36
KUSOMA KUSOMA SURA SURA ZENYE ZENYE SIJDA SIJDA ZA ZA W W AJIBU AJIBU KA KA TIKA TIKA SALA SALA Kimeandikwa na: Shaikh Abdul-Karim al-Bahbahani Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba Selemani Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page i

Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Kuna tofauti kati ya Shia na Sunni juu ya suala hili, na halikadhalika kuna tofauti ndani ya madhehebu za Sunni zenyewe. Wanazouni wa Kiislamu kama kawaida ya wanadamu, wamehitilafiana katika hukumu ndogondogo katika matendo ya ibada, lakini kama ilivyo, tofauti ndogo kati ya wanazuoni kwa wafuasi inakuwa ni mlima wa tofauti na kusababisha zogo lisilo na maana. Mambo ambayo wanazuoni wetu wamehitilafiana si katika asili au misingi ya dini, na isitoshe ni mambo machache sana ukilinganisha na yale tunayokubaliana nayo. Ili kupata ufafanuzi wa suala hili, ungana na jopo la wanazuoni ambao wamelichambua suala hili kwa uzuri sana kwa kutumia vyanzo sahihi vya Kiislamu ambavyo ni Qur’ani na Sunna.

Citation preview

Page 1: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

KUSOMAKUSOMA SURASURA ZENYEZENYE

SIJDASIJDA ZAZA WWAJIBU AJIBU

KAKATIKATIKA SALASALA

Kimeandikwa na:Shaikh Abdul-Karim al-Bahbahani

Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba Selemani

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page i

Page 2: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

©Haki ya kunakili imehifadhiwa na:AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 978 - 9987 - 512 - 54 - 6

Kimeandikwa na:Shaikh Abdul-Karim al-Bahbahani

Kimetarjumiwa na:Hemedi Lubumba Selemani

Kimepangwa katika Kompyuta na:Hajat Pili Rajab

Toleo la kwanza: Januari, 2010Nakala: 1000

Kimetolewa na kuchapishwa na:Alitrah Foundation

S.L.P. 19701 Dar es Salaam, TanzaniaSimu: +255 22 2110640

Simu/Nukushi: +255 22 2127555Barua Pepe: [email protected]

Tovuti: www.alitrah.orgKatika mtandao: www.alitrah.info

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page ii

Page 3: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page iii

Page 4: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

YALIYOMOHukmu ya kusoma sura hizo ndani ya sala.............................2

Dalili za Rai ya Mahanafi..........................................................2

Rai ya madhehebu mengine na dalili zao juu ya hilo...............4

Rai ya Imamiya na dalili zao juu ya hilo..................................7

Muhtasari wa uchunguzi..........................................................21

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page iv

Page 5: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

NENO LA MCHAPISHAJI

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabukiitwacho, Qira’atu ‘l-’Aza’im Fi ‘s-Swalah. Sisi tumekiita, KusomaSura zenye Sijda za Wajibu katika Sala.

Kitabu hiki kimeshughulikia suala la usomaji wa sura ambazo ndaniyake kuna aya za “sijda wajibu.”

Kuna tofauti kati ya Shia na Sunni juu ya suala hili, na halikadhalikakuna tofauti ndani ya madhehebu za Sunni zenyewe.

Wanazouni wa Kiislamu kama kawaida ya wanadamu,wamehitilafiana katika hukumu ndogondogo katika matendo yaibada, lakini kama ilivyo, tofauti ndogo kati ya wanazuoni kwawafuasi inakuwa ni mlima wa tofauti na kusababisha zogo lisilo namaana. Mambo ambayo wanazuoni wetu wamehitilafiana si katikaasili au misingi ya dini, na isitoshe ni mambo machache sanaukilinganisha na yale tunayokubaliana nayo.

Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huuwa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapouwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayohayana nafasi tena katika akili za watu.

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page v

Page 6: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemani (Lipumba)kwa kukubali jukumu hili la kukiftarjumi kitabu hiki. Vileviletunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyinginehadi kufanikisha kuchapishwa kwake.

Mchapishaji: Al-Itrah FoundationS. L. P. 19701Dar-es-Salaam, Tanzania.

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page vi

Page 7: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

NENO LA JUMUIYA

Hakika mirathi ya Ahlul-Bait ambayo imehifadhiwa na kambi yao nawafuasi wao dhidi ya upotovu inaonyesha ni kambi iliyokusanya ainambalimbali za taaluma za kiislamu.

Kambi hii imeweza kulea nafsi mbalimbali zilizo tayari kunywa kuto-ka kwenye chemchemu hiyo, na kuupa umma wa kiislamuwanavyuoni wakubwa wenye kufuata nyayo za ujumbe wa Ahlul-Bait.

Wanavyuoni waliokusanya vidodosa na maswali mbalimbali ya mad-hehebu na mitazamo tofauti ya kifikira kuanzia ndani ya desturi yakiislamu hadi nje ya desturi hiyo, huku wao wakitoa majibu na utatuzimakini juu ya maswali hayo ndani ya karne zote.

Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait imefanya hima kutetea utukufuwa ujumbe wa Uislamu na ukweli wake ambao umechafuliwa namakundi, madhehebu na wanaharakati mbalimbali wenye chuki naUislamu.

Jumuiya imefuata nyayo za Ahlul-Bait na za wafuasi wa kambi yaonjema ambayo imefanya hima kujibu madai yenye kuendelea nadaima ikijaribu kubaki ndani ya msitari wa mapambano kwa kiwan-go kinachohitajika ndani ya kila zama.

Hakika uzoefu ambao umehifadhiwa ndani ya vitabu vya wanavyu-uoni wa kambi ya Ahlul-Bait katika dhamira hii ni wa aina ya pekee,kwa sababu una akiba ya kielimu inayotegemea akili na hoja, hukuukijiepusha na matamanio na upendeleo uliokatazwa.

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page vii

Page 8: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

Unazungumza na wasomi na wanafikra wenye fani maalumu,mazungumzo ambayo yanakubalika kiakili na yanapokewa na maum-bile yaliyo salama.

Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait limekuja kuwapawatafuta ukweli hatua mpya ya uzoefu wa thamani katika ulingo wamazungumzo na maswali na kujibu hoja za utata zilizotolewa zamazilizopita au zinazotolewa leo kwa njia ya Tovuti, na hasa kwa kupe-wa nguvu na baadhi ya duru zenye chuki dhidi ya Uislamu naWaislamu.

Ikijiepusha na uchochezi uliokatazwa, na ni yenye kuhangaikiakuzishauri akili zenye kufikiria na nafsi zenye kutafuta haki, iliziweze kufikia kwenye haki ambayo inatolewa na Kambi ya Ahlul-Bayt ulimwengu mzima, ndani ya zama ambazo akili inaerevuka nanafsi na roho zinaboreka kwa kasi ya pekee.

Ni lazima tugusie kuwa mfululizo huu wa tafiti hizi umeandaliwa naKamati maalumu toka jopo la wanachuoni watukufu, hivyo tunatoashukurani njema kwa hawa wote na kwa wasomi na wahakiki kwakila mmoja miongoni mwao kwa kupitia sehemu ya tafiti hizi nakutoa mchango wao wa thamani kuhusu tafiti hizi.

Na sote tunategemea na kutaraji kuwa tutakuwa tumetoa kile tuli-chokiweza katika juhudi za kutekeleza baadhi ya wajibu tulionaombele ya ujumbe wa Mtukufu Mola Wetu Mlezi ambaye alimtumaMtume Wake na uongofu na dini ya haki ili aipe ushindi dhidi ya dinizote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi.

Jumuiya ya kimataifa ya Ahlu-BaitKitengo cha utamaduni

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page viii

Page 9: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 1

Page 10: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

HUKMU YA KUSOMA SURA HIZO NDANI YA SALA

Nazo kwa mujibu wa Fiqhi ya kishia ni Sura As-Sajda, Fuswilat, An-Najmi na Al-A’laq. Na wala haijumuishi maeneo mengine ya Aya zili-zo na sijda. Bila shaka madhehebu za kiislamu zimetofautiana kuhusuhukmu ya sijda itokanayo na kisomo, kwa yule aliyesoma moja yaAya zilizo na sijda akiwa ndani ya Swala yake.

Mahanafi wamesema: “Inajuzu kusoma, na aliye ndani ya Swalaatakapoisoma ni wajibu kwake haraka sana kusujudu ndani yaSwala.”

Madhehebu mengine yamesema: “Inaruhusiwa kuisoma ndani yaSwala lakini ni karaha kufanya hivyo. Na si wajibu kusujudu, kwanikwao wao haujathibiti wajibu wa sijda itokanayo na kisomo.”

Imamiya wanasema: “Hairuhusiwi kusoma moja ya Sura hizo nnendani ya Swala, na Swala hubatilika kwa hilo, kutokana na wajibu wakusujudu uliyomo humo.”

Uchambuzi huu umetengwa ili kudurusu rai hizi tatu na kubainishadalili zake na hatimaye kuteua iliyo sahihi, ile inayoungwa mkono nadalili ya Kitabu na Sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

DALILI ZA RAI YA MAHANAFI

Abu Hanifa na wafuasi wake wametetea wajibu wa sijda ya kisomokwa kutumia dalili mbalimbali, kati ya hizo ni kauli ya Allah:

Kusoma Sura Zenye Sijda

2

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 2

Page 11: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

“Basi wana nini hawaamini. Na wanaposomewa Qur’ani hawasu-judu.” (Surat Al-Inshiqaq: 20 - 21).

Hapo akawalaumu kwa kuacha kwao kusujudu na akawakemea, nahilo likaonyesha wajibu wa kusujudu.1 Na kati ya hizo ni kauli yaMtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Sijda ni wajibu kwa aliyeisikia na kwaaliyeisoma.”2

Na kati ya riwaya hizo ni ile riwaya iliyopokewa na Abu Hurairakutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kuwa alisema: “Mwanadamuasomapo Aya ya sijda Shetani hujitenga huku akisema: ‘Ole wangu!Mwanadamu ameamriwa kusujudu na amesujudu, anapata pepo.Nami niliamriwa kusujudu nikakataa, ninapata moto.’”

Amesema ndani ya kitabu Fat’hul-Qadiir: “Na asili ni kuwa mwenyehekima anaponukuu maneno ya asiyekuwa na hekima bila yakuyakanusha, basi hilo huwa ni dalili ya usahihi wake. Hivyo Aya nidhahiri kwenye wajibu, zaidi ya hapo ni kuwa Aya za sijda nazozinaonyesha hivyo, kwa sababu zenyewe zina vifungu vitatu:

Kifungu chenye amri iliyo wazi ikiamuru. Kifungu chenye hikaya yajinsi makafiri walivyopinga, kwani waliamrishwa kufanya hivyo. Nakifungu kingine kina hikaya ya kitendo cha manabii walivyosujudu.Na vyote kuanzia kutekeleza amri, kuwafuata manabii na kuwapinga

Kusoma Sura Zenye Sijda

3

1. Sharhu Fathul-Qadiir cha Muhammad bin Abdul-Wahid Juz. 1, Uk. 465.Pia tazama Al-Mughniy cha Ibnu Qadamah Juz. 1, Uk. 652. Al-Wahiy Al-Kabiir Juz. 2, Uk. 200, chapa ya Darul-Kutub Al-Il’miyyah.

2. Sharhu Fathul-Qadiir cha Muhammad bin Abdul-Wahid Juz. 1, Uk. 466.

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 3

Page 12: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

makafiri, ni wajibu, ila pale dalili itakapobainisha kuwa moja - kati yahivyo vitatu - si wajibu…..”3 Baada ya kuthibiti wajibu wake kwao,imekuwa kuutekeleza ni wajibu kwa kila anayeisoma Aya ya sijda,bila kuwepo tofauti baina ya yule anayekuwa katika hali ya Sala nanyingineyo. Sijda ya kisomo inapokuwa wajibu ndani ya Sala, kwaowao huchukua sifa ya Sala.4

RAI YA MADHEHEBU MENGINE,NA DALILI ZAO JUU YA HILO

Madhehebu mengine ya kisunni yenyewe yameona kuwa sijda yakisomo si wajibu, wakasema kuwa yenyewe ni mustahabu. IbnuQadamah amesema: “Hakika sijda ya kisomo ni Sunna iliyotiliwamkazo, na wala si wajibu kwa imamu wetu, Malik, Al-Awzaiy, Al-Laythi na Shafiy. Nayo ndio madhehebu ya Umar na mwanayeAbdullah.”5

Al-Mawridiy amesema: “Ni mustahabu kwa anayeisoma au kuisikiatoka kwa anayeisoma, kusujudu kwa ajili yake, awapo ndani ya Salaau nje ya Swala. Na wala si wajibu kwake, sawa awe msomaji aumsikiaji, na hii ndio kauli ya Umar na ndio madhehebu ya Malik.”6

Kusoma Sura Zenye Sijda

4

3. Sharhu Fathul-Qadiir cha Muhammad bin Abdul-Wahid Juz. 1, Uk. 466,chapa ya Daru Ihyait-Turathil-Arabiy.4. Sharhu Fathul-Qadiir cha Muhammad bin Abdul-Wahid Juz. 1, Uk. 470,chapa ya Daru Ihyait-Turathil-Arabiy.5. Al-Mughniy Juz. 1, Uk. 652.6. Al-Wahiy Al-Kabiir cha Ali bin Muhammad Al-Mawridiy Juz. 2, Uk. 200,chapa ya Darul-Kutub Al-Il’miyyah.

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 4

Page 13: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

Na Ibnu Hazmi anesena mfano wa hayo ndani ya kitabu Al-Mahalliy.7

Ibnu Qadamah ametetea rai ya masunni wengi kwa kusema: “Natunayo riwaya aliyoipokea Zayd bin Thabit, amesema: ‘Nilisoma (An-Najmi) kwa Mtume na hakusujudu yeyote yule miongonimwetu.’Nayo inakubalika na kwa kuwa yenyewe ni ijmai ya sahaba.Bukhari na Al-Athram wamepokea kutoka kwa Umar kuwa alisomasiku ya Ijumaa akiwa juu ya mimbari Sura Nahli mpaka alipofika Ayaya sijda, akashuka akasujudu, na watu wakasujudu. Ilipowadia Ijumaailiyofuata akaisoma tena mpaka alipofika Aya ya sijda, akasema:‘Enyi watu! Hakika tunapita kwenye sijda, hivyo atakayesujuduatakuwa amepatia, na ambaye hatosujudu si dhambi kwake.’ Na Umarhakusujudu.

Na katika lafudhi nyingine: “Hakika Allah hakutuwajibisha kusujuduila tupendapo wenyewe.”

Na katika riwaya ya Al-Athram: “Akasema: ‘Ni wajibu juu yamitume wenu, hakika Allah hakuifaradhisha juu yetu ila tutakapo.’

Akaisoma wala hakusujudu na akawazuia kusujudu. Na hili lilikuwambele ya kundi kubwa na hakuna yeyote aliyekanusha wala kunukuukinyume chake.

Ama Aya, yenyewe imewalaumu wao kwa kuacha kusujudu kwa kulekutoamini ubora wake wala sheria yake, na kipimo chao kinatengukakwa sijda ya sahau, kwani yenyewe kwao si wajibu.”8

Kusoma Sura Zenye Sijda

5

7. Al-Mahalliy Juz. 5, Uk. 10, chapa ya Darul-Jayli.8. Al-Mughniy Juz. 1 Uk. 652.

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 5

Page 14: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

Al-Mawridiy ametetea kauli yake kwa kusema: “Dalili yetu ni riwayaya Atau bin Yasar iliyopokewa kutoka kwa Zayd bin Thabit, kuwa ali-soma Sura Najmi mbele ya Mtume wa Allah (s.a.w.w.) na hakusu-judu. Hivyo lau kama ingekuwa ni wajibu basi Mtume wa Allah ange-sujudu na angemwamuru Zayd kufanya hivyo. Na imepokewa kuwa:Kuna mtu mmoja aliisoma Aya ya sijda mbele ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) kisha akasujudu, na akaisoma mwingine lakini yeyehakusujudu, Mtume akasema: ‘Ulikuwa imamu wetu, lau kama unge-sujudu tungesujudu.’ Ndani ya kisa hicho kuna dalili mbili:Mojawapo: Hakika yeye hakumwamuru kusujudu na aliridhiakuiacha kwake. Ya pili: ‘Lau kama ungesujudu tungesujudu’ ipo kati-ka hali ya hiari na kufuata hiari hiyo.

Shafiy amepokea kuwa Umar bin Khattab alisoma Aya ya sijda juu yamimbari siku ya Ijumaa, kisha akasujudu. Akaisoma tena Ijumaa iliy-ofuata, watu wakajiandaa kusujudu, akasema: “Enyi watu! Ni wajibujuu ya mitume wenu, hakika Allah hajaifaradhisha kwetu ilatutakapo.’

Pia Shafiy amepokea kutoka kwake kuwa alisema: “Atakayesujuduatakuwa amefanya jambo jema, na ambaye hatosujudu hana dhambi.”Hivyo kauli yake hii mbele ya hadhara ya kundi la muhajirina naanswari, na wao kutompinga, ni dalili ya kuwa wao wamekubalianakwa ijmai kuwa yenyewe si wajibu.

Na kwa sababu katika baadhi ya hali sijda ni wajibu kutekelezwa namsafiri, hivyo ikalazimu isiwe wajibu kiasili kama ilivyo sijda yaSunna. Na kwa kuwa yenyewe ni Swala isiyo ya wajibu, hivyo ikalaz-imu hata sijda yake kiasili isiwe wajibu iwapo utakariri kuisoma Ayahiyo. Na kwa kuwa sijda hiyo imekuwa si wajibu unapokariri kuiso-ma (Aya hiyo), imekuwa pia si wajibu uanzapo kuisoma, kama ilivyotohara. Na kwa sababu kila sijda ambayo haibatilishi Sala kwa

Kusoma Sura Zenye Sijda

6

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 6

Page 15: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

Kusoma Sura Zenye Sijda

7

kuiacha ni Sunna kama ilivyo sijda ya sahau.

Ama kauli yake:

“Na wanaposomewa Qur’ani hawasujudu.” (Sura Al-Inshiqaq:21).

Muradi wake ni makafiri, kwa kule kufuatiwa na ahadi ya adhabuambayo haimsitahiki yule aliyeacha sijda ya kisomo. Na kauli yake:“Hawasujudu.” Inamaanisha hawaitakidi, hivi huoni kauli yake:“Bali waliokufuru wanakanusha tu.” (Sura Al-Inshiqaq: 22). Amakipimo chao, chenyewe ni batili kwa sijda ya sahau. Zaidi ya hapo nikuwa maana ya sijda ya Swala ni ile iliyoratibiwa ndani ya nyakatimaalumu.”9

Hii ndio rai yao katika asili ya sijda ya kisomo. Ama kusoma ndani yaSwala zile Aya za sijda zikiwemo Sura nne zenye Aya zilizo na sijda,ni jaizi kwao na hawana maneno katika hilo. Kisha wanatenganishahukmu ya suala hilo kati ya Swala ya jamaa na ile ya mtu mmoja.

RAI YA IMAMIYA NA DALILI ZAO JUU YA HILO

Imamiya wametoa dalili juu ya rai yao kuhusu mas’ala hii kwa kutu-mia dalili ambazo tutazinukuu kutoka kwenye vyanzo vyao maarufu,moja baada ya nyingine, baada ya kuondoa zile dalili zilizo mahsusikwao, ambazo wametumia kuthibitisha hilo. Nazo ni riwaya zili-zopokewa kutoka kwa Maimamu wa Ahlul-Bait (a.s.) kuhusu kadhiahii.

9. Al-Wahiy Al-Kabiir Juz. 2 Uk. 200 – 201.

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 7

Page 16: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

As-Sayyid Al-Murtaza amesema katika kitabu Al-Intiswar: “Na kige-zo cha kuzuia hilo ukiachia mbali ijmai iliyojikariri, ni kuwa kilamoja kati ya Sura hizi ina sijda ya wajibu isiyo na shaka, hivyo aki-isujudu atakuwa amezidisha (sijda) ndani ya Swala, na kama ataiachaatakuwa amevuruga wajibu.”10

Sheikh Tusy amesema ndani ya kitabu Al-Khilaaf kuhusu kutoruhusi-wa kusoma Sura hizo ndani ya Swala: “Dalili yetu ni ijmai ya kundiletu na habari zao, na pia dhima yenye kushughulishwa na Swala kwayakini, na wala haiondoki ila kwa yakini mfano wake, nayo ni kuso-ma Sura isiyo na Aya yenye sijda ya wajibu….”11.

Na akathibitisha wajibu wa kufanya sijda katika Sura zenye Ayayenye sijda ya wajibu, kwa kutumia dalili mbalimbali, ya kwanza ni:“Ijmai ya kundi, hakika wao hawatofautiani kuhusu hilo.”12

Al-Alamah Al-Hilliy ametoa dalili ndani ya kitabu At-Tadhkirah juuya kutoruhusiwa kusoma ndani ya Swala zile Sura zenye Aya zenyesijda ya wajibu, akasema: “……Na ni kwa kuwa sijda ya kisomo niwajibu, na kuzidisha sijda kunabatilisha (Swala).

Na Sunni wamekubaliana kuwa inajuzu kiasili. Na hakika inakuwa nihoja lau kama tu hakijajitokeza kipingamizi.”13

Mwandishi wa kitabu Al-Jawahir ameongeza kusema: “Wajibu wasijda ya kisomo unaweza kupatikana toka ndani ya kauli yake:

Kusoma Sura Zenye Sijda

8

10. Al-Intiswar: 146.11. Al-Khilaaf, Juz. 1, Uk. 426, chapa ya Jamaatul-Mudarrisiin- Qum.12. Al-Khilaaf, Juz. 1, Uk. 431, chapa ya At-Tadhkirah, Juz. 3, Uk. 146.13. Jamaatul-Mudarrisiin- Qum.

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 8

Page 17: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

“Na wanaposomewa Qur’ani hawasujudu.” (Sura Al-Inshiqaq:21)Kwa kuzingatia kuwa ni lawama kwa kuacha kusujudu kwa ajili yakisomo cha Qur’ani. Na baada ya ijmai na mengineyo haina sehemuila Sura nne zilizotajwa zilizo mahsusi…”14

Ni wazi kuwa rai ya Imamiya imejengeka juu ya misingi miwili: Wakwanza: Wajibu wa kusujudu pindi usomapo Aya yenye sijda katikaSura nne zenye Aya zilizo na sijda ya wajibu.

Wa pili: Swala hubatilika kwa kule kuleta sijda kwa ajili ya Aya yenyesijda ya wajibu, kwa kuzingatia kuwa sijda hiyo ni ziada iliyo nje yaasili ya Swala.

Na ni maalumu kuwa mukalafu analazimika kuitimiza Swala nakutoibatilisha kwa kuiletea kitendo cha nje pindi awamo ndani yaSwala, hivyo inalazimu kutokutenda mfano wa kitendo hicho, kwakuwa chenyewe wakati huo kitakuwa ni miongoni mwa mifano halisiya wazi kabisa yenye kupingana na lengo. Hivyo misingi yote hiimiwili kwa pamoja inazaa hali ya kutokuruhusiwa kusoma Surazenye Aya zenye sijda ya wajibu ndani ya Swala.

Mahanafi wamewaafiki Imamiya katika msingi wa kwanza, hukuwenyewe wakipanua wajibu hadi katika kila Aya yenye sijda ndani yaQur’ani Tukufu. Na wamewakhalifu katika msingi wa pili, na masun-ni wengine wamewakhalifu katika misingi yote miwili.

Kusoma Sura Zenye Sijda

9

14. Jawahirul-Kalaam, Juz. 10, Uk. 214, chapa ya Najaf Tukufu.

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 9

Page 18: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

Licha ya kuwa masunni, kuanzia mahanafi hadi wengineo wametoadalili mbali mbali tulizozitaja huko mwanzo juu ya kukhalifu kwaomisingi hiyo miwili, ila ni kuwa uchunguzi wa kina wa kielimuunatuongoza kuamini utimilifu wa misingi hiyo miwili, na kutosihikwa mjadala na upinzani uliotolewa juu yake.

Ama kukhalifu kwao msingi wa kwanza ni kuwa wao wamedai kuwasijda ya kisomo cha Sura hizo si wajibu, kwa mujibu wa dalili, nazoni:

Wamepinga kuwa Aya hii:

“Na wanaposomewa Qur’ani hawasujudu.” (Sura Al-Inshiqaq:21)inaonyesha wajibu wa kusujudu.Riwaya ya Atau bin Yasar.

Riwaya ya mtu mmoja aliyoipokea toka kwa Mtume wa Allah(s.a.w.w.) kuhusu hilo.

Riwaya kutoka kwa Umar bin Khattab kuhusu hilo, inaonyesha ijmaiya sahaba juu ya kutowajibika kusujudu.

Hakika kila sijda isiyobatilisha Sala kwa kuiacha ni Sunna.

Hakika kule kutekeleza sijda ya kisomo ukiwa juu ya mnyama kwamsafiri anayeweza kuteremka kunaonyesha kuwa yenyewe ni musta-habu.

Hizi ndio hoja na dalili ambazo wamezitumia kutetea kuwa sijda yakisomo si wajibu, na sisi hapa tutazijadili ili tuone kiwango cha nguvuzake.

Kusoma Sura Zenye Sijda

10

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 10

Page 19: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

Ama kupinga kwao Aya kuonyesha wajibu ni madai yasiyo na hoja.Na pia ila ya upinzani wao kuwa msemezwa katika Aya ni makafiri,nayo pia si sahihi. Kwa sababu kipimo ni ule mjumuisho wa lafudhina si sababu, kama wasemavyo wafasiri, na kuwa sababu haiifungihukumu, kama wasemavyo wanataaluma wa misingi ya sheria, balimsemezwa katika Aya ni mjumuisho wa muumini na kafiri, hiyo nikwa sababu kitu kilichokua maudhui yaliyopelekea Aya kushuka nikule kutokusujudu kwa ajili ya jambo ambalo lenyewe tu lilivyolinastahiki sijda, bila kujali usadikisho na imani, nalo ni kisomo chaQur’ani Tukufu.

Na ni wazi kuwa ubaya wa hali hii unaongezeka pale inapokuwa kulekutokusujudu kunaambatana na ukanushaji wa kiburi, hivyo makafiriwakawa ndio wasemezwa wa mwanzo katika Aya, japokuwa mse-mezwa wake wa asili ni mjumuiko wa kafiri na muumini.

Kwani ni wazi kuwa sijda haitekelezwi ila na muumini, na wala hai-ingii akilini Aya iwalaumu makafiri kwa kutokumsujudia Allahwakati wa kusoma kitabu Chake, ilihali wao bado wana hali ya ukafirina ukinzani.

Na hakika Aya imewalaumu wao (makafiri) kwa kutokusadiki kwaona kutoamini kwao Aya za Allah. Haistahiki kwa mwanadamu kuami-ni tu bali inastahiki kwake pia kusujudu pindi asomapo Aya hizo,hivyo Aya ilianza kulaumu kule kutoamini na ikamalizia kulaumukule kutokusujudu:

“Basi wana nini hawaamini. Na wanaposomewa Qur’ani hawasu-judu.” (Sura Al-Inshiqaq: 20 - 21).

Kusoma Sura Zenye Sijda

11

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 11

Page 20: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

Hivyo kinachotafutwa na Aya kutoka kwa makafiri ni imani, usadik-isho na kukubali, kisha baada ya kuamini, kusadikisha na kukubaliwanaombwa watekeleze amri mpya, nayo ni kusujudu pindiwasomapo Aya za Kitabu Kitukufu. Kama ilivyo amri kwa upande wawaumini wengine.

Na kwa kuwa ijmai imesimama juu ya msingi wa kutokuwepo wajibuwa sijda kwa ajili ya kusoma Qur’ani Tukufu, hivyo ili kukusanyabaina ya Aya na ijmai hii, inakuwa ni wajibu kusujudu wakati wakusoma Aya mahsusi, nazo ni zile zenye maana ya amri ya kusujudu,hivyo Aya ikaonyesha kwa ukamilifu bila doa ule wajibu wa sijda yakisomo.

Ama riwaya ya Atau bin Yasar kutoka kwa Zayd bin Thabit,wameipokea Bukhari na Muslim katika Sahih zao. Na maelezo yayake katika Bukhari ni kutoka kwa Ibnu Qusayt, kutoka kwa Atau binYasar, kuwa alimpa habari kuwa alimuuliza Zayd bin Thabit, akadaikuwa alisoma mbele ya Mtukufu Mtume: “Wan-Najmi” na hakusu-judu.15

Na katika Sahih Muslim ni kutoka kwa IbnuQusayt, kutoka kwa Atau bin Yasar, kuwa alimpa habari kuwaalimuuliza Zayd bin Thabit kuhusu kusomwa na imamu, akasema:“Haina wajibu wowote wa kusomwa na imam.” Na akadai kuwa yeyealisoma kwa Mtume wa Allah: “Wan-Najmi” na hakusujudu.16

Ni kuwa riwaya inatunukulia Sunna ya kitendo cha Mtume (s.a.w.w.),na kuna riwaya nyingine inatunukulia Sunna ya kitendo chake(s.a.w.w.) kikionyesha kuwa yeye alisujudu katika Sura An-Najmi.Riwaya hiyo kaipokea Abdullah bin Umar na ameitaja Bukhari kati-

Kusoma Sura Zenye Sijda

12

15. Sahih Bukhar Juz. 2 Uk. 32, chapa ya Darul-Fikr.16. Sahih Muslim Juz. 2 Uk. 88, chapa ya Darul-Fikr.

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 12

Page 21: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

ka Sahih yake kwenye mlango wenye jina “Mlango wa sijda yaNajmi.” 17

Maarufu ni kuwa Sunna ya kitendo ni fumbo huwa haitumikikuthibitisha wajibu wala mustahabu, bali hutumika kuthibitisha ilehali ya kuthibiti jambo kisheria, (bila ya kujua hili lililothibiti kishe-ria ni mustahabu au ni wajibu).

Kama ambavyo riwaya ya Abdullah nayo haionyeshi wajibu, kwanihuenda kusujudu kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa ni kwa ajiliya mustahabu. Kama ambavyo pia riwaya ya Atau bin Yasarhaionyeshi kutokuwa wajibu, kwani huenda Mtukufu Mtume(s.a.w.w.) alisujudu baada ya hapo, na hasa ukizingatia kuwa mpokeziambaye ni Atau amenukuu jibu kutoka kwa Zayd bin Thabit, ambaloyeye (Atau) amelisifu kwa “Anadai”, neno ambalo hutumika kumaan-isha maneno ambayo bado hayajathibitika, nayo ni sawa na madaimatupu, na ni kama ndani ya nafsi ya Atau mna shaka dhidi yamaneno ya Zayd.

Ama riwaya ya mtu ambaye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia:“Lau kama ungesujudu tungesujudu.” Aliyoyataja mwandishi wakitabu Al-Hawiy Al-Kabiir, yenyewe haina nyororo ya wapokezi,hivyo haina mazingatio yoyote.

Ama dai la ijmai ya sahaba kuhusu suala hili, ijmai iliyotokana namaneno ya Umar bin Khattab na kunyamaza kwa sahaba, iliyopoke-wa ndani ya Sahih Bukhar18 na Sunanul-Bayhaqiy19 , iwapo itasihibasi itahusu Aya mbili tu ‘49 na 50’ katika Sura Nahli. Kwa sababu

Kusoma Sura Zenye Sijda

13

17. Sahih Bukhari Juz. 2 Uk. 32, chapa ya Darul-Fikr.18. Sahih Bukhari Juz. 2 Uk. 33 - 34, chapa ya Darul-Fikr.19. Sunanul-Bayhaqiy Juz. 2 Uk. 320, milango ya sijda ya kisomo, mlangowa ambaye hajaona wajibu wa sijda ya kisomo.

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 13

Page 22: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

ilivyotajwa ndani ya Sahih Bukhari ni kuwa Umar bin Khattab aliso-ma Sura Nahli ndani ya Ijumaa mbili zilizotajwa, akasujudu katikaIjumaa ya kwanza na akakataza kusujudu katika Ijumaa ya pili, kwasababu madhehebu yametofautiana kuhusu idadi ya maeneo yenyesijda ndani ya Qur’ani Tukufu. Kwa mujibu wa madhehebu ya Ahlul-Bait si wajibu kusujudu kila sehemu ya Qur’ani iliyo na amri ya kusu-judu au maana yake, bali kuna maeneo maalumu ambayo ndio wajibukusujudu na si mengine.

Na itikadi ya Ahlul-Bait ni kuwa sijda ni wajibu katika sehemu nne,nazo ni Aya zenye sijda zinazopatikana katika Sura As-Sajda, An-Najmi, Al-A’laq na Fuswilat. Hiyo ni kinyume na mahanafi ambaowanaona kuwa ni wajibu kusujudu katika kila sehemu yenye sijda yakisomo katika Qur’ani, ambazo idadi yake kwao wao inafikia sehemukumi na nne.20

Na ni mustahabu katika maeneo mengine ya sijda ya Qur’ani Tukufu,nayo ni moja ya maeneo mengine kumi, yakiwemo maeneo hayoyaliyotajwa ya Sura Nahli, hivyo ijmai hii ya sahaba haikatazi wajibuwa sijda ya Sura zenye Aya zilizo na sijda ya wajibu, bali inathibitishakuwa katika sehemu hii ya Qur’ani Tukufu (Aya mbili za Sura Nahli),sijda ni mustahabu, nayo inaunga mkono madhehebu ya Ahlul-Bait.

Ama kauli yao kuwa kila sijda ambayo haibatilishi Swala kwakuiacha ni mustahabu, kauli hiyo ni sahihi katika sijda ya Swala. Nakitendo cha kuivusha hukmu hadi kwenye sijda ya kisomo ni kufanyaulinganisho (Qiyas), na ulinganisho ni batili kwa mujibu wa baadhi yamadhehebu ya kisunni, achia mbali Imamiya. Na wenye kusema ulin-ganisho ni sahihi wanaona kuwa kulinganisha sijda ya kisomo nasijda ya Swala ni ulinganisho batili.21

Kusoma Sura Zenye Sijda

14

20. Al-Fiqhi Alal-Madhahib Al-Arbaa Wamdh’hab Ahlil-Bayti Juz. 1, Uk.605.21. Umdatul-Qariy Juz. 7, Uk. 96, chapa ya Darul-Fikr.

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 14

Page 23: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

Ama kitendo cha msafiri kufanya sijda ya kisomo kwa kuashiriaawapo juu ya mnyama, na kutokulazimika kuteremka kwa ajili yake,hakionyeshi mustahabu, kwani kila faradhi ina sifa zake mahsusi,hivyo hakuna kizuizi kwa sijda ya kisomo kuwa na sifa hii. Na laukama maneno ya mpinzani yatasihi, basi itawajibika kusema kuwaSwala ya maiti ni mustahabu, kwani yenyewe haina sijda wala rukuu.

Ama maneno ya Al-Mawridiy ambayo kasema: “Asili yake ni sijda yaSunna, na ni kwa kuwa ni Swala isiyokuwa ya wajibu, hivyo imelaz-imu hata sijda yake isiwe wajibu kiasili iwapo atakariri kuisoma Ayahiyo, na kwa kuwa imekuwa si wajibu unapokariri kuisoma basiimekuwa si wajibu pia uanzapo kuisoma.”

Haijafahamika ndani ya maneno yake maana yenye kuingia akiliniwala hoja ipatikanayo. Hivi ni ipi maana ya kusema: Asili katika sijdaya kisomo ni sijda ya Sunna, na kuwa sijda ya Sunna ni Swala isiyoya wajibu?

Kisha Swala ya Sunna japokuwa yenyewe binafsi si wajibu lakiniinapokosa nguzo zake kama vile sijda na rukuu huwa batili, na wakatihuo huo haiitwi Swala hata isemwe kuwa sijda yake si wajibu. Hivyoni lazima kuleta nguzo za Swala ili mukalafu alipwe thawabu juu yahilo. Na yule asiyeleta nguzo yoyote miongoni mwa nguzo ni sawa nayule ambaye hajaileta Sunna yenyewe, hivyo yeye hana kosa kwakuwa Sunna si wajibu, na si mwenye kupata thawabu kwa kuwa yupokwenye hukmu ya mtu ambaye hajaleta Sunna yenyewe.

Kisha nini maana ya kauli yake: “Atakapokariri kusoma Aya hiyo.”22

Kwani hakuna aliyesema kuwa sijda ya kisomo ni wajibu wakati wakuikariri Aya. Na kila anayesema wajibu au mustahabu anaona hilo ni

Kusoma Sura Zenye Sijda

15

22. Al-Hawiy Al-Kabiir cha Al-Mawridiy Juz. 3, Uk. 201, kitabu cha Swala,mlango wa sifa ya Swala na idadi ya sijda za Qur’ani.

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 15

Page 24: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

wakati wa kusoma Aya, na hakuna anayesema kuwa hilo ni wakati wakuikariri tu.

Kwa maelezo haya zinabatilika zile dalili walizozitaja juu ya sijda yakisomo, kuwa si wajibu. Na inathibiti kuwa Aya inaonyesha wajibutimilifu, na zaidi ya hapo ni kauli ya Uthman bin Affan ambayokaipokea Bukhari akisema: “Hakika sijda ni juu ya mwenyekuisikia.”23 Na Ibnu Abu Shayba amepokea ndani ya kitabu chakeAl-Musannaf24 kutoka kwa Ibnu Umar kuwa alisema: “Sijda ni juu yamwenye kuisikia.”

Na Al-Ayniy ameandika dalili nyingine juu ya wajibu wa sijda yakisomo ndani ya ufafanuzi wake wa Sahih Bukhar, nayo ni ile aliy-oipokea Ibnu Abu Shayba kutoka kwa Hafsa, kutoka kwa Hujjaj,kutoka kwa Ibrahim na Nafiu na Said bin Jubair, kuwa wao wamese-ma: “Atakayesikia Aya ya sijda ni juu yake kusujudu.” Na kutoka kwaIbrahim kwa njia sahihi: “Mtu atakaposikia Aya ya sijda ilihali akiwaanaswali basi asujudu.”

Na kutoka kwa As-Shaabiy: “Sahaba wa Abdullah walikuwa wasiki-apo Aya ya sijda husujudu, sawa wawe ndani ya Swala au nje.”

Shaabah amesema: “Nilimuuliza Hamada kuhusu mtu anayesali kishaakasikia Aya ya sijda, akasema: Asujudu. Na Al-Hakam alisemamfano wa hayo. Na ametusimulia Hashim: Alitupa habari Mughirakutoka kwa Ibrahim, kuwa alikuwa akisema: “Mwenye janabaakisikia Aya ya sijda akoge kisha aisome na kusujudu, na kamahawezi kusoma kwa ufasaha basi asome Aya nyingine, kisha asu-judu.” Na ametusimulia Ubaydullah bin Musa kutoka kwa Aban Al-

Kusoma Sura Zenye Sijda

16

23.Sahih Bukhari, Juz. 2 Uk. 33.24. Al-Musannaf, cha Ibnu Abu Shayba Juz. 1, Uk. 457.

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 16

Page 25: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

Attar, kutoka kwa Qatadah kutoka kwa Said bin Al-Musayyab kutokakwa Ibrahim, kuhusu mwenye hedhi asikiapo Aya ya sijda, akasema:“Ataashiria kwa kichwa chake na aseme: ‘Ewe Allah nimesujudu kwaajili Yako.’”

Na kutoka kwa Hasan kuhusu mtu aliyesahau sijda mwanzoni mwaSwala yake na hakuikumbuka mpaka alipofika mwishoni mwa rakaaya Swala yake, akasema: “Atasujudu sijda tatu.” Na kama hakuikum-buka mpaka alipomaliza Swala yake kabla ya kutoa salamu, akasema:“Atasujudu sijda moja madamu tu hajazungumza, na kamaatazungumza basi ataianza Sala mwanzo.”

Na kutoka kwa Ibrahim: “Atakaposahau sijda basi aisujudu popotepale atakapoikumbuka ndani ya Swala yake.” Na Mujahid aliulizwakuhusu mtu anayeshakia sijda ilihali akiwa ameketi, hajui ameshasu-judu au la, mujahid akasema: “Ukitaka isujudu, na utakapomalizaSwala yako sujudu sijda mbili ilihali ukiwa umeketi. Na ukitakausisujudu, na mwishoni mwa Swala yako sujudu sijda mbili ilihaliukiwa umeketi.”25

Haya ndio maneno yote kuhusu msingi wa kwanza.

Ama msingi wa pili, ambao ni kubatilika Swala kwa sijda ya kisomo,hilo ni kati ya mambo yaliyo wazi kabisa, kwa sababu mukalafu ame-jituma yeye mwenyewe kwa hiari yake kufanya sijda hii ndani yaSwala, kwa ajili ya kusoma kwake moja ya sura hizo ndani ya Swala,hivyo ameleta jambo lililo nje ya asili ya Swala, na tayari wanazuoniwa sheria ya kiislamu wamesema kuwa, Sala hubatilika kwa kule kui-wekea amali nyingi.

Kusoma Sura Zenye Sijda

17

25. Umdatul-Qariy Juz. 7 Uk. 95, chapa ya Darul-Fikr.

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 17

Page 26: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

Al-Jazairiy amesema ndani ya kitabu Al-Fiqhi Ala Madhahib Al-Arbaa kuwa: “Swala hubatilika kwa kuiwekea amali nyingi ambazosi katika jinsia ya Swala, nazo ni zile zinazomfanya mtazamaji aonekuwa mtendaji wake hayumo ndani ya Swala…..Ama mwenye kusaliatakapotenda amali ya ziada iliyo nje ya jinsia ya Swala, kama vilekuzidisha rukuu au sijda, basi ikiwa ni kwa kukusudia, kichache aukingi, vyote hubatilisha. Na kama ni kwa kusahau basi Swala yakehaibatiliki kwa namna yoyote ile.”26

Kwa ajili hiyo Shafiy amesema: “Mwenye kuswali atakaposoma Ayaza sijda ndani ya Swala, na akawa kwa sijda hiyo anakusudia sijda yakisomo, Swala yake imebatilika.”27

Kauli hiyo inakaribiana na kauli ya Imamiya. As-Sayyid MuhammadKadhim Al-Yazdiy (r.a.) amesema ndani ya kitabu Al-Ur’watu Al-Wuthqa: “Hairuhusiwi kusoma moja ya Sura zenye Aya zilizo na sijdaya wajibu ndani ya Swala ya faradhi, na lau kama ataisoma makusu-di, basi atalazimika kuianza upya Swala.”28

Hayo yote ni kuachia mbali tofauti iliyopo kati ya kauli mbili upandewa mambo mawili: Upande wa kwanza wa tofauti iliyopo ni kuwa,mashafi wanahukumu ubatilifu wa Swala kwa aliyesoma Aya ya sijdahuku akikusudia kufanya sijda ya kisomo, ilihali wanafiqhi waImamiyya wao wanahukumu ubatilifu wa Swala kwa yule aliyesomamoja ya Sura hizo kwa makusudi, yaani ambaye hajasahau na wala sijahili wa hukmu yake, bali ni mjuzi mwenye kumbukumbu, hata

Kusoma Sura Zenye Sijda

18

26. Al-Fiqhi Alal-Madhahib Al-Arbaa Wamdh’hab Ahlil-Bayti Juz. 1 Uk.430. Al-Fiqhi Alal-Madhahib Al-Khamsa cha Sheikh Muhammad JawadMughniyah: 145.27. Al-Fiqhi Alal-Madhahib Al-Arbaa Wamdh’hab Ahlil-Bayti Juz. 1, Uk.602.28. Al-Ur’watul-Wuthqa Juz. 1, Uk. 644, Faslu ya 24 kuhusu kisomo.

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 18

Page 27: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

kama atakuwa hajakusudia kufanya sijda ya kisomo.

Na upande wa pili wa tofauti ni kuwa mashafi wanahukumu ubatilifuwa Swala kwa yule aliyesujudu sijda ya kisomo hivi sasa, ama yuleambaye hajasujudu hana tatizo lolote. Wanaafikiana na Imamiya kati-ka kuhukumu usahihi wa Swala katika sura kama hii, lakini wao(Imamiyya) wanamwona mtu huyo kuwa ni mwasi, na wanahukumukuwa anatakiwa kurudia Swala kwa ajili ya tahadhari (ihtiyat) yawajibu, kwa mujibu wa baadhi,29 na tahadhari (ihtiyat) ya Sunna kwamujibu wa wengine.30

Na kinashangaza sana kitendo cha mahanafi kukhalifu katika kifunguhiki, kwa sababu yule atakayesoma Aya ya sijda ndani ya Swalaatakuwa yeye mwenyewe amejiweka kati ya mambo mawili yenyekugongana.

La kwanza: Wajibu wa kutimiza Swala na kutoruhusiwa kuibatilisha.

La pili: Wajibu wa kufanya sijda ya kisomo haraka iwezekanavyondani ya Swala.

Ukichukua kukiri kwa mahanafi kuwa sijda ya kisomo ni wajibu, basivipi tena inakubalika kwao kusema kuwa, inaruhusiwa kusoma Ayaya sijda, ambayo matokeo yake ya lazima yanapelekea kubatilishaSala? Je hii si kumpa ujasiri mwenye kusali abatilishe Sala yake? Jemwenye kusali si kaamriwa kutokubatilisha Sala yake?

Kuifanyia kazi kauli hii kunapelekea kuwapo mgongano katikahukmu za kisheria, jambo ambalo linaonyesha kuwepo dosari kwenyemsimamo huo wa kisheria. Na ni wazi kuwa mgongano huu

Kusoma Sura Zenye Sijda

19

29. Minhajus-Salihiin cha As-Sayyid Al-Khui Juz. 1 Uk. 164.30. Minhajus-Salihiin cha As-Sayyid Sistaniy Juz. 1 Uk. 206.

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 19

Page 28: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

haukomei kwenye Fiqhi ya mahanafi tu, wanaotoa fatwa ya wajibuwa kufanya sijda ya kisomo ndani ya Swala, bali inahusu hata mad-hehebu mengine ya kisunni, wale wanaoamini kuwa inajuzu kufanyasijda ya kisomo ndani ya Sala, ijapokuwa fiqhi ya mahanafiinachukua daraja la juu kabisa. Kwa sababu kusema inajuzu sijda yakisomo ndani ya Sala, inamaanisha sheria imekataza sijda ya kisomokwa kigezo kuwa yenyewe ni ziada iliyo nje ya asili ya Swala, nakuwa yenyewe (sheria) wakati huohuo imeruhusu kuitekeleza ndaniya Swala. Upuuzi huu unafichua dosari za msimamo wa kifiqhi zili-zopelekea kuficha kwa ndani mfano wa matokeo kama haya, na kishakuyanasibisha na sheria.

Imam (a.s.) alielezea uhalisia wa sheria pindi Zarara alipotoa habaritoka kwa Imam Al-Baqir au As-Sadiq, kuwa mmoja wao alisema:“Msisome yoyote ile kati ya Sura zenye Aya zilizo na sijda ya wajibundani ya Swala ya faradhi, kwani kwa hakika sijda ni kuleta ziadakatika Sala ya faradhi.”31

Kusoma Sura Zenye Sijda

20

31. Al-Wasailu Juz. 4 Uk. 779, mlango wa 40 kati ya milango yakisomo,hadithi ya 1.

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 20

Page 29: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

MUHTASARI WA UCHUNGUZI

Kwa muhtasari ni kuwa maoni kuhusu suala la sijda ya kisomo nimatatu:

Kauli isemayo inajuzu kusoma Aya ya sijda ndani ya Swala, na niwajibu kusujudu kwa ajili ya kisomo, nayo ni kauli ya mahanafi.

Kauli isemayo inajuzu kusoma na inajuzu kusujudu kwa ajili ya kiso-mo, nayo ni kauli ya madhehebu mengine ya kisunni.Kauli isemayo hairuhusiwi kusoma Sura nne zilizotajwa huko nyuma,na kuzisoma kunabatilisha Sala, nayo ni kauli ya Imamiya.

Na iko wazi kuwa kauli ya Imamiya inategemea misingi miwili: Wakwanza: Wajibu wa kusujudu kwa ajili ya kusoma Sura hizo. Nakutokana na uchambuzi huo tayari utimilifu wake umeshakuwa wazi.Mjadala na hoja zote zilizotolewa dhidi yake zimethibitika kuwa sisahihi.

Wa pili: Swala hubatilika kwa kule kuleta sijda ya kisomo ndani yaSwala, na kuwa mukalafu atajiweka yeye mwenyewe kati ya mambomawili yenye kugongana: Uharamu wa kubatilisha Swala na wajibuwa kuleta sijda ya kisomo itakayopelekea Swala yake kubatilika. Kwaajili hiyo inalazimu kusema ni haramu kusoma moja ya Sura zenyeAya zilizo na sijda ya wajibu uwapo ndani ya Swala.

Kusoma Sura Zenye Sijda

21

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 21

Page 30: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWANA AL-ITRAH FOUNDATION

1. Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanzampaka Thalathini

2. Uharamisho wa Riba3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili5. Hekaya za Bahlul6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)8. Hijab vazi Bora9. Ukweli wa Shia Ithnaashari10. Madhambi Makuu11. Mbingu imenikirimu12. Abdallah Ibn Saba13. Khadijatul Kubra14. Utumwa15. Umakini katika Swala16. Misingi ya Maarifa17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia18. Bilal wa Afrika19. Abudharr20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu21. Salman Farsi22. Ammar Yasir23. Qur'an na Hadithi24. Elimu ya Nafsi25. Yajue Madhehebu ya Shia

Kusoma Sura Zenye Sijda

22

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 22

Page 31: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu27. Al-Wahda28. Ponyo kutoka katika Qur'an. 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii30. Mashukio ya Akhera31. Al Amali32. Dua Indal Ahlul Bayt33. Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna.34. Haki za wanawake katika Uislamu35. Mwenyeezi Mungu na sifa zake36. Amateka Na Aba'Khalifa37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s)38. Adhana.39 Upendo katika Ukristo na Uislamu40. Nyuma yaho naje kuyoboka41. Amavu n’amavuko by’ubushiya42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya swala mbili44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya46. Kusujudu juu ya udongo47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s)48. Tarawehe49. Malumbano baina ya Sunni na Shia50. Kupunguza Swala safarini51. Kufungua safarini52. Umaasumu wa Manabii53. Qur’an inatoa changamoto54. as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm55. Uadilifu wa Masahaba

Kusoma Sura Zenye Sijda

23

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 23

Page 32: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

56. Dua e Kumayl57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume

Muhammad (s)61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili63. Kuzuru Makaburi64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu67. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne68. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano69. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita70. Tujifunze Misingi Ya Dini71. Sala ni Nguzo ya Dini72. Mikesha Ya Peshawar73. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu74. Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia

iliyonyooka75. Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake76. Liqaa-u-llaah77. Muhammad (s) Mtume wa Allah78. Amani na Jihadi Katika Uislamu 79. Uislamu Ulienea Vipi?80. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 81. Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 82. Urejeo (al-Raja’a )83. Mazingira

Kusoma Sura Zenye Sijda

24

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 24

Page 33: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

84. Utokezo (al - Badau) 85. Sadaka yenye kuendelea 86. Msahafu wa Imam Ali87. Uislamu na dhana88. Mtoto mwema89. Adabu za Sokoni90. Johari za hekima kwa vijana91. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza92. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili93. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu94. Tawasali95. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia96. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu97. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi98. Swala ya maiti na kumlilia maiti99. Shiya na Hadithi (kinyarwanda)100. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu101. Hadithi ya Thaqalain102 Fatima al-Zahra103. Tabaruku104. Sunan an-Nabii105. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)106. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili)107. Mahdi katika sunna108. Kusalia Nabii (s.a.w)109. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza110. Ujumbe - Sehemu ya Pili

Kusoma Sura Zenye Sijda

25

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 25

Page 34: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

111. Ujumbe - Sehemu ya Tatu112. Ujumbe - Sehemu ya Nne113. Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa114. Iduwa ya Kumayili115. Maarifa ya Kiislamu.116. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza117. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili118. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu119. Ukweli uliopotea sehmu ya Nne120. Ukweli uliopotea sehmu ya Tano121. Johari zenye hekima kwa vijana122. Safari ya kuifuata Nuru123. Idil Ghadiri124. Myahudi wa Kimataifa125. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi126. Visa vya kweli sehemu ya Kwanza127. Visa vya kweli sehemu ya Pili128. Muhadhara wa Maulamaa129. Mwanadamu na Mustakabali wake130. Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Kwanza131. Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Pili132. Khairul Bariyyah133. Uislamu na mafunzo ya kimalezi134. Vijana ni Hazina ya Uislamu.135. Yafaayo kijamii

Kusoma Sura Zenye Sijda

26

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 26

Page 35: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

136. Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu137. Taqiyya138. Vikao vya furaha 139. Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje?140. Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Kwanza141. Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Pili142. Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza143. Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah144. Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu145. Kuonekana kwa Allah146. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt

(Sehemu ya Kwanza)147. Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili)148. Ndugu na Jirani149. Ushia ndani ya Usunni150. Maswali na Majibu151. Mafunzo ya hukmu za ibada 152. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No1153 Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 2154. Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 3155. Abu Huraira

Kusoma Sura Zenye Sijda

27

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 27

Page 36: Kusoma sura zenye sijda za wajbu katika sala

BACK COVERKitabu hiki kimeshughulikia suala la usomaji wa sura ambazo ndaniyake kuna aya za “sijda wajibu.”

Kuna tofauti kati ya Shia na Sunni juu ya suala hili, na halikadhalikakuna tofauti ndani ya madhehebu za Sunni zenyewe.

Wanazouni wa Kiislamu kama kawaida ya wanadamu, wamehitilafi-ana katika hukumu ndogondogo katika matendo ya ibada, lakini kamailivyo, tofauti ndogo kati ya wanazuoni kwa wafuasi inakuwa nimlima wa tofauti na kusababisha zogo lisilo na maana. Mamboambayo wanazuoni wetu wamehitilafiana si katika asili au misingi yadini, na isitoshe ni mambo machache sana ukilinganisha na yaletunayokubaliana nayo.

Ili kupata ufafanuzi wa suala hili, ungana na jopo la wanazuoniambao wamelichambua suala hili kwa uzuri sana kwa kutumia vyan-zo sahihi vya Kiislamu ambavyo ni Qur’ani na Sunna.

Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah FoundationS.L.P. 19701 Dar es Salaam, TanzaniaSimu: +255 22 2110640Simu/Nukushi: +255 22 2127555Barua Pepe: [email protected]: www.alitrah.orgKatika mtandao: www.alitrah.info

Kusoma Sura Zenye Sijda

28

Kusoma sura zenye sijda wajbu Lubumba & Dr. Kanju.qxd 7/2/2011 10:51 AM Page 28