10
Kenya KIPSAINA CRANE AND WETLANDS CONSERVATION GROUP Empowered lives. Resilient nations. Miradi y Equator Wanafijiji na Maendeleo Himili ya Jamii

KIPSAINA CRANE AND WETLANDS CONSERVATION GROUP · Miche ya miti ya asili hupewa wakaazi wa eneo hili kupanda ili kuongeza idadi ya miti na kuunda kinga maalum ya eneo chepechepe,

  • Upload
    others

  • View
    14

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Kenya

KIPSAINA CRANE AND WETLANDS CONSERVATION GROUP

Empowered lives. Resilient nations.

Miradi y EquatorWanafijiji na Maendeleo Himili ya Jamii

MIRADI YA UNDP EQUATOR Kote duniani, jamiii zinazidi kubuni mbinu zinazonuiwa kuyakidhi mahitaji yao ya kila siku na ya kimazingira. Kuna kazi chache ambazo zimechapishwa za kuelezea kinagaubaga hizo mbinu bunifu na vile zilianzishwa,vile ziliathiri wakaaji wa sehemu mbali mbali na vile zimekuwa zikibadilika pindi wakati unapotita. Wachache wamejitokeza kuelezea wazi wazi juu ya miradi yao, na hata wale ambao wamefanya hivyo ni wakuu wa vijiji ambao wamefanya kuelezea kufaulu kwao.

Mradi huu wa Equator Katika unadhamiria kujaza hili pengo kama njia moja ya kuadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwake. Masimulizi juu ya huu mradi ni baadhi tu ya mingi ambayo imefaulu na kushinda tuzo za Equator baada ya kukaguliwa na kutathiminiwa katika kitengo cha makundi ya kijamii yanayo hifadhi mazingira na kuinua maisha ya wanafijiji. Miradi hii inakusudiwa kuwa mifano ya kuiwa na kuwatia shime kuzungumzia ilivyofaulu ili kuhamasisha ulimwengu juu ya uhifadhi wa mazingira.

Bonyeza katika ramani ya miradi ya Equator ili upate kupata habari zaidi

WahaririMhariri Mkuu : Joseph CorcoranMuhariri Meneja : Oliver HughesWahariri Waliochangia : Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Erin Lewis, Whitney Wilding

Wahandishi Waliochangia Edayatu Abieodun Lamptey, Erin Atwell, Toni Blackman, Jonathan Clay, Joseph Corcoran, Larissa Currado, Sarah Gordon, Oliver Hughes, Wen-Juan Jiang, Sonal Kanabar, Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Rachael Lader, Patrick Lee, Erin Lewis, Jona Liebl, Mengning Ma, Mary McGraw, Gabriele Orlandi, Juliana Quaresma, Peter Schecter, Martin Sommerschuh, Whitney Wilding, Luna Wu

Uchoraji Oliver Hughes, Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Amy Korngiebel, Kimberly Koserowski, Erin Lewis, John Mulqueen, Lorena de la Parra, Brandon Payne, Mariajosé Satizábal G.

ShukraniEquator ingependa kuwashukuru wanachama wa Kipsaina Crane and Wetlands Conservation Group, haswa mwongozo na mchango wa Maurice Wanjala. Picha ni za Kipsaina Crane and Wetlands Conservation Group, ramani ni za CIA World Factbook na Wikipedia. Masimulizi juu ya mradi huu yalitafsiriwa kwa Kiswahili na Dr. Ken Ramani.

Nukuu ziadaUnited Nations Development Programme. 2012. Kipsaina Crane and Wetlands Conservation Group, Kenya. Equator Initiative Case Study Series. New York, NY.

MAELEZO KUHUSU MRADI HUUKikundi hiki cha kijamii kimekuwa kikijishughulisha na mradi wa kuhifadhi maeneo chepechepe kwa kutumia mbinu tofauti tangu mwaka wa 1990 katika mbuga ya kitaifa ya kinamasi cha Saiwa,ambayo pia ndio makao ya asilimia 25 ya Korongo wenye taji la kijivu kichwani na wanaokabiliwa na tishio la kuangamizwa nchini Kenya. Katika miaka ya themani upandaji wa miti aina ya mikalitusi kulichangia pakubwa kukauka kwa kinamasi cha Saiwa na kuathiri sana makazi ya ndege hawa.

