanuel Caulk, Shule za umma za kata ya Fayette

Darasa 1 - Fayette County Public Schools · “simple Machines” na Allen Fowler ama mafunzo ya hadithi katika vitabu vya fiction kama vile “Frog and Toad Are Friends” (Chura

  • Upload
    others

  • View
    18

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

1Shule za umma za kata ya Fayette

Darasa 1

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza

Muhtasari wa yale watoto wanastahili kufahamu na kuweza kufanya na njia za familia kuongeza masomo

nyumbani.

“Tunaamini familia ni wenzetu. Niwa kwanza na waelimishaji wa watoto wenye nguvu zaidi . Pamoja

tutahakikisha mafanikio ya wanafunzi wote.”

-Mrakibu Emmanuel Caulk, Shule za umma za kata ya Fayette

Darasa 12

Kuhusu mwongozo wetu wa kujifunza:

Mwongozo huu unawakilisha baadhi ya vitu muhimu mtoto wako anapaswa kujuana kuweza kufanya kufikia MWISHO wa mwaka wa shule katika usanaa wa lugha yaKiingereza (ELA) na Hesabu. Malengo ya kujifunza inasaidia familia na walimu kujualini wanafunzi wanahitaji msaada zaidi na lini wanahitaji changamoto zaidi.

Familia zinaweza kufanya nini?

Kuna mengi ya kufanya kumsaidia mtoto wako kujifunza na kusaidia kuwatayarishakwa maisha yao ya mbeleni. Haya ni mambo machache ambayo yatawasaidiawanafunzi kufanikiwa:

1. Shiriki na mtoto wako jinsi masomo yalivyo muhimu kwako. Waambie elimu inastahili, kwamba ni msingi wa mafanikio.

2. Fanya shule iwe kipaumbele kwa kumpeleka mtoto wako shuleni kwa wakati kila siku.

3. Hudhuria mikutano ya mzazi-mwalimu na shughuli zingine za shule inapowezekana.

4. Shiriki na shule kujenga kuheshimiana. 5. Himiza uhuru; ruhusu watoto wako wafanye makosa na wakubali wajibu wa

chaguo lao. 6. Jadiliana na mtoto wako kuhusu nini kinatendeka shuleni. 7. Wasiliana mara kwa mara na walimu wa mtoto wako kuhakikisha mtoto

wako anafanya maendeleo kwa mwaka mzima. 8. Una haki ya kujua jinsi mtoto wako anavyoendelea; usisite kuwasiliana na

mwalimu wake kama una mswali.

Kuzungumza na Mwalimu wa Mtoto wako

Ni muhimu kuwasiliana na mwalimu wa mtoto wako na shule mara kwa mara kuhusumaendeleo ya mtoto wako kuhusu malengo ya masomo. Hapa kuna mifano yamaswali ya kuuliza:

■ Mtoto wangu ana nguvu wapi na ni wapi anahitaji kuboresha? ■ Maendeleo ya mtoto wangu yanapimwa vipi katika mwaka mzima? ■ Naweza kuona mifano ya kazi za mtoto wangu? Vipi wanafikia ama hawafikii

malengo ya masomo? ■ Mtoto wangu yuko njiani kufikia malengo ya kiwango cha darasa? Kama

sivyo, misaada gani shule itatoa? Naweza kufanya nini nyumbani? ■ Mtoto wangu yuko kwa ama juu ya matarajio ya masomo? Kama ndivyo, nini

kingine shule inaweza kutoa? Naweza kufanya nini nyumbani? ■ Mtoto wangu anajifnuza Kiingereza. Kukua kwa lugha ya mtoto wangu

kunasaidiwa vipi shuleni?

Shule za umma za kata ya Fayette 3

Kuzungumza na Mtoto wako

Hii inasikika kama kawaida? “Shule ilikuwaje leo?” “Sawa” “Ulifanya nini?” “Hakuna” Hiyo ni sawa, endelea kuuliza!

Wanafunzi ambao wazazi wao wanazungumza nao kuhusu shule hufanya vizurikimasomo katika shule. Hapa kuna njia unaweza kumhusisha mtoto wako na usaidiemafaniko yake:

■ Teua wakati kila siku kuzungumza na mtoto wako kuhusu shule.■ Uliza mtoto wako akueleze jambo moja walisoma leo. Nini mtoto wako anafaikiri

kuwa inavutia sana? Nini inaonekana ngumu?■ Tizama ama pitia makaratasi na miradi ambayo mtoto wako analeta nyumbani

kutoka shuleni. Uliza mtoto wako: unajuaje hivo? Unadhani nini? Unatambua nini? Kwa nini uliifanya vile ama hivi? Kuna njia nyingine ya kupata jawabu hilo?

