28
1 HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWENYE SHEREHE YA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, KUMBUKUMBU YA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE NA WIKI YA VIJANA KITAIFA TAREHE 14/10/2013 MKOANI IRINGA Mheshimiwa Anne Makinda, Spika wa Bunge; Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo; Mheshimiwa Zainab Mohamed, Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na watoto - Zanzibar; Waheshimiwa Mawaziri na Nanaibu Mawaziri; Mheshimiwa Dkt. Christine Ishengoma, Mkuu wa Mkoa wa Iringa; Waheshimiwa Wabunge na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi; Makamu Mwenyekiti wa CCM (wa Mkoa) na Viongozi wa Vyama vya Siasa mliopo;Waheshimiwa Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa, Viongozi wa Serikali wa Ngazi mbalimbali za Taifa na Mkoa; Wageni Waalikwa; Ndugu Wananchi;

HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

  • Upload
    others

  • View
    16

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

1

HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE,

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWENYE

SHEREHE YA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU,

KUMBUKUMBU YA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS

KAMBARAGE NYERERE NA WIKI YA VIJANA KITAIFA

TAREHE 14/10/2013 MKOANI IRINGA

Mheshimiwa Anne Makinda, Spika wa Bunge;

Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari,

Vijana, Utamaduni na Michezo;

Mheshimiwa Zainab Mohamed, Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi

wa Jamii, Vijana, Wanawake na watoto - Zanzibar;

Waheshimiwa Mawaziri na Nanaibu Mawaziri;

Mheshimiwa Dkt. Christine Ishengoma, Mkuu wa Mkoa wa

Iringa;

Waheshimiwa Wabunge na Wajumbe wa Baraza la

Wawakilishi;

Makamu Mwenyekiti wa CCM (wa Mkoa) na Viongozi wa

Vyama vya Siasa mliopo;Waheshimiwa Mabalozi na

Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa, Viongozi wa Serikali

wa Ngazi mbalimbali za Taifa na Mkoa;

Wageni Waalikwa;

Ndugu Wananchi;

Page 2: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

2

Mabibi na Mabwana;

Shukrani

Niruhusuni nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu,

mwingi wa rehema, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha

kukutana tena mwaka huu kuadhimisha Kilele cha Mbio za

Mwenge wa Uhuru, kumbukumbu ya Baba wa Taifa hayati

Mwalimu Julius Nyerere na Wiki ya Vijana. Namshukuru sana

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, na viongozi wenzake pamoja na

wananchi wa Iringa kwa kutupokea vizuri na ukarimu wenu. Pia

nawapongeza kwa kukubali kuwa wenyeji wa maadhimisho

haya. Kazi ya kuandaa sherehe kubwa kama hizi siyo jambo

jepesi hata kidogo. Bahati nzuri mambo yamefana sana kama

tunavyoshuhudia sote. Hongereni sana.

Pongezi Wizara

Ndugu wananchi;

Niruhusuni pia nitoe pongezi nyingi kwa Mheshimiwa Dkt.

Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na

Page 3: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

3

Michezo na Mheshimiwa Zainab Omary, Waziri wa Uwezeshaji,

Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto wa Zanzibar

kwa uongozi wao makini wa shughuli za Mbio za Mwenge.

Kama tujuavyo shughuli za Mbio za Mwenge husimamiwa na

Wizara zetu hizi mbili. Tunawapongeza kwa kazi nzuri

waifanyayo. Ni ukweli ulio wazi kuwa kila mwaka tunashuhudia

mambo yakiwa bora zaidi kuliko mwaka uliopita. Mcheza kwao

hutunzwa. Hongereni sana.

Pamoja na Mawaziri napenda kuwatambua viongozi na

wafanyakazi wote wa Wizara zetu mbili waliohusika na Mbio za

Mwenge kwa kazi yao nzuri tunayojivunia sote. Aidha,

nawapongeza Wakuu wa Mikoa na Wilaya, viongozi na

watumishi wa Serikali zetu mbili na wajumbe wote wa kamati

mbalimbali walioshiriki katika kuratibu Mbio za Mwenge wa

Uhuru mwaka huu. Wamefanya kazi nzuri inayostahili

kupongezwa na kila mmoja wetu.

