Upload
others
View
4
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
1
HALMASHAURI YA WILAYA MASASI (Barua zote zitumwe kwa Mkurugenzi Mtendaji)
Simu: 2510031, S.L.P. 60,
Fax: 2510045. Masasi, E-mail: [email protected] Mtwara,
Kumb. Na. MDC/E.40/3/ Tarehe: 28/02/2018.
Mh. Mwenyekiti,
Baraza la Madiwani,
Halmashauri ya Wilaya
MASASI.
YAH: KUWASILISHA RASIMU YA MPANGO NA BAJETI YA HALMASHAURI
KWA MWAKA 2018/2019
Mh. Mwenyekiti,
Naomba kuwasilisha rasimu ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri kwa kipindi cha 2018/2019
ulioandaliwa kwa kufuata vipaumbele vyenye kujibu matarajio ya Serikali ya awamu ya Tano
vilivyomo kwenye Hotuba ya Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokuwa
akizindua Bunge la Tanzania. Pamoja na sheria ya Bajeti ya mwaka 2015 namba 11 iliyoanza
kutumika mwezi Julai, 1 2015. Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2015 hadi 2020, Mpango wa
Maendeleo wa miaka mitano 2015/2016 – 2020/2021 na miongozo mingine ya kitaifa, Wizara
Mama TAMISEMI, Kimkoa na Kiwilaya yote kwa pamoja ikiwa na lengo la kuwatumikia
wananchi na kuwaletea maendeleo endelevu.
Mh. Mwenyekiti, Bajeti ya 2018/2019 imejikita zaidi katika kutekeleza mambo yafuatayo:-
1. Kuzingatia matumizi ya mfumo mpya wa ‘‘Web Based PlanRep’’ utakaotumiwa
na Mamlaka za Serikali za Mitaa- MSM katika maandalizi ya Mipango na Bajeti
ya mwaka wa fedha 2018/19 badala ya mfumo wa zamani wa PlanRep ya kawaida
(uk.17 ya Mwongozo wa Bajeti 2018/19);
2. Kutenga bajeti kwa ajili ya kutekeleza masuala mtambuka kama vile jinsia,
UKIMWI na virusi vya UKIMWI, watu wenye ulemavu, masuala ya lishe, ulinzi
wa Mtoto, Vijana na Wazee pamoja na mazingira ya Mabadiliko ya Tabia Nchi
(uk. 14 ya Mwongozo wa Bajeti 2018/19);
3. Kuendelea kutenga bajeti kwa ajili ya shughuli za ufuatiliaji na tathmini (M&E)
(uk. 20 ya Mwongozo wa Bajeti 2018/19);
2
4. Kuweka kipaumbele kwa kutenga bajeti kwenye miradi ya maendeleo
inayoendelea (uk. 11 ya Mwongozo wa Bajeti 2018/19);
5. Kutenga bajeti kwa ajili ya maandalizi na uchaguzi wa viongozi wa ngazi za
msingi za Kijiji/Mtaa na kitongoji kwa Mwaka 2019 (Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa) uk. 17 ya Mwongozo wa Bajeti 2018/19
6. MSM kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kusaidia vikundi vya
ujasiriamali vya wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu kwa mchanganuo
ufuatao:- Wanawake 4%, Vijana 4% na 2% watu wenye ulemavu (uk. 18 ya
Mwongozo wa Bajeti 2018/19)
7. Kutenga asilimia 40 mpaka 60 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kutumika katika
miradi ya maendeleo na kipaumbele kitolewe kwenye kuwekeza ili kuimarisha
vyanzo vikuu vya mapato (uk. 18 ya Mwongozo wa Bajeti 2018/19) (kiambatisho
Na. 2) Halmashauri kutenga 60% ya fedha zake za Mapato ya Ndani kwa ajili ya miradi
ya maendeleo na 40% Matumizi mengineyo. Sanjari na hilo imeelekezwa kuwa
asilimia 40 ya fedha za Mapato zinazotokana na kilimo zikatumike kwenye Idara
husika kwa machanganuo ufuatao (20% Kilimo, 15% Mifugo na 5% Uvuvi).
8. Kutenga bajeti kwa ajili ya kupanga matumizi bora ya ardhi katika maeneo ya
Mijini na Vijijini na kushughulikia migogoro ya ardhi ili kuzuia migogoro ya
wakulima na wafugaji (uk.17 ya Mwongozo wa Bajeti 2018/19);
9. Kutenga bajeti kwa ajili ya ukarabati na ujenzi ili kuimarisha miundombinu ya
kiuchumi na kijamii katika sekta zote mfano Afya, Elimu, Kilimo, Maji n.k
kipaumbele kikiwa kwenye miradi ambayo haijakamilika iliyoanzishwa kwa
nguvu za wananchi (uk. 18 ya Mwongozo wa Bajeti 2018/19); na
10. Kuainisha, kupanga, kuandaa maandiko na bajeti kwa miradi ya kimkakati
itakayotelezwa katika Mwaka wa fedha 2018/19 yenye lengo la kuongeza mapato.
Mfano wa miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa stendi za mabasi, masoko, maeneo
ya maegesho, machinjio, miradi ya umwagiliaji, miundombinu mbalimbali ya
kutolea huduma pamoja na fursa zilizopo katika sekta mbalimbali (uk. 11 &19 ya
Mwongozo wa Bajeti 2018/19).
11. Kutenga bajeti asilimia 20 ya mapato ya ndani ikijumuisha GPG kwa ajili ya
uendeshaji wa Serikali za Vijiji, Mitaa
12. Kutenga bajeti kwa ajili ya kununua mashine za kieletroniki za malipo (POS);
13. Kutenga bajeti kwa ajili ya kuendesha makazi ya wazee kwa Halmashauri zenye
makazi hayo
3
14. Halmashauri zihakikishe zinatenga fedha za ujenzi wa Hospitali na ukarabati wa Vituo
vya kutolea huduma vilivyopo ili kuleta tija na kuboresha huduma za Afya.
15. Halmashauri kutenga fedha za kuimarisha masuala ya ulinzi na usalama na kuendesha
vikao vya kisheria, pamoja na masuala ya kupambana na Rushwa.
16. Kuweka kipaumbele cha kukuza Uchumi kwa kufufua Viwanda. Halmashauri
inategemea kuimalizia miradi ya usindikaji wa Alizeti na Viwanda vidogo vidogo vya
Korosho na mihogo ilikuwa haijakamilika.
A: MAPITIO YA MAPATO NA MATUMIZI 2017/2018
Mhe, Mwenyekiti,
Katika bajeti ya mwaka 2017/2018 Halmashauri ilikadiria kukusanya na kutumia jumla ya Tshs
30,560,442,000.00 kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali vya mapato. Kati ya makisio hayo,
Tshs 26,390,816,000.00 ilikuwa ni Ruzuku toka serikali Kuu, na Tsh 4,169,626,000.00 kutoka
Mapato ya ndani ya Halmashauri. Kufuatia maagizo na miongozo mbalimbali kutoka Serikali
kuu ya kututaka kushusha Ushuru wa mazao kutoka asilimia 5 hadi asilimia 3 na kuondolewa
kwa baadhi ya vyanzo vya mapato kumepelekea kushuka kwa mapato ya ndani kutoka Tshs.
4,169,626,000.00 hadi kufikia Tshs. 2,484,576,000. Kiasi kilichopungua ni Tshs.
1,685,050,000.00 sawa na asilimia 40.41 ya maksio ya awali:- (Tshs. 960,000,000 Export levy,
Tshs. 473,000,000 Korosho, Tshs. 100,000,000 Ufuta, Tshs. 10,000 Karanga, Tshs. 80,000,000
Mbaazi, Tshs. 12,000,000 mahindi, Tshs. 40,000 mpunga na Tshs. 60,000,000 choroko) pia
Halmashauri ililazimika kuondoa kiasi cha Tshs. 1,371,650,000.00 fedha za mfuko wa barabara
na hivyo kufanya Bajeti ya Halmashauri kupungua hadi Tshs. 27,503,742,000.00. Kati ya
makisio hayo, Tshs 25,019,166,000.00 ni Ruzuku toka serikali Kuu, na Tsh 2,484,576,000
kutoka Mapato ya ndani ya Halmashauri.
Mhe, Mwenyekiti,
Kupungua kwa mapato ni dhahili kuwa kutaathiri pia matumizi; upungufu huu utaathiri miradi
na kwa asilimia hiyo hiyo pia zitaathiri matumizi mengineyo, hata hivyo itatutaka pia kupunguza
matumizi kwa kiasi kikubwa ili kuenenda na Bajeti yetu 2017/18 na kuifikisha mwisho.
4
Mhe. Mwenyekiti, hadi Disemba 31 2017, Halmashauri ilikuwa imekusanya jumla ya Tshs.
11,963,860,240.81 toka vyanzo vyake mbalimbali vya mapato, Fedha hizo ni sawa na asilimia
43.50 ya makisio yaliyoidhinishwa baada ya mapitio.
Jedwali Na.1 Mchanganuo wa mapato kwa kila fungu:-
Eneo Makisio
2017/2018
Mapitio ya
Vyanzo vya
Mapato-Ndani
Mapato Halisi
hadi Desemba
2017
Asilimia
(%)
Mapato ya Ndani 4,169,626,000.00 2,484,576,000.00 1,259,648,936.81 50.70
Jumla ya mapato
ya ndani
4,169,626,000.00 2,484,576,000.00 1,259,648,936.81 50.70
Ruzuku - Mishahara 19,264,953,000.00 19,264,953,000.00 8,530,783,600 44.28
Ruzuku–Matumizi
mengineyo
1,043,086,000.00 1,043,086,000.00 618,504,600 59.30
Mfuko wa Pamoja
(Miradi ya
Maendeleo)
6,082,777,000.00 4,711,127,000.00 1,554,923,104 33.01
Jumla ya vyanzo
vya nje
26,390,816,000.00 25,019,166,000.00 10,704,211,304.00 42.78
Jumla Kuu 30,560,442,000.00 27,503,742,000.00 11,963,860,240.81 43.50
Fedha
zilizopokelewa nje
ya bajeti
- 4,950,737,634.84
-
Jumla Kuu 30,560,442,000.00 27,503,742,000.00 16,914,597,875.65 61.50
B: MATUMIZI:
Mhe. Mwenyekiti,
Kwa upande wa Matumizi, mwaka 2017/2018 Halmashauri ilikadiria kutumia Tshs
30,560,442,000.00. Kati ya matumizi hayo 4,169,626,000.00 ni kutokana na vyanzo vya ndani,
Tsh 26,390,816,000.00 ni kutokana na Ruzuku toka serikali Kuu kwa ajili ya Mishahara,
Matumizi mengineyo na Miradi ya Maendeleo. Wakati wa mapitio ya nusu mwaka 2017/18,
bajeti ya Halmashauri ilishuka hadi kufikia Tshs. 27,503,742,000.00 kutokana na sababu
zilizotajwa hapo juu.
Mhe. Mwenyekiti hadi kufikia Disemba, 31 2017 Halmashauri imetumia jumla ya Tshs
10,794,650,958.71 sawa na asilimia 39.25 ya makisio yaliyoidhinishwa baada ya mapitio.
5
Jedwali Na.2 Mchanganuo wa Matumizi kwa kila fungu
Eneo MAKISIO
2017/2018
Mapitio Halisi hadi
Desemba 2017
MATUMIZI HADI
DESEMBA
% YA
MATUMIZI
HADI
DESEMBA
Mapato ya Ndani 4,169,626,000.00 2,484,576,000.00 631,451,618.95 25.41
Jumla ya
mapato ya ndani
4,169,626,000.00 2,484,576,000.00 631,451,618.95 25.41
Ruzuku -
Mishahara
19,264,953,000.00 19,264,953,000.00 8,467,214,133.79 43.95
Ruzuku–
Matumizi
mengineyo
1,043,086,000.00 1,043,086,000.00 517,970,028.97 49.66
Mfuko wa
Pamoja (Miradi
ya Maendeleo)
6,082,777,000.00 4,711,127,000.00 1,178,015,177 25.00
Jumla ya vyanzo
vya nje
26,390,816,000.00 25,019,166,000.00 10,163,199,339.76 40.62
Jumla Kuu 30,560,442,000.00 27,503,742,000.00 10,794,650,958.71 39.25
Fedha
zilizopokelewa
nje ya bajeti
- 3,729,600,787.36
Jumla Kuu 30,560,442,000.00 27,503,742,000.00 14,524,251,746.07 52.81
C: MAPITIO YA VYANZO VYA MAPATO YA NDANI NA MAREKEBISHO YAKE KUFIKIA
DISEMBA, 2017.
Mhe. Mwenyekiti, Jedwali Na.3 hapa chini linaonyesha mapato halisi ya fedha za ndani hadi kufikia
Disemba 31, 2017.
Jedwali Na. 3
MAELEZO MAKISIO
2017/2018
Mapitio ya Vyanzo
vya Mapato-Ndani
2017/18
JUMLA YA
MAPATO JULAI -
DISEMBA 2017
ASILIMIA
%
Mfuko wa Elimu na
Usafirishaji wa mazao
1,530,000,000.00 570,000,000 134,946,840.00 23.67
Ushuru wa Mazao:
Korosho 1,430,000,000.00 957,000,000 955,410,993.50 99.83
Ufuta 250,000,000.00 150,000,000 18,344,000.00 12.23
Karanga 25,000.00 15,000 175,000.00 1166.67
Mbaazi 200,000,000.00 120,000,000 3,902,500.00 3.25
Mahindi 30,000,000.00 18,000,000 7,613,000.00 42.29
Mpunga 100,000.00 60,000 0.00 0.00
Nyanya 16,000,000.00 16,000,000 5,050,250.00 31.56
Choroko 150,000,000.00 90,000,000 6,044,000.00 6.72
6
Mapato kupitia
vyanzo Vengine
Ushuru wa Huduma 16,232,000.00 16,232,000 17,494,271.83 107.78
Hoteli na nyumba za
wageni
3,240,000.00 3,240,000
9,007,669.98 278.01
Ada ya Shule
Sekondari
64,260,000.00 64,260,000
36,334,000.00 56.54
CHF na BIMA 160,000,000.00 160,000,000 7,536,925.00 4.71
Papo kwa Papo 75,000,000.00 75,000,000 7,854,000.00 10.47
Maombi ya Zabuni 15,000,000.00 15,000,000 150,000.00 1.00
Land survey service
fee
53,000,000.00 53,000,000 3,400,000.00 6.42
Ada ya Magulio 4,080,000.00 4,080,000 0.00 0.00
Ushuru wa Soko 3,600,000.00 3,600,000 0.00 0.00
Ushuru wa Machinjo
na Majosho
5,170,000.00 5,170,000 263,500.00 5.10
Ushuru wa Kokoto 30,850,000.00 30,850,000 6,893,000.00 22.34
Leseni ya Vileo 10,075,000.00 10,075,000 331,200.00 3.29
Leseni za Biashara 47,945,000.00 47,945,000 10,864,680.00 22.66
Mazao ya Misitu 10,241,000.00 10,241,000 673,573.00 6.58
Faini na Tozo 25,000,000.00 25,000,000 2,900,000.00 11.60
Mapato mengineyo 39,808,000.00 39,808,000 24,459,533.50 61.44
JUMLA MAPATO
YA NDANI
4,169,626,000.00 2,484,576,000 1,259,648,936.81 50.70
D. MAKSIO YA MAPATO NA MATUMIZI MWAKA 2018/2019.
Mhe. Mwenyekiti, kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi
inategemea kukusanya na kutumia Tshs. 38,003,668,225.98 kutoka vyanzo mbalimbali vya
Halmashauri. Katika Fedha hizo Tshs. 2,784,169,432.00 ni mapato ya Ndani ya Halmashauri na
Ruzuku toka Serikali Kuu ni Tshs. 35,219,498,793.98 kwa ajili ya Mishahara, Matumizi
mengineyo na Miradi ya Maendeleo.
Mhe. Mwenyekiti, kwa upande wa mapato ya ndani, Halmashauri imejipanga kukusanya jumla ya
Tshs 2,784,169,432.0 kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali vya mapato. Kiasi hiki
kinategemea kupanda kwa asilimia 12.06 ukilinganisha na mapitio ya 2017/2018 hali hii
imetokana na kuondolewa kwa baadhi ya vyanzo vya mapato na kupungua kutoka asilimia 5 hadi
3 ya ushuru wa mazao.
7
E. MAPATO YA NDANI: I
Kwa mwaka wa fedha 2018/19 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imepanga kukusanya
jumla ya shilingi 2,784,169,432.00 (Tshs 1,847,681,432.00 mapato yasiyolindwa na
Tshs 936,488,000.00 mapato lindwa) kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali vya
mapato, fedha hizo zitagawanywa katika sekta mbalimbali ili kutekeleza shughuli za
kiutawala na miradi ya maendeleo.
A: VYANZO VISIVYOLINDWA
KASMA MAELEZO MAKISIO
2018/2019
110815 Ushuru wa Mazao:
Halmashauri inakisia kukusanya TSh. 1,455,474,000 kutoka chanzo cha Ushuru
wa mazao kwa mchanganuo ufuatao:
Zao Tani
Tegemewa
(2018/19)
Bei kwa
kilo
3% ya bei
kwa kilo
Kiasi tegemewa
Korosho 28,000 1,450 43.50 1,218,000,000
Ufuta 1,800 2,000 60.00 108,000,000
Mbaazi 2,400 800 40.00 96,000.000
Nyanya 1,000 **1,000 **1,000 2,000,000
Choroko 600 800 40.00 24,000,000
Mahindi 1,200 300 6.00 7,200,000
Mpunga 2.5 800 40 100,000
Karanga 5.8 1,000 30 174,000
Jumla 1,455,474,000
1,455,474,000
140384 Faini na adhabu:
Halmashauri ya Wilaya ya Masasi inatarajia kukusanya TSh. 12,000,000/= kwa
wastani wa TSh 1,000,000/= kwa mwezi.
12,000,000
140283 Ada za Zabuni:
Halmashauri ya Wilaya ya Masasi inatarajia kukusanya jumla ya TSh.
8
KASMA MAELEZO MAKISIO
2018/2019
7,500,000/= kutokana na uuzaji wa zabuni mbalimbali, wastani.
Vitabu vya Zabuni 50 x 100,000/= Tshs 5,000,000/=
Quotation 50 x 50,000/= Tshs 2,500,000/=
7,500,000
140376 Ushuru wa Mazao ya Misitu:
Halmashauri inatarajia kukusanya jumla ya TSh 5,020,700/= kutokana na
maliasili zilizopo katika Wilaya kama ifuatavyo:
Ushuru wa misitu
(ushuru wa 5%)
Mbao m3 675@6,000 Tshs 4,050,000/=
Mkaa gunia 1,000@720 Tshs 720,000/=
Kuni m3 130@1350 Tshs 175,500/=
Miaa kg 2,350@32 Tshs 75,200/=
Jumla Tsh 5,020,700/=
5,020,700
110851
Ushuru wa Huduma (Service Levy):
Halmashauri inategemea kukusanya TSh. 29,040,000/= kutokana na huduma zinazotolewa na Wafanyabiashara (Viwanda) ndani ya Wilaya.
Chanzo Ushuru/mwezi Miezi Jumla
Ndanda spring 300,000 12 3,600,000
Ndanda Abbey 140,000 12 1,680,000
Ndanda Printing 80,000 12 960,000
Lulindi (Makonde) 50,000 12 600,000
Drumax 200,000 12 2,400,000
Airtel 50,000 12 600,000
Tigo 50,000 12 600,000
Vodacom 50,000 12 600,000
Halotel 50,000 12 600,000
NMB Ndanda 120,000 12 1,440,000
Nanganga Petrol station 90,000 12 1,080,000
29,040,000
9
KASMA MAELEZO MAKISIO
2018/2019
Ndanda Mission Petrol Station
80,000 12 960,000
Mkalapa Petrol Station 70,000 12 840,000
Yokod Oil International 100,000 12 1,200,000
Wakandarasi 200,000 12 2,400,000
Wazabuni 150,000 12 1,800,000
Ndanda workshop 120,000 12 1,440,000
Pepsi 100,000 12 1,200,000
Cocacola 110,000 12 1,320,000
TBL 160,000 12 1,920,000
SBL 150,000 12 1,800,000
JUMLA 29,040,000
110852 Hoteli na Nyumba za Wageni:
Halmashauri inakisia kukusanya TSh. 5,040,000/= kutokana na nyumba 27 za
kulala wageni pamoja na hoteli wastani wa TSh. 420,000/= kila mwezi x miezi 12
5,040,000
140370
Leseni za Vileo (Other Business Licence Fees):
Halmashauri inakisia kukusanya TSh 10,075,000/= kutokana na
1. Leseni za pombe za kigeni Halmashauri ina jumla ya grocery 120 @
80,000 Tshs 9,600,000
2. Leseni za pombe za kienyeji; jumla ya vilabu 95 @ 5,000 sawa na
Tshs.475,000/=
10,075,000
140353
Kokoto,Mawe na Mchanga (Madini ya Ujenzi)
Halmashauri inakadiriwa kukusanya kiasi cha Tshs 69,886,732/= kutoka mradi
wa uuzaji wa kokoto, mawe na mchanga.
- Vitalu vya Halmashauri 6 x 2,302,455 Tshs 13,814,732/=
- Drumax Kokoto tani 6,996 x 2,000 = Tshs 13,992,000/=
- Msanga kokoto tani 2,040 x2,000 = Tshs 7,000,000/=
- Msanga Mawe tani 3,500 x2,000 = Tshs 4,080,000/=
- Mkolopola – Mawe tani 1,000 x 2,000 = Tshs 2,000,000/=
69,886,732
10
KASMA MAELEZO MAKISIO
2018/2019
- Chikundi – Mchanga tani 1,000 x 2,000 = Tshs 2,000,000/=
- Mkalipinde-Mchanga tani 1,000 x 2,000= Tshs 2,000,000/=
- Mitesa Mawe tani 1,000 x 2,000 = sh 2,000,000/=
- Mitesa Kokoto tani 1,000 x 2,000= sh 2,000,000/=
- Maendeleo Mawe tani 500 x 2,000 = sh 1,000,000/=
- Maendeleo Kokoto tani 500 x 2,000 = sh 1,000,000/=
- Mkangaula Kokoto tani 500 x 2,000 = 1,000,000/=
- Chigugu – Mchanga tani 1,000 x 2,000 = Tshs 2,000,000/=
- Ahmed Samri (Mpodipodi) kokoto tani 3,000 x 2,000 = Tshs 6,000,000
- Mkalapa Mawe tani 1000x 2,000 = shs 2,000,000/=
- Liloya Mchanga tani 4,000 x 2,000 = shs 8,000,000/=
140371
Leseni za Biashara
Kiasi cha Tshs 57,295,000.00 zinakadiriwa kukusanywa kutokana na utoaji wa
leseni za biashara kama ifuatavyo:-
Vioski 350 @ 20,000/= 7,000,000.00
AMCOS Matawi Makuu 42 @ 40,000/= 1,680,000.00
Maduka ya vifaa vya ujenzi 75@ 65,000/= 4,875,000.00
Maduka ya Jumla 22 @ 100,000/= 2,200,000.00
Maduka ya rejareja 500 @ 50,000/= 25,000,000.0
0
Viwanda vya Maji 3 @ 300,000/= 900,000.00
Maduka ya dawa baridi 35 @ 100,000/= 3,500,000.00
Maduka ya pembejeo za kilimo/mifugo 10@ 60,000/= 600,000.00
Migahawa 70@ 5,000/= 350,000.00
Salon za kunyoa/kusuka nywele 30 @ 5,000/= 150,000.00
Bucha za nyama/samaki 20 @ 30,000/= 600,000.00
57,295,000.00
11
KASMA MAELEZO MAKISIO
2018/2019
Nyumba za kulala wageni 27 @ 80,000/= 2,160,000.00
Machine za kusaga nafaka 100 @ 20,000/= 2,000,000.00
Machine za kuranda mbao 8 @ 80,000/= 640,000.00
Viwanda vya kukamua mafuta 1 @ 100,000/= 100,000.00
Viwanda vya korosho 6 @ 100,000/= 600,000.00
Huduma za fedha kwenye simu 30@ 15,000/= 450,000.00
Pool tables 166 @ 15,000/= 2,490,000.00
Gereji za Pikipiki na uchomeleaji mageti 100@ 20,000/= 2,000,000.00
JUMLA 57,295,000.00
140291 Ushuru wa Magulio (Mnada)
Halmashauri inatarajia kukusanya kiasi cha Tshs.3,600,000/= kutokana na
ushuru wa magulio 34 @ 25,000 x 12
10,200,000
140292 Ushuru wa Soko
Halmashauri inatarajia kukusanya kiasi cha Tshs 5,400,000 kutokana na ushuru
wa soko katika kata za:-
1. Lulindi Tsh.5,000 x siku 360 = 1,800,000.00
2. Ndanda Tsh.5,000 x siku 360 = 1,800,000.00
3. Chidya shs 5,000 x siku 360 = 1,800,000.00
5,400,000
140368
Mapato Mengineyo
Halmashauri inatarajia kukusanya kiasi cha Tshs. 31,000,000/= kutokana na
ukusanyaji wa vyanzo mbalimbali vya mapato ambavyo havijajulikana
31,000,000
140293
Ushuru wa Machinjio na Majosho
Halmashauri inatarajia kukusanya kiasi cha Tshs 2,592,000/= kutokana na
ushuru wa machinjio
Machinjio
Ng’ombe 5@1000 X 12 x 12 = 720,000/=
Mbuzi 10@ 500X30x12= 1,800,000/=
2,520,000/=
3,780,000
12
KASMA MAELEZO MAKISIO
2018/2019
Kuogesha
Mifugo 200@200X2X12= 960,000/=
Leseni za uvuvi wa samaki/Kibali cha kusafirisha Samaki.
Wavuvi 30@10,000 Tsh 300,000/=
120110
Ada ya usajili wa vikundi
Halmashauri inatarajia kukusanya ada za usajili wa vikundi 192@ 20,000
Tshs. 3,840,000 kwa ajili ya vikundi ambavyo vinajisajili kwa mara ya
kwanza
3,840,000
Ada ya Upimaji Mashamba
Halmashauri inatarajia kukusanya Tsh. 53,000,000.00 ikiwa ni ada ya
upimaji mashamba. Vijiji 166 x watu 7 x 65,000/=)
75,530,000
Stendi ya Mabasi Ndanda
Halmashauri inatarajia kukusanya Tshs 66,600,000./= kutoka katika stendi
ya mabasi Ndanda wastani wa shs. 5,550,000/=kwa mwezi
Mabasi makubwa 20 x2 x siku 30 x2,000 x12 = shs.28,800,000/=
Mabasi madogo 40 x2 siku 30 x 1,000 x 12 = shs 28,800,000/=
Magari madogo binafsi 10 x siku 30 x 500 x12 = shs 1,800,000/=
Pikipi/ Bajaji 20 x siku 30 x 300 x 12 = shs 2,160,000/=
Choo 14,000 x siku 30 x 12 = shs 5,040,000/=
66,600,000
A. JUMLA YA MAPATO HALISI (PROPER OWN SOURCE) 1,847,681,432
13
B. VYANZO LINDWA /PROTECTED REVENUE SOURCES
120106 CHF
Halmashauri inakadiria kukusanya Tshs.150,000,000/= kutoka kwenye kaya
15,000 kwa Tshs 10,000 kwa kaya kwa mwaka wa fedha 2018/2019
150,000,000
USER FEES
Halmashauri inakadiria kukusanya Tshs.40,000,000/= kutoka kwenye Vituo vya
kutolea huduma za Afya kwa mwaka wa fedha 2018/2019
40,000,000
120105 NHIF
Kiasi cha Tshs. 75,008,000.00 kinatarajiwa kukusanywa kutoka mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya
75,008,000
120103 Ada ya shule za Sekondari (A’Level)
Halmashauri inatarajia kukusanya Tshs.81,480,000.00 ikiwa ni ada ya shule za
sekondari (A’Level) kutoka
Ndanda Sekondari. Wanafunzi 978 x 70,000 = 68,460,000.00,
Chidya Sekondari Wanafunzi 120 x 70,000 = 8,400,000.00
Ndwika Sekondari Wanafunzi 66 x 70,000 = 4,620,000.00
81,480,000
110815
Ushuru wa mazao ( Mfuko wa Elimu)
Halmashauri inakisia kukusanya TSh. 590,000,000.00 kutokana na Ushuru wa
mazao (Mfuko wa Elimu) kwa mchanganuo ufuatao:-
Zao Tani
Tegemewa
(2018/19)
Bei kwa
kilo
Ushuru
kwa kilo
Kiasi tegemewa
Korosho 28,000 1,450 20.00 560,000,000.00
Ufuta 1,800 2,000 5.00 9,000,000.00
Mbaazi 2,400 800 5.00 12,000,000.00
Mahindi 1,200 300 5.00 6,000,000.00
Choroko 600 1,200 5.00 3,000,000.00
JUMLA 590,000,000.00
590,000,000
B. JUMLA YA MAPATO LINDWA (PROTECTED SOURCES) 936,488,000
JUMLA KUU (A&B) 2,784,169,432
14
Muhtasari wa Makadirio ya Mapato Kutokana na Mafungu mbalimbali.
Fungu/Maelezo Makadirio 2018/2019
Vyanzo vya Halmashauri 2,784,169,432.00
JUMLA 2,784,169,432.00
Vyanzo vingine:
Ruzuku – Mishahara 27,803,058,753.00
Ruzuku – Matumizi Mengineyo 3,786,711,990.98
Ruzuku ya Fidia 129,880,000.00
Mfuko wa Pamoja (Miradi ya Maendeleo) 3,499,848,050.00
JUMLA NDOGO 35,219,498,793.98
JUMLA KUU 38,003,668,225.98
Mlinganisho wa Mategemeo ya Miradi ya Maendeleo 2017/18 & 2018/19
S/N JINA LA MRADI 2017/2018 2018/2019
1 Ruzuku ya Maendeleo (LG-
CDG) Fedha za Ndani
1,400,444,000.00 1,400,444,000.00
2 Mfuko wa Jimbo 76,975,000.00 76,975,000.00
3 Mfuko wa Barabara (ROAD
FUND)
1,371,650,000.00 0.00
4 Elimu bila Malipo Sekondari 945,128,000.00 113,762,500.00
5 Ruzuku ya Maji (RWSSP ) 342,931,000.00 342,931,000.00
6 Ujenzi wa ukumbi na ofisi za
Halmashauri
600,000,000.00 600,000,000.00
7 Mfuko wa pamoja wa Afya 532,622,000.00 0.00
8 Elimu bila malipo Msingi 730,353,000.00 342,882,000.00
9 USAID BORESHA AFYA 0.00 615,953,550.00
10 UNICEF 82,674,000.00 6,900,000.00
JUMLA MIRADI YA MAENDELEO 6,082,777,000.00 3,499,848,050.00
15
Mhe. Mwenyekiti, makadirio ya mwaka huu ni jumla Tshs. 38,003,668,225.98 ukilinganisha na
mwaka jana Tshs 27,503,742,000.00 Makadirio haya yamepanda kwa asilimia 38.18 ya
makadirio ya mwaka 2017/2018. Mapato ya ndani ni Tshs 2,784,169,432.00 Kiasi hiki
kinategemea kupanda kwa asilimia 12.06 ukilinganisha na mapitio ya 2017/2018.
F: MAKISIO YA MATUMIZI 2018/2019.
Mhe. Mwenyekiti, kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri inakadiria kutumia
jumla Tsh 38,003,668,225.98 kwa mchanganuo ufuatao:-
i) Mishahara Tsh 27,803,058,753.00
ii) Matumizi mengineyo Tsh 3,916,591,990.98
iii) Miradi ya Maendeleo Tsh. 3,499,848,050.00
iv) Mapato ya ndani Tsh 2,784,169,432.00
JUMLA Tsh. 38,003,668,225.98
G: MAKISIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2018/2019 KAMATI
MBALIMBALI KAMA IFUATAVYO:
S/N KAMATI
OC -
SERIKALI
KUU
OC - MAPATO
YA NDANI MISHAHARA
MIRADI
JUMLA MAPATO
YA NDANI
NDANI
(SERIKALI
KUU)
NJE
(WAHISA
NI)
1
Elimu,
Afya na
Maji
3,673,296,993.96 422,488,000 24,289,786,468 590,000,000 1,313,629,550 965,784,550 31,254,985,558.98
2
Ujenzi,
Uchumi
na
Mazingira
119,006,000.00 48,000,000 973,709,420 493,072,573 0.00 0.00 1,633,787,993
3
Fedha
Utawala
Mipango
124,289,000.00 984,608,859 2,539,562,865 226,000,000 1,220,433,950 0.00 5,094,894,674
4 Kuthibiti
Ukimwi 0 0 0 20,000,000 0.00 0.00 20,000,000
JUMLA KUU 3,916,591,993.96 1,455,096,859 27,803,058,753 1,329,072,573 2,534,063,500 965,784,550 38,003,668,225.98
NB: Fedha za mapato ya ndani zitakazotumika kwenye miradi ya Maendeleo kwa asilimia 60 ya
makusanyo yote.
Kamati ya Elimu, Afya na Maji Tshs 590,000,000.00
Kamati ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira Tshs 493,072,573.00
Kamati Fedha, Utawala na Mipango Tshs 226,000,000.00
Kamati ya Kudhibiti Ukimwi Tshs. 20,000,000.00
16
H: CHANGAMOTO:
Mhe. Mwenyekiti, pamoja na Bajeti hii, Halmashauri imepata changamoto mbalimbali
wakati wa utekelezaji wa mpango na bajeti ya 2017/2018.
1. Kupungua kwa mapato ya ndani kwa asilimia 40.41 na hii itafanya Halmashauri
kushindwa kutekeleza bajeti yake kama ilivyokuwa imejipangia kabla ya mabadiliko
hayo.
2. Fedha za miradi na matumizi mengineyo toka Serikali Kuu kupokelewa kiasi kidogo.
3. Halmashauri kutokuwa na usafiri wa uhakika baada ya kuchomewa magari tarehe 26
Jan 2013.
I: UFUMBUZI:
Mhe. Mwenyekiti, rasimu hii 2018/19 inalenga kutafuta mbadala wa vyanzo vya mapato
kama ifuatavyo.
Kujenga Ghala la mazao ambalo litakuwa chanzo cha mapato cha Halmashauri.
Kuongeza juhudi za ukusanyaji wa mapato ya ndani
Kuongeza au kupanua standi ya Ndanda
Mhe. Mwenyekiti, Naomba kuidhinishiwa jumla ya Tsh. 38,003,668,225.98 kati ya fedha
hizo, Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango inategemea kukusanya na kutumia jumla ya
Tshs. 5,094,894,674.00, Kamati ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira jumla ya Tshs.
1,633,787,993.00, Kamati ya Elimu, Afya na Maji jumla ya Tshs. 31,254,985,558.98 na
Kamati ya kudhibiti UKIMWI jumla ya Tshs. 20,000,000.00
Mhe. Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Jeremiah J. Lubeleje
KNY. MKURUGENZI MTENDAJI (H/W),
MASASI
17
KIAMBATISHO CHA MCHANGANUO WA MAPATO NA MATUMIZI YA BAJETI
YA HALMASHAURI YA WILAYA
(2018/2019-2020/2021)
I. MISHARAHA:
Kwa mwaka wa fedha 2018/19 kiasi cha Tshs. 27,803,058,753.00 kimeombwa kwa ajili ya
mishahara ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya yetu na kitatumika kwa mchanganuo wa
kiidara kama ifuatavyo:-
S/N KIFUNGU IDARA JUMLA
1 5004 Mshahara GSs and Above 1,910,249,595.00
2 5006 Utawala na Elimu Watu wazima 323,184,060.00
3 5007 Elimu Msingi 15,835,875,960.00
4 5008 Elimu Sekondari 5,301,903,898.00
5 5010 Huduma za Afya 670,890,480.00
6 5011 Huduma – Kinga 324,389,280.00
7 5012 Vituo vya Afya 1,037,329,200.00
8 5013 Zahanati 650,517,600.00
9 5014 Ujenzi 149,973,080.00
10 5017 Maji Vijijini 145,695,990.00
11 5031 Mishahara ya Watendaji wa Vijiji (VEOs) 629,313,270.00
12 5033 Kilimo 479,042,880.00
13 5034 Mifugo 344,693,460.00
JUMLA KUU MSHAHARA 27,803,058,753.00
18
II. MAKISIO YA MATUMIZI YA MAPATO YA NDANI II:
Jumla ya Tsh. 2,784,169,432.00 zinategemewa kukusanywa na kugawanywa katika Sekta
mbalimbali za Halmashauri ili kutekeleza shughuli mbalimbali za Kiutawala na Miradi
mbalimbali ya Halmashauri kama ifuatavyo:-
S/N KASMA IDARA JUMLA
1 500 Mishahara 168,228,000.00
2 500B Utumishi 199,348,600.00
3 500C Madiwani 473,438,000.00
4 503A Sera, Mipango & Usimamizi 21,000,000.00
5 514A Sheria 8,000,000.00
6 500A Uchaguzi 6,000,000.00
7 515A Ukaguzi wa Ndani 16,399,259.20
8 502A Fedha Utawala 17,195,000.00
9 502B Fedha Final Accounts 20,000,000.00
10 502C Fedha Matumizi 15,000,000.00
11 502D Fedha Mapato 18,000,000.00
12 516A Ugavi 7,000,000.00
13 502E Biashara na Uchumi 7,000,000.00
14 506D Ushirika na Masoko 6,000,000.00
15 507D Elimu (M) Utamaduni 6,000,000.00
16 512A Ardhi Utawala 4,000,000.00
17 512G Maliasili Uwindaji 4,000,000.00
18 512F Maliasili Utawala 4,000,000.00
19 519A Maliasili Nyuki 2,000,000.00
20 518A Habari na Mawasiliano 8,000,000.00
21 527A Maendeleo ya Jamii 11,000,000.00
22 501A Mazingira 9,000,000.00
23 517A Upimaji wa Mashamba 8,000,000.00
24 509B Kuendesha shughuli za Kuboresha Elimu 90,000,000.00
25 508A LISHE 20,000,000.00
26 527B UKIMWI 20,000,000.00
27 527B Mchango wa Wanawake na Vijana (8%) 147,814,514.56
19
28 527B Watu wenye ulemavu 36,953,628.64
29 509B Kuboresha miundombinu ya Elimu (Elimu
Msingi na Sekondari)
590,000,000.00
30 5010 Huduma za Afya (CHF-150,000,000 &
75,008,000 NHIF)
225,008,000.00
31 509B Ada-Elimu Sekondari 81,480,000.00
32 500A Ununuzi wa samani na vifaa vya mawasiliano
vya ukumbi wa Halmashauri
22,000,000.00
33 500A Kukarabati Choo cha Halmashauri ya Wilaya 4,000,000.00
34 500A Kununua Gari la Mkurugenzi Mtendaji 150,000,000.00
35 500A Michango ya Kisheria na uendeshaji wa Miradi
ya Wahisani wa maendeleo ndani ya halmashauri
(Enzkreis, JICA na AGA KHAN
30,000,000.00
36 506B Miradi ya Maendeleo – KILIMO, MIFUGO NA
UVUVI (40% ya Produce cess)
Ujenzi wa Ghala -253,965,130.00
308,304,430.00
37 500A Fedha kwa ajili ya Maafa 20,000,000.00
JUMLA MATUMIZI MAPATO YA NDANI 2,784,169,432.00
20
III. MATUMIZI MENGINEYO (OC):
Kwa mwaka wa fedha 2018/19 Halmashauri yetu inaomba jumla ya shilingi 3,916,591,990.98 ili
kugharamia matumizi mengineyo ya kiidara kama inavyoonesha katika mchanganuo ufuatao:-
S/N KIFUNGU IDARA JUMLA
1 500A Utawala 80,385,000.00
3 503E Biashara na Uchumi 10,000,000.00
4 505A Ukaguzi wa Ndani 15,904,000.00
5 500B Mipango 18,000,000.00
5 507C Elimu watu Wazima 6,000,000.00
6 507A Elimu Utawala 19,502,000.00
7 507B Elimu Msingi 1,044,040,934.00
8 509B Elimu Sekonari 1,423,423,959.00
9 512A Ardhi Utawala 10,000,000.00
10 508A Afya 107,273,000.00
11 508A Afya - MSD 365,000,000.00
12 508A Afya - HSBF 687,824,999,98
11 511A Ujenzi 22,693,000.00
12 510A Maji 20,232,000.00
13 512F Maliasili Utawala 10,000,000.00
14 519B Maliasili Nyuki 10,000,000.00
15 527A Maendeleo ya Jamii 10,000,000.00
16 506A Kilimo 26,548,600.00
17 506D Ushirika 10,000,000.00
18 505A Mifugo 9,764,400.00
19 501A Mazingira 10,000,000.00
JUMLA MATUMIZI MENGINEYO (OC) 3,916,591,990.00