4
Mshirika aeleza jambo Mwalimu (aliyeshika kitabu) baada ya kufungua shule rasmi Jarida la Maendeleo Molo Tol. 7 2009 “juhudi za amani na kuhusika kwa jamii kimaendeleo” Wakulima wazuru Chuo cha Kilimo cha Ol Joro Orok mnamo Machi 18, 2009 Katika mwezi wa Machi, Mtandao wa NECOFA wajkishirikiana na FKSW walitayarisha safari ya wakulima 34 hadi wilaya ya Nyandarwa ili kujifunza mbinu mpya na bora katika juhudi za kupigana na ukiwa na njaa. Wakulima hawa walitoka maeneo ya Mau Narok, lare, Kuresoi, Keringet, Molo na Olenguruone katika wilaya ya Molo. Pia kulikuwa na washiriki kutoka mashule mbalimbali. Wakiwa huko waliweza kujifunza njia na mbinu za kuboresha mazao shambani hasa ukuzaji wa nyanya ndani ya majumba ya makaratasi(green house). Ukulima wa aina hii husaidia katika kuhifadhi maji na kuzuia magonjwa mbalimbali yanayodhuru mmea huu wa nyanya. Pia waliweza kutembelea baadhi ya wakulima wilayani Nyahururu(eneo la Kifathi) ambao wanaendeleza kilimo chao kwa kutumia mbinu hii mpya. Wakulima hawa walijifunza kuwa hata mtu akiwa na shamba ndogo linaweza kumpatia mapato mengi. Shirika la Utafiti la Chakula la Slow Food Shirika la Chakula la Slow Food lina makao yake makuu katika nchi ya Italiano, na linahusika na kupigania vyakula vya kitamaduni vinavyoendelea kutokomea. Kufikia mwisho wa mwaka wa 2008,. Utafiti wa vyakula ulianzishwa katika wilaya ya molo. Utafiti huu pia ulishirikisha kamati ya MISCC, ambapo jamii mbalimbali zinazofanya kazi na MISCC zilitumiwa. Katika mwanzo wa mwezi wa Machi 2009, MISCC ilipokea wageni kutoka shirika la Slow Food. Baadhi ya vyakula vinavyofanyiwa utafiti ni marenge katika tarafa ya Lare, kuku aina ya “muchunu’ katika eneo la tarafa ya Elburgon. Kuna matarajio kuwa vyakula hivi vitakuwa katika orodha ya vyakula vinavyofanyiwa utafiti na shirika la Slow Food. Kuanzishwa kwa Shule ya Chekechea katika Kambi ya Tuinuane ya Molo Saw Mill Mnamo siku ya Jumatano tarehe 25 Februari 2009, waathiriwa wa Tuinuane Molo Saw Mill walianzisha shule ya chekechea. Washikadao mbali mbali walialikwa katika tukio hili. Kamati ya MISCC iliwakilishwa na kikundi cha Maendeleo Endelevu, Mtandao wa Ecofarming in Africa(NECOFA) na Friends of Kenya Schools and Wildlife (FKSW). MISCC ilisaidia katika kununua ploti ya kujenga shule hiyo kwa mchango wa shilingi elfu ishirini na tano (Kshs 25,000). Pia MISCC ilisaidia ujenzi wa dawati za kusomea ikiwa ni pamoja na kuahidi kulipa mwalimu wa shule hiyo. Jambo hili lilipokelewa sana na wana kijiji hao kwa vile watoto wao walikuwa na fursa ya kuhudhuria masomo.Mwenyekiti wa kambi hiyo Bw. Martin Kamau aliongeza kuwa tayari walikuwa wamepokea makaratasi, vitabu na kalamu kutoka kwa washikadao wengine kuashiria kuwa masomo yangeanza bila shida yoyote. Shule hiyo ilianzishwa rasmi na Bi. Gwen Meyer ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la Friends of Kenya Schools and Wildlife. Watoto wa shule hii walionekana wenye furaha na wakiwa tayari kwa masomo. Kongamano la Kutathmini Mikakati la MISCC Kamati ya MISCC ilitathmini mipango yake kati ya tarehe 3 na 7 Februari 2009. Kongamano hili lilichukua muda wa siku tano na lilihudhiriwa na washiriki 19, kutoka wanakamati wa MISCC, wawakilishi wa jamii mbalimbali(wanawake kwa wanaume), maofisa kutoka wizara ya kilimo, chuo cha ukulima cha baraka, pamoja na mashule. Kongamano liliongozwa na Bw. Karangathi wa Maendeleo Endelevu Action Program(MEAP) pamoja na Bi. Priscilla Nzamalu wa Mtandao wa Ecofarming in Africa(NECOFA). Kufikia mwisho wa kongamano washirika wote walikubaliana umuhimu wa kuwa na mafunzo mengi, hasa katika nyanja za kuandika mahitaji ya miradi pamoja na kuchunguza na kutathmini maendeleo ya miradi. Kongamano la mbinu za kuandika juu ya miradi mnamo tarehe 25 hadi 27 Machi 2009 MISCC iliandaa kongamano la jinsi ya kuandika miradi kati ya Machi 25 hadi 27 2009. Kongamano hili lilipendekezwa na mkutano wa tathmini wa MISCC wa mwezi wa Februari. Washiriki walitoka kamati ya MISCC, na washiriki wake, wanajamii na wakulima. Walifunzwa namna ya kuandika miradi, namna ya kukuza mstakabali mwema na watu, ufadhili, kutambua makosa pamoja na mengine mengi. Katika mwisho wa kongamano, washirika walipendekeza pawe na mafunzo Uk 1