Kichocheo cha kutaka kubadilisha mtindo huo kilitokana na juhudi za kiongozi mmoja katika Parokia ya kanisa Katoliki eneo hilo, ambaye aliwahamasisha wakaazi kuanza kuhifadhi eneo lipatalo kilomita tano kutoka kwa kinamasi hiki. Juhudi hizo zilishirikisha kuwashinikiza kukoma kulima kwenye vipande vidogo vidogo vilivyokuwa kando mwa kinamasi chenyewe na kuanza kupanda miti ya asili aina mbalimbali ikiwemo aina ya Acacia kwenye mipaka yake. Hatua hii ilisaidia sana eneo hilo chepechepe kurejelea hali yake ya awali na kuwezesha uleaji wa Korongo wenye afya nzuri. Kiasi cha idadi yao kuongezeka kufikia 35 kulingana na hesabu iliyofanywa katika eneo chepechepe la Kipsaina mnamo Desemba 2009.

MUHTASARIULISHINDA TUZO YA EQUATOR: Mwaka 2006

ULIANZISHWA: Mwaka 1990

ENEO: Magharibi mwa Bonde la Ufa, Kenya

WANAOFAIDI: Kipsaina na jamii za karibu

MAZINGIRA: Mbuga ya kitaifa ya Kinamasi cha Saiwa

3

KIPSAINA CRANE AND WETLANDS CONSERVATION GROUPKenya

YALIYOMOHistoria na Mandhari 4

Majukumu Makuu na Ubunifu 5

Matokeo ya Kimazingira 7

Matokeo ya Kijamii 7

Matokeo ya Kisera 8

Jinsi ya Kudumisha Mradi Huu 9

Maono 9

Wahisani 9

4

Kikundi cha Kipsaina Cranes and Wetlands Conservation kilianza kazi yake mwaka 1990, na kilisajiliwa rasmi kama kikundi cha kijamii katika mwaka 1991. Kikundi hiki kinajishughulisha na mradi wa kuhifadhi maeneo chepechepe kwa kutumia mbinu za kulinda mazingara tofauti tofauti katika mbuga ya Kitaifa yenye Kinamasi cha Saiwa inayopatikana magharibi mwa Kenya. Kinamasi hiki kinapatikana nyanda za chini zilizoko wilayani Trans Nzoia kati ya Mlima Elgon na miinuko ya Cherangani, pembeni mwa Bonde la Ufa. Mito mingi hupitia katika eneo hili ikielekeza maji yake kwenye ziwa Victoria na kati ya mito hii ni ile ya Saiwa na Kipsaina ambayo imechangia kuwepo kwa msitu na kinamasi kaskazini mwa mji wa Kitale. Kinamasi cha Saiwa ambacho kiliwekwa rasmi kwenye gazeti la serikali mnamo 1974, ndicho kinaunda Mbuga ndogo ya Kitaifa nchini. Kuanzia 1991 mpaka 2003, lengo kuu la kikundi hiki lilikuwa ni Kinamasi cha Saiwa, lakini tangu hapo lengo letu limepanuliwa zaidi na sasa tunaangazia sana eneo la kilomita tano kutoka Saiwa mpaka kijiji cha Kipsaina. Kulinda mbuga ndogo ya kitaifa ya Kenya.

Kikundi hiki kilianza kwa kukabiliana na uharibifu wa wanadamu wa mifumo mbalimbali ya ikolojia katika kinamasi cha Saiwa na eneo zima la Kipsaina. Mbuga nzima pamoja na wanyama pori wote walitishiwa kuangamia kutokana na mitindo wa maisha ya wakaazi wa eneo hili ikiwemo uvunaji wa changarawe, ulishaji wa mifugo kupita kiasi, uchimbaji mitaro ya kuondoa maji ili kukausha sehemu yenyewe, kuwaua wanyama pori kutokana na kemikali za mbolea zilizotumika katika ukuzaji mimea pamoja na desturi haramu ya kukata kuni katika sehemu iliyolindwa.

Eneo linaloambatana na mto Kipsaina lilitumika kwa shughuli za ukulima, jambo lililosababisha kupungua kwa ukubwa wa mto mwenyewe na hata kuwafanya wanyama pori kuhamia kwingineko. Kikundi hiki cha uhifadhi wa Kipsaina kilibuniwa kwa madhumuni ya kukabiliana na changamoto hizi na kukiwezesha kinamasi hiki

kuwa chenye kutegemea jamii ya eneo hili kukitunza na kukihifadhi ili kuzuia kuangamia kwake. Kazi kubwa ya kikundi hiki ilikuwa kuhamasisha wakaazi wa eneo hili kukomesha shughuli zao za ukulima maeneo chepechepe na kazi hii ilitekelezwa sana na kiongozi mkuu wa parokia ya kanisa la kikatoliki eneo hili ambaye alifanikiwa kuwaaminisha wakaazi wa Kipsaina kuhifadhi na kukitunza kinamasi cha Saiwa katika mazingara yake ya asili.

