36
KIWANGO CHA KUANGAMIA Uhalifu, Ufisadi na Kuangamizwa kwa Ndovu wa Tanzania

KIWANGO CHA KUANGAMIA

Embed Size (px)

Citation preview

KIWANGO CHAKUANGAMIA Uhalifu, Ufisadi naKuangamizwa kwa

Ndovu wa Tanzania

ENVIRONMENTAL INVESTIGATION AGENCY (EIA)

62/63 Upper Street, London N1 0NY, UKTel: +44 (0) 20 7354 7960 Fax: +44 (0) 20 7354 7961email: [email protected]

www.eia-international.org

EIA US

P.O.Box 53343Washington DC 20009 USATel: +1 202 483 6621Fax: +202 986 8626email: [email protected]

UTANGULIZI

MGOGORO WA UJANGILI WA NDOVU BARANI AFRIKA

CHANZO: TANZANIA

FAILI ZA KESI ZA EIA:

NCHI ZA KUSAFIRISHIA

SOKO KUU: UCHINA

HITIMISHO NA MAPENDEKEZO

2

3

5

18

26

28

33

YALIYOMO

1

JALADA LA MBELE:Mafuvu ya ndovu waliouawa, Hifadhi ya Taifa yaQuirimbas, kaskazini mwa Msumbiji, Oktoba 2012.© EIA / Mary Rice

JALADA LA NYUMA:© EIA / Mary Rice

SHUKRANI

Shukrani za dhati ziendee Wakfu wa Rufford, na kwaBrian kikosi cha matbaa ya Emmerson Press kwamsaada wao.

Imesanifiwa na:www.designsolutions.me.uk

Novemba 2014

2

© X

XXXX

XXXX

XXXX

XXXX

XXXX

X

Serikali ilihitimisha kwamba bila hatuakali kuchukuliwa nchi ingepoteza ndovuwake wote na heshima kimataifa. Mwaka1989, baada ya kubainika kwambahaingeweza kukabiliana na janga hilipeke yake ikiwa inakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa washirikamuhimu, Tanzania ilipendekeza marufuku ya kimataifa ya biashara yapembe za ndovu wote wa Afrika.Tanzania ilipongezwa kama mtetezi wa ndovu wa Afrika na kiongozi wa uhifadhi duniani.

Marufuku hiyo ilifanikiwa kwa muongommoja. Tatizo la ujangili lilidhibitiwa naidadi ya ndovu ilirejea hali yake aukuimarika. Nchini Tanzania, idadi yandovu iliongezeka kwa karibu ndovu142,788 kufikia 2006, huku zaidi ya nusu ya idadi hiyo ikiwa katika Hifadhiya Selous.

Hata hivyo, viashiria vyote vilivyoletawasiwasi miaka ya 1980 vimerudi tenana ndovu wa Tanzania wanauawa kwawingi ili kukidhi mahitaji ya biashara

iliyochipuka ya pembe za ndovu.

Tanzania ina nafasi muhimu katika hiibiashara haramu. Ingawa ongezeko laujangili lilianza 2009, ushahidi unaonyesha kwamba hali hii ilianzamiaka minne mapema na kuonyeshailivyoimarika kuliko ilivyofikiriwa. Kati2009-13, idadi ya ndovu imeshuka sana.Idadi ya ndovu katika Hifadhi ya Selousilipungua kwa asilimia 66 katika kipindicha miaka minne tu. Katika kipindi hiki,Tanzania imepoteza ndovu zaidikutokana na ujangili kuliko nchi nyingine yoyote. Mwaka 2013 peke yake,ilipoteza ndovu 10,000, sawa na ndovu30 kila siku.

Ndovu wa Tanzania wanaendeleakuwindwa na majangili ili kutoshelezamahitaji ya soko la magendo la pembeza ndovu hususan Uchina. Takwimu zapembe zilizonaswa inahusisha Tanzaniana idadi kubwa ya pembe zinazotokanchini kuliko nchi nyingine yoyote. Piainahusishwa mara kwa mara na uhalifuunaohusu shehena kubwa za pembe za

ndovu zilizonaswa sehemu mbalimbalikama Hong Kong, Vietnam, Ufilipino,Malaysia, Sri Lanka na Taiwan. Janga laujangili nchini Tanzania linafanikishwana ushirikiano wa magenge sugu,ambayo mara nyingi yanaongozwa naraia wa Uchina, na ufisadi miongoni mwa baadhi ya maafisa wa Serikali ya Tanzania.

Ripoti hii inaonyesha kwamba bila hatuamadhubuti za kumaliza kabisa ujangilikuchukuliwa haraka, mustakabali wandovu wa Tanzania na sekta ya utalii iko hatarini. Biashara ya pembe zandovu lazima ikomeshwe katika ngazizote za uhalifu, kuna haja ya kurekebisha mfumo wote wa mahakamana wadau wote, ikiwa ni pamoja na jamii zinazonyonywa na na magenge ya ujangili na watekelezaji, kuwezeshwa.Biashara zote za pembe za ndovu zipigwe marufuku kali, hasa nchiniUchina.

Shirika La Upelelezi wa MazingiraNovemba 2014

UTANGULIZIJanga la ujangili nchini Tanzania miaka 25 iliyopita lilianishwa na ongezekola uhalifu, ufisadi, kuenea kwa silaha, utepetevu katika mfumo wa mahakamana mtazamo kwamba nchi ya Tanzania ilikuwa ngome ya wahalifu. Kati ya1977-1987, Tanzania ilipoteza zaidi ya ndovu 50,000, ambayo ni asilimia 50 yaidadi yote ya ndovu wake.

Vuvu la tembo aliyeuawakatika hifadhi ya Selous, 2010

Maisha ya ndovu wa Afrika yako hatarinikadri ujangili unavyoongezeka na kueneabarani. Aina zote za jamii ya ndovu waKiafrika, ndovu wa msitu (L. a. cyclotis)na ndovu wa nyikani (L. a. Africana),wanakabiliwa na kupungua kwa idadi yaona wako katika hatari ya kuangamizwakabisa.1 Ingawa mwaka 1979 kulikuwa nazaidi ya ndovu milioni 1.3 barani Afrikamwaka, leo hii idadi ya ndovu inakadiriwakupungua hadi 419, 000.2

Mwaka 2011 pekee, Ndovu 25,000 wabarani Afrika waliripotiwa kuuawa, huku22,000 wakiuawa mwaka 2012.3 Takwimuhizi ni makadirio na idhibati ya uharibifumkubwa unaoweza kutokea.4 Kwa mfano,takwimu nyingine zinaonyesha kwambaidadi ya ndovu waliouawa mwaka 2011 ni40,000.5 Ongezeko la ujangili ni tisho lamoja kwa moja kwa uhai wa ndovu kwasababu kasi ya mauaji inazidi idadi yandovu wanaozaliwa, hivyo kuongeza wasiwasi wa kuangamizwa kabisa katikakipindi cha muongo ujao.6

Kiwango hiki cha mauaji hakijawahikushuhudiwa tangu miaka ya 1980, wakati ujangili wa ndovu ulienea koteAfrika, hali iliyosababisha kupitishwa kwamarufuku ya biashara ya kimataifa yapembe za ndovu mwaka 1989 chini yaMkataba wa Umoja wa Mataifa waBiashara ya Kimataifa ya Viumbe vilivyoKatika Hatari ya Kuangamia ya Wanyamana Mimea (CITES) kwa kuorodheshandovu wa Afrika katika Kiambatisho cha I cha CITES.

Ingawa marufuku hiyo ilipunguza ujangilina idadi ya ndovu ikaanza kuongezeka,baadaye manufaa haya yalidhoofishwa.

Mwaka 1997, idadi ya ndovu nchiniBotswana, Namibia na Zimbabwe iliwekwakwenye orodha ya CITES Kiambatisho chaII na mauzo ya "kimajaribio" ya takribantani 50 za pembe za ndovu kutoka nchi hizi barani Afrika hadi Japan yalifanyikamwezi Aprili mwaka 1999. Mauzo hayayalifuatwa na mauzo mengine “ya maramoja” ya tani 102 za pembe za ndovu kutoka Botswana, Namibia, Afrika Kusini, na Zimbabwe hadi Uchina na Japanmwishoni mwa mwaka 2008. Aidha, hivisasa wanachama wa CITES wanajadili"mikakati ya kufanya maamuzi kuhusubiashara ya pembe za ndovu ya siku zausoni" ambayo ina uwezo wa kuwezeshabiashara ta mara kwa mara ya pembe zandovu. Mchakato huu unafanyika licha ya mgogoro wa ujangili unaondelea barani Afrika.

Hivi sasa, kuna Mifumo miwili ya CITESiliyopewa mamlaka ya kufuatilia ujangilina biashara haramu ya pembe za ndovu –Mfumo wa Usimamizi wa Ujangili waNdovu (MIKE) na Mfumo wa Taarifa yaBiashara ya Ndovu (ETIS). Mifumo yoteinanakili ongezeko kubwa, hususankuanzia mwaka 2006 huku ongezekokubwa zaidi la mauaji likishuhudiwakuanzia mwaka 2011.

Mwaka 2011, mfumo wa MIKE ulirekodikiwango cha juu zaidi cha ujangili tangumfumo wa kufuatilia ulianza muongommoja uliotangulia. Takwimu zilionyeshakwamba asilimia 7.4 ya jumla ya idadi yandovu katika maeneo ya ufuatiliaji waliuawakinyume cha sheria, jumla ya ndovu17,000 ikilinganishwa na ndovu 11,500katika mwaka 2010.7 Utafiti wa kisayansiuliochapishwa Agosti mwaka 2014

3

MGOGORO WA UJANGILI WA NDOVU BARANI AFRIKA

HAPO JUU:Ndovu aliyeuawa, Hifadhi yaTaifa ya Ruaha, Tanzania,Septemba, 2014.

ulichambua data iliyokusanywa na MIKE na kugundua kwamba katikakipindi cha muongo uliopita, idadi yandovu waliouawa kinyume cha sheriailiongezeka kutoka asilimia 25 hadi katiya asilimia 60-70.8

Kipimo cha Idadi ya Ndovu WaliouawaKinyume cha Sheria (PIKE) hupima idadiya mizoga ya ndovu inayosababishwa na ujangili. Kipimo hiki huanzia 0.0kuonesha hakuna ujangili hadi 1.0ambapo mizoga yote ilitokana naujangili. Kiwango cha juu zaidi chaujangili kinapatika Afrika ya Kati, ikiwana kipimo cha PIKE cha 0.9. Hali hiiimethibitishwa na tafiti zinazooneshakwamba idadi ya ndovu wa misitu nchiniAfrika ya Kati imeshuka kwa zaidi yaasiliamia 65 kati ya mwaka 2002-13.9

Katika ukanda wa Afrika Mashariki,kiwango cha PIKE kimeongezeka maratatu 0.2-0.6 kati ya mwaka 2006-11.Kwa mfano, zaidi ya asilimia 60 ya mizoga iliyopatikana katika maeneo yaufuatiliaji wa MIKE nchini Kenya ilitokana na ujangili.

Si jambo la kushangaza kwamba, datainayoonesha kuongezeka kwa viwangovya ujangili inathibitishwa na ongezekola biashara haramu ya pembe za ndovu.Kwa mujibu wa takwimu za ETIS,biashara haramu ya pembe za ndovuimeongezeka mara tatu tangu mwaka1998.10 Ongezeko hili limekithiri hususan katika kipindi cha mwaka2011-13, huku tani 116 za pembe zandovu zikinaswa katika kipindi hiki.11

Pia data za ETIS zinaonesha kuibukakwa kanda ya Afrika Mashariki kamachanzo kikubwa cha pembe haramu zandovu, hususan Kenya na Tanzania. Kati ya mwaka 2009-11, nchi hizi mbilizilisafirisha tani 16 kati ya tani 34 za

shehena kubwa zaidi za pembe za ndovuzilizonaswach (zenye uzani wa kilo 500au zaidi) kote duniani, ikiwa ni tani 35.Kwa jumla, Tanzania ndio ilikuwa chanzo cha iliyosafirisha nje asilimia 37ya pembe za ndovu zilizonaswa wakatiwa kipindi hiki, ikifuatwa na Kenyaikiwa na asilimia 27.12

Data za pembe zilizonaswa inashadidianafasi ya Uchina kuwa soko kubwakabisa la pembe haramu za ndovu, hukuHong Kong, Vietnam, Ufilipino naMalaysia kama nchi zinazotumikakusafirishia pembe za ndovu kutokaAfrika. Kati ya mwaka 2009-13, theluthimbili za visa 76 vya pembe za ndovu zilizonaswa zilitokea Asia, hali inayoonesha kutoimarika kwa usalamawa bandari za Afrika Mashariki. Hali hii ilibadilika mwaka 2013 wakati aslimia 80 ya jumla ya visa 18 vya kukamatwa kwa kiasi kikubwa chapembe za ndovu zenye jumla ya uzaniwa tani 41, zilitokea katika nchi tatu tuza Afrika Mashariki -. Tanzania, Kenyana Uganda.13

Kuongezeka kwa ujangili wa ndovu nausafirishaji wa shehena kubwa za pembeza ndovu kunaonesha kuhusika kwamakundi ya uhalifu wa kupangwa katikabiashara haramu ya pembe za ndovu inayozidi kuchipua, yakisaidiwa na ufisadi katika hatua muhimu katikabiashara hii ya magendo. Kwa ujumla,Afrika Mashariki inapoteza idadi kubwaya ndovu kadri makundi ya uhalifuyanavyolenga ndovu waliobaki kwa ukatili ili kutosheleza masoko ya Asiayasiyotosheka hususan, Uchina. Ikiwahali hii itaachwa iendelea katika kasiyake ya sasa, ni idadi ya ndovu wachachetu watasalia Afrika katika kipindi chamuongo ujao.

4

HAPA CHINI:Pembe za ndovu zinazosafirishwakutoka Tanzania na Kenya hadiUchina zilizonaswa na Maafisa waForodha wa Hong Kong,Oktoba 2012.

© H

ong

Kong

Cus

tom

s an

d Ex

cise

HALI ILIVYO NCHINI TANZANIA Hali ya sasa ya idadi ya ndovu waTanzania ni mbaya na imekithiri. Nchiimepoteza nusu ya ndovu wake katikakipindi cha miaka mitano na theluthimbili tangu mwaka 2006. Ushahidiuliopo unaonesha kwamba tangu wakatihuo nchi imepoteza ndovu wengikutokana na ujangili kuliko nchi yoyotebarani Afrika na ndio chanzo kikubwacha pembe haramu za ndovu zilizonaswakote duniani. Idadi yake ndovu ambaowalikuwa wengi awali imeangamizwa namakundi ya wahalifu.

Hali kama hii ilishuhudiwa miaka ya1970 na ’80, Tanzania ilipokumbwa naongezeko la ujangili wa ndovu, haliiliyosababisha idadi yake kupunguakutoka 110,000 hadi 55,000.14 Baada yakupitishwa kwa marufuku ya biasharaya pembe za ndovu mwaka 1989, idadiya ndovu nchini Tanzania iliongezekahadi karibu 142,788 kufikia mwaka2006, huku zaidi ya nusu ya ndovu haowakipatikana katika Hifadhi ya Selous,hifadhi ambayo imeorodheshwa katikaUrithi wa Asili wa Dunia.15

Mwaka 2009, ilikadiriwa kuwa idadi ya ndovu nchini Tanzania ilikuwaimepungua hadi karibu 109,051.16 Halihii ya kupungua kwa idadi ya ndovuimeendelea kwa kasi ya kutisha, hukuutafiti wa idadi ya ndovu wa hivi karibuniuliofanywa mwaka 2013 ukionyeshakiwango kikubwa cha kupungua kwandovu. Idadi ya ndovu katika hifadhi yaSelous ilipungua kwa asilimia 66 kwamuda wa miaka minne tu kutoka 38,975mwaka 2009 hadi 13,084 mwaka 2013,kiwango cha chini kuwahi kurekodiwatangu mwaka 1976 wakati zaidi ya

ndovu 100,000 walikuwa wakiishi katika Hifadhi ya Selous.17 Katika hifadhi ya Ruaha-Rungwa, idadi imepungua kwa asilimia 37 kutoka31,625 mwaka 2009 hadi 20,090 katika mwaka 2013.18

Sababu kuu ya janga hili ni ujangiliunaolenga kutosheleza biashara yapembe za ndovu. Majangili wanachangiaasilimia 60 hadi 90 ya vifo vya ndovukatika hifadhi za wanyamapori nchiniTanzania.19 Kwa mfano, asilimia 90 yamizoga yote iliyopatikana katika eneo laRuaha-Rungwa mwaka 2011, ilitokanana ujangili.20 Katika mwaka 2013 pekeyake kutokana na ujangili, Tanzaniailiripotiwa kupoteza ndovu 10,000, sawana ndovu 30 kila siku.21

Kiasi kikubwa cha pembe za ndovuhusafirishwa nje ya Tanzania ilikupelekwa katika masoko haramubarani Asia. Data ya pembe zilizonaswa inaonyesha kwambaTanzania imeshiriki katika usafirishajiwa shehena kubwa za pembe za ndovukuliko nchi yoyote.22 Hivi karibuniINTERPOL iligundua kwamba kiasikikubwa cha pembe za ndovu zinazofikamasoko ya kimataifa barani Asia hutoka nchini Tanzania.23

Kiwango cha ujangili wa ndovu nausafirishaji wa pepmbe za ndovu nchini Tanzania kina athari mbaya kwauchumi na usalama wa nchi. Utalii,unaongozwa na safari za wanyamapori,ni chanzo kikubwa cha pato la Tanzania,ikileta takriban Dola bilioni 2 kilamwaka.24 Kupungua kwa idadi ya ndovuna uwepo wa majangili waliojihami katika maeneo ya hifadhi wanawezakuwa pingamizi katika kukua kwa sekta utalii.

5

CHANZO: TANZANIA

“Ndovu waliokuwawengi wanaangamizwana magenge yasiyona huruma ili... Kutosheleza mahitaji ya biasharaya pembe za ndovu.”

KUVAMIWA KWA SELOUS Hifadhi ya Selous iliyo kusini mwaTanzania ni moja ya maeneo makubwana ya zamani yanayolindwa baraniAfrika. Ikiwa na ukubwa wa kilomitamraba 50,000, hifadhi ya Selous nimaarufu kwa upekee wake wa makazianuwai ya wanyama, ikiwa na eneolenye miti ya Miombo, misitu ya kandokando ya mito, chemichemi nanyika, ambayo ni makazi ya aina nyingiza wanyama ikiwa ni pamoja na ndovu,kiboko, simba, twiga na mamba.

Ilhali katika hali halisi Selous hailindwi.Ndovu wake wamekuwa wakiwindwavibaya na magenge yanayowindawanyamapori kwa sababu ya idadi yakeiliyokuwa kubwa hivyo kuwapa pembe,ulinzi ambao hupati rasililimali zakutosha na ulinzi ambao hujaimarikadhidi ya ujangili, na ukaribu wake nabandari kuu za Bahari ya Hindi hivyokutoa njia rahisi ya kuzisafirisha.

Matokeo yake ni kwamba, idada yandovu imepungua kwa kasi kutoka70,406 katika mwaka 2006 hadi 13,084pekee mwaka 2013, kiasi cha chinikuwahi kunakiliwa.25 Hifadhi ya Selousimeathirika sana kwa sababu ya kuuawakwa ndovu nchini Tanzania na kwamujibu wa uchambuzi wa DNA wapembe za ndovu zilizonaswa, ndio mbugainayowindwa sana barani Afrika kulingana na idadi ya ndovu wanaouawa.

Dalili za hatari zilibainika mwaka 2010,wakati ambao ndovu 31,000 waliuawakatika kipindi cha miaka mitatu tu.26

Ripoti za magazeti zilieleza mizoga iliyozagaa katika hifadhi huku askari wa wanyamapori wakishiriki katikaujangili huo.27 Katika kujibu madai haya,aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara yaWanyamapori alisema kuwa kiwangocha ujangili kilikuwa kidogo.28

Mwaka 2010, maafisa wa EIA walitembelea hifadhi ya Selous na kupitia mahojiano na wanakijiji, walipata maelezo kuhusu maeneo yabiashara ya pembe za ndovu katikahifadhi, njia za magendo na jinsi askariwa wanyamapori na polisi wa eneo hiliwanavyohusika.29

Licha ya hali hii, Serikali ya Tanzaniaimeshindwa kupambana na ujangili katika Hifadhi ya Selous na ndovuwengine 25,000 waliuawa kati ya 2010-13. Sababu kuu ya kiwango hikikikubwa cha vifo vya ndovu ni ujangili.Mwaka 2011, theluthi mbili za mizogailiyoonekana katika maeneo ya ufuatiliaji katika Hifadhi ya Selous ilisababishwa na ujangili.30

Sababu inayochangia ni ukosefu warasilimali hali ambayo imeacha hifadhiya Selous bila ulinzi. Kufikia mwaka2005, mpango wa kubakisha mapato

ulikuwa ukitekelezwa, ambao kiasikikubwa cha mapato kilichotokana nasafari za kupiga picha na kuwindaziligharamia shughuli za hifadhi, ikiwani pamoja na shughuli za kuzuia ujangili,hivyo kuzalisha mapato ya Dola milioni2.8 za Marekani kila mwaka. Mpangohuo ulipofutiliwa mbali, mfuko huoulipungua hadi Dola za Marekani800,000 kufikia mwaka 2009.31 Mwakahuo huo, safari za kupiga picha katikahifadhi ya Selous zilileta mapato ya Dolamilioni 1.5.

Kiwango cha pembe za ndovuwanaowindwa katika hifadhi ya Selouszimechochea biashara haramu ya pembeza ndovu kinathibitishwa na uchambuziwa DNA wa pembe zilizonaswa. Njia hiiinahusisha kulinganisha aina za jeni zapembe za ndovu zinazonaswa na ramaniya marejeleo ya DNA ili kuonesha chanzocha eneo la kijiografia la pembe hizo.

Uchambuzi wa shehena kubwa za pembeza ndovu zilizonaswa kuanzia mwaka2006 unaonesha kwamba hifadhi zaSelous na Niassa ndizo hifadhi zenyeviwango vikubwa vya ujangili baraniAfrika; Niassa ni hifadhi iliyo kaskazinimwa Msumbiji ikipakana na Selous.

Matokeo yanaonesha kwamba hifadhi yaSelous-Niassa ndiyo ilikuwa chanzo chaidadi kubwa ya pembe zilizonaswa; taninne nchini Taiwan mwaka 2006, tani 2.6mjini Hong Kong mwaka 2006, tani tanonchini Ufilipino mwaka 2009, tani 1.5nchini Sri Lanka mwaka 2012, tani 2.6nchini Malawi mwaka 2013, tani 1.9nchini Uganda mwaka 2013 na tani mojanchini Singapore mwaka 2014.32

Juni mwaka 2014, Kamati ya Urithi waDunia ya UNESCO iliorodhesha Selouskatika Orodha ya Maeneo ya Urithi waDunia Yaliyo Hatarini kutokana naujangili ulioenea unaoangamizawanyamapori33

6

HAPA CHINI:Hifadhi ya Selous:kitovu kikubwa cha ujangili wapembe za ndovu,

Njia za baadhi ya shehenakubwa zinazosafirishwa kutokaTanzania kama nchi ya kutokaau kutokana na uchambuzi wa DNA.

7

UHALIFU WA DUNIA YOTE:

SHEHENA YA PEMBE ZILIZONASWACOLOMBO, MEI, 2012

Pembe za ndovu zilizosafirishwa ardhiniKupitia Uganda na Kenya zilinaswanchini Sri Lanka

NJIA:

kutoka kaskazini mwa Tanzania hadiUganda, kisha Kenya katika mpaka waMalaba Mombasa, Colombo, zilikuwa zikisafirishwa kuelekea Dubai

PEMBE ZILIZONASWA ZANZIBAR,AGOSTI, 2011

PEMBE ZILIZONASWA ZANZIBAR,NOVEMBA, 2013

PEMBE ZILIZONASWA HONG KONG,AGOSTI, 2011

HAI PHONPEMBE ZILIZONASWA HAIPHONG, MACHI, 2009

PEMBE ZILIZONASWA MANILA,MACHI, 2009

8

Tani 11 zilizosafirishwa kutoka Tanzaniahadi Vietnam na Ufilipino

NJIA:Dar es Salaam, UAE, Bandari ya Klang(Malaysia), Hai Phong (Vietnam)

Tani 11 zilizosafirishwa kutoka Tanzaniahadi Vietnam na Ufilipino

NJIA:Shehena sawa na ilie ya Hai Phong

Pembe zilizonaswa Zanzibar zikisafirishwa kwenda Asia

NJIA:

Dar, Zanzibar, Malaysia

Tani 2.9 za pembe zilizofichwa ndaniya makaka zilizohusishwa na Wachinamjini Dar

NJIA:

Zanzibar, tayari kupakiwa kwenyemeli iliyokuwa ikielekea Ufilipiosafarini kwenda Uchina

Maafisa wa Hong Kong walinasa tani1.9 za pembe zikisafirishwa kwendaGuangdong, Uchina

NJIA:

Tanzania hadi Malaysia na Hong Kong,safarini kuelekea mkoa wa Guangdong(Uchina)

PEMBE ZA NDOVU ZILIZONASWA KATIKABANDARI YA KAOHSIUNG, JULAI, 2006

Shehena mbili zenye uzani wa tani 5.5za pembe za ndovu zilinaswa kwamuda wa siku chache

NJIA:Tanga (Tanzania), Bandari ya Penang(Malaysia), Cebu (Ufilipino),Kaohsiung (Taiwan)

9

UDHAIFU WA UONGOZI NAUTEKELEZAJIKiini cha janga la ndovu nchini Tanzaniani uongozi dhaifu, ufisadi na uhalifu.Ushirikiano kati ya viongozi fisadi namashirika ya uhalifu ndio chanzo chakiwango cha juu cha ujangili na biashara ya magendo ya pembe za ndovu nchini, na hii inatatiza juhudi zautekelezaji ambapo kiasi kwamba niwashukiwa wachache sana hushtakiwamahakamani.

Uwajibikaji uko katika ngazi za juu zaSerikali ya Tanzania . Rais JakayaKikwete aliposhika hatamu mwaka2005, nchi ilikuwa na takriban ndovu142,000. Kufikia wakati atang'atukamadarakani mwishoni mwa mwaka2015, idadi hiyo ya ndovu itakuwaimepungua hadi karibu 55,000.

Kinyume na nchi nyingine za Afrikazinazoshuhudia viwango vya juu vyaujangili Tanzania inafurahia amani nahaijashuhudia ghasia zozote. Ingawamakundi ya waasi na magaidi yanahusishwa na ujangili wa ndovu nabiashara ya pembe za ndovu katikaAfrika ya Kati na Afrika Magharibi naKenya, vitisho kama hivi havipatikaninchini Tanzania.34

Badala yake, magenge ya kimataifa yauhalifu yanatumia pengo linalotokana naufisadi uliokithiri na udhaifu wa utwala

nchini Tanzania kupora urithi asili wakipekee wa nchi. Mwaka 2005, Tanzaniailiorodheshwa katika nafasi ya 88 katiya nchi 158 katika Kielezo cha Mtazamowa Ufisadi na Shirika la TransparencyInternational; kufikia mwaka 2013ilishuka hadi nafasi ya 111 kati ya nchi177.35 Kielezo cha utawala wa Afrikakulingana na vigezo kama vile utawalawa sheria, haki za binadamu na nfasi zauchumi za kudumu kiliorodheshaTanzania katika nafasi ya 15 mwaka2014, lakini ndio nchi ya pekee katiks15 zilizoshuhudia kushuka kwa alamazake kwa miaka mitano iliyopita.36

Ufisadi ndio nguzo kuu inayowezeshakatika kila hatua ya mchakato wakusafirisha pembe za ndovu. Kuanziaaskari wa mbuga za wanyamaporiambao hutoa taarifa muhimu kuhusudoria na maeneo ambayo makundi yandovu yanapatikana na maafisa wapolisi wanaokodisha silaha nakusafirisha pembe za ndovu, na maafisawa Mamlaka ya Mapato Tanzaniaambayo huruhusu makasha ya pembe zandovu kusafirishwa nje kutoka kwenyebandari ya nchi.

Katika ngazi za juu, wanasiasa wachama tawala (CCM) na wafanyabiasharawenye ushawishi mkubwa hutumiaushawishi wao kuwalinda wafanyibisharawa magendo ya pembe za ndovu. Mwaka2013 waziri wa zamani wa Maliasili naUtalii, Khamis Kagasheki, alitajaWabunge wanne wa CCM kwa kuhusika

HAPO JUU:Akiba ya Tanzania ya pembeza ndovu mwaka 1988, wakatiwa ujangili wa awali

katika ujangili wa meno ya ndovu. Pia alidokeza kuhusu kuhusika kwangazi ya juu, alinukuliwa akisema:“Biashara hii inahusisha mabwenyenyena wanasiasa ambao wamebuni mtandao mkubwa.”37

Mwaka 2012, orodha ya siri iliyotajawashukiwa waliochangia ongezeko laujangili wa kuwinda meno ya ndovu ilipatiwa Rais kutoka kwa vyanzo vyaujasusi. Orodha hiyo ilikuwa na majinaya vigogo serikalini na wafanyabisharaambao kutokana na ushawishi waokatika chama tawala, wanachukuliwakuwa hawawezi kushtakiwa. Si jambola ajabu kwamba wengi wa watu waliokatika orodha hii hawajachunguzwawala kukamatwa.38

Mashirika ya kimataifa pia yameelezakuhusu mchango na namna ufisadiunavochangia katika kudhoofishautawala wa sheria nchini Tanzania.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Madawaya Kulevya na Uhalifu (UNODC)inaelezea jinsi masoko haramu katikaukanda wa Afrika Masharikiyanavyoshirikiana na viongozi, kwakusema: "Maafisa hawa fisadi ni nguzomuhimu katika kuelewa mazingiramagumu ya Afrika Mashariki kwa uhalifu wa kupangwa. Wafanyabiasharawa magendo huvutiwa na bandariambazo udhibiti haujaimarika au ambazomaafisa wanaweza kupokea rushwa.”39

Aidha, ripoti ya Jopo la Wataalamukuhusu pendekezo la Tanzania lakuuza hifadhi yake ya pembe za ndovukatika mkutano wa CITES mwaka2010, lilihitimisha kuwa "kudorora kwauwezo wa Tanzania kuzuia usafirishajiwa shehena kubwa za pembe za ndovukutoka nchini inaakisi kuhatarishwakwa utekelezwaji wa sheria yawanyamapori kama sababu ya uhabawake wa rasilimali”.40

Idara ya Wanyamapori - wasimamizi wa mbuga wasio na ufanisi

Wizara ya Maliasili na Utalii (MNRT)imepewa jukumu la kulinda na kuhifadhi urithi wa asili wa Tanzaniana inasimamia idara nne: Mamlaka yaHifadhi za Taifa (TANAPA), Idara yaWanyamapori (WD), Misitu na Ufugajiwa Nyuki, na Utalii. Kati ya Idara hizonne, ni Mkurugenzi wa Idara yaWanyamapori pekee huteuliwa na Rais.

Kwa ujumla, ndovu kaskazini mwaTanzania hupatikana katika hifadhi zataifa chini ya mamlaka ya TANAPA,ambayo huzalisha mapato yake nainachukuliwa kuwa na ufanisi kwakiasi fulani. Maeneo mengi yawanyamapori kusini na magharibi mwaTanzania, mengi yakiwa hifadhi zawanyamapori, husimamiwa na Idara ya

Mapungufu ya Idara ya Wanyamapori katika kulinda kikamilifuwanyamapori wa Tanzania ni bayana katika matumizi mabaya yasekta ya uwindaji nchini. Maamuzi yote muhimu, ikiwa ni pamojana kutenga vitalu vya mgao wa kuwinda, yanatolewa naMkurugenzi.

Ukosefu wa takwimu za ukweli kuhusu idadi ya wanyamapori na jinsi walivyoenea ina maana kwamba vitalu vya mgao wa kuwinda hayajakitwakwenye misingi ya kiekolojia hivyo basi kwa ujumla yanaoenekana kuwa siendelevu. Mchakato wa kugawa vitalu na maeneo ya uwindaji si wazi naunashawishiwa na ufisadi, huku ugavi wa vitalu ili kuzalisha mapato zaidiukizidi viwango endelevu. Marekani ilisitisha uagizaji wa pembe za ndovukutoka Tanzania katika mwaka 2014 kwa sababu ya ukosefu huu wa takwimu

Ingawa wawindaji wengi nchini Tanzania wanatii sheria na kufadhili juhudi zakupambana na ujangili, kuna mifano ya wawindaji wengi wasio na maadiliwanaotumia ushawishi wao kukiuka sheria kwa jeusi na kuangamiza wanyapori wa Tanzania.

Mtu aliyetajwa mara kwa mara kuhusiana na shughuli za uwindaji wa ujeuri niMohsin M Abdallah Shein, anayejulikana pia kama Sheni. Jina lake lilitajwakatika ripoti ya uchunguzi wa Rais ya 1996 iliyomtaja kwa tuhuma za ufisadina kudai kwamba alitumia rushwa kupata vitalu vya uwindaji na kukwepa kodi.Anadaiwa kumiliki vitalu 16 vya mgao wa uwindaji katika hifadhi za wanyamapori vinavyomilikiwa na kampuni nne tofauti: Royal Frontiers ofTanzania Ltd, Game Frontiers of Tanzania Ltd, Western Frontiers of TanzaniaLtd na Northern Hunting and Enterprises Ltd. Hii inakiuka sheria kuhusu upeowa idadi ya vitalu vya uwindaji mtu yeyote anaweza kukodisha.

Wakati wa kikao cha Bunge Julai 2012, ilibainika kwamba Game Frontiers ofTanzania Ltd ilikuwa na mkataba na Uranium Resources PLC na WesternMetals Ltd mwaka 2007, kuruhusu kuingia katika vitali vya uwindaji vya kijijicha Mbarang'andu. Chini ya masharti ya Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori,ni kinyume cha sheria kwa mtu yeyote aliyepewa kitalu cha uwindajikumkodishia mtu mwingine. Licha ya ushahidi wa kukiuka sheria, GameFrontiers of Tanzania Ltd ilisalia na leseni yake na imepewa vitalu vya kuwinda katika kipindi cha 2013-18.

Mfano wazi wa ukiukwaji wa uwindaji ulitokea Mei mwaka 2014, ukihusishakampuni inayoitwa Green Mile Safaris (GMS). Wakiwa katika safari ya kuwindakatika maeneo ya hifadhi ya Selous iliyopangwa na kampuni ya GMS mwaka2012, kundi kutoka Falme za Kiarabu (UAE), mambo kadhaa ya uhalifu nayanayokiuka maadili ya uwindaji yalinaswa katika picha zilizopigwa na kampuni ya GMS yenyewe. Baada ya picha hizo kufichuliwa kwa Bunge laTanzania, Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu alifutilia mbali leseniya GMS. Tangu wakati huo kumekuwa na shinikizo kwa Serikali kubatilishauamuzi huo na inaaminika kwamba kampuni ya GMS inaendesha shughuli zake tena chini ya jina la Shangri-La Safaris.

SEKTA YA UWINDAJI

10

11

Wanyamapori (WD). Ujangili wa ndovuumekithiri zaidi katika hifadhi kama vileSelous, ikilinganishwa na hifadhi za taifa.

TANAPA inafadhiliwa vizuri kwa hivyoaskari wake wa wanyamapori wana vifaabora na ufanisi mkubwa. Ikilinganishwana idara nyingine, Idara ya Wanyamaporiinakabiliwa na tatizo la kiwango kidogocha pesa ambazo hazitoshi kulinda eneolenye ukubwa mara tano zaidi ya lile lahifadhi za taifa. Kwa wastani, kuna askariwa wanyamapori mmoja kwa kila eneola ukubwa wa kilomita 168 mraba, hukukiwango kinachopendekezwa ni askarimmoja kwa kila kilomita 25 mraba.41

Hali imedorora zaidi kutokana nakuhusika kwa baadhi ya askari wawanyamapori katika ujangili. Mapemamwaka 2014, Wizara iliwaachisha kaziaskari 21 wa wanyamapori kwa sababuya kushirikiana na majangili kufuatiauchunguzi wa ndani uliofanywa.42

Mawaziri waliofuata wamejitahidi kukabiliana na mazoea ya ndani ya Idaraya Wanyamapori na wakati mwinginemaamuzi ya waziri hukosolewa naKatibu wa Kudumu au Mkurugenzi waIdara ya Wanyamapori kutokana nautata na mgongano wa itifaki ya uon-gozi. Wakurugenzi wa Idara yaWanyamapori hubadilishwa kwa kasi yakushangaza; kuanzia mwaka 2007,kumekuwa na teuzi nane, huku nusu yateuzi hizi zikiwa ni katika kiwango cha'kaimu' kwa vipindi virefu. Hii ina

maana kwamba maamuzi yanahairishwakwa miezi kadhaa, wakati mwinginemiaka kadhaa. Ni nadra kwawafanyakazi wenye utovu kuachishwakazi bali wao hupewa majukumumengine.

Kutokana na uhaba wa rasilimali, ufisadina mazoea, Idara ya Wanyamaporiimeshindwa kutekeleza wajibu wake wakulinda na kuhifadhi wanyamapori wakipekee wa Tanzania, na hivi sasa idarahaiko katika hali nzuri ya kutekelezawajibu huu.

Utendakazi wa MNRT umekosolewavikali na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali mara kadhaa. Mwaka 2013,ukaguzi ulionyesha kwamba MNRTilishindwa kutekeleza wajibu wake wakutekeleza sheria za wanyamapori,ukosoaji huu ulielekezwa kwa Idara yaWanyamapori kwa kuruhusu vitalu vyamgao wa uwindaji kuongezwa mara kadhaa na kuripoti visa vichache vyaujangili. Ukaguzi huo uligundua kwambaIdara ya Wanyamapori haikufanyauchambuzi rasmi ili kutambua na kuweka kwenye ramani maeneoyaliyokuwa katika hatari ya ujangili nakwamba doria zilikuwa tendaji wakatiwa dharula.43 Pia ilibainika kwamba usimamizi wa akiba ya pembe za ndovuna bidhaa nyingine za wanyamaporiulikuwa duni, huku kiwango kikubwacha pembe za ndovu zikipotea katikahali isiyoeleka.44

“Idara yaWanyamaporiimeshindwakutekeleza wajibuwake wa kulinda nakuhifadhi viumbehai wa kipekee waTanzania”

1976

1979

1986

1989

1990

1991

1993

1994

1995

1996

1998

2002

2006

2007

2009

2013

120,000

100,000

80,000

60,000

40,000

20,000

0

Idad

i ya

ndov

u

Mwaka

SELOUS

RUAHA

IDADI YA NDOVU WATANZANIA 1979:NDOVU 316,300

IDADI YA NDOVU TANZANIA, 2013:NDOVU 50500

KIELELEZO CHA 1: IDADI YA NDOVU NCHINI TANZANIA HIFADHI ZA SELOUS NA RUAHA 1976-2013

12

SERA YA PEMBE ZA NDOVU Kufuatia ushahidi wa ongezeko laujangili dhidi ya ndovu tangu mwaka2006, Serikali ya Tanzania imejaribumara tatu kupata kibali kutoka kwaCITES ili iuze akiba yake ya pembe zandovu. Wakati wa hatamu ya RaisKikwete serikali yake imetafutakukubaliwa kuuza pembe za ndovu katika kila kikao cha CITES. Sera hiiimesababisha ukandamizaji wa habarikuhusu ujangili na idadi ya ndovu.

Kabla ya Kikao cha CITIES cha mwaka2007, shirikika la EIA liliwasilishamatokeo ya utafiti wake kwa Waziri waMaliasili na Utalii, Jumanne Maghembe,matokeo yaliyoonyesha kushiriki kwaviongozi mbalimbali wa Serikali katikabiashara haramu ya pembe za ndovu,huku mfanyabiashara mmoja akisemakwamba hangeweza kununua kiasikikubwa cha pembe za ndovu alipozihitaji kutoka kwa afisa mkuu wa serikali wa Idara ya Wanyamaporikatika hifadhi ya Selous. HatimayeTanzania iliondoa pendekezo lake.

Mwaka 2010, wakati kulikuwa naongezeko la ujangili katika hifadhi yaSelous na kunaswa kwa shehena ya tani11 za pembe za ndovu mwaka 2009nchini Vietnam na Ufilipino kutokaTanzania, Serikali ilijaribu tena kutafutaidhini ya kuuza pembe za ndovu. Wakatihuu pendekezo lilifika katika kikako chaCITES lakini lilibwagwa chini kupitiakura iliyopigwa. Jaribio la tatu lilifanywamwaka 2013, kwa mara nyingine lilipuuza makusudi kiwango cha janga la ujangili unaoikabili nchi. Nchi ilipogundua kwamba haingepata uungwajimkono wa kutosha, pendekezo liliondolewakabla ya kikao cha CITES.

Tangu wakati huo kumekuwa na dalilikwamba Serikali ya Tanzania inajaribukuongeza juhudi za kukabiliana naujangili na biashara ya pembe za ndovu.Kwa mara ya kwanza katika miaka yahivi karibuni, serikali ya Tanzania ilinasa pembe za ndovu nyingi sanandani ya nchi katika mwaka 2013 kulikozile zilizonaswa katika nchi nyingine.Katika mwaka huo huo, operesheni yakukabiliana na ujangili iliyooitwaOperesheni Tokomeza Ujangili ilizinduliwa kwa amri ya Rais, aliyeitangaza mapema mwaka huo.Awali, operesheni hiyo iliyohusisha ofisi mbalimbali za serikali ilionekanakufanikiwa, na kutia nguvuni zaidi yawashukiwa 900 na kufanikiwa kunasapembe za ndovu na bunduki. Hata hivyo,iilipata pigo kubwa kutokana na msururu wa ukiukwaji wa haki zabinadamu uliotekelezwa na jeshi lakulinda nchi dhidi ya jamii za wafugaji.Matokeo yake yalikuwa ni kuahairishwakwa operesheni hiyo kabla ya washukiwawa ngazi ya juu kutiwa mbaroni naWaziri Kagasheki alilazimika kujiuzulu,

hatma ambayo Waziri wa Ulinzi, ambayeaskari wake walitekeleza dhulma hiihaikumpata.

Mwanzoni mwa mwaka 2014, Serikaliya Tanzania hatimaye ilikubali kiwangocha janga la ujangili na ilitoa takwimuzilizowashangaza wengi za utafiti waidadi ya ndovu katika hifadhi za Selousna Ruaha-Rungwa kwa namna waziambayo haikutarajiwa. Katika mahojianoya televisheni, Rais Kikwete alibadilishania na kuomba marufuku ya biashara ya pembe za ndovu, akisema kuwakulegeza marufuku hiyo kungehalalishaujangili.45 Waziri wa sasa, LazaroNyalandu, ameomba usaidizi na ufadhilizaidi wa angalau Dola milioni 50 kutokakwa jumuiya ya kimataifa, kugharamiashughuli za kupambana na ujangili, naamerejesha mpango wa kubakisha mapato katika hifadhi ya Selous.

Hata hivyo, matatizo ya kimfumo yapokatika ofisi zilizopewa jukumu lakupambana na ujangili na magendo yapembe za ndovu ambao kama hautatafutiwa mwafaka, utafanya halikuwa mbaya zaidi.

HAPA CHINI:Pembe za ndovu zilizonaswaHong Kong mwaka 2003.

Mwaka 1961, rais wa kwanza wa Tanzania na mwanzilishi wa chama tawala cha CCM, Mwalimu Julius Nyerere,alitoa hotuba ya kihistoria katika kikao cha Uhifadhi wa Mazingira na Maliasili ambacho kilijulikana kamaAzimio la Arusha. Hotuba hiyo ilichochea mwito wa haja kubwa ya kuhifadhi urithi wa asili wa Afrika.

Azimio linasema: “Uhai wa wanyamapori ni sula linalotuhusu sana sotebarani Afrika. Viumbe hawa wakiwa wanaishi maeneo ya mapori, sio muhimutu kama chanzo cha maajabu na mvuto, bali ni sehemu muhimu ya maliasiliyetu na mustakabali na uhai wetu. Katika kukubali dhamana ya wanyamaporiwetu, tunatamka kwa dhati kwamba tutafanya kila tuwezalo ili kuhakikishakwamba vitukuu wetu wataweza kufurahia urithi huu mwingina wa thamani.”

Hatimaye Nyerere alifanyia maneno haya kazi. Akiwa anakabiliwa na ujangiliuliokithiri mwisho mwa miaka 1980, aliona tatizo la ujangili kama tisho lausalama na alimhamisha Costa Mlay, wa Idara ya Usalama, hadi katika Idaraya Wanyamapori kufuatilia biashara haramu ya pembe za ndovu. Mlay alifanywa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori mwaka 1989 na – kwausaidizi wa Neyere kisha, Rais Mwinyi – alizindua Operesheni Uhai ili kukabiliujangili na kuvuruga usafirishaji wa pembe za ndovu kwa kufunga barabarazilizoelekea katika viwanja vya ndege, bandari na mipaka. Mwaka 1989,Tanzania, chini ya uongozi wa Mlay, iliwasilisha pendekezo lililopitishwa baadaye katika kikao cha wanachama wa CITES mjini Lausanne ili kuorodhesha ndovu wa Afrika katika Kiambatisho cha I, pendekezo hili lilipitisha marufuku ya biashara ya pembe za ndovu kote duniani.

Hatimaye Nyerere aliyafanyia kazi maneno haya kwa vitendo. Akiwa anakabiliwa na ujangili uliokithiri mwishoni mwa miaka ya 1980, aliona tatizohilo kama tishio la usalama na akazindua Operesheni Uhai nchini kote ili kukabiliana na ujangili. Pia Serikali yake iligundua kwamba tishio hilolingeendelea huku biashara haramu ya pembe za ndovu ikiendelea. Mwaka 1989, Tanzania iliwasilisha pendekezo lililopitishwa baadaye katikakikao cha CITES ili kuorodhesha ndovu wa Afrika katika Kiambatisho cha I,kufuatia pendekezo hili marufuku ya biashara ya pembe za ndovu kote duniani ilipitishwa.

Kuna haja tena ya moyo huu kwa sababu Tanzania inakabiliwa na tishiosawa na lile la miaka ya 1980.

Watu wafuatapo, wote wenye uhusiano wa chama cha CCM, wametajwa katika vyombo vya habari nchiniTanzania au Bunge kwa kushiriki katika biashara ya pembe za ndovu:

• mwaka 2008, polisi walipekua lori kusini mwa Tanzania na kupata shehena ya pembe za ndovu. Gari hilo lilimilikiwa na Usangu Safaris, kampuni ya uwindaji inayomilikiwa na familia ya Nawab Mulla, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya;46

• mwaka 2013, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alitajwa Bungeni kwa madai ya kuhusika katika biashara ya magendo ya pembe pembe za ndovu kutoka Tanzania kwenda Vietnam mwaka 2009, kwa sababu ya kumiliki moja ya kampuni za meli zilizohusika katika kusafirisha shehena hiyo. Alikanusha madai hayo;47

• mwaka 2013, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Khamis Kagasheki, alitaja Wabunge wanne wa chama cha CCM kwa shutuma za ujangili wa ndovu. Wabunge wote walikuwa kutoka kusini mwa Tanzania ambako hifadhi ya Selous inapatikana. Walioshutumiwa walikuwa Faith Mitambo (Mbunge wa Liwale), Miriam Kasembe (Mbunge wa Massassi), Mtutura Abdallah Mtutara (Mbunge wa Tunduru Kusini) na Vita Kawawa (Mbunge wa Namtumbo).48

13

© P

ublic

dom

ain

/ UK

Nat

iona

l Arc

hive

s

KUHUSIKA KWA WANASIASA

WASIA ULIOSAHAULIWA

14

ECO 03/2009, ECO 04/2009(Tanzania, Vietnam, Ufilipino)

ECO 08/2010 (Dar, Zanzibar, Hong Kong)

ECO 01/2011 (Zanzibar, Vietnam)

ECO 10/2011 (Zanzibar, Malaysia)

ECO 08/12(Dar, Hong Kong)

ECO 06/2013 (Tanzania) na 07/2013 (Malawi)

ECO 13/2013 (Mikocheni jijiniDar) na ECO 19/2013 (Zanzibar)na ECO 21/2014 (washukiwa waziada Watanzania), na ECO23/2014 (WashukiwaWachina/Wazanzibari)

ECO 02/2014 (Bandari ya Dar)

Wafanyabiashara sita kutoka kwa mawakala wa mizigonchini Tanzania walishtakiwa kwa kosa la kuuza pembeza ndovu nchini Vietnam na Ufilipino mwaka 2009.

Kiasi cha pembe za ndovu: tani 11 takriban ndovu 1640 (kilo 6.7 kwa kila ndovu)

Mchina Huang Guo Lin, maarufu “Alimu”, alishtakiwa naZanzibar associates kwa kusafirisha pembe za ndovukwenda Hong Kong.

Kiasi cha pembe za ndovu: kilo 1,504.4takriban ndovu 225

Li Guibang

Kiasi cha pembe za ndovu: kilo 2,005.6takribani ndovu 300

Kunaswa kwa pembe za ndovu katika Bandari yaMalindi, mjini Zanzibar, ambazo zilitoka Dar es Salaamna zilikuwa zikisafirishwa kwenda Malaysia.

Kiasi cha pembe za ndovu: kilo 1,895takriban ndovu 283

Mtanzania Hassan Othman na wengine walishatakiwakwa tuhuma za magendo ya pembe za ndovu zili-zonaswa mjini Hong Kong, zikiwa zimefichwa ndani yambegu za alizeti.

Kiasi cha pembe za ndovu: kilo 1,300 takriban ndovu 194

Matukio mawili yaliyohusiana ya pembe zilizonaswa, za kwanza nchini Malawi na nyingine nchini Tanzania.Afisa wa uvuvi jijini Dar, Bw. Selamani IsanzuChasama/Chassema alitiwa mbaroni

Kiasi cha pembe za ndovu: kilo 3,729Takriban ndovu 557

Novemba 2013; wafanyakazi watatu wa Kichina walitiwambaroni kwa kupatikana na kilo 1,899 za pembe zandovu katika nyumba moja mtaani Mikocheni. Pembenyingine zilinaswa katika Bandari ya Malindi nchiniZanzibar na kusababisha kukamatwa kwa Wazanzibari. Mwaka 2014, Watanzania wawili walikamatwa kwa kosaka kuuza pembe za ndovu. Pia, mashtaka yalifunguliwadhidi ya watuhumiwa watatu waliotoroka

Kiasi cha pembe za ndovu: kilo 4,814Takriban ndovu 719

Desemba mwaka 2013: Mchina kwa jina Yu Bo na mshirika wake Mtanzania walikamatwa katika bandariya Dar, wakati wa ziara ya Wanamaji wa Uchina, wakiwa na meno 81 ya ndovu.

Kiasi cha pembe za ndovu: kilo 303Takribani ndovu 45

Inaonekana upande wa mashatakaumeshindwa kuendelea.Washukiwa waliachiwa huru.

Mawakala waliotuhumiwa walirejeshwakwenye orodha ya mawakala wa mizigo.

Huang aliachiliwa kwa dhamana; bado kesiinaendelea kusikilizwa miaka minne baa yakosa kufanyika.

Alilakamatwa Januari 2011, alifikishwamahakamani kujibu mashtaka kuhusu pembezilizonaswa Agosti 2009 nchini Vietnam.Machi mwaka 2011, aliachiliwa kwa dhamanaya Tsh milioni 80; bado kesi imepangwakusikilizwa lakini hajafika mahakamani. Zanzibar shipper Ramadhan Makame Panducharged. Prosecution ongoing.

Msafirishaji wa shehena kutoka ZanzibarRamadhan Makame Pandu alishtakiwa.Kesi inaendelea.

Othman yuko kizuizini, kesi inaendeleamahakamani, kumekuwa na ucheleweshajikatika ombi la kutafuta usaidizi wa kisheriakutoka Hong Kong.

Selemani Isanzu Chasama yuko kizuizini, kesi inaendelea. Ombi lilitumwa Malawi iliMsafirishaji Charles Kaunda ahukumiwe katika nchi aliyofanya kosa.

Kesi ya wafanyakazi wa Kichina watatuinaendelea waliotiwa mbaroni katika eneo la tukio. Inasemekana Wazanzibari walihamishwa hadi Tanzania Bara kushtakiwamahakamani. Wauzaji wawili Watanzaniawako kizuizini.

Watuhumiwa muhimu wa kesi ECO 23/2014walitoroka nchini, na ilani za INTERPOL zimetolewa.

Mashtaka dhidi ya mtanzania yalitupiliwambali lakini Yu Bo alipatwa na hatia Machi2014. Faini aliyotozwa ya Tsh bilioni 9.78(sawa na mara 10 zaidi ya thamani ya pembehizo, kulingana na hesabu katika sokonyeusi) haikulipwa na alihukumiwa kifungocha miaka 20.

JEDWALI LA KESI:

Nambari ya kesi nchini Tanzania Maelezo ya kesi Mustakabali wake kufikia Oktoba 2014

Jumla ya kesi hizi: tani 26.5 za pembe za ndovu au ndovu 3963 waliouawa

Mshukiwa mmoja amepatikana na hatia mahakamani

© A

delie

peng

uin

| Dre

amst

ime.

com

UTAFITI WA KESI ZA TANZANIA- MAGENGE YA MAGENDO YAPEMBE ZA NDOVU Ndovu wa Tanzania wanaangamizwakwa kasi ili kukidhi mahitaji ya masokomakubwa ya pembe za ndovu baraniAsia, hususan Uchina. Haya ni makosaya jinai dhidi ya mazingira ya muongouliopita.

Mitandao mikubwa ya uhalifu inayojumuisha majangili wa Tanzania na walanguzi, maafisa fisadi naWafanyabiashara kutoka Uchina wanajilimbikizia faida za mamilioni yamadola kila mwaka, huku kiasi kikubwakikiwaendea wafanyabiashara haramuwa Uchina. Mitandao hii iko mikoanikama vile hifadhi ya Selous, vituo vyaukusanyaji na bandari za kusafirishianchini Tanzania, wafanyabishara wamagendo katika nchi za usafirishaji nawauzaji katika soko la Uchina.

Hadi hivi karibuni, jitihada za ofisi za utekelezaji nchini Tanzania zikishirikiana na wenzao kutoka Asia zakukabiliana na kutibua mitandao hii yauhalifu hazijatosha na hazijafanikiwakikamilifu. Hii inadhihirika kupitiakushindwa kwa ofisi za Tanzania kugundua na kunasa kiasi kikubwa cha pembe za ndovu zinazosafirishwakutoka nchini.

Tanzania ni ya kipekee kwa sababukaribu shehena zote za pembe za ndovuzinazosafirishwa nje ya nchi ni pembeghafi zilizofichwa katika makashayanayosafirishwa kupitia bandari tatutu;Dar es Salaam, Zanzibar na Mombasakatika nchi jirani ya Kenya. Licha yaviwango hivi vikubwa vinavyohitajikushughulikiwa kwa dharura, kufikiamwaka 2013 pembe nyingine za ndovukutoka Tanzania zilinaswa nje ya nchikuliko zilizonaswa ndani ya nchi.49

Hii imekuwa ndiyo hali halisi kwa zaidiya muongo mmoja. Mwaka 2010,iliripotiwa kuwa tangu mwaka 2002pembe zote za ndovu, zaidi ya tani moja,zilizonaswa zilizohusu Tanzania zili-naswa baada ya kuondoka nchini, ikiwani thuluthi mbili ya jumla ya uzani wapembe zote za ndovu zilizonaswa katikavisa vilivyohusisha Tanzania.50 Takwimuza Idara ya Wanyamapori zinaoneshakwamba kuanzia mwaka 2009-14 tani22.6 za pembe za ndovu zilinaswa ndaniya Tanzania.51 Hifadhidata ya EIA yavisa vikubwa vya pembe za ndovu zilizonaswa kote duniani inaonyeshakwamba katika kipindi hicho, tani 40.7za pembe za ndovu kutoka Tanzania zilinaswa nje ya nchi.52 Hali kama hiiinaonyesha uzembe na ufisadi uliokithirikatika udhibiti wa bandari za Tanzania.

Mbali na wingi wa pembe za ndovu zinazosafirishwa nje ya Tanzania bila

© A

lex

Hoff

ord

“Kufikia Oktobamwaka 2014, ni kesimoja tu ambayohukumu ya kifungocha kutumikiagerezani imetolewa”

15

kizuizi chochote, mamlaka husikazinaponasa kiasi kikubwa cha pembe za ndovu ndani ya nchi kwa kawaidawahusika wakuu huwa hawatiwi kizuizinina ni nadra kuwapata watuhumiwa nahatia kwa sababu ya mchakato mgumuwa mahakama usioeleweka. Takwimu za Idara ya Wanyamapori zinaonyeshakuwa kuanzia mwaka 2001-09, kati yavisa 118 vya watu waliotiwa mbaroni natani 12 za pembe ghafi za ndovu ni visa10 pekee vilivyohukumiwa, huku fainiikiwa ni wastani ya Dola 110 na hukumu kati ya miezi 18-60.53 Takwimuza hivi majuzi kutoka Idara yaWanyamapori kati ya mwaka 2010-14zinaonyesha kuimarika kwa idadi yakesi zinazofikishwa mahakami, au hataadhabu zinazotolewa. Kesi 2899 kati yawatuhumiwa 5675, kesi 44 zilishiakuwahuku watuhumiwa 128 kifungo chajela, wastani wa muda kutumikia kifungoukiwa miezi 14. Kesi nyingine 1,181 ziliishia kutozwa faini kwa watuhumiwa1,567 kutozwa wastani wa TSh 475,000(Dola 275). EIA imekuwa ikifuatilia kesizinazohusishwa na pembe nyingi zandovu zinazonaswa na zinazohusuTanzania tangu mwaka 2009; KufikiaOktoba 2014, hukumu ya kutumikiakifungo cha jela imetolewa mara moja tukatika kesi moja (tazama Jedwali).

Njia ya Kusafirishuwa Magendo -kutoka Selous hadi Uchina

Kwa sababu ya utekelezaji usiodhabitina viwango vya ugunduzi wa chinikupindukia, pamoja na ukosefu wamashtaka yaliyo na msingi dhabiti, nibayana kwamba makundi ya ujangiliyamelenga wanyamapori wa Tanzaniakwa ukatili mkubwa. Faida inayotokanana uuzaji wa pembe za ndovu ni kubwana uwekezekano wa kukamatwa ukochini. Tatizo hili halipo Tanzania pekee;wahusika wa shehena kubwa za pembeza ndovu zilizonaswa nchini Kenya,Vietnam, Hong Kong, Ufilipino, SriLanka na Uchina huwa ni nadra kushtakiwa. Katika ugavi wa biasharaya pembe za ndovu, kutoka maeneo yavijijini hadi masoko ya mwisho katikamiji mikubwa ya Uchina, ufisadi nimuhimu katika kuwezesha biashara hii.

Katika miaka mitano iliyopita, biasharaya usambazaji kutoka hifadhi ya Selousna masoko kuu nchini Uchina imeibukakuwa njia kubwa zaidi ya usafirishaji ya pembe haramu za ndovu koteulimwenguni.

Safari huanza katika vijiji kadhaa viungani mwa hifadhi ya Selous kusinimwa Tanzania. Katika vituo muhimukama vile Mloka, Tunduru, Namtumbo,Liwale na Kilwa, wafanyabiashara wangazi ya chini, kwa kawaida kutoka Dares Salaam, huagiza pembe za ndovukutoka kwa majangili wa maeneo haya,na hata kuwauzia silaha. Katika baadhi

ya matukio, majangili hutoka maeneomengine hulipwa na waangalizi wa maeneo haya, ikiwa ni pamoja namaafisa wa serikali. Katikati ya mwaka2014, kundi la majangili kutoka Arushakaskani mwa Tanzania walilipwa naaskari polisi mjini Mloka, sehemu kuuya kuingia Hifadhi ya Wanyamapori yaSelous. Askari polisi hao waliwapa silaha na kusafirisha pembe hizo zandovu kutoka kwa majangili hao baadaya majangili hao kuua ndovu watano.Mara nyingi meno ya ndovu hukatwakatika vipande na kufukiwa mpakawanunuzi wawasili.

Pembe nyingi za ndovu zinazowindwakatika hifadhi ya Selous husafirishwa

HAPO JUU:Pembe za ndovu kutoka Selouszikiuwa, mwaka 2010.

HAPO JUU:Mwaka 2013, uvamizi katikanyumba ya makazi mtaa waMikocheni mjini Dar es Salaamulipata kilo 1,899 za pembe za ndovu.

16

17

hadi Dar es Salaam, aidha katikabarabara kuu inayoelekea kaskazini au baharini kwa kutumia majahazi yakawaida. Pikipiki zinazotumia vichochoro husafirisha pembe za ndovu hadi maeneo zinapochukuliwakaribu na barabara kuu. Kutoka hapoaidha pembe hizo husafirishwa katikamagari ya kibinafsi, aghalabu yenyesehemu maalum zilizojengewa ndani, au katika mabasi ambayo hupata pesazaidi kwa kusafirisha pembe za ndovukuliko abiria.

Pembe ghafi za ndovu zikifika Dar esSalaam kutoka kusini mwa nchi, kwakawaida huwekwa katika makazi viunganimwa jiji. Kiasi kikubwa cha pembe zandovu kinapoagizwa, hiki kiwango kidogo huwekwa pamoja, aghalabu katika mabohari katika maeneo yaviwandani kama vile Changombe karibuna bandari, lakini wakati mwingine katikaviwanja vya majumba yaliyojitenga.

Magendo ya pembe za ndovu hupakiwakatika makasha ya kusafirishwa, kamabandari ya kusafirishia ni Dar es Salaamau Mombasa, au husafirishwa hadiZanzibar ambapo huwekwa katikamakasha iwapo Zanzibar ndio bandari yakusafirishia. Njia zinazotumika kufichazinafanana na shehena za kawaidaambazo husafirishwa kutoka Tanzaniakuelekea Asia; plastiki chakavu, mazaoya kilimo kama vile mbegu za alizeti aumaharage, na mazao ya baharini kamavile samaki waliokaushwa, mwani aumakaka.

Mara nyingi, magendo ya pembe zandovu husafirishwa kutoka Tanzaniabila kizuizi chochote. Mtandao wa

maafisa wa forodha na mawakala wamizigo huhakikisha hati zote zimekamilishwa na maafisa wa forodhahulipwa. Makasha hupakiwa kwenyemeli chache zinazotoka Afrika Masharikizikielekea Asia ya Mashariki, kama vileCMA-CGM au Pacific InternationalLines. Njia za usafirishaji zinawezakuhusisha msururu wa nchi zakusafirishia, kwa kawaida Milki yaFalme za Kiarabu na Malaysia, kabla yakufika vituo muhimu vya kusafirishia,ikiwa ni pamoja na Haiphong nchiniVietnam, Manila nchini Ufilipino na HongKong. Kutoka bandari hizi pembe hizoharamu husafirishwa aidha majini au nchikavu hadi soko la mwisho nchini Uchina.

Uchambuzi wa data na EIA wa pembezilizonaswa unaonyesha ni mara ngapinjia hii imetumika na mbinu zilizotumikakwa muda wa miaka mitano iliyopita,huku kukiwa na mabadiliko machachekwa sababu ya shughuli za utekelezaji.Hata hivyo, tangu mwaka 2013kumekuwa na ishara za kutia moyo zakuimarika kwa juhudi za kukabiliana namakundi yanayoendesha biashara yapembe za ndovu nchini Tanzania. Katikamwaka huo, kwa mara ya kwanzapembe nyingi za ndovu zilinaswa ndaniya Tanzania kuliko zilizonaswa nje yanchi. Halikadhalika, kundi dogo lamaafisa watekelezaji wenye ari kutokakitengo cha askari polisi na upeleleziwametibua mitandao kadhaa kupitiamsururu wa mashambulizi katika mejengo jijini Dar es Salaam na bandarini. Bado haijulikani kama juhudi hizi zitaishia kwa watuhumiwakushtakiwa na kuhukumiwa ili kuzuiamakundi ya uhalifu kutekeleza ujangiliau kama hii ni hali ya muda mfupi.

HAPA CHINI:Dar es Salaam, bandari kubwazaidi ya Tanzania: kivukiokikubwa za shehena za pembeza ndovu.

18

Kwa kutumia upelelezi wa siri, upelelezi wa hivi karibuniukiwa ni wa Septemba 2014, na uchambuzi wa kina wamatukio makubwa ya kunaswa kwa pembe za ndovu, EIA imechora taswira kamili ya namna viwango hivi vya shehenakubwa vya ujangili na magendo ya pembe za ndovuhutekelezwa na imetambua watu muhimu wanaohusika.

Katika uchunguzi wa hivi karibuni, EIA iligundua kwambautekelezaji bora katika mwaka 2013 umekuwa na athari katikashughuli za baadhi ya makundi ambayo yanauza pembe zandovu, ambayo yamekuwa maangalifu sana kwa sababu yakunaswa kwa pembe nyingi za ndovu katika nyumba moja jijini Dar es Salaam mwezi Novemba 2013, zilizohusisha raiawatatu kutoka Uchina, na hukumu ya miaka 20 ya kuhudumujela aliyohukumiwa muuzaji wa Kichina Machi 2014.

Lakini kama uchambuzi wa kesi hiyo unavyoonyesha hapachini, washukiwa wengi wanaochangia katika janga la ujangilinchini Tanzania hawajapatikana au hawajafunguliwamashataka, na baadhi ya makundi yanayohusika sana hayajaadhibiwa.

Kunaswa kwa Shehena Katika Bandaru yaHaiphong na Manila

Machi 2009, maafisa wa forodha katika bandari kubwa yaHaiphong kaskazini mwa Vietnam walikagua kasha lililokuwalimetoka Dar es Salaam na kusafirishwa kupitia njia isiyoeleweka ya Umoja wa Falme za Kiarabu na Bandari yaKlang nchini Malaysia. Kasha lililosajiliwa kama lenye plastikichakavu lilipatikana na tani 6.2 za pembe za ndovu, kiasikikubwa cha shehena moja kuwahi kugunduliwa katika kipindicha miaka saba.

Hata hivyo, iligunduliwa kwamba kasha lililonaswa nchiniVietnam ilikuwa moja kati ya matatu yaliyosafirishwa kutokaDar es Salaam na kundi moja. Siku chache baadaye menginemawili yalizuiliwa katika bandari ya Manila nchini Ufilipino,licha ya jaribio la kubadilisha maelezo ya bidhaa na eneo

lilipokuwa likisafirishwa. Kasha lililonaswa Manila lilikuwa natani 4.5 za pembe za ndovu, kumaanisha kwamba kundi lililohusika lilijaribu kusafirisha magendo ya tani 11 za pembeza ndovu kutoka Tanzania katika operesheni moja, kiasikikubwa zaidi kuwahi kuripotiwa. Baadaye uchambuzi wa DNAwa pembe za ndovu nchini Ufilipino ulionyesha kwambapembe hizo zilitoka hifadhi za Selous na Niassa.

Ilibainika kwa haraka kwamba kampuni ya Puja Ltdiliyosafirisha makasha yote matatu ilikuwa kampuni ya bandia. Mwezi Juni, maafisa sita kutoka Mamlaka ya MapatoTanzania (TRA), ambayo hutekeleza majukumu ya forodha,walitiwa mbaroni kwa kushiriki njama ya kuruhusu makashahayo kufichwa katika eneo la viwanda karibu na bandari nakuruhusu usafirishaji wake.

Mwezi uliofuata, watu sita waliohusishwa na kampuni nne zamizigo (Team Freight Tanzania, Kigoma MN Enterprises,Uplands Freight Forwarders na Nectar Logistics) zilizohusishwana magendo hayo walikamatwa. Kampuni ya pekee iliyoshirikikatika usafirishaji wa makasha hayo ilikuwa Team Freight.Kwa mujibu wa vyanzo vya askari polisi, mmoja wa watuhumiwawakuu alikuwa raia wa Kongo kwa jina Bavon Muyumba, aliyesafiri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo naTanzania. Kampuni ya Muyumba ndio ilishirikiana na kampunimbili za mizigo kutoka Tanzania kusafirisha magendo hayo yapembe za ndovu. Makasha hayo yaliagizwa na Shaaban YasinYabulula, Mkurugenzi Mtendaji wa Kigoma MN Enterprises,Desemba 19, 2008. Tarehe 23 Disemba , meli nambari CMA-CGM ilisafirisha makasha hayo matatu hadi ua unaomilikiwana Team Freight Tanzania, katika barabara ya Bandari Road.Makasha hayo yalichukuliwa na kupakiwa kwenye meli.Stakabadhi za ankara na risiti za kuegesha makasha hayomatatu ziliandaliwa kwenye kompyuta inayomilikiwa na TeamFreight. Makasha yalijazwa na kuidhinisha na kampuni yaTeam Freight. Muyumba hakuwahi kutiwa mbaroni.

Uchunguzi uliofanywa na EIA uligundua kwamba Team Freightilikuwa ikitumia nambari ya mawasiliano sawa na kampuniinayoiwa Mussa Enterprises, ambayo mwaka 2006 ilisaidiawapelelezi wa EIA kugundua magendo kwa sababu ya tajriba

EIA imekuwa ikichunguza usafirishaji wa pembe za ndovu nje ya Tanzaniatangu ongezeko la sasa la ujangili wa ndovu ulianza mwaka 2006.

FAILI ZA KESI ZA EIA:

DNA ya pembe zilizonaswainachukuliwa kutoka kwa pembe zilizonaswazikisubiri kuharibiwaUfilipino, Juni, 2013.

19

yake katika kugundua magendo ya pembe za ndovu. Team Freightpia imetuhumiwa kwa ulaghai wa uuzaji wa madini ya shabayanayosemekana kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nje yaDar es Salaam, tuhuma zinazoeleza uhusiano wake na Muyumba.

Mwaka 2013, baada ya watuhumiwa wote kuachiliwa kwa dhamana,kesi iliangaziwa tena wakati Mbunge kwa jina Abdulrahman Kinana,Katibu Mkuu wa chama tawala cha CCM, lituhumiwa kuhusika katikausafirishaji wa kasha lililokuwa likielekea Vietnam. Ilidaiwa kwambakampuni kwa jina Sharaf Shipping Agency, inayomilikiwa na Kinanana wengine, iliandaa hati za usafirishaji. Kinana alikana madai hayo.54

Katika mwaka huo huo, taarifa za magazeti zilidai kesi hiyo ilitupiliwa mbali na mahakama kwa sababu ya ukosefu waushirikiano kutoka kwa seriakli ya Vietnam, ilhali ushirikiano kamahuo uliwahi kutokea kuhusu shehena iliyonaswa Manila baada yamaafisa wa utekelezaji kutoka Tanzania waliporuhusiwa kuonapembe za ndovu zilizonaswa na hati husika bila tatizo mwaka 2010.

Mwaka 2014, kampuni za mizigo zilizotuhumiwa katika kesi hiyozilirejeshwa kwenye orodha ya TRA ya mawakala wa mizigo wenyekibali cha kuhudumu baada ya kusimamishwa 2009. Faili ya kesihiyo iliripotiwa kupotea na inaonekana kwamba hakuna yeyoteatashtakiwa. Miaka mitano baada ya shehena kubwa zaidi yapembe za ndovu kunaswa, hakuna jitihada zozote zimefanywa ilikukamilisha uchunguzi na kuwatambua watuhumiwa wakuu, hatawawezeshaji kama maafisa wa TRA na mawakala wa mizigo hawajashtakiwa.

Kwa mujibu wa CITES, shehena kubwa za pembe za ndovu zilizonaswa "zinatoa fursa bora kwa wahusika wa biashara hii yamagendo kutambuliwa na kushtakiwa mahakami. Mara nyingi nafasikama hizi huwa hazitumiwi ipasavyo”.55 Huu ni mfano wa udhaifukatika upande wa utekelezaji haki.

Kunaswa kwa Shehena ya Pembe za NdovuMtaani MikocheniIjapokuwa kisa cha Haiphong na Manila kinaonyesha mapungufu yautekelezaji ya vyombo vya dola, kisa cha kunaswa kwa shehenakubwa ya meno ya ndovu kilichotokea katika nyumba ya makazi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa 2013 ni ushuhuda wa operesheniyenye ufanisi mkubwa wa polisi wa Tanzania na ofisi za ujasusikatika kuvuruga biashara ya magendo ya pembe za ndovu.

Tarehe 2 Novemba, 2013 polisi walivamia jumba moja mataa waMikocheni B kitongoji cha Dar es Salaam na wakafanikiwa kupatapembe 706 za ndovu zenye uzani wa zaidi ya tani 1.8. Raia watatuwa Kichina waliopatikana katika nyumba hiyo- Huang Gin, Xu Fujiena Chen Jinzhan - walizuiliwa katika eneo la tukio baada yakujaribu kuwapa askari waliowakamata rushwa ya Dola 50,000.Aidha, katika nyumba hiyo kulikuwa na kiasi kikubwa cha pesa,mizani na gari la aina ya basi ndogo lililokarabatiwa mahsusi lenyesehemu za kuficha pembe na vibao viwili vya nambari za usajili wamagari. Pembe hizo zilikuwa katika harakati ya kupakiwa katikamagunia yaliyokuwa na makaka ya konokono na vitunguu saumu ilikuzificha pembe za ndovu.

Uvamizu huu ulitokana na kazi ngumu ya ujasusi na kufuatiliawashukiwa iliyofanywa na askari polisi kwa miezi kadhaa. Baada yanyumba kuchunguzwa ilibainika kwamba kampuni kwa jina EvergoInternational iliendesha shughuli zake katika nyumba hiyo na hatizilizopatikana zilionyesha kwamba shehena za kwanza zilikuwazimesafirishwa kutoka Zanzibar. Kwa mujibu wa habari zaupelelezi, tarehe 13 Novemba makasha yaliyokuwa yakisubirikupakiwa kwenye meli ya Kota Hening katika bandari ya Zanzibar

kusafirishiwa Ufilipino kabla ya kusafirishwa kwenda Uchina yalikaguliwa. Pembe 1,023 za ndovu zenye uzani wa tani 2.9 zilizofichwa ndani ya makaka ya konokono zilipatikana ndani yakasha hilo. Watu sita, walitiwa nguvuni nchini Zanzibar kufuatiaugunduzi huo, huku washukiwa wawili kati ya sita wakiwa nimaafisa wa TRA na wawili waliohusishwa na kampuni ijulikanayokama Island Sea Food, ambayo ilikuwa wakala wa usafirishaji.

Mei 2014, kesi hiyo ilipanuliwa zaidi Watanzania wawili - SalviusMatembo na Julius Manase - walipokamatwa jijini Dar es Salaambaada ya kusakwa na polisi kwa kusambaza pembe 706 za ndovuzilizogunduliwa katika nyimba moja mtaa wa Mikocheni. Matembo,ambaye ni mkazi wa eneo la Mbezi jijini Dar es Salaam lakiniambaye ni mzaliwa wa kusini mwa Tanzania, alikiri kuhusika katikabiashara ya pembe za ndovu tangu miaka ya 1990; kufikia mwaka2005, alikuwa wakala muhimu akinunua pembe za ndovu kutokakwa watu aliowajua katika maeneo ya kusini mwa Tanzania na kuziuza kwa wateja kutoka Asia wanaoishi jijini Dar es Salaam.

Kupitia operesheni hii iliyoongozwa na ujasusi wa hali ya, askaripolisi wa Tanzania walitimbua mtandao muhimu unaojumuishamaeneo ya kusini mwa Tanzania, Dar es Salaam na Zanzibar. Katikanyumba iliyo mtaani Mikocheni, watuhumiwa walitumia biashara ya kuagiza vitunguu saumu na asidi ya limau kutoka Uchina naKusafirisha samaki wa bahari ili kuficha shughuli zao za biasharaya pembe za ndovu na kueleza kutuma na kupokea mizigo.Uchunguzi wa kampuni unaonyesha uhusiano kati ya Evergo nakampuni nyingine inayoitwa YQP International huku kampuni kadhaa zikiwa Hong Kong na Uchina. Msururu wa malipo uliofanyikabaina ya kampuni mbalimbali, huku dola nusu milioni taslimu zikilipwa katika mojawapo wa akaunti husika kwa siku moja.

Uchambuzi wa kesi unaonesha kwamba ingawa raia watatu waUchina walizuiliwa katika nyumba ambayo ilihusika katika jaribio lamagendo ya pembe za ndovu, wao si viongozi wa kundi hilo labiashara haramu. Vile vile, wafanyakazi wa kampuni ya Island Sea

FAILI ZA KESI ZA EIA:

© IT

N

Raia wa Uchina waliotiwambaroni wakati wauvamizi katika nyumbamoja mtaa wa Mikocheni,Dar Novemba, 2013.

20

Food walipanga usafirishaji wa shehena kutoka Zanzibar hukuwakiwaficha wamiliki halisi wa pembe hizo za ndovu.

Kumbukumbu za mahakama zinaonyesha kuwa, watuhumiwawakuu ni Deng Jiyun, Zhang Mingzhi, wote raia wa Uchina, na IdrisKai Hamisi kutoka Zanzibar.56 Inaaminika kwamba Deng nimfanyakazi wa zamani katika ubalozi wa Uchina nchini Zanzibar.Kesi hii ilipofichuliwa, watatu hao walikimbilia Uchina. Zhang naDeng wameorodheshwa kwenye hifadhidata ya orodha ya ilaninyekundu ya INTERPOL ya watu wanaosakwa.57

Njia ya Malawi

Njia ya mmagendo ya pembe za ndovu kutoka Tanzani iligunduliwamwaka 2013 wakati lori lilikaguliwa katika nchi jirani ya Malawi nalikapatikana na pembe za ndovu. Tarehe 24 Mei, 2013 kikosi chabarabarani cha Mamlaka ya Mapato ya Malawi kilipekua lori katikaeneo kati ya Bwengu na Phwezi. Dereva alisema kwamba lorililikuwa likisafirisha saruji kutoka Tanzania. Baada ya kukaguliwa,pembe 781 za ndovu zenye uzani wa tani 2.6 zilipatikana zikiwazimefichwa chini ya mifuko ya saruji.58

Lori likimilikiwa na kuendeshwa na Charles “Chancy” Kaunda.Aliendesha lori hilo kutoka Lilongwe hadi Dar es Salaam nchiniTanzania, safari iliyomchukua angalau saa 20, ambapo alichukuapembe hizo za ndovu kutoka nyumba moja ya makazi. Akiwa njiani kurudi, alifanikiwa kuvuka mpaka wa Songwe bila ugumuwowote na alikuwa safarini kurudi Lilongwe aliposimamishwa namaafisa wa kitengo cha barabarani cha Mamlaka ya Mapato yaMalawi (MRA).

Uchunguzi uliofanywa na serikali ya Tanzania ulibaini kuwa nyumba ambayo pembe hizo za ndovu zilitolewa ilikuwa mtaa wamabwenyenye; Mbezi Makabe, ambapo nyumba kama hizohugharimu kodi ya dola Dola 3,000 kwa mwezi. Uvamizi uliofanywakatika nyumba hiyo ulifanikiwa kunasa pembe 347 za ndovu zenyeuzani wa takriban tani moja na mifuko ya saruji. Mwenye nyumbaambaye alikuwa afisa wa uvuvi kwa jina Selemani Isanzu Chasama,

aliwekwa kizuizini. Alipohojiwa, alidai kwamba aliendesha shughulihizo kwa niaba ya Mbunge wa CCM.

Utafiti wa baadaye unaonyesha kwamba Kaunda ni mkurugenzi wakampuni inayopatikana jijini Lilongwe ya kukodisha magari. Vyanzovya ndani vinadai kwamba kampuni hii inamilikiwa na wafanyabiashwawa asili ya Kichina wanaoishi jijini Lilongwe, na kaunda anatumiwakuficha wamiliki halisi. Hii si mara ya kwanza nchi ya Malawi imetumiwa kama kituo cha kusafirisha nje pembe za ndovu; utafitiwa kina uliofanywa na EIA mwaka 2002 ulionyesha kwamba kunamakundi makubwa ya biashara ya magendo mjini Lilongwe ambayo

© M

RA

Pembe 781 kutoka Tanzaniazilizonaswa nchini Malawi,Mei 2013.

Pembe zilizonaswa nchiniMalawi zilionekana zilitokakatika nyumba hii mtaa waMbezi jijini Dar es Salaam.

21

yalikuwa yakisafirisha nje pembe za ndovu kutoka Zambia hadi Asiakupitia Lilongwe. Yakiongozwa na raia mmoja wa Malaysia kwa jina"Peter" Wang, kundi hilo lilikuwa limesafirisha angalau shehena 19za pembe za ndovu kwenda bara Asia mpaka shehena moja , yenyeuzani wa tani saba, iliponaswa mjini Singapore mwezi Juni 2002.59

Kulingana na kesi za awali za pembe za ndovu matukio yausafirishaji nje yanayohusisha nchi ya Malawi, heunda pembe zilizopatikana katika lori Mei mwaka 2013 zingefichwa katika kasha mjini Lilongwe na kusafirishwa nje kutoka bandari yaMsumbiji ya Beira. Uchambuzi wa DNA wa pembe zilizonaswa, baadhi zikiwa na urefu wa mita 1.6, unaonyesha kwamba zilitolewahifadhi za Selous na Niassa, huku nyingine zikitoka hifadhi yaRuaha na Mikumi.60

Kufikia Oktoba 2014, Chasama alikuwa korokoroni akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake. Mustakabali wa mchakato wa kisheriadhidi ya Kaunda nchini Malawi bado huwezi kubashiriwa. Kuna ripotikwamba alitozwa faini na Mamlaka ya Mapato ya Malawi (MRA) lakinihaijulikani kama amefunguliwa mashtaka. Serikali ya Tanzaniaimeomba ashtakiwe nchini Tanzania alikotekeleza kosa hilo.

Ziara ya Jeshi la Wanamaji wa Uchina

Mwishoni mwa Desemba 2013, bandari ya Dar es Salaam ilipataziara rasmi ya kikosi maalum cha jeshi la wanamaji kutoka Uchinaambacho kilikuwa safarini kuelekea Uchina baada ya kushika doriaya kupambana na uharamia katika Ghuba ya Aden. Ziara hiyo yasiku nne, ambayo ilijumuisha manowari ya Jinggangshan naHengshui, ilihusu shughuli kadhaa kati ya wanamaji na maafisakutoka nchi hizo mbili, “pamoja na kubadilishana utamaduni”.61

Ziara hii ilichochea kuongezeka kwa biashara ya pembe za ndovukwa wafanyabiashara kutoka Dar es Salaam. Muuzaji mmoja kutokasoko la Mwenge la wachonga vinyago alijigamba kwamba alipataDola 50,000 baada ya kmuuzia afisa wa meli. Wakati huo raiammoja wa Kichina alikuwa korokoroni, Yu Bo, hakubahatika; alitiwakizuizini tarehe 30 Desemba akijaribu kuingia bandari ya Dar esSalaam katika lori lililopakiwa pembe 81 za ndovu zenye uzani wakilo 303, zikiwa zimefichwa chini ya vinyago vya mbao.

Yu Bo alikuwa akipanga kusafirisha pembe hizo kwa afisa wa cheo cha wastani wa kikosi maalum cha wanamaji waliotia nanga bandarini. Jioni hiyo, magari mawili yaliwasili katika lango la bandari, yote yakiwa yamebeba pembe za ndovu zilizofichwa.Rushwa ya jumla ya Shilingi milioni 35 za Tanzania (Dola 20,000)ililipwa ili kuruhusu magari hayo kupita bila kukaguliwa. Lakini Yu Bo alisimamishwa katika kituo cha pili cha kukagua mizigobaada ya taarifa kutoka kwa muuzaji ambaye hakuridhika na kiasialicholipwa na pembe hizo zilipatikana.62

Ripoti ilisema kwamba Yu Bo aliingia Tanzania tarehe 26 Novembana akawasiliana na magenge yanayouza pembe za ndovu akitakapembe za hizo. Pembe hizo zilikuwa zimefichwa katika eneo la sokola Mwenge mpaka wakati zilisafirishwa.63

Katika hali isiyo ya kawaida, kesi dhidi ya Yu Bo iliharakishwa kupitia kwa mfumo wa mahakama; na kufikia mwezi Machi, alipatikana na hatia na kupewa faini ya kubwa zaidi kuwahi kutolewa ya Shilingi milioni 978 za Tanzania (Dola 5,600,000). Pesa hizi zilikadiriwa baada ya kuzidisha thamani ya pembe zilizonaswa mara 10, kiwango cha juu cha faini inayoruhusiwa,thamani ya pembe za ndovu ikiwa Dola 1,860 kwa kila kilo, bei

FAILI ZA KESI ZA EIA:©

Xu

Mia

obo

/ Xi

nhua

Pre

ss /

Cor

bis

Kikosi Maalum cha Wanamajiwa Uchina kilitia nanga katikabandari ya Dar es SalaamDesemba, 2013.

Paul “Paulo” Gavana naSuleiman Mochiwa,Septemba, 2014.

Nova "Chikawe ni kiongoziwa wafanyabiasha wapembe za ndovu katikasoko la Mwenge.

22

kamili ya magendo. Aliposhindwa kulipa faini hiyo, alihukumiwakutumikia kifungo cha miaka 20 jela.64 Kufikia mwezi Oktoba 2014,alikuwa gerezani akikata rufaa.

Kituo cha Biashara cha Mwenge

Soko la Wachongaji la Mwenge jijini Dar es Salaam ni maaruufu kwawageni wanaotafuta vinyago vya mbao na michoro ya kitamaduniya tinga tinga. Pia ni kituo muhimu kwa biashara ya pembe zandovu, licha ya kuangaziwa mara kwa mara na vyomba vya habarinchini na vya kimataifa.65

Wakati wa ziara ya upeleezi ya mwaka 2006, wapelelezi wa EIAwalipewa vinyago vya pembe za ndovuu viliyochongwa na ambazohazijachongwa na wafanyabiashara kadhaa nje ya soko la Mwenge,huku chanzo kikuu kikisemekana kuwa Selous na kaskazini mwaMsumbiji. Katika ziara ya pili ya Septemba 2014, wapelelezi wa EIAwaligundua kwamba biashara ilikuwa ikifanywa kwa siri, nawafanyabiashara wakiwa wangalifu zaidi kuliko hapo awali nahakuna hawakuna bidhaa za pembe za ndovu zilikuwa zikiuzwasokoni humo.

Hali hii ilitokana na shughuli za utekelezaji za hivi karibuni katikasoko hilo na kwingineko mjini Dar es Salaam. Majasusi kutoka njeya eneo hili waliwatia mbaroni wafanyabiashara katika soko hiliwaliowauzia bidhaa za pembe za ndovu.

Licha ya hali ya tahadhari, wachunguzi wa EIA waligundua kwambasoko la Mwenge bado ni eneo muhimu kwa mawasiliano yawanunuzi na wauzaji wa pembe za ndovu. Mikutano hupangwamaeneo mengine kujadili kiwango, bei na jinsi ya kusafirishapembe za ndovu.

Kundi la wafanyabiashara lenye siri kubwa ndilo linatawalabiashara ya pembe za ndovu nje ya soko la Mwenge. Watu wannewaliotiwa mbaroni- Novatus "Nova" Chikawe, Paulo Gavana, DeusMbopo na Roberto - wote ni wa kabila la Makonde, wanaotoka eneola kusini mwa Tanzania na kaskazini mwa Msumbiji. Watu hawawamekuwa katika soko hili tangu mwaka 2006 na wanalindwa nana maafisa wa askari polisi wa kituo cha polisi cha eneo hilo.

Uhusiano wake na kusini mwa Tanzania husaidia katika kutafutapembe za ndovu kutoka eneo hilo. Nova ndiye kiongozi wa kundihili na hujigamba kwa kuwauzia watu kutoka Ubalozi wa Uchinanchini Tanzania pembe za ndovu, ilhali Deus husimamia mawasiliano na polisi.

Septemba 2014, wapelelezi wa siri kutoka EIA walikutana na Paulokatika hoteli moja nje ya soko la Mwenge. Paulo aliandamana namwanamume mmoja kwa jina Suleiman, ambaye alimtambulishakama binamu yake. Ingawa Paulo alieleza kwamba biashara yake nikuuza Vinyago vya Mpingo, Suleiman ni wakala wa huduma zakusafirisha mizigo. Wote walikubali kuhusika katika biashara yapembe za ndovu lakini walisema shughuli hiyo sasa ilifanywa kwasiri kubwa kutokana na operesheni za utekelezaji za hivi karibunina kwa sasa wanauza ndani ya nchi tu badala ya kuzisafirisha njeya nchi. Wakati wa majadiliano kuhusu uuzaji wa magendo nje yabandari ya Dar es Salaam, Suleiman alisistiza umuhimu wa kuwa nauhusiano mwema na maafisa wa forodha ili kuepuka matatizo yoyote na alikiri kwamba kuongezeka kwa matumizi ya mashini zakuskani mizigo bandarini ilifanya usafirishaji wa magendo kuwamgumu. Paulo alidai kwamba raia wa Kichina aliyekamatwa katikanyumba moja mtaani Mikocheni, Huang Gin, alikuwa mnunuzi wamara kwa mara wa pembe za ndovu sokoni.

Wote walieleza kuwa uuzaji wa pembe za ndovu na wafanyabiashara katika soko la Mwenge uliongezeka wakati waziara ya Rais wa Uchina Xi Jinping nchini Tanzania Machi 2013.Ujumbe mkubwa wa Serikali ya Uchina na wafanyabiasharawaliozuru walitumia fursa hiyo kupata kiasi kikubwa cha pembe zandovu kiasi kwamba bei yake ilipanda. Wafanyabiashara hao wawiliwalidai wakwamba wiki mbili kabla ya ziara hiyo ya kiserikali,wanunuzi wa asili ya Kichina walianza kununua maelfu ya kilo zapembe za ndovu, ambazo baadaye zilitumwa Uchina katika mifukoya kidiplomasia katika ndege ya Rais.

Suleiman alisema: “Bei ilikuwa juu sana kwa sababu mahitajiyalikuwa juu. Mgeni akijja, ujumbe wote, huo ndio wakati biasharahuwa nyingi.” Aliongeza kuwa bei kwa kila kilo ilipanda mara mbilihadi Dola 700 wakati wa ziara hiyo.

© R

eute

rs

Ziara ya kiserikali ya Rais waUchina mjini Dar es Salaam,Machi 2013.

Soko la Mwenge: kitovu chamuda mrefu cha biasharaya pembe za ndovu jijini Dar es Salaam.

23

Madai kama hayo yalitolewa na muuzaji mwingine katika soko laMwenge, akizungumza na waandishi wapekuzi mwaka 2010 kuhusuziara ya Rais wa Uchina Februari 2009: “Je, unanajua Rais waUchina Hu Jintao alipozuru Tanzania? Wao huja kuchukua vitu vingi.Lakini hiyo si kazi ya Hu Jintao, ni ujumbe wote. Kisha waohuelekea moja kwa moja hadi uwanja wa ndege, kwa sababu hakuna mtu hukagua begi za wageni mashuhuri”66 Mwaka 2006,wapelelezi wa EIA waliambiwa na wauzaji wa Mwenge kwambamaafisa katika Ubalozi wa Uchina walikuwa wanunuzi wakubwa wapembe za ndovu.

Uhusiano na Zanzibar

Uchunguzi wa EIA na uchambuzi wa shehena kubwa zilizonaswaunaonyesha kwamba Zanzibar imeibuka kuwa kituo kikubwa chakusafirisha shehena kubwa za pembe za ndovu nje ya Tanzania.Zanzibar inarejelea visiwa viwili - Unguja na Pemba - ambazo zinauhuru fulani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katikakarne ya 19, eneo hili lilikuwa na kituo cha biashra ya watumwa napembe za ndovu. Siku hizi inajulikana kama kivutio cha utalii, lakinisifa zake za zamani kama kituo cha biashara ya pembe za ndovuzimeanza kurudi.

Bandari kuu ya Malindi kisiwani Zanzibar inapendwa sana makundiya magendo nchini Tanzania kama njia ya kusafirishia pembe zandovu ughaibuni. Sababu ya bandari hii kupendwa ni dhahirishahiri; ni rahisi kupata kibali cha kusafirisha shehena

ikilinganishwa na bandari ya Dar es Salaam, sheria kuhusu biasharaya viumbe vilivyo katika hatari ya kuangamizwa ni tofauti ikilinganishwa na Tanzania bara, ina njia za meli zinazoelekea Asia,ukosefu wa vidhibiti vyenye ufanisi na maafisa fisadi bandarini.

Huchukua siku chache kupata kibali cha kusafirisha bidhaa kutokaZanzibar ikilinganishwa na majuma kadhaa katika bandari ya Dar esSalaam na meli husafirisha bidhaa mara kwa mara kati ya bandarihizo mbili. Majahazi ya kawaida pia hutumiwa kusafirisha mizigokutoka Tanzania bara, ikiwa ni pamoja na Kilwa upande wa Kusini,hadi eneo fulani karibu na bandari ya Malindi. Kuna mtandao wamawakala wa wasafirishaji mizigo kote kwenye bandari ambaowako tayari kutumia majina yao kama mawakili kwenye hati ilikuficha wamiliki halisi.

Sheria msingi ya wanyamapori ya Zanzibar, Sheria ya Usimamizi na Kuhifadhi Misitu (FRMCA) Kifungu.10 ya 1996, inalinda wanyamapori wanaopatikana ndani ya Zanziba pekee, hii ina maanakwamba ndovu, ambao hawako katika hatari ya kuangamizwahawajajumuishwa katika kundi hili. Hali hii pia inasababisha matatizo katika utekelezaji wa sheria ya CITES. Ijapokuwa askaripolisi na Idara ya Wanyamapori kutoka bara inonekana kuwa namamlaka ya kuchunguza uhalifu wa wanyamapori mjini Zanzibar,msingi wa kisheria kwa ajili ya uchunguzi huu haujafafanuliwa.Halikadhalika, adhabu zinazoelezwa chini ya FRMCA ni ndogo sana,huku adhabu ya juu sana kwa mtuhumiwa mwenye hatia ikiwa nikufungwa jela kwa muda usiozidi miezi sita au faini isiyopunguaShilingi 300,000 za Tanzania (Dola 185).67

Shehena kubwa za pembe za ndovu zimenaswa Zanzibar katikakipindi cha miaka mitano iliyopita; moja ya shehena hizo ilinaswaAgosti 2011. Kati ya pembe 1041 za ndovu zilizonaswa zikiwazimefichwa ndani samaki waliokaushwa zikisafirishwa kwendaMalaysia, na pembe zilizonaswa Novemba 2013 za uzani wa tani 2.9zilizofichwa ndani ya makaka na zilizohusishwa na tukio la nyumbaya makazi mtaani Mikochen. Shehena zaidi za pembe za ndovuzimenaswa Asia baada ya kusafirishwa kutoka Zanzibar. Angalaushehena sita zimenaswa katika bandari za Haiphong, Vietnam naHong Kong tangu 2009. Katika kila tukio, pembe zilikuwa zimefichwa katika makasha ya mazao ya baharini kama samakiwaliokaushwa, mwani na makaka.68

Agosti 2009, meli ya Kivietinamu, Vinashin Mariner, ilitia nangakatika bandari ya Haiphong ambapo kasha moja lililokuwa limesajiliwa kuwa na makaka ya konokono, lilikaguliwa na likapatikana na zaidi ya tani mbili za pembe za ndovu. Shehenahiyo ilikuwa imetoka Zanzibar. Hati zilionyesha wakala wa mizigoRamadhan Makame Pandu kutoka zanzibar, ambaye iliripotiwakwamba alikamatwa Desemba 2009.69 Januari 2011, raia wa KichinaLi Guibang alikamatwa jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kuhusikana shehena iliyonaswa Haiphong. Li alitajwa kuwa “mtu muhimu”aliyeratibu usafirishaji wa pembe za ndovu hadi Asia.70 DLicha yahadhi yake kama “mtu muhimu”, Li aliachiliwa kwa dhamana yashilingi milioni 80 za Tanzania (Dola 46,500) na Mahakama Kuu yaTanzania mwezi Machi 2011 na akatorokea nchini Kenya, akisaidiwana Salvius Matembo, mhusika wa biashara ya pembe za ndovuambaye baadaye alitiwa mbaroni kufuatia pembe za ndovu zilizonaswa Mikocheni.

Baadaye mwaka huo, pembe 1,041 za ndovu zilinaswa mwezi Agosti2011 katika bandari ya Malindi huko Zanzibar. Mzigo huo ulikuwaumewasili kutoka Dar es Salaam katika meli ya Tanzania ya MVBuraq; pembe hizo zilikuwa zimepakiwa ndani ya samakiwaliokaushwa kutoka Mwanza kaskazini mashariki mwa Tanzania.Wakala huyohuyo wa meli Ramadhan Makame Pandu alikuwa amepokea mzigo huo katika bohari yake karibu na soko la mboga

FAILI ZA KESI ZA EIA:©

ww

w.g

loba

lpub

lishe

rstz

.com

Bandari ya Malindi,Zanzibar: kituo chakusafirishia pembekwenda Asia.

“Mshukiwa muhimu” Li Guibangalitiwa mbaroni mwaka 2011kwa tuhuma za kusafirishapembe za ndovu hadi Vietnam,lakini aliachiliwa kwa harakakwa dhamana na akatoroka.

24

na matunda la mji wa Zanzibar. Iliripotiwa katika vyombo vyahabari kuwa mmiliki halisi wa pembe hizo alikuwa mtu kwa jina “Mr Lee” kutoka Dar es Salaam.71 Kufikia Oktoba 2014, Pandualikuwa bado kizuizini akisubiri kesi isikilizwe huku kukiwa nafununu kwamba Li alirudi Dar es Salaam.

Mnamo Septemba 2010, maafisa wa Forodha katika bandari ya HongKong walinasa makasha mawili yaliyokuwa yamebeba tani 1.5 yapembe zandovu zilizosafirishwa kutoka Zanzibar zikiwa zimeandikwakama dagaa wa baharini.72 Raia wa Uchina Huang Guo Lin, maarufukama Alimu, alikamatwa na kushatkiwa kwa kuuza pembe za ndovukinyume cha sheria na kujaribu kuwapa askari waliomtia nguvuni rushwaya shilingi milioni 17.5 za Tanzania (Dola 10,000).73 Hatimaye Huang aliachiliwa kwa dhamana na miaka minne baadaye kesi haijakamilika.

Kisadfa, Septemba 2014 wapelelezi wa siri wa EIA walikutana nawakala wa usafirishaji kutoka Zanzibar kwa jina SM Rashid. Mmiliki,Suleiman Rashid, alidokeza kwamba alikuwa wakala wa usafirishaji washehena iliyozuiliwa Hong Kong mwaka 2010. Kwa sababu jina lake lilionekana kwenye hati za usafirishaji, alikamatwa na kuwekwa kizuizini kwa muda wa mwezi mmoja mpaka ilipobainika kwambahakujua kilichokuwemo ndani ya makasha hayo. Aliongeza kuwamakasha mawili yaliyonaswa yalikuwa sehemu ya shehena tano zilizosafirishwa hadi Hong Kong ya ria huyo mmoja wa Uchina, lakinimawili hayakugunduliwa. Aidha, Rashid alikiri kupanga shehena zaawali za plastiki zilizosafirishwa na wateja wa Kichina hadi bandari yaHaiphong nchini Vietnam, njia iliyothibitishwa kwamba inatumiwakusafirisha magendo ya pembe za ndovu.

Kukua kwa umaarufu wa Zanzibar kama kivukio cha kusafirishamagendo ya pembe za ndovu kumechochewa na ongezeko la nakuibuka kwa makundi mengi ya uhalifu wa wanyamapori kutoka kusinimwa Uchina, ambayo hutumia bandari kama kivukio cha shehena zapembe za ndovu zinazosafirishwa kwenda Uchina.

Katika kipindi cha muongo uliopita, mtandao wenye siri kubwa wawanyabiashara kutoka eneo la Maoming Mkoa wa Guangdong nchiniUchina limetawala biashara ya pembe za ndovu kutoka AfrikaMashariki na Magharibi, huku Zanzibar ikiwa ni moja ya ngome kuu.Kundi hili kutoka Maoming limewang'oa wafanyabiashara kutokaPutian katika mkoa wa Fujian nchini Uchina ambao walitawala biasharahii kutoka kwa biashara hii.

Watu wengi wanaoshiriki katika biashara hii wanatoka mji waShuidong, katika eneo la Maoming. Shuidong ni kituo kikubwa chabiashara katika matango ya bahari, chakula ghali sana nchini Uchina.Wafanyabiashara wengi wa pembe za ndovu walio Zanzibar walikujaZanzibar kwanza kufanya biashara ya matango ya bahari na sasawanaitumia kuficha magendo ya pembe za ndovu.

Septemba 2014, wapelelezi wa siri wa EIA walikutana na mfanyabiasharawa matango ya bahari anayeishi Zanzibar kwa jina Wei Ronglu, kutokaShuidong. Mwanzoni, Wei alikataa kuhusika katika biashara ya pembeza ndovu lakini alionekana kuwa na maarifa mengi kuhusu biasharahiyo. Alieleza jinsi utekelezaji wa hivi karibuni ulikuwa umetatizabiashara ya pembe za ndovu lakini aliongeza kwamba makundi mawilimakuu yanayomilikiwa na watu kutoka Shuidong yalikuwa yakiendeshabiashara hiyo kutoka Zanzibar.

Alisema kwamba mwaka 2013, kundi moja lilifanikiwa kutuma hadimakasha 20 ambamo pembe za ndovu zilikuwa zimefichwa na zikafikishwa Uchina, kwa kawaida hupitia Hong Kong. Alidai kwambakwa wastani, moja kati ya makasha 20 ya pembe za ndovu hunaswa;na kila shehena huwa na kati ya tani mbili hadi tatu za pembe zandovu, huku bidhaa za thamani ya chini kama makaka na samakiwaliokaushwa wakitumiwa kuficha pembe za ndovu. Matango ya

bahari huwa hayatumiwi kwa sababu gharama ya kupoteza pembe za ndovu na matango iwapo shehena itanaswa itakuwa kubwa zaidi.

Makundi ya Shuidong yana uangalifu mkubwa na hutumiaWatanzania wanaowaamini kuendesha shughuli zao. Ushirika waaina hii unaweza kuchukua mwaka kuujenga. Jukumu laWatanzania ni kupanga usafirishaji na kusimamia uhusiano namaafisa fisadi bandarini. Mabosi kutoka Uchina hutulia nahawawasiliani na shehena hadi wapate Hati ya Kuchukulia Mizigo,ili kuruhusu makasha yakifika Asia, mara shehena inapopakiwakwenye meli . Mara nyingi siku ya kupakia mzigo, makundi hayahuchunguza shughuli hiyo kwa umbali ili wahakikishe hakuna matatizo yoyote katika dakika za mwisho. Mara nyingi huwawamekata tikiti za ndege tayari kuondoka Tanzania siku hiyoendapo lolote litatokea.

Mipango kabambe huwekwa ili kutunza muda wa kusafirisha nje ilikuhakikisha kwamba maafisa wa forodha wanaolipwa na makundihaya wako tayari siku ya kuondoka. Kawaida ada inayolipwa kuhakikisha shehena haitakaguliwa kabla ya kusafirishwa ni Dola70 kwa kila kilo ya pembe za ndovu. Makundi ya Shuidong hutumia akaunti za benki kusini mwa Uchina ili kugharamia shughuli hii.'Wawekezaji' wa kuaminiwa hulipa kabla ya bidhaa kusafirishwa ilikulipia gharama za kupata na kusafirisha pembe za ndovu na kishahulipwa mara pembe za ndovu zinaposambazwa na kuuzwa nchiniUchina na wanachama wa ndani wa makundi haya.

Wei alithibitisha kwamba raia watatu wa Kichina waliotiwa mbaronikatika nyumba ya makazi mtaani Mikocheni walikuwa kutokaShuidong lakini walikuwa wa ngazi ya chini na walifanya kosa lakupakia pembe za ndovu mahali walikuwa wakiishi. Baada ya kukutana na Wei, wapelelezi wa EIA waliwasiliana na yeye kwa njiaya simu mara kadhaa. Alikubali kupanga mkutano na wanachamawa kundi hilo kutoka Maoming, akiwataja kama ndugu zake nakusema kwamba itahitaji kulipa Dola milioni 1.3 mdio mkutamoufanyike.

Uchunguzi wa EIA unaonesha kwamba kampuni zinazoongozwa nawahalifu kutoka Uchina zimechagua bandari ya Zanzibar makusudikama kivukio kikuu cha usafirishaji wa pembe za ndovu kwasababu ya ulegevu wa udhibiti wake na urahisi wa baadhi yamaafisa wake kuchukua rushwa. Mfanyakazi mmoja wa bandarialisema Zanzibar ndio bandari kubwa zaidi Afrika ya kusafirisha njepembe za ndovu.

Matango ya bahari yathamani kubwa yakikaushwanje mjini Zanzibar, tayarikusafirishwa kwenda Uchina .

Niassa

Hufadhi ya Taifa ya Niassa kaskazini mwa Msumbiji inapakana naHifadhi ya Selous katika nchi jirani ya Tanzania. Pia Niassa imepatwana janga la ujangili wa ndovu, huku Watanzania wakihusishwakatika baadhi ya matukio na pembe za ndovu kuvuka mpakaambao hujadhibitiwa ardhini na kwa kutumia boti ndogo.

Mwaka 2009, idadi ya ndovu katika hifadhi ya Niassa ilikuwa20,374 lakini kufikia mwaka 2013 idadi hiyo ilipungua hadi ndovu13,000, asilimia 36 kila mwaka. Katika wiki mbili za kwanza zamwezi wa Septemba 2014 peke yake, ndovu 22 waliuawa katikahifadhi ya Niassa.74 Katika mwezi huo, ujangili wa ndovu ulitangazwa kuwa "janga la kitaifa" huku ndovu watano wakiuawakila siku.75 Utafiti wa angani katika hifadhi ya Niassa wa mwaka2011 ulihesabu ndovu 12,026 na mizoga 2627. Sensa ya mwaka2013 katika Hifadhi ya Kitaifa ya Quirimbas iliyo karibu na Niasailipata ndovu 854 hai na mizoga 811.76

Ushahidi wa kutosha unaonesha kushiriki kwa magenge yaujangili kutoka Tanzania na wafanyabiashara wa pembe za ndovukatika mauji ya ndovu kaskazini mwa Msumbiji. Inakadiriwakwamba karibu nusu ya majangili wanaowinda katika Hifadhi yaNiassa ni Watanzania, wakisaidiwa na maafisa fisadi kutoka nchizote mbili.77 Mapema September 2014, watu sita wa genge lamajangili walitiwa mbaroni katika eneo la Niassa baada ya uchunguzi wa miaka 10 uliofanywa na askari polisi na askari wawanyamapori. Genge hilo lilikamatwa lilipokuwa likisafirishapembe 12 za ndovu na walinyang'anywa bunduki za kuwinda.Wanne kati ya majangili walioshikwa walikuwa raia wa Tanzania.Mmoja wa genge hilo alikiri kuua ndovu 39 katika hifadhi yaNiassa mwaka 2014.78 Mwaka 2011, maafisa kutoka Hifadhi ya Taifaya Quirimbas aliambia EIA kuhusu uwepo wa Watanzania katikaeneo hilo, ambao waliwalaumu kwa kuanza kutumia sumu kamanjia ya kuwaua ndovu.79

Data ya shehena zilizonaswa na mazungumzo na wafanyabi-ashara wa soko la Mwenge inaonyesha kwamba baadhi ya pembeza ndovu zinazotoka kaskazini mwa Msumbiji huvuka mpaka nakuingia Tanzania na huwa sehemu ya shehena ambazohusafirishiwa hadi Asia. Mwaka 2006, wafanyabiashara kadhaakatika soko la Mwenge walidai kwamba walitoa pembe zao zandovu kutoka Msumbiji. Aidha, uchambuzi wa DNA unaonyeshakwamba baadhi ya shehena ya pembe 781 zilizonaswa nchiniMalawi mwaka 2013 katika lori lililotoka Tanzania zilitolewa katikaHifadhi ya Niassa.80

Pia pembe za ndovu zilizowindwa kwa ujangili kutoka hifadhi zaNiassa na Quirimbas husafirishwa moja kwa moja nje ya Msumbijikwenda Asia kupitia bandari ya karibu ya Pemba. Kampuni nyingikutoka Uchina za kukata miti na wafanyabiashara wa mbao wanapatikana katika eneo hili na kiwango kikubwa cha magogona mbao zinazosafirishwa kwenda Uchina hutoa njia rahisi yakuficha magendo ya pembe za ndovu.

Mapema mwaka 2011, operesheni ya utekelezaji ilipata makasha161 ya magogo yaliyopigwa marufuku yakiwa tayari yamepakiwakwenye meli tayari kwa safari ya bandari ya Pemba. Pia uvamizihuo ulinasa pembe 166 za ndovu zikiwa zimefichwa ndani yamagogo katika baadhi ya shehena. Wafanyakazi wawili wa kampuniya Kichina ya kukata magogo iliyohusishwa na shehena hiyo walitoroka nchini.81 Julai mwaka 2009, maafisa wa forodha katikabandari ya Haiphong nchini Vietnam walinasa kilo 600 za pembeza ndovu zikiwa zimefichwa katika shehena ya mbao. Shehenahiyo ilikuwa imetoka katika bandari ndogo ya Mocimboa da Praiakaskazini mwa Msumbiji na ilikuwa ikisafirishwa na kampuni inayomilikiwa na serikali ya Uchina kwa jina Senlian Corporation.82

FAILI ZA KESI ZA EIA:

25

HAPO JUU:Idadi ta ndovu katika hifadhiya Niassa wamepungua kwaasilimia 36 tangu 2009.

26

Mara nyingi mizigo ya pembe za ndovuzinazosafirishwa kutoka Tanzania katikamakasha ya kusafirisha hatimaye hadiUchina hufuata njia ambazo ni ngumukueleweka zinazochapitia nchi nyingikuanzia Mashariki ya Kati, Asia yaKusini na Asia ya Kati. Katika matukiofulani, kupitia nchi nyingine katikasafari huwa ni ratiba za safari ya meliambazo huendeshwa na kampuni zinazosafirisha mizigo kutoka Tanzania.Kwa mfano, kampuni ya meli ya CMA-CGM hutumia Port Klang nchiniMalaysia kama kituo cha kusafirishiashehena zinazotoka Afrika Masharikizikisafirishwa hadi Asia. Kampuninyingine za meli hutumia bandari yaMilki ya Falme za Kiarabu ili kuunganisha njia za Afrika Mashariki na kuendelea na safari hadi Asia.

Nchi tatu zinaweza kutumiwa na katikasafari inayotumiwa na wafanyabiasharaya megendo kusafirisha shehena yapembe za ndovu, Athari yake ni kwambahali hii huficha chanzo cha mzigo katikajitihada za kuepuka hatari katika ofisi zaforodha katika bandari ambayo mzigounapaswa kusafirishwa. Kwa mfano,Oktoba mwaka 2013 maafisa wa forodhakatika bandari ya Haiphong, kaskazinimwa Vietnam, walinasa shehena mbiliza pembe za ndovu zenye jumla ya uzaniwa tani 4.4, zilizosafirishwa kama makaka. . Ingawa njia hii ya kufichwahuhusishwa na shehena za pembe zandovu mjini Zanzibar, Hati yaKuchukulia Mizigo ilikuwa ya kutokabandari ya Port Klang nchini Malaysiaikielekea Haiphong, hivyo basi kufanikiwa kuficha asili ya mzigo.

Kati ya mwaka 2009-13, nchi hizo zakusafirishia mizigo ambazo mara nyingihuhusishwa na magendo ya pembe zandovu - Hong Kong, Vietnam, Malaysiana Ufilipino -. zilihusika katika asilimia62 ya shehena kubwa zilizonaswa, jumlaya tani 41 za pembe za ndovu.83

Uchunguzi uliofanywa na EIA unaonyeshakwamba bandari muhimu zaidi kati

kusafirisha magendo ya pembe za ndovukutoka Tanzania hadi Uchina ni HongKong na Haip Hong nchini Vietnam.Umaarufu wa bandari hizi mbili si kwasababu ya njia za meli; huchaguliwamakusudi na makundi yanayouzamagendo ya pembe za ndovu wakitafutanjia salama kabisa za kufikia soko nchini Uchina.

Hong Kong

Hong Kong hutumika kama kituo kikubwacha kusafirishia pembe haramu za ndovukwenda Uchina. Kati ya mwaka 2009-14,mamlaka ya Hong Kong ilinasa angalautani 18 za pembe za ndovu, na thuluthimbili za pembe hizo zilinaswa tangumwaka 2012.84 Tanzania imeibuka kamachanzo kikubwa cha pembe za ndovuzilizonaswa Hong Kong.

Faida kubwa kwa wanaoendeshabiashara ya pembe za ndovu ni wingi wamizigo inayopitia bandari ya Hong Kong,ambayo ndiyo bandari tatu duniani kwawingi wa mizigo, mwaka 2012 jumla yamakasha milioni 23 yalipitia katika bandari hii.85 Wingi wa makasha naumuhimu wa kukagua mizigo kwa haraka ina maana kwamba ni makashamachache sana hukaguliwa.

Sababu nyingine muhimu ni kuwepo kwamawakala wataalam wa mizigo katikabandari ya Hong Kong wenye uzoefu,ujuzi na watu wanaosongeza mizigo,ikiwa ni pamoja na magendo, hadiUchina. Mara nyingi mchakato huu unatumia ulaghai na/au kubadilisha hatiza kusafirisha mizigo ili kuficha chanzohalisi cha mizigo, hivyo kuifanya kuwavigumu kuifuatilia. Kwa mfano mapemamwaka 2014 wachunguzi wa EIAwakipeleleza biashara ya mbao zamwaridi mti ambao ni marufuku kutokaAfrika na Asia hadi Uchina walikutanana mawakala kadhaa wa utaratibu wausafirishaji mjini Hong Kong ambaowalikuwa wakisafirisha mbao kwendaUchina.86 Wakala mmoja alikuwa tayari

© H

ong

Kong

Cus

tom

s an

d Ex

cise

NCHI ZA KUSAFIRISHIAHAPO JUU:Agosti, 2011:Kilo 1,898 za pembe za ndovuzilinaswa Hong Kong, zikiwa katika magunia ya chumvi.

27

kusafirisha magogo ya mwaridi hadibandari za Mkoa wa Guangdong nchiniUchina kwa ada ya Dola 2,300 kwa kilatani, mti ambao chini ya CITES haupaswikukatwa. Wakala huyo alikuwa tayarikutoa ridhaa ya Dola 6,500 kwa kila taniiwapo shehena hiyo ingenaswa.

Uwepo wa makundi yanayosafirishapembe za ndovu katika nchi nyingi bainaya Hong Kong na Guangdong unadhihirikakupitia kisa kinachohusu kunaswa kwamakasha mawili katika bandari ya HongKong Oktoba 2012. Ukaguzi wa makashahayao, moja kutoka Tanzania na linginekutoka Kenya, ulipata tani 3.8 za pembeza ndovu. Makasha hayo hayakukaguliwakwa bahati na sibu bali yalichaguliwakufuatia operesheni ya ujasusi wa miezisita iliyofanywa na maafisa wa utekelezaji katika Mkoa wa Guangdong,waliokuwa wakichunguza magendo yapembe za ndovu zilizoingia miji yaShenzhen, Zhongshan na Dongguan.Kunaswa kwa sehehena hii kulipelekeakutiwa mbaroni kwa watuhumiwa nchiniUchina, ikiwa ni pamoja na mkazi mmojawa Hong Kong.87

Ingawa kugundua magendo ya wanyamapori ni moja ya kipaumbele chaforodha ya Hong Kong na ushirikiano nawenzao kutoka Uchina umekuwa naufanisi, hadi sasa shehena kubwa zapembe za ndovu zilizonaswa Hong Konghazijapelekea kufunguliwa kwa mashtaka yoyote.

Haiphong Haiphong ndiyo bandari kuu ya kimataifainayofanya kazi kaskazini mwa Vietnam.Inatumika pia kama njia ya magendokadhaa, ikiwa ni pamoja na bidhaachakavu za elektroniki, bidhaa zinazotokana na wanyamapori na mbaozinazokatwa kinyume cha sheria zikisafirishwa kwenda Uchina.

Kwa kawaida bidhaa zinazowasiliHaiphong zikielekea Uchina husafirishwabarabarani zikiwa na mhuri wa forodhaya Haiphong ili zikaguliwe katika kivukiokikuu cha Mong Cai, kilicho kati ya Mkoawa Quang Ninh nchini Vietnam naGuangxi nchini Uchina. Katika visa vingiambavyo pembe za ndovu hunaswa,mawakili huwa ni mawakala wa mizigowalio Haiphong au Mong Cai.

Kivukio cha Mong Cai kina makundimengi ya wahalifu, wanaosadiwa namaafisa fisadi wa forodha na kudhibitimpaka ambao hutoza ada fulani ilikuruhusu mizigo kupitia mipaka ambayosi rasmi. Ufuatiliaji wa kina wa eneo lampaka wa Mong Cai umebaini kwambakati ya magari 16,800 yanayoelekeaUchina, ni asilimia mbili pekee yaliyotumiakivukio ramsi cha kimataifa.88

Hakuna sababu zozote za kiuchumi zakutumia njia ya Haiphong-Mong Cai

kusafirisha mizigo hadi kusini mwaUchina. Uchanganuzi wa gharama zakusafirisha kasha moja la samakiwaliokaushwa kutoka Tanzania hadiGuangdong unaonyesha kwamba njia yamoja kwa moja kutoka Dar es Salaamhadi Guangzhou kupitia Shenzhenitagharamu Dola 1,683 kwa wastani,ikilinganishwa na Dola 2,480 kusafirishakasha moja kutoka Dar es Salaam hadiGuangzhou kupitia Haiphong na MongCai.89 Sababu kuu ya kutumia njia hii nikunufaika kutokana na udhibiti ambao siimara na wingi wa mawakala fisadiwanaopatikana Mong Cai.

Mapema 2014, wachunguzi wa EIAwaliokuwa wakifuatilia usafirishaji wamiwaridi kutoka Vietnam hadi Uchinawaliambiwa kwamba, kutokana nakuongezeka kwa uangalizi kwenye kituocha Mong Cai, shughuli za magendozilikuwa zihamishiwe maeneo yamagharibi hadi kivukio cha mpaka waLang Son. Hali hii inaonekana kwambailihusu usafirishaji wa pembe za ndovupia. Manamo Oktoba 2013, maafisa waforodha ya Haiphong walinasa tani mbiliza pembe za ndovu katika shehenailisajiliwa kama makaka. Hati za forodhazilionyesha kwamba kasha hilo lilikuwalisafirirshwe tena hadi Uchina kupitiaLang Son.90

Visa vya kunaswa kwa pembe za ndovupia vilifanyika mpakani katika Mkoa waGuangxi. Mapema mwaka 2009, raia sitawa Kichina walikamatwa kwa kusafirishamagendo ya pembe za ndovu kutokaVietnam kupitia Guangxi na Guangdonghadi Mkoa wa Fujian, nchini Uchina.Mshukiwa mkuu, Li Zhiqiang kutokaXianyou Mkoa wa Fujian, alikuwa amesafiri hadi Haiphong kukagua pembehizo za ndovu, ambazo zilisafirishwa katika lori la jokofu la kusafirisha samakiwaliokaushwa hadi Guangdong ambapozilihamishiwa kwenye masunduku yambao tayari kwa safari ya kwenda Fujian,mojawapo wa vituo vya biashara yapembe za ndovu nchini Uchina.91 Aprili2011, askari waliokuwa katika doriakwenye barabara kuu walikagua lorikaribu na mpaka wa Vietnam likielekeakatika mji wa Nanning na kupata pembe707 za ndovus.92

Ingawa Haiphong inatajwa mara kwamara kama kitovu cha usafirishaji wapembe za ndovu zinazopelekwa Uchina,hakujakuwa na mtu anayehusishwa nashehena zilizonaswa bandarini aliyeshtakiwa na hakuna ushahidiwowote unaonyesha kwamba maafisa wa serikali ya Vietnam wanashiriki taarifa za ujasusi na nchi ambako pembehizo hutoka barani Afrika au na sokolengwa la Uchina. Maafisa wa Tanzaniawalipoomba ruhusa ya kusafiri hadiVietnam kuchunguza tani sita za pembeza ndovu zilizonaswa Machi 2009 katikabandari ya Haiphong, walikatazwa vibalivya kusafiri.

“Kufikia sasa, nyingiya shehena kubwa za pembe za ndovuzilizonaswa HongKong hazijapelekeawatuhumiwa kufunguliwa mashtaka.”

28

Mbali na janga la ujangili dhidi ya ndovu nchini Tanzania, pembe za ndovuhutengeneza bidhaa za mapambo yathamani kubwa nchini Uchina, sokokubwa zaidi la pembe haramu za ndovu duniani.93

Ongezeko linaloshuhudiwa la biasharaharamu ya pembe za ndovu nchiniUchina ni matokeo ya visababishi kadhaa vinavyohusiana: kubuniwa kwasoko tofauti lililohalalishwa la pembe zandovu nchini Uchina kupitia maamuzi yaCITES, nafasi ya Serikali ya Uchina nasekta hiyo katika kuchochea mahitaji yabidhaa za pembe za ndovu, na kushindwakusimamisha usafirishaji wa pembeharamu za ndovu kupitia Hong Kongkuelekea Uchina.

Tatizo hili limekuwa likiongezeka tangumwishoni mwa miaka ya 1990. Mwaka1999, nusu ya jumla ya pembe za ndovuzilizonaswa kote duniani zilikuwa zikisafirishwa kwenda Uchina.94 Mwaka2000, EIA ilikuwa mojawapo wamashirika ya kwanza kuonya dhidi yaongezeko la pembe za ndovu nchiniUchina baada ya uchunguzi mjiniGuangdong uliobaini biashara mpya iliyoingia katika soko hilo.95

Ingawa sheria ya Uchina inaruhusubiashara ya pembe za ndovu zilizopatikana kabla ya marufuku kutolewa, kiwango cha pembe za ndovu

zilizorekodiwa na EIA katika msururuwa uchunguzi, pamoja na taarifa kutokakwa mazungumzo na vyanzo bidhaa hii,inaonyesha bayana kwamba kufikiamwaka 2002 soko nchini Uchina lilitegemea pembe za ndovu zilizosafirishwa kama magendo, ambazoziliingia katika soko ambalo udhibiti wakesi imara nchini kinyume cha sheria.96

Uchunguzi nchini Uchina pia ulionyeshajukumu la Serikali katika biashara hii,hususan ni viwanda vya kuchongapembe za ndovu na maduka yanayomilikiwa na serikali. Uchunguziwa EIA kwa mfano ulianika wazi vyanzovya pembe za ndovu vya kutiliwa shakazinazouzwa na kampuni ya Uchina mjiniGuangzhou, Yue Ya, ambayo ilisambazapembe za ndovu kwa Maduka ya Urafikiyanayomilikiwa na Serikali. Mbali nahayo, iliripotiwa kwamba kati ya mwaka1990 hadi 2004, pembe haramu zandovu zilizonaswa na Serikali ya Uchinaziliuzwa katika soko la ndani na, mweziNovemba 2004, mamlaka katika mkoawa Guangdong zilipiga mnada wa takriban tani moja ya pembe haramu zandovu kwa wafanyabiashara wa ndani.97

Uchunguzi na utafiti wa EIA uliofanywakati ya 1999-2005 ulionyesha kukuakwa nafasi ya Uchina katika katikabiashara haramu ya pembe za ndovu,ikiwa ni pamoja na:

SOKO KUU: UCHINA

“Kufikia 2002 sokonchini Uchina lilitegemea pembeharamu za ndovu,ambazo zilikuwa zikiuzwa kwa urahisikatika soko la magendo ambalohalidhibitiwi”

29

• Uchunguzi na utafiti wa EIA uliofanywa kati ya 1999-2005 ulionyesha kukua kwa nafasi ya Uchina katika katika biashara haramu ya pembe za ndovu, ikiwa ni pamoja na:

• Uchunguzi wa EIA uliofanywa Hong Kong, Shanghai na Beijing mwaka 2002 uligundua kwamba biashara ya pembe za ndovu mjini Hong Kong ilikuwa imepungua lakini ilikuwa ikiongezeka nchini Uchina ambapo raia wa Kichina ndio walikuwa wanunuzi wakuu. Ingawa Serikali ya Uchina ilikuwa imeanzisha mpango wa kuweka alama ili kudhibiti biashara haramu ya pembe za ndovu na kuzuia biashara hii haramu, Shirika la EIA lirekodi visa vya biashara haramu ya pembe za ndovu mjini Beijing, Tianjin na Guangzhou ambapo pembe 'mpya' za ndovu kutokaAfrika zilikuwa zikiuzwa. Mfanyabiashara mmoja aliambia wachunguzi wa EIA kwamba njia za kidiplomasia zilitumiwa mara nyingi kusafirisha pembe za ndovu ndani ya Uchina kinyume cha sheria;

• Hati ya Serikali ya Uchina ambayo wachunguzi wa EIA walifanikiwa kupata ya mwaka 2003 ilionyesha kwamba utafiti wa akiba ya Serikali ya pembe za ndovu uliofanywa mwaka uliotangulia uligundua kwambatani 110 za pembe za ndovu zilikuwa zimepotea, na ikaongeza kwamba kiwango kikubwa kiliuzwa kinyume cha sheria;98

• Mwaka 2005, wachunguzi wa EIA mjini Guangzhou walinakili matatizo sugu katika mfumo wa kuidhinisha na kudhibiti pembe za ndovu nchini Uchina. Wafanyabiashara walikuwa wakiuza pembe za ndovu bila vibali halali na walitoa habari za kina kuhusu magendo ya pembe za ndovu.

Ingawa kwa upande mwingine baadhiya wafanyabiashara walionekana wakiuza pembe za ndovu kulingana na sheria kwa sababu ya kuogopa kushikwa, kuliwa na wafanyabiashara wakubwa waliokuwa radhi kuuza pembe za ndovu kinyume cha sheria.

Mienendo ya Soko

Mwaka 2002, Uchina ilikosoa uamuzi wa mauzo ya "majaribio" ya pembe zandovu nchini Japan kama sababu kuu yaongezeko la kiasi kikubwa cha pembe zandovu zinazoingia nzhini kinyume chasheria, ikihoji kwamba mauzo hayo yaliwachanganya watumiaji wengi nchiniUchina: “Wachina wengi hawaelewiuamuzi huo na wanaamini kwambabiashara ya pembe za ndovu kimataifaimerudishwa.”99

Hata hivyo, kufikia mwaka 2005 nchi yaUchina ilikuwa imeamua kwamba ilitakapia kufaidika kutokana na biashara yapembe za ndovu na ikaanza kampeni yakutaka kuuzwa kwa hifadhi nyingine yapembe za ndovu ambazo ingenunua.Katika hali hii ya kuongezeka kwaujangili na magendo ya pembe za ndovu,wanachama wa CITES walikubalikuuzwa kwa akiba nyingine ya pembe zandovu mwaka 2008, wakati huu kwaUchina na Japan. Iliafikiwa kwambapembe hizo ziuzwe kwa msingi kwambaUchina itatekeleza kanuni kali za kudhibiti biashara ya pembe za ndovunchini na kwamba uuzaji wa akiba halaliungejaza soko la Uchina na pembe zandovu za bei ya chini, hivyo kumalizasoko la magendo ya pembe za ndovu.Kwa kweli, waliopigia upatu mauzo hayawalishindwa kuelewa uwezekano waongezeko la matumizi ya bidhaa zapembe za ndovu nchini Uchina. Tanguwakati huo, uchunguzi wa EIA namashirika mengine kadhaa umeonyeshakushindwa kwa mauzo ya 2008 kufikialengo lolote lilitarajiwa.100

China ilinunua tani 62 za pembe zandovu katika mnada wa CITES.Kampuni nne za pembe za ndovu zinazomilikiwa na Serikali- ChinaNational Arts & Crafts GroupCorporation (pia inayojulikana kamaGongmei), Beijing Ivory Carving Factory,Guangzhou Daxin Ivory Factory naBeijing Mammoth Art Co Ltd - zilishirikina zilinunua pembe za ndovu katikamauzo hayo.101 Pembe hizo za ndovu zilisambazwa kwa kampuni nyingineyenye kibali kupitia minada ya ndani,lakini ni mnada mmoja tu ulifanyikakatika kipindi cha 2009-11. Tani 40 katiya jumla ya pembe zilizonunuliwa naUchina katika mnada huo, zilinunuliwana kundi la Gongmei. Wakati huo huo,juhudi zilifanywa na Serikali, viwandana vyombo vya habari nchini Uchina ilikukuza matumizi ya pembe za ndovu

HAPA CHINI:Bidhaa za thamani za pembe za ndovu zikionyeshwamjini Guangzhou, nchiniUchina, 2010.

30

kama urithi wa utamaduni na kamauwekezaji wenye faida kubwa.

Shirika la Usimamizi wa Misitu laUchina (SFA) ndilo lenye jukumu la kudhibiti biashra yote halali ya pembe zandovu, hasa kupitia mfumo wa usajiliuliozinduliwa mwaka 2003 ambao ulihakikishs vyombo vyote vinavyohusikana pembe za ndovu halali vinapaswakutangaza hadharani Cheti cha Usajilikatika eneo wanaloendeshea shughulihiyo na bidhaa zote halali za pembe zandovu zinapaswa kuuzwa zikiwa na Kadi ya Utambulisho wa Bidhaa zaPembe za Ndovu. Kwa bidhaa za pembeza ndovu zenye uzani wa zaidi ya kilo50, Kadi ya Utambulisho wa Bidhaa zaPembe za ndovu lazima iwe na picha yabidhaa hiyo.

Mwaka 2004, viwanda tisa vya kuchonga vinyago vya pembe za ndovuna maduka 31 yaliruhusiwa na SFAkuzalisha na kuuza ‘pembe halali zandovu’, ambazo wakati huo zilidaiwakujumuisha pembe za ndovu kabla yamarufuku kuwekwa.102 Kufuatiaongezeko la pembe zaidi za ndovu kutoka CITES mwaka 2008, sasa kunazaidi ya viwanda na maduka 180 yapembe za ndovu, maduka mengi yakiwaBeijing, Shanghai, Guangzhou na Fujian.Hivyo basi, kampuni nne zinazomilikiwana serikali ambazo zilinunua pembe zandovu zilizonadiwa zinafanya kazi kamamuungano wa ukiritimba, kwa kuuzatani tano pekee za pembe ambazomwaka mmoja baada ya mnada, kunafaida kubwa ya Dola 1,500 kwa kilokutoka bei ya kununua ya dola 157 kwa kilo.103

Uchunguzi wa EIA uliofanywaGuangdong mwaka 2010 ulibaini kwamba wauzaji wa pembe za ndovuwanaoaminika kuwa asilimia 90 yawauzaji wa pembe za ndovu eneo hilowalipata mizigo yao kutoka kwa vyanzoharamu.104 Mifumo ya Uchina ya udhibitiwa ndani ni duni na dhana kwambamauzo halali yangepunguza mahitaji yapembe haramu za ndovu si ukweli.

Uchunguzi wa EIA MjiniGuangdong na Fujian

Novemba 2010 na Septemba 2013,wapelelezi wa EIA walizuru mkoa waGuangdong na Fujian, mikoa miwili yakusini mwa Uchina inayojulikana kamakitovu kikubwa katika magendo yapembe za ndovu na vituo vya kuchonga.Visa vikubwa vya shehena za pembe zandovu zilizonaswa nchini Uchina katikamiaka ya karibuni vimetokea katikamikoa hii miwili.

Mwaka 2010, wapelelezi wa EIA walikutana na wakikutana nawafanyakazi wa kampuni nne kati yasaba zilizopewa kibali cha kuzalisha na

kuuza pembe za ndovu katika mkoa waGuangdo. Mmoja wa wafanyabiasharahao kutoka Guangzhou- aliiambia EIAkwamba viwanda vyenya leseni hulazimika kununua ugavi uliotengwakila mwaka kutoka kwa kampuni chachezinazojulikana, ambazo huongeza bei zapembe za ndovu. Alilalamika kuwa ugaviwa Serikali ni ghali mno na pembe zinazosambazwa hazitoshi.Hali ambayoilibainika katika bei ya kuuza ya bidhaaza pembe za ndovu katika maduka yenye leseni mjini Guangzhou, ambayoghali sana ikilinganishwa na madukamengine.

Mwaka 2013, wachunguzi wa EIAwalikutana na wafanyakazi wa kampuni tano kati ya nene zilizopewaleseni na SFA katika Mkoa wa Fujian.Mazungumzo yalionyesha kwambapembe ghafi za ndovu kutoka kwamanda huo zilikuwa zikiuzwa hadi dola3,000 kwa kilo. Mfanyabiashara mmojaalidokeza kwamba FSA sasa inawatakawauzaji wenye leseni kuuza buidhaa zandovu kwa bei isiyopungua RMB 40,000kwa kilo (Dola 6,500) la sivuo wataadhibiwa kwa kupatiwa mgaomdogo wa kuzalisha, mgao wa kilamwaka uliowekwa na SFA.

Katika Mkoa wa Guangdong na Fujian,bei ya malighafi ya pembe za ndovu katika soko nyeusi iko chini kuliko beiya pembe za ndovu 'halali' na imekuwaikipanda kwa kasi. Wapelelezi wa EIAwakiwa ziarani hivi karibuni nchiniUchina waligundua kwamba ingawamalighafi halali ya pembe za ndovu nichache, pembe haramu za ndovu zinapatikana kwa urahisi ndizohupatikana kwa wingi.

Mwaka 2010 wachunguzi wa EIAwalikutana na wazalishaji na wauzaji wapembe za ndovu ambao hawana vibalipamoja na wafanyabiashara wenyeleseni. Mazungumzo haya yalionyeshasoko huru ambalo halidhibitiwi ipasavyo,

HAPO JUU:Duwei karibu na Xianyoumkoa wa Fujian, kitovumuhimu cha uzalishaji nabiashara ya pembe za ndovu.

31

huku Guangzhou ikiwa ndicho kituokikuu. Wafanyabiashara walizungumziamtandao wa wauzaji mjini Guangdong,wanaodhibitiwa na 'bosi watatu wenyeushawishi'. Makundi haya yanahamishanjia za kusafirisha magendo kama vilekupitia kaskazini mwa Vietnam, nambinu za kisasa kama vile kufichapembe za ndovu katika masanduku yachuma yanayoning'inia chini ya meli, na hata hubadilisha bei ya bidhaa sokonikwa kuweka akiba kubwa ya pembe za ndovu.

Wapelelezi wa EIA walipozuru Mkoa waFujian mwaka 2013, kituo kinginemuhimu cha kusafirisha magendo nchiniUchina, kulikuwa na wasiwasi dhahirimiongoni mwa wafanyabiashara wapembe za ndovu - shughuli za utekelezajiwa hivi karibuni ambazo zimepelekeakutiwa mbaroni kwa watu mashuhurizimewafanya wafanyabiashara kuwa natahadhari zaidi. Hata hivyo, EIAilithibitisha kuwa ingawa biashara haramu ya pembe za ndovu imekuwa yasiri zaidi bado inaendelea kustawi; “kilamfanyabiashara aliye ndani anajua niwapi pa kupata bidhaa,” alidai mfanyabiashara asiye na kibali wapembe za ndovu.

Mkoani Fujian, biashara ya pembe zandovu imeenea kote kwenye mkoa lakiniiko zaidi katika vituo vya kuzalishakama vile Fuzhou, Putian na Xianyou.Huko, pembe za ndovu huzalishwa naviwanda vya kuchonga kama kawaidaambavyo pia hutengeneza samani navinyago vya mwaridi nchini Uchina.105

Vituo vikuu ni pamoja na Minhou karibuna Fuzhou, Baxia, na Duwei karibu naXianyou, ambapo wauzaji hupata bidhaazao na wasafirishaji wa pembe za ndovuhuficha magendo yao. Duru zinaarifukwamba mjini Xianyou peke yakekulikuwa na mitandao nane iliyokuwaikiendesha biashara ya pembe za ndovu

kabla ya operesheni za utekelezaji mwak 2012. Kwa kawaida vinyagovilivyokamilika husambazwa ndani yamitandao ya wafanyabiashara wakuaminiwa na aghalabu huishia katikamiji kama vile Beijing na Shanghai.Kubadilisha kati ya magogo ya mwaridina biashara ya pembe za ndovukunaonyesha kukutana kwa aina zauhalifu wa wanyamapori; njia sawa zausafirishaji wa magendo zinatumia nausafirishaji wa shehena za mbao zinatoanafasi mwafaka ya kuficha pembe za ndovu.

Pia EIA ilinakili ushahidi kuhusu jinsiwafanyabiashara walio na kibaliwanavyoshirki katika soko la magendoya pembe za ndovu na kutumia pengolinaloachwa na mfumo wa usajili waSerikali. Wakati wa mkutano na kampuni halali wa bidhaa za ndovu yaFujian Zhengang ilibainika kwambakampuni hiyo ilizalisha bidhaa zenyenambari zinazofanana ikitumia chetikimoja ili kukwepa mgao mdogouliowekwa wa kuzalisha.

Mkutano wa baadaye na mmiliki wakampuni kutoka Duwei ya FulingCarving alithibitisha kuwa hapo awaliZhengang aliwahi kununua pembe haramu za ndovu kinyume kutokakwake. Kampuni nyingine yenye leseni,Xianyou Senyi Xianshi Crafts Ltdiliyokuwa ndio kwanza imepewa kibalicha hadhi ya biashara, lakini mmilikiwake Fang Zhishun, aliyekuwa piamwakilishi wa Jiji la Putian katikaChama cha Kitaifa cha People'sCongress aliwaambia wachunguzi waEIA kwamba alikuwa na mipango yakutafuta pembe haramu za ndovu nakutumia leseni yake kuuza bidhaa hizokatika mfumo halali. Wakati wa mkutano huo alipigia muuzaji wa magendo ya pembe za ndovu simu mara kadhaa.

“Huku Serikali yaUchina ikikuza uchongaji wa vinyagovya pembe za ndovukama sehemu yaurithi wa utamaduniwa nchi, utamadunihuu unatishiakuangamiza urithi wa asili wa Afrika”

HAPO JUU:Kiwanda cha kuchongapembe za ndovu chaZhengang, mkoani Fujian,Agosti, 2013.

32

Mwaka 2013, msururu wa visa vya ufanisi wa operesheni zautekelezaji zilibainika maafisa wa forodha kutoka Xamienwalipofanikiwa kunasa takriban tani 12 za pembe haramu zandovu zilizokuwa zikisafirishwa kutoka Afrika na kutiwa mbaroni kwa wafanyabiashara wenye leseni.106

Mwaka 2011, maafisa wa forodha katika bandari ya Shishi, katika Mkoa wa Fujian, walikagua kasha lililotiliwa shakalililowasili bandarini na halikuchukuliwa kwa muda wa siku.Ndani ya kasha hilo kulikuwa na magunia 10 ya pembe zandovu; jina la hati ya kusafirisha alikuwa mtu kutoka Shishikwa jina He. Maafisa wa forodha walianza kumfuatilia He, yeyena washirika wake.

Ilionekana Hehe alikuwa akiwasiliana na Chen Buzhong, mmilikiwa wa kampuni kubwa ya pembe za ndovu ya Fujian PuxiangCrafts, na mwanachama wa Kamati ya Taifa ya KuchongaPembe za Ndovu ya Uchina. Ili apate faida kubwa, Chen alitumia wadhifa wake katika biashara ya pembe halali zandovu kama njama ya kuficha uagizaji wa pembe za ndovukutoka Afrika kinyume cha sheria. Uchunguzi ulionyeshakwamba Chen alikuwa akishirikiana na mwanamke mmoja aitwaye Chao Hsiu-Chin, ambaye walikutana Afrika Kusinimwishoni mwa 2010. Chao, mzaliwa wa Taiwan , maarufu kama"Sophia", ndiye alikuwa mshirika wa Chen kutoka Afrika, aliyeratibu usafirishaji wa mizigo hadi Asia. He ambaye nimshirika wa Chen alisaidia katika mchakato wa kuandaa hatiza kusafirisha mizigo iliyowasili nchini Uchina; nambari zakasha zilibadilishwa kupitia ujumbe wa husika chombowalikuwa kubadilishana kupitia ujumbe wa maandishi.

Baada ya washukiwa kuhojiwa maafisa wa forodha walipatavielelezo vilivyowasaidia shehena nyingine za pembe za ndovuzilizopakuliwa katika bandari ya Shishi. Kwa jumla, shehenasita za pembe za ndovu kutoka bandari mbalimbali barani

Afrika, zote zikiwa na njia tofauti ya kuficha ukweli wa shehena: kasha moja likiwa limetoka Tanzania ndani ya shaba(ikiwa imesajiliwa kuwa ilitoka Kinshasa); mawili kutoka Nigeriandani ya korosho; moja kutoka Kenya katika ngozi za ng'ombe(kupitia Hong Kong); moja kutoka Ivory Coast ndani ya mbaona moja kutoka Togo ndani ya mbao. Iligunduliwa kwambamakasha yote yalikuwa ya Chen, kwa jumla, Chen na washirikawake walikuwa wameagiza tani 7.7 za pembe za ndovukinyume cha sheria.107

Awali Kesi iliyofunguliwa baada ya makasha haya kupatikanailmpata Chen na hatia na akahukumiwa kifungo cha maisha,lakini baadaye hukumu hiyo ilipunguzwa hadi miaka 15 baadaya rufaa, He alihukumiwa kifungo cha miaka saba na Zhaomiaka 15.

Hata hivyo, Chen si mfanyabiashara wa pembe halali za ndovupeke yake ambaye amehusishwa na matumizi mabaya yamfumo wa biashara ya pembe halali za ndovu; Yao Quan’an,mmiliki wa kampuni ya Zhongshan Yixingxin Crafts Ltd, piaalishukiwa kusafirisha magendo ya zaidi ya tani moja yapembe za ndovu kutoka Afrika mwaka 2011.

Kama mhusika mkuu aliyepanga, Yao hakuonekana kwenyehati za kusafirisha mzigo kwa sababu biashara hiyo ilifanywana mtandao wa mawakala wa usafirishaji na forodha, na kampuni za siri. Shehena moja ya pembe za ndovu ilikuwaimefichwa ndani ya kibodi chakavu na ziliingia Jieyang, nchiniUchina, kupitia Malaysia na Hong Kong. Shehena nyingine iliwasili kutoka bandari ya Quanzhou kama karatasi ya kufungia kutoka Taiwan. Wu Jianlang, mhusika muhimu,alisafiri hadi Hong Kong na Taiwan kupanga utaratibu wakusafirisha mizigo akitumia mitandao yake. Yao na Wu walihukumiwa miaka 14 na 12 mtawalio gerezani na mwaka2013 leseni zao za pembe za ndovu zilifutiliwa mbali.

© C

CTV,

Leg

al R

epor

t, 10

/01/

2014

Chen Buzhong alihukumiwakifungo cha miaka 15 kwatuhuma za kusafirishamagendo ya tani 7.7 yapembe za ndovu wa Afrikahadi Uchina.

Sanamu iliyochongwa kutoka kwa pembe haramu za ndovu iliyoonyeshwa kwawapelelezu mjini Xianyou.

UHUSIANO WA PEMBE HALALI NA PEMBE HARAMU ZA NDOVU

Ijapokuwa mfumo wa ndani wa kudhibii pembe za ndovu una mapungufu mengi, vyombo vya utekelezajivya Uchina vinajaribu kuzuia kumiminika kwa pembe haramu za ndovu zinazoingia nchini humo.

EIA INAPENDEKEZA KWAMBA SERIKALI YA TANZANIAITEKELEZE HATUA ZIFUATAZO HARAKA KAMA KIPAUMBELE:

1. Ifanye uchambuzi wa DNA wa shehena za pembe zote za ndovu zenye uzani wa zaidi ya kilo 500 zilizonaswa ndani ya nchi. Hii ni pamoja na pembe zilizonaswa Mikocheni jijiniDar (kilo 1,899) na Zanzibar (kilo 2,915kg) mwishoni mwa mwaka 2013

2. Ihesabu na kuharibu akiba ya Serikali ya pembe zote za ndovu zilizonaswa ndani ya Tanzania. Kutekeleza ahadi zinazotolewa kwa umma na maafisa wakuu serikalini, ya hivi karibuni ikiwa ni Mei 2014, ya kufanya hesabu ya akiba yote ili zisitumiwe kwa ajili ya biashara haijatimizwa

3. Iunde jopo kazi la wataalamu ili kuchunguza wafanyabiashara wakuu wa pembe za ndovu na maafisa fisadi wanaowezesha biashara hiyo. Kuafikia lengo hili, mambo kadhaa ya mfumo wa mahakama yanafaa kutekelezwa, ikiwa ni pamoja na:

• kupanua ukusanyaji wa ushahidi katika upelelezi kubuni sheria ya kudhibiti fedha zinazotokana na uhalifu na kupambana na ufisadi dhidi ya wafanyabiashara ya pembe za ndovu

• kushiriki habari za ujasusi mapema na utekelejazi na nchi chanzo, nchi za kusafirishia na soko linalolengwa kama vile Uganda, Kenya, Msumbiji, Uchina (ikiwa ni pamoja na Hong Kong), Vietnam, Malaysia na Sri Lanka ilikuonyesha mafanikio katika kusambaratisha ujangili

• kutumia vyombo vya kimataifa kuwatangaza na kuwapata watuhumiwa, na kusisitiza kushatakiwa kwa washukiwa kama hao, ikiwa ni pamoja na wale waliotajwakatika ripoti hii

• kutumia wataalamu na mashirika muhimu, ikiwa ni pamoja na Polisi wa Tanzania, Mamlaka ya Mapato Tanzania ikiwa ni pamoja na idara ya Forodha na Mamlaka ya Bandari ya Tanzania, Idara ya Wanyamapori ya Tanzani, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Idara ya Usalama wa Taifa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, waendesha mashitaka, mahakama na vyombo vingine maalumu kutoka Tanzania bara na Zanzibar

4. Kubuni na kuwawezesha watu na shirika lingine la kukagua mizigo inayosafirishwa nje ya nchi katika bandari zote za Tanzania na Zanzibar

5. Kuharakisha mchakato wa kufanyia marekebisho sheria ya Zanzibar ili kuruhusu utekelezaji wa ndani wa CITES

EIA INAPENDEKEZA KWAMBA SERIKALI YA UCHINA ITEKELEZEMAMBO YAFUATAYO KAMA HATUA ZA DHARURA:

1. Kupitisha na kutekeleza marufuku ya ndani ya biashara ya pembe za ndovu, mara moja.

2. Kuchunguza na kuwafungulia mashtaka watu muhimu wanaofanya magendo kuptia magenge ya uhalifu wa kupangwa

3. Kuchunguza na kuwafungulia mashtaka wanaotumia bidhaa za pembe za ndovu kama rushwa mbadala

4. Kukuza na kudumisha hamasisho zenye athari kubwa za kupunguza mahitaji ya pembe za ndovu

5. Kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania, Kenya, Msumbiji na nchi nyingine muhimu barani Afrika, na kwa ushirikiano na serikali hizi za kitaifa, kubuni na kusambaza ujumbe wa kuhimiza dhidi ya ujangili, kununua na magendo ya bidhaa za wanyamapori kwa wananchi na raia wa Uchina, wanaozuru au wanaoishi katika hizi.

EIA INAPENDEKEZA KWAMBA NCHI ZA KUSAFIRISHIA NA SOKO:

1. Ziharakishe Machakato wa Kutoa Usaidizi kwa Tanzania katika maswali yote ya uchunguzi na maombi ya kisheria kuhusu biashara ya pembe za ndovu

EIA INAPENDEKEZA KWAMBA JAMII YA WAHISANI:

1. Ifanye hatua za kupiga vita ufisadi na kuimarisha usimamizi wa umma nguzo kuu katika fedha zote

HITIMISHO NA MAPENDEKEZOIjapokuwa kumekuwa na mafanikio mdogo katika kupambana na mambofulani ya biashara haramu ya pembe za ndovu nchini Tanzania, ahadi kadhaaza msingi zilizotolewa katika mikutano ya kimataifa, bado hazijatekelezwa.

33

1. George Wittemyer et al. Illegal killing for ivory drives global decline in African elephants, PNAS 2014

2. IUCN African Elephant Specialist Group (AfESG), African Elephant Database, 2013

3. CITES, New figures reveal poaching for the illegal ivory trade could wipe out a fifth of Africa’s elephants over nextdecade, 2/12.2013

4. National Geographic – A Voice for Elephants, Elephant declines vastly underestimated, 16/12/2013

5. Colorado State University, Study: More than 100,000 African elephants killed (18/08/2014); Douglas Hamilton et al study estimation of 100,000 elephants poached in last three years

6. University of Washington, Center for Conservation Biology,Tracking Poached Ivory

7. UNEP, CITES, IUCN, TRAFFIC, Elephants in the Dust – The African Elephant Crisis, 2013

8. Colorado State University, 2014 op cit9. Wildlife Conservation Society press release, New data

shows continued decline of African forest elephants, 12/2/2014

10. UNEP, CITES, IUCN, TRAFFIC, 2013 op cit11. CITES SC65 Doc. 42.1, Elephant Conservation, Illegal Killing

And Ivory Trade, 201412. United Nations Office on Drugs and Crime, Transnational

organised crime in East Africa – a threat assessment, 201313. CITES press release, Elephant poaching and ivory

smuggling figures released today, 13/06/201414. Ripoti ya Taasisi ya Tanzania ya Kuwalinda Tembo (TEPS)

Iliyowasilishwa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, Apr. 2013

15. CITES Cop15, Doc. 68 kiambatisho cha 6a, 201016. Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Sera

ya Usimamizi wa Ndovu Tanzania 2010-2015, Juni 201017. Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori, Sensa ya Angani ya

Wanyama Wakubwa katika Hifadhi ya Selous-Mikumi - Hali ya Idadi Ndovu wa Kiafrika, 2013

18. Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori, Sensa ya Angani ya Wanyama Wakubwa katika Hifadhi ya Ruaha-Rungwa - Hali ya Idadi ya Ndovu wa Kiafrika, 2013

19. Radio ya Taifa, Majangili Waangamiza Kundi la Ndovu wa Tanzania, 25/10/2012

20. UNEP, CITES, IUCN, TRAFFIC, 2013, op cit.21. Daily Nation, Tanzania leading source of illegal ivory in

East Africa – INTERPOL, 26/2/201422. TRAFFIC press release, More than 1,000 ivory tusks seized

in Tanzania, 26/08/201123. INTERPOL (Feb. 2014), Elephant Poaching and Ivory

Trafficking in East Africa: Assessment for an Effective LawEnforcement Response

24. ETurboNews, Tanzania march for Elephants and Rhinos to coincide Nyerere Day, 29/9/14

25. Tawiri, 2013, op cit26. CITES CoP15, 2010, op cit27. This Day, Selous: The Killing Fields, 26/10/200928. The Spectator, Will China kill all Africa’s elephants?,

24/03/1029. EIA, Open Season – The burgeoning illegal ivory trade in

Tanzania and Zambia, 201030. UNEP, CITES, IUCN, TRAFFIC, 2013, op cit31. TAWIRI, 2010 op cit32. Dr. Sam Wasser, Center for Conservation Biology,

University of Washington, pers comm, 201433. UNESCO, Poaching Put’s Tanzania’s Selous Game Reserve

on List of World Heritage in Danger, 18/6/201434. UNEP, CITES, IUCN, TRAFFIC, 2013 op cit35. Transparency International, Corruption Perceptions Index,

201336. Ibrahim Index of African Governance, 201437. Mail & Guardian, Corrupt officials ensure the battle against

poaching remains futile, 8/08/201338. Daily Mail, Haul of shame: This shocking photo shows for

the first time the biggest stockpile of illegal ivory on earth, 22/03/14

39. UNODC, Transnational organised crime in Eastern Africa – a threat assessment, September 2013

40. CITES, 2010, op cit41. Tanzania Daily News, Forest Guards Need Military Skills,

13/10/201442. Citizen, ujangili: Govt. mateke nje maafisa 21, 2014/09/01SSC43. Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania, Ripoti ya Utendaji Kuhusu Usimamizi wa Wanyamapori katika Mbuga za Wanyamapori na Maeneo Yanayodhibitiwa ya Wanyamapori, Desemba 2013

44. Ripoti ya Kila Mwaka ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kuhusu taarifa za fedha za Serikali Kuu ya mwaka ulioishia Juni 2013, Machi 2014

45. CNN, Tanzania’s bloody ivory, 13/2/201446. This Day, CCM leader’s family firm in illegal poaching

trade?, 9/06/200847. The Citizen, CCM bigwigs under fire over ivory deal gone

sour, 30/04/201348. Mawio, Wabunge CCM Watajwa Ujangili, 4/10/201349. CITES press release, 2014, op cit50. CITES, 2010, op cit51. Wildlife Division, Ivory Confiscated in Tanzania, 201452. EIA ivory seizure database, 201453. CITES, 2010, op cit54. The Guardian, Kinana refutes ivory trafficking claims made

by opposition MPs, 8/05/201355. CITES Standing Committee 61, Doc. 44.1, 201156. Case reference Eco 23/2014, Kisutu Magistrates Court

Records, 201457. INTERPOL, Red List, /www.interpol.int/notice/search/

wanted, accessed 20/10/201458. Nyasa Times, Malawi Revenue Authority seizes 781 ivory

pieces, 1/06/201359. EIA, Back in Business, 200260. Sam Wasser, 2014, op cit61. China Military Online, 15th Chinese naval task force visits

Tanzania, 31/12/201362. Daily News, Two held over attempt to smuggle 81 tusks,

4/01/201463. Daily News, Self-confessed poacher files against sentence,

2/04/201464. Daily News, Chinese “poacher” fails to pay fine, jailed 20

years, 19/03/201465. Independent Television News, ITV News goes undercover

to expose Tanzania’s illegal ivory trade, 10/02/201466. The Spectator, Will China kill all of Africa’s elephants

24/03/201067. DLA Piper, Empty threat: does the law combat illegal

wildlife trade? 201468. EIA, Ivory Seizure Database, 201469. Lusaka Agreement Task Force press release, Suspect of

illegal export of ivory tusks arrested in Zanzibar, 18/12/2009

70. Lusaka Agreement Task Force, Another kingpin of illegal

elephant ivory trafficking arrested in Tanzania, 6/01/201171. IPP Media, Wachuuzi bandarini wadai kuguundua meno ya

Tembo, 25/08/201172. Hong Kong Customs and Excise, Customs seize

unmanifested ivory tusks, 10/09/201073. Case number Eco 8/2010, Kisutu Magistrates Court,

2/10/201374. Mail & Guardian, Mozambique elephants obliterated,

3/10/201475. Mozambique News Agency, Elephant census under way,

23/09/201476. Mozambique News Agency, Elephant poaching “a national

disaster”, 22/09/1477. Mozambique News Agency, 22/09/2014, op cit78. Associated Press, Mozambique logs a rate victory against

poachers, 14/09/201479. Pers comm, Head of Enforcement, Quirimbas NP,

November 201180. Sam Wasser, 2014, op cit81. News 24, Chinese flee Mozambique over ivory smuggling,

7/06/201182. EIA, Appetite for Destruction, 201283. TRAFFIC International, ETIS Report of TRAFFIC, CoP16 Doc.

53.2.2 (Rev. 1), 201384. EIA, Ivory seizures database, 201485. World Shipping Council, Top 50 world container ports, 201486. EIA, Routes of Extinction, 201487. ABC News, Largest ever ivory seizure in Hong Kong,

21/10/201288. Financial Times, Vietnam-China smuggling surges,

29/05/201289. Wildlife Conservation Society, In Plain Sight, March 201290. Tuổi Trẻ News, Vietnam seizes 2 tons of smuggled

elephant tusks (10/10/201391. Guangdong Province Higher Peoples’ Court, 201192. Xinhua, 18/04/201193. UNEP et al, 2013, op cit94. CITES Secretariat, Illegal Trade in Ivory and other Elephant

Specimens, CoP12 Doc. 34.1, 200295. EIA, Lethal Experiment, 200096. EIA, Back in Business, 200297. CITES Secretariat, Control of Trade in African Elephant

Ivory, SC53 Doc. 20.1, 200598. EIA, China, Ivory Trade and the Future of Africa’s

Elephants, 200899. Bryan Christy, Blood Ivory, National Geographic, October

2012100. EIA, Blood Ivory, 2012101. Yufang Gao and Susan G. Clark, Elephant ivory trade in

China: Trends and drivers, Biological Conservation, 2014102. State Forestry Administration, 2004 Notification No. 1,

13/04/2004103. Southern Weekly, China’s black market drives global illegal

ivory trade, 2011104. EIA, 2012, op cit105. People’s Daily, Illegal ivory spreads across the country

with Hongmu, 6/02/2012106. South China Morning Post, Xiamen customs smash

HK$767m ivory smuggling ring, 6/11/2013107. CCTV, Legal Report, 10/01/2014

MAREJELEO

34

ENVIRONMENTAL INVESTIGATION AGENCY (EIA)

EIA - LONDON

62/63 Upper StreetLondon N1 0NY, UK

Tel: +44 (0) 20 7354 7960 Fax: +44 (0) 20 7354 7961

email: [email protected]

www.eia-international.org

EIA - WASHINGTON, DC

PO Box 53343Washington, DC 20009 USA

Tel: +1 202 483-6621Fax: +1 202 986-8626

email: [email protected]

www.eia-global.org