65
KIDATO CHA NNE 2019 Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 1 MADA YA 1 KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI Uundaji wa Maneno Lugha hukua na kubadilika kila wakati kulingana na maendeleo ya jamii. Kigezo kimojawapo cha kukua na kubadilika kwa lugha ni kuongezeka kwa msamiati. Ili msamiati uongezeke katika lugha sharti maneno mapya yaundwe. Njia za Uundaji Maneno Uundaji wa Msamiati hutokea kwa njia mbalimbali zifuatazo: 1. Kubadili mpangilio wa herufi. 2. Kuambatanisha maneno. 3. Kutohoa maneno ya lugha nyingine. 4. Uambishaji wa maneno. 5. Kufanikisha sauti, umbo, mlio na sura. Kuunda msamiati kwa kubadili mpangilio wa herufi Neno hujengwa kwa vitamkwa au herufi. Neno jipya lenye maana tofauti huweza kuundwa kwa kubadili mpangilio wa neno lingine Mfano Neno lima, lina herufi l, i, m, a, herufi hizi huweza kujenga maneno kama mali, kumi,imla, mila. Neno tua lina herufi t, u, a, herufi hizi zina weza kujenga maneno kama:- tatu, tua, viatu, tatua. Njia ya kuambatanisha maneno Kuna njia tatu za kuambatanisha meneno Njia ya kurudufisha au kukariri neno

KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

  • Upload
    others

  • View
    575

  • Download
    15

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 1

MADA YA 1

KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI

Uundaji wa Maneno

Lugha hukua na kubadilika kila wakati kulingana na maendeleo ya jamii. Kigezo

kimojawapo cha kukua na kubadilika kwa lugha ni kuongezeka kwa msamiati. Ili

msamiati uongezeke katika lugha sharti maneno mapya yaundwe.

Njia za Uundaji Maneno

Uundaji wa Msamiati hutokea kwa njia mbalimbali zifuatazo:

1. Kubadili mpangilio wa herufi.

2. Kuambatanisha maneno.

3. Kutohoa maneno ya lugha nyingine.

4. Uambishaji wa maneno.

5. Kufanikisha sauti, umbo, mlio na sura.

Kuunda msamiati kwa kubadili mpangilio wa herufi

Neno hujengwa kwa vitamkwa au herufi. Neno jipya lenye maana tofauti huweza

kuundwa kwa kubadili mpangilio wa neno lingine

Mfano

Neno lima, lina herufi l, i, m, a, herufi hizi huweza kujenga maneno kama

mali, kumi,imla, mila.

Neno tua lina herufi t, u, a, herufi hizi zina weza kujenga maneno kama:-

tatu, tua, viatu, tatua.

Njia ya kuambatanisha maneno

Kuna njia tatu za kuambatanisha meneno

Njia ya kurudufisha au kukariri neno

Page 2: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 2

Mfano; barabara, sawasawa, polepole, katikati, vilevile.

Njia ya uundaji wa Msamiati kwa kuunganisha maneno mawili tofauti

Nomino na Nomino

Punda + mlia unapata Pundamilia

Bibi + Shamba unapata Bibishamba

Afisa + Elimu unapata Afisaelimu

Mwana + Siasa unapata Mwanasiasa

Bata + maji unapata Batamaji

Kuunganisha kitenzi na Nomino/Jina

Changa + moto changamoto

Chemsha + bongo chemshabongo

Piga + mbizi pigambizi

Zima + moto zimamoto

Kuunganisha maneno mawili na kudondosha baadhi ya herufi

Mfano

Baraza la Kiswahili Tanzania BAKITA

Mzaliwa wa mahali Fulani MZAWA

Chama cha Mapinduzi CCM

Nyamamfu NYAMAFU

Page 3: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 3

Kutohoa maneno kutoka lugha nyingine

Kila lugha na tabia ya kuchukua maneno lugha nyingine ili kukidhi mahitaji ya

Msamiati. Maneno kutoka lugha nyingine yanapoteuliwa hubadilishwa

kimatamshiili ya fuate kanuniza Kiswahili.

Maneno yanayotoholewa kutoka lugha nyingine husanifishwa na asasi za lugha ya

Kiswahili ndipo ya ruhusiwe kutumiwa rasmi.

Mfano

Neno la Kiswahili Lugha ya Mwanzo Neno Lililotoholewa

Kijerumani Schule

Salama Kiarabu Salaam

Duka Kihindi Dukan

Karoti Kiingereza Carrot

Shati Kiingereza Shirt

Picha Kiingereza Picture

Papai Kihispania Papaya

Meza Kireno Mezi

Shukrani Kiarabu Shukran

Page 4: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 4

Ngeli Kihaya Engeli

Ikulu Kinyamwezi Ikulu

Ng'atuka Kizanaki Ng'atuka

Ndafu Kichaga Ndafu

Namba

Kuunda maneno kwa njia ya uambishaji wa maneno

Hii ni njia ya kubandika viambishi awali na tamati kwe nyekiini. Ujenzi wa

maneno hutokana na mzizi mmoja kuonesha maana tofauti ingawa maana zina

husiana.

Mfano mzizi: -lim-.Tukipachika viambishi awali na tamati tunapata maneno kama

lima, analima, walilima, kilimo, limiana,halitalimwa na ukulima.

Kufananisha sauti, sura au tabia

Mfano

Kengele - utokana na sauti ya kengele inapo pigwa

Pikipiki - hutokana na muungurumo wa pikipiki

Ndizi mkono wa tembo – Ndizi inayo fananishwa na mkono wa mnyama

tembo

Chubwi - Jiwe au chura atumbukiapo katika kina cha maji.

ZOEZI

Maana ya pili ya neno komba ni mtu mlevi sana iliyopatikana kwa kuhamisha

maana ya neno, maana yake halisi ni___.

Page 5: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 5

A Aina ya ndege

B Aina ya mdudu

C Aina ya mnyama

D Aina ya samaki

Bainisha njia ya uundaji wa maneno iliyotumika kuunda neno \"MKURABITA\":

A Njia ya urudifishaji

B Njia ya uhulutishaji

C Njia ya kuangalia kazi ya kitu

D Njia ya kufupisha maneno

___ ni mfano wa neno lililoundwa kutokana na kufananisha sauti.

A BAKITA

B Kengele

C Shule

D Analima

___siyo neno lililoundwa kwa kufananisha sauti, sura au tabia.

A Beberu

B Kengele

C Kifaru

Page 6: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 6

D Mfuniko

___ ni mfano wa neno lililotoholewa kutoka katika lugha ya Kinyamwezi.

A Ikulu

B Ng‟atuka

C Ndafu

D Ngeli

Mazingira yanayoelezea Kuhitaji Maneno Mapya

Mabadiliko mengi yanatokea kila siku katika nyanja mbalimbali za kimaisha-

mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa, kisayansi na kiteknolojia. Katika mazingira kama

haya, watu watahitaji kuwasiliana, lugha itahitaji kuunda maneno ili kuwasilisha

dhana mpya zilizoibuka. Kwa mfano, maneno kama vile nywila, kisakuzi, udukuzi,

puku, talakirishi n.k yameundwa ili kuwasilisha dhana za kiteknoljia kwa

Kiswahili.

ZOEZI

Faida za kuongeza msamiati ni pamoja na hizi zifuatazo isipokuwa___.

A kuwasiliana bila tatizo

B taaluma kujitosheleza kimsamiati

C kujitosheleza kimawasiliano

D kuongeza watumiaji

Msamiati mpya unaundwa kwa lengo la___.

A Kusanifisha lugha

Page 7: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 7

B Kuimarisha lugha

C Kuwasilisha dhana mpya

D Kuongeza msamiati katika lugha

Mabadiliko ya ___yamesababisha uhitaji wa neno 'nywila'.

A Utamaduni

B Uchumi

C Siasa

D Sayansi na teknolojia

Uundwaji wa maneno kama vile plasta, vidonge na asprini yametokana na

mabadiliko katika fani ya___.

A Sheria

B Tiba

C Sanaa

D Uandishi

Mabadiliko ya mfumo wa kisiasa na kiutawala yamesababisha kuundwa kwa

neno___.

A Sidii

B Kiotomotela

C Mafisadi

D Tarakilishi

Page 8: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 8

Undaji wa Maneno katika Miktadha mbalimbali

Mabadiliko ya kimaendeleo yanafanya lugha ihitaji maneno ya kuyafikisha na

kutumiwa na jamii. Ili kukidhi mahitaji hayo, maneno mapya yanazuka. Maneno

hayo yanaweza kuwa katika fani mbalimbali, kama vile sayansi na teknolojia,

siasa, utamaduni na uchumi kulingana na mkondo wa maendeleo. Mfano wa

msamiati ni kama vile fedha, ushuru, kumpyuta, ukoloni, hospitali, suruali n.k

ZOEZI

Neno pembejeo linapatikana katika muktadha wa___.

A Sayansi na teknolojia

B Kijamii

C Kisiasa

D Kiuchumi

___ ni neno linalopatikana katika muktadha wa kisiasa ambalo hutambulisha cheo

cha kiongozi wa juu kabisa Tanzania.

A Luteni

B Mfalme

C Rais

D Kanali

Maneno yafuatayo yameundwa kutokana na maendeleo katika muktadha ya

kiutamaduni, isipokuwa:

A Suruali

Page 9: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 9

B Uma

C Dansi

D Walalahoi

___ni mfano wa neno lililotoholewa kutoka katika lugha ya Kihindi.

A shule

B bajia

C beseni

D hisani

Ifuatayo ni mifano ya maneno yaliyoundwa katika muktadha wa sayansi na

teknolojia sipokuwa___.

A bunduki, nyukilia

B umeme, bunduki

C zahanati, asprini

D kikokotozi, redio

MADA YA 2

UKUAJI NA UENEAJI WA KISWAHILI ENZI YA WAINGEREZA NA

BAADA YA UHURU

Ukuaji na ueneaji wa Kiswahili katika enzi ya Waingereza

Mambo waliyochangia Waingereza katika Ukuaji wa Kiswahili nchini Tanzania

Waingereza walipochukua koloni la Tanganyika kutoka kwa Wajerumani walikuta

Kiswahili kimeimarika na kinatumika katika maeneo mengi ya nchi. Kwa kuwa

nao walihitaji kutawala hawakupuuzia matumizi ya Kiswahili katika utawala wao

Page 10: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 10

japo hawakutumia Kiswahili kwa lengo la kukikuza lakini walijikuta wanakieneza

na kukikuza bila ya wao kukusudia.

Waingereza walitumia Kiswahili kama nyenzo ya kusaidia shughuli zao za

kiutawala. Hata hivyo kuna mambo waliyofanya waingereza yaliyosaidia kukua na

kuenea kwa Kiswahili, mambo hayo ni kama yafuatayo:

Shuguli za kiuchumi

Shuguli za kiuchumi wakati wa Waingereza zilihusisha kilimo na biashara. Kwa

upande wa klimo, Waingereza waliendesha kilimo cha mazao mbalimbali, na

walitumia mfumo wa kuajiri vibarua kutoka sehemu mbalimbali za nchi. Vibarua

hao walijulikana kwa jina la manamba.

Katika mkusanyiko wa vibarua hawa waliokuwa na usuli wa makabila

tofautitofauti, lugha pekee iliyoweza kuwaunganisha ni Kiswahili ikizingatiwa

kwamba Kiswahili kiliteuliwa kuwa lugha rasimi katika mawasiliano ya kiutawala.

Walilazimika kuzungumza Kiswahili kwani bila hivyo mawasiliano yasingeweza

kufanyika kwa urahisi.

Hata hivyo kupitia shuguli za kilimo maneno mapya ya Kiswahili yaliweza

kuzaliwa, kwa mfano: yadi, belo, belingi, bani, mtama n.k, kwa hiyo kupitia

shughuli hizi Kiswahili kilizidi kukua.

Shuguli za kiutamaduni

Shughuli hizi ni kama vile uigizaji wa tamthiliya za kigeni, uchezaji wa mziki wa

kigeni hususani twisti. Tamthiliya za kigeni zilikuwa zikiigizwa majukwaani kwa

lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili.

Shughuli za kidini

Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio wa wamishonari

waliokuwa na lengo la kueneza dini ya kikristo.