Lengo kuu lilikuwa kuanza kurekebisha sehemu zilizokuwa zimeathirika sana ndani na nje mwa kinamasi kwa kupanda miti, huku malengo mengine yakiwa katika kuwafidia wakaazi kwa manufaa waliyokuwa wakipata kutoka eneo hilo chepechepe. Hili lilishirikisha kuwapa vitu mbadala vikiwemo maji safi ya matumizi, nyasi kavu kama chakula cha mifugo yao badala ya kuwalisha kwenye eneo chepechepe pamoja na kuwafunza mbinu zingine za kujipatia riziki ya kila siku badala ya kutegemea ukulima pekee. Kikundi cha Kipsaina kilianzisha ukulima ambao hauathiri mazingara ya eneo hili kama vile ufugaji wa samaki, upanzi wa miti, ufugaji wa nyuki, ufugaji wa kuku na hata ufugaji wa sungura pamoja na uuzaji wa vinyago, kozi za uelekezaji wa watalii ili kuinua utalii katika eneo hili. Kupitia mbinu hizi mbadala za kujikimu kimaisha, kikundi hiki kimefanikiwa kurekebisha eneo hili chepechepe na hata kuimarisha maisha ya wakaazi wake.

Jambo kubwa la kujivunia kutoka kwa shughuli hizo ni kurejea kwa wingi kwa aina mbalimbali ya wanyama pori katika maeneo haya chepechepe, wakiwemo paa maarufu kama Sitatunga na Korongo wenye kofia ya rangi ya kijivu.Kazi nyingi ya kikundi cha Kipsaina imekuwa ikifadhiliwa sana na wakfu wa International Crane Foundation, na eneo hili limeangaziwa sana na vyombo vya habari vya kimatifa kama vile BBC na African Wildlife Foundation ambavyo vimekuwa vikirekodi vipindi kuhusu eneo lenyewe. Kutambulika kwa kikundi hiki katika ngazi za kimataifa kumekifanya kuwa mfano bora wa kikundi cha kijamii kinachotumia mbinu za kinyumbani katika jitihada za kuhifadhi mazingara nchini Kenya.

Historia na Mandhari

55

Majukumu Makuu na Ubunifu

Mtindo uliotumika na kikundi cha Kipsaina katika uhifadhi ulitegemea sana kuwahusisha wakaazi wa eneo hili, na ulihushisha utunzaji wa eneo chepechepe kwa ujumla hadi mbuga ya kitaifa ya Kinamasi cha Saiwa. Shughuli hii iliwahusisha sana wakaazi wa eneo hili kwa vile maeneo chepechepe yalikuwa yakitumika kwa ukulima, ulishaji mifugo pamoja na kuwa chanzo cha maji ya matumizi huku msitu ukikatwa kwa ajili ya kuni na mbao. Ili kukomesha shughuli hizo za kibinadamu katika eneo hili na kusitisha uharibifu zaidi wa mazingara kikundi cha Kipsaina kililazimika kubadilisha mitindo ya maisha ya wakaazi wa hapa kwa kuwahamasisha juu ya umuhimu wa kuhifadhi maeneo muhimu kama haya kwa kuanzisha miradi ambayo ingewezesha uhifadhi huo na hata kuwafunza juu ya mbinu mbadala za kujikimu kimaisha.Sehemu ya kwanza ya shughuli hii iliafikiwa kupitia ushirikiano na waumini wa kanisa moja la eneo hili; ambako uhifadhi wa maeneo chepechepe ulichukuliwa kama jukumu nzima la wakaazi wote wanaomiliki mashamba hapa.Hili lilikuwa jambo muhimu sana katika kuanzisha na kuendeleza mpango wenyewe lakini baadaye ukapigwa jeki kutokana na manufaa yaliyopatikana kutoka kwa mbinu mbadala za kujikimu kimaisha ambazo haziathiri mazingara.