Page 4: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

4

Kwa namna ya pekee nawapongeza ndugu Juma Ali Sumai,

kiongozi wa Mbio za Mwenge na Wakimbiza Mwenge wenzake

kwa kutimiza kwa ufanisi wa hali ya juu jukumu kubwa na zito

la kukimbiza Mwenge wa Uhuru nchi nzima. Nawapa pole

nyingi kwa changamoto mbalimbali walizokumbana nazo katika

safari ya kilomita nyingi. Kazi hiyo wameimaliza salama na leo

wameukabidhi Mwenge ukiwa salama. Nawapongeza sana kwa

kuufikisha ujumbe wa Mwenge kwa uhodari mkubwa.

Waheshimiwa Mawaziri;

Ndugu wananchi;

Nafurahi kusikia kuwa kama ilivyokuwa miaka iliyopita,

mwaka huu watu walijitokeza kwa wingi kila mahali Mwenge

wa Uhuru ulipopita. Pia nimeambiwa ujumbe wa Mwenge

ulifikishwa kwa ufasaha na kwamba umepokelewa vizuri. Miradi

mingi ya maendeleo imezinduliwa na kuwekewa mawe ya

msingi.

Page 5: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

5

Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati

kabisa wananchi wa Tanzania kwa ushiriki wao mzuri katika

Mbio za Mwenge. Ushiriki wao ni kielelezo tosha cha kutambua

umuhimu wa Mwenge wa Uhuru na cha moyo wa uzalendo kwa

nchi yetu na kuwaenzi waasisi wa taifa letu. Kwa niaba ya

Serikali nawahakikishia kuwa tutaendelea kuwahimiza viongozi

wa ngazi mbalimbali kuhakikisha kuwa miradi yote

iliyozinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi wakati wa mbio za

Mwenge wa Uhuru inaendelea kutekelezwa kama

ilivyokusudiwa.

Kwa namna ya pekee nawapongeza waandishi na vyombo

vya habari kwa kuwa nasi bega kwa bega kuhamasisha watu na

kueneza ujumbe wa Mwenge. Mchango wao umesaidia sana

kufanikisha malengo ya Mbio za Mwenge kwani siku zote

wapotoshaji hawakosekani.

Page 6: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

6

Kumbukumbu ya Baba wa Taifa

Ndugu Wananchi;

Kama mjuavyo siku ya kilele cha Mbio za Mwenge pia ni

siku ya kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa

letu la Tanzania kilichotokea miaka 14 iliyopita. Ni siku ambayo

tunawajibika kukumbuka mema mengi aliyoifanyia nchi yetu,

mafundisho yake na urithi aliotuachia. Nia yetu ni kutaka watu

wasimsahau kiongozi wetu huyu maalum na muhimu sana

katika historia ya nchi yetu.

Miongoni mwa mambo ya kukumbuka hasa wakati huu wa

Mchakato wa Katiba Mpya ni (jambo la busara kutumia muda

wetu) kujikumbusha mawazo ya Mwalimu kuhusu umoja wa

nchi yetu pamoja na Muungano wa Zanzibar na Tanganyika.

Hotuba zake na maandishi yake kuhusu mambo hayo yana

mafundisho mengi mazuri ambayo tukiyaelewa vyema na

kuyazingatia yatatusaidia sana katika mjadala na ukamilishaji wa

mchakato wa Katiba mpya.

Page 7: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

7

Mimi naamini fikra za Mwalimu na mtazamo wake kuhusu

umoja wetu na Muungano bado vina maana hata leo. Tujiepushe

na kuyapuuza tusije tukawa na Katiba itakayolibomoa taifa

badala ya kulijenga. Ninaposema hivyo sipendi nieleweke kuwa

sitaki mabadiliko ila napenda tuwe makini katika kufanya

mabadiliko. Nataka tufanye mabadiliko yatakayotupeleka mbele

na siyo kuturudisha nyuma.

