64
HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010 http://kiswahili.irib.ir -1- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu HUD-HUD Jarida la Radio Tehran Toleo la Tatu Julai – Septemba 2010 Mchapishaji: Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran Mkurugenzi: Muhammad Baraza Mhariri Mkuu: Ahmed Rashid Makala zimehaririwa na: Jopo la Wahariri Wasanifu Kurasa: Ahmed Rashid, Mahboubeh Asgari Msanifu Jalada: Ahmed Rashid Anwani: Idhaa ya Kiswahili, Sauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran P.O.Box 19395/6767 Tehran Islamic Republic of Iran Simu: +98 21 2010 544 Fax: +98 21 2010 544 Barua-pepe: [email protected] Tovuti: http://kiswahili.irib.ir YALIYOMO Tahariri………………………………..2 Kiongozi Muadhamu Alaani Jinai za Wazayuni …………………………….3 Ijue Qur’ani (2)……………………….7 Ramadhani, Mwezi wa Neema na Baraka…………………………………12 Wanawake katika Uislamu…………15 Saumu na Siha………………………..20 Iran Yafanikiwa Kutengeneza Manowari ya Kivita…………………..22 Imam Khomeini (MA) na Mtazamo wa Mustakabali……………………………24 Siku ya Quds, Siku ya Kupaza Sauti dhidi ya Wazayuni……………………28 Visa vya Kuelimisha………………….34 Abu Ali Sina Mtaalamu na Msomi Aliyeng’ara katika Uga wa Elimu…..37 Bustani ya Malenga…………………...42 Kijue Kitabu Hiki……………………..44 Ramadhani, Mwezi wa Toba na Kuitakasa Nafsi……………………….46 Swala, Ibada Inayomjenga Mja……….50 Ikhlasi katika Amali………………….54 Barua za Wasomaji……………………57 Matangazo Redioni…………………..61 Matangazo katika Satalaiti…………62

Jarida Hudu-Hud 3

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -1- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Kwa jina la Allah, Mwingi

wa rehema, Mwenye kurehemu

HUD-HUD

Jarida la Radio Tehran

Toleo la Tatu Julai – Septemba 2010

Mchapishaji:

Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Mkurugenzi: Muhammad Baraza

Mhariri Mkuu: Ahmed Rashid

Makala zimehaririwa na:

Jopo la Wahariri

Wasanifu Kurasa: Ahmed Rashid, Mahboubeh Asgari

Msanifu Jalada: Ahmed Rashid

Anwani:

Idhaa ya Kiswahili, Sauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

P.O.Box 19395/6767 Tehran

Islamic Republic of Iran Simu: +98 21 2010 544 Fax: +98 21 2010 544

Barua-pepe: [email protected] Tovuti: http://kiswahili.irib.ir

YALIYOMO Tahariri………………………………..2 Kiongozi Muadhamu Alaani Jinai za Wazayuni …………………………….3 Ijue Qur’ani (2)……………………….7 Ramadhani, Mwezi wa Neema na Baraka…………………………………12 Wanawake katika Uislamu…………15 Saumu na Siha………………………..20 Iran Yafanikiwa Kutengeneza Manowari ya Kivita…………………..22 Imam Khomeini (MA) na Mtazamo wa Mustakabali……………………………24 Siku ya Quds, Siku ya Kupaza Sauti dhidi ya Wazayuni……………………28 Visa vya Kuelimisha………………….34 Abu Ali Sina Mtaalamu na Msomi Aliyeng’ara katika Uga wa Elimu…..37 Bustani ya Malenga…………………...42 Kijue Kitabu Hiki……………………..44 Ramadhani, Mwezi wa Toba na Kuitakasa Nafsi……………………….46 Swala, Ibada Inayomjenga Mja……….50 Ikhlasi katika Amali………………….54 Barua za Wasomaji……………………57 Matangazo Redioni…………………..61 Matangazo katika Satalaiti…………62

Page 2: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -2- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

TAHARIRI Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

يا أيها الذين آمنوا كتب عليكم الصيام كما كتب على الذين من قبلكم لعلكم تتقونEnyi mlioamini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyoandikiwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu. (al Baqarah: 183). Naam, mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi wa saumu, mwezi wa nuru, mwezi wa maghufira, mwezi wa baraka, mwezi wa taqwa, mwezi wa neema zisizo na kikomo. Kumi la kwanza la mwezi huu mtukufu ni la rehema, kumi lake la pili ni la maghufira na kumi lake la tatu na la kuepushwa na moto. Mapenzi makubwa yaliyoje hayo ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake. Kila nukta ya mwezi wa Ramadhani imejaa umaanawi na uchaji Mungu. Ni mwezi wa kujitakasa, ni mwezi wa kujiweka mbali na maasi, ni mwezi wa kupendana na kusameheana, ni mwezi wa udugu. Amma lakini, inasikitisha mno kuona mgeni huyo azizi anakaribishwa na kuagwa na baadhi ya watu, kwa maasi yaliyorembeshwa kwa jina la “Vunja Jungu!” Hii inasikitisha sana! Ukimuuliza huyo “Mvunja Jungu” ni jungu la nani na lipi hilo analolivunja hubaki kukodoa macho asijue la kunena. Tabia chafu ya “Vunja Jungu” si kufu ya Waislamu, basi natujiepushe nayo. Toleo hili la tatu la Hud-Hud ni maalumu kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Tumekuandalieni makala mbalimbali juu ya mwezi huo. Zimo na makala nyinginezo. Tumeendelea kupokea barua kutoka kwa wasikilizaji na wasomaji wa jarida hili kwa njia ya barua za posta na barua-pepe. Baadhi ya barua hizo tumezichapisha humu kama tulivyofanya kwa toleo la pili la jarida hili. Tunakaribisha maoni na mapendekezo yenu. Mhariri

*HUD-HUD – Jarida la Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran hutolewa bila malipo mara moja kila miezi mitatu. Maoni yaliyomo si lazima yawe yanawakilisha misimamo ya

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

SWT: Subhanahu Wata’ala, m.y. ametakasika na ametukuka. SAW: Swallallaahu ‘Alayhi Wa-aalih, m.y. rehema za Allah ziwe juu yake na kwa Aali zake. AS: ‘Alayhis/’Alayhas/‘Alayhimus Swalaam, m.y. amani iwe juu yake/yao. MA: Mwenyezi Mungu amrehemu.

Page 3: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -3- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Kiongozi Muadhamu Alaani Jinai za Wazayuni Dhidi ya Msafara wa Meli

za Gaza

Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, siku ya Jumanne ya Juni Mosi 2010 alitoa ujumbe muhimu kuhusiana na jinai na ukatili mkubwa uliofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya msafara wa meli zilizokuwa na misaada ya kibinaadamu kwa ajili ya wananchi wa Ukanda wa Ghaza. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya

Kiislamu alisema kuwa, shambulizi hilo la Wazayuni dhidi ya Msafara wa Uhuru (Freedom Flotilla) ni sawa na kushambulia utu wa wanaadamu wote duniani. Alisisitiza kuwa, leo hii kadhia ya Palestina si tu si suala la Waarabu wala Waislamu pekee, bali sasa imekuwa ni kadhia ya haki za binaadamu inayowahusu walimwengu wote na kwamba waungaji mkono wa utawala jeuri na katili wa Kizayuni hasa Marekani, Uingereza na Ufaransa, wanapaswa kutoa majibu ya kukinaisha juu ya jinai za utawala huo dhalimu. Ifuatayo ni matini kamili ya riSwala hiyo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Page 4: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -4- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Bismillahir Rahmanir Rahim.

Shambulio la kigaidi na kikatili la utawala wa Kizayuni dhidi ya msafara wa meli zilizokuwa na misaada ya kibinaadamu, ni kongwa nyingine katika mnyororo wa jinai kubwa zilizorundikana kwenye faili la jinai za utawala huo mshari na khabithi katika muongo huu wa saba wa maisha yake yaliyojaa nakama. Huu ni mfano wa wazi wa vitendo vya jeuri na visivyo na chembe ya huruma ambavyo wanatendewa Waislamu wa eneo hili hususan kwenye ardhi madhulumu za Palestina kwa makumi ya miaka sasa. Mara hii msafara huo haukuwa wa Kiislamu wala wa Kiarabu bali ulikuwa ni wa watu wenye utu na ubinaadamu kutoka kona mbali mbali za dunia. Bila ya shaka shambulio hilo la kijinai litakuwa limewatimizia hoja watu wote kwamba Uzayuni ni sura mpya ya ukatili mkubwa zaidi kuliko ufashisti sura ambayo hivi sasa inaoneshwa na Wazayuni kwa uungaji mkono na msaada wa madola yanayodai kupigania uhuru na haki za binaadamu yakiongozwa na serikali ya Marekani.

Waislamu wa Uturuki wakishiriki katika maziko ya wahanga wa jinai za Israel

Marekani na Uingereza, Ufaransa na madola mengine ya Ulaya yanaunga mkono jinai hizo ambazo ndiyo dhati ya Wazayuni kwa kutumia hila za kisiasa, vyombo vya habari, jeshi na uchumi. Siku zote madola hayo yako nyuma ya maafa

Page 5: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -5- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Hivi sasa tena kadhia ya Palestina si kadhia ya Kiarabu tu wala si suala la Kiislamu tu, bali ni kadhia muhimu mno katika suala zima la haki za binaadamu kwenye ulimwengu wetu huu.

yanayofanywa na Wazayuni, hivyo yanapaswa kutoa majibu ya kina na yabebe jukumu la jinai za Wazayuni hao. Watu wenye hisia za utu katika kila kona ya dunia wanapaswa kutafakari na kuona jinsi hali ya hatari kabisa inavyoutishia ubinaadamu leo hii katika eneo nyeti la Mashariki ya Kati. Waone ni kiasi gani utawala wa kiwendawazimu, wa kikatili na wa umwagaji wa damu unavyoikalia kwa mabavu nchi ya Palestina na kuwafanyia ukatili mkubwa wananchi madhulumu wa ardhi hizo. Kwa miaka mitatu sasa watu milioni moja na nusu, wanawake na watoto wadogo wa Ghaza wamezingirwa na Wazayuni na kufungiwa njia zote wa kuingiza vyakula, madawa na kuendeshea maisha yao ya kila siku. (Watu wenye fikra huru wakae na kufikiria) ni nini maana ya jambo hilo. Mtu anaweza kuyaeleza vipi mauaji, vifungo na mateso ya kila leo wanayofanyiwa vijana wa Ghaza na wa Ukingo wa Magharibi? Hivi sasa tena, kadhia ya Palestina si kadhia ya Kiarabu tu wala si suala la Kiislamu tu, bali imekuwa ni kadhia muhimu mno katika suala zima la haki za binaadamu kwenye ulimwengu wetu huu. Kazi ya kupigiwa mfano na ya kupongezwa ya kupelekwa msafara wa meli huko Ghaza inabidi iendelee kwa mara nyingi na kwa makumi ya sura na mbinu tofauti. Utawala katili wa Kizayuni na waungaji mkono wake hasa Marekani na Uingereza bila ya shaka sasa wanaiona na kuihisi nguvu isiyoshindika ya azma, nia ya kweli na mwamko wa hisia za kibinaadamu kote ulimwenguni. Tawala za nchi za Kiarabu nazo ziko katika mtihani mgumu hivi sasa. Wananchi walioamka wa nchi za Kiarabu wanataka kuona tawala zao zinachukua hatua madhubuti na zisizotetereka dhidi ya Wazayuni. Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) hazipaswi kutulia ila baada ya kuhakikisha kuwa mzingiro wa Ghaza umeondolewa kikamilifu, (na ila baada

Page 6: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -6- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

ya) kumekomeshwa kitimilifu uporaji wa nyumba na ardhi za Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi pamoja na kuhakikishwa kuwa wamepandishwa kizimbani watenda jinai kama vile Benjamin Netanyahu na Ehud Barack. Taifa lenye kupigana jihadi la Palestina, wananchi na serikali ya kidemokrasia ya Ghaza nayo inapaswa kujua kuwa, adui yao khabithi hivi sasa amedhii na kudhoofika mno. Shambulizi la baharini lililofanywa na Wazayuni siku ya Jumatatu si tu si ishara ya kuwa na nguvu, bali hata ni ushahidi wa kuchanganyikiwa na kuemewa utawala huo ghasibu. Suna ya Mwenyezi Mungu imethibiti tena hapa kwamba madhalimu wako mwishoni mwa njia yao iliyojaa nakama na wanajipeleka kwa mikono yao kwenye hatima yao ya maangamizi na kutoweka kabisa. Mashambulizi dhidi ya Lebanon na baadaye katika Ukanda wa Ghaza yaliyofanywa kwenye miaka ya huko nyuma ni miongoni mwa hatua hizo za kipunguwani ambazo zimewaburuta magaidi wa Kizayuni karibu kabisa na shimo la kuangamia. Shambulio dhidi ya msafara wa kimataifa wa misaada katika maji (ya kimataifa ya bahari) ya Mediterranean nalo ni hatua nyingine ya kiwendawazimu mithili ya hatua za huko nyuma. Makaka na madada wa Palestina! Mtegemeeni Mwenyezi Mungu Mwingi wa hekima, Mwenye nguvu. Ziaminini nguvu zenu na ziongezeni mbinde na nguvu hizo. Kuweni na yakini kuwa hatima ya yote, ushindi ni wenu nyinyi. Jueni kuwa:

لقوي ه ه من ینصره إن اللـ .عزیز ولینصرن اللـ (Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anayemsaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu). Sayyid Ali Khamenei 11/Khordad/ 1389 (Hijria Shamsia) 17 Mfunguo Tisa 1431 (Hijria Qamaria) 01/Juni/2010 (Milaadia). Kwa hisani ya mtandao binafsi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei. http://swahili.khamenei.ir

Page 7: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -7- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Katika sehemu ya kwanza ya makala ya Ijue Qur'ani Tukufu tulisema kuwa kuna udharura kwa Muislamu kupata maarifa ya jumla kuhusiana na kitabu kitakatifu cha Qur'ani na kuelewa kwa muhtasari yaliyomo ndani yake. Vilevile tuliahidi kwamba mfululizo huu utakuwa dirisha la kutuwezesha kuchungulia na kutamaza yaliyomo ndani ya kitabu cha mwisho cha Mwenyezi Mungu SW. Makala yetu ya leo itaendeleza mada tuliyoianza katika toleo lililopita ya kutoa utangulizi wa baadhi ya masuala uhimu yanayohusu kitabu cha Qur'ani Tukufu. Majina ya Qur'ani na Sura Zake

Page 8: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -8- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Qur'ani Tukufu ina majina mengi kama al Kitabu, al Furqan na al Dhikr. Kitabu hiki kina sura 144. Neno "sura" katika lugha ya Kiarabu lina maana ya nyumba katika jengo kubwa ambalo lina nyumba kadhaa. Kwa maana hii, msomaji wa Qur'ani anapofungua kitabu hicho na kusoma sura fulani huwa ameingia katika jengo kubwa na kisha kuingia katika moja ya nyumba zake. Anapokamilisha sura na kuingia katika nyingine huwa kana kwamba amefungua mlango wa kuingia katika nyumba nyingine ya jengo adhimu la Qur'ani.

Yumkini neno hilo pia likawa limetokana na neno "Sur" ambalo lina maana ya "ukuta" unaotenganisha kiwanja kimoja na kingine au nyumba na nyingine. Mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu Jalaluddin Suyuti ameandika kitabu cha "al Ittiqan fii Ulumil Qur'ani" kwamba sura ni sehemu ya Qur'ani Tukufu sawa kabisa na mji ambao umegawanyika katika sehemu na maeneo mengi kwa kuta zake. Anasema kila sura ina vipengee kadhaa ambavyo huitwa aya na jumla ya sura zote za Qur'ani zina zaidi ya aya elfu 6.

Page 9: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -9- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Sura zote za Qur'ani Tukufu zinaanza na Bismillahiir Rahmanir Rahim isipokuwa sura ya Tauba ambayo ndiyo sura pekee ya kitabu hicho isiyokuwa na Bismillahi. Sababu kama zinavyosema hadithi na wanazuoni wa elimu ya tafsiri ya Qur'ani ni kwamba Bismillahil Rahmanir Rahim ni baraka, rehema na amani ya Mwenyezi Mungu SW, na haina maana neno hilo la amani kufungua sura ambayo imeteremshwa kwa ghadhabu za Mwenyezi Mungu. Sura ya Tauba inaanza kwa aya zinazotangaza ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na kujitoa katika dhima na kujiweka mbali kwao na washirikina waliovunja ahadi zao na kumkasirisha Mola Muumba. Wanahistoria na wafasiri wa Qur'ani wameandika kuwa baada ya washirikina wa Makka kukiuka ahadi yao kwqa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Mwenyezi Mungu aliteremsha sura hii akitangaza ghadhabu zake na kujiweka mbali na nao akitangaza vita dhidia ya wale waliokikuka mtataba na ahadi zao.

Wanazuoni wa tafsiri na historia ya Kiislamu akiwemo Jalaluddin Suyuti katika kitabu cha al Durrul Manthur wanasema: "Mtume alimpa Abubakr aya za mwanzoni mwa sura hiyo ya Tauba ili akazisome kwa washirikina.

Page 10: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -10- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Baadaye kidogo alimtuma Imam Ali bin Abi Twalib ili achukue aya hizo kutoka kwa Abubakr na akazisome yeye kwa washirikina waliokiuka ahadi zao. Hadithi zinasema Abubakr alirejea kwa Mtume na kuuliza kulikoni. Mtume alimjibu kwa kusema: "Hatekelezi kazi zangu ila mimi mwenyewe au mtu anayetokana nami." Sura ndefu zaidi ya Qur'ani Tukufu ni suratul Baqara ambayo ina aya 286, na sura fupi zaidi ya kitabu hicho ni al Kauthar yenye aya tatu. Qur'ani, Kitabu cha Uongofu Qur'ani Tukufu ndiyo kitabu kikubwa zaidi cha kumwongoza mwanadamu katika maisha yake yote. Kitabu hicho kimezungumzia na kugusia masuala mbalimbali yanayohusu saada na ufanisi wa mwanadamu hapa duniani na huko akhera. Masuala yanayohusu ulimwengu na vilivyomo, siasa, uchumi, kutafakari katika viumbe, maadili na akhlaki yamezungumziwa mno katika kitabu hicho kuliko masuala mengine. Ukweli huo unaonekana wazi pale tunapoyatupia jicho majina na vichwa vya sura za kitabu hicho. Kwa mfano utaona kwamba sura 31 za Qur'ani kama Baqara, Naml, Qamar, Asr, Falaq na kadhalika zinazungumzia maumbile na muundo wa ulimwengu. Baadhi ya sura za Qur'ani zinazozungumzia masuala ya kijamii na kisiasa ni kama al Ahzab, Muminuun, al Shuraa, Nisaa, na al Shuaraa. Vilevile karibu sura 17 za Qur'ani zinajadili masuala mbalimbali ya kifalsafa na kihistoria zikiwemo sura za Al Imram, Anbiyaa, Yunus, Bani Israeil na Maryam. Sura nyingine yapata tano za kitabu hicho kitukufu zinazungumzia masuala ya kiuchumi na mambo mengine yanayohusiana na kadhia hiyo.

Page 11: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -11- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Makki na Madani Miongoni mwa masuala mengine muhimu ya kujua kuhusiana na Qur'ani Tukufu ni kutambua aya na sura zilizoteremshwa Makka na zile zilizoteremshwa Madina na vilevile aya zilizoteremshwa Makka kuhusu watu wa Madina na kinyume chake, yaani aya zilizoteremshwa Madina kuhusu watu wa Makka. Kigezo kikuu kinachotumiwa na wanazuoni waliowengi katika kutofautisha baina ya sura zilizoteremshwa Makka na za Madina au Makki na Madani kama zinavyoitwa kiistilahi, ni kwamba aya na sura zilizoteremshwa kabla ya Bwana Mtume kuhajiri na kuhamia Madina zinaitwa Makki, yaani sura za Makka hata kama ziliteremkwa akiwa nje ya Makka. Na sura zilizoteremshwa akiwa baada ya hijra na Mtume kuhamia Madina zinaitwa Madani, japokuwa sura hizo ziliteremshwa kwa mtukufu huyo akiwa mahala pengine. Hivyo basi kigezo cha kupambanua kati ya sura zilizoteremshwa Makka na za Madina ni hijra na kuhama Mtume kutoka Makka kwenda Madina. Suala jingine ambalo linaweza kusaidia msomaji wa Qur'ani kutambua sura zilizoteremshwa Makka au Madina ni kutadabbari na kutaamali vyema na kwa makini ndani ya aya za sura husika. Hii ni kwa sababu baadhi ya sura zina maana ambazo zinanasibiana na matukio ya kabla ya hijra na kuhama Mtume kwenda Madina na baadhi ya nyingine zinanasibiana na matukio ya baada ya hijra. Kwa mfano aya zinazowalingania washirikina na kuwaita katika dini tukufu ya kiislamu na kuwataka waache kuabudu masanamu zinaoana zaidi na zama za Makka na kabla ya Mtume SAW kuhamia Madina. Yaani sura hizo zinanasabiana zaidi na kipindi cha Makka wakati Mtume Muhammad SAW alipokuwa akikabiliana na waabudu masanamu. Na zile zinazozumgumzia masuala ya vita vya kujihami, sheria na kanuni na sheria za adhabu ziliteremshwa Madina baada ya Uislamu kuenea na kuasisi dola mjini Madina. Njia hiyo ya kutadabari na kutafakari vilivyo ndani ya aya za sura mbalimbali za Qur'ani inaweza kumsaidia msomaji kwa kiwango fulani kujua na kutambua sura zilizoteremshwa Makka na zile zilizoteremshwa Madina.

Page 12: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -12- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Wema na huruma huongezeka mwezi wa Ramadhani, mtoto wa Kiislamu akiomba dua huku Muislamu mwingine wa Pakistan akipanga futari msikitini mjini Karachi.

Na Salum Bendera Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa tisa katika mpangilio wa miezi ya Hijria. Mwezi huu unahesabiwa kuwa mwezi ulio bora kuliko miezi mingine. Mwezi huu ni mwezi wa Mwenyezi Mungu, mwezi ilimoshushwa Qur’ani, mwezi wa toba, mwezi wa kujitakasa na mwezi wa kujilea na kujizoesha. Ni wazi kuwa miezi yote ni ya Mwenyezi Mungu, lakini pia ni wazi kuwa kuna miezi mingine ni mitukufu kuliko mingine kama inavyoonesha Qur’ani tukufu, amesema Mwenyezi Mungu mtukufu;

شھر رمضان الذي أنزل فیھ القرآن ھدى للناس وبینات من الھدى والفرقان

Page 13: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -13- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

"Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge." al-Baqarah 2:185

Katika mwezi huu milango ya mbinguni na milango ya peponi hufunguliwa huku milango ya motoni ikifungwa na mashetani kufungwa. Ni mwezi ambao umechaguliwa na Mwenyezi Mungu SWT kuwa mwezi wa kufunga, kitendo cha ibada ambacho Mwenyezi Mungu SWT kakifanya ni chake maalum.

Yeye Mwenyezi Mungu ameubariki mwezi huu juu ya miezi mingine yote na kuwa ni mwezi wa rehma, baraka na msamaha kwa waumini wote. Kwa kweli mwezi huu ni mwezi uliobora zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa malezi kwa nyoyo za binaadamu na kujifundisha na kujizoesha juu ya malezi ya kumtii mola wako.

Na imekuja katika hadithi kutoka kwa Mtume SAW na Maimamu AS kwamba, Usingizi wa mtu aliyefunga ni ibada, na kuvuta kwake pumzi na kunyamaza kwake ni tasbihi,na amali zake ni zenye kukubaliwa, na dua zake ni zenye kujibiwa, na harufu ya mdomo wake mbele ya Allah SWT ni nzuri kuliko harufu ya manukato, na mfungaji hunyanyuliwa daraja za peponi, na Malaika humuombea dua mpaka muda anaofutari (kufuturu) na mfungaji ana furaha mara mbili, furaha ya kwanza wakati anapofutari na furaha ya pili wakati atapokutana na Mola wake. Adhama ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani inadhihirika zaidi pia katika hotuba ya Bwana Mtume SAW mashuhuri kama hotuba ya Shaabani. Mtume anasema katika sehemu ya hotuba hiyo kwamba: Enyi watu hakika umekujieni mwezi wa Mwenyezi Mungu kwa baraka na rehema na msamaha, mwezi ambao mbele ya Mwenyezi Mungu ni bora ya miezi yote, na michana yake ni bora ya michana yote, na usiku wake ni bora ya nyusiku zote, na saa zake ni bora ya saa zote, mwezi ambao mumealikwa katika ugeni wa Mwenyezi Mungu (SWT) na mumekuwa katika mwezi huu miongoni mwa watu waliotukuzwa na Mwenyezi Mungu, pumzi zenu katika mwezi huu ni tasbihi, usingizi wenu ni ibada, na vitendo vyenu ni vyenye kukubaliwa, na dua zenu ni zenye kujibiwa, basi muombeni Mola wenu kwa nia iliyo safi na nyoyo zilizo safika, akupeni tawfiki ya kuufunga mwezi wa Ramadhani na kukisoma kitabu chake (Qur’ani), kwani mtu muovu kabisa ni yule ambaye atanyimwa msamaha wa Mwenyezi Mungu katika mwezi huu mtukufu. Enyi watu! hakika milango ya pepo katika mwezi huu imefunguliwa, muombeni Mola wenu asiifunge, na milango ya moto imefungwa, muombeni Mola wenu asiifungue, na mashetani wamefungiwa, muombeni Mola wenu asiwaachilie.

Page 14: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -14- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Ramadhani na Matukio Katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani kulitokea matukio mengi. Hata hivyo katika makala hii nitashiria baadhi tu ya matukio hayo.

1. Kufariki dunia Bibi Khadija bint Khuweilid. Bibi Khadija bint Khuweilid mke wa Bwana Mtume SAW alifariki tarehe 10 ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Fadhila na utukufu wa bibi huyu unajulikana. Bibi Khadija alikuwa na mchango mkubwa katika kusimama na kuendelea kwa dini tukufu ya Kiislamu. Mtume amenukuliwa akisema kwamba, Uislamu umesimama na kupata nguvu kwa upanga wa Imam Ali na mali ya Bibi Khadija.

2. Kuzaliwa Imam Hassan bin Ali AS. Imam Hassan al-Mujtaba ambaye ni mjukuu wa Bwana Mtume SAW alizaliwa tarehe 15 ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika mwaka wa pili Hijria. Imam Hassan ndiye mtoto wa kwanza wa Imam Ali na Bibi Fatima naye ni mmoja wa viongozi wa mabarobaro wa peponi.

3. Vita vya Badr. Vita mashuhuri vya Badr vilivyopiganwa baina ya Waislamu na washirikina wa Makka vilitokea katika mwezi wa Ramadhani katika mwaka wa pili Hijria.

4. Kukombolewa Makka (Fat’ h Makka). Moja ya matukio muhimu katika historia ya Uislamu ni kukombolewa Makka yaani kukombolewa mji wa Makka na Waislamu kupata ushindi dhidi ya washirikina wa mji huo.

5. Kupigwa upanga Imam Ali AS. Tarehe 19 Ramadhani ndio siku ambayo Abdul Rahman bil Muljim alimpiga Imam Ali upanga wa kichwa. Tukio hili lilitokea ndani ya msikiti wa al-Kufa nchini Iraq wakati Imam alipokuwa anasali Swala ya alfajiri.

6. Kufa shahidi Imam Ali bin Abi Talib AS. Imam Ali ambaye ni jemadari wa Uislamu alikufa shahidi tarehe 21 ya mwezi wa Ramadhani, ikiwa ni siku tatu tu tangu alipopigwa upanga msikitini.

7. Kuteremeshwa Qur'ani tukufu. Moja ya tukio muhimu katika mwezi wa Ramadhani ni kuteremshwa Qur'ani tukufu ndani ya mwezi huu. Mwenyezi Mungu anasema:

“Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu. Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri? Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu. Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jamboAmani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.” al Alaq 97: 1-5

Page 15: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -15- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Wanawake Katika

Bibi Fatimatuz Zahraa AS ni kigezo bora cha kufuata na wanawake wote ulimwenguni Wapenzi wasomaji katika toleo letu lililopita tulizungumzia juu ya Bibi Asia aliyekuwa mke wa Firauni. Katika toleo hilo tutazungumzia sifa na utukufu wa Bibi Fatima al Zahra AS. Miongoni mwa wanawake ambao wametukuzwa duniani na akhera ni binti huyo wa Mtume Mtukufu na Bibi Khadija bint Khuwailid, mke kipenzi wa Mtume na mtoto wa nne wa kike wa Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Page 16: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -16- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Baadhi ya lakabu zake ni al Zahra, Siddiqa, Twahira, Mubarakah, Zakiyyah, Raadhiyah, Mardhiyya, Muhaddathah na Batul. Ijapokuwa viumbe wote ni uthibitisho wa uwepo wa Muumba na wote wameumbwa kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, lakini viko baadhi ya viumbe huwa fakhari ya uumbaji wa Allah kutokana na Mwenyezi Mungu kuwapa zingatio maalumu. Ndio maana katika historia kunashuhudiwa viumbe watukufu kama Bibi Fatima al Zahra AS ambaye ni moja ya miujiza ya Mwenyezi Mungu kwa walimwengu ili kuwaonesha walimwengu dalili zilizo wazi za uwepo wa Mwenyezi Mungu Mmoja asiye na mshirika na anayestahiki kuabudiwa na viumbe wote. Ni kwa sababu hiyo ndio maana Bwana Mtume Muhammad SAW akanukuliwa akisema: "Faatimah ni kipande cha mwili wangu, ni nuru ya jicho langu, ni tunda la moyo wangu, ni moyo na ni roho yangu. Yeye ni hurulaini katika sura ya mwanaadamu, kila anaposimama kufanya ibada, Mwenyezi Mungu anawaambia malaika Wake: Mwangalieni mja wangu aliye bora - Faatimah - amesimama mbele Yangu na dhati yake yote inatetemeka kutokana na unyenyekevu wake mkubwa Kwangu na amesimama kuniabudu kwa moyo wake wote. Bibi Fatima al Zahra alizaliwa na kulelewa katika nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ambako Malaika wa wahyi na ufunuo walikuwa wakiingia na kutoka wakileta ujumbe wa Mola Mlezi. Alikulia katika nyumba ambayo ndiyo pekee sauti ya Allahu Akbar (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa) ilikuwa ikisikika katika zama za awali za Uislamu. Baada ya kuolewa na Imam Ali bin Abi Twalib AS alitambulika kuwa mwanamke kigezo bora cha kuigwa na watu wote katika maisha ya ndoa, ibada na mwenendo mzuri. Baada ya kazi za nyumbani, Bibi Fatima alikuwa akijipinda kwa ibada, dua na kumtaradhia Mola Karima. Imam Ja'far Swadiq AS ananukuu kutoka kwa babu yake Imam Hassan bib Ali mwana wa Bibi Fatima AS akisema kwamba: "Mama alikuwa akisimama katika mihrabu ya ibada katika usiku za kuamkia Ijumaa hadi asubuhi. Alikuwa akiwaombea dua waumini wa kike na kiume bila ya kusema lolote kuhusu yeye mwenyewe. Siku moja nilimuuliza: "Mama! Kwa nini hauiombei nafsi yako kama unavyowaombea dua watu wengine? Alisema: "Mwanangu mpenzi! Jirani kwanza kisha nyumbani." Tasbihi na dhikri ambazo ni maarufu kwa jina la Tasbihatu Zahra alizofundishwa na baba yake kipenzi yaani Mtume Muhammad SAW ni maarufu katika vitabu vya wanazuoni wa Shia na Suni. Elimu na maarifa ya Bibi Fatima AS Tokea awali Bibi Fatima alijifunza elimu na maarifa katika nyumba na ufunuo na wahyi. Elimu na mambo yote ya siri aliyokuwa akifunzwa na baba yake yalikuwa yakiandikwa na mume wake Ali bin Abi Twalib AS. Bibi Fatima

Page 17: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -17- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

alikusanya elimu na maarifa hayo aliyoambiwa na baba yake na kuandikwa na Imam Ali katika tabu kubwa lililokuwa maarufu kwa jina la 'Mas'hafu Fatima'. Bibi huyu mtakatifu alifanya jitihada kubwa za kuwafunza wanawake wa Kiislamu maarifa ya dini hiyo. Alishika Qur'ani tukufu na kuanisika na kitabu hicho. Imepokelewa kwamba hata mtumishi wake, Bibi Fedha, ambaye pia alikuwa mwanafunzi mkubwa wa mtukufu huyo hakuwahi kuzungumza lolote au kujibu swali na maneno ya mtu yeyote bila ya kutumia aya za Qur'ani. Katika kipindi cha miaka 20 alitumia aya za Qur'ani kueleza jambo au kuwasilisha muradi na makusudio yake. Bibi Fatima AS alikuwa akifanya jitihada kubwa za kueneza maarifa ya Kiislamu na hakusita au kuchoka katika uwanja huo. Siku moja mwanamke mmoja alienda kwa Bibi Fatima na kusema: "Nina mama bibi kizee ambaye amekosea katika Swala yake na amenituma ili nikuulize masiala kuhusu Swala hiyo. Bibi Zahra alisikiliza swali lake na akampa majibu ya masiala hayo. Mwanamke huyo alienda na kurudi kwa mara kadhaa akiuliza maswali na kupewa majibu. Hali hiyo ilikariri mara kumi na mara zote Bibi Fatima alikuwa akitoa majibu kwa maswali hayo kwa utanashati na moyo mkunjufu. Mwanamke huyo aliona haya kwa kuhisi kwamba alikuwa akimsababishia usumbufu Bibi Fatima al Zahra na kwa msingi huo alisema: "Sitakusumbua tena." Bibi Fatima alimjibu kwa kusema: "Njoo tena na uliza maswali yako, wala sioni usumbufu wowote kutokana na maswali hayo. Hakika nimemsikia baba yangu Mtume wa Mwenyezi Mungu SAW akisema: "Siku ya Kiyama maulamaa watafufuliwa pamoja nasi na watapewa mavazi ya thamani kadiri ya elimu na maarifa yao, watapewa malipo na thawabu kwa kiwango cha juhudi wanazofanya katika kuwaongoza waja wa Mwenyezi Mungu." Kwa upande wa ibada Bibi Fatima al Zahra AS alikuwa akipitisha sehemu ya usiku kwa ibada na kumtaradhia Mola Muumba. Swala zake za usiku zilikuwa ndefu kiasi kwamba miguu ya mtukufu huyo ilikuwa ikivimba kwa kusimama sana katika Swala. Hassan al Basri aliyefariki dunia mwaka 110 Hijria anasema: "Hakuna mtu katika umma aliyekuwa akifanya ibada kwa wingi, kuipa mgongo dunia na kumcha Mungu zaidi ya Fatima bint Muhammad AS." Mkufu wenye baraka Siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu SAW alikuwa ameketi msikitini akizungukwa na masahaba zake. Mze mmoja aliyekuwa na nguo chakavu na hali ya kusikitisha aliingia msikitini hapo huku akiwa taabani kutokana na uzee na udhaifu wa mwili. Mtume alimwendea na kumjulia hali. Mzee huyo alisema: "Mimi ni maskini dhaifulhali, nina njaa ninaomba chakula, sina mavazi naomba nguo na ni fukara naomba kutatuliwa shida zangu." Mtume alimwambia: "Kwa sasa sina chochote lakini 'mwelekezaji katika kheri na mema ni sawa na mtenda wema'. Baada ya hapo Mtume alimuelekeza kwenye nyumba ya Bibi Fatima AS.

Page 18: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -18- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Mzee huyo alielekea kwenye nyumba ya Bibi Fatima al Zahra iliyokuwa karibu mno na msikiti wa Mtume SAW na akamweleza matatizo yake. Bibi Fatima pia alisema: "Sisi pia kwa sasa hatuna chochote hapa nyumbani. Kisha alifungua mkufu aliokuwa amepewa zawadi na binti ya Hamza bin Abdul Muttalib RA na akampa mzee huyo maskini kisha akasema: "Uza mkufu huu na inshallah utapata muradi wako." Mzee fukara alichukua mkufu na akaelekea kwenye msikiti wa Mtume. Mtume SAW alikuwa bado ameketi na masahaba zake. Mzee fukara alisema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Bibi Fatima kanipa mkufu huu ili niuuze na kutumia mapato yake katika kukidhi haja na matatizo yangu." Mtume alilia baada ya kusikia maneno hayo. Sahaba Ammar bin Yasir alisema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Unaniruhusu ninunue mkufu huu?" Mtume alisema: "Namuomba Mwenyezi Mungu asimuadhibu mtu yeyote atakayenunua mkufu huu."

Ammar alimuuza mzee Mwarabu: "Mkufu huo unauuza kiasi gani?" Alisema: Ninauuza kwa thamani ya chakula cha mkate na nyama kitakachonishibisha, vazi litakalositiri mwili na dinari moja itakayokuwa masurufu ya kunifikisha nyumbani kwangu." Ammar bin Yasir alisema: "Ninanunua mkufu huu kwa dinari 20 za dhahabu, chakula, nguo na mnyama wa kupanda. Kisha sahaba Ammar alimchukua fukara huyo nyumbani kwake na akumpa chakula, nguo, mnyama wa kusafiria na dinari 20 za dhahabu. Aliuchukua mkufu huo akautia uturi na akaufunga kwenye kitambaa. Alimwambia hadimu wake kwamba:

Page 19: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -19- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

"Mpelekee Mtume wa Mwenyezi Mungu mkufu huu na wewe pia nimekutoa zawadi kwa mtukufu huyo." Mtume Muhammad SAW pia aliurejesha mkufu na hadimu yule aliyeachiwa huru na Ammar kwa Bibi Fatima AS. Hadimu alikwenda wa Bibi Fatima na kumpa mkufu. Bibi Fatima al Zahra alimwambia hadimu yule: "Nimekuachia huru kwa ajili ya Mwenyezi Mungu." Mtumishi huyo alicheka. Bibi Fatima aliuliza sababu na siri ya kicheko hicho. Alijibu: "Ewe binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hakika baraka za mkufu huu zinanifanya nicheke. Umemshibisha mwenye njaa, ukamvisha mtu asiyekuwa na nguo, umemtajirisha fukara, ukampa kipando mtu ambaye hakuwa nacho na kumuachia huru mtumwa kisha ukarejea kwa mwenye nao." Katika kipindi kikubwa cha maisha yake ndoa na Bibi Fatima AS, Imam Ali bin Abi Twalib AS alitumia wakati wake mwingi akiwa katika medani za vita na jihadi ya kulinda mipaka ya utawala mchanga wa Kiislamu. Wakati huo mke wake mwaminifu alichukua majukumu yote ya kuendesha nyumba na kulea watoto. Si hayo tu, bali Bibi Fatima al Zahra AS alifanya hima kubwa katika kusaidia pia familia za wapiganaji wengine wa Kiislamu au familia za mashahidi waliouawa katika vita vya jihadi na kupigania dini ya Kiislamu. Alikuwa pia akiwahamasisha wanawake wa Kiislamu katika kutibu majeruhi wa vita vya jihadi wa familia na ndugu zao. Maisha ya Bibi Fatima al Zahra AS yamejaa ibra na mafundisho mengi. Wengine wanaishi kwa ajili ya mali, wengine kwa ajili ya watoto wengine kwa ajili ya uluwa na ziko sababu nyingine nyingi zinazowafanya watu waishi kwa ajili yake, lakini sababu bora zaidi ya maana ya maisha ni imani kwa Mwenyezi Mungu. Maisha ya Bibi Fatima al Zahra AS yalijaa imani kwa Mwenyezi Mungu. Bwana Mtume Muhammad SAW amenukuliwa akisema: "Kwa yakini Mwenyezi Mungu ameujaza imani moyo na viungo vyote vya binti yangu Fatima." Hakika anayefuatilia maisha ya Bibi Fatima AS anakuta kuwa yeye ni chuo kamili katika njanya mbalimbali za maisha. Hivyo anapasa kuwa ni kigezo chema kwa wanawake wote, na hata wanaume pia. ngawa Bibi huyo mtukufu aliishi maisha mafupi, na mwanzo wa kujenga jamii ya Kiislamu Madina alikuwa ni mdogo kwa umri, lakini alikuwa na fahamu na utambuzi wa elimu ya kiuchamungu, ya kidini na umaasumu uliokamilika, kiasi kwamba alitekeleza majukumu muhimu katika ukuaji wa jamii mpya ya Kiislamu. Hii ndio sababu Bibi Fatima AS ni kigezo bora cha kufuata na wanawake wote ulimwenguni.

Swala za Swalamu za Mwenyezi Mungu, Malaika, na Mitume Wake zimshukie Bibi Fatimatuz Zahra AS.

Page 20: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -20- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Kufunga kumeamrishwa katika dini mbalimbali ikiwepo dini tukufu ya Uislamu, Uyahudi na Ukiristo. Mbali na dini mbalimbali kuamuru wafuasi wao wafunge kama moja ya ibada muhimu, wataalamu wengi wa masuala ya tiba wamekuwa wakiamini kuwa kufunga ni miongoni mwa tiba asilia na inaleta faida kubwa kiafya. Kufunga kuna faida tele kwa afya na kwa siha ya mwili. Uislamu unawataka wafuasi wake wawe wenye afya njema, wasafi, walio imara kiimani na kimwili na mwenye nguvu. Bwana Mtume Mtukufu Muhammad SAW ametilia nguvu hoja hiyo pale aliposema kwamba: "Fungeni mpate siha." Hii leo pia wataalamu wa masuala ya afya wamethibitisha faida kemkem mtu anazoweza kuzipata mtu kwa kufunga, zinazouinufaisha mwili na akili. Kuna baadhi ya madaktari wanasema kuwa kufunga kunamfaidisha mtu kisaikolojia na kimwili. Mbali na saumu kumfanya anayefunga awe na stamina ya njaa na aweze kuvumulia matatizo na awe na subra, pia husaidia kupunguza mafuta ya ziada mwilini. Faida za kufunga haziishii hapo bali pia saumu ni njia ya kuponya magonjwa mbalimbali yakiwemo yale yanayohusiana na mfumo wa chakula kama vile maumivu ya tumbo sugu, kuvimba utumbo mkubwa, ugonjwa wa ini, kukosa choo na matatizo mengineyo kama vile unene wa kupindukia, kuziba mishipa ya moyo (arteriosclerosis), shinikizo la damu, asthma, diphtheria na kadhalika. Lakini kabla hatujaendelea na mada yetu hii hebu sasa tueelezee kwa undani kitaalamu jinsi kitendo cha kufunga kinavyoufaidisha mwili. Kufunga kitaalamu huanza pale mwili unapokosa chakula kwa masaa 12 hadi 24. Kikemia kufunga hakuanzi hadi pale sukari aina ya carbohydrate iliyohifadhiwa mwilini inapoanza kutumiwa kama chanzo cha kuzalisha nguvu. Kufunga huko huendelea madamu tu mafuta na carbohydrate iliyohifadhiwa iendelee kunyofolewa na kubadilishwa kuwa nguvu, bila kutumiwa protini iliyohifadhiwa. Pale protini inapoanza kutumiwa na kubadilishwa kuwa nguvu (suala ambalo hupelekea misuli kupungua) kitaalamu tunasema kuwa mtu ameanza kukabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula mwilini au kwa kimombo starving. Faida za kufunga zinaweza kufahamika kwa kujua jinsi mwili unavyofanya kazi wakati chakula kinapokosekana.

Wakati mwili unapoishiwa na nguvu inayotokana na chakula, huanza kutegemea hazina yake ya chakula kilichohifadhi na kitendo hicho

Page 21: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -21- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

huitwa Autolysis. Autolysis ni kuvunja vunja mafuta yaliyohifadhiwa mwilini ili kutengeneza nguvu, kitendo ambacho hufanywa na ini. Hali hiyo hupunguza mafuta ya ziada mwilini ambayo ndio sababu kuu ya magonjwa mengi kama vile shinikizo la damu, mshituko wa moyo na kadhalika.

Kufunga pia husaidia kuondoa sumu mwilini. Suala hilo

hurahisishwa na kufunga kwani chakula kisipoingia mwilini, mwili hubadilisha mafuta yaliyohifadhiwa kuwa nishati na kupitia kitendo hicho kemikali nyinginezo na sumu zenye madhara kwa mwili pia hutoka katika utumbo, ini, figo, mapafu na ngozi. Hizi ni sumu ambazo hutokana na vyakula tunavyokula na mazingira yetu, na huingia mwilini na kuhifadhiwa pamoja na mafuta.

Faida nyingine ya saumu kitiba ni kuupumzisha mfumo wa chakula.

Wakati mtu anapokuwa hali, nguvu inayotumiwa na mfumo wa chakula ambao huwa umepumzika huelekezwa kwenye metabolism na mfumo wa kulinda mwili. Kitendo hicho husaidia mfumo wa kulinda mwili uweze kufanya kazi zake vyema zaidi na kupambana na ugonjwa au vile visivyotakiwa mwilini. Pengine hii ndiyo sababu wanyama wanapopata jeraha huacha kula, na wanadamu hupoteza hamu ya kula wanapopatwa na magonjwa kama vile mafua. Kwa sababu mwili huielekeza nguvu yake yote kwenye mfumo wa ulinzi wa mwili ili kupambana na vijidudu. Faida hiyo mtu huipata pia anapofunga.

Wakati wa kufunga vilevile joto la mwili hupungua kwa kiasi

kikubwa. Hii hutokana na kupungua kasi ya metabolism na kusimama kazi nyingi zinazofanywa na mwili. Kwa kupungua kiwango cha sukari au glukosi katika damu, mwili hutumia glukosi inayohifadhiwa kwenye ini. BMR (basal metabolis rate) hupungua ili kuhifadhi nishati mwilini. Pia homoni mbalimbali huzalishwa wakati mtu anapokuwa amefunga zikiwemo homoni za kukua na za kuzuia seli zisizeeke. Hivyo njia mojawapo ya kuzuia uzee na kuwa na maisha marefu ni kufunga.

Kwa kuzingatia maelezo hayo yote tunaweza kusema kuwa, saumu ina faida kubwa kiafya kwa mwanadamu.

Page 22: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -22- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Iran Yafanikiwa Kutengeneza Manowari ya Kivita

Na Mubarak Henia Manowari ya kivita yenye uwezo wa kutokomeza makombora na iliyotengenezwa na wataalamu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeng'oa nanga katika Ghuba ya Uajemi katika sherehe zilizohudhuriwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatollah Sayyed Ali Khamenei. Manoari hiyo ya Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inajulikana kama Jamaran na ina rada za kisasa na uwezo wa kushiriki katika vita vya kielektroniki. Jamaran ni manoari yenye uwezo wa kusheheni aina kadhaa za makombora ya kuhujumu meli na ya kutungua makombora na ndege za adui. Meli hiyo inayoenda kwa kasi kubwa pia ina eneo la kutua helikopta.

Page 23: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -23- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Utengenezaji na uzinduzi wa meli hiyo ya kisasa kabisa ya kivita ni hatua kubwa katika sekta viwanda vya manoari za kivita nchini Iran. Aidha Iran sasa imejiunga na nchi chache duniani zenye uwezo wa kujitengenezea manoari za kivita.

Ayatullah Khamenei ameashiria hatua ya wataalamu Wairani ya kutengeneza manoari ya kivita ijulikanayo kama Jamaran na kusema, 'Mafanikio haya ni natija ya matumaini, kujiamini na kumtegemea Mwenyezi Mungu'. Amesema mafanikio hayo yataimarisha azma, irada na matumaini ya kizazi cha vijana nchini Iran na kupelekea kupatikana mafanikio makubwa zaidi nchini.

Mdadisi wa mambo kutoka Lebanon amesema mafanikio ya utengenezaji wa manoari hiyo kuimeimarisha nafasi ya Jamhuri ya Kiislamu katika kukabiliana na vitisho vya Marekani. "Manoari ya kivita ya Jamaran inaimarisha uwezo wa Iran kukabiliana na sera za Marekani kivita na vitisho," alisema Mostafa Etrisi. Baada ya kuzinduliwa manoari hiyo ilifanyiwa majaribio yaliyofana katika Ghuba ya Uajemi. Kombora la Nour kutoka manoari hiyo lilifanyiwa kutoka meli hiyo. Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Admeli Habibollah Sayyari amesema: "Manoari ya Jamaran imefanyia majaribio aina mbali mbali za silaha ikiwa ni pamoja na makombora erevu". Manoari ya Jamaran ya kiwango cha Mowdge vile vile ina aina kadhaa ya makombora ya kukabiliana na adui aliye baharini, nchi kavu na angani. "Manoari ya Jamaran vile vile inaweza kurusha aina mbali mbali ya topedo kukabiliana na maadui walio ndani ya maji, " alisema Admeli Sayyari. Kamanda huyo wa jeshi la wanamaji la Iran anasema manoari ya Jamara pia inaweza kutekeleza majukumu sita kwa mpigo kutokana na teknolojia ya juu iliyotumika kuitengeneza.

Page 24: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -24- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Imam Khomeini (MA) na Mtazamo wa Mustakabali

Imetarjumiwa na Mubarak Henia

Miaka 21 iliyopita Juni 4 Radio ya BBC ilitangaza kuwa: “Leo ameaga dunia mtu ambaye kifo chake kitawapa usingizi mnono wengi katika ulimwengu wa Magharibi”. Siku hiyo Wamagharibi walidhani kuwa, kwa kuaga dunia Imam Khomeini, njia na malengo yake pia yalikuwa yamefikia ukingoni. Walidhani kuwa, kwa mara

Page 25: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -25- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

nyingine wangeendeleza sera zao za kibeberu, uvamizi na kupora mali za wengine bila kujali. Lakini leo baada ya kupitia miongo miwili tokea aliporejea kwa Mola wake Imam Khomeini, madola ya kibeberu yanazidi kushangazwa na namna fikra za Imam Khomeini zilivyokita mizizi miongoni mwa Walimwengu. Hamid Malakuti, Mkuu wa Idara ya Utamaduni katika Ubalozi wa Iran nchini Sudan anasema hivi: “Siku moja nilikuwa nikifanya kazi katika ofisi yangu nilipopokea simu. Hapo nikasikia sauti ya kijana aliyesema: “Mimi ni Khomeini”. Nilistaajabu na kusema: “Tafadhali rudia tena maneno yako”. Kwa mara ya pili akasema kwa sauti kubwa: “Mimi ni Khomeini”. Nilimualika ofisini kwangu na alipokuja niliona ni kijana Msudani mwenye umri wa miaka 28 aliyekuwa na uso wa furaha na bashasha. Nilimuomba anifafanulie zaidi kuhusu maisha yake na alianza kwa kusema: “Jina langu ni Khomeini na nilizaliwa mwaka 1982 katika mji wa Khartoum.

