325
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Kumi na Moja – Tarehe 16 Aprili, 2019 (Bunge lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Tukae. Katibu. NDG. ATHUMAN B. HUSSEIN – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2019/2020. NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwa mwaka wa fedha 2019/2020. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA (MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Makamu

MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

  • Upload
    others

  • View
    46

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA________

MAJADILIANO YA BUNGE_________

MKUTANO WA KUMI NA TANO

Kikao cha Kumi na Moja – Tarehe 16 Aprili, 2019

(Bunge lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua

MWENYEKITI: Tukae. Katibu.

NDG. ATHUMAN B. HUSSEIN – KATIBU MEZANI:

HATI ZA KUWASILISHA MEZANI

Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:-

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA:

Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA:

Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira) kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YAKATIBA NA SHERIA (MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA):

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba naSheria kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Makamu

Page 2: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

wa Rais (Muungano) kwa mwaka wa fedha 2018/2019pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapatona Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YAVIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA (MHE. KANALI (MST)MASOUD ALI KHAMIS):

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara na Mazingira kuhusu utekelezaji wa majukumu yaOfisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) kwa mwaka wa fedha2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio yaMapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

MHE. LATHIFAH H. CHANDE (K.n.y. MSEMAJI MKUU WAKAMBI RASMI YA UPINZANI KWA OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA - MHE. ALLY SALEH ALLY):

Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano naMazingira) kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisihiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020.

MWENYEKITI: Ahsante. Katibu.

NDG. ATHUMAN B. HUSSEIN – KATIBU MEZANI: Maswali.

MASWALI NA MAJIBU

MWENYEKITI: Waheshimiwa, tutaanza na Ofisi, yaWaziri Mkuu swali la Mheshimiwa Paschal Yohana Haonga.

Na. 88

Madai ya Wastaafu Waliokuwa Wanachama wa PSPF

MHE. PASCHAL Y. HAONGA aliuliza:-

Kuna watumishi katika Halmashauri nyingi za Wilayanchini walikuwa wanachama wa PSPF wamestaafu zaidi ya

Page 3: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

mwaka mmoja na hawajalipwa fedha zao za kiiunuamgongo (pension) na kwa sasa wanaishi maisha ya taabuna mateso makali:-

(a) Je, ni lini sasa Serikali itawalipa wastaafu hawa?

(b) Inasemekana kwamba Serikali imetumia vibayafedha za PSPF ikiwa ni pamoja na kukopesha baadhi ya watuna taasisi: Je, Serikali haioni kwamba hii inaweza kuwa sababumojawapo ya kucheleweshwa mafao kwa wastaafu?

(c) Fedha za kiinua mgongo ni mali ya Mtumishianayestaafu: Je, kwa nini Mifuko ya Pensheni isiwakopeshewastaafu watarajiwa angalau 40% ya fedha hizo bila ribapale inapobaki miaka 10 kabla ya kustaafu?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANANA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa PaschalYohana Haonga, Mbunge wa Mbozi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka kufikia tarehe 28Februari, 2019 Mfuko mpya wa PSSF ulikuwa umekamilishakulipa malimbikizo ya deni la wastaafu lilorithiwa kutoka Mfukowa PSPF ambapo jumla ya wastaafu 9,971 wamelipwa stahikizao zilizofikia kiasi cha shilingi bilioni 888.39. Aidha, Mfukoumekamilisha mfumo wa ulipaji mafao utakaowezeshakufanya malipo katika ngazi ya mkoa na hivyo kuwezeshamfuko kulipa mafao ndani ya muda uliowekwa kisheria wasiku 60 tangu mwanachama anapowasilisha madai.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mifuko ya Hifadhi ya Jamiiinaendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Bunge iliyoanzishamfuko husika. Sheria hiyo pamoja na mambo mengineinasimamia muundo wa utawala na mfumo wa maamuzi nausimamizi wa uwekaji wa fedha za mifuko. Aidha, sheria

Page 4: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

inaipa Bodi ya Wadhamini ya mfuko jukumu la kusimamiauwekezaji wa fedha za mfuko kwa uhuru. Hivyo basi, siyo kwelikwamba Serikali inaweza kuingilia uendeshaji wa mifuko aukufanya maamuzi ya uwekezaji ikiwemo kukopesha taasisiau watu binafsi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii,imekuwa mikopo yenye masharti nafuu kwa wanachamawake kupitia vikundi vya kuweka na kukopa (SACCOS) katikamaeneo ya kazi. Kwa mujibu wa Mwongozo wa Uwekezajiwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifukoinaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 yarasilimali za mfuko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria za Mifuko ya Hifadhiya Jamii zinaruhusu wanachama kutumia sehemu ya mafaoyao kama dhamana kwa ajili ya kujipatia mkopo wa nyumbakutoka katika mabenki na taasisi za fedha nchini i l ikuwawezesha kuboresha makazi wakati wa kipindi chautumishi wao.

Aidha, Kanuni Na. 24 na 25 ya kanuni mpya za Mafaoya Hifadhi ya Jamii za mwaka 2018 zimetoa wigo mpana zaidikwa wanachama waliochangia kwa miaka isiyopungua 10kuweza kupata huduma hii tofauti na hapo awali ambaponi wanachama waliokuwa wametimiza umri kuanzia miaka55 ndio waliweza kupatiwa mikopo ya kujenga vyumba.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Haonga.

MHE. PASCHAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swalila kwanza, kwa kuwa mtumishi anapokuwa anaajiriwa, maraya kwanza na kwenye salary slip yake inaonesha mudaatakaostaafu, hivyo inakuwa siyo suala ambalo ni la ghafla,lakini Serikali imekuwa ikichelewa sana kuwalipa watumishihawa: Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka inapokuwawamesababisha ucheleweshwaji wa mafao kwa watumishiwa Umma inataikiwa walipe kwa riba? (Makofi)

Page 5: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pil i, katikaHalmashauri ya Mbozi kuna watumishi 35 wamestaafu tokaSeptemba, 2018, hadi sasa hawajalipwa fedha zao nawanaidai Serikali na wanaishi maisha magumu sana: Je, nilini sasa Serikali itaacha kuwatesa watumishi hawa wanaoishimaisha ya taabu sana kwa sababu ya ucheleweshaji wafedha zao? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANANA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): MheshimiwaMwenyekiti, katika swali lake la kwanza Mheshimiwa Haongaamezungumza kuhusu ucheleweshwaji wa ulipaji wa mafao.Kwa mujibu wa sheria ambayo tumeipitisha hapa ndaniBungeni hivi sasa, inautaka mfuko kulipa mafao ya mstaafundani ya siku 60.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zilikuwepo changamotonyingi hapo awali, nyingi sio kwambwa zinasababishwa namfuko husika lakini pia wale wastaafu katika namna mojaama nyingine katika uandaaji wa nyaraka na kufuatilia taarifazao imekuwa pia ikileta changamoto. Baada ya kuunganishamifuko hii na kwa kutumia sheria mpya, hivi sasa PSSFwameweka utaratibu na motto wao ni kwamba wanalipamafao tangu jana.

Mheshimimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwondoehofu Mheshimiwa Mbunge kwamba hivi sasa zoezi la ulipajiwa mafao kwa wastaafu linafanyika kwa kiwango kikubwasana na kwa idadi ambayo nimesema tayari imeshalipwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili kuhusu watumishikatika Jimbo lake la Mbozi, kwa sababu hii inakwenda caseby case, nisilisemee kwa ujumla, lakini nichukue tu fursa hiikumwambia Mheshimiwa Haonga kwamba ofisi yetu iko wazi,kama kuna madai ya watumishi ambao mpaka hivi sasabado hawajalipwa mafao yao, basi anaweza kuyasilisha ilisisi Ofisi ya Waziri Mkuu tuweze kufuatilia mkoa husika tujue

Page 6: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

changamoto ni nini na baada ya hapo tuweze kutatuachangamoto yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhamira ya Serikali kulipamafao yao kwa wakati kabisa ili kuwafanya watumishi hawawaishi katika maisha ya amani.

MWENYEKITI: Ahsante Waheshimiwa, tunaendelea naOfisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Mheshimiwa BonnahKamoli.

Na. 89

Hitaji la Masoko la Segerea

MHE. BONNAH M. KALUWA aliuliza:-

Wananchi wa Kata za Kinyerezi, Bonyokwa, SegereaLiwiti, Kipawa, Kimanga, Kisukulu na Tabata wamekuwawakitumia fedha na muda mwingi kwenda kutafuta bidhaana huduma katika masoko ya Buguruni na Kariakoo kutokanana kukosa huduma hizo katika maeneo yao:-

(a) Je, kwa nini Serikali isijenge soko kubwa katikaeneo mbadala lililo katikati na linaloweza kufikiwa nawananchi hao kwa wakati?

(b) Je, kwa nini Soko la Kinyerezi lililozinduliwa naMwenge mwaka 2017 lisifunguliwe ili kutoa huduma kwawananchi wanaozunguka soko hilo na maeneo ya karibu?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwa niaba yaWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Bonnah Kamoli, Mbunge wa Segerea, lenyesehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

Page 7: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri yaManispaa ya Ilala iliweka kipaumbele cha kutekeleza mradiwa kimkakati wa ujenzi wa Soko la Kisutu utakaogharimutakribani shilingi bilioni 12.17. Mpaka sasa mradi huoumepatiwa jumla ya shilingi bilioni 3.92 na ujenzi unaendelea.Aidha, katika mwaka wa fedha 2019/2020, Halmashauri yaManispaa ya Ilala imetenga shilingi milioni 200 kwa ajili yakujenga masoko mengine ndani ya Manispaa ya Ilala.Halmashauri inashauriwa kutumia fursa ya miradi ya kimkakatina kuandaa andiko la mradi wa kujenga masoko katika Kataya Kinyerezi, Bonyokwa, Segerea, Liwiti Kipawa, Kimanga,Kisukulu na Tabata ili kupata fedha za utekelezaji.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, Soko la Kinyerezilililozinduliwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 limepangwakuanza kutumika Mei, 2019 baada ya matengenezo ya chooambacho kilikuwa hakijakamilika kwa wakati huo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kamoli.

MHE. BONNAH M. KALUWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na majibu mazuri ambayo ameyajibu MheshimiwaNaibu Waziri; kwa kuwa Serikali imeanzisha miradi ya kimkakatikatika mikoa mingine na ukizingatia katika Jimbo la Segereakuna wananchi wengi sana ambao wanakaribia 1,300,000;je, Serikali ina mpango gani kujenga masoko ambayoyatakuwa yanawasaidia wananchi ili wasiweze kwendambali kama hivyo alivyosema Kisutu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, nimemsikiaMheshimiwa Waziri anaongelea kuhusiana na Soko laKinyerezi. Kutokana na kwamba nilifanya ziara mwezi uliopita,hilo soko mpaka sasa hivi kwanza linavuja, halafu piahalijamaliziwa vizuri. Kwa hiyo, haliwezi kuzinduliwa mwaka2019 kama anavyosema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo, kuna Katanyingi ambazo hazina masoko kama Kata ya Kisukulu, Kataya Kipawa na Kata nyingine: Je, Serikali ina mpango gani

Page 8: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

kuhusiana na hizo Kata nyingine kuhakikisha kwambazinapata masoko?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu. Soko la Kisutumwongeze hela.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaMwenyekiti, nakuelewa, nakushukuru. Swali la kwanzaningeomba niseme tu kwamba utaratibu unaotumika kuibuamiradi ya kimkakati ni Halmashauri husika, inakaa nawataalam wake, wanaandika andiko, wanaliwasilisha Ofisiya TAMISEMI pamoja na Wizara ya Fedha; wataalam waWizara ya Fedha wanaenda kufanya tathimini ya andikolenyewe, gharama zake na mrejesho kwa maana ya faidaitakayopatikana na baada ya hapo wataruhusiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hii ya kuwa namasoko ya Kinyerezi na maeneo mengine, itategemeaHalmashauri ya Manispaa ya Ilala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili nilitaka tuniseme kwamba inawezekana ni kweli Mheshimiwa Mbungeanasema, sasa nimwelekeze Mkurugenzi wa Manispaa yaIlala aende akafanye utaratibu wa kukarabati na kurekebishasoko hilo ili liendane na ambavyo nimejibu katika swali langula msingi, kwamba Kinyerezi ilizinduliwa mwaka 2017 na Mbioza Mwenge wa Uhuru lakini Mei mwaka huu linatakiwa lianzekufanya kazi. Mkurugenzi aweke pesa pale ili liweze kufanyakazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja anayoizungumzaMheshimiwa Mbunge hapa, soko la Kisutu ni kweli lipo kwenyemkakati, limesharuhusiwa na Serikali na fedha imeshatolewa.Naomba nimhakikishie, kwa kadri anavyojua kwamba lazimalisimamiwe; na Mheshimiwa Mbunge nimridhishe kwambayeye katika Manispaa ya Ilala ana ujenzi wa machinjio yakisasa kabisa ya Vingunguti ambayo ipo pia kwenye mpangomkakati katika eneo hilo. Ahsante.

Page 9: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

MWENYEKITI: Ahsante kwa majibu mazuri. MheshimiwaQambalo.

MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Mji wa Karatu ni Mji wa Kitalii na hauna soko lauhakika. Hivi sasa wananchi wa Karatu kwa kutumia mapatoyao ya ndani wameanza kujenga soko lenye hadhi ya Mjihuo: Je, Serikali iko tayari sasa kuunga mkono jitihada zawananchi hao ili soko hilo likamilike?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri kwa kifupi sana.Mheshimiwa Mlinga na Mheshimiwa Catherine wajiandae.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Katika Mkoa wa Manyara tayarituna mradi wa kimkakati katika Wilaya ya Hanang’. Kwa hiyo,namwomba Mheshimiwa Mbunge kama nilivyosema katikajibu langu la msingi, fedha zipo, Serikali ipo tayari kutoaushirikiano. Cha muhimu, Halmashauri husika ikae na kutoaandiko, likija hapa kwenye tathmini hili jambo litafanyika. Sisitunakusudia kuweka masoko, stendi na majengo mbalimbaliya kimkakati ili baada ya kuwekeza katika maeneo hayo,Halmashauri zetu zipate mapato ya kutosha ili kuwezekuendeleza na kutekeleza miradi ya maendeleo kwawananchi wetu.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, pesa zipo,andikeni maandiko. Pelekeni maandiko TAMISEMI,mtajengewa miradi ya kimkakati.

Mheshimiwa Mlinga halafu Mheshimiwa Catherine.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Kata yangu ya Mahenge Mjiniambapo ndiyo Mji wenyewe ulipo, kuna shida kubwa ya soko.Wananchi walijitolea wakajenga soko, Serikali ikatia helazake.

Page 10: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2018 Mwenge ulikujaukafungua hilo soko, lakini mpaka leo hii soko hilo halijaanzakutumika. Kwa hiyo, Mwenge umedanganywa, Mbungekadangaywa, wananchi wamedanganywa. Je, lini Serikaliitasimamia ufunguaji wa soko hilo ili wananchi wapatekulitumia?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, anataka kujua ni linisoko litafunguliwa? Mwenge haujapita kwako?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaMwenyekiti, nakuhsukuru. Hili jambo tumelipokea, tutalifanyiakazi tuone tatizo liko sehemu gani ili liweze kufanya kazi.

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Catherine.

MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Kwa kuwa imekuwa ni ahadi ya muda mrefuya Serikali kujenga Soko la Mto wa Mbu Wilayani MonduliMkoani Arusha, lakini mpaka sasa hakuna chochotekinachoendelea na wananchi wa Mto wa Mbu wamekuwawakipata taabu: Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Soko laMto wa Mbu Mkoani Arusha? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Ni kweli hili suala hata MheshimiwaMbunge wa Jimbo la Monduli, Mheshimiwa Julius Kalangaameniuliza jana. Kama nilivyosema, namwomba MheshimiwaMbunge wakae na Halmashauri yao, fedha zipo kamaulivyosema. Ni kuandika andiko na sisi Ofisi ya Rais, TAMISEMItupo tayari kusaidia utaalaam na namna ya kuboreshapamoja na Hazina ili andiko likamilike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua kuna wapiga kurawengi sana pale Mto wa Mbu, tungependa wapate sokozuri, wapate kipato, pia wachangie kodi katika maendeleo

Page 11: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

ya Watanzania wenzetu. Kwa hiyo, naomba MheshimiwaMbunge tuwasiliane hili jambo liweze kufanyiwa kazi. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na Ofisi yaMakamu wa Rais (Muungano na Mazingira), MheshimiwaCapt. Abbas Ali Hassan Mwinyi, Mbunge wa Fuoni, kwa niabayake Mheshimiwa Khadija.

Na. 90

Changamoto za Muungano

MHE. KHADIJA HASSAN ABOUD (K.n.y. MHE. ABBAS A.H. MWINYI) aliuliza:-

Changamoto za Muungano wetu bado zipo licha yavikao vya Kamati za pamoja kati ya SMT na SMZ kukutanamara kwa mara:-

(a) Je, ni changamoto zipi zilizopata ufumbuzi tanguSerikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani?

(b) Je, changamoto hizo ni ngapi?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa NchiOfisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), naombakujibu swali la Mheshimiwa Abbas Ali Hassan Mwinyi, Mbungewa Fuoni, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka2015 mpaka 2019 Serikali ya Awamu ya Tano iliyoingiamadarakani, changamoto mbili zimepatiwa ufumbuzi. Hojazilizopatiwa ufumbuzi katika kipindi cha Serikali Awamu yaTano ni utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia nakutoa VAT kwa asilimia sifuri kwa umeme unaouzwa na

Page 12: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

TENESCO kwa ZECO ikiwa ni pamoja na kufuta deni la kodiya VAT lililofikia shilingi bilioni 22.9 kwa umeme uliouzwa kwaZECO.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na juhudi hizo, Ofisiya Makamu wa Rais imeendelea kuitisha vikao vya kisekta,kutafuta ufumbuzi wa changamoto zil izobakia nazinazoendelea kujitokeza. Sekta hizo ni Sekta ya Fedha,Uchukuzi, Biashara, Mifugo, Uvuvi na Nishati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja zilizojadiliwa ni pamojana Taarifa ya Mapendekezo ya Tume ya Pamoja ya Fedha,hisa za SMZ zilizokuwa katika Bodi ya Sarafu ya Afrika Masharikina mgawanyo wa mapato yanayotokana na faida ya BenkiKuu, usajili wa vyombo vya moto, upatikanaji wa fursa zamasoko Tanzania Bara, ushirikiano kati ya Taasisi ya Viwangona Zanzibar (ZBS) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS),Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) na Mamlakaya Chakula na Dawa ya Zanzibar (ZFDA), ZBS kupatiwa nakalaya usaili kiwango cha Afrika Mashariki ili kurahisisha usaili wakiwango hicho kwa wakati; Leseni za viwanda, Zanzibar kuwadesignated member country wa mashirika ya AfricanRegional Intellectual Property Organization (ARIPO) na Worldna World Intellectual Property Organisation (WIPO) naupatikanaji wa fursa za miradi inayohusisha maendeleo yaviwango na ubora wa bidhaa kwa maendelo ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania ikiwemo miradi inayohusumaendeleo ya wajasiriamali na kuzuiwa kwa bidhaa ya majiya kunywa inayozalishwa Zanzibar kuingia Tanzania Bara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali zote mbili za SMZ naSMT zimeendelea kuhakikisha kuwa makubaliano yaliyofikiwana pande mbili yanatekelezwa na kuhakikisha kuwachangamoto zinazojitokeza zinashughulikiwa ipasavyo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Khadija Aboud.

MHE. KHADIJA HASSAN ABOUD: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwamajibu mazuri ya Serikali. Pamoja na hayo napenda kuchukua

Page 13: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

nafasi hii kuipongeza sana Serikali ya Jamhuri ya Muunganokwa kutatua baadhi ya changamoto muhimu ambazozilikuwa zinazikumba Serikali zetu hizi mbili, ikiwemo yakuondosha VAT kwenye suala la umeme, naipongeza sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sina swali la nyongeza,isipokuwa naendelea kuishauri Serikali kila inapoona inafaakwa wakati muafaka kuendelea kutatua changamoto hiziza Muungano. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, hamna swali la nyongeza.Ahsante kwa ushauri mzuri, Serikali imepokea.

Waheshimiwa Wabunge tunaendelea naMheshimiwa Mbarouk Salum Ali, swali namba 91.

Na. 91

Elimu Juu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

MHE. JUMA KOMBO HAMAD (K.n.y. MHE. MBAROUKSALUM ALI) aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa elimu kwaWatanzania hususan kizazi kipya, kuhusu Muungano waTanganyika na Zanzibar ili kutoa uelewa wa pamoja nadhamira njema za Muungano huo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbarouk Salum Ali,Mbunge wa Wete, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua kwamba,karibu asilimia 80 ya kizazi cha sasa kimezaliwa baada ya

Page 14: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

Muungano na hivyo kuna haja ya kutoa elimu ya Muunganokwa wananchi wote, hususan vijana wa Kitanzania. Elimu hiini muhimu kwa mustakabali wa Muungano kwani inaongezaari ya uraia, uzalendo na kujenga undugu wa Kitaifa kati yawananchi wa pande mbili za Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwaka 2018/2019, ofisiimetoa elimu ya Muungano kupitia vipindi vya redio natelevision, ili kuhakikisha makundi mbalimbali yanapata elimuya Muungano, hususan vijana. Katika Mwaka wa Fedha 2017/2018, shughuli za elimu ya Muungano, hususan kwa vijana,zilitolewa kupitia kongamanko la vijana, hususan fursa zilizopokatika Muungano ambapo ilifanyika Zanzibar tarehe 22Oktoba, 2017. Wanafunzi wa shule za msingi zilizopo Dodomailifanyika tarehe 18 Aprili, 2018 na Kongamano la Vyuo vyaElimu ya Juu vilivyopo Dodoma, itafanyika tarehe 21 Aprili,2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, ofisi ilishiriki katikamaonesho ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Dunianiiliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia tarehe 31 haditarehe 6 Juni, 2018, ambapo wananchi walipata fursa zakujulishwa kuhusu masuala ya Muungano. Pamoja na kazihizo, ofisi ilishiriki katika vipindi vya redio, television na magazetikatika kutoa elimu ya Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutambua faidazitakazopatikana kwa kutoa elimu ya Muungano, Serikalikupitia Ofisi ya Makamu wa Rais, itaendelea kutoavipaumbele katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 na imetengafedha kwa ajili ya kutoa elimu ya Muungano kwa vijanakupitia makongamano na warsha, ambayo yamelengawanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo vya elimuya juu Tanzania Bara na Zanzibar.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbarouk.

MHE. JUMA KOMBO HAMAD: Mheshimiwa Mwenyekiti,ni mara kadhaa maafisa mbalimbali ambao wanatumiamagari ambayo yamekuwa na namba za Zanzibar

Page 15: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

wamekuwa wakikumbana na vikwazo vya TRA pamoja naPolisi kwamba, namba hizo ni namba za kigeni wakatianapotembea Tanzania Bara. Naomba nimuulizeMheshimiwa Waziri, je, yupo tayari sasa kutenga mudamahususi kuwapa taaluma Polisi pamoja na TRA kuonakwamba, Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano waTanzania?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, je, MheshimiwaWaziri yuko tayari sasa kuambatana na sisi au na mimikwenda kuangalia namna Maafisa wa TRA wanavyofanyakazi pale bandarini kwamba, unapokuja tu na kilo tano zasukari kutoka Zanzibar au Tv ya nchi 21 unatakiwa ulipe kodi?Je, hili yupo tayari kwenda kulishuhudia Bandari ya Zanzibarili kutoa mwongozo na taaluma kwa ajili ya shughuli hizo zakibiashara?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS –MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nichukue fursa hii kujibu swali la nyongeza la MheshimiwaMbarouk, kwa niaba yake Mheshimiwa Juma ameuliza vizurisana:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza niko tayari kwayote mawili, lakini kwa ufafanuzi zaidi hili la vyombo vya motokwa sababu, bado lipo tayari kwenye majadiliano na vikaovinaendelea, nadhani baada ya hivyo vikao sasa nitakuwatayari kwa ajili ya kutoa hiyo elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili, niko tayarikuambatana na wewe na Wabunge wengine ambaowanatoka Zanzibar kwenda kushiriki kwa pamoja kuhakikishakwamba, eneo hili tunalifanyia ufumbuzi. Ahsante sana.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Maryam.

MHE. MARYAM SALUM MSABAHA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Napenda kuuliza swali dogo la

Page 16: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

nyongeza. Kwa kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais watumishiwengi wanakaimu.

Je, Serikali ina mikakati gani kuhakikisha watumishihawa sasa, wale wanaokaimu wanapandishwa madaraja?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nishukuru. Nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbungekama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza Serikali ina dhamiraya dhati kabisa kuhakikisha maeneo yote ambayo watumishiwanakaimu waweze kufanya kazi yao kwa ukamilifu. Natakanimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tayari ofisi yetuimeshafanya utaratibu wa kuomba kibali kwa ajili yakuhakikisha watumishi wote wale au maeneo yote, positionzote ambazo zinakaimiwa ziweze kupata watalaam ambaowako kamili. Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mary Mwanjelwa, NaibuWaziri, Utawala Bora.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHIWA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru ili nami niweze kufafanua swali la MheshimiwaMbunge, Maryam Msabaha. Pamoja na majibu mazuri sanaya Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira), naomba nifafanue kidogo juu yasuala zima la kuhusu watumishi kukaimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli watumishiwamekuwa wakikaimu kwa muda mrefu sana na nimekuwanikilizungumza hili kwamba, hii ni kutokana na watumishiwengi wamekuwa wakikaimishwa na waajiri wao kienyeji nanafasi za kukaimu ni kukaimu tu sio kwamba, ni nafasi yakuthibitishwa au ni kwamba, umeshapewa ile kazi.

Page 17: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi nafasi za kukaimu zikokatika uwezo wa madaraka kwa maana ya superlativesubstantive post. Kwa maana hiyo, sisi kama Serikali, tumetoawaraka kwamba, kukaimu mwisho miezi sita. Kwa maana hiyowaajiri wote nchini wanapaswa kuomba kibali na kamaunataka mtumishi aendelee kukaimu basi tuandikie tenabarua. Kukaimu lazima iwe kulingana na level ya ile nafasiambayo unastahili kukaimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Wizara ya Elimu, Sayansi naTeknolojia, Mheshimiwa Janeth Maurice Masaburi.

Na. 92

Serikali Kuwekeza kwenye Vyuo vya Ufundi

MHE. JANETH M. MASABURI aliuliza:-

Nchi za China na Singapore zinefanikiwa kwa kiwangokikubwa kwa kuwekeza kwenye ujenzi wa Vyuo vya Ufundi:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kutenga bajeti yakutosha ili kuwekeza kwenye Vyuo vya Ufundi ambavyovitasaidia vijana wengi kupata ujuzi na kujiajiri?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIAalijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waElimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali laMheshimiwa Janeth Maurice Masaburi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimuwa nchi kuwekeza katika elimu ya ufundi na mafunzo yaufundi stadi ili kufikia azma ya uchumi wa kati unaotegemea

Page 18: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

viwanda ifikapo mwaka 2025. Serikali inaendelea na mpangowa ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi vya mikoa mitano katikaMikoa ya Geita, Rukwa, Njombe, Simiyu na Kagera, pamojana vyuo vya ufundi stadi vya wilaya 13. Aidha, kupitia mradiwa Education Skills for Productive Jobs (ESPJ) vyuo vyote 54vya Maendeleo ya Wananchi vinakarabatiwa ambapoawamu ya kwanza vyuo 20 vitakarabatiwa na ukarabati upokatika hatua za umaliziaji. Vilevile kupitia mradi huu Chuo chaUfundi wa Kati (Technical College) kitajengwa katika Mkoawa Dodoma kuanzia Mwaka wa Fedha 2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, kupitia mradi wa EastAfrican Skills for Transformation and Regional IntergrationProject Serikali inatarajia kuzijengea uwezo taasisi za ChuoCha Ufundi Arusha, Taasisi ya Teknolojia Dar-es-Salaam (DIT)tawi la Dar-es-Salaam na Mwanza, pamoja na Chuo ChaTaifa Cha Usafirishaji (NIT), ili kuwa vivutio vya umahiri katikasekta za nishati, teknolojia ya habari na mawasiliano,usafirishaji na uchakataji wa mazao ya ngozi. Serikaliitaendelea kuwekeza katika elimu ya ufundi na mafunzo yaufundi stadi kadri uchumi utakavyoruhusu, ili kuongeza fursana ubora wa elimu na mafunzo hayo nchini kwa lengo lakuleta tija zaidi na manufaa kwa Taifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Masaburi.

MHE. JANETH M. MASABURI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Natambua Serikali imefanya vizuri sana katikasekta hii ya elimu, lakini nina maswali madogo ya nyongeza.Swali la kwanza, kwa kuwa, hivi sasa kwa wastani kwawahitimu wa vyuo vikuu ni kati ya 10 kwa mmoja kwawahitimu wanaohitimu vyuo vya ufundi, yaani wasimamizi 10kwa mtendaji kazi mmoja badala ya msimamizi mmoja kwawatendaji kazi 10. Je, Serikali inasema nini juu ya hili?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, katika umuhimuhuo wa vyuo vya ufundi ambako ndiko kunakozalisha kundikubwa la watenda kazi ambalo kundi hili ndilo linajiajirilenyewe. Je, Serikali inasema nini juu ya kuweka uwekezajimkubwa katika vyuo vya ufundi?

Page 19: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili yanyongeza ya Mheshimiwa Janeth Masaburi kwa pamoja,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ukweli kwamba, kwasasa hakuna uwiano mzuri kati ya watendaji au wafanyakazikatika sekta ya ufundi katika ile maana ya kwamba, walewatendaji wa kada ya kati pamoja na kada ya chini na walewa ngazi za juu. Serikali ndio maana imechukua maamuzi yakuongeza udahili katika vyuo vyetu ili tuendelee kuwapatawataalam wengi ambao baadae watatusaidia kujazaombwe hili na hivyo kurekebisha hali hiyo, ili tuwe na uwianomzuri katika wafanyakazi wetu katika sekta ya ufundi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la pili kwamba,Serikali inafanya nini kuwekeza katika vyuo vya ufundi. Kamanilivyosema kwenye jibu langu katika swali la msingi, Serikaliinachukua hatua kadhaa za makusudi kuhakikisha kwamba,tunaongeza, sio tunaongeza vyuo vingi, lakini vileviletunaongeza udahili pamoja na ubora wa vyuo hivyoambavyo vinatoa fani mbalimbali za ufundi. Ndio maanatunapozungumza sasa tunajenga vyuo 13 vya wilaya, lakinitutajenga vyuo vitano vya mikoa, ambavyo vile vya mikoavyenyewe vinagharimu shilingi bilioni 118, lakini pia hatujaishiahapo, tunakarabati Vyuo vyote 54 vya Wananchi viletunaviita FDCs.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo ni kuweza kuwa navyuo vingi vyenye ubora mzuri, ili tuongeze udahili, ilituendelee kuwapata mafundi wengi kwa sababu,watatusaidia katika azma yetu ya kujenga uchumi waviwanda, lakini vilevile kuongeza fursa za ajira. Kwa sababu,kama mnavyofahamu ni rahisi vijana wengi kujiajiri wakisomaufundi; lakini pia, tunaendelea kujenga vyuo vya ufundi wakati na ndio maana tumewekeza katika kujenga chuokikubwa Dodoma, chuo ambacho kina hadhi kama ilivyo DITna Arusha Technical College.

Page 20: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Dau, MheshimiwaShekilindi ajiandae.

MHE. MBARAKA K. DAU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kuniona. Wananchi wa Mafia kwakushirikiana na Mbunge wao wamejenga chuo cha kisasakabisa cha VETA na kukamilisha taratibu zote, lakini mpakaleo Wizara haijatoa usajili. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri sasaatakuwa tayari kutoa usajili kwa ajili ya VETA ya Mafia?

MWENYEKITI: Majibu Mheshimiwa Waziri.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la MheshimiwaDau, Mbunge wa Mafia, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Dau amekuwaakifuatilia sana suala la VETA ya Mafia. Kwa kweli, kuna wakatihata mimi na yeye kidogo tulitofautiana kwa sababu, alionakwamba, hatufanyi kazi kwa kasi ambayo anaitaka kwa hiyo,nampongeza sana kwa sababu, amekuwa akifuatilia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, VETA ya Mafia imekuwa nachangamoto mbili kubwa ambayo ni changamoto ya vifaa,hasa kwenye fani za ushonaji, lakini vilevile Walimu ambaowana viwango vinavyohitajika, ili VETA iweze kusajiliwa.Nimemwahidi Mheshimiwa Mbunge na ninaendelea vilevilekumwahidi kupitia Bunge lako Tukufu kwamba, Wizara yanguiko tayari kusaidiana na yeye pamoja na wananchi wakewa Mafia ili changamoto hizo tuweze kuziondoa na tuwezekutoa usajili mapema kwa ajili ya chuo chake.

MWENYEKITI: Ahsante, ameshakuelewa. MheshimiwaShekilindi, jiandae Mheshimiwa Susan Lyimo.

MHE. SHAABAN O. SHEKILINDI: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana. Wilaya ya Lushoto ni wilayakongwe na bahati nzuri Waziri Mheshimiwa Ndalichakoalitembelea Wilayani ya Lushoto na akaona hali halisi ilivyo.Je, ni lini Mheshimiwa Waziri utatuma wataalam wake

Page 21: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

kwenda kuona majengo yale ya Halmashauri, ili ikimpendezatuweze kuanza sasa kukarabati majengo yale na watotowetu waanze kusoma masomo ya VETA?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri kwa kifupi sana,anataka kujua ni lini tu, mwambie.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongezala Mheshimiwa Shekilindi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimwahidiMheshimiwa Mbunge kwamba, leo hii tukitoka mimi na yeyetutapanga ni lini tutawapeleka hao watendaji kule.

MWENYEKITI: Ahsante, majibu sahihi. MheshimiwaLyimo.

MHE. SUSAN A. LYIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri anapojibu anaelezeasuala zima la kujenga vyuo kila wilaya na mkoa, lakinihawajazungumzia changamoto kubwa ya tatizo kubwa laWalimu wa ufundi stadi. Je, wanapojenga hivi vyuo kila mkoana kila wilaya wana Walimu kwa sababu, wana Chuo kimojatu cha Ualimu wa Ufundi Stadi kule Morogoro, ni liniwataongeza au waapanua chuo kile au kujenga chuokingine, ili tupate Walimu bora ambao wataweza kuhimili aukwenda kwenye hivi vyuo ambavyo vinajengwa?

MWENYEKITI: Mhesimiwa Waziri kwa kifupi, ni lini?Jiandae Mheshimiwa Hongoli.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la MheshimiwaSusan Lyimo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba, kunaupungufu huo na Serikali inatambua na tumeanza hatua zamakusudi kuhakikisha kwamba, tunaongeza upatikanaji waWalimu katika vyuo vyetu vya ufundi.

Page 22: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

MWENYEKITI: Mheshimiwa Hongoli.

MHE. JORAM I. HONGOLI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.Zamani tulikuwa na shule za msingi ambazo zilikuwa zinatoamafunzo ya ufundi, lakini pia, tulikuwa na sekondari za ufundi.Je, ni kwa nini sasa Wizara isizifufue zile shule angalau kilakata iwe na shule moja ambayo inatoa mafunzo ya ufundi, ilikuwawezesha vijana ambao hawajafanikiwa kwendasekondari kupata stadi na mwisho wakaweza kujiajiri navilevile tukateua sekondari katika kila tarafa sekondari mojaiwe sekondari ya ufundi, ili vijana wanaokosa kuendelea nakidato cha tano waweze kujiajiri?

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Waziri. JiandaeMheshimiwa Mwamoto.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongezala Mheshimiwa Hongoli kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba, kuna hajaya kuongeza fursa za mafunzo ya ufundi katika ngazimbalimbali na ndio maana Serikali inajaribu kwa kuanziakujenga vyuo, lakini badaye tutaangalia uwezekano wakurudi kwenye shule za sekondari na shule za msingi ambazoni za ufundi. Kwa sasa zipo shule baadhi za sekondari ambazozinatoa ufundi vilevile.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mwamoto,ajiandae Mheshimiwa Magereli.

MHE. VENANCE M. MWAMOTO: MheshimiwaMwenyekiti, swali langu limeshaulizwa.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Magereli.

MHE. LUCY S. MAGERELI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nimeshukuru kwa maelezo ya Mheshimiwa Waziri aliyoyatoakuhusu umuhimu wa elimu ya ufundi na Halmashauri ya

Page 23: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

Wilaya ya Kigamboni ni wilaya mpya ambayo ina fursa nyingisana zinaweza kuwasaidia vijana kujiajiri wenyewe. Je, Serikaliina mpango gani wa kujenga chuo cha ufundi katikaHalmashauri ya Kigamboni, ili kuwaepusha vijana wetu nagharama kubwa ya nauli wanayolipa katika kivuko kuvukakwenda mjini kutafuta huduma hiyo?

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Waziri, majibu kwakifupi.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la MheshimiwaMagereli, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema Serikali inampango wa kujenga vyuo vya ufundi vya wilaya katikaWilaya zote ikiwemo na Wilaya ya Kigamboni. Naombanimshauri vilevile Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wenginewote kwamba, pale ambapo wao wenyewe na wananchiwao watakuwa wameanzisha jitihada ya kujenga chuoinakuwa ni rahisi sisi kuja kuongezea kuliko tunapoendeleakusubiri nchi nzima tujenge.

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa Wabunge,tunaendelea Wizara ya Kil imo. Swali l inaulizwa naMheshimiwa Martin Alexander Msuha.

Na. 93

Vyama vya Ushirika vya Msingi

MHE. MARTIN M. MSUHA aliuliza:-

Hivi karibuni Serikali ilibadilisha mfumo wa ununuzi nauuzaji kahawa kwamba ni lazima kupitia Vyama vya Ushirikavya Msingi:-

Je, ni Vyama vingapi vya Msingi vya Ushirika (AMCOs)vimeundwa Wilayani Mbinga kufuatia kubadilishwa kwamfumo huo?

Page 24: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA)alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waKilimo, kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Martin Msuha,Mbunge wa Mbinga Viji j ini, naomba kutoa maelezoyafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Vyama vya Ushirikahuanzishwa na wananchi kutokana na mahitaji yao, hivyo,kupelekea kuwepo kwa aina mbalimbali za Vyama vyaUshirika kama vile vyama vya ushirika vya mazao ya kilimona masoko, mifugo, uvuvi, viwanda, nyumba, fedha namadini kwa mujibu wa Sheria ya Ushirika Na. 6 ya mwaka2013.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Serikali imeelekezabiashara ya zao la kahawa na mazao mengine ya biasharakufanyika kupitia Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)badala ya wanunuzi binafsi kwenda kwa wakulima moja kwamoja. Utaratibu huu utawawezesha wakulima kunufaika nakilimo cha kahawa kwa kuzalisha kahawa yenye ubora nakuzwa kupitia minada ambapo wanunuzi watashindanishwana hivyo kupelekea mkulima kupata bei nzuri na yenye tija.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi sasa Mkoa wa Ruvumauna jumla ya Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Kahawa 67na Chama Kikuu cha Ushirika kimoja (MBIFACU) ambavyovimeansihwa na wakulima wa kahawa katika Mkoa waRuvuma. Aidha, Wilaya ya Mbinga ina jumla ya Vyama vyaUshirika vya Msingi vya Kahawa 58 ambavyo ndivyovitasimamia na kuendesha biashara ya kahawa katika Wilayaya Mbinga.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msuha.

MHE. MARTIN M. MSUHA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Nashukuru kwa majibu ya Serikali lakini pia

Page 25: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

nichukue fursa hii kuishukuru Serikali kwa kupeleka mnada wakahawa Wilayani Mbinga kuanzia msimu ujao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina maswali mawili yanyongeza. Swali la kwanza, kumetokea changamoto kadhaakatika mfumo huu mpya ikiwemo kuchelewesha malipo kwawakulima, wakulima kulipwa bei tofauti lakini pia kukosekanakwa uaminifu kwa baadhi ya watendaji wa AMCOS. Je,Serikali imejipangaje kutatua kero hizi kwenye msimu ujao wakahawa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kumekuwepomabadiliko ya bei msimu kwa msimu, je, Serikali inajipangajeama ina mpango gani wa kuanzisha Mfuko wa KuimarishaBei ya Kahawa (Price Stabilization Fund) ili kuondokana natatizo hili la mabadiliko ya mara kwa mara ya bei ya kahawa?Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa kifupisana.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA):Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili yanyongeza ya Mheshimiwa Martin Msuha, Mbunge wa MbingaVijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanzaanataka kujua changamoto zilizojitokeza katika msimuuliopita hasa ya kuchelewesha malipo kwa wakulima pamojana wakulima kulipwa bei tofauti na bei ambayo ilitangazwana Serikali ama iliyouzwa mnadani. Kwanza nichukue nafasihii kumpongeza Mheshimiwa Msuha kwa ufuatiliaji wawakulima wa kahawa nchi nzima kupitia wakulima hawa waMbinga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kujibu swali lakenapenda kusema kwamba madai yake ni ya kweli, mimimwenyewe nilifika katika Mkoa wa Ruvuma na tuliongea nawakulima walithibitisha hilo. Kilichotokea mwaka jana kamaunavyokumbuka, ndiyo ulikuwa mwaka wa kwanza kutumia

Page 26: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

mfumo huu wakulima wenyewe kwenda kuuza kahawa yaoMoshi kupitia vyama vyao vya ushirika. Kwa hiyo, kahawa ilewalivyokoboa na kuipeleka mnadani ilichelewa sana kuuzikakutokana na anguko kubwa la bei katika soko la dunia nakatika soko la mnada hapa nchini. Kwa sababu waliendakuuza wenyewe, ilikuwa hamna namna nyingine lazimawasubiri mpaka kahawa iuzwe ndipo walipwe. Hata hivyo,kadiri watakavyoendelea kuuza kwenye mnada ndivyo hivyowakulima wataweza kulipwa pesa zao kwa kuzingatia namauzo kwenye mnada.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la piliamesema kwamba tumejipangaje. Mwaka huu tumejipangakupeleka minada hiyo katika kanda zao lakini pili ni kuruhusuwakulima wenyewe kupitia vyama vyao vya ushirika kamawakipata soko la moja kwa moja kuuza nje ya nchi tutatoavibali hivyo ili wauze moja kwa moja. Kwa taarifa tu nikwamba mpaka sasa tumeshapata wanunuzi ambao wapotayari kuingia mkataba na Serikali kwa ajili ya kuuza kahawahiyo kupitia mnada wa moja kwa moja (direct export market)kwa ajili ya kahawa hiyo na tayari mahitaji ya wanunuzi waleni makubwa kuliko uzalishaji uliopo nchini.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Selasini,Mheshimiwa Nape na Mheshimiwa Bulembo.

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Zao la kahawa lina matatizo makubwa sana nchinzima na matatizo yanayolikabili ni pamoja na pembejeona bei yenyewe ya kahawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi hapa Dodoma tulikuwana kikao cha wadau na Mheshimiwa Waziri uliongea vizurisana, uzalishaji unapungua kila mara na maeneo menginekwa mfano kwangu kule Rombo wanaamua kung’oakahawa ile ya zamani wanapanda ndizi na kabichi. Je, nimkakati gani ambao Serikali inao kuwasaidia wakulima ilikunyanyua kiwango cha uzalishaji wa kahawa yetu ambayokatika soko la dunia inasemekana ni kahawa tamu sanaukilinganisha na kahawa kutoka maeneo mengine?

Page 27: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, kwa kifupi ajiandaeMheshimiwa Nape, Mheshimiwa Bulembo na MheshimiwaMaftaha.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA):Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Napenda kujibu swali lanyongeza la Mheshimiwa Selasini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, anataka kujua Serikali tunamkakati gani wa kuongeza tija na uzalishaji wa zao la kahawaili kuvutia bei nzuri kwa wakulima. Mkakati wa kwanza nikwamba sasa hivi tupo kwenye mazungumzo ya makampuniambayo yanatengeneza mbolea kama OCP kutokaMorocco ili kujenga kiwanda kikubwa cha mbolea hapanchini ili kurahisisha upatikanaji wa mbolea na pembejeozingine kwa ajili ya kupunguza gharama za uzalishaji kwawakulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kupitia Shirika letu laMaendeleo la Taifa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo,tunawawezesha wakulima kwa kuwapa mikopo na Serikaliinadhamini zaidi ya asilimia 80 ya matrekta na nyenzo zingineza kilimo kwa ajili ya kupunguza gharama za uzalishaji kwawakulima. Lengo ni kuongeza tija na uzalishaji, kamaalivyosema tuna miaka zaidi ya kumi hatujaweza kuongezauzalishaji wa kahawa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kifupisana, Mheshimiwa Nape.

MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo lanyongeza. Pamoja na kupongeza ziara nzuri ya MheshimiwaRais Magufuli kwa baadhi ya Mikoa ya Kusini ambayo inalimakorosho, Serikali itakubaliana na mimi kama ilivyotokeakwenye kahawa mabadiliko ya mfumo wa ununuzi wakorosho yameathiri mapato ya Halmashauri ambazo zilikuwazinategemea ushuru wa korosho. Halmashauri nyingi kwaasilimia 70 mpaka 80 zilikuwa zinategemea mapato haya.Serikali ipo tayari kufanya tathmini ya madhara

Page 28: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

yatakayojitokeza baada ya maagizo ya Mheshimiwa Raiskwamba pesa hizi zisidaiwe na hivyo kuangalia namna yakufidia ili hizi Halmashauri zisiathirike zaidi? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA):Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali moja lanyongeza la Mheshimiwa Nape, Mbunge wa Mtama, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la msingi anasemakwamba, je, Serikali ipo tayari kufanya tathmini ya atharizi l izopatikana kwa kushuka mapato ya Serikali yaHalmashauri? Kwanza nichukue nafasi hii kusema kwambaSerikali haijabadili mfumo wa ununuzi wa korosho hapa nchi.Kama mnavyofahamu tuliingia kwenye mfumo huo baadaya wakulima wenyewe kukataa kuuza katika mnadauliokuwa halali kwa wanunuzi wale kutokana na bei ambayohaikuwavutia zaidi ya minada mitatu minne. Kama Serikalitusingeweza kuangalia hali ile iendelee ndiyo maana tuli-intervene ili kuhakikisha wakulima hawa wanapata bei nzuriwanayostahili. Wakati ule tunaingia tulikuwa tunafahamu beini ndogo lakini tulienda kuwalipa wakulima bei ya Sh.3,300ambayo ilikuwa huwezi kuipata mahali popote duniani zaidiya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, swali lake la kamatupo tayari kufanya tathmini, napenda kusema kwamba tupotayari na tumeshaanza kufanya tathmini hiyo lakini mapatoyale ya Halmashauri ni ya Serikali na iliyolipa ni Serikali, kwahiyo, Serikali haiwezi kumlipa Serikali mwenzie. Msimu ujaotutajipanga vizuri na mfumo utakuwa kama ulivyokuwa,mapato ya Halmashauri watayapata kupitia mfumoutakaokuwepo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Bulembo.

MHE. ALHAJ ABDALLAH M. BULEMBO: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Kutokana na swali la msingi,

Page 29: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

niipongeze Wizara ya Kilimo na Waziri Mkuu kwa kaziwaliyoifanya Kagera. Wakulima wa kahawa Mkoa wa Kagerawa Muleba, Misenyi na Bukoba Vijijini kupitia KDCU na KCUmpaka leo kuna ambao hawajalipwa malipo yao yakupeleka kahawa KDCU na KCU. La pili, bado kuna wakulimandani wana kahawa…

MWENYEKITI: Swali ni moja tu Mheshimiwa.

MHE. ALHAJ ABDALLAH M. BULEMBO: MheshimiwaMwenyekiti, naomba Serikali itoe tamko kwa wale wakulimaambao hawajalipwa haki yao, ni lini watalipwa haki yao?(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA):Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongezala Mheshimiwa Alhaj Abdallah Bulembo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kuna baadhi yawakulima waliouza kupitia Vyama vya Ushirika vya KCU naKDCU hawajalipwa malipo yao mpaka sasa hata wale waTarime Vijijini katika Mkoa wa Musoma. Kama nilivyojibukwenye swali la msingi, walioenda kuuza kahawa ile niwakulima wenyewe kupitia vyama vyao vya ushirika kwenyemnada wa Moshi, kwa hiyo watalipwa baada ya kahawayao kuuzwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilichotokea katika msimuwa mwaka jana kahawa ilianguka sana sokoni kwa hiyowakulima wale waliona siyo busara kuuza kwa bei ya chinikuliko gharama za uzalishaji walizoingia. Pia, kahawa hiiambayo ikikobolewa inatoka madaraja zaidi ya matano,wakati mwingine inachelewa kwa sababu imeuzwa darajamoja, madaraja mengine hayajauzwa. Kwa hiyo, wanasubiriili kuuza kahawa yote na kwenda kuwalipa wakulima nawanachama wao. Kwa hiyo, naomba waendelee kuwa nasubira kwa sababu kahawa hiyo wameuza wenyewe kilawanapouza watalipwa.

Page 30: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Bulembo kuwa nasubira, Mheshimiwa Maftaha.

MHE. MAFTAHA A. NACHUMA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Kumekuwa na utaratibu wa hizi AMCOSzetu kuajiri ama kutokuwa na vigezo vya wale ambaowanaajiriwa kwamba hawawekewi elimu ni kiwango ganina kwa kiasi kikubwa wahasibu ndiyo wanakuwa ni watupekee wenye elimu kiasi ambacho kinapeleka kufanyahujuma nyingi sana kwenye hizi AMCOS. Naomba kujuaSerikali ina mkakati gani kuhakikisha kwamba wale ambaowanafanyia kazi hizi AMCOS wanawekewa vigezo vya kielimuili wakulima wasiweze kuibiwa kama ilivyo hivi sasa? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu yakoni mazuri sana lakini fanya kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA)Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la MheshimiwaMaftaha, Mbunge wa Mtwara Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza Serikali tulishaanzampango huo tangu msimu uliopita kwa mfano Chama Kikuucha Ushirika Tunduru tulianza kuajiri Wahasibu wenye degreemoja na kuendelea kwa ajili ya kuongoza vile vyama vyaushirika. Utaratibu ule tutaendeleza nchi nzima kupitia vyamavyote vya ushirika ili tupate Wahasibu wenye weledi ili kuwezakuwahudumia wakulima wetu.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana swali la Mheshimiwa Conchesta Leonce Rwamlaza.

Na. 94

Ujenzi wa Masoko ya Nkwenda na Murongo

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA aliuliza:-

Serikali ilikuwa na mradi wa kujenga masoko katikaeneo la Nkwenda na Murongo katika Wilaya ya Kyerwa lakini

Page 31: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

masoko hayo hayajakamilika na yametelekezwa. Je, Serikaliilikuwa na malengo gani kujenga masoko hayo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA)alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waKilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa ConchestaLeonce Rwamlaza, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, masoko ya Nkwenda naMurongo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ni kati yamasoko matano ya kimkakati yaliyopangwa kujengwakupitia Mradi wa Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo Wilayani(District Agricultural Sector Investment Project – DASIP) naujenzi ulianza kutekelezwa mwaka 2006/2007 hadi mwakaDesemba, 2013. Masoko mengine yapo katika Halmashauriza Busoka (Kahama), Kabanga (Ngara) na Sirari (Tarime).Mradi huo uligharamiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrikana Serikali ya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la ujenzi wa masokohayo ya kimkakati ilikuwa ni kuanzisha mfumo thabiti wamasoko utakaoongeza tija na pato kwa wakulima ndani yaWilaya husika. Mfumo huu ulijenga mazingira wezeshikibiashara katika maeneo ya mpakani ili kurahisisha biasharana majirani zetu na kuinua hali za kiuchumi za wananchi wamaeneo hayo na uchumi wa taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi mradi wa DASIPunafungwa Desemba 2013/2014, kazi ya ujenzi wa masokohayo ilikuwa haijakamilika na yalikuwa katika hatuambalimbali za ujenzi. Kwa kuzingatia umuhimu wa masokohayo ya kimkakati katika Halmashauri husika, Serikaliimepanga kukamilisha ujenzi wa masoko hayo na menginenchini kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya KilimoAwamu ya Pili (ASDP II). Katika bajeti ya mwaka 2019/2020

Page 32: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

Serikali imetenga shilingi bilioni 2.9 kuendelea na ujenzi wamasoko hayo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Conchesta.

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuulizamaswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, Mhandisialiyekuwa anasimamia kujenga Soko la Nkwenda alikuja naFuso mbili akahamisha nondo, mabati na saruji akidaianapeleka vifaa hivyo vya ujenzi katika Soko la Sirari katikaMkoa wa Mara na Serikali ina taarifa ya tuhuma za huyuMhandishi. Je, ni hatua zipi zilichukuliwa dhidi ya Mhandisihuyu ambaye kwa kweli alikuwa kikwazo katika ukamilishajiwa soko hilo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa katikamajibu ya Serikali imesemwa kwamba masoko hayayalijengwa kimkakati ili kuweza kusaidia wananchi kufanyabiashara na nchi zilizo jirani na maeneo ambayo yamejengwamasoko hayo. Je, sasa ni lini Serikali itayakamilisha? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa kifupi naajiandae Mheshimiwa Gekul.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA)Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili yanyongeza ya Mheshimiwa Conchesta Rwamlaza, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanzaanasema kwamba huyu Mhandisi alipeleka magarikuhamisha vitu hivyo na kwamba Serikali tunayo taarifa naanataka kujua kwamba tumechukua hatua gani. Mpakasasa tulishavielekeza vyombo vyetu vya ulinzi na kiuchunguzikuendelea kuchunguza tuhuma na jinai hiyo ili ikithibitikaamefanya jambo hili hatua za kisheria zitachukuliwa dhidiyake.

Page 33: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili ni lini masokohayo yatakamilika, kama nilivyojibu kwenye swali lake lamsingi, kwenye bajeti hii tumetenga zaidi ya shilingi bilioni2.9, Waheshimiwa Wabunge mkitupitishia harakaiwezekanavyo kuanzia Julai 1, tutaanza kutekeleza ujenzi wamasoko hayo yote.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Gekul.

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niipongeze Serikalina niishukuru kwa moyo wa dhati kwa kutusaidia kutujengeajengo kubwa la NFRA pale Babati kwa ajili ya kununuamahindi na kuyachakata. Bahati mbaya mwaka huu tanguJanuari mvua hazinyeshi Kanda ya Kaskazini na hali si nzuri,hatuna maharage wala mahindi. Naomba nifahamu Serikaliimejipanga vipi kwa ajili ya kukabiliana na hali hii ambayowananchi wanakwenda kukabiliana nayo ya ukosefu wamahindi na maharage ili wananchi wetu wapate mazaohayo kwa bei rahisi na wasiingie katika baa la njaa?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, wewe mzoefujibu kwa kifupi sana.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA):Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Mheshimiwa Gekulanataka kujua kwamba Serikali tumejipanga vipi katikakukabiliana na tishio la upungufu wa chakula nchini kutokanana ukame uliopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kwanza tumetengashilingi bilioni 15 kupitia Wakala wetu wa Taifa (NFRA) kwakuendelea kununua mahindi kwa ajili ya kuyahifadhi kwa ajiliya kuja kuyasambaza au kupeleka sehemu ambazo zitakuwana mahitaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia sasa hivitumeshawaelekeza wataalam wetu wamesambaa nchi

Page 34: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

nzima kufanya tathmini ya kina kujua athari iliyoletwa namabadiliko ya tabianchi hususan huu ukame ili kujua athariiko kiasi gani ili tuweze kuongeza mikakati mingine. Piatumetenga zaidi ya shilingi bilioni tisa kupitia Bodi yetu yaNafaka na Mazao Mchanganyiko kuendelea kununuamahindi na mazao mengine kukabiliana na hali hiyo.

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na Wizara yaMambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Jaku Hashim Ayoub.

Na. 95

Uchakavu wa Vituo vya Polisi – Unguja na Pemba

MHE. JAKU HASHIM AYOUB aliuliza:-

Kumekuwa na kilio cha uchakavu wa vituo vya polisikwa upande wa Unguja na Pemba:-

(a) Je, ni vituo vingapi vipya vya polisi vilivyojengwakwa upande wa Unguja na Pemba?

(b) Je, vituo hivyo vimejengwa na kampuni gani na nivigezo gani vilivyoangaliwa katika ujenzi wa vituo hivyo?

(c) Je, ni lini Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri pamojana Katibu Mkuu wa Wizara watafuatana nami kwendakuviona vituo hivyo vilivyochakaa?

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali laMheshimiwa Jaku Hashim Ayoub, Mbunge wa Baraza laWawakilishi, lenye sehemu (a), (b) na (c), kwa pamoja, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mikoa ya Unguja naPemba vituo vingi vimejengwa au kukarabatiwa katika miakatofauti, vikiwemo Vituo vya Mwembe Madafu na Mbwenikatika Mkoa wa Mjini Magharibi, Kituo cha Mchanga Mdogo

Page 35: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

Mkoani Kaskazini Pemba, Vituo vya Chwaka na JambianiMkoa wa Kusini Unguja na Vituo vya Chakechake naMtambile Mkoa wa Kusini Pemba. Aidha, kuna ujenziunaoendelea kwa sasa wa Vituo vya Chukwani, Dunga naMkokotoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, majengo mengi ya vituo hivivya polisi ujenzi ulikuwa ni wa ushirikiano wa wananchi naJeshi la Polisi. Hata hivyo, tunatambua mkandarasi aitwayeAlbatina Construction Company Ltd anayejenga Kituo chaPolisi Mkokotoni ambaye kazi yake bado inaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua kuwepona uchakavu wa vituo vingi vya polisi katika Mikoa ya Ungujana Pemba kama vile vituo vya Mkoani Pemba, Kengeja,Micheweni, Konde, Mahonda, Nungwi, Kiwengwa na Kibojeambapo hali ya kifedha ikiruhusu vitakarabatiwa. Viongoziwa Wizara wataambatana na Mheshimiwa Mbunge JakuHashim Ayoub tarehe 3/7/2019 kwenda kuviona vituo hivyovilivyochakaa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Jaku.

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Kwanza nimpe pole sana Mheshimiwa Wazirikwa kuvamiwa Kituo chake cha Polisi cha Madema…

MWENYEKITI: Waheshimiwa, muda wetu umekwisha.Mheshimiwa Jaku.

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Tarehe 25 Julai, 2017, naomba kunukuu Hansard,“taratibu hizo zilishafanyika kama nilivyokwambia sasa. Tarehe9 Novemba, “Serikali inatambua deni hilo.” Tarehe 8Novemba, 2017 mwaka wa Fedha 2017, “Jeshi la Polisilimetenga jumla ya shilingi bilioni 2.2 kwa ajili ya kupunguzamadeni ikiwemo mkandarasi.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naona ni aibu kwaSerikali yangu kupata aibu na hili deni ni la muda mrefu. Je,

Page 36: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

Mheshimiwa Waziri, hesabu hata ulipochaguliwa weweJimboni kwako ulianzia kwa kura moja ukafika hapa. Kamamimi, Serikali yangu kupata aibu nami ninaipenda nikotayari…

MWENYEKITI: Mheshimiwa, uliza swali.

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: …niko tayari kuanzakuchangia shilingi milioni moja kwa ajili ya kituo. Je,Mheshimiwa Waziri yuko tayari kuchukua shilingi milioni moja,kupokea mchango huu ili tufuatane kupeleka deni hilo nahizi hapa? Maana yake deni limeshakuwa la muda mrefu.Yuko tayari kupokea shilingi milioni moja kufuatana namikupeleka hizi fedha za deni? (Kicheko/Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Jaku, michango ni nje yaBunge. Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaMwenyekiti, katika Ilani hii ya CCM ujenzi wa vituo vya Polisina makazi ya Askari tumeweka utaratibu kwamba tutahusishawadau. Ninashukuru sana wewe Bungeni kujitokeza kuwamdau kwa mujibu wa ilani hii. Hivyo naomba mchango wakouuwasilishe kwa Inspekta Jenerali wa Polisi ili tuendelee naujenzi wa vituo vya Polisi hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ni kweli kabisa kwambadeni la huyu Mkandarasi limekuwa la siku nyingi. NimhakikishieMheshimiwa Jaku, ambaye najua akifuatilia jambo lake niking’ang’anizi, ni moto wa kuotea mbali; na kwa kweli sikusiyo nyingi hatutakubali jambo analolisema kwamba Serikaliyetu inatiwa aibu. Ndiyo maana Wakandarasi wengi nchiniwanapenda kufanya kazi na Serikali na Serikali yetu inalipamadeni yake na deni lake limeshahakikiwa, awe na subirawakati wowote tutaweza kumlipa Mkandarasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Nkamia.

Page 37: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

MHE. JUMA S. NKAMIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Naomba niulize swali mojadogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Chemba ni mojakati ya wilaya mpya. Tumeanza kujenga kituo cha Polisi kwasababu huduma nyingi za Polisi zinapatikana kwenye Wilayamama ya Kondoa: Je, Serikali ina mchango gani kuhakikishakwamba tunakamilisha ujenzi wa Kituo cha Polisi paleChemba ambao tayari tumeuanza?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, mna mpango gani?Jibu kwa kifupi sana.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaMwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la MheshimiwaJuma Selemani Nkamia, Mshabiki wa Simba namba moja,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jeshi la Polisi katika muundowake na utoaji wa huduma, tunayo Mikoa 35 ya Kipolisi,tunazo Wilaya 182 za Kipolisi na pia tunazo Tarafa 610 zaKipolisi na tuna Kata na Shehia 4,410. Kwa hiyo, tunaompango mkakati kuhakikisha kwamba huduma hizizinakwenda kwenye maeneo yote hayo; na bado tuna mikoamipya na wilaya mpya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie MheshimiwaJuma Nkamia kwamba Wilaya ya Chemba ni miongoni mwawilaya ambazo mikakati yetu ndani ya Jeshi la Polisitunakwenda kujenga kituo cha Polisi katika Wilaya yaChemba.

MWENYEKITI: Ahsante. Jibu hilo linakwenda kwaWabunge wote ambao majengo yao hayajajengwa.

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasil iano,Mheshimiwa Jacqueline Ngonyani.

Page 38: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

Na. 96

Barabara ya Likuyufusi – Mkenda (Km 123)

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI aliuliza:-

Barabara ya Likuyufusi – Mkenda yenye urefu wakilometa 123 inayounganisha nchi mbili za Tanzania naMsumbiji, bado haijaanza kujengwa kwa kiwango cha lami:-

Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara hiyo kwakiwango cha lami?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, napenda kujibu swali laMheshimiwa Jacqueline Ngonyani Msongozi, Mbunge wa VitiMaalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Likuyufusi –Mkenda yenye urefu wa kilometa 123 ni barabara kuuinayounganisha nchi mbili za Tanzania na Msumbiji nainahudumiwa na Wizara yangu kupitia Wakala wa BarabaraNchini (TANROADS).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kwa kutambuaumuhimu wa barabara hii iliamua kuifanyia upembuzi yakinifuna usanifu wa kina kwa lengo la kuijenga barabara hiyo kwakiwango cha lami, kazi ambayo ilikamilika mwaka 2013. KatikaMwaka wa Fedha 2018/2019 shilingi bilioni 5.86 zimetengwakwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwangocha lami.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuwepo kwa uchimbaji nausafirishaji wa makaa ya mawe katika Kijiji cha Muhukurukilicho kilometa 74 kutokea Songea katika barabara hiyo,kumesababisha kuongezeka kwa magari mengi na mazitoyanayobeba makaa ya mawe. Kufuatia hali hiyo, Serikali

Page 39: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

kupitia Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) imeamuakufanya mapitio ya usanifu wa kina (Design Review) ili kukidhimahitaji halisi yaliyojitokeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kazi hiyokukamilika, Serikali itaendelea kutafuta fedha zaidi kwa ajiliya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ngonyani.

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swalimoja dogo la nyongeza, lenye sehemu (a) na (b) kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuriya Serikali, naomba nichukue nafasi hii kumpongeza piaMbunge wa Jimbo la Peramiho, dada yangu, MheshimiwaJenista Mhagama, kwa namna ambavyo amekuwaakifuatil ia ujenzi wa barabara hii na hata alipokujaMheshimiwa Rais, alijaribu kusema pale ili barabara hii iwezekujengwa. (Makofi)

(a) Swali langu la kwanza; ni kwa nini Serikaliinachukua muda mrefu sana kufanya upembuzi yakinifu lakinipia na usanifu wa kina? Barabara hii imechukua karibu miakakumi kupitia maneno hayo ya upembuzi na usanifu. Ni liniSerikali itamaliza upembuzi huu na usanifu huu ili barabarahii ianze kujengwa? (Makofi)

(b) Swali la pili; licha ya Serikali kuonesha kwambaimetenga shilingi bilioni 5.86, lakini fedha hizi hazikuwezakwenda kwa mwaka 2018/2019: Je, Serikali haioni kwambakutokupeleka fedha hizi inaendelea kucheleweshamaendeleo kupitia barabara hii kwa wananchi wa Mkoa waRuvuma, hususan Jimbo la Peramiho? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, kwa kifupi sana,muda wetu umekwisha.

Page 40: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Mwenyekiti,uniruhusu tu nimpongeze Mheshimiwa Jacqueline, lakininimpongeze Mbunge wa Peramiho kwa kufuatilia kwasababu amekuwa akifuatilia sana jambo hili. Nimhakikishietu Mheshimiwa Mbunge mwuliza swali kwamba inachukuamuda mrefu kwa sababu kwanza mtandao wa barabara nimkubwa, mahitaji ya ujenzi ni makubwa na tunaendeleakutafuta fedha na kutenga fedha. Hata mwaka unaokujatutaliomba Bunge lako liweke fedha kwa ajili ya ujenzi wabarabara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunawasiliana na wenzetuwa Wizara ya Fedha. Tukipata fedha tu mara mojatutatangaza na kuanza kujenga barabara hii. Kwa hiyo, kwamajibu hayo, Mheshimiwa Jacqueline avute subira kidogo,tumejipanga vizuri, mahitaji ni makubwa, tunakuja Peramihokuhakikisha kwamba tumewaunga wananchi wa…

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Kemi.

MHE. KEMILEMBE J. LWOTA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi ya kuweza kuuliza swali dogo lanyongeza. Barabara ya Nyakato Steel – Igombe, kilometa 18na Barabara ya Mwaloni – Kirumba, kilometa 1.2 zimekuwazikisuasua na ujenzi wake kwa muda mrefu sana. MheshimiwaAngeline Mabula, amekuwa akifuatilia barabara hizi kwamuda mrefu lakini bado hatujapata majibu sahihi ya Serikali.Ni lini sasa barabara hizi zitakamilika na wananchi wa Mkoawa Mwanza, hususan Wilaya ya Ilemela waweze kupatabarabara safi na salama?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, kwa kifupi. JiandaeMheshimiwa Nsanzugwanko.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Mwenyekiti,natambua changamoto za barabara za Ilemela, nami

Page 41: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

nimekwenda, nimeona. Nitoe tu maelekezo na wito kwaMameneja wetu kule kwenye Mkoa wa Mwanza kwambawasimamie kwa ukaribu nami nitakwenda kuhakikishakwamba maeneo haya; na yapo maeneo siyo haya tualiyoyataja Mheshimiwa Mbunge, yapo maeneo mengikwenye Jimbo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sanaMheshimiwa Angeline Mabula kwa sababu amekuwaakifuatilia sana, ilinichukua siku nzima, mtandao ni mkubwasana kwenye Jimbo lake, mjini lakini…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu mazuri namuhimu, fanya ziara naye.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru, nitakwenda. (Makofi)

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: MheshimiwaMwenyekiti, nami naomba niulize swali dogo la nyongeza.

MWENYEKITI: Jiandae Mheshimiwa Mama Salma.

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: …barabara yakutoka Tabora kwenda Kigoma ambayo inatuunganisha naTabora bado haijakamilika; na kipande cha kutokaMalagarasi mpaka Uvinza ambacho kilikuwa na Mkandarasiwa Abu Dhabi Fund tumesikia kuna matatizo ya kiufundi: Je,Mheshimiwa Waziri unasema nini juu ya jambo hilo?Vinginevyo barabara hii haitakamilika mpaka tufike mwaka2020. (Makofi)

MWENYEKITI: Kwa kifupi Mheshimiwa Waziri.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Mwenyekiti,Mheshimiwa Nsanzugwanko anafahamu, tumezungumzamara nyingi sana juu ya barabara hizi. Niseme tu kwa ufupi,Chagu – Kazilambwa pamoja na barabara ya Malagarasi –

Page 42: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

Uvinza zitakamilisha mtandao wa barabara kutoka Taborakwenda Kigoma tukikamilisha vipande hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutazungumza tu naMheshimiwa Mbunge tuone kama kuna changamoto, basitujue nini kinachoendelea. Kwa kifupi tunakwenda kujengabarabara hii. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mama Salma.

MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Barabara za lami hugharimu pesa nyingi zaSerikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mara tubarabara hizo zinapojengwa, hubomolewa na kupitishwamiundombinu mingine, hatimaye hazirejeshwi katika uborawake:-

Je, Serikali inatuambia nini juu ya jambo hili? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweliujenzi wa barabara unachukua fedha nyingi, lakini nisemetu shughuli zozote zitakazohusisha kukata barabara lazimazifanyike kwa mujibu wa sheria. Kwa hiyo, kama kuna mtuanakata barabara na kuacha uharibifu ni makosa. Naminielekeze viongozi wote, Mameneja wote wa Mikoa; mtuambaye atafanya shughuli za kibinadamu na kuharibubarabara bila kurejesha kwa ubora wake na bila kupata kibalikwa mujibu wa sheria ni makosa, wachukue hatua kwamujibu wa sheria.

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa muda wetumdogo. Tunaendelea na Wizara ya Fedha na Mipango,Mheshimiwa Juma Othman Hija.

Page 43: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

Na. 97

Kushuka kwa Thamani ya Shilingi

MHE. JUMA OTHMAN HIJA aliuliza:-

Thamani ya Shil ingi ya Tanzania inaendeleakuporomoka kila siku, kuporomoka huko kunachangia kwakiasi fulani ugumu wa maisha kwa wananchi wa kawaidakatika kupanga mipango yao ya kimaisha:-

Je, Serikali ina mkakati gani ya kudhibiti mporomokohuo?

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waFedha na Mipango napenda kujibu swali la MheshimiwaJuma Othman Hija, Mbunge wa Tumbatu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, thamani ya shilingi dhidi yasarafu nyingine hutegemea nguvu za soko, yaani ugavi namahitaji. Sababu za kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi yafedha za kigeni ni pamoja na tofauti ya mfumuko wa bei katiya Tanzania na nchi wabia katika biashara, mauzo kidogonje ya nchi, mahitaji makubwa ya kuagiza bidhaa na hudumakutoka nje; kupungua kwa misaada na mikopo kutoka nje;kuimarika kwa fedha za kigeni kutokana na kuimarika kwauchumi wa nchi wabia katika biashara na kuzuka kwabiashara ya kuhisia na kuotea ya sarafu za kigeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha miakamiwili iliyopita, sababu zote hizi hazikuwepo na hivyo thamaniya shilingi yetu dhidi ya Dola ya Marekani ilikuwa tulivuikilinganishwa na sarafu nyingine dhidi ya Dola ya Marekani.Kwa mfano, thamani ya shilingi ilipungua kwa wastani wa 2%kwa mwaka 2017/2018 na 2016/2017 ikilinganishwa nawastani wa 22% mwaka 2015/2016.

Page 44: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

Mheshimiwa Mwenyekiti, kiujumla shilingi ilikuwa imaraikilinganishwa na sarafu nyingine kama vile Franc ya Rwandailiyopungua kwa wastani wa 5% na shilingi ya Ugandailiyoshuka kwa 3.8% katika kipindi kama hicho. Utulivu wathamani ya shilingi ulitokana na utekelezaji thabiti wa seraza fedha na bajeti pamoja na kudhibiti mfumuko wa bei.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuimarisha utulivu wathamani ya shilingi dhidi ya fedha za kigeni, Serikaliinatekeleza mikakati ifuatayo:-

(i) Kuhakikisha kuwa ongezeko la ujazi wa fedhalinaendana na ukuaji wa shughuli za uzalishaji;

(ii) Kuongeza uzalishaji wa bidhaa na huduma ndaniya nchi;

(iii) Kuongeza mauzo ya bidhaa na huduma nje yanchi, na;

(iv) Kudhibiti hali ya wasiwasi katika soko la fedhaza kigeni inayosababishwa na hisia pamoja na biashara yakuotea ambapo Benki Kuu hununua na kuuza fedha za kigenikatika soko la jumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuliarifu Bungelako Tukufu kwamba jukumu la kuimarisha thamani ya shilingini shirikishi na pia lina wadau wengi na hivyo kila mmojaanahitajika kushiriki kwa nafasi yake ili kuleta mafanikio kwanchi. Aidha, wadau wakuu ni Serikali pamoja na wananchi.Serikali ina majukumu makuu mawili:-

(i) Serikali kupitia Benki Kuu ina jukumu la kutekelezana kusimamia Sera ya Fedha ili kudhibiti mfumuko wa bei,viwango vya kubadilisha fedha na ujazi wa fedha katika soko;na

(ii) Kuandaa na kusimamia sera thabiti za kibajeti,kuhakikisha nchi inakuwa na amani na utulivu na kujengamiundombinu wezeshi kwa ajili ya kuchochea uzalishaji.

Page 45: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, wananchi ambaondio wawekezaji, wana jukumu la kuzalisha kwa wingi bidhaana huduma mbalimbali hususan zile zinazoipatia nchi fedhaza kigeni na/au zinazoipunguzia nchi mzigo wa mahitaji yafedha za kigeni.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Othman Hija.

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Namshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yakemazuri na ya kutosheleza kabisa, lakini nina swali moja dogola nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni Serikali imekuwana zoezi la kuyafungia maduka ya Bureau De Change nchinzima. Je, zoezi hili ni miongoni mwa mikakati ya kuimarishafedha yetu au ni kwa madhumuni gani? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa kifupisana.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, napenda kujibu swali moja la Mheshimiwa JumaOthman Hija, Mbunge wa Tumbatu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama alivyouliza je, ulikuwani mkakati wa kuhakikisha thamani ya fedha yetu. Kamanilivyoeleza kwenye jibu langu la msingi moja ya kazi za benkikuu ni kuhakikisha kwamba thamani ya fedha yetu inakuwaimara na katika mikakati ya kuhakikisha hilo, ni kuhakikishakunakuwa na usimamizi imara na madhubuti wa madukayetu ya kubadilisha fedha na hilo ndilo lilikuwa lengo la zoezilililofanyika.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, muda wetuumekwisha, tumeshaongoza dakika ishirini ya maswali na hiitunamwomba Mheshimiwa Waziri wa Nchi, MheshimiwaJenista, mara nyingi Kiti huwa kinasema majibu ya Serikali nimarefu mno, jaribuni kuyapunguza, mnajibu vizuri very clear,

Page 46: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

lakini yanakuwa ni marefu mno, jibu moja linachukua dakikanne, kwa hiyo, tunaomba mjaribu kulitazama hilo.

Wageni waliopo Bungeni asubuhi hii, wageni waliopojukwaa la Spika Wageni 38 wa Mheshimiwa JanuaryMakamba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira) ambao ni Mhandisi JosephMalongo, Katibu Mkuu; Balozi Joseph Sokoine, Naibu KatibuMkuu; Profesa William Mwegoha, Mkurugenzi Mazingira; Dkt.Gwamaka Mafwenga, Mkurugenzi Mkuu NEMC; ProfesaEsnath Chaggu, Mwenyekiti wa Bodi NEMC; Ndugu JumaMkomi, Katibu wa Makamu wa Rais; Ndugu Paul Sangawe,Mkurugenzi – Sera na Mipango; Ndugu Sifuni Msangi, KaimuMkurugenzi Muungano; Ndugu Mosoud Balozi, Msaidizi waMakamu wa Rais, Mambo ya Nje; Ndugu Nehemia Mandia,Msaidizi wa Makamu wa Rais siasa; wameambatana naviongozi wa Maafisa wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Ofisihiyo. (Makofi)

Wageni wa Waheshimiwa Wabunge ni wageni wawiliwa Mheshimiwa Angelina Mabula, Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ambao ni Askofu RichardMsingwa kutoka Jijini Mwanza na Engineer Marko Kotta,kutoka Jijini Dodoma, Karibuni. (Makofi)

Mgeni wa Mheshimiwa Japhary Michael kutokaMkoani Kilimanjaro, Mchungaji Yohana Mbogo. Karibu.(Makofi)

Wageni 79 wa Mheshimiwa Fatma Toufiq ambao niwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma wakiongozwana Ndugu Mashaka Mahangi, Karibuni Bungeni. (Makofi)

Wageni 35 wa Mheshimiwa Anna Lupembe ambaoni wanamaombi wa Mkoa wa Dodoma wakiongozwa naMchungaji Obadia Chitalya, Karibuni. (Makofi)

Wageni 31 wa Mheshimiwa Lolesia Bukwimba ambaoni kwaya ya ushindi kutoka Jijini Dodoma wakiongozwa naBishop Julius Nassary, Karibuni. (Makofi)

Page 47: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

Wageni watatu wa Mheshimiwa Zainabu Mndolwaambao ni watoto wake kutoka Jijini Dar es Salaam nduguAhmed Baabad, Ndugu Ayman Baabad na Ndugu HairatSweleh. Karibuni. (Makofi)

Wageni 42 wa Mheshimiwa Augustine Vuma ambazoni wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)wakiongozwa na Ndugu Lutakonya Essau. Karibuni. (Makofi)

Mgeni wa Mheshimiwa Vedastus Mathayo ambayeni mjukuu wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, NduguSophia Nyerere. (Makofi)

Mwenyekiti wa ibada ya Chapel ya Bunge,Mheshimiwa Anna Lupembe anaomba kuwatangaziaWaheshimiwa Wabunge wote kuwa, wanatangaziwakuhudhuria ibada katika Chapel ya Pius Msekwa leo siku yaJumanne, tarehe 16 Aprili, mara baada ya kusitisha shughuliza Bunge saa saba mchana. Waheshimiwa Wabunge wotemnakaribishwa. Waziri wa Nchi.

MHE. AIDA J. KHENANI: Mwongozo wa Spika.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mwongozo wa Mwenyekiti.

MWENYEKITI: Waziri wa Nchi, zimeni microphone zenuhizo, kaeni chini, wote zimeni microphones.

HOJA YA KUTENGUA KANUNI

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kutoa maelezo ya Hoja ya KutenguaKanuni za Bunge chini ya Kanuni ya 153(1) ya Kanuni zaKudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016, naomba kutoa hojaifuatayo:-

KWA KUWA tarehe Mosi Aprili, 2019, Kamati ya Kanuniilikutana na kufanya marekebisho katika Nyongeza ya Naneya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Januari, 2016.

Page 48: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

Marekebisho hayo yanalenga kuongeza msukumo, ufanisi nakasi ya kudhibiti ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa kuiwezeshaKamati ya Masuala ya UKIMWI kuwa na jukumu la kusimamiashughuli za Serikali za kudhibiti ugonjwa wa Kifua Kikuu.Jukumu hilo lilikuwa linatekelezwa na Kamati ya Huduma naMaendeleo ya Jamii;

NA KWA KUWA Kamati ya Masuala ya UKIMWI niKamati mahususi yenye jukumu la kusimamia Shughuli zaSerikali kuhusu utekelezaji wa masuala ya UKIMWI; nakwakuwa, ushahidi wa kitakwimu umeonesha mahusianomakubwa baina ya ugonjwa wa UKIMWI na ugonjwa waKifua Kikuu;

NA KWA KUWA Kamati ya Masuala ya UKIMWIimeonesha ufanisi mkubwa katika kusimamia shughuli zaSerikali kuhusu utekelezaji wa sera na mikakati ya kudhibitiugonjwa wa UKIMWI nchini;

NA KWA KUWA Kamati ya Kanuni baada ya kuzingatiauhusiano baina ya ugonjwa wa UKIMWI na ugonjwa wa KifuaKikuu, iliona umuhimu wa kufanya marekebisho ya kifungucha 10 cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu zaBunge kwa lengo la kuwezesha Kamati ya masuala ya UKIMWIkusimamia shughuli za Serikali za kudhibiti ugonjwa wa KifuaKikuu katika nchi yetu ya Tanzania;

NA KWA KUWA marekebisho haya yalifanyika kwamujibu wa Kanuni ya 155(3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge,Toleo la Januari, 2016;

NA KWA KUWA Kanuni 156(1) inakataza marekebishoya Kanuni kuanza kutumika kabla ya kuchapishwa nakuingizwa kwenye toleo la Kanuni za Bunge linalofuata;

NA KWA KUWA Kanuni ya 156(2) inaelekeza kwambaSpika ataagiza Kanuni zilizofanyiwa marekebisho zichapishweupya kwenye gazeti la Serikali kwa madhumuni ya kuingizamabadiliko yaliyofanyika;

Page 49: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

NA KWA KUWA mabadiliko yaliyofanywa ni madogona jambo linalofanya kuwe na uzito mdogo wa kuwa na Toleojipya la Kanuni;

NA KWA KUWA hata bila kuwepo kwa chapisho jipyaupo urahisi wa kufanya rejea ya Kanuni bila ya kuwa na Toleojipya;

NA KWA KUWA mchakato wa kuandaa nakuchapisha toleo jipya la kanuni utagharimu fedha nyingiambazo zinaweza kutumika katika mahitaji mengine;

NA KWA KUWA muda si mrefu kamati ya Kanuni ndaniya Bunge letu Tukufu inatarajia kuanza mchakato wa kufanyamapitio ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016,ambapo inatazamiwa yatakuwepo mabadiliko makubwa yaKanuni na kwamba Kamati itaandaa mapendekezo yamarekebisho ya kanuni ambayo iwapo yatapitishwa naBunge yataingizwa kwenye Toleo Jipya na marekebisho hayoyatachapishwa kwenye gazeti la Serikali.

HIVYO BASI Bunge linaazimia kwamba Kanuni 156(1)na Kanuni ya 156(2) zinazoweka sharti la kuingiza mabadilikoya Kanuni kwenye Toleo jipya la Kanuni na sharti la kuzichapaupya kwenye gazeti za Serikali zitenguliwe ili kuwezeshamabadiliko yaliyofanyika katika kifungu cha 10, NyongezaNane ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016,yaanze kutumika bila kuchapisha Toleo jipya na kulitangazakwenye gazeti la Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kutoa maelezohayo, naomba sasa kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.

MWENYEKITI: Hoja imeungwa mkono, WaheshimiwaWabunge hii Kanuni ni muhimu na hii Kamati ya UKIMWI kwamara ya kwanza imeonesha kazi nzuri sana ndani ya Bungehili, sasa nitawaoji kuhusu mabadiliko haya ya Kanuni.

Page 50: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

MWENYEKITI: Walioafiki wameshinda. Kwa hiyo,marekebisho ya Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu zaBunge, Toleo la 2016 yatakuwa, Kamati ya Masuala ya UKIMWIitatekeleza majukumu yafuatayo:-

(i) Kusimamia utekelezaji ya masuala yanayohusu UKIMWIkatika sekta zote;

(ii) Kusimamia shughuli za Serikali za kudhibiti na kutokomezaugonjwa wa Kifua Kikuu;

(iii) Kufuatilia utekelezaji wa Sera na Mipango ya Serikalikuhusu UKIMWI Kifua Kikuu na udhibiti wa dawa za kulevya;

(iv) Kujadili na kutoa mapendekezo na ushauri kuhusu hatuaza kudhibiti UKIMWI, Kifua Kikuu na dawa za kulevya; na

(v) Kushughulikia bajeti ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzaniana Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa zaKulevya.

Kwa hiyo, sasa Mwenyekiti wa Kamati hiki kitu kinakujakwenu moja kwa moja, muendelee nacho.

Mheshimiwa Lubeleje Mwenyekiti wa Wabunge waMkoa wa Dodoma anawaomba Wabunge wote waDodoma, kuhudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM,Mkoa wa Dodoma, saa tano asubuhi.

Mkuu wa Mfuko wa Faraja Fund Bungeanawatangazia Wabunge wote Wanafaraja,mnakumbushwa kuchangia Mfuko wa Faraja, tafadhaliwasiliana na Joseph Mhagama, Afisa Mtendaji Mkuu. Katibu.

MWONGOZO WA SPIKA

MHE. AIDA J. KHENANI: Mwongozo.

Page 51: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

MWENYEKITI: Waheshimiwa muda wetu leo mdogo,haya nitachukua Mheshimiwa Khenani na Mbarouk wawilitu. Mheshimiwa Khenani.

MHE. AIDA J. KHENANI, Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Naomba Mwongozo wako kwa Kanuni ya 68(7).katika michango ambayo inaendelea ndani ya Bunge kutokakwenye hotuba ya Waziri Mkuu upande huu wa Upinzani,michango yetu kwa maandishi inakuja, lakini kwa maana yavideo hazifiki na zikifika zinakuwa nusu. Sasa linapotokeatatizo kama hilo tumeomba Kiti chako mara kadhaa, ninikinatokea, kama kuna shida ya mitambo ya Bunge tujuekwamba mitambo hiyo inaruka upande wa Opposition tu,lakini upande wa CCM haifanyi kazi hiyo. TunaombaMwongozo wako nini kinasababisha michango yetuisionekane.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mbarouk.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Tanzania tuna Majiji matano, lakini kwa bahatimbaya mambo mengi yamekuwa yakianzia Dar es Salaam,mfano ni suala la vitambulisho hivi vya wajasiriamali, leo katikavyombo vya habari wametangaza kwamba katika Jiji la Dares Salaam, Mgambo wa Jiji wamekuwa wanakamatawafanyabiashara wadogo wadogo hawa na kuwasumbuapamoja na kuchukua bidhaa zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka kujua tuMwongozo wako wakati huku kuna vitambulisho, lakini hapohapo sasa Mgambo wa Jiji nao wamekuwa wanawakamatawafanyabiashara na kuwasumbua, sasa tuelekee wapikwamba umuhimu ni kupata vitambulisho au Halmashauriza Majiji nazo zinakuwa zinang’ang’ania hasa kuwasumbuawafanyabishara kutaka mapato. Naomba Mwongozo wako.

MWENYEKITI: Ahsante nina miongozo miwili,Mwongozo wa kwanza ni wa Mheshimiwa Khenani, hilinitalifuatilia kwa sababu majibu yake sinayo hapa mezani.

Page 52: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

Pia jambo la Mheshimiwa Mbarouk kwa mujibu waKanuni halijatokea ndani ya Bunge leo. Kwa hiyo sinaMwongozo juu ya hilo.

Katibu.

NDG. ATHUMANI HUSSEIN – KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Makamu wa Rais,

Muungano na Mazingira

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa MazingiraMheshimiwa January Makamba.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, baadaya Bunge lako Tukufu kupokea taarifa iliyowasilishwa naMwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara na Mazingira na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumuya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Mapitio ya Utekelezajiwa Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa mwaka 2018/2019;na Malengo ya Ofisi kwa mwaka 2019/2020, naomba kutoahoja kwamba, Bunge lako Tukufu sasa likubali kupokea,kujadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi yaOfisi ya Makamu wa Rais kwa mwaka 2019/2020.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote napendakumshukuru Mwenyezi Mungu aliyenijalia afya, uzima nakuniwezesha kuwasilisha hotuba hii. Napenda sanakumshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kuniamini katikanafasi hii na kuendelea kuongoza vizuri nchi yetu nakumpongeza kwa mafanikio yaliyopatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumshukuruMakamu wa Rais kwa kutupa miongozo na maelekezoyaliyotuwezesha kutekeleza majukumu yetu katika Ofisi yaMakamu wa Rais, nampongeza pia Mheshimiwa Dkt. Ali

Page 53: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

Mohamed Shein Rais wa Zanzibar kwa kazi nzuri anayoifanyakwa hekima na Busara zake zilizowezesha Muungano wetukudumu. Pia nampongeza sana Mheshimiwa KassimMajaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania kwa hotuba yake kwanza aliyoitoa hapa Bungeambayo imetoa mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwakaujao, lakini pia kwa uongozi wake dhabiti hapa Bungeni napia katika shughuli za kila siku za Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nimpongeze sanaMheshimiwa Spika, Naibu Spika, wewe pamoja na Wenyevitiwenzako kwa kuliongoza Bunge letu vizuri. Napenda vile vilekuwapongeza sana na kuwashukuru Wenyevitiwanaoziongoza wanaotusimamia katika Ofisi ya Makamu waRais pamoja na Makamu Wenyeviti wa Kamati zote mbiliViwanda, Biashara na Mazingira na Katiba na Sheria pamojana Wajumbe wa Kamati hizo kwa kazi nzuri wanazozifanyakwa kushirikiana na sisi kwa kutuongoza na kutushauri, lakinizaidi kwa kupokea na kujadili na kupitisha taarifa yautekelezaji wa mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedhauliopita na makadirio kwa mwaka wa fedha unaokuja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nijadili kuhusumakusanyo na mapato kwa mwaka wa fedha uliopita. Ofisiya Makamu wa Rais haina vyanzo vya mapato. Hata hivyo,Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira hadikufikia mwezi Machi, mwaka huu lilikuwa limekusaya mapatoya jumla ya Sh.10,430,060,727.00.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bajeti iliyoidhinishwa kwamwaka unaoisha wa fedha kwa mwaka 2018/2019, kwaFungu 26, jumla ya Sh.6,485,991,000.00 ziliidhinishwa kwa ajiliya Fungu 26. Hadi mwezi Machi pesa zilizopokelewa niSh.4,572,810,578.05. Kwa Fungu 31 fedha zilizoidhinishwa naBunge Sh.15,065,422,523.28. Hadi mwezi Machi, fedhazilizopokelewa zilikuwa ni Sh.7,937,894,492.78 ambayo ni sawana asilimia 52.7.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ofisi imeendelea kutekelezamajukumu yake kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya

Page 54: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Dira yaMaendeleo ya Nchi yetu kwa mwaka 2020 – 2025, Mpangowa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/2017 – 2020/2021, Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi, Malengoya Maendeleo Endelevu, Sera ya Taifa ya Mazingira, Sheriaya Usimamizi wa Mazingira na maelekezo na miongozombalimbali iliyotolewa na viongozi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijaendelea, niombehotuba yetu iliyogawiwa kwa Waheshimiwa Wabungeiingizwe katika hansard kama hotuba rasmi iliyotolewa naOfisi ya Makamu ya Rais na hapa nasoma muhtasari tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, masuala ya Muungano.Muungano wetu ndiyo utambulisho wa Taifa letu na kielelezocha umoja wetu, bila Muungano hakuna Tanzania. Ili kuuenzina kuimarisha Muungano wetu, ofisi imetekeleza majukumuambayo imekabidhiwa kikatiba na kisheria ya kuratibuutekelezaji wa masuala ya Muungano na kuimarishaushirikiano katika masuala yasiyo ya Muungano kati ya Serikalizetu mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedhaunaokwisha kazi zifuatazo zimefanyika. Kwanza, kuratibuvikao vya kamati ya pamoja; kuratibu utekelezaji wa masualaya kiuchumi, kijamii na kisiasa; kuratibu masuala yasiyo yaMuungano ili kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali zetu mbililakini pia kutoa elimu kwa umma kuhusu Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ya Pamoja. Katikamwaka unaokwisha ofisi iliratibu na kufanya kikao cha Kamatiya Pamoja tarehe 9 Februari, 2019 hapa Dodoma. Kikao hichokilitanguliwa na vikao vya mbalimbali vya Sekretarieti,Makatibu Wakuu pamoja na Mawaziri. Hoja zilizowasilishwakatika kikao hicho ni pamoja na mapendekezo ya utaratibuwa vikao vya Kamati ya Pamoja; Mwongozo wa Ushirikishwajiwa Zanzibar kwenye masuala ya kimataifa; na hojazinazohusu fedha na biashara baina ya Zanzibar na TanzaniaBara.

Page 55: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

Mheshimiwa Mwenyekiti, kikao hicho kilikuwa namafanikio mengi lakini kadhaa ni yafuatayo. Kwanza,tulipitisha utaratibu wa mpya wa vikao vya Kamati ya PamojaKushughulikia Masuala ya Muungano ambapo tulipitishamfumo mpya wenye lengo la kuimarisha na kuongeza ufanisiwa vikao hivi ikiwa ni pamoja na uwezo na urahisi wa kufuatiliamaagizo na maelekezo yanayotolewa na Kamati hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu huu mpya ambaoumepitishwa umeanzisha Kamati mbili za Kamati ya Pamojaambapo ni Kamati ya Fedha, Uchumi na Biashara na Kamatiya Katiba, Sheria na Utawala. Kamati hizi zimepewamajukumu ya kutafuta ufumbuzi wa haraka kwachangamoto zinazohitaji utatuzi wa haraka badala ya kusubirimlolongo mrefu wa kikao cha Kamati ya Pamoja. Pia katikautaratibu huu mpya tumeurasimisha na tumewezeshaMakatibu Wakuu Viongozi kuwa sehemu ya vikao rasmi vyaKamati ya Pamoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya changamotozilizokuwa zinalalamikiwa na Zanzibar kwenye Muungano niushiriki na ushirikishwaji mdogo wa Zanzibar kwenye masualaya Kimataifa na Kikanda. Katika moja ya mafanikio ya kikaohiki ni kwamba tumepitisha Mwongozo wa Ushiriki wa SMZkatika masuala mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile changamoto yaongezeko la gharama za umeme kutoka TANESCO kwendaZECO lilipatiwa ufumbuzi ambapo imekubalika kuwa Kodi yaOngezeko la Thamani (VAT) itatozwa kwa kiwango chaasilimia sifuri (0%) kwenye umeme unaouzwa na TANESCO.Vilevile, mapendekezo ya deni linalofikia shilingi bilioni 22.9na lenyewe limefutwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kikao cha Kamati ya Pamojapia kilijadili na kuzipatia ufumbuzi hoja za biashara kati yaZanzibar na Tanzania Bara ambazo baadhi yake ni gharamaza kushusha mizigo; viwanda vya Zanzibar kupata lesenikutoka BRELA na upatikanaji wa fursa za ushiriki katika miradi

Page 56: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

ya maendeleo ya viwango na ubora kwa bidhaa namaendeleo ya wajasiriamali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka unaokwisha,Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeendelea kupata gawiola asilimia 4.5 ya fedha za Misaada ya Kibajeti (GeneralBudget Support - GBS), faida ya Benki Kuu, Mfuko waMaendeleo ya Jimbo na Kodi ya Mapato yatokanayo naAjira (PAYE). Hadi kufikia mwezi Machi, jumla ya shilingi bilioni36.79 zimepelekwa kwenye Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibarkatika maeneo yote hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedhaunaokwisha Ofisi imefanya ufuatiliaji wa miradi inayofadhiliwana Mfuko wa Maendeleo wa Jimbo katika Majimbo 16 katiya 32 yaliyoko Unguja. Matokeo ya ufuatiliaji huo yanaoneshakuwa miradi mingi ikiwemo ya maji na umeme inakidhimahitaji kwa kuongeza huduma muhimu za kijamii na hivyokuboresha maisha ya watu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendeleakuwawezesha wananchi wa pande zote mbili za Muunganokushiriki katika shughuli za kiuchumi na kijamii kupitiautekelezaji wa miradi na programu mbalimbali zamaendeleo. Miradi hiyo imefanikiwa kuinua hali ya wananchi,kukuza uchumi na kupunguza umaskini wa kipato na kuinuaubora wa maisha na ustawi wa watu kwa pande zote mbiliza Muungano. Miradi hiyo hufadhiliwa na Serikali ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Washirika waMaendeleo. Baadhi ya Miradi ya hiyo ni pamoja na Miradiya TASAF, MIVARF, MKURABITA, Kurejesha Ardhi Iliyoharibikana Kuongeza Uzalishaji wa Chakula na Kuongeza Tija naUzalishaji wa Zao la Mpunga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedhaunaokwisha, Ofisi kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu waPili wa Rais wa Zanzibar imeendelea kuhamasisha Sekta zisizoza Muungano kukutana na kujadili masuala yanayohusu sektazao na kubadilishana utaalam na wataalam ili kuleta ufanisina uwiano wa maendeleo kati ya pande zote mbili za

Page 57: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

Muungano. Katika kipindi hiki vikao tisa (9) vya sekta zisizo zaMuungano vimekaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedhaunaokwisha, Ofisi imeendelea kuelimisha umma kuhusuumuhimu na faida zinazotokana na Muungano kupitiavyombo vya habari ikiwemo televisheni na magazeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu hifadhi ya mazingira,ni muhimu itambulike kwamba sekta zote za uzalishaji malihapa nchini zinategemea hifadhi ya mazingira na hivyomazingira ni muhimu sana na yanatoa mchango mkubwasana katika ukuaji wa uchumi na ustawi wa Watanzania. Hatahivyo, shughuli zisizo endelevu zinazofanywa kwa namnaisiyoendelevu zinachangia kwa kiasi kikubwa katika uharibifuwa mazingira na kusababisha uharibifu wa ardhi; ukosefu wamaji salama kwa wananchi wa mijini na vijijini; uchafuzi wamazingira; upotevu wa bioanuai na makazi; uharibifu wamifumo ikolojia; uharibifu wa misitu; mabadiliko ya tabianchi;kuongezeka kwa viumbe vamizi na kuongezeka kwa taka zakielektroniki; kuongezeka kwa taka za kemikali; kuwepo kwauchafuzi utokanao na shughuli za utafutaji na uchimbaji wamadini, mafuta na gesi; na kukosekana kwa udhibiti wamazao yatokanayo na teknolojia ya uhandisi jeni (GMOs).

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kulinda na kuhifadhimazingira na kukabiliana na changamoto ya mazingiranchini, Ofisi imeendelea kusimamia utekelezaji wa sera, sheria,mikakati mbalimbali ya hifadhi ya mazingira na mikataba yakimataifa ya mazingira pamoja na utoaji wa elimu kuhusumazingira. Katika kutekeleza azma hiyo, kwa mwaka wafedha unaokwisha, yafuatayo yamefanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, tumeandaa Serampya ya Mazingira. Sera ya Mazingira tuliyonayo ni ya mwaka1997, ina miaka 22 na imepitwa na wakati, kwa hiyo,tunaandaa sera mpya na bora zaidi itakayoweza kutupanguvu na uwezo wa kusimamia mazingira kwa ufanisi zaidi.Sera hiyo sasa iko kwenye ngazi ya Kikao cha Makatibu

Page 58: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

Wakuu na baadaye itapelekwa kwenye Baraza la Mawazirikwa ajili ya kupitishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Ofisi imeendeleakusimamia utekelezaji wa Sheria ya Mazingira. Katika kipindicha utekelezaji wa sheria hii, changamoto kadhaazimejitokeza ikiwemo kutoandaliwa kwa baadhi ya kanuni;uwezo mdogo wa kitaasisi zinazosimamia utekelezaji waSheria ya mazingira ikiwemo Wizara za kisekta na Serikali zaMitaa; na uelewa mdogo kuhusu wajibu na majukumu yawadau katika utekelezaji wa sheria hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, i l i kukabiliana nachangamoto hizi, juhudi mbalimbali zimechukuliwa na Ofisiyetu ikiwemo pamoja na kutekeleza Mradi wa Kujenga Uwezowa Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira. Mradi huuunaofadhiliwa na Serikali ya Sweden na ni wa miaka mitatu(3) na una thamani ya dola milioni 3. Mradi huu utatusaidiakufanya kazi mbalimbali katika kusimamia vizuri Sheria yaMazingira. Hadi kufikia sasa, Ofisi imeratibu uteuzi waWakaguzi wa Mazingira wapatao 487 watakaosaidiakuimarisha utekelezaji wa Sheria ya Mazingira katika ngaziya Serikali za Mitaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tuzo ya Rais ya Hifadhi yaMazingira. Ofisi yetu imekamilisha Mwongozo ambaoutaboresha Tuzo hii. Awali Tuzo hii ilihusu maeneo machacheya kutunza miti na vyanzo vya maji, maboresho haya sasayatatoa mtazamo mpana zaidi kuhusu Tuzo hii na kuanziamwakani tunaweza kuanza kuitoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ripoti ya Tatu ya Hali yaMazingira nchini. Sheria ya Mazingira inatutaka sisi Ofisi yaMakamu wa Rais kila baada ya miaka miwili kuwasilisha Ripotiya Hali ya Mazingira nchini, hatujafanya hivyo kwa miakakadhaa sasa lakini katika mwaka wa fedha ujao tutawasilisharipoti hiyo kwa sababu imekwishakamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mfuko wa Taifa waDhamana ya Mazingira. Katika kipindi cha mwaka

Page 59: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

unaokwisha, Ofisi iliainisha mapendekezo ya maeneo yayanayohitajika kufanyiwa marekebisho ya sheria ili kuwezeshaMfuko huu kuanza kazi kwa ufanisi. Matarajio yetu ni kwambamabadiliko haya yatapitishwa ili Mfuko huu uweze kuanzakazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Maadhimisho ya Siku yaMazingira Duniani. Tumekuwa tunatumia Maadhimisho hayakama fursa ya kutoa elimu kwa umma kuhusu mazingira.Mwaka juzi tulifanya Butiama, mwaka jana tulifanya Dar esSalaam na mwaka ujao tutafanya Mkoani Mwanza. Uteuziwa Mkoa wa Mwanza umezingatia changamoto mbalimbalizinazolikabili Jiji hili ikiwa ni pamoja na uharibifu wa ardhi katikaBonde la Ziwa Victoria pamoja na uharibifu wa mazingira yandani ya Ziwa lenyewe unaosababishwa na shughuli za kijamiina kiuchumi. Kufanyika kwa Maadhimisho haya katika Mkoawa Mwanza kutatoa fursa kwa wananchi wa Mkoa huokushiriki na kuelimika zaidi na kuhamasishwa kuhifadhimazingira ya Bonde la Ziwa Victoria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupunguza matumizi yamkaa unaotokana na miti. Asilimia 80 ya miti inayokatwahapa nchini inakatwa kwa ajili ya kutengeneza mkaa. Ofisiyetu katika kipindi cha mwaka wa fedha unaokwishaimeendelea kushirikiana na taasisi nyingine na Wizarazinazosimamia sekta hii kupunguza matumizi ya mkaaunaotokana na miti. Vilevile, tumeendelea kushirikiana nawadau wengine katika kuandaa maonyesho na mashindanoya teknolojia mbadala. Imani yetu ni kwamba katika mwakaujao wa fedha basi maonyesho haya na uvumbuzi huuutasaidia kupunguza matumizi ya mkaa nchini ili kuokoa misituyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matumizi ya mifuko yaplastiki. Naomba hapa nitumie muda mrefu kidogo kuelezea.Hatimaye Serikali kupitia tamko la Mheshimiwa Waziri Mkuuimeamua kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastikikuanzia tarehe 1 Juni, 2019. Uamuzi huu ni mkubwa na wakihistoria na wa kijasiri. (Makofi)

Page 60: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

Mheshimiwa Mwenyekiti, kufuatia tamko hili, Ofisi yetuimeandaa kanuni zitakazochapishwa katika Gazeti la Serikaliambazo zitaainisha utaratibu mzima wa suala hili ikiwemokuweka adhabu kwa mtu atakayekiuka makatazo haya.Vilevile Ofisi yetu imeunda Kikosi Kazi cha Taifa kinachohusishataasisi mbalimbali za umma ikiwemo Mamlaka ya Viwanjavya Ndege, NEMC, Mamlaka ya Mapato Tanzania, Shirika laViwango Tanzania, TFDA, Jeshi la Polisi, Ofisi ya Mkemia Mkuuwa Serikali, TAMISEMI na nyinginezo ili kusimamia na kuratibukwa pamoja zuio hili la matumizi ya mifuko ya plastiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kikao na wawekezajiwa mifuko ya plastiki ambacho nilikiongoza jana tarehe 15Aprili, 2019 tukishirikiana na Mawaziri, Mheshimiwa Kakundana Mheshimiwa Kairuki, wazalishaji wa mifuko mbadalawameihakikishia Serikali kuwa wana uwezo wa kuzalishamifuko mbadala itakayokidhi mahitaji ya nchi. Ofisiitaendelea kuhamasisha umma kuhusu jambo hili ili tuwezekufanikiwa. Naomba Waheshimiwa Wabunge waungemkono jitihada hizi kwa mustakabali wa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nifafanue zaidi kwakusema kwamba uchumi mpana zaidi utakaoshirikisha watuwengi zaidi na ajira nyingi zaidi na mapato mengi zaidi upokwenye mifuko mbadala kuliko mifuko ya plastiki. Vilevile ilikuhakikisha tunafanikiwa, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamuwa Rais ameelekezwa kuwasiliana na Katibu Mkuu wa Ofisiya Rais, TAMISEMI ili kuhakikisha kwamba kila Halmashauriinapata maelekezo mahsusi kuhusu hatua za kuchukuakuhakikisha kwamba tunafanikiwa katika ngazi zote zautawala katika nchi yetu kuanzia vitongoji, vijiji, mitaa namaeneo yote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile napenda kutoaufafanuzi zaidi kwamba katika jambo hili vifungashio kadhaahasa vinavyotumika katika sekta ya ujenzi, kilimo, afyahavitahusika katika katazo hili. Pia napenda kutoa wito kwawale wanaohusika na kuzalisha bidhaa za kwenye chupa zaplastiki basi utaratibu utawekwa kuhamasisha ukusanyaji wa

Page 61: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

chupa zile na urejelezaji (recycling) ili tukiondoa plastiki vileviletuweze kupunguza matumizi ya chupa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango Mkakati wa Taifawa Kudhibiti Viumbe Vamizi (Invasive Species). Viumbe vamizini changamoto kubwa na mpya ya mazingira nchini. Viumbehawa husababisha athari kubwa katika uchumi hususankatika sekta kuu za uzalishaji kama vile kilimo, uvuvi, mifugo,maji, maliasili na utalii na hivyo kuathiri ajira na maendeleoya Taifa kwa ujumla. Pia huathiri afya za binadamu na mifugopamoja na mazingira kwa kuharibu mifumo ya kiikolojia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafiti zinaonyesha kwambahapa nchini kwetu kuna takriban aina 220 ya viumbe vamizina Tanzania imeathirika zaidi ya nchi nyingine katika ukandawa Afrika Mashariki na Kati. Kwa kuzingatia hili, hatua zaharaka zisipochukuliwa kuwadhibiti viumbe hawa, uchumi wanchi na ustawi wa wananchi utaendelea kuathirika kwa kasikubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kukabiliana na atharihii katika mwaka wa fedha unaokwisha, Ofisi yetu iliundaKikosi Kazi cha Kitaifa kwa ajili ya kuandaa Mpango Mkakatiwa Taifa wa Kudhibiti Viumbe Vamizi. Mpango huo utasaidiakudhibiti kuongezeka na kusambaa kwa viumbe hawa naMpango huo tayari umepitishwa katika ngazi ya MakatibuWakuu na unangoja Baraza la Mawaziri ili uweze kupitishwana kutekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, usimamizi wa taka zenyemadhara. Taka hatarishi zinazozalishwa viwandani, migodini,hospitalini na baadhi ya maeneo ya biashara, Ofisiimeendelea kudhibiti uzalishaji na utupaji wa taka hizi kwamujibu wa sheria na kanuni zilizowekwa. Ofisi yetu inabadilishakabisa utaratibu wa kutoa vibali vya kuruhusu biashara yataka zenye madhara ikiwemo vyuma chakavu, pamoja nataka nyinginezo. Lengo ni kupunguza na kuondoa biasharaholela ya vyuma chakavu inayochangia kuharibumiundombinu ya nchi yetu. Kwa hiyo, tutaendelea na jambohili katika mwaka ujao wa fedha.

Page 62: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu kwa umma kuhusuusimamizi na hifadhi ya mazingira. Ofisi ilikamilisha maandaliziya Mfumo wa Taarifa kuhusu Mazingira (CentralEnvironmental Information System) unaoendana na mfumowa teknolojia ya simu kuwawezesha watumiaji kupokea nakutoa taarifa zinazohusu mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi nyingine zilizofanyikakatika mwaka unaokwisha ni maandalizi ya kutangazamaeneo ya mazingira lindwa na maeneo na nyeti pamojana kuandaa orodha, kuunda Kamati ya Kitaifa, kuandaavigezo na kujadili maeneo yanayopendekezwa. Vileviletuliendelea na kazi za juhudi za kuokoa Ikolojia ya Bonde laMto Ruaha na kuandaa mapendekezo ya kukabiliana nachangamoto zinazokabili utekelezaji wa Kampeni yaUpandaji Miti kwa kushirikiana na sekta husika, hasa sekta yamaliasili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tuliendelea kutoatathmini ya mazingira kimkakati; kuratibu na utekelezaji wamikataba ya Kimataifa na ya Kikanda kuhusu Mazingira;kuendelea na kazi ya udhibiti wa taka ngumu nchini hususankuandaa Mwongozo wa Uwekezaji katika Taka Ngumu ilikuhamasisha uwekezaji na kuongeza jitihada za kuboreshausimamizi wa taka hizo hapa nchini. Katika utekelezaji waMwongozo huo, Ofisi ya Rais – TAMISEMI ndiyo ina jukumumuhimu kabisa la kudhibiti taka kwenye masoko na kwenyemiji yetu. Hivyo ndiyo ina jukumu la kufuatilia utekelezaji waMwongozo huo ili kuleta ufanisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Mfuko waMazingira wa Dunia (GEF) katika mwaka unaokwisha tuliratibushughuli za Mfuko huo kwa kufanya ufuatiliaji wa utekelezajiwa miradi iliyofadhili na Mfuko huo. Vilevile tuliwasilishakwenye Sekretarieti ya GEF kwa ajili ya kupata ufadhili nchinikwa awamu ijayo ya mfuko huo ambapo katika awamu hiiTanzania imetengewa fedha kiasi cha Dola za Kimarekanimilioni 24.

Page 63: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kazi za NEMC; Barazala Taifa la Hifadhi la Mazingira ambalo ndiyo msimamizi mkuuwa uzingatiaji na utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi waMazingira limeendelea kutekeleza majukumu yake kamaifuatavyo:-

Moja, ni kuhakikisha kwamba Sheria ya Mazingirainazingatiwa ipasavyo. Katika kutekeleza shughuli zamaendeleo hapa nchini, Baraza limetekeleza kazi zifuatazo:-

Kwanza, Baraza limefanya ukaguzi katika maeneoyanayostahili kufanyiwa ukaguzi kwa mujibu wa Sheria yaMazingira. Hata hivyo, ukaguzi huo umebaini kwamba asilimia40 tu ya miradi ndiyo inayozingatia Sheria ya Mazingira namingine inakabiliwa na changamoto mbalimbali za uharibifuwa mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Baraza limechukua hatuastahiki kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira kwa miradiiliyokiuka sheria na kanuni. Hatua hizo ni pamoja na kutoaushauri, maelekezo, maonyo, amri za katazo, amri zaurejeshaji wa mazingira lakini pia tumewafikisha Mahakamaniwatu ambao hawakuzingatia Sheria za Mazingira nahawakuzingatia maelekezo ya Baraza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka katikamwaka unaokwisha NEMC imeendelea kupokea malalamikoyanayohusu uchafuzi wa mazingira na kuyafanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kuhusu tathmini yaathari kwa mazingira (EAI), naomba eneo hili nilizungumziekwa kirefu kidogo kwa sababu ni eneo ambalo limekuwalinalalamikiwa hata na viongozi wetu. Niseme kwamba sualala uchelewashaji na gharama za utoaji wa vyeti vya mazingiratumelishughulikia kwa ukamilifu sana. Tumefanya mamboyafuatayo ili kurahisisha kuharakisha na kupunguza utoaji wavyeti.

Kwanza, tumeweka kanuni mpya za kupunguzagharama za kufanya EIA kwenye miradi kutoka shilingi milioni

Page 64: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

10 kwa miradi ya watu wa kawaida hadi kwenda shilingimilioni nne na chini zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumefanya hivi kwa msingikwamba EIA siyo chanzo cha mapato bali ni huduma. Kwahiyo, kuanzia sasa cheti cha mazingira kitagharimu gharamaya shughuli ya kufanya ile kazi na siyo chanzo cha mapato.Vile vile tumepunguza sana muda wa kupata cheti. KwenyeSheria ya Mazingira muda uliowekwa kwa kawaida ni siku149.

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda niseme kwambashughuli za kufanya EIA zipo ndani ya sheria na ni siku 149,lakini tumeweka utaratibu mpya wa kupunguza sana siku hizona kuhakikisha kwamba watu wanapata vyeti kwa haraka.Kwa mfano, kwenye sheria, Waziri anapaswa kukaa na chetihicho kwa siku 30, lakini tumekubaliana kwamba chetikitakapofika kwenye ofisi yangu hakitachukua siku nnekitakuwa kimeondoka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile tumeamua kuwekautaratibu mpya wa kutoa vyeti vya muda (ProvisionalEnvironmental Clearance - PIC) ambapo cheti hiki ambapocheti unakipata ndani ya siku saba na kitakuwezesha kuanzashughuli za uwekezaji wakati mchakato wa EIA unaendelea;kwa sababu tunaamini kwamba kuna watu wamezingatiasheria lakini wanahitaji vibali vingine na wanahitaji ku-mobilizena kuanza kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tumewekautaratibu kwamba pale utakapoomba na paletutakapofanya checklist kuhakikisha kwamba kiwanja chakokipo mahali salama, unakimiliki, basi tutakupa cheti uanzeuwekezaji wakati mchakato unaendelea. Ingawa cheti hikicha muda haki-guarantee kwamba utapata cheti chakudumu, lakini kinakuwezesha kuanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile tumepitia upyakanuni za tathmini ya athari kwa mazingira ili kuondoa vikwazovinavyowakwaza wawekezaji katika kuanza kushughuli zao.

Page 65: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

Pia tumepitia upya kanuni zinazodhibiti wataalamwanaofanya EIA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima ifahamike kwambamchakato huu wa EAI unahusu NEMC na consultant binafsiambao wakati mwingine wao ndio wanacheleweshawawekezaji lakini lawama zinakuja kwa NEMC. Kwa hiyo,tunapitia kanuni zinazowadhibiti ili kuhakikisha kwambahawacheleweshi wawekezaji na pia wanawatoza gharamaambazo siyo kubwa na vile vile tunaondokana nachangamoto za udanganyifu zinazoweza kufanywa naconsultants hawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tumewachukulianidhamu watumishi wa NEMC ambao walikuwawandanganyifu ambao walikuwa wanapaka matope Barazana kusumbua wawekezaji na kuwalaghai. Hivi tunavyongea,watumishi wanane wa NEMC wapo Mahakamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tumepata uongozimpya, Mkurugezi Mkuu mpya na Bodi mpya ya NEMC. Imaniyetu ni kwamba hatua zote hizi zitatusaidia kuhakikisha nakuharakisha mchakato wa kupata vyeti. Malalamiko yaNEMC ukiyasikia sasa hivi, basi hayakutokea sasa hivi, nimalalamiko ya nyuma kwa sababu kazi kubwa na nzuriinafanyika sasa hivi na sisi tunaamini kwamba usimamizi wamazingira katika uwekezaji ni jambo muhimu na la msingisana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuhakikisha kwambamchakato wa miradi wa Kitaifa na Kimataifa unakwenda kwakasi inayokubalika, Baraza limekuwa linashauriana nawahusika katika kila hatua ya utekelezaji. Kwa mfano, mradiwa bomba la mafuta kutoka Uganda, Baraza limeshapokeatathmini ya athari kwa mazingira na imefanyiwa kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa ujenzi wa Uwanjawa Mpira hapa Dodoma, cheti kimeshatolewa; mradi waStriegler’s Gorge na wenyewe umepatiwa cheti. Baraza kwakushirikiana na TANESCO wanaratibu na kusimamia

Page 66: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

utekelezaji wa mpango wa utekelezaji wa mazingira wakatiwote wa utekelezaji wa mradi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile ofisi yetu pamoja naNEMC, ili kuhakikisha kwamba mchakato EIA unafanyika kwaufanisi, tumeshirikiana na Kituo cha Sayansi na Mazingira chaIndia ili kuandaa miongozo ya kurahisisha mapitio ya miradiya majengo na Sekta ya Ujenzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile tunaangalia uwezowa Waziri mwenye dhamana ya mazingira kukasimu kwamamlaka za Serikali na Wizara za Kisekta, baadhi ya vyetivingine, kwa mfano, vituo cha mafuta pamoja na miradimidogo midogo ili kuharakisha upatikanaji wa vyeti kwamiradi ya aina hiyo ambapo siyo kila mradi hapa nchiniunakuja kwa Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika mwaka fedhaunaokwisha, Baraza limeendelea kutoa elimu kwa Ummakuhusu mazingira kwa kutumia vyombo vya habari namafunzo kwa wadau mbalimbali. Kazi hiyo bado inaendeleana kazi ya Elimu kwa Umma kuhusu Mazingira bado ni kubwa,kwa hiyo, Baraza litaendelea na kazi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia NEMC imeendeleakutekeleza ajenda ya Utafiti katika Mazingira (NationalEnvironmental Research Agenda) kwa kufanya tafitimbalimbali hapa nchini. Vile vile Baraza limefanya tathminiya mmomonyoko wa fukwe za Kigamboni na utafiti wa kinakuhusiana na tatizo la kujaa kwa maji ya mvua katika maeneoya makazi ya Mlandizi na ripoti za utafiti huo zimeandaliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile tumeangalia kwakina na kuandaa kikosi kazi kwa ajili ya kuangalia tatizo laupatikani wa mchanga katika Mkoa wa Dar es Salaam namikoa ya jirani na uharibifu wa miundombinu na mitokutokana na uhitaji mkubwa sana wa mchanga ambaounaharibu mazingira. Ripoti ya Kamati hiyo inatatolewa nahatua zitachukuliwa.

Page 67: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Baraza la Taifa la Hifadhiya Mazingira limeendelea kusimamia maeneo, kuratibushughuli za (Man And Biospher Reserve) tano hapa nchini naBaraza limeanza maandalizi ya Kongamano la Kisayansikuhusu hifadhi hai (biosphere reserves). Kongamano hilolinatarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu 2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Mazingira imetoanafasi ya kuhifadhi baadhi ya maeneo ambayo yanapaswakuhifadhiwa kutokana na unyeti wake kimazingira na Ofisiya Makamu wa Rais ilitembelea maeneo mbalimbali nchiambayo hayana hifadhi yoyote lakini yanahitaji hifadhi kwamujibu wa Sheria ya Mazingira na Baraza pamoja na Ofisizimeendelea kufanya maandalizi kwa ajili ya kuyahifadhimaeneo hayo nyeti. Tunaziomba Halmashuri zote nchini kamakuna maeneo kama kuna maeneo ambayo wanadhani ninyeti na hayana hifadhi yoyote, basi tupo tayari kufanya naokazi kuyahifadhi kwa kutumia Sheria za Mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uratibu wa miradiinayotekelezwa kwa fedha za washirika wa maendeleo, kwamwaka unaokwisha Baraza limeendelea kutekeza miradimbalimbali kwa ajili hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwaka fedhaunaokwisha Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Barazatumeendelea kusimamia sheria na kanuni na taratibu zautumishi wa Umma sambamba na kuwezesha watumishiwake kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Katika kipindihiki, watumishi wamehudhuria mafunzo mbalimbali ya mudamrefu na mfupi ndani na nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutekeleza majukumuyetu, ofisi yetu ilikumbana na changamoto kadhaa zikiwemoupatikanaji wa rasilimali zinazoendana na mahitaji halisi yaofisi; pili, uelewa mdogo wa wadau kuhusu masuala yaMuungano na umuhimu wa hifadhi ya mazingira; nyingine niupatikanaji wa takwimu sahihi za mazingira; na kutokuwa nawataalam wa kutosha.

Page 68: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, tulichukua hatuakadhaa katika kukabiliana nazo. Hatua hizo ni pamoja nakuandaa miradi na kuiwasilisha kwa wadau wa maendeleokwa ajili ya kupata fedha, kuendelea kutoa elimu kwa Ummakupitia vyombo vya habari na maonyesho ya Kitaifa kuhusumasuala ya Muungano na umuhimu wa kuhifadhi mazingira,pamoja na kuhamasisha wadau hususan Serikali za Mitaa nasekta binafsi kushiriki katika masuala ya mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile tumeandaa taarifaya hali ya mazingira pamoja na kuandaa maandikombalimbali ya kupata ufadhili kwa ajili ya eneo la ukusanyajitakwimu, lakini vile vile tumeendelea kutoa mafunzo kwawataalam pamoja na kuajiri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni malengo na maombiya fedha za matumizi kwa mwaka fedha unaokuja. Katikakuimarisha na kuuenzi Muungano, Ofisi yetu imepangakutekeleza majukumu na malengo yafuatayo:-

Kwanza, kuendelea kuratibu vikao vya Kamati yapamoja; pili, kufuatilia utekelezaji wa miradi na programu zamaendeleo zinazotekelezwa pande zote mbili za Muungano;tatu, kutoa elimu ya Muungano kwa makundi tofauti ya kijamiiikiwa ni pamoja na kuandaa warsha na mafunzo mbalimbali;nne, kuhamasisha Wizara, Idara na Taasisi zisizo za Muunganozenye majukumu yanayoshabihiana kuendelea kushirikianakatika kuimarisha Muungano wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu hifadhi ya mazingirakatika kusimamia na kuhifadhi mazingira kwa ajili ya kizazicha sasa na kijacho, katika mwaka ujao wa fedha Ofisiimepanga kufanya mambo yafuatayo:-

Kwanza kukamilisha Sera mpya ya Taifa ya Mazingiraambayo ni mapitio ya Sera ya mwaka 1997. Vile viletumepanga kukamilisha na kuchapisha nakala za ripoti yaTaifa ya hali mazingira nchini na kuiwasilisha Bungeni kwamujibu wa sheria. Pia tutaendelea kuhamasisha na kutoaelimu ili kuhakikisha kwamba matumizi ya mkaa wa kukatwa

Page 69: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

kwa miti kwa kweli yanapungua kwa kiasi kikubwa kwasababu yanaharibu sana mazingira yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme, kwa mujibuwa mamlaka niliyopewa katika Sheria ya Mazingira kifungucha 13, tutaweka utaratibu sasa na tunafanya maandalizikwamba kila Taasisi ya Umma na binafsi, inayolisha watuwanaozidi 300 itakatazwa kutumia kuni na mkaa wa kukatakwenye misitu yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nirudie. Tutawekautaratibu kwenye kanuni na tangazo la Gazeti la Serikalikwamba kila Taasisi ya Umma au binafsi inayolisha watu zaidiya 300 kwa siku, italazimika aidha kupata mkaa kwenyeshamba lake yenyewe au kutumia nishati mbadala. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu kama Chuo Kikuucha Dodoma kuna wanafunzi 30,000, kila siku wanakula maratatu na kila siku vyakula hivyo mara tatu ni mkaa na kuniunaotoka katika misitu wa asili; kuna Kambi za Jeshi, kunahospital kuna shule, makambi ya wakimbizi na kadhalika. Kwahiyo, tutalazimisha; naomba niurudie; kila taasisi inayolishawatu wanaozidi 300, aidha, italazimika kupata mkaa na kunikwenye shamba lake yenyewe au kutumia nishati mbadala.Mamlaka ya kuandika kanuni hiyo ninaya kupitia Sheria yaMazingira, kifungu cha 15. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mifuko ya plastiki.Kama nilivyosema hapo awali, tumeanza na imani yetu nikwamba tutafanikiwa. Kwa hiyo, tunasubiri kanuni zitokekwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili tuzichapishena tuanze utekelezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, dhamira yetu ni kutekelezazoezi hili bila bugudha, bila usumbufu, bila kupigana virungu,kwa sababu tumefanya maandalizi ya muda mrefu wa kwawadau wote; na imani yangu ni kwamba Watanzania wotewatalipokea jambo hili kama jambo jema kwa ustawi wa nchiyetu. Imani yetu ni kwamba uchumi mpya utakaoibuka wa

Page 70: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

mifuko mbadala utasaidia kutoa mapato zaidi kwawananchi, ajira zaidi na hifadhi ya mazingira vile vile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu viumbe vamizi. Hili nijambo jipya ambalo ofisi yetu imeamua kulishughulika kuanziamwaka uliopita wa fedha na tumeandaa na kwa kwelininayo faraja kubwa sana kwa wataalam wetu waliofanyakazi kwa zaidi ya miezi miwili kwenda kila kona ya nchi yetukuangalia viumbe vamizi kwenye maeneo ya malisho,maeneo ya kilimo, maeneo ya maji na kutengeneza mkakatimkubwa na mzuri wa kupambana na invasive species.Tanzania itakuwa ni nchi ya pili Afrika ukiondoa South Africaambayo ina mkakati mahususi wa kupambana na viumbevamizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, imani yetu nikwamba mkakati huo utapitishwa na utatumika kwa ajili yakuilinda nchi yetu.

Waheshimiwa Wabunge, nadhani mnafahamu kipindimvua ikiwa inanyesha, ukipita maeneo Kongwa na Gairoulikuwa unaona maua mengi mazuri pembeni mwabarabara. Yale maua ni viumbe vamizi, yanaenea nakuondoa kabisa maeneo ya kilimo na hamna shughuliinayoweza kufanyika. maua hayo yamevamia maeneomengi ya nchi yetu na kuondoa ardhi muhimu kwenyeuzalishaji wa chakula na malisho. Kwa hiyo, ni tishio kubwa lamazingira la Kitaifa, nasi ofisi yetu tumeamua kulichukulia kwauzito huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu upandaji wa miti,katika mwaka ujao wa fedha, Ofisi yetu itaendeleakuhamasisha na kufuatilia utekelezaji wa kampeni yaupandaji miti. Kwa kweli hapa tutaomba kushirikiana na sektayenyewe husika yenye dhamana ya miti. TFS, TAFORI,Tanzania Tree Seed Agency, vyote vipo chini ya Wizara yaMaliasili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ili zoezi hili lifanyikena vifanikiwe vizuri, ushirikiano kati ya Ofisi ya Makamu ya

Page 71: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

Rais, Wizara ya Maliasili na TAMISEMI ni muhimu. Jukumu laupandaji wa miti siyo la ofisi moja peke yake, nasi tutafanyakazi kwa pamoja kuhakiksha kwamba ile dhamira yetu yamiti milioni moja na nusu kila Halmashauri, inatimia na kunaufuatiliaji kweli kwamba miti hiyo inapandwa na siyo takwimutu kwenye karatasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu tuzo ya Rais yaHifadhi ya Mazingira, katika mwaka ujao wa fedha tutaanzakutoa tuzo rasmi. Naomba nizungumzie sasa suala la mita 60ambalo limezungumzwa sana na limewagusa watu wengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mnavyofahamu,yalitoka maelekezo kwamba watu wasizuiwe kufanyashughuli katika maeneo ya ndani ya mita 60 na kwambatungalie upya sheria hiyo. Sheria ya Mazingira ni kweliimekataza kutofanyika kwa shughuli za kibinadamu zakudumu au ambayo asili yake inaweza kuhatarisha mazingiraau kuathiri vibaya ulinzi wa mazingira ndani ya mita 60 yamito, kingo za mito, bwawa na miambao ya asili ya ziwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, katika kifunguhicho hicho kinachofuatia, kimebaini kwamba kunauwezekano kukatokea uhitaji wa shughuli za kibanadamu zakutafuta ridhiki kufanyika. Ndiyo maana kifungu hichokimetoa nafasi kwa Waziri mwenye dhamana ya mazingirakutengeneza mwongozo wa namna na aina ya shughulizinazoweza kufanyika ndani ya mita 60.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa kutumiakifungu hiki, ofisi yetu sasa inaandaa mwongozo wa aina nanamna ya shughuli za riziki zinazoweza kufanyika ndani yamita 60. Mwongozo huo tutauleta kwa ajili ya kupitishwa.Inawezekana kabisa tukaruhusu kilimo katika mita 60 lakinitukataza matumzi ya mbolea za kemikali au tukakatazakwamba tusiende mita 10 au 20 au tukakataza aina fulaniya mazao, lakini tukaruhusu watu watafute riziki ndani ya mita60 kwa sababu sheria imetoa nafasi hiyo kwa Waziri mwenyedhamana ya mazingira.

Page 72: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi ni jirani na Kenya na tuna-share baadhi ya rasilimali za mazingira. Baadhi ya rasilimalihizo ni pamoja na Ziwa Chala, Ziwa Jipe, Ziwa Natron na MtoMara. Nilipoenda Kenya nilikutana na Waziri mwenzengu waMazingira, nilimwomba naye mkutano na kuna manenoyalikuwa yanazungumzwa kuhusu Mto Mara na Kenyakujenga miradi kule itakayozuia maji yasitiririke na hivyokuathiri Hifadhi ya Serengeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati nzuri tuliwekeanamkataba kuhusu usimamizi wa pamoja wa rasilimali hizi.Baadhi ya mambo tuliyokubaliana ni kwamba tutaundakamati ya pamoja ya ngazi ya wataalam na ngazi yaMawaziri, tutafanya tathmini ya kina ya rasilimali za mipakani,tutaanda mikataba wa pamoja wa usimamizi wa rasilimalizote ambazo tuna-share na vilevile tutandaa mpango wapamoja wa utafutaji wa fedha na rasilimali hizo. Hadi sasaKamati ya wataalam kwa upande wa Tanzania imeundwana tunangoja wenzetu wa Kenya walete wataalam wao iliwaweze kuja na tuanze kazi hiyo.

Tunaamini jambo hili litasaidia nchi hizi kufanya kazi kwapamoja, lakini kuimarisha ujirani mwema na urafiki na unduguuliopo kati yetu na ndugu zetu Wakenya kwa kushirikianakatika jambo hili la kuhifadhi rasilimali za pamoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kuhusu usimamizi wamazingira katika ngazi za mikoa na Mamlaka za Serikali zaMitaa; Sheria ya Mazingira inatoa jukumu kubwa na wajibumkubwa kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuimarisha uratibuna usimamizi wa mazingira, mazingira yotetunayoyazungumza yapo kwenye Tawala za Mikoa na Serikaliza Mitaa, kwenye vitongoji, vijiji, mitaa na kata, kwa hiyotumeamua sasa tufanye kazi na wenzetu wa Tawala za Mikoana Serikali za Mitaa ili na wenyewe jambo la mazingirawaliweke katika vipaumbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kwa ajili hiyo sasautekelezaji uratibu na ufuatiliaji wa hifadhi ya mazingirautauhusu uundaji wa Kamati za Mazingira katika ngazi ya jiji,

Page 73: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

manispaa, wilaya, miji, kata, vijiji, mtaa na vitongoji pamojana kuhakikisha kwamba Kamati hizi zinafanya kazi nauandaaji wa utekelezaji wa mipango ya mazingira katikaMamlaka za Serikali za Mitaa, kama Tawala za Mikoa naSerikali za Mitaa haitoi umuhimu kwa mazingira, basi tusahaukabisa kuhusu hifadhi ya mazingira nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi nyingine ambazotunazitekeleza katika hifadhi ya Mazingira kwenye Ofisi yetuni:-

(i) Kutoa mafunzo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wizaraza Kisekta;

(ii) Kuanzisha mfumo wa utoaji vyeti na leseni za mazingirakwa njia ya mtandao;

(iii) Kuratibu utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi ili chakuokoa mfumo wa Ikolojia wa Bonde la Mto Ruaha ambachotulikiunda na kazi hiyo inaendelea;

(iv) Tutaendelea kuelimisha umma kuhusu hifadhi yamazingira pamoja na matumizi salama ya bioteknolojia yakisasa (GMO);

(v) Tutaendelea Vilevile, kuandaa na kuchapisha Mkakatiwa Mawasiliano ya Elimu ya Umma kuhusu Hifadhi yaMazingira.

(vi) Tutasimamia na kuratibu na kuendelea kufuatiliaUtekelezaji wa Mikataba ya Kimataifa ambayo Tanzania niMwanachama;

(vii) Tutaendelea kutoa vyeti vya (EIA) pamoja na StrategicEnvironment Assessment;

(viii) Tutaendelea kufatilia utekelezaji wa mikakati iliyopo chiniya Mikataba ya Kitaifa tuliyoridhia;

Page 74: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

(ix) Tutaendelea kuwezesha mchakato wa kuridhia Mikatabana Itifaki za Kimataifa ambazotumezisaini;

(x) Tutaendelea kutekeleza miradi ya hifadhi na usimamiziwa mazingira na mabadiliko ya tabiachi iliyopo chini yaMikataba ambayo sisi ni washiriki; na

(xi) Tutaendelea kuandaa miradi ya kuhifadhi mazingira nakuiwasilisha kwa wafadhili kwa ajili ya kutafuta fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Malengo ya Baraza la Taifala Kusimamia Hifadhi ya Mazingira kwa mwaka unaokujakatika kutekeleza utekelezaji wa Sheria ya Mazingira, Barazalimepanga pamoja na mambo mengine kufanya yafuatayo:-

(i) Kuendelea na ukaguzi na ufuatialiaji jambo ambalo niwajibu wake na kuchukua hatua stahiki;

(ii) Kuendelea kufanya mapitio ya nyezo na miongozombalimbali;

(iii) Kuboresha mfumo wa kutoa vyeti;

(iv) Kuendelea kusajili miradi ya mazingira;

(v) Kufanya tathimini ya mifumo ya Ikolojia;

(vi) Kuendelea na ajenda ya Taifa ya utafiti;

(vii) Kufanya mapitio ya miradi iliyowasilishwa;

(viii) Kuandaa miongozo ya usimamizi wa mazingira katikamaeneo lindwa na nyeti; na

(ix) Kazi nyinginezo ambazo ni wajibu wake kKisheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu miradi yamaendeleo kwa mwaka unaokuja tutaendelea kutekelezamiradi mbalimbali ya maendeleo kama ilivyoodheshwakatika kitabu chetu ambacho tumewakabidhi, lakini vile vile

Page 75: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

tutaendelea kusimamia mikataba mbalimbali ambayoTanzania ni mwanachama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hitimisho, nchi yetu ni yaMuungano na Muungano huo, una umuhimu wa kipekee kwaTaifa na umekuwa ni utambulisho wa Taifa letu na kielelezocha umoja wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Muungano huu sasaunatimiza miaka 55 tangu kuasisiwa kwake na katika kipindicha miaka 55 maingiliano, mashirikiano, udugu na ujamaaumeendelea kuimarika na hamna namna yoyote ambapoMuungano huu unaweza kurudi nyuma au maingiliano hayayanaweza kurudi nyuma. Natoa wito kwa Watanzania wotekuendelea kuuthamini, kuuenzi, na kuulinda na kuudumishaMuungano huu ili jitihada za kusukuma mbele maendeleoya nchi yetu ya kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa faida yapande zote mbili yaendelee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, chini ya uongozi wa Rais wetu,Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Makamu waRais, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Mheshimiwa Dkt. AliMohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi, Muungano huu unaendelea kuimarika nakushamiri. Chini ya uongozi wao, naomba nirudie hakunachangamoto yoyote ya Muungano inayowezakutufarakanisha, kututenganisha na kuturudisha nyuma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedhaujao Ofisi na Serikali kwa ujumla itaendelea kuyafanyia kazimambo yote yanayoleta changamoto katika utekelezaji wamasuala ya Muungano. Naomba niseme hapa, kwambatusitumie changamoto za Muungano kuupa jina bayaMuungano, tusitumie changamoto za Muungano kuhojiuhalali na umuhimu wa Muungano. Changamoto hizizilikuwepo, zipo na zitaendelea kuwepo hata zikiisha zote leo,miaka kumi, miaka mitano ijayo zitakuja nyingine. Chamuhimu ni taratibu na mifumo ya kushughulikia changamotohizi za Muungano na sisi tunaamini kwamba kwa wakati huu

Page 76: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

tumeweka mfumo na utaratibu bora zaidi wa kushughulikiachangamoto hizo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na umuhimu wamazingira na mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu, nijukumu la kila Mtanzania kuhakikisha kwamba mazingirayanalindwa. Napenda kutoa wito kwa WaheshimiwaWabunge pamoja na wananchi kwa ujumla kuunga mkonojitihada za Serikali katika kulinda na kuhifadhi mazingira.Naomba niseme hapo pia kwamba, hatua zote zamaendeleo tunazochukua mambo yote tunayojengayatakuwa hayana maana kama kutafuta riziki na ustawikutakuwa hakuwezekani, kwa sababu tumeharibu mazingirayetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kila kitu tunachofanyatunapolima, tunapofuga, tunapovua, common denominatorni mazingira, ndiyo ukweli wenyewe. Kwa hiyo bila hifadhiya mazingira afya za watu, riziki zetu, na shughuli nyingizinazoajiri ikiwemo Kilimo zitaathirika, kwa hiyo naomba Bungehili, wajishike kabisa, kama wadau wakubwa wa hifadhi yamazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naomba nimalizekabisa kwa kuwashukuru wote walionisaidia kuhakikishakwamba tunatekeleza majukumu ya Ofisi yetu. Napendakumshukuru Rais wetu kwa uongozi wake, na dira namwelekeo aliotupatia kuhusu majukumu yetu. Namshukurusana Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais,kwa uongozi wake uliotuwezesha kutekeleza na kwa kwelikwa ulezi wake, hasa kwangu mimi binafsi na watumishi waOfisi ya Makamu wa Rais, najisikia fahari san, na kwa kwelinadeka kwamba mtu ambaye naripoti kwake ni mama naMakamu wa Rais ambaye anatulea vizuri na kutufundishavizuri kuhusu uongozi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuwashukuru sana,ndugu yang una rafiki yangu Mheshimiwa Mussa RamadhaniSima, Naibu Waziri, ananisaidia na anafanya kazi nzuri sana…

Page 77: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, omba pesa, mudawako umekwisha.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Namshukuru Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu,na Watendaji wote wa Ofisi, Mhandisi Joseph K. Malongo,na Balozi Joseph E. Sokoine na Watendaji wote wa Ofisi yaMakamu wa Rais; na wa NEMC kwa kweli kwa kazi nzuriwanayoifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashukuru pia Wafadhiliwote ambao tumewaorodhesha na washirika wa maendeleoambao wametusaidia Ofisi yetu katika kufanikisha majukumuyake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maombi ya fedha, ili Ofisiyetu iweze kutekeleza majukumu na malengo yaliyopangwa,naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu liidhinishemaombi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2019/2020, kamaifuatavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, fungu 26 Makamu wa Raisnaomba Bunge lako Tukufu liidhinishe Makadirio ya Matumiziya Sh.7,855,093,000/= fedha za Matumizi ya Kawaida na kiasihiki kinajumuisha mishahara ya watumishi ambayo niSh.1,120,128,000/= na fedha za Matumizi Mengineyo ambayoni Sh.6,734,965,000/=.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Fungu 31 - Ofisi ya Makamuwa Rais, naomba Bunge lako Tukufu, liidhinishe makadirio yamatumizi ya Sh.29,066,298,442/= kwa Fungu hili. Kiasi hikikinajumuisha Sh.9,847,374,000/= fedha za Matumizi yaKawaida na Sh.19,218,915,442/= fedha za Miradi yaMaendeleo. Bajeti ya Matumizi ya Kawaida inajumuishaSh.2,759,365,000/= fedha za mishahara na Sh.7,088,009,000/=fedha za Matumizi Mengineyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Fedha za MatumiziMengineyo zinajumuisha Sh.2,808,957,000/= Ruzuku ya

Page 78: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

Mishahara ya watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi naUsimamizi wa Mazingira. Aidha, fedha za Miradi yaMaendeleo zinajumuisha Fedha za Ndani Sh.1,000,000,000/=na Fedha za nje Sh.18,218,915,442/=.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.(Makofi)

HOTUBA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WARAIS MHE. JANUARY Y. MAKAMBA (MB.), WAKATI WAKUWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA

MATUMIZI KWA MWAKA 2019/2020 - KAMAILIVYOWASILISHWA MEZANI

A. UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, baada ya Bunge lako Tukufukupokea taarifa iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati yaKudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira naMwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba naSheria kuhusu Mapitio ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi yaMakamu wa Rais kwa mwaka 2018/19; na Malengo ya Ofisiya mwaka 2019/20, naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lakoTukufu sasa likubali kupokea, kujadili na kupitisha Makadirioya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwamwaka 2019/20.

