Upload
others
View
0
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
Karibu katika Jarida la STEP! Julai– Septemba 2015
Southern Tanzania Elephant Program (STEP) ni mradi wa uhifadhi wa tembo ulioko kusini mwa
Tanzania. Tunafanya kazi na mamlaka za uhifadhi wanyamapori na jamii inayoishi maeneo ya hifadhi
ili kuwahifadhi tembo na binadamu kuendelea kuishi na tembo kwa uvumilivu. Pia tunafanya tafiti
husika za kisayansi za uhifadhi. Tunayo furaha kushiriki na wewe baadhi ya habari tangu Julai hadi
Septemba 2015.
Mpango wa anga na uhesabuji mpya wa idadi ya Tembo Ruaha-Rungwa
Timu ya STEP ya marubani Charles na Anne Nagy
wameanza mpango wetu wa anga. Wakifanya
ufuatiliaji na uangalizi kwa ndege katika hifadhi
ya Taifa ya Ruaha kwa ndege ndogo (ijulikanayo
kama “Skubie”. Tangu mwezi wa tisa, kwa
mwaliko wa Taasisi ya Utafiti Wanyamapori
Tanzania (TAWIRI) na Wizara ya Maliasili na
Utalii, timu ya marubani imekuwa ikiruka kama
sehemu ya uhesabuji upya wa Tembo (2015)
katika Ruaha-Rungwa.
Timu ya STEP inafanya kazi kwa karibu na timu ya sensa, kuruka kwa saveyi ya awali kupitia transekti
kuthibitisha kuwepo/kutokuwepo kwa tembo hai na mizoga katika hifadhi. Wakiruka chini na taratibu,
na kwa kuweza kuona kwa umakini mkubwa kuliko ndege za Cessna zilizotumika katika sensa kubwa.
Mpango huu wa kuruka kima cha chini kwa ndege ndogo umepangwa kwa pamoja kuongeza thamani
na uhakiki wa sensa kwa kuongeza ufasaha na uwiano kwa matokeo ya mwisho. Mbinu ya kuruka
kilomita 10 kwa 10 inaleta ufasaha kutoa alama zinazoonekana za shughuli haramu na kutoa taarifa
haraka kwa timu za askari wa wanyamapori ardhini.
SOUTHERN
TANZANIA
ELEPHANT
PROGRAM
Kulinda amani ya baadaye ya Tembo wa
kusini mwa Tanzania na kwingineko
Pia tunayo furaha kusaidia kazi ya utafiti ya Mkuu wa Ruaha Dr Alex Epaphras na watafiti toka mradi
wa Hali, UC Davis, South Carolina Zoo, na WCS. Kwa kuruka ukanda wa chini kubaini makundi ya nyati
na viota vya ndege wala mizoga walio hatarini kutoweka.
Kama sehemu ya sensa awamu ya pili STEP pia ilisaidia kutayarisha camera katika Ruaha-Rungwa.
Takwimu za camera zitasaidia kuchunguza mabadiliko katika tabia za Tembo kwa ajili ya
uwindaji/ujangili, na uwezekano wa kubaini kuonekana kwa tembo toka katika anga ndani ya maeneo
mbalimbali.
Tathmini ya Tembo kwa eneo Pori la Akiba Selous
Mtafiti wa Tembo wa STEP, Lameck, na wasaidizi wake Athumani na Serafino
wamerejea hivi karibuni toka Pori la akiba la Selous, ambapo walikamilisha
saveyi ya tembo kwa kuangalia kinyesi, kwato na vipimo vya fuvu umbali wa
kilomita 900 za barabarani. Timu ilipitia changamoto nyingi - ikiwemo
kuharibika kwa gari mara nyingi katika saveyi ya Matambwe, Kingupira, na
kusini mwa Selous (Kalulu). Takwimu hizi sasa zitapitiwa ili kujua mgawanyo wa
umri na jinsia wa Selous na uelekeo tangu saveyi iliyopita mwaka 2009.
Tunapenda kuwashukuru Idara ya Wanyamapori, Utawala wa Pori la Akiba la
Selous na Lake Manze Camp kwa ushirikiano wao na kusaidia katika saveyi .