Jarida la Maendeleo Molo Tol. 7 2009 · Ol Joro Orok mnamo Machi 18, 2009 Katika mwezi wa Machi, Mtandao wa NECOFA wajkishirikiana na FKSW walitayarisha safari ya wakulima 34 hadi

  • Upload
    others

  • View
    3

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Jarida la Maendeleo Molo Tol. 7 2009 · Ol Joro Orok mnamo Machi 18, 2009 Katika mwezi wa Machi, Mtandao wa NECOFA wajkishirikiana na FKSW walitayarisha safari ya wakulima 34 hadi

Mshirika aeleza jambo

Mwalimu (aliyeshika kitabu) baada ya kufungua shule rasmi

Jarida la Maendeleo Molo Tol. 7 2009“juhudi za amani na kuhusika kwa jamii kimaendeleo”

Wakulima wazuru Chuo cha Kilimo cha Ol Joro Orok mnamo Machi 18, 2009

Katika mwezi wa Machi, Mtandao wa NECOFA wajkishirikiana na FKSW walitayarisha safari ya wakulima 34 hadi wilaya ya Nyandarwa ili kujifunza mbinu mpya na bora katika juhudi za kupigana na ukiwa na njaa.

Wakulima hawa walitoka maeneo ya Mau Narok, lare, Kuresoi, Keringet, Molo na Olenguruone katika wilaya ya Molo. Pia kulikuwa na washiriki kutoka mashule mbalimbali.

Wakiwa huko waliweza kujifunza njia na mbinu za kuboresha mazao shambani hasa ukuzaji wa nyanya ndani ya majumba ya makaratasi(green house). Ukulima wa aina hii husaidia katika kuhifadhi maji na kuzuia magonjwa mbalimbali yanayodhuru mmea huu wa nyanya.

Pia waliweza kutembelea baadhi ya wakulima wilayani Nyahururu(eneo la Kifathi) ambao wanaendeleza kilimo chao kwa kutumia mbinu hii mpya. Wakulima hawa walijifunza kuwa hata mtu akiwa na shamba ndogo linaweza kumpatia mapato mengi.

Shirika la Utafiti la Chakula la Slow FoodShirika la Chakula la Slow Food lina makao yake

makuu katika nchi ya Italiano, na linahusika na kupigania vyakula vya kitamaduni vinavyoendelea kutokomea. Kufikia mwisho wa mwaka wa 2008,. Utafiti wa vyakula ulianzishwa katika wilaya ya molo. Utafiti huu pia ulishirikisha kamati ya MISCC, ambapo jamii mbalimbali zinazofanya kazi na MISCC zilitumiwa.

