96

Click here to load reader

Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

a

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA

MAENDELEO YA KILIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU

WA TANZANIA BARA (1961 - 2011)

KILIMO KWANZA“Tumethubutu, Tumeweza, Tunazidi Kusonga Mbele”

kilimo miaka 50.indd akilimo miaka 50.indd a 11/16/11 10:34:23 AM11/16/11 10:34:23 AM

Page 2: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

b

kilimo miaka 50.indd bkilimo miaka 50.indd b 11/16/11 10:34:23 AM11/16/11 10:34:23 AM

Page 3: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

i

KAULI YA WAZIRIKwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyenzi Mungu kwa kunipa uhai na kuniwezesha kuungana na Watanzania wenzangu katika maadhimisho haya ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Katika kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa nchi yetu, hatuna budi kuwakumbuka waasisi na viongozi wa Taifa letu ambao wametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya kilimo tunachojivunia leo. Tangu Uhuru wa Tanzania Bara upatikane nchi yetu imepitia awamu nne za uongozi. Awamu ya kwanza iliongozwa na Baba wa Taifa na Rais wa Kwanza Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alikuwa mstari wa mbele na mhimili mkubwa

wa kuwaongoza Watanzania katika kudai Uhuru na hatimaye kuupata hapo Desemba 9, 1961. Mara baada ya nchi yetu kupata Uhuru, Serikali ilitoa kipaumbele cha kwanza katika kuendeleza kilimo kama uti wa mgongo wa uchumi wetu. Kilimo kiliajiri zaidi ya asilimia 90 ya wananchi wote na mazao ya katani, kahawa na pamba yaliongoza kulipatia Taifa fedha za kigeni. Hivyo ilibidi kilimo kiendelezwe kwa kutumia mbinu mbalimbali za kisiasa, kijamii na kiuchumi. Kati ya miaka ya 1961 na 1980, zilibuniwa kaulimbiu na maazimio mbalimbali kama vile “Chakula ni Uhai”, “Siasa ni Kilimo”, “Kilimo cha Kufa na Kupona”, “Mvua za Kwanza ni za Kupandia” ili kuhamasisha maendeleo ya kilimo, pamoja na kuhamasisha kilimo cha ujamaa. Awamu ya Pili iliongozwa na Rais Ali Hassan Mwinyi ambapo tulishuhudia mageuzi ya kiuchumi ambayo yalikuwa kichocheo kikubwa katika maendeleo ya kilimo ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa Sera ya Kilimo ya mwaka 1983. Awamu ya tatu ya uongozi ilikuwa chini ya Rais Benjamin William Mkapa ambapo katika awamu hiyo kilimo kilipata msukumo wa kipekee na kuwa chenye mafanikio. Katika awamu hiyo utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Kilimo na Mifugo ya mwaka 1997 na uanzishwaji wa Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo ulishuhudia kilimo kikikua kutoka chini ya asilimia 3 hadi asilimia 6. Awamu ya nne ya uongozi ambayo ipo chini ya Rais Daktari Jakaya Mrisho Kikwete, kilimo kimeendelea kupewa kipaumbele kikubwa, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP) na Programu ya Mageuzi na Modenaizesheni ya Ushirika (CRMP) ambazo zimekuwa chachu ya kuleta mapinduzi ya kijani hapa nchini. Jambo kubwa la kujivunia kutokana na kilimo ni kuwa kwa sasa asilimia 95 ya mahitaji ya Taifa ya chakula kinazalishwa hapa hapa nchini. Aidha, Serikali imeweka mfumo wa kuhifadhi chakula kwa ajili ya matumizi wakati upungufu unapotokea. Akiba ya Taifa ya Chakula imekuwa ikiongezeka kila mwaka na uwezo wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula unatarajia kufi kia tani 400,000

kilimo miaka 50.indd Sec2:ikilimo miaka 50.indd Sec2:i 11/16/11 10:34:24 AM11/16/11 10:34:24 AM

Page 4: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

ii

ifi kapo mwaka 2015 kutoka uwezo wa kununua na kuhifadhi tani 150,000 mwaka 2009. Aidha, mikakati mbalimbali inaendelea kutekelezwa hususan kuongeza eneo la kilimo cha umwagiliaji, matumizi ya zana bora za kilimo na kuongeza upatikanaji wa pembejeo zinazohitajika katika kuongeza uzalishaji na tija. Katika Miaka 50 ya Uhuru wa nchi yetu, pamoja na kuwa na changamoto nyingi za kisiasa, kijamii na kiuchumi, kilimo chetu kimeendelea kuwa nguzo kuu na mhimili wa Uchumi wa Taifa letu. Hivyo, tunapoadhimisha Miaka 50 ya Uhuru tunayo sababu ya kwenda kifua mbele tukiwa na kaulimbiu yetu inayosema KILIMO KWANZA- “Tumethubutu, Tumeweza, Tunazidi Kusonga Mbele”. Kutokana na uzoefu tulioupata kwa miaka 50, napenda kuwahakikishia Watanzania kuwa tutasonga mbele kwa haraka, tujitosheleze kwa chakula na tuwe wazalishaji wakubwa wa mazao ya chakula na biashara, tutakaotegemewa na majirani zetu wa EAC, SADC na soko la kimataifa. Katika miaka 50 ijayo vizazi vyetu vitajivunia Taifa tajiri linalojitegemea kiuchumi, kijamii na lenye nguvu za kisiasa hapa duniani.

Profesa Jumanne A. Maghembe (Mb.)WAZIRI WA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA

kilimo miaka 50.indd Sec2:iikilimo miaka 50.indd Sec2:ii 11/16/11 10:34:25 AM11/16/11 10:34:25 AM

Page 5: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

iii

MUHTASARI

Mwaka huu wa 2011, nchi yetu inaadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara uliopatikana tarehe 9 Desemba, 1961 kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza. Katika kuadhimisha miaka hiyo 50 tangu Uhuru, juhudi mbalimbali zimefanyika na zinaendelea kufanyika ili kuendeleza sekta ya kilimo. Juhudi hizo ni pamoja na tafi ti mbalimbali za kilimo, huduma za ugani, mafunzo ya wataalam, mafunzo ya wakulima, ujenzi wa miundombimu ya umwagiliaji, mipango ya matumizi bora ya ardhi, matumizi ya zana bora na maendeleo ya ushirika. Muundo wa Wizara inayosimamia sekta ya kilimo umekuwa ukibadilika katika vipindi tofauti kukidhi mahitaji ya kipindi husika. Kiuongozi, kuanzia mwaka 1961 mpaka sasa (2011), Wizara imeongozwa na Mawaziri 16 na Naibu Mawaziri 8 (Jedwali Na. 1). Waziri wa kwanza aliyeongoza Wizara alikuwa Mheshimiwa Dereck Bryceson. Kwa sasa (2011) Wizara inaongozwa na Mheshimiwa Profesa Jumanne Maghembe na Naibu Waziri Mheshimiwa Injinia Christopher Chiza. Katibu Mkuu wa kwanza wa Wizara alikuwa Bwana Ibrahim Sapi Mkwawa. Tangu Uhuru hadi sasa (2011), Wizara inayosimamia kilimo imeongozwa na Makatibu Wakuu 22 na Naibu Makatibu Wakuu sita. Katibu Mkuu wa Wizara wa sasa (2011) ni Bwana Mohamed S. Muya akiwa na Naibu Makatibu Wakuu wawili ambao ni Bibi Sophia Kaduma na Injinia Mbogo Futakamba. Katika muundo wa sasa Wizara ina Idara 10 ambazo ni Utafi ti na Maendeleo; Mafunzo; Maendeleo ya Mazao; Matumizi Bora ya Ardhi; Zana za Kilimo; Umwagiliaji na Huduma za Ufundi; Sera na Mipango; Utawala na Rasilimali Watu; Usalama wa Chakula; na Maendeleo ya Ushirika. Pia, Wizara ina vitengo nane ambavyo ni Sheria; Fedha na Uhasibu; Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) , Ukaguzi wa Ndani; Usajili wa Haki Miliki za Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu; Mawasiliano Serikalini; Mazingira; na Ugavi na Manunuzi. Vilevile, Wizara ina wakala, mamlaka na taasisi tisa na inasimamia bodi tisa za mazao. Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika ina majukumu ya kuhakikisha Taifa linajitosheleza kwa chakula na kwamba kilimo kinatoa mchango mkubwa katika uchumi na katika kuondoa umaskini. Katika kuhakikisha kwamba hayo yanatekelezwa, Wizara inaongozwa na Dira pamoja na Dhamira ya kutoa huduma bora za kilimo na ushirika, kujenga uwezo wa Serikali za mitaa, na kuweka mazingira mazuri kwa wadau na sekta binafsi ili kuchangia ipasavyo katika uzalishaji wenye tija kwa maendeleo endelevu ya kilimo na ushirika. Ndani ya kipindi cha Miaka 50 ya Uhuru yamekuwepo mabadiliko ya sera na mikakati ambayo yamekuwa yakianzishwa ili kutekeleza azma ya Serikali ya kuinua uchumi wa nchi kupitia sekta ya kilimo. Mabadiliko makuu ya sera yalitokea baada ya kutangazwa kwa Azimio la Arusha la mwaka 1967 lililosisitiza Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ambalo katika utekelezaji wake kaulimbiu mbalimbali zilibuniwa. Kaulimbiu hizo ni pamoja na Azimio la Iringa la “Siasa ni Kilimo” la mwaka 1972 lililosisitiza uanzishwaji wa mashamba makubwa ya vijiji yatakayoendeshwa kwa

kilimo miaka 50.indd Sec2:iiikilimo miaka 50.indd Sec2:iii 11/16/11 10:34:25 AM11/16/11 10:34:25 AM

Page 6: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

iv

kutumia zana bora, wanyamakazi na kilimo cha umwagiliaji. Azimio hilo lilifuatiwa na Operesheni Vijiji ambayo ilikuwa na lengo la kuwaweka wananchi pamoja ili wapate huduma muhimu kama vile maji, elimu na afya. Operesheni Vijiji kwa upande wa sekta ya kilimo iliambatana na kuanzishwa kwa mashamba makubwa ya vijiji na mashamba ya bega kwa bega. Mwaka 1974 ilizinduliwa “Kampeni ya Kilimo cha Kufa na Kupona” ambayo ililenga kuongeza uzalishaji wa chakula katika ngazi ya Kaya. M a z i n g i r a mbalimbali ya kiuchumi na kijamii yaliyoipata nchi yetu mwishoni mwa miaka ya 70 yalichangia kutofi kiwa kwa baadhi ya malengo ya kuimarisha kilimo kama ilivyotarajiwa. Hivyo, mwaka 1982 Serikali iliagiza ufanyike uchambuzi wa kubaini upungufu wa kisera uliosababisha kutofi kiwa kwa malengo ya kujitosheleza kwa chakula. Uchambuzi huo uliwezesha upatikanaji wa sera ya kwanza ya kilimo ya mwaka 1983 ambayo ililenga katika kuhakikisha upatikanaji wa chakula katika ngazi ya kaya na kuboresha kiwango cha lishe na maisha ya Watanzania. Sera hiyo ilifanyiwa marekebisho na kuunganishwa na sera ya mifugo na kupatikana kwa Sera ya Kilimo na Mifugo ya mwaka 1997 ambayo pia imefanyiwa marekebisho na ikishapitishwa itajulikana kama Sera ya Taifa ya Kilimo ya mwaka 2009. Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDS) wa mwaka 2001, ambao unatekelezwa kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP) kuanzia mwaka 2006, ikiwa na malengo makubwa mawili ambayo ni (i) Kuwawezesha wakulima na wafugaji kuongeza uzalishaji na tija (ii) Kujenga mazingira bora ya kisera na kisheria ili kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi katika kilimo. Azimio la Kilimo Kwanza na Programu Kabambe ya Kuendeleza Kilimo Afrika (Comprehensive Africa Agriculture Development Program –CAADP) inalenga kuongeza rasilimali ili kuleta mapinduzi ya kilimo kwa kasi zaidi. Aidha, katika kuendeleza ushirika Sera ya kwanza ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania ilipitishwa mwaka 1997 kwa ajili ya kutoa malengo ya jumla na mikakati muhimu kuhakikisha kwamba makundi ya watu maskini katika jamii yanakuwa na chombo cha kuaminika cha kuwezesha kufi kia malengo yake ya kiuchumi na kijamii. Sera ya Maendeleo ya Ushirika ya mwaka 2002 ilipitishwa, ili kuzingatia upungufu uliotokana na Sera ya Maendeleo ya Ushirika ya mwaka 1997. Sera hiyo inatekelezwa kupitia Programu Kabambe ya Mageuzi na Modenaizesheni ya Ushirika (CRMP) na Sheria ya Vyama vya Ushirika Na.20 ya mwaka 2003. Mwaka 2010, Serikali ilikamilisha utayarishaji wa Sera ya Taifa ya Umwagiliaji inayoweka dira na mwelekeo katika kuendeleza kilimo cha umwagiliaji nchini. Sera hiyo pia inatoa mwongozo utakaowezesha kuharakisha uwekezaji na usimamizi thabiti katika kilimo cha umwagiliaji, kuleta ufanisi katika kuendeleza miundombinu ya umwagiliaji, kutoa fursa kwa sekta binafsi kutoa huduma na kuwekeza katika umwagiliaji, kuhakikisha matumizi bora na endelevu ya rasilimali ya maji na kuainisha majukumu ya Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, sekta binafsi na Taasisi mbalimbali katika kufanikisha uendelezaji wa kilimo cha umwagiliaji nchini. Mafanikio yaliyopatikana ni kuwa, kilimo kinaendelea kukua kila mwaka tangu

kilimo miaka 50.indd Sec2:ivkilimo miaka 50.indd Sec2:iv 11/16/11 10:34:25 AM11/16/11 10:34:25 AM

Page 7: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

v

Uhuru na kinaendelea kuchangia katika uchumi na kuondoa umaskini. Katika kipindi cha miaka 50 iliyopita vituo vya utafi ti wa kilimo vimezalisha teknolojia mbalimbali za kilimo kwa lengo la kuongeza uzalishaji, tija na kipato kwa mkulima na Taifa kwa ujumla. Hiyo ni pamoja na ubunifu na utoaji wa mbegu bora za mazao mbalimbali ya biashara, chakula, mboga na matunda zenye sifa ya kutoa mavuno mengi na bora, kustahimili ukame, kukomaa haraka na zenye ukinzani dhidi ya magonjwa. Mbegu hizo ni pamoja na aina 33 za mahindi, 21 maharage, 20 pamba, 18 mpunga, 16 korosho, 15 kahawa, 13 muhogo, 13 ngano, 12 ufuta, 11 karanga, 6 viazi vitamu na 7 mtama. Mbegu nyingine ni aina 7 mboga za asili, 5 viazi mviringo, 5 shayiri, 4 kunde, 4 dengu, 3 mbaazi, 6 nyanya, 2 choroko, 2 uwele, 2 soya, 3 miwa, 2 zabibu, 1 alizeti, 1 tumbaku, 7 parachichi, 6 migomba, 5 kabichi, 4 vitunguu na 4 mafyurisi. Utoaji wa aina tofauti za mbegu bora za mazao unaenda sambamba na utoaji wa teknolojia husishi za mbinu za kilimo bora zilizofanyiwa utafi ti wa ukuzaji wa mazao hayo. Pia, kila mwaka vituo vya utafi ti huzalisha mbegu ya awali (breeders’ seed) ya aina bora za mbegu zilizotolewa ambazo hupelekwa kwa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kwa uzalishaji zaidi ili kuwafi kia wakulima. Idadi ya wataalam wa fani mbalimbali za kilimo imeongezeka kwa kiwango kikubwa tangu Uhuru. Kwa mfano, idadi ya watafi ti wazalendo katika kituo cha mafunzo na utafi ti cha KATRIN kilichoanzishwa mwaka 1963, wameongezeka kwa asilimia 500 na watafi ti wasaidizi kwa asilimia 1000. Mafanikio katika upande wa mafunzo, ni ongezeko la idadi ya vyuo vya kilimo na wahitimu. Mwaka 1961, ni chuo kimoja tu kilikuwa kinatoa mafunzo ya muda mrefu ngazi ya Stashahada. Miaka 50 baada ya Uhuru (2011) vyuo 14 vina uwezo wa kutoa mafunzo hayo katika fani/michepuo mitano (5) tofauti. Tangu mwaka 1995 hadi Novemba, 2010 vijana 7,604 walihitimu mafunzo ya miaka miwili ngazi ya Stashahada na Astashahada. Hiyo inaenda sambamba na ongezeko la idadi ya wakulima waliopatiwa mafunzo katika vyuo vya kilimo, uboreshaji wa mitaala ya kufundishia, kuandaliwa kwa maandiko nane ya rejea, kukarabatiwa kwa miundombinu ya vyuo na mafunzo kutolewa kwa kuzingatia vigezo vya ubora vilivyoainishwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE). Katika Miaka 50 ya Uhuru kumekuwa na mafanikio ya kuridhisha katika kuongeza upatikanaji na matumizi ya zana bora za kilimo hapa nchini. Jitihada hizo zimelenga kupunguza matumizi ya jembe la mkono na kupunguza harubu inayotokana na zana duni za kilimo. Maksai wanaotumika katika kilimo wamekuwa wanaongezeka kutoka 320,000 mwaka 1970 hadi kufi kia 1,542, 000 mwaka 2010, ambapo majembe yanayokokotwa na maksai yaliongezeka kutoka 140,000 hadi kufi kia 620,000 katika kipindi hicho. Trekta kubwa zinazotumika katika kilimo zimeongezeka kutoka 2,580 mwaka 1960 hadi kufi kia 7,823 mwaka 2010. Aidha, Serikali inatoa mikopo yenye masharti nafuu kupitia Mfuko wa Pembejeo (AGITF) na dirisha dogo la kilimo katika Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) kwa ajili ya kuwawezesha wakulima kupata zana bora za kilimo. Kuanzia mwaka 2003 hadi Mei, 2011 jumla ya trekta kubwa 671 na trekta ndogo za mkono 212 zenye thamani ya shilingi bilioni 23.34 zilikopeshwa kwa wakulima kupitia Mfuko wa Pembejeo.

kilimo miaka 50.indd Sec2:vkilimo miaka 50.indd Sec2:v 11/16/11 10:34:25 AM11/16/11 10:34:25 AM

Page 8: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

vi

Kuhusu matumizi bora ya ardhi na hifadhi ya mazingira, wakulima wadogo katika maeneo ya nyanda za juu wameweza kutumia kilimo kinachozingatia hifadhi ya udongo na maji mashambani. Kwa mfano wakulima wa maeneo ya Wilaya za Moshi, Hai na Rombo wameweza kuongeza uzalishaji wa mahindi shambani kutoka tani 1.3 hadi tani 2.6 kwa hekta, alizeti toka tani 0.6 hadi tani 1.1 kwa hekta na maharage toka tani 0.7 hadi tani 1.2 kwa hekta. Aidha, sera, mikakati, sheria na kanuni za usimamizi wa mazingira ya kilimo zimeendelea kutekelezwa kwa mafanikio. Tangu Uhuru mazao makuu ya biashara kama chai, pamba, kahawa, tumbaku, mkonge, korosho, sukari na pareto yamekuwa na mchango mkubwa kwa Taifa hasa katika kuliingizia pato la fedha za kigeni na ajira (mashambani na viwandani). Uzalishaji wa mazao hayo umekuwa ukipanda na kushuka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, mabadiliko ya kisera, upatikanaji wa pembejeo na mabadiliko ya bei katika soko la dunia. Kuhusu mazao ya chakula yakijumuisha yale ya nafaka, mbegu za mafuta na bustani uzalishaji wake umekuwa ukipanda kila mwaka isipokuwa zao la ngano. Hivyo, hali ya chakula imeendelea kuwa ya kuridhisha ambapo katika miongo minne iliyopita nchi iliweza kujitosheleza kwa chakula kwa kati ya asilimia 88 hadi asilimia 111. Kuhusu mazao ya bustani, thamani ya mauzo ya nje imeongezeka kutoka dola milioni 19.1 mwaka 2007 hadi dola milioni 32.2 mwaka 2008, sawa na ongezeko la asilimia 68.4. Akiba ya chakula ya Taifa imeendelea kutumika kupunguza makali ya njaa katika maeneo yaliyoathirika na ukame na upungufu wa chakula. Katika mwaka 2010/2011 Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umefanikiwa kwa kiwango kikubwa kununua mahindi ya ziada kutoka kwa wakulima ambapo kiasi cha tani 180,964.082 zimenunuliwa ikiwa ni asilimia 90.5 ya lengo la kununua tani 200,000. Kutokana na jitihada hizo akiba ya Taifa ya Chakula hadi tarehe 30 Juni, 2011 ni tani 228,713.8. Kuhusu kilimo cha umwagiliaji, eneo linalomwagiliwa limeongezeka kutoka hekta 2,600 mwaka 1970 hadi hekta 345,690 mwaka 2011. Aidha, uzalishaji na tija wa mazao (hasa Mpunga) katika skimu za umwagiliaji umeongezeka. Kwa mfano, uzalishaji wa mpunga kwa skimu za Lower Moshi na Ndungu umeongezeka kutoka tani 3 hadi 7 kwa hekta (Kielelezo Na.8). Hali ya ushirika nchini imeendelea kuimarika kutokana na utekelezaji wa CRMP. Idadi ya wanachama wa Vyama vya Ushirika imeongezeka kutoka milioni 1.8 mwaka 2009 hadi milioni 2.1 mwaka 2010. Idadi ya Vyama vya Ushirika wa Mazao imeongezeka kutoka 2,616 mwaka 2006 hadi vyama 2,821 mwaka 2009. Aidha, kumekuwepo ongezeko la idadi ya Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo (SACCOS), kutoka 1,876 mwaka 2006 hadi 5,344 mwaka 2010. Idadi ya wanachama wa SACCOS nayo imeongezeka kutoka 820,670 hadi 911,873 katika kipindi hicho. Vilevile katika kipindi hicho, hisa za wanachama ziliongezeka kutoka shilingi bilioni 33.5 hadi shilingi bilioni 36.7, akiba na amana za wanachama nazo ziliongezeka kutoka shilingi bilioni 148.1 hadi shilingi bilioni 176.6, mikopo iliyotolewa kwa wanachama nayo iliongezeka kutoka shilingi bilioni 383.5 hadi shilingi bilioni 463.4. Mikopo hiyo ilikuwa kwa ajili ya mitaji

kilimo miaka 50.indd Sec2:vikilimo miaka 50.indd Sec2:vi 11/16/11 10:34:25 AM11/16/11 10:34:25 AM

Page 9: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

vii

ya biashara, kilimo, ufugaji, ujenzi wa nyumba, karo za shule, ununuzi wa trekta ndogo za mkono (power tillers) na kubwa. Aidha, vyama vya ushirika vimeimarika kibiashara na vimeweza kuchangia katika maendeleo ya jamii. Pamoja na jitihada za Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo, kilimo bado kinakabiliwa na changamoto nyingi ambazo hazinabudi kupangiwa mikakati mipya ya kufanikisha azma ya kuleta mapinduzi ya kijani nchini. Tangu nchi yetu ipate Uhuru kilimo kimekabiliwa na changamoto zifuatazo.i. Mabadiliko ya mara kwa mara ya miundo ya taasisi za sekta ya kilimo ii. Ardhi ya kilimo kutotambulika kisheria hivyo kubadilishwa matumiziiii. Upungufu wa rasilimaliiv. Mabadiliko ya tabianchiv. Ushiriki hafi fu wa sekta binafsi katika kilimovi. Ushiriki hafi fu wa vijana katika kilimovii. Kupungua kwa nguvu kazi kutokana na maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI

(VVU) na ugonjwa wa UKIMWIviii. Uwezo mdogo wa wakulima kununua zana bora na pembejeo za kilimoix. Miundombinu duni katika maeneo ya uzalishaji wa mazao ya kilimox. Kiwango kidogo cha usindikaji wa bidhaa za kilimoxi. Msukumo wa kuzalisha mazao ya nishati mbadala na madhara yake unakinzana na

lengo kuu la kuzalisha mazao ya chakulaxii. Gharama kubwa ya ujenzi wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliajixiii. Matumizi madogo ya teknolojia sahihi na za kisasa kwa wakulima walio wengixiv. Uvamizi wa visumbufu vya mimea xv. Vyama vya ushirika kukosa mitajixvi. Elimu duni ya ushirikaxvii. Usimamizi hafi fu wa sera ya soko huruxviii. Idadi ndogo ya wataalam wa kilimo na ushirikaxix. Kukosekana kwa mikopo yenye masharti nafuu ya kuendeleza kilimo Mwelekeo katika kipindi cha miaka 50 ijayo (2011-2061) umejikita katika kuendelea kutekeleza majukumu ya Wizara kupitia mipango na mikakati iliyopo na inayotarajiwa kubuniwa ili kilimo pamoja na ushirika viweze kutoa mchango unaotarajiwa katika harakati za kufi kia malengo ya Maendeleo ya Milenia, Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini (MKUKUTA II) na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025. Mwelekeo umejikita katika maeneo ya kimkakati yafuatayo:-i. Kuongeza uzalishaji na tija katika sekta ya kilimoii. Kuimarisha upatikanaji wa masoko ya bidhaa za kilimoiii. Kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na kuboresha mfumo wa masokoiv. Kuendelea kuboresha uwezo wa Wizara kutoa huduma za kilimov. Kuimarisha sera, mikakati na usimamizi katika sekta ya kilimovi. Kuboresha uratibu katika sekta ya kilimovii. Kuzingatia masuala mtambuka katika kilimo na ushirika

kilimo miaka 50.indd Sec2:viikilimo miaka 50.indd Sec2:vii 11/16/11 10:34:25 AM11/16/11 10:34:25 AM

Page 10: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

viii

viii. Kuimarisha mawasiliano ya habari za kilimo na serikali mtandaoix. Kuboresha huduma na kupunguza maambukizi ya VVU/UKIMWIx. Kuimarisha na kuwezesha asasi za wananchi katika kilimoxi. Kuimarisha mfumo wa ukusanyaji, uchambuzi, na usambazaji wa takwimu na

taarifa za vyama vya ushirika na kilimo.

kilimo miaka 50.indd Sec2:viiikilimo miaka 50.indd Sec2:viii 11/16/11 10:34:25 AM11/16/11 10:34:25 AM

Page 11: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

ix

MAANA YA VIFUPISHOAGITF Mfuko wa PembejeoASA Wakala wa Mbegu za KilimoASARECA Chama cha Kuendeleza Kilimo katika nchi za Mashariki na

kati mwa AfrikaASDP Programu ya Kuendeleza Sekta ya KilimoASDS Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya KilimoCAADP Programu Kabambe ya Kuendeleza Kilimo AfrikaCAT Mamlaka ya Kahawa TanzaniaCBD Mkataba wa Kimataifa wa Kuhifadhi BioanuaiCOASCO Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya UshirikaCORDEMA Mfumo wa Kushughulikia Mahitaji ya WatejaCRDB Benki ya Ushirika na Maendeleo VijijiniCRMP Programu Kabambe ya Mageuzi na Modenaizesheni ya

UshirikaDADPs Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya WilayaDIDF Mfuko wa Kuendeleza Umwagiliaji Ngazi ya WilayaDRD Idara ya Utafi ti na MaendeleoDRT Idara ya Utafi ti na MafunzoEAAFRO Taasisi ya Utafi ti wa Kilimo na Misitu ya Afrika MasharikiEAC Jumuiya ya Afrika MasharikiFARA Jukwa la Utafi ti wa Kilimo AfrikaGAPEX Shirika la Kuuza Nje Mazao ya KilimoHODECT Baraza la Kuendeleza Mazao ya Bustani TanzaniaKATC Kituo cha Mafunzo ya Kilimo cha KilimanjaroKATRIN Kituo cha Utafi ti na Mafunzo cha KilomberoLAMP Mradi wa Hifadhi ya Ardhi BabatiMATI Chuo cha Mafunzo cha Wizara ya KilimoMKUKUTA Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kuondoa UmaskiniNACTE Baraza la Taifa la Elimu ya UfundiNAEP Programu ya Kuimarisha Huduma za UganiNAFCO Shirika la Taifa la Kilimo na ChakulaNALERP Mradi wa Taifa wa Kuboresha Huduma za Ugani katika

Kilimo na MifugoNAPB Bodi ya Mazao ya KilimoNBC Benki ya Taifa ya BiasharaNDC Shirika la Maendeleo ya TaifaNFRA Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya ChakulaNIDF Mfuko wa Kuendeleza Umwagiliaji Ngazi ya TaifaNIDP Mpango wa Kitaifa wa Kuendeleza UmwagiliajiNIMP Mpango Kabambe wa Taifa wa Umwagiliaji

kilimo miaka 50.indd Sec2:ixkilimo miaka 50.indd Sec2:ix 11/16/11 10:34:25 AM11/16/11 10:34:25 AM

Page 12: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

x

NMB Benki ya Taifa ya Wananchi Wenye Kipato cha Chini NMC Shirika la Usagishaji la TaifaOTC Vituo vya Kufundishia WanyamakaziPPP Ubia kati ya Serikali na Sekta binafsiRUBADA Mamlaka ya Kuendeleza Bonde la Mto Rufi jiSADC Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi kwa nchi za Kusini mwa

AfrikaSACCOS Vyama vya Ushirika vya Akiba na MikopoSAGCOT Mradi wa Ukanda wa Kilimo wa Kusini mwa TanzaniaSCAPA Mradi wa Hifadhi ya Udongo na Kilimo - Mseto ArushaSECAP Mradi wa Hifadhi ya Mmomonyoko wa udongo na Kilimo

- Mseto LushotoSGR Hifadhi ya Chakula ya TaifaSUDECO Shirika la Maendeleo ya SukariTaCRI Taasisi ya Utafi ti wa Kahawa TanzaniaTAHA Chama cha Wakulima wa Mazao ya Bustani TanzaniaTALIRO Taasisi ya Utafi ti wa Mifugo TanzaniaTANITA Kampuni ya Kusindika KoroshoTANRICE Kituo Mahiri cha Utafi ti wa MpungaTANSEED Kampuni ya Mbegu TanzaniaTARO Taasisi ya Utafi ti wa Kilimo TanzaniaTCMB Bodi ya Masoko ya KahawaTDV Dira ya Maendeleo ya TaifaTEHAMA Teknolojia ya Habari na MawasilianoTFC Kampuni ya Mbolea TanzaniaTORITA Taasisi ya Utafi ti wa Tumbaku TanzaniaTOSCI Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa MbeguTPRI Taasisi ya Utafi ti wa Viuatilifu Ukanda wa KitropikiTRAMA Kampuni ya Kuunganisha Trekta TanzaniaTRIT Taasisi ya Utafi ti wa Chai TanzaniaTTPM&B Bodi ya Usindikaji na Mauzo ya TumbakuUAC Shirika la Kilimo UyoleWFP Shirika la Mpango wa Chakula Duniani

kilimo miaka 50.indd Sec2:xkilimo miaka 50.indd Sec2:x 11/16/11 10:34:25 AM11/16/11 10:34:25 AM

Page 13: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

xi

YALIYOMO1. UTANGULIZI ........................................................................................ 1 2. HISTORIA YA WIZARA ......................................................................... 2 2.1 Muundo na Majukumu ya Wizara .................................................... 2 2.1.1 Dira .................................................................................... 2 2.1.2 Dhamira ............................................................................ 2 2.1.3 Majukumu ......................................................................... 3 2.2 Mabadiliko ya Uongozi na Utawala ................................................ 53. SERA, MIKAKATI, PROGRAMU NA SHERIA ..................................... 9 3.1 Sera za Kilimo ................................................................................... 9 3.2 Sera za Ushirika ............................................................................... 9 3.3 Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo ....................................... 10 3.4 Programu za Kuendeleza Kilimo na Ushirika .................................. 10 3.4.1 Programu ya Kuendeleza Kilimo (ASDP) ......................... 10 3.4.2 Programu Kabambe ya Mageuzi ya Ushirika ..................... 10 3.5. Maazimio na Kaulimbiu za Kuhamasisha Kilimo ........................... 11 3.6 Sheria za Kilimo na Ushirika ........................................................... 124. HUDUMA ZA KILIMO ........................................................................ 14 4.1 Kufanya Utafi ti wa Kilimo ............................................................... 14 4.1.1 Hali ya Utafi ti Kabla ya Uhuru ........................................ 14 4.1.2 Hali ya Utafi ti wa Kilimo Baada ya Uhuru ....................... 14 4.1.3 Majukumu Makuu ya Utafi ti wa Kilimo .......................... 15 4.2 Kutoa Mafunzo ya Kilimo ................................................................. 17 4.2.1 Uboreshaji Vyuo vya Mafunzo ......................................... 17 4.3 Kuboresha Ushauri na Elimu kwa Wakulima .................................. 18 4.4 Kuimarisha Udhibiti wa Visumbufu vya Mazao na Mimea ............. 18 4.5 Kuongeza Uzalishaji wa Mazao ya Biashara .................................... 19 4.5.1 Mkonge ............................................................................ 20 4.5.2 Chai ................................................................................. 20 4.5.3 Pamba ................................................................................. 20 4.5.4 Sukari ............................................................................... 21 4.5.5 Tumbaku ............................................................................. 21 4.5.6 Korosho .............................................................................. 21 4.5.7 Kahawa ............................................................................. 22 4.5.8 Pareto ................................................................................... 22 4.6 Kuongeza Uzalishaji wa Mazao ya Chakula, Mbegu za Mafuta na Mazao ya Bustani ........................................................... 23 4.7 Kusimamia Upatikanaji wa Pembejeo za Kilimo ............................ 23 4.7.1 Uzalishaji na Usambazaji wa Mbegu Bora ...................... 23 4.7.2 Mbolea .............................................................................. 24 4.7.3 Ruzuku ya Pembejeo ......................................................... 24 4.8 Kuongeza Uhakika na Usalama wa Chakula ................................... 24

kilimo miaka 50.indd Sec2:xikilimo miaka 50.indd Sec2:xi 11/16/11 10:34:26 AM11/16/11 10:34:26 AM

Page 14: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

xii

4.9 Kusimamia Akiba ya Chakula ya Taifa ............................................. 25 4.10 Kuimarisha Matumizi Bora ya Ardhi ya Kilimo .............................. 25 4.11 Kuongeza Matumizi ya Zana Bora za Kilimo .................................. 27 4.12 Kuongeza Matumizi ya Kilimo cha Umwagiliaji ............................. 28 4.12.1 Kilimo cha Umwagiliaji Kabla ya Miaka ya 1990 .............. 28 4.12.2 Kilimo cha Umwagiliaji Kuanzia Miaka ya 2000 ............. 295. MAENDELEO YA USHIRIKA ............................................................... 30 5.1 Maendeleo ya Ushirika kabla ya Uhuru ........................................... 30 5.2. Maendeleo ya Ushirika Baada ya Uhuru ......................................... 30 5.3 Maendeleo ya Ushirika katika Mfumo wa Soko Huru .................... 30 5.3.1 Kuimarisha Nguvu za Kiuchumi za Vyama vya Ushirika ........................................................................ 31 5.3.2 Kuangalia Mfumo wa Vyama vya Ushirika Nchini .......... 31 5.3.3 Uchaguzi wa Viongozi na Maadili .................................... 31 5.3.4 Kufuatilia Kesi za Ushirika ............................................... 31 5.3.5 Kutambua Vikundi Vidogo Vidogo (Pre-Cooperatives) .... 31 5.3.6 Mabadiliko Katika Sheria Nyingine Za Nchi ..................... 31 5.3.7 Kuendana na Programu ya Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa ........................................................... 316. MAFANIKIO YA KILIMO NA USHIRIKA .............................................. 32 6.1 Kilimo kimeendelea Kukua na Kuchangia katika uchumi .............. 32 6.2 Kuongezeka kwa Teknolojia za Kilimo Kutokana na Utafi ti ......... 32 6.2.1 Utafi ti wa Mazao ............................................................ 32 6.2.2 Utafi ti wa Udongo ............................................................ 36 6.2.3 Teknolojia na Masuala Mtambuka ................................... 37 6.2.4 Uenezaji wa Matokeo ya Utafi ti .......................................... 38 6.3 Kuongezeka kwa Wataalam wa Kilimo ........................................... 40 6.3.1 Kuongezeka kwa Idadi ya Wakulima Waliopatiwa Mafunzo 40 6.3.2 Mitaala ya Kufundishia Imeboreshwa .............................. 41 6.3.3 Maandiko ya Rejea Yameandaliwa .................................... 41 6.3.4 Miundombinu ya Vyuo Imekarabatiwa ............................ 41 6.3.5 Mafunzo Yanatolewa kwa Kuzingatia Vigezo vya Ubora ............................................................................... 41 6.4 Kuongezeka kwa Matumizi ya Zana Bora za Kilimo ........................ 41 6.4.1 Matumizi ya Wanyamakazi Yameongezeka ........................ 42 6.4.2 Upatikanaji na Matumizi ya Trekta Umeongezeka ........... 42 6.4.3 Mikopo Yenye Masharti Nafuu Inapatikana ...................... 42 6.4.4 Matumizi ya Zana za Kilimo Hifadhi Yameongezeka ........ 42 6.5 Kuimarika kwa Matumizi Bora ya Ardhi ya Kilimo .......................... 43 6.5.1 Wakulima Wanaolima kwa Matuta Wameongezeka ........... 43 6.5.2 Elimu ya Hifadhi ya Udongo na Maji Imetolewa kwa Wakulima .......................................................................... 43 6.5.3 Tathmini ya Ubora na Uwezo wa Ardhi Imefanyika .......... 43

kilimo miaka 50.indd Sec2:xiikilimo miaka 50.indd Sec2:xii 11/16/11 10:34:26 AM11/16/11 10:34:26 AM

Page 15: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

xiii

6.5.4 Miradi ya Hifadhi na Matumizi Bora ya Ardhi ya Kilimo Imetekelezwa .................................................... 43 6.6 Kuimarika kwa Hifadhi ya Mazingira katika Kilimo ........................ 44 6.7 Ongezeko la Uzalishaji na Ubora wa Mazao Makuu ya Biashara ............................................................................................. 45 6.7.1 Mkonge .............................................................................. 46 6.7.2 Chai .................................................................................... 46 6.7.3 Pamba ................................................................................. 47 6.7.4 Sukari ................................................................................. 48 6.7.5 Tumbaku ............................................................................. 48 6.7.6 Korosho ............................................................................... 49 6.7.7 Kahawa ............................................................................... 49 6.7.8 Pareto .................................................................................. 49 6.8 Nchi Imeendelea Kujitosheleza kwa Chakula .................................. 50 6.9 Uzalishaji wa Mazao ya Bustani Umeongezeka ................................ 52 6.10 Akiba ya Taifa ya Chakula Imeongezeka .......................................... 52 6.11 Kuongezeka kwa Tija ya Kilimo cha Umwagiliaji ............................ 52 6.12 Kuimarika kwa Uongozi wa Vyama vya Ushirika ............................. 54 6.13 Vyama vya Ushirika wa Mazao Vimeongezeka ................................. 55 6.14 Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo Vimeongezeka ............... 55 6.15 Kuimarika kwa Vyama vya Ushirika Kibiashara ............................. 55 6.16 Vyama vya Ushirika vimechangia maendeleo ya jamii ..................... 567. CHANGAMOTO ZA KILIMO NA USHIRIKA .......................................... 58 7.1 Mabadiliko ya Miundo na Taasisi za Sekta ya Kilimo ...................... 58 7.2 Ardhi ya Kilimo Haitambuliki Kisheria ............................................ 58 7.3 Upungufu wa Rasilimali ................................................................... 59 7.4 Mabadiliko ya Tabianchi .................................................................... 59 7.5 Ushiriki Hafi fu wa Sekta Binafsi Katika Kilimo .............................. 59 7.6 Ushiriki Hafi fu wa Vijana katika Kilimo ......................................... 60 7.7 Kupungua kwa Nguvukazi Kutokana na VVU/UKIMWI ................ 60 7.8 Uwezo Mdogo wa Wakulima Kugharamia Zana za Kilimo .............. 60 7.9 Uwezo Mdogo wa Wakulima Kugharamia Pembejeo ....................... 61 7.10 Ubovu wa Miundombinu .................................................................... 61 7.11 Kiwango Kidogo cha Usindikaji wa Bidhaa za Kilimo ..................... 61 7.12 Msukumo wa Kuzalisha Mazao ya Nishati Mbadala ......................... 62 7.13 Matumizi Madogo ya Teknolojia Sahihi na za Kisasa ....................... 62 7.14 Uvamizi wa Visumbufu wa Mimea na Mazao ................................... 62 7.15 Upungufu wa Uratibu wa Sekta ya Kilimo ........................................ 63 7.16 Upungufu wa Mitaji kwa Vyama vya Ushirika ................................. 63 7.17 Elimu Duni ya Ushirika ..................................................................... 63 7.18 Usimamizi Hafi fu wa Sera ya Soko Huru .......................................... 63 7.19 Idadi Ndogo ya Maafi sa Ushirika ...................................................... 63 7.20 Kukosekana kwa Mikopo ya Kilimo yenye Masharti Nafuu ............ 63

kilimo miaka 50.indd Sec2:xiiikilimo miaka 50.indd Sec2:xiii 11/16/11 10:34:26 AM11/16/11 10:34:26 AM

Page 16: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

xiv

8. MWELEKEO WA KILIMO NA USHIRIKA (2011-2061) ......................... 65 8.1 Utangulizi .......................................................................................... 65 8.2 Mwelekeo wa Miaka 50 Ijayo ........................................................... 66 8.2.1 Kuongeza Uzalishaji na Tija katika Sekta ya Kilimo .......... 66 8.2.2 Kuimarishwa Upatikanaji wa Masoko ya Bidhaa za Kilimo ............................................................................... 67 8.2.3 Kuongeza Thamani ya Mazao ya Kilimo na Mfumo wa Masoko ......................................................................... 68 8.2.4 Kuendelea Kuboresha Uwezo wa Wizara kutoa Huduma .. 68 8.2.5 Kuimarisha Sera, Mikakati na Usimamizi katika Sekta ya Kilimo ............................................................. 68 8.2.6 Kuboresha Uratibu katika Sekta ya Kilimo ....................... 68 8.2.7 Kuzingatia Masuala Mtambuka katika Kilimo .................. 69 8.2.8 Kuimarisha Mawasiliano ya Habari za Kilimo .................. 69 8.2.9 Kuboresha Huduma na Kupunguza Maambukizi ya VVU/UKIMWI .............................................................. 69 8.2.10 Kuimarisha na Kuwezesha Asasi za Wananchi katika Kilimo 69 8.2.11 Kuimarisha Mfumo wa Ukusanyaji, Uchambuzi, Uhifadhi na Usambazaji wa Takwimu na Taarifa za Kilimo na Vyama vya Ushirika ......................................... 69 8.3 Hitimisho ........................................................................................... 70

kilimo miaka 50.indd Sec2:xivkilimo miaka 50.indd Sec2:xiv 11/16/11 10:34:26 AM11/16/11 10:34:26 AM

Page 17: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

1

1. UTANGULIZI Mwaka huu wa 2011, nchi yetu inaadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara uliopatikana tarehe 9 Desemba, 1961 kutoka kwa Wakoloni wa Kiingereza. Tangu tupate Uhuru tumefanya mambo mengi katika kuendeleza jamii ya Watanzania. Mojawapo ya maeneo ya kujivunia ni sekta za kilimo na ushirika zinavyochangia kujenga uchumi wa nchi yetu. Katika kipindi chote cha Miaka 50 ya Uhuru, sekta hii imeendelea kuwa mhimili wa ukuaji wa uchumi. Katika kuadhimisha miaka 50 tangu nchi yetu ipate Uhuru taarifa hii inalenga kueleza juhudi mbalimbali zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika katika kuendeleza sekta ya kilimo. Juhudi hizo ni pamoja na utafi ti wa kilimo, huduma za ugani, mafunzo ya wataalam, mafunzo ya wakulima, ujenzi wa miundombimu ya umwagiliaji, matumizi ya zana bora za kilimo na maendeleo ya ushirika. Aidha, taarifa hii inaeleza mafanikio, changamoto na matarajio ya miaka 50 ijayo.

Viongozi wakuu wanaoongoza Wizara kwa sasa (2011)

Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (MB)WAZIRI

Mhe. Eng. Christopher Chiza (MB)NAIBU WAZIRI

Bibi Sophia KadumaNAIBU KATIBU MKUU

Bwana Mohamed MuyaKATIBU MKUU

Eng. Mbogo FutakambaNAIBU KATIBU MKUU

kilimo miaka 50.indd Sec1:1kilimo miaka 50.indd Sec1:1 11/16/11 10:34:26 AM11/16/11 10:34:26 AM

Page 18: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

2

2. HISTORIA YA WIZARA2.1 Muundo na Majukumu ya WizaraWakati tunapoadhimisha Miaka 50 ya Uhuru, Wizara inayosimamia kilimo imekuwa ikibadilika kimuundo kuanzia mwaka 1961 hadi 2011 kama inavyoonekana katika Jedwali Na. 1. Mwaka 1974 Wizara ilikuwa na Idara kuu nne ambazo ni Idara ya Kuendeleza Mifugo, Idara ya Kuendeleza Mazao, Idara ya Maendeleo ya Utumishi, na Idara ya Mipango ya Kilimo. Hadi kufi kia mwaka 2011, muundo wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika una Idara 10 ambazo ni Utafi ti na Maendeleo; Mafunzo; Maendeleo ya Mazao; Matumizi Bora ya Ardhi; Zana za Kilimo; Umwagiliaji na Huduma za Ufundi; Sera na Mipango; Utawala na Rasilimali Watu; Usalama wa Chakula; na Maendeleo ya Ushirika. Wizara pia ina vitengo nane ambavyo ni Sheria; Fedha na Uhasibu; Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) , Ukaguzi wa Ndani; Usajili wa Haki Miliki za Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu; Mawasiliano Serikalini; Mazingira; na Ugavi na Manunuzi. Aidha, Wizara ina Wakala zifuatazo: Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) na Wakala wa Maendeleo ya Wakulima Wadogo wa Chai Tanzania. Taasisi zingine chini ya Wizara ni Mfuko wa Pembejeo, Mamlaka ya Kuendeleza Bonde la Mto Rufi ji (RUBADA), Utafi ti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (TPRI), Ukaguzi na Udhibiti wa Mbegu Bora za Kilimo (TOSCI) na Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO). Aidha, mchakato unaendelea wa kuanzisha Mamlaka ya Mbolea na Mamlaka ya Usalama wa Chakula. Wizara pia inasimamia Bodi tisa za Mazao ya Pamba, Korosho, Tumbaku, Kahawa, Sukari, Chai, Pareto, Mkonge na Nafaka na Mazao Mchanganyiko. Katika kufanikisha utafi ti wa kahawa, chai, na tumbaku, Wizara inashirikiana na taasisi binafsi zifuatazo:- Taasisi ya Utafi ti wa Kahawa (TaCRI), Taasisi ya Utafi ti wa Chai (TRIT) na Taasisi ya Utafi ti wa Tumbaku (TORITA).

2.1.1 DiraKuwa kiini cha kutoa miongozo ya kisera, huduma za kilimo cha kisasa chenye tija, faida, ushindani kibiashara na mfumo wa ushirika wenye nguvu ifi kapo mwaka 2025.

2.1.2 Dhamira Kutoa Huduma bora za kilimo na ushirika, kujenga uwezo wa Serikali za Mitaa, kuweka mazingira mazuri kwa wadau na sekta binafsi ili kuchangia ipasavyo katika uzalishaji wenye tija kwa maendeleo endelevu ya kilimo na ushirika.

kilimo miaka 50.indd Sec1:2kilimo miaka 50.indd Sec1:2 11/16/11 10:34:27 AM11/16/11 10:34:27 AM

Page 19: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

3

Jedwali Na. 1: Mabadiliko ya Muundo wa Wizara Tangu Mwaka 1961 hadi 2011

Mwaka Muundo wa Wizara Maelezo1961 Wizara ya Kilimo Kuanzia mwaka 1963 ushirika ulikuwa chini ya

Wizara ya Biashara na Vyama vya Ushirika. 1964 Wizara ya Kilimo Misitu na

Wanyama Pori1967 Wizara ya Kilimo na Vyama vya

Ushirika1968 Wizara ya Kilimo, Vyakula na

Vyama vya Ushirika1980 Wizara ya Kilimo Mifugo iliundiwa Wizara yake1984 Wizara ya Kilimo na Maendeleo

ya MifugoMwaka 1985, ushirika ulikuwa chini ya Wizara ya Serikali za Mitaa na Vyama vya Ushirika

1990 Wizara ya Kilimo Katika kipindi hicho ushirika ulibaki kuwa chini ya Wizara ya Serikali za Mitaa Vyama vya Ushirika na Masoko. Mifugo ilikuwa ndani ya Wizara ya Kilimo.

2000 Wizara ya Kilimo na Chakula Mifugo ilihamishiwa Wizara ya Maji na Mifugo. Wakati huo ushirika uliundiwa Wizara iliyoitwa Wizara ya Ushirika na Masoko

2005 Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika

Wizara ya Ushirika na Masoko ilivunjwa. Idara ya Masoko ilihamishiwa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko. Mifugo iliundiwa Wizara iliyoitwa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo.

2008 Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika

Idara ya Umwagiliaji ilihamishiwa Wizara ya Maji na Umwagiliaji

2010 Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika

Idara ya Umwagiliaji ilirudishwa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika.

2.1.3 MajukumuWizara ya Kilimo Chakula na Ushirika ina majukumu ya kuhakikisha Taifa linajitosheleza kwa chakula na kwamba kilimo kinatoa mchango mkubwa katika uchumi na kuondoa umaskini. Katika kufanikisha majukumu hayo Wizara inatekeleza yafuatayo:(i) Kubuni na kuratibu utekelezaji wa sera za kilimo, chakula na ushirika (ii) Kuratibu matumizi bora ya ardhi katika kilimo (iii) Kujenga uwezo wa Halmashauri za Wilaya katika kutoa huduma za ugani kwa wakulima (iv) Kufanya utafi ti wa kilimo (v) Kuendeleza kilimo cha umwagiliaji (vi) Kudhibiti magonjwa, wadudu, ndege na wanyama waharibifu wa mazao (vii) Kusimamia hifadhi ya Taifa ya chakula (viii) Kujenga uwezo wa Halmashauri

kilimo miaka 50.indd Sec1:3kilimo miaka 50.indd Sec1:3 11/16/11 10:34:27 AM11/16/11 10:34:27 AM

Page 20: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

4

za Wilaya katika kudhibiti upotevu wa mazao baada ya mavuno (ix) Kusimamia na kuratibu hali ya usalama wa chakula nchini (x) Kuendeleza rasilimali watu katika fani za kilimo na ushirika (xi) Kusimamia na kuratibu Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP), (xii) Kusimamia Bodi na Asasi zilizo chini ya Wizara (xiii) Kuendeleza ushirika na vikundi vya uzalishaji na (xiv) Kusimamia na kuratibu Programu ya Mageuzi na Modenaizesheni ya Ushirika (CRMP)

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (wa pili kushoto) akikagua mafanikio ya mradi wa uzalishaji wa mahindi mkoani Mtwara, mwaka 1975

kilimo miaka 50.indd Sec1:4kilimo miaka 50.indd Sec1:4 11/16/11 10:34:27 AM11/16/11 10:34:27 AM

Page 21: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

5

2.2 Mabadiliko ya Uongozi na Utawala Kuanzia mwaka 1961 mpaka sasa (2011), Wizara imeongozwa na Mawaziri 16 na Naibu Mawaziri 9 (Jedwali. Na. 2a-b). Waziri wa kwanza aliyeongoza Wizara alikuwa Mheshimiwa Dereck Bryceson. Kwa sasa (2011) Wizara inaongozwa na Mheshimiwa Profesa Jumanne Maghembe na Naibu Waziri Mheshimiwa Injinia Christopher Chiza. Katibu Mkuu wa kwanza wa Wizara alikuwa Bwana Ibrahim Sapi Mkwawa. Tangu Uhuru hadi sasa (2011), Wizara inayosimamia kilimo imeongozwa na Makatibu Wakuu 22 na Naibu Makatibu Wakuu watano. Katibu Mkuu wa Wizara wa sasa (2011) ni Bwana Mohammed S. Muya akiwa na Naibu Makatibu Wakuu wawili ambao ni Bibi Sophia Kaduma na Injinia Mbogo Futakamba (Jedwali Na. 2b-c).

Mheshimiwa Abdul Jumbe (wa tano kutoka kushoto) akipata maelezo katika skimu ya umwagiliaji ya Kitere Mkoani Mtwara, mwaka 1975

kilimo miaka 50.indd Sec1:5kilimo miaka 50.indd Sec1:5 11/16/11 10:34:27 AM11/16/11 10:34:27 AM

Page 22: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

6

Jedwali Na.2a: Mawaziri na Naibu Mawaziri Walioongoza Wizara (1961 – 2011)

MWAKA WIZARA WAZIRI NAIBU WAZIRI1962-1963 Wizara ya Kilimo Mhe. Dereck Bryceson

1963-1964 Wizara ya Kilimo Misitu na

Wanyama

Mhe. Edward Barongo

1965-1968 Wizara ya Kilimo Misitu na

Wanyama

Mhe. Dereck Bryceson

1968-1970 Wizara ya Kilimo na

Ushirika

Mhe. Dereck Bryceson

1971-1974 Wizara ya Kilimo Mhe Joseph Mungai1975-1980 Wizara ya Kilimo Mhe. John Samwel Malecela1981-1984 Wizara ya Kilimo Mhe. Profesa John Machunda1985-1987 Wizara ya Kilimo Mhe. Paul Bomani Mhe. Frederick Sumaye1987-1989 Wizara ya Kilimo Mhe. Jackson Makwetta Mhe. Frederick Sumaye

Mhe. Amran Mayagila1990-1991 Wizara ya Kilimo na

Maendeleo ya Mifugo

Mhe. Anna Abdalah Mhe. Frederick Sumaye

1992-1993 Wizara ya Kilimo na

Maendeleo ya Mifugo

Mhe. Amran Mayagila Mhe. Frederick Sumaye

1993 -1994 Wizara ya Kilimo na

Maendeleo ya Mifugo

Mhe. Jackson Makwetta Mhe. Frederick Sumaye

1994-1995 Wizara ya Kilimo Mhe. Frederick Sumaye Mhe. Charles Kabeho1996-1997 Wizara ya Kilimo Mhe. Paul Kimiti Mhe. Njelu Kasaka1998-2000 Wizara ya Kilimo Mhe. William Kusila Mhe. Ismail Ivwata

Mhe. Ezekiah Chibulunje2001-2005 Wizara ya Kilimo na

Chakula

Mhe. Charles N. Keenja Prof. Pius Mbawala

2006-2007 Wizara ya Kilimo Chakula

na Ushirika

Mhe. Joseph Mungai Mhe. Dkt. Mathayo David

Mathayo

Mhe. Eng. Christopher

Kajoro Chizza2007-2008 Wizara ya Kilimo Chakula

na Ushirika

Mhe. Stephen Wasira Mhe. Dkt. Mathayo David

Mathayo

Mhe. Eng. Christopher

Kajoro Chiza2008 Wizara ya Kilimo Chakula

na Ushirika

Prof. Peter M. Msolla Mhe. Dkt. Mathayo David

Mathayo2008 -2010 Wizara ya Kilimo Chakula

na Ushirika

Mhe. Stephen M. Wasira Mhe. Dkt. Mathayo David

MathayoDesemba

2010 hadi sasa

(2011)

Wizara ya Kilimo Chakula

na Ushirika

Mhe. Prof. Jumanne Maghembe Mhe. Eng. Christopher

Kajoro Chiza

kilimo miaka 50.indd Sec1:6kilimo miaka 50.indd Sec1:6 11/16/11 10:34:28 AM11/16/11 10:34:28 AM

Page 23: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

7

Mhe. Dereck Bryceson(1961-1963; 1965-1970)

Mhe. John Machunda(1981-1984

Mhe. Amran Mayagila(1992 – 1993)

Mhe. Charles Keenja(2001-2005)

Mhe. Joseph Mungai(1971-1974; 2006-2007)

Mhe. Jackson Makwetta(1987-1989; 1993-1994)

Mhe. Paul Kimiti(1996-1997

Mhe. Stephen Wasira (1990; 2007-2008;

2008-2010)

Mhe. Edward Barongo(1963-1964)

Mhe. Paul Boman(1985 -1986))

Mhe. Frederick Sumaye(1994-1995)

Mhe. Prof. Peter Msolla(2008)

Mhe. John Malecela(1975-1980)

Mhe. Anna Abdallah(1991)

Mhe. William Kusila(1998 – 2000)

Mhe. Prof. Jumanne Maghembe

(2010)

Kielelezo Na.1: Picha za Mawaziri Walioongoza Wizara Tangu Mwaka 1961-2011

kilimo miaka 50.indd Sec1:7kilimo miaka 50.indd Sec1:7 11/16/11 10:34:28 AM11/16/11 10:34:28 AM

Page 24: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

8

Jedwali Na. 2b: Makatibu Wakuu wa Wizara (1961 – 2011)

Na Jina Kipindi cha uongoziIbrahim Sapi MKWAWA 01.12.1962 – 1964Gerald M. RUGARABAMU 02.03.1964 – 1967David Albert MWAKOSYA 23.02.1967 – 1968Ernest Albert MULOKOZI 25.03.1968 – 01.11.1970Timothy APIYO 05.11.1970 – 12.02.1972Awina MUSHI 18.02.1972 – 12.02.1977Dkt. Said Abdallah MADALALI 13.02.1977 – 06.11.1980David D. MASANJA 07.11.1980 – 27.02.1983Prof. Simon Michael MBILINYI 28.02.1983 – 23.04.1984Dkt. Said Abdallah MADALALI 07.11.1980 – 23.04.1984Prof. Simon Michael MBILINYI 24.04.1984 – 03.04.1985Ernest Abel MULOKOZI 04.04.1985 – 17.11.1988Abdi H. MSHANGAMA 18.11.1988 – 12.04.1990Peter J. NGUMBULU 13.04.1990 – 13.11.1990Dkt. Ben MOSHI 14.11.1990 – 13.12.1992Raphael MHAGAMA 14.12.1992 – 19.12.1995T. P. MAGERE 19.03.1997 – 09.10.1998Raphael O. S. MOLLEL 20.12.1997 – Desemba 1998Peter BARIE 19.10.1998 – 01.02.2001Wilfred W. NGIRWA 01.02.2001 – 21.01.2006Peniel M. LYIMO 21.01.2006 – Desemba 2008Mohamed S. MUYA Desemba 2008 hadi sasa (2011)

Jedwali Na. 2c: Naibu Makatibu Wakuu Walioongoza Wizara (1961 – 2011)

NA JINA KIPINDI CHA UONGOZI1 Kamaiko Yuda Mpupuwa 1984-19902 Rudovick Remisho 1991-19923 Mohammed S. Muya 2005-20084 Sophia E. Kaduma 2008 hadi sasa (2011)5 Injinia Mbogo Futakamba 2010 hadi sasa (2011)

kilimo miaka 50.indd Sec1:8kilimo miaka 50.indd Sec1:8 11/16/11 10:34:32 AM11/16/11 10:34:32 AM

Page 25: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

9

3. SERA, MIKAKATI, PROGRAMU NA SHERIAKatika kipindi cha miaka 50 tangu nchi yetu ipate Uhuru, kilimo kimeongozwa na sera, mikakati, programu na sheria mbalimbali. Kuanzia mwaka 1961 kilimo kiliongozwa na Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa miaka mitatu (1961-1964). Mpango wa Pili wa Maendeleo ambao pia ulikuwa muhimu kwa maendeleo ya kilimo nchini ulianza kutekelezwa mwaka 1965. Kuanzia mwaka 1982, uchambuzi wa kina ulifanyika ili kubaini upungufu wa kisera katika kukiwezesha kilimo kukidhi matarajio ya kiuchumi na kujitosheleza kwa chakula. Kufuatia hatua hiyo sera, mikakati, programu na kaulimbiu zilibuniwa ili kufi kia malengo hayo.

3.1 Sera za KilimoSera ya Kilimo ya Mwaka 1983 ilitungwa ikiwa na lengo la kuhakikisha upatikanaji wa chakula katika ngazi ya kaya na kuboresha kiwango cha lishe na maisha ya jamii nzima ya Tanzania. Kutokana na haja ya kukidhi mageuzi ya kiuchumi yaliyotokea katika miaka ya 1983/1984, Sera ya Kilimo ya mwaka 1983 ilihuishwa na kuunganishwa na Sera ya Mifugo ya mwaka 1986 na ikapatikana Sera ya Kilimo na Mifugo ya mwaka 1997. Mabadiliko ya kisera, mikakati na mifumo mbalimbali ya kiuchumi ambayo imekuwa ikitokea kati ya miaka ya 1990 hadi mwishoni mwa miaka ya 2000, Serikali ililazimika kuandaa sera nyingine ya kilimo ya mwaka 2009. Sera hiyo imezingatia changamoto na fursa za kiuchumi zinazoendelea kujitokeza, ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira ya kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi na Serikali katika kilimo. Mwaka 2010, Serikali ilikamilisha utayarishaji wa Sera ya Taifa ya Umwagiliaji inayoweka dira na mwelekeo katika kuendeleza kilimo cha umwagiliaji nchini. Sera hiyo pia inatoa mwongozo utakaowezesha kuharakisha uwekezaji na usimamizi thabiti katika kilimo cha umwagiliaji, kuleta ufanisi katika kuendeleza miundombinu ya umwagiliaji, kutoa fursa kwa sekta binafsi kutoa huduma na kuwekeza katika umwagiliaji, kuhakikisha matumizi bora na endelevu ya rasilimali ya maji na kuainisha majukumu ya Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, sekta binafsi na Taasisi mbalimbali katika kufanikisha uendelezaji wa kilimo cha umwagiliaji nchini.

3.2 Sera za UshirikaSera ya kwanza ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania ilipitishwa mwaka 1997 kwa ajili ya kutoa malengo ya jumla na mikakati muhimu kuhakikisha kwamba makundi ya watu maskini katika jamii yanakuwa na chombo cha kuaminika cha kuwezesha kufi kia malengo yake ya kiuchumi na kijamii. Sera ya Maendeleo ya Ushirika ya mwaka 2002 ilipitishwa ili kuzingatia upungufu uliotokana na Sera ya Maendeleo ya Ushirika ya mwaka 1997. Pamoja na mambo mengine sera hiyo ilizingatia umuhimu wa kuweka mazingira muafaka kwa vyama vya ushirika kufanya shughuli zake na kumudu ushindani katika mfumo mpya wa kiuchumi, juhudi za vikundi vya kiuchumi vya wakulima vinavyoanzishwa kutokana na nguvu mpya za mahusiano ya uzalishaji kama msingi muhimu wa maendeleo ya ushirika katika mazingira ya uchumi wa soko huru. Aidha, sera hiyo inaangalia upya majukumu ya Serikali katika kuvisaidia vyama vya ushirika

kilimo miaka 50.indd Sec1:9kilimo miaka 50.indd Sec1:9 11/16/11 10:34:33 AM11/16/11 10:34:33 AM

Page 26: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

10

ambavyo vinamilikiwa na kusimamiwa na wanachama wenyewe kwa mujibu wa maadili na misingi ya ushirika inayotambuliwa kimataifa.

3.3 Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya KilimoMwaka 2001, Serikali ilizindua Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo (Agricultural Sector Development Stretegy – ASDS) ambao ulizingatia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 (Tanzania Development Vision 2025 -TDV) ambayo inaitaka sekta ya kilimo iendeshwe kisasa, kibiashara, kwa faida na tija kwa kuzingatia matumizi endelevu ya maliasili ili kilimo kiwe nguzo ya kuunganisha na kuziwezesha shughuli za sekta nyingine.

3.4 Programu za Kuendeleza Kilimo na Ushirika3.4.1 Programu ya Kuendeleza Kilimo (ASDP)Katika kutekeleza ASDS Serikali iliandaa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (Agricultural Sector Development Program –ASDP). ASDP ni Programu ya miaka saba iliyoanza kutekelezwa mwaka 2006 ikiwa na malengo makuu mawili yafuatayo: (i) Kuwawezesha wakulima na wafugaji kuongeza tija na uzalishaji ili kupata faida na kuongeza kipato (ii) Kujenga mazingira bora ya kisera na kisheria ili kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi katika kilimo. Aidha, Programu hiyo ina mikakati ya kuleta mapinduzi ya kijani nchini kwa lengo la kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya kilimo. Malengo mengine ya ASDP ni pamoja na kuratibu mabadiliko ya sera yanayotokea katika Wizara zinazohusiana na kilimo (Agrucultural Sector Lead Ministries - ASLMs), kuangalia mahitaji halisi ya sekta, kuingiza mipango ya kilimo katika mchakato wa utayarishaji wa mipango ya maendeleo ya wilaya na kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi. Katika kuzingatia Sera ya Kupeleka Madaraka Wilayani, ASDP inatekelezwa kupitia Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (District Agricultural Development Plans- DADPs) ambayo ni sehemu ya Mipango ya Maendeleo ya Wilaya. Pamoja na mafanikio yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wa ASDP, Serikali imeona umuhimu wa kuongeza msukumo zaidi katika kuendeleza kilimo. Aidha, mnamo tarehe 8 mwezi Julai, 2010, Tanzania iliungana na nchi nyingine duniani kuweka saini Programu Kabambe ya Kuendeleza Kilimo Afrika (Comprehensive Africa Agriculture Development Program –CAADP). Juhudi zote hizo ni kuhakikisha kuwa Tanzania katika siku zijazo inakuwa na uzalishaji na akiba ya kutosha ya chakula pamoja na ziada kwa ajili ya kuuza nchi za nje.

3.4.2 Programu Kabambe ya Mageuzi ya Ushirika Programu Kabambe ya Mageuzi na Modenaizesheni ya Ushirika (CRMP) ni mkakati wa kuwezesha sekta ya ushirika kutekeleza Sera ya Maendeleo ya Ushirika ya mwaka 2002 pamoja na Sheria ya Vyama vya Ushirika Na.20 ya mwaka 2003. CRMP inatoa mwelekeo na dira ya mfumo wa ushirika wa Tanzania kuwa na Vyama vya Ushirika imara na endelevu, vyenye uwezo wa kukidhi mahitaji ya kiuchumi na kijamii ya wanachama. CRMP inatekelezwa kwa miaka kumi (10) kuanzia 2005 hadi 2015 na malengo yake ni haya yafuatayo:- (i) Kuhimiza na kuwezesha kuibua mfumo wa ushirika

kilimo miaka 50.indd Sec1:10kilimo miaka 50.indd Sec1:10 11/16/11 10:34:33 AM11/16/11 10:34:33 AM

Page 27: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

11

ambao msingi wake ni vyama vya msingi na wanachama (ii) Kuhamasisha kuwepo kwa viongozi wa ushirika wanaowajibika kwa wanachama na ambao ni wabunifu kibiashara (iii) Kujasirisha wanachama kwa kuwawezesha kupata elimu na stadi zinazohitajika ili waendeleze vyama vyao (iv) Kuhimiza na kuhamasisha uanzishwaji na uendelezaji wa vyama vya ushirika vyenye nguvu za kiuchumi na endelevu (v) Kuhimiza na kuwezesha mabadiliko katika mfumo wa Vyama vya Akiba na Mikopo; na Benki za Ushirika ili vyombo hivyo viweze kuwahudumia wanachama kikamilifu (vi) Kuhamasisha na kuhimiza uanzishwaji wa Vyama vya Ushirika vya aina mbalimbali kulingana na mahitaji ya wanachama, jamii na Taifa (vii) Kuimarisha uwezo wa Idara, Taasisi na Asasi mbali mbali zinazohusika na maendeleo ya ushirika nchini.

3.5. Maazimio na Kaulimbiu za Kuhamasisha KilimoKatika vipindi tofauti tangu Uhuru, kumekuwa na maazimio na kaulimbiu mbalimbali zilizolenga kuhamasisha kilimo. Mwaka 1967 Azimio la Arusha liliweka njia kuu za uchumi mikononi mwa umma. Katika kutekeleza Azimio la Arusha, mashamba makubwa yaliyokuwa yakimilikiwa na watu binafsi yalitaifi shwa na kuwa chini ya mashirika ya umma. Aidha, mwaka 1972, Azimio la Iringa la Siasa ni Kilimo liliweka msukumo katika kuanzisha mashamba makubwa ya vijiji vya ujamaa ambayo yaliendeshwa kwa kuzingatia kanuni za kilimo bora. Mwaka 1974, kampeni ya Kilimo cha Kufa na Kupona ililenga katika kuongeza uzalishaji wa chakula katika ngazi ya kaya. Mwaka 1982 kulikuwa na kampeni ya Kilimo ni Uti wa Mgongo wa Taifa ikiwa na lengo la kuhamasisha wadau kuhusu umuhimu wa kilimo katika uchumi na maisha ya Watanzania. Azimio la Kilimo Kwanza lilizinduliwa na Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Agosti 3, 2009, katika viwanja vya maonyesho ya Siku kuu ya wakulima (Nane Nane) vilivyopo Nzuguni mjini Dodoma. Kilimo Kwanza ni azma maalum ya kitaifa ya kuongeza kasi ya kuleta mapinduzi ya kilimo nchini. Azimio la Kilimo Kwanza linajumuisha sera na mikakati inayolenga katika kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili kilimo chetu na pia kutumia fursa nyingi zilizopo. Kwa misingi hiyo, Kilimo Kwanza ni mhimili muhimu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na inaweka msukumo zaidi katika kufanikisha malengo yetu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Nguzo kuu katika kufanikisha Kilimo Kwanza zinahusisha kutekeleza mambo kadhaa ambayo miongoni mwake ni kukuza kilimo cha kisasa na cha kibiashara kuanzia kwa wakulima wadogo hadi wakulima wakubwa; kuweka mkakati wa muda mfupi na mrefu wa upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya kilimo kwa masharti nafuu; kuboresha mipango ya ugawaji wa ardhi; kubuni sera za kuboresha mazingira ya uwekezaji, vivutio pamoja na kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika kilimo. Nguzo nyingine zinahusisha utekelezaji wa programu za maendeleo ya viwanda, maendeleo ya rasilimali watu na kukuza uelewa wa matumizi ya teknolojia za kisasa kwa wakulima katika ngazi zote. Pia, msisitizo umewekwa katika kuongeza matumizi ya pembejeo za kilimo na matumizi ya mitambo na mashine; upatikanaji wa pembejeo muhimu kwa wakati muafaka kwa ajili ya kuongeza mazao ya kilimo, ufugaji na uvuvi; kuwa na mpango madhubuti wa

kilimo miaka 50.indd Sec1:11kilimo miaka 50.indd Sec1:11 11/16/11 10:34:33 AM11/16/11 10:34:33 AM

Page 28: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

12

kuboresha miundombinu ikiwemo miradi mikubwa ya kilimo cha umwagiliaji maji, barabara za vijijini na uhifadhi bora ili kupunguza hasara zinazotokana na uharibifu wa mazao baada ya mavuno. Aidha, azimio limezingatia suala zima la kuimarisha masoko ya mazao ili mkulima apate soko la uhakika na lenye tija.

3.6 Sheria za Kilimo na UshirikaTangu Uhuru zimekuwepo sheria mbalimbali ambazo zimekuwa ni msingi wa kuendeleza kilimo na ushirika (Jedwali Na. 3). Aidha, Wizara imekuwa ikitekeleza sheria hizo kupitia kanuni mbalimbali zinazoambatana na sheria hizo.

Mheshimiwa Frederick Sumaye, Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tatu akiwa katika ziara ya kuzindua mojawapo ya miradi ya umwagiliaji

kilimo miaka 50.indd Sec1:12kilimo miaka 50.indd Sec1:12 11/16/11 10:34:33 AM11/16/11 10:34:33 AM

Page 29: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

13

Jedwali Na. 3: Sheria za Kilimo na Ushirika (1961-2011)

Mwaka Sheria Maelezo1961-19701971-1980 Sheria ya Mamlaka ya kuendeleza

Bonde la Mto Rufi ji (Rufi ji Basin Development Authority Act), ya Mwaka 1975Sheria ya Taasisi ya utafi ti wa madawa ( TPRI) ya mwaka 1979;

Inafanyiwa marekebisho

1981-19901991-2000 Sheria ya Usalama wa Chakula ya

mwaka 1991 (imefanyiwa marekebisho mwaka 2009);

Inasimamia na kuratibu usalama wa chakula nchini.

Sheria ya Mfuko wa Pembejeo ya mwaka 1994

Inafanyiwa marekebisho

Sheria ya Pareto ya mwaka 1997 (imerekebishwa mwaka 2009)

Usimamizi na uratibu wa sekta ya Pareto.

Sheria ya Chai ya mwaka 1997 Usimamizi na uratibu wa sekta ya chai. Imerekebishwa mwaka 2009;

Sheria ya Mkonge ya mwaka 1997 (imerekebishwa mwaka 2009);

Usimamizi na uratibu wa sekta ya Mkonge.

Sheria ya Kudhibiti Visumbufu vya Mimea (“The Plant Protection Act”) Na.13 ya mwaka 1997

Inafanyiwa marekebisho

2001 – 2010 Sheria ya Sukari ya mwaka 2001 (imerekebishwa mwaka 2009);

Usimamizi na uratibu wa sekta ya sukari.

Sheria ya Pamba ya mwaka 2001 (imerekebishwa mwaka 2009)

Usimamizi na uratibu wa sekta ya pamba.

Sheria ya Kahawa ya mwaka 2001 (imerekebishwa mwaka 2009)

Usimamizi na uratibu wa sekta ya kahawa.

Sheria ya Tumbaku ya mwaka 2001 (imerekebishwa mwaka 2009)

Usimamizi na uratibu wa sekta ya tumbaku.

Sheria ya Hakimiliki za Wagunduzi wa Mbegu Mpya ya mwaka, 2002 (The Plant Breeders Rights Act

Kulinda hakimiliki za wagunduzi wa mbegu mpya

Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 20 ya mwaka 2003

Kuwezesha utekelezaji wa sera ya maendeleo ya ushirika ya mwaka 2002

Sheria ya Mbegu Na. 18 ya mwaka 2003

Usimamizi wa uzalishaji, uagizaji toka nje na uingizaji nchini mbegu zote za mazao ya kilimo

Sheria ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, ya Mwaka 2009 (The cereal and Other Produce Act, 2009)

Kusimamia mazao ya Nafaka na mengineyo ambayo hayakuwa na Bodi maalumu.

Sheria ya Mbolea ya mwaka 2009 (The Fertilizers Act)

Kudhibiti ubora wa mbolea zote.

Sheria ya sekta ndogo ya Korosho ya mwaka 2009 ( The Cashewnuts Industry Act)

Usimamizi na uratibu wa sekta ya korosho.

kilimo miaka 50.indd Sec1:13kilimo miaka 50.indd Sec1:13 11/16/11 10:34:33 AM11/16/11 10:34:33 AM

Page 30: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

14

4. HUDUMA ZA KILIMO4.1 Kufanya Utafi ti wa KilimoUtafi ti katika sekta ya kilimo ni muhimu katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini. Umuhimu huo unatokana na juhudi zinazofanyika katika uboreshaji wa teknolojia zenye faida kiuchumi na zinazokubalika katika eneo husika. Utafi ti wa kilimo una malengo makuu matano yafuatayo: (i) Kuongeza uzalishaji na tija kutokana na matumizi ya teknolojia bora zilizopatikana (ii) Kuongeza ufanisi kwa kutumia zana bora zilizotokana na utafi ti (iii) Kuzalisha aina za mbegu zenye mavuno mengi na bora ambazo pia zinastahimili ukame na visumbufu vya mimea na mazao (iv) Kutafi ti na kupendekeza njia mpya za usindikaji ili kuongeza thamani ya mazao na kupunguza hasara inayotokana na uharibifu wa mazao baada ya mavuno (v) Kushirikiana na wadau mbalimbali wanaojihusisha na utafi ti wa kilimo na matumizi ya teknolojia husika.

4.1.1 Hali ya Utafi ti Kabla ya UhuruKituo cha kwanza cha utafi ti kilianzishwa na Wakoloni wa Kijerumani mwaka 1902 huko Amani-Tanga. Chini ya utawala wa Waingereza (1918-1961) vituo kadhaa vya utafi ti vilijengwa kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya wakulima wa mashamba makubwa waliokuwa wakijihusisha na uzalishaji wa mazao makuu ya biashara. Katika kipindi hicho mwaka 1932 Kituo cha utafi ti Ukiriguru kilianzishwa kwa ajili ya utafi ti wa pamba. Vituo vingine ni Lyamungu (1934: kahawa), Mlingano (1934: mkonge), Ilonga (1943: pamba), Nachingwea (1956: korosho na karanga) na Maruku (1947: kahawa). Waingereza walikigeuza kituo cha utafi ti Amani kuwa Taasisi ya Kilimo ya Afrika Mashariki mnamo mwaka 1944. Vituo hivyo viliendeshwa na watafi ti wa kigeni, na kwa ujumla utafi ti haukuwanufaisha wakulima wadogo wazalendo kutokana na kutakiwa kufuata matakwa ya wamiliki wa mashamba makubwa kwa ajili ya kuinua uzalishaji wa mazao hasa ya biashara waliyokuwa wakijihusisha nayo.

4.1.2 Hali ya Utafi ti wa Kilimo Baada ya UhuruAwamu ya kwanza ya uongozi katika Tanzania huru ilitimiza jukumu lake la kuleta tija katika sekta ya kilimo kwa kujenga vituo zaidi vya utafi ti. Sera na mtazamo katika nyanja ya utafi ti ilifanyiwa mabadiliko makubwa kwa lengo la kutatua matatizo ya wakulima wadogo wazalendo, wakulima wa kati na wakulima wenye mashamba makubwa. Vituo kadhaa vilivyoanzishwa kipindi hiki ni KATRIN (1963, mpunga), Uyole (1970, mazao mbalimbali), Hombolo (1972, mtama), Naliendele (1972, korosho, mbegu za mafuta; na ikachukua majukumu ya Nachingwea), Makutopora (1979, zabibu) na Selian (1980, ngano, shayiri). Mfumo mzima wa utafi ti uliathiriwa kwa kiasi kikubwa na kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (East African Community- EAC) mnamo mwaka 1977, ambapo kabla ya kuvunjika kwake baadhi ya shughuli za utafi ti muhimu kwa nchi wanachama ziliratibiwa na Taasisi ya Utafi ti wa Kilimo na Misitu ya Afrika Mashariki (East African Agricultural and Forestry Research Organisation-EAAFRO) iliyokuwa imeanzishwa mwaka 1948 jijini Nairobi. Kituo cha Kibaha kilianzishwa na EAC mwaka 1970 kwa ajili ya kuratibu utafi ti wa miwa kwa nchi za Afrika Mashariki. Vilevile, utafi ti

kilimo miaka 50.indd Sec1:14kilimo miaka 50.indd Sec1:14 11/16/11 10:34:33 AM11/16/11 10:34:33 AM

Page 31: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

15

wa chai ulikuwa chini ya EAC huko Kericho-Kenya. Mara baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki taasisi ya kitaifa ya utafi ti wa kilimo (Tanzania Agricultural Research Organisation, TARO) pamoja na ile ya utafi ti wa mifugo (Tanzania Livestock Research Organisation, TALIRO) ziliundwa kwa sheria za bunge Na. 2 (TALIRO) na 3 (TARO) za mwaka 1980. Pia, Shirika la Kilimo Uyole (Uyole Agricultural Centre, UAC) na kituo cha Utafi ti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (Tropical Pesticides Research Institute, TPRI) zilifanywa taasisi zinazojitegemea chini ya Wizara yenye dhamana ya kilimo ambayo iliendelea kuwa mwangalizi mkuu wa shughuli za utafi ti katika sekta hiyo. Kabla ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, TPRI ilikuwa miongoni mwa vituo vya mwanzo kabisa vilivyoanzishwa na Waingereza wakati wa kipindi cha utawala wao. Chini ya muundo huo mpya wa utafi ti uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Kwanza, tafi ti mbalimbali muhimu katika sekta ya kilimo zilifanyika na kutoa matokeo muhimu yaliyotumika kuongeza uzalishaji. Miongoni mwa matokeo muhimu ya wakati huo ni pamoja na kuzalishwa kwa aina ya mbegu mpya na bora za mazao mbalimbali hususan pamba, mahindi, mpunga, ufuta na karanga (Jedwali. Na. 4) sambamba na teknolojia husishi za mbinu bora mbalimbali za ukuzaji wa mazao. Katika kipindi cha kwanza cha Serikali ya Awamu ya Pili (1985-1990), mabadiliko katika mfumo wa utafi ti yalifanyika ambapo TARO na TALIRO (na baadaye UAC) zilivunjwa mwaka 1989 na utafi ti ukaanza tena kusimamiwa moja kwa moja na Wizara yenye dhamana ya kilimo kupitia Idara ya Utafi ti na Mafunzo ikiongozwa na Kamishna. Idara hiyo mpya ilijumuisha utafi ti wa mazao na mifugo chini ya Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo na iliundwa sambamba na mfumo wa kanda saba za utafi ti. Mwaka 2001 utafi ti wa mazao na mifugo ulitenganishwa na kila moja ikawa chini ya wizara yenye dhamana ya kilimo au mifugo. Utafi ti kwa upande wa kilimo ulikuwa chini ya Idara ya Utafi ti na Mafunzo ikiongozwa na Mkurugenzi (DRT). Mwaka 2007 majukumu ya utafi ti na mafunzo yalitenganishwa na kuunda Idara ya Utafi ti na Maendeleo chini ya Mkurugenzi. Mwaka mmoja baadaye shughuli za utafi ti na mafunzo ziliunganishwa tena na kuunda Idara ya Utafi ti na Mafunzo chini ya Mkurugenzi. Hata hivyo muundo huo haukudumu kwani mwaka mmoja baadaye utafi ti na mafunzo vilitenganishwa tena na kuunda idara ya sasa inayoshughulikia utafi ti wa kilimo, yaani Idara ya Utafi ti na Maendeleo (Division of Research and Development, DRD) ikiongozwa na Mkurugenzi chini ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika. Idara hiyo huratibu na kusimamia utafi ti wa kilimo (yaani mazao; hifadhi ya udongo na maji; kilimo-mseto/kilimo-misitu; uhandisi-kilimo; teknolojia za hifadhi; na mifumo ya kilimo/sayansi-jamii/uchumi); na kusambaza matokeo ya utafi ti kwa washauri wa kilimo, wakulima, sekta binafsi na wadau wengine.

4.1.3 Majukumu Makuu ya Utafi ti wa Kilimo Katika mfumo wa sasa, Wizara hutekeleza majukumu ya utafi ti kupitia kanda 7 zenye jumla ya vituo 16 vya utafi ti (Kiambatisho Na.2) ambavyo ni hazina kubwa ya

kilimo miaka 50.indd Sec1:15kilimo miaka 50.indd Sec1:15 11/16/11 10:34:34 AM11/16/11 10:34:34 AM

Page 32: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

16

teknolojia mbalimbali za kuboresha kilimo (Jedwali Na.4). Majukumu makuu ya utafi ti yameainishwa chini ya programu zifuatazo:

4.1.3.1 Utafi ti wa Mazao(a) Kubuni na kutathmini aina za mbegu bora za mazao zenye kutoa mavuno mengi na bora, kustahimili ukame, ukinzani dhidi ya visumbufu vya mimea, na zinazokidhi viwango vya ubora na matakwa ya walaji; (b) Kutafi ti na kupendekeza mbinu bora za uzalishaji wa mazao ili kumwezesha mkulima kuongeza mavuno na tija; (c) Kutafi ti njia bora za kukinga mazao dhidi ya visumbufu vya mimea (magonjwa, wadudu na magugu); (d) Kuzalisha mbegu za awali (breeders’ seed) na kuzipeleka kwa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA); (e) Kukusanya na kuhifadhi vyanzo vya vinasaba vya mimea kwa ajili ya kuboresha mazao; (f) Kufanya utafi ti juu ya njia mbalimbali za bioteknolojia zinazofaa; na (g) Kuhifadhi na kusambaza teknolojia za utafi ti wa mazao kwa wakulima na wadau wengine.

4.1.3.2 Programu Maalum za Utafi ti (udongo, kilimo-mseto/miti, zana za kilimo)(a) Kuandaa, kuchapa na kusambaza ramani za udongo kwa wilaya zote nchini kwa kipimo cha 1:100,000 hadi 1:250,000; (b) Kuandaa na kusambaza ramani za kanda za ikolojia-kilimo zinazoonyesha ubora wa mazao yanayofaa kulimwa kikanda; (c) Kuhakiki na kusambaza teknolojia za matumizi bora ya mbolea za asili na viwandani, teknolojia za kuweza kupanda mazao ya mikunde baada ya kupanda mpunga wa mabondeni na kutokomeza viduha, (d) Kuwapatia wakulima mafunzo mbalimbali kuhusu matumizi bora ya mbolea na hifadhi maji; na (e) Kufanya utafi ti kilimo-misitu (agroforestry) na kusambaza teknolojia zake.

4.1.3.3 Utafi ti wa Mifumo ya Kilimo, Uchumi na Sayansi Jamii(a) Kushughulikia mahitaji ya wateja (wakulima) kupitia CORDEMA (Client Oriented Management Approach); (b) Kufanya utafi ti kuhusu matumizi ya teknolojia mbalimbali kwa wakulima; (c) Kufanya utafi ti wa jinsi mahitaji mbalimbali ya wakulima yanavyowasaidia watafi ti kuzalisha mbegu bora zinazokubalika kwa wakulima; (d) Kuoanisha gharama na faida za kilimo cha mazao mbalimbali yanayolimwa; (e) Kufanya utafi ti namna ya kusambaza teknolojia mbalimbali kutoka vituo vya utafi ti; (f) Kufanya tathmini ya athari za UKIMWI katika kilimo; na (g) Kufanya tathmini ya matatizo ya kilimo kwa wakulima. Katika kuboresha kilimo na kuhakikisha utafi ti unafanyika na kuwafi kia walengwa, Wizara imeweka utaratibu wa kufuatilia na kutathmini shughuli za utafi ti katika kanda zake saba ili mipango ya utafi ti iweze kutekelezwa kwa ufanisi, na kutambua changamoto zilizopo ili kuweka mikakati ya kukabiliana nazo. Licha ya utafi ti unaofanywa na Wizara kupitia Idara ya Utafi ti na Maendeleo (DRD), taasisi nyingine za utafi ti pia zimechangia maendeleo ya sekta. Kwa kutumia utaratibu wa ubia kati yake na sekta binafsi (Public-Private-Partnership-PPP) na wadau wengine, Wizara hushirikiana na Taasisi ya Utafi ti wa Kahawa (Tanzania Coffee Research

kilimo miaka 50.indd Sec1:16kilimo miaka 50.indd Sec1:16 11/16/11 10:34:34 AM11/16/11 10:34:34 AM

Page 33: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

17

Institute -TaCRI), Taasisi ya Utafi ti wa Chai (Tea Research Institute of Tanzania-TRIT) na Taasisi ya Utafi ti wa Tumbaku (Tobacco Research Institute of Tanzania -TORITA). Pia, TPRI ni taasisi inayojitegemea chini ya Wizara. Mafanikio na changamoto za utafi ti katika sekta ya kilimo katika Miaka 50 ya Uhuru na dira ya utafi ti katika miaka 50 ijayo inajumuisha DRD na taasisi zote zinazofanya utafi ti wa kilimo.

4.2 Kutoa Mafunzo ya KilimoMafunzo ya kilimo yamekuwa yakitolewa katika vyuo vya kilimo kwa lengo la kuboresha uzalishaji wa mazao ya chakula na ya biashara. Katika nyakati tofauti vyuo vya kilimo vililenga kutoa wataalamu ambao walitarajiwa kutoa ushauri kwa wakulima, kupata wataalamu wa ngazi ya kati katika taasisi za utafi ti na mashamba ya kuzalisha mbegu na kupata wakulima watakaojiajiri katika tasnia ya kilimo. Programu za mafunzo ya kilimo yalianza tangu enzi za ukoloni ambapo Chuo cha Kilimo Ukiriguru (MATI Ukiriguru) katika mkoa wa Mwanza kilianza kutoa mafunzo ya muda mfupi katika stadi za kilimo cha zao la pamba tangu mwaka 1939. Vyuo vingine vilivyoanzishwa kabla ya uhuru ni Mpwapwa, Tengeru, Tumbi na Morogoro. Zaidi ya kutoa mafunzo ya muda mfupi vyuo hivyo vilijishughulisha na utafi ti wa mazao na tiba za mifugo. Hadi mwaka 1996 Serikali ilikuwa na vyuo 16 vya kilimo na mifugo. Vyuo vya Kilimo vilivyoongezeka baada ya Uhuru wa Tanzania Bara ni MATI Nyegezi (Mwanza), MATI Ilonga (Kilosa), MATI Maruku (Kagera), MATI Mlingano (Tanga), MATI Mubondo (Kigoma), MATI Mtwara, HORTI Tengeru (Arusha), MATI Uyole (Mbeya) na KATC Moshi. Vyuo vya Mifugo ni pamoja na LITI Buhuri (Tanga) na LITI Madaba (Ruvuma). Hadi mwaka 2011 baada ya mabadiliko kadhaa ya sera na miundo katika Serikali, Vyuo vya Kilimo (MATIs) vilivyo chini ya usimamizi wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika ni 13. Vyuo vya mifugo (LITIs) viko chini ya mamlaka ya Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.

4.2.1 Uboreshaji Vyuo vya Mafunzo Kuanzia mwaka 2000 Serikali ilirejesha utaratibu wa kugharimia mafunzo ya muda mrefu ngazi ya Stashahada kupitia Programu ya Kuimarisha Huduma za Ugani (National Agriculture Extension Programme -NAEP II). Waliofaidika na mpango huo walikuwa ni maafi sa ugani waajiriwa waliokuwa na Astashahada. Baada ya NAEP II kufi kia tamati mwaka 2002 Serikali iliendelea kugharimia mafunzo hayo yaliyolenga kuhakikisha kuwa maafi sa ugani wote wa ngazi ya kijiji wanakuwa na elimu ya Stashahada ya Kilimo na Tiba ya Mifugo. Hivyo katika kipindi hicho, Serikali ilitumia shilingi bilioni 1.098 kwa ajili ya kugharamia ufufuaji, ukarabati na uboreshaji wa miundombinu katika vyuo vyote vya kilimo. Mwaka 2007, Serikali ilianza kutekeleza programu maalum ya miaka mitano (2007 – 2012) ambapo vyuo 15 vya kilimo (13 vya Serikali na viwili vya binafsi) vinashiriki katika utekelezaji. Vyuo binafsi vinavyoshiriki utekelezaji ni Kilacha (Dayosisi ya Kanisa Katoliki Moshi) na Igabiro (Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Mkoani Kagera). Utekelezaji wake unagharimiwa na Serikali kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP). Zoezi hilo linalenga kuviwezesha vyuo vya kilimo kufundisha na kupata maafi sa ugani katika ngazi ya Astashahada na Stashahada wapatao 12,227 ili ifi kapo mwaka 2012 wawepo maafi sa ugani 15,082 watakaohudumia wakulima katika Vijiji 12,227 na Kata 2,855 kwa Tanzania Bara.

kilimo miaka 50.indd Sec1:17kilimo miaka 50.indd Sec1:17 11/16/11 10:34:34 AM11/16/11 10:34:34 AM

Page 34: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

18

4.3 Kuboresha Ushauri na Elimu kwa WakulimaHuduma za Ugani nchini zilianza wakati wa Ukoloni ambapo msisitizo mkubwa ulikuwa kuongeza uzalishaji wa mazao makuu ya biashara ambayo ni pamba, mkonge, chai, kahawa, pareto na korosho. Baada ya Uhuru kati ya mwaka wa 1962 na 1967, Serikali ilitumia mbinu kuu mbili za kuongeza tija katika kilimo. Mojawapo ya mbinu hizo ilizingatia kutoa huduma za ugani kwa wakulima katika vijiji vyao vya asili na mbinu nyingine ilikuwa kuwahamishia wakulima katika makazi maalum ya kilimo. Matumizi ya mbinu hizo mbili yalilenga kuongeza kasi ya uzalishaji wa mazao hayo. Mabadiliko makubwa ya huduma za ugani yalitokea mwaka 1972 ambapo Sera ya Madaraka Mikoani ilianza. Usimamizi na utekelezaji wa Huduma za Ugani ulihamishwa kutoka Serikali Kuu na kupelekwa kwa Wakurugenzi wa Maendeleo wa Mikoa na Wilaya kupitia Ofi si ya Waziri Mkuu. Aidha, katika miaka ya 1973 na 1978 Bodi na Mamlaka za Mazao, pamoja na Vyama vya Ushirika vilianza kutoa huduma za ugani. Mabadiliko mengine yalitokea mwaka 1983 ambapo usimamizi na utekelezaji wa huduma za ugani ulirejeshwa Wizara ya Kilimo. Mwaka 1988 ulianzishwa Mradi wa Taifa wa Kuboresha Huduma za Ugani katika Kilimo na Mifugo (National Agriculture and Livestock Extension Rehabilitation Project - NALERP). Lengo kuu la mradi huo lilikuwa kuwawezesha wakulima na wafugaji kwa pamoja kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo na mifugo. Katika kufi kia lengo hilo watalaam wa ugani wa ngazi ya Taifa, Mkoa, Wilaya, Tarafa, Kata na Vijiji walipewa vitendea kazi. Programu ya Taifa ya Huduma za Ugani (NAEP II) ilianzishwa mwaka 1995 msukumo mkubwa ukiwa kumwezesha mkulima kubaini matatizo yake, kuyachambua, kuweka katika kipaumbele, kuangalia rasilimali aliyonayo, na kuandaa mkakati na programu ya kutatua matatizo. Mwaka 1997, Serikali ilirudisha majukumu hayo Serikali za Mitaa na Halmashauri za Wilaya. Kuanzia mwaka 1998, huduma za ugani zinaendeshwa kupitia vikundi vya wakulima, miradi ya kilimo, Wakala wa Huduma za Pembejeo, Vyuo vya Mafunzo ya Kilimo, Vyuo vya Wakulima (FTCs) na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs), Vyama vya Wakulima, Mashirika yasiyo ya Serikali (Non Government Organizations - NGOs), mashirika ya kijamii (Community Based Organizations – CBOs), mashirika ya dini, makampuni ya zana za kilimo, wataalam binafsi wa kilimo, vyombo vya habari, maonyesho ya kilimo na siku za wakulima.

4.4 Kuimarisha Udhibiti wa Visumbufu vya Mazao na MimeaWizara inahusika na kusimamia udhibiti wa milipuko ya visumbufu vihamavyo hususan nzige, kwelea kwelea, viwavijeshi na panya. Aidha, Wizara pia hutoa ushauri kuhusu mbinu endelevu za udhibiti wa visumbufu vya mimea na mazao. Jukumu lingine la Wizara ni uzalishaji wa wadudu maadui wa visumbufu kwa ajili ya udhibiti wa kibiolojia. Katika kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Hifadhi ya Mimea na Mazao ya mwaka wa 1997, Wizara inasimamia utekelezaji wa karantini ya mimea na uagizaji, utengenezaji na matumizi ya viuatilifu. Katika kipindi cha Miaka 50 tangu Uhuru, visumbufu mbalimbali vya mimea na mazao viliendelea kudhibitiwa kwa lengo la kupunguza upotevu wa mazao na uharibifu

kilimo miaka 50.indd Sec1:18kilimo miaka 50.indd Sec1:18 11/16/11 10:34:34 AM11/16/11 10:34:34 AM

Page 35: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

19

wa mazingira. Visumbufu hivyo ni dumuzi, kidung’ata wa muhogo, gugu maji, nondo mgongo almasi, nzi wa matunda, nzi mweupe, utitiri wa muhogo, funza wa mabua, nzige wekundu, kwelea kwelea, viwavijeshi, panya na kiduha. Magonjwa mengine yanayodhibitiwa ni mnyauko wa migomba (Banana Wilt) na mnyauko fusari wa mibuni. Katika udhibiti wa nzige Wizara inashirikiana na Mashirika ya Kimataifa ya Kudhibiti Nzige ambayo ni International Red Locust Organisation for Central and Southern Africa (IRLCO-CSA) na Desert Locust Control Organisation for East Africa (DLCO-EA).

Wakulima wakiwa katika mafunzo kuhusu mbinu za kilimo bora kupitia shamba darasa

4.5 Kuongeza Uzalishaji wa Mazao ya BiasharaMazao makuu ya biashara yanayozalishwa nchini Tanzania kabla na baada ya Uhuru ni pamoja na chai, kahawa, tumbaku, pamba, mkonge, pareto, sukari na korosho. Uzalishaji wa mazao hayo umekuwa ukipanda na kushuka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, mabadiliko ya kisera, upatikanaji wa pembejeo na mabadiliko ya bei katika soko la dunia. Mara baada ya Uhuru Serikali ilichukua jukumu la kusimamia uzalishaji wa mazao hayo ikiwa ni pamoja na kuruhusu wakulima wadogo kuanza kilimo cha mazao ya biashara kwa lengo la kuongeza mchango wa mazao hayo katika uchumi. Mwaka 1967 lilipotangazwa Azimio la Arusha asilimia kubwa ya mashamba ya wakulima binafsi yalitaifi shwa na kuwa chini ya usimamizi wa Serikali. Mwanzoni mwa miaka ya 1970, sheria zilitungwa na kuweka usimamizi wa mazao hayo kuwa chini ya mashirika ya umma ambayo yalipewa jukumu la kumiliki na kuendesha mashamba hayo. Hadi mwaka 1975 kulikuwa na Mashirika 12 chini ya Wizara ambayo ni Mamlaka ya Pamba, Mamlaka ya Mkonge, Mamlaka ya Korosho, Mamlaka ya Tumbaku, Mamlaka ya Chai, Mamlaka ya Maendeleo ya Mifugo, Bodi ya Kahawa, Bodi ya Pareto, Shirika la Taifa

kilimo miaka 50.indd Sec1:19kilimo miaka 50.indd Sec1:19 11/16/11 10:34:34 AM11/16/11 10:34:34 AM

Page 36: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

20

la Kilimo na Chakula (NAFCO), Shirika la Maendeleo ya Sukari, Shirika la Taifa la Usagishaji (NMC) na Shirika la Kuuza Nje Mazao ya Kilimo (GAPEX). Usimamizi wa mazao makuu ya biashara katika vipindi tofauti tangu nchi ipate uhuru ni kama ifuatavyo.

4.5.1 MkongeZao la mkonge ni zao la kihistoria nchini Tanzania, ambalo lililetwa mnamo mwaka 1893 na mtafi ti wa Kijerumani. Shamba la kwanza lilianzishwa mwaka 1900 katika kitongoji cha Bushiri Wilayani Pangani kabla ya kusambaa katika mikoa ya Morogoro, Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Lindi, Mtwara, Arusha, Mara, Shinyanga na Mwanza. Baada ya Uhuru zao hilo liliifanya Tanganyika na baadaye Tanzania kuongoza katika mauzo ya nje ulimwenguni ambapo rekodi ya juu kabisa ilikuwa tani 230,000 ya mwaka 1964 ambayo ilikuwa ni sawa na asilimia 65 ya mauzo yote ya nje ya nchi. Usimamizi wa zao la mkonge mwaka 1961 ulikuwa chini ya Muungano wa Wakulima wa Mkonge (ushirika), ukafuatiwa na Shirika la Mkonge Tanzania, Mamlaka ya Mkonge na sasa Bodi ya Mkonge Tanzania.

4.5.2 ChaiHistoria ya kilimo cha chai nchini inaanzia mwaka 1902, wakati wakoloni wa Kijerumani walipoingiza zao hilo katika kituo cha utafi ti wa kilimo kilichopo Amani mkoani Tanga. Uzalishaji wa chai kibiashara ulianza kwenye mashamba makubwa ya chai katika wilaya za Rungwe, Njombe, Mufi ndi, Muheza na Bukoba. Baadaye, mashamba mengine yalipandwa chai huko Korogwe na hadi mwaka 1961 eneo lililokuwa limepandwa chai na wakulima wakubwa lilikuwa hekta 7,797. Wilaya nyingine zinazolima zao la chai kwa sasa ni Muleba, Lushoto, Kilolo, Ludewa na Tarime. Mwaka 1961, usimamizi wa zao la chai ulikuwa chini ya Bodi ya Chai Tanganyika, ambapo mwaka 1968 ulikuwa chini ya Mamlaka ya chai ambayo pia ilipewa jukumu la kuwaendeleza wakulima wadogo wa chai kuzalisha, kusindika na kuuza chai. Mwaka 1997 iliundwa Wakala wa Maendeleo ya Wakulima Wadogo wa Chai kwa ajili ya kuendeleza zao la chai, wakati usimamizi ulibaki kuwa chini ya Bodi ya Chai.

4.5.3 PambaPamba iliingizwa nchini Tanzania na wakoloni wa Kijerumani mwaka 1903, lakini uzalishaji wa zao hilo kibiashara ulianza mwaka 1922. Pamba ilianza kuzalishwa Kanda ya Mashariki katika mikoa ya Morogoro, Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Manyara, Iringa na Mbeya. Miaka michache baadaye zao la pamba lilienezwa katika mikoa ya Kanda ya Magharibi kwa sasa ikijumuisha mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Tabora, Singida, Kagera na Kigoma. Hadi mwaka 1930 uzalishaji wa pamba ulikuwa marobota 7,200 ambapo marobota 4,000 yalikuwa yakizalishwa katika Kanda ya Mashariki na marobota 3,200 yalizalishwa katika Kanda ya Magharibi. Baada ya Tanganyika kupata Uhuru mwaka 1961, chombo kilichokuwa na dhamana ya kusimamia na kuendeleza zao la pamba kilikuwa ni Lint and Seed Marketing Board of Tanganyika. Mara baada ya Azimio la Arusha uzalishaji wa pamba uliongezeka kwa kiasi kikubwa. Hii ilitokana na kuanzishwa kwa Bodi ya Pamba ambayo ilipunguziwa

kilimo miaka 50.indd Sec1:20kilimo miaka 50.indd Sec1:20 11/16/11 10:34:34 AM11/16/11 10:34:34 AM

Page 37: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

21

majukumu ikabaki na jukumu la kusimamia maendeleo ya zao la pamba na shughuli za ununuzi kufanywa na Vyama vya Ushirika. Mwaka 1976; usimamizi wa zao la pamba ulikuwa chini ya Mamlaka ya Pamba na kuanzia mwaka 1984; ulikuwa chini ya Bodi ya Pamba (TCMB). Aidha, mwaka 1991; usimamizi wa pamba ulikuwa chini ya Tanzania Cotton Lint & Seed Board (TCL & SB) na kuanzia mwaka 1993 ulifanywa kuwa chini ya Bodi ya Pamba.

4.5.4 SukariMara baada ya Uhuru National Sugar Board (NSB) ilianzishwa ili kusimamia uuzaji wa sukari nchini na uagizaji wa sukari toka nchi za nje. Baadaye majukumu hayo yalihamishiwa Shirika la Kilimo na Chakula (National Agriculture and Food Corporation-NAFCO) ambalo pia lilihusika na mazao mengine ya chakula. Mwaka 1974 Serikali iliweka msukumo katika kuendeleza zao la sukari kwa kuanzisha Shirika la Maendeleo ya Sukari (Sugar Development Corporation-SUDECO). SUDECO ilipewa majukumu ya kusimamia uzalishaji, uuzaji na uagizaji wa zao la sukari. Aidha SUDECO ilikuwa na jukumu la kusimamia mashamba na viwanda vyote vya sukari nchini kwa niaba ya Serikali. Serikali ilibinafsisha kazi ya uzalishaji na uuzaji wa sukari kati ya mwaka 1998/99 na 2001/02. Kuanzia mwaka 2001 majukumu ya kuendeleza, kuhamasisha na kusimamia zao la sukari yaliwekwa chini ya Bodi ya Sukari Tanzania.

4.5.5 TumbakuZao la tumbaku liliingizwa nchini mwaka 1930 kutokea Nyasaland (sasa Malawi) na kuanza kulimwa mkoani Ruvuma. Kuanzia mwaka 1949 uzalishaji ulifanyika katika maeneo ya Tabora, Kahama, Mpanda na Chunya. Maeneo yanayozalisha tumbaku yameongezeka mwaka hadi mwaka, ambapo hadi mwaka 2011 inalimwa katika mikoa 10 ya Tanzania bara ambayo ni Tabora, Shinyanga, Rukwa/Katavi, Mbeya, Kigoma, Kagera, Singida, Iringa, Ruvuma na Mara. Usimamizi wa zao la tumbaku mwaka 1960 na mara baada ya Uhuru ulikuwa chini ya Bodi ya Tumbaku ya Tanganyika. Mwaka 1983, usimamizi wa zao hilo ulibadilika na kuwa chini ya Bodi ya Usindikaji na Mauzo ya Tumbaku (Tanzania Tobacco Processing and Marketing Board-TTP&MB). Kuanzia mwaka 1993, usimamizi wa zao la tumbaku uliwekwa chini ya Bodi ya Tumbaku Tanzania.

4.5.6 KoroshoKatika Miaka 50 ya Uhuru, usimamizi wa zao la korosho umepita katika mabadiliko ya kisheria na miundo mbalimbali. Mwaka 1962 zao la korosho lilikuwa linasimamiwa na chombo kilichojulikana kama Southern Region Cashewnut Board. Kuanzia mwaka 1963 kulifanyika mabadiliko na chombo hicho kujulikana kama Southern Agricultural Products Board. Mwaka 1964 usimamizi wa zao la korosho ulikuwa chini ya National Agricultural Products Board, ambao ulidumu hadi mwaka 1974 kilipoundwa chombo kingine kilichoitwa Cashewnut Authority of Tanzania. Kuanzia mwaka 1985 Tanzania Cashewnut Marketing Board ilianza kusimamia zao la korosho hadi mwaka 1993. Kuanzia mwaka 1993 hadi 2011, Bodi ya Korosho Tanzania (BKT) ndiyo msimamizi wa zao la korosho kwa mujibu wa sheria.

kilimo miaka 50.indd Sec1:21kilimo miaka 50.indd Sec1:21 11/16/11 10:34:34 AM11/16/11 10:34:34 AM

Page 38: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

22

Jitihada za kuongeza ubanguaji wa korosho unaonyesha kuwa mwaka 1963 ulifanywa na mitambo chini ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na baadaye kufanywa na Tanganyika Italian Company Ltd (TANITA) kupitia kiwanda cha Dar es Salaam na mwaka 1968 kiwanda kingine kilichojengwa Mtwara kiliitwa Mtwara Cashew Company. Ujenzi wa viwanda vingine zaidi uliendelea chini ya usimamizi wa Bodi ya Korosho Tanzania na hadi kufi kia Desemba 31, 2001 kulikuwa na jumla ya viwanda 12 na kisima cha kutunzia mafuta ya korosho cha CNSL kilichojengwa Mtwara. Upungufu wa korosho kutoka tani 140,000 hadi tani 16,000 kwa mwaka ulisababisha viwanda vya ubanguaji kufungwa. Baadhi ya matatizo yaliyolikumba zao la korosho hivi sasa yamepata ufumbuzi au yamo kwenye mchakato wa kupata ufumbuzi.

4.5.7 KahawaMara baada ya Uhuru kahawa ilienea na kulimwa katika maeneo mengi ya nchi ambapo mpaka mwaka 2011 zao hilo linalimwa katika mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Kigoma, Rukwa, Ruvuma, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mbeya, Tanga na Morogoro. Mara baada ya Uhuru Serikali iliunda Bodi ya kwanza ya kusimamia zao la kahawa iliyoitwa Tanganyika Coffee Board kwa lengo la kusaidia kuongeza tija kwa wakulima wadogo wa kahawa kwani mfumo wa awali chini ya chama kilichoitwa Tanganyika Association of Coffee Traders Agency (TACTA) ulikuwa kwa maslahi ya wakulima wenye mashamba makubwa. Katika kipindi kati ya mwaka 1961 na 1976 chombo cha usimamizi wa zao hilo kilijulikana kama Bodi ya Kahawa Tanganyika. Mwaka 1977, iliundwa Mamlaka ya Kahawa Tanzania (Coffee Authority of Tanzania - CAT). Mwaka 1984 Serikali iliweka usimamizi wa zao la kahawa chini ya Bodi ya Masoko ya Kahawa (Tanzania Coffee Marketing Board-TCMB). Mwaka 1993, usimamizi wa zao hilo uliwekwa chini ya Bodi ya Kahawa Tanzania.

4.5.8 ParetoZao la pareto liliingizwa nchini kutoka Kenya miaka ya 1930. Kuanzia mwaka 1930 hadi 1950 zao hilo lilikuwa likilimwa na wazungu katika mashamba makubwa (estates), maeneo ya Nyanda za Juu Kaskazini ikijumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Tanga. Kiwanda cha kusindika pareto kilijengwa Arusha (Tanganyika Extract Company Limited) katika miaka ya 1960. Wakati wa utekelezaji wa Azimio la Arusha mashamba makubwa yalitaifi shwa, hivyo wakulima wadogo (small scale growers) wakaanza uzalishaji wa pareto katika Nyanda za Juu Kusini, mikoa ya Iringa na Mbeya. Uzalishaji wa pareto katika Nyanda za Juu Kaskazini ulipungua miaka ya 1970, wakati uzalishaji Nyanda za Juu Kusini uliongezeka na Serikali ililazimika kujenga kiwanda cha pareto Mafi nga mkoani Iringa na kukifunga kile cha Arusha. Mwanzoni mwa mwaka 1998 Bodi ya Pareto Tanzania ilianzishwa na kupewa jukumu la kusimamia sera na sheria katika sekta ya pareto, ambapo shughuli zote za ununuzi, usindikaji na uuzaji nje (export) zilihamishiwa sekta binafsi.

kilimo miaka 50.indd Sec1:22kilimo miaka 50.indd Sec1:22 11/16/11 10:34:34 AM11/16/11 10:34:34 AM

Page 39: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

23

4.6 Kuongeza Uzalishaji wa Mazao ya Chakula, Mbegu za Mafuta na Mazao ya BustaniMazao ya chakula yaliyotiliwa mkazo tangu mwaka 1961 ni pamoja na yale ya nafaka kama vile mahindi, mtama, uwele, mpunga, ngano, na ulezi. Mazao mengine ya chakula ni yale ya aina ya mikunde, muhogo na ndizi. Mazao ya mbegu za mafuta yanayotiliwa mkazo ni alizeti, karanga, ufuta, michikichi na pamba. Aidha, mazao ya bustani ni pamoja na matunda, mboga, viungo na maua. Katika kuongeza uzalishaji wa mazao hayo jitihada mbalimbali zimekuwa zikitekelezwa na Serikali. Juhudi hizo ni pamoja na kuongeza upatikanaji wa mbolea, mbegu bora, kuimarisha huduma za ugani, matumizi ya zana bora za kilimo na kupanua kilimo cha umwagiliaji. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na wadau kama Tanzania Horticulture Association (TAHA) imekuwa ikitoa mafunzo kwa wakulima na watalaam kuhusu uendelezaji wa mazao ya bustani. Mafunzo hayo yanahusu mbinu za uzalishaji bora ili kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao ya bustani. Wizara pia kwa kushirikiana na wadau ilianzisha Baraza la kuendeleza Mazao ya Bustani (Horticultural Development Council of Tanzania- HODECT) na kulisajili Machi 2007. Lengo ni kuwa na mfumo wa kuratibu uzalishaji wa mazao ya bustani na kazi zinazofanywa na wadau mbalimbali. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na HODECT na wadau wengine imeandaa mkakati wa kuendeleza mazao ya bustani (Tanzania Horticulture Development Strategy)

4.7 Kusimamia Upatikanaji wa Pembejeo za KilimoPembejeo za kilimo ni pamoja na mbegu bora, mbolea na viuatilifu. Tangu nchi ipate Uhuru zimekuwepo jitihada mbalimbali za kuongeza upatikanaji wa mbegu bora, mbolea na viuatilifu ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara. 4.7.1 Uzalishaji na Usambazaji wa Mbegu BoraMwaka 1973, kampuni ya kwanza ya mbegu bora iliyoitwa Tanzania Seed Company (TANSEED) ilianzishwa kwa lengo la kuzalisha na kusambaza mbegu bora nchini. TANSEED iliweza kufi kisha kiwango cha uzalishaji wa tani 6,781 na ilipofi ka mwaka 1998/1999 uzalishaji huo ulipungua hadi kufi kia tani 589.4 za mbegu bora zikijumuisha mazao ya nafaka, mikunde na mbegu za mafuta. Baada ya kufi lisika kwa kampuni ya TANSEED mwaka 1990 Serikali iliruhusu makampuni binafsi ya ndani na nje ya nchi kuwekeza katika kuzalisha na kusambaza mbegu bora. Hadi mwaka 2011 kuna jumla ya makampuni 53 ambayo yamesajiliwa kisheria nchini. Aidha, mwaka 2006, Serikali ilianzisha Wakala wa Mbegu za Kilimo (Agricultural Seed Agency) kwa lengo la kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa mbegu bora nchini. Mahitaji ya mbegu bora yamefi kia tani 120,000 kwa mwaka iwapo kila mkulima atatumia mbegu bora. Hata hivyo, upatikanaji umeongezeka kutoka tani 6,781 mwaka 1980 hadi tani 17,000 mwaka 2011. Lengo la Serikali ni kuongeza upatikanaji pamoja na matumizi ya mbegu bora ili yafi kie tani 60,000 za mazao ya nafaka, mikunde na mbegu za mafuta ifi kapo mwaka 2015.

kilimo miaka 50.indd Sec1:23kilimo miaka 50.indd Sec1:23 11/16/11 10:34:35 AM11/16/11 10:34:35 AM

Page 40: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

24

4.7.2 MboleaKabla ya kuanza kwa utekelezaji wa sera ya mfumo wa soko huru mwaka 1985, Serikali ilihusika moja kwa moja na uagizaji, usambazaji na uuzaji wa mbolea za viwandani kupitia Kampuni ya Mbolea ya Tanzania (Tanzania Fertilizer Company-TFC) na Vyama vya Ushirika. Baada ya mfumo wa soko huru kuanza idadi ya waagizaji na wasambazaji wa mbolea iliongezeka. Aidha, udhibiti wa ubora wa mbolea ulisimamiwa na Sheria ya Mbolea na Chakula cha Mifugo ya mwaka 1962. Hali hiyo ilisababisha Serikali kutunga Sheria Mpya ya Mbolea Na. 9 ya mwaka 2009 ili kukidhi mabadiliko ya kijamii na kiuchumi kulingana na soko huru.

4.7.3 Ruzuku ya PembejeoRuzuku ya pembejeo ilianza mwaka 1974 wakati wa kutekeleza Mradi wa Mahindi wa Taifa (National Maize Programme) ambao uliishia mwaka 1986. Mwaka 1980 ruzuku ilipanuliwa na kuhusisha mazao mengine chini ya Mpango wa Mbolea wa Taifa (National Fertilizer Programme). Mpango huo uliongeza matumizi ya mbolea kutoka tani 70,392 kwa miaka ya 1970 hadi kufi kia tani 91,303 mwaka 1994. Mwaka 1991 kiwanda cha mbolea cha Tanga kilifungwa na Serikali ilijitoa katika biashara ya pembejeo (ikiwemo mbolea). Hali hiyo ilisababisha kupanda kwa bei ya mbolea na matumizi kushuka toka wastani wa tani 91,303 mwaka 1994 hadi kufi kia tani 61,289 mwaka 1998. Mwaka 2003/2004, Serikali ilirejesha mpango wa kutoa ruzuku ya mbolea kwa kuingia mkataba na makampuni ya mbolea ili yaweze kusambaza pembejeo kwenye vituo vikuu na kuziuza kwa bei iliyokubaliwa baina ya Serikali na makampuni. Madhumuni ya Serikali kurejesha ruzuku kwenye pembejeo ilikuwa kuhakikisha kila mkulima anapata pembejeo kwa bei nafuu ili kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo. Mwaka 2008/2009 Serikali ilianza kutoa ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa kutumia mfumo wa vocha kwa lengo la kuhakikisha mbolea inawafi kia wakulima kwa bei nafuu.

4.8 Kuongeza Uhakika na Usalama wa ChakulaTangu tupate Uhuru lengo kuu la Serikali katika kuhakikisha Taifa linajitosheleza kwa chakula ilikuwa ni kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula. Sheria ya Mazao (Agricultural Produce Act) ya mwaka 1962 na ile ya Food Security Assistance Scheme (1976) zililenga katika kupunguza uagizaji wa chakula kutoka nje ya nchi. Matokeo yake yalikuwa ni uanzishwaji wa Ghala la Taifa la Nafaka (SGR) chini ya Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC) na pia uundwaji wa Kitengo cha Uratibu wa Mazao na Tahadhari ya Njaa (Crop Monitoring and Early Warning Unit) kilichokuwa chini ya Wizara ya Kilimo. Mwaka 1984 ulianzishwa Mkakati wa Taifa wa Chakula ambao ulilenga kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na kuboresha hali ya lishe ya watu walio katika makundi hatarishi. Mwaka 1986 vipengele mbalimbali vilivyosababisha uhaba wa chakula vilitambuliwa na kupendekeza hatua za kuvirekebisha ili kuboresha utekelezaji wa huduma muhimu. Sheria ya Usalama wa Chakula (The Food Security Act) ilihamisha shughuli mbalimbali zinazohusiana na mazao ya chakula kutoka Shirika la Usagishaji la Taifa kwenda Wizara ya Kilimo na Chakula chini ya Idara ya usalama wa chakula. Aidha, mwaka 1995 Programu Maalumu ya Taifa ya Usalama wa Chakula

kilimo miaka 50.indd Sec1:24kilimo miaka 50.indd Sec1:24 11/16/11 10:34:35 AM11/16/11 10:34:35 AM

Page 41: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

25

ilianzishwa chini ya ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO). Programu hiyo ililenga kuongeza uzalishaji wa mazao makuu ya chakula kwa kuboresha huduma za ugani. Programu hiyo ilitekelezwa chini ya mradi uliolenga vikundi maalumu vya wakulima vilivyoteuliwa. Programu hiyo ilitekelezwa kwa mafanikio katika maeneo ya majaribio (pilot areas) na mafanikio hayo yameenezwa na kutumika katika maeneo mbalimbali nchini. Ili kuweka msukumo zaidi katika kusimamia usalama wa chakula, mwaka 2000 Idara ya Usalama wa Chakula ilianzishwa chini ya Wizara ya Kilimo na Chakula ikiwa na majukumu yafuatayo:- (i) Kubuni sera, kuandaa mikakati na kuratibu utekelezaji wa Programu za Usalama wa Chakula (ii) Kuratibu hali ya chakula nchini na kutoa tahadhari ya njaa (iii) Kufanya tathmini mbalimbali za kisera kuhusu usalama wa chakula (iv) Kutoa huduma za hifadhi ya mazao kwa lengo la kupunguza upotevu wa mazao ya chakula baada ya mavuno (v) Kuhamasisha matumizi ya mazao mbalimbali ya chakula kwa lengo la kupanua wigo wa aina ya vyakula vikuu vinavyotumiwa na jamii (vi) Kuhamasisha usindikaji wa mazao ya chakula katika maeneo ya uzalishaji kwa lengo la kuongeza ubora, muda na eneo la matumizi (vii) Kuhamasisha usindikaji kwa lengo la kuongeza thamani.

4.9 Kusimamia Akiba ya Chakula ya TaifaChimbuko la uanzishwaji wa akiba ya chakula ya Taifa lilitokana na ukame ulioikumba nchi yetu miaka ya 1973 hadi 1975 na kusababisha baa kubwa la njaa, hali ambayo iliifanya nchi kutegemea chakula kutoka nje ya nchi kilichoagizwa kibiashara pamoja na chakula cha msaada kutoka kwa nchi wahisani. Baada ya baa hilo la njaa, Serikali iliamua kubuni mkakati pamoja na kuanzisha chombo mahususi kinachomilikiwa na Serikali ambacho kilipewa jukumu la kununua na kuhifadhi chakula cha akiba. Chombo cha kwanza kuundwa kwa madhumuni hayo ni Bodi ya Mazao ya Kilimo (National Agricultural Produce Board - NAPB) mwaka 1973 na baadaye likaanzishwa Shirika la Usagishaji la Taifa (National Milling Corporation - NMC). Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC) lilikuwa na majukumu makuu mawili ambayo ni kuendesha biashara ya chakula (commercial role), na kusambaza chakula kwa waathirika wa njaa (social role). Katika miaka ya 1990 Serikali ilichukua hatua ya kuondoa SGR kutoka NMC; na kuwekwa chini ya usimamizi wa Wizara ya Kilimo. Mwaka 1990/91 SGR ilikuwa na kiasi cha tani 107,000 za mahindi kwa ajili ya akiba ya chakula ya Taifa. Shughuli za SGR zimeendelea kuimarishwa ambapo mwaka 2008 ulianzishwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (National Food Reserve Agency-NFRA). NFRA inafanya kazi katika kanda saba ambazo ni Arusha, Dodoma, Kipawa, Makambako, Shinyanga, Songea na Sumbawanga. NFRA kwa sasa ina jumla ya maghala 30 yenye uwezo wa kuhifadhi nafaka mita za ujazo 241,000 katika maeneo muhimu ya uzalishaji na usambazaji nchini.

4.10 Kuimarisha Matumizi Bora ya Ardhi ya KilimoKabla ya ukoloni ardhi ilikuwa ikitumiwa na kusimamiwa kimila. Ardhi iligawanywa kwa matumizi mbalimbali na kupewa majina ya utambuzi. Kwa mfano “Ngitili” lilimaanisha eneo la hifadhi ya malisho ya mifugo nyakati za ukame katika jamii za wafugaji mkoani

kilimo miaka 50.indd Sec1:25kilimo miaka 50.indd Sec1:25 11/16/11 10:34:35 AM11/16/11 10:34:35 AM

Page 42: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

26

Shinyanga. Jamii nzima iliwajibika kusimamia matumizi yaliyopangwa na kuhakikisha kila eneo linatumiwa ilivyokusudiwa. Aina za udongo pia zilitambuliwa na kupewa majina ya utambuzi, kwa mfano, mkoani Tabora udongo mwekundu ulijulikana kama "Kikungu", "Ipwisi" kwa udongo hudhurungi na "Ibushi" kwa udongo mweusi, na matumizi yanayofaa (suitability) kwa aina hizo za udongo yalijulikana. Wakati nchi ikiwa chini ya utawala wa Ujerumani (1891-1917) kulikuwa na uwekezaji katika kuandaa ramani zilizotumika zaidi katika kusaidia harakati za kijeshi na ukusanyaji wa kodi, na pia ujenzi wa barabara na reli kwa lengo la kurahisisha harakati za kusafi risha rasilimali mbalimbali za nchi yakiwemo madini, magogo ya miti ya thamani na wanyamapori. Aidha, ardhi nzuri na yenye rutuba ilitumika katika kuendesha kilimo cha mazao ya biashara kama pamba, katani (maeneo tambarare), kahawa (kwenye ardhi ya miinuko). Mfumo huu wa uzalishaji wa mazao maalumu na matumizi ya ardhi ya kilimo uliendelezwa chini ya utawala wa Waingereza na kufi kia mwaka 1910 kulikuwa na mashamba makubwa 54 ya zao la katani. Ujenzi wa reli ya Tanga-Moshi uliwawezesha walowezi wa kikoloni kutwaa na kumiliki ardhi ya Usambara Mashariki na kulima zao la kahawa na hatimaye kwenye miteremko ya mlima Kilimanjaro. Maeneo ambayo hawakupewa walowezi yalitangazwa kuwa hifadhi ya misitu. Kati ya mwaka 1923 na1961 wakulima wa kizungu walikuwa wamepewa ardhi yenye ukubwa wa zaidi ya eka milion tatu. Aidha, hifadhi ya ardhi kwa wakati huo ilijikita katika mambo yafuatayo:- (i) kuhifadhi ardhi na kudhibiti mmomonyoko wa udongo mashambani (ii) kudhibiti idadi ya mifugo ( stocking levels) na (iii) kudhibiti visumbufu vya mimea. Wakati wa utawala wa Waingereza sheria ya ardhi iliyotumika ilijulikana kama Land Ordinance ya mwaka 1923 ambapo jamii ya wazawa walinyimwa jukumu la kusimamia ardhi yao kwa kuwa ardhi ilitangazwa kuwa mali ya Mfalme (Crown Land). Sheria hiyo ilizaa mifumo miwili ya ugawaji ardhi yaani leasehold na customary ambao upo hata leo. Aidha, utekelezaji wa sheria hiyo uliondoa haki ya wazawa kusimamia matumizi ya ardhi yao na hivyo kusababisha kuporomoka kwa mifumo endelevu ya asili ya usimamizi na matumizi ya rasilimali ardhi. Wakati wa vita vya pili vya dunia uzalishaji wa kilimo ulilenga mazao maalumu hususan katani, mpira, na pamba. Mashamba makubwa yenye miundombinu ya kilimo yalianzishwa mwaka 1942 kwa zao la ngano ambapo hekta 8000 zililimwa kwenye mikoa ya Kilimanjaro na Arusha. Ilipokaribia mwishoni mwa vita hiyo zilianzishwa skimu chache za wakulima wakubwa (large peasant farming schemes) ambapo pamoja na mambo mengine zilijihusisha na udhibiti wa mmomonyoko wa udongo mashambani. Miongoni mwa skimu hizo ni (i) Sukumaland Development Scheme iliyoanzishwa mwaka 1947 kusini mwa Ziwa Viktoria (Geita), na ililenga uzalishaji wa zao la pamba; na (ii) Mbulu Development Scheme iliyolenga kuhesabu mifugo na kulazimisha kupunguza idadi pale ilipozidi uwezo wa ardhi na upatikanaji endelevu wa malisho. Pia zilianzishwa skimu za kuhifadhi udongo kwenye mitelemko ya milima ya Uluguru, Usambara na Upare ambapo wakulima walilazimishwa kulima matuta ya meza (bench terraces). Ulazimishaji huo haukukubalika miongoni mwa jamii zilizohusika, hivyo maendeleo hayakuwa mazuri.

kilimo miaka 50.indd Sec1:26kilimo miaka 50.indd Sec1:26 11/16/11 10:34:35 AM11/16/11 10:34:35 AM

Page 43: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

27

Ingawa taratibu mbalimbali za kupanga na kusimamia matumizi ya ardhi zilikuwepo nchini kabla ya uhuru, mifumo na malengo yake vilitofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine, na kazi zilizopangwa zililenga zaidi kwenye maeneo yaliyolimwa mazao ya biashara kama kahawa, chai, katani, karanga na tumbaku. Kazi hizo zilihusisha (i) upimaji udongo (soil surveys) (ii) tathmini ya ubora wa ardhi (land resource inventories) (iii) upimaji wa mashamba (farm boundary surveys) (iv) uandaaji wa mipango ya kina ya matumizi ya ardhi mashambani (farm lay-out) na (v) hifadhi ya udongo na maji mashambani (soil and water conservation). Katika Miaka 50 ya Uhuru, usimamizi wa mipango ya hifadhi ya udongo na maji mashambani na matumizi bora ya ardhi ya kilimo ni mojawapo ya shughuli za Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika. Katika kuleta matumizi endelevu ya rasilimali ardhi, Wizara imekuwa ikitekeleza kazi hizo kwa kuzingatia majukumu ya Wizara nyingine za sekta ya ardhi ambazo pia husimamia na kuratibu matumizi ya ardhi iliyo chini ya mamlaka husika. Wizara imekuwa ikielimisha wakulima na maafi sa ugani juu ya teknolojia mbalimbali za hifadhi ya udongo na maji mashambani. Aidha, Wizara imekuwa ikishiriki katika shughuli za upimaji wa mashamba ya wakulima wanaotaka kupata hati miliki za ardhi yao. Katika kuimarisha uwezo wa utoaji wa huduma zinazohusu matumizi bora ya ardhi ya kilimo mwaka 2010 Wizara ilianza kupeleka wataalamu wa fani hiyo kwenye vituo vya kanda ili washirikiane na wataalamu wa mikoa na Halmashauri katika kuwahudumia wananchi. Kanda tano (Ziwa, Nyanda za Juu Kusini, Mashariki, Kati na Kaskazini) kati ya saba zina wataalam hao. Uimarishaji wa vituo vya kanda utaendelea kutegemea upatikanaji wa rasilimali watu na fedha.

4.11 Kuongeza Matumizi ya Zana Bora za KilimoMatumizi ya zana bora za kilimo ni muhimu katika kuondoa umaskini kwa kuwawezesha wakulima kupanua maeneo wanayolima pamoja na kuongeza uzalishaji na kipato. Kabla ya uhuru kuanzia miaka ya 1930, trekta nyingi ziliingizwa nchini kwa ajili ya kutayarisha na kulima mashamba. Mwaka 1950 kulikuwa na trekta 2,057 zilizokuwa zinatumika nchini na ziliongezeka hadi kufi kia trekta 2,580 mwaka 1960 kabla ya Uhuru. Baada ya Uhuru, Serikali ilianzisha skimu 40 za makazi katika maeneo mbalimbali nchini ambapo zana za kilimo hasa trekta zilitumika kwa ajili ya kutayarisha na kulima mashamba. Zaidi ya asilimia 60 ya gharama ya uwekezaji wa Serikali katika skimu hizo za makazi ulikuwa ni kwa ajili ya trekta na zana zake. Katika kipindi hicho Serikali iliendelea na juhudi nyingine za kuongeza matumizi ya zana za kilimo. Kwa mfano mwaka 1963, Serikali iliingiza nchini trekta 159 ambazo zilitumiwa na Shirikisho la Vyama vya Ushirika la Viktoria (Victoria Federation of Cooperative Union) kwa lengo la kukodisha kwa wakulima katika mashamba makubwa ya pamba. Katika miaka ya 1970, vituo vya kukodisha trekta vya mikoa na wilaya vilianzishwa na mikopo nafuu ilitolewa kwa wakulima, vijiji vya ujamaa pamoja na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kununua trekta na zana zake kupitia iliyokuwa Benki ya

kilimo miaka 50.indd Sec1:27kilimo miaka 50.indd Sec1:27 11/16/11 10:34:35 AM11/16/11 10:34:35 AM

Page 44: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

28

Ushirika na Maendeleo Vijijini (CRDB) pamoja na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC). Hali hiyo iliinua kwa kiasi kikubwa matumizi ya zana bora za kilimo kwani idadi ya trekta zilizokuwa zinatumika nchini ilifi kia 9,000 katika mwaka 1975. Sambamba na kuhimiza matumizi ya trekta, Serikali iliendelea kuhimiza matumizi ya wanyamakazi. Kwa mfano, mwaka 1972 Azimio la Iringa la Siasa ni Kilimo, lilielekeza Serikali kuongeza matumizi ya wanyamakazi ambapo vituo 80 vya kufundishia matumizi ya wanyamakazi (OTC) vilianzishwa nchini kote. Aidha, viwanda viwili vya kutengeneza zana za kukokotwa na wanyamakazi vilianzishwa ambavyo ni Ubungo Farm Implements (UFI) kilichoanzishwa mwaka 1970 kikiwa na uwezo wa kutengeneza majembe ya mkono 2,500,000 na plau zinazokokotwa na maksai 30,000 kwa mwaka. Aidha, Kiwanda cha Zana za Kilimo (ZZK) katika mkoa wa Mbeya kilianzishwa mwaka 1984 kikiwa na uwezo wa kutengeneza majembe ya mkono 1,500,000 na plau 10,000 za kukokotwa na maksai kwa mwaka. Katika mwaka 1981, Serikali ilianzisha kampuni ya kuunganisha trekta aina ya Valmet (Tanzania Tractor Manufacturing Company Limited-TRAMA) ambayo ilikuwa na uwezo wa kuunganisha trekta 300 hadi 500 kwa mwaka. Pia mradi wa zana za kilimo wa Morogoro (The Morogoro Mechanization Project) ulianzishwa mwaka 1984 ambapo trekta 150 aina ya FIAT ziliingizwa na kukopeshwa kwa wakulima, Serikali za vijiji na vyama vya ushirika. Aidha, kati ya mwaka 1984 na 1994 trekta 308 aina ya Kubota ziliingizwa nchini na kusambazwa kwa vyama vya ushirika na wakulima binafsi katika mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kuendeleza kilimo hasa cha zao la mpunga. Mwaka 1985 uingizaji wa trekta ulipungua kutokana na sababu mbalimbali kutoka wastani wa trekta 1,143 kwa mwaka hadi trekta 49 mwaka 1996, sambamba na kufungwa kwa viwanda vya UFI na ZZK kutokana na kupanda kwa gharama za uendeshaji. Katika kipindi cha mwaka 1995 hadi 2011, Serikali imeweka msukumo wa kuendeleza kilimo cha wanyamakazi na trekta kwa kuhamasisha sekta binafsi, na kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wakulima kupitia Mfuko wa Pembejeo. Mfuko huo ulianzishwa mwaka 1994 kwa lengo la kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa wakulima na wasambazaji wa pembejeo za kilimo na mifugo nchini.

4.12 Kuongeza Matumizi ya Kilimo cha UmwagiliajiLengo la kutumia kilimo cha umwagiliaji ni kuwa na uhakika wa uzalishaji wenye tija wa mazao kwenye maeneo ambayo kuna uhaba wa mvua au mvua hazinyeshi kwa mtawanyiko mzuri na kwa wakati kulingana na kipindi cha uzalishaji wa mazao. Hapa Tanzania kilimo cha umwagiliaji kilianza miaka mingi iliyopita hata kabla ya kuingia kwa utawala wa kikoloni. Baada ya Uhuru kumekuwepo na mikakati mbalimbali ya kuongeza matumizi ya kilimo cha umwagiliaji.

4.12.1 Kilimo cha Umwagiliaji Kabla ya Miaka ya 1990Mipango katika miaka 10 ya awali baada ya Uhuru ilikuwa ni kuendeleza eneo la hekta 10,000 kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji kwa nchi nzima ambapo hadi mwaka 1970 hekta 2,600 zilikuwa zimeendelezwa. Katika kuongeza kasi ya kupanua kilimo cha umwagiliaji, kati ya mwaka 1975 na 1979 Serikali za mikoa ziliwezeshwa kuendeleza

kilimo miaka 50.indd Sec1:28kilimo miaka 50.indd Sec1:28 11/16/11 10:34:35 AM11/16/11 10:34:35 AM

Page 45: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

29

umwagiliaji katika programu na miradi mbalimbali hapa nchini. Mwaka 1980 malengo ya kuendeleza umwagiliaji yalipitiwa na kufanyiwa tathmini ambapo msisitizo ulikuwa katika kuendeleza na kukarabati skimu za umwagiliaji za vijiji kupitia Mradi wa Kitaifa wa Kuendeleza Umwagiliaji Vijijini nchini kote. Skimu za umwagiliaji zilizolengwa ni zile zilizokuwa na maeneo ya ukubwa wa hekta 200 hadi 2,000 ili kufi kia hekta 150,000 ifi kapo mwaka 1985.

4.12.2 Kilimo cha Umwagiliaji Kuanzia Miaka ya 2000Mpango wa kitaifa wa kuendeleza Umwagiliaji (National Irrigation Development Plan- NIDP) uliandaliwa mwaka 1994, ukiwa na lengo la kutambua kwa ukamilifu matatizo na changamoto za umwagiliaji na namna ya kuzipatia ufumbuzi. Serikali ilitekeleza mapendekezo ya NIDP ambapo mwaka 2002 ilifanyiwa mapitio na matokeo yake ukaandaliwa Mpango Kabambe wa Taifa wa Umwagiliaji (National Irrigation Master Plan -NIMP). Katika mpango huo ilibainishwa kuwa eneo linalofaa kuendelezwa kwa kilimo cha umwagiliaji ni hekta milioni 29.4. Kati ya eneo hilo, hekta milioni 2.3 zina uwezekano mkubwa wa kuendelezwa (High development potential), hekta milioni 4.8 zina uwezekano wa kati wa kuendelezwa (Medium development potential) na hekta milioni 22.3 zina uwezekano mdogo wa kuendelezwa (Low development potential). Mtawanyiko wa maeneo yenye uwezekano wa kuendelezwa kilimo cha umwagiliaji Tanzania Bara umeonyeshwa katika ramani (Kiambatisho Na. 9); na mgawanyo wa maeneo hayo kimkoa umeonyeshwa katika Kiambatisho Na. 3. Kasi ya kuimarisha kilimo cha umwagiliaji nchini ilichukua sura mpya tangu kuanza kutekelezwa kwa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP) Julai 2006, ambapo Halmashauri za Wilaya ndiyo wamekuwa watendaji wakuu wa kazi za uendelezaji wa kilimo cha umwagiliaji kupitia Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (District Agricultural Development Plans - DADPs). Aidha, mwaka 2009/2010, Serikali ilikamilisha utayarishaji wa miongozo ya kiufundi ya kutekeleza miradi ya umwagiliaji kupitia Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (The Comprehensive Guidelines for Irrigation Scheme Development under District Agricultural Development Plans). Miongozo hiyo imetawanywa kwenye Halmashauri zote ili itumike kuibua na kutekeleza miradi ya umwagiliaji. Miradi inayopitishwa na Halmashauri hutekelezwa kwa fedha za Mfuko wa Kuendeleza Umwagiliaji ngazi ya Wilaya (District Irrigation Development Fund-DIDF), na Mfuko wa Kuendeleza Umwagiliaji ngazi ya Taifa (National Irrigation Development Fund-NIDF).

kilimo miaka 50.indd Sec1:29kilimo miaka 50.indd Sec1:29 11/16/11 10:34:35 AM11/16/11 10:34:35 AM

Page 46: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

30

5. MAENDELEO YA USHIRIKA5.1 Maendeleo ya Ushirika kabla ya UhuruHistoria ya Vyama vya Ushirika Tanzania inaanzia mwaka 1925 wakati chama cha kwanza cha Kilimanjaro Native Planters Association (KNPA) kilipoanzishwa huko Kilimanjaro. KNPA kilianzishwa na wakulima wadogo wa zao la kahawa. KNPA kilizingatia misingi muhimu ya ushirika ambayo ni (i) Uongozi wa kidemokrasia (ii) Uanachama ulio wazi na wa hiari. Mwaka 1932 KNPA ilibadilishwa na kuanzisha Kilimanjaro Native Co-operative Union Limited (KNCU). Hadi kufi kia mwaka 1960 KNCU ilikuwa na vyama vya msingi 62, vikiwemo 55 vya kahawa na 7 vya pamba. Mwaka 1960 Vyama vya Ushirika vya Pamba vilianzisha Chama Kikuu cha Tambarare Co-operative Union Limited. KNCU ilijihusisha na mambo ya jamii na kwa muda mfupi kiliweza kujenga shule na vyuo mbalimbali, maktaba, vituo vya afya na hoteli. KNCU kilikuwa Chama Kikuu cha Ushirika cha mfano kilichochochea maeneo mengine Tanganyika kuanzisha vyama vya ushirika.

5.2. Maendeleo ya Ushirika Baada ya UhuruMara baada ya Uhuru, Serikali ilitoa msukumo mkubwa wa kuanzishwa vyama vikuu katika mikoa na kuufanya ushirika kuwa ni nyenzo ya maendeleo ya uchumi vijijini na kutekeleza Sera ya Ujamaa na kujitegemea. Mwaka 1972, wakati wa utekelezaji wa sera ya madaraka mikoani ilielekeza kila mkoa uwe na chama kikuu cha ushirika. Mwaka 1976, Serikali ilivunja vyama vyote vya ushirika vya msingi vya vijijini pamoja na vyama vikuu. Shughuli za vyama vya msingi zilichukuliwa na vijiji na zile za vyama vikuu zilikabidhiwa kwenye Mamlaka za Mazao, Mashirika ya Biashara ya Mikoa, Mashirika ya Maendeleo ya Wilaya na Shirika la Usagishaji la Taifa. Hata hivyo, Serikali kwa kutambua umuhimu wa Vyama vya Ushirika iliunda upya ushirika mwaka 1984.

5.3 Maendeleo ya Ushirika katika Mfumo wa Soko Huru Msukumo wa ushirika kuanzia miaka ya 1990, ilikuwa kuweka mazingira muafaka kwa vyama vya ushirika, kufanya shughuli zake na kumudu ushindani katika mfumo mpya wa kiuchumi, juhudi za vikundi vya kiuchumi vya wakulima vinavyoanzishwa kutokana na nguvu mpya za mahusiano ya uzalishaji kama msingi muhimu wa maendeleo ya ushirika katika mazingira ya uchumi wa soko huru. Kuanzia miaka ya 2000 Serikali iliweka mkazo katika kuvisaidia vyama vya ushirika ambavyo vinamilikiwa na kusimamiwa na wanachama wenyewe kwa mujibu wa maadili na misingi ya ushirika inayotambuliwa kimataifa. Aidha, Serikali ilizingatia matatizo ya kimuundo na kihistoria ya vyama vya ushirika katika mazingira ya uchumi huru, na kuweka mazingira muafaka ili vyama viweze kufanya shughuli kwa ushindani na ufanisi zaidi. Kutokana na kuwepo kwa mabadiliko makubwa ya sera za nchi za kiuchumi kulikuwa na haja ya mabadiliko ya Sheria ili kuviwezesha vyama vya ushirika kuendeshwa kulingana na mahitaji ya wakati huo. Sheria ya Ushirika Na. 20 ya mwaka 2003 imeweka mazingira ya kufufua, kuendeleza na kuimarisha vyama vya ushirika. Kwa ujumla baada ya sheria hiyo pamoja na mambo mengine msisitizo umeelekezwa

kilimo miaka 50.indd Sec1:30kilimo miaka 50.indd Sec1:30 11/16/11 10:34:35 AM11/16/11 10:34:35 AM

Page 47: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

31

katika mambo yafuatayo:-

5.3.1 Kuimarisha Nguvu za Kiuchumi za Vyama vya UshirikaSheria inatilia mkazo nguvu za kiuchumi za vyama vya ushirika (economic viability) ili kuondokana na hali ya utegemezi ya vyama vya ushirika.

5.3.2 Kuangalia Mfumo wa Vyama vya Ushirika NchiniSheria inawapa wanachama wa vyama vya ushirika uwezo na mwongozo wa kuweka mfumo unaokidhi mahitaji yao. Sheria inatambua kwamba kuna umuhimu wa kuwa na vyama vya msingi na shirikisho, kuwepo kwa vyama vya kati na kilele kutegemea matakwa na maamuzi ya wanachama.

5.3.3 Uchaguzi wa Viongozi na MaadiliSheria imeweka utaratibu wa uchaguzi wa viongozi na ajira ya Watendaji unaozingatia maadili ya uongozi (code of conduct) na utendaji makini katika vyama vya ushirika. Ufuatiliaji wa maadili umeanza kuibua heshima ya ushirika ambayo ilikuwa imepotea.

5.3.4 Kufuatilia Kesi za UshirikaSheria hiyo ina kipengele kinachowapa uwezo Maafi sa Maalum (Special Prosecutors) kusimamia Vyama vya Ushirika Mahakamani ambao watawezesha uendeshaji wa haraka wa kesi zinazohusu ushirika.

5.3.5 Kutambua Vikundi Vidogo Vidogo (Pre-Cooperatives)Sheria inatambua vikundi vya uzalishaji na uchumi, Akiba na Mikopo n.k. na umuhimu wa kuvilea hadi kufi kia kuwa vyama vya ushirika kamili. Nia kubwa katika kutekeleza jambo hilo ni kutambua mfumo wa ushirika unaotokana na wananchi wenyewe.

5.3.6 Mabadiliko Katika Sheria Nyingine Za NchiSheria ya Ushirika ya mwaka 2003 imebadilishwa ili kwenda sambamba na mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na kisheria yanayotokea nchini.

5.3.7 Kuendana na Programu ya Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za MitaaSheria imeainishwa ili iendane na progamu ya uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa (Local Government Reform Programme) wa kupeleka madaraka ya udhibiti na usimamizi wa vyama vya ushirika karibu zaidi na pale vyama vilipo.

kilimo miaka 50.indd Sec1:31kilimo miaka 50.indd Sec1:31 11/16/11 10:34:35 AM11/16/11 10:34:35 AM

Page 48: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

32

6. MAFANIKIO YA KILIMO NA USHIRIKA 6.1 Kilimo kimeendelea Kukua na Kuchangia katika uchumiTangu mwaka 1961, ukuaji wa sekta ya kilimo umekuwa ukipanda na kushuka kutokana na sababu mbalimbali, kubwa ikiwa ni mabadiliko ya hali ya hewa. Kuanzia miaka ya 1970 hadi mwishoni mwa miaka ya 1990, kilimo kilikuwa kikikua kwa wastani wa asilimia 3.1 kwa mwaka. Kutokana na sera na mikakati ya kuendeleza sekta ya kilimo iliyoandaliwa na Serikali, kuanzia mwaka 1995 kilimo kilianza kuongeza kasi ya ukuaji. Kwa mfano katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 1995 hadi 2005 kilimo kilikua kutoka wastani wa asilimia 2.1 hadi wastani wa asilimia 6. Mwaka 1961 wakati tunapata uhuru, mchango wa kilimo katika mapato ya fedha za kigeni ulikuwa ni zaidi ya asilimia 75. Kadhalika, idadi ya Watanzania waliokuwa wanaendesha maisha yao kwa kutegemea kilimo ilikuwa ni zaidi ya asilimia 90 kati ya Watanzania milioni 9.8. Mchango wa sekta ya Kilimo katika Pato Ghafi la Taifa (Gross Domestic Product – GDP) ulikuwa zaidi ya asilimia 70, wakati kilimo kilikuwa kinachangia karibu asilimia 81 ya mapato ya mauzo ya nje. Mapato kutokana na mauzo ya mazao ya kilimo yalikuwa Dola za Marekani Milioni 115 mwaka 1961. Kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 iliyopita yaani kutoka mwaka wa 1998 mpaka 2010, mchango wa kilimo katika pato la Taifa ni wastani wa asilimia 27.2. Ukuaji huo unaonyesha kuwa kilimo bado kinachangia kiasi kikubwa katika uchumi ingawa kiwango cha uchangiaji kimekuwa kikishuka kutokana na kukua kwa sekta nyingine hususan madini, viwanda, ujenzi na huduma.

