16
November, 2019 KITINI NAMBA 4: Z A K I L I M O H A I Z A U F U G A J I W A K U K U MWONGOZO WA MBINU

KITINI NAMBA 4: MWONGOZO WA MBINU ZA KILIMO HAI ZA … · 2020. 6. 2. · Idadi ya kuku Vifo Baki Mwezi Jogoo majike Vifaranga. jogoo jike vifaranga jogoo Jike Wa tano, 2019 20 78

  • Upload
    others

  • View
    11

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: KITINI NAMBA 4: MWONGOZO WA MBINU ZA KILIMO HAI ZA … · 2020. 6. 2. · Idadi ya kuku Vifo Baki Mwezi Jogoo majike Vifaranga. jogoo jike vifaranga jogoo Jike Wa tano, 2019 20 78

November, 2019

KITINI NAMBA 4: ZA KILIMO HAI ZA UFUGAJI WA KUKU MWONGOZO WA MBINU

Page 2: KITINI NAMBA 4: MWONGOZO WA MBINU ZA KILIMO HAI ZA … · 2020. 6. 2. · Idadi ya kuku Vifo Baki Mwezi Jogoo majike Vifaranga. jogoo jike vifaranga jogoo Jike Wa tano, 2019 20 78
Page 3: KITINI NAMBA 4: MWONGOZO WA MBINU ZA KILIMO HAI ZA … · 2020. 6. 2. · Idadi ya kuku Vifo Baki Mwezi Jogoo majike Vifaranga. jogoo jike vifaranga jogoo Jike Wa tano, 2019 20 78

1

YALIYOMO

UTANGULIZI ..................................................................................................................................................................... 2

A. Matarajio ya mwongozo ................................................................................................................................. 2

B. Uandishi wa mwongozo ................................................................................................................................. 2

MADA YA KWANZA: BANDA BORA LA KUFUGIA KUKU. .............................................................................. 3

1:1.Umuhimu wa kuwa na banda bora la kuku. ............................................................................................... 3

1:2. Sifa za Banda bora la kuku. .............................................................................................................................. 3

1:3. Ukubwa wa banda ............................................................................................................................................... 3

1:4 Vifaa vya kujengea banda ................................................................................................................................. 3

1:5. Muonekano wa banda ....................................................................................................................................... 4

MADA YA PILI: LISHE NA UCHANGANYAJI BORA WA CHAKULA. ............................................................ 4

2:1 Umuhimu wa lishe bora. ................................................................................................................................... 4

2:2: Mambo ya kuzingatia katika kuchanganya chakula cha kuku. ....................................................... 5

MADA YA TATU: MIFUMO YA UFUGAJI KUKU. ................................................................................................. 5

MADA YA NNE: UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU. .............................................................................................. 6

5:1 Umuhimu wa kumbu kumbu. .............................................................................................................................. 6

5:2 Aina za kumbukumbu. ...................................................................................................................................... 7

1. Kumbukumbu za uzalishaji .......................................................................................................................... 7

2. Kumbukumbu ya matibabu na chanjo. .................................................................................................... 7

3. Kumbukumbu ya mapato na matumizi. .................................................................................................. 7

MADA YA TANO: MAGONJWA NA TIBA ............................................................................................................... 8

Njia za jumla za kudhibiti magonjwa ya kuku .............................................................................................. 10

NAKALA/ VITABU REJEA ........................................................................................................................................... 11

Page 4: KITINI NAMBA 4: MWONGOZO WA MBINU ZA KILIMO HAI ZA … · 2020. 6. 2. · Idadi ya kuku Vifo Baki Mwezi Jogoo majike Vifaranga. jogoo jike vifaranga jogoo Jike Wa tano, 2019 20 78

2

UTANGULIZI

A. Matarajio ya mwongozoWafugaji wataweza

- Kujenga banda bora la kufugia kuku- Tengeneza lishe bora- Tunza kumbukumbu vizuri za ufugaji- Kutibu magonjwa kulingana na yalivyoelekezwa- Watafanya uchaguzi sahihi wa ufugaji kulingana na maeneo Yao.- Kutambua na kudhibiti magonjwa- Kuwa mabalozi wazuri wa ufugaji kuku kwa mbinu za kilimo hai

B. Uandishi wa mwongozo- Mwongozo umeandikwa Kwa kulejea nakala mbalimbali za ufugaji pamoja na uzoefu

wa wafugaji wenyewe katika matumizi ya mimea dawa katika kudhibiti na kutibu ma-gonjwa.

- Mwongozo umelenga magonjwa yanayopatikana na yaliyothibika kuwa sumbufu Kwawalengwa.

Page 5: KITINI NAMBA 4: MWONGOZO WA MBINU ZA KILIMO HAI ZA … · 2020. 6. 2. · Idadi ya kuku Vifo Baki Mwezi Jogoo majike Vifaranga. jogoo jike vifaranga jogoo Jike Wa tano, 2019 20 78

3

MADA YA KWANZA: BANDA BORA LA KUFUGIA KUKU.

1:1.Umuhimu wa kuwa na banda bora la kuku. Usalama dhidi ya maadui zao. Mfano; nyoka , kicheche n.k Hupunguza mazalia ya vimelea na visumbufu. Hurahisisha utoaji huduma mbalimbali. Mfano: chakula, matibabu. Ni rahisi kutenga kuku wasiofaa.

1:2. Sifa za Banda bora la kuku. Liwe imara Lisiwe na vitundu vitundu wala nyufa. Liwe na sehemu ya kuku kutagia, kuhatamia na kulelea vifaranga. Liwe na vichanja kwaajili ya kuku kupumzika na kulala. Liwe na nafasi ya kutosha kulingana na idadi ya kuku. Lenye mwanga na hewa ya kutosha. Mtu afanye usafi akiwa amesimama.

1:3. Ukubwa wa banda Ukubwa wa banda utategemea na idadi ya kuku, umri/aina ya kuku Mfano, Kuku wakubwa mia moja huitajia eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 20

(urefu wa mita 5 na upana wa mita 4).

1:4 Vifaa vya kujengea banda 1. Vifaa vya kujengea sakafu: Saruji, Udongo, Mbao, Mianzi na fito.2. Vifaa vya kujengea kuta: Fito udongo, matofali, mawe, mabati, mabanzi, mbaona mianzi.

Page 6: KITINI NAMBA 4: MWONGOZO WA MBINU ZA KILIMO HAI ZA … · 2020. 6. 2. · Idadi ya kuku Vifo Baki Mwezi Jogoo majike Vifaranga. jogoo jike vifaranga jogoo Jike Wa tano, 2019 20 78

4

3. Vifaa vya kujengea paa: Nyasi, makuti, matete, wavu, matofali, miti, mabanzi na mabati.4. Vifaa vya kujengea wigo: Mbao, mianzi, matete, wavu, matofali, miti, mabanzina mabati.5. Vifaa vya kujengea dirisha: Mianzi, fito, nyaya (kashata), tenga.

1:5. Muonekano wa banda 1. Urefu na upana – itategemeana na idadi ya kuku waliopo. Mfano, banda lenye urefu wa

futi sita na upana wa futi Saba, linaweza kufuga kuku ishirini na moja.2. Kimo cha banda – jumla na paa, iwe futi Saba au 8.3. Ukubwa wa ukuta toka kwenye msingi- iwe futi 3.4. Ukubwa wa dirisha kuanzia kwenye msingi- futi 4.( kama kuku watakuwa wanakaa

ndani muda wote, banda liwe na madirisha nyuma na mbele . endapo banda litakuwalinatumika kwa kulala tu usiku, madirisha yawekwe mbele tu.

MADA YA PILI: LISHE NA UCHANGANYAJI BORA WA CHAKULA.

Lishe bora ni mchanganyiko wa vyakula vya kulinda, kujenga na kutia nguvu mwilini. Kama vilivyo orodheshwa kwenye jedwali hapo chini:

Aina ya vyakula Mfano wa vyakula Kazi

Vyakula vya kutia nguvu mwilini ( wanga )

Nafaka na pumba zake. Kuku hupata nguvu ya kutaga, kupiga kelele, kupandana, na kinga mwili kuwa na uwezo wa kupambana na vimelea vya magonjwa.

Vyakula vya ku-jenga mwili( protini )

Pumba za dagaa,mimea jamii ya kunde ,wadudu, masalia ya sa-maki,mashudu, n.k

Kuwezesha utagaji mzuri wa mayai, ukuaji mzuri wa vifaranga, uzalishwaji bora wa mbegu za uzazi kwa jogoo na jike.

Vyakula vya kulin-da mwili ( vitamin )

Mbogamboga. Kulinda mwili dhidi ya magonjwa.

Vyakula kuhimali-sha mifupa ( madini )

Unga wa Maganda ya ma-yai, unga wa chokaa, unga wa mifupa.

Mifupa kuwa imara, kuzuia kuku kula mayai, kuzuia kutagwa kwa yai lenye ganda laini.

2:1 Umuhimu wa lishe bora. Upunguza vifo vya kuku Kwa kuimarisha kinga ya mwili. Upunguza gharama za matibabu Uchochea uzalishaji bora wa mayai na nyama.

Page 7: KITINI NAMBA 4: MWONGOZO WA MBINU ZA KILIMO HAI ZA … · 2020. 6. 2. · Idadi ya kuku Vifo Baki Mwezi Jogoo majike Vifaranga. jogoo jike vifaranga jogoo Jike Wa tano, 2019 20 78

5

2:2: Mambo ya kuzingatia katika kuchanganya chakula cha kuku. 1. Epuka kutumia malighafi zilizoharibika/vunda.2. Zingatia vipimo sahihi za malighafi.3. Kuku wapewe virutubisho kulingana na mahitaji ya mwili/rika la kuku.4. Chakula kichanganywe vizuri.5. Hifadhi chakula kwenye mazingira ya hewa Safi na yasiyo na unyevu nyevu.

Mfano wa mchanganyiko wa chakula kulingana na umri wa kuku. (Chakula cha kilo 100).

Umri Vyakula vya kujenga mwili

Vyakula vya kutia nguvu mwilini

Vyakula vya ku-jenga na kuhimali-sha mifupa

Jumla

Vifaranga

( siku 0-60)

Kilo 20 Kilo 75 Kilo 5 Kilo 100

Wanaokuwa

(wiki 5-19)

Kilo 18 Kilo 77 Kilo 5 Kilo 100

Wakubwa

(wiki 20 na zaidi

Kilo 16 Kilo 79 Kilo 5 Kilo 100.

MADA YA TATU: MIFUMO YA UFUGAJI KUKU.

1. UFUGAJI HURIA Kuku hujitafutia chakula na maji Huwa na uhuru wa kuzunguka huku na kule Hutumika zaidi Kwa wafugaji wadogo /waishio vijijini.

Faida

Haina gharama kubwa Kuku hupata mazoezi ya kutosha Kuku huwa huru kula chakula anachokipenda

Changamoto

Kuku huwa kwenye hatari dhidi ya maadui zao – wezi, wanyama, ndege n.k Ni ngumu kudhibiti magonjwa na ukuaji hafifu Upotevu wa mayai kutokana na kutaga vichakani

Page 8: KITINI NAMBA 4: MWONGOZO WA MBINU ZA KILIMO HAI ZA … · 2020. 6. 2. · Idadi ya kuku Vifo Baki Mwezi Jogoo majike Vifaranga. jogoo jike vifaranga jogoo Jike Wa tano, 2019 20 78

6

2. UFUGAJI WA NUSU NDANI- Kuku hufugwa sehemu zilizozungushiwa uzio.

Faida Gharama nafuu kulinganisha na ufugaji wa ndani Rahisi kutunza kumbukumbu Kuku huwa salama dhidi ya maadui zao Rahisi kudhibiti magonjwa.

Changamoto Gharama za ujenzi wa uzio na vifaa kwaajili ya chakula na maji ni kubwa Njia hii inahitaji eneo kubwa

3. UFUGAJI WA NDANI YA BANDA- Kuku hufugwa ndani ya banda wakati wote na hupatiwa maji na chakula

Faida Kuku wengi hufugwa eneo dogo Rahisi kutunza kumbukumbu Kuku huwa salama dhidi ya maadui zao Rahisi kudhibiti magonjwa.

Changamoto Gharama za mwanzo zinahitajika mtaji mkubwa Njia hii inahitaji eneo kubwa

MADA YA NNE: UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU.

5:1 Umuhimu wa kumbu kumbu.- Kumbukumbu humuwezesha mfugaji kutambua magonjwa sumbufu katika mifugo yake ,

hivyo, atabuni mbinu mbalimbali za kukabiliana nayo- Mfugaji ataweza kubaini aina za dawa zenye ufanisi katika kutibu mifugo na kupanga mika-

kati ya uendelevu wa dawa hizo.- Kiwango cha chakula kinachotumika Kwa kuku, kitaweza fahamika. Kufahamika Kwa ki-

wango cha chakula, kuna muwezesha mfugaji kupanga bajeti ya chakula cha mwaka mzi-ma.

- Kumbukumbu humuwezesha mfugaji kufanya tathimini ya mafanikio katika ufugaji wake.- Mfugaji ataweza kuchagua kuku bora wa kuzalisha na kuendeleza vizazi.

Page 9: KITINI NAMBA 4: MWONGOZO WA MBINU ZA KILIMO HAI ZA … · 2020. 6. 2. · Idadi ya kuku Vifo Baki Mwezi Jogoo majike Vifaranga. jogoo jike vifaranga jogoo Jike Wa tano, 2019 20 78

7

5:2 Aina za kumbukumbu.

1. Kumbukumbu za uzalishaji

2. Kumbukumbu ya matibabu na chanjo.Tarehe ugonjwa Dawa tumika Gharama Maoni

2-3-2017 Homa ya matumbo Majani ya mpa-pai.

hakuna Alipona

3. Kumbukumbu ya mapato na matumizi.Tarehe Mauzo Mapato. Tshs Matumizi Maoni

kuku Mayai kuku mayai Kuku chinjwa

Mayai liwa.

10 15 150,000/= 7500/=

Idadi ya kuku Vifo Baki

Mwezi Jogoo majike Vifaranga. jogoo jike vifaranga jogoo Jike

Wa tano, 2019

20 78 50 2 5 0 18 73

Page 10: KITINI NAMBA 4: MWONGOZO WA MBINU ZA KILIMO HAI ZA … · 2020. 6. 2. · Idadi ya kuku Vifo Baki Mwezi Jogoo majike Vifaranga. jogoo jike vifaranga jogoo Jike Wa tano, 2019 20 78

8

MADA YA TANO: MAGONJWA NA TIBA

Ugonjwa dalili Tiba/kinga

Homa ya matumbo. - Kifaranga hutoa kinyesi cha njano

- Kuku mkubwa kuhara chokaa.

- Vifaranga hufiandani ya yai kablaya kuanguliwa nahata vikianguliwahuwa dhaifu

Majani ya mwarubaini.

Ponda ponda mwarubaini kiasi cha nusu kilo, changanya kwenye lita moja ya maji. Acha kwa masaa 12 na kisha uchuje na kuwapa ku-ku. Fanya hivyo kwa muda wa wiki mbili.

Kumbuka: kila siku andaa mchanganyiko mpya.

Muharo wa damu. - Kuku kuhara kin-yesi chenyemchanganyiko nadamu/ rangi yaudongo/ugoro

Kitunguu swaumu.Ponda ponda punje 5 za kitunguu swaumu, changanya kwenye lita moja za maji.

Muhimu

Changanya mchanganyiko mpya kila siku kwa mfululizo wa siku 14.

Ndui - Vidonda /vipelesehemu zisizokuwana manyoya (kichwani, mi-guuni).

Chanja kuku wakiwa na umri wa mwezi mmoja.

Kitoga/kideri. Muharo wa kijanikibichi.

Vifo vingi Kwakipindi kifupi.

Shingo kupinda Kizunguzungu,

chanja kuku wafikishapo umri wa siku 7 na 21.kisha, rudia kila baada ya miezi 3

Kumbuka Fuata mashariti ya chanjo Kwa

Page 11: KITINI NAMBA 4: MWONGOZO WA MBINU ZA KILIMO HAI ZA … · 2020. 6. 2. · Idadi ya kuku Vifo Baki Mwezi Jogoo majike Vifaranga. jogoo jike vifaranga jogoo Jike Wa tano, 2019 20 78

9

Kutembea kin-yume nyume

Ute mdomoni napuani

Kutaga mayai yenye ganda laini. .

matokeo mazuri.

Kikohozi Kupiga chafya, Kutokwa maka-

masi. kukoroma

1. Ponda ponda tangawizi mojana kitunguu swaumu kimoja

2. Changanya kwenye lita mojaza maji.

3. Koroga vizuri dawa ikolee.4. Chuja na wape kuku.

Muhimu: Watibu kwa muda wa siku 14. Kila siku tengeneza mchanganyiko mpya.

Macho - Jicho kuvimba, hutokwa na majimaji.

- Jicho huwa nausaha ulioganda.

- Husababisha vifokutokana na kukukutokula.

1. Osha jicho kwa maji safi nayenye mchanganyiko wachumvi (kipimo: kijiko kimojacha chakula kwa maji lita moja.)na kama kuna usaha ulioganda ,hakikisha unauondoa.

2. Kamulia robo nzima ya limaokubwa kwenye jicho.

3. Funga jicho kwa muda wa da-kika tatu,

Fanya hivyo kwa mfululizo wa wiki mbili.( hadi kuku atapopona )

Page 12: KITINI NAMBA 4: MWONGOZO WA MBINU ZA KILIMO HAI ZA … · 2020. 6. 2. · Idadi ya kuku Vifo Baki Mwezi Jogoo majike Vifaranga. jogoo jike vifaranga jogoo Jike Wa tano, 2019 20 78

10

Minyoo - Manyoya huwa hafifu.

- Hupungua uzito nakukonda

- Kuharisha.- Hudumaa- Minyoo yaweza

kuonekana kwenyekinyesi.

1. Majani ya mpapai:ponda pondamajani (kangomba mbili),changanya kwenye lita moja zamaji. Chuja na wape kuku.

2. Kitunguu swaumu

Ponda ponda punje tatu za ki-tunguu, changanya kwenye lita mbili za maji. ( hutumika kama tiba na kinga )

Viroboto - Wadudu kwenyengozi ya macho.

- Ngozi ngumu

Mafuta ya mgando, kupikia: paka mafuta sehemu zilizo na viroboto.

Njia za jumla za kudhibiti magonjwa ya kuku - Nunua kuku bora (wasiokuwa na dalili zozote za magonjwa)- Kamilisha ratiba nzima ya chanjo.- Hakikisha mazingira ya kuku, vyombo vya chakula na maji vipo katika hali ya usafi kwa muda

wote- Kuku wale chakula kilichobora.- Tenga na watibu kuku wagonjwa hadi wapone ndipo uwachanganye na wenzake.- Usimchanganye kuku mgeni moja moja kwa wenyeji. Mtenge Kwa muda wa wiki mbili Ili ku-

baini Kama anamaambukizi yoyote na kisha mtibu kulingana na ugonjwa uliobainika.- Epuka mwingiliano wa kuku wako na wa majirani. Vivyo hivyo, si vizuri watu kuingia hovyo

bandani kwako.wanaweza kuwa chanzo cha vimelea- Kama umetoka kwenye banda lilio na maambukizi ya magonjwa, hakikisha unabadilisha ma-

vazi kabla ya kuingia kwenye banda lako.- Hakikisha mizoga yote inafukiwa au kuchomwa na kuzikwa.- Kuku wapate tiba lishe kila siku- Kwa udhibiti wa minyoo, kuku wanywe maji yaliyo na mchanganyiko wa kitunguu swaumu

kila siku.

Page 13: KITINI NAMBA 4: MWONGOZO WA MBINU ZA KILIMO HAI ZA … · 2020. 6. 2. · Idadi ya kuku Vifo Baki Mwezi Jogoo majike Vifaranga. jogoo jike vifaranga jogoo Jike Wa tano, 2019 20 78

11

NAKALA/ VITABU REJEA - Training notes for community animal health workers –village poultry, small scale livestock

and livelihood. P.o.box 1604, lilonge, Malawi- Medicinal plants extracts widely used in the control of Newcastle disease

.www.ethnopharmacological.org.- The benefits of garlic for poultry. By Susan Burek, Herbalist.- Ufugaji bora wa kuku (Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania – toleo la tano, 2006).- Ufugaji bora wa kuku wa kienyeji ( wizara ya maendeleo ya Mifugo na Uvuvi -2008 )

Page 14: KITINI NAMBA 4: MWONGOZO WA MBINU ZA KILIMO HAI ZA … · 2020. 6. 2. · Idadi ya kuku Vifo Baki Mwezi Jogoo majike Vifaranga. jogoo jike vifaranga jogoo Jike Wa tano, 2019 20 78
Page 15: KITINI NAMBA 4: MWONGOZO WA MBINU ZA KILIMO HAI ZA … · 2020. 6. 2. · Idadi ya kuku Vifo Baki Mwezi Jogoo majike Vifaranga. jogoo jike vifaranga jogoo Jike Wa tano, 2019 20 78
Page 16: KITINI NAMBA 4: MWONGOZO WA MBINU ZA KILIMO HAI ZA … · 2020. 6. 2. · Idadi ya kuku Vifo Baki Mwezi Jogoo majike Vifaranga. jogoo jike vifaranga jogoo Jike Wa tano, 2019 20 78

SHUK RANI

Kitini hiki cha “ K itabu cha mafunzo cha mbinu za kilimo hai za ufugaji wa kuku” kimeandaliwa

na shirika la SWISSAID Tanzania. Kitini hiki kimepitiwa na kuidhinishwa na wawakilishi wa

O�si ya Kilimo ya Mkoa wa Mtwara, Ministry of Agriculture Training Institute (MATI) Nal-

iendele, Sustainable Agriculture Tanzania (SAT), Tanzania Organic Agriculture Movement

(TOAM), Tanzania Alliance for Biodiversity (TABIO), Tanzania O�cial Seed Certi�cation Insti-

tute (TOSCI-Mtwara), Shirika la Uhifadhi Misitu Asilia Tanzania (TFCG), wawakilishi wa waku-

lima na SWISSAID Tanzania katika warsha iliyofanyika tarehe 25 – 27 September 2019 katika

Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara. Pia, msaada wa kifedha kutoka Ubalozi wa Ufaransa nchini

Tanzania, Liechtenstein Development Service (LED) na Swiss Agency for Development and Co-

operation (SDC) umefanikisha kwa kiwango kikubwa katika kugharamia uandaaji, kupitia na

kukamilisha uchapishaji wa kitini hiki.

“Kitini hiki cha mafunzo kipo chini ya hati miliki ya kimataifa nambari 4.0 (CC BY-NC-DC 4.0), hairuhusiwi kuuzwa ama kunakiriwa pasipo idhini ya mmiliki.”

"This training manual is licensed under a Creative Commons Attribution-Non Commercial-NoDerivatives 4.0 International (CC BY-NC-ND 4.0) license"