Uhifadhi kupitia upanzi miti

Ufanisi mkubwa wa kikundi cha Kipsaina umepatikana kupitia uwezo wake wa kukuza miche ya miti ya asili na kisasa kwa wingi. Kwa sasa kikundi hiki kina uwezo wa kutoa miche 100,000 kwa mwaka, ikiwemo zaidi ya miti 20 aina mbalimbali.Mpango huu umewashirikisha wahusika mbali wa eneo hili wakiwemo wanafunzi wa shule, vikundi vya kina mama, waumini wa makanisa pamoja na vikundi vya vijana. Miche ya miti ya asili hupewa wakaazi wa eneo hili kupanda ili kuongeza idadi ya miti na kuunda kinga maalum ya eneo chepechepe, ili hali ile miche ya miti ya kisasa huuzwa ili kuleta mapato yanayotumika kufadhili shughuli za kikundi za kutekeleza malengo yake.

Upanzi wa miti pembeni mwa maeneo chepechepe pamoja na maeneo kavu yaliyokando wa maeneo haya kumechangia pakubwa kukabiliana na tatizo la mmomonyoko wa udongo na hili limesaidia sana katika kuendelea kuwa kwa makazi ya wanyama pori wanaorejea kwa wingi.

Sehemu kumi mpya zitakazotumika kwa kupanda miche ya miti katika wilaya kumi zinazopakana na eneo hili zinapangwa kuanzishwa ili kuongeza manufaa ya kupitia mradi huo wa upanzi wa miti kwa kutumia ujuzi wa wanachama wa kikundi cha Kipsaina. Sehemu hizi zitatambuliwa kwa kutumia vigezo kama vile uwezo au uwepo wa makazi ya wanyama pori. Kikundi hiki kinapania kukuza miche millioni moja ambapo miche 100,000 itapandwa katika kila sehemu mpya. Wahusika wengine kama vile waumini wa makanisa, wanafunzi, vikundi vya kina mama na vijana waliokaribu na sehemu hizi mpya watatumika katika miradi hii. Kufikia sasa sehemu tatu zimetambuliwa katika maeneo ya Trans-Nzoia, Bungoma, na msitu wa Kakamega.

Uwekazaji ili kuimarisha hali ya maisha na uhamasishaji Katika mbuga ya kitaifa ya Kinamasi cha Saiwa na eneo, shughuli za kibinadamu zenye madhara zimepungua kupitia hatua mbalimbali zilizochukuliwa. Hatua kubwa iliyofanikisha shughuli hii ni ufadhili wa kifedha kutoka kwa Disney Worldwide Conservation Fund kupitia wakfu wa International Crane Foundation mnamo 2003. Mojawapo wa uzinduzi ulikuwa kuwapa wakulima miche ya miti ya kupanda bila malipo na pia kuwafunza umuhimu wa kusitisha kukata miti katika maeneo chepechepe kwa ajili ya kuni. Vyanzo vipya vya maji vimepatikana kutokana juhudi hizo za kuhifadhi vyanzo vya maji katika mbuga ya kitaifa jambo ambalo limepunguza matumizi ya maji yanayopatikana katika maeneo yanayostahili kuhifadhiwa.

Mipango pana ya kuwahamasisha wakaazi kupitia mafunzo, semina ilikuwa muhimu katika juhudi za kuwarai wakulima kukoma kulisha mifugo wao katika mbuga. Ili kufanikisha hili, kikundi cha

66

Kipsaina kilianzisha upanzi wa nyasi ndefu kando mwa mito ili kuzuia mmomonyoko wa udongo na pia nyasi zenyewe kutumika kama chakula cha mifugo wa wakulima hao badala ya kuendelea kuwalisha kwenye kinamasi cha Saiwa.

Walionufaika sana na jitihada hizi za kikundi cha Kipsaina ni wakaazi wa maeneo yanayopatika katika nyanda za juu na chini mwa Saiwa na Kipsaina. Wengi wa wakaazi hawa ambao ni wanawake na vijana wameshawishika na kuanza kutumia mbinu mbadala za kujikimu kimaisha.Mafunzo yamekuwa yakitolewa katika kituo cha kutolea maelezo cha kikundi hiki ambako wakaazi wamepata fursa ya kujionea jinsi ya kufuga nyuki, samaki, kuku na sungura pamoja na ukulima wa mbinu za kisasa zisizoathiri mazingara miongoni mwa vitu vingi.

Mafunzo haya yametiwa nguvu sana na mafunzo ya ziada kuhusu mazingara kutoka kwa vijana wa eneo hili. Mwanzoni shule 16 zikiwemo shule za msingi kumi na sita za upili zilipewa miche ya miti na mizinga ya nyuki katika juhudi za kuwahusisha vijana kwenye uhifadhi. Shule hizi pia hushiriki mashindano ya michezo ya kuigiza yenye mada kuhusu utunzaji wa mazingara.Uhamasisho wa umuhimu wa kuhifadhi eneo chepechepe pia umeenezwa kwa jamii nzima kupitia nyimbo na michezo ya kuigiza hasa wakati wa sherehe

za kuadhimisha siku kuu ya Mazingara (World Environment Day) na siku kuu nyingine za kitaifa.