Sayyid Hamid Malakuti (kulia) mwambata wa utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Sudan na kushoto ni raia wa Sudan anayejulikana

kwa jina la Khomeini. Baba yangu alikuwa mfuasi wa Imam Khomeini na wakati mtoto wake alipozaliwa aliamua kumpa jina la Khomeini. Nami kila wakati ninapokutana na

Page 26: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -26- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

jamaa na marafiki huwa ninaona fakhari kubwa kujitambulisha kwa jina hili.” Kijana huyo Msudani anaongeza: “Nawaambia vijana wote Wairani kuwa wana bahati kwa kuwa na kiongozi kama huyu. Fuateni mkondo wake na mtapata ushindi. Imam Khomeini na Ayatullah Khamenei ni chanzo cha fahari kwa wanaadamu wote huru duniani. Ifahamike kuwa hata kama Imam Khomeini MA aliaga dunia, lakini kuna maelfu ya Khomeini wengine katika maeneo yote ya dunia, wamezaliwa na kuinukia kwa fikra zake na mapenzi yao kwake ni ya kina na yanazidi kuimarika." Je, Khomeini alikuwa nani, na ni vipi vijana hata walio katika nukta za mbali kutoka Iran, kwa fahari wanajiarifisha kama Khomeini? Dunia inashuhudia mwanaadamu wa leo akielekea zaidi upande wa dini na umaanawi. Weledi wa mambo wanaamini kuwa, kwa kiwango kikubwa muelekeo huu ni mojawapo ya athari za jitihada zisizo na kikomo za Imam Khomeini. Ukweli kuwa raghba ya umaanawi miongoni mwa wanaadamu wa leo imedhihiri ni jambo linaloashiria kuwa kumbukumbu ya Imam Khomeini miongoni mwa fikra za watu ingali hai. Imam Khomeini aliamini kuwa mataifa ya dunia yana kiu cha umaanawi na kwamba yakipata muongozo wa wahyi basi wataelekea katika ucha Mungu. Robert Macwand mwandishi Mmarekani anaitaja karne ya 21 kuwa karne ya kutafuta umaanawi na anatoa takwimu zinazotabiri kuwa: “Karne ya 21 itakuwa duru mpya ya msisimuko wa kidini na katika hali ya sasa hakuna nguvu ya kijamii iliyo na uwezo zaidi ya dini”. Weledi wa mambo wametoa sababu mbali mbali kuhusu muelekeo mpya wa kidini katika jamii zilizostawi kiviwanda. Wengi wanaamini kuwa, muelekeo huu wa maadili mema na umaanawi unatokana na aina fulani ya kujielimisha pamoja na kuwepo mwamko katika mataifa. Imam Khomeini, mwanazuoni mwenye hekima, arif na mwanasiasa wa karne ya 21 aliingia katika medani ya mapambano makubwa ya kihistoria kwa ikhlasi na hisia ya kutekeleza wajibu wa kidini ili kubadilisha muelekeo potofu katika jamii. Akiwa na mwenge wa imani na kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu Moja, Imam Khomeini alifanikiwa kuibua wimbi kubwa la harakati ya wanaadamu na akatoa wito kwa mataifa yaliyokuwa yamedhulumiwa na kudhofishwa, kuinuka na kukabiliana na wakandamizaji. Mitazamo na fikra za Imam Khomeini hazikuwa kwa ajili ya kundi moja tu la watu katika jamii. Aliwaita wanaadamu wote kufuata mafundisho ya dini ya kweli na aliamini kuwa msingi wa ujumbe wa mitume ulikuwa ni kumstawisha mwanaadamu.

Page 27: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -27- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Katika wasia wake, Imam Khomeini ameainisha njia ambayo ikifuatwa, mwanaadamu atafikia malengo ya juu anayoyakusudia. Mwanzoni mwa wasia wake wenye thamani na maana tele, anasherehesha maana ya Hadhiti ya Thaqalain au vizito viwili ambayo Waislamu walio wengi wanaikubali. Kwa mtazamo wa Imam Khomeini, mataifa yanaweza kustawi, kupata saada na kueneza uadilifu duniani kwa kutekeleza mafundisho ya Quran Tukufu na kuwapa wanaadamu wacha Mungu na wanaostahiki uwezo wa kutawala nchi. Kuhusiana na hili, Imam Khomeini anaarifisha utawala wa kidini kwa mbinu bora zaidi na kusema serikali kama hiyo inayoendeshwa na wacha Mungu inaweza kuudhaminia Ummah wa Kiislamu saada ya dunia na akhera. Aina hii ya serikali katika dhati yake inapingana na udhalimu, ufisadi na hujuma. Ni wazi kuwa serikali inapoendeshwa kwa msingi wa thamani za kimaanawi na kidini, maslahi ya madola ya kibeberu huwa hatarini. Kwa sababu hiyo hakuna shaka kuwa serikali ya Kiislamu inapoanzishwa hukabiliwa na changamoto nyingi sana kutoka kwa maadui na njama zao zisizo na kikomo. Lakini watu ambao humuweka Mwenyezi Mungu mbele hudumu katika njia hii na hutegemea msaada wa Mwenyezi Mungu katika harakati zao. Imam Khomeini katika wasia wake anawausia watu wote hivi: "Kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu chukueni hatua za kujitambua, kujitosheleza na kupata uhuru katika sekta zote. Hakuna shaka kuwa mkono wa Mwenyezi Mungu uko nanyi."

Imam Khomeini (Quddisa Sirruhu) alikuwa na mapenzi makubwa kwa bara la Afrika.

Page 28: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -28- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Imetarjumiwa na Salum Bendera Siku ya Kimataifa ya Quds ni siku ya kutangaza himaya na uungaji mkono wa wapenda haki ulimwenguni kwa wananchi madhulumu na wanaokandamizwa wa Palestina. Hayati Imam Khomeini MA mwasisi na mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu aliitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani kila mwaka kuwa ndio siku ya kimataifa ya Quds, siku ya kupaza sauti dhidi ya maadui Wazayuni. Hatua ya hayati Imam Khomeini ya kuitangaza Ijumaa ya

Page 29: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -29- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

mwisho ya kila mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds ilitoa bishara ya harakati tofauti ya kurejesha mapambano ya taifa la Palestina katika njia sahihi. Tunapotazama kwa ujumla ujumbe wa Imam kuhusu siku hiyo tunaelewa vyema umuhimu wa mtazamo wake kuhusu kadhia hiyo. Imam Khomeini anasema katika ujumbe huo kwamba:

Kwa Jina la Allah Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu

"Ninatoa wito kwa Waislamu wote duniani na serikali za Kiislamu kuungana kwa ajili ya kukata mkono wa utawala ghasibu wa Israel na wasaidizi wake. Ninatoa wito kwa Waislamu wote duniani kuichagua Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, ambayo ni miongoni mwa siku za Laylatul Qadr na inaweza kuwa na umuhimu mkubwa mno kwa mustakabali wa wananchi wa Palestina, kuwa Siku ya Quds na kufanya marasimu ya kutangaza mshikamano wa kimataifa wa Waislamu katika kutetea haki za kisheria za wananchi wa Palestina." “Kwa hakika mapambano dhidi ya Uzayuni hususan Israel, ilikuwa moja ya nguzo kuu za fikra za kisiasa za hayati Imam Khomeini. Moja ya nukta zenye umuhimu mkubwa katika kadhia hii ni sisitizo la uzingatiaji makhsusi la Imam kwa mitazamo ya pamoja ya wanafikra huru duniani kutoka makundi na mirengo yote. Mwelekeo huu ulio fauka ya mipaka ya kidini na utaifa unaandaa mazingira mazuri kwa wanaadamu kutafakari kwa kina kuhusu kadhia ya Palestina na kuleta uwiano na umoja katika jamii ya Kiislamu na pia kuifungamanisha jamii ya kimataifa na suala la Palestina. Imam Khomeini anasema: Siku ya Quds ni Siku ya Kimataifa na si siku inayoihusu Quds peke yake…" Hatua ya Imam Khomeini ya kuitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kama Yaum al-Quds (Siku ya Quds) ni kumbu kumbu ya mwaka ya masaibu ya Wapalestina walionyang’anywa ardhi yao. Ni jambo lisilo na shaka kwamba, kwa Waislamu wote Masjidul Aqsa huko Beitul Muqaddas inachukua sehemu muhimu sana baada ya Makka na Madina; kwani ndicho kilichokuwa kibla cha kwanza cha Waislamu. Siku ya Quds huwakumbusha Waislamu wote kwamba, waonevu wamekanyaga kwa nguvu ardhi za Waislamu na hamu yao kubwa ya kutawala haishii Beitul Muqaddas peke yake, bali mpaka kwenye sehemu kubwa za ardhi za Kiislamu kama ilivyo dhahiri sasa kwa matukio katika Iraq na Afghanistan. Hivyo tunaadhimisha siku ya Quds katika muktadha huu. Katika Siku ya Kimataifa ya Quds wapenda haki kote ulimwenguni huadhimisha siku hii kwa maandamano, makongamano na hutuba na kupaza sauti ya kuwaunga mkono Wapalestina wanaokandamizwa na ambao wameporwa haki zao za kimsingi sambamba na ardhi yao kukaliwa kwa mabavu na maadui Wazayuni. Waislamu

Page 30: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -30- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

na wapenda haki kote ulimwenguni hutumia fursa ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds kuonesha mshikamano wao pamoja na ndugu zao wa Palestina, na pamoja na watu wote wanaoonewa ulimwenguni, ambao wanafanywa wakumbane na masaibu mfano wa yale ya Wapalestina.

Maandamano ya Waislamu wa Nigeria dhidi ya Israel Umuhimu wa Siku ya Quds kwa Mtazamo wa Imam Khomeini Baada ya kupita karibu miaka mia moja, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalivunja kimya cha ulimwengu kuhusiana na suala la Palestina; na kwa kutumia muelekeo unaozingatia uhalisia wa mambo, uliosimama juu ya misingi ya itikadi na mafundisho ya Kiislamu ambayo ndiyo dira ya kila Muislamu mwenye fikra huru, yakabuni mkakati sahihi na wa muda mrefu wa kudai kurejeshwa haki zilizoghusubiwa za taifa la Palestina, na ambao utavuruga mahesabu ya Wazayuni yaliyopangwa kwa zaidi ya karne moja; na badala yake kuleta suhulu ya kiadilifu itakayowezesha kuwarejeshea wanamapambano hao (Wapalestina) wa kupigiwa mfano katika historia ya kupigania uadilifu na ardhi za mababu zao. Hakuna shaka yoyote kuwa wananchi wa mataifa mengine hawatokosa kufaidika na hidaya itakayopatikana kwa kuwepo mlingano wa

Page 31: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -31- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

nguvu, ambayo si kitu kingine bali ni uthabiti wa kudumu katika eneo, na watafanya jitihada kwa ajili ya kufanikisha malengo matukufu ya Mapinduzi makubwa ya Imam Khomeini MA.

Kutangaza Imam Khomeini siku ya Kimataifa ya Quds kuliweka wazi msimamo wa Mapinduzi ya Kiislamu katika sura ya mpango wa kistratijia, wa kukabiliana na mpango wa Wazayuni, wa kutaka kuwatokomeza kikamilifu Wapalestina pamoja na madhihirisho yote ya Kiislamu ya ardhi ya Palestina. Hatua hiyo inaonyesha tadbiri ya mwanasiasa mweledi ambaye wito wake wa kupambana na batili katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa ugeni wa Mwenyezi Mungu umebaki katika kumbukumbu ya historia ya Waislamu; siku hiyo ya mshikamano wa Waislamu na wenye fikra huru wote duniani, ni ya kukabiliana na utawala ambao kichwani mwake una ndoto ya kupanua mipaka yake ulimwenguni, na ambao kubakia kwake kunahatarisha amani na uSwalama wa dunia. Umuhimu wa kuzungumzia suala la Palestina na kubuni fikra ya kuanzisha moja ya siku za kimataifa kuwa ni Siku ya Quds, unatokana na kuwa kwake siku hiyo nembo kubwa ya kidini iliyovuka mpaka

Page 32: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -32- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

wa mitazamo finyu ya utaifa na ukabila kwa ajili ya kutumikia malengo matukufu ya Palestina. Hatua hiyo ya Imam Khomeini imepelekea kuitoa fikra ya kuushughulikia mgogoro wa Palestina katika ngazi rasmi na za kiserikali na kuielekeza kwenye ngazi ya wananchi, mataifa na fikra za walio wengi duniani. Nayo Intifadha ya wananchi wa Palestina ni mojawapo ya madhihirisho ya kupigania haki kwa mtazamo wa Kiislamu, ikiwa imepata ilhamu na kufuata mfano wa Mapinduzi ya Kiislamu, na ikazidi kupata nguvu na mwamko maradufu kutokana na mafanikio makubwa iliyopata harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Lebanon ya kuwatimua Wazayuni katika ardhi yao. Kutokea Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kulivuruga mahesabu yote ya wakoloni. Na kutokana na uongozi, uamshaji na msimamo imara wa Imam Khomeini MA, mbinu za mapambano na Israel zikachukua muelekeo mpya. Kutokana na kulielewa barabara suala la Palestina na kutambua nafasi kuu ya wananchi na athari ya kuchukua hatua za mtawalia na za kishujaa za kuupinga utawala wa Israel, Imam Khomeini aliwafanya Wazayuni hao wakabiliwe na hali ngumu zaidi. Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ulidhihirisha wazi kwamba, kulikubali suala la msingi la kutambua haki za taifa za Palestina na kulirejeshea haki zake hizo, ndiyo njia pekee ya ufumbuzi wa mgogoro huo wa kihistoria. Kwa kutumia tajiriba ya Mapinduzi ya wananchi wa Iran na kufuata kigezo cha mapambano yenye mpangilio maalumu katika kuhamasisha matabaka tofauti ya jamii, Wapalestina walianzisha harakati iliyoratibiwa kwa umakini zaidi, ya maandamano makubwa ya akina mama, watoto, viongozi wa dini na wanafikra wakiwa katika safu moja ya kukabiliana na mtutu wa bunduki kwa kutumia mawe, virungu na hata mikono mitupu; na kwa kutumia vituo vya misikiti na Swala za Ijumaa wakaleta mabadiliko makubwa katika sura na mwenendo wa mapambano. Kuingia kwa awamu hii muhimu ya mapambano na kujitokeza kivitendo wananchi na kwa uelewa kamili, kuliliweka suala la Palestina katika hali tofauti kabisa ambayo ilipelekea kuanza kwa vuguvugu la Intifadha. Intifadha ya kwanza ambayo ilikuwa maarufu kama "Intifadha Kubwa" ilianza mwaka 1987 na kuendelea hadi mwaka 1991. Intifadha ya pili iliyoanza mwaka 2000 ilijulikana kama "Intifadha ya al Aqsa." Endapo tutatupia jicho matukio ya kisiasa na kiutamaduni ya eneo la Mashariki ya Kati hususan katika masuala muhimu likiwemo suala la Palestina, tunang’amua kwamba, Mapinduzi ya Kiislamu yakiwa kama kigezo na umbo jipya la mapambano ya kiraia (ya wananchi) yameweza kuwa na nafasi muhimu baina ya Waislamu na harakati za mapambano katika maeneo mbalimbali ulimwenguni na hivyo kuwa na taathira chanya katika kuleta mwamko baina ya

Page 33: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -33- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Waislamu na wanadamu wenye fikra huru kwa ujumla. Kuhusiana na hilo, nafasi maalumu iliyonayo Palestina katika mazungumzo na miamala ya Imam Khomeini-ambapo kilele cha kuzingatia suala hilo ni kuichagua siku na kuipa jina la Siku ya Kimataifa ya Quds-ni jambo la kutaamali, kutadabari na kuchunguza; kwani bila shaka taathira ya muamala huu una umuhimu wa hali ya juu kwa suala la Palestina. 1- Ubunifu wa Imam Khomeini (Quddisa Sirruh) katika kuichagua Siku ya Kimataifa ya Quds ni sisitizo la upinzani wa ulimwengu wote wa Kiislamu dhidi ya uwepo wa utawala vamizi kwa jina la ‘’Israel’’. Siku hii imekuwa ni chimbuko la kusafisha nyoyo na aina fulani ya kuwa na mtazamo mmoja katika Ulimwengu wa Kiislamu ambao ni dhihirisho la wito wa Imam Khomeini wa kuweko umoja wa kalima. Ni kwa namna hii ambapo hatua ya kwanza hupigwa kwa ajili ya umoja wa Kiislamu na kuweko njia kwa ajili ya kufikia katika umma mmoja ambao hauna ubaguzi na tofauti za kimadhehebu. 2- Siku ya Quds ni vita vikubwa kabisa vya kisaikolojia dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na ni moja ya wenzo mkubwa kabisa wa mashinikizo ambao yamkini ukatumiwa dhidi ya tamaa na uchu wa utawala huo ghasibu. Siku ya Kimataifa ya Quds ni tukio muhimu ambalo hutia alama ya ulizo juu ya uhalali wa utawala huo. Kukaririwa kila mwaka kwa tukio hili sambamba na kuufanya ulimwengu wa Kiislamu kuwa na muelekeo kwa fikra za kiistratejia za Imam Khomeini, harakati hiyo huwaonyesha walimwengu kwamba, utawala huo si halali na wakati huo huo huzing’arisha nyoyo za waumini kwa matukufu ya Palestina. Katika upande mwingine, kuonekana picha za mamia kwa maelfu ya waandamanaji katika pembe mbalimbali za dunia hupelekea kutokea ukosefu wa amani wa kisaikolojia ndani ya mipaka ya utawala huo ghasibu. 3- Siku ya Quds imelitoa suala la Palestina katika engo ya kitaifa na kulionyesha katika engo ya Kiislamu na kimataifa; daima utawala wa Kizayuni wa Israel ulikuwa ukifanya njama za kutaka kulidogosha suala hili na kulionyesha kwamba, ni mvutano wa kikaumu baina ya Waarabu na Israel. Kutangazwa msimamo wa Imam Khomeini akiwa shakhsia mahiri wa kielimu na kidini katika ulimwengu wa Kiislamu kulileta moyo mpya katika harakati ya Kiislamu iliyokuwa imesahaulika na hivyo kuimarisha mapambano dhidi ya Israel, hali ambayo iliwafanya wanamapambano wa Kipalestina badala ya kuchagua vitu kama mrengo wa kushoto, mrengo wa utaifa (nationalism) na hata muelekeo wa Magharibi na mapatano, wafikirie tu chaguo la Uislamu, mapambano na istikama.