Katika mwanzo wa mwezi wa Machi 2009, MISCC ilipokea wageni kutoka shirika la Slow Food. Baadhi ya vyakula vinavyofanyiwa utafiti ni marenge katika tarafa ya Lare, kuku aina ya “muchunu’ katika eneo la tarafa ya Elburgon. Kuna matarajio kuwa vyakula hivi vitakuwa katika orodha ya vyakula vinavyofanyiwa utafiti na shirika la Slow Food.

Kuanzishwa kwa Shule ya Chekechea katika Kambi ya Tuinuane ya Molo Saw Mill

Mnamo siku ya Jumatano tarehe 25 Februari 2009, waathiriwa wa Tuinuane Molo Saw Mill walianzisha shule ya

chekechea. Washikadao mbali mbali walialikwa katika tukio hili. Kamati ya MISCC iliwakilishwa na kikundi cha Maendeleo Endelevu,

Mtandao wa Ecofarming in Africa(NECOFA) na Friends of Kenya Schools and Wildlife (FKSW). MISCC ilisaidia katika kununua ploti ya kujenga shule hiyo kwa mchango wa shilingi elfu ishirini na tano (Kshs 25,000). Pia MISCC ilisaidia ujenzi wa dawati za kusomea ikiwa ni pamoja na kuahidi kulipa mwalimu wa shule hiyo. Jambo hili lilipokelewa sana na wana kijiji hao kwa vile watoto wao walikuwa na fursa ya kuhudhuria masomo.Mwenyekiti wa kambi hiyo Bw. Martin Kamau aliongeza kuwa tayari walikuwa wamepokea makaratasi, vitabu na kalamu kutoka kwa washikadao wengine kuashiria kuwa masomo yangeanza bila shida yoyote.

Shule hiyo ilianzishwa rasmi na Bi. Gwen Meyer ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la Friends of Kenya Schools and Wildlife. Watoto wa shule hii walionekana wenye furaha na wakiwa tayari kwa masomo.

Kongamano la Kutathmini Mikakati la MISCC

Kamati ya MISCC ilitathmini mipango yake kati ya tarehe 3 na 7 Februari 2009. Kongamano hili lilichukua muda wa siku tano na lilihudhiriwa na washiriki 19, kutoka wanakamati wa MISCC, wawakilishi wa jamii mbalimbali(wanawake kwa wanaume), maofisa kutoka wizara ya kilimo, chuo cha ukulima cha baraka, pamoja na mashule. Kongamano liliongozwa na Bw. Karangathi wa Maendeleo Endelevu Action Program(MEAP) pamoja na Bi. Priscilla Nzamalu wa Mtandao wa Ecofarming in Africa(NECOFA). Kufikia mwisho wa kongamano washirika wote walikubaliana umuhimu wa kuwa na mafunzo mengi, hasa katika nyanja za kuandika mahitaji ya miradi pamoja na kuchunguza na kutathmini maendeleo ya miradi.

Kongamano la mbinu za kuandika juu ya miradi mnamo tarehe 25 hadi 27 Machi 2009

MISCC iliandaa kongamano la jinsi ya kuandika miradi kati ya Machi 25 hadi 27 2009. Kongamano hili lilipendekezwa

na mkutano wa tathmini wa MISCC wa mwezi wa Februari. Washiriki walitoka kamati ya MISCC, na washiriki wake, wanajamii na wakulima. Walifunzwa namna ya kuandika miradi,

namna ya kukuza mstakabali mwema na watu, ufadhili,

kutambua makosa pamoja na mengine mengi. Katika mwisho wa kongamano, washirika walipendekeza pawe na mafunzo

Uk 1

Page 2: Jarida la Maendeleo Molo Tol. 7 2009 · Ol Joro Orok mnamo Machi 18, 2009 Katika mwezi wa Machi, Mtandao wa NECOFA wajkishirikiana na FKSW walitayarisha safari ya wakulima 34 hadi

Wagonjwa wapokea madawa

Shughuli za maabara

Bw. Kinuthia akipokea usaidizi wa kununua ploti

Jarida la Maendeleo Molo Tol. 7 2009“juhudi za amani na kuhusika kwa jamii kimaendeleo”

zaidi juu ya kuandika bajeti, kuripoti na kutathmini miradi. Ilikubaliwa kuwa kikao kingine kitaandaliwa.

Kliniki ya Afya ya Zahanati ya Kokwa yafanyika mnamo tarehe 8 Februari 2009Mnamo Februari 8,2009, Mtandao wa Ecofarming in Africa(NECOFA) Friends of Kenya Schools and Wildlife pamoja na wizara ya afya katika eneo la Marigat waligharamia huduma za bure za afya katika kisiwa cha Kokwa mojawapo ya visiwa katika Ziwa Baringo, Kenya. Ziwa hili la Baringo linapatikana katika mkoa wa Bonde la Ufa kilomita 120 kutoka mji wa Nakuru na kilomita 20 kutoka mji wa Marigat. Kisiwa hiki kina idadi ya watu takribani 1200 ambao ni kutoka jamii ya Ilchamus mojawapo wa jamii ndogo zaidi hapa nchini Kenya. Jamii ya ilchamus inaishi katika sehemu kame katika wilaya ya Baringo na katika

eneo la Kokwa kama takribani familia 200 kila moja ikiwa na watu 5.Wahudumu katika

shughuli hii muhimu walitoka Hospitali ya Molo, ya kiserikali naya kibinafsi , hospitali ya

wilaya ya Molo na hospitali ya wilaya ya Marigat.

Walisiaidiana na maofisa kutoka NECOFA na FKSW.Madawa na vifaa vingine vilivyotumika katika

shughuli hiyo vilinunuliwa na wizara ya afya, zahanati za watu binafsi pamoja na NECOFA na FKSW. Maendeleo Endelevu Action Program walisaidia katika kurekodi shughuli hiyo. Baadhi ya shughuli zilizofanyika ni:• Kutibiwa maradhi mbalimbali.• Kupewa madawa• Kuchunguzwa shida za macho• Upimaji katika maabara• Kunyolewa kwa watu wazima na watoto ili kuzuia

maradhi ya ngozi kichwani.• Elimu ya kiafya kwa watoto wa shule ya msingi ya

Kokwa juu ya matumizi ya taweli za hedhi.

• Elimu ya lishe bora.

Kati ya saa nne na saa nane unusu, jumla ya wagonjwa 281

walikuwa

wamehudumiwa. Wahudumu walijigawa kulingana na huduma maalum, wakakaa chini ya miti karibu na zahanati Kwanza wanajamii walijiandikisha, kiwango cha mpigo wa moyo kikachukuliwa kwa kila mmoja wao na baadaye mtu alikuwa na hiari ya kumwona daktari kama alikuwa na shida kubwa ama kutembelea mojawapo ya vituo vingi vilivyokuwa chini ya miti. SIku hiyo watu 121 walinyolewa na vinyozi. Magonjwa yaliyoonekana kuwa sugu kwa watoto wa chini ya miaka 5 ni pumu na kuhara. Watoto wa umri wa kuenda shule kati ya miaka 5-18, maradhi ya pumu, maradhi ya macho, viungo na ngozi mtawalia ndio yalionekana kuwa shida. Wagonjwa kati ya miaka 18-55 walikuwa na matatizo ya kuumwa na mifupa na viungo. Maradhi mengine yalikuwa ya pumu.

Shughuli hii ilikuwa ya kufana na jamii nzima ya Kokwa ilishukuru sana kwa huduma hiyo.

Kikundi cha akina Mama cha Karunga chazinduliwa

Akina mama wa kikundi cha karunga kutoka ELburgon walikuwa na furaha isiyo kifani baada ya kutembelea mbuga la wanyama la Ziwa Nakuru mnamo tarehe 10 Januari 2009. Safari hii ilitayarishwa na Molo Lamb and Wool Project (Mradi wa kondoo na manyoya) ambao ni mradi mmoja unaoendeshwa na Mtandao wa Ecofarming in Africa (NECOFA) wakishirkiana na Friends of Kenya Schools and Wildlife. Katika mradi huu wa kondoo na manyoya, jamii husokota manyoya na kushona vinyago vya wanyama, mikeka na vikapu pamoja na bidhaa zingine, lengo lao hasa ni kujipatia mapato pamoja na maarifa katika kazi husika. Kiini cha safari hii ni kuwezesha wanakikundi kujifunza mengi ili waweze kuboresha bidhaa zao katika siku za halafu. Waliweza kuona wanyama wengi ambao wamekuwa wakitenegeneza vinyago vyao lakini hawakuwa wamewaona wakiwa hai. Wamekuwa wakiwaona katika picha lakini sasa wanatarajiwa kutengeneza vinyago hivi vyema zaidi. Kikundi cha Friends of Kenya Schools and Wildlife pia kilifadhili safari hiyo, pia kikundi hiki hujishughulisha na uuzaji wa bidhaa zitokanazo na manyoya katika nchi ya Amerika.

Wengi watamani kuwa na nyumba zao lakini kwa wakimbizi ni zaidiTangu kuanzishwa kwa oparesheni Rudi Nyumbani kwa waathiriwa, familia nyingi zimeweza kurudi katika maakazi yao ya awali lakini bado kuna wengi ambao hulima mashamba yao wakiwa kwenye kambi

Uk 2

Page 3: Jarida la Maendeleo Molo Tol. 7 2009 · Ol Joro Orok mnamo Machi 18, 2009 Katika mwezi wa Machi, Mtandao wa NECOFA wajkishirikiana na FKSW walitayarisha safari ya wakulima 34 hadi

Jarida la Maendeleo Molo Tol. 7 2009“juhudi za amani na kuhusika kwa jamii kimaendeleo”

zilizojengwa karibu na mashamba yao. Jambo la kusikitisha ni kuwa sio wote waliokuwa na mashamba ambayo wangeweza kurudi, baadhi yao walikuwa maskwota katika mashamba ya watu na wengine walikuwa wamepanga vyumba kwenye vituo vya kibiashara.

Baada ya vita kutokea, kidogo walichokuwa nacho kiliharibiwa au kuibiwa na kwa hivyo hawana chochote, watu hawa bado wako kwenye kambi za wakimbizi. Ni kweli kuwa shida hunoa akili za mtu, baada ya serikali kulipa kila jamii kima cha shilingi elfu kumi, baadhi ya wakimbizi waliokuwa kwenye kambi ya Molo Saw Mill waliweza kuungana na kwa kupitia pesa hizi waliweza kununua ploti kwa kila mmoja wao.Waliweza kulipa awamu ya kwanza katika maeneo yaKibunja na shamba la Mitoni. Awamu nyingine watalipa baada ya kupata msaada kutoka kwa serikali au wafadhili wengine. Wakati kikundi cha MISCC walipata habari hizi, kiliamua kufadhili ploti mbili, moja ya familia ya Bw. Kinuthia na nyingine ya mayatima watano wambao pia ni waathiriwa.

Msaada mdogo lakini wa manufaaKikundi cha MISCC kilionelea vyema kuwapa watoto 8 ambao pia ni waathiirwa wa vita walivyozuka hapa nchiini Kenya mwanzoni mwa mwaka 2008. Zawadi hizi zilikuwa nguo au mavazi wakati wa msimu wa kusherehekea krisimasi

na mwaka mpya.Kati ya watoto hawa ni mayatima ambao walipoteza wazazi kwenye vita hivy. Hawa ni:kuanzia kushoto, msichana Spinicah Moraa wa miaka 16, Wycliff Onduso wa miaka

15, Dennis Ayoti wa miaka 10, George Mbugua wa miaka 14 na Joshua Nyakundi wa miaka 17. Watoto hawa wanasoma shule ya msingi ya St Marys Boys, Mjini Molo.

Wengine walinufaika ni familia ya Bw. David Kinuthia Muiruri. Bw. Kinuthia na dadake ni viema. Bw. Kinuthia hutumia kigari cha kusukumwa(Wheelchair) lakini dadake hajawahi kutembea kwa vile hajanufaika na kigari kama hicho. Pia wao ni waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi na wanaishi katika kanisa la New Testament. Walionufaika ni Zaphania Gitau mwenye umri wa miaka 12, Monicah Wanjiru wa miaka 13, Judy Nyokabi wa miaka 16 na mama yao Rose Wambui.

Mikutano ya kuleta amani katika wilayaMkutano wa amani tarafa ya Elburgon

MISCC ilifanya mkutano wake wa kila mwezi mnamo tarehe 3 Oktoba 2008. katika mkutano huo iliamuliwa kuwa kila tarafa ifanye mikutano yake ya amani ili kuendeleza kuhimiza juhudi za amani.

Wakiongozwa na Bi. Lucy Ndungu, Johnson Kimotho, John Kemoi na Teresia Kitakita wote kutoka tarafa ya Elburgon, walipanga mkutano wa amani mnamo tarehe 14 Oktoba 2008. Kikao hiki kilikuwa na wahusika 26 kutoka maeneo mbalimbali ya tarafa ya Elburgon akiwemo naibu wa kiongozi wa maendeleo ya kijamii(CDA), wanaume, wanawake, vijana na viongozi wa kidini.

Wote walipendezwa kuwa shamba(kijiji) cha Tegat lililoko Elburgon, halikuathiriwa na ghasia za baada ya Uchaguzi. Chifu mstaafu John Thogoto alihimiza umuhimu wa kuwa na amani na maendeleo na kuwa bila mojawapo jamii haiwezi kupata ufanisi.

Wahusika wote walikubaliana kuwa amani ni muhimu kwa maendeleo yoyote kupatikana. Kwa hivyo njia ya pekee ni kuendeleza amani popote pale.

Mikutano ya amani katika tarafa ya Kuresoi na KeringetMkutano wa amani ulifanyika katika tarafa ya Kuresoi, Murinduko mnamo tarehe 7 Novemba 2008. Mkutano ulikuwa na wahusika 39 kutoka sehemu mbalimbali za tarafa hiyo. Taraffa ya Keringet ilifanya mkutano wake wa amani mnamo tarehe 14 Disemba 2008 Langwenda.Wahusika 26 walihudhuria. Kwenye mikutano yote miwili umuhimu wa kuishi pamoja na marishiano ulihimizwa.

Mbio za nyika za amani za OlenguruoneTukio la kuleta amani liliandaliwa na Baraza la wazee la Kamii ya Kuresoi Kipsigis. Tukio au shughuli hii ya amani ililileta pamoja watu zaidi ya elfu tatu mnamo tarehe 28 Novemba 2008. Mbio hizi zilifadhiliwa na kamati ya MISCC Benki ya National tawi la Molo, Hazina ya kenya ya fedha kwa

Wanawake, kampuni ya Majani chai ya Kiptagich na EMO. Baadhi ya mbio zilifanyika ni kilomita2 kwa wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka 50, kilomita 2 kwa wanawake wenye umri wa miaka 45

pamoja na mchezo wa kandanda kwa watoto wenye umri wa miaka 14 kurudi chini. Wakimbiaji walianzishwa rasmi katika

Uk 3

Page 4: Jarida la Maendeleo Molo Tol. 7 2009 · Ol Joro Orok mnamo Machi 18, 2009 Katika mwezi wa Machi, Mtandao wa NECOFA wajkishirikiana na FKSW walitayarisha safari ya wakulima 34 hadi

Jarida la Maendeleo Molo Tol. 7 2009“juhudi za amani na kuhusika kwa jamii kimaendeleo”

kampuni ya majani chai ya kiptagich namwenyekiti wa baraza la Wazee la Kuresoi Kipsigis Bwana Koromicha.

Mashinadno yalidhamiria kuleta amani miongoni mwa jamii mbalimbali na pia kuleta maridhiano. Waliohutubia maelfu ya watu waliohudhuria tukio hili walisizitia umuhimu wa amani miongoni mwa jamii zote. Miongoni mwao ni Bw. Ombaso , Afisa wa Maswala ya Kitamaduni katika wilaya ya Nakuru, Bw. Karangathi Njoroge wa MISCC na Bw. Chemeswot aliyekuwa mgeni rasmi.

MISCC Yahusika katika sherehe za kuadhimisha siku ya Chakula DunianiSherehe za siku ya chakula duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ziliadhimishwa katika Kiptagich Olenguruone. Sherehe hizi zilitayarishwa na Jopo la Washikadao katika wilaya ya Molo wakiongozwa na mkuu wa kilimo wilayani Molo. Waliokuwa na vibanda vya kuonyesha bidhaa mbalimbali ni Benki ya Equity, Faulu kenya, Makundi ya wakulima pamoja na wengineo.

MISCC ilionyesha vyakula vingi vikiwemo uyoga. Pia walihimiza watu kupanda mimea yao kwa kutumia mbolea ya mimea (kujiandalia kwa kutumia majani na kinyezi cha wanyama), na pia umuhimu wa kupanda na kutumia vyakula vya kienyenji(kitamaduni) hasa walieleza umuhimu wake kiafya na kama dawa za maradhi mbalimbali.

Kikao cha kutathmini cha tarehe 10 Disemba 2008Kikao cha kutathmini kilifanyika mnamo tarehe 10 Disemba kwenye kikao wahusika walikumbaliana kuwa waendelea kufanya mikutano ya amani katika maeneo yao. Ilikubaliwa kuwa watakuwa mabalozi wa amani na kwamba watatumia kila nafasi kuhubiri amani miongoni mwao.

Mkutano wa tathmini wa Machi 20, 2009Mkutano wa kwanza wa tathmini wa mwaka 2009

ulifanyika mnamo tarehe 20, Machi 2009. Wahusika waliripoti kuwa marithiano na utangamano unarejea na wakulima wamo mbioni kwa maandalizi ya upanzi pindi mvua inyeshapo. Hata hivyo bado kuna changamoto chache kama vileukosefu wa mbegu na wizi wa mifugo. Kikao kilikubaliana kuwa mikutano ya amani itafanyika mashinani kwa mfano Kamwaura, Sirikwa, Sachangwani, Sondu Riverm Mauche na Kaplelach.

MISCC na washikadao wengineMISCC ilishiriki katika mkutano wa kutoa maoni wa

hadhara uliotayarishwa na kikundi cha Abantu cha Maendeleo

mnamo tarehe 22 Oktoba 2008. Lengo ni kuleta jamii mbalimbali pamoja ili kutafuta suluhisho la kudumu katika vita vya kikabila kwenye eneo la Molo..

Bi Lucy Ndung’u na Carlos Njogu walipata mafunzo kutoka kwa UNHCR kuhusiana na mikinzano na fujo za kijinsia kati ya tarehe 28 na 31 Oktoba 2008.

Wana MISCC ni miongoni mwa Wakenya 59 waliohudhuria mkutano wa Terra Madre World Meeting 2008. Mkutano huo ni wa vyakula vya kijamii na hufanyika baada ya miaka miwili mjini Turin, Italia.

Mkutano huleta pamoja wakulima, vijana, wapishi na washikadao wengine wanahusiana na kilimo na vyakula ulimwenguni. MISCC ilitumia fursa hiyo kujitangaza na shughuli zake mbalimbali ulimwenguni.

VifupiFKSW – Friends of Kenya Schools and WildlifeMEAP - Maendeleo Endelevu Action ProgramMISCC – Jopo unganishi la mashirika yasiyokuwa

ya serikali katika eneo la Molo Tol - Toleo

Kwa habari zaidi wasiliana na Jopo la MISCCKupitia NECOFA – KenyaS.L.P 819, [email protected] miscc.wordpress.comSimu rununu: 0722647112/0722906453

Uk 4