2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote ninapendakuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyenijaliaafya njema na kuniwezesha kuwasilisha Hotuba ya Bajeti yaOfisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira kwamwaka 2019/20 mbele ya Bunge lako Tukufu. Aidha,ninamshukuru kwa dhati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendeleakuniamini kusimamia masuala ya Muungano na Mazingira.Pia, ninapenda kutoa pongezi kwa mafanikio makubwayaliyopatikana chini ya uongozi wake makini na thabiti.Mafanikio hayo yanajidhihirisha katika utekelezaji wa miradimikubwa ya kitaifa ya maendeleo. Mafanikio hayo ni dalilitosha kuwa nchi ipo katika njia sahihi ya kufikia malengo

Page 79: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

tuliyojiwekea katika kutekeleza Mpango wa Maendeleo waMiaka Mitano 2016/17 – 2020/21 na Dira ya Taifa yaMaendeleo 2025 ya kuwa nchi yenye kipato cha kati ifikapomwaka 2025.

3. Mheshimiwa Spika, kwa dhati ninapenda kumshukuruMheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maelekezoanayotupa katika kusimamia masuala ya Muungano nakuhifadhi Mazingira. Uongozi wake thabiti unadhihirishwa namatokeo ya kazi nzuri inayofanywa ya kuudumishaMuungano wetu pamoja na kuhifadhi na kusimamiaMazingira. Aidha, kwa namna ya pekee ninapendakumshukuru Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein Rais waZanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kazi nzurianayofanya ya kuuenzi na kuudumisha Muungano wetu.

4. Mheshimiwa Spika, ninamshukuru na kumpongezaMhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu waJamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa hotuba yake nzuriambayo imetoa mwelekeo wa kisera katika utekelezaji washughuli za Serikali kwa kipindi cha mwaka 2019/20. Aidha,nampongeza kwa uongozi wake thabiti katika kusimamiashughuli za Serikali ndani na nje ya Bunge lako Tukufu. Pianinawashukuru Waheshimiwa Mawaziri wote kwa ushirikianowalionipa katika kutekeleza majukumu ya kusimamia shughuliza Muungano na Mazingira.

5. Mheshimiwa Spika, ninapenda kutoa shukrani napongezi za dhati kwa Bunge lako tukufu kwa kazi nzuriambayo limeifanya kwa kipindi cha uongozi wako. Aidha,ninakupongeza wewe binafsi Mheshimiwa Job YustinoNdugai (Mb.), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania, kwa kuliongoza Bunge letu kwa hekima na busarakubwa. Ninampongeza pia Mheshimiwa Dkt. Tulia AcksonMwansasu (Mb.), Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwakukusaidia kuliongoza Bunge letu kwa weledi na uadilifu.

6. Mheshimiwa Spika, ninapenda kutoa shukrani zanguza dhati kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya

Page 80: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

Viwanda, Biashara na Mazingira Mheshimiwa SuleimanAhmed Saddiq (Mb.) na Makamu wake Mhe.Kanali (Mst.)Masoud Ali Khamis (Mb.) na Mwenyekiti wa Kamati yaKudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria MheshimiwaMohamed Omary Mchengerwa (Mb.) na MakamuMwenyekiti Mhe. Najma Murtaza Giga (Mb.) pamoja naWaheshimiwa wajumbe wa Kamati hizo kwa kupokea, kujadilina kupitisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwamwaka 2018/19 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisiya Makamu wa Rais kwa mwaka 2019/20.

7. Mheshimiwa Spika, kwa masikitiko makubwa,ninaungana na Waheshimiwa Wabunge wenzangu kutoapole kwa ndugu, marafiki na wananchi wa Jimbo la KorogweVijijini, kwa kifo cha Mheshimiwa Stephen Hilary Ngonyanialiyekuwa Mbunge wao kilichotokea mwezi Julai, 2018 naMheshimiwa Kasuku Bilago aliyekuwa Mbunge wa Jimbo laBuyungu kilichotokea mwezi Mei, 2018. Aidha, ninatoa poleza dhati kwa wananchi kwa ujumla kwa kuwapoteza nduguzao na mali kutokana na ajali na maafa yaliyotokea sehemumbalimbali hapa nchini. Ninaomba Mungu azilaze roho zamarehemu mahali pema peponi. Amina.

8. Mheshimiwa Spika, ninawapongeza wabunge wotewaliochaguliwa na kuteuliwa kisha kuapishwa katika kipindicha mwaka huu wa fedha. Uadilifu wao na tabia ya kujitumana kufanya kazi kwa bidii ndio sababu kubwa ya kuwasehemu ya wawakilishi wa wananchi katika Bunge hili tukufu.

9. Mheshimiwa Spika, sasa ninaomba kutoa maelezo yautekelezaji wa kazi za Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kipindicha mwaka 2018/19 na malengo ya mwaka 2019/20.

B. UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA2018/19

Makusanyo ya Mapato kwa Mwaka 2018/1910. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Makamu wa Rais hainavyanzo vya mapato. Hata hivyo, Baraza la Taifa la Hifadhi naUsimamizi wa Mazingira hadi kufikia Machi, 2019 lilikuwa

Page 81: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

limekusaya mapato ya jumla ya sh. 10,430,060,727.00kutokana na tozo na faini.

Bajeti Iliyoidhinishwa kwa Mwaka 2018/1911. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, jumla yaSh. 6,485,991,000.00 ziliidhinishwa kwa ajili ya Fungu 26. Katiya fedha hizo, Sh. 5,432,325,578.05 zilikuwa ni ajili ya MatumiziMengineyo na Sh. 1,053,666,000.00 zilikuwa za Mishahara.Aidha, Fungu 31 liliidhinishiwa Sh.15,065,422,523.28. Kati yafedha hizo Sh. 10,002,082,523.28 ni za Matumizi ya Kawaidana Sh. 5,063,340,000.00 ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.Bajeti ya Matumizi ya Kawaida inajumuisha fedha zamishahara kiasi cha Sh. 2,924,993,000.00 na Sh.7,077,089,523.28 fedha za Matumizi Mengineyo. Fedha zaMatumizi Mengineyo zinajumuisha Sh. 3,017,072,000.00 ruzukuya mishahara kwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi waMazingira (NEMC) na Sh. 4,060,017,523.28 kwa ajili ya MatumiziMengineyo.

Fedha Zilizopokelewa na Kutumika Hadi Machi, 201912. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanzia Julai2018 hadi Machi 2019, jumla ya Sh. 4,572,810,578.05zilipokelewa kwa ajili ya kutekeleza majukumu yaliyopo chiniya Fungu 26. Kati ya fedha hizo Sh. 3,911,669,578.05zilipokelewa kwa ajili ya Matumizi Mengineyo na Sh.661,141,000.00 kwa ajili ya Mishahara. Aidha, hadi Machi,2019, jumla ya Sh 4,365,447,196.20 zilikuwa zimetumika. Katiya fedha hizo kiasi Sh. 3,704,306,196.20 zilitumika kwa ajili yaMatumizi Mengineyo na Sh. 661,141,000.00 kwa ajili yaMishahara.

13. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2019 Fungu 31lilipokea jumla ya Sh. 7,937,894,492.78 ambayo ni sawa naasilimia 52.7 ya bajeti iliyoidhinishwa. Kati ya fedha hizo Sh.5,405,152,561.18 zilipokelewa kwa ajili ya Matumizi ya Kawaidana Sh. 2,400,099,489.50 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Katiya fedha zilizopokelewa kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida,kiasi cha Sh. 1,652,371,000.00 ni kwa ajili ya Mishahara, Sh.2,331,102,003.28 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo ya Ofisina kiasi cha Sh. 1,554,322,000.00 ni fedha za ruzuku kwa Baraza

Page 82: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC. Aidha,Ofisi imetumia jumla ya Sh. 7,266,452,050.68 sawa na asilimia91.5 ya fedha zilizopokelewa. Kiasi hiki kinajumuisha fedhakwa ajili ya Matumizi ya Kawaida Sh. 5,405,152,561.18. naFedha za Miradi ya Maendeleo Sh.1,861,299,489.5. Fedha kwaajili ya Matumizi ya Kawaida zilizotumika zinajumuisha, Sh.2,198,459,561.18 za Matumizi Mengineyo ya Ofisi,Sh.1,652,371,000.00 Mishahara ya Watumishi wa Ofisi na Sh.1,554,322,000.00 ruzuku ya Mishahara kwa Baraza la Taifa laHifadhi na Usimamizi wa Mazingira.

14. Mheshimiwa Spika, Ofisi imeendelea kutekelezamajukumu yake kwa kuzingatia matakwa ya Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977; Dira yaTaifa ya Maendeleo 2025; Mpango wa Pili wa Taifa waMaendeleo wa Miaka Mitano (2016/17 – 2020/21); Ilani yaUchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi - CCM (2015 – 2020);Malengo ya Maendeleo Endelevu (Sustainable DevelopmentGoals – SDG 2030); Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 1997;Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004; naMaelekezo na Miongozo mbalimbali inayotolewa na ViongoziWakuu wa nchi.

MASUALA YA MUUNGANO

15. Mheshimiwa Spika, Muungano wetu ndio utambulishowa Taifa letu na kielelezo cha umoja wetu. Bila Muunganohakuna Tanzania. Ili Kuuenzi na kuuimarisha Muungano Ofisiimeendelea kutekeleza majukumu ambayo imekabidhiwakikatiba na kisheria ya kuratibu utekelezaji wa masuala yaMuungano na kuimarisha ushirikiano katika masuala yasiyoya Muungano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).Katika mwaka 2018/19, kazi zifuatazo zilitekelezwa: - Kuratibuvikao vya Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ ya kushughulikiaMasuala ya Muungano; Kuratibu utekelezaji wa masuala yakiuchumi, kijamii na kisiasa; Kuratibu masuala yasiyo yaMuungano ili kuimarisha ushirikiano kati ya SMT na SMZ; naKutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya Muungano.

Page 83: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ ya Kushughulikia Masualaya Muungano16. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Ofisiiliratibu na kufanya kikao cha Kamati ya Pamoja ya SMT naSMZ ya Kushughulikia Masuala ya Muungano tarehe 9Februari, 2019 Jijini Dodoma. Kikao hiki kilitanguliwa na vikaovya Sekretarieti ya Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ tarehe6 Februari, 2019; Makatibu Wakuu wa SMT na SMZ tarehe 8Februari, 2019; na Mawaziri wa SMT na SMZ tarehe 9 Februari,2019.

17. Mheshimiwa Spika, hoja zilizojadiliwa katika kikaohicho ni pamoja na: - Mapendekezo ya Utaratibu wa Vikaovya Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ ya kushughulikiaMasuala ya Muungano; Mwongozo wa Ushirikishwaji wa SMZkwenye Masuala ya Kimataifa na Kikanda; na Hoja za Fedhana Biashara baina ya Zanzibar na Tanzania Bara. Kikao hichokilikuwa na mafanikio yafuatayo: - Kupitishwa kwa Utaratibuwa Vikao vya Kamati ya Pamoja ya Kushughulikia Masualaya Muungano wenye lengo la kuimarisha na kuongeza ufanisiwa vikao vya Kamati ya Pamoja ikiwa ni pamoja na kufuatiliamaagizo na maelekezo yanayotolewa na Kamati hiyo.Utaratibu huo pia, umeainisha Kamati mbili ambazo ni Kamatiya Fedha, Uchumi na Biashara na Kamati ya Katiba, Sheriana Utawala zilizopewa jukumu la kuzipatia ufumbuzichangamoto zinazohitaji utatuzi wa haraka badala ya kusubiriutaratibu wa kawaida wa vikao vya Kamati ya Pamoja vyaSMT na SMZ. Kamati hizo zitawasilisha taarifa za utekelezajikatika vikao vya Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ.

18. Mheshimiwa Spika, katika Kikao hicho pia ulipitishwaMwongozo Kuhusu Ushiriki wa SMZ katika masuala mbalimbaliya Kimataifa na Kikanda. Mwongozo huo umezingatiamaeneo ya mikutano ya kimataifa na kikanda, nafasi zamasomo ya elimu ya juu na mafunzo mengine nje ya nchi nautafutaji wa fedha za misaada na mikopo ya kufadhili miradimbalimbali ya maendeleo.

19. Mheshimiwa Spika, changamoto ya ongezeko laGharama za Umeme kutoka TANESCO kwenda ZECO

Page 84: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

ilipatiwa ufumbuzi ambapo imekubalika kuwa, kodi yaongezeko la thamani (Value Added Tax-VAT) itatozwa kwakiwango cha asilimia sifuri (0%) kwenye umeme unaouzwana TANESCO. Vilevile, malimbikizo ya deni la VAT lililokuwalimefikia Sh. Bilioni 22.9 kwa shirika la ZECO kwenye umemeuliouzwa na TANESCO limefutwa.

20. Mheshimiwa Spika, kikao cha Kamati ya Pamoja piakilijadili na kuzipatia ufumbuzi hoja za biashara baina yaZanzibar na Tanzania Bara ambazo ni: - Gharama za kushushamizigo (landing fees); Viwanda vya Zanzibar kupata lesenikutoka Wakala wa Usajili na Utoaji Leseni za Biashara (BusinessRegistrations Licensing Agency-BRELA); na Upatikanaji wafursa za ushiriki katika miradi ya maendeleo ya viwango naubora wa bidhaa na maendeleo ya wajasiriamali.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano naMazingira Mhe. January Makamba akihutubia wakati wakikao cha Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ kujadili masualaya Muungano kilichofanyika Februari 9, 2019 katika ukumbiwa Kambarage, jengo la Hazina Square, Dodoma.

Uratibu wa Masuala ya Kiuchumi, Kijamii na Kisiasai. Gawio kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar21. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar imeendelea kupata gawio la asilimia4.5 ya fedha za Misaada ya Kibajeti (Government BudgetSupport - GBS); faida ya Benki Kuu; Mfuko wa Maendeleo yaJimbo; na kodi ya mapato yatokanayo na ajira (Pay As You

Page 85: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

Earn – PAYE). Hadi kufikia Machi, 2019 jumla ya Sh. bilioni 36.79zimepelekwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kati ya fedhahizo, Sh. bilioni 14.00 ni PAYE, Sh. bilioni 1.4 ni fedha za Mfukowa Maendeleo ya Jimbo, Sh. bilioni 5.64 ni fedha za Misaadaya Kibajeti (GBS) na Sh. bilioni 15.75 ni gawio la Benki Kuu.

ii. Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo yaJimbo, Zanzibar

22. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19 Ofisiimefanya ufuatiliaji wa miradi inayofadhiliwa na Mfuko waMaendeleo ya Jimbo kwa Majimbo 16 kati ya 32 yaliyopoUnguja, Zanzibar. Majimbo hayo ni Nungwi, Mkwajuni, Chaani,Donge, Mahonda, Bumbwini, Mfenesini, Bububu, Welezo,Mwera, Fuoni, Kijitoupele, Mwanakwerekwe, Kiembesamaki,Paje na Makunduchi. Matokeo ya ufuatiliaji huo yanaoneshakuwa, miradi mingi ikiwemo ya maji na umeme inakidhimahitaji kwa kuongeza huduma muhimu za kijamii na hivyokuboresha maisha ya wananchi.

Ujenzi wa minara minne (4) na matenki manne (4) namabomba katika maeneo ya Magogoni na Mikarafuni-Unguja

iii. Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo23. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuwawezeshawananchi wa pande zote mbili za Muungano kushiriki katikashughuli za kiuchumi na kijamii kupitia utekelezaji wa miradi

Page 86: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

na programu za maendeleo. Miradi na Programu hizozimefanikiwa kuinua hali ya wananchi, kukuza uchumi nakupunguza umaskini wa kipato na kuinua ubora wa maishana ustawi wa jamii wa pande zote mbili za Muungano. Miradihiyo hufadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo. Katikamwaka 2018/19 utekelezaji wa Miradi na Programu hizo nikama ifuatavyo: -

a) Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tanzania Social ActionFund - TASAF)

24. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, TASAF IIIimeendelea na utekelezaji wa Mpango wa kunusuru KayaMaskini Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar. Programuzilizotekelezwa ni:- kutengeneza na kuboresha Mifumo yakutambua, kuandikisha na kutunza kumbukumbu zaWalengwa; Uhawilishaji ruzuku kwa kaya maskini; Uandikishajina utoaji ajira za muda ili kuongeza kipato kwa kaya maskini;na uwekezaji wa miradi ya kukuza uchumi wa kaya. Aidha,TASAF III imeendelea kujenga uwezo wa viongozi, watendajina wasimamizi wa Mipango katika maeneo yote yautekelezaji. Katika mwaka 2018/19 kiasi cha Sh.305,337,803,999.00 ziliidhinishwa kwa ajili ya kutekelezaprogramu za mradi. Hadi kufikia Machi, 2019 Sh.125,795,098,700.00 zilitumika kwa upande wa Tanzania Barana Sh. 3,512,043,950.00 kwa Tanzania Zanzibar.

b) Programu ya Miundombinu ya Masoko, UongezajiThamani na Huduma za Fedha Vijijini (MarketInfrastructure, Value Addition and Rural Finance -MIVARF)

25. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, MIVARFimeendelea na mpango wa kupunguza umaskini nakuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kwa kuwezesha kaya zavijijini kuongeza kipato na usalama wa chakula. Kazizilizotekelezwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wazalishajina kuwaunganisha na masoko ya mazao na taasisi za fedha.Katika mwaka 2018/19 Sh. 22,912,124,648.00 ziliidhinishwa nahadi kufikia Machi, 2019 kiasi cha Sh. 10,278,334,000.00

Page 87: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

zilitumika Tanzania Bara na Sh. 1,150,504,026.00 TanzaniaZanzibar.

c) Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara zaWanyonge Tanzania (MKURABITA)

26. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19 kazimbalimbali za kurasimisha rasilimali ardhi na biasharazinazomilikiwa na wananchi ili waweze kuzitumia kupunguzaumaskini na hatimaye kuchangia Pato la Taifa kazi zilifanyika.Kazi hizo ni pamoja na; Kuratibu utekelezaji wa mapendekezoya maboresho ya kisheria na kitaasisi; Kusimamia na kuratibushughuli za urasimishaji; Kujenga uwezo wa urasimishajibiashara na uanzishwaji wa vituo vya biashara; Kujengauwezo wa urasimishaji Ardhi Mjini; Kujenga uwezo waurasimishaji Ardhi Vijijini; na kukamilisha ujenzi wa Masjala zaArdhi. Jumla ya Sh. 1,411,694,987.00 ziliidhinishwa kwa mwaka2018/19. Hadi kufikia Machi, 2019 Sh. 288,252,127.00 zilitumikaTanzania Bara na Sh. 69,843,000.00 Tanzania Zanzibar.

d) Mradi wa Kurejesha Ardhi Iliyoharibika na KuongezaUzalishaji wa Chakula (Land Degradation and FoodSecurity- LDFS)

27. Mheshimiwa Spika, mradi huu unafadhiliwa na Mfukowa Dunia wa Mazingira (Global Environment Facility - GEF)kupitia Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo(International Fund for Agriculture Development - IFAD).Thamani ya mradi ni dola za Marekani milioni 50 ambapodola za Marekani milioni 7.156 zinatoka GEF na mchango wanchi (in-kind) ni kiasi cha dola za Marekani milioni 42.94. Fedhazinazotolewa na GEF zinalenga kuchangia katika kukabilianana Mabadiliko ya Tabianchi, na Hifadhi ya Bioanuai naUsimamizi Endelevu wa Ardhi. Mradi wa LDFS utatekelezwakwa kipindi cha miaka mitano kuanzia Julai, 2017 hadiSeptemba, 2022. Mradi huu utatekelezwa katika maeneoyenye changamoto za ukame katikati ya nchi na pwaniambayo ni Kata ya Haubi katika Halmashauri ya Kondoa,Mkoani Dodoma; Kata ya Sigili katika Halmashauri ya Nzega,Mkoani Tabora; Kata ya Mpambala Halmashauri yaMkalama, Mkoani Singida; Kata ya Sukuma, katikaHalmashauri ya Magu Mkoani Mwanza na Shehia 8 katika

Page 88: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

Wilaya ya Micheweni, Kaskazini Pemba. Jumla ya Sh.1,230,033,688.96 ziliidhinishwa katika mwaka 2018/19. Hadikufikia Machi, 2019 kiasi cha Sh. 667,907,922.17 kilitumikaTanzania Bara na kiasi cha Sh.158,583,866.70 kwa upande waZanzibar.

Sehemu ya miche ya Mikoko iliyopandwa katika ufukwe waeneo la Kisiwa-Panza, Mjini Pembae) Mradi wa Kuongeza Tija na Uzalishaji wa Zao laMpunga (Expanded Rice Production Project - ERPP)28. Mheshimiwa Spika, mradi huu unachangia utekelezajiwa Mpango wa Uwekezaji kwenye Sekta ya Kilimo Tanzania(Tanzania Agriculture and Food Security Investment Plan -TAFSIP) chini ya Mpango Kabambe wa Maendeleo ya KilimoAfrika (CAADP). Kwa upande wa Tanzania Bara, mradiunatekelezwa katika Halmashauri za Mvomero, Kilosa naKilombero Mkoani Morogoro na kwa upande wa Zanzibarunatekelezwa Kibonde Mzungu, Mtwango, Koani,Mchangani, Bandamaji (Unguja); na Machigini,Kwalempona, Ole, Dobi – 1 na Dobi – 2 (Pemba). Katikamwaka 2018/19 jumla ya Sh. 22,731,651,587.00 ziliidhinishwaili kutekeleza kazi za mradi huu. Hadi kufikia Machi, 2019 jumlaya Sh. 728,072,250.00 zilitolewa na kutumika Tanzania Barana kiasi cha Sh. 227,860,253.00 Tanzania Zanzibar.

Uratibu wa Masuala Yasiyo ya Muungano Kati ya SMT na SMZ29. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Ofisi kwakushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibarimeendelea kuhamasisha Sekta zisizo za Muungano za SMT

Page 89: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

na SMZ kukutana na kujadili masuala yanayohusu Sekta zao,kubadilishana utaalam na wataalam ili kuleta ufanisi nauwiano wa maendeleo kwa pande mbili za Muungano.Katika kipindi hiki vikao tisa (9) vimefanyika katika Sekta yaSerikali za Mitaa, Elimu, Maji, Habari, Utamaduni, Sanaa naMichezo, Ardhi, Nishati, Fedha na Mipango na Uchukuzi.

Elimu ya Muungano kwa Umma30. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Ofisiimeendelea kuelimisha Umma kuhusu umuhimu na faidazinazotokana na Muungano kupitia vyombo vya habariikiwemo redio, televisheni na magazeti. Ofisi pia, ilitoa elimuya Muungano kwa Maafisa Viungo (Focal Persons) kutokaWizara za SMT katika kikao kilichofanyika tarehe 18 Oktoba,2018, Dodoma.

HIFADHI ENDELEVU YA MAZINGIRA

31. Mheshimiwa Spika, Sekta zote za uzalishaji malizinategemea mazingira na hivyo kufanya sekta hii kuwa namchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi. Uwepo warasilimali kwa ajili ya mahitaji ya sasa na vizazi vijavyoutategemea namna uhifadhi wa mazingira unavyozingatiwa.Shughuli zisizo endelevu zinachangia kwa kiasi kikubwa katikauharibifu wa mazingira na kusababisha; Uharibifu wa ardhi;Ukosefu wa maji safi na salama kwa wananchi wa mijini navijijini; Uchafuzi wa mazingira; Upotevu wa bioanuai namakazi; Uharibifu wa mifumo ikolojia ya majini; Uharibifu wamisitu; Mabadiliko ya tabianchi; Kuongezeka kwa ViumbeVamizi; Kuongezeka kwa Taka za Kielektroniki; Kuongezekakwa taka za kemikali; Kuwepo kwa uchafuzi utokanao nashughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini, mafuta na gesi;na Kukosekana udhibiti wa mazao yatokanayo na Teknolojiaya uhandisi jeni.

32. Mheshimiwa Spika, katika miaka ya hivi karibuni,imedhihirika kuwa mazingira yetu si salama kutokana na kasiya uharibifu wa mazingira unaoshuhudiwa katika sehemumbalimbali za nchi. Ushahidi huo ni pamoja na kuongezekakwa hali ya jangwa na ukame, mafuriko, kuongezeka kwa

Page 90: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

magonjwa ya kuambukiza na mabadiliko ya hali ya hewa,kasi ya ukataji miti, kuongezeka kwa Viumbe Vamizi nakuongezeka kwa matumizi ya zebaki katika Sekta ya madinihususan wachimbaji wadogo wa dhahabu. Maendeleoendelevu hayawezi kupatikana bila kutunza mazingira.Pamoja na Serikali kuchukua jitihada kubwa katika utunzajina usimamizi wa mazingira, hali ya mazingira nchini bado siya kuridhisha.

33. Mheshimiwa Spika, hali hiyo inachangiwa nachangamoto nyingi zinazoikabili sekta hii ikiwemo: uhaba warasilimali fedha, uhaba wa rasilimali watu wa kusimamiautekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, Sura 191katika ngazi zote; uelewa mdogo wa jamii kuhusu umuhimuna wajibu wa kuhifadhi mazingira; kutokuwa na takwimusahihi za mazingira kwa wakati; kutokutengwa kwa maeneomaalum ya kutupa taka; na utegemezi wa nishati ya kuni namkaa.

34. Mheshimiwa Spika, katika kulinda na kuhifadhimazingira ya nchi yetu na kukabiliana na changamoto zamazingira nchini, Ofisi imeendelea kusimamia utekelezaji waSera, Sheria na Mikakati mbalimbali ya hifadhi ya mazingirana mikataba ya kimataifa ya mazingira pamoja na utoaji waelimu kuhusu mazingira. Katika kutekeleza azma hiyo kwamwaka 2018/19 yafuatayo yamefanyika; -

Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 1997 na Mkakati waUtekelezaji35. Mheshimiwa Spika, mwaka jana niliarifu Bunge lakoTukufu kuwa Ofisi inaendelea na hatua za kuboresha Sera yaMazingira ya Taifa ya Mwaka 1997 na Mkakati wa utekelezaji.Aidha, katika mwaka 2018/19 rasimu ilijadiliwa katika ngaziya Sekretariati ya Baraza la Mawaziri. Kwa kuwa Sera hii nimtambuka pamoja na maoni mengine ushauri uliotolewa naSekretarieti ilikubaliwa kupata maoni zaidi kutoka kwa wadau.Kazi hiyo imefanyika na baada ya kujiridhisha kuwa maoniya wadau yamezingatiwa Rasimu ya Sera itajadiliwa katikangazi inayofuata ambayo ni kikao cha Makatibu Wakuu (Inter- Ministerial Technical Committee - IMTC).

Page 91: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, Sura ya 19136. Mheshimiwa Spika, Ofisi inaratibu utekelezaji wa Sheriaya Usimamizi wa Mazingira ambayo ilitungwa mwaka 2004.Katika kipindi cha utekelezaji wa Sheria hii changamotokadhaa zimejitokeza ikiwemo kutoandaliwa kwa baadhi yaKanuni na Miongozo; uwezo mdogo wa Taasisi zinazosimamiautekelezaji wa Sheria ikiwemo Wizara za Kisekta na Mamlakaza Serikali za Mitaa; na uelewa mdogo kuhusu wajibu namajukumu ya wadau katika utekelezaji wa Sheria hii. Ilikukabiliana na changamoto zipo juhudi mbalimbali ambazoofisi imepanga kuchukua ikiwa ni pamoja na kutekeleza Mradiwa Kujenga Uwezo wa Utekelezaji wa Sheria ya Usimamiziwa Mazingira unaofadhiliwa na Serikali ya Sweden. Mradi huuuna thamani ya Dola za Marekani Milioni tatu (3) nautatekelezwa kwa muda wa miaka mitatu (2019/20 -2021/22). Baadhi ya shughuli zitakazotekelezwa ni pamoja nakuandaa Kanuni na Miongozo; kuendesha mafunzo kwaMamlaka za Serikali za Mitaa na Wizara za Kisekta; nakuanzisha mfumo wa utoaji vyeti na leseni za mazingira kwanjia ya mtandao. Hadi kufikia sasa, Ofisi imeratibu uteuzi waWakaguzi wa Mazingira wapatao 487 watakaosaidiakuimarisha utekelezaji wa Sheria ya usimamizi wa mazingirakatika ngazi ya Serikali za Mitaa.

Tuzo ya Rais ya Hifadhi ya Mazingira37. Mheshimiwa Spika, Ofisi imekamilisha Mwongozo wakushiriki Tuzo ya Rais ya Kuhifadhi Mazingira. Awali Tuzo hiiilihusu masuala ya kupanda na kutunza miti na kuhifadhivyanzo vya maji pekee. Maboresho ya tuzo yamefanyika ilikuwa na mtazamo mpana wa hifadhi ya mazingira.Maboresho hayo yameongeza masuala yafuatayo: -Uzalishaji endelevu viwandani, matumizi ya nishati mbadala,uchimbaji madini endelevu, kilimo na ufugaji endelevu,usimamizi wa taka, afya na usafi wa mazingira.

Ripoti ya Tatu ya Hali ya Mazingira Nchini38. Mheshimiwa Spika, napenda kulitaarifu Bunge lakoTukufu kuwa Ofisi imekamilisha rasimu ya Ripoti ya Tatu yaHali ya Mazingira nchini na sasa kinachofanyika ni kupitisharasimu hiyo katika ngazi mbalimbali za Serikali ikiwa ni pamoja

Page 92: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

na Kamati ya Mazingira ya Baraza la Mawaziri kabla yakuwasilishwa Bungeni ili kukidhi matakwa ya Sheria yaUsimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004 Kifungu 175 (1).

Mfuko wa Taifa wa Dhamana ya Hifadhi ya Mazingira39. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2018/19, Ofisi iliainisha mapendekezo ya maeneo ya kufanyiwamarekebisho katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, 2004ili kuwezesha Mfuko wa Taifa wa Dhamana ya Hifadhi yaMazingira kufanya kazi kwa ufanisi. Kwa kuwa Sera ya Taifaya Mazingira (1997) inafanyiwa maboresho, kipaumbele nikukamilisha Sera ili maeneo yote yatakayohitaji maboreshokwenye Sheria yafanyike kwa pamoja. Ni matarajio yetu kuwaMaboresho ya Sera pamoja na Sheria yatasaidia kwa kiasikikubwa juhudi za Serikali kusimamia masuala ya mazingiranchini na hivyo kuwa na maendeleo endelevu.

Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani40. Mheshimiwa Spika, Dunia huadhimisha Siku yaMazingira tarehe 5 Juni kila mwaka ili kutoa hamasa kwa watukutunza mazingira. Kitaifa, maadhimisho ya Siku ya MazingiraDuniani kwa mwaka 2018 yalifanyika Mkoani Dar es Salaamkatika viwanja vya Mnazi mmoja. Serikali iliamua Mkoa waDar es Salaam uwe mwenyeji wa Maadhimisho haya kwalengo la kuwapa fursa wananchi wa Jiji la Dar es Salaamkuelimishwa na kuhamasishwa kupambana na changamotoza uharibifu wa mazingira unaolikumba Jiji la Dar es Salaam,kama vile: -mafuriko; uchafuzi wa mazingira utokanao namifuko ya plastiki; kubomoka kwa kuta na kingo za fukwe zabahari ya Hindi; pamoja na utumiaji wa kiasi kikubwa chanishati ya mkaa.

41. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka huu Maadhimisho yaSiku ya Mazingira Duniani Kimataifa yatafanyika nchini Chinakatika mji wa Hangzhou kaulimbiu ikiwa ni Uchafuzi wa Hewa(Air Pollution). Kitaifa maadhimisho haya yatafanyika MkoaniMwanza. Uteuzi wa Mkoa wa Mwanza umezingatiachangamoto zinazolikabili jiji hili ikiwa ni pamoja na uwepowa uharibifu wa ardhi katika Bonde la Ziwa Victoria pamojana uharibifu wa mazingira ya ndani ya Ziwa hilo

Page 93: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

unaosababishwa na shughuli za kijamii na kiuchumi. Kufanyikakwa maadhimisho ya kitaifa Mkoani humo kutatoa fursa kwawananchi wa Mkoa huo na Mikoa jirani kuelimishwa nakuhamasishwa kuhifadhi mazingira ya Bonde la Ziwa Victoriapamoja na mazingira yake.

Kupunguza Matumizi ya Mkaa Unaotokana na Miti42. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea na jitihada zakupunguza matumizi ya mkaa unaotokana na miti kwakushirikiana na Taasisi za Serikali kuandaa mipango kazi kwakila Taasisi ya kupunguza matumizi ya mkaa unaotokana namiti. Aidha, Ofisi imeendelea kushirikiana na wadau wamazingira kutoa mafunzo kwa washindi wa Tuzo ya Teknolojiaya Mkaa Mbadala kwa lengo la kukuza teknolojia na ubunifuwao ili bidhaa zao ziweze kuwa za kiwango kinachokubalikakitaalam na kibiashara na hatimaye kuwafikia wananchiwengi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Bw. Leonard Kushokamfano wa hundi yenye thamani ya shilingi za kitanzaniamilioni 300 mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano lateknolojia ya nishati mbadala wa mkaa mwaka 2018

Page 94: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

Matumizi ya Mifuko ya Plastiki

43. Mheshimiwa Spika, ili kutimiza azma ya kupigamarufuku matumizi ya mifuko ya plastiki Ofisi ilihamasishawajasiriamali na wawekezaji kuwekeza katika uzalishaji wamifuko mbadala ikiwemo vikapu vya asili, mifuko ya karatasina nguo ili kutumia fursa hiyo kukidhi mahitaji ya soko.Kampeni za uhamasishaji zilifanyika katika mikoa ya Dar esSalaam na Mwanza kwa lengo la kuwatambua wadauwanaozalisha mifuko mbadala na kupata maoni kuhusunamna ya kujenga mazingira wezeshi kwa wadau kuwekezazaidi katika uzalishaji wa mifuko mbadala.

44. Mheshimiwa Spika, kufuatia tamko la Serikali la kupigamarufuku uzalishaji, uingizaji, uuzaji, usambazaji na utumiajiwa mifuko ya plastiki kuanzia tarehe 01 Juni, 2019, Ofisiimeandaa kanuni zitakazochapishwa katika Gazeti la Serikalichini ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004na kutoa adhabu kwa kila mtu atakayekiuka matakwa yaKanuni. Vilevile, Ofisi imeunda Kikosi Kazi cha Taifa kwa ajiliya kusimamia uzingatiaji wa Kanuni. Kikosi kazi hichokinahusisha wajumbe kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi naUsimamizi wa Mazingira, Mamlaka ya Mapato Tanzania, Idaraya Uhamiaji, Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege, Shirika laViwango Tanzania, Mamlaka ya Chakula na Dawa, Jeshi laPolisi, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Rais Tawalaza Mikoa na Serikali za Mitaa na Wizara ya Mambo ya Ndaniya Nchi.

45. Mheshimiwa Spika, katika kikao na wawekezaji wamifuko mbadala kilichofanyika tarehe 15 Aprili, 2019wamenihakikishia kuwa wana uwezo wa kuzalisha mifukombadala kukidhi mahitaji ya nchi. Aidha, Ofisi itaendeleakuhamasisha umma juu ya jambo hili ili liweze kuzingatiwa.Ninaomba Waheshimiwa Wabunge kuunga mkono jitihadahizi kwa mustakabali wa nchi yetu.

Page 95: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

Kikao cha Wadau wa Mifuko mbadala ya Plastikikilichofanyika jijini Mwanza

Kuokoa Ikolojia ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu46. Mheshimiwa Spika, katika kunusuru Ikolojia ya Bondela Mto Ruaha Mkuu, kwa mwaka 2018/19, Wizara na Mikoahusika imetekeleza majukumu yake ya kulinda ikolojia yabonde hili ambapo jumla ya vyanzo vya maji 5,373 katikamikoa saba vilitambuliwa na kati ya hivyo, vyanzo 652viliwekewa mipaka ya kudumu; jumla ya kaya 1,218 kutokaMikoa ya Iringa na Njombe zilizovamia maeneo ya hifadhiziliondolewa, baiskeli 18 zilikamatwa na kiasi cha Sh.98,994,000.00 kilikusanywa kama faini kutokana na makosaya uharibifu wa mazingira kwa Mkoa wa Tabora. Vilevile,jumla ya mifugo 4,303 ikiwemo ngombe, mbuzi na kondookwa Mikoa ya Iringa na Tabora ilikamatwa, mabanioyapatayo 7 yasiyo katika ubora yalivunjwa, madaraja 3 yakienyeji ya kuchepusha maji yalibomolewa na matanurumakubwa 6 ya mkaa yalibomolewa.

Page 96: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan (katikati), Waziri wa Nchi Ofisi yaMakamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. JanuaryMakamba pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo MhandisiJoseph Malongo wakipitia taarifa ya maendeleoya kikosi kazi cha kuokoa mfumo-ikolojia wa bonde lamto Ruaha Mkuu

47. Mheshimiwa Spika, ili kuimarisha hifadhi na usimamiziwa ikolojia ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu, TANAPA imewekavigingi vikubwa (beacons) 52 na vigingi vidogo (intermediatebeacons) 357 ili kuimarisha mipaka. Aidha, NEMC, Tume yaUmwagiliaji (NIRC) na Mamlaka ya Bonde la Rufij iwameainisha mipaka kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Na.28 la terehe 14 Machi, 2008 na kupokea maoni ya wananchikuhusu mapendekezo ya marekebisho ya mipaka kwa GN.Na. 28 la terehe 14 Machi, 2008. Katika Mkoa wa Iringa Vijiji58 na Mkoa wa Mbeya Vijiji 20 viliwezeshwa kuandaa nakusimamia Mipango ya Matumizi ya Ardhi. Aidha, miradimikubwa nane (8) ya umwagiliaji imebainika kuanzishwa bilakufanya Tathimini ya Athari kwa Mazingira. Miradi hiyo niMAMCOS, Mwashikamile, Nguvu Kazi, Mnazi, Kapunga SmallHolder, Igowole, Bwawa la Lwanyo na Mwendamtitu. Miradiyote imepewa amri ya kufanya Ukaguzi wa Mazingira(Environmental Audit); Tathmini imefanyika kwenye Mito ya

Page 97: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

Mswiswi na Chimala Wilayani Mbarali na jumla ya vibali 15vimefanyiwa mapitio; Tathimini ya Mazingira Kimkakati (TMK)ilifanyika kwa Bonde zima la Mto Rufiji; na kazi ya kupitia vibalivya watumia maji 20 katika Mito ya Mbarali na Mswiswilimefanyika na wahusika wote 20 wamepewa notisi iliwajenge miundombinu sahihi kuzuia upotevu wa maji.

Kutangaza Maeneo ya Mazingira – Lindwa na Nyeti48. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia matakwa ya Sheriaya Mazingira hatua za makusudi za kushirikisha wananchipamoja na viongozi wao katika kujadili na kuamua maeneoyanayopendekezwa kuwa maeneo Lindwa au Nyeti yaMazingira. Katika mwaka 2018/19 Serikali kwa kushirikiana nawadau hao imeandaa orodha ya maeneo Nyeti hapa nchini;Kutathmini hali ya maeneo hayo na kuandaa taarifa za awali;Kuunda Kamati ya Kitaifa ya kuanzisha Maeneo Lindwa auNyeti; na Kuandaa vigezo vya kubainisha na kuanzishamaeneo Lindwa ya mazingira nchini. Aidha, Serikali inafanyatathmini ya hali ya Milima na Vilima hapa nchini ili kufuatiliana kutathmini mabadiliko yake. Hatua hii inajumuishaukusanyaji wa takwimu za mifumo ikolojia.

Mpango Mkakati wa Taifa wa Kudhibiti Viumbe Vamizi(Invasive Species)49. Mheshimiwa Spika, Viumbe Vamizi ni changamotokubwa na mpya ya mazingira nchini. Viumbe hawahusababisha athari kubwa katika uchumi hususan katikasekta kuu za uzalishaji kama vile, kilimo, uvuvi, mifugo, maji,maliasili na utalii na hivyo kuathiri ajira na maendeleo ya taifakwa ujumla. Pia huathiri afya ya binadamu, mifugo pamojana mazingira kwa kuharibu mifumo ikolojia. Tafiti zinaoneshakuna takriban aina 220 ya Viumbe Vamizi nchini na Tanzaniaimeathirika zaidi ya nchi nyingine katika ukanda wa AfrikaMashariki na Kati. Kwa kuzingatia hali hiyo hatua za harakazisipochukuliwa kuwadhibiti, uchumi wa nchi na ustawi wawananchi utaendelea kuathirika kwa kasi kubwa.

50. Mheshimiwa Spika, Ili kukabiliana na athari hizo katikamwaka 2018/19, Ofisi iliunda Kikosi Kazi cha Kitaifa kwa ajiliya kuandaa Mkakati wa Taifa wa Kudhibiti Viumbe Vamizi.

Page 98: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

Mkakati huo utasaidia kudhibiti kuongezeka na kusambaakwa viumbe hawa nchini ambao ni tishio kubwa kwabioanuai. Mpango Mkakati huo umebainisha hatua zakuchukua ili kukabiliana na changamoto hii pamoja nakuainisha majukumu ya kila Sekta husika. Mkakati huuutajadiliwa katika kikao cha Kamati ya Mazingira ya Barazala Mawaziri ili kuwa na uelewa wa pamoja wa majukumu yaSerikali na wadau katika utekelezaji wa mkakati huo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja nawajumbe wa kikosi kazi cha Kuandaa Mkakati wa kutatuachangamoto za viumbe vamizi nchini mara baada ya uzinduziuliofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano chaMwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam

Kampeni ya Upandaji miti51. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2018/19, Mkakati wa Taifa wa Upandaji wa Miti ( 2016 – 2021)umeendelea kutekelezwa. Hata hivyo, utekelezaji wakeumekumbwa na changamoto ya upatikanaji wa rasilimalifedha. Changamoto nyingine ni pamoja na: uwasilishwaji watakwimu zisizo akisi hali halisi ya upandaji na utunzaji miti katikaHalmashauri za Wilaya; Ufuatiliaji na utunzaji hafifu wa miti

Page 99: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

iliyopandwa; na upandaji wa miti isiyo rafiki kuendana naeneo husika. Ili kuimarisha utekelezaji wa Mkakati huo Serikaliinaandaa mapendekezo ya kukabiliana na changamoto hizoikiwa ni pamoja na kutafuta namna bora ya kuratibu nakusimamia utekelezaji wa Mkakati huo.

Udhibiti wa Taka Ngumu Nchini52. Mheshimiwa Spika, uchafuzi wa mazingira utokanaona taka ngumu umeendelea kuwa changamoto katikamaeneo ya mijini. Hii inachangiwa na uwezo mdogo waMamlaka za Serikali za Mtaa na miundombinu hafifu yausimamizi wa taka za aina hii. Katika mwaka 2018/19, Ofisiimeandaa Mwongozo wa Uwekezaji katika Taka Ngumu ilikuhamasisha uwekezaji na kuongeza jitihada za kuboreshausimamizi wa taka hapa nchini. Mwongozo huo umeainishafursa za uwekezaji zilizopo na taratibu za kuomba vibali naleseni. Baadhi ya fursa zilizopo ni pamoja na ukusanyaji nausafirishaji wa taka ngumu; urejelezaji wa taka; viwanda vyauzalishaji mboji; uzalishaji wa umeme kutokana na takangumu; ujenzi na uendeshaji wa madampo ya kisasa namitambo ya kutibu majitaka; na uteketezaji wa taka hatarishi.

53. Mheshimiwa Spika, shughuli hizi zinafanyika katikamaeneo ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, hivyo jukumu lausimamizi na udhibiti wa taka ngumu katika maeneo hayo nila TAMISEMI. Hivyo, Ofisi ya Rais – TAMISEMI ina jukumu lamuhimu sana kufuatilia utekelezaji wa Mwongozo huo ilikuleta ufanisi.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na MazingiraMussa Sima (mwenye kofia) akikagua dampo la Halmashauri yaMji wa Njombe katika ziara iliyofanyika katika Mikoa ya Nyandaza Juu Kusini.

Page 100: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

Usimamizi wa Taka Zenye Madhara54. Mheshimiwa Spika, taka hatarishi zinazalishwaviwandani, migodini, hospitalini na baadhi ya maeneo yabiashara. Ofisi imeendelea kudhibiti uzalishaji na utupaji wataka zenye madhara kwa mujibu wa Kanuni za Udhibiti waTaka zenye Madhara za mwaka 2009. Aidha, Serikali inapitiautaratibu wa kusimamia taka zenye madhara kwa lengo lakuziboresha ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu wa kudhibitiusafirishaji wa vyuma chakavu nje ya nchi. Vile vile, Serikaliimeimarisha udhibiti katika vituo vya forodha pamoja nakuimarisha ushirikiano na Taasisi zenye dhamana. Lengo nikupunguza na kuondoa biashara holela ya vyuma chakavuinayochangia kuhujumu na kuharibu miundombinu. Aidha,kwa kushirikiana na maafisa mazingira wa Halmashauri naBaraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)imeendelea kutoa vibali vya kukusanya, kuhifadhi, kusafirishana kurejeleza taka kwa kampuni zilizokidhi vigezo. Hadi kufikiamwezi Machi, 2019 vibali 87 kati ya maombi 107 vimetolewa.

Tathmini ya Mazingira Kimkakati (TMK)55. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2018/19 Ofisi imeandaa Mwongozo wa ufundishaji kwa ajili yakujenga uwezo kwa wadau katika kutumia Mwongozo waTathmini ya Mazingira Kimkakati. Mwongozo huo umetafsiriwakatika lugha ya kiswahili ili kujenga uelewa kwa wadau wengi.Mwongozo huu una lengo la kuwezesha Mipango, Mikakati,Sera, na Miradi Mikubwa kufanyiwa Tathmini ya MazingiraKimkakati ili kuhakikisha kuwa uchumi wa viwanda unakuakatika hali endelevu.

56. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19 Ofisiimesajili mipango saba (7) ya Tathmini ya Mazingira Kimkakatiambayo ripoti zake zimekamilika na nyingine zinaendeleakuandaliwa na ziko katika hatua mbalimbali za ukamilishaji.Mipango iliyosajiliwa na kupata idhini ni:- Mradi wa kufuaUmeme wa Rufiji (Rufiji Hydropower Project); Uboreshaji waMpango kabambe wa Taifa wa Umwagiliaji (UpdatingNational Irrigation Master Plan); Mpango Kabambe wa Usafirikatika Jiji la Dar es Salaam, (Dar es Salaam Transport MasterPlan); na Sera, Mikakati, Sheria na kanuni za Uvuvi wa Bahari

Page 101: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

Kuu (Policy for Deep Sea Fisheries; Policy ImplementationStrategy; Deep Sea Fishing Authority Act; and Deep SeaFishing Authority Regulations); Aidha, Mipango iliyosajiliwaambayo ipo katika mchakato wa kukamilisha tathimini nakupatiwa idhini ni:- Mpango Kabambe wa Mji wa Serikali(Government City Master Plan); Mpango Kabambe waMafuta na Gesi (Oil and Gas Master Plan); na MpangoKabambe wa eneo la Viwanda Handeni (Handeni IndustrialPark Limited, Master Plan).

Mfuko wa Mazingira wa Dunia (Global Environmental Facility)57. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19 Ofisiimeendelea kuratibu shughuli za Mfuko wa Mazingira waDunia hapa nchini kwa kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wamiradi mitatu iliyopata ufadhili kutoka GEF ambayo ni Mradiwa Kukabiliana na Ujangili Nchini (Combating Poaching andIllegal Wildlife Trade in Tanzania Through IntegratedApproach) unaotekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii;Mradi wa kuzuia Uharibifu wa Ardhi na Kuongeza Usalamawa Chakula Katika Maeneo Kame ya Nyanda za Kati(Reversing Land Degradation Trends and Increasing FoodSecurity in Degraded Ecosystems of Semi-arid Areas of CentralTanzania) unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais; naMradi wa Kukuza Matumizi ya Bio-Ethanol kama NishatiMbadala kwa Kupikia (Promotion of Bio-Ethanol as AlternativeClean Fuel for Cooking in the United Republic of Tanzania)ambao unatekelezwa na Wizara ya Nishati.

58. Mheshimiwa Spika, Ofisi kwa kushirikiana na wadauimeandaa miradi mitano (5) na kuiwasilisha katika Sekretarietiya GEF kwa ajili ya kupata ufadhili chini ya Awamu ya Sabaya mfuko huo (GEF – 7th Replenishemnt Cycle). Katika awamuhii Tanzania imetengewa fedha kiasi cha Dola za Kimarekanimilioni 24 ambazo zitatumika katika kuandaa na kutekelezamiradi inayolenga kuhifadhi mazingira kwa kuzingatiavipaumbele vya nchi pamoja na matakwa ya Mikataba yaKimataifa inayohusu mazingira ambayo nchi yetu nimwanachama. Miradi iliyowasilishwa ni pamoja na: Programuya Hifadhi Endelevu ya Ziwa Tanganyika (The Lake TanganyikaRegional Environmental Programme); Integrated Land Use

Page 102: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

and Restoration Program for Tanzania’s Productive ForestLandscape; Integrated Land Cape Management in the DryMiombo Woodlands in Tanzania; Sustainable CitiesProgramme; na Programu ya Ufadhili wa Miradi Midogo (GEFSmall Grants Programme).

Uratibu na Utekelezaji wa Mikataba ya Kimataifa na yaKikanda ya Mazingira59. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2018/19, Ofisi kwa kushirikiana na Wizara za kisekta na Wadau waMaendeleo imeratibu na kutekeleza Mikataba ya mazingiraya Kimataifa na Kikanda. Mikataba hiyo ni:-

Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi na Itifaki ya Kyoto60. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19 Ofisiimeratibu utekelezaji wa miradi minne mikubwa ya kuhimilimabadiliko ya tabianchi. Miradi hiyo ni:- Mradi wa KujengaUwezo wa Jamii za Pwani Kuhimili Athari za Mabadiliko yaTabianchi; Mradi wa Kuhimili Athari za Mabadiliko yaTabianchi katika Jiji la Dar es Salaam; Mradi wa Kuhimili Athariza Mabadiliko ya Tabianchi kupitia Hifadhi ya Ikolojia(Ecosystem Based Adaptation for Rural Resilience; na Mradiwa Kupunguza Uharibifu wa Ardhi na Kuboresha Usalama waChakula katika Maeneo Kame Nchini (Reversing LandDegradation Trends and Increasing Food Security inDegraded Ecosystem of Semi Arid Areas of Tanzania-LDCFS).

61. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Ofisiimeendelea kutekeleza Mradi wa Kujenga Uwezo wa Jamiiza Pwani Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi. Kupitia mradi huuukuta wa Mto Pangani Tanga umeendelea kujengwa hadikufikia mita 795 kati ya mita 950 zilizopangwa kujengwa.Lengo la ujenzi huu ni kukabiliana na mmomonyoko wa fukweutokanao na kuongezeka kwa kina cha bahari (sea level rise).Aidha, mikoko imepandwa katika Wilaya ya Kibiti (hekta 208).Vilevile, miundombinu ya kuvuna maji ya mvua imejengwakatika Shule za Sekondari Kingani na Matipwili katika Wilayaya Bagamoyo. Kazi nyingine zilizofanyika ni ujenzi wa matanki10 ya kuhifadhi maji ya visima ya ujazo wa lita 15,000 kila moja.

Page 103: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

62. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Ofisiimeendelea kutekeleza mradi wa Kuhimili Mabadiliko yaTabianchi katika Jiji la Dar es Salaam. Kupitia mradi huu ujenziwa mfereji wenye urefu wa mita 550 katika eneo la Mtoni,Temeke, Dar es Salaam uliobomolewa na mvua kubwa mweziAprili, 2018 ulijengwa upya na kukamilika; miche ya mikokoilipandwa kwa ajili ya kuziba mapengo yaliyojitokeza katikaeneo la Mbweni na Kigamboni; na Tathmini ya Mwisho yaMradi na Ukaguzi wa mradi ulifanyika.

63. Mheshimiwa Spika, Ofisi ilianza utekelezaji wa Mradiwa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi katika maeneo ya Vijijinikupitia Mfumo Ikolojia (Ecosystem-Based Adaptation for RuralResilience in Tanzania). Mradi huu ni wa miaka mitano (5)kuanzia mwaka 2018 hadi 2022 na unafadhiliwa na Mfukowa Mabadiliko ya Tabianchi kwa nchi Masikini (LeastDeveloped Countries Fund – LDCF) kupitia Mfuko wa Duniawa Mazingira (Global Environment Facility – GEF). Mradiunatekelezwa katika Wilaya nne (4) Tanzania Bara na Wilayamoja (1) Tanzania Zanzibar. Wilaya hizo na Mikoa yake nipamoja na: Mpwapwa (Dodoma), Kishapu (Shinyanga),Simanjiro (Manyara), Mvomero (Morogoro) na Kaskazini AUnguja (Kaskazini Unguja).

64. Mheshimiwa Spika, lengo la mradi huu ni kuongezauhimilivu wa kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi kupitiamifumo ikolojia katika maeneo ya vijijini. Kufikiwa kwa lengohili kutachangia katika kupunguza hatari za athari zaMabadiliko ya Tabianchi kwa jamii zinazoishi vijijini. Kupitiauboreshaji wa mifumo ikolojia, mradi utachangia pia katikakuongeza uzalishaji wa chakula, kuboresha ufugaji nakuboresha uhifadhi wa mazingira katika Wilaya husika zamradi. Mradi utawanufaisha wananchi wapatao 1,468,035katika Kaya 298,631 katika Wilaya zinazotekeleza mradi. Mradiutaongoa hekari 9,200, kati ya hizo hekari 3,000 ni maeneoya vyanzo vya maji (watershed) na maeneo ya misituyaliyoharibika; hekari 6,000 zitaongolewa na kutumika katikakuboresha nyanda za malisho (rangeland rehabilitation) kwaajili ya mifugo; na hekari 200 zitaongolewa katika maeneoyaliyoko kando ya Mito iliyoharibiwa (riverbank rehabilitation).

Page 104: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

Aidha, mradi unatarajia kuendesha Kilimo Rafiki kwa Hali yaHewa (Climate Smart Agriculture – CSA) ambacho kitafanyikakatika Vijiji vinavyotekeleza kilimo kinachohimili mabadilikoya tabianchi.

Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kueneakwa Hali ya Jangwa na Ukame65. Mheshimiwa Spika, nchi yetu inakabiliwa na kueneakwa hali ya jangwa na ukame katika maeneo mengi. Sualahili kwa sasa linachochewa zaidi na janga la Mabadiliko yaTabianchi. Katika kipindi cha mwaka 2018/19, Ofisi imeratibumaandalizi ya Programu ya Kitaifa yenye madhumuni yakufanya tathmini ya maeneo yaliyoathirika ili kuwekashabaha ya kuzuia uharibifu wa ardhi (Land DegradationNeutrality Target Setting) ifikapo mwaka 2030 katikakutekeleza maazimio ya nchi wanachama. Uandaaji washabaha hizi ni mojawapo ya utekelezaji wa Makubalianoya Mkutano wa Kumi na Mbili wa Nchi Wanachama waMkataba uliofanyika Jijini Ankara nchini Uturuki mwaka 2015.

66. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Ofisi ilianzautekelezaji wa Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika naKuongeza Uhakika na Usalama wa Chakula katika MaeneoKame ya Pwani ya Tanzania kwa ufadhili wa Mfuko waMazingira wa Dunia (Global Environment Facility - GEF) kupitiaMfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (InternationalFund for Agricultural Development - IFAD). Lengo la mradihuu ni kuboresha mifumo ya Ikolojia ya Kilimo ambayoitawezesha kuongeza uzalishaji wa chakula na kuchangiakuboresha Mazingira katika Wilaya husika za mradi. Madi huuunatekelezwa katika Vijiji ishirini na tano (25) katika Kata sita(6) Wilaya tano (5) na Mikoa mitano (5) kama ifuatavvyo: -Mkoa wa Tabora ni vijiji vya Lyamalagwa, Sigili, Bulambuka,Iboja na Bulende vilivyoko kata ya Sigili, Wilaya ya Nzega.Mkoa wa Mwanza ni vijiji vya Lumeji, Iseni na Nyang’hangavilivyoko kata ya Sukuma, Wilaya ya Magu. Mkoa wa Singidani vijiji vya Mpambala, Nyahaa, Lugongo, Mkiko na Mungulivilivyoko kata ya Mpambala, Wilaya ya Mkalama. Mkoa waDodoma ni vijiji vya Ntomoko, Haubi, Mafai na Mwisangavilivyoko kata ya Haubi, Wilaya ya Kondoa. Katika Mkoa wa

Page 105: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

Kaskazini Pemba mradi unatekelezwa katika Wilaya yaMicheweni, Kata ya Micheweni, Shehia za Micheweni Mjini,Micheweni Chamboni, Kwale/Majenzi, Shumba Mjini na MjiniWingwi. Katika Kata ya Kiuyu mradi unatekelezwa katikaShehia ya Kiuyu Mbuyuni na katika Kata ya Maziwa Ng’ombeunatekelezwa katika Shehia za Maziwa Ng,ombe naShanaka.

Mkataba wa Hifadhi ya Bioanuai

67. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2018/19, Ofisi imeendelea kuratibu na kusimamia utekelezaji waMkataba wa Hifadhi ya Bioanuai na Itifaki zake. Ofisiimeandaa Ripoti ya Sita ya utekelezaji wa Mkataba waKimataifa wa Hifadhi ya Bioanuai ambayo itawasilishwakatika Sekretarieti ya Mkataba kwa ajili ya kuandaa taarifaya Hali ya Bioanuai Duniani (Global Biodiversity Outlook).Pamoja na mambo mengine ripoti imebainisha hali yabioanuai nchini; changamoto zinazosababisha upotevu wabioanuai; hatua na Mikakati iliyochukuliwa kutekelezaMkakati na Mpango Kazi wa Taifa wa Hifadhi ya Bioanuainchini (National Biodiversity Strategy and Action Plan, NBSAP).Aidha, katika kipindi hiki, Ofisi kwa kutumia wakaguzi waMatumizi Salama ya Bioteknolojia ya Kisasa imeendeleakusimamia na kukagua shughuli za utafiti wa mazao ya kilimoyaliyofanyiwa mabadiliko ya kijenetiki katika Kituo cha Utafitiwa Kilimo Makutupora, Dodoma.

68. Mheshimiwa Spika, Ofisi imeendelea kukuza uelewawa jamii kuhusu matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasakwa kutumia vyombo vya habari kama redio na luninga.Vilevile, Ofisi imeendesha mafunzo kwa wataalam kutokaSekta zinazohusika na matumizi ya bioteknolojia ya kisasa,mafunzo hayo pamoja na mambo mengine yalihusishamaeneo yafuatayo: utambuzi wa mazao yaliyoboreshwavinasaba (GMOs Detection); tathmini ya uwezekano wakutokea kwa madhara kwa mazingira (Environmental RiskAssessment); na tathmini ya usalama wa chakula chabinadamu na wanyama (Food and Feed Assessment).

Page 106: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

Mkataba wa Nairobi Kuhusu Hifadhi, Usimamizi na Uendelezajiwa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibiya Bahari ya Hindi69. Mheshimiwa Spika, Ofisi imeendelea kuratibuutekelezaji wa Mkataba wa Nairobi pamoja na Itifaki zake.Katika mwaka 2018/19 Ofisi iliratibu uandaaji wa miradi yautekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mkataba wa Nairobi waUhifadhi wa Mazingira ya Bahari Magharibi ya Bahari ya Hindikutokana na vyanzo na shughuli zinazofanyika nchi kavu (TheStrategic Action Programme for the Protection of the WesternIndian Ocean from Land-Based Sources and Activities -WIOSAP). Kupitia uratibu huu, Ofisi ilipokea maandiko ya awaliya miradi ya mfano kumi (10) kutoka kwa wadau mbalimbaliwanaojihusisha na uhifadhi wa mazingira ya bahariinayolenga kupunguza uchafuzi wa bahari kutokana na majitaka, usimamizi wa maeneo nyeti ya bahari (Managementof critical habitat) na usimamizi endelevu wa mitiririko ya mito(Sustainable Management of River Flows). Maandiko hayoyalipitiwa na timu ya wataalamu katika ngazi ya Kitaifa nakupata maandiko bora matatu (3) ambayo yamewasilishwaSekretarieti ya Mkataba kwa ajili ya kupitiwa na kuboreshwakatika ngazi ya Kikanda.

70. Mheshimiwa Spika, Ofisi imefanya mapitio ya Mkakatiwa Kuhifadhi Mazingira ya Ardhi na Vyanzo vya Maji wamwaka (2006) na Mkakati wa Hatua za Haraka za KuhifadhiMazingira ya Bahari, Ukanda wa Pwani, Maziwa, Mito naMabwawa wa mwaka (2008). Mikakati hii imefanyiwa mapitioya utekelezaji kwa kipindi cha miaka mitano (2019 -2024).Mapitio ya Mikakati hii yamebainisha changamoto mpyaambazo hazikuwa zimebainishwa wakati wa maandalizi yaMikakati hii mwaka 2006 na 2008. Changamoto mpyazilizobainishwa ni pamoja na: Mabadiliko ya Tabianchi;Viumbe Vamizi; Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na GesiBaharini na kwenye Maziwa; na ongezeko la uchafuzikutokana na Taka za Plastiki. Aidha, Mikakati hii imeainishahatua na mipango ya utekelezaji ili kutatua changamoto hizo.

71. Mheshimiwa Spika, mapitio ya Mikakati hii namaandalizi ya mipango ya utekelezaji katika kipindi cha

Page 107: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

mwaka (2019 - 2024) yalishirikisha wadau kutoka Wizara zaKisekta, Vyuo vya Elimu ya Juu na Taasisi za Utafiti, Mamlakaza Serikali za Mitaa, Sekta binafsi na Mashirika Yasiyo yaKiserikali. Ushiriki huu wa wadau ulisaidia katika kutoamwongozo na kusanifu Mikakati ya utekelezaji inayoendanana utekelezaji wa Sera, Mipango na Mikakati yao pamojana kujenga uwezo wao katika kuutekeleza Mkakati huu.

Mkataba wa Basel Kuhusu Udhibiti wa Usafirishaji na Utupajiwa Taka za Sumu Kati ya Nchi na Nchi72. Mheshimiwa Spika, kuhusu utekelezaji wa Mkatabawa Basel, Ofisi imeendelea kutoa elimu kwa Umma kupitiavyombo vya habari kuhusu taratibu za kukusanya, kusafirishana kurejeleza taka hatarishi na taratibu zinazotakiwa ilikusafirisha taka nje ya nchi kwa madhumuni mbalimbaliikiwemo kurejelezwa au kuteketezwa. Vilevile, Ofisiimeendelea kudhibiti uingizaji na usafirishaji wa taka zenyemadhara baina ya nchi kupitia Tanzania kwa kuzingatiaKanuni na Matakwa ya Mkataba wa Basel.

Mkataba wa Stockholm Kuhusu Udhibiti wa KemikaliZinazodumu Katika Mazingira kwa Muda Mrefu73. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Ofisiimeendelea kuratibu utekelezaji wa Mkataba wa Stockholmkatika kuzuia madhara ya kemikali zinazodumu kwenyemazingira kwa muda mrefu. Ofisi imeratibu zoezi la kukusanyasampuli za mafuta ya transfoma zinazomilikiwa na TANESCOna ZECO yanayodhaniwa kuwa na kemikali aina ya“Polychlorinated Biphynels” (PCBs) ambayo imethibitika kuwaina madhara katika mazingira na inapaswa kuondoshwaifikapo mwaka 2025 kulingana na matakwa ya Mkataba huu.Sampuli hizo zitawasilishwa katika kituo cha Africa Institutekilichopo Pretoria, Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi kablaya kuondoshwa kwa kemikali hizo. Vilevile, Ofisi kwakushirikiana na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu waSerikali na Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika nchi za Kitropiki(Tropical Pesticides Research Institute - TPRI) imetoa mafunzokwa maafisa ugani na Taasisi za Serikali na zisizo za Serikalizinazojishughulisha na uchimbaji wa gesi nchini kuhusu udhibitiwa kemikali.

Page 108: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

74. Mheshimiwa Spika, Ofisi kwa kushirikiana na wadauwengine imeendesha zoezi la ukusanyaji wa taarifa za haliya uchomaji wa taka kwenye madampo makubwa katikaMajiji yote nchini. Lengo la taarifa hizi ni kuandaa Mpangowa kuhamasisha mbinu bora na rafiki kwa mazingira zakupunguza uzalishaji wa kemikali zinazodumu kwenyemazingira kwa muda mrefu zitokanazo na uchomaji wa taka.