Page 34: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -34- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Imetarjumiwa na Abdul Fatah Mussa Iddi Kama ilivyokuwa ada na desturi yake ya kila siku, kijana mmoja wa Kiyahudi alikuwa amekaa juu ya paa la nyumba yao. Kila baada ya muda alikuwa akiinuka na kwenda kuchungulia kutokea huko huko juu alikokuwa, kwenye kichochoro kilichokuwa kinaishia kando ya nyumba yao. Alionekana kama kwamba alikuwa anamsubiri mtu apite kwenye uchochoro huo. Mwishowe subira yake ilitoa tija aliyoitarajia; na naam alimwona kutokea mbali mtu aliyekuwa akielekea upande wa nyumbani kwao. Mtu huyo alizidi kukaribia mpaka akafika kando ya nyumba yao Myahudi huyo. Bila kupoteza muda Myahudi aliinuka alipokuwa, na haraka haraka akainua beseni lililojazwa jivu na kujongea nalo hadi kwenye kona ya paa na kummiminia kichwani yule mtu aliyekuwa akipita kando ya nyumba yao. Mpita njia huyo aliyefanyiwa kitimbi hicho hakuwa mtu mwingine ghairi ya Nabii Muhammad saw. Bwana Mtume hakuonyesha hasira wala hisia za kuchukizwa na kitendo hicho cha kijana wa Kiyhaudi. Kwa utulivu alijikumta jivu lililokuwa limemtapakaa kichwani na mwilini, kisha bila kusema chochote, akashika njia na kwenda zake. Pamoja na kwamba hiyo ilikuwa ndio desturi na kawaida ya kila siku ya Myahudi huyo kumfanyia Bwana Mtume uovu huo, lakini nabii huyo wa rehma hakubadilisha njia yake hiyo. Naye Myahudi hakusita kuendeleza vitimbi na maudhi yake hayo aliyokuwa akimfanyia Bwana Mtume; na kubwa zaidi ni kwamba uovu aliokuwa akiutenda ulikuwa ukimpa raha na buraha ya aina yake.

Masahaba ambao walikuwa wakijua yaliyokuwa yakijiri kati ya Bwana Mtume na Myahudi, mara kadhaa walimwomba mtukufu huyo awaruhusu wamtie adabu

Visa hivi unavyovisoma hapa mpenzi msomaji, si vile visa vya ngano za kubuni za alfu lela ulela, wala si vya hadithi

za kutunga za Paukwa Pakawa au za matukio ya uvumi na tetesi za sadiki ukipenda. Ni visa vya matukio ya kweli,

yaliyotokea katika maisha ya viongozi halisi wa wanaadamu, yaani Manabii wa Mwenyezi Mungu. Visa

ambavyo ni kigezo na ruwaza njema kwa mimi na wewe, ya kuweza kubadilisha maisha yetu na kutufanya tupate

fanaka na saada ya leo hapa duniani na kesho huko akhera.

Page 35: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -35- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

kidogo kijana huyo wa Kiyahudi. Lakini Bwana Mtume hakuwaruhusu kufanya hivyo. Aliendelea kustahamili na kuyavumilia maudhi ya Myahudi. Nao masahaba walipobaini kuwa Bwana Mtume ana lengo muhimu analofuatilia katika kadhia hiyo wakaacha kutaaradhia, na badala yake wakaendelea kufuatilia mkasa huo kwa madhumuni ya kutaka kujua nini utakuwa mwisho wake. Siku nyingine ya kupita Bwana Mtume kwenye uchochoro unaopakana na nyumba ya Myahudi ikawadia, naye kama kawaida akawa anapita kando ya nyumba hiyo. Lakini kinyume na matarajio, siku huyo hakukuwepo na habari za Myahudi wala beseni la majivu. Siku nyingine pia alipopita Bwana Mtume mahala hapo hakukuwepo alama yoyote ya Myahudi wala vitimbi vyake vilivyozoeleka. Kuona hivyo Bwana Mtume aliwaambia masahaba zake: “Kitambo sasa hakuna habari zozote za rafiki yetu wala beseni lake la majivu;” kwa hivyo akawaagiza wafuatilie habari zake ili kujua lililomfika. Baada ya kupita na kuuliza uliza masahaba walibaini kuwa Myahudi yule alikuwa amepatwa na maradhi yaliyomweka kitandani, kiasi kwamba alikuwa hawezi hata kuuinua mguu hapa na pale. Wakati habari hiyo ilipomfikia Bwana Mtume, mtukufu huyo aliwaambia masahaba zake: Sasa ni wakati mzuri wa kwenda kumtembelea na kumjulia hali rafiki yetu huyu, hivyo jitayarisheni tupate kwenda kumtizama. Masahaba walistaajabu kusikia maneno hayo, kiasi kwamba mmoja wao aliwauliza wenzake kwa udadisi: “Mnadhani Mtume anafuatilia kitu gani hasa?” Sahaba mwenzake alimjibu kwa kumwambia: “Badala ya maswali hayo ni afadhali tumfuate Mtume ili tujue siri ya kadhia hii.” Hivyo kwa pamoja wakafuatana na Bwana Mtume hadi nyumbani kwao kijana wa Kiyahudi. Wakati mama wa Myahudi aliposikia mlango wa nyumba yao unagongwa na kwenda kuufungua, alishangaa alipomwona Bwana Mtume na idadi kadhaa ya masahaba zake wamesimama mlangoni. Mshangao uliompata mama huyo wa Kiyahudi ulimfanya ashindwe kutamka chochote, akabaki anawaza na kujiuliza

Page 36: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -36- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

akilini mwake, 'hivi Mtume alikuwa na shida gani na wao?' Wakati Bwana Mtume alipobaini hali hiyo ya mshangao na bumbuwazi iliyompata mama wa Kiyahudi alimwelekea kwa heshima na kumwambia: “Ni muda sasa rafiki yetu, yaani mwanao amepatwa na maradhi, hivyo tumekuja kumjulia hali.” Mama wa kijana yule wa Kiyahudi ambaye hakuweza kusema chochote aliamua kujongea kando ili kumpisha Bwana Mtume na masahaba zake wapite. Walielekea hadi kwenye chumba alimokuwa akiugulia Myahudi yule. Wakati Myahudi alipofumbua macho, hakuyaamini macho yake kwa kile alichokiona. Alifunua kinywa chake kwa tabu na kusema: “Ni kweli haya ninayoyaona?” Ni kweli huyu Muhammad, Mtume wa Uislamu, ndiye aliyekuja kunijulia hali mimi, mtu ambaye kila siku nimekuwa nikimmwagia majivu kichwani?! Mtume alimtuliza Myahudi kwa kuanza kumjulia hali yake. Myahudi aliona aibu kubwa kiasi kwamba hakuweza kumtizama Bwana Mtume usoni. Hata hivyo uso wa Bwana Mtume ulionyesha upendo na huruma; na muamala wake kwa Myahudi huyo ulikuwa wa mithili ya watu wanaojuana kwa miaka na miaka. Mlahaka mzuri na wa ucheshi wa Bwana Mtume ulimwathiri mno Myahudi na kuibadilisha kabisa hali yake kiasi kwamba hakuweza kuficha hali ya majuto aliyokuwa nayo na akasema: ”Kitendo changu cha kumvunjia heshima Mtume wa Uislamu kilikuwa ni ujinga na upumbavu mkubwa. Sikuwa nikijua kwamba Uislamu ni dini ya upendo na udugu. Kwa kuwa sasa nimelitambua hilo nami pia naukubali wito wa Muhammad na naamua kuwa Muislamu. Baada ya Myahudi kusilimu, hapo ndipo masahaba walipoelewa hikima ya subira aliyokuwa nayo Bwana Mtume SAW kwa utovu wa adabu aliokuwa akifanyiwa na Myahudi. Kwa kuwa mtukufu huyo alikuwa akifahamu kwamba sehemu kubwa ya upinzani, vitimbi na vitendo vya maudhi vilivyokuwa vikifanywa dhidi yake vilitokana na ujinga na ujahili, ndiyo maana mara nyingi alikuwa akionyesha usamehevu na upole katika kuamiliana na wapinzani wa haki. Kwa hakika akhlaqi na tabia ya Nabii ya rehma Muhammad saw ilikuwa mithili ya tabibu mwenye huruma katika kumchukulia mgonjwa wake kwa ajili ya kumjulisha kile kinachomtaabisha. Na ndiyo maana alikuwa akiwausia masahaba zake kwa kuwaambia: “Kila mwenye kuwahurumia watu, Mwenyezi Mungu atamrehemu naye mtu huyo. Basi wahurumieni watu wote walioko katika ardhi.”

Page 37: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -37- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Mtaalamu na Msomi Aliyeng’ara Katika Uga wa Elimu

Imehakikiwa na Salum Bendera

Dini tukufu ya Kiislamu inasifika kwa utajiri na turathi aali za utamaduni na ustaarabu sanjari na mafunzo yke yasiyo na nakisi. Utajiri wa dini hii ambayo ndio ya haki mbele ya Mwenyezi Mungu, unatokana na lulu na johari za mfundisho yake ambayo ni dafina yenye thamani mno. Sehemu nyingine ya utajiri wa dini hii ni kuwa na wasomi na wanazuoni staid ambao wametopea na kutabahari katika nyuga tofauti za kielimu. Mmoja kati ya wataalamu wakubwa na waliong'ara katika elimu na msanifu wa jengo la Ustaarabu wa Kiislamu ni Abu Ali Sina. Abu Ali Sina ambaye kutokana na kuibuka kwake katika pande zote za wanahekima na wanafalsafa, katika ulimwengu wa mashariki ni mashuhuri kwa jina la Sheikhur-Rais. Alikuwa ni mwanafalsafa mwenye mtazamo uliokamilika, mwanasayansi mkubwa, mhakiki asiyechoka, mwenye kuchambua nadharia kwa kina, tabibu aliyebobea, mshairi na malenga stadi, mhariri na mtaalamu wa muziki. Mtaalamu huyu wa Kiislamu ameandika vitabu vingi sana, ambavyo kila kimoja kati ya vitabu hivyo, kilikuwa cha aina yake na cha kipee katika fani ya elimu ya

Page 38: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -38- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

zama hizo. Mtaalamu huyo kutokana na kipaji cha hali ya juu alichokuwa nacho visa na ngano mbalimbali ziliandikwa kuhusiana na sifa za juu za kibinadamu alizokuwanazo. Baadhi ya hadithi na visa hivyo hadi leo vingali vinazungumzwa na kuhadithiwa na watu. Abu Ali Sina alizaliwa katika mwaka 370 Hijria, mwafaka na mwaka 980 Miladia. Alizaliwa katika ukoo mmoja mtukufu huko katika mji wa Balakh, ambao hivi sasa kijiografia unapatikana nchini Afghanistan. Katika kipindi cha utoto na kuinukia kwake, alijishughulisha na kujifunza Qur'ani Tukufu na fasihi. Akiwa na umri wa miaka 10, Abu Ali Sina alikuwa tayari amehifadhi Qur'ani yote, na maudhui nyingi za kifasihi, jambo ambalo liliwastaajabisha wengi. Baba yake Abu Ali Sina yaani mzee Abdalla bin Sina ambaye alilipa umuhimu mkubwa suala la mafunzo na malezi ya mwanawe, alifanya juhudi kubwa kwa ajili ya kumpatia mwanawe suhula zote za kielimu. Mwanzoni alimpeleka Ibn Sina kwa mtu ambaye, alizifahamu vyema hisabati za Kihindi ili ajifunze elimu hiyo ya hisabati. Wakati huo, mtaalamu aliyejulikana kwa jina la Abuu- Abdallah Natali, alielekea katika mji wa Bukhara na baba yake Ibn Sina akamkaribisha na kumuweka nyumbani kwake na hapo Ibn Sina akaanza kujifunza elimu ya falsafa kutoka kwa mtaalamu huyo. Abu Ali Sina alijifunza kutoka kwa Abu Abdallah Natali taaluma nyepesi ya mantiki, lakini hakufunzwa taaluma nzito za elimu na mwanazuoni huyo. Baada ya kujifunza elimu ya hisabati na kuzielewa elimu za mantiki na falsafa, Ibn Sina akaanza kujishughulisha na elimu za Maumbile na Tiba na kwa haraka na kwa kasi ya ajabu sana akaweza kujifunza elimu hizo, kiasi kwamba, alipofikisha umri wa miaka 16, tayari alikuwa amekwishapata umaarufu katika elimu ya Tiba. Itibari na umaarufu wake katika elimu ya Tiba, ukampelekea siku moja kuitwa mbele ya Mkuu wa Bukhara Nuh bin Mansour Samani, ili akamtibu. Kufanikiwa kwake kumtibu Mkuu wa Bukhara, kukapelekea Ibn Sina kupewa idhini ya kutumia maktaba ya Nuh bin Mansour Samani, maarufu kwa jina la Hazina ya Wataalamu. Katika maktaba hiyo kubwa na ya kipekee, Abu Ali Sina aliweza kuvipata vitabu vingi vilivyozungumzia elimu mbalimbali ambavyo ilikuwa ni adimu na nadra mno kuvipata katika maktaba nyingine. Vitabu ambavyo hadi wakati huo alikuwa bado hajavisikia kutoka kwa mtu yeyote yule hata majina yake. Ibn Sina akaanza kuvisoma vitabu hivyo na kuweza kustafidi navyo vizuri na kupata maalumati mengi sana. Baada ya kupita siku na masiku, siku moja Abu Ali Sina alimwambia mwanafunzi wake Abu Abdi Juzjazi kuwa, kwa vile nilipotimia umri wa miaka 18 au 19, niliweza kujifunza kikamilifu elimu zote za kutumia maarifa, kama vile mantiki, Elimu za Maumbile, Hisabati,

Page 39: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -39- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Jiometri, Nujumu, Muziki, Tiba na elimu nyingi nyinginezo na kutokea hapo kukawa hakuna chochote katika elimu ambacho sikukijua, sikuweza tena kumkubali mtu yeyote awe mwalimu wangu. Kipaji cha kuhifadhi cha Ibn Sina na upeo mpana wa maarifa na elimu yake, vilikuwa ni vya kushangaza mno. Inasemekana kuwa, baada ya moto kuiteketeza Maktaba ya Bukhara, watu wakawa wanasema, hazina ya wataalamu haikuteketea, bali vitabu vyake vyote vimehamishiwa katika kifua cha Ibn Sina, yaani Sheikhr-Rais. Hivyo Ibn Sina akiwa na umri wa miaka 18, kwa kuwa kwake na ufahamu mkubwa na wa ajabu na kipaji cha juu, aliweza kujifunza elimu mbalimbali na wakati alipofikisha umri wa miaka 21 aliandika kitabu chake cha kwanza kuhusiana na elimu ya falsafa. Baba yake alifariki dunia, wakati Abu Ali Sina akiwa na umri wa miaka 22. Hivyo ili kuendesha maisha yake, Ibn Sina akalazimika kufanya kazi. Katika kipindi hicho hali ya kisiasa ikaanza kuwa mbaya katika mji wa Bukhara na hivyo kumfanya Ibn Sina aondoke mjini humo na kuelekea katika mji wa Gurganj, uliokuwa mji mkuu wa Khorazmi-Shahian. Akiwa huko alijumuika pamoja na matabibu na wataalamu kadhaa wa kadhaa wa utawala. Haukupita muda, Sultan Mahmoud-Ghaznawi akaivamia Khorazmi na kuiungusha katika utawala silsila ya Kifalme ya Khorazmi. Sultan Ghaznawi alimuamuru waziri ampelekee watalaamu wote waliokuweko huko Khorazmi akiwemo Abu Ali Sina. Hata hivyo, Ibn Sina kwa kumuhofia Sultani Ghaznawi aliyekuwa akipinga mitazamo yake, aliamua kutoroka na baada ya safari ndefu akawasili mjini Hamedani, Iran. Hadi mwaka 411 Hijria alilazimika Ibn Sina kufanya kazi katika serikali ili kuweza kuendesha maisha yake, hata hivyo hakughafilika na masomo ya kielimu na ilikuwa ni katika kipindi hicho, ndipo alipoandika baadhi ya vitabu vyake kama vile Shifaa. Ibn Sina baada ya kipindi hicho kupita, alielekea katika mji mwingine wa Iran wa Isfahan na akiwa katika anga tulivu ya mji huo, ambao ulikuwa moja ya vituo muhimu vya Elimu ya Utamaduni wakati huo, akaanza kujishughulisha na kutalii; na katika kipindi cha miaka 15 alichoishi katika mji wa Isfahani, aliweza kuandika baadhi ya vitabu vyake muhimu. Kipindi cha utulivu na amani kilichokuwa kikitawala mjini Isfahan kilikuja kuhitimishwa na uvamizi wa Masoud Ghaznawi na kupelekea vitabu vingi vya Ibn Sina kupotea moja kwa moja. Kufuatia ghasia na hali ya machafuko mjini humo, Ibn Sina akadhoofika mno kiafya na hivyo akarejea tena mjini Hamedan

Page 40: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -40- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

na katika mwaka 428 Hijria, yaani akiwa na umri wa miaka 58 akaiaga dunia baada ya kupatwa na maradhi na kuzikwa katika mji huo huo wa Hamedan, ambao kijiografia leo hii unaopatikana magharibi mwa Iran. Umri mfupi wa Ibn Sina, kwa mukhtasari unaweza kuelezwa kama ni umri wa uvumbuzi na uhakiki. Ibn Sina daima na katika hali yoyote ile, hakuwa akikaa burebure, bali alikuwa akijishughulisha na kazi. Kwa mujibu wa takwimu za wahakiki, Ibn Sina aliandika vitabu karibu 456, kwa kutumia lugha za Kifarsi na Kiarabu ambapo baadhi ya vitabu hivyo ameviandika yeye binafsi na vyengine vimenasibishwa naye. Hivi sasa katika orodha ya maktaba za dunia, kuna vitabu 160 vilivyoandikwa na Abu Ali Sina. Hata kama Ibn Sina ameandika vitabu kadhaa wa kadhaa katika fani mbalimbali za elimu, lakini barani Ulaya katika kipindi cha karne nyingi, mtaalamu huyo alikuwa maarufu zaidi katika elimu ya tiba.

Sehemu alipozikwa Ibnu Sina – Hamedan magharibi mwa Iran.

Page 41: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -41- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Kitabu chake kikubwa na maarufu cha sheria ni mjumuiko wa kustaajabisha wa maalumati yote ya tiba ambao ulizikusanya pamoja natija za utafiti na uvumbuzi zilizo bora za matibabu wa Kigiriki, Kihindi, Kiirani na Kiarabu. Njia za uvumbuzi alizozitumia katika katika kitabu chake hicho cha sheria, katika kuyatafutia majina masuala magumu na uwezo wake mkubwa wa kiakili katika ubunifu wa mambo yote hayo yamekifanya kitabu hicho cha sheria kuwa kitabu bora zaidi na kisicho na mfano wala mithili. Kitabu hicho kina sifa maalumu na kilitumiwa na matabibu wengi kama ni marejeo kwa kipindi cha karne kadhaa. Kitabu kingine mashuhuri mno cha Abu Ali Sina ni Kitabu cha Uponyo na Kanuni ya Tiba, ambavyo vilikuwa ni vitabu rejea vya udaktari katika Vyuo Vikuu katika nchi za Waislamu na Bara Ulaya mpaka katika karne ya 18.

Ibn Sina alikuza mfumo wa utabibu uliochanganya na uzoefu wake na ule wa utabibu wa Kiislamu, mfumo wa utabibu wa akina Galen, na wengineo na utabibu wa kale wa Kifursi, Kiarabu na wa Kihindi. Ibn Sina anachukuliwa kama baba wa udaktari wa sasa, hasa katika kuanzisha mfumo wa majaribio na kuchukua hima maalumu katika masomo ya tiba na kuvumbua kwake maumbile ya kuambukizana magonjwa. George Sarton, baba wa historia ya sayansi ameandika katika Utangulizi wa Historia ya Sayansi: “Mmoja wa wasimamizi maarufu wa kilimwengu kati ya Waislamu na mtu mashuhuri katika masomo ya Kiislamu ni Ibn

Sina, aliyejulikana Magharibi kama Avicenna. Kwa muda wa miaka elfu moja amebaki katika umaarufu wa kiasili kama mwanafalsafa mkubwa zaidi na mwanachuoni wa utabibu katika historia. Kazi yake muhimu zaidi katika udaktari ni Qanun na waraka kuhusu dawa za magonjwa ya moyo. Kitabu chake ‘Qanun Fiyt Twib’ (The Canon of Medicine) ni kikubwa sana katika masuala ya utabibu.

Page 42: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -42- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

HEKO KUMI LA REHEMA

1. Bismillahi ‘Aliyyun, Ya Ilahi Ya Rahimu Bismillahi Qawiyyun, nguvu ni Zako Qayyumu Bismillahi Ghafurun, toba ni Kwako Hakimu Heko kumi la rehema, Allah katujaalia. 2. Rehema Zako Rabana, zeleya kila mahala Rehema za Subhana, zenda kwa hata kabwela Rehema za Maulana, kwa ‘asi na mcha Mola Heko kumi la rehema, Allah katujaalia. 3. Awali ya Ramadhani, kumi limejaa heba Kwa kusoma Qur’ani, na kukithirisha toba Wokovu kwa waumini, Rabbi utupe haiba Heko kumi la rehema, Allah katujaalia. 4. Tufunge tukihimidi, rehema zako Rabbana Tufunge tukikunadi, turehemu Ewe Bwana Tufunge tukiburudi, Amina Rabbi Amina Heko kumi la rehema, Allah katujaalia. 5. Tukitaja jina Lako, tuburudike nafusi Tukiona waja Wako, tukukumbuke Mkwasi Tukiwa na Peke Yako, tujiepushe kuasi Heko kumi la rehema, Allah katujaalia. 6. Tukwogope hadharani, na zaidi faraghani Kubali wetu ugeni, Ilahi Ya Rahmani Bila ya Kwako Manani, twende kwa mwengine nani? Heko kumi la rehema, Allah katujaalia. 7. Takabali zetu dua, saumu na Swala pia Waja tumejaa doa, pumzi zinafifia Hatutendi kwa kujua, Ya Rabbi twakulilia Heko kumi la rehema, Allah katujaalia.

Na Ahmed Rashid.

NI KUMI LA GHUFURANI

Allah jina takatifu, naanza ya Rahmani Kwa jina Lako Latwifu, baraka za

Ramadhani Samehe hai na wafu, sote tuwe neemani

Rabi turuzuku toba, ni kumi la ghufurani. ***

Turudi Kwake Raufu, Yaayyuha waumini Tusijifanye vipofu, kuasi wetu Manani Tujipange safusafu, kwa toba misikitini

Rabbi turuzuku toba, ni kumi la ghufurani. ***

Allah Rabbi utuafu, tumezama madhambini Mja kiumbe dhaifu, hajali jema ni nini Hutesa hata siafu, amshinda hayawani

Rabbi turuzuku toba, ni kumi la ghufurani. ***

Nyoyo zetu zi jafafu, ni kavu hatubaini Rutubaye ni hafifu, tarutubishwa na nini Kama si zako Arifu, kwa wajao samahani Rabi turuzuku toba, ni kumi la ghufurani.

*** Tutende uadilifu, amri ya yetu dini

Tusione takilifu, kurejea kwa Rabbani Nyoyo ziingie khofu, tujue tu masikini

Rabi turuzuku toba, ni kumi la ghufurani. ***

Mola wetu ni Latifu, twaasi tu madhambini Atusamehe Raufu, huruma nyingi pomoni

Kumi hili takatifu, fursa tusitupeni Rabi turuzuku toba, ni kumi la ghufurani.

*** Leo hai kesho mfu, zitajapita awani

Bila ya Mola kukhofu, hakuna cha nusurani Toba kitu maalufu, tutubu dhambi jamani Rabi turuzuku toba, ni kumi la ghufurani.

Na Ahmed Rashid.

Page 43: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -43- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

RABI TWEPUSHE NA NARI

1. Hamdu za Maulana, Muumba janna na nari Wokovu Ya Rabbana, maasi yamekithiri Viumbe twatafunana, kimetuzidi kiburi

Yatuaga Ramadhani, Rabi twepushe na Nari.

2. Kumi la mwisho mwungwana, jiweke mbali na shari Ya shetani mwenye lana, asi wa Allah Qahari

Atujia kwa mapana, kuzishawishi suduri Yatuaga Ramadhani, Rabi twepushe na nari.

3. Tutiye moyo dhamiri, tusijifanye hodari Jahanamu kali nari, huwakumba majabari Huchoma na kuadhiri, wakosefu makafiri

Yatuaga Ramadhani, Rabi twepushe na nari.

4. Saumu ituathiri,tutubu dhambi tukiri Wanojitia ghururi, Haawiya yawasubiri

Watachomwa matajiri, wa inda wenye viburi Yatuaga Ramadhani, Rabi twepushe na nari.

5. Nyoyo zikose sururi, kuasi si ufakhari Pokea langu shauri, sijitie ujabari

Mja ngia tahayuri, hakuna jambo la siri Yatuaga Ramadhani, Rabi twepushe na nari.

6. Mwenzangu ngia nadhari, utende lilo la kheri Tambua Mola Qahari, yuko nawe huna siri

Alijua la dhahiri, na la batini vizuri Yatuaga Ramadhani, Rabi twepushe na nari.

7. Jahanamu yavinjari, yawangoja majeuri Na wale wasofikiri, wapenda umashuhuri Wala hawangii ari, kurejea kwa Ghafuri

Yatuaga Ramadhani, Rabi twepushe na nari.

8. Wakiasi hawajali, wapenda sifa titiri Nyoyo kama majabali, kamwe hazingii nuri Hawasimami kusali, wamwasi Allah dhahiri Yatuaga Ramadhani, Rabi twepushe na nari.

9. Nakhatimisha qauli, kiyama siku hatari Funga ziwe maqubuli, hiyo siku ya hashiri Twakuomba ya Jalali, Ya Alimu ya Jabbari

Yatuaga Ramadhani, Rabi twepushe na nari.

Na Ahmed Rashid

Page 44: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -44- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Na Mussa Said Abdul Rahman

Kitabu cha ‘Kanuni za Ndoa na Maadili ya Familia’ kina jumla ya kurasa 229, ambapo mwandishi wa kitabu hiki ni mwanachuoni mkubwa nchini Iran, ameelezea kwa undani mambo mengi ambayo yanapaswa kuzingatiwa na wanandoa. Mwandishi amefanya juhudi kubwa za kufanya utafiti wa kina wa somo la mfumo wa maadili ya familia na uhusiano wa mume na mke, kwa mtazamo wa dini ya Kiislamu, na kuchanganua haki za mke na mume katika ndoa. Kitabu hiki kina mafundisho mazuri kwa jamii yetu ambayo imemomonyoka mno kimaadili kwa kuiga tamaduni za

kimagharibi ambazo zimewapotosha wengi, hasa tabaka la vijana. Pamoja na kuandikwa kwa mtazamo wa Kiislamu, lakini ni kitabu ambacho kitawafaa pia hata wasio Waislamu, kwani kinazungumzia maisha ya ndoa kwa ujumla. Ni

Jina la kitabu: ‘ Kanuni za Ndoa na Maadili ya Familia.’

“Principles Marriage & Family Ethics”. Kimeandikwa na: Ayatullah Ibrahim Amini

Kimetarjumiwa na: Bwana Salman Shou Kimehaririwa na Dr. M.S. Kanju

Kimetolewa na kuchapishwa na: Al-Itrah Foundation/ Tanzania.

Page 45: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -45- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

jambo la kusikitisha kuona kwamba wazazi huwaozesha watoto wao bila ya kuwafundisha kanuni na misingi ya ndoa na maadili ya familia. Matokeo yake wamekuwa wakitumbukia kwenye mizozo na migogoro isiyokwisha katika maisha yao ya ndoa, na hatimaye ni kutolewa talaka za kiholela. Mwandishi wa kitabu, amejaribu kukigawa kitabu chake katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza inahusu wajibu wa wanawake kwa waume zao na sehemu ya pili inazungumzia wajibu wa wanaume kwa wake zao. Bila shaka mwanamme ameumbwa kwa ajili ya mwanamke na hali kadhalika mwanamke ameumbwa kwa ajili ya mwanaume. Kila mmojawapo anao mvuto kwa mwenzake kama ilivyokuwa sumaku. Ndoa na kuanzisha maisha ya pamoja ni hamu ya kawaida ya mwanadamu na ya kukubaliana silika zao. Ndoa inahesabiwa kuwa mojawapo ya neema kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mlezi. Mkataba mtakatifu wa ndoa ni kamba ya Mwenyezi Mungu inayoziunganisha nyoyo, huzibembeleza zinapokuwa zimefadhaika na kuzielekeza njozi zisizo na mantiki kwenye lengo lililo bora. Mwenyezi Mungu Mlezi ameitaja neema hii kwenye Qur’ani Tukufu pale aliposema:” Na katika Ishara zake ni kuwa Amekuumbieni wenza kutokana na nafsi zetu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri” ( Qur’an 30:21). Mtume Mtukufu Muhammad SAW anasema: “ Mwanaume ambaye hakuoa hata kama ni tajiri kwa hakika ni masikini na mhitaji; na hivyo hivyo kwa mwanamke”. Aidha ameongeza kwa kusema kuwa: “ Hakuna taasisi katika Uislamu iliyobuniwa na Mwenyezi Mungu ambayo anaipendelea na kuipenda zaidi kuliko ndoa.” Pamoja na kwamba Mwenyezi Mungu Mwenye huruma amewajaalia wanadamu neema yenye thamani kubwa kama hii, wao hawaifurahii, na wakati mwengine kwa sababu ya ujinga na ubinafsi, huugeuza muungano huu wa upendo na uliobarikiwa kuwa jela yenye giza au hata Jahannam iwakayo moto! Kama wanandoa wanafahamu wajibu wao na kutenda matendo yao kufuatana na maelekezo yake, bila shaka nyumba hiyo itakuwa mahali pa urafiki na kufanana na Pepo. Mwanamme anapotaka kuoa, kamwe asifikirie kwamba ndoa ni kama kununua mali au kukodi mfanyakazi wa kike, bali akubali kwamba ndoa ni mkataba wa urafiki, uaminifu, wema, ushirikiano na muungano katika maisha ya pamoja ya familia. Mwanamke pia lazima afahamu falsafa ya maisha ya mume wake na matakwa yake. Asifikiri kwamba ndoa ni kama kumwajiri mtumishi kwa lengo la kutimiza mahitaji bila ya mapatano na masharti. Wazazi nao wanakuwa na nafasi kubwa katika kufanikisha maisha ya wanandoa wao. Kwa hakika kitabu hiki kimeandikwa kwa kutegemea misingi ya Qur’an Tukufu, hadith za Mtukufu Mtume SAW na Maimamu Watoharifu AS, takwimu za kawaida na uzoefu wa mwandishi.

Page 46: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -46- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Mwezi wa Toba na Kuitakasa Nafsi

Na Amir Ibrahim Rutajengwa Saumu ni ibada yenye taathiri kubwa mno za kiroho, kimalezi, kijamii na kiafya kwa mwanadamu. Uislamu umefaradhisha ibada hiyo ya kuacha kula, kunywa na kujiepusha na mambo mengine kadhaa ya halali kwa Waislamu waliobaleghe katika nyakati za mchana za mwezi mzima wa Ramadhani kwa malengo na falsafa maalumu. Moja ya faida kubwa za ibada hiyo ni somo la usawa na udugu kati ya watu wote wa jamii. Kwani kwa kutekeleza ibada hiyo matajiri na watu wanaojiweza kimaada huhisi hali ya watu wanaosumbuliwa na njaa na umaskini katika jamii zao, suala ambalo bila shaka huimarisha hisia za huruma, mshikamano na kutenda wema katika nafsi zao. Imam Jaafar Sadiq AS ambaye ni mmoja wa Maimamu watukufu katika kizazi cha Mtume wetu Muhammad SAW ameashiria moja ya falsafa za funga kwa kusema: “Saumu imewajibishwa katika Uislamu kwa ajili ya kuleta usawa kati ya maskini na matajiri.” Ibada ya saumu huimarisha irada na azma na kumpa mwanaadamu uwezo wa kudhibiti matamanio yake ya kinafsi. Tunaweza kusema kuwa lengo kuu la ibada ya funga na saumu katika Uislamu ni kumpa mwanaadamu uwezo wa kushika hatamu za nafsi yake na kudhibiti matakwa na matamanio ya nafsi. Kwani wakati mwanaadamu analazimika kushibisha matakwa yake kwa njia sahihi anawajibika pia kudhibiti matamanio yake ya nafsi na kuyaepusha na upotofu. Hivyo basi, kadiri mwanadamu anavyoweza kudhibiti matakwa na matamanio yake ya kinafsi ndivyo anavyopata uwezo mkubwa zaidi na kinyume chake, anaposalimu amri mbele ya matamanio yake ya kinafsi huwa dhaifu na dhalili zaidi. Wanaadamu ambao daima huwa na uwezo wa kudhamini mahitaji yao ya kimaisha na hawajawahi kuonja mashaka ya njaa, kiu na matatizo mengineyo, huwa mithili ya mti uliooteshwa katika maeneo ya maji, hewa safi na ardhi nzuri yenye rutuba na mbolea kandokando ya mto. Mti wa aina hii huwa na maisha mafupi na uwezo mdogo wa kustahamili mashaka. Kwani pale unapokosa maji

Page 47: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -47- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

kwa muda mfupi tu hunyauka na huenda ukakauka kabisa. Kinyume chake, mti unaoota majangwani na katikati ya miamba na kukumbwa na tufani, joto na baridi kali huwa na uwezo mkubwa wa kustahamili mashaka na matatizo mbalimbali. Vivyo hivyo ibada ya funga kwa mwanadamu ambayo huzidisha nguvu na uwezo wake wa kukabiliana na hali tofauti na kuupa moyo nuru, usafi na utakasifu. Saumu na siha Ibada ya saumu pia ina faida nyingi za kiafya na matabibu wengi wamezungumzia na kubainisha taathira za ibada hiyo katika afya ya mfungaji na kuzuia kwake aina mbalimbali za maradhi. Mtume wetu Mtukufu anasema katika sentensi fupi lakini yenye maana kubwa kwamba: “Fungeni ili mupate siha.” Mtawala mashuhuri wa kizazi cha Bani Abbas Haroun Rashid alikuwa na tabibu Mkristo aliyesifika kwa kuwa hodari katika fani hiyo. Siku moja tabibu huyo alimwambia msomi mmoja Muislamu kwamba: Mimi sijapata lolote linalohusiana na tiba katika kitabu chenu kitukufu, akimaanisha Qur’ani. Tabibu Mkristo aliendelea kumwambia msomi wa Kiislamu kwamba, hali hii inakinzana na madai yenu pale mnaposisitiza kwamba elimu zenye faida ni za aina mbili: "Elimu ya dini na taalumu ya tiba." Mwanazuoni wa Kiislamu alijibu kwa kusema: "Mwenyezi Mungu amezungumzia sheria zote za tiba katika nusu ya aya ya kitabu chake kwa kusema: Kuleni na kunyweni na msifanye israfu, kwa maana kwamba msipite kipimo" Aliendelea kusema kwamba: Mtume wetu Mtukufu pia amezungumzia elimu ya tiba katika hadithi fupi kwa kusema: Utumbo ni nyumba ya maradhi yote, na kufunga ndiyo kinara wa dawa zote."

Page 48: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -48- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Baada ya kusikia maneno hayo, tabibu Mkristo alimwambia msomi Muislamu kwamba: Hakika Qur’ani na Mtume wenu hakumbakishia Galinos chochote cha kusema katika elimu ya tiba." Mwisho wa kunukuu. Galinos huyo aliyetajwa na tabibu Mkristo alikuwa mashuhuri sana katika masuala ya tiba kwenye Ugiriki ya zamani. Saumu huchoma kalori za ziada ambazo hazitumiwi na mwili na kuupa mfumo wa mmeng’enyo wa mwanadamu fursa ya kupumua na kupumzika. Mfumo huo ambao unafanya kazi katika kipindi chote cha mwaka mzima unahitajia fursa na kupumzika. Mapumziko hayo ya muda ya utumbo na mfumo wa mmeng’enyo huzidisha uSwalama na uzima wa mwili.

Hivi ni miongoni mwa vitu ambavyo havikosekani katika kitanga cha futari nchini Iran. Funga halisi Ibada hiyo ya funga vilevile huwa na taathira kubwa mno kwa nafsi pale inapotekelezwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na bila ya kuingiliwa na riyaa. Imamu Sajjad Zainul Abidin anasema kuhusu faida za saumu kwamba: “Na haki ya saumu juu yako ni kutambua kwamba funga ni pazia la Mwenyezi Mungu aliloliweka katika ulimi, masikio, macho, viungo vya uzazi na tumbo lako

Page 49: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -49- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

kukulinda na Moto wa Jahanam; na imepokewa katika hadithi (ya Mtukufu Mtume SAW kuwa "Funga ni ngao ya kujikinga na moto wa Jahannam.” Hivyo basi, kama utavituliza viungo vya mwili wako na kuviweka katika pazia hili, unaweza kuwa na matumaini kwamba vimelindwa, na ukiviacha huru na kuendeleza harakati zisizokuwa na faida na kutupilia mbali pazia hilo kwa kutazama mambo ya haramu na kuvuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, hutakuwa na uhakika kwamba havitapasua pazia hilo.” Hapa Imamu Sajjad AS anaeleza haki za funga na umuhimu wake na kuashiria funga na saumu halisi. Imamu anasisitiza katika hadithi hiyo kwamba funga si kuacha kula na kunywa pekee bali hiyo ni funga ya kidhahiri tu na funga muhimu zaidi ni ile ya roho na batini ya nafsi. Imam Sajjad anasisitiza kwamba mwanadamu hapaswi kutosheka kwa kuacha kula na kunywa bali macho, masikio, roho, ulimi, miguu na viungo vyake vyote vinapaswa pia kufunga. Kwa maana kwamba mwanadamu anapaswa kuzuia ulimi kusema maneno machafu na yasiyosahihi kama kusengenya, urongo, kuwatuhumu wenzake na kadhalika. Vilevile anapaswa kuzuia masikio yake kusikiliza upuuzi na haramu. Kwa ujumla viungo vyake vyote vinapaswa kujiepusha na mambo machafu na ya upuuzi. Kwani funga iliyofanywa na Mwenyezi Mungu SW kuwa ngao ya moto wa Jahannam ni ile inayofungwa kwa ikhlasi, nia safi na kuwa saumu halisi na ya kweli. Ni wazi kuwa masuala kama vile kusema uongo, kusengenya, kutazama haramu na kadhalika huifanya saumu ipoteze maana yake halisi. Kujiepusha na mambo hayo pia huisafisha roho na kumkurubisha mwanadamu kwa Mola wake Muumba. Hii kwa hakika ndio takwa ambayo ndiyo matunda muhimu zaidi ya ibada ya funga. Mwenyezi Mungu SW anasema katika aya ya 183 ya Suratul Baqarah kwamba:

***

یا أیھا الذین آمنوا كتب علیكم الصیام كما كتب على الذین من قبلكم لعلكم تتقون

Enyi mlioamini! Mmefaradhishiwa saumu kama walivyofaradhishiwa

waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu.

****

Tunamuomba Mola SWT atujaalie kutekeleza ibada hiyo kama inavyostahiki na kupata neema na baraka za mwezi mtukufu, Aamin Yaa Rabbal Alamiin.

Page 50: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -50- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

(Sehemu ya Tatu)

Katika makala iliyopita tulisema kuwa ibada ni wenzo unaoleta mlingano wa kiroho na kinafsi na kumpa mwanadamu utulivu wa roho. Kumtegemea Mwenyezi Mungu Hakimu na Muweza humpa mwanadamu uwezo wa kusimama kidete na kuwa ngangari katika misukosuko na matatizo ya kimaisha. Hata hivyo baadhi ya watu hawajui ni kwa nini wanapaswa kumuabudu Mwenyezi Mungu Mmoja, kumuomba na kuwa na uhusiamo wa karibu na Mola wao Mlezi?

Page 51: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -51- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Kundi jingine la watu linaamini kwamba mwanadamu ambaye ndiye kiumbe kamili, anaweza kushinda na kutatua matatizo yake yote kwa kutegemea kazi na akili yake mwenyewe. Kundi hili linaona kuwa maendeleo ya sayansi na teknolojia yanatosha kumfikisha mwanadamu katika saada na ufanisi wa milele. Hapana shaka kuwa mwanadamu ni kiumbe tata na cha kustaajabisha ambacho kinakabiliana na njia nyingi tofauti. Kiumbe huyo anaweza kufuata njia ya ukamilifu na saada ya milele au kuchagua njia ya kuporomoka na kuangamia. Moja ya masuala hatari mno kwa kiumbe huyo ni mghafala na kusahau nafsi yake. Kwa maneno mengine ni kuwa, wakati mwanadamu anapojitambua kuwa mwenye nguvu na muweza katika ulimwengu huu, hukumbwa na hali ya mghafala na kuchupa mipaka na hisia hiyo humuelekeza katika maangamizi. Qur'ani Tukufu inasema:

أن رآه استغنى* كال إن اإلنسان لیطغى "Si hivyo, hakika mwanadamu huwa jeuri. Akijiona ametajirika." (al Alaq: 6-7). Kinyume chake pale mwanadamu anapojitambua kuwa kiumbe tegemezi chenye mfungamano na nguvu ya azali ya Mwenyezi Mungu, huanza harakati za kuelekea kwake na kujiepusha na uasi na ghururi. Katika upande mwingine hapana shaka kuwa elimu na teknolojia ni nyenzo zinazomuwezesha na kumpa nguvu mwanadamu. Hata hivyo elimu na sayansi peke yake haviwezi kutatua matatizo ya mwanadamu asiyekuwa na uhusiano na Mola wake Mlezi na asiyefungamana na mafundisho ya dini na maadili mema ya kibinadamu. Ushahidi hai wa ukweli huo ni watawala na wamiliki wa mali na madaraka wa leo wanaotumia matunda ya elimu na sayansi katika kukidhi matamanio yao na kuwakandamiza watu wengine. Mawasiliano ya daima ya mwanadamu na Mola Muumba, kumuomba na kumuabudu yeye humtayarishia kiumbe huyo uwanja mzuri wa ustawi na maendeleo katika nyanja mbalimbali za kiroho na kimaada. Hamu hiyo ya ibada na kutaka kunong'ona na Mola Muumba hutokana na kiu na haja ya mwanadamu kwa nguvu mutlaki na kamili. Ibada na maombi kama hayo huwa na taathira kubwa katika maisha ya mwanadamu. Vilevile imethibitika kwamba watu wanaorukuu na kumsujudia Mwenyezi Mungu peke

Page 52: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -52- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

yake huwa na ezi, utukufu na heshima mbele ya wanadamu wenzao. Tabibu mashuhuri wa Kifaransa Dakta Alexis Carrel ameandika kuwa: "Baada ya tajiriba yenye machungu na mashaka tumejifunza kwamba ukosefu wa hisi ya maadili mema na masuala ya kiroho katika sehemu kubwa ya watu wenye ushawishi katika taifa fulani hutayarisha uwanja wa kutoweka taifa hilo. Hakika jamii iliyopoteza haja ya kuomba na kuabudu, haitasalimika na ufisadi na hatimaye kuangamia." Mwanafikra huyo wa Ufaransa anasema katika sehemu nyingine kwamba: "Saada na ufanisi wa mwanadamu hudhaminiwa kwa kukuza fikra sambamba na roho ya kiumbe huyo. Ustaarabu wa Ulaya umekumbwa na kasoro ya kwamba umestawisha ubongo kupita kiasi na kuacha roho ikiwa tupu. Kwa sababu hiyo, imani na hisi ya kupenda maadili mema imedhoofika na kutoweka." Mwisho wa kunukuu.

Swala, Dhihirisho la Mawasiliano ya Mja na Mola wake Mawasiliano bora zaidi ya mja na Mwenyezi Mungu SWT hudhihirika katika Swala. Swala ni mfungamano uliojaa ikhlasi wa mwanadamu na Mola Mlezi na

Page 53: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -53- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

nembo kubwa ya uchaji na utiifu na imani ya mja haikamiliki bila ya ibada na mawasiliano hayo. Qur'ani tukufu haijatoa umuhimu na mazingatio makubwa zaidi kwa ibada nyingine yoyote kama ilivyo Swala na imehimiza mno juu ya umuhimu wa kutekelezwa ibada hiyo katika nyakati zote hata wakati wa vita, kama zinavyosema aya za 102 na 103 za suratu Nisaa. Qurani Tukufu imetumia neno "Swalat" kumaanisha ibada ya Swala. Neno hilo katika lugha ya Kiarabu lina maana ya kuzingatia, kuwa makini na kuomba. Neno hilo na minyambuliko yake limetajwa karibu mara 114 katika Qur'ani Tukufu. Katika aya nyingi za Qur'ani zinazozungumzia ibada hiyo, Mwenyezi Mungu SW anamuhutubu Mtume wake Mtukufu Muhammad SAW akimuamuru kusimama kwa ajili ya Swala. Katika aya ya 14 ya suratu Twaha Mwenyezi Mungu anasema:

إنني أنا اللھ ال إلھ إال أنا فاعبدني وأقم الصالة لذكري "Kwa yakini Mimi ndiye Mwenyezi Mungu, hakuna aabudiwaye kwa haki ila Mimi, basi niabudu na usimamishe Swala kwa kunitaja." Je, Mwenyezi Mungu Anahitaji Swala na Ibada Zetu? Mwenyezi Mungu ni muweza na mkamilifu mutlaki na hana haja na Swala na maombi ya waja wake. Qur'ani Tukufu inasisitiza ukweli huo na kueleza kwamba faida za ibada na maombi hayo ya mja yanarejea kwa mja mwenyewe. Ibada na maombi humwelekeza mwanadamu kwenye njia ya kufikia ukamilifu na saada ya milele. Iwapo tutatafakari vyema tutaona kwamba mara nyingi shughuli na purukushani za kila siku na matatizo ya kimaisha humghafilisha mwanadamu na kumsahaulisha chanzo cha ulimwengu huu. Kumsahau Mwenyezi Mungu huwa na maana ya kujitenga na asili na kupoteza utambulisho wa mwanadamu. Kwa ujumla roho ya mwanadamu inahitajia usafi na kupigwa msasa, jambo ambalo haliwezekani ila kwa njia ya kuelekea daima kwa Mwenyezi Mungu Mmoja, kukumbuka uwezo na adhama yake isiyokuwa na mwisho na kusalimu amri mbele ya maamrisho na makatazo yake. Mwanadamu anayesimama kwa ajili ya Swala mbele ya Mola Muweza na mudiri wa dunia nzima na kutaja sifa na majina yake, viungo vyake hujipamba kwa sifa hizo. Wakati huo Mola Mlezi humpa msaada na auni mja wake na kumuongoza katika njia iliyonyooka.

Page 54: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -54- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Na Hussein Hassan Awali kabisa, ni vyema kujua hapa nini maana ya neno 'Ikhlas' kilugha na kisheria. Mabingwa wa lugha wanasema, Ikhlas ni nia njema, ukweli, unyoofu na uaminifu. Aidha, Ikhlas ni Sura ya 112 katika Kitabu Kitukufu cha Qur'ani. Amma kifikihi neno hilo linamaanisha kufanya amali 'lillahi', yaani kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah SWT Peke Yake. Kwa tathmini ya haraka haraka, Ikhlas ni kinyume cha 'Riyaa' au kufanya amali kwa kujinesha kwa watu au kutaka sifa, cheo, nafasi au hadhi machoni mwa wanaadamu. Katika ulimwengu wa hivi sasa, ni jambo zito mno kumtambua mtu aliye na asiye na ikhlasi ingawa sisi wanaadamu hatustahili kumhukumu yeyote yule awe mja mwema au mwovu, letu ni kumnasihi akiwa muovu na kumuombea mema akiwa mwema.

Page 55: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -55- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Pengine katika kuelezea umuhimu wa ikhlasi, itakuwa ni vyema nikisimulieni kisa kifupi ambacho ni maarufu kwa wengi wetu. Ni matumaini yangu kisa hiki kitakuwa ni ibra kwetu sisi ili tujitenge kikamilifu na riyaa, jambo ambalo hubatilisha ikhlasi ya amali zetu ni sawa tu iwe tunafanya kwa kutua au kutojua. Naam, katika utawala wa nyuma wa Umar bin Abdul-Aziz, siku miongoni mwa siku, alitoka jamaa kunyoosha miguu akiwa katika hali ya kujipumbaza. Mara huyo! Akajipata katika bustani yenye kupendeza. Katika pita pita zake, akaona mtufaha wenye matufaha yaliyo mbivu na yenye kuvutia. Hakuchelewa jamaa yule, na pengine kwa njaa yake, akatunda tufaha moja na kuanza kulibugia. Mara akagutuka jamaa yule na kufahamu kuwa anakula tunda hilo pasi na idhini ya mwenye bustani ile. Duh! Afanyeje Shekhe huyu na tayari ashalimega upande mmoja? Kweli kajikosea mwenyewe kwa kuwa kala ambacho si halali yake, kamkosea mwenye bustani kwa kula mali yake bila idhini na zaidi, kamkosea Mola wake kwa wizi. Lakini hakuna mtu aliyemuona, si bora angeendelea na safari yake tu. La! haiwezekani kwa watu wacha Mungu. Jamaa yule akajiondokea taratibu akionekana mnyonge na uso wake kasawijika huku amekibeba kila kipande kilichobaki cha tunda lile. Akaamua kumtafuta mwenyewe na akauliziaulizia hadi mwishowe akaonyeshwa nyumbani kwa mwenye bustani ile. Baada ya mazungumzo marefu kati yeke na mwenye bustani ile, mwafaka ukapatikana kwamba, atasamehewa kwa sharti moja tu, lakini zito kweli. "Ili ni kusamehe, basi wewe utamuoa binti yangu, ambaye ni kipofu, kiziwi, bubu na pia miguu yake haiwezi kutembea." Akasema mwenye bustani. Ah! Ingekuwaa wewe

Page 56: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -56- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

ungefanyaje na ushayavulia tayari hivyo basi huna budi kuyaoga. "Nenda katika kile chumba, mkeo yumo humo." Akazidi kumwambia. Mara alipofika mlangoni, desturi ya Muislamu yoyote ule akatoa Swalamu. Mara sauti ya binti ikajibu kutoka mle chumbani: "WaalaykumusSwalam Warahmatullahi Wabarakaatuh!" Shekhe yule akapigwa na bumbuwazi akaanza kujiuliza, vipi binti huyu kajibu Swalamu na nimeambiwa kuwa hazungumzi, na mwanzo kanisikia vipi nikitoa Swalamu? Akastaajabu yule kijana. "Baba yako kanidanganya," kijana yule akamwambia binti. Akatabasamu yule binti na kumjibu kuwa, hajakudanganya babangu, ndio, kasema mimi ni kipofu kwa kuwa sitizami ila katika kuisoma Qur'ani na kutazama tu ninakoruhusiwa na sheria ya dini yangu, uziwi wangu ni kuwa, si sikizi ila yanayonikaribisha mimi kwa Allah SWT, ububu wangu ni kuwa sizungumzi ila kwa yanayofungamana na kauli ya Allah na kauli ya Rasuul SAW, na pia mimi ni kiwete kwa kuwa sitembei ila katika njia ya ibada na inayonikurubisha kwa Mola wangu Mlezi. Tabasamu pana likapamba sura ya yule kijana na mzee yule mwenye bustani akawafungisha nikahi. Naam kisa chenyewe ni waadhih, kiko wazi kabisa na wala hakihitaji maelezo, sherehe wala ufafanuzi. Lakini kikubwa tulichojifunza ni kuwa, ikhalasi inalipa, na sio hapa tu duniani bali pia kesho katika maisha ya milele. Ni muhimu kujua kuwa, asiye na ikhlasi katika amali zake, basi hana tawhidi, asiye na tawhidi hana dini na asiye na dini maisha yake ya ulimwenguni humporomokea na atakwenda kupata hasara isiyo na mithili siku ya malipo. Inshaallah, Allah SWT atujaaliye tuwe ni miongoni ma wenye ikhalas katika amali zetu. Amin!!

Page 57: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -57- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Nafurahishwa na Makala za jarida hili, zina manufaa mno hasa kuhusu masuala ya kidini, kiafya na ya kisiasa. Ongezeni nafasi ya marafiki katika jarida hilo kwani jambo hilo litaunganisha umma wa Waislamu kutoka kona mbali mbali za dunia. Jabir Ali Jabir - Dar es Swalaam , Tanzania. Nimefurahi kwa zawadi mlizonitumia. Zimenifikia na ninaomba tuzidi kuwasiliana katika uwanja huo wa kubadilishana khabari. Ally Youssuf Ibrahim – Kigali , Rwanda. Uongozi wa gazeti la An-nuur pamoja na wafanyakazi wote wanatoa shukrani zao za dhati

kwa ushirikiano mwema wa Radio Tehran na gazeti hili kwa kututumia majarida pamoja na kalenda mbali mbali mlizokuwa mkitutumia kwa mda mrefu, naomba leo nichukue fursa hii kukushukuruni kwa kina pamoja na dua kuwaombea, Allah awape moyo wa Subra na utendaji mwema. lengo ni tufikie lengo. Azza Ahmed wa Gazeti la Kiislamu An-nuur - Dar es Swalaam, Tanzania. Napenda kutoa pongezi na shukrani zangu za kipekee kwa uongozi mzima wa radio Tehran na watangazaji wake kwa kuendelea kutujuza kila uchao kwa lile linalojiri ulimwenguni. Kwa hakika nina furaha isiyo kifani kwa zawadi mpya ambayo nimeipokea hivi karibuni ya Jarida jipya la Hud-Hud ambalo limesheheni mambo mbalimbali yenye manufaa hapa duniani na huko Akhera. Masoud Khamis Hamed Elbimany – Pemba, Zanzibar, Tanzania.

Page 58: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -58- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Tumepokea nakala za Hud-Hud toleo la pili na tunashukuru sana. Iqbal Gitau Kuraia – Mombasa, Kenya. Nashukuru sana kwa jarida la Hud-Hud toleo la pili. Nimelipata kwa njia nzuri. Hakika ndani yake muna kila mada ambayo ni muhimu kwetu. Imam Hamad Badi Faraj – Taita, Kenya.

Nashukuru nimepata Jarida la HUD HUD katika hali nzuri sana. Nimependezwa sana na makala za Mwanahisabati KHORAZMI, Sayansi na Teknolojia nchini Irani pamoja na historia ya Mapinduzi ya ya Kiislamu ya Iran. Ramadhani Abdul Swaibu - Ifakara, Tanzania.

Nachukua fursa hii kukiri kupokea majarida mawili yenye jina la HUD-HUD toleo la pili, ama kwa hakika sina budi kukupongezeni kwa juhudi zenu za dhati kabisa katika kufikisha yale yaliyo mema kwa sisi viumbe wenzenu ambao kwa nyakati kadhaa huwa tunaghafilika na kusahau wajibu wetu kwa Allah kabisa. Juma I. Zuberi – Dar es Swalaam, Tanzania.

Napenda kutoa Swalaam zangu za dhati kwa Mhariri Mkuu na uongozi wa Radio Tehran kwa fikra na hatimaye kuanzisha jarida maridhawa la HUD-HUD ambalo ni kioo cha jamii kote duniani. Kwangu mimi ni mara ya pili kutumiwa jarida hilo, na mara zote nimekuwa nafurahia makala mbalimbali yaliyomo katika jarida hilo la HUD-HUD. Abubakari Mohamed Seif - Mtwara, Tanzania.

Page 59: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -59- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Shukrani zangu za dhati zikufikyeni hapo mlipo, nimefurahi sana kwa mara nyingine kupokeya jarida la Hud Hud la Radio Tehran. Nimepata majarida mawili toleo la pili, January-March 2010 ahsanteni sana. Nimefurahi kuona barua yangu na wanabaraza wenzangu zimechapishwa kwenye toleo hilo la pili. Mola ajaaliye liwe jarida la kheri kwetu na Allah aidumishe Idhaa yetu ya Kiswahili, Sauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na wakaazi wake, Amin. Khamisa Mohamed Al Rabiee – Sur, Oman.

Napenda kuwajulisha kuwa nimepokea gazeti la kwanza la Hud Hud la Oktoba Disemba 2009. Hakika natoa pongezi tu kwa juhudi zenu. Mwenyezi Mungu akuzidishieni imani na kazi njema. Hilal Nasor Zahor al Kindy, Amrat, Oman. Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu. Shukrani kwa zawadi maridadi ya toleo la pili la jarida la HUD-HUD. Wengi walishangaa mno kwani Iran ni mbali sana. Kupitia kwalo ni kumwona

mwasisi wa jamhuri ya kiislamu ya Iran imam Khomeini (quddisa sirruh), mwana hisabati na mnajimu(Khorazmi), picha nzuri sana ya msikiti wa ''Raya'' ulioko Indonesia. Nimejifunza mengi kama mashambulizi ya Ghaza,bustani ya malenga,uzayuni katika kioo cha historia,taswira ya mwanamke katika Qur'an tukufu,miaka kumi na tano ya Idhaa ya Kiswahili Redio Tehran na manufaa na faida ya ndizi kwa afya yetu. Mwisho ni kuwashukuru wote haswa wakurugenzi, watangazaji na wasikilizaji wa Redio hii. Pia nchi ya Iran kuwekeza hapa Kenya na ushirikiano wa KBC na Radio Tehran upande wa kubadilisha vipindi. Ni mimi wenu, Barasa S. Wafula, Bungoma Agricultural Training Centre, Bungoma, Kenya.

Page 60: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -60- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

AsSwalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh. Naomba nitumie fursa hii kukushukuruni wahusika wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio Tehran kwa kuweza kuniagizia zawadi mbalimbali likiwemo jarida la Hud-Hud. Jarida hili limeniwezesha kujua kwa undano chanamoto zinazoukumba ulimwengu wa Kiislamu. Naomba nihitimishe kwa kumuomba Allah ayalinde Mapinduzi matukufu ya Kiislamu ya Iran kwani Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni nuru ya dunia kutokana na kutetea kwake haki na usawa miongoni mwa watu na baina ya mataifa ya dunia. Wabillahit Tawfiq. Taze S. Kabavako, Kigoma, Tanzania.

Anwani ya Posta: Idhaa ya Kiswahili – Redio

Tehran P.O.Box 19395/6767 Tehran,

Islamic Republic of Iran P.O.Box 7898 Dar es Swalaam,

Tanzania P.O.Box 59595 Postal Code 00200 au 49170 Postal Code

00100 Nairobi, Kenya

Tovuti na Barua-pepe http://kiswahili.irib.ir;

[email protected]

Simu: (+98-21) 22162913, 22010544

Fax: (+98-21) 22010544.

Page 61: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -61- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Masafa Mafupi FM Wakati wa Kusikika

Eneo

Khz M MHz UTC Tehran Afrika Mashariki

Tehran 100.7 12.00

Kenya, Tanzania,Uganda,Congo, Rwanda, Burundi, na Ghuba ya

Uajemi 13640 22

Kenya, Tanzania,Uganda,Congo, Rwanda, Burundi, na Ghuba ya

Uajemi 15260 19

4:00-5:00

12:30-1:30 Asubuhi

Kenya, Tanzania,Uganda,Congo, Rwanda, Burundi 15240 19 13:00-

14:00

Kenya, Tanzania,Uganda,Congo, Rwanda, Burundi 17660 16

8:30-9:30

5:30-6:30 Mchana

Kenya, Tanzania, Uganda, Congo, Rwanda, Burundi,

Kenya, Ghuba ya Uajemi na Bahari ya Oman

6130 49

Kenya, Tanzania,Uganda,Congo, Rwanda, Burundi 7365 41

17:30-18:30

2:30-3:30 Usiku

Kupitia satalaiti 19:30-20:30 22:30-23:30

Page 62: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -62- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

HOTBIRD 8 (13°E)

Frequency : 12437 MHz Polarization : Horizontal S/ Rate : 27.5MSym/s FEC : 3/4

Huduma PID ya Huduma

Aina ya Huduma

Jina la Mtandao ID ya Huduma

Studio110-111 98 Audio01 IRIB1/IRIB2 9730

Studio114 87 Audio01 IRIB4/IRIB5 7931

ASIASAT 2 (100.5° E)

Frequency : 3660 MHz Polarization:

Vertical S/ Rate :

27.5MSym/s FEC : ¾

Huduma PID ya Huduma

Aina ya Huduma

Jina la Mtandao ID ya Huduma

Studio110-111 661 Audio02 AL-ALAM 7

Nilesat 102 (7°W)

Frequency : 11919 MHz Polarization:

Horizontal S/ Rate :

27.5MSym/s FEC : 3/4

Huduma PID ya Huduma

Aina ya Huduma

Jina la Mtandao

ID ya Huduma

Studio110-111 1002 Audio01 al-Alam Radio

2525

BADR 4 (26°E) - (ARABSAT)

Frequency : 11996 MHz Polarization:

Horizontal S/ Rate :

27.5MSym/s FEC : 3/4

Huduma PID ya

Huduma Aina ya Huduma

Jina la Mtandao ID ya Huduma

Studio110-111 4420 Audio al-Alam Radio1

43

Page 63: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -63- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Jumamosi Jumapili Jumatatu Jumanne Jumatano Alkhamisi Ijumaa

Qur’ani Qur’ani Qur’ani Qur’ani Qur’ani Qur’ani Qur’ani

Habari /Ripoti

/Mahojiano

Habari /Ripoti

/Mahojiano

Habari /Ripoti

/Mahojiano

Habari /Ripoti

/Mahojiano

Habari /Ripoti

/Mahojiano

Habari /Ripoti

/Mahojiano

Habari /Ripoti

/Mahojiano

Uchambuzi wa Kisiasa

Uchambuzi wa Kisiasa

Uchambuzi wa Kisiasa

Uchambuzi wa Kisiasa

Uchambuzi wa Kisiasa

Uchambuzi wa Kisiasa

Uchambuzi wa Kisiasa

Darsa ya Qur'ani

B/Wasikilizaji Jifunze Kiafarsi

Swala Uliza Ujibiwe

B/Wasikilizaji Iran Juma Hili

Macho Yetu

Magazetini

Macho Yetu Magazetini

Macho Yetu

Magazetini

Macho Yetu

Magazetini

Macho Yetu

Magazetini

Macho Yetu Magazetini

Macho Yetu

Magazetini

Mafanikio ya Iran katika

Sayansi

Iran Juma Hili Imam Khomeini

Ulimwengu wa

Michezo

Maadili Bora

Aliyefikia Kilele cha Historia

Hapa na Pale

Leo katika Historia

Leo katika Historia

Leo katika Historia

Leo katika Historia

Leo katika Historia

Leo katika Historia

Leo katika Historia

Muhtasari wa Habari

Muhtasari wa Habari

Muhtasari wa Habari

Muhtasari wa Habari

Muhtasari wa Habari

Muhtasari wa Habari

Muhtasari wa Habari

Kuaga Kuaga Kuaga Kuaga Kuaga Kuaga Kuaga

Page 64: Jarida Hudu-Hud 3

HUD-HUD [email protected] Julai - Septemba 2010

http://kiswahili.irib.ir -64- Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran

Jumamosi Jumapili Jumatatu Jumanne Jumatano Alkhamisi Ijumaa

Qur'ani Qur'ani Qur'ani Qur'ani Qur'ani Qur'ani Qur'ani

Habari /Ripoti

/Mahojiano

Habari /Ripoti

/Mahojiano

Habari /Ripoti

/Mahojiano

Habari /Ripoti

/Mahojiano

Habari /Ripoti

/Mahojiano

Habari /Ripoti

/Mahojiano

Habari /Ripoti

/Mahojiano

Uchambuzi wa Kisiasa

Uchambuzi wa Kisiasa

Uchambuzi wa Kisiasa

Uchambuzi wa Kisiasa

Uchambuzi wa Kisiasa

Uchambuzi wa Kisiasa

Uchambuzi wa Kisiasa

B/Wasikilizaji Jifunze Kifarsi

Swala Uliza Ujibiwe

B/Wasikilizaji Iran Juma Hili

Darsa ya Qur’ani

Afrika Wiki Hii

Imam Khomeini

Ulimwengu wa

Michezo

Maadili Bora

Aliyefikia Kilele wa Historia

Hapa na Pale

Mafanikio ya Iran

Leo katika Historia

Leo katika Historia

Leo katika Historia

Leo katika Historia

Leo katika Historia

Leo katika Historia

Leo katika Historia

Muhtasari Muhtasari Muhtasari Muhtasari Muhtasari Muhtasari Muhtasari

Kuaga Kuaga Kuaga Kuaga Kuaga Kuaga Kuaga

Jina Kamili Kiwango cha Elimu Anwani Kamili ya Posta

Maoni