Ustawishaji wa utalii katika eneo la Kipsaina bado unaendelea lakini linalodhihirika wazi ni mapato makubwa yatakayopatikana kupitia mpango huu. Kwani mwanzoni watalii waliotembelea Mbuga ya Kitaifa ya Kinamasi cha Saiwa walipitia Kipsaina jambo ambalo liliinua sana soko la vinyago katika sehemu hii na kuwaletea mapato wakaazi kwa wingi. Kwa sasa, barabara mpya iliyojengwa imebadilisha taswira ya eneo hili kwa kulifanya kuwa rahisi kufikiwa. Mbali na hayo, kikundi cha Kipsaina kimetafakari uwezakano wa kujenga sehemu muhimu za kujionea wanyama pori katika eneo hili. Kwa kufanya hivyo itakuwa rahisi kwa watalii kuwaona paa wanaofahamika kama Sitatunga ambao huishi majini na pia nchi kavu pamoja na Korongo wenye kofia ya rangi ya kijivu katika eneo hili.

Katika kumalizia, kikundi cha Kipsaina pia kimeshiriki katika utafiti wa mbinu mbadala za kimaisha katika eneo kwa ushirikiano na mabingwa wa utafiti na wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Moi, Kenyatta na Nairobi kutoka Kenya, na wale chuo kikuu cha Makerere kutoka Uganda.

“Ningependa kuwashauri wakenya na hata jamii za kimataifa kuchangia katika juhudi za kuhifadhi mazingara. Kwani tukishindwa kufanya hivyo hatima yetu itakuwa taabani.Mwanadamu

aliumbwa wa mwisho na kukabidhiwa dunia kuitunza bali sio kuiharibu.” Maurice Wanjala, Kipsaina Crane and Wetlands Conservation Group

Kinamasi cha Saiwa, 1990 Kinamasi cha Saiwa, 2006

7

Matokeo

MATOKEO YA KIMAZINGIRABustani ya miche inayotumika kama sehemu ya kutolea mafunzo ya maelezo na kikundi cha Kipsaina, kina miche aina 15 ya miti ya kiasili pamoja na aina tano ya kisasa. Hii inajumuisha: Prunus Africana, Cordia Africana, Melia, Albizia Gummifra, Sizygium, acacia, Bischovia, Olea (Olea Africana and Olea Welwich), Graveria, Spathodea Nilotica, Markhamia Lutea, seda, mnazi (jamii ya Phonex), Melidia Dura, Vitex Kinyensis, Croton Megalcarpus, Maesopis Eminii, ash, Eucalyptus Grandis, cypress, na Caleantra. Uenezaji wa aina mbalimbali ya miti hii na nyingine ya jamii tofauti katika maeneo yanayozingira eneo hili chepepe, yamekuwa matokeo makubwa ya shughuli za kikundi cha Kipsaina za kuhifadhi maeneo muhimu yaliyokuwa yakikaribia kuangamia.

Aina hii ya miti ilichaguliwa kutokana na manufaa yake mengi tofauti tofauti, ikiwemo uwezo wake wa kuhimili na kukua kwa haraka katika sehemu tofauti za ulimwengu na pia uwezo wa kuenea kwa haraka. Ubora huu umeifanya miti hii kuwa nguzo muhimu katika kuunda kinga kwa maeneo chepechepe. Mingi ya miti hiyo ina manufaa ya kutoa dawa za kutumiwa na wanadamu, inaweza kutumika katika kutoa mbao pamoja na makaa. Mingine kati ya miti ya asili kama vile mikalutusi na seiprus huuziwa wakulima kwa bei nafuu ili kuwapa nao pia nafasi ya kuipanda katika mashamba yao kwa sharti kuwa hawaipandi maeneo yaliyo chepechepe. Aina nyingine ya miti inaweza kutumiwa kwa kuwafuga nondo wa kulisha mifugo au hata kutumika kuwekea mizinga ya nyuki. Nayo miti ya Acacia huwa mizuri sana kwa kutumika na korongo kujenga viota vyao na mahala pa kupumzikia. Mbuga ya kitaifa ya Kinamasi cha na eneo chepechepe la Kipsaina ni makazi asili ya asilimia 25 ya Korongo wenye kofia la rangi ya kijivu nchini Kenya. Kulingana na hesabu za hivi karibuni katika eneo hili iliyofanyika mwezi Desemba 2009 ilipatikana kuwa Korongo 35 wanaishi eneo hili. Ndege wengine wanaopatikana eneo hili wanajumuisha Turaco wa rangi ya samawati na wale wa rangi ya

kijivu pamoja na ndege wanaojulikana kama Ibis. Na ni asilimia 78 ya ndege hawa wameonekana katika eneo hili lililochini ya uhifadhi. Pia kuna paa 22 aina ya Sitatunga na kikundi kidogo cha familia ya nyani sita aina ya De Brazza, Vervet na Mbega (Colubus). Eneo hili pia ni makao ya aina nyingine ya wanyama wakiwemo Nguchiro wa majini, majoka makubwa meusi na kijani kibichi, pamoja na Cobra. Pia kuna mimea aina mbalimbali kama vile Tipha, nyasi aina ya Sedge miongoni mwa nyingine. Idadi hii ya wanyama na ndege ni ya juu ikilinganishwa na wakati juhudi za kuhifadhi zilikuwa ndio zimeanzishwa katika mwaka wa 2003 wakati eneo hili lilionekana kuathirika sana kutokana na shughuli za kibinadamu. Aina hii ya wanyama tofauti wamekuwa wakirejea wenyewe kutokana na kuimarika kwa makazi yao kutokana na shughuli za kujitolea kwa kikundi cha Kipsaina za kuhifadhi maeneo haya; hata mimea ya asili imeongezeka kiasi cha kutaka kuwepo na mipango ya kudumu kwa ajili ya mradi huu. Usimamizi na ufuatiliaji wa mradi huu wa mbinu mbadala za kimaisha katika eneo hili hutekelezwa na wanafunzi wa shule kwa ushirikiano na walimu wao. Jukumu lao haswa huwa katika kutambua jamii mpya za wanyama na mimea, kuwahesabu ndege aina ya Korongo angalau mara mbili kwa mwaka kwa ushirikiano pia na wenye kujitolea.

MATOKEO YA KIJAMIIMatokeo ya kiuchumi kwa jamii kutokana na kazi za kikundi cha Kipsaina yaliathirika sana kutokana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 nchini ambazo zilikithiri sana katika mkoa wa Bonde la Ufa. Hata hivyo kikundi cha Kipsaina kimefanikiwa kuendeleza shughuli za kuleta mapato katika maeneo bunge kadhaa iliyokusudia, hatua ambayo imechangia kupatikana kwa manufaa mengi ya kijammi na kiuchumi kwa wakaazi wake. Shughuli hizi zilijumuisha uuazaji wa vinyago na bidhaa nyingine za kitamaduni kwa watalii pamoja na biashara nyingine ambazo hazikuathiri mazingara. Katika mwaka wa 2003, wakfu wa International Crane Foundation kwa ushirikiano na kikundi cha serikali, ulifanya zoezi la kukagua

mradi uliofadhiliwa na fedha kutoka kwa shirika la Disney Worldwide Conservation Fund, wakizingatia sana mradi wa ukulima wa samaki ulioanzishwa na kikundi hiki. Kikundi cha Kipsaina kilikuwa kikifanya uchunguzi wa ukulima wa samaki wa jinsi moja ambao ulishirikisha ukulima wa samaki wa kiume pekee katika kidimbwi kimoja, ukulima ambao ulichangia kupatikana kwa samaki wakubwa. Kwa wakati huo, samaki mmoja aliuzwa kwa Sh 250 na kila kidimbwi kilikuwa na idadi ya samaki wapatao 1000. Wakulima walitarajia kupata mapato ya Sh 250,000 kutoka kila kidimbwi. Ukulima huu wa samaki na shughuli nyingine kama ufugaji wa nyuki na kuku ulisaidia kupunguza shughuli za kibinadamu za kujipatia riziki kutoka maeneo chepechepe.

Katika mfano, kikundi cha Kipsaina kilifanya kazi kwa ushirikiano na kikundi cha kina mama cha Bwayi, kwa kukisaidia na samaki wa kufuga, miche ya miti ya kupanda. Kwa bahati mbaya miradi hii ilianguka kufuatia ghasi za baada ya uchaguzi wa 2007. Sehemu ya kikundi hiki ya kukuza miche ya miti na hata kutumia kuwapa mafunzo wakaazi iliathirika baada ya wanachama wa kikundi kuondoka lakini kwa sasa sehemu hiyo imeanza kurejelea hali yake ya awali.Dhamira kuu ya kikundi hiki cha Kipsaina ya kuendelea kuwasawishi wakaazi kujishughulisha na shughuli za maisha ambazo haziathiri mazingara zitaendelea kuwanufaisha kiuchumi na kijamii mbali na dhamira hii kuwa kigezo kikuu cha ufanisi wa shughuli za kikundi hiki.

MATOKEO YA KISERAKikundi cha Kipsaina kimejihusisha sana katika uungaji mkono wa kubuniwa kwa sera za ustawi kutoka kwa idara mbalimbali za serikali. Kufanya kazi na Mamlaka ya Mazingara (NEMA), wizara ya Kilimo

pamoja na idara nyingine za serikali katika ngazi tofauti kuanzia mashinani hadi wilaya na jata kufikia kitaifa kumekipa kikundi hiki sauti katika uundaji na ubunifu wa sera zinazowahusu wakaazi na mazingara yao. Kwa mfano kikundi cha Kipsaina kimeandaa mikutano ya mazingara katika ngazi ya wilaya na hata ilikabidhiwa kipande cha ardhi na wizara ya kilimo kwa minajili ya kuendeleza upandaji wa miche ya miti.

Mkuregenzi wa kikundi hiki ni mwanachama wa NEMA, ambayo imekuwa ikitumia Kipsaina kama mfano wa kuiga katika jitihada za uhifadhi wa mazingara nchini Kenya. Kushirikishwa katik idara hii ya kitaifa kumekipa kikundi hiki nafasi kushiriki katika mazungumzo ya kuleta uwiano katika tofauti za kisheria zilizoibuka kati ya idara mbalimbali za serikali. Kwa mfano sheria kuhusu kilimo, maji na haki za mashamba ambazo ziliibua tofauti katika kueleza bayana kati ya mali ya kibinafsi na umma: ushirikiano katika kufafanua sheria hizi kulipitishwa baada ya kufanyika kwa ushawishi wa pamoja ambako Kipsaina ilikuwa mstari wa mbele. Hivi karibuni kikundi cha Kipsaina kimekuwa kikijaribu kuwashawishi wahusika kuleta mabadiliko katika sera ya wanyama pori ambako kinataka wakulima wawe wakifidiwa mimea yao inapoharibiwa na wanyama hao. Mara nyingi wanachama wa kikundi cha Kipsaina wamehisi kuwa wanakabiliwa na upungufu wa vifaa maalumu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya uhamasishaji na uungaji mkono wa maswala muhimu yanayowahusu. Hata hivyo hili lilishughulikiwa mnamo mwaka 2010 wakati shirika la ufadhili la World Wildlife Fund lilipowaalika wanachama wanne kwa mafunzo kuhusu kutafuta ushawishi juu ya maswala ya mashamba kama sehemu ya maandalizi ya kukaribisha katiba mpya mwaka wa 2010. Kikundi hiki kimeendelea kuwa mstari wa mbele katika maswala ya uhifadhi wa mazingara nchini Kenya hasa kupitia ushirikiano wake na NEMA.

8

9

Jinsi ya Kudumisha Mradi Huu

JINSI YA KUDUMISHA MRADI HUUKatika njia za kujifadhili, kikundi cha Kipsaina kimekuwa kitegemea sana mapato kutoka kwa uuzaji wa miche ya miti ya asilia ili kuendeleza shughuli zake.Biashara hii ndio imekuwa chanzo pekee ya fedha kwa kikundi hiki kwa sasa,hata hivyo ufadhili uliotolewa na wakfu wa International Crane Foundation katika mwaka wa 2003 ndio fedha pekee kutoka nje ambazo kikundi hiki kilipokea pamoja na mafunzo ambayo wakfu huo umekuwa ukiwapa wanachama wakati mwingine. Licha ya uchache huo wa ufadhili juhudi za uhifadhi za kikundi hiki zimekuwa za kuvutia. Ufanisi wa kikundi hiki ambao umeshuhudiwa mpaka sasa umetokana na ushirikiano mzuri kati ya kikundi na wakaazi wa maeneo husika. Na hili limechangia sana kuwa mstari wa mbele katika shughuli ambazo zimetekelezwa na baadhi ya wanachama katika maswala ya ustawi wa jamii. Kati ya wanachama hawa ni pamoja na Maurice Wanjala ambaye ndiye nguzo muhimu katika ushawishaji wa uhifadhi na ustawi kwa kuwahusisha wakaazi. Pia alikuwa nguzo muhimu katika kuundwa kwa kikundi na amekuwa mkuregenzi wake tangu kilipobuniwa. Ushirikiano wake na Parokia ya Kanisa Katoliki, ambayo alianzisha katika eneo la Kipsaina umechangia sana kukubalika kwa undani kwa kazi yake katika shule nyingi na hata wakaazi wa eneo hili. Kikundi cha Kipsaina kimekuwa kikishirikisha waumini jambo ambalo limefanya kuendelea kwa miradi ya uhifadhi wa maeneo chepechepe na vitongoji vyake.

Mbali na hayo, ili kuendelea kudumu siku zijazo na kuimarisha juhudi zake za ustawi, kikundi cha Kipsaina kinahitaji sana kusaidiwa ili kukiwezesha kudumu. Mojawapo wa usaidizi huo ni ufadhili wa kukiwezesha kununua vifaa vya kisasa kwa ajili ya miradi yake kama vile miche ya miti zaidi. Ufadhili pia unahitajika katika kufanikisha kuwapa mafunzo wanachama wake katika nyanja mbalimbali za kisayansi, utafiti kuhusu kudidimia kwa aina fulani ya wanyama katika eneo la Kipsaina pamoja na utafiti wa nyasi bora za kupanda kando mwa mito.

MAONOMtindo sawa wa utenda kazi wa kikundi cha Kipsaina umeanzishwa katika miji ya Bungoma na Eldoret ambako upanzi wa miche ya miti umezinduliwa. Awali katika sehemu hizi paa almaarufu Sitatunga walikuwa wakiwindwa na wawindaji haramu na vinamasi kukaushwa lakini sasa mafunzo yaliyoanza kutolewa na wanachama wa Kipsaina kwa kuuhamasiha umma umuhimu wa utunzaji wa mazingara kumeonekana kusaidia na kukomesha uharibifu huo. Wanachama wa Kipsaima walifanikiwa kuwashawishi wakaazi wa sehemu hizi kuhifadhi vinamasi kwa manufaa ya kuendeleza utalii badala ya kuvikausha kwa ajili ya ukulima hasa kutokana na kuwa karibu na barabara kuu ya Kapsabet-Eldoret.Mafunzo hayo yalifanikishwa kwa ushirikiano kati yetu na mpango wa kutunza maeneo chepechepe ya ziwa Victoria (Lake Victoria Wetlands Management Programme). Na miradi zaidi mwenza inatarajiwa kuanzishwa katika sehemu kumi zitakazoanzishwa kama mahala pa kupanda miche za miti.

WAHISANIWashirika wengi wamekuwa wakishirikiana nasi katika kufanikisha juhudi zetu za uhifadhi na ufanisi wa ustawi. Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya washirika wetu:

• Wakfu wa International Crane Foundation ambao wamekuwa mstari wa mbele katika washirika kwa kufanya kazi nasi tangu 1992.

• UNDP Equator Initiative• Endangered Wildlife Trust• World Wildlife Fund• Shirika la Wanyama Pori Nchini (KWS)• Makavazi ya Kitaifa ya Kenya• Wizara ya Kilimo • Mamlaka ya Mazingara (NEMA)• Kituo cha Utafiti wa Misitu (KEFRI)• Mpango wa uhifadhi wa maeneo chepechepe ya Ziwa

MAREJELEO YA ZIADA

• International Crane Foundation spotlight on Kipsaina: savingcranes.org/the-kipsaina-crane-and-wetlands-conservation-group.html • Kipsaina Crane and Wetlands Conservation Group PhotoStory (Vimeo) vimeo.com/15780448 (English) vimeo.com/15780521 (Swahili)

Equator InitiativeEnvironment and Energy GroupUnited Nations Development Programme (UNDP)304 East 45th Street, 6th Floor New York, NY 10017Tel: +1 646 781 4023www.equatorinitiative.org

Mradi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa ndio unaoendesha miradi ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa kote ulimwenguni kwa kutoa mwito wa mageuzi na kuelekeza mataifa kwa maarifa, na malighafi ili kusaidia watu kujiimarisha kimaisha.

Mradi huu wa Equator huleta pamoja Umoja wa Mataifa , serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, wafanyibiashara na makundi ya mashinani ili kutambua na kuimaliza maendeleo himili kwa watu na jamii kwa jumla.

©2012 Haki Zote ni za Mradi wa Equator

Masimulizi kuhusu miradi mingine, bonyeza hapa: