Upload
others
View
32
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
MAELEZO YA METHALI ZA KISWAHILI
Adhabu ya kaburi, aijuaye
maiti
m.y.
mat.
taz.
Taabu na dhiki ya kaburini, aijuaye maiti.
Methali hii inatufahamisha kuwa aijuaye taabu na
dhiki ya jambo lolote ni yule aliyehusika nalo.
Kitanda usichokilalia hujui kunguni wake
Afadhali dooteni, kama ambari
kutanda
Dooteni:
Ambari
Kutanda
m.y
mat.
Dhaifu, kibaya
Kitu cha thamani kinachopatikana Pwani na
kinatumiwa kwa manukato au dawa
Kuenea, iliyo nyingi
Afadhali kibaya kidogo ulichonacho, kuliko kingi
kizuri usichonacho wala huna njia ya kukipata.
Methali hii hutumiwa kumnasihi mtu akinai na
atosheke na alichonacho, ingawa kidogo na duni.
Afya ni bora kuliko mali m.y
mat.
Afya ya kiwiliwili imeshinda aina yoyote ya mali
Inatumiwa methali hii, kwa mfano, kumnasihi
mtu ambaye kutwa kucha yumo mbioni tu
kutafuta mali bila ya kujali afya yake.
Ahadi ni deni m.y
mat.
Miadi ni kama deni, lazima utimize.
Methali hii hutumika kumuasa mtu kuwa akitoa
ahadi kufanya jambo sharti atomize. Siyo aseme
tu bali atende.
Ahangaikaye sana na jua ajua ajua
m.y
mat.
Anajua
Ahangaikaye sana na jua anajua alifanyalo,
hahangaiki bure.
Methali hii inatumiwa kwa mtu anayelihangaikia
sana na kulishughulikia. Mtu huyo hafanyi hivyo
bure, ila ana azma fulani ambayo anaijua
mwenyewe.
Aisifuye mvua imemnyea m.y
mat.
taz.
Anayetoa sifa ya mvua, mvua hiyo imemnyeshea.
Methali hii inatufundisha kuwa mtu anaposimulia
jambo kwa makini na usawa, ni kwamba jambo
hilo limempata.
Alisifuye jua limemwangazia.
Ajabu ya kondoo kucheka kioo m.y
mat.
taz.
Ajabu ya kondoo kumcheka yule amwonaye
ndani ya kioo na kumbe anajicheka mwenyewe.
Methali hii inatumiwa kwa mtu anayemcheka
mwenziwe na ilhali yeye na huyo anayemcheka
wamo katika hali moja. Akifanya hivyo huwa
kama anajicheka mwenyewe.
Ajabu ya ngamia kucheka nundu ya ng’ombe.
Nyani haoni kundule.
Ajabu ya ngamia kucheka
nundu ya ng’ombe
m.y
mat.
Ajabu ya ngamia, ambaye mwenye nundu kubwa
zaidi, kucheka nundu ya ng’ombe.
Inatumiwa methali hii kwa mtu anayeicheka ila au
upungufu wa mwenziwe na yeye anayo ila au
upungufu kama ule au zaidi ya ule.
taz. Ajabu ya kondoo kucheka kioo.
Nyani haoni kundule.
Ajali haina kinga Kinga
m.y
mat.
taz.
Kizuizi
Mungu akitaka ufikwe na ajali au jambo, hakuna
la kukukinga – utafikwa tu na jambo hilo.
Inatumika methali hii kwa kumpoza mtu
aliyefikwa na jambo baya au ajali.
Cha kuvunda hakina ubani
Cha kuvunjika hakina rubani.
Chombo cha kuzama hakina usukani.
Ajizi nyumba ya njaa Ajizi:
m.y
mat.
Usiri
Kutoweza kukata shauri kufanya jambo – mtu
kusema jambo hili au kazi hii nitaifanya kesho,
mara kesho kutwa – huku ndiko kunakosababisha
njaa.
Methali hii inatumiwa kwa mtu asiyeweza kukata
shauri mara moja akafanya jambo, hasa muhimu,
likesha.
Ajuaye misonoe ni alalaye naye Misonoe:
m.y
mat.
Misono yake, mikoromo yake
Ajuaye misono yake mgonjwa anapougua ni yule
anayelala naye ili kumwuguza.
Hutumika kwa maana ya kuwa ajuaye taabu ya
jambo ni yule anayehusika nalo.
Akiba si mbi, ingawa ya kumbi,
siku ya kivumbi hutia motoni
Mbi:
Kumbi:
Siku ya
kivumbi:
m.y
mat.
Mbovu, mbaya
La nazi
Siku ya taabu au balaa
Akiba si mbaya hata akiba hiyo ikiwa kitu duni,
kisicho thamani kama kumbi, kwani huenda hilo
ukalihitaji na likakufaa siku ya haja, pengeni kwa
kuashia moto.
Methali hii inakufahamisha kuwa akiba yoyote
iliyohifadhiwa ijapo si kitu cha thamani,
taz.
usiidharau kwani iko siku itakuja kukufaa.
Hakuna akiba mbovu
Akili ni mali m.y
mat.
Akili ni mali, maana bila ya akili huwezi kufanya
jambo likatengemaa au likaenda sawa; na ukiwa
nayo ndiyo chanzo cha kupatia mali n.k. na
kufanyia kila jambo.
Methali hii aghalabu hutumika kwa mtu
anayefanya jambo la kipumbavu. Watu husema:
Tazama upumbavu anaofanya fulani; ama kweli:
Akili ni mali.
Akili nyingi huondoa maarifa m.y
mat.
Kujitia akili nyingi au uwerevu mwingi wakati
mwingine huondoa busara na hekima ya mtu, na
baada ya mtu kufanya jambo likatengenea,
huliharibu.
Hutumiwa methali hii kwa mtu asiyesikia nasaha
na mashauri ya wenziwe katika kufanya jambo;
anahisi fikra zake tu ndio sawa. Mwishowe mtu
huyo anashtukia jambo lake limemharibikia.
Akipenda chongo huita kengeza m.y
mat.
Mtu anapopenda, basi huyo apendwaye hata
akiwa ana chongo, huambiwa si chongo hiyo, ni
kengenza tu.
Inatumiwa methali hii kwa mtu asiyeona ila
zozote za mwenziwe jinsi anavyompenda –
mabaya ya huyo mwenziwe yeye huyaona mazuri.
Akosaye la mama hata la mbwa
huamwa
Huamwa:
m.y
mat.
Hukamwa
Anayekosa titi la mamaye kunyonya, kwa sababu
ya dhiki huambiwa hata la mbwa aweza
kunyonya.
Methali hii huambiwa mtu kwa kumfahamisha
kuwa ikiwa kakikosa kizuri alichokuwa akikitaka,
basi atumiye hicho kibaya alichokipata, ama
vyote huenda akavikosa.
Akufaaye kwa dhiki ndiye
rafiki
Akufaaye kwa taabu ndiye
sahibu
Sahibu
m.y
mat.
Rafiki
Akufaaye wakati wa taabu na dhiki ndiye rafiki
hasa, si yule unayemwona wakati wa raha tu.
Methali hii inatunasihi tuchague marafiki zetu
vema – wale watufaao wakati wa dhiki ndio
marafiki hasa.
Akufukuzaye hakwambii toka m.y
mat.
Asiye na haja nawe tena si lazima akufukuze au
akwambie kwa maneno, bali kwa vitimbi au kwa
mabadiliko ya tabia.
Methali hii inakufahamisha kuwa ikiwa hutakiwi
pahala utaona kwa dalili na vitendo, si lazima
uambiwe kwa maneno.
Akumulikaye mchana usiku
atakuchoma
m.y
mat.
Anayethubutu kukukaribia na kijinga cha moto
mchana na kukumulika usoni, basi ikiwa usiku
hata kukuchoma anaweza.
Methali hii inatumika kumtahadharisha mtu na
mwenziwe ambaye kaweza kumfanyia uwovu
japo mdogo; mwishowe hata ovu kubwa anaweza
kumfanyia.
Aliye juu mngoje chini m.y
mat.
Taz.
Aliye juu ana siku yake atashukashini – mngoje tu
huko chini.
Methali hii aghalabu hutumiwa kwa mtu aliye na
madaraka ya juu lakini anayewadhulumu, au
kuwakandamiza, au kuwadharau wenziwe wa
chini. Iko siku atakuwa si chochote.
Mpanda ngazi hushuka.
Aliye kando haangukiwi na mti Kando:
m.y
mat.
Pembeni
Aliye na hadhari na kukaa pembeni mti
unapoanguka, basi mtu huyo haangukiwi na mti
huo.
Huambiwa mtu methali hii kumfahamisha kuwa
asipojitia katika balaa isiyomhusu basi taabu
haimfiki, atakuwa katika salama.
Aliyekueka kitini, ndiye
aliyeniweka chini
m.y
mat.
Aliyekuweka katika cheo hicho au kukupa utajiri
huo wewe ndiye aliyenifanya mimi maskini, naye
ni Mungu
Hutumiwa methali hii kumwambia mtu mwenye
kujivuna na kumkandamiza mwenziwe aliyekuwa
chini ambaye hana uwezo au madaraka kama
yeye.
Aliyekunyima kunde
amekupunguzia mashuzi
m.y
Aliyekunyima kitu ambacho kitakuletea hasara,
ijapo una haja nacho, hiyo itakuwa ni faida
mat.
taz.
kwako, maana atakupunguzia taabu na dhiki.
(Watu wengi wanaitikadi kuwa kunde
zinasababisha tumbo kuwa yabisi na kuleta
mashuzi)
Methali hii hutumiwa aghalabu kumpoza mtu
anayesikitika kwa kukikosa kitu fulani ambacho
akitarajia kukipata.
Aliyekunyima mbaazi kakupunguzia mashuzi.
Aliyekunyoa shungi kakupunguzia kuchana.
Aliyekunyima mbaazi
kakupunguzia mashuzi
m.y
mat.
taz.
Aliyekunyima mbaazi, ambazo mara nyingi
husababisha riyahi tumboni kwa yule aliyezila,
basi kakupunguzia balaa ya kujamba.
Methali hii huweza kutumiwa kumliwaza mtu
ambaye kanyimwa au kanyang’anywa kitu na
wenziwe.
Aliyekunyima kunde amekupunguzia mashuzi.
Aliyekunyoa shungi kakupunguzia kuchana.
Aliyekunyoa shungi
kakupunguzia kuchana
Shungi:
m.y
mat.
taz.
Furushi la nywele
Aliyekunyoashungi la nywele amekupunguzia
taabu ya kuzichana, maana sasa nywele hizo
zimekuwa kidogo zaidi.
Huwza kutumiwa methali hii kumliwaza mtu
ambaye amenyang’anywa kitu chake ambacho
kwa hakika hakihitajii sana.
Aliyekunyima kunde amekupunguzia mashuzi
Aliyekunyima mbaazi kakupunguzia mashuzi
Aliyekutweka ndiye
atakayekutua
Kutweka
m.y
mat.
kubebesha
Aliyekutweka mzigo huyo huyo ndiye
atakayekutua mzigo wako.
Methali hii hutumika kuambiwa mtu aliyejitakia
taabu
Aliyekwelekeza chanda aweza
na kukupiga kofi
Chanda
m.y
mat.
Kidole
Anayeweza kukunyooshea kidole akakutukana
basin a kukupiga pia aweza. (Kumnyoshea mtu
kidole wakati unaposema naye si jambo la
heshima)
Methali hii inatuasa kuwa tuwe na hadhari na mtu
anayetuvunjia heshima au anayetufanyia ubaya
kwa jambo dogo. Tusidharau tukasema hayo ni
madogo, kwani mara nyingine ataweza kufanya
makubwa zaidi
Aliyeshiba hamkumbuki
mwenye njaa
m.y
Tajiri mwenye nafasi hamkumbuki maskini
mwenye njaa au taabu yoyote.
mat.
Methali hii inamsihi mtu kuwa ajisaidie
mwenyewe asitumai msaada wa tajiri aliyekuwa
akimtumainia.
Aliyezowea kupokea kutoa ni
vita
m.y
mat.
Yule mwenye tabia ya kupokea yeye kila siku vya
watu,chake huwa hatoi, ila kwa taabu na mashaka.
Methali hii huweza kuambiwa mtu mgumu,
bahili, aliyezoea kupokea vya watu tu, lakini
chake hatoi.
Aliyezowea tumbaku tambuu
haiwezi
m.y
mat.
Mwenye uraibu wa kutumia tumbaku ukimpa
tambuu atumie itakuwa wamsumbua kwani si
uraibu aliouzowea.
Methali hii hutumiwa kwa mtu ambaye hawezi
kugeuza mazoea yake ya siku zote kwa kupata
jambo jingine jipya ambalo pengine ni zuri zaidi
kuliko hilo la zamani.
Amani haiji ila kwa ncha ya
upanga
m.y
mat.
taz.
Amani wakati mwingine haiji ila kwa kutumia
nguvu.
Methali hii inamnasihi mtu ambaye anaonewa na
mwenziwe au wenziwe, kuwa apinge maonevu
hayo – hapo ndio atapata suluhu na salama.
Dawa ya moto ni moto.
Naije baa iondoe baa.
Sumu ya neno ni neno.
Anayejitahidi hufaidi m.y
mat.
Anayejitahidi ndiye anayefaidi matunda ya
jitihada yake.
Methali hii inatufahamisha kuwa yeyote
anayefanya bidii na jambo lolote bila shaka
atafanikiwa, kwa kupata alilolikusudia.
Anayejitia lisilomuhusu hupata
lisilo mridhi
Lisilomridhi
m.y
mat.
Lisilompendeza
Anayeingingilia jambo lisilomhusu hupata jambo
asiloliridhi, yaani jambo la kumuudhi.
Hutumiwa methali hii kumnasihi mtu asijitie
katika mambo yasiyomhusu.
Angurumapo samba mcheza ni
nani?
m.y
mat.
Samba anapotoka uwanjani na kunguruma, nani
anayethubutu kuchezacheza mbele yake?
Methali hii hutumika kwa maana ya kuwa watu
mara nyingi hunung’unikanung’unika nyuma
kuhusu mkubwa au kiongozi wao lakini
anapojitokeza huyo kiongozi hakuna
anayethubutu kumkabili na kumnung’ung’ikia.
Apendapo hushona asipopenda
hurarua
Hurarua:
m.y
mat.
Huchanachana
Mtu akiwa ana mapenzi ya kupenda kitu, hata
kama kibaya hukisifu, na iwapo ni kizuri kwa
hakika, lakini yeye hakipendi, atakitaja kwa
vibaya.
Methali hii hutumiwa kwa mtu mwenye tabia ya
kusifu akipendacho sana na kukiponda kile
asichokipenda.
Apendwaye akajua haachi
kujishaua
Kujishaua:
m.y
mat.
Kuringa
Apendwaye na anajua kuwa anapendwa haachi
kuringa.
Mfano wa methali hii ni mtoto, ambaye anajua
kuwa anapendwa sana na wazazi wake. Mtoto
huyo huringa na kufanya atakavyo nyumbani
kwao.
Asazacho mwizi mganga atwae Asazacho:
m.y
mat.
Anachokisaza, anachokibakisha
Anachokibakisha mwizi baada ya kukuibia huwa
hufanyi akili ukakiweka kikakufaa mbeleni, lakini
wakipeleka kwa mganga akufanyie uganga wa
kumroga mwizi.
Methali hii inahimiza mtu ajuapo mali yake
sehemu fulani, imepotea kwa njia fulani, basi
afanye bidii ili ile sehemu iliyobaki, iwe salama
isije ikapotea kwa jambo jingine.
Asiyefawa na wake hufawa na
wa mwenziwe
m.y
mat.
Asiyesaidiwa na mtu wake mwenyewe, yaani
aliyemhusu, wakati mwingine husaidiwa na mtu
au jamaa ya mwenziwe.
Methali hii hutumiwa kwa mtu ambaye alitumai
kusaidiwa na jamaa yake katika shida, lakini
asisaidiwe, na akatokea mtu mbali ndiye
akamsaidia.
Asiyefunzwa na mamaye
hufunzwa na ulimwengu
m.y
mat.
Kijana asipopata mafunzo ya kutosha kutokana na
mzazi wake, hufunzwa na ulimwengu wakati
zinapompata taabu za dunia.
Methali hii hutumiwa kwa kijana ambaye kila
akifunzwa na wakubwa zake hafunziki.
Inapomfika balaa, kijana huyu, watu husema:
Asiyefunzwa na mamaye……
Asiyejua maana haambiwi
maana
m.y
mat.
Asiyejua maana, yaani faida ya jambo,
usijisumbue bure kumweleza, kwani hafuati.
Inatumiwa methali hii kwa maana kuwa wajipa
taabu bure kumweleza juha jambo la busara
ambalo wakati mwingine ni la faida kwake.
Asiyejua utu si mtu m.y
mat.
Asiyefahamu mwendo mzuri wa kibinadamu kwa
binadamu wenziwe, basi huyo si mtu.
Hutumiwa kwa kumsema mtu ambaye ingawa
amefanyiwa wema hata hamjali au kumtia
maanani huyo aliyemfanyia.
Asiyekubali kushindwa si
mshindani
Mat. Hutumiwa kwa mtu ambaye mkaidi, anajua
hakika ameshindwa, lakini anaona aibu kukubali
kuwa ameshindwa; mtu kama huyu hapati faidi ya
kujua mambo kwani hakuna atayechukua taabu ya
kujadiliana naye na kumfahamisha makosa yake
atakapoyafanya.
Asiyekujua hakuthamini m.y
mat.
Asiyekujua hakufahamu heshima yako, asili yako
na thamani yako kwa jumla.
Methali hii hutumiwa inapokuwa mtu
anayetukuzwa na watu wanaomjua, anafanyiwa
jambo la dharau na mtu, pengine duni, asiyemjua
utukufu wake. Haya huweza kumfika mtu, kwa
mfano anapokwenda ugenini.
Asiyekuweko na lake haliko m.y
mat.
Asiyekuweko watu waliopo humsahau na
hawamkumbuki kwa lolote.
Methali hii inatufahamisha kuwa ukitaka
ukumbukwe na ufanyiwe jambo fulani basi
hakikisha uwepo na kuonekana na watu hao
unaowatumainia kukufanyia hilo jambo, au
watakusahau.
Asiye na bahati habahatishi m.y
mat.
Aliye kwa desturi hana bahati habahatishi kufanya
jambo, akibahatisha jambo lake halitengenei,
huharibika.
Aghalabu hutumiwa kwa mtu ambaye anahisi
amefanya jambo jema lakini hakupata shukrani ila
ubaya tu kwa huyo aliyemfanyia.
Asiyeogopa ng’ombe ni
ng’ombe yeye
m.y
Asiyeogopa au kujihadhari na ng’ombe kuwa
labda anaweza kumdhuru, basin aye ni ng’ombe
mat.
pia. (Waswahili humwita mtu mjinga asiye na
nadhari “Ng’ombe”)
Methali hii hutumiwa kwa maana ya kuwa
asiyejihadhari na mjinga basi na yeye mjinga pia.
Asiyesikia la mkuu huvunjika
guu
guu:
m.y
mat.
Mguu
Asiyesikia shauri la mkubwa wake, aliyemzidi
kwa maarifa na umri, basi hufikwa na balaa.
Methali hii inatusihi tusikize shauri tunalopewa na
watu wazima,kama vile wazazi wetu, kwani
wametuzidi kwa maarifa.
Aumwaye na nyoka akiona
ung’ongo hushtuka
m.y
mat.
Mtu aliyewahi kuumwa na nyoka, siku nyingine
atakuwa na hadhari na uwoga, kwani akiona
ung’ongo au kuti huruka kwa hofu.
Methali hii inatufahamisha kuwa aliyepatikana na
taabu fulani mara ya kwanza, siku nyingine
huhofu asipatikanena taabu namna hiyo mara
nyingine.
Baada ya dhiki faraja Faraja:
m.y
mat.
taz.
Nafuu
Baada ya dhiki na taabu mara nyingi huja nafuu
na raha.
Methali hii hutumiwa kumpoza mtu aliyepatikana
na shida.
Mla cha uchungu na tamu hakosi.
Mstahimilivu hula mbivu.
Zito hufuatwa na pesi.
Bandu bandu humaliza gogo m.y
mat.
Gogo naliwe kubwa vipi lakini unapolichanja na
kubadnua kipande kimoja kimoja kidogo kidogo
mwisho gogo hilo humalizika.
Methali hii hutumiwa kumpa nasaha ambaye
anafanya usiri kuifanya kazi fulani kwa sababu
labda anaiona kubwa sana – yaani hata kazi ikiwa
kubwa vipi, ikifanywa kidogo kidogo mwisho
humalizika.
Barua ni nusu ya kuonana m.y
mat.
Mnapoandikiana barua kujuliana hali na mtu aliye
mbali huwa ni kama mlioonana nusu – yaani bora
kuliko kutoandikiana barua kabisa.
Unaweza kuitumia methali hii unapoagana na mtu
anayekwenda safari ya mbali, ili kumhimiza
akuandikie barua atapokuweko huko
taz.
anakokwenda.
Waraka ni nusu ya kuonana.
Baya, baya lako si jema la
mwenzako
m.y
mat.
taz.
Kibaya chako ni bora kuliko kizuri cha mwenzio.
Methali hii inamfahamisha mtu kuwa kizuri cha
mwenziwe hakiwezi kumfaa maana hakipati,bora
kibaya chake mwenyewe.
Bura yangu sibadilina reheani.
Bendera hufuata upepo m.y
mat.
taz.
Bendera hufuata kule upepo unakoelekea, iwapo
ni kaskazini ama kusini.
Methali hii hutumiwa kwa mtu ambaye hashiki
mahali pamoja, yeye anafuata aambiwalo tu; mara
huandama huku mara huku kama bendera
kwakufuata upepo unapoelekea.
Maji hufuata mkondo.
Bura yangu sibadili na rehani Bura:
m.y
mat.
taz.
Aina ya kitambaa hapo zamani, ambacho
kilikuwa si cha thamanisana.
Nguo yangu (bura), iliyo duni lakini inanifaa,
sibadilishi na nguo bora (rehani) ambayo hainifai
na kwa hivyo haina faida kwangu.
Methali hii inamfunza mtu kuwa bora chake
kibaya kimfaacho kuliko kizuri cha mwenziwe,
ambacho hakina faida kwake.
Baya, baya lako si jema la mwenzako.
Chaka la samba halali nguruwe Chaka:
m.y
mat.
Mwitu mkubwa
Sehemu ya mwitu anamokaa samba, nguruwe
halali, au hakai kwa kituo, mahali hapo.
Methali hii inatumiwa na mtu kwa maana ya
kuwa hawezi kupakaa mahali fulani kwa sababu
ya maonevu ya aliyemzidi nguvu.
Cha (La) kuvunda hakina
(halina) ubani
Kuvunda:
m.y
mat.
Kuoza
Kilichoozandio kimeoza, hakiachi kunuka, hata
ukifukiza ubani, harufu haiondoki.
Inatumika methali hii kwa maana ya kuwa jambo
likishaharibika na aibu kutapakaa ndio
Taz.
imetapakaa, hakuna liwezalo kufanyika kuizuia
isitapakae.
Ajali haina kinga.
Cha kuvunja hakina rubani.
Chombo cha kuzama hakina usukani.
Cha kuvunja hakina rubani Kuvunja;
Rubani:
m.y.
mat.
Taz.
Chombo kupanda mwamba na kuvunjika baharini
Mtu aongozaye chombo baharini (au angani)
Chombo kilichojaaliwa kuvunjika na pengine
kuzama basi kitavunjika tu, rubani hata afanye
nini hataweza kukisaidia kisivunjike.
Inatumiwa kwa maana ya kuwa jambo
likishajaaliwa kuharibika, hata likipata mtu wa
kuliongoza, litaharibika tu hakuna kinga.
Ajali haina kinga.
Cha kuvunga hakina ubani.
Chombo cha kuzama hakina usukani.
Cha mlevi huliwa na mgema Mgema:
m.y.
mat.
Anayepanda mnazi kugema tembo
Rasilimali ya mlevi hupotea ikaenda kwa mgema
ambayeni mwuza tembo. Cha mjinga huliwa na
mwerevu.
Watu husema methali hii kumweleza mtu ambaye
pato lake lote anamtumilia mtu mwingine bila ya
kupata faida yoyote kwake.
Chanda chema huvishwa pete Chanda:
m.y.
mat.
Taz.
Kidole
Kidole kizuri kilichoumbika huvishwa pete ili
kizidi kupendeza.
Watu husema hivyo wanapohisi mtu fulani ni
mwema; yafaa apewe tuzo kwa jambo zuri
analolifanya, ambalo linafurahisha watu au
linaleta faida na sifa.
Mcheza kwao hutuzwa.
Changu ni bora kuliko chetu m.y.
mat.
Maana yake ni kuwa kitu changu mimi peke
yangu, ambacho nina amri nacho na ninaweza
kukisarifu ninavyotaka, ni bora kuliko kitu chetu
sisi, cha watu wengi, ambacho siwezi kukifanya
nitakavyo mpaka tukubaliane sote.
Methali hii inakufahamisha kuwa kitu chako
mwenyewe ni bora kuliko kitu cha shirika.
Chema chajiuza kibaya
(kibovu) chajitembeza
m.y.
mat.
Kitu kizuri kinajiuza chenyewe bila ya
kutembezwa, lakini kibaya sharti kijitembeze, na
papo pengine kisinunuliwe.
Methali hii aghalabu hutumiwa kwa mtu
anayependa kujisifu. Watu wanapochoka na
majisifu yake husema methali hii.
Chema hakidumu m.y.
mat.
Kizuri hakidumu.
Methali hii hutumiwa, kwa mfano, kwa mtu
mwenye kufanya matendo mazuri na mwenye
msaada sana kwa watu. Mtu huyu aghalabu hakai
sana au hadumu, katika hali hiyo inayomwezesha
kufanya matendo mazuri. Watu waliomkalia kwa
ubaya humfisidi tu kwa uovu wao.
Chendacho kwa mganga
hakirudi
m.y.
mat.
Kinachokwenda kwa mganga, ikiwa ni pesa au
kitu kingine, basi tujue kuwa kitu hicho hakipati
mwenyewe tena.
Methali hii huambiwa mtu aliyetoa amana yake
kumpa mtu ambaye anajulikana jambazi – yaani
hiyo hairudi kwa mwenyewe tena.
Chombo cha kuzama hakina
usukani
m.y.
mat.
Taz.
Chombo kama jahazi au meli kikishajaaliwa
kuzama kitazama tu, hakina nahodha wala
baharia.
Kama: cha kuvunda hakina ubani.
Ajali haina kinga.
Cha kuvunda hakina ubani.
Cha kuvunja hakina rubani.
Chombo kilichopikiwa samaki
hakiachi kunuka vumba
Vumba:
m.y.
mat.
Taz.
Harufu ya samaki
Sufuria au chungu kilichozoea kupikiwa samaki
kila siku hata ukikisafisha vipi kitanuka vumba.
Methali hii hutumiwa kwa mtu, ambaye alikuwa
tajiri, lakini sasa amefilisika; mtu huyo aghalabu
huwa anayo mali imesalia, japo kidogo.
Jungu kuu halikosi ukoko.
Chururu si ndo-ndo-ndo Chururu:
Ndo-ndo-ndo
m.y.
mat.
Mlio wamaji yanapomiminika kwa wingi
Mlio wa matone ya maji yanapodondoka, hasa
kwenye ndoo au debe, tone baada ya tone.
Ni heri mtu apate maji haba kwa matumizi ya kila
siku kuliko maji mengi ya mara moja au ya siku
moja.
Methali hii hutumika kwa maana ya kuwa bora
mtu kupata kidogo kidogo kila siku kuliko wingi
wa mara moja na kukosa. Kwa mfano afadhali
mtu apate kitu cha matumizi japo ni kidogo cha
kila siku kuliko kupata kingi cha mara moja
kikiisha iwe basi.
Dalili ya mvua ni mawingu m.y.
mat.
Dalili, yaani alama ya kuonesha kuwa itanyesha
mvua ni kuyaona mawingu ya mvua angani. Dalili
ya kupata ulilokusudia, kwanza ni kuiona ishara
ya kukuonesha kuwa hicho kitu kipo tayari
kukufika.
Hutumiwa kwa maana ya kuwa jambo likitaka
kuwa, huwepo ishara (dalili) kwanza inayoonesha
kuwa jambo hilo litatokea. Watu husema methali
hii wanapoiona dalili kama hiyo.
Dau la mnyonge haliendi joshi Dau;
Joshi:
m.y.
mat
taz
Aina ya chombo cha majini
Chombo cha baharini kwenda kwa kasi/kina
kirefu
Chombo cha mtu mnyonge hakiendi kina kirefu
kwa sababu hakijakamilika au kinavuja, au tanga
bovu.
Methali hii hutumika mtu anapoona jambo lake
halinyoki au haliendi ipasavyo kwa sababu ya
kukosa pesa au kwa kuwa hali yake ni duni.
Jahazi la mkata haliendi joshi.
Dawa ya moto ni moto m.y.
Dawa ya mtu akutendeaye uovu na wewe
umtende uovu namna hiyo hiyo.
mat
taz
Huambiwa mtu ili kumnasihi kuwa asikubali
kuonewa pasipo sababu.
Amani haiji ila kwa ncha ya upanga
Naije baa iondoe baa
Sumu ya neno ni neno
Debe tupu haliachi kutika Kutika
m.y.
mat
Kutikisika na kufanya kelele
Debe tupu haliachi kutikisika na kupiga kelele
hasa linapopigwa na upepo.
Hutumiwa methali hii kwa mfano, kusemwa mtu
mwenye maneno mengi tu lakini hafanyi jambo
lolote la maana. Pia husemwa mtu anayependa
kujionesha tajiri, mfano kwa kuzilizaliza pesa
mfukoni.
Donda ndugu laisha dawa Donda
ndugu:
m.y.
mat
Donda la siku nyingi, lisilopona
Donda la siku nyingi hata ukilifanyia dawa namna
gani huwa halisikii dawa, na kupoa huwa ni kwa
bahati sana.
Methali hii hutumiwa kwa mtu aliye na tabia
mbaya na amezama kabisa katika tabia yake hiyo.
Mtu huyo huwa ametolewa tamaa tena kuwa kuna
dawa ya kumwachisha tabia yake mbovu.
Dua la kuku haimpati mwewe Mwewe:
m.y.
mat
Aina ya ndege kama tai, anayependa kula watoto
wa kuku.
Dua la kuku la kumwapiza mwewe, kwa sababu
amemlia wanawe halimfiki au halimdhuru huyo
mwewe, yeye anaendelea vile vile na tabia yake
ya kukamata kuku.
Methali hii huweza kutumiwa kwa mfano
mwanafunzi anayemlaani mwalimu aliyempa
adhabu kali kwa kosa alilolifanya. Wanafunzi
wenziwe huweza kumwambiya, “Bure unalaani
na kumwapiza mwalimu na kumwombea dua
baya. Dua la kuku……”
Dunia mti mkavu ukiulemea
utakubwaga
Utakubwaga:
m.y.
Utakutupa chini
Dunia ni kama mti mkavu, ambao ukiwa huna
hadhari na ukauegemea sana basi mti huo
utakatika na wewe utaanguka chini.
mat Methali hii hutumiwa kumnasihi mtu atahadhari
asiitegemee sana dunia. Asione sasa anajiweza
akaponda rasilimaliyake, akawa jeuri n.k. dunia
ghafla inaweza kumgeukia na kumtupa, akawa
hana mbele hana nyuma, hohe hahe.
Eleza haja upate haja m.y.
mat
Eleza waziwazi haja yako upate kutimiziwa hiyo
haja.
Methali hii huambiwa mtu ambaye anaomba
jambo fulani kwa mwenziwe lakini hamfunulii
waziwazi haja yake, anazungukazunguka. Huyo
mwenziwe huweza kumwambia: Eleza haja……
Embe dodo sawasawa na
kisukari
Dodo:
Kisukari:
Mat
Aina ya embe ambayo huzaa kwa wingi
Aina ya embe ambazo ni ghali zaidi kuliko dodo
Methali hii hutumiwa kumnasihi mtu, kwa mfano,
kuwa bora achukue kitu hiki ambacho ni rahisi
kukipata, tena ni kizuri kama hicho akitakacho
yeye lakini ni taabu au adimu kukipata.
Enga kabla ya kujenga Enga
m.y.
mat
Angalia
Angalia mbele kwanza kabla ya kujenga. Inabidi
kufikiri kwanza na kupanga kabla hujaanza
kujenga nyumba.
Methali hii inatumiwa kwa maana ya kuwa
inatubidi tufikiri mbele matokeo ya jambo kabla
ya kulianza hilo jambo.
Fadhila za punda, mashuzi Fadhila:
m.y.
mat
Shukrani
Ukimfanyia punda wema shukrani zake hukulipa
mashuzi.
Hutumiwa methali hii kumsema mtu aliyefanyiwa
wema akalipa uovu.
Fahali wawili hawakai zizi moja Fadhila:
Zizi:
m.y.
Ng’ombe dume
Boma la ng’ombe
Mafahali wawili hawakubali kukaa katika zizi
moja, watagombana tu, kwa sababu kila mmoja
atataka awe yeye ndiye mfalme wa zizi.
mat Inatumika methali hii inapokuwa jambo au kazi
fulani inatarajiwa kufanywa na watu wawili
wenye madaraka sawasawa. Watu hao wawili
lazima watateta.
Fimbo ya mbali haiui nyoka m.y.
mat
Fimbo inayokufaa unapotaka kumwua nyoka ni
ile uliyonayo karibu, iliyopo mbali haikufai kitu.
Methali hii inatufahamisha kuwa kinachofaa
wakati wa haja ya ghafla ni kile kilicho karibu
nas, si kilicho mbali tusichokipata. Kwa mfano
ukitokewa na haja ya ghafla ukataka kumkopa
mtu pesa. Akakwambia, “Hapa sina ziko
nyumbani; nikakuchukulie?” Waweza
kumwambia, “Haja yangu ni hivi sasa; fimbo ya
mbali haiui nyoka.”
Fuata nyuki, ule asali m.y.
mat
Ukiitaka asali, huna budi kufuata nyuki mpaka
kwenye mzinga ukaitafute.
Methali hii inamnasihi mtu kuwa aandamane na
mtu au watu wenye manufaa, ikiwa mali, elimu,
busara n.k. ili naye anufaike kwa manufaa haya;
ijapo atapata taabu.
Fumbo mfumbie mjinga
mwerevu huling’amua
m.y.
mat
Kumdanganya mdanganye mjinga, mwerevu mara
hutambua.
Mtu huitumia methali hii kumweleza mwenzake
kuwa ingawa hamfunulii kweli akamwambia
kinaga ubaga, yeye kishatambua anavyokusudia.
Gae huwa chombo wakatiwe Wakatiwe:
m.y.
mat
Kwa wakati wake
Gae ingawa kwa desturi halithaminiwi na
hutupwa, hutumiwa kuwa chombo cha kutilia
maji n.k. – wkati chombo kizima kinahitajiwa na
hakipatikani.
Methali hii inamnasihi mtu asidharau kitu kibovu,
au hafifu; kuna wakati huweza akakihitajia.
Ganda la mua la jana chungu
kaona kivuno
m.y.
mat
taz
Ganda la mua lililotupwa jana, yaani limeshaanza
kukauka, basi mdudu chungu kupata ganda hilo
anaona kama amevuna mazao.
Methali hii hutumiwa kwa mtu aliyepata kitu
kidogo tu, lakini kwa sababu hakuzoea kupata,
hicho kidogo anakiona kikubwa sana.
Maskini akipata, matako hulia mbwata.
Gota (gonga) gogo usikize mlio m.y.
mat
Lipige hilo gogo usikilize kuwa litalia mlio wa
aina gani?
Kwa ada za Kiswahili, atakaye kuoa hupeleka
posa, yaani ujumbe rasmi kwa wazee wa huyo
msichana amtakaye. Lakini kabla ya ujumbe
rasmi haujaenda huyo mtu, “hugonga gogo”
kwanza – yaani huulizauliza chini chini kama
hiyo posa yake itakubaliwa au la. Huu ni mfano
mmoja wa matumizi ya methali hii. Inatuhimiza
tufanye uchunguzi kwanza kabla ya kuanza
kufanya jambo muhimu.
Haba na haba hujaza kibaba Haba
m.y.
mat
taz
Punje ya nafaka, kidogo
Punje moja moja ukizikusanya mwishowe huwa
nyingi za kuweza kujaza kibaba kizima.
Methali hii inatufunza tusidharau kitu kidogo.
Kwa mfano, pesa kidogo kidogo tukizikusanya
mwishowe pesa hizo huwa nyingi.
Tone na tone huwa mchirizi.
Hakuna akiba mbovu m.y.
mat
taz
Hakuna kitu kibovu kisichofaa kabisa kabisa.
Hutokea haja mtu akakihitaji.
Methali hii inatuhimiza tuweke akiba ya vitu, pesa
n.k. ijapokuwa vitu tunavyovihisi sasa havina
thamani.
Akiba si mbi ingawa ya kumbi
Hakuna jambo lisilokuwa na
mwisho
Mat Methali hii hutumiwa kwa mfano kumpoza mtu
ambaye yumo katika mateso na dhiki; yaani ni
kama kumwambia kuwa dhiki yake itamalizika tu,
haitaendelea maisha.
Hakuna mchele ukosao ndume Ndume:
m.y.
mat
(za mchele) punje ambazo zingali zina maganda
Mchele kabisa haukosi kuwa na ndume ijapo
kidogo.
Mchele kabisa haukosi ndume, yaani zile punje
ambazo zingali na maganda yake kama mpunga
ambao haujatwangwa, zinazopatikana katika
mchele. Na pia hapana mahali katika taifa
pakosapo kiongozi (mkubwa).
Hakuna mume wa waume m.y.
mat
Hakuna mume ashindaye waume wote.
Mtu akijifanya ana nguvu sana kushinda watu
ajue anajidanganya, kwani kuna mwengine
anamshinda, na amshindaye yeye, kuna
mwengine amshindaye pia, n.k.
Methali hii hutumika kwa mtu ajionaye hakuna
anayemshinda kwa ujasiri au ushujaa au nguvu
n.k.
Hamadi ni ilo kibindoni
(Hamadi kibindoni)
Hamadi:
Kibindoni:
m.y.
mat
Tamko la mtu anaposhtuka
Mkunjo wa nguo inayofungwa kiunoni, kama
kikoi au shuka
Ukishtuliwa (na adui au mnyama mbaya) na
kushtuka, yataka silaha iweko kibindoni, haiku
mbali.
Methali nii inamfahamisha mtu kuwa wakati wa
haja au dhiki kinachomfaa ni kile alichonacho
mkononi, yaani karibu naye. Pia methali hii
inamhimiza mtu aweke akiba, kwani ndiyo
itakayomfaa akitokewa na haja ya ghafla.
Hapana masika yasiyo na mbu Masika:
m.y.
mat
Majira ya mvua nyingi
Masika kabisa hayakosi mbu (kwa sababu ya
mvua na tope nyingi zinazokuwepo)
Methali hii inatufahamisha kuwa kila wakati huja
na taabu na shida zake, kama vile wakati wa
masika unavyokuja na mbu.
Hapana msiba usiokuwa na
mwenziwe
Msiba:
m.y.
mat
Jambo la huzuni, maafa
Hakuna msiba unaokuja peke yake, basi
ukamalizika. Mara nyingi husababisha misiba
mingine ambayo hufuata.
Hutumiwa methali hii inapokuwa mtu anafikwa
na msiba baada ya msiba.
Haraka haraka haina Baraka Mat
Taz
Methali hii inakufahamisha kuwa unapotaka
kufanya jambo ulifanye kwa makini na utulivu;
ukifanya pupa halinyoki.
Mwenda pole hajikwai
Mwenye pupa hadiriki kula tamu
Samba mwenda pole ndiye mla nyama
Taratibu ndiyo mwendo.
Hasira hasara Hasira:
m.y.
mat
Hamaki, ghadhabu, chuki
Hasira huweza kumletea mtu hasara
Methali hii hutumiwa kumnasihi mtu aliyeshikwa
na hasira kuwa apoe, ama hiyo hasira yake
inaweza kumsababishia akafanya jambo ambalo
litamletea majuto na hasara baadaye.
Hasira za mkizi tijara ya mvuvi Mkizi:
Tijara;
m.y.
mat
Aina ya samaki
Faida, manufaa
Chuki na ghadhabu anazozifanya mkizi zinampa
manufaa mvuvi. (mkizi hurukaruka kwa hasira, na
mara nyingi, katika kuruka kwake, hujiingiza
mwenyewe ndani ya chombo cha mvuvi).
Methali hii hutumiwa kumtahadharisha mtu kuwa
hasira zake kumfanyia aliyemshinda kwa nguvu
hazina maana, kwani kwanza atamshinda kisha
aondoke na sifa.
Hayawi hayawi huwa m.y.
mat
Hayatakuwa hayatakuwa, mwisho wake
yanakuwa.
Hutumiwa methali hii kwa maana ya kuwa mtu
akipuuza jambo na akasema haliwi au halitokei,
huja pengine likatokea ghafla, akabakia majuto tu.
Heri kujikwaa dole kuliko
kujikwaa ulimi
Kujikwaa
ulimi:
m.y.
Kuteleza ulimi
Heri mtu kujikwaa kidole aumiye kidogo, kuliko
kujikwaa ulimi, yaani kusema jambo baya.
mat Hutumiwa methali hii kumtahadharisha mtu
yasimtoke maneno ovyo ambayo yanaweza
kumtia matatani.
Heri nitakula na nini kuliko
nitakulani
m.y.
mat
Afadhali nitakula na nini (yaani kuwa na chakula
bila ya kitoweo cha kutoelea) kuliko nitakula nini
(kuliko kukosa chakula kabisa ukawa unajiuliza:
nitakula nini?)
Hutumiwa kumnasihi mtu kuwa bora kidogo
alichopata kuliko kukosa kabisa kabisa.
Heri nusu shari kuliko shari
kamili
m.y.
mat
Afadhali kupata taabu ndogo kuliko taabu kubwa,
iwapo ni lazima upate taabu hiyo.
Hutumiwa kumnasihi mtu kuwa bora alikabili
jambo fulani dogo linalomchukiza kuliko
kukumbana na balaa kubwa zaidi baadaye.
Heshima kitu cha bure m.y.
mat
Heshima ni kitu kinachopatikana bila kununuliwa
Mfano huu hutumiwa kumnasihi mtu awe na
heshima na adabu.
Hiari yashinda utumwa m.y.
Mat
Mtu akiachiwa alifanye jambo kwa hiari yake
mwenyewe basi huweza kulifanya vizuri zaidi
kuliko akilazimishwa
Methali hii inatufahamisha kuwa binadamu
akilazimishwa kwa nguvu kufanya jambo,
halifanyi vizuri kama akiachwa afanye kwa hiyari
yake.
Hucheka kovu asiyefikwa na
jeraha
m.y.
mat
Mtu hucheka kovu la jeraha kwa mwenziwe kwa
sababu yeye hajapata kufikwa hata na kidonda.
Methali hii hutumiwa kumwelezea mtu ambaye
anamcheka na kutomjali mwenziwe aliyefikwa na
maafa kwa sababu yeye hakupata kufikwa na
mashaka kama hayo.
Ihsani iandame imani Ihsani:
m.y
mat
Wema
Fadhila ifuate huruma, ziwe zinaandamana
pamoja.
Methali hii inatunasihi kuwa tukifanyiwa wema,
basi tomwonee huruma na imani huyo mwema
wako; nawe ujaribu kumlipa kwa wema vile vile.
Ikiwa hujui kufa tazama kaburi m.y
Iwapo kufa hukujui uangalie kaburi lilivyo.
mat Methali hii hutumiwa kumwambia mtu ambaye
hajapatikana na taabu fulani kuwa amtazame mtu
mwenye dhiki kama hiyo; yuko haligani? Hapo
ndipo atakapojua dhiki hiyo ilivyo.
Iliyopita si ndwele ganga ijayo Ndwele:
Ganga:
m.y
mat
Ugonjwa
Tibu, agua
Ugonjwa uliopita si maradhi tena, jaribu kuyatibu
maradhi yajayo, kwani hayo ndiyo muhimu.
Methali hii hutumiwa, kunasihi kuwa balaa
iliyopita ndiyo imekwisha pita. Kitu muhimu ni
kufikiri njia za kuikabili balaa ijayo.
Imara ya chombo ni nanga m.y
mat
Chombo, kama jahazi au meli, kinahitaji nanga
ndiyo kiwe imara.
Methali hii hutumiwa aghalabu kumwambia mtu
kuwa akitaka kufanya jambo ambalo linahitaji
pesa, ni lazima awe nazo za kutosha, ama jambo
lake halitafanikiwa.
Inuka twende ni watu
waaganao
m.y
mat
Yule anayemwambia mwenziwe ainuke waende
mahali huwa wameshaagana kimbele.
Hutumiwa wakati watu wawili wanapotaka
kufanya jambo fulani ni lazima kwanza
washirikiane na wakubaliane. Methali hii
inatahadharisha kuwa tuwaonapo watu, tuseme
wawili au zaidi, wanataka kufanya jambo fulani,
basi watu hao wamekwisha agana kwanza, yaani
wamekwisha kubaliana kabla na kushirikiana.
Ituuzayo tia iyo isokuwako si
dawa
Ituuzayo:
Iyo:
m.y
mat
Inayochuruzika
Hiyo
Tumia dawa hiyo mbaya uliyonayo iliyo mbali
haifai.
Methali hii inamnasihi mtu chake kibaya
asikidharau kwani huja siku kikamfaa kikashinda
kizuri cha mbali.
Ivute ngozi ingali mbichi Ingali
Bado
m.y
mat
Wahi kuivuta ngozi haraka kabla bado
haijakauka.
Methali hii hutumika kuelezwa mtu kuwa afanye
haraka kulitengeneza jambo kabla
halijaharibika.kwa mfano, mtoto awahiwe kwa
malezi mema angali bado mdogo.
Uwahi udongo ungali maji.
Jahazi la mkata haliendi joshi Mkata
Joshi
m.y
mat
taz
Maskini
Jahazi kwenda kwa kasi
Jahazi la maskini haliendi sawasawa kama
linavyotakiwa.
Methali hii hutumia mtu anapoona jambo lake
haliendi sawa kwa sababu ya ukosefu wa pesa au
kwa sababu hali yake ni duni.
Dau la mnyonge haliendi joshi.
Jazaa ya ihsani ni ihsani Jazaa
Ihsani
m.y
mat
Malipo, fadhila, zawadi
Wema, hisani
Malipo ya wema ni wema
Methali hii inamnasihi mtu kuwa anapofanyiwa
wema wa aina yoyote, naye alipe wema.
Jifya moja halisimamishi
chungu
Jifya
m.y
mat
taz
Moja kati yam awe matatu ya kuwekea chungu
juu.
Jiwe moja haliwezi kusimamisha chungu kikaa
sawasawa.
Methali hii aghalabu hutumia mtu anapotaka
kufahamisha kuwa kazi fulani inahitaji watu
wengi kuifanya, haiwezekani kufanywa na mtu
mmoja.
Kidole kimoja hakivunji chawa.
Kijiti kimoja hakisimamishi jengo.
Jino la pembe si dawa ya pengo m.y
mat
Jino la kutengeneza kwa mfupa au pembe
haliwezi kuwa kama jino la kuumbwa nalo ijapo
litaziba pengo.
Methali hii inatufahamisha kuwa kitu chochote
ambacho umekizowea na unakipenda, kikikutoka
kikapotea, hata ukipata badili yake hakiwezi
kufidia cha kwanza.
Jisaidie Mungu akusaidie m.y
Sharti mwenyewe ujisaidie ndipo Mungu naye
akusaidie.
mat Methali hii hutumika kumtia mtu hima ili afanye
jitihada wakati afanyapo jambo, asikae tu,
akatumai Mungu atamsaidia.
Jitihada haiondoi kudura Kudra
m.y
mat
Nguvu au uwezo wa Mungu
Bidii haiondoi uwezo wa Mungu
Methali hii huweza kutumika, kwa mfano mtu
kumwambia adui yake kwamba hata akifanya
bidii namna gani ili yeye apatikane na shida
iwapo Mungu hataki, haiwi. Pia methali hii
hutumiwa kumliwaza mtu ambaye ingawa
amejitahidi kulifanya jambo, hakufanikiwa; na ni
kama kumwambia, “Kweli umejitahidi uwezavyo,
lakini Mungu ndiye mwenye uwezo wa kufanya
atakalo liwe, na mara hii hakutaka; basi usife
moyo.
Jogoo la shamba haliwiki mjini M.y
Mat
Jogoo linalotoka shamba likiletwa mjini huogopa
kuwika.
Methali hii inakufahamisha kuwa hata ikiwa
kwenu unasema na kufanya utakalo kwa marefu
na mapana, huwezi kufanya hivyo ugenini; yafaa
ufanye kila jambo kwa hadhari.
Jungu kuu halikosi ukoko Jungu
m.y
mat
taz
Chungu kikubwa
Chungu kilicho kikubwa hakikosi ukoko ijapo
kidogo
Methali hii inatujulisha kwamba mtu aliyekuwa
tajiri hata akiharibikiwa na kufilisika, hakosi
akiba yoyote japo ndogo.
Chombo kilichopikiwa samaki hakiachi kunuka
vumba.
Kaa mkuu ng’ombe wa maji
akiinua gando mwelemeze
nanda
m.y
mat
Kaa mkubwa ni kama ng’ombe wa majini, akiinua
mguu mwelemeze kigongo cha panda
Methali hii hutumiwa kutukanya kuwa
tusimdharau mtu mwenye uwezo katika mazingira
yake mwenyewe, kwani ingawa pengine
anaonekana mdogo lakini katika mazingira yake
huwa na nguvu na akitaka huweza kuleta madhara
makubwa.
Kamba hukatikia pabovu m.y
mat
Kamba hukatikia mahali penye ishara ya ubovu
Mtu hutumia methali hii aghalabu jambo
linapoharibika na lawama akatupiwa yeye aliye
mnyonge, asiye na bahati, ingawa pengine yeye si
mkosa.
Kazi mbi si mchezo mwema Mbi
m.y
mat
Mbaya
Kazi mbaya ni bora kuliko mchezo mzuri,
usiokuletea faida.
Methali hii hutumiwa kwa maana ya kuwa kazi
ijapo ni mbaya na duni lakini inayokupatia pesa ni
bora kuliko kukaa bure na kuzurura bila faida.
Aghalabu huambiwa methali hii mtu asiyependa
kufanya kazi, anapenda kuzurura tu, na anasa na
mchezo huu na huu.
Kelele za mwenye nyumba
hazimuudhi mpangaji
m.y
mat
Maneno ya kila siku ya mwenye nyumba huwa
mpangaji ameyazoea na wala hayamuudhi.
Hutumiwa methali hii kwa maana ya kuwa mtu
akiwa ana haja fulani kwako, yaani ni muhitaji,
kila utakalomwambia yeye huridhia, ilia pate haja
yake.
Kenda ni karibu na kumi Kenda
m.y
mat
Tisa
Tisa iko karibu na kumi
Hutumiwa, kwa mfano, kumhimiza mtu afanye
bidii zaidi maana kazi aliyoifanya iko karibu
kumalizika, hasa inapokuwa mtu mwenyewe
anaonesha kuchoka na ameanza kupunguza bidii
yake.
Kibaya chako si kizuri cha
mwenzako
m.y
mat
Chako ambacho hukipendi, ni bora kuliko kizuri
cha mwenzako.
Methali hii hutumiwa kwa maana ya kuwa chako
ambacho hukipendi na unakiona duni, kina
manufaa zaidi kwako kuliko cha mwenzako
kizuri, ambacho una tamaa ya kukipata. Aghalabu
methali hii hutumiwa kwa mtu anayetamani vya
watu, ilhali anavyo vyake kama hivyo lakini
havithamini, anaviona duni.
Kichwa cha kuku hakistahimili
kilemba
m.y
mat
Kichwa cha kuku, kwa udogo wake, hakiwezi
kuvumilia uzito wa kilemba.
Methali hii hutumiwa kwa mtu ambaye hastahili
kupata ukubwa kwa kukosa akili, kwa sababu
alipokwisha kupata madaraka, akaanza kuchafua
mambo. (Kilemba, kwa Waswahili ni nguo
inayompa heshima na ukubwa aliyekivaa).
Kidole kimoja hakivunji chawa m.y
mat
taz
Kidole kimoja hakiwezi kumvunja chawa na
kumwua (Chawa, kwa desturi huvunjwa kwa
kubanwa baina ya kucha mbili za vidole gumba)
Methali hii hutumiwa kwa maana ya kuwa pesa
kidogo haziwezi kufanya jambo la gharama
kubwa na pia kazi yenye kuhitaji watu wengi mtu
mmoja haiwezi.
Jifya moja halisimamishi chungu
Kijiti kimoja hakisimamishi jingo.
Kigumba kwa nguruwe kwa
mwanadamu kiuchungu
Kigumba
m.y
mat
Chuma cha mkuki au mshale
Mshale kumpiga nguruwe ni sawa lakini kwa
mwanadamu si sawa.
Methali hii hutumiwa kumtoa mtu makosa na ni
kama kumwambia, “Siku uliponikosea mimi
nilivumilia, lakini sasa mimi nimekukosea wewe,
unahamaki na huwezi kustahimili.”
Kijiti kimoja hakisimamishi
jengo
m.y
mat
taz
Kijiti kimoja hakiwezi kujenga nyumba
ikasimama
Methali hii hutumiwa kwa maana ya kuwa kazi au
jambo linalohitaji watu wengi haliwezi
kukamilika kwa kufanywa na mtu mmoja.
Jifya moja halisimamishi chungu.
Kidole kimoja hakivunji chawa.
Kikulacho ki nguoni mwako m.y
mat
Kikulacho (kwa mfano, kunguni au chawa) kipo
ndani ya nguo yako uliyoivaa.
Hutumiwa methali hii kwa maana ya kuwa
anayekuandama kwa ubaya aghalabu ni yule
anayekujua vizuri kwa sababu hayuko mbali
nawe.
Kila kufuli ina ufunguo wake Mat
Taz
Methali hii hutumika aghalabu kwa maana ya
kuwa kila mtu ana mtu wake anayemweza
kusema naye hata akasikia rai.
Kila mtu kwa mtuwe.
Kila shetani na mbuyu wake.
Kila likuepukalo mja, lina heri
nawe
Mja
Mat
Mwanadamu
Hutumiwa methali hii kumliwaza mtu ambaye
alikuwa na haj asana na kitu akakikosa. Ni kama
kumwambia: Usione vibaya ukasikitika, pengine
kitu hicho ni shari kwako; Mungu atakupa chenye
heri nawe.
Kila mtu kwa mtuwe m.y
mat
taz
Kila binadamu ana mtu wake
Methali hii inatufahamisha kwamba duniani kila
mtu ana mtu amwezaye kumwambia jambo
akasikiliza. Basi ikiwa una haja kubwa kwa mtu
mtafute anayemweza mtu huyo, amkabili na
kumweleza haja yako.
Kila kufuli ina ufunguo wake.
Kila shetani na mbuyu wake.
Kila ndege huruka kwa ubawa
wake
m.y
mat
Kila ndege huruka angani kwa kutumia ubawa
wake, si kwa kutumia ubawa wa ndege mwingine.
Methali hii aghalabu hutumiwa katika kumnasihi
mtu, na ni kama kumwambia, “Kila mtu ana
bahati yake, usitegemee bahati ya mwenzio;
usione fulani anafanya jambo hili wala haingii
matatani tena linamnyokea, ukafikiri na wewe
ukifanya utaongokewa vile vile.”
Kila shetani na mbuyu wake m.y
mat
taz
Kila shetani ana mbuyu wake ambao ndio makao
yake (Itikadi ya kienyeji ni kuwa mashetani
hupenda kukaa kwenye mibuyu)
Methali hii aghalabu hutumika kwa maana ya
kuwa kila binadamu ana binadamu mwenziwe
wanaosikilizana, ambaye akisema naye hawezi
kumvunja wakati wowote.
Kila kufuli na ufunguo wake.
Kila mtu na mtuwe.
Kiliacho pa, kijutie Paa
m.y
mat
Mlio wa, mfano, sahani ya kigaye inapoanguka
juu ya sakafu na kupasuka.
Kinacholiwa pa! inafaa ukisikitikie.
Inatumika methali hii kwa maana ya kuwa
kinachoingia athari ya kuvunjika au kuharibika,
hata kama si chako, inafaa ukisikitikie.
Kimumunye (mumunye)
huharibikia ukubwani
m.y
mat
Kimumunye huharibika wakati kinapopevuka.
(Mumunye hupikwa linapokuwa change.
Likipevuka hutupwa)
Mfano wa matumizi ya methali hii ni mtu ambaye
tangu kuinukia kwake hajafanya kosa fulani lakini
katika utu uzima wake ameharibika na kuanza
kufanya kosa hilo.
Kinga na kinga ndipo moto
uwakapo
Kinga
m.y
mat
Kipande cha ukuni kilicho na moto
Kikuni cha moto na kikuni cha moto ndipo
hufanya moto uwake.
Watu wanaposhirikiana kwa nia moja kulifanya
jambo fulani hunyoka, na lao walilokusudia
likawa. Methali hii inahimiza watu wawe wamoja
na washirikiane.
Kinolewacho hupata m.y
mat
Kinachonolewa, ikiwa kisu, panga, n.k hupata
makali.
Methali hii hutumiwa kwa maana ya kuwa, kwa
mfano, mtu anapoambiwa neno lilo kwa lilo ijapo
hataki, ni lazima mwisho wake atasikia na afuate.
Pia, mtu akiwa anafanya jambo hilo kwa hilo,
mwishowe ataweza tu kulifanya, hata ikiwa
mwanzo likimshinda.
Kipendacho moyo ni dawa m.y
mat
Kinachopenda roho yako ni kama dawa.
Methali hii hutumiwa kwa mtu ambaye anakitaka
sana kitu ingawa pengine ni kibaya. Watu
husema; mpeni maana kipendacho moyo ni dawa.
Labda kwa kukipata hicho kitu moyo wake utatua.
Kipya kinyemi ingawa kidonda Kinyemi Kitu cha kupendeza, chenye kufurahisha.
m.y
mat
Kipya chapendeza ijapokuwa ni kibaya, kama
kidonda.
Methali hii hutumiwa kwa mtu aliyepata kitu
kipya ambacho si kizuri hivyo, lakini akakienzi
zaidi kuliko kizuri alichokuwa nacho tangu
zamani. Pia, watu hutumia methali hii
wanapomwona mtu anapenda kuvaa nguo hiyo
hiyo mara nyingi kwa sababu ni mpya.
Kiraka cha jamvi ni kanda Kanda
m.y
mat
Fuko lililosukwa kwa minyaa
Kiraka kinachofaa kuziba mpasuko wa jamvi,
hukatwa katika kanda. (Jamvi na kanda yote
hufanywa kwa minyaa).
Mwenye fedha ashindane na mwenye fedha; na
maskini kwa maskini. Kila mmoja kwa kadiri
yake.
Methali hii inatufahamisha ya kuwa amfaye
maskini wakati wa dhiki ni maskini mwenziwe.
Kwa hivyo maskini akiwa na haja hupata msaada
kwa maskini mwenziwe, mtu wa hali moja na
yeye.
Kitanda usichokilalia hujui
kunguni wake
m.y
mat
taz
Kitanda ambacho hujalala juu yake huwezi kujua
kama kina kunguni wengi au kidogo, wakali au si
wakali n.k. Yule anayekilalia kitanda hicho ndiye
ajuaye hasa adhabu ya kunguni wake.
Methali hii inatufahamisha kuwa shida
inayompata mwenzio huwezi kujua taabu yake
maana haikukufika wewe.
Adhabu ya kaburi aijuaye maiti.
Kitema kuni temato Tema
m.y
mat
Chanja kuni
Ukichanja kuni, chanja kwa vizuri.
Methali hii inamnasihi mtu akiazimia kulifanya
jambo lolote alifanye sawasawa na kwa vizuri.
Kitokacho matumboni ki
uchungu
m.y
mat
Kinachotoka katika matumbo kina uchungu (kwa
mfano, mwana).
Methali hii hutumika kwa maana ya kuwa
chochote mtu anachokipatia taabu ni lazima
akionee uchungu na akilinde sana, kama mtu
anavyomwonea uchungu mwana aliyemzaa
mwenyewe.
Kivuli cha fimbo hakimfichi
mtu jua
m.y
mat
Kivuli cha fimbo, kwa sababu ya udogo wake,
hakimzibi mtu jua.
Methali hii hutumiwa mtu anapokuwa anahisi
kuwa anachokipata ni kidogo sana, hakitoshi
kabisa kwa mahitaji yake; kwa mfano, anapotaka
kukopa shilingi elfu kwa mahitaji yake,lakini
akapata mia tu.
Kivumacho hakidumu Kivumacho
m.y
mat
Kinachotajwa
Kinachotajwa sana huwa hakina maisha marefu.
Hutumiwa methali hii kumsema mtu ambaye
anatajwa sana hasa kwa ubaya. Huwa hana
mwisho mwema, aghalabu madhara humfika.
Kufa kwa wengi ni arusi m.y
mat
Kufa kwa watu wengi ni furaha.
Mashaka yanayowapata watu wengi mwanadamu
huona kidogo ni afadhali kuliko kumfika yeye
peke yake. Na hii ni tabia tu ya mwanadamu
ilivyo. Basi ikiwa maafa fulani yamewafika watu
wote, watu husema: kufa kwa wengi……
Kuinamako ndiko kuinukako m.y
mat
Upande unaoinama ndio upande utakaoinuka.
Hutumika methali hii katika kumliwaza aliye
chini kuwa asife moyo maadamu yu hai;
apendapo Mola iko siku yake naye atakuwa juu
afurahike.
Kuishi kwingi ni kuona mengi m.y
mat
Mtu akiishi sana huona mambo mengi.
Methali hii hutumiwa aghalabu na watu wazima
wanapoona mambo ya kushangaza au ya
kustaajabisha, ambayo pengine hawakupata
kuyaona kabla. Hapo ndio husema: Kuishi kwingi
ni kuona mengi.
Kukopa arusi kulipa matanga Matanga
m.y
mat
Siku za msiba na kumlilia mtu aliyefariki.
Kukopa ni furaha kama arusi lakini kulipa ni
msiba kama matanga.
Unaweza kuitumia methali hii, kwa mfano
kumwambia mtu aliyekujia kwa furaha na
bashasha kutaka umkopeshe, lakini sasa anafanya
udhia, hataki kukulipa.
Kuku havunji yai lake m.y
mat
Kuku ni taabu kulivunja yai lake.
Methali hii hutumiwa kwa maana ya kuwa mtu
hamdhuru mtu wake hata kama hampendi. Kila
mmoja hukionea uchungu kitu chake hata kama ni
kibaya.
Kuku mgeni hakosi kamba
mguuni
m.y
mat
Kuku ambaye ni mgeni hakosi alama katika mguu
wake. (Kuku akiwa mgeni aghalabu hufungwa
kamba mpaka apazowee pale pahala ndipo
huachiliwa. Alama ya kamba hiyo huwepo bado
mguuni kwa muda)
Methali hii inatufahamisha kuwa mgeni anapofika
nchi au mji wa watu, aghalabu hujulikana tu, kwa
sura, tabia au hata mwendo wake.
Kulenga si kufuma Kulenga
Kufuma
m.y
mat
Kutunga shabaha
Kupiga, mfano kwa mkuki
Kutunga shabaha (kwa madhumuni, kwa mfano,
ya kumpiga mnyama kwa mkuki au mshale) si
kupiga.
Hutumika methali hii kwa maana ya kuwa
kuazimia tu kufanya jambo si sawasawa na
kulifanya hasa hilo jambo na kuliweza.
Huambiwa mtu anayejisifu tu: “Nitafanya hivi,
nitafanya hivi”; naye hafanyi lolote.
Kumwashia taa kipofu
wamaliza mafuta yako
Mat Hutumika methali hii kwa maana ya kwamba
kumweleza mjinga jambo la maana wapoteza
wakati wako bure kwani unayosema
hatatamwingia akilini – ni sawa na kumwashia taa
kipofu, ilhali haoni.
Kunguru mwoga hukimbiza
ubawa wake
m.y
mat
taz
Kunguru mwenye uwoga hukimbiza bawa, asije
akadhurika.
Methali hii inamnasihi kila mtu ambaye hapendi
kujitia katika balaa isiyomhusu, ajitenge mbali ili
matata yakitokea awe salama
Mie nyumba ya udongo, sihimili kishindo
Kuni juu ya uchaga zacheka
zilizo motoni
Uchaga
m.y
mat
Pahala pa kuwekea kuni
Kuni zilizo juu ya uchaga ati zacheka kuni
ambazo ziko motoni (na ilhali mwishowe nazo
zitaishia humo humo motoni)
Hutumika methali hii kwa kuwastaajabia watu
wengine kuwa kuwacheka wenzio ambao wako
katika shida, na hali wao kumbe mashaka yale
yale yawangojea.
Kupanda mchongoma kushuka
ndiyo ngoma
Mchongoma
m.y
mat
Namna ya mti wenye miiba
Kupanda juu ya mchongoma ni rahisi lakini
kushuka ndio udhia.
Methali hii hutumika kwa mfano
kumtahadharisha mtu asijisemee maneno ovyo,
kwa sababu mara nyingine huweza kutoa neno
ambalo linaweza kuzusha balaa kubwa.
Hutumika pia, kumtahadharisha mtu asichokoze
na kujitia katika balaa, kwani akisha kujiingiza
pengine itakuwa taabu sana kutoka.
Kupata si uwerevu na kukosa si
ujinga
m.y
mat
Kupata utajiri si werevu na kuwa maskini si
upumbavu.
Hutumika methali hii kwa maana ya kuwa kupata
na kukosa vyote vyatokana na Mungu, si kwa
uhodari wala si kwa ujinga wake mwanadamu.
Lake mwanadamu ni kufanya bidii tu amtegemee
Mungu.
Kupewa usikubali waja taka
usipwe
m.y
mat
Kupewa ukakataa, utakuja wakati utake unyimwe.
Methali hii hutumika kumkanya mtu anayepewa
kitu akakikataa. Utakuja wakati akihitajie akose,
iwe ni kujuta.
Kupotea njia ndiyo kujua njia m.y
mat
Ukipotea njia mara mbili tatu mwishowe ndio
utaijua.
Methali hii hutumika kumnasihi mtu aendelee na
kulifanya jambo, asione kuwa amekosea mara
mbili tatu, akavunjika moyo; akiendelea
mwishowe atafanikiwa.
Kuregarega si kufa, kufa ni
kuoza utumbo
Kuregarega
m.y
mat
Kulegea, kutokuwa imara; k.m. kwa sababu ya
ugonjwa
Kuugua na kulegea kwa maradhi sio kufa; kufa
hasa ni mtu afikapo kuoza tumbo (yaani sehemu
nyingine za mwili, kama mikono, miguu na
kadhalika, huweza kuoza lakini mtu bado yu hai)
Mtu mgonjwa au dhaifu akiitumia hii methali ni
kama kusema: “Msinione hivi nimeregea mkaona
nimekwisha, siwezi kitu. Bado ni hai, sikufa; na
maadamu ni hai ninaweza kufanya la kufanya.
Kutaataa siyo dawa ya kufa Kutaataa
m.y
mat
Kuhangaika au kutapatapa huku na kule, kama
mgonjwa.
Kutaataa (kama vile mgonjwa anapokata roho)
hakuzuwii mauti yasije.
Mgonjwa akishajaaliwa kufa, hata akihangaika na
kutapatapa vipi ili ajiepushe na mauti, yatamfika
tu. Methali hii inapotumika ni kama kusema:
“Jambo hili limekwisha haribika wala hakuna njia
ya kulitengeneza. Kuhangaika kujaribu
kulitengeneza ni kujisumbua tu.”
Kutoa ni moyo usambe ni
utajiri
Usambe
m.y
mat
Usiseme
Kutoa yataka uwe na moyo wa kutoa, usiseme
yataka utajiri
Methali hii inatufahamisha kuwa asiye tajiri
huweza kutoa chache kusaidia jambo au mtu,
ilhali tajiri mwenye nacho, asitoe chochote,
akaona ubahili kutoa.
Kuuliza si ujinga m.y
mat
Kuuliza ili kutaka kujua jambo, si upumbavu.
Methali hii inatusihi tuulize ikiwa jambo hatulijui,
hapo ndipo tutaponufaika. Tusipouliza tukajua,
tutabaki na ujinga wetu.
Kuva m’va na mvuvi Kuva
M’va
m.y
mat
Kuvua
Vua
Kuvua samaki vua na mvuvi
Methali hii hutumiwa kumnasihi mtu kuwa
anapotaka kweli kujua jambo ajifunze kwa mtu
mjuzi wa jambo lile.
Kuzima koleo si mwisho wa
uhunzi
m.y
mat
Usimwone mhunzi amezima koleo zake ukadhani
hafanyi tena kazi ya uhunzi; yaani, usimwone mtu
kaacha ule mwenendo wake wa desturi, ukadhani
ndio kaacha kabisa kabisa.
Methali hii inakutahadharisha kuwa usione mtu
mbaya anakuonesha vitendo vyema ukafikiri
unyama wake amekwisha uwacha; la, jihadhari
naye.
Kwa mwenda wazimu
kumeingia mlevi
m.y
mat
Nyumbani kwa mwenda wazimu ameingia mlevi.
Hutumika methali hii kuwaelezea, kwa mfano,
watu wawili ambao wanashindana na kupigizana
kelele kwa jambo ambalo halina maana, mfano
wa mwenda wazimu anayeshindana na mlevi.
Kwa shujaa huenda kilio kwa
mwoga huenda kicheko
m.y
mat
Shujaa hupambana na balaa akaishia vilio na
masikitiko; mwoga huikimbia balaa na huishia
kucheka kwa furaha.
Methali hii hutumika kumnasihi mtu kuwa asijitie
ushujaa wa ujinga wa kulikabili jambo ambalo
anajua hakika atashindwa na matokeo yake ni
maafa na vilio. Bora awe mwoga avuke salama.
Kwenye miti hakuna wajenzi m.y
mat
Mahali penye miti mingi aghalabu hapana
wajenzi.
Methali hii hutumiwa, kwa mfano, kwa mtu
ambaye ana ujuzi fulani au mali, lakini ujuzi ule
au mali ile haitumii kwa njia ya manufaa kwake
au kwa watu wengine.
Leo ni leo, asemaye kesho ni
mwongo
m.y
mat
Jambo la leo nalifanywe leo, asemaye tufanye
kesho ni mwongo – yaani hana azma kweli ya
kufanya jambo.
Methali hii inatuhimiza tufanye mambo yetu
yaliyo muhimu tuyamalize; tusiwe na ajizi ya
kusema tutafanya kesho, kesho……..
Methali hii aghalabu hutumia wanawake, kwa
mfano harusini, wanaposhangilia kwa vigelegele
na kelele.
Liandikwalo halifutiki m.y
mat
Linaloandikwa na Mungu liwe litakuwa tu,
haliwezi kufutika.
Methali hii hutumiwa pengine kumliwaza mtu
aliyefikwa na maafa, na ni kama kumwambia:
Haya yaliyotokea yameshaandikwa, yaani
yamekwisha jaaliwa, na Mungu, na wewe
binadamu huna uwezo wa kuyafuta, au
kuyageuza, atakayo Mungu. Lililobaki ni
kumshuru tu.
Liandikwalo ndilo liwalo m.y Linaloandikwa na Mungu ndilo linalokuwa.
mat
Yaani jambo ambalo limeshakadiriwa na Mungu
kuwa ndilo hilo litakuwa ikiwa baya au zuri. Mtu
aghalabu hutumia methali hii anapoona mambo
yamemzonga na hana njia thabiti ya kuyatatua.
Hapo humwachia Mungu afanye apendavyo, na
husema: Liandikwalo…..
Lipitalo hupishwa m.y
mat
Jambo la kupita tu si la kudumu huachwa likapita.
Methali hii inatujulisha kuwa haifai kukumbuka
tena, kwa mfano, jambo baya lililopita; bora
kulisahau. Mtu huweza kutumia methali hii, kwa
mfano, kuwanasihi watu wawili walioteta,
anapojaribu kuwapatanisha.
Lisemwalo lipo ikiwa halipo
lipo nyuma laja (linakuja)
m.y
mat
Linalosemwa huwa liko na iwapo haliko liko
njiani linakuja
Jambo linaposemwa sana na watu katika mji
huwa liko jambo hilo na iwapo halipo basi
litatokea. Hutumiwa methali hii inapokuwa jambo
limevuma na kuenea katika mji au kijiji, lakini
kuna wanaosema kuwa uvumi huo ni uwongo.
Ndipo watu husema: Lisemwalo lipo……..
Lisilo budi hutendwa m.y
mat
Ambalo halina budi kufanywa hufanywa.
Methali hii inatufahamisha kuwa likiwa jambo
lishabidi liwe basin i lazima lifanywe maana
lisipotendwa huharibika.
Maji hufuata mkondo Mkondo
Mat
Taz
Nguvu za maji yanayoelekea upande fulani.
Methali hii hutumiwa aghalabu kwa mtu ambaye
anayefuata tu fikira au mwenendo wa watu
wengine bila ya kujiuliza kwanza kama afanyavyo
ndivyo au sivyo.
Bendera hufuata upepo.
Maji ukiyavulia nguo yaoge m.y
mat
taz
Maji unapoyavulia nguo ni bora uyaoge.
Ikitumiwa methali hii kwa mtu ni kama
kumwambia. “Maadamu umekwisha jitayarisha
kufanya jambo hili, basi bora ulikabili ulifanye na
ulimalize.”
Mchungulia bahari si msafiri.
Maji ya kifuu bahari ya chungu Chungu
m.y
mat
Mdudu chungu
Maji yaliyomo katika kifuu mdudu chungu
huyaona mengi kama bahari.
Mfano: dhiki au taabu ambayo mtu fulani anaiona
kubwa, mtu mwengine mwenye uwezo au nguvu
zaidi huweza kuiona dhiki hiyo si chochote si
lolote.
Maji ya moto hayachomi
nyumba
m.y
mat
Maji hata yawe moto kiasi gani hayawezi
kuteketeza nyumba.
Methali hii hutumika kwa maana ya kuwa vitimbi
na vituko vya mtu mnyonge kumfanya mtu
mwenye nguvu havimshitui au kumdhuru huyo
mwenye nguvu.
Majuto ni mjukuu m.y
mat
Masikio ni kama mfano wa mjukuu kwa sababu
huja baada ya kitendo.
Methali hii hutumiwa kumnasihi mtu kuwa kabla
ya kufanya jambo yataka kwanza afikirie, siyo
afanye tu kwani mara nyingine jambo hilo lina
hatari na hasara, na alifanyapo atakuja kujuta
mwishowe.
Mali bila daftari hupotea bila
habari
Daftari
m.y
Mat
Kitabu
Mali isiyodhibitiwa kwa kuandikwa kitabuni
sawasawa, hupotea bila kujulikana.
Methali hii hutumiwa kwa mtu mwenye dhamana
ya kushika pesa, lakini haweki hesabu barabara ya
pesa zinazopatikana na zinazotumika.
Akitahamaki pesa zote zimepotea.
Mambo ni kangaja huenda
yakaja
Kangaja
m.y
mat
Aina ya matunda kama chenza lakini ni madogo.
Mambo mengine huweza kutokea kwa ghafla tu
kama kangaja ambazo zina desturi ya miaka
mingine kuonekana na miaka mingine kupotea
kabisa.
Hutumika methali hii kwa maana ya kuwa jambo
au kitu usichokitumainia kuja kabisa, huenda
mara kwa ghafla kikatokea.
Manahodha wengi chombo
huzama
m.y
mat
Wakuu wa chombo wakiwa wengi katika jahazi
au meli, chombo hicho kitazama kwa kuwa kila
mmoja anatoa amri yake dhidi ya mwengine.
Methali hii hutumika kwa mfano, jambo
linapoharibika kwa sababu ya kuendeshwa na
viongozi wengi ambao kila mmoja anajiona ana
nguvu kushinda mwengine.
Maneno makali yavunja mfupi m.y Maneno mabaya ya kuudhi, uchungu wake ni
mat
kama yanayoweza kuvunja mfupa.
Methali hii hutumiwa kuonesha vipi maneno ya
kumtia mtu uchungu yanavyoweza kumuathiri
binadamu.
Maneno matamu humtoa nyoka
pangoni
m.y
mat
Maneno mazuri yaweza kumlainisha hata nyoka
akatoka pangoni bila matata.
Hutumika methali hii kuonesha vipi maneno
matamu ni muhimu mtu anapohitaji kitu au jambo
fulani kwa mwenziwe, hata ikiwa mtu huyo ni
anayemwogopa kama nyoka.
Maskini akipata, matako hulia
mbwata
m.y
mat
taz
Maskini anapopata pesa kidogo tu, watu wote
watapata habari, jinsi ya majisifu yake.
Methali hii hutumiwa kwa mfano kwa mtu
ambaye alikuwa hana lake hana chake, lakini sasa
amepata cheo kidogo, ama pesa kidogo, anaudhi
watu kwa majivuno yake.
Anda la mua la jana chungu kaona kivuno.
Maskini hana miko m.y
mat
Maskini hana kizuizi cha chakula fulani
Methali hii hutumika kwa maana ya kuwa mtu
mnyonge au maskini aghalabu hawezi kuchagua
akasema hiki nataka na hiki sitaki.
Mavi ya kale hayaachi kunuka m.y
mat
Mavi hata yakiwa ya zamani, hayaachi kutoa
harufu
Methali hii hutumika kwa maana ya kuwa jambo
ovu, hata ikiwa limepita zamani, halisahauliki
kabisa kabisa.
Mbio za sakafuni huishia
ukingoni
Ukingoni
m.y
mat
Pembezoni, kandokando, mwisho wa sakafu n.k.
Mbio za kwenye sakafu humalizikia ukingoni.
Aghalabu hutumika methali hii kwa mtu
anayeifanya kazi fulani kwa vishindo na kwa
hamu na mwishowe kazi hiyo asiimalize.
Mchagua jembe si mkulima m.y
mat
taz
Anayechagua kila aina ya jembe ilia pate zuri,
huyo si mlimaji barabara.
Methali hii hutumiwa kumwambia mtu akiwa ni
muhitaji wa kazi, si sawa achague kazi.
Imemlazimu afanye kazi yoyote ili aondoe shida
yake wakati wa dhiki iliyomkabili.
Mshoni hachagui nguo.
Mchagua nazi huangukia
koroma
Koroma
m.y
mat
Nazi ambayo haijapevuka
Anayechagua sana nazi mwishowe huangukia
nazi mbaya (koroma)
Methali hii yatumika kwa yule anayependa sana
kuchagua vitu kwa tamaa kuwa atapata kizuri
zaidi, lakini mwishowe hupata kibovu zaidi.
Mcheka kilema hafi
hakijamfika
Kilema
m.y
mat
Kasoro ya kiungo cha mwili
Anayemdhihaki kiumbe mwenye upungufu au ila
fulani, ajue naye kuna siku mambo yatamfika.
Methali hii hutumika kumhadharisha yule
anayemcheka mwenziwe kwa msiba wowote
uliomfika, ajue naye hana salama, kwani
binadamu heshi kufikwa na mambo mpaka siku
ya kufa.
Mchungulia bahari si msafiri m.y
mat
taz
Ukiazimia kusafiri na ukihofu bahari jinsi ilivyo
huwezi kusafiri (yaani unakwenda ukiichungulia
tu bahari, lakini kuingia hutaki).
Inatumika methali hii kumnasihi mtu kuwa
akiazimia kufanya jambo awache uwoga na
alifanye. Yataka ukitia nia kufanya kitu, fanya.
Maji ukiyavulia nguo yaoge.
Mdomo siri ya gunda Gunda
m.y
mat
Baragumu
Siri yote ya mdomo yajulikana na gunda, maana
vitu hivi viwili vinatumika pamoja.
Inatumika methali hii kwa maana ya kuwa siri ya
mtu, kwa mfano, hujulikana na yule
aliyeambatana naye sana. Kwa mfano, aibu ya
mke husitiriwa (hufichwa) na mumewe, ijapo awe
na kasoro fulani, kabisa haitangazi.
Meno ya mbwa hayaumani m.y
mat
Meno ya mbwa hayashikani kama vile ya
mnyama mwingine.
Inatumika methali hii kwa maana ya kuwa mtu
hamdhuru mtu wake. Hata wakiteta namna gani
lakini mtu wake hawezi kumwepuka wala
kumdhuru.
Mfa maji haachi kutapatapa m.y
mat
Anayezama katika maji haachi
kuhangaikahangaika katika kujaribu kujisaidia
ingawa ndiyo anakufa.
Hutumika methali hii kwa maana ya kuwa
anayepatikana na shida yoyote, haachi kujitetea
na kujisaidia hata ikiwa ndiyo kujitetea huko
hakutasaidia kitu.
Mgaagaa na upwa hali wali
mkavu
Mgaagaa
Upwa
m.y
Mat
Anayekwenda huku na kule.
Ufuo wa bahari
Anayehangaika huku na kule (yaani, kwa mfano,
mvuvi aliyekosa samaki baharini) ufuoni kutafuta
kitoweo hakosi japo kidogo cha kutowelea wali
wake.
Hutumika methali hii kumtia mtu moyo
alihangaikie jambo au alifanyie jitihada kikweli
atafaulu.
Mgema akisifiwa tembo hulitia
maji
m.y
mat
Mgema anapojua anasifiwa, tembo lake huzidi
kuliharibu kwa kuliongeza maji.
Methali hii hutumika, kwa mfano, kumsema mtu
ambaye akisifiwa kwa jambo fulani, lakini sifa
hizo badala ya kuzidi kumtengeneza zimemfanya
aharibu jambo asifiwalo.
Mgeni aje mwenyeji apone m.y
mat
Akitokea mgeni kwenye nyumba watu wote
hunufaika kwa kula vinono (mgeni afike ili
anayempokea mgeni asalimike).
Watu hutumia methali hii wanapotaraji mgeni –
yaani angalau watu watanufaika kwa kuja mgeni
huyo.
Mgeni pofu ingawa ana macho
yake
m.y
mat
Mgeni ni kama kipofu hata kama ana macho yake
kamili.
Methali hii inatuonya kuwa mgeni hata kama ni
mwerevu, huwa kama mjinga au kipofu na ni
tofauti na mwenyeji, maana ni lazima aongozwe
kwa takriban kila jambo ijapo anaona na akili
yake timamu. Pia, methali hii inamwonya mgeni
kuwa baadhi ya mambo ayaonayo ugenini hata
kama hayampendezi, ajifanye kama hayaoni.
Mgomba haushindwi na
mkunguwe
m.y
mat
Mgomba hauwezi kushindwa kuuchukua mkungu
wake wa ndizi, hata uwe mzito vipi.
Methali hii hutumika, kwa mfano, kwa maana ya
kuwa mwana vyovyote atakavyokuwa – akiwa
mwovu, mgonjwa au mvivu, na kadhalika – mzazi
hatashindwa na mwanawe kwa sababu
kamlazimu.
Mgonjwa haulizwi dawa m.y
mat
Mgonjwa haulizwi kama anataka kunywa au kula
dawa, hupewa tu.
Methali hii inatufunza kwamba ikiwa mwenzetu
ana haja kubwa na tunajua kuwa mwenzetu ni
muhitaji, haina maana kumwuliza, “Unataka kitu
fulani?” tumsaidie tu kwa haja yake ikiwa
tunaweza.
Mie nyumba ya udongo, sihimili
kishindo
m.y
mat
taz
Mimi ni kama nyumba ya udongo sistahimili
msukosuko (kwa sababu nyumba ya udongo si
imara)
Hutumia mtu methali hii kwa kumaanisha kuwa
yeye hapendelei balaa, na ni kama kusema, “Mimi
ni mnyonge wala nguvu sina za kuweza
kuvumilia dharuba au taabu.”
Kunguru mwoga hukimbiza ubawa wake
Milima haikutani lakini
binadamu hukutana
m.y
mat
Milima haimkiniki kuweza kukutana, lakini
wanadamu madhali ni wahai, huweza kukutana
tena hata ikiwa wako mbali mbali kwa siku
nyingi.
Methali hii aghalabu huambiana watu
wanapoagana kwa kwenda safari ndefu na tamaa
ya kuonana tena ni ndogo; na ni kama kupeana
moyo kuwa tamaa ya kuonana ingawa ni ndogo
isiondoke kabisa.
Mja hatindi rehema ali hai
duniani
Hatindi
m.y
mat
Hakati
Mtu hakati tamaa naye bado yu hai duniani
Methali hii inatufunza kuwa binadamu asikate
tamaa angali yu hai duniani, lake na asubiri, na
atapata. Hutumika methali hii kuzidi kumtia mtu
moyo, asikate tamaa na jambo alifanyalo.
Mja wa hiana ana laana Hiana
m.y
mat
Udhalimu, uchoyo, unyimaji
Mtu mwenye hiana, huyo pia ni mwenye laana, ni
mwovu.
Inatumika methali hii kutuhadharisha na watu
wenye hiana.
Mjinga akierevuka mwerevu yu
mashakani
m.y
mat
Mjinga akitoka ujingani, mwerevu yumo taabuni.
Inatumika methali hii kuwatahadharisha wale
wanaojiona werevu na kuwahadaa wenziwao
kuwa watapata taabu hao wanaohadaiwa
watakapoerevuka na kutambua kuwa
wanahadaiwa.
Mkamia maji hayanywi m.y
mat
Aliye na hamu sana kunywa maji kama vile
jangwani, hawahi kuyafika na kuyanywa.
Hutolewa methali hii wakati mtu fulani
anapokuwa na hamu ya jambo fulani sana na
akafanya kila bidii katika kulifanya au kulipata
jambo lile, lakini alipokuwa tayari kulifanya au
kulipata mara likatokea jambo jingine la kupinga.
Ndipo hutamkwa: Mkamia maji hayanywi.
Mkataa kikoa ni mchawi Kikoa
m.y
mat
Jumla ya watu wanaoshirikiana
Anayekataa umoja ni adui kama mchawi.
Methali hii inatufahamisha kuwa anayekataa
kuungana na wenziwe wakashirikiana pamoja
kwa heri na shari, huyo ni mtu mwovu mfano wa
mchawi.
Mkono mmoja haulei mwana m.y
mat
Mkono mmoja pekee hauwezi kumlea mtoto.
Methali hii hutumika wakati mtoto anayelelewa
na baba tu au mama tu, anapoharibika. Watu
husema: Mkono mmoja haulei mwana, yaani
mzazi mmoja pekee hawezi kulea mwana.
Mkono mtupu haurambwi m.y
mat
Mkono usio na kitu chochote cha kurambwa
haurambwi.
Methali hii inamfahamisha mtu, kwa mfano, kuwa
akitaka jambo fulani afanyiwe au alipate, basi
sharti naye mkono wake uwe wazi, yaani awe
taz
tayari naye kutoa kitu.
Mkono utowao ndio upatao
Mkono utoao ndio upatao m.y
mat
taz
Mkono utoao kumpa mtu kitu, ndio unaopata kitu.
Methali hii inatumika kutukumbusha kuwa yule
unayempa chako, ndiye atakayekupa chake, lakini
ukijifanya mgumu au mchoyo hupati cha mtu.
Yaani ukitoa nawe utapata.
Mkono mtupu haurambwi
Mkulima hasahau jembe
kiselema
Kiselema
m.y
mat
Jembe butu la zamani
Mkulima halisahau jembe jembe butu la zamani.
Methali hii inatukumbusha kuwa kile kitu
ambacho kina kasoro fulani hatukitumii, huja siku
kikafaa na tukakihitajia.
Mkulima ni mmoja walaji ni
wengi
m.y
mat
Mkulima huwa ni mmoja lakini wanaokula
mavuno yake ni watu wengi
Methali hii inatufahamisha kwamba anayetoa
jambo la faida huwa aghalabu ni mtu mmoja kati
ya watu wengi, likaja likawafaa watu wengi au
umma mzima.
Mla cha mwenziwe na chake
huliwa
m.y
mat
taz
Anayekula cha watu afahamu kuwa na chake pia
kitaliwa.
Aghalabu methali hii hutumiwa kwa maana ya
kuwa mwenye kudhulumu pia hudhulumiwa.
Mla kuku wa mwenziwe maguu yamlekele
(miguu humwelekea).
Mla cha uchungu na tamu
hakosi
m.y
mat
taz
Anayekula kibaya na kizuri pia hakosi, atakula.
Hutumika methali hii hasa katika kumliwaza
aliyepatikana na maafa, na ni kama kumwambia,
“Stahamili tu hii taabu, baadaye bila ya shaka
raha itakuja.”
Baada ya dhiki faraja.
Mstahamilivu hula mbivu
Zito hufuatwa na pesi.
Mla kuku wa mwenziwe maguu
yamlekele (miguu humwelekea)
m.y
Aliyekula kuku wa jirani yake akumbuke kuwa
alama za miguu za huyo kuku zinaonesha
zimeelekea kwake.
mat
taz
Methali hii inatufunza tusimdhulumu mtu na
chake, hasa mtu aliye karibu na wewe kwa ujirani,
kwa urafiki, au kwa udugu.
Mla cha mwenziwe na chake huliwa.
Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa
nawe
Mla
Mzaliwa
m.y
mat
Rafiki
Ndugu yako mnayekaa pamoja, mkala pamoja
wakati wote, hakubali kufa kwa ajili yako, lakini
ndugu mliyezaliwa tumbo moja yu tayari kufa
kwa ajili yako, unapokabiliwa na hatari.
Methali hii inatufahamisha thamani ya ndugu na
kuwa ingawa tunathamini marafiki, lakini
tuthamini ndugu zaidi.
Mla ni mla leo, mla jana kala
nini?
m.y
mat
Anayekula leo ndiye mlaji kweli, aliyekula jana
kala nini?
Hutumika methali hii kwa maana ya kuwa yule
mwenye nacho leo ndiye wa kuhesabika;
aliyekuwa nacho zamani na sasa hana tena si wa
kuhesabika. Hutumika methali hii kuambiwa wale
wanaojinasibu kuwa zamani walikuwa na hiki na
kile, au walikuwa na utajiri au madaraka fulani.
Mnyonge kupata haki ni
mwenye nguvu kupenda