■ Pongeza mtoto wako kwa kazi ngumu na bidii, sio tu kwa “majibu sahihi”.■ Uliza maswali kuhusu mtoto wako anafikiria nini: Unajuaje? Unafikiri nini?

Unatambua nini? Uliifanya hivyo kwa nini? Kuna njia nyingine ya kupata jawabu hilo?

Kusaidia kujifunza mbali na nyumbani

Kujifunza hakusimami wakati wanafunzi wanaacha shule. Hapa kuna njia ambazounaweza kusaidia kujifunza nje ya darasani:

■ Somea mtoto wako, soma na mtoto wako, na uhimize wakati wa familia wa kusoma—katika lugha ambayo unajisikia starehe.

■ Tengeneza mahali patulivu na starehe na uunde ratiba ya kila mara kwa wanafunzi wako kufanya kazi za shuleni za kufanyia nyumbani ama shughuli nyingine.

■ Hakikisha wewe na mtoto wako mko na kadi ya maktaba na mnahudhuria shughuli za kusoma kwa familia nzima.

■ Jaribu kuanzisha ratiba ya mara kwa mara ya kufanya homework ama shughuli zingine za kujifunza.

■ Tumia mwongozo huu kulenga malengo machache ya kujifunza, jaribu maoni kadha ya kujifunza nyumbani.

Darasa 14

Nini mwanafunzi wako anapaswa kujua na kuweza kufanyakatika sanaa ya Lugha ya Kiingereza (ELA):

Msingi wa Ustadi/Lugha

□ Fuata sheria za majadiliano, kama vile kusikiliza wengine, kuzungumza mmoja mmoja, na kuuliza maswali ili kuelewa ni nini mtu mwingine amesema.

□ Chagua maneno kwa vikundi, kama vile tofauti (furaha/huzuni) na vitu vinavyoishi (mbwa, paka, miti).

□ Tambua maana sawa ya neno lenye maana mengi, kulingana na sentensi ama aya ambapo neno linatumika (kwa mfano, kuamua kama neno popo linamaanisha mnyama anayepepea ama klabu inayotumika kwa besiboli).

Kusoma na Fasihi

□ Tumia foniki na ujuzi mwingine kutambua mambo yasiyo ya kawaida wakati unasoma, kama vile picha, maneno yanayojulikana katika neno, na dalili za yaliyopo.

□ Tambua wazo kuu na maelezo muhimu katika vitabu vya nonfiction kama vile “simple Machines” na Allen Fowler ama mafunzo ya hadithi katika vitabu vya fiction kama vile “Frog and Toad Are Friends” (Chura na mwanawe ni marafiki) na Arnold Lobel.

□ Tambua tofauti mbali mbali katika hadithi; wahusikia, makao, ploti, tatizo/suluhisho na mtindo wa vituko kwenya hadithi.

□ Kadiria ni nini kitafanyika mara katika hadithi na eleza kama au la makadirio yalikuwa sawa.

□ Soma kwa sauti na sahihi vitabu vya kiwango ya gredi-yako (hakuna makosa), haraka, na mfululizo.

Kuandika

□ Andika na uonyehse hadithi ambazo zina mwanzo , katikati, na mwisho na tumia sentensi wenya muundo kamilifu, herufi kubwa, nafasi, na alama.

□ Jaribu kuandika maneno ambayo haelezi ukitumia maarifa ya sauti za herufi.

□ Andika kuhusu mada, peana ukweli kadhaa, na peana baadhi ya hisia za kufunga.

Shule za umma za kata ya Fayette 5

Jinsi ya kuhimiza kujifunza ELA nyumbani

□ Soma kwa sauti kwa watoto wako kila siku. Read aloud to your child every day.□ Tengeneza flashi kadi ukitumia maneno ambayo mtoto wako anajifunza shuleni.

Tumia kadi kufanya michezo kama Nenda vua (Go Fish) ama kumbukumbu (Memory).

□ Unapokuwa ukisoma hadithi, simama na kumuuliza mtoto wako nini kitafanyika baadaye.

□ Unda hadithi na mtoto wako ukitumia vibaraka ama wanyama waliojazwa ukitumia sauti tofauti kwa wahusika tofauti.

□ Baada ya kusoma vitabu vya nonfiction ama makala, zungumza kuhusu uliyojifunza.

□ Himiza mtoto wako kuleta vitabu nyumbani kutoka shuleni na kuvisoma kwa sauti. Msaidie kutambua maneno magumu na toa maoni kwamba asome tena ili kupata uzoefu (kusoma kwa haraka, sawa, na vizuri).

□ Uliza mtoto wako aandike kuhusu jambo maalum kwake, kama vile sherehe ya kuzaliwa.

Tafadhali ungana na mwalimu wa mtoto wako na uulize kuhusu rasilimali za masomoya nyumbani zinazohusika na programu za kipekee za kusoma na kuandika.

Darasa 16

Nini mwanafunzi wako anapaswa kujua na kuweza kufanyakatika Hesabu:

□ Suluhisha kuongeza na kutoa katika masuala ya maneno katika hali ya kuongeza ma kuondoa kutoka kwa.

□ Suluhisha matatizo kwa kufikiri kuhusu uhusiano kati ya nambari, kwa mfano: 5 + 5 + 10, hiyo 6 + 5 + 11.

□ Tumia vyombo, michoro, na maandishi kuonyesha mbinu na ufumbuzi.

□ Kiakili ongeza na kuondia ndani ya 10. Kwa mfano: Kama nina tano na ninataka 8, ninahitaji ngapi zaidi?”

□ Eleza na ufananishe miundo.

□ Vunja muundo ili kuunda nyingine mpya. Kwa mfano: ukitumia vitalu, tambua kuwa pembetatu 6 zinatengeza hexagoni.

□ Ndani ya 120, hesabu mbele na kurudi nyuma kwa moja na kumi kuanzia kwenya nambari yeyote.

□ Sema na kuandika wakati ukitumia saa ya analog na ya digital kwa masaa na kwa nusu saa.

□ Pima urefu wa kitu ukitumia chombo kifupi kama kitengo cha urefu (pini za karatasi, mapeni).

□ Kusanya, onyesha, na eleza data. Kwa mfano: tengenewa picha, chati, ama grafu ambayo inaonyesha ni wanyama wangapi wako katika kikombe cha kupasua .

□ Tumia kalenda kutambua tarehe, miezi, na siku za wiki.

Shule za umma za kata ya Fayette 7

Njia za kuhimiza masomo ya Hesabu nyumbani

□ Hesabu na ufananishe ukusanyaji wa vifaa na mtoto wako. Kwa mafano: hesabu coins, vikundi vya wanyama ama magari, ama picha katika vitabu. Uliza ni vikundi vipi vya vifaa vina zaidi, vikundi vipi vina vichache.

□ Tundika kalenda sehemu ambayo mtoto wako ataiona na kuitumia kirahisi. Onyesha tarehe muhimu za familia yako, kama vile siku za kuzaliea ama safari za familia. Jadili na mtoto wako ni nini kinatendeka katika tarehe ya leo na uliza, “jana ilikuwa tarehe ngapi?” ama “siku ngapi zimebakia hadi tuende kwenye soko Jumamosi?”

□ Fanya michezo na himiza uzoefu wa kuongeza na kuondoa. Kwa mfano: Hi Ho Cherry-o, uno, Dominoes, Chutes na Ngazi, ifunge juu , (mkusanyiko/kumbukumbu), Go Fish (Nenda vua), blink.

□ Pima umbali na kiasi cha vitu katika nyumba yako kama vile klipu za karatasi ma vijiti ya popsiko. Kabla kupima, uliza mtoto wako akadirie, “Unadhani kujaza hii meza kwa urefu itachukua Klipu ngapi za karatasi?”

□ “Pamoja, zunguka na kuangalia ndani ya nyumba kutambua miundo tofauti. Wacha mtoto wako aeleze miundo kulingana na tabia zake. Kwa mfano: uliza maswali kama vile, hii fremu ya mstatili ya picha ina pande ngapi“?

Tafadhali ungana na mwalimu wa mtoto wako na uulize kuhusu rasilimali za masomo yanyumbani zinazohusika na programu za kipekee za hesabu kwa shule yako.

FAYETTE COUNTY PUBLIC SCHOOLS1126 Russell Cave RoadLexington, KY 40505

859-381-4100 www.fcps.net

Brosha hii imechapishwa na shule za umma za kata ya fayette.

Ilitengenezwa Fall 2016