6.2 Kuongezeka kwa Teknolojia za Kilimo Kutokana na Utafi ti Katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, vituo vya utafi ti wa kilimo vimezalisha teknolojia mbalimbali za kilimo kwa lengo la kuongeza uzalishaji, tija na kipato kwa mkulima na Taifa kwa ujumla.

6.2.1 Utafi ti wa Mazao Utafi ti umetoa aina mbalimbali za mbegu bora za mazao ya chakula, biashara na yale ya bustani. Mbegu hizo ni pamoja na aina 33 za mahindi, 21 maharage, 20 pamba, 18 mpunga, 16 korosho, 15 kahawa, 13 muhogo, 13 ngano, 12 ufuta, 11 karanga, 8 viazi vitamu na 7 mtama. Mbegu nyingine ni aina 7 za mboga za asili, 6 viazi mviringo, 5 shayiri, 4 kunde, 4 dengu, 6 mbaazi, 3 nyanya, 2 choroko, 2 uwele, 2 soya, 3 miwa, 2 zabibu, 1 alizeti, 1 tumbaku, 7 parachichi, 6 migomba, 5 kabichi, 4 vitunguu na 4 mafyurisi (Jedwali. Na. 4). Mbegu hizo zina sifa ya kutoa mavuno mengi, kustahimili ukame, kukomaa haraka na ukinzani dhidi ya magonjwa. Utoaji wa aina tofauti za mbegu bora za mazao huenda sambasamba na teknolojia husishi kuhusu mbinu bora zilizotafi tiwa za ukuzaji wa mazao na kupendekezwa pamoja na kupelekwa kwa wakulima kwa uzalishaji wa mazao hayo. Pia, kila mwaka vituo vya utafi ti huzalisha mbegu ya awali (breeders’ seed) kwa kila aina ya mbegu bora ambazo hupelekwa kwa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kwa uzalishaji wa mbegu bora kwa matumizi ya mkulima. Mafanikio yaliyopatikana yanaendana na mafanikio ya shughuli za utafi ti zinazoendelea. Mifano halisi ni katika maeneo yafuatayo:

kilimo miaka 50.indd Sec1:32kilimo miaka 50.indd Sec1:32 11/16/11 10:34:35 AM11/16/11 10:34:35 AM

Page 49: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

33

6.2.1.1 Utafi ti wa MahindiKatika kanda ya Nyanda za Juu Kusini utafi ti wa mahindi umefanikiwa kutoa mbegu chotara (hybrids) aina sita zenye tija kubwa; nazo ni H6302 na H 614 kupitia enzi za Jumuiya ya Afrika Mashariki; UH615 (mwaka 2001), UH6303 (mwaka 2004), UHS 5210 na UHS5350 (mwaka 2009). Mbegu bora isiyo chotara (OPV) aina ya TMV2 pia ilitolewa katikati ya miaka ya 1980. Pia vizazi kwa ajili ya kuunda mbegu bora vimekuwa vikiandaliwa na programu hii kwa miaka yote tangu ilipoanza shughuli zake rasmi mwishoni mwa miaka ya 1960. Vinasaba vitaendelea kusaidia katika kukabiliana na changamoto zitakazokuwa zinajitokeza katika siku zijazo.

6.2.1.2 Utafi ti wa Zao la PambaMbegu aina tatu za pamba zinazostahimili minyoo ya pamba ambazo zimeshaonyesha matokeo mazuri ni NTA 93-2/91(01)2, NTA 93-4/91(01)2 na F 135/91(01)4. Majaribio yanaendelea kabla ya mbegu hizo kuthibitishwa kwa matumizi ya wakulima.

6.2.1.3 Utafi ti wa Mazao ya Mbegu za Mafuta na Jamii ya KundeUtafi ti unaoendelea katika Kituo cha Ilonga wenye nia ya kutoa mbegu bora mpya za mazao mbalimbali umefi kia hatua nzuri kwa baadhi ya mazao. Mfano ni aina nne za kunde (IT00K-1263, IT99K-1122, IT99K-7-21-2-2-1, IT99K-573-1), aina nne za mbaazi, (ICEAP 00554, ICEAP 00557, ICEAP 00932, ICEAP 00053), moja ya soya (TGX 1895-33F) na nyingine ya alizeti (PI 364860). Utafi ti unaoendelea katika kituo cha Naliendele umetambua aina mpya za karanga (ICGV SM 90704 na ICGV SM 99568). Aina hizo zina uwezo wa kuhimili magonjwa yanayoshambulia majani. Tathmini ya upokeaji na utumiaji wa teknolojia za karanga na ufuta miongoni mwa wakulima zimeongezeka kutoka wastani wa asilimia 10 mwaka 2006 hadi wastani wa asilimia 60 mwaka 2010 katika mikoa ya kusini ya Lindi na Mtwara. Mbegu ya mbaazi aina ya ICEAP 000557 inaendelea kufanya vizuri katika majaribio na msimu wa 2010/11 iliingizwa katika majaribio yatakayowezesha kuisajili kama mbegu bora. Watafi ti wakishirikiana na wataalam wa kilimo wa wilaya za Masasi, Nachingwea, Nanyumbu na Tunduru, mbegu hiyo imepandwa kwenye mashamba ya mfano ili wakulima waweze kuiona na kutambua ubora wake. Aidha, utafi ti wa njugumawe (Bambara groundnuts) unafanyika ili kuziba pengo la uhaba wa mbegu bora za zao hilo.

kilimo miaka 50.indd Sec1:33kilimo miaka 50.indd Sec1:33 11/16/11 10:34:35 AM11/16/11 10:34:35 AM

Page 50: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

34

Jedwali Na. 4: Aina ya Mbegu za Mazao Zilizobuniwa na Kutolewa na Utafi ti wa Kilimo(1961-2011)

Miaka Zao Aina ya Mbegu Iliyotolewa Kituo/Taasisi

1961-1971 Pamba IL 54, IL 66 Ilonga

UK 61, UK63, UK64, UK66, UK68, UK 69 UK70, UK71 Ukiriguru

Mahindi Katumbili, UCA (Ukiriguru Composite A) Ukiriguru

ICW (Ilonga Composite W) Ilonga

Ufuta Lindi White, Morada, Improved Morada, Morada 2, SSBS 4, SSBS 7 Naliendele

Karanga Red Mwitunde, Natal Common Naliendele

1972-1981 Mahindi Tuxpeno Ilonga

Mpunga Afaa Mwanza, Supa India, Kihogo Red Sel.No.7 Ilonga (kwa ushirikiano na KATRIN & Ukiriguru)

Mtama Serena, Lulu Ilonga

Ngano Mbuni, Tai, Joli, Viri, Kweche, Trophy Selian

Maharage Kabanima Uyole

Choroko Nuru, Imara Ilonga

Viazi mviringo Baraka, Sasamua Uyole

Nyanya Money Maker, Maglobe, Rossae, Roma (Recommended) Uyole

Vitunguu Red Creole, Bombay Red, Indian Khakhi Uyole

Kabichi Drum Head, Copenhagen, Glory of Enkhuizen (Recommended) Uyole

Peaches Dabaga Na.4, Flordabelle, Flordagold, Sunred Nectarine (Recommended) Uyole

Migomba Pazi, Jamaica, Uganda, Cavendish (Recommended) Uyole

Pamba IL 74 Ilonga

UK74, UK77 Ukiriguru

Miwa EA 70-97 SRI-Kibaha

1982-1991 Mahindi Staha, TMV-1, Kito-ST, Katumani-ST Ilonga

TMV-2 Uyole

H512, H612, H613, H6302, H614, Kilima-ST C (Recommended) Uyole

Mpunga KATRIN, Selemwa KATRIN

IR54, IR64, Subarimati (Recommended) KATRIN

Mtama Tegemeo Ilonga

Ngano Mbayuwayu, Azimio, Tausi, Selian-87 Selian

Juhudi Uyole

Maharage Lyamungo 85, Lyamungo 90 Selian

Uyole 84, Uyole 90, Ilomba Uyole

Kunde Fahari, Tumaini, Vuli 1 Ilonga

Ufuta Bora Naliendele

Karanga Nyota, Johari Naliendele

Viazi mviringo Kikondo, Subira, TANA, Bulongwa Uyole

Nyanya CAL-J, Rossal (Recommended) Uyole

Parachichi Weisal, Fuerte, Ex-Tengeru, Haas (Recommended) Uyole

Pamba IL 85, ALAI 90. Ilonga

UK82, UK91 Ukiriguru

1992-2001 Mahindi UH615 Uyole

CH 1, CH 2 Dakawa

Mtama Pato, Macia Ilonga

Uwele Okoa, Shibe Ilonga

Shayiri Kibo Selian

Alizeti Kobe Ilonga

Ufuta Naliendele 92, Ziada 94, Zawadi 94 Naliendele

Karanga Pendo, Sawia Naliendele

Maharage Selian 94, Jesca, Selian 97 Selian

Uyole 94, Uyole 96, Uyole 98 Uyole

Soya Uyole Soya 1 Uyole

Mbaazi Komboa Ilonga

Viazi vitamu Simama, Mavuno, Vumilia, Jitihada, Sinia Naliendele

kilimo miaka 50.indd Sec1:34kilimo miaka 50.indd Sec1:34 11/16/11 10:34:35 AM11/16/11 10:34:35 AM

Page 51: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

35

Miaka Zao Aina ya Mbegu Iliyotolewa Kituo/Taasisi

Nyanya Tengeru 97, Tanya HORTI-Tengeru

Pamba Mkombozi. Ilonga

Tumbaku PD4 Tumbi

2002-2011 Mahindi Bora Ilonga

UH6303, UHS 5350, UHS 5210 Uyole

Staha-ST C (Recommended) Uyole

Lishe-K1, Lishe-H1 (chotara), Lishe-H2 (chotara), Situka-1, Situka-M1, Selian-MH07 (chotara), Vumilia-K1, Selian H208 (chotara), Selian H308 (chotara), Vumilia H1

Selian

Mpunga TXD 85, TXD 88, TXD 306 (SARO 5) KATRIN (kwa ushirikiano na Dakawa)

NERICA 1, NERICA 2, NERICA 4, NARICA 7, WAB450-12-2BLB-DV4 KATRIN (kwa ushirikiano na Dakawa, Ukiriguru, Uyole & Naliendele)

Kalalu, Mwangaza SUA (kwa ushirikiano na Uyole)

Mtama Wahi, Hakika Ilonga

Ngano Riziki C1 Selian

SIFA Uyole

Shayiri Chiriku, Riziki C1, RV 593, Lumbesa Selian

Maharage Selian 05, Selian 06, Cheupe Selian

Wanja, Uyole 03, Uyole 04, BILFA-Uyole, Urafi ki, Njano-Uyole Uyole

Soya Uyole, Soya 2 Uyole

Kunde Vuli 2 Ilonga

Mbaazi Tumia, Mali. Ilonga

Dengu Mwanza 1, Ukiriguru1, Mwanza 2, Mwangaza Ukiriguru

Pamba UK08, UKM08 Ukiriguru

Karanga Mangaka 2009, Mnanje 2009, Masasi 2009, Nachingwea 2009, Naliendele 2009

Naliendele

Ufuta Lindi 02, Mtwara 09 Naliendele

Muhogo Rangi mbili, Meremeta, Mkombozi, Belinde, Kasala, Suma, Nyakafulo and Kyaka

Ukiriguru

Kiroba, Kibaha, Hombolo 95, Mumba, Naliendele 90 SRI-Kibaha (kwa ushirikiano na Naliendele)

Viazi vitamu Ukerewe, Mataya, Kiegea SRI-Kibaha (kwa ushirikiano na Naliendele)

Viazi mviringo Tigoni (Recommended) Uyole

Miwa N 19 & N25 SRI-Kibaha

Nyanya Meru, Kiboko, Duluti , Tengeru 2010 HORTI-Tengeru

Kabichi Glory FI, Prucktor (Recommended) Uyole

Vitunguu Mang’ola Red (Recommended) Uyole

Zabibu Makutupora Red; Chenin Nyeupe VRTC-Makutupora

Loshuu/fi giri Rungwe & Arumeru HORTI-Tengeru

Nyanya chungu/ ngogwe

DB 3 HORTI-Tengeru

Mnafu Olevolosi & Nduruma HORTI-Tengeru

Mchicha Madiira 1 & Madiira 2 HORTI-Tengeru

Parachichi Simmonds, Ikulu, Ex-Mwaikokesya (Recommended) Uyole

Migomba FHIA 17 , FHIA 23 SUA (kwa ushirikiano na Uyole)

Korosho AC 1, AC 4, AC 4/17, AC 4/285, AC 43, AC 10, AC 14, AC 34, AC 10/129, AC 10/220, AC 22, AZA 2, AZA 17, AZA 17/79, AZA 17/156, AZA 17/158

Naliendele

Kahawa (Robusta) Muleba 1, Maruku 1, Bukoba 1, Maruku 2 TaCRI

Kahawa (Arabica) N 39-1, N39-2, N39-3, N39-4, N39-5, N39-6, N39-7, KP 423-1, KP 423-2, KP 423-3, KP 423

TaCRI

kilimo miaka 50.indd Sec1:35kilimo miaka 50.indd Sec1:35 11/16/11 10:34:36 AM11/16/11 10:34:36 AM

Page 52: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

36

6.2.1.4 Utafi ti wa Zao la MpungaUtafi ti unaofanyika katika kituo cha KATRIN umetoa mbegu bora za mpunga kama vile KATRIN, Selemwa, Afaa Mwanza, Supa na Kihogo Sel. No. 7. Aidha, kwa kushirikiana na kituo cha Chollima (Dakawa) na vituo vingine, kituo cha KATRIN kimetoa mbegu bora aina ya TXD 85, TXD 88, TXD 306 (SARO 5), IR54 na Subarimati. Aina hizo za mpunga ni kwa ajili ya wakulima wanaotegemea kilimo cha umwagiliaji na wale wa ukanda wa chini wanaotegemea mvua. Matumizi ya mbegu hizo yameongeza uzalishaji kati ya asilimia 200 na 400 ikilinganishwa na mbegu za asili zilizokuwa zikitumiwa hapo awali. Mbegu za maeneo ya miinuko aina ya NERICA zimeshaidhinishwa ki-Taifa ili zitumike kwenye maeneo yanayotegemea mvua. Mbegu hizo ni NERICA1, NERICA2, NERICA4, NERICA7 na WAB450-2-12-BL1-DV4. Mbegu hizo zina uwezo wa kuongeza mavuno kwa kiasi cha asilimia 70 ikilinganishwa na mbegu za asili. Aina nyingine ya mbegu zinazolimwa katika maeneo hayo ni Dunduli ya Milimani na Afrika. Aidha, utafi ti umebaini kuwa mbegu za Lunyuki, Mwangaza, IR47686-15-5-1, Gigante, WABIS 844 na IRAT 252 zina ukinzani dhidi ya ugonjwa wa ’Kimyanga’ (Rice Yellow Mottle Virus-RYMV). Aina hizo za mbegu zitatumika katika utafi ti kwa ajili ya kuboresha mbegu za asili zisizo na ukinzani dhidi ya ugojwa wa ‘Kimyanga’, unaoleta hasara ya mavuno kwa kiwango cha kati ya asilimia 20 na 100 kutegemea aina ya mbegu. Pindi mbegu hizo zitakapokuwa tayari kutumika zitaongeza mavuno kwa asilimia 40 ukilinganisha na zile zisizo na ukinzani.

6.2.1.5 Utafi ti wa Zao la ZabibuKupitia Kituo cha Makutopora, takriban aina 300 za mizabibu ziliingizwa nchini kutoka Ulaya na Asia kwa ajili ya majaribio ya kukidhi mazingira ya Tanzania. Aina ya zabibu zilizosajiliwa ni Makutopora Red na Chenin White. Aina sita za zabibu zipo katika hatua za mwisho za utafi ti ili ziweze kusajiliwa. Aina hizo zinajulikana kama Regina; kwa ajili ya matunda ya mezani, Beauty Seedless; kwa ajili ya kukausha (raisins), Ruby Seedless; kwa ajili ya kukausha, Alphonce Lavallee; kwa ajili ya matunda ya mezani, Makutupora White; kwa ajili ya matunda ya mezani na Syrah; kwa ajili ya kutengeneza mvinyo mwekundu na juisi. Aidha, aina hizo zina sifa za kutoa mavuno mengi, kustahimili ukame na magonjwa.

6.2.1.6 Utafi ti wa Zao la KoroshoUtafi ti wa mbegu bora aina za chotara (cashew hybrids) katika Kituo cha Naliendele umeonyesha kuwa mbegu hizo zinatoa mavuno wastani wa kilo 10 kwa mti wa mkorosho zikilinganishwa na mbegu zinazotumika sasa. Kwa mfano mbegu bora aina ya AC-4 inatoa mavuno wastani wa kilo 6 kwa mti wa mkorosho. Pia aina hizo za mbegu bora zimeonyesha kuwa na ukinzani wa magonjwa ya mikorosho. Vinasaba (germplasm) kutoka Msumbiji aina ya MATRIZ96, 1.18VM, 8.4NAS na 11.9PA vimeonyesha kuzaa korosho zenye ukubwa wa wastani wa gramu 15 hadi 18 kwa korosho moja na miti yake kuwa na uwezo wa kutoa mavuno kilo 8 hadi 27 kwa mti mmoja. Uzaaji huo haujawahi kutokea kwa mbegu zilizowahi kufanyiwa majaribio na hivyo aina hizo zitatumika kama mbegu mama katika utafi ti wa mbegu bora za mikorosho. Katika ukanda wa Makonde, mbegu aina za AC10/220 na AC4/4 ziliendelea kufanya vizuri na kuonekana bora kuliko mbegu nyinginezo zilizojaribiwa katika ukanda huo. Aina 32 za mbegu chotara na 25

kilimo miaka 50.indd Sec1:36kilimo miaka 50.indd Sec1:36 11/16/11 10:34:36 AM11/16/11 10:34:36 AM

Page 53: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

37

za mbegu bora fupi za vinasaba vya Kibrazili zitafanyiwa majaribio zaidi na Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu (TOSCI) ili kuthibitisha ubora wake kabla hazijaidhinishwa kwa matumizi ya wakulima.

6.2.1.7 Utafi ti wa Zao la KahawaTaasisi ya Utafi ti wa Kahawa (TaCRI) inatarajia kupendekeza aina 5 za kahawa aina ya arabika zenye ukinzani wa kudumu kwa magonjwa ya chulebuni na kutu ya majani ili zitumike rasmi na wakulima mwishoni mwa mwaka 2011. TaCRI inadhamiria kupendekeza aina fupi za kahawa chotara zenye uwezo wa kuzaa mara tatu hadi nne zaidi ya aina zilizokuwepo (N39 na KP423), na zaidi ya mara mbili hadi tatu ya aina mpya za kahawa chotara zilizopendekezwa mwaka 2005. Aina hizo pia zina sifa ya kuwa na ukinzani dhidi ya magonjwa ya chulebuni na kutu ya majani, na sifa nyingine za ubora. Aina hizo zitazalishwa kwa kutumia vikonyo au mbegu chotara.

6.2.1.8 Utafi ti wa Zao la ChaiTaasisi ya Utafi ti wa Chai (TRIT), imefanikiwa kuweka mazingira mazuri ya upatikanaji wa vipando bora vya michai kwa kuingia makubaliano na taasisi za utafi ti za nchi jirani ambapo vipando zaidi ya 44 vinafanyiwa tathmini kabla ya kupelekwa kwa wakulima. TRIT pia imeweza kutafi ti na kusambaza teknolojia za kisasa za matumizi ya maji na hifadhi ya ardhi. Mashamba makubwa ya chai Wilayani Mufi ndi na Njombe yanamwagiliwa kutokana na utafi ti uliofanywa na Taasisi hiyo.

6.2.2 Utafi ti wa UdongoMafanikio makubwa yamepatikana kwenye utafi ti wa udongo na raslimali ardhi, pamoja na matumizi bora ya udongo na maji (Soil and Water Management Research). Baadhi ya mafanikio katika eneo hili ni kama ifuatavyo:a. Ramani pamoja na taarifa za udongo, ekolojia mbalimbali na mazao yanayostawi

zimetengenezwa kwa wilaya zaidi ya 120 nchini na zinapatikana kupitia tovuti (http://www.kilimo.go.tz) ya Wizara kwa ajili ya matumizi ya wadau.

b. Tathmini ya udongo na mazingira zimefanywa katika mashamba ya mkonge hususan Kigombe, Mwera, Kwamdulu, Pongwe, Tungi, Kwafungo, Ngombezi, Amboni, Bombwera, Kwamgwe na Kwashemshi na ushauri kutolewa kuhusu mbinu za kuboresha uzalishaji wa zao la mkonge.

c. Utafi ti umefanywa na ushauri kutolewa kuhusu uanzishwaji na uendelezwaji wa kilimo cha umwagiliaji katika maeneo ya Matipwili, Mkindo, Kitivo na Bagamoyo.

d. Utafi ti ulifanywa na ushauri kutolewa kuhusu kilimo cha chai katika mashamba ya Amani, Bulwa na Kwamkoro.

e. Utafi ti umefanywa kuonyesha maeneo yanayofaa kwa kilimo cha kahawa kwa nchi nzima.

f. Ramani zimetengenezwa kuonyesha mifumo ya kilimo (farming systems) kwa kanda za Mashariki, Magharibi, Kati, Kusini, Kaskazini, Ziwa na Nyanda za Juu Kusini.

kilimo miaka 50.indd Sec1:37kilimo miaka 50.indd Sec1:37 11/16/11 10:34:36 AM11/16/11 10:34:36 AM

Page 54: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

38

6.2.2.1 Utafi ti wa Matumizi Bora ya Mbolea za Asili na za ViwandaniKituo cha Utafi ti Mlingano kimefanya utafi ti mbalimbali na kutoa mapendekezo kuhusu matumizi bora ya mbolea katika maeneo mbalimbali hapa nchini (National fertilizer recommendations). Mapendekezo yanayotumika kwa sasa yalitolewa mwaka 1993 na marekebisho yake yanaendelea.

6.2.2.2 Maabara Kuu ya Udongo na Mifumo ya Taarifa za Kijiografi aMaabara Kuu ya Udongo iliyopo Mlingano ni ya Kitaifa na ina uwezo wa kupima sampuli 5,000 za udongo kwa mwaka. Sampuli za udongo hupimwa kwa ajili ya kuelewa aina za udongo na namna maeneo husika yanavyoweza kutumiwa kwa kilimo, ufugaji, hifadhi ya mazingira na mengineyo. Maabara ya Mifumo ya Taarifa za Kijiografi a (Geographical Information Systems-GIS) ilianzishwa mwaka 1998 kwa ajili ya kukusanya, kuchambua, kuhifadhi, na kutoa maelezo ya kitaalam kwa maliasili zinazohusiana na kilimo (maji, udongo na mimea) na jinsi zinavyoweza kutumika katika uzalishaji na utunzaji endelevu wa mazingira.

6.2.3 Teknolojia na Masuala MtambukaPamoja na utoaji wa aina tofauti za mazao na teknolojia husishi, kuna masuala mtambuka ambayo yanaongeza ufanisi na uhifadhi katika uzalishaji na matumizi ya mazao mbalimbali ikiwa ni pamoja na yafuatayo:6.2.3.1 Matumizi na Utengenezaji wa VyakulaKituo cha Ilonga kimetoa na kusambaza kwa wakulima matumizi na njia za kutengeneza vyakula mbalimbali kutokana na mazao ya mtama, kunde, soya na mbaazi; hivyo kuchangia katika kuongeza uzalishaji wa mazao hayo ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa soko.6.2.3.2 Mikataba ya Kufanya Utafi ti na Halmashauri za WilayaBaadhi ya vituo vya utafi ti vimeingia mikataba na Halmashauri za wilaya kufanya utafi ti unaolenga kutatua matatizo yaliyoibuliwa na wakulima. Kwa mfano, katika Kituo cha Ilonga jumla ya mikataba 19 ya utafi ti imekamilishwa kwa ajili ya wilaya za Muheza, Kilosa, Ulanga na Kilombero. Kituo cha Naliendele kwa kushirikiana na Halmashauri za wilaya kimeweza kuzalisha tani 35 za karanga na tani 30 za ufuta daraja la kuazimiwa (Quality Declared Seed - QDS) kwa kutumia vikundi vya wakulima 50 vinavyofanya utafi ti shirikishi (Participatory Variety Selection -PVS).

6.2.3.3 Njia Sahihi za Kuhifadhi Udongo na MajiNjia za kuhifadhi udongo na maji zimeainishwa ikiwa ni pamoja na uvunaji wa maji mashambani na utumiaji wa matuta ya kufunga. Jembe la makucha (Magoye Ripper) na plau katika kutayarisha mashamba ni njia mojawapo ya kuongeza ufanisi wa matumizi ya maji na hifadhi ya udongo. 6.2.3.4 Utafi ti wa Udongo Unaolenga Mazingira Tofauti NchiniLicha ya utafi ti wa kitaifa wa udongo unaofanyika kupitia Kituo cha Mlingano, vituo vingine vinafanya tafi ti mbalimbali za matumizi ya ardhi, uboreshaji wa rutuba ya udongo na lishe bora ya mimea kuendana na mazingira mbalimbali nchini. Aina mbalimbali za vyanzo vya virutubisho vya mimea vimejaribiwa ikiwa ni pamoja na mbolea za viwandani, samadi na mimea aina ya mikunde. Kwa mfano, kilimo-mseto cha mtama na mbaazi kwa kuzingatia idadi ya mistari ya mtama na mbaazi kimeonyesha mafanikio katika kuboresha udongo na kuongeza mavuno. Aidha, utafi ti umefanyika kuhusu uzalishaji na utunzaji wa samadi, uzalishaji wa mboji pamoja na matumizi yake.

kilimo miaka 50.indd Sec1:38kilimo miaka 50.indd Sec1:38 11/16/11 10:34:36 AM11/16/11 10:34:36 AM

Page 55: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

39

6.2.3.5 Udhibiti Husishi wa VinamiziUdhibiti wa gugu chawi “KIDUHA” katika mazao ya nafaka kwa kutumia aina za mbegu zenye ukinzani, uvunaji maji na kuboresha rutuba ya udongo kwa pamoja (integrated approach) umeonyesha mafanikio makubwa. Miaka ya 1994 hadi 1998, tathmini ya viuatilifu vitokanavyo na mimea ulipendekeza matumizi ya utupa, mbono na mwarobaini. Utafi ti wa pamba unaolenga kuchunguza aina za kilimo kinachoweza kupunguza ugonjwa wa mnyauko fuzari na minyoo, mafanikio yaliyopatikana ni kuwa kilimo cha mzunguko wa pamba na mahindi au mtama au mihogo kila baada ya miaka mitatu hupunguza ugonjwa huo. Mwaka 1969 utafi ti ulifanyika kuainisha maeneo safi yasiyo na ugonjwa wa mnyauko fuzari kwa ajili ya uzalishaji mbegu safi za kupandwa na wakulima na ramani kuchorwa. Mwaka 1987 hadi 2011 utafi ti umefanyika kuainisha maeneo safi yasiyo na ugonjwa wa mnyauko fuzari kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu za pamba na baadhi ya sehemu za ramani zinazoonyesha kuenea kwa ugonjwa ziliboreshwa. Sehemu kubwa ya utafi ti huo ulifanywa na Kituo cha Utafi ti Ukiriguru. Huko Ilonga, Kituo kimefanya uchunguzi wa mdudu hatari wa pamba aitwaye Funza Mwekundu (Cotton Red Bollworm) kusini mwa Tanzania na kupanua eneo lililoko kwenye karantini kulingana na kubainika kwa mdudu huyo hadi kusababisha kusitishwa kwa kilimo cha pamba mkoani Mbeya katika juhudi za kumdhibiti. Utafi ti uliofanyika ulionyesha kuwa kilimo cha pamba kwenye sehemu alipo mdudu huyu hakina tija.

6.2.3.6 Udhibiti wa DumuziTasisi ya Utafi ti wa Viuatilifu kwa Ukanda wa Kitropiki (TPRI) ilifanya utafi ti wa kuangamiza dumuzi aliyewasababishia wakulima usumbufu wa muda mrefu na upungufu wa chakula. Elimu ilitolewa na watafi ti wa TPRI kwa wakulima kuhusu matumizi sahihi ya kiuatilifu (Actellic Super Dust), na hatimaye kuokoa upotevu wa chakula na mazao ya nafaka kwa kiasi kikubwa. Aidha, TPRI ilihusika katika kubuni mchanganyiko wa viambato amalifu (active ingredients) vya kiuatilifu vumbi cha kudhibiti dumuzi. Kiuatilifu hicho kwa sasa ni maarufu kwa wakulima.

6.2.4 Uenezaji wa Matokeo ya Utafi ti Utafi ti hautakuwa na maana ikiwa matokeo yake hayatawafi kia walengwa ili teknolojia bora ziweze kutumika kubadilisha maisha yao. Kuna njia mbalimbali ambazo Wizara imefanikisha usambazaji wa matokeo ya utafi ti kwa wadau mbalimbali. Baadhi ni zifuatazo:a. Kupitia njia mbalimbali za mawasiliano kama vile televisheni, redio, magazeti,

maonyesho ya wakulima (agricultural shows), ziara za wakulima (field visits), maonyesho ya wakulima shambani (fi eld days), machapisho (kama vile vipeperushi, mabango, vijarida, magazeti), mikutano ya wadau, mafunzo kwa wakulima na mashamba ya maonesho. Kituo cha Ilonga, kwa mfano, kinachapisha na kusambaza vipeperushi na vijarida zaidi ya 40,000 vinavyohusu njia bora za uzalishaji wa mazao mbalimbali na kusambaza machapisho hayo kwenye wilaya zote za Kanda ya Mashariki. Aidha, kutokana na uhamasishaji kupitia Kituo cha Naliendele, wakulima zaidi wanalima ufuta na soko lake limeendelea kuimarika na Tanzania iliuza nje zaidi ya tani 50,000 mwaka 2009/10.

kilimo miaka 50.indd Sec1:39kilimo miaka 50.indd Sec1:39 11/16/11 10:34:36 AM11/16/11 10:34:36 AM

Page 56: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

40

b. Kwa kipindi cha mwaka 1961 hadi 2011 kumekuwa na machapisho ya kisayansi (scholarly publications) yaliyotayarishwa kwa nia ya kueneza matokeo na teknolojia zitokanazo na utafi ti. Machapisho hayo yanapatikana katika taarifa za utafi ti za robo mwaka na za mwaka (quarterly and annual reports), vitabu/vijitabu, taarifa za mikutano ya kitaifa na kimataifa (proceedings), majarida (journals & newsletters), vipeperushi (brochures) na mabango (posters).

c. Vitengo maalum vya kuunganisha utafi ti na wadau katika kila kanda (ZIELUs) na kwa kushirikiana na Kitengo cha Habari na Hifadhi ya Nyaraka za Utafi ti (IDU) vimesaidia kufanikisha jukumu la usambazaji wa matokeo ya utafi ti.

d. Kwa kushirikiana na FARA na ASARECA Idara ya Utafi ti na Maendeleo imeanzisha tovuti ya kusaidia kusambaza shughuli na matokeo ya utafi ti wa kilimo Tanzania. Tovuti inajulikana kama eRAILS na inapatikana kwa anuani ifuatayo http://www.erails.tz/net

6.3 Kuongezeka kwa Wataalam wa KilimoMwaka 1961, kulikuwa na chuo kimoja tu kilichokuwa kinatoa mafunzo ya muda mrefu ngazi ya Stashahada. Miaka 50 baada ya Uhuru (2011) vyuo 14 vina uwezo wa kutoa mafunzo hayo katika fani/michepuo mitano (5) tofauti. Tangu mwaka 1995 hadi Novemba 2010 wataalam 7,604 wamehitimu mafunzo ya miaka miwili ngazi ya Stashahada na Astashahada. Katika kipindi cha Miaka 50 ya Uhuru kumekuwepo na ongezeko kubwa la idadi ya watafi ti na wataalam wengine wazalendo katika fani mbalimbali za kilimo. Kwa mfano, imeripotiwa kwamba katika Kituo cha KATRIN kuna ongezeko la watafi ti wazalendo kwa asilimia 500 na ongezeko la watafi ti wasaidizi kwa asilimia 1000. Vilevile, kwa kipindi cha mwaka 1961 na 1965 muda mfupi mara baada ya Uhuru, asilimia 96 ya taarifa za utafi ti ziliandaliwa na watafi ti wa kigeni na takribani asilimia tatu (3%) pekee ya taarifa za utafi ti ndizo ziliandaliwa na watafi ti wa kizalendo. Kufi kia mwaka 1990, asilimia 50 ya taarifa za utafi ti ziliandaliwa na watafi ti wa kizalendo. Ingawaje hakuna tathmini nyingine kama hiyo iliyofanyika tangu mwaka 1990 ni wazi kwamba asilimia imeongezeka kwa kiwango kikubwa kwani mara nyingi, japo siyo mara zote idadi ya machapisho ya utafi ti yanaenda sambamba na idadi ya watafi ti.6.3.1 Kuongezeka kwa Idadi ya Wakulima Waliopatiwa MafunzoWakulima 42,137 walifaidika na mpango wa mafunzo ya muda mfupi katika Vyuo vya Kilimo kati ya mwaka 1995 na 2010. Mafunzo hayo yaligharimiwa na Serikali pamoja na Taasisi/Asasi zisizo za kiserikali na watu binafsi (Wakulima/Wafugaji). Mada kuu zilizofundishwa ni kuhusu kilimo cha umwagiliaji, matumizi ya wanyamakazi katika kilimo, kilimo cha biashara, ujasiriamali, uchakataji na usindikaji wa mazao ya kilimo. Aidha, hadi mwezi Machi 2010 jumla ya wakulima 7,543 kutoka skimu za umwagiliaji 27 zikiwemo mbili kutoka Tanzania Visiwani, walikuwa wamefaidika kupitia utekelezaji wa mradi wa TCSDIA/TANRICE unaogharimiwa na Serikali ya Tanzania na Japan. Mradi unalenga kuwafi kia wakulima 15,000 wa zao la mpunga katika skimu za umwagiliaji 40 ifi kapo Juni 2012.

kilimo miaka 50.indd Sec1:40kilimo miaka 50.indd Sec1:40 11/16/11 10:34:36 AM11/16/11 10:34:36 AM

Page 57: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

41

6.3.2 Mitaala ya Kufundishia ImeboreshwaMitaala minane inayoongoza utekelezaji wa programu nane za Stashahada iliboreshwa kwa kuingiza mada muhimu zilizohitajika kwa kuzingatia matakwa ya wadau na umuhimu wa Vyuo vya Kilimo “kwenda na wakati”. Mada mpya zilizoingizwa ni pamoja na matumizi ya mbinu shirikishi katika utoaji wa huduma za ugani, mbinu za mawasiliano, ujasiriamali, kilimo cha biashara, VVU/UKIMWI na hifadhi ya maliasili na mazingira. Vyuo vya Kilimo kwa kushirikiana na bodi za mazao ya biashara, viliandaa mitaala kwa ajili ya mafunzo rejea ya muda mfupi ya maafi sa ugani wa mazao ya pamba, korosho, kahawa, chai na tumbaku. Vile vile, vyuo hivyo kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) vilirekebisha mitaala minne na kuiweka kwenye mfumo wa moduli ili kutimiza masharti ya elimu ya ufundi (NTA level 4, 5 na 6). Mitaala hiyo ni ya kilimo mseto, uzalishaji mazao, kilimo cha mazao ya bustani na kilimo cha umwagiliaji.

6.3.3 Maandiko ya Rejea YameandaliwaVitabu 13 vya rejea (reference books) viliandaliwa na kuchapishwa kwa ajili ya matumizi ya wakufunzi katika vyuo vya kilimo, maafi sa ugani na wakulima. Vitabu hivyo viliandaliwa kwa kushirikiana na wataalam na mabingwa katika fani mbalimbali.

6.3.4 Miundombinu ya Vyuo ImekarabatiwaKati ya mwaka 1995 na 2005; ukarabati wa miundombinu ya vyuo ulifanyika kwa lengo la kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia. Miundombinu hiyo ni ofi si, madarasa, maktaba, maabara, karakana, mabwalo ya chakula, mabweni, nyumba za watumishi, mifumo ya maji na umeme, vitengo vya mifugo na barabara za mashambani. Kufuatia ukarabati huo vyuo vinane (8) ambavyo ni KATC Moshi, Igurusi, Ilonga, Mlingano, Mtwara, Tumbi, Ukiriguru na Uyole viliongeza udahili wa wanafunzi kutoka 229 hadi 778. Aidha, vyuo vilivyofanyiwa ukarabati kupitia utekelezaji wa programu maalum ya kuimarisha huduma za ugani (2007 hadi 2012) ni Mtwara, Ukiriguru na Maruku. Kupitia ukarabati uliofanyika nafasi za bweni katika vyuo zimeongezeka na kuwa zaidi ya 3,000 kwa wakati mmoja.

6.3.5 Mafunzo Yanatolewa kwa Kuzingatia Vigezo vya UboraKwa kuzingatia sifa husika (utoaji wa mafunzo ya kilimo ngazi ya Stashahada- National Technical Award level 5-6), vyuo 10 vya Wizara vimetambuliwa na kusajiliwa na Baraza la Elimu ya Ufundi nchini (NACTE); Vyuo vya Inyala, Maruku na KATRIN viko mbioni kutimiza masharti yatakayoviwezesha kupata usajili. Sanjari na hilo, wakufunzi wa vyuo wamesajiliwa (Technical Teachers) utaratibu ambao utawawezesha kuingia kwenye mfumo wa ajira unaozingatia fani na uzoefu wao kazini na hivyo kuwahakikishia maslahi bora zaidi.

6.4 Kuongezeka kwa Matumizi ya Zana Bora za KilimoKutokana na mikakati mbalimbali ya Serikali, katika Miaka 50 ya Uhuru kumekuwa na mafanikio ya kuridhisha katika kuongeza upatikanaji na matumizi ya zana bora za kilimo hapa nchini. Jitihada hizo zimelenga kupunguza matumizi ya jembe la mkono na harubu zinazotokana na zana duni za kilimo. Mafanikio yamekuwa katika maeneo yafuatayo:-

kilimo miaka 50.indd Sec1:41kilimo miaka 50.indd Sec1:41 11/16/11 10:34:36 AM11/16/11 10:34:36 AM

Page 58: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

42

6.4.1 Matumizi ya Wanyamakazi Yameongezeka Kumekuwa na ongezeko la ujumla la matumizi ya wanyamakazi katika kilimo na usafi rishaji katika maeneo mbalimbali nchini. Idadi ya maksai wanaotumika katika kilimo imekuwa inaongezeka kutoka 320,000 mwaka 1970 hadi 1,542,000 mwaka 2010 ambapo majembe yanayokokotwa na maksai yameongezeka kutoka 140,000 hadi 620,000 katika kipindi hicho.

6.4.2 Upatikanaji na Matumizi ya Trekta Umeongezeka. Idadi ya trekta kubwa zinazotumika katika kilimo imeongezeka kutoka 2,580 mwaka 1960 hadi 7,823 mwaka 2010. Aidha, kiasi cha trekta kubwa zinazoingizwa nchini kwa mwaka kimeongezeka kutoka trekta 210 mwaka 1982 hadi 2,846 mwaka 2010/2011. Pia, kuna trekta ndogo za mikono 3,400 zinazotumika nchini; teknolojia ambayo ilikuwa haitumiki kabla ya Uhuru. Aidha, Serikali imekuwa ikiwawezesha wakulima kupata zana bora za kilimo zikiwemo trekta kubwa na ndogo kupitia Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (DADPs). Katika kipindi cha miaka miwili (2009/10 hadi 2010/11) wakulima wamepatiwa jumla ya trekta ndogo 3,562 na trekta kubwa 169 zenye thamani ya shilingi bilioni 28.4 kwa utaratibu wa wakulima kuchangia asilimia 20 ya gharama za ununuzi wa trekta hizo.

6.4.3 Mikopo Yenye Masharti Nafuu InapatikanaSerikali katika mwaka 2010 ilifanikiwa kupata mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za Kimarekani milioni 40 kutoka India uliowezesha kuingiza nchini trekta 1,860 na zana zake, trekta ndogo za mikono 400 na pampu za kusukuma maji 1,100 ambazo zinauzwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa - SUMA JKT. Wizara imetayarisha mwongozo kwa ajili ya watumiaji wa trekta kubwa na trekta ndogo za mikono (powertillers) ili kuwawezesha wakulima kuzitumia kwa usahihi na hivyo kuongeza tija. Mpango huo utaongeza uzalishaji na tija katika kilimo. Aidha, Serikali kupitia Mfuko wa Pembejeo imeendelea kutoa mikopo kwa ajili ya kununua trekta mpya na kuzikarabati zile zilizoharibika. Kuanzia mwaka 2003 hadi Mei, 2011 jumla ya trekta kubwa 671 na ndogo za mikono 212 zenye thamani ya shilingi bilioni 23.34 zimekopeshwa kwa wakulima kupitia Mfuko huo. Serikali katika mwaka wa 2010 imeanzisha dirisha dogo la kilimo katika Benki ya Rasilimali Tanzania (Tanzania Investment Bank-TIB) kwa ajili ya kutoa mikopo ya miradi ya kilimo ikiwemo ya kununua pembejeo na zana za kilimo kwa masharti nafuu. Hadi Mei, 2011 jumla ya trekta kubwa 100 na trekta ndogo za mikono 82 zimekopeshwa kwa wakulima.

6.4.4 Matumizi ya Zana za Kilimo Hifadhi YameongezekaWakulima wamehamasishwa kuanza kutumia zana bora za kilimo hifadhi kwa lengo la kupunguza mkandamizo wa udongo, kuongeza rutuba na kuwezesha udongo kuhifadhi unyevunyevu na hivyo kuwa na kilimo endelevu kinacholinda mazingira. Mashamba darasa 285 yenye wakulima 3,645 yameanzishwa katika Wilaya za Moshi Vijijini, Arumeru, Karatu, Babati, Hanang, Kilosa, Mvomero, Kongwa na Kiteto. Aidha, majembe tindo ya kukokotwa na wanyamakazi (rippers) na mashine za kupanda bila

kilimo miaka 50.indd Sec1:42kilimo miaka 50.indd Sec1:42 11/16/11 10:34:36 AM11/16/11 10:34:36 AM

Page 59: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

43

kukatua (direct seeders) zimeanza kutengenezwa hapa nchini kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wake.

6.5 Kuimarika kwa Matumizi Bora ya Ardhi ya Kilimo Katika kipindi cha Miaka 50 ya Uhuru wakulima wadogo katika maeneo ya nyanda za juu wameweza kutumia kilimo kinachozingatia hifadhi ya udongo na maji mashambani. Hilo limeongeza tija ya uzalishaji wa mazao shambani. Baadhi ya maeneo yaliyoonyesha mafanikio ni wakulima wa maeneo ya Wilaya za Moshi, Hai na Rombo ambao wameweza kuongeza uzalishaji wa mahindi shambani kutoka tani 1.3 kwa hekta moja hadi tani 2.6 kwa hekta, alizeti toka tani 0.6 mpaka tani 1.1 kwa hekta na maharage toka tani 0.7 mpaka tani 1.2 kwa hekta.

6.5.1 Wakulima Wanaolima kwa Matuta WameongezekaWakulima wa maeneo ya nyanda za juu wanaotumia kilimo cha kuhifadhi udongo na maji mashambani kama vile matuta ya ngazi wameongezeka kwa asilimia kubwa kulingana na sehemu walipo. Baadhi ya maeneo hayo ni katika Halmashauri zifuatazo; Babati, Same, Lushoto, Korogwe, Mvomero na Morogoro vijijini ambayo wakati wa Ukoloni yalikuwa na upinzani mkubwa. Wakulima katika wilaya zilizotajwa wameongezeka kwa asilimia 67.

6.5.2 Elimu ya Hifadhi ya Udongo na Maji Imetolewa kwa WakulimaWadau wa kilimo hususan wakulima wamepewa elimu kwa njia mbalimbali kama vile mafunzo kwa vitendo na kupitia maonyesho mbalimbali ya kitaifa. Wadau wengi wa kilimo wamehamasishwa juu ya umuhimu, kanuni na njia mbalimbali za hifadhi ya udongo na maji mashambani, na mpango wa matumizi bora ya ardhi.

6.5.3 Tathmini ya Ubora na Uwezo wa Ardhi ImefanyikaKutokana na kuongezeka kwa wataalam maeneo ya kilimo yaliyofanyiwa tathmini ya ubora na uwezo wa ardhi yameongezeka ikilinganishwa na wakati nchi inapata uhuru. Baadhi ya Halmashauri zilizofanyiwa tathmini ya udongo kwa ukamilifu ni Mbulu, Maswa, Kahama, Biharamulo na Ngara.

6.5.4 Miradi ya Hifadhi na Matumizi Bora ya Ardhi ya Kilimo ImetekelezwaWizara imeshiriki katika kutekeleza miradi ya hifadhi na mpango wa matumizi bora ya ardhi ya Kilimo (Regional Integrated Development Projects-RIDEPs) katika maeneo mbalimbali nchini. Baadhi ya miradi hiyo ni Hifadhi ya Ardhi Dodoma (HADO), Hifadhi Ardhi Shinyanga (HASHI), Hifadhi ya Udongo na Kilimo Mseto Arusha (SCAPA), Hifadhi ya Mmomonyoko wa Udongo na Kilomo Mseto Lushoto (SECAP), na Hifadhi ya Ardhi Babati (LAMP).

kilimo miaka 50.indd Sec1:43kilimo miaka 50.indd Sec1:43 11/16/11 10:34:37 AM11/16/11 10:34:37 AM

Page 60: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

44

Kilimo Mseto kwenye matuta yaliyoimarishwa na nyasi (Guatemala grass) huongeza uzalishaji wa mazao shambani. Pichani ni mashamba ya wakulima

yenye zao la pareto katika tarafa ya Songwe, wilayani Mbeya vijijini

6.6 Kuimarika kwa Hifadhi ya Mazingira katika KilimoWizara kwa kushirikiana na wadau wa kilimo imeendelea kutekeleza sera, mikakati, sheria na kanuni za usimamizi wa mazingira. Wizara pia imekuwa ikijihusisha na uratibu na utekelezaji wa mikataba ya Kimataifa inayohusu mazingira kama, mabadiliko ya tabianchi; kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame; udhibiti wa kemikali zinazoharibu tabaka la hewa ya Ozoni na hifadhi ya bayoanuai. Kupitia ushauri wa wataalam wa mazingira, Wizara imezingatia matumizi ya mbegu zinazostahimili ukame, wadudu waharibifu na magonjwa. Kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya Wizara kupitia Kitengo cha Mazingira, imefanikiwa kuhamasisha shughuli za hifadhi ya mazingira katika kazi za maendeleo ya kilimo kwa kusudio la kuongeza uzalishaji na kuwa na kilimo endelevu na chenye tija. Aidha, elimu imeendelea kutolewa kuhusu matumizi bora ya teknolojia endelevu za kilimo zinazozingatia hifadhi ya mazingira kupitia maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, na maadhimisho mengine ya kitaifa pamoja na vyombo vya habarí na machapisho mbalimbali. Wizara imewakilishwa ipasavyo katika mikutano mbalimbali ya Kimataifa na kushiriki katika utekelezaji wa makubaliano mbalimbali (Bilateral & Multilateral Agreements) ya Kimataifa ya hifadhi ya mazingira.

kilimo miaka 50.indd Sec1:44kilimo miaka 50.indd Sec1:44 11/16/11 10:34:37 AM11/16/11 10:34:37 AM

Page 61: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

45

6.7 Ongezeko la Uzalishaji na Ubora wa Mazao Makuu ya Biashara Tangu Uhuru mazao ya biashara yamekuwa na mchango mkubwa kwa Taifa hasa katika kuliingizia fedha za kigeni na ajira (mashambani na viwandani). Uzalishaji wa mazao hayo umekuwa ukipanda na kushuka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, mabadiliko ya sera, upatikanaji wa pembejeo na mabadiliko ya bei katika soko la dunia (Kielelezo Na. 3).

Kielelezo Na. 3: Mwenendo wa uzalishaji wa mazao makuu ya biashara kwa kipindi

cha Miaka 50 ya Uhuru (1961-2011) Tani/mwaka

Chanzo: Bodi za Mazao ya Biashara

Mara baada ya Uhuru, uzalishaji wa mazao ya biashara uliongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na juhudi za Serikali kushirikisha wakulima wadogo katika uzalishaji. Vilevile, ongezeko hilo la tija lilitokea zaidi katika kipindi cha miaka ya 1968 hadi miaka ya 1999, wakati Mamlaka za mazao zilikuwa zinasimamia shughuli za uzalishaji na uendelezaji wa mazao. Aidha, mtikisiko wa kiuchumi ulisababisha bei ya mazao hayo katika soko la dunia kushuka na hivyo uzalishaji kupungua. Hata hivyo, Serikali imefanya juhudi kubwa kukabiliana na hali hiyo, ambapo uzalishaji wa mazao makuu ya biashara hadi mwaka 2010, umekuwa ukipanda. Thamani ya mauzo ya nje ya mazao makuu ya biashara imekuwa ikipanda na kushuka kutokana na mabadiliko ya bei na mahitaji ya mazao hayo katika soko la nje (Kielelezo Na.4)

kilimo miaka 50.indd Sec1:45kilimo miaka 50.indd Sec1:45 11/16/11 10:34:37 AM11/16/11 10:34:37 AM

Page 62: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

46

Kielelezo Na. 4: Mwenendo wa mapato ya baadhi ya mazao makuu ya biashara mwaka 2003 hadi 2008.

Chanzo: Wizara ya Fedha na Uchumi6.7.1 MkongeBaada ya Uhuru zao la mkonge liliifanya Tanganyika na baadaye Tanzania kuongoza katika mauzo ya nje ulimwenguni ambapo rekodi ya juu kabisa ilikuwa tani 230,000 ya mwaka 1964 ambayo ilikuwa sawa na asilimia 65 ya mauzo yote ya nje ya nchi kwa wakati huo. Uzalishaji wa zao hilo ulianza kushuka katika miaka ya 1970 baada ya kugundulika kwa nyuzi za nailoni ambazo zilipunguza soko la singa za katani katika soko la dunia. Mwaka 1971, uzalishaji ulipungua kwa asilimia 21 na kufi kia tani 181,108. Hadi kufi kia mwaka 1997, uzalishaji ulipungua zaidi na kufi kia tani 22,180. Mahitaji ya mkonge yalianza kuongezeka tena katika kipindi cha miaka ya 2000, ambapo uzalishaji wa mkonge umeongezeka hadi kufi kia tani 33,028 mwaka 2007/2008. Katika kipindi cha Miaka 50 ya Uhuru tasnia ya mkonge imeweza kutekeleza miradi mingi ya utafi ti wa bidhaa za mkonge. Mpaka sasa zao la Mkonge limewezesha uzalishaji wa gesi inayotumika kuzalishia umeme wa Kilo Watt 150 katika maeneo ya Hale mkoani Tanga.

6.7.2 ChaiKatika kipindi cha Miaka 50 ya Uhuru, kumekuwa na mafanikio ya kuridhisha katika tasnia ya Chai nchini. Mafanikio hayo yamechangiwa na usimamizi madhubuti wa zao la chai unaofanywa na Bodi ya Chai pamoja na mikakati ya kuliendeleza zao hilo iliyowekwa na Wakala wa Maendeleo ya Wakulima Wadogo wa Chai. Mara baada

kilimo miaka 50.indd Sec1:46kilimo miaka 50.indd Sec1:46 11/16/11 10:34:37 AM11/16/11 10:34:37 AM

Page 63: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

47

ya Uhuru wakulima wadogo waliruhusiwa kuanzisha kilimo cha chai na ushiriki wao umechangia kwa kiasi kikubwa katika ongezeko la uzalishaji wa chai (Jedwali Na. 5).

Jedwali Na. 5: Ongezeko la Eneo na Uzalishaji na Tija Katika Tasnia ya Chai.

Mwaka Eneo Uzalishaji Tija

(hekta) Tani) Wakulima wakubwa(tani/hekta)

Wakulima wadogo (tani/hekta)

1972/1973 5,878 11,613 1,259 281

2009/2010 22,721, 32,799 2048 849

Chanzo: Wakala wa Wakulima Wadogo wa Chai Tanzania

Kuanzishwa kwa Wakala kumeleta mageuzi makubwa katika tasnia ya chai, ambapo kupitia taasisi hiyo Serikali imewawezesha wakulima wadogo kuongeza tija na kupanua maeneo ya kilimo cha chai kwa kuwapatia ruzuku ya miche bora. Aidha, bei ya majani mabichi ya chai imepanda kutoka shilingi 55 kwa kilo kwa mwaka 1992 hadi shilingi 180 kwa kilo kwa mwaka 2009/2010. Vilevile wakulima wadogo wamewezeshwa kuanzisha mfuko wa Wakfu ambao utasaidia katika kutatua matatizo ya uzalishaji hususan upatikanaji wa pembejeo, ununuzi wa hisa na ujenzi wa viwanda. Licha ya mafanikio hayo uwepo wa Wakala unajionyesha kutokana na ongezeko la uwekezaji katika kilimo cha chai kupitia miradi inayoibuliwa na wakulima wa chai kupitia jamii na vikundi vyao. Wakala imekuwa ikishirikiana na Halmashauri za Wilaya zinazolima chai kuainisha maeneo ya kilimo cha chai yanayoweza kuwekwa katika Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (DADPs). Tangu nchi ipate uhuru, mchango wa Bodi ya Chai Tanzania katika tasnia ya chai ni pamoja na kuwepo kwa ongezeko la ujenzi wa viwanda vya kusindika chai ambavyo kwa sasa idadi yake imefi ka 19, ambapo wakulima wadogo pia wamewezeshwa kununua hisa katika viwanda hivyo. Aidha, viwanda vya kuchanganya na kufunga chai kwenye vikasha na ambavyo vinaendesha biashara ya kununua, kuchanganya na kuuza chai hapa nchini vimefi kia saba. Vilevile, kumekuwa na uzingatiaji wa kanuni za afya na ubora wa chai kutokana na ukaguzi wa mara kwa mara katika viwanda vya kusindika na kuchanganya chai. Mbali na mafanikio hayo, wawekezaji wa ndani na nje wameanza kujitokeza kuwekeza katika tasnia ya chai.

6.7.3 PambaMara baada ya Uhuru uzalishaji wa pamba uliongezeka kwa kasi ambapo mwaka 1966 ulifi kia tani 237,600. Uzalishaji ulipungua zaidi mwishoni mwa miaka ya 1970 na mwanzoni mwa miaka ya 1980 na kufi kia tani 127,910 kwa mwaka. Kati ya mwaka 1984 hadi 2010, uzalishaji uliendelea kupanda katika maeneo ya kanda ya magharibi na kufi kia tani 162,882. Katika kanda ya mashariki uzalishaji umepungua kwa kiasi kikubwa na kufi kia tani 636. Bei anayolipwa mkulima imeongezeka kutoka asilimia 28 kabla ya soko huru hadi asilimia 60 kwa sasa. Aidha, kumekuwa na ufanisi katika

kilimo miaka 50.indd Sec1:47kilimo miaka 50.indd Sec1:47 11/16/11 10:34:38 AM11/16/11 10:34:38 AM

Page 64: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

48

uchambuaji wa pamba ambapo idadi ya viwanda vya kuchambua pamba iliongezeka kutoka viwanda 37 vilivyokuwepo kabla ya soko huru hadi viwanda 80 mwaka 2011.

6.7.4 SukariKatika kipindi cha Miaka 50 ya Uhuru kumekuwa na ongezeko katika uzalishaji wa sukari. Kutokana na mahitaji ya sukari kuongezeka mwaka hadi mwaka, uzalishaji wa sukari mwaka 1963/64 ulikua na kufi kia tani 51,802. Uzalishaji huo uliongezeka na kufi kia tani 120,353 mwaka 1992/93. Hadi mwaka 2010/11, uzalishaji wa sukari nchini umeongezeka na kufi kia tani 304,135.

6.7.5 TumbakuUzalishaji na ubora wa zao la tumbaku nchini katika kipindi cha miaka 50 umekuwa na mafanikio makubwa. Ongezeko hilo la uzalishaji limetokana na matumizi ya mbegu bora za tumbaku. Pia ubora wa tumbaku umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na matumizi ya teknolojia mpya ya mabani ya kukaushia tumbaku (Brazilian barns na rocket barns). Hali hiyo imesababisha kuongezeka kwa kiasi kikubwa cha uzalishaji wa tumbaku kutoka tani 3,000 wakati wa Uhuru (1961), hadi tani 120,400 kwa mwaka 2011 (kielelezo Na.5). Vilevile, kutokana na kuimarika kwa ubora bei ya tumbaku imepanda kutoka shilingi 7.4 kwa kilo mwaka 1977/78, shilingi 1,264 mwaka 2007/2008 na kufi kia shilingi 3,422 mwaka 2009/2010.

Kielelezo Na 5. Uzalishaji wa Tumbaku kwa Kipindi cha Miaka ya 1961 hadi 2010

Chanzo: Bodi ya Tumbaku Tanzania

kilimo miaka 50.indd Sec1:48kilimo miaka 50.indd Sec1:48 11/16/11 10:34:38 AM11/16/11 10:34:38 AM

Page 65: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

49

6.7.6 KoroshoMwaka 2006/2007 uzalishaji wa korosho ulikuwa tani 92,573 ambao mwaka 2010/2011 umefi kia tani 121,135. Ongezeko hilo limechangiwa na kuongezeka kwa kaya za wakulima wa korosho kutoka 180,000 miaka ya 1960 na 1970 hadi kaya 300,000 mwaka 2011. Katika kipindi hicho, ekari zilizopandwa mikorosho katika mikoa na wilaya mbalimabali nazo ziliongezeka kutoka ekari 300,000 hadi ekari 500,000. Kwa mantiki hiyo, kwa sasa kuna wilaya 36 zinazolima korosho nchini kote. Kiuchumi, zao la korosho limekuwa likitoa mchango mkubwa katika kulipatia Taifa fedha za kigeni ambapo kiwango kwa mwaka 2009/10 kilifi kia asilimia 10 ya mapato yanayotokana na kilimo. Ubora wa korosho za daraja la kwanza umeongezeka hadi asilimia 97 ya korosho zote zinazozalishwa nchini. Aidha, bei ya korosho anayolipwa mkulima imeongezeka na kufi kia shilingi 1,600 kwa kilo moja ya korosho baada ya gharama zote kutolewa. Wakati mwaka 2005/2006 kiasi cha korosho zilizobanguliwa kilikuwa asilimia 10, kiasi hicho kimeongezeka hadi kufi kia asilimia 40 ya korosho zote zinazozalishwa nchini. Ongezeko hilo limechangiwa na kuanzishwa kwa viwanda vidogo na vya kati vinavyoendeshwa na wajasiriamali na wakulima katika vijiji na miji midogo. Kuhusu viwanda vikubwa vilivyobinafsishwa mwanzoni mwa miaka ya 2000, sita kati yake vinaendelea kufanya kazi vizuri ambapo viwili viko Newala, viwili Mtwara, kimoja Tunduru na kimoja Mtama katika wilaya ya Lindi Vijijini. Mafanikio mengine ni kuboreshwa kwa upatikanaji wa takwimu kutokana na matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi ya Mazao Ghalani na usimamizi wa usafi rishaji korosho nje.

6.7.7 KahawaZao la kahawa katika kipindi cha Miaka 50 ya Uhuru limebaki kuwa ni miongoni mwa mazao makuu ya biashara hapa nchini. Kahawa ilishawahi kuchangia hadi asilimia 40 katika pato la Taifa, wakati hali ya sasa zao hilo linachangia wastani wa dola za Kimarekani milioni 100 kwa mwaka. Katika kipindi cha mwaka 1975 hadi 1984, wastani wa uzalishaji kwa mwaka ulikuwa tani 52,164. Hata hivyo, uzalishaji ulipungua kidogo katika kipindi cha miaka ya 1985 hadi 1994 ambapo ulikuwa wastani wa tani 49,116 kwa mwaka. Kutokana na usimamizi makini wa sheria unaofanywa na Bodi ya Kahawa Tanzania, uzalishaji wa kahawa uliongezeka kutoka tani 34,100 mwaka 2005 hadi tani 68,000 mwaka 2009. Aidha, ubora wa kahawa katika daraja la kwanza hadi la tano umeongezeka kutoka asilimia 32 mwaka 2002 hadi asilimia 56 mwaka 2008. Unywaji wa ndani wa kahawa umeongezeka kutoka asilimia 2 mwaka 2003 hadi asilimia 7 mwaka 2008.

6.7.8 ParetoUzalishaji wa pareto umekuwa ukiongezeka na kushuka kutegemea bei katika soko la dunia, pamoja na mabadiliko ya sera. Kati ya mwaka 1959/1960 na mwaka 1966/1967 uzalishaji wa pareto uliongezeka kutoka tani 1,618 hadi tani 6,015. Katika mwaka 1998/1999 uzalishaji ulishuka hadi tani 578. Baada ya ubinafsishaji wa sekta ya pareto; uzalishaji uliongezeka haraka kutoka tani 1,850 mwaka 2000/2001 hadi tani 2,800 mwaka 2005/2006; na tani 3,200 mwaka 2008/2009 hadi tani 4,560 mwaka 2010/2011.

kilimo miaka 50.indd Sec1:49kilimo miaka 50.indd Sec1:49 11/16/11 10:34:38 AM11/16/11 10:34:38 AM

Page 66: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

50

Aidha, kumekuwa na ongezeko la ubora wa zao la pareto kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha sumu (pyrethrin content) katika pareto inayozalishwa na wakulima kutoka wastani wa asilimia 1.10 mwaka 1978/1979 hadi asilimia 1.6 mwaka 2010/2011.

6.8 Nchi Imeendelea Kujitosheleza kwa ChakulaHali ya chakula nchini imeendelea kuwa ya kuridhisha mwaka hadi mwaka kwa viwango tofauti. Tangu nchi yetu ipate Uhuru sehemu kubwa ya mahitaji ya chakula yanatokana na uzalishaji wa ndani, na kiasi kidogo kinachobaki kimekuwa kikitoka nje ya nchi. Uzoefu unaonyesha kuwa katika misimu inayokuwa na mvua za kutosha, Tanzania imekuwa na uwezo wa kuzalisha chakula cha kutosheleza mahitaji na kuuza ziada katika nchi za jirani. Uchambuzi unaotokana na kigezo cha Uwiano wa Kujitosheleza kwa Chakula (Food Self Suffi ciency Ratio - FSSR) katika miongo minne iliyopita unaonyesha kwamba nchi iliweza kujitosheleza kwa chakula kwa kati ya asilimia 88 hadi asilimia 111 (Jedwali Na. 6; Kielelezo Na. 6 &7). Kiwango hicho cha kujitosheleza kwa chakula kutokana na uzalishaji wa ndani ya nchi ni cha juu ikilinganishwa na nchi nyingi za bara la Afrika. Aidha, uchambuzi umeonyesha kuwa katika baadhi ya miaka viwango vya kujitosheleza kwa chakula vilikuwa chini ya asilimia 100. Hali hiyo haimaanishi kwamba, maeneo yote ya nchi yalikuwa yameathiriwa na upungufu wa chakula katika viwango vinavyofanana. Upungufu wa chakula katika baadhi ya maeneo katika miaka hiyo ulitokana na sababu mbalimbali kama vile mafuriko yaliyosababishwa na mvua za El Nino, na ukame kama ilivyokuwa katika miaka ya 1971/1972, 1993/1994 na 2002/2003, ambao ulisababisha upungufu mkubwa wa chakula katika miaka iliyofuata. Hata hivyo, katika miaka ambayo uzalishaji umekuwa chini ya kiwango, Serikali imekuwa ikifanya juhudi kubwa ya kuhakikisha wananchi walio na upungufu wanapata chakula. Miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kununua na kusambaza chakula, kuhamasisha wafanyabiashara kuingiza chakula kutoka nje ya nchi na kupokea misaada kutoka kwa wahisani mbalimbali. Kwa kipindi cha 2004/05 hadi 2008/09 hali ya chakula ilikuwa nzuri na Taifa lilijitosheleza kwa wastani wa asilimia 102.4. Katika msimu wa mwaka 2009/10 Taifa lilijitosheleza kwa asilimia 102 lakini kulikuwa na upungufu wa nafaka wa tani milioni 1.3 uliotokana na uzalishaji mdogo wa mazao hayo wa tani milioni 5.2 ikilinganishwa na mahitaji ya nafaka ya jumla ya tani milioni 6.5. Pamoja na hali ya chakula ki-Taifa kuwa nzuri kwa wastani, kumekuwa na maeneo machache katika baadhi ya mikoa ambayo yamekuwa na upungufu. Maeneo ambayo yamekuwa yakikumbwa na upungufu wa chakula wa mara kwa mara ni kama vile maeneo ya Karatu, Monduli, Meru, Arusha (v), Ngorongoro, Simanjiro, Same, Rombo na Mwanga. Maeneo mengine ni Manyoni, Singida (v), Iramba, Uyui, Bahi, Chamwino, Mpwapwa, Kongwa, Meatu, Kishapu, Bariadi, Bukombe, Magu, Bunda, Rorya, Musoma (v), Musoma (m) na Iringa (v).

kilimo miaka 50.indd Sec1:50kilimo miaka 50.indd Sec1:50 11/16/11 10:34:38 AM11/16/11 10:34:38 AM

Page 67: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

51

Jedwali Na. 6: Mwenendo wa Hali ya Chakula Kitaifa Miaka ya 1995 hadi 2010

Mwaka 1995/96 1996/97 1997/98 1998/99 1999/00 2000/01 2001/02 2002/03 2003/04 2004/05

Asilimia 110 117 88 109 108 92 94 102 88 103

Mwaka 2005/06 2006/07 2007/08 2008/09 2009/10 2010/11 2011/12 2012/13 2013/14 2014/15

Asilimia 102 112 106 105 102 111

Kielelezo Na. 6: Hali ya kujitosheleza kwa chakula mwaka 1995 hadi 2010

Chanzo: Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika

Kielelezo Na. 7: Uzalishaji wa baadhi ya mazao ya chakula

Chanzo: Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika

kilimo miaka 50.indd Sec1:51kilimo miaka 50.indd Sec1:51 11/16/11 10:34:38 AM11/16/11 10:34:38 AM

Page 68: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

52

6.9 Uzalishaji wa Mazao ya Bustani UmeongezekaKuanzia miaka ya 1980, uzalishaji wa mazao ya bustani umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka (Kiambatisho Na. 7). Hiyo ni kutokana na umuhimu na manufaa ya mazao hayo kiuchumi na kijamii. Uzalishaji wa mazao hayo umeonyesha mafanikio makubwa hasa katika ongezeko la uzalishaji, ubora wa maua na mboga unaokidhi viwango vya masoko ya nje pamoja na kulipatia Taifa mapato. Hadi mwaka 2008, thamani ya mauzo ya nje ya mazao ya bustani ilikuwa dola za Kimarekani milioni 32.2 ikilinganishwa na dola za Kimarekani milioni 19.1 mwaka 2007, sawa na ongezeko la asilimia 68.4. Ongezeko hilo lilitokana na kupanda kwa wastani wa bei ya mazao ya bustani katika soko la dunia. Vilevile, Wizara kwa kushirikiana na wadau ilianzisha Baraza la kuendeleza mazao ya bustani (Horticultural Development Council of Tanzania- HODECT) na kusajiliwa Machi 2007. Lengo ni kuwa na mfumo wa kuratibu kazi zinazofanywa na wadau mbalimbali katika kuendeleza na kuongeza uzalishaji wa mazao ya bustani hapa nchini.

6.10 Akiba ya Taifa ya Chakula ImeongezekaKatika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru Serikali imeweka mkazo katika kununua na kuhifadhi chakula kwenye maghala yake ambacho kimekuwa kikitumika kupunguza makali ya njaa katika maeneo yaliyoathirika na ukame na hivyo kuwa na upungufu wa chakula. Mwaka 1990/1991 akiba ya Taifa ya chakula chini ya Kitengo kilichojulikana kama Strategic Grain Reserve-SGR ilikuwa ni tani 107,000 za mahindi. Kitengo cha SGR kimeendelea na majukumu ya kununua, kuhifadhi na kutoa chakula cha msaada katika maeneo yenye upungufu wa chakula ndani na nje ya nchi kwa mafanikio makubwa. Kwa mfano mwaka 2001/2002, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitoa msaada wa mahindi tani 2000, kwa Serikali ya Malawi na tani 2,000 kwa Serikali ya Zambia. Mwaka 2002/2003, Serikali pia ilitoa msaada wa tani 4,000 za mahindi kwa Serikali ya Zimbabwe. Aidha, Serikali ya Kenya iliuziwa na SGR tani 3,000 za mahindi katika mwaka 2007/2008, wakati Shirika la Chakula Duniani (WFP) limekuwa likinunua mahindi ya SGR kila mwaka na kuyasafi risha nchi jirani kwa ajili ya kulisha wakimbizi. Hali hii imetujengea heshima kubwa ya kiuchumi na kisiasa katika historia ya Tanzania huru. Kitengo cha SGR kimetekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa na hivyo mwaka 2008, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula uliundwa kwa lengo la kuhakikisha usalama wa chakula ili kukabiliana na upungufu wa chakula kwa kununua, kuhifadhi, kutoa msaada wa chakula kinapohitajika na kuuza ziada ya akiba ya chakula kwa lengo la kupata mapato ya kununulia akiba mpya kwa kuzingatia ufanisi na tija. Katika mwaka 2010/2011, Wakala umefanikiwa kwa kiwango kikubwa kununua mahindi ya ziada kutoka kwa wakulima ambapo kiasi cha tani 180,964.082 zilinunuliwa ikiwa ni asilimia 90.5 ya lengo la kununua tani 200,000. Kutokana na jitihada hizo akiba ya Taifa ya Chakula hadi tarehe 30 Juni, 2011 ni tani 228,713.8.

6.11 Kuongezeka kwa Tija ya Kilimo cha UmwagiliajiKabla ya Uhuru, Serikali ya kikoloni ilianzisha shamba la umwagiliaji kwa kilimo cha mpunga huko Kilangali, mkoani Morogoro likiwa na ukubwa wa hekta 1,000. Hadi

kilimo miaka 50.indd Sec1:52kilimo miaka 50.indd Sec1:52 11/16/11 10:34:39 AM11/16/11 10:34:39 AM

Page 69: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

53

mwaka 1970 hekta 2,600 zilikuwa zimeendelezwa ambazo ni asilimia 26 ya malengo ya miaka 10 ya kuendeleza hekta 10,000. Skimu za umwagiliaji zilizojengwa ni zile zilizokuwa na maeneo ya ukubwa wa hekta 200 hadi 2,000; kwa lengo la kufi kia hekta 150,000 ifi kapo mwaka 1985. Katika kusimamia utekelezaji wa kazi hiyo, mwaka 1981 Idara ya Umwagiliaji iliunda kanda sita za umwagiliaji na Kanda ya saba iliundwa mwaka 2003/04 ili kufi kisha huduma kwa wananchi wengi zaidi katika wilaya. Kanda hizo ni Mbeya (Mbeya, Iringa na Rukwa); Kilimanjaro (Kilimanjaro, Arusha na Tanga); Mwanza (Mwanza, Mara, Kagera na Shinyanga); Tabora (Tabora, Kigoma); Mtwara (Mtwara, Lindi na Ruvuma); Morogoro (Morogoro, Pwani na Dar es Salaam); na Kanda ya Kati inayojumuisha mikoa ya Dodoma, Manyara na Singida.

Miundombinu ya umwagiliaji iliyojengwa katika baadhi ya skimu za umwagiliaji nchini

Mwaka 2001/2002, eneo la skimu za umwagiliaji lililoendelezwa kwa kujengewa miundombinu ya umwagiliaji bora lilikuwa hekta 191,900. Eneo hilo liliongezeka hadi hekta 331,490 mwaka 2010/2011. Eneo linalomwagiliwa baada ya kujengewa miundombinu ya umwagiliaji hadi sasa ni jumla ya hekta 345,690 ambalo ni asilimia moja nukta moja (1.1%) ya eneo lote linalofaa kwa umwagiliaji. Jumla ya hekta 49,398 bado zinatumia umwagiliaji wa asili na hivyo zikijumuishwa na eneo lililojengewa miundombinu linafanya jumla ya eneo linalomwagiliwa nchini kufi kia hekta 380,888. Kati ya eneo lililoendelezwa, hekta 276,261 ni za wakulima wadogo ambazo hutumika kwa kilimo cha mazao ya mpunga, mahindi, maharage na mboga. Hekta 55,229 ni za wakulima wakubwa wa kibiashara kwa kilimo cha chai, kahawa, miwa, mpunga, mboga na maua. Hali ya uzalishaji wa mazao (hasa Mpunga) inatofautiana kutoka skimu moja hadi nyingine. Kwa baadhi ya skimu, takwimu zinaonyesha kuwa uzalishaji wa mavuno yatokanayo na umwagiliaji ni mkubwa na wenye tija. Kwa mfano uzalishaji wa mpunga kwa skimu za Lower Moshi na Ndungu umekuwa ni kuanzia tani 3 hadi 7 kwa hekta

kilimo miaka 50.indd Sec1:53kilimo miaka 50.indd Sec1:53 11/16/11 10:34:39 AM11/16/11 10:34:39 AM

Page 70: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

54

(Kielelezo Na.8). Aidha, ufanisi wa matumizi ya maji kwa umwagiliaji umeongezeka kutoka kati ya asilimia 10 na 15 kwenye skimu za asili na kufi kia asilimia 30 kwa skimu zilizoboreshwa miundombinu ya umwagiliaji.

Kielelezo Na 8: Uzalishaji wa Mpunga kwa Eneo Katika Baadhi ya Skimu za Umwagiliaji

Chanzo: Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika

6.12 Kuimarika kwa Uongozi wa Vyama vya UshirikaUtekelezaji wa CRMP umejikita katika kujenga mifumo ya Taasisi (vyama vya ushirika). Katika kipindi cha mwaka 2005/2006 hadi mwaka 2009/2010 ufufuaji wa vyama vya ushirika vilivyokuwa vimeshindwa kuwahudumia wanachama wake kwa kuviwezesha kufanya biashara kwa kujitegemea ulianza. Mwaka 2007/2008, ufufuaji uliviwezesha vyama vya ushirika kununua mazao ya korosho kutoka kwa wakulima na kuwapa bei nzuri. Aidha, ubora wa mazao ya wakulima yaliyouzwa kupitia vyama hivyo uliongezeka na hivyo kuvutia wanunuzi na kuongeza ushindani. Kati ya mwaka 2005 na 2010, kupitia Programu hiyo uratibu umeendelea kuimarishwa ikiwa ni pamoja na kusimamia chaguzi za viongozi wa vyama vya ushirika vya msingi, vyama vikuu, kilele na shirikisho. Lengo limekuwa kuhakikisha chaguzi hizo zinafanyika kwa kuzingatia matakwa ya Sheria ya Ushirika ya mwaka 2003 ambayo inawawezesha wanachama wa vyama hivyo kuchagua viongozi waadilifu na wanaowajibika. Vile vile, viongozi mbalimbali wa ushirika waliochaguliwa wamepata mafunzo ya utawala bora katika vyama vya ushirika na hivyo kuimarisha utendaji na uwajibikaji katika vyama husika.

kilimo miaka 50.indd Sec1:54kilimo miaka 50.indd Sec1:54 11/16/11 10:34:39 AM11/16/11 10:34:39 AM

Page 71: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

55

6.13 Vyama vya Ushirika wa Mazao VimeongezekaIdadi ya wanachama wa Vyama vya Ushirika imeongezeka kutoka milioni 1.8 mwaka 2009 hadi milioni 2.1 mwaka 2010. Idadi ya Vyama vya Ushirika wa Mazao imeongezeka kutoka 2,616 mwaka 2005 hadi vyama 2,821 mwaka 2009.

6.14 Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo VimeongezekaKumekuwepo ongezeko la idadi ya Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo (SACCOS), kutoka 1,876 mwaka 2006 hadi 5,344 mwaka 2010. Idadi ya wanachama wa SACCOS nayo imeongezeka kutoka 820,670 hadi 911,873 katika kipindi hicho. Hisa za wanachama ziliongezeka kutoka shilingi bilioni 33.5 hadi shilingi bilioni 36.7. Akiba na amana za wanachama nazo ziliongezeka kutoka shilingi bilioni 148.1 hadi shilingi bilioni 176.6, ambapo mikopo iliyotolewa kwa wanachama iliongezeka kutoka shilingi bilioni 383.5 hadi shilingi bilioni 463.4. Mikopo hiyo ilikuwa kwa ajili ya mitaji ya biashara, kilimo, ufugaji, ujenzi wa nyumba, karo za shule, ununuzi wa trekta ndogo (power tillers) na kubwa.

6.15 Kuimarika kwa Vyama vya Ushirika KibiasharaKatika kipindi cha 2009/2010, vyama vya ushirika vinavyoshughulika na zao la tumbaku vilisambaza kwa wakulima wa tumbaku jumla ya tani 22,941 za aina mbalimbali za mbolea. Hii ni baada ya kutenganishwa kwa shughuli za usambazaji wa pembejeo na ununuzi wa tumbaku ambapo vyama vya ushirika kwenye maeneo ya uzalishaji wa zao hilo vilipewa jukumu la kusambaza pembejeo na jukumu la ununuzi lilielekezwa kwa makampuni binafsi. Hali kadhalika, vyama vya ushirika vya tumbaku vimekuwa vikidhamini wakulima kupata mikopo ya pembejeo na zana bora. Mathalani, mwaka 2009/2010 wakulima 20 (wilaya ya Chunya 19 na Manyoni 1) walidhaminiwa kupata mikopo ya kununulia trekta kubwa kutoka benki ya CRDB. Aidha, vyama vya ushirika vilipata mikopo ya jumla ya shilingi bilioni 53 sawa na dola za Kimarekani milioni 40.8 kwa ajili ya ununuzi wa pembejeo katika kipindi hicho kutoka benki za CRDB na NMB. Vyama vilivyopata mikopo ni; CHUTCU (Mbeya), CETCU (Singida), LATCU (Rukwa), KACU (Shinyanga), SONAMCU (Ruvuma) na WETCU (Tabora). Vyama karibu vyote vimelipa mikopo hiyo isipokuwa KACU ambacho kinaendelea na taratibu za kukamilisha malipo ya mkopo wake. Mfumo wa stakabadhi ghalani, katika msimu wa mwaka 2009/2010 umeendelezwa katika mikoa yote inayolima Korosho - Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani, Dar es Salaam na Tanga ambapo wakulima wameendelea kupata bei nzuri kwa vyama kulipa wakulima kati ya shilingi 1,000 hadi shilingi 1,050 kwa kilo ikilinganishwa na kipindi cha kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani walipokuwa wanapata bei kati ya shilingi 200 hadi shilingi 250 kwa kilo. Vyama Vikuu vya Ushirika vya KDCU (Karagwe), KCU (Kagera) na KNCU (Kilimanjaro) vilichukua mikopo kutoka benki ya CRDB ya jumla ya shilingi bilioni 8.8 na vinashiriki vizuri kukusanya na kuuza kahawa ya wakulima ambapo msimu wa mwaka 2009/2010 jumla ya kilo 15,729,524 zilikusanywa. Kati yake kilo 4,688,000 ni za kahawa hai ya robusta (organic coffee) ambazo zimeuzwa katika soko maalum (fair trade) nje ya nchi kwa bei ya shilingi 3,800 kwa kilo na kulipa mikopo yote ya benki

kilimo miaka 50.indd Sec1:55kilimo miaka 50.indd Sec1:55 11/16/11 10:34:39 AM11/16/11 10:34:39 AM

Page 72: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

56

katika kipindi hicho. Aidha, vyama hivyo vinalipa kodi Serikalini ambapo msimu wa mwaka 2009/2010 vyama hivyo vitatu pekee vililipa jumla ya shilingi milioni 330.7 Kwa zao la pamba, chama Kikuu cha Ushirika cha Nyanza (NCU) katika msimu wa 2009/10 kiliweza kufanya biashara ya pamba na kulipa mkopo wa benki ya CRDB wa kununulia zao la pamba kwa asilimia 100. Aidha, watendaji mbalimbali wa SACCOS wameendelea kupata mafunzo kwa lengo la kuboresha utendaji wao wa kazi. Kutokana na haja ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wanachama wake baadhi ya SACCOS zimeanza kutumia mifumo ya kompyuta ambayo imeboresha utunzaji wa takwimu na kumbukumbu za vyama na kusaidia wanachama kupata huduma kwa wakati.

6.16 Vyama vya Ushirika Vimechangia Maendeleo ya Jamii na Jumuiya.Mbali na michango isiyoonekana kama vile kutoa viongozi katika ngazi mbalimbali Serikalini vyama vya ushirika vimeleta manufaa yafuatayo:-a. Vyama vikuu vya KNCU, KCU, KDCU, MCU na SHIRECU kwa nyakati tofauti

vilianzisha shule za Sekondari 10 na kati ya hizo zimefi kia kidato cha sita.b. Vyama vilivyotajwa hapo juu vimeendelea kutoa ufadhili kwa watoto wa wakulima

wanaoshindwa kulipa karo za shule.c. Vyama vikuu ya KDCU, KCU na TFC vinamiliki asilimia 92 za hisa ya kiwanda

cha kahawa TANICA ambacho kinaongeza thamani ya kahawa inayouzwa ndani na nje ya nchi.

d. Vyama vinavyolima kahawa vinamiliki asilimia 90 ya hisa za viwanda vya kahawa vya Mbozi na Mbinga.

e. Vyama vya KCU na KDCU vinamiliki viwanda vya kukoboa kahawa (coffee curing).

f. Vyama vya ushirika katika maeneo yanayolima pamba vinamiliki viwanda 25 vya kuchambua pamba.

g. KNCU inaendesha mradi wa utalii wa ikolojia.h. Vyama vya KDCU, KCU na KNCU vinamiliki hoteli kubwa katika miji yao ya

mikoa.i. Vyama vya ushirika vya msingi vya Kilimanjaro na vya Wilaya za Bukoba na

Muleba vimeanzisha benki za ushirika zinazoitwa KCBL na KFCB ambazo zinatoa huduma kwa wakulima, wanachama wa vyama vya ushirika na wafanyabiashara.

Vyama vya Ushirika vilishawahi kumiliki Benki ya Ushirika kitaifa ambayo baadaye ilibadilishwa na kugawanywa kuwa National Bank of Commerce na sehemu nyingine kuwa Cooperative and Rural Development Bank.

kilimo miaka 50.indd Sec1:56kilimo miaka 50.indd Sec1:56 11/16/11 10:34:39 AM11/16/11 10:34:39 AM

Page 73: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

57

Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mojawapo ya mashamba ya mpunga uliostawi vizuri mkoani Morogoro.

kilimo miaka 50.indd Sec1:57kilimo miaka 50.indd Sec1:57 11/16/11 10:34:40 AM11/16/11 10:34:40 AM

Page 74: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

58

7. CHANGAMOTO ZA KILIMO NA USHIRIKA Pamoja na jitihada kubwa za Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo, kilimo bado kinakabiliwa na changamoto nyingi ambazo hazinabudi kupangiwa mikakati mipya ya kufanikisha azma ya kuleta mapinduzi ya kijani nchini. Tangu nchi yetu ipate Uhuru kilimo kimekabiliwa na changamoto zifuatazo:-

7.1 Mabadiliko ya Miundo na Taasisi za Sekta ya KilimoMiundo ya Wizara na Taasisi zake imekuwa ikibadilika tangu mwaka 1961. Kwa mfano mwaka 1961 Wizara ilianza kama Wizara ya Kilimo ikijumuisha Mazao, mifugo, misitu, wanyama pori na ushirika. Mwaka huu wa 2011 tunapoadhimisha Miaka 50 ya Uhuru Wizara inaitwa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika. Hali hii imefanya kuwepo na mabadiliko ya sera, mikakati na programu za utekelezaji katika sekta hizo ambazo kwa kiasi fulani yamepunguza ufanisi na ufi kiwaji wa malengo ya kilimo. Baadhi ya huduma za sekta ya kilimo kama utafi ti, ugani na umwagiliaji zimeathirika zaidi na mabadiliko hayo.

7.2 Ardhi ya Kilimo Haitambuliki KisheriaTanzania kumekuwa na sheria nyingi zinazolinda ustawi na maendeleo ya sekta mbalimbali. Kwa mfano sheria ya misitu inalenga kuhifadhi na kutunza misitu nchini. Sheria nyingine ni kama zile za wanyapori, madini na nyinginezo. Tangu nchi ipate Uhuru hapajawahi kuwa na sheria inayolenga kulinda na kutunza maeneo ya ardhi inayofaa kwa kilimo. Matokeo yake ardhi inayofaa kwa kilimo imekuwa ikihamishiwa matumizi mengine kama misitu, hifadhi ya wanyama pori, madini, maendeleo ya makazi na matumizi mengine. Hali hiyo, imesababisha upungufu wa ardhi inayofaa kwa kilimo mwaka hadi mwaka na hivyo kuhatarisha upatikanaji wa maeneo yanayofaa kwa kilimo katika siku zijazo. Hali hiyo isipodhibitiwa, kuna hatari miaka ijayo kutokuwa na ardhi inayofaa kwa ajili ya matumizi ya kilimo na hivyo kuhatarisha upatikanaji wa chakula na mazao mengine kwa ajili ya ustawi wa Taifa na vizazi vijavyo. Kuna haja kubwa sasa ardhi inayofaa kwa kilimo ipimwe na itambuliwe kisheria ili iweze kulindwa. Wakulima wengi wa Tanzania wanalima kilimo cha kujikimu (subsistence farming). Wengi wao hawana uwezo wa kufanya mchakato wa umiliki wa ardhi kisheria. Tatizo hili limesababisha wakulima kutokopesheka kutoka taasisi za fedha na hivyo, kutokuwa na mitaji ya kutosha ya kuendeleza sekta ya kilimo. Pia, wakulima wengi hawana uelewa juu ya umuhimu wa kumiliki ardhi kisheria. Kutokana na hali hiyo, kuna haja ya kuweka mikakati itakayowezesha wananchi kumilikishwa ardhi ambayo pia inaweza kutumika kama dhamana wanapohitaji kupata mikopo kutoka taasisi za fedha. Kutokana na ardhi za taasisi za Wizara kutopimwa na kupatiwa hati tumeshuhudia miaka ya karibuni kumekuwa na uvamizi wa ardhi ya taasisi hizo kwa ajili ya matumizi mbalimbali ambayo hayakukusudiwa katika kuendeleza kilimo. Uvamizi huo unahatarisha mipango ya sasa na ya baadaye ya kuendeleza shughuli za kilimo kama utafi ti, uzalishaji mbegu bora, na mengineyo katika vituo hivyo. Mathalani uendelezaji wa kituo cha Mpiji (Wilayani Bagamoyo) kwa ajili ya kuzalisha miche ya miembe umezoroteshwa na uvamizi unaoendelea kwa ajili ya watu kujenga makazi. Hivyo, hatua za haraka hazinabudi kuchukuliwa kuhakikisha maeneo yote ya Serikali yanapimwa na yanamilikiwa kisheria.

kilimo miaka 50.indd Sec1:58kilimo miaka 50.indd Sec1:58 11/16/11 10:34:40 AM11/16/11 10:34:40 AM

Page 75: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

59

7.3 Upungufu wa RasilimaliWakati tunapata Uhuru mwaka 1961 kulikuwa na upungufu mkubwa wa rasilimali watu katika nyanja zote za sekta ya kilimo. Watalaam wa ugani, watafi ti na walimu katika vyuo vya kilimo walikuwa wachache. Hali hiyo kwa muda wa miaka 50 imeendelea kuboreshwa kwa kusomesha wagani, watafi ti na walimu wa kilimo ndani na nje ya nchi. Hata hivyo, jitihada hizo hazijaweza kutosheleza mahitaji ya kuwa na wataalam wa kilimo hususan katika maeneo ya kata na vijiji. Upungufu mwingine wa rasilimali ni ufi nyu wa fedha za kuendeshea na kuboreshea miundombinu ya utafi ti, huduma za ugani, mafunzo na ujenzi wa miundombinu kama ya umwagiliaji, barabara vijijini, mawasiliano na masoko. Kwa mfano, uwekezaji katika miundombinu ya umwagiliaji kunahitaji mtaji mkubwa na upatikanaji wa fedha na rasilimali nyingine za ujenzi wa miundombinu hiyo katika wakati muafaka. Uzoefu unaonyesha kwamba mara nyingi fedha za ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji hazipatikani katika kipindi kile ambacho kinafaa kwa kujenga miundombinu hiyo, hususan wakati wa kiangazi. Kwa kuzingatia hali hiyo kuendeleza kilimo cha umwagiliaji kunahitaji mpango maalum wa namna ya kupata fedha kwa kiasi kinachotakiwa na kwa wakati muafaka.

7.4 Mabadiliko ya TabianchiKatika miaka 50 tangu nchi yetu ipate Uhuru, dunia imeshuhudia mabadiliko makubwa ya hali ya hewa ambayo yamekuwa ni chanzo cha ukame, mafuriko na kuongezeka kwa visumbufu vya mimea hivyo kupunguza uzalishaji katika kilimo. Mabadiliko ya hali ya hewa na kilimo cha kutegemea mvua inayonyesha kwa mtawanyiko usio mzuri ni moja ya changamoto ambazo inabidi kuwekewa mikakati ya muda mfupi na mrefu na kuitekeleza kwa mpangilio unaofaa. Aidha, udhibiti wa visumbufu vya mimea na mazao na milipuko ya magojwa na wadudu waharibifu unategemea kwa kiasi kikubwa utabiri wa mabadiliko ya tabianchi. Kwa upande wa utafi ti wa kilimo, kuongeza tija kwa mbegu bora (uzaaji) katika ikolojia isiyotabirika kwa nyakati zijazo na kulenga sifa mahsusi kwa soko la mazao mbalimbali hasa mahindi bado ni changamoto ambayo inabidi ipewe mikakati ya kipaumbele kwa vipindi vifupi na virefu katika utekelezaji wa programu za utafi ti wa mbegu bora.

7.5 Ushiriki Hafi fu wa Sekta Binafsi Katika KilimoMara baada ya Uhuru sekta binafsi haikupewa msisitizo kujihusisha katika shughuli za kiuchumi. Hali hiyo ilijitokeza wakati wa utekelezaji wa Azimio la Arusha kwa kutaifi sha njia kuu za uchumi ikiwa ni pamoja na mabenki, makampuni binafsi, majumba, viwanda, mashamba makubwa na kuziweka mikononi mwa umma hivyo kudhoofi sha ushiriki wa sekta binafsi kuendelea kuwekeza katika kilimo. Serikali katika kuendesha shughuli hizo ilikumbana na matatizo mengi ya utawala na usimamizi, hivyo kuhitaji tena ushiriki wa sekta binafsi. Hata hivyo, kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo na Azimio la Kilimo Kwanza, sekta binafsi imepata tena msukumo na kipaumbele kushiriki katika maeneo mbalimbali ya utafi ti, uzalishaji, usindikaji na utafutaji wa masoko. Pamoja na jitihada hizo bado hapajawa na mwitikio mkubwa wa sekta binafsi kujitokeza kuwekeza katika sekta ya kilimo. Kuhusu utafi ti, sekta binafsi inajishughulisha zaidi na mazao ya biashara ambayo utafi ti wake ulipewa kipaumbele tangu wakati wa mkoloni badala ya

kilimo miaka 50.indd Sec1:59kilimo miaka 50.indd Sec1:59 11/16/11 10:34:40 AM11/16/11 10:34:40 AM

Page 76: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

60

kuingia kwenye utafi ti wa mazao ambayo bado hayajafanyiwa utafi ti wa kutosha lakini yana uwezekano wa kukuza tija ya kilimo, kwa mfano mazao ya bustani na matunda. Hiyo imekuwa ni changamoto kubwa ambayo imepunguza tija na mchango wa sekta ya kilimo katika kukuza uchumi. Vile vile, sekta binafsi inasita kuwekeza kwenye miradi mikubwa ambayo gharama za mwanzo ni kubwa (mfano umwagiliaji) kwa kuogopa kupata hasara au kuchukua muda mrefu kupata faida.

7.6 Ushiriki Hafi fu wa Vijana katika Kilimo Tangu nchi yetu ipate Uhuru tunayo mambo mengi ya kujifunza, ambayo mengi yanaweza kuwa yamesababishwa na utekelezaji wa baadhi ya sera. Kwa mfano, utekelezaji wa sera ya ujamaa na kujitegemea kulitoa nafasi kwa vijana kupata elimu na mafunzo yaliyowatayarisha vijana pindi wakimaliza shule waweze kujitegemea. Aidha, Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria kwa vijana wasomi, na kwa kujitolea kwa vijana waliokuwa wanamaliza elimu ya msingi, kulikuwa kunaweka mazingira muafaka kwa vijana kushiriki katika kulijenga Taifa lao kupitia njia mbalimbali ikiwemo kilimo. Kufutwa kwa mafunzo ya elimu ya kujitegemea na pia kuondolewa kwa nafasi ya JKT kumezalisha vijana ambao baada ya kumaliza elimu ya msingi wamekuwa hawana shughuli rasmi ya kujipatia kipato na wale waliomaliza elimu ya sekondari na chuo wamekuwa wakipendelea zaidi kufanya kazi maeneo ya mijini. Madhara yake yamekuwa ni makubwa katika maeneo ya vijijini ambako ndiyo kitovu cha uzalishaji kwa upande wa sekta ya kilimo. Vijana wengi sasa wanakilimbilia mijini kwa lengo la kujihusisha na biashara ndogo ndogo (wamachinga) na shughuli za kilimo zimeshindwa kuwavutia vijana kama ni miongoni mwa shughuli muhimu za kiuchumi. Hali na mvuto katika kilimo ingeweza kubadilika kwa kuweka mikakati itakayoweka vivutio vya kuwafanya vijana kujihusisha zaidi na shughuli za uzalishaji mali hususan kilimo kwa kutoa mafunzo, mikopo na kuwamilikisha ardhi. Kwa hali ilivyo sasa, maeneo mengi ya shughuli za kilimo yanamilikiwa na wazee wengi wao wakiwa ni wanawake ambao si nguvu kazi pekee ya kutumainiwa ikiwa tunahitaji kuongeza kasi katika ukuaji wa sekta ya kilimo.

7.7 Kupungua kwa Nguvukazi Kutokana na VVU/UKIMWIMaambukizi ya VVU na UKIMWI yamekuwa kikwazo katika maendeleo ya sekta ya kilimo kutokana na kupoteza nguvukazi na rasilimali ambazo zingetumika katika uzalishaji. Kwa mfano, wagonjwa wa UKIMWI wanashindwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji na hivyo kuhatarisha uhakika wa chakula na jitihada za kupunguza umaskini. Vile vile rasilimali kubwa kutoka mfuko wa Serikali inatumika katika kuhudumia waathirika wa VVU/UKIMWI kama kununua madawa ya kurefusha maisha na matibabu ya magonjwa nyemelezi. Rasilimali hizo zingeweza kutumika katika maendeleo mengine ambayo yangechochea ukuaji wa kilimo na uchumi kwa ujumla.

7.8 Uwezo Mdogo wa Wakulima Kugharamia Zana za Kilimo Pamoja na jitihada za kuhamasisha matumizi ya zana bora za kilimo, bado wakulima walio wengi wanatumia zana duni za kilimo hususan jembe la mkono. Hii inachangiwa na wakulima kuwa na uwezo mdogo kifedha kutokana na uzalishaji mdogo na bei ndogo

kilimo miaka 50.indd Sec1:60kilimo miaka 50.indd Sec1:60 11/16/11 10:34:40 AM11/16/11 10:34:40 AM

Page 77: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

61

ya mazao wanayopata hasa yanapouzwa wakati wa mavuno. Aidha, wakulima wengi wanashindwa kununua zana bora za kilimo kutokana na bei yake kuwa kubwa. Kwa mfano kwa miaka 25 iliyopita bei ya trekta la Hp 70 na zana zake (plau, haro na tela) imeongezeka kutoka shilingi 460,000 (mwaka 1984) hadi shilingi 35,000,000 mwaka 2010. Ongezeko hilo la gharama ya trekta haiendani na kasi ya upandaji wa bei ya mazao shambani (farm gate price). Kukosekana kwa mikopo na masharti magumu ya mabenki yanafanya wakulima wengi kukosa mikopo na hivyo kushindwa kumudu gharama za ununuzi wa zana. Wakulima kuwa na elimu ndogo na utaalam mdogo wa matumizi ya zana bora kumeendelea kupunguza kasi ya matumizi ya zana bora.

7.9 Uwezo Mdogo wa Wakulima Kugharamia Pembejeo Baada ya kubaini wakulima walio wengi hawamudu gharama kubwa za pembejeo (mbegu, mbolea na viuatilifu), Serikali imelazimika kuweka mpango wa kutoa ruzuku ya pembejeo kwa baadhi ya mazao. Katika kutekeleza mpango huo changamoto mbalimbali zilijitokeza. Miongoni mwa changamoto hizo ni:- a. Idadi ndogo ya wakulima wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo kwa mazao ya

chakula. b. Wilaya kuwa na uwezo mdogo katika kuwashauri wakulima kuhusu matumizi ya

pembejeo mbalimbali kufuatana na mazingiza yao; kwa mfano, aina ya mbolea za kutumia, kiwango cha kutumia na aina ya mazao yanayofaa kulimwa, hivyo wakulima kutonufaika kikamilifu na ruzuku hiyo.

c. Baadhi ya mawakala kufanya udanganyifu na hivyo kuzorotesha azma ya Serikali ya kuwafi kishia wakulima pembejeo kwa bei nafuu.

d. Baadhi ya wakulima kushindwa kufi dia tofauti ya bei.

7.10 Ubovu wa MiundombinuKutokuwepo kwa miundombinu muhimu na ya kuvutia uwekezaji katika kilimo imekuwa kikwazo cha kukua kwa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara. Hii ni pamoja na kutokuwepo kwa umeme wa uhakika ambao umechangia kwa kiasi kikubwa kukatisha tamaa wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika uzalishaji na usindikaji wa mazao. Vilevile, hali mbaya ya barabara katika maeneo ya mashambani imekuwa sababu kuu ya mazao hayo kuharibika na kuchelewa kuyafi kisha sokoni. Pia, licha ya nchi yetu kuwa kubwa kieneo, inavyo viwanja vichache vya ndege kwa ajili ya kusafi rishia mazao yanayoharibika haraka kama yale ya bustani (maua, matunda, mboga). Hata vile viwanja vya ndege vichache vilivyopo havina vifaa maalum vya kuhifadhia mazao tayari kwa kusafi rishwa.

7.11 Kiwango Kidogo cha Usindikaji wa Bidhaa za KilimoGharama kubwa na ukosefu wa vifaa vya usindikaji imekuwa ni sababu kuu ya upotevu mkubwa wa mazao mara baada ya kuvunwa. Wakulima wengi bado hawajajengewa uwezo wa matumizi ya teknolojia rahisi za usindikaji na uhifadhi wa mazao. Pia, kama ilivyoainishwa hapo awali (7.5) bado kuna ushiriki hafi fu wa sekta binafsi katika eneo hili ambalo lina uwezo mkubwa pia wa kutoa ajira kwa vijana na hivyo kukabili changamoto nyingine (kama inavyosomeka katika kipengele cha 7.6 ).

kilimo miaka 50.indd Sec1:61kilimo miaka 50.indd Sec1:61 11/16/11 10:34:40 AM11/16/11 10:34:40 AM

Page 78: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

62

7.12 Msukumo wa Kuzalisha Mazao ya Nishati Mbadala Msukumo katika kilimo cha mazao ya nishati mbadala na utekelezaji wake bila ufafanuzi wa kutosha wa sera kuna uwezekano wa kuathiri uzalishaji wa mazao ya chakula. Hii ni kwa sababu kilimo hiki kinatumia eneo la ardhi pamoja na nguvu kazi ambayo ingeelekezwa katika kuzalisha mazao ya chakula. Vilevile, mpaka sasa Tanzania haijawa na viwanda vya kusindika pamoja na kuwa na mitambo inayotumia nishati hiyo. Ufafanuzi wa sera unatakiwa kusisitiza matumizi ya nishati mbadala inayotokana na masalia (by-products) ya mazao ya chakula na biashara badala ya mazao ya nishati pekee.

7.13 Matumizi Madogo ya Teknolojia Sahihi na za KisasaKuna wakulima ambao hawajapata fursa ya kujua, kupokea na kutumia teknolojia mpya zitokanazo na utafi ti kama mbegu bora za mazao mbali mbali, matumizi bora ya mbolea, teknolojia husishi na nyinginezo. Hii inaweza kusababishwa na yafuatayo: (a) Ufahamu mdogo hasa kwa wakulima wadogo unawafanya kutozingatia kanuni za

kilimo hivyo kutumia mbinu duni za uzalishaji na kusababisha taifa kuchelewa kufi kia malengo ya kupunguza umaskini hususan maeneo ya vijijini. Kwa kiwango fulani, hali hiyo inasababishwa na (i)Udhaifu wa mifumo ya kuunganisha utafi ti-ugani-mkulima ili kusambaza matokeo ya utafi ti kwa ufanisi zaidi. Wakati mwingine watafi ti wanalazimika kufanya kazi ya ugani wakati muda huo ungetumika katika kubuni teknolojia mpya kwa ufanisi zaidi (ii)Mfumo hafi fu wa uzalishaji na usambazaji wa mbegu bora za kilimo. Utafi ti umebaini kwamba kuna ukosefu wa mfumo mzuri wa uzalishaji na usambazaji wa mbegu bora za kilimo zinazotolewa kutokana na shughuli za utafi ti nchini. Madhara ya hali hiyo inasababisha utafi ti uonekane kama hauna matokeo tarajio (impact). Ukosefu wa mbegu bora ni moja ya sababu zinazoathiri kilimo hapa nchini na barani Afrika.

b) Ingawaje juhudi zimefanyika katika miaka ya karibuni kutumia teknolojia za kisasa kama bayoteknolojia katika utafi ti wa kilimo, ni wazi kwamba bado hazijatumika kikamilifu kuharakisha upatikanaji wa teknolojia za kilimo kama mbegu bora. Inachukua takribani miaka kumi kupata mbegu mpya kwa utafi ti wa kawaida na matumizi ya mbinu mbalimbali za bayoteknolojia itapunguza muda kwa kiwango kikubwa.

c) Pia, wananchi wengi (wakiwemo wataalam na wakulima) hawajajengewa uwezo juu ya matumizi ya teknologia za kisasa hasa mfumo wa kisasa wa habari na mawasiliano (TEHAMA) ili kuweza kuongeza ufanisi katika uzalishaji na upatikanaji wa taarifa za masoko.

7.14 Uvamizi wa Visumbufu vya Mimea na Mazao Kuongezeka kwa visumbufu vya mimea (magonjwa, magugu, wadudu, ndege na wanyama waharibifu) kutokana na mabadiliko ya tabianchi na sababu nyingine hupunguza uzalishaji wa mazao. Hiyo inatokana na wakulima wengi kutokuwa na uwezo wa kukabiliana na maradhi na wadudu waharibifu wa mazao. Mfano mzuri ni uvamizi wa magonjwa na wadudu hatari wa mazao kama baka bakteria, mnyauko fuzari, alternaria na minyoo fundo ya mizizi ya pamba. Visumbufu hivyo vimeongeza mahitaji ya rasilimali zaidi kwa ajili ya udhibiti.

kilimo miaka 50.indd Sec1:62kilimo miaka 50.indd Sec1:62 11/16/11 10:34:40 AM11/16/11 10:34:40 AM

Page 79: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

63

7.15 Upungufu wa Uratibu wa Sekta ya Kilimo Mfumo wa upatikanaji na usambazaji wa takwimu mbalimbali zinazohusiana na sekta ya kilimo kama hali ya chakula upo katika mamlaka tofauti. Mamlaka hizo ni pamoja na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Halmashauri za wilaya, sekretariati za mikoa, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, na Wizara ya Afya pamoja na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA). Hali hiyo inaendana na kuwepo na upungufu wa uratibu baina ya sekta hizi na kukosa mfumo imara wa mawasiliano na hivyo kujitangaza ipasavyo kwa lengo la kuwaelimisha wadau mbalimbali kuhusu hali ya mazao na chakula nchini. Hiyo ni pamoja na upatikanaji wa taarifa za masoko kwa wale wanaosafi risha mimea na mazao ndani na nje ya nchi. 7.16 Upungufu wa Mitaji kwa Vyama vya UshirikaKwa muda mrefu vyama vya ushirika vimeathiriwa na ukosefu wa mitaji ya ndani ya kutosheleza uendeshaji wenye tija wa shughuli zake. Athari kubwa zimeonekana katika biashara ndogo zinazofanywa na vyama hivyo hususan kwenye eneo la mazao pamoja na uwezo mdogo wa SACCOS kutoa mikopo ya kutosha kwa wanachama wake. Hali hiyo ilichangiwa na mabadiliko katika sera za uchumi na fedha ambapo benki za biashara zinazotegemewa na vyama kutoa mikopo zilipobinafsishwa zimekuwa zikitoa umuhimu wa chini kwa ushirika.7.17 Elimu Duni ya UshirikaWanachama wengi katika ngazi mbalimbali za vyama vya ushirika hawaifahamu vema dhana ya ushirika. Hali hii inachangia kuwafanya washindwe kuwajibika na pia kujua haki zao ndani ya ushirika wao.7.18 Usimamizi Hafi fu wa Sera ya Soko HuruKasoro katika usimamizi wa Sera ya soko huru na uwezo mdogo wa ushindani kwa vyama vya ushirika inatokana na mfumo wa soko huru ulipoanza ulivikuta vyama vya ushirika vikiwa havina maandalizi. Pia, upungufu katika usimamizi wa taratibu za soko huru umetoa mianya kwa wafanyabiashara binafsi kujinufaisha kwa njia za udanganyifu.7.19 Idadi Ndogo ya Maafi sa UshirikaMaendeleo ya Ushirika yameathiriwa kwa kiasi kikubwa na kuwepo kwa idadi ndogo ya Maafi sa Ushirika. Idadi hiyo ndogo imetokana na kupungua kwa vyuo vilivyokuwa vinatoa elimu kwa watumishi wanaoajiriwa na Idara ya Maendeleo ya Ushirika. Chuo kilichokuwa kinategemewa kimepanuka na kuwa Chuo Kikuu na hivyo kutoa wahitimu waliobobea katika fani nyingine.7.20 Kukosekana kwa Mikopo ya Kilimo yenye Masharti Nafuu Kukosekana kwa mikopo yenye masharti nafuu kutoka taasisi za fedha nchini yanasababisha wakulima wengi kukosa mitaji, hivyo kushindwa kumudu gharama za ununuzi wa zana na pembejeo za kilimo. Pia, wakulima wanashindwa kuendeleza kilimo kwa kutumia mikopo ya kugharamia skimu za umwagiliaji. Hilo linaathiri azma ya Taifa ya kuleta mapinduzi ya kijani.

kilimo miaka 50.indd Sec1:63kilimo miaka 50.indd Sec1:63 11/16/11 10:34:40 AM11/16/11 10:34:40 AM

Page 80: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

64

Ujenzi wa banio katika skimu ya umwagiliaji ya Pawaga katika Wilaya ya Iringa vijijini, Mkoa wa Iringa

kilimo miaka 50.indd Sec1:64kilimo miaka 50.indd Sec1:64 11/16/11 10:34:40 AM11/16/11 10:34:40 AM

Page 81: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

65

8. MWELEKEO WA KILIMO NA USHIRIKA (2011-2061)8.1 UtanguliziKatika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania bara, Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika imejipanga kuendelea kutekeleza majukumu yake kupitia mipango na mikakati iliyopo na inayotarajiwa kubuniwa ili kilimo pamoja na ushirika viweze kutoa mchango unaotarajiwa katika harakati za kufi kia malengo ya Maendeleo ya Milenia, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini (MKUKUTA II). Katika kutufi kisha huko, Wizara inaendelea kutekeleza Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP), na Programu Kabambe ya Mageuzi na Modenaizesheni ya Ushirika (CRMP). ASDP ambayo ilianza kutekelezwa tangu mwaka 2006 ni programu ya miaka saba na itatekelezwa hadi mwaka 2012/2013. Katika kuongeza uwezo na rasilimali zinazohitajika katika kilimo Julai 8, 2010, Tanzania ilisaini Programu ya Kuendeleza Kilimo Afrika (CAADP) ambayo malengo yake makuu ni kuondoa umaskini, kuongeza wigo wa eneo la kilimo cha umwagiliaji, masoko na miundombinu. Aidha, mwaka 2009 Serikali ilizindua Azimio la Kilimo Kwanza ambalo ni azma maalum ya kitaifa ya kuongeza kasi ya kuleta mapinduzi ya kijani kwa kushirikisha kikamilifu sekta binafsi kama ilivyoainishwa katika Sera Shirikishi ya Pamoja yaani (Public- Private Partnership Policy-PPP-Policy). Juhudi nyingine ambazo zimeanza kutekelezwa ni zile zinazohusu utekelezaji wa mradi wa Ukanda wa Kilimo wa Kusini mwa Tanzania (Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania-SAGCOT) ambao utasaidia kupunguza umaskini miongoni mwa wananchi hususan wanaoishi vijijini kwa kuwaongezea mavuno ya mazao yao. Utekelezaji wa SAGCOT ni sehemu ya Kilimo Kwanza wenye lengo la kukuza ajira miongoni mwa Watanzania. SAGCOT itawawezesha maelfu ya wakulima na wafanyabiashara wadogo kufaidika na shughuli za kilimo baada ya kuuza na kununua mazao yatakayotokana na mradi huo. Kupitia SAGCOT zaidi ya ajira mpya 400,000 zinatarajiwa kupatikana na hivyo kuwatoa katika lindi la umaskini zaidi ya wananchi milioni mbili wanaoishi katika mikoa ya kusini. SAGCOT ni mpango mkakati wa kuleta mapinduzi ya kilimo unaotekelezwa kwa pamoja kati ya Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo yakiwemo mashirika ya Kimataifa. SAGCOT inatarajiwa kutekelezwa katika mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Iringa, Rukwa na Morogoro. Kwa mara ya kwanza SAGCOT ilizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mwezi Mei, 2010 na kutangaza kuwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini inaweza kuwa ghala la Taifa na kuzalisha ziada inayoweza kuuzwa nje na kuwapatia wananchi fedha za kigeni. Aidha, Serikali kuanzia mwaka 2011/12 itaanza kutekeleza Mpango wa Kwanza wa Taifa wa Maendelo wa Miaka 5 katika kipindi cha 2011/12 hadi 2015/16 ili kutekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025. Mpango wa pili wa miaka 10 ambao utatekelezwa kuanzia 2016/17 hadi 2025/26 unaodhamiria kukifanya kilimo chetu kuwa cha kisasa, kibiashara chenye tija, faida na ushindani katika kanda ya Afrika Mashariki na Kati na kitakachochangia kuongeza kipato na kupunguza umaskini kwa Watanzania ifi kapo mwaka 2025.

kilimo miaka 50.indd Sec1:65kilimo miaka 50.indd Sec1:65 11/16/11 10:34:41 AM11/16/11 10:34:41 AM

Page 82: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

66

8.2 Mwelekeo wa Miaka 50 IjayoMwelekeo wa kilimo katika miaka 50 ijayo ni kuhakikisha kuwa kinaendelea kuwa cha kisasa chenye tija, faida, ushindani kibiashara kikanda na kimataifa, kisichotegemea mvua na kinachoongeza kipato na kupunguza umaskini kwa Watanzania pamoja na kuhakikisha usalama wa chakula nchini. Wizara itatakiwa kutekeleza maeneo ya kimkakati ili kufi kia azma hiyo. Hivyo, katika miaka 50 mingine ijayo ya Uhuru (2011-2061) Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika itajikita katika maeneo yafuatayo ya kimkakati.

