18
EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA DARASA VII KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA MWANAFUNZI: _____________________ MAELEKEZO 1. Kumbuka kuandika majina yako matatu kwa usahihi. 2. Jibu maswali yoe kulingana na maelekezo. 3. Soma maswali kwa ufasaha kabla ya kuyajibu. SHULE YA MSINGI MARTIN LUTHER S. L. P 1786 Dodoma. Simu. +255 26 2395029, +255 784 449098 Fax +255 26 2395030 (www.martinlutherschooldodoma.com) “Quality Education for the New Generation”

DARASA VII KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA …JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA DARASA VII – KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA

  • Upload
    others

  • View
    75

  • Download
    8

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: DARASA VII KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA …JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA DARASA VII – KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

DARASA VII – KAZI YA NYUMBANI

KISWAHILI

JINA LA MWANAFUNZI: _____________________

MAELEKEZO

1. Kumbuka kuandika majina yako matatu kwa usahihi.

2. Jibu maswali yoe kulingana na maelekezo.

3. Soma maswali kwa ufasaha kabla ya kuyajibu.

SHULE YA MSINGI MARTIN LUTHER S. L. P 1786 Dodoma. Simu. +255 26 2395029, +255 784 449098

Fax +255 26 2395030 (www.martinlutherschooldodoma.com)

“Quality Education for the New Generation”

Page 2: DARASA VII KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA …JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA DARASA VII – KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, OFISI YA RAISI

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA SHULE YA MSINGI MARTIN LUTHER

KISWAHILI, KAZI YA NYUMBANI, APRILI, 2020

JINA: ____________________________DARASA LA VII: _______ SEHEMU “A”: MSAMIATI. Andika herufi ya jibu sahihi 1. Mtu anayefundisha chuo kikuu huitwaje ……..

A. mkurugenzi B .mhadhara C. profesa D. mkufunzi E. Mhenga. [ ]

2. Mzee John amemletea mwanae KIZIBAO. Neno kizibao limetumika likiwa na maana ipi? A. Suti nyenye mikono mirefu B. shati lenye mikono mifupi C. Jaketi kubwa D. Koti lenye mikono mirefu E .Koti fupi lisilo na mikono. [ ]

3. Kaka anapenda kujisomea c humbani kwake. Katika sentensi hii neno gani limetumika kama kitenzi kisaidizi?....... A. anapenda B. kujisomea C. kaka D. kwake E. chumbani. [ ]

4. Mtu mwenye mguu mbovu na anatembea kwa kuchechemea anaitwa?..........

A. Kengeza B. kiwete C. masinini D. kiguru E. kikono. [ ]

5. Kinyume cha neno mzalendo?............. A. muungwana B. mchoyo C. haini D. jambazi E. mwanajeshi. [ ]

6. Babu yangu amekuwa ……kwani amekuwa na umri wa miaka mia moja. A. ajuza B. manju C. hafifu D. mgane E. buda. [ ]

7. Neno lenye maana sawa na “Kiambaza” ni ……….

A. jiko B. kifungo C. dhamana D. ukuta E. hukumu. [ ]

8. Nimetuma ujumbe lakini sijapata mrejesho wowote. Neno lililopigiwa mstari lina maana sawa

na neno lipi?........... A. asante B. ushauri C. mwaliko D. jibu E. mawasiliano. [ ]

9. Ng’ombe dume aliyehasiwa ambaye hutumika kwa kufanya kazi kama v ile kuvuta mkokoteni

au kukokota plau huitwa …..A. mbuguma B .beberu C. maksai D .gegedu E. fahali. [ ]

10. Muziki, maigizo, ushairi na vichekesho kwa neno moja ni?....................... A. nyimbo B. marimba C. sinema D. zeze E. sanaa. [ ]

Page 3: DARASA VII KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA …JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA DARASA VII – KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

11. Wewe utazungumza kwa…………….ya mwalimu mkuu. A. njia B. niaba C. mara D. kwa sababu E. badala [ ]

12. Mtoto wa kuku anaitwa kifaranga, je mtoto wa ng’ombe ni .......... A. Kinda B. Kuku C. Mwewe D. Ndama [ ]

13. Mtoto wa Shangazi au Mjomba ninamwita...... A. dada B. kaka C. shangazi D. Binamu. [ ] 14. Mawaidha ni…. A. masikitiko B. maono C. ushauri D. maradhi E. marathi [ ]

15. Kutembea kwa matao ni kutembea kwa mwendo wa …..

A. kasuku B. maringo C. polepole D. haraka haraka E. kuchechemea. [ ]

16. Mzee yule ana kibiongo. Kibiongo ni …..... A. nundu B. pua kubwa C. jicho moja D. mfupi E. toinyo [ ]

17. Kinyume cha neno HASIMU ni …… A. adui B. rafiki C. ghadhabu D. aghalabu E. mzazi [ ]

18. Mtu anayesaliti nchi au serikali huitwa ….........

A. haini B. fedhuli C. mzalendo D. kaidi E. fisadi [ ] 19. Wanafunzi wote walipoelezwa walielewa isipokuwa Tino ambaye ni ….

A. bilula B. renge C. damsi D. gomesi E. luja [ ]

20. Msichana yule ana nywele za …... A. singa B. katani C. mafuta D. mnato E. marashi [ ] 21. Stadi wa kutunga na kuimba nyimbo katika ngoma ni ……..

A. magumu B. kungwi C. manju D. nyakanga E. mahiri [ ]

22. ..............ni mchezo kukimbia kwa miguu. A. Siasa B. Upepo C. Rede D. Riadha [ ]

A. huruma B. uwongo C. uoga D. haya E. imani . [ ]

23. Neno Msimu lina maana ya …… A. muda B. mvua C. majira D. masika E. kipupwe [ ] 24. Sehemu ya juu inayofunika nyumba huitwa…… A. ghorofani B. dari C .boriti D. bati E. paa [ ] 25. Neno Motisha lina maana sawa na… A. rushwa B. posho C. ajira D. mashahara E. zawadi [ ]

26. ……..za chama chetu haziruhusu ubaguzi. A. siasa B. sera C. shughuli D .harakati E. staha [ ] 27. Neno Kabumbu, kisawe chake ni ..... A. Ukungu B. Kandanda C.Niti D. Kikapu E. Muziki [ ] 28. Mtu anayetengeneza majembe, mapanga, visu, huitwa ……

A. mwashi B. makenika C .fundi D. mhunzi E. sonara [ ]

Page 4: DARASA VII KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA …JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA DARASA VII – KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

29. Neno machweo lina maana sawa na …… A. adhuhuri B .asubuhi C .magharibi D. mchana E .alasiri [ ]

30. Uhodari wa kufanya jambo ni …… A. umaarufu B. umahiri C. ukongwe D. utaratibu E. ushujaa [ ]

31. Neno lenye maana sawa na “Mithilisha” ni …….. A. ridhisha B. mathalani C. fananisha D. madhalani [ ]

32. ……ya kuhifadhi vitabu imeharibika. A. droo B. lafu C. lavu D. rafu E .dawati [ ]

33. Rukia anafanya kazi yake kwa umakini, badala ya kutumia neno “umakini” unaweza kutumia neno lipi kati ya haya yafuatayo? A. busara B. hekima C. uangalifu D. umahiri E. hekima [ ]

34. Neno moja linalotumika kutaja mchuzi wa samaki, mchuzi wa nyama, mchuzi wa dagaa ni ……. A. nyama B. kitoweo C. mboga D. mchuzi E. mahanjumati. [ ]

35. Kisawe cha neno bibi ni …… A. ajuza B. kikongwe C. mkongwe D. nyanya E. kinyanya [ ]

36. Ugonjwa wa utapiamlo husababishwa na ukosefu wa ….. A. malezi B. chanjo C. maziwa D. chakula bora E. nishati. [ ]

37. Kinyume cha neno mtafaruku ni ………... A. mwafaka B. ugomvi C. ghasia D. ujamaa E. mvutano. [ ]

38. Mtu asiyeweza kutembea anaitwaje? A. bubu B. kiziwi C. kiwete D. kilema E. kipofu. [ ]

39. Yupi kati ya hawa lazima awe mwanamke? A. mpwa B. kitukuu C. kaka D. shangazi E. kining’ina [ ]

40. Neno TABIBU lina irabu ngapi? A. mbili B. tatu C. moja D. nne E. sita. [ ]

41. Mtu anayekimbia nchi yake kwa kuhofia usalama wake huitwa ...... A. Mhamiaji B.Mwizi C. Mkimbizi D .Fukara E .Safari. [ ]

42. Kazi yako ina walakini. Neno ‘walakini’ lina maana gani? A. kasolo B. kasumba C. kasoro D .safi E. uchoyo. [ ]

43. Wanyama kama vile ng’ombe na mbuzi hufugwa kwenye ........ A. zuzu B. shimo C. zizi D. kiota E. mzinga [ ]

44. Mshitakiwa aliomba mahakama impe …….

Page 5: DARASA VII KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA …JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA DARASA VII – KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

A. mdhamana B. dhamana C. thamana D. samana E. zamana. [ ]

45. Maji yalijaa ………ndani ya ndoo. A. tele B .sana C. pomoni D. juu E. hadi. [ ]

46. Mzanie ni kitukuu changu. Kwa hiyo Mzanie ni mtoto wa ……. A. mpwawangu B. mjukuu wangu C. mtoto wa mtoto wangu D. binamu yangu E. baba na mama mkubwa. [ ]

47. Kinyume cha neno pomoni ni ........ A. jaa B. mwagika C. miminika D. ongezeka E. mwaga [ ]

48. Maji ya matunda yaliyokamuliwa huitwa .......... A. zabibu B. matamu C .sharubati D. asali E. maziwa [ ]

49. Neno haba lina maana sawa na ..... A. kiasi B. kidogo C. wastani D. rasharasha E. zaidi [ ]

50. Mlinzi wa mlangoni huitwa .... A. Bawaba B. Bawabu C. Baharia D. Banati E. bubu [ ]

51. a, e, i, o, u. kwa pamoja huitwa ..... A. Irabu B. silabi C. neno D. maneno E. sentensi [ ]

52. Ng’ombe jike huitwa maksai ........... A. kweli B. si kweli C. ni kweli D. sijui E. ni sahihi [ ]

53. Neno televisheni linafanana na ......... A. redio B. Komputa C. runinga D. simu E. tochi [ ]

54. Kirefu cha neno MWISHOWE ni....... A. juu yake B. chini yake C. pembeni D. mwisho wake [ ]

55. Baada ya msemaji kutoa ..........wageni waliondoka na kurudi makwao.

A. fahari B. Posa C. Barua D. Mahari E. Mali [ ]

56. Yule bwana amelima kwa bidii na amevuna ..........mwingi sana.

A. mipunga B. Mchele C. Mpunga D. wali E. Michele [ ]

SEHEMU B: Sarufi. Chagua herufi ya jibu sahihi na uweke kivuli katika karatasi yako ya kujibia.

57. Wangapi wanapenda kuimba? Neno wangapi limetumika kama……… A .Kivumishi B. Kielezi C. Kiwakilishi D .kitenzi E .Kiunganishi [ ]

58. Dada ameandika hadithi nzuri. Sentensi hii iko katika kauli gani?............ A. Kutenda B. Kutendea C .Kutendeka D .Kutendwa E. Kutendana [ ]

59. Kiambishi cha wakati katikaneno “Wanaandika” ni…… A. –ndika B. –na- C. wana D. wa E. –and- [ ]

Page 6: DARASA VII KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA …JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA DARASA VII – KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

60. Mtoto mchanga analia sana. Neno lililopigiwa mstari limetumika kama aina gani ya maneno? A. Kiwakilishi B. Kitenzi C. nomino D. kivumishi E. kielezi. [ ]

61. Johari ametunukiwa nishani ya shaba. Sentensi hii iko katika kauli gani?............. A. Kutendwa B. kutendewa C. kutenda D. kutendeana E. kutendea. [ ]

62. Kyaruzi ni mtoto wa mjukuu wangu; hivyo kyaruzi ni nani kwangu………. A. kilembwekeze B. Kitukuu C .Kining’ina D .Mjukuu E. kilembwe. [ ]

63. Neno ndoo lipo katika ngeli gani?.......... A. KI-VI B. LI-YA C. I-ZI D. A-WA E. U-YA [ ]

64. Yandilo alinitembelea jana kwa……kunijulia hali………… A. dhumini la B. zumuni la C. dhumini ya D. madhumuni ya E. mazumuni ya [ ]

65. Neno mbarika lina silabi ngapi?............ A. 1 B. 3 C. 5 D. 6 E. 2 [ ]

66. Siku ile ya maandamano kulikuwa na ………..wa pikipiki. A. msululu B. msururu C. msuluru D. msurulu E. msusulu [ ]

67. Katika neno “sitakuwepo” kiambishi kipi kinaonyesha ukanushi?.......... A. ta- B. - we C. ku- D. –po- E. si- [ ]

68. Mvutano kati ya wanakijiji na viongozi wao ulikuwa haujapatiwa ……Neno linalo kamilisha sentensi hii ni…. A. ugunduzi B. ufunguzi C. ufumbuzi D. uvamizi E. uchunguzi. [ ]

69. Kipi ni kinyume cha neno ‘gwiji’…… A. mwerevu B .asiye hodari C. mwanamuziki D. mwimbaji E. hodari [ ]

70. Mwalimu aliwaambia kuwa wasome kwa bidii. Sentensi hii ipo katika kauli ipi? ………. A. taarifa B .timilifu C. halisi D. shurutia E. masharti [ ]

71. Mjomba anafanya kazi ya kupakia na kupakua shehena katika meli, kwa hiyo yeye ni …… A. kuli B. nahodha C. baharia D. kondakta E. mali [ ]

72. Katika maneno yafuatayo ni lipi lina maana zaidi ya moja…………. A. kaa B. rika C. imba D. chake E. mwashi [ ]

73. Sisi ni wanafunzi makini. Kiwakilishi katika sentensi hii ni cha aina gani?.............

A. sifa B. nafsi C. pekee D. jumla E. kirejeshi [ ]

74. Ondoka hapa haraka. Hii ni tungo inayoonesha……. A. ombi B. onyo C. amri D. unyenyekevu E. upole [ ]

75. Neno lipi ni tofauti na maneno mengine kati ya yafuatayo?.............

Page 7: DARASA VII KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA …JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA DARASA VII – KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

A. Seng’enge B .wigo C. barabara D. ukuta E. uzio. [ ]

76. Watu waliokusanyika pamoja ili kuabudu huitwa…… A . Wajenga kanisa B. waabudio C .waumini D. waswalishwa E. wakereketwa [ ]

77. Haruni ni mtoto mtukutu. Neno lililotumika kama kitenzi ni…….. A. Haruni B. ni C. mtoto D. mtukutu E. hakuna [ ]

78. Lahaula! Sijawahi kumuona nyoka mkubwa hivi. Neno “lahaula!” limetumika kama……… A. kielezi B. kivumishi C. kihisishi D. kitenzi E. kiungo [ ]

79. Neno “walituhamasisha” lina silabi ngapi?...... A. saba B. tano C. nne D. sita E. nane [ ]

80. Katika neno “wataimba” kiambishi kinachoonesha nafsi ni kipi?...... A. wa B. ta C. imb- D. a E. I [ ]

81. Neno mtoto lipo katika ngeli gani?........ A. A-WA B. LI-YA C. KI-VI D. I-ZI E. LI-ZI [ ]

82. Pepe amemchezea vibaya Messi. Katika sentensi hii mtenda ni nani?.......... A. mpira B. Messi C. Pepe D. vibaya E. uwanja [ ]

83. Kipya kinyemi ingawa kidonda. Neno ingawa limetumka kama.… A. U B. V C. N D. W E. T [ ]

84. Je, katika neno amekufa, mzizi wa neno hilo ni….. A. -kuf- B. -fa- C. -f- D. -mekuf E. -ku- [ ] 85. Unapounganisha herufi za konsonanti na irabu tunapata………..

A. neno B. sentensi C. tungo D. silabi E. sauti [ ]

86. Sentensi ipi ni sahihi zaidi kisarufi kati ya hizi zifuatazo…….. A. Wamekopeshwa gari tano B. Wamekopeshwa magari matano C. Wamekopeshwa tano gari D. Gari tano wamekopeshwa E. Matano magari wamekopeshwa [ ]

87. “Ningeliwahi mapema nisingeli chelewa basi” Maumbo haya “nge” na “ngali” hutumika tu katika wakati gani?........ A. uliopo B. uliopita C. ujao D. mtimilifu E. nyakati zote [ ]

88. Alisema yeye hana ubaya na mtu. Neno lililotumika kama kiwakilishi katika sentensi hii ni lipi?........

A. yeye B. alisema C. hana D. ubaya E. mtu [ ]

89. Kipi ni kisawe cha neno wali……… A. chakuula B. mlo C. wali D. ugali E. ubwabwa [ ]

90. Kipindi cha miaka mia moja huitwa……… A. muhula B. karne C. muongo D. zama E. milenian [ ]

91. Baba yangu ni mwenyekiti wa kijiji. Neno “mwenyekiti” ni nomino ya aina gani?........ A. dhahania B. kawaida C. pekee D. jumla E. mguso [ ]

Page 8: DARASA VII KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA …JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA DARASA VII – KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

92. Ng’ombe dume huitwa…… A. Mori B. Fahali C. Fahari D. Gegedu E. Mbuguma [ ]

93. Andika kinyume cha neno nadra…………………….

A. mara dufu B. anglau C. agharabu D. aghalabu E. mara chache [ ]

94. Neno gani kati ya haya yafuatayo lina maana ya utajiri?...........

A. ukwasi B. ubosi C. umwinyi D. umaskini E. ukata [ ]

95. Alikuwa anajibu kihuni. Neno “kihuni” limetumika kama aina gani ya maneno?........

A. kielezi B. kiwakilishi C. kivumishi D. kitenzi E. kihisishi [ ]

96. Ooh! Pole ndugu yangu ni mapenzi ya Mungu. Kihisishi katika sentensi hiyo ni kipi?

A. mapenzi B. ndugu C. Mungu D. ooh! E. yangu [ ]

97. “Mganga anatibu magonjwa” sentensi hiyo ipo katika kauli gani? A. kutenda B. kutendwa C. kutendewa D. kutendeka E. kutendana [ ]

98. Wangapi wamechelewa shuleni? Katika sentensi hiyo neno “wangapi” limetumika kama aina

gani ya maneno? A. kiulizi B. kiwakilishi C. kielezi D. kitenzi E. kivumishi [ ] 99. Kati ya sentensi zifuatazo ipi ina maana sahihi zaidi? A. Mtamu ni huu wali. B. Huu wali mtamu ni.

C. Wali huu ni mtamu. D. Wali ni mtamu huu. E. Ni wali mtamu huu. [ ] 100. Ni neno lipi kati ya haya yafuatayo ni kisawe cha neno “magonjwa?”

A. shida B. balaa C. maradhi D. malazi E. UKIMWI [ ] 101. Neno linalojumuisha herufi ka, ba, cha, da, mbe ni lipi kati ya haya yafuatayo:

A. irabu B. konsonanti C. vitanza ndimi D. ambatano E. silabi [ ] 102. “Samatta hucheza mpira uwanjani” sentensi hii ikiwa katika hali ya kuendelea itakuwa ipi kati ya hizi

zifuatazo? A. Samatta atacheza mpira uwanjani. B. Samatta amecheza mpira uwanjani. C. Samatta anacheza mpira uwanjani. D. Samatta alicheza mpira uwanjani. E. Samatta hucheza mpira uwanjani. [ ]

103. Hakuna masika yasiyokuwa na mbu. Kitenzi “hakuna” kipo katika hali ipi?

A. mazoea B. timilifu C. ukanushi D. kuendelea E. hasira [ ] 104. Mapengo anamcheka kiziwi. Neno “mapengo” limetumika kama aina gani ya neno?

A. mtu ambaye hana meno B. msanii C. nomino D. kuvumishi E. kelezi [ ]

Page 9: DARASA VII KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA …JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA DARASA VII – KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

105. Wanamuziki wanaimba na kucheza usiku kucha. Kielezi katika sentensi hii ni kipi? A. wanamuziki B. wanaimba na kucheza C. usiku kucha D. wimbi wa muziki E. na mchana [ ]

106. Aliruka kamba na kukimbia. Katika sentensi hii mtenda ni nafsi ipi?

A. ya tatu wingi B. ya pili wingi C. ya tatu umoja D. ya pili umoja E. ya kwanza umoja [ ] 107. Kipi ni kinyume cha neno “shaibu” kati ya haya yafuatayo?

A. aibu B. jasiri C. mtabiri D. mwalimu E. ajuza [ ] 108. Mwanafunzi………atakayefeli mtihani huu ataadhibiwa vikali. Ni neno lipi lanakamilisha sentensi hiyo?

A. yoyote B. wote C. yeyote D. wotewote E. yote [ ] 109. Kondoo aliyenunuliwa jana jioni atachinjwa kesho asubuhi. Hii ni aina gani ya sentensi?

A. tegemezi B. tata C. ambatano D. sahili E. changamano [ ] 110. Wingi wa neno “shule” ni upi? A. mashule B. mashuleni C. shuleni D. shule E. vishule [ ] 111. Umoja wa sentensi isemayo “kucha zetu zinapendeza” ni upi?....................

A. ukucha wangu unapendeza B. kucha yangu inapendeza C. kucha zangu zinapendeza D. kucha wangu anapendeza E. ukucha umependeza huo [ ]

SEHEMU C: METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI: Chagua herufi ya jibu sahihi. 112. Alisamehewa lakini alijipalia mkaa baada ya kujigamba hadharani kuwa hawamuwezi.

“Kujipalia mkaa” maana yake ni ipi?....... A. kupakia mkaa B. kujiepusha na matatizo C. kujitia matatizoni D. kujinufaisha E. kujisifu [ ]

113. Joyce ameota mizizi kwenye uongozi wa mtaa. Sentensi hii ina maana gain?

A. Joyce ameugulia kwenye uongozi B. Joyce amekuwa na kiburi C. Joyce ni kiongozi mzuri D. Joyce amekuwa kwenye uongozi kwa muda mrefu E. Uongozi umemshinda [ ]

114. Maana ya nahau “andika meza” ni ipi? A. chora mezani B. andika neno meza

C. andika neno D. andaa chakula mezani E. andika irabu juu ya meza [ ] 115. Nina mwanangu nikimkata hakatiki. Tegua kitendawili hiki..............…..

A. kamba B. chuma C. maji D. kuni E. beseni [ ] 116. Kamilisha methali ifuatayo: Jina jema……. A. ni faida ya wenye jina B. hupendwa na wengi

C. husikia toka mbali D. hung’aa gizani E. ni lenye tabia nzuri [ ] 117. Chausiku alinihadaa aliponiambia angenipa kitabu. Neno lililopigiwa mstari lina maana gani?

A. alinidanganya B. alinisingizia C. alinirudishia D. aliniahidi E. alinisengenya [ ]

Page 10: DARASA VII KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA …JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA DARASA VII – KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

118. Lila na fila havitngamani. Maana ya methali hii ni kuwa…… A. Huyo fila na ndugu yake Lila hawapendani B. Ukikaa mahali utawaona lila na fila wakipita C. ukimwona Fila ujue Lila yuko karibu D. Ucha Mungu na ujambazi haviwezi kukaa pamoja E. Fila anamkimbiza Lila [ ]

119. Maana ya nahau ana ndimi mbili ni ipi? A. kigeugeu B. ni mtu mnene C. mlafi D. mnafiki E. mlaji [ ]

120. Methali ipi unaweza kuitumia badala ya “mzahamzaha hutumbua usaha”………

A. polepole ndiyo mwendo B. kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi C. akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki D. usipoziba ufa utajenga ukuta E. haraka haraka haina Baraka [ ]

121. Nahau mwaga unga ina maana gani?............... A. kumwaga unga wa ugali B. kudondosha sima C. kufukuzwa kazi D. kupewa madaraka E. kuchukua unga wa ngano [ ]

122. Babu huanika sembe usiku, asubuhi huiondoa. Kitendawili hiki kina maana gani? (a) mawingu (b) mwezi (c) nyota (d) umande (e) giza [ ]

123. ……………huliwa na mchwa. Mwanzo wa methali hii ni upi? (a) mali ya bahili (b) ukitunza vibaya (c) kutwanga nisile (d) baniani mbaya (e) umekuwa jeta [ ]

124. Vijana wengi wamejibweteka wengine wakifanya juhudi. Maana ya kujibweteka ni......... (a) kukaa bila kazi (b) kuogopa (c) kutokuwa na shida (d) kutokushirikiana (e) kukosa maarifa [ ]

125. Kifungu kipi cha maneno kinakamilisha methali isemayo “Aliyekunyoa shungi” kakuepushia…………. (a) kuchana (b) kusuka (c) kuosha (d) kuumia (e) gharama [ ]

126. Ngozi ivute ingali maji na udongo upate ungali maji. Methali hizi…………… (a) zinakinzana (b) zinafahana (c) zina maana sawa (d) zinalingana (e) zina sawa [ ]

127. Meli ilitia nanga bandarini. Maneno yaliyopigiwa mstari yana maana ya………..

(a) zama (b) ogelea (c) ibuka (d) ondoka (e) simama [ ] 128. Gari langu halitumii mafuta. Jibu lake ni lipi? (a) punda (b) toroli

(c) maksai (d) miguu (e) ngamia [ ] 129. ‘‘Samaki mkunje angali mbichi.’’ Methali ipi inafanana na hii……

(a) mtoto mkaidi hafaidi mpaka siku ya idi (b) kuliza si ujinga (c) usipoziba ufa utajenga ukuta (d) mali bila daftari hupotea bila kujua (e) bandu bandu humaliza gogo [ ]

130. Kibarua chake kimeota nyasi. Hii ina maana kuwa…………. (a) kazi anayoifanya sasa haifai (b) wamemuhamishia sehemu nyingine ya kazi (c) wamemtoa kazi za ofisini sasa anafyeka nyasi

Page 11: DARASA VII KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA …JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA DARASA VII – KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

(d) ameachishwa kazi (e) amepandishwa cheo [ ] 131. Mfalme hushuka kwa kelele. Tegua kitendawili hiki

(a) mvua (b) upepo (c) mwangwi (d) jaji (e) meli [ ] 132. “Mwenda pole hajikwai.” Methali ipi kati ya zifuatazo haifanani na hiyo?

A. Kawia ufike B. Polepole ndiyo mwendo C. Haraka haraka haina Baraka D. Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha E. Hamadi kibindoni silaha iliyo mkononi [ ]

133. “Kidagaa kimemwozea”. Msemo huu una maana gani?..............

A. kukwepa kulipa deni B. kutowajibika kulipa C. kuelemewa na jambo D. kupoteza tumaini E. kulipa deni maradufu [ ]

134. Malizia methali ifuatayo, “Usiku ni………………...

A. mrefu B. libasi bora C. giza nene D. kanda la sufi E. mfupi [ ]

135. Tegua kitendawili kifuatacho, “Nikitembea walio wafu huniamkia walio hai hukaa kimya.” A. Mjusi na mdudu B. Shoka msituni C. Punda na mzigo wake D. Kobe na gamba lake E. Majani makavu na mabichi [ ]

136. Nahau “Kula mwata”, ina maana gani?............. A. pata shida B. pata matumaini C. msaada D. upeo E. kuwa na akili nyingi [ ]

137. Methali ipi inakinzana na methali isemayo “Palipo na wengi hapaharibiki neno.” A. nyama ya usiku hainoni B. Hisani haiozi C. Wingi si hoja D. Ngoja ngoja yaumiza matumbo E. Moto hauzai moto [ ]

138. Nahau isemayo, “Amevimba kichwa” ina maana gani?................ A. kupata mafanikio makubwa B. kukabidhiwa madaraka ya juu C. kuwa na hali ya hasira D. kuwa na hali ya huzuni E. kuwa na tabia ya majivuno [ ]

139. Methali hii, “Kila mtoto na koja lake” ina maana gani?............... A. kila binadamu anamapungufu yake B. kila mtoto ana matatizo yake

C. kila mtoto ana mapungufu yake D. kila mtoto ana wazazi wake E. kila binadamu ana tabia yake [ ]

140. Tegua kitendawili kifuatacho, “Napanda mti na kichaa wangu” A. ngoma B. macho C. kivuli D. mwangwi E. moto [ ]

141. Nahau isemayo “Ana Inda” ina maana gani?.........

A. mkarimu B. mtu mwenye huruma C. mchoyo D. anashirikiana na watu E. mtaratibu [ ]

142. “Mambo mema na mabaya hayafungamani”. Kifungu hichi cha maneno kinatoa maana

ya methali ipi kati ya zifuatazo?............. A. Gogo la mbuyu si la mvule B. Liwapo lako ni jema la mwenzio ni baya

Page 12: DARASA VII KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA …JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA DARASA VII – KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

C. Lila na fila havitengamani D. Lako ni lako, likikufika lina wenzako E. Padogo pako si pakubwa pa mwenzako [ ]

143. “Tatizo la utoro limeota mizizi katika shule yetu”. Usemi “kuota mizizi” una maana gani?

A. kuibuka B. kuchipuka C. kushamiri D. kuongezeka E. kuenea [ ] 144. Tegua kitendawili kisemacho, “Anatengeneza mchuzi mtamu lakini hapiki”

A. muwa B. supu C. mama D. nyuki E. mpishi [ ]

145. Hayakamatiki hayafumbatiki…….. A. mayai B. maji C. majani D. mawe E. miib a [ ] 146. Baada ya kutafakari sana, nikakata shauri kuendelea na masomo. Kukata shauri ni……….

A. kujiuzulu B. kuamua C. kushauriana D. kukataa E. tafakari [ ]

147. Alimpaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Maana yake ni………………. A. sifa za uongo B. sifa za kweli C. sifa zote D. kuchua mgongo E. kumsuta mtu [ ]

148. Penye miti hakuna wajenzi. Methali ipi ina maana sawa na hiyo?.......

A. Ukiona vyaelea vimeundwa B. Elimu ni bahari C. Upele humwota asiye na kucha D. Mchagua jembe si mkulima E. Akufaae kwa dhiki ndiye rafiki [ ]

149. Ni methali ipi utamweleza mtu ambaye akipata kitu kidogo hujisifu na kuishiwa baada ya muda mfupi?..... A. Subira yavuta heri B. Bandubandu humaliza gogo C. Ivumayo haidumu D. Baada ya dhiki faraja E. Dalili ya mvua ni mawingu [ ]

150. Kiangazi chote hulala usingizi yakija masika hukesha…………………. A. nyoka B. kaa C. samaki D. boga E. chura [ ]

151. Kiti cha dhahabu hakikaliwi na mtu. Kitendawili hiki kina maaga gani?......... A. moto B. barafu C. nyuki D. jua E. maji [ ]

152. Kuwa na kichwa kikubwa ni nahau yenye maana ipi?............. A. Kuwa mzee B .Kuwa na kiburi C .Kuwa na nywele nyingi D .Kuwa na uso mpana E. Kutojiandaa. [ ]

153. Tegua kitendawili kisemacho kondoo wangu mnene kachafua njia nzima……….. A. Ng’ombe B .Firigisi C .Konokono D .jongoo E. Kinyonga. [ ]

154. Kamilisha methali hii, mpiga ngumi ukutani. …….. A. hukimbia sana B. huumiza mkonowe C. huvimba mkono D. hutokeza upande E. huishia kulia. [ ]

155. Uchungu wa mwana aujuaye mzazi, methali hii ina maana sawa na ipi kati ya zifuatazo?..........

A. Bendera hufuata upepo B. Nazi mbovu harabu ya nzima C. Kitanda usicholalia hujui kunguni wake D .Mgaagaa na upwa hali wali mkavu

Page 13: DARASA VII KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA …JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA DARASA VII – KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

E. mtoto umleavyo ndivyo akuavyo [ ]

156. Daktari aliitwa mara ilipoonekana dada anachungulia kaburi. Nahau iliyopigiwa mstari inamaanisha …….

A .kuteseka B. Kuumwa C .kuingia ndani ya kaburi D. Kuugua sana hadi kukaribia kufa E. Kulia [ ]

157. “Macho” ni jibu la kitendawili kipi? …… A .hausimiki hausimami B. popote niendapo ananiona C .Huangaza ulimwengu mzima D. popoo mbili zavuka mto. E .ni mweusi siku zote. [ ]

158. Anayeonja asali huchonga mzinga. Maana ya methali hii ni ……

A .mtu atakaye kula asali, itambidi pia ale mzinga B .Mtu anaye kula asali ndiye achongaye mzinga C. mtu anayetaka raha lazima kwanza apate taabu D. ukichonga mzinga utapata asali nyingi E. aghalabu mtu akipendezwa na kitu hujitahidi akipate chake mwenyewe. [ ]

159. Maana ya nahau kutundika miguu begani ni ……

A. kujistarehesha B. kuweka miguu juu sana C. kuumiza wengine D. kutembea kwa kasi E. kujiweka kando [ ]

160. Mzazi hana miguu, mzaliwa ana miguu. Jibu la kitendawili ni …..…… A. mototo na mama B. jivu na moto C. mpunga na bonde D .yai na kifaranga E. kuku na yai. [ ]

161. ……………ukamshika mkono. Mwanzo sahihi wa methali hii ni upi? A. Usile chakula B .Usile na mototo C. Usile na kipofu D. Usiache mbachao E. Usile chakula [ ]

SEHEMU “D”: UTUNGAJI “A” Umepewa habari yenye sentensi nne (4) zilizoandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo. Zipange

sentensi hizo ili ziwe na matiririko wenye mantiki kwa kutumia herufi A, B, C, D.

162. Hivyo mazoezi huleta afya, kwa hiyo ni muhimu kwa kila mmoja wetu kufanya mazoezi. [ ] 163. Mtu asiyefanya mazoezi anapata maradhi ya moyo, atanenepa kupita kiasi, kwa hiyo

atapata ugonjwa wa kuuwma mgongo na magoti. [ ]

164. Mazoezi ya viungo yanachangamsha misuli ya mwili, mifupa na ubongo. [ ]

165. Lakini mtu anayefanya mazoezi anaepuka magonjwa ya moyo na msukumo wa damu. [ ]

“E” Umepewa habari yenye sentensi 4 zilizoandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo. Zipange sentensi hizo ili ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kutumia herufi A, B, C, D. 166. Vilevile matunda huongeza damu mwilini. [ ]

167. Hivyo matunda yana umuhimu mkubwa katika miili yetu.

Page 14: DARASA VII KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA …JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA DARASA VII – KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

168. Lakini watu wasiokula matunda hupata maradhi kama vile ugonjwa wa fizi, macho na ngozi. [ ]

169. Kula matunda kunasaidia kuponyesha magonjwa na vidonda haraka, pia husaidia macho kuona vizuri katika mwanga hafifu. [ ]

“F” Umepewa habari yenye sentensi nne (4) zilizoandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo katika swali la 47-50. Zipange sentensi hizo ili ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A, B, C na D. 170. Hewa ndiyo yenye umuhimu wa kwanza ikifuatiwa na chakula. [ ]

171. Maji ni moja kati ya vitu vitatu muhimu sana vinavyotuwezesha kuishi [ ]

172. Kusingelikuwa na maji maisha ya binadamu na ya viumbe wengine yasingeliwezekana. [ ] 173. Vitu vingine ni hewa na chakula [ ]

SEHEMU “G”: UFAHAMU. “A” Soma habari ifuatayo kwa umakini kisha jibu maswali yafuatayo.

Mdharau biu hubiuka yeye. Watu wengi walitubeza sana. Walidhani sisi Waafrika hatuwezi kuandaa

mashindano ya soka ya kombe la dundia. Sina shaka walitahayari na kubaki vinywa wazi baada ya kujionea

kweli hayawi hayawi huwa.

Afrika kusini ilishinda kura na kuchaguliwa kuwa taifa litakalo andaa mashindano hayo kwa mwaka

2010. Viwanja vya kisasa vilijengwa na matayarisho kabambe yakafanyika.

Muda ulipo wadia, wachezaji walijimwaga viwanajani kupigania ushindi katika mchezo huo maarufu wa

kandanda. Afrika nayo haikujiweka nyuma. Iliwakilishwa na Ghana, Afrika kusini, Algeria, Cameroon na Ivory

coast.

Wakati wa mchezo mamia ya maelfu ya mashabiki walio kwea pipa na kutua Afrika kusini kusherekea kombe la dunia, walitia fora. Walikuwa wakishangilia na kuwatia moyo wachezaji. Mioyoni mwao walikuwa na matumaini na ushindi wa timu walizozishabikia. Nasi Waafrika tukiongozwa na ari na hamasa za uzalendo, tulishangilia timu zetu kwa shangwe na nderemo. Kwani mcheza kwao hutuzwa. Wachezaji walihamasishwa kucheza kufa na kupona ili timu zao zishinde.

Hatimaye Uhispania iliibuka mshindi wa kwanza, washindi walitunzwa kombe, medali na pesa.

Walioshindwa walitiwa moyo na kutakiwa kujitahidi kufika katika michuano ijayo, aidha waliombwa wasikate tamaa kwa vile asiyekubali kushindwa si mshindani. MASWALI. 174. Watu wangapi walikwea pipa na kutua Afrika kusini kuangalia kombe la dunia?..........

A. Milioni mbili B .Mamia ya maelfu C. Wachache D. Waafrika E. Elfu hamsini [ ] 175. Kisawe cha neno mshindi kama lilivyotamkwa kwenye habari ni …….

Page 15: DARASA VII KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA …JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA DARASA VII – KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

A .shujaa B. dhaifu C. mshindwa D. bingwa E. jasiri [ ]

176. Wachezaji walisubiri mashindano kwa hamu na ghamu. Kifungu cha maneno kilichopigiwa mstari kinamaanisha……………… A. muda mrefu B. shauku kubwa C. muda mfupi D. kukosa matumaini E. wasiwasi mwingi [ ]

177. Umoja wa neno mashabiki ni ……..

A. mtazamaji B. mashabiki C. mhusika D. shabiki E. mshangiliaji. [ ]

178. Habari hii ina jumla ya aya ngapi?……….. A. Tano B .Tatu C .Sita D. Nne E. Hakuna haya [ ]

179. Mdharau biu hubiuka yeye, methali hii kama ilivyotumika katika habari ina maana ipi?……… A. Tuwadharau Waafrika B .Tusiwe na tabia ya kudharau watu C .Tusichome biu D .Tujitahidi kufanya mazoezi E. Ni muhimu kushindana kila wakati. [ ]

180. Afrika iliwakilishwa na nchi mbalimbali katika mashindano ya kombe la dunia isipokuwa……. A .Ghana B .Tanzania C .Afrika kusini D. Ivory coast E. Algeria. [ ]

181. Nchi ipi iliibuka mshindi wa kwanza katika mashindano hayo?................ A. Tanzania B .Afrika C .Uhispania D .Cameroon E .Nigeria. [ ]

182. Methali ipi kati ya hizi haikutumika katika habari hii?

A. Hayawi hayawi huwa B .asiyekubali kushindwa C .Mdharau biu hubiuka yeye D .Mcheza kwao hutuzwa E. Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni. [ ]

183. Kucheza kufa na kupona maana yake ni…… A .Kufanya bidii kupita kiasi B. kuuana bila kujali C. kuumizana mchezoni D. kuzubaa E. kuuliza. [ ]

“H” Soma habari ifuatayo kwa makini kisha jibu swali la 41 – 45 kwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi.

Katika mapambano ya kudai Uhuru, viongozi wengi wa Afrika walifanikiwa kuzikomboa nchi zao. Mara

baada ya Uhuru wa nchi zao wapo mashujaa wa Afrika walioibuka ambao walitaka Uhuru na Umoja wa Bara

lote la Afrika. Miongoni mwa mashujaa waliotaka Uhuru na Umoja wa Bara la Afrika ni Kwame Nkrumah wa

Ghana na Mwalimu Julius K. Nyerere wa Tanzania. Hawa ndio waliokuwa vinara wa kutaka kuunganisha Afrika.

Wao waling’amua mapema kuwa umoja ni nguvu utengano ni udhaifu pia walitambua kuwa fimbo ya

mnyonge ni umoja.

Kwame Nkrumah alitaka nchi za Afrika ziungane chini ya Raisi mmoja kwa bara lote. Lengo lake lilikuwa ni kuunda taifa kubwa lenye nguvu kiuchumi hatimaye kisiasa ili kuweza kukabiliana na nguvu za mataifa ya ulaya, yaani alitaka Afrika iwe na sauti moja na msimamo mmoja. Kwa hiyo alihamasisha na kuhimiza muungano wa Umoja wa bara la Afrika. Shujaa wa pili ni Mwalimu Julius K. Nyerere wa Tanzania. Nyerere

Page 16: DARASA VII KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA …JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA DARASA VII – KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

alipigania haki za wanyonge popote duniani. Aliwasha mwenge wa Uhuru na kusema maneno haya “Tunawasha mwenge wa Uhuru na kuweka juu ya Mlima Kilimanjaro. Umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hapana matumaini, Upendo mahali ambapo pana chuki na heshima ambapo pamejaa dharau”.

Kutokana na msimamo, ujasiri na uwezo wake Nyerere alijijengea heshima kubwa barani Afrika na sehemu mbalimbali duniani. Mataifa mengi duniani yalimtambua kama ni mtu muhimu mwenye mawazo ya kujenga na mpenda usawa. Kama Nkrumah, Nyerere naye alitaka Afrika iungane na kuwa na umoja wa Afrika. Hata hivyo yeye alipendelea muungano huo uje polepole hatua kwa hatua. Kuhusu ukombozi wa Afrika, Nyerere alitaka bara lote likombolewe kwani aliamini kwamba uhuru wetu hauwezi kuwa kamili hadi bara lote la Afrika limekuwa huru. Matokeo yake Tanzania iliweza kuteuliwa kuwa makao makuu ya kamati ya ukombozi kusini mwa Afrika na Nyerere akachaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo na katibu wa kamati alikuwa Brigedia Mstaafu Hashim Mbita. Mwalimu Nyerere kupitia kamati hiyo alivisaidia sana vyama vya ukombozi katika nchi za Msumbiji, Angola, Namibia, Zimbabwe na Afrika kusini. MASWALI

184. Wataje viongozi mashujaa wawili waliokuwa mstari wa mbele kuunda umoja wa

Afrika…………………………………...........................................................……………………………………

185. Ni nani aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya ukombozi? …………………………………………..

186. Ni nani alitaka nchi za Afrika ziungane chini ya Rais mmoja kwa bara lote la Afrika?..............................

187. Katibu wa kamati ya ukombozi alikuwa ni nani? ………………………………………………………………

188. Nchi gani iliweza kuteuliwa kuwa makao makuu ya kamati ya ukombozi kusini mwa Afrika?......................

“C” Soma habari ifuatayo kwa usahihi kisha jibu swali la 41 – 45 kwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi.

Siku moja wakati wa somo la Kiswahili, Amadori alimuuliza swali mwalimu. Alianza kwa kusema, “Mwalimu nimeona kwenye karatasi swali linasema, Fupisha habari ifuatayo. Kufupisha habari ni nini?” Mwalimu akajibu “Fupisha maana yake ni punguza urefu.” Na kufupisha habari maana yake ni kupunguza urefu wa habari. Tunafupisha habari kwa sababu taarifa zinatakiwa kuwa fupi bila kuharibu au kupotosha ujumbe au taarifa kutoka kwa mtoaji. Kisha mwalimu aliendelea kufafanua kwamba katika ufupishaji wa habari tunapata taarifa na kuandika mambo ya msingi na ya muhimu tu. Hivyo habari inakuwa fupi lakini inatoa taarifa kamili kuhusu jambo linalohusika. Ufupisho mzuri wa habari huwa theluthi moja ya habari nzima. Maana yake ni kwamba kama aya ina mistari 12 ufupisho utakuwa na takribani mistari minne. Pia kama habari ina maneno sitini, ufupisho utakuwa na maneno kiasi cha ishirini hivi.

MASWALI

Page 17: DARASA VII KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA …JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA DARASA VII – KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA

EPUKA COVID-19 OSHA MIKONO MARA KWA MARA APRILI 2020 HAIUZWI HAIUZWI HAIUZWI

“Elimu ni uzima wangu” (Mithali 4:13)

189. Kutokana na habari uliyoisoma, nani aliyeuliza swali kuhusu kufupisha habari?........................................ ............................................................................................................................. .......................................

190. Kulingana na habari ya mwandishi anasema kufupisha habari maana yake ni nini?……………………………….

191. Amadori alimuuliza swali mwalimu wa somo gani?............................................................................... .....

192. Ufupisho wa habari huwa………………………………………………..ya habari nzima.

193. Badala ya kutumia maneno “ufupisho wa habari” unaweza pia kutumia maneno yapi yakaleta maana sawa? ……….................................................................................................................... ....................

SEHEMU I: USHAIRI.

1. Korona gonjwa hatari, watu wote jihadhari, Kijana uwe tayari, epuka ujihadhari, Wazee pia tayari, kuzikimbia athari, Korona gonjwa hatari, kwa vijana na wazee.

2. Matangazo kutolewa, kwajamii yote pia, Elimu imetolewa, mtaani bila udhia, Matibabu kutolewa, ndugu yangu zingatia, Korona gonjwa hatari, kwa vijana na wazee

194. Shairi hili lina mizani mingapi?..................................................................................

195. Mtunzi wa shairi anaitwa malenga. Hivyo Malenga wa shairi hili ametunga shairi la……................………

196. Shairi hili linahusu nini ................................................................................................... ...... 197. Pendekeza kichwa cha shairi hili ........................................................................................ 198. Je, ugonjwa uliotajwa unawakumba kina nani? ......................................................................

199. Taja njia za kujikinga na ugonjwa uliotajwa kwenye shairi hapo juu

(i) .................................................................. ..........................

(ii) .............................................................................................

(iii) .............................................................................................

200. Mtunzi wa shairi anaposema tujihadhari ana maana ................................................... ............................

Page 18: DARASA VII KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA …JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA DARASA VII – KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA

KUWA MAKINI NA COVID-19 NAWA MIKONO YAKO KILA MARA APRILI 2020