Athumani, Askari wa Selous, na Lameck Serafino akitengeneza Landrova ya STEP lililopewa
jina la utani “Labda” kwa usumbufu wake
Timu ya field ya STEP ikitayarisha Camera “Fundi” Athumani akiwa anafunga Camera
Kuchunguza mgogoro baina ya binadamu na Tembo, Hifadhi ya Taifa ya Ruaha
Mwezi wa saba na wa nane, timu yetu wachapakazi, Jenipha,
Kennedy na Kepha walisafiri kwa basi, pikipiki, na kwa miguu katika
vijiji 33 vinavyopakana na hifadhi ya Taifa Ruaha kwenda kuwahoji
viongozi wa vijiji na wakulima kuhusu mgogoro baina ya binadamu
na Tembo. Takwimu walizokusanya zitasaidia kubaini eneo
linaloathiriwa zaidi na tembo kuharibu mazao na vyanzo vingine vya
migogoro na kuamua kwa kiasi gani tunaweza kusaidia kwa
baadaye zaidi mradi wa fensi ya mizinga ya nyuki ambayo zinaweza
kuzuia uvamizi na kutoa chanzo mbadala cha mapato dhidi ya
ujangili. Pia kuwa utafiti wa kwanza mkubwa wa mgogoro wa
binadamu na Tembo katika eneo hilo, saveyi hii ilikuwa ni uzoefu
mzuri kwa timu ambayo mahojiano yao na watu ilivutia mtazamo
na fikra za watu katika uhifadhi na mambo ya kijamii na uchumi
yanayowakabili maeneo ya vijijini mwa Tanzania, na kutoa mwanya wa suluhisho la kudumu dhidi ya
migogoro ya binadamu na tembo.
Habari mpya za Udzungwa: ufuatiliaji wa Tembo na kitabu kipya
Habari njema toka Udzungwa ni kuwa tumeanza ufuatiliaji wa Tembo kwa kushirikiana na Udzungwa.
Watafiti wa STEP Paulo na Jose watatembea kilomita 22 kila mwezi kurekodi na kupima kinyesi cha
Tembo ili kuelewa mgawanyiko na demografia ya Tembo (kwa kupima kinyesi kutambua umri wa
Tembo), na kuelewa matokeo ya matishio kama ukataji miti na ujangili.
Kujifunza zaidi kuhusu utafiti wa muda mrefu wa
STEP Udzungwa soma kitabu chapisho jipya
Udzungwa: Tales of Discovery in an East African
Rainforest ambapo Trevor Jones na Katarzyna
Nowak wamechangia kuandika sura kadhaa kuhusu
Tembo na Primates wa kipekee wa Udzungwa.
Picha: Paulo anapima transekti ya kinyesi cha tembo kwa
kutumia kifaa maalum; Jose anapima diameta ya kinyesi ili
kupima Umri.
Safari ya mafunzo na mashauriano Amboseli na Samburu
Meneja wa Fildi Josephine, Mtafiti wa Tembo Lameck, na Dereva Peter walisafiri kuelekea Kenya kwa
mafunzo na mashauriano na miradi miwili ya muda mrefu ya utafiti na uhifadhi wa Tembo. Kwanza
walitembelea mradi wa muda mrefu ulimwenguni wa utafiti wa Tembo – Mradi wa Utafiti wa Tembo
Amboseli (AERP) – ambapo walitumia siku tatu katika fildi kuwatambua umri tembo wakiwa na Norah
Njiraini, mmoja kati ya wasaidizi wa muda mrefu wa utafiti katika mradi. Timu pia ilijifunza toka kwa
mwanasayansi mkazi katika AERP, Dr. Vicki Fishlock, namna mradi unavyomudu takwimu zake za
muda wa miaka arobaini, zaidi sana “ID Database” yake ya Tembo kubwa na jinsi wanavyohifadhi
takwimu za maisha ya kila tembo kuanzia kuzaliwa hadi kufa.
Timu pia ilielekea hifadhi ya Taifa ya Samburu kaskazini mwa Kenya kutembelea kambi ya utafiti ya
Save the Elephants (STE). Ikiwemo kujifunza kuhusu kazi yao ya muda mrefu ya ufuatiliaji tembo,
tulitambulishwa matumizi ya teknolojia yao ya collar kuelewa uelekeo wa Tembo katika maeneo ya
kaskazini mwa Kenya.
Amboseli na Samburu ni mifano bora ya nini yaweza kuwa matokeo ya ufuatiliaji ya muda mrefu wa
Tembo kwa maana ya kuongeza ufahamu wa wanyama hawa wazuri, na kulinda usalama wa Tembo
katika ukanda unaotishia wa Afrika mashariki. Safari ilitujaza na mawazo ya namna ya kuendeleza
utafiti wetu, uhifadhi, uenezaji na ushauri kusini mwa Tanzania. Shukrani nyingi kwa kila mmoja
Amboseli na Samburu kwa kutushirikisha maarifa yenu, na kila mmoja aliyechangia kufanya uzoefu
huu uwezekane.
Kampeni mpya ya Tembo: “OKOA Tembo wa Tanzania”
STEP inajivunia kusaidia kampeni ya “OKOA Tembo wa Tanzania”, ambayo inalenga kupaza sauti za
Watanzania dhidi ya Ujangili wa Tembo na kuhoji utekelezaji wa ndani kumaliza tatizo hili. Kampeni
inaitaka Serikali ya Tanzania kuwakamata na kuwashitaki wafanyabiashara wakubwa wa meno ya
Tembo nchini, kuweka msukumo kwa serikali ya China kufunga soko la meno ya Tembo na kuharibu
ghala ya meno ya Tembo. Wanakampeni wa OKOA wamekuwa bize mwezi wote wa Septemba,
wakihudhuria matamasha ya Amani ya FEMA sehemu mbalimbali nchini, wakiunda vikundi vya OKOA
na pia kufanya mahojiano kwa Televisheni na Radio nyingi.
Fahamu zaidi kuhusu kampeni kwa kutembvelea tovuti www.okoatembowatanzania.org, na kwenye
ukurasa wa Facebook OKOA Tembo wa Tanzania ambao tayari una watu 50,000 wanaoufuatilia!
Matamasha la Jazz kwaajili ya Tembo
Mwezi wa tisa, matamasha ya muziki wa Jazz kumshirikisha Floris Kappeyne Trio na DazzJazz
yalifanyika huko Dar es salaam kuisaidia STEP. Kwa pamoja, matamasha haya yalikusanya shilingi
milioni saba na nusu kwa mpango wa anga wa STEP na mradi wa Binadamu na Tembo. Shukrani nyingi
kwa walioshiriki matamasha haya, waandaaji wetu, kwa balozi wetu Dar, Andy Perkin, na kwa
wanamuziki wenye vipaji. Shukrani za pekee kwenu Belia Klaassen kwa kuandaa matamasha haya.
Lameck akiwa anaongea na wanafunzi kuhusu Kampeni
ya OKOA – Nane Nane, Arusha
Wadau wa “OKOA Tembo Club” - Ilula, Iringa
Floris Kappeyne Trio na DazzJazz wakiburudisha katika onyesho
dogo.
Habari za Tembo
Mwezi wa nane, iliripotiwa kuwa raia watatu wa China walikamatwa na mabegi 14 ya pembe za ndovu huko uwanja wa ndege wa Zurich, wakiwa wamesafirisha moja kwa moja kutokea Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam. Watu watano, wafanyakazi wa uwanja wa ndege na wanajeshi wa Tanzania wameshitakiwa kwa kuhusika. Cha kushtusha, Mamlaka za Uswizi ziliwaruhusu wachina kurudi China, na bado hakuna habari za kuwarejesha Tanzania kushitakiwa.
Inaonekana hata hivyo kuwa kukamatwa kwa wingi wafanyabiashara wa meno ya Tembo kunaanza kufanyika nchini Tanzania. Asante kwa kazi ya kishujaa ya wakiwemo wengineo, the National and Transnational Serious Crimes Investigation Unit (NTSCIU). Habari za karibuni mpaka tunaandika hii, ni kuwa raia wa China, Yang Feng Glan ameshitakiwa kwa kufanya biashara ya pembe za ndovu na kufadhili uuwaji wa Tembo kwa miaka mingi. Sote tunaamini kuwa kukamatwa na kuzuiliwa kwake kutafungua mianya ya kuwakamata wanamtandao wenzake bila kujali wanaweza kuwa na nguvu kiasi gani.
Hongera kwa Taasisi ya Wanyamapori Kenya (Kenya Wildlife Service) ambao mwezi wa tisa walimalizia kuchoma hadharani akiba yao ya meno ya tembo, ikishuhudiwa na Asasi za kiraia na washuhudiaji wa kimataifa kama hatua nyingine ya utayari kwao kuharibu ghala lote hadi mwishoni mwa mwaka huu.
Kuisaidia STEP.
STEP hutegemea zaidi ukarimu kwa namna ya pekee kutoka kwa wafadhili wetu -mnatusaidia kufanya mengi kwa ajili ya tembo. Tafadhali fikiria kutusaidia kwa kutumia njia zifuatazo:
Fuatilia STEP kwenye Facebook,Twitter, na tovuti yetu na shirikisha wengine shughuli zetu
Saidia kujenga ufahamu kwa tisheti zetu za “Okoa Tembo wa Tanzania” (Tsh 30,000) na mifuniko ya magurudumu (Tsh 80,000)
Wasaidie wakulima vijijini kwa kununua Asali rafiki wa Tembo (inapatikana Butcher Shop, Dar)
Changia katika nyanja za kazi yetu kwa chaguo lako
Asante sana kwa msaada wako!
Registered not-for-profit No. 112972
SOUTHERN
TANZANIA
ELEPHANT
PROGRAM