126
i  HOTUBA YA MHESHIMIWA BALOZI DKT. AUGUSTINE PHILIP MAHIGA (MB), WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI AKIWASILISHA MAKADIRIO YA BAJETI YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017

Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

Embed Size (px)

Citation preview

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 1/126

i

 

HOTUBA YA MHESHIMIWA BALOZI DKT.AUGUSTINE PHILIP MAHIGA (MB), WAZIRIWA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WAAFRIKA MASHARIKI AKIWASILISHA

MAKADIRIO YA BAJETI YA MAPATO NA

MATUMIZI YA WIZARA KWAMWAKA WA FEDHA 2016/2017

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 2/126

ii  

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 3/126

iii

 

YALIYOMO

ORODHA YA VIFUPISHO……………………………  iv 

UTANGULIZI…………………………………………… 

 TATHMINI YA HALI YA DUNIA…………………….  6 

MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAWIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2015/2016..  12 

ILIYOKUWA WIZARA YA MAMBO YA NJE NAUSHIRIKIANO WA KIMATAIFA…………………….  12

 

 TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA…………….…  65 

Chuo cha Diplomasia…………………………… 

65 

Kituo cha Kimataifa cha Mikutano chaArusha………………………………………………  

66 

Mpango wa Kujitathmini Kiutawala BoraBarani Afrika………………………………………  68 

ILIYOKUWA WIZARA YA USHIRIKIANO WAAFRIKA MASHARIKI………………………………….  70 

USIMAMIZI WA MAPATO NA MATUMIZI………..  107 

CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA KATIKAUTEKELEZAJI WA BAJETI KWA MWAKA WAFEDHA 2015/2016……………………………………  108 

SHUKRANI……………………………………………….  110 

MALENGO YA WIZARA KWA MWAKA WA

FEDHA 2016/2017……………………………………. 111 

MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YAWIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017… 

113 

HITIMISHO………………………………………………. 

115 

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 4/126

iv

 

ORODHA YA VIFUPISHO

AfDB – African Development Bank

COMESA – Common Market for Easternand Southern Africa

FAO – Food and Agriculture

OrganizationIAEA – International Atomic Energy

AgencyILO – International Labour

OrganizationIMF – International Monetary FundIOM – International Organization for

MigrationPSPF – Public Sector Pension Fund

SADC – Southern African DevelopmentCommunity

UNDP – United Nations DevelopmentProgamme

UNEP – United Nations EnvironmentProgamme

UNESCO – United Nations EducationalScientific and CulturalOrganization

UNFPA – United Nations PopulationFund

UN-HABITAT – United Nations Human

Settlement ProgrammeUNHCR – United Nations High

Commission

for Refugees

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 5/126

v

 

UNICEF – United Nations Children’sEmergency Fund

UNIDO – United Nations Industrial

Development OrganizationUNWTO – United Nations World Tourism

OrganizationUTT – Unit Trust of TanzaniaWHO – World Health OrganizationWWF – World Wildlife Fund

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 6/126

vi

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 7/126

1

 

UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, kutokana na Taarifa iliyowasilishwa leo Bungeni naMwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge yaMambo ya Nje, Ulinzi na Usalama naomba kutoahoja kwamba Bunge lako Tukufu likubalikujadili na kupitisha Makadirio ya Mapato naMatumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka waFedha 2016/2017.

2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote 

nakushukuru kwa fursa hii adhimu yakuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu kwamara ya kwanza Bajeti ya Wizara ya Mambo ya

Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Aidha,naomba nitumie nafasi hii adhimu kumpongezakwa dhati Mheshimiwa Dkt. John Pombe

 Joseph Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Raiswa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania kufuatia Uchaguzi Mkuuuliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015.

3. Mheshimiwa Spika,  naungana nawalionitangulia kumpongeza Mheshimiwa Raiskwa uongozi wake madhubuti na makiniunaoakisi kauli mbiu yake ya ‘Hapa Kazi Tu’. Sisisote ni mashahidi wa namna uongozi wakeulivyogusa si tu wananchi wa Tanzania bali pia

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 8/126

ulivyopokelewa na kuwa mfano wa kuigwa katikanchi za bara la Afrika na duniani kwa ujumla.Sifa zake zinasikika kila pembe ya dunia na

kutufanya tutembee kifua mbele. Nampongezasana kwa kumteua Mheshimiwa Samia Suluhukuwa Mgombea Mwenza na baadae kuchaguliwakuwa Makamu wa Rais wa kwanza mwanamkekatika historia ya nchi yetu. Kuchaguliwa kwakekumeidhihirishia dunia hatua kubwa ambayonchi yetu imepiga katika kumpa fursa sawa

mwanamke.

4. Mheshimiwa Spika, nichukue nafasi hiipia kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Ali MohamedShein kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Serikali

 ya Mapinduzi Zanzibar kwa kipindi cha pilikatika uchaguzi ulioendeshwa kwa amani nausalama. Kadhalika, nampongeza MheshimiwaKassim Majaliwa Majaliwa (Mb), kwa kuteuliwakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania. Wizara yangu imefaidika sana nauongozi wao na miongozo mbalimbaliwanayoitoa katika utekelezaji wa majukumu

 yetu.

5. Mheshimiwa Spika, niungane nawenzangu walionitangulia kuwashukuru nakuwapongeza watoa hoja waliozungumza kabla

 yangu wakiongozwa na Mheshimiwa KassimMajaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa

 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 9/126

Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango (Mb), Waziriwa Fedha na Mipango ambao hotuba zaozimeweka msingi mzuri kwa kuainisha dira na

masuala muhimu ya kitaifa na kimataifaambayo baadhi yake yanaangukia katikamajukumu ya Wizara yangu. Kama alivyoahidiMheshimiwa Rais kujenga ‘Tanzania yaViwanda’ na kama ilivyotafsiriwa katika Mpangowa Pili wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka2016/2017 hadi 2020/2021, Wizara yangunayo imejielekeza katika kutekeleza ‘Azma yaSerikali ya kujenga Uchumi wa Viwanda’. 

6. Mheshimiwa Spika, kama unavyofahamu,Wizara hii ni mpya baada ya kuunganishwa kwazilizokuwa Wizara mbili za Mambo ya Nje na

Ushirikiano wa Kimataifa na Wizara yaUshirikiano wa Afrika Mashariki. Kwa ajili hiyo,namshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe

 Joseph Magufuli kwa kuniteua kuwa Mbunge naWaziri wa kwanza wa Wizara hii. Napendakumuahidi mbele ya Bunge lako Tukufu kuwanitatumia ujuzi na uzoefu mkubwa niliouvuna

katika nyanja za diplomasia ya kikanda nakimataifa kuendelea kuipaisha diplomasia ya Tanzania.

7. Mheshimiwa Spika, kazi yanguimefanywa kuwa nyepesi zaidi kutokana naushirikiano mzuri na ushauri tunaoupata mara

kwa mara kutoka kwenye Kamati ya Kudumu ya

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 10/126

Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalamachini ya uongozi wa Mheshimiwa Balozi AdadiMohammed Rajab (Mb), na Makamu wake

Mheshimiwa Kanali Mstaafu Masoud Ali Khamis(Mb) pamoja na Wajumbe wote wa Kamati hiyo.Wamekuwa wa msaada mkubwa sana kwaWizara yangu katika utekelezaji wa majukumu.

8. Mheshimiwa Spika, ukiniona nasimamambele ya Bunge lako Tukufu kwa kujiamini nikwa sababu ninao nyuma yangu viongoziwenzangu, watendaji na wafanyakaziwanaonisaidia kutekeleza majukumu yangu kwaufanisi mkubwa. Napenda kumshukuruMheshimiwa Dkt. Susan Alphonce Kolimba,Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianowa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi AzizPonary Mlima, Katibu Mkuu, Mheshimiwa BaloziRamadhan Muombwa Mwinyi, Naibu KatibuMkuu, Wakurugenzi, Mabalozi, Maafisa naWafanyakazi walioko Makao Makuu, Balozini naOfisi ya Zanzibar kwa msaada mkubwawanaonipatia. Uzalendo wao, ari yao na imani

 yao kwangu, vinanipa kila sababu ya kuaminikuwa malengo tuliyojiwekea katika Bajeti hiitutayatekeleza kwa ufanisi mkubwa.

9. Mheshimiwa Spika , mwisho lakini simwisho kwa umuhimu,  namshukuru kwadhati mke wangu mpendwa Mama Elizabeth

Mahiga, Watoto na familia yangu yote kwa

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 11/126

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 12/126

TATHMINI YA HALI YA DUNIA

Hali ya Uchumi, Siasa na Usalama Duniani

12. Mheshimiwa Spika,  hali ya duniaimeendelea kuwa ya mchanganyiko wamatumaini na mashaka. Katika kipindi chamwaka mmoja uliopita dunia imepiga hatuakwenye masuala kadhaa ya msingi kwa ustawina mustakabali wa dunia. Katika kipindi hiki

tumeshuhudia kusainiwa kwa Mkataba wa Pariskuhusu Tabianchi mwezi Desemba, 2015 ambaoumesubiriwa kwa muda mrefu. Kusainiwa kwaMkataba huu kunatoa matumaini kwa nchi zaAfrika na zile zinazoendelea kwa kuwepo kwauhakika katika Kudhibiti na Kukabili athari nachangamoto za tabianchi. Hii ni kutokana na

ukweli kuwa nchi zetu zinaathirika zaidi naathari za tabianchi wakati ni wachangiajiwadogo sana wa tatizo hilo. Kusainiwa kwaMkataba huu kunatoa fursa kwa nchi maskinikufidiwa na kujengewa uwezo katikakukabiliana na changamoto hizo. Hili ni jamboambalo nchi yetu imekuwa mstari wa mbele

kulipigania na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya MrishoKikwete aliongoza jitihada hizi akiwa Mwenyekitiwa Kamati ya Wakuu wa Nchi wa Umoja waAfrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi.

13. Mheshimiwa Spika,  jambo lingine lakutia matumaini ni kusainiwa kwa Malengo ya

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 13/126

Maendeleo Endelevu ambayo yanachukuanafasi ya Malengo ya Milenia ya mwaka 2000 -2015 ambayo utekelezaji wake ulifikia tamati

mwezi Septemba, 2015. Majadiliano kati ya nchizetu yaliyofikia malengo haya yalizingatia uzoefukatika utekelezaji wa Malengo ya Milenia, haja

 ya kumalizia viporo vya Malengo ya Milenia naumuhimu wa kuhakikisha kuwa malengomapya yanazingatia mahitaji ya leo na keshokwa kuhakikisha kuwa ni endelevu. Malengo yaMaendeleo Endelevu ndio mwongozo wa agenda

 ya maendeleo duniani kote na ndiyo yatakayokuwa rejea ya majadiliano namakubaliano mengine duniani. Sisi tumejipangavyema kutekeleza malengo hayo na bahati nzuri

 yanashabihiana kwa kiwango kikubwa na Dira yetu ya Taifa ya 2025 na Mpango wa Pili waMaendeleo 2016/2017 – 2020/2021.

14. Mheshimiwa Spika, katika kipindi chamwaka mmoja uliopita kumekuwa pia namatukio ambayo yana mwelekeo mzuri kwaustawi wa amani na usalama duniani. Kwa

kuwa yako mengi, niruhusu niyataje mawilimakubwa. Kwanza, ni hatua ya nchi zaMarekani na Cuba kuamua kurejesha urafikiwao baada ya kuwepo kwa vikwazo vyaMarekani dhidi ya Cuba kwa zaidi ya miaka 50.Hatua hii ni muhimu na tunaungana nawapenda amani kote duniani kumpongeza Rais

Barack Obama wa Marekani na Rais Raul

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 14/126

Castro wa Cuba. Ikumbukwe kuwa Marekani naCuba ni rafiki wa Tanzania, na Tanzaniaimekuwa mstari wa mbele kupinga vikwazo vya

Marekani dhidi ya Cuba. Ni faraja kuwauhasama huo umekwisha, kwani kuondolewakwa vikwazo vya Marekani dhidi ya Cubakutawezesha Cuba kushiriki kikamilifu katikauchumi wa Dunia, na hali kadhalika itaimarishaushirikiano mzuri wa kiuchumi tulionao kati

 yetu na Cuba. Makubaliano hayo yamemaliza

mabaki ya misuguano ya vita baridi ya miongo ya nyuma na kuendeleza amani duniani.

15. Mheshimiwa Spika,  tukio la pili, nikuondolewa kwa vikwazo vilivyowekwa dhidi yaIran kuhusu Mpango wa Iran wa Nyuklia tarehe16 Januari, 2016, kufuatia Shirika la Kimataifa

la Nguvu za Atomiki kuthibitisha kuwa Iranimekamilisha hatua zote ilizopewa naWanachama wa Kudumu wa Baraza la Usalamala Umoja wa Mataifa na Ujerumani. Hatua hiinayo ni muhimu sana kwa kuwa inaondoa hali

 ya mashaka iliyokuwa imetanda katika eneo laMashariki ya Kati kuhusu nchi ya Iran

kutengeneza silaha za nyuklia. Mashaka hayondiyo ambayo yamekuwa yakiyumbisha sanadunia kiuchumi kwa kuathiri bei za mafuta.Iran ni nchi rafiki ambayo tunashirikiana nayokiuchumi. Hivyo, kuondolewa kwa vikwazo hivyokunatoa fursa ya kukua kwa ushirikiano wa

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 15/126

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 16/126

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 17/126

11 

Mashariki kuwa Msuluhishi wa Mgogoro wa

Burundi. Uteuzi wa Viongozi wetu Wastaafu wa

Kitaifa ni ushahidi kuwa kauli ya Tanzania

inasikilizwa na kuheshimika kwenye majukwaa

 ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

18. Mheshimiwa Spika, Macho na masikio

 ya dunia yameelekezwa huko Asia-Pacific

kutokana na fukuto la mgogoro wa umiliki wa

eneo la Bahari ya Kusini mwa Chinaunaohusisha nchi za China, Brunei, Vietnam,

Malaysia na Ufilipino. Pamoja na kuwa

kijiografia eneo hili laweza kuonekana ni mbali

sana na nchi yetu, athari za mgogoro huo

zitagusa kila pembe ya dunia kama

hautamalizika kwa njia za amani. Eneo hilo ndiopenye kitovu kikubwa cha ukuaji wa uchumi,

uzalishaji na biashara katika kipindi hiki

ambacho uchumi wa dunia kiujumla

unasuasua. Tanzania inaamini kuwa njia ya

uhakika ya kumaliza mgogoro wa Bahari ya

Kusini mwa China ni kupitia mazungumzo

baina ya nchi na nchi na kanda. Kwa sababu

hiyo, tunaunga mkono juhudi za utatuzi wa

mgogoro huo kwa njia ya mazungumzo na

mashauriano. Tunaitaka Jumuiya ya Kimataifa

na vyombo vyake kuzingatia Azimio Na. 298 la

mwaka 1982 la Mkataba wa Umoja wa Mataifa

wa Sheria ya Bahari. 

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 18/126

12 

MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU

YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA

2015/2016

ILIYOKUWA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA

USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

19. Mheshimiwa Spika,  kabla ya kuelezautekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wafedha 2015/2016, naomba uniruhusu niainishekwa ufupi majukumu ya iliyokuwa Wizara yaMambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifakama ifuatavyo:- 

i. Kubuni na Kusimamia Utekelezaji waSera ya Nchi ya Mambo ya Nje;

ii. Kusimamia Mikataba na Makubaliano ya Kimataifa;

iii. Kuratibu Masuala ya Uhusiano baina ya Tanzania na nchi mbalimbali,Ushirikiano wa Kimataifa, Bara laAfrika na Kikanda;

iv. Kulinda na kuendeleza Maslahi ya Taifa

 ya Kiuchumi na Mengineyo nje ya nchi;v. Kusimamia masuala yanayohusu Kingana Haki za Kibalozi kwaWanadiplomasia waliopo nchinikulingana na Mkataba wa Vienna wamwaka 1961;

vi. Kusimamia na kuratibu masuala ya

Itifaki na Uwakilishi;

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 19/126

13 

vii. Kuanzisha na Kusimamia Huduma zaKikonseli;

viii. Kuratibu shughuli za Tume za Pamojaza Kudumu za Ushirikiano; na

ix. Kusimamia utawala na Maendeleo yaUtumishi Wizarani na kwenye Balozizetu.

20.  Mheshimiwa Spika,  katika kutekeleza

majukumu hayo kwa mwaka wa fedha

2015/2016, Wizara ilitengewa kiasi cha Shilingi170,367,129,238.00. Kati ya fedha hizo, Shilingi162,367,129,238.00 ni kwa ajili ya Matumizi yaKawaida na Shilingi 8,000,000,000.00 ni kwaajili ya bajeti ya maendeleo. Katika fedhazilizotengwa kwa Matumizi ya Kawaida, shilingi153,698,142,238.00 ni kwa ajili ya Matumizi

Mengineyo na Shilingi 8,668,987,000.00 

ni kwaajili ya mishahara ya Watumishi.

21.  Mheshimiwa Spika,  katika mwaka wa

fedha 2015/2016, Wizara na Balozi zakeilitarajia kukusanya maduhuli ya kiasi chashilingi 20,036,019,000.00. Hadi kufikia tarehe

30 Aprili 2016, Wizara imefanikiwa kukusanyakiasi cha shilingi 16,296,907,020.00 ikiwa nisawa na asilimia 81.3 ya makisio ya makusanyo

 yote ya maduhuli kwa mwaka wa fedha2015/2016.

22.  Mheshimiwa Spika, hadi kufikia tarehe

30 Aprili, 2016 Wizara ilipokea jumla ya Shilingi

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 20/126

14 

126,407,697,224.00 sawa na asilimia 77.8 yabajeti iliyopitishwa na Bunge. Kati ya fedha hizoShilingi 117,783,609,614.00 ni kwa ajili ya

Matumizi Mengineyo na Shilingi8,624,087,610.00 ni kwa ajili ya mishahara yaWatumishi. Hadi hivi sasa, Wizara badohaijapokea mgao wowote wa fedha za bajeti yamaendeleo.

23.  Mheshimiwa Spika,  katika kipindi chamwaka wa fedha 2015/2016, Wizaraimetekeleza majukumu yake kama ifuatavyo:-

Kubuni na Kusimamia Utekelezaji wa Sera yaMambo ya Nje

24.  Mheshimiwa Spika,  Wizara kwakushirikiana na Balozi zake, Taasisi nyingine zaSerikali na sekta binafsi imeendelea kubuni nakusimamia utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje

 yenye lengo la kukuza uchumi wa nchi kupitiadiplomasia ya uchumi iliyo endelevu. Aidha,

 jukumu hili limepewa uzito zaidi naMheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniawakati alipozindua Bunge la 11 la Jamhuri yaMuungano wa Tanzania ambapo aliziagiza Balozizetu kushiriki Mikutano inayofanyika nje kwaniaba ya Wizara, Idara na Taasisi nyingine za

Serikali. Jukumu hili kubwa limetekelezwa

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 21/126

15 

ipasavyo na Balozi zetu na hivyo kupunguzagharama kubwa za safari ambazo zingefanywana Watumishi wa Wizara, Idara na Taasisi za

Serikali. 

25.  Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu nakufanikisha ziara za Viongozi Wakuu wa Kitaifahapa nchini kutoka nchi za Vietnam naMsumbiji. Wizara pia iliratibu ziara za viongozimbalimbali kutoka nchi za Saudi Arabia, Oman,

Qatar, Ujerumani, Norway, Umoja wa Falme zaKiarabu, Sweden, Finland, Ireland, Czech, Italia,na Urusi. Pamoja na mambo mengine ziara hizozililenga kuimarisha, mahusiano ya biashara nauwekezaji kati ya nchi yetu na nchi hizo. Aidha,baadhi ya nchi hizo tayari zina mikataba yaUshirikiano na Tanzania na nyingine

zimeanzisha ushirikiano kwa mara ya kwanza.

26.  Mheshimiwa Spika, Wizara kwakushirikiana na wadau mbalimbali ilifanikishakufanyika makongamano na maonesho yabiashara na uwekezaji yaliyolenga kutangazafursa za biashara na uwekezaji zilizopo hapa

nchini. Makongamano hayo yalijumuishawafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania nanchi za Oman, Urusi, Rwanda, Ujerumani,China, India, Czech, Comoro, Misri naSingapore.

27.  Mheshimiwa Spika, kutokana na

makongamano hayo, Tanzania iliweza

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 22/126

16 

kutangaza fursa zake mbalimbali katikabiashara na uwekezaji na kufanikisha

 yafuatayo:-

(a) Kusainiwa kwa mkataba wa makubaliano ya ushirikiano baina ya Chama chaWafanyabiashara, wenye Viwanda naWakulima Tanzania na Chama chaWafanyabiashara wa Oman wa kuanzishaKampuni ya Uwekezaji kati ya Tanzaniana Oman. Kampuni hiyo imeanzishwakwa lengo la kutafuta fursa za uwekezaji

 Tanzania na Oman na imeazimia kuanzana mtaji wa Dola za Marekani milioni 25ambazo zitatumika kutoa mikopo kwawawekezaji. Mkataba huo ulisainiwamwezi Aprili 2016, Dar es Salaam wakatiwa Kongamano la Biashara na Uwekezajibaina ya Tanzania na Oman;

(b)Serikali ya Oman pia imeanzamazungumzo na kiwanda cha sukariKagera kwa nia ya kuingia makubaliano

 yatakayowezesha Serikali ya Omankuwekeza katika kiwanda hicho. Hatuahii inalenga kukiwezesha kiwandakuzalisha tani laki nne za sukari ambazozitauzwa hapa nchini na hivyo kupunguzatatizo la upungufu wa sukari. Ongezekohili la uzalishaji pia litawezesha

kuzalisha hamira, spiriti na umeme.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 23/126

17 

Hamira itauzwa Oman na sehemunyingine wakati umeme utaingizwa katikagridi ya taifa; na

(c) Kuanzishwa kwa Kiwanda chautengenezaji wa pikipiki katika eneo laUkanda Maalum wa Kiuchumi waBagamoyo kupitia Kampuni yaGuanghzhou Fekon Motorcycle Co. Ltd.

 ya China. Aidha, Kampuni hiyo imeahidi

kufungua Chuo maalum kwa ajili yamafunzo ya ufundi wa pikipiki namakenika. Vilevile, mwekezaji huyoameahidi kutoa nafasi kwa ajili ya vijanawa Tanzania kwenda China kupata ujuziwa masuala hayo katika kiwanda mamakilichopo China. Makubaliano hayo

 yalifanyika wakati wa kongamano labiashara na uwekezaji baina ya Afrika naChina lililofanyika mwezi Agosti 2015mjini Guangzhou China.

28. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa

kushirikiana na wadau mbalimbali katikautekelezaji wa Sera ya Mambo ya Njeimefanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbalikatika sekta za miundombinu, nishati, viwanda,kilimo na mifugo. Baadhi ya miradiiliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwakatika mwaka wa fedha 2015/2016 ni pamoja

na:-

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 24/126

18

 

(a) Mradi wa barabara ya Ndundu-Somanga yenye urefu wa kilomita 60 uliozinduliwamwezi Agosti, 2015. Barabara hiyo

imejengwa kwa ufadhili wa Mfuko waMaendeleo wa Kuwait kwa kushirikianana Mfuko wa Umoja wa Nchizinazozalisha Mafuta Duniani na Serikali

 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

(b) Mradi wa ujenzi wa Barabara ya Kidahwe-

Uvinza yenye urefu wa kilomita 76.6uliozinduliwa mwezi Septemba, 2015.Barabara hiyo imejegwa kwa ushirikianowa Serikali ya Umoja wa Falme zaKiarabu kupitia Mfuko wa Maendeleo waAbu Dhabi kwa gharama ya Dola zaMarekani milioni 57 pamoja na mchango

wa fedha za ndani;

(c) Mradi wa Daraja la Kikwete kwenye mtoMalagarasi mkoani Kigoma lililozinduliwamwezi Septemba, 2015. Daraja hilolimejengwa kwa ushirikiano wa Serikali

 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na

Serikali ya Jamhuri ya Korea kupitiaMfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo yaUchumi wa Jamhuri ya Korea;

(d)Mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ukamandana Unadhimu cha Tengeru, Arushakilichozinduliwa mwezi Agosti 2015

ambao ulitekelezwa kwa ushirikiano na

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 25/126

19 

Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu;na

(e) Mradi wa ujenzi wa bandari mpya yaBagamoyo na Eneo Huru la Kiuchumiuliozinduliwa Oktoba 2015. Mradi huoutatekelezwa kwa ushirikiano baina yaSerikali ya Tanzania, China na Oman.

29. Mheshimiwa Spika,  katika hatua

nyingine Wizara imeendelea kuzungumza nakuwashawishi wadau mbalimbali wa maendeleoili kusaidia jitihada za Serikali katikakukabiliana na changamoto ya ujangili hapanchini, hususan upatikanaji wa vifaa kwa ajili

 ya kufanyia doria kwenye Mbuga na Hifadhi za Taifa. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu

kwamba katika kipindi hiki, Serikali yaUjerumani imeipatia Tanzania ndege mbilindogo kwa ajili ya kupambana na ujangili.

 Tunaamini kuwa ndege hizo zitaongeza ari naufanisi kwa askari wetu katika utekelezaji wamajukumu yao ya kuendesha doria katikaHifadhi za Taifa na Mapori ya Akiba yaliyopo

nchini. Vilevile, nchi nyingi za Ulaya, Marekanina Mashirika ya Kimataifa kama vile WorldWildlife Fund , Frankfurt Zoological Society  zimeonyesha utayari wa kuisaidia Tanzania kwahali na mali katika kulinda hifadhi zawanyamapori.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 26/126

20 

30. Mheshimiwa Spika,  Kadhalika,  Wizara 

kwa kushirikiana na wadau wengine,imefanikisha majadiliano na Serikali ya

Ufaransa kwa ajili ya kusaidia mpango wamaboresho ya jengo la abiria (Terminal II)  katikaUwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JuliusNyerere. Serikali ya Ufaransa kupitia Shirikalake la Maendeleo imekubali kuipatia Serikali ya

 Tanzania kiasi cha Euro  Milioni  65   kwa ajili yaukarabati na uboreshaji wa uwanja huo.

31.  Mheshimiwa Spika, Wizara kwakushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo

 ya Ufundi imeendelea kutafuta fursa za masomonje ya nchi ili kuliwezesha Taifa kuwa na hazinakubwa ya wataalam katika sekta mbalimbali.Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwanchi rafiki za Algeria, Malaysia, Indonesia,Pakistan, Iran, Malta, Misri, Sri Lanka, BruneiDarussalam, Canada, Ujerumani, Uingereza,Marekani, Uholanzi, Ubelgiji, Oman, Urusi,Australia, Japan, China, Cuba, Ufaransa,

 Thailand, Uswisi na Korea pia zimeendelea

kushirikiana nasi katika kuwajengea uwezoWatanzania kupitia ufadhili wa mafunzo yamuda mrefu na mfupi katika fani mbalimbali.

32. Mheshimiwa Spika , Wizara imeratibuna kufanikisha upatikanaji wa mkopo wamasharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 20

kutoka Serikali ya Italia, kupitia Shirika la

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 27/126

21 

Maendeleo la nchi hiyo. Mkopo huo utatumikakutekeleza mradi wa Technical and LabourMarket Support Programme   unaolenga

kuimarisha na kukuza elimu ya Ufundi kwakuvijengea uwezo vyuo vya ufundi ili kutoamafunzo yanayokidhi mahitaji ya soko la ajira.Vyuo vitakavyonufaika na mradi huo ni pamojana Chuo cha Ufundi Dar es Salaam, Chuo chaUfundi Arusha na Chuo Kikuu cha Sayansi na

 Teknolojia Mbeya. 

33. Mheshimiwa Spika , Wizara inaendeleana juhudi za kuwatafutia fursa za ajira nakuwaandalia mazingira mazuri watanzaniawanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi.Kufuatia Mkataba wa ajira baina ya Tanzania naQatar, Watanzania wapatao 250 wamekwendaQatar kufanya kazi kuanzia mwezi Desemba,2015. Timu za pande zote mbili zinaendelea nauratibu wa kuwapata Watanzania watakaowezakunufaika na fursa hiyo. Aidha, Wizara piainaendelea kuwasaidia Watanzania kupata kazikatika makampuni mbalimbali nje ya nchi

mathalani katika Mashirika ya Ndege yanayofanya safari zake hapa nchini. Katikamwaka wa fedha 2015/2016, Watanzania 18walipata kazi katika Shirika la Ndege laEmirates na jitihada kama hizo zinaendeleakufanyika kwa mashirika mengine. Nichukuefursa hii kutoa wito kwa vijana wa Tanzania

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 28/126

22 

kujitokeza na kuomba kazi katika Mashirika yaKimataifa.

34. Mheshimiwa Spika, 

Wizara iliratibu na

kufanikisha makubaliano kati ya  Tanzania na

Poland yaliyofanyika mwezi Oktoba 2015,

ambapo Poland ilikubali kutoa mkopo wa

masharti nafuu wa kiasi cha Dola za Marekani

milioni 110. Makubaliano hayo yatawekwa saini

baina ya Shirika la Maendeleo la Taifa kwaupande wa Tanzania na kampuni ya URSUS ya

Poland. Kati ya fedha hizo, kiasi cha Dola za

Marekani milioni 55 zitatumika kwa ajili ya

uanzishaji kiwanda cha kuunganisha matrekta

hapa nchini yanayotengenezwa na kampuni

hiyo. Chini ya makubaliano hayo kampuni hiyoitafundisha vijana wetu kuunganisha na

kutengeneza matrekta. Aidha, kiasi cha Dola za

Marekani Milioni 55 kitatumika kwa ajili ya

ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mazao.

Nafurahi kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa

utekelezaji wa miradi hii miwili utaanza hivi

karibuni.

35. Mheshimiwa Spika , katika suala zima

la utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje

inayoweka msisitizo katika Diplomasia ya

Uchumi, Tanzania itaendelea kujenga

mahusiano ya karibu na mashirika mbalimbali

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 29/126

23 

 ya kimataifa kama vile Benki ya Dunia;

mashirika yasiyo ya kiserikali yenye nguvu za

kiuchumi na kisiasa; na makampuni ya

kimataifa ya mafuta, nishati, mawasiliano na

miundombinu ili kupata mitaji na teknolojia

inayohitajika nchini kwetu.

Kusimamia Mikataba na Makubaliano yaKimataifa

36. Mheshimiwa Spika , katika kipindi cha

mwaka wa fedha 2015/2016 Wizara iliratibu na

kusimamia uwekwaji saini wa mikataba

ifuatayo:- 

(a)Hati za Makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na

Serikali za Sri – Lanka, Serbia, Ghana,

Malta, Qatar, Kuwait na Morocco

kuhusu masuala ya Usafiri wa Anga

 yaliyotiwa saini mwezi Oktoba, 2015;

(b) Hati ya Makubaliano kati ya Wizara na Taasisi ya Maendeleo ya Miundombinu

kuhusu kuendeleza viwanja na nyumba

zinazomilikiwa na Serikali nje ya nchi,

uliowekwa saini tarehe 08 Desemba,

2015 – Dar es Salaam;

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 30/126

24 

(c) Mkataba wa Uenyeji kati ya Tanzania na

 Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kuhusu

Makao Makuu ya Kamisheni ya Kiswahili

 ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki

 yaliyoko Zanzibar. Mkataba huo

uliwekwa saini tarehe 28 Desemba,

2015; na

(d) Mkataba wa Ushirikiano kati ya

 Tanzania na Ufalme wa Saudi Arabiakatika nyanja za uchumi, biashara,

uwekezaji, michezo na vijana uliosainiwa

tarehe 24 Machi, 2016.

37. Mheshimiwa Spika , Wizara inaendelea

kufuatilia utekelezaji wa mikataba hiyo ilikusimamia maslahi ya nchi.

Kuratibu Masuala ya Uhusiano baina yaTanzania na nchi mbalimbali, Ushirikiano waKimataifa, Bara la Afrika na Kikanda

Ushirikiano wa Kimataifa

Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka2030

38. Mheshimiwa Spika,  mwaka 2015

utakumbukwa sana na Jumuiya ya Kimataifa

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 31/126

25 

kutokana na makubaliano na maamuzi muhimu

 ya kimataifa yaliyofikiwa. Miongoni mwa

makubaliano hayo ni kupitishwa kwa Ajenda

Mpya ya Maendeleo kwenye Mkutano Maalum

wa Umoja wa Mataifa wa Wakuu wa Nchi na

Serikali uliofanyika New York, Marekani mwezi

Septemba, 2015. Katika Mkutano huo, viongozi

hao walikubaliana kuwa na dira mpya ya

maendeleo ya dunia ijulikanayo kama Ajenda ya

Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030 yenye jumla ya Malengo 17 na shabaha 169. Ajenda

hii mpya ya maendeleo endelevu inarithi

Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya miaka 15

 yaliyomalizika mwaka 2015.

39. Mheshimiwa Spika,  malengo hayo yamejikita katika kutokomeza umaskini;

kuhifadhi mazingira; kupambana na mabadiliko

 ya tabianchi; na kushirikisha makundi yote

kwenye jamii katika masuala ya maendeleo.

Ninajivunia kuwa Tanzania ilitoa mchango

mkubwa sana katika ngazi mbalimbali kipindichote cha majadiliano yaliyopelekea kupatikana

kwa malengo hayo na hivyo kuhakikisha kuwa

vipaumbele vya nchi vinakuwepo kwenye Ajenda

hiyo mpya ya Maendeleo. Tanzania ilikuwa ni

miongoni mwa nchi 30 zilizounda Kikundi Kazi

kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 32/126

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 33/126

27 

Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Majaliwaalipata nafasi ya kufafanua hatua mbalimbali zakisiasa, kisheria na utawala ambazo Serikali ya

 Tanzania inachukua katika kupambana natatizo hilo sugu la rushwa na pia kuonyeshaushirikiano wa kitaifa katika kuimarisha juhudihizo. 

Usimamizi wa Amani Duniani

42. Mheshimiwa Spika,  miongoni mwamasuala yanayoiletea heshima kubwa nchi yetuni suala la ulinzi na utetezi wa amani nausalama kwenye ukanda wetu na sehemumbalimbali duniani. Hadi sasa Tanzaniaimepeleka askari, wanawake kwa wanaume zaidi

 ya 2,328 kwenye misheni saba tofauti zakulinda amani za Umoja wa Mataifa na badotunaendelea kufanya hivyo. Tunayafanya yotehaya kwa kuwa tunaamini amani ndiyo msingiwa maendeleo na ustawi wa binadamu. Pia,tunatimiza wajibu wetu kama sehemu ya

 Jumuiya ya Kimataifa katika kuhakikisha kuwa

dunia inakuwa sehemu nzuri na salama yakuishi.

43. Mheshimiwa Spika , Taifa linajivuniasana Askari wetu wanaofanya kazi hizo zakulinda amani kwani pamoja na kushambuliwamara kadhaa, wamekuwa wakiifanya kazi hiyo

kwa umahiri, kujitoa, bidii na weledi mkubwa.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 34/126

28 

Ndiyo maana haishangazi kuona Watanzaniambalimbali wakiwa wanateuliwa kushikanyadhifa za juu kwenye misheni hizo za kulinda

amani. Ninatoa pongezi za pekee kwa askariwetu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Polisina raia walioshiriki kwa vipindi mbalimbalikatika vikosi vya kulinda amani vya Umoja waMataifa na Umoja wa Afrika.

44. Mheshimiwa Spika , pamoja na kazi

nzuri inayofanywa na askari hawa wazalendo,hivi karibuni tumepokea tuhuma kwambabaadhi ya askari wetu wamehusika kudhalilishakijinsia wanawake huko Jamhuri yaKidemokrasia ya Kongo. Tanzania ilizichukuliatuhuma hizi kwa uzito mkubwa sana na iliundatimu ya uchunguzi kutoka Jeshi la Wananchi

wa Tanzania ndani ya siku tano badala ya sikukumi zinazotakiwa na Umoja wa Mataifa baada

 ya Nchi husika kupokea taarifa za tuhuma. Tuhuma hizi zimeisikitisha sana Serikali naendapo zitathibitika hatua kali za kinidhamudhidi ya wale wote waliohusika zitachukuliwa. Ilikuhakikisha kuwa vitendo kama hivyo

vinaepukwa siku zijazo, Tanzania itajiunga nakusimamia kikamilifu “Kigali Principles”  ambazoni mwongozo wa jumla kwa nchi zinazopelekaaskari wa kulinda amani kwenye vikosi vyaUmoja wa Mataifa.

45. Mheshimiwa Spika, maendeleo ya

kisayansi na teknolojia yamesababisha

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 35/126

29 

kuongezeka kwa hali ya uhatarishi kutokana nambinu za kiuhalifu zinazotumiwa na wahalifuwenye mitandao ya kimataifa. Mathalan,

tumeshuhudia ongezeko la tishio la ugaidiAfrika Mashariki, biashara haramu ya dawa zakulevya, uvuvi haramu katika Bahari ya Hindina mzunguko wa silaha ndogondogo. Wizara

 yangu kupitia Jumuiya za Kikanda na Kimataifana ushirikiano tulionao na nchi zilizondelea,tunaratibu jitihada za kitaifa za kukabiliana na

uhalifu wa kimataifa. Kwa mfano, kupitiaMkutano wa Baraza la Mawaziri wa NchiWanachama wa SADC uliofanyika Gaborone,Botswana mwezi Agosti, 2015 Nchi Wanachamazilikubaliana kuandaa Mkakati wa SADC wakukabiliana na Ugaidi, Mkakati wa SADC wakukabiliana na ujangili na Mkakati wa SADC wakukabiliana na uzagaaji wa silaha ndogondogo.

46. Mheshimiwa Spika , katika kuendeleza

 jitihada za kupambana na uharamia baharini,

Wizara iliratibu ushiriki wa Serikali katika

Mkutano wa Tatu wa Majadiliano ya Bahari ya

Hindi uliofanyika mwezi Machi, 2016 nchini

Indonesia. Pamoja na mambo mengine, Mkutano

huo ulijadili changamoto zinazoukabili Ukanda

huo ikiwemo vitendo vya uharamia, uhalifu wa

kutumia silaha, usafirishaji haramu na ugaidi

wa majini ambavyo vinaathiri maendeleo ya

uchumi. Kutokana na kuwepo kwa changamoto

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 36/126

30 

hizo, Mkutano ulifikia Makubaliano

 yajulikanayo kama Padang Consensus  

 yanayozitaka Nchi Wanachama kuandaa

mikakati mbalimbali kwa kutumia sheria za

kimataifa zilizopo katika kupambana na vitendo

hivyo haramu. Tanzania imejipanga kutekeleza

makubaliano hayo kupitia Kamati ya Kitaifa ya

Usalama Majini iliyo chini ya Uenyekiti wa

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na

Nchi Kavu.

47. Mheshimiwa Spika, Tanzania ni mhanga

wa biashara haramu ya silaha ndogondogo

kutokana na kuzungukwa na nchi zenye

machafuko hasa kwenye Ukanda wa Maziwa

Makuu. Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo,Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali

imekuwa ikichukua hatua madhubuti za

kukabiliana na changamoto hiyo ikiwemo

kutunga sheria na kanuni za kudhibiti biashara

hiyo haramu; kuweka alama silaha

zinapoingizwa nchini na kuzisajili; na kuchoma

silaha haramu. Jitihada hizi pia zinafanyika

kimataifa ikiwemo kusaini mikataba mbalimbali

kama vile Mkataba wa Kimataifa wa Kudhibiti

Biashara ya Silaha. Aidha, jitihada hizi zinapewa

nguvu zaidi na lengo la 16 la Agenda 2030 ya

Maendeleo Endelevu ambalo linazitaka nchi

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 37/126

31 

kupunguza ufadhili na usambazaji haramu wa

silaha ndogondogo ifikapo mwaka 2030.

Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Paris

48. Mheshimiwa Spika,  katika miaka yahivi karibuni tumekuwa mashuhuda wa athariza mabadiliko ya Tabianchi yanayosababishakuwepo kwa ongezeko la ukame; mvua nyingizinazoleta mafuriko; kuzama kwa baadhi ya

visiwa; vimbunga na tufani kubwa; kupotea kwabaadhi ya mimea na wanyama na kuongezekakwa kina cha bahari. Hali hii sio tu inapotezamaisha ya binadamu wengi na mali zao, bali piainaturudisha nyuma kwenye jitihada zetu zamaendeleo na kutokomeza umaskini. Ni kwamsingi huo, Tanzania kama ilivyo nchi nyingi

zinazoendelea imeunga mkono kupatikana kwaMkataba mpya unaolenga kudhibiti mabadiliko

 ya tabianchi. Mkataba huo ulikubaliwa wakatiwa Mkutano wa 21 wa Nchi Wanachama waMkataba wa Mabadiliko ya Tabianchiuliofanyika Paris, Ufaransa mwishoni mwamwaka 2015. Mkataba huo tofauti na mingine

iliyopita una mamlaka ya kisheria kuzibana nchizilizoendelea na zenye viwanda vingi kupunguzagesijoto.

49. Mheshimiwa Spika,  Mkataba huouliokubaliwa na nchi zote, ulitiwa saini tarehe22 Aprili, 2016 kwenye Makao Makuu ya Umoja

wa Mataifa, New York na nchi 175 zikiwemo zile

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 38/126

32 

kubwa ambazo zilikuwa zikipinga Mikatabailiyopita. Tanzania ilikuwa ni miongoni mwanchi zilizotia saini Mkataba huo. Naomba

nichukue fursa hii kuzisihi nchi zote hasa zilezilizoendelea na zinazotoa gesijoto kwa wingikuheshimu makubaliano hayo ili kupunguzaathari za mabadiliko ya tabianchi na kuitunzadunia yetu kwa manufaaa ya vizazi vya sasa navijavyo. Aidha, ninawaasa Watanzania wotekulinda misitu yetu, uoto asilia na wanyamapori

wetu kwa manufaa ya Taifa letu.

50. Mheshimiwa Spika, sitawezakuhitimisha hoja hii ya Mkataba wa Paris bilakumpongeza binti wa Kitanzania, GetrudeClement, mwenye umri wa miaka 16 ambayealipata nafasi ya kulihutubia Baraza Kuu laUmoja wa Mataifa kwa niaba ya vijana dunianiwakati wa hafla ya utiaji saini Mkataba huo.Ninaona fahari kuwa nafasi hiyo alipewa mtotowa Kitanzania miongoni mwa vijana wengiduniani kutokana na uwezo mkubwa alionao.Binti huyo ameliletea heshima Taifa na napenda

kutumia nafasi hii kuwasihi watoto na vijanawengine hapa nchini kuweka jitihada kwenyemasomo na shughuli zao wanazozifanya ili sikumoja nao wapate nafasi kama hizi nakupeperusha vizuri bendera ya Taifa. Mtotohuyu awe mfano kwa kizazi kipya chaWatanzania ambao watakuwa makini katika

kulinda urithi wa mazingira yetu.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 39/126

33 

Uteuzi wa Watanzania kwenye Mashirika naTaasisi za Kimataifa

51. Mheshimiwa Spika, kutokana namahusiano mazuri tuliyonayo na nchi nyingine,Watanzania wameendelea kupewa nafasimuhimu kwenye mashirika na taasisi zakimataifa. Suala linalozidi kuipa sifa nchi yetuna kuthibitisha imani iliyowekwa na Jumuiya yaKimataifa kwa nchi hii na watu wake.

52.  Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifuBunge lako Tukufu kuwa mwezi Februari 2016,Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliteuliwa na Bw. Ban Ki-moon, Katibu Mkuuwa Umoja wa Mataifa kuwa mmoja wa wajumbewa Jopo la Ngazi za juu la kumshauri KatibuMkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala yaUwezeshaji wa Wanawake Kiuchumi. Aidha,mwezi Januari 2016, Mheshimiwa JakayaMrisho Kikwete, Rais wa Awamu ya Nne wa

 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliteuliwakuwa Mwakilishi wa Umoja wa Afrika kwenyeutatuzi wa mgogoro wa Libya. Uteuzi wa Mhe.Kikwete unalenga kusaidia juhudi za Umoja waAfrika katika kurejesha amani na utulivu nchiniLibya kwa kutumia uzoefu wake. Pia katikamwezi huo wa Januari, Mhe. Kikwete,alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mwenza wa  Jopo

la Watu Mashuhuri la Umoja wa Mataifa lenye

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 40/126

34 

 jukumu la kutoa mwongozo wa agenda ya kinamama na watoto wakati huu wa mpito kutokaMalengo ya Milenia kwenda Malengo ya

Maendeleo Endelevu.

53.Mheshimiwa Spika, uteuzi haukuishia tukwa viongozi hawa wa Kitaifa, Watanzaniawengine pia wameendelea kuchaguliwa nakuteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali kubwakwenye Mashirika na Taasisi za Kimataifa. Hawa

ni pamoja na Dkt. Agnes Kijazi, MkurugenziMkuu, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzaniaalichaguliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Shirikala Hali ya Hewa Duniani; Bw. Gabriel Rugalemaambaye ameteuliwa kuwa Mwakilishi Mkazi waShirika la Chakula na Kilimo Duniani nchiniSierra Leone; Profesa Kennedy Gastorn ambayeni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaamKitivo cha Sheria, alichaguliwa kuwa KatibuMkuu wa Jumuiya ya Mashauriano ya Masuala

 ya Kisheria katika nchi za Asia na Afrika nafasiambayo ataanza kuitumikia mwezi Agosti 2016;na Balozi Wilfred Ngirwa alichaguliwa kuendelea

na nafasi yake ya Mwenyekiti Huru wa Baraza laShirika la Chakula na Kilimo Duniani. Pia, Bw.Donatius Kamamba, alichaguliwa kuwa Mjumbekwenye Kamati ya Urithi wa Dunia ya Shirika laUmoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,Sayansi na Utamaduni na Dk. Frannie Leautieralichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Benki

 ya Maendeleo ya Afrika.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 41/126

35

 

Kuratibu Masuala ya Ushirikiano BaraniAfrika

Umoja wa Afrika

54. Mheshimiwa Spika,  Wizara kwakushirikiana na Ubalozi wetu wa Addis Ababa,Ethiopia, imeendelea kuratibu ushiriki wa

 Tanzania katika shughuli mbalimbali za Umojawa Afrika. Mwezi Januari 2016, Tanzania

ilishiriki kwenye Mkutano wa 26 wa Wakuu waNchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyikaAddis Ababa, Ethiopia. Mheshimiwa SamiaSuluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri

 ya Muungano wa Tanzania aliongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo. Kaulimbiu yamkutano huo ilikuwa ni “Mwaka wa Haki za

Binadamu Afrika, hususan Haki za Wanawake”. Wakati wa uzinduzi wa kaulimbiu hiyo, NchiWanachama zilihimizwa kuridhia na kutekelezaItifaki na sera mbalimbali zilizoundwa na Umojahuo kwa lengo la kulinda, kukuza na kutekelezahaki za wanawake Afrika. Itifaki hizo ni pamojana Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na

Watu na Sera ya Umoja wa Afrika kuhusuMasuala ya Jinsia. Mkutano huo pamoja namasuala mengine pia ulijadili ripoti ya Baraza laAmani na Usalama la Umoja wa Afrika kuhusuhali ya amani na usalama Barani Afrika.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 42/126

36 

55. Mheshimiwa Spika,  mwezi Novemba,2015 Tanzania iliteuliwa na Umoja wa Afrikakusimamia uzinduzi wa Jeshi la Pamoja la

Afrika la Kulinda Amani Barani Afrika. Mimimwenyewe nilisimamia uzinduzi huo. Tanzaniavilevile iliendelea kutoa mchango wake katikakutafuta suluhu ya migogoro barani Afrika.

 Tanzania ikiwa Mwenyekiti wa Jumuiya yaAfrika Mashariki, ilieleza hatua mbalimbalizilizochukuliwa na Jumuiya ya Afrika Masharikikatika kutatua mgogoro wa Burundi. Mchangowa Tanzania katika Umoja wa Afrika kuhusumgogoro wa Burundi kwa kiasi kikubwa uliwezakusaidia Umoja huo kuwa na taswira mpya yanamna ya kutafuta suluhu ya kudumu ikiwemokutoa kipaumbele katika mazungumzo

 yanayohusisha pande zinazohasimiana nchiniBurundi chini ya usimamizi wa Jumuiya yaAfrika Mashariki badala ya uamuzi wa awali wakupeleka majeshi ya Umoja huo nchini Burundi. 

56. Mheshimiwa Spika , napendakulifahamisha Bunge lako Tukufu kwamba

 Tanzania ilichaguliwa kuwa mjumbe wa Barazala Amani na Usalama la Umoja wa Afrika kwavipindi viwili mfululizo kuanzia mwaka 2012hadi mwezi Januari, 2016. Hii inatokana namchango wake mkubwa katika kusuluhishamigogoro barani Afrika. Katika uchaguzi wawajumbe wapya wa Baraza hilo uliofanyika

mwezi Januari 2016, Kenya, Rwanda na Uganda

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 43/126

37 

zilichaguliwa kuwakilisha ukanda wa AfrikaMashariki.

Mkutano wa Tatu wa Ushirikiano kati yaAfrika na India

57. Mheshimiwa Spika, Wizara pia iliratibuushiriki wa Tanzania kwenye Mkutano wa Tatuwa Ushirikiano kati ya Afrika na India,uliofanyika New Delhi, India mwezi Oktoba,

2015. Katika Mkutano huo, pamoja na masualamengine, India iliahidi kuisaidia Afrika katikakuendeleza miundombinu; umwagiliaji;kuongeza thamani ya rasilimali; kuanzishaviwanda; na teknolojia ya habari namawasiliano. Aidha, Serikali ya India iliahidikutoa mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za

Marekani bilioni 10, ruzuku ya misaada ya Dolaza Marekani milioni 600 na kuchangia Dola zaMarekani milioni 100 kwa ajili ya Mfuko waMaendeleo. Vilevile, India iliahidi kutoa nafasi50,000 za ufadhili wa masomo kwa wanafunziwa Afrika nchini India kwa miaka mitano ijayo.Ili kunufaika na fursa hizi, nchi za Afrika

zinatakiwa kuwasilisha andiko la miradimbalimbali ya vipaumbele kwa Serikali ya India.

58. Mheshimiwa Spika,  napenda kuliarifu

Bunge lako Tukufu kwamba kufuatia mkutano

huo, tayari Serikali imeandaa na kuwasilisha

miradi ya kipaumbele ikiwemo miradi 17 ya maji

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 44/126

38 

pamoja na Mradi wa Serikali Mtandao. Aidha,

miradi mingine itakayowasilishwa ni pamoja na

mradi wa ujenzi wa atamizi kwa ajili ya viwanda

vidogo na vya kati katika kila mkoa; mradi wa

ujenzi wa reli itakayotumika kusafirisha abiria

katika Jiji la Dar es Salaam; na mradi wa kilimo

cha umwagiliaji – Zanzibar.

Mkutano wa Sita wa Wakuu wa Nchi na

Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati yaChina na Afrika

59. Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu na

kushiriki Mkutano wa Sita wa Wakuu wa Nchi

na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya

China na Afrika uliofanyika mwezi Desemba

2015, Jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Katika

mkutano huo Serikali ya China ilitangaza

mpango mpya wa miaka mitatu kuanzia 2016

hadi 2018 wa ushirikiano kati ya China na

Afrika ambao umeweka kipaumbele katika

kuendeleza sekta ya viwanda barani Afrika. Tanzania ni miongoni mwa nchi nne za mfano

zilizochaguliwa na China kwa ajili ya kujenga

viwanda vya mfano. Nchi nyingine zilizomo

kwenye mpango huo ni Afrika Kusini, Ethiopia

na Kenya. 

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 45/126

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 46/126

40 

Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa MaziwaMakuu

Mikutano ya Jumuiya ya Nchi za Ukanda waMaziwa Makuu.

62. Mheshimiwa Spika,  katika kipindi hikiWizara iliratibu na kushiriki katika Mkutano waMawaziri wa Sheria wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu

uliofanyika Livingstone, Zambia mwezi Agosti,2015. Mkutano huo ulipokea taarifa kutokaNchi Wanachama kuhusu hatua zilizofikiwakatika kuridhia na kutekeleza Itifaki za Jumuiya

 ya nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu hususanItifaki nne zinazopewa kipaumbele katikautekelezaji wake kwa sasa. Itifaki hizo ni; Itifaki

 ya Ushirikiano wa Kiulinzi; Itifaki ya Ushirikianowa Kimahakama; Itifaki ya Kuzuia UvunajiHaramu wa Maliasili na Itifaki ya KuzuiaUnyanyasaji wa Kijinsia dhidi ya Wanawake naWatoto. Mkutano huo ulibaini itifaki hizohazijatekelezwa kikamilifu na nchi zotewananchama. Hivyo, nchi wanachama

zilikubaliana kutekeleza itifaki hizo kikamilifu.

63. Mheshimiwa Spika,  katika kutekelezaItifaki hizo Serikali imechukua hatuambalimbali zikiwemo kutunga Sheria yakudhibiti uhalifu wa njia ya mawasiliano; Sheria

 ya kurudishiana wahalifu waliokimbilia nchinyingine; kuanzisha vitengo maalum katika

Kuratibu Masuala ya Ushirikiano wa Kikanda

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 47/126

41 

viwanja vya ndege vya Kimataifa nchini ilikudhibiti usafirishaji holela wa Maliasili;kuanzisha Mpango wa Mataifa wa kuwalinda

wanawake na watoto dhidi ya unyanyasaji wakujinsia na kuanzisha kitengo maalum katikavituo vya polisi Wilaya zote nchinikushughulikia kesi za uonevu wa kijinsia.

64. Mheshimiwa Spika, Wizara pia iliratibuushiriki wa wataalamu wa Tanzania katika

Mkutano wa Jumuiya ya Nchi za Maziwa Makuuuliofanyika Luanda, Angola mwezi Januari,2016. Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwakatika Mkutano huo ni kutathmini hali yaulinzi na usalama katika nchi za eneo laUkanda wa Maziwa Makuu hususan katikanchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia yaKongo na Sudan Kusini. Pamoja na mambomengine Jumuiya hiyo imekuwa ikifanya kazikwa karibu na Taasisi za Kikanda katikakuratibu shughuli za kutatua migogoro. Kwamfano, mgogoro wa Burundi kwa kushirikianana Jumuiya ya Afrika Mashariki, mgogoro wa

 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwakushirikiana na Jumuiya ya Maendeleo yaKusini mwa Afrika pamoja na mgogoro waSudan Kusini kwa kushirikiana na Jumuiya yaUshirikiano wa Maendeleo ya Nchi za Masharikina Pembe ya Afrika.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 48/126

42 

65. Mheshimiwa Spika,  Jumuiya hiyo yaNchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ambayo

 Tanzania ni mwanachama inatambua uhusiano

mkubwa uliopo kati ya uvunaji haramu warasilimali na kushamiri kwa migogoro. Hivyo,nchi wanachama zimesaini Itifaki ya Ulinzi,Usalama na Maendeleo pamoja na Itifaki yaKupinga Uvunaji Haramu wa Rasilimali ambazokwa pamoja zinazitaka nchi zote 12 wanachamakutii taratibu zinazotambulika kikanda zauvunaji rasilimali ambapo Cheti ya Kikanda chakuthibitisha uvunaji huo hutolewa. Hii kwakiasi kikubwa imesaidia kudhibiti makundi yawaasi kujipatia fedha kwa njia za uvunajiharamu wa rasilimali kwa lengo la kufadhilishughuli zao.

66.  Mheshimiwa Spika,  jitihada hizo zapamoja zimepelekea kutengamaa kwa hali yaulinzi na usalama katika nchi za maziwamakuu. Kwa mfano, idadi ya wakimbiziwanaoingia nchini imepungua kutoka kati yawakimbizi 200 hadi 300 kwa siku kwa mwezi

Novemba, 2015 hadi kufikia wakimbizi kati ya100 hadi 120 kwa siku kwa mwezi Mei, 2016.Hadi sasa Tanzania inahifadhi jumla yawakimbizi 136,000 kutoka Burundi na wengine2,360 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia yaKongo. Bado idadi hii ni kubwa na Serikaliinaendelea kushirikiana na wadau wengine

katika jitihada za kutatua migogoro katika

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 49/126

43 

ukanda wetu wa Maziwa Makuu ili hatimayewakimbizi hao waweze kurejea nchini mwao.

Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa AfrikaMkutano wa 35 wa Wakuu wa Nchi waJumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika

67. Mheshimiwa Spika,  Wizara iliratibu nakushiriki katika Mkutano wa 35 wa Wakuu wa

Nchi na Serikali wa Jumuiya ya MaendeleoKusini mwa Afrika uliofanyika mwezi Agosti2015 Gaborone, Botswana. Mkutano huoulijadili masuala ya siasa, uchumi, uwekezaji,kijamii, ulinzi na usalama katika Kanda.

68. Mheshimiwa Spika, pamoja na Mkutano

huo kuiteua Tanzania kuwa MakamuMwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi naUsalama wa Jumuiya hiyo, Nchi Wanachamaziliazimia yafuatayo:-

i. Serikali ya Lesotho pamoja na washirikawengine wa kisiasa nchini humokuandaa mapema iwezekanavyompango wa utekelezaji wa mabadiliko

 ya Katiba na Sekta ya Ulinzi;

ii. Kuhakikisha kuwa kunakuwepo naongezeko la uwakilishi wa wanawake

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 50/126

44 

katika nafasi mbalimbali za maamuzi ya juu Serikalini na sekta binafsi;

iii. Kutekeleza kikamilifu Sera ya Kilimo yaKanda na Itifaki zingine ili kusaidiakuongeza kasi ya uzalishaji, biasharana ushindani katika sekta ya kilimo; na

iv. Sekretariati kufuatilia kwa karibu kwakushirikiana na Nchi Wanachamakuhakikisha UKIMWI na magonjwamengine ya kuambukiza hayaendeleikuwa tishio kwenye Sekta ya Afyakatika Kanda.

69. Mheshimiwa Spika,  kutokana na nchi

 yetu kujijengea sifa ya umahiri na weledi katikamasuala ya siasa, ulinzi na usalama barani

Afrika na katika Kanda, katika mkutano huo,

 Tanzania iliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti 

wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama

kwa kipindi cha mwaka 2015/2016. Kutokana

na uteuzi huo, Tanzania kwa mara nyingineitakuwa Mwenyekiti wa Asasi hiyo katika kipindi

cha Agosti 2016 hadi Agosti 2017 ikiwa ni mara

 ya tatu kupewa wadhifa huo. Uteuzi huu

unaonyesha imani ya wanachama wa SADC

waliyonayo kwa Tanzania katika kutatua

migogoro na kusimamia amani katika kanda

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 51/126

45 

hiyo na unaendelea kuijengea nchi yetu

heshima kubwa na kuiweka juu katika medani

za Kikanda na Kimataifa. 

Mkutano wa dharura wa Viongozi Wakuu waNchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwaAfrika wanaosimamia Asasi ya Siasa, Ulinzina Usalama

70. Mheshimiwa Spika , Tanzania ilishirikikwenye Mkutano wa Dharura wa ViongoziWakuu wa Nchi za Jumuiya ya MaendeleoKusini mwa Afrika wanaosimamia Asasi yaSiasa, Ulinzi na Usalama uliofanyika Gaborone,Botswana tarehe 18 Januari, 2016 kwa ajili yakujadili hali ya kisiasa nchini Lesotho. Ujumbe

wa Tanzania kwenye Mkutano huo uliongozwana Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa,Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa

 Tanzania. Pamoja na mambo mengine, Mkutanohuo uliielekeza Serikali ya Jamhuri ya Lesothokuitoa kwa umma ripoti ya Tume Huru yaUchunguzi ya SADC na kuhakikisha kuwa

inatekeleza kwa uadilifu mapendekezo yaliyomokatika taarifa hiyo ili kuboresha hali ya siasa,ulinzi na usalama nchini humo. Vilevile,Viongozi Wakuu walisisitiza umuhimu wakusimamia kwa dhati utekelezaji wa Mikataba

 yote mitatu ya amani iliyosainiwa kwa ajili yakurejesha amani nchini humo. Taarifa ya

utekelezaji wa mapendekezo yaliyomo katika

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 52/126

46 

ripoti hiyo itawasilishwa kwenye Mkutano wa 36wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliopangwakufanyika mwezi Agosti, 2016 Mbabane,

Swaziland.

Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Nchi zaJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika

71. Mheshimiwa Spika , Wizara iliratibu nakushiriki katika Mkutano wa Baraza la Mawaziriwa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrikaambao ulifanyika Gaborone, Botswana mweziMachi, 2016. Pamoja na masuala mengine,Mkutano huo ulijadili hatua ya utekelezaji yaMpango wa Kikanda wa Maendeleo 2015 - 2020;hatua ya utekelezaji wa Mpango wa Kikanda waMaendeleo ya Viwanda; na Mtangamano waUtatu wa Eneo Huru la Biashara la COMESA-EAC-SADC. Mkutano huo pia ulipokea taarifa yautekelezaji wa maamuzi ya vikao vya Baraza laMawaziri ambayo ilihusisha jumla ya maeneokumi. Taarifa hiyo inaonyesha kuwa utekelezajiwa maeneo hayo unaendelea vizuri. 

72. Mheshimiwa Spika , Mkutano huo pia,ulipokea maombi ya Serikali ya Visiwa vyaComoro na Serikali ya Burundi ya kutakakujiunga na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwaAfrika. Hivi sasa Sekretarieti inaendelea na zoezila kutathmini maombi ya nchi hizo kulingana na

taratibu, kanuni na sheria za Jumuiya za kuwa

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 53/126

47 

mwanachama. Taarifa ya tathmini hiyo itatolewakwenye Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchiambao umepangwa kufanyika mwezi Agosti,

2016, Mbabane, Swaziland.

Jumuiya ya Nchi za Mwambao wa Bahari yaHindi

73. Mheshimiwa Spika,   Tanzania imeendeleakuwa mwanachama wa mstari wa mbele katika

kuimarisha ushirikiano wa nchi zilizo katikamwambao wa Bahari ya Hindi kupitia Jumuiya

 ya Nchi hizo.

Mkutano wa Kwanza wa Mawaziri kuhusu‘Blue Economy’  

74. Mheshimiwa Spika,  Wizara ilishiriki

katika Mkutano wa Kwanza wa Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Mwambao wa Bahari yaHindi kuhusu Blue Economy   uliofanyika mweziSeptemba, 2015 nchini Mauritius. Mkutano huoulijadili maeneo manne ya kipaumbele kuhusumatumizi endelevu ya rasilimali zitokanazo nabahari. Maeneo hayo ni Fisheries andAquaculture ; Renewable Ocean Energy; Seaportand Shipping; na  Seabed Exploration andMinerals . Mkutano huo pia ulidhamiria kuundamifumo madhubuti yenye Sera, Sheria naMikakati ya Matumizi Endelevu ya Rasilimali zaBahari na kusimamia Dhana ya Uchumi wa

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 54/126

48 

Bahari ili kukuza uchumi na kuleta maendeleoendelevu kwa Nchi Wanachama.

75. Mheshimiwa Spika , katika kutekelezamaazimio ya mkutano huo, Mamlaka yaKusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu kwakushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi

 Tanzania inaendelea kufanya utafiti wakutambua maeneo yenye samaki wengi hususanaina ya Jodari pamoja na majaribio ya kuwekavifaa vya kuvutia samaki katika Bahari ya Hindi.Utafiti huu unaohusisha maeneo ya Mafia,Zanzibar na Bagamoyo unalenga kuwapunguziawavuvi muda wa kutafuta samaki, kupunguzagharama za mafuta na kuwaongezea kipato.Vilevile, taarifa za utafiti huo zitatolewa kwawawekezaji wa ndani na nje ya nchi ili wajekuwekeza katika uvuvi wa Bahari Kuu ya

 Tanzania.

Kulinda na kuendeleza Maslahi ya Taifa yaKiuchumi na Mengineyo nje ya nchi

Mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa

Mataifa

76. Mheshimiwa Spika,  Wizara iliratibu na

kushiriki kwenye Mkutano wa 70 wa Baraza

Kuu la Umoja wa Mataifa uliofanyika New York,

Marekani, mwezi Septemba, 2015 ambapo

Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 55/126

49 

wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa

 Tanzania alipata nafasi ya kulihutubia Baraza

hilo na kueleza msimamo wa nchi kwenye

masuala mbalimbali duniani, yakiwemo ya

kiuchumi na maendeleo, amani na usalama,

pamoja na mahusiano yetu na nchi nyingine.

Aidha, Mheshimiwa Kikwete alifanya

mazungumzo na nchi marafiki na washirika

wetu wa maendeleo na kukubaliana masuala

mbalimbali yenye manufaa kwa nchi ikiwemoufadhili wa miradi ya maendeleo.

Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali waJumuiya ya Madola

77. Mheshimiwa Spika,  Wizara iliratibu na

kushiriki kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchina Serikali wa Jumuiya ya Madola uliofanyika

Malta mwezi Novemba, 2015. Tanzania ilishiriki

kikamilifu kwenye majadiliano mbalimbali

 yaliyofanyika na hivyo tamko la mwisho ya

mkutano liliakisi maslahi ya nchi hususan

kwenye masuala ya amani na usalama; haki zabinadamu na utawala bora; maendeleo

endelevu; mabadiliko ya tabianchi; biashara na

usawa wa kijinsia na kumwezesha Mwanamke.

78. Mheshimiwa Spika ,  kwa mara yakwanza baada ya miaka 66, Jumuiya ya Madola

ilimchagua mwanamke mwenye asili ya Afrika,

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 56/126

50 

Mheshimiwa Baroness Patricia Scotland mzaliwawa Dominica na mwenye uraia pacha waDominica na Uingereza kuwa Katibu Mkuu wa

sita wa Jumuiya hiyo ambapo alianza kazitarehe 1 Aprili, 2016. Vipaumbele alivyoainishaMheshimiwa Scotland ni pamoja nakushughulikia unyanyasaji dhidi ya wanawakena watoto wa kike; athari za mabadiliko ya

 Tabianchi; biashara na utawala bora; nakuanzisha majadiliano na nchi wanachamakuhusu kutokufanya suala lamahusiano/mapenzi ya jinsia moja kuwa kosala jinai. Alisisitiza kuwa nchi haziwezikulazimishwa kufuata suala hili lakiniataanzisha majadiliano na lazima pawepo namakubalino ya pande zote. Wizara itaendelea

kufuatilia kwa makini ajenda zake ilikuhakikisha masuala ambayo yanapingana nasheria, mila na desturi za nchi yetu hayawisehemu ya majadilino ya Jumuiya.

Mkutano wa 10 wa Nchi Wanachama wa

Shirika la Biashara Duniani

79. Mheshimiwa Spika, Wizara pia iliratibuna kushiriki kwenye Mkutano wa 10 waMawaziri wa Nchi Wanachama wa Shirika laBiashara Duniani uliofanyika mwezi Desemba2015, Nairobi, Kenya. Katika Mkutano huo

 Tanzania ilitetea maslahi yake hasa kuhusumasuala ya biashara ya kilimo na mazao yake

ikiwemo pamba kwa kushirikiana na makundi

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 57/126

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 58/126

52 

Wachumi, Wahadhiri na Wakufunzi katikanyanja mbalimbali na pia wafanyabishara;ambao wote hawa wametawanyika sehemu

mbalimbali duniani.

81. Mheshimiwa Spika,  Wizara iliratibu nakushiriki katika Kongamano la Pili la Diasporalililofanyika Jijini Dar es Salaam mwezi Agosti,2015. Lengo la Kongamano hilo lilikuwa nikuhamasisha Diaspora kushiriki katika kukuzasekta ya biashara ndogondogo na za kati nakuboresha mahusiano kati ya Diaspora naWajasiriamali waliopo nchini. Aidha, Wizaraimeendelea kuratibu makongamano mengine yakibiashara na uwekezaji yanayofanyika nje yanchi kama yale yanayoandaliwa na Jumuiya ya

Watanzania wanaoishi nchini Marekani.

82. Mheshimiwa Spika,  Wizara iliratibuziara ya kitabibu ya Madaktari Watanzania kwakushirikiana na madaktari wenzao wa kiafrikawaishio nchini Marekani mwezi Julai 2015.Madaktari hao walitoa huduma za matibabu na

ushauri katika hospitali za Mwananyamala (Dares Salaam) na Mnazi Mmoja (Zanzibar) kwamagonjwa ya moyo, saratani na kinywa. Aidha,walitoa msaada wa madawa na vifaa tiba vyenyethamani ya Dola za Marekani 300,000 kwenyehospitali hizo na kukabidhi mashine ya kupimasaratani ya matiti yenye thamani ya Dola za

Marekani 200,000 katika Hospitali ya Lugalo.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 59/126

53

 

83. Mheshimiwa Spika,  naomba kutumianafasi hii kuwapongeza na kuwashukurumadaktari hao kwa moyo wao wa dhati wa

kujitolea. Aidha, ningependa kuwahamasishaDiaspora wengine kuiga mifano hiyo. Wizara

 yangu iko tayari kushirikiana nao wakati wote.

84. Mheshimiwa Spika,  napenda kuliarifuBunge lako Tukufu kuwa katika kuitikia wito wakuchangia maendeleo ya nchi yetu, uwekezajiwa Diaspora katika Benki ya CRDB, Mfuko waPensheni wa PSPF na Mfuko wa Mitaji wa UTTumefikia Shilingi Bilioni 26 mwaka 2015.Aidha, uwekezaji wa Diaspora katika mifukomingine ya hifadhi za jamii, sekta za afya,viwanda na utalii umeongezeka.

85. Mheshimiwa Spika,  katika kuhakikishakwamba tunaweka mazingira wezeshi kwaDiaspora, Wizara yangu imekamilisha hatua zaawali za kutengeneza Sera ya Diaspora kwaushirikiano na Mfuko wa Jumuiya ya Nchi zaAfrika, Karibiani na Pasifiki. Sera hii itatoa

mwongozo kwa wadau na kuleta uelewa wapamoja kuhusu mikakati bora ya kuwatambuaDiaspora na kuwawezesha kuchangiamaendeleo ya nchi. Rasimu ya Sera hiyoitawasilishwa kwa wadau kwa ajili ya maoni naushauri. Ni matarajio ya Serikali kuwaushirikishwaji wa Diaspora kama moja ya

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 60/126

54 

wadau wa maendeleo utawawezesha kuchangiakatika maendeleo ya nchi yetu kwa kuletateknolojia mpya; na kuongeza uwekezaji kwenye

sekta mbalimbali kama vile viwanda, masoko yamitaji, kilimo na utalii. Ushirikishwaji huo waDiaspora utaiwezesha nchi kufikia malengo yakuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

86. Mheshimiwa Spika,  Wizara kwakushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania na

wadau wengine inaandaa mfumo sahihi wakutambua na kurahisisha uingiaji wa fedhakutoka kwa Diaspora ili kuwa na takwimusahihi za mchango wa Diaspora kwenyekuongeza Pato la Taifa.

Kusimamia masuala yanayohusu Kinga naHaki za Kibalozi kwa Wanadiplomasia walioponchini kulingana na Mkataba wa Vienna wamwaka 1961

87. Mheshimiwa Spika,  Wizara imeendeleakushirikiana na mamlaka mbalimbali nchini ili

kuhakikisha kuwa, jamii ya wanadiplomasiawaliopo nchini wanapata haki zao kamailivyoainishwa katika Mkataba wa ViennaKuhusu Mahusiano ya Kidiplomasia wa mwaka1961. Wizara inasimamia kikamilifu utekelezajiwa Mkataba huo kwenye vipengele muhimu vyakinga na haki za kibalozi na wategemezi wao.

Pamoja na jamii ya kibalozi kuwa na kinga na

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 61/126

55 

upendeleo maalum, Wizara inahakikisha kuwa jamii hizi zinaheshimu na kufuata sheria,kanuni na taratibu za nchi yetu.

Kusimamia na Kuratibu Masuala ya Itifaki naUwakilishi

88. Mheshimiwa Spika,  mara baada yakuundwa kwa Serikali ya Awamu ya Tano,nilikutana na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika

 ya Kimataifa waliopo nchini. Kwa niaba yaMheshimiwa Rais, nilitumia fursa hiyokuwapatia taarifa ya masuala mbalimbali

 yanayohusu umuhimu wa ushirikiano wa Tanzania na nchi nyingine na kutoa Dira yaSerikali ya Awamu ya Tano. Wizara yanguitaendelea kuwa na vikao vya mara kwa mara nawanadiplomasia hawa kwa lengo la kuimarishazaidi ushirikiano.

89. Mheshimiwa Spika,  Wizara iliratibuziara za Viongozi wa Kitaifa wa Awamu ya Nnenje ya nchi ambao ni Rais wa Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais waZanzibar na Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi, Waziri Mkuu wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Makamu wa Kwanzawa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibarna Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya

Mapinduzi ya Zanzibar. Baadhi ya ziara za

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 62/126

56 

Viongozi hao zilifanywa katika nchi za Uswisi,Australia, Marekani, Misri, India, Kenya,Uganda, Botswana, Vietnam, Uingereza na

Italia. Vilevile, Wizara iliratibu ziara za Viongoziwa Kitaifa wa Awamu ya Tano nje ya nchizilizofanyika katika nchi za Afrika Kusini,Botswana, Ethiopia, Rwanda, Uganda, UingerezaZambia, Comoro na Papua New Guinea.

90. Mheshimiwa Spika, ziara hizo zimekuwana mafanikio ikiwa ni pamoja na kukuza nakuimarisha mahusiano kati ya nchi yetu na nchihizo, zimetangaza fursa za uwekezaji, biashara,utalii na kuwahamasisha Diaspora kuwekezanyumbani. Pia zinaimarisha uhusiano kati yasekta binafsi za hapa nchini na taasisi

mbalimbali za nje.

91. Mheshimiwa Spika,  Wizara imeendeleakuratibu na kufanikisha uwasilishaji wa hati zautambulisho za Mabalozi kutoka nchimbalimbali. Katika kipindi hiki Mabaloziwaliowasilisha hati zao za utambulisho ni

pamoja na Qutar, Argentina, India, Denmark,Uswisi, Uturuki, Finland, Sweeden, Ubelgiji,Hispania, Msumbiji, Uganda, Misri, Israeli,Ufilipino, Jamhuri ya Korea, Umoja wa Ulaya,Palestina, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,

 Jamhuri ya Namibia, Brazil, Jamhuri ya Czechna Jamhuri ya Sudan Kusini. 

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 63/126

57 

Kuanzisha na Kusimamia Huduma za

Kikonseli

92. Mheshimiwa Spika,  Wizara imeendeleakutoa huduma za kikonseli kwa kurahisishaupatikanaji wa viza kwa maafisa na watendajiwa Serikali, Vyama vya Siasa na Taasisinyingine zinazostahili huduma hiyo. Aidha,Wizara imeendelea kuratibu matumizi yaUkumbi wa Watu Mashuhuri wa Uwanja wa

Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, kwawatu wanaostahili wakiwemo Mabalozi naWakuu wa Mashirika ya Kimataifa, viongozi waSerikali na baadhi ya Wafanyabiashara hapanchini. Vilevile, Balozi zetu nje zimeendeleakutoa Viza kwa raia wa nje wanaoitembelea

 Tanzania na kushirikiana na mamlaka nyinginekutafuta ufumbuzi wa matatizo mbalimbali

 yanayowakabili Watanzania waishio nje ya nchi. 

93. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea 

kulinda maslahi ya Watanzania wanaofanya kazikwenye Balozi mbalimbali na Mashirika ya

Kimataifa hapa nchini. Katika kutekeleza jukumu hilo, Wizara yangu imebaini kuwepokwa changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi yaWatanzania wanaofanya kazi katika Balozi namashirika hayo kutokuwa na mikataba ya ajira.Hivyo, natoa rai kwa ofisi za Kibalozi naMashirika ya Kimataifa yaliyopo hapa nchini

kutoa mikataba kwa waajiriwa wao ili kukidhi

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 64/126

58 

matakwa ya kisheria. Vilevile, nawaasaWatanzania wanaofanya kazi katika Balozi naMashirika ya Kimataifa wahakikishe wana

mikataba ya ajira ili kulinda maslahi yao.

94. Mheshimiwa Spika,  Wizara imeendelea

kutoa huduma za kikonseli kwa Watanzaniawaliopo nje ya nchi. Naomba kutumia fursa hiikuwasihi Watanzania hao kuhakikishawanajisajili katika Balozi zetu na Konseli, napale ambapo hatuna ofisi za ubalozi wajisajilikatika ofisi za ubalozi wa Uingereza kamailivyoainishwa kwenye hati za kusafiria.

95. Mheshimiwa Spika,  niruhusu nitumie

fursa hii kuliarifu Bunge lako Tukufu naWatanzania kwa ujumla kwamba miaka yakaribuni pamejitokeza wimbi la Watanzaniawanaokwenda nje ya nchi kwa ahadi zakupatiwa ajira. Kwa upande wa India, Thailand,Malaysia na China, ahadi hizo za ajira zimekuwazikitolewa na watu wasio waaminifu ambaowana mtandao wa biashara ya kusafirisha

binadamu. Mtandao huo unahusisha raia wa Tanzania waliopo ndani na nje ya nchi kwakushirikiana na raia wa kigeni waliopo kwenyenchi hizo. Watu hao wanachofanya ni pamojana kuwatafuta wasichana wenye umri kati yamiaka 18 na 24, kuwatafutia vibali vya safari nakuwalipia nauli za kuwafikisha kwenye nchi

husika kwa kuwalaghai kuwa wanakwenda

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 65/126

59 

kufanya kazi katika hoteli, migahawa, madukamakubwa au kazi za nyumbani. Matokeo yake,wanapofika kwenye nchi hizo wasichana hao

wanakuta kuwa ahadi walizo ahidiwa sio zakweli na badala yake wanalazimishwa kukubalikufanya kazi za ukahaba ili kurejesha fedhawalizogharimiwa kufika huko. Kwa taarifatulizonazo, mtandao huo wa biashara yaukahaba huwataka wasichana hao kurejeshakiasi cha Dola za Marekani kati ya 5,000 hadi6,000 kiasi ambacho sio rahisi kupata kwa kazihizo ikizingatiwa kwamba mapatano na malipo

 ya kazi hiyo hayafanywi na wahusika balimadalali wa mtandao huo. Madalaliwaliowapeleka vijana hao kwenye nchi hizohuwanyang’anya hati zao za kusafiiria ilikuwadhibiti wasitoroke hadi kipatikane kiasicha fedha walizogharimwa. Kwa kuwa hawanafedha na namna nyingine ya kuishi wasichanahao wamelazimika kukubali kufanya biasharahiyo.

96. Mheshimiwa Spika,  baadhi ya vijana

hao, waliweza kuwatoroka madalali hao, nakukimbilia kwenye ofisi zetu za Ubalozi kutafutamsaada. Kwa bahati mbaya Mheshimiwa Spika,Balozi zetu hazina fungu la kuhudumiaWatanzania wanaopata shida ughaibuni namatokeo yake maafisa wa Ubalozi kwa moyo wakibinadamu wamekuwa wakitoa fedha zao

wenyewe kusaidia kununua tiketi za

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 66/126

60 

kuwarejesha Watanzania waliofanikiwakuchomoka kwenye makucha ya makuadi waukahaba. Katika jitihada za kukabiliana na

tatizo hilo, Wizara imeanzisha mazungumzo naShirika la Kimataifa la Uhamaji ili wasaidiekuwarudisha nyumbani vijana hao. 

97. Mheshimiwa Spika,  ni wazi kwambavitendo hivyo ni vya kinyama na vinakiuka haki

 ya binadamu. Ifahamike pia kwamba usafirishaji

wa binadamu ni uhalifu kwa mujibu wa makosa ya kupangwa ya Azimio la Umoja wa Mataifa NA.55/25 la mwaka 2003 la kuzuia, kukomesha nakuadhibu usafirishaji wa binadamu hasa kwawanawake na watoto chini ya Itifaki yake.

98. Mheshimiwa Spika, 

Kutokana naushirikiano kutoka kwa Jumuiya za Watanzaniawaishio nchini Thailand na India, pamoja nabaadhi ya wahanga wa biashara hiyo haramu,Serikali imepata majina ya baadhi ya wahusikawa mtandao huo na tayari mawasiliano naSerikali za nchi hizo yamefanyika ili

kuwakamata wahusika wote na kuwafikishakatika mkondo wa sheria. Kwa hapa nyumbani,uchunguzi unaendelea kwa kushirikiana naBalozi za nchi ambazo wasichana wetuwanapelekwa ili kubaini watu wote waliosehemu ya mtandao huo hususan walewanaowezesha upatikanaji wa vibali vya

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 67/126

61 

kusafiria kwenye Balozi hizo ili kuwakamata nakuwachukulia hatua kali za kisheria. Piatumeziomba Balozi hizo ziwe makini zaidi

kudhibiti uombaji wa vibali vya kusafiria kwashughuli mbalimbali na kuwataka wahusikakuthibitisha uwezo wa kifedha zitakazowawezesha kutalii, kufanya shughuli ama kuishikatika nchi wanazokwenda ili kuudhibitimtandao wa biashara ya watu. 

99. Mheshimiwa Spika,  Vilevile, kupitiaBunge hili, ninatoa wito kwa Watanzania wote,tuwe makini pale tunapopata fursa za kazi nje

 ya nchi. Kama nilivyosema hapo awali, nimuhimu kuzingatia na kujiridhisha na masuala

 yote ya msingi yanayohusiana na ajira za nje,

ikiwa ni pamoja na; kuwepo na mkataba rasmiwa ajira unaotambuliwa na Mamlaka husikazilizopo nchini na za Nchi unayotaka kwenda,kujisajili kweye ofisi za Ubalozi wa Tanzaniauliopo katika nchi hizo na kutokubali kuwekahati yako ya kusafiria kama rehani. 

100. Mheshimiwa Spika , nasikitika kuliarifuBunge lako Tukufu kuwa bado kunaWatanzania kadhaa wanatumikia vifungo nawengine kati yao wanakabiliwa na adhabu yakifo katika magereza ya nchi mbalimbali dunianibaada ya kukutwa na hatia ya makosa yakujihusisha na biashara haramu ya madawa ya

kulevya. Idadi yao ni kama ifuatavyo: Brazil (41),

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 68/126

62 

China (266), Iran (68), India (9), Nepal (4), Oman(3), Thailand (14) na Umoja wa Falme za Kiarabu(3). Naomba kuchukua nafasi hii kuwasihi

Watanzania kujiepusha na biashara hiyo kwakuwa hasara zake ni kubwa kwa familia zao na

 Taifa kwa ujumla.

Kuratibu shughuli za Tume za Pamoja za

Kudumu za Ushirikiano

101. Mheshimiwa Spika , Wizaraimeendelea kuratibu Mikutano ya Tume zaPamoja za Kudumu za Ushirikiano ambazokimsingi hutoa fursa kwa nchi zetu kujadilianakwa kina kuhusu masuala muhimu katikanyanja zote za mahusiano na kuweka mikakati

 ya pamoja ya maendeleo.

102. Mheshimiwa Spika , mwezi Februari2016, Wizara ilifanya kikao cha Tume ya Pamoja

 ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania naZambia kilichofanyika hapa nchini. Katika kikaohicho, pande zote mbili zilikubaliana kuimarisha

ushirikiano katika masuala ya Ulinzi naUsalama Mipakani; kuanzisha Mashauriano yaKidiplomasia; Kupunguza Msongamano wamagari katika mpaka wa Tunduma/Nakonde;na kuanzisha majadiliano ya kutotoza kodi marambili kwenye bidhaa zinazotoka na kuingiakatika nchi hizo.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 69/126

63 

103. Mheshimiwa Spika , Vilevile, mweziAprili 2016, Wizara iliratibu na kushiriki kwenyeKikao kingine cha Tume ya Pamoja ya Kudumu

 ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwandakilichofanyika Mjini Gisenyi, Rwanda. Katikakikao hicho nchi hizi zimekubalianakushirikiana katika kukamilisha mapema ujenziwa miundombinu ya ushoroba wa kati kama vileujenzi wa reli ya kati katika kiwango chakimataifa kwa kushirikiana na wadau, kukuzaushirikiano katika sekta ya anga hususan baina

 ya Shirika la Ndege la Rwanda na Shirika laNdege la Tanzania, kuimarisha ushirikianokatika sekta za sayansi na teknolojia, afya,kilimo, ufugaji, utalii na elimu. Mkutano huoumezidi kuimarisha urafiki na ushirikiano kati

 ya Tanzania na Rwanda kufuatia ziara yakirafiki ya Mheshimiwa Dkt. John PombeMagufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

 Tanzania nchini Rwanda mwezi Aprili, 2016.

104. Mheshimiwa Spika, Wizara imeratibuna kushiriki vikao vya Ujirani Mwema kati ya

 Tanzania na nchi za Msumbiji, Uganda naZambia. Vikao hivyo ni muhimu katika kukuzamahusiano katika sekta mbalimbali kati ya

 Tanzania na nchi husika. Aidha, Vikao hivyovinasaidia kutatua matatizo mengi ya mpakanina kurasimisha biashara baina ya nchi yetu nanchi tunazoshirikiana nazo.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 70/126

64 

Kusimamia utawala na Maendeleo yaUtumishi Wizarani na kwenye Balozi zetu

105. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hikiWizara iliajiri watumishi 42, ambapo maafisa 30kati ya hao walipelekwa katika mafunzo maalum

 ya Jeshi la Kujenga Taifa yenye lengo lakuwajengea uwezo, uadilifu na uzalendo katikakazi; mtumishi mmoja alibadilishwa kada;iliwapandisha vyeo watumishi 59; nailiwathibitisha kazini watumishi 15. Aidha,napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa,katika kipindi hiki ulifanyika uteuzi wa mabalozikuiwakilisha nchi yetu katika nchi za Uholanzi,Malawi, Kuwait, Japan, Uingereza na Zimbabwe.Vilevile, Wizara imejaza nafasi za Wakurugenzi

zilizokuwa wazi.106. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea

kutekeleza mpango wa mafunzo wa miakamitatu 2013/2014 - 2015/2016. Katika kipindihiki jumla ya watumishi 43 walihudhuriamafunzo ndani na nje ya nchi. Kati ya hao,Watumishi 24 walihudhuria mafunzo ya muda

mrefu na watumishi 19 walihudhuria mafunzo ya muda mfupi. Wizara imeshaanza kuandaampango mwingine wa mafunzo wa miaka mitatuambao utaanza kutekelezwa kuanzia mwezi

 Julai 2016 baada ya mpango wa sasa kuishamuda wake mwezi Juni 2016.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 71/126

65 

107. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hikiWizara imewarejesha nyumbani Mabaloziwatano na watumishi tisa baada ya kustaafu na

wengine kumaliza muda wao wa kufanya kaziUbalozini. Aidha, Wizara iliwapeleka vituoniNaibu Mabalozi watatu na watumishi thelathini.Zoezi la kuwarudisha Mabalozi na watumishiwanaostaafu na wanaomaliza muda wao nakupeleka mbadala wao ni endelevu na Wizaraitaendelea kulitekeleza kadri inavyopata fedha.

TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA

108. Mheshimiwa Spika , Wizara yanguinasimamia taasisi tatu ambazo ni Chuo chaDiplomasia kilichopo Kurasini Jijini Dar es

Salaam, Mpango wa Kujitathmini KiutawalaBora Barani Afrika na Kituo cha Kimataifa chaMikutano cha Arusha, ambacho piakinasimamia Kituo cha Mikutano cha Kimataifacha Julius Nyerere kilichopo Dar es Salaam.

Chuo cha Diplomasia

109. Mheshimiwa Spika , Chuo kimeendeleakutekeleza majukumu yake ya kutoa mafunzo,kufanya tafiti, kutoa ushauri wa kitaaluma nakendesha kozi fupi kwenye nyanja za diplomasiana uhusiano wa kimataifa. Katika kutekeleza

 jukumu hilo, Chuo kimejizatiti katika kutimiza

na kutekeleza viwango vilivyowekwa na Baraza

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 72/126

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 73/126

67 

na vyanzo vyake mbalimbali vya mapatoikiwemo Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha

 Julius Nyerere kilichopo Dar es Salaam

ambacho kinatarajiwa kukusanya mapato yaShilingi 3,051,000,000.00.

113. Mheshimiwa Spika , Kituo kinategemeakukopa shilingi bilioni 2.4 kwa ajili ya miradi yamaendeleo ya ujenzi wa jengo la maonesho naupanuzi wa Hospitali. Miradi yoteinayotekelezwa imeombewa kibali cha Msajili waHazina.

114. Mheshimiwa Spika , Kituo kinaendeleakufanya taratibu za kuwezesha kujengwa kituomahsusi cha mikutano kitakachoitwa Kituo chaKimataifa cha Mikutano cha Mlima Kilimanjaro.

 Taarifa ya upembuzi yakinifu ya mradi wa ujenziwa Kituo hicho iliandaliwa na WataalamuWashauri kutoka Chuo Kikuu cha Dar esSalaam. Taarifa hiyo ilionyesha kwamba mradihuo ni muhimu na wenye manufaa kiuchumi nakijamii kwa taifa. Aidha, makadirio ya awali ya

ujenzi wa kituo hicho ni Dola za marekanimilioni 248. Kwa hivi sasa Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha kinaendelea namazungumzo na mifuko ya hifadhi ya jamiiiliyopo nchini ili iweze kushiriki katikakutekeleza mradi huo. Ni matarajio ya Wizarakuwa kuwepo kwa Kituo hicho kutakuwa

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 74/126

68 

suluhisho sahihi la mahitaji ya mikutano yakimataifa na maonesho hapa nchini. 

Mpango wa Kujitathmini Kiutawala BoraBarani Afrika

115. Mheshimiwa Spika ,  Wizaraimeendelea kuratibu utekelezaji wa Mpango waKujitathmini Kiutawala Bora Barani Afrika kwaupande wa Tanzania wenye lengo la kuzisaidianchi za Kiafrika kuhakikisha kuwa changamotozinageuzwa kuwa fursa za maendeleo na mambomazuri ya kuendelezwa kwa faida ya nchi

 yenyewe na hata kuwa mfano wa kuigwa nanchi nyingine. Mpango huo unaratibiwa kwamujibu wa miongozo ya Wakuu wa Nchi na

Serikali wa nchi za Afrika.

116. Mheshimiwa Spika, katika kipindi chamwaka wa fedha 2015/2016, Taasisi ya Mpangowa Kujitathmini Kiutawala Bora Barani Afrikakwa upande wa Tanzania imeendelea kutekelezashughuli zifuatazo:-

i. Kusimamia utekelezaji wa Mpango kazi

wa kuondoa changamoto za utawala bora

zilizobainishwa kwenye ripoti ya Mpango

wa Kujitathmini Kiutawala Bora Barani

Afrika kwa upande wa Tanzania. Taasisi

imeendelea kupokea na kuchambua

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 75/126

69

 

taarifa mbalimbali za utekelezaji kutoka

Wizara, Idara na Wakala wa Serikali

zilizoguswa na Ripoti ya Mpango wa

Kujitathmini Kiutawala Bora Barani

Afrika kwa upande wa Tanzania;

ii. Kuandaa taarifa ya utekelezaji ya mwaka

kuhusu hatua zilizochukuliwa ili kutatua

changamoto zilizojitokeza kwenye ripoti

 ya Mpango wa Kujitathmini KiutawalaBora Barani Afrika kwa upande wa

 Tanzania. Taarifa hiyo inatarajiwa

kuwasilishwa kwenye vikao vya Wakuu

wa Nchi za Kiafrika wanaoshiriki kwenye

mchakato wa Mpango wa Kujitathmini

Kiutawala Bora Barani Afrika;

iii. Kuendelea kutoa taarifa kwa wananchi

 juu ya matokeo ya tathmini ya utawala

bora kwa nchi yetu kupitia vyombo

mbalimbali vya habari na majukwaa

mengineyo; na

iv. Kutafsiri ripoti ya Mpango wa

Kujitathmini Kiutawala Bora Barani

Afrika kwa upande wa Tanzania katika

lugha ya Kiswahili na kuandaa chapisho

la muhtasari.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 76/126

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 77/126

71 

118. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wafedha 2015/2016 Wizara hiyo iliidhinishiwaShilingi 26,666,436,300.00. Kati ya fedha hizo,

Shilingi 24,047,468,300.00 ni kwa ajili yaMatumizi Mengineyo na Shilingi2,618,968,000.00 ni kwa ajili ya mishahara yawatumishi. Kiasi kilichotengwa kwa ajili yamatumizi mengineyo kimejumuisha mchangowa Tanzania katika Jumuiya ya AfrikaMashariki wa kiasi cha Shilingi18,570,055,300.00.

119. Mheshimiwa Spika,  hadi kufikiatarehe 30 Aprili 2016, Wizara ilipokea jumla yaShilingi 19,003,440,860.00, sawa na asilimia71.26 ya fedha zote zilizotengwa. Kati ya fedhahizo Shilingi 15,506,375,000  zilitumika kulipamchango wa Tanzania kwenye Jumuiya yaAfrika Mashariki, Shilingi 1,689,936,160.00zilitumika kulipa mishahara ya watumishi naShilingi 1,807,129,700.00 zilitumika kutekelezashughuli za Wizara.

Kusimamia na kuratibu utekelezaji waMkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki naItifaki zake

120. Mheshimiwa Spika,  kamaunavyofahamu Mtangamano wa Jumuiya yaAfrika Mashariki umepiga hatua kubwa ambapo

Nchi wanachama wa Jumuiya zimefikia

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 78/126

72 

makubaliano na kuendelea kuyatekelezamakubaliano hayo kwenye nyanja zote zakiuchumu, kijamii, kiutamaduni na kwa kiasi

fulani kisiasa pia na hivyo kutufanya tusilale nakutakiwa kuwa makini katika kila hatuatunazopiga. Itakumbukwa kuwa Jumuiya yetuilianzishwa rasmi Julai 2000 baada ya NchiWanachama kukamilisha kuridhia Mkataba waUanzishaji wa Jumuiya ya Afrika Masharikiuliotiwa saini na Wakuu wa Nchi Wanachama

tarehe 30 Novemba, 1999. Aidha, hivi sasa Nchizote Wanachama zinatekeleza Mkataba huu naItifaki zake kubwa tatu (3) na zile mbalimbali zakisekta. Maeneo yaliyobaki ambayo tunaendeleana majadiliano ni Umoja wa Fedha na Shirikishola Kisiasa.

121. Mheshimiwa Spika,  juhudi hizi sasazinamaanisha kuwa eneo lote la nchi sita (6) za

 Jumuiya ya Afrika Mashariki kimsingilimeungana katika nyanja mbalimbali na hivyokutoa motisha ya ushindani mkubwa wa ndani

 ya Jumuiya kiuchumi na kimaendeleo. Kwa

kutambua kuwa Tanzania ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitia Wizara yangu ameelekeza Wimbo na Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki zitumike hapa

nchini.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 79/126

73

 

122. Mheshimiwa Spika,  napendakuchukua nafasi hii kupitia Bunge lako Tukufukutoa wito wa kuongezwa kwa matumizi ya

Bendera ya Jumuiya ya Afrika Masharikikwenye Ofisi zote za Umma nchini zikiwemo zaSerikali Kuu, Serikali za Mitaa na Taasisi zaUmma (tukiwemo sisi Waheshimiwa Wabungekwenye Magari yetu na ofisi zetu Majimboni) nazile za sekta binafsi sambamba na Bendera ya

 Taifa letu Tukufu. Aidha, natoa rai kwa Taasisiza Serikali na vyombo vya habari viwezekuutumia Wimbo wa Jumuiya ya AfrikaMashariki pale ambapo Wimbo wa Taifa letu

 Tukufu unapigwa.

123. Mheshimiwa Spika,  ni imani yangu

kuwa hatua hii itasaidia kuwajengeaWatanzania uelewa, kuifahamu vyema Jumuiya yetu na hatimae waweze kujiandaa, kushiriki nakupata manufaa yanayoendana na fursa zilizopokibiashara, kiuchumi, kiuzalishaji, kijamii nakiutamaduni kwa kuzingatia uwepo wa Sokokubwa la Afrika Mashariki na fursa zinginezo.

124. Mheshimiwa Spika,  wito huu ni moja ya utekelezaji wa Mkakati wetu wa mawasilianowa Wizara ambao unalenga kuwapa fursaWananchi wetu ya kujiandaa, kuiendesha,kuitumia Jumuiya yao na kutimiza matakwa yaIbara ya 7(a) ya Mkataba wa Uanzishaji wa

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 80/126

74 

 Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo inasisitizakuwa “Jumuiya yetu hii imejengwa katikaWananchi na ushirikiano wa kimasoko”. Aidha,

hatua hizi zinalenga katika kuendeleza juhudiza Mheshimiwa Dkt. John Pombe JosephMagufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

 Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuhakikisha kuwa Jumuiya hii inakuwa kweli ni Jumuiya yaWananchi wetu, kutambua uwepo wake nawanufaike nayo katika kubadilisha maisha yao.

Mkutano wa 17 wa Viongozi Wakuu wa NchiWanachama na Mikutano ya 32 na 33 yaBaraza la Mawaziri la Jumuiya ya AfrikaMashariki

125. Mheshimiwa Spika,  katika kipindihiki Wizara iliratibu na kushiriki katikaMkutano wa 17 wa Wakuu wa NchiWanachama wa Jumuiya ya Afrika Masharikiuliofanyika mwezi Machi 2016 Jijini Arusha,

 Tanzania. Katika Mkutano huo Tanzania

iliteuliwa kwa mara ya pili mfululizo kuwaMwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Masharikihadi mwezi Novemba 2016. Aidha, Mkutanohuo uliridhia Jamhuri ya Sudan Kusinikujiunga na Jumuiya ya Afrika Masharikiambapo tarehe 15 Aprili, 2016 nchi hiyo ilisainiMkataba wa Kujiunga na Jumuiya hiyo.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 81/126

75 

126. Mheshimiwa Spika, kadhalika, katikamkutano huo Wakuu wa Nchi walizindua rasmiPasi mpya ya kielektroniki ya Kusafiria ya

 Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuelekezamatumizi ya hati hii mpya kuanza rasmi tarehe1 Januari, 2017. Pasi hii inaipandisha hadhiPasi ya sasa ya Afrika Mashariki kutumikakusafiria nje ya Afrika Mashariki. NchiWanachama zimekubaliana kuziondoa hati zakusafiria zilizopo sasa katika kipindi cha miezi

24 kuanzia tarehe 1 Januari, 2017 hadi tarehe31 Desemba, 2018. Hati hizo zitakuwa naalama za jumla za kiusalama na kila NchiMwanachama imeruhusiwa kuongeza alamazake za kiusalama katika Pasi hizo. Idara zaUhamiaji katika nchi wanachama zitaendeleana jukumu la utoaji wa hati hizo kwa raia wanchi zao.

127.  Mheshimiwa Spika, Mkutano wa 32wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya AfrikaMashariki ulifanyika tarehe 14 Agosti, 2015 nakufikia maamuzi mbalimbali ikiwa ni pamojana kuidhinisha ajira kwa Mwanasheria Mkuu

wa Jumuiya, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakalawa Usalama wa Anga na Mkurugenzi waMipango katika Jumuiya.

Umoja wa Forodha

128. Mheshimiwa Spika,  Wizara imeendelea

kuratibu utekelezaji wa hatua ya kwanza ya

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 82/126

76 

Mtangamano ambayo ni Umoja wa Forodha waAfrika Mashariki kama ifuatavyo: 

Kanuni Mpya za Utambuzi wa Uasili waBidhaa

129. Mheshimiwa Spika , katikakuziwezesha Nchi Wanachama wa Jumuiya yaAfrika Mashariki kunufaika zaidi na hatua hii yaUmoja wa Forodha, mabadiliko yamefanywa

katika kanuni za utambuzi wa uasili wa bidhaa.Katika mabadiliko hayo, Nchi Wanachamazimeacha kutumia vigezo sawa kwa bidhaa zote,na sasa zitatumia vigezo tofauti kulingana nabidhaa husika. Mabadiliko haya ni fursa kubwakwa viwanda vya Tanzania ambavyo vingi badoni vidogo na vilikuwa haviwezi kufikia vigezo vya

uasili wa bidhaa. Aidha, katika kipindi hiki, nchiWanachama wa Jumuiya zilikamilishamwongozo wa kutumika katika kurahisishautekelezaji wa kanuni hizo.

Uondoaji wa Vikwazo Visivyo vya Kiforodha

130. Mheshimiwa Spika,  katika kuwekamazingira wezeshi ya biashara katika Jumuiya,Wizara imeendelea kuratibu uondoaji waVikwazo Visivyo vya Kiforodha kupitia Kamati yaKitaifa na Kikanda ya uondoaji wa vikwazohivyo. Katika mwaka wa fedha 2015/2016vikwazo 16 viliripotiwa vimeondolewa, kati ya

hivyo vinne (4) viliihusu Tanzania. Vikwazo

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 83/126

77 

hivyo ni tozo ya Dola za Marekani 200 kwa kilakontena la kemikali; kutopewa upendeleo waushuru wa forodha kwa chumvi na bidhaa za

plastiki kutoka Kenya; na upimaji wa malorimatupu.

131. Mheshimiwa Spika , ili kuharakishauondoaji wa vikwazo visivyo vya kiforodha,Wizara imekuwa na utaratibu wa kuitishamikutano ya pande mbili husika. Katika kipindi

hiki Wizara ilifanya mikutano na Kenya naBurundi ambayo ilichangia kuharakishauondoaji wa vikwazo visivyo vya kiforodhavikiwemo vile vilivyotajwa hapo juu. Vilevile,tumekubaliana na Kenya kufanya utafiti juu yatozo zinazotozwa na mamlaka za Serikali zamitaa za nchi zetu zinazoathiri biashara baina

 yetu kwa lengo la kurazinisha tozo hizo.

Mwenendo wa Biashara ya Bidhaa kati yaTanzania na Nchi Wanachama wa Jumuiya yaAfrika Mashariki

132. Mheshimiwa Spika,  nafasi ya Tanzania katika Soko la Jumuiya imeendeleakupanda kutoka asilimia 18 mwaka 2010 hadiasilimia 26 mwaka 2014 na tunategemeakufanya vizuri zaidi kutokana na juhudizinazoendelea za kudhibiti ulanguzi wa mazaona bidhaa mipakani, utekelezaji wa sheria mpya

 ya uasili wa bidhaa, kuondoa vikwazo visivyo

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 84/126

78 

vya kiforodha na kuimarisha uzalishajiviwandani. Kwa mujibu wa Taarifa ya Biashara

 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka

2014, biashara ndani ya Jumuiya imekua nakufikia Dola za Marekani bilioni 5.63 kwamwaka 2014 ikilinganishwa na Dola zaMarekani bilioni 3.72 kwa mwaka 2010. Aidha,biashara baina ya Tanzania na NchiWanachama imeendelea kuimarika nakuongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni0.69 mwaka 2010 na kufikia Dola za Marekanibilioni 1.49 mwaka 2014. Kwa mwaka 2013kiwango cha biashara kiliongezeka zaidikulingana na hali ya mahitaji ya soko nakupanda kwa uzalishaji kwenye sektambalimbali. Tanzania imeendelea kuwa na urarichanya wa biashara katika Jumuiya ya AfrikaMashariki kama inavyoonekana katikaKiambatisho Na. 1.

133. Mheshimiwa Spika,  wafanyabiasharawa Tanzania wamendelea kuchangamkia fursazitokanazo na Umoja wa Forodha wa Afrika

Mashariki. Wafanyabiashara hao wamefanikiwakuuza kwa wingi katika Soko la AfrikaMashariki bidhaa za viwandani kama viletransfoma, waya za umeme, vyandarua, sarujina magunia; na bidhaa za kilimo kama vilemahindi, mchele, katani, mbogamboga, asali nachakula cha mifugo. Hii inaashiria kuendelea

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 85/126

79 

kuimarika kwa biashara ya bidhaa za viwandanina mazao ya kilimo.

134. Mheshimiwa Spika,  bidhaazilizonunuliwa kwa wingi kutoka NchiWanachama ni pamoja na kemikali kwa ajili yaviwanda vya nguo, vipodozi na sabuni; dawa zabinadamu na mifugo; vipuri vya magari; vifunikovya chupa za vinywaji; sabuni; vifaa vyakufanyia usafi; vifungashio; mabanda maalum

 ya kilimo cha mbogamboga na maua (greenhouse); na vyumba vya baridi kwa ajili yakuhifadhia bidhaa mbalimbali.

Umoja wa Fedha

135. Mheshimiwa Spika,  NchiWanachama wa Jumuiya ya Afrika Masharikizimeendelea kutekeleza Mpangokazi  wa MiakaKumi wa Kuelekea katika Eneo la Sarafu Mojaulioanza kutekelezwa mwaka 2014 nautakaokamilika mwaka 2024. Katika kutekelezaMpangokazi huo, Nchi Wanachama

zimekamilisha majadiliano ya Muswada waSheria ya uanzishwaji wa Taasisi ya Fedha yaAfrika Mashariki na Taasisi ya Takwimu yaAfrika Mashariki. Maandalizi ya majadiliano yamuswada wa Kamisheni ya Ufuatiliaji naUsimamizi ya Afrika Mashariki yataanza katikakipindi hiki cha mwaka wa fedha.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 86/126

80 

136. Mheshimiwa Spika,  matarajio yaNchi Wanachama wa Jumuiya ya AfrikaMashariki ni kuifikia hatua hii muhimu ya

kuanzisha matumizi ya sarafu moja kwenyeeneo la Jumuiya ifikapo mwaka 2024. Hatua hiiitafikiwa mara baada ya Nchi Wanachamaangalau watatu (3) kufikia vigezo vya kiuchumivilivyoainishwa kwenye Itifaki ya Umoja waFedha. Aidha, hatua hiyo itatanguliwa nauanzishwaji wa Benki Kuu ya Afrika Masharikiambayo pamoja na majukumu mengine itakuwana majukumu ya kuchapisha na kusambazasarafu hiyo ya Afrika Mashariki.

Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki

137. Mheshimiwa Spika,  Shirikisho la

Kisiasa ni hatua ya nne na ya mwisho katikamtangamano wa Afrika Mashariki ambayoinategemea sana misingi imara itokanayo nautekelezaji wa hatua za mwanzo zamtangamano. Katika kipindi cha mwaka fedha2015/2016, Nchi Wanachama ziliendelea namajadiliano ya modeli ya shirikisho ambayoitatumika katika kuandaa Rasimu ya Katiba yaShirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki.

138. Mheshimiwa Spika, rasimu hiyo,

inatarajiwa kutumika katika kuelimisha na

kuhamasisha wananchi wa Afrika Mashariki

kuhusu aina ya Shirikisho linalotarajiwa

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 87/126

81 

kuundwa ili kuleta uelewa wa pamoja na

uungwaji mkono wa hatua hiyo wakati ukifika.

Aidha, kwa kuwa Shirikisho la Kisiasa ni

mchakato, Nchi Wanachama zimeendelea na

utekelezaji wa shughuli zinazounda msingi wa

Shirikisho hilo ikiwemo masuala ya utawala

bora, uimarishaji wa demokrasia na utawala wa

sheria.

Ushirikiano na Kanda nyingine za Kiuchumi

Majadiliano ya Kuanzisha Eneo Huru laBiashara la Utatu wa Soko la Pamoja laMashariki na Kusini mwa Afrika, Jumuiya yaAfrika Mashariki na Jumuiya ya MaendeleoKusini mwa Afrika

139.  Mheshimiwa Spika,  juhudi za

kuziunganisha Jumuiya za COMESA, EAC na

SADC ili kuwa eneo moja huru la kibiashara

zimefika hatua nzuri. Mkutano wa Tatu wa

Wakuu wa Nchi za COMESA, EAC na SADCuliofanyika tarehe 10 Juni, 2015 Jijini Sharm El

Sheikh, Misri ulihitimishwa kwa Wakuu wa Nchi

na Serikali kutia saini Azimio la Uanzishwaji wa

Eneo Huru la Biashara; na Mkataba wa

Uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 88/126

82 

140. Mheshimiwa Spika,  kufuatia

kusainiwa kwa mkataba huo, Viongozi Wakuu

wa Nchi Wanachama wa Jumuiya hizo

walikubaliana kukamilisha majadiliano ya

maeneo yaliyosalia katika kipindi cha miezi 6

hadi 12 baada ya uzinduzi rasmi wa eneo huru

la biashara. Maeneo hayo ni uondoshwaji wa

kodi kwenye bidhaa, utambuzi wa uasili wa

bidhaa, usuluhishi wa migogoro ya kibiashara

na kupunguziana ushuru.

Majadiliano ya Uhuru wa Wafanyabiasharakusafiri katika Eneo la Utatu

141. Mheshimiwa Spika,  ili kurahisisha

na kuwezesha wafanyabiashara kusafiri katikaEneo hilo la Utatu, Nchi Wanachamazimeendelea na majadiliano ya kuandaaMkataba wa Uhuru wa Wafanyabiasharakusafiri kwenye eneo hilo. Mkataba huounatarajiwa kuidhinishwa ifikapo Desemba,2016. 

Majadiliano ya Uendelezaji wa Viwanda katikaEneo la Utatu

142. Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibuushiriki wa Tanzania katika kukamilishaRasimu ya Mpango wa Maeneo ya Ushirikianokatika Maendeleo ya Viwanda; na Mpangokazi

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 89/126

83 

kwa ajili ya Utekelezaji wa utaratibu waUshirikiano katika eneo la Utatu.  Maeneo

 yaliyoboreshwa ni Sera na Mikakati kutoka

Kanda zote tatu; Uzingatiaji wa uendelezaji waviwanda unaojali utunzaji wa mazingira; naUtambuaji Kisheria na Umiliki wa Hakizinazotokana na Uvumbuzi na Ubunifu katikamaendeleo ya Viwanda. Aidha, Nchi Wanachamazimekubaliana kushirikiana katika maeneo yauratibu na uhamasishaji wa pamoja wa sera ya

maendeleo ya viwanda na uongezaji thamanibidhaa baina ya nchi Wanachama; naUendelezaji wa Viwanda Vidogo na vya Kati nakujenga uwezo wa utaalam katika kuendelezaViwanda.

Ubia wa Kiuchumi kati ya Nchi za Jumuiya yaAfrika Mashariki na Umoja wa Ulaya

143. Mheshimiwa Spika,  Wizaraimeendelea kuratibu majadiliano ya Mkataba waUbia wa Kiuchumi baina ya Nchi za Jumuiya yaAfrika Mashariki na Umoja wa Ulaya. Malengo

 ya ubia huu ni kuimarisha ushirikiano wakikanda, kuleta maendeleo endelevu nakuziwezesha nchi za Afrika, Karibiani naPasifiki kupata misaada ya kimaendeleo ilikukabiliana na changamoto za uzalishaji nakuweka muda wa kuondoa vikwazo vyabiashara.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 90/126

84 

144. Mheshimiwa Spika , nchi za Jumuiya

 ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya

zilikamilisha mapitio ya kisheria ya Mkataba wa

Ubia wa Kiuchumi baina ya nchi hizo. Hatua

inayoendelea ni Nchi za Jumuiya ya Afrika

Mashariki kutafsiri mkataba huo katika lugha

 ya Kiswahili wakati Umoja wa Ulaya unatafsiri

mkataba huo katika lugha 21 zinazotumiwa na

 Jumuiya ya Ulaya. Baada ya kukamilika kwa

mchakato wa kufanya tafsiri, Nchi Wanachamawa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa

Ulaya zitasaini Mkataba huo, pamoja na

kuuridhia ili utekelezaji wake uanze.

145. Mheshimiwa Spika, ili kuweka

mazingira wezeshi ya kukuza na kuendelezaviwanda vya nguo na ngozi ndani ya Jumuiya,

Mkutano wa 17 wa Wakuu wa Nchi Wanachama

ulielekeza Nchi Wanachama kuhakikisha

zinapunguza uingizaji wa nguo na viatu

vilivyotumika kutoka nje ya Jumuiya na

kusitisha uagizaji wake katika kipindi chamiaka mitatu kuanzia mwaka huu wa fedha.

Aidha, Wakuu wa Nchi walielekeza Nchi

wanachama kupiga marufuku utaratibu wa

kuuza ngozi na bidhaa za ngozi ghafi nje ya

 Jumuiya ya Afrika Mashariki.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 91/126

85 

Kujengea uwezo na upatikanaji wa masokokwa Wajasiriamali wadogo

146. Mheshimiwa Spika, Maonesho ya 16 ya Juakali/Nguvukazi yaliyofanyika tarehe 30Novemba hadi 6 Disemba 2015 katika Viwanjavya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam katikamaonesho hayo jumla ya wajasiriamali 734kutoka Nchi zote wanachama walishiriki. Kati yahao, wajasiriamali 395 walikuwa ni washiriki

kutoka Tanzania. Lengo la maonesho hayo nikujenga uwezo wa wafanyabiashara wadogokupata masoko ya bidhaa zao katika NchiWanachama. Napenda kutoa rai kwawajasiriamali wa Tanzania kushiriki katikaMaonesho ya 17 ya Juakali/Nguvukazi

 yaliyopangwa kufanyika mwezi Novemba 2016

nchini Kenya.

Uendelezaji wa Miundombinu ya Kiuchumi

147. Mheshimiwa Spika, Wizaraimeendelea kuratibu utekelezaji wa programu na

miradi ya kitaifa yenye sura ya Kikandailiyoainishwa katika Mipango ya Jumuiya yaAfrika Mashariki ya Uendelezaji waMiundombinu ya Kiuchumi. Hatua zilizofikiwakatika uendelezaji wa programu na miradi hiyoni kama ifuatavyo:

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 92/126

86 

Ujenzi wa Vituo vya Kutoa Huduma kwaPamoja Mipakani 

148. Mheshimiwa Spika , Wizaraimeendelea kuratibu ujenzi wa vituo vya kutoahuduma kwa pamoja mipakani. Hadi sasa vituoviwili (2) kati ya saba (7) vinavyojengwa kwauratibu wa Jumuiya ya Afrika Masharikivimekamilika na kuzinduliwa. Vituo hivyo nikituo cha Holili/Taveta mpakani mwa Tanzania

na Kenya; na kituo cha Rusumo mpakani mwa Tanzania na Rwanda.

149. Mheshimiwa Spika , vilevile, Wizarailiratibu ukamilishaji wa Kanuni za Utekelezajiwa Sheria ya Jumuiya ya KusimamiaUendeshaji wa Vituo vya Kutoa Huduma kwaPamoja Mipakani. Kanuni hizo zimepitishwa naMkutano wa 33 wa Baraza la Mawaziri la

 Jumuiya uliofanyika mwezi Februari, 2016. Ilikupata uelewa wa pamoja kuhusu Vituo vyaKutoa Huduma kwa Pamoja Mipakani, Wizarailiratibu na kushiriki katika mafunzo kwa

maafisa wa Serikali, sekta binafsi nawawakilishi wa jamii kwa Vituo vya Horohoro naSirari. Taarifa kuhusu vituo vingine na hatuazilizofikiwa ili kuwezesha kuanza kutoa hudumastahiki ni kama inavyoonesha katikaKiambatisho Na. 2. 

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 93/126

87 

150. Mheshimiwa Spika,  Wizaraimeendelea kuratibu ukamilishaji wa ujenzi waDaraja la Kimataifa la Rusumo ikiwa ni sehemu

 ya kurahisisha usafirishaji wa bidhaa nakuimarisha vituo vya kutoa huduma za pamojamipakani katika ushoroba wa kati. Daraja hilolenye uwezo wa kupitisha magari manne kwawakati mmoja yenye uzito wa tani 56 kila mojalilizinduliwa rasmi na Mhe. Dkt. John Pombe

 Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na Mhe. Paul Kagame,Rais wa Jamhuri ya Rwanda tarehe 6 Aprili,2016.

Uendelezaji wa Mtandao wa Barabara 

151.Mheshimiwa Spika,

  hatua zilizofikiwakatika uendelezaji wa mtandao wa barabara zaKikanda katika mwaka 2015/2016 ni kamaifuatavyo:

Mradi wa Barabara ya Arusha – Holili/Taveta – Voi

152. Mheshimiwa Spika,  mradi huu

unahusu uendelezaji wa mtandao wa barabara

unaoziunganisha nchi za Tanzania na Kenya

kupitia mpaka wa Holili/Taveta yenye urefu wa

kilomita 234.3. Kwa upande wa Tanzania,

awamu ya kwanza ya ujenzi wa barabara hiyo

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 94/126

88 

kwa kiwango cha lami unahusisha upanuzi wa

sehemu ya kutoka Arusha hadi Tengeru yenye

urefu wa kilometa 14.1 kuwa njia nne na

barabara ya mzunguko wa kusini mwa Jiji la

Arusha yenye urefu wa kilometa 42.41. Aidha,

kwa upande wa Kenya mradi unahusisha ujenzi

wa barabara mpya ya lami yenye urefu wa

kilomita 100 kutoka Taveta hadi Mwatate.

Gharama za mradi kwa upande wa Tanzania ni

takriban Shilingi bilioni 209.61 ambapo kati yahizo Benki ya Maendeleo ya Afrika itatoa Shilingi

bilioni 190.21 na Serikali ya Tanzania itatoa

Shilingi bilioni 19.4.

153. Mheshimiwa Spika, Jiwe la Msingi la

Ujenzi wa Barabara hiyo liliwekwa mwezi Machi,2016 na Mheshimiwa Dkt. John PombeMagufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

 Tanzania na Mheshimiwa Uhuru MuigaiKenyatta, Rais wa Jamhuri ya Kenya.

Uwianishaji wa Uzito wa Magari Katika

Barabara

154. Mheshimiwa Spika,  Sheria yaUdhibiti wa Uzito wa Magari ya Mwaka 2013iliyopitishwa na Bunge la Afrika Masharikiimeridhiwa na Nchi zote Wanachama. NchiWanachama zimekamilisha majadiliano ya

kuandaa Kanuni za kuwezesha utekelezaji wa

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 95/126

89 

Sheria hizo ambazo zilipitishwa katika Mkutanowa 33 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiyauliofanyika Jijini Arusha mwezi Februari, 2016. 

Mkakati wa Kuwezesha Sekta ya Uchukuzi

155. Mheshimiwa Spika,  NchiWanachama wa Jumuiya ya Afrika Masharikizimeidhinisha utekelezaji wa Mkakati wa

Kuwezesha Sekta ya Uchukuzi. Mkakati huounazitaka Nchi Wanachama pamoja na masualamengine kuwianisha mitaala ya mafunzo yaudereva wa magari ya biashara; usajili wavyombo vya moto; na madaraja ya leseni. NchiWanachama zimekamilisha rasimu za mitaala yamafunzo ya udereva wa magari ya biashara. 

Sekta ya Mawasiliano

156. Mheshimiwa Spika,  Wizarainaendelea kuratibu utekelezaji wa Mpango waKutatua Changamoto ya Gharama Kubwa zaMaunganisho ya Simu za Mkononi katika Nchi

Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Masharikikama ulivyoridhiwa na Wakuu wa Nchi wa

 Jumuiya hiyo mwezi Februari, 2015. Katikakutekeleza mpango huo, yamefanyika mapitio yaKanuni zinazotumika katika mfumo wakuongoza sekta ya mawasiliano nchini. Wizara

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 96/126

90 

 ya kisekta inafanya tathmini ya changamotozilizoibuliwa na wadau kuhusu mpango huo.

Sekta ya Hali ya Hewa

157. Mheshimiwa Spika,  Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Ushirikianokatika Huduma za Hali ya Hewa ilisainiwa naMawaziri wanaosimamia masuala ya Jumuiya

 ya Afrika Mashariki kutoka Nchi Wanachamakatika Mkutano wa 33 wa Baraza la Mawaziri la

 Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika mweziFebruari, 2016. Itifaki hiyo inatoa mwongozowa ushirikiano wa Nchi Wanachama katikakubadilishana taarifa na ujuzi katika masuala

 ya hali ya hewa. Nchi Wanachamazimekubaliana kuridhia Itifaki hiyo kabla yamwezi Julai, 2016.

Sekta ya Bandari na Usafiri Majini

158. Mheshimiwa Spika,  katika jitihadaza kurahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa

katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, NchiWanachama zinaendelea na maandalizi yaMkakati wa Usafiri wa Majini wa AfrikaMashariki. Katika kutekeleza azma hiyo, Utafitiwa Awali wa Hali ya Usafiri wa Majini na Sekta

 ya Bandari umekamilika. Ripoti ya Utafiti huo,pamoja na mambo mengine, imebainisha

changamoto katika utekelezaji wa miradi ya

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 97/126

91 

kuendeleza Bandari katika mwambao wa Bahari ya Hindi, Maziwa na Uanzishaji wa BandariKavu. Changamoto hizo ni pamoja na uhaba wa

rasilimali fedha zinazohitajika katika kutekelezaMiradi iliyoainishwa katika Mipango Mikuu yakuendeleza Bandari za Nchi Wanachama nahaja ya kuwianisha Mifumo ya Kitaasisi naUdhibiti katika Sekta ya Usafiri wa Majinimiongoni mwa Nchi Wanachama ili kuwa naviwango vinavyofanana katika udhibiti wa

vyombo vya majini. Maoni ya Ripoti hiyo yatasaidia katika maandalizi ya Mkakati waAfrika Mashariki wa Usafiri wa Majini. 

Sekta ya Nishati

159. Mheshimiwa Spika , wakati waMkutano wa Kilele wa Wakuu wa NchiWanachama wa Jumuiya ya Afrika Masharikiuliofanyika mwezi Machi 2016, Rais wa Jamhuri

 ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Uganda walifanya Kikao cha pamoja kujadilimasuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi

wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutokaHoima, Uganda mpaka bandari ya Tangalitakalokuwa na urefu wa kilometa 1,410.

160. Mheshimiwa Spika , kufuatia  Kikaohicho cha Marais wawili, wataalam wa pandezote mbili waliendelea na majadiliano

 yaliyopelekea Serikali ya Uganda kutoa tamko

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 98/126

92 

rasmi kwenye Mkutano wa 13 wa Ushoroba waKaskazini uliofanyika mwezi Aprili, 2016 JijiniKampala kuwa bomba hilo litajengwa kupitia

 Tanzania. Mradi huo utagharimu Dola zaMarekani bilioni nne na kukamilika baada yamiaka mitatu hadi minne. Mradi huounatarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa mojatakriban 1,500 na ajira zisizo za moja kwa moja20,000. Aidha, Benki ya Maendeleo ya Afrikaimeidhinisha msaada wa kiasi cha Dola za

Marekani 1,691,130 kwa ajili ya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa Mradi mwingine waBomba la Mafuta la Mbarara - Mwanza - Isaka -Dar es Salaam. Fedha za nyongeza Dola zaMarekani 95,600 zinahitajika ili kukamilishaupembuzi yakinifu huo. Hivyo, kila NchiMwanachama imetakiwa kuchangia kiasi chaDola za Marekani 19,120 kabla ya mwisho wamwezi Juni, 2016 ili kukamilisha upembuzi

 yakinifu wa Mradi huo.

Ushirikiano Katika Sekta za Huduma zaJamii

Sekta ya Elimu, Utamaduni na Michezo

Urazinishaji wa Mitaala

161. Mheshimiwa Spika ,  Wizara imeendeleana uratibu wa zoezi la urazinishaji wa Mitaala

kwa ngazi zote za Elimu pamoja na mafunzo ya

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 99/126

93 

ualimu kwa shule za awali, msingi nasekondari.

Shindano la Insha la Jumuiya

162. Mheshimiwa Spika,  Wizara iliratibuushiriki wa Tanzania katika shindano lauandishi wa Insha la Jumuiya ya AfrikaMashariki lililoshirikisha wanafunzi wa shule za

sekondari kutoka nchi tano (5) Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nafurahi kuliarifuBunge lako Tukufu kuwa kijana MtanzaniaSimon Mollel Sabaya kutoka Shule ya Sekondari

 ya Mzumbe aliibuka mshindi wa kwanza katikashindano hilo. Huu ni ushahidi kuwa vijanawetu wanaweza na wanauelewa wa Jumuiya

 yetu. Naomba nitumie fursa hii kutoa pongezikwa kijana huyu na kuwatia moyo vijanawengine waendelee kushiriki kwenyemashindano haya ili waweze kuliletea sifa Taifaletu.  Natoa wito kwa walimu na wazazikuwahamasisha wanafunzi kushiriki katikashindano hilo ili kukuza uelewa wao katikamasuala ya Jumuiya. Wizara yangu kwakushirikiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki;Wizara za Elimu, Sayansi na Teknolojia; naWizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa naMichezo itaanzisha kampeni ya kuongeza uelewawa Jumuiya katika shule na vyuo.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 100/126

94 

Mdahalo wa Nne wa Wanafunzi wa VyuoVikuu

163. Mheshimiwa Spika,  Wizara iliratibuushiriki wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya

 Tanzania katika mdahalo wa Nne (4) waWanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Nchi Wanachamawa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyikamwezi Desemba 2015, Kampala, Uganda. Lengola mdahalo huo ni kupata washindi wawili

kutoka kila Nchi Mwanachama wa Jumuiyaambao watakuwa Mabalozi wa Nchi zao katikamasuala ya Jumuiya. Kwa upande wa Tanzania,washindi wa mwaka 2015 ni RaphaelKambamwene wa Chuo Kikuu cha Dar esSalaam na Lucy Peter Funja wa Chuo Kikuu chaArdhi. Aidha, Wizara inaendelea na jukumu la

kuwapatia taarifa Mabalozi haozitakazowawezesha kutoa elimu kwa ummahususan kwa vijana wenzao.

Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki

164. Mheshimiwa Spika,  napendakulifahamisha Bunge lako Tukufu kwambaKamisheni ya Kiswahili ya Afrika Masharikiimeshahamia rasmi katika Makao Makuu yake

 yaliyopo Zanzibar. Hii ni kufuatia kusainiwakwa Mkataba wa Uenyeji baina ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na Sekretarieti ya

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 101/126

95 

 Jumuiya ya Afrika Mashariki tarehe 28Desemba, 2015.

Mradi wa Hifadhi ya Mazingira Katika Bondela Ziwa Victoria Awamu ya Pili

165. Mheshimiwa Spika,  katikakukabiliana na athari za mazingira zinazotokanana shughuli za binadamu katika Bonde la ZiwaVictoria zilizosababisha pamoja na mambomengine kupungua kwa kina cha maji nasamaki katika ziwa, Wizara imeendelea nauratibu wa utekelezaji wa shughuli za Mradi waUsimamizi wa Mazingira katika Bonde la ZiwaVictoria. Katika kipindi hiki, Benki ya Duniailiongeza muda wa miaka miwili na nusu

kuanzia mwezi Juni 2015 hadi mwezi Desemba2017 na mkopo wa Dola za Marekani milioni 10ambazo zitatumika kukamilisha miradi ambayoilikuwa haijakamilika katika Awamu ya Pili yaMradi iliyofikia ukomo wake mwezi Juni 2015na kuandaa Awamu ya Tatu. Vilevile, udhibitiwa magugumaji katika Ziwa Victoria

umeendelea ambapo magugumaji yamepunguaZiwani kutoka hekta 520 mwezi Septemba, 2009hadi hekta 104 mwezi Novemba, 2015. Mradiumeendelea na shughuli za udhibiti wa utupajitaka na uhamasishaji wa uzalishaji boraviwandani ambapo Jumla ya viwanda 118 sawana asilimia 86 vimepata mafunzo ya uzalishaji

bora viwandani.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 102/126

96

 

Programu ya Hifadhi ya Mazingira kwaKuboresha Sera, Mabadiliko ya Tabianchi,Utafiti na Maendeleo ya Kiuchumi

166. Mheshimiwa Spika,  katikakuhakikisha kunakuwa na matumizi endelevu

 ya rasilimali maji katika Bonde la Mto Mara, Wizara yangu imefanikisha utiaji saini wa Hati

 ya Makubaliano ya Usimamizi wa pamoja warasilimali maji katika Bonde la Mto Mara kati ya

 Tanzania na Kenya. Makubaliano hayo yatasaidia kupunguza athari za mazingirazinazosababishwa na shughuli za binadamukatika bonde hilo.

Mradi wa Idadi ya Watu, Afya na Mazingira waJumuiya

167. Mheshimiwa Spika,  ili kujengauelewa wa pamoja kwa wananchi katikamasuala ya idadi ya watu, afya na mazingirakwa ajili ya kuleta maendeleo endelevu, Wizaraimeendelea kuratibu ushiriki wa Tanzania

katika maandalizi ya Mpango Mkakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Masuala yaIdadi ya Watu, Afya na Mazingira. Mpango huoutakapokamilika utatoa mwongozo wakuzingatia masuala ya idadi ya watu, afya namazingira katika utekelezaji wa miradi yamaendeleo katika Nchi Wanachama.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 103/126

97 

Sekta ya Jinsia na Maendeleo ya Jamii

168. Mheshimiwa Spika,  nafasi yawanawake, watoto na vijana imeendelea kupewakipaumbele katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.Kwa muktadha huo, Wizara imeendeleakuratibu programu na miradi inayolengakuyajengea uwezo makundi hayo ili kunufaikana fursa mbalimbali zinatokanazo naMtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Aidha, progamu hizi zimetoa fursa kwa makundihayo kutoa maoni yao ya namna bora yakuendeleza mtangamano. Vilevile, Jumuiya yaAfrika Mashariki inakamilisha Sera ya Watoto ya

 Jumuiya.

Ushirikiano katika Siasa, Ulinzi na Usalama

169. Mheshimiwa Spika,  naombakuchukua nafasi hii kulifahamisha Bunge lako Tukufu kuwa Jumuiya ya Afrika Masharikiimepata Katibu Mkuu mpya Balozi LiberatMfumukeko kutoka Jamhuri ya Burundiatakeyeiongoza Jumuiya kwa Kipindi cha miakamitano ijayo. Aidha, naomba kumshukuru

Balozi Dkt. Richard Sezibera kutoka Jamhuri yaRwanda kwa mchango wake mkubwa katikakuiendesha Jumuiya kwa kipindi cha miakamitano iliyopita.

Ushirikiano katika Siasa

170. Mheshimiwa Spika,  katika kipindi

hiki tumeendelea kushuhudia kushamiri kwa

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 104/126

98 

demokrasia katika Nchi Wanachama wa Jumuiya.  Kwa kuzingatia kwamba  demokrasiani moja ya misingi mikuu ya Jumuiya ya Afrika

Mashariki, Wizara yangu imeendelea kuratibuushiriki wa Tanzania katika timu ya waangaliziwa uchaguzi mkuu kutoka Jumuiya ya AfrikaMashariki kushiriki katika uangalizi wauchaguzi mkuu katika Nchi Wanachama. Katikakipindi hiki, Nchi tatu Wanachama wa Jumuiyazilifanya uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge.Nchi hizo ni Jamhuri ya Burundi, Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na Jamhuri ya Uganda.

 Jamhuri ya Burundi ilifanya Uchaguzi wakemwezi Julai, 2015 ambapo Rais PierreNkurunziza aliibuka mshindi wa Uchaguzi huo.Aidha, kwa upande wa Uchaguzi Mkuu wa

 Tanzania, Wizara iliratibu ushiriki wa waangaliziwa uchaguzi kutoka Jumuiya ya AfrikaMashariki waliokuja kufanya uangalizi ambapoMheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufulialipata ushindi katika uchaguzi huo.

171. Mheshimiwa Spika,  Wizara pia

iliratibu ushiriki wa Tanzania katika timu yawaangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya kwenyeuchaguzi mkuu wa Uganda uliofanyika mweziFebruari, 2016. Katika uchaguzi huo,Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafuwa Awamu ya Pili alipewa heshima ya kuwaKiongozi wa timu hiyo kutoka Jumuiya ya Afrika

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 105/126

99 

Mashariki ambapo Mheshimiwa Rais YoweriKaguta Museveni aliibuka mshindi.

172. Mheshimiwa Spika,  katikakuwashirikisha zaidi wananchi wa AfrikaMashariki kuchangia maoni yao katika maamuzimbalimbali ya uendeshaji wa Jumuiya,  Wizara

 yangu iliwawezesha Wananchi wa Tanzaniakupitia asasi zao kushiriki katika Mkutano waKatibu Mkuu wa Jumuiya na Asasi Zisizo zaKiserikali na Sekta Binafsi uliofanyika mweziMachi, 2016 Dar es Salaam, Tanzania. Maazimio

 ya Mkutano huo yalikuwa ni pamoja nakuliomba Baraza la Mawaziri la Jumuiyakuharakisha matumizi ya vituo vya utoaji wahuduma kwa pamoja mipakani, utekelezaji wahimaya moja ya forodha; na kushirikisha sektabinafsi katika ngazi zote za mchakato wauchaguzi ili kuweka mazingira mazuri yakufanya shughuli zao.

Bunge la Afrika Mashariki

173. Mheshimiwa spika, Wizara iliratibuna kushiriki katika mikutano ya Bunge la AfrikaMashariki, ambapo Bunge hilo lilijadili nakupitisha Miswada ya Sheria za Jumuiya,Maazimio na Taarifa mbalimbali. Miswadailiyopitishwa ni pamoja na Muswada wa Sheria

 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Kupunguza

na Kukabiliana na Majanga wa mwaka 2012;

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 106/126

100 

Muswada wa Sheria ya Jumuiya ya AfrikaMashariki ya Miamala ya Kielektroniki wamwaka 2014; Muswada wa Sheria ya Jumuiya

 ya Afrika Mashariki wa Tasnia ya Ubunifu naUtamaduni wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamwaka 2015; na Muswada wa Sheria ya

 Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Usimamizi naUhifadhi wa Misitu wa mwaka 2015.

174. Mheshimiwa spika, aidha, Miswadailiyosomwa Bungeni kwa mara ya kwanza ni:Muswada wa Sheria ya Jumuiya ya AfrikaMashariki ya Usawa wa Jinsia na Maendeleo wamwaka 2016; Muswada wa Sheria ya Jumuiya

 ya Afrika Mashariki ya Kulinda Watoa Taarifawa mwaka 2016; Muswada wa Sheria ya

 Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Mafao yaKustaafu kwa baadhi ya Wakuu wa Taasisi za

 Jumuiya ya Afrika Mashariki wa mwaka 2016;Muswada wa Sheria ya Jumuiya ya AfrikaMashariki wa Marekebisho ya Sheria yaUsimamizi wa Forodha ya Afrika Mashariki wamwaka 2016; na Muswada wa Sheria ya

 Jumuiya ya Afrika Mashariki wa KuzuiaUsafirishaji Haramu wa Binadamu wa mwaka2016.

175. Mheshimiwa spika,  Vilevile, Bungelilitoa Maazimio kwa Nchi Wanachama wa

 Jumuiya ya Afrika Mashariki na kusisitiza

Kuridhia Itifaki ya Umoja wa Afrika ya

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 107/126

101 

kuanzisha Bunge la Afrika;  Kuridhia Itifaki yaSheria ya Ushauri ya Umoja wa Afrikainayohusiana na Bunge la Afrika; Kumpongeza

Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania kwa ushindi wakekatika uchaguzi Mkuu pamoja na wananchi wa

 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwakudumisha Amani na Demokrasia wakati waUchaguzi;  Azimio la Bunge la Kuzitaka NchiWanachama wa Jumuiya ya Afrika Masharikikuchukua hatua za haraka katika kudhibitiUsafirishaji haramu wa binadamu; na Azimio laBunge la kuwashukuru Wake wa Viongozi waNchi Waanzilishi wa Jumuiya ya AfrikaMashariki.

176. Mheshimiwa spika, 

Kamati yaBunge la Afrika Mashariki ya Masuala yaKikanda na Utatuzi wa Migogoro ilifanya ziara yaUangalizi na tathmini ya changamoto zautekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja katikaKanda ya Kati mwezi Novemba 2015. Kamati

hiyo na Uongozi wa Wizara ilijadili hali halisi yautekelezaji wa makubaliano ya Itifaki hiyohususan katika kanda ya kati ambapo kati yamasuala yaliyoibuliwa ni kuhusu afya yaWananchi katika kutumia uhuru wa watu wa

 Jumuiya kuingia na kutoka Nchi za Jumuiyaambapo walisisitiza kuhusu umuhimu wa

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 108/126

102 

Chanjo ya Homa ya Manjano ili kuzuiauambukizaji wa ugonjwa huo.

177. Mheshimiwa Spika,  Kamatimbalimbali za Bunge la Afrika Masharikizilifanya mikutano ya kukusanya maoni yawadau kuhusu utungwaji wa sheria mbalimbaliza Jumuiya ambapo Kamati ya Mawasiliano,Biashara na Uwekezaji ilikusanya maoni yaMuswada wa Sheria ya Sectional Properties Bill,

2016 , Kamati ya Kilimo, Maliasili na Mazingirailikusanya maoni kuhusu Muswada wa Sheria

 ya Usimamizi na Uhifadhi wa Misitu wa AfrikaMashariki wa mwaka 2015 na Kamati yaGeneral Purpose ilikusanya  maoni kuhusuMuswada wa Sheria ya Watu Wenye Ulemavuwa mwaka 2015.

178. Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibuProgramu ya Wabunge wa Tanzania katikaBunge la Jumuiya ya kutoa elimu kwa ummailiyohusisha Vyombo vya Habari, Taasisi zaElimu, Asasi za Kiraia, Wabunge na Maafisa waSerikali mwezi Aprili, 2016. Lengo la programu

hiyo pamoja na mambo mengine nikuhamasisha umma juu ya fursa zitokanazo na

 Jumuiya ili kunufaika nazo.

Ushirikiano katika Ulinzi

179. Mheshimiwa Spika,  ili  kuimarisha

uwezo wa vyombo vya ulinzi na usalama vya

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 109/126

103 

Nchi Wanachama katika urejeshaji amaniwakati wa machafuko, kukabiliana na ugaidi,uharamia na majanga, Wizara iliratibu ushiriki

wa Tanzania katika zoezi la kijeshi kwa vyombovya ulinzi na usalama kutoka nchi Wanachamawa Jumuiya ya Afrika Mashariki la Vituo vyaKamandi lijulikanalo kama ‘ Ushirikiano Imara

2016’ . Zoezi hilo lilifanyika mwezi Machi 2016nchini Kenya.

Ushirikiano katika Usalama

180. Mheshimiwa Spika,  kwa kuzingatiakuwa amani na usalama ni nguzo kuu kwamaendeleo ya kijamii na uchumi katika

 Jumuiya, Wizara yangu iliratibu ushiriki wa Tanzania katika mkutano wa Wakuu waUpelelezi toka Jeshi la Polisi, Wasajili wa Magari,Wakuu wa Kupambana na Madawa ya Kulevyana Wakuu wa Vitengo vya Kupambana naBiashara Haramu ya Watu uliofanyika mweziDesemba 2015 Nairobi, Kenya. Mkutano huoulitoa fursa kwa wakuu hao kubadilishana

uzoefu na taarifa za mienendo ya uhalifu katikamaeneo yao na kupanga mpango wa pamoja waoperesheni za kupambana na uhalifu. Aidha,Nchi Wanachama zinaendelea kutekelezaMkakati wa Kikanda wa Amani na Usalama.

181. Mheshimiwa Spika , napenda

kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa Jamhuri ya

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 110/126

104 

Sudan Kusini imejiunga rasmi na Jumuiya nahivyo kuifanya idadi ya Nchi Wanachamakuongezeka kutoka tano hadi sita. Nchi ya

Sudan Kusini, iliwasilisha rasmi maombi yakujiunga na Jumuiya mwezi Novemba, 2011.Nchi Wanachama zilikamilisha mchakato wauhakiki kuthibitisha iwapo nchi hiyo inakidhivigezo kulingana na matakwa ya Mkataba waUanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Mkutano wa 17 wa Wakuu wa Nchi Wanachama

uliofanyika mwezi Machi 2016 jijini Arushauliridhia nchi hiyo kujiunga na Jumuiya.

182. Mheshimiwa Spika, Wakuu wa Nchiwanachama wa Jumuiya walimpa heshimaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naMwenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa NchiWanachama wa Jumuiya kusaini Mkataba wa

 Jamhuri ya Sudan Kusini kujiunga na Jumuiyakwa niaba yao. Zoezi la utiaji saini Mkatabahuo, lilifanyika Dar es Salaam tarehe 15 Aprili,2016.

183. Mheshimiwa Spika, kujiunga kwa Jamhuri ya Sudan Kusini kumeifanya Jumuiyakuwa na jumla ya watu zaidi ya milioni 160, hiini fursa ya kipekee kwa sekta binafsi hapanchini katika kuendeleza na kukuza biasharazao. Naomba kuchukua nafasi hii kuishauri

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 111/126

105 

sekta binafsi hapa nchini kuchangamkia fursazitokanazo na kupanuka kwa soko la Jumuiya.

Kutoa elimu ya Mtangamano wa AfrikaMashariki ili Wananchi waweze kuelewa nakutumia fursa zitokanazo na Mtangamano.

184. Mheshimiwa Spika,  Wizaraimeendelea kutekeleza Mkakati wake waMawasiliano kwa kutoa Elimu kwa Umma

kuhusu fursa zilizopo katika Jumuiya ya AfrikaMashariki na jinsi ya kunufaika nazo. Wizarailitumia maonesho mbalimbali kama vile ya Wiki

 ya Utumishi wa Umma, Saba Saba, Nane Nane,Maonesho ya Biashara Zanzibar, maonesho yaSiku ya Mara, Maonesho ya Siku yaWafanyakazi Duniani na Juakali/Nguvu Kazi ya

 Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoa elimu kwaUmma. Jumla ya nakala za machapisho 11,046

 yenye taarifa muhimu na fursa zipatikanazokwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki

 yalisambazwa na jumla ya wananchi 7,387walitembelea Mabanda ya Wizara ili kupata

taarifa na ufafanuzi wa masuala yamtangamano. Taarifa za maonesho hayozilisambazwa kupitia vyombo mbalimbali vyahabari ikiwemo Luninga, tovuti na blogu yaWizara. Vilevile, makala ya Televisheni yenyeujumbe wa fursa mbalimbali za Jumuiya yaAfrika Mashariki ilioneshwa katika Luninga za

TBC1, Star TV, Channel 10 na Clouds TV .

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 112/126

106

 

185. Mheshimiwa Spika,  Wizara yanguiliweka mabango saba katika mipaka yaNamanga, Horohoro, Holili, Sirari, Mutukula,

Rusumo na Kabanga yenye kuelezea taratibu zakufuatwa na wafanyabiashara wakati wa kuuzana kununua bidhaa ndani ya Jumuiya ya AfrikaMashariki. 

186. Mheshimiwa Spika,  Wizarailiendesha mikutano ya elimu kwa umma katikaMikoa ya Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Tanga,Mara, Kagera, Mtwara, Lindi na katika mipaka

 ya Mutukula, Rusumo, Kabanga, Holili naNamanga. Aidha, Wizara iliendesha warsha yaWaandishi wa Habari wa Zanzibar kwa lengo lakuwaelimisha juu ya fursa na masuala yaMtangamano ili waweze kufikisha taarifa sahihiza Mtangamano kwa wananchi.

Kuimarisha Utendaji na Kujenga Uwezo waWizara

187. Mheshimiwa Spika,  Wizara

iliendelea kuimarisha uwezo wa kiutendaji kwakupandisha vyeo watumishi 20 baada yakukidhi Vigezo vya Kisheria kamavilivyoainishwa katika Miundo yao ya Utumishipamoja na kutengewa fedha katika Makisio yaIkama na Bajeti ya Mishahara ya Wizara kwamwaka wa fedha 2015/2016. Aidha, Wizara

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 113/126

107 

iliwabadilisha kada jumla ya watumishi watatuwa kada tofauti baada ya kujiendelezakitaaluma wakiwa kazini na kupata sifa stahiki.

Vilevile, watumishi 29 wamethibitishwa kazinina watumishi 15 wa kada mbalimbaliwalithibitishwa katika vyeo vyao vipya baada yakukidhi vigezo.

188. Mheshimiwa Spika ,  katikakuhakikisha kuwa Wizara inawajengea uwezowa kitaaluma watumishi wake ili wawezekutekeleza majukumu yao kwa weledi naufanisi, Wizara iliandaa na kutekeleza mpangomdogo wa mafunzo kwa mwaka wa fedha2015/2016 ambao hadi kufikia mwezi Februari2016 watumishi wawili (2) walihudhuriamafunzo ya muda mrefu na watumishi tisa (9)walihudhuria mafunzo ya muda mfupi. Mpangohuu mdogo ni utekelezaji wa mpango wamafunzo wa Wizara wa miaka mitatu kuanziamwaka 2015/2016 hadi 2017/2018.

USIMAMIZI WA MAPATO NA MATUMIZI

189. Mheshimiwa Spika, Wizaraimeendelea kuimarisha usimamizi nauwajibikaji katika Mapato na Matumizi ya Fedhaza Umma kwa kuzingatia sheria na kanuni zafedha za umma. Napenda kuliarifu Bunge lako

 Tukufu kwamba, Wizara imeendelea kupata Hati

Safi ya Ukaguzi wa Hesabu. Kwa mujibu wa

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 114/126

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 115/126

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 116/126

110 

kwenye taasisi za kikanda na kimataifazinapotangazwa;

iv. Kuendelea kuratibu uondoaji wavikwazo visivyo vya kiforodha nchini ilikuwavutia wafanyabiashara kutokandani ya Jumuiya kununua bidhaazinazozalishwa nchini na kutumiabandari zetu kikamilifu; na

v. Wizara itaendelea kuimarisha Balozizetu na kufungua ofisi za uwakilishikwenye maeneo yenye maslahi kwataifa.

SHUKRANI

192. Mheshimiwa Spika, Wizara imefanikiwakutekeleza sehemu ya majukumu yaliyotajwahapo juu kwa ushirikiano na washirika wamaendeleo kutoka nchi na asasi mbalimbali zakitaifa, kikanda, kimataifa pamoja na sektabinafsi. Naomba nitumie fursa hii kuwashukuruwashirika wetu wote wa maendeleo ikiwa ni

pamoja na Australia, Brazil, Canada, China,Cuba, Denmark, Finland, India, Italia, Ireland,

 Japan, Korea Kusini, Kuwait, Malaysia,Marekani, Malta, Norway, Oman, Poland, Qatar,Sweden, Ubelgiji, Ufaransa, Uhispania,Uholanzi, Uingereza, Ujerumani, Umoja waFalme za Kiarabu, Ureno, Urusi, Uswisi,

Uturuki, Umoja wa Ulaya, AfDB, African

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 117/126

111 

Capacity Building Facility, FAO, IAEA, ILO, IMF,IOM, Investment Climate Facility forAfrica,UNDP, UNEP, UN-HABITAT, UNWTO,

UNHCR, UNICEF, UNFPA, UNESCO, UNIDO,WHO, TradeMark East Africa, The Association ofEuropean Parliamentarians with Africa, WorldBank na WWF kwa mchango wao mkubwakatika kufanikisha utekelezaji wa Diplomasia yauchumi.

MALENGO YA WIZARA KWA MWAKA WA

FEDHA 2016/2017

193. Mheshimiwa Spika,  katika mwakawa fedha 2016/2017, pamoja na mambomengine, Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki imepangakutekeleza malengo makuu muhimu kulinganana majukumu yake kama ifuatavyo:-

i. Kuitangaza nchi yetu kama moja yanchi duniani zenye mazingira mazurikwa ajili ya uwekezaji kutokana na

historia yake ya miaka mingi ya amani,umoja, utulivu na mshikamano wakitaifa;

ii. Kuongeza uwakilishi wetu nje ya nchikwa kufungua Balozi mpya, Ofisi zaKikonseli na kuimarisha rasilimali watuna fedha;

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 118/126

112 

iii. Kuendelea kusimamia, kufuatilia nakuratibu utekelezaji wa mikatabambalimbali iliyosainiwa kati ya nchi

 yetu na nchi nyingine na ile yamashirika ya kikanda na kimataifa;

iv. Kukamilisha mchakato wa kuitambua jumuiya ya watanzania wanaoishiughaibuni na kuweka utaratibuutakaowawezesha kuchangia maendeleo

 ya taifa;

v. Kuratibu majadiliano kuhusu maeneo ya ushirikiano katika uendelezaji wamiundombinu ya kiuchumi, kijamii nakuendeleza ushirikiano katika sekta zauzalishaji;

vi. Kuratibu utekelezaji wa Mpango Kaziwa miaka kumi wa Umoja wa Fedhakatika kuelekea kwenye eneo la SarafuMoja ya Jumuiya ya Afrika Mashariki;

vii. Kuratibu majadiliano na kusimamiautekelezaji wa makubaliano ya

ushirikiano wa kiuchumi kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya nyingine za Kikanda kuhusukuanzisha Eneo Huru la Kibiashara naKiuchumi;

viii. Kuratibu, kushiriki na kusimamia

majadiliano na utekelezaji wa

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 119/126

113 

makubaliano katika maeneo ya siasa,ulinzi na usalama;

ix. Kuratibu, kushiriki na kusimamiamajadiliano na utekelezaji wa hatua zaMtangamano wa Afrika Mashariki; na

 x. Kutoa Elimu kwa Umma kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki na fursazinazopatikana katika Jumuiya hiyo.

MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA

WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017

194. Mheshimiwa Spika,  ili kuwezakutekeleza kikamilifu majukumu, kwa mwakawa fedha 2016/2017 Wizara imepangiwa bajeti

 ya kiasi cha shilingi 151,396,775,000.00 Kati yafedha hizo shilingi 143,396,775,000.00 ni kwaajili ya Matumizi ya Kawaida na shilingi8,000,000,000.00 ni kwa ajili ya bajeti yaMaendeleo.

195. Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya

Matumizi ya Kawaida ya Wizara kwa mwaka wafedha 2016/2017, shilingi 133,056,021,000.00ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo na shilingi10,340,754,000.00  ni kwa ajili ya Mishahara.Kati ya fedha za Matumizi Mengineyo shilingi720,160,000.00  ni kwa ajili ya Mpango waKujitathmini Kiutawala Bora Tanzania, shilingi

3,154,721,000.00 ni kwa ajili ya fedha za

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 120/126

114 

Mishahara na Matumizi Mengineyo ya Chuo chaDiplomasia na shilingi 686,298,378.00  ni kwaajili ya Mahakama ya Afrika ya Haki za

Binadamu na Watu.

196. Mheshimiwa Spika,  katika fedha za

bajeti ya maendeleo za kiasi cha shillingi8,000,000,000.00 zilizopangwa kwa mwaka wafedha 2016/2017, kiasi cha shilingi2,375,250,000.00 zitatumika kufanikisha ujenzi

wa jengo la ofisi ya Wizara ambalo ni sehemu yaKituo cha Mikutano ya Kimataifa cha JuliusNyerere; shilingi 1,316,435,000.00 zitatatumikakukamilisha ukarabati jengo la ghorofa tisa (9),makazi ya Balozi na Mkuu wa Utawala Ubaloziwa Tanzania Maputo, Msumbiji; shilingi2,172,880,000.00 zitatumika kukarabati makazi

 ya Balozi na watumishi yaliyopo Stockholm,Sweden; shilingi 1,813,871,000 zitatumikakukarabati majengo mawili yanayomilikiwa naSerikali yaliyopo Khartoum, Sudan na shilingi321,564,000.00  kwa ajili ya kuboresha mfumowa mawasiliano kati ya Wizara na Balozi za

 Tanzania nje.

197. Mheshimiwa Spika,  katika mwakawa fedha 2016/2017, Wizara kupitia Balozizake, inatarajia kukusanya kiasi cha shilingi24,001,150,000.00 kama maduhuli ya Serikali.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 121/126

115 

HITIMISHO

198. Mheshimiwa Spika, ili kuweza

kutekeleza kikamilifu majukumu yaliyotajwahapo juu, kwa mwaka wa fedha 2016/2017,naomba Bunge lako Tukufu liidhinishe jumla yaShilingi 151,396,775,000.00. Kati ya fedha hizoShilingi 143,396,775,000.00. ni kwa ajili yaMatumizi ya Kawaida na Shilingi8,000,000,000.00. ni kwa ajili ya Bajeti yaMaendeleo.

199. Mheshimiwa Spika, naombakuchukua nafasi hii kukushukuru wewe binafsi,na Waheshimiwa Wabunge kwa kunisikiliza.

200. Mheshimiwa Spika, naomba kutoahoja. 

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 122/126

116

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 123/126

117

 

Kiambatisho Na. 1

Kielelezo Na. 1: Urari wa biashara

0.00

200.00

400.00

600.00

800.00

1000.00

1200.00

US$Mil

Mwaka

Urari 

wa 

Biashara

Mauzo Nje

Manunuzi Nje

 

Chanzo:  Taarifa ya Biashara ya Afrika Mashariki, 2014 

Tufe Na. 1: Mgao wa Soko Baina ya Nchi Wanachama, 2014

Chanzo : Taarifa ya Biashara ya Afrika Mashariki, 2014

     U     S      $     M     i     l

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 124/126

118

  Kiambatisho Na.2

Hatua Iliyofikiwa Katika Ujenzi wa Vituo Vya Utoaji wa

Huduma kwa Pamoja Mipakani (One Stop Border Posts- OSBPs)  

Na. Kituo Hatua ya UjenziIliyofikiwa kwa upande waTanzania

1. Holili/Taveta(Tanzania na Kenya)

Ujenzi umekamilika. Kituohiki kinafanya kazi kwamfumo wa kutoa huduma

kwa pamoja kuanzia mweziMei, 2015. Uzinduzi rasmiwa Kituo hiki ulifanyikamwezi Februari, 2016, HoliliMkoani Kilimanjaro.

2. Sirari/Isebania(Tanzania na Kenya)

Ujenzi umekamilika naMaafisa wamehamiakwenye majengo.  Hatahivyo, kituo hakijaanza

kufanya kazi kwa mfumowa kutoa huduma kwapamoja kwa kuwa majengo

 yake hayajaunganishwakwa mifumo ya Teknolojia

 ya Habari na Mawasilianoili kuwezesha Maafisa wa

 Tanzania kutoa hudumawakiwa upande wa Kenya

na Maafisa wa Kenya kutoahuduma wakiwa upande wa

 Tanzania.

3. Mutukula/Mutukula(Tanzania na Uganda)

Ujenzi wa kituo hiki kwa

upande wa Tanzania

umekamilika  ambapo

maafisa wamehamia

kwenye jengo. Upande wa

Uganda ujenzi upo kwenye

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 125/126

119

  Kiambatisho Na.2

hatua za mwisho.

4. Namanga/Namanga(Tanzania na Kenya).

Ujenzi wa Kituo hiki kwaupande wa Tanzania

umekamilika tangu mwezi

Januari, 2015 

 Taasisi zinazotoa huduma

mpakani zimeshindwa

kuhamia kwenye Kituo hiki

kutokana na changamoto

 ya samani, upatikanaji wamaji ya uhakika na

kutokamilika kwa Mfumo

wa TEHAMA. Jengo la

upande wa Kenya ujenzi

upo katika hatua za mwisho

kukamilika.

Matarajio ni kuwachangamoto zilizobainishwa

zitapatiwa ufumbuzi na

Kituo kuanza kutoa

huduma mwanzoni mwa

mwaka 2016/2017.

5. Kabanga/Kobero(Tanzania na Burundi).

Ujenzi kwa pande zote mbiliunaendelea.

6. Rusumo/Rusumo(Tanzania na Rwanda)

Ujenzi umekamilika. Kituohiki kilizinduliwa rasmi naRais wa Jamhuri yaMuungano wa TanzaniaMhe. Dkt John Pombe

 Joseph Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mhe.Paul Kagame tarehe 6Aprili, 2016.

8/16/2019 Hotuba Ya Bajeti ya Wizara ya Mambo Ya Nje 2016

http://slidepdf.com/reader/full/hotuba-ya-bajeti-ya-wizara-ya-mambo-ya-nje-2016 126/126

  Kiambatisho Na.2

Kituo hiki kilianza kutoa

huduma kwa mfumo wakutoa huduma kwa pamoja

mpakani tarehe 1 Machi,

2016 baada ya kukamilika

kwa miundombinu ya maji,

umeme na uwekaji wa

samani upande wa

 Tanzania.

7. Horohoro/Lungalunga,(Tanzania na Kenya).

Ujenzi kwa upande waTanzania umekamilika  na

maafisa wamehamia

kwenye jengo. Kituo

hakijaanza kufanya kazi

kwa mfumo wa kutoa

huduma kwa pamoja kwa

kuwa majengo

hayajaunganishwa na

Mfumo ya Teknolojia ya

Habari na Mawasiliano.