52
Page 1 of 52 HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI NDUGU KABWE ZUBERI ZITTO (MB), WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI, KUHUSU MAPENDEKEZO YA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014 (Inatolewa chini ya Kanuni ya 105(8) ya kanuni za Bunge Toleo la mwaka 2013) _________________________________ 1. UTANGULIZI Mheshimiwa Spika, Bajeti ya serikali kimsingi ni ‘policy instrument’ inayotolewa kama mpango wa hati ya mapato na matumizi. Aidha hati hujumuisha makadirio ya makusanyo na matumizi ambayo Serikali imetayarisha na fedha iliyotumia au ambayo itatumika kwa mwaka ujao. Bajeti ya Serikali huoanisha makadirio ya fedha yanayohitajiwa na Wizara zote, idara zinazojitegemea, Wakala na Serikali za Mitaa kwa mwaka husika wa fedha. Bajeti ya Serikali ina sehemu tatu, yaani; makadirio ya mapato, matumizi ya kawaida ya kila siku na matumizi ya maendeleo. Matumizi ya kawaida na ya maendeleo ndiyo hufanya jumla ya fedha yote inayotumiwa na Serikali kwa mwaka wa fedha unaohusika. Bajeti ya Serikali pia inajulikana kama Taarifa ya Mwaka wa Fedha ya nchi.

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

  • Upload
    others

  • View
    29

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 1 of 52

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI NDUGU

KABWE ZUBERI ZITTO (MB), WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI, KUHUSU

MAPENDEKEZO YA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA

SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014

(Inatolewa chini ya Kanuni ya 105(8) ya kanuni za Bunge Toleo la

mwaka 2013)

_________________________________

1. UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, Bajeti ya serikali kimsingi ni ‘policy instrument’

inayotolewa kama mpango wa hati ya mapato na matumizi. Aidha

hati hujumuisha makadirio ya makusanyo na matumizi ambayo

Serikali imetayarisha na fedha iliyotumia au ambayo itatumika kwa

mwaka ujao. Bajeti ya Serikali huoanisha makadirio ya fedha

yanayohitajiwa na Wizara zote, idara zinazojitegemea, Wakala na

Serikali za Mitaa kwa mwaka husika wa fedha. Bajeti ya Serikali ina

sehemu tatu, yaani; makadirio ya mapato, matumizi ya kawaida ya

kila siku na matumizi ya maendeleo. Matumizi ya kawaida na ya

maendeleo ndiyo hufanya jumla ya fedha yote inayotumiwa na

Serikali kwa mwaka wa fedha unaohusika. Bajeti ya Serikali pia

inajulikana kama Taarifa ya Mwaka wa Fedha ya nchi.

Page 2: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 2 of 52

Mheshimiwa Spika, katika Bajeti Mbadala za mwaka 2011/12 na

2012/13 Kambi Rasmi ya Upinzani ilipendekeza masuala kadhaa ili

kusaidia kuongeza mapato ya Serikali kwa upande mmoja na kwa

upande wa pili kusaidia kupunguza umasikini wa kipato kwa

wananchi wa kawaida na hivyo kuboresha maisha yao. Masuala

tuliyoyapendekeza ni pamoja na:

1. Kupunguza misamaha ya kodi hadi kufikia asilimia moja ya

pato la Taifa kama wenzetu wa Uganda na Kenya. Serikali

ilikubaliana na pendekezo hili kwa maneno lakini imeshindwa

kulitekeleza licha ya kutoa ahadi za kufanya hivyo kila mwaka.

Hivi sasa misamaha ya kodi imefikia asilimia 4.3 ya Pato la Taifa.

2. Kuongeza makusanyo ya mapato ya ndani hadi kufikia asilimia

20 ya Pato la Taifa. Katika Bajeti ya Mwaka huu Serikali

inatarajia kufikia lengo hili ambalo lilitolewa na Kambi ya

Upinzani Bungeni katiika bajeti zilizopita licha ya miaka yote

kubezwa kwamba haiwezekani. Iwapo Misamaha ya kodi

ikipunguzwa, utoroshaji fedha nje ukadhibitiwa na ukwepaji

kodi katika idara ya forodha ukapunguzwa, Tanzania inaweza

kukusanya asilimia 25 ya Pato la Taifa kama mapato ya ndani.

Bajeti mbadala ya upinzani inaelekea huko.

3. Kuongeza Kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wa

umma hadi Tsh 315,000 kwa Mwezi. Inashangaza kuwa katika

mwaka wa fedha 2013/14 Serikali imeshindwa hata kutangaza

Page 3: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 3 of 52

kima cha chini licha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania kueleza katika hotuba yake katika sherehe za Mei

Mosi huko Mbeya na Waziri wa Utumishi kuahidi kuwa kima cha

chini kitatangazwana Waziri wa Fedha.

4. Kuweka kiwango cha chini cha kodi ya Mapato kwa

mwananchi (PAYE) kuwa asilimia tisa (9) na kitozwe kwa

mapato yanayozidi Tshs 150,000. Kwa mwaka wa pili mfululizo

Serikali imeendelea kuwahadaa wafanyakazi nchini kwa

kushusha kiwango hicho kwa asilimia moja tu.

5. Kuifanyia marekebisho sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka

2004 kwa kufuta sehemu ya Kodi ya Mapato inayotoa fursa

kwa kampuni za madini kutumia sheria ya Kodi ya Mapato ya

mwaka 1973 iliyofutwa (grandfathering). Pendekezo letu

lilikuwa na lengo la kutaka kuweka mfumo wa ‘straightline

method of depreciation’ ya asilimia 20 badala ya sasa ambapo

Kampuni za Madini ufanya ‘100 percent depreciation’ kwenye

mitambo yao mwaka wa kwanza na hivyo kuchelewesha

kulipa ‘Corporate Tax’. Pendekezo hili ambalo lingeipatia

Serikali mapato mengi na kwa sasa bado halijatekelezwa kwa

Kampuni za madini zenye mikataba.

6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama

tulivyofanya kwa mwaka uliopita na kwamba kila mwenye

nyumba ya kupangisha lazima atambuliwe na kulipa kodi

inavyostahili kutokana na biashara ya kupangisha

Page 4: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 4 of 52

nyumba/vyumba. Serikalibado haijatekeleza pendekezo hili,

hakuna sera ya nyumba na hivyo Serikali kupoteza mapato

mengi sana kwenye sekta ya nyumba, kodi za nyumba kuwa

juu sana na kuumiza vijana wanaoanza maisha na kutozwa

kwa mwaka mzima.

7. Kushushwa kwa tozo ya kuendeleza stadi (skills development

levy – SDL) kutoka asilimia sita (6) ya sasa mpaka asilimia nne

(4). Katika pendekezo hilo tulishauri kuwa waajiri wote walipe

kodi hii ikiwemo Serikali na Mashirika ya Umma. Serikali

imechukua pendekezo hili kwenye mapendekezo ya Bajeti ya

mwaka 2013/14 lakini bila kuhusisha mwajiri Mkuu, Serikali. Ni

vema kodi hii ilipwe na waajiri wote nchini na ishuke kuwa

asilimia 4.

8. Kuwepo na utaratibu wa kuweka stiker maalumu kwa kazi za

sanaa zinazotolewa na mamlaka za serikali kuonyesha uhalali

wa muuzaji wa kazi hizo ili wasanii wanaozitengeneza

wanufaike na kazi zao. Pendekezo hili lilikubaliwa na Serikali na

hivi sasa TRA na COSOTA wameanza kufanya kazi hii ili

kuhakikisha wasanii wetu wanafaidi jasho lao.

9. Kuzuia kabisa kusafirisha ngozi ghafi kwenda nje ya nchi na

badala yake kuwe na mpango wa kuziongezea thamani na

kuzitumia ngozi ghafi hapa nchini ili kuleta tija katika uchumi

wa taifa kwa kutengeneza ajira na kuongeza thamani ya

mauzo nje. Serikali iliamua kupandisha ushuru. Kambi ya

Page 5: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 5 of 52

Upinzani Bungeni inaamini kuwa kuna haja kubwa ya kuzuia

kuuza mazao ghafi nje ili kukuza ajira za ndani na kuongeza

thamani ya mauzo yetu nje.

10. Kujenga Mazingira ya ukuaji wa uchumi vijijini (rural

growth) kwa kuboresha miundombinu ya umeme, barabara,

maji na Umwagiliaji. Tulipendekeza kutumia shilingi bilioni 450

kila mwaka kwa ajili ya kutekeleza azma hii. Fedha hizi

zitasimamiwa na Mamlaka ya Maendeleo Vijijini (Rural

Development Authority) ambayo nayo tulipendekeza iundwe

chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Pendekezo hili Serikali imelidharau

na madhara yake ni kuwa maendeleo ya vijijini hayana uratibu

mzuri na hivyo kusahaulika kabisa.

11. Kukarabati Reli ya Kati na matawi yake ya Tanga - Arusha

na Mpanda. Tuliitaka serikali kutenga Tsh 443 bilioni kwa

RAHCO kwa ajili ya maendeleo ya reli nchini. Serikali imetenga

fedha kidogo sana kwenye miundombinu ya Reli. Mwaka huu

tunapendekeza kodi maalumu ya kuendeleza Reli.

12. Kujenga uwezo wa viwanda vya ndani ili kuviwezesha

kuzalisha na kuuza nje bidhaa za kilimo na mifugo

zilizoongezewa thamani. Tuliitaka serikali kupiga marufuku

uuzaji nje wa korosho ghafi kama ilivyovyo kwa ngozi ghafi kwa

kuanzia. Serikali haijaweka mkakati wowote wa kuhakikisha

korosho yote nchini inabanguliwa kabla ya kuuzwa nje.

Page 6: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 6 of 52

13. Kuboresha elimu na afya hasa kwa shule na

zahanati/Vituo vya Afya vilivyo katika maeneo ya vijijini kwa

kutoa motisha kwa wafanyakazi wa sekta hizi walio kwenye

Halmashauri za Wilaya. Tulipendekeza pia kuanzishwa kwa

posho za mazingira magumu ya vijiji sawa kwa kiwango cha

mara moja na nusu ya mishahara yao. Serikali haijatekeleza

pendekezo hili.

14. Kuanzisha pensheni ya uzeeni kwa wazee wote nchini

wenye umri wa zaidi ya miaka 60. Serikali ipo kimya kuhusu

suala hili muhimu sana kwa wazee nchini.

15. Kuanzisha Chuo Kikuu cha Mtwara (Mtwara University for

Petroleum Studies) ili kufundisha wataalamu wa kutosha wa

sekta ya Mafuta na Gesi na kuliandaa Taifa kuwa na wasomi

mahiri wa maeneo hayo na hivyo kufaidika na utajiri wa

Mafuta na Gesi uliopo nchini kwetu. Serikali ipo kuhusu

pendekezo hili ambalo lingeweza hata kupunguza matatizo

haya yanayoendelea mkoani Mtwara.

16. Kupunguza mzigo wa matumizi ya magari ya Serikali kwa

kupiga mnada baadhi ya ‘mashangingi’ na kuweka mfumo

wa kukopesha magari kwa watumishi wote wa umma

wanaostahili magari kama alivyofanya Gavana wa Benki Kuu

ya Tanzania. Katika Bajeti ya serikali ya mwaka ujao wa fedha

imeahidi kuwakopesha watumishi wake magari lakini hakuna

uhakika iwapo hilo liotafanyika.

Page 7: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 7 of 52

17. Aidha tulipendekeza hatua ili kuweza kukabiliana na

ukwepaji wa kodi unaofanywa na makampuni makubwa ya

kimataifa (Multinational Corporations) na hatimaye

kuliongezea taifa mapato. Hatua hizo ni pamoja na:

(i) Kutunga sheria kwa kuimarisha zaidi sheria ya Kodi ya

Mapato ya mwaka 2004 kwamba, mikopo ya makampuni

kwenye uwekezaji, kwa sababu za kikodi, isizidi asilimia 70

ya mtaji wote uliowekezwa na hii ianze mara moja bila

kujali mikataba iliyopo. Pendekezo hili limetekelezwa

kikamilifu.

(ii) Kutunga sheria kuhakikisha kwamba riba kwenye mikopo

kutoka Makampuni yanayohusiana (sister companies)

haitaondolewa kwenye kutoza kodi (not tax deductible).

Pendekezo hili limetekelezwa kikamilifu.

(iii) Kuhakikisha kwamba serikali inakusanya kodi kwa

kiwango cha asilimia 30 kama ‘ongezeko la mtaji’

(‘capital gains’) kutokana na mauziano ya Kampuni

yoyote ambayo mali zake zipo Tanzania. Pendekezo hili

limetekelezwa kikamilifu. Hata hivyo Wizara ya Nishati na

Madini imeshindwa kushirikiana na TRA kupata kodi ya

tshs 329 bilioni kutoka kampuni ya Mantra Resources

baada ya kuuza mradi wa Mkuju Uranium.

Page 8: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 8 of 52

Mheshimiwa Spika, baadhi ya mapendekezo yetu yalichukuliwa na

Serikali ya CCM na kuyafanyia kazi kama nilivyoonyesha hapo juu.

Kwa yale ambayo yalitekelezwa vizuri yameleta matokeo mazuri.

Lakini kuna mapendekezo mengine serikali imeyachukua lakini

imeshindwa kuyatekeleza kama ambavyo tulishauri. Licha ya

mapendekezo yaliyotekelezwa vizuri kuleta sifa kwa serikali, Kambi

Rasmi ya Upinzani itaendelea kuwaonyesha njia serikali na CCM ya

namna bora na rahisi ya kuiondoa nchi katika giza hili la uchumi na

lindi la umasikini lililotengenezwa na Serikali hii ya CCM kwa

makusudi lakini sasa inashindwa kuwa na mkakati makini wa kuweza

kutoka.

2. DENI LA TAIFA (FUNGU 22)

Mheshimiwa Spika, Deni la Taifa limeendela kuwa changamoto

kubwa Kwa uchumi wetu. Kukua Kwa Deni la Taifa kusababisha

bajeti ya Serikali kuendelea kuwa tegemezi na hivyo kushindwa

kutatua kero za kiuchumi za wananchi. Kwa bahati mbaya

wananchi wengi hawaelewi undani wa deni la taifa na athari zake

katika maisha yao ya kawaida. Jambo la kusikitisha ni kwamba

Serikali imekuwa ikitumia mwanya wa wananchi kutokufahamu kwa

undani athari za deni la taifa kuendelea kukopa mikopo mikubwa

yenye masharti ya kibiashara (kwa maana ya riba kubwa).

Kuendelea kukopa Kwa namna hiyo kunaendelea kuwabebesha

walipa kodi wa Tanzania mzigo mkubwa wa madeni ambayo

Page 9: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 9 of 52

yanazidi kufanya hali ya maisha kwa wananchi iendelee kuwa

ngumu kwa kuwa Serikali inatumia fedha nyingi kulipa madeni

badala ya kuzitumia fedha hizo kugharamia miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa

Hesabu za Serikali, deni la taifa liliongezeka kwa asilimia 38 kutoka

Shilingi trilioni 7.6 mwaka 2008 mpaka Shilingi trilioni 10.5 mwaka

2009/2010. Mwaka 2010/2011 deni hilo liliendelea kuongezeka

kutoka shilingi trilioni 10.5 na kufikia kiasi cha shilingi trilioni 14.441

Aidha, katika mwaka wa fedha 2011/2012 deni hilo liliendelea

kuongezeka zaidi kutoka shilingi trilioni 14.441 na kufikia kiasi cha

shilingi trilioni 16.975. Kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa

Taifa mwaka 2012, deni la taifa liliongezeka kwa kasi ya ajabu

kutoka shilingi trilioni 18.8 (Desemba 2011) hadi kufikia shilingi trilioni

22.7 (Desemba, 2012).

Mheshimiwa Spika, hata hivyo kwa mujibu wa hotuba ya Bajeti ya

Waziri wa Fedha aliyoisoma Juni 13, 2013 akiwasilisha bungeni

mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi

kwa mwaka 2013/2014, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi machi

2013, deni la Taifa lilikuwa limeongezeka tena na kufikia shilingi

trilioni 23.7. Kati ya hizo shilingi trilioni 18.3 zinawakilisha deni la nje,

ikiwa ni sawa na asilimia 77 ya deni lote la Taifa.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa

na CHADEMA inatumia fursa hii kuwajulisha wananchi wote wa

Page 10: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 10 of 52

Tanzania kwamba hali duni ya maisha waliyo nayo na umasikini

mkubwa walio nao unasababishwa kwa kiasi kikubwa na Serikali

kukopa mno nje jambo ambalo linaongeza ugumu wa maisha.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapenda pia kuwajulisha

wananchi kwamba jukumu la kulipa deni la taifa kimsingi ni la

wananchi na wanalilipa kwa njia mbali mbali zikiwemo kodi

mbalimbali jambo ambalo linafanya maisha yao yaendelee kuwa

magumu.

Kwa mfano ukichukuwa jumla ya deni la taifa, ukaligawanya kwa

idadi ya wananchi wote wa Tanzania, utakuta kwamba kila mtu

(bila kujali mtoto mchanga, mzee, mlemavu, mwanafunzi, asiye na

ajira nk) anadaiwa kiasi cha shilingi 526,977 kama inavyoonyeshwa

kwenye jedwali Na 1 hapa chini;

Jedwali Na. 1 Mgawanyo wa Deni la Taifa kwa Kila Mtanzania

DENI LA TAIFA1 IDADI YA WATU TANZANIA2

Shilingi 23,673,530,000,000 44,928,923

Deni la taifa ÷ Idadi ya Watu = Deni la Taifa kwa kila mtu

Hivyo; Sh. 23,673,530,000,000 ÷ 44,928,923 = Sh. 526,977

1 Deni la Taifa kwa Mujibu wa Hotuba ya Waziri wa Fedha ya tarehe 13 Juni, 2013 ni Shilingi Trilioni 23.7

2 Kwa Mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya 2012, Idadi ya Watu Tanzania ilikuwa ni 44,928,923

Page 11: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 11 of 52

Mheshimiwa Spika, ikiwa mtanzania masikini anayeishi chini ya dola

moja au shilingi 1,500 kwa siku angeamua kulipa deni hili kwa

shilingi 500 kwa siku ili abaki na shilingi 1,000 za kutumia kwa siku hiyo,

itamlazimu kulipa shilingi 15,000 kwa mwezi kama malipo ya deni la

taifa. Hii ina maana kwamba kwa mwaka mmoja atalazimika kulipa

180,000. Kwa maana hiyo, iwapo kila mtu angechukua jukumu la

kulipa deni hili la taifa kwa kiwango hicho, ingechukua miaka mingi

kumaliza kulilipa deni hilo.

Mheshimiwa Spika, kiasi hiki cha fedha cha shilingi 15,000 ambacho

kila mtanzania atatakiwa alipe kila mwezi kwa ajili ya deni la Taifa

kingekuwa kinabaki kwa mwananchi na akakifanyia ujasiriamali

angeweza kuondokana kabisa na umasikini. Hii ni kwa sababu

kiwango hicho hakina riba na atakuwa anakipata kwa miaka mitatu

mfululizo. Lakini kwa sababu Serikali imeamua kuwafukarisha

wananchi wake kwa kukopa kupita kiasi, sasa mwananchi

analazimika kurudi nyuma kimaendeleo kwa kutoa shilingi 15,000 kila

mwezi kwa miaka mitatu mfululizo kulipa deni la taifa. Fedha hizo

hazimjengi mwananchi kiuchumi bali zinambomoa kwa kuwa

zinatoka bila faida yoyote kwake.

Page 12: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 12 of 52

Mheshimiwa Spika, serikali imekuwa ikijinasibu kuwa inakopa fedha

hizi kwa ajili ya mitradi ya maendeleo. Lakini inashangaza kuwa

fedha hizo zilizokopwa zimetumika lakini miradi hiyo ambayo

imetumia fedha hizi haijaleta hayo maendeleo ambayo serikali

imekuwa ikiyasema na kumwondolea mwananchi wa kawaida

umasikini. Fedha hizo zimeendelea kutumika zikimwongezea

mwananchi deni na umasikini. Hii inathibitishwa na uhalisia kwamba

licha uchumi kukua kwa kasi ya asilimia saba kwa mwaka kwa

miaka kumi mfululizo, umasikini umepungua kwa asilimia mbili tu na

idadi ya watu masikini wa kutupwa imeongezeka kwa kiwango cha

watu milioni mbili na nusu katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Mheshimiwa Spika, hali ya hatari zaidi ni kwamba kuna madeni

mengine ambayo hayajajumuishwa kwenye Deni la Taifa na hivyo

kulifanya Deni halisi la Taifa kuwa kubwa kuliko linaloonyeshwa

kwenye taarifa mbalimbali za Serikali na ile ya CAG. Kwa mfano,

kuna madai ya PSPF ya shilingi bilioni 716.6 kati ya madai ya shilingi

trilioni 6.5 ambayo Serikali imekubali kuyalipa.

Mheshimiwa Spika, katika taarifa hiyo ya CAG ya mwaka 2012, kuna

jumla ya shilingi bilioni 619 ambazo zipo kwenye Deni la Taifa lakini

hazina vithibitisho. Katika ripoti yake Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa

Hesabu za Serikali ameandika: “Uhakiki wa mchanganuo wa

madeni ya Taifa kama ulivyokuwa tarehe 30 Juni 2012 ulibaini

kuwepo kwa marekebisho ya Deni ya shilingi 619.8 bilioni ambao

uongozi haukuweza kutoa maelezo ya kuridhisha”.

Page 13: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 13 of 52

Udhaifu kama huu unazua hisia kwamba kitengo cha Deni la Taifa

kinatumika kuiba fedha za umma kwa kisingizio kwamba ni malipo

ya Deni la Taifa. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na

CHADEMA inaitaka Serikali kutoa maelezo yaliyonyooka mbele ya

Bunge hili kuelezea ni kwanini shilingi bilioni 619.8 zimeongezwa

kwenye deni la taifa bila maelezo wala vielelezo vyovyote?

Uhimilivu wa Deni la Taifa

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa muda

mrefu imekuwa ikiitaka Serikali ipunguze au iachane kabisa na

mikopo yenye masharti ya kibiashara ambayo inazidi kuliongeza

Deni la Taifa. Kinyume na nia hii njema ya Kambi ya Upinzani ya

kujitegemea kibajeti, Serikali hii ya CCM imeendelea kupuuza

mawazo haya mazuri kwa kisingizio kwamba Deni la Taifa ni himilivu

na kwamba nchi yetu inakidhi vigezo vya kimataifa vya

kukopesheka.

Mheshimiwa Spika, kwa taarifa ni kwamba baadhi ya vigezo vya

kimataifa ambavyo Serikali inasema Tanzania imekidhi na hivyo

inaweza kukopesheka vimeshapitiliza ukomo wake na kwa maana

hiyo deni la taifa sio himilivu tena (Tazama Jedwali Na. 3).

Jedwali Na. 3 Matokeo ya Upimaji wa Uhimilivu wa Deni la Taifa

Kiashiria Matokeo (Asilimia) Ukomo

Deni la Taifa kwa sasa/Pato

la Taifa

18.9 50

Page 14: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 14 of 52

Chanzo: Kitabu cha Hali ya Uchumi 2012 uk. 77

Mheshimiwa Spika, matokeo ya upimaji wa uhimilivu wa deni la

taifa uliofanywa na Serikali kwa kutumia kigezo cha asilimia ya

uwiano wa Deni la Taifa na Pato la Taifa si ya kweli kwani kwa

kutumia hesabu rahisi tu za kugawanya na kutafuta asilimia ambazo

mwanafunzi wa darasa la pili anaweza kufanya ni kwamba tayari

tumeshavuka ukomo wa kukopesheka. Hii ni kwa sababu uwiano wa

deni la taifa na pato la taifa kwa sasa ni asilimia 53 wakati ukomo

wa kukopesheka ni asilimia 50. (Tazama Jedwali Na. 3)

Jedwali Na. 3 Uchambuzi wa Ustahimilivu wa Deni la Taifa

Kiashiria Matokeo (asilimia) Ukomo

Deni la Taifa ÷ Pato la Taifa

23.7tr ÷44.7tr = 0.53 0.53x100 = 53.02%

50

Chanzo: Uchambuzi wa Kambi ya Upinzani

Utata katika Deni la Taifa (Fungu 22)

Mheshimiwa Spika, mfumo wa sasa wa kuweka pamoja malipo ya

Deni la Taifa na malipo kutoka mfuko mkuu wa Hazina hauweki

uwazi wa kutosha. Jambo lenye utata katika fungu 22 - Deni la Taifa

- ni kwamba fungu hilo linajumuisha huduma za Mfuko Mkuu wa

Hazina (Consolidated Fund Services - CFS). Kwa mujibu wa

Randama ya Wizara ya Fedha, Idara ya Mhasibu Mkuu, Fungu 22 –

Deni la Taifa - jumla ya shilingi 870,717,882,000 zimetengwa ndani ya

Page 15: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 15 of 52

Mfuko Mkuu wa Hazina (ambazo zimechanganywa pamoja na Deni

la Taifa) kwa ajili ya ajili ya malipo mbalimbali kama ilivyooneshwa

kwenye jedwali Na 4.

Jedwali Na 4. Bajeti kwa ajili ya CFS Others

S/N NDANI YA CFS OTHERS KUNA MATUMIZI YAFUATAYO FEDHA

ZILIZOTENGWA

2013/2014

1. Mishahara ya Majaji, Makamishna wa Tume ya Haki za

Binadamu na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za

Serikali

6,311,772,000

2. Mafao ya Wastaafu wanaofanya kazi kwa Mkataba 3,757,060,000

3. Stahili za Majaji 1,844,840.000

4. Michango ya Mwajiri kwa Watumishi wa Serikali Kuu na

Serikali za Mitaa kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

556,809,310,000

5. Malipo ya Pensheni kwa ajili ya wastaafu hai, Mirathi,

watumishi walio katika Mikataba Serikalini na Stahili za

Majenerali kwa kila mwezi

213,498,000,000

6. Gharama za Huduma za Benki (bank charges) 6,400,000,000

7. Ada ya Usimamizi wa Amani za Serikali 1,700,000,000

8. Riba ya Mapungufu kati ya Mapato na Matumizi (Interest on

net deficit position)

80,000,000,000

9 Gharama za usafiri na malazi na posho kwa ajili ya uhakiki

na usuluhuishi wa taarifa za madeni.

396,900,000

JUMLA 870,717,882,000

Chanzo: Randama ya Wizara ya Fedha (Fungu 22) uk. 17

Page 16: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 16 of 52

Mheshimiwa Spika, mbali ya hayo fungu 21 kasma 290700

“contingencies non-emergency” kasma ndogo 290704: Domestic

Debts - Sh 436,721,151,000 ambayo matumizi yake yanaonyeshwa

kama: gharama za upigaji kura za maoni, kuhuisha Daftari la

wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi ujao, kulipia madeni ya

wakandarasi na watumishi, gharama za Bunge la Katiba, deni la

HESLB kwa mfuko wa PSPF, mfuko wa maendeleo ya Jimbo, Ukaguzi

wa shule za msingi na Ssekondarina mengine mengi. Kambi Rasmi ya

Upinzani inaona kuwa matumizi haya hayana mtiririko unaoeleweka.

Kambi inaamini kuwa kuna uwezekano mkubwa fungu hili likatumika

kuweka fedha ambazo badaye zitakuja kukwapuliwa na wajanja.

Hivyo basi, inamtaka Mheshimiwa Waziri wa Fedha atoe uchambuzi

wa gharama ya kila kimoja kwani kurundika mambo yote kwenye

kapu moja kunaweza kusababisha jambo moja kulipwa hata mara

kumi na kusiwepo ushahidi wake wa malipo na pia watu wakikosa

ushahidi wa kuhoji.

Mheshimiwa Spika, kitendo cha kuchanganya deni la taifa na

matumizi haya ya fedha yanayohusu Mfuko Mkuu wa Hazina

kunaweza kutoa mwanya mkubwa wa ubadhirifu na matumizi

mabaya ya fedha za umma kwa kisingizio cha Deni la Taifa. Kwa

sababu hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na

CHADEMA inataka mambo makubwa mawili yafanyike kama kama

ifuatavyo:

Page 17: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 17 of 52

1. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali afanye

ukaguzi maalum (Special Audit) katika kitengo cha Deni la

Taifa (fungu 22) ili tuweze kujua mikopo hii tunayoichukua

kila wakati inatumika kufanyia nini, na miradi iliyotekelezwa

kama ni miradi ya kipaumbele kwa mujibu wa mpango

wa taifa wa maendeleo. Aidha, ukaguzi huu maalum

utatuwezesha kama taifa kujua kiwango halisi cha Deni la

Taifa ambalo tunadaiwa.

2. Serikali itenganishe haraka iwezekanavyo deni halisi la

Taifa na matumizi mengine yanayohusu Mfuko Mkuu wa

Hazina (Consolidated Fund Services – Others) ili kuziba

mianya ya ubadhirifu au matumizi mabaya ya fedha za

umma kwa kisingizio cha Deni la Taifa. Tunapendekeza

kwamba Fungu namba 22 liwe la Deni la Taifa pekee na

Fungu lingine litengenezwe kwa ajili ya CFS.

3.0 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI.

3.1 KODI KWENYE MAFUTA

Mheshimiwa Spika, Waziri wa Fedha ameendeleza utaratibu wa kila

mwaka wa kupandisha kodi kwenye bidhaa zile zile ikiwemo mafuta

bila kutilia maanani kuwa kufanya hivyo kunahatarisha maisha ya

wananchi kwani kutaongeza gharama ya karibu kila kitu. Hotuba ya

Page 18: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 18 of 52

bajeti iliyowasilishwa na Serikali haijalenga kabisa katika kukuza

ustawi wa wananchi badala yake imejikita katika kuongeza mzigo

mkubwa wa umasikini kwa wananchi, kuongeza mfumuko wa bei

na kuzorotesha uchumi wa Tanzania kama nitakavyoelezea hapa

chini.

Wakati Bajeti ya mwaka 2012/13 ililenga kupunguza gharama za

maisha kwa mwananchi, Bajeti ya Mwaka 2013/14 kwanza haina

malengo mahususi na pili inafuta mafanikio yote yaliyopatikana

katika sera ya Bajeti ya mwaka uliotangulia.

Mheshimiwa Spika, moja ya vyanzo vipya vya mapato kwa mujibu

wa hotuba ya bajeti ya Waziri wa Fedha ni pamoja na ongezeko la

ushuru wa mafuta kama ifuatavyo.

i. Ushuru wa Dizeli umeongezwa kutoka shilingi 215 kiwango cha

sasa kwa lita hadi shilingi 217.

ii. Ushuru wa Petroli umeongezwa kutoka shilingi 339 kiwango cha

sasa kwa lita hadi shilingi 400, ikiwa ni ongezeko la shilingi 61.

Mheshimiwa Spika, Bajeti imeongeza pia tozo kwenye mafuta (fuel

levy). Kwa mujibu wa maneno ya Waziri kwenye hotuba yake ni

kwamba ameongeza tozo kwenye petroli peke yake lakini ukweli ni

kwamba, ongezeko hilo litaiathiri pia bei ya dizeli na hii ni kwa mujibu

wa Sheria ya Ushuru wa Barabara na Mafuta Sura 220 (the Road

and Fuel Tolls Act). Neno ‘fuel’ limetafsiriwa kama ‘petroli aina ya

supa, au kawaida, na dizeli kwa matumizi ya kuendeshea gari’

Page 19: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 19 of 52

("fuel" means petrol, whether super or regular, and diesel for use in

the propulsion of a vehicle).

Mheshimiwa Spika, kwa mapendekezo hayo ya Serikali, shilingi 63

kwa lita inaongezeka kwenye gharama za mafuta. Hii itaathiri bei ya

mafuta ya dizeli na petroli, na si petroli peke yake. Hata hivyo, hilo si

ongezeko peke. Kuna ongezeko zaidi lipo kwenye mapendekezo ya

Serikali kupitia hotuba ya Waziri wa Fedha Ukurasa wa 77 la ushuru

wa Petroli (petroleum levy) wa kiwango cha shilingi 50 kwa lita.

Mheshimiwa Spika, ni vyema Bunge lako tukufu na wananchi

wakaelewa kwamba ‘petroleum’ inahusisha nishati zote za mafuta

katika hali ghafi kwa kuwa aina nyingine zote za mafuta

zinatengezwa kutokana na petroleum), ikiwa ni pamoja na gesi

katika hali kimiminika (liquid gas), grisi (grease), parafini (paraffin)

dizeli, mafuta ya taa, mafuta ya ndege.

Na kwa mujibu wa Sheria ya Uhifadhi wa Petroleum - the Petroleum

(Conservation) Act, Sura ya 392, Petroleum imetafisiriwa kama

("petroleum" includes any inflammable liquid or liquid gas made

from petroleum, coal, schist, shale, peat, or any other bituminous

substance or from any product of petroleum).

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa hotuba hiyo, majumuisho ya

maongezeko mahusui ya moja kwa moja ya ushuru katika mafuta

ya dizeli, petroli, na mafuta ya taa, na ongezeko la ujumla la

petroleum yanatoa jumla inayoonekana kwenye jedwali hapa chini.

Page 20: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 20 of 52

AINA YA

MAFUTA

ONGEZEKO

MAHUSUSI

(shilingi)

FUEL LEVY

(shilingi)

ONGEZEKO LA

JUMLA(PETROLEUM)

(shilingi)

JUMLA

(shilingi)

Dizeli 2 63 50 115

Petroli 61 63 50 174

Mafuta

ya taa

- - 50 50

Mheshimiwa Spika, ongezeko hili ni dhahiri kuwa linakwenda

kuongeza gharama za usafirishaji mali, gharama za usafirishaji

chakula, gharama za uzalishaji malighafi na bidhaa kwenye

viwanda vidogo na vikubwa, yanaenda kuongeza mfumuko wa bei,

na matokeo yake kupaisha gharama za maisha kwa jumla yake na

kudumisha umasikini nchini.

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na

CHADEMA inapinga kubadilisha sheria ya Petroli sura 392 na

kuongeza kitu kinaitwa ‘Petrolium Levy’ kwa ajili ya kuongeza shilingi

50 kwa kila lita ya mafuta na ziweze kupelekwa REA. Kiasi ambacho

kitakusanya kupitia ushuru huu ni shilingi bilioni 123.725 kwa mwaka

ujao wa fedha.

Page 21: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 21 of 52

Hatupingi wazo la kuongeza fedha kwa ajili ya REA, siku zote kambi

ya Upinzani imekuwa ikitaka REA kuwezeshwa zaidi ili kubadilisha

maisha ya wananchi vijijini kwa kuwapa nishati ya Umeme. Fedha

hizi zingeweza kupatikana kwa njia nyingine ambazo hazimuumizi

mwananchi. Serikali imekwepa jukumu la kupunguza matumizi yasio

ya lazima ili kupata fedha za miradi ya maendeleo na badala yake

inakwenda kwenye njia rahisi lakini zenye kumuumiza mwananchi.

Ikumbukwe kwamba mwaka 2012/13 Bunge lilitenga zaidi ya shilingi

bilioni 300 kwa ajili ya umeme vijijini lakini fedha zote hizo

hazikwenda REA na badala yake zikaenda kununua mafuta ya

kuendesha mitambo ya kukodi ili kuzuia mgawo wa umeme.

Hakuna dhamana yeyote kuzuia fedha hizi zitakazopatikana

kutokana na kuongeza ushuru wa mafuta kwenda kuwanufaisha

asilimia 18 tu ya Watanzania ambao wameunganishwa kwenye

mtandao wa umeme.

Mheshimiwa Spika, katika hotuba ya Bajeti Mheshimiwa Waziri

amependekeza kufanywa kwa marekebisho ya sheria ya ushuru wa

mafuta na kuongeza kodi ya fuel levy kutoka shilingi 200 kwa lita

hadi shilingi 263 kwa lita kiasi ambacho ni sawa na ongezeko la

asilimia 31.5. Waziri wa Fedha amesema hatua hii inalenga

kuiongezea serikali mapato ya kiasi cha shilingi bilioni 155.893 katika

mwaka ujao wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya

barabara. Kambi ya Upinzani Bungeni inapinga nyongeza hii kwani

itaongeza gharama za maisha kwa mwananchi.

Page 22: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 22 of 52

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza

kwamba Bunge likatae mapendekezo yote ya kuongeza kodi

kupitia The Road and Fuel Tolls act Sura ya 220, Sheria ya Ushuru wa

Bidhaa Sura 147 eneo la Ushuru za bidhaa za Petroli na Sheria ya

Utafutaji Mafuta, sura ya 392. Mapendekezo haya ya Serikali

yataongeza gharama za maisha kwa mwananchi masikini. Mapato

yatakayopotea kutokana na kukataa mapendekezo haya

yatafidiwa na hatua za kiutawala na kikodi tutakazopendekeza

ikiwemo kupunguza matumizi, kupunguza misamaha ya kodi na

kuzuia utoroshaji fedha.

3.4 SHERIA YA KODI YA MAPATO – sura 332 NA USHURU WA BIDHAA –

SURA 147

Mheshimiwa Spika, Serikali inapendekeza mabadiliko kwenye sheria

ya kodi ya mapato ikiwemo kupunguza kiwango cha chini cha

kulipa PAYE na kuanza kutoza kodi kwenye huduma za kusafirisha

fedha kwa kupitia simu za mkononi. Vile vile Serikali inataka

kubadilisha sheria ya ushuru wa bidhaa kwa kuwalipisha kodi

wananchi asilimia 14.5 kwenye huduma zote za simu za mkononi (all

mobile phone services) na kwamba asilimia 2.5 ziende kugharamia

elimu nchini.

Mheshimiwa Spika, ushuru wa bidhaa huu ni janga jingine kwa

wananchi, kwani mpaka sasa wananchi wamekuwa wakitozwa

Page 23: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 23 of 52

pesa nyingi na kampuni kugharamia simu za mkononi, huku kampuni

zikikwepa kodi kwa kutokutoa taarifa sahihi juu ya kiasi gani cha

faida yanapata, na wakati huo Serikali haina uwezo wa kujua ni kiasi

gani hasa cha simu zinazopigwa na faida halisi ambayo kampuni hizi

zinaipata.

Mheshimiwa Spika, Kilio cha wananchi ni kampuni za simu kulipa

kodi ya mapato na sio kuhamisha ulipaji kodi na kuwabebesha

watumiaji. Serikali badala ya kupambana na kampuni zenye nguvu

kwa kuweka utaratibu wa kudhibiti matumizi yao ya uwekezaji,

imeamua kumlalia mwananchi mnyonge kwa kuongeza ushuru na

hivyo kuongeza gharama za mawasiliano.

Mheshimiwa Spika, Serikali inapanga pia kutoza kamisheni ya

asilimia 10 kwa mawakala wa huduma za mihamala ya pesa kwa

njia ya simu (mobile money transfer/transactions) kama njia ya

kuongeza mapato. Katika hotuba ya msemaji wa Kambi Rasmi ya

Upinzani wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia tuliitaka

Serikali itoze kodi na ushuru kwenye pesa kwa njia ya simu, lakini

tulitahadharisha kwamba mzigo huo wa kodi usibebeshwe kwa

wananchi bali kampuni za simu. Kwamba kampuni zilipe kutokana

na faida zinazozipata kwa sababu kwa mujibu wa sheria (the

Banking and Financial Institutions Act, 2006). Lakini cha ajabu Serikali

hii ya CCM imendelea kuziogopa kampuni za simu na imezua

pendekezo ya kuwatoza asilimia 10 mawakala, huku ikiziacha

kampuni zikipeta.

Page 24: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 24 of 52

Mheshimiwa Spika, Tozo hili jipya kwenye usafirishaji wa fedha ni tozo

linayobagua (discriminatory) kwa misingi kwamba wanaotuma

fedha kwa njia za mabenki hawatozwi kodi kama hii. Ni dhahiri

mabenki yanapiga vita mobile money transfer na hivyo Serikali

imeshawishiwa na mabenki kuongeza gharama za utumaji fedha ili

kuua sekta hii inayokua kwa kasi na inayohudumia wananchi

masikini kabisa.

Katika Azimio la Bunge kuhusu Watanzania wanaotorosha fedha na

kuzihifadhi nje ya nchi, Bunge liliazimia kwamba Serikali ianzishe kodi

ya ‘financial transaction tax’ ili kuweza kusimamia vizuri utumaji na

upokeaji wa fedha katika njia za mabenki. Kambi ya pinzani

inapendekeza kuwa tozo hili jipya kwenye mobile money transfer

litumike iwapo tu tozo kama hili litawekwa kwenye utumaji fedha

kwa njia za benki na njia nyinginezo. Vingenevyo tozo hili ni la

kibaguzi na linapendelea watu wenye uwezo mkubwa dhidi ya

wanyonge na hivyo tunatoa wito kuwa pendekezo hili lisikubaliwe

na Bunge.

Aidha, tunaendelea kupinga ongezeko hili la ushuru kwa kuwa sekta

hii ya mawasiliano ndio inaongoza katika kuchangia fedha nyingi

kwenye pato la taifa kuliko sekta nyingine yeyote hapa nchini. Sekta

hii huchangia asilimia 36.5 ya pato la taifa. Kwa mfano kwa mwaka

2012/2013 sekta hii ilichangia shilingi bilioni 287 wakati pombe, hasa

bia, ikichangia shilingi bilioni 214 na sigara shilingi bilioni 99.

Page 25: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 25 of 52

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza

mabadiliko ya Sheria ya Mawasiliano (EPOCA) ya mwaka 2009 ili

kuipa TCRA mamlaka ya kufanya ukaguzi wa uwekezaji

unaofanywa na kampuni za simu hapa nchini kwa lengo la kuzuia

ukwepaji kodi unatokana na kudanganya gharama za uwekezaji.

Kupitia TMAA ianyokagua migodi Serikali imeweza kuokoa kodi

nyingi sana. Hivyo tunataka TCRA ifanye kazi hiyo ya kukagua

gharama za uwezekaji zinazofanywa na kampuni za simu. Kambi ya

upinzani Bungeni inatarajia kuwa sekta ndogo ya mawasiliano

itaweza kuchangia sio chini ya asilimia 10 ya mapato ya ndani.

3.4.1 PAYE

Mheshimwia Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza

kushusha PAYE kutoka asilimia 14 ya sasa mpaka asilimia 9 na

kiwango cha chini cha kutoza PAYE kiwe ni Sh 250,000 kwa mwezi. Hii

itawezesha wananchi wa kipato cha chini kubakia na fedha za

kutosha na kutumia kwenye matumizi ili kuchochea uzalishaji nchini.

Uamuzi wa Serikali wa kushusha PAYE kwa asilimia moja tu (sawa na

shilingi 1,900 kwa mwezi) ni kiini macho na haina maana yeyote na

kwa kweli ni matusi kwa wafanyakazi wa Tanzania.

3.4.2 Tax Returns

Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba kwa kuwa

utaratibu wa vitambulisho vya taifa umeanza na tayari sehemu

fulani ya wananchi wamepewa vitambulisho na kwa kuwa kwa

Page 26: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 26 of 52

kupitia mfumo wa TIN na usajili wa magari kuna watanzania wengi

sana wana rekodi za kikodi ni vema sasa sheria ya kodi ya mapato

sura 332 ifanyiwe marekebisho ili kulazimisha kila mwananchi ajaze

‘tax return’ awe au asiwe na kipato. Hii itawezesha sana kupanua

wigo wa kodi kwa kuongeza idadi ya walipa kodi hapa nchini ili

kufikia lengo la anagalua Watanzania milioni 4.5 ambao wanalipa

kodi kutoka milioni moja wa sasa.

3.4.3 Kodi ya Ongezeko la thamani (VAT)

Mheshimiwa Spika, Serikali inapendekeza mabadilko kadhaa

kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani VAT ikiwemo kuondoa ushuru

wa gharama sifuri kwenye viwanda vya nguo na kuweka unafuu wa

VAT (kutoka jedwali la kwanza kwenda jedwali la tatu). Pia Serikali

inapendekeza kufanya mabadiliko kwa kuondoa msamaha wa VAT

kwenye sekta ya Utalii.

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza

kwamba mfumo mzima wa ‘zero rating’ uondolewe na badala yake

kwa bidhaa zenye umuhimu na zilizopo kwenye jedwali la kwanza

zipelekwe jedwali la tatu kama ‘special relief’. Pendekezo hili

linatokana na ukweli kwamba mfumo wa ‘zero rating’ hauonyeshi

mafanikio makubwa, hupoteza mapato kwa sababu ya kutumika

vibaya na kuwa na tatizo la cash flow kwa wazalishaji wengi.

Nchi jirani ya Kenya, katika muswada wake wa sheria ya VAT,

imependekeza kuondoa mfumo mzima wa ‘zero rating’.

Page 27: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 27 of 52

4.0 UWEKEZAJI NA MISAMAHA YA KODI

Mheshimiwa Spika, Kwa muda mrefu sana tumekuwa tukijadiliana

kuhusu misamaha ya kodi kama kivutio cha uwekezaji nchini. Serikali

kupitia sheria ya uwekezaji nchini hutoa nafuu lukuki kwa wawekezaji

ili kuleta mitaji yao nchini. Tanzania inatoa pia nafuu za kisekta,

mathalani kilimo kinapata nafuu ya asilimia ishirini (20%) ya mtaji kwa

kuandaa mashamba. Kampuni za uchimbaji madini zinazochimba

madini ya dhahabu, shaba, makaa ya mawe, lime, nickel n.k

yanapata nafuu ya asilimia mia moja (100%). Utalii inapata nafuu ya

asilimia kumi (10%).

Mheshimiwa Spika, pamoja na uvutiaji wa uwekezaji toka nje kupitia

motisha za kikodi; bado fursa za ajira ni ndogo, bado hakuna urari

wa biashara, bado maendeleo ni kidogo sana katika teknolojia. Na

hii ni tasfiri kwamba motisha za kodi zinazotolewa kwa wawekezaji

hazitoi matunda yanayokusudiwa, badala yake zimeendelea

kuinyima mapato serikali.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali ya

CCM ifahamu kuwa si motisha za kodi peke yake zinazoweza

kuwavutia wawekezaji, bali hali ya utulivu wa kiuchumi na kisiasa,

uwepo wa rasilimali za asili na rasilimali watu, utulivu wa soko la

ndani, uimara wa pesa ya ndani (local currency), uwazi na

kutokuwepo kwa rushwa, ni vigezo ambavyo kwa pamoja

vinawavutia wawekezaji.

Page 28: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 28 of 52

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa kitabu cha utafiti wa Mamlaka

ya Mapato Tanzania (‘Lessons From Selected Cases of Tax

Simplification Reforms and Tax Expenditure Budgeting’) cha mwezi

Machi 2012, Tanzania ni moja nchi zenye huruma katika kulipisha

kodi vyanzo vyake kiasi cha kuzorotesha uwezo wake wa kukusanya

mapato yake ya ndani na hivyo kushindwa kutekeleza miradi yake

ya maendeleo. Kwa mujibu wa taarifa za TRA (TRA Monthly Revenue

Report) misamaha ya kodi kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani

(VAT) na Ushuru wa Forodha (custom) peke yake imeipotezea

Tanzania wastani wa asilimia 4.3 (4.3%) ya Pato la Taifa kati ya

mwaka 2006/2007 - 2010/2011.

Mheshimiwa Spika, asilimia 4.3 (4.3%) ya pato la Taifa ni sawa na

Shilingi za kitanzania trillion moja, bilioni mia tisa ishirini na mbili, milioni

mia nane hamsini na tisa, kaki tano na tisa elfu (1,922, 859, 509,000/-

). Wakati Serikali inapoteza fedha zote hizi kama misamaha ya kodi,

Serikali hiyo hiyo inakwenda kukopa Uchina kiwango kama hicho

cha fedha kwa ajili ya kujenga bomba la kusafirisha gesi asilia

kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, kiasi hicho cha pesa kingetosha kulipa deni la

Shilingi 33,442,156,55, madai yote ya walimu ya malimbikizo ya

mishahara, likizo, uhamisho, masomo, matibabu, kujikimu, ajira

mpya, na mengineyo na kubaki kiasi cha Shilingi 1,919,515,293,345

pesa ambazo zingeweza kutumika kulipa askari polisi wote nchini,

madaktari na watabibu, askari magereza wote.

Page 29: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 29 of 52

Mheshimiwa Spika, kiasi hicho kingeweza, kama mbadala, kutumika

kujenga shule, kununua vitabu, kujenga zahanati na kununua dawa,

kujenga viwanda na hivyo kupanua ajira. Kuboresha maisha ya

wakulima na wafugaji, kupeleka nishati ya umeme vijijini n.k.

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza

kwamba misamaha yote ya Kodi iwekwe wazi na ikaguliwe na

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Ikumbukwe

kwamba misamaha ya kodi ni ruzuku ya Serikali kwa wanaofaidika

na misamaha, hivyo ni matumizi kama matumizi mengine yeyote ya

Serikali na hivyo ni lazima yakaguliwe na ukaguzi wake kuwekwa

wazi kama taarifa nyingine za CAG.

Mheshimiwa Spika, Suala la kuweka wazi misamaha ya kodi na

kufanyiwa ukaguzi lilishughulikiwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za

Serikali, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na

Mamlaka ya Mapato Tanzania ambapo suala hili lilikubalika na

Waziri wa Fedha alipaswa kuliwekea utaratibu wa kisheria kwenye

Sheria ya Fedha mwaka huu. Jambo la kushtusha ni kwamba Serikali

imekaa kimya kabisa kuhusu jambo hili na hivyo kuonyesha kwamba

Serikali imewekwa mfukoni na wanaofadika na misamaha hii.

Hakuna namna nyingine ya kueleza zaidi ya kusema kwamba

Serikali imeshindwa nguvu na makampuni, taasisi na watu binafsi

wanaopinga mabadiliko kwenye mfumo wa misamaha ya kodi,

wanaopinga uwazi na wanaopinga ukaguzi wa misamaha yao.

Page 30: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 30 of 52

Kama si hivyo, basi ni vema Mheshimiwa waziri wa Fedha

akalibainisha suala hilo katika Sheria ya fedha na aeleze hivyo

kinaga ubaga katika majumyuisho yake.

4.1 UKWEPAJI KODI

Mheshimiwa Spika, Tanzania ni moja ya nchi za Afrika zenye tatizo

kubwa la ukwepaji wa kodi unaofanywa na kampuni kubwa za

kimataifa zilizowekeza, kampuni za ndani na watu binafsi. Watu na

kampuni wanaokwepa kodi hutoa taarifa za uongo juu ya mauzo

na faida zao, na kuonyesha kwa udanganyifu kuwa wamepata

hasara. Tafiti nyingi ikiwemo Ripoti ya Benki ya Dunia (2008)

zinaonyesha kuwa ukwepaji kodi ni tatizo kubwa Tanzania kuliko nchi

tunazopakana nazo.

Kwa mujibu wa ripoti Benki ya Dunia kampuni nyingi Tanzania hutoa

taarifa kwa kiwango cha asilimia 69 tu ya mauzo yake, ukilinganisha

na asilimia 77 nchini Uganda, na asilimia 86 huko Kenya. Kampuni

hapa nchini zinakuwa na vitabu viwili vya hesabu; kimoja

wanaandika hesabu za kweli na kingine wanaandika taarifa za

uongo kwa madhumuni ya kupunguza kodi. Lakini hiyo ni njia moja

tu.

Mheshimiwa Spika, njia nyingine inayotumika na kampuni hizo

kukwepa kodi ni kutotoa taarifa za mauzo ya nje, kufanya biashara

Page 31: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 31 of 52

nje ya nchi kimagendo (kupitia njia za panya). Kwa mujibu wa

Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (East African Business Council)

mwaka 2008 kiasi cha biashara ya thamani ya Dola za Marekani

milioni 602 ($ 602 Milioni) zilifanyika kwenye mpaka wa Kenya na

Tanzania, pale Namanga peke yake.

Mheshimiwa Spika, mfano mmoja dhahiri wa ukwepaji kodi kwenye

mauzo ya nje umeonyeshwa na utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia

katika Bandari ya Dar es Salaam na Bandari nyingine hapa nchini

kuhusu mauzo nje ya zao la korosho ghafi. Mwaka 2011 Tanzania

iliuza kwenda nchini India korosho kiasi cha tani 80,000 kwa mujibu

wa taarifa za Mamlaka ya Mapato Tanzania na Benki Kuu ya

Tanzania. Hata hivyo, idara ya Forodha ya India inaonyesha katika

mwaka huo, nchi hiyo ilikuwa imenunua tani 120,000 za korosho

kutoka Tanzania. Hii maana yake ni kwamba jumla ya tani 40,000 ya

korosho ambazo ni sawa na theluthi moja ya korosho zote

zilizopaswa kuwa zimeuzwa nchini India na nusu ya korosho

zilizoripotiwa kuwa Tanzania imeuza nchini India hazikuripotiwa na

hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa sana kiwango cha kodi

ambacho serikali ilipaswa kukusanya. Pia, tofauti hiyo ilipunguza urari

wa mauzo nje.

Mheshimiwa Spika, hivi karibuni tumeshuhudia taarifa za ukwepaji

mkubwa sana wa kodi ya forodha kufuatia wafanyabiashara wasio

waaminifu kutumia vibaya mfumo wa kutoa mizigo. Ikumbukwe

kwamba Bunge lako tukufu katika mwaka wa fedha wa 2008/09

Page 32: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 32 of 52

lilipinga mfumo wa kuruhusu wafanyabiashara wakubwa kutoa

mizigo yao bila kukaguliwa.

Bidhaa nyingi zilizoagizwa hazikulipiwa kodi kwa sababu ama

hazikuwa zimeorodheshwa kwenye nyaraka zilizowasilishwa idara ya

forodha au kulifanyika udanganyifu wa aina ya bidhaa. Kwa mujibu

wa taarifa za TRA, ukaguzi wa mizigo uliofanyika kati ya Aprili na Juni

2013 unaonyesha kwamba jumla ya shilingi bilioni nne ziliokolewa.

Mheshimiwa Spika, kuna mtandao mzito wa wafanyabiashara

wakubwa hapa nchini kwa kushirikiana na maafisa wa forodha

wanafanya njama za kukwepa kodi. Kumekuwa na vita vya

kibiashara miongoni mwa wafanyabiashara, vita ambayo

imewagawa maafisa wa forodha wasio waaminifu na kujikuta

kufanya kazi za wafanyabishara wakubwa.

Kumekua na uonevu mkubwa dhidi ya wafanyabiashara wadogo

na wanaoibukia unaofanywa na wafanyabaishara wakubwa na wa

muda mrefu. Hakuna haki kabisa katika ukaguzi wa mizigo jambo

linalosababisha wafanyabiashara wadogo wengi wa Kariakoo

kuumizwa kutokana na hila za wafanyabishara wakubwa

wanaoshirikiana na maofisa wa idara ya forodha.

Mheshimiwa Spika, hii inathibitishwa na Taarifa ya ukaguzi wa

thamani ya Fedha (Value for Money Audit Tanzania Revenue

Authority’s New Customs system) iliyotayarishwa na Bert

Cunningham kutoka Canada. Taarifa hiyo inaonyesha kuwa maofisa

Page 33: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 33 of 52

wa forodha wanashirikiana na mawakala wa mizigo na wafanya

biashara (Clearing and Forwarding Agents) kuonyesha kiwango

kidogo cha mizigo inayoingizwa nchini au thamani ndogo ya mizigo

kwa lengo la kukwepa kulipa kodi stahiki.

Kutokana na ukosefu wa maadili, rushwa na uzembe wa maafisa wa

forodha, Taifa hupoteza mapato ya zaidi ya asilimia 15 ya kiwango

kinachokusanywa na Idara ya Forodha kwa mwaka. Katika mwaka

wa Fedha 2012/13 jumla ya shilingi bilioni 477 zimepotea kupitia

idara ya forodha peke yake.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ina mashaka

makubwa sana kwamba ukwepaji kodi kwenye eneo la kodi ya

forodha ni mkubwa mno kuliko inavyoripotiwa hivi sasa. Vyombo vya

habari vinavyoandika habari hizi, vinaandika kutokana na taarifa

ambazo zimekipata kuitoka kwa chanzo chao ambacho aghalabu

huwa hakina taarifa zote na za kina. Hivyo, ni dhahiri kuwa

kinachoandikwa ni sehemu tu na ukweli wote hausemwi. Kambi ya

Upinzani Bungeni, kwa mujibu wa kanuni ya 117 italeta hoja Bungeni

kutaka kuundwa kwa kamati teule ya Bunge kuchunguza ‘Mfumo

wa Forodha na ukwepaji kodi katika idara ya Forodha ya Mamlaka

ya Mapato Tanzania’ kwa lengo la kuhakikisha ukwepaji kodi

unadhibitiwa na wahujumu wote wanachukuliwa hatua stahili za

kisheria.

Page 34: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 34 of 52

Mheshimiwa Spika, suala la ukwepaji wa kodi linahusu pia

wanasiasa wakiwamo Wabunge. Ni dhahiri wabunge wana stahili za

kisheria za kupata msamaha wanapoagiza magari yao nk. Tunatoa

wito kwa wabunge ambao ni wafanyabiashara waliosajili biashara

zao katika Kituo cha Uwekezaji yaani TIC na kupata vyeti vya

misamaha ya kodi wawe wa kwanza kuhakikisha kuwa hawatumii

misamaha hiyo vibaya.

Hatuwezi kuwa mbele kukemea misamaha ilhali sisi wenyewe

tunaitumia vibaya misamaha hiyo. Ni dhahiri kabisa kwamba

inapaswa kuwa ni aibu kwa mbunge kutumia msamaha wa kodi

aliopata kununua kitanda, magodoro na mambo kama hayo. Sisi

wabunge tutembee kwenye maneno yetu ikibidi hata kwa kukataa

misamaha hii mikubwa ya kodi tunayopewa. Natumai baada ya

CAG kuanza kukagua misamaha ya kodi kama matumizi mengine

yeyote ya Serikali tutashuhudia aibu kubwa tutakayopata kwa

kutumia vibaya misamaha ya kodi.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa dunia ipo kwenye ajenda ya kuzuia

utoroshaji mkubwa wa fedha kupitia ‘tax havens’ ambapo licha ya

kwamba kuna fedha zinazotokana rushwa katika utoroshaji huu

lakini pia kuna fedha nyingi zinazotokana na ukwepaji wa kodi (Tax

evasion and tax avoidance). Taarifa ya Benki ya Maendeleo ya

Afrika (The joint report from the African Development Bank (AfDB)

and Global Financial Integrity (GFI)) iliyotolewa jijini Marrakech nchini

Morocco inaonyesha kuwa jumla ya dola za Marekani trilioni 1.4

Page 35: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 35 of 52

zimetoroshwa kutoka Afrika kati ya mwaka 1980 mpaka 2009 na

hivyo kulifanya bara hili kuwa ‘net creditor’ kwenye dunia. Sehemu

kubwa ya Fedha hizi ni kodi inayokwepwa na kampuni kubwa

zinazowekeza katika bara la Afrika. Sehemu nyingine ya fedha hizi

zinatokana na udanganyifu katika akaunti ya Deni la Taifa ambapo

madeni na riba za uwongo hulipwa kutoka Afrika.

Mheshimiwa Spika, wakati dunia nzima ipo kwenye kampeni kubwa

dhidi ya ukwepaji kodi unaofanywa na kampuni kubwa duniani

zinazowekeza kwenye nchi zinazoendelea, Tanzania ipo kimya

kabisa kana kwamba hakuna linalotokea. Licha ya kwamba Bunge

la Tanzania ni Bunge la Kwanza katika nchi za SADC kupitisha Azimio

kuchunguza utoroshwaji wa Fedha (Azimio la Bunge namba 9/2012),

Serikali ya Tanzania imekaa kimya kabisa kupaza sauti yake kuhusu

ukwepaji kodi mkubwa.

Tanzania inapoteza mapato ya ndani sawa na asilimia tano (5) ya

Pato la Taifa kupitia kodi za kimataifa ambayo ni sawa na shilingi

trilioni mbili kila mwaka. Uchunguzi unaonyesha kwamba katika

orodha ya walipa kodi wakubwa 10, kampuni saba zinatumia ‘tax

havens’ kukwepa kodi. Katika kampuni kubwa tatu za simu hapa

nchini kampuni mbili zimesajiliwa ‘tax havens’ za Uholanzi na

Luxembourg na hivyo kukwepa kodi mbalimbali hapa nchini.

Kampuni moja kubwa ya madini hapa nchini ina kampuni dada tisa

(9) katika offshore hali kadhalika kampuni moja kubwa ya kutafuta

mafuta na gesi hapa nchini. Katika mahojiano na gazeti la Financial

Page 36: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 36 of 52

Times la Uingereza la mwezi June, 2013 kampuni ya African Barrick

Gold imetangaza kufunga baadhi ya kampuni zaidi ya 24 iliyoyasajili

maeneo kama Cayman Islands.

Mheshimiwa Spika, bila Serikali ya Tanzania kuamua kwa dhati

kusafisha nyumba yake, hata juhudi kubwa zinazofanywa na asasi

za kiraia kama Oxfam, ActionAid, Tax Justice Network nk katika

kupambana na ukwepaji kodi na utoroshaji wa fedha hazitafua

dafu. Wakati nchi za G8 zinaweka mipango ya kutusaidia na sisi

kama nchi tuweke mipango yetu wenyewe. Kambi ya Upinzani

Bungeni inapendekeza hatua za awali zifuatazo zichukuliwe ili

kukabiliana na utoroshaji mkubwa wa fedha unaotokana na

ukwepaji wa kodi;

(i) Tanzania ijiondoe kabisa katika mfumo wa kodi

unaopendekezwa na OECD (OECD model treaty) kwani

mkataba huu wa kikodi unalinda kampuni kubwa za nje dhidi

ya nchi changa kama Tanzania.

(ii) Tanzania ijondoe katika mikataba yote ya kikodi na nchi

ambazo ni ‘tax havens’ kama Mauritius, Uingereza (City of

London and British overseas territories), Luxembourg,

Netherlands n.k.

(iii) Kampuni yoyote ya ndani na nje yenye kampuni dada

zilizosajiliwa kwenye ‘tax havens’ zitangaze bayana na kuweka

Page 37: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 37 of 52

wazi hesabu zao kwa miaka mitano iliyopita kwa ukaguzi wa

TRA na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

(iv) Bunge litunge sheria kudhibiti matumizi ya ‘tax havens’

yanayofanywa na kampuni za uwekezaji na haswa kwenye

sekta za Mawasiliano, Madini, Mafuta na Gesi na nyinginezo.

5.0 MAENDELEO YA MICHEZO

Mheshimiwa Spika, maendeleo mazuri ya michezo katika taifa

lolote, ni utambulisho mzuri wa taifa hilo katika mataifa mengine

kutokana na ushirikiano wa kimichezo na mataifa hayo. Pamoja na

mambo mengine, michezo katika nchi yetu inaweza kutumika

kutengeneza fursa za kiuchumi kwa kuitangaza nchi yetu duniani

katika sekta za utalii na uwekezaji. Ukiacha mbali suala la manufaa

ya kiuchumi yanayoweza kupatikana kupitia michezo, michezo pia

inawajengea vijana wetu afya na hivyo kuwa na taifa la watu

wakakamavu. Kwa upande mwingine, michezo pia ni ajira.

Inasikitisha kwamba katika hotuba nzima ya Waziri wa Fedha,

hapakuwa na mpango wowote wa kukuza michezo hapa nchini

bila hata kujali kwamba timu yetu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ipo

katika nafasi nzuri sana hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote

katika kuweza kufuzu kucheza fainali za kombe la Dunia mwakani.

Page 38: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 38 of 52

Mheshimiwa Spika, Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika

barua yake ya tarehe 5/4/2013 iliomba Kamati ya Bajeti kuangalia

namna ya kusaidia kupata fedha za kujenga michezo na hasa

kusaidia Taifa Stars katika juhudi zake za kuelekea kufuzu kwenye

michuano ya kombe la Dunia huko Brazil. Hata hivyo Wizara ya

Fedha haikutoa hata senti tano kwa ajili hiyo. Kamwe hatuwezi

kufanikiwa kwenye michezo bila kuwekeza na kutegemea juhudi za

dharura za kamati za kusaidia ushindi. Tukitaka tung’ae kwenye

michezo ni lazima tuwekeze sana na kuwekeza ni gharama,

gharama ambayo thamani yake ni kubwa sana kwa nchi.

Mheshimiwa Spika, licha ya michezo kuliingizia taifa mapato kupitia

asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) inayotokana na

viingilio katika michezo mbalimbali, hakuna uwekezaji wowote wa

maana uliofanyika kwenye michezo jambo ambalo ni hatari kwa

uhai na maendeleo ya michezo hapa nchini. Aidha hakuna

mipango madhubuti ya muda mrefu kuhusu maendeleo ya michezo

hapa nchini.

Kutowepo kwa mipango madhubuti na ya muda mrefu,

kumeshababisha timu zetu kufanya vibaya katika mashindano

mengi ya kimataifa na hivyo kulifanya taifa letu lionekane kuwa ni

taifa dhaifu au kichwa cha mwendawazimu kama alivyopata

kusema Rais Mstaafu was Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi.

Kambi Rasmi ya Upinzani, inatoa angalizo kwa Serikali kwamba,

kamwe hatuwezi kufanikiwa katika michezo kwa mipango ya

Page 39: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 39 of 52

kukurupuka. Aidha ni aibu kwa Serikali kukusanya kodi kutokana na

michezo, halafu vijana wetu wanakosa fedha ya nauli kwenda nchi

nyingine kwa mashindano ya michezo mpaka wafanye harambee

ya kukusanya fedha kwa wahisani. Hivyo, Kambi Rasmi ya Upinzani

Bungeni inayoongozwa na CHADEMA inapendekeza mambo

yafuatayo yafanyike ili kunusuru tasnia ya michezo hapa nchini;

1. Timu yoyote itakayowakilisha taifa katika mashindano

yoyote ya kimichezo igharamiwe na Serikali kwa asilimia

100.

2. Viwanja vyote vya Michezo hapa nchini viundiwe Wakala

wa Serikali, Wakala wa maendeleo ya michezo (Sports

Development Agency). Wakala huo uwe na majukumu ya

kujenga viwanja vipya na kusimamia viwanja hivyo kwa

niaba ya Serikali. Viwanja vyote vya michezo vilivyoporwa

na CCM kama Lake Tanganyika – Kigoma, Ali Hasan Mwinyi

- Tabora, Kirumba – Mwanza, Maji Maji – Songea nk

virejeshwe Serikalini mara moja chini ya Wakala wa Viwanja

vya Michezo. Wakala pia ujenge academies za michezo

maeneo kama vile Mbeya, Tanga, Mtwara, Mwanza,

Manyara na Dar es Salaam ili kukuza vipaji vya watoto na

vijana.

3. Mashirika yote ya Umma, hasa mashirika makubwa yawe

na timu za michezo. Ushauri uliotolewa na IMF na Benki ya

Dunia dhidi ya Mashirika ya Umma kuwa na timu ulikuwa

Page 40: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 40 of 52

ushauri usio wa maana. Wenzetu Uganda kwa mfano,

Mamlaka ya Mapato Uganda (URA) wana timu katika ligi

Kuu, ambayo ni moja ya timu mahiri katika ukanda huu wa

bara la Afrika.

4. Serikali ianzishe Mfuko Maalum wa Michezo (Sports Fund).

Pia, Serikali ianzishe Kodi ya Maendeleo ya Michezo (Sports

Development Levy). Kodi hii ipatikane kama ifuatavyo:

Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya asilimia 18 iliyokuwa

ikikatwa kwenye viingilio katika michezo mbalimbali

iondolewe na badala yake kiasi hichohicho kiingizwe

kwenye Mfuko wa Michezo (Sports Fund) utakaoanzishwa.

5. Matumizi ya Mfuko wa michezo yawe kama ifuatavyo:

i. Asilimia 50 ya fedha zitakazokusanywa

zitumike kujenga miundombinu ya michezo

(Sports Infrastructure) kupitia kwa Wakala

wa Maendeleo ya Michezo na Academies.

ii. Asilimia 50 inayosalia itumike kuhudumia

maandalizi ya timu za Taifa.

6.0 UKUSANYAJI WA MAPATO YA ZIADA.

6.1 BANDARI YA DAR-KAMA KICHOCHEO CHA UCHUMI

Mheshimiwa Spika, Bandari ya Dar es Salaam ni mlango mkuu wa

biashara kwa asilimia 90 kwa nchi sita zisizokuwa na bandari za

Page 41: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 41 of 52

Zambia, Malawi, Rwanda, Burundi, Uganda na eneo la Mashariki ya

nchi ya DRC. Toleo la tatu la taarifa ya Benki ya Dunia (Tanzania

Economic Update) la mwezi Mei, 2013 inaonyesha kwamba Bandari

ya Dar es Salaam inapoteza fedha na muda mwingi sana kwa

watumiaji wa bandari hiyo kwa kulinganisha na Bandari yoyote

katika mwambao wa Afrika ya Mashariki.

Mheshimiwa Spika, taarifa hiyo ya Benki ya Dunia inasema kwamba

familia za kawaida zingeweza kuepuka matumizi ya takriban dola za

Marekani 147 au asilimia 8.5 kwa mwaka kama Bandari ya Dar es

salaam ingekuwa inafanyakazi kama inavyofanyakazi Bandari ya

Mombasa.

Mheshimiwa Spika, kutokana na utafiti ni kwamba kama Bandari ya

Dar es Salaam itaboreshwa na kubadili mtizamo (mind set) wa

watendaji wake katika uwajibikaji ni dhahiri kwamba bandari ina

fursa za kuongeza mapato ya Serikali yapatayo dola za Marekani

bilioni 1.8 au shilingi trilioni 2.93 kwa mwaka au ongezeko la asilimia

saba la pato la Taifa.

Kambi rasmi ya Upinzani inapendekeza kuimarisha ufanisi wa

Bandari kwa mwaka huu wa fedha 2013/2014 na kufikia ufanisi wa

asilimia hamsini (50%) jambo ambalo litawezesha kuongeza mapato

ya ndani ya kiasi cha shilingi trilioni 1.46

6.2 Kudhibiti misamaha ya kodi

Page 42: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 42 of 52

Mheshimiwa Spika, katika mapendekezo ya namna bora ya

kuongeza mapato ya serikali, Kambi Rasmi ya Upinzani

tunapendekeza yafanyike marekebisha katika Sheria ya Uwekezaji

na kuweka udhibiti wa thabiti katika kutoa misamaha na nafuu za

kodi, tofauti na hali ilivyo sasa ambapo asilimia 4.3 ya pato la taifa

linapotea kwa misamaha ya kodi. Kiwango hiki ni sawa na shilingi

Trilioni Moja, Bilioni Mia tisa ishirini na mbili, milioni mia nane hamsini

na tisa, Laki tano na tisa elfu (1,922, 859, 509,000/-).

Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na CHADEMA

inapendekeza kudhibiti misamaha hiyo ili kuishusha na kufikia asilimia

moja (1%) ya pato la taifa. Jambo hilo ni muhimu lifanyike kwa

sababu kwa kufanya hivyo nchi itakuwa imeokoa shilingi Trilioni

moja, Bilioni mia tano arubaini na tano, milioni mia sita themanini na

mbili, laki nane na elfu sabini na tisa (1,545, 682, 879, 000).

6.3 Kodi ya Mauzo na Manunuzi ya Bidhaa kutoka Nje

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na

CHADEMA inapendekeza kuanzishwa kwa kodi maalumu (Special

Railways development levy) ya manunuzi na mauzo ya bidhaa nje.

Tunapendekeza tozo ya asilimia moja (1 %) ya bei ya bidhaa

zinazoagizwa toka nje na asilimia 0.5 (0.5%) ya thamani ya bidhaa

kwa zile zinazouzwa nje. Mapato ya tozo hii maalumu yote yatumike

kujenga miundombinu ya Reli hapa nchini.

Page 43: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 43 of 52

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taarifa ya Hali ya Uchumi wa

Taifa mwaka 2012 Tanzania iliagiza bidhaa kutoka nje ya nchi zenye

thamani ya dola za Marekani milioni 10,324.9 ambazo ni sawa na

shilingi 16,519,840,000,000 (bei ya kubadilisha dola 1 ni sawa na

shilingi 1,600). Kwa maana hiyo, asilimia moja ya mapato ya

manunuzi yote ya nje ni shilingi bilioni 165.2. Mauzo ya bidhaa nje ya

nchi kwa mwaka 2012 yalikuwa dola za Mmarekani milioni 5,912.3

ambazo ni sawa na shilingi trilioni 9.456 na asilimia 0.5 ya kiasi hicho

ni shilingi bilioni 47.298.

Mheshimiwa Spika, kutokana na kodi hii ya mauzo na manunuzi ya

bidhaa kutoka na kwenda nje ya nchi, iwapo tozo hiyo ingekuwepo,

serikali ingekusanya kiasi cha shilingi bilioni 212.498 mwaka 2012.

7.0 VIPAUMBELE VYA BAJETI YA MATUMIZI 2013/2014

Mheshimiwa Spika, kutokana na mapendekezo tuliyoyatoa, Kambi

Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA

inapendenkeza kuwa vipaumbele vya Bajeti ya mwaka ujao wa

fedha vingekuwa kama ifuatavyo:

(i) Kujenga Mazingira ya ukuaji wa uchumi vijijini (rural

growth) kwa kuboresha miundombinu ya umeme,

barabara, maji na miundombinu ya umwagiliaji.

Tunapendekeza kutumia shilingi bilioni 450 kila mwaka

katika eneo hili. Fedha hizi zitasimamiwa na Mamlaka ya

Maendeleo Vijijini (Rural Development Authority – to be

established) itakayokuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Page 44: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 44 of 52

(ii) Kukarabati Reli ya Kati na matawi yake ya Tanga - Arusha

na Mpanda. Tutatenga Tsh 212.498 bilioni kwa RAHCO

kwa ajili ya Reli. Fedha za ujenzi wa Reli zitakuwa ni fedha

endelevu kutoka Railways Development Fund

itakayotokana na tozo maalumu tunayopendekeza.

(iii) Kuboresha Elimu na Afya hasa kwa Shule na

Zahanati/Vituo vya Afya vya Vijijini kwa kutoa motisha

kwa wafanyakazi wa Sekta hizi walio kwenye Halmashauri

za Wilaya. Tunapendekeza posho za Mazingira ya Vijiji

sawa na mara moja na nusu ya Mishahara yao.

(iv) Kuongeza Kima cha chini cha Mshahara kwa

Wafanyakazi wa Umma mpaka Tsh 315,000 kwa Mwezi

(v) Kuanzisha Pensheni ya uzeeni kwa Wazee wote nchini

wenye umri wa zaidi ya miaka 60.

(vi) Kupunguza mzigo wa matumizi ya magari ya Serikali kwa

kupiga mnada baadhi ya ‘mashangingi’ na kuweka

mfumo wa kukopesha Magari kwa watumishi wote wa

umma wanaostahili magari.

(vii) Kuanzisha Chuo Kikuu cha Mtwara (Mtwara University for

Petroleum Studies) ili kuzalisha wataalamu wa kutosha wa

Sekta ya Mafuta na Gesi na kuliandaa Taifa kuwa na

wasomi mahiri wa maeneo hayo na hivyo kufaidika na

Utajiri wa Mafuta na Gesi uliopo nchini kwetu.

Page 45: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 45 of 52

8.0 SURA YA BAJETI MBADALA KWA MWAKA 2013/14

Mheshimiwa Spika, kambi rasmi ya upinzani bungeni katika kupanga

bajeti yake imezingatia heshima ya taifa kwa kuhakiki nchi inaweza

kutumia vema rasilimali zake na kufuta utegemezi. Naomba kunukuu

maneno ya Abraham Lincoln anayesema; “You cannot help people

permanently by doing for them, what they could and should do for

themselves”. Kwa tafsiri ya haraka haraka anamaanisha kuwa

hauwezi kuwasaidia watu kwa kuwafanyia, wakati wote, kile

ambacho wanaweza na wanapaswa kukifanya. Leo hii, kama nchi

tunategemea kuendelea kusaidiwa na mataifa wahisani kwa vitu

ambavyo tunauwezo wa kuvifanya na tunapaswa kuvifanya. Pia

tunajenga taifa tegemezi lisilo na heshima mbele ya dunia na kujipa

matumaini ya kuwa bado tunao uwezo wa kukopesheka. Ni lazima

kuongeza wigo wa kodi ili kuondokana na utamaduni wa

kupandisha kodi zile zile kila mwaka na hivyo kuonekana kana

kwamba hatuna ubunifu wowote.

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia heshima ya taifa letu kambi rasmi

imependekeza bajeti mbadala ya mwaka 2013/2014 yenye jumla

ya makusanyo ya ndani ya shilingi billion 15,698.937 kwa kujikita

katika kupanua wigo wa mapato ya ndani na kuachana na mikopo

yenye masharti ya kibiashara ili kupunguza mzigo mkubwa

ulioingizwa katika deni la taifa. Asilimia 75.8 ya bajeti nzima ni

mapato ya ndani ikijumuisha mapato ya halmashauri. Hivyo ni

Page 46: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 46 of 52

asilimia 24.2 tu ya bajeti ndio itatukana na misaada ya kibajeti na

mikopo isiyo na riba za kibiashara.

Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya upinzani bungeni inapendekeza

kuondoa kabisa mikopo yenye masharti ya kibiashara na

kupendekeza vyanzo mbadala vya mapato ili kuondokana na adha

ya madeni na kukusanya mapato yetu ya ndani kugharimia

uendeshaji wa bajeti, pia kupunguza matumizi yasio ya lazima na

fedha hizo kuelekezwa katika miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, kutokana na ongezeko kubwa la matumizi yasiyo

ya lazima katika bajeti ya serikali, kambi rasmi ya upinzani

imependekeza kupunguza asilimia 30 ya gharama za posho za

vikao, semina, usafiri, viburudisho, mafuta na vilainishi. Kwa mwaka

2012/2013 serikali inatumia shilingi billion 681 kwa matumizi yasiyo ya

lazima na 2013/2014 imepanga kutumia shilingi bilioni 714 (kwa

mujibu wa taarifa ya Shirika la Sikika) sawa na ongezeko la asilimia

tano kinyume na kauli ya Waziri Mkuu ya kupunguza gharama za

matumizi yasiyo ya lazima. Hivyo kambi imedhamiria kuwepo na

punguzo hilo la shilingi bilioni 214 kutoka katika eneo hili ambazo

zitaelekezwa katika miradi ya maendeleo.

JEDWALI LA VYANZO VYA MAPATO MBADALA.

Page 47: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 47 of 52

CHANZO CHA MAPATO. MAKISIO SHILINGI BILIONI

Kuongeza Ufanisi wa bandari ya

Dar Es Salaam

1,465.000

Marekebisho ya kodi za misitu 220.416

Kupunguza misamaha ya kodi 1,545.000

Kodi ya 0.5% kwenye Mauzo na

ya 1% manunuzi ya nje kwa ajili

ya kujenga Reli

212.498

Kuzuia ukwepaji kodi

unaofanywa na Kampuni za

kimataifa

718.500

Jumla 4,161.414

SURA YA BAJETI MBADALA YA MWAKA 2013/2014.

MAPATO % SHILINGI BILIONI

A Mapato ya ndani 15,315.485

i)Mapato ya Kodi (TRA) 13,855.851

ii)Mapato yasiyo ya Kodi 1,459.634

B Mapato ya Halmashauri 383.452

C Mikopo na misaada ya Kibajeti 1,163,131

D Mikopo na Misaada ya miradi

ya maendeleo ikijumuisha MCA

(T)

2,692,069

Page 48: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 48 of 52

E Mikopo ya ndani 1,156,400

Jumla ya Misaada na mikopo.

5,011.600

JUMLA YA MAPATO YOTE 20,710.537

MATUMIZI

E Matumizi ya Kawaida 13,132.121

(i) Deni la Taifa 3,319.156

(ii) Mishahara 5,706.399

(iii) Matumizi Mengineyo 4,106.566

Wizara 3,352,316

Mikoa 49,701

Halmashauri 704,549

H Matumizi ya Maendeleo 7,578.416

(i)Fedha za ndani 6,537.467

(ii)Fedha za Nje 1,040,949

JUMLA YA MATUMIZI YOTE. 20,710.537

Page 49: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 49 of 52

TOFAUTI KATI YA BAJETI YA SERIKALI NA BAJETI MBADALA YA KAMBI

RASMI YA UPINZANI.

BAJETI MBADALA YA KAMBI YA

UPINZANI 2013/2014

BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA

2013/2014

Bajeti yenye kuondoa mikopo

yenye masharti ya kibiashara ili

kulipunguzia taifa mzigo wa

madeni.

Bajeti yenye mikopo ya shilingi

1.156 trilioni yenye masharti ya

kibiashara

Bajeti yenye kujikita katika

utekelezaji wa mpango wa

maendeleo kwa kutenga zaidi

ya asilimia 41 ya mapato ya

ndani kugharimia miradi ya

maendeleo.

Bajeti inayopingana na

mpango wa maendeleo wa

taifa kwa kutenga asilimia 22.4

kinyume na matakwa ya

mpango wa serikali ambao

unahitaji asilimia 35.

Imeanzisha kodi maalum ya

michezo na wakala wa

maendeleo ya michezo

Haijali michezo na wala sio

kipaumbele chake

Kulipa pensheni kwa wazee

wote kuanzia miaka 60 na

kuendelea.

Bajeti isiyo na mfumo wa

pensheni kwa wazee.

Kushusha kiwango cha chini

cha kodi ya mapato (PAYE)

kutoka 14% mpaka 9%

Haijali wafanyakazi, kodi ya

mapato (PAYE) imeendelea

kuwa kubwa 13%

Kupunguza matumizi yasiyo ya Ina matumizi yasiyokuwa ya

Page 50: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 50 of 52

lazima kwa kuondoa 30% ya

OC kwenye wizara na idara .

lazima kiasi cha shilingi bilioni

214

Bajeti inayojitegemea kwa

makusanyo ya mapato ya

ndani ya asilimia 75.8

Bajeti tegemezi kwa asilimia

37.8 kutokana na kukopa kwa

kiwango kikubwa.

Bajeti yenye punguzo la

misamaha ya kodi na kufikia 1%

ya pato la taifa

Bajeti yenye misamaha ya kodi

kiasi cha 4.3% ya pato la taifa

(sawa na shilingi trilioni 1.922)

Bajeti itakayokabiliana na

mfumuko wa bei kwa bidhaa

muhimu

Bajeti isiyozingatia mfumuko wa

bei

Bajeti yenye maslahi bora kwa

wafanyakazi kwa kuongeza

kima chini cha mshahara

kuanzia 315,000

Bajeti iliyo na kima cha chini

cha shilingi 170,000

kisichoendana na gharama za

maisha kwa sasa.

Bajeti inayofuta ongezeko la

kodi kwenye mafuta ya dizeli na

petroli

Bajeti inayoongeza kodi kwenye

mafuta, dizeli 6.1% na petroli

8.5%

Bajeti inayoondoa ongezeko la

kodi kwenye ngano na hivyo

bidhaa za ngano kama mikate,

maandazi, chapati kutopanda

bei

Bajeti inayoongeza bei ya

ngano kwa 10% na hivyo

kutowajali wananchi wa

kipatyo cha chini wanaotumia

bidhaa hizi kwa wingi

Inafuta ongezeko la kodi Inaongeza kodi kwenye simu za

Page 51: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 51 of 52

kwenye matumizi ya simu za

mkononi

mkononi na hivyo mtumiaji

kutakiwa kulipa kodi

/tozo/ushuru wa 36.5%

9.0 HITIMISHO.

Mheshimiwa Spika, wakati waziri wa fedha alipokuwa anawasilisha

hotuba yake ya bajeti wiki iliyopita wapo wabunge ambao

walikuwa wanapiga makofi kuashiria kuwa waliridhika na hotuba ya

bajeti na walikuwa wanaiunga mkono.

Aidha, baada ya mawasilisho yake hayo wananchi wa kada

mbalimbali kuanzia wasomi, wafanyakazi, wanasiasa, wakulima na

wafanyabiashara pamoja na makundi mbalimbali ya kijamii katika

maeneo mbalimbali ya nchi yetu wamekuwa wakipaza sauti zao

kuhusiana na jinsi ambavyo bajeti ya serikali itakavyokwenda

kuongeza gharama za maisha na kuwafanya waendelee kuogelea

kwenye wimbi la umasikini katika nchi yenye rasilimali za kutosha.

Mheshimiwa Spika, ni rai yangu na ya kambi rasmi ya upinzani kuwa

sisi wabunge wote bila kujali itikadi zetu tusikilize kilio cha watanzania

wenzetu hawa na tuwe na huruma juu ya maisha yao na

tutakapokuwa tunajadili bajeti hii tuangalie maslahi ya taifa letu na

wananchi wetu kwa kuhakikisha kuwa tunatimiza wajibu wetu wa

kuisimamia serikali ili itimize wajibu wake wa kutoa huduma kwa

wananchi wake. Nawashauri waheshimiwa wabunge wenzangu

Page 52: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI … · Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita

Page 52 of 52

kuwa kamwe tusikubali kuwaongezea wananchi mzigo wa gharama

za maisha kwa kukubaliana na serikali katika kupandisha kodi

kwenye bidhaa za mafuta, ngano, matumizi ya simu za mkononi,

malighafi za sabuni na kodi zozote ambazo zitawaumiza wananchi

wetu. Tuiambie serikali itumie vyanzo vingine vya mapato kwa ajili ya

kupata fedha za kujiendesha bila ya kuwaumiza wananchi wetu.

Sote tutimize wajibu wetu kwa taifa letu. Njia hizo zipo na baadhi

tunmezipendekeza kupitia hotuba yetu hii na hotuba zilizopita. Ni

jukumu la serikali kuhakikisha kuwa inayachukua mapendekezo

haya na kuyatekeleza kwa ajili ya kumwokoa mwananchi masikini.

Imeshajidhihirisha kuwa pale ambapo serikali imeyachukua

mapendekezo yetu na kuyatekeleza kwa ufanisi, kumekuwepo na

mabadiliko chanya. Serikali isione aibu kuyachukua mapendekezo

yetu na kuyatekeleza kwa sababu tunayatoa kwa moyo wa

uzalendo wa kulisaidia taifa letu na watu wake. Sisi si wabinafsi.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo kwa niaba ya kambi ya

upinzani naomba kuwasilisha.