8.2.1 Kuongeza Uzalishaji na Tija katika Sekta ya KilimoChini ya mkakati huu, mazao ya kipaumbele yatakayopewa msukumo ni pamoja na yale ya chakula, biashara na bustani. Kilimo cha umwagiliaji kitapewa kipaumbele ili Taifa liendelee kujitosheleza kwa Chakula na ziada ya kuuza katika masoko ya ndani na nje ya nchi. Katika mkakati huo, uzalishaji wa mpunga unategemea kuongezeka hatua kwa hatua, kati ya asilimia 75 hadi 100 kwa kuanza na skimu 28 za umwagiliaji katika awamu ya kwanza. Wakulima katika skimu hizo watawezeshwa kupata mbolea, mbegu bora, huduma za ugani, zana bora za kilimo na elimu kuhusu matumizi bora ya ardhi na maji. Aidha, uzalishaji wa mpunga pia utategemea kuongezeka kutokana na uwekezaji utakaofanywa na Mamlaka ya Kuendeleza Bonde la Mto Rufi ji (RUBADA) kwa kushirikiana na sekta binafsi ya AGRCA na kupitia utekelezaji katika Kituo Mahiri cha Utafi ti wa Mpunga (Regional Rice Centre of Excellence) kilichopo KATRINI- Ifakara. Kupitia utafi ti katika kituo hicho, aina ya mpunga wenye tija unaolimwa kwa kutumia mvua (Upland rice) utapatikana. Tija na uzalishaji wa mazao ya mahindi, mbegu za mafuta, mazao ya bustani na mazao asilia ya biashara unategemea kuongezeka kutokana na ongezeko la matumizi ya pembejeo muhimu kama mbolea, mbegu bora na miche bora pamoja na kuimarisha huduma za ugani. Upatikanaji wa mbegu bora kupitia Wakala wa Mbegu za Kilimo (Agricultural Seed Agency – ASA), utaongezeka kwa kupanua uwezo wa mashamba ya Serikali wa kuzalisha zaidi kutokana na ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji pamoja na kuendeleza mkataba wa kuzalisha mbegu kati ya ASA, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Magereza. Aidha, TOSCI itaendelea kujengewa uwezo ili kusimamia udhibiti wa mbegu bora. Mambo mengine yatakayozingatiwa katika utekelezaji wa mkakati huu ni pamoja na:-a. Kuimarisha utafi ti wa kilimo, mafunzo na huduma za ugani kwa kuboresha

miundombinu ya vituo vya utafi ti na kuongeza mafunzo na ajira za wataalam wa kilimo

b. Kuboresha vituo vya utafi ti vinavyotafi ti bayoteknolojia kwa lengo la kuja kuanzisha kituo cha bayoteknolojia ambacho kitatumika kuzalisha mbegu na miche kibiashara

c. Kuhamasisha upanuaji wa mashamba mapya na uzalishaji wa miche na mbegu bora kwa kushirikiana na Halmashauri za wilaya na bodi za mazao hususan kwa mazao ya chai, pamba, pareto, korosho na kahawa

kilimo miaka 50.indd Sec1:66kilimo miaka 50.indd Sec1:66 11/16/11 10:34:41 AM11/16/11 10:34:41 AM

Page 83: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

67

d. Kuimarisha udhibiti wa visumbufu vya mimea ili kupunguza upotevu wa mazao ambao ungesababishwa na visumbufu hivyo

e. Kupanua eneo linalomwagiliwa kwa kuendelea kujenga skimu na mabwawa kwa kutumia fedha za DADPs, Mfuko wa Umwagiliaji wa Wilaya na Taifa (District Irrigation Development na National Development Funds).

f. Wakulima wa skimu za umwagiliaji watawezeshwa kuongeza thamani ya zao la mpunga kwa kutumia mashine za kukoboa, kuchambua mawe na kupanga mchele kulingana na madaraja ya ubora.

8.2.2 Kuimarishwa Upatikanaji wa Masoko ya Bidhaa za Kilimo Kupitia mkakati huo upatikanaji wa masoko ya bidhaa za kilimo utaimarishwa kwa kuboresha huduma za kukagua viwango vya viuatilifu kwenye mazao na bidhaa za kilimo kwa kujenga uwezo wa TPRI ili iweze kutoa vyeti vya usafi wa mazao na bidhaa za kilimo vinavyotambulika kitaifa (Accredited Laboratories). Ujenzi wa miundombinu ya masoko ya mipakani (Strategic Boarder Markets) utafanyika kwa ajili ya maghala ya kuhifadhia mazao ya wakulima. Maghala hayo yatatumika kwa ajili ya stakabadhi ghalani na baadaye kuanzisha Mfumo wa Soko la Bidhaa (Commodity Exchange). Mambo mengine yatakayotekelezwa ni kutoa elimu ya ujasiriamali kuhusu namna ya kuendesha biashara ya kilimo cha mazao. Mafunzo hayo yatatolewa kwa wakulima kwa kutumia njia mbalimbali vikiwemo Vituo vya Rasilimali za Kilimo vya Kata (Ward Agricultural Resources Centre). Aidha, Vyama vya Ushirika vitaendelea kuhamasishwa ili kuunganisha nguvu za kukabiliana na mashindano katika biashara ya kuuza mazao ya kilimo nje ya nchi. Jitihada nyingine zitahusu uimarishaji wa usimamizi wa ubora wa mazao kupitia bodi za mazao na vituo vya mipakani vya ukaguzi wa mazao na mimea na kujenga maabara ya kupima kiwango cha sumu kilichomo kwenye pareto ya wakulima kupitia Bodi ya Pareto. Utaratibu huo utaweza kumlinda mkulima kwa kumpatia bei nzuri kulingana na kiwango halisi cha sumu iliyo kwenye pareto yake. Aidha, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) utaongezewa uwezo wa kununua na kuhifadhi mazao na pia kuiwezesha Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kununua mazao hayo. Katika mpango huo vikundi vya wakulima vitaanzishwa na kuwafundisha namna ya kujadiliana juu ya bei ya mazao na bidhaa zao na namna ya kuwawezesha kupata taarifa za bei katika masoko mbalimbali kwa kutumia mtandao wa simu. Kupitia msaada wa PHRD wakulima katika skimu 20 za umwagiliaji watawezeshwa kujenga maghala, kununua mashine za kukoboa, kuchambua, kupanga mchele katika madaraja na kufungasha. Aidha, maghala yatakayojengwa yatatumika kuanzisha mfumo wa stakabadhi za maghala. Vilevile wakulima watafundishwa elimu ya biashara, utunzaji wa kumbukumbu na manejimenti ya fedha. Sambamba na hayo Wizara itaendelea kushirikiana na Shirika la Chakula Duniani (WFP) katika kutekeleza Mpango wa Purchase for Progress (P4P).

kilimo miaka 50.indd Sec1:67kilimo miaka 50.indd Sec1:67 11/16/11 10:34:41 AM11/16/11 10:34:41 AM

Page 84: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

68

8.2.3 Kuongeza Thamani ya Mazao ya Kilimo na Mfumo wa MasokoMkakati huu unalenga katika kuwezesha wakulima kuongeza thamani ya mazao yao kwa ajili ya kupata bei nzuri na soko la uhakika. Katika kutekeleza hilo, Wizara itawawezesha wajasiliamali wa mazao ya kilimo kama vile wasindikaji wa mazao, kuboresha na kusambaza teknolojia za kuhifadhi mazao ya kilimo. Mambo mengine yanayotarajiwa kutekelezwa katika mkakati huo ni kuhimiza na kushawishi matumizi mbalimbali ya nafaka kama vile kuchanganya unga wa muhogo na ngano, kusaidia usagishaji na ufungashaji wa nafaka na mazao mengine ya kilimo kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula. Aidha, Wizara itatoa mikopo ya vifaa vya usindikaji kupitia Mfuko wa Pembejeo na kufanya tafi ti za teknolojia rahisi za usindikaji.

8.2.4 Kuendelea Kuboresha Uwezo wa Wizara kutoa HudumaWizara itaendelea kujipanga kuboresha huduma zake kwa wateja wake kwa kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara katika ngazi zote kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali. Aidha, Wizara itafanya ukarabati na ujenzi ili kuongeza vituo vya utafi ti na vyuo vya mafunzo ya kilimo. Wizara itaendelea kuwezesha upatikanaji wa vitendea kazi kwa watumishi wake. Aidha, Wizara itawezesha mafunzo ya Wahandisi wa Umwagiliaji na Mafundi Sanifu (Irrigation Technicians) wa umwagiliaji katika vyuo vinavyotoa mafunzo husika hapa nchini. Lengo la jitihada hizo zote ni kuongeza upatikanaji wa watumishi wa fani hiyo ili waweze kusimamia ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji na kusimamia matumizi mazuri ya maji ambayo ni pembejeo muhimu katika Kilimo. Aidha, utaratibu wa muda wa kupata wataalam wa umwagiliaji kupitia mpango wa South South Corperation utaendelea kutekelezwa kadri itakavyoonekana inafaa.

8.2.5 Kuimarisha Sera, Mikakati na Usimamizi katika Sekta ya KilimoKuanzia mwaka 2011/2012, Wizara imepanga kuanza kutekeleza Sera mpya ya Taifa ya Kilimo baada ya kupitishwa. Baada ya sera hiyo kuanza kutumika mambo kadhaa yatafanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na kupitia upya sheria za kilimo ili ziendane na matamko ya Sera ya Taifa ya Kilimo na azma ya Kilimo Kwanza. Jukumu lingine litahusu kufanya uchambuzi wa Sera mbalimbali (Policy analysis) na kutumia matokeo ya chambuzi hizo kusaidia kufanya maamuzi yenye manufaa kwa wakulima na Taifa. Aidha, Wizara itaimarisha utekelezaji wa mikataba na itifaki za Kikanda na Kimataifa zilizoridhiwa.

8.2.6 Kuboresha Uratibu katika Sekta ya KilimoKutokana na umuhimu wa kilimo katika maendeleo ya Taifa, miradi na programu mbalimbali zimeanza kuandaliwa kama vile SAGCOT, Feed the Future programme, na Bread Basket Initiative. Miradi na program hizo zinahitaji uboreshaji wa uratibu uliopo unaotumika kutekeleza ASDP. Hivyo Wizara imekusudia kuimarisha na kuongeza timu ya uratibu, ikiwa ni pamoja na kuoanisha nguvu na rasilimali zilizopo, kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ili ijumuishe mipango na programu hizo, na kuboresha mfumo wa ukusanyaji takwimu na kuanzisha benki ya takwimu (data bank) itakayokuwa na taarifa za miradi na programu hizo.

kilimo miaka 50.indd Sec1:68kilimo miaka 50.indd Sec1:68 11/16/11 10:34:41 AM11/16/11 10:34:41 AM

Page 85: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

69

8.2.7 Kuzingatia Masuala Mtambuka katika KilimoWizara kwa kutambua umuhimu wa masuala mtambuka katika kilimo, itaendelea kuzingatia sheria ya mazingira na masuala ya jinsia katika utekelezaji wa shughuli za kilimo. Aidha, Wizara imejipanga kuwawezesha vijana kujihusisha na shughuli za kilimo kwa kuwawezesha kuzalisha kibiashara na kwa faida.8.2.8 Kuimarisha Mawasiliano ya Habari za KilimoWizara inatambua kwamba mawasiliano ya habari ni muhimu katika kuwafahamisha wadau mbalimbali kuhusu sera, mikakati, mafanikio na changamoto za kilimo. Katika kutekeleza hayo, Wizara imepanga kuimarisha mawasiliano ya ndani na nje ya Wizara ili kufanikisha kuongeza uelewa na ushiriki wa wadau katika kutekeleza sera na mikakati hiyo. Aidha, mkakati huo utaongeza matumizi ya maarifa na teknolojia mbalimbali zilizothibitika kuwa na manufaa kwa wakulima. Katika kufanikisha hayo Wizara itaendelea kutekeleza mkakati wa mawasiliano, kwa kujenga uwezo wa ofi si za mawasiliano za kanda (ZIELU) pamoja na Kitengo cha Elimu kwa Mkulima cha Ukulima wa Kisasa. 8.2.9 Kuboresha Huduma na Kupunguza Maambukizi ya VVU/UKIMWI.Wizara imepanga kuendelea kutoa huduma kwa wanaoishi na virusi vya UKIMWI na elimu ya kuzuia maambukizi mapya. Mkakati huo unalenga kulinda nguvukazi ya wataalam wa kilimo ili waendelee kutoa huduma kupitia taaluma zao hatimaye Wizara iweze kufi kia malengo yake pamoja na yale ya kitaifa. 8.2.10 Kuimarisha na Kuwezesha Asasi za Wananchi katika KilimoKatika kuimarisha na kuwezesha Asasi za Wananchi katika kilimo, Wizara kupitia Ushirika, imepanga kuendelea na jitihada zilizoanza za kuimarisha uongozi na usimamizi katika vyama vya ushirika na kuwezesha kuwepo kwa weledi na utaalam katika vyama vya ushirika kuhusiana na masoko na mnyororo wote wa kuongeza thamani ya mazao (value addition chain) ya wananchi. Aidha, masuala mengine yatakayozingatiwa ni pamoja na kuweka mazingira yatakayowezesha kukua kwa ushirikiano baina ya Vyama vya Ushirika hususan katika nyanja za uzalishaji, masoko, mitaji, teknolojia na habari, na kuviwezesha vyama vya ushirika kuimarisha biashara za mazao. Jitihada zingine ni kuimarisha SACCOS na mabenki ya ushirika ili yaweze kufi kisha huduma zake kwa watu wenye kipato duni, vijana na walemavu sambamba na kuhamasisha vijana wanaoshiriki katika kilimo kuunda vyama vya ushirika kwenye maeneo ya uzalishaji, ili kujipatia masoko na mitaji pamoja na kuwezesha bodi za vyama vya ushirika kupata mafunzo ya kuwawezesha kutekeleza kikamilifu majukumu wanayokabidhiwa.8.2.11 Kuimarisha Mfumo wa Ukusanyaji, Uchambuzi, Uhifadhi na Usambazaji

wa Takwimu na Taarifa za Kilimo na Vyama vya UshirikaKwa kutambua umuhimu wa kuwa na takwimu sahihi katika kuendeleza kilimo, Wizara itaendelea na utekelezaji wa jukumu la kukusanya takwimu za ushirika, kuzichambua na kuzisambaza kwa wanaushirika. Aidha, Wizara itaendesha mafunzo kwa maafi sa ushirika kuhusu ukusanyaji wa takwimu na umuhimu wa takwimu pamoja na kuanzisha mfumo wa kuhifadhi takwimu za ushirika.

kilimo miaka 50.indd Sec1:69kilimo miaka 50.indd Sec1:69 11/16/11 10:34:41 AM11/16/11 10:34:41 AM

Page 86: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

70

8.3 HitimishoTaarifa hii ya Miaka 50 imejikita katika kuangalia maendeleo ya kilimo na ushirika tangu kupatikana kwa Uhuru wa Tanzania Bara. Taarifa inaonyesha kwa kifupi jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kilimo kinatoa mchango unaokusudiwa katika kuzalisha chakula cha kutosha, na kinatoa mchango kwenye uchumi kwa lengo la kuwaondolea umaskini wananchi wake. Taarifa pia imezingatia michango iliyotolewa na taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara. Vilevile, taarifa imezingatia masuala machache muhimu kati ya mengi yaliyoko kwenye taarifa zilizowasilishwa na taasisi mbalimbali. Ni mategemeo kuwa wakati tunaadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, kila taasisi itachapisha taarifa zinazohusu shughuli zinazotekelezwa chini ya usimamizi wake na kuainisha mafanikio, changamoto na mwelekeo wa miaka 50 ijayo kwa mapana yake. Taarifa hizo ni muhimu kwa ajili ya manufaa ya sasa na baadaye tunapoendelea kutekeleza mikakati ya kutuwezesha kufi kia malengo ambayo sekta ya kilimo inategemewa na Taifa. Kwa mantiki hiyo, shukrani za pekee ziwaendee Wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi zilizochangia taarifa na kuwezesha kukamilika kwa chapisho hili. Ni mategemeo ya Wizara kuwa taarifa hii itasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuwaelimisha na kuwashirikisha wananchi kwenye masuala mbalimbali na kupata uzoefu wa namna sekta ya kilimo inavyopaswa kutoa fursa ya kuwaendeleza Watanzania katika Miaka mingine 50 ijayo ya Uhuru wa nchi yetu. KILIMO KWANZA - “Tumethubutu, Tumeweza, Tunazidi Kusonga Mbele”.

kilimo miaka 50.indd Sec1:70kilimo miaka 50.indd Sec1:70 11/16/11 10:34:41 AM11/16/11 10:34:41 AM

Page 87: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

71

kilimo miaka 50.indd Sec1:71kilimo miaka 50.indd Sec1:71 11/16/11 10:34:41 AM11/16/11 10:34:41 AM

Page 88: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

72

Kiambatisho Na. 2: Kanda na Vituo vya Utafi ti wa Kilimo

Kanda Mikoa Husika Vituo vya Utafi ti na Mwaka Vilipoanzishwa

Tafi ti Zinazofanyika

Mashariki Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Tanga

ARI-Ilonga, Kilosa (Makao Makuu ya Kanda)

1943 Pamba, mahindi, kunde, mbaazi, choroko, soya, mtama, uwele, alizeti, udongo, mifumo ya kilimo & uchumi-jamii

KATRIN, Ifakara 1963 Mpunga, viungo

Chollima-Dakawa, Morogoro

1982 Mpunga, mahindi, mboga-mboga (bamia, nyanya, matango, mchicha na nyanya chungu)

ARI-Mikocheni, DSM

1996 Minazi, matumizi ya bayoteknolojia katika kilimo, mifumo ya kilimo & uchumi-jamii

SRI-Kibaha, Pwani 1970 Miwa, muhogo na viazi vitamu

ARI-Mlingano, Tanga

1934 Udongo & hifadhi maji, matumizi ya ardhi, mkonge, viungo & vikolezo

Magharibi Kigoma, Tabora ARI-Tumbi, TaboraVituo vidogo: Seatondale-Iringa, Mtanila

1930 Mahindi, mpunga, mtama, maharage, mihogo, michikichi, karanga, alizeti, tumbaku, miti ya malisho, uchumi-jamii, ngombe wa maziwa

Kaskazini Arusha, Kilimanjaro, Manyara

ARI-Selian, Arusha (Makao Makuu ya Kanda)

1980 Ngano, maharage, shayiri, mahindi, udongo& hifadhi maji, mifumo ya kilimo & uchumi-jamii, kilimo-misitu, uhandisi-kilimo/zana.

HORTI-Tengeru, Arusha

1952 Mazao ya bustani (horticultural crops)

Nyanda za Juu Kusini

Iringa, Mbeya, Rukwa, Ruvuma

ARI-Uyole, Mbeya (Makao Makuu ya Kanda)

1970 Mahindi, maharage, mboga mboga, matunda, pareto, viazi mviringo, soya, udongo& hifadhi maji, mifumo ya kilimo & uchumi-jamii, kilimo-misitu, uhandisi-kilimo/zana.

Kifyulilo-Mufi ndi 1986

Kusini Lindi, Mtwara ARI-Naliendele, Mtwara (Makao Makuu ya Kanda)Kituo kidogo: Mtopwa

1972 Korosho, karanga, ufuta, alizeti, soya, mazao aina ya mizizi (muhogo na viazi vitamu), mifumo ya kilimo & uchumi-jamii, udongo, kilimo-mseto

Kati Dodoma, Singida VRC-Makutupora, Dodoma (Makao Makuu ya Kanda)

1979 Zabibu

Hombolo, Dodoma 1972 Mtama, uwele

Ziwa Kagera, Mara, Mwanza, Shinyanga

ARI-Ukiriguru, Mwanza (Makao Makuu ya Kanda)

1932 Pamba, mpunga, viazi vitamu, mihogo, mahindi, dengu, mbaazi

ARI- Maruku, Bukoba

1947 Migomba, mahindi, muhogo, viazi vitamu/ mviringo, maharage, vanilla, ulezi, mpunga, matunda, viungo, soya, magimbi, viazi vikuu, udongo& hifadhi maji, mifumo ya kilimo & uchumi-jamii, kilimo-misitu.

kilimo miaka 50.indd Sec1:72kilimo miaka 50.indd Sec1:72 11/16/11 10:34:41 AM11/16/11 10:34:41 AM

Page 89: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

73

Kiambatisho Na. 3: Mgawanyo wa Maeneo Yanayoweza Kumwagiliwa Kimkoa

NA. MKOA Eneo Linalofaa Kuendelezwa Kwa Umwagiliaji

(Irrigation Development Potential ) (Ha)

Uwezekanowa

Juu (High)

Uwezekano Wa

Kati (Medium )

Uwezekano Wa

Chini (Low)

Jumla

1 Arusha/Manyara* 455,300 758,300 2,626,400 3,840,000

2 Dar Es Salaam - - 68,900 68,900

3 Dodoma 1,200 68,900 2,015,400 2,085,500

4 Iringa 163,600 1,091,500 1,125,000 2,380,100

5 Kagera 96,300 59,000 1,063,200 1,218,500

6 Kigoma 160,300 107,400 271,100 538,800

7 Kilimanjaro 238,500 109,600 231,600 579,700

8 Lindi - 19,600 1,704900 1,724,500

9 Mara 210,100 576,500 123,400 910,000

10 Mbeya 285,100 499,700 884,800 1,669,600

11 Morogoro 376,800 602,400 574,300 1,553,500

12 Mtwara - - 1,332,700 1,332,700

13 Mwanza 98,500 165,000 1,013,000 1,276,500

14 Pwani 83,000 171,800 961,700 1,216,500

15 Rukwa 27,000 79,800 888,900 995,700

16 Ruvuma 23,200 283,700 1,617,800 1,924,700

17 Shinyanga 80,400 215,500 1,821,200 2,117,100

18 Singida - - 1,348,900 1,348,900

19 Tabora - - 1,517,000 1,517,000

20 Tanga - - 1,151,300 1,151,300

JUMLA 2,299,300 4,808,900 22,341,700 29,449,900

NB: * Mpango Kabambe wa Taifa wa Umwagiliaji (NIMP) ulikamilishwa Mwaka 2002 kabla ya kugawanywa kwa Mkoa wa Arusha kuwa mikoa miwili ya Arusha na Manyara. Inatarajiwa Kutenganisha maeneo haya wakati wa kupitia upya (updating) Takwimu za NIMP.

Chanzo: Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika

kilimo miaka 50.indd Sec1:73kilimo miaka 50.indd Sec1:73 11/16/11 10:34:42 AM11/16/11 10:34:42 AM

Page 90: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

74

Kiambatisho Na. 4: Idadi ya trekta Zilizoingizwa Nchini Hadi 2011

S/no. Mwaka Idadi

1 1982 210

2 1983 263

3 1984 495

4 1985 1143

5 1986 407

6 1987 289

7 1988 536

8 1989 338

9 1990 241

10 1991 369

11 1992 273

12 1993 180

13 1994 73

14 1995 58

15 1996 49

16 1997 309

17 1998 665

18 1999 440

19 2000 431

20 2001 375

21 2002 274

22 2003 246

23 2004 272

24 2005 356

25 2006 445

26 2007 464

27 2008 472

28 2009 627

29 2010 1,860

Chanzo: Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika

kilimo miaka 50.indd Sec1:74kilimo miaka 50.indd Sec1:74 11/16/11 10:34:42 AM11/16/11 10:34:42 AM

Page 91: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

75

Kiambatisho Na. 5: Hali ya Ubanguaji Korosho Nchini

Na. Jina la Kiwanda

Uwezo wa kubangua (tons) (installed capacity)

Malengo ya kubangua msimu wa 2011/2012 (Tani)**

Mtaji unaotakiwa kununua korosho ghafi (Tsh)*

1. Agrofocus 10,000 8,000 16,000,000,000

2. Bucco 20,000 0 0

3. Lindi Farmers Co Limited 10,000 2,000 4,000,000,000

4. Safa Petrolium 10,000 0 0

5. Olam (T) Ltd 30,000 25,000 50,000,000,000

6. Mohamed Enterprises 10,000 6,000 12,000,000,000

7. Premier Cashew 8,000 0 0

8. Mtwara Cashew Company 10,000 0 0

9. Micronix 20,000 0 0

10. Export Trading Co Limited 10,000 8,000 16,000,000,000

11. UVUKI 4,000 2,000 4,000,000,000

12. Demros 300 600 1,200,000,000

13. River Valley 2000 1,500 3,000,000,000

14. Southern Jumbo Nuts 1000 1,100 2,200,000,000

15. Perfect Kernels Processing Factory (Masasi)

2,000 1,000 2,000,000,000

16. Masasi High Quality Farmers Products

1000 600 1,200,000,000

17. Kitama Cooperative Society 500 300 600,000,000

JUMLA 149,800 56,100 112,200,000,000

* Gharama za fedha za mtaji wa kununulia korosho ghafi zimekokotolewa kwa kutumia bei ya shilingi 2,000 kwa kilo

** Kiasi kitaongezeka kadri viwanda vipya na vile vinavyoendelea kukarabatiwa vitakapoanza kufanya kazi

Chanzo: Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika

kilimo miaka 50.indd Sec1:75kilimo miaka 50.indd Sec1:75 11/16/11 10:34:42 AM11/16/11 10:34:42 AM

Page 92: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

76

Kiambatisho Na. 6: Uzalishaji Mazao ya Chakula Kati ya 1990/91 na 2009/2010 (Tani)

Mwaka Mahindi Mtama Uwele Mchele Ngano Mikunde Muhogo Ndizi

1990/91 2,270,500 745,400 250,150 294,000 75,700 369,235 1,168,800 633,900

1991/92 2,290,180 628,333 277,791 398,541 65,948 297,382 1,916,136 793,701

1992/93 2,282,150 719,140 210,250 640,910 59,430 405,840 1,708,220 810,180

1993/94 2,214,559 496,936 218,200 614,300 59,440 273,555 1,802,270 834,342

1994/95 2,566,600 838,800 411,000 722,100 75,300 378,400 1,492,200 651,100

1995/96 2,662,700 882,420 366,960 734,210 83,900 474,940 1,498,400 641,000

1996/97 1,831,236 501,281 347,000 549,800 78,000 374,100 1,425,500 603,100

1997/98 2,600,484 583,178 235,832 1,039,801 111,472 461,970 1,824,524 835,768

1998/99 2,451,766 561,031 194,372 506,192 82,373 528,195 1,795,375 751,601

1999/00 2,009,320 596,823 218,997 508,355 32,791 673,711 1,238,893 702,543

2000/01 2,578,562 742,243 167,121 564,000 89,323 732,926 1,445,457 779,414

2001/02 2,704,849 830,367 206,490 640,189 76,527 682,951 1,721,670 752,072

2002/03 2,321,951 487,891 138,985 712,555 73,716 850,373 1,320,698 706,156

2003/04 3,232,400 820,100 215,101 586,274 74,269 905,682 1,538,475 738,633

2004/05 3,218,540 714,339 220,940 759,386 101,912 885,804 1,846,387 990,574

2005/06 3,423,025 711,631 227,905 805,067 109,531 1,049,919 2,052,767 1,169,151

2006/07 3,302,058 971,198 193,975 872,193 82,784 1,155,985 1,732,978 1,027,535

2007/08 3,555,833 861,386 202,810 875,119 92,399 1,125,503 1,797,455 982,366

2008/09 3,326,200 709,305 220,377 867,619 95,124 1,116,312 1,972,148 1,073,149

2009/10 4,475,416 788,800 372,297 1,699,825 62,130 1,254,035 1,464,046 974,898

Chanzo: Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika

kilimo miaka 50.indd Sec1:76kilimo miaka 50.indd Sec1:76 11/16/11 10:34:42 AM11/16/11 10:34:42 AM

Page 93: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

77

Kiambatisho Na. 7: Wastani wa Uzalishaji wa Mazao ya Bustani 2000/01 na 2009/10

Zao 2000/01 2001/02 2002/03 2003/04 2004/05 2005/06 2006/07 2007/08 2008/09 2009/10

Chungwa 139,500 145,000 155,865 168,854 170,542 177,881 181,550 210,000 251,040

Maembe 145,000 146,000 154,302 255,000 257,550 309,174 334,986 300,000 394,000

Papai 2,300 3,000 4,320 4,680 4,727 4,930 5,032 6,038 6,820

Nanasi 218,000 200,000 181,629 196,765 198,733 207,284 211,560 245,600 275,650

Ndizi 245,000 455,000 380,593 500,000 505,000 617,204 682,330 787,966 775,650

Mapera 400 600 2,000 2,166 2,188 2,282 2,329 2,795 5,550

Limau 700 1,200 3,155 7,200 7,272 9,331 9,500 10,500 6,720

Kakara 1,200 1,700 1,391 3,000 3,030 3,849 4,259 5,111 2,090

Machenza 10,000 10,300 20,310 20,502 22,527 22,636 22,490 27,100 28,545 Parachichi 4,800 5,500 5,366 5,813 5,871 6,124 6,250 7,500 36,420 Mafyurisi 3,200 3,800 4,685 5,076 5,127 5,347 5,458 6,200 5,550 Matunda damu

16,000 18,000 16,818 18,219 18,401 19,193 19,589 20,800 21,000

Matundamiwa 1,500 1,750 1,620 2,800 2,828 3,000 3,200 3,840 4,150 Matofaa 3,900 4,020 3,860 5,070 5,121 5,751 6,066 7,279 2,590 Loquat 135 170 91 920 929 1,34 1,558 1,870 1,425 Mafenesi 100 150 74 1,200 1,212 1,781 2,066 2,479 2,500 MbogaNyanya 120,000 130,500 132,801 342,000 145,420 151,750 206,595 237,914 250,000

Kabichi 220,700 223,550 185,832 259,300 261,893 299,923 216,835 209,282 256,635

Vitunguu 170,000 170,500 126,132 136,643 138,010 143,948 147,601 137,121 150,500

Mchicha 13,500 14,600 10,877 18,520 18,705 22,619 2,090 2,600 3,700

Bamia 120 200 342 560 566 678 736 883 1,250 Karoti 1,500 2,000 1,365 2,700 2,727 3,408 2,362 2,514 3,750

Njegere 230 280 2,673 2,896 2,925 3,050 2,428 2,554 2,750 Spinachi 580 570 576 624 630 657 674 809 1,271 B’nganya 1,880 1,900 1,750 3,400 3,434 4,276 2,714 2,900 3,120 Pilipili 3,100 3,300 2,973 4,470 4,515 5,286 2,694 2,700 1,485

Maharage machanga

1,710 1,750 836 3,450 3,485 4,809 2,800 2,970 3,050

Viungo Kitunguu saumu

90 150 50 568 574 657 680 944 1,050

Tangawizi 300 380 254 3,400 3,434 2,614 2,495 2,700 15,063

Iliki 450 560 432 5,100 5,151 2,870 3,589 3,205 740

Maua

Mauaridi 0 0 0 0 0 4,792 5,550 6,659 7,200

Vipingili 0 0 0 0 0 1,070 1,348 1,618 2,150

Chanzo: Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika

kilimo miaka 50.indd Sec1:77kilimo miaka 50.indd Sec1:77 11/16/11 10:34:42 AM11/16/11 10:34:42 AM

Page 94: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

78

Kiambatisho Na. 8: Uzalishaji wa Mbegu za Mafuta Kati ya 2000/01 na 2007/08 (Tani)

Mwaka Alizeti Karanga Ufuta

2000/2001 80,870 206,800 25,707

2001/2002 104,400 289,500 55,100

2002/2003 112,440 255,100 22,485

2003/2004 106,312 163,360 49,163

2004/2005 88,854 125,311 74,989

2005/2006 373,391 783,775 221,421

2006/2007 369,803 408,058 155,794

2007/2008 418,317 396,769 46,767

2008/2009 310,584 349,306 90,063

2009/2010 328,533 475,918 146,919

2010/2011** 666,030 600,300 326,660

** Malengo

Chanzo: Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika

kilimo miaka 50.indd Sec1:78kilimo miaka 50.indd Sec1:78 11/16/11 10:34:43 AM11/16/11 10:34:43 AM

Page 95: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011)

79

Kiambatisho Na. 9: Ramani inayoonyesha mtawanyiko wa maeneo yanayofaa kuendelezwa kwa kilimo cha umwagiliaji Tanzania Bara

kilimo miaka 50.indd Sec1:79kilimo miaka 50.indd Sec1:79 11/16/11 10:34:43 AM11/16/11 10:34:43 AM

Page 96: Maendeleo ya Sekta ya Kilimo katika kipindi cha Miaka 50

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE

80

kilimo miaka 50.indd Sec1:80kilimo miaka 50.indd Sec1:80 11/16/11 10:34:43 AM11/16/11 10:34:43 AM