92
KIDATO CHA PILI 2019 Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 1 MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO Uundaji wa maneno ni ujenzi au uzalishaji au utengenezaji wa maneno mapya. Uundaji wa maneno mapya husaidia kuongeza msamiati katika lugha ili kukidhi mahitaji ya mawasiliano. Uundaji wa maneno mapya husababishwa na mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni na maendeleo ya kisayansi yanayotokea katika jamii. Kwa mfano tunayo maneno mapya, kama vile ufisadi, uwekezaji, ukeketaji, ujasiriamali na mengine mengi kutokana na mabadiliko ya kijamii. Kutumia Uambishaji Kubainisha Mofimu katika Maneno Uambishaji wa maneno ni kitendo cha kupata maneno kwa kubandika Mofimu kwenye kiini cha neno, uambishaji kutokea kabla ya kiini cha neno au mzizi wa neno. Mfano kiini pig- unaweza kuunda maneno kama inapiga, anayepiga, mpigaji, amepigika nk. MOFIMU Fasili ya mofimu ni: Mofimu ni neno au sehemu ya neno yenye maana kisarufi, ambayo haiwezi kugawanyika zaidi bila kupoteza maana. Kwa mfano: maneno (a) babu, hewa mofimu kila neno lina Mofimu moja AINA ZA MOFIMU 1. Mofimu huru 2. Mofimu tegemezi

MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

  • Upload
    others

  • View
    22

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 1

MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO

Uundaji wa maneno ni ujenzi au uzalishaji au utengenezaji wa maneno mapya.

Uundaji wa maneno mapya husaidia kuongeza msamiati katika lugha ili kukidhi

mahitaji ya mawasiliano. Uundaji wa maneno mapya husababishwa na mabadiliko

ya kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni na maendeleo ya kisayansi yanayotokea

katika jamii. Kwa mfano tunayo maneno mapya, kama vile ufisadi, uwekezaji,

ukeketaji, ujasiriamali na mengine mengi kutokana na mabadiliko ya kijamii.

Kutumia Uambishaji

Kubainisha Mofimu katika Maneno

Uambishaji wa maneno ni kitendo cha kupata maneno kwa kubandika Mofimu

kwenye kiini cha neno, uambishaji kutokea kabla ya kiini cha neno au mzizi wa

neno. Mfano kiini pig- unaweza kuunda maneno kama inapiga, anayepiga, mpigaji,

amepigika nk.

MOFIMU

Fasili ya mofimu ni: Mofimu ni neno au sehemu ya neno yenye maana kisarufi,

ambayo haiwezi kugawanyika zaidi bila kupoteza maana. Kwa mfano:

maneno

(a) babu, hewa

mofimu

kila neno lina Mofimu moja

AINA ZA MOFIMU

1. Mofimu huru

2. Mofimu tegemezi

Page 2: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 2

MOFIMU HURU

Haya ni maneno kamili ambayo huwezi kugawa zaidi bila kupoteza maana.

Mfano:Baridi, kofia, hewa, kaka, mama, sana, maji. Maneno haya hayawezi

kugawanyika zaidi na yakaendelea kuwa na maana hiyohiyo kisarufi.

MOFIMU TEGEMEZI

Ni vipande vidogovidogo vya maneno vyenye maana kisarufi. Mofimu hii maneno

yamejengwa kwa kubandika vipashio kadhaa vya kisarufi ambavyo huweza

kubadilishwa na maana ya neno ikabadilika.

Mfano: neno anapika lina mfano tegemezi ufuatazo

a -na- -pik- -a

1 2 kiini 3

Mofimu zinazobadilika kwenye kiini cha neno huitwa Viambishi.

Katika lugha ya Kiswahili viambishi hutokea kabla na baada ya kiini cha neno.

Mfano

Wanapendana = Wa-na-pendan-a kiini cha neno ni-pend-.

Mofimu zilizobadilisha baada ya kiini –an-na-a viambishi vinavyotokea kabla ya

kiini cha neno huitwa viambisha awali au tangulizi. Viambisha vinavyotokea baada

ya kiini cha neno huitwa viambishi tamati au fuatishi.

Mfano 1

Angalia mifano ifuatayo:

Neno Viambisha Awali Kiini Viambisha Tamati

Page 3: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 3

Unapendelea u-na- -penda- el-e-a

Waliongozana wa-li- -ongoz- an-a

Analima a-na- -lim- -a

anayeiimbisha a-na-ye -imb- -ish-a

Test Yourself

Dhima za Mofimu

Baadhi ya dhima za uambishaji ni kama ifuatavyo:

1. Kuonyesha upatanisho wa usanifu maana ya maneno yanayozalishwa

kutofautiana katika msingi wa kusanifu tu, lakini uhusiano wa maneno hayo

hutokana na kiini au mzizi wake uleule.Mfano;Fundisha kiini chake ni fund.

Unaweza kuzalisha maneno mengine kwa kutumia mzizi/kiini kilichopo

kama vile fundishana, mafundisho, mfundishaji, fundishwa, fundishana.

2. Uambishaji huonyesha nafsi

3. Uambashaji huonyesha njeo (muda)

4. Uambishaji huonyesha urejeshi

5. Uambishaji huonyesha ukanushi

6. Uambishaji huonyesha hali mbalimbali za kitenzi

Vitenzi vikiambishwa huweza kujenga/kuunda/kuzalisha vitenzi vingine au

nomino.

Page 4: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 4

Mfano 2

Vitenzi Kiini Nomino Vitenzi

Cheza -

chez-

Mchezaji,

mchezo wanacheza/atamchezea

Piga -pig- Mpigaji,

Mpiganaji

watanipiga,

aliyempiga/wanaompiga

Uambishaji hutumika kuzalisha viwakilishi na vielezi.

Neno (Kiwakilishi) Kiini Kielezi

Huyu, Huyo Hu Humu, humo

Wangu, wako, wake wa

Hii, hizo, hiki hi

Viambishi awali vina dhima ya kudokeza nafsi, njia, idadi urejeshi na

ukanushi.Mfano: Hawakulima

Ha-, kiambishi cha ukanushi

Ku-, kiambishi njeo/wakati

Viambishi tamati vina dhima mbalimbali hudokeza hali ya utendekaji, ukamilishaji

au kimalizio cha neno na kauli za matendo kama vile kutendwa,

kutendewa,kutendeka nk.

Dhima:Ukanusho, kutendeana, agizo na mtendwa, ukamilisho, usababishi.

Page 5: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 5

Mfano 3

Neno Viambishi Tamati

Anapiga -a

Wanapigana -an

Asipigwe -w

Amempigisha -ish-

Viambishi tamati vina dhima ya kutambulishwa mapema/nomino zilizoundwa

kutokana na vitenzi.

Neno Kiini Viambishi Tamati

Piga pig- -o

Mchezo chez- -o

Mtembezi tembe- -z-i

Mfiwa -fi- -us-a

ZOEZI

Katika neno “analima”, mofimu {-a-}, {-na-}, {-lim-} zina dhima gani kwa

pamoja?

A Kileksika

B Uyakinishi

Page 6: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 6

C Kisarufi

D Ukanushi

___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟.

A Kuonesha njeo

B Kuonesha wingi

C Kuonesha urejeshi

D Kuonesha nafsi

Katika neno „aliyebarikiwa‟, mofimu {-ye-} ina kazi ya___

A Kuonesha hali

B Ukanushi

C Uyakinishi

D Urejeshi

Mofimu {-hu-} katika neno „hucheza‟ ina dhima ya kuonesha hali ya___

A Kuendelea

B Mazoea

C Masharti

D Utimilifu

Katika kitenzi „analima‟, mofimu {-na-} ina dhima ngapi?

Page 7: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 7

A Tano

B Mbili

C Tatu

D Nne

Kutumia Mnyumbuliko

Mazingira yanayosababisha Mahitaji ya Maneno Mapya

Mnyumbulisho ni neno linalotokana na neno nyumbua. Kunyumbua kitu ni kuvuta,

kuongeza urefu wa kitu hicho.

Kunyumbua katika lugha ya Kiswahili ni kuongeza vinyumbulishi katika katika

kiini ili kupata msamiati mpya. Hivyo basi, mnyumbulisho ni njia mojawapo na

inasaidia kuunda maneno kwa njia ya kunyumbulisha.

Viambishi vinapochukuliwa katika kiini cha neno, basi neno hilo huwa

limenyumbulishwa. Kwa mfano neno lima kiini chake lim- huweza

kunyumbulishwa na kupata maneno mengine mpya, kama lim-ishwa, lim-ia, lim-

w-a.

Pia maneno ya mnyumbulisho yanaweza kuundwa kwa kuongeza viambishi

kwenye shina, kwa mfano:

Neno Kiini Shina Maneno ya Mnyumbuliko

Elekea elek eleka Elekeana, elekea, elekwa, elekesha

Shikishana shik shikisha Shikishana, shikisha, shikishaneni

Kwa ujumla tunawaza kusema kuwa maneno ya kawaida hunyumbulika. Hivyo

kiini/mzizi au shina moja huweza kuzalisha maneno mengine mengi ambayo

yanatokana na msingi mmoja wa maana.

Page 8: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 8

ZOEZI

Neno lipi kati ya haya halijaundwa kutokana na mabadiliko ya harakati za kisiasa?

A Utandawazi

B Ugatuzi

C Ufisadi

D Udukuzi

Ni mazingira gani yamesababisha kuundwa kwa neno „nywila‟?

A Kisiasa

B Kiuchumi

C Kiutamaduni

D Kisayansi na teknolojia

___ni neno lililoundwa kutokana na mabadiliko ya kiutamaduni.

A Ukeketaji

B Ubeberu

C Ubepari

D Ujamaa

Mabadiliko ya kisayansi na kiteknolojia yamesababisha kuundwa kwa neno gani

kati ya haya?

A Ubepari

Page 9: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 9

B Ugatuzi

C Ufisadi

D Luninga

Neno „itifaki‟ limeundwa kutokana na mabadiliko ya___.

A Kisiasa

B Kiutamaduni

C Kiuchumi

D Kisayansi

Dhima ya Uambishaji na Mnyambulikoa wa Maneno

Dhima ya uambishaji ni kuleta upatanisho wa kisarufi, kuonesha idadi na umoja na

wingi katika ngeli za majina, kuonesha njeo na kuonesha urejeshi pamoja na hali

mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi kabla ya mzizi wa neno. Aidha dhima ya

mnyambuliko ni kuonesha matokeo ya tendo na kuzalisha kauli mbalimbali kwa

kupachika viambishi baada ya mzizi wa neno.

ZOEZI

Ipi kati ya hizi siyo dhima ya uambishaji wa maneno?

A Kuleta upatanisho wa kisarufi

B Kuonesha umoja na wingi katika ngeli

C Kuonesha njeo

D Kubadili kategoria ya neno

Kuonesha matokeo ya tendo na kuzalisha kauli mbalimbali ni mojawapo ya dhima

ya___.

Page 10: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 10

A Unominishaji

B Uambishaji

C Unyambulishi

D Uyakinishi

___ni neno lililohama kategoria baada ya unyambulishaji wa kitenzi „penda‟.

A Pendeza

B Pendo

C Pendaneni

D Pendezesha

Viambishi vilivyoongezwa baada ya mzizi {fagi-} katika kitenzi fagiliwa

vinaonesha dhima gani ya mnyambuliko?

A Kuonesha urejeshi

B Kuonesha idadi

C Kuzalisha kauli

D Kuonesha njeo

___ni dhima ya uambishaji inayooneshwa na kiambishi {-o-} katika kitenzi

„waliotutafuta‟.

A Kuonesha urejeshi

B Kuonesha umoja

Page 11: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 11

C Kuonesha idadi

D Kuonesha hali mbalimbali

Kuunda Maneno mbalimbali kwa kutumia Mnyambuliko

Uundaji wa maneno mbalimbali kwa kutumia mnyambuliko hufanyika kwa

kupachika viambishi baada ya mzizi wa neno na hivyo kulifanya neno husika

liweze kuonesha matokeo mbalimbali ya matendo pamoja na kuzalisha kauli

mbalimbali za matendo.

ZOEZI

Maneno ya mnyambuliko „zalika‟, „twalika‟ na „kalika‟ yameundwa kwa kutumia

kinyambulishi___.

A {-ek-}

B {-ik-}

C {-lik-}

D {-lek-}

Neno „piga‟ linaweza kunyumbuliwa na kuwa maneno yafuatayo, isipokuwa:

A Pigisha

B Anapiga

C Pigiwa

D Pigisha

___ni neno ambalo halijaundwa kwa kutumia kinyambulishi {-an-}.

A Tuhumiana

Page 12: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 12

B Oana

C Saidiana

D Shindana

Neno lipi kati ya haya linatokana na kiambishi cha mnyambuliko {-ek-}?

A Elekezwa

B Somesha

C Somea

D Someka

___siyo neno la mnyumbuliko wa neno „fumba‟.

A Fumbata

B Fumbiana

C Fumbia

D Wamefumba

Kutumia Maneno ya Mnyambuliko katika Miktadha mablimbali

Maneno ya mnyambuliko hutumika katika miktadha mbalimbali ambapo miktadha

hiyo hujitokeza katika kauli mbalimbali za vitenzi. Kauli hizo ni kauli ya kutenda,

kauli ya kutendwa, kauli ya kutendewa, kauli ya kutendea, kauli ya kutendeka,

kauli ya kutendesha, kauli ya kutendana, na kauli ya kutendama.

ZOEZI

Yafuatayo ni maneno ambayo hutumika katika muktadha unaorejelewa na kauli ya

kutendewa, isipokuwa:

Page 13: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 13

A Zolewa

B Limiwa

C Imbika

D Somewa

Kitenzi „yatazoleka‟ hutumiwa katika muktadha wa kauli ya ___.

A Kutendewa

B Kutendea

C Kutendeka

D Kutendwa

Ni viambishi gani kati ya hivi ni vya muktadha wa kauli ya kutendwa?

A {-ian-} na {-an-}

B {-w-}, {-liw-} na {-lew-}

C {-e-}, {-li-} na {-le-}

D {-ik-}, {-ek-}, {-lik-} na {-lek-}

Ni muktadha gani ambao tendo hufanywa kwa niaba au faida ya mtu mwingine?

A Muktadha wa kutendesha

B Muktadha wa kutendea

C Muktadha wa kutendana

D Muktadha wa kutendeka

Neno „tungama‟ hutumika katika muktadha wa___.

Page 14: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 14

A Kufungamanisha

B Kutendewa

C Kutendwa

D Kutendana

MADA YA 2 MATUMIZI YA LUGHA KATIKA MIKTADHA

MBALIMBALI

Matumizi ya lugha ni namna ambavyo wazungumzaji wa lugha hutumia lugha kwa

kuzingatia mila, desturi na kaida mbalimbali za jamii inayohusika.

Rejesta

Kwa ujumla tunaweza kufasili rejesta kama mtindo wa lugha kutegemeana na kazi

fulani, muktadha wa matumizi, lengo na uhusiano wa wanaowasiliana. Katika

muktadha rasmi rejesta hurejelea upande mmoja kama vile, msamiati wa kiufundi,

adabu maalum na matumizi ya lugha fasaha, mfano katika elimu, mahakamani na

kadhalika.

Kuwasiliana kwa kutumia Rejesta

Rejesta za Mitaani

Haya ni mazungumzo yanayozungumzwa magengeni nayo hueleweka na

wazungumzaji wenyewe. Ni lugha ambayo huchipuka kutokana na kikundi cha

watu ambacho ni kidogo. Mfano wa maneno yanayotumika sana mitaani ni kama

vile “Mshikaji” (rafiki) Demu” (mwanamke)n.k. Kwa ujumla lugha ya mitaani ni

lugha isiyo sanifu, ni lugha iliyojaa maneno ya mitaani ambayo yanaeleweka kwa

wazungumzaji wenyewe.