Mkataba wa Vienna na Itifaki ya Montreal Kuhusu KemikaliZinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni75. Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa Mkataba waVienna na Itifaki ya Montreal Kuhusu KemikaliZinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni, Ofisi iliendelea kuratibuutekelezaji wa Mkataba na Itifaki yake inayohusu udhibiti wakemikali zinazomong‘onyoa Tabaka la Ozoni. Kazizilizotekelezwa ni pamoja na: Kuendesha mafunzo kwamaafisa forodha na mafundi mchundo 40 kuhusu teknolojiampya na njia sahihi za kuhudumia vifaa vinavyotumia kemikalizinazoharibu Tabaka la Ozoni; Kutoa elimu kwa Umma kuhusuutekelezaji wa Itifaki ya Montreal na kemikali mbadala wakatiwa maadhimisho ya Siku ya Ozoni tarehe 16 Septemba, 2018;na kuendelea kuhamasisha wafanyabiashara, watumiaji nawaingizaji wa kemikali nchini kupunguza kiasi cha uingizajina utumiaji wa kemikali ambazo zitaondolewa katika sokokutokana na kubainika kuongeza joto angani(Hydrochrolofluorocarbons - HCFCs). Aidha, Ofisi imeratibuukusanyaji wa takwimu za uingizaji na matumizi ya kemikalimbadala zinazoharibu Tabaka la Ozoni. Takwimu hizizinaendelea kutusaidia kupanga mikakati ya kusitishamatumizi ya kemikali zinazoharibu Tabaka la Ozoni.

Mkataba wa Minamata Kuhusu Udhibiti wa Matumizi yaZebaki76. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha mwaka 2018/19, Ofisi imeendelea kuratibu utekelezaji wa Mkataba waMinamata unaohusu udhibiti wa matumizi ya zebaki kwa ajiliya kulinda afya ya binadamu na mazingira. Aidha, Ofisiimekamilisha Rasimu ya Mpango-Kazi wa Kitaifa waKupunguza Matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo wadhahabu nchini pamoja na kuandaa Kanuni za zebaki.

Page 109: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi (Green Climate Fund –GCF)77. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Ofisiiliendelea kuhimiza suala la Taasisi za Umma na Sekta binafsihapa nchini kupata ithibati (accreditation) katika Mfuko waMabadiliko ya Tabianchi (GCF). Aidha, Wizara ya Fedha naMipango ilifanya tathmini ya Kitaasisi yenye lengo lakuangalia jinsi mifumo, taratibu, Kanuni na miongozo ya fedhahapa nchini, inavyokidhi mahitaji na vigezo vya usajili vyaGCF. Mwezi Januari mwaka 2019, Wizara iliendesha warshaya wadau kwa ajili ya kupokea, kujadili, na kuhakiki (validate)rasimu ya taarifa ya tathmini. Vilevile, Ofisi ya Rais, Tawala zaMikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mwezi Februari, 2019iliwasil isha rasmi maombi ya kupata ithibati kwenyeSekretarieti ya GCF.

78. Mheshimiwa Spika, Ofisi iliendelea kuratibu uchambuziwa miradi chini ya ufadhili wa Mfuko wa Mabadiliko yaTabianchi (Green Climate Fund - GCF). Katika kipindi hikiuchambuzi wa miradi mitatu ulifanyika. Kati ya miradi hiyomradi mmoja ambao umekidhi vigezo uliwasilishwa GCF kwaajili ya kupatiwa fedha za utekelezaji. Aidha, katika kipindihiki Ofisi iliwezesha ukamilishaji wa Mikataba ya kifedha kwaajili ya utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Simiyu wenyegharama ya kiasi cha Sh. bilioni 250. Ofisi ilisimamia uwekajisaini wa Mkataba wa Kifedha kati ya GCF na KfW. Tukio hilolilifanyika tarehe 12 Desemba, 2018 huko Katowice, Polandwakati wa Mkutano wa 24 wa Nchi Wanachama waMkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na MazingiraMussa Sima akihutubia wakati wa Mkutano wa Mabadiliko ya tabiaNchi (COP24/CMP14/CMA1.3) uliofanyika Katowice-Poland.

Page 110: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

Itifaki ya Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika kuhusuUsimamizi Endelevu wa Mazingira79. Mheshimiwa Spika, Tanzania ni Mwanachama waJumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na inashirikikatika kutekeleza Mikataba na Itifaki mbalimbalizinazopitishwa na nchi wanachama wa Jumuiya. Katikakipindi cha mwaka 2018/19, Ofisi imeanza utaratibu wakuridhia Itifaki ya SADC kuhusu Usimamizi Endelevu waMazingira ikiwa ni pamoja na kukusanya maoni ya wadauna kuandaa andiko kabla ya kuanza taratibu ya kuridhia itifakihiyo.

Elimu kwa Umma Kuhusu Usimamizi na Hifadhi ya Mazingira80. Mheshimiwa Spika, Ofisi ilikamilisha maandalizi yaMfumo wa Taarifa kuhusu Mazingira (Central EnvironmentalInformation System) utakaoendana na mfumo wa teknolojiaya simu kuwawezesha watumiaji kupokea na kutoa taarifazinazohusu masuala ya Mazingira.

BARAZA LA TAIFA LA HIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA81. Mheshimiwa Spika, Baraza la Taifa la Hifadhi naUsimamizi wa Mazingira ambalo ndio msimamizi mkuu wauzingatiaji na utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa MazingiraSura ya 191 limeendelea kutekeleza majukumu yake kamaifuatavyo:-

Uzingatiaji na Usimamizi wa Sheria ya Mazingira82. Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha Sheria ya Usimamiziwa Mazingira inazingatiwa ipasavyo katika kutekelezashughuli za maendeleo hapa nchini, Baraza limetekeleza kazizifuatazo:-

i) Ukaguzi wa Maeneo ya Uwekezaji na Mazingira83. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19 Barazalimefanya ukaguzi katika viwanda, machinjio ya wanyama,migodi (yakiwemo machimbo ya mchanga na kokoto),hifadhi ya vyanzo vya maji, mashamba, vituo vya mafuta,maghala ya kuhifadhi kemikali na taka hatarishi, madampo,hoteli, mifumo ya maji taka, taasisi za elimu na afya, majengoya biashara na makazi ili kupima uzingatiaji na usimamizi wa

Page 111: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

Sheria ya Usimamizi wa Mazingira nchini. Katika ukaguzi huojumla ya miradi 4,853 ilikaguliwa ambapo miradi 1,627 ni yaviwanda sawa na asilimia 34. Ukaguzi huo ulibaini kuwaasilimia 40 ya miradi inazingatia Sheria na baadhi ya miradikuwa na changamoto za kimazingira kama:- kutiririshamajitaka kwenye vyanzo vya maji na mazingira; Kutumiarasilimali za misitu ya asili kwa ajili ya kuni na majengo;Kutokuwa na mifumo ya kuhifadhi na kusimamia taka ngumu;Uzalishaji wa hewa chafu; Udhibiti na Uhifadhi duni wa takahatarishi; Upigaji wa kelele na mitetemo zaidi ya viwangovinavyokubalika kimazingira; na baadhi ya viwandakuanzishwa kwenye makazi ya watu.

84. Mheshimiwa Spika, Baraza limechukua hatua stahikikwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, Sura ya191, kwa miradi iliyokiuka Sheria na Kanuni zake. Hatua hizoni pamoja na kutoa ushauri, maelekezo, maonyo, amri zakatazo, amri za urejeshaji wa mazingira na kuwafikishamahakamani

ii) Kushughulikia Malalamiko ya Kimazingira85. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19 Barazalimeendelea kupokea malalamiko yanayohusu uchafuzi wamazingira kutoka kwa wananchi na kuyashughulikia kwamujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, Sura 191 naKanuni zake. Katika kipindi hiki zaidi ya malalamiko 701yamepokelewa kutoka maeneo mbalimbali nchini nakuyapatia ufumbuzi. Baadhi ya malalamiko yalihusu:- Kelelekutoka katika karakana; Nyumba za ibada; Kumbi za starehe;Viwanda na utengenezaji wa matofali; Utiririshaji wa majitakakutoka kwenye maeneo mbalimbali ya uzalishaji; Uchimbajiwa mchanga katika vyanzo vya maji na maeneo mengineyo;na uchafuzi wa mazingira kutokana na uanzishwaji wamachinjio ya wanyama kwenye makazi ya watu.

Ukaguzi wa Sampuli86. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Barazakwa kushirikiana na Maafisa wa Bodi ya Maji ya Bonde laZiwa Rukwa, lilichukua sampuli thelathini (30) za tope/tabakikutoka kwenye vijito mbalimbali vya maji vinavyopatikana

Page 112: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

kwenye maeneo ambayo ni maarufu kwa uchimbaji mdogowa madini katika Wilaya ya Chunya. Sampuli hizozimepelekwa kwenye maabara ya SGS – Mwanza kwa lengola kuchunguza uwepo wa viambata vya kemikali za sumu(hasa Zebaki). Matokeo ya vipimo hivyo yatatoa majibu sahihiya hali halisi na taarifa zitatolewa kwa Umma. Aidha, sampulisita (6) za tabaki na maji zilichukuliwa katika fukwe karibu naeneo la uchakataji wa gesi asilia (Mnazi Bay - Mtwara) kwaajili ya ufuatiliaji.

Mafunzo kwa Wakaguzi wa Mazingira

87. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19 Barazalimetoa mafunzo kwa Wakaguzi wa Mazingira (EnvironmentalInspectors) 194 kutoka Kanda za Mashariki, Kusini, Nyanda zaJuu Kusini na Ziwa; Wizara ya Maji; na Wizara ya Mambo yaNdani. Mafunzo haya yatawawezesha Wakaguzi kusimamiavilivyo Sheria ya mazingira katika maeneo yao ya utendaji.

Uteketezaji wa Kemikali/Taka Hatarishi

88. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Barazakwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali kama Mamlaka yaChakula na Dawa (TFDA), Mamlaka ya Maabara ya MkemiaMkuu wa Serikali (GCLA) na Serikali za Mitaa (LGAs),limesimamia uteketezwaji (incineration) wa taka hatarishi kiasicha tani 90. Uteketezaji huo umefanyika kwa kutumiamtambo wa uteketezaji taka (incinerator) wa Safe wasteulioko Mkuranga na Tindwa Medical and Health Service uliokoKisarawe. Vile vile, makampuni 45 yalipewa miongozo nakusimamiwa katika uteketezwaji wa taka hatarishi hususanikemikali, madawa ya binadamu yaliyomaliza muda wamatumizi na mabati ya asbestos. Aidha, Baraza kwakushirikiana na Taasisi ya Usajili na Utafiti wa Viuatilifu nchini(TPRI) lilifanya ukaguzi wa eneo lenye madawa chakavu yakilimo (Obsolete Pesticides) lililoko Arusha na kuhakikishamadawa hayo yamehifadhiwa (Safeguarding ObsoletePesticides Stockpiles) katika utaratibu maalum na hivyokuondoa uwezekano wa kusababisha athari za kiafya nakimazingira.

Page 113: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM)

i) Usajili wa Miradi na Utoaji wa Vyeti vya Mazingira

89. Mheshimiwa Spika, ili kufanyia kazi changamotozilizojitokeza katika utoaji wa vyeti vya Tathimini ya Athari kwaMazingira katika Miradi ya Maendeleo utaratibu wa utoajiwa vyeti hivyo umeboreshwa. Baraza limeweka utaratibu wakutoa Kibali cha Awali cha Mazingira (ProvisionalEnvironmental Clearance) ili kuwawezesha wawekezajikuendelea na maandalizi ya awali ya mradi wakati mchakatowa TAM unaendelea. Kibali hicho kinatumika kwa miradi yaviwanda, kilimo na miradi mingine ya kipaumbele kwa Serikali.Mpaka sasa jumla ya Vibali saba (7) vya Awali vya Mazingiravimetolewa. Utaratibu huu utasaidia kuharakisha uwekezajikatika Sekta ya viwanda nchini. Vilevile Serikali inaandaautaratibu utakaowezesha kuwa na namba za simu (hot lines)zitakazowezesha wawekezaji kutoa taarifa au malalamikokuhusiana na maombi wanayoyawasilisha ili yawezekufanyiwa kazi kwa wakati. Utaratibu huu utawezesha Ofisikufanyia kazi maoni yanayotolewa na hivyo kuboreshataratibu zinazotumika kutoa vyeti hivi kila inapohitajika.

Katika mwaka 2018/19 Baraza limesajili jumla ya miradi 1,254ya maendeleo kwa ajili ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira(TAM) na Ukaguzi wa Mazingira, ambapo jumla ya miradi 455ilikamilika na kupatiwa vyeti vya mazingira. Vilevile, Ofisiimefanya maboresho ya Kanuni katika mchakato wa TaMna kupunguza idadi ya siku. Miradi yenye athari ndogo kwamazingira itatumia jumla ya siku 35 tu kupata cheti ambaposiku 21 zitakuwa kwa ajili ya NEMC kukamilisha taratibu husika,na siku 14 ni kwa ajili ya Waziri mwenye dhamana ya mazingirakutoa maamuzi. Aidha, Miradi yenye athari kubwa kwamazingira itapata kibali cha muda ndani ya siku 14 na sasamchakato wa TAM utatumia siku 88 kutoka siku 149 zilizokuwazikitumika awali. Aidha, gharama ya usajili wa miradi ya TAMimepungua na haitozwi kwa kiwango cha asilimia yagharama ya mradi kama ilivyokwa awali. Kwa sasa gharamaza usajili wa mradi zinaanzia Sh. Milioni 4 kwa miradi midogona kwa miradi mikubwa gharama haizidi Sh. milioni 50.

Page 114: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

90. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha mchakato wamiradi ya kitaifa na kimataifa inakwenda kwa kasiinayokubalika, Baraza limekuwa likishauriana na wahusikakatika kila hatua ya utekelezaji. Mfano wa miradi hiyo ni: Mradiwa ujenzi wa Bomba la mafuta (East Africa Crude Oil Pipeline- EACOP). Baraza limepokea ripoti ya Tathmini ya Athari kwaMazingira na Kamati ya kupitia ripoti hii imeteuliwa; Mradiwa ujenzi wa Uwanja wa Mpira Dodoma (Dodoma SportsComplex) ulipewa cheti cha Mazingira tarehe 31 Julai 2018;na Mradi wa kufua Umeme wa Rufiji (Rufiji HydropowerProject) umeshapatiwa cheti cha TAM. Baraza kwakushirikiana na TANESCO litaratibu na kusimamia utekelezajiwa mpango wa usimamizi wa mazingira wakati wote wautekelezaji wa mradi.

ii) Kuandaa Miongozo kuhusu TAM91. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha mchakato waTAM unatekelezwa kwa ufanisi, Baraza kwa kushirikiana naKituo cha Sayansi na Mazingira cha India limeandaamiongozo itakayosaidia kurahisisha mapitio ya miradi yamajengo na Sekta ya ujenzi. Miongozo hii iko katika hatua zamwisho ambapo wadau watashirikishwa kutoa maoni kablaya kupitishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza.

Aidha, Baraza kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maabara yaMkemia Mkuu wa Serikali – Mbeya, Ofisi ya Madini ya Mkoawa Mbeya na Wilaya ya Chunya, Sekretarieti ya Mkoa waMbeya, Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Mamlaka ya Afyana Usalama Mahala pa Kazi (Mbeya) na wawakilishi wawachimbaji wadogo kutoka Wilaya ya Chunya limeandaautaratibu wa kurahisisha mchakato wa kuandaa maandikoya Tathimini ya Athari kwa Mazingira kwa miradi ya wasafishajiwadogo wa dhahabu (elusion plants) katika Wilaya yaChunya. Utaratibu huu utawapunguzia gharama za kufanyaTAM wawekezaji hao wadogo katika Sekta ya madini.

Elimu kwa Umma Kuhusu Hifadhi ya Mazingira92. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Barazalimeendelea kutoa elimu kwa Umma kwa kutumia vyombovya habari na mafunzo kwa wadau kuhusu masuala ya

Page 115: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

mazingira ili kujenga uelewa kwa jamii kuhusu masuala yamazingira. Aidha, Baraza lilishiriki katika maadhimishombalimbali na muhimu kimazingira ili kukuza na kukuzauelewa wa jamii kwa lengo la kuboresha uwajibikaji katikakutunza na kuhifadhi Mazingira. Maadhimisho hayo ni pamojana Siku ya Maonesho ya Viwanda na Biashara na Maoneshoya Nane Nane. Pia Baraza liliendesha warsha ya kuelimishawadau kuhusu Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka2004 pamoja na Kanuni zake ambapo jumla ya wachimbajiwadogo 70 wa dhahabu pamoja na wamiliki 23 wa viwandavya kukoboa mpunga katika Mikoa ya Mbeya na Songwewalielimishwa.

Ajenda ya Taifa ya Utafiti katika Mazingira (NationalEnvironmental Research Agenda - NERA)93. Mheshimiwa Spika, Baraza limeendelea kutekelezaAjenda ya Taifa ya Utafiti katika Mazingira (NationalEnvironmental Research Agenda - NERA) kwa kufanyatathmini ya lindimaji/dakio (catchment) la Bonde la Wami-Ruvu. Mkutano wa wadau unaandaliwa ili kutengenezaMpango wa Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira ya dakiohilo. Vile vile, Baraza limefanya ufuatiliaji wa bomba kuu lamafuta (TAZAMA pipeline) ili kupata taarifa ya hali yamazingira na bioanuai zilizopo na kupendekeza njia bora zauhifadhi.

94. Mheshimiwa Spika, Baraza pia limefanya tathmini yammomonyoko wa fukwe za Kigamboni kufuatia malalamikoyaliyowasilishwa na wananchi na kutoa mapendekezo yanamna bora ya kukabiliana na hali hiyo. Aidha, Baraza kwakushirikiana na Wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Dar esSalaam na Ardhi limefanya utafiti wa kina kuhusiana na tatizola kujaa kwa maji ya mvua katika makazi eneo la Mlandizi,Halmashauri ya Kibaha. Ripoti ya utafiti huo inaandaliwa kwaajili ya kuwasilishwa katika Mamlaka husika kwa utekelezaji.Rasimu 85 za maandiko ya miradi ya kuhimili mabadiliko yatabianchi zilipokelewa na kupitiwa. Jumla ya miradi mitatu(3) i l ipitishwa baada ya kukidhi vigezo. Miradi hiyoimewasilishwa kwenye Sekretarieti ya Bodi ya Mfuko waMabadiliko ya Tabianchi kwa ajili ya hatua zaidi.

Page 116: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

Mipango ya Hifadhi ya Mazingira katika Maeneo Maalum95. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19 Barazalimeendelea kuratibu shughuli zote za Hifadhi Hai (Man andBiosphere Reserves - BRs) tano (5) ambazo ni Serengeti,Ngorongoro, Ziwa Manyara, Usambara Mashariki na JozaniChwaka Bay iliyopo Zanzibar. Aidha, Baraza limeanzamaandalizi ya Kongamano la Kisayansi kuhusu Hifadhi Hai(Biosphere Reserves) nchini. Kongamano hili linatarajiwakufanyika mwezi Agosti, 2019.

96. Mheshimiwa Spika, Baraza lilitembelea Mikoa sita(Singida, Tabora, Geita, Mara, Manyara na Arusha)kuthibitisha taarifa za maeneo yaliyopendekezwa kutengwakama maeneo Nyeti na Lindwa (EPA and ESAs). Maeneoyaliyotembelewa na kuridhiwa na wananchi ili yatangazwekuwa maeneo Nyeti ni pamoja na Msitu wa Mwalimu Nyererena Mlima Mkendo yaliyoko Mkoa wa Mara pamoja naSingidani, Kindai na Munang yaliyoko Mkoa wa Singida.Baraza liko katika mchakato wa kuainisha na kuyapimamaeneo hayo il i kupata ukubwa na ‘geographicalcoordinates’ kwa ajili ya kuyatambua. Aidha, mazungumzona wadau muhimu yanaendelea ili kujiridhisha na taarifazilizopatikana kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho yakuyatangaza maeneo hayo kuwa maeneo Lindwa.

Uratibu wa Miradi Inayotekelezwa kwa Fedha za Washirikawa Maendeleo Nchini97. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19 Barazalimeendelea kutekeleza na kuratibu miradi miwili (2) kwakupitia fedha za wafadhili. Miradi hiyo ni:

i. Mradi wa Kuhifadhi Lindimaji la Bonde la Kihansipamoja na dakio lake (Kihansi Catchment ConservationManagement Project - KCCMP). Baadhi ya kazi zilizofanyikakatika mradi huu ni pamoja na zoezi la uwekaji mipaka katikaeneo la Kihansi ambalo linatarajiwa kutangazwa kuwa eneolindwa la kimazingira (Environmental Protected Area –EPA) ;na Kuendesha maabara za vyura, kurejesha na kufuatiliamaendeleo ya vyura waliorejeshwa kwenye makazi yao yaasili pamoja na mazingira yake.

Page 117: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

ii. Mradi wa Kujenga Uwezo kwenye SektaZinazoshughulika na Nishati (Energy Sector Capacity BuildingProject - ESCABP). Baadhi ya kazi zilizofanyika katika mradihuu ni pamoja na kuweka (installation) kituo cha taarifa zamazingira (Environmental Information Centre) ambachokitakuwa na maktaba ya vitabu mango (hard copies) nanakala tete (e-library); na kuboresha maabara ya mazingirakwa ajili ya kufanya vipimo vya mazingira kwa mujibu waViwango vya Mazingira (Environmental Standards).

MASUALA MTAMBUKA, (UTAWALA NA MAENDELEO YARASILIMALI WATU)

98. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Ofisi yaMakamu wa Rais imeendelea kusimamia Sheria, Kanuni naTaratibu za Utumishi wa Umma sambamba na kuwawezeshawatumishi wake kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Katikakipindi hiki watumishi 33 wamehudhuria mafunzo ya mudamrefu na mfupi ndani na nje ya nchi. Kati ya hao 17wamehudhuria mafunzo ya muda mrefu na watumishi 16wamehudhuria mafunzo ya muda mfupi.

99. Mheshimiwa Spika, Ofisi imefanikiwa kuajiri watumishiwapya saba (7) wa kada mbalimbali kwa lengo la kujazanafasi zilizo wazi ili kuongeza nguvukazi na kuwezeshautekelezaji wa majukumu kwa ufanisi zaidi. Watumishi wawili(2) wamebadilishwa vyeo kwa kuzingatia sifa, miundoinayotawala kada zao na Mfumo Wazi wa Utendaji Kazi naUpimaji (OPRAS). Aidha, watumishi nane (8) wamethibitishwakazini baada ya kumaliza muda wa majaribio. Vilevile, taarifana kumbukumbu za watumishi zimeboreshwa kwa asilimia miamoja (100%) kupitia mfumo wa taarifa za watumishi namishahara (Human Capital Management Information System– HCMIS).

100. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19 Ofisiimeendelea kuimarisha utawala bora, demokrasia na dhanaya ushirikishwaji watumishi pahala pa kazi katika mipangoya Ofisi kupitia vikao vya Idara na vitengo, vikao vyamenejimenti na vya Baraza la wafanyakazi. Aidha, mazingira

Page 118: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

ya utendaji kazi yameboreshwa kwa kuwezesha upatikanajiwa vifaa na vitendea kazi kwa kuzingatia upatikanaji wafedha. Vilevile, ujenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais katika mjiwa Serikali Ihumwa, Dodoma unaendelea.

Usimamizi wa Ofisi, Maslahi na Maendeleo ya Watumishi -NEMC101. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2018/19 Baraza limewapatia watumishi wake vitendea kazi kamakompyuta na samani za Ofisi ili kuboresha utendaji kazi. Pia,Baraza limefanya tathmini ya utendaji kazi wa watumishiwake kwa kupitia mfumo wa OPRAS na kufanya vikao vyawafanyakazi wote ili kujadili na kutatua changamotozinazowakabili. Vilevile, Baraza limewawezesha wafanyakazikushiriki katika semina, mikutano na mafunzo mbalimbalindani na nje ya nchi ili kuwajengea uwezo katika masualaya mazingira. Aidha, Baraza limeboresha mifumo ya kifedhana kujiunga na Mfumo wa Serikali wa Kielektroniki waUkusanyaji wa Mapato na Malipo Mtandao (Government e-Payment Gateway - GePG).

CHANGAMOTO NA MIKAKATI ILIYOPO102. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumu yetuOfisi i l ikumbana na changamoto kadha zikiwemo; -Upatikanaji wa rasilimali fedha zinazoendana na mahitajihalisi ya Ofisi; Uelewa mdogo wa wadau kuhusu masuala yaMuungano na umuhimu wa kuhifadhi na kutunza mazingira;Upatikanaji wa takwimu sahihi za mazingira; na kutokuwa nawataalam wa kutosha. Hata hivyo tulichukua hatua katikakukabiliana nazo ikiwa ni pamoja na ;-Kuandaa miradi nakuiwasilisha kwa Wadau wa Maendeleo kwa ajili ya kupatafedha za utekelezaji; Kuendelea kutoa elimu kwa ummakupitia redio, luninga, magazeti, machapisho, maadhimishona maonyesho ya kitaifa kuhusu Masuala ya Muungano naumuhimu wa kuhifadhi mazingira, pamoja na kuhamasishawadau hususan Serikali za Mitaa na sekta binafsi kushirikikatika masuala ya mazingira; Kuandaa taarifa ya Hali yaMazingira pamoja na kuandaa maandiko ili kupata ufadhilikatika eneo la ukusanyaji takwimu; kutoa mafunzo kwawataalam pamoja na kuajiri.

Page 119: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

C. MALENGO NA MAOMBI YA FEDHA ZA MATUMIZI YAKAWAIDA NA MAENDELEO KWA MWAKA 2019/20Masuala ya Muungano103. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha na kuuenziMuungano katika mwaka 2019/20 Ofisi imepanga kutekelezamajukumu na malengo yafuatayo: -

i) Kuratibu vikao vya Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZya kushughulikia masuala ya Muungano pamoja na ufuatiliajiwa maelekezo na maagizo yanayotolewa katika vikao;

ii) Kufuatilia utekelezaji wa miradi na programu zamaendeleo zinazotekelezwa pande zote za Muungano,kuhakikisha gawio la asilimia 4.5 ya fedha za Misaada yaKibajeti (GBS), faida ya Benki Kuu, Mfuko wa Maendeleo yaJimbo na PAYE linapelekwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibarpamoja na ziara za kikazi ili kuimarisha Muungano’;

iii) Kutoa elimu ya Muungano kwa makundi tofauti yakijamii ikiwa ni pamoja na kuandaa warsha namakongamano ili kuendelea kuamsha ari ya kuuenzi, kuulindana kuuimarisha Muungano ambao umedumu miaka 55; na

iv) Kuhamasisha Wizara, Idara na Taasisi zisizo zaMuungano zenye majukumu yanayoshabihiana kuendeleakufanya vikao angalau mara mbili kwa mwaka ili kupunguzachangamoto za kisekta kwa ustawi wa Muungano wetu.

Hifadhi ya Mazingira104. Mheshimiwa Spika, katika kusimamia na kuhifadhiMazingira kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho katika mwaka2019/20 Ofisi imepanga kutekeleza majukumu na malengoyafuatayo:-

Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 1997105. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Ofisiimepanga kukamilisha mapitio ya Sera ya Taifa ya Mazingiraya Mwaka 1997 na Mkakati wake wa Utekelezaji. Lengo lamapitio hayo ni ni kuboresha Sera ya Taifa ya Mazingira kwakuhakikisha masuala mapya ya kimazingira yanazingatiwa ili

Page 120: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

kujumuishwa katika Mkakati wa utekelezaji. Aidha, kwakuzingatia maboresho ya Sera Ofisi itakamilisha Marekebishoya Sheria ikiwa ni pamoja na kuwezesha Mfuko wa Taifa waDhamana ya Hifadhi ya Mazingira kusajiliwa na kuanzakufanya kazi kama inavyostahili. Ni matarajio yetu kuwaMaboresho ya Sera pamoja na Sheria yatasaidia kwa kiasikikubwa juhudi za Serikali kusimamia masuala ya mazingiranchini na hivyo kuwa na maendeleo endelevu.

Ripoti ya Tatu ya Hali ya Mazingira Nchini

106. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Ofisiitachapisha nakala za Ripoti ya Tatu ya Hali ya Mazingira yaMwaka 2018 kwa lengo la kuzisambaza kwa wadau na kutoaelimu kwa umma kuhusu hali ya mazingira nchini. Vilevile Ofisiitaandaa Ripoti hiyo katika lugha nyepesi ili kurahisisha utoajiwa elimu. Ripoti hii ina takwimu na taarifa muhimuzitakazosaidia katika Mipango ya kuhifadhi mazingira nchini.Ripoti hiyo itawasilishwa Bungeni kwa mujibu wa Sheria yaUsimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004 Kifungu 175 (1).

Kuhamasisha Matumizi ya Nishati Mbadala

107. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Ofisiitaendelea kuelimisha na kuhamasisha umma ili kuhakikishakuwa, mkaa mbadala unatumiwa na kukubalika na watuwengi ikiwa ni pamoja na kuwa na viwango vinavyokubalikakitaaalam. Ofisi kwa kushirikiana na taasisi za elimu na zautafiti, itatumia kazi za washindi kuweka viwango vya uborawa mkaa mbadala unaozalishwa hii ikiwa ni pamoja na:kiwango cha nishati joto (calorific values); aina ya vifungashio(packaging materials); uzito wa mkaa (density) pamoja nakujua usalama wa kiafya kwa mkaa unaozalishwa kulinganana aina ya viambata (ingredients) vinavyotumikakutengeneza mkaa husika. Pia Taasisi zote za Serikalizitahamasishwa kupunguza kwa kiasi kikubwa matumizi yamkaa na kuni na kuongeza matumizi ya nishati mbadalahususan gesi ya kwenye mitungi (Liquified Petroleum Gas –LPG.

Page 121: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

Mifuko ya Plastiki108. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Ofisiitaendelea kusimamia uzingatiaji wa Kanuni zinazoandaliwachini ya usimamizi wa Sheria ya Mazingira, kutoa elimu nakuhamasisha wadau mbalimbali wakiwemo wamiliki waviwanda vya mifuko ya plastiki ili kuhakikisha utekelezaji watamko la Serikali la kupiga marufuku uingizaji, uuzaji, uzalishajina utumiaji wa mifuko ya plastiki linatekelezwa kwa ufanisi.Aidha, nichukue fursa hii kuwahimiza wawekezaji kuendeleakutumia fursa hii kuwekeza katika teknolojia ya uzalishaji wamifuko mbadala.

Viumbe Vamizi109. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Ofisi kwakushirikiana na wadau itaratibu utekelezaji wa MpangoMkakati wa Taifa wa Kudhibiti Viumbe Vamizi (2019 - 2029).Mkakati huo unalenga kuimarisha juhudi za Serikalikukabiliana na ueneaji wa viumbe hao na athari zakeambazo zinaendelea kuongezeka kwa kasi nchini na hivyokuathiri sekta kuu za uchumi ambazo ndiyo msingi wauzalishaji na ajira. Juhudi hizo zitakwenda sambamba nautoaji elimu kwa umma juu ya jambo hili ili kuhakikisha wadauwanaunga mkono juhudi za Serikali katika kupambana natatizo hili. Nachukua fursa hii kuomba wadau wa mazingiraikiwa ni pamoja na sekta binafsi, Washirika wa Maendeleo,Mashirika na Asasi zisizo za Serikali kuunga mkono juhudi zaSerikali kukabiliana na tatizo hili.

Kampeni ya Upandaji Miti110. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Ofisiitaendelea kuhamasisha na kufuatilia utekelezaji wa kampeniya upandaji miti kwa kushirikiana na Sekta zinazohusika katikaHalmashauri za Wilaya Nchini ili kukabiliana na changamotombalimbali zinazokwamisha kufikiwa kwa malengo yakampeni hii. Baadhi ya masuala yatakayopewa kipaumbeleni pamoja na kuhamasisha wananchi kupanda miti yamatunda ambayo pamoja na kuhifadhi mazingira itasaidiakukuza kipato na kuimarisha afya kwa jamii. Juhudi hizozitakwenda sambamba na kusisitiza juu ya utunzaji wa mitiya asili.

Page 122: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

Tuzo ya Rais ya Hifadhi ya Mazingira111. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Serikaliitaendesha mashindano ya Tuzo ya Rais ya Hifadhi yaMazingira kwa kutumia Mwongozo wa Tuzo ulioboreshwa.Baadhi ya masuala yalioongezwa katika mwongozo huo ilikuuboresha ni pamoja na uzalishaji endelevu viwandani,matumizi ya nishati mbadala, uchimbaji madini endelevu,kilimo na ufugaji endelevu, usimamizi wa taka, afya na usafiwa mazingira. Aidha washindi wa Tuzo hii wanatarajiwakupewa Tuzo zao wakati wa kilele cha maadhimisho ya Sikuya Mazingira Duniani, tarehe 5 Juni, 2020;

Uzuiaji wa Shughuli za Binadamu katika Baadhi ya Maeneo112. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia Sheria yaMazingira ya Mwaka 2004 Kifungu cha 57 (1) kinakatazakutofanyika shughuli yoyote ya kibinadamu ya kudumu auambayo kwa asili yake inaweza kuhatarisha au kuathiri vibayaulinzi wa mazingira na au utunzaji wa bahari au kingo za mito,bwawa, au miambao ya asili ya ziwa. Hata hivyo, Kifungu 57(2) kinampa mamlaka Waziri mwenye dhamana ya mazingirakuweka miongozo ya kuendesha shughuli za binadamu ndaniya maeneo yaliyoelezwa. Kwa kuzingatia hilo Ofisi inaandaaMiongozo itakayotoa ufafanuzi kuhusu aina ya shughulizinazoweza kutekelezwa katika maeneo hayo. Lengo nikuhakikisha kuwa kunakuwa na uwiano kati ya uongezaji wakipato cha wananchi pamoja na uzingatiaji wa uhifadhi wamazingira katika eneo lililolengwa.

Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Maji Zinazovuka MipakaKati ya Kenya na Tanzania113. Mheshimiwa Spika, Tanzania na Kenya ni nchi jiranizinazomiliki kwa pamoja baadhi ya Maziwa na Mito ikiwemo,Ziwa Chala, Ziwa Jipe, Ziwa Natron na Mto Mara. Kwa mudamrefu nchi hizi mbili zimekuwa kwenye changamoto zamatumizi yasiyo endelevu kwa rasilimali hizo na hivyokusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira unaopelekeaupungufu wa utiririshaji maji, kupungua kwa kina cha majikwa baadhi ya Mito na Maziwa na kuongezeka kwa magugumaji kunakohatarisha bioanuai ya maeneo haya. Il ikukabiliana na changamoto hizo nchi za Kenya na Tanzania

Page 123: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

zimekubaliana masuala yafuatayo; Kuunda Kamati yapamoja katika ngazi ya Wataalam na Mawaziri; Kufanyatathmini ya kina ya rasilimali za mipakani; na KuandaaMkataba wa usimamizi wa rasilimali hizo pamoja na Mpangowa utafutaji wa rasilimali fedha. Hadi sasa Kamati ya pamojaya Wataalam kwa ajili ya kutoa mwongozo wa kitaalam wausimamizi wa rasilimali za mipakani zinazomilikiwa kwapamoja imeshaundwa na kuanza kazi.

114. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20 Serikaliitaendelea kuratibu kazi chini ya Kamati hizi kwa kushirikianana Serikali ya Kenya.

Uratibu wa Usimamizi wa Mazingira Katika Ngazi ya Mikoana Mamlaka za Serikali za Mitaa115. Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kutekeleza Sheriaya Mazingira, Ofisi itaendelea kushirikiana na Wizara yenyedhamana ya Tawala za Mikoa na Mamlaka ya Serikali yaMitaa ili kuimarisha uratibu wa usimamizi wa Mazingira kwakuhakikisha uteuzi wa wataalam wa usimamizi wa mazingirakatika ngazi za Miji, Wilaya, Manispaa, Jiji na Mikoaunaendelea kufanyika. Maafisa hao ni kiungo katikautekelezaji, usimamiaji na ufuatiliaji wa Sheria ya Mazingiraya mwaka 2004 katika maeneo hayo na hivyo wana wajibuwa kushauri Serikali za Mitaa kuhusu utekelezaji wa Sheria hii.Aidha, utekelezaji, uratibu na ufuatiliaji utahusisha uundaji waKamati za Usimamizi wa Mazingira za Jiji, Manispaa, Wilaya,Mji, Kata, Kijiji, Mtaa na Kitongoji pamoja na kuhakikisha kuwazinafanya kazi na uandaaji na utekelezaji wa Mipango yaMazingira ya mamlaka ya Serikali za Mitaa.

116. Mheshimiwa Spika, Kazi nyingine zitakazotekelezwakatika hifadhi ya mazingira ni pamoja na:-

i) Kuendesha mafunzo kwa Mamlaka za Serikali zaMitaa na Wizara za Kisekta; na kuanzisha mfumo wa utoajivyeti na leseni za mazingira kwa njia ya mtandao;ii) Kuratibu utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kaziili kuhakikisha hali ya Mfumo Ikolojia ya Bonde la Mto RuahaMkuu inaendelea kuimarika;

Page 124: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

i) Kuelimisha Umma kuhusu Hifadhi na Usimamizi waMazingira pamoja na matumizi salama ya bioteknolojia yakisasa (GMO) kupitia vyombo vya habari ikiwemo redio,luninga na magazeti. Vilevile, Ofisi itaandaa na kuchapishaMkakati wa Mawasiliano na Elimu kwa Umma kuhusu Hifadhiya Mazingira;

ii) Kusimamia, Kuratibu na Kufuatilia Utekelezaji waMikataba ya Kimataifa ya Mazingira ambayo Tanzania niMwanachama na kuandaa msimamo wa nchi na kuratibuushiriki katika mikutano ijayo ya nchi wanachama waMikataba ya kimataifa ya hifadhi ya mazingira;

iii) Kutoa vyeti vya Tathmini ya Athari za Mazingira (TAM)kwa miradi na Tathmini ya Mazingira Kimkakati (SEA) nakufuatilia utekelezaji wa suala hili kwa mujibu wa Sheria yaMazingira ya Mwaka 2004;

iv) Kuratibu utekelezaji wa Mikakati iliyopo chini yaMikataba ya Kimataifa tuliyoridhia;

v) Kuwezesha mchakato wa kuridhia Mikataba na Itifakiza Mazingira ambazo Tanzania imesaini;

vi) Kutekeleza miradi ya hifadhi na usimamizi wamazingira na Mabadiliko ya Tabiachi iliyopo chini yaMikataba ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini na ufuatiliaji;na

vii) Kuandaa miradi ya kuhifadhi mazingira na kuiwasilishakwa wafadhili kwa ajili ya kupatiwa fedha kutoka kwenyeMifuko na Mashirika yanayohusika na kuhifadhi mazingira.

Malengo ya Baraza la Taifa la Kusimamia na KuhifadhiMazingira117. Mheshimiwa Spika, Baraza katika kusimamiautekelezaji wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 limepangakutekeleza yafuatayo katika mwaka 2019/20: -i) Kufanya ukaguzi na ufuatialiaji wa Miradi ya Uwekezajina kuchukua hatua stahiki kwa wataokiuka Sheria pamoja

Page 125: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

na kushughulikia malalamiko wa wananchi kwa mujibu waSheria ya Usimamizi wa Mazingira na Kanuni zake;

ii) Kuandaa na kufanya mapitio ya nyezo na miongozombalimbali inayohusu uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira naKanuni zake;

iii) Kuendesha maabara ndogo ya kimazingira kwa ajiliya kupima sampuli kwa hatua za awali katika kubaini uchafuzikatika mazingira;

iv) Kuboresha mfumo na mchakato wa TAM ili kuwezeshaupatikanaji wa vyeti kwa haraka zaidi na kuendelea kutoamiongozo kwa wadau ili kuhakikisha TAM inazingatiwa kablaya uwekezaji kufanyika;

v) Kuendelea kusajili miradi kwa ajili ya mchakato waTAM, kusajili wataalam wa TAM na Wakaguzi wa Mazingirapamoja na kufanya vikao vya kinidhamu ili kufuatiliamienendo yao katika kutoa ushauri kwenye masuala yaMazingira;

viii) Kufanya tathmini ya mifumo ikilojia katika bonde lamaji la Rufiji katika eneo la mradi wa umeme wa Rufiji;

viii) Kuendelea kutekeleza Ajenda ya Taifa ya Utafiti katikaMazingira kwa kufanya tafiti na tathmini mbalimbali zamazingira pamoja na kufuatilia shughuli za Kuhimili Mabadilikoya Tabianchi;

ix) Kufanya mapitio ya miradi inayowasilishwa na wadauna kuiwasilisha kwenye Mfuko wa Kuhimili Mabadiliko yaTabianchi ili iweze kupata ufadhili;

x) Kuandaa miongozo ya usimamizi wa mazingira katikamaeneo lindwa na nyeti (Environmental Protected Areas -EPAs and Environmental Sensitive Areas - ESAs);xi) Kufanya ufuatiliaji wa karibu wa shughuli zinazofanyikakatika Mradi wa Uzalishaji Umeme wa Rufiji ili kuhakikishahifadhi ya mazingira na usalama mahali pa kazi unazingatiwa;

Page 126: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

xii) Kuimarisha Usimamizi wa taka ngumu na kuboreshaudhibiti wa utupaji wa taka hatarishi kwa kushirikiana nawadau;

xiii) Kuongeza wigo wa mapato kwa kupitia utekelezajiwa kanuni ya Tozo pamoja na uandaaji wa Miradi yaMaendeleo;

xiv) Kuendelea na kampeni za elimu ya mazingira kwaumma na kuifanya NEMC ijulikane zaidi kwa jamii;

xv) Kuanza ujenzi wa Ofisi za kudumu katika kiwanja chaBaraza kilichopo eneo la Njendengwa, Dodoma; na

xvi) Kuanzisha Ofisi ya Kanda ya Magharibi na kuimarishaOfisi za Kanda zilizopo kwa kuongeza watumishi na vitendeakazi ili kuongeza ufanisi.

Miradi ya Maendeleo

118. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20 miradimikubwa ifuatayo ya hifadhi na usimamizi wa mazingiraimepangwa kutekelezwa: -

i. Mradi wa Kurejesha Ardhi Iliyoharibika na KuongezaUsalama wa Chakula Katika Maeneo Kame Tanzania

119. Mheshimiwa Spika, katika mradi huu kazi zifuatazozitatekekelezwa:- Kuandaa Mpango wa matumizi bora yaardhi kwa vijiji 17 katika Halmashauri tano ambazo ni Magu(3), Nzega (5), Mkalama (5) na Kondoa (4) na Wilaya yaMicheweni katika Shehia 8; Kuanzisha mashamba darasakwa wakulima kuhusu kilimo, hifadhi na mbinu bora za kilimorafiki kwa mazingira; Kutoa mafunzo ya uboreshaji naurutubishaji wa udongo, mbinu za kilimo cha misitu (agro-forest) na kilimo cha makinga maji; Kuchimba, kukarabati nakujenga mabwawa na visima na ununuzi wa matanki yakuhifadhi maji; Kupanda miti kwa kuzingatia mpango wamatumizi bora ya ardhi wa vijiji; na Kutambua teknolojia namaeneo yanayofaa kwa uvunaji wa maji ya mvua.

Page 127: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

ii. Mradi wa Kuhimili Athari ya Mabadiliko ya Tabia NchiKupitia Mifumo ya Ikolojia

120. Mheshimiwa Spika, katika mradi huu kazi zifuatazozitatekekelezwa:- Kujenga uwezo wa kuhimili mabadiliko yatabianchi kwa kuimarisha mifumo ya ikolojia; Kufanya tathminiya athari za mabadiliko ya tabianchi na kutoa mapendekezoya kukabiliana na athari hizo; Kuunda mfumo wa ujuzi kuhusukuhimili mabadiliko ya tabianchi (Formulation of AdaptationKnowledge Management System); Kuendesha mafunzo kwawadau wa mradi kuhusu umuhimu wa Ikolojia katika kuhimilimabadiliko ya tabianchi; Kuandaa mipango ya matumizibora ya ardhi na Kutoa elimu ya matumizi ya majiko banifuna sanifu kwenye maeneo ya utekelezaji wa mradi.

iii. Mradi wa Kusaidia Utekelezaji na Usimamizi wa MbinuJumuishi za Mazingira Katika Kuongoa na KurejeshaIkolojia Iliyoharibika na Hifadhi ya Bioanuai

121. Mheshimiwa Spika, katika mradi huu kazi zifuatazozitatekelezwa: - Kuhuisha masuala ya hifadhi ya Bioanuai namatumizi endelevu ya huduma za ikolojia katika Sekta zauzalishaji; Kuwezesha matumizi endelevu na usimamizi waardhi katika mifumo ya uzalishaji (kilimo, safu, na misitu); naKuongoa na kurejesha Ikolojia iliyoharibika katika sekta ndogoya misitu.

iv. Mradi wa Kusimamia Uhifadhi na Matumizi Endelevu yaBonde la Ziwa Nyasa

122. Mheshimiwa Spika, katika mradi huu kazi zifuatazozitatekelezwa:- Kuwezesha uzalishaji wa mkaa endelevupamoja na matumizi ya majiko sanifu na banifu; kutoamafunzo kwa vikundi kuhusu usimamizi endelevu wa uvuvipamoja na kuendeleza ujasiliamali; Kutoa mafunzo kwawachimbaji wadogo wadogo wa madini na mchangakuhusu uchimbaji endelevu; Kuanzisha na kujenga uwezo kwajumuia za watumia maji (Establishment/Strengthening ofWater Users Association) kwa ajili ya usimamizi endelevu warasilimali za maji; na Kusaidia utekelezaji wa mipango shirikishiya usimamizi wa misitu.

Page 128: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

123. Mheshimiwa Spika, Miradi mingine itakayotekelezwana Ofisi katika mwaka 2019/20 ni pamoja na:- Mradi waKujenga Uwezo wa Taasisi Kusimamia na Kupunguza Athariza Mazingira kwa Jamii za Vijijini Katika Sehemu zenye Ukame;Mradi wa Kujenga Uwezo wa Kutekeleza Sheria ya Mazingira;Mradi wa Kujenga Uwezo wa Kitaasisi Kupunguza KemikaliZinazomong’onyoa Tabaka la Ozone; Mradi wa KutekelezaMpango wa Ufuatiliaji na Udhibiti wa Taka Zinazodumu KatikaMazingira Kwa Muda Mrefu; Mradi wa Kujenga Uwezo waKitaasisi wa Kusimamia Kemikali na taka nchini; na Mradi waKuhuisha Uhusiano Kati ya Afya na Mazingira na Uwezo waKisheria na Kitaasisi Katika Udhibiti wa Kemikali na Taka.

HITIMISHO NA SHUKRANI

124. Mheshimiwa Spika, nchi yetu ni ya Muungano ambaouna umuhimu wa pekee kwa Taifa na umekuwa niutambulisho wa Taifa letu na kielelezo cha umoja wetu katikakudumisha Amani na Usalama wa nchi yetu. Mwaka huuMuungano wetu unatimiza miaka 55 tangu kuasisiwa kwake.Ninatoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kuuthamini,kuuenzi, kuulinda na kuudumisha Muungano ili jitihada zakusukuma mbele maendeleo kiuchumi, kisiasa na kijamii kwafaida za pande zote mbili.

125. Mheshimiwa Spika, chini ya uongozi wa Rais wetu,Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Makamu waRais, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, pamoja naMheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar naMwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Muungano wetuunaendelea kuimarika na kushamiri. Chini ya uongozi waohakuna changamoto yoyote inayoweza kutufarakanisha,kututenganisha wala kuturudisha nyuma. Katika mwaka 2019/20 Ofisi na Serikali kwa ujumla itaendelea kuyafanyia kazimambo yote yanayoleta changamoto katika utekelezaji wamasuala yanayohusu Muungano na kutoa elimu kuhusuMuungano ili uendelee kuimarika.

126. Mheshimiwa Spika, kutokana na umuhimu wamazingira katika mustakabali wetu na maendeleo ya uchumi

Page 129: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

wa viwanda, ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha kuwamazingira na maliasili za nchi yetu zinalindwa na kuhifadhiwa.Ninapenda kutoa wito kwa Waheshimiwa Wabunge pamojana wananchi kwa ujumla kuunga mkono juhudi za Serikalikatika kulinda na kuhifadhi mazingira kwa manufaa ya kizazicha sasa na kijacho.

127. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Ofisiimejipanga kuipa elimu ya mazingira kipaumbele kwa jamiiili kuhakikisha mazingira yanalindwa na kutunzwa. Aidha, Ofisiitahakikisha masuala yote yanayohusu uharibifu wa mazingirayanapatiwa ufumbuzi. Vilevile, Ofisi itaendelea kutoamiongozo ya hifadhi ya mazingira katika nyanja mbalimbalikwa lengo la kuhifadhi mazingira kwa kuangalia mifumo yaikolojia, mifumo ya uzalishaji mali, na mifumo ya uchumi yamatumizi ya rasilimali asili.

128. Mheshimiwa Spika, ninaomba nitumie nafasi hiikuwashukuru walionisaidia kufanikisha utekelezaji wamajukumu ya Ofisi. Shukrani zangu za dhati na za kipekee nikwa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wake nadira na mwelekeo aliotupatia kuhusu majukumu yetu. Aidha,ninamshukuru Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu waRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongoziwake makini uliotuwezesha kutekeleza majukumu yetu.Ninapenda kumshukuru Mheshimiwa Mussa Ramadhani Sima,(Mb.), Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, kwa ushirikianoanaonipa katika utekelezaji wa kazi za Ofisi. Vilevile,ninapenda kuwashukuru Mhandisi Joseph K. Malongo, KatibuMkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais; Balozi Joseph E. Sokoine,Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais; Ndugu AliMufuruki, Mwenyekiti wa Mfuko wa Taifa wa Dhamana yaMazingira na Wajumbe wa Bodi ya Mfuko huo; Dkt.SamuelMafwenga Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhina Usimamizi wa Mazingira; Wakuu wa Idara na Vitengo; naWafanyakazi wote wa Ofisi ya Makamu wa Rais na Barazakwa michango yao katika kufanikisha utekelezaji wamajukumu. Pia ninawashukuru wale wote waliotuwezeshakutekeleza majukumu ya Ofisi kwa kipindi kilichopita, na

Page 130: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

ambao wamesaidia katika kuandaa Mpango na Bajeti yamwaka 2019/20.

129. Mheshimiwa Spika, Ofisi imefanikisha utekelezaji wamajukumu yake kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo.Ninapenda kuwataja baadhi ya washirika wa maendeleoambao Ofisi imefanya nao kazi kwa karibu kama ifuatavyo:Serikali ya Norway; Serikali ya Canada; Serikali ya Sweden;Serikali ya Italia; Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Korea; Umojawa Nchi za Ulaya (European Union - EU); Shirika la Mpangowa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (United NationsDevelopment Programme - UNDP); Shirika la Umoja waMataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (United NationsEducational, Scientific and Cultural Organization - UNESCO);Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP); Mfuko waMazingira wa Dunia (Global Environment Facility - GEF); Shirikala Umoja wa Mataifa la Huduma za Miradi (United NationsOffice for Project Services - UNOPS); Benki ya Dunia (WorldBank - WB); Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfricanDevelopment Bank - AfDB); Shirika la Umoja wa Mataifa laMaendeleo ya Viwanda (United Nations IndustrialDevelopment Organization - UNIDO); Shirika la Kimataifa laMisaada ya Maendeleo la Denmark (Danish InternationalDevelopment Agency - DANIDA); World Wide Fund for Nature- WWF; Mfuko wa Kimataifa wa Kuendeleza Kil imo(International Fund for Agricultural Development - IFAD);Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi (Green Climate Fund -GCF); Shirika la Kilimo na Chakula Duniani ( Food andAgriculture Organization - FAO); Shirika la Ushirikiano waKimataifa la Ujerumani (Gesellschaft fiir InternationaleZusammenarbeit - GiZ); Kikundi cha Washirika wa Maendeleokinachoshughulikia Mazingira (Development Partners Groupon Environment - DPGE); Asasi Zisizo za Kiserikali (AZISE); naSekta binafsi. Aidha, ninapenda nitumie fursa hii kuwaombawashirika wa maendeleo kuendelea kutoa ushirikiano katikakipindi kijacho ili tuweze kufanikiwa zaidi katika kulinda nakuimarisha Muungano wetu na kulinda na kuhifadhi mazingirayetu.

Page 131: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

MAOMBI YA FEDHA

130. Mheshimiwa Spika, i l i Ofisi iweze kutekelezamajukumu na malengo yaliyopangwa, ninaomba kutoa hojakwamba Bunge lako Tukufu liidhinishe maombi ya fedha kwamwaka 2019/20, kama ifuatavyo:

Fungu 26: Makamu wa Rais

131. Mheshimiwa Spika, ninaomba Bunge lako Tukufuliidhinishe Makadirio ya Matumizi ya Sh. 7,855,093,000 fedhaza Matumizi ya Kawaida kwa mwaka 2019/20. Kiasi hikikinajumuisha fedha za Mishahara ya watumishi Sh.1,120,128,000 na fedha za Matumizi Mengineyo Sh.6,734,965,000.

Fungu 31: Ofisi ya Makamu wa Rais132. Mheshimiwa Spika, ninaomba Bunge lako Tukufu,liidhinishe makadirio ya matumizi ya Sh. 29,066,298,442 kwaFungu hili. Kiasi hiki kinajumuisha Sh. 9,847,374,000 fedha zaMatumizi ya Kawaida na Sh. 19,218,915,442 fedha za Miradiya Maendeleo. Bajeti ya Matumizi ya Kawaida inajumuishaSh. 2,759,365,000 fedha za Mishahara na Sh. 7,088,009,000fedha za Matumizi Mengineyo. Fedha za Matumizi Mengineyozinajumuisha Sh. 2,808,957,000 Ruzuku ya Mishahara yawatumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi waMazingira. Aidha, fedha za Miradi ya Maendeleo zinajumuishaFedha za Ndani Sh. 1,000,000,000 na Fedha za Nje Sh.18,218,915,442.

133. Mheshimiwa Spika, ninaomba kutoa hoja.

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Waziri, hojaimeungwa mkono.

Sasa namwita Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu yaBunge ya Katiba na Sheria, ajiandae Mwenyekiti wa Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira.(Makofi)

Page 132: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

MHE. NAJMA MURTAZA GIGA - MAKAMU MWENYEKITIWA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba kwaupekee kabisa nimshukuru Mwenyezi Mungu kwakutuwezesha katika kila jambo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Kanuni ya99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Januari, 2016,naomba kuwasilisha taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bungeya Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa Bajeti Ofisi yaMakamu wa Rais, Muungano kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na maoni na Kamati kuhusu makadirio yamapato na matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu cha 6(2)(c) chaNyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo laJanuari, 2016, kimeipa Kamati ya Katiba na Sheria jukumu lakusimamia shughuli za Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ofisi ya Makamu wa RaisMuungano ina Mafungu mawili ya bajeti, ambayo ni Fungu26 Ofisi binafsi ya Makamu wa Rais na Fungu 31 Ofisi yaMakamu wa Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa hii inatoa maelezokuhusu maeneo manne kama yanavyoonekana hapo chini.Taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyotengewafedha kwa mwaka wa fedha 2018/2019. Fungu 26 - Ofisi Binafsiya Makamu wa Rais, kwa kuzingatia muundo wa majukumuya Ofisi Binafsi ya Makamu wa Rais Muungano, hakukuwa nabajeti ya miradi ya maendeleo katika fungu hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Fungu 31, Ofisi ya Makamuwa Rais, Muungano katika kutekeleza Kanuni ya 98(1) yaKanuni za Kudumu za Bunge, Kamati ya Katiba na Sheriailipokea taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleoinayosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano naorodha ya Miradi hiyo ni kama ifuatavyo:-.

Page 133: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi Na. 6309 – Ujenzi waOfisi na Nyumba ya Makazi ya Makamu wa Rais Zanzibaryaani (Construction of Vice President Office and Residencein Zanzibar), ambao uliidhinishiwa Shilingi Bilioni Moja na MradiNa. 6389 – Ujenzi na Ukarabati wa Ofisi na Makazi ya Makamuwa Rais (Luthuli II) (Construction and Rehabilitation of VicePresident Office Luthuli II and State Lodges), ambaouliidhinishiwa Shilingi milioni mia tano thelathini na nne na lakinane.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Taarifa yaOfisi ya Makamu wa Rais - Muungano ya tarehe 20 Machi,2019, kwa kipindi cha Julai, 2018 hadi Machi, 2019, Mradi Na.6389 wa Ujenzi na Ukarabati wa Ofisi na Makazi ya Makamuwa Rais (Luthuli I I) ulikuwa umepokea fedha zotezilizoidhinishwa na Bunge, Shilingi milioni mia tano thelathinina nne na laki nane sawa na asilimia 100. Hata hivyo, MradiNa. 6309 haujapokea kiasi chochote cha Fedhazilizoidhinishwa na Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Uchambuzi wa Taarifa yaOfisi ya Makamu wa Rais-Muungano Kuhusu Utekelezaji waMpango wa Bajeti na Uzingatiaji wa Maoni ya Kamati Kwamwaka wa fedha 2018/2019. Kamati imepokea nakuchambua Taarifa za Utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka wafedha 2018/2019 na uchambuzi wa Makadirio ya Mapato naMatumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano. Naombakulijulisha Bunge lako Tukufu kuhusu uchambuzi huo kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Uchambuzi wa Mapitio yaUtekelezaji wa Mpango wa Bajeti kwa mwaka wa fedha2018/2019; uchambuzi uliofanywa na Kamati katika Mapitioya Utekelezaji wa Mpango wa Bajeti ya Ofisi ya Makamu waRais - Muungano kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 ulitazamamlinganisho wa kiasi cha fedha kilichoidhinishwa na BungeAprili, 2018 na kiwango ambacho kimepokelewa hadi Machi,2019 katika Robo ya Tatu ya mwaka huu wa fedha 2018/2019.

Page 134: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi huu piaulitazama kiasi cha fedha kilichoidhinishwa kwa mwaka wafedha 2018/2019 na kiasi cha fedha kilichopokelewa katikaMiradi ya Maendeleo hadi kufikia mwezi Machi, 2019. Lengola kufanya tathmini ya namna hii ni kufahamu Mwelekeo waMpango wa Bajeti ya Mapato na Matumizi ya Serikali katikamwaka wa fedha 2019/2020 ili kujua vipaumbele vya kibajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Upatikanaji wa fedha zaMatumizi ya Kawaida kutoka Hazina; Fungu 26 - Ofisi Binafsiya Makamu wa Rais; katika mwaka wa fedha 2018/2019Fungu hili lilitengewa Shilingi bilioni sita, milioni mia nnethemanini na tano, laki tisa tisini na moja elfu mia tano sabinina nane na senti tano kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Katiya fedha hizo, Shilingi bilioni moja na milioni hamsini na tatu,laki sita sitini na sita elfu ilikuwa ni kwa ajili ya mishahara, naShilingi bilioni tano, milioni mia nne thelathini na mbili, laki tatuishirini na tano elfu, mia tano sabini na nane na senti tanoilikuwa ni fedha za Matumizi Mengineyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi wa Kamatiumebaini kuwa, katika kipindi cha kuanzia Mwezi Julai, 2018hadi mwezi Machi, 2019, jumla ya Shilingi bilioni nne, milionimia tano sabini na mbili, laki nane na kumi elfu, mia tanosabini na nane na senti tano zilikuwa zimepokelewa kwa ajiliya Mishahara na Matumizi Mengineyo. Kiasi hicho cha fedhakilichopokelewa ni sawa na asil imia 70.5% ya Bajetiiliyoidhinishwa na Bunge katika Fungu 26.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati inaipongeza Hazinakwa kutoa Fedha zilizoidhinishwa na Bunge kwa wakati, hatuaambayo imesaidia Ofisi Binafsi ya Makamu Rais - Muunganokutekeleza Majukumu yake kwa wakati na kwa ufanisiuliokusudiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Fungu 31 - Ofisi ya Makamuwa Rais; katika mwaka wa fedha 2018/2019, Fungu hili kwaujumla lilitengewa Shilingi bilioni kumi na milioni mbili,themanini na mbili elfu, mia tano ishirini na tatu na senti ishirinina nane kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida.

Page 135: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi wa Kamatiumebaini kuwa, katika kipindi cha Julai, 2018 hadi Machi,2019, Ofisi hiyo ilipokea Shilingi bilioni tano, milioni mia tanothelathini na saba, laki saba tisini na tano elfu na tatu nasenti ishirini na nane, sawa na asilimia 55.4% ya bajeti yaMatumizi ya Kawaida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi huu unaoneshakuwa kumekuwa na Mwenendo mzuri na wa kuridhishakuhusu upatikanaji wa fedha za Bajeti ya Matumizi yaKawaida, kwa Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano kwaMafungu yote yaani Fungu 26 na Fungu 31.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Maoni ya Kamati ni kwambahali hii ya upatikanaji wa fedha kwa wakati inatakiwakuendelea na kuzingatiwa na Serikali kwa mwaka wa fedha2019/2020, ili kurahisisha usimamizi na utekelezaji wa shughulimbalimbali za Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano kwawakati na kwa ufanisi. Kwa hatua hii, Kamati inaipongezaHazina na Serikali kwa ujumla kwa kutoa fedha za matumiziya kawaida kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Uchambuzi wa Utekelezajiwa Bajeti ya Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 -Fungu 31; Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano iliidhinishiwaShilingi bilioni moja, milioni mia tano thelathini na nane nalaki nane kwa ajili ya Miradi Miwili ya Ujenzi wa Ofisi na Makaziya Makamu wa Rais (Zanzibar) (Mradi Na.6309) na Mradi waKujenga na kukarabati Ofisi ya Makamu wa Rais Luthuli II (Dares Salaam) (Mradi Na. 6389).

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi wa Kamatiumebaini kuwa, katika kipindi cha Julai, 2018 hadi Machi,2019, Mradi Na. 6389 wa Ujenzi na Ukarabati wa Ofisi naMakazi ya Makamu wa Rais(Luthuli II) ulikuwa umepokeaasilimia 100 ya fedha zote zilizoidhinishwa na Bunge, ambazoni Shilingi milioni mia tano thelathini na nane na laki nane.Aidha, Kamati imebaini kuwa, Mradi Na. 6309 haukuwaumepokea kiasi chochote cha fedha zilizoidhinishwa naBunge.

Page 136: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

Mheshimiwa Mwenyekiti, maoni ya Kamati ni kuwa,Miradi hii imechukua muda mrefu, hivyo, Serikali ihakikisheMradi Na. 6309 unaanza na kukamilika katika mwaka huuwa fedha wa 2019/2020.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi wa Mpango wamakadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha2019/2020; Kamati ilipokea na kuchambua Mpango na Bajetiya Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano kwa mwaka wafedha 2019/2020, tarehe 20 Machi, 2019, ambayo imelengakutekeleza masuala ya Muungano kwa vipaumbelevilivyoainishwa katika taarifa hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na vipaumbelehivyo, Kamati inatoa rai kwa Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano kuhakikisha kwamba vipaumbele vyake vinaakisimwendelezo wa kuimarisha na kulinda Muungano wetu kwamanufaa ya Watanzania wote na kudumisha udugu, umojana mshikamano wa Watanzania wa pande zote mbili zaMuungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati inaipongeza sanaSerikali, ya Awamu ya Tano kwa kuendeleza jitihada za dhatiza Awamu ya Nne na zilzotangulia katika kutatuachangamoto mbalimbali za Muungano kwa manufaa yapande zote mbili na wananchi wake kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi wa Makadirio naMatumizi kwa mwaka wa fedha 2019/2020; Fungu 26 - OfisiBinafsi ya Makamu wa Rais, katika mwaka wa fedha 2019/2020 Ofisi hii inaomba kuidhinishiwa jumla ya shilingi bilionisaba milioni mia nane hamsini na tano na tisini na tatu elfukwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Matumizi ya Mengineyo.Kati ya fedha hizo shilingi bilioni moja milioni mia moja ishirinilaki moja ishirini na nane elfu ni kwa ajili ya Mishahara nashilingi bilioni sita milioni mia saba thelathini na nne laki tisasitini na tano elfu ni fedha za Matumizi Mengineyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi wa Kamatiumebaini kwamba bajeti ya Fungu 26 imeongezeka kwa kiasi

Page 137: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

cha Sh.1,369,101,422 ikilinganishwa na bajeti iliyoidhinishwana Bunge kwa mwaka wa fedha 2018/2019. Ongezeko hiloni sawa na asilimia 21.11% ya bajeti ya Fungu 26 kwa mwakawa fedha 2018/2019. Ongezeko hili linatokana na mahitajihalisi ya Ofisi hiyo hususan gharama za utoaji huduma kwaOfisi Binafsi ya Makamu wa Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Fungu 31 - Ofisi ya Makamuwa Rais. Katika mwaka wa fedha 2019/2020, Ofisi ya Makamuwa Rais (Fungu 31) inaomba kuidhinishiwa jumla yaSh.5,357,575,560 kwa ajili ya Matumizi ya Mishahara naMatumizi Mengineyo. Kati ya fedha hizo, Sh.1,931,624,000 nikwa ajili ya Mishahara na Sh.3,425,951,560 ni fedha zaMatumizi Mengineyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi wa Kamatiumebaini kwamba bajeti ya Matumizi ya Kawaida kwa Fungu31 imeongezeka kwa asilimia 4.5% ikilinganishwa na bajetiiliyoidhinishwa na Bunge chini ya Fungu hili kwa mwaka wafedha 2018/2019. Kama ilivyoelezwa hapo juu, ongezeko hililinatokana na mahitaji halisi ya Ofisi hiyo ikiwa ni pamoja nauratibu wa vikao vya Kamati ya Pamoja kati ya Serikali yaMuungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar (SMZ) na uanzishwaji wa Ofisi ya Makamu wa RaisZanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango wa Maendeleokwa mwaka wa fedha 2019/2020 (Fungu 31). Kwa upandewa Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano, Mradi mmoja waMaendeleo unaendelea kuombewa fedha kwa mwaka wafedha 2019/2020. Mradi huo ni Mradi Na.6309 wa Ujenzi waOfisi na Makazi ya Makamu wa Rais Zanzibar ambaounaombewa Sh.1,000,000,000. Kamati inapendekeza fedhahizo zitolewe kwa wakati kwa mwaka huu wa fedha 2019/2020 ili kurahisisha ukamilishaji wa mradi huo muhimu. Aidha,kuhusu kuanza utekelezaji wa Mradi huo kabla ya mwakahuu wa fedha kuisha, Kamati inashauri Serikali itoe fedha

Page 138: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

zilizopangwa na kuidhinishwa kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ili kuwezesha utekelezaji wa shughuli zilizopangwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maoni na ushauri wa Kamati.Kamati ina maoni na ushauri kama ifuatavyo:-

(i) Kamati imeridhishwa kwa kiasi kikubwa nautekelezaji wa maoni na mapendekezo ya Kamatiyaliyotolewa na Kamati kwa Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano) katika mwaka wa fedha 2018/2019, ikiwa nipamoja na kuendelea na ukarabati wa magari na mitamboyote inayotumiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano.Aidha, Kamati inaipongeza Serikali kwa kununua magarimapya kwa lengo la kurahisisha utekelezaji wa majukumumbalimbali chini ya Ofisi hii muhimu. (Makofi)

(ii) Kamati inapongeza juhudi za Ofisi ya Makamuwa Rais (Muungano) kwa kushirikiana na Mamlaka husika zapande mbili za Muungano katika kuendelea kutatuachangamoto mbalimbali katika sekta ya biashara baina yapande mbili za Muungano, hatua ambayo itachochea ukuajiuchumi kwa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

(iii) Kamati inaendelea kuishauri Serikalikuendelea kuratibu utekelezaji wa Waraka wa Mgao waMuda wa Ajira (Quota) ambapo Taasisi za Muunganozinatakiwa kuzingatia matakwa ya Waraka huo pindi fursaza ajira zinapopatikana.

(iv) Kamati inaishauri Serikali kuendelea nautekelezaji wa mpango wake wa kuongeza na kuboreshavitendea kazi chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais-Muunganokwa lengo kurahisisha utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi hiyokwa wakati na kwa ufanisi zaidi.