Ndugu wananchi;

Pamoja na kuadhimisha siku ya kifo cha Baba wa Taifa

(Mwalimu Julius Nyerere), nadhani ni vyema pia tukawa

tunaikumbuka siku ya kuzaliwa kwake yaani tarehe 13 Aprili

(1922). Nisingependa kujiingiza katika mjadala wa siku ipi bora

zaidi kwani zote ni siku muhimu katika historia ya maisha ya

mwanadamu. Tofauti yake ni kuwa siku ya kuzaliwa ni ya furaha

na siku ya kufa ni ya majonzi. Kama tutakubaliana tuikumbuke

na siku yake ya kuzaliwa pengine siku hiyo tungeiita Nyerere

Day. Tuiadhimishe siku hiyo kusheherekea maisha yake kwa

Page 8: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

8

kujadili kazi zake na kufanya shughuli mbalimbali kuenzi

mambo mema aliyosimamia na kuifanyia nchi yetu na dunia kwa

ujumla.

Kauli Mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2013

Ndugu Wananchi;

Kama alivyoeleza Mheshimiwa Waziri kila mwaka Mbio za

Mwenge wa Uhuru huwa na ujumbe maalum unaobebwa na

kauli mbiu ya mwaka huo. Mwaka huu ujumbe ulikuwa

“Watanzania ni Wamoja: Tusigawanywe kwa Msingi wa

Tofauti Zetu za Dini, Itikadi, Rangi na Rasilimali”. Ujumbe

huu ni muafaka kabisa hasa ukikumbuka misukosuko na

majaribu makubwa nchi yetu iliyopitia mwaka huu. Hivyo

kutumia Mbio za Mwenge wa Uhuru kukumbushana haja na hoja

za kuziba nyufa zilizoanza kujitokeza ni jambo la busara sana. Ni

jambo la kuungwa mkono na kila mwananchi na hasa kila

mzalendo.

Page 9: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

9

Bahati nzuri upepo huo mbaya umepita na tuombe usirudi

tena. Hivi sasa hali ni shwari na Watanzania tunaendelea

kushirikiana vizuri bila ya kubaguana kwa dini zetu, vyama vya

siasa na kadhalika kama tulivyozoea kuishi miaka yote.

Waliotaka kutufarakanisha hawakufanikiwa lakini, lazima tuwe

makini kwani wanaweza kujaribu tena kutugawa ama kwa yale

yale au mambo mengine.

Ndugu wananchi;

Kwa kweli nafarijika sana kuona Watanzania wakiendelea

kukataa ushawishi na uchochezi wa kugawanywa kwa misingi ya

dini au mambo mengine. Ndugu zangu naomba tuendelee hivyo

na hayo ndiyo mafundisho mema na urithi aliotuachia Baba wa

Taifa tunayemkumbuka leo. Tukigawanyika, nchi yetu

itavurugika na sote tutakuwa tumeharibikiwa. Dhambi kubwa ya

kubaguana kwa misingi yo yote ile ni kupotea kwa amani na

utulivu. Bila amani, hatuwezi kuishi kwa furaha katika nchi yetu

hii nzuri. Bila amani, jamii haiwezi kujishughulisha kwa

Page 10: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

10

ukamilifu na shughuli za kujiletea maendeleo. Amani

ikituponyoka nchi yetu itayumba na hakuna atakayebaki salama.

Napenda kuwahakikishia wananchi wenzangu wote, kuwa

sisi Serikalini tutaendelea kufanya kila tuwezavyo kujenga,

kulinda na kudumisha umoja na mshikamano wetu ambao ndio

msingi mkuu wa kuwepo kwa amani na utulivu nchini.

Tutaendelea kukemea kwa nguvu zetu na uwezo wetu wote

vitendo vinavyosababisha mmomonyoko wa umoja na

mshikamano wetu. Serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria

dhidi ya mtu au kikundi cha watu watakaojihusisha na vitendo

vya kuvuruga amani ya nchi yetu. Naomba Watanzania

wenzangu mtuelewe hivyo. Napenda kusisitiza na kuwasihi

kuwa tuendelee kuaminiana, kuheshimiana na kuvumiliana

pamoja na tofauti zetu.

