38
Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com 1 Itikadi Sahihi Shaykh ´Abdul-´Aziyz Ibn ´Abdullaah Ibn Baaz Mfasiri: Mbwana Ahmad Mchapaji Katika Kompyuta: Abu Bakr al-Khatwiyb al-Atrush

Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Itikadi Sahihi - Imaam Ibn Baaz

Citation preview

Page 1: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

1

Itikadi Sahihi

Shaykh ´Abdul-´Aziyz Ibn ´Abdullaah Ibn Baaz

Mfasiri:

Mbwana Ahmad

Mchapaji Katika Kompyuta:

Abu Bakr al-Khatwiyb al-Atrush

Page 2: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

2

Sifa njema Anastahiki Allaah pekee (Subhaanahu wa Ta´ala), rehema na amani zimshukie Mtume ambaye hakuna mtume mwengine baada yake. Pia rehema na amani ziwafikie jamaa na Maswahaba wake. Ilipokuwa itikadi sahihi ndio msingi wa dini ya Kiislamu, nimeonelea iwe ndio maudhui ya mhadhara huu.

Ni jambo lenye kujulikana kwa hoja za Kishari´ah katika Qur-aan na Sunnah [1] kwamba metendo na maneno hayakubaliwi isipokuwa pale tu yatakapotokana na Itikadi Sahihi. Iwapo Itikadi sio sahihi, basi matendo na meneno yanayotokana na Itikadi hio ni batili, kama Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), Alivyosema:

�������� ���� وه� �� ا���ة � ا� � و � �$#� "�!���ن ��

”Na yeyote anayeikufuru (anayeikataa) imani, basi yameporomoka matendo yake na yeye huko Akhera ni miongoni mwa wenye kuhasirika.” [2]

Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

������ � ا %�&�$'�(�% ���) و*+0� أ.�آ, (��1 � ��2%� أو�� إ+) وإ3 ا� و

”Na kwa yakini yamefunuliwa kwako na kwa waliokuwa kabla yako: Bila ya shaka ukimshirikisha Allaah ’amali zako zitaanguka, na lazima utakuwa miongoni mwa wenye hasara. [3]

Aayah za Qur-aan katika kuelezea maana hii ni nyingi.

Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake mwaminifu (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) zinafahamisha kwamba Itikadi sahihi, kwa ufupi inapatikana katika kumwamini:

(1) Allaah,

(2) Malaika Wake,

(3) Vitabu Vyake,

Page 3: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

3

(4) Mitume Wake,

(5) Siku ya Mwisho na

(6) Qadari; kheri na shari yake.

Mambo haya sita ndio misingi ya Itikadi sahihi ambayo kimeshuka nayo Kitabu cha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwa Itikadi hio, Allaah Ametuma Mtume wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam). Yanachipuka kutokana na misingi hii mambo yote ya ghaibu [4] yanayopasa kuaminiwa na mambo yote aliyoyaletea habari Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam).

----------------------------------- [1] Sunnah ni kila jambo ambalo linahusiana na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) iwe ni kauli au vitendo au nyamazio (Mtume kupata habari kuwa jambo fulani limefannywa naye asiseme lolote akanyamaza).

[2] al-Maaidah, 5

[3] az-Zumar, 65

[4] Mambo ya kiitikadi yasiyoonekana yaliyojificha

Hoja za misingi hii sita ni nyingi sana. Miongoni mwa hoja hizo ni neno Lake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

5$67��� وا+�م ا��� وا�" � : � %���@ ا�?�ق وا�=�ب وـ$�% ا1 A$ه�Bا و�C�D أن %��%+E ا�+F+�%G وا$'�ب وا

”Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi. Bali wema ni wa anayemuamini Allaah na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii.” [5]

Na kauli yake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

�F ���� و 67$'� وآ'�� ور��� F�#& Iق "+� أ�" � : K@ن آ�G L� � ر%"F� وا �+ � ا�%��ل "�� أ&Nل إ:���Cر

Page 4: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

4

”Mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake na Mitume Wake. Hatutofautishi baina ya yeyote katika Mitume Wake.” [6]

Na kauli Yake Allaah :

� �@ و1 � �Gا : �Gا "��� ور��� وا$'�ب ا%2ي &N%ل 3�� ر��� وا$'�ب ا%2ي أ&Nل : ��2%�� أ��PC ا�ا+R" IST %@T ��� و 6S$'� وآ'�� ور��� وا+�م ا��� ���" �#$�

”Enyi ambao mmeamini, mwaminini Allaah na Mtume Wake na Kitabu Ambacho Amekiteremsha huko nyuma. Na yeyote anayemkufuru Allaah na Malaika Wake na Vitabu Vyake na Mitume Wake na Siku ya mwisho, basi amepotea upotevu ulio mbali.” [7]

Na kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) :

إن� ذ�" +�* ا���ـ� ��() إن� ذ�" �� آ �ب أ�� ���� أن� ا���ـ� ���� �� �� ا��� �ء وا��رض

”Hivi hujui kuwa Allaah Anayajua yaliyomo katika mbingu na ardhi? Bila shaka hayo yapo katika Kitabu. Bila shaka hayo kwa Allaah ni mepesi.” [8]

----------------------------------- [5] al-Baqarah, 177

[6] al-Baqarah, 185

[7] an-Nisaa, 136

[8] al-Hajj, 70

Ama hadiyth sahihi (za Mtume) juu ya misingi hii ni nyingi sana. Miongoni mwa hadiyth hizo ni hadiyth mashuhuri aliyoipokea Imaam Muslim katika kitabu chake ”Swahiyh Muslim” katika hadiyth ya kiongozi wa waumini ´Umar Ibn al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anhu) kwamba Jibriyl alimuuliza Mtume (Swalla

Page 5: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

5

Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu Imani na Mtume akamjibu kwa kusema:

”(Imani) ni kumwamini Allaah na Malaika Wake na vitabu Vyake na Mitume Wake na Siku ya Mwisho na kuiamini Qadar; kheri na shari yake.” [9]

Kutokana na misingi hii sita yanachipuka mambo yote yanayompasa Muislamu kuyaitakidi katika haki ya Allaah na katika mambo ya Akhera na yasiyokuwa hayo miongoni mwa mambo ya Ghaibu.

1. KUMUAMINI ALLAAH

Ni katika kumuamini Allaah kuamini kuwa Yeye ndiye Mungu wa kweli, Anayestahiki kuabudiwa badala ya kila kisichokuwa Yeye kwa sababu Yeye ndiye Muumba wa waja, Mfadhili wao, Mwenye kuzisimamia riziki zao, Allaah kuzijua siri na dhahiri zao, Allaah uwezo wa kumpa thawabu mwenye utiifu na kumuadhibu mwenye kufanya uasi. Kwa ajili ya kuabudu huku ndio Allaah Ameumba watu na majini na kuwaamuru hivyo kama Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Alivyosema:

�F رFزق و � أر�� أن �(R��ن APG ��ون � أر��R+ �% و � ���, ا�Y% واE&X إ�+'� إن% ا�%� ه� ا�%ز%اق ذو ا��%ة ا

”Na Sikuumba majini na watu ila tu kwa kutaka waniabudu. Sitaki kutoka kwao riziki yoyote na wala sitaki wanilishe. Bila shaka Allaah ndiye tu Mtoaji riziki, Mwenye nguvu kubwa.” [10]

-----------------------------------

[9] Ameipokea hadiyth hii Imaam Muslim

[10] adh-Dhaariyaat, 56-58

Page 6: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

6

Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

D A$%�R'%��ن A$��1 � ��2%�وا ر"%$A ا%2ي ���$A وا� �� أ��PC اG%�س ا� S� A$%$A اcرض ��ا.� واa%��ء "�Gء وأ&Nل � اa%��ء �ء �_��ج "� � ا[%��ات رز1� @RB 2ي%ا

RYD��ا �� أ&�ادا وأ&'RD A���ن

“Enyi watu, muabuduni Mola wenu ambaye Amekuumbeni nyinyi na waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuokoka. Ambaye Amewafanyieni ardhi kuwa ni busati na mbingu kuwa ni paa na Akateremsha kutoka mawinguni maji (mvua) ambayo Akatoa kwa maji hayo riziki zenu katika matunda. Hivyo basi msimfanyie Allaah washirika na ilihali nyinyi mnajua (kuwa Allaah Hana mshirika).” [11]

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Amewatuma Mitume na akateremsha vitabu ili kuiweka wazi haki hii, kuilingania na kuyatahadharisha yale yanayopingana na haki hii, kama Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Alivyosema:

��ا ا(%��eتG'Bوا ���وا ا�� "�G]R �� آ@F أ %5 ر%I�� أن ا�� و

“Na hakika tulipeleka katika kila Ummah Mtume (ili kuwafundisha watu) kuwa wamuabudu Allaah na jiepusheni na Twaaghuut.” [12]

Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

�ون��� إ+� أ&%� � إ� إ%� أ&� ����& �% � ر%��ل إ (��1 � �G��أر � و

”Na Hatukupeleka kabla yako Mtume yeyote ila (tulikuwa) tunampa wahyi kwamba hakuna mwenye haki ya kuabudiwa ila Mimi (Allaah) tu, hivyo niabuduni.” [13]

Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

GF� &�2� و"?+� A$ �G%&إ ���وا إI% ا�RD %Iأ �+�� A+$��ن % � ,�Fg� %Ah �D��: ,�$� ا� آ'�ب أ

“(Hiki) ni kitabu zimetengenezwa vizuri aayah zake kasha zimefafanuliwa vyema kutoka kutoka kwa (Allaah) Mwenye hekima, Mwenye ujuzi (wa kila jambo ili) kwamba msimwabudu (yeyote) isipokuwa Allaah tu. Hakika mimi kwenu ni muonyaji, mtoaji habari njema kutoka kwake.” [14]

Page 7: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

7

-----------------------------------

[11] al-Baqarah, 21-22

[12] an-Nahl, 36

[13] al-Anbiyaa, 25

[14] Huud, 1-2

Uhakika wa kuabudu ni kumkusudia Allaah Pekee kwa yote ambayo Amewataka waja wamuabudu kwayo, ikiwa ni pamoja na kuomba, kuogopa, kutaraji, kuswali, kufunga, kuchinja, kuweka nadhiri na aina zingine za ´Ibaadah zisizokuwa hizo. Inatakiwa kumfanyia Allaah tu `Ibaadah hizo kwa njia ya kumnyenyekea, kutaraji rehema Zake, kuogopa adhabu Yake pamoja na kumpenda Yeye Allaah kikamilifu na kuunyenyekea utukufu Wake.

Sehemu kubwa ya Qur-aan Tukufu imeshuka ili kuufafanua msingi huu mkubwa, kama kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) isemayo kwamba:

i����F� ا�%� ا ���F� أ%� ا �g�� �%�� ا����

”Basi muabudu Allaah ukimsafia Dini Yeye tu. Hakika Dini Safi ni ya Allaah tu.” [15]

Na kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

j�%إ� %Iوا إ��RD %Iأ (C"3 رk1و

”Na Mola wako Ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu,” [16]

Na kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

��F� و� آj� ا$���ون� ا �+g�� �%� ��د��ا ا

Page 8: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

8

”Basi mwombeni Allaah mkimsafia Dini Yeye tu, na wangachukia makafiri.” [17]

Katika ”Swahiyh al-Bukhaariy” na ”Swahiyh Muslim” imepokelewa kutoka kwa Mu´aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anhu) akisema kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

-----------------------------------

[15] az-Zumar, 2-3

[16] al-Israa, 23

[17] Ghaafir/al-Muumin, 14

”Haki ya Allaah iliyopo kwa waja ni kwamba (wanatakiwa) wamwabudu Yeye na wasimshirikishe naye kitu chochote.” [18]

Ni katika kumuamini Allaah kuyaamini Yale yote Aliyoyafaradhisha Allaah kwa waja Wake, ikiwa ni pamoja na nguzo tano za Uislamu ambazo ni:

1. Kukiri moyoni na kutamka kinywani kuwa hakuna mwenye haki ya kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah Mmoja tu na kwamba Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) ni Mtume wa Allaah.

2. Kusimamisha Swalah

3. Kutoa Zakaah

4. Kufunga Ramadhaan

5. Kuhiji Nyuma tukufu ya Allaah kwa mwenye uwezo wa kwenda.

Page 9: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

9

Pia ni katika kumuamini Allaah kuziamini faradhi nyingine zisizokuwa hizo na ambazo zimeletwa na Shari´ah tukufu ya Kiislamu.

Muhimu na kubwa zaidi katika nguzo hizi tano ni ile ya kukiri kuwa hakuna mwenye haki ya kuabudiwa ila Allaah tu na kwamba Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) ni Mtume wa Allaah. Kukiri huku kunataka ´ibaadah ifanywe kwa nia safi ya kumkusudia Allaah Pekee na kutomfanyia mwingine asiyekuwa Yeye. Hii ndio maana ya ”Laa ilaaha Ila Allaah”, kwani maana yake ni ”Hakuna mwabudu wa haki ila Allaah tu.” Vyote vinavyoabudiwa badala ya Allaah, sawa iwe ni mwanaadamu au malaika au jini au kingine kisichokuwa hivyo, basi hivyo vinaabudiwa kwa batili.

Muabudiwa wa haki ni Allaah Pekee, kama Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Alivyosema:

@l�����ن � دو&� ا� � ذ) "_ن% ا�%� ه� ا*Cm وأن%

”Hivi ni kwa sababu hakika Allaah ndiye wakweli, na hakika wanachokiomba ni cha uongo.” [19]

-----------------------------------

[18] Ameipokea hadiyth hii Imaam Bukhaariy na Imaam Muslim

[19] Luqmaan, 30

Umeshapita ufafanuzi wa kwamba Allaah Aliyetakasika Amewaumba wanaadamu na majini kwa ajili ya msingi huu wa kumuabudu Yeye tu, Amewaamuru kuutekeleza, Amewatumia Mitume Wake kwa msingi huo na kuvitemresha vitabu Vyake kwa msingi huo. Lizingatie hilo vizuri na kulitafakari ili ukudhihirikie ujinga mkubwa wa kutoujua msingi huu; ujinga ambao wametumbukia katika huo Waislamu wengi mpaka wakaviabudu vitu vingine pamoja na Allaah na kuielekeza haki Yake safi kwa asiyekuwa Yeye. Allaah ndiye wa kuombwa msaada!

Page 10: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

10

Ni katika kumuamini Allaah Aliyetakasika kuamini kuwa Yeye ndiye Muumba wa ulimwengu, Mtekelezaji wa mambo ya walimwengu wa ujuzi na uwezo wake kama Anavyotaka, Mmilikaji wa dunia na Akhera, Mola wa walimwengu wote. Hakuna Muumba wa Mola mwengine asiyekuwa Yeye. Amewatuma Mitume na kuteremsha vitabu ili kuwafanya waja wawe wema na walingania yale yenye uwokovu na wema kwao hapa duniani na Akhera. Yeye Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) katika yote hayo hana mshirika, kama Alivyosema:

وه8 +�* آ4 2�ء وآ(4 ا���ـ� 6�5� آ4 2�ء

“Allaah ndiye Muumba wa kila kitu na Yeye juu ya kila jambo ni mtegemewa.” [20]

Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

��إن% ر"%$A ا�� ا%2ي m�� اa%��وات واcرض �� �'%5 أ�%�م Ah% ا�'�ى 3�� اR�ش �=?� ا�%+@ ا�P%Gر �(��+��R��رك ا�� ربC اD � cوا m��� ا Iأ j� �[+[� وا?%E� وا��� وا�YCGم �a%�ات "_

”Hakika Mola wenu ni Allaah Aliyeziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kisha Akastawi juu ya ’Arshi. Huufunika usiku kwa mchana, ufuatao upesi upesi. Na jua, na mwezi, na nyota zinazotumika kwa amri yake. Fahamuni! Kuumba na amri ni Zake. Ametukuka kabisa Allaah, Mola wa viumbe vyote. [21]

Na katika kumuamini Allaah pia kuamini Majina Yake mazuri na Sifa Zake tukufu zilizopo katika kitabu chake kitukufu na zilizothibiti kunukuliwa kwa Mtume wake Mwaminifu. Inapasa kuamini Majina na Sifa hizo bila ya kubadilisha maana (tahriyf) au kukanusha maana (taatwiyl) au kuainisha namna (takyiif) au kufananisha (tamthiyl). Bali inapasa majina na Sifa hizo zithibitishwe kama zilivyokuja bila ya kufafanua umbile, pamoja na kumamini maama Zake tukufu zinazofahamisha na ambazo ndio Sifa za Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Inapasa kumsifu Allaah kwa sifa hizo katika njia inayofaa kwake bila ya kumfananisha na viumbe vyake katika Sifa yoyote kati ya Sifa Zake, kama Alivyosema:

[20] az-Zumar, 62

Page 11: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

11

[21] al-´Aaraf, 54

Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

�+g�+E آ�[�� .�ء وه� اq+�%a ا

”Hapana kitu kama mfano Wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.” [22]

Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

[�ل إن% ا�� A�R� وأ&'RD I A���نcا �� kD S��"�ا

”Basi msimpigie Allaah mifano. Hakika Allaah Anajua, na nyinyi hamjui.” [23]

Hii ndio Itikadi ya watu wa Sunnah na Jama´ah (Ahlus-Sunnah Wal-Jama´ah) katika Maswahaba wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) na waliowafuatia wao kwa wema. Hio pia ndio Itikadi aliyoinukuu Imaam ´Abul-Hassan al-Ash´ariy (Rahimahu Allaah) katika kitabu chake ”al-Maqaalaat ’an-Aswhaabil-Hadiyth wa-Ahlis-Sunnah” na pia wameinukuu Wanachuoni wengine wenye elimu na imani.

Amesema Imaam al-Awzaaiy´ (Rahimahu Allaah) kwamba aliulizwa Imaam az-Zuhriy na Mak´huul kuhusu aayah za Qur-aan zinazozungumzia Sifa za Allaah wakasema:

”Zipitisheni (zithibitisheni) kama zilivyokuja.”

Naye Waliyd bin Muslim (Rahimahu Allaah) amesema kwamba aliulizwa Imaam Maalik, Awzaaiy´, Layth bin Sa’ad na Sufyaan ath-Thawriy kuhusu Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) zinazozungumzia Sifa za Allaah na wote (Rahimahum Allaah) walisema:

”Zipitisheni kama zilivyokuja, bila ya kuainisha namna.”

Page 12: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

12

Na Imaam Awzaaiy´ (Rahimahu Allaah) amesema kuwa:

”Tulikuwa tukisema na ilihali Taabi´iyna wapo, kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Yuko juu ya ’Arshi Yake na tunaziamini Sifa za Allaah zilizokuja katika Sunnah za Mtume.”

[22] ash-Shuraa, 11

[23] an-Nahl, 74

Wakati alipoulizwa Rabi’a bin Abi ´Abdir-Rahmaan Shaykh wa Imaam Maalik kuhusu kulingana sawa [kulikotajwa katika Surah al-´Aaraaf, aayah 54] alisema kwamba:

”Kulingana sawa kunajulikana na namna (aina) yake haijulikani na ujumbe unatoka mwa Allaah na ni juu yetu kuuamini.”

Naye Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) alipoulizwa juu ya suala hilo na Allaah kulingana sawa juu ya ‘Arshi yake alisema:

”Kulingana sawa kunajulikana na namna yake haijulikani na kuamini ni wajibu na kuulizia ni Bid´ah.”

Halafu alimwambia yule mtu aliyemuuliza kwamba:

”Mimi sioni isipokuwa kwamba wewe ni mtu muovu tu.”

na akaamuru yule mtu atolewe nje.

Page 13: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

13

Maana ya Maimamu katika suala hili ni mengi mno. Haiwezekani kuyanukuu yote katika mnasaba huu wa haraka. Yeyote anayetaka kufahamu zaidi katika suala hilo ayarejee yale waliyoyaandika Wanachuoni wa Sunnah, mfano:

a) KItabu ”as-Sunnah” cha ´Abdullaah bin al-Imaam Ahmad

b) Kitabu “at-Tawhiyd” cha Imaam mkubwa Muhammad bin Khuzaymah

c) Kitabu “as-Sunnah” cha Abul-Qaasim Al-Laalikaaiy atw-Twabariy

d) Kitabu “as-Sunnah” cha Abu Bakr bin Abi-‘Aaswim

e) Jawabu la Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah kwa watu wa Humaat [24]. Jawabu hilo ni adhimu na lenye faida sana. Katika jawabu hilo Shaykh (Rahimahu Allaah) ameweka wazi Itikadi ya watu wa Sunnah na Jama´ah. Amenuku maneno yao mengi pia amenukuu hoja za Kishari´ah za kiakili juu ya usahihi wa waliyoyasema watu wa Sunnah na ubatili wa waliyoyasema wapinzani wao.

-------------------------------

[24] Jawabu hilo lipo kwenye kijitabu na kinaitwa “ar-Risaalah al-Hamaawiyyah.

Vile vile kitabu cha Shaykh kiitwacho “at-Tadmuuriyyah” ni adhimu pia, kwani amelieleza kwa urefu suala hili na kuifafanua Itikadi ya watu wa Sunnah kwa hoja zake za Kishari´ah na za kiakili. Pia amewajibu wapinzani kwa hoja

Page 14: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

14

zinazodhihirisha haki na kuivunja batili kwa mtu mwenye elimu anayetafakari hayo kwa lengo jema na nia ya kutaka kujua haki.

Kila anayewapinga watu wa Sunnah katika yale wanayoyaitakidi kuhusu majina na Sifa za Allaah, basi hapana budi atatumbukia katika kuzipinga hoja za Kishari´ah na za kiakili pamoja na kutumbukia katika utata wa wazi katika anayoyathibitisha na kuyakanusha.

Ama watu wa Sunnah wao wamemthibitishia Allaah yale ambayo Allaah Amejithibitishia katika Qur-aan tukufu au yale ambayo Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) amemthibitishia Allaah katika Sunnah zake sahihi. Wamethibitisha uthibitisho usiokuwa na ufananisho na wamemuepusha Allaah na kufanana na viumbe, muepusho usiokuwa na kukanusha maana. Kwa kufanya hivyo watu wa Sunnah wamesalimika na utata na wamezitekeleza hoja zote. Hii ndio kanuni ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa mtu ambaye ameshikamana na haki ambayo kwayo Allaah Amemtuma Mtume Wake akatoa juhudi zake katika hilo na akamtakasia Allaah nia yake katika kuifuata haki hiyo ili Allaah amuwezeshe kuifuata haki na kumdhihirishia hoja zake kama Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Alivyosema:

�%� gD#�ن @�� =� X�ذا ه� زاهm و$A ا�+� @l�� "@ &�2ف "�*Fm 3�� ا

”Bali tunaitupa kweli juu ya uongo ikauvunja na mara ukatoweka. Na ole wenu kwa mnayoyazua.” [25]

--------------------------------

[25] al-Abnbiyaa, 18

Page 15: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

15

Na Imaam al-Haafidhw Ibn-Khathiyr katika tafsiri yake mashuhuri amesema maneno mazuri katika suala hili wakati akiifasiri kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) isemayo:

و� �_�D&) "�[@ إ%� �G0Bك "�*Fm وأ�a#D �a+�ا

”Wala hawatakuletea mfano wowote, ila na Sisi tutakuletea (jawabu) kwa haki, na tafsiri iliyo bora.” [26]

Ni vizuri hapa kuyanukuu maneno hayo kwa sababu ya faida yake kubwa. Amesema al-Haafidhw Ibn-Kathiyr (Rahimahu Allaah) kwamba:

”Watu katika suala hili wana kauli nyingi sana. Hapa sio mahali pa kuzichambua isipokuwa tu sisi katika suala hili tunafuata madhehebu ya as-Salafus-Swaalih (wema waliotangulia) Maalik, Awzaaiy´, ath-Thawriy, al-Layth bin Sa’ad, ash-Shaafi’iy, Ahmad, Is-haaq bin Raahawayh na Maimaam wengine wa Kiislamu wasiokuwa hao, wa zamani na wa sasa. Madhehebu hayo ni kuthibitisha Majina na Sifa za Allaah kama zilivyokuja bila ya kuainisha namna. Bali ilivyo ni kama walivyosema Maimaam akiwemo Nu´aym bin Hammaad al-Khuzaa’iy Shaykh wa Imaam al-Bukhaariy ambaye amesema ”Yeyote anayemfananisha Allaah na viumbe Vyake basi amekufuru na hakuna kufananisha katika sifa Alizojisifia Allaah au alizomsifia Mtume Wake. Hivyo basi yeyote anayemthibitishia Allaah Majina na Sifa zilizokuja katika aayah za wazi (za Qur-aan) na Hadiyth sahihi (za Mtume) katika njia inayowiana na utukufu wa Allaah na akazikanusha kasoro, basi huyo amefuata njia ya uongofu.” [27]

2. KUAMINI MALAIKA

Kuamini Malaika kunajumuisha kuwaamini Malaika kwa ujumla na kwa ufafanuzi. Hivyo Muislamu anaamini kuwa Allaah Ana Malaika Aliowaumba ili wamtii, na amewasifu kuwa wao ni:

R� j����ن_" A�ل وه��" �&���a� � ?#��ن �'+?� �F A3 وهkDار �� �% � "+� أ���AP و � ��#AP و� �?#�Rن إ A�R�

”Hawamtangulii kwa neno, nao wanafanya amri Zake. Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawamwombei yeyote ila yule Anayemridhia Yeye, nao kwa ajili ya kumwogopa wananyenyekea.” [28]

Page 16: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

16

--------------------------------

[26] al-Furqaan, 33

[27] Ibn-Kathiyr, tafsiyr surah al-´Aaraaf: 54

[28] al-Anbiyaa, 17-28

Malaika wako aina nyingi. Miongoni mwao kuna waliopewa jukumu la kuibeba ’Arshi. Kuna watumishi wa Peponi na Motoni na kuna waliopewa jukumu la kuyahifadhi matendo ya waja.

Tunawaamini kwa ufafanuzi Malaika ambao Allaah na Mtume Wake wamewataja kwa majina, kama Jibriyl, Mikaaiyl, Maalik mtumishi wa Motoni na Israafiyl aliyepewa jukumu la kupuliza parapanda na ambaye ametajwa katika hadiyth sahihi [za Mtume].

Imethibiti katika hadiyth sahihi iliyonukuliwa kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

”Wameumbwa Malaika kutokana na nuru na wameumbwa majini kutokana na wako la moto na ameumbwa adamu kutokana na kile mlichotajiwa [29].” [30]

3. KUAMINI VITABU

Page 17: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

17

Ni wajibu kuamini kwa ujumla kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Ameteremsha vitabu kwa Mitume Wake ili kuiweka wazi haki na kuihubiri, kama Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Alivyosema:

�a� APR ا$'�ب وا�+Nان +��م اG%�س "� �GN&ت وأ�GF+��" �G��ر �G��أر ��

”Kwa hakika Tuliwatuma Mitume wetu kwa dalili waziwazi, na Tukateremsha Kitabu pamoja nao na Mizani, ili watu wasimamie uadilifu,” [31]

Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

+*$A "+� اG%�س �+�� Fm*�?F��� و 2Gر�� وأ&Nل APR ا$'�ب "� �+F+�%G�ة ��uR ا�� ا�آ�ن اG%�س أ %5 وا ا�'�#�ا �+�

”Watu wote walikuwa ni Ummah mmoja. Allaah Kkapeleka Manabii wabashiri na waonyaji. Na pamoja nao Akateremsha Kitabu kwa Haki, ili kihukumu baina ya watu katika yale waliyokhitalifiana.” [32]

--------------------------------

[29] Tulichotajiwa ni kwamba Mtume Aadam ameumbwa kutokana na udongo. Tazama Qur-aan, kwa mfano surah as-Sajdah, 7 au surah Swaad, 71.

[30] Imepokea hadiyth hii na Imaam Muslim

[31] al-Hadiyd, 25

[32] al-Baqarah, 213

Pia tunaviamini kwa ufafanuzi vile vitabu Alivyovitaja Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Miongoni mwa vitabu hivyo ni kama Tawrat, Injiyl, Zabuur Na Qur-aan.

Qur-aan tukufu ndio kitabu bora zaidi, cha mwisho, kinachovitawala vitabu vyote na ndio kinachovisadikisha. Qur-aan pamoja na Sunnah sahihi zilizonukuliwa kutoka kwa Mtume wa Allaah ndio mambo yanayoupasa Ummah wote kuyafuata na kutekeleza Shari´ah zake. Hiyo ni kwa sababu Allaah Aliyetukuka Mmemleta Mtume Wake Muhammad ili awe Mtume kwa watu na

Page 18: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

18

majini. Pia Ameteremsha kitabu pamoja naye ili kitabu hicho kiwe hakimu kati ya watu na kukifanya kuwa ni dawa kwa magonjwa yaliyo katika nyoyo. Pia Qur-aan ni ufafanuzi wa kila jambo, ni muongozo na ni rehema kwa Waumini, kama Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Alivyosema:

���ن �D A$%�R�j�R واD%��ا %D�� رك�� j�GN&وهـ2ا آ'�ب أ

”Na hichi ni Kitabu Tulichokiteremsha, kilichobarikiwa. Basi kifuateni, na mcheni (Allaah), ili mrehemewe.” [33]

Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

�+��a��F@$F .�ء وه�ى ور�5� و"?�ى �&�+�D ب�'$�G ��+) ا%N&و

”Na Tumekuteremshia Kitabu hiki kinachobainisha kila kitu, na ni uongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu.” [34]

Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

�) اa%��وات واcرض I إـ� إI% ه� �*+ـ� و��+, �1@ �� أ��PC اG%�س إ&�F ر��ل ا�� إ+$�R+�B A ا%2ي �ون'PD A$%�R j�R�%Dوا �D���وآ ���" � L� 2ي% F�F اcا F��%G �Gا "��� ور��� اv�

”Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote, niliyetumwa na Allaah Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Hapana mungu ila Yeye Anayehuisha na Anayefisha. Basi muaminini Allaah na Mtume Wake asiyejua kusoma na kuandika, ambaye anamuamini Allaah na maneno yake. Na mfuateni yeye ili mpate kuongoka.” [35]

Aayah za Qur-aan katika kuelekeza maana hii ni nyingi sana.

--------------------------------

[33] al-An´aam, 155

[34] an-Nahl, 89

[35] al-´Aaraaf, 158

Page 19: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

19

4. KUAMINI MITUME

Inapasa kuwaamini Mitume kwa ujumla na kwa ufafanuzi. Tunaamini kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Ametuma kwa waja Wake Mitume wanaotokana na wao; Mitume wanaotoa habari njema na wanaotoa habari za maonyo na wanaoihubiri haki. Yeyote anayewaitika Mitume atapata wema na yeyote anayewapinga atapata hasara na majuto. Mtume wa mwisho na bora zaidi ni Mtume wetu Muhamad bin ´AbdiLlaah. Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

��ا ا(%��eتG'Bوا ���وا ا�� "�G]R �� آ@F أ %5 ر%I�� أن ا�� و

”Na kwa hakika kwa kila ummah Tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Allaah, na muepukeni Twaaghuut.” [36]

Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

@�C�� اR" 5%Y� ���?F��� و 2Gر�� S0% �$�ن �G%�س 3�� اC S�Cر

”Mitume hao ni wabashiri na waonyaji, ili watu wasiwe na hoja juu ya Allaah baada ya kuletewa Mitume.” [37]

Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

�+F+�%G$A و$� ر%��ل ا�%� وAD�� ا�BFر �F ��� أ"� أ%�* %� آ�ن

”Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Allaah na Mwisho wa Manabii;” [38]

Mtume yeyote ambaye Allaah Amemtaja katika Mitume hao au kutajwa kwake kumethibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah, basi tunamwamini kwa njia ya ufafanuzi na kuainisha; kama Mtume Nuuh, Huud, Swaalih, Ibraahiym na wengineo Allaah Awafikishie, pia Amfikishie Mtume wetu rehema na amani bora na tukufu.

Page 20: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

20

--------------------------------

[36] an-Nahl, 36

[37] an-Nisaa, 165

[38] al-Ahzaab, 40

5. KUAMINI SIKU YA MWISHO

Ama kuamini Siku ya Mwisho, huingia humo kuyaamini mambo yote yatakayotokea baada ya kufa; mambo ambayo Allaah na Mtume Wake wameyaeleza – kama mtihani wa kaburi (fitnatul-qabri); mateso na neema zake. Pia huingia humo kuamini yatakayotokea Siku ya Qiyaamah ikiwa ni pamoja na shida na mateso, swiraat [39], mizani, kuhesabiwa, malipo, kutolewa vitabu kwa watu ambapo kuna atakayechukua kitabu chake kwa mkono wa kulia na kuna atakayechukua kitabu chake kwa mkono wa kushoto au nyuma ya mgongo wake. Pia huingia katika kuiamini Siku ya Mwisho kuamini kisima cha maji cha Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa salam), kuamini Pepo, moto, na Waumini watamuona Mola wao, Naye Allaah Atawasamehe na kuamini mambo mengine yasiyokuwa hayo na ambayo yametajwa katika Qur-aan tukufu na Sunnah sahihi za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa saallam). Ni wajibu kuyaamini yote hayo na kuyasadiki katika njia ambayo Allaah na Mtume Wake wameifafanua.

6. KUAMINI QADAR

Ama kuamini Qadar kunajumuisha kuamini mambo manne:

Page 21: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

21

A) Allaah Ameyajua yaliyotokea na yatakayotokea. Anazijua hali za waja Wake, riziki zao, muda wao wa kuishi, matendo yao na mambo yao mengine yasiyokuwa hayo. Hakuna chochote katika hayo kinachofichikana kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kama Alivyosema:

A+�� �ء. F@$" �%� إن% ا

”Hakika Allaah ni Mjuzi wa kila kitu.” [40]

------------------------------

[39] Swiraat ni njia nyembamba watakayo tahiniwa watu kwa kupita kwenda Peponi.

[40] al-Mujaadilah, 7

Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

� أ��ط "$@F .�ء ���� 1 �%�'R���ا أن% ا�%� 3�� آ@F .�ء 1��� وأن% ا….

”…. ili mjue kwamba Allaah ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu, na kwamba Allaah Amekizunguka kila kitu kukijua vilivyo kwa ilimu Yake.” [41]

B) Jambo la pili ni kwamba Allaah Ameandika kila alichokikadiria na kukihukumu, kama Alivyosema:

|+#��&� آ'�ب G�و APG � GD�i ا_رض �G��� �1

”Hakika SisiT kiasi cha kila kinachopunguzwa na ardhi kutokana nao. Na Kwetu kipo Kitabu kinachohifadhi yote.” [42]

Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

�+� وآ@% .�ء أ�j�G+g �� إ �م

”Na kila kitu Tumekihifadhi katika daftari asli lenye kubainisha.” [43]

Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

Page 22: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

22

�+a� �%� � �� اa%��ء وا_رض إن% ذ) �� آ'�ب إن% ذ) 3�� ا A�R� �%� أA�RD A أن% ا

”Je! Hujui kwamba Allaah Anayajua yaliomo mbinguni na katika ardhi? Hakika hayo yamo Kitabuni. Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi.” [44]

-----------------------------------

[41] at-Twalaaq, 12

[42] Qaaf, 4

[43] Yaasiyn, 12

[44] al-Hajj, 70

C) Jambo la tatu ni kuamini utashi wa Allaah unaoendelea. Anayoyataka Allaah huwa, na Asiyoyataka hayawi, kama Alivyosema:

� �?�ء @R#� �%� إن% ا

”Hakika Allaah Hutenda Apendayo” [45]

Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

إ&%�� أ j� إذا أراد .+�0 أن ���ل � آ� �+$�ن

”Hakika amri Yake Anapotaka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa.” [46]

Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

�+��R و � D?�ؤون إ%� أن �?�ء ا�%� ربC ا

”Wala nyinyi hamtotaka isipokuwa Atake Allaah Mola wa walimwengu wote.” [47]

D) Jambo la nne ni kuamini kuwa Allaah ndiye Muumba wa vyote vilivyopo. Hakuna Muumba wala Mola isipokuwa Yeye tu, kama Alivyosema:

Page 23: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

23

m آ@F .�ء وه� 3�� آ@F .�ء وآ+@�� �%� ا

”Allaah ndiye Muumba wa kila kitu, na Yeye ndiye Mlinzi juu ya kila kitu.” [48]

[45] al-Hajj, 18

[46] Yaasiyn, 82

[47] at-Takwiyr, 29

[48] az-Zumar, 62

Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

F� اa%��ء وا_رض � إ� إ%� ه� �_&3% A$1��ز �%�e m+� ا�� � �� أ��PC اG%�س اذآ�وا &R�, ا�%� ��+$A ه@ LD�$�ن

”Enyi watu! Kumbukeni neema za Allaah juu yenu. Je, yupo muumba mwengine asiyekuwa Allaah anayekupeni riziki kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Hapana mungu ila Yeye tu. Basi wapi mnakogeuzwa?” [49]

Kwa watu wa Sunnah na Jama´ah, kuamini Qadar kunajumuisha kuamini mambo yote haya manne, kinyume cha baadhi ya watu wa bid´ah wanaokanusha baadhi ya mambo hayo.

Inaingia katika kumwamini Allaah kuitakidi kuwa imani ni maneno na vitendo. Imani inaongezeka kwa utiifu na inapungua kwa kufanya maasi. Pia haifai kumfanya Muislamu yeyote kuwa ni kafiri kwa sababu ya kutenda jambo lolote katika maasi ambayo sio Shirki na sio Ukafiri, kama zinaa, wizi, kula ribaa, kunywa ulevi, kuwadharau wazazi na madhambi mengine makubwa yasiyokuwa hayo, maadamu Muislamu huyo hajaitakidi uhalali wa madhambi hayo. Hii kwa mujibu wa kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwamba:

�� �?�ء ( إن% ا�� I �=#� أن �?�ك "� و�=#� � دون ذ

Page 24: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

24

”Hakika Allaah Hasamehi kushirikishwa na kitu. Lakini Yeye Husamehe yasiyokuwa hayo kwa Amtakaye.” [50]

Hii pia ni kwa mujibu wa vile ilivyothibiti katika hadiyth zilizonukuliwa kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba Allaah Atamtoa katika Moto kila ambaye katika moyo wake mna chembe ndogo ya Imani.

Ni katika kumuamini Allaah kupenda kwa ajili ya Allaah, kuchukia kwa ajili ya Allaah, kufanya urafiki kwa ajili ya Allaah na kufanya uadui kwa ajili ya Allaah. Muumini anatakiwa awapende Waumini na kuwafanya marafiki, awachukie makafiri na kuwafanya maadui. [51]

--------------------------------

[49] Faatwir, 3

[50] an-Nisaa, 116

[51] Tazama kwa mfano Surah al-Mujaadilah, 22 au surah al-Mumtahinah, 1-6

Waumini wakubwa wa Ummah huu ni Maswahaba wa Mtume wa Allaah. Watu wa Sunnah na Jama´ah wanawapenda Maswahaba, wanawafanya marafiki na wanaitakidi kuwa wao ni watu bora zaidi ya Mtume kwa mujibu wa kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) isemayo kwamba:

”Watu bora zaidi ni karne yangu, halafu ni wale ambao wanawafuatia hao, halafu ni wale ambao wanawafuatia hao.” [52]

Watu wa Sunnah na Jama´ah wanaitakidi pia kuwa Maswahaba bora zaidi ni Abu Bakrr as-Swiyddiyq, halafu ´Umar al-Faaruuq, halafu ´Uthmaan Dhun-Nuurayn, halafu ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhum jamai´ah). Baada ya hao ni Maswahaba waliosalia kati ya Maswahaba kumi waliokwishapewa habari njema

Page 25: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

25

za kupata Pepo, halafu ni Maswahaba waliosalia. Tunamuomba Allaah Awawie radhi wote.

Watu wa Sunnah na Jama´ah wanazinyamazia tofauti zilizojitokeza kwa Maswahaba na kuitakidi kuwa Maswahaba katika kutofautiana huko walikuwa wakijitahidi. Mwenye kupatia ana malipo mara mbili na mwenye kukosea ana malipo mara moja.

Watu wa Sunnah na Jama´ah wanawapenda watu wa familia ya mtume (Ahlul-Bayt) wanaomuamini Mtume; wanawapenda wao na pia wanawapenda na kuwaenzi wake wa Mtume wa Allaah ambao ni Mama wa Waumini, na wanawaombea radhi wote.

Watu wa Sunnah na Jama´ah wanajiepusha na mwenendo wa Raafidhah [53] ambao wanawachukia Maswahaba wa Mtume wa Allaah na kuwatukana. Pia wanachupa mipaka kwa watu wa familia ya Mtume na kuwatukuza zaidi ya daraja aliyowapa Allaah. Aidha watu wa Sunnah na Jama´ah wanajitenga na mwenendo wa Nawaasib wanaowaudhi watu wa familia ya Mtume kwa kauli na vitendo.

---------------------------------------

[52] Ameipokea hadiyth hii Imaam Muslim

[53] Raafidhah (Rawaafidh) ni katika vikundi vya Mashia. Miongoni mwa Itikadi za kikundi hichi ni kuamini kuwa Swahaba ´Aliy bin Abi Twaalib aliusiwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) awe kiongozi wa Waislamu baada ya kufa Mtume. Kwa msingi huo, kikundi hichi huamini kuwa Swahaba wengi, akiwemo Abu Bakr, ´Umar na ´Uthmaan watu ambao hawakumpa ´Aliy uongozi baada ya kufa Mtume ni madhalimu. Na madai hayo ni uongo wa dhahiri.

Yote tuliyoyataja katika maneno haya mafupi kuhusu Itikadi Sahihi ambayo kwayo Allaah Amemtuma Mjumbe Wake Muhammad (Swalla Allahu ´alayhi wa

Page 26: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

26

sallam), ndio Itikadi ya kikundi kilichookoka; Watu wa Sunnah na Jama´ah, kikundi ambacho Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Amekielezea kwa kusema:

”Halitoacha kundi katika Ummah wangu kuwa juu ya haki ni lenye kunusuriwa. Hatowadhuru mwenye kuwafedhehesha mpaka ije amri ya Allaah (Qiyaamah).” [54]

Pia amesema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam):

”Wamegawanyika Mayahudi katika mapote 71, wakagawanyika Wakristo katika mapote 72 na Ummah wangu utagawanyika mapote 73. Yote hayo yataingia motoni ila moja tu)) Maswahaba waliuliza: Ni lipi hilo, ewe Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wa Allaah! Akasema: ((Ni lile nililokuwemo mimi na Swahaba zangu.” [55]

Hiyo ndio Itikadi sahihi ambayo inapasa kushikamana nayo, kuidumisha na kujihadhari na kila lililo (dhidi yake) yani kinyume na hayo.

Ama waliojitenga na Itikadi hii na kwenda kinyume nayo wako aina nyingi. Kuna wanaoabudu masanamu, Malaika, mawalii, majini, miti, mawe nk. Hawa hawakuuitakidi wito wa Mitume bali wamewapinga na kuwafanyia inaad – yaani jeuri, kama walivyofanya Maquraysh na Waarabu wengine kwa Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam). Vitu walivyokuwa wakiviabudu Maquraysh na Waarabu walikuwa wakiviomba kuwatatulia shida, kuponya wagonjwa na kupata ushindi kwa maadui. Pia walikuwa wakichinja na kuviwekea nadhiri hivyo walivyokuwa wakiviabudu. Wakati Mtume wa Allaah alipowakataza kufanya hivyo na kuwaamuru waitakase ´Ibaadah kwa Allaah Pekee walilishangaa hilo, walilikataa na kusema:

@RB5 أPv�ا إ�P ا��Y�ب ?�ء ه2ا إن% وا

”Amewafanya miungu wote kuwa ni Mungu Mmoja tu? Hakika hili ni jambo la ajabu.” [56]

--------------------------------

Page 27: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

27

[54] al-Bukhaariy na Muslim

[55] Ameipokea hadiyth hii: Imaam Ahmad, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na ad-Daarimiy

[56] Swaad, 5

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) hakuacha kuwahubiria kwa Allaah, kuwatahadharisha na Shirk na kuwafafanulia uhakika wa da´wah aliyokuwa akiwahubiria mpaka Allaah Akawaongoza Aliowaongoza miongoni mwao. Halafu waliingia katika Dini ya Allaah kwa makundi. Dini ya Allaah ikashinda dini nyingine baada ya da´wah ya mfululizo na Jihaad ndefu kutoka kwa Mtume wa Allaah, Maswahaba wake na waliowafuatia hao kwa wema.

Hali baadaye ilibadilika na watu wengi wakakumbwa na ujinga mpaka wengi wao wakarudi kwenye dini ya ujinga kwa kuchupa mipaka katika kuwaadhimisha Mitume na mawalii; kuwaomba, kuwataka msaada na aina nyingine za ushirikina zisizokuwa hizo. Watu hawakuijua maana ya ”Laa Ilaaha Ila Allaah” kama makafiri wa Kiarabu walivyojua maana yake. Tunamuomba Allaah msaada!

Ushirikina huu bado ungali ukienea kati ya watu hadi wakati wetu huu, kwa sababu ya kuzidiwa na ujinga na kuwa mbali na kipindi cha utume. Dhana ya hawa waliokuja nyuma ni dhana ile ile ya watu wa mwanzo. Dhana yao ni kule kusema kwao kuwa:

� .#�Rؤ&� هـILءG� ��ا

”Hawa ndio waombezi wetu kwa Allaah!” [57]

� Aه��R& �%+��F"�&� إ 3ز#3 ا�%� إ

”Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu kumkaribia Allaah.” [58]

Page 28: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

28

[57] Yuunus, 18

[58] az-Zumaar, 3

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Ameibatilisha dhana hii na kufafanua kuwa mtu yeyote anayemaubudu asiyekuwa Allaah vyovyote awavyo, basi mtu huyo amemfanyia Allaah Shirk na amekuwa kafiri, kama Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Alivyosema:

�ون�R�و � � ا�� دون I AهC�k� Iو APR#G� ن�� .#�Rؤ&� هـILء و���G� ��ا

”Nao, badala ya Allaah, wanaabudu wasiowadhuru wala kuwanufaisha, na wanasema: Hawa ndio waombezi wetu kwa Allaah!” [59]

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Amewaradi kwa kusema:

��0Fن 1@GDأ ���*�&� اcرض �� وI اa%��وات �� I A�R� "�� ا� 3�RD�آ�ن ��%� و?�

”Sema: Je! Mnamwambia Allaah asiyo yajuaya katika mbingu wala katika ardhi? Subhaanahu wa Ta'ala! Ametakasika na Ametukuka na hao wanaomshirikisha naye.” [60]

Katika aayah hizi Allaah Amebainisha kuwa kumuabudu asiyekuwa Yeye ikiwa ni Mitume au mawalii au wengine ni Shirki kubwa sana japo wanaoifanya wataiita kwa jina jingine. Pia Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Amesema:

��2% � أو+�ء دو&� � اD%2�وا وا Aه��R& �%+��F"�&� إ 3ز#3 ا�%� إ

”Na wale wanaowafanya wenginewe kuwa ni walinzi wakisema: Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu kumkaribia Allaah.” [61]

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Amewaradi kwa kusema:

� �� "+A$*� APG ا�%� إن% Aإن% ��'�#�ن �+� ه �%��ي � اP� � آ#%�ر آ�ذب ه�

Page 29: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

29

”Hakika AllaahA bainayao katika wanayokhitalifiana. Hakika Allaah Hamwongoi aliye mwongo kafiri.” [62]

[59] Yuunus, 18

[60] Yuunus, 18

[61] az-Zumar, 3

[62] az-Zumar, 3

Kwa kauli hio Allaah Ameweka wazi kuwa ´Ibaadah yao ya kumuabudu asiyekuwa Allaah kwa kuomba, kuogopa, kutaraji na ´Ibaadah nyingine kama hizo ni kumkufuru Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Allaah Amebainisa kuwa ni waongo katika kusema kwao kuwa miungu yao inawakurubisha Kwake.

Miongoni kwa Itikadi za kikafiri zinazopingana na Itikadi Sahihi na kutofautiana na yale waliyokuja nayo Mitume ni Itikadi wanazoitakidi makafiri katika wakati wetu wa sasa, makafiri ambao ni wafuasi wa Marks na Lenin na wahubiri wengine wa ukafiri wasiokuwa hao. Ni sawa waziite itikadi hizo Ujamaa au Ukomunisti au Ba’ath [63] au majina mengine. Miongoni mwa misingi ya makafiri hawa ni kuwa hakuna Mungu na maisha ni uyakinifu (material).

Miongoni mwa misingi yao pia ni kukanusha kuwepo Akhera, Pepo, Moto na kuzikanusha dini zote. Yeyote atakayevitupia macho vitabu vyao na kuyapitia mambo yao atalijua hilo kwa yakini. Ni jambo lisilokuwa na shaka kwamba Itikadi hii inapingana na dini zote inawapelekea wafuasi wake kwenye mwisho mbaya duniani na Akhera.

Miongoni mwa Itikadi zinazopingana na Itikadi Sahihi ni Itikadi wanayoitakidi baadhi ya al-Baatwiniyyah [64] na baadhi ya watu wa Tasawwuf [65] kwamba

Page 30: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

30

baadhi ya watu wanaoitwa kuwa ni mawalii (wapenzi wa Allaah) wanashirikiana na Allaah katika matendo na kuwa na taathira katika mambo ya ulimwengu. Wanawaita mawalii hao kuwa ni Aqtaab, Autaa (nguzo, vigingi), agh-Waath (waokozi) na majina mengine waliyowaundia miungu yao hiyo. Hii ni Shirki mbaya sana katika Rubuubiyyah (matendo ya Allaah). Shirki hio ni mbaya zaidi kuliko shirki ya Waarabu wa wakati wa Ujaahiliyyah. Makafiri wa Kiarabu hawakufanya shirki katika matendo ya Allaah (Rubuubiyyah) bali walifanya shirki katika kuabudu (Uluuhiyyah).

[63] Ba’ath ni nadharia ya kisiasa iliyoanzishwa katika nchi za Kiarabu. Pamoja na malengo mengine. Nadharia hii ina madhumuni ya kuleta Umoja wa Kiarabu, uhuru na ujamaa.

[64] Baatwiniyyah ni mojawapo ya madhehebu ya Mashia. Wafuasi wa madhehebu haya huamini kuwa Shari´ah za Qur-aan tukufu zina nje (dhaahir) na ndani (baatin). Nje ya Shari´ah hizo sio makusudio bali makusudio ni ndani ambayo haifahamiki isipokuwa tu kupitia kwa kiongozi aliyekingwa asitende dhambi (Imaam Maa´aswuum).

[65] Tasawwuf, wafuasi wake wakujulikana kama Masufi, ni nadharia ya kuitakidi ambayo miongoni mwa malengo yake ni kumtaka Muumini aelekee kwa Allaah tu na kujiepusha na mambo ya kilimwengu. Pia wafuasi wa nadharia hii wanaamini kwamba dini ni nje na ndani. Nje ni matendo ambayo hutendwa na kila mtu na ndani ni daraja ya juu ambayo hawaifikii daraja hiyo isipokuwa tu wateule (mawalii) maalum.

Ushirikina wapo pia ulikuwa ni katika wakati wa raha tu, ama katika wakati wa shida walikuwa wakimtakasia Allaah ´Ibaadah, kama Alivyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwamba:

g��+� ا�%� د��ا ا#�) �� رآ��ا X�ذا � ��F���F إY& 3%�هA ���%� ا�?�آ�ن هA إذا ا

”Na wanapopanda katika marikebu, humwomba Allaah kwa kumsafia utiifu. Lakini Anapowaokoa wakafika nchi kavu, mara wanamshirikisha.” [66]

Ama matendo ya Allaah (Rubuubiyyah) makafiri wa Kiarabu walikuwa wakikiri kuwa ni ya Allaah Pekee, kama Allaah (Subhaanahuwa wa Ta´ala) Alivyosema:

Page 31: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

31

�0'AP و_� �% AP��� %���+ �%�L��$�ن �_&%3 ا

”Na ukiwauliza ni nani aliyewaumba? Bila ya shaka watasema: ”Allaah!” Basi ni wapi wanakogeuziwa?” [67]

Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

@1 � A$1��ز �F � ا*�% ���ج و � وا�g"cر اq�%a ���) أ %� واcرض اa%��ء F+� ا�+%, و���ج ,ا� F�*�"F� و � ا� � cن ا���+a� ��D'%��ن أS� ��@ ا

”Sema: Ni nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Au ni nani anayemiliki kusikia na kuona? Na nani amtoaye hai kutoka maiti, na akamtoa maiti kutoka aliye hai? Na nani anayeyadabiri mambo yote? Watasema: Allaah. Basi sema: Je! Hamchi (Allaah)?” [68]

Aayah nyingine katika kueleza maana hii ni nyingi.

--------------------------------

[66] al-’Ankabuut, 65

[67] az-Zukhruf, 87

[68] Yuunus, 31

Ama washirikina wa baadaye wamewazidi washirikina wa mwanzo katika sehemu mbili:

a) Baadhi yao wamefanya shirki katika matendo ya Allaah (Rubuubiyyah)

b) Ushirikina wao unafanyika katika wakati wa raha na wakati wa shida, kama ambavyo anaweza akayajua hayo mtu atakayejumuika nao, akachunguza hali zao na kuona wanayoyafanya katika kaburi la Husayn, Badawiy na makaburi mengine huko Misri, kaburi la Ibn ´Arabiy huko Shaam, kaburi la ´Abdul-Qaaqiyr al-Jalayniy huko Iraq na makaburi mengine mashuhuri ambayo watu

Page 32: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

32

wengi wamechupa mipaka katika kuyaadhimisha na kuyapa haki nyingi za Allaah.

Ni wachache wanaoyakataza hayo na kuwabainishia watu hakika ya Tawhiyd ambayo kwa Tawhiyd hio Allaah Amemtuma Mjumbe Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) na Mitume wengine kabla yake, Allaah Awafikishie rehema na amani. Inna LiLlaahi wa Inna Ilayhi raaji`uun. Tunamuomba Allaah Awarudishe wanaofanya hayo kwenye uongofu, Awapelekee kwa wingi kati yao madaa´iyyah wa uongofu na awasaidie viongozi wa Waislamu na Wanachuoni wao ili waipige vita shirki hii na kuiangamiza. Hakika Yeye Allaah ni Msikivu, Aliye karibu.

Miongoni mwa Itikadi zinazopingana na Itikadi Sahihi katika mlango wa majina na sifa za Allaah ni Itikadi za watu wa bid´ah ikiwa ni pamoja na Jahmiyyah [69], Mu´utazilah [70] na wanaowafuata hao katika kuzikana sifa za Allaah, kumtenga Allaah na Sifa za ukamilifu na kumsifu kwa sifa za visivyokuwepo, visivyokuwa na uhai na vilivyo muhali. Amekatasika Allaah na maneno yao kutakasika kukubwa.

--------------------------------

[69] Jahmiyyah ni nadharia ya kiitikadi ambayo pamoja na mambo mengine wafuasi wake wanaitakidi kwamba Imani ni Itikadi ya moyoni tu ya kumuamini Allaah na Mtume Wake hata kama mtu hakuithibitisha Imani hiyo kwa kutamka na kutekeleza faradhi.

[70] Mu´utazilah ni kikundi kimojawapo kilichojitenga na Itikadi. Miongoni mwa Itikadi zao ni kwamba matendo ya mwanadamu yanatokana na yeye mwanadamu mwenyewe na wala sio kwa Qadar, Utashi na Uwezo wa Allaah. Pia wao huzikanusha baadhi ya sifa za Allaah.

Pia huingia katika mkumbo huo wale wanaokana baadhi ya sifa za Allaah na kuthibitisha baadhi yake, kama Ashaa´irah [71]. Inawalazimu katika sifa walizozithibitisha mfano wa hoja walizozikimbia katika sifa walizozikana na kuzipotosha ushahidi wake. Kwa kufanya hivyo, wamezipinga hoja za kusikia

Page 33: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

33

(Qur-aan na Hadiyth za Mtume) na za kiakili, na wamejikanganya kujikanganya kuliko wazi.

Ama watu wa Sunnah na Jama´ah wao wamemthibitishia Allaah Sifa za Majina Alivyojithibitishia Yeye Mwenyewe au kuthibitishiwa na Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) kwa njia ya ukamilifu. Pia wamemtakasa Allaah na kufanana na viumbe vyake kutakasa kusikokuwa na kukana maana (Ta’atwiyl). Hivyo wamezitumia hoja zote na hawakupotosha wala kukanusha maana. Wamesalimika na mkanganyo ambao wengine wametumbukia katika mkanganyo huo, kama ulivyotangulia ufafanuzi wa hayo. Hii ndio njia ya uokovu na wema katika dunia na Akhera na ndio njia iliyonyooka na ambayo ilifuatwa na maimamu na Salaf (wema waliotangulia) wa Ummah huu. Hakuna kitakachowafanya wawe wema watu wa mwisho wa Ummah huu isipokuwa tu kile kilichowafanya kuwa wema watu wa mwanzo wa Ummah huu na ambacho ni kufuata Qur-aan na Sunnah na kuacha yanayokwenda kinyume na viwili hivyo.

MAMBO YANAYOTENGUA UISLAMU

Ndugu yangu Muislamu, jua kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Amewajibisha kwa waja wote kuingia katika Uislamu, kushikamana nao na kujihadhari na kila linalokwenda kinyume na Uislamu. Allaah pia Amemtuma Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) ili kulihubiri hilo. Aidha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Amewafahamisha kuwa yeyote anayemtii Yeye ameongoka na yeyote anayempinga amepotea. Katika aayah nyingi Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Amehadharisha sababu za kuritadi na aina nyingine za ushirikina na ukafiri.

Page 34: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

34

[71] Ashaa´irah ni wafuasi wa Imaam Abul-Hasan Ash´ariy kabla ya kurudi kwake katika Itikadi ya watu Sunnah na Jama´ah. Awali, Imaam Abul-Hasan alikuwa katika Itikadi ya Mu´utazilah, lakini baadae aliikana Itikadi hiyo na kurudi katika Itikadi Sahihi ya watu wa Sunnah na Jama´ah. Hata hivyo, jambo la kusitikisha ni kwamba wanaojinasibisha na Imaam huyu wanamfuata katika nadharia za kiitikadi za awali ambazo yeye mwenyewe baadae amezikana.

Wanachuoni pia, Allaah Awarehemu katika mlango wa hukumu ya Murtadd (aliyetoka katika Uislamu) wametaja kwamba Muislamu anaweza kutoka katika Dini yake kwa kutenda aina nyingi ya mambo yanayohalalisha damu yake na mali yake. Kwa kutenda mambo hayo mtu anakuwa yuko nje ya Uislamu. Hatari zaidi katika mambo hayo na ambayo hutokea sana ni mambo kumi. Katika maelezo yafuatayo tutakutajia mambo hayo kwa ufupi ili ujihadhari nayo na pia umhadharishe mwenzako kwa kutaraji salama za uzima wa kuepukana nayo. Pamoja na hayo, utatajwa ufafanuzi kidogo baada yake.

1. La kwanza katika mambo kumi yanayotengua Uislamu ni kufanya Shirki katika kumuabudu Allaah. Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

�?�ء �� ذ) دون � و�=#� "� �?�ك أن �=#� I ا�� إن%

”Hakika Allaah Hasamehi kushirikishwa na kitu. Lakini Yeye Husamehe yasiyokuwa hayo kwa Amtakaye.” [72]

Na Amesema Allah (Subhaanahu wa Ta´ala):

�� �?�ك � إ&%� �" ���%م �� �� �و اG%�ر و _واj اGY%5 ��+� ا �+��%~� � أ&�gر

”Yule atakayemshirikisha Allaah. Hakika Allaah Atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na waliodhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru.” [73]

Ni miongoni mwa Shirki kuwaomba watu waliokufa, kuwataka uokovu, kuweka nadhiri na kuchinja kwa ajili yao.

Page 35: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

35

2. Jambo la pili ni kuwa mtu yeyote anayeweka katikati yake na kati ya Allaah wakaa kati (mediators) anawaomba, kuwataka uombezi na kuwategema basi huyo amekufuru kwa mujibu wa makubaliano ya Wanachuoni wote.

--------------------------------

[72] an-Nisaa, 116

[73] al-Maaidah, 72

3. Jambo la tatu ni kwamba mtu yeyote asiyeitakidi ukafiri wa makafiri au akiutilia shaka ukafiri wao au akiitakidi kuwa madhehebu yao ni sahihi basi mtu huyo amekufuru.

4. Jambo la nne ni kwamba mtu yeyote anayeitakidi kuwa muongozo usiokuwa wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) ni mkamilifu zaidi kuliko wa Mtume au kwamba shari’ah zisizokuwa za Mtume ni nzuri zaidi kuliko shari’ah zake, basi mtu huyo ni kafiri.

5. Jambo la tano ni kwamba mtu yeyote anayechukia jambo katika mambo aliyokuja nayo Mtume japokuwa analitekeleza, basi mtu huyo amekufuru kwa mujibu wa kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

(�� ا�%� أ&Nل � آ�ه�ا "_&%AP ذ�_� APأ���

”Hayo ni kwa sababu waliyachukia Aliyoyateremsha Allaah, basi Akaviporomosha vitendo vyao.” [74]

6. Jambo la sita ni kwamba mtu yeyote anayelifanyia istihzai (dharau) jambo lolote la Dini ya Mtume au thawabu zake au mateso yake, basi mtu huyo amekufuru. Ushahidi ni kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

Page 36: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

36

@1 ��� RD'2روا �6NP'aD Iن آA'G ور��� و:D��� أ"�1 AD�#آ �R" A$&��إ�

”Sema: Mlikuwa mkimfanyia maskhara Allaah na Ishara Zake na Mtume Wake? Msitoe udhuru; mmekwisha kufuru baada ya kuamini kwenu!” [75]

7. Jambo la saba ni uchawi. Miongoni mwa uchawi ni as-Swarf [76] na al-’Atwf [77]. Mtu yeyote mwenye kufanya hayo au akayaridhia basi amekufuru. Ushahidi ni kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

� F�R���ن و � و �روت ���'%3 أ I��� ��%&5 &*� إG'� S� �#$D

”Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru.” [78]

--------------------------------

[74] Muhammad, 9

[75] at-Tawbah, 65-66

[76] as-Swarf ni vitendo vya kichawi ambavyo hukusudiwa kwavyo kumbadilisha mtu katika jambo analolipenda, kama vile kumfanya mtu asimpende mkewe n.k.

[77] al-’Atwf ni vitendo vya kichawi ambavyo hukusudiwa kwavyo kumfanya mtu apende jambo asilolipenda kwa kutumia njia za kishaytwaan.

[78] al-Baqarah, 102

8. Jambo la nane ni mtu kusaidiana na kushirikiana na makafiri dhidi ya Waislamu. Ushahidi ni kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

� �%AP و'� A$GF �%&X� APG �ي I ا�� إن% P� �م��+� ا�%~ا

”Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Allaah Hawaongoi watu wenye kudhulumu.” [79]

9. Jambo la tisa ni kwamba mtu yeyote anayeitakidi kuwa baadhi ya watu wana hiari ya kutoka katika shari’ah ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu

Page 37: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

37

´alayhi wa aalihi wa sallam) basi mtu huyo ni kafiri, kwa ushahidi wa kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwamba:

� �'� و� �+e مS�!ا �Gد� ��� @��� �G � ا���ة �� وه� ������ا

”Na anayetafuta dini isiyokuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye khasara.” [80]

10. Jambo la kumi ni kuipuuza Dini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Mtu kuwa hajifunzi Dini wala haitekelezi. Ushahidi ni kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

� �%� أA�� و �F��ت ذآv" �F"ر %Ah أ��ض �PG� �%&إ � �+ �Y� G'���ن ا

”Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anayekumbushwa kwa Ishara za Mola wake , kisha akazikataa? Hakika Sisi tutajilipiza kwa wakosefu.” [81]

Hakuna tofauti katika mambo yote hayo yanayotengua Uislamu kati ya mtu anayefany mzaha, anayefanya kweli na anayefanya kwa woga, isipokuwa tu mtu aliyetezwa nguvu. Mambo yote haya ni miongoni mwa mambo hatari sana na yaanyotokea sana. Inatakikana kwa Muislamu ajihadhari nayo na kuyaogopa, kwa usalama wake.

--------------------------------

[79] al-Maaidah, 51

[80] al-‘Imraan, 85

[81] as-Sajdah, 22

Na huingia katika lile jambo la nne mtu anayeitakidi kuwa:

a) Mifumo na sheria wanazoziweka watu ni bora zaidi kuliko shari´ah za Kiislamu, au kwamba:

Page 38: Itikadi Sahihi - Shaykh Ibn Baaz (PDF)

Itikadi Sahihi www.alhidaaya.com

38

b) Mfumo wa Kiislamu haufai kutekelezwa katika karne ya ishirini, au kwamba:

c) Mfumo wa Kiislamu ndio uliosababisha Waislamu kuwa nyuma, au kwamba:

d) Uislamu uhusishwe tu na uhusiano kati ya mtu na Mola wake bila ya kuingilia mambo mengine ya maisha.

Aidha huingia katika lile jambo la nne mtu anayeona kuwa kutekeleza Shari´ah za Allaah katika kukata mkono wa mwizi au kumpiga mawe mzinifu aliyehifadhika ni jambo lisilowiana na wakati wa sasa.

Pia huingia katika fungu hilo kila mtu anayeitakidi kuwa inafaa kutumia sheria zisizokuwa za Allaah katika Mu’amaalaat (mambo yasiyo ya Ki’ibaadah) na adhabu au mengine, hata hakuitakidi kuwa sheria hizo ni bora zaidi kuliko Shari´ah za Allaah. Hii ni kwa sababu, kwa Itikadi yake hiyo atakuwa amehalalisha mambo Aliyoharamisha Allaah. Kila anayehalalisha aliyoyaharamisha Allaah katika mambo yanayojulikana katika Dini kwa lazima kama zinaa, pombe, ribaa na kuhukumu kwa kutumia sheria zisizokuwa za Allaah, basi mtu huyo ni Kafiri kwa makubaliano ya Wanachuoni wote.

Tunamuomba Allaah Atulinde na mambo yanayosababisha hasira Zake na adhabu kali. Pia tunamuomba Allaah Amfikishie rehema na amani kiumbe Wake bora zaidi Muhammad, na Jamaa na Maswahaba wake.