(v) Kwa upande wa fedha za maendeleo kuhusuMradi Na.6309, Kamati inashauri kuwa, fedha hizo kiasi chaSh.1,000,000,000 kwa mradi huo zinazoombwa kuidhinishwana Bunge lako Tukufu, zitolewe zote kwa wakati kwa mwaka

Page 139: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

wa fedha 2019/2020 ili kurahisisha ukamilishaji wa mradi huomuhimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nihitimishe kwakukupongeza wewe mwenyewe kwanza binafsi kwa kasi yakuliendesha Bunge hili. Pia napenda nitumie fursa hiikumpongeza Spika, Mheshimiwa Job Ndugai na Naibu Spika,Mheshmiwa Dkt. Tulia Ackson, kwa weledi na umahiri waokatika kuliongoza Bunge. Niwapongeze pia Wenyeviti waBunge kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kushauri na kusaidiakuendesha vikao vya Bunge. Wote kwa pamoja nawaombeaafya na uzima katika kutekeleza majukumu tuliyopewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti napenda kumpongeza nakumshukuru Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,Mheshimiwa Januari Makamba, Naibu Waziri, MheshimiwaMussa Ramadhan Sima, Watendaji Wakuu na Wataalamwote wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ushirikiano waliotoakwa Kamati wakati wa uchambuzi wa Bajeti ya Ofisi yaMakamu wa Rais-Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya pekeenapenda kuwashukuru Wajumbe wa Kamati kwa ushirikianona michango yao mizuri wakati wa kupitia na kuchambuaBajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano. Naombamajina yao kama yalivyo katika taarifa hii yaingie katikaTaarifa Rasmi ya Bunge (Hansard).

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa lakini si kwaumuhimu, napenda kumshukuru Katibu wa Bunge, NduguStephen Kagaigai kwa kuiwezesha Kamati kukamilisha kaziyake bila kukwama. Aidha, napenda kumshukuru Mkurugenziwa Kamati za Bunge, Ndugu Athuman Hussein, MkurugenziMsaidizi, Ndugu Angelina L. Sanga, Katibu wa Kamati hii,Ndugu Stanslaus Kagisa na Msaidizi wa Kamati Ndugu RaheliMasima kwa kuihudumia vyema Kamati pamoja nakukamilisha taarifa hii kwa wakati. Napenda kuwashukuruMakatibu Muhtasi wa Idara ya Kamati za Bunge kwakuchapa taarifa hii. Napenda pia kuwashukuru Watendaji

Page 140: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

wote wa Kitengo cha Taarifa Rasmi za Bunge (Hansard) kwakuhakikisha Taarifa hii inatoka kwa wakati na kwa ubora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayo,naliomba Bunge lako Tukufu sasa lijadili na kuidhinishaMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu waRais - Muungano, kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kamayalivyowasilishwa na Mheshimiwa Waziri wa Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha na naungamkono hoja hii.

TAARIFA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NASHERIA KUHUSU UTEKELEZAJI WA BAJETI YA OFISI YA

MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO) KWA MWAKA WA FEDHA2018/2019; PAMOJA NA MAONI YA KAMATI KUHUSU

MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA OFISI HIYO KWAMWAKA WA FEDHA 2019/2020 - KAMA

ILIVYOWASILISHWA MEZANI______________________

UTANGULIZIMheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 99 (9) ya Kanuniza Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016, naombakuwasilisha Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katibana Sheria kuhusu Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Makamuwa Rais-Muungano kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019,pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapatona Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020.

Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 6 (2) (c) cha Nyongeza yaNane ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016,kimeipa Kamati ya Katiba na Sheria jukumu la kusimamiashughuli za Ofisi ya Makamu wa Rias - Muungano.

Aidha, Kifungu cha 7(1) (a) cha Nyongeza ya Nane ya Kanuniza Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016 kinatoa Jukumukwa Kamati zote za Kisekta kushughulikia bajeti za Wizarainazozisimamia. Jukumu hil i la Uchambuzi wa Bajeti

Page 141: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

linaendana sambamba na jukumu la ukaguzi wa Miradi yaMaendeleo iliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha2018/2019 kwa mujibu wa Kanuni ya 98(1) ya Kanuni zaKudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano inaMafungu 2 ya Bajeti ambayo ni:-

i) Fungu 26 - Ofisi Binafsi ya Makamu wa Rais, na

ii) Fungu 31 - Ofisi ya Makamu wa Rais,

Mheshimiwa Spika, Taarifa hii inatoa maelezo kuhusu maeneoManne yafuatayo:-i) Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa mwakawa fedha unaoisha;

ii) Mapitio ya Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Bajetikwa Mwaka wa Fedha 2018/2019;

iii) Uchambuzi wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisiya Makamu wa Rais – Muungano kwa Mwaka wa Fedha2019/2020 na;

iv) Maoni na Ushauri wa Kamati

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEOILIYOTENGEWA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019

Fungu 26: Ofisi Binafsi ya Makamu wa Rais.Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia Muundo na Majukumu yaOfisi Binafsi ya Makamu wa Rais (Muungano), hakukuwa naBajeti ya Miradi ya Maendeleo katika Fungu hili.

Fungu 31: Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano;Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Kanuni ya 98 (1) yaKanuni za Kudumu za Bunge, Kamati ya Katiba na Sheriailipokea taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleoinayosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano.Orodha ya Miradi hiyo ni kama ifuatavyo:-

Page 142: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

i) Mradi Na. 6309 – Ujenzi wa Ofisi na Nyumba ya Makaziya Makamu wa Rais Zanzibar (Construction of Vice PresidentOffice and Residence in Zanzibar), ambao uliidhinishiwaShilingi Bilioni Moja (1,000,000,000/=), na

ii) Mradi Na. 6389 – Ujenzi na Ukarabati wa Ofisi naMakazi ya Makamu wa Rais (Luthuli II) (Construction andRehabilitation of Vice President Office Luthuli II and StateLodges), ambao uliidhinishiwa Shilingi Milioni Mia TanoThelathini na Nne na Laki Nane (538,800,000/=).

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Taarifa ya Ofisi ya Makamuwa Rais - Muungano ya tarehe 20 Machi, 2019, kwa kipindicha Julai, 2018 hadi Machi, 2019, Mradi Na.6389 wa Ujenzi naUkarabati wa Ofisi na Makazi ya Makamu wa Rais(Luthuli II)ulikuwa umepokea fedha zote zilizoidhinishwa na Bunge,Shilingi Milioni Mia Tano Thelathini na Nne na Laki Nane(538,800,000/=) sawa na asilimia 100%. Hata hivyo, Mradi Na.6309 haujapokea kiasi chochote cha Fedha zilizoidhinishwana Bunge.

UCHAMBUZI WA TAARIFA YA OFISI YA MAKAMU WA RAIS-MUUNGANO KUHUSU UTEKELEZAJI WA MPANGO WA BAJETI NAUZINGATIAJI WA MAONI YA KAMATI KWA MWAKA WA FEDHA2018/2019

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipokea na kuchambua Taarifaza Utekelezaji wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 nauchambuzi wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi yaMakamu wa Rais - Muungano kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, kwa mujibu wa Kanuni ya 98 (2) ya Kanuni za Kudumuza Bunge Toleo la Januari 2016, tarehe 20 Machi, 2019.Naomba kulijulisha Bunge lako Tukufu kuhusu uchambuzi huokama ifuatavyo:-

Uchambuzi wa Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango wa Bajetikwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Mheshimiwa Spika, uchambuzi uliofanywa na Kamati katikaMapitio ya Utekelezaji wa Mpango wa Bajeti ya Ofisi ya

Page 143: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

Makamu wa Rais - Muungano kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 ulitazama mlinganisho wa kiasi cha fedhakilichoidhinishwa na Bunge Aprili 2018 na kiwango ambachokimepokelewa hadi Machi 2019 katika Robo ya Tatu yaMwaka huu wa Fedha 2018/2019. Uchambuzi huu piaulitazama kiasi cha fedha kilichoidhinishwa katika Mwaka waFedha 2018/2019 na kiasi cha Fedha kilichopokelewa katikaMiradi ya Maendeleo hadi kufikia Mwezi Machi 2019. Lengola kufanya tathmini ya namna hii ni kufahamu Mwelekeo waMpango wa Bajeti ya Mapato na Matumizi ya Serikali katikaMwaka wa Fedha 2019/2020 ili kujua vipaumbele vya kibajeti.

Upatikanaji wa fedha za Matumizi ya Kawaida kutoka Hazina

FUNGU 26: Ofisi Binafsi ya Makamu wa RaisMheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2018/2019 Fungu26 la Ofisi Binafsi ya Makamu wa Rais lilitengewa Shilingi BilioniSita, Milioni Mia Nne Themanini na Tano, Laki Tisa Tisini naMoja Elfu Mia Tano Sabini na Nane na Senti Tano(6,485,991,578.05/=) kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Katiya fedha hizo, Shilingi Bilioni Moja na Milioni Hamsini na Tatu,Laki Sita Sitini na Sita Elfu (1,053,666,000/=) ilikuwa ni kwa ajiliya Mishahara, na Shilingi Bilioni Tano, Milioni Mia NneThelathini na Mbili, Laki Tatu Ishirini na Tano Elfu, Mia TanoSabini na Nane na Senti Tano (5,432,325,578.05/=) ilikuwa nifedha za Matumizi Mengineyo.

Mheshimiwa Spika, uchambuzi wa Kamati umebaini kuwa,katika kipindi cha kuanzia Mwezi Julai, 2018 hadi mwezi Machi2019, Jumla ya Shilingi Bilioni Nne, Milioni Mia Tano Sabini naMbili, Laki Nane na Kumi Elfu, Mia Tano Sabini na Nane naSenti Tano(4,572, 810,578,.05), zilikuwa zimepokelewa kwa ajiliya Mishahara na Matumizi Mengineyo. Kiasi hicho cha Fedhakilichopokelewa ni sawa na asilimia 70.5% ya Bajetiiliyoidhinishwa na Bunge katika Fungu 26.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaipongeza Hazina kwa kutoaFedha zilizoidhinishwa na Bunge kwa wakati, hatua ambayoimesaidia Ofisi Binafsi ya Makamu Rais-Muungano kutekelezaMajukumu yake kwa wakati na kwa ufanisi uliokusudiwa.

Page 144: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

FUNGU 31: Ofisi ya Makamu wa RaisMheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2018/2019 Fungu31 la Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ujumla lilitengewa ShilingiBilioni Kumi na Milioni Mbili, Themanini na Mbili Elfu, Mia TanoIshirini na Tatu na Senti Ishirini na Nane (10,002,082, 523.28/=)kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida.

Mheshimiwa Spika, Uchambuzi wa Kamati umebaini kuwa,katika kipindi cha Julai, 2018 hadi Machi, 2019 Ofisi hiyoilipokea Shilingi Bilioni Tano, Milioni Mia Tano Thelathini naSaba, Laki Saba Tisini na Tano Elfu na Tatu na Senti Ishirini naNane(5,537,795,003.28) sawa na asilimia 55.4% ya bajeti yaMatumizi ya Kawaida.

Mheshimiwa Spika, Uchambuzi huu unaonyesha kuwakumekuwa na Mwenendo mzuri na wa kuridhisha kuhusuupatikanaji wa fedha za Bajeti ya Matumizi ya Kawaida, kwaOfisi ya Makamu wa Rais-Muungano kwa Mafungu yote (Fungu 26 na Fungu 31).

Mheshimiwa Spika, Maoni ya Kamati ni kwamba hali hii yaupatikanaji wa fedha kwa wakati inatakiwa kuendelea nakuzingatiwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, ilikurahisisha usimamizi na utekelezaji wa shughuli mbalimbaliza Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano kwa wakati na kwaufanisi. Kwa hatua hii, Kamati inaipongeza Hazina na Serikalikwa Ujumla kwa kutoa Fedha za Matumizi ya Kawaida kwawakati.

Uchambuzi wa Utekelezaji wa Bajeti ya Maendeleo kwaMwaka wa Fedha 2018/2019 - FUNGU 31

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muunganoiliidhinishiwa Shilingi Bilioni Moja, Milioni Mia Tano Thelathinina Nane na Laki Nane (1,538,800,000/=) kwa ajili ya MiradiMiwili ya Ujenzi wa Ofisi na Makazi ya Makamu wa Rais(Zanzibar) (Mradi Na.6309) na Mradi wa Kujenga nakukarabati Ofisi ya Makamu wa Rais Luthuli II (Dar es Salaam)(Mradi Na.6389).

Page 145: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

Mheshimiwa Spika, Uchambuzi wa Kamati umebaini kuwa,katika kipindi cha Juai, 2018 hadi Machi, 2019, Mradi Na.6389wa Ujenzi na Ukarabati wa Ofisi na Makazi ya Makamu waRais(Luthuli II) ulikuwa umepokea asilimia 100% ya fedha zotezilizoidhinishwa na Bunge,ambazo ni Shilingi Milioni Mia TanoThelathini na Nane na Laki Nane (538,800,000/=). Aidha,Kamati imebaini kuwa, Mradi Na. 6309 haujapokea kiasichochote cha Fedha zilizoidhinishwa na Bunge.

Mheshimiwa Spika, maoni ya Kamati ni kuwa, Miradi hiiimechukua muda mrefu, hivyo, Serikali ihakikishe MradiNa.6309 unaanza na Kukamilika katika mwaka huu wa Fedha,2019/2020.

UCHAMBUZI WA MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NAMATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipokea na kuchambua Mpangona Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano kwaMwaka wa Fedha 2019/2020 tarehe 20 Machi 2019, ambayoimelenga kutekeleza masuala ya Muungano kwavipaumbele vifuatavyo:-

i) Kuratibu vikao vya Kamati ya Pamoja ya Serikali yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar (SMZ) vya Kushughulikia masuala yaMuungano,

ii) Kuratibu masuala ya kijamii na kiuchumi pamoja nakufuatilia utekelezaji wa program na Miradi ya Maendeleokwa pande mbili za Muungano,

iii) Kutoa elimu kwa Umma kuhusu Muungano kwamakundi mbalimbali ya kijamii, na

iv) Kuratibu masuala yasiyo ya Muungano kupitia vikaovya ushirikiano kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduziya Zanzibar zenye majukumu yanayoshabihiana.

Page 146: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

Mheshimiwa Spika, pamoja na vipaumbele hivyo, Kamatiinatoa rai kwa Ofisi ya Makamu wa Rais kuhakikisha kwambavipaumbele vyake vinaakisi mwendelezo wa kuimarisha nakuulinda Muungano wetu kwa manufaa ya Watanzania wotena kudumisha Udugu, Umoja na Mshikamano wa Watanzaniawa pande zote mbili za Muungano.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaipongeza Serikali ya Awamuya Tano kwa kuendeleza jitihada za dhati za Awamu Nnezilizotangulia, katika kutatua changamoto mbalimbli zaMuungano, hususan, kuendelea kurahisisha mwingiliano wakibiashara baina ya Pande mbili za Muungano kwa kuzitafutiaufumbuzi kero mbalimbali za kikodi na kisheria kwa manufaaya pande zote mbili na wananchi wake kwa ujumla.

Uchambuzi wa Makadirio ya Matumizi kwa Mwaka wa Fedha2019/2020

Fungu 26: Ofisi Binafsi ya Makamu wa RaisMheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 OfisiBinafsi ya Makamu wa Rais (Fungu 26) inaomba kuidhinishiwajumla ya Shilingi Bilioni Saba, Milioni Mia Nane Hamsini naTano na Tisini na Tatu Elfu (7,855,093,000/=) kwa ajili yaMatumizi ya Kawaida na Matumizi Mengineyo. Kati ya fedhahizo, Shilingi Bilioni Moja, Milioni Mia Moja Ishirini, Laki MojaIshirini na Nane Elfu (1, 120,128,000/=) ni kwa ajili yaMishahara, na Shilingi Bilioni Sita,Milioni Mia Saba Thelathinina Nne, Laki Tisa Sitini na Tano Elfu (6,734,965,000/=) ni fedhaza Matumizi Mengineyo.

Mheshimiwa Spika, uchambuzi wa Kamati umebainikwamba, Bajeti ya Fungu 26 imeongezeka kwa kiasi chaShilingi Bilioni Moja, Milioni Mia Tatu Sitini na Tisa, Laki Mojana Moja Elfu, Mia Nne Ishirini na Mbili (1,369,101,422)ikilinganishwa na Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwa Mwakawa Fedha 2018/2019, Ongezeko hilo ni sawa na asilimia21.11% ya Bajeti ya Fungu 26 kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019. Ongezeko hili linatokana na mahitaji halisi ya Ofisi Ofisihiyo hususan gharama za utoaji huduma kwa Ofisi Binafsi yaMakamu wa Rais.

Page 147: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

Fungu 31; Ofisi ya Makamu wa RaisMheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 Ofisiya Makamu wa Rais (Fungu 31) inaomba kuidhinishiwa jumlaya Shilingi Bilioni Tano, Milioni Mia Tatu Hamsini na Saba, LakiTano Sabini na Tano Elfu, Mia Tano Sitini (5,357,575,560/=) kwaajili ya Matumizi ya Mishahara na Matumizi Mengineyo. Katiya fedha hizo, Shilingi Bilioni Moja,Milioni Mia Tisa Thelathinina Moja, Laki Sita Ishirini na Nne Elfu (1,931,624,000/=) ni kwaajili ya Mishahara, na Shilingi Bilioni Tatu, Milioni Mia Nne Ishirinina Tano, Laki Tisa Hamsini na Moja Elfu, Mia Tano Sitini,(3,425,951,560/=) ni fedha za Matumizi Mengineyo.

Mheshimiwa Spika, Uchambuzi wa Kamati umebainikwamba, bajeti ya Matumizi ya Kawaida kwa Fungu 31imeongezeka kwa asilimia 4.5% ikilinganishwa na Bajetiiliyoidhinishwa na Bunge chini ya Fungu hili kwa Mwaka waFedha 2018/2019. Kama ilivyoelezwa hapo juu, Ongezeko hililinatokana na mahitaji halisi ya Ofisi hiyo ikiwa ni pamoja nauratibu wa vikao vya Kamati ya Pamoja kati ya Serikali yaMuungano wa Tanzania(SMT) na Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar (SMZ) na uanzishwaji wa Ofisi ya Makamu wa RaisZanzibar.

Mpango wa Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020(FUNGU 31).

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano, Mradi mmoja wa Maendeleo unaendeleakuombewa Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. Mradihuo ni Mradi Na. 6309 wa Ujenzi wa Ofisi na Makazi yaMakamu wa Rais Zanzibar ambao unaombewa Shilingi BilioniMoja (1,000,000,000/=)

Mheshimiwa Spika, Kamati inapendekeza Fedha hizo zitolewekwa wakati kwa Mwaka huu wa Fedha 2019/2020 ilikurahisisha ukamilishaji wa mradi huo muhimu. Aidha, kuhusukuanza utekelezaji wa Mradi huo kabla ya mwaka huu wafedha kuisha, Kamati inashauri Serikali itoe fedhazilizopangwa na kuidhinishwa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 ili kuwezesha utekelezaji wa shughuli zilizopangwa.

Page 148: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

MAONI NA USHAURI WA KAMATIMheshimiwa Spika, ninaomba sasa kutoa maoni na ushauriwa Kamati kuhusu masuala mbalimbali yaliyojitokeza katikauchambuzi wa Taarifa ya utekelezaji wa Bajeti kwa Mwakawa Fedha 2018/2019 pamoja na Taarifa za Makadirio yaMapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 waOfisi ya Makamu wa Rais - Muungano kama ifuatavyo:-

i) Mheshimiwa Spika, Kamati imeridhishwa kwa kiasikikubwa na utekelezaji wa maoni na mapendekezo yaKamati yaliyotolewa na Kamati kwa Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano) katika Mwaka wa Fedha 2018/2019, ikiwa nipamoja na kuendelea na ukarabati wa Magari na Mitamboyote inayotumiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano.Aidha, Kamati inaipongeza Serikali kwa kununua Magarimapya kwa lengo la kurahisisha utekelezaji wa Majukumumbalimbali chini ya Ofisi hii muhimu.

ii) Mheshimiwa Spika, Kamati inapongeza juhudi za Ofisiya Makamu wa Rais (Muungano) kwa kushirikiana naMamlaka husika za pande mbili za Muungano katika kutatuachangamoto mbalimbali katika Sekta ya biashara baina yaPande mbili za Muungano, hatua ambayo itachochea ukuajiUchumi kwa Mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

iii) Mheshimiwa Spika, Kamati inaendelea kuishauriSerikali kuendelea kuratibu utekelezaji wa Waraka wa Mgaowa Muda wa Ajira (Quota) ambapo Taasisi za Muunganozinatakiwa kuzingatia matakwa ya Waraka huo pindi fursaza Ajira zinapopatikana.

iv) Mheshimiwa Spika, Kamati inaishauri Serikalikuendelea na utekelezaji wa mpango wake wa kuongezana kuboresha vitendea kazi chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano kwa lengo kurahisisha utekelezaji wa Majukumuya Ofisi hiyo kwa wakati na kwa ufanisi zaidi.

v) Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Fedha zaMandeleo kuhusu Mradi Na.6309, Kamati inashauri kuwa,Fedha hizo kiasi cha Shilingi Bilioni Moja (1,000,000,000/=) kwa

Page 149: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

Mradi huo zinazoombwa kuidhinishwa na Bunge lako Tukufu,zitolewe zote kwa wakati kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020ili kurahisisha ukamilishaji wa mradi huo muhimu.

HITIMISHOMheshimiwa Spika, napenda nikupongeze kwa umahiri wakokatika kasi ya kuliendesha Bunge hili katika kuishauri vemaSerikali kwa manufaa ya Wananchi wa Tanzania, pia,nikushukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuwasilisha Maoni yaKamati kwa niaba ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katibana Sheria.

Mheshimiwa Spika, napenda kumpongeza Naibu SpikaMheshmiwa Dkt. Tulia Ackson, Mb, kwa weledi na umahiriwake katika kukusaidia kuongoza Bunge. Niwapongeze piaWenyeviti wa Bunge kwa kazi nzuri wanayoifanya yakukushauri na kukusaidia kuendesha vikao vya Bunge. Wotekwa pamoja tunawaombea afya na uzima katika kutekelezamajukumu mliyopewa.

Mheshimiwa Spika, napenda kumpongeza na kumshukuruWaziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. JanuariMakamba, (Mb), Naibu Waziri, Mhe. Mussa RamadhanSima,(Mb), Watendaji Wakuu na Wataalam wote wa Ofisi yaMakamu wa Rais kwa ushirikiano waliotoa kwa Kamati wakatiwa uchambuzi wa Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee napendakuwashukuru Wajumbe wa Kamati kwa ushirikiano namichango yao mizuri wakati wa kupitia na kuchambua Bajetiya Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano. NAOMBA MAJINAYAO KAMA YALIVYO KATIKA TAARIFA HII YAINGIE KATIKATAARIFA RASMI YA BUNGE (HANSARD).

1. Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa, Mb – Mwenyekiti2. Mhe. Najma Murtaza Giga, Mb – Makamu /Mwenyekiti3. Mhe. Joseph Kizito Mhagama, Mb - Mjumbe;4. Mhe. Makame Mashaka Foum, Mb - Mjumbe;5. Mhe. Asha Abdallah Juma, Mb - Mjumbe;

Page 150: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

6. Mhe. Amina Saleh Mollel, Mb - Mjumbe;7. Mhe. Wanu Hafidh Amer, Mb - Mjumbe;8. Mhe. Prof. Jumanne Abdallah Maghembe, Mb - Mjumbe;9. Mhe. Dkt. Mathayo David Mathayo, Mb - Mjumbe;10. Mhe. Nimrod Elirehemah Mkono, Mb - Mjumbe;11. Mhe. Susan Peter Maselle, Mb - Mjumbe;-12. Mhe. Alfredina Apolinary Kahigi, Mb - Mjumbe;13. Mhe. Latifah Hassan Chande,Mb - Mjumbe;14. Mhe. Ally Abdulla Saleh, Mb - Mjumbe;15. Mhe.Jacqueline Kandidus Ngonyani Msongozi,Mb- Mjumbe;16. Mhe. Bupe Nelson Mwakang’ata, Mb - Mjumbe;17. Mhe. Sixtus Raphael Mapunda, Mb - Mjumbe;18. Mhe. Hassan Seleman Kaunje, Mb - Mjumbe;19. Mhe. Yahaya Omary Massare, Mb - Mjumbe;20. Mhe. Upendo Furaha Peneza, Mb - Mjumbe;21. Mhe. Tundu Antiphas Mughwai Lissu, Mb – Mjumbe;22. Mhe. Emmanuel A.Mwakasaka, Mb – Mjumbe;23. Mhe. Dkt. Suzan Alphonce Kolimba, Mb – Mjumbe;

Mheshimiwa Spika, mwisho, kabisa lakini si kwa umuhimunapenda kumshukuru Katibu wa Bunge, Ndg. StephenKagaigai kwa kuiwezesha Kamati kukamilisha kazi yake bilakukwama. Aidha, napenda kumshukuru Mkurugenzi waKamati za Bunge Ndg. Athuman Hussein, Mkurugenzi MsaidiziNdg. Angelina L. Sanga, Katibu wa Kamati hii, Ndg. StanslausKagisa na Msaidizi wa Kamati Ndg. Raheli Masima kwakuihudumia vyema Kamati pamoja na kukamilisha taarifa hiikwa wakati. Napenda kuwashukuru Makatibu Muhtasi waIdara ya Kamati za Bunge kwa kuchapa taarifa hii. Napendapia kuwashukuru Watendaji wote wa Kitengo cha TaarifaRasmi za Bunge (Hansard) kwa kuhakikisha Taarifa hii inatokawa wakati na kwa ubora.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo naliomba Bungelako Tukufu sasa lijadili na kuidhinisha Makadirio ya Mapatona Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais -Muungano, kwaMwaka wa Fedha 2019/2020 kama yalivyowasilishwa naMheshimiwa Waziri hivi punde.

Page 151: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na naunga mkonohoja hii.

Mohamed Omary Mchengerwa, Mb.MWENYEKITI,

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA16 APRILI, 2019

MWENYEKITI: Ahsante. Sasa namwita Mwenyekiti waKamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara naMazingira.

MHE. KANALI MST. MASOUD ALI KHAMIS - K.n.y.MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA,BIASHARA NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwaniaba ya Mwenyekiti, naomba kuwasilisha Taarifa ya Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingirakuhusu utekelezaji wa majukumu ya Uhifadhi wa Usimamiziwa Mazingira chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira,Fungu 31 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na maonikuhusu Makadirio na Mapato ya Matumizi ya mwaka wafedha 2019/2020.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote, napendakumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema kwakutujalia uhai kuweza kufikia siku ya leo ambapo tumekutanakwa ajili ya kujadili bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais –Mazingira. Kwa kuzingatia umuhimu wa yaliyomo kwenyetaarifa hii pamoja na muda wa kutoa maoni, naomba taarifayote ya Kamati kama ilivyo katika kitabu iiingie katikakumbukumbu za taarifa za Bunge yaani Hansard

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Kanuni ya99(9) ya Kanuni za Bunge, Toleo la Januari, 2016, naombakuwasilisha Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge yaViwanda, Biashara na Mazingira kuhusu utekelezaji wamajukumu ya hifadhi na usimamizi wa mazingira chini ya Ofisiya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Fungu 31 kwa

Page 152: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

mwaka 2018/2019 na makadirio ya mapato na matumizi yamwaka 2019/2020.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuliarifu Bungelako Tukufu kuwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara na Mazingira ilizingatia matakwa ya Kanuni ya 98(1)ya Kanuni za Kudumu za Bunge ambapo ilifanya ziara katikabaadhi ya miradi ya maendeleo iliyotengewa fedha katikamwaka wa fedha 2018/2019, kwa lengo la kujionea hali halisiya utekelezaji wa miradi hiyo. Vilevile, Kamati ilipokea nakujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Makamuwa Rais - Mazingira kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamojana kuchambua Mpango na Bajeti kwa mwaka fedha wa2019/2020 kama inavyoelekezwa na Kanuni ya 98 (2)ikisomwa pamoja na kifungu cha 7(1)(a) cha Nyongeza yaNane ya Kanuni za Kudumu za Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa hii inalengakuliomba Bunge lako Tukufu kuidhinisha maombi ya fedhakwa ajili ya Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, lakini piakutoa mapendekezo kwa Bunge kuhusu masuala kadhaaambayo Kamati inaamini ni muhimu yakafanyiwa kazi ilikuboresha shughuli za hifadhi na usimamizi wa mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa hii inatoa maelezokuhusu maeneo yafuatayo. Moja, mapitio ya utekelezaji waMpango wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2018/2019. Mbili,matokeo ya ukaguzi ya miradi ya maendeleo. Tatu uzingatiajiwa ushauri wa Kamati kuhusu bajeti ya Ofisi ya Makamu waRais Mazingira mwaka wa fedha 2018/2019. Nne, uchambuziwa mpango wa makadirio ya mapato na matumizi ya fedhakwa mwaka 2019/2020. Tano, maoni na ushauri wa Kamati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi wa taarifa yautekelezaji wa Mpango wa Bajeti wa mwaka 2018/2019.Katika kutekeleza masharti ya Kanuni ya 98(2) ya Kanuni zaBunge, Toleo la Januari, 2016, Kamati ilichambua taarifa yautekelezaji wa Mpango wa Bajeti ya Ofisi ya Makamu waRais – Mazingira kwa mwaka wa fedha 2018/2019. Katikauchambuzi huo, Kamati i l itumia mapitio ya taarifa

Page 153: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

zilizowasilishwa, matokeo ya ziara za ukaguzi wa miradi yamazingira pamoja na mahojiano wakati wa vikao. Lengo lanjia hizo lilikuwa ni kujiridhisha kuhusu ukusanyaji wa mapato,utekelezaji wa malengo/kazi na upatikanaji wa fedhaikilinganishwa na kiasi kilichoidhinishwa na Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tarehe 17 Aprili, 2018, Bunge lakoTukufu lilijulishwa kuwa katika mwaka wa fedha 2018/2019,Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira – NEMClilipanga kukusanya Sh.18,877,446,995 kutoka vyanzo vyandani vya Baraza. Lengo hili la makusanyo lilikuwa limezidilengo la mwaka wa fedha 2017/2018 kwa asilimia 20.4.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi wa Kamatiumebainisha kuwa hadi kufikia tarehe 14 Machi, 2019, NEMCilikuwa imekusanya SH.10,430,060,727 kiasi ambacho nipungufu ya lengo kwa asilimia 44.8 ya kiasi kilichopangwakukusanywa kwa mwaka huu wa fedha. Takwimu hizozinaonesha kuwa katika robo moja ya kipindi cha utekelezaji,NEMC itakusanya asilimia 44.8 ya lengo la makusanyo jamboambalo si la kawaida/uhalisia. Aidha, Takwimu hizi zinaashiriakuwa lengo hili lilipangwa bila kuzingatia uhalisia wa uwezowa NEMC wa kukusanya na upungufu huu unaashiriakukwama kwa utekelezaji wa baadhi ya majukumu ya NEMCkwa mwaka wa fedha 2018/2019. Kutokana na uwezekanomdogo wa kukusanya asilimia 44.8 iliyobaki kwa mwaka wafedha unaoishia, Kamati imeishauri NEMC kupanga lengo lamakusanyo kwa kuzingatia uwezo wake wa kukusanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwaka wa fedha 2018/2019, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira iliidhinishiwa jumlaya Sh.8,118,494,000.00 kwa ajili ya matumizi ya hifadhi nausimamizi wa mazingira. Hadi kufikia tarehe 14 Machi, 2019,Ofisi hii ilikuwa imepokea Sh.4,167,969,635.79 tu, sawa naasilimia 51.3 ya fedha zote zilizokuwa zimeidinishwa na Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi wa Kamatiumebaini kuwa kiasi kilichopokelewa ni pungufu kwa asilimia48.7. Kwa kipindi hiki cha robo ya nne ya mwaka wa Fedha2018/2019 il itarajiwa zaidi ya asil imia 75 ya fedha

Page 154: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

zilizoidhinishwa na Bunge ziwe zimepokelewa tofauti na ilivyosasa ambapo ni asilimia 51.3 tu ndiyo ilikuwa imepokelewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, uchambuzi waKamati ulibaini kuwa kati ya Sh.3,524,540,000.00 ya fedha zaMiradi ya Maendeleo ni Sh.1,861,299,489.50 tu ndizozimepokelewa kwa aji l i ya utekelezaji wa Miradi yaMaendeleo, kiasi hicho ni fedha za nje. Vilevile, Kamati ilibainikuwa katika fedha za maendeleo kulikuwa na fedha za ndaniambazo ni Sh.1,461,200,000.00 lakini hadi kufikia robo ya tatuya mwaka wa fedha 2018/2019 zilikuwa hazijapokelewakabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi huuunadhihirisha kuwa baadhi ya majukumu ya usimamizi wamazingira yameshindwa kutekelezwa ipasavyo hususanimiradi ya maendeleo. Mwenendo wa upatikanaji wa fedhakwa ajili ya shughuli za hifadhi ya mazingira si wa kuridhishakwa upande wa fedha za Miradi ya Maendeleo hususanifedha za ndani. Kamati inaishauri Serikali kuweka mikakatina msisitizo katika kuwezesha shughuli za usimamizi wamazingira kwa kutenga fedha za kutosha zikiwepo fedha zandani na kuzipeleka kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafurahi kulijulisha Bungelako Tukufu kuwa kwa mwaka wa fedha 2018/2019, kazizilizopangwa kuhusiana na hifadhi na usimamizi wa mazingirazilitekelezwa. Hata hivyo, Kamati inaendelea kuisisitiza Ofisiya Makamu wa Rais-Mazingira kuongeza juhudi katikamajukumu sita kama ilivyooneshwa katika taarifa hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Maoni ya Jumla kuhusuutekelezaji wa bajeti. Matokeo ya uchambuzi wa taarifa yautekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais – mazingirakuhusu hifadhi na usimamizi wa mazingira yanaonesha kuwaupatikanaji wa fedha za uendeshaji wa shughuli za Idara yaMazingira (fedha za matumizi ya kawaida) umekuwa mzuriukil inganisha na upatikanaji wa fedha za Miradi yaMaendeleo hususani fedha za ndani ambapo hadi kufikiatarehe 14 Machi, 2019, kati ya fedha zote za Miradi ya

Page 155: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

Maendeleo ni fedha za nje tu ndizo zilikuwa zimepokelewajambo ambalo halitoi picha nzuri kwa wahisani wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha2018/2019, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Fungu 31,iliidhinishiwa Sh.3,524,540,000.00 kwa ajili ya kutekeleza Miradiya Maendeleo. Kati ya fedha hizo, Sh.1,461,200,000.00 ni fedhaza ndani na Sh.2,063,340,000.00 fedha za nje. Kamati ilipatafursa ya kutembelea Mradi wa Kuhimili Mabadiliko yaTabianchi - Bagamoyo (Mradi Namba 5301); Mradi wa Ujenziwa Ofisi za NEMC (Mradi Namba 6507) na shughuli za uhifadhimazingira katika Ziwa Manyara. Ufafanuzi wa miradi yamaendeleo na shughuli za mazingira zilizotembelewa nakukaguliwa na Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingirakwa mwaka wa fedha 2018/2019 ni kama ilivyoonekanakatika taarifa ya kamati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ilipata fursa yakutembelea hifadhi ya mazingira Manyara kwa lengo lakujionea hali ya mazingira katika eneo la hifadhi ambayoinahusisha na Ziwa Manyara na kuangalia changamoto namkakati wa Serikali katika kukabiliana na athari za kimazingirakatika eneo hilo la hifadhi. Shughuli za hifadhi na mazingirakatika Ziwa Manyara zinatekelezwa na TANAPA nazinahusisha kutoa elimu ya mazingira na sheria, usimamizi wamazingira katika ngazi za Wilaya na Halmashauri ya Mkoawa Manyara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uhifadhi wa Mazingira katikaZiwa Manyara unakumbana na changamoto ya ukosefu wafedha za kwa ajili ya kutekeleza shughuli za uhifadhi nausimamizi wa mazingira katika eneo la hifadhi, jambolinalopelekea athari za uharibifu unaofanywa kuendelea nakupelekea kuhatarisha eneo la hifadhi hususani ZiwaManyara. Pia Shughuli za binadamu (kilimo kisichofuatakanuni za kitaalamu, uwepo wa mifugo mingi) katika maeneoya karibu na Ziwa Manyara zinazopelekea mmomony’okowa udongo na kupelekea tope jingi kuelekea ziwani nakupunguza kina cha maji kupelekea kukauka kwa ziwa.Takwimu zinasema katika kipindi cha miaka 35 ya karibuni

Page 156: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

(1980-2015) hali imezidi kuwa mbaya ambapo matukio yakukauka Ziwa yalikuwa 7 wakati kati ya mwaka (1920-1970)ziwa liliripotiwa kukauka mara tatu tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto nyingine nimabadiliko ya tabianchi ambayo hupelekea ukame nakukauka kwa vyanzo vya maji yatiririkayo kwenda ziwani nakupelekea kukauka kwa Ziwa manyara. Vilevile, shughuli zakibinadamu katika eneo la hifadhi zisizolenga matumiziendelevu ya rasilimali za asili jambo linalopelekea kuharibumfumo Ikolojia ya Tarangire na Ziwa Manyara na kuviwekakatika hatari ya kutoweka na mimea vamizi/wageni katikabaadhi ya vyanzo vya maji vya Ziwa Manyara ambavyohupelekea maji kushindwa kufika ziwani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya ziara katika ZiwaManyara Kamati ilikuwa na maoni na ushauri ufuatao:-

(i) Kwa kuwa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004inampa mamlaka Waziri mwenye dhamana ya kusimamiamazingira kuliingiza katika orodha ya maeneo lindwa eneololote linaloonekana lipo katika hatihati za kutowekea, Serikaliifanye haraka kuanza mchakato wa kuliingiza Ziwa Manyarakatika maeneo lindwa. Hatua hii ichukuliwe kwa maziwa yoteambayo yapo katika hatari ya namna hii likiwepo ziwa Jipena Chala.

(ii) Serikali kuangalia namna ya kuwasaidia nakuwasimamia wakulima na wafugaji kufanya shughuli zaombali na miinuko. Shughuli hizi zimekuwa zikiporomoshaudongo na tope katika Ziwa Manyara.

(iii) Ziwa Manyara na Bioanuai zipatikanazo katika ziwahili ni moja ya kivutio kikubwa kinachovuta utalii katika Hifadhiya Manyara, changamoto zinazopelekea kukauka kwa ZiwaManyara kunahatarisha na kupelekea kupungua kwashughuli za utalii katika Hifadhi ya Manyara. Serikali ifanyejitihada za makusudi kuhakikisha wanalinusuru Ziwa Manyara.

Page 157: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

(iv) Kuna udhaifu katika kusimamia Sheria za Mazingirana Sheria ndogondogo za Vijiji na Halmashauri jambolinalotoa mianya kwa baadhi ya watu kuendelea shughulizao katika eneo la hifadhi. Kamati inaishauri Serikali kuongezakasi ya kufutilia na kusimamia matakwa ya sheria ili kuzuiashughuli zisizo endelevu katika eneo la hifadhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kukamilisha ziaraza ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo ya mwaka 2018/2019,Kamati ilikuwa na maoni ya jumla kuhusu utekelezaji wa miradihiyo na inashauri mambo yafuatayo:-

(i) Serikali kulipa uzito suala la hifadhi ya mazingira kwakutenga fedha za maendeleo na kuzipeleka kwa wakati. Kwasasa asilimia kubwa ya Miradi ya Maendeleo ya Mazingirainatekelezwa kwa kutumia fedha za wafadhili jambo ambalosi sahihi sana.

(ii) Sekta asili (kilimo, ufugaji na uvuvi) kwa kiasi kikubwandiyo zinategemewa katika uchumi wa nchi yetu namaendeleo ya sekta hizi kwa kiasi kikubwa yanategemeauhifadhi wa mazingira. Jambo la kushangaza shughuli hizi hizizimekuwa zikiendeshwa bila kuzingatia taratibu za kitaalamu.Kamati inashauri Serikali kuongeza kasi ya kuielimisha jamiikuhusu umuhimu wa kutunza mazingira, pia kuwa na matumiziendelevu ya rasilimali za asili hususani misitu na vyanzo vyamaji.

(iii) Sheria ya Mazingira inayotekelezwa sasa ni yamwaka 2004 lakini inatekelezwa kwa kuzingatia Sera ya Taifaya Mazingira ya mwaka 1997. Sera hii ni ya zamani takribanimiaka 22 na haijahusisha mabadiliko mengi ambayoyameendelea kutokea katika mazingira mfano mabadilikoya tabianchi na viumbe vamizi. Kamati inashauri Serikalikukamilisha mchakato wa kuandaa Sera mpyaitakayoendana na mazingira ya sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati pia i l ifuatil iauzingatiaji wa ushauri iliyoutoa wakati wa kuchambua taarifaya utekelezaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira mwaka

Page 158: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

wa fedha 2017/2018, pamoja na Makadirio ya Mapato naMatumizi ya Ofisi kwa mwaka wa fedha 2018/2019. Kamatiilitoa ushauri kwenye maeneo mbalimbali na kutoa maagizokumi na mbili (12). Naomba kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwaSerikali imejitahidi kuzingatia ushauri wa Kamati na kutekelezamaagizo hayo. Hata hivyo, kuna maeneo manne ambayoserikali haikuyatekeleza ipasavyo kama inavyoainishwakwenye taarifa hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uchambuzi waMpango wa Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwakawa Fedha 2019/2020; kabla ya kuchambua Makadirio yaMapato na Matumizi katika jukumu la kuhifadhi na kusimamiamazingira, Kamati ilipitia maelezo ya Waziri kuhusu kazizilizopangwa kutekelezwa kwa mwaka 2019/2020. Lengolilikuwa ni kufuatilia tija inayoweza kupatikana kutokana namalengo yaliyopangwa na ofisi hii kwa fedha zinazoombwakatika kifungu 5003.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ililinganisha malengoya mwaka wa fedha 2018/2019 na 2019/2020 na katikaulinganisho huo Kamati ilibaini yafuatayo:-

Moja, malengo yote yaliyozingatia hati idhini yaSerikali iliyoainishwa majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais,Mazingira.

Pili, lengo Na.2 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 nalengo la 12 kwa mwaka wa fedha 2019/2020 yanaendanana kwamba yote yanajielekeza kwenye udhibiti wa utupajitaka ngumu na hatarishi.

Tatu, lengo linahususha udhibiti wa taka ngumu kwamwaka wa fedha 2019/2020, ni mwelekeo wa uzingatiaji waushauri uliowahi kutolewa na Kamati hii kwa mwaka wa fedha2017/2018.

Mheshimiwa wenyekiti, aidha, agizo la Waziri Mkuualilolitoa akihitimisha hoja Bungeni tarehe 9/4/2019, linatoanguvu ya msisitizo kama ilivyotolewa na Kamati ya mwaka

Page 159: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

2017/2018. Kwa uchambuzi huo, Kamati inaipongeza Serikalikwa kupokea ushauri uliotolewa na Kamati na kutoa mudawa kutosha kwa wawekezaji hao kuanzia Agosti, 2017 hadiMei, 2019 na ni matumaini ya Kamati kuwa wawekezaji haowatakuwa wametumia vizuri muda uliotolewa na Serikali,hivyo kuweza kutumia teknolojia nyingine na kuwezeshakuzalisha mifuko mbadala.

Aidha, Kamati inaishauri Ofisi ya Makamu wa Rais,Mazingira, kufuatilia utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu nakuhakikisha ifikapo tarehe 30 Mei, 2019 matumizi ya mifukoya plastiki yatakuwa yamefika mwisho. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uchambuzi waMakadirio ya mapato. Katika mwaka wa fedha 2019/2020,Ofisi ya Makamu wa Rais chini ya Fungu 31 inalengakukusanya jumla ya shilingi bilioni 18.2 kutoka katika vyanzovya ndani vya Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi waMazingira (NEMC) ambayo ni ada, faini zitokanazo nashughuli za usimamizi wa mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi wa Kamatiulibaini kuwa, kiasi kinachotengwa kukusanywa kinakaribianakabisa na malengo ya mwaka wa fedha 2018/2019 ambapoyalitekelezwa kwa asilimia 55.2 tu hadi kufikia robo ya tatuya mwaka wa fedha, kipindi ambacho walipaswa kukusanyaasilimia 75.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na uchambuzihuu, Kamati inaishauri Serikali mambo yafuatayo:-

Moja, kupanga lengo la makusanyo kwa kuzingatiakasi na uwezo wake wa kukusanya; pili, wakati wa kupangalengo la makusanyo, izingatie changamoto zilizokwamishakufikia lengo la makusanyo la mwaka wa fedha uliotangulia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati inatambua kuwawingi wa mapato yatokanayo na shughuli za mazingira nimkubwa, lakini kasi ya ukusanyaji bado ni ndogo. Kamatiinashauri Serikali kuiongezea NEMC uwezo kwa kuwapatia

Page 160: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

matumizi na vitendea kazi ili waweze kuongeza kasi yaukaguzi na hatua ambayo itaongeza mapato kwa Barazapia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni uchambuzi wabajeti ya matumizi. Bajeti ya matumizi kwa ajili ya shughuli zaHifadhi na Usimamizi wa Mazingira hutengwa katika Fungu31 - Ofisi ya Makamu wa Rais. Kamati ilijulishwa kuwa jumlaya shilingi bilioni 22.7 zinaombwa kwa ajili ya kutekelezamajukumu muhimu. Kiasi hiki ni ongezeko la asilimia 179.71ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi wa Kamatiulibaini kuwa ongezeko la bajeti ya shughuli za Hifadhi yaUsimamizi wa Mazingira kwa mwaka wa fedha 2019/2020 linaathari katika fedha za miradi ya maendeleo ambayoimeongezeka kutoka shilingi bilioni 3.52 mwaka 2018/2019mpaka shilingi bilioni 18.2 mwaka wa fedha 2019/2020.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni maoni ya jumlakuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wafedha 2019/2020. Tanzania ni nchi mwanachama wamikataba mingi ya Kimataifa inayohusishwa na mambo yaMazingira. Kupitia mikataba hiyo, nchi hii ina fursa ya kupatafedha za maendeleo kwa kuandika maandiko ya miradi nakuyawasilisha katika Taasisi za Mazingira Duniani. Kamatiimebaini kuwa kama nchi, haijatumia fursa hiyo ipasavyo,kwa kuwa hatujaandika maandiko ya kutosha ambayoyanawezesha upatikanaji wa fedha hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa mwenendo waupatikanaji wa fedha kwa ajili ya shughuli za uhifadhi nausimamizi wa mazingira siyo wa kuridhisha, hivyo basi, Kamatiinaishauri Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira,Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)na wadau wengine wa mazingira kuchangamkia fursa hii kwakuongeza kasi na kuandaa maandiko ya kutosha yenyeuhalisia na kuyawasilisha katika taasisi za Kimataifa kila fursainapotokea. Juhudi hizo zitapelekea kuongezeka kwa fedhaza uhifadhi na utunzaji wa mazingira nchini.

Page 161: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hili, Kamatiinaishauri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira kuwatambuawadau wote wa mazingira hususan NGO’s ambaowanatumia fursa hii kupata fedha za miradi. Umuhimu wakuwatambua wadau hawa ni kuwawezesha Ofisi ya Makamuwa Rais, Mazingira kuweza kuwafuatilia na kuhakikisha fedhawanazozipata zinatumika kutekeleza miradi inayokusudiwa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yafuatayo ni maoni naushauri wa Kamati: Hali ya Mazingira nchini siyo ya kuridhisha.Tafiti zimeonesha kuwa tafiti zilizofanyika na kubainisha halimbalimbali zinaashiria jambo hili. Kamati ilipata fursa wakatiwa ziara zake za ukaguzi wa miradi, kutembelea nakushuhudia hali isiyo ya kuridhisha ya mazingira katika baadhiya maeneo nchini. Kamati imebainisha maeneo machachetu ambayo yanadhihirisha hali mbaya ya mazingira kwalengo la kutoa picha ya kuathirika kwa mazingira ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo hayo ni pamojana:-

Moja, athari za mabadiliko ya tabia nchi, ambazozimeshadhihirika katika maeneo mbalimbali nchini. Athari hizoni pamoja na ukame, mafuriko, kuenea kwa magonjwa yakuambukiza, kuongezeka kwa ujazo wa maji baharini,kuharibu kingo za bahari na fukwe, kumezwa kwa visiwavidogo kwenye bahari na kuathiri water table, kuyeyuka kwabarafu katika vilele vya milima kama vile Mlima Kilimanjaro,uharibifu wa madaraja, barabara, reli na makazi kutokanana mafuriko,

Pili, hali ya ukame na jangwa nchini; tafiti zinaoneshakuwa asilimia 61 ya nchi ipo hatarini kugeuka jangwa. Baadhiya Mikoa iliyoathirika zaidi na hali ya ukame nchini ni pamojana Dodoma, Singida, Shinyanga, Simiyu, Manyara na baadhiya maeneo ya Mikoa wa Kilimanjaro. Kwa kiasi kikubwa halihii inatokana na matumizi ya yasiyo endelevu ya rasilimaliasili nchini.

Page 162: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

Tatu, takwimu za ukataji wa misitu zinaonesha kuwa,msitu wenye ukubwa wa kiwanja cha mpira hufyekwa kilabaada ya dakika moja. Takwimu hizi zimepelekea Tanzaniakuwa katika ya nchi tano za juu (top five) zinazoongoza kwaukataji wa misitu duniani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania imeingia katikaorodha ya nchi zenye upungufu wa maji ikilinganishwa namahitaji, hali hiyo ni moja ya kiashiria cha uharibifu wamazingira katika vyanzo vya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baadhi ya maziwa yaliyopokwenye hatari ya kupotea ni Ziwa Manyara, Jipe na Chala.Kupotea kwa maziwa haya kwa kiasi kikubwa kimechangiwana shughuli za kibinadamu zinazoendeshwa katika maeneoya ziwa ambapo hupelekea uharibifu wa mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hayo ni baadhi tu yamaeneo ambayo yameonekana kuwa hali ya mazingiranchini siyo ya kuridhisha. Hivyo basi, Kamati inaishauri Serikalikuchukua jitihada za kimakusudi kwa lengo la kunusuru nchikutokana na athari zitokanazo na uharibifu wa mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kufanya ziara yaukaguzi wa miradi ya maendeleo na kuchambua utekelezajiwa bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira mwaka2018/2019, pamoja na mapendekezo na mapato ya mwakawa fedha 2019/2020 ya ofisi hii, Kamati imekuwa na maonina ushauri kadhaa kwa Serikali. Ni imani ya Kamati kuwa,maoni na ushauri huu yatafanyiwa kazi hivyo kupelekeakuboresha shughuli za uhifadhi na usimamizi wa mazingiranchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa miaka kadhaatumeshuhudia Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingiraimeendelea kutengewa bajeti ndogo ukilinganisha naukubwa wa jukumu walilonalo la uhifadhi wa Mazingira. Kunavyanzo mbalimbali vya mapato ambavyo vinatokana namazingira lakini vyanzo hivi vinaingia katika mfuko ambaohaurudishi katika shughuli za hifadhi ya mazingira.

Page 163: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ilifahamishwa naOfisi ya Makamu wa Rais, Mazingira kuwa vyanzo hivivimeshaainishwa na kuwasilishwa katika Baraza la Mawaziri.Kamati inaisisitiza Serikali kuhakikisha katika mwaka wa fedha2019/2020, kwa kuanzia na angalau na vyanzo vitano tuvichangie katika Mfuko wa Mazingira kwa asilimia tano.Hatua hii itasaidia kupunguza utegemezi wa ruzuku ya Serikalikatika kutekeleza majukumu ya usimamizi wa mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati inaishauri Serikalikuwa, baada ya kupitisha vyanzo hivi vya mapato ya Mfuko,ifanye maboresho katika Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004Sura ya 191 ili iwezeshe kutambua na kusimamia utekelezajiwa sekta zote zinazotakiwa kuchangiwa na mfuko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Mazingiraimemtambua na kumpa majukumu makubwa AfisaMazingira. Pamoja na kuwa Afisa Mazingira anapewamajukumu na Sheria ya Mazingira na analengwa kumsaidiaMkurugenzi wa Mazingira, lakini ni mwajiriwa wa Halmashaurina anaripoti kwa Mkurugenzi wa Halmashauri. Aidha, taarifaya kazi anazozifanya Afisa wa Mazingira ili zimfikie Mkurugenziwa Mazingira ni lazima zipitie TAMISEMI.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, kwa namna yapekee, napenda kuwashukuru Wajumbe wote wa Kamati yaBunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ambaowamewezesha kutoa maoni, michango na mawazo yaombalimbali katika kukamilisha taarifa hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchukua nafasi hiikumpongeza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Rais, Muunganona Mazingira, Mheshimiwa January Makamba; Naibu Waziriwa Wizara hiyo, Mheshimiwa Mussa Ramadhan Sima, ,Makatibu Wakuu na Watendaji wote wa Wizara kwa kutoaufafanuzi mzuri wakati wa uchambuzi wa bajeti hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kumshukuruMheshimiwa Naibu Spika kwa kutoa maelekezo mbalimbaliambayo wakati wote yamefanikisha kazi za Kamati hii. Aidha,

Page 164: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

napenda kukushukuru wewe mwenyewe kwa kutupa nafasiya kutoa taarifa hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Katibu waBunge Ndugu Stephen Kagaigai, Mkurugenzi wa Idara yaKamati za Bunge Athumani Hussein, Mkurugenzi Msaidizi waSehemu ya Fedha na Uchumi Bwana Michael Chikokoto,Makatibu wa Kamati Bi. Zainab Mkamba na Bi. MwajumaRamadhani pamoja na Msaidizi wa Kamati Bi. PaulinaMavunde kwa kuratibu shughuli za Kamati hadi taarifa hiikukamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya,sasa naliomba Bunge lako Tukufu likubali kuidhinishaMakadirio na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, MazingiraFungu 31 kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ambayo ni kiasicha shilingi 22,708,713,882.00 kwa ajili ya kutekeleza shughuliza hifadhi na usimamizi wa mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha nanaunga mkono hoja. (Makofi)

TAARIFA YA KAMATI KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YAVIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA KUHUSU UTEKELEZAJIWA MAJUKUMU YA UHIFADHI NA USIMAMIZI WA AZINGIRACHINI YA OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MAZINGIRA) FUNGU

31 KWA MWAKA 2018/2019 PAMOJA NA MAONI KUHUSUMAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA

MWAKA 2019/2020 - KAMA ILIVYOWASILISHWA MEZANI______________

1.0 UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 99(9) ya Kanuniza Bunge, Toleo la Januari, 2016, naomba kuwasilisha Taarifaya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara naMazingira kuhusu utekelezaji wa majukumu ya hifadhi nausimamizi wa Mazingira chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira) Fungu 31 kwa Mwaka 2018/2019na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mwaka 2019/2020.

Page 165: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

Mheshimiwa Spika, Kamati ilizingatia matakwa ya Kanuni ya98(1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge ambapo ilifanya ziarakatika baadhi ya miradi ya maendeleo iliyotengewa fedhakatika mwaka wa fedha 2018/2019, kwa lengo la kujioneahali halisi ya utekelezaji wa miradi hiyo. Vilevile, Kamatiilipokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi yaMakamu wa Rais Mazingira kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019pamoja na kuchambua Mpango na Bajeti kwa MwakaFedha wa 2019/2020 kama inavyoelekeza na Kanuni ya 98(2) ikisomwa pamoja na kifungu cha 7(1)(a) cha Nyongezaya Nane ya Kanuni za kudumu za Bunge.

Mheshimiwa Spika, taarifa hii inalenga kuliomba Bunge lakotukufu kuidhinisha maombi ya Fedha kwa ajili ya Ofisi yaMakamu wa Rais - Mazingira, lakini pia kutoa mapendekezokwa Bunge kuhusu masuala kadhaa ambayo Kamati inaaminini muhimu yakafanyiwa kazi yatasidia kuboresha shughuli zahifadhi na usimamizi wa Mazingira.

2.0 UCHAMBUZI WA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MPANGONA BAJETI YA MWAKA 2018/2019 NA MATOKEO YAUKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO ILIYOTENGEWAFEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019

2.1 Utekelezaji wa Mpango wa Bajeti kwa mwaka wafedha 2018/2019

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza masharti ya Kanuni ya98(2) ya Kanuni za Bunge, Toleo la Januari, 2016, Kamatiilichambua Taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Bajeti yaOfisi ya Makamu wa Rais – Mazingira kwa Mwaka wa Fedha2018/2019. Katika uchambuzi huo, Kamati ilitumia mapitio yataarifa zilizowasilishwa, matokeo ya ziara za ukaguzi wa Miradiya Mazingira pamoja na mahojiano wakati wa vikao. Lengola njia hizo lilikuwa ni kujiridhisha kuhusu ukusanyaji wamapato, utekelezaji wa malengo/kazi na upatikanaji wafedha ikilinganishwa na kiasi kilichoidhinishwa na Bunge.

Page 166: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

2.1.1 Makusanyo ya MapatoMheshimiwa Spika, tarehe 17 Aprili, 2018 Bunge lako tukufulilijulishwa kuwa, katika Mwaka wa Fedha 2018/2019 Barazala Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira – NEMC lilipangakukusanya Shilingi 18,877,446,995 kutoka vyanzo vya ndanivya Baraza. Lengo hili la Makusanyo lilikuwa limezidi lengo laMwaka wa Fedha 2017/2018 kwa asilimia 20.4.

Uchambuzi wa Kamati umebainisha kuwa hadi kufikia tarehe14 Machi, 2019, NEMC il ikuwa imekusanya Shil ingi10,430,060,727 kiasi ambacho ni pungufu ya lengo kwaasilimia 44.8 ya kiasi kilichopangwa kukusanywa kwa mwakahuu wa fedha. Takwimu hizo zinaonesha kuwa katika robomoja ya kipindi cha utekelezaji, NEMC itakusanya asilimia 44.8ya lengo la makusanyo jambo ambalo si la kawaida/uhalisia.Aidha, Takwimu hizi zinaashiria kuwa;-

i) Lengo hili lilipangwa bila kuzingatia uhalisia wa uwezowa NEMC wa kukusanya;

ii) Upungufu huu unaashiria kukwama kwa utekelezajiwa baadhi ya majukumu ya NEMC kwa Mwaka wa Fedha2018/2019;

Mheshimiwa Spika, kutokana na uwezekano mdogo wakukusanya asilimia 44.8 iliyobaki kwa Mwaka unaoishia wafedha, Kamati imeishauri NEMC kupanga lengo la makusanyokwa kuzingatia uwezo wake wa kukusanya.

2.1.2 Upatikanaji wa fedha kutoka Hazina

Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019, Ofisiya Makamu wa Rais – Mazingira iliidhinishiwa jumla ya Shilingi8,118,494,000.00 kwa ajili ya matumizi ya Hifadhi na Usimamiziwa Mazingira. Hadi kufikia tarehe 14 Machi, 2019 Ofisi hiiilikuwa imepokea shilingi 4,167,969,635.79 tu, sawa na asilimia51.3 ya fedha zote zilizokuwa zimeidinishwa na Bunge.

Uchambuzi wa Kamati umebaini kuwa kiasi kilichopokelewapungufu kwa asilimia 48.7. Kwa kipindi hiki cha robo ya nne

Page 167: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

ya Mwaka wa Fedha 2018/2019 ilitarajiwa zaidi ya asilimia 75ya fedha zilizoidhinishwa na Bunge ziwe zimepokelewa tofautina ilivyo sasa ambapo ni asilimia 51.3 tu ndio ilikuwaimepokelewa.

Aidha, uchambuzi wa Kamati ulibaini kuwa kati ya shilingi3,524,540,000.00 ya fedha za Miradi ya Maendeleo ni shilingi1,861,299,489.50 tu ndizo zilikuwa zimepokelewa kwa ajili yautekelezaji wa Miradi ya Maendeleo, kiasi hicho ni fedha zanje.Vilevile, Kamati ilibaini kuwa katika fedha za maendeleokulikuwa na fedha za ndani ambazo ni shilingi 1,461,200,000.00lakini hadi kufikia robo ya tatu ya Mwaka wa Fedha 2018/2019 zilikuwa hazijapokelewa kabisa.

Mheshimiwa Spika, Uchambuzi huu unadhihirisha kuwabaadhi ya majukumu ya usimamizi wa mazingirayameshindwa kutekelezwa ipasavyo hususani miradi yamaendeleo.

Mheshimiwa Spika, mwenendo wa upatikanaji wa fedha kwaajili ya shughuli za hifadhi ya mazingira si wa kuridhisha kwaupande wa fedha za miradi ya maendeleo hususani fedhaza ndani. Kamati inaishauri Serikali kuweka mikakati namsisitizo katika kuwezesha shughuli za usimamizi wa mazingirakwa kutenga fedha za kutosha zikiwepo fedha za ndani nakuzipeleka kwa wakati.

2.1.3 Utekelezaji wa kazi zilizopangwa kwa mwaka2018/2019

Mheshimiwa Spika, ili kuiwezesha Kamati kujiridhisha nadhamira ya Bunge kuiidhinisha Bajeti kwa ajili ya Shughuli zaUsimamizi na Hifadhi ya Mazingira, Kamati ilijulishwa kuhusuutekelezaji wa kazi zilizopangwa kutekelezwa kwa mwakawa fedha 2018/2019. Jumla ya kazi Kumi na Sita (16)zilipangwa kutekelezwa na taarifa ya Waziri ilibainisha hatuailiyofikiwa katika utekelezaji huo.

Page 168: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

Nafurahi kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa kwa mwaka wafedha 2018/2019, kazi zilizopangwa kuhusiana na Hifadhi nausimamizi wa mazingira zilitekelezwa. Hata hivyo, Kamatiinaendela kuisisitiza Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingirakuongeza juhudi katika majukumu yafuatayo;-

i) Kukamilisha mchakato wa mapitio ya Sera ya Taifaya Mazingira 1997 na mkakati wa utekelezaji wake kwa lengola kuihuisha iweze kuendana na mazingira halisi ya sasa yamazingira (ihusishe mabadiliko yote yaliyotokea katikamazingira ambayo hayakuwepo miaka ya 1997) ili iwezekuboresha usimamizi wa shughuli za mazingira;

ii) Kukamilisha maandalizi ya Mkakati wa Taifa wakudhibiti Viumbe vamizi (Inversive Alien Species) kwa lengola kuokoa maisha ya binadamu, mazingira na bioanuai zotena athari za viumbe vamizi ambazo miaka ya hivi karibunizimeendelea kushamiri;

iii) Kukamilisha Ripoti ya Tatu ya Hali ya Mazingira Nchinina kuiwasilisha Bungeni kama inavyoelekezwa na Sheria yaUsimamizi wa Mazingira Mwaka 2004. Sheria ya Mazingirainaelekeza kuwa Ripoti ya Hali ya Mazingira Nchini iwasilishweBungeni kila baada ya miaka miwili lakini kwa kipindi kirefusasa haijawasilishwa;

iv) Kukamilisha mchakato wa kuokoa Ikolojia ya Bondela Mto Ruaha Mkuu kwa lengo la kulinusuru kwa kuwa lipohatarini kupotea kutokana na shughuli mbalimbali zakibinadamu zinazoendeshwa katika eneo la bonde bilakuzingatia taratibu na sheria;

v) Kuendelea kulisimamia Baraza la Taifa la Hifadhi naUsimamizi wa Mazingira – NEMC kuhakikisha wanaongeza kasiya ukaguzi wa uzingatiaji wa Sheria ya Usimamizi waMazingira, Sura 191 na kanuni zake kwa lengo la kudhibiti nakupunguza kasi ya uharibifu wa mazingira;

vi) Kuongeza jitihada katika kutekeleza kampeni zaUpandaji miti hususani katika maeneo ambayo yameathirika

Page 169: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

sana na ukame, sambamba na hili Ofisi ya Makamu wa Rais– Mazingira iweke utaratibu wa ufuatiliaji wa miti iliyopandakatika kampeni mbalimbali za upandaji miti na zawadizitolewe kwa maeneo ambayo kampeni hizo zimefanikiwa(wahusika wameitunza mpaka kukua); na

vii) Kundelea kusimamia utekelezaji wa masharti yamikataba mbalimbali ya kimataifa ambayo Ofisi hii imeridhiakwa niaba ya nchi, kwa kuwa mikataba hii imekuwa yamanufaa sana kwa Tanzania na kwa kiasi kikubwa kwaniinasaidia kupata fedha za kupambana na athari za uharibifuwa mazingira.

2.2 Maoni ya Jumla kuhusu utekelezaji wa Bajeti

Mheshimiwa Spika, matokeo ya uchambuzi wa taarifa yautekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingirakuhusu hifadhi na Usimamizi wa Mazingira yanaonesha kuwaUpatikanaji wa fedha za uendeshaji wa shughuli za Idara yaMazingira (fedha za matumizi ya kawaida) umekuwa mzuriukil inganisha na upatikanaji wa fedha za Miradi yaMaendeleo hususani fedha za ndani ambapo hadi kufikiatarehe 14 Machi, 2019, kati ya fedha zote za Miradi yaMaendeleo ni fedha za nje tu ndizo zilikuwa zimepokelewajambo ambalo halitoi picha nzuri kwa wahisani wetu.

2.3 Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo2.3.1 Mapitio ya Taarifa za utekelezaji wa Miradi ya

Maendeleo

Mheshimiwa Spika, Kanuni ya 98(1) ya Kanuni za Kudumu zaBunge inazitaka Kamati za Sekta, kutumia siku zisizozidi sabakwa kutembelea na kukagua miradi ya Maendeleo. Kamatiya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, ilifanya ziarakatika baadhi ya miradi ya maendeleo ya Uhifadhi naUsimamizi wa Mazingira kwa lengo la kujionea hali halisi yautekelezaji wa miradi hiyo.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2018/2019 Ofisiya Makamu wa Raisi - Mazingira Fungu 31, iliidhinishiwa shilingi

Page 170: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

3,524,540,000.00 kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleokati ya fedha hizo Shilingi 1,461,200,000.00 ni Fedha za ndanina Shilingi 2,063,340,000.00 fedha za nje.

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipata fursa ya kutembelea Mradiwa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi - Bagamoyo (MradiNamba 5301), Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za NEMC (MradiNamba 6507) na shughuli za Uhifadhi mazingira katika ZiwaManyara, maelezo ya utekelezaji wa miradi hiyo ni kamayanavyoonekana katika taarifa hii.

a) Mradi wa Mabadaliko ya Tabianchi Bagamoyo (MradiNamba 5301)Mheshimiwa Spika, tarehe 18 Machi, 2019 Kamati ilitembeleaMradi Namba 5301 wa kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwaeneo la Bagamoyo. Lengo la Kamati kutembelea Mradi huuni kubaini namna Mabadiliko ya tabianchi yameathirimazingira yetu na kwa namna Serikali inakabiliana na atharizake.

Mheshimiwa Spika, mabadiliko ya tabianchi ni jambo dhahirina athari zake zimeendelea kuonekena katika maeneombalimbali Duniani. Ongezeko la usawa wa bahari (sea levelrise) kwa sentemita 19 katika kipindi cha miaka 50 iliyopita nimoja za athari za mabadiliko ya Tabiachi. Kwa Tanzaniaongezeko la usawa wa bahari limechangia uharibifu wamwambao wa Pwani hususani katika maeneo ya KisiwaPanza Zanzibar, Mto Pangani, Fungu la Nyani Rufuji, na baadhiya visima vya maji baridi katika maeneo ya Bagamoyokuharibiwa na maji chumvi. Katika kutambua hilo, Ofisi yaMakamu wa Rais-Mazingira inatekeleza Miradi mbalimbaliikiwemo Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi(Mradi namba 5301).

Mheshimiwa Spika, kama nilivyokwisha eleza kuwa athari yaMabadiliko ya Tabianchi katika Pwani ya Bagamoyo imeathirivisima vya asili baada ya kina cha maji ya bahari kuongezekana kufikia usawa wa meza ya maji (water table) na kupelekeamaji hayo ya bahari kuingia katika visima vya asili na kuletamadhara kwa watumiaji wa maji ya visima hivyo. Kwa

Page 171: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171

Bagamoyo mradi huu umehusisha ujenzi wa visima vikubwavya maji masafi na ujenzi wa miundombinu ya uvunaji majiya mvua.

Mradi unatekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingirachini ya ufadhili wa Least Development Countries Fund-LDCFna umegharimu takriban jumla ya Shilingi 1,171,668,189/=

Mheshimiwa Spika, wakati wa ziara ya Kamati Mradi ulikuwaumekamilika na kazi zifuatazo zilikuwa zimetekelezwa:-

i) Ujenzi wa miundombinu ya uvunaji maji ya mvua katika shuleya Sekondari ya Kingani Matipwili;

ii) Uchimbaji wa visima na ujenzi wa matanki kumi (10) katikamaeneo ya Ukanda wa Pwani wa Bagamoyo; na

iii) Mafunzo ya ufahamu wa kuhimili mabadiliko ya tabianchina athari zake kwa wakazi wa Ukanda wa Pwani waBagamoyo.