Page 11: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

11

Mapambano Dhidi ya UKIMWI

Ndugu wananchi;

Pamoja na ujumbe huu maridhawa ambao kimsingi ndiyo

ujumbe mkuu wa Mbio za Mwenge tangu kuasisiwa kwake,

mwaka huu wananchi waliendelea kuhimizwa kuendeleza

mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI, rushwa na dawa za

kulevya. Tangu ugonjwa wa UKIMWI uingie nchini kwetu

mwaka 1983, inakadiriwa kuwa zaidi ya ndugu zetu milioni 2

wamepoteza maisha kutokana na maradhi haya. Hali kadhalika

zaidi ya watoto milioni 1.3 wamekuwa yatima na watu zaidi ya

milioni 1.5 wanaishi na VVU hivi sasa. Bahati mbaya karibu

asilimia 65 ya hao ni wanawake.

Kitaifa, takwimu zinaonesha kuwa maambukizi ya UKIMWI

yanazidi kupungua kutoka asilimia saba mwaka 2005 hadi

asilimia 5.7 mwaka 2010 na kufikia asilimia 5.1 mwaka 2012.

Hapa Iringa napo maambukizi yamekuwa yanapungua ingawaje

bado yapo juu na kwamba ni Mkoa wa pili nchini kuwa na

Page 12: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

12

kiwango cha juu cha maambukizi. Takwimu zinaonesha kuwa

kiwango cha maambukizi Mkoa wa Iringa ni asilimia 9.1,

wanaume asilimia 6.9 na wanawake asilimia 10.9. Mkoa wa

Njombe ndiyo unaoongoza ukiwa na asilimia 14.8.

Kwa sababu ya maradhi haya idadi ya watoto yatima ni

kubwa katika mkoa huu (inakadiriwa kuwa waliopo ni 3400).

Inahuzunisha sana kusikia au kuona baadhi ya watoto hawa

wamelazimika kukatisha masomo yao baada ya wazazi wao

kufariki ili kuwalea wadogo zao. Kwa ajili hiyo, wamelazimika

kufanya kazi zisizostahili kufanywa na watu wa umri wao.

Wapo pia wazee ambao kwa umri wao wanahitaji kulelewa lakini

wamebaki peke yao na wakati mwingine wanalazimika kulea

watoto walioachwa na watoto wao.

Ndugu wananchi;

Nilishaagiza viongozi siku za nyuma na leo narudia tena

kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango

thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha

Page 13: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

13

kupata fursa ya kukua na kuishi kama watoto wengine. Jambo

moja muhimu nililolisisitiza ni kuwa tuhakikishe kuwa vijana

hawa wanapata elimu ambayo ndiyo ufunguo wa maisha yao.

Ndugu wananchi;

Tuongeze ari, nguvu na kasi ya kupambana na gonjwa hili

hatari. Ni kweli tunapata mafanikio lakini hayatoshi. Kiwango

bado ni cha juu mno. Nawaomba viongozi wa Serikali, dini, asasi

za kijamii, wanasiasa na wananchi tuendelee kuhamasisha jamii

kujiepusha na ugonjwa huu. Tuwahimize watu wajitokeze

kupima wajue mustakabali wao, waepuke ngono nzembe na hasa

hasa wawe na subira na waaminifu kwa ndoa zao au wapenzi

wao. Sisi katika Serikali tutaendelea kutimiza wajibu wetu wa

kuelimisha na kuhakikisha kuwa dawa za kufubaza vijijidudu

vya UKIMWI zinapatikana bure kwa waathirika waliofikia hatua

ya kutumia dawa hizo.

Page 14: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

14

Natoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Iringa kuongeza

juhudi maradufu kutokana na ukweli kwamba kiwango cha

maambukizi kiko juu mno. Watu waendelee kujitokeza kwa

wingi kupima kwa hiari ili kujua afya zao. Katika zoezi la

kupima kwa hiari hapa Iringa, watu 388,071 wamejitokeza

kupima. Jambo hili ni jema sana. Napenda pia kuchukua fursa

hii kuwasihi akina mama wajawazito wawe mstari wa mbele

kupima VVU ili wale walioathirika waitumie ipasavyo huduma

ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa

mtoto. Huduma hii inamfanya mtoto anayezaliwa na mama

aliyeathirika kuwa salama. Huduma hii ipo kote nchini na

inatolewa katika hospitali zote za Serikali.

Ndugu wananchi;

Ombi langu maalum kwa wanaume, kote nchini ambao

bado hawajafanyiwa tohara wajitokeze kwa wingi kufanya hivyo.

Madaktari wanasema kuwa mwanaume aliyefanyiwa tohara

anapunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya kuambukizwa VVU

Page 15: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

15

wakati wa kujamiiana. Naomba ieleweke kuwa sisemi mtu

akifanyiwa tohara hapati UKIMWI. La hasha. Ninachosema ni

kwamba ukimlinganisha na yule ambaye hakufanya hivyo,

uwezekano wa kuambukizwa unapungua. Wanasema asiye na

tohara ana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata michubuko

ambayo hurahisisha virusi kuingia kwenye mwili wake. Narudia

kusisitiza mtu akipata tohara asidhani yuko salama kabisa. Watu

wote lazima wachukue tahadhari stahiki.

Ndugu wananchi;

Ombi langu la pili ni kwa watu wanaotumia dawa za

kufubaza virusi vya UKIMWI wasiache kuzitumia. Wakiacha

kwa sababu yo yote ile wanavipa vijidudu nafasi kujiimarisha na

hivyo kuhatarisha maisha yao. Ombi langu la tatu ni kwa jamii

kuendelea kuwasaidia na kuwahudumia wenzetu ambao

wameathirika badala ya kuwanyanyapaa na kuwatenga. Na,

muhimu zaidi tuwasaidie watoto yatima na wazee ambao

wameachwa bila msaada wowote.

Page 16: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

16

Nawataka viongozi wote katika ngazi mbalimbali washiriki

kwa ukamilifu katika mapambano dhidi ya maradhi ya UKIMWI.

Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Afya na TACAIDS waendelee

kuongoza mapambano hayo bila kuchoka. Mimi bado naamini

Tanzania bila UKIMWI inawezekana iwapo tutazingatia masharti

ya kuepuka ugonjwa huu na kuwahudumia ipasavyo

walioathirika. Ushindi hauko mbali sana.

Mapambano dhidi ya Rushwa

Ndugu wananchi;

Mwaka huu, katika Mbio za Mwenge wa Uhuru wananchi

waliendelea kukumbushwa wajibu wao katika kupambana na

rushwa, kwa kauli mbiu isemayo “chukua hatua dhidi ya

rushwa sasa”. Ujumbe huu unakwenda sambamba na juhudi za

serikali za kupambana na rushwa nchini. Tunafahamu kuwa

rushwa ni adui wa haki na kikwazo kikubwa cha maendeleo ya

jamii na taifa. Nchi ikiwa imegubikwa na vitendo vya rushwa

itakosa maendeleo stahiki na watu watadhulumiwa haki zao.

Page 17: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

17

Hizo ndizo sababu kuu zilizoifanya serikali yetu ichukie

rushwa na kuchukua hatua za kupambana na uovu huu, tangu

nchi yetu ilipopata uhuru mpaka sasa. Kazi hiyo ngumu na yenye

changamoto nyingi inaongozwa na Taasisi ya Kuzuia na

Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Serikali imechukua na

itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha chombo

hiki ili kiweze kutimiza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.

Matokeo yake TAKUKURU sasa ina mtandao mpana zaidi. Ina

ofisi kila Mkoa na kila Wilaya, watumishi wameongezeka na

vitendea kazi pia.

Nafurahi kuona kuwa mafanikio ya kutia moyo yanaendelea

kupatikana ingawaje kazi iliyo mbele yetu bado ni kubwa. Sote

tunasoma na kusikia kupitia vyombo vya habari taarifa za

watumishi wa serikali, taasisi za umma pamoja na watu wengine

wanavyokamatwa na TAKUKURU kwa kujihusisha na vitendo

vya rushwa. Tangu mwaka 2006, kesi 63 zinazohusu rushwa

kubwa zimefikishwa Mahakamani. Baadhi zimeisha na

wahusika waliopatikana na hatia wameadhibiwa kwa mujibu wa

Page 18: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

18

sheria. Zipo pia tulizoshindwa, ni sawa katika nchi inayoheshimu

utawala wa sheria. Nyingine zinaendelea. Vile vile juhudi za

TAKUKURU zimeokoa fedha nyingi za umma. Kwa mfano, kwa

kipindi cha miaka mitatu, yaani kati ya 2010 hadi 2013, zaidi ya

shilingi bilioni 28 zimeokolewa ambazo zingeweza kunufaisha

watu wachache wanaoendeleza vitendo vya rushwa badala ya

taifa.