Katika harakati hizi walitumia lugha ya Kiswahili ili kufanikisha malengo yao

ikizingatiwa kwamba Kiswahili kilikuwa kimeshaenea vya kutosha wakati wa

utawala wa Mjerumani, kwa hiyo wamishonari wa Kiingereza waliendelea

kukiimarisha zaidi.

Page 11: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 11

Pia shughuli za kidini zilipelekea kutafsiriwa kwa vitabu mbalimbali vya kidini

kama vile Biblia na vitabu vingine. Tafsiri ya vitabu hivi ilikuwa ni kutoka katika

lugha ya kiingereza kwenda katika lugha ya Kiswahili. kwa kufanya hivi Kiswahili

kiliweza kuingiza msamiati mwingi sana na hivyo kukuza lugha ya Kiswahili.

Wamishonari walilazimika kujifunza Kiswahili hukohuko kwao ili wanapokuja

huku Afrika Mashariki wasipate tabu ya kujifunza Kiswahili. Kwa sababu hii

wamishonari waliokuwa wamekwishajifunza lugha ya Kiswahili walitunga kamusi

za Kiswahili – Kiingereza ili kuwasaidia wenzao pia kujifunza Kiswahili; kwa njia

hii waliweza kukikuza Kiswahili.

Shughuli za kisiasa

Shughuli za kisiasa hasa katika uanzishwaji wa vyombo mbalimbali vya kiutawala,

jeshi, polisi, mahakama, boma n.k. Kufuatia uanzishwaji wa vyombo hivi msamiati

mwingi wa Kiswahili uliweza kuzuka na hivyo kukuza Kiswahili.

Shughuli za kiutawala

Makampuni ya uchapishaji yalianzishwa (East African literature Bureau), na

kamati ya lugha iliundwa (Interterritorian language committee). Hatua hii

iliimarisha matumizi ya lugha ya Kiswahili hali iliyosaidia kukua kwa lugha ya

Kiswahili.

Shuguli za ujenzi wa reli na barabara

Shughuli hizi pia zilisaidia kuibuka kwa msamiati mpya kama vile, reli, stesheni,

tiketi n.k.

Usanifishaji wa Kiswahili

Usanifishaji wa lugha ya Kiswahili pia lilikua ni jambo jingine muhimu sana

lililosaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Lengo la usanifishaji wa Kiswahili

lilikuwa ni kuleta ulinganifu wa matumizi ya lugha ya Kiswahili katika ukanda wa

Afrika Mashariki.

Page 12: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 12

UENEAJI WA KISWAHILI

Ukuaji na Ueneaji ni maneno mawili yenye maana zinazokaribiana lakini

zinazotofautiana. Ukuaji humaanisha ongezeko la msamiati katika lugha na ueneaji

ni uongezekaji wa matumizi ya lugha kieneo. Kwa hiyo hapa tutaangalia yale

mambo yaliyosababisha Kiswahili kitumike katika eneo kubwa. Mambo hayo ni

haya yafuatayo:

Vyombo vya habari

Vyombo vya habari vilivyokuwepo kwa wakati huo ni redio, magazeti na majarida

mbalimbali. Kwa upande wa redio kulikuwepo na redio Tanganyika iliyoanza

kurusha matangazo yake kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Na magazeti

yaliyokuwa yakichapishwa wakati huo ni pamoja na: Mambo leo, Sauti ya Pwani,

Kiongozi na Habari za leo. Magazeti haya yote yalikuwa yakichapishwa kwa lugha

ya Kiswahili. Kwa hiyo kwa kutumia vyombo vya habari (redio na magazeti)

kiswahili kiliweza kuenea.

Kilimo

Kupitia kilimo watu waliweza kukutana pamoja, watu wa makabila tofautitofauti.

Kwa hiyo katika kipindi chote walichokaa kwenye makambi ya mashambani

waliweza kujifunza Kiswahili na walipomaliza muda wao walirudi nyumbani

wakiwa wamejifunza lugha mpya na hivo kwa njia hii waliweza kuieneza lugha ya

Kiswahili.

Muundo wa jeshi la kikoloni (KAR)

Jeshi la KAR liliundwa na watu kutoka makabila mablimbali, na lugha iliyokuwa

ikitumika jeshini ni Kiswahili, askari hawa walisaidia kueneza lugha ya Kiswahili

ndani na nje ya nchi kwani kila walipokwenda walikuwa wakizungumza Kiswahili.

Mfumo wa elimu

Chini ya utawala wa Waingereza Kiswahili kilitumika katika masomo yote kwa

ngazi ya shule ya msingi, na pia kilitumika kama somo kwa ngazi ya shule za

sekondari. Kwa hiyo hii pia ilichangia kuenea kwa lugha ya Kiswahili

Harakati za kudai uhuru

Page 13: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 13

Chama cha TANU kilianzisha harakati za kudai uhuru, harakati hizo ziliendeshwa

kwa lugha ya Kiswahili. Kwa hiyo kupitia harakati hizo Kiswahili kiliweza kuenea

kwa kiwango kikubwa.

Tathimini ya maendeleo ya Kiswahili wakati wa Waingereza

Licha ya maendeleo ya lugha ya Kiswahili katika utawala wa Waingereza, pia

kulikuwa na changamoto zilizoikabili lugha ya Kiswahili katika kupiga hatua ya

maendeleo. Changamoto hizo ni kama zifuatazo:

Kutofundishwa kwa Kiswahili shule zote nchini

Wakati wa utawala wa Waingereza Kiswahili kilifundishwa katika shule za watoto

wa kiafrika tu, wakati katika shule za watoto wa kizungu Kiswahili

hakikufundishwa. Kwa hiyo suala hili lilifanya Kiswahili kipewe msukumo mdogo

sana na hivyo kuhafifisha ukuaji wake.

Kutotumika kwa Kiswahili kama lugha ya kufundishia

Lugha ya Kiswahili ilitumika kufundishia katika shule za msingi pekee ilihali

lugha ya kiingereza ilitumika kuanzia shule za sekondari hadi elimu ya juu. Hali

hii ilisababisha watu kujitahidi sana kujifunza kiingereza; kwa kuzungumza

kiingereza ilikuwa na ishara kwamba wewe ni msomi, na hivyo kutokana na hali

hii Kiswahili kilendelea kukua polepole sana.

Kukosekana kwa vyombo vya kizalendo vya kukuza Kiswahili

Vyombo vilivyokuwa vinahusika na masuala ya ukuzaji wa Kiswahili wakati wa

ukoloni vilikuwa vimeanzishwa na wakoloni wenyewe, kwa mfano Kamati ya

Lugha ya Afrika Mashariki (Inter-Territorial Swahili Language commitee) na

Shirika la maandiko la Afrika Mashariki (East African Literature Bureau). Katika

hali kama hii ukuzaji wa Kiswahili ulikosa msukumo mkubwa wa kizalendo.

Kasumba ya kuthamini Kiingereza

Wananchi walikuwa na kasumba kwamba mtu anayezungumza Kiingereza

alichukuliwa kuwa ni mtu mwenye maendeleo na msomi, kwa hiyo hali hii

ikapelekea watu kutothamini Kiswahili na hivyo Kiswahili kudharaulika.

Page 14: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 14

ZOEZI

Maneno kama vile tiketi, titi, stesheni na treni yaliongezwa katika Kiswahili

kipindi cha Waingereza kupitia shughuli ya___.

A Biashara

B Uchumi

C Ujenzi wa reli

D Usanifishaji

Lengo la Waingereza kukuza lugha ya Kiswahili lilikuwa ni nini?

A Kueneza dini

B Kutumia Kiswahili katika Shughuli zote

C Kurahisisha shuguli za utawala

D Kuelimisha watoto wao

Shughuli za ___ zilichangia ukuaji wa Kiswahili kipindi cha Waingereza kwa

kuongeza maneno kama vile yadi, belo na belingi.

A Kidini

B Kisiasa

C Kiuchumi

D Kiutawala

Maneno yaliyoongezeka kutokana na shughuli za kidini wakati wa Waingereza ni

pamoja na___.

Page 15: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 15

A Belo

B Mkatukumeni

C twisti

D Rakaa

Kampuni ya uchapishaji wa vitabu (EALB) ilianzishwa mwaka gani?

A 1930

B 1947

C 1948

D 1849

Ukuaji na Ueneaji wa Kiswahili baada ya Uhuru

Shughuli mbalimbali zinazowezesha Kukua na Kuenea kwa Kiswahili nchini

Baada ya uhuru kuna harakati mbalimbali zilizochukuliwa na serikali ya Tanzania

katika kukiendeleza na kukikuza kiswahili. Harakati hizo ni pamoja na

kupendekezwa kuwa lugha rasmi 1962. Mkwaka 1964 kiswahili kilipendekezwa

kuwa lugha ya taifa na kuwa kitatumika katika shughuli zote za kiserikali na kitaifa

mfano katika elimu hususani elimu ya msingi.

Kuundwa kwa Chombo cha usanifishaji ambacho kilikuwa na kazi ya kuhimiza

maendeleo ya kiswahili, kutayarisha kamusi na vitabu mbalimbali vya sarufi na

fasihi ya lugha ya kiswahili na kuandaa wataalamu watakaoshughulikia

usanifishaji wa Kiswahili

Pia baada ya uhuru kulianzishwa Taasisi mbalimbali zitakazoshughulikia lugha ya

kiswahili. Mfano:- BAKITA, TUKI, TUMI, UKUTA, UWAVITA, Idara ya Chuo

Kikuu Cha Dar es Salaamu.

Page 16: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 16

Baada ya uhuru nchini Tanzania kiswahili kilienea kwa kasi kubwa sana. Kuna

sababu mbalimbali ambazo zilichangia kukua na kuenea kwa kiswahili hapa

nchini. Baadhi ya sababu hizo ni pamoja na kuteuliwa kwa kiswahili kuwa lugha

ya Taifa, Kiswahili kitumike katika Elimu, mfano kuwa lugha ya kufundishia

katika shule za msingi. Kuundwa kwa vyombo mbalimbali vya kukuza na kuneza

kiswahili, Kiswahili kuwa Lugha rasmi na lugha ya Taifa, shughuli mbalimbali za

kidini, shughuli za kisiasa na kiutawala na shughuli za kiutamaduni na uchapishaji

wa vitabu na majarida mbalimbali.

Kiswahili kuwa lugha ya taifa

Baada ya uhuru mwaka 1962 kamati iliundwa ili kuangalia uwezekano wa kutumia

kiswahili katika shughuli zote rasmi, mfano bungeni na shughuli zote za kiofisi.

Pia kiswahili kiliteuliwa kuwa lugha ya taifa 1964 ambapo katika shughuli zote za

kitaifa zitaendeshwa kwa kutumia lugha ya kiswahili. Hivyo kiswahili kilihimizwa

kutumika katika mawasiliano yote hasa katika shughuli za umma na Wizara zote,

Serikali na Bunge, kiswahili kiliendelea kupanda hadhi zaidi wakati wa Azimio la

Arusha la mwaka 1967 kwani azimio hilo lilitungwa na kuandikwa kwa lugha ya

kiswahili.

Kuundwa kwa vyombo vya ukuzaji na uenezaji wa Kiswahili

Tanzania baada ya uhuru ilifanya jitihada za kuunda vyombo mbalimbali vya

kukuza na kueneza Kiswahili katika nyanja mbalimbali mfano wa vyombo hivyo

ni UWAVITA BAKITA, TUKI, Taasisi ya Elimu,TAKILUKI na Chama cha

Kiswahili Chuo Kikuu Dar es Salaam.

Kutumika katika elimu

Kiswahili licha ya kutumika katika shughuli mbalimbali za kiserikali,

kilipendekezwa kutumika katika shule za Msingi na kufundishwa katika elimu ya

sekondari kama somo na katika vyuo vikuu wanatoa shahada mbalimbali za lugha

ya kiswahili. Pia katika Elimu ya watu wazima ambao hawakujua kusoma na

kuandika. Watu hawa walijifunza masomo mbalimbali kwa lugha ya kiswahili na

kuwafanya watu wengi kujua kusoma, kuandika na kuzungumza lugha ya kiswahili

fasaha. Kampeni hii ilikuwa kwa nchi nzima ambapo walijifunza elimu ya Afya,

Page 17: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 17

Siasa, Kiswahili, Kilimo na ufundi kwa lugha ya Kiswahili na kuwafanya watu

wengi kuzungumza kiswahili sanifu.

Vyombo vya habari

Tangu uhuru ulipopatikana kuna vyombo mbalimbali vya habari vilivyoanzishwa.

Vyombo hivi hutumika kueneza kiswahili kwa kiasi kikubwa na hufikiwa na watu

wengi licha ya kuwepo kwa changamoto za kiuchumi. Vyombo hivyo ni magazeti

na majarida mbalimbali ambayo huandikwa kwa lugha ya kiswahili lakini kuna

redio na runinga ambazo matangazo yake hutangazwa kwa lugha ya kiswahili.

Hivyo kukifanya kiswahili kuenea kote ndani na nje ya nchi.

Biashara

Shughuli za kibiashara nchini husaidia kuenea na kukua kwa kiswahili kutokana na

kuwepo kwa makabila tofauti tofauti ambapo wafanyabiashara huweza

kuunganishwa kwa lugha ya kiswahili. Hivyo kiswahili hudumishwa na kutumika

katika biashara hizo.

Shughuli za siasa na utawala

Tangu wakati wa harakati za kupigania uhuru kiswahili kimetumika kama nyenzo

muhimu kuwaunganisha wananchi. Shughuli za kisiasa zimetumia lugha hii katika

kujiimarisha; mfano wakati wa chama kimoja, Azimio la Arusha na Mfumo wa

vyama vingi Kiswahili kimetumika kama njia kuu ya mawasiliano. Pia katika

utawala chama kinachotawala kimekuwa na harakati za kukiendeleza kiswahilli

katika nyanja zote. Ambapo kiswahili kimekuwa kikitumika katika shughuli zote

za kiutawala. Hivyo shughuli za kisiasa na kiutawala zimechangia kwa kiasi

kikubwa katika kukuza, kukieneza na kukiendeleza kiswahili.

Uandishi na uchapishaji wa vitabu

Kuibuka kwa waandishi wa vitabu mbalimbali vya kiswahili vya sarufi na fasihi

ambavyo vilichambua kwa kina mambo mabalimbali yahusuyo lugha ya kiswahili

na utamaduni wake, mfano :- F Nkwera, Shabani Robart, Mathias Mnyapala na

Shaffi Adam Shaffi. Waandishi wengine chipukizi walijitokeza na wanaendelea

kujitokeza katika tasnia hii ya uandishi wa vitabu.

Page 18: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 18

Shughuli za kiutamaduni

Shughuli za kiutamaduni zimechangia kueneza kukuza na kuendeleza lugha ya

Kiswahili. Shughuli hizo ni pamoja na harusi, misiba, matanga na sherehe

mbalimbali za kijamii ambazo zimesaidia kukiendeleza Kiswahili kwa kuwa

huwakutanisha watu tofautitofauti katika shughuli hizo, ambapo huwalazimu

kutumia lugha ya kiswahili katika mawasiliano na kufanya kiswahili kuendelea.

Pia katika Sherehe mbalimbali vikundi vya sanaa na muziki vinavyotumia lugha ya

kiswahili kutumbuiza. Vikundi vingine huandaa nyimbo zao kwa ajili ya kukieneza

Kiswahili.

Vyombo vya Ukuzaji na Uenezaji wa Lugha ya Kiswahili

Tangu Tanzania ipate uhuru hadi sasa kuna vyombo kadha wa kadha

vilivyoanzishwa kwa ajili ya kukuza na kueneza Kiswahili baadhi ya vyombo

hivyo ni hivi vifuatavyo:

BAKITA

Hii ni taasisi ya serikali iliyoundwa kwa sheria ya Bunge Na.27 ya mwaka 1967

kwa madhumuni ya kukuza Kiswahili. Kutokana na sheria hii Baraza ndilo mratibu

wa kusimamia asasi zote na mawakala wote wanaokuza Kiswahili katika Jamhuri

ya Muungano wa Tanzania.

BAKITA imekuwa na mchango mkubwa sana katika ukuzaji na uenezaji wa lugha

ya Kiswahili kupitia majukumu yake. Majukumu ya Baraza kama

yalivyofafanuliwa katika sheria hiyo ni haya yfuatayo:

Kuratibu na kusimamia maendeleo na matumizi ya Kiswahili nchini

kote. Katika kufanya hivi Baraza lina jukumu la kuhakikisha Kiswahili

kinaendelea na kuhakikisha kuwa matumizi ya Kiswahili yanakuwa sahihi.

Kushirikiana na vyombo vingine nchini vinavyojihusisha na maendeleo

ya Kiswahili na kuratibu shughuli zao. Vyama vya Kiswahili kama vile

CHAKAMA, CHAWAKAMA vina mchango mkubwa wa kukuza na

kueneza lugha ya Kiswahili kwa kushirikiana na BAKITA. Ushirikiano wa

BAKITA na vyama hivi waweza kuwa ni wa kuto ushauri, au msaada wa

kifedha, kwa mfano BAKITA imekuwa ikiwasaidia CHAWAKAMA pale

Page 19: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 19

wanapokuwa wanataka kufanya makongamano nap engine wanahitaji

msaada wa kifedha, kwa hiyo BAKITA imekuwa ikiwasaidia kifedha.

Kuhimiza matumizi ya Kiswahili katika shughuli rasmi na za

kawaida. BAKITA imekuwa ikiandaa vipindi mbalimbli redioni ili

kuhimiza matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili.

Kushirikiana na mamlaka zinazohusika kuthibitisha tafsiri sanifu za

istilahi. Katiaka uundaji wa istilahi, BAKITA imekuwa ikichapisha vitabu

mbalimbali ikionesha istilahi sanifu zilizoingizwa katika lugha ya Kiswahili.

kwa hiyo kupitia jukumu hili Kiswahili kimekuwa kinakua.

Kutoa huduma za tafsiri na ukalimani kwa serikali, mashirika ya

serikali na yasiyo yaserikali na asasi nyingine. Kupitia tafsiri

zinazofanywa na BAKITA Kiswahili kimekuwa kikikuwa na kuenea.

Kuchapisha jarida au toleo linalohusu lugha na fasihi ya

Kiswahili. Machapisho haya ya BAKITA yanaendelea kukifanya Kiswahili

kukua kwa kuongeza msamiati mpya na hivyo watu wanaposoma

machapisho hayo wanajifunza msamiati mpya na hivyo kufanya Kiswahili

kukua.

Kushirikiana na mashirika ya kitaifa, asasi na watu binafsi, kufuatilia,

kushauri na kusimamia shughuli zinazolenga kukuza Kiswahili nchini

Tanzania.

Kutoa ushauri kwa waandishi na wachapishaji ili watumie Kiswahili

fasaha. Kwa kufanya hivi matumizi bora ya Kiswahili yanakuwa

yanaimarika.

Kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuthibitisha

vitabu vya Kiswahili vitakavyotumika shuleni na vyuoni kabla

havijachapishwa. Hili pia ni jamabo linaloimarisha matumizi ya Kiswahili

sanifu.

Page 20: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 20

TAKILUKI

Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni (TAKILUKI) ilianzishwa mwaka 1979

kwa lengo la kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Zanzibar, ili

kutimiza lengo hilo TAKILUKI inajishughulisha na kazi zifuatazo:

Kuratibu na kuendesha mafunzo ya lugha ya Kiswahili visiwani Zanzibar,

kuendesha mafunzo ya lugha ya Kiswahili kwa wazawa na wageni, kuhariri

miswada mbalimbali ili kuthibitisha ufasaha wa Kiswahili na kufanya tafiti

za Kiswahili katika Nyanja zake zote, hususani katika uwanja wa sarufi na

fasihi.

Pia TAKILUKI wana kazi ya kuandaa istilahi za taaluma mbalimbali, kutoa

huduma za taaluma mbalimbali, kutoa huduma za tafsiri na ukalimani kwa

lugha mabalimbali kwa mashirika, idara, wizara, taasisi, kampuni na watu

binafsi, kufundisha lugha za kigeni na kuandika vitabu mbalimbali vya

Kiswahili.

Pia hujishughulisha na utoaji wa ushauri wa kitaaluma kwa watunzi wa

vitabu ili waweze kuandika kazi zenye ubora, na kushirikiana na wadau

wengine wa Kiswahili kama vile, mashirika, wizara, taasisi, vyuo na watu

binafsi katika kuendesha shuguli za ukuzaji wa Kiswahili, mathalani

kuandaa na kuendesha semina, warsha na kozi fupifupi za Kiswahili.

Vilevile hujishugulisha na usimamizi na ufuatiliaji wa matumizi sahihi ya

lugha ya Kiswahili katika vyombo vya habari na katika shughuli mbalimbali

za serikali na za kawaida.

TUKI/TATAKI

Majukumu ya TUKI ni pamoja na kuunda sera muafaka za kustawisha Kiswahili

na pia kufanya utafiti katika lugha ya Kiswahili.

Majukumu mengine ya TUKI ni kuhariri, kuchapisha vitabu na kutawanya vitabu

na majarida ya kitaaluma katika Kiswahili.

Page 21: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 21

Kwa sasa TATAKI inatoa shahada ya awali na uzamili katika lugha ya Kiswahili,

kwa njia hii inawaandaa wataalamu wa lugha ya Kiswahili ambao watatumika

sehemu mbalimbali za ulimwengu kufundisha lugha ya Kiswahili.

CHAUKIDU

CHAUKIDU ni kifupi cha Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani, makao

makuu ya chama hiki kwa sasa yapo chuo kikuu cha Wisconsin-Madison,

Marekani

Madhumuni makuu ya CHAUKIDU ni: Kuwajumuisha pamoja wakuzaji wa

Kiswahili duniani kote kwa lengo la kuchochea kasi ya malengo mahususi

yafuatayo:

Kukuza Kiswahili katika nyanja zote ambamo lugha hii inatumika au

inaweza kutumika na kuongeza ufanisi wa mawasiliano katika ufundishaji

na utafiti wa maarifa ya aina zote, uandishi/utangazaji wa habari, uandishi

wa vitabu, uchapishaji vitabu na majarida, utayarishaji wa safari za mafunzo

katika Afrika ya Mashariki na Kati, n.k.

Kusambaza habari na matokeo ya utafiti kwa kutumia machapisho

mbalimbali na teknolojia ya mtandao wa kompyuta juu ya vipengele

mbalimbali vya Kiswahili na masuala yanayohusiana na Kiswahili.

Kuwajumuisha wanachama kwa ajili ya kubadilishana mawazo na tajiriba

zao katika masuala mbalimbali yanayohusu Kiswahili (k.v. uboreshaji wa

ufundishaji, utangazaji, utafiti, uandishi, nk.) kwa njia ya KIKAO wa kila

mwaka, warsha au semina au kongamano maalumu, na hata kwa njia ya

mtandao.

Kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kujivunia, kuendeleza, na

kuheshimu Kiswahili.

Kushauri ama kushinikiza serikali za nchi ambamo Kiswahili

kinazungumzwa kutambua thamani iliyobebwa na maliasili hii ili kuunda

sera muafaka za kukiendeleza kadri ya uwezo wake kwa manufaa ya

maendeleo ya serikali na watu wake kijamii, kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni,

kielimu, n.k.

Page 22: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 22

CHAWAKAMA

CHAWAKAMA husimama badala ya Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili vyuo

vikuu Afrika Mashariki. Chama hiki kilianzishwa mwaka 2004 kwa lengo la

kukuza na kueneza Kiswahili katika eneo lote la Afrika Mashariki kupitia

wanafunzi wanaosoma Kiswahili vyuoni. Wanachama wa chama hiki ni wale

wanosoma Kiswahili na hata wale wenye mapenzi ya lugha ya Kiswahili pia

wanaweza kujiunga na chama hiki.

Chama hiki kina utaratibu wa kuandaa makongamano ambapo wanachama wake

kutoka nchi zote za Afrika Mashariki hupata fursa ya kukutana mara moja kila

mwaka. Pamoja na utaratibu wa chama kuandaa makongamano pia uanzishwaji

wake umeambatana na malengo kadhaa ambayo ndiyo dira inayoiongoza chama

kwa mujibu wa katiba, malengo hayo ni haya yafuatayo:

1. Kuwapa wanachama nafasi ya kujadili, kuimarisha, kuendeleza na kukuza

vipawa vyao vya lugha na fasihi ya Kiswahili.

2. Kuamsha ari ya mapinduzi ya utamaduni wa lugha ya kiswahili.

3. Kueneza lugha ya kiswahili ndani na nje ya nchi.

4. Kushirikiana na vyama vingine katika juhudi za kuendeleza na kuimarisha

lugha ya kiswahili ndani na nje ya nchi wanachama.

5. Kuwaunganisha wanafunzi wa kiswahili Afrika Mashariki na kati katika

kukikuza kiswahili.

6. Kushirikiana na asasi mbalimbali zinazojihusisha na ukuzaji na uenezaji wa

kiswahili ndani na nje ya nchi kama vile BAKITA, TATAKI, TAKILUKI,

UWAVITA, CHAKAMA, BAKIZA n.k.

7. Kuchapisha kijarida cha chama na machapisho mengine ili kusaidia kueneza

taaluma ya kiswahili.

8. Kuweka kumbukumbu ya wataalamu wa kiswahili kwa nia ya kuwatumia

katika kufanikisha malengo ya chama na wadau wa Kiswahili.

Page 23: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 23

9. Kuratibu makongamano na mijadala mbalimbali inayohusiana na taaluma ya

kiswahili.

Pamoja na malengo hayo, lengo kuu la chama hiki ni kueneza Kiswahili lakini sasa

wanakienezaje? Wanachama wa chama hiki ambao ni nchi wanachama wa jumuia

ya Afrika mashariki wanakawaida ya kuandaa makongamano kwa ngazi ya kitaifa

na ngazi ya kimataifa.

Kwa ngazi ya kitaifa kila nchi huandaa kongamano kila mwaka ambalo

linawakutanisha wanachama wote kutoka vyuo mbalimbali katika nchi husika.

Katika kongamano hilo mada mbalimbali zinazohusu lugha ya Kiswahili na

mustakabali wake hujadiliwa lakini pia maazimio mbalimbali huchukuliwa juu ya

maendeleo ya chama. Sasa katika mijadala kama hii inatoa nafasi ya Kiswahili

kukua kwani makala mbalimbali huandikwa ambazo pia husomwa na watu

mbalimbali. Makala hizi pia zimekuwa zikichapishwa katika majarida ya chuo

husika na pia zimekua zikichapishwa mtandaoni ambapo hutoa fursa kubwa kwa

watu wengi zaidi kuzifikia na kusoma, hivyo kwa njia hiyo Kiswahili kinakua

kimeenea.

ZOEZI

Kiswahili kilienea kwa kasi sana katika kipindi gani?

A Kipindi cha Waingereza

B Wakati wa kupigania uhuru

C Baada ya uhuru

D Kipindi cha Waarabu

Ni wakati gani ambapo Kiswahili kilitumika katika elimu?

A Kabla ya uhuru

B Wakati wa waingereza

Page 24: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 24

C Wakati wa waarabu

D Baada ya uhuru

Kuenea kwa kasi kwa lugha ya Kiswahili baada ya uhuru kulichangiwa na lugha

hii kuteuliwa kuwa___

A Lugha ya taifa

B Lugha ya kimataifa

C Lugha sanifu

D Lugha ya Afrika

Lipi kati haya siyo msamiati uliotokana na vita kati ya Tanzania na Uganda na

kusababisha ukuaji wa Kiswahili?

A Dikteta

B Ubia

C Nduli

D Walokole

Shaaban Robert na Mathias Mnyampala walichangia sana ukuaji wa Kiswahili

baada ya uhuru kwa njia ya___.

A Utunzi wa nyimbo

B Uandishi wa vitabu

C Siasa

Page 25: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 25

D Uandishi wa habari

Dhima ya kila Asasi inayokuza Kiswahili

Mafanikio na Changamoto Zinazovikabili Vyombo vya Ukuzaji wa Kiswahili

Mafanikio

Vyombo vya ukuzaji wa Kiswahili vimejitahidi sana kukuza lugha ya

Kiswahili, kwa hali ya Kiswahili ilivyo sasa ni matokeo ya juhudi za

vyombo hivyo. Mafanikio ya vyombo hivyo ni pamoja na haya yafuatayo:

Machapisho ya lugha ya Kiswahili ni mengi sana nchini na nje ya nchi,

kufanya mafunzo ya Kiswahili, kukua kwa matumizi ya Kiswahili na

kuongezeka kwa idadi ya watumiaji wa Kiswahili nchini.

Matumizi ya lugha ya Kiswahili katika sehemu rasmi hasa katika ofisi za

serikali na ofisi za watu binafsi inadhihirisha mafanikio ya jitihada za

vyombo hivi kuhimiza matumizi ya lugha ya Kiswahili.

Kufundshwa kwa lugha ya Kiswahili kama taaluma kwa ngazi ya shahada ya

awali, uzamili na uzamivu. Hizi ni jitihada za TATAKI katika kuhakikisha

kunapatikana wataalamu wa lugha ya Kiswahili, hivi sasa TATAKI

wanafundisha lugha ya Kiswahili kwa ngazi ya shahada ya awali, uzamili na

uzamivu.

Matumizi ya lugha ya Kiswahili katika vyombo mabalimbali vya kimataifa,

matumizi ya lugha ya Kiswahili katika vikao vya Umoja wa Afrika na pia

ufundishwaji wa lugha ya Kiswahili katika vyo mabalimbali Duniani ni

ishara tosha ya kuonesha mafanikio ya jitihada za vyombo vya ukuzaji na

uenezaji wa Kiswahili.

Changamoto

Vyombo hivi vinakabiliwa na upungufu wa wataalam. Wataalamu wengi

waliobobea katika taaluma za Kiswahili wanakimbilia nje ya nchi wakidhani

huko ndiko kuna maslahi mazuri zaidi.

Page 26: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 26

Upungufu wa fedha za kuendeshea shughuli za ukuzaji wa Kiswahili katika

vyombo hivi pia limekuwa ni tatizo sugu. Kwa hiyo shughuli za ukuzaji wa

Kiswahili zinakuwa zinakwenda taratibu.

Taasisi hizi pia zinashindwa kujitangaza vizuri kutokana na kwamba hazina

vyombo vya habari binafsi ambavyo vingeweza kutumika kutangaza

shughuli zao. Jambo hili limesababisha vyombo hivi kushindwa kutoa elimu

ya Kiswahili kwa kutumia vyombo vya habari kutokana na kwamba

gharama za kufanya hivyo ni kubwa.

Vyombo hivi baadhi havina ofisi za kudumu, na hivyo kuhamahama jambo

ambalo linaathiri utendaji kazi wa vyombo hivyo.

ZOEZI

Kukuza ari ya kupenda somo la Kiswahili lilikuwa ni dhumuni la kuanzishwa

kwa___.

A. BAKITA

B. UKUTA

C. TUKI

D. Chama cha Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

___ni chombo kikuu chenye dhima ya kusimamia shughuli za ukuzaji wa lugha

nchini.

A. UKUTA

B. BAKITA

C. TAKILUKI

D. TATAKI

Page 27: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 27

Baada ya uhuru kuna asasi ziliundwa kwa ajili ya kukuza na kueneza Kiswahili

ambazo ni___.

A. CHAUMA, TATAKI

B. CHAKIMA, TUKI

C. CHAKAM, BAKITA, TUKI

D. BAKITA, TUKI, TAKILUKI, CHAWAKAMA

Chama cha Kiswahili cha Afrika kiliundwa mwaka gani?

A. 1964

B. 1963

C. 1970

D. 1978

Ni taasisi gani ina dhumuni la kufanya tafiti za Kiswahili katika nyanja zake zote

za fasihi na sarufi?

A. Taasisi ya Elimu Tanzania

B. CHAKA

C. TATAKI

D. Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima

MADA YA 3 UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI

Uhakiki wa Ushairi, Tamthiliya na Riwaya

Dhana ya Uhakiki

Page 28: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 28

Uhakiki ni kitendo cha kutathmini, kueleza, kuainisha na kutoa maoni juu ya kazi

fulani ya fasihi kwa kuongozwa na kaida maalum. Kwa kiwango cha elimu ya

sekondari mhakiki anafanya kazi ya uhakiki ili kuonesha mambo yanayojitokeza

kama vile, dhamira, migogoro, ujumbe, falsafa, mtazamo, msimamo n.k

Dhima ya Mhakiki na Nafasi ya Mhakiki

Uhakiki ni kazi ambayo ina mchango mkubwa sana katika kazi za fasihi. Kwa

msingi huo uhakiki una dhima zifuatazo:

Husaidia wasomaji kuilewa kazi ya fasihi kwa urahisi;Watunzi wa kazi

za fasihi hutofautiana katika matumizi ya lugha na taswira, hivyo mhakiki

anapofanya kazi ya uhakiki anamsaidia msomaji kuelewa vipengele hivi kwa

kuvifafanua kwa lugha rahisi.

Husaidia ukuaji wa kazi za fasihi;Mhakiki anapoonesha ubora na udhaifu

wa kazi ya mtunzi fulani, watunzi wengine pia watafunguka kifikra na

kutunga kazi iliyobora zaidi.

Uhakiki hukuza uelewa wa mhakiki; Kwa kuhakiki kazi mbalimbali za

fasihi, mhakiki hujiongezea maarifa ya lugha pamoja na mambo

yanayotokea katika jamii.

Nafasi ya Mhakiki

Mhahiki ana nafasi kubwa katika kazi za fasihi, Mhakaki ndiye anafafanua kazi ya

fasihi ili hadhira iweze kumwelewa vizuri mtunzi wa kazi hiyo. Kwa hiyo hapa

mhakiki anasaidia kurahisisha mawasiliano kati ya hadhira na mtunzi.

Vilevile mtunzi huwaonyesha watunzi ubora na udhaifu wa kazi zao. Kwa kufanya

hivyo huwawezesha watunzi kufanya kazi bora zaidi.

Hatua za Kufuata wakati wa Kufanya Uhakiki

Vilevile mtunzi huwaonyesha watunzi ubora na udhaifu wa kazi zao. Kwa kufanya

hivyo huwawezesha watunzi kufanya kazi bora zaidi.

Kwanza ni kuisoma kazi ya fasihi; hapa mhakiki anatakiwa kuisoma kazi husika ya

fasihi kwa kina na kuielewa vizuri.

Page 29: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 29

Pili ni kuainisha na kuchambua mambo muhimu yanayojitokeza katika kazi hiyo

katika vipengele vya fani na maudhui.

Tatu ni kutoa tathimini au kuelezea ubora na udhaifu wa kazi inayohusika.

UHAKIKI WA MASHAIRI

Shairi ni utungo wa kisanaa wenye mpangilio maalum wa lugha ya mkato

unaowasilisha mawazo au ujumbe kuhusu mwanadamu au mazingira yake na

hufuata utaratibu fulani.

Mashairi yapo ya aina mbili:

1. Mashairi huru

2. Mashairi ya arudhi

Mashairi ya arudhi

Haya ni mashairi yanayofuata kanuni za kimapokeo au arudhi za utunzi wa

mashairi. Arudhi/kanuni hizi ni pamoja na:

1. Kugawika kwa shairi katika beti

2. Beti kuwa na idadi maalum ya mishororo.

3. Mishororo ya ubeti kugawika katika vipande

4. Mishororo kuwa na ulinganifu wa mizani

5. Shairi kuwa na urari wa vina

6. Shairi kuweza kuimbika / kuwa na mahadhi au mapigo.

7. Kuwepo kwa kipokeo katika shairi

8. Kuwa na mtiririko wa mantiki na mawazo au muwala

9. hairi kuwa na utoshelezo wa beti / kujisimamia kimaana.

Page 30: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 30

Mashairi huru

Pia hujulikana kama mashairi ya kimapinduzi. Haya ni mashairi yasiozingatia

lazima ya arudhi na hivyo huwa na muundo huru. Sifa zake kuu huweza kuwa:

1. Lugha ya muhtasari

2. Lugha yenye mahadhi

3. Lugha ya kisanii iliyo na mafumbo na taswira

4. Mara nyingine hugawika katika beti.

5. Mishororo kamilifu (inayojitosheleza) na ile isiyo kamilifu (mishata)

Sifa za Mashairi

Mashairi huwa na sifa maalum zinazoyatambulisha kama kazi ya kishairi, yawe ya

kimapokeo au kimapinduzi.

Sifa hizi ni kama vile:

1. Mashairi hutumia lugha ya mkato / muhtasari

2. Ni sanaa au kazi iliyobuniwa kwa ufundi

3. Huwa na mpangilio maalum kuanzia mistari hadi beti.

4. Hutumia lugha teule na msamiati teule uliosheheni tamathali, taswira na

jazanda.

5. Mashairi huwa na sifa ya kuweza kuimbika hivyo shairi ni wimbo na wimbo

ni shairi.

Dhima ya mashairi

1. Kupasha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya upole na mvuto

2. Kuelimisha na kuzindua jamii.

3. Kuendeleza na kukuza kipawa cha utunzi.

4. Kuhifadhi msamiati wa lugha ya Kiswahili na Sanaa ya fasihi.

Page 31: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 31

5. Kuburudisha hadhira na wasomaji.

6. Kuwasilisha hisia za ndani za mtu na mawazo

Hatua za uhakiki wa mashairi

1. Soma shairi polepole na kwa makini kupata maana ya jumla.

2. Soma shairi tena kwa utaratibu ukizingatia maneno na vipande mbalimbali

na kuchunguza maana ya kila mojawapo

3. Pitia maswali yote kwa makini ukitilia maanani aina ya majibu

yanayotarajiwa.

4. Soma shairi tena ukipigia mstari kwa penseli sehemu zinazoelekea kujibu

maswali.

5. Toa majibu kamilifu kulingana na swali kwa lugha ya mtiririko.

Vipengee vya Uchambuzi Wa Mashairi

1. Anwani/kichwa cha shairi – Huwa ni muhtasari wa shairi katika neno au

sentensi moja. Anwani ni kidokezo muhimu cha kinachozungumziwa katika

shairi. Anwani huweza kuwa ya moja kwa moja, fumbo, kinaya, kibwagizo

au sehemu ya kibwagizo. Ikiwa shairi halina anwani, basi lipewe anwani

inayoafikiana na maudhui au dhamira kwasentensi isiyozidi maneno 6.

2. Maudhui – Haya ni masuala makuu au mambo muhimu yanayohusu

mwanadamu au mazingira yake yanayozungumziwa katika shairi. Kwa

mfano: malezi, siasa, usalama, unyanyasaji, ufisadi n.k. Maudhui

hung‟amuliwa kwa wepesi kutokana na kisa kilichomo katika shairi.

3. Dhamira / shabaha - Ni lengo kuu la mshairi katika kusanifu utungo wake.

Dhamira ya mtunzi huwa ni ujumbe kwa kifupi anaoutambua msomaji

kutokana na mwelekeo wa usemaji wa mtunzi katika shairi. Mfano: Baada

ya kusoma shairi, unaweza kung‟amua mtunzi alitaka kusisitiza kauli

kuwa uongozi mbaya haufai, misitu ni uhai n.k. Dhamira hutokana na

mwelekeo wa mawazo ya mshairi au falsafa yake.

Page 32: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 32

4. Mbinu na tamathali za lugha - Ni mbinu za uandishi na tamathali za usemi

zilizotumiwa na mshairi katika shairi. Mfano:Mazda / ziada / zidi -

kurefusha maneno;enda kuwa enenda. Inksari / muhtasari - Ni kufupisha

maneno;aliyefika kuwa alofika. Utohozi – Mbinu ya kugeuza msamiati /

maneno ya lugha geni ili yaandikike na kutamkika kana kwamba ni ya

Kiswahili. Mfano: Time - taimu; One – Wani. Mbinu hii vilevile

huitwa ukopaji au uswahilishaji.

ZOEZI

Mfano wa kazi za fasihi andishi ni___.

A Ngonjera, nyimbo na methali

B Ushairi, riwaya na tamthiliya

C Riwaya, maigizo na tamthiliya

D Hadithi, ngano na tarihi

Moja wapo ya dhima ya mhakiki kwa wasomaji wa kazi za fasihi ni___.

A Kumsifia mwandishi

B Kuelimisha hadhira

C Kusaidia wasomaji kuilewa kazi ya fasihi

D Kumkosoa msomaji

Umuhimu wa mhakiki katika kazi ya fasihi ni pamoja na___.

A kuwakosoa waandishi

B Kuwaelimisha wasomaji

Page 33: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 33

C kushawishi wasomaji

D kufichua maovu ya waandishi

Ni kitendo gani kati ya hivi hakifanyiki katika uhakiki?

A Kubeza

B Kutathmini

C Kutoa maoni

D Kuainisha

Kipi kati ya hivi hakifanyiki katika uhakiki wa mbinu ambazo msanii ametumia

kuwasilisha kazi yake?

A Mtindo

B Msimamo

C Matumizi ya lugha

D Muundo

Taarifa Muhimu za Mwandishi wa kila Kitabu

Mwandishi wa fasihi ni mtu anaeweza kubuni kazi ya fasihi na kuiweka katika

maandishi. Unaposoma kazi za fasihi ni lazima ujue taarifa muhimu za mwandishi

wa kazi hiyo, ambazo ni jina, kwa sababu kila utakapokua unajibu swali ni lazima

utaje jina la mwandishi wa kitabu. Falsafa na utamaduni kujua msimamo wake, na

muundo kujua mpangilio wa matukio, mtindo kujua upekee wake na matumizi ya

lugha.

ZOEZI

Ni kipengele gani amacho huelezea mwelekeo wa ujumla wa mawazo ya

mwandishi kuhusiana na jambo fulani?

Page 34: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 34

A Falsafa

B Mtindo

C Mtazamo

D Msimamo

Mwandishi wa fasihi ni nani?

A Mtu naeweka habari katika maandishi

B Mbunifu wa kazi za fasihi na kuweka kimaandishi

C Mtu anaenakili maandishi

D Mwanafasihi

Kipengele kinachotoa taarifa ambayo hubeba mawazo ya mwandishi ni ___.

A Dhamira

B Mtindo

C Falsafa

D Mtazamo

NI muhimu kujua falsafa ya mwandishi___

A Kujua siasa yake

B Ili kujua msimamo wake

C Kubaini kufaulu na kufeli kwake

D Ili kujua matatizo yake

Zifuatazo si taarifa muhimu kufahamu kuhusu mwandishi

Page 35: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 35

A Desturi

B Msimamo

C tamaduni na mila

D Umri na lugha

MADA YA 4 KUTUNGA KAZI ZA FASIHI ANDISHI

Utungaji wa Mashairi

Mambo ya Kuzingatia katika Utungaji wa Mashairi

Utungaji/uandishi wa kubuni ni ule unatokana na hisia ambazo zinamsukuma

mtunzi ili atunge kazi yake. Hisia zinaungana na wazo ambapo vitu hivyo

vinamsumbua akilini na kumkosesha raha. Mwandishi wa kubuni anataka

aliwasilishe wazo lake ili hadhira ifahamu kilichopo moyoni mwake. Mwandishi

hukosa usingizi na hivyo hulazimika kuamka na kuandika kile kinachomsukuma

akilini mwake.

Uandishi wa kubuni unamtaka mtunzi atumie milango yake ya fahamu

kinagaubaga. Kuna milango ya fahamu mitano ambayo ni pamoja na: kuona,

kunusa, kusikia, kuhisi, na kuonja.

Kuona: je, mhusika unayemfikiria kichwani mwako unamwonaje? Umbo

lake ni la kuvutia au kuchusha? Je, macho yake yakoje – je ni ya golori au

la? Ni makubwa au madogo? Je, ni mlemavu wa macho?

Kunusa: pua zako zinakufanya usikie harufu gani? Je, ni harufu mbaya au

nzuri? Je, ni uvundo au marashi? Je, mhusika wako ananuka kikwapa au

uturi? Je, ananuka mdomo?

Kuhisi: je, unapokaa karibu naye unajihisi nini? Je, unapata mhemko

wowote au huhisi chochote? Je, akikupapasa mwilini mwako unajisikia nini?

Akikugusa bega unajisikia nini?

Page 36: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 36

Kuonja: je, ukiweka kitu hicho mdomoni unaonjaje – ni chungu au tamu?

Je, ina pilipili au masala? Je, kuna chumvi au sukari? Je, kitu hicho kina

ukakasi au uchachu?

Kusikia: je, sauti unayoisikia ikoje? Inamtoa nyoka pangoni? Inakufanya

ukose usingizi? Je, ni sauti nzuri au mbaya? Ni nyororo au nzito? Kama ni

sauti ya muziki – je, iko chini au juu (kelele)?

Uzoefu wa Mwandishi

Uzoefu ni hali ya kukaa au kujishughulisha na jambo au kitu kwa muda mrefu.

Mwandishi ana uzoefu (uzoevu) wa kukabiliana na maisha kwa kiasi gani? Je, ni

matatizo gani ambayo umekutana nayo katika maisha yako? Je, ni mafanikio gani

umekutana nayo katika maisha yako? Kwa mfano, katika ajali ya MV Spice (2011)

kuna baadhi ya watu waliokolewa na magodoro ya Tanzania? Magodoro haya yana

nailoni na je kama yasingekuwa na nailoni? Uzoevu/uzoefu wako ukoje?

Uchunguzi/utafiti

Uchunguzi unapaswa ufanywe na mwandishi ili aweze kuandika jambo au tukio

bila kuongopa. Kwa kufanya udanganyifu, mwandishi atapoteza imani yake kwa

wasomaji wa kazi zake.

Uchunguzi ili ufahamu au ujue mtu, mnyama, mdudu na kadhalika – anatembeaje,

anakulaje, analalaje, anaishije, anachekaje, analiaje, anazaaje, anahusianaje na

wenzane na mazingira yake? Haya ni maswali muhimu katika kumwezesha mtunzi

kufanya utafiti wa kina ili ajue kitu anachotaka kukiandika akiandikaje na

akiwasilishaje ili aweze kuikamata hadhira yake.

Mwandshi baada ya kuzingatia mambo haya sasa anaweza kuanza kutunga kazi

yake. Hapa sisi tutajikita zaidi katika utunzi wa mashairi. Kabala hatujaenda katika

hatua ya utunzi ni muhimu kujua dhana ya shairi kwa ujumla wake, na baada ya

hapo tutakuwa tumekwisha pata maarifa yakutosha juu ya mashairi ambayo

yatatuwezesha kutunga mashairi.

Dhana ya shairi

Page 37: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 37

Shairi ni kipande cha maandishi kilichopangwa kwa utaratibu katika mistari. Sauti

za silabi hufanana zikiwa kati au mwisho mwa mstari. Maandishi hayo yakisomwa

huleta ujumbe na hisia fulani ya kimaisha.

Mpango wa maneno ya shairi, ambao huweza kuimbwa hutoa picha wazi, maana

halisi na burudani ya kimuziki. Nyimbo nyingi za makabila zimepangiliwa kishairi

ijapokuwa hazikuandikwa

Mashairi yana umbo ambalo huonekana kwa mpangilio wa sauti na idadi ya

maneno katika mistari. Umbo hili hutofautisha shairi na tenzi. Kuna mambo

kadhaa yanayotakiwa kufahamika kuhusu shairi, nayo ni:

1. Beti – Kifungu kimoja cha shairi ambacho kina uzani sawa.

2. Vina – Ni mwisho wa mistari ambayo huwa na silabi zenye sauti

ileile mwishoni mwa sentensi.

3. Mizani – Ni idadi zilizo sawa za silabi katika kila mstari, ubeti hadi ubeti.

4. Kituo – Huu ni mstari wa mwisho wa ubeti. Kuna vituo vya aina tatu:Kituo

cha bahari – ni mstari unaotoka mwanzo hadi mwisho bila kubadilika katika

kila ubeti;Kituo cha kimalizio – ni kituo ambacho mstari wa mwisho maneno

yake hubadilika ubeti hadi ubeti;Kituo nusu bahari – ni mstari wa mwisho

ambao maneno yake nusu hubadilika na nusu hubaki kama ulivyo ubeti hadi

ubeti.

Katika mashairi (ya kimapokeo), kila mstari lazima uwe umekamilika na ubeti uwe

na maana kamili.

Vipengele vya fani katika mashairi

Vipengele vya fani katika shairi ni pamoja na:

Jina / anwani

Mandhari

Wahusika

Muundo –tathnia, tathlitha, tarbia, tathamisa, sabilia n.k

Page 38: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 38

Mtindo – pindu, msisitizo, beti kubadilishana vina, kurudiwa kipande kizima

cha mstari wa mwisho kikiwa ni chanzo cha ubeti unaofuatia.

Vipengele vya Maudhui kati mashairi

Vipengele vya maudhui ni pamoja na: migogoro, ujumbe, falsafa, msimamo,

mtazamo, na dhamira za mwandishi.

Matumizi ya ushairi ni pamoja na: kuomboleza, kubembeleza, kuliwaza,

kufundisha, kuburudisha, kukosoa, na kadharika.

Baada ya hapa sasa unaweza kuanza kutunga shairi lako la kwanza.

ZOEZI

Mtiririko wa maelezo ya shairi ambayo hutolewa kwa kuzingatia utangulizi, kiini

na mwisho huitwa___.

A Muwala

B Kituo

C Beti

D Urari wa mistari

Ni jambo gani la kuzingatia katika utunzi wa shairi ili kuweza kuchochea hisia za

wasomaji?

A Muwala

B Urari wa vina

C Lugha ya kishairi

D Taswira

Page 39: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 39

___hutokana na jambo linalojadiliwa katika shairi na huzingatiwa katika utunzi.

A Anwani ya shairi

B Beti

C Muundo

D Mizani

Utungaji unatokana na___.

A Mawazo ya mhakiki

B Mazingira yanayomzunguka mwandishi

C Mawazo ya mwandishi

D Mawazo ya watu

Silabi zinazounda mistari ya beti za mashairi huitwa___.

A Beti

B Vina

C Kichwa cha shairi

D Mizani

MADA YA 5 UANDISHI

Uandishi wa Insha za Kiada

Insha ni kifungu cha maandishi kilichoandikwa kutokana na mtazamo wa

mwandishi katika kujadili juu ya mada fulani. Mwandishi anaweza kuandika

kuipinga mada hiyo au kuishadidia mada hiyo. Kuna aina mbili za insha, insha za

kaida (zisizo za kisanaa) na insha za kisanaa.

Page 40: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 40

Insha za kaida ni insha zinazotumia lugha ya kawaida kuelezea mambo

mbalimbali katika jamii, mfano juu ya mazingira, uchumi, biashara, historia n.k.

Muundo wa Insha za Kaida

Katika uandishi wa insha, muundo wake unakuwa na vitu vifuatavyo:

1. Kichwa cha insha; kichwa cha insha hudokeza kile ulichokijadili katika

insha yako. Kwa mfano: Madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya n.k

2. Utangulizi; Mambo yaliyopo katika utangulizi ni pamoja na kutoa fasili ya

maneno muhimu na kuelezea kwa muhtasari mambo ambayo utakwenda

kuyajadili katika insha yako.

3. Kiini cha insha; katika kiini ndipo kuna maelezo ya kina juu ya kile

unachokijadili katika insha yako, maelezo haya yanakuwa katika aya kadhaa

kulingana na idadi ya hoja ulizonazo katika mjadala wako.

4. Hitimisho; hapa ndipo kuna muhtasari wa kile kilichojadiliwa katika kiini

cha insha au inaweza kuwa ni msimamo juu ya kile kilichohadiliwa katika

insha.

Mambo ya kuzingatia katika uandishi wa insha

Taratibu za uandishi zinapozingatiwa insha pia itasomeka vizuri na pia itakuwa na

mtiririko mzuri wa mawazo.

Epuka kutumia vifupisho vya maneno visivyo rasmi.Uandishi wa insha ni

suala rasmi, kwa hiyo katika uandishi wake inatakiwa kuzingatia kuepuka

kutumia vifupisho ambavyo sio majumui yaani havijulikani. Kwa mfano

maandishi kama, xamahani (samahani), ckatai (sikatai) na mengine

yafananayo kama hayo ni lazima yaepukwe katika uandishi wa insha.

Andika utangulizi unaovuta umakini wa msomaji. Hiki ni kipangele cha

muhimu sana, msomaji anapoona kwamba kwenye utangulizi hakuna kitu

kinachomvutia hataendelea kuhangaika kusoma insha hiyo.

Page 41: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 41

Andika kiini cha insha kwa mpangilio mzuri Unatakiwa kuandika insha

yako katika mpangilio mzuri huku kila wazo kuu likipewa aya yake na

kuwepo na mtiririko mzuri wa mawazo.

Andika hitimisho la insha likiwa linahitimisha mawazo

yaliyokwishajadiliwa katika kiini.Hakikisha unapofanya hitimisho epuka

kudokeza wazo jipya ambalo linazua mjadala mpya, hakikisha hitimisho

lako linabeba mawazo uliyokwisha yajadili katika insha yako na wala

yasiwe mawazo yanayotoka nje ya kile ulichokijadili.

ZOEZI

Muundo wa insha ya kiada huwa na vipengele vingapi muhimu?

A Sita

B Vitano

C Vinne

D Vitatu

Ni sehemu gani katika muundo wa insha za kiada huonesha mapendekezo ya

mwandishi kuhusiana na jambo lililojadiliwa?

A Kichwa cha insha

B Hitimisho

C Kiini cha insha

D Utangulizi

Fasili ya maneno muhimu hutolewa katika kipengele gani ndani ya insha ya kiada?

A Kiini cha insha

Page 42: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 42

B Hitimisho

C Utangulizi

D Kichwa cha insha

___ni sehemu katika muundo wa insha ya kiada ambayo hubainisha kwa undani

jambo linalozungumziwa.

A Kiini cha insha

B Hitimisho

C Kichwa cha insha

D Utangulizi

___huzingatia wazo kuu la insha ya kiada na wakati mwingine kupigiwa mstari.

A Kiini cha insha

B Utangulizi

C Kichwa cha insha

D Hitimisho

Uandishi wa Insha za Kiada

Uandishi wa Hotuba

Hotuba ni insha ambayo hutoa maneno halisi ya mzungumzaji/kiongozi

anapozungumzia hadhira, kuhusu jambo fulani. Insha ya hotuba huandikwa katika

hali ya usemi halisi na mwandishi hatakiwi kuweka alama za kunukuu anapoanza

insha yake.

Hotuba inaweza kutolewa na kiongozi wa kisiasa, utawala, kidini, kikundi, shirika

fulani, daktari, n.k. Hadhira katika hotuba husheheni wageni waalikwa,

Page 43: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 43

wanachama, wafuasi, wananchi, n.k ambao wanahusishwa katika mada

inayorejelewa katika hotuba hiyo.

Muundo wa Hotuba

Hutuba inakuwa na muundo ufuatao:

Anwani

Anwani, mada au kichwa cha hotuba hurejelea mada ya hotuba. Pia mada inaweza

kutaja hadhira.

Hotuba ya Waziri wa Afya kuhusu madhara ya ukimwi kwa wananchi.

Hotuba ya Mwalimu Mkuu kwa Wazazi

Utangulizi

Anza hotuba yako kwa kuwatambua waliohudhuria KIKAO (hadhira).

Wataje kwa majina/vyeo vyao kuanzia yule wa cheo cha juu hadi wa chini,

mabibi na mabwana. Kumbuka kwamba hauhitajiki kuwasalimia.

Kuwatambua kwa majina pekee kunatosha.

Jitambulishe kwa hadhira yako hasa ikiwa unazungumzia hadhira isiyokujua

au wageni.

Tanguliza mada yako.

Kwa mfano:

Waziri wa Kilimo, Mkuu wa Wilaya, Mhe. Mbunge, wanachama wa kikundi hiki

cha Mazingira, mabibi na mabwana. Ni matumaini yangu kwamba nyote mu

buheri wa afya. Mimi ni mwakilishi wa Kikundi cha Mazingira na jioni ya leo

kuna jambo muhimu ambalo ningependa sote tulifahamu ili kuboresha mazingira

yetu kwa …

Kiini

Hakikisha kuna mtiririko wa hoja kuanzia mwanzo hadi mwisho

Page 44: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 44

Ujumbe wako wote unapaswa kuwa katika usemi halisia wala si wa taarifa.

Tamati

Hakikisha kwamba mwisho wa hotuba yako unatambulika.

Unaweza kumaliza kwa shukurani

ZOEZI

Kipi kati ya hivi siyo kipengele katika muundo wa hotuba?

A Muhtasari

B Kiini

C utangulizi

D Tamati

___ni sehemu katika muundo wa hotuba ambapo msisitizo na shukrani hutolewa.

A Hitimisho

B Kichwa cha hotuba

C Utangulizi

D Kiini

Shukrani katika hotuba hutolewa katika kipengele gani kati ya hivi?

A Anwani

B Utangulizi

C Hitimisho

Page 45: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 45

D Kiini

___ni kipengele cha muundo wa hotuba ambacho hurejelea mada ya hotuba.

A Tamati

B Anwani

C Kiini

D Utangulizi

Muundo wa hotuba una sehemu___.

A Nne

B Tano

C Tatu

D Sita

Uandishi wa Risala

Risala ni hotuba fupi inayosomwa mbele ya kiongozi kwa niaba ya kundi fulani la

watu hasa hasa wanafunzi, wafanyakazi, washiriki, wanachama, mafundi n.k ili

kutoa maelezo ya haja zao mbalimbali na mahitaji yao au kuonyesha msimamo wa

kundi hilo kwa kiongozi.

Muundo wa Risala

Utanguizi

Cheo cha kiongozi anayehusika

Kundi linalowakilishwa

Kiini

Page 46: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 46

Maelezo ya hali halisi ya maswala na msimamo wa kundi linalowakilishwa.

Mapendekezso na hatua zinazotakiwa kuchukuliwa.

Hitimisho

Shukrani

Tanbihi: Kama vilivyosemwa awali risala ni hotuba fupi lakini inachukua mambo

muhimu tu na kuyaeleza. Hivyo risala yenyewe huwa ni maelezo ya muhtasari kwa

jambo linalohitaji maelezo marefu Katika hotuba. Utungaji wa risala unahitaji

uangalifu sana na lugha ya heshima iliyo wazi kueleweka kwa kiongozi.

Mfano wa risala:

Ndugu Mgeni rasmi, Walimu, Wanafunzi wenzetu, Wazazi, Wageni waalikwa,

Mabibi na Mabwana.

Kwa niaba ya wanafunzi wa kidato cha nne, tunayo heshima na furaha kubwa ,

kukukaribisha ili ushiriki nasi katika siku hii muhimu na kusikia mafanikio

mbalimbali kwa kipindi chote cha masomo yetu hapa shuleni.

Shukrani zetu za pekee na za dhati ziende kwa uongozi mzima wa Shule na

walimu wetu wote kwa jinsi walivyojitoa kwa moyo wa kutufundisha, hivyo

tumefundishika vyema; kwasababu tupo tofauti sana na tulivyokuja hapa mwezi

januari 2009.

Ndugu mgeni rasmi, tulianza kidato cha kwanza tukiwa wanafunzi 120; wasichana

60 na wavulana 60. Mpaka leo tunapohitimu tupo wanafunzi 90; kati yao wavulana

ni 43, na wasichana 47. Wengine wameshindwa kuhitimu nasi siku ya leo

kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro, ujauzito na kuhama shule.

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema wa Baraka kwa ulinzi wake

kwetu hadi leo hii tunahitimu kidato cha nne.

Ndugu mgeni rasmi, elimu hii ya kidato cha nne imetupatia msingi mzuri wa

kujiunga na Elimu ya juu, pia imetujengea uwezo mzuri wa kujitambua na kufikiri,

kufanya kazi vizuri na kufanya maamuzi sahihi; pia imetuwezesha sisi wanafunzi

kupata elimu ya mambo mbalimbali kupitia masomo tunayo fundishwa hapa

shuleni, mfano; tumepata elimu ya uraia, historia ya mambo mbalimbali katika

Page 47: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 47

nchi yetu na dunia kwa ujumla, pia tumeweza kupata uelewa kuhusu afya na

magonjwa, usalama katika mazingira yetu, Kilimo, Maumbile ya nchi, hali ya

hewa, misitu, na viwanda. Vilevile tumeelewa umuhimu wa kusoma vitabu

mbalimbali kwa lengo la kupata ujuzi wa kuinua uchumi wetu wa taifa.

Ndugu mgeni rasmi, mafanikio hayo yamepatikana kwasababu ya ushirikiano

mzuri kati yetu na walimu wetu. Tangu tujiunge na shule hii tukiwa kidato cha

kwanza tumefanya majaribio na mitihani ya mara kwa mara jambo lililo tusaidia

kuinua taaluma yetu.Tunawashukuru sana walimu wetu, tuna waahidi kufanya

vizuri katika mitihani yetu ya Taifa ya kidato cha nne mwaka huu, na Mungu

awabariki sana.

Ndugu mgeni rasmi, tumepata changamoto mbalimbali wakati wa maisha yetu ya

kielimu hapa shuleni, kama ifuatavyo;

Ndugu mgeni rasmi, tuna changamoto ya upungufu wa vitabu vya kiada na ziada;

hii imepelekea kushindwa kujisomea vizuri, kwani kitabu kimoja kinatumiwa na

wanafunzi zaidi ya ishirini (20).

Ndugu mgeni rasmi, changamoto nyingine ni upungufu wa vifaa vya maabara, hii

inapelekea kuchangia kifaa kimoja, hivyo tuna tumia muda mwingi sana kujifunza

na kumuelewa mwalimu.

Ndugu mgeni rasmi, pia kuna changamoto ya upungufu wa walimu, hasa wa

masomo ya sayansi; hii imepelekea kutomaliza „syllabus‟ kwa wakati.

Ndugu mgeni rasmi, pia kuna changamoto ya upungufu wa samani za shule, kama

vile; madawati kwa ajili ya wanafunzi, viti na meza kwa ajili ya walimu; hii

imepelekea baadhi ya wanafunzi wenzetu kukaa wawili kwenye dawati moja.

Ndugu mgeni rasmi, maji ni changamoto hapa shuleni, kwani shule haina kisima

cha maji, hii imepelekea shule kununua maji kwa gharama kubwa, ambayo

hayatoshelezi mahitaji ya shule, kama vile usafi; hususani kwa upande wa vyoo,

bila kuwa na maji ya kutosha tutapata magonjwa ya mlipuko, kama vile

kipindupindu.

Ndugu mgeni rasmi, changamoto ya vifaa vya michezo; kama unavyojua kuwa

michezo ni afya, shule yetu ina upungufu mkubwa wa vifaa vya michezo kama

Page 48: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 48

vile; mipira ya miguu, pete na mikono, pia hatuna milingoti ya chuma kwaajili ya

magoli ya viwanja vya michezo yote tunayocheza hapa shuleni.

Ndugu mgeni rasmi, tunashukuru uongozi wa shule hii, walimu na wazazi ambao

wamekuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo ya shule yetu; kwa

upande wa masomo ya sayansi; shule imeweza kutenga chumba kimoja cha darasa

kitumike kama maabara japo kuwa kuna upungufu mkubwa wa vifaa.

Ndugu mgeni rasmi, tunayo matumaini kwamba maombi yetu umeyasikiliza na

utayaatekeleza, maana tunajua kwamba wewe unaweza kupitia Hlimashauri unayo

isimamia, asante sana.

Mwisho tunaomba msamaha wa dhati toka moyoni mwetu kwa Walimu,

Wanafunzi wenzetu na Wazazi pale tulipoenda kinyume na matazamio yenu,

kwani watu wakiishi pamoja tofauti lazima ziwepo, tunatumaini mtapokea

msamaha wetu, nasi hatuna jambo lolote baya kwenu.

Ndugu mgeni rasmi, tuna kushukuru sana kwa kufika katika Mahafali yetu, kwani

tunatambua kuwa unamajukumu mengi ambayo umeyaacha na kuwepo hapa

kwaajili yetu.

ZOEZI

Muundo wa risala una sehemu kuu nne. Ni ipi kati ya hizo hukazia malengo ya

risala?

A Kiini cha risala

B Hitimisho

C Utangulizi

D Mwanzo wa risala

Ni kipi kati ya hivi hutajwa katika utangulizi wa risala?

Page 49: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 49

A Shukrani

B Jina la mwandishi

C Salamu

D Msisitizo wa malengo

___sio mojawapo ya kipengele cha muundo wa risala.

A Utangulizi

B Shukrani

C Hitimisho

D Kiini

___ni sehemu katika muundo wa risala inayoonesha malengo ya risala.

A Hitimisho

B Utangulizi

C Kiini cha insha

D Mwanzo wa risala

Risala ya kidato cha nne ilionekana kuwa bora zaidi kwa sababu

walizingatia___wa risala.

A Urefu

B Ufupi

C Mtindo

D Muundo

Page 50: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 50

UANDISHI WA KUMBUKUMBU/TAARIFA ZA VIKAO

1. Taarifa za kikao

Kumbukumbu za kikao ni muhtasari wa mambo yaliyojadiliwa na kukubaliwa

katika kikao. Ni muhimu kuandika kumbukumbu za kikao ili kusaidia na

kurahisisha utekelezaji wa mambo yaliyoamuliwa. Pia kumbukumbu za kikao

hutumika kwa ajili ya marejeleo kwa vizazi vya baadaye.

Namna ya kuandika kumbukumbu za kikao

Katika kuandika kumbukumbu mwandishi hana budi kuzingatia mambo

yafuatayo:

(a) Kichwa cha kumbukumbu

Kichwa cha kumbukumbu kioneshe kuwa kikao kinahusu nini, kilifanyikia

wapi na tarehe gani.

(b) Mahudhurio

Mwandishi anapaswa kuandika orodha ya majina ya watu waliohudhuria kikao

na wasiohudhuria. Kama kikao kinahudhuriwa kwa mara ya kwanza

mahudhurio yatakuwa na majina ya waliohudhuria tu.

(c) Uteuzi wa viongozi

Iwapo kikao kinahudhuriwa kwa mara ya kwanza wajumbe hupaswa kuteua

viongozi wa kikao hicho ambao ni Mwenyekiti na Katibu kabla ya kuanza kwa

kikao. Kikao hakiwezi kuanza pasipo viongozi wa kusimamia mijadala yote

katika kikao husika.

(d) Ufunguzi wa kikao

Baada ya kuteua viongozi, Mwenyekiti aliyeteuliwa hufungua kikao rasmi na

kuanzisha mijadala ya kikao cha siku hiyo na siku zijazo hadi itakapokuwa

vinginevyo

(e) Ajenda

Page 51: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 51

Hapa huandikwa ajenda zilizojadiliwa kwenye kikao. Mambo yaliyojadiliwa

katika kila ajenda yaandikwe kwa muhtasari. Kwa kila ajenda kauli ya

kukubaliwa au kukataliwa itamkwe wazi.

(f ) Mengineyo

Hapa huandikwa ajenda ambazo hujitokeza katika kikao lakini hazikupitia kwa

Mwenyekiti na zinastahili kujadiliwa kama ajenda.

(g) Yatokanayo

Hapa huandikwa mambo ambayo yamejitokeza katika kikao na hayana

uhusiano na ajenda za kikao. Kwa mfano masuala mtambuka kama mjumbe

kulipia gharama za kikao,taarifa ya dharura inayoweza kumfanya mjumbe

aondoke kabla ya kikao kuahirishwa, n.k

(h) Kuahirisha kikao

Baada ya majadiliano ya ajenda, Mwenyekiti huahirisha kikao. Mwandishi wa

kumbukumbu azingatie muda kikao kilipoahirishwa.

Baada ya kikao mwandishi apitie tena kumbukumbu hizo na aziandike vizuri na

kuzihifadhi kwa ajili ya marejeleo ya kikao kijacho. Kumbukumbu hizo zitiwe

saini na Mwenyekiti na Mwandishi (katibu) kisha wakati wa kikao kingine

zisambazwe na kusomwa na wajumbe wa mkutano. Baadaye zithibitishwe na

wajumbe na Mwenyekiti na atie saini ya kuthibitishwa huko.

Ufuatao ni mfano wa kumbukumbu za kikao kinachofanywa kwa mara ya

kwanza:

KUMBUKUMBU ZA KIKAO CHA KWANZA CHA WANAFUNZI WA

KIDATO CHA NNE KUHUSU MAHAFALI KILICHOFANYIKA TAREHE

5/4/2017 KATIKA UKUMBI WA SHULE KUANZIA SAA 4:00 ASUBUHI

HADI SAA 6:00 MCHANA.

(a) Mahudhurio

Page 52: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 52

Waliohudhuria (orodhesha majina yao)

-

-

-

-

-

-

-

-

-

Wasiohudhuria (orodhesha majina yao)

-

-

-

-

-

-

-

-

-

(b) Uteuzi wa viongozi

Kiranja wa darasa aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa kikao na katibu wake ni

kiranja msaidizi. Wajumbe wote walikubaliana na uteuzi huo.

(c) Kufungua kikao

Kiranja wa darasa ambaye aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa kikao hicho

alifungua kikao mnamo saa 4:00 asubuhi kwa kuwaeleza wajumbe madhumuni

ya kikao hicho.

(d) Ajenda

- Siku na mahali pa mahafali

- Mgeni rasmi

- Zawadi

Page 53: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 53

- Michango ya sherehe

- Uteuzi wa kamati

Siku na mahali pa mahafali

Wajumbe walijadiliana na kukubaliana kwa pamoja kuwa mahafali yafanyike

jumamosi ya pili kabla ya kuanza kwa mitihani ya kitaifa ili kuwawezesha

waalikwa wote kuhudhuria lakini pia kutoa muda wa kutosha kwa wahitimu

kujiandaa kwa mitihani yao.

Kuhusu mgeni rasmi

Wajumbe walikubaliana kuwa jukumu la kutafuta mgeni rasmi apewe mkuu wa

shule.

Kuhusu zawadi

Wajumbe walijadiliana na kukubaliana kuwa zawadi zitapangwa na kuamuliwa

na kamati itakayoundwa.

Michango ya sherehe

Kikao kiliazimia kwa pamoja kuwa ili kupata pesa za kufanikishia mahafali kila

mjumbe apewe fomu maalumu itakayoandaliwa ili kuchangisha toka kwa

ndugu, jamaa na marafiki kiasi chochote atakachoguswa mtu kuchangia.

Uteuzi wa kamati

Wanafunzi wafuatao walichaguliwa ili wafanye mipango ya kuandaa na

kusimamia sherehe ya mahafali yao. Wanafunzi hao ni;

- Mtungi

- Baraka

- Mujuni

- Byoma

- Shukuru

- Sikudhani

- Kachacha

- Stumai

Page 54: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 54

- Tamasha

- Kaitaba

Wajumbe hao walikubaliana na uteuzi huo na wakaahidi kupeana majukumu.

(f) Mengineyo

Wajumbe walisisitiza kwamba kamati ifanye mipango kwa kuzingatia kwamba

muda uliobaki ni mfupi. Walipendekeza kwamba kufanyike mkutano wa

kuwapatia wajumbe taarifa kuhusu mgawanyo wa majukumu.

(g) Yatokanayo

Mjumbe mmoja aliwaburudisha wajumbe kwa vinywaji na nyama choma ya

mbuzi katika kumbukumbu yake ya kuzaliwa.

(h) Kuahirisha kikao

Mwenyekiti aliahirisha kikao kwa kuwaomba wajumbe wengine wawe na

ushirikiano kwa wenzao katika kufanikisha mahafali hayo. Kikao liahirishwa

saa 6:00 mchana. Kikao kijacho kitakuwa 12/4/2017 kuanzia saa 9:00 mchana

hadi saa 12:00 jioni.

Mwenyekiti…………………….Tarehe…………………………........

Katibu………………………….Tarehe……………………………….

Ikiwa kikao kinafanyika kwa mara ya pili:

Kikao cha pili na kuendelea huwa na muundo ufuatao:

1. Kichwa cha kikao

2. Mahudhurio

3. Kusomwa na Kuthibitishwa taarifa za kikao kilichotangulia

4. Kufungua kikao

5. Ajenda

6. Mengineyo

7. Yatokanayo

Page 55: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 55

8. Kuahirisha kikao

9. Majina & saini za viongozi

ZOEZI

Kumbukumbu za mkutano huchukuliwa na nani?

A Mwenyekiti

B Mjumbe

C Walioalikwa

D Katibu

Tarehe ya mkutano huandikwa katika kipengele gani wakati wa uchukuaji wa

kumbukumbu za mkutano?

A Ajenda

B Mahudhurio

C Mengineyo

D Kichwa cha kumbukumbu

Kichwa cha kumbukumbu za mkutano hutaja mambo yafuatayo isipokuwa___.

A Tarehe

B Gharama

C Mahali

D Muda

“Waliohudhuria ni wanafunzi 3 wa kidato cha 3B.” Sentensi hii hubainisha nini?

Page 56: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 56

A Ajenda

B Kichwa cha kumbukumbu

C Mengineyo

D Mahudhurio

Hoja zitakazorejelewa katika mkutano huitwa___.

A Mapendekezo

B Maazimio

C Maafikiano

D Ajenda

MADA YA 6 : UFAHAMU

Ufahamu wa Kusikiliza

Ufahamu wa kusikiliza ni zaidi ya kusikiliza tu kile kilichosemwa; badala yake ni

uwezo wa mtu kuelewa maana ya maneno anayoyasikia na kuweza kuhusiana nayo

kwa namna fulani. Kwa mfano mwanafunzi anaposikiliza hadithi, ufahamu mzuri

wa kusikiliza humsaidia kuielewa hadithi hiyo, kuikumbuka, kuijadili, na hata

kuisimulia tena kwa maneno yake mwenyewe.

Kujibu Maswali ya Habari Uliyosikiliza

Ufahamu wa kusikiliza unahusisha michakato kadhaa katika kuelewa na kupata

maana ya kile kinachozungumzwa. Michakato hii inahusisha:

Kuelewa vizuri sarufi ya lugha ile inayozungumzwa

Kuelewa vyema maana ya maneno ya mhusiaka anayezungumza

Page 57: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 57

Kuelewa sintaksia (muundo wa maneno) ya sentensi kwa namna

zinavyowasilishwa.

Katika ufahamu wa kusikiliza, msikilizaji hana budi kuzingatia mambo yafutayo:

1. Kuwa makini na kuelekeza akili yote kwa mzungumzaji ili kuweza kusikia

kila anachokisema.

2. Kutilia maanani vidokezo vya maana ili kubaini iwapo msemaji anaongeza

jambo jipya, anatofautisha, anafafanua au anahitimisha hoja.

3. Msomaji anatakiwa kuandika baadhi ya mambo anayoona kuwa ni ya

muhimu ili kumasidia kukumbuka hapo baadae.

4. Kuwa makini na ishara mbambali za mwili kama vile kurusha mikono,

kutingisha kichwa, kutingisha mabega au hata kupepesa macho. Ishara hizi

huwa zinachangia kwa kiasi kikubwa kupata maana katika mazungumzo.

ZOEZI

___ husaidia kupata maana ya maneno na misemo ili kujibu maswali ya habari

unayoisikiliza.

A Kusikiliza kwa makini

B Matumizi ya neno

C Wazo kuu

D Msomaji

Ni kipi afanye msikilizaji ili aweze kubaini mawazo makuu katika habari

anayoisikiliza?

A Kuuliza maswali

B Kusikiliza kwa makini

Page 58: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 58

C Kufuatilia ishara

D Kuandika

Ipi siyo ishara ya mwili inayotoa maana katika kujibu maswali ya habari

inayosikilizwa?

A Kukaa kimya

B Kupepesa macho

C Kutingisha kichwa

D Kutingisha mabega

Inapaswa kuzingatia vidokezi vya maana ili kujibu maswali ya habari uliyosikiliza.

Ipi si kazi ya vidokezi vya maana?

A Kutofautisha

B Kuhitimisha

C Kuonesha mtiririko

D Kurahisisha

Yafuatayo hufanyika katika ufahamu wa kusikiliza, isipokuwa:

A Kuzingatia ishara

B Kuandikwa kwa ufupi yasemwayo

C Kuzingatia vidokezi vya maana

Page 59: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 59

D Kuzingatia matini

Kufupisha Habari

FIli kuandika ufupisho mzuri wa habari uliyoisikiliza yafuatayo hayana budi

kuzingatiwa; kusikiliza habari kwa makini ili kuielewa vizuri, kuandika mawazo

makuu yanayojitokeza katika kila aya, kuyaunganisha mawazo makuu na

kuiandika habari kwa maneno yako, kuhesabu idadi ya maneno kama inazidi na

kuandika idadi hiyo mwisho wa ufupisho upande wa kulia chini kidogo.

ZOEZI

___ yapaswa yaunganishwe ili kuandika ufupisho mzuri wa habari.

A Mawazo makuu

B Maneno magumu

C Maneno ya kila aya

D Matamshi ya mzungumzaji

___siyo jambo la kuzingatiwa katika kuandika ufupisho unaofaa wa habari

iliyosikilizwa.

A Uunganishaji wa mawazo makuu

B Vidokezo vya maana

C Mawazo makuu

D Idadi ya maneno

___hupatikana baada ya kuyatambua mawazo makuu na kuyafupisha.

A Nafsi

B Kiini cha habari

Page 60: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 60

C Kichwa cha habari

D Njeo

Katika kufupisha habari uliyosikiliza kipi katika haya ni cha kuzingatia?

A Ishara za mwili

B Aya

C Matamshi ya mzungumzaji

D Mawazo makuu

Katika ufupisho wa habari uliyosikiliza ni muhimu kubainisha___.

A Njeo

B Kichwa cha habari

C Swali

D Nafsi

Ufahamu wa Kusoma

Ufahamu wa kusoma ni ule mtu anaoupata kwa njia ya kusoma makala, kifungu

cha habari, kitabu au gazeti.

Kujibu Maswali kutokana na Habari ndefu uliyosoma

Jibu maswali kutokana na habari ndefu uliyosoma

Kuna vipengele viwili vinavyounda mchakato wa ufahamu wa kusoma:

Uelewa wa msamiati na

Uelewa wa matini

Page 61: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 61

Ili kuilelewa habari/matini ni lazima msomaji awe na uwezo wa kuelewa msamiati

uliotumika katika matini hiyo. Endapo maneno yaliyotumika hayataeleweka

vilevile matini yote hataeleweka.

Katika ufahamu wa kusoma, msomaji anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:

1. Kubaini mawazo makuu; msomaji anaposoma habari fulani au kitabu

inatakiwa ajiulize, Je, kinachoongelewa hapa ni nini? Ni jambo gani hasa

analolizungumzia mwandishi? Msomaji akiwa na maswali haya akilini

mwake basi itakuwa rahisi kwake kuielewa habari hiyo.

2. Kuzingatia alama za uakifishi; msomaji ni lazima azingatie alama za

uakifishi, kwa kufanya hivyo itamsaidia kuelewa ujumbe wa habari hiyo na

endapo hatazingatia alama za uakifishaji anaweza kupotosha maana ya

mwandishi.

3. Kubaini maana ya maneno na misemo mbalimbali; habari nyingine huwa

zina maneno ya kisanaa hivyo ni muhimu msomaji kubaini maana ya

maneno hayo katika muktadha wa habari hiyo, hii itamsaidia kuelewa vyema

maana ya mwandishi.

4. Vilevile msomaji anatakiwa kumakinikia kile anachokisoma, kila kipengele

anachokisoma inampasa akielewe vizuri.

Kwa kuzingatia haya yote msomaji atakuwa na uelewa mzuri juu ya habari

aliyoisoma na pia anaweza kufupisha habari hiyo aliyoisoma.

Kufupisha habari

Kufupisha habari ni kuandika upya habari uliyoisoma kwa maneno machache

lakini bila kupotosha ujumbe wa habari ya kwanza.

Ufupisho wa habari huwa na sifa hizi:

1. Huwa ni mfupi kuliko habari ya mwanzo

2. Huwa na ujumbe uleule uliokuwa katika habari ya mwanzo

3. Hujumuisha mawazo makuu yaliyodondolewa kutoka kwenye habari ya

mwanzo

Page 62: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 62

4. Mawazo haya sharti yapangwe katika mtririko wenye mantiki

Hatua za kufuata katika kuandika ufupisho

Ili kuweza kufanikiwa kufupisha habari kwa ufanisi hatua zifuatzo sharti zifuatwe:

Kuisoma au kuisilikiza habari kwa makini ili kuielewa vizuri

Kutambua na kubaini mawazo makuu yanayojitokeza katika kila aya

Kuyaunganisha mawazo makuu na kuandika au kuelezea ufupisho wa habari

hiyo kwa maneno yako mwenyewe bila kupostosha maana ya habari ya

kwanza.

Kuhesabu idadi ya maneno ya ufupisho ili kuyapunguza ikiwa yanazidi idadi

iliyotakiwa.

Kama muda unaruhusu pitia tena habari ya mwanzo na pitia tena ufupisho ili

kujiridhisha kuwa hujaacha taarifa yoyote ya muhimu.

ZOEZI

___ni ujumbe wa msingi katika habari unaopaswa kuzingatiwa.

A Ishara

B Misemo

C Mawazo makuu

D Lugha ya mwandishi

Nini huweza kuhafifisha maana ya mwandishi katika habari ikiwa

hakitazingatiwa?

A Aina ya insha

B Urefu wa insha

C Alama za uandishi

Page 63: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 63

D Idadi ya maneno

Mbinu gani itaepusha kutoka maelezo marefu na yasiyohitajika wakati wa kujibu

maswali ya habari ndefu uliyosoma?

A Kujibu kwa ufupi

B Kuwa mtulivu

C Kuelewa swali

D Kusoma kwa makini

___ siyo mojawapo ya vidokezo vya maana vinavyotumika katika kuhitimisha

habari.

A Hivyo

B Hatimaye

C Hata hivyo

D Kwa hiyo

Msomaji afanye nini ili asome habari ndefu kwa ukamilifu bila kuruka baadhi ya

aya na kujibu maswali yake?

A Kuwa mtulivu

B Kujibu kwa ufupi

C Kuelewa swali

D Kusoma kwa makini

Kufupisha Habari ndefu uliyosoma

Ili kuweza kuandika ufupisho wa habari ndefu uliyoisoma hatua zifuatazo sharti

zifuatwe, kusoma habari kwa makini na kuielewa vizuri, kubaini mawazo makuu,

Page 64: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 64

kuandika ufupisho wa habari kwa maneno yako, kuhesabu idadi ya maneno na

kupunguza yaliyozidi na kupitia tena habari ya mwanzo na ya mwisho kama muda

unaruhusu. Aidha ufupisho wa habari huwa ni mfupi na una ujumbe uleule wa

habari ya mwanzo.

ZOEZI

Zifuatazo ni hatua za kufuata ili kuandika ufupisho wa habari, isipokuwa:

A Kuisoma habari kwa makini

B Kuandika ufupisho kwa maneno yako

C Kuhesabu maneno

D Kubaini mawazo makuu

___ni kuandika upya habari uliyoisoma kwa maneno machache bila kupotosha

ujumbe wa habari ya kwanza.

A Kufupisha habari

B Ufahamu

C Uandishi

D Insha

Ipi ni hatua ya mwisho ya kuzingatia katika kuandika ufupisho wa habari

uliyosoma?

A Kuhesabu idadi ya maneno

B Kutambua mawazo makuu

C Kusoma kwa makini

Page 65: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI · lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Shughuli za kidini Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio

KIDATO CHA NNE 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 65

D Kuandika idadi ya maneno

Kipi kati ya hivi ni muhimu kujumuishwa katika ufupisho wa habari ndefu

uliyosoma?

A Viunganisha

B Misemo

C Vielezi

D Mawazo makuu

Maneno yaliyozidi katika ufupisho hupunguzwa baada ya___.

A Kuhesabu idadi ya maneno

B Utambuzi wa mawazo makuu

C Kubaini mawazo makuu

D Kuandika idadi ya maneno