Mheshimiwa Spika, changamoto kubwa katika utekelezaji waMradi ilikuwa ni ufinyu wa Bajeti, jambo lililopelekea malengoya kuchimba visima 17 na miundombinu mitatu (3) ya kuvunamaji ya mvua kutofikiwa na badala yake kuchimba visima10 na miundombinu ya kuvuna maji ya mvua miwili (2) tu. PiaMradi ulikabiliwa na Mvua nyingi za masika zilizopelekeabaadhi ya maeneo ya miradi kushindwa kufikika nakupelekea kuchelewa kukamilika. Vilevile, kuwepo nachangamoto ya nguvu ndogo ya umeme (Low voltage) waTANESCO katika maeneo matatu ya visima hali iliyopelekeamiradi ya eneo hilo kuchelewa kukamilika.

Mheshimiwa Spika, maoni na Ushauri wa Kamati kuhusuutekelezaji wa Mradi Namba 5301, Fungu 31 unaohusuMabadiliko ya Tabianchi Wilayani Bagamoyo ni;-

i) Serikali itumie mradi huu kama mfano, na kwa kupitiaWizara ya Maji na Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Serikaliijipange kutafuta miradi mingine mingi ya aina hii ili kupunguza

Page 172: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

172

changamoto ya maji, lakini pia kuwaokoa wananchikuendelea kutumia maji yasiyo salama; (kwa sasa mradiumetekelezwa katika maeneo machache tu wakati atharimabadiliko ya tabianchi imeharibu visima vingi vya asili nakusababisha upungufu wa maji kwa wakazi wa eneo lote laUkanda wa Pwani ya Bagamoyo.)

ii) Kamati za maji ziangalie namna ya kuyatibu (treat)maji ya mvua yanayovunwa na kuhifadhiwa katika matankikwa muda mrefu, kwa lengo la kulinda afya za watumiaji.Kama inavyofahamika maji ya mvua baada ya muda mfupihuota ukungu na kuzalisha vijidudu;

iii) Kwa maeneo ambayo mradi unatekelezwa,wananchi wapatiwe elimu ya kutosha juu ya mradi huoikihusianishwa na mabadiliko ya Tabianchi na waelimishwejinsi ya kutunza mradi huo ili uweze kuwa mradi endelevu;

iv) Kwa mradi ya namna hii ambayo inatekelezwa katikahalmashauri zetu ni vema tukatumia wahandisi wahalmashauri kwa lengo la kupunguza gharama, kutokana naukweli kwamba fedha zinazotumika kumlipa mhandisi mshaurini nyingi na kupelekea kuongezeka kwa gharama za mradi;na

v) Kamati ya Maji ya vijiji husika kuangalia namna nzuriya kuendesha mradi ili wananchi wapate maji kwa gharamanafuu na vilevile kupunguza urasimu wa upatikanaji wa maji.

b) Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za NEMC (Mradi Namba6507);

Mheshimiwa Spika, Kamati ilitembelea Mradi Namba 6507ujulikanao kama Ujenzi wa Ofisi ya Baraza la Taifa la Uhifadhina Usimamizi wa Mazingira – NEMC. Mradi wa Ujenzi wa Ofisiza NEMC ulianzishwa kwa lengo la kupunguza gharama yaBaraza itokanayo na kodi ya pango.

Tangu kuundwa kwa Baraza mwaka 1983 halikuwahikupatiwa ofisi za Serikali na ilikuwa ikipanga katika majengo

Page 173: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

173

mbalimbali, juhudi za NEMC kupatiwa ofisi za Serikalizilishindikana na mnamo mwaka 2009 Katibu Mkuu Kiongozialiiagiza Bodi ya NEMC kutafuta ofisi za kudumu na ndipoBaraza lilipochukua uamuzi wa kununua kiwanja na kujengajengo lake katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Ujenzi wa mradi huo ulipewa Namba 6507, mradiumetekelezwa kupitia ruzuku kutoka Serikalini pamoja namakusanyo ya ndani Baraza. Mradi umehusisha ununuzi waviwanja vinne (vitatu Dar es salaam Mikocheni na kimojaDodoma) pamoja na ujenzi wa jengo la ghorofa mbili katikaviwanja vya Mikocheni- Dar es Salaam. Mradi umegharimujumla ya shil ingi 5,564,364,893.00 ambazo shil ingi1,650,000,000.00 ni ruzuku kutoka Serikalini na shilingi3,253,464,893.00 ni fedha za ndani za Baraza na 660,900,000.00ni Msaada kutoka Benki ya Dunia.

Mchanganuo wa fedha za Mradi ni shilingi 660,900,000.00 kwaajili ya Ujenzi wa jengo, shilingi 4,903,464,893.00 kwa ajili yaviwanja vinne ambapo viwanja vitatu vipo Dar es SalaamMikocheni na kiwanja kimoja kipo Dodoma.

Hali ya Mradi wakati wa Ziara ya Kamati;-

Wakati wa ziara ya Kamati ilikuta mradi umekamilika ambapo

i) Jengo la ghorofa mbili likukuwa limejengwa;

ii) Mashine za kisasa kwa aji l i ya utafiti zi l ikuwazikiendelea kufungwa katika jengo hilo; na

iii) Baadhi ya watumishi walikuwa wameanza kuhamiakatika jengo jipya kitendo kilichopunguza msongamanouliokuwepo katika majengo yaliyokuwa yakitumika awali.

Mheshimiwa Spika, Changamoto katika utekelezaji wa Mradihuu ilikuwa ni mabadiliko ya mpango wa awali wa ujenzi wajengo ambalo lililengwa kutumika upande mmoja kwa ajiliya ofisi na upande mwingine kwa ajili ya Biashara. Mabadilikohaya yalipelekea kuchelewesha utekelezaji wa mradi sababu

Page 174: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

174

Baraza lililazimika kuanza upya mchakato wa upatikanaji wamchoro wa jengo jipya;

Mheshimiwa Spika, Kamati pia ilifahamishwa changamotoza Baraza katika utekelezaji wa Majukumu ya Baraza ambapomoja ya changamoto kubwa ni upungufu wa watumishiambao ni wataalamu wa masuala ya mazingira jambolinalopelekea kushindwa kutekeleza jukumu la ukaguzi wamasuala ya mazingira kwa ufanisi. Makadirio ya Baraza iliwaweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi wanahitajiangala wafanyakazi 2000 na lakini kwa sasa wanawafanakazi 250. Kamati iliielekeza Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira kuongeza kazi ya ufwatiliaji wa maombi ya vibaliwaliyoyapeleka Utumishi, kwa kuwa Baraza limepewamajukumu makubwa sana na Sheria ya Mazingira lakini bilakuwa na watumishi wa kutosha hawataweza tekelezamajukumu hayo kwa ufanisi.

Mheshimiwa Spika, Kamati imepongeza Serekali na Barazakwa kutekeleza wa mradi huu, kwa kuwa jengo hili limeipaBaraza sehemu ya kufanyia kazi lakini pia imelipa Barazahadhi inayostahili. Hapo awali Ofisi za Baraza hazikuwa nahadhi ya ofisi, walikuwa wanatumia nyumba walizozikutawakati wananunua viwanja na kupelekea baadhi ya ofisikuwa katika stoo ya nyumba hizo. Hatua hii ilikuwa ikipelekeabaadhi ya wawekezaji hususani kutoka nje ya nchi kukosaimani na huduma za Baraza.Aidha, kwa kuwa Serikali imejipanga kuhamia Dodoma naimezielekeza Taasisi zake kuhamia Dodoma pia, Kamatiinaishauri Serikali kuziwezesha taasisi hizi kifedha ili ziwezekujenga ofisi zake kama ilivyofanya kwa Wizara. Hatua hiiitaondoa gharama za kodi.

c) Shughuli za Uhifadhi mazingira katika Ziwa Manyara;

Kamati ilipata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Ziwa Manyarakwa Lengo la kujionea Hali ya Mazingira katika eneo la hifadhiambayo inahusisha na ziwa manyara, changamoto namkakati wa Serikali katika kukabiliana na athari za kimazingirakatika eneo hilo la hifadhi.

Page 175: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

175

Shughuli za Uhifadhi wa Mazingira katika Ziwa Manyarazinatekelezwa na TANAPA na zinahusisha Kutoa elimu yamazingira na sheria ya usimamizi wa mazingira katika ngaziya wilaya na Halmashauri za Mkoa wa Manyara; Kufanyaufuatiliaji wa wachimbaji wadogo na wakubwa ili wawezekufanya uchimbaji kwa kufuata taratibu na sheria zilizopo;na Kutengeneza mabwawa (makingia maji) kuzunguka eneola ziwa ya kupokea maji ya mvua yanayotoka katika maeneoya miinuko kwa lengo la kuchuja tope, kwa lengo lakupunguza uingiaji wa tope katika ziwa;

Shughuli za uhifadhi wa Mazingira katika Ziwa Manyarazinakumbana na Changamoto zifuatazo;-

i) Ukosefu wa fedha za kwa ajili ya kutekeleza shughuliza uhifadhi na usimamizi wa mazingira katika eneo la Hifadhi,jambo linalopelekea athari za uharibifu unaofanywakuendelea na kupelekea kuhatarisha eneo la hifadhi hususaniziwa Manyara;-

ii) Shughuli za binadamu (kilimo kisichofuata kanuni zakitaalamu, uwepo wa mifugo mingi) katika maeneo ya karibuna Ziwa Manyara zinazopelekea mmomony’oko wa udongona kupelekea tope jingi kuelekea ziwani na kupunguza kinacha maji kupelekea kukauka kwa ziwa. Takwimu zinasemakatika kipindi cha miaka 35 ya karibuni (1980-2015) hali imezidikuwa mbaya ambapo matukio ya kukauka Ziwa yalikuwa 7wakati kati ya mwaka (1920-1970) ziwa liliripotiwa kukaukamara tatu tu;

iii) Mabadiliko ya Tabianchi ambayo hupelekea ukamena kukauka kwa vyanzo vya maji yatiririkayo kwenda ziwanina kupelekea kukauka kwa ziwa manyara;

iv) Shughuli za kibinadamu katika eneo la hifadhizisizolenga matumizi endelevu ya rasilimali za asili jambolinalopelekea kuharibu mfumo Ikolojia ya Tarangire na ZiwaManyara na kuviweka katika hatari ya kutoweka. Piakuharibika maeneo ya shoroba na maeneo ya mtawanyikowa wanyamapori; na

Page 176: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

176

v) Mimea vamizi/wageni katika baadhi ya vyanzo vyamaji vya ziwa manyara ambavyo hupelekea maji kushindwakufika ziwani; hali hii pia hupunguza vyanzo na upatikanajiwa maji kwa ajili ya mazingira, wanyamapori na mahitaji yajamii zinazozunguka hifadhi (mfano wa mimeo hiyo niMikaratusi, Misanduku).

Mheshimiwa Spika, baada ya ziara katika Ziwa ManyaraKamati ilikuwa na maoni na ushauri ufuatao;-i) Kwa kuwa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004inampa mamlaka Waziri mwenye dhamana ya kusimamiamazingira kuliingiza katika orodha ya maeneo Lindwa eneololote linaloonekana lipo katika hatihati za kutowekea. Serikaliifanye haraka kuanza mchakato wa kuliingiza ziwa manyarakatika maeneo Lindwa kwa lengo la kuliweka katika usimamizimaalumu na kulitoa katika hatari ya kupotea. Hatua hiiichukuliwe kwa maziwa yote ambayo yapo katika hatari yanamna hii likiwepo ziwa Jipe na Chala

ii) Serikali kuangalia namna ya kuwasaidia nakuwasimamia wakulima na wafugaji kufanya shughuli zaombali na miinuko. Shughuli hizi zimekuwa zikiporomoshaudongo na tope katika Ziwa Manyara na hivyo kupekekeakupungua kwa kina cha ziwa na kuliondolea uwezo wakutunza maji kwa muda mrefu.

iii) Ziwa Manyara na Bioanuai zipatikanazo katika ziwahili ni moja ya kivutio kikubwa kinachovuta utalii katika Hifadhiya Manyara, changamoto zinazopelekea kukauka kwa ziwaManyara kunahatarisha na kupelekea kungua kwa shughuliza utalii katika Hifadhi ya Manyara. Serikali ichukue jitihadaza makusudi kuhakikisha wanalinusuru Ziwa Manyara naBioanuai zote zinazopatikana katika ziwa hili;

vi) Kuna udhaifu katika kusimamia Sheria za Mazingirana Sheria ndogondogo za Vijiji na Halmashauri jambolinalotoa mianya kwa baadhi ya watu kuendelea shughulizao katika eneo la hifadhi; Kamati inaishauri Serikali kuongezakasi ya kufutilia na kusimamia matakwa ya sheria ili kuzuiashughuli zisizo endelevu katika eneo la hifadhi.

Page 177: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

177

2.3.2 Maoni ya Jumla kuhusu utekelezaji wa Miradi yaMaendeleo kwa mwaka wa Fedha 2018/2019

Mheshimiwa Spika, baada ya kukamilisha ziara za ukaguziwa miradi ya maendeleo, Kamati ilishauri mambo yafuatayo:-

i) Serikali kulipa uzito suala la hifadhi ya Mazingira kwakutenga fedha za maendeleo na kuzipeleka kwa wakati, kwasasa asilimia kubwa ya Miradi ya Maendeleo ya Mazingirainatekelezwa kwa kutumia fedha za wafadhili jambo ambalosi sahihi sana. Kwa mfano katika Mwaka wa Fedha 2018/2019hadi kufikia robo ya tatu ya Mwaka, fedha za ndani kwa ajiliya Miradi ya Maendeleo zilikuwa hazijatolewa kabisa.

ii) Sekta asili (kilimo, ufugaji na uvuvi) kwa kiasi kikubwandio zinategemewa katika uchumi wa nchi yetu, namaendeleo ya sekta hizi kwa kiasi kikubwa yanategemeauhifadhi wa mazingira, jambo la kushangaza shughuli hizi hizizimekuwa zikiendeshwa bila kuzingatia taratibu za kitaalamu.Kamati inashauri Serikali kuongeza kasi ya kuielimisha jamiikuhusu umuhimu wa kutunza Mazingira, pia kuwa na matumiziendelevu ya rasilimali za asili hususani misitu na vyanzo vyamaji;

iii) Sheria ya Mazingira inayotekelezwa sasa ni ya Mwaka2004 lakini inatekelezwa kwa kuzingatia Sera ya Taifa yaMazingira ya Mwaka 1997. Sera hii ni ya zamani takribanimiaka 22, na haijahusisha mabadiliko mengi ambayoyameendelea kutokea katika mazingira mfano mabadilikoya Tabia nchi na viumbe vamizi. Kamati inasishauri Serikalikukamilisha mchakato wa kuandaa Sera mpyaitakayoendana na mazingira ya sasa.

3.0 UZINGATIAJI WA USHAURI WA KAMATI KUHUSU BAJETIYA OFISI YA MAKAMU WA RAIS - MAZINGIRA MWAKAWA FEDHA 2018/2019.

Mheshimiwa Spika, wakati wa kupitia na kuchambua taarifaya utekelezaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira kwamwaka wa fedha 2018/2019 Kamati ilitoa ushauri kwenye

Page 178: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

178

maeneo mbalimbali na kutoa maagizo Kumi na Mbili (12).Naomba kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa Serikali imejitahidikuzingatia ushauri wa Kamati na kutekeleza maagizo hayo,hata hivyo kuna maeneo ambayo serikali haikuyatekelezaipasavyo kama inavyoainishwa kwenye taarifa hii;-

i) Serikali ifanye Tathimini ya Athari kwa Mazingira- EIAkatika maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya wachimajiwadogo wa madini kabla ya kuwakabidhi ili kuepusha athariza kimazingira zinazoweza kujitokeza. Maelezo ya Serikalikuhusu utekelzaji wa agizo hili ni kuwa Ofisi ya Makamu waRais- Mazingira kwa kushirikiana na NEMC wanaendeleokusimamia Sheria ya Mazingira na kuhakikisha kila mradiunaotaka kutekelezwa unafanyiwa EIA na unafuata mashartiya EIA. Maelezo haya hayaendani na agizo la Kamati, Kamatiinaendelea kusisitiza Serikali juu utekelezaji wa agizo hili kwalengo la kuepusha athari za kimazingira zinazoweza kujitokezakatika maeneo ya wachimbaji wadogo (wachimbajiwadogo hawana uwezo wa kufanya EIA ni vema Serikaliikafanya ukaguzi huo)

ii) Serikali iendelee kutoa elimu kwa jamii kukusu athariza kuharibu vyanzo vya maji ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu,na kuliingiza bonde hilo katika orodha ya maeneo lindwakwa kutumia Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004. Kamatiinaendelea kusisitiza kuhusu utekelezaji wa agizo hili hususanikatika kipengele cha kuliingiza Bonde lote la Mto Ruaha Mkuukatika orodha ya maeneo lindwa kwa sasa kipandekilichopita katika hifadhi tu ndio kinalindwa sehemu iliyobakihaijahifadhiwa. Sheria ya Mazingira inampa Waziri mwenyedhamana ya Mazingira mamlaka ya kuliingiza eneo lolotekatika orodha ya maeneo lindwa pale eneo hilolinapoonekena kuwa katika hatihati ya kupotea. Kutokanana changamoto zilizopo katika maeneo ya bonde hili, Kamatiinaishauri Serikali kutumia Sheria hii na kuliweka bonde lotekatika maeneo lindwa lakini pia kuunda chombo chausimamizi wa bonde ambacho ni Mamlaka ya Hifadhi yaBonde la Mto Ruaha Mkuu. Hatua hii itasaidia kulinda bondeletu lakini pia itatoa uhakika wa maji katika Mradi Mkubwawa Umeme unaoenda kutekelezwa (Stigler’s Gorge).

Page 179: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

179

iii) Serikali ihakikishe kuwa katika Mwaka wa Fedha 2018/2019 Mfuko wa Mazingira unawezeshwa na kuanza kufanyakazi kikamilifu. Maelezo ya Serikali kuhusu utekelezaji wa agizohili hayaridhishi, Kamati inatambua kuwa changamotokubwa ya Mfuko wa si marekebisho ya Sheria pekee bali kunachangamoto ya vyanzo vya mapato ya mfuko pia. Kwa kuwamchakato wa maboresho ya sheria unaendelea. Kamatiinaishauri Serikali kutatua nah ii changamoto ya vyanzo vyamapato kwa kupitisha vyanzo vyote vya Mapato yatokanayona shughuliza uchafuzi wa mazingira kuchangia walau kwaasilimia tano katika mfuko wa Mazingira kwa lengo lakuuwezesha mfuko kutekeleza majukumu yaliyokusudiwa.

iv) Machinjio yahamishwe kutoka kwenye makazi yawatu na ukaguzi wa mara kwa mara ufanyike ili kuhakikishawanaoziendesha wanafuata Sheria inayosimamia machinjiohayo na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira kwa ajili ya kulindaafya za walaji. Kamati inaendeleo kusisitiza juu ya utekelezajiwa agizo hili na kuongeza kasi ya ukaguzi kwani kuna baadhiya maeneo bado mazingira za machinjio si yakuridhisha.

4.0 UCHAMBUZI WA MPANGO WA MAKADIRIO YA MAPATONA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020

4.1 Uchambuzi wa malengo/mpango

Mheshimiwa Spika, kabla ya kuchambua makadirio yaMapato na Matumizi katika jukumu la kuhifadhi na kusimamiamazingira, Kamati ilipitia maelezo ya Waziri kuhusu kazizilizopangwa kutekelezwa kwa mwaka wa fedha 2019/2020.Lengo lilikuwa ni kufatilia tija inayoweza kupatikana kutokanana malengo yaliyopangwa na Ofisi hii kwa fedhazinazoombwa katika kifungu 5003. Kamati ililinganishamalengo ya Mwaka wa Fedha 2018/2019 na 2019/2020 nakatika ulinganisho huo kamati ilibaini yafuatayo:-

i. Malengo yote yalizingatia hati idhini ya serikaliiliyoainisha majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais- mazingira.

Page 180: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

180

ii. Lengo namba mbili (ii) kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na lengo namba kumi na mbili (xii) kwa mwaka wa fedha2019/2020 yanaendana na kwamba yote yanajielekezakwenye udhibiti wa utupaji wa taka ngumu na hatarishi.

iii. Lengo linalohusu udhibiti wa taka ngumu kwa mwakawa fedha 2019/2020 ni muendelezo wa uzingatiaji wa ushauriuliowahi kutolewa na Kamati hii kwa mwaka wa fedha 2017/2018. Aidha, agizo la Waziri Mkuu alipokuwa akihitimisha hojayake bungeni tarehe 9/4/2019, Linatoa nguvu na msisitizokama ilivyotolewa na Kamati 2017/2018.

Mheshimiwa Spika, kwa uchambuzi huo Kamati inaipongezaSerikali kwa kupokea ushauri uliotolewa na Kamati na kutoamuda wa kutosha kwa wawekezaji hao, kuanzia Agosti, 2017hadi Mei, 2019, na ni matumaini ya Kamati kuwa wawekezajihao watakuwa wametumia vizuri muda uliotolewa na Serikali.Hivyo, kuweza kutumia teknolojia nyingine na kuwezakuzalisha mifuko mbadala.Aidha, Kamati inaishauri Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingirakufuatilia utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu na kuhakikishaifikapo tarehe 30 Mei, 2019 matumizi ya mifuko ya plastikiyatakuwa yamefikia mwisho.

4.2 Uchambuzi wa Makadirio ya mapato

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2019/2020, Ofisiya Makamu wa Rais-Mazingira chini ya Fungu 31 inalengakukusanya jumla ya Shilingi 18,218,915,442.00 kutoka katikavyanzo vya ndani vya Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamiziwa Mazingira – NEMC ambavyo ni ada na faini zitokanazona shughuli za usimamizi wa mazingira.

Uchambuzi wa Kamati ulibaini kuwa kiasi kinacholengwakukusanywa kinakaribiana na kabisa na malengo ya Mwakawa Fedha 2018/2019 ambalo yalitekelezwa kwa asilimia 55.2tu hadi kufikia robo ya tatu ya Mwaka wa Fedha, kipindiambacho walipashwa kukusanya asilimia 75. Kutokana nauchambuzi huu kamati inaishauri Serikali mambo yafuatayo:-

Page 181: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

181

i) kupanga lengo la makusanyo kwa kuzingatia kasi nauwezo wake wa kukusanya.

ii) Wakati wa kupanga lengo la makushanyo izingatiechangamoto zilizokwamisha kufikia lengo la makusanyo laMwaka wa Fedha uliotangulia na kuzitatua.Vilevile, Kamati inatambua kuwa wigo wa mapatoyatokanayo na shughuli za Mazingira ni mkubwa lakini kasiya ukusanyaji bado ni ndogo. Kamati inaishauri Serikalikuiongezea NEMC uwezo kwa kuwapatia watumishi navitendea kazi ili waweze kuongeza kasi ya ukaguzi na hatuaambayo itaongeza mapato ya Baraza pia.

4.3 Uchambuzi wa Bajeti ya Matumizi

Mheshimiwa Spika, Bajeti ya matumizi kwa ajili ya shughuli zaHifadhi na Usimamizi wa Mazingira hutengwa katika Fungu31 Ofisi ya Makamu wa Rais. Kamati ilijulishwa kuwa jumla yashilingi 22,708,713,882.00 zinaombwa kwa ajili ya kutekelezamajukumu hili muhimu, Kiasi hicho ni ongezeko kwa asilimia179.71 ikilinganishwa na Bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019.

Uchambuzi wa Kamati ulibaini kuwa ongezeko la Bajeti yashughuli za Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira kwa Mwakawa Fedha 2019/2020 linaathari katika fedha za miradi yamaendeleo ambayo imeongezeka kutoka 3,524,540,000.00Mwaka 2018/2019 mpaka shilingi 18,218,915,442.00 Mwakawa Fedha 2019/2020.

4.4 Maoni ya jumla kuhusu Makadirio ya Mapato naMatumizi kwa mwaka wa fedha 2019/2020

Mheshimiwa Spika, Tanzania Nchi mwanachama wamikataba mingi ya kimataifa inayohusiana na mambo yaMazingira. Na kupitia mikataba hiyo nchi ina fursa ya kupatafedha za maendeleo kwa kuandika maandiko ya miradi nakuyawasilisha katika taasisi za mazingira duniani.

Mheshimiwa Spika, Kamati imebaini kuwa kama nchihatujaitumia fursa hiyo ipasavyo, kwa kuwa hatujaandika

Page 182: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

182

maandiko yakutosha ambayo yanawezesha upatikanaji wafedha hizo.

Kwa kuwa, mwenendo wa upatikanaji wa fedha kwa ajili yashughuli za uhifadhi na usimamizi wa mazingira si wakuridhisha. Hivyo basi Kamati inaishauri Serikali kupitia Ofisiya Makamu wa Rais – Mazingira, Baraza la Taifa la Hifadhi naUsimamizi wa Mazingira – NEMC na wadau wengine wamazingira kuchangamkia fursa hii kwa kuongeza kasi nakuandaa maandiko ya kutosha yenye uhalisia nakuyawasilisha katika taasisi za kimataifa kila fursa inapotokea.Juhudi hizo zitapelekea kuongezeka kwa fedha za uhifadhina utunzaji wa mazingira nchini.

Sambamba na hilo Kamati inaishauri Ofisi ya Makamu waRais-Mazingira kuwatambua wadau wote wa mazingira(hususani NGO’s) ambao wanatumia fursa hii na kupatafedha za miradi. Umuhimu wa kuwatambua wadau hao nikuiwezesha Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira kuwezekuwafuatilia na kuhakikisha fedha wanazozipata zinatumikakutekeleza miradi/shughuli zilizokusudiwa.

5.0 MAONI NA USHAURI WA KAMATI5.1 Hali ya Mazingira

Mheshimiwa Spika, Hali ya Mazingira nchini si ya kuridhisha,tafiti zimefanyika na kubainisha hali mbalimbalizinazodhihirisha jambo hili. Kamati ilipata fursa wakati wa ziarazake za ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutembelea nakushuhudia hali isiyo ya kuridhisha ya mazingira katika baadhiya maeneo nchini. Kamati imebainisha maeneo machachetu ambayo yanadhihirisha hali mbaya ya mazingira kwalengo la kutoa picha ya kuathirika kwa mazingira ya Nchi.Maeneo hayo ni pamoja na;-

i) Athari za Mabadiliko ya Tabianchi, ambazozimekwisha dhihirika katika maeneo mbalimbali nchini. Atharihizo ni pamoja na ukame, mafuriko, kuenea kwa magonjwaya kuambukiza, kuongezeka kwa ujazo wa maji ya bahari(kuharibu kingo za bahari na fukwe; kumezwa kwa visiwa

Page 183: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

183

vidogo kwenye bahari; na kuathiri wáter table), kuyeyuka kwabarafu katika vilele vya milima mirefu kama vile MlimaKilimanjaro, uharibifu wa madaraja, barabara, reli na makazikutokana na mafuriko;

ii) Hali ya ukame na jangwa nchini, tafiti zinaonyeshakuwa asilimia 61 ya nchi ipo hatarini kugeuka jangwa. Baadhiya Mikoa iliyoathirika zaidi na hali ya ukame nchini ni pamojana Dodoma, Singida, Shinyanga, Simiyu, Manyara na baadhiya maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro. Kwa kiasi kikubwa halihii inatokana na matumizi ya yasiyoendelevu ya rasilimali asilinchini.

iii) Takwimu za ukataji wa misitu zinaonesha kuwa, msituwenye ukubwa wa kiwanja cha mpira hufyekwa kila baadaya dakika moja, takwimu hizi zimeipelekea Tanzania kuwakatika ya nchi tano za juu (top five) zinazoongoza kwa ukatajiwa misitu (deforestation) Duniani;

iv) Hali ya rasilimali maji, Tanzania imeingia katika orodhaya nchi zenye upunguvu wa maji ukilinganisha na mahitaji(water stressed country). Hali hiyo ni moja ya kiashiria chauharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji;

vii) Hatari ya kupotea kwa baadhi ya maziwa nchini,baadhi ya maziwa yaliyopo kwenye hatari ya kupotea ni ZiwaManyara, Jipe na Chala. Kupotea kwa maziwa haya kwakiasi kikubwa kumechengiwa na shughuli za kibinadamuzinazoendeshwa katika maeneo ya ziwa ambazo hupelekeauharibifu wa mazingira.

Mheshimiwa Spika, hayo ni baadhi tu ya maeneo ambayoyanaonesha kuwa hali ya mazingira nchini si ya kuridhisha.Hivyo basi Kamati inaishauri Serikali kuchukua jitihada zamakusudi kwa lengo la kuinusuru nchi kutokana na atharizitokanazo na uharibifu wa mazingira.

Page 184: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

184

5.2 Maoni na Ushauri

Mheshimiwa Spika, baada ya kufanya ziara za Ukaguzi waMiradi ya Maendeleo na kuchambua utekelezaji wa Bajetiya Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira 2018/2019, pamojana mapendekezo ya Mapato kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 ya Ofisi hii Kamati imekuwa na Maoni na Ushauri kadhaakwa Serikali. Ni imani ya Kamati kuwa maoni na ushauri huuutafanyiwa kazi hivyo kutapelekea kuboresha shughuli zauhifadhi na usimamizi wa mazingira nchini.

i) Mfuko wa Mazingira

Mheshimiwa Spika, kwa miaka kadhaa tumeshuhudia Ofisiya Makamu wa Rais-Mazingira imeendelea kutengewa bajetindogo ukilinganisha na ukubwa wa jukumu walilonalo lauhifadhi na usimamizi wa Mazingira.

Mheshimiwa Spika, dhana ya kuanzishwa kwa Mfuko waMazingira ilikuwa ni kuisaidia Serikali kuisimamia Sekta Binafsikuchangia katika shughuli za uhifadhi na usimamizi wamazingira. Mfuko huu umeanzishwa tangu mwaka 2007 lakiniunashindwa tekeleza majukumu yake mpaka sasa.

Mheshimiwa Spika, kuna vyanzo mbalimbali vya mapatoambavyo vinatokana na mazingira lakini vyanzo hivi vinaingiakatika mifuko ambayo hairudishi katika shughuli ya hifadhiya mazingira. Kamati ilifahamishwa na Ofisi ya Makamu waRais-Mazingira kuwa vyanzo hivi vimekwisha ainishwa nakuwasilishwa katika Baraza la Mawaziri. Kamati inaisisitizaSerikali kuhakikisha katika mwaka wa fedha 2019/2020, kwakuanzia walau vyanzo vitano tu vichangie katika Mfuko waMazingira kwa asilimia tano (5). Hatua hii itasaidia kupunguzautegemezi wa ruzuku ya Serikali katika kutekeleza majukumuya usimamizi wa mazingira.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaishauri Serikali kuwa baada yakupitisha vyanzo hivi vya mapato ya Mfuko, ifanye maboreshokatika Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 Sura ya 191 ili iweze

Page 185: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

185

kutambua na kusimamia utekelezaji Sekta zote zinazotakiwakuchangia katika mfuko.

ii) Afisa Mazingira

Mheshimiwa Spika, Sheria ya Mazingira imemtambua nakumpa majukumu makubwa Afisa Mazingira. Pamoja nakuwa Afisa Mazingira anapewa majukumu na Sheria yaMazingira na analengwa kumsaidia Mkurugenzi wa Mazingiralakini ni muajiriwa wa Halmashauri na anaripoti kwaMkurugenzi wa Halmashauri. Aidha, taarifa ya kazianazofanya Afisa Mazingira ili zimfikie Mkurugenzi waMazingira ni lazima zipitie TAMISEMI.

Mheshimiwa Spika, mlolongo huu unapelekea ucheleweshajiwa taarifa lakini pia unakwamisha utekelezaji wa shughuli zamazingira. Kamati inaishauri Serikali kuondoa mlolongo huomrefu na badala yake Afisa Mazingira awe anaripoti mojakwa moja kwa Mkurugenzi wa Mazingira kwa masuala yoteyanayohusu mazingira. Jambo hil i si j ipya limekuwalikitekelzwa na Maafisa Maji wa Halmashauri zote, waowanaripoti moja kwa moja Wizara ya Maji.

Pia, Kamati inashauri Serikali kwa siku za usoni kuangalianamna ya kuwahamisha maafisa mazingira wote kuwa chiniya Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira. Hatua hii itasaidiauratibu wa shughuli za hifadhi na usimamizi wa mazingira.

iii) Elimu ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira

Mheshimiwa Spika, katika suala la uhifadhi na usimamizi wamazingira asilimia sabini (70) ya jukumu lao ni kutoa elimu ilikujenga uelewa kwa jamii kuhusu uhifadhi wa mazingira naathari za kuharibu mazingira; na asilimia thelathini (30) iliyobakini kutekeleza miradi/shughuli za kupambana na mabadilikoya Tabianchi kama vile ujenzi wa ukuta kwenye kingo zabahari na mito, kampeni za upandaji wa miti n.k. Kamatiinaishauri Serikali kuongeza kasi ya kusambaza elimu yauhifadhi wa mazingira. Elimu hii iende sambamba na ainaya shughuli za kijamii zinazofanyika katika maeneo husika kwa

Page 186: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

186

kuwa aina ya uharibifu wa mazingira inategemea aina yashughuli za binadamu katika eneo husika. Mfano aina yauharibifu unaofanywa na wakulima ni tofauti na uharibifuunaofanywa na wafugaji.

iv) Utekelezaji wa Sheria ya Namba 20 ya Mazingirakuhusu Mita 60

Mheshimiwa Spika, kifungu namba 57 cha Sheria ya Mazingiraya Mwaka 2004 kinampa Waziri mwenye dhamana namasuala ya Mazingira, mamlaka ya kutunga Kanuni namiongozo mbalimbali ambayo itasaidia katika kusimamiashughuli za usimamizi wa mazingira katika maeneo ya owevuyani bahari, mito na mabwawa. Kamati imebaini kuwa kunaupungufu katika Kanuni na Miongozo zilizotungwa kwa lengola kusimamia maeneo hayo jambo linaloleta changamotokatika utekelezaji wa sheria hii na kupelekea migogoro namalalamiko kwa baadhi ya maeneo. Kamati inaishauri Serikalikupitia kwa Waziri mwenye dhamna ya mazingira kurekebishakanuni na miongozo hii ili iweze kuelekeza kwa uwazi ni kwajinsi gani wananchi wanaokaa pembezoni mwa bahari, mitona mabwawa wanaweza kufanya shughuli zao bila yakuharibu mazingira.

Mheshimiwa Spika, Pia Kamati inaishauri Serikali kuzielekezaHalmashauri zote ambazo zina maeneo owevu, kuainishamaeneo yote na kuorodhesha shughuli zinazoweza kufanyikakatika eneo husika, kisha kuwasilisha maombi kwa Wazirimwenye dhamna ya Mazingira ili waweze kutumia maeneohayo. Sambamba na hilo Halmashauri hizo ziwajibikekusimamia maeneo hayo.

v) Utekelezaji wa Majukumu ya Baraza la Taifa la Hifadhina Usimamizi wa Mazingira- NEMC.

Mheshimiwa Spika, Kumekuwa na malalamiko ya mudamrefu juu ya utendaji wa NEMC. Uchambuzi wa Kamatiumebaini kuwa malalamiko haya yametokana na uzamaniwa kanuni na taratibu za uendeshaji wa shughuli za Barazahususani uendeshaji wa Tathimini ya Athari za Mazingira – EIA.

Page 187: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

187

Mheshimiwa Spika, Kamati inatambua mabadiliko makubwayaliyofanywa na Mheshimiwa Rais katika Baraza, kuanziaMwenyekiti wa Bodi ya Baraza na Mkurugenzi Mkuu waBaraza na inamatumaini kuwa uendeshaji wa Barazautaimarika na malalamiko yatafika mwisho. Pamoja namabadiliko hayo Kamati inaishauri Serikali kulisimamia Barazakufanya mapitio ya kanuni na taratibu za utekelezaji washughuli zake na kuziboresha kuhakikisha zinaendana namazingira halisi ya sasa.

Mheshimiwa Spika, moja ya eneo ambalo linahitaji sanamaboresho ni hatua zinazofuatwa wakati wa kuomba cheticha Tathimini ya Athari za Mazingira – EIA. Baadhi ya hatuazilizowekwa si za lazima na haziendani na wakati kwani duniaya sasa ni ya kidigitali.

vi) Vibali vya Tathimini ya Athari za Mazingira – EIA

Mheshimiwa Spika, kwa muda mrefu NEMC imekuwaikilalamikiwa juu ya ucheleweshaji wa vibali vya Tathimini yaAthari za Mazingira – EIA. Kamati inatambua kuwa kupatakibali cha EIA ni mchakato na unachukua muda, lakiniinatambua pia kuwa si muda mrefu kama unaolalamikiwana baadhi ya wadau (mpaka miaka mitatu). Kamatiinaishauri Serikali kuhakikisha inaisimamia NEMC kupunguzaurasimu katika kutoa vibali na EIA kwa lengo la kuisaidiaSerikali kujenga mazingira mazuri ya Uwekezaji ukizingatiakuwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuliameelekeza kuwa Mwaka 2019 ni Mwaka wa Uwekezaji.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa nchi inajielekeza kwenyeuwekezaji, kuna haja kubwa ya kuangalia upya gharama zaEIA katika miradi mikubwa ya uwekezaji. Gharama zaTathimini ya Athari za Mazingira - EIA kwa miradi mikubwa yauwekezaji ni kubwa na zinalipwa kwa wakati mmoja. Kamatiinashauri Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira kupitia upyagharama hizo na kuziboresha. Pia, Kamati inashauri kwambawajaribu kugawanya gharama ambazo mteja anapaswakulipa, ili aweze kulipa kwa awamu, jambo hilo linawezakutekelezwa kwa kuangalia hatua za uwekezaji kama vile

Page 188: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

188

hatua za awali, kati na mwisho. Hatua hii itatoa unafuu kwawawekezaji wetu kwa kuwa gharama za awali za kuanzauwekezaji zitakuwa zimepungua.

vii) Nguvu ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka2004

Mheshimiwa Spika, Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004imejipambanua vizuri na imegawa majukumu/wajibu kwa kilamtu kuanzia ngazi ya Serikali mpaka kufikia kwa wananchi.Kamati imebaini kuwa changamoto ipo katika usimamizi wautekelezaji wa Sheria hii. Wahusika waliotajwa na Sheria tenahususani mamlaka za Serikali hazichukui nafasi zao nakutekeleza majukumu yao. Kamati inaishauri Serikali kupitiakwa Waziri mwenye dhamana kutumia mamlaka yake yakisheria kuwawajibisha wale wanaopuuzia majukumu yao.

viii) Taarifa ya Hali ya Mazingira NchiniMheshimiwa Spika, kifungu 175 cha Sheria ya Mazingira yaMwaka 2004 kinamuelekeza Mkurugenzi wa Mazingirakuandaa na kutoa taarifa kuhusu hali ya usimamizi wamazingira nchini kila baada ya miaka miwili na taarifa hiyoinapaswa kuwasilishwa Bungeni. Takribani miaka mitano (5)sasa kuanzai mwaka 2014 hadi 2019, taarifa hii haijaandaliwawala kuwasilishwa Bungeni. Kamati inaishauri Serikalikusimamia taarifa hii kuhakikisha inakamilika na kuwasilishwaBungeni kabla ya Mwaka wa fedha 2019/2020 haujaisha kwalengo la kutoa picha ya hali ya mazingira nchini, lakini piakuwapa Wabunge nafasi ya kuijadili na kuishauri Serikali.

6.0 HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee, napendakuwashukuru Wajumbe wote wa Kamati ya Bunge yaViwanda, Biashara na Mazingira ambao wameweza kutoamaoni, michango na mawazo yao mbalimbali katikakukamilisha taarifa hii. Orodha yao ni kama inavyosomekahapa chini.i. Mhe. Suleiman Ahmed Sadiq, Mb Mwenyekitiii. Mhe. Kanal (Mst.) Masoud Ali Khamis, Mb M/Mwenyekitiiii. Mhe. David Cecil Mwambe, Mb Mjumbe

Page 189: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

189

iv. Mhe. Gimbi Dotto Masaba, Mb Mjumbev. Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mb Mjumbevi. Mhe. Kiteto Zawadi Koshuma, Mb Mjumbevii. Mhe. Hawa Subira Mwaifunga, Mb Mjumbeviii. Mhe. Munira Mustafa Khatibu, Mb Mjumbeix. Mhe. Mussa Rashid Ntimizi, Mb Mjumbex. Mhe. Godbless Jonathan Lema, Mb Mjumbexi. Mhe. Omary Ahmad Badwel, Mb Mjumbexii. Mhe. Kmamis Ali Vuai, Mb Mjumbexiii. Mhe. Zainabu Mndolwa Amiri, Mb Mjumbexiv. Mhe. Josephine Johnson Genzabuke, Mb Mjumbexv. Mhe. Sylvestry F. Koka, Mb Mjumbexvi. Mhe. Gibson Blasius Meiseyeki, Mb Mjumbexvii. Mhe. Shamsia Azizi Mtamba, Mb Mjumbexviii. Mhe. Ahmed Juma Ngwali, Mb Mjumbexix. Mhe. Richard Mganga Ndassa, Mb Mjumbexx. Mhe. Jafar Sanya Jussa, Mb Mjumbexxi. Mhe. Machano Othman Said, Mb Mjumbexxii. Mhe. Kalanga Julius Laizer, Mb Mjumbe

Mheshimiwa Spika, naomba kuchukua nafasi hii kumpongezaWaziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Rais-Muungano na Mazingira,Mhe. January Y. Makamba, Mb, Naibu waziri wa wizara hiyoMhe. Mussa Ramadhan Sima, Mb, Makatibu Wakuu naWatendaji wote wa Wizara kwa kutoa ufafanuzi mzuri wakatiwa uchambuzi wa Bajeti hii.

Mheshimiwa Spika, naomba nikushukuru sana wewe naMheshimiwa Naibu Spika kwa kutupatia maelekezombalimbali ambayo wakati wote yamefanikisha kazi zaKamati. Aidha, napenda pia kumshukuru Katibu wa BungeNdg. Stephen Kagaigai, Mkurugenzi wa Idara ya Kamati Bw.Athumani Hussein, Mkurugenzi msaidizi Sehemu ya Fedha naUchumi Bw. Michael Chikokoto, makatibu wa Kamati Bi.Zainab Mkamba na Bi Mwajuma Ramadhani pamoja naMsaidizi wa Kamati Bi. Paulina Mavunde kwa kuratibu shughuliza Kamati hadi taarifa hii kukamilika.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya, sasa naliombaBunge lako Tukufu likubali kuidhinisha Makadirio ya Mapato

Page 190: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

190

na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Fungu31 kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 ambayo ni kiasi chaShilingi 22,708,713,882.00 kwa ajili ya kutekeleza shughuli zahifadhi na usimamizi wa mazingira.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na naunga mkonohoja.

Suleiman Ahmad Sadiq, (Mb)MWENYEKITI

KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA,BIASHARA NA MAZINGIRA

16 Machi, 2019

MWENYEKITI: Ahsante. Sasa namwita Msemaji waMkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani juu ya Ofisi ya Makamuwa Rais, Muungano na Mazingira.

MHE. LATHIFAH H. CHANDE K.n.y. MSEMAJI MKUU WAKAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA OFISI YA MAKAMUWA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: MheshimiwaMwenyekiti, kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa Kambi yaUpinzani Bungeni, napenda kuwasilisha hotuba kuhusuMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu waRais, Muungano na Mazingira kwa mwaka 2019/2020.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumshukuruMwenyezi Mungu mwingi wa Rehema, kwa kutujaalia sotekuwa hapa kwenye Mkutano huu wa bajeti katika Bunge hilila Kumi na Moja. Pamoja na hujuma na njama zilizofanywana zinazoendelea kufanywa kwa kuwarubuni baadhi yaWabunge wenzetu kuhamia upande wa pili, bado Upinzanikwa ujumla na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni iko imarana inachapa kazi kwa weledi mkubwa zaidi. Kwani tunaamini,kesho yetu ni bora kuliko jana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa shukrani za dhati kwaKiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani kwa kuniamini na

Page 191: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

191

kunipa fursa hii ya kuwa Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi yaUpinzani katika Ofisi hii ya Makamu wa Rais na hivyokusimama hapa na kutoa mtazamo wa Kambi kwa hojailiyopo mbele yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naushukuru pia uongozimzima wa Kambi Rasmi ya Upinzani na WaheshimiwaWabunge wote kwa msaada wao na ushirikiano wao katikamatayarisho ya wasilisho hili. Aidha, nawashukuru Watanzaniawenzangu na wadau wa mazingira kutoka pande zote mbiliza Muungano kwa kunipa hoja ambazo zimenisaidia sanakatika kukamilisha hotuba hii ya wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho lakini siyo kwaumuhimu, naishukuru familia yangu kwa kunivumilia na kunipamoyo wa kazi nikiwa ndani ya Bunge na nje ya Bunge. Piakwa Ofisi ya Spika, shukrani zangu haziwezi kuwa na ukomo,naitukuza kila fursa niliyopewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu masuala yaMuungano; ukweli ni kuwa masuala ya Muunganoyameelezwa vizuri katika Ibara ya (4)(3) na kuorodheshwakatika Nyongeza ya Kwanza ya Katiba. Kuna hoja ambazokwa miaka yote imekuwa ni kilio kutoka upande wa pili waMuungano na kupelekea kuundwa kwa Tume kadhaa ilikutatua kero hizo za Muungano. Kero hizo ambazo zimekuwazinapigiwa kelele miaka yote ni mafuta na gesi asilia, mamboya Muungano, ajira za Wazanzibar katika Taasisi zaMuungano, uwezo wa Zanzibar kukopa nje, gawio la Zanzibarkatika mali za Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki, Mfuko waPamoja wa Fedha, utozwaji kodi mara mbili kwawafanyabiashara wa Zanzibar. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar peke yake ama kwa kushirikiana na Serikali yaMuungano, zimechukua hatua kadhaa za kutafuta ufumbuziwa kero za Muungano. Kwa upande wa Serikali ya MapinduziZanzibar, miongoni mwa hatua ilizochukua na ambazozinajulikana ni pamoja na kuunda Kamati mbalimbali.

Page 192: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

192

Mheshimiwa Mwenyekiti, miongoni mwa Kamatizilizoundwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kushughulikiakero za Muungano kati ya mwaka 1990 na 2003 ni pamojana zifuatazo: Kamati ya Baraza la Mapinduzi (Kamati yaAmina) ya 1992; Kamati ya Rais ya Kupambana na Kasoro zaMuungano (Kamati ya Shamhuna, 1997; Kamati ya RaisKuchambua Ripoti ya Kisanga (Kamati ya Salim Juma);Kamati ya Rais ya Kuandaa Mapendekezo ya Serikali yaMapinduzi Zanzibar juu ya Kero za Muungano (Kamati yaRamia ya mwaka 2000); Kamati ya Baraza la Muungano juuya Sera ya Mambo ya Nje; Kamati ya Rais ya Wataalamu juuya Kero za Muungano ya mwaka 2001; Kamati ya Baraza laMuungano ya Jamuiya ya Afrika Mashariki; Kamati ya Mafuta;Kamati ya Madeni baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibarna Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Kamati yasuala la Exclusive Economic Zone, Kamati ya masuala yaFedha na Benki Kuu na Kamati ya Masuala ya Simu ya mwaka1996 hadi mwaka 1999.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Serikali ya MapinduziZanzibar pia imewahi kuajiri mtaalamu wa mambo ya fedha,Dkt. Courtrey Blackman na mtaalam wa masuala ya mafutakatika kutafuta suluhu ya mambo hayo yanayoyumbishaMuungano wetu, lakini kamati zote hizo hazikuzaa matunda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaamini kabisa tatizo kubwa liko kwenye Muundo waMuungano na suluhu ya tatizo hilo ni kubadilisha muundo iliMuungano wetu uimarike zaidi na kuwa wenye manufaa kwapande zote washirika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mbali na baadhi ya Kamatihizo za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar peke yake, Serikali yaMuungano Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibarzimeunda Tume, Kamati na kuajiri wataalamu mbalimbali ilikutafuta suluhisho la kero mbalimbali za Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miongoni mwa Tume naKamati hizo ni kama zifuatazo: Kamati ya Mtei, Tume yaNyalali, Kamati ya Shellukindo, Kamati ya Bomani, Kamati ya

Page 193: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

193

Shellukindo ya pili ya kuandaa muafaka juu ya mambo yaMuungano baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikaliya Muungano Tanzania, Kamati ya Harmonisation, Kamatiya masuala ya simu ambayo ilikuwa ni Kamati ya Kusila.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Serikali ya MapinduziZanzibar na Serikali ya Muungano Tanzania zimefanya vikaovya pamoja visivyopungua 80 katika ngazi mbalimbali ilikuzungumzia kero za Muungano. Aidha, Serikali hizi mbilimwaka 1994 ziliomba msaada wa IMF ili kuzishauri kuhusianana Benki Kuu, mgawanyo wa misaada na uhusiano wakifedha (intergovernmental fiscal relationship).

Mheshimiwa Mwenyekiti, mbali ya juhudi zote hizo,tarehe 14 Novemba, 2000 wakati Mheshimiwa Rais BenjaminMkapa alipokuwa akizundua Bunge aliahidi kuzipatiaufumbuzi kero za Muungano ndani ya siku 60. Tokea ahadiilipotolewa hadi leo ni miaka 19 imepita, Serikali zinazoongozani zile zile za Chama cha Mapinduzi. Kuchelewa huko kutatuakero hizo, kunaonesha dhahiri kwamba Serikali za CCMhazijatoa kipaumbele kwa Muungano huu kuendeleakuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume ya Pamoja ya Fedha(Joint Finance Commission) ni asasi ya Muungano iliyoundwakwa mujibu wa Ibara ya 134 ya Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania ya mwaka 1977, na Sheria ya Tumeya Pamoja ya Fedha, sura 140 ya mwaka 1996.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume ya Pamoja ya Fedha(Joint Finance Commission), ni asasi ya Muungano iliyoundwakwa mujibu wa Ibara ya 134 ya Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Sheria ya Tumeya Pamoja ya Fedha, Sura 140 ya mwaka 1996). Tumeilizinduliwa rasmi tarehe 5 Juni, 2003, baada ya Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania kuteua Makamishnasaba. Aidha, Tume ina Sekretarieti ambayo ni chombo kikuukiutendaji. Tume hii ilikuwa njia mojawapo ya kutatua keroza kifedha kati ya zile kero kuu za Muungano, lakini kwa

Page 194: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

194

masikitiko makubwa hata Tume hiyo ambayo ni chombo chakiutendaji kimeshindwa kutimiza azma ya uanzishwaji wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Katiba, Tumeya Pamoja ya Fedha ina majukumu yafuatayo:-

(a) Kuchambua mapato na matumizi yanayotokana na,au yanayohusu utekelezaji wa Mambo ya Muungano nakutoa mapendekezo kwa Serikali mbili kuhusu mchango namgao wa kila mojawapo ya Serikali hizo;

(b) Kuchunguza kwa wakati wote mfumo wa shughuli zafedha wa Jamhuri ya Muungano na pia uhusiano katikamambo ya kifedha kati ya Serikali mbili;

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Ibara ya 133 yaKatiba inaeleza kuwa:

“Serikali ya Jamhuri ya Muungano itatunza akauntimaalum itakayoitwa “Akaunti ya Fedha ya Pamoja” naambayo itakuwa ni sehemu ya Mfuko Mkuu wa Hazina yaSerikali ya Jamhuri ya Muungano ambamo kutawekwa fedhayote itakayochangwa na Serikali mbili kwa kiasikitakachoamuliwa na Tume ya Pamoja ya Fedha kwa mujibuwa Sheria iliyotungwa na Bunge, kwa madhumuni ya shughuliza Jamhuri ya Muungano kwa mambo ya Muungano”.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya msingi hapa yakuomba majibu kutoka Serikalini ni je, hiyo Akaunti ya Pamojaimeshafunguliwa? Kwa kuwa toka uwepo wa Tumeimeshindwa kutatua kero za kifedha zinazohusiana naMuungano na hivyo malalamiko kuzidi kurundikana, ni wazikuwa chombo hiki licha ya kuwa ni chombo cha kikatibakimekosa uhalali kwa wananchi wa kuendelea kutengewafedha za walipa kodi katika kufanya kazi zake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni muda muafaka sasakama ambavyo wanazuoni mbalimbali wa masuala hayaya Muungano walivyo na wanavyozidi kushauri kuwa tatizoni muundo wa Muungano, hivyo vyombo vyote

Page 195: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

195

vitakavyoundwa kwa nia njema ya kuleta suluhu vitashindwakufanya kazi iliyopo na inayokusudiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinatoa rai kuwa ili matatizo au kero za Muungano ziishehatuna budi kurejea kwenye mapendekezo yaliyotolewakatika rasimu ya pili ya Katiba iliyotolewa na Tume yaMarekebisho ya Katiba iliyokuwa chini ya Uenyekiti wa JajiMstaafu Joseph Sinde Warioba kuhusiana na Muundo waMuungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ufupi naomba kunukuu“Ibara ya 60(1) ya Rasimu ya Pili ya Katiba kama wananchiwalivyohitaji muundo wa Muungano wetu utakavyokuwa:Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa na muundo washirikisho lenye Serikali tatu ambazo zitakuwa ni:

(a) Serikali ya Muungano;

(b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na

(c) Serikali ya Tanganyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzanikupitia sera yake ukurasa wa 13 na 14, Sura ya 2.4 inaelezawazi aina na muundo wa Muungano na kueleza malengoyatakayofikiwa kuwa ni kila nchi mshirika wa Muunganoitakuwa na mamlaka kamili katika kumiliki na kutumia rasilimalina maliasili zake; isipokuwa masuala yote ya msingi ya jumlakama vile Katiba ya Shirikisho la Jamhuri ya Muungano,Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ulinzi na Usalama,Uraia, Sarafu ya Benki Kuu, Mfumo wa Elimu, Mahakama yaKatiba na Bunge la Shirikisho yatashughulikiwa na Serikali yaShirikisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaamini juu ya kuurudisha Muungano karibu zaidi nawananchi kwa kuwashirikisha kwa njia mbali mbali, kuchaguana kuyatambua yale wanayoyataka katika Muungano waoili yaheshimiwe.

Page 196: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

196

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na uhifadhi nauendelevu wa mazingira. Mazingira ni dhana panainayojumuisha vitu vyote vinavyotuzunguka, iwe ni sekta yamaji (maziwa, bahari, mito, mabwawa aina na mbinu zakupata rasilimali ziishizo kwenye maji - aina ya uvuvi nakadhalika), sekta ya kilimo(matumizi bora ya uhifadhi wa ardhi- aina za mitambo ya kilimo inayotumika, matumizi ya mbolea,matumizi ya dawa), sekta ya misitu, sekta ya viwandani (jinsimabaki ya viwandani yanavyohifadhiwa na aina yateknolojia inayotumika katika uzalishaji), sekta ya afya (takazinavyotunzwa na kuteketezwa) na kadhalika. Maisha yabinadamu na viumbe vingine yanategemea sana hali yamazingira, ndiyo maana nimeyaita mazingira kuwa kitalu chamaisha. Kutokana na umuhimu huo usio na shaka, mazingirani miongoni mwa masuala mtambuka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, licha ya Serikali kutambuaumuhimu wa mazingira; na kuweka sheria, kanuni namiongozo ya ulinzi na uhifadhi wa mazingira kama vile Seraya Mazingira ya mwaka 1997, Sheria ya Mazingira ya mwaka2004, Mpango Kazi wa Taifa wa Mazingira (NationalEnvironmental Action Plan, 2013), MKUKUTA awamu ya piliwa mwaka 2010; Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 pamojana kuridhia Mikataba mbalimbali ya Kimataifa kuhusuuhifadhi na utunzaji wa mazingira; bado suala la utunzaji nauhifadhi wa mazingira halijapewa umuhimu na uzitounaostahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ikumbukwe kwambashughuli yoyote inayofanywa na binadamu katika uso wadunia, ina athari za moja kwa moja au zisizo za moja kwamoja katika mazingira. Athari hizo zinazosababishwa nabinadamu katika mazingira, baadaye hugeuka na kuathiritena maisha ya binadamu na viumbe vingine pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniilidhani kwamba jambo hili ambalo linagusa karibu kila sektaambayo binadamu anafanya shughuli za kuendesha maishayake lingepewa uzito angalau hata wa kujadiliwa siku mbililakini limepewa siku moja tu.

Page 197: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

197

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni jambo la aibu kwa Serikalihii kutegemea fedha za nje kukabiliana na majangayanayotokana na uharibifu wa mazingira na mabadilko yatabia nchi. Kwa mfano, kipindi hiki cha mvua ambapomafuriko yamebomoa nyumba nyingi za wananchi; mazaomashambani yameharibiwa vibaya na miundombinu yabarabara na madaraja yameharibiwa vibaya, wananchiwamepoteza maisha kwa kusombwa na maji tusubiri fedhaza nje ambazo hatujui zitatolewa lini kukabiliana na majangahayo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyoeleza hapoawali, mazingira ni suala mtambuka (cross cutting issue); lipokila mahali na madhara yatokanayo na uharibifu wamazingira yanagusa karibu sekta zote, hivyo ni rai ya KambiRasmi ya Upinzani Bungeni kwa Serikali, kutenga fedha zakutosha kutunza na kuhifadhi mazingira yetu; lakini pia kwaajili ya kukabiliana na athari zitokanazo na uharibifu wamazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tathmini ya jumla yautekelezaji wa bajeti ya maendeleo kwenye utunzaji nauhifadhi wa mazingira ni kama ifuatavyo:-

Jumla ya fedha iliyoidhinishwa na Bunge kwa Mwakawa Fedha 2017/2018 ilikuwa shilingi bilioni 6.788, lakini fedhailiyotolewa na kutumika (ambayo ni ya nje tu) hadi kufikiatarehe 8 Machi, 2018 ilikuwa ni shilingi bilioni 1.7, sawa naasilimia 25 tu ya bajeti ya maendeleo iliyoidhinishwa naBunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa utekelezaji huo duni wabajeti, ni wazi kwamba Serikali haiko makini kabisa katikasuala hili la mazingira. Tafsiri ndogo ya takwimu nilizozitoa nikwamba Serikali imeweka rehani maisha ya wananchi kwawahisani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ningependakuzungumzia kuhusiana na uchumi wa kijani. Uchumi wa kijanini uboreshaji wa uchumi na ustawi wa jamii unaozingatia

Page 198: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

198

uzalishaji na matumizi yasiyoharibu mazingira. Ukiangalia hatiidhini inaonesha kuwa moja ya kazi za Ofisi ya Makamu waRais ni “Promotion of Cleaner Production and GreenEconomy”

Mheshimiwa Mwenyekiti, imethibitika kuwa Tanzaniainapoteza zaidi ya hekta 372,000 kila mwaka eneolinalokadiriwa kuwa sawa na ukubwa wa nchi ya Rwanda,kutokana na ukataji miti kwa matumizi ya nishati ya kuni namkaa, uchomaji wa misitu unaofanywa na baadhi ya raiawasio waaminifu kwenye hifadhi mbalimbali nchini. Jambohilo lina athari kubwa katika mkakati wa nchi yetu wa kujikitakatika uchumi wa kijani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ukweli kwamba zaidi yaasilimia 90 ya nishati inayotumika katika familia za Tanzaniawanategemea nishati inayotokana na miti na mabaki yamazao ya shambani au taka zingine zaidi ya zile za plastikikwa matumizi ya kila siku ya majumbani kwao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa vijijiniasilimia mbili kutoka kwenye umeme na asilima naneinayotokana na bidhaa za petroli. Kati ya nishati hiyo kuni namkaa ndio chanzo kikuu cha nishati kwa wananchi waishiomijini na vijijini. Kambi Rasmi ya Upinzani inauliza uchumi wagesi tulioaminishwa kuwa upo na ndio mwarobaini wakututoa hapa kwenye matumizi makubwa ya nishatiitokanayo na miti upo au umeondoka katika Awamu hii yaTano?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukuaji wa uchumiunaozingatia matumizi yasiyo endelevu ya maliasili haunamanufaa katika dunia ya leo. Watu wanapaswa kuachanana mbinu za kizamani za ukuaji wa uchumi wa matumizishinikizi ya rasilimali, ambapo maendeleo yamekuwayakigharimu mazingira; badala yake, wanapaswa kufuatambinu mpya ambazo tija huongezwa kwa kutumia nakusimamia maliasili kwa ufanisi zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shughuli za kiuchumi lazimazizingatie athari za muda mrefu kwa mazingira na haja ya

Page 199: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

199

kuhifadhi urithi wetu wa pamoja kwa faida ya vizazi vijavyo.Uchumi wa kijani huchochea ukuaji wa uchumi, mapato, naajira. Tena husaidia kuimarisha mazingira na kuongeza tijakwa wananchi. Aidha, aina hii ya uchumi huleta maendeleoya kiuchumi ya muda mrefu na yanayotoa fursa kwa watuwengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika baadhi ya sektamuhimu kama vile kilimo, ujenzi, misitu na usafiri, uchumi wakijani hutengeneza ajira nyingi zaidi kuliko ambazo zipo katikahali ya kawaida. Katika sekta kama vile uvuvi; uchumi wakijani utalazimisha kushuka kwa mapato na ajira katika mudamfupi na wa kati ili kujazia hifadhi asilia, lakini hali hii hubakiaya muda mfupi na baadaye sekta hukua na kutoa tija kubwakwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jitihada za maendeleonchini Tanzania lazima zifanywe kwa kuzingatia uhalisia wamambo. Kwanza, zaidi ya asilimia 75 ya wananchi wa nchihii huishi vijijini. Hivyo, jitihada madhubuti za kupunguzaumaskini na kuleta maendeleo lazima zilenge wakazi nauchumi wa vijijini ili kuwa na matokeo mazuri. Kuna uhusianomkubwa kati ya watu maskini hasa wa vijijini na mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinasema kwa muktadha huo wa uchumi wa kijani, ni kweliuwekezaji wa mradi wa kuzalisha umeme unaotokana nanguvu za maji (Stiegler’s Gorge) uliopelekea kufyekwa kwamisitu kwenye eneo ambalo ni sawa na ukubwa wa Mkoawa Dar es Salaam, Ofisi hii ya Makamu wa Rais inatoa kauligani kuhusiana na utekelezaji wa mradi huo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchumi wa kijani sio kamaunaishia kwenye kufyeka misitu tu bali pia matumizi sahihi naendelevu ya pembejeo za kilimo kama vile (mbolea namadawa) yanayotumiwa kwenye kilimo ili ardhi isiharibike nahivyo kushindwa kuhimili uzalishaji wa mazao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niongelee mabadilikoya tabianchi. Mabadiliko ya tabianchi ni mabadiliko ya

Page 200: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

200

mfumo wa hali ya hewa yanayosababishwa na kazi za mojakwa moja au zisizo za moja kwa moja za binadamu, ambazozinaongeza gesi joto (greenhouse gases) na kubadilishamchanganyiko wa viwango vya gesi katika angahewa ladunia, ambayo pia ni nyongeza ya mabadiliko ya asili yamfumo wa hali ya hewa yaliyotathminiwa na kulinganishwakwa muda mrefu (usiopungua miaka thelatini na zaidi).

Mheshimiwa Mwenyekiti, mabadiliko ya tabianchikwa kiasi kikubwa (zaidi ya 95%) yanasababishwa na shughuliza kibinadamu ikiwemo uzalishaji wa viwanda unaotoa gesiukaa (carbon dioxide) kwa kiwango kikubwa sana. Matokeoau athari za mabadiliko ya tabianchi ni kuongezeka kwa joto,mvua kubwa na za muda mfupi, mafuriko, mvua ya maweikiambatana na upepo mkali, mvua fupi zisizo za msimu naukame wa muda mrefu na unaojirudia mara kwa mara. Tabiahizi zote zimeshajitokeza hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mabadiliko ya tabianchi nijambo linalohusu sekta zote za uchumi katika nchi, iwekwenye kilimo, mifugo, uvuvi, miundombinu ya barabara,misitu, afya kwa kuzuka magonjwa mapya, sekta yawanyapori na kadhalika, hivyo jambo hili ni jambo kubwasana kuliko ambavyo Serikali inavyolichukulia kwa urahisisana. Uwekezaji unaofanywa unaweza kuwa kazi bure kamahatutawekeza vya kutosha katika kukabiliana na mabadilikoya tabianchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mabadiliko ya tabianchi,ambayo pia huchangiwa na uharibifu mkubwa wa mazingiraumeleta athari kubwa katika sekta mbalimbali za maendeleoya jamii na sekta zingine ziko katika hatari ya kuathirika pia.Sekta hizi ni nishati, kilimo na usalama wa chakula, maji,mifugo (kwa kuzuka kwa magonjwa ya milipuko, ukosaji wamalisho na maji), uvuvi…

MWENYEKITI: Mheshimiwa, nenda kwenye maombi yapesa.

Page 201: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

201

MHE. LATHIFAH H. CHANDE – K.n.y. MSEMAJI MKUU WAKAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA OFISI YA MAKAMUWA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA : Kambi Rasmi inaitakaSerikali kulieleza Bunge hili ni kwa nini kila mara inashindwakutenga kutoa fedha za ndani ikiwa kulikuwa na Mkakati waKitaifa wa Kupambana na Mabadiliko ya Tabia Nchi au ndiokusema Mkakati huo haukuwa na kipengele cha bajeti kwaajili ya kuutekeleza? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinatoa wito kuwepo kwa uwazi zaidi katika hatua za utatuziwa changamoto za Muungano na pia hatua shirikishi katikaviwango mbalimbali ili kuondosha dhana kuwa Muunganohuu ni wa viongozi zaidi na sio wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi zaidi ingepaswakubuniwa ambayo ni ile Tanzania kuwa na uchumi endelevuna wenye kutoa ajira kwa wananchi wengi (Uchumi wa kijanini uboreshaji wa uchumi na ustawi wa jamii unaozingatiauzalishaji na matumizi yasiyoharibu mazingira).

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhahiri kwamba Tanzaniabado ina fursa nyingi katika kuifanya nchi yetu kuwa kwenyeuchumi wa kijani na fursa hiyo ilikuwa ni kuifanya Tanzaniakutumia rasilimali gesi kwa kiwango kikubwa ili kudhibitimatumizi ya nishati itokanayo na miti hapa nchini ili juhudizinazofanywa na Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo zaKiserikali matunda yake kuonekana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani, naomba kuwasilishahii hotuba yot eiliyoko hapa mbele yangu na imeikabidhikwenu. Nashukuru sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante.

Page 202: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

202

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANIBUNGENI, ALLY SALEHE ALLY (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA

MAPATO NA MATUMIZI YA OFISI YA MAKAMU WA RAISMUUNGANO NA MAZINGIRA KWA MWAKA WA 2019/2020 -

KAMA ILIVYOWASILISHWA MEZANI

(Inatolewa chini ya kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Bunge,Toleo la mwaka 2016)

A. UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumshukuru MwenyeziMungu, Mwingi wa Rehema, kwa kutujaalia sote kuwa hapakwenye mkutano huu wa bajeti katika Bunge hili la 11. Pamojana hujuma na njama zilizofanywa na zinazoendeleakufanywa za kuwarubuni baadhi ya wabunge wenzetukuhamia upande wa pili bado Upinzani kwa ujumla na KambiRasmi ya Upinzani Bungeni ni imara na inachapa kazi kwaweledi mkubwa zaidi, kwani tunaamini Kesho yetu ni borakuliko jana.

2. Mheshimiwa Spika,Natoa shukrani za dhati kwaKiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani kwa kuniamini nakunipa fursa hii kuwa Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi yaUpinzani katika Ofisi hii ya Makamu wa Rais na hivyokusimama hapa na kutoa mtazamo wa Kambi kwa hojailiyopo mbele yetu. Naushukuru pia uongozi mzima wa KambiRasmi ya Upinzani na waheshimiwa wabunge wote kwamsaada wao na ushirikiano wao katika matayarisho yawasilisho hili. Aidha, nawashukuru Watanzania wenzangu nawadau wa mazingira kutoka pande zote mbili za Muunganokwa kunipa hoja ambazo zimenisaidia sana katika kukamilishahotuba hii ya wananchi.

3. Mheshimiwa Spika,Mwisho lakini si kwa umuhimuniishukuru familia yangu kwa kunivumilia na kunipa moyo wakazi nikiwa ndani ya Bunge na nje ya Bunge, pia na kwa ofisiya Spika, shukrani zangu haziwezi kuwa na ukomo. Naitukuzakila fursa niliyopewa.

