Upload
wanachuoni
View
266
Download
6
Embed Size (px)
DESCRIPTION
Fataawa Za Wanachuoni (30)
Citation preview
1
فتاوى العلماءFataawa Za Wanachuoni
[30]
Imefasiriwa Na Kutayarishwa Na:
Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush
©
2
Dibaji:
Hizi ni Fataawa za wanachuoni mbali mbali ambazo nimezikusanya ili
kuweza kuwasahilishia ndugu zetu Waislamu na khaswa wale watafutaji
elimu. Fataawa ni mchanganyiko kuhusiana na masuala mbali mbali ya
Tawhiyd, ´Aqiydah, Manhaj, Fiqh na mengineyo.
Hivyo, ninamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) ziweze kuleta faida kwa ndugu
zetu Waislamu, na ninamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) Ajaalie kazi hii niwe
nimeifanya kwa kutafuta Radhi Zake (Subhaanahu wa Ta´ala), na Amlipe kila
Aliyeisambaza kwa ndugu mwengine na Awalipe ndugu wasomaji wote kwa
jumla.
Tanbihi: Fataawa zote hizi tumezifasiri kwa njia ya Video na zinapatikana
Youtube waweza kusoma na huku wasikiliza. Kwa mwenye kutaka hizo
Fataawa za Video aende Alhidaaya au Youtube kwa juu sehemu ya kutafuta
aandike au kukopi kichwa cha habari cha Fatwa (kama ilivyo hapo chini kwa
kila Fatwa ina kichwa chake cha habari) na atafute itajitokeza In Shaa Allaah.
Jazaakumu Allaahu Khayra
Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad , na ahli zake na
Maswahabah zake na watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.
3
Fataawa zilizomo:
1) Mwanamke Anataka Kufunza Kidogo Alichokipata Kwa Wanazuoni
2) Wanyama Wangapi Mtu Atachinja Akipata Watoto Mapacha?
3) Masharti Ya Mwanamke Kutoka Na Kwenda Sokoni
4) Lipi Lakufanya Fataawa Mbili Zikigongana?
5) Lipi Lakufanya Fataawa Mbili Zikigongana?
6) Kusoma Kiarabu Katika Madrasah Ya Mchanganyiko
7) Kununua Au Kuuza Simu Za Camera
8) Kumsomea Mtu Ruqyah Kwa Kitabu Cha Aayah Na Hadiyth
9) Kufanya Kazi Kwenye Mgawaha Wanapohudumia Nguruwe Na Pombe
10) Kuashiria Mkono Anapotoa Mtu Salaam Na Uko Unaswali
11) Khawaarij Wanaokufurisha Watawala
12) Je Kusoma Kwa Kupangilia Suurah Ni Wajibu?
13) Hukumu Ya Mahram Kafiri Kwa Mke Wangu
14) Hukumu Ya Swawm Ya Pamoja (Kundi)
15) Hukumu Kwa Anaemtetea Abu Ishaaq al-Huwayniy
16) Shaykh Dr. as-Suhaymiy Kuhusu ´Aliy al-Halabiy Kuipiga Radd al-Lajnah ad-
Daa´imah
17) ´Allaamah Shaykh Rabiy´ Kuhusu Usaamah al-Quusiy Na Abul-Hasan
18) Kunyoa Ndevu Ni Kujifananisha Na Wanawake Na Ni Laana
19) Vitabu Vinasomwa Kwa Wanachuoni
20) Vipi Mzazi Afanye Uadilifu Kati Ya Mtoto Wa Kiume Na Wa Kike?
21) Wanaume Waliolaaniwa Wanaojifananisha Na Wanawake Na Makafiri
22) Upi Wajibu Wetu Kwa Aliyekataa Kutoa Zakaah?
23) Umekumbusha Yatosha!
24) Swali Lako Halina Faida Kwa Sasa!
25) Swalah Ya Usiku Ina Idadi Rakaa Maalumu?
26) Hukumu Ya Kula Nyama Ya Mtu Asiyeswali
27) Aliyeacha Swalah Ni Lazima Atoe Shahaadah Atapoanza?
28) Unyenyekevu Wa Shaykh ´Abdul-Muhsin al-´Abbaad
29) Ni Wajibu Kutahadharisha Dhidi Ya Watu Wa Bid´ah
30) Mkutano Wa Shaykh al-Albaaniy Na Shaykh Ibn ´Uthamiyn
31) Hukumu Ya Kumpa Zakaah Mume Wako
32) Je Mwanamke Anaweza Kumuomba Mwanaume Kumuoa?
33) Iko Wapi Demokrasia Ya Hawa Makafiri?
34) Hili Ni Swali La Ajabu Sijawahi Kusikia Maishani
35) Dalili Ya Qur-aan Inayofuta Vitabu Vilivyotangulia
36) Je, al-Ikhwaan al-Muslimuun Ni Katika Ahl-us-Sunnah?
37) Hukumu Ya Mwanamke Kuzuru Makaburi -1-
38) Baina Yetu Sisi Na Nyinyi Ni Vitabu Vya Salaf
39) Sifa Na Tabia Za Mja Zimeumba Na Allaah
4
40) Ni Lazima Kwa Muadhini Awe Twahara
41) Mume Ana Wake Wawili Kumuacha Mmoja
42) Madhehebu Manne Ni Katika Makundi 72 Ya Motoni?
43) Kupigana Jihaad Pamoja Na Ahl-ul-Bid´ah
44) Kuweka Mlio Wa Simu Wa Adhaana, Qur-aan Au Dhikr
45) Kupiga Radd Watu Wa Bid´ah Ambao Wanalingania Watu Katika Bid´ah Zao
46) Kumsimamishia Mtu Hoja Kabla Ya Kumhukumu Kuwa Ni Mtu Wa Bid´ah
Wanachuoni waliomo:
1) Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
2) Imaam Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
3) Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
4) ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
5) ´Allaamah Ahmad bin Yayhaa an-Najmiy
6) ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
7) ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
8) ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
9) ´Allaamah ´Abdul-Muhsin al-´Abbaad
10) Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
11) Shaykh Swaalih bin Sa´iyd as-Suhaymiy
12) Shaykh Abu ´Abdul-Haaliym ´Abdul-Haadiy
5
Bismillaahi Rahmaani Rahiym
1) Mwanamke Anataka Kufunza Kidogo Alichokipata Kwa Wanazuoni
Swali:
Naishi Uingereza na nimekwishasoma baadhi ya vitabu vya wanachuoni, je
naweza kuwafunza watu kiasi hichi kidogo ambacho nimepata katika kusoma
vitabu hivyo?
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Ni wajibu kwanza kunibainishia uliyoyaandika na ukayapata kwa baadhi ya
hao wanachuoni ambao yawezekana kweli ulipata kwao, likidhihirika kwako
hilo - ni wajibu kwako kufunza hichi ambacho ulipata kwao - namna hii,
kidogo kidogo.
Chanzo: http://youtu.be/hwoIo0Pra8M
2) Wanyama Wangapi Mtu Atachinja Akipata Watoto Mapacha?
Swali:
Ni wangapi itachinjwa kwa mapacha wawili?
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Ikiwa ni mapacha wakiume, ni minyama minne. Na ikiwa ni wakike minyama
itakuwa ni miwili. Na ikiwa ni wakiume na wakike minyama itakuwa mitatu;
mwanamume miwili na wakike mmoja. Lakini huenda baadhi ya watu
wakafikiria kuwa kufanya 'Aqiyqah ni wajibu na sivyo, ´Aqiyqah ni Sunnah
mustahaba na sio wajibu.
6
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=109
3) Masharti Ya Mwanamke Kutoka Na Kwenda Sokoni
Swali:
Yapi masharti ya mwanamke kutoka [kwenda] sokoni?
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Atoke na Mahram ambaye ni mkubwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam) kasema kuwa Shaytwaan huyaweka macho yake kwa mwanamke
anapotoka. Inatakiwa kwa Muislamu (mume) kutomsikiliza mke wake kutoka
kwenda sokoni isipokuwa awe pamoja naye Mahram. Na awe amejisitiri na
ajiepushe na mahala ambapo kumejaa watu wengi.
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=6
4) Lipi Lakufanya Fataawa Mbili Zikigongana?
Swali:
Je inajuzu kwa wanawake kuswali mbele ya safu ambayo Imamu anaswali
ikiwa Msikiti umejaa na hawawezi kuswali sehemu ya wanawake, wanaswali
nje ya Msikiti na wakifanya hivyo itakuwa safu yao mbele ya Imaau?
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Hili ni kosa wala haifai. Ima wawe nyuma ya wanawake au waswali
majumbani kwao. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kakataza na
kwamba bora ya Swalah ya mwanamke ni katika nyumba yake.
7
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=108
5) Lipi Lakufanya Fataawa Mbili Zikigongana?
Swali:
Upi msimamo wa mtafutaji elimu (wanafunzi) anayeanza kwa Fataawa
ambazo zinatofautiana?
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Aulize wanachuoni wa Sunnah na awaombe kutoka kwao dalili, ataekuwa na
dalili kwa kauli yake huyu ndiye ambaye inafaa kuchukua [kauli yake].
Chanzo: http://youtu.be/yEvubNcN3_0
6) Kusoma Kiarabu Katika Madrasah Ya Mchanganyiko
Swali:
Kuna dada anasoma lugha ya kiarabu katika Madrasah mchanganyiko na
ndio Madrasah yalioko karibu yake. Je, inajuzu kwake kusoma katika
Madrasah haya mpaka atapopata njia ingine ajifunze lugha?
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Uhakika ni kwamba Madrasah mchanganyiko ni fitina sawa kwa vijana na
wasiokuwa vijana. Kusoma kwake kwa haya Madrasah ni makosa na Mtume
kakataza hili.
8
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=110
7) Kununua Au Kuuza Simu Za Camera
Swali:
Ipi hukumu ya kuuza simu za Camera na Bluetooth? Na ipi hukumu ya
kununua pia ikiwa mtu huyo haitumii Camera hii kwa kupiga picha viumbe
vyenye roho?
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Haijuzu kuziuza wala kuzinunua. Hata yule mwenye anaziuza hana uhakika
kwa yule anayezitumia, huenda ni mmoja katika watu wake wa nyumbani
akapiga nazo picha.
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=186
8) Kumsomea Mtu Ruqyah Kwa Kitabu Cha Aayah Na Hadiyth
Swali:
Muulizaji kutoka Ufaransa, mke wangu ni mgonjwa sana kwa majini na
uchawi, inajuzu kwangu kumsomea Matn ya al-Uswuul ath-Thalaathah kwa
kuwa iko na Aaayah na Hadiyth?
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Ruqyah inakuwa kwa Aayah za Qur-aan na Sunnah ambazo ziko na dawa.
Msomee al-Faatihah, al-Kursiy, Aayah mbili za mwisho katika Suurat-ul-
9
Baqarah na Aayah za wachawi, na Qul-HuwaLlaahu Ahad, na
A´udhubiLlaahi KalimaatiLlaahi at-Tammah, min kulli Shaytwaani
wahammah, wamin kulli ´aynin lammah. Haya ndo yanayopasa.
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=180
9) Kufanya Kazi Kwenye Mgawaha Wanapohudumia Nguruwe Na
Pombe
Swali:
Nafanya kazi katika mgahawa ambapo mmiliki wake ni kafiri, kunapikwa
vyakula vya Haramu - kama vile pombe na nyama ya nguruwe. Ipi hukumu
ya kazi hii?
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Tunachokunasihi ewe Muislamu ambaye unashahidilia ya kwamba hapana
Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allaah na kwamba Muhammad ni
Mtume wa Allaah, pamoja na hayo unafanya kazi ya kuhudumia nyama ya
nguruwe na pombe n.k. Najikinga kwa Allaah kutokana na hilo. Je
humuogopi kweli Allaah katika nafsi yako? Na ukawa mwenye kutafuta riziki
kwa njia nzuri na kujiweka mbali na mfano [wa kazi] kama hizi. Haikustahiki
[kazi] kama hii ewe Muislamu.
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=855
10) Kuashiria Mkono Anapotoa Mtu Salaam Na Uko Unaswali
Swali:
10
Hukumu ya kurudisha Salaam kwa ishara kwa mwenye kuswali ni khaswa
katika Swalah ya mwenye kuswali peke yake au Swalah ya Jamaa´ah? Na je
hukumu inabadilika wakati [Swalah] ya Naafil [Sunnah] na faradhi?
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Yote hayo yanajuzu na wala hukumu zake hazibadiliki. Hukumu ya faradhi
na Naafil, zole mbili [zajuzu]. Akitoa Salaam mtu, atafanya namna hii [ishara]
na mkono wake.
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=3
11) Khawaarij Wanaokufurisha Watawala
Swali:
Ipi hukumu ya mwenye kuwakufurisha watawala wa kiarabu katika wakati
huu?
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Hii ndo hali ya Khawaarij ambao wanawakufurisha watu kwa madhambi.
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=190
12) Je Kusoma Kwa Kupangilia Suurah Ni Wajibu?
Swali:
11
Je ni sharti unaposoma Suurah iwe kwa mpangilio katika kukhatimu Qur-aan
au hapana?
Muulizaji:
Shaykh anamaanisha mpangilio.
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Kusoma kwa mpangilio ndio bora zaidi, na ikiwa hakufanya hivyo hakuna
ubaya. Mpangilio wa Suurah si lazima. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam) aliwahi kuswali Swalah ya usiku akasoma al-Baqarah,
kisha an-Nisaa kisha al-´Imraan.
Chanzo: http://youtu.be/lOgpcjTWgpU
13) Hukumu Ya Swawm Ya Pamoja (Kundi)
Swali:
Ipi hukumu ya Swawm ya kundi? Kama kukusanyika kundi la watu na
kukubaliana kufunga masiku maalumu kama Jumatatu na alkhamisi na hivyo
kwa jili ya kusaidizana katika wema na taqwa; kwa kuwa mtu ni dhaifu katika
nafsi yake anapata nguvu kwa ndugu zake. Ipi hukumu ya hilo?
Imaam Ibn ´Uthaymyniyn:
Naona kuwa si katika Sunnah na ni aina ya Bid´ah, ikiwa watakubaliana hilo.
Kwa kuwa ikiwa tunakataa Takbiyra za pamoja au Dhikr za pamoja kwa
mfano, hii pia ni Swawm na Swawm ni ´Ibaadah. Haifai kuwa pamoja (kundi).
Lakini ikiwa bila ya makubaliano hakuna neno. Kwa mfano imetokea
tumefunga siku ya Jumatatu hivyo wakasema baadhi yetu kuwaambia
12
wengine, waliofunga futari itakuwa kwa fulani na tunakubaliana kufuturu
kwake hili halina neno; kwa kuwa si jambo lililopangwa na mkusanyiko wetu
sio ´Ibaadah. Kukusanyika kwa ajili ´Ibaadah au kuwa pekee ni katika jambo
yaliyo katika Shari´ah. Na kwa hili lau kama Allaah Asingetuwekea Shari´ah
kuswali Jamaa´ah, tusingeliswali Jamaa´ah, ingekuwa kuswali Jamaa´ah ni
Bid´ah. Lakini Allaah Katuwekea hilo katika Shari´ah. Hali kadhalika Swawm
ya pamoja (kundi) na kukubaliana hilo kabla, ni aina katika Bid´ah. Baadhi
ya watu wanaweza kuuliza kuhusu Swawm ya Ramadhaan, je situnafunga
pamoja? Ni kweli, lakini hivyo ndivyo ilivofaradhishwa. Imefaradhishwa
kufunga watu wote katika mwezi huu. Mimi naona mtu aache njia hii na mtu
awe mwenye kumuomba Allaah (´Azza wa Jalla) na ajihesabu nafsi yake. Na
ikiwa mtu hawezi kufanya ´Ibaadah ila mpaka apate msaada katika fimbo -
yaani mpaka waifanye wengine - azima yake itakuwa dhaifu.
Chanzo: http://youtu.be/uG05kNiMttU
14) Hukumu Ya Mahram Kafiri Kwa Mke Wangu
Swali:
Je, inajuzu kwa mke wangu kujidhihirisha mbele ya baba yangu kafiri? Na ni
hukumu inayotumika kwa kila Mahram ambaye ni kafiri?
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Anasema:
"Au wanawake wenzao". (33:55)
Yaani haijuzu kuonesha mapambo yao isipokuwa kwa wanawake Waislamu,
ama wanawake ambao si wa kiislamu haijuzu kwao kuonesha mapambo yao.
Hali kadhalika kwa baba ambaye ni kafiri, haifai kudhihirisha mapambao
mbele yake. Lakini kama kuacha wazi uso wake, mikono yake; ilimradi tu
hajiachii moja kwa moja mbele yake hili halijuzu.
13
Chanzo: http://youtu.be/ypuLD4v0gfQ
15) Hukumu Kwa Anaemtetea Abu Ishaaq al-Huwayniy
Swali:
Ipi rai yako kwa yule anayemtakasa Abu Ishaaq al-Huwayniy na anamtetea?
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Abu Ishaaq al-Huwayniy ana changanya, na yule anayemtakasa huenda
hajafikiwa na mchanganyiko huu. Akhabarishwe.
Chanzo: http://youtu.be/2evKwYL7zs8
16) Shaykh Dr. as-Suhaymiy Kuhusu ´Aliy al-Halabiy Kuipiga Radd al-
Lajnah ad-Daa´imah
Shaykh Dr. Swaalih bin Sa´iyd as-Suhaymiy:
Wenye haki ni al-Lajnah ad-Daa´imah. Na ´Aliy [bin] Hassan katika qadhiya
hii alichanganya mambo. Alikosea kuipiga Radd al-Lajnah. Kwa kuwa
hakuyafahamu maneno ya al-Lajnah, kamwe. Alikosea kupiga Radd al-
Lajnah. Alikosea. Na kaidhulumu nafsi yake. Kafungua njia ya kuikashifu al-
Lajnah bila ya kujua. Kafanya kosa, kafanya kosa, kafanya kosa, kosa mara
elfu. Na yuko na msemo ambao wanaingia humo Murji-ah. Yuko na msemo
ambao kunakhofiwa kuutumia Murji-ah. Mfano kwa kusema kwake wakati
fulani kuwa kuna kufuru ya matendo na Itikadi na mtu hakufuru ila
akianguka tu katika kufuru ya Itikadi. Hili si sahihi. Hata Shaykh wake,
14
Shaykh [Muhammad] Naaswir-ud-Diyn [al-Albaaniy] kwa fadhila zake na
cheo chake, hatukubaliani nae katika qadhiya hii. Kuna kufuru ya matendo
ambayo inamtoa mtu katika Uilsamu. Kama kumtukana Allaah na Mtume
Wake, kusujudia sanamu, kukejeli Sunnah. Yote haya ni kufuru inayomtoa
mtu katika Uislamu.
Chanzo: http://youtu.be/mgnF8jnDuWw
17) Allaamah Shaykh Rabiy´ Kuhusu Usaamah al-Quusiy Na Abul-
Hasan
´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy:
Usaamah al-Quusiy kama mnavyojua, alikuwa Salafiy wa kweli In Shaa
Allaah. Kisha kulipokuja fitina za Abul-Hasan, akatumbukia humo. Kisha
akaendelea kuathirika na fitina hizi, mpaka akafikia katika daraja ambayo -
tunamuomba Allaah Awakinge Waislamu nayo na yeye pia. Na mimi
siwanasihi kudhudhuria mihadhara na duruus zake, mpaka atubie kwa
Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) katika aliyotumbukia humo. Hakika ni katika
aliyeathirika na fitina za Abul-Hasan, na alisaidia fitina zake na kufanya
mambo ya kuipatia nguvu. Na mfano wa hilo ni ziara yake katika shirika hii
na mialiko yao kwake. Haya ni mambo nimeona na kuzama kwake zaidi
katika fitina. Na jitihada katika njama zao (za kuwadanganya watu) kuwa
mbali na Rabiy´ na ndugu zake (katika Wanachuoni), bali hata katika Manhaj
yenyewe ya Salaf. Abul-Hasan kazua misingi mingi na yote ni batili, na Abuu
Haatim (Usaamah al-Quusiy) hajakosoa katika hayo lolote. Isitoshe kwa sasa
anatakasa, kutetea na kuwasifia watu wa Bid´ah - kwa masikitiko makubwa.
Kaenda mbali zaidi katika fitina, hii imekuja kuwa kama ilivyokuwa tabia
yake. Tunamuomba Allaah Tawfiyq na tunamuomba Atusamehe sote. Kwa
hali yoyote jiwekeni mbali naye na mihadhara yake mpaka atubie kwa Allaah
na arudi katika Manhaj Salaf.
Chanzo: http://youtu.be/xghBDNTEUJA
15
18) Kunyoa Ndevu Ni Kujifananisha Na Wanawake Na Ni Laana
´Allaamah al-Fawzaan:
Haijuzu kwa mwanaume kujifananisha na wanawake katika mavazi yao,
kutembea kwao, kuongea kwao, kujipendezesha kwao wanawake. Haijuzu
kwake hilo kwa kuwa yeye ni mwanamume. Yahitajika kwake nguvu na
ukakamavu, hakuhitajiki kwake ulaini na kujiachia achia hivi ilihali ni
mwanamume. Asifike kwa sifa za wanaume. Kadhalika katika kujifananisha
na wanawake ni kunyoa ndevu, hii ni aina kubwa katika aina za kujifananisha
na wanawake. Kunyoa ndevu akawa mwanaume kama mwanamke. Kitu
kinachomtofautisha mwanaume na mwanamke ni ndevu. Hivyo [mwanaume]
akinyoa ndevu zake huwezi kutofautisha kati ya uso wa mwanamke na uso
wa mwanamume. Inatoweka alama inayowapambanua. Huku ni
kujifananisha wanaume kwa wanawake. Kamuumba nazo mwanaume na
kumnyima nazo mwanamke. Hivyo kamlaani Mtume ( وسلم ليهع هللا صلي )
anayelifanya. Na laana ni dalili ya kuonesha kuwa ni dhambi kubwa katika
madhambi makubwa. Ni wajibu kwa wanaume kujitofautisha na wanawake,
na ni wajibu kwa wanawake kujitofautisha na wanaume. Huu ndo wajibu.
كر وليس كاأل نثى الذ
“Na mwanamume si sawa na mwanamke.” (al-´Imraan 03:36)
Ama akiwa mwanamume kama mwanamke au mwanamke kama
mwanamume, hali itabadilika, laa hawla walaa Quwwata illa biLlaah. Na yeye
kajifananisha na sifa ya wanawake. Lakini ukimwambia wewe [unafanana] ni
kama mwanamke atakukasirikia au anaweza hata kukuua, ukimwambia
[mnyoa ndevu] wewe ni kama mwanamke, atakuua au atakupiga. Ilihali yeye
mwenyewe ndo anafanya jambo hili, anakuwa kama mwanamke.
Chanzo: http://youtu.be/hmwTFUaAgvM
19) Vitabu Vinasomwa Kwa Wanachuoni
16
Swali:
Mwanafunzi anaeanza [kusoma] unamnasihi nini kwa vitabu katika elimu ya
tafsiri?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni kama tulivyosema tatizo si vitabu, vitabu vipo vingi wa Alhamdulillaah.
Lakini tatizo ni kupatikana mwanachuoni ambae utasoma kwake kitabu hiki.
Ukipata mwanachuoni ambae utasoma kwake, kitabu kitakuwa sahali. Ni juu
yake kushikamana na vitabu vyenye tafsiri ya zamani; tafsiri ya Ibnu-Jariyr,
tafsiri ya Ibnu-Kathiyr, tafsiri ya al-Baghawiy. Tafsiri za zamani ambazo
zimeegemea nususi [dalili] za kuaminika. Tafsiri ya Qur-aan kwa Qur-aan,
tafsiri ya Qur-aan kwa Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam),
tafsiri ya Qur-aan kwa tafsiri ya Maswahabah, tasfiri ya Qur-aan kwa kauli za
Taabi´iyn, tafsiri ya Qur-aan kwa lugha yake ilivyoteremka. Na haya
yanapatikana katika [vitabu vya] tafsiri ambazo nimewatajia.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13840
20) Vipi Mzazi Afanye Uadilifu Kati Ya Mtoto Wa Kiume Na Wa Kike?
Swali:
Vipi kwa mzazi afanye uadilifu katika matumizi baina ya watoto, je kijana
apewe zaidi kuliko msichana?
´Allaamah al-Fawzaan:
Matumizi baina ya watoto kwa uadilifu ni kumpa kila mmoja kile
anachokihitaji. Mtoto wa kike utampa kile anachokihitaji na wa kiume
anachokihitaji katika matumizi. Si kwamba kuwapa sawa, hapana! Kila mmoja
ana haja [mahitajio] yake. Matumizi ya mkubwa si kama matumizi ya mtoto
mdogo. Mtoto matumizi yake huwa madogo, lakini mkubwa huwa zaidi.
17
Atapewa kila mmoja kile anachokihitaji katika fungu, nyumba na
anayoyahitaji katika mambo yake na kazi zake.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13840
21) Wanaume Waliolaaniwa Wanaojifananisha Na Wanawake Na
Makafiri
Swali:
Yaliyopokelewa kwa Mtume ( وسلم عليه هللا صلي ) kulaani wanaume
wanaojifananisha na wanawake, je anaingia katika laana yule anayenyoa
ndevu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni kila sampuli ya kujifananisha. Huku [kunyoa ndevu] ni kujifananisha kwa
sampuli mbili:
- Mtume ( وسلم عليه هللا صلي ) kasema "Wakhalifuni wamajusi, zirefusheni ndevu
na punguzeni masharubu.
- Na ni kujifananisha na wanawake pia. Kwa hiyo kuna kujifananisha namna
mbili. Ni kujifananisha na wanawake na kujifananisha na makafiri.
Chanzo: http://youtu.be/iUyYPwZ8pQI
22) Upi Wajibu Wetu Kwa Aliyekataa Kutoa Zakaah?
Swali:
Ipi dhambi kwa yule anayechukulia sahali suala la kutoa Zakaah?
18
´Allaamah al-Fawzaan:
Ichukuliwe kutoka kwake. Akikataa kuitoa kwa khiyari ichukuliwe kutoka
kwake kwa nguvu, hata ikifikia hii katika kupigana. Ikiwa atahitaji kupigana.
Kama walivyopigana Maswahabah na waliokataa kutoa Zakaah. Ama
akikataa na kusema hakuna uwajibu wa kutoa Zakaah mtu ana khiyari, huyu
karitadi na kutoka katika Dini ya Kiislamu. Kwa kuwa kamkadhibisha Allaah,
na Mtume Wake na Ijmaa´ ya Waislamu. Aliyekataa uwajibu wa kutoa Zakaah
karitadi, na anayekubali uwajibu wake lakini kakataa [kutoa] kwa ubakhili
huyu atalazimishwa kutoa hata kama itakuwa kwa nguvu.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13840
23) Umekumbusha Yatosha!
Swali:
Mimi daima huwanasihi watu kutosengenya na huwatakaza, ninapomnasihi
mtu mara moja mpaka mbili. Je, inajuzu kwangu kukariri nasaha kutokana na
kwamba kuna mtu aliyenambia: Umeshawanasihi mara mbili yatosha.
ما ولنا على فإن بين البلغ رس الم
“Basi hakika juu ya Mtume wetu ni kufikisha (Ujumbe wake) kwa uwazi tu.”
(64:12) Ipi rai yako kwa hili?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio lakini usikae nao. Ukiwanasihi na wasikubali usikae nao. Kwa kuwa
ukikaa nao huku ni kuwasapoti.
Chanzo: http://youtu.be/ENGZ8fbqv6M
19
24) Swali Lako Halina Faida Kwa Sasa!
Swali:
Nilimtaliki mke wangu kwa sababu alitoka nyumbani kwa kuvaa vibaya, je
nimekosea katika hili?
´Allaamah al-Fawzaan:
Wewe umeshamtaliki, maadamu umeshamtaliki mambo yamekwisha. Ilikuwa
uulize tangu mwanzo. Kwa sasa swali hili halina faida.
Chanzo: http://youtu.be/iJspPajK9pU
25) Swalah Ya Usiku Ina Idadi Rakaa Maalumu?
Swali:
Swalah ya usiku ina idadi Rakaa ngapi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haina idadi, unaswali [Rakaa] utazoweza kisha utahitimu kwa kuswali Witr.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13840
26) Hukumu Ya Kula Nyama Ya Mtu Asiyeswali
20
Swali:
Mimi baba yangu haswali na anatuchinjia siku ya ´Iyd, ipi hukumu ya uchinjo
huu akichinja yeye au akimpa mwengine achinje?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Akichija yeye itakuwa Haramu kutokana na kauli sahihi ya wanachuoni. Kwa
kuwa mwenye kuacha Swalah huchukuliwa ni kafiri, kutokana na Hadiyth:
"Ahadi iliyopo baina yetu sisi na wao [makafiri] ni Swalah, atakayeiacha
amekufuru.
"Hakuna baina ya mja na kufuru na Shirki ila ni mtu kuacha Swalah."
Kaipokea Hadiyth hii Muslim. Kutoka Hadiyth ya nani? Jaabir. Na wakichinja
wengine katika wanaoswali, hakuna ubaya In Shaa Allaah.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=pXOBiW2zkC4
27) Aliyeacha Swalah Ni Lazima Atoe Shahaadah Atapoanza?
Swali:
Akitubia mtu na kurejea kwa Mola Wake kwa kuwa alikuwa haswali, je ni
lazima atamke Shahaadah mbili na kufanya ghusl [kukoga]?
Imaam Ibn ´Uthaymiyn:
Akitubia mtu ambaye alikuwa haswali kwa Allaah (´Azza wa Jalla) na
akaanza kuswali, atakuwa Muislamu kwa Swalah yake. Kwa kuwa mwenye
kukufuru kwa kuacha kitu fulani, anakuwa Muislamu kwa kufanya kitu
hicho. Na katika kila Swalah hio, atakuwa akisema "ash-Hadu an laa ilaaha
illa Allaah wa ash-Hadu anna Muhammad ´abduhu wa Rasuuluh". Ama
kufanya Ghusl, msingi wake umejengeka katika uwajibu wa Ghusl wakati
21
anasilimu kafiri. Na wanaosema kwamba kafiri anaesilimu si wajibu kufanya
Ghusl, hivyo itakuwa si wajibu kwa mtu huyu kufanya Glusl. Na bila shaka ni
bora zaidi kufanya Ghusl ili atoke katika Khilaaf hii [ya wanachuoni] na awe
katika usalama.
Chanzo: http://youtu.be/PNfsXRKm_9M
28) Unyenyekevu Wa Shaykh ´Abdul-Muhsin al-´Abbaad
Swali:
Hii ni bishara njema. Shaykh wetu nimeona usingizini kuwa naingia
nyumbani, nikamuona Shaykh al-Albaaniy kajinyoosha nikamuuliza:
"Shaykh wetu, nani wa kurejea kwake baada yako?"
Akasimama na kwenda kwenye mlango na akafungua mlango na akaashiria
kwa mkono wake wa kulia na akanyoosha kidole chake cha shahada na
kuashiria mahala, na akasema:
"al-´Abbaad, al-´Abbaad."
Akaendelea kukariri mpaka nikashtuka na mimi nikafurahi.
´Allaamah al-´Abbaad:
Allaahu Musta´aan. Ninasema Allaahu Musta´aan mimi sistahiki nafasi kama
hii, mimi siwezi kusimama nafasi kama hii. Ndoto hii inaweza kuwa na taabiri
(maana) nyingine.
Chanzo: http://youtu.be/sYIjpAVD3MY
22
29) Ni Wajibu Kutahadharisha Dhidi Ya Watu Wa Bid´ah
Shaykh Abu ´Abdul-Haaliym ´Abdul-Haadiy:
Kama alivyosema al-´Allaamah Ibn al-Qayyim (Rahimahu Allaah) na Salaf na
maimamu kuhusu kutahadharisha watu na Bid´ah. Kwa nini? Kwa kuwa
madhara ya Bid´ah na kuiharibu Dini ni mabaya na ni jambo la wajibu katika
mambo ya uwajibu mkubwa na ni Jihaad kubwa. Kasema Shaykh-ul-Islaam
Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah):
“Hakika kutahadharisha watu na maimamu wa Bid´ah kwa watu wakukhalifu
Qur-aan na Sunnah au ´Ibaadah zinazokhalifu Qur-aan na Sunnah, kubainisha
hali zao na kutahadharisha Ummah dhidi yao ni wajibu kutahadharisha watu
na Ahl-ul-Bid´ah.”
Ni wajibu juu yako ewe mja wa Allaah kutadharisha watu dhidi ya watu wa
Bid´ah. Anasema Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah):
"Hakika kubainisha hali zao, na kuhadharisha Ummah dhidi yao ni wajibu
kwa makubaliano ya wanachuoni."
Kulisemwa kuambiwa Ahmad bin Hanbal:
"Mtu anafunga, anaswali na kufanya I´tikaaf - yaani anafunga Swawm za
Sunnah, Swalah za Sunnah na kufanya I´tikaaf. Je ni bora au [mtu mwenye]
kuwaongelea watu wa Bid´ah?
Akasema: "Akisimama na kuswali na kufanya I´tikaaf ni faida yake
mwenyewe, na akiongelea watu wa Bid´ah faida ni ya Waislamu na hili ndio
bora zaidi."
Na ni wajibu kwa maulamaa wa Ummah kutahadharisha watu dhidi ya watu
wa Bid´ah na watu wa Ahwaa (matamanio), kwa kuwa ni Jihaad enyi waja
wa Allaah, bali ni katika aina bora ya Jihaad katika njia ya Allaah (Jalla wa
´Alaa). Kasema Imaam al-Baghawiy katika Sharh-us-Sunnah:
"Katwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu mgawanyiko
wa Ummah huu na kujitokeza Ahwaa na Bid´ah na kuokoka kwa yule
atayefuata Sunnah zake na Sunnah za Maswahabah wake (Radhiya Allaahu
´anhum)".
23
Waislamu wajue wakimuona mtu kashikamana na kitu katika Ahwaa na
Bid´ah au anachukia kitu katika Sunnah huku akiamini hivyo, mtu huyo
inatakiwa kumhama [kumsusa] na kujiweka nae mbali kabisa na amuache yu
hai au maiti, asimtolee Salaam atapokutana nae wala asimjibu atapoanza
[kukutolea yeye], mpaka hapo atapoacha Bid´ah zake na kurejea katika haki...
Na makatazo ya kumsusa ndugu yako zaidi ya siku tatu katika yaliyotokea
baina ya watu wawili, hili halihusiana na mambo ya haki ya Dini. Watu wengi
wanadhani kuwa kumhama mtu hata ikiwa kwa watu wa Bid´ah, isizidi siku
tatu. Maana ya Hadiyth si hii, fahamu Hadiyth hii vizuri. Makusudio ya
Hadiyth hii:
"Si halali kwa muumini kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu."
Hili si kwa watu wa Bid´ah na Ahwaa. Bali hili linahusiana wakati watu
wawili wanapokwaruzana katika mambo ya kidunia au ya kawaida tu... Baina
yako wewe na yeye. Ama watu wa Bid´ah na watu wa Ahwaa, wanasusiwa
sawa waliohai na waliokufa mpaka watubie kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa). Na
kwa hili anasema Imaam al-Baghawiy:
"Kuwasusia watu wa Bid´ah na matamanio ni jambo la daima (milele) mpaka
hapo watapotubia."
Na si kwamba ni siku tatu, mambo gani siku tatu? Bali ni wajibu kwako
kuwahama [kuwasusia] daima mpaka watapotubie, khaswa ikiwa ni wale
vigogo wa Bid´ah na Ahwaa. Hapa enyi ndugu, lazima tutanabahishe mambo
mawili. Tusiwabadiy´ na kutafsiyq khaswa kama wafanyavyo baadhi ya
vijana wanapoona mtu katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kaanguka katika
Bid´ah moja kwa moja wanamhukumu kuwa ni mtu wa Bid´ah na yuko hivi
na vile, na unamsafiki, na kumbadiy´ na kumsusa, hapana ewe mja wa Allaah.
Si kila mwenye kutumbukia katika Bid´ah, Bid´ah huanguka juu yake.
Anaweza kutumbukia katika Bid´ah naye ni mjinga hajui, anaweza
kutumbukia katika Bid´ah naye kalazimishwa hilo, kama jinsi baadhi ya vijana
wamenguka na Jamaa´at-ut-Tabliygh, al-Ikhwaan al-Muslimuun
wakawadanganya huku wakidhani kuwa wako katika haki. Ni juu yako
kuwabainishia kuwa wako katika Bid´ah, na kwamba kitendo ambacho
wakoemo ni Bid´ah. Uwabainishie kwa dalili katika Qur-aan na Sunnah za
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama (baada ya
kumfikishia haki) akaleta kiburi na ukaidi, huyu ndiye Mubtadiy´ (mtu wa
Bid´ah). Mtu wa Bid´ah ni mtu ambaye kaanguka katika Bid´ah akanasihiwa
24
lakini akaleta kiburi na ukaidi. Na si (kumhukumu) kabla hujamsimamishia
haki ewe mja wa Allaah. Ama kwa yule anayekubali haki, tutamshika mkono
na Dini ni nasaha kama ilivokuja katika Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam). Na anasema Imaam ash-Shawkaaniy katika
Fathiyl Qadiyr katika tafsiri Kauli ya Allaah (Jalla wa ´Alaa):
ون الذين رأيت وإذا وض وا حتى عنه م فأعرض آياتنا في يخ وض ا غيره حديث في يخ د فل ياان الش ي نسينك وإم تقع
كرى المين القوم مع بعد الذ الظ
“Na unapowaona wanaoziingilia Aayah zetu, basi jitenge nao mpaka
waingilie mazungumzo mengine. Nakama Shaytwaan akikusahaulisha, basi
baada yakutanabahi usikae pamoja na watu madhaalimu.” (06:68)
Anasema (Rahimahu Allaah) - fahamu Aayah hii vizuri na uzingatie maana
yake nayo ni Aayah kubwa. Anasema Imaam ash-Shawkaaniy (Rahimahu
Allaah) kama ilivo katika kitabu Fathiyl Qadiyr:
"Katika Aayah hii kuna mawaidha makubwa kwa yule mwenye kukaa na
watu wa Bid´ah."
Kama wasemavyo baadhi ya vijana leo, tunaangalia maslahi na madhara
(kabla ya kuwasusa watu wa Bid´ah). Yako wapi maslahi? Je ni wewe mwenye
kujua maslahi na madhara? Mwenye kujua maslahi na madhara ni maulamaa
ewe mja wa Allaah, ewe mja wa Allaah acha kucheza, acha kucheza ewe mja
wa Allaah. Vijana wengi wanasema, tunaangalia maslahi na madhara - anakaa
na watu wa Bid´ah, anatembea na watu wa Bid´ah, anacheka na watu wa
Bid´ah na anasema:
"Ni kwa ajili ya maslahi na madhara"
Maslahi na madhara hayakadiriwi na wewe?? Ni maulamaa wangapi
waliokuwa katika Sunnah, kwa kukaa kwao na watu wa Bid´ah na Hawaa
wamepotea na hili lipo ewe mja wa Allaah. Ni watu wangapi katika wale
wanaodai kuwa wana elimu walipoanza kukaa na watu wa Hawaa na
wakajichanga nao wamepotea, kama ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq,
Adnaan ´Ar´uur na wengine wengi katika makundi haya na katika watu hawa
wanaodai kuwa wana elimu - wamepotea katika Manhaj kwa kukaa nao na
watu wa Bid´ah na wamekuwa na wao sasa wanalingania watu katika Bid´ah.
Hivyo ni lazima tufahamu Aayah hii kuna mawaidha makubwa kwa ambaye
anakaa na watu wa Bid´ah ambao wanageuza Maneno ya Allaah na
25
wanafanya mchezo na Kitabu Chake na Sunnah za Mtume na wanazikejeli
kwa matamanio yao ya kipotofu na Bid´ah zao chafu. Basi ikiwa mtu hawezi
kuwakataza na kubadilisha walioemo, basi angalau kwa uchache mtu aache
kukaa nao na hilo ni jambo rahisi kwako, jiweke mbali na watu wa Bid´ah na
hilo ni rahisi kwako na si gumu.
Chanzo: http://youtu.be/4VaMwbrbfDY
30) Mkutano Wa Shaykh al-Albaaniy Na Shaykh Ibn ´Uthamiyn
Swali:
Mmeshawahi kukutana na Shaykh Muhammad bin ´Uthaymiyn katika
mkutano wa kielimu au wa kawaida?
Imaam al-Albaaniy:
Nilipata heshima kwa kupata mgeni wake nyumbani kwa mkwe wangu Dr.
Ridhwaa Na´saan Makkah. Nadhani ilikuwa wakati wa Hajj.
Muulizaji:
Hamjawahi kukutana wakati mwingine tena?
Imaam al-Albaaniy:
Siwezi kukumbuka zaidi ya mara hii.
Muulizaji:
Kama kwamba nadhani alinambia ni wakati ulipita ´Unayzah na Buraydah...
26
Imaam al-Albaaniy:
Ni kweli. Ila sidhani kama nilikutana nae.
Muulizaji:
Nadhani hata mlikunywa kahawa nyumbani kwake.
Imaam al-Albaaniy:
Sikumbuki. Yeye ndiye aliyekwambia?
Muulizaji:
Ndio na alinambia kuwa ulikuwa na Zuhayr ash-Shaawaysh.
Imaam al-Albaaniy:
Ndio ni kweli nilikuwa kule na Zuhayr ash-Shaawaysh. Inawezekana ilikuwa
ni wakati sijamjui Shaykh vizuri. Inawezekana ndio maana sikuweza
kumkumbuka, tofauti wakati alinizuru Makkah. Mimi nakumbuka hilo vizuri.
Alikuwa na wanafunzi wawili. Mmoja wao aliniuliza swali kuhusiana na
elimu ya Hadiyth. Kwa kweli napenda tabia ya Shaykh, urafiki wake, maadili
yake na jinsi anavyofanya awezavyo kwa kuepuka Taqliyd [kufuata kichwa
mchunga] tofauti na maulamaa wengi katika miji yote.
Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Källa: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (301)
27
31) Hukumu Ya Kumpa Zakaah Mume Wako
Swali:
Kuna mwanamke ambaye anamiliki dhahabu na zimefika niswaab, je inajuzu
kwake kuwapa Zakaah dada zake au kwa mume wake kwa kuzingatia ya
kwamba hamiliki mali yoyote zaidi ya dhahabu hii anayoimiliki ?
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Ndio, inajuzu kwake kulipa Zakaah kuwapa dada zake ikiwa ni mafakiri.
Umaskini wa kuhitajia, yaani ikiwa hawana kile cha kuwatosheleza. Inajuzu
pia kulipa Zakaah kumpa mume wake ikiwa ni fakiri kama alivyosema
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa Zaynab mke wa ´Abdullaah
bin Mas´uud: Aliposema je inajuzu kumpa (mume wangu) Zakaah? Akasema
"Na´am."
Chanzo: http://youtu.be/4j-DmV2wYzY
32) Je Mwanamke Anaweza Kumuomba Mwanaume Kumuoa?
Swali:
Je inajuzu kwa mwanamke akimpata mwanaume mwenye msimamo katika
Manhaj ya Salaf-us-Swaalih kuiwasilisha nafsi yake kwake kwa ajili ya ndoa,
na ipi nasaha yako?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Kwa hakika, kutafuta mwanaume mzuri ni jambo ambalo Shari´ah yalisisitiza,
kwa kuwa maisha ya ndoa yana umuhimu na athari yake, kutafuta kwake
mwanamke mwanaume mwema ni dalili ya wema wake. Mwanamke huyu,
kama kuna uwezekano maneno yakawa baina ya walii wake na baina ya huyo
anayetaka kumchumbia hili ni bora. Atamwachia jambo hili msimamizi wake.
28
Na ikiwa hawezi kuongea na msimamizi wake, atamtumia dada yake
mkubwa kama mama au dada na mfano wa hao, kisha anaweza kuwakilisha
qadhiya hii na lengo (la ndoa) ili asije kumkosa mwanaume mzuri. Hili halina
makosa. Ama ikiwa makusudio ya yeye kujiwasilisha, ni mazungumzo, au
kwa uhusiano ambao unajulikana hivi leo, kama kuoneshana mapicha,
kupeana mapicha, na kupigiana masimu; hili madhara yake yako wazi kwa
watu. Muhimu ni kuwa, ombi lake ni zuri lakini inatakiwa iwe kwa sura nzuri
na ya heshima. Si kwa maana ambayo imezoeleka leo kama kwa intanet na
simu n.k. Ikiwa itatokea kuongea nae kwa njia ya simu lengo lake la ndoa,
hivyo inatakiwa iwe neno moja tu. Nako ni kuwakilisha ombi la ndoa na
inatosha hivo. Ama kukalia mazungumzo, hili halijuzu mpaka hapo
atapokuwa mke wake.
Chanzo: http://youtu.be/1LFJ8HjGHsg
33) Iko Wapi Demokrasia Ya Hawa Makafiri?
Swali:
Ipi hukumu kwa anayesema kuweka demokrasia ni katika dharurah na
mambo ya muhimu katika zama hizi, la sivyo tutafikwa na yaliyoifika Iraaq?
´Allaamah al-Fawzaan:
Demokrasia ni madhehebu ya makafiri. Na Waislamu Allaah Hakuwapa haja
ya kitu kama hichi. Wao wako na uadilifu, uadilifu wa Kiungu. Wana uadilifu
wa Kiungu. Hawana haja ya "demokrasia" kama wasemavyo. Wanadanganya,
hakuna demokrasia. Hawana ila chuma na moto (unyama). Hawana
demokrasia. Huu ni uongo mtupu. Katika Uislamu kuna kitu kinachoitwa
uadilifu. Alhamdulillaah. Ama wanayodai na kujivunia, si sahihi. Hawana
chochote ila chuma na moto, na kushambulia manyumba na kushambulia
wale wasioafikiana na matakwa yao. Tunawaambia wale wanaosema kuna
"demokrasia", iko wapi demokrasia Afghanistan? Iko wapi demokrasia
Palestina? Iko wapi demokrasia mnayosema? Iko wapi demokrasia
29
Chechenia? Iko wapi? Iko wapi demokrasia? Mnashambulia miji yote na watu
wake. Mnaua watoto, wanawake, wazee na watu wote wanapokhalifu amri
zenu. Iko wapi Demokrasia?
Chanzo: http://youtu.be/PHdRay1KTKw
34) Hili Ni Swali La Ajabu Sijawahi Kusikia Maishani
´Allaamah Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy:
Hili ni swali la ajabu sana sijawahi kusikia maishani mwangu, anasema:
Imaam Msikitini kwetu anasema kuwa al-Albaniy ni myahudi.
Mimi nadhani mtu huyu ni mmoja katika watu wawili:
- Ima hamjui ni nani al-Albaaniy
- Na ima ni Shaytwaan mgonjwa.
Hatoki katika watu hawa wawili. Muinuko wa al-Albaaniy haukuinuka kwa
kuwa ni al-Albaaniy tu, hapana. Kainuka kwa na kupanda daraja, na dunia
kukithiri kumtaja, kwa kulinda kwake Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam). Wallaahi, kisha wallaahi, kisha wallaahi, hata mapua yetu
yakishindiliwa katika vumbi, sijui katika zama hizi aliyezilinda Sunnah za al-
Mustwafaa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hata kwa 1/10
kwa juhudi alizoweka. Ni ushahidi nitaoulizwa mbele ya Allaah (Tabaaraka
wa Ta´ala). Mtu huyu aliishi karibu miaka tisini. Miaka yote hii alikuwa ni
mwenye kuzilinda Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Allaah Akanyanyua utajo wake katika Athaar, na katika minbar, minbar ya
Msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kunasemwa: "[Hadiyth
hii] kaisahihisha al-Albaaniy, kaidhoofisha al-Albaaniy na pia kasema ni
hasan." Tunamshukuru Allaah (Subhaahahu wa Ta´ala) kwa fadhila hii
ambayo Allaah Katuneemesha kwa huduma hii ya kulinda Sunnah za Mtume
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika zama hizi ambazo wamekuwa
wachache wenye kujishughulisha na fani hii, fani ya Hadiyth za Mtume
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tunamuombea Allaah (Subhaanahu wa
30
Ta´ala) kwa Shaykh al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) msamaha mkubwa kwa
Mola Wake (Tabaaraka wa Ta´ala). Na mtu huyu atakutana na Mola Wake na
atakutana na malipo yake kwa Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) ikiwa hatotubia
kwa hili.
Chanzo: http://youtu.be/Uj6oXO9wjQk
35) Dalili Ya Qur-aan Inayofuta Vitabu Vilivyotangulia
Swali:
Je kuna dalili katika Kitabu inayothibitisha kuwa Qur-aan imevifuta vitabu
vilivyotangulia?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hili linahitajia dalili katika Qur-aan. Je, hujasoma Kauli ya Allaah:
ها يا ق ل ول إني الناس أي م هللا رس لك له الذي جميعا إليك ماوات م و إال إلـه ال واألرض الس فآمن وا وي ميت ي حيـي ه
وله ي النبي بالل ورس األ م
“Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote, niliyetumwa
na Allaah Mwenye Ufalme wa mbingu na ardhi. Hapana mungu ila Yeye
anayehuisha na anayefisha. Basi muaminini Allaah na Mtume wake asiyejua
kusoma na kuandika. (07:158)
Ni nani Mtume asiyejua kusoma na kuandika? Ni Muhammad (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam).
ون م تهتد وه لعلك بع ي الذي ي ؤمن بالل وكلماته وات األ م
“Ambaye anamuamini Allaah na maneno Yake. Na mfuateni yeye ili mpate
kuongoka.” (07:158)
Angalia.
ي وه وكلماته بالل ي ؤمن الذي األ م بع م وات ون لعلك تهتد
31
“Ambaye anamuamini Allaah na maneno Yake. Na mfuateni yeye ili mpate
kuongoka.” (07:158)
Ni dalili ya kwamba ambaye hamuamini hatoongoka na kuwa ni kafiri na
mpotofu. Je, hii haifuti yaliyotangulia?
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2515
36) Je, al-Ikhwaan al-Muslimuun Ni Katika Ahl-us-Sunnah?
Imaam Muhammad Naaswirud-Diyn al-Albaaniy:
Hivyo mimi nikasema hakuna mtu awezae kusema kuwa al-Ikhwaan al-
Muslimuun ni katika Ahl-us-Sunnan, kwa kuwa wanaiharibu Sunnah.
Chanzo: http://youtu.be/U6hPdNVqc6w
37) Hukumu Ya Mwanamke Kuzuru Makaburi -1-
Swali:
Huyu dada anauliza, je inajuzu kwangu kuzuru makaburi - yaani kumzuru
kaka yangu (Rahimahu Allaah)? Tangu kaka yangu afe huwa nikienda daima
kumzuru, napeleka uvumba na humaliza muda mrefu niko nae, humrehemu
na humuombea daima kuingia Peponi. Je hili linajuzu?
Imaam Ibn Baaz:
Hili halijuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kawalaani wanawake
wenye kuzuru makaburi, wanawake hawazuru makaburi. Hali kadhalika
32
kwenda makaburini na manukato, yote haya ni munkari. Lakini muombee
nyumbani, muombee nyumbani kwako unaposujudu. Muombe Allaah
Amrehemu, mtolee Swadaqah. Ama kwenda kumzuru hapana, wanawake
hawazuru makaburi. Ni juu yako kuomba Tawbah kwa uliyoyafanya, ni juu
yako kuomba Tawbah kwa uliyoyafanya kabla. Na kumuombea Du´aa
itakuwa nyumbani Alhamduli Allaah.
Chanzo: http://youtu.be/9TgK44ou16I
38) Baina Yetu Sisi Na Nyinyi Ni Vitabu Vya Salaf
´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy:
Shikamaneni nyote katika kamba ya Allaah na itawasaidia katika hili, na
itawafanya kuwa kama jua, kwa kurejea katika ufahamu wa Salaf-us-Swaalih,
na (ufahamu wao) kama nilivyowaambia umeenea na upo mbele yenu (katika
Kitabu cha Allaah, Sunnah, duruus za wanachuoni). Na hii ni changamoto
kwa yule atayekengeuka hili, sisi tunawapa changamoto watu wa Bid´ah na
watu wa matamanio; watu wa Bid´ah wa kiitikadi, na watu wa Bid´ah wa
kisiasa. Tunasema:
"Baina yetu sisi na nyinyi ni Salaf, baina yetu sisi na nyinyi ni Vitabu (vya
Salaf).
Alikuwa Ahmad akisema kuwaambia watu wa bid´ah:
"Baina yetu sisi na nyinyi ni Swalah ya janaza (yaani kifo).”
Na sisi tunasema hali kadhalika:
"Baina yetu sisi na nyinyi ni vitabu.”
Vitabu vipo. Allaah Alimwambia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam):
وراة فأت وا ق ل نت م إن فاتل وها بالت صادقين ك
“Leteni Tawrat muisome ikiwa nyinyi ni wasema kweli.” (03:93)
33
Hivyo (Mayahudi) walikuwa wakileta Tawrat na ilikuwa ni yenye
kuwadhalilisha. Na kwa hawa (watu wa Bid´ah), tutaleta vitabu vya Salaf,
Qur-aan na Sunnah, tunaleta vitabu vya al-Bukhaariy, Muslim, Abuu
Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa´iy, na alivyoandika Ahmad na wengineo.
Tutavileta (na kuona) ni nani aliye katika njia ya watu hawa, na ni nani
aliyeitupa na kuwakhalifu? Kama Allaah Alivyowapa changamoto Mayahudi
walete Tawrat, na wakati Tawrat ililetwa ikawafedhehesha. Sisi tunawapa
hawa watu (wa Bid´ah) walete vitabu vya Salaf, ili tumuweke wazi nani mtu
wa Bid´ah ni sisi au wao, na kubainisha ni nani mpotofu ni sisi au wao. Je wao
wanaweza kweli kutupa changamoto? Je wao wanaweza kufungua midomo
yao kwa kuthubutu kusema hivi? Sisi tunafungua midomo yetu kwa ushujaa
mkubwa, tunampa changamoto kila anayesema sisi hatuko katika Manhaj ya
Salaf-us-Swaalih. Sisi wallaahi tunalingania katika Manhaj ya Salaf-us-
Swaalih, katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam) na tunawaleta katika ´Aqiydah yetu, ´Ibaadah yetu
na msimamo wetu (kuhusiana kati ya) viongozi, makundi, mapote katika
Kitabu cha Allaah na katika Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam). Ama kwa wengine (watu wa Bid´ah) wako katika hila na
upambaji. Wallaahi hukuti kwao isipokuwa hila tu na michezo kama ya
watoto.
Chanzo: http://youtu.be/HEs47e56TTA
39) Sifa Na Tabia Za Mja Zimeumba Na Allaah
Swali:
Ipi rai yako kwa anayesema kuwa sifa ya ukarimu anayosifika nayo
mwanaadamu imeumbwa?
´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy:
Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye Aliyemuumba binaadamu na tabia
yake. Ukarimu, ushujaa n.k. [sifa] hizi zimeumba Allaah kwa waja Wake.
34
Chanzo: http://youtu.be/QN188c3AVAs
40) Ni Lazima Kwa Muadhini Awe Twahara
Swali:
Je ni lazima kwa mwenye kutoa adhaana asiwe na hadathi kubwa wala
ndogo?
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Ama hadathi kubwa ni sharti [mtu awe Twahara], lakini hadathi ndogo si
lazima. Inajuzu kuadhini bila ya kuwa na Twahara [Wudhuu].
Chanzo: http://youtu.be/6RacSh4v6wE
41) Mume Ana Wake Wawili Kumuacha Mmoja
Swali:
Akimtaliki mwanamume mmoja katika wake zake, ni wajibu kwake
kuheshimu haki za kitandani kwake mpaka itapoisha eda yake?
´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy:
Hapana! Hapana!
Chanzo: http://youtu.be/9EpD2KvFZTo
35
42) Madhehebu Manne Ni Katika Makundi 72 Ya Motoni?
Swali:
Imethibiti kwa Mtume ( وسلم عليه هللا صلي ) kuwa amesema:
"Wamegawanyika Wakristo katika mapote 72 na Ummah wangu
utagawanyika mapote 73. Yote hayo yataingia motoni ila moja tu".
Je, anaingia katika tishio hili mtu ambaye atajinasibisha na madhehebu
maalum, kwa mfano madhehebu mane?
Imaam Ibn ´Uthaymiyn:
Hapana, hawatoingia humo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)
alimaanisha ni yale makundi ambayo yatawapoteza wengine. Na madhehebu
mane hayawapotezi wengine.
Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Chanzo: Liqaa' al-Baab al-Maftuuh (129 B)
Tarehe: 1417-02-11/1996-06-27
43) Kupigana Jihaad Pamoja Na Ahl-ul-Bid´ah
Swali:
Muislamu akiwa katika safu ya vita baina ya makafiri - mayahudi, manaswara
na washirikina na baina ya wanaouwakilisha Uislamu, lakini hao
wanaouwakilisha Uislamu ni katika makundi potofu. Upi msimamo wa
Muislamu katika vita hivi ?
36
Imaam Ibn ´Uthaymiyn:
Ni wajibu apigane. Akiwepo katika safu ni lazima apigane.
Muulizaji:
Hata kama atakuwa na kundi potofu?
Imaam Ibn ´Uthamiyn:
Anapigana kwa ajili ya Uislamu na si kwa ajili ya kundi hili potofu. Si hivyo?
Ni wajibu kwake kupigana, kutokan na kauli ya Allaah:
"Enyi mlioamini! Mkikutana na jeshi, basi kueni imara, na mkumbukeni
Allaah sana ili mpate kufanikiwa". (08:45)
Na Anasema tena Allaah (´Azza wa Jalla):
"Enyi Mlioamini! Mkikutana na waliokufuru vitani msiwageuzie mgongo. Na
atakaye wageuzia mgongo wake siku hiyo - isipokuwa kwa mbinu za vita au
kuungana na kikosi - basi atakuwa amestahiki ghadhabu ya Allaah. Na pahala
pake ni Jahannamu, na huo ni mwisho muovu". (08:15-16)
Isitoshe kasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kukimbia siku ya
mapigano ni katika madhami ya kuangamiza.
Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Liqaa' al-Baab al-Maftuuh (128 B)
Tarehe: 1417-02-04/1996-06-20
44) Kuweka Mlio Wa Simu Wa Adhaana, Qur-aan Au Dhikr
Swali:
37
Je inajuzu kuweka mlio wa simu sauti ya adhaana au Aaayah tukufu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana! Zisitumiwe Adhkaar katika simu kwa ajili ya tanbihi ya maongezi.
Huu ni mtihani kwa Dhikr, mtihani kwa Qur-aan. Weka mlio usiokuwa na ala
wala muziki wala, kwa jili tu ya kukushtua [kuwa kuna mtu anapiga].
Chanzo: http://youtu.be/M072XtKRRXc
45) Kupiga Radd Watu Wa Bid´ah Ambao Wanalingania Watu Katika
Bid´ah Zao
Swali:
Kuhusiana na Radd, baadhi ya watu wanasema asipigwe Radd kila mtu,
akasema:
"Huyu akipigwa Radd na huyu, yupi atakayebaki?"
Je, hili ni sahihi?
Imaam Ibn ´Uthamiyn:
Hapana, makusudio si haya. Ni masuala tu ya Ijtihaad ndo watu haifai
wapigane Radd wao kwa wao. Kwa mfano mmoja anasema nyama ya ngamia
inavunja Wudhuu na mwingine haoni hivyo. Hapa hapahitajiki kupigana
Radd. Lakini masuala ya Fiqh ambayo msingi wake watu wametofautiana na
ni sehemu ya Ijtihaad za wanachuoni, hatuwezi kusema kila mwenye
kukhalifu rai fulani apigwe Radd. Kama tulivyosema tukifungua mlango huu,
kila mtu anapiga na kupigwa Radd.
Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
38
Liqaa' al-Baab al-Maftuuh (127 B)
Tarehe: 1417-01-27/1996-06-13
46) Kumsimamishia Mtu Hoja Kabla Ya Kumhukumu Kuwa Ni Mtu Wa
Bid´ah
Swali:
Masuala ya Tabdiy´ [kumtia mtu katika Bid´ah] ni sharti kwanza
kumsimamishia mtu hoja, kwa kuwa kuna watu wanatoa dalili kwa maneno
ya Shayk-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) katika Minhaj-us-
Sunnah an-Nabawiyyah isemayo hapewi hukumu ya Tabdiy´ kwa mtu ila
baada ya kutimia masharti na kutokuwepo vikwazo. Kwa mtazamo mwingine
ana maneno mengine ambayo wanayatolea dalili ambao hawakubaliani na
kauli hii. Je, maneno haya ni kweli kwa Shaykh-ul-Islaam na ipi kauli yenye
nguvu kwa masuala ya Tabdiy´? Ni lazima kwanza kumsimamishia mtu hoja
ili mtu achukuliwe kweli kuwa ni Mubtadiy´?
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Kumekithiri maongezi kuhusiana na hili. Tabdiy´ haitokani na Iqaamat-ul-
Hujjah. Bali anasihiwe. Ikiwa Bid´ah zake ziko wazi, anasihiwe mtu wa
Bid´ah. Na wala hakusemwi nimemsimamishia hoja. Kumsimamishia mtu
hoja inahitajika wakati tu wa Takfiyr [kumkufurisha mtu], ama Tabdiy´
hapana. Na wakati Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) alipomuuliza mtu
akasema Ibn Abiy Qutaylah Makkah kasema watu wa Hadiyth ni watu
wabaya, akasema:
"Zindiyq (mnafiki)! Zindiyq! Zindiy!".
Alitoa vumbi kwenye nguo yake na mikono yake na kusema:
"Zindiyq! Zindiyq! Zindiy!".
Hakusema kwanza itabidi nimsimamishie hoja [Iqaamat-ul-Hujjah].
Kumfanyia mtu Tabdiy´ si sharti kwanza kumsimamishia mtu hoja.
39
´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=127300
Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad , na ahli zake na
Maswahabah zake na watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.