30
DESEMBA, 2016 BARAZA LA HABARI TANZANIA

KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

  • Upload
    others

  • View
    0

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

1

DESEMBA, 2016

BARAZA LA HABARI TANZANIA

UCHAMBUZI WA SHERIA YA HAKI YA KUPATA TAARIFA,

2016

Page 2: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

32

CONTENTS1. Utangulizi ................................................................................................................3

2. Viwango vya Kimataifa/Kikanda, Katiba na namna Bora ya Upatikanaji wa Taarifa. ....................................................................................4

3. Sheria ya Kupata Taarifa ya Mwaka 2016 na Sera ya Habari na Utangazaji ya Mwaka 2003 na Mpango wa Uwazi Serikalini. ...20

2. Upungufu na Udhaifu wa Sheria hii .........................................................25

3. Mapendekezo Muhimu .................................................................................30

4. Hitimisho .............................................................................................................30

Page 3: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

3

1. Utangulizi Uchambuzi huu umegawanyika katika sehemu saba. Sehemu

ya kwanza ni utangulizi, sehemu ya pili inazungumzia namna sheria hii inavyoendana na viwango vya Kimataifa/Kikanda, Katiba na namna bora (best practices) ya upatikanaji wa taarifa. Sehemu ya tatu inalinganisha Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa na Sera ya Habari na Utangazaji, ya mwaka 2003 pamoja na mpango wa uwazi serikalini. Sehemu ya nne inaangalia kiwango ambacho mapendekezo ya CoRI yameakisiwa katika Sheria hii. Sehemu ya tano inaonyesha udhaifu na upungufu wa Sheria hii, ambapo sehemu ya sita inatoa mapendezo na sehemu ya saba ni hitimisho.

Sheria hii ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Septemba 7, 2016 na kuidhinishwa na Rais John Pombe Magufuli, Septemba 23, 2016. Kwa mujibu wa kifungu cha 2(1), Sheria hii inatumika Tanzania Bara pekee. Kwa kifupi, hii ni Sheria inayohusu haki ya kupata taarifa, kupanua wigo wa taarifa ambayo jamii inaweza kuipata ili kukuza uwazi na uwajibikaji wa wenye taarifa pamoja na mambo mengine yanayohusiana na hayo.1

Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa ni ndogo sana ukilinganisha na sheria nyingine za nchi. Sheria hii imegawanyika katika sehemu nne na vifungu 24. Sehemu ya kwanza ina vifungu vya awali, sehemu ya pili inazungumzia haki ya kupata taarifa, sehemu ya tatu inazungumzia upatikanaji wa taarifa na sehemu ya nne inazungumzia vifungu vinavyotoa masharti ya jumla.

Kwa ujumla vifungu vingi vya Sheria hii viko sawa na vinakidhi viwango vinavyokubalika. Hata hivyo kuna baadhi ya vifungu ambavyo havikidhi viwango na hivyo kuingilia haki ya kupata taarifa kama ilivyoelezwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mikataba ya Haki za Binadamu iliyoridhiwa au kusainiwa na Tanzania. Vifungu

1 Angalia sehemu ya Mwanzo ya Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa, 2016.

Page 4: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

54

hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote.

Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu lengo au dhumuni la Sera ya Habari na Utangazaji ya mwaka 2003 la kuhakikisha upatikanaji wa taarifa pasipo na vikwazo. Sababu kuu ni baadhi ya vifungu vya sheria hii ambavyo vinaminya haki ya kupata taarifa kwa kuzuia watu wasio raia kupata taarifa, kuweka mazingira mapana ya kuminya upatikanaji wa taarifa pamoja na ada kwa ajili ya kupata taarifa. Kwa pamoja hivi ni vikwazo katika upatikanaji wa taarifa. Bila kujali upungufu huo, pia sheria hii inaendana na malengo ya mpango kazi wa uwazi serikalini wa mwaka 2014 - 2016 japokuwa kuna vifungu vichache ambavyo haviakisi malengo hayo kama itakavyonekana katika uchambuzi huu.

Pia kwa kiwango kikubwa mapendekezo yaliyotolewa na CoRI kuhusu sheria hii hayakuchukuliwa. Ni mapendekezo machache ambayo yameakisiwa ndani ya sheria hii. Kwa hiyo kuna haja ya kushawishi marekebisho ya sheria hasa kuhusu vifungu vyenye matatizo ili viendane na viwango vinavyokubalika kimataifa. Pia, wadau wa sekta ya habari wanaweza kufungua shauri la kikatiba katika Mahakama Kuu kupinga baadhi ya vifungu vya sheria hii vinavyokinzana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2. Viwango vya Kimataifa/Kikanda, Katiba na namna Bora ya Upatikanaji wa Taarifa.

Sehemu hii ya uchambuzi inalinganisha vifungu vya sheria ya Haki ya Kupata Taarifa ya mwaka 2016 na viwango vya kimataifa, Kikanda, Kikatiba na namna bora ya upatikanaji wa taarifa. Inaeleweka kuwa serikali inatunza taarifa si kwa ajili yake yenyewe bali ni kwa niaba ya umma na hivyo vyombo vya umma vinatakiwa kutoa taarifa hizo pale vinapohitajika kufanya hivyo. Kwa mantiki hiyo na kwa mujibu wa kanuni, sheria zinazohusu taarifa ni lazima zitambue dhana kuu kuwa

Page 5: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

5

Serikali ipo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.2

Vyombo mbalimbali vya kimataifa vinatambua umuhimu wa haki ya uhuru wa kupata taarifa ikiwa ni pamoja na haja ya kuwa na sheria madhubuti kwa ajili ya kulinda utoaji wa haki hiyo. Vyombo hivyo ni pamoja na Umoja wa Mataifa (U.N), Muungano wa Nchi za Amerika (OAS), Baraza la Ulaya (CE) na Umoja wa Afrika (AU).3

Mchunguzi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa maoni na kujieleza, amezungumzia kuhusu umuhimu wa uhuru wa kupata taarifa katika ripoti zake za kila mwaka tangu mwaka 1997. Kwa kiasi kikubwa, katika ripoti yake ya mwaka 1998, mchunguzi huyo alisema wazi kuwa haki ya kupata taarifa zinazotunzwa na nchi zimeunganishwa katika haki ya uhuru wa kujieleza: “ Haki ya kutafuta, kupokea na kutoa taarifa inaweka wajibu kwa nchi kuhakikisha upatikanaji wa taarifa hasa taarifa zile zinazotunzwa na serikali katika kila aina au mifumo ya uhifadhi.4

Chini ya sheria za kimataifa haki hii hutolewa chini ya Ibara ya 19 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa, 1966 na Ibara ya 9 ya Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu, 1981. Ibara hizi mbili zinatoa haki ya mtu kutafuta na kupokea taarifa.5

Mwaka 2002, Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ilipitisha Azimio la Kanuni za Uhuru wa Kujieleza Afrika. Azimio hilo linasisitiza haki ya kupata taarifa kutoka katika vyombo vya umma. Azimio hilo linatamka wazi kuwa vyombo vya umma vinatunza taarifa sio kwa ajili yao wenyewe bali kwa niaba ya umma na kila mmoja ana haki ya kupata taarifa hizo kwa mujibu wa taratibu za kisheria. Azimio hilo linaenda mbali zaidi na kutamka kwamba-6

2 https://www.article19.org/resources.php/resource/3024/en/international-standards:-right-to-information ilivyotembelewa tarehe 5 Desemba 2016.3 Inapatikana katika tovuti iliyotajwa hapo juu.4 Inapatikana katika tovuti iliyotajwa hapo juu.5 Inapatikana katika tovuti iliyotajwa hapo juu.6 https://www.article19.org/resources.php/resource/3024/en/international-standards:-right-to-information

Page 6: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

76

• Haki ya kupata taarifa italindwa kwa mujibu wa kanuni zifuatazo:

Kilamtuanahakiyakupatataarifakutokakatikavyombovya umma;

Kilamtuanahakiyakupatataarifakutokakatikavyombobinafsi ambazo ni muhimu kwa ajili ya kupata au kulinda haki yoyote;

Kilaombilataarifalitakapokataliwakuwenahakiyakukatarufaa katika chombo huru au mahakama;

Vyombovyaummavinawajibuwakuchapishataarifamuhimu na zenye maslahi kwa umma hata kama hakuna maombi ya kufanya hivyo;

Mtuyoyoteasipeweadhabukwakutoataarifakwanianjemajuu ya matendo maovu au taarifa zinazoonyesha tishio kubwa kwa afya, usalama au mazingira. Adhabu itolewe tu pale ambapo ni lazima kwa ajili ya kulinda maslahi ya jamii na ni muhimu katika jamii ya kidemokrasia;

Sheriazinazotamkataarifafulanikuwazasirizifanyiwemabadiliko ili ziendane na kanuni za uhuru wa kupata taarifa; na

Kilamtuanahakiyakupata,kuongezaaukusahihishataarifa zake binafsi bila kujali kuwa zinatunzwa na vyombo vya umma au binafsi.

Ukilinganisha vifungu vya Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa ya mwaka 2016 na kanuni hii, utagundua kuwa sheria hii inaruhusu upatikanaji wa taarifa zinazotunzwa na vyombo vya umma au binafsi, vilivyosajiliwa na vinavyotumia pesa za umma. Hii inatamkwa chini ya kifungu cha 2(2) (a) na (b) (i) cha sheria hii. Kanuni hii hapo juu inataka upatikanaji wa taarifa hata kwa vyombo binafsi ikiwa tu taarifa hiyo ni muhimu kwa ajili ya kupata au kulinda haki.1 Kipengele hiki kinakosekana katika sheria hii ambayo inaruhusu utolewaji wa taarifa kwa vyombo binafsi vinavyotumia fedha za umma pekee. Huu ni upungufu.

kama ilivyotembelewa tarehe 5 Desemba 2016.

Page 7: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

7

Kwa undani zaidi, kanuni hiyo hapo juu, inasema kwamba kila mtu bila kujali uraia wake ataweza kupata taarifa zinazotunzwa na vyombo vya umma. Hii inamaanisha kwamba hakuna ubaguzi wa aina yoyote unaoruhusiwa katika kutoa/kupata taarifa.

Chini ya sheria hii ya upatikanaji wa taarifa ya 2016, taarifa zinaruhusiwa kutolewa kwa raia wa Tanzania pekee. Kifungu cha 5 (1) kinatamka wazi kuwa kila mtu ataweza kupata taarifa kutoka kwa mwenye taarifa. Hata hivyo kifungu kidogo cha 5(4) kinatamka wazi kuwa maana ya mtu ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hiyo, hii inamaanisha kuwa ni raia pekee wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio wanaweza kupata taarifa kutoka katika vyombo vya umma au binafsi vinavyotumia pesa za umma. Hii inaweza kuwa na athari kubwa zaidiyaifikiriwavyo.KwamujibuwaSheriayaUraiayamwaka1995, maana ya neno raia ni mtu au binadamu (natural persons) mwenye sifa za kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na kwa mantiki hiyo, sheria hii inazuia makampuni/mashirika/ asasi, taasisi za kimataifa na raia wa kigeni kupata taarifa kwa kuwa hawatambuliki kama raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni ukiukwaji wa wazi kabisa wa kanuni tajwa hapo juu inayotaka kila mtu aruhusiwe kupata taarifa. Kwa mfano hakuna sababu za msingi za kuzuia raia wa kigeni kupata taarifa kwa kuwa kuna taarifa ambazo zinaweza kuwa na umuhimu kwao kama vile za uhamiaji, uwekezaji n.k. Njia rahisi ilikua ni kuzuia au kutaja aina ya taarifa wanazoweza kupata na zile ambazo hawawezi kupata na si vinginevyo.

Kanuni nyingine katika azimio hili ni wajibu wa kuchapisha taarifa. Kanuni hii inatajwa katika ibara ya IV (2) ya Azimio la Kanuni za Uhuru wa Kujieleza Afrika la mwaka 2002. Kanuni hii inasema hivi, vyombo vya umma vina wajibu wa kuchapisha taarifa muhimu. “Uhuru wa kupata taarifa haumaanishi tu kuwa vyombo hivi vinatakiwa kukubali maombi ya kutoa taarifa lakini pia kuchapisha na kusambaza nyaraka mbalimbali zenye taarifa zenye maslahi pana ya umma. Vyombo hivi ni lazima vifanye hivyo kwa kuwa kufanya kinyume na hapo kunamaanisha kuwa taarifa hizo zitapatikana tu kwa wale ambao wameomba, ilihali ni taarifa

Page 8: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

98

muhimu kwa kila mtu. Zaidi ya hayo, uchapishwaji wa taarifa kwa ujumla unapunguza gharama na muda kuliko kutoa taarifa kwa kila maombi yanapoletwa.7

Wigo wa kuchapisha taarifa unategemea rasilimali zilizopo, lakini kiwango cha taarifa kinachochapishwa kinatakiwa kuongezeka kila mara, ukizingatia kuwa teknolojia mpya imefanya uchapishaji na usambazaji wa taarifa kuwa rahisi zaidi.

Chini ya sheria hii ya Upatikanaji wa Taarifa, wajibu wa kuchapisha taarifa unatolewa kwenye kifungu cha 9(1), lakini wigo wa taarifa zinazotakiwa kuchapishwa ni mdogo sana. Namna bora ya uchapishaji wa taarifa unaonesha kuwa, pamoja na mambo mengine, vyombo vinavyotunza taarifa vinatakiwa kuchapisha bajeti au mipango yao ya kifedha, mikataba mbalimbali n.k. Kwa bahati mbaya hili halijazungumziwa kabisa katika sheria hii ya Upatikanaji wa Taarifa ya mwaka 2016.

Tukiachana na Azimio hili, pia kuna sheria ya Mfano ya Upatikanaji wa Taarifa ya Afrika (African Model Law on the Right to Access Information). Sheria hii ilitungwa ili isaidie nchi nyingine kutunga sheria zao zitakazoakisi viwango vinavyokubalika kimataifa na kikanda kuhusu haki ya kupata taarifa. Sheria hii ya mfano inatamka viwango vya chini kabisa ambavyo nchi inatakiwa kuvizingatia. Sasa tulinganishe vifungu vya Sheria ya Kupata Taarifa ya mwaka 2016 na sheria hii ya mfano ili tuone kama vinaendana.

Kifungu cha 2(1) (b) cha sheria ya Mfano kinaruhusu kupata taarifa kutoka kwa vyombo binafsi ikiwa tu taarifa hizo zinahitajika ili kusaidia katika upatikanaji au ulinzi wa haki yoyote. Kama tulivyoona hapo mwanzo, chini ya sheria ya Kupata Taarifa, ya mwaka 2016, upatikanaji wa taarifa kutoka katika vyombo binafsi unaruhusiwa kwa vyombo vile tu ambayo vinatumia pesa za umma kujiendesha na si vyombo vingine. Hii ni kinyume na kanuni na iko chini kabisa ya kiwango kinachokubalika. Kuna mazingira ambayo taarifa

7 https://www.article19.org/resources.php/resource/3024/en/international-standards:-right-to-information kama ilivyotembelewa tarehe 5 Desemba 2016.

Page 9: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

9

zinaweza kuwa ni muhimu sana katika kupata au kulinda haki ya mtu, na taarifa hizo zikawa ziko chini ya vyombo binafsi. Kwa hiyo ni muhimu kuruhusu upatikanaji wa taarifa katika mazingira hayo kama ilivyotanabaishwa katika sheria ya Mfano.

Kifungu cha 4(1) cha sheria ya Mfano, kinatamka ukuu wa sheria hii dhidi ya sheria nyingine yoyote inayozuia upatikanaji wa taarifa. Inatamkwa wazi kuwa sheria hii itakuwa kuu dhidi ya sheria nyingine yoyote inayohusiana na upatikanaji wa habari. Hii ni muhimu sana kwa ajili ya kulinda haki hiidhidiyaukiukwajiunowezakufanywanamaafisawaserikali kwa kutumia sheria nyingine kinzani. Ni bahati mbaya kuwa sheria ya Kupata Taarifa haijatamka chochote kuhusu ukuu wake dhidi ya sheria nyingine. Madhara ya kukosekana kwakifungukinachotamkahivyonikuruhusumaafisawaserikalikujifichanyumayakivulichasheriazinazotakausiriwa baadhi ya taarifa na kuminya upatikanaji wa aina fulani ya taarifa.

Katika wajibu wa kuchapisha taarifa, sheria hii ya Mfano, inatoa wigo mpana sana. Pamoja na mambo mengine, Sheria hii inamtaka kuwa mwenye taarifa atatakiwa kuchapisha mikataba, bajeti na mipango ya matumizi.8 Sheria ya Kupata Taarifa 2016, haikidhi kiwango hiki. Wajibu wa kuchapisha taarifa katika kifungu cha 9 cha sheria ya Kupata Taarifa haihusishi mikataba na mipango ya fedha kama inavyotakiwa kwenye sheria ya Mfano.

Kifungu cha 8(1) (a) na (b) cha Sheria ya Mfano kinaweka wajibu kwa mwenye taarifa kupeleka ripoti ya mipango ya uchapishaji na utekelezaji wa vifungu vya sheria kila mwaka kwa chombo maalum cha usimamizi. Hili halijazungumziwa kabisa katika sheria ya Upatikanaji wa Taarifa. Kwanza, sheria haianzishi chombo chochote cha usimamizi. Pili, sheria haiweki wajibu kwa mwenye taarifa kupeleka ripoti ya utekelezwaji wa sheria hii kwa chombo chochote. Huu ni upungufu mkubwa

8 Hii inatamkwa katika vifungu vya 7(g) na (f).

Page 10: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

1110

na unaweza kuathiri utekelezwaji madhubuti wa Sheria hii na hasa hasa haki ya kupata taarifa.

Kifungu kingine muhimu cha Sheria ya Mfano ni kifungu cha 12(1), ambacho kinampa kila mtu haki ya kupata taarifa. Kifungu hiki hakibagui kati ya raia na wasiokuwa raia. Inatoa nafasi sawa kwa wote. Hii ni tofauti na vifungu vya 5(1) & (4) vya sheria ya upatikanaji wa taarifa ambavyo vinaruhusu haki hii kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee. Kwa kifupi, sheria ya Kupata Taarifa haijakidhi kiwango hiki.

Zaidi ya hayo, Sheria ya Mfano inatoa wigo mpana katika namna ambavyo maombi ya kupata taarifa yanaweza kufanywa. Chini ya kifungu cha 13(1), sheria inatamka kwamba katika kuomba taarifa, maombi yanaweza kufanywa kwa maandishi au kwa njia ya mdomo. Kwa hiyo sio lazima maombi yafanywe kwa maandishi tu. Lakini chini ya sheria ya Kupata Taarifa, maombi ya kupata taarifa ni lazima yawe kwenye maandishi. Hii ni kwa sababu mtu anayeomba taarifa atawajibika kujaza fomu maalum. Hakuna njia nyingine mbadala ya kuomba taarifa kwa njia ya mdomo.

Pia, chini ya kifungu cha 15(1) cha Sheria ya Mfano, muda ambao maombi ya kupata taarifa yanatakiwa kuwa yameshughulikiwa ni ndani ya siku 21. Muda huu ni mfupi na unasaidia katika kuhakikisha kuwa maombi ya taarifa yanafanyiwa kazi kwa haraka. Sheria ya Kupata Taarifa imeweka muda mrefu zaidi wa siku 30 kinyume na Sheria ya Mfano.

Kuhusu ucheleweshwaji au uzuiaji wa muda wa upatikanaji wa taarifa, Sheria ya Mfano inaweka namna bora zaidi. Chini yakifungucha19(1)(a)na(b),inatamkwawazikuwaafisawahabari anaweza kuzuia kwa muda upatikanaji wa taarifa, ikiwa kama, taarifa zinahohitajika zimeandaliwa ili ziwasilishwe bungeni kwanza. Hata hivyo uzuiaji huo hautakiwi kuzidi siku tano za vikao vya bunge. Hii inamaanisha kuwa mwenye taarifa anaweza kuzuia kwa muda upatikanaji wa taarifa kwa siku tano tu za vikao vya bunge na si zaidi ya hapo.

Page 11: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

11

Pia, upatikanaji wa taarifa unaweza kuzuiwa kwa muda kuhusiana na taarifa zinazotakiwa kuwasilishwa kwanza kwenye chombo mahsusi cha umma. Cha kufurashisha ni kwamba, taarifa hizo zinaweza kupatikana mara tu baada ya kuwasilishwa katika chombo hicho au baada ya siku 45. Hii ni njia nzuri sana kwa sababu inaondoa uwezekano wa kuzuia upatikanaji wa taarifa kwa kipindi kisichojulikana. Ni bahati mbaya sana kuwa kifungu cha 16 (1) cha sheria ya Kupata Taarifa, kinaruhusu mwenye taarifa kuzuia upatikanaji wa taarifa bila ya kuwa na kikomo cha muda wa zuio. Hii ni hatari sana, kifungu hiki kinaweza kutumika kunyima upatikanaji wa aina fulani ya taarifa.

Ili kufanikisha haki ya kupata taarifa, upatikanaji wa taarifa hautakiwi kuwa na gharama kubwa. Wadau wengi wamekuwa wakitetea hoja kuwa upatikanaji wa taarifa uwe ni bure au kwa gharama ndogo ili kila mtu aweze kupata haki hii. Kuipa nguvu jambo hili, kifungu cha 23 (2) cha Sheria ya Mfano kinazungumza wazi kabisa kuwa mwenye taarifa anaweza kumtozamwombataarifakiasikidogochaadaikiwanifidiaya gharama za kutoa au kutengeza nakala za taarifa hiyo. Hii ni nzuri kwa kuwa inalenga kuhakikisha kuwa wenye taarifa hawatumii nafasi hii kama vyanzo vya kujiongezea mapato. Kifungu hiki kinaenda mbali zaidi na kusema kuwa, maombi ya taarifa zenye maslahi kwa umma yasitozwe ada yoyote, kwa maana nyingine iwe ni bure kupata taarifa za namna hiyo. Hii inatamkwa katika kifungu cha 23 (b) cha Sheria ya Mfano. Kwa upande mwingine Sheria ya Kupata Taarifa ina kifungu kinachotaka utozaji wa ada kwenye maombi ya kupata taarifa. Kitu cha kushangaza ni kuwa, Sheria inasema tu kuwa mwenye taarifa anaweza kutoza ada. Sheria haiweki viwango vya ada inayoweza kutozwa wala haiweki namna au mazingira ambayo baadhi ya taarifa zenye maslahi kwa umma zinaweza kupatikana pasipokuwa na utozaji wa ada.

Mwisho kabisa, sehemu ya tano ya Sheria ya Mfano, (kutoka kifungu cha 45-81) kinaazisha chombo maalumu cha

Page 12: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

1312

usimamizi wa utekelezwaji wa Sheria ili kuipa nguvu haki ya kupata taarifa. Haijulikani ni kwa sababu gani, sheria ya Kupata Taarifa haijaanzisha chombo chochote cha kusimamia utekelezwaji wa sheria hii. Nchi nyingi zenye sheria ya Kupata Taarifa zimekuwa na vyombo maalum vya usimamizi wa sheria hizi, kwa mfano nchi kama Uingereza, India na Afrika ya Kusini zina vyombo maalum vya kusimamia utekelezwaji wa sheria hizo. Na imeonekana kuwa vyombo hivi vimekuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha kuwa sheria hizi zinatekelezwa ipasavyo.

Hata kama hatutaki kuamini, lakini ukweli unabaki kuwa Sheria ya Kupata Taarifa ya mwaka 2016 haikidhi kwa kiasi kikubwa viwango vilivyomo kwenye Sheria ya Mfano vya upatikanaji wa taarifa Afrika. Vifungu muhimu ambavyo vinahakikisha upatikanaji madhubuti wa haki ya kupata taarifa havimo kwenye sheria hii ya Kupata Taarifa. Mtu unaweza kushawishika kusema kuwa sheria hii ilitungwa ikiwa na malengo mengine tofauti na kutoa haki ya kupata taarifa.

Pia, kuna kanuni nyingine ambazo zinajulikana kama Kanuni za Uhuru wa kupata Taarifa za Jumuiya ya Madola. Kanuni hizi zilitungwa katika mkutano wa 11 wa Mawaziri wa nchi za Jumuiya ya Madola huko Trinidad na Tobago mwezi Mei mwaka 1999. Kanuni ya 2 inatamka kuwa sheria za utoaji wa taarifa ni lazima zitungwe kwa kuzingatia kanuni ya uwazi ya kutoa taarifa ya Jumuiya za Madola kwa kiwango cha juu.”9 Kanuni ya uwazi inataka kuwe na upatikanaji wa taarifa zote zilizo chini ya vyombo vya umma, na taarifa hizo zinaweza kuzuiwa katika mazingira machache sana. Kipengele kingine cha kanuni hii kinataka wigo wa sheria kuhusu haki ya kupata taarifa kuwa mpana sana. Kila mtu na sio raia pekee, afaidike na haki hii na kila mtu anayeomba taarifa hatakiwi kuelezea maslahi yoyote katika taarifa hiyo au sababu za kwa nini anaomba taarifa hizo. Taarifa zilizomo kwenye vyombo husika zinatakiwa kuelezewa kwa upana bila kujali namna, tarehe,

9 https://www.article19.org/resources.php/resource/3024/en/international-standards:-right-to-information Kama ilivyotembelewa tarehe 5 Desemba 2016.

Page 13: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

13

mtu aliyezitoa au kuandaa na kama ni za siri au la.10

Katika sheria hii ya Kupata Taarifa, hasa kifungu kifungu cha 5(1) & 5(4) kinaminya haki ya kupata taarifa kwa kuruhusu raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee kupata taarifa. Hii ni kinyume na kanuni za kimataifa na viwango vinavyokubalika katika haki ya upatikanaji wa taarifa.

Pia kuna kanuni inayohusu mazingira ambayo upatikanaji wa taarifa unaweza kuminywa. Kanuni hii inasema kuwa mazingira ambayo upatikanaji wa taarifa unaweza kuminywa yanatakiwa yawe machache na wigo usio mpana, hasa hasa yawe ni mazingira ambayo taarifa zinaweza kusababisha madhara au kulinda maslahi ya umma.” Uwekaji wa mazingira haya ni moja kati ya mambo magumu wanayokumbana nayo watungaji wa sheria za habari na ni moja kati ya maeneo yenye matatizo katika sheria nyingi zilizopo. Katika mifano mingi, sheria ambazo ni madhubuti zinaharibiwa kwa kuwa na mazingira ya uminywaji wa haki ambayo ni mapana au yasiyokuwa na mipaka. Kwa upande mwingine, ni muhimu pia kuhakikisha kuwa taarifa zote za siri zenye maslahi kwa taifa zinalindwa kisheria, vinginevyo vyombo vinaweza kutakiwa kutoa taarifa hizo hata kama hali hii itasababisha madhara.11

Nchi wanachama wanaweza kuweka mipaka katika upatikanaji wa taarifa zilizomo kwenye nyaraka rasmi. Hata hivyo mipaka hii ni lazima iwekwe kisheria, iwe ni ya lazima katika jamii ya kidemokrasia na kuwe na uwiano kati ya mpaka na lengo linalokusudiwa ili kulinda:

• Usalama wa Taifa, ulinzi na uhusiano wa kimataifa; • Usalama wa Umma; • Uzuiaji, uchunguzi na uendeshaji wa kesi dhidi ya vitendo

vya jinai; • Usiri na mambo mengine halali binafsi;10 https://www.article19.org/resources.php/resource/3024/en/international-standards:-right-to-information kama ilivyitembelewa tarehe 5 Desemba 2016.11 Inapatikana katika tovuti iliyotajwa hapo juu..

Page 14: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

1514

• Maslahi ya uchumi au biashara aidha ya binafsi au umma; • Usawa wa kuhusu mwenendo wa mahakama; • Asili; • Ukaguzi na usimamizi wa mamlaka za umma; • Sera za uchumi, fedha na Sera za viwango vya kubadilishia

fedha wa nchi; • Usiri wa majadiliano ndani ya mamlaka za umma wakati

wa uandaaji wa mambo mbalimbali.

Hata hivyo haiwezi kuwa halali kuzuia upatikanaji wa taarifa eti kisa tu zinahusiana na moja kati ya mambo hayo yaliyotajwa hapo juu. Kwa mujibu wa sheria, taarifa itazuiwa tu ikiwa inaweza kuleta madhara katika jambo hilo.

Sheria hii ya Kupata Taarifa inatoa mazingira mengi ambayo taarifa zinaweza kuzuiwa chini ya vifungu vya 6(1),(2) & (3). Baadhi ya mazingira ni sawa lakini mengine hayako sawa kwa mujibu wa kanuni za kimataifa. Mazingira mengine ni mapana sana na hivyo kuwa katika hatari ya kutumika vibaya. Kwa mfano, chini ya vifungu vya 6(1) (2) na (3) mtu mwenye taarifa anaweza kukataa kutoa taarifa, kama akiona kuwa, kwa mujibu wa sheria hii, utoaji wa taarifa hizo hautakiwi kwa maslahi ya umma. Sheria haitoi au kuelezea maana ya maslahi ya umma au kitu gani kinaweza kuwa ni masilahi ya umma. Huu ni wigo mpana sana ambao unaweza kutumika vibaya kuzuia baadhi ya taarifa. Pia, kuzuia upatikanaji wa taarifa zinahusiana na uhusiano wa nje kwa kigezo kuwa zinahusiana na usalama wa taifa, inaleta ukakasi na ni ngumu kueleweka.

Kanuni nyingine inahusiana na urahisishaji wa upatikanaji wa taarifa. Kanuni hii inatamka kwamba maombi ya taarifa ni lazima yashughulikiwe haraka na kwa haki pia ni lazima kuwe na chombo huru cha kupitia maombi yote yaliyokataliwa. Upatikanaji madhubuti wa taarifa unataka mambo mawili, kwanza sheria itoe mwongozo wa mchakato mzima wa kutolea maamuzi maombi ya taarifa na pili kuwe na mfumo huru wa kupitia maombi yaliyokataliwa.12 Kwa

12 https://www.article19.org/resources.php/resource/3024/en/international-standards:-right-to-

Page 15: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

15

kawaida maombi yanafanywa kwa maandishi, hata hivyo sheria lazima iweke namna nyingine ya kutuma maombi kwa watu ambao hawawezi kutuma kwa maandishi, kwa mfano vipofu au watu wasiojua kusoma na kuandika. Hii inaweza kufanyika kwa kuvitaka vyombo husika kuwasaidia katika kuweka maombi yao kwenye maandishi. Pia sheria lazima iweke muda maalum wa kushughulikia maombi ya taarifa, ambao unatakiwa kuwa mfupi iwezekanavyo. Majibu ya maombi lazima yawe katika notisi ya maandishi na ielezee ada kama imetozwa, kama taarifa zote au chache zimetolewa au kuzuiwa, sababu za zuio na taarifa nyingine kuhusu haki ya rufaa. Pia inapendekezwa kuwa sheria inatakiwa kuwapa waomba taarifa haki ya kuamua namna bora ya kupata taarifa, aidha kwa kukagua rekodi mbalimbali au kupewa nakala ya rekodi hizo.13

Mwisho, sheria itoe haki ya kukata rufaa kutoka kwa vyombo hivi kwenda mahakamani. Ni mahakama pekee yenye uwezo wa kuweka viwango vya utaoaji wa taarifa katika maeneo yenye utata na hivyo kuhakikisha kuwa kunakuwa na mfumo mzuri wa utoaji wa taarifa hizo.14

Mambo yanayohusiana na namna ya kushugulikia maombi ya taarifa na muda wa kufanya hivyo yameelezwa chini ya vifungu vya 11, 12, 13, na 14. Haki ya kukataa rufaa imeelezwa pia chini ya kifungu cha 19(4). Hata hivyo muda wa kushughulikia maombi chini ya sheria hii bado ni mrefu. Muda wa siku 30 ni mrefu ukizingatia kuwa baadhi ya taarifa zinaweza kuwa zinahitajika kwa matumizi ya haraka. Zaidi ya hayo, hii inakwenda kinyume na hali ya utoaji huduma kwa sasa kama ilivyoelezwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja (Client Service Charter) kati ya OfisiyaWaziriMkuu,TawalazaMikoanaSerikalizaMitaanawateja wake. Hii inasisitiza utoaji wa huduma kwa haraka.

Kanuni ya mwisho ni kuhusu ada inayotozwa kwenye maombi ya taarifa. Kanuni hii inataka kuwa gharama za kuomba taarifa

information kama ilivyotembelewa tarehe 5 Desemba 2016.13 https://www.article19.org/resources.php/resource/3024/en/international-standards:-right-to-information Kama ilivyotembelewa tarehe 5 Desemba 2016.14 Inapatikana katika tovuti iliyotajwa hapo juu.

Page 16: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

1716

zisiwe za juu sana na kufanya watu washindwe kuzimudu. Ada zinatakiwa kutokuwa kubwa kiasi kwamba watu washindwe kuzimudu, kwa kawaida sheria huwa zinaruhusu utozaji wa ada katika kutoa taarifa15. Lakini kila sheria inakuwa na namna ya kipekee ya utozaji wa ada hizo. Kuna sheria zinazotozaadakwakiwangochakufidia tugharamayakudurufu nyaraka za taarifa. Nyingine zinaweka ada ndogo kwa taarifa zenye maslahi ya umma au taarifa binafsi. Na nyingine zinaweka kikomo cha taarifa zinazoweza kupatikana bure, kwa mfano kurasa 100 za kwanza hutolewa bure, na ada huanza kutozwa kwa kurasa zinazozidi. Bila kujali namna sheria inavyotoza ada, kitu cha msingi ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na mamlaka inayoweka viwango vya ada ili kuleta usawa na sio kila mwenye taarifa kuachwa aamue kiwango cha ada atakachotoza.16

Kifungu cha 21 cha sheria hii ya Kupata Taarifa kinazungumzia ada ya upatikanaji wa taarifa, hata hivyo kifungu hakihitaji kiwango cha ada kitakachotozwa au namna ada hiyo itakavyotozwa. Kwa lugha nyingine, mwenye taarifa amepewa uwezo wa kuamua kiwango cha ada atakachotoza. Hii ni kinyume na viwango vinavyokubalika.

Angalizo: Kama ilivyoonekana katika uchambuzi hapo juu, baadhi ya vifungu vya sheria hii havikidhi viwango na namna bora ya upatikanaji wa taarifa. Kuna vipingamizi visivyokuwa na lazima kwenye haki ya kupata habari kinyume na/au chini ya kiwango kinachokubalika kimataifa.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Haki ya kupata taarifa inatamkwa katika Ibara ya 18 (1) na (2). Ibara hii inatamka kuwa kila mtu ana haki ya kutafuta na kupokea taarifa. Kwa mantiki hiyo sheria ya Kupata Taarifa ni lazima iipe nguvu kusudio la Ibara hii ya Katiba kwa kutengeza mazingira ambayo watu wanaweza kupata taarifa pasipo kuwa na ubaguzi wowote.

15 Inapatikana katika tovuti iliyotajwa hapo juu.16 Inapatikana katika tovuti iliyotajwa hapo juu.

Page 17: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

17

Kama tulivyoona hapo juu, kifungu cha 5(1) na (4) cha sheria ya Kupata Taarifa kinaminya haki hii kwa kuruhusu raia pekee kupata taarifa. Watu wasio raia wamezuiwa kupata taarifa chini ya sheria hii. Hii ni kinyume na ibara ya 18 ya Katiba. Hivyo inatosha kabisa kusema kuwa kifungu cha 5(1) na (4) cha sheria hii ipo kinyume na Katiba. Kwa hiyo inapendekezwa kuwa kifungu hiki kinaweza kupingwa mahakamani kwa kukiuka Katiba.

Pia ni muhimu kuangalia namna bora ya upatikanaji wa habari kutoka nchi mbalimbali duniani. Hii inafanywa kwa lengo la kutambua mapungufu yaliyopo chini ya sheria hii ya Upatikanaji wa Habari kwa kulinganisha namna sheria hii inavyotoa haki ya upatikanaji wa habari na kile kinachofanywa katika nchi nyingine zilizofanya vizuri katika nyanja hiyo.

Namna bora ya kuhakikisha upatikanaji wa taarifa inaonesha kuwa sheria nyingi za upatikanaji wa taarifa zinaunda chombo cha usimamizi wa utekelezwaji wa sheria hiyo. Hii inaweza kuwa tume huru,AfisaMlinziwa Takwimu/Taarifa auMsimamizi Maalum. Sababu za kuanzishwa kwa vyombo hivi ni kukuza haki ya upatikanaji wa taarifa na pia kusikiliza rufaa dhidi ya ukiukwaji wa haki hii.

Kwa mfano katika nchi za Sweden, Norway na New Zealand, Sheria za Kupata taarifa zinampa msimamizi maalum haki ya kusimamia utekelezwaji wa haki ya kupata taarifa. Maana yaMsimamizimaalumniafisaanayeteuliwakuchunguzamalalamiko ya watu dhidi ya vitendo vya ukiukwaji wa sheria unaofanywanamaafisawaummaauvyombovyaumma.Inaripotiwa kuwa mfumo huu wa kutumia msimamizi maalum ni kati ya mifumo inayofanya kazi vizuri ulimwenguni, hasa katika usimamizi wa sheria.

Nchini Afrika ya Kusini, Tume ya Haki za Binadamu imepewa jukumu la kusimamia utekelezwaji wa haki ya upatikanaji wataarifa.MaafisawaHabariwanatakiwakupelekaripotikila mwaka kwenye Tume ya Haki ya Binadamu.17 Kati ya mambo wanayotakiwa kuripoti ni idadi ya maombi ya

17 Soma kifungu cha 38 cha Sheria ya Kukuza Haki ya Kupata Habari, ya mwaka 2000.

Page 18: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

1918

taarifa waliyopokea, idadi ya maombi yaliyokubaliwa, idadi ya maombi yaliyokataliwa pamoja na rufaa. Pia, Tume ya Haki za Binadamu inatakiwa kupeleka ripoti bungeni kila mwakakuhusutaarifahizoinazopokeakutokakwamaafisawa habari.18 Kwa kifupi, sheria ya Kupata Taarifa ya nchini Afrika ya Kusini inaweka mfumo wa usimamizi wa kuhakikisha kila kifungu cha sheria kinatekelezwa. Mfumo wa namna hii unakosekana katika sheria yetu ya Kupata Taarifa.

Zaidi ya hayo, Sheria ya Kupata Taarifa ya Afrika ya Kusini inaruhusu upatikanaji wa taarifa kutoka katika vyombo binafsi au watu binafsi ikiwa taarifa hizo zinahitajika kwa ajili ya upatikanaji au ulinzi wa haki yoyote.19 Hii ni namna bora kabisa ya upatikanaji wa taarifa, ambayo sheria yetu ya upatikanaji wa habari ilitakiwa kuwa nayo.

Jambo zuri zaidi, Sheria hii ya Afrika ya Kusini ina kifungu kinachoipa ukuu dhidi ya sheria nyingine yoyote inayozuia upatikanaji wa taarifa. Ni bahati mbaya kuwa sheria yetu ya Kupata Taarifa haina kifungu kama hicho. Hii ni hatari ukizingatia kuwa baadhi ya wenye taarifa wanaweza kutumia vifungu vya sheria nyingine kuminya au kuzuia upatikanaji wa taarifa fulani. Pia, sheria hii ya Afrika ya Kusini ina kifungu kinachotamka wazi kuwa wakati wa kuomba taarifa, mwombaji hatawajibika kutoa sababu za kuomba taarifa hizo. Kifungu cha namna hii hakipo katika sheria Kupata Taarifa ya 2016. Kwa maneno mengine, sheria yetu iko kimya kuhusu jambo hili.

Nchi nyingine inayoweza kuwa mfano bora ni Uingereza. Uingereza kuna Kamishna wa Habari na Baraza la Habari (Information Tribunal) kwa ajili ya kusimamia utekelezwaji wa haki ya kupata taarifa. Zaidi ya hapo, Katibu wa Nchi, Jaji Mkuu na Kamishina wamepewa kazi ya kusaidia mamlaka za umma katika utekelezaji wa majukumu yao chini ya sheria ya Kupata Taarifa. Kwa mfano, Katibu wa nchi na Jaji Mkuu

18 Soma kifungu cha 84, cha sheria iliyotajwa hapo juu.19 Soma kifungu cha 50, cha sheria iliyotajwa hapo juu.

Page 19: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

19

wanatkiwa kutoa mwongozo wa namna bora ya mamlaka za umma kutekeleza majukumu yao chini ya sheria.20 Muhimu zaidi, chini ya kifungu cha 49 cha sheria hiyo, Kamishina anatakiwa kupeleka ripoti bungeni kuhusu utekelezaji wa majukumu yake chini ya sheria hii.

Nchi nyingine inayoweza kuwa mfano bora ni India. India ina Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa ya mwaka 2005. Sheria hii inaanzisha Tume mbili za kusimamia utekelezwaji wa sheria hii. Tume hizi ni Tume Kuu ya Habari na Tume ya Habari ya Majimbo.21 Kwa ujumla, tume hizi zinapokea malalamiko ya watu walioomba taarifa kutoka katika vyombo mbalimbali vya umma.22 Pia, tume hizi zinatakiwa kutoa ripoti kila mwaka kwa serikali husika kuhusu utekelezwaji wa haki ya kupata taarifa.23

Tunachoweza kujifunza kutoka katika mifano ya namna bora ya upatikanaji wa taarifa katika nchi hizi ni kuwa kuna haja ya kuwa na vyombo maalum vya usimamizi wa utekelezwaji wa sheria ya Kupata Taarifa. Pia, vyombo hivi vinaweza kupokea na kuamua malalamiko mbalimbali yanayohusiana na upatikanaji wa taarifa. Ni bahati mbaya sana kuwa sheria yetu haijaanzisha chombo chochote cha usimamizi. Jambo jingine ni kuwa hata mfumo wa kushughulikia malalamiko ulioanzishwa chini ya sheria yetu haukidhi viwango vinavyokubalika. Ilitakiwa kuwe na vyombo huru vya kufanya shughuli hiyo kama vile ilivyo India. Utoaji wa ripoti kuhusu utekelezwaji wa sheria ni jambo muhimu katika kuhakikisha utekelezwaji madhubuti wa sheria. Kuna haja ya kuwa na kifungu kinachowataka wenye taarifa kuripoti bungeni au kwenye chombo kingine chochote huru.

20 Soma kifungu cha 45 and 46, cha sheria iliyotajwa hapo juu.21 Zinaanzishwa na vifungu vya 12 na 13 vya Sheria ya Habari ya Mwaka 2005.22 Kifungu cha 18, cha sheria iliyotajwa hapo juu.23 Kifungu cha 25, cha sheria iliyotajwa hapo juu.

Page 20: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

2120

3. Sheria ya Kupata Taarifa ya Mwaka 2016 na Sera ya Habari na Utangazaji ya Mwaka 2003 na Mpango wa Uwazi Serikalini.

Sera ya Habari na Utangazaji ya Mwaka 2003, inataka uondoaji wa vikwazo katika upatikanaji wa taarifa. Kwa mfano, maelezo ya sera chini ya Aya ya 2.4.1 inatamka wazi kuwa ina lengo la kuondoa vikwazo vya upatikanaji wa taarifa kutoka serikalini na taasisi zake. Sera hii pia inaitaka serikali kuhakikisha inaondoa vikwazo vya upatikanaji wa taarifa katika taasisi zake. Pia, wajibu huu wa serikali unarudiwa tena kwenye maelezo ya sera chini ya Aya za 2.4.2 and 2.1.1. Kiujumla Serikali inatakiwa kuondoa vikwazo vyote vinavyozuia upatikanaji wa taarifa na kuhakikisha kuwa watu wanapata taarifa bila vikwazo. Hata hivyo ukiangalia vifungu vya sheriahii,utaonawazikuwalengohililakiserahalijafikiwaipasavyo. Hii ni kwa sababu sheria hii ina baadhi ya vifungu ambavyo vinaweza kuwa kikwazo katika upatikanaji wa habari. vifungu kama vile vinavyotoza ada katika upatikanaji wa habari, kuweka mazingira mapana ya uminyaji au uzuiaji wa taarifa fulani. Kwa ujumla vifungu hivi ni vikwazo kwa wananchi katika kupata haki yao ya kupata habari.24

Kuhusiana na mpango wa uwazi serikalini (Open Government Partnership (OGP), Tanzania ilijiunga na mpango huu Septemba mwaka 2011. Lengo lilikua ni kufanya shughuli za serikali kuwa wazi zaidi kwa wananchi na hivyo kuboresha utoaji wa huduma, ushughulikiaji wa mambo mbalimbali, kupambana na rushwa na kujenga imani kwa wananchi. Kama ilivyoelezewa katika mpango wa uwazi serikalini wa Tanzania wa mwaka 2012/2013, juhudi za serikali zimeelekezwa katika maeneo muhimu manne nayo ni uwazi, uwajibikaji, ushirikishwaji wa wananchi na teknolojia na ubunifu. 25.

24 Soma maelezo ya sera chini ya Aya ya 2.1.1, 2.4.1 na 2.4.2 ya Sera ya Habari na Utangazaji ya mwaka 2003.

25 Tembelea http://www.opengovpartnership.org/country/tanzania kama ilivyotembelewa tarehe 4

Page 21: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

21

Katika uwazi, lengo ni kuboresha tovuti mbalimbali za serikali ili kuwawezesha wananchi kupata taarifa kwa haraka na bure. Pia bajeti za wananchi zitolewe katika lugha rahisi na inayoeleweka. Lengo likiwa kuwafanya wananchi waelewe bajeti ya Taifa.26

Kwa sasa Tanzania ina mpango mpya wa uwazi serikalini wa mwaka 2014-2016. Chini ya Aya ya 3.1 ya mpango kazi huu wa uwazi serikalini 2014-2016, inatamkwa wazi kuwa uhuru wa kupata taarifa ni nguzo muhimu kwa serikali yenye uwazi na haki ya demokrasia. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inaitambua haki hii, lakini hakuna sheria inayoipa uhai au kuelezea zaidi haki hii. Katika kutekeleza jambo hilo, Tanzania iliaidi kutunga sheria yakupatataarifaifikapoDesemba2014.(Hatahivyosheriahiihaikuweza kutungwa mwaka 2014 na badala yake ilitungwa na kupitishwa mwaka 2016 ).

Mpango wa uwazi serikalini unaenda mbali zaidi na kutamka kuwa sheria ya Kupata Taarifa itatungwa kulingana na viwango vya kimataifa na itakuwa na mambo yafuatayo:-

(i) Utambuzi wa haki za binadamu wa kupata taarifa pamoja na dhahania ya uwazi wa taarifa zilizoko kwenye vyombo vya umma yakiwemo makampuni au mashirika yanayomilikiwa na serikali, vyombo binafsi vinavyofanya kazi za umma au kutumia pesa za umma;

Sheria ya Kupata Taarifa ya Mwaka 2016 inatimiza masharti haya chini ya kifungu cha 2(2) ambacho kinaruhusu upatikanaji wa taarifa zilizoko kwenye vyombo vya umma au binafsi vinavyotumia pesa za umma.

Desemba 2016.26 Tembelea http://www.opengovpartnership.org/country/tanzania kama

ilivyotembelewa tarehe 4 Desemba 2016.

Page 22: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

2322

(ii) Wajibu wa kuchapisha taarifa mara kwa mara;

Hii inaelezewa chini ya kifungu cha 9 cha sheria, ingawaje wigo wa taarifa zinazotakiwa kuchapishwa ni mdogo sana.

(iii) Mwenendo madhubuti wa uombaji na ushughulikiaji wa maombi ya taarifa ambao ni rahisi, bure na wa haraka (Ukiwa na muda maalumu wa kushughulikia maombi).

Mwenendo huu unaelezewa katika vifungu vya 10, 11,12,13,14,15,16,17, 18 na 19 vya sheria. Ingawaje kuna upungufu, mwenendo mzima uko sawa kama inavyotakiwa na mpango wa uwazi serikalini.

(iv) Mazingira machache yanayoruhusu uminywaji wa taarifa ili kuzuia madhara, kulinda usalama na maslahi ya umma;

Hii inatamkwa chini ya kifungu cha 6 cha sheria. Kifungu cha 6(2) & (3) kinatoa mazingira ambayo taarifa zinaweza kuminywa au kuzuiwa. Ingawaje wigo wa mazingira haya sio mpana sana ila kuna mazingira mengine yako chini ya kiwango kinachokubalika. Kwa mfano kuweka taarifa zinazohusu uhusiano na nchi za nje au shughuli za nje kama ni taarifa za usalama inakosa mantiki. Kuna haja ya kuweka sawa mazingira ya uminyaji wa taarifa, kwa mfano kifungu kingewekwa kuwa taarifa hizo zitazuiwa iwapo zinahusiana na usalama wa taifa lakini sio kuzizuia kijumla. Uzuiaji huu wa jumla unawanyima haki wananchi kujua au kupata taarifa kuhusu serikali yao.

(v) Haki ya Kukata Rufaa

Hii inatamkwa chini ya kifungu cha 19(4) cha sheria. Kifungu hiki kinampa mtu haki ya kukata rufaa katika Mahakama Kuu.

Page 23: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

23

(vi) Ulinzi dhidi ya uvujishaji au utoaji wa taarifa kwa nia nzuri na adhabu dhidi ya kuzuia upatikanaji wa taarifa;

Hii inaelezewa chini ya kifungu cha 23(1) na (2) cha sheria hii. Kifungu hiki kinatoa kinga ya mashitaka dhidi ya utoaji wa taarifajuuyamambomaovu.Adhabudhidiyaafisaanayezuiaupatikanaji wa taarifa inatolewa chini ya kifungu cha 22, ingawaje adhabu hizi ni kwa ajili ya mtu mwingine atakayezuia utoaji wa taarifa na sio mwenye taarifa mwenyewe.

(vii) Wajibu wa kuripoti maombi ya taarifa yaliyopokelewa pamoja na adhabu za kukataa kutoa taarifa pasipo kuwa na sababu zinazokubalika.

Hili halijazungumziwa katika sheria hii. Hakuna kifungu chochote kinachomtaka mwenye taarifa kutoa ripoti ya maombi aliyopokea vile vile hamna kifungu kinachotamka adhabu zinazohusina na kukataa kutoa taarifa pasipokuwa na sababu zinazokubalika.

Mpaka hapa tunaweza kusema kuwa kwa kiwango kikubwa sheria hii ya Upatikanaji wa Habari imeendana na mpango wa uwazi serikalini. Hata hivyo kuna baadhi ya mambo ambayo sheria haijayaelezea sawa sawa kama uchambuzi unavyoonesha hapo juu.

1. Mlinganisho kati ya Mapendekezo ya Wadau kwenye Muswada wa 2011, na Mapendekezo ya CoRI na Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa, 2016.

Mwaka 2011, wadau wa habari walitoa mapendekezo ya Muswada juu ya mambo wanayotaka yaingizwe kwenye Muswada wa Haki ya Kupata Taarifa wa mwaka 2011. Mswada huo wa mapendekezo ulikua na sehemu saba na vifungu 44.

Kiujumla, mapendekezo ya wadau kwenye Mswada wa Haki ya Kupata Taarifa wa mwaka 2011 hayakuzingatiwa kwa kiasi kikubwa hasa katika sheria ya Haki ya Kupata Taarifa 2016. Vifungu vichache sana vimechukuliwa na

Page 24: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

2524

hata hivyo vimefanyiwa marekebisho kwa kupunguzwa baadhi ya mambo. Kwa mfano mapendekezo yafuatayo yameakisiwa ndani ya Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa ya mwaka 2016:-

Upatikanaji wa taarifa kutoka katika vyombo vya umma na binafsi kama ilivyotamka katika kifungu cha 8(1) cha mapendekezo kimeakisiwa ndani ya kifungu cha 2(2) cha Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa lakini kimerekebishwa kidogo. Chini ya sheria hii, vyombo binafsi vyenye wajibu wa kutoa taarifa ni vile tu vinavyotumia pesa za umma na si vinginevyo.

Pia wajibu wa kuchapisha taarifa kama ilivyotamkwa chini ya kifungu cha 12 cha Muswada wa mapendekezo kimechukuliwa ndani ya kifungu cha 9 cha sheria ya Haki ya Kupata Taarifa. Hata hivyo, wakati Muswada wa mapendekezo ulitaka uchapishwaji wa taarifa ufanywe ndani ya kipindi cha miezi 12, Sheria hii inataka uchapishwaji ufanywe ndani ya kipindi cha miezi 36. Pia, Muswada ulitaka lugha ya uchapishwaji wa taarifa iwe ni Kiswahili lakini sheria ya Haki ya Kupata Taarifa ya 2016, haina kipengele cha lugha ya uchapishwaji wa taarifa. Kwa kifupi haizungumzii lugha ya kuchapisha taarifa hizo.

Vifungu vya 37 na 38 vya Muswada ambavyo vinalinda watoa taarifa za maovu kwa nia njema zimechukuliwa kiasi katika kifungu cha 23 an 24 cha sheria ya Haki ya Kupata Taarifa ambavyo navyo vinalinda watoa taarifa za maovu kwa nia njema.

Kama ilivyotanguliwa kusemwa hapo awali, sheria hii haikuchukua mapendekezo mengi ya wadau. Kwa mfano hakuna Tume ya Habari kama ilivyopendekezwa katika vifungu vya 21, 22, 23, 24, 25, 26, 27, 28, 29, 30, 31, 32 vya mapendekezo ya wadau. Pia, kama Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI) ulivyopendekeza chini ya kifungu cha 42 cha Muswada wa mapendekezo yao, pia halijaanzishwa.

Page 25: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

25

Kwa hiyo, tunaweza kusema kuwa kwa kiwango kikubwa mapendekezo ya wadau wa habari hayajachuliwa katika Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa ya mwaka 2016. Vifungu vichache vimechukuliwa na kufanyiwa mabadilliko kidogo.

Kuhusu mapendekezo ya CoRI bado hali ni ile ile. Mapendekezo mengi ya CoRI hayajachukuliwa na yale machache yaliyochukuliwa yamefanyiwa marekebisho. Kwa mfano mapendekezo kuwa kifungu cha 6(6) cha Sheria ya Haki ya kupata Taarifa kitoe kikomo cha juu cha adhabu ya kifungo kimechukuliwa. Hata hivyo pendekezo la kuwa faini iwekwe kama adhabu mbadala haijachukuliwa.

Mapendekezo juu ya kifungu cha 18(1) ambacho kilikua kinazuia matumizi ya taarifa za umma, kimefanyiwa marekebeisho na sasa sio kosa la jinai kutumia taarifa hizo kwa umma, hata hivyo kifungu hicho kinaazisha kosa jipya la upotoshaji wa taarifa. Zaidi, mapendekezo kuwa mwenye taarifa atoe notisi au ashughulikie maombi ndani ya muda uliopangwa yamechukuliwa chini ya kifungu cha 11(1) cha sheria hii. Bila kuathiri kilichozungumzwa hapo juu, mapendekezo mengi mazuri ya CoRI hayakuchukuliwa, kwa mfano kifungu cha 21 kinaendelea kuweka gharama za kupata taarifa, hakuna muda wa kuanza kwa matumzi ya sheria hii chini ya kifungu cha 1 kama ilivyopendekezwa. Upatikanaji wa taarifa umeminywa kwa watu wasio raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya kifungu cha 5(4). Mbaya zaidi, kuna mazingira mapana ya uzuiaji wa taarifa chini ya kifungu cha 6(2) kinyume na mapendekezo ya CoRI.

2. Upungufu na Udhaifu wa Sheria hii Baada ya uchambuzi wa kina wa vifungu vya sheria hii, kuna

upungufu na udhaifu ambao umegundulika kama ifuatavyo:-

5.1 Upatikanaji wa Habari

Kifungu cha 5(1) kinasema kuwa kila mtu atakuwa na haki

Page 26: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

2726

ya kupata taarifa. Hata hivyo kifungu cha 5(4) kinaminya maana ya MTU na kumaanisha raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hii inamaainsha kwamba watu ambao sio raia hawawezi kupata taarifa. Pili, watu kwa mujibu wa kisheria kama vile makampuni, mashirika, asasi, na mashirika ya kimataifa hawawezi kupata taarifa kwa sababu hawaingii chini ya maana ya raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pendekezo: Kifungu kifanyiwe mabadiliko. Maana ya neno MTU limaanishe watu wote wa asili na wa kishera bila kuweka mipaka kwenye uraia au kama mbadala neno mtu libadilishwe na neno kila mmoja au kila mtu.

5.2 Wajibu wa Kuchapisha Taarifa

Kifungu cha 9(1) (a) (b) na (c) kinaweka wajibu kwa mwenye taarifa kuchapisha baadhi ya taarifa ndani ya kipinmdi cha miezi 36 baada ya sheria kuanza kufanya kazi. Mwenye taarifa anatakiwa kuchapisha muundo wake na kazi zake anazofanyaikiwemokazizamaofisawakeaukamatizaushauri, pamoja na maelezo ya jumla ya taarifa zote zilizoko chini yake.

Pia, kifungu hiki hakizungumzii wajibu wa kuchapisha taarifa kila baada ya kipindi fulani. Kifungu hiki kilitakiwa kitoe wajibu wa kuchapisha taarifa kila baada ya muda fulani, kwa mfano kila baada ya mwaka. Kifungu hakijatoa mwongozo juu ya lugha ya kuchapisha taarifa hizo. Kifungu hiki kilitakiwa kiyatamke haya yote kwa uwazi.

Pendekezo: Kifungu kifanyiwe mabadiliko ili kuongeza wigo wa taarifa zinazotakiwa kuchapishwa kujumuisha bajeti, mipango ya kifedha na mikataba ya watu mbalimbali. Pia, kifungu kiweke wajibu wa kuchapisha taarifa hizo kwa vipindi maalum na kwa lugha ya Kiswahili ili watu wengi wapate kuelewa.

Page 27: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

27

5.3 Muda wa Kushughulikia Maombi

Kifungu hiki kinatamka kuwa wakati taarifa zitakapoombwa, mwenye taarifa, atawajibika haraka iwezekanavyo lakini katika kipindi kisichozidi siku 30 kumtaarifu mwombaji kama taarifa alizoomba zipo na anaweza kuzipata kama upatikanaji wake unaruhusiwa. Kikomo cha siku 30 ni kikubwa sana ukizingatia kuwa kuna taarifa zinahitajika kwa matumzi ya haraka. Tatizo kubwa linaloweza kujitokeza kwa uwekaji wa kikomo cha siku thelathini ni baadhi ya wenye taarifa kuchukulia muda huu kama ni muda wa kawaida ambao maombi yanabidi yashughulikiwe na hivyo kuchelewesha utoaji wa taarifa. Sheria ingeweka muda mfupi zaidi ili kuhakikisha kuwa maombi ya taarifa yanashughulikiwa kwa haraka.

Pendekezo: Kifungu kifanyiwe marekebisho kwa kuweka muda mfupi zaidi wa kushughulikia maombi vinginevyo baadhi ya wenye taarifa wanaweza kuzembea au kuwa wavivu katika kushughulikia maombi kwa kigezo kuwa muda uliowekwa kisheria bado haujakwisha.

5.4 Uzuiaji wa Muda wa Upatikanaji Taarifa

Kifungu hiki kinampa mwenye taarifa uwezo wa kuzuia kwa muda upatikanaji wa taarifa mpaka litokee tukio fulani wakati atakapoona inafaa kufanya kwa mujibu wa maslahi ya umma au kwa sababu madhubuti za kiutawala.Kifungu hiki ni kipana sana na kinaweza kutumiwa vibaya na wenye taarifa. Namna bora ilikua ni kuweka kikomo cha uzuiaji huo, kwa mfano miezi mitatau n.k.

Pendekezo: Kifungu kifanyiwe marekebisho ili kuweka muda wa uzuiaji wa upatikanaji wa taarifa, vinginevyo kifungu hiki kinaweza kutumika kunyima upatikanaji wa aina fulani ya taarifa.

Page 28: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

2928

5.5 Matumizi ya Taarifa

Kifungu hiki kinaanzisha kosa la kuharibu taarifa. Kifungu hiki kinaelezea kuwa mtu yoyote atakayepokea taarifa kutoka kwa mwenye taarifa hatakiwi kuharibu taarifa hizo.Kama mtu akiharibu taarifa hizo atakua anafanya kosa la jinai. Kifungu hakisemi kuharibu taarifa hizo kwa nia au lengo gani. Ni maoni yetu kuwa kifungu hiki ni kipana sana na kina weza kuwa na tafsiri nyingi.

Pendekezo: Kifungu kifanyiwe marekebisho ili kitamke sababu za kuharibu taarifa hizo. Kwa mfano kinaweza kusema kuwa ni kosa la jinai kuharibu taarifa kwa lengo la kuudanganya au kuupotosha umma n.k.

5.6 Marejeo ya Maamuzi

Kifungu cha 19(1) kinazungumzia marejeo ya maamuzi ya mwenye taarifa kukataa kutoa taarifa. Mtu asiyeridhishwa na maamuzi hayo anaweza kuomba marejeo kwa mkuu wa taasisi husika. Wakati mwenendo wa marejeo haya uko sawa kwa kiasi kikubwa, lakini tatizo linaweza kujitokeza pale mtu anaposoma kifungu cha 7(3) cha sheria hii. Kwa mujibu wa kifungu hiki, kama mkuu wa taasisi atashindwa kumteuaafisahabari,yeyemwenyeweatawajibikakufanyakazikamaafisahabari.Sasa,katikamazingiraambayomkuuwataasisiatafanyakazikamaafisahabari,kifungucha19(1)kinapoteza lengo lake, kwa maana lengo la watungaji wa sheria hii ilikua ni kumpa nafasi mtu wa juu zaidi kupitia maamuzi ya mtu wa chini aliyekataa kutoa taarifa.

Pendekezo: Kifungu kifanyiwe marekebisho na kutamka wazi kuwa katika mazingira ambayo mkuu wa taasisi atafanyakazikamaafisahabaribasimaombiyamarejeoyamaamuzi yafanywe kwa waziri husika.

Page 29: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

29

5.7 Ada za Upatikanaji wa Taarifa

Kifungu cha 21 kinatamka wazi kuwa mwenye taarifa anaweza kutoza ada kwa ajili ya kutoa taarifa. Kifungu hakiweki kikomo cha ada hiyo na wala hakitoi mwongozo juu ya utozwaji au ukokotoaji wa ada hiyo. Namna bora inaonesha kwamba sheria inatakiwa kutoza ada inayolingana na gharama za utaoaji wa taarifa hizo. Kwa kawaida kuna idadi ya kurasa ambazo zinatakiwa kutolewa bure, pia haiwezi kuwa sawa kutoza ada kwa taarifa zilizoombwa kwa njia ya barua pepe. Kifungu hiki kikiachwa kama kilivyo, baadhi ya wenye taarifa wanaweza kugeuza jambo hili kama chanzo mbadala cha mapato.

Pendekezo: Kifungu hiki kifanyiwe marekebisho na kuweka kikomo cha ada inayoweza kutozwa. Ada iwe ni kwa ajili yakufidiagharamazautoajiwataarifa.Piakifunguhichokitamke wazi kuwa Waziri atatunga kanuni za namna ada hii itakavyotozwa ili kuleta usawa na sio kila mwenye taarifa kuamua kutoza ada kwa kiwango chake.

5.8 Kutaja Sababu za Maombi ya Taarifa

Hakuna kifungu katika sheria hii kinachozuia mtu anayeomba taarifa asilazimike kutoa sababu za maombi hayo. Sheria inatamka tu kuwa maombi ya taarifa yatafanywa kwa kujaza fomu maalumu. Fomu hii itakuwa kwenye kanuni zitakazotungwa na waziri na hivyo kuna uwezekano wa kuwa na kipengele kinachomtaka mwomba taarifa kutoa sababu za maombi hayo.

Pendekezo: Sheria ifanyiwe marekebisho na kuwa na kifungu kinachotamka wazi kuwa mwomba taarifa hatatakiwa kutaja sababu za kuomba taarifa hizo. Jambo hili ni lazima liwekwe kisheria na si kuachwa kwenye mikono ya wenye taarifa kuamua kwa mujibu wa utashi wao.

Page 30: KUPAT AARIF 20164 5 hivi ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha haki ya kupata taarifa inapatikana bila vikwazo vyovyote. Zaidi ya hayo, Sheria hii pia imeshindwa kuipa nguvu

3130

3. Mapendekezo Muhimu ❑ Sheria ifanyiwe marekebisho ili kuruhusu kila mtu, raia

na wasio raia, pamoja na makampuni/taasisi/mashirika kupata taarifa.

❑ Sheria ifanyiwe marekebisho na kuwekwa kifungu kitakachohakikisha kuwa upatikanaji wa taarifa unakuwa kwa gharama ndogo au katika baadhi ya mazingira iwe ni bure.

❑ Mwenendo wa marejeo chini ya kifungu cha 19(1) ufanyiwe marekebisho kwa kutambua uwezekano wa kuomba marejeo moja kwa moja kwa waziri katika mazingira ambayo mkuu wataasisiatakuwapiakamaafisahabariwataasisikwamujibu wa kifungu cha 7(3) cha sheria.

❑ Sheria ifanyiwe marekebisho ili kuweka kikomo cha muda wa zuio la muda la upatikanaji wa taarifa chini ya kifungu cha 16 cha sheria.

❑ Sheria ifanyiwe marekebisho kuongeza wigo wa taarifa zinazotakiwa kuchapishwa chini ya kifungu cha 9(1) kujumuisha bajeti au mipango ya kifedha, mikataba na watu wengine n.k. Hii itaongeza kiwango cha uwazi serikalini.

❑ Sheria ifanyiwe marekebisho ili kuweka kifungu kinachotaka watu wote wanoomba taarifa wasitakiwe kutoa sababu za kuomba taarifa hizo.

❑ Wadau wanaweza kwenda mahakamani kupinga baadhi ya vifungu vya sheria hii ambavyo vinakiuka Ibara ya 18 ya Katika ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotoa haki ya kila mtu kutafuta, kupata na kutoa taarifa .

4. Hitimisho Japokuwa vifungu vingi vya sheria hii viko sawa, kuna baadhi

ya vifungu ambavyo vinazuia haki hii ya kupata taarifa. Sheria hii kama ilivyo, inanyima haki ya kupata taarifa kwa watu