Naomba wananchi waendelee kutoa taarifa zitakazosaidia

kuwatambua na kuwakamata watoaji na wapokeaji rushwa.

Tukumbuke kuwa mafanikio katika mapambano haya

hayategemei Serikali au TAKUKURU peke yake. Ni mapambano

ambayo jamii ikijihusisha kwa ukamilifu ushindi mkubwa

utapatikana. Yanatuhusu sote kwani tukishinda, matunda yake

yatawafaidisha watu wote. Pia, napenda kutumia nafasi hii

kutoa wito kwa taasisi na idara zote za serikali zinazohusika moja

kwa moja katika vita dhidi ya rushwa zitimize ipasavyo wajibu

wake. Aidha pakiwepo na ushirikiano mzuri na mshikamano wa

dhati miongoni mwetu kwa hakika ushindi utapatikana.

Page 19: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

19

Tukifanya hivyo nina imani tutapata mafanikio makubwa zaidi

tena kwa haraka.

Dawa za Kulevya

Ndugu Wananchi;

Tatizo la biashara na matumzi ya dawa za kulevya

limeendelea kuwa moja ya changamoto kubwa zinazolikabili

taifa letu. Serikali imeendelea kufanya jitihada kubwa

kupambana na changamoto hiyo. Yapo mafanikio

yanayopatikana lakini bado tuna kazi kubwa ya kufanya mbele

yetu. Ukubwa wa kazi hiyo unaletwa na ule ukweli kwamba

watu wanaohusika ni wengi na wanazidi kuongezeka kila

kukicha kwa tamaa ya kupata utajiri wa haraka. Isitoshe wakati

wote washiriki wake wanabuni mbinu mpya za kusafirisha,

kusambaza na kuuza dawa hizo haramu. Pia ni kazi hatari kwani

wapambanaji kupoteza maisha si jambo la ajabu.

Pamoja na changamoto hizo, kwa vile matumizi ya dawa za

kulevya yana athari mbaya kwa watu wanaotumia na jamii kwa

Page 20: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

20

ujumla, Serikali haitachoka kufanya kila tuwezalo kupambana na

uhalifu huu mpaka ushindi upatikane. Wakibadili mbinu na sisi

tutabadili maarifa ya uchunguzi na utambuzi mpaka tuwapate.

Tutawahami ipasavyo watu wanaojitolea muhanga kupambana

na uovu huu. Mafanikio yanaendelea kupatikana. Kwa mfano,

kuanzia Januari hadi Septemba, mwaka huu (2013) watu 2000

(wafanya biashara na watumiaji wa dawa za kulevya)

wamekamatwa na aina mbalimbali ya dawa za kulevya ikiwa ni

pamoja na kilo 681 za dawa hatari ya heroine, zimekamatwa.

Watu hao kama wasingekamatwa wangeendelea kuuza na

kusambaza dawa za kulevya na kuathiri maelfu ya watu na hasa

vijana ambao ni nguvu kazi muhimu ya taifa letu na warithi wa

jamii na taifa wa kesho. Inatia uchungu sana kuona kuwa

tegemeo letu hilo linaangamizwa na watu wachache wenye

uroho usio na kifani wa kujipatia utajiri wa haraka, tena kwa

gharama yoyote ile.

Page 21: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

21

Ndugu wananchi;

Kwa niaba yenu, napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi

zangu za dhati kwa viongozi na wafanyakazi wote wa Tume ya

Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya na vyombo vingine

vya dola kwa kazi kubwa na nzuri inayoendelea kufanyika ya

kukabiliana na tatizo hili. Katika mapambano yetu

tunashirikiana na nchi na taasisi za nchi mbalimbali duniani.

Hivyo basi nazipongeza kwa dhati nchi na taasisi hizo rafiki kwa

ushirikiano wao ambao umetusaidia kupata mafanikio haya kiasi

tunayojivunia leo. Naomba ushirikiano huu uendelee kwani

umetusaidia kwa namna nyingi na umekuwa wa manufaa

makubwa.

Ndugu wananchi;

Nilishawahi kusema siku za nyuma kuwa ni makusudio

yangu na ya serikali kuanzisha chombo chenye uwezo na nguvu

kubwa zaidi ya kupambana na tatizo la dawa za kulevya nchini.

Mchakato wa kuunda chombo hicho umeanza na unaendelea

Page 22: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

22

vizuri. Hivi sasa tunayo Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za

Kulevya. Chombo hicho kipya kitakuwa na nguvu kubwa zaidi

kuliko Tume na hata kuliko kikosi kazi cha vyombo vyote vya

dola nilichokiunda kuipa Tume meno.

Ndugu wananchi;

Ili juhudi hizo zifanikiwe na ushindi upatikane itategemea

sana msaada, ushirikiano na ushiriki wa wananchi. Nawaomba

sana ndugu zangu wananchi wenzangu mshirikiane na vyombo

vya dola katika kupambana na usafirishaji, uuzaji na usambazaji

wa dawa za kulevya. Baadhi yenu mnawajua watu

wanaojihusisha na biashara hii haramu. Watajeni

washughulikiwe ipasavyo.

Wiki ya Vijana

Ndugu wananchi;

Kama nilivyosema awali leo pia tunaadhimisha wiki ya

vijana. Nimepata fursa ya kutembelea mabanda ya maonesho ya

Page 23: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

23

vijana ili kuona shughuli wanazozifanya. Nimefurahi na

kufarijika sana na kile nilichokiona. Vijana wanafanya kazi nzuri

na kwa kweli ni uamuzi wa busara kuwashirikisha katika sherehe

hizi kwani wanapata fursa ya kuonesha kazi wanazozifanya

katika kuboresha maisha yao na kuleta maendeleo ya taifa. Hii

pia ni nafasi nzuri kwa vijana kukutana, kufahamiana na

kubadilishana mawazo, ujuzi na taarifa muhimu zinazohusu

maisha na maendeleo yao. Kwa kuzingatia umuhimu na faida ya

maonesho haya, ni vyema kuangalia uwezekano wa

maadhimisho ya Wiki ya Vijana yakafanyika katika ngazi ya

Mikoa na kuhitimishwa Kitaifa kama tulivyofanya leo.

Ndugu wananchi;

Mimi na wenzangu Serikalini tunatambua na kuthamini

sana nafasi na mchango wa vijana katika kuchochea maendeleo

ya nchi yetu. Ndio maana Serikali inawekeza sana katika elimu

na mafunzo yao. Ndiyo maana pia Serikali imeamua katika

mwaka huu wa fedha kuongeza uwezo wa bajeti ya Wizara ya

Page 24: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

24

Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ili iweze kuwahudumia

vijana vizuri zaidi. Tutaendelea kuongeza bajeti hiyo ili Wizara

iweze kuwaongezea vijana mitaji ya biashara kupitia Mfuko wa

Taifa wa Maendeleo ya Vijana.

Nimefurahi kumsikia Mheshimiwa Waziri akiahidi hapa

kwamba baadhi ya vijana walioshiriki katika maonesho

niliyoyaona leo watafikiriwa kupewa mikopo kwa mujibu wa

taratibu zilizowekwa. Nawasihi vijana watakaopata mikopo

kupitia Mfuko huu pamoja na mifuko mingine ya uwezeshaji

wahakikishe wanaitumia vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa na

kuirejesha kwa wakati ili wengine nao wapate.

Maendeleo ya Mkoa wa Iringa

Ndugu wananchi;

Jana jioni nilipokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa wa Iringa

kutoka kwa Mkuu wa Mkoa, Dokta Christine Ishengoma. Natoa

pongezi nyingi kwa wananchi wa Iringa kwa juhudi zenu na

mafanikio mnayoyapata katika kujiletea maendeleo. Mkoa

Page 25: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

25

umeendelea kuwa wa kutegemewa katika kulipatia taifa chakula

hasa mahindi na sasa mwelekeo ni mzuri kwa mazao ya chai,

mpunga, mboga na matunda. Nawaomba muendelee na juhudi

zenu. Ongezeni maarifa na matumizi ya zana za kisasa na

pembejeo za kilimo ili tija iongezeke mpate mavuno mengi zaidi.

Mtatosheleza mahitaji yenu na mtapata ziada kubwa

itakayotumika kwingineko nchini na hata kuuzwa nje ya nchi.