Page 203: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

203

B. MASUALA YA MUUNGANO4. Mheshimiwa Spika,Ukweli ni kuwa masuala yaMuungano yameelezwa vizuri katika Ibara ya (4)(3) nakuorodheshwa katika nyongeza ya kwanza ya Katiba. Kunahoja ambazo kwa miaka yote imekuwa ni kilio kutoka upandewa pili wa Muungano na kupelekea kuundwa kwa tumekadhaa ili kutatua kero hizo za Muungano. Kero hizo ambazozimekuwa zinapigiwa kelele miaka yote ni;

• Mafuta na Gesi Asilia• Mambo ya Muungano• Ajira za Wazanzibari katika Taasisi za Muungano• Uwezo wa Zanzibar Kukopa Nje• Gawio la Zanzibar katika Mali za Bodi ya Sarafu ya

Afrika Mashariki (EACB)• Mfuko wa Pamoja wa Fedha• Utozwaji Kodi mara mbili kwa Wafanyabiashara wa

Zanzibar

5. Mheshimiwa Spika, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) peke yake ama kwa kushirikiana na Serikali yaMuungano, zimechukua hatua kadhaa za kutafuta ufumbuziwa Kero za Muungano. Kwa upande wa SMZ, miongoni mwahatua ilizochukua na ambazo zinajulikana ni pamoja nakuunda Kamati mbali mbali. Miongoni mwa Kamatizilizoundwa na SMZ kushughulikia Kero za Muungano kati yamwaka 1990 na 2003 ni pamoja na zifuatazo:

(a) Kamati ya Baraza la Mapinduzi (Kamati ya Amina) ya 1992.(b) Kamati ya Rais ya Kupambana na Kasoro za Muungano(Kamati ya Shamhuna, 1997).(c) Kamati ya Rais Kuchambua Ripoti ya Kisanga (Kamati yaSalim Juma).(d) Kamati ya Rais ya Kuandaa Mapendekezo ya SMZ juu yaKero za Muungano. (Kamati ya Ramia, 2000).(e) Kamati ya BLM juu ya Sera ya Mambo ya Nje.(f) Kamati ya Rais ya Wataalamu juu ya Kero za Muungano(2001).(g) Kamati ya BLM ya Jamuiya ya Afrika Mashariki.(h) Kamati ya Mafuta

Page 204: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

204

(i) Kamati ya Madeni baina ya SMZ na SMT.(j) Kamati ya Suala la Exclusive Economic Zone (EEZ)(k) Kamati ya Masuala ya Fedha na Benki Kuu.(l) Kamati ya Rais ya Masuala ya Simu – (1996 – 1999)

Aidha, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pia imewahi kuajirimtaalamu wa mambo ya fedha, Dr. Courtrey Blackman naMtaalam wa masuala ya mafuta katika kutafuta suluhu yamambo hayo yanayoyumbisha Muungano wetu, lakinikamati zote hizo hazikuzaa matunda.

6. Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaaminikabisa tatizo kubwa liko kwenye Muundo wa Muungano nasuluhu ya tatizo hilo ni kubadilisha Muundo ili Muungano wetuuimarike zaidi na kuwa wenye manufaa kwa pande zotewashirika.

7. Mheshimiwa Spika,Mbali na baadhi ya Kamati hizoza SMZ peke yake, SMT na SMZ zimeunda Tume, Kamati naKuajiri Wataalamu mbali mbali ili kutafuta suluhisho la Kerombali mbali za Muungano. Miongoni mwa Tume na Kamatihizo ni kama zifuatazo:

(a) Kamati ya Mtei(b) Tume ya Nyalali(c) Kamati ya Shellukindo(d) Kamati ya Bomani(e) Kamati ya Shellukindo 2, ya kuandaa Muafaka juu yaMambo ya Muungano baina ya SMZ na SMT.(f) Kamati ya Harmonisation.(g) Kamati ya Masuala ya Simu (Kamati ya Kusila)

Aidha SMZ na SMT zimefanya vikao vya pamojavisivyopungua 80 katika ngazi mbali mbali ili kuzungumzia Keroza Muungano. Aidha Serikali hizi mbili mwaka 1994 ziliombamsaada wa IMF ili kuzishauri kuhusiana na Benki Kuu,mgawano wa misaada na uhusiano wa kifedha(intergovernmental fiscal relationship). Mbali ya juhudi zotehizo, tarehe 14 Novemba, 2000 wakati Rais Benjamin Mkapaalipokuwa akizundua Bunge aliahidi kuzipatia ufumbuzi Kero

Page 205: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

205

za Muungano ndani ya siku 60!! Tokea ahadi ilipotolewa hadileo ni ni miaka 19 imepita. Serikali zinazoongoza ni zile zile zaChama cha Mapinduzi. Kuchelewa huko kutatua kero hizokunaonesha dhahiri kwamba Serikali za CCM hazijatoakipaumbele kwa muungano huu kuendelea kuwepo.

a. TUME YA PAMOJA YA FEDHA -Joint FinanceCommission-JFC

8. Mheshimiwa Spika,Tume ya Pamoja ya Fedha (JointFinance Commission – JFC) ni asasi ya Muungano iliyoundwakwa mujibu wa Ibara ya 134 ya Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania (ya mwaka 1977) na Sheria ya Tumeya Pamoja ya Fedha Sura 140 ya mwaka 1996). Tumeilizinduliwa rasmi tarehe 5 Juni, 2003, baada ya Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania kuteua Makamishnasaba. Aidha Tume ina Sekretarieti ambayo ni chombo kikuukiutendaji. Tume hii ilikuwa ni njia mojawapo ya kutatua keroza kifedha kati ya zile kero kuu za Muungano lakini kwamasikitiko makubwa hata Tume hiyo ambayo ni chombo chakiutendaji kimeshindwa kutimiza azma ya uanzishwaji wake.

9. Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa Katiba, Tume yaPamoja ya Fedha ina majukumu yafuatayo:

a) Kuchambua mapato na matumizi yanayotokana na, auyanayohusu utekelezaji wa Mambo ya Muungano na kutoamapendekezo kwa Serikali mbili kuhusu mchango na mgaowa kila mojawapo ya Serikali hizo;

b) Kuchunguza kwa wakati wote mfumo wa shughuli za fedhawa Jamhuri ya Muungano na pia uhusiano katika mamboya kifedha kati ya Serikali mbili;

10. Mheshimiwa Spika, aidha, Ibara ya 133 ya Katibainaeleza kuwa; “Serikali ya Jamhuri ya Muungano itatunzaakaunti maalum itakayoitwa Akaunti ya Fedha ya Pamojana ambayo itakuwa ni sehemu ya Mfuko Mkuu wa Hazina yaSerikali ya Jamhuri ya Muungano ambamo kutawekwa fedhayote itakayochangwa na Serikali Mbili kwa kiasikitakachoamuliwa na Tume ya Pamoja ya Fedha kwa mujibu

Page 206: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

206

wa Sheria iliyotungwa na Bunge, kwa madhumuni ya shughuliza Jamhuri ya Muungano kwa mambo ya Muungano”.

11. Mheshimiwa Spika, hoja ya msingi hapa ya kuombamajibu kutoka Serikalini ni je hiyo Akaunti ya Pamojaimeshafunguliwa?

12. Mheshimiwa Spika,kwa kuwa toka uwepo wa Tumeimeshindwa kutatua kero za kifedha zinazohusiana naMuungano na hivyo malalamiko kuzidi kurundikana, ni wazikuwa chombo hiki licha ya kuwa ni chombo cha kikatibakimekosa uhalali kwa wananchi wa kuendelea kutengewafedha za walipa kodi katika kufanya kazi zake.

13. Mheshimiwa Spika, ni muda mwafaka sasa kamaambavyo wanazuoni mbalimbali wa masuala haya yamuungano walivyo na wanavyozidi kushauri kuwa tatizo nimuundo wa Muungano, hivyo vyombo vyotevitakavyoundwa kwa nia njema ya kuleta suluhu vitashindwakufanyakazi iliyopo na inayokusudiwa.

14. Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inatoarai kuwa ili matatizo au kero za Muungano ziishe hatuna budikurejea kwenye mapendekezo yaliyotolewa katika rasimu yapili ya KATIBA iliyotolewa na Tume ya Marekebisho ya Katibailiyokuwa chini ya Uenyekiti wa Jaji Mstaafu Joseph SindeWarioba kuhusiana na Muundo wa Muungano.

15. Mheshimiwa Spika,Kwa ufupi naomba kunukuu “Ibaraya 60(1) ya Rasimu ya Pili ya Katiba kama wananchiwalivyohitaji Muundo wa Muungano wetu utakavyokuwa:Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa na Muundo washirikisho lenye Serikali tatu ambazo ni;-

a. Serikali ya Muungano

b. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na;

c. Serikali ya Tanganyika.

Page 207: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

207

16. Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani kupitiasera yake uk. 13 &14 Sura ya 2.4 inaeleza wazi aina naMuundo wa Muungano na kueleza malengo yatakayofikiwakuwa ni kila nchi mshirika wa Muungano itakuwa na mamlakakamili katika kumiliki na kutumia rasilimali na maliasili zake;isipokuwa masuala yote ya msingi ya jumla kama vile Katibaya Shirikisho la Jamhuri ya Muungano, Mambo ya nje naushirikiano wa Kimataifa, Ulinzi na Usalama, Uraia, Sarafu yaBenki Kuu, Mfumo wa Elimu, Mahakama ya Katiba na Bungela Shirikisho yatashughulikiwa na Serikali ya Shirikisho.

17. Mheshimiwa Spikia, Kambi Rasmi ya Upinzani inaaminijuu ya kuurudisha Muungano karibu zaidi na wananchi kwakuwashirikisha kwa njia mbali mbali, kuchagua nakuyatambua yale wanayoyataka katika Muungano wao iliyaheshimiwe.

C. UHIFADHI NA UENDELEVU WA MAZINGIRA18. Mheshimiwa Spika, mazingira ni dhana panainayojumuisha vitu vyote vinavyotuzunguka, iwe ni sekta yamaji (maziwa, bahari, mito, mabwawa aina na mbinu zakupata rasilimali ziishizo kwenye maji-aina ya uvuvi n.k), sektaya kilimo(matumizi bora ya uhifadhi wa ardhi-aina zamitambo ya kilimo inayotumika, matumizi ya mbolea,matumizi ya madawa), sekta ya misitu(upandaji wa miti naukataji wa misitu) sekta ya viwandani (Jinsi mabaki yaviwandani yanavyohifadhiwa na aina ya teknolojiainayotumika katika uzalishaji), sekta ya afya (Takazinavyotunzwa na kuteketezwa) n.k. Maisha ya binadamuna viumbe vingine yanategemea sana hali ya mazingira,ndiyo maana nimeyaita mazingira kuwa kitalu cha maisha.Kutokana na umuhimu huo usio na shaka, mazingira nimiongoni mwa masuala mtambuka.

19. Mheshimiwa Spika, licha ya Serikali kutambuaumuhimu wa mazingira; na kuweka sheria, kanuni namiongozo ya ulinzi na uhifadhi wa mazingira kama vile Seraya Mazingira ya mwaka 1997, Sheria ya Mazingira ya mwaka2004, Mpango Kazi wa Taifa wa Mazingira (NationalEnvironmental Action Plan 2013), MKUKUTA awamu ya Pili

Page 208: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

208

mwaka 2010; Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 pamojana kuridhia mikataba mbali mbali ya kimataifa kuhusuuhifandhi na utunzaji wa mazingira; bado suala la utunzajina uhifadhi wa mazingira halijapewa umuhimu na uzitounaostahili.

20. Mheshimiwa Spika, ikumbukwe kwamba shughuliyoyote inayofanywa na binadamu katika uso wa dunia, inaathari za moja kwa moja au zisizo za moja kwa moja katikamazingira. Athari hizo zinazosababishwa na binadamu katikamazingira, baadaye hugeuka na kuathiri tena maisha yabinadamu na viumbe vingine pia.

21. Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani ilidhanikwamba jambo hili ambalo linagusa karibu kila sekta ambayobinadamu anafanya shughuli za kuendesha maisha yakelingepewa uzito angalau hata wa kujadiliwa siku mbili lakinilimepewa siku moja tu.

22. Mheshimiwa Spika, ni jambo la aibu kwa Serikali hiikutegemea fedha za nje kukabiliana na majangayanayotokana na uharibifu wa mazingira na mabadilko yatabia nchi. Kwa mfano, kipindi hiki cha mvua ambapomafuriko yamebomoa nyumba nyingi za wananchi; mazaomashambani yameharibiwa vibaya miundombinu yabarabara na madaraja yameharibiwa vibaya, wananchiwamepoteza maisha kwa kusombwa na maji tusubiri fedhaza nje ambazo hatujui zitatolewa lini kukabiliana na majangahayo?

23. Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza hapo awali,mazingira ni suala mtambuka (cross cutting issue); lipo kilamahali na madhara yatokanayo na uharibifu wa mazingirayanagusa karibu sekta zote, hivyo ni rai ya Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni kwa Serikali ,kutenga fedha za kutoshakutunza na kuhifadhi mazingira yetu; lakini pia kwa ajili yakukabiliana na athari zitokanazo na uharibifu wa mazingira.

24. Mheshimiwa Spika, tathmini ya jumla ya utekelezajiwa bajeti ya maendeleo kwenye utunzaji na uhifadhi wa

Page 209: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

209

mazingira ni kama ifuatavyo:- Jumla ya fedha iliyoidhinishwana Bunge kwa mwaka wa fedha 2017/18 ilikuwa shilingi bilioni6.788, lakini fedha iliyotolewa na kutumika (ambayo ni ya njetu) hadi kufikia tarehe 8 Machi, 2018 ilikuwa ni shilingi bilioni1.7 sawa na asil imia 25 tu ya bajeti ya maendeleoiliyodhinishwa na Bunge.

25. Mheshimiwa Spika, kwa utekelezaji huo duni wabajeti, ni wazi kwamba Serikali haiko makini kabisa katikasuala hili la mazingira. Tafsiri ndogo ya takwimu nilizozitoa nikwamba Serikali imeweka rehani maisha ya wananchi kwawahisani.

D. UCHUMI WA KIJANI (Green economy)26. Mheshimiwa Spika, Uchumi wa kijani ni uboreshaji wauchumi na ustawi wa jamii unaozingatia uzalishaji na matumiziyasiyoharibu mazingira. Ukiangalia hati idhini inaonesha kuwamoja ya kazi za Ofisi ya Makamu wa Rais ni “Promotion ofCleaner Production and Green Economy”

27. Mheshimiwa Spika, imethibitika kuwa Tanzaniainapoteza zaidi ya hekta 372,000 kila mwaka eneolinalokadiriwa kuwa sawa na ukubwa wa nchi ya Rwanda,kutokana na ukataji miti kwa matumizi ya nishati ya kuni namkaa, uchomaji wa misitu unaofanywa na baadhi ya Raiawasio waaminifu kwenye hifadhi mbalimbali nchini. Jambohilo linaathari kubwa katika mkakati wa nchi yetu wa kujikitakatika uchumi wa kijani.

28. Mheshimiwa Spika, ni ukweli kwamba zaidi ya asilimia90 ya nishati inayotumika katika familia za Tanzaniawanategemea nishati inayotokana na miti na mabaki yamazao ya shambani au taka zingine zaidi ya zile za plastikikwa matumizi ya kila siku ya majumbani kwao.

29. Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa vijijini asilimia 2kutoka kwenye umeme na asilima 8 inatokana na bidhaa zapetroli1. Kati ya nishati hiyo kuni na mkaa ndio chanzo kikuucha nishati kwa wananchi waishio mijini na Vijijini. Kambi Rasmiya Upinzani inauliza uchumi wa gesi tulioaminishwa kuwa upo

Page 210: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

210

na ndio muharobaini wa kututoa hapa kwenye matumizimakubwa ya nishati itokanayo na miti upo au umeondokakatika awamu hii ya Tano?

30. Mheshimiwa Spika, ukuaji wa uchumi unaozingatiamatumizi yasiyo endelevu ya maliasili hauna manufaa katikadunia ya leo. Watu wanapaswa kuachana na mbinu zakizamani za ukuaji wa uchumi wa matumizi shinikizi yarasilimali, ambapo maendeleo yamekuwa yakigharimumazingira; badala yake, wanapaswa kufuata mbinu mpyaambazo tija huongezwa kwa kutumia na kusimamia maliasilikwa ufanisi zaidi.

31. Mheshimiwa Spika, shughuli za kiuchumi lazimazizingatie athari za muda mrefu kwa mazingira na haja yakuhifadhi urithi wetu wa pamoja kwa faida ya vizazivijavyo22Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uzinduzi wa jukwaala uchumi wa kijani mjini iringa tarehe 08 mei, 2012

. Uchumi wa kijani huchochea ukuaji wa uchumi, mapato,na ajira. Tena husaidia kuimarisha mazingira na kuongeza tijakwa wananchi. Aidha aina hii ya uchumi huleta maendeleoya kiuchumi ya muda mrefu na yanayotoa fursa kwa watuwengi.

32. Mheshimiwa Spika,Katika baadhi ya sekta muhimukama vile kilimo, ujenzi, misitu, na usafiri, uchumi wa kijanihutengeneza ajira nyingi zaidi kuliko ambazo zipo katika haliya kawaida. Katika sekta kama vile uvuvi; uchumi wa kijaniutalazimisha kushuka kwa mapato na ajira katika muda mfupina wa kati ili kujazia hifadhi asilia, lakini hali hii hubakia yamuda mfupi na baadaye sekta hukua na kutoa tija kubwakwa wananchi.

33. Mheshimiwa Spika,Jitihada za maendeleo nchiniTanzania lazima zifanywe kwa kuzingatia uhalisia wa mambo.Kwanza, zaidi ya asilimia 75 ya wananchi wa nchi hii huishivijijini. Hivyo, jitihada madhubuti za kupunguza umaskini na

Page 211: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

211

kuleta maendeleo lazima zilenge wakazi na uchumi wa vijijiniili kuwa na matokeo mazuri.Kuna uhusiano mkubwa kati yawatu maskini hasa wa vijijini na mazingira.

34. Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani inasemakwa muktadha huo wa uchumi wa kijani, ni kweli uwekezajiwa mradi wa kuzalisha umeme unaotokana na nguvu za maji(Stigler’s Gorge) uliopelekea kufyekwa kwa misitu kwenyeeneo ambalo ni sawa na ukubwa wa Mkoa wa Dar esSalaam, Ofisi hii ya Makamu wa Rais inatoa kauli ganikuhusiana na utekelezaji wa mradi huo?

35. Mheshimiwa Spika, uchumi wa kijani sio kama unaishiakwenye kufyeka misitu tu bali pia matumizi sahihi na endelevuya pembejeo za kilimo kama vile (mbolea na madawa)yanayotumiwa kwenye kilimo ili ardhi isiharibike na hivyokushindwa kuhimili uzalishaji wa mazao.

E. MABADILIKO YA TABIANCHI36. Mheshimiwa Spika, mabadiliko ya tabianchi nimabadiliko ya mfumo wa hali ya hewa yanayosababishwana kazi za moja kwa moja au zisizo za moja kwa moja zabinadamu, ambazo zinaongeza gesi joto (Greenhouse Gases)na kubadilisha mchanganyiko wa viwango vya gesi katikaangahewa la dunia, ambayo pia ni nyongeza ya mabadilikoya asili ya mfumo wa hali ya hewa yaliyotathminiwa nakulinganishwa kwa muda mrefu (usiopungua miaka thelatinina zaidi).

37. Aidha, Mheshimiwa Spika, Mabadiliko ya tabianchikwa kiasi kikubwa (zaidi ya 95%) yanasababishwa na shughuliza kibinadamu ikiwemo uzalishaji wa viwanda unaotoa gesiukaa (carbon dioxide) kwa kiwango kikubwa sana. Matokeoau athari za mabadiliko ya tabianchi ni:

• kuongezeka kwa joto• mvua kubwa na za muda mfupi• mafuriko• mvua ya mawe ikiambatana na upepo mkali• mvua fupi zisizo za msimu

Page 212: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

212

• ukame wa muda mrefu na unaojirudia mara kwamara.

Tabia hizi zote zimeshajitokeza hapa nchini.

38. Mheshimiwa Spika, mabadiliko ya tabianchi ni jambolinalohusu sekta zote za uchumi katika nchi, iwe kwenye kilimo,mifugo,uvuvi, miundombinu ya barabara, misitu, afya kwakuzuka magonjwa mapya, sekta ya wanyapori n.k. hivyojambo hili ni jambo kubwa sana kuliko ambavyo Serikaliinalichukulia kwa urahisi sana. Uwekezaji unaofanywaunaweza kuwa kazi bure kama hatukuwekeza vya kutoshakatika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

39. Mheshimiwa Spika, mabadiliko ya tabianchi, ambayopia huchangiwa na uharibifu mkubwa wa mazingira umeletaathari kubwa katika sekta mbalimbali za maendeleo ya jamiina sekta zingine ziko katika hatari ya kuathirika pia. Sekta hizini nishati, kilimo na usalama wa chakula, maji, mifugo (kwakuzuka kwa magonjwa ya milipuko, ukosaji wa malisho namaji), uvuvi, misitu, wanyamapori, afya, miundombinu, utalii,n.k.

40. Mheshimiwa Spika, Tanzania tayari imeshuhudiamadhara ya mabadiliko ya tabianchi, Mabadiliko ya misimuya uzalishaji kwa wananchi yanachangia kwa kiasi kikubwakatika shughuli za kiuchumi. Kila mabadiliko ya tabianchiyanayotokea kila mwaka yanapelekea gharama za uchumikuongezeka kwa asilimia 1 ya pato la Taifa . Na kadri madharayanavyozidi, inazidi kupunguza ukuaji wa uchumi na hivyokuendelea kuathiri maisha ya mamilioni ya watanzania3.Athari za mabadiliko ya tabianchi ni zaidi ya uharibifu wamazingira;huathiri na kurudisha nyuma juhudi za maendeleoya nchi hususani zinazotegemea maliasili kama Tanzania.

41. Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani inasemakwamba mabadiliko ya Tabianchi sio nadharia za kwenyevitabu tu kama ambavyo watu wengi pamoja na Serikaliinavyoamini, bali ni jambo la uhalisia usiokuwa na hatachembe ya mashaka kama ripoti mbalimbali za kisayansizinavyothibitisha.

Page 213: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

213

42. Mheshimiwa Spika,wakati nchi yetu imeridhiamikataba ya kimataifa kuhusu namna ya kukabiliana naathari za kimazingira na mabadiliko ya tabia nchi; lakinikinachofanyika ndani hasa suala la kutenga na kutekelezabajeti kuhusu masuala hayo bado, tuko nyuma sana.

43. Mheshimiwa Spika,ni ukweli kwamba Tanzaniaimekuwa inachukua hatua mbalimbali katika kuelezeamabadiliko ya tabianchi kwa muktadha wanchi yetu nahivyo kutayarisha nyaraka muhimu za mkakati kama vile “TheNational Climate Change Strategy (2012) and the ZanzibarClimate Change Strategy (2014)” ambazo zinaeleza kwa kinahatua za kuchukua katika kukabiliana na Mabadiliko yaTabianchi.

Kambi Rasmi inaitaka Serikali kulieleza Bunge hili ni kwa ninikila mara inashindwa kutenga kutoa fedha za ndani ikiwakulikuwa na Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana naMabadiliko ya Tabia Nchi. Au ndio kusema Mkakati huohaukuwa na kipegele cha bajeti kwa ajili ya kuutekeleza?

F. MAPITIO YA BAJETI ZA UTEKELEZAJI MIRADI YAMAZINGIRA NA MABADILIKO YA TABIANCHI 2018/19-2020

44. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa mabadiliko yaTabianchi nisuala mtambuka na sio tu linaathiri sekta moja, ilikukabiliana na suala hili nguvu toka pande zote inatakiwakutumika. Ofisi ya Waziri Mkuu, Fungu 37 miradi inayohusukujiandaa kwa majanga na mabadiliko ya Tabianchihaikupata hata senti moja;

I. Mradi wa kujenga uwezo wa kujiandaa na kukabilimaafa ambao ulitengewa jumla ya shilingi 176,530,200 zakutoka nje, lakini hadi Febr 2019 hakuna hata shilingiiliyopokelewa na kutolewa.

II. Mradi wa kuimarisha upatikanaji wa taarifa zaMabadiliko ya Tabianchi na mifumo ya Tahadhari, uliokuwaumetengewa jumla ya shilingi 286,923,269 fedha za nje, lakinifedha hizo hazikupatikana.

Page 214: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

214

45. Mheshimiwa Spika, kwa bahati mbaya sanaukiangalia mpango wa maendeleo kwa fungu hilo 37 miradini hiyo hiyo ya toka mwaka wa fedha 2017/18 hadi 2019/20kwa Kasma 5306 na Kasma 6575 inaombewa kuidhinishiwafedha za nje shilingi 36,577,565,737. Fedha za ndani kwakasma zote za Miradi ya Maendeleo hakuna hata shilingimoja ya fedha za ndani.

46. Mheshimiwa Spika, miradi hii kwa kiwango kikubwainahusu usalama wa wananchi na mali zao, lakini kitendocha Serikali kutegemea fedha za utekelezaji wa miradi hiikutoka nje, maana yake ni kuweka rehani usalama wawatanzania na mali zao. Jambo hili kwa kweli halikubali nalinatakiwa kukemewa kwa nguvu zote.

47. Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa Ofisi ya Makamuwa Rais Mazingira fedha za maendeleo zilizotengwa zilikuwani shilingi 5,063,340,000 lakini hadi mwezi Machi 2019 zilitolewani shilingi 2,400,099,489.50 zikiwa ni fedha za nje. Bajeti hiyoya shilingi bilioni 5.063, asilimia 69.6 zilikuwa ni fedha zamazingira na tabianchi lakini hadi Februari 2019 hakuna hatasenti moja ya fedha za ndani iliyotolewa.

48. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka huu wa fedha miradihiyo inayohusu mazingira na mabadiliko ya Tabianchiinaombewa jumla ya shilingi 18,218,915,441.73. Katika fedhahizo zinazoombwa hakuna hata shilingi moja ya fedha zandani inayoombwa, hili nalo ni jambo la kujiuliza kama kweliSerikali yetu inaona umuhimu wa mazingira na mabadilikoya tabianchi? Tukumbuke kuwa miradi yote inayojengwakama hatukuwa na mpango mahususi wa kukabiliana namabadiliko ya tabianchi inaweza kuwa ni kazi bure kwamuda mfupi sana.

G. MAOMBI YA FEDHA KWA MWAKA 2019/201949. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Makamu wa Rais inaombakuidhinishiwa shilingi bilioni 7.86 kwa Fungu 26, na shilingi bilioni29.07 kwa fungu 31 kwa ajili ya matumizi ya kawaida namatumizi ya miradi ya maendeleo. Kambi Rasmi ya Upinzaniinatoa angalizo tu, kwani mwaka wa bajeti unaomalizika

Page 215: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

215

Fungu 26 iliidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni 6.5 na kwa fungu31 iliidhinishwa jumla ya shilingi bilioni 15.065.

50. Mheshimiwa Spika, kati ya hizo zilizoombwa walipewakwa fungu 31 walipokea asilimia 52.7 hadi mwezi Februari,2019. Kambi Rasmi ya Upinzani inauliza ni kwa nini muombekubwa zaidi wakati mnaona uwezo ni mdogo au kipaumbelecha Serikali sio Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi?

H. HITIMISHO51. Mheshimiwa Spika, Ofisi hii ya Makamu wa RaisMuungano na Mazingira ndiyo yenye mamlaka kamakutakuwa na dhamira na nia njema ya kuhakikisha kwambaKero na malalamiko ya Muungano zinamalizika. Pili ndiyoyenye mamlaka ya kuhakikisha kuwa Tanzania tunaingiakwenye uchumi wa kijani, kama ambavyo imeelezwa hapoawali.

52. Mheshimiwa Spika, kwa masikitiko makubwa nikwamba ofisi hii inashindwa kusimama kwa miguu yake nakuhakikisha yale yote yaliyomo kwenye Hati Idhiniinayasimamia kwa ukamilifu wake na badala yakemalalamiko ya Muungano bado ni kitendawili japokuwatunaambiwa vikao vya pamoja vinakaa, lakini matunda yavikao hivyo hayaonekani kwa wananchi.

53. Mheshimiwa Spika, tumepokea taarifa kuwa vilevinavyoitwa vikao vya kutatua kero za Muungano kupitiaKamati ya Pamoja vinaelekea kurasimishwa zaidi kwakutengenezewa ratiba yake na kuundiwa kamati mbili yaaniile ya Uchumi na Fedha na ile ya Sheria na Utawala katikania ya kutekeleza maamuzi kadri yanavyofikiwa.

54. Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inatoawito kuwepo kwa uwazi zaidi katika hatua za utatuzi wachangamoto za Muungano na pia hatua shirikishi katikaviwango mbali mbali ili kuondosha dhana kuwa Muunganohuu ni wa viongozi zaidi na sio wananchi

Page 216: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

216

55. Mheshimiwa Spika, Miradi zaidi ingepaswa kubuniwaambayo ni ile Tanzania kuwa na uchumi endelevu na wenyekutoa ajira kwa wananchi wengi (Uchumi wa kijani niuboreshaji wa uchumi na ustawi wa jamii unaozingatiauzalishaji na matumizi yasiyoharibu mazingira).

56. Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kwamba Tanzania badoina fursa nyingi katika kuifanya nchi yetu kuwa kwenyeuchumi wa kijani, na fursa hiyo ilikuwa ni kuifanya TANZANIAkutumia rasilimali gesi kwa kiwango kikubwa ili kudhibitimatumizi ya nishati itokanayo na miti (kuni na Mkaa) hapanchini ili juhudu zinazofanywa na Taasisi mbalimbali za Serikalina zisizo za Kiserikali matunda yake kuonekana.

57. Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, kwaniaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani, naomba kuwasilisha.

………………………………Latifah H.Chande (Mb)

K.N.Y MSEMAJI MKUU – KAMBI RASMI YA UPINZANI-OFISI YAMAKAMU WA RAIS

MUUNGANO NA MAZINGIRA16 Aprili, 2019

MWENYEKITI: Sasa tunaanza na uchangiaji, tunaanzana Mheshimiwa Dkt. Sware dakika tano, anakuja MheshimiwaHawa dakika tano halafu atakuja Mheshimiwa Najma naedakika tano.

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kwa nafasi. Nitaanza kwa kutafakarikwa pamoja. Ni dhahiri kwamba Taifa letu bado halijatambuathamani ya mazingira na afya ya mazingira na hili lipolinajionesha dhahiri ndani ya Serikali baina yetu sisi hapaWabunge hata na jamii inayotuzunguka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema haya kwa sababuukiangalia tu kwa Wizara zilizopita humu ndani WaheshimiwaWabunge tulikuwa tunagombania nafasi za kuchangia kama

Page 217: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

217

ni TAMISEMI au ni Utawala Bora au ni Ofisi ya Waziri Mkuu navitengo vyake lakini sasa kama tulikuwa tunakimbilia kuteteashule, barabara, vyakula, afya na kadhalika tulitakiw atujuekwamba kiini kinachotubeba sisi kama Taifa na afya nauchumi wa Taifa, ni mazingira. Mazingira ndiyo kiini chamaendeleo. Tungelitambua hilo tukaisimamia Serikaliipasavyo tungetoka kwenye huu umaskini, kwa sababu haliya umaskini inajengwa na vitu vikuu vitatu, uchumi duni,utawala bora na uharibifu wa mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi Tanzania mazingira ndiyoyanayotubeba, kwa sababu hata hao wananchi wetu hukuvijijini asilimia 96 wanategemea maliasili, zaidi ya asilimia 90wanategemea nishati kutoka kwenye maliasili. Kamatunaongelea viwanda, maji safi na salama inategemea nahali ya mazingira iliyopo. Kama mazingira yanachechemeahatutakaa tukote katika dimbwi la umaskini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulitunga Sera ya Taifa yaMazingira ya mwaka 1997 kama Mheshimiwa Waziri husikaalivyosema na iliainisha mambo sita makuu ya uharibifu wamazingira. Tuliainisha changamoto za uharibifu za vyanzo vyamaji, hii tunaangalia mito, mabwawa, bahari na kadhalika;tuliainisha uharibifu mkubwa wa maji safi ambayo yanaendakujenga uchumi kwa sababu kusipokuwa na wananchiwanaopata maji safi inaenda kuharibu afya yao binafsi,mifugo au na chochote kinachotegemea maji safi; tuliainishauharibifu wa ardhi, ardhi ndiyo iliyobeba miundombinuambayo tunaitegemea sisi aidha sekta za kil imo navinavyobebwa na kilimo au ni shughuli za madini nakadhalika; na tuliainisha kwamba kuna upotevu mkubwa wamakazi ya viumbepori na bioanuwai. Hivi vyote kwa ujumlawake ni nguzo hizo sita ambazo zinabeba shughuli zakiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miaka 22 i l iyopitaMheshimiwa Waziri umesema haya na sasa hivitunachanganua hii sera kwa upya wake, ardhi inasemaje,uharibufu wa ardhi upo katika percent ngapi na una-reflectvipi hali ya uchumi? Kwa sababu unapoharibu ardhi

Page 218: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

218

inamaana unaharibu na uzalishaji ambao unategemeanana ile ardhi. Kama unaharibu vyanzo vya maji hupati majisafi au maji yanayotakiwa unaenda kuwa reflected kwenyeshughuli za kiuchumi. Tunalia kila siku kuhusu bajeti ya majihaitoshi, sasa tungeweza ku-link kuhusu upatikanaji wa maji,budget wise na upatikanaji maji kwenye kutunza vyanzo vyamaji na njia za maji basi tungeweza kwenda sambamba nakukuza uchumi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sera yetu imeainisha mambosita makubwa ambayo bado hayana ufumbuzi kwa sababubado tunaharibu mazingira, sasa nayo yanakuwa reflectedkwenye uchumi wetu. Uchumi wa mtu mmoja mmojaunategemea na hayo mazingira kwa sababu kila mtuanayategemea mazingira hayo. Mfano tu mfupi, usipokuwana maji safi kwanza ukinywa maji machafu au maji hayakosalama jamii hiyo husika inapata maradhi, kwa hiyo, inaendaku-reflect bajeti ya afya, bdo tunazidi kuididiza. Kama hupatimaji kwa ajili ya kilimo chako cha umwagiliaji unategemeamvua na sasa hivi kuna mabadiliko ya tabianchi ina maanauzalishaji wako utakuwa wa wasiwasi hutakaa utoke. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiweza kuipa nguvu Sheriayetu ya Mazingira ambayo imeainisha mambo makuumanne, kuna utafiti, uelimishaji na kadhalika, hii sekta inawezaikatutoa hapa kwenye dimbwi la umaskini.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante kwa mchango mzuri. (Makofi)

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: MheshimiwaMwenyekiti, naomba tuwape bajeti inayotakiwa, ahsante.(Makofi)

MWENYEKITI: Tunaendelea na Mheshimiwa Hawa.

MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia katika Ofisi ya

Page 219: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

219

Makamu wa Rais na nitajikita zaidi kwenye suala zima lamazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe masikitikoyangu makubwa sana kuhusiana na bajeti ya Wizara hii.Kama ambavyo hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzaniimesema imekuwa ni mazoea kwa Ofisi ya Makamu wa RaisMazingira kutokutengewa bajeti ya kutosha na hata hiyokidogo ambayo inawekwa haifiki kama ilivyokusudiwa, hivyokupelekea ufanyaji kazi katika hii kuwa mgumu kulikoambavyo tunatarajia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyotunafahamu suala zima la mazingira ndiyo roho za sisiWatanzania. Tunapodharau mazingira tutegemee tutapataelimu na afya tunajidanganya. Bila mazingira hakuna afya,elimu na miundombinu vinginevyo tunajisumbua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nil isikia hotuba yaMheshimiwa Waziri Mkuu wakizungumzia kuhusiana na sulazima la ukatazaji wa matumizi ya mifuko ya plastiki. Bahatinzuri niko kwenye Kamati ya Mazingira, suala hili lilianza mudamrefu na sisi kama Kamati tulijaribu sana kuishauri Serikali nakuangalia ni kwa namna gani wanaweza wakafanya ilikusaidia hawa wenye viwanda ambao wanatengenezamifuko ya plastiki waweze kutengeneza kwa teknolojia yakisasa. Teknolojia za kisasa zipo ambapo mifuko hii minginewatu wanatengeneza na inaoza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kama Serikaliimejiandaaje baada kuzuia matumizi haya kwa nchi jiraniambazo zinazalisha kwa wingi kuliko tunavyozalisha Tanzaniamifuko ya plastiki kuingia nchini kwetu? Kwa sababu ni ukweliusiopingika Tanzania tunazalisha mifuko ya plastiki kwaasilimia 30 peke yake lakini asilimia 70 ya mifuko ya plastikiinayoingia nchini kwetu ni mifuko inayotoka nje ya nchi. Je,Serikali imejipanga namna gani kuhakikisha kwamba mifukohii haiwezi kuingia nchini Tanzania na matumizi ya mifuko yaplastiki yakaendelea. (Makofi)

Page 220: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

220

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini wakati tunakatazamifuko ya plastiki tumejiandaa na vifungashio vya aina gani?Kwa sababu nachokiona hapa ni makatazo tu lakinihatujaambiwa kwamba tunakwenda kutumia mifuko ya ainagani, leo tutakuwa tunabeba mikononi bidhaa amatutakuwa tunafanyaje? Kwa hiyo, tungeomba sana Wazirianapokuja hapa atuambie ili Watanzania wajue baada yamifuko ya plastiki kukatazwa tarehe 1 sijui Mei au Julai, niniambacho kitatumika mbadala badala ya mifuko hii yaplastiki? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala ya mazingira nimtambuka kama nilivyosema, kwa hiyo lisiishie kwenyemasuala ya mifuko ya plastiki peke yake, je, suala la mkaalimefikia wapi mpaka sasa? Kwa sababu ya kupata mkaawatu wanakata sana miti. Leo tunaambiwa nchi inakwendakuwa jangwa kwa asilimia 61, hii ni asilimia kubwa sana kwanchi ya Tanzania, tunapoelekea vizazi vyetu vitakuja kukutanchi imeshakuwa jangwa, hali ni mbaya kweli kweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunapofikiria zaidimifuko ya plastiki, mimi huwa nasema vitu vidogo vidogoMheshimiwa Waziri anajua, tusing’ang’anie na vitu vidogovidogo kama mifuko ya plastiki tuangalie uhalisia wamazingira, vitu vingi zaidi vinategemea mazingira yetu. Kamamazingira hayataboreshwa tusije tukategemea hivi vyoteambavyo tunavifanya vitaendelea kuwepo kwa sababu nilazima vitapotea kutokana na kwamba mazingira siyo rafiki,tunakwenda kuingia kwenye ukame wa hali ya juu. Kamaambavyo mmeshuhudia kuna maeneo ambayo mvuahazijanyesha kabisa, kuna maeneo kama kwenye Mikoa yetuya Tabora tulikuwa tunapata mvua misimu miwili, leo Taboraukienda ni msimu mmoja tu ndiyo mnapata mvua na mvuazenyewe siyo za zinatosheleza, hali ni mbaya kweli kweli kilamaeneo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sana Serikaliiangalie upya kuhakikisha kwamba bajeti inayotakiwa katikaOfisi ya Makamu wa Rais inapelekwa kama ilivyokusudiwakuliko kutegemea bajeti za wafadhili. Hawa wafadhili leo

Page 221: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

221

umeomba bajeti ya asilimia 40 unaletewa bajeti asilimia 10,mwisho wa siku mambo yanakuwa hayaendi ama hawaletikabisa. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante kwa mchango mzuri.Tunaendelea na Mheshimiwa Najma, ajiandae MheshimiwaJosephine Genzabuke, wote dakika tano tano.

MHE. NAJMA MURTAZA GIGA: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kwa kunipa dakika hizo tano. Kwanzakabisa, naanza kwa kuunga mkono hoja hii ya Wizara yaMuungano. Nitumie fursa hii kumuunga mkono sana nakuwapongeza Waziri wa Muungano, Mheshimiwa JanuaryMakamba na Naibu Waziri wake Mheshimiwa Mussa, kwakazi nzuri wanayofanya lazima niwapongeze. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia natumia fursa kwakipekee kabisa kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa namnaambavyo ameondoa changamoto iliyokuwa inatukabilimuda mrefu ya deni la ZECO. Hilo lazima tushukuru sana nakupongeza na hii inathibitisha kwamba Mheshimiwa Rais nimuumini wa kweli wa Muungano wetu. Hilo lazima tulioneshena Watanzania lazima waelewe hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo mazuriyanayofanywa na Mheshimiwa Janauary na timu nzima,napenda kusema kwamba sote tunaupenda Muungano,mimi ndiyo muumini wa kwanza wa Muungano. Katikakuupenda Muungano tunaomba hayo ambayommeyakusudia na kuyaendeleza muyafanyie kaziinavyostahiki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nisisitize maeneomatatu kwa haraka haraka. Fursa za kiuchumi Zanzibar nijambo linalopigiwa makelele siku zote. Miaka ya 1985 mpakatunakwenda 2000 wenzetu wa Tanzania Bara walikuwawanakuja kufanya biashara Zanzibar, wanabeba mali kule

Page 222: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

222

na wanatunufaisha Wazanzibari. Sijui kimetokea nini hapakatikati, ndugu zetu wa Tanzania Bara mnahamia Rwanda,Burundi, Kenya na Uganda mnatuacha jirani zenu, hebuangalieni hapo tunakwenda wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, ni kwenye masualaambayo tunaungana, nakwenda kwenye Balaza la Mitihanila Taifa, hapo bado hapajakaa vizuri. Kuna communication,coordination na cooperation ndogo, tuweke sawa hapo.Balaza la Mitihani lile na chombo maalum kinachotambulikakisheria ili ku-coordinate, cooperate na ku-communicatebaina ya Wizara zetu mbili, tutakwenda vizuri, tunaupendaMuungano. Pia NACTE kwenye elimu ya juu, tuangaliekinachotambulika Tanzania Bara na Zanzibar kitambulike.Tunaomba tufanye hayo kwani tutakwenda vizuri naMuungano wetu Mheshimiwa January na timu yako. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine zuri kabisa, naombaniliseme kwa Watanzania wote kuhusu Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania. Katiba ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania imejenga misingi imara ambayo inawezakulidumisha Taifa letu miaka mia ijayo. Kwa hiyo, yalemarekebisho madogo madogo ambayo tunaombayanaendelea kufanyika siku zote isiwe ni neno la kuletamjadala. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaendelea namarekebisho madogo madogo, Katiba yetu iko vizuri natutakwenda nayo vizuri hata miaka mia ijayo kwa sababukila kilicho ndani ya Katiba ile kinatafsirika vizuri. Hiyoimplementation ni jambo lingine wala siingilii lakini Katibayenyewe kama Katiba inatufaa na ndiyo maana ikatufikishamiaka 55 hii na tukiwa tunasifiwa na mataifa yoteulimwenguni kwa Muungano ambao tunao, kwa ninitusiringe? Lazima turinge na Taifa letu kwa sababu Muunganowetu ni mzuri, uko very unique, inatakiwa na mataifa yotewaige kwetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ili tuweze kuendelezahaya, hizo changamoto tuzimalize kwa muda unastahiki ili

Page 223: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

223

tuweze kujivunia zaidi Muungano wetu na kuupenda zaidiMuungano wetu. Mimi naipenda Zanzibar, naipendaTanzania Bara lakini nakupenda Muungano zaidi kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Genzabuke,dakika tano na ajiandae Mheshimiwa Saada Mkuya, dakikatano.

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwanza napendaniipongeze Serikali ya Awamu ya Tano kwa jinsi inavyofanyakazi. Naomba nimpongeze Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisiya Makamu wa Rais, Mheshimiwa January Makamba, Naibuwake, Katibu Mkuu pamoja na watendaji wote wa Wizara hiikwa hotuba waliyotuletea leo hapa Bungeni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nitazungumzia kuhusumazingira. Kuanzia 1995, Mkoa wa Kigoma ulipata na wimbikubwa la wakimbizi lakini pamoja na Mikoa ya jirani ikiwemoKagera na Rukwa. Kutokana na wimbi kubwa la wakimbizikufika katika mikoa hiyo ni ukweli usiopingika yametokeamadhara makubwa ya uharibifu wa mazingira. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, walipoingia watu kutokaBurundi kwa mara ya kwanza katika Wilaya ya Kasulu walifikiakatika Kambi moja ya Mtabila, wakati huo mazingirayaliharibika kwani miti mingi ilikatwa. Kwa hiyo, unawezakuona ni jinsi gani mazingira yalivyoweza kuharibika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata waliporudishwawalienda tena kwenye Kambi moja ya Nyarugusu ambayoni kubwa, ina wakimbizi wa kutoka DRC na Warundi. Kwahiyo, ni jinsi gani unaweza kuona mazingira katika Mkoa waKigoma yalivyoharibika na kule Kibondo vilevile ipo Kambiya Nduta lakini Kakonko iko Kambi ya Mtendeli. Kwa hiyo,naiomba Serikali kwa kushirikiana na Shirika la UNHCRkuangalia ni jinsi gani zinaletwa pesa kwa ajili ya kunusuru

Page 224: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

224

mazingira katika mikoa hiyo ambayo ilipokea wakimbizi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naiomba Serikali iwezekuipatia Ofisi ya Makamu wa Rais pesa za kutosha kwa ajiliya kuweza kufanya ziara katika mikoa hiyo lakini kuwezakupeleka pesa kwa ajili ya kukabiliana na tatizo hili lamazingira. Ukienda kuangalia jinsi misitu ilivyoteketea, kwakweli ni kilio kikubwa sana na wakati mwingine uharibifu wamazingira unaendelea siyo kwamba eti mazingirayanahifadhiwa, hapana. Bado tuna kila sababu yakuhakikisha Wizara hiyo inapatiwa pesa ili kwenda kunusurumikoa ile ambayo imeathirika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Muungano, naombawanafunzi waendelee kufundishwa umuhimu wa Muunganokuanzia darasa la kwanza mpaka vyuo vikuu. Kwa sababuwatoto wakianza kufundishwa wakiwa bado ni watotowataendelea kuupenda tangu mwanzo mpakawatakapoendelea kuwa wakubwa na wataendeleakuulinda kwa nguvu zao zote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, naungamkono hoja, ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Saada, dakika tano.

MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipatia nafasi hii na naunga mkono hojana nazipongeza Serikali zote mbili za Jamhuri ya Muunganowa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibarkwa kuona kuna nia ya dhati kabisa ya kutatua changamotoza Muungano. Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Waziritunawapongeza pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa ni dakika tano,itabidi niende haraka haraka. Katika kitabu cha MheshimiwaWaziri, ukurasa wa 14 ameelezea kuhusiana changamoto yaongezeko na gharama za umeme ambapo Serikali yaAwamu ya Tano imehakikisha kwamba changamoto hii

Page 225: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

225

inaondoka na tunaipongeza sana kwa hilo. Hata hivyo,changamoto hii ya VAT si kwamba inakwenda moja kwamoja kuondoa gharama za umeme kwa mwananchi wakawaida wa Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaombaMheshimiwa ukiwa mwenye dhamana ya kuratibu masualaya Muungano, Wizara ya Nishati ihakikishe kwamba yuleConsultant ambaye amepewa kazi ya kuangalia gharamaza umeme anamaliza kazi hii mapema zaidi ili wananchi sasawaweze kunufaika kutokana na kupungua kwa gharamahizo. Hii VAT imeondoka lakini haijaondoa hizo gharama kamavile ambavyo tulitarajia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, MheshimiwaWaziri amejikita zaidi sasa kuendelea kutoa elimu. Mchangiajialiyemaliza kuongea Mheshimiwa Genzabuke amesisitiza jinsigani Wizara iangalie hii elimu inapelekwa katika shule zamsingi, sekondari na vyuo vikuu. Naamini Mheshimiwa Waziriwakati hilo l inaendelea mimi nadhani elimu kuhusuMuungano ianzie humu ndani katika Bunge letu Tukufu kwasababu bado tunaona hata baadhi ya Wabunge ile conceptya Muungano haijatuingia sawasawa. Ndiyo maana hatabaadhi tu ya kauli zinaweza zikawa zinatoka ambazo unahisikwamba huyu mtu bado hajafahamu hasa nini maana yaMuungano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hilo hata katika ngazi yawatendaji linatokea. Changamoto zinazoonekana ni kwasababu ya issue za Muungano hazijawa mainstreamed. Kamatumeweza ku-mainstream issue za HIV, gender na mazingira,Muungano ni issue ambayo inatakiwa kuwa mainstreamed,wether iko kwenye eneo ambalo taasisi zetu zinafanya kazikwenye Muungano au katika taasisi ambazo siyo zaMuungano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaloliona sasa hiviMheshimiwa Waziri anayeshughulika na Muungano yeyendiye anakuwa responsible kuangalia masuala ya Muunganolakini Wizara ambazo tunaziona tu kikawaida kwamba siyo

Page 226: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

226

Wizara za Muungano lakini moja kwa moja lolote linalofanyikakatika Wizara zile linaathiri upande mwingine wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania.

Kwa hiyo, Muungano huu siyo Muungano ambaoanausimamia Mheshimiwa January Makamba ni Muunganoambao sote tunakiwa tusimamie katika maeneo yetutunayofanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kumekuwa nautaratibu Mawaziri ambao wanachaguliwa katika Taasisi zaMuungano mara moja wanakwenda Zanzibar, wanamwonaMheshimiwa Rais na viongozi wengine lakini I do hope hilohaliishii kwenye kwenda kumuona Mheshimiwa Rais,linatakiwa liwe katika kazi zetu za kila siku. Bahati mbaya waleambao wameji-term kwamba Wizara zao siyo za Muunganohatuwaoni kwenda Zanzibar labda siku ya Sherehe zaMapinduzi, tunaomba sana hii nchi yetu ni Jamhuri yaMuungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ukurasa wa 16 wahotuba ya Mheshimiwa Waziri ameeleza mambo mengiyaliyopatikana ikiwa ni pamoja na gawio la Benki Kuu.Tunashukuru sana Benki Kuu ya Tanzania imeendelea kutoagawio. Hii ni taasisi ya Muungano na inasimamia fedha zaSerikali lakini bado Mheshimiwa Waziri kuna taasisi zaMuungano na gawio halitolewi. Kuna taasisi ambazo zinaoperate katika Muungano lakini hatuoni gawio kwendaZanzibar. Kwa mfano, Mashirika yetu kama TCRA, AICC, NIC,TTCL, bado gawio haliendi Zanzibar. Hizi ni taasisi zaMuungano na inatakiwa gawio linatolewa kwa Serikali yaJamhuri na Zanzibar ipate.

MWENYEKITI: Ahsante kwa mchango mzuri.

MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana na naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, niliombwaMwongozo na Mheshimiwa Khenani kuhusu kutopata clip

Page 227: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

227

zake na hii nafikiri wengi wanalalamika lakini tarehe 9 Mei,2019, Kiti kilitoa ruling hapa, haki ya Mbunge ni Hansard, clipna vitu vingine ni privilege tu basi. Kwa hiyo, tumieni PRkuzipata hizo clip mnazoziomba, haki yako ni Hansard, ukikosaHansard una haki ya kulalamika.

Waheshimiwa Wabunge, vilevile kulikuwa naMwongozo mwingine, Mheshimiwa Mkuchika inakuhusu hii,kuhusu ustaarabu wa michango inayochangishwa ndani yaBunge kutangazwa. Kuna michango hapa imekusanywa natimu moja huko nje na Wabunge wengi wametoa lakinitaarifa rasmi ya mchango ile mpaka leo hamna.

WABUNGE FULANI: Eeeh.

MWENYEKITI: Sasa tunaomba wahusika wa michangoile…

WABUNGE FULANI: Ya nani?

MWENYEKITI: Anajua huyu, Club ya Yanga waliombamichango kwa Wabunge humu, kwa hiyo, Wabungewanataka kupata taarifa ya michango yao. (Kicheko)

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nje yaBunge hiyo.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, baada yamaneno hayo, nasitisha shughuli za Bunge mpaka saa 11.00jioni.

(Saa 7.00 Mchana Bunge lilisitishwa hadi Saa 11.00 jioni)

(Saa 11.00 jioni Bunge lilirudia)

MWENYEKITI: Tukae, Katibu!

Page 228: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

228

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano

na Mazingira

(Majadiliano Yanaendelea)

MWENYEKITI: Waheshimiwa tunaanza na MheshimiwaJaku Hashim ajiandae Mheshimiwa Khamis Mtumwa.

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti,bila kupoteza muda, nianze kwa ni-declare interest kwambamimi ni mmoja wa wanaohitaji Muungano na Wazanzibarwengi wanauhitaji, lakini niformula tu ya kuuendeshamuungano huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, nichukue fursa hiikuwashukuru sana viongozi wetu wawili wakubwa;Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na MheshimiwaRais Dkt. Ali Mohamed Shein kwa ushirikiano mkubwa wakutatua tatizo la mazingira ya hali ya VAT ya umeme natumefikia mahali muafaka; mwezi huu wa Aprili, aliwahikuzungumza Mheshimiwa Najma hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nimpongeze sanaMheshimiwa Waziri, ndugu yangu Mheshimiwa JanuaryMakamba, pamoja na kuambiwa na Mawaziri wenzake niMzanzibar, akubali hivyo hivyo. Ameonesha uwezo mkubwasana katika Mawaziri ambao wameitwa Zanzibar wakafikakwa wakati, mmojawapo ni yeye. Haya ndiyo malezi mazuribinadamu anatakiwa kulelewa. Ameonyesha ushirikiano kwahali na mali bila kujali mvua wala jua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sitamfanyia hakiMheshimiwa Naibu Waziri wake tumemshuhudia sana katikakutatua matatizo hayo. Pia nitakuwa sijamfanyia haki nduguyangu, jirani yangu Mheshimiwa Keissy. Nakushukuru sana kwautulivu wake alioonesha kwa kipindi kirefu baada ya kero hizi

Page 229: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

229

za Muungano. Ametulia sana Mheshimiwa Keissy, namshukurusana na huu ndiyo uungwana.

Mheshimiwa Mwenyekiti,…

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: …nataka kuuliza…

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: …nini Muungano?…

MHE. ALLY K. MOHAMED: Taarifa.

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: …maana ya formula yaMuungano?

MHE. ALLY K. MOHAMED: Nataka nimpe taarifa huyu.

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: …umuhimu wa kuunganani watu kuwa pamoja, kushirikiana katika nyanja mbalimbalikatika kuungana kiuchumi…

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: …ulinzi,…

MWENYEKITI: Taarifa

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: …maendeleo

MWENYEKITI: Taarifa.

Page 230: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

230

T A A R I F A

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti,nampa taarifa mzungumzaji, anasema mimi nimetulia mudamrefu. Mimi sikuwa napinga Muungano, nilikuwa napingahabari ya bidhaa kutoka Zanzibar ambazo hazilipiwi ushuru,ndiyo nilikuwa napinga. Mambo mengine mimi…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Jaku, unapokea taarifahiyo?

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba afute kauli yake. Kule Wazanzibar wanalipa ushuru,vinginevyo kwa vyovyote vile kungekuwa hakuna Serikali palebila kulipa ushuru. Naomba umruhusu afute kauli yake kwaSerikali ya Mapinduzi Zanzibar. Siyo kauli ya kiungwanaaliyoitumia. Hiyo siyo kauli ya kiungwana, yeye atetee mamboyake kule Nkasi; maji hakuna, barabara ndiyo vya kutetea.Wazanzibar wapo wenyewe wasemaji.Wakuu wa Duniawalishirikiana katika Jumuiya za Afrika Mashariki waliombaEuropean Union kwa mashirikiano makubwa sana, lakinijambo la kushangaza na la kusikitisha, nije katika bidhaa zabiashara hasa kutoka upande wa Zanzibar kuja kutafuta sokohili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni geti kubwa la Bandariya Tanzania Bara na ndiyo soko kubwa lenye walaji wengiwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kati. Hili suala limekuwa nila muda mrefu, vinginevyo labda ifutwe hii kauli. Kuna mahaliKenya inataka kwenda, Rwanda inataka kwenda na Burundiinataka kwenda, lazima ipite katika gateway kubwa hii yaBandari ya Dar es Salaam. Sasa patafutwe njia. Hili sualalimekuwa la muda mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Zanzibar wapo katikaJukuiya ya Afrika Mashariki, vinginevyo, watumwe Wabungewetu wa Afrika Mashariki na Kati wapeleke hoja binafsiZanzibar itolewe katika hili. Hili ni soko lenye walaji karibumilioni mbili na kuendelea. Hili ni jambo la kufikiriwa.

Page 231: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

231

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha kushangazaMheshimiwa Waziri Dkt. Mpango lilitokea tatizo la Kenya,bidhaa za Kenya kuja huku ilikuwa maziwa sijui na cigarretena bidhaa za hapa kwenda kule, tatizo likatatuliwa maramoja. Sisi ndugu wa damu. Mheshimiwa January utapa kazikubwa sana haya mambo, lazima ufuatilie; na yote utakuwamasuuli hata kwa Mwenyezi Mungu. Haya ni mambo yakuyafikiria. Mmetatua kero za mbali za karibu mmeziacha!Lah, hii siyo halali, mlifikirie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bila kupoteza muda,Mheshimiwa Dada yangu Mheshimiwa Saada aliyazungumzaMashirika ya Muungano. Kwanza naipongeza sana Benki Kuu.Katika Shirika linalotoa pesa wakati, BoT; 4.5 ile inapatikanakwake tofauti na Mashirika mengine. Mheshimiwa NaibuWaziri yupo, Waziri wako hayupo, hii 4.5 tulikuwanayo yamkataba tu, ni ya muda. Zanzibar imekua, population imekua,IMF walitumia kutokana na kigezo cha watu lakini mlifikirie.Mheshimiwa January lifuatilie suala hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mapato ya NBC,Zanzibar imo. Kuna Benki ya NMB, Zanzibar imo; kuna PostalBank, Zanzibar imo; kuna TTCL, Zanzibar imo; kuna TCRA,Zanzibar imo; kuna TCAA, Zanzibar imo; imepata nini? Hayani matatizo. Zanzibar imepata lini? Haielekei.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ajira za mambo yaMuungano Mheshimiwa January; kuna Jeshi, kuna migration,kuna Polisi, kuna Mambo ya Nje. Mnapogawa hizi kazi mfikiriemtapeleka namna gani Zanzibar, zinahitajika, Ajira imekuwaissue. Muungano wetu keshokutwa Mungu akijaalia unatimizamiaka 55, twende vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa uchumi siyo sualala Muungano, ndiyo hoja yangu ilipo; Zanzibar ina haki yakeya kutumikia Wazanzibar wake na Tanzania Bara ina haki yakutumikia.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

Page 232: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

232

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Khamis Mtumwa,jiandae Mheshimiwa Juma Kombo.

MHE. KHAMIS MTUMWA ALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nianze kwa kukushukuru kwa kunipa nafasi nami nichangieWizara hii ya Muungano na Mazingira. Pia naomba nichukuefursa hi kumpongeza kwa dhati kabisa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John PombeJoseph Magufuli na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Sheinkwa kuhakikisha kwamba wanaulinda, kuuhifadhi nakuutetea muungano wetu huu mpaka sasa unafika miaka55. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia napenda kuchukua fursahii kumpongeza Waziri Mkuu na Makamu wa Rais kwa kazikubwa wanayoifanya ya kuhakikisha kwambawanazikusanya kero hizi za Muungano na kuwezakuzifanyiakazi hatua baada ya hatua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile napenda kuchukuafursa hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziriwake pamoja na Katibu Mkuu kwa kuweza kuzichanganuana kuzitafuta kero hizi na hatimaye tunaona matokeo yakeya kuweza kutatuliwa moja hadi moja kwa kadri ya sikuzinavyokwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijielekeze sasakwenye suala zima la umuhimu wa Muungano wetu.Muungano wetu huu ni wa historia na unatusaidia sanapande zote mbili ya Tanzania Bara na ya Zanzibar na hasakwenye suala zima la kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshuhudia mambombalimbali ya kibiashara yanafanyika pande mbili hizi nawatu hunufaika, lakini bado kuna kikwazo kikubwa chakufanya double taxation ambayo inafanyika Zanzibarukipeleka kitu ukileta Tanzania Bara ulipie tena ushuru maraya pili. Hii bado ni kero na tunaipigia kelele sana na Wabungewengi wa Zanzibar wanaipigia kelele hii kwa sababu bado

Page 233: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

233

inaonekana haitendi haki kwa pande zote mbili zaMuungano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia napenda kuzungumzakuhusiana na suala la ushiriki na ushirikiano mdogo kuhusumasuala ya Kitaifa na kikanda. Kama Mheshimiwa Wazirialivyoelezea katika kitabu chake hiki, amefanya juhudi zakuunda Kamati ya kuweza kuhakikisha kwamba changamotohizi zinafanyiwa kazi za kielimu, nafasi za masomo na vilevileamezungumza kuhusiana na suala la utafutaji wa fedha kwamasuala ya mambo ya nje ya misaada na mikopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile ametuambiamasuala mbalimbali yameundiwa Kamati ambayoatahakikisha kwamba soon tunaona matokeo yake.Napenda sana kumshauri Mheshimiwa Waziri tutakapokujakwenye bajeti ya mwakani, changamoto hizi tusiwetunazirejea tena kila siku katika Bunge letu hili Tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naomba nizungumziekuhusiana na suala la Elimu ya Muungano. Wenzanguwametangulia kusema kwamba ipo haja ya kutoa taalumakwa yale ambayo yanatatuliwa katika Serikali yetu ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania kuhusiana na zile kero zaMuungano, kwa sababu vijana wanaoamkia sasa hivi badowana mentality kichwani kwamba Muungano siyo mzuri, auunatunyonya sana kule Zanzibar. Kiukweli Muungano unafaida kubwa sana za kiuchumi, kisiasa na kijamii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kukiwa na utoaji waelimu katika maeneo mbalimbali hasa kule Zanzibar juu yachangamoto ambazo zinatatuliwa na umuhimu waMuungano wetu, mimi nina imani kwamba muungano huuutazidi kudumu zaidi ya miaka 100 badala ya miaka 55 hiituliyofikia sasa hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia napenda kuzungumziasuala la ushirikiano kuhusiana na masuala mbalimbali yaMuungano hasa katika Taasisi hizi za ukaguzi. Tumeshuhudiakwamba Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) hufanya

Page 234: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

234

ukaguzi katika Taasisi mbalimbali au katika Taasisi za Ubalozibila kushirikiana na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu Zanzibar. Suala hili tumeshalizungumza sana kwambawale wenzao ni vyema kwamba wakashirikiana nao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, madhali hili suala siyo laMuungano lakini ni vyema zaidi wakaenda kukagua katikaTaasisi za Muungano ambazo zipo nje hasa Ubaloziwawashirikishe na wenzetu kule ili wapate exposure namambo mengine ambayo wataweza kujifunza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri aliniahidisiku moja kwamba tutafuatana mimi naye twende kuleZanzibar, tuone, tukae na Taasisi ambayo inahusiana na Ofisiya Mdhibiti na Mkaguzi kuangalia zile changamoto zaoambazo zinawakabili, lakini alitingwa na kazi. Naamini baadaya Bunge hili au baada ya kujibu hoja zetu hizi tutafuatana ilituone tatizo hili pia linatatuka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nampongezaMheshimiwa Waziri; baada ya kauli ya Meshimiwa Waziri Mkuukusema kwamba ikifiuka tarehe 1 Juni, 2019 suala la mifukoya plastic ni marukufu, Mheshimiwa Waziri na Naibu wake naKatibu Mkuu wake wamefanya jitihada ya haraka kuonanana wadau na kuweza kuzungumzia mambo mbalimbaliambayo…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante kwa mchango mzuri.Mheshimiwa Juma Kombo, ajiandae Mheshimiwa Mtolea.

MHE. KHAMIS MTUMWA ALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja. (Makofi)

MHE. JUMA KOMBO HAMAD: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nami nafasi hii ya kuchangia mawili,matatu.

Page 235: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

235

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote tumshukuruMwenyezi Mungu mwingi wa rehema ambaye ametupaafya, bado tupo na tunaendelea na pia nakushukuru kwakunipa fursa hii ya kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na msemo waKiswahili, watu wa Pwani tunakuwa na msemo tunasemakwamba, “ukipenda boga, basi upende na mti wake.” Siyosahihi kwamba unapenda boga, lakini mti wake unautiamoto. Hii itakuwa siyo sahihi na wala haikubaliki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia udugu siku zote nikufaana na siyo kufanana. Kama kufanana, miaka 50tumefanana vya kutosha, lakini sasa tunatakiwa tuwe namwelekeo mpya kabisa wa kufaana hususan katika masualamazima ya kiuchumi. Kama tutajaribu kuimba na kusifu tumasuala ya Muungano lakini bila kusaidiana kiuchumi, bilakupeana fursa zaidi za kiuchumi, kwa kweli Muungano huuutakuwa hauna mwendo mwema na hauna afya kwaWatanzania hususan wale walioko Zanzibar kwa maana yaWazanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba kimsingi niukweli usiopingika kwamba Muungano kama Muungano nimuhimu na hakuna anayekataa hata mmoja. Siyo kwelikwamba kuna Wazanzibar fulani hawataki Muungano, siyokweli kabisa. Wazanzibar wanataka Muungano. Kamaalivyosema Kaka yangu Mheshimiwa Jaku tunahitajiMuungano ambao utakuwa na maslahi kwa pande zotembili. Hatuhitaji Muungano ambao umejikita maslahi yaupande mmoja hii itakuwa siyo muungano. Naomba Mawaziriwatakapokuja ku-wind up kwanza waje wanijibu masualamawili ambayo tumekuwa tukiyazungumza mara kwa marapale tunapopata fursa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza ni kuhusiana navyombo vya moto. Kwa kweli tumekuwa tukipata taabu sanaWazanzibar, hasa sisi Wabunge, tumekuwa tukibughudhiwasana na TRA na Polisi kwa sababu tu tuna magari yamesajiliwakwa namba za Zanzibar. Hii siyo halali. (Makofi)

Page 236: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

236

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi kwenye mchezo ule waSimba na Mazembe ya Congo, tuliwakuta Wakongowanahojiwa kwenye vyombo vya habari. Walikuja hapa namagari yao na wakafanya shughuli zao Dar es Salaam,Tanzania hii hii na halafu wakaondoka na magari yao. Leohakuna Mzanzibar anayethubutu kuja Tanzania Bara na gariyake akatumia, hii siyo haki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi binafsi na-declarekwamba ipo siku nilifukuzwa na TRA na Polisi usiku Dar esSalaam. Nasimama, wananiambia tuna wasiwasi na gariyako. Kwa nini? Unatumia namba za kigeni. Aah,nikashangaa, nikamwuliza wewe nani? Mimi Afisa wa TRA.Hii namba ya wapi? Namba ya Zanzibar. Hivi Zanzibar leo ninchi ya kigeni na Dar es Salaam? Ananiambia kwani Zanzibarni Tanzania Bara. Nikataka kujua kumbe hivi kuna nchi inaitwaTanzania Bara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi ni vitu ambavyovinahitaji majibu. Naomba Mheshimiwa Waziri atakapokujaanipe jibu sahihi juu ya suala hili kwamba ni lini sasa bughudhahii na adhabu hii itaondoka kwa Wazanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ambalo natakaMheshimiwa Waziri aje anijibu kwa kina ni suala la uwepo waAccount ya Pamoja ya Fedha ambayo imetajwa wenyeKatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 133.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba sanaMheshimiwa Waziri, mwaka juzi 2017 tulizungumza suala hiliakaahidi kwamba linakwenda kutatuliwa; mwaka jana 2018,tulizungumza suala hili akaahidi kwamba linakwendakutatuliwa. Leo tunataka commitment ya Serikali kwamba nilini sasa suala hili linakwenda kumalizwa na tuone Accountya Pamoja ya Fedha ambayo itashughulika na mgawanyosahihi wa mapato ya Muungano baina ya Zanzibar naTanzania Bara au Tanganyika unakwenda sawa.

Page 237: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

237

Mheshimiwa Mwenyekiti, yote haya yanakuja kwasababu moja; hakuna siku Serikali ya Chama cha Mapinduziimekuwa na nia njema na Muungano huu. Hiyo ndiyo kaulisimple kabisa, ndiyo kauli rahisi. Siku Muungano huuunaundwa uliundwa kwa siku mbili baina ya Mwalimu Nyererena Karume, lakini tunazungumzia kero ya Muungano tenaambayo iko ndani ya Katiba inachukua miaka 50, nia njemaiko wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuwezi kuimba tukwamba tuna nia njema, tunataka kutatua kero zaMuungano, sijui tunafanyeje, wakati nia njema hakuna.Vijana wetu hao, wote vijana; Mheshimiwa Makamba naMheshimiwa Mussa, wote wana utashi wa kuona kero zaMuungano zinatatuliwa. Tena hata ukizungumza nao unahisikwamba wanaumia na wako tayari kuona kero za Muunganozinatatuliwa. Ushirikiano wanaopata bila shaka ni tatizo,Serikali haiko tayari kuona kero hizi zinatatuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Muunganolimekuwa na shida na ndiyo maana zipo taarifa zinasemana ni sahihi kabisa, hata mgogoro uliokuwepo katika miakaya 1970 baina ya Mwalimu Nyerere na Karume sababu ilikuwani Muungano. Hata mgogoro uliomwondoa Jumbe kwenyemadaraka kama Rais wa Zanzibar akafukuzwa Urais,akafukuzwa nafasi zote sababu ilikuwa ni Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata Mashehe ambao leowako jela kwa mwaka wa sita sasa; siyo ugaidi, wala siyosuala la uanaharakati, wala siyo suala lolote, ni kwa sababuwalisimama na Wazanzibar kudai maslahi zaidi…

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. JUMA KOMBO HAMAD: …ya kiuchumi kwa ajili…

MWENYEKITI: Taarifa. Mheshimiwa Kombo kaa chinikwanza.

Page 238: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

238

T A A R I F A

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nataka nimpe taarifa mzungumzaji, anaposema kwambaChama cha Mapinduzi hawana nia njema na Muungano huuna Chama cha Mapinduzi sasa hivi kina umri wa zaidi yamiaka 51 na Chama cha Wananchi CUF walipojaribu kujana Muungano wa Shirikisho, Chama cha Mapinduzi ndiyokilisimama imara kupinga Muungano ule wa shirikisho. Kwahiyo, suala la kusema Chama cha Mapinduzi hakina nianjema na Muungano huu, siyo sawa sawa. (Makofi)

MWENYEMITI: Ahsante. Mheshimiwa Kombo, taarifahiyo.

MHE. JUMA KOMBO HAMAD: Mheshimiwa Mwenyekiti,Kuchauka ndugu yangu wewe umekwenda juzi CCM…

MWENYEKITI: Jibu taarifa yake. Mengine yaache.

MHE. JUMA KOMBO HAMAD: …hayo mapenzi yakona CCM yamekuja lini? Au kwa sababu Mbunge! Subiri keshokutwa CCM wakuangushe halafu uanze kuimba imba huko.(Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba nia njemandiyo itakayodumisha Muungano. Naomba niseme moja nakatika hili naomba Mheshimiwa Jenista anisikilize vizuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, fursa ya mazungumzoambayo ipo sasa kwenda kutatua changamoto hizi zaMuungano, baada ya muda hazitakuwepo tena na tutakujakushuhudia mambo mengine ambayo hayastahili. Kwasababu unapobana fursa za kiuchumi za Zanzibar, vizazivinavyokuja havitakubali kuona kwamba wao hawa-enjoyfursa za kiuchumi kama zile ambazo wenzao Watanzania Barawanazipata ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Hili hawatalikubali. Kwa hiyo, ushauri wangu ni kwambatutumie fursa ambayo ipo, tutumie nafasi ambayo sasa hivitunayo ili kutatua changamoto hizi tukiwa na nia njema ya

Page 239: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

239

kwenda kwenye Muungano ambao utadumu na utadumishausawa na haki kwa pande hizi mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalizie mchangowangu kwa kusema kwamba, suala la mazingira Wizara hiibahati mbaya sana hakuna fedha ya ndani ambayoimetengwa katika kuendeleza suala la mazingira ndani yanchi yetu ya Tanzania. Fedha yote inayotegemewa ni yamisaada kutoka nje. Hii inadhihirisha au inaonyesha kwambani kiasi gani Serikali haiko serious na kuendeleza suala lamazingira katika nchi yetu ya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana wakati wakupitisha bajeti na Waheshimiwa Mawaziri pamoja naCabinet iwe serious na suala la mazingira kwa sababu nimuhimu na ni suala ambalo linagusa binadamu na viumbevyote vilivyomo ndani ya Tanzania yetu. Bila mazingira sahihina bila kudumisha mazingira, Taifa hili litatupotea na tutakujakujutia nafasi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, ahsantesana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Nilimwita Mheshimiwa Mtolea.Jiandae Mheshimiwa Mattar

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Dakika 10 eh?

MWENYEKITI: Dakika tano.

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Kwanza niwapongeze sana Mawaziriwanaosimamia Wizara hii kwa namna ambavyo wanajitoakuhakikisha wanasimamia Muungano, lakini pia upande wamazingira. Waendelee kufanya ziara nyingi kwa sababumazingira kwa kweli yameharibika kwa kiasi kikubwa naMuungano unahitaji kusemewa kwa kiasi kikubwa.

Page 240: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

240

Mheshimiwa Mwenyekiti, pale kwangu kuna tatizomoja; kuna mtaro mmoja unatiriri nafikiri ni maji ya sumu,nimeshawahi kulizungumza hili hapa Bungeni na leo ni maraya pili. Kwenye Kata ya Sandari kule Temeke Mikoroshini, kunamtaro wa mfereji wa Mpogo, yake maji yanaoneka yanatokakwenye moja kati ya viwanda vilivyoko Vingunguti, nyumbazil izokuwa pembeni bati zinaharibika na matofaliyanamung’unyuka. Hali hii inaonesha kabisa kwamba palekuna sumu inatembea na kama matofali yanamung’unyukamaana yake afya za watu wanaoishi pale ziko kwenye hiichangamoto kubwa. Kwa hiyo, naomba hil i jambowalichukue na walifanyie kazi kwa haraka. Sisi kamaHalmashauri tumeshatenga fedha ya kuujenga ule mfereji,lakini haiondoi ukweli kwamba maji yanayotiririka yanakuwana sumu. Hilo moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, naitaka Wizara wawewanatupa taarifa za mara kwa mara za uchafuzi wamazingira katika Jiji la Dar es Salaam. Tunapata taarifaambazo zinaleta sintofahamu kidogo, kuna wakatitunaambiwa kwamba mabonde yale hayafai hata kwakulima mbogamboga za majani, kuna wakati tunaambiwawater table ya Dar es Salaam yote imechafuka hata maji yavisima tunayoyatumia si mazuri. Sasa ni vizuri wakawawanatuandalia taarifa za wazi na za kina ili tujue kitu kipitufanye na kitu kipi tusifanye. Maana yake sasa tukiendasokoni tunaogopa michicha tunaogopa matembele, tunahisiyamelimwa kwenye yale maeneo ambayo yana sumu.Ikiwezekana waweke hata mabango tujue kwamba eneohili linastahili, eneo hili halistahili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine, sheria ambazozinatumika na NEMC kwa kuwaadhibu wanaochafuamazingira, ziangaliwe upya, inawezekana ni za Ulaya sana.Kwa mfano, mtu mwenye garage anatakiwa aweamesakafia na kuwe na system ya kutofautisha maji na oil.Garage zetu nyingi hazijasakafiwa, kwa hiyo kinachofanyikani kama tumetengeneza mwanya wa watu kupiga fedha.Leo mtu anapelekewa notice kwamba hii garage uisakafiendani ya siku 14, jambo ambalo haliwezekani. Akija siku ya

Page 241: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

241

pili, yule mtu atakachofanya ili asitozwe faini ya milioni tano,atamuona tu pembeni huyu mtu, kwamba bwanausiniandikie, chukua hii milioni moja, chukua hii laki mbili, sasawatu wataishi hivi mpaka lini? Lazima tuwe na sheria ambazozinaendana na mazingira yetu, je tuna uwezo kwenye kilacar wash kuwa na hiyo system ya kuchuja maji na oil. Magariyetu yenyewe ya mitumba, likisimama tu hapo linavuja oil,mtu anatakiwa awe na system ya kuchuja hiyo kitu, hiiinawezekana vipi? Kwa hiyo, tuziangalie hizi sheria kama kwelini rafiki na zinaweza kutekelezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mwisho ni laMuungano; nimeshtushwa sana, mtu aliyesimama hapakusema kwamba Serikali ya Chama cha Mapinduzi haiutakiMuungano tena na yeye anasimama akitoka CUF. CUFwanaamini kwenye madaraka kamili, mamlaka kamili,mamlaka kamili maana yake Zanzibar isimame kama nchitofauti na Tanzania Bara isimame kama nchi tofauti, sasahapa ni nani asiyeupenda Muungano? Kwa hiyo, nafikirikwenye jambo hili la Muungano, ni vizuri tukawa wakweli,kwamba hizi nchi mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani,zinahitajiana sana whether tuko ndani au nje ya Muungano.(Makofi)

MHE. JUMA KOMBO HAMAD: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,sasa tumekubali tuko ndani ya muungano ni vizuri….

MWENYEKITI: Taarifa.

MHE. JUMA KOMBO HAMAD: Mheshimiwa Mwenyekiti,suala la mamlaka ya Zanzibar ambayo ni kupata fursa zaidiza kiuchumi hususan katika nyanja za kimataifa, haliharamishikutokuwepo Muungano. Tuna mifano mingi, tuna EuropeanUnion, ni Muungano una nchi kadhaa, lakini kila nchi si inamamlaka yake! Kwa hiyo, suala la kujadili, MheshimiwaMtolea, suala la kusema kwamba eti kwa sababu kuna watuwanazungumzia suala la kwamba Zanzibar iwe na mamlaka

Page 242: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

242

kamili, hawataki Muungano, hii siyo sahihi. Suala la mamlakakamili ni suala la kuwepo kwa Serikali tatu….

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mtolea endelea.

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,mimi siipokei hiyo taarifa yake. Tunapozungumzia Muunganowa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, tunazungumzia kitutofauti sana. Huwezi kufananisha na miungano mingine hiyosijui ya European Union na sehemu nyingine. Huu ni muunganowa kipekee, una historia ya kipekee na mazingira yake ni yakipekee. Sasa ukianza kusema kwamba tunakosa fursa, sikweli na wakati mwingine eti mtu anasema kwambatumechoka kubebwa kwenye koti la Muungano, hivialiyebebwa anaweza akaanza kuchoka kabla yaaliyembeba? Maana yake aliyekubeba anavumilia kwasababu anafahamu thamani ya anachokifanya. Mamaakimbeba mtoto, si kwamba eti mtoto aanze kuchoka etimama hajachoka, lakini Mama anaendelea kumbeba kwasababu anajua ni jukumu lake na ndicho Tanzania Barawanachokifanya… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsate. Mheshimiwa Mattar hayupoenh?

MICHANGO KWA MAANDISHI

MHE. ZAINAB M. AMIR: Mheshimiwa Mwenyekiti, awaliya yote napenda kumpongeza Mheshimiwa Januari YusuphMakamba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira kwa kazi kubwa anayoifanyapamoja na Naibu Waziri Mheshimiwa Mussa Sima bilakuwasahau wafanyakazi wa Wizara hiii kwa kusimamia nakutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na umuhimu wamazingira naishauri Serikali itenge fedha za ndani katika bajeti

Page 243: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

243

ili kuweza kutekeleza majukumu yake na sio kutenga fedhaza wahisani kutoka nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri katika kampeni yaupandaji miti Serikali ione haja sasa ya kupanda miti yenyefaida zaidi ya moja, nashauri ipandwe miti mingi ya matundakwanza tutahifadhi mazingira pia yatapatikana matundaambayo ni muhimu kwa binadamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mifuko ya plastiki si vizuri kwamazingira na naunga mkono usitishwaji wake. Ushaurimaelekezo ya awali ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ni kutumiaKiwanda cha Mgololo kutengeneza mifuko mbadala nakiwanda hicho hutumia malighafi ya misitu (miti).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ihamasishewananchi kila mkoa kuanza kulima kilimo cha miti ambayoitatumika katika viwanda vitakavyotengeneza mifuko hiyokikiwemo Kiwanda cha Mgololo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya mita 60 ipitiweupya maana kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchimaeneo ikiwemo mito maziwa (Victoria) na kadhalika nakusababisha migongano isiyo ya lazima katika ya Serikali nawananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna utupwaji hovyo wachupa za maji, juice pembezoni mwa barabara kuu ziendazomikoani. Serikali ifanye utaratibu wa kutoa elimu hususan kwawafanyakazi wa magari ya abiria licha ya kuwa na vyombondani ya mabasi vya kuhifadhia taka, lakini bado utupwajiupo na unaharibu mazingira. Hivyo, wafanyakazi hao wamagari ya abiria wapewe elimu ya kutosha ya uhifadhi wamazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali na Wizara ya Nishatiili kupunguza ukatwaji wa miti ambayo hutumika kusambazaumeme mijini na vijijini na Wizara ya Nishati ianze mara mojautumiaji wa nguzo za zege ambazo kila mara imeahidi

Page 244: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

244

kutumia ili sasa kuepuka kukata miti mingi ambayo itapelekeanchi kugeuka jangwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naomba Munguampe Mheshimiwa Waziri umri mrefu na afya njema katikakuyatekeleza majukumu yako ya kila siku.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Mwenyekiti,nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema.Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ndiyo uliozaa jinaTanzania na ni wa kihistoria Afrika na duniani kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zipo nchi zinataka kufanyaMuungano kama huu lakini zimeshindwa na pia zipo nchiziliungana na baadaye muungano huo ulivunjika na sasazinafanyika bidii za kujiunga upya na mfano ni Jumuiya yaAfrika Mashariki iliyovunjika mwaka 1977 na sasa bidii na juhudizinafanyika kuunda upya muungano huo (East AfricaCommunity) kwa nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda,Burundi na Southern Sudan. Ni mategemeo yangu Muunganowa watu wa pande hizi (Tanganyika na Zanzibar) utadumu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, faida, changamoto namustakabali; Watanzania kwa miaka mingi wamekuwa naumoja na mshikamano katika nyanja mbalimbali ambapokwa kutekeleza haya ndiyo tunapata neno Muungano.Kihistoria tokea miaka mingi iliyopita tangu dunia iumbwe,makabila na watu wa maeneo mbalimbali katikaTanganyika, wamekuwa na ushirikiano na mahusiano yakaribu. Mfano ni katika harakati za kuondoa uonevu,ukandamizaji na ubaguzi uliokuwa ukifanywa na WakoloniWajerumani mnamo mwaka 1905 hadi mwaka 1907.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika Vita ya Minongekatika maeneo ya Ukanda wa Pwani Tanga, Pwani, Dar esSalaam na Zanzibar, mikoa hii makabila yake yalishirikianakuondoa uonevu hali iliyopelekea kutokea Vita ya Kwanzaya Dunia (1st World War 1914-1918). Hii yote ni kuoneshanamna muungano ulivyokuwa na umuhimu na faida kwajamii. Hivyo, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulianzia

Page 245: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

245

miaka mingi na hadi katika Mapinduzi ya Zanzibar 1964.Mchango mkubwa ulitokea Tanganyika (Tanzania Bara) nakufanikiwa kuondoa ukandamizaji uliokuwa ukifanywa naWakoloni wa Kiarabu katika Visiwa vya Unguja na Pemba(Zanzibar).

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi na ushauri; Serikaliizifanyie kazi kero zote za Muungano na kuzipatia ufumbuziwa haraka; Sera ya kulinda viwanda vya ndani ifanye kazipande zote za Muungano, mfano Kiwanda cha SukariMahonda kiruhusiwe kupata soko la sukari na bidhaa zakeupande wa Tanzania Bara. Magari yaliyosajiliwa Zanzibaryaruhusiwe kutumika Tanzania Bara bila vikwazo vyovyote;kero na changamoto zinazofanyiwa kazi, taarifa zakeziwekwe wazi na isiwe siri; gawio la Pato la Taifa, deni laTANESCO, suala la FIFA, Exclusive Zone katika Bahari Kuuyafanyiwe kazi na yaishe; suala la mafuta ya gesi, zote hizi nisekta ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi na kupata ufumbuzi.Mfumo wa Serikali tatu (Serikali ya Muungano, Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Shirikisho ndio ufumbuziwa kudumu).

Mheshimiwa Mwenyekiti, mazingira ni neno lenyemaana pana sana ambalo bado Watanzania wengihawajalielewa maana yake na bahati mbaya bado Serikalihaijatoa elimu ya kutosha kwa kutumia vyombo vya habari,vipeperushi na Taasisi zake katika jamii ya Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mazingira katika Tanzaniayanaingiliana sana na shughuli za uzalishaji mali (kutafuta riziki)kwa wananchi wake kama vile kilimo, uvuvi, ufugaji nashughuli za viwandani. Sheria nyingi na Kanuni zinatungwabila kuwashirikisha wananchi ili wazielewe na kuzifanyia kazi,badala yake Sheria zinatumika kuwakandamiza wananchina pale wawakilishi wao tunapotetea (Wabunge, Madiwanina Wenyeviti wa Serikali za Mitaa) tunajibiwa ignorance oflaws is not a defence na inaonekana Serikali inatumia makosayanayofanywa na wananchi kujipatia faini (fedha) na kuwachanzo cha mapato ya Serikali.

Page 246: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

246

Mheshimiwa Mwenyekiti, wafugaji, wakulima nawawindaji wamekuwa wahanga wakubwa katika suala zimala mazingira, hivyo Serikali katika hili ifanye kazi ya ziada kwakutoa elimu ya kutosha. Sheria ya kuacha mita 60 ya vyanzovya maji katika shughuli za uzalishaji mali ni mpya, iwekwevizuri na itolewe elimu ya kutosha ili kuondoa mkanganyikouliopo hususan pale ambapo sheria imekuta mwananchiameshaanza kufanya kazi (kabla Sheria kuanzishwa), Serikaliimfidie kwa eneo litakalotwaliwa na sheria hii katika ngazi zaSerikali za Vijiji, Serikali za Mitaa, Halmashauri za Manispaana Halmashauri za Majiji kwa thamani ya fedha katika soko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika bajeti ya Ofisi yaMakamu wa Rais, Muungano na Mazingira inatengewafedha ndogo sana na mfano katika bajeti ya 2018/2019, bajetiiliyotengwa hadi mwaka wa fedha unaoishia ni shilingi bilioni1.7 tu ndiyo iliyopokelewa hali inayoonesha Serikali haitiliimaanani suala la Mazingira.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru sana kwa kupata muda huu kuwezakuchangia kwa maandishi. Namshukuru Mwenyezi Mungu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa pongezi sana kwaMheshimiwa Rais, Makamu wa Rais na Mheshimiwa Wazirina Makamu wa Waziri kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Viumbe Vamizi.Kuhusu hasa gugu la Kongwa ambalo linaharibu malisho yamifugo ni la muda mrefu sasa ingawaje Serikali inajitahidikukabiliana nalo, lakini bado ni tatizo. Mheshimiwa Wazirinashauri jitihada zaidi zitumike ili kutokomeza kabisa guguhili la Kongwa. Naomba maelezo zaidi kwa niaba ya wafugajina Serikali na hasa kuhusu gugu hili lililoenea katika Ranchya Kongwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu gugu karoti ambalolinaenea kwa kasi hasa Mikoa ya Kaskazini. Gugu hili ni hatari,Mheshimiwa Waziri anafahamu gugu hili linahatarisha na hasakatika kil imo mazao na malisho. Mheshimiwa Waziri

Page 247: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

247

ningependa kujua kwa niaba ya wakulima na wafugajimikakati inayoendelea ya haraka ili kutokomeza gugu karoti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu vyanzo vya maji naupandaji miti rafiki ya vyanzo vya maji. Natoa pongezi zajitihada zinazoendelea kunusuru vyanzo vya maji. Nashaurielimu izidi kutolewa kuhusu vyanzo vya maji na kupanda mitirafiki ili kulinda vyanzo vya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Morogoro tunamatatizo ya maji na hasa Halmashauri ya MorogoroManispaa. Sababu mojawapo ikiwa ni uharibifu wa vyanzovya maji na ukataji miti katika Milima ya Uluguru. MheshimiwaWaziri kwa jitihada zake za kulinda mazingira, naombaakaliangalie tatizo hili, ili kunusuru vyanzo vya maji milima yaUluguru (Morogoro) kwa madhumuni ya upatikanaji wa majina uhai wa mito kama ilivyokuwa zamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa pongezi kwaMheshimiwa Rais, Waziri Mkuu na Mheshimiwa Waziri kwakulisimamia suala hili la mifuko ya karatasi. Kama MheshimiwaWaziri alivyoelekeza kupitia kwenye mkutano (15/04/2019) nakwenye hotuba yake ya bajeti. Nashauri Mheshimiwa Wazirina watalaam wake walisimamie kwa ukamilifu ili tuwezekuondokana na tatizo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo la ukataji miti nauchomaji mkaa bado ni tatizo. Elimu zaidi inatakiwa kwawananchi kuhusu faida na hasara za kutunza mazingira, hasakwa kupanda miti na kukata miti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, gunduzi kuhusu nishatimbadala na hasa zinazooneshwa wakati wa maonesho yaSiku ya Wakulima – Nane Nane zipewe kipaumbele kwakuwaendeleza na kuwawezesha wagunduzi hawa wa nishatimbadala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna tatizo la fedha katikaofisi hii ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Page 248: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

248

Nashauri fedha zote zilizoombwa wakati wa bajeti hii zitolewekwa wakati ili waweze kufanya kazi zao vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkonohoja.

MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Mwenyekiti,pongezi kwa Serikali Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Makamuwa Rais, Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Waziri,Mheshimiwa Naibu Waziri na Makatibu Wakuu kwa kazi nzuriwanazozifanya za ujenzi wa Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, NEMC; naomba Serikaliwaangalie utendaji wa NEMC kwani washauri wanachukuafedha nyingi kuliko Serikali. Waangalie mradi gani unahitajiupembuzi wa muda mrefu na mengine kama imeshapitishwana Halmashauri NEMC wapitishe kwa haraka. NEMC na taasisinyingine kama EWURA na wengine wakae pamoja nakutafuta njia nyepesi ya kuwasaidia wawekezaji wa mafuta(naweka maslahi wazi ni mdau). Badala ya kulipa malipomakubwa mara moja, nashauri katika kukuza na kuendelezauwekezaji waweke tozo ambazo zinaweza kulipwa kilamwaka, hii itasaidia hata wawekezaji wadogo kuwezakumudu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mifuko ya plastic;naipongeza Serikali kwa uamuzi wake wa kupiga marufukukwani mazingira yetu yaliharibika vibaya kutokana na mifukokujaa ardhini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Muungano; naipongezaSerikali kwa kujitahidi kutatua kero za Muungano kwa kiasitulichofikia inatia moyo sana. Tudumishe Muungano wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja kwaasilimia mia moja.

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kupata nafasi ya kuchangia. Matumizi ya mifukoya plastic; ni jambo jema kwa Serikali kutoa tamko mwisho

Page 249: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

249

wa kutumia mifuko ya plastic ni 1/6/2019. Tamko pekeehalitoshi, ni vizuri Waziri atueleze ni lini suala hili litatumikakisheria ili yeyote anayetumia mifuko hiyo ajue kuna faini yakulipa au anaweza kufungwa jela. Bila sheria kuna baadhiya watu wataendelea kutumia mifuko hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona kabisa mwaka huumvua mfano kaskazini bado hazijanyesha lakini kwa kisingiziocha mabadiliko ya tabianchi, lakini ni wazi kuwa miti imekuwaikikatwa ovyo kwa matumizi ya mkaa, wengine kwa ajili yakilimo. Siku zilizopita vijijini (Serikali za Vijiji) ilikuwa ni lazimakupanda miti na ilikuwa hairuhusiwi kulima kando ya mito,lakini sasa hivi ni jambo la kawaida kufanya hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri shule zote za msingina sekondari katika kila vijiji wawe na vitalu vya kupandamiti na iwe kabisa ni elimu kuanzia shule za awali kuhusuumuhimu wa kutunza mazingira kwa kupanda miti na wajueukikata mti lazima uwe umepanda mti mwingine. Wazeewetu walisomesha vijana wao kwa kukata mti na kuuza mbaolakini walihakikisha kuna mti mwingine pembeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nashauri kila halmashauriziwe na vitalu vya miti ikiwezekana ya matunda pia ambayoyatatumika kujenga afya na kuongeza kipato kwa wananchina uuzwe kwa bei nafuu ili kila mwananchi aweze kununua.

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: MheshimiwaMwenyekiti, naunga mkono hoja hii ya Waziri. Hata hivyo,ninayo machache ya kushauri; ni dhahiri bila kutunzamazingira nchi yetu itapata matatizo mengi na makubwa.Mkoa wa Kigoma na hasa Halmashauri ya Mji Kasuluulibahatika kutembelewa na timu ya wataalam wa mazingirana vyanzo vya maji. Timu hii ilimaliza kazi na kutoa ripoti yakemwaka 2017. Kazi kubwa iliyofanyika ni pamoja nakutembelea vyanzo vya maji vilivyopo Halmashauri ya Mji waKasulu. Vyanzo kadhaa vilifanyiwa tathmini na utafiti wa kinabaada ya taarifa ile ya kitaalam niliamini kwamba hatua zautekelezaji zimechukuliwa.

Page 250: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

250

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona hotuba yako yaBajeti 2019/2020, ukurasa wa 83 (xi) kwamba moja ya kazizitakazotekelezwa mwaka huu ni kupitia miradi iliyowasilishwana wadau ili ipate wafadhili wa Mfuko wa Kuhimili Mabadilikoya Tabianchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Je mradi wa ulinzi wa vyanzovya maji zaidi ya 25 katikaHalimashauri ya Kasulu Mjini nisehemu ya mkakati huu? Naomba Wizara yako ifahamukwamba maji yanayotiririka kutoka uwanda wa juu wa HeruJuu, Buhigwe maji hayo hatimaye hutiririka hadi ZiwaTanganyika. Ulinzi wa vyanzo hivi si tu kwamba ni muhimu nijambo la lazima, tafadhali hatua sasa zichukuliwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ulinzi wa ardhi oevu yaMalagarasi; eneo hili maarufu Malagarasi wetland linahitajikulindwa. Eneo hili kwa kiasi kikubwa linakumbwa na uvamiziwa ng’ombe wengi kutoka baadhi ya maeneo ya nchi yetuna wakati fulani nchi jirani. Eneo hili la Ramsar Site litapotea,urithi wetu utapotea na rasilimali hii itaangamia pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vizuri Wizara ya Maliasilina Utalii, TAMISEMI, Mambo ya Ndani na Wizara hii waje nampango mkakati wa kulinda eneo hili, lisipolindwa ndani yamiaka mitano mpaka saba shida itakuwa haiwezikurekebishika tena.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwatakie Wizara hii kazinjema katika kulinda mazingira ambayo ni uhai wa Taifa letu.

MHE. ANTHONY C. KOMU: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri, Naibu Wazirina Watendaji wote katika Wizara hii kwa kazi wanazozifanyakatika mazingira mazuri kutokana na kutokuwa na rasilimaliza kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mazingira ni sualala kufa na kupona kutokana na umuhimu wake kwa viumbevyote duniani ikiwa ni pamoja na sisi binadamu.

Page 251: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

251

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu haijatoa uzitounaostahili kibajeti kwa eneo hili. Nichukue fursa hii kuiombaWizara kufuatilia maombi yangu ya mara kwa mara ya kujaJimboni kwangu kuona athari mbalimbali zinazosababishwana mabadiliko ya tabianchi ukanda wa tambarare katikaKata za Arusha Chini, Mabogini, Old Moshi Magharibi naKahe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri yetu imefanyajitihada na kupata mshirika toka Ujerumani Jiji la Kiel ambalolinatusaidia sana kufanikisha mradi wa mazingira wenye lengola kurejesha miti ya asili ambayo ni rafiki wa mazingira katikaeneo letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe sana MheshimiwaWaziri aje aone jitihada hii, aitambue na Serikali ione jinsi yakuchangia na kupanua mradi huu kuhusu manufaa yamaeneo mengine katika Taifa.

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nawapongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuuna wafanyakazi wote kwa kazi wanazozifanya, hongerenisana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Urambo ina MtoUgalla. Mto huu ni muhimu sana kwa uhai wa wananchi lakinipia uhai wa Mto Malagalasi ambao unapata maji kutokaMto Ugalla. Serikali ina mpango gani wa kuondoa maguguyaliyovamia Mto Ugalla?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya wananchi waUrambo, naomba Serikali yetu isome tena barua rasmiiliyotumwa Wizarani kuhusu magugu yaliyovamia Mto Ugallana kuchukua hatua za kuokoa mto huo harakaiwezekanavyo. Aidha, tunaomba semina za kuelimishawananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira na kuachakukata miti hovyo.

MHE. SILAFU J. MAUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kutoa pongezi za dhati kwa Waziri, Naibu Waziri na

Page 252: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

252

wataalamu wote wa Wizara hii kwa kufanya kazi yao yaudhibiti wa uharibifu wa mazingira na kukabiliana namabadiliko ya tabianchi kwa dhati na weledi pamoja nakutopelekewa fedha kama zilivyopitishwa na kuidhinishwana Bunge kutoka Hazina.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu eneo kubwalimeathiriwa na uharibifu wa mazingira na tabianchi nakupelekea vipindi vyetu vya masika (mvua) kubadilika namvua kuwa ndogo na mazao ya mahindi, mpunga nakadhalika kukosa maji (mvua) na kufanya uzalishaji kuwamdogo. Mfano mwaka huu mazao yamekubwa na ukame,hivyo nashauri Serikali ijipange namna ya kukabiliana naukosefu wa chakula nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri kila Halmashaurikubaini miinuko (milima) iliyokuwa kipara yaani hakuna mitikuweka mkakati wa kupanda miti na kuweka kanuni zakulinda miinuko hiyo. Pia, kwa vile athari ni kubwa kwa nchi,ni vema bajeti ya Wizara hii katika Fungu 31 na 26, zikatolewakwa asilimia zaidi ya 85 kwani hali ya mazingira yetu ni mbaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mazingira yasipoboreshwakwa uharaka zaidi, lengo la maendeleo ya uchumi waviwanda halitakuwa lenye mafanikio na endelevu kwa vizazivijavyo. Tufanye jitihada za kufufua na kuboresha mazingiraili tupate mvua za kutosha na kupunguza athari za upepo(kuezuliwa na kubomoa majengo) ya wananchi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nashauri tupateMaafisa wa Mazingira wa kutosha ili watoe elimu na iwe elimuendelevu kwa wananchi wetu na tuwe na ushindani kwenyeHalmashauri zetu. Wataalam hawa wasiwe na urasimumkubwa wa kufikisha mapendekezo kwa Mkurugenzi waMazingira kutokana na waliyoyaona katika utekelezaji waowa majukumu ili kusaidia kutatua changamoto za mazingirakatika maeneo yao. Tuwe na kanuni na miongozo yakurejesha hali ya mazingira yetu kwa haraka tusiwe naurasimu? Chelewa chelewa tutakuta mazingira

Page 253: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

253

yameharibika kwa kiasi kikubwa na kuwa jangwa nagharama ya kuyarejesha itatushinda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikalitushughulikie haraka suala hili, hali ni mbaya sana. Naombatuone umuhimu wa kuongeza bajeti yetu ndani. Pia tuwekemikakati maalum ya kupanda miti rafiki ya kulinda mazingirana vyanzo vya mito, maziwa na bahari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ziwa Rukwa nalo limejazwana udongo unaoteremka kwenye milima na kushuka kwenyeBonde la Rukwa hadi kuingia Ziwa Rukwa. Hivyo nalo likombioni kina chake kutoweka. Naomba nalo lipewekipaumbele ili kulinusuru na hali hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, suala la mazingiratuliangalie upya na kuliwekea mikakati kwani tunahitajimazingira kwa ajili ya urithi wa vijana wetu. Naunga mkonohoja.

MHE. AUGUSTINO M. MASELE: MheshimiwaMwenyekiti, naunga mkono hoja ya Mheshimiwa Waziri waNchi, Ofisi ya Makamu wa Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa napendakuchangia zaidi katika suala la mazingira hasa juu ya uharibifuwa mazingira unaotokana na ukataji wa miti hovyo kwamatumizi mbalimbali ikiwemo uchomaji wa mkaa, kuni,utayarishaji wa mashamba na kadhalika. Uharibifu huuunafanyika bila ya kuwepo hatua madhubuti za kuhakikishanchi yetu haiwi jangwa. Watanzania walio wengi hawanadestruli ya kupanda miti ni mabingwa wa kukata miti nahawaelewi kuhusu uharibifu wa mazingira. Ifike mahali Serikaliichukue hatua kali kabisa dhidi ya Watanzania wenzetuwanaoharibu mazingira kwa kukata miti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri zitungwe sheria zakumtaka kila Mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18kupangiwa utaratibu wa kupanda miti angalau 10 kwamwaka kwa kuwa miti ndiyo chanzo cha mvua na hifadhi ya

Page 254: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

254

mazingira. Bila kuchukua hatua za makusudi, Tanzaniainakwenda kugeuka jangwa ndani ya kipindi kifupi. Hivyo basini wajibu wa Serikali kuchukua hatua madhubuti kukabilianana hali hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ongezeko kubwa la watuna wanyama wafugwao kunachangia kwa kiwango kikubwauharibifu wa mazingira. Kuna umuhimu mkubwa kuingizamasomo yanayohusiana na uhifadhi wa mazingira katikamitaala ya elimu nchini kuanzia chekechea hadi chuo kikuu.Madhara ya uharibifu wa mazingira ni pamoja na ukame,mafuriko na mmomonyoko wa ardhi. Ipo sababu ya msingikabisa kwa Serikali kusisitiza umuhimu wa kuwatakaWatanzania kujenga tabia ya kupenda mazingira kwa kuzuiaukataji miti badala yake wawe wanapanda miti katikamashamba yao na kwenye makazi yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina ushauri ufuatao:-

(i) Uzazi wa mpango upewe kipaumbele;

(ii) Idadi ya mifugo inayohamahama ipunguzwe;

(iii) Watanzania wanaofanya biashara ya mkaa wapewemasharti ya kuwa na mashamba ya kupandwa kwa ajili yaukataji miti ya kuchoma mkaa; na

(iv) Kila Mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18apewe malengo ya kupanda angalau miti 10 au zaidi katikamashamba na kwenye viwanja vya makazi, maeneo yabiashara na makazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. SUZANA C. MGONUKULIMA: MheshimiwaMwenyekiti, mabadiliko ya tabianchi ni suala mtambuka nasiyo tu linaathiri sekta moja. Ili kukabiliana na suala hili, nguvutoka pande zote inatakiwa kutumika. Ofisi ya Waziri Mkuu,Fungu 37, miradi inayohusu kujiandaa kwa majanga namabadiliko ya tabianchi haikupata hata senti moja. Kwa

Page 255: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

255

maana hii, nchi yetu ya Tanzania hatuoni kama hili ni tatizona kama tunaona ni tatizo kwa nini basi tusione ni wakatikama Taifa kuyalinda mambo ya mazingira kwa kutumiafedha zetu ili kuondokana na tatizo la ukame.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uchafuzi wamazingira kutokana na taka ngumu ni changamoto katikamaeneo ya mijini kutokana na uwezo mdogo wa Mamlakaza Serikali za Mtaa na miundombinu hafifu ya usimamizi wataka za aina hii hasa mifuko ya plastiki au rambo. Nchi yetuTanzania ina Kiwanda cha Karatasi Nyororo Mkoani Iringa,Wilaya ya Mufindi, kinatoa karatasi za kiwango cha juuambazo zinasafirishwa nchi jirani. Kwa nini Serikali isichukuemaamuzi magumu kuwekeza katika utengenezaji wa mifukoya kaki katika kiwanda hicho na kwa kufanya hivyo mapatoya Serikali yataongezeka, wakati huo matumizi ya mifuko yaplastiki itakoma na hali ya mazingira itakuwa salama. Nimipango ambayo kama nchi hatupaswi kulialia, hapa niuamuzi mgumu ambao unatakiwa kufanyika kulinusuru Taifaletu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna sheria ya utunzaji wavyanzo vya maji ambayo inaelekeza shughuli za kibinadamuzisifanyike kandokando na mito, nashauri sheria hii isimamiwekwa umakini kwani kuna maeneo mengine wanaambiwawafanye shughuli zao ndani ya mita 60 na maeneo menginemita 100. Nashauri watu wote waelekezwe umbali ufananekama ni mita 60 au mita 100, kauli iwe moja tu kwa kuwanchi ni moja na watu ni wamoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kukauka kwa MtoRuaha Mkoani Iringa kunasababishwa na wakulima wampunga Mbarali ambao baada ya kumwagilia mashambayao wanaacha maji yanatiririka ambapo kungekuwa nausiamamizi mkali wa kuhakikisha kila mwenye shamba baadaya kumaliza kumwagilia maji wanayarudisha kwenye mto.Kadri Mto Ruaha Mkuu unavyozidi kukauka wanyama waMbuga ya Ruaha, Mkoani Iringa watahama na mbuga hiindiyo mbuga kubwa kuliko mbuga zote Tanzania. Nini kauli

Page 256: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

256

ya Serikali kuhusu hatma ya mbuga hiyo? Nataka kauli yaSerikali wakati wa kuhitimisha.

MHE. MBARAKA K. DAU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa fursa hii na naanza kwa kuunga mkono hoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru nakumpongeza mtoa hoja Mheshimiwa Waziri kwa wasilisho zuri.Nianze kuchangia hotuba hii kwa kurejea kitabu cha hotubaukurasa wa 50 juu ya mkataba wa Nairobi kuhusu hifadhi,usimamizi na uendelezaji wa mazingira ya bahari na ukandawa pwani ya bahari ya Hindi. Mkataba huu unatakakuhakikisha tunalinda na kupambana na uchafuzi wamazingira ya bahari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafiti zinaonesha ifikapomwaka 2035 eneo la pwani ya bahari ya Tanzania litakuwana mifuko mingi ya plastiki na takataka nyingine kuliko samakibaharini. Nashukuru sana tamko la Mheshimiwa Waziri Mkuuna leo Mheshimiwa Waziri wa Mazingira kwa kupiga marufukumatumizi ya mifuko ya plastiki. Hatua hii imekuja wakatimuafaka kwani hali ya mazingira ya pwani yetu ni mbayana inaathiri wananchi hususani sisi tunaoishi kwenye visiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni matumizi yamkaa, kama lilivyoelezwa kwa uzuri kwenye kitabu chahotuba ukurasa wa 29, kasi ya ukataji miti kwa uchomaji wamkaa imekuwa ikiongezeka siku hata siku. Nashauri bei yagesi ipungue ili wananchi waweze kuacha matumizi ya mkaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upandaji wa miti kamalilivyojadiliwa kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri, ukurasawa 37 ni jambo jema. Naishauri Serikali yangu iongeze fedhakwenye kampeni za upandaji miti. Ni ukweli usio na shakakasi ya ukataji miti imekuwa kubwa sana hivyo ipo haja yakuongeza fedha kwa ajili ya kampeni za upandaji miti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho nikuharibika kwa ikolojia ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu kamalilivyoelezwa kwenye kitabu cha hotuba ukurasa wa 50.

Page 257: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

257

Ikolojia ya Mto Ruaha Mkuu ndiyo inayotiririsha maji kwenyeMto Rufiji na hatimaye maji hayo ndiyo tegemeo kwenyeuzalishaji wa umeme kwenye mradi wa Rufiji Hydro Project.Kwa msingi huu, ni muhimu ikolojia hii kutunzwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na naungamkono hoja.

MHE. LUCIA M. MLOWE: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kuchangia katika hoja hii, kama ifuatavyo. Kwanza,ni matumizi ya mifuko ya plasitiki. Baada ya katazo la mifukoya plasitiki, naomba Serikali itoe njia mbadala ya mifuko hiiya plasitiki. Serikali itoe maelekezo ya vifaa vitakavyotumikabadala ya plasitiki. Mfano, vitengenezwe vifungashio kwakutumia karatasi za kawaida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi sasa kuna ukatajimkubwa sana wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa. NiombeSerikali ipunguze bei ya gesi ili wananchi waweze kutumiagesi badala ya kuni na mkaa ambao unasababisha uharibifuwa mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, masuala ya Muungano,naomba wananchi waendelee kupata elimu juu yaMuungano huu. Hata wanafunzi wafundishwe masuala yaMuungano ili kuendelea kuenzi juhudi za waasisi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. RUTH H. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti,namshukuru Mungu kunipa fursa hii ili nitoe mchango wangukwenye eneo hili la mazingira. Utunzaji wa mazingira nimuhimu sana kwa uhai wa binadamu. Utunzaji wa misitu,vyanzo vya maji, usafi wa mazingira ni sehemu ya uhai wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitajikita zaidi kwenyeutunzaji wa misitu kwa sababu ndiyo chanzo kikubwakinachovuta mvua, hivyo kupata maji ya mvua kwa ajili yakilimo na vilevile maji kwenye mito, maziwa kwa ajili ya ustawiwa jamii. Bado Serikali haijawekeza vya kutosha katika

Page 258: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

258

utunzaji wake. Tumeshuhudia misitu ambayo imetunzwa kwamuda mrefu ikikatwa kiholela. Tumeshuhudia makaziyakijengwa au shughuli za kibinadamu katika misitumbalimbali nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli wananchi wengibado wanatumia nishati ya kuni na mkaa kwa matumizi yanyumbani, ni kweli pia kwamba uchomaji mkaa umekuwachangamoto kubwa katika kuteketeza misitu na watumiajiwengi wa mkaa wanaishi mjini. Ni kwa nini sasa Serikali hii yaAwamu ya Tano isifanye maamuzi magumu kwa kutoa ruzukukwenye mitungi ya gasi iliyojazana mjini ili kuwezeshawatumiaji wengi waweze kununua mitungi hiyo kwa bei nafuusana na kuachana na matumzi ya mkaa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua kuna usambazaji wagesi asilia kwa baadhi ya makazi na viwanda mbalimbalilakini zoezi hili ni la muda mrefu sana mpaka kuja kusambaaeneo kubwa la nchi. Utatuzi wa haraka wa kuinusuru misituyetu na vyanzo vya maji ni matumizi ya mitungi ya gesi yamajumbani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni matumaini yangukwamba Serikali itachukua hatua ili kunusuru mazingira nauhai wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,awali ya yote, napenda kuunga mkono hutuba ya KambiRasmi ya Upinzani, naishauri Serikali izingatie ushauri uliotolewakatika hotuba ile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala uchafuzi wa mazingirana kukosekana kwa usimamizi mzuri unasababisha uharibifuwa mazingira. Nani asiyejua uidhinishaji/usajili unaofanywawa viwanda ambavyo ni hatari kwa mazingira yetu? Hivyobasi, pamoja na kauli ya Waziri Mkuu kupiga marufuku utumiajiwa mifuko ya plastiki, je, kauli hiyo imeenda sambamba naufungaji viwanda vinavyozalisha mifuko hiyo? Je, kauli ya

Page 259: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

259

Waziri Mkuu inaenda sambamba na utoaji wa elimu kwawananchi hasa vijijini? Nina mashaka makubwa na faini/vifungo watakavyopata wananchi hasa vijijini. NaishauriSerikali itangaze kufunga viwanda vya utengenezaji mifukohiyo mara moja na elimu itolewe kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa ukataji wa mitiunakithiri kila mwaka na hakuna jitihada za upandaji miti haliambayo inasababisha mabadiliko makubwa ya hali ya hewa.Serikali iweke mkazo katika upatikanaji wa gesi na umemevijijini na mijini kwa matumizi ya viwanda, magari namajumbani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nashauri Serikaliipeleke miradi ya ufugaji nyuki kwa wananchi vijijini. Ahsante.

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kuchangia suala la uhifadhi na uendelevu wamazingira. Dhana hii ni pana na inajumuisha vitu vyotevinavyotuzunguka katika sekta mbalimbali kama vile maji,kilimo, nishati na kadhalika. Bado sekta hii ya utuzaji wamazingira na uhifadhi haijapewa umuhimu na uzitounaostahili, kwani utekelezaji wake unakumbana nachangamoto kadha wa kadha hasa upatikanaji wa rasilimalifedha zinazoendana na Ofisi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Iringa hasaHalmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa sehemu kubwa ni kamekwa sababu ya matumizi mabaya ya mbolea yachumvichumvi bila kufuata ushauri wa wataalam pamoja nakukata miti hovyo. Nashauri Wizara itenge fedha kwa ajili yakutoa elimu kwa umma kupitia luninga, redio vipeperushi nawadau hususan Serikali za Vijiji na Vitongoji pamoja na sektabinafsi kueleza madhara ya uharibifu huo wa mazingira,ikiwemo Operesheni Kata Mti Panda Mti itengewe fedha pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mifuko ya plastiki. WaziriMkuu alivyokuwa akihitimisha hoja ya Wizara yake, alipigamarufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia miezi miwiliijayo. Hata hivyo, nitaomba Mheshimiwa Waziri wa Mazingira

Page 260: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

260

anavyohitimisha hoja yake aje na mbinu mbadala kuhusuvifungashio vitakavyotumika katika nchi yetu na namnawatakavyoweza kuzibiti mifuko itokayo nje ya nchi yetu.Vilevile ashirikiane na wahusika wa viwanda vilivyokuwavikitengeza mifuko hiyo ili kuona namna watakavyoshirikiananao kufanya kazi mbadala kwa sababu ughafla wa taarifahiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kampeni ya upandaji miti.Katika Mkoa wa Iringa kuna ustawi wa miti, matunda namboga mboga. Nashauri Serikali iweze kutenga fedha ilikusaidia kampeni ya upandaji miti ya matunda ambayopamoja na kuhifadhi mazingira itasaidia wananchi kupatakipato na kuboresha afya zao. Kwa mfano, wananchiwakipatiwa miti ya miparachichi na apple (matufaa) itakuzasana pato kwa wananchi na kuhifadhi mazingira.

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nichukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano na Mazingira),Mheshimiwa Naibu Waziri, viongozi wote katika ofisi kwahotuba yao nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeze MheshimiwaWaziri kwa uamuzi wake wa kupiga marufuku matumizi yamifuko ya nylon ifikapo tarehe 1/6/2019. Kimsingi jambo hililimekuwa ni kubwa kuliko faida ya mapato ya kodi ambayoSerikali imekuwa ikipata kutoka kwa wazalishaji nawafanyabiashara wa mifuko hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na uamuzi huumkubwa wenye manufaa mapana kwa Taifa, binafsi naonakama taarifa ya sitisho la matumizi ya mifuko hiihalijatangazwa sana. Nimemsikia Mheshimiwa Waziri akisemakwamba wamekaa na wadau wa mifuko hii kwa mudamrefu, lakini naamini kutokana na uamuzi huu mzuri waSerikali, nina ushauri kwamba ofisi yako kupitia vyombombalimbali vya habari, kupitia Watendaji mbalimbali Serikalinihususan katika Halmashauri zetu, nao wawe sehemu ya

Page 261: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

261

kusambaza katazo hili kwa sababu siyo wananchi wotewanatazama TVs, wanasikiliza Redio na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani itakuwa ni busarasana kuhakikisha wafanyabiashara wa kada zote pamojana watumiaji wanapata taarifa hii kwani ni takribani miezimiwili tu imebaki kufikia mwisho wa matumizi ya mifuko yaplasitiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiacha katazo hili muhimu,Mheshimiwa Waziri amesema katika hotuba yake kwamba,baadhi ya bidhaa zitaendelea kutumia mifuko ya nylon,kama vifungashio vya dawa na kadhalika. Nadhani kwaumuhimu siku za usoni kuhakikisha matumizi yote ya plasitikiau nylon yanapigwa kabisa marufuku kwa kuzingatia athariza mazingira na hata uzalishaji wa mazao umepungua kwasababu ya ardhi imeathirika kwa matumizi ya mifuko hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naipongeza Serikali kwajitihada kubwa za ofisi yako kwa namna inavyokabiliana nauharibifu wa mazingira hususan ukataji wa miti ovyo. Naiombaofisi yako pia itoe katazo la wananchi wote kulima kwenyemilima. Kama ambavyo katazo la kufanya shughuli za kilimokwenye vyanzo vya maji, pia kulima kwenye milimakumekuwa na athari za kuleta mabadilikoo ya tabia nchihususan kwa mvua kupungua, pia tumeshuhudia kuonavyanzo vyote vya maji vinachafuliwa na maji ya mvuayanayochanganyika na udongo kutoka milimani. Naiombasana Serikali itazame katika hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa suala la mazingirani suala mtambuka, napongeza maelezo ya MheshimiwaWaziri kusema Halmashauri zetu zina wajibu mkubwa wakusimamia suala la mazingira. Swali hapa ni je, Halmashaurizetu zina watumishi wa kutosha kusimamia mazingira? Je,Serikali inajipangaje kuhakikisha Halmashauri zinapelekawatumishi wenye elimu na weledi wa kutosha juu yamazingira? Ni vyema tukajipanga katika eneo hili.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

Page 262: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

262

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nianze mchango wangu kwa kumshukuru Mungukwa kunipa uhai na kuniwezesha kushika kalamu nakuchangia hoja hii. Pia napenda kuipongeza Serikali kwa kujana hoja ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plasticnchini. Kwa hili, pongezi kwanza zimwendee MheshimiwaWaziri Mkuu kwani yeye ndiye kwa kwanza kuja na tamkohili. Vilevile, nampongeza Mheshimiwa Waziri mwenyedhamana kwa kuona umuhimu wa jambo hili na kuamuakuchukua hatua, tena niseme hatua hii imecheleweshwasana hapa nchini, kwani athari za kimazingira juu ya matumiziya mifuko hii ya plastic ni kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nizungumzie uharibifuwa mazingira utokanao na shughuli za kibinadamu kama vilekilimo cha kuhamahama, biashara ya mazao ya misitu naujenzi wa miundombinu mbalimbali za kimaendeleo. Mfano,katika Wilaya ya Liwale, Wilaya hii imezungukwa na misitu yaasili; na kwa kuwa huko nyuma hali ya miundombinu yabarabara ilikuwa siyo mizuri, uharibufu wa misitu hii haukuwamkubwa sana lakini kwa sasa uvunaji wa magogo, mbao namkaa ni biashara inayokua kwa kasi sana na ni uvunajiusiozingatia sheria na kuwaachia wananchi wa Liwalejangwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kiasi cha ushuru Halmashauriinachopata hakiwezi kurudisha uoto wa asili wa misitu hiyokwani miti imekuwa ikipandwa pembeni mwa majengo yataasisi za Umma kama shule, hospitali na kadhalika, lakini kuleambako miti hii imekatwa kunabaki kuwa jangwa. Hivyo,napendekeza Wizara ya Maliasili na Wizara ya Mazingirazikafanye kazi kwa pamoja kutafuta namna bora ya kuonamisitu au miti inarudishiwa kupandwa pale mti ulipokatwana Ikiwezekana fedha za upandaji miti ziongezwe nazikasimamiwe moja kwa moja na Halmashauri husika. Kiasicha asilimia tano cha sasa kinachotokana na uvunaji wamazao ya misitu kifanyiwe marekebisho ili kiendane na ainaau kiasi cha uharibifu unaotokea, hivyo Halmashauri iwezekupanda miti ya kutosha.

Page 263: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

263

Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu zaidi inahitajika juu yautunzaji wa mazingira hasa kwenye utunzaji wa vyanzo vyamaji. Ufugaji wa samaki pembezoni mwa mito ni boraukapigwa marufuku, kwani mito mingi sasa imeanza kukaukabaada ya watu kuchimba mabwawa ya samaki pembezonimwa mito. Urinaji wa asali kwa njia za kizamani unachangiakwa kiasi kikubwa uharibifu wa misitu kwa kuchoma moto nakuharibu maisha ya viumbe vingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba nichangiekidogo kuhusu Muungano wetu. Kwa kuwa Muungano huuni wa muda mrefu, kizazi cha leo hakina uelewa wa kutoshakwa nini nchi hizi mbili; Tanganyika na Zanzibar ziliamuakuungana na faida za Muungano wetu na hivyo, kutambuadhamira ya Waasisi wetu. Ndiyo maana kizazi hiki kimeishiakuangalia changamoto tu za Muungano bila kuangalia faidazake kwa pande zote mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo basi, nazishauri Serikalizote mbili za Muungano kuwekeza zaidi kwenye elimu yakuelimisha jamii ya leo kuelewa Muungano. Pia palepanapotokea changamoto, basi Serikali zote mbili zichukuehatua za haraka kutatua changamoto hizo kabla hazijaotasugu na kuchafua sura nzuri ya Muungano wetu, tenanyingine zinapaswa zitatuliwe na ngazi za Taasisi za chinikama zile za Uhamiaji, TRA na ZRA. Hivyo, naiomba Serikalikulinda na kudumisha Muungano huu kwa gharama yoyoteile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba nizungumzejuu ya uchafuzi wa mazingira unaofanywa na viwandavinavyotoa moshi au vumbi mawinguni. Jambo la viwandavinavyorusha moshi angani na teknolojia iliyopitwa na wakatihuchangia kwa kiwango kikubwa uchafuzi wa hali ya hewaikiwa ni pamoja na magari yanayotoa moshi kupita kiwango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda vinavyotoa moshinashauri viwe vinatozwa tozo za uchafuzi wa mazingira ili iwekama ni juhudi za kulinda mazingira, kwani sasa nchi zawenzetu viwanda hivi sasa haviko tena na pale vilipo,

Page 264: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

264

teknolojia yake haitoi tena huo moshi. Hivyo basi, imefikawakati sasa kuazima teknolojia hiyo ili kulinda mazingira yetu.Viwanda hivi ni kama vile vya cement, chuma na viwandavya nafaka kama ngano na vile vya kuchakata kokoto naMarumaru.

MHE. DKT. CHRISTOPHER K. CHIZA: MheshimiwaMwenyekiti, nampongeza Mheshimiwa Makamu wa Rais,Waziri na wasaidizi wenu wote kwa kazi nzuri katika masualaya Muungano na Mazingira. Kipekee, naipongeza Serikali kwahatua yake ya kuondoa mifuko ya plastiki sokoni ifikapotarehe 31 Mei, 2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchangia katikamaeneo matatu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania siyo kisiwa. Kwakuwa nchi nyingi zilizoendelea zinaratibu matumizi mazuri yambegu za GMO, nashauri wataalam waendelee kufanyautafiti wa kitaalam hususan kwenye mbegu za mazaozinazotumia teknolojia ya GMO ili kujua faida na madharayanayotokana na teknolojia hiyo badala ya kuchukua uamuziwa jumla wa kuikataa teknolojia ya GMO. Kwa mfano, utafitiumeonesha kuwa uzalishaji wa pamba kwa kutumiateknolojia ya GMO umeongezeka maradufu katika nchizinazozalisha pamba kwa GMO (Wizara ya Kilimo wanazotakwimu).

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiongeza uzalishaji wapamba tutawezesha upatikanaji wa malighafi kwa ajili yaviwanda vya nguo tunavyoanzisha sasa. Hata hivyo,kutakuwa na haja ya kufanya utafiti wa kina kuhusu matumiziya mafuta ya kula yanayotokana na pamba itakayozalishwakwa teknolojia ya GMO.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matumizi makubwa ya majini yale ya kilimo cha umwagiliaji kwa sababu consumptiveuse ya mimea inayomwagiliwa ni kubwa kuliko matumizi yanyumbani (domestic use), viwandani na yale ya miradi yakuzalisha umeme ambayo consumptive use ni sawa na

Page 265: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

265

hakuna kwa sababu karibu maji yote yanayotumikakuendesha mitambo yanarudishwa kwenye mto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu ni kushirikianakwa karibu na Wizara inayohusika na kilimo cha umwagiliajina Wizara ya Maji, makampuni makubwa ya miwa (sukari)na mashamba makubwa ili wazingatie mambo muhimuyafuatayo:-

(a) Matumizi sahihi ya maji kwa mazao husika (crop waterrequirements) na water rights ili kuepuka matumizi makubwayanayosababisha vyanzo vya mito kukauka.

(b) Kulinda uharibifu wa ardhi kwa chumvi na kuwa nakilimo endelevu. Kila mradi wa umwagiliaji, hasa ile yaflooding iwe na miundombinu ya kutoa maji ya ziadashambani (drainage systems) kwa sababu ukosefu wamiundombinu hiyo husababisha chumvi kuongezeka (salinity)na ardhi inaharibika. Gharama za kurejesha ardhiinayoharibika kwa salinity ni kubwa sana.

(c) Usimamizi wa sheria nyingine zinazoshabihiana naSheria ya Mazingira, mfano Sheria ya Rasilimali za Maji ya 2009.Wenye viwanda vinavyotumia maji ni lazima waheshimusheria hii pamoja na sheria nyingine. Katika miaka ya 1990,kulikuwa na mgogoro mkubwa kwenye Kiwanda cha KaratasiMjini Moshi (Kibo Pulp and Paper Board). Tatizo lilianza paleambapo kiwanda kilipewa water right kwa ajili ya kutumiakiwandani kuzalisha karatasi. Katika kiwanda hicho, matumizimengine yalikuwa ya kemikali ya aluminium sulphateambayo ina sumu (toxic).

Sheria ya Rasilimali Maji iliwataka wenye kiwanda kujengamtambo wa kusafisha maji (treatment plant) kabla yakuyarudisha maji katika Mto Karanga baada ya kuyatumiakiwandani. Kiwanda hakikufanya hivyo badala yakekilichepusha maji katika mfereji na kuwapelekea wakulimawa mpunga. Matokeo yake yalikuwa mawili; moja, wakulimawaliwashwa na sumu ya Al2(SO4)3; pili, mazao ya mpungayalipungua.

Page 266: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

266

Mheshimiwa Mwenyekiti, inawezekana suala hilililisharekebishwa kwa sababu wanamazingira waliingilia.Ushauri wangu ni kwamba sheria zote ambazo zinashabihianana utunzaji wa mazingira, zisimamiwe vizuri na zieleweke kwangazi zote katika Serikali za Mitaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana nami kuchangia kwenye Wizara hii nyeti namuhimu ya Muungano na Mazingira. Wilaya yetu ya Kilosa niWilaya Kongwe sana hapa nchini; na kwa kweli changamotokubwa sana tunayoipata kila mwaka ni mafuriko ya marakwa mara ambayo yanasababisha vifo, uharibifu mkubwawa mashamba, mali na miundombinu mbalimbali katikaWilaya ya Kilosa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sababu kubwa ya mafurikohayo ni kupasuka kwa bwawa la Kidete ambapo mvuazinaponyesha kidogo tu yanamwagika kwa wananchi lakinipia kupoteza ulekeo wa mto Miyombo ambao ni mtounaopita kwenye kata nyingi za Wilaya ya kilosa yenyeMajimbo ya Kilosa kati na Mikumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaiomba sana Serikaliitusaidie pesa ili kujenge bwawa hili muhimu la Kidete kwakuwa Waziri wa Maji alishafanya ziara na kuahidi kuwa pesazimeshatengwa na wapo kwenye mchakato wa kumalizanana mkandarasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mto Miyombotunaomba sana tujengewe tuta katika Kata ya Masanzeiliyopo Jimbo la Mikumi ambapo kwa ujenzi huu wa tuta nimuhimu sana na utasaidia sana kuzuia maji yasiende kwenyemakazi ya wananchi na kuepusha maafa ambayoyanatokea mara kwa mara kwenye kata hii pamoja na KataMagomeni na kuleta maafa makubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tunaiomba sana Serikalikuchonga kingo za Mto Miyombo hasa kwenye maeneo ya

Page 267: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

267

Kata ya Kilangali ili kuzuia maji kuingia kwenye maeneo yawananchi (makazi na mashamba yao) na kuyaharibu vibayasana kutokana na mto huu kupoteza uelekeo mara kwa marakwa kuzidiwa na maji mengi ambayo yanatiririka kwa wingisana hasa kipindi kama hiki cha masika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho naomba sanaSerikali iongeze bajeti ya Wizara hii hasa kwenye mfuko wamazingira ili kuwezesha Wizara hii kutimiza majukumu yakemuhimu sana kwa Taifa hili kwenye masuala muhimuyahusuyo mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,hoja yangu kubwa kwa Mheshimiwa Waziri wa Mazingira ninamna Wizara inavyoachia mifugo hasa ng’ombe kuharibumazingira yetu kwa kiwango kikubwa. Mkoa wa Lindi ni mojaya mhanga mkubwa wa hali hii; mifugo inaingia bilakuzingatia uwezo wa mazingira yaliyopo katika eneo husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Lindi ipo hatarinikugeuka jangwa. Jimbo langu la Mchinga ni kielelezo chahoja hii. Wafugaji wanavamia maeneo yote oevu ya Jimbola Mchinga kama vile bonde la Mbwenkulu na eneo la bondela Mkoa lililopo katika Kata za Mvuleni na Kitomanga. Wizaralazima ishirikiane na Wizara ya Mifugo katika kupangamaeneo mbalimbali hapa nchini. Uchungaji holela wa mifugoyetu utapelekea kuligeuza Taifa letu kuwa jangwa sikuchache zijazo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja yangu ya pili ni kuhusumiti adimu ya mikoko na mkakati wa nchi wa upandajimikoko. Kutokana na umuhimu wa miti hii, Serikali inapaswakuongeza juhudi katika kuilinda na kuongeza miti ya mikoko.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: MheshimiwaMwenyekiti, kauli za wanasiasa zinakua kikwazo katika ustawiwa Mazingira yetu. Sheria ya mita 60 kama ikifanywa kamasiasa na kuruhusiwa kuharibu vyanzo vya maji, itakuwa kiama

Page 268: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

268

kwa nchi yetu, kwani itaharibu mazingira, kusababishaupotevu wa mvua na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vipi vifungashio vya mikate,ni sehemu ya katazo hilo? Kwa nini tusitoe muda maalumkwa wazalishaji hawa? Naomba ku-declare interest kwambamimi nazalisha mikate na kutumia mifuko hiyo. Badohakujawa na mbadala sokoni na wafanyabiasharawashanunua mizigo na hata kubadilisha mashines.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Wizara ije itusaidiekutengeneza kingo za bonde la Mto Msimbazi kwani bondelinazidi kukua na kutafuna majengo na makaazi ya watu.Tunaomba Wizara itoe kipaumbele kwa mto huu.Tunawaombeni sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nishati mbadala kama gesizishushwe bei hata kupunguza kodi ili wananchi wengiwatumie gesi badala ya kuni na mkaa kama ilivyo sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vikundi vya akina mamaviwe motivated na Wizara. Wale wanaozalisha mkaambadala binafsi, naikaribisha Wizara kutembelea mradi waakina mama wa Tabata wanaozalisha mkaa mbadala.Karibu mtunishe mfuko wao waweze kupata mashine yakisasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Wizara isaidiewabunifu kubuni zaidi mashine za kuzalisha mkaa mbadala.

MHE. SONIA J. MAGOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza nianze kwa kuipongeza Wizara kuona umuhimu wamazingira na afya kwa wananchi kwa kutoa tamko lakusitisha matumizi ya mifuko ya plasitikic kuanzia tarehe 1 Juni,2019. Kama tujuwavyo, mazingira bora na usafi ni kiunganishikikubwa cha kuondoa umasikini na kukuza uchumi wa nchina kuleta maendeleo kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jamii ni lazima ihamasishwekuwa rafiki wa mazingira na waelimishwe kuwa uharibifu wa

Page 269: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

269

mazingira ndiyo unaopelekea kuharibika kwa miundombinu,upungufu wa maji, matatizo ya kiafya, upungufu wa mazaokutokana na uharibifu wa rutuba katika udongo. Vile vilekukosekana kwa mvua na ongezeko la joto vyote hivyovinachangiwa na uharibifu wa mazingira hayo. Elimu yakutosha kwa wananchi ni lazima iendelee kutolewa kwa kasiili wajue umuhimu wa kutunza mazingira. Maana ukiangaliavijijini suala hili la elimu ya mazingira bado sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna changamoto nyingineya wazoa taka mitaani. Unapomwambia Mtanzania wakawaida, yaani mwenye maisha duni atoe shilingi 5,000/= ilitaka zake zibebwe kila wiki, hapa suala la utunzaji wamazingira tunaweza kulifanya kuwa gumu. Serikali iangalieinafanya nini katika hili ili kila mtu aweze kumudu kutoa takakila wiki (gharama za wazoaji taka).

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia suala la mitaro katikamitaa yetu; watu wamekuwa wakikamatwa kwa kumwagamaji nje ya nyumba zao na wakati mwingine kutozwa fainihadi shilingi 50,000/= ili mradi tu pakiwa pabichi hata kamani maji safi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kutunza mazingira nakuweka urahisi na amani kwa wananchi ili wawe rafiki namazingira yao, Serikali iwatengezee mazingira mazuri yakuyatunza. Kama hilo la kuwa na mitaro mitaani, tozo yashilingi 5,000/= kwa wanaomwaga maji ovyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kusikiliza hotubahii, pia nimeona upungufu kwa sehemu kubwa ya hotubakugusa mazingira kuliko Muungano na hiyo kupelekeakuziacha changamoto nyingi za Muungano bila majibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile Serikali iangalieuwezekano wa kupeleka elimu ya Muungano kwenyevyombo vya habari ili watu wengi wajifunze na kupata majibuya maswali waliyonayo, ikibidi elimu hii ianzie Shule za Msingi,watoto wakue na uelewa wa Muungano.

Page 270: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

270

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia changamoto zinazokuaaddressed zipatiwe ufumbuzi ili tuudumishe Muungano wetuna kuondoa malalamiko yanayokuwa yanajirudia rudia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MWENYEKITI: Tumemaliza uchangiaji, sasa tunaanzaupande wa Serikali. Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha,jiandae Naibu Waziri Mazingira na jiandae Mtoa Hoja.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa fursa hii. Nianze kwakuwapongeza sana kaka yangu Mheshimiwa January, Waziri,pamoja na Naibu Waziri kaka yangu Mheshimiwa Sima kwakazi kubwa ambayo wanaendelea kuifanya kwenye Wizarahii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme mambomachache sana baada ya pongezi, kwenye hotuba hii nahoja hii iliyowekwa mezani na Mheshimiwa Waziri wa NchiOfisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na jambo la kwanzaambalo limeonekana kwenye vitabu vyote vitatu, kitabu chaUpinzani, kitabu cha Kamati zote mbili za Kudumu za Bungewalipoongelea fedha ambazo zimetolewa, hasa fedha zamaendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha hizi hutolewakulingana na jinsi zinavyopatikana, kwa hiyo zikipatikana thenmgao unafanyika nani apate nini kulingana na majukumuya Ofisi husika na kama ilivyooneshwa kwenye vitabu hivibajeti ilipitishwa na sisi hasa hii sehemu ya kujenga na kufanyaukarabati wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Luthuli, Tunguu naWete-Pemba. Tumetoa kiwango hiki cha fedha shilingi milioni538.4 ndizo ambazo zimetolewa kwa ajili ya ukarabati waOfisi hii, lakini ninachoomba kusema hapa ni pale ambapovitabu vyote vimesisitiza kwamba fedha hii iliyotolewa nifedha ya nje hakuna fedha ya ndani.

Page 271: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

271

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeanza kwa kusematunatoa fedha hizi kulingana na upatikanaji wa fedha husika.Katika hili mkononi mwangu nimebeba kitabu cha hotubaya bajeti ya Serikali nzima aliyoisoma Mheshimiwa Waziri waFedha na Mipango. Ndugu zangu tunapojadili jambo hilitusioneshe kwamba kuna mtu ambaye hapewi kwa sababuya aina fulani ya Wizara yake, hapana. Vyanzo vya mapatovya bajeti kuu wa Serikali vimetajwa kwenye kitabu hiki. Mojaya vyanzo vya mapato kama ilivyoelezwa, tuna mapato yandani na tuna mapato ya nje ambayo kwenye mapato yanje tuna misaada na mikopo nafuu, tuna misaada na mikoponafuu kwa ajili ya miradi ya maendeleo, tuna misaada namikopo nafuu ya kisekta kwa hiyo tunapoongelea jambo hilituiongelee bajeti ya Serikali kama ilivyowasilishwa na vyanzovyake vya mapato kuliko kusema fedha za ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zinapopatikana kwenyekapu, Mfuko Mkuu wa Hazina zinapoingia fedha hizizinagawiwa kutokana na mgao ambao kwahiyo haingii akilinitunaposema kwamba huyu apewe fedha za ndani wakatitayari ana fedha za nje na Wizara nyingine haina fedha zanje, kwa hiyo kwa kuwa tu tunataka na huyu aonekane anafedha za ndani basi tulazimishