106
HOTUBA YA WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI MHESHIMIWA PROF. JOYCE LAZARO NDALICHAKO (MB.) AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2016/17 DODOMA MEI, 2016

HOTUBA YA WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA · PDF filei hotuba ya waziri wa elimu, sayansi, teknolojia na ufundi mheshimiwa prof. joyce lazaro ndalichako (m b.) akiwasilisha bungeni

Embed Size (px)

Citation preview

i

HOTUBA YA WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI,TEKNOLOJIA NA UFUNDI MHESHIMIWA PROF.JOYCE LAZARO NDALICHAKO (MB.)AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YAMATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2016/17

DODOMA MEI, 2016

ii

“Natambua juhudi kubwa zimefanyika katika upanuzi waelimu ya awali, msingi, sekondari na vyuo vikuu.Serikali ya awamu ya tano, itajielekeza katika kuongezaubora wa elimu inayotolewa ikiwa ni pamoja nakuongeza mkazo katika masomo ya sayansi.”

Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakatiakifungua rasmi Bunge la 11, tarehe 22 Novemba2015.

i

YALIYOMO

YALIYOMO.....................................................................

i

VIFUPISHO ................................................................ iii

1.0 UTANGULIZI ..................................................... 1

2.0 DIRA, DHIMA NA MAJUKUMU YA WIZARA YAELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI........................................................................... 4

DIRA NA DHIMA YA WIZARA .......................... 4MAJUKUMU YA WIZARA .................................. 4

3.0 VIPAUMBELE VYA WIZARA YA ELIMU,SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI ............. 6

4.0 MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI KWAMWAKA 2015/16 ................................................ 8

5.0 MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMUKWA MWAKA 2015/16 NA MPANGO NABAJETI KWA MWAKA 2016/17 .......................... 10

5.1 UTUNGAJI NA UTEKELEZAJI WA SERAYA ELIMU ................................................. 10

5.2 UPATIKANAJI WA FURSA ZA ELIMUNA MAFUNZO ......................................... 14

5.3 KUINUA UBORA WA ELIMU NAMAFUNZO ............................................... 16

5.4 TAFITI NA HUDUMA KWA JAMII ............. 36

5.5 SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU…. 40

5.6 URATIBU WA TAASISI NA WAKALA ........ 49

ii

5.7 USIMAMIZI WA UTEKELEZAJI WAPROGRAMU NA MIRADI ......................... 67

6.0 SHUKRANI ......................................................... 83

7.0 MAOMBI YA FEDHA KWA MWAKA 2016/17… 86

VIAMBATISHO ........................................................... 88

iii

VIFUPISHO

DAAD Deutscher Akademischer AustauschDienst

DfID Department for InternationalDevelopment

EU European UnionFDC Folk Development CollegesICT Information and Communication

TechnologyKKK Kusoma, Kuandika na KuhesabuLANES Literacy and Numeracy Education

SupportMMES Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya

SekondariNACTE National Council for Technical

EducationNECTA National Examination Council of

TanzaniaOR-TAMISEMI

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa naSerikali za Mitaa

OVC Orphans and Vulnerable ChildrenSIDA Swedish International Development

AgencySLADS School of Library Archives and

Documen- tation StudiesSTHEP Science, Technology and Higher

Education Project

iv

SWASH Schools Water Sanitation and HygieneTEHAMA Teknolojia ya Habari na MawasilianoTET Taasisi ya Elimu TanzaniaUDSM University of Dar es SalaamUNESCO United Nations Educational Scientific

and Cultural Organization

UNICEF United Nations Children’s FundVETA Vocational Education and Training

AuthorityVVU Virusi Vya Ukimwi

1

1.0 UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwana Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge yaHuduma na Maendeleo ya Jamii ndani ya Bunge lakoTukufu, ambayo imechambua Bajeti ya Wizara yaElimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, naomba kutoahoja kwamba sasa Bunge lako likubali kupokea nakujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Kazi za Wizara kwamwaka 2015/16 na Mpango wa Utekelezaji wa Bajetikwa mwaka 2016/17. Aidha, naliomba Bunge lakoTukufu likubali kupitisha Makadirio ya Mapato naMatumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia naUfundi kwa mwaka wa fedha 2016/17.

2. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee kabisana kwa heshima kubwa napenda kutoa shukranizangu za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe JosephMagufuli kwa imani kubwa aliyoonesha kwangu kwakuniteua kuwa Mbunge na Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi. Ninatambua ukubwa wadhamana aliyonipa na changamoto zilizopo katikaSekta hii. Napenda kumhakikishia Mheshimiwa Raisna wananchi wote kwa ujumla kuwa nitafanya kazihii kwa uadilifu na umahiri wa hali ya juu, ilikuhakikisha kuwa tunakidhi matarajio ya Watanzaniakatika sekta hii ya elimu ambayo ndiyo uti wamgongo wa maendeleo ya taifa letu.

2

3. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hiikumpongeza sana Mhe. Dkt. John Pombe Magufulikwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania wa Awamu ya Tano. Aidhanampongeza kwa uongozi wake wenye kuzingatiauwajibikaji na utendaji wenye tija kwa kazi kubwaanayoifanya ya kuwatumikia kwa moyo wa dhatiwananchi wote.

4. Mheshimiwa Spika, Napenda pia kumpongeza kwadhati Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwakuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na kwa kuandika historiamuhimu sana ya kuwa Makamu wa kwanzamwanamke tangu nchi yetu ilipopata uhuru. Vilevile,nitumie fursa hii kumpongeza Mheshimiwa MajaliwaKassim Majaliwa, kwa kuteuliwa na Rais na baadayekuthibitishwa na Bunge lako kuwa Waziri Mkuu waJamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha,nawapongeza Mheshimiwa Job Ndugai (Mb) naMheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) kwakuchaguliwa kuwa Spika na Naibu Spika wa Bungehili la 11 pamoja na Wenyeviti wote wa Bunge.

5. Mheshimiwa Spika, napenda pia kuwapongezaMheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kwakuchaguliwa kuwa Rais wa Serikali ya Mapinduziya Zanzibar kwa kipindi cha Pili na MheshimiwaBalozi Seif Ali Iddi kuwa Makamu wa Pili wa Rais.

3

6. Mheshimiwa Spika, ninapenda kuishukuru Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleoya Jamii chini ya Mwenyekiti wake MheshimiwaPeter Serukamba, kwa ushauri mzuri waliotupatiawakati wa maandalizi ya Bajeti hii. Wizara yanguimezingatia na itaendelea kuzingatia ushauri namaelekezo ya Kamati kwa lengo la kuleta ufanisikatika utendaji wa Sekta ya Elimu, Sayansi, naTeknolojia. Aidha, napenda kumshukuru Waziri kivuliwa Wizara hii, Mheshimiwa Susan Lyimo, kwaushirikiano wake.

7. Mheshimiwa Spika, Hotuba yangu imegawanyikakatika sehemu kuu Saba: Sehemu ya Kwanza niUtangulizi; Sehemu ya Pili ni Dira, Dhima naMajukumu ya Wizara; Sehemu ya Tatu ni Vipaumbelevya Wizara kwa mwaka 2016/17; Sehemu ya Nne niMapitio ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwaMwaka 2015/16; Sehemu ya Tano ni Mapitio yaUtekelezaji kwa mwaka 2015/16 na Mpango na Bajetikwa Mwaka 2016/17; Sehemu ya Sita ni Shukrani;na sehemu ya Saba ni Maombi ya Fedha.

4

2.0 DIRA, DHIMA NA MAJUKUMU YA WIZARAYA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NAUFUNDI

DIRA NA DHIMA YA WIZARA

8. Mheshimiwa Spika, Dira ya Wizara ni kuwa naMtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa, stadi,umahiri, uwezo na mitazamo chanya ili kuwezakuchangia katika kuleta maendeleo ya Taifa. Aidha,Dhima ya Wizara ni kuinua ubora wa elimu namafunzo na kuweka mifumo na taratibuzitakazowezesha kupata idadi kubwa ya Watanzaniawalioelimika na wanaopenda kujielimisha zaidi iliwaweze kuchangia katika kufikia malengo yamaendeleo ya Taifa letu.

MAJUKUMU YA WIZARA

9. Mheshimiwa Spika, Majukumu ya Wizara ya Elimu,Sayansi, Teknolojia na Ufundi ni kama ifuatavyo:

(i) kutunga na kutekeleza Sera za Elimu, Utafiti,Huduma za Maktaba, Sayansi, Teknolojia,Ubunifu na Uendelezaji wa Mafunzo yaUfundi;

(ii) kuendeleza Elimumsingi kwa Kutoa Ithibatiya Mafunzo ya Ualimu na Maendeleo yaKitaalamu ya Walimu;

(iii) kubainisha Vipaji na Kuviendeleza;

5

(iv) kusimamia Uendelezaji wa Mafunzo katikaVyuo vya Maendeleo ya Wananchi;

(v) kusimamia Mfumo wa Tuzo wa Taifa;

(vi) kuainisha Mahitaji ya Nchi katika Ujuzi naKuuendeleza;

(vii) kuweka Viwango vya Taaluma ya Ualimu;

(viii) kusimamia Ithibati na Uthibiti wa Shule;

(ix) kusimamia Huduma za Machapisho yaKielimu;

(x) kutegemeza/kuimarisha utumiaji wa Sayansi,Uhandisi, Teknolojia na Hisabati;

(xi) kuendeleza Wataalamu wa ndani katikaSayansi, Teknolojia na Ubunifu;

(xii) kuratibu utafiti katika Sayansi na Teknolojia;

(xiii) uendelezaji wa Rasilimaliwatu na UongezajiTija ya Watumishi walio chini ya Wizara; na

(xiv) kuratibu Shughuli za Idara, Mashirika,Wakala, Programu na Miradi iliyo chini yaWizara.

6

3.0 VIPAUMBELE VYA WIZARA YA ELIMU,SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI

10. Mheshimiwa Spika, Dira ya Maendeleo ya Taifa(2025) imelenga kuifanya Tanzania kuwa nchi yakipato cha kati ifikapo mwaka 2025. Katika juhudiza kufikia lengo hili, Wizara ya Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi ina jukumu la kuandaawataalamu wenye ujuzi na maarifa watakaotoamchango wenye tija kwa maendeleo ya nchi yetu.Wizara yangu inatambua kuwa utekelezaji wa azmaya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwa na uchumiwa viwanda inategemea kwa kiasi kikubwa ufanisikatika Sekta ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Uborawa rasilimali watu ni jambo la msingi sana katikakuhakikisha kuwa tija na ufanisi vinakuwepo katikaSekta zote muhimu ili kuchochea kasi ya ukuajiuchumi na hatimaye kuiwezesha nchi yetu kufikiauchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

11. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia mwelekeo huo,katika mwaka 2016/17, vipaumbele vya Sekta yaElimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi ni kamaifuatavyo:

(i) kuinua ubora wa elimu na mafunzo katikangazi zote za elimu na mafunzo nchini;

(ii) kuimarisha mifumo na usimamizi wa Ithibatina Uthibiti wa Ubora wa Elimu na mafunzo;

7

(iii) kuongeza upatikanaji na ushiriki katika fursaza elimu na mafunzo; na

(iv) kuimarisha tafiti na matumizi ya Sayansi,Teknolojia na Ufundi kwa lengo la kuongezachachu ya maendeleo.

8

4.0 MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETIKWA MWAKA 2015/16

12. Mheshimiwa Spika, naomba nianze kutoa tathminiya utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa mwaka wafedha 2015/16 kuanzia tarehe 1 Julai, 2015 haditarehe 30 Aprili, 2016.

Ukusanyaji wa Maduhuli Kwa Mwaka 2015/16

13. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16, Wizarailikusudia kukusanya jumla ya Shilingi286,074,571,684.47 ambapo Shilingi9,268,457,100.00 zilitarajiwa kukusanywa na Idarawakati Shilingi 276,806,114,584.47 zilitakiwakukusanywa na Taasisi zilizo chini ya Wizara.Makusanyo ya maduhuli hadi kufikia tarehe 30 Aprili,2016 yalikuwa ni jumla ya Shilingi199,422,233,349.12 ambayo ni sawa na asilimia69.7 ya makadirio. Kati ya fedha hizo, Shilingi5,723,343,678.36 zilikusanywa na Idara na Shilingi193,698,889,670.76 zilikusanywa na Taasisi zilizochini ya Wizara.

Matumizi ya Kawaida na Maendeleo kwa Mwaka2015/16

14. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha2015/16 bajeti ya Wizara ilikuwa ni Shilingi1,094,195,824,888.49 (Matumizi ya kawaida

9

Shilingi 511,525,227,000.00 na Matumizi yamaendeleo Shilingi 582,670,597,888.49). Hadikufikia tarehe 30 Aprili, 2016 fedha ambazozimekwishatolewa na Hazina zilikuwa Shilingi789,460,338,381.61 (Matumizi ya kawaida Shilingi351,284,829,898.00 na Matumizi ya MaendeleoShilingi 438,175,508,483.61) sawa na asilimia72.15 ya bajeti ya Wizara. Aidha, fedha zilizotumikahadi kufikia tarehe 30 Aprili 2016 zilikuwa ni Shilingi694,148,943,065.89 (Matumizi ya kawaida Shilingi313,796,049,657.61 na Matumizi ya maendeleoShilingi 380,352,893,408.28) sawa na asilimia 87.9ya fedha zilizotolewa.

10

5.0 MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMUKWA MWAKA 2015/16 NA MPANGO NABAJETI KWA MWAKA 2016/17

15. Mheshimiwa Spika, mwaka 2015/16, Wizara ililengakusimamia utekelezaji wa mambo makuu yafuatayo:

(i) utungaji na utekelezaji wa Sera za Elimu;

(ii) upatikanaji wa fursa za elimu na mafunzo;

(iii) ithibati ya Shule;

(iv) uthibiti ubora wa elimu;

(v) mafunzo ya Ualimu, hususan wa Sayansi,Hesabu, Ufundi (ikiwemo ufundi sanifumaabara), Lugha na KKK;

(vi) uratibu wa shughuli za Taasisi na Wakala; na

(vii) usimamizi wa utekelezaji wa programu namiradi mbalimbali.

5.1 UTUNGAJI NA UTEKELEZAJI WA SERA YAELIMU

16. Mheshimiwa Spika, mojawapo kati ya majukumuya msingi ya Wizara yangu ni kubuni na kutungaSera mbalimbali za kusimamia Elimu, Mafunzo yaUfundi, Sayansi, Teknolojia, Ubunifu, Huduma zaMaktaba na Utafiti.

11

Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo (2014)

17. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha2015/16, yafuatayo yalifanyika:

(i) kutafsiri Sera ya Elimu na Mafunzo (2014) kwalugha ya Kiingereza na kukamilisha maandaliziya Mkakati wa Utekelezaji wa Sera ya Elimu;

(ii) kufanya uchambuzi wa mahitaji ya mabadilikoya sheria ili kutekeleza Sera ya Elimu naMafunzo (2014);

(iii) kuhuisha mitaala ya elimu ya awali, elimu yamsingi na elimu ya sekondari. Aidha, vitabu vyakiada vya Darasa la Kwanza vinavyoendana naMtaala uliohuishwa vinasambazwa kwenyeMikoa na Halmashauri zote nchini; na

(iv) ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wamajukumu ya Wizara.

Utekelezaji wa Elimumsingi bila Malipo

18. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza azma yaSerikali ya kutoa Elimumsingi bila Malipo, Wizarayangu ilitoa Waraka wa Elimu Namba 6 wa mwaka2015 kwa lengo la kutoa mwongozo wa namna yakutekeleza Elimumsingi bila malipo. Waraka waElimu Na. 6 umeweka bayana majukumu ya wadauwote muhimu katika utoaji wa Elimumsingi bilaMalipo ambapo imeainishwa kuwa wazazi

12

wanatakiwa kufanya yafuatayo:

(i) kununua sare za shule na michezo, vifaa vyakujifunzia, chakula kwa wanafunzi wa kutwana kugharamia matibabu kwa watoto wao.

(ii) kulipia nauli ya kwenda shule na kurudi kwawanafunzi wa kutwa.

(iii) kulipa nauli za wanafunzi wakati wa likizo;kununua vifaa kwa ajili ya malazi shuleni navifaa vya kujifunzia.

19. Mheshimiwa Spika, natoa wito kwa wazazi nawalezi kuunga mkono juhudi za Serikali zakuhakikisha kuwa watoto wote wanapata elimu. Nimuhimu wazazi mkawawezesha watoto wenukupata mahitaji ya shule na muhimu zaidi mjengeutamaduni wa kukagua madaftari ya watoto wenu ilikujiridhisha kama wanafundishwa shuleni.

20. Mheshimiwa Spika, serikali hutoa fedha ya chakulakwa wanafunzi wa bweni tu. Hivyo, kama kunashule za sekondari ambazo zimesajiliwa kama shuleza kutwa lakini wamejenga Hosteli na miundombinuinayokidhi vigezo vya kuwa shule za bweni, MaafisaElimu wazitambue na wawasilishe maombi kwenyeWizara yangu ya kuomba kuzibadilisha hadhi.Endapo zitakuwa zimekidhi vigezo muhimuzitabadilishwa na kuwa shule za bweni. Kwakufanya hivyo, wanafunzi wataweza kutengewa

13

fedha ya chakula kama ilivyoainishwa kwenyeWaraka wa Elimu Na. 6 wa mwaka 2015.

Mpango wa Utekelezaji wa Sera ya Elimu naMafunzo (2014) kwa mwaka 2016/17

21. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizarayangu itaendelea na utekelezaji wa Sera ya Elimu naMafunzo (2014) na Mkakati wake. Wizara itafanyamabadiliko ya Sheria ya Elimu na kupitia Sheria,Kanuni na Taratibu za taasisi zilizo chini ya Wizara,hususan Baraza la Mitihani, Taasisi ya ElimuTanzania, Taasisi za Ithibati na Uthibiti, Bodi yaMikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu na Mamlakaya Elimu Tanzania kwa lengo la kuimarishautekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo (2014) kwaufanisi. Aidha, Wizara itakamilisha taratibu zauundwaji wa Bodi ya Kitaalamu ya Walimu.

22. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizarayangu itaendelea kuimarisha Mpango wa matumiziya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji. Vilevile,Wizara itatoa mwongozo wa kuwatambua nakuwaendeleza wanafunzi wenye vipaji, vipawa namahitaji maalumu na wenye kasi kubwa ya kujifunzamasomo ya Sayansi na Hisabati ili kuwezakuwaendeleza katika fani mbalimbali za teknolojia.

14

Sera ya Sayansi, Teknolojia naUbunifu

23. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizarayangu imedhamiria kuimarisha na kuongeza kasiya ukuaji wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwakukamilisha mapitio ya Sera zifuatazo:

(i) Sera ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia yamwaka 1996 na kutunga sera mpya ya Taifa yaSayansi, Teknolojia na Ubunifu;

(ii) Sheria Na. 7 ya mwaka 1986 iliyoanzisha Tumeya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)na kutunga sheria mpya ya Maendeleo yaSayansi, Teknolojia na Ubunifu; na

(iii) Sheria Na. 7 ya mwaka 2003 iliyoanzisha Tumeya Nguvu za Atomiki (Tanzania Atomic EnergyCommission - TAEC).

5.2 UPATIKANAJI WA FURSA ZA ELIMU NAMAFUNZO

Udahili wa wanafunzi vyuoni

24. Mheshimiwa Spika, Serikali ina lengo la kuendeleakuongeza fursa za Elimu na Mafunzo ili kuandaarasilimali watu itakayochangia maendeleo ya taifa.Kupitia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya UfundiStadi, Wizara iliendelea kuratibu udahili wawanafunzi ambapo kwa mwaka 2015 wanafunzi

15

189,687 walidahiliwa katika vyuo mbalimbali vyaufundi. Aidha, kwa kupitia Baraza la Elimu ya Ufundiwanafunzi 75,186 walidahiliwa kwenye vyuombalimbali kupitia mfumo wa pamoja wa udahili.

25. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kupitia Tume yaVyuo Vikuu imeendelea kuratibu udahili wawanafunzi wanaojiunga na Elimu ya Juu kupitiaMfumo wa Udahili wa Pamoja (Central AdmissionSystem) wa kudahili wanafunzi wa Digrii ya kwanza.Katika mwaka 2015/16 wanafunzi 65,064 wa Digriiya kwanza walidahiliwa wakiwemo wanawake22,225 sawa na asilimia 34.2 na kufanya jumla yawanafunzi wote wa elimu ya juu kufikia 210,000.Wanafunzi hao walidahiliwa katika vyuo vikuu na vyuovikuu vishiriki 49 na Taasisi zisizo vyuo vikuu 21 (kamailivyo kwenye kiambatisho Na. 1).

Elimu Maalum

26. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia kwamba elimuni haki ya msingi ya kila Mtanzania, Wizara yanguimeendelea kupanua fursa za elimu na mafunzo kwakuimarisha elimu kwa wanafunzi wenye mahitajimaalum. Katika mwaka 2015/16, Wizara yanguiliendesha mafunzo kwa walimu 142 kuhusuufundishaji wa Sayansi na Hisabati kwa wanafunziwasioona. Aidha, kupitia Chuo Kikuu Huria chaTanzania wanafunzi 45 viziwi na wasioona walipewamafunzo ya kutumia TEHAMA katika kurahisisha

16

kujifunza ili waweze pia kupata maarifa na taarifambalimbali zilizoko kwenye mtandao.

27. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17 Wizarayangu itafanya yafuatayo:

(i) kununua vifaa mbalimbali vya wanafunzi wenyemahitaji maalum. Vifaa hivyo ni pamoja namashine za nukta nundu, fimbo nyeupe, viti vyamagurudumu, visaidizi vya kusikia, na vifaa vyavituo maalum vya msaada wa kitabibu;

(ii) kukarabati na kufanya matengenezo ya vifaavya wanafunzi walemavu; na

(iii) kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya maabarana vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwawanafunzi wenye mahitaji maalum wa shuleza msingi na Sekondari.

5.3 KUINUA UBORA WA ELIMU NA MAFUNZO

28. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inatambuakwamba elimu bora ina nafasi ya pekee katikakufanikisha ujenzi wa msingi wa uchumi wa kisasawa taifa linalojitegemea. Ili kukidhi azma hii, Wizarayangu imeimarisha na kuboresha mfumo wa ithibatina uthibiti wa shule na vyuo, mafunzo ya ualimu,mazingira ya kufundishia na kujifunzia pamoja nahuduma za maktaba.

17

Ithibati ya Shule za Msingi na Sekondari

29. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imeendeleakusimamia ithibati ya shule kwa lengo la kuzipatiashule idhini ya kufundisha masomo husika,kuthibitisha Wamiliki na Mameneja wa Shule nakutoa vibali vya ujenzi wa shule zisizo za Serikali.Hadi kufikia Aprili, 2016 shughuli zifuatazo zilifanyika:

(i) shule 174 zikiwemo shule za awali 4, msingi115 na sekondari 55 zilisajiliwa;

(ii) kutoa vibali kwa Wamiliki 151 na Mameneja154 wa shule na vibali vya ujenzi wa shule 201zisizo za Serikali;

(iii) kufuta vibali vya ujenzi kwa shule 37 kwa kuwavilikuwa vimeombwa zaidi ya miaka kumiiliyopita, na hapakuwa na jitihada za kuendeleana ujenzi na kuanza taratibu za kusajili shulehizo; na

(iv) Wamiliki na Mameneja wa shule 13 walifutiwauthibitisho kutokana na shule zao kubadiliumiliki.

30. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2016/17, Wizarayangu itafanya yafuatayo katika ithibati ya shule;

(i) kuhuisha na kuandaa Mwongozo wa Usajili waShule za Serikali na zisizo za Serikali kulinganana mahitaji ya sasa;

18

(ii) kusajili shule za Awali, Msingi na Sekondarikwa kutilia mkazo uanzishwaji wa shule zenyemwelekeo wa Sayansi, Kilimo, Teknolojia naUfundi; na

(iii) kusajili vituo vinavyotoa Elimu Nje ya MfumoRasmi na Elimu Huria.

Uthibiti wa Ubora wa Shule za Msingi na Sekondari

31. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inatambuakwamba, uthibiti ubora wa shule ni jambo muhimusana katika kuimarisha ubora wa elimu na mafunzoyanayotolewa katika shule za msingi na sekondari.Hadi kufikia Aprili, 2016, shule 7,882 kati ya 17,242ambayo ni sawa na asilimia 46 ya shule zilizolengwazilifanyiwa ukaguzi. Aidha, walimu 292 waliteuliwakuwa Wathibiti Ubora wa Shule na kupangwa katikaofisi za Kanda na Wilaya kwa lengo la kuimarishaukaguzi wa shule.

32. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inafuatilia kwakaribu na kuhakikisha kwamba watoto wotewanafundishwa vema na wanaweza kumudu stadiza kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) kuanziahatua za mwanzo. Katika kutimiza azma hii WathibitiUbora wa Shule wapatao 1,435 wamepatiwamafunzo ya stadi za kufundisha KKK ili wawezekufuatilia utekelezaji wake katika shule za msingina kutoa msaada kwa walimu wanapofundisha.

19

Vilevile, Wizara ilifungua ofisi za Uthibiti Ubora waShule na kupeleka Wathibiti Ubora wa Shule katikaHalmashauri za Wanging’ombe, Makambako, Kaliua,Nyasa, Geita (Mji), Njombe (Mji), Nyangh’wale,Ikungi, Kalambo, Mbogwe, Buligwe, Gairo,Chemba, Majinga, Momba, Bumbuli, Handeni (M),na Mkarama. Ofisi hizi zimesaidia walimu nawadau wa elimu kupata huduma za Wathibiti Uborawa Shule kwa karibu zaidi.

33. Mheshimiwa Spika, katika uthibiti ubora wa shulekwa mwaka 2016/17, Wizara imepanga kufanyayafuatayo:

(i) kufuatilia ubora wa utoaji elimu katika shule10,818 na kutoa ushauri kwa lengo lakuboresha ufundishaji;

(ii) kutoa ushauri wa kitaalamu na kitaaluma kwawadau wa elimu;

(iii) kukamilisha ujenzi wa ofisi za uthibiti uborakatika Wilaya za Hai, Masasi, Mtwara Mjini,Namtumbo, Urambo na Sumbawanga Mjini;

(iv) kufuatilia ufundishaji katika elimu ya awali nastadi za KKK kwa wanafunzi wa Darasa la I naII;

(v) kuandaa kiunzi cha Uthibiti Ubora wa Shule(Basic Education Quality AssuranceFramework) na kutekeleza mapendekezo ya

20

uimarishaji wa mfumo wa ukaguzi;

(vi) kuhuisha mwongozo wa Wathibiti Ubora,kuchapa na kusambaza kwa Wathibiti Uborawote; na

(vii) kununua na kugawa pikipiki kwa WaratibuElimu Kata wa Mikoa 18 na kuchangia mafutakwa ajili ya magari na pikipiki zilizonunuliwachini ya Mpango wa LANES.

Ithibati na Uthibiti wa Elimu ya Ufundi naMafunzo ya Ufundi Stadi

34. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2015/16, Wizarayangu iliendelea kusimamia ubora wa Elimu yaUfundi nchini kwa kupitia Baraza la Taifa la Elimu yaUfundi. Baraza lilivifanyia tathmini na kuvisajili vyuo70, kutoa ithibati kwa Vyuo 23 vya Ufundi; nakuhakiki jumla ya Wakufunzi 807 ili kubaini uhalaliwao wa kufundisha katika ngazi husika. Aidha,Baraza limetambua Idara 35 na kuzipatia ithibati yakuendesha programu za mafunzo.

35. Mheshimiwa Spika, ili kuimarisha elimu ya ufundinchini, Baraza liliendesha mafunzo ya kuhakikiubora wa mafunzo vyuoni kwa wafanyakazi 30 waBaraza na kwa wakufunzi 22 wa vyuo pamoja nakukagua jumla ya vyuo 35 ili kutathmini ubora wautoaji wa mafunzo. Aidha, Baraza liliidhinishamitaala 93 inayozingatia umahiri ikiwemo 42 ya

21

ngazi ya Cheti, 34 ya Diploma, 16 ya Digrii na 1Digrii ya uzamili. Baraza pia limetoa mafunzo ya jinsiya kutumia mitaala inayozingatia umahiri kwawakufunzi 417 wa vyuo.

36. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizarayangu kupitia Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundiitaendelea kukagua na kusajili vyuo vya ufundikulingana na maombi na mahitaji ya nchi. Barazapia litaendelea kusajili wakufunzi ili kuhakiki sifa zaopamoja na kukagua na kutoa ithibati kwa vyuo vyaufundi na kutambua idara zenye uwezo wakuendesha programu mbalimbali za ufundi.

37. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizarayangu pia kupitia Baraza la Taifa la Elimu yaUfundi litafanya shughuli zifuatazo:

(i) tathmini ya ubora wa mafunzo katika vyuo 60na kuboresha miongozo na taratibu za usajilina utoaji ithibati kwa vyuo vya ufundi.

(ii) litadahili wanafunzi 90,000 katika ngazi yaCheti, Diploma na Digrii kupitia mfumo wapamoja wa udahili.

(iii) litajengea uwezo vyuo 60 katika kujihakiki nakusimamia ubora wa mafunzo vyuoni, kupimana kuhakiki ubora wa mitaala ya vyuo vya ufundikatika ngazi zote,

22

(iv) litatengeneza mfumo wa kielektroniki wakupokea na kuhakiki mitaala, kufanya tafitizenye lengo la kuboresha utoaji wa mafunzo yaelimu ya ufundi,

(v) kuratibu mafunzo ya kutumia mitaalainayozingatia umahiri kwa walimu 400,

(vi) kuandaa moduli za mafunzo kwa walimukuhusu kuandaa, kupitia, kufundisha nakupima mitaala ya elimu ya ufundi.

Uthibiti Ubora wa Vyuo vya Elimu ya Juu

38. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imeendeleakusimamia ubora wa elimu ya juu kupitia Tume yaVyuo Vikuu Tanzania. Katika mwaka 2015/16, Tumeya Vyuo Vikuu ilikagua na kutathmini vyuo vikuu 15nchini kwa lengo la kusimamia ubora. Katika ukaguzihuo, ilibainika kuwa Chuo Kikuu cha Mt. YosefuKampasi ya Songea (Koleji za Kilimo, Teknolojia naTEHAMA) na Kampasi ya Arusha hazikukidhiviwango vya ubora stahiki. Changamoto zilizobainikani pamoja na vyuo kutokuwa na wahadhiri wenyesifa stahiki na mitaala kutoandaliwa ipasavyo.Mazingira ya kufundishia na kujifunzia kutokidhivigezo hususan ukosefu wa mafunzo kwa vitendokutokana na kutokuwepo kwa maabara.

23

Kufutwa kwa Ithibati kwa Chuo cha Mt Yosef

39. Mheshimiwa Spika, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzaniakwa kutumia mamlaka yake kisheria ilifuta usajili waKoleji za Songea na Kampasi ya Arusha. Kutokanana hatua hiyo, jumla ya wanafunzi 3,585 waliokuwakwenye vyuo hivyo walihamishiwa kwenye Vyuovingine. Hata hivyo, imekuwepo changamoto katikakupokelewa kwa wanafunzi hao kwani vyuovilivyowapokea vimeona hawakuwa wamesoma kwakiwango cha kutosha ukilinganisha na mwaka wamasomo waliokuwepo. Ili kuhakikisha wanapatamaarifa stahiki kwa miaka waliyopo, baadhi ya vyuovimewarudisha mwaka wakati vingine vimelazimikakuwapa mafunzo ya ziada kukabiliana namapungufu kitaaluma waliyoyabaini.

40. Mheshimiwa Spika, Hali hiyo inathibitisha kuwaelimu iliyokuwa ikitolewa katika Chuo cha Mt Yosefhaikuwa inakidhi viwango hali iliyosababisha kuwepokwa migogoro ya wanafunzi ya mara kwa marakatika chuo hicho. Napenda kuchukua nafasi hiikuviagiza vyuo vyote vya elimu kuhakikishavinaendeshwa kwa kufuata Sheria. Kanuni naTaratibu. Wizara yangu haitasita kuchukua hatua kalidhidi ya chuo kitakachokwenda kinyume na taratibu.

24

Wanafunzi wa Kidato cha 4 waliokuwawanachukua Digrii Katika chuo cha Mt. Yosef

41. Mheshimiwa Spika, naomba sasa nizungumziesuala la wanafunzi 424 wa Mt Yosef walioondolewachuoni. Suala hili liliwasilishwa katika Bunge lakotukufu siku ya tarehe 17/05/2015 na Mh CosatoDavid Chumi (Mbunge wa Mafinga). Kwa mujibu waKanuni 28(11) aliwasilisha maelezo binafsi akitakaSerikali kutoa ufafanuzi kuhusu hatua hiyo. Nitatoaufafanuzi wa kina ili sababu za uamuzi huo ziwezekueleweka ipasavyo.

42. Mheshimiwa Spika, katika zoezi la kuwahamishawanafunzi wa Mt. Yosef kampasi ya Arusha,ilibainika kuwa walikuwepo wanafunzi ambaowalidahiliwa kujiunga na Digrii ya Ualimu kwamasomo ya Sayansi wakati hawakuwa na sifastahiki. Wanafunzi hao walikuwa wamemaliza Kidatocha Nne wakiwa na ufaulu hafifu ambapomwanafunzi aliyepata ‘D’ nne sawa na Divishen IVya pointi 31 alipewa fursa ya kudahiliwa kwenyeDigrii ya Ualimu wa Sayansi.

43. Mheshimiwa Spika, jambo la kusikitisha zaidi nikuwa katika kudahili wanafunzi hao kwenye Digrii yaSayansi, masomo ya msingi aliyoyasomamwanafunzi hayakuzingatiwa. Kwa mfano, wapowaliochukua mkondo wa Biashara yaani masomo yaBook-keeping na Commerce lakini walidahiliwa

25

kusoma Sayansi. Aidha, wapo ambaohawakuchukua kabisa mkondo wa Sayansi yaanimasomo ya Sayansi lakini walidahiliwa. Vilevile,wapo wanafunzi waliofeli masomo ya Sayansi Kidatocha Nne lakini wakadahiliwa kuchukua Digrii yaSayansi ya Ualimu kama inavyooneshwa katikamifano ifuatayo:

S/N INDEX UFAULU KWA MASOMO

1 S2123/0043/2011CIV-D,HIS-F,GEO-D,KIS-F,ENG-D,PHY-D,CHE-F,BIO-D,MAT-F

2 S0194/0027/2012CIV-C,HIS-D,GEO-D,BIB-D,KIS-D,ENG-D,BIO-D,MAT-F,COM-D,BOO-F

3 S0348/0068/2005CIV-D,HIS-F,GEO-D,KIS-F,ENG-D,PHY-F,CHE-D,BIO-D,AGR-F,MAT-F

4 S0353/0091/2009CIV-D,HIS-D,GEO-F,KIS-D,ENG-F,PHY-F,CHE-D,BIO-D,AGR-C,MAT-F

5 S2295/0019/2012CIV-D,HIS-C,GEO-D,KIS-D,ENG-D,BIO-C,COM-D,MAT-F

44. Mheshimiwa Spika, kutokana na wanafunzi kuwana sifa za aina hiyo ambazo hazitoshelezi hatakujiunga na mafunzo ya Cheti cha Ualimu, Serikalikupitia Tume ya Taifa ya Vyuo Vikuu, imefuta udahiliwao wa Digrii ya Ualimu wa Sayansi. Serikaliimesikitishwa sana na na kitendo hicho cha kudahiliwanafunzi hao kujiunga na Digrii ya Ualimu waSayansi wakati hawana sifa stahiki. Katika mwaka2013/14 walipodahiliwa kwa ufaulu wa Kidato cha 4kwa kiwango cha angalau ‘D’ nne, sifa za kujiungana Cheti cha Ualimu zilikuwa ziko juu zaidi. Aidha,wanafunzi hao walipewa mikopo licha ya kutokuwana sifa stahiki.

45. Mheshimiwa Spika, kutokana na hali hiyo, Serikaliimeunda Kamati ya kuchunguza mchakato mzima

26

wa uanzishwaji wa programu hiyo na sababu zawanafunzi wasio na sifa kudahiliwa. Hatua kalizitachukuliwa dhidi ya wote watakaobainikakuhusika na suala hilo.

Mafunzo ya Ualimu

46. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inatambuaumuhimu wa kuwa na walimu wenye sifa, maarifa naweledi katika kuinua viwango na ubora wa elimu.Katika mwaka 2015/16 Wizara yangu iliendelea najuhudi za kuongeza walimu, hususani walimu waSayansi na Hisabati ili kukabiliana na upungufu wawalimu wapatao 22,000 uliopo sasa. Walimu tarajali5,690 walidahiliwa kwa ngazi ya Diploma ya Ualimuwa masomo ya Hisabati na Sayansi katika ChuoKikuu cha Dodoma na vyuo vya ualimu vya Kleruu,Monduli na Korogwe. Aidha, Wizara imeendeleakutilia mkazo sifa za kudahili wanafunzi katikaprogramu za Ualimu, ambapo ufaulu wa chini niDaraja la Tatu katika mtihani wa kuhitimu Kidato chaNne na Kidato cha Sita.

47. Mheshimiwa Spika, ili kuimarisha uwezo wakitaaluma wa wakufunzi wa Sayansi na Hisabatikatika vyuo vya ualimu, Wizara yangu kupitia ufadhiliwa China Trust Fund na UNESCO – Tanzania imetoamafunzo ya TEHAMA kwa wakufunzi 20 na kuwekamiundombinu ya TEHAMA kwa vyuo vya Mondulina Tabora. Miundombinu hii imeimarisha ufundishaji

27

na ujifunzaji wa masomo ya Sayansi na Hisabati.

48. Mheshimiwa Spika kwa kutambua kwambawanafunzi wanaojiunga na elimu ya sekondariwanahitaji mafunzo kabilishi ya lugha ya kiingereza,Wizara yangu imetoa mafunzo kwa walimu 2,485 washule za sekondari kwa lengo la kuwawezesha walimuhao kumudu kuwasaidia wanafunzi wa Kidato chaKwanza. Aidha, vitabu 26,000 vya wawezeshaji nawalimu vimeandaliwa na kusambazwa kwenyewilaya 37 na mikoa 5 ya majaribio.

49. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17 Wizarayangu itaendelea kutoa mafunzo tarajali (Pre-service) ya walimu wa elimu ya awali pamoja nawale wa masomo ya Ufundi kwa shule za sekondariza ufundi na mafunzo ya Ufundi Sanifu wa Maabarakwa ajili ya maabara za shule za Sekondari. Aidha,Wizara yangu itaendelea kuendesha mafunzo kazinikwa Walimu wa Elimu Maalumu, Elimu ya Ufundi nakwa masomo yote ya Elimumsingi.

Uboreshaji wa Mazingira ya Kufundishia naKujifunzia

Elimumsingi na Sekondari

50. Mheshimiwa Spika, Mazingira ya kufundishia nakujifunzia yana mchango mkubwa katika kuinuaubora wa elimu katika ngazi zote. Katika mwaka

28

2015/16, Wizara imeandaa mpango wa ukarabatiwa shule kongwe za sekondari nchini ambapo katikaAwamu ya Kwanza shule 33 zitakarabatiwa. Shulehizi ni Ihungo, Ilboru, Kilakala, Mwenge, Msalato,Mzumbe, Nganza, Pugu, Same, Tabora Boys naTabora Girls. Shule nyingine ni Azania, Jangwani,Kantalamba, Mpwapwa, Tosamaganga, Malangali,Milambo, Nangwa, Kibiti, Minaki, Ifakara, SongeaBoys, Ndanda, Kigoma, Kibaha na Shule za Ufundiza Bwiru Boys, Ifunda, Iyunga, Moshi, Mtwara,Musoma na Tanga.

51. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kwa kushirikianana wabia wa maendeleo na OR-TAMISEMIimewezesha shule 250 za msingi na sekondarikatika wilaya 25 kuunganishwa kwenye mtandao wa“internet” na kupatiwa kompyuta mpakato, Projectorna kompyuta endeshi (Server) kwa ajili ya matumiziya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji.

52. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizarayangu kupitia Mamlaka ya Elimu itaendelea nauimarishaji wa miundombinu ya Shule na Vyuo vyaUalimu, ikiwemo ukarabati wa shule za sekondari7 kongwe pamoja na ujenzi wa nyumba 30 zawalimu zenye uwezo wa kuchukua walimu 180,katika maeneo yasiyofikiwa kwa urahisi. Wizara piaitajenga vyumba 25 vya madarasa na matundu 200ya vyoo katika shule zenye uhitaji mkubwa.

29

Elimu ya Juu

53. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inatambuaumuhimu wa mchango wa elimu ya juu katika juhudiza kufikisha nchi yetu katika uchumi wa kati ifikapomwaka 2025. Kwa kuzingatia hilo, Wizara yanguimekuwa ikiongeza majengo na kukarabatimiundombinu ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ilikuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunziakwa lengo la kuinua ubora na kuongeza fursa kwawanafunzi wengi zaidi kujiunga na Elimu ya Juu.Katika mwaka 2015/16 baadhi ya shughulizilizofanyika katika taasisi za elimu ya juu ni pamojana:

(i) Kukamilisha ujenzi wa maabara kwa ajili yaKitivo cha Sayansi- Chuo Kikuu cha Sokoinecha Kilimo unaogharimiwa na Mradi waEnhancing Pro-poor Innovation in NaturalResources and Agricultural Value-chain(EPINAV). Mradi huu umekamilika kwa asilimia75. Aidha, Chuo kimekarabati maktaba namaabara na kupeleka maji Kampasi yaSolomon Mahlangu; na

(ii) kukarabati vituo vya Mikoa ya Temeke, Mbeya,Bungo na Kinondoni vinavyosimamiwa naChuo Kikuu Huria cha Tanzania.

30

54. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizarayangu itaendelea kuboresha mazingira yakufundisha na kujifunzia kwa kufanya yafuatayo:

(i) kukiwezesha Chuo Kikuu Huria cha Tanzaniakukarabati miundombinu katika mikoa yaRuvuma, Rukwa, Kilimanjaro, Singida, Mara naPwani;

(ii) kukarabati hosteli za wanafunzi, kumbi zamihadhara, Kituo cha Polisi, nyumba zawahadhiri pamoja na miundombinu ya majitakakatika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam;

(iii) kukarabati hosteli za wanafunzi Kampasi kuuna ujenzi wa majengo ya madarasa na ofisi zakampasi ya Mbeya ya Chuo Kikuu cha Mzumbe;

(iv) kujenga maabara katika Chuo Kikuu cha Ardhiambayo itakuwa na matumizi mbalimbali (Mult-purpose Laboratory) pamoja na kukarabatihosteli za wanafunzi;

(v) kukarabati kumbi za mihadhara, maabara nahosteli za wanafunzi katika Chuo Kikuu chaSokoine cha Kilimo;

(vi) kukarabati majengo na miundombinu minginekatika Kampasi Kuu ya Chuo Kikuu chaUshirika Moshi na Kampasi ya Kizumbi;

(vii) kukamilisha ujenzi wa jengo la Utawala nakuanza ujenzi wa Maabara za Sayansi ilikuongeza fursa kwa wanafunzi zaidi kudahiliwa

31

katika mafunzo ya Sayansi katika Chuo KikuuKishiriki cha Elimu Dar es Salaam;

(viii) kujenga madarasa na Hosteli kwa Chuo cha“Earth Sciences” pamoja na Chuo cha “Naturaland Mathematical Sciences” katika Chuo Kikuucha Dodoma;

(ix) kukamilisha jengo la Mihadhara la Chuo KikuuKishiriki cha Elimu Mkwawa na kukarabatimiundombinu ya Chuo hicho;

(x) kujenga na kuweka samani katika jengo laMaktaba ya Chuo Kikuu cha Sayansi naTeknolojia Mbeya ili kuendana na ongezeko laudahili;

(xi) kukamilisha ujezi wa jengo la ghorofa kumikatika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam nakuweka umeme na samani katika Kampasi Kuuna kukarabati miundombinu ya majitaka kwaKampasi ya Mwanza ambayo itaanza kutoamafunzo katika ngazi ya cheti katika fani yautunzaji na usindikaji wa ngozi kuanzia hatuaya mnyama akiwa hai, akichinjwa hadi kufikiahatua ya uchunaji na usindikaji wa ngozi; na

(xii) kuendeleza ujenzi wa Hosteli katika Kampasiya Kivukoni ya Chuo cha Kumbukumbu yaMwalimu Nyerere na kununua samani kwa ajiliya Kampasi ya Bububu, Zanzibar.

32

55. Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea na mpangowa uanzishwaji wa Chuo Kikuu cha Kilimo naTeknolojia cha Mwalimu Julius K. Nyerere. Utaratibuwa ujenzi wa Kampasi kuu ya Butiama utaanzamwaka wa 2016/17. Kuhusu kutumia majengo yaShule ya Sekondari Oswald Mang’ombe, Wizaraimefanya mazungumzo na wamiliki kukamilishauhamishaji wa miliki ya majengo kisheria. Aidha,tunawashukuru wamiliki pamoja na MheshimiwaNimrod Mkono kwa mchango wao katika kukuzaelimu nchini.

Kampasi Mpya ya Mloganzila

56. Mheshimiwa Spika, napenda kutoa taarifa kuwaujenzi wa hospitali ya kufundishia ya Kampasi mpyaya Mloganzila ya Chuo cha Afya na SayansiShirikishi cha Muhimbili (MUHAS) iliyojengwa kwaushirikiano wa Serikali yetu na Serikali ya KoreaKusini inatarajiwa kukamilika mwezi Juni 2016.Hospitali hii itakuwa na uwezo wa kubeba wagonjwa571 wa kulazwa kwa wakati mmoja.

57. Mheshimiwa Spika, pamoja na juhudi za Serikalikukamilisha Awamu ya Kwanza ya ujenzi wahospitali hii, bado kuna changamoto ya majengomengine ya chuo kama madarasa, maabara,maktaba, majengo ya utawala, mabweni yawanafunzi, nyumba za wafanyakazi n.k. Majengohaya ni muhimu ili Kampasi hii ya Chuo ikamilike na

33

hivyo Chuo kiweze kuongeza udahili wa wanafunzikutoka 3,000 wa sasa na kufikia wanafunzi 15,000kitakapokamilisha Awamu ya Pili. Katika mwaka2016/17 Wizara inalenga kutafuta fedha kwa ajili yakuanza awamu ya pili ya ujenzi ambapo tayariandiko la kutafuta fedha kutoka kwa wafadhili nawawekezaji limeandaliwa.

Ujenzi wa Kituo Mahiri cha Magonjwa ya Moyo –Mloganzila

58. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17 Wizarayangu itaanza ujenzi wa Kituo Mahiri chaMagonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu cha AfrikaMashariki katika eneo la Mloganzila.

Huduma za Maktaba

59. Mheshimiwa Spika, huduma bora za Maktabazinachangia katika utoaji wa Elimu bora katika nchiyoyote ile. Wizara yangu kupitia Bodi ya Hudumaza Maktaba ina jukumu la kuanzisha, kusimamia,kuongoza, kuimarisha, kutunza na kuendelezaMaktaba za Umma. Uendelezaji wa huduma zaMaktaba, unaanzia ngazi ya Kijiji, Wilaya hadi Mkoapamoja na kutoa mafunzo na kuendesha mitihaniya Taaluma ya Ukutubi. Katika mwaka 2015/16Wizara kupitia Bodi ya Huduma za Maktabaimefanya yafuatayo:

34

(i) imeendelea kuimarisha huduma za Maktabakwa kusambaza vitabu vya rejea 68,000 kwamasomo yote katika maktaba za mikoa.

(ii) imetoa ushauri wa kitaalamu kuhusuuanzishaji na uendeshaji wa Maktaba katikashule 28 (17 za msingi na 11 za sekondari),vyuo 5 na Halmashauri za Wilaya 4 ambazo niMkinga, Longido, Kongwa na Ushirombo.

60. Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na upungufu wawataalam wa Maktaba katika asasi na taasisi zaelimu nchini, Wizara kupitia Chuo cha Ukutubi naUhifadhi Nyaraka (SLADS) Bagamoyo, imeratibuutoaji wa mafunzo kwa wanafunzi 1,363; wakiwemoCheti 390; Diploma 773 na kozi ya miezi mitatu“Elementary Library Course” 200. Wanafunzi hawawatakapohitimu wataongeza idadi ya wataaalam waMaktaba katika maeneo yaliyo na uhitaji mkubwa wawakutubi, ikiwa ni pamoja na Shule, Vyuo vyaUalimu na Maktaba za Umma. Aidha, ukarabatimdogo umefanyika katika Maktaba za mkoa waMtwara na Tanga.

61. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kutoawito kwa Halmashauri zote nchini pamoja na wadaukuona umuhimu wa kuanzisha maktaba nakuhamasisha wananchi kujenga utamaduni wakusoma vitabu, vijarida na machapisho mbalimbali.Wizara yangu iko tayari kutoa ushauri wa kitaalamu

35

kuhusu uanzishwaji na uendeshaji wa maktaba.

62. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizarakupitia Bodi ya Huduma za Maktaba itafanyayafuatayo:

(i) itaimarisha na kuinua ubora wa huduma zamaktaba katika mikoa 21 kwa kuongezamachapisho/vitabu 40,000 ya watu wazima nawatoto ili kuongeza ari ya usomaji katika jamii;

(ii) itatoa ushauri wa kitaalamu juu ya uanzishajina uendeshaji wa Maktaba za Shule, Vyuo,Taasisi na Halmashauri za Miji, Manispaa naWilaya nchini;

(iii) itatoa mafunzo ya Ukutubi na Uhifadhi Nyarakakwa walengwa 700 wa Cheti, 700 wa Diplomana 500 wa mafunzo ya muda mfupi kwa ajili yawafanyakazi wa Maktaba;

(iv) itaendeleza miundombinu ya Chuo cha Ukutubina Uhifadhi Nyaraka (SLADS), Bagamoyo kwakujenga maktaba ya chuo pamoja nakukarabati majengo ya maktaba za Tabora,Tanga na Rukwa; na

(v) itaanza matayarisho ya ujenzi wa majengo yamaktaba za mikoa ya Singida na Shinyanga ilikutoa fursa kwa wananchi wa mikoa hiyokupata machapisho na huduma nyingine zamaktaba za umma.

36

5.4 TAFITI NA HUDUMA KWA JAMII

Utekelezaji wa Tafiti na Huduma 2015/16

63. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu ina jukumu lakufanya tafiti na kutoa huduma kwa jamii kupitiaVyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu. Katikamwaka wa fedha 2015/2016, Wizara yangu kupitiaVyuo Vikuu imefanya tafiti mbalimbali zenyematokeo makubwa kwa jamii kama ifuatavyo:

Chuo Kikuu cha Sokoine

(i) udhibiti wa magonjwa ya mifugo yaletwayona kupe, mbung’o na minyoo kwa wafugaji waasili, ambapo wafugaji hao sasa wamefanikiwakuongeza kipato kutokana na kupungua kwamagonjwa ya mifugo yao;

(ii) kutumia Panya Buku kutatua matatizo ya jamiiikiwa ni pamoja na kutambua wagonjwa yakifua kikuu kwa kasi kubwa na kwa usahihizaidi ya darubini. Aidha, utafiti umegunduakuwa wanyama hao wanafundishika na wanaouwezo wa kutumika kutegua mabomu katikajamii zilizokumbwa na vita. Panya haowameweza kutegua mabomu katika nchi zaCambodia, Msumbiji, Jamhuri ya Lao, Vietnamna Thailand, ambapo nchi hizo sasazimetangaza kwamba hazina tena tishio la

37

mabomu baada ya kuwatumia panya hao; na

(iii) uzalishaji wa mbegu bora za maharage zenyekustahimili magonjwa na ukame, kuzaa vizurina kuiva kwa muda mfupi. Matokeo ya utafitihuu yamesambazwa kwa wakulima ambapowanatumia mbegu bora za maharage (SUA 90,ROJO, Mshindi na Pesa) na wamewezakuongeza uzalishaji na kipato chao.

Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi ShirikishiMuhimbili

(i) utafiti wa majaribio ya chanjo ya VVU awamuya II, uliohusisha nchi za Tanzania na Msumbiji(Tanzania Mozambique Vaccine – TaMoVac II).Chanjo hii ilijaribiwa na kuthibitishwa kuwasalama na ina uwezo wa kufanya mwiliutengeneze viashiria vya kinga. Pia majaribiohayo yamewezesha wanasayansi kubaini dozisahihi ya chanjo na namna ya kuitoa ili iwezekufanya kazi katika kiwango kinachotakiwa;

(ii) matibabu ya ugonjwa wa Malaria na kuboreshamfumo wa matibabu ya ugonjwa kwa lengo lakupunguza athari zitokanazo na Malaria hasakwa akina mama wajawazito na watoto; na

(iii) ugonjwa wa Selimundu ambapo utafiti huoumebaini mbinu bora zaidi za kuhudumiawenye tatizo hilo.

38

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Tafiti zifuatazo zilifanyika:

(i) ufuatiliaji wa mienendo ya Tembo kwakutumia teknolojia ya GPS (Global PositioningSystem) inayoonesha mahali tembo alipokwa wakati wote. Matokeo ya utafiti huuyanasaidia kukabiliana na tatizo la ujangili watembo. Utafiti huu umewezesha ulinzi watembo kufanyika kwa ufanisi mkubwa zaidi;

(ii) utafiti kuhusu kilimo cha uyoga pori kwamatumizi ya chakula na biashara, ambaoumewezesha wakulima wapatao 4,000 kulimaaina tano za uyoga na hivyo kuongezauzalishaji wa zao hili na kujiongezea kipato;na

(iii) ufugaji wa samaki wa maji baridi aina yaTilapia katika maji chumvi ambao umewasaidiawakulima wa Rufiji kuweza kufuga aina hii yasamaki katika maeneo yao na hivyo kuongezakipato cha kaya.

64. Mheshimiwa Spika, Napenda kuchukua fursa hiikuwajulisha wananchi na wadau mbalimbaliwanaweza kusoma na kuona matokeo ya tafiti hizokwenye tovuti za vyuo husika.

39

Malengo ya Tafiti na Huduma 2016/17

65. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kupitia vyuovikuu itaendelea kufanya tafiti na kutoa ushauri kwajamii kwa kutumia fedha za Serikali na wadau wamaendeleo. Katika mwaka 2016/17 baadhi ya tafitizitakazofanyika zitakuwa kama ifuatavyo:

(i) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitaendeleakusimamia miradi 12 ya utafiti inayofadhiliwa naSida kuhusu rasilimali maji (water resources);sayansi za bahari na rasilimali zake; usalamawa chakula (Food Security); mabadiliko yatabianchi; utalii; biashara ya rasilimali za kilimo;kujenga uwezo katika Hisabati, na Sayansi zaMolekali Biolojia (Molecular Biosciences) na“Nishati Joto”;

(ii) Chuo Kikuu cha Ardhi, kitafanya tafiti na kutoaushauri wa kitaalam kuhusu matumizi bora yaardhi, ujenzi, usanifu majengo na usimamizi wamazingira;

(iii) Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, kitafanyatafitina kutoa ushauri wa kitaalam na kuchapamakala kwa lengo la kusambaza elimuinayokidhi mahitaji ya sasa ya jamii ilikupunguza umaskini;

(iv) Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi chaMuhimbili, itaendelea na tafiti za: afya ya akinamama na watoto, majaribio ya chanjo dhidi ya

40

maambukizi ya VVU, uchunguzi wa kifua kikuu(TB); malaria; magonjwa makuu ya tropikiyasiyopewa kipaumbele (Neglected TropicalDiseases) na magonjwa yasiyoambukiza(magonjwa ya moyo, kisukari, selimundi n.k); na

(v) Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) naTaasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansina Teknolojia (NM-AIST) vitafanya tafiti nneambazo zinaviandaa kuwa vituo mahiri vyautafiti na taaluma katika Ukanda wa AfrikaMashariki na Kusini. Tafiti hizo ni SUA(Innovative Rodent Management and BiosensorTechnology Development; na InfectiousDisease Surveillance) na NM-AIST(Miundombinu ya Maji na Nishati Endelevu; naya pili ni kuhusu Maendeleo na Elimu Endelevuya Kilimo).

5.5 SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU

66. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inatambuaumuhimu wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu pamojana matumizi yake katika kuleta maendeleo ya nchi.Wizara imefanya yafuatayo katika mwaka 2015/16:

(i) imekamilisha uandaaji wa Mpango waMaendeleo ya Sayansi na Teknolojia namkakati wa utekelezaji ambao uliandaliwakupitia mpango wa Matokeo Makubwa Sasa.

41

(ii) imesimamia majadiliano ya Mkataba waUshirikiano kati ya Serikali ya Tanzania naSerikali ya Zambia katika masuala ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu na kufanya Mikutano yakuhamasisha umuhimu wa kuwa na dawati lasayansi, teknolojia na ubunifu kwa wadau.

(iii) iliendesha Kambikazi ya Maabara ambapomatokeo yake yamekuwa msingi wa kuandaaprogramu za utekelezaji wa mpango wamaendeleo ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.

(iv) katika kuongeza idadi ya wanafunzi wa kikewanaojiunga na masomo ya Sayansi, Wizarayangu pia iliendesha mafunzo maalumu yakuongeza uwezo wa kitaaluma wa wanafunziwa kike 305 ambao hatimaye walijiunga nakozi katika Vyuo vya Elimu ya Juu na Ufundivitano (5) vya Tanzania Bara na Zanzibar.

67. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizarayangu imepanga kuanzisha maabara na kupanuavituo vya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu pamojana kufadhili miradi mipya na inayoendelea na utafitikatika maeneo ya TEHAMA, Kilimo, Afya, Viwandana Maliasili. Aidha, Wizara itashirikiana na ofisi zaHalmashauri ili kubaini wagunduzi na wabunifu ilikuboresha vipaji vyao. Vilevile, kituo chakuendeleza ubunifu na ujasiriamali katika fani yaTEHAMA kitajengwa kwenye Taasisi ya Afrika yaNelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia pamoja

42

na kuanzisha Kituo mahiri cha “AgriculturalBiotechnology” katika Chuo Kikuu cha Sokoine.

Taasisi zinazohusika na Sayansi Teknolojia naUbunifu

68. Mheshimiwa Spika, naomba sasa nitumie fursa hiikueleza utekelezaji wa masuala ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu yaliyofanywa na Taasisi zetuza Sayansi na Teknolojia:

Tume ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH)

69. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kwa mwaka2015/16 kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia,imefanya yafuatayo:(i) imeratibu mtandao wa kuunganisha Vyuo

Vikuu na Taasisi za Utafiti na Maendeleoambapo taasisi 28 zimeunganishwa.

(ii) imeendelea kuhawilisha teknolojia mbalimbalinchini ambazo zimewezesha ujenzi wamaabara ndogo yenye uwezo wa kutoamachapisho mbalimbali kwa njia ya kidijitalikwa kutumia teknolojia ya 3D “printers”ambazo zimetengenezwa hapa nchinikutokana na mabaki ya vifaa vingine vyakielektroniki. Ubunifu huu umefanyika katikaAtamizi ya BUNI ambayo inasimamiwa naTume.

43

(iii) imesimamia Kituo cha kuendeleza ubunifu(BUNI Innovation Hub) ambacho kimekuwakikiendesha mpango maalum wa kuandaawaatamizi watarajiwa (pre-incubationprogram) kwa wanafunzi wa vyuo vikuukupitia mafunzo kwa vitendo (field practicaland Internship program).

(iv) kushirikiana na Serikali ya MapinduziZanzibar imeimarisha Atamizi ya TEHAMA(ICT Incubator) iliyopo katika Taasisi yaSayansi na Teknolojia ya Karume, na Atamiziya Usarifu wa Mazao ya Kilimo (AgribusinessIncubator) iliyopo katika Kituo cha utafiti waKilimo cha Kizimbani, Zanzibar. Atamizi yaUsarifu wa mazao ya kilimo inalengakuongeza mnyororo wa thamani katikakubiasharisha mazao mbalimbali ya kilimo namifugo.

(v) Imetoa huduma za maktaba mtandao (e-library) na;

(vi) kutoa taarifa za utafiti kupitia tovuti ya utafiti(Research web).

70. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17 Wizarayangu kupitia Tume ya Sayansi na Tekonlojiaitafanya yafuatayo:

(i) kuendelea kugharimia tafiti zenye kulengakutatua matatizo ya wananchi;

44

(ii) kuanzisha mfumo wa kitaifa wa kufadhili tafitiza masomo baada ya Digrii ya uzamivu (postdoctoral research);

(iii) kuanzisha mfumo wa kufuatilia viwango,ubora na maadili ya utafiti katika taasisi zautafiti na maendeleo;

(iv) kuhamasisha uanzishwaji wa atamizi katikavyuo vya elimu ya juu; na

(v) kujenga maabara ya kutunza maarifa namachapisho.

Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam -(DIT)

71. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutoamafunzo ya teknolojia kwa wanafunzi nawafanyakazi wa viwandani ili waweze kujiongezeaujuzi mpya katika taaluma mbalimbali. Katika mwaka2015/16 Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam,ilidahili wanafunzi wapya 1,386 ambapo 654walikuwa ni Diploma ya Uhandisi, 648 Digrii yaKwanza ya Uhandisi na 84 Digrii ya Uzamili yaUhandisi na kufanya Taasisi kuwa na jumla yawanafunzi 4,187 Wanawake 541 na wanaume3,646. Aidha, Taasisi ilianzisha kozi mpya zaDiploma ya Biotechnology, Digrii ya Uhandisi katikaMafuta na Gesi, Digrii ya Uzamili ya Matumizi ya

45

Teknolojia ya Ukokotoaji katika fani za Sayansi naUhandisi na kupata ithibati kutoka NACTE.

72. Mheshimiwa Spika, pamoja na mafunzo yaliyotajwa,Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam imejenga nakuendelea kuukarabati mtandao wa mawasiliano watiba mtandao (Telemedicine) unaounganishahospitali 7 za Taifa Muhimbili, Rufaa Mbeya, Amana,Temeke, Mwananyamala, Tumbi Kibaha naBagamoyo.

73. Mheshimiwa Spika: katika mwaka wa fedha2016/17, Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaamitatekeleza mambo yafuatayo:

(i) kuanzisha kozi mpya ya Diploma ya UhandisiUjenzi na Barabara (Civil and HighwayEngineering);

(ii) kufundisha kozi mpya ya Digrii ya Uzamili katikaNishati Endelevu (MEng. Sustainable Energy);

(iii) kuendesha mafunzo ya awali (pre-entry) ilikupata wanafunzi wa kike 65 wasio na vigezovya kutosha kudahiliwa katika kozizinazoendeshwa na Taasisi;

(iv) kuendelea kuhudumia mradi wa matibabumtandao (Telemedicine) kwa kushirikiana naWizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, JinsiaWazee na Watoto; na

(v) kuanza kufundisha kozi za Diploma za bidhaa za

46

ngozi (Leather goods) na Sayansi na Teknolojiaya Maabara (Science and LaboratoryTechnology) na kuendelea na utoaji wa kozi fupina za kitaalam katika Teknolojia ya ngozi nabidhaa zake katika Kampasi ya Mwanza.

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia chaMbeya

74. Mheshimiwa Spika, Chuo hiki kina majukumu yakutoa mafunzo, kufanya utafiti na kutoa ushauri wakitaalamu na kitaaluma. Katika mwaka 2015/16,Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeyakilitekeleza yafuatayo:

(i) kudahili wanafunzi 3,682 ikiwa ni ongezeko lawanafunzi 82 kutoka kwa wanafunzi 3,600waliodahiliwa mwaka 2014/15 ambayo ni sawana ongezeko la asilimia 2;

(ii) kuajiri wafanyakazi katika fani mbalimbali(wafanyakazi 43 wameajiriwa kuanzia mweziJulai 2015 mpaka Januari 2016);

75. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17 ChuoKikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kitaendeleakuongeza udahili wa wanafunzi kuhamasishawanafunzi wa kike katika shule za sekondari kusomamasomo ya sayansi ili hatimaye waweze kujiunga navyuo vya ufundi.

