50
Mkusanyiko wa vifaa kwa mazingira yenye changamoto: Kupeleka utengenezaji mashuleni

Kupeleka utengenezaji mashuleni

  • Upload
    ubcedo

  • View
    429

  • Download
    14

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Shukrani kwa msaada kutoka Senta ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (SKUM) Msaada wa Mabadilishano katika Utafiti kwa Kanada na Afrika (MUKA) kuwa na uwezo wa kusanifu na kufanyia jaribio njia ya maendeleo ya kitaaluma kuwasaidia walimu kurekebisha ufanyaji kazi wao. Kupeleka Utengenezaji Mashuleni: Mkusanyiko wa Vifaa kwa Ajili ya Ugunduzi na Mabadiliko Katika kufundisha na Kujifunza ni matokeo ya kazi ya (MUKA) iliyopatiwa msaada.

Citation preview

Mkusanyiko  wa  vifaa  kwa  mazingira  yenye  changamoto:  

Kupeleka  utengenezaji    mashuleni  

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     2  

Kupeleka  utengenezaji  mashuleni:  Mkusanyiko  wa  vifaa  kwa  ajili  ya  ugunduzi  na  mabadiliko  katika  kufundisha  na  kujifunza  imeandaliwa  na  

Dkt.  Susan  Crichton  na  Dkt.  Lilian  Vikiru      

1

Shukrani  2015    Msaada  wa  Mabadilishano  katika  Utafiti  wa  Kikanada  na  Kiafrika  –  Senta  ya  Kimataifaya  ya  Utafiti  wa  Maendeleo  (SKUM)      Senta  ya  Ugunduzi  Katika  Kujifunza  –  Kitivo  cha  Elimu  |  UBC  Okanagan    Chuo  Kikuu  cha  Aga  Khan  –  Taasisi  ya  Maendeleo  ya  Elimu,  Afrika  ya  Mashariki  (CKAK-­‐TME,  AM)                    

2

Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni:  Mkusanyiko  wa  Vifaa  kwa  ajili  ya  Ugunduzi  na  Mabadiliko  katika  Kufundisha  na  Kujifunza    imeandaliwa  na  Dkt.  Susan  Crichton  na  Dkt.  Lilian  Vikiru  chini  ya  leseni  ya  Creative  Commons  Attribution-­‐NonCommercial  4.0  International  License.  CC  licensing  information:  http://creativecommons.org/licenses/by-­‐nc-­‐sa/4.0/deed.en_CA      

   Imetokana  na:    Siku  ya  Kutengeneza  Mkusanyiko  wa  Vifaa  na  Dkt.  Susan  Crichton  na  Deb  Carter,  PhD  (c)  ipo  chini  ya  leseni  ya  a  Creative  Commons  Attribution-­‐NonCommercial-­‐ShareAlike  4.0  International  License.      CC  licensing  information:  http://creativecommons.org/licenses/by-­‐nc-­‐sa/4.0/deed.en_CA    Based  on  a  work  at  http://innovativelearningcentre.ca/our-­‐space/maker-­‐days/  and    http://innovativelearningcentre.ca/careg-­‐project-­‐page/          

Dkt.  Susan  Crichton   Dkt.  Lilian  Vikiru  

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     3  

Karibu  

1

Walimu  wote  mara  nyingi  wamekuwa  wakihaingaika  kubadili  hata  jambo  muhimu  sana  katika  ufundishaji  wao  darasani.  Huu  ni  uhalisia  hasa  kwa  wale  walio  katika  mazingira  yenye  changamoto  ambapo  walimu  wengi  wanafundisha  kwa  namna  walivyofundishwa  wao-­‐mara  nyingi  hutumia  “akili  isiyowezatafsiri  dhana/kujenga  maana”  matendo  ambayo  mwalimu  ni  kitovu  cha  maarifa,  ufundishaji  wa  kukariri/kurudiarudia.      Tunatumia  neno  mazingira  yenye  changamoto,  kuliko  nchi  zinazoendelea  au  mazingira  ya  nchi  za  ulimwengu  wa  tatu,  kama  njia  ya  kuelezea  mahali  ambapo  mtu  mmoja  mmoja  na  vikwazo  au  anapata  kwa  nadra  au  hapati  huduma  za  kisasa  kama  vile  umeme,  maji,  afya,  simu,  mtandao  na  teknolojia  zinazohusiana  na  hizo  zinazoibuka  kutokana  na  hali  anuai  au  vikwazo  vya  kimazingira.      Tunatambua  kuwa  changamoto  za  kimazingira  zinatokea  duniani  kote,  inatofautiana  tu  katika  ukubwa  wake,  mambo  yanayosababisha,  muda  wake,  Jiografia  na  kudumu  kwake.  Walimu  katika  mazingira  ya  changamoto  wana  kazi  ya  kukatisha  tamaa.  Changamoto  wanazokutana  nazo,  kama  vile  madarasa  makubwa,  wanafunzi  wenye  uwezo  tofauti  darasani,  kiwango  cha  chini  cha  elimu,  ukosekanaji  wa  vifaa,  kiwango  kidogo  cha  ruzuku  na  kutokuwepo  kwa  fursa  za  kujisomea  katika  taaluma  zao.      Mwaka  1916,  mwelimishaji/mwalimu  mashuhuri    John  Dewey  alisema,  “endapo  tunawafundisha  wanafunzi  

Aenean  eget  urna  

2

wa  sasa  kama  tulivyofundisha  wanafunzi  wa  jana,  tunawaibia  watoto  wetu  wa  kesho.”    Duniani,  nchi  zinapambana  kufanya  mabadiliko  thabiti  yakudumu.  Harakati  kama  zile  za  malengo  ya  millennia  ya  umoja  wa  mataifa  (http://www.un.org/millenniumgoals/)  zihamasisha  elimu  ya  msingi  kwa  wote  na  mabadiliko  darasani  ambayo  mwanafunzi  ndiye  kitovu  cha  maarifa,  uwepo  wa  ushahidi,  na  imehamasisha  ujifunzaji  shirikishi  na  uliochangamka.    Kwa  mfano,  nchini  Tanzania  kwa  sasa,  walimu  wanahitajika  kufikia  matokeo  makubwa  sasa,  ambayo  ni  muhimu  katika  harakati  za  nchi  za  mabadiliko  kwenye  elimu.    Hata  hivyo,  walimu  hawajapatiwa  fursa  za  mafunzo  ya  kuendeleza  taaluma  zao  ili  kufanyia  kazi  malengo  ya  jitihada/harakati  ndani  ya  utendaji  wa  darasani.    Kazi  yetu  inapendekeza,  walimu  wanahitaji  mafunzo  ya  kitaaluma  ya  kina  na  endelevu,  ili  kuwawezesha  kuwa  wa  kwanza  kupata  uzoefu  jinsi  mabadiliko  haya  yanavyoweza  kuwa  na  namna  ambavyo  watayatumia  kwenye  madarasa  yao.    Shukrani  kwa  msaada  kutoka  Senta  ya  Kimataifa  ya  Utafiti  wa  Maendeleo  (SKUM)  Msaada  wa  Mabadilishano  katika  Utafiti  kwa  Kanada  na  Afrika  (MUKA)  kuwa  na  uwezo  wa  kusanifu  na  kufanyia  jaribio  njia  ya  maendeleo  ya  kitaaluma  kuwasaidia  walimu  kurekebisha  ufanyaji  kazi  wao.  Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni:  Mkusanyiko  wa  Vifaa  kwa  Ajili  ya  Ugunduzi  na  Mabadiliko  Katika  kufundisha  na  Kujifunza  ni  matokeo  ya  kazi  ya  (MUKA)  iliyopatiwa  msaada.  Tunatoa  shukrani  kwa  taasisi  na  watu  waliotusaidia  hadi  kufikia  hapa:      • Idara  ya  elimu  –  Wilaya  ya  Mvomero,  Mko  wa  

Morogoro      • Walimu  katika  eneo  la  Turiani  kwa  kuhudhuria  

warsha,  hususani  Veronica  Mdapo  na  Fatuma  Jumbe.  • Mussa  Mohamed  na  Veronica  Sarungi    kwa  ari  ya  

ushirikiano  na  kunyumbulika  • Taasisi  ya  Maendeleo  ya  Elimu,  Chuo  Kikuu  cha  

AgaKhan,  Afrika  ya  Mashariki  (TME,  CKAK,  AM)    • Senta  ya  Ugunduzi  katika  Kujifunza  (SUKILC)  –  Kitivo  

cha  Elimu  –  Chuo  Kikuu  cha  Britishi  Kolumbia  (CKBK),  Kampasi  ya  Okanagan      

Tunatoa  fomati  mbili  (PDF  na    MS  Word)  na  Lugha  rasmi  mbili    (Kiswahili  na  English)  tukitumaini  kuwa  itakusaidia  wewe  kupeleka  utengenezaji  kwenye  muktadha  wako    na  kufanya  mabadiliko  yenye  tija  na  wanafunzi  wako.    

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     4  

Yaliyomo  katika  boksi  la  vifaa  

1

1.  Kuimarisha  Taaluma    1.1.  Usuli  1.2.  Harakati  za  Mtengenezaji  –  Mtazamo  wa  Kidunia  1.3.  Harakati  za  Mtengenezaji-­‐Mtazamo    Katika  Muktadha  wa  Kutengeneza  Kwenye  Mazingira  yenye  Changamoto  1.4.  Kutengeneza  na  Maendeleo  1.5.  Kuhusianisha  

1.5.1.  Kutengeneza  na  Kujifunza  Kwa  Kushiriki  Kikamilifu     1.5.2.  Kutengeneza  na  Kujenga  

1.5.3.  Kutengeneza  na  Matokeo  Makubwa  Sasa  

      1.5.4.  Kutengeneza  na  Kufikiri  kwa  Kuona  1.6.  Kufikiri  juu  ya  Kusanifu    

1.6.1.  Utangulizi  1.6.2.  Kuunganisha  kwenye  Elimu  

1.7.  Upimaji/Tathmini  1.8.Njia  za  Kuelewa  kwa  kutumia  maarifa  ya  asili    1.9.  Kujifunza  Kitaaluma  –  Kutengeneza  Kisa  Mkasa  kwa  Uzoefu  wa  Kina  na  Endelevu  

 2.   Kuwezesha  Warsha  ya  Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni  

2.1.  Ajenda  za  mfano    2.2.  Vipengele  vya  Warsha      

2.2.1.  Changamoto  ya  Kubuni    2.2.2.  Mchakato  wa  Kufikiri  Kubuni  –Karatasi  ya  Kufanyia  kazi  Washiriki  2.2.3.  Mchakato  wa  Kufikiri  Kubuni  –  Kiongozi  cha  Mwezeshaji  2.2.4.  Maelezo  kuhusu  sampuli  2.2.5.  Matembezi  ya  Galari  2.2.6.  Tafakari  2.3.  Tathmini  ya  Warsha  ya  Kujifunza  Kitaalamu    

 3.   Dondoo  na  Maoni  ya  Kuwezesha  Warsha  yako  

3.1.  Uundaji  wa  Makundi  3.2.  Dondoo  rahisi  za  Kuchora  3.3.  Dondoo  za  kutengeneza  Sampuli  ya  Zana  3.4.  Sehemu  Zilizopendekezwa  za  Mahali  pa  Mtengenezaji  –  Vifaa  na  Mali  ghafi  zinazohitajika  kwa  ajili  ya  warsha  yako  

Kutengeneza  ni  njia  muhimu  yakutambulisha  Sayansi,  Teknolojia,  Uhandisi,

-­‐Ujuzi  wa  Mtumiaji  –  (STUHx)  

2

4.  Maelezo  juu  ya  Sampuli  –  Zana  kutoka  Warsha  zilizopita  

4.1.    Tufe  lenye  sitaha  tatu  4.2.  Vibao  vidogo/vyembamba  kwa  ajili  ya  kuunganisha  na  kupata  maumbo  anuai...  Tangrams    4.3.    Bata    4.4.    Nyumba    4.5.    Maumbo  ya  Herufi  

 5.  Viambatisho  

5.1.  Mchakato  wa  Fikra  Bunifu-­‐Kiongozi  cha  Mwezeshaji  5.2.  Mchakato  wa  Fikra  Bunifu  –Karatasi  ya  Kufanyia  kazi  Washiriki    

 6.  Rejea  za  Kwenye  Mtandao  Zilizopendekezwa  ili  Zitafutwe    

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     5  

1.  Kuimarisha  Taaluma  

1

Harakati  za  Kutengeneza  na  vyumba  vya  madarasa  vinaonekana  ni  marafiki  sahihi.    Kujifunza  kwa  kuchunguza/kuuliza,  kujifunza  kwa  kutafuta  majibu  ya  tatizo,  kujenga  dhana,  kujifunza  kutokana  na  uzoefu,  ujifunzaji  unaomgusa  Reggio  zote  zinapigania  njia  za  kufanya  kwa  mikono  ili  kuwezesha  kufikiri  na  kujifunza  kwa  kuonekana.    Pindi  kufikiri  kukiwa  kwa  kuonekana  na  dhahiri,  kuna  ushahidi  kuwa  kujifunza  kumefanyika.  Kutengeneza  ni  njia  ya  kufundisha  kwa  kuongoza/kuelekeza  (Crichton  &  Carter,  2015)  na  namna  ya  kufikiri  ambako  kunaunganisha  mawazo  na  ubunifu  na  fikra  bunifu,  utatuzi  wa  tatizo,  na  pia  muhimu  zaidi,  kutafuta  tatizo  (Dougherty,  2013).    Kutengeneza  na  mahali  pa  mtengenezaji  haviwezi  kuongezwa  kirahisi  mahali  pa  shule  na  kujumuishwa  katika  mtaala  ambao  tayari  umesongamana  kupita  kiasi.  Kuleta  utengenezaji  mashuleni  sio  kuhusu  kuongeza  kozi  nyingine  au  somo.  Ila  ni,  njia  halisi  ya  kutekeleza  ushiriki  timilifu,  kujifunza  kwa  kushiriki  kikamilifu  madarasani.  Kutengeneza  ni  njia  yenye  maana  kubwa  ya  kuunganisha  STUH  (Sayansi,  Teknolojia,  Uhandisi,  Hisabati  na  Ubunifu  –Uzoefu  wa  mtumiaji)  na  kusaidia  kulenga  mtu  mmoja  mmoja,  kujifunza  kwa  kutengeneza  dhana  kuzunguka  mtaala.  

 1.1.  Usuli  Kwa  sasa,  asilimia  hamsini  ya  maudhui  tuliyopata  yalikuwa  kwenye  mtandao-­‐katika  mfumo  wa  dijitali.  “Wingu  la  kidijitali”.  Kidunia,  upatikanaji  wa  habari  unabadilika:  kuna  zaidi  ya  simu  bilioni  moja  za  teknolojia  ya  juu,  na  jumla  ya  maarifa  ya  binadamu,  katika  njia  ya  Wikipedia,  inapatikana  bila  kuwasha  mtandao  katika  hali  ya  kupakuliwa  (http://www.labnol.org/software/download-­‐wikipedia-­‐offline/20012/).    Kwa  sababu  tuna  matatizo  machache  ya  kufikia  au  kupata  taarifa  au  kutafuta  fursa  ya  kuwasiliana  na  wengine,  kimsingi  tunafanya  chochote  tunachofikiria  na  kuweka  mipango,  dondoo  na  watu  wakutusaidia  kwenye  mtandao.  Hii  inajulikana  kama  mtandao  wa  vitu-­‐vitu  vinaunganishwa  kwa  njia  ya  muundo  na  matumizi  yake.    Tupo  katika  wakati  wenye  maendeleo  ya  binadamu  ambapo  elimu  ya  dijitali  (namna  ya  kutumia  teknolojia  kama  vile  simu  za  mkononi  na  kompyuta  ndogo  za  

2

kisasa)  haitoshi;  ufasaha  katika  dijitali  (kwa  nini  na  wakati  gani  kuvitumia)  ni  muhimu.    Tuna  uwezo  wa  kujifunza  kwa  njia  ya  mfumo  rasmi  au  usio  rasmi,  wakati  wowote,  mahali  popote,  na  katika  muundo  wowote  tuutakao.    Fursa  za  kujifunza  kwa  namna  fulani  zimekuwa  hazinyumbuliki.    Tunaweza  kuongeza  ujuzi  wa  kalkulasi,  kujifunza  kujenga  kichujio  thabiti  cha  maji  na  kisichokuwa  na  gharama  kubwa  (www.cawst.org),  au  kubuni  hita  ya  maji  inayotumia  nguvu  ya  jua  kwa  kutumia  taarifa  tunazoweza  kuzipata  kwa  kutumia  vyombo  mbalimbali  (yaani,  simu  za  mkononi,  kompyuta  ndogo  za  kisasa,  na  kompyuta  za  kawaida),  majukwaa  (yaani  Androidi,  ‘Apple’,  ‘Windows’),  na  njia  za  mawasiliano  (yaani  ‘wikis’,  tovuti,  video).      Walimu  au  waelimishaji  wanakabiliwa  na  changamoto  kutoka  kwenye  serikali  zao  na  sekta  za  biashara  kusaidia  wanafunzi  kupata  ujuzi  muhimu  katika  nyakati  za  sasa.  Wanaambiwa  kuwa  ujuzi  huu  lazima  uwepo  katika  hali  yakufikiwa,  mnyumbuliko,  mazingira  ya  kunyumbulika  ya  kujifunza  lakini  ni  mara  chache  walimu  wamepatiwa  uono  wa  mara  moja  juu  ya  namna  mazingira  ya  kujifunzia  yanaweza  yakaonekana  au  wamepewa  maoni  yakivitendo  ya  namna  wanavyoweza  kutumia  katika  muktadha  wa  kwao.          Shirika  la  Ushirikiano  wa  Kiuchumi  na  Maendeleo  (SUKM)  linaelezea  mazingira  yenye  ubora  wa  juu  ya  kujifunzia  kuwa  ni:    • Mwanafunzi  kuwa  kitovu  cha  maarifa,  yenye  

umuhimu,  na  bado  walimu  wawe  na  majukumu  anuai.    

• Muundo  na  ubunifu  thabiti,  unahitaji  ueledi  wa  hali  ya  juu  kusaidia  udadisi  wa  wanafunzi  na  kujifunza  kwa  kujitegemea.  

• Kwa  undani  na  kwa  kila  mtu,  kuwa  makini  juu  ya  utofauti  wa  mahitaji  maalum  miongoni  mwa  makundi  na  kutoa  mrejesho  uliorekebishwa  kwa  wakati  na  mwalimu  husika.  

• Mchanganyiko  ili  kuchukulia  na  kuwa  makini  juu  ya  utofauti  wa  mahitaji  maalum  binafsi  na  yakikundi.    

• Yenye  ushirikiano  ili  wanafunzi  waweze  kufanya  kazi  kwa  kushirikiana  katika  hali  ya  vikundi  na  kuunganisha  hadi  kwenye  jamii  zao  katika  ukubwa  wake  (OECD,  2011).  

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     6  

   3

 Mazingira  yenye  ubora  wa  juu  yakujifunzia  yameelezewa  na  OECD  na  wengine  wanaungana  na  kile  ambacho  Pink  (2005)  anaita  dhana  ya  kipindi  –  muda  ambao  mantiki  na  fikra  nyoofu  zinathaminiwa,  hususani  pindi  zinapokuwa  zimeunganishwa  na  ubunifu  na  uvumbuzi.    Upelelezi,  ujumi  wa  kuonekana,  kutafuta  na  kufumbua  tatizo  vimekuwa  vikibainishwa  kuwa  ni  ujuzi  muhimu  katika  zama  za  dhana.        Hatch  (2014),  mwandishi  wa  kitabu  Maker  Manifesto,  anapendekeza  kuwa  kama  sehemu  ya  zama  za  dhana,  kiuhalisia  tunaingia  kwenye  mapinduzi  mapya  ya  viwanda.  Ikiwa  mapinduzi  ya  kwanza  yalichochewa  na  

viwanda  vilivyoimarishwa  na  mvuke  na  pili  kwa  umeme,  zama  za  dhana  zinaimarishwa  na  upatikanaji  wa  habari  usio  na  kikomo;  maendeleo  ya  kuongezeka  kwa  bei  yakuridhisha,  vifaa  thabiti,;  na  uwezo  wa  kupata    nyenzo  anuai  zinazopatikana  duniani  kote  na  vifaa  vya  kutengenezea  vitu.  Hatch  anapendekeza  harakati  za  utengenezaji  kiuhalisia  ni  mtandao  wa  vitu  (angalia  uwasilishaji  hapo  chini).  Anadai  kiuhalisia  ni  kubwa  kuliko  toleo  la  kwenye  mtandao  kwa  sababu  inajumuisha  vitu  vya  asili  vilivyounganishwa  kupitia  kifaa  cha  kunasa  kwenda  kwenye  mtandao  wa  intaneti.    1.2.  Harakati  za  Utengenezaji  –  Mtazamo  wa  Kidunia    Wote  tunahitaji  kutengeneza.    Ina  mizizi  kutoka  kwenye  udadisi  juu  ya  dunia  na  shauku  yetu  kutengeneza  vitu  na  tena  kutengeneza  hivyo  vitu  kwa  ustadi/ubora  zaidi.    Wazazi  wetu  wa  mwanzo  kabisa  waliongoza  njia  ya  kutengeneza  pindi  walipounda  vitu  vya  mwanzo  vya  mikono  Afrika  ya  mashariki  na  kufanya  majaribio  kwa  

Intaneti  (mtandao)  ya/wa  vitu    

4

moto.  Waliendelea  kutengeneza  vitu  na  kufanya  vitu  hivyo  bora  zaidi  pindi  walipobadilika  kutokana  na  maeneo  mapya  na  kusambaa/kuenea  kuzunguka  dunia.    Kwa  sasa,  kuna  shauku  mpya  katika  kujifunza  namna  ya  kutengeneza  vitu-­‐inafahamika  kama  Harakati  za  Fanya-­‐Wewe-­‐Mwenyewe  (FWM).    Watu  wanazidi  kuchoshwa  na  vilivyotengenezwa  kirahisi/uduni,  People  are  growing  tired  of  cheaply  made,  vifaa/bidhaa  za  kutumika  mara  moja  tu  bila  kufanyiwa  matengenezo  au  kubadilishwa.  Inaongezeka  sana,  watu  wanarudi  kwenye  njia  za  asili  za  kufanya  mambo.  Wengi  wanaachana  na  vyakula  vyakuhifadhiwa  kwenye  vifaa,  ambavyo  vina  virutubisho  haba  au  vilivyotengenezwa  bila  viwango  lakini  kwa  gharama  kubwa,  vilivyofanywa  kuwa  vigumu  na  vifaa  vyake  haviwezi  badilishwa  na  kutumika  tena.      Kidunia,  tunadai  kurudisha  hitaji  letu  la  kutengeneza,  na  tunarasimisha  hili  kuwa  harakati.    Tunaandaa  warsha  shirikishi  (mahali  pa  mtengenezaji),  kutoa  muda  wa  video  za  kufundishia  kwa  njia  ya  mtandao    (mfano.  ‘You  Tube’,  ‘Intractable’  -­‐  www.Instructables.com),  na  kutoa  warsha  (kazi  za  kuboresha  taaluma),  kuondoa  ubinafsi  wetu  na  kuirekebisha  dunia  inayotuzunguka.    Utofauti  uliopo  kwa  sasa  ni  kuwa  tulikuwa  tunatumia  njia  ya  fikra  bunifu  yenye  kumlenga  mwanadamu  kubuni  vitu  ambavyo  vina  thamani  kutengenezwa  na  vinalenga  mahitaji  halisi.    Waelimishaji/walimu  wana  jukumu  la  kufanya  katika  badiliko  hili  kutengeneza  kwa  kutambulisha  fikra  sanifu  na  kujifunza  kwa  kushiriki  kikamilifu  katika  kuandaa  vifaa  na  kazi  za  shuleni-­‐hii  tunaita  Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni.    1.3.  Harakati  za  Utengenezaji  –Mtazamo  katika  Muktadha  wa  Kufundisha  na  Kujifunza  kwenye  Mazingira  yenye  Changamoto.  Wakati  elimu  imekuwa  ikitambulika  kama  ufunguo  katika  mabadiliko  chanya  ya  mtu  mmoja  mmoja  na  jamii,  inaweza  tu  ikapata  kutumika  kwa  kazi  hii  endapo  itatolewa  katika  njia  iliyo  sahihi.  Kama  ilivyoonekana  hapo  mwanzo,  njia  ya  mwalimu  kuwa  kitovu  cha  maarifa  na  kurudiarudia  matendo  sio  lazima  ipelekee  kujifunza.  Kufundisha  na  kusikiliza  sio  lazima  ipelekee  kujifunza.  Ujifunzaji  wakimageuzi  unahitaji  kujifunza  kwa  utimilifu  ambapo  wanafunzi  wanarekebisha  utaratibu  wa  maana  kwa  kutafakari  ki  umakinifu  juu  ya  uzoefu  wao.  Hatua  ya  kwanza  ni  yakuandaa  mazingira  rafiki  ambayo  yanaruhusu  kupata  uzoefu,  kutafakari  kwa  makini,  na  kutengeneza  maana  juu  ya  uzoefu  wao.  Kufundisha  na  kutengeneza  kunatakiwa  kupelekee  kujifunza  kwa  kushiriki  kikamilifu  ambapo  itakuwa  yakimageuzi.  

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     7  

5

 Kutengeza  katika  muktadha  wa  shule  kunawakilisha  fursa  kubwa  kwa  ujifunzaji  wa  kimageuzi  ambapo  wanafunzi  wanaweza  wakatafakari  changamoto  katika  muktadha  wao.  Wanashiriki  katika  kuuliza  na  kueleza  wanayatambua  kama  ni  masuala  yenye  umuhimu  ya  kuyakabili.    Kwa  njia  ya  mazungumzo,  wanayachukulia  matatizo  ya  wenzao  na  kushauriana  juu  ya  utatuzi  na  kufikiri  kutengeneza  ufumbuzi  wake.  Katika  mchakato  wote  huu,  mwanafunzi  anachukua  nafasi  katika  kazi  ambapo  mwalimu  anawezesha  na  kutoa  muongozo  kwa  njia  ya  upimaji  usiorasmi  wa  maendeleo  yao.  Mwalimu  na  wanafunzi  wanajifunza  kutoka  kwenye  mchakato,  wanaelezea  uelewa  wao  kwa  kubuni  na  kuandaa  ufumbuzi  kwa  pamoja.  Ujifunzaji  huu  unaweza  ukahifadhiwa  kwa  hatua  zilizochukuliwa  na  pia  ushahidi  kwenye  majibu/ufumbuzi  uliofikiwa.    Muktadha  ni  kigezo  muhimu  katika  kubaini  kile  kinachounda  elimu  bora.  Wakati  vigezo  vingine  ni  vyakidunia,  undani  wake  unategemea  muktadha.  Kwa  mfano,  mawazo  juu  ya  kufikia  ubora  wa  elimu  unahitajika  kuakisi  muktadha  ili  yaweze  kufanikiwa.    Mazingira  yenye  changamoto  yapo  kila  mahali-­‐inaweza  kuwa  ni  eneo  duni  la  mjini  au  lenye  maisha  duni,  lisilofikika  kijijini,  lisilo  rafiki  lenye  jiografia  ngumu/tata,  eneo  lenye  hali  ngumu  kiuchumi  na  huduma  za  kijamii.  Muktadha  unaweza  kuwa  ni  muunganiko  wa  masuala  yanayofanya  ugumu  kwa  walimu  na  wanafunzi  kupata  uzoefu  wa  elimu  bora.  Baadhi  ya  masuala  haya  ni  pamoja  na  wingi  wa  watu,  mahitaji  maalum  tofauti  ya  wanafunzi,  kukosekana  kwa  vifaa,  ruzuku  isiyotosheleza,  kukosekana  kwa  fursa  za  kujiendeleza  kitaaluma  na  mengine  mengi  yanayohusiana  nayo.  Mazingira  au  muktadha  kama  huu  unafanya  mageuzi  katika  elimu  yaliyoongelewa  hapo  juu  kuwa  na  ugumu  fulani  lakini  sio  kuwa  hayawezekani.  Kiuhalisia,  yanatoa  fursa  ya  kufanyika  kwa  ujifunzaji  wa  kimageuzi  ambapo  elimu  inaitikia/inaakisi  mahitaji  ya  mtu  mmoja  mmoja  na  jamii  bila  uwepo  wa  suluhisho/utatuzi  kutoka  nje  ambao  unaweza  kuwa  hauendani  na  muktadha  husika.  

 Harakati  za  utengenezaji  zimekuwa  zikifanikiwa  katika  mazingira/muktadha  tofauti  tofauti,  ikiwemo  yale  yenye  changamoto.  (kwa  mfano;  Hifadhi  ya  wenyeji  nchini  Kanada,  vijijini  Tanzania).  Katika  muktadha  hizi,  kwa  ujumla  mchakato  unabaki  kuwa  ule  ule-­‐kuhamasisha  mchakato  wa  fikra  bunifu  na  kutengeneza.    Lengo  la  

6

kuanzisha  mahali  pa  mtengenezaji  katika  kituo  cha  walimu  cha  zana/vifaa  ni  kuwawezesha  waelimishaji  kufikiri  juu  ya  hali  ya  baadaye  ya  elimu  kwa  kushiriki  kutafakari  fikra  bunifu  na  kupata  ufumbuzi  kwa  ugunduzi  timilifu,  kuitikia  changamoto  za  njia  za  ufundishaji  katika  mazingira  yao.  Njia  hii  inaendana  na  mageuzi  ya  sasa  ya  elimu  kama  vile  Matokeo  Makubwa  Sasa  (BRN)  nichini  Tanzania.  Mambo  ya  msingi  katika  mageuzi  haya  ni  kuhakikisha  kwamba  wanafunzi  hawahudhurii  tu  shuleni  bali  wanasoma  kikamilifu;  walimu  wanamotisha  ya  kutumia  muda  zaidi  darasani  kufundisha;  na  yawepo  matokeo  yenye  ushahidi.  Harakati  za  utengenezaji  zinawajengea  walimu  uwezo  wa  kufikiri  na  kutekeleza  elimu  chini  ya  jitihada  hizo.      Zama  hizi  za  maarifa  zinatoa  aina  tofauti  ya  ufahamu  (kusoma  na  kuandika).  Kando  ya  kujua  lugha  ya  kiasili-­‐  kuna  haja  ya  kujumuisha  ujuzi  zaidi  ya  huo  unaowakilisha  njia  tofauti  za  kufahamu  na  kuelezea  ujifunzaji.  Aina  mpya  za  ufahamu  zinahusisha  vyombo  vya  habari,  dijitali,  nafasi/uhusika  wa  anga,  kisayansi,  uelewa  wa  hisabati  ambao  ni  muhimu  katika  kufikia  na  kutumia  maarifa  mengi  ambayo  mwanafunzi  anayapata  kwa  urahisi.  Uelewa/ujuzi  zaidi  ya  mmoja  unaungana  na  intelijensi  zaidi  ya  moja  iliyoongelewa  na  Gardner.    Utambuzi  na  kuendelea  kwa  ujuzi  zaidi  ya  mmoja  katika  njia,  inahakikisha  kuwa  intelijensi  zaidi  ya  moja  miongoni    mwa  wanafunzi  inazingatiwa.  Pia  inahamasisha  wanafunzi  kushirikiana  na  kufanya  kazi  kwa  kuelewana.  Hatimaye  inapelekea  ubunifu  na  ugunduzi  kwa  kuwa  wanafunzi  wanapanua  fikra  zao  na  kutumia  ujuzi  wao.  Uhalisia  wa  mazingira  ambayo  walimu  na  wanafunzi  

Aina  mpya  ya  ujuzi  wa  maarifa  hutambulishwa  wakati  wa  kutengeneza  

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     8  

 

7

wanafanya  kazi  yanaweza  yakajulisha  na  kusaidia  ubunifu  au  ukawa  kikwazo  katika  uvumbuzi  na  ubunifu.    Uwezo  wa  kukabiliana  na  matendo  yaliyopo  ni  mwitikio  wa  mazingira  halisi.  Neno  ‘leapfrog’  liliazimwa  kutoka  kwenye  uenezi  wa  teknolojia.  Mfano  ni  muktadha  

8

ambapo  simu  za  mkononi  zilipanda  thamani  haraka  zaidi  ya  simu  za  mezani  kwa  kuruhusu  watumiaji  kuanza  kutumia  teknolojia  mpya.    Mahsusi,  kubadilishana  ujumbe  wenye  taarifa  anuai,  kufanya  miamala  ya  fedha  kwenye  simu  ni  baadhi  ya  matumizi  ya  teknolojia  ambayo  yalikuwa  yamechukua  nafasi  kwa  sababu  ya  kuenea  zaidi  kwa  matumizi  ya  simu  za  mkononi.    Vivyo  hivyo,  maarifa,  taarifa,  ujuzi  na  matendo  yaliyochukuliwa  kutoka  njia  za  kiasili  za  kujua  zinaweza  kuchangia  kwenye  uvumbuzi  na  ubunifu  katika  njia  ambayo  inaruhusu  matendo  ya  kielimu.  Aina  ya  maarifa  ya  asili  inahusisha  imani  na  desturi  za  asili,  uchongaji  wa  vifaa,  sanaa,  kutumia  zana  za  ufundi  toka  kwenye  mazingira  –  mimea  na  wanyama,  mifumo  ya  kujifunza,  uainishaji,  sheria,  aina  za  mawasiliano  na  mpangilio.  Njia  ya  kiasili  ya  kutambua  ni  chimbuko  la  usuli  wa  muktadha  wa  maarifa  

 

Elimu  ni  lengo  na  pia  ni  kichocheo  cha  maendeleo    

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     9  

9

na  ujuzi  ambao  mwanafunzi  anauleta  darasani.  Pia  maarifa  ya  asili  yanatoa  msingi  na  chimbuko  la  Lugha,  hisabati  na  maudhui  ya  kisayansi  kwa  kuendeleza  umahiri  wa  mwanafunzi  katika  miaka  ya  mwanzo.  Maarifa  haya  yanatengeneza  msingi  ambapo  mwanafunzi  anajenga  ujifunzaji  mpya.  Baadhi  ya  maarifa  yanaweza  yakaendelezwa  wakati  mwanafunzi  akiwa  anashirikishwa  kama  mwanamageuzi  wa  biashara  fulani.  Zaidi,  maarifa  ya  asili  yanatambua  uthabiti  na  upatikanaji  wa  vitu  vya  kiasili.  Utumiaji  wa  vitu  hivyo  (ikiwemo  rasilimali  watu)  ni  muhimu  katika  kuendeleza  ufumbuzi  wakudumu.      Katika  kutafuta  ubunifu,  uhusiano  na  uthabiti  wa  ufumbuzi  na  matumizi,  uzingatiaji  makini  unatakiwa  kufanywa  juu  ya  muktadha.  Uelewa  wa  hali  ya  fikra  kiasili  ya  ujumi,  uhitaji  na  uwezokano  wa  ufumbuzi  wa  tatizo  ni  muhimu.  Ufumbuzi  unaopendekezwa  unatakiwa  kumilikiwa,  ukubalike  na  udumu  kwa  watumiaji.  Ufumbuzi  pendekezwa  unatakiwa  ukubalike  na  usiwe  wakuamuriwa.  

 1.4.  Kutengeneza  na  Maendeleo  Kwa  pamoja  elimu  ni  lengo  na  chachu  ya  maendeleo.  Umuhimu  wa  elimu  umeakisiwa  katika  kujumuishwa  kwake  kwenye  Malengo  ya  Maendeleo  ya  Millennia  (MMM).    Moja  kati  ya  MMM  ni  kufikia  Elimu  ya  Msingi  kwa  Wote  kwa  huhakikisha  kuwa  ifikapo  mwaka  2015,  wanafunzi  kila  mahali,  wavulana  na  wasichana  kwa  pamoja  watakuwa  na  uwezo  wa  kumaliza  masomo  ya  elimu  ya  msingi  kikamilifu"  (UN,  2015).    Zaidi  ya  hapo,  

10

MMM  yanathibitisha  kutambua  kuwa  elimu  ni  chombo  katika  kufikiwa  kwa  malengo  menginie  ya  maendeleo  ya  millennia,  utambuzi  ni  kuwa  “  kuelimisha  watoto  kunawapa  kizazi  kijacho  chombo  cha  kupambana  na  

 

 

   

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     10  

   

11

umasikini  na  kuzuia  magonjwa,ikiwepo    malaria    na  ukimwi"  (UN,  2015).    Kwa  masikitiko  makubwa,  tathmini  ya  malengo  ya  millennia  ya  umoja  wa  wataifa,  mafanikio  yaliyofikiwa  hadi  sasa  yanaonesha  kuwa  dunia  haijaweza  fikia  malengo  ya  mwaka  2015  ya  elimu  ya  msingi  kwa  wote.  Imekiri  kuwa  pamekuwa  na  ubora  fulani  wa  kufikika  kwa  elimu,  lakini  imethibitishwa  kuwa  matokeo  ya  ujifunzaji  na  elimu  yenye  uhusiano  ni  muhimu  ili  iweze  kuchangia  katika  maendeleo.  Mchango  wa  mawazo  uliotolewa  katika  boksi  la  vifaa/mkusanyiko  wa  vifaa  ina  uhusiano  wa  moja  kwa  moja  kwenye  njia  ambazo  

12

tunaweza  kufanya  kazi  kuifanya  elimu  kuwa  yakuhusika  zaidi  na  kuwa  zalishi  kwa  watoto.    Kusudio  la  hatua  inayofuata  ya  Malengo  ya  Umoja  wa  Mataifa  ya  Millenia  ni  Melengo  Endelevu  ya  Maendeleo  (MEM).    MEM  inatambua  uhitaji  wa  kila  nchi  kulenga  changamoto  mahsusi  inahitaji  kukabiliana  nazo  ili  kupata  uhusiano  wa  kimuktadha  na  maendeleo  endelevu  (UN,  2014).    Tunaona  ‘kutengeneza’  kama  kunafaa  kiasili  katika  mashule  kwa  kuwa  inaunganisha  ugunduzi,  ubunifu,  kubaini  tatizo,  kutafuta  ufumbuzi  kulingana  na  muktadha  mahsusi.      1.5.  Kutengeneza  Uhusiano/Uhusiano  uliopo    Kutengeneza  kunaweza  kutumika  kama  njia  elekezi  iliyo  bora.    Unaanzia  kwa  kutumia  Njia  ya  Kufikiri  na  Kubuni.  Utengenezaji  unaangazia  utamaduni  mpya  katika  kujifunza  ambako  hakujawekewa  mipaka  katika  madarasa  ya  kiasili.      

1.5.1.  Kutengeneza  na  Kujifunza  kwa  Kushiriki  Kikamilifu.  Utamaduni  huu  mpya  wa  kujifunza  kwa  kushiriki  kikamilifu  unahusisha  katika  mchezo,  kuuliza  na  fikra  (Thomas  &  Brown,  2011).    Ikiwa  kama  njia  elekezi,  kutengeneza:  • Kunasisitiza  ushirikianao,  ugunduzi,  ubunifu  na  

kufikiri  kwa  umakinifu.  • Ni  mchakato  wa  kubaini  tatizo  na  kufumbua  tatizo.  • Kiasili  inapelekea  kujifunza  kwa  kushiriki  kikamilifu-­‐

wanafunzi  kujadiliana  na  kutengeneza  vitu.  • Kupelekea  kushirikishwa  kwa  mwanafunzi  (uwezo  wa  

kufiriki,  hisia,  tabia,  kijamii  na  kiutamaduni)  –  ushirikishwaji  wa  karibu  wa  mwanafunzi  unathibitika  wakati  wanafunzi  wanakuwa  wadadisi,  wenye  shauku  na  kwa  hiyo  wana  motisha  kusoma  zaidi.  

• Ni  yenye  malengo  na  hivyo  kuwa  na  motisha  ya  hali  ya  juu.  

• Inafanya  kwa  pamoja  mchakato  na  matokeo  kuwa  muhimu.    

• Kuhakikisha  kuwa  kujifunza  kunapatikana  katika  mchakato.  

 1.5.2.  Kutengeneza  na  Kujenga  

Ufunguo  katika  elimu  bora  unaweka  mazingira  rafiki  yakujisomea  (OECD,  2011).  Mazingira  haya  yanapelekea  kujifunza  kwa  kushiriki  kikamilifu  ambapo  wanafunzi  wanaweza  wakashirikiana  kwa  pamoja  kujenga  maarifa  katika  njia  ambazo  zinaendana  na  muktadha  pia  zenye  kufaa.  Kujifunza  kunahusisha  kupata  maarifa  mapya  au  kurekebisha  na  kuimarisha  maarifa  yaliyopo.  Kwa  mujibu  

Tunaona  utengenezaji  kama  wakufaa  kiasili  mashuleni  

Kutengeneza  kunaunganisha  ugunduzi,  ubunifu,  kubaini  tatizo  na  ufumbuzi  wake  

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     11  

13

wa  mawazo  ya  wajengaji  maana,  inamtaka  kila  mmoja  kushiriki  katika  mchakato  wa  kujenga  maana  katika  dunia  yao.  Wanafunzi  hawasharabu  maarifa  yaliyokwisha  jengwa  tayari  kwa  ajili  yao  toka  kwa  walimu,  lakini  wanapatiwa  fursa  za  kujenga  maarifa  kwa  kila  mmoja  mmoja  na  kwa  kushirikiana.      Ili  kufanikisha  hili,  waelimishaji/walimu  wafuasi  wa  kujenga  maana  wanashikilia  imani  zifuatazo:  • Kujifunza  lazima  iwe  ni  mchakato  wenye  kushirikisha  

kikamilifu  –  wanafunzi  hutumia  data  za  ufahamu  kujenga  maana  (hii  inatambua  untelijensi  zaidi  ya  moja  kama  chanzo  cha  data  za  ufahamu)  

• Wanafunzi  wanajifunza  kusoma  kupitia  kujenga  maana  na  mfumo  wa  maana-­‐kutengeneza  utaratibu  fulani-­‐mpangilio,  madarasa,  makundi,  makundi  ya  sanaa  za  maonesho  

• Ujenzi  wa  maana  unatakiwa  uwe  kwa  pamoja  ushirikishe  muonekano  na  ubongo/ufahamu    –  inahusisha  uwakilishi  mwonekano  wa  nje  wa  maana  ya  mtu  fulani  iliyo  na  maelezo  ya  uchaguzi  tunoufanya  na  kwa  nini.  

• Lugha  ni  kitu  muhimu  sana  katika  kujifunza  –  tunajenga  maana  katika  lugha  ambayo  tupo  nayo  huru  zaidi,  na  hivyo  umuhimu  wa  kuchagua,  kwa  mfano,  lugha  ya  asili  kwa  kufundishia  au  kuelezea  ujifunzaji.  

• Kujifunza  ni  kazi  ya  kijamii  –  elimu  ya  asili  ilimbagua  mwafunzi,  elimu  endelevu  hutambua  kujifunza  kama  ni  juhudi  za  kijamii  (waamini  wa  ujenzi  wa  maana-­‐kijamii)  ambapo  wanafunzi  wanafanya  kazi  kwa  ushirikiano  kujenga  maana  ambayo  ina  maana  katika  muktadha  fulani.  

• Kujifunza  hapatokei  angani-­‐bali  kunafanyika  katika  muktadha  husika-­‐na  hivyo  kuhitajika  kwa  maarifa  yakufaa  na  yenye  uhusiano  na  muktadha.  Maarifa  yaliyoingizwa  toka  nje  yanaweza  yasiwe  yakufaa  au  na  uhusiano  na  mazingira  husika  hivyo  kukosa  thamani  yakuchukuliwa  kuwa  ni  maarifa  katika  muktadha/mazingira  yaliyokusudiwa.  

• Kujifunza  kunahitaji  maarifa-­‐kuna  haja  ya  wawezeshaji  na  wanafunzi  kuanzia  katika  maarifa  waliyonayo  kabla  ya  darasani/maarifa  ya  awali.  Kwa  mfano,  maarifa  ya  asili  ni  chanzo  kikubwa  cha  maarifa  ya  awali  yanayotoa  ujumbe  kwa  ujengaji  wa  maarifa  mapya  kwa  sababu  yana  uhusiano  wa  kimazingira  na  yanafaa.  

• Kujifunza  kunachukua  muda  –  sio  kitu  cha  papo  kwa  papo.  Inahitaji  mpango,  vitendo,  tafakari  na  kurudia  

14

umaizi  mpya  na  ufahamu  unaotokea  wakati  wa  awamu  hizi.  

• Kujifunza  kunahitaji  motisha  –  wanafunzi  wanahitaji  sababu  za  wao  kujifunza.  Mchakato  wa  kujifunza  na  matokeo  yake  (ujengaji  mpya)  unaleta  motisha  ya  kujifunza.  

 Ujengaji,  kwa  hiyo  unawakilisha  kujifunza  kama  mchakato  wa  ujuzi  wa  vitu  na  kutafakari  katika  ujuzi  huo.  Inaendeleza  ufahamu  kiundani  na  wenye  kudumu.    

1.5.3.  Kutengeneza  na  Matokeo  Makubwa  Sasa  Tanzania,  kama  wengine  wanoendelea  kiuchumi  inakusudia  kuvuka  kutoka  uchumi  wa  chini  kwenda  uchumi  wa  kati.  Ili  kufikia  hili,  imechukua  Modeli  ya  Maendeleo  kutoka  Malaysia  (Matokeo  Makubwa  Sasa)  na  ikazindua  kuanzishwa  kwa  Matokeo  Makubwa  Sasa  (BRN).  Mkakati  huu  unalenga  maeneo  makuu  manne  na  elimu  ni  mojawapo.  Elimu  inachukuliwa  kuwa  wakala  muhimu  katika  kuleta  kichocheo  kwenye  maendeleo.  Hata  hivyo,  ili  elimu  iweze  kutimiza  mamlaka  ya  uwakala,  baadhi  ya  mageuzi  ni  muhimu.      Ni  muhimu  kukumbuka  kuwa  wakati  Tanzania  ime  rekodi  mafanikio  yakuonekana  kwenye  upatikanaji  wa  elimu  ya  msingi  ndani  ya  miaka  10  iliyopita,  pamekuwa  na  kukithiri  kwa  kushuka  katika  ubora  wa  elimu,  na  kuzua  swali  endapo  wanafunzi  wanajifunza  au  wanahudhuria  tu  shule.  (Ripoti  ya  Benki  ya  dunia  Julai  2014;  Ripoti  ya  UWEZO  2011-­‐2014).  Chini  ya  jitihada  za  BRN,  Benki  ya  dunia  na  marafiki  wa  maendeleo  nchini  Tanzania  wanalenga  kuinua/kuboresha  matokeo  ya  kujifunza  kwa  kukabiliana  na  mambo  mahsusi  yanayopelekea  matokeo  mabovu  ya  ujifunzaji.  

Kujifunza  ni  kazi  ya  kijamii  (ya  umoja)  

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     12  

 

15

 Hususani  kwa  kuzingatia  kujifunza,  wanapendekeza  kuhakikisha;  • Walimu  wapatiwe  motisha  ya  kutumia  muda  zaidi  

darasani  kufundisha  • Data  zimekusanywa  na  matokeo  yanaangaliwa  kila  

mara  ili  elimu  iweze  kusimamiwa  kwa  ufanisi    • Wanafunzi  wengi  wajifunze  kusoma,  kuandika  na  

kufanya  hesabu  za  msingi  kufikia  mwisho  wa  darasa  la  pili  (Benki  ya  Dunia,  2014)  

 Wakati  hatua  zimekuwa  zikichukuliwa  kutenganisha  kile  kinachohitajika  kufanyika,  mchakato  halisi  wa  kuwamotisha  walimu,  kuwashirikisha  wanafunzi  na  kukusanya  data  ni  suala  linahusiana  na  mbinu/njia  za  ufundishaji.  Njia  elekezi  ya  kufundisha  iliyopendekezwa,  kutengeneza  inaweza  kutoa  suluhisho  kwa  makusudio  haya  mazuri  na  yanaweza  kutimia  (angalia  kipengele  cha  2.5).  Kwa  kutengeneza,  walimu  wanaweza  kuwa  na  sababu  ya  kukaa  kwa  muda  mrefu  darasani  na  wanafunzi  watashirikishwa  zaidi;  kuna  fursa  nyingi  za  kukusanya  data  ambazo  zinathibitisha  mchakato  wa  kujifunza  na  zinatoa  data  halisi  kwa  tathmini  endelevu  na  tamati.  Data  hizo  zinatoa  mrejesho  kwa  uongozi  wa  shule  na  wadau  wengine  kwa  pamoja  juu  ya  mafanikio  na  maeneo  ambayo  yanahitaji  kuangaliwa  kwa  ukaribu  na  kutoa  mchakato  unaoendeleza  kwa  pamoja  ujuzi  wa  kusoma  na  kuandika  (kwa  ufahamu  mpana  wa  kusoma  na  kuandika    angalia  Kalantzis  na  Cope,  2012)  na    kufanya  hisabati  kwa  vitendo  na  kwa  njia  ya  ushahidi.  Hatimaye,  mchakato  wa  kutengeneza  unaleta  ujifunzaji  bora  kwa  mwalimu  na  mwanafunzi  ambao  unaendana  na    muktadha  na  utaimarisha  elimu  kutimiza  jukumu  lake  la  uwakala  katika  kuendesha  maendeleo.    

1.5.4.  Kutengeneza  na  Kufikiri  kwa  Kuona      Mizizi  yake  ni  katika  nadharia  na  vitendo  ya  ujenzi  wa  maana,  kutengeneza  ni  njia  bora  sana  ya  kutoa  ushahidi  wa  mchakato  wa  fikra  unaotokea  wakati  wa  kujifunza.  Katika  hatua  mbalimbali  mchakato  wa  kufikiri  na  kubuni,  kuna  uwakilishi  wa  nje  wa  mchakato  wa  kufikiri.  Kutokea  nje,  washiriki  wanashirikishana  mitazamo  yao  juu  ya  masuala  fulani  na  kupitia  mazungumzo  wanafikiria  jambo  walilolipata  kutoka  kwa  mwenzao/wenzao.  Baada  ya  hapo  kupitia  mchakato  wa  uwezo  wa  kuhisi  maono  ya  mwingine  wanaweza  wakashughulika  kutafuta  majibu  au  ufumbuzi  fulani.  Mazungumzo  yanabainisha  ufikiriaji  wa  kirafiki  au  mtu  na  mtu,  ufupisho  unaelezea  fikra  na  majibu/ufumbuzi  unaopendekezwa    (katika  kuchora  na  maelezo/ufafanuzi)  unawakilisha  mchakato  wa  utatuzi  

16

wa  tatizo  –ambapo  ni  mwitikio  wa  hitaji  lililoelezewa.  Zaidi  ya  hapo,  majadiliano  ya  kushauriana  yanatoa  ushahidi  wa  tathmini  ya  fikra  juu  ya  majibu/ufumbuzi  unaopendekezwa  na  mchoro  wa  mwisho  ni  ushahidi  wa  wazo  la  pamoja.  Sampuli  kifani/sampuli  ya  awali  ni  ushahidi  dhahiri  wa  mchakato  wa  kufikiri.  Tathmini  ya  mwisho  binafsi  na  ya  washiriki  wengine  iliyoelezewa  katika  tafakari  inatoa  ushahidi  wa  kulingana  kati  ya  jambo  la  awali  lililoshirikishwa  na  ufumbuzi  uliowasilishwa.  (Angalia  kipengele  cha  2.5.)  

 1.6.  Fikra  Bunifu      “Kufikiri  juu  ya  ubunifu  kwa  ujumla  kunazingatia  uwezo  wa  kuunganisha  uwezo  wa  kuhisi  maono  ya  mwingine  kwa  muktadha  wa  tatizo,  ubunifu  katika  kuzalisha  umaizi/utambuzi  na  majibu  au  ufumbuzi,  na    kutazama  jambo  kimaantiki  kuchambua  na  kuendana  na  ufumbuzi  kulingana  na  muktadha”  (Wikipedia,  n.d.).    Mchakato  wa  usanifu  unamlenga  binadamu  ambapo  unamzingatia  mtumiaji  zaidi  kuliko  tatizo  pekee  au  matokeo.    Fikra  bunifu  ni  sehemu  muhimu  ya  kusudio  la  mchakato  tunaoutumia  katika  warsha  za  kupeleka  utengenezaji  mashuleni.    Tumetambua  kuwa  mara  nyingi  watu  kama  watu  wakipewa  tatizo  walitatue,  huwa  wanakimbilia  kwenye  ufumbuzi/majibu  bila  ya  kuzingatia  mambo  yote  yanayochangia  ugumu  na  uwezekano  wa  majibu/ufumbuzi.        

1.6.1.  Utangulizi  Fikra  bunifu  ni  mchakato  ambapo  mbunifu  anaweza  akacheza  na  kitu  (kucheza  au  kwa  makusudi  kucheza  na  fikra/mawazo  yaliyounganishwa)  na  kuongea  kwa  ushirikiano  ndani  ya  makundi  yao,  kujadili,  kutafiti  na  kupeleleza  njia  mbadala  au  fursa  zilizopo.    Fikra  bunifu  au  aina  ya  mawazo  yanayoendeleza  ubunifu  na  ugunduzi.    Mawazo  ya  ubunifu  yanashabihiana  vyema  na  kutengeneza  kwa  kusaidia  watengenezaji  kuzingatia  kile  ambacho  wangependa  kukitengeneza  na  kile  kinachoweza  kuhitajika.    Ina  waruhusu  watengenezaji  “kupambana  na  matatizo  makubwa  ya  dunia  kwa  ubunifu  na  kutimiza  mahitaji  muhimu  zaidi  ya      kibinadamu  ”  (Hatch,  2014,  uk.  10).  Kama  alivyowahi  kusema  Walt  Disney,  mgunduzi  wa  Mickey  Mouse,  “Ni  aina  ya  kufurahisha  kufanya  kisichowezekana!”    Mchakato  wa  mawazo  ya  ubunifu  unahusisha  muunganiko  wa  maamuzi  na  kazi  ambazo  humfahamisha  msanifu/mbunifu.    “Usanifu/ubunifu  sio  tu  unafanya  vitu  kuwa  vizuri,  ila  inafanya  vitu  vifanye  kazi”  (Dadich,  2013).    Ubunifu  bora  unaweza  kuelezewa  na  kanuni  kumi  

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     13  

17

(Vitsoe,  2013).      Zinajumuisha    • Ubunifu  mzuri  ni  wakiuvumbuzi  • Ubunifu  mzuri  hufanya  bidhaa  kuwa  na  thamani  zaidi  • Ubunifu  mzuri  ni  ujumi  • Ubunifu  mzuri  hufanya  bidhaa  ieleweke  • Ubunifu  mzuri  hauna  kikwazo  • Ubunifu  mzuri  ni  nyoofu/aminifu  • Ubunifu  mzuri  unadumu  kwa  muda  mrefu  • Ubunifu  mzuri  ni  kamilifu  hadi  mwisho  wa  utondoti  • Ubunifu  mzuri  ni  rafiki  kwa  mazingira  • Ubunifu  mzuri  ni  usanifu  mdogo  kadri  

inavyowezekana.    

18

Kubuni  wazo  ni  mchakato  kwa  ajili  ya  kutatua  matatizo,  na  kipekee  inajumuisha  hatua  saba:  fasili,  tafiti,  jenga  wazo,  sampuli  kifani,  kuchagua,  utekelezaji,  na  kujifunza.        Fasili  • Kuamua  ni  jambo  gani  unalojaribu  kulitatua  • Kukubaliana  juu  ya  hadhira  ni  nani  • Bainisha  kipi  kitakachofanya  mradi  ufanikiwe.    Utafiti  

• Pitia  upya  historia  ya  suala/tatizo;  jaribu  kubainisha  kwa  nini  ni  tatizo?  

• Kusanya/shirikisha  mifano  ya  jitihada/majaribio  mengine  kutatua  tatizo/suala  hilo  hilo  

• Zungumza  na  watu  wenye  tatizo  hilo  au  waliowahi  kukumbana  na  tatizo  hilo  

Dhana/wazo  • Onyesha  mahitaji  na  motisha  kwa  watumiaji  wako.  

 

Mara  kwa  mara,  waelimishaji  wamekuwa  wakihitajika  kuwa  wabunifu  wa  uzoefu  wa  kujifunza      

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     14  

   

19

• Zalisha  mawazo  mengi  kadri  inavyowezekana  kuhudumia  mahitaji  yaliyooneshwa  

• Chora  dhana/mawazo  mengi  kadiri  iwezekanavyo  • Usiamue  wala  kujadili  juu  ya  mawazo/dhana  • Wakati  wakubungua  bongo,  kuwa  na  mazungumzo  

au  usaili  mmoja  tu  kwa  wakati  

Sampuli  kifani/Sampuli  ya  awali  • Unganisha,  tanua,  na  fasili  mawazo.  • Unda  kielelezo  zaidi  ya  kimoja  • Omba  mrejesho  kutoka  kwa  kundi  lenye  watu  

tofautitofauti,  wajumuishe  watumiaji  wako  • Washirikishe  wenzako  sampuli  kifani  yako  • Hifadhi  maamuzi  na  endeleza  kutopendelea  upande  

wowote    • Unda  na  wasilisha  kazi  halisi  ya  sampuli  kifani/vifani  

20

Chagua  • Pitia  upya  lengo  • Weka  pembeni  hisia  na  umiliki  wa  mawazo  • Epuka  kufikiri  kwa  makubaliano  • Kumbuka:  suluhisho/ufumbuzi  unaoweza  kutendeka  

sio  wakati  wote  ni  bora  • Chagua  mawazo  yenye  uwezo/nguvu  zaidi  

Tekeleza  • Tengeneza  maelezo  ya  sampuli  • Fanyia  kazi/tekeleza  • Jaribu  wazo  lako  na  watumiaji  wenzako  

Kujifunza  • Kusanya  mrejesho  kutoka  kwa  m/watumiaji  • Bainisha  kama  ufumbuzi/majibu  yamefikia  malengo  • Jadili  kipi  kinachoweza  kuboreshwa  • Pima  mafanikio;  kusanya  data  • Nyaraka    

Ingawaje  ubunifu  wakati  wote  unategemea  ladha  ya  mtu  binafsi,  wafikiriaji  wa  ubunifu  wana  misingi  ya  pamoja,  inayowaongoza  kuendesha  ugunduzi:  misingi  hii  kiujumla  ni  ubunifu,  uwezo  wa  kutumia  mikono  yote  miwili  kwa  usawa,  kufanya  kazi  kwenye  timu,  malengo  kwa  mtumiaji  wa  mwisho,  udadisi  (Wikipedia,  n.d.).  

Shule  ya  Stanford  inatoa  mlolongo  mrefu  wa  zana  za  ubunifu  wa  mawazo.    Tafadhali  peleleza/tembelea  http://dschool.stanford.edu/dgift/  

1.6.2.  Kuunganisha  kwenye  Elimu  Kuna  ongezeko  la  waelimishaji/walimu  kuhitajika  kuwa  wabunifu  wa  uzoefu  wa  kujifunza  kama  ilivyopendekezwa  na  ripoti  ya  OECD  iliyoshirikishwa  katika  kipengele  cha  1.2.  Harakati  za  utengenezaji-­‐mtazamo  wa  kidunia.  Huu  ni  mhamo  kutoka  majukumu  yaliyopita  kama  watekelezaji  au  wafasili  wa  mtaala.    Njia  bora  ya  kushirikisha  ubunifu  wa  mawazo  darasani  ni  kuutumia  kuwasaidia  wanafunzi  kwa  makusudi  kutafuta  uhusiano  kati  ya  uzoefu  wa  ujifunzaji  halisi  na  matatizo  ya  kimtaala.        Kwa  sababu  ya  msisitizo  juu  ya  uwezo  wa  kuhisi  maono  ya  wengine,  ubunifu  wa  mawazo  unawaalika  walimu  na  wanafunzi  kulenga  katika  ubunifu  uliyojikita  kwa  binadamu  na  kufiriki  juu  ya  vitu  vya  msingi  vyakuzingatia.    Inalandana  vizuri  sana  na  mradi  wa  STEMx  wenye  misingi  ya  kushirikisha  mchakato  wa  kufikiri  kwa  ubunifu  –  

Fikra  bunifu  na  kutengeneza  muunganiko  wakupendeza!    

Sampuli  kifani:  unganisha,  kuza  na  rekebisha  mawazo.    

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     15  

21

dhania,  jenga,  cheza,  shirikisha,  tafakari,  (Resnick,  2007)  kwenye  utendaji  wao  ambapo  “unaakisi  njia  ya  asili  ambayo  watoto  wadogo  wanajifunza  na  kucheza”  (Martinez  &  Stager,  2013).  Fikra  bunifu  na  kutengeneza  vinalandana  vizuri  sana!        Angalizo  moja  hata  hivyo,  kama  ilivyo  kwa  kila  mchakato,  heshimu/fuata  hatua.  Amini  mchakato.  Hakuna  njia  ya  mkato  katika  ugunduzi!    1.7.  Upimaji  Upimaji  ni  sehemu  muhimu  ya  mtaala.  Kimsingi,  upimaji  unatakiwa  kufanyika  kwa  wakati  mmoja  na  ufundishaji        na  ujifunzaji  wakati  wote  wa  uwezeshaji  wa  kozi.  Katika  mchakato  wa  kutengeneza,  upimaji  unasaidia  kama      nguvu  ya  kuendesha  inayofanya  utengenezaji  uwe  kwenye  mstari  na  kuhakikisha  kwamba  kuna  ushahidi  wa  kujifunza  (au  kutokuwepo  kwa  ushahidi).      Upimaji  endelevu  unaojulikana  pia  kuwa  ni  upimaji  kwa  ajili  ya  kujifunza  ndio  unaendesha  machakato  kutoka  hatua  moja  hadi  nyingine.  Upimaji  endelevu  uliofanywa  na  wewe,  wenzako  na  wawezeshaji  unachangia  kukamilisha  matokeo/bidhaa.  Upimaji  endelevu  unafanywa  wakati  wanafunzi  wanashirikishana  mawazo,  wanapochora  na  kushiriki  katika  mchakato  wa  kuunda  sampuli  kifani/mfano.  Wakati  wa  kipindi  hiki,  mwalimu  anaweza  kusimamia  na  kusaidia  wanafunzi  kuhakikisha  kuwa  wanapata  matokeo  mazuri.  Upimaji  endelevu  unachangia  kuzalisha  sampuli  kifani  ambayo  baadaye  inatathminiwa  na  mhusika  mwenyewe,  washiriki  wengine  na  mwezeshaji  wakati  wa  matembezi  ya  galari.  Bidhaa  halisi,  rekodi  ya  maelezo  ya  sampuli  inaweza  ikatumiwa  kwa  upimaji  na  ushahidi  wa  uwezo  wa  wanafunzi.  

 1.8.    Njia  za  Kiasili  za  Ufahamu/Kuelewa  Utendaji  wa  ujengaji  dhana  unatoa  motisha  ya  ujengaji  wa  maarifa  kutoka  maafira  ya  mwanzo  (angalia  kipengele  cha  1.5.2.).  Njia  za  kiasili  za  kujua/kuelewa  (au  hazina  ya  maarifa  ya  kiasili)  ni  chanzo  bora  cha  maarifa  ya  mwanzo/awali.  Wanafunzi  wanakuja  shuleni  na  akiba  ya  kiasili  ya  kufahamu  ambao  unawakilisha  njia  ya  maisha  ya  jamii.  Maarifa  hayo  yanajumuisha:    imani  na  desturi  za  asili,  utengenezaji/uundaji  wa  vitu  (vifaa,  sanaa,  ufundi),  zana  za  kimazingira  (mimea  na  wanyama),  mifumo  ya  kujifunza,  uainishaji,  sheria,  vifaa,  aina  za  mawasiliano  na  

22

taasisi.  Imani  na  desturi  za  asili  kwa  mfano,  inaweza  ikatoa  mwanzo  mzuri  kwa  ujuzi  anuai  wa  lugha  ambapo  ufundi  na  vifaa  vinaweza  kuvutia  ubunifu  husika  na  ujumi  kwa  usanifu  mpya  au  ulioboreshwa.  Uainishaji  na  zana  za  kimazingira  inawezakuwa  hatua  nzuri  ya  kuanzia  kwa  ujuzi/ufahamu  wa  hisabati  na  sayansi.  Nyongeza  ya  hapo,  maarifa  ya  awali  yanawezakuwa  ufunguo  wa  kubainisha  kile  ambacho  kina  landana  na  muktadha  na  kinachofaa,  kitu  muhimu  cha  kuzingatiwa  kwa  ugunduzi  endelevu  na  kuingilia  kati.    

 

 

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     16  

   

23

1.9.  Kitaaluma  –  Kutengeneza  Kisa  Mkasa  kwa  Uzoefu  wa  Kina  na  Endelevu    Utafiti  juu  ya  ufundishaji  bora  na  nadharia  ya  mabadiliko  ya  kielimu  ipo  wazi  –  walimu  wanahitaji  fursa  endelevu  za  kujifunza  kama  wanahitajika  kutumia  njia  mpya,  kufuata  harakati  za  Wizara  ya  Elimu,  na  kuendelea  kulandana  na  kuwa  imara/na  wenye  sauti  katika  kazi  zao.    Walimu  lazima  washiriki  katika  mafunzo  ya  kudumu  kwenye  kazi  zao,  ni  kwa  sababu  hiyo  hiyo  ambayo  wataalamu  wengine  kama  vile  wanafizikia  na  manesi  wanafanya-­‐ili  kubakia  wakisasa,  kusoma  njia  mpya,  na  kuunda  jamii  ya  wataalamu  kiutendaji  na  kusaidia.    Kwa  walimu  wengi,  kufikiwa  na  maendeleo  ya  kitaaluma  ni  vigumu  kutokana  na  gharama  za  usafiri  na  upatikanaji  wake.    Pia,  kwa  mara  nyingi  kwa  ujumla  wake,  mafunzo  ya  kitaaluma/maendeleo  ya  kitaaluma  yanatolewa  katika  hali  ya  ‘kukaa  na  kupokea’  mfumo  wa  usomaji  usioshirikishi.    Boksi  hili  la  vifaa/mkusanyiko  huu  wa  vifaa,  kupeleka  utengenezaji  mashuleni:  boksi  la  vifaa  kwa  ajili  ya  ugunduzi  na  mabadiliko  katika  kufundisha  na  kujifunza,  unatoa  njia  mbalimbali.    Umesanifiwa  kukusaidia  kuwezesha  kisa  mkasa  kwa  mawazo  ya  kina  kwa  mafunzo  ya  kitaaluma  kwa  walimu  wanaojifunza.  Inaweza  pia  ikatumika  na  waelimishaji/walimu  wengine  kuwatambulisha  kwenye  Ubunifu  wa  wazo  na  kutengeneza.      Kipengele  cha  2.1.  Kinatoa  sampuli  ya  ajenda  kwa  undani  wa  siku  moja  wa  tukio  la  maendeleo  ya  kitaaluma.    Kipengele  cha  Undani  wa  siku  kinahitaji  washiriki  kuzingatia  kwa  makini  na  kushiriki  kikamilifu  katika  usanifu  wa  mawazo  na  kutambua  tatizo  kwa  ubunifu.  Katika  sehemu  muhimu  ya  siku  ni  utamaduni  wa  kutengeneza  ambao  “unathamini  kujifunza  kwa  ujuzi  wa  moja  kwa  moja  na  uwezo  wa  kufikiri  na  faida  za  kijamii  ambazo  zinaongezeka  kutoka  uundaji  wa  kitu  cha  kushirikishana"  (Martinez  &  Stager,  2013).    Pia  ina  unganisha  fikra  bunifu  na  kutengeneza  kwa  ujuzi  wa  kimtaala  unaotakiwa  kwa  Afrika  ya  mashariki.    Mafunzo  ya  kitaaluma  kwa  undani  yanatambua  kuwa  ni  vigumu  kushirikishana  vitu  vya  msingi  ambavyo  hatujawahi  kuwa  na  uzoefu  navyo  kwa  kina.  Kama  walimu  watapeleka  utengenezaji  mashuleni  kwao,  tunaamini  waelimishaji/walimu  wanahitaji  kushiriki  kikamilifu  katika  uzoefu  wa  siku  nzima  kuwasaidia  kujisikia  jasiri  na  kumiliki  mawazo  ya  fikra  bunifu,  kufumbua  tatizo,  kutengeneza  kwa  kushirikiana,  kuheshimiana/kuchukuliana  na  kuhakiki/kukosoa  kwa  moyo  mkunjufu/kiurafiki,  na  kutafakari.  

24

 Rejea    Crichton,  S.  &  Carter,  D.  (2015).  Taking  Making  Into  the:  An  Immersive  Professional  Development  Approach.  In  M.  Niess  &  H.  Gillow-­‐Wiles  (Eds.).  Handbook  of  Research  on  Teacher  Education  in  the  Digital  Age.  IGI  Global.    Dadich,  S.  (August,  2013).    The  age  of  invisible  design    has  arrived.    Retrieved  from  http://www.wired.com/design/2013/08/the-­‐age-­‐of-­‐invisible-­‐design/      Dougherty,  D.  (2013).  The  maker  mindset.  In  M.  Honey  &  D.  Kanter  (Eds.),  Design,  Make,  Play:  Growing  the  Next  Generation  of  STEM  Innovators  (pp.  7-­‐11).  New  York,  NY:  Routledge.    Hatch,  M.  (2014).    The  Maker  Schools  Movement  Manifesto:  Rules  for  Innovation  in  the  New  World  of  Crafters,  Hackers,  and  Tinkerers.    NY:  McGraw-­‐Hill.  Kalantzis,  M.  and  Cope,  B.  (2012)  Literacies.CUP  Martinez,  S.  &  Stager,  G.  (2013).    Invent  to  learn:  Making,  tinkering,  and  engineering  in  the  classroom.    Torrance,  CA:  Constructing  Modern  Knowledge  Press.    Organization  for  economic  co-­‐operation  and  development  (OECD).  (May  2011).    Innovative  learning  environments  –  A  leading  OECD/CERI  project.    Retrieved  from  http://www.innovations.sa.edu.au/files/links/ILEMay.pdf    Resnick,  M.  (2007).    All  I  really  need  to  know  (about  creative  thinking)  I  learned  (by  studying  how  children  learn)  in  kindergarten.    Paper  presented  at  the  Proceedings  of  the  6th  ACM  SIGCHI  conference  on  Creativity  &  Cognition.  Thomas,  D  and  Brown,  J.S.  (2011)  .  A  New  Culture  of  Learning:  Cultivating  the  Imagination  for  a  World  of  Constant  Change.  Createspace  Independent  Publishing  platform    Vitsoe.  (2013).    Dieter  Rams:  ten  principles  for  good  design.    Retrieved  from  https://www.vitsoe.com/us/about/good-­‐design      United  Nations,  2015  http://www.un.org/millenniumgoals/    United  Nations,  2014  https://sustainabledevelopment.un.org/topics/sustainabledevelopmentgoals/      Wikipedia.  (n.d.).    Design  thinking.    Retrieved  from  http://en.wikipedia.org/wiki/Design_thinking    

25

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     17  

2.  Uwezeshaji  wa  Warsha  ya  Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni  

Changamoto  ya  Ubunifu  wa  Sampuli  Ubunifu  huu  wa  sampuli  ulitumika  wakati  wa  jaribio  na  walimu  Turiani,  mkoa  wa  Morogoro.    Usuli  Walimu  wa  shule  za  vijijini  na  zile  zisizofikika  kwa  urahisi  mara  nyingi  huhangaika  kutafuta  zana  za  kufaa  kusaidia  ujifunzaji  ambao  mwanafunzi  ni  kitovu  cha  maarifa,  ujifunzaji  shirikishi.    Wakati  wote  wanasahau  kuwa  zana  zilizonyingi  zenye  thamani  kubwa  zimekaa/zinapatikana  mbele  yao  au  nje  tu  ya  milango  ya  madarasa  yao.        Sabubu/Misingi  ya  Ubunifu  Walimu  Tanzania  wanatarajiwa  kupata  Matokeo  Makubwa  Sasa  katika  madara  yao.  Wengi  wanapambana/wanahangaika  kufahamu  maana  ya  elimu  ya  matokeo  ilivyo  na  namna  ya  kuendeleza  kazi  za  kujifunza  kwa  ushiriki  kwa  ajili  ya  wanafunzi  wao.    Kazi  yako  Kundi  lako  limepewa  kazi  ya  kuunda  sampuli  ya  zana  ya  kujifunzia  inayosaidia  wanafunzi  kujifunza  ustadi  muhimu  unaopelekea  Matokeo  Makubwa  Sasa.    Sampuli  yako  ya  zana  lazima  ihamasishe  na  kusaidia  ujifunzaji  ambapo  mwanafunzi  anakuwa  ni  kitovu  cha  maarifa,  ujifunzaji  shirikishi.    Mafanikio  ya  Sampuli  ya  Zana  yako  Yatabainishwa  na  :  • Sampuli  inaweza  kutengenezwa  kwa  kutumia  vifaa  

vilivyopo?  • Sampuli  inaweza  kutengenezwa  kwa  kutumia  vitu  

vinavyopatikana/vilivyopo  katika  mazingira  ya  asili?  • Sampuli  inasaidia  ujifunzaji  muhimu  wa  ustadi/uhodari  

kundi  lako  lilipochagua  wakati  wa  kazi  ya  fikra  bunifu?  • Walimu  wengine  wanaweza  wakatengeneza  maana  juu  ya  

sampuli  na  kuona  faida  yake  kwenye  madarasa  yao?    Vigezo  • Lazima  utumie  vitu/vifaa  kutoka  kwenye  Mkusanyiko  wa  

Vifaa  vya  Utengenezaji  ulivyoshirikishwa.  • Lazima  utumie  vitu  unavyoweza  kuvipata  katika  mazingira  

yanayokuzunguka  • Lazima  ukamilishe/ujaze  karatasi  ya  Maelezo  ya  Sampuli  • Lazima  uwe  na  sampuli  unayoifanyia  kazi  kwa  ajili  ya  

matembezi  ya  galari      

1

Lengo  la  warsha  ni  kuhamasisha  washiriki  kupata  uzoefu  wa  kutengeneza  kupitia  fikra  bunifu  na  shughuli  za  kufanya  kwa  mikono.  Hali  ya  kurudia  rudia  ya  njia  ya  kushiriki  kwa  undani  huwa  inawezekana  kwa  kuletekeza  kupeleka  warsha  ya  utengenezaji  kwenye  mashule  zaidi  ya  siku  2-­‐3  mfululizo.  Ukiweza  kufanikisha  hilo,  tunapendekeza  utumie  ujenda  moja  kila  siku.  Hii  inaruhusu  washiriki  kupata  uelewa  wa  kina  wa  mchakato.  Tuligundua  kazi  yao  inaboreka/inaimarika  kila  wakirudia  mchakato  wa  kubuni,  kutengeneza  na  kutafakari  hatua.    Kupeleka  utengenezaji  kwenye  mashule  hutambulisha  washiriki  katika  kutengeneza  na  uendelezaji  wa  vifaa/vitu  kwa  kulenga  elementi  tano  zinazotofautiana  huku  bado  zikihusiana:  • Changamoto  ya  ubunifu    • Mchakato  wa  fikra  bunifu  • Majibu/ufumbuzi  wa  ubunifu  kupitia  utengenezaji  

wa  kushirikiana  • Matembezi  ya  galari  • Tafakari    

2.1.  Ajenda  ya  Sampuli  

Mwisho  wa  sehemu  hii  (Kurasa  21  na  22),  Ajenda  ya  Sampuli  na  muda  uliopendekezwa,  usomaji  wa/vitabu  vya  awali  na  vitu/vifaa  vinavyohitajika  vimetolewa.    

2.2.  Elementi  za  Warsha  

2.2.1.  Changamoto  ya  ubunifu  

Fikra  bunifu  na  kutengeneza  ni  mchakato  na  shughuli  za  kufurahisha.  Lakini,  walimu  wanahitaji  kitu  fulani  kufikiri  na  kutengeneza  wakati  wanapounda/kuumba  vitu/vifaa  vya  elimu.  Hapa  ndipo  changamoto  ya  ubunifu  inapotumika.  Changamoto  ya  ubunifu  inalenga  kila  kundi  la  walimu  katika  kazi,  inaruhusu  mwezeshaji  kushirikisha  kundi/kikundi  katika  mchakato  wa  ubunifu.      Katika  kazi  ya  kufundisha  na  kujifunza,  tunajua  kuwa  kumaliza  mtaala  kirahisi  kwa  kutumia  njia  ya  muongozo  wa  mwalimu,  inachangia  kidogo  katika  kuboresha  kujifunza  na  pia  inasaidia  kwa  uchache  udadisi.  Ilipendekezwa  kuwa  chini  ya  asilimia  10  ya  kile  kilichofundishwa  kinahifadhiwa  miaka  miwili  baadaye  

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     18  

 

2

(Lambert,  2012).  Kufundisha  kwa  kutumia  zaidi  njia  ya  kujifunza  kwa  ghibu  (kukariri)  sio  jibu.    Nchi  kama  vile  Singapo  tayari  wameshabadilisha  kabisa  sera  zao  za  taifa  na  kufuata/  kutekeleza  harakati  kama  vile  Fundisha  Kidogo  Jifunze  Zaidi.  Harakati  hizi  zilianza  mwaka  2006  kama  njia  ya  kusaidia    “walimu  na  mashule  kulenga  kwenye  misingi  ya  kufundisha  kikamilifu,  ili    …  wanafunzi  washirikishwe,  kujifunza  kwa  kuelewa,  na  waendelezwe  kwa  ujumla,  mbali  ya  kujiandaa  kwa  majaribio  na  mitihani.  …  [imezitaka  shule  kubadilika  juu  ya]  mtaala  (kipi  cha  kufundisha),  njia  za  kufundisha  (sayansi  ya  kufundisha)  (namna  ya  kufundisha)  na  upimaji  (kwa  kiasi  gani  wanafunzi  wamejifunza)”  (Wizara  ya  Elimu  ya  Singapo,  2015).  Wakati  sio  mashabiki  wakuu  wa  ushindani    wa  juu  wa  mitihani,  matokeo  ya  PISA  ya  mwaka  2012,  ambapo  ilikuwa  mwaka  wa  kwanza  kupima  ufumbuzi  wa  tatizo  kwa  ubunifu,  imeiweka  Singapo  #1  …  Kanada  ilikuwa  ya  5th  ilifuatiwa  na  Finlendi  7th  na  Amerika  13th  (http://www.oecd.org/pisa/singapore-­‐and-­‐korea-­‐top-­‐first-­‐oecd-­‐pisa-­‐problem-­‐solving-­‐test.htm).  Sampuli  za  aina  za  maswali  yalioulizwa  yanaweza  kupatikana  kwenye  http://www.oecd.org/pisa/test/.      Tunaona  njia  ya  makusudi  ya  kupeleka  utengenezaji  kwenye  mashule  yetu  ni  kwa  kukusudia  kuunganisha  mchakato  wa  kutengeneza  (kusanifu,  kutengeneza,  kufanya  jaribio,  kutafakari)    kufikiri  kwa  kina  changamoto  ya  ubunifu  kwa  ustadi  unaohitaji  washiriki  kupata  uwezo  wa  kuhisi/kubainisha  mawazo  ya  mwingine  na  kuzingatia  mawazo  mapya.  Changamoto  ya  ubunifu  inatoa  maudhui  ya  mitaala.    Kuunda  changamoto  ya  ubunifu  Uzoefu  wetu  unapendekeza  kuna  njia  tatu  za  msingi/awali  kuunda  changamoto  ya  ubunifu:    • Kama  swali  la  udadisi    • Kama  tatizo  linalohitaji  ufumbuzi  • Kama  hali  ya  kucheza      1. Udadisi    unaruhusu  mtaala  kuweza  

kuchunguzwa/kupelelezwa  kwa  ujuzi  wa  usomaji  halisi  (Alberta  Learning,  2004)  –  mchango  mkuu  wa  KUTENGEZA  kwenye  kazi  za  kufundisha  na  kujifunza.  Ujifunzaji  halisi  unahamasisha  wanafunzi  kudadisi  katika  vitu  ambavyo  ni  halisi  na  vinavyowavutia  wao.  Inaweka  kazi  za  kujifunza  kama  matatizo  yanayohitaji  ufumbuzi.  Edutopia  ina  tovuti  ya  vifaa  

3

vya  kushirikiana/kutumia  kwa  pamoja,  dondoo  na  mawazo  juu  ya  ujifunzaji  uliojikita  kwenye  tatizo/fumbo.  (http://links.edutopia.mkt5094.com/ctt?kn=17&ms=NzE3NDM0OAS2&r=MjcyODg5NjI0MjMS1&b=0&j=OTMyNDg3NjYS1&mt=1&rt=0)  

 2. Ufumbuzi  wa  tatizo  ni  “mchakato  wa  kifikra/kiakili  

uliolekezwa  kufanikisha  lengo  pindi  ambapo  hakuna  njia  ya  jibu  la  moja  kwa  moja  kwa  mtatua  tatizo/fumbo”  (Mayer  &  Wittrock,  2006,  uk.  287).  Wanaeleza  wanafunzi  wanahitaji  aina  tano  za  maarifa  kuweza  kuwa  wafumbuzi  wa  matatizo  wenye  mafanikio:  

 • Uhalisia:  maarifa  juu  ya  tabia  za  elementi  au  

matukio,  kama  vile  kuna  senti  100  kwenye  dola  ya  Kanada;  

• Dhana:  maarifa  ya  aina,  kanuni  au  modeli,  kama  vile  kujua  mahali  gani  thamani  inamaanisha  katika  hisabati  au  namna  gani  hewa  yenye  joto  inaongezeka  kwenye  sayansi;  

• Mikakati  :  maarifa  ya  njia  za  jumla,  kwa  mfano  namna  ya  kuvunja  tatizo  kuwa  katika  sehemu  au  namna  ya  kutafuta  tatizo  linalofanana;  

• Hatua:  maarifa  ya  hatua  mahsusi,  kama  vile  namna  ya  kukokotoa  kuzidisha  kwa  njia  ndefu  au  namna  ya  kubadili  waneno  kutoka  hali  ya  umoja  kwenda  wingi;  na  

• Imani:  utambuzi  wa  tatizo  la  mtu-­‐ujuzi  wa  kulitatua  (kama  vile  “mimi  sio  mzuri  wa  hisabati”)  au  kuhusu  asili  ya  utatuzi  wa  tatizo  (mf,  “kama  mmojawapo  hawezi  kufumbua/kutatua  tatizo  moja  kwa  moja,  mhusika  hataweza  kabisa  kulitatua”).    

3. Matukio  ya  maonesho  ni  mtindo  wa  habari  au  simulizi.  Yanaweza  yakatumika  kutambulisha  wanafunzi  katika  kazi  mradi.  Lengo  la  mfano  wa  tukio  ni  kuweka  mandhari  ya  kazi  mradi  na  kuunda  pointi  ya  kuanzia  kwa  pamoja.  Mfano  wa  tukio  pia  una  vigezo  vya  kazi  mradi,  kuorodhesha  jambo  lolote  linalozuia,  hali  maalumu  na  muda/vikwazo  vya  muktadha.  Matukio  ni  njia  za  ubunifu  za  kudhania  “tofauti  ya  wakati  ujao”  au  njia  mbadala  ya  kufanya  kitu  fulani.  Yanasaidia  wanafunzi  kupata  taswira  ya  muktadha  kwa  ajili  ya  kazi  kwa  kuwa  wakati  wote  inahusisha  mazingira,  jamii,  ufundi/utaalam,  siasa  na  

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     19  

4

masuala  ya  uchumi.      Kwa  nini  tunapendelea  matukio  ya  changamoto  ya  usanifu  Tulishirikishana  kwa  ufupi  njia  tatu  za  kuunda  changamoto  ya  usanifu.  Kuna  njia  zingine  nyingi,  na  tuna  uhakika  utapata  moja  ambayo  inakufaa  vizuri  zaidi  kwa  mtindo  wako  wa  kufundisha.  Tunapendelea  kuziweka  changamoto  za  usanifu  kama  shughuli  za  maendeleo  za  siku  ya  mtengenezaji  mtaalam  zinakamilishwa  katika  vikundi  vidogo  vya  watu  wane.  Tukio  linasaidia  njia  ya  kikundi.  Kipekee,  tunajaribu  kufanya  makundi  mchanganyiko  na  kujaribu  kufanya  ujifunzaji  wenye  kuhusisha  masomo  mbalimbali  kadiri  inavyowezekana.      Matukio  ya  maonesho  yanajumuisha  sehemu  zifuatazo  • Maelezo  ya  jumla  ambayo  yanatoa  usuli  kwa  ajili  ya  

changamoto.  • Sababu  za  kimaantiki  zinazotoa  muktadha  wa  

hisabati  kuwa  kwa  nini  changamoto  ni  muhimu.  • Mfano  wa  tukio  linaloweka  changamoto  ndani  ya  

kundi  ambalo  limeulizwa  kutatua/kufumbua.  • Viashiria  vya  mafanikio  vinavyotoa  vigezo  kwa  

namna  ufumbuzi  wa  ubunifu  utakavyopimwa/utakavyotathminiwa  au  tathmini  ya  wawashiriki  wengine  wakati  wa  matembezi  ya  galari.    

• Vigezo  au  kanuni  na  mipaka  ambayo  makundi  yanatakiwa  kufuata  au  kuzingatia.  

 2.2.2.  Mchakato  wa  Fikra  Bunifu  –  Karatasi  ya  Kazi  ya  Washiriki  

Pindi  utakapokuwa  umeandaa  washiriki  wako  katika  makundi  madogo,  unaweza  ukaanza  kazi  ya  kubuni  wazo.  Kwa  dondoo  juu  ya  namna  ya  kuandaa  makundi,  angalia  sehemu  ya  3.1  Kuunda  makundi.      Karatasi  ya  mfano  ya  kazi  imejumuishwa  kwenye  sehemu  ya  5.2.  Kama  bajeti  yako  inaruhusu,  tafadhali  chapa  nakala  moja  ya  karatasi  hii  ya  kazi  kwa  kila  mshiriki.  Karatasi  ya  kazi  inatakiwa  ichapwe  pande  zote  mbili  kwenye  karatasi  yenye  ukubwa  wa  A3.  Kama  huwezi  pata  kinukuzi  au  huwezi  kumudu  kutoa  nakala,  washirikiki  wanaweza  wakatengeneza  matoleo  yao  wenyewe  ya  karatasi  ya  kazi  kwa  kutumia  karatasi  tupu  ya  ukubwa  wa  A3.    Sehemu  ya  5.1.  inatoa  mwongozo  wa  mwezeshaji  kukusaidia  kufuata  muda  katika  hatua  za  mchakato  na  inatoa  maelekezo  kwa  washiriki.  Tafadhali,  pitia  upya  

5

mwongozo  kabla  ya  kuwezesha  warsha  yako,    

2.2.3.  Mchakato  wa  Fikra  bunifu  –  Mwongozo  wa  Mwezeshaji  

Fikra  bunifu  ni  mchakato  unaowezeshwa  na  uliopangiwa  muda.  Unahitaji  washiriki  wa  warsha  kufanya  kazi  kwenye  makundi  madogo  kuzingatia  ufumbuzi  kwa  changamoto  ya  ubunifu.  (Sehemu  2.5.2).  Mchakato  wa  fikra  bunifu  ulianzishwa  katika  chuo  kikuu  cha  Stanford  karibu  na  bonde  la  Silicon    –    moyo/kiini  cha  ugunduzi  wa  usanifu  na  maendeleo  ya  kompyuta.    Mapema  kabla  ya  kuanza  kwa  kazi  ya  fikra  bunifu,  unaweza  ukahitaji  kutambulisha  kwa  washiriki  dondoo  rahisi  za  uchoraji  (Sehemu  3.2).  Watu  wazima  wengi  hawapo  tayari  kuchora,  kwa  hiyo  huu  ni  wakati  muafaka  kuwasaidia  kukumbuka  furaha  waliyokuwa  nayo  wakiwa  watoto  wakichora  dunia  yao.  Pia,  kwa  sababu  washiriki  wanaenda  kutengeneza  sampuli  kifani/awali  (modeli  za  vitu  halisi  vilivyopimwa)  michoro  ni  muhimu  sana  kuliko  dhana  dhahania  zilizoelezewa  kwa  maneno  tu.    Wambie  washiriki  juu  ya  sehemu  zote  za  mchakato  ili  usichukue  njia  ya  mkato:  •  Changamoto  ya  ubunifu  • Mchakato  wa  kufikiri  juu  ya  ubunifu  • Maelezo  ya  sampuli    • Matembezi  ya  galari  • Tafakari    Hakikisha  unasoma  maelekezo  yafuatayo  kabla  ya  kuwezesha  warsha  yako.  Utahitaji  kuwa  na  chombo  cha  kutunza  wakati  (simu  ya  mkononi  inafaa  sanaa,  hususani  kama  itakuwa  saa  ya  kidijitali).    

2.2.4.  Maelezo  ya  Sampuli  Karatasi  ya  maelezo  ya  sampuli  inatoa  tafakari  kwa  washiriki.  Tafakari  ni  jambo  muhimu  la  ujifunzaji  wa  kitaaluma  na  ukuaji.  Walimu  /waelimishaji  wanahitaji  fursa  kusoma  ili  kuwa  watendeji  wa  kutafakari  –mtu  ambaye  hufikiri  juu  ya  kile  walichokifanya  na  kujaribu  kusaidia  matendo  yao  katika  matokeo  mahsusi  au  ujuzi.      Kazi  ya  kuelezea  sampuli  inaalika/inakaribisha  washiriki  wa  warsha  kuzingatia  changamoto  ya  ubunifu  waliyopewa  na  kutafakari  juu  ya  mpango  sanifu  na  kazi  za  utengenezaji.  Pia  ni  kifaa  kwa  ajili  ya  kuchangia  mawazo  bora  ya  vifaa.  Mwalimu  mratibu  wa  kituo  cha  maarifa  cha  walimu  ambaye  ni  mwenyeji  wa  warsha  

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     20  

6

anaweza  akahitaji  kukusanya  maelezo  ya  sampuli  na  kuunda  benki/hifadhi  ya  vifaa  vya  mawazo  bora  zaidi  na  mifano  ya  walimu  wanaotembelea  kituo  cha  maarifa  cha  walimu  kwa  ajili  ya  kukitumia.  

2.2.5.  Matembezi  ya  galari    Matembezi  ya  galari  ni  njia  ya  kusherehekea  kitendo  cha  ubunifu  na  kutengeneza.  Matembezi  ya  galari  inawafanya  washiriki  wote  kuona  namna  mchakato  wa  uundaji  unavyowezakustaajabisha.  Washiriki  wana  fursa  ya  kuona  tofauti  gani  ufumbuzi/majibu  yalivyo,  kukumbuka  kila  mmoja  alianza  na  changamoto  ya  ubunifu  unaofanana,  mchakato  wa  ubunifu  na  fursa  sawa  ya  kufikia/kupata  vifaa  na  vitendea  kazi.    Matembezi  ya  galari  ni  aina  ya  kukua  kwa  taaluma  na  tafakari.  Washiriki  wanatakiwa  kuhamasishwa  kuuliza  maswali  rahisi,  magumu  kwa  nidhamu  na  kutoa  maoni.    Kipekee,  katika  matembezi  ya  galari,  mwanakikundi  mmoja  kutoka  kila  kikundi  anakaa  na  sampuli  kifani  ya  kikundi,  kujibu  maswali  na  kutoa  maelezo  ya  tatizo  na  mchakato.  Wanakikundi  wanahamasishwa  kuonesha  onesho  la  kikundi  chao  ili  wanakikundi  wote  waweze  kuona  sampuli  kifani  ya  kila  kikundi.  

 

2.2.6.  Tafakari  Tafakari  ni  elementi  muhimu  ya  ukuaji  kitaaluma.  Muda  lazima  utolewe  kwa  washiriki  kufikiri  juu  ya  ujifunzaji  na  namna  itakavyoweza  kutoa  taarifa  juu  ya  utendaji  wao.      Tafakari  ya  washiriki  pia  ni  muhimu  kwa  ajili  ya  

7

mwezeshaji  wa  warsha  kwa  kuwa  zinatoa  maono  juu  ya  ujifunzaji  wa  washiriki,  changamoto  za  warsha,  umuhimu  wa  hatua  inayofuata  kwenye  ujifunzaji  wa  kikundi,  na  mapendekezo  kwa  ajili  ya  warsha  zitakazofuata.  Pindi  washiriki  wakikamilisha  tafakari  zao  kwenye  #8  ya  karatasi  ya  washiriki  ya  fikra  bunifu,  unaweza  ukahitaji  kutumia  muda  kutafakari  juu  ya  warsha  na  kuandaa/kuplani  mabadiliko.    2.3.  Tathmini  ya  Warsha  ya  Kitaalam  ya  Kujifunza    Mrejesho  wa  washiriki  ni  muhimu  kwa  kuwa  unajifunza  kutoka  katika  ujuzi  wa  uwezeshaji  wako  na  kufanya  mabadiliko  yoyote  muhimu  kwa  ajili  ya  warsha  ijayo.  Tathmini  ya  warsha  inawezakuwa  inahitajika  kutoka  kwa  wafadhili  endapo  utakuwa  umepokea  msaada  kwa  ajili  ya  warsha  yako.    Washiriki  hawahitaji  fomu  maalumu  kwa  ajili  ya  tathmini;  unaweza  ukayapandika  maswali  ya  tathmini  kuzunguka  chumba  na  kuwapa  washiriki  kipande  cha  karatasi.  Ni  juu  yako  kuamua  endapo  utahitaji  washiriki  wako  kuandika  majina  yao  katika  fomu  ya  tathmini.    Sampuli  ya  maswali  ya  tathminini  ya  warsha  yanaweza  kujumuisha:  • Tafadhali  tafakari  juu  ya  ujifunzaji  wako  binafsi.  

   

Maelezo  ya  Sampuli    Kichwa:    Ujuzi  wa  Kimtaala:      Maelezo  ya  Sampuli:      Mapendekezo  ya  jinsi  ya  kutumia  Darasani:      Hatua  za  kutengeneza  hii  Sampuli:      Mapendekezo  kwa  ajili  ya  Tathmini:      

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     21  

8

Fupisha  uzoefu  wako  wakati  wa  warsha  na  tuambie  ni  mawazo  gani  makuu  unayapeleka  shuleni  kwako  kutoka  kwenye  warsha  hii?  

• Utatumiaje  ujifunzaji  wako  kutoka  katika  warsha  hii?  • Tafadhali,  pendekeza  njia  ambazo  

zinawezakuboresha  warsha  hii.  • Msaada  gani  zaidi  utakaouhitaji  ili  Kupeleka  

Utengenezaji  kwenye  Shule  Yako?    

9

 Rejea  Alberta  Learning.  (2004).  Focus  on  inquiry:  a  teacher’s  guide  to  implementing  inquiry-­‐based  learning.  Edmonton,  AB:  Learning  Resource  Centre.  Retrieved  from  http://education.alberta.ca/media/313361/focusoninquiry.pdf      Edutopia.  (2013).  Problem  based  learning  (2013).  Retrieved  from  http://links.edutopia.mkt5094.com/ctt?kn=17&ms=NzE3NDM0OAS2&r=MjcyODg5NjI0MjMS1&b=0&j=OTMyNDg3NjYS1&mt=1&rt=0  

 

Mayer,  R.  E.,  &  Wittrock,  R.  C.  (2006).  Problem  solving.  In  P.  A.  Alexander  &  P.  H.  Winne  (Eds.),  Handbook  of  educational  psychology  (2nd  ed.,  pp.  287–304).  Mahwah,  NJ:  Erlbaum.  

1

 Mada  ya  Ajenda  

 Muda  

uliopendekezwa  

Marejeo  ya  Mkusanyiko  wa  vifaa  kwa  mapendekezo  ya  

vitabu  vya  awali  kwa  wawezeshaji  

 Vifaa  Vinavyohitajika  

1. Karibu  • Utambulisho  wa  

wageni  na  wenyeji    

• Usajili  • Kuweka  sawa  

mazingira  

Dakika  10   Sehemu  ya  1.9.    Mafunzo  ya  kitaalamu  –  Kutengeneza  kisa  kwa  ajili  ya  Uzoefu  wa  Kina  na  Kurudiarudia      Sehemu  ya  3.4.  Mapendekezo  ya  Sehemu  ya  Mahali  pa  Utengenezaji  

Karatasi  za  Usajili  

2. Utangulizi  wa  harataki  za  utengenezaji  

Dakika  10     Sehemu  ya  1.2.  Harakati  za  Utengenezaji  -­‐  Mtazamo  wa  kiulimwengu    

Karatasi  la  Bango  na  kalamu    Karatasi  na  kalamu  ya  risasi  kwa  ajili  ya  washiriki  

3. Kuunganisha  utengenezaji  na  mabadiliko  kwenye  kufundisha  na  kujifunza  

Dakika  15     Sehemu  ya  1.3.  Harakati  za  Utengenezaji-­‐mtazamo  wa  kimazingira,  hasa  mazingira  yenye  changamoto      Sehemu  1.5.1.  Kutengeneza  na  kujifunza  kwa  kushiriki  kikamilifu  

Karatasi  la  Bango  na  kalamu      

Karatasi  na  kalamu  ya  risasi  kwa  ajili  ya  washiriki    

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     22  

2

 Mada  ya  Ajenda  

 Muda  

uliopendekezwa  

Marejeo  ya  Mkusanyiko  wa  vifaa  kwa  mapendekezo  ya  

vitabu  vya  awali  kwa  wawezeshaji  

 Vifaa  Vinavyohitajika  

4. Kuunda  Vikundi   Dakika  5  –  10   Sehemu  ya  3.1.  Uundaji  wa  Vikundi  

Karatasi  nyembamba  ndogo  na  kalamu  za  risasi    

5. Utangulizi  wa    kufikiri  juu  ya  ubunifu  

Dakika  10   Sehemu  ya  1.9.  Kufikiri  juu  ya  Ubunifu  

Karatasi  na  kalamu  ya  risasi  kwa  washiriki  

6. Kazi  ya  kufikiri  juu  ya  ubunifu  

Dakika  60     Sehemu  ya  2.2.1.  Andaa  changamoto    Sehemu  ya  5.2.  Mchakato  wa  kufikiri  juu  ya  ubunifu–  karatasi  ya  kufanyia  kazi  washiriki      Sehemu  ya  5.1.  Mchakato  wa  Kufikiri  juu  ya  ubunifu    –  Mwongozo  wa  Mwezeshaji  

Chombo  cha  majira/wakati  (simu  ya  mkononi)    Nakala  za  kifungu  2.2.1  kwa  kila  meza    Nakala  za  sehemu  ya  2.2.2  kwa  kila  mshiriki    Nakala  za  sehemu  ya  2.2.3  kwa  kila  mwezeshaji  

7. Kazi  ya  Kutengeneza   Dakika  120     Sehemu  ya  3.3.  vidokezo  vya  kutengeneza  sampuli  za  vifaa    Sehemu  ya  2.2.4.  Maelezo  ya  Sampuli    Sehemu  ya  3.4.  Sehemu  zilizopendekezwa  za  mahali  pa  mtengenezaji  

• Nakala  ya  sehemu  ya  2.2.4  kwa  kila  mshiriki  

• Mahali  pa  mtengenezaji  • Vifaa  vinavyohitajika  

8. Matembezi  ya  galari     Dakika  20     Sehemu  ya  2.2.5.  Matembezi  ya  Galari    

• Sampuli  za  awali  zilizokamilika    

• Maelezo  yaliyokamilika  kuhusu  Sampuli  

9. Tafakari   Dakika  15   Sehemu  ya  2.2.6.  Tafakari   Karatasi  ya  washiriki  ya  kufikiri  juu  ya  ubunifu  

10. Hitimisho  • Mrejesho  wa  

siku  • Kusafisha  na  

kukusanya  vifaa    • Mazungumzo  ya  

hatua  inayofuata    

15  Dakika  15   Sehemu  ya  2.3.Tathmini  ya  warsha  ya  mafunzo  ya  kitaalamu  

Karatasi  na  kalamu  kwa  ajili  ya  washiriki      

 

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     23  

3.  Vidokezo  na  Mapendekezo  ya  Kuwezesha  Warsha  Yako  

1

Kwa  miaka  mingi  sasa  tumejifunza  baadhi  ya  vidokezo  ambavyo  vinaweza  kukusaidia  kuwezesha  warsha  yako.  Kitu  kimoja  tulichojifunza  kupitia  warsha  za  kupeleka  utengenezaji  mashuleni  ni  umuhimu  wa  mipango  makini.  Vidokezo  katika  sehemu  ya  3  vimetolewa  kama  mapendekezo  tu  kwa  kuwa  kila  kikundi  na  mahali  vitakuwa  tofauti.    3.1.  Uundaji  wa  Makundi  Warsha  hii  iliandaliwa  ili  kusaidia  ujifunzaji  wenye  juhudi  katika  vikundi  vidogo  vidogo.    Wakati  washiriki  wanawasili  wanaweza  kukaa  kwenye  makundi  ya  watu  wanne  kwenye  meza  mahali  popote  ndani  ya  chumba/darasa.  Kabla  ya  kazi  ya  kufikiri  juu  ya  ubunifu  kuanza,  ni  lazima  mwezeshaji  awahoji  washiriki  ili  kuona  ni  maeneo  yapi  ndani  ya  somo  yatawasilishwa.  Mgawanyo  wa  mwanzo  wa  vikundi  ni  lazima  uwe  kwa  masomo  kuliko  shule  au  ngazi  ya  darasa.  Jaribu  kuweka  mchanganyiko  mbali  mbali  katika  makundi  (kwa  mfano;  jinsi,  umri,  miaka  ya  ufundishaji  n.k).  Isipokuwa  kama  kumejitokeza  tatizo,  tunashauri  vikundi  viwe  ni  hivyo  hivyo  muda  wote  wa  warsha.          3.2.  Vidokezo  vya  Michoro  Rahisi  Watu  wazima  wengi  husita  kuchora.  Wengine  hawajawahi  kabisa  kujifunza  vidokezo  na  mbinu  za  kutengeneza  michoro  rahisi.  Si  kwamba  ni  muhimu  tu  kwa  walimu  kuhamasisha  wanafunzi  wao  kuchora,  bali  ni  muhimu  kwa  walimu  kuigwa  na  kuwafundisha  vidokezo  hivi  vingi  kwa  ajili  ya  kuhamasisha  ubunifu  na  kuona  kifikra.  Tunapochora  tunatumia  upande  mwingine  wa  ubongo  wetu  na  hii  huturuhusu  kufikiri  kikamilifu  zaidi  na  kuja  na  mawazo  tofauti  na  bunifu.      Uchoraji  unaweza  kuwa  rahisi.  Unahitaji  tu  maumbo  na  mawazo  pendekezwa……  macho  yetu  yatajaza  sehemu  zote  na  kila  kitu  kilichokosekana.    Kuchora  watu  na  kuonesha  matendo  yanayoweza  kufanywa  na  watu  hao  inaweza  kuwa  na  ugumu  

2

kidogo.  Hata  hivyo,  kuna  vidokezo  vichache  vya  msingi  unaweza  kuzingatia.        Kidokezo  cha  #1  –  tambua  mwili  wa  binadamu  ni  sawia.  Tunatumia  uwiano  wa  1:8  kwa  watu  wazima  na  1:5  kwa  watoto.  Hii  ina  maana  kwamba  ukubwa  wa  mwili  na  miguu  ni  sawa  na  makadirio  ya  vichwa  vyao  saba!  (http://www.drawinghowtodraw.com/drawing-­‐lessons/drawing-­‐faces-­‐lessons/proportions-­‐human-­‐figures-­‐bodies.html    

Dondoo  #1:  Tambua,  mwili  wa  binadamu  una  uwiano      

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     24  

3

Kidokezo  cha  #2  –  katika  mifano  hapo  chini,  zingatia  sifa  kadhaa:  • Michoro  yote  huanza  na  mstatili  rahisi.  Mstatili  

unaweza  kuwa  mwembamba  kuonyesha  watu  wembamba  au  mpana  kuonyesha  watu  wanene.    

• Mikono  ni  lazma  iambatanishwe  juu  ya  mstatili;  miguu  kwa  chini.    Kona  za  juu  na  chini  za  mstatili  hutengeneza  mabega  na  maungio  ya  nyonga.  

• Mikono  inahitaji  kupinda  kidogo  kwenye  kiwiko  au  ipinde  zaidi  kuonesha  kitendo.  

• Miguu  inahitajika  kupinda  kidogo  kwenye  magoti  au  kupinda  zaidi  kuonyesha  kukimbia,  kuruka  au  matendo  mengine.    

• Baada  ya  maumbo  kuchorwa  kwa  uwiano  sahihi  kufuatia  hatua  hizo  hapo  juu,  unaweza  kuyavalisha  nguo  au  kuongeza  vitu  kama  kofia  au  michoro  hiyo  inaweza  kushika  au  kutupa  vitu  

• Ongezea  pua  kuonyesha  ni  uelekeo  upi  mchoro  wako  unaangalia.  

 

 

3.3.  Vidokezo  vya  kuunda  vifaa  vya  Sampuli    Walimu  wengi  huangaika  kutengeneza  vifaa  vinavohakikisha  ujifunzaji  unaohamasisha  juhudi.    Wakati  tuna  tambulisha  hatua  za  uundaji  madarasani,  tunataka  tuandae  wanafunzi  wetu  pamoja  na  vifaa  ambavyo  vinahamasisha  ubunifu,  ushiriki  zaidi  na  maonyesho  yenye  ushahidi  wa  misingi  ya  ujifunzaji.  Sehemu  ya  4  inatoa  maelezo  ya  Sampuli  ya  vifaa  vilivyotengezwa  katika  warsha  iliyopita    

4

Vifaa  kwa  ajili  ya  ujifunzaji  wa  kushiriki  kikamilifu  vinawezakuwa  • Vifaa  vya  hisabati    vilivyotengenezwa  kusaidia  

kuelewa  kuhesabu    • Vikaragosi  vya  kuhamasisha  mazungumzo  • Vinyago  ili  kusaidia  ujifunzaji  wa  lugha  • Kadi  za  herufi  kuhamasisha  utambuzi  wa  herufi  

na  matamshi    • Kadi  za  kuhesabia  ili  kuhamasisha  ujuzi  wa  

kuhesabu    • Matofali  ya  kujengea  ili  kusaidia  uelewa  wa  

kusoma,  kuandika  na  hisabati  • Tangram/Fumbo/chemsha  bongo  ya  jiometri  

kwa  ajili  ya  maarifa  kuhusiana  na  anga  na  muundo  

• Makazi  ya  mdudu  kwa  ajili  ya  uchunguzi  • Tufe  la  Dunia  kwa  ajili  ya  Jiografia  • Na  mawazo  mengi,  mengi  zaidi  

3.4.  Mapendekezo  juu  ya  mahali  pa  mtengenezaji–  Nyenzo  na  Zana  zinazohitajika  kwenye  warsha  yako      Zana  za  Mikono  • Ubao  mdogo  wa  plasta  (hutumika  katika  ujenzi  

wa  nyumba)  • Jozi  tatu  za  koleo  pamoja  na  kikatio  cha  waya  • Vibanio  viwili  vidogo    • Kipimapembe    • Rula  10  za  chuma  ndogo  (12”)  • Visu  10  vyenye  nyembe  zinazoweza  kubadilishwa  baada  ya  kutumika  • Jozi  moja  ya  mkasi    Vitu  vya  kutumika  • Waya  wa  kufungia  • Kipande  cha  mti  kirefu,  chembamba,  laini  cha  

kuvutia  ulimu  chini  • Kibaniko  cha  mwanzi  • Kigundishio  chenye  utepe  pande  mbili  kama  

kitapatikana  • Gundi  ngumu  ya  kugundishia  • Gundi  ya  Maji    • Unga  wa  ngano  uliotiwa  maji  kwa  ajili  ya  

kuchanganya  na  karatasi  ili  kuigundisha  badala  ya  kutumia  gundi  halisi.  

• Bakuli  la  plastiki  la  lita  3  kwa  ajili  ya  

Dondoo  #2:  Kuongeza  vitu  kwenye  mchoro    

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     25  

5

kuchanganyia  maji,  unga  na  karatasi.  • Vijiti  vidogo  vidogo  vya  mti  • Ubao  wa  kugundishia  karatasi  • Gazeti  • Chupa  za  plastiki  za  ujazo  tofauti  tofauti    • Vifuniko  vya  chupa  • Plastiki  laini  iliyotengenezwa  tena  kwa  matumizi  

baada  ya  matumizi  ya  awali  • Vitu  vilivyopatikana  ambavyo  vinaweza  

kutumika    • Chati  na  karatasi  za  manila    • Gundi  ya  utepe  kwa  ajili  ya  chati  na  karatasi  za  

manila    

6

• Msumari  bapa  (usio  na  kichwa)  kwa  ajili  ya  kubandikia  karatasi  

 Vifaa  vya  Warsha  (Angalia  sehemu  ya  5.  Viambatanisho)  • Nakala  ya  karatasi  ya  kufanyia  kazi  ya  kufikiri  

kwa  ubunifu  kwa  ajili  ya  washiriki.  • Karatasi  za  A3  kwa  ajili  ya  washiriki  • Karatasi  za  Chati/bango  kitita  • Kalamu  maalumu  za  Kuandikia  kwenye  karatasi  

za  Chati/bango    • Kalamu  za  risasi  kwa  ajili  ya  washiriki  Kichongeo  cha  kalamu  ya  risasi  

Uchoraji  unawezakuwa  rahisi  sana.  

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     26  

4.  Maelezo  ya  Sampuli/Kifani  –  Zana/Nyenzo  Kutoka  Warsha  Iliyopita  

1

4.1.    Tufe  lenye  sitaha  tatu  (urefu,  kimo  na  kitako)    Kichwa  cha  habari:    Kutengeneza  tufe  lenye  sitaha  tatu  (urefu,  kimo  na  kitako)  (http://www.progonos.com/furuti/MapProj/Normal/ProjPoly/Foldout/Dodecahedron/Files/Res3/gnDod-­‐s500_pof-­‐bw.pdf)        Ustadi  wa  mitaala  kwa  Shule  za  Tanzania:  Malengo  ya  Masomo  ya  Jamii:  • Kuthamini  utegemezi  kati  ya  binadamu  na  mazingira  • Kuimarisha  ari  ya  umoja  wa  nchi  na  ushirikiano  kati  ya  jamii  za  kitanzania  na  zile  za  pande  nyingine  za  

dunia.  • Kuwa  na  uwezo  wa  kutambua  na  kusimulia  matukio  ya  Tanzania  na  yale  yanayotokea  katika  nchi  zingine      Darasa  la  Tatu  • Shule  yetu  –  Picha  na  Ramani;  sehemu  kuu  za  dira  Darasa  la  nne  • Wilaya  Yetu  –  Ujuzi  wa  kusoma  Ramani;  sura  na  tabia  ya  eneo,  hali  ya  hewa  na  uoto  wa  asili;  sura  ya  dunia,  

tabia  ya  hali  ya  hewa  na  uoto  wa  asili;  rasilimali  za  asili  Darasa  la  Tano  • Ujuzi  wa  kusoma  Ramani;  Pande  8  za  Dira;  Alama  za  Ramani;  Onyesha  Tanzania;  Sura  ya  dunia;  Hali  ya  

Hewa;  Uoto  wa  asili;  Mawakala  wa  ukoloni;  Uchumi  wetu;  Utalii;  Biashara  Darasa  la  Sita  • Ujuzi  wa  kusoma  Ramani;  Dunia;  mahali  na  sura  ya  nchi  katika  Afrika  ya  mashariki;  hali  ya  hewa;  biashara  

na  masoko;  Eneo  la  nchi  za  Afrika  ya  Kusini;  Uvamizi  wa  kikoloni;  Bara  la  Afrika;  Ukimbizi  katika  Afrika;  Afrika  na  Mashirika  ya  Kimataifa  

Darasa  la  Saba  • Dunia  yetu  –  sura  ya  nchi;  hali  ya  hewa;  mawasiliano  na  Usafirishaji    Maelezo  ya  Sampuli:  Ramani  ya  dunia  iliyo  na  mipaka  ya  kisiasa  imeainishwa  na  umewekewa  utambulisho,  ramani  inaweza  ikakatwa  na  kugundishwa  kutengeneza  mwonekano  wa  sitaha  tatu  (12  sided  http://mathworld.wolfram.com/Dodecahedron.html)  tufe  lenye  muonekano  ambapo  duara  kuu  zinaonekana  kama  mstari  mnyoofu  (http://en.wikipedia.org/wiki/Gnomonic_projection).  Mwonekano  ambapo  duara  kuu  zinaonekana  kama  mstari  mnyoofu  ni  umbo  la  zamani  zaidi  la  ramani.    Mapendekezo  kwa  Matumizi  ya  Darasani:  • Kuelewa  nafasi  ya  Tanzania  katika  Dunia  • Kuelewa  Dunia  ni  duara  • Kuonyesha  uhusiano  kati  ya  nusu  dunia  kaskazini  na  Kusini  • Kuonyesha  njia  za  biashara  na  umbali  –  kimkoa,  kitaifa,  kibara,  kimataifa  • Kujenga  taswira  ya  mawazo  dhahania  (mipaka,  pointi  za  dira,  latitudo,  longitudo,  n.k..)  • Kulinganisha  ramani  sawa  kwa  tufe  lenye  sitaha  tatu  –  nini  hakipo  na  kilichoongezeka  kwa  miundo  yote?  

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     27  

     

2

• Ongea  kuhusu  mwonekano  tofauti  wa  ramani  na  mwelekeo.  Zalisha  maswali  (Kwa  mfano;  kwanini  siku  zote  Kaskazini  inakuwa  juu  ya  ramani  nyingi  wakati  Tanzania  na  nchi  zingine  nyingi  zipo  ncha  ya  kusini?  

 Hatua  za  kutengeneza  Sampuli  hii  • Pakua    Ramani  

(http://www.progonos.com/furuti/MapProj/Normal/ProjPoly/Foldout/Dodecahedron/Files/Res3/gnDod-­‐s500_pof-­‐bw.pdf)  au  nakala  ya  ramani  uliyopewa  kwenye  ukurasa  wa  29.  

• Itategemea  dhamira  ya  matumizi  yako,  toa  nakala  ya  ramani  kwa  kila  mwanafunzi.  Ukubwa  pendekezwa  ni  karatasi  ya  A3    

• Tumia  penseli  kuongeza  weusi  kwenye  mistari  ya  nakala  zilizo  chapishwa.      • Tumia  penseli  ya  rangi  au  rangi  za  maji  ku  onyesha  vielelezo  halisi  vya  mikoa,  nchi  au  mada  yoyote  

inayopelekea  utumie  ramani.    • Ikate  ramani  kwa  uangalifu.  Hakikisha  haukati  nembo  ambazo  zitatumika  badae  kugundisha  ramani  ya  tufe  

la  Dunia  pamoja.  • Kunja  ramani  kwa  uangalifu,  tengeneza  tufe  lenye  pande  12  • Gundisha  tufe  juu  juu  kwa  pamoja  na  bila  kutumia  nguvu  anza  kuiwekea  vijikaratasi  vya  ziada.  Hii  

itaongeza  uzito  na  uthabiti  wa  tufe  lililokamilika.  • Kamilisha  kugundisha  tufe.        Mapendekezo  juu  ya  Upimaji    Darasa  la  tatu  • Onyesha  Tanzania  ilipo  kwenye  Ramani  na  kisha  kwenye    tufe  la  Dunia    • Onyesha  pande  kuu  za  dira  kwenye  ramani  na  kwenye  ramani  ya  tufe  la  dunia  Darasa  la  nne  • Onyesha  sehemu  kwenye  ramani  na  kwenye  tufe  la  dunia    • Tambua  hali  ya  hewa  ya  kanda  mbalimbali  na  uoto  wa  asili  wa  mikoa  iliyopo  kwenye  ramani  na  tufe  la  

Dunia  • Onyesha  sura  muhimu  zinazoonekana  (Mfano;  Kisiwa  cha  Zanziba,  Mlima  Kilimanjaro,  Dodoma)  • Tambua  maeneo  yenye  uwezekano  wa  rasilimali  za  asili    Darasa  la  tano  • Tafuta  maeneo  mbali  mbali  kwenye  ramani  na  tufe  la  Dunia  • Tambua  pointi  nane  za  dira    • Tumia  alama  mbali  mbali  za  ramani  kutambua  maeneo  kwenye  ramani  na  tufe  la  Dunia    • Tambua  Tanzania  na  sura  zake  muhimu  za  asili    • Elezea  ni  kwa  jinsi  gani  mahali/sehemu  inavyoathiri  hali  ya  hewa    • Onesha  mahali  asilia/halisi  pa  wakoloni  na  wasilisha  jinsi  walivyokuja  Afrika  ya  mashariki  • Mawakala  wa  ukoloni  • Elezea  ni  kwa  jinsi  gani  mahali/sehemu  inavyoathiri  uchumi  wetu    • Tambua  maeneo  ya  utalii    • Elezea  kwa  jinsi  gani  mahali  huathiri  biashara    Darasa  la  Sita  • Tafuta  sehemu  mbalimbali  kwenye  ramani  na  tufe  la  Dunia  • Tambua  sura  za  asili  za  Afika  Mashariki  • Elezea  athari  ya  mahali  juu  ya  hali  ya  hewa  

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     28  

3

• Elezea  athari  za  mahali  juu  ya  uchumi  na  biashara  • Tambua  nchi  za  Afrika  Kusini    • Onyesha  njia  za  uvamizi  wa  kikoloni  –  zionyeshe  chimbuko  la  mahali  na  makoloni    • Tambua  bara  la  Afrika  • Onyesha  mahali  pa  chimbuko  la  wakimbizi  na  elekeza  njia  walizopitia  Afrika    • Eleza  madhara  ya  mahali  juu  ya  uhusiano  wa  Afrika  na  ushiriki  kwenye  ushirikiano  wa  kimataifa    Darasa  la  Saba  • Tafuta  maeneo  tofauti  tofauti  kwenye  Ramani  na  kwenye  tufe  la  Dunia    • Elezea  athari  ya  mahali/eneo  kwenye  hali  ya  hewa  • Elezea  athari  ya  mahali  kwenye  mawasiliano  na  usafirishaji  (kwa  mfano;  Mfumo  wa  kebo  ya  chini  ya  maji  

ya  Afrika  ya  Mashariki  ni    undersea  fibre  optic  (mkongo  wa  chini  ya  bahari)  mfumo  wa  kebo  unaounganisha  nchi  ndani  ya  Afrika  ya  Mashariki  na  dunia  yote  (http://en.wikipedia.org/wiki/EASSy)    

 

Ramani  inaweza  kupakwa  rangi,  kukatwa  na  kuunganishwa  kwa  gundi  kuunda  tufe  lenye  sitaha  tatu  (3D),  tufe  lenye  umbo  la  sura  kumi  na  mbili .  

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     29  

   

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     30  

4

 4.2.  Tangram  *  Ni  mchezo  wa  watoto  ambao  ni  fumbo  la  kijiometri,  lenye  vipande  saba  vya  mraba  vilivyokatwa  ambavyo  

hupangwa  kutengeneza  maumbo  mengine*  

Title:  Tangram  na  maumbo  ya  kijiometri  http://www.activityvillage.co.uk/tangrams      Ujuzi  wa  Mitaala  Ndani  ya  Mashule  ya  Tanzania:  • Maarifa  kuhusiana  na  anga/maeneo  ya  maumbo  na  ukubwa  • Kubainisha  na  kufumbua  kwa  kupima  na  kujenga.  • Kubainisha  mistatili  na  miraba    Maelezo  ya  Sampuli:  Tangram  ni  mraba  ambao  umekatwa  vipande  7.    Changamoto  ni  kuweza  kutumia  vipande  hivyo  saba  kuunda  tena  mraba  huo  na  maumbo  mengine  magumu.    Mapendekezo  ya  Kutumia  Darasani:  • Tambulisha  tangram  darasani  kama  njia  ya  kuelewa  maumbo  ya  jometri      • Wanafunzi  watengeneze  jozi  za  tangram  zao  kwa  kutumia  karati  ngumu  yakubandikia  au  plastiki  bapa  

ambayo  ni  rahisi  kukata.      • Wapatie  maumbo  tofauti  tofauti  ya  tangram  ili  wanafunzi  wafanyie  kazi/  wafanyie  mazoezi    • Wakumbushe  wanafunzi  mara  zote  kutumia  vipande  vyote  7.    • Tumia  tangram  kama  mchezo  kuhamasisha  tendo  la  ujifunzaji  wa  kushiriki  kikamilifu  • Tumia  tangram  kama  fumbo  kwa  ajili  ya  kutatua  tatizo      Hatua  za  kutengeneza  sampuli  hii  • Toa  nakala  za  maumbo  ya  mchezo  wa  tangaram    • Wanafunzi  wakate  maumbo  hayo    

 Mapendekezo  ya  Upimaji    • Upimaji  usio  rasmi  –  chunguza  njia  za  wanafunzi  za  utatuzi  wa  tatizo    • Upimaji  endelevu  –  waulize  wanafunzi  kutengeneza  maumbo  ya  msingi  na  kurekodi  namba  ya  hatua  

wanazotumia  kukamilisha  kazi.  Ongeza  ugumu  wa  maumbo    

Modeli  ya  kiolezo/mpangilio  wa  mchezo  wa  Tangram    Zingatia:  Kabla  ya  kutoa  nakala  kwa  ajili  ya  wanafunzi,  kuza  mraba  huu  katika  ukubwa  unaoutaka  lakini  hakikisha,  unabaki  kuwa  mraba.      Zingatia:  Tangram  zinaweza  kutengenezwa  kwa  kutumia  karatasi,  karatasi  ngumu  ya  kubandikia,  plastiki,  ubao  wa  mti  au  kitu  chochote  bapa  na  imara.  

 

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     31  

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     32  

 

5

4.3.  Bata    

 Kichwa  cha  habari:  Bata    Ujuzi  wa  Mitaala:    Kingereza  Darasa  la  1  na  2  1.  Kuunda  sentensi,  uliza  na  jibu  maswali  rahisi  kuhusu  mazingira  yaliyo  karibu  (nyumbani  na  shuleni)  

o Tambua  na  taja  majina  ya  vitu  o Elezea  vitu  o Tambua  sehemu  za  mwili  

Darasa  la  3  na  4  1.  Kuelewa  na  kutumia  misemo  inayotumika  mara  kwa  mara  kwenye  familia,  shule  na  mazingira  na  hali  maalum    2.  Wasiliana  kwa  kazi  rahisi  za  kila  siku  zinazohitaji  ubadilishanaji  rahisi  wa  habari  kwa  kutumia  ujuzi  wote  (nne)  wa  lugha.  

o Kuelezea  mfanano  o Kuelezea  Maeneo  o Kuelezea  Ubora  kwa  kuzingatia  ukubwa    

 Kiswahili  Darasa  la  1  na  2  1.  Kuelewa  na  Kutumia  sentensi  rahisi  kwa  mahitaji  ya  mawasiliano  ya  kila  siku    2.  Kuwasiliana  kwa  urahisi  kuhusu  mambo  yaliyomo  kwenye  mazingira  ya  karibu  sana  

o Tambua  na  taja  majina  ya  vitu  vilivyomo  kwenye  mazingira  ya  karibu    

o Tambua  Rangi  tofauti  tofauti    o Elezea  vitu  kwa  kuzingatia  ubora    

Darasa  la  3  na  4  1.  Kusikiliza  na  Kuongea  ili  kukidhi  mahitaji  ya  mtu      

2.  Kuwasiliana  kwa  usahihi  kwa  lugha  ya  Kiswahili  kuhusu  mambo  ya  kila  siku  katika  muktadha  tofauti      Sayansi  Darasa  la  1  na  2  1.  Thamini  na  tumia  kanuni  za  kisayansi  na  teknolojia  katika  maisha  ya  kila  siku  

o Taja,orodhesha  na  elezea  tabia  za  viumbe  hai,  chora  na  tengeneza  vifani  vya  viumbe  hai  o Tambua  na  igiza  sauti  za  wanyama  mbalimbali  o Taja  vyanzo  vya  chakula    o Elezea  makazi  ya  asili  ya  wanyama  tofauti  tofauti  

Darasa  la  3  na  4  

 

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     33  

   

6

o Fafanua  makazi  ya  asili  ya  Viumbe  hai  o Fafanua  kuhsu  mwendo  miongoni  mwa  viumbe  hai      Hisabati    

Darasa  1  na  2  1. Tambua  namba  2. Kuhesabu      3. Kuandika  namba  1,  2  

 Maelezo  ya  Sampuli:  Kifani  cha  bata  kilichotengenezwa  na  soksi  za  zamani/zilizotumika,  vipande  vya  nguo  na  sponji,  vijiti,  kadi  za  maboksi,  vifungo,  karatasi,  gundi  na  uzi.  Kifani  kimepakwa  rangi  nyeusi/kijivu  na  nyeupe  ili  kufanya  aonekane  kama  bata  halisi.  Bata  ni  miongoni  mwa  wanyama  wafugwao  nyumbani  hasa  katikati  mwa  Tanzania  na  ni  rahisi  zaidi  kutambuliwa  na  watoto  katika  maeneo  haya.  Pia,  sio  wanyama  haramu/wenye  miiko  –  hivyo  watoto  wanaweza  kuwashika  kwa  urahisi  na  kuongea  kuhusu  bata.      Mapendekezo  kwa  ajili  ya  matumizi  darasani:  • Kusababisha  mazungumzo  ya  vitu  vilivyomo  kwenye  mazingira    • Kutoa  misingi  ya  mjadala  juu  ya  upendeleo  binafsi/mtu  binafsi  • Kuchochea  mazungumzo  juu  ya  tabia  za  viumbe  hai  na  sehemu  za  miili  ya  viumbe  hai    • Chochea  wanafunzi  watambue,  wataje  na  waainishe  vitu  katika  mazingira  yao    • Kufundisha  namba  rahisi  1  na  2    • Kuanzisha  mazungumzo  ya  wanyama  mbalimbali  na  jinsi  wanavyolia    • Kuanzisha  mazungumzo  juu  ya  wanyama  mbali  mbali  wafugwao  nyumbani    • Kuhesabu  hadi  4  • Kuhusianisha  umbo  la  bata  na  namba  2    Hatua  za  kutengeneza  Sampuli  hii    Vifaa  vya  kutengeneza  sampuli  hii  vinawezakutokana  na  vile  vilivyotupwa  na  vifaa  vinavyoweza  kutumika  tena  baada  ya  matumizi  ya  awali.  • Kwanza  kusanya  vifaa  vyote  vinavyohitajika  • Kata  vipande  vya  nguo  na  sponji/sifongo  • Weka  vipande  vilivyokatwa  ndani  ya  Soksi–  tengeneza  umbo  inavyotakiwa.    • Tumia  kipande  cha  nguo  kuunda  sehemu  nyembamba  na  pana  ya  mwili  wa  bata.  • Tengeneza  matundu  mawili  kwa  chini  ya  mwili    • Tumia  kipande  cha  boksi  kutengeneza  mabawa-­‐  penyeza  vipande  hivyo  vya  boksi  ndani  ya  mwili  • Tumia  vipande  viwili  vya  mti  kutengeneza  mdomo  na  tumia  kisu  ili  kurekebisha  umbile  la  mdomo  liwe  

lakufaa.  • Chukua  vijiti  viwili  na  bandika  kipande  cha  boksi  kilichoundwa  kama  mguu  wa  bata.  • Penyeza  vijiti  hivyo  kwenye  matundu  mawili  • Unganisha  mdomo  kwenye  kichwa    • Bandika  viungo  viwili  kwa  ajili  ya  macho  • Gundisha  viambatisho  

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     34  

   

7

• Paka  rangi  modeli/sampuli  kwa  rangi  zakufaa  (nyeupe,  nyeusi  au    kijivu)    Mapendekezo  ya  Upimaji        • Unda  maelezo  kuhusu  Kifani    • Eleza  rangi  ya  Kifani    • Tambua/  Taja/  Elezea  kifani    • Sema  makazi  ya  asili  ya  kifani    • Taja  na  Tambua  (kwa  kugusa  au  kuonyesha)  sehemu  mbali  mbali  za  mwili  wa  kifani    • Hesabu  idadi  ya  miguu  na  macho  ya  Kifani    • Elezea  matumizi  ya  mnyama  huyo    • Elezea  mnyama  huyo  huwa  anakula  nini    • Elezea  mfanano  na  utofauti  kati  ya  kifani  cha  mnyama  na  wanyama  wengine  waliopo  kwenye  mazingira  

yao  • Chora  picha  ya  Bata    • Tengeneza  kifani  chako  rahisi  cha  bata      

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     35  

8

4.4.    Nyumba    Kichwa  cha  habari:  Nyumba    Ujuzi  wa  mitaala:  Kingereza      Darasa  la  1  na  2    1. Unda  sentensi,  uliza  na  jibu  maswali  rahisi  kuhusu  mazingira  jirani  (Nyumbani  na  Shuleni)    2. Chukua  nafasi  katika  mazungumzo  rahisi    

o Tambua  na  taja  Vitu    o Elezea  Vitu    o Hesabu    o Panga  vitu  vyenye  sifa  moja  pamoja  kwa  mfano;  maumbo  na  rangi    

Darasa  la  3,  4  na  5    1.  Elewa  na  tumia  misemo  inayotumika  mara  kwa  mara  kwenye  familia,  shule  na  mazingira  na  hali  halisi  

waliyomo  2.  Wasiliana  kwa  kazi  rahisi  za  kila  siku  zinazohitaji  ubadilishanaji  rahisi  wa  habari/taarifa  kwa  kutumia  sehemu  

nne  za  ujuzi  wa  lugha  o Onyesha  mfanano  o Onyesha  mahali    o Onyesha  ubora  kwa  kuzingatia  ukubwa    o Kuhesabu    

 Darasa  la  5  

1. Kuelewa  taarifa  zilizowasilishwa  na  wengine  ndani  ya  mazingira  yao  halisi  2. Wasiliana  na  watu  wengine  kwa  usahihi  na  kwa  hali  inayofaa  katika  mazingira  halisi  kwa  kutumia  

maelezo  rahisi  yanayojumuisha  sehemu  nne  za  ujuzi  wa  lugha  Uliza  juu  ya  na  toa  sababu  Onyesha  ulinganishi    Kutumia  vivumishi  vya  maumbo/muonekano    

Kiswahili  Darasa  la  1  na  2  1.  Kuelewa  na  kutumia  sentensi  rahisi  kwa  mahitaji  ya  mawasiliano  ya  kila  siku    2.  Kuwasiliana  kuhusu  mambo  yaliyomo  kwenye  mazingira  halisi    

o Tambua  na  taja  majina  ya  vitu  vilivyomo  kwenye  mazingira  halisi  

o Tambua  rangi  mbali  mbali    o Elezea  vitu  kwa  kigezo  cha  ubora    

o Kuhesabu  vitu    o Tofautisha  umoja  na  wingi    

 Darasa  la  3  na  4  1.  Kusikiliza  na  kuongea  ili  kukidhi  mahitaji  ya  mtu  mwingine    2.  Kuwasiliana  kwa  usahihi  kwa  lugha  ya  Kisawahili  kuhusu  mambo  ya  kila  siku  katika  muktadha  tofauti  tofauti    

Kupeleka  vifaa  (Nyumba)  darasani    

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     36  

   

9

o Kuelezea  vitu  kwa  kigezo  cha  ukubwa    o Linganisha  na  onyesha  tofauti  kwa  kulinganisha  vitu    o Tofautisha  vitu    

Sayansi  Darasa  la  1  na  2  1.  Fahamu  vyema  na  tumia  kanuni  za  kisayansi  na  teknolojia  katika  maisha  ya  kila  siku    

o Taja,  orodhesha,  elezea  tabia  za  vitu,  michoro  na  tengeneza  vifani  vya  vitu      o Kuelezea  makazi  ya  asili  ya  watu    o Kuweka  mazingira  yawe  safi  na  salama  

Darasa  la  3  na  4    o Kuelezea  makazi  ya  asili  ya  viumbe  hai  o Kuweka  mazingira  safi  na  salama      Hisabati  

Darasa  la  1  na  2  1. Kutambua  namba  2. Kuhesabu    3. Kuandika  namba  4. Tambua,  umbo  bapa  la  pande  nne,  pembe  tatu,  maduara  

Darasa  la  3  na  4  o Kuchora  na  kukata  maumbo  bapa    maumbo  ya  ndege  ya  pembe  nne,  pembe  tatu  na  duara  o Kupima  urefu  wa  maumbo  na  vitu    o Kuelezea  tabia  za  mistatili,  mraba  na  pembetatu  o Kutafuta  mzunguko  na  eneo  la  mraba  na  mstatili    o Kutambua  aina  za  pembe  –  kali,  mraba    

Ujuzi  wa  Ufundi  Stadi      Darasa  la  1-­‐4  

o Kuelewa  na  kutumia  ujuzi  wa  Sanaa  ya  uchoraji,  mapambo  na  ufinyanzi  o Kuchora  maumbo  na  vitu  kwa  kutumia  kiolezo/Kigezeo  o Oanisha  maumbo  na  violezo  o Kufinyanga  kwa  udongo    o Kupamba  vifani/modeli      o Kuchora  picha  za  vitu  halisi    o Kupaka  rangi  kwa  kutumia  rangi  za  maji  

Historia  1. Elewa  familia    2. Elewa  maendeleo  yanayofanywa  na  jumuiya  zao  

o Mahitaji  ya  msingi  ya  familia    o Kazi  na  wajibu  katika  familia  na  jumuiya  o Kuelewa  mila,  desturi  na  tamaduni  zinazohusiana  na  makazi  

Jiografia  o Tambua  shughuli  zinazoathiri  mazingira,  athari  zake,  na  kuchukua  njia  zakufaa  za  kutunza  na  kuyalinda  

mazingira  hayo    o Kuelewa  mahusiano  yaliyopo  kati  ya  watu  na  mazingira,  na  utumie  maarifa  hayo  kwa  maendeleo  ya  

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     37  

10

kijamii  na  kiuchumi.  o Kuelezea  mazingira    o Tambua  vitu  vilivyomo  katika  mazingira  ya  nyumbani  na  shuleni    

 Maelezo  ya  Sampuli/Kifani:  Kifani  cha  nyumba  kilichotengenezwa  kutokana  na  kadi  za  maboksi  yaliyotumika,  vijiti,  matete,  majivu,  rangi  na  gundi.  Kifani  hiki  ni  kiwakilishi  cha  aina  za  nyumba  za  sasa  zinazopatikana  katika  mazingira  (Tanzania  Vijijini).    Pia,  inawakilisha  kile  ambacho  kinafikiriwa  kuwa  ni  nyumba  za  kisasa  hasa  sehemu  za  vijijini  ambapo  baadhi  ya  aina  za  nyumba  za  kitamaduni  kama  vile  Manyatta  (zilizotengenezwa  kwa  udongo,kinyesi  cha  ng’ombe  na  fito)  au  nyumba  za  udongo  za  duara  bado  zinaweza  kuonekana.        Mapendekezo  ya  Matumizi  Ndani  ya  Darasa:  • Kukuza  msamiati  katika  Kingereza  na  Kiswahili    • Kufanya  mazoezi  ya  kuhesabu    • Kufanya  mazoezi  ya  kutambua  maumbo  • Kufanya  mazoezi  ya  kutambua  rangi    • Kufanya  mazoezi  ya  kupima  urefu,  upana,  mzingo  na  eneo    • Kuanzisha  mazungumzo/mjadala  kuhusu  mazingira,  uhifadhi  na  utunzaji    • Kuanzisha  mazungumzo  juu  ya  makazi  ya  asili  • Kuanzisha  mazungumzo  juu  ya  maendeleo    • Kuanzisha  mazungumzo  juu  ya  utengenezaji  wa  vifani  • Kufanya  mazoezi  juu  ya  matumizi  ya  maneno  ya  kuelezea  • Kuanzisha  mazungumzo  juu  ya  mahusiano  yaliyopo  kati  ya  watu  na  vitu  vingine  vilivyopo  kwenye  mazingira      Hatua  za  Kutengeneza  Kifani  Hiki  Baadhi  ya  vitu  vinavyohitajika  katika  utengenezaji  wa  kifani  hiki  vinaweza  kupatikana  katika  mazingira  bila  gharama  yoyote  au  kwa  gharama  za  chini  kabisa.  Kwa  mfano;  vipande  vya  maboksi  yaliyotumika,  vijiti,  matete,  na  majivu.  Rangi  na  gundi  vinaweza  kununuliwa      • Kwanza  kusanya  vifaa  vyote  vinavyohitajika  • Chora  mchoro  wa  kifani  kilichokusudiwa  kutengenezwa  (kwa  kuzingatia  kila  kitu  (utondoti  unaohitajika)  

kinachohitajika    • Kata  vipande  vya  maboksi  yaliyotumika  katika  maumbo  ya  mstatili  kwa  ajili  ya  sehemu  ya  mbele  na  nyuma  

ya  nyumba    • Chora  alama  zilizochaguliwa  mahali  pa  madirisha  na  milango  juu  ya  vipande  hivyo  • Kata  sehemu  tatu  katika  kila  alama  za  mchoro  wa  dirisha  na  mlango,  acha  upande  mmoja  ambao  utakuwa  

unaunganika  na  ukuta  ili  kufanya  milango  na  madirisha  kufunga  na  kufunguka.  Hii  itasaidia  katika  kutoa  nafasi  nyingi  zaidi  za  mazoezi  na  ujifunzaji  wa  msamiati    

• Tumia  matete  kutengeneza  sura  ya  kiunzi  cha  nyumba  • Kata  kipande  kingine  cha  boksi  kwa  ajili  ya  paa  • Chuna  karatasi  la  upande  mmoja  ili  kupata  sura  yenye  mikunjomikunjo  • Tumia  gundi  na  vijiti  kushikanisha  vipande  vya  maboksi  kwenye  kiunzi    • Changanya  maji  na  majivu  na  upake  kwenye  kifani  cha  nyumba  –  hii  itafanya  kadi  za  maboksi  kuwa  ngumu  

zaid  na  pia  kuilinda  isivunjike  • Acha  kifani  kikauke    

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     38  

   

11

• Chagua  rangi  za  nyumba  na  upake  kifani  cha  nyumba  • Kata  kipande  kingine  cha  boksi  kitakachofanywa  kama  msingi  (sakafu)  ya  nyumba      • Paka  majivu  pia  na  ukiache  kikauke  • Shikiza  msingi  na  sehemu  nyingine  ya  kifani    Mapendekezo  ya  Tathimini    • Unda  sentensi  kuhusu  kifani  • Eleza  rangi  za  kwenye  kifani  • Tambua/taja/elezea  kifani  • Taja  na  tambua  (kwa  kugusa  au  kuonyesha)  sehemu  tofauti  tofauti  za  kifani  • Hesabu  idadi  ya  madirisha,  pande,  pembe,  maumbo  n.k  ya  kifani  • Elezea  matumizi  ya  nyumba  • Elezea  nyumba  halisi  zinajengwa  kwa  vitu  gani/zinatengenezwa  na  nini?    • Elezea  mfanano  na  utofauti  kati  ya  kifani  cha  nyumba  na  nyumba  nyingine  zilizopo  kwenye  mazingira  yako  

halisi    • Chora  picha  ya  nyumba  • Tengeneza  kifani  rahisi  cha  nyumba  

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     39  

12

4.5.  Maumbo  ya  Herufi    

Title:  Maumbo  ya  Herufi    Ujuzi  wa  Mitaala:    Kiingereza    Darasa  la  1  na  2  

o Tambua  na  orodhesha  majina  ya  vitu  katika  mazingira  yako  halisi  o Elezea  vitu  o Kuhesabu  o Tambua  herufi  za  alfabeti  za  Kingereza    o Tofautisha  herufi  kubwa  na  ndogo  o Tumia  herufi  za  alfabeti  kutamka  na  kuandika  maneno  mafupi    

 Darasa  la  3,  4  na  5  

1. Elewa  na  tumia  misemo  inayotumika  mara  kwa  mara  kwenye  familia,  shule,  hali  na  mazingira  ya  kawaida    

2. Kuwasiliana  kwa  urahisi  utaratibu  wa  shughuli  unaohitaji  kubadilishana  taarifa  rahisi  kwa  kutumia  sehemu  nne  za  ujuzi  wa  lugha    

o Tahajia  za  maneno,  kusoma  na  kuandika  maneno  mafupi  na  sentensi      o Kuelezea  mahali  o Kuelezea  ubora  kwa  kuzingatia  ukubwa  o kuhesabu  

 Kiswahili  Darasa  la  1  na  2  1.  Kuelewa  na  kutumia  sentensi  rahisi  kwa  ajili  ya  mahitaji/matumizi  ya  kila  siku  2.  Kuwasiliana  kirahisi  kuhusu  mambo  yaliyomo  kwenye  mazingira  halisi  

o Kutambua  alfabeti  za  herufi    o Kutofautisha  herufi  kubwa  na  ndogo  o Unda,  kusoma  na  kuandika  silabi,  maneno  mafupi  

na  sentensi    

o Kutambua  na  kuorodhesha  vitu  katika  mazingira  halisi    

o Tambua  rangi  tofauti  o Kuelezea  vitu  kwa  kigezo  cha  ubora  o Kusoma    

 Darasa  la  3  na  4  1.  Kusikiliza  na  kuongea  ili  kukidhi  mahitaji  ya  mtu  mwingine    2.  Kuwasiliana  kw  usahihi  kwa  lugha  ya  Kiswahili  kuhusu  mambo  ya  kila  siku  mahali  tofaut  tofauti    

o Kuelezea  vitu  kwa  kigezo  cha  ukubwa  

Maumbo  ya  herufi  yaliyotengenezwa  kwa  chupa  za  maji  zilizotumika.  

 

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     40  

     

13

o Linganisha  na  tofautisha  kwa  kulinganisha  vitu  o Tofautisha  vitu    o Kusoma  aya    o Kusoma  kwa  ufahamu  na  furaha    o Kuandika  maelezo  ya  matukio  kwa  ufupi  o Hisabati  (Kadi  za  hisabati  zinaweza  kuwa  badala  ya  kadi  za  herufi  )  

 Darasa  la  1  na  2  1.  Kutambua  na  Kusoma  namba  2.  Kusoma  majina  ya  namba  3.  Kuhesabu    4.  Kuandika  namba  5.  Kupanga  namba        Maelezo  ya  Sampuli/Kifani:  Maumbo  ya  herufi  (yanaweza  kuwa  maumbo  ya  namba)  hutengenezwa  kutokana  na  chupa  za  plastiki  zilizotumika  na  vipande  vya  karatasi  ambapo  herufi  au  namba  huandikwa.  Matumizi  ya  chupa  za  plastiki  zilizotumika  kwenye  maeneo  yenye  changamoto  huwa  na  faida  mara  mbili;  ya  kuweka  mazingira  safi  na  hupunguza  gharama  za  kutengenezea  vifaa  vya  kujifunzia  kwani  gharama  huwa  za  chini  au  bure  lakini  vifaa  vinakuwa  vya  kudumu  sana.  Ni  muhimu  chupa  iwe  angavu  (isiyo  na  rangi)  au  yenye  rangi  ya  kutosha  kuonyesha  herufi  kwa  urahisi.  Kwa  kuongezea,  mapambo  yoyote  hayatakiwi  kuingiliana  na  kile  kinachotakiwa  kusomwa.        Mapendekezo  ya  Matumizi  Ndani  ya  Darasa:  • Kukuza  uwezo  wa  wanafunzi  katika  kutambua  herufi  • Kukuza  uwezo  wa  kutofautisha  herufi  kubwa  na  ndogo    • Kukuza  uwezo  wa  wanafunzi  kusoma  herufi,  maneno  na  

sentensi  • Kukuza  msamiati  katika  lugha  zote  Kingereza  na  

Kiswahili  • Kufanya  mazoezi  ya  tahajia  za  maneno,  uundaji  wa  

maneno  na  uundaji  wa  sentensi    • Kujifunza  kwa  kupitia  michezo  kwa  mfano;  kujihusisha  

na  utafutaji  wa  maneno,  ushindani  wa  tahajia  za  

maneno,  mafumbo  rahisi  ya  maneno  • Kufanya  mazoezi  ya  utambuzi  wa  rangi  –  kwa  dhumuni  

hili,  karatasi  au  herufi  zinaweza  kuwa  na  rangi  tofauti  tofauti  

• Kufanya  mazoezi  ya  maneno  ya  kuelezea    Hatua  za  Kutengeneza  Kifani  Hiki  Baadhi  ya  vifaa  vyakutengenezea  kifani  hiki  vinaweza  kupatikana  kwenye  mazingira  bila  gharama  au  kwa  gharama  nafuu  kwa  mfano,  chupa  za  maji  za  plastiki  zilizokwisha  tumika.  Kalamu  na  karatasi  zinaweza  kununuliwa  pamoja  na  kisu  cha  kukatia  maumbo.      • Kwanza  kusanya  vifaa  vyote  vinavyohitajika  –  unaweza  kupata  msaada  wa  wanafunzi  wakati  wa  kukusanya  

Vipande  vya  chupa  vinaweza  kujumuisha  herufi,  namba,  silabi  au  maneno.  

 

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     41  

14

chupa  za  maji  za  plastiki  zilizo  tupu  • Kata  sehemu  za  chini  za  chupa  (kadiri  ya  sentimeta  6  au  nchi  2.5)    • Hakikisha  ukataji  ni  wa  usawa/ulisawazishwa    –  epuka  ncha  kali    • Kata  vipande  vya  karatasi  isiyo  na  maandishi  au  manila  (kadiri  ya  sentimeta  4  kwa  4)  

• Andika  herufi  za  alfabeti  kwenye  vipande  vya  karatasi.  Herufi  au  namba  moja  kwa  kila  umbo.  • Uwe  na  herufi  nyingi  hasa  za  irabu  na  konsonanti  zinazopendwa  kutumiwa  zaidi  (kwa  kutengeneza  

maneno,  herufi  nyingi  zinahitajika)  • Chomeka  vipande  vya  karatasi  ndani  ya  chupa  moja  iliyokatwa    • Funika  kipande  hicho  cha  chupa  kwa  kutumia  kipande  cha  chupa  nyingine  iliyokatwa  ili  kutengeneza  

umbo  lenye  kipande  cha  karatasi  ndani  yake        Mapendekezo  ya  Upimaji    • Tambua  herufi  kwa  kuchagua  herufi  sahihi  kutoka  kwenye  fungu  • Sema  majina  ya  herufi  zinazoonyeshwa  • Tengeneza  maneno  rahisi  kwa  kupanga  maumbo  ya  herufi  • Tengeneza  silabi  kwa  kupanga  maumbo  ya  herufi  • Tengeneza  sentensi  rahisi,  beti  na  mashairi      • Oanisha  herufi  kubwa  na  herufi  ndogo  zinazolingana/husiana  • Kamilisha  fumbo  rahisi  la  maneno  kwa  kutumia  matofali  • Unda  maneno  yanayoanza  na  herufi  za  kufanana  • Soma  herufi,  silabi,  maneno  na  sentensi  zinazoonyeshwa  kwenye  seti  ya  maumbo  • Elezea/tambua  rangi  za  herufi  mbalimbali  zilizowasilishwa  • Nakili  herufi  na  maneno  kutoka  kwenye  maumbo  • Katika  vikundi,  tengeneza  benki  ya  maneno  kutoka  kwenye  maumbo  ya  herufi  kulingana  na  mwongozo.  

Mfano:  maneno  yanayoanza  au  kuishia  na  herufi  maalum;  maneno  yanayohusisha  kitu  (Vitu)    • uthern  hemisphere?    

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     42  

       

5.  Viambatisho  

1

5.1.  Mchakato  wa  Kufikiri  juu  ya  Ubunifu–  Mwongozo  wa  Mwezeshaji    Kufikiri  juu  ya  ubunifu  ni  mchakato  wakuwezeshwa  na  uliopangiwa  muda.    Warsha  hii  inahitaji  washiriki  kufanya  kazi  katika  vikundi  vidogo  vidogo  kuzingatia  ufumbuzi  kwa  changamoto  ya  ubunifu  (sehemu  ya  2.5.2).    Mchakato  wa  kufikiri  juu  ya  ubunifu  ulianzishwa  katika  chuo  kikuu  cha  Stanford  karibu  na  bonde  la  Silicon  –  kiini  cha  ubunifu  wa  ugunduzi  na  maendeleo  ya  kompyuta.    Kabla  ya  kuanza  kazi  ya  kufikiri  juu  ya  ubunifu,  unaweza  kutambulisha  vidokezo  vya  uchoraji  rahisi  kwa  washiriki  wako  (sehemu  ya  3.2).    Watu  wazima  wengi  huwa  hawataki  kuchora,  kwa  hiyo  ni  wakati  mzuri  kuwasaidia  kukumbuka  burudani/furaha  waliyokuwa  nayo,  kama  watoto  wakichora  dunia  yao.    Pia,  kwa  sababu  washiriki  wanategemewa  kutengeneza  vifani  (modeli  za  vitu  halisi  zenye  vipimo)  michoro  husaidia  zaidi  kuliko  dhana  za  kidhahania  zinazoelezeka  kwa  maneno  tu.  

2

 Waambie  washiriki  juu  ya  sehemu  zote  za  mchakato  ili  kutochukua  njia  ya  mkato:  • Changamoto  ya  ubunifu/kubuni  • Mchakato  wa  kufikiri  juu  ya  ubunifu  • Maelezo  ya  sampuli    • Matembezi  ya  Galari  • Tafakari  

 Hakikisha  umesoma  maelekezo  yafuatayo  kabla  ya  kuwezesha  warsha  yako  ya  kwanza.  Utahitaji  kuwa  na  kifaa  cha  kuhesabia  muda  (simu  ya  mkononi  inafanya  kazi  vizuri,  hususani  kama  ina  saa  ya  kidijitali).        

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     43  

 Hatua   Maelekezo  

Wote  /  kikundi  cha  watu  4  /  na  patna(mbia)  /  mtu  binafsi  

 Muda  

1.     Wambie  washiriki  kitendo  hiki  kitachukua  dk  60  na  kuna  weza  kuwa  na  muingiliano  wakati  kitakapoanza.  

Wote   Dakika  5  

2.   Kuandaa  washiriki  katika  vikundi  vidogo  vidogo  –  washiriki  4  kwa  kila  kikundi  ni  barabara      

Wote   Dakika  10  

3.   Toa  nakala  ya  changamoto  ya  ubunifu  kwa  kila  kikundi  (sehemu  ya  2.2.1.)    Karibisha  yeyote  katika  kila  kundi  kuwasomea  washiriki  wenzake  nakala  hiyo  kwa  sauti.    Uliza  kama  kuna  swali  lolote  kuhusu  mchoro.  

Wote   Dakika  10    

4.   Wape  washiriki  nakala  za  kitini  cha  karatasi  ya  kufanyia  kazi  ya  kufikiri  juu  ya  ubunifu  (Kifungu  5.2).    hakikisha  kila  mshiriki  ana  kalamu  ya  risasi.  

Wote   Dakika  5  

5.   • Wambie  washiriki  kutafuta  #1  nukuu  za  usaili    (uwezo  wa  kutambua  maono  ya  mwenzako)  katika  karatasi  zao  za  kufanyia  kazi.  

• Wambie  washiriki  wachague  patna/mbia  kutoka  kwenye  vikundi  vyao  na  kukaa  nao  pamoja  wakati  wote  wa  kazi  ya  kufikiri  juu  ya  ubunifu.      

• Wambie  washiriki  wawahoji  patna/wabia  wao  ili  kufahamu  ni  mada  ipi  ambayo  wanafuzi  wao  huiona  kuwa  na  changamoto?  Uliza  maswali  mengi  kujaribu  kupata  uwezo  wa  kutambua  wazo  la  mwingine  ya  kwa  nini  wanafunzi  wanapata  shida  na  mada  hiyo.    

• Wambie  wanakili  nukuu  za  usaili/mahojiano  yao  kwenye  #  1  ya  karatasi  zao  za  kufanyia  kazi      

• Simamia  makundi  ili  kuhakikisha  mshiriki  mmoja  anafanya  mahojiano  na  kurekodi    

Tegesha  saa  yako  kwa  dakika  4  kwa  ajili  ya  hatua  hii.  

Mbia   Dakika  4    

6.   • Muda  ukiisha,  waambie  wabia  kubadilishana  majukumu  na  kuanza  mahojiano/kuandika  nukuu  tena  za  mahojiano    

Tegesha  saa  yako  kwa  dakika  4  kwa  ajili  ya  hatua  hii.  

Patna/mbia   Dakika  4  

7.   • Wambie  wabia/patna  kupitia  upya  nukuu  zao  na  wawaulize  patna  wao  watoe  maelezo  zaidi,  habari,  mifano  juu  ya  matatizo  ambayo  wanafunzi  wanayo  katika  mada.  Waulize  kile  ambacho  wameshakijaribu-­‐ni  kipi  kilifanikiwa  ni  kipi  hakikufanikiwa.  

• Anza  mchakato  wa  mahojiano  upya,  kuanzia  na  mhojaji  wa  kwanza  kutoka  hatua  ya  5.    Wambie  warekodi  nukuu  zao  kwenye  #2  usaili/mahojiano  ya  kina  (uwezo  wa  kutambua  maono  ya  mwenzako).  

• Tegesha  saa  yako  kwa  dakika  3  katika  hatua  hii.  

Mbia/patna   Dakika  3    

 

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     44  

 

 Hatua   Maelekezo  

Wote  /  kikundi  cha  watu  4  /  na  patna(mbia)  /  mtu  binafsi  

 Muda  

8.   • Muda  ukipita,  wambie  wabia/patna  kubadilishana  majukumu  na  kuanza  mahojiano/mchakato  wa  kuchukua  nukuu  tena.      

Tegesha  saa  yako  kwa  dakika  3  katika  hatua  hii.  

Mbia     Dakika  3  

9.   • Wambie  washiriki  kuonesha  #3  kuelezea  jambo  kwenye  karatasi  yao  ya  kufanyia  kazi.      

• Kufanya  kazi  mtu  mmoja  mmoja,  wanahitaji  kubainisha  lengo  na  matarajio  ya  patna  wao.    LENGO  =  ni  nini  patna  anajaribu  kufanya  kuwasaidia  wanafunzi  wake?      

• Pia,  rekodi  umaizi  wowote  ambao  umeupata.    Umaizi  =  amejifunza  kitu  fulani  juu  ya  tatizo  au  changamoto  za  wanafunzi?  

Tegesha  saa  yako  kwa  dakika  3  katika  hatua  hii    

Mtu  binafsi   Dakika  3    

10.   • Wambie  washiriki  wachore  mawazo  5  ya  kuwasaidia  patna  wao  juu  ya  changamoto  waliyonayo.    Tumia  #4  wachore  mawazo  5  kwenye  makaratasi  yao  ya  kufanyia  kazi.  Wahamasishe  washiriki  kuchora  kuliko  kutumia  maneno  kuelezea  mawazo  yao.  

Tegesha  saa  yako  kwa  dakika  10  katika  hatua  hii        

Mtu  binafsi     Dakika  10  

11.   • Wambie  washiriki  kushirikishana  michoro  yao  5  na  patna/wabia  wao.      

• Wambie  warekodi  mrejesho  wa  patna  wao  na  maoni  kwenye  #5  pata  mrejesho  kutoka  kwa  patna  wako.        

Tegesha  saa  yako  kwa  dakika  5  katika  hatua  hii                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                      

Mbia   Dakika  5    

12.   • Pindi  muda  utakapoisha,  wambie  patna  wabadilishane  majukumu  na  fanya  mchakato  tena.      

Tegesha  saa  yako  kwa  dakika  5  katika  hatua  hii    

Mbia/patna   Dakika  5  

13.   • Kwa  kuzingatia  mrejesho  kutoka  kwa  wabia,  wambie  washiriki  kutumia  #6  kubuni  upya  wazo  lako.    Inaweza  ikawa  muunganiko  wa  mawazo  yote  au  wazo  lililoboreshwa,  au  wazo  lililoboreshwa  kutokana  na  mrejesho  wa  mbia/patna;  

•  Tena,  sisitiza  washiriki  uhitaji  wa  kuchora  mawazo  yao.  Tegesha  saa  yako  kwa  muda  wa  dakika  5  katika  hatua  hii  

Mbia   Dakika  5    

14.   • Wambie  wabia  kushirikishana  #6,  michoro  ndani  ya  vikundi  vidogo.  

• Kumbuka  makundi  ya  vigezo  vya  changamoto  ya  kubuni.  • Wambie  kila  kundi  dogo  kuchagua  mchoro  mmoja  ili  kufanya  

kifani/sampuli  

Kikundi  cha  watu  4  

Dakika  15    

 

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     45  

 Hatua   Maelekezo  

Wote  /  kikundi  cha  watu  4  /  na  patna(mbia)  /  mtu  binafsi  

 Muda  

15.   • Pindi  kila  kikundi  kitakapochagua  ubunifu  wa  kifani,  wambie  wabuni  kwenye  #7  chora  wazo  la  kikundi.      

Pindi  mchoro  huu  ukiwa  umekamilika,  kundi  linaweza  kuchunguza  eneo/mahali  pa  mtengenezaji    na  kutumia  vifaa  na  vitu  vilivyopo  kutengeneza  vifani  vyao.  

Kikundi  cha  washiriki  4    

Muda  utatofautina  kwa  kikindi  

16.   • Saidia  vikundi  kutumia  vifaa  na  vitu  vya  mahali  pa  mtengenezaji.      

Wahamasishe  kuhimiza  kwa  ajili  ya  utondoti  na  kujaribu  vifani  vyao.  

Kikunndi  cha  wanne    

Masaa  2  au  Muda  utakaopatikana  

17.   • Pindi  makundi  yakishaanza  kumaliza  vifani  vyao,  wahamasishe  kuanza  kusafisha  maeneo  yao  na  kurudisha  vifaa  mahali  pa  mtengenezaji.  

• Hamasisha  kuhifadhi  vitu  vilivyokwishatumika  na  kuvitumia  tena.  

Hakikisha  unahesabu  vifaa  vyote  na  hakikisha  kila  kifaa  kimerudishwa.  

Kikundi  cha  washiriki  4  

 

18.   • Wape  washiriki  wote  nakala  ya  maelezo  ya  sampuli  na  elezea  vipengele  (Sehemu  ya  2.2.4).  

•  Wambie  wakamilishe  karatasi  hii  kabla  ya  matembezi  ya  galari.      Safisha  meza  zote  na  andaa  kifani  na  maelezo  ya  sampuli  kwa  ajili  ya  matembezi  ya  galari.  

Mtu  binafsi  na  kikundi  cha  watu  4  

Dakika  15    

19.   Matembezi  ya  gallari    • Mwagize  kila  mshiriki  1  kutoka  kwa  kila  kikundi  kubaki  katika  

meza  yao  na  kuelezea  kazi  yao  kwa  makundi  mengine.      • Washiriki  wa  makundi  mengine  wanaweza  wakazunguka  

chumba  na  kuongea  na  wawakilishi  kutoka  kwa  kila  kikundi.  • Wakumbushe  makundi  kufuata  taratibu  wafikapo  kwenye  

meza.  Wakumbushe  washiriki  kuuliza  maswali  mazuri  na  yaheshima  kwa  kila  mwakilishi  wakikundi.  Hii  ni  fursa  ya  kushirikishana  wazo,  kurudiarudia  na  mafunzo  ya  kitaaluma.  

Wote   Dak.  30    Muda  unategemea  na  kiwango  cha  shauku  au  ari  

20.   Tafakari  • Wambie  washiriki  kurudi  kwenye  makundi  na  kushirikishana  

kile  ambacho  wemejifunza.  Wambie  kukamilisha  #8  tafakari  kwenye  karatasi  zao  za  kufanyia  kazi.  

Mtu  mmoja  mmoja  

Dak.  10    

 

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     46  

     

1

5.2.  Mchakato  wa  Kufikiri  juu  ya  Kubuni  –  Karatasi  ya  Kufanyia  Kazi  Washiriki  Mara  baada  ya  kuwapanga  washiriki  wako  kwenye  vikundi  vidogo  vidogo,  unaweza  kuanza  kazi  ya  kufikiri  kubuni.    Kwa  vidokezo  juu  ya  jinsi  gani  ya  kupanga  vikundi  vyako,  angalia  sehemu  ya  3.1.  Uundaji  wa  makundi        Kama  bajeti  yako  inaruhusu,  tafadhali  toa  nakala  1  ya  hii  karatasi  ya  kufanyia  kazi  kwa  kila  mshiriki.  Karatasi  ya  kufanyia  kazi  inatakiwa  itolewe  pande  

2

zote  mbili  za  karatasi  ya  A3.  Kama  huwezi  kupata  mashine  ya  kutolea  nakala  au  huwezi  kumudu  kutoa  nakala,  washiriki  wanaweza  kutengeneza  karatasi  zao  za  kufanyia  kazi  kwa  kutumia  karatasi  za  A3.    Sehemu  ya  5.1.    Kinakupa  wewe  mwezeshaji  muongozo  wa  kupanga  muda  wa  hatua  za  mchakato  na  kutoa  maelezo  kwa  washiriki.  Tafadhali  pitia  mwongozo  kabla  hujawezesha  mchakato  huu.  Pia  unahitaji  kifaa  cha  kutegesha  muda  kusaidia  kusimamia  kazi  ya  kufikiri  juu  ya  ubunifu  (kwa  mfano  simu  ya  mkononi).    

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     47  

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     48  

   

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     49  

6.  Tembelea  Vifaa/Zana  za  Kimtandao  Zilizopendekezwa  Kumbuka:  Kwa  bahati  mbaya  vifaa  vyote  hivi  vinahitaji  kufikika  na  upatikanaji  bora  wa  mtandao  wa  intaneti.  

1

 Programu  za  bure  za  Kompyuta  Autodesk  123D  (http://www.123dapp.com/)    Program  ya  modeli  ya  sitaha  tatu  imejumuishwa  na  maudhui  na  huduma  za  kutengeneza.  Pia  inauhusiano  na  miradi,  mitindo  na  modeli.  

 Scratch  (http://scratch.mit.edu/)      Kwa  kukwaruza,  unaweza  uka  programu  habari  yako  ya  kushirikisha  watu,  michezo  na  katuni  hai  —  na  kuwashirikisha  wengine  kwenye  jamii  ya  mtandao  juu  ya  utengenezaji  wako.    Kukwaruza  kunawasaidia  watoto  kujifunza  kwa  ubunifu,  kuwaza  kwa  mpangilio  na  kufanya  kazi  kwa  ushirikiano-­‐ujuzi  muhimu  katika  maisha  ndani  ya  karne  ya  21.    Kukwaruza  ni  mradi  wa  muda  mrefu  wa  watoto  wadogo  wa  chini  ya  kundi  la  MIT  Media  Lab.  Inatolewa  bure.    

 Vifaa  vya  Kuchunguza  Arduino  (http://www.arduino.cc/)  Arduino  ni  chanzo  cha  bure  cha  jukwaa  la  kielekroniki  cha  sampuli  chenye  kunyumbulika,  rahisi  kutumia  vifaa  na  programu  zake  za  kompyuta.  Ipo  kwa  kuwalenga  wasanii,  wabunifu,  wenye  upendeleo  wa  jambo  fulani  na  yeyote  yule  mwenye  shauku  ya  kutengeneza  vifaa  vyakuingiliana  au  mazingira.    Mahali  pa  kuangalia  Adafruit  (http://www.adafruit.com/)    Mahali  pa  vifaa  na  mawazo  ya  miradi.  

 Yakuelekeza  (www.Instructables.com)    Mahali  pa  kushirikishana  kile  unachotengeneza  na  wenzako.    ..Yakuelekeza  ina  uelekeo  kwa  miradi  mbali  mbali.    Vifaa  vya  kuvumbua  kujifunza  (http://www.inventtolearn.com/resources/)  inaorodhesha  vifaa  mbalimbali  vilivyoorodheshwa  kwenye  kitabu.    Kwa  vipindi,  wanatoa  huduma  bure  kupakua  vitabu  vyao.    Khan  Academy  (https://www.khanacademy.org/)      Saiti  ya  kujifunza  –  ni  bure.    Yaliyomo  maktaba  yanahusisha  hisabati,  mada  za  sayansi  kama  vile  baiolojia,  kemia,  fizikia  na  sayansi  ya  jamii  iliyo  na  orodha  ya  masuala  ya  fedha  na  Historia.      Vitu  vya  Kusoma  Vumbua  kusoma  -­‐  kutengeneza,  kutengeneza  vilivyoharibika,  na  uhandisi  ndani  ya  darasa(http://www.inventtolearn.com/)  Sylvia  Libow  Martinez  &  Gary  Stager    Kutumia  teknolojia  kutengeneza,  kutengeneza  vilivyoharibika,  au  kuboresha  vitu  tunavyohitaji  inaleta  uhandisi,  ubunifu,  na  sayansi  ya  kompyuta  kwenye  watu  wengi.  Kwa  bahati  mbaya  kwa  walimu,  harakati  za  utengenezaji  zinapitiliza  kwenye  mwinamo  wa  asili  wa  watoto  na  nguvu  ya  kujifunza  kwa  vitendo/kutenda.  

 Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni     50  

       

2

 Tengeneza  baruti/silaha  (http://makezine.com/)    Ulibuniwa  baada  ya  makanika  maarufu,  kutengeneza  silaha  ni  kwenda  kwenye  kiwanja  husika  cha  matengenezo  ya  vitu  vyote-­‐kuanzia  mawazo  kwenda  kwenye  vitu.  

 Maeneo  ya  kutembelea    MIT  Center  for  Bits  to  Atoms  (http://cba.mit.edu/about/)    Senta  ya  MIT  ya  chembe  na  atomi  ni  juhudi  inayohusisha  masomo  anuai  kuchunguza  mpaka  kati  ya  sayansi  ya  kompyuta  na  sayansi  ya  asili.    Stadi  za  CBA  namna  ya  kubadili  data  kuwa  vitu  na  vitu  kuwa  data.      MIT  Media  Lab  –  Lifelong  Kindergarten  (http://llk.media.mit.edu/)  Nyumbani  pa  mkwaruzo  –  Mitch  Resnick  na  timu  yake  ya  ubunifu  wa  vifaa  na  programu  za  kompyuta  za  kusaidia  ubunifu,  kuunda  na  kujifunza.    Taasisi  ya  Ubunifu  ya  Stanford  Hasso  Plattner    –  d.school  (http://dschool.stanford.edu/)  Nyumbani/mahali  pa  Kufikiri  juu  ya  ubunifu  …  Shule  ilianzishwa  na  Profesa  David  Kelley  wa  uhandisi  wa  makanika  mwaka  2004.    Ni  mradi  wa  kushirikiana  kati  ya  chuo  kikuu  na  Taasisi  ya  Hasso  Plattner  ya  chuo  kikuu  cha  Potsdam  Ujerumani.  Kama  ilivyo  kwa  shule  zingine  za  ubunifu,  inaunganisha  shughuli  na  mafunzo  ya  usimamizi  kuwa  uhandisi  wa  kiasili  na  matokeo  ya  ubunifu  wa  elimu.    

 Senta  ya  Ujifunzaji  wa  Uvumbuzi    (SUU)–  Kitivo  cha  Elimu,  Chuo  Kikuu  Cha  British  Columbia  Waazilishi  wa  Kupeleka  Utengenezaji  Mashuleni  –  Njia  ya  kina  ya  ujifunzaji  wa  kitaaluma  (www.innovativelearningcentre.ca)