14
Mabaraza ya wanafunzi ni chombo kilichoundwa/kinachoundwa na wanafunzi ili kuweza kushughulikia ustawi wao shuleni Kwa kifupi ni uongozi wa wanafunzi kwa ajili ya wanafunzi. Ili chombo hiki kiweze kufanya kazi zake vizuri na kwa uhuru, lazima uongozi wa shule na walimu kwa ujumla wakiunge mkono na kukisaidia chombo hiki kwa hali na mali.

Mabaraza ya wanafunzi ni chombo kilichoundwa/kinachoundwa ... ya Mabaraza.pdf · baadaye juu ya utekelezaji wa ahadi zao kwao; Wanafunzi waelekezwe na kuhimizwa kutekeleza maelekezo

  • Upload
    others

  • View
    14

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Mabaraza ya wanafunzi ni chombo kilichoundwa/kinachoundwa na wanafunzi ili kuweza kushughulikia ustawi wao shuleni

Kwa kifupi ni uongozi wa wanafunzi kwa ajili ya wanafunzi.

Ili chombo hiki kiweze kufanya kazi zake vizuri na kwa uhuru, lazima uongozi wa shule na walimu kwa ujumla wakiunge mkono na kukisaidia chombo hiki kwa hali na mali.

Unapofika wakati wa uchaguzi, hatua zifuatazohutakiwa kufuatwa:

Uongozi wa shule hutoa matangazo ya nafasizinazotakiwa kugombewa na kubandikwakwenye mbao za matangazo;

Uongozi wa shule huandaa fomu maalum zakuomba kugombea nafasi zilizotangazwa;

Uongozi wa shule na walimu huhamasishawanafunzi ili waweze kuchukua fomu zakugombea uongozi;

Wanafunzi kuchukua fomu za uongozi na kuzijaza;

Fomu zilizojazwa kurudishwa kwa uongozi wa shule;

Uongozi wa shule kuteua kamati maalum ya uchambuzi wa nafasi mbalimbali na kufanya uteuzi. Kamati hiyo iwe na walimu na wanafunzi wasiozidi wanne(4);

Baada ya uteuzi, majina ya wateule na nafasizao kutangazwa kwa wanafunzi wote nakubandikwa kwenye mbao za matangazo;

Uongozi wa shule kuandaa mkutano wawanafunzi wote na kuwapa nafasi waombauongozi kujieleza mbele ya wanafunziwenzao na kuomba kura;

Tangu siku hiyo ya mkutano, wagombeawakiambatana na wapambe wao waendeleekufanya kampeini siku nzima na sikuinayofuata itumike kufanya kampeini;

Siku inayofuata iwe ya uchaguzi. Wanafunzi wafanye uchaguzi na upigaji kura uwe wa siri;

Kamati ziundwe za kuhesabu kura huku zikishuhudiwa na mawakala wa wagombea;

Matokeo ya uchaguzi yatangazwe na uongozi wa wanafunzi uzinduliwe rasmi.

Kutibu majeraha yauchaguzi;

Mafunzo kwaviongozi wawanafunzi juu yawajibu na Hakizao.

Wakati wa Kampeini, uongozi wa shule na walimu wawaelekeze wagombea ili watoe ahadi(yaani watawafanyia nini) pindi watakapochaguliwa.

Viongozi wawe na kumbukumbu ya ahadi zao.

Vilevile wanafunzi watunze ahadi walizoahidiwa na wagombea ili waweze kufuatilia utekelezaji wake na kuwahoji;

Viongozi wajitahidi kutimiza ahadi walizotoa kwawanafunzi, watambue wazi kuwa watahitajiwabaadaye juu ya utekelezaji wa ahadi zao kwao;

Wanafunzi waelekezwe na kuhimizwa kutekelezamaelekezo yanayotolewa na uongozi katikaserikali ya wanafunzi;

Wanafunzi, kupitia uongozi wao wanawasilianana uongozi wa shule, viongozi wa jamii namaofisa wa serikali juu ya mambo yanayohusikana ubora wa Elimu yao (Mawasiliano hayoyanaweza kuwa ya ana kwa ana, kwamazungumzo, kwa barua ama mikutano);

Wanafunzi wa kike wawashawishi wanafunziwa kiume ili wawapigie kura;

Viongozi, kwa kusaidiwa na uongozi wa shulena walimu, wawaongoze wanafunzi kushirikimikutano ya jamii, kuunda vilabu vyamasomo na michezo, kufanya makongamano, Kufanya mikutano ya Baraza ya wanafunzi piakuwa na Bunge la Watoto;

Wapewe nafasi ya kuhoji na kujengewa ujasiriwa kuongea juu ya wajibu wao na haki zao;

Uongozi wa shulena walimuwawahamasishewanafunzi wa kike kugombea nafasi zauongozi katikashule, vilabu vyamasomo namichezo, Bunge la Watoto na katikajamii;

Wanafunzi wakiumewawahamasishewanafunzi wa kike ili washirikikugombea uongozikatika shule nakatika jamii.

Haya yote yatafanyikaiwapo wanafunziwenyewe watatambua, watapenda, watajitambua nakujiamini kuwawanaweza , hivyokuchukua hatua zakushiriki katika mambo mbalimbaliyanayowahusu

yakiwemo ya uongozi.

1. Mpango wa maendeleo ya Milenia

2. Mwongozo wa Uundaji wa Mabaraza ya Watoto /2002

3.Mkata wa Umoja wa Kimataifa wa haki za watoto(Kifungucha 12 na 13) na Mkataba wa Africa wa Haki za WatotoKifungu cha 7,8na 9

4. Sheria ya Mtoto No.21/2009 (Ibara II Kifungu cha 11.)

5. Sera ya Elimu

6. Miongozo ya Walimu wakuu

7. PPP

8. MMEM NA MMES

9. Waraka na Sheria ya Elimu

10.Sera ya Maendeleo ya Vijana.