Mazungumzo ya Kwenye Shughuli Maalum (Rejesta za Mahali)

Mazungumzo ya kwenye shughuli maalumu hayafanywi kiholela, bali yanafuata

taratibu na kanuni maalum zinazojitokeza katika mazingira haya. Kutokana na

kutumiwa kwake kwa muda mrefu kwenye mazingira yale yale.

Page 15: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 15

Mazungumzo ya kwenye shughuli maalumu ni kama vile mazungumzo ya:

Maofisini au mahali popote pa kazi

Mahakamani

Hotelini

Hospitalini

Msikitini

Kanisani n.k

Mazungumzo ya mahotelini yana utaratibu wake ambao katika hali ya kawaida

inaweza isieleweke.

Nani wali kuku?

B: Mimi

Chai moja wapi?

B: Hapa

Katika mazungumzo haya A anapouliza “Nani wali kuku”, ana maana kuwa nani

anahitaji kula wali na nyama ya kuku”. Hapa hana maana ya kumwainisha mtu

aitwaaye “wali kuku”.

Kwa upande wa lugha ya mahakamani ni tofauti na lugha ya hotelini. Lugha ya

mahakamani inasisitiza usahihi ili kuondoa migongano miongoni mwa

wanaohusika.

Mfano:

Wakili wa Utetezi: Nakuuliza jaribio la kutaka kupindua serikali litakuwa kosa la

namna gani katika sheria za Tanzania?

Kamishna Msaidizi: (Baada ya kupewa kitabu cha sheria za Tanzania na

kukisoma) Ni kosa la uhaini.

Page 16: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 16

Wakili wa Utetezi: Ulichukua muda mrefu kufikia jibu hili. Washitakiwa wawili

hawahusiani na makosa haya?

Kamishna Msaidizi: Sijui.

Kimsingi hii ni hali ya kawaida kabisa katika mahojiano ya mahakamani. Mara

nyingi mahojiano katika mahakama hayaendi haraka sana. Kila mtu anayehusika –

hakimu, mwendesha mashtaka, wakili, mdaiwa, shahidi, n.k. hujieleza kwa wazi

wazi bila kujali urefu wa maelezo.

Rejesta Zinazohusu Watu

Rejesta zinazohusu watu ni yale mawasiliano yasiyo rasmi, ni yale maongezi ya

kawaida ya kila siku au mazungumzo rasmi; kwa mfano mazungumzo kati ya:

Vijana wenye rika moja,

Wazee wenyewe,

Wanawake wenyewe,

Wanaume wenyewe,

Mwalimu na mwanafunzi,

Meneja na wafanyakazi wake,

Mtu na mpenzi wake, n.k.

Mazungumzo miongoni mwa marafiki wa rika moja huzungumza lugha ambayo

wao wenyewe wanaielewa na sio rahisi kwa mtu wa rika lingine kuielewa lugha

hiyo.

Mfano:

'Basi, Master jana wikiendi ilikuwa kibaridi sana. Basi nilizamia infoo kwenye

zinga la mnuso huko saiti za upanga. Nilifika getini nikakuta baunsa kanyuti

chedro likisubiri kumtoa noma kila mzamiaji. Alikuwa mnoko kishenzi. Akatema

mkwara mbuzi, nikajibu kwa mkwaradume....akabloo mimi ndani‟.

Maana ya Maneno

Page 17: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 17

Wikiendi – Mwisho wa wiki

Kibaridi –tulivu

Kuzamia infoo – Kuingia mahali bila kualikwa

Zinga la Mnuso –sherehe kubwa

Saiti –sehemu

Baunsa limenyuti chedro – Ni mlinzi wa mlangoni ametulia pembeni

Noma – Hatari

Mnoko kishenzi – kinaa sana

Mkwara mbuzi – Vitisho dhaifu (Sani, Toleo Na 49).

Mtu asomapo maelezo hayo, mara moja unaona jinsi vijana hawa wa rika moja

waishio mjini wanavyozungumza Kiswahili. Si rahisi kwa mzungumzaji wa

Kiswahili sanifu kuielewa kirahisi lugha hiyo.

ZOEZI

„Chai moja wapi?‟ hii ni rejesta inayotumika katika muktadha gani?

A Hotelini

B Dukani

C Hospitalini

D Darasani

___tofauti husababisha kuwepo kwa aina mbalimbali za rejesta.

A Watu

B Lugha

Page 18: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 18

C Wahusika

D Miktadha

„Je mshtakiwa una utetezi wowote?‟ rejesta hii hutumika wapi?

A Mahakamani

B Kanisani

C Msikitini

D Shuleni

Mazungumzo kati ya mwalimu na mwanafunzi ni aina gani ya rejesta?

A Lugha ya kitarafa

B Rejesta za mitaani

C Rejesta zinazohusu watu

D Rejesta za mahali

___ni rejesta ambazo hudumu kwa muda mfupi tu na baadae hufifia.

A Lugha za kitarafa

B Rejesta za mitaani

C Rejesta za mahali

D Rejesta zinazohusu watu

Dhima za Rejesta

Katika kipengele cha utambulisho wa kijamii tunaangalia namna aina ya lugha ya

mazungumzo inavyoweza kujidhihirisha miongoni mwa watumiaji wake au

Page 19: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 19

kuwatambulisha na kuwatofautisha wanajamii husika. Pia katika utambaulisho wa

kijamii tunaangalia vile ambavyo mtu hutambulika katika jamii kulingana na

namna anavyoongea kulingana na hadhi, tabaka, na jinsi ambavyo mtu huyo

anavyoweza kusababisha mshikamano au mwachano katika mazungumzo. Kwa

mfano jamii itamtambua mwanajamii kuwa ni msomi kulingana na mtindo wa

lugha ya mazungumzo anaoutumia, au ni mtu wa mtaani kulingana na lugha

anayotumia.

Rejesta, ina nafasi kubwa sana katika maendeleo ya kiuchumi kwa mtu binafsi na

taifa kwa ujumla. Hii ni kutokana na kwamba, madhumuni makuu ya mawasiliano

katika biashara ni kuwavutia wateja na kuwafanya kuamini kuwa bidhaa ama

huduma wanazouziwa ni za kiwango cha juu na ni thamani bora kwa pesa zao.

Hivyo lugha ya biashara (rejesta), kwa kawaida ni lugha ya kutangaza uzuri wa

bidhaa au huduma, huwa na sentensi au vifungu vifupi, mfano “Okoa mapesa

chungu mbovu” pia huwa na lugha ya kupumbaza na kuaminisha, mfano “Kunywa

XYZ kufumba na kufumbua afya yako itakurudia”.

Pia rejesta inasaidia sana kurahisisha mawasiliano miongoni mwa wazungumzaji

katika masuala mbalimbali ya kibiashara na hata katika huduma mbalimbali za

kijamii. Mfano hospitalini “mbili mara tatu”, hotelini “kuku wali tafadhali”, sokoni

“kata nusu” na maeneo mengine.

Baadhi ya rejesta hutumika kupunguza idadi ya maneno hivyo kufanya

mazungumzo yawe mafupi na yanayoeleweka kwa urahisi mfano rejesta za

hotelini kama vile:- Muuzaji: wapi ng‟ombe? Mteja: hapa Muuzaji: wapi chai

chapati? Mteja: hapa.

Pia katika kutolea elimu ya dini kanisani na msikitini rejesta ina nafasi kubwa

katika kujenga maadili.

Vilevile rejesta ina nafasi ya kupamba mazungumzo, wazungumzaji wengi

wanapozungumza hapa na pale hupenda kutumia maneno tofautitofauti ili kufanya

mazungumzo yawe ya kuvutia. Mfano mazungumzo miongoni mwa vijana:

Kijana 1: Niaje? Nakuona umechili

Kijana 2: mzuka jembe. Kama kawa… kama dawa!

Page 20: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 20

Misimu

Kuwasiliana kwa Kutumia Misimu

Misimu ni semi za muda na mahali maalum ambazo huzuka na kutoweka

kutegemea mazingira maalum. misimu inayodumu huweza kuingia katika methali,

nahau au misemo ya lugha ya jamii hiyo.

Chanzo cha misimu

Misimu huzuka kulingana na mabadiliko ya kihistoria yanayoikumba jamii

husika katika nyakati mbalimbali.

Misimu huzuka kutokana na haja ya watu kuelezea hisia zoa juu ya matukio

mbalimbali yaliyotokea katika vipindi fulani kwa mfano, njaa, mafuriko,

vita n.k.

Aina za misimu

1. Misimu ya pekee. Hii ni misimu ambayo huelezea mahusiano ya kikundi

kimoja kutoka katika utamaduni mmoja, na hujulikana miongoni mwao

pekee.

2. Misimu ya kitarafa. Misimu hii hujulikana na watu wengi katikia eneo

kubwa, yaweza kuwa ni kata, wilaya au tarafa.

3. Misimu zagao. Ni misimu iliyoenea nchi nzima au pengine kuvuka mipaka

ya nchi, misimu hii husikika redioni, magazetini na hata kwenye vitabu.

Msimu uliokita mizizi sana huweza kusanifishwa na kuwa msamiati rasmi.

Sifa za misimu

Huzuka na kutoweka kufuatana na mabadiliko ya jamii

Ni lugha isiyo sanifu

Ina chuki

Ni lugha ya mafumbo

Ina maana nyingi

Page 21: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 21

Dhima ya misimu

Hutumika kupamba lugha

Hutumika kukuza lugha

Hutumika kutunza historia ya jamii fulani

Hutumika kuibua hisia mbalimbali za wazungumzaji

Hufurahisha na kuchekesha

ZOEZI

___za wazungumzaji huakisiwa na misimu.

A Matukio

B Maisha

C Lugha

D Hisia

___ni maneno yasiyo rasmi ambayo huzuka katika kipindi fulani na kupotea.

A Lahaja

B Istilahi

C Rejesta

D Misimu

Miktadha ya misimu ni___.

A Mazingira rasmi

B Mazingira yasiyokuwa rasmi

C Mazingira ya shughuli maalumu

Page 22: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 22

D Mazingira rasmi

Ni aina gani ya misimu ambayo huenea nchi nzima na hata kuvuka mipaka ya

nchi?

A Rejesta

B Misimu ya kitarafa

C Misimu za gao

D Misimu ya pekee

Lipi kati ya haya si mojawapo ya maeneo finyu ambayo hutumia misimu?

A Kijiji

B Tarafa

C Mtaa

D Darasani

Lugha ya Mazungumzo na ya Maandishi

Sifa ya Lugha ya Kimazungumzo

Lugha ya mazugumzo ni maongezi ya watu wawili au zaidi bila kutumia

maandishi. Lugha ya mazungumzo ambayo ndiyo lugha kongwe zaidi ya lugha ya

maandishi ina dhima kubwa ya kufanikisha mawasiliano miongoni mwa watu au

kikundi fulani. Lugha hii ya mazungumzo ilianza punde tu binadamu alipoanza

kukabiliana na mazingira yake, hivyo kimsingi lugha ya mazungumzo ndiyo nguzo

kuu ya kufanikisha shughuli zote za kibinadamu kutokana na nafasi yake

kimatumizi.

Faida ya lugha ya mazungumzo

Mzungumzaji anaweza kukaa ana kwa ana na msikilizaji, hivyo hukuza

uhusiano.

Page 23: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 23

Mzungumzaji anaweza kutumia ishara za mwili katika kusisitiza maelezo

yake.

Mzungumzaji anaweza kupata nafasi ya kuuliza au kuulizwa maswali.

Mzungumzaji anaweza kuonesha hisia zake kwa kulia, kupaza sauti,

kupunguza sauti, kuonyesha furaha huzuni au hasira.

Mzungumzaji anaweza kuuliza maswali, kuona hisia za mzungumzaji kwa

kusikiliza lugha zinazotolewa na kuangalia ishara za mwili zinazotumika.

Mzungumzaji anaweza kupata nafasi ya kufuta usemi wake, kuongezea

jambo au kutoa maelezo ya ziada.

Mzungumzaji anaweza kubadilisha lugha yake kulingana na mazingira

aliyomo.

Mzungumzaji anao uhuru wa kutumia lugha ya mitaani, misimu kulingana

na muktadha.

Matatizo ya lugha ya mazungumzo

Maelezo lazima yahifadhiwe kichwani, hivyo kama mtu hana kumbukumbu,

taarifa zilizotolewa hupotea na kusahaulika.

Mtumiaji wa lugha ya mazungumzo anaweza kurudiarudia vipengele fulani

na hivyo kuichosha hadhira.

Ujumbe unaweza usieleweka kama unatolewa kwenye kelele nyingi

Lugha ya maandishi

Hii ni lugha inayowasilishwa kwa njia ya maandishi. Lugha ya maandishi

huzihusiha pande mbili, mwandishi na msomaji. Lugha ya maandishi sharti iwe

fasaha ili msomaji anaposoma maandishi hayo, apate kuelewa kila kitu, yaani

asibaki akijiuliza maswali.

Lugha ya maandishi huambatana na alama za uakifishaaji, hii husaidia maandishi

kusomeka vizuri na kueleweka kwa urahisi

Page 24: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 24

Ubora wa lugha ya maandishi

Lugha ya maandishi huwawezesha watu walio mbali kuwasiliana.

Lugha ya maandishi hustawisha sarufi ya lugha na misingi yake, kwa sababu

mwandishi anahakikisha kwamba anazingatia vizuri kanuni za kisarufi ili

msomaji wake aweze kumwelewa.

Ili kuhakikisha maelezo yake yanaeleweka mwandishi analazimika kuandika

kwa uwazi na kwa kuzingatia kanuni na miiko yote ya uandishi.

Udhaifu wa lugha ya maandishi

Lugha hii hutumiwa na wale tu wanaojua kusoma na kuandika.

Lugha ya maandishi haina msisimko uletwao na lafudhi na matamshi.

Msomaji hukosa vidokezo vingi ambavyo katika lugha ya mazungumzo

huchangia katika mawasiliano.

Lugha ya maandshi inamnyima mwandishi nafasi ya kupima welewa wa

msomaji kwa kuwa hamwoni.

Dhima ya lugha ya mazungumzo na lugha ya maandishi

Lugha ya mazungumzo na lugha ya maandshi zote zina umuhimu wa pekee katika

maisha ya kila siku kwa sababu ndizo zinzaowezesha watu kuwasiliana kwa namna

mbalimbali.

Umuhimu wa lugha ya maandshi pia hutokana na dhima yake kwa watu.

Maandishi yanaweza kuhifadhiwa na kusambazwa kwa watu wengi hata walio

mbali. Maandishi yanahifadhi kumbukumbu na kwa muda mrefu. Kwa hali hii,

watu wa vizazi vingine wanaweza kusoma na kujua mambo yaliyofanyika karne

nyingi zilizopita.

Tofauti kati ya lugha ya mazungumzo na lugha ya maandishi

1. Lugha ya mazungumzo huwezesha mawasiliano ya ana kwa ana lakini lugha

ya maandishi haiwezeshi mawasiliano ya ana kwa ana.

Page 25: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 25

2. Lugha ya mazungumzo haihitaji maandalizi wakati lugha ya maandishi

huhitaji maandalizi. Mwandishi atalazimika kupata muda wa kuandika

pamoja na kuandaa vifaa kama vile kalamu, karatasi n.k

3. Lugha ya mazungumzo hailazimiki kuzingatia kanuni za kisarufi, lakini

lugha ya maandshi hutakiwa kuzingatia kanuni za kisarufi.

Tofauti nyingine kati ya lugha ya maandishi na lugha ya mazungumzo huweza

kuonyeshwa katika jedwali lifuatalo.

Kipengele Mazungumzo Maandishi

Muktadha

1. Wahusika

huonana

2. Viungo vya mwili

hutumika

3. Maandalizi na

matumizi

hufanyika wakati

mmoja

1. Wahusika

hawaonani

2. Viungo vya

mwili havitumiki

3. Maandalizi

hufanyika kabla

ya matumizi

Mada Hazina uzito mkubwa Huelekea kuwa na uzito

mkubwa.

