34
M W O N G O Z O W A M A F U N Z O O YA KILIMO MSETO November, 2019 KITINI NAMBA 3:

KITINI NAMBA 3: MWONGOZO WA MAFUNZOO YA KILIMO … › fileadmin › 02_documents › 15...mazao (Alley cropping), uchanganyaji wa miti ya kudumu na mazao na mfumo wa kuchanganya bila

  • Upload
    others

  • View
    11

  • Download
    4

Embed Size (px)

Citation preview

  • MWONGOZO WA MAFUNZOO YA KILIMO MSETO

    November, 2019

    KITINI NAMBA 3:

  • 2

    YALIYOMO 1. KILIMO MSETO/MISITU (AGROFORESTRY) NI NINI? ............................ 3 2. UMUHIMU AU LENGO LA KILIMO MSETO .............................................. 3 3. KILIMO MSETO HUFANYIKA WAPI NA KWA WAKATI GANI?............. 4 4. JINSI YA KUFANYA KILIMO MSETO ......................................................... 5

    4.1 Vitu vya msingi kwenye kilimo mseto ............................................... 5

    4.2 Mgawanyiko wa mifumo ya kilimo mseto ........................................ 6

    5. TABIA YA MITI INAYOFAA KWA KILIMO MSETO .................................. 9 6. UHUSIANO WA KIUTENDAJI KATI YA MITI, MAZAO NA MIFUGO .... 11

    6.1 Ni jinsi gani mazao yananufaika na uchanganyaji na miti (ni jinsi gani miti hustawisha udongo) .................................................................. 11

    6.2 Ni kwa namna gani miti inanufaika na mchanganyiko wa mazao na miti. ............................................................................................................... 14

    6.3 Ni kwa vipi mifugo hunufaika na kilimo mseto.............................. 15

    7. Upandaji miti na ukaaji wake shambani ................................................ 15 8. KITALU CHA MICHE YA MITI .................................................................. 18

    8.1 Kitalu cha Miti ni nini? ....................................................................... 18

    8.2 Umuhimu wa kitalu ............................................................................ 18

    8.3 Uanzishaji wa kitalu cha miti............................................................. 18

    8.4 Kuandaa miche kwa ajili ya kupanda shambani ............................ 23

    8.5 Jinsi ya kupanda miche ya miti shambani ....................................... 23

    9. MAMBO YANAYOATHIRI MCHANGANYIKO WA MITI NA MAZAO KWENYE KILIMO MSETO .............................................................................. 25 10. MABADILIKO YA TABIA NCHI NA KILIMO MSETO .............................. 27 11. MAMBO MUHIMU YA KUYAJUA KWENYE KILIMO MSETO (MUHTASARI) ................................................................................................. 29

  • 3

    1. KILIMO MSETO/MISITU (AGROFORESTRY) NI NINI?

    Ni kilimo kilicho hai, kilimo chenye kuhusishwa na mazingira bora, mfumo wa usimamizi wa maliasili (mfano: misitu) ambao, kwa kupitia mchanganyiko wa miti mashambani au kwenye ardhi ya kilimo, hupanua wigo na kuongeza uzalishaji na hivyo kuongeza uchumi katika ngazi ya familia hadi Taifa na kuongeza faida katika utunzaji wa mazingira katika ngazi zote za watumiaji wa ardhi. (Picha 1: Chanzo – USDA United States Department of Agriculture)

    2. UMUHIMU AU LENGO LA KILIMO MSETO

    (a) Husaidia kuongeza rutuba kwenye udongo na hakuna ushindani, hivyo huongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na mazao mengine shambani.

    (b) Husaidia kuongeza kipato cha kutoka shambani kwa kuwa aina mbali mbali za mazao hupatikana kwa mara moja.

    (c) Husaidia kupunguza uharibifu wa mazingira pale miti inaponyonya hewa chafu ya kaboni angani.

    (d) Mahitaji ya mazao ya miti kwa wanajamii ni mengi na hii hupelekea uharibifu na au utowekaji mkubwa wa misitu; kwa hiyo upandaji wa

  • 4

    miti mashambani husaidia kupunguza kasi hiyo ya uharibifu kwa kuwa mazao ya miti hupatikana pia mashambani.

    (e) Ongezeko la watu limesababisha pia kuwepo na ushindani wa ardhi yenye rutuba, kukosekana kwa ardhi hiyo ndiko kunakosababisha uharibifu mkubwa wa misitu, urutubishaji ardhi kwa njia za kiasili hufanya kutumika kwa muda mrefu bila kuchoka

    (f) Hupunguza gharama za kurutubisha ardhi ukilinganisha na njia nyingine za kutumia mbolea za viwandani.

    (g) Miti ni chanzo cha upatikanaji wa malighafi za viwanda na nishati kwa ajili ya jamii.

    (h) Upandaji miti ni moja ya utekelezaji wa Sera mbalimbali za serikali.

    3. KILIMO MSETO HUFANYIKA WAPI NA KWA WAKATI GANI? Maeneo yenye ardhi finyu kwa maana ya uhaba au shida ya ardhi yanafaa sana kufanyika kilimo mseto kwa kuwa mazao ya aina tofauti tofauti huweza kupatikana kwenye eneo moja kwa wakati mmoja au nyakati tofauti.

    Aidha eneo linaweza kuwa dogo mfano wa bustani moja au eneo la shamba lenye ukubwa wa kadri kwa ajili ya kurahisisha usimamizi na kuona matokeo ya kazi inayofanywa kwa urahisi.

  • 5

    4. JINSI YA KUFANYA KILIMO MSETO

    4.1 Vitu vya msingi kwenye kilimo mseto a) Aina ya miti – Mimea yenye asili ya miti o Mimea yenye shida moja inayokua kwa zaidi ya mita 6 o Vichaka (Mimea miti yenye mashina zaidi ya moja chini ya mita 6) o Miti ya mizabibu o Mianzi nk. b) Mazao ya kilimo c) Wanyama

    Matarajio ya Mkulima kwenye kilimo Mseto

    Tija (Productivity) kwenye Mazao (kwa maana ya uzalishaji wa kutosha)

    • Uendelevu (Sustainability) wa upatikanaji wa mazao na chakula

    • Kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na ya

    Mchoro 1. Mistari ya Miti na Mazao shambani

    (Alleys) (Chanzo: ICRAF – A tree for all reason)

    Picha 2: Mistari ya miti ya Grevelia na mahindi

    kwenye eneo moja. (Chanzo: Daisy Ouya/ICRAF)

  • 6

    ardhi ya kilimo (Adaptability & mitigation)

    4.2 Mgawanyiko wa mifumo ya kilimo mseto

    a) Mfumo wa Ukuaji wa pamoja (Simultaneous systems) ambapo miti au vichaka vya miti na mazao hupandwa na kukua pamoja katika eneo moja katika mipangilio tofauti tofauti; mfano kuhusisha miti kwenye shamba la mazao, safu ya miti kama ua ikichanganywa na mazao (Alley cropping), uchanganyaji wa miti ya kudumu na mazao na mfumo wa kuchanganya bila utaratibu maalum.

    b) Mfumo wa kupanda kwa utaratibu (Sequential systems)

    Hapa miti na mazao hupandwa kwa mzunguko; mfano inahusisha mzunguko wa upumzishaji shamba kwa kuliacha liote pori au kulipanda miti au kupanda aina nyingine ya mazao. Hata hivyo baadhi ya mifumo mingine kama vile ule wa shamba la miti lililovunwa na kuruhusu upandaji wa mazao ya chakula halafu baadaye tena kupanda miti ndani na mazao kukoma kupandwa baada ya miti kufunga (taungya) ni mfano mmojawapo, mchanganyiko wa mzunguko kwenye mistari, mzunguko kwenye eneo dogo lililopandwa miti, na uelewa wa mazao kwenye eneo lililopandwa miti unakuwa na tabia za pamoja kama zilivyo kwenye mfumo wa ukuaji wa pamoja au mfumo wa upandaji kwa utaratibu.

    Hata hivyo, kuna mifumo mingine ambayo mizunguko ya miti kwenye maeneo, huunganisha matokeo ya pamoja ya tabia za mfumo wa ukuaji wa pamoja na mfumo wa upandaji kwa utaratibu. Kwa maelezo mengine katika kuelezea kilimo mseto na mifumo yake ya kufuatwa, kuna aina muhimu kuu tatu za kukielezea kilimo mseto na mgawanyo wake kwenye matumizi ya ardhi:

  • 7

    Mifumo ya upandaji kwa utaratibu:

    i. Miti inayoota kwa pamoja na Mazao (Agrisilviculture) - hutumika zaidi kuliko agrosilviculture. - Hii inaelezea muunganiko wa miti na mazao tu mfano; 1. Miti kwenye shamba 2. Miti kwenye shamba lililopumzishwa 3. Miti kwenye mipaka na Miti kwenye Misitu, Ardhi yenye miti na

    mashamba madogo ya miti (Taungya – Mazao yaliyopandwa kwenye eneo la msitu iliyovunwa na baadaye miti kupandwa wakati mazao yanaendelea kuota)

    4. Miti pembezoni mwa njia za maji.

    Picha 3: Miti kwenye shamba la kahawa

    (Chanzo: Greentumble sustainable farming)

  • 8

    ii. Miti kwenye malisho na ardhi za ranchi (Silvipastoral) – Miti inayoota kwa pamoja na malisho ya mifugo.

    iii. Miti inayoota kwa pamoja na mazao na malisho ya mifugo (Agrosilvopastoral) hutumika zaidi kuliko agrisilvipastoral.

    Kumbuka: Kwenye mifumo ya kilimo mseto kuna maingiliano ya kiikolojia na kiuchumi katika madaraja tofauti tofauti.

    Mifumo mingineyo:

    iv. Aquasilviculture – kilimo cha kwenye maji pamoja na miti v. Entomosilviculture – Wadudu na Misitu

    – Apiculture – Ufugaji wa nyuki – Sericulture (Ufugaji wa Nondo wa hariri)

    Picha 4: Miti na Malisho, mifugo na miti katika eneo moja (Chanzo: https://drkarkiu.blogspot.com/2015/07/agroforestry-training-in-tuskegee.html)

    https://drkarkiu.blogspot.com/2015/07/agroforestry-training-in-tuskegee.html

  • 9

    5. TABIA YA MITI INAYOFAA KWA KILIMO MSETO Matumizi mengi/zaidi ya

    moja mfano. Uwezo wa kutoa miti kwa ajili ya nishati (kuni, mkaa), malisho, nguzo, mbao, mbolea ya majani na kurutubisha udongo, kukinga upepo, kuzuia mmomonyoko wa udongo n.k. (Mchoro 2 Chanzo: ICRAF – A tree for all reason)

    Ukuaji wa haraka – Uwezo wa kuzalisha majani mengi. Kuwa na mzizi mkuu, Kuwa na mizizi michache na ya kwenda chini

    zaidi ambapo hupunguza ushindani wa rutuba na mazao ya chakula, mfano baadhi ya migunga.

    • Kumbuka: Mifano ya miti isiyofaa kwa kilimo mseto ambayo ina ushindani na mazao ya chakula ni pamoja na Mipaini (Pines), Mikaratusi (Eucalyptus spp)., Miwati (Acacia mearnsii) ambayo mizizi yake hutawanyika juujuu na majani yake kutokuoza kwa urahisi. Tunaposema miti isiyo na ushindani na mazao, Ina maana ni juu

    na chini ya ardhi Yaani; juu ya ardhi ushindani ni wa mwanga na nafasi.

    Chini ya ardhi mfano. Ushindani wa rutuba, hewa na maji Rahisi kuota tena baada ya kukatwa/ kuvunwa. Yenye utamu na virutubisho pale inapotumika kama malisho ya

    mifugo. Uwezo wa kuchukua Nitrogen iliyopo angani na kuibadilisha kuwa

    mbolea kwa ajili ya mazao.

  • 10

    Uwezo wa kuwa na mazao yenye thamani kuinua uchumi ambayo yaweza kutumika au kuuzwa kama vile matunda, nguzo n.k.

    Yenye kuwa na Kivuli chepesi na cha kutosha kuruhusu mwanga kupenya. Miti yenye kivuli kikubwa hushindania mwanga kwa yale mazao yanayohitaji mwanga wa jua kukua (Mfano wa mti unaofaa ni kama Faidherbia albida).

    (Picha 5: Chanzo: (Agroforestry_in_Masaka__VI_Agroforestry) Baadhi ya miti kwa asili ina kivuli kinene lakini kivuli kinaweza

    kupunguzwa na kufaa kwa kilimo mseto, mfano wa miti hiyo ni: Grevillea (G. robusta), Makhamia (M. lutea), Mruka (C. abyssinica), Mfurufuru (Croton spp)., Kaliandra (C. calothyrsus), Panga uzazi (Terminalia spp), Zambarau (Syzigium), n.k.

    • Mfano wa mazao yanayoshindania mwanga ni pamoja na: Nafaka (Mahindi, Mtama, uwele, serena, ulezi nk.), Viazi vitamu

    • Mfano wa mazao yanayovumilia kivuli – Viazi mviringo, Migomba/ndizi, Kahawa.

    Isiwe ya kuficha Wadudu na Magonjwa. Iwe na majani ya kuweza kuoza kwa haraka. Isiwe na sumu kwenye majani au mizizi kuzuia uotaji wa mazao

    mengine. • Kumbuka: Mti unaofahamika zaidi ni bora kuliko ule usiofahamika

  • 11

    • Mkulima anashauriwa aipende miti vinginenyo haitaweza kuendelezwa.

    Mfano wa miti muhimu: Mkuungo (Terminalia spp), Mnyanza (Albizia vsicolar) Mng'onga (Balanites), Mlonge (Moringa oloifera), Kigelia africana, Calliandra calothyrsus, Sesbania sesban, Mgunga (Acacia spp), Mgirivea (Grevillea robusta), Mvulugu (Croton macrostachyus), Mnyenya (Cordia abyssinica), Matalawanda (Markhamia lutea), n.k.

    • Kutafuta miti inayopatikana kwenye mazingira husika

    6. UHUSIANO WA KIUTENDAJI KATI YA MITI, MAZAO NA MIFUGO

    6.1 Ni jinsi gani mazao yananufaika na uchanganyaji na miti (ni jinsi gani miti hustawisha udongo)

    6.1.1 Kuongeza rutuba kwenye udongo kwa:

    a) Kuchukua hewa ya Nitrogen angani • Miti mingi ya jamii ya kunde na michache isiyo jamii ya kunde

    (mfano miti ya mivinje (Casuarinas spp) ina uwezo wa kuchukua hewa ya Nitrogen kutoka angani kupitia njia ya kufaana (kutumia mimea mingine) bakteria au Uyoga kwenye mizizi na kutengeneza Nitrate ambayo ndiyo mimea hutumia na kustawi.

    Kumbuka: Kazi inayofanywa na majani ya kawaida ya kufunika udongo inafanana na ile inayofanywa na majani yanayodondoka ardhini kutoka kwenye miti.

    b) Kazi ya Majani yanapokuwa yamefunika udongo

    - Kupunguza mmomonyoko wa udongo kuwa kiwango cha chini

    - Huzuia magugu

  • 12

    - Huoza na kuongeza kiasi cha mboji kwenye udongo. - Huimarisha mwonekano wa udongo na uwezo wa udongo

    kushika maji. - Huwa na faida za kiikolojia katika kujitengeneza kwa udongo

    Hata hivyo, ufunikaji wa majani;

    - Huwa na hatari ya moto - Husababisha kutokuwepo na uwiano mzuri wa madini

    muhimu pale majani ya aina fulani yanapotumika kwenye ufunikaji, yanapooza huongeza aina fulani ya madini kuliko aina nyingine.

    c) Mizizi ya mimea/miti huchangia 20 hadi 30 % zaidi ya majani. - Mizizi midogomidogo ina maisha mafupi zaidi ila inapokufa

    na kuoza huongeza nitrogen inayoweza kutumika na mimea mingine kama mazao ya chakula.

    - Ukatiaji wa majani ya miti na baadaye kuota tena husababisha kwa muda mfupi kuongezeka kwa kufa kwa mizizi ila inapokufa inaongeza mbolea hai kwenye udongo.

    - Ufaji wa mizizi hutokea kwa kiasi kikubwa kukisababishwa na upungufu katika uzalishaji wa chakula.

    - Kwa mimea inayochukua hewa ya nitrogen, huitumia kwa makuzi yake ambayo hutengenezwa na mizizi.

    Mfano – mimea ya Sesbania hutengeneza hadi kg 80 kwa/hekta/kwa mwaka.

    6.1.2 Kuhifadhi maji kwenye udongo a) Miti huongeza uwezo wa udongo kushikilia maji kwa:

    Inapoongeza maozea na maozea yanakuwa kama sponji inayoweza kunyonya na kushikilia maji

  • 13

    Majani yanayodondoka ardhini hupunguza kukauka kwa udongo kunakoweza kusababishwa na upepo. b) Husaidia kupunguza kasi ya upepo na hivyo kupunguza ukaushaji

    ardhi. Ukaushaji wa ardhi husababishwa na ongezeko la joto pamoja na

    uvumaji wa upepo. Mizizi ya miti husaidia kupenyeza maji kwenye udongo.

    c) Huweka kivuli cha kadri kwenye eneo la wazi kipindi cha mazao Hivyo, kupungua kwa ukaukaji wa eneo.

    6.1.3 Uchukuliwaji wa rutuba na mmea Mizizi ya miti hupenya ndani zaidi ardhini kuliko ile ya mazao Wakati wa miamba kubadilika kuwa udongo, baadhi ya madini

    huenda chini zaidi lakini huchukuliwa na mizizi ya miti na kuletwa juu mfano ni Phosphorus, Potassium, aina ndogo ndogo za virutubisho n.k.

    Pia kufuatia uvujajibaadhi ya madini hupotea kwenye udongo kwa kwenda mbali ila hurejeshwa na mizizi ya miti.

    6.1.4 Hifadhi ya Udongo Miti hupunguza kasi ya mmomonyoko wa udongo kwa njia tofauti

    tofauti

  • 14

    Mizizi hushikilia udongo kwa pamoja – Hii huwa na uzito hasa pale miti inapokuwa imepandwa kwa kufuata contua.

    (Picha 6: Chanzo: elimu.net/Secondary/Kenya/KCSE)

    • Majani ya miti yanapokuwa yamedondoka ardhini, pia kinga ya matawi ya miti pale inapozuia matone ya mvua kuanguka na kukutana na ardhi. Badala ya maji ya mvua kuingia ardhini, pale pasipokuwa na miti maji hupotea kwa kutiririkia bondeni (run-off).

    • Miti au vichaka iliyopandwa kwa kubanana kufuata kontua, husaidia katika kuzuia mmomonyoko wa udongo unaosababishwa na maji au upepo.

    6.2 Ni kwa namna gani miti inanufaika na mchanganyiko wa mazao na miti. • Mbegu za miti zilizopandwa na mazao zina nafasi kubwa ya

    kukua vizuri kwa sababu zina nafasi sawa ya uangalizi kama ilivyo kwenye mazao.

    Zinakuwa • Zimezingirwa na kumwagiliwa maji na hivyo kulindwa zisiliwe

    na mifugo au wanyama pori • Hupaliliwa pamoja na mazao

    http://www.elimu.net/Secondary/Kenya/KCSE

  • 15

    • Kupata huduma zote za kilimo hai kwa maana ya matumizi mbolea za asili au dawazilizotengenezwa kiasili.

    • Mwanzo mazao kama vile mahindi huilinda miti michanga iliyopandwa dhidi ya upepo.

    6.3 Ni kwa vipi mifugo hunufaika na kilimo mseto • Miti mingi ya kilimo mseto ni chakula kizuri kwa mifugo, mara

    nyingi miti hii ina protini kwa ajili ya mifugo, mfano ni miti ya Mpogoro (kwa kibena) (Faidherbia albida), Calliandra, Mkikwajukwaju (Prosopsis spp).

    • Kipindi cha ukame wakati malisho ya mifugo yakiwa hayapatikani, miti huendelea kutoa malisho kwa ajili ya mifugo.

    7. Upandaji miti na ukaaji wake shambani Mkulima ni lazima kujali matumizi ya eneo la shamba lake ila siyo

    kwa shughuli nyingine tofauti na za kilimo. Afahamu tu kuwa, miti iliyopandwa inahitaji huduma za upunguziaji wa matawi ili kupunguza kivuli kitakachoweza kuathiri mazao ya chakula yaliyopandwa shambani. (Mchoro 3 Chanzo: ICRAF – A tree for all reason)

    Kumbuka: Maandalizi ya eneo kuwezesha makuzi ya haraka ya miti na afya nzuri ni ya muhimu kufanyika.

  • 16

    Uwezekano wa Upangiliaji a) Mtawanyiko wa miti shambani.

    Aina ya miti kwa eneo linalofaa Uanzishaji na nafasi

    Uanzishaji • Upandaji wa mbegu moja kwa moja shambani haushauriwi sana kwa

    kuwa unaweza kutokumbuka ni wapi ulizisia. • Uandaaji wa Kitalu kupata miche ya kupanda ndiyo njia inayohitajika

    Nafasi • Nafasi ya upandaji miti inatakiwa iwe pana ya kutosha ili kuruhusu

    uotaji mzuri wa mazao. • Angalau wastani wa mita 3 hadi 4 kwa kuanzia.

    b) Mistari ya miti shambani (syn. Hedgerows in cropland) • Mazao hupandwa kati ya mistari ya miti au vichaka (miti

    yenye urefu wa chini ya mita 6) ambapo miti hutiishwa na kuwekwa kwa nafasi inayokubalika shambani.

    • Kitendo hiki husaidia kuongeza rutuba kwenye udongo na hasa kwa kuwa sera ya SWISSAID wakishirikiana na TFCG kwa wakulima ni kutumia mbolea na dawa za asili.

    Uanzishaji na nafasi

    Uanzishaji • Usiaji mbegu wa moja kwa moja • Miche kutoka kitaluni • Mpangilio kwa eneo tambarare – Mistari ielekezwe Mashariki

    kwenda Magharibi kama jua linavyotoka na kuzama ili kuepusha vivuli vya miti kuwa juu ya mazao.

    • Kwenye miteremko miti ifuate kontua.

  • 17

    Nafasi • Kwa miti mikubwa nafasi iwe - m6 x m8 (yaani, m6 ni kwenye

    mstari – mti na mti, m8 ni umbali kati ya mstari na mstari) hii itaruhusu shughuli za kilimo kufanyika vizuri.

    • Kwa mistari ya Sesbania sesban – sentimita 10 kati ya mche na mche huwa na matokeo mazuri ya urutubishaji.

    • Calliandra calothyrsus – sentimita 25 mche na mche kwenye mstari hufanya vizuri kwenye urutubishaji.

    Mbinu na taratibu za usimamizi • Unahitaji usimamizi wa kina mfano ukataji na upunguziaji wa

    matawi ya mwanzo hufanyika kati miezi 6 - 18 baada ya kuanzisha au kupandikiza.

    • Ukatiaji wa mara kwa mara unategemea mazao yaliyopandwa kama ni yale yanayohitaji kivuli au mwanga na aina ya miti. (Mchoro 4:Chanzo: World Agroforestry center) • Majani kwa ajili ya malisho au mbolea

    ya majani – Ukatiaji wa matawi unahitajika mara kwa mara, angalau kila mwezi.

    • Pale unapokuwa unahitaji kuni/miti ya kusimamishia nyanya – upunguziaji ni baada ya mwaka (japo kunaweza kukawepo kupungua kwa mazao kutokana na kivuli).

  • 18

    8. KITALU CHA MICHE YA MITI

    8.1 Kitalu cha Miti ni nini? Ni kipande cha ardhi kilichotengwa na kuandaliwa ili kuwezesha upatikanaji wa miche ya miti ambapo mbegu husiwa na kuchipua na kupatiwa malezi yanayostahili ili zikue katika afya nzuri na kupandwa katika maeneo yaliyokusudiwa.

    8.2 Umuhimu wa kitalu Miche inaangaliwa

    kwa makini zaidi. Miche inahudumiwa

    kwa urahisi. Haya yote huwezekana kwa sababu kitalu huwa ni eneo dogo na mara nyingi liliochaguliwa karibu na makazi ya mkulima

    8.3 Uanzishaji wa kitalu cha miti

    8.3.1 Sifa za eneo zuri la kuweka kitalu

    i. Liwe ni eneo lilipo karibu na uangalizi ii. Chanzo cha maji pia kiwe karibu

    iii. Lisiwe ni eneo lenye kuweka magugu kama ndago iv. Lisiwe eneo lenye kusimamisha maji v. Liwe ni eneo lenye mwinuko wa kiasi ili kuweza kuruhusu maji

    kutiririka kwa urahisi na viriba kutokuanguka pindi vikipangwa. vi. Lisiwe ni eneo lililopo karibu na mifugo, na kama mifugo ni lazima

    kuwepo, basi litengenezewe uzio.

    Picha 7: Mfano wa Kitalu cha miche ya miti (miembe) ikisubiri ubebeshwaji

  • 19

    vii. Lisiwe ni eneo lenye wadudu waharibifu au magonjwa yanayoweza kushambulia miche.

    8.3.2 Aina za vikulia mimea Kikulia mmea ni kitu chochote chenye uwezo wa kushikilia mmea na au kuupatia chakula ili uweze kustawi. Mfano wa kikulia mmea ni udongo, mboji, pumba za mpunga, maranda ya mbao, kokoto, moramu, mchanga, n.k.

    a. Sifa za kikulia mmea Kiwe na uwezo wa kushikilia mmea. Kiweze kutoa virutubisho na maji kwa mmea. Kiweze kuhifadhi unyevu wa kutosha. Kisituamishe maji. Kipitishe hewa ya kutosha. Kiruhusu mizizi kupenya kwa urahisi. Kisiwe na wadudu au vimelea vya magonjwa. Kiweze kupatikana kwa urahisi na kwa gharama nafuu. Kiweze kudumu kwa kipindi chote cha kukuza mche

    b. Kutengeneza aina za vikulia mmea Kikulia mmea hutofautiana kutokana na eneo na eneo. Ila kikulia mmea

    chenye mchanganyiko wa orodha hii kinashauriwa. Udongo wa msituni (chini ya miti) au kutoka shamba lenye rutuba:

    Huu hutoa virutubisho vya madini muhimu kwa ukuaji wa miche pia hushikilia mizizi inayokua – Unaweza kuwekwa sehemu 5.

    Pumba za mpunga au mabaki ya randa – kama yanapatikana: Hutumika kuweka mzunguko mzuri wa hewa na maji ndani ya kikulia mmea hivyo kuruhusu mizizi kupumua na kuchukua maji na virutubisho. Weka sehemu 1.

    Samadi au Mboji: Hii hutumiwa kutoa virutubisho vya kukuzia miche na kuimarisha mizizi na hivyo hutumika kama mbolea. Weka sehemu 2.

  • 20

    • Mchanga: Mchanga unafanya kazi ya kuongeza upitivu wa maji na mzunguko wa hewa kwenye mizizi. Weka sehemu 1.

    • Mfinyanzi: Unafanya kazi ya kushikilia chembechembe za udongo zisitawanyike na pia kushikilia maji. Weka sehemu 1.

    Kumbuka: Kuchanganya vizuri na weka maji ya wastani kuweza kuchanganya kwa

    beleshi na vile vile mchanganyiko uwezekukaa kwenye kiriba bila kumwagika wakati kiriba kinaponyanyuliwa. Pasipo kuwa na toroli, uchanganyaji wa kikulia mmea kinaweza tengenezwa katika uwiano huo huo kwa kutumia chombo kingine kama ndoo au debe.

    Kiwango cha samadi au mboji kinaweza kubadilika kulingana na rutuba ya udongo wa msituni uliotumika.

    8.3.3 Usiaji wa Mbegu Mbegu zinaweza kusiwa kwenye kitalu cha mbegu ambacho huandaliwa pembeni au kupandwa moja kwa moja kwenye vitalu vya kukuzia.

    a. Kitalu cha Mbegu Huandaliwa pembeni kwa kutengenza kingo kisha kujaza huko kikulia mmea kilichoandaliwa. Vifaa vinavyoweza kutengenezea kingo ni pamoja na Matofali, Mawe, Magogo, Mabanzi, Mbao, n.k.

    b. Vitalu vya kukuzia Hapa ni mahali ambapo miche iliyochipuka kwenye kitalu cha mbegu huamishiwa kwa uangalizi hadi muda wa kupelekwa shambani. Vifaa vinavyoweza

    Picha 8: Mfano wa viriba vilivyopangwa na Kitalu cha mbegu pembeni – Chanzo Mumbaka DG

  • 21

    kuandaa ni pamoja na Viriba, maboksi, Mianzi, Mifuko, Chupa za maji, majani makavu ya migomba, n.k.

    8.3.4 Uhamishaji miche iliyoota kwenda vitalu vya kukuzia Uotaji wa mbegu baada ya kusiwa unatofautiana na aina ya miti na kama mbinu za ushawishi wa uharakishaji kuota umetumika. Mbinu zitumikazo katika uharakishaji kwenye kuota kwa mbegu upo wa namna mbalimbali:

    i. Ulowekaji wa mbegu kwenye maji ya kawaida kwa masaa 24 kisha kuzisia

    ii. Ulowekaji wa mbegu zenge gamba gumu kwenye maji ya moto kukoroga hadi maji yapoe na kuziacha kwa saa 24

    iii. Kuzichoma kwenye moto iv. Kuzigonga kwa kutumia kitu kigumu

    Mara mbegu zinapokuwa zimeota huendelea kupewa huduma hadi miche inapokuwa imetengeneza majani mawili ya mwanzo kabisa (Picha 9: Chanzo – Mumbaka DG). Baada ya hapo, miche huanza kuhamishiwa kwenye vitalu vya kukuzia

    (Transplanting). Uhamishaji wa miche

    kwenye vitalu vya kukuzia unafanikiwa vizuri kama hatua zifuatazo zitafuatwa:

    a) Tumia keni yenye vitundu kama vya mvua kumwagilia maji kwenye kitalu cha mbegu na kwenye vitalu vya kukuzia

    b) Chukua Karai lenye maji au kipande cha nguo/gunia lililolowekwa kwenye maji kwa ajili ya kubebea miche itakayong’olewa.

    c) Tumia kijiti kilichochongwa mfano wa penseli kung’olea miche (Dibar)

  • 22

    d) Wakati wa ung’oaji miche, shika majani na siyo shina la mche, kama wakati wa kushika jani moja lilikatika, shika la pili.

    e) Tumia kijiti kile kile kilichotumika kung’olea miche kupandikiza kwa kufanya yafuatayo: Weka shimo katikati ya kiriba au pale palipokusudiwa kuwekwa

    mche lililosimama wima Angalia mzizi wa mche usiwe mrefu sana au kuwa na matawi

    yatakayozuia kupenya vizuri kwenye kashimo kalikowekwa. Ukiwa umeshikilia jani la mche wakati wa kuhamisha, punguza urefu

    wa mzizi au matawi ya mzizi kwa ufanisi mzuri wa upandaji, epuka kuruhusu kujikunja kwa mzizi mkuu wa mche.

    Hakikisha kimo cha kuingia kwenye shimo ni kile kile kilichotoka kung’olewa

    Ingiza kijiti cha kupandia kwa upande (kimshazari) kikikutana na shimo lililowekwa mche na kisha uubane mche vizuri.

    Hakikisha vifuko vya hewa havipo kati ya mche na shimo, hakikisha mche umeshikana vizuri na udongo.

    Ukimaliza kupanda miche mwagilia tena maji na hakikisha ipo katika kivuli

    8.3.5 Ukatiaji wa mizizi Mizizi ya miche iliyopo kwenye viriba hukua zaidi hadi kupitiliza viriba na kushikana na ardhi.

    Upogoleaji au ukatiaji wa mizizi ni muhimu na hufanyika ili kuifanya miche iliyopo kitaluni kukaa vizuri na kuleta urahisi kipindi cha kuihamisha kuipeleka shambani.

    Picha 10: Umwagiliaji maji kwenye kitalu Chanzo - Mumbaka DG

  • 23

    Mizizi inaweza kupogolewa kwa kutumia Panga, Kisu, Mkasi au waya wa piano. Shughuli ya upogoleaji mizizi inaweza kufanyika angalau kila baada ya mwezi mmoja au kama njia rahisi ya usogezaji miche inashauriwa kufanyika angalau kila baada ya wiki mbili.

    8.3.6 Ulinzi wa bustani Ulinzi wa bustani ni muhimu hasa kukilinda na wanyama wanaofugwa kama Ng’ombe, Mbuzi, Kondoo, mbwa kuku n.k Kitalu kinaweza kuzungushiwa uzio.

    8.4 Kuandaa miche kwa ajili ya kupanda shambani

    8.4.1 Kiasi au ukubwa mche Mche hupelekwa kupanda shambani unapokuwa urefu wa sentimita 15 na usizidi sentimita 100 kutegemeana na ukuaji na aina ya mmea.

    8.4.2 Kuimarisha miche Kuimarisha miche ni ile hali ya kuinyima maji na kivuli mwishoni mwa kipindi chake kwenye bustani. Hali hii huiwezesha miche kuimarika na kuzoea hali ya kawaida iwapo shambani.

    8.5. Jinsi ya kupanda miche ya miti shambani

    Mashimo: Chimba shimo lenye upana na urefu wa kutosha. Kwa wastani shimo liwe kina cha futi moja na upana futi moja (Picha 11: Chanzo Mumbaka DG), hii ni kwa maeneo udongo tifutifu na ambao hutunza unyevu unyevu kwa muda mrefu. Maeneo yenye hali ya ukame shimo linapaswa liwe na futi mbili upana na kimo cha futi mbili. Unapochimba shimo,

  • 24

    tenganisha udongo wa juu wenye rutuba na ule wa chini usio na rutuba au wenye rutuba kidogo.

    a) Ongeza mbolea kwenye ule udongo wa juu kisha uurudishe kwenye

    shimo hadi shimo lijae au kama halikujaa, ongezea na ule usio na rutuba hadi shimo lijae.

    b) Simamisha kijiti katikati ya hilo shimo (Picha 12: Chanzo Mumbaka DG) na endelea kuandaa mashimo mengine. Sababu ya kuweka kijiti ni kuonyesha katikati ya shimo ili usilipoteze pindi mvua

    zitakapokuwa zimenyesha. Kumbuka mashimo huandaliwa mapema kabla ya mvua na baada ya mvua kuingia ardhini kama futi moja hivi ndipo miche ya miti hupandwa. Wakati wa kupanda, ondoa kijiti kilichokuwa kinaonysha katikati ya shimo kisha uweke mche.

  • 25

    8.4.3 Kuweka mche ndani ya shimo Kata na ondoa kiriba/ Kifuko/Kikapu (iwapo hakiozi) kutoka kwenye mche.

    Usipande mche ukiwa kwenye kikapu (Kiriba/mfuko) kisichooza kwani kitauzuia mche usikue. Weka mche ndani ya shimo na usimamishe kwa kujaza udongo kwenye shimo. Shindilia kwa uangalifu na sehemu ya kutuamisha maji pindi mvua zikinyesha.

    9. MAMBO YANAYOATHIRI MCHANGANYIKO WA MITI NA MAZAO KWENYE KILIMO MSETO

    a) Tabia ya eneo Tabia ya eneo kama vile hali ya hewa na hali ya udongo zinaweza zikawa na madhara kwenye hali halisi na uwezo wa miti au vichaka kwenye mchanganyiko na mazao. Mchakato wa kuchanganya miti na mazao unatawaliwa na rutuba, uondoaji wa magugu na ushindani wa rasilimali za ukuzaji ambapo uhusiano wa hivi ni kipimo cha tija kwenye mazao.

    b) Tabia ya majani ya miti Uwepo wa tofauti ya tabia ya majani kwenye miti kunachangia matokeo ya muda mfupi. Kwa mfano, mti wa aina ya mgunga (Faidherbia albida) una utaratibu wake wa kudondosha majani ambao ni wa tofauti na miti mingine. Hauna ushindani wa namna yoyote na mazao kwa sababu una mahitaji makubwa ya maji na rutuba kwa muda tofauti na ule wa mazao (Ong et al., 1992).

    Picha 13: Mche ukishindiliwa kwa

    umakini baada ya kupandwa –

    Chanzo: CCIAM in Tanzania

  • 26

    c) Miti/Vichaka miaka na nafasi Kwa mfumo wa uotaji wa pamoja kwenye kilimo mseto, tija ya mazao hupungua kadri kivuli cha miti kinavyopungua kufuatia umri wa miti na ushindani wa pamoja wa mwanga kama matokeo ya kivuli baada ya kupanuka kwa matawi ya mti na ushindani wa maji unaotokana na maendeleo ya mfumo wa mizizi ya mti/vichaka (Yin and He, 1997; Nyadzi, 2004).

    d) Usimamiaji wa Miti/Vichaka (i) Nafasi ya upandaji na ukatiaji wa matawi Ukatiaji wa mizizi na mashina ya miti/vichaka ni muhimu; uchaguzi wa miti/vichaka inayodondosha majani na yenye mizizi mikuu ambayo hutumia maji kidogo kipindi cha kiangazi itapunguza ushindani na mazao. Usimamizi wa aina hii unatekelezwa kwa madhumuni ya kuhakikisha miti ama vichaka vinachukua tu rasilimali ambazo hazichukuliwi na mazao ya shamba.

    Kielelezo kuonyesha jinsi ya upangaji wa miti mahindi

    na mazao ambayo hayana ushindani mkubwa wa rutuba

    ya udongo (Chanzo: GLOWS-FIU, 2015)

  • 27

    (ii) Uchanganyaji wa miti na vichaka Kama ilivyosemwa mwanzo, upandaji miti wa nafasi kubwa utaweza kupunguza hali ya ushindani. Hata hivyo, upana mkubwa wa uoteshaji wa miti, husababisha kuharibika kwa uwezo wa miti kuongeza mbolea kwenye udongo kwa sababu ya ujengaji hafifu wa majani.

    10. MABADILIKO YA TABIA NCHI NA KILIMO MSETO

    Hapa tunajaribu kuangalia uhusiano uliopo kati ya mabadiliko ya hali ya hewa na kilimo cha mchanganyiko wa miti na mazao. Mazingira mazuri ni yale yanayokuwa na misitu iliyohifadhiwa vizuri au maeneo yaliyopandwa miti kwa kuwa uwepo wa misitu iliyohifadhiwa ama miti iliyopandwa katika maeneo mbalimbali ni chanzo kizuri cha upatikanaji wa mvua ambayo husaidia katika uwepo wa chemchem za maji ya matumizi na umwagiliaji wa mazao yetu mashambani.

    Chanzo cha Mabadiliko ya tabianchi Mabadiliko ya hali ya hewa ni tatizo la kidunia linalotokana na

    matukio ya kiasili na shughuli za kibinaadamu ambazo hubadilisha muundo wa anga la dunia kwa kuongeza gesijoto.

    Ukataji wa miti hovyo na uharibifu wa misitu kupitia upanuzi wa mashamba, mabadiliko ya matumizi ya ardhi, mioto kichaa kwenye misitu nk ni chanzo pia.

  • 28

    Madhara ya Mabadiliko haya ni kama yanavyoonekana kwenye picha Chanzo: Athari za mabadiliko ya tabianchi – ucsusa.org/global-warming/science

    Jinsi ya kupunguza Kuzuia ufyekaji wa misitu na uharibifu wake kunaweza kupunguza

    Kabondioksidi (gesijoto) na hivyo kuifanya dunia kuwa ni sehemu nzuri ya kuishi. Misitu inaweza kumsaidia binaadamu kukabiliana na mazingira yake pale ambapo huduma nyingi zitokanazo na misitu zitakuwa zinapatikana. Baadhi ya mikakati ya kukabiliana na haya ni:

    Kuweka mikakati ya uhifadhi wa misitu iliyopo Kupanda miti kwenye maeneo ya wazi, mipakani, maeneo ya

    taasisi, na mashambani kwa mifumo ya Kilimo mseto, na kuendeleza kilimo hai/ikolojia.

    Kuhamasisha jamii kutokuendea na maandalizi mabaya ya mashamba kama matumizi ya moto (Acha kuchoma moto hovyo) n.k.

    http://www.ucsusa.org/global-warming/sciencehttp://www.ucsusa.org/global-warming/science

  • 29

    • Kujitahidi kufanya kilimo hai; yaani kuacha kutumia madawa (sumu) na mbolea za viwandani na badala yake yatumike madawa na mbolea za asili ambazo hazina madhara kimazingira.

    Jinsi ya kurekebisha

    • Kutoa elimu ya mabadiliko ya hali ya hewa na jinsi yanavyohusishwa na umaskini wa wanajamii

    • Miti iliyosimama au misitu inatusaidia kurekebisha hali ya hewa kwa utoaji wa huduma za thamani za kimazingira ama kiikolojia. Kwa hivyo uhifadhi wa misitu ni wa muhimu pamoja na upandajiwa miti.

    • Ulimaji wa mazao yanayostahimili ukame kwa kutumia mbinu za kilimo ikolojia (HAI) ili kupambana na hali ngumu ya kimazingira inayoweza kusababishwa na Ukame, Mafuriko, mvua zisizo za wakati, ukosefu wa chakula bora, n.k.

    • Misitu na au miti hutumika kama sehemu ya kuhifadhi hewa ya ukaa (hewa chafu) pale inapokuwa inaitumia hewa hiyo kwenye kujitengenezea chakula chake yenyewe.

    • Kutoa zawadi au motisha kwa wale wanaojitolea kuhifadhi misitu 11. MAMBO MUHIMU YA KUYAJUA KWENYE KILIMO MSETO

    (MUHTASARI)

    • Jamii kujua ni na kuweza kutoa maelezo ya nini maana ya Kilimo mseto na malengo yake.

    • Aina ya miti inayofaa kwa kilimo mseto na mipangilio yake shambani.

    • Jinsi ya upatikanaji wa miche ya miti na namna ya kuiotesha shambani

    • Usimamizi wa Miti shambani ili iweze kutimiza lengo kusudiwa • Uhusiano uliopo kati ya misitu/miti na Mazingira na jinsi

    kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

  • SHUKRANI

    Kitini hiki cha “Kilimo Mseto” kimeandaliwa na shirika la Kuhifadhi Misitu Asilia Tanzania (Tanzania Forest Conservation Group - TFCG) kwa kushirikiana na SWISSAID Tanzania. Kitini hiki kimepitiwa na kuidhinishwa na wawakilishi wa O�si ya Kilimo ya Mkoa wa Mtwara, Ministry of Agriculture Training Institute (MATI) Naliendele, Sustainable Agriculture Tanzania (SAT), Tanzania Organic Agriculture Movement (TOAM), Tanzania Alliance for Biodiversity (TABIO), Tanzania O�cial Seed Certi�cation Institute (TOSCI-Mtwara), Tanzania Forest Conservation Group (TFCG) wawakilishi wa wakulima na SWISSAID Tanzania katika warsha iliyofanyika tarehe 25 – 27 September 2019 katika Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara. Pia, msaada wa kifedha kutoka Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Liechtenstein Development Service (LED) na Swiss Agency for Development and Cooperation (SDC) umefanikisha kwa kiwango kikubwa katika kugharamia uandaaji, kupitia na kukamilisha uchapishaji wa kitini hiki.

    “Kitini hiki cha mafunzo kipo chini ya hati miliki ya kimataifa nambari 4.0 (CC BY-NC-DC 4.0), hairuhusiwi kuuzwa ama kunakiriwa pasipo idhini ya mmiliki.”

    "This training manual is licensed under a Creative Commons Attribution-Non Commercial-NoDerivatives 4.0 International (CC BY-NC-ND 4.0) license"

    Blank PageBlank PageBlank Page