Sisi katika Serikali tutaendelea kuwasaidia kwa upande wa

upatikanaji wa pembejeo, zana za kilimo, masoko, huduma

mbalimbali zikiwemo za ugani, fedha na kadhalika. Mkoa wa

Iringa utanufaika kupitia Mpango wetu wa Matokeo Makubwa

Sasa (Big Result Now) na SAGCOT.

Ndugu wananchi;

Serikali itaendelea kununua mahindi ya wakulima kupitia

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula. Hata hivyo ni vyema

nikaeleza wazi kuwa Hifadhi ya Taifa ya Chakula haitanunua

mahindi yote yaliyovunwa nchini. Ukomo wetu kwa sasa ni tani

Page 26: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

26

250,000 lakini tunaendelea kupanua uwezo wa maghala hadi

kufikia tani 400,000 ifikapo mwaka 2015. Tayari Hifadhi ya Taifa

wameshanunua tani 209,000 hivyo bado tani 41,000. Hivyo

nashauri wenzetu wa sekta binafsi nao wajitokeze kununua

mahindi ya wakulima.

Kwa kuwa hakuna kizuizi cha kuuza nje wanaweza kufanya

hivyo wakipenda. Hata hivyo, sisi tungependa kwanza wauze

hapa nchini. Naomba ieleweke kuwa hatutawauzia watu akiba

yetu ya mahindi katika Hifadhi ya Taifa ya Chakula kwa ajili ya

kuuza nje.

Ndugu wananchi;

Pamoja na kuendeleza kilimo katika Mkoa wa Iringa,

tutaendelea kuboresha barabara, na huduma za umeme, maji,

elimu na afya. Ninyi ni mashahidi kwamba utekelezaji wa ahadi

ya kujenga barabara ya lami kutoka Iringa hadi Dodoma

unakwenda vizuri na ukarabati wa barabara ya Morogoro –

Page 27: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

27

Tunduma kupitia Iringa na Mbeya umekamilika. Tunajipanga

kutekeleza ahadi zetu kwa baadhi ya barabara za Mkoa huu.

Kwa upande wa umeme vijijini tunaendelea kuvipatia

umeme vijiji 38 vya Mkoa huu na wakati huo huo tunajiandaa

kuvipatia umeme vijiji vingine 86. Tutaendelea kuongeza

upatikanaji wa maji vijijini na mijini. Aidha, tumeanza kutekeleza

mkakati kabambe wa kuboresha elimu kwa shabaha ya kutoa

fursa ya elimu kwa vijana wetu wengi na kuongeza kiwango cha

ufaulu. Haya yote tunayafanya chini ya mkakati mpya wa

kupata Matokeo Makubwa Sasa. Tutaongeza mara dufu juhudi za

kuboresha huduma ya afya.

Hitimisho

Ndugu wananchi;

Kabla ya kumaliza hotuba yangu niwakumbushe

Watanzania wenzangu kuwa mwaka ujao ni wa aina yake katika

nchi yetu. Kwanza tunasherehekea miaka 50 ya Mapinduzi

Matukufu ya Zanzibar, pili, tunasherehekea miaka 50 ya

Page 28: HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT - Tanzania...kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha 13 kupata fursa ya kukua

28

Muungano. Na tatu, kama mambo yatakwenda sawa tutapata

Katiba Mpya. Niwaombe Watanzania wenzangu tujiandae vyema

kufanikisha mambo yetu hayo matatu ya kihistoria. Naomba

nimalize kwa kuwashukuru tena wananchi na viongozi wa Mkoa

wa Iringa kwa kufanikisha sherehe hii muhimu. Nawashukuru

pia wadau mbalimbali ambao wamechangia kwa hali na mali

kufanya sherehe hizi zifanikiwe na kufana sana kama hivi.

Napenda kutumia nafasi hii pia kuwatakiwa ndugu zetu

Waislamu na Watanzania wenzangu wote heri ya Sikukuu ya Idd

El Hajj.

Baada ya kusema hayo sasa natamka rasmi kwamba

shughuli za Mbio za Mwenge wa Uhuru, kumbukumbu ya Baba

wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Wiki ya Vijana

kwa mwaka 2013 zimefikia kilele chake.

Asante sana kwa kunisikiliza.