Mpangilio

wa mada na

mawazo

Hautabiriki. Unaelekea

kutokuwa na mtiririko.

Hutabirika. Huelekea

kuwa na mtiririko.

Mjadala wa

mada

Hauelekei kuwa na kina.

Hazichujwi kwa

uaangalifu.

Unaelekea kuwa na

kina. Huchujwa.

Page 26: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 26

Dhima ya matumizi ya lugha

Dhima kuu ya lugha ni kupashana habari, ujuzi na maarifa mbalimbali. Vilevile

lugha husaidia kujenga uhusiano mwema baina ya watu. Uhusiano huo unaweza

kuwa wa kijamii, kielimu, kibiashara, kihuduma, kisiasa, kiuchumi n.k. Kwa hiyo,

kujua jinsi ya kuitumia lugha kama inavyotakiwa, kunasaidia kufikisha vizuri

ujumbe unaotakiwa bila kuupotosha. Vilevile kunasaidia kuepuka migongano, hasa

ya kijamii kwa kuwa utakuwa umetumia lugha kwa mujibu wa mila na desturi za

jamii inayohusika.

Mambo ya kuzingatia katika matumizi ya lugha

1. Mada inayozungumziwa:Mada za mazungumzo zipo nyingi. Kuna mada za

kijamii, kwa mafano ndoa, unyago, mapenzi, kifo, matanga, burudani,

muziki n.k. Kuna mada za kibiashara kwa mfano bidhaa, kodi, vibali, fedha,

hasara, faida n.k. Kwa hiyo, ili mazungumzo yaweze kwenda vizuri,

wazungumzaji wanatakiwa kuzingatia mada husika.

2. Muktadha wa mazungumzo:Mazungumzo yanaweza kuathiriwa na

miktadha tofauti. Kwa mfano kuna miktadha ya kidini, kiganga, huzuni,

sherehe, kisiasa, kielimu, kibiashara n.k. Mazungumzo yanaweza kufanyika

mjini, kijijini, ugenini, shuleni, dukani, hotelini n.k

3. Malengo ya mazungumzo hayo:Malengo ya mazungumzo nayo yanaathiri

matumizi ya lugha. Kwa mfano, lengo linaweza kutoa taarifa, kuhoji,

kukejeli, kutia moyo n.k. Sasa jinsi lugha itakavyotumika katika kutoa

taarifa ni tofauti na itakavyotumika katika kutia moyo au kukejeli.

4. Uhusiano uliopo baina ya wazungumzaji:Matumizi ya lugha huweza

kuathiriwa pia na mahusiano ya wazungumzaji. Kuna mazungumzo baina ya

watoto, wanafunzi, wazee, viongozi, marafiki n.k. Upo uhusiano wa daktari

na mgonjwa, mwalimu na mwanafunzi, mnunuzi na muuzaji. Kwa hiyo

mazingira baina ya pande hizi mbili yatategemea uhusiano wao, kwa hiyo

kaida za uhusiano huu utapaswa kuzingatiwa. Kwa hiyo, kwa kuzingatia

mambo haya manne, itawafanya wazungumzaji wawe makini katika uteuzi

wa maneno, miundo, mifano na kina cha ufafanuzi wa maelezo au habari

inayozungumzwa.

Page 27: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 27

ZOEZI

Zifuatazo ni taratibu za uandishi ambazo huambatana na lugha ya kimaandishi,

isipokuwa:

A Matumizi ya lafudhi

B Matumizi ya vituo

C Matumizi ya herufi kubwa

D Matumizi ya aya

Mtu anapoonesha umahiri wa lugha katika mazungumzo ina maana kuwa lugha ya

kimazungumzo ina sifa ya___

A Mabadiliko

B Uhai

C Uhuru

D Maandalizi ya awali

Lugha ya mazungumzo ina sifa ya kutokuwa na gharama, hii ni kwa sababu___

A Haina maandalizi

B Ni hai

C Inahitaji kuwa na ala za sauti tu

D Inahitaji kalamu na karatasi

Sifa gani ya lugha ya kimazungumzo hudhihirika pale mzungumzaji anapoonesha

hali ya hisia zake?

A Utajiri wa wahusika

B Uhusiano na hadhira

C Sifa ya mabadiliko

Page 28: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 28

D Uhai

Lugha ya mazungumzo inapowakutanisha ana kwa ana msikilizaji na mzungumzaji

inadhihirisha sifa ya___

A Uhai

B Uhusiano kati ya hadhira

C Utajiri wa wahusika

D Uhuru

Dhima ya Lugha ya Kimazungumzo na ya Kimaandishi

Lugha ya kimazungumzo na ya kimaandishi zina dhima kuu ya kupasha habari,

ujuzi, na maarifa mbalimbali, husaidia kujenga uhusiano mwema baina ya watu,

kufikisha ujumbe unaotakiwa vizuri bila kupotosha, kufundishia ujuzi, kuchochea

maendeleo, kuhifadhi historia ya jamii na kueleza mawazo au hisia za watu.

ZOEZI

Lugha ya kimazungumzo inapotumika kutofautisha jamii moja na nyingine huwa

na dhima ya ___.

A Kutolea maarifa

B Utambulisho

C Kuchochea maendeleo

D Kujenga umoja

Lugha ya kimazungumzo inapowaleta watu karibu huwa na dhima ya___.

A Kujenga umoja

B Kueneza umoja

C Kuvunja umoja

D Kutetea umoja

Page 29: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 29

___ni dhima inayotofautisha lugha ya kimazungumzo na ya kimaandishi.

A Kupasha habari

B Kuhifadhi kumbukumbu

C Kufikisha ujumbe mahususi

D Kuchochea maendeleo

Lugha ya kimazungumzo na kimaandishi zina dhima moja kuu ambayo ni___

A Kuwasiliana

B Kuchochea maendeleo

C Kuunganisha watu

D Kuhifadhi taarifa

Ipi ni dhima kuu ya lugha ya kimazungumzo?

A Kupasha habari na maarifa

B Kujenga uhusiano katika jamii

C Kuchochea maendeleo

D Kuhifadhi kumbukumbu

Lugha ya Kimazungumzo na ya Kimaandishi katika Miktadha Sahihi

Matumizi ya lugha ya kimazungumzo na ya kimaandishi katika muktadha sahihi

huongozwa na mambo yafuatayo, ambayo ni mada inayozungumzwa, muktadha au

mahali mazungumzo hayo yanapofanyika, malengo ya mazungumzo hayo na

uhusiano uliopo kati ya wazungumzaji.

ZOEZI

___ ni kipengele cha muhimu ambapo uteuzi wa maneno unazingatia ni nani

anahusika katika mazungumzo.

Page 30: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 30

A Uhusiano baina ya wahusika

B Mazingira

C Mada

D Malengo ya mazungumzo

Miongoni mwa vitu vya kuzingatia katika lugha ya kimazungumzo ni mada. Ipi

kati ya hizi ni mada ya kijamii?

A Bidhaa

B Unyago

C Fasihi

D Uhandisi

Ni muktadha gani ambao uhusisha matumizi ya risala katika lugha ya

mazungumzo?

A Kidini

B Baa

C Dukani

D Msibani

Yafuatayo ni mambo yanayotawala lugha ya kimazungumzo na kimaandishi,

isipokuwa:

A Mada

B Istilahi

C Uhusiano baina ya wahusika

D Muktadha

Page 31: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 31

Kipi kati ya hivi ni cha kuzingatia wakati wa matumizi ya lugha ya mazungumzo

katika mikatdha mbalimbali?

A Mawazo ya mwandishi

B Alama za uandishi

C Herufi

D Matamshi

Matamshi na Lafudhi ya Kiswahili

Matamshi ni namna ambavyo mtu anatamka neno au jinsi mtu anavyozungumza

lugha. Unaposema fulani ana matamshi mazuri ya Kiswahili utakuwa unamaanisha

anazungumza Kiswahili fasaha.

Neno moja linaweza kuzungumzwa/kutamkwa kwa namna tofauti na watu

mbalimbali kutokana na sababu mbali mbali, sababu hizo ni pamoja na eneo la

kijiografia anakotoka huyo mtu, kabila lake, kundi lake la kijamii mfano msanii au

mwanasiasa, na elimu aliyonayo. Hizi zote zinaweza zikawa ni sababu za kufanya

watu watofautiane katika matamshi.

Lafudhi Mbalimbali za Kiswahili

Dhana ya matamshi huhusisha

Sauti za lugha husika

Mkazo

Kiimbo

Sauti za lugha ya Kiswahili

Sauti za lugha ya Kiswahili hujumuisha irabu na konsonanti, ambazo kwa ujumla

huunda sauti 24, irabu tano na konsonanti 19 (konsonanti x na q hazipo katika

matamshi ya kiswahili). Sauti za Kiswahili hutamkwa kama zilivyoandikwa, kwa

mfano maneno “data” au “dengue” wewe unayatamkaje? Wengi huyatamka kama

Page 32: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 32

yalivyo hata kama wakiwa wanazungumza kiingereza, hii ni kwa sababu maneno

ya Kiswahili hutamkwa kama yalivyoandikwa.

Kwa hiyo unapotamka maneno ya Kiswahili ni sharti uzingatie sauti asilia za lugha

ya Kiswahili. Kuna watu huwa wanaandika hivi “xaxa”, hii huwa unaitamkaje? Au

“ucjal” huwa unaitamkaje? Kwa kufuata matamshi asilia ya Kiswahili “ucjal”

itatamkwa “uchijal” sijui itakuwa ina maana gani sasa. Na pengine umekuwa

ukitumia maandishi ya namna hii hata kwenye insha zako ukidhani upo sahihi au

ni kwa mazoea tu, sasa kwa kuwa umejua matamshi sahihi ya Kiswahili ni yapi,

utajifunza kuyatumia kwa usahihi katika maandishi rasmi na yasiyo rasmi.

Mkazo

Katika lugha ya Kiswahili kuna namna ya kutamka maneno ili kuleta maana mbali

mbali, kwa mfano neno “barabara” litaleta maana husika kulingana na jinsi

lilivyotamkwa. Hivyo, mkazo ni pale silabi inapotamkwa kwa kukazwa. Maneno

ya Kiswahili huwa na silabi moja ambayo hutamkwa kwa nguvu zaidi kuliko silabi

nyingine. Unapotamka silabi iliyotiwa mkazo, sauti hupandishwa juu kiasi.

Maneno mengi ya Kiswahili, hasa yale yenye asili ya Kibantu hutia mkazo katika

silabi ya pili kutoka mwisho.

Kwa mfano:ba’bu, maya’i, rama’ni (mimi nilikuwa nikitamka ra’mani), baraba'ra

(njia).

Baadhi ya maneno yenye asili ya kigeni, huwa na mkazo katika silabi nyingine.

Kwa mfano: bara'bara (sawa sawa), Alha’misi

Kiimbo

Ni utaratibu maalum wa upandaji na ushukaji wa mawimbi ya sauti unaojitokeza

katika utamkaji wa lugha fulani.

Katika utaratibu wa utamkaji, dhana ya Kiimbo huandamana pia na dhanna

ya kidatu ( yaani , kiwango cha juu, cha chini au cha kati cha sauti katika usemaj),

Kwa hivyo ni muhimu hapa kueleza tofauti zilizopo baina ya kiimbo na kidatu.

Wakati kiimbo kina maana ya kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti ya

Page 33: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 33

lugha, kidatu kina maana ya kiwango cha sauti isikikayo, wakati wa utamkaji ama

kuwa juu, kuwa katikati au kuwa chini.

Aina za viimbo

Kiimbo cha maelezo: Kiimbo cha maelezo ni kile ambacho kwa kawaida

msemaji wa lugha akiwa kwenye kidatu chochote kile mawimbi sauti ya

usemaji wake yanakuwa takriban katika mstari ulionyooka. Mfano,

Mwalimu anafundisha.

Kiimbo cha maulizo: Kiimbo cha kuuliza hujitokeza kwa kutumia viwango

tofauti vya kidatu kutegemeana na aina ya swali linaloulizwa. Mfano,

mwalimu anafundisha?

Kiimbo cha amri: kiimbo cha amri hakitofautiyani sana na kiimbo cha

maulizo. Kiimbo cha amri, mzungumzaji hutumia kidatu cha juu zaidi

kuliko ilivyo katika kiimbo cha maelezo. Mfano, njoo hapa!

Lafudhi ya Kiswahili

Lafudhi ni matamshi ya msemaji wa lugha fulani ambayo yanatokana na athari za

kimazingira. Mazingira hayo yanaweza kuwa eneo atokalo mtu, mahali

alikosomea, kiwango chake cha elimu, tabaka lake la kijamii na kadhalika.

Lugha ya Kiswahili ni lugha ya pili kwa watumiaji wengi wa afrika mashariki, kwa

hiyo hii inafanya kuwatambua wazungumzaji wa Kiswahili kulingana na makabila

yao au maeneo wanakotoka. Kwa mfano, kwa hapa Tanzania tunaweza

kuwatambua watu wa mwanza kwa lafudhi yao, watu wa mtwara kwa lafudhi yao,

watu wa pemba kwa lafudhi yao au watu wa Musoma kwa lafudhi yao.

Mifano

1. Usiniretee maswara ya ubaguzi wa kikabira hapa (Wakuria)

2. Amemupiga mutoto ya watu juu amemuibia mfaranga makumi mawili

(Wakongo)

3. Ukikaa nchale, ukichimama nchale (Wamakonde)

4. Wewe unakamuaga mang‟ombe tu moja kwa moja (Wasukuma)

Page 34: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 34

5. Mbona unakuwa kinganganizi, nilishakwambia sikupendi lakini wewe bado

unaningangania tu! (Wahaya)

ZOEZI

Neno lipi kati ya haya linaonesha lafudhi ya mzungumzaji wa Kiswahili kutoka

jamii ya Wapare?

A Thatha

B Thelathini

C Sasa

D N'toto

„Hifi ni fiatu fyangu‟ hii ni lafudhi ya watu wa jamii gani?

A Wanyakyusa

B Wayao

C Wamakua

D Wapare

___ ni tungo ya Kiswahili yenye lafudhi ya Kimakonde.

A N‟toto amekuja.

B Juma amemupiga mutoto.

C Riereze riondoke.

D We mitu kabila gani?

Ipi kati ya hizi ni tungo ya Kiswahili yenye lafudhi ya kihaya?

A Riambie riende.

B E bhatoto hamuyambo.

C Toa ukyafu hapa.

Page 35: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 35

D Wewe mbona kinganganizi.

___ni tofauti ya matamshi ya wasemaji wa lugha ambayo husababishwa na athari

ya mazingira.

A Mkazo

B Mtindo wa lugha

C Lafudhi

D Utata

Utata katika Mawasiliano

Utata ni hali ya neno au sentensi kuwa na maana zaidi ya moja. Kwa hiyo tungo

tata ni tungo ambayo inaweza kuwa na maana zaidi ya moja.

Sababu za Utata

Utata katika tungo hutokea kwa sababu zifuatazo:

1. Neno kuwa na maana zaidi ya moja, kwa mfano neno mbuzi, kata n.k.

2. Kutozingatia taratibu za uandishi, Mfano; Tulimkuta Nyammy na rafiki yake,

Mazala vs Tulimkuta Nyammy na rafiki yake Mazala. Katika sentensi hizi

alama (,) ndio huleta tofauti, sentensi ya kwanza inamaana kulikuwa na watu

wawili Nyammy na rafiki yake aitwaye Mazala na sentensi ya pili isiyo na

alama (,) inamaanisha kulikuwa na watu wawili Nyammy na mtu mwingine

ambaye ni rafiki yake Mazala

3. Kutumia maneno bila kuzingatia muktadha wa matumizi ya maneno hayo.

4. Utamkaji wa maneno. Wakati mwingine utata unaweza kujitokeza katika

matamshi tu, ili hali katika maandishi utata hauonekani. Kwa mfano;

Mimina wewe, katika maandishi linaweza kuandikwa mimi na wewe, na

hivyo kuondoa utata.

5. Mjengo wa maneno. Utata huu huzuka katika vitenzi kama pigia. Chanzo

cha utata katika kitenzi hiki ni kiambishi –i-. Kiambishi hiki kinaweza

Page 36: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 36

kumaanisha: kwa ajili ya…, kwa sababu ya.., kwa kutumia chombo fulani..,

au mahali fulani.

Mfano:

Alimpigia ukorofi wake (kwa sababu ya)

Alimpigia kiatu (kifaa)

Alimpigia ndani (mahali)

Mifano ya utata katika tungo

1. Patience amemwandikia Lilian barua:Sentensi hii huweza kuwa na maana

kuwa Patience ameandika barua kwenda kwa Lilian au Patience ameandika

barua kwa niaba ya Lilian

2. Umefanikiwa kununua mbuzi?Sentensi hii huweza kumaanisha ununuzi

wa mbuzi mnyama au mbuzi kifaa cha kukunia nazi.

3. Alimkuta amelala kwenye nyumba ya wageni:Sentensi hii huweza

kumaanisha, nyumba ya mtu lakini inatumika kwa ajili ya wageni kwa

malipo au ni nyumba inayomilikiwa na watu ambao ni wageni katika eneo

lile.

4. Attu ametumwa na Aritamba:Sentensi hii inaweza kueleweka

kumaanisha, Aritamba amemtuma Attu au Attu na Aritamba wametumwa

wote kwa pamoja.

ZOEZI

Zifuatazo ni sababu za utata, isipokuwa:

A Kutumia maneno ya picha

B Umahiri wa lugha

C Neno kuwa na maana zaidi ya moja

D kutumia maneno bila kuzingatia muktadha husika

Page 37: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 37

Neno „mbuzi‟ ni tata, kwa sababu___

A Ni neno la Kiswahili

B Lina maana iliyofichika

C Lina maana moja tu

D Lina maana zaidi ya moja

Mojawapo ya sababu za utata ni mjengo wa maneno. Ni aina gani ya maneno

ambayo mjengo wake huleta utata?

A Vitenzi

B Viwakilishi

C Viunganishi

D Vihisishi

Tungo ipi inaonesha sababu ya utata ya kutozingatia mukutadha wa matumizi ya

meneno?

A Mwajuma ametumwa na Rama.

B Ana uma.

C Anampigia ujeuri wake.

D Juma anabuni.

Utata unaojitokeza katika maneno husababishwa na neno kuwa na___.

A Maana zaidi ya moja

B Maana mbili tu

C Maana zaidi ya mbili

D Maana moja tu

Page 38: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 38

MADA YA 3 : UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI

Fasihi simulizi kama zilivyo kazi nyingine za fasihi andishi hufanyiwa uhakiki.

Uhakiki huu huzingatia vipengele vya fani na maudhui ili kubainisha usanaa wa

kazi husika pamoja na kile ilichokusudia kufikishwa kwa hadhira.

Uhakiki wa Ushairi

Mashairi kama kazi nyingine za kifasihi huhakikiwa kwa kutumia vigezo sawa na

vinavyotumika katika kazi nyingine za kifasihi. Vigezo hivyo ni kwa kuzingatia

vipengele vyake viwili yaani fani na maudhui.

Vipengele vya Fani na Maudhui katika Kuhakiki Ushairi

Vipengele vya fani

Uhakiki wa fani za ushairi ni uchambuzi wa kina na kuziweka wazi mbinu za

kisanaa alizotumia mshairi katika kutunga kazi yake. Vipengele muhimu vya

kuhakiki katika fani ya ushairi ni kama vifuatavyo:

Mtindo

Jambo la kuonyesha hapa ni kwamba iwapo shairi ni la kimapokeo ama ni la

kisasa.

Muundo

Katika kuhakiki muundo wa shairi mhakiki inatakiwa aweke wazi mambo

yafutayo:

1. Idadi ya beti

2. Idadi ya mistari na aina ya vibwagizo

3. Idadi ya vipande

4. Idadi ya mizani

5. Aina na mpangilio wa vina

Page 39: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 39

Wahusika

Ikiwa shairi limehusisha wahusika ni vema pia mhakiki awabainishe

Matumizi ya lugha

Katika kipengele hiki mhakiki huchunguza:

1. Mpangilio wa maneno. Mf. Wengi wari badala ya wari wengi

2. Matumizi ya : Mazida – kurefusha neno mfano, kiwembe badala ya

wembe; Ikisari – kufupisha neno mfano siombe badala ya

usiombe; Tabdila – kubadilisha mwendelezo wa neno mfano kujitanuwa

badala ya kujitanua.

3. Matumizi ya methali, misemo na nahau

4. Matumizi ya lugha ya picha

5. Matumizi ya tamathali za semi kama vile takriri, sitiari n.k

6. Mbinu nyingine za kisanaa

Mhakiki anapochunguza vipengele vya fani, jambo muhimu la kuzingatia ni jinsi

vipengele hivyo vinavyosaidia kuwasilisha maudhui.

Vipengele vya maudhui

Ili kuhakiki na kupata maudhui ya shairi inatakiwa kulisoma shairi kwa kulielewa

zaidi. Baada ya kupata picha fulani kuhusu shairi na kutafakari maana za maneno

muhimu, itatubidi tuelewe vipengele vya maudhui, ambavyo ni dhamira, mtazamo,

msimamo, falsafa ya mwandishi, ujumbe na maadili, migogoro na muktadha.

ZOEZI

Kipi kati ya hivi siyo kipengele cha fani katika uhakiki wa ushairi wa fasihi

simulizi?

A Mtindo

B Muundo

Page 40: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 40

C Ujumbe

D Wahusika

Mawazo ya kisiasa na kiutamaduni huakikiwa katika kipengele gani cha maudhui

ya ushairi?

A Ujumbe

B Falsafa

C Migogoro

D Dhamira

Mafunzo mbalimbali yanayopatikana katika shairi huakikiwa katika kipengele gani

cha maudhui?

A Ujumbe

B Migogoro

C Dhamira

D Falsafa

___ni kipengele cha maudhui ya ushairi kinachobainisha mivutano na misiguano

iliyopo ndani ya shairi.

A Dhamira

B Mtazamo

C Falsafa

D Migogoro

___ ni kipengele cha fani kinachoonesha kama shairi ni la kimapokeo au la kisasa.

A Mtindo

B Muundo

Page 41: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 41

C Matumizi ya lugha

D Wahusika

Uhakiki wa Maigizo

Igizo huhakikiwa kwa namna lilivyo katika maumbo yake yote mawili yaani fani

na maudhui.

Vipengele vya Fani na Maudhui katika Kuhakiki Maigizo

Fani

Uhakiki wa fani katika maigizo unajihusisha na ufundi uliotumiwa. Ufundi huu

unajumuisha mambo kadhaa kama ifuatavyo:

Mtindo

Mtindo ni sura ya maigizo inayojitokeza kupitia mpangilio wa maneno na vitendo.

Inabidi mhakiki achunguze kama kazi ni:

1. Mchezo wa jukwaani – wenye mpangilio wa mazungumzo baina ya watu na

matendo yao.

2. Majigambo

3. Vichekesho – mpangilio wa maneno yanayowasilisha ujumbe kwa

kuchekesha.

4. Mazungumzo – maongezi ya kujibizana baina ya watu.

5. Ngonjera – mpangilio wa tungo za kishairi ambapo watu wawili au makundi

mawili hukinzana.

6. Miviga – sherehe za kitamaduni kama vile matambiko

Pamoja na haya, mtindo hutegemea lengo la maigizo ambalo laweza kuwa

kuelimisha, kukejeli, kuburudisha, kuonya, kukosoa na kadhalika.

Mandhari

Page 42: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 42

Mazingira ya kutendea ni kipengele muhimu cha fani. Mhakiki hana budi kujiuliza

iwapo utendaji unadhihirisha wakati au mahali halisi. Jambo hili huweza

kutekelezwa kupitia vifaa, maleba, maneno n.k.

Wahusika

Maswali ya mhakiki kuuliza ni:

Wamejitokeza kikamilifu?

Wanaaminika?

Matumizi ya lugha

Vigezo anavyotumia mhakiki kuchunguza lugha ni:

Kama usemaji ni wa kisanaa, yaani unatumia picha, tamathali za semi,

methali, nahau n.k.

Kama lugha imetumika vile inavyotumiwa katika jamii. Mfano: kiimbo,

mkazo, miguno, vihisishi n.k.

Matumizi ya maneno ya ajabu kama yale yanayotumiwa na waganga.

Maleba na vifaa

Hivi huakisi mandhari na husaidia kuzua mukatadha. Kwa hiyo ni muhimu

kuchunguza kama vimetumiwa ipasavyo.

Matumizi ya ala

Matumizi ya ala kama ngoma, baragumu, au sauti zingine ili kuamsha hisia za

hadhira ni jambo muhimu kuchunguza.

Mbinu nyingine

Mhakiki anapaswa pia kuchunguza matumizi ya nyimbo, uchezaji ngoma,

usimulizi na mbinu nyingine katika kuibua hisia za watazamaji.

Page 43: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 43

Maudhui

Kwa upande wa maudhui, mhakiki wa maudhui hutakiwa kuchunguza vipengele

vyote vya kimaudhui ambavyo ni dhamira, migogoro, maadili, mtazamo na

msimamo wa fanani pamoja na ujumbe bila kusahau kipengele cha falsafa. Yote

hayo kwa pamoja ndiyo humsaidia mhakiki kubaini ukinzani wa igizo na maisha

halisi ya jamii ambayo huwa ndiyo hadhira ya igizo hilo.

ZOEZI

Ni kipengele gani cha maudhui ambacho hubainisha tofauti ambazo hujitokeza

katika maigizo?

A Dhamira

B Ujumbe

C Migogoro

D Falsafa

Matumizi ya mbinu nyingine ni kipengele cha fani katika maigizo ambacho huwa

na vipengele vifuatavyo, isipokuwa:

A Uchezaji ngoma

B Matumizi ya ala

C Usimulizi

D Matumizi ya nyimbo

___ni kipengele cha maudhui ambacho huonesha busara na hekima za mtunzi wa

maigizo.

A Dhamira

B Ujumbe

C Falsafa

D Migogoro

Page 44: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 44

Nasaha atoazo mtunzi wa maigizo uhakikiwa katika kipengele gani cha maudhui?

A Dhamira

B Mafunzo

C Falsafa

D Mgogoro

___ni kipengele cha fani ambacho hubainisha vitendo na mjengo wa visa katika

maigizo.

A Mandhari

B Mtindo

C Matumizi ya lugha

D Muundo

MADA YA 4 : UHIFADHI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI

Ili kitu kidumu ni lazima kihifadhiwe; fasihi simulizi kama sanaa kutokana na

umuhimu wake katika jamii nayo huhufadhiwa kwa ajili ya faida ya kizazi kijacho.

Katika mada hii utaweza kujifunza umuhimu wa fasihi simulizi katika jamii.

Utajifunza njia mbalimbali zitumikazo katika uhifadhi wa fasihi simulizi pia

utaweza kubainisha ubora na udhaifu wa kila njia.

Njia za kuhifadhi Fasihi Simulizi

Kuhifadhi Fasihi Simulizi

Umuhimu wa kazi za fasihi simulizi

Ingawa kila utanzu wa fasihi una umuhimu wake, kwa pamoja tanzu zake zote zina

umuhimu mkubwa katika jamii.

Kwaza fasihi hutumika kama chombo cha kuwaelimisha watu. Kupitia fasihi

andishi na fasihi simulizi, watu hupata maarifa ya kutambua mambo maovu na

Page 45: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 45

namna ya kuyakwepa. Licha ya haya, wanajamii hujifunza njia za kujitawala,

kuzalisha mali na kuishi kwa misingi ya haki, usawa na demokrasia.

Pili, fasihi ni nyenzo ya kutoa mafunzo kuhusu mambo kama vile historia, dini,

siasa, jiografia na tiba. Kwa hiyo watu hujifahamisha juu ya maumbile na asili

yake, mazingira, utawala, uchumi, sheria n.k.

Aidha fasihi huwapa watu mazoezi na kuimarisha uwezo wao wa kuzungumza kwa

ufasaha, kuimba nyimbo kwa ufundi, kuigiza mambo kwa ustadi, kucheza ngoma

kwa umahiri, kughani mashairi kwa mvuto na kusimulia matukio kwa mtindo

ufaao.

Fasihi hufahamisha, huhifadhi na hurithisha mambo kuhusu utamaduni kutoka

kizazi kimoja hadi kingine. Mambo hayo ni pamoja na mila, desturi, falsafa, imani

na itikadi. Pia hudumisha maarifa ya kijadi kama vile tiba, sayansi ya kilimo,

uhifadhi wa mazingira na sayansi ya utabiri wa hali ya hewa.

Umuhimu mwingine wa fasihi unatokana na kutumika kwake kama chombo cha

kuburudisha na kupumbaza. Watu wanaposoma kazi mbalimbali za fasihi hupata,

msisimko wa kimwili na kiakili. Kadhalika fasihi hugusa hisia za watu na

kuwafanya wafurahi au wahuzunike.

Istoshe fasihi hudumisha na kukuza lugha. Watu hupanua msamiati wao na miundo

ya lugha kupitia kazi zake. Hivyo fasihi inakuwa kama hazina ya maneno na dafina

ya kanuni za kisarufi.

Kutokana na umuhimu huu ndio maana fasihi huhifadhiwa ili isipotee. Na uhifadhi

huu hufanyika kwa njia mabalimbali.

ZOEZI

___ni njia ambayo kazi za fasihi simulizi uhifadhiwa katika programu.

A Njia ya makazi

B Njia ya vinasasauti

C Njia ya maandishi

D Njia ya kompyuta

Page 46: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 46

___ni njia ya kuhifadhi fasihi simulizi inayohitaji gharama kubwa na ujuzi wa juu.

A Njia ya makazi

B Njia ya kompyuta

C Njia ya vinasasauti

D Njia ya maandishi

Rediokaseti hutumika katika njia ipi kati ya hizi za kuhifadhia fasihi simulizi?

A Njia ya vinasasauti

B Njia ya makazi

C Njia ya maandishi

D Njia ya mkanda wa video

Mikeka na picha za kuchora uhifadhiwa katika njia gani ya kuhifadhi fasihi

simulizi?

A Njia ya maandishi

B Njia ya kompyuta

C Njia ya makazi

D Njia ya kichwa

Ipi kati ya hizi ni njia kongwe inayotumika kuhifadhi fasihi simulizi?

A Njia ya vinasasauti

B Njia ya kutumia kichwa

C Njia ya maandishi

D Njia ya kanda za video

Ubora na Udhaifu wa kila Njia ya Kuhifadhi kazi za Fasihi Simulizi

Fasihi simulizi inaweza kuhifadhiwa kwa njia zifuatazo:

Page 47: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 47

Kichwani

Hii ndio njia ambayo imekuwa ikitumiwa kuhifadhi kazi za fasihi tangu kale na

inaendelea kutumika hadi leo. Kwa kutumia njia hii kazi ya msanii hukaa kwenye

ubongo wa msanii, naye huweza kuiwasilisha kazi hiyo, wakati wowote bila

gharama yoyote.

Ubora wake

Uwasilishaji wa kazi hiyo unaweza kufanyika wakati wowote bila kuhitaji

kufanyika maandalizi yoyote, hususani ya kiufundi.

Hakuna gharama yoyote wakati wa uwasilishaji wa kazi ya fashi. Msanii

hahitaji kugharimia kitu chochote ili waweze kuitoa kichwani, ni uamzi

wake tu, anaweza kuimba papo kwa papo.

Kazi ya fasihi iliyohifadhiwa kichwani ni hai. Hii ni kwa sababu msanii

anakuwa ana kwa ana na hadhira yake. Kutokana na matumizi ya mbinu

tofauti za kisanaa kama vile kucheza, kubadili sauti, miondoko na

mengineyo mengi, kazi yake inapata uhalisia zaidi mbele ya hadhira.

Udhaifu wake

Uwezekano wa kazi kupotea au kuharibika hasa katika fani ni mkubwa. Kwa

mfano msanii anapokuwa amefariki dunia kazi anayokuwa ameihifadhi

kichwani nayo hupotea. Ndio maana katika baadhi ya jamii kazi za kifasihi

zimepotea. Hii ni kwa sababu wasanii wanapoondoka duniani hondoka na

fani hizo.

Kazi inapohifadhiwa kichwani ni rahisi kubadilika. Hii inatokea pale

ambapo msanii anasahau baadhi ya maneno kutokana na umri wake au

sababu nyinginezo

Njia ya maandishi

Maandishi ni njia moja wapo inayotumika kuhifadhia kazi za fasihi. Njia hii

imeanza kutumika baada ya watu kujua kusoma na kuandika. Uhifadhi wa kazi za

fasihi kwa njia hii hupitia njia mbili kubwa. Hatua ya kwanza ni kubuni kisa au

wazo; na hatua ya pili ni kuliweka wazo hilo katika maandishi. Kazi za fasihi

Page 48: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 48

simulizi zinazoweza kuhifadhiwa katika maandishi ni hadithi, nyimbo, mashairi,

ngonjera, majigambo n.k

Ubora wake

Kazi iliyohifadhiwa inaweza kudumu kwa muda mrefu

Kazi iliyohifadhiwa inaweza kufikia hadhira hata ya mbali na aliko msanii.

Kazi iliyohifadhiwa katika maandshi haipotezi fani yake na maudhui yake

bali huendelea kuwa katika asili yake ya awali hadi msanii atakapoamua

kuibadilisha.

Udhaifu wake

Hii njia ni kwa ajili ya watu wachache tu wanaojua kusoma na kuandika.

Wasanii wanaoweza kutumia njia hii ni wale tu wanaojua kusoma na

kuandika.

Ni aghali sana kuhifadhi kazi za kifasihi kwa njia ya maandishi. Msanii

atalazimika kununua vifaa vinavyohitajika katika maandishi ambavyo ni

kalamu, karatasi, meza. Kwa hiyo ni aghali.

Uwasilishaji wake si hai kwani hakuna kuonana ana kwa ana kati ya hadhira

na fanani. Kwa hiyo msomaji hawezi pata vionjo vya msanii hivyo itambidi

ajibunie yeye mwenyewe.

Wahusika pia hawawezi kuonekana, endapo ni igizo mabalo limehifadhiwa

katika maandishi, hivyo ubora wa kazi ya msanii huchujuka.

Njia ya vinasasauti

Vinasasauti ni miongoni mwa vyombo vinavyotumika kuhifadhi kazi za fasihi

simulizi. Hii ni njia iliyoendelea kuliko ile ya maandishi.

Ubora wake

Kazi ya msanii huweza kuwafikia watu hata walio mbali na alipo mtunzi.

Page 49: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 49

Ikihifadhiwa katika vinasasauti kama vile tepurekoda au CD ubora wake

huwa haupotei wala kuharibika endapo vifaa hivyo vitatunzwa vizuri.

Sauti ya mtunzi unaiskia moja kwa moja

Unaweza kusikia vionjo vya msanii

Udhaifu wake

Njia hii ni aghali kutumia, kununua vinasasauti ni gharama.

Uwasilishaji wake si hai, ingawa unaweza sikia sauti ya msanii au wahusika

lakini hahawezi kuonekana.

Kazi yoyote ya kifasihi inapohifadhiwa katika vinasasauti, kwa mfano

nyimbo, huwa ni mali ya msanii husika, mtu yeyote haruhusiwi kuitumia

kama mali yake binafsi bila kuruhusiwa na msanii.

Njia ya kompyuta

Njia hii imeanza kutumika katika miaka ya hivi karibuni baada ya watu kuanza

kujua na mna ya kutumia kompyuta.

Ubora wake

Njia hii ni ya uhakika zaidi kwa vile shuguli za kisanaa zinazohusika

huhifadhiwa katika kompyuta na hutolewa pale zinapokuwa zinahitajika.

Udhaifu

Msanii au wasanii wanohusika hawawasiliani na hadhira papo kwa papo.

Hivyo hadhira hukosa kuuliza maswali katika vipengele vinavyotatiza.

Ili kuhifadhi kazi ya fasihi kwa kutumia njia hii ni sharti msanii awe anajua

kutumia kompyuta.

Pia ni aghali sana, kuzingatia kwamba kununua komputa ni gharama kubwa.

Njia ya kanda za video

Msanii huweza kutumia kanda ya video kuhifadhi kazi yake.

Page 50: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 50

Ubora wake

Kwanza wasnii na vifaa wanavyotumia huonekana

Sauti zao na milio ya ala wanazotumia husikika na pia huonekana kwa

hadhira. Hii angalau huipa uhai kazi ya msanii mbele ya hadhira.

Huweza kudumu kwa muda mrefu endapo kanda ya video iliyotumika

kuhifadhi kazi ya msanii itatunzwa vizuri.

Udhaifu wake

Uhifadhi wa njia hii ni aghali, msanii atahitajika kununua, kanda ya video,

kumlipa mpiga picha na mzalishaji pia.

Watu wanoweza kunufaika na njia hii ni wacheche mno na wengi wao ni

wale wenye uwezo wa kumiliki televisheni ambao kimsingi hupatikana

maeneo ya mijini.

Ingawaje hadhira wanaweza kumwona msanii lakini hawawezi kuwasiliana

nae ana kwa ana, hivyo kukosa kuuliza swali pindi wanapohitaji kufanya

hivyo.

ZOEZI

Njia ipi ya kuhifadhi fasihi simulizi ina udhaifu wa wahusika kusikika bila ya

kuonekana na hadhira?

A Njia ya kompyuta

B Njia ya kichwa

C Njia ya maandishi

D Njia ya vinasasauti

Fani ya kazi ya fasihi simulizi huweza kupotea endapo itahifadhiwa kwa kutumia

njia ipi?

Page 51: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 51

A Njia ya kanda za video

B Njia ya maandishi

C Njia ya vinasasauti

D Njia ya kichwani

Ipi ni njia yenye udhaifu wa wahusika kutokuonekana pale kazi ya fasihi simulizi

inapowasilishwa?

A Njia ya kichwani

B Njia ya kompyuta

C Njia ya vinasasauti

D Njia ya kanda za video

Ipi kati ya njia zifuatazo haitumii gharama yoyote katika kuhifadhi fasihi simulizi?

A Njia ya kanda za video

B Njia ya kompyuta

C Njia ya vinasasauti

D Njia ya kutumia kichwa

Kubadilika kwa kazi iliyohifadhiwa ya fasihi simulizi wakati wa uwasilishaji ni

udhaifu wa___

A Njia ya kichwani

B Njia ya vinasasauti

C Njia ya kanda za video

D Njia ya maandishi

Umuhimu wa kuhifadhi kazi za Fasihi Simulizi

Faida ya Kuhifadhi Fasihi Simulizi

Page 52: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 52

Njia zote za uhifadhi wa kazi za fasihi simulizi zina umuhimu mkubwa katika

ukuzaji na uendelezaji wa utamaduni katika jamii. Kama ambavyo tumekwishaona,

kazi za fasihi simulizi huelimisha, huburudisha, hurithisha maarifa, maadili, pia ni

vielelezo vya utamaduni wetu wa asiili. Kwa ajili hiyo ni muhimu kuzihifadhi kazi

hizo zisiharibike wala kupotea ili ziendelee kutumika kutoka kizazi kimoja hadi

kingine.

Ni muhimu ziendelee kuwepo ili kuhifadhi utamaduni wetu na huku vikitumika

kama vivutio vya watalii.

Kazi za fasihi simulizi kwa upande mwingine ni sehemu ya ajira. Kwa mfano,

shughuli mabalimbali za kisanaa kama vile ngoma, maigizo na utunzi wa vitabu,

vinawapatia vipato baadhi ya wasanii. Hivyo ni muhimu zihifadhiwe.

Kazi za fasihi simulizi pia ni kichocheo cha umoja na maelewano miongoni mwa

jamii. Yote hayo kwa ujumla wake yanabainisha kuwepo na haja ya kuendelea

kuzikusanya, kuzifanyia kazi, kuziendeleza, na kuzihifadhi kazi za fasihi simulizi.

ZOEZI

Fasihi simulizi iliyohifadhiwa ina faida gani katika lugha?

A Pambo la lugha

B Kiwakilishi cha lugha

C Ni ghala ya lugha

D Ni kivutio cha lugha

Kando na faida ya kuburudisha, kazi za fashi simulizi kama vile ngoma na maigizo

zina faida gani kwa utamaduni wa jamii?

A Kutambulisha

B Kuelimisha

C Kurithisha

D Kufundisha

Page 53: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 53

Zifutazo ni faida za kuhifadhi kazi za fasihi simulizi, isipokuwa:

A Kivutio cha utalii

B Kutoa ajira

C Kurithisha utamaduni

D Kudumaza utamaduni

Fasihi simulizi ikihifadhiwa vizuri huwa dafina ya lugha, hii ina maana ya___

A Kivutio cha lugha

B Ghala ya lugha

C Msamiati wa lugha

D Sarufi ya lugha

Kazi za fasihi simulizi zitakuwa na faida kwa vizazi vijavyo endapo____.

A Zitasambazwa

B Zitafundishwa

C Zitahifadhiwa

D Zitauzwa

MADA YA 5 : UTUNGAJI WA KAZI ZA KIFASIHI

Kazi za fasihi simulizi hazikutokea tu, zilitungwa. Mtu fulani alikaa na akatunga

kazi fulani ambayo inajulikana katika jamii. Katika mada hii utajifunza kanuni

mbalimbli zinazohusika na utunzi wa kazi za fasihi simulizi. Pia utapata fursa ya

kujifunza jinsi ya kutunga kazi mbalimbali za fasihi simulizi kama vile ngonjera,

methali , nahau, vitendawili na kazi nyingine. Utajifunza pia kanuni zinazoongoza

utunzi wa kila kazi ya fasihi simulizi.

Page 54: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 54

Mashairi

Kanuni za Utungaji wa Mashairi

Uandishi wa kubuni unamtaka mtunzi atumie milango yake ya fahamu

kinagaubaga. Kuna milango ya fahamu mitano ambayo ni pamoja na: kuona,

kunusa, kusikia, kuhisi, na kuonja.

Kuona: je, mhusika unayemfikiria kichwani mwako unamwonaje? Umbo

lake ni la kuvutia au kuchusha? Je, macho yake yakoje – je ni ya golori au

la? Ni makubwa au madogo? Je, ni mlemavu wa macho?

Kunusa: pua zako zinakufanya usikie harufu gani? Je, ni harufu mbaya au

nzuri? Je, ni uvundo au marashi? Je, mhusika wako ananuka kikwapa au

uturi? Je, ananuka mdomo?

Kuhisi: je, unapokaa karibu naye unajihisi nini? Je, unapata mhemko

wowote au huhisi chochote? Je, akikupapasa mwilini mwako unajisikia nini?

Akikugusa bega unajisikia nini?

Kuonja: je, ukiweka kitu hicho mdomoni unaonjaje – ni chungu au tamu?

Je, ina pilipili au masala? Je, kuna chumvi au sukari? Je, kitu hicho kina

ukakasi au uchachu?

Kusikia: je, sauti unayoisikia ikoje? Inamtoa nyoka pangoni? Inakufanya

ukose usingizi? Je, ni sauti nzuri au mbaya? Ni nyororo au nzito? Kama ni

sauti ya muziki – je, iko chini au juu (kelele)?

Uzoefu wa Mwandishi

Uzoefu ni hali ya kukaa au kujishughulisha na jambo au kitu kwa muda mrefu.

Mwandishi ana uzoefu (uzoevu) wa kukabiliana na maisha kwa kiasi gani? Je, ni

matatizo gani ambayo umekutana nayo katika maisha yako? Je, ni mafanikio gani

umekutana nayo katika maisha yako? Kwa mfano, katika ajali ya MV Spice (2011)

kuna baadhi ya watu waliokolewa na magodoro ya Tanzania? Magodoro haya yana

nailoni na je kama yasingekuwa na nailoni? Uzoevu/uzoefu wako ukoje?

Page 55: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 55

Uchunguzi/utafiti

Uchunguzi unapaswa ufanywe na mwandishi ili aweze kuandika jambo au tukio

bila kuongopa. Kwa kufanya udanganyifu, mwandishi atapoteza imani yake kwa

wasomaji wa kazi zake.

Uchunguzi ili ufahamu au ujue mtu, mnyama, mdudu na kadhalika – anatembeaje,

anakulaje, analalaje, anaishije, anachekaje, analiaje, anazaaje, anahusianaje na

wenzane na mazingira yake? Haya ni maswali muhimu katika kumwezesha mtunzi

kufanya utafiti wa kina ili ajue kitu anachotaka kukiandika akiandikaje na

akiwasilishaje ili aweze kuikamata hadhira yake.

Mwandishi baada ya kuzingatia mambo haya sasa anaweza kuanza kutunga kazi

yake. Hapa sisi tutajikita zaidi katika utunzi wa mashairi. Kabala hatujaenda katika

hatua ya utunzi ni muhimu kujua dhana ya shairi kwa ujumla wake, na baada ya

hapo tutakuwa tumekwisha pata maarifa yakutosha juu ya mashairi ambayo

yatatuwezesha kutunga mashairi.

Dhana ya shairi

Shairi ni kipande cha maandishi kilichopangwa kwa utaratibu katika mistari. Sauti

za silabi hufanana zikiwa kati au mwisho mwa mstari. Maandishi hayo yakisomwa

huleta ujumbe na hisia fulani ya kimaisha.

Mpango wa maneno ya shairi, ambao huweza kuimbwa hutoa picha wazi, maana

halisi na burudani ya kimuziki. Nyimbo nyingi za makabila zimepangiliwa kishairi

ijapokuwa hazikuandikwa.

Mashairi yana umbo ambalo huonekana kwa mpangilio wa sauti na idadi ya

maneno katika mistari. Umbo hili hutofautisha shairi na tenzi. Kuna mambo

kadhaa yanayotakiwa kufahamika kuhusu shairi, nayo ni:

1. Beti – Kifungu kimoja cha shairi ambacho kina uzani sawa.

2. Vina – Ni mwisho wa mistari ambayo huwa na silabi zenye sauti

ileile mwishoni mwa sentensi.

3. Mizani – Ni idadi zilizo sawa za silabi katika kila mstari, ubeti hadi ubeti.

Page 56: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 56

4. Kituo – Huu ni mstari wa mwisho wa ubeti. Kuna vituo vya aina tatu:Kituo

cha bahari – ni mstari unaotoka mwanzo hadi mwisho bila kubadilika katika

kila ubeti;Kituo cha kimalizio – ni kituo ambacho mstari wa mwisho maneno

yake hubadilika ubeti hadi ubeti;Kituo nusu bahari – ni mstari wa mwisho

ambao maneno yake nusu hubadilika na nusu hubaki kama ulivyo ubeti hadi

ubeti.

Katika mashairi (ya kimapokeo), kila mstari lazima uwe umekamilika na ubeti uwe

na maana kamili.

Vipengele vya fani katika mashairi

Vipengele vya fani katika shairi ni pamoja na:

Jina / anwani

Mandhari

Wahusika

Muundo –tathnia, tathlitha, tarbia, tathamisa, sabilia n.k

Mtindo – pindu, msisitizo, beti kubadilishana vina, kurudiwa kipande kizima

cha mstari wa mwisho kikiwa ni chanzo cha ubeti unaofuatia.

Vipengele vya Maudhui kati mashairi

Vipengele vya maudhui ni pamoja na: migogoro, ujumbe, falsafa, msimamo,

mtazamo, na dhamira za mwandishi.

Matumizi ya ushairi ni pamoja na: kuomboleza, kubembeleza, kuliwaza,

kufundisha, kuburudisha, kukosoa, na kadharika.

ZOEZI

Mstari wa mwisho katika kila ubeti wa shairi huitwa___

A Mizani

B Anwani

Page 57: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 57

C Vina

D Kibwagizo

___ siyo sifa ya lugha inayotumika katika utunzi wa shairi.

A Mpangilio wa maneno usio wa kawaida

B Lugha inayoeleweka kwa urahisi

C Maneno ya mkato

D Lugha inayotoa picha au taswira

Jambo gani analolizingatia mtunzi wa shairi ili kuweka usiri katika shairi?

A Vituo

B Anwani

C Maana ya shairi

D Aina na idadi ya wahusika

Jina lingine la kichwa cha shairi ni___.

A Anwani

B Kituo

C Idadi ya mizani

D Maana ya shairi

Utunzi wa shairi kwa kuzingatia alama mbalimbali hujikita katika matumizi ya___.

A Anwani

B Idadi

C Vituo

D Mpangilio wa maneno

Page 58: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 58

Kuigiza Ngonjera

Katika kuigiza ngonjera muigizaji hana budi kuzingatia fani yenye kanuni

zifuatazo; mtindo wa mashairi ya kimapokeo, muundo wa mashairi ya kimapokeo

wenye mizani, vina, vipande, mishororo na beti, kuteua mandhari kutegemeana na

mada, kuwepo kwa wahusika wawili au zaidi au makundi mawili au zaidi na

matumizi ya lugha ya kishairi.

ZOEZI

Muigizaji wa ngonjera hana budi kuzingatia mambo yafuatayo katika fani ya

ngonjera, isipokuwa:

A Vina

B Mizani

C Kituo

D Maonyesho

Suluhisho la tatizo linaloongelewa katika ngonjera hupatikana___mwa ngonjera.

A Mwanzoni

B Mwishoni

C Katikati

D Katikati na mwishoni

Kila ubeti katika utunzi wa ngonjera yapaswa uwe na___la kuwasilisha.

A Mambo mawili

B Jambo moja

C Mambo manne

D Mambo matatu

Muundo unaotumika katika ngonjera ni wa mashairi ya___.

Page 59: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 59

A Masivina

B Kimapokeo

C Mapingiti

D Kisasa

Ni lugha gani ambayo inapaswa kutumika katika kuigiza ngonjera?

A Lugha ya tamthiliya

B Lugha ya mitaani

C Lugha ya kishairi

D Lugha ya nathari

Maigizo

Kanuni za Utungaji wa Maigizo

Maigizo ni tendo la kuiga sura, tabia, matendo na mazungumzo ya watu au viumbe

wengine yaani kuiga jinsi walivyoumbwa, wanavyotembea, wanavyovaa,

wanavyosema n.k

Kanuni na hatua za kutunga maigizo

1. Kuchagua wazo, tendo, visa au tukio la kuigizwa:Ni lazima jambo hilo

liwe na uzito, umuhimu au athari fulani katika jamii. Matukio hubainika

kutokana na utafiti. Matukio yanayoweza kuwa kiini cha kutungiwa maigizo

ni kama vile matumizi mabaya ya simu za mkononi, mitindo ya mavazi,

madhara ya uganga wa kienyeji, madhara ya UKIMWI n.k.

2. Kuchagua muktadha au mahali pa kutendeka kwa jambo:Muktadha

waweza kuwa ofisini, shuleni, kijijini, mjini, barabarani, kwenye daladala

n.k

Page 60: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 60

3. Kuamua mtindo wa kuwasilisha jambo la kuigizwa:Hapa mtunzi

anaweza kutumia fumbo, vichekesho, historia, tanzia n.k. Inashauriwa

mtunzi kuchanganya mbinu ili kuongeza mvuto.

4. Kupanga hoja kuu zinazojenga maudhui ya igizo:Maudhui hujikita katika

migogoro au mivutano. Suluhisho la mivutano hupatikana pale migogoro

inapofikia kilele. Kwa mfano jamabazi sugu anapokamatwa.

5. Kuweka mpangilio wa maonyesho:Maonyesho hujumuisha vitendo na

hoja zinazokamilisha sehemu inayobeba aina moja au zaidi ya maudhui.

Sehemu kadhaa nazo hukaa zikajenga kitendo ambacho hubeba jambo

mojawapo muhimu. Katika migawanyo hii yapasa mtunzi atunge kauli na

vitendo vinavyoandamana navyo.

6. Kubuni wahusika na kuweka aina au idadi yao kulingana na

matukio:Mtunzi anashauriwa kutumia wahusika wanaohitilafiana. Kwa

mfano wazee, vijana, wanawake, wanaume, wanene, wafupi n.k. Mtunzi

akishawateua anaweza kuwatungia kauli na zamu za matendo katika sehemu

mbalimbali.

7. Ni muhimu pia kwa mtunzi kuwaumba wahusika wake na kuamua

maleba yao:Uamuzi huu yapasa ufanywe kwa kuzingatia mazingira. Kwa

mfano siku hizi sio lazima wahusika wazee kuvaa ngozi, kutumia mkongojo

na kuvuta mtemba.

8. Urefu wa maigizo ni suala la kuamliwa kutegemea tukio

9. Kutunga maelezo kuhusu mandhari:Maumbile ya wahusika na vitendo

vyao, ni muhimu kuelezwa katika mabano.

10. Kuandika maigizo na kuhariri:Ni muhimu kutumia lugha ya

kimazungumzo inayovutia, yenye kuleta taharuki na yenye utamu unaoeleza

maadili kwa mnato.

ZOEZI

___hujumuisha vitendo na hoja zinazokamilisha sehemu inayobeba maudhui

katika maigizo.

Page 61: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 61

A Mbinu

B Mada

C Tukio

D Maonyesho

Aina na idadi ya wahusika katika utunzi wa maigizo hutegemea___.

A Matukio

B Maonyesho

C Mada

D Mtindo

Ni kanuni gani katika utungaji wa maigizo ambayo hukazia umuhimu na uzito wa

jambo husika kwa jamii?

A Kupanga hoja kuu

B Kuamua mtindo

C Kuchagua muktadha

D Kuchagua wazo

___ siyo mtindo unaotumiwa kuwasilisha maigizo.

A Vichekesho

B Tanzia

C Fumbo

D Majibizano

Uamuzi wa mavazi ya kuigizia katika maigizo unapaswa ufanywe kwa

kuzingatia___

Page 62: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 62

A Visa

B Mazingira

C Hoja

D Mada

MADA YA 6 : UANDISHI

Insha za Hoja

Insha za hoja ni insha zinazoelezea jambo fulani katika hali ya kujenga hoja

ambazo zinatetea msimamo fulani alionao mwandishi wa insha hiyo juu ya jambo

analolizungumzia. Hoja ni maelezo bayana yanayotolewa na mwandishi kutetea

msimamo wake.

Katika uandishi wa insha za aina hii, mwandishi hutakiwa kuonesha ni jambo gani

ambalo analiunga mkono na ni lipi ambalo hakubaliani nalo.

Ili hoja zote zipate kueleweka ni sharti zipangwe katika mtiririko wa mawazo ulio

sahihi kiasi kwamba mtu aisomapo anapata kuelewa ni mada gani mwandishi

anaijadili na ana msimamo gani kuhusu mada hiyo.

Muundo wa Insha za Hoja

Katika uandishi wa insha, muundo wake unakuwa na vitu vifuatavyo:

1. Kichwa cha insha; kichwa cha insha hudokeza kile ulichokijadili katika

insha yako. Kwa mfano: Madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya n.k

2. Utangulizi; Mambo yaliyopo katika utangulizi ni pamoja na kutoa fasili ya

maneno muhimu na kuelezea kwa muhtasari mambo ambayo utakwenda

kuyajadili katika insha yako.

3. Kiini cha insha;katika kiini ndipo kuna maelezo ya kina juu ya kile

unachokijadili katika insha yako, maelezo haya yanakuwa katika aya kadhaa

kulingana na idadi ya hoja ulizonazo katika mjadala wako.

Page 63: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 63

4. Hitimisho; hapa ndipo kuna muhtasari wa kile kilichojadiliwa katika kiini

cha insha au inaweza kuwa ni msimamo juu ya kile kilichohadiliwa katika

insha

ZOEZI

___ni sehemu katika muundo wa insha za hoja ambapo mada hujadiliwa.

A Utangulizi

B Hitimisho

C Kiini cha insha

D Kichwa cha insha

Mkazo wa jambo lililojadiliwa katika insha hutolewa katika___.

A Kichwa cha insha

B Hitimisho

C Utangulizi wa insha

D Kiini cha insha

Maelezo mafupi yanayodokeza mada inayojadiliwa katika insha za hoja hutolewa

katika sehemu ya___

A Kiini cha insha

B Hitimisho

C Utangulizi

D Kichwa cha insha

Kipi kati ya hivi ni muhimu kuandikwa kwa herufi kubwa katika muundo wa insha

za hoja?

A Utangulizi wa insha

B Kichwa cha insha

Page 64: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 64

C Kiini cha insha

D Hitimisho la insha

Muhtasari na msisitizo wa kile kilichojadiliwa katika insha za hoja hutolewa katika

kipengele gani?

A Hitimisho

B Kiini cha insha

C Utangulizi

D Kichwa cha insha

Barua Rasmi

Dhima ya Barua Rasmi

ZOEZI

Ipi ni dhima ya barua rasmi inapotumika kuwaita watu kuhudhuria sherehe au

harusi?

A Kuomba kazi

B Kutoa mwaliko

C Kuagiza vitu

D Kutoa taarifa

Barua rasmi zinapoandikwa na kutunzwa kwa matumizi ya baadae huwa na dhima

ya___

A Kuweka kumbukumbu

B Kuomba kazi au huduma

C Kutoa malalamiko

D Kutoa taarifa

Page 65: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 65

Barua rasmi hutumika kurahisisha mawasiliano katika shughuli za___.

A Kisiasa

B Kiutamaduni

C Kijamii

D Kiofisi

Barua rasmi huwa na dhima gani inapoandikwa na mtu ili kukiri kosa?

A Kuombea cheo

B Kutolea malalamiko

C Kuombea msamaha

D Kuombea kazi

Barua rasmi huweza pia kuitwa___.

A Barua za magazetini

B Barua za kiofisi

C Barua za simu

D Barua za maandishi

Barua rasmi ni barua zinazohusu mambo rasmi ya kiofisi. Dhima za barua rasmi ni

kutoa taarifa, kuomba kazi au huduma, kuagiza vitu na kutoa mwaliko kwa mfano

kwa kiongozi fulani wa nchi, kutoa malalamiko na kuweka kumbukumbu au

marejeo.

Muundo wa Barua Rasmi

Barua rasmi au barua ya kiofisi/kibiashara huzingatia mtindo rasmi wa barua. Kwa

kawaida huwa na sehemu zifuatazo:

1. Anwani ya mwaandishi -huwekwa juu kabisa na huwa katika upande wa

kulia wa karatasi.

Page 66: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 66

2. Tarehe ya barua hiyo- tarehe huandikwa chini ya anwani ya mwandishi

3. Anuwani ya mpokeaji- Anwani ya anayeandikiwa huwa katika upande wa

kushoto wa karatasi, na huwekwa msitari mmoja chini ya tarehe.

4. Salamu- Chini ya anwani ya mpokeaji, barua huanza kwa kumrejelea

mpokeaji kama bwana au bi. Ni makosa kumsalimia mpokeaji wa barua

rasmi au kumwuliza hali yake.Ndugu Bwana Meshaki, => taja jina lake

ikiwa mnajuana na unayemwandikia. Kwa Bw/Bi, => Ikiwa humjui

mpokeaji wa barua, tumia bw/bi

5. Mada- Kichwa cha barua rasmi huja pindi tu baada ya salamu.

Hutangulizwa na maneno kama vile YAH:(yahusu). Ni sharti kichwa

kiandikwe kwa herufi kubwa na kipigiwe mstari. Kichwa kinapaswa kuwa

kifupi na kinachoelezea mada ya barua kiukamilifu.

6. Utangulizi– Hukaa chini kidogo ya mada ya barua. Haya ni maelezo mafupi

yasiyozidi aya moja ambayo huelezea kusudi kuu la barua kama kidokezo.

7. Ujumbe- Ujumbe wa barua rasmi lazima uwe mfupi na unaotumia lugha

rasmi.

8. Tamati– mwandishi humalizia kwa maneno ya hitimisho kama vile: Wako

mwaminifu, [jina], Sahihi

ZOEZI

Kipengele cha wadhifa wa mwandishi katika muundo wa barua rasmi huandikwa

baada ya kipengele cha___

A Hitimisho la barua

B Jina kamili la mwandishi

C Tarehe

D Kiini cha barua

Kipengele gani cha muundo wa barua rasmi kinachotoa msisitizo na kutia mkazo

kile kilichoandikwa?

Page 67: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 67

A Kichwa cha barua

B Mwisho wa barua

C Utangulizi wa barua

D Kiini cha barua

Wadhifa wa mwandikiwa barua hutajwa katika kipengele gani cha muundo wa

barua rasmi?

A Kiini cha barua

B Anwani ya mwandikiwa

C Anwani ya mwandishi

D Tarehe

Vifuatavyo ni vipengele katika muundo wa barua rasmi, isipokuwa:

A Anwani ya mwandishi

B Namba ya kumbukumbu ya barua

C Tarehe

D Maamkizi

___ni kipengele cha muundo wa barua rasmi kinachorahisisha urejeaji wa barua

katika majalada.

A Mwanzo wa barua

B Namba ya kumbukumbu ya barua

C Anwani ya mwandishi

D Tarehe

Page 68: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 68

Simu

Dhima ya Simu ya Maandishi

Simu za maandishi ni aina ya barua fupi ambazo husafirishwa kwa haraka sana

kuliko barua za kawaida.

Simu hizo huandikwa kwenye fomu maalumu ambazo hutolewa na shirika la

posta. Simu za maandishi hujulikana kama telegram.

Kwa kawaida simu za maandishi hutumika kutuma ujumbe wa dharura. Kuandika

simu za maandishi ni njia ya haraka ya kufikisha ujumbe kwa sababu, baada ya

kuandika simu yako ujumbe humfikia huyo unayemtumia katika muda usiozidi

siku tatu.

Gharama za simu za maandishi hutozwa kulingana na idadi ya maneno

yaliyotumika. Kwa hiyo ujumbe unaotumwa huandikwa kwa maneno machache ili

kuepuka kutozwa gharama kubwa.

Mfano wa simu ya maandishi:

MUSA KINGAMBE SLP 5299 DSM

NJOO HARAKA DADA MGONJWA

LINGIDO

ZOEZI

Simu ya maandishi ina dhima gani inapowezesha watu walio mbali kuwasiliana

kwa urahisi?

A Kuokoa gharama

B Kurahisisha mawasiliano

C Kuokoa muda

D Kuonesha umuhimu wa ujumbe

Simu ya maandishi ina dhima zifuatazo, isipokuwa:

Page 69: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 69

A Kutoa mwaliko

B Kurahisisha mawasiliano

C Kufikisha ujumbe kwa haraka

D Kuokoa muda

Gharama ya simu ya maandishi hutozwa kulingana na___.

A idadi ya maneno

B umuhimu wa ujumbe

C muda uliotumika

D ukubwa wa maneno

Kutokana na dhima ya kuokoa muda na kuepusha gharama simu maandishi huwa

na___.

A Maneno mengi

B Maneno machache

C Maneno magumu

D Maneno rahisi

Simu za maandishi hutolewa na nani?

A Benki

B Mamlaka ya mawasiliano

C Posta

D Makampuni ya simu

Kuandika Simu za Maandishi kwa Kuzingatia Muundo na Taratibu za Uandishi

Page 70: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 70

Muundo wa kuandika simu za maandishi una mambo yafuatayo ya kuzingatia

ambayo ni anwani ya mpelekewa taarifa, ujumbe na jina la mwandishi au mtuma

simu. Mambo mengine ya kuzingatia ni kuandika maneno yote kwa herufi kubwa

ili kurahisisha usomaji na kuandika simu ya maandishi katika karatasi maalumu

ambayo hutolewa na posta.

ZOEZI

___ ni aina ya barua fupi ambazo husafirishwa kwa haraka sana kuliko barua za

kawaida.

A Barua rasmi

B Simu ya maandishi

C Simu ya mdomoni

D Simu ya magezetini

Muundo wa simu za maandishi una sehemu ngapi muhimu?

A Sita

B Nne

C Tatu

D Tano

___katika simu ya maandishi huwa ni mfupi na unaoeleweka kwa urahisi.

A Ukurasa

B Hitimisho

C Utangulizi

D Ujumbe

Jina lingine la simu ya maandishi ni___.

A Telegramu

Page 71: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 71

B Simu ya haraka

C Simu ya mkononi

D Simu ya dharura

Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia katika muundo wa simu ya maandishi,

isipokuwa:

A Ujumbe

B Anawani ya mpelekewa taarifa

C Tarehe

D Jina la mwandishi

Kadi za Mialiko

Kadi za mialiko ni aina ya karatasi ngumu zinazopeleka taarifa fupi za kumwomba

mtu ahudhurie katika sherehe fulani kama vile harusi, ubatizo mahafali n.k

Muundo wa Kadi ya Mialiko

Mambo muhimu yanayotakiwa kuonyeshwa katika kadi ya mwaliko:

1. Jina la mwandishi au mwalikaji

2. Jina la mwalikwa, ni muhimu kuandika cheo chake kama vile: Profesa, Bi.,

Bw. Bw&Bi n.k

3. Lengo la mwaliko

4. Mahali pa kufanyika shughuli

5. Tarehe ya mwaliko

6. Wakati wa shughuli

7. Jina na anwani ya mtu atakayepelekewa majibu.

Mialiko huweza kuandikwa kwa namna mbili yaani kama barua au kadi. Jina la

mwalikwa katika kadi ya mwaliko hutakiwa kuanza na maneno ya heshima kama

Page 72: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 72

vile Bwana….Bi…..au Ndugu…ikiwa waalikwa ni mume na mke kadi itaanza na

Bwana na Bibi.

Mfano wa Kadi ya Mwaliko

Familia ya Marandu wa Mto wa Mbu

Wanapenda kukualika/kuwaalika Profesa/Dkt/Shekhe/Padri/Bi/Bw/Bw&Bi………

kwenye harusi ya kijana wao mpendwa Ibahim Joseph itakayofanyika huko Mto wa

Mbu katika ukumbi wa simba siku ya Jumapili tarehe 9/12/2016 sasa 8.00 mchana

hadi saa 3.00 usiku

Kufika kwako ndio mafanikio ya sherehe hii.

Majibu kwa (wasiofika tu)

Joseph Marandu

Simu: 0717104507

ZOEZI

___huandikwa kwa ufupi na kwa uwazi katika kadi za mialiko.

A Tarehe ya mwaliko

B Jina la mwalikaji

C Mahali pa kufanyia shughuli

D Lengo la mwalikaji

Katika kadi ya mwaliko, majina ya vyeo kama vile „Profesa na Shekhe‟ hufuatana

na___.

A Terehe ya mwaliko

B Jina la mwalikwa

Page 73: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 73

C Lengo la mwalikaji

D Jina la mwandishi

___ni kipengele katika muundo wa kadi za mialiko kinachotoa nafasi ya kutoa

majibu kwa aliyeandika.

A Jina la mwalikwa

B Lengo la mwalikaji

C Jina ya mwandishi

D Jina na anwani

___ni aina ya karatasi ngumu zinazopeleka taarifa fupi za kumwomba mtu

ahudhurie katika sherehe fulani.

A Barua za kirafiki

B Barua rasmi

C Kadi za mwaliko

D Barua za magezetini

Kipi kati ya hivi siyo kipengele katika muundo wa kadi za mialiko?

A Tarehe ya mwaliko

B Lengo la mwalikaji

C Kichwa cha habari

D Jina la mwandishi

Uandishi wa Dayalojia

Dhana ya Dayolojia

Dayalojia ni mazungumzo au majibizano baina ya watu wawili au zaidi

wanaozungumza kwa kupokezana. Kama zilivyo kazi nyingine za utunagaji,

dayalojia inaweza kuwasilishwa kwa nijia ya mazungumzo au maandishi.

Page 74: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 74

Katika kutunga dayalojia mtunzi hana budi kujifanya kama mhusika katika

dayalojia hiyo. Kwanza anapaswa kutafakari kwa makini mada anayokusudia

kuandikia dayalojia, kutayarisha na kupanga mawazo kimantiki na kwa mtiririko

na kufikiria wahusika na kuwapangia majukumu kulingana na matendo yao. Kwa

mfano kama mhusika ni mkulima, lugha anayopewa, vifaa anavyosemekana

kuvitumia na mandhari aliyomo ni lazima vifanane na hali ya mkulima halisi.

Mambo ya kuzingatia katika dayalojia ni pamoja na haya yafuatayo:

1. Kutoa maelezo ya ufafanuzi katika mabano ili kumfahamisha

2. Kuwa na mazungumzo ya mkato na yasiyozidiana sana kati ya wahusika.

Mhusika mmoja asitawale mazungumzo kupita wengine.

3. Kutumia vihisishi ili kufanya dayalojia iwe ya kusisimua

4. Pawepo mwingiliano wa mazungumzo ya wahusika na kudakia maneno ili

dayalojia iwe na uhalisia.

Mfano wa dayalojia

Wambura:

(Anaonekana mwenye furaha,anamwita rafiki yake,

Anna)Wow, Anna! Tumekutana tena, siamini macho

yangu! (wanakumbatiana wote wakiwa na nyuso za

furaha).

Anna:

(Anatabasamu huku ameshikilia mkono wa kulia wa

Wambura, anaonesha shauku kuu)Wambura! Bado

unanikumbuka? Nina furaha sana kwa kweli, ni muda

mrefu sana.

Wambura:

(Anachekelea)Aaaah, nahisi kama naota Neema, siamini

kama nimekutana na wee leo hii ni muda mrefu sana,

nimefurahi kwa kweli.

Page 75: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 75

Anna: (Anachekelea)

Wambura: Mbona wachekelea tu….

ZOEZI

Mwingiliano wa mazungumzo ya wahusika na kudakia maneno huifanya dayalojia

iwe na___.

A Uhalisia

B Mvuto

C Mashiko

D Ukinzani

Wahusika katika dayalojia wanapaswa kupangiwa majukumu kulingana na nini?

A Matendo yao

B Maelezo yao

C Mitazamo yao

D Msimamo wao

Lugha na maneno ya wahusika katika dayalojia hutegemea___.

A Shughuli walizopewa

B Mtunzi

C Sarufi

D Msimamo wa wahusika

Mtunzi wa dayalojia anapaswa kujifanya kuwa___.

Page 76: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 76

A Hadhira

B Muulizaji

C Mhusika

D Mhakiki

Wahusika katika dayalojia huzungumza kwa___.

A Kukejeli

B Madaha

C Kupokezana

D Kugombana

MADAYA 7 USIMULIZI

Usimulizi ni jumla ya maelezo yanayotolewa na mtu au watu wengi kuhusu tukio

fulani. Tukio hilo linaweza kutokea katika wakati mfupi uliopita au zamani kidogo.

Usimuliaji wa Matukio

Njia za Usimulizi wa Matukio

Usimulizi hufanyika kwa njia kuu mbili yaani kwa njia ya maandishi na kwa njia

ya masimulizi ya mdomo. Kila njia hutegemea kwa namna msimuliaji anavyoweza

kuwasiliana na msikilizaji. Ikiwa msimuliaji na msikilizaji hawakukaribiana, njia

ambayo itatumika ni ile ya maandishi. Kwa mfano kama utahitaji kumweleza mtu

aliyembali kuhusu tukio fulani la kusisimua utalazimika kutumia maandishi, yaani

utatumia njia ya kumwandikia barua.

Lakini kama unamsimulia mtu ambaye yupo karibu nawe, utatumia njia ya

mazungumzo ya ana kwa ana.

Taratibu za usimulizi wa matukio

Usimulizi wa matukio dhamira yake ni kumweleza mtu au watu tukio ambalo wao

hawakulishuhudia. Hivyo katika usimulizi msimuliaji hutakiwa kutoa maelezo

Page 77: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 77

muhimu ambayo yatawawezesha watu hao kulielewa tukio linalosimuliwa

sawasawa na huyo anayeshuhudia.

Mambo muhimu ya kutaja katika usimulizi wa matukio ni pamoja na haya

yafuatayo:

1. Aina ya tukio – msimuliaji atatakiwa kubainisha katika maelezo yake aina

ya tukio. Kwa mfano, kama ni harusi, ubatizo, ajali ya barabarani au

mkutano.

2. Mahali pa tukio – ili msimuliaji aweze kuielewa habari inayosimuliwa, ni

lazima kumwelewesha ni mahali gani tukio hilo limetokea. Kwa mfano,

kama ni mjini inafaa kutaja hata jina la mtaa.

3. Wakati – katika usimulizi ni muhimu pia kutaja muda ambao tukio

limetendeka kama ni asubuhi, mchana au jioni bila kusahau kutaja muda

halisi yaani ilikuwa saa ngapi.

4. Wahusika wa tukio – ni muhimu kutaja tukio limehusisha watu gani, wingi

wao, jinsia yao, umri wao n.k.

5. Chanzo cha tukio – kila tukio lina chanzo chake hivyo ni muhimu kutajwa

katika usimulizi.

6. Athari za tukio – athari za tukio nazo ni sharti zibainishwe. Kama ni ajali,

je watu wangapi wameumia; wangapi wamepoteza maisha n.k.

7. Hatima ya tukio – msimuliaji katika usimulizi wake ni lazima abainishe

baada ya tukio kutokea na kushughulikiwa hatima yake ilikuwaje. Kwa

mfano, kama tukio ni ajali ya barabarani hatima yake inaweza kuwa

majeruhi kupelekwa hospitalini na dereva aliyehusika kukamatwa.

Kwa hiyo misingi hii ya usimulizi hufanya usimulizi wa tukio kuwa na sehemu

kuu tatu:

Utangulizi – sehemu hii huwa na maelezo tu ya utangulizi ambayo hulenga

kuvuta hisia na umakini wa msikilizaji au wasikilizaji. Kwa kawaida

utangulizi wa tukio huwa ni maneno machache kiasi yasiyozodi aya moja.

Page 78: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 78

Kiini – kiini cha usimulizi huelezea tukio halisi kuanzia chanzo chake,

wahusika, muda, mahali na athari za tukio.

Mwisho – mwisho wa usimulizi ni matokeo yanayoonyesha matokeo ya

mwisho ya tukio linalohusika, wakati mwingine matukio haya yanaweza

kuambatana na maelezo ya msimuliaji kuhusu mtazamo au maoni yake

binafsi juu ya tukio ambalo amesimulia.

Mbinu za usimulizi

Ili habari inayosimuliwa ipate kueleweka vizuri, sharti msimuliaji ajue mbinu za

kusimulia katika hali inayovuta hisia za msikilizaji wake.

Baadhi ya mbinu hizo ni uigizi, utumizi wa lugha fasaha inayozingatia lafudhi

sahihi ya Kiswahili.

Kwa upande wa uigizi msimuliaji atatakiwa kuigiza mambo muhimu

yanayohusiana na tukio ambalo anasimulia. Nayo ni kama vile milio, sauti na

matendo.

Kwa upande wa usimulizi ambao unafanyika kwa njia ya maandishi, sharti

usimulizi huo uwe na kichwa cha habari. Kichwa cha habari kinatakiwa kuandikwa

kwa maneno yasiyozidi matano, yaliyoandikwa kwa herufi kubwa.

Kwa vile usimulizi wa tukio huwa unahusu tukio lililopita, maelezo yake mengi

huwa katika wakati uliopita.

ZOEZI

Kipi kati ya hivi ni cha muhimu katika njia ya usimulizi wa kutumia maandishi?

A Kichwa cha habari

B Watazamaji

C Lafudhi

D Msikilizaji

Page 79: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 79

___hutakiwa kuandikwa kwa herufi kubwa katika njia ya usimulizi wa kutumia

maandishi.

A Kiini

B Utangulizi

C Kichwa cha habari

D Hitimisho

___ni maelezo ambayo hulenga kuvuta hisia na umakini wa msikilizaji katika njia

za usimulizi wa matukio.

A Mahali pa tukio

B Kiini cha usimulizi

C Hitimisho

D Utangulizi

___ni kipengele katika usimulizi ambacho hutaja aina ya watu, wingi wao na umri

wao.

A Wakati

B Mahali pa tukio

C Wahusika wa tukio

D Aina ya tukio

___ ni jumla ya maelezo yanayotolewa na mtu au watu wengi kuhusu tukio fulani.

A Ufahamu

B Ufupisho

C Ngonjera

D Usimulizi

Page 80: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 80

MADA YA 8 UFAHAMU

Ufahamu ni dhana inayorejelea kujua na kulielewa jambo kwa usahihi na kuweza

kulielezea upya kwa usahihi bila kupoteza maana yake ya msingi. Ufahamu wa

mtu waweza kupimwa katika kusikiliza jambo au katika kusoma.

Ufahamu wa Kusikiliza

Ufahamu wa kusikiliza ni zaidi ya kusikiliza tu kile kilichosemwa; badala yake ni

uwezo wa mtu kuelewa maana ya maneno anayoyasikia na kuweza kuhusiana nayo

kwa namna fulani. Kwa mfano mwanafunzi anaposikiliza hadithi, ufahamu mzuri

wa kusikiliza humsaidia kuielewa hadithi hiyo, kuikumbuka, kuijadili, na hata

kuisimulia tena kwa maneno yake mwenyewe.

Kujibu Maswali ya Ufahamu kutokana na Habari uliyoisikiliza

Jibu maswali ya ufahamu kutokana na habari uliyoisikiliza

Ufahamu wa kusikiliza unahusisha michakato kadhaa katika kuelewa na kupata

maana ya kile kinachozungumzwa. Michakato hii inahusisha:

Kuelewa vizuri sarufi ya lugha ile inayozungumzwa

Kuelewa vyema maana ya maneno ya mhusiaka anayezungumza

Kuelewa sintaksia (muundo wa maneno) ya sentensi kwa namna

zinavyowasilishwa.

Katika ufahamu wa kusikiliza, msikilizaji hana budi kuzingatia mambo yafutayo:

1. Kuwa makini na kuelekeza akili yote kwa mzungumzaji ili kuweza kusikia

kila anachokisema.

2. Kutilia maanani vidokezo vya maana ili kubaini iwapo msemaji anaongeza

jambo jipya, anatofautisha, anafafanua au anahitimisha hoja.

3. Msomaji anatakiwa kuandika baadhi ya mambo anayoona kuwa ni ya

muhimu ili kumasidia kukumbuka hapo baadae.

Page 81: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 81

4. Kuwa makini na ishara mbambali za mwili kama vile kurusha mikono,

kutingisha kichwa, kutingisha mabega au hata kupepesa macho. Ishara hizi

huwa zinachangia kwa kiasi kikubwa kupata maana katika mazungumzo.

Kufupisha kwa Mdomo Habari uliyoisikiliza

Ili kuweza kufupisha kwa mdomo habari uliyoisikiliza yapo mambo ya kuzingatia.

Mambo hayo ni kubaini mawazo makuu yanayopaswa yajitokeze katika habari

iliyofupishwa, kupanga maelezo kwa usahihi katika usemaji, kuzingatia kichwa

cha habari ambacho kinapaswa kihusiane na ufupisho na wazo kuu na mwisho ni

kusema ufupisho kwa ufasaha na kwa lugha ambayo ni nzuri.

ZOEZI

Lipi kati ya haya ni muhimu kuzingatia katika ufupisho wa kusema kwa mdomo?

A Matumizi ya lugha fasaha

B Idadi ya maneno

C Aina ya matini

D Aina ya maswali

Nini kinapaswa kibainishwe katika kila aya ya habari unayoisikiliza ili kuifupisha

kwa mdomo?

A Idadi ya mistari

B Mawazo makuu

C Maneno ya ziada

D Ishara za mwili

Kupanga maelezo kwa usahihi katika kufupisha habari kwa mdomo kunasaidia

nini?

A Kusema kwa ufupi

B Mtiririko wa mawazo

Page 82: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 82

C Kuelewa kichwa cha habari

D Kuelewa wazo kuu

Kichwa cha habari katika habari iliyofupishwa ni lazima kihusiane na ___.

A Vidokezo vya maana

B Idadi ya maneno

C Maneno ya mzungumzaji

D Wazo kuu

Ufupisho wa kusema kwa mdomo hutokana na___.

A Mtiririko wa hoja

B Mawazo makuu

C Maswali

D Habari uliyoisikiliza

Ufahamu wa Kusoma

Ufahamu wa kusoma ni ule mtu anaoupata kwa njia ya kusoma makala, kifungu

cha habari, kitabu au gazeti.

Kusoma kwa Sauti kwa kuzingatia Lafudhi ya Kiswahili

Kuna vipengele viwili vinavyounda mchakato wa ufahamu wa kusoma:

Uelewa wa msamiati na

Uelewa wa matini

Ili kuilelewa habari/matini ni lazima msomaji awe na uwezo wa kuelewa msamiati

uliotumika katika matini hiyo. Endapo maneno yaliyotumika hayataeleweka

vilevile matini yote hataeleweka.

Katika ufahamu wa kusoma, msomaji anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:

Page 83: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 83

1. Kubaini mawazo makuu; msomaji anaposoma habari fulani au kitabu

inatakiwa ajiulize, Je, kinachoongelewa hapa ni nini? Ni jambo gani hasa

analolizungumzia mwandishi? Msomaji akiwa na maswali haya akilini

mwake basi itakuwa rahisi kwake kuielewa habari hiyo.

2. Kuzingatia alama za uakifishi; msomaji ni lazima azingatie alama za

uakifishi, kwa kufanya hivyo itamsaidia kuelewa ujumbe wa habari hiyo na

endapo hatazingatia alama za uakifishaji anaweza kupotosha maana ya

mwandishi.

3. Kubaini maana ya maneno na misemo mbalimbali; habari nyingine huwa

zina maneno ya kisanaa hivyo ni muhimu msomaji kubaini maana ya

maneno hayo katika muktadha wa habari hiyo, hii itamsaidia kuelewa vyema

maana ya mwandishi.

4. Vilevile msomaji anatakiwa kumakinikia kile anachokisoma, kila kipengele

anachokisoma inampasa akielewe vizuri.

Kwa kuzingatia haya yote msomaji atakuwa na uelewa mzuri juu ya habari

aliyoisoma na pia anaweza kufupisha habari hiyo aliyoisoma.

ZOEZI

Katika kusoma kwa sauti kwa kuzingatia lafudhi ya Kiswahili ni alama gani ya

kituo huonesha hali ya furaha?

A Alama ya kuuliza

B Alama ya mshangao

C Alama ya koma

D Alama ya nukta

Kusoma kwa sauti kwa kuzingatia lafudhi ya Kiswahili humaanisha kuzingatia___.

A Matini za Kiswahili

B Fasihi

Page 84: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 84

C Usahihi wa matamshi ya Kiswahili

D Matamshi ya lugha zote

Ipi siyo mojawapo ya alama za vituo zinazopaswa kuzingatiwa na msomaji pale

anaposoma kwa sauti?

A Nukta

B Kidahizo

C Nukta pacha

D Mkato

___huonesha kupanda na kushuka kwa sauti katika kusoma kwa sauti kwa

kuzingatia lafudhi ya Kiswahili.

A Msito

B Vituo

C Kiimbo

D Matamshi

Usomaji wa sauti kwa kuzingatia lafudhi ya Kiswahili husaidia___.

A kuwa mkalimani mzuri

B Kuokoa muda

C Kujifunza maneno ya lugha

D Kufaulu mitihani

Kujibu Maswali kutokana na Habari uliyoisoma

Ili kujibu maswali yanayotokana na habari uliyoisoma inatakiwa kuzingatia

mambo yafuatayo; kubaini mawazo makuu, kuzingatia alama za uandishi, kubaini

maana ya maneno na misemo mbalimbali na kutilia maanani vidokezo vya maana.

Page 85: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 85

Aidha mawazo yanapaswa kuelekezwa katika jambo linalosomwa, kujiuliza

maswali kadri unavyosoma na kuandika ufupisho.

ZOEZI

Vidokezi vya maana kama vile „lakini, isipokuwa na hata hivyo‟ hutumika ___

A Kutofautisha

B Kuongeza wazo

C Kuonesha mtiririko

D Kuhitimisha

Maana ya mwandishi katika habari inaweza kupotoshwa endapo msomaji

hatazingatia___

A Idadi ya maneno

B Aya

C Alama za uandishi

D Aina ya insha

Msomaji anapaswa afanye nini kadri anavyosoma ili kujibu maswali yatokanayo

na habari husika?

A Kuhesabu maneno

B Kujiuliza maswali

C Kusoma kwa sauti

D Kukaa kimya

Yafuatayo yanapaswa yazingatiwe katika usomaji ili kujibu maswali ya habari

husika, isipokuwa:

A Aina ya ufahamu

B Mawazo makuu

Page 86: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 86

C Alama za uandishi

D Vidokezi vya maana

Mbinu ipi husaidia kuelewa hitaji la swali wakati wa kujibu maswali ya habari

uliyoisoma?

A Kukosa umakini

B Kujibu kwa urefu

C Kusoma kwa makini

D Kukaa kimya

Kufupisha Habari uliyoisoma

Ili kuandika ufupisho mzuri wa habari uliyosoma yapaswa kuzingatia yafuatayo:

kuisoma habari uliyopewa zaidi ya mara moja, kubainisha mawazo makuu,

kuandika ufupisho kwa lugha fasaha na yenye mtirirko mzuri wa hoja, kuhesabu

idadi ya maneno na kuhakikisha haizidi idadi inayotakiwa na kupitia habari ya

mwanzo na kisha ufupisho ili kuona kama taarifa muhimu haijaachwa au

kusahaulika.

ZOEZI

Kutambua mawazo makuu katika habari ni sawa na ___ mawazo makuu.

A Kufafanua

B Kuandika

C Kubaini

D Kueleza

Katika ufupisho wa habari uliyoisoma ni muhimu kuonesha___.

A Maswali

B Njeo

Page 87: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 87

C Kichwa cha habari

D Nafsi

___ni kitendo cha kuifanya habari ndefu kuwa fupi na kwa maneno machache pia.

A Kubainisha mawazo

B Ufahamu

C Ufupisho

D Kufupisha habari

___hufanyika ili kuhakikisha idadi ya maneno haizidi ile inayohitajika katika

ufupisho wa habari.

A Kupitia habari yote

B Kupunguza mawazo makuu

C Kuhesabu maneno

D Kurudia habari

Kipi kati ya hivi hakitakiwi kukosa kwenye habari iliyofupishwa?

A Mawazo makuu

B Vivumishi

C Vielezi

D Maneno ya ziada

Kusoma kwa Burudani

Huu ni usomaji ambao lengo lake kuu huwa ni kujiburudisha tu. Katika usomaji

wa aina hii, msomaji hujisomea zaidi magazeti, majarida na vitabu tofauti na vile

vinavyotumika darasani.

Page 88: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 88

Wakati mwingine sio lazima msomaji awe na vitabu vyote ambavyo anahitaji

kuvisoma au magazeti na majarida. Inapotokea hivyo, msomaji anaweza kwenda

maktaba kuazima kitabu nachokihitaji.

Ingawa lengo la msomaji huwa ni kujiburudisha tu, lakini pia hujiongezea maarifa.

Hii ni kwa sababu, magazeti, majarida na vitabu sambamba na kutumia lugha

sanifu huelezea mambo mabalimbali yanayoihusu jamii.

Msomaji kutokana na kusoma vitabu na majarida mbalimbali hujiongezea kiwango

cha welewa wa lugha na mambo mengine ya kijamaii yanayojadiliwa humo.

Ni jambo zuri kwa msomaji kujijengea tabia ya kujipima ili aweze kuelewa

kiwango cha maarifa aliyopata katika kujisomea. Kujipima huku kunaweza

kufanywa kwa kujiundia utaratibu w kuweka kumbukumbu ya vitu au makala

zilizosomwa na kufanya ufupisho wa kila makala.

Utaratibu unaopendekezwa katika kujipima na kujiwekea kumbukumbu ya usomaji

wa burudani ni kama ufuatao:

1. Tarehe...

2. Jina la kitabu/makala/gazeti....

3. Mchapishaji......

4. Mwaka/tarehe ya uchapishaji.....

5. Ufupisho wa habari(yasizidi maneno 20)

6. Fundisho/ujumbe mkuu ni.....

7. Jambo lililokuvutia sana......

8. Maoni kwa ujumla kama yapo...

ZOEZI

Kupitia usomaji wa burudani msomaji huweza kuelewa kiwango cha maarifa

aliyopata kwa kuwa na tabia ya___.

Page 89: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 89

A Kukariri

B Kununua vitabu

C Kuazima vitabu

D Kujipima

Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia katika usomaji wa burudani, isipokuwa:

A Kuweka kumbukumbu

B Kuandaa vitabu au makala

C Kujiburudisha

D Kufanya ufupisho wa kinachosomwa

___ni mojawapo ya kipengele cha kujiwekea kumbukumbu katika usomaji wa

burudani.

A Mawazo makuu

B Utangulizi

C Fundisho kuu

D Kiini cha habari

___ni mahali maalumu ambapo msomaji anaweza kuazima kitabu kwa ajili ya

kujisomea kwa burudani.

A Ofisini

B Maabara

C Dukani

D Maktaba

Lipi kati ya haya ni jambo la kuzingatia katika usomaji wa burudani?

Page 90: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 90

A Kujipima

B Kujiandaa kwa mtihani

C Kujibu maswali

D Kuweka kumbukumbu

Matumizi ya Kamusi

Kamusi ni kitabu cha marejeo chenye msamiati uliokusanywa kutoka kwa

wazungumzaji wa jamii fulani na kupangwa katika utaratibu maalumu, kisha

kufafanuliwa kwa namna ambayo wasomaji wanaweza kuelewa. Au kamusi ni

orodha ya maneno yaliyo katika karatasi au nakala tepe yaliyopangwa kialfabeti na

kutolewa maana pamoja na maelezo mengine na kuhifadhiwa katika kitabu,

santuri, simu, tarakilishi au katika mfumo wowote wa kielekroniki.

Jinsi ya Kutumia Kamusi

Maneno yanayoingizwa katika kamusi hupangwa kwa utaratibu wa alfabeti.

Maneno yanayoanza na herufia, yote huwekwa chini ya herufiA. Maneno

yanayoanza na herufi fulani nayo hupangwa katika utaratibu wa alfabeti kwa

kuzingatia herufi ya pili, ya tatu, nne au tano ya neno kama mfano hapa chini

unavyoonyesha.

Mfano:ja, jabali, jabiri, jadhibika, jadi.

Maneno yote yanaanza na herufi [j]. herufi ya pili kwa maneno yote ni [a]. herufi

ya tatu ni [b] na [d]. Kwa kuwa [b] hutangulia [d] katika mpangilio wa alfabeti

maneno yenye [b] kabla ya yale yenye [d]. Kwa kuwa maneno yenye herufi [b] ni

mawili itabidi tutazame herufi ya nne ya hya maneno ili tuchague

litakaloorodheshwa mwanzo. Neno „jabali‟ litaorodhewshwa kabla ya „jabiri‟ kwa

kuwa [a] (herufi ya nne) ya „jabali‟ hutangulia [i] ya „jabiri‟ ambayo pia ni herufi

ya nne. Kisha tunatazama maneno yenye [d] kama herufi ya tatu. Hapa tunaangalia

pia herufi ya nne ili kubaini neno litakaloandikwa mwanzo kati ya „jadhibika‟ na

„jadi‟. Kwa kuwa [h] hutangulia [i] basi „jadhibika‟ huorodheshwa mwanzo ndipo

lifuatiwe na „jadi‟.

Page 91: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 91

Kwa hiyo hivi ndivyo unavyopaswa kutafuta neno kwenye kamusi. Nenda kwenye

herufi ya neno ulalotafuta alafu litafute kwa kufuata mlolongo huo huo wa herufi

ya kwanza kuorodheshwa.

Neno linaloorodheshwa kwenye kamusi ili lifafanuliwe linaitwa kidahizo.

Kidahizo huandikiwa maelezo ya kukifafanua. Maelezo haya ni matamshi ya

kidahizo, maana ya kidahizo, kategoria ya kisarufi, sentensi ya mfano wa matumizi

ya kidahizo n.k. Kidahizo pamoja na maelezo yake ndio huitwakitomeocha

kamusi.

Kutafuta maana unayoitaka

Neno linaweza kuwa na maana moja au zaidi ya moja. Maana inapokuwa moja

mtumiaji kamusi hana tatizo kwani hiyo ndiyo atakayoipata na kuichukua. Lakini

neno linapokuwa na maana zaidi ya moja, mtumiaji kamusi hutatizika asijue ni ipi

aichague. Ili kupata maana inayosadifu itafaa mtumiaji kamusi kutafuta maana

ambayo inahusiana na muktadha wa neno linalotafutwa.

Mfano:kifungonm vi-

kitu cha kufungia

kitu kinachotumiwa kufungia vazi kama vile shati, gauni, suruali n.k

adhabu ya mtu kuwekwa jela kwa muda fulani

Iwapo mtumiaji aliona neno „kifungo‟ kwa muktadha wa: “Juma alihukumiwa

kifungo cha miaka kumi baada ya kupatikana na hatia ya kubaka….” Maana ya

mukatadha huu itakuwa ni ile maana ya 3 kwa sababu ndiyo yenye kuhusiana na

muktadha ambapo neno kifungo limetumika na wala sio maana ya 1 wala ya 2.

ZOEZI

Neno lipi kati ya haya yafuatayo linatangulia kuorodheshwa katika kamusi?

A Mdukuzi

B Mdubiri

C Mdoya

Page 92: MADA YA 1 UUNDAJI WA MANENO€¦ · ___ni kazi ya mofimu {mi-} katika nomino „miji‟. A Kuonesha njeo B Kuonesha wingi C Kuonesha urejeshi ... mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi

KIDATO CHA PILI 2019

Maeda T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 92

D Mdumizi

Maneno katika kamusi hupangwa katika utaratibu wa___

A Namba

B Herufi

C Alfabeti

D Kategoria

___ni alfabeti ambayo haina maneno katika kamusi ya Kiswahili.

A Alfabeti T

B Alfabeti X

C Alfabeti Z

D Alfabeti Y

Neno “wanacheza” hupatikana katika kamusi kwa kuangalia ___.

A Alfabeti

B Viambishi awali

C Shina la neno

D Viambishi tamati

Neno unganifu katika kamusi linahesabiwa kama___

A Maneno matatu

B Neno moja

C Maneno manne

D Maneno mawili