8
4 Shule za umma za kata ya Fayette Darasa la 4 Mwongozo wa Familia wa Kujifunza Muhtasari wa yale watoto wanastahili kufahamu na kuweza kufanya na njia za familia kuongeza masomo nyumbani. “Tunaamini familia ni wenzetu. Niwa kwanza na waelimishaji wa watoto wenye nguvu zaidi . Pamoja tutahakikisha mafanikio ya wanafunzi wote.” - Mrakibu Emmanuel Caulk, Shule za umma za kata ya Fayette

Darasa la 4 · Eleza maoni ya kitabu, hadithi, ama jarida aliyosoma ukitumia maelezo ya kuunga mkono. Tambua maana ya nahau za kawaida (maneno yanayoonyesha mawazo mbali na maana

  • Upload
    others

  • View
    22

  • Download
    2

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Darasa la 4 · Eleza maoni ya kitabu, hadithi, ama jarida aliyosoma ukitumia maelezo ya kuunga mkono. Tambua maana ya nahau za kawaida (maneno yanayoonyesha mawazo mbali na maana

4Shule za umma za kata ya Fayette

Darasa la 4

Mwongozo wa Familia wa Kujifunza

Muhtasari wa yale watoto wanastahili kufahamu na kuweza kufanya na njia za familia kuongeza masomo

nyumbani.

“Tunaamini familia ni wenzetu. Niwa kwanza na waelimishaji wa watoto wenye nguvu zaidi . Pamoja

tutahakikisha mafanikio ya wanafunzi wote.”

- Mrakibu Emmanuel Caulk, Shule za umma za kata ya Fayette

Page 2: Darasa la 4 · Eleza maoni ya kitabu, hadithi, ama jarida aliyosoma ukitumia maelezo ya kuunga mkono. Tambua maana ya nahau za kawaida (maneno yanayoonyesha mawazo mbali na maana

Darasa la 42

Kuhusu mwongozo wetu wa kujifunza:

Mwongozo huu unawakilisha baadhi ya vitu muhimu mtoto wako anapaswa kujuana kuweza kufanya kufikia MWISHO wa mwaka wa shule katika usanaa wa lugha yaKiingereza (ELA) na Hesabu. Malengo ya kujifunza inasaidia familia na walimu kujualini wanafunzi wanahitaji msaada zaidi na lini wanahitaji changamoto zaidi.

Familia zinaweza kufanya nini?

Kuna mengi ya kufanya kumsaidia mtoto wako kujifunza na kusaidia kuwatayarishakwa maisha yao ya mbeleni. Haya ni mambo machache ambayo yatawasaidiawanafunzi kufanikiwa:

1. Eleza na mtoto wako jinsi masomo yalivyo muhimu kwako. Waeleze elimu inastahili, kwamba ni msingi wa mafanikio.

2. Fanya shule iwe kipaumbele kwa kumpeleka mtoto wako shuleni kwa wakati kila siku. Kwa kufanya hivyo unaonyesha kwamba ni kipaumbele.

3. Shirikiana na shule kujenga kuheshimiana. 4. Himiza uhuru; ruhusu watoto wako wafanye makosa na wakubali wajibu wa

chaguo lao. 5. Jadiliana na mtoto wako kuhusu nini kinatendeka shuleni. 6. Wasiliana mara kwa mara na walimu wa mtoto wako kuhakikisha mtoto

wako anafanya maendeleo kwa mwaka mzima. 7. Hudhuria mikutano ya mzazi-mwalimu na shughuli zingine za shule

inapowezekana. 8. Una haki ya kujua jinsi mtoto wako anavyoendelea; usisite kuwasiliana na

mwalimu wake kama una mswali.

Kuzungumza na Mwalimu wa Mtoto wako

Ni muhimu kuwasiliana na mwalimu wa mtoto wako na shule mara kwa mara kuhusumaendeleo ya mtoto wako kuhusu malengo ya masomo. Hapa kuna mifano yamaswali ya kuuliza:

■ Mtoto wangu ana nguvu wapi na ni wapi anahitaji kuboresha? ■ Maendeleo ya mtoto wangu yanapimwa vipi katika mwaka mzima? ■ Naweza kuona mifano ya kazi za mtoto wangu? Vipi wanafikia ama hawafikii

malengo ya masomo? ■ Mtoto wangu yuko njiani kufikia malengo ya kiwango cha darasa? Kama

sivyo, misaada gani shule itatoa? Naweza kufanya nini nyumbani? ■ Mtoto wangu yuko kwa ama juu ya matarajio ya masomo? Kama ndivyo, nini

kingine shule inaweza kutoa? Naweza kufanya nini nyumbani? ■ Umesoma IEP ya mtoto wangu? Ni makao gapi yanayofanyiwa mtoto

wangu? ■ Mtoto wangu anajifnuza Kiingereza. Kukua kwa lugha ya mtoto wangu

kunasaidiwa vipi shuleni?

Page 3: Darasa la 4 · Eleza maoni ya kitabu, hadithi, ama jarida aliyosoma ukitumia maelezo ya kuunga mkono. Tambua maana ya nahau za kawaida (maneno yanayoonyesha mawazo mbali na maana

Shule za umma za kata ya Fayette 3

Kuzungumza na Mtoto wako

Hii inasikika kama kawaida? “Shule ilikuwaje leo?” “Sawa” “Ulifanya nini?” “Hakuna” Hiyo ni sawa, endelea kuuliza!

Wanafunzi ambao wazazi wao wanazungumza nao kuhusu shule hufanya vizurikimasomo katika shule. Hizi ni baina ya njia za kumhusisha mtoto wako na kusaidiakatika mafaniko yao:

■ Tenga wakati fulani kila siku kuzungumza na mtotowako kuhusu shule. Uliza mtoto wako ni darasa gani alipendelea zaidi leo. Kwa nini? Ni kitu gani kimoja angeweza kubadilisha kuhusu siku hiyo? Kwa nini?

■ Uliza mtoto wako akueleze kitu kimoja walijifunza wamejifunza leo. Ni nini mtoto wako anafikiri inavutia sana? Ni nini inaonekana kuwa ngumu?

■ Pitia makaratasi na miradi ambayo mtoto analeta nyumbani kutoka shuleni. Uliza mtoto wako akueleze inaonyesha mafunzo gani?

■ Sifia mtoto wako kwa kazi ngumu na juhudi, sio wakati tu “majibu ni sahihi”.■ Uliza maswali kuhusu mtoto wako anawaza nini? Unafikiri nini? Unatambua nini?

Uliifanya hivyo kwa nini? Kuna njia nyingine ya kupata jibu hilo?

Kusaidia mafunzo mbali na shule

Mafunzo hayapaswi kusimama wakati wanafunzi wanaache shule. Wanafunzihutumia mda mwingi nje ya shule kuliko katika shule. Hizi ni baina ya njia ambazounaweza kusaidia masomo nje ya shule:

■ Somea mtoto wako, soma na mtoto wako, na uhimize mda wa familia kusoma pamoja — katika lugha unayoipendelea.

■ Tenga wakati mtulivu na mahali starehe kwa mwanafunzi wako kufanya kazi za shule za nyumbani ama shughuli zingine za masomo.

■ Jaribu kutengeneza ratiba ya kawaida ya kufanya kazi za shule za nyumbani na shughuli zingine za masomo.

■ Tumia muongozo huu kwa malengo machache ya masomo; jaribu mapendekezo kadhaa ya masomo ya nyumbani.

■ Himiza mtoto wako kutumia ubishi wenye maana kutetea maoni yao. Kwa mfano, kama mtoto wako anataka nyongeza ya mapato, muulize kufanya utafiti kuhusu jinsi mapato yanapeanwa. Kisha kulingana na utafiti, eleza ni kwa nini wanahitaji nyongeza ya mapato yao na saidia maombi yao ukitumia maelezo na ukweli.

■ Zungumza kuhusu taarifa pamoja. Chagua hadithi moja, isome na mtoto wako na mjadiliane maana yake.

■ Zungumza na mtoto wako kuhusu lengo lao. Wanataka kufanya nini wakimaliza sekondari? Sikiliza wanavyosema na uwape mawaidha ili kusaidia kufikia malengo yao.

Page 4: Darasa la 4 · Eleza maoni ya kitabu, hadithi, ama jarida aliyosoma ukitumia maelezo ya kuunga mkono. Tambua maana ya nahau za kawaida (maneno yanayoonyesha mawazo mbali na maana

Darasa la 44

Ni nini mwanafunzi wako anapaswa kujua na kuwezakufanya katika sanaa ya lugha ya kiingereza (ELA):

Lugha□ Eleza maoni ya kitabu, hadithi, ama jarida aliyosoma ukitumia maelezo ya

kuunga mkono. □ Tambua maana ya nahau za kawaida (maneno yanayoonyesha mawazo mbali na

maana hakika ya neno) kama vile “tone katika ndoo” ama “kipande cha keki”.□ Fikiria maana ya neno lisilo la kawaida kwa kutumia ufahamu wa viambishi vya

kawaida katika neno (kama vile de-, ex-, na pre-) na vimalizio vya maneno (kama vile –er, -ly, na –ous).

□ Fupisha na ujibu taarifa iliyotolewa katika majadiliano.

Kusoma na Fasihi □ Tofautisha chanzo na athari katika hadithi za ukweli katika kitabu ama jarida. □ Tambua mandhari au mafunzo katika hadithi. □ Tambua mashairi, mtindo, marudio, tashibiha, mifano, na picha hisia katika shairi. □ Linganisha mawazo, wahusika, matukio, na vikao katika hadithi kutoka kwa mila

tofauti.

Kuandika□ Andika maoni ya hadithi, ukitumia maelezo kutoka kwa maneno ya kitabu

kusaidia mawazo yao. □ Kusanya habari kutoka sehemu nyingi na uandike muhtasari wa utafiti ukitumia

maneno yao wenyewe na mpangilio sahihi. □ Andika hadithi fupi ambayo ina mazungumzo na maelezo ya wahusika na

matukio.

Page 5: Darasa la 4 · Eleza maoni ya kitabu, hadithi, ama jarida aliyosoma ukitumia maelezo ya kuunga mkono. Tambua maana ya nahau za kawaida (maneno yanayoonyesha mawazo mbali na maana

Shule za umma za kata ya Fayette 5

Jinsi ya Kuhimiza Masomo ya ELA Nyumbani

□ Kusanya nahau pamoja na mtoto wako kama vile “usihesabu vifaranga wako kabla kuzaliwa,” na “inanyesha paka na mbwa.” Zungumza kuhusu semi hizi zinamaanisha nini haswa.

□ Soma hadithi zisizo kweli, hadithi za kweli (jarida, vitabu vyenye habari/taarifa), na mashairi pamoja na mtoto wako. Jadili mandari ama mafunzo wakati unaposoma hadithi na zungumza kuhusu nini mnachojifunza mnaposoma hadithi. Ukisoma shairi, jadili jinsi mshairi anatumia maneno kutengeneza picha.

□ Jadili nini mtoto wako amejifunza katika sayansi. Tambua jambo ambalo anapendelea sana kama vile wanyama ambao wanabadilisha rangi, na tafuta habari kuhusu mada pamoja katika mtandao na maktaba.

Tafadhali ungana na mwalimu wa mtoto wako na uulize kuhusu rasilimali za masomoya nyumbani zinazohusika na programu za kipekee za kusoma na kuandika.

Page 6: Darasa la 4 · Eleza maoni ya kitabu, hadithi, ama jarida aliyosoma ukitumia maelezo ya kuunga mkono. Tambua maana ya nahau za kawaida (maneno yanayoonyesha mawazo mbali na maana

Darasa la 46

Ni nini mwanafunzi wako anatakiwa kujua na kuwezakufanya katika hesabu:

□ Fikiri kuhusu na utatue hesabu za kuzidisha na kugawanya ukitumia ujuzi ya kufikiria, ukweli wa nambari za kawaida na vifaa tofauti (sama vile safu – mpangilio wa vitu, picha, ama nambari katika kolamu na row).

□ Zidisha na ugawanye nambari nyingi katika mifano rahisi. Kwa mfano, zidisha 1,638 x 7 ama gawanya 6,966 kwa 6.

□ Endelea kujenga ufahamu wa mfumo wa nambari haid 10,000 na zaidi. Tumia ufahamu huu wakati unapoongeza, kuondoa, na kulinganizah nambari kubwa. Elewa sehemu ya nambari ambayo inaeleza mamoja, makumi, mamia, na kadhalika.

□ Tambua mviringo na eneo la miundo tofauti na uzipe jina lenye kipimo sawa na kitengo, kama vile fiti ama fiti mraba.

□ Elewa kwamba fraksheni inaweza kuwa sehemu nzima au nusu ya kitu fulani.

□ Elewa na uweke usawa ( dhamani sawa) fraksheni. Kwa mfano, kutambua kwamba ¼ ni chache kuliko 3/8 kwa sababu 2/8 (ambayo ni sawa na ¼) ni chache kuliko 3/8.

□ Kuelewa nukta rahisi kulingana na fraksheni. Kwa mfano: kuandika tena 0.62 kama 62/100.

□ Tambua kipimo cha pembe kulingana na kulia (90-digrii) pembe. Kwa mfano: pembe ya digrii 30 ni 1/3 ya pembe ya digrii 90.

□ Kusanya, wakilisha, chambua, na tafsiri data.

Page 7: Darasa la 4 · Eleza maoni ya kitabu, hadithi, ama jarida aliyosoma ukitumia maelezo ya kuunga mkono. Tambua maana ya nahau za kawaida (maneno yanayoonyesha mawazo mbali na maana

Shule za umma za kata ya Fayette 7

Jinsi ya Kuhimiza Masomo ya Hesabu Nyumbani

□ Tatua hesabu ya kuzidisha pamoja. Uliza mtoto wako alivyoitatua. Linganisha na jinsi ulivyoitatua. Uliza kama kuna njia nyingine ya kuitatua. Jaribu njia tofauti za tutatua matatizo mengine.

□ Angalia miundo katika magazini, magazeti, na vitu vya kila siku. Jadiliana kama miundo ina pembe za digrii 90 (pembe kulia), chini ya digrii 90 (pembe kali), ama zaidi ya digii 90 (pembe obtusi).

□ Ambia mtoto wako atatute eneo la juu ya meza, juu ya deski, ama mkeka katika nyumba yako. Kabla kupima, kila mmoja wenu anaweza kukadiri vitengo vya mraba vingapi vinaweza kuwa na ulinganishe makadirio na majibu.

□ Unapopika ama kubeki, ambia mtoto wako apime viungo na ataje fraksheni. Uliza utahitaji kiasi gani cha viungo kama utahitaji kuzidisha recipe mara mbili.

□ Tengeneza grafu inayoonyesha muda jua inapotokea ama inapotua katika Lexingon, ukitumia data kutoka kwa gazeti ama kwenye mtandao.

Tafadhali ungana na mwalimu wa mtoto wako na uulize kuhusu rasilimali za masomo yanyumbani zinazohusika na programu za kipekee za hesabu.

Page 8: Darasa la 4 · Eleza maoni ya kitabu, hadithi, ama jarida aliyosoma ukitumia maelezo ya kuunga mkono. Tambua maana ya nahau za kawaida (maneno yanayoonyesha mawazo mbali na maana

FAYETTE COUNTY PUBLIC SCHOOLS1126 Russell Cave RoadLexington, KY 40505

859-381-4100 www.fcps.net

Brosha hii ilichapishwa na Shula za Umma za Kata ya Fayette.

Iliundwa Fall 2016