47

Tume ya Nguvu za Atomiki

76. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16 Wizarayangu kupitia Tume ya Nguvu za Atomiki imeendeleana jukumu lake la kudhibiti mionzi katika migodi navituo vya huduma kwa kufanya yafuatayo: kukaguamigodi 3 na vituo 72 kati ya vituo 100 sawa naasilimia 72 na kuhakikisha kuwa viwango vya mionzivinavyotumika kwenye sehemu za kazi na vyakulavinadhibitiwa. Hili lilifanywa kwa kupima viwango vyamionzi kwa wafanyakazi 840 kutoka katika vituo 300vya uzalishaji pamoja na kupima mionzi kwenyevyakula na mbolea kwa sampuli zipatazo 6,633.

77. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwavyanzo vya mionzi vinadhibitiwa na haviathirimazingira na afya za viumbe hai, Wizara kupitiaTume ya Nguvu za Atomiki imesajili vyanzo vyamionzi vipatavyo 1045 na vituo vinavyomiliki vyanzovya mionzi vipatavyo 1032. Kati ya vyanzo hivyo,387 vina viasili vya mionzi (radioactive materials).Aidha, Tume pia kwa kushirikiana na Mamlaka yaMawasiliano Tanzania imeweza kupima mionziitokayo katika minara ya simu katika mikoa ya Dares Salaam, Morogoro, Dodoma, Arusha, Mwanza,Mbeya, Lindi na Mtwara. Vituo vipatavyo 294vimepimwa na matokeo ya vipimo yameoneshaviwango vya mionzi viko chini ya viwango vyausalama vya kimataifa.

48

78. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizarayangu itaendelea na mikakati ya kuhakikisha kuwawananchi na viumbe hai hawaathiriwi na mionzihatarishi hasa kwenye sehemu za kazi kwa kufanyaukaguzi wa migodi 5 mikubwa inayofanya kazi ilikubaini hali ya usalama inayoendelea katika migodihiyo. Aidha, vituo 120 vyenye vyanzo vya mionzivitakaguliwa ili kubaini hali ya usalama kwawafanyakazi 1,700 na umma kwa ujumla. Ukaguzihuu utasaidia kuandaa taratibu (standard operatingprocedures) za kufanya kazi katika maabara.

79. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kupitia Tume yaNguvu za Atomiki kwa mwaka 2016/17, itaendeleana udhibiti wa mionzi hatarishi kwa kusajili vituovyenye vyanzo vya mionzi vipatavyo 1045 pamojana kupokea na kutathimini maombi 450 ya lesenimbalimbali ili kuona kama yanakidhi matakwa yaSheria na Kanuni za Usalama na Kinga ya Mionziya mwaka 2004. Aidha, Tume itakusanya mabaki yamionzi katika vituo vyote na kuyahifadhi katikamaabara maalum na kutafuta mabaki ya mionzikatika viwanda vinavyokusanya vyuma chakavu. Vilevile, Tume itaimarisha mfumo wa kielektroniki katikakutoa vibali, na kuwa na vifaa vya kupimia mionzikatika vituo 2, ambavyo ni Namanga na bandari yaDar es salaam pamoja na kuanzisha vituo vya kandaya kusini katika mikoa ya Ruvuma na Mbeya.

49

5.6 URATIBU WA TAASISI NA WAKALA

80. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu ina Taasisi naWakala za elimu, Sayansi na Teknolojiainazozisimamia. Naomba sasa kutoa maelezokuhusu Taasisi na Wakala hizo:

Tume ya Taifa ya Vyuo Vikuu Tanzania

81. Mheshimiwa Spika, Tume ya Vyuo Vikuu piaimefanya mapitio ya miongozo mbalimbali ya uthibitiubora ili kuthibiti na kusimamia ithibati ya elimu yajuu nchini. Miongozo hiyo inajumuisha ya uhakikiubora wa programu za masomo ya elimu ya juu nautoaji wa mafunzo katika ngazi ya Digrii za juu(postgraduate training). Miongozo hii imewezeshavyuo vya elimu ya juu kutoa elimu yenye viwangovinavyokidhi ubora kitaifa na kimataifa na mahitaji yasoko la ajira na jamii ya sasa na ya baadae.

82. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizarakupitia Tume ya Vyuo Vikuu imepanga kufanyayafuatayo:

(i) kusimamia ubora wa elimu ya Vyuo Vikuu vyotenchini kwa kufanya ukaguzi na tathmini zamara kwa mara vyuoni na pia mipango yakuanzisha/kuhuisha Vyuo Vikuu 20 ilikusimamia ubora wa elimu itolewayo na VyuoVikuu nchini;

50

(ii) kuendelea kuratibu na kusimamia udahili wawanafunzi wapatao 65,000 watakaojiunga naVyuo Vikuu kupitia mfumo wa udahili wapamoja (CAS), ili kufikia lengo la kuwa nawanafunzi wapatao 300,000 kwenye Taasisiza Elimu ya Juu nchini ifikapo mwaka 2017;

(iii) kuboresha mfumo wa ukusanyaji taarifambalimbali toka vyuo vya elimu ya juu nchini ilikurahisisha upatikanaji wa taarifa sahihi kwawakati zitakazosaidia katika kufikia maamuzisahihi ya utekelezaji wa mipango yamaendeleo ya elimu ya juu nchini;

(iv) kutathimini programu 200 za masomo katikaVyuo Vikuu nchini;

(v) kuendelea kuratibu na kuandaa Maonesho yakumi na moja ya Elimu ya Juu, Sayansi naTeknolojia ili kuelimisha umma kuhusumalengo, maendeleo na mchango wa Taasisiza Elimu ya Juu katika maendeleo ya kiuchumina kijamii nchini;

(vi) Kuendelea kuratibu mafunzo ya wanataalumakutoka vyuo vikuu nchini wanaoendelea namasomo ya Uzamivu nchini Ujerumani (DAAD)kwa lengo la kukabiliana na changamoto zaupungufu wa wanataaluma wenye sifa stahikikatika vyuo vikuu nchini; na

(vii) Kuanza ujenzi wa ofisi za kudumu za Tumekatika kiwanja cha Uporoto, Dar es Salaam.

51

Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu(ADEM)

83. Mheshimiwa Spika, Wakala wa Maendeleo yaUongozi wa Elimu una majukumu ya kuandaa nakuendesha mafunzo ya muda mfupi na mrefu katikauongozi na uendeshaji wa elimu; kufanya utafiti,kuandaa na kusambaza makala na vitabupamojana kutoa ushauri wa kitaalamu katika mamboyanayohusu uongozi na uendeshaji wa elimu. Katikamwaka 2015/16, Wakala wa Maendeleo ya Uongoziwa Elimu, umefanya yafuatayo:

(i) umetoa mafunzo ya Uongozi na Usimamizi waElimu kwa ngazi ya Cheti kwa Walimu Wakuu881 ambao wanaendelea na mafunzo katikaMikoa ya Mbeya, Njombe na Iringa; na ngazi yaDiploma ya Uongozi wa Elimu (DEMA) kwawalimu 815;

(ii) umetoa mafunzo ya Diploma ya Ukaguzi waShule kwa Wathibiti Ubora wa Shule 332 wamwaka wa kwanza na 118 wa mwaka wa pili;

(iii) umekamilisha uanzishaji wa Kampasi ya Mbeyaambapo wanachuo 70 wameanza mafunzo yaDiploma ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu(Diploma in Education Management andAdministration);

(iv) umeendesha mafunzo ya Muda Mfupi yaUongozi na Uendeshaji wa Elimu kwa Walimu

52

Wakuu 10,870 na Waratibu Elimu Kata 2,480,juu ya Uongozi wa Shule na Usimamizi waUfundishaji wa Kusoma, Kuandika naKuhesabu (KKK);

(v) Maafisa Elimu Sekondari kutoka Halmashauri179 wamepata mafunzo ya Uongozi wa Elimuna Udhibiti wa Majanga katika Elimu;

(vi) umefanya utafiti wa kubaini mahitaji yamafunzo kwa walimu na wadau wenginekuhusu Uthibiti wa Ubora wa Elimu ili kuwezakuanzisha Digrii ya Menejimenti na Uthibiti waElimu (Bachelor in Education Management andQuality Assurance);

(vii) umetoa huduma ya Ushauri wa Kitaalamu juuya Uongozi na Menejimenti ya Elimu kwaWizara ya Elimu na Mafunzo ya AmaliZanzibar, UNICEF, Rufiji Social DevelopmentInitiative, Equip(T) na SHIPO; na

(viii) umeandaa makala mbalimbali kwa wadau wakeambazo ni pamoja na Moduli ya Uongozi naUthibiti wa Majanga kwa Maafisa ElimuSekondari na Moduli ya Uongozi wa Shule naUsimamizi wa Ufundishaji KKK kwa WaratibuElimu Kata na Walimu Wakuu.

53

Uratibu wa Shughuli za UNESCO nchini

84. Mheshimiwa Spika, Tume ya UNESCO inamajukumu ya kuratibu na kutekeleza programu zaUNESCO nchini. Tume hii inatekeleza programukatika nyanja za Elimu, Sayansi Asilia, Sayansi Jamii,Utamaduni, Mawasiliano na Habari. Katika mwaka2015/16, Tume ya Taifa ya UNESCO, ilifanya mapitioya Toleo la 12 la Jarida la UNESCO Tanzania nakusambaza nakala 600 kwa wadau wa ndani na njeya nchi kwa lengo la kutoa taarifa kuhusu shughulizilizotekelezwa na Tume hiyo. Aidha, Tumeimefanikiwa kuunganisha shule 10 za sekondari nachuo kimoja cha ualimu nchini kwenye mtandao washule nyingine duniani ili ziweze kubadilishanauzoefu wa kielimu kupitia mtandao wa shule waUNESCO Associated Schools Project Network(ASP- Net).

85. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2016/17 Wizarayangu kupitia Tume ya Taifa ya UNESCOitatekeleza yafuatayo:

(i) kutathmini miradi yote ya kielimu itakayopataufadhili wa UNESCO makao makuu na ileitakayopata ufadhili kutoka kwa wafadhiliwengine kupitia UNESCO;

(ii) kuendelea kutangaza na kuratibu ‘fellowships’na ‘sponsorship’ zitakazoletwa nchini kwalengo la kukuza weledi na uzoefu wa

54

wafanyakazi wa kada mbalimbali;

(iii) kuendelea na jitihada za kuunganisha Serikaliya Tanzania na UNESCO kupitia Wizara; na

(iv) kuendesha semina wezeshi zitakazojengauwezo wa wadau katika kushiriki shughulimbalimbali ikiwepo kuwa mstari wa mbelekatika kutimiza malengo ya maendeleo yadunia na maendeleo endelevu ifikapo 2030.

Taasisi ya Elimu Tanzania

86. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inatambuaumuhimu wa kuandaa mitaala bora ili elimuitolewayo iwe na viwango vinavyokubalika kitaifa nakimataifa. Wizara imekuwa ikitekeleza jukumu hilikupitia Taasisi ya Elimu Tanzania. Aidha, Taasisi hiiinalo jukumu la kutoa miongozo kuhusu vifaa vyakufundishia na kujifunzia, kutoa mafunzo kwawalimu kazini na kufanya utafiti na ufuatiliaji wautekelezaji wa mitaala katika ngazi za elimu yaAwali, Msingi, Sekondari na Ualimu.

87. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2015/16, Taasisiya Elimu Tanzania imetekeleza yafuatayo:

(i) imeboresha Mtaala wa Elimu ya Awali na Elimuya Msingi Darasa la III hadi VII ili uendane nadhana ya elimumsingi na kuandaa Mihtasari naMiongozo ya Elimu ya Awali na Elimumsingi

55

Darasa III – VI kwa masomo ya Kiswahili,English, Hisabati, Stadi za Kazi, Sayansi naTeknologia, Maarifa ya Jamii, Uraia na Maadilina Lugha ya Kifaransa;

(ii) imekusanya maoni ya wadau kuhusu mahitajiya utekelezaji wa mtaala wa elimu ya sekondariKidato cha 1-4 uliofanyika katika mikoa 26 yaTanzania Bara ambapo Wilaya 52 na taasisimbalimbali zilifikiwa;

(iii) imeandika na kusimamia uchapaji wa nakala6,862,800 za vitabu 6 vya kiada kwa Darasa laKwanza. Wizara imeweza kubaini kasoro zakiuchapaji kwenye nakala 2,807,600. Mchapajiamewajibishwa kurudia kazi hiyo kwa gharamazake;

(iv) imefanya tathmini ya vitabu vya ziadavilivyoandikwa na wachapishaji mbalimbalivitakavyotumika shuleni katika ngazimbalimbali za elimumsingi, sekondari navyuo vya ualimu ambapo jumla ya vitabu 146vimefanyiwa tathmini kwa ajili ya kupewaithibati; na

(v) imeandaa Mwongozo wa Walimu Washauri waVituo Shikizi (Satelite Schools) kwa ajili yamaandalizi ya shule za awali katika maeneoambayo ni magumu kufikika.

56

88. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Taasisiya Elimu Tanzania imelenga kutekeleza yafuatayo:

(i) kutayarisha vitabu vya kiada vya Elimumsingina sekondari vinavyozingatia mtaalaulioboreshwa;

(ii) kuhuisha na kuboresha mtaala wa elimu yaMsingi na Sekondari Kidato cha 1-4;

(iii) kuhuisha na kuboresha mtaala wa sekondariKidato cha 5-6;

(iv) kuhuisha na kuboresha mtaala wa elimu yaufundi; na

(v) kufanya tafiti za kielimu kuhusu mitaalainayotumika katika vyuo vya mafunzo ya elimuya ualimu kwa lengo la kubaini ulinganifu wakena mitaala ya elimumsingi na sekondari.

Baraza la Mitihani la Tanzania

89. Mheshimiwa Spika, ili kusimamia upimaji na UtoajiTuzo, Serikali kupitia Baraza la Mitihani la Tanzania(NECTA), liliendesha mitihani ya upimaji endelevukwa watahiniwa 1,037,305 wa Darasa la Nne; naKidato cha Pili watahiniwa 396,770; mitihani yakumaliza Elimu ya Msingi kwa watahiniwa 763,606;na Kidato cha Nne watahiniwa 448,373 pamoja naupimaji wa Maarifa (QT) kwa watahiniwa 19,547.

57

90. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17 Barazala Mitihani la Tanzania litaboresha mfumo wake waukusanyaji na uchakataji takwimu pamoja nakuweka mfumo wa kumtambua mwanafunzi kwanamba maalumu ili kuweza kufuatilia maendeleoya mwanafunzi kuanzia anapoandikishwa mpakaanapomaliza mzunguko wa masomo. Baraza pialitaendelea kuimarisha utendaji wake kwa kusimikamashine mbili za kufunga bahasha zenye karatasi zamitihani (Auto Poly Wrapping and Packingmachines) ili kuondokana na hatari na gharamaza ufungaji wa mitihani kwa kutumia mikono nakuimarisha usalama wa Mitihani kwa kupunguzaidadi ya watu wanaoshiriki katika maandalizi yamitihani.

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA)

91. Mheshimiwa Spika, Mamlaka ina majukumu yakuratibu, kudhibiti, kugharimia, kutoa na kukuzamafunzo ya ufundi stadi nchini. Katika mwaka2015/16, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya UfundiStadi, ilifanya yafuatayo:

(i) ilikamilisha taratibu za uandaaji wa Michoro yaujenzi wa chuo cha Wilaya ya Karagwepamoja na kuandaa Hadidu za Rejea (TOR) naombi kwa ajili ya pendekezo (RFP) nakuwapatia washauri elekezi kwa ajili ya ujenzi

58

wa vyuo vya Wilaya za Chunya, Korogwe,Kilindi na Ukerewe.

(ii) iliendelea na ukarabati wa miundombinu yavyuo vya ufundi stadi vya mikoa ya Tanga,Mwanza, Moshi, Kihonda (Morogoro) pamojana chuo cha walimu wa ufundi stadi chaMorogoro.

(iii) imenunua mitambo na zana za kisasa zakufundishia na kujifunzia na zimeanza kutumikakatika vyuo vya ufundi stadi vinne vya; Moshi-fani ya uchoraji majengo; Tanga- Vifaa vya faniya Umeme wa majumbani na viwandani;Mwanza-fani ya TEHAMA na umeme; naMakete-vifaa vya fani ya ufundi magari.

(iv) ilitoa mafunzo kwa wanafunzi 400 waliopatamafunzo nje ya mfumo rasmi wa elimu namafunzo (informal apprentices) katika Mikoaya Mbeya na Dar es Salaam pamoja nakuwapatia mafunzo walimu wa ufundi 567katika ngazi ya Cheti na Walimu 27 katika ngaziya Diploma.

(v) ilitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi389 (wanaume 253 na wanawake 136)wanaofanya kazi katika Sekta Rasmi kwamakampuni 17 kupitia mpango unaojulikanakama ”Skills Enhancement Programme”.

(vi) ilitoa mafunzo katika vikundi mbalimbali vyasekta isiyo rasmi kwa washiriki wapatao 878

59

(Wanaume 344 wanawake 534) katikakutekeleza mpango wa mamlaka wa kuboreshana kuimarisha ufanisi wa utendaji kazi katikaSeka isiyo rasmi.

92. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwamafunzo ya ufundi stadi yanatolewa katika kiwangocha ubora unaotakiwa na soko la ajira, tayari mamlakaimeimarisha eneo la ukaguzi kwa kuwajengea uwezowakaguzi wapatao 66 (22 toka viwandani na 44 tokavyuoni) kwa mwaka huu wa fedha.

93. Mheshimiwa Spika,katika mwaka 2016/17Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadiitatekeleza yafuatayo:

(i) kuendelea na ujenzi wa Chuo cha UfundiStadi cha Mkoa wa Njombe na kuwapataWakandarasi na kuanza ujenzi wa Vyuovya Ufundi Stadi vya mikoa ya Geita,Simiyu na Rukwa;

(ii) kuanza ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi vyaWilaya za Namtumbo, Chunya, Kilindi naUkerewe;

(iii) kukamilisha ukarabati wa miundombinu yaVyuo vya Ufundi Stadi vya Tanga, Mwanza,Moshi, Kihonda na Chuo cha Mafunzo yaUalimu wa Ufundi cha Morogoro;

(iv) kuanza ukarabati wa vyuo vya Wilaya ya

60

Karagwe na Korogwe;

(v) kusambaza vifaa vya kufundishia na kujifunziakatika Vyuo vya Ufundi stadi vya Iringa;Arusha Oljoro; Morogoro–Kihonda, Mkoa waMbeya; Mkoa wa Mwanza; na Chuo cha Ufundistadi Singida pamoja na Chuo cha Walimu waUfundi Stadi cha Morogoro; na

(vi) Kuendelea kufanya tathmini na utahini kwamafundi stadi wa nje ya mfumo rasmi wamafunzo (informal apprentices) kwa kuongezaidadi ya fani na kuwajengea walimu wa ufundistadi uwezo katika eneo hili.

94. Mheshimiwa Spika, pamoja na shughuli hizo Wizarayangu kupitia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo yaUfundi Stadi itatekeleza yafuatayo:

(i) maandalizi ya awali kwa ajili ya kujenga vyuovipya vya wilaya katika wilaya ya Chato naNyasa;

(ii) ujenzi wa bweni la wasichana katika chuo chaVETA Makete;

(iii) ujenzi wa bweni la wasichana katika chuo chaVETA Mbeya;

(iv) kukamilisha ujenzi wa chuo cha ufundi stadikatika Halmashauri ya wilaya ya Busokelo namaandalizi ya kuanza mafunzo katika chuohicho ifikapo 2017;

61

(v) ukarabati wa Chuo cha Ufundi Stadi cha katikaHalmashauri ya wilaya ya Ruangwa; na

(vi) kuviwezesha vyuo viwili vya maendeleo yaWananchi (Folk Development Colleges) vyaKibondo na Kasulu pamoja na Chuo kimojacha Ufundi Stadi cha Nkowe ili kuimarishamafunzo ya ufundi stadi.

Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi

95. Mheshimiwa Spika, kufuatia kuhamishiwa kwenyeWizara yangu Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi(FDC),Wizara imedhamiria kuvitumia Vyuo hivyo ilikuimarisha utoaji wa Mafunzo ya Ufundi stadi kwamaendeleo ya wananchi. Hivyo, katika mwaka wafedha 2016/17, Wizara yangu imepanga kubainishahali halisi ya miundombinu katika vyuo vyote vyaFDC, na kuainisha Vyuo ambavyo vitawezakutumika kutoa mafunzo ya Ufundi Stadi katika haliyake ya sasa kwa kuzingatia mahitaji ya jamiihusika.

96. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizarayangu kwa kutumia fedha zilizokuwa zimetengwachini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto itaanza ukarabati wa vyuo vyaIlula, Newala na Kilosa. Aidha, itajenga vyoo katikavyuo vya Buhangija, Bariadi na Kisarawe. Vilevileitaunganisha umeme katika vyuo vya Mwanhala,

62

Malya, Rubondo, Ulembwe, Munguri na Msingi.Wizara pia itashughulikia upatikanaji wa hatimiliki wavyuo vya Kilwa Masoko, Chisalu, Kisarawe, Chilala,Arnautoglu, Musoma, Mwanva, Ikwiriri, Msingi naIfakara.

Mamlaka ya Elimu Tanzania

97. Mheshimiwa Spika, katika kugharimia Elimumsingihapa nchini, Serikali kupitia Mamlaka ya ElimuTanzania inayosimamia mfuko wa Elimu nchini,imeweza kukusanya jumla ya Shilingi33,647,048,003.00/= ambapo vyanzo vyake niTozoya Elimu (Education Levy) kiasi cha Shilingi30,486,481,326.00 na mapato ya ndani ni Shilingi3,160,566,677.00.

98. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha2015/2016, Mamlaka ya Elimu Tanzania iliwezeshautekelezaji wa yafuatayo:

(i) Kuwajengea uwezo walimu na wanafunzi waHisabati, Biologia, Kingereza na Kiswahiliambapo walimu 15,000 na wanafunzi 6,000walinufaika;

(ii) ilijenga mabweni 11 katika shule za Muyenzi(Ngara), Moyowasi (Kibondo), Mkongo (Rufiji),Endasak (Hanang), Shelui (Iramba),Kishamapanda (Busega), Kilumba (Nyasa),Mbuga (Mpwapwa), Kisiwani (Same), Kibaigwa

63

(Kongwa), na Ufana (Babati); na

(iii) Imegharimia uchapishaji wa vitabu 558,720 vyajinsi ya kujibu maswali ya mitihani ya Kidatocha Pili na cha Nne na Miongozo 75,360 katikakufanikisha mpango wa Matokeo MakubwaSasa (BRN). Vitabu hivi vimewezesha walimuna wanafunzi kutambua mada ngumu na kutoamiongozo kwa walimu na watahiniwa kuhusunamna ya kujibu maswali ya mitihani hiyo.

99. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17,Mamlaka ya Elimu Tanzania itatekeleza yafuatayo:

(i) ukarabati wa majengo ya Shule kongwe 7 zaSekondari pamoja na kuzipatia vifaa vyamaabara;

(ii) kuliwezesha Baraza la Mitihani kununuamitambo ya uchapishaji na ufungaji mitihani ilikuboresha na kufanikisha shughuli za uandaajina utoaji wa mitihani; na

(iii) kutoa motisha kwa wanafunzi 10 watakaofanyavizuri na shule za msingi na sekondari 3000zitakazofanya vizuri. Aidha, katika kupunguzachangamoto za nyumba za walimu, Wizaraitajenga nyumba za walimu 50 zitakazowezeshawalimu 300 kupata makazi katika maeneoyasiyofikika kirahisi.

64

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu yaJuu

100. Mheshimiwa Spika, Mikopo ya Wanafunzi wa Elimuya Juu ni nyenzo kubwa katika kuongeza wataalamkatika ngazi ya elimu ya juu nchini. Wizara kupitiaBodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, ilitoaMikopo kwa wanafunzi wanaodahiliwa kusomeamasomo ya kipaumbele kama vile Udaktari naUalimu wa Sayansi na Hisabati. Mikopo hiyo piaimekua ikitolewa kwa wanafunzi wanaosomea faniadimu kama vile Uhandisi wa mafuta na gesi pamojana Uhandisi umwagiliaji. Aidha, Serikali imeendeleakutoa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma masomomengine kwa kuzingatia viwango vya uhitaji.

101. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16 hadikufikia Machi 2016, jumla ya wanafunzi 124,243walikuwa wamepatiwa mikopo ya kiasi cha Shilingi467,425,257,529.00. Idadi hii ilijumuisha wanafunzi54,072 wa mwaka wa kwanza na 70,171wanaoendelea na masomo. Aidha, Bodi pia ilitoaMikopo kwa wanafunzi 7,996 wa Diploma ya Ualimuwa Hisabati na Sayansi na pamoja na wanafunzi270 wa mafunzo ya sheria. Aidha, wanafunzi 685wanaosomea nje ya nchi kwa makubaliano yaushirikiano baina ya Tanzania na nchi rafiki (Algeria,Ujerumani, Cuba, Misri, Msumbiji, China na Urusi)hukopeshwa fedha za kujikimu.

65

102. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17,wanafunzi 1,957 wanaosomea udaktari wa binadamuwamepatiwa ruzuku kwa kiasi cha Shilingi5,514,656,888.00. Idadi hii inahusisha wanafunziwanaoendelea na wanafunzi wapya kwenye fani hiiya udaktari wa binadamu.

Mwongozo wa Utoaji Mikopo

103. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kupitia Bodi yaMikopo ya Elimu ya Juu, imeboresha mwongozowa utoaji mikopo kwa ajili ya mwaka 2016/17.Mwongozo huo unalenga kuondoa au kupunguzamalalamiko kutoka kwa wanafunzi wasiopata mikopokwa kuwapa kipaumbele waombaji wenye uhitajimkubwa. Aidha, waombaji waliodahiliwa kwenye faniza vipaumbele vya kitaifa na masomo menginewatapatiwa mikopo kwa kuzingatia matokeo yaupimaji uwezo (Means Testing).

104. Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha kuwa wadauwa Bodi ya Mikopo wanapata taarifa sahihi nakupunguza malalamiko, katika mwaka 2016/17Wizara yangu itaendelea kuendesha kampeni yaelimu kwa umma, ili kuelimisha wadau juu yahuduma zitolewazo na Bodi hiyo.

66

Urejeshwaji Mikopo

105. Mheshimiwa Spika, kiwango cha urejeshwajimikopo bado kipo katika kiwango kisichoridhisha.Changamoto zilizopo ni pamoja na kutokuwepo kwamikakati thabiti ya ufuatiliaji wa wakopaji, udhaifukatika Sheria ya Bodi ya Mikopo ambapo, makato yamarejesho ya mikopo kutoka kwenye mshahara siya lazima (statutory deductions). Aidha bado kunamwitikio mdogo kutoka kwa wanufaika kujitokezakuanza kurejesha mikopo yao pamoja na waajirikutokutimiza majukumu yao ya kuwasilisha taarifaza wanufaika wa Mikopo.

106. Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na changamotona kuongeza kasi ya marejesho ya mikopo katikamwaka 2016/17, Wizara yangu kupitia Bodi yaMikopo imeweka mikakati ya kuongeza ukusanyajina kasi ya marejesho ya mikopo kwa kushirikianakwa karibu na mamlaka nyingine za Serikali kwenyekukusanya marejesho; na kuendelea kutoa elimustahiki kwa wadau kuhusu urejeshwaji wa mikopohii. Aidha Sheria ya Bodi ya Mikopo inafanyiwamarekebisho ili kuongeza kiwango cha urejeshwaji.

107. Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi hiikuwakumbusha wanufaika wote wa mikopo kufanyamarejesho ili watanzania wengine wenye uhitajiwaweze kunufaika. Nawasihi wale wenye uwezowalipe kwa mkupuo mmoja ili kupunguza utegemezi

67

wa Bodi ya Mikopo kwa Serikali. Kwa kufanyahivyo, fedha zinazotengwa kwenye Bodi ya Mikopozingeweza kutumika kuimarisha sekta ya elimukatika maeneo mengine muhimu. Aidha, napendakuchukua fursa hii kuwapongeza wale wotewaliojitokeza kulipa mikopo yao kwa mkupuo mmoja.

5.7 USIMAMIZI WA UTEKELEZAJI WAPROGRAMU NA MIRADI

108. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16, Wizarayangu imeendelea kusimamia utekelezaji wa miradina programu mbalimbali zinazotekelezwa katikangazi zote za Elimu na Mafunzo.

Programu ya Maendeleo ya Elimu yaSekondari Awamu II (MMES II)

109. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imeendeleakutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Elimu yaSekondari (MMES II) kwa ushirikiano na Ofisi yaRais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa tangumwaka 2010 hadi sasa. Mradi huu umelengakuboresha miundombinu ya shule za sekondari1,200; kuhakikisha kuwepo kwa walimu wa kutoshana kuboresha ufundishaji hususani katika masomoya Hisabati, Sayansi na Lugha. Malengo mengineni kusimamia matumizi sahihi ya rasilimali fedhakwenye shule kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vyakufundishia na kujifunzia pamoja na kujenga uwezo

68

wa Wakala na Taasisi za Elimu ili kutekeleza mikakatiya kielimu iliyopo na ile ijayo.

110. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana naOR-TAMISEMI imeimarisha mfumo wa takwimu kwaajili ya kukusanya, kuchakata na kuhifadhi takwimu.Aidha, mfumo na zana zilizokuwa zinatumika katikaukusanyaji takwimu zimefanyiwa mapitio nakuboreshwa ili kukidhi mahitaji ya takwimu za elimu.

111. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2015/16, Wizaraimetekeleza yafuatayo:

(i) imetoa mafunzo kwa walimu 3,419 wa shule zasekondari wa masomo ya Sayansi, Hisabati naLugha; na

(ii) imefanya mapitio ya mwongozo wa mafunzona moduli za ufundishaji na ujifunzaji kwawalimu wa masomo ya Sayansi, Hisabati naLugha yenye lengo la kuhakikisha kuwa elimubora yenye viwango vya kimataifa inatolewakwa wanafunzi wa Kitanzania.

112. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha2016/17, Wizara inalenga kutekeleza yafuatayo:

(i) kutoa mafunzo kwa walimu 7,000 wa masomoya Sayansi, Hisabati na Lugha pamoja nakununua vifaa vya TEHAMA vya kufundishiana kujifunzia kwa Vituo 50 vya TEHAMA

69

vilivyopo kwenye Shule za Sekondari;

(ii) kufanya ufuatiliaji na tathmini ya miundombinuya shule za sekondari 408 itakayojengwakupitia Halmashauri mbalimbali nchini;

(iii) kufanya tathmini ya MMES II na kuandaaAndiko la Mpango wa Maendeleo ya Elimu yaSekondari Awamu ya Tatu (MMES III);

(iv) kukagua matumizi ya fedha za MMES IIkwenye Wizara na Halmashauri;

(v) kugharimia uchapaji wa vitabu vya Sayansi naHisabati; na Kiongozi cha Mwalimu kwawanafunzi wasioona na wenye uono hafifu;

(vi) kuhakiki uchakataji na uboreshaji wa mfumo waukusanyaji takwimu za elimu na kutegemezamatumizi ya takwimu; na

(vii) kuwezesha na kutegemeza shughuli za MMESII zinazohusiana na mpango wa MatokeoMakubwa Sasa (BRN).

Mradi wa Kusaidia Stadi za Kusoma, Kuandikana Kuhesabu (Literacy and Numeracy EducationSupport (LANES)

113. Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kuhakikishakwamba watoto wanaojiunga na elimu ya msingiwanamudu vema stadi za Kusoma Kuandika naKuhesabu, Wizara yangu inaendelea na uratibu wa

70

utekelezaji wa Programu wa Kukuza Stadi za KKK.

114. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa fedha2015/16, Wizara imetekeleza yafuatayo:

(i) imegharimia mapitio ya Mitaala ya Elimu yaAwali na Msingi kwa lengo la kwendasambamba na dhana ya Elimumsingi;

(ii) imegharimia mafunzo kuhusu mabadiliko yaufundishaji na ujifunzaji wa Stadi za KKK kwaWathibiti Ubora wa Shule 1,500. Aidha, magari38 yamenunuliwa na kugawiwa katika Wilayaambazo hazikuwa na magari na hivyokuwawezesha Wathibiti Ubora wa Shulekuzifikia shule nyingi zaidi na kwa urahisi; na

(iii) imegharimia mafunzo ya menejimenti nauongozi wa shule kwa Waratibu Elimu Kata2,480 na Walimu wakuu wa Shule za Msingi10,870. Kupitia mafunzo haya Walimu Wakuuwa shule za msingi sasa wataweza kuandaana kutekeleza Mipango ya Maendeleo yaShule kwa ufanisi zaidi (Whole SchoolDevelopment Plan).

115. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa fedha2016/17, Wizara yangu kupitia programu hiiitatekeleza yafuatayo:

(i) itaimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa stadi

71

za KKK kwa kutoa mafunzo kabilishi kwawalimu 22,955 wa Darasa la III & IV kuhusianana mtaala uliohuishwa;

(ii) itakamilisha mpango wa kuimarishamiundombinu ya matumizi ya mfumo wakielektroniki kwenye Halmashauri zote nchini.Mfumo huu utasaidia upatikanaji wa takwimuza ngazi ya shule moja kwa moja kwenyemtandao na hivyo kupunguza kwa kiasikikubwa gharama za ukusanyaji wa takwimukwenye mifumo isiyo ya kisasa;

(iii) itagharimia usimikaji mfumo wa kielektroniki waukusanyaji taarifa za wanafunzi chini ya Barazala Mitihani Tanzania ili kurahisisha upatikanajiwa taarifa hizo wakati wa Mitihani. Utaratibuhuu utaisaidia Serikali kupunguza matumizimakubwa ya fedha za ukusanyaji taarifa chiniya mfumo wa TSM9;

(iv) itawezesha kamati za shule kupata mafunzo yakuandaa mipango ya maendeleo ya shule kwalengo la kuziwezesha kutekeleza majukumuyake kwa ukamilifu ili kuharakisha maendeleoya shule;

(v) itahamasisha jamii kushiriki kwenye utekelezajiwa mpango wa LANES kupitia vyombo vyahabari na utoaji taarifa kwa umma, machapisho,matamasha na vikundi vya watoto (childrens3Rs Clubs);

72

(vi) kutoa nafasi za masomo na tafiti ili kuongezaufahamu wa masuala ya elimu ya awali;

(vii) kuajiri mtaalamu elekezi kuandaa nakutekeleza katika ngazi ya majaribio maudhuiya kieletroniki ya KKK ili yatumike kuongeza ariya kujifunza kwa watoto;

(viii) kufanya tathmini ya Sekta ya Elimu na kutumiamapendekezo yake kutengeneza Mpango waMaendeleo wa Elimu wa miaka mitano 2016/17hadi 2020/21;

(ix) kufuatilia na kutathmini mipango ya Sekta yaElimu; na

(x) kuimarisha usimamizi, utekelezaji na ufuatiliajiwa mipango ya LANES kwa kutoa mafunzoya matumizi bora ya rasilimali fedha kwaWatendaji na Wakurugenzi pamoja na kununuavifaa vya uendeshaji kwa Idara, Taasisi navitengo vinavyotekeleza LANES.

Mradi wa Huduma ya Maji, Elimu ya Afya na Usafiwa Mazingira Shuleni “School Water, Sanitationand Hygiene (SWASH)”

116. Mheshimiwa Spika, lengo la Mradi wa Hudumaya Maji, Afya na Usafi wa Mazingira ni kuboreshamiundombinu ya vyoo bora, upatikanaji wa majisafi na salama pamoja na utoaji wa elimu ya afyana kutunza mazingira ya shule. Katika mwaka

73

2015/16, miundombinu ya vyoo vya shule za msingi1,087 iliboreshwa; shule 2,531 ziliunda vikundi vyausafi ambavyo hutoa elimu ya afya shuleni; nakuweka vifaa vya kunawia mikono shuleni. Aidha,timu za usafi wa mazingira za mikoa 10 (Dar esSalaam, Morogoro, Ruvuma, Njombe, Iringa, Tanga,Kilimanjaro, Pwani, Dodoma na Mtwara) ya TanzaniaBara zilipatiwa elimu elekezi kuhusu utumiaji waMwongozo wa Huduma ya Maji, Elimu ya Afya naUsafi wa Mazingira shuleni.

117. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, mradiwa SWASH umelenga kufikia jumla ya shule 4,200(za msingi 3,500 na 700 za sekondari). Aidha,Serikali itashirikisha wadau mbalimbali wa elimu ilikupata rasilimali fedha ili kutatua tatizo la ukosefu wavyoo bora shuleni.

118. Mheshimiwa Spika, mradi huu pia umelengakutekeleza yafuatayo:

(i) kufanya ufuatiliaji na tathmini ya ujenzi wavyoo bora kwenye shule zilizopatiwa fedha zamradi, kujenga uwezo wa utekelezaji naupanuzi wa mradi kwa waratibu wa mradingazi ya Mkoa na Halmashauri na kuwezeshakuandaa mfumo wa ukusanyaji takwimu zataarifa za upatikanaji maji, vyoo bora na vifaavya unawaji mikono;

74

(ii) kukusanya takwimu za vyoo, maji na elimuya usafi wa mazingira shuleni ili kupangamipango ya muda mfupi na mrefu ya kuboreshamiundombinu ya vyoo na mifumo ya majikatika mikoa 14; na

(iii) kufanya mapitio ya Mpango Mkakati wahuduma ya maji, afya na usafi wa mazingira,kuchapa miongozo, kugharimia ununuzi wavitendea kazi na kuendesha harambee kwaajili ya ujenzi wa vyoo na miundombinu yamaji safi na taka.

Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu(Mpango wa Ugharimiaji - Lipa Kulingana naMatokeo (Programme for Results – P4R)

119. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutekelezaprogramu mpya ya kufadhili sekta ya elimu inayoitwa“Lipa Kulingana na Matokeo” (P4R) kwa kushirikianana Washirika wa Maendeleo ambao ni Benki yaDunia, DfID na Sida. Programu hii inalenga kujengauwezo wa Serikali wa kutekeleza vipaumbele vyakeilivyojiwekea. Programu ilianza kutekelezwamwaka 2014/15 ambapo mpaka sasa jumla yaShilingi bilioni 90 zimepatikana kutokana na Serikalikutekeleza vipaumbele vyake kwa ufanisi. Aidha,kupitia programu hii, Wizara imelenga kuhakikishamadai yote ya walimu yasiyo ya mishaharayanalipwa. Kupitia programu hii, hadi kufikia mweziAprili, 2016 jumla ya walimu 63,409 wa shule za

75

msingi na sekondari wameshalipwa madai yaoyanayofikia Shilingi bilioni 22.24.

120. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizarayangu itatumia fedha zitakazopatikana kupitiaprogramu hii kusaidia kuboresha mazingira yakufundishia na kujifunzia kwa kufanya ukarabatimkubwa kwa shule kongwe za sekondari nchini.Kwa hivi sasa uchambuzi wa mahitaji ya ukarabati(conditional survey) wa shule 22 za awamu yakwanza unafanyika na ukarabati unategemewakuanza mwezi Agosti, 2016.

121. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17 Serikaliimejipanga kuhakikisha kuwa shule zetu za sekondarizina vifaa vya maabara na vitabu vya kutoshaambapo tayari Wizara yangu imetangaza zabuni yaununuzi wa vifaa hivyo vya maabara na uchapajiwa vitabu hivyo, ambavyo vitasambazwa nchini kote.Maabara zote zilizojengwa na Halmashauri kwakushirikiana na wananchi zitapatiwa vifaa vyamaabara. Ununuzi wa vifaa vya maabara utafanyikakwa awamu tatu ambapo awamu ya mwishoinategemewa kukamilika mwaka wa fedha 2018/19.Nia ya Serikali katika mpango huu ni kuhakikishakuwa elimu inayotolewa inakidhi viwango nawanafunzi wanapatiwa zana zote muhimu katikakujifunza.

76

122. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kuzihamasishaHalmashauri ambazo hazijakamilisha maabarazikamilishe ili ziweze kunufaika na mpango huu waWizara yangu wa kutoa vifaa vya maabara.

Mradi wa Kutegemeza Elimu ya Ufundi naMafunzo ya Ufundi Stadi na Elimu ya Ualimu

123. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inatekelezamradi wa kutegemeza Elimu ya Ufundi na Mafunzoya Ufundi Stadi na Elimu ya Ualimu unaolengakuongeza udahili, usawa na ubora katika maeneohayo. Hii inahusisha pia kujenga uwezo wawakufunzi na walimu wa sekondari na vyuo vyaUalimu katika masomo ya Sayansi na Hisabati.Katika mwaka wa fedha 2015/16 mradi umefadhiliwalimu 5 wa Chuo cha Ufundi Arusha, watatu katikangazi ya Digrii ya uzamili na wawili katika ngazi yauzamivu. Aidha, wanataaluma 162 wa vyuo vyaufundi vilivyosajiliwa na NACTE wamejengewauwezo katika kuendeleza mitaala, kufundisha nakutathmini mafunzo yanayozingatia umahiri ili kuinuaubora wa Elimu na Mafunzo yatolewayo katika Vyuovya Ufundi.

124. Mheshimiwa Spika, mradi huu umewezeshaununuzi wa kompyuta 400 kwa ajili ya vyuo 40 vyaufundi. Aidha, katika mwaka 2016/17 mradiunalenga kukarabati vyuo sita vya ualimu wa

77

Sayansi vya Dakawa, Tabora, Kleruu, Butimba,Mpwapwa na Marangu ambapo kwa mwaka2015/2016 uchambuzi wa awali wa mahitaji yaukarabati umefanyika. Vilevile, mradi utagharimiaukarabati wa Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi chaMorogoro na kununua vifaa vya maabara kwa ajili yamafunzo ya ufundi kwenye fani za gesi na mafutakwa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Mkoawa Mtwara.

125. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha2016/17, mradi huu utawezesha ununuzi wa vifaambalimbali vya kufundishia na kujifunzia katika vyuovya Ufundi Stadi vya Mikoa ya Mtwara, Njombe,Geita, Simiyu na Rukwa ili kuinua ubora wa Elimu naMafunzo yatolewayo katika Vyuo vya Ufundi naMafunzo ya Ufundi Stadi. Aidha, mradi pia utaanzaujenzi na ukarabati wa majengo ya hosteli namadarasa katika Chuo cha Ualimu wa Ufundi StadiMorogoro.

Mradi wa Ukarabati na Upanuzi wa Vyuo vyaUalimu vya Ndala, Shinyanga, Kitangali naMpuguso (Upgrading of Teachers’ Colleges)

126. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizarayangu itatekeleza Mradi wa Ukarabati na Upanuziwa Vyuo vya Ualimu vya Shinyanga, Mpuguso,Ndala na Kitangali ambao unalenga kuinua uborawa elimu ya msingi na sekondari. Lengo la mradi

78

huu ni kuboresha mazingira ya kusomea kwa walimuwaliopo, kusaidia kuvutia walimu wapya nakuhakikisha kuwa walimu wanafunzi wana motishaya kupata ujuzi ili waweze kutoa elimu bora kwawanafunzi wao mara watakapohitimu. Idadi yawatakaohitimu baada ya kukamilika kwa ukarabatiwa vyuo hivi vinne inatarajiwa kufikia wanachuo3,300 kwa mwaka.

Mradi wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu(STHEP)

127. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha miundombinuna ufundishaji wa Elimu ya Juu, Wizara imetekelezaMradi wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu kwaAwamu ya Pili, kuanzia mwezi Septemba 2014 hadiJanuari 2016. Mradi huu umepata ufadhili wa Benkiya Dunia. Vyuo na Taasisi za Elimu ya Juuzilizonufaika katika mradi huu ni;(i) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,(ii) Chuo Kikuu cha Ardhi,(iii) Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,(iv) Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo,(v) Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar,(vi) Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Dar es

Salaam,(vii) Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa,(viii) Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam,(ix) Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,(x) Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi; na(xi) Tume ya Vyuo Vikuu.

79

128. Mheshimiwa Spika, malengo ya mradi huu yalikuwani kujenga uwezo wa wanataaluma na watumishi waVyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu kwakudhamini mafunzo katika ngazi ya uzamili nauzamivu, kujenga miundombinu mipya ya vyuo vikuuna kufanya ukarabati wa majengo katika Taasisi.Mradi pia ulisaidia ununuzi wa vifaa na samani zakufundishia na kujifunzia kulingana na vipaumbelevya Taasisi husika.

129. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Aprili, 2016mradi umegharimia masomo ya wanataaluma 188wa ngazi ya uzamivu (asilimia 30 ni wanawake); nawanataaluma 208 wa ngazi ya uzamili (asilimia 28ni wanawake). Zaidi ya asilimia 60 ya wanufaikawamehitimu mafunzo yao na wanaendelea na kazikatika Taasisi zao na waliobaki wako katika hatua zamwisho za kuhitimisha mafunzo yao.

130. Mheshimiwa Spika, mradi pia umejenga majengomapya 25 ya kufundishia na kujifunzia, na piaumefanyia ukarabati majengo yaliyokuwepo katikavyuo vikuu 7. Ujenzi na Ukarabati huo umeviongezeavyuo vikuu uwezo wa kuchukua wanafunzi wa elimuya juu 47,622 zaidi ikilinganishwa na kabla ya mradi.Aidha, wakutubi, wataalamu wa maabara nawatumishi wengine 1,794 katika taasisi za ARU,DUCE, DIT, OUT, MUCE, SUA, na UDSM walipatamafunzo ya muda mfupi ya kuwaongezea ujuzikatika maeneo yao. Vile vile wananchi 2,194

80

wanaozunguka vyuo wamenufaika na miundombinuya kitafiti iliyojengwa kama vile mitambo yakusafisha maji taka iliyojengwa Chuo Kikuu chaArdhi, Dar es Salaam.

131. Mheshimiwa Spika, mradi pia umewezesha ununuziwa vifaa vya maabara 5,634 vinavyotumiwa nawanafunzi 16,600 wa elimu ya juu. Kwa upande waTEHAMA vifaa 1,831 vilivyonunuliwa vimewezakusaidia wanafunzi takriban 5,400 katika fanimbalimbali za elimu ya juu. Aidha, vitabu 6,121vilisambazwa kwenye Taasisi na vilipunguza tatizo laupungufu wa vitabu kwa kiasi kikubwa. Hatua hizizimechochea ongezeko na ubora wa wanafunziwanaohitimu katika fani ya Sayansi na Teknolojiakutoka wahitimu 3,353 kwa mwaka 2007 hadi kufikiawanafunzi zaidi ya 8,294 mwaka 2015.

132. Mheshimiwa Spika, mradi pia umewezesha ujenziwa mfumo wa kielektroniki kwa ajili ya udahili wawanafunzi wa Elimu ya Juu nchini. Mfumo huuumewezesha waombaji kuchagua programu katikavyuo mbalimbali kwa ufanisi kupitia mtandao nasimu za mkononi. Aidha, mfumo huu umesaidiakuondoa tatizo la wanafunzi kudahiliwa katika chuozaidi ya kimoja pamoja na kubaini wanaotumiamatokeo ya kughushi kwa kuwa mfumo huuumeunganishwa na Baraza la Mitihani la Tanzania(NECTA). Mfumo huu umepunguza kwa kiasikikubwa gharama za maombi ya udahili katika vyuo

81

vya elimu ya juu kwa kuwa mwombaji anaomba nakulipia mara moja tu.

Mradi wa Elimu na Kukuza Stadi za Kazi na Ujuzi(Education and Skills for Productive JobsProgram– ESPJ)

133. Mheshimiwa Spika, baada ya kukamilisha mradi waSayansi, Teknolojia na Ubunifu, Wizara imeandaamradi mpya utakaoanza mwaka 2016/17 kwa ajili yakukuza stadi za kazi na ujuzi. Mradi huuumeandaliwa ili kuwezesha utekelezaji wa Mkakatiwa Kitaifa wa Kukuza na kupanua stadi za kazi naujuzi. Mkakati huu uliandaliwa na Wizara yangu kwakushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi Vijana na Ajira, na Walemavu. Mradi utajikitakatika kuongeza fursa za upatikanaji wa stadi zakazi na kuongeza ujuzi katika sekta sita zakipaumbele za kukuza uchumi ambazo ni kilimona kilimo uchumi, utalii, uchukuzi, ujenzi, nishatina madini; na TEHAMA. Uchaguzi wa sekta hiziumezingatia mahitaji makubwa ya waajiri katikasekta hizo, mchango wa sekta katika uchumi,upungufu mkubwa wa wataalamu, uwezo wakuongeza ajira; na mahusiano kati ya sekta hizi nanyingine.

82

134. Mheshimiwa Spika, lengo kuu la mradi wa ESPJ nikuimarisha na kupanua upatikanaji na ukuzaji waubora wa stadi za kazi na ujuzi katika ngazi za ufundina ufundi stadi, elimu ya juu na sekta isiyo rasmikwenye maeneo lengwa. Aidha, mradi unalengakuimarisha mfumo wa kitaasisi wa kusimamia,kuratibu na kugharimia uendelezaji stadi za kazikatika ngazi ya kitaifa na kisekta kwa kushirikiana nasekta binafsi. Jumla ya wanafunzi watakaopatamafunzo katika mradi inatarajiwa kuwa zaidi ya47,000 kwa miaka mitano. Mradi huu wa miakamitano kuanzia mwaka 2016/17 unagharimiwa naSerikali kupitia mkopo wa Dola za Kimarekani milioni120 kutoka Benki ya Dunia.

83

6.0 SHUKRANI

135. Mheshimiwa Spika, napenda kutambua mchangomkubwa wa viongozi wenzangu katika Wizara. Kwanamna ya pekee namshukuru sana MheshimiwaMhandisi Stella Martin Manyanya (Mb) Naibu Waziri,kwa ushirikiano mkubwa anaonipa. Aidha,namshukuru Katibu Mkuu, Bi. Maimuna KibengaTarishi; Manaibu Makatibu Wakuu; Profesa SimonSamwel Msanjila na Dkt. Leonard Douglas Akwilapo,Kamishna wa Elimu, Wakurugenzi, Wakuu waVitengo na Wakuu wa Taasisi mbalimbali zilizo chiniya Wizara yangu kwa ushirikiano wao katikakutekeleza majukumu yetu ya kila siku. Napenda piakuwashukuru, Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi,Watumishi wa Wizara, Wanataaluma, Wanafunzi nawadau wote wa Elimu kwa ushirikiano wao katikakuendeleza Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.

136. Mheshimiwa Spika, napenda kuwashukuru wadauwote wa sekta ya elimu, sayansi, teknolojia na ufundiwakiwemo Washirika wa Maendeleo, viongozimbalimbali na kwa namna ya pekee wananchi ambaowamechangia sana katika kufanikisha utekelezaji wamipango ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.

137. Mheshimiwa Spika, washirika mbalimbali waMaendeleo na wadau wa Elimu wamechangia katikakufanikisha mipango ya Elimu, Sayansi, Teknolojia

84

na Ufundi kwa kuwa si rahisi kuwataja wote.Napenda kuchukua fursa hii kwa niaba ya Wizarayangu, kuwashukuru na kuwatambua baadhi yaokama ifuatavyo: Serikali za Algeria, Canada, China,Cuba, India, Italia, Japan, Urusi, Denmark, Finland,Norway, Marekani, Mauritius, Msumbiji, Misri,Norway, Sweden, Uingereza, Ujerumani, KoreaKusini, Uturuki na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

138. Mheshimiwa Spika, napenda pia kuyashukurumashirika yaliyochangia katika kufanikisha programuza Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi ambayopamoja na: Aga Khan Education Services, Airtel,Barclays Bank, Benki Kuu, Benki ya Dunia, Benki yaMaendeleo ya Afrika, Benki ya Taifa ya Biashara,British Council, Campaign for Female Education(CAMFED), Care International, ChildrenInternational, Children’s Book Project,Commonwealth Secretariat, Benki ya CRDB, DAAD,DfID, Education Quality Improvement Programme(EQUIP(T)), FEMINA, Ford Foundation, GIZ, GlobalPartnership for Education, International LabourOrganisation (ILO), International ReadingAssociation, Irish Aid, Inter University Council ofEast Africa (IUCEA), Japan InternationalCooporation Agency (JICA), Korea InternationalCooporation Agency (KOICA), National MicroFinance Bank (NMB), Peace Corps, PlanInternational, Rockefeller, Swedish InternationalDevelopment Agency (Sida), Sight Savers

85

International, Tanzania Education Network /Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET), Tigo,Umoja wa Nchi za Ulaya, United NationsDevelopment Programme (UNDP) , UNESCO,UNICEF na WaterAid.

86

7.0 MAOMBI YA FEDHA KWA MWAKA 2016/17

139. Mheshimiwa Spika, ili kuwezesha utekelezaji wamalengo yaliyopangwa katika mwaka 2016/17,Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundiinaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi1,396,929,798,625.00 ili kutekeleza majukumu yakekwa ufanisi.

140. Mheshimiwa Spika, katika maombi haya:

(i) Shilingi 499,272,251,000.00 zinaombwa kwaajili ya Matumizi ya Kawaida ya Wizaraambapo Shilingi 386,904,995,000.00 ni kwaajili ya mishahara na Shilingi112,367,256,000.00 ni kwa ajili ya MatumiziMengineyo;

(ii) Shilingi 84,132,297,000.00 zinaombwa kwa ajiliya Matumizi ya Kawaida ya Idara na Vitengo.Kati ya hizo, Shilingi 57,246,945,000.00 ni kwaajili ya mishahara, na Shilingi26,885,352,000.00 ni kwa ajili ya MatumiziMengineyo;

(iii) Shilingi 415,139,954,000.00 zinaombwa kwaajili ya Matumizi ya Kawaida ya Taasisi. Kati yahizo, Shilingi 329,658,050,000.00 ni kwa ajili yamishahara, na Shilingi 85,481,904,000.00 nikwa ajili ya Matumizi Mengineyo; na

(iv) Shilingi 897,657,547,625.00 zinaombwa kwa

87

ajili ya Miradi ya Maendeleo. Kati ya hizo,Shilingi 620,693,856,575.00 ni fedha za ndanina Shilingi 276,963,691,050.00 ni fedha kutokakwa washirika wa maendeleo.

141. Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Wizara yangu,napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwakobinafsi na kwa Waheshimiwa Wabunge kwakunisikiliza. Hotuba hii inapatikana pia katika tovutiya Wizara kwa anwani ya: http://www.moe. go.tz.

142. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

89

VIAMBATISHO

Kiambatisho Na.1: Udahili kwa Vyuo vya Elimu ya Juu vya Umma - Mwaka waMasomo 2015/16

Na. Taasisi Ke Me Jumla1 Ardhi University 407 722 11292 Arusha Technical College 13 69 823 Center for Foreign Relations Dar es Salaam 85 106 1914 College of African Wildlife Management Mweka 49 135 1845 College of Business Education 497 610 11076 Community Development Training Institute 146 102 2487 Dar es Salaam Institute of Technology 112 579 6918 Dar Es Salaam Maritime Institute 7 85 929 Dar es Salaam University College of Education 527 1441 1968

10 Eastern Africa Statistical Training Centre 22 63 8511 Institute of Accountancy Arusha 346 399 74512 Institute of Adult Education 157 147 304

90

Na. Taasisi Ke Me Jumla13 Institute of Finance Management 1002 1629 263114 Institute of Rural Development Planning 255 385 64015 Institute of Social Work 432 227 65916 Institute of Tax Administration 30 99 12917 Mbeya University of Science and Technology 124 929 105318 Mkwawa University College of Education 337 1179 151619 Moshi Cooperative University 479 602 108120 Muhimbili University of Health and Allied Sciences 187 418 60521 Mzumbe University 1542 1668 321022 National Institute of Transport 455 1529 198423 Open University of Tanzania 193 441 63424 Sokoine University of Agriculture 703 1838 254125 State University of Zanzibar 469 348 81726 Tanzania Institute of Accountancy 1293 1387 268027 The Mwalimu Nyerere Memorial Academy DSM 403 534 93728 University of Dar es Salaam 1884 3792 567629 University of Dodoma 2252 5702 7954

91

Na. Taasisi Ke Me Jumla30 Water Development Management Institute 37 174 21131 Zanzibar Institute of Financial Administration 71 72 143

Jumla 14,516 27,411 41,927Kiambatisho Na.2: Udahili kwa Vyuo vya Elimu ya Juu vya Binafsi - Mwaka waMasomo 2015/16

Na. Taasisi Ke Me Jumla1 Aga Khan University 25 3 282 Algerian Scholarships 8 44 523 Archbishop James University College 161 524 6854 Archbishop Mihayo University College of Tabora 121 291 4125 AbdulRahman Al-Sumit Memorial University 154 111 2656 Catholic University of Health and Allied Sciences 211 294 5057 Centre for Development Cooperation (Arusha) 1 1 28 Eckernforde Tanga University 26 43 699 Hubert Kairuki Memorial University 138 136 27410 Institute of Procurement and supply 7 8 1511 International Medical and Technological University 98 223 321

92

Na. Taasisi Ke Me Jumla12 Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology 8 7 1513 Jordan University College 293 431 72414 Josiah Kibira University College 61 286 34715 Kampala International University Dar es Salaam Conventional 382 783 116516 Kilimanjaro Christian Medical College 248 383 63117 Marian University College 92 282 37418 Mount Meru University 76 136 21219 Mount Meru University(Mwanza Centre) 27 49 7620 Mozambique Scholarships 11 36 4721 Muslim University of Morogoro 273 681 95422 Mwenge Catholic University 315 848 116323 Ruaha Catholic University 241 656 89724 Sebastian Kolowa Memorial University 179 412 59125 St Johns University of Tanzania (Msalato Centre) 1 2 326 St Johns University of Tanzania (St. Mark’s Centre) 29 30 5927 St. Augustine University in Tanzania Mbeya Center 113 265 37828 St. Augustine University of Tanzania 640 1218 185829 St. Augustine University of Tanzania(Arusha Centre) 108 209 31730 St. Augustine University of Tanzania(Bukoba Centre) 29 101 130

93

Na. Taasisi Ke Me Jumla31 St. Francis University College of Health and Allied Sciences 70 162 23232 St. Johns University of Tanzania 529 880 140933 St. Joseph University College of Agricultural Sciences and Technology 125 355 48034 St. Joseph University College of Health and Allied Sciences 173 307 48035 St. Joseph University College of Management and Commerce 1 136 Stefano Moshi Memorial University College 85 116 20137 Stella Maris Mtwara University College 124 140 26438 Teofilo Kisanji University 190 451 64139 Teofilo Kisanji University Dar es Salaam College 68 46 11440 Teofilo Kisanji University(Tabora Centre) 3 10 1341 Tumaini University Makumira 311 645 95642 Tumaini University Dar es Salaam College 375 290 66543 Tumaini University Mbeya Center 33 125 15844 Unique Academy Dar es Salaam 8 52 6045 United African University of Tanzania 10 49 5946 University of Arusha 142 177 31947 University of Bagamoyo 80 158 23848 University of Iringa 351 553 90449 Zanzibar University 416 324 740

Jumla 7,709 15,428 23,137

94

Kiambatisho Na.3Udahili wa Wanafunzi kwenye vyuo vya Ufundi Stadi - mwaka 2014/15

Sekta ya MafunzoChini ya Darasa la VII Darasa la VII

Kidato chaIV

Kidato cha VIna zaidi

JumlaKuu

%

Auto Motive 210 16273 32633 3957 53073 28%

ICT 9461 9441 22988 3025 44915 24%

Other Trades and Subjects 2324 7559 9836 1482 21201 11%

Hospitality and Tourism 178 3321 15895 1055 20449 11%

Business Administration 1378 2078 10201 835 14492 8%

Electrical 17 1886 7863 30 9796 5%

Construction 159 4170 4210 51 8590 5%

Clothing and Textiles 123 5154 1774 9 7060 4%

Agriculture and Food Processing 22 1144 2736 54 3956 2%

Mining 48 1211 1534 517 3310 2%

Mechanical 11 594 1707 1 2313 1%

Printing 3 280 283 0%

Lab Technology 44 179 223 0%

Pedagogy/Andragogy/Training oftrainers

12 14 26 0%

Jumla Kuu 13931 52890 111850 11016 189687 100%

Asilimia 7.34% 27.88% 58.97% 5.81% 100.00%

95

Kiambatisho Na.4: Ongezeko la Udahili kijinsi kwenye Vyuo vya Ufundi Stadi vyaSerikali na Binafsi kwa mwaka 2010 - 2014

Idadi ya Vituo Usajili

Serikali BinafsiJumla ya Usajili

Mwaka

Serik

ali

Bin

afsi

Jum

laMe Ke

Jum

la

Me Ke

Jum

la

Me Ke

Jum

la

Was

tani

Asi

limia

laO

ngez

eko

2010/11 149 523 672 16372 6751 23123 36314 45403 81717 52686 52154 104840

2011/12 164 586 750 23519 10072 33591 40980 46777 87757 64499 56849 121348 16508 14%

2012/13 173 586 759 21811 15173 36984 63436 45091 108527 85247 60264 145511 24163 17%

2013/14 179 670 849 37986 12022 50008 54849 49496 104345 102559 61518 164077 18566 11%

2014/15 189 705 894 44573 14650 59223 64573 65891 130464 109146 80541 189687 25610 14%

Wastani 171 614 785 16512 5334 21846 52030 50532 102562 82827 62265 145093 16969 12%

96

Kiambatisho Na.5: Chati inayoonesha idadi ya Wanafunzi (kijinsi) waliojiunga naVyuo Vya Ufundi Stadi mwaka 2010/11 – 2014/15

97

Uchambuzi wa udahili katika vyuo vya ufundi stadi vya serikali na vile vya binafsi unaoneshakuwa idadi ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo hivi imeongezeka kutoka 104,840 mwaka2010 hadi 189,687 mwaka 2015; sawa na ongezeko la asilimia 12.

Kiambatisho Na.6

Idadi ya Wanafunzi wenye Mahitaji maalum (kijinsi) waliojiunga na Vyuo vyaMaendeleo ya Wananchi na Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadimwaka 2012 – 2014

2012/13 2013/14 2014/15Aina yaUlemavu Me Ke

Jumla %Me Ke

Jumla %Me Ke

Jumla %

Physical 53 64 117 44% 127 128 255 35% 17 16 33 10%Deaf 25 34 59 22% 73 260 333 46% 50 57 107 33%

Mental 9 15 24 9% 17 21 38 5% 101 30 131 40%Albino 15 23 38 14% 35 35 70 10% 11 13 24 7%Multiple 10 10 20 7% 0 0 0 0% 4 4 8 2%Blind 3 0 3 1% 5 9 14 2% 7 12 19 6%Autism 1 1 2 1% 2 4 6 1% 2 1 3 1%Deaf-Blind 1 3 4 1% 5 5 10 1% 2 0 2 1%Jumla Kuu 117 150 267 100% 264 462 726 100% 194 133 327 100%Asilimia 44% 56% 100% 36% 64% 100% 59% 41% 100%

98

Kiambatisho Na.7Upangaji wa Shule za msingi na Sekondari kwa kiwango cha ufaulu kwa mwaka2014& 2015Mtihani Mwaka Kijani % Njano % Nyekundu %

2015 2,022 12.562 8,603 53.448 5,471 33.992014 913 5.7541 6,697 42.207 8,257 52.039PSLETofauti 1,109 6.8079 1,906 11.241 -2,786 -18.0492015 325 7.0438 3,503 75.921 786 17.0352014 186 4.2206 3,732 84.683 489 11.096CSEETofauti 139 2.8232 -229 -8.762 297 5.939

99

Kiambatisho Na.8

Mwendo wa Usajili kijinsi kwenye Vyuo vya Ufundi Stadi vya Serikali na Binafsikwa mwaka 2010 - 2014

Idadi ya Vituo Usajili

Serikali BinafsiJumla ya Usajili

Mwaka

Serik

ali

Bin

afsi

Jum

la

Me Ke

Jum

la

Me Ke

Jum

la

Me Ke

Jum

la

Was

tani

Asi

limia

laO

ngez

eko

2010/11 149 523 672 16372 6751 23123 36314 45403 81717 52686 52154 104840

2011/12 164 586 750 23519 10072 33591 40980 46777 87757 64499 56849 121348 16508 14%

2012/13 173 586 759 21811 15173 36984 63436 45091 108527 85247 60264 145511 24163 17%

2013/14 179 670 849 37986 12022 50008 54849 49496 104345 102559 61518 164077 18566 11%

2014/15 189 705 894 44573 14650 59223 64573 65891 130464 109146 80541 189687 25610 14%

Wastani 171 614 785 16512 5334 21846 52030 50532 102562 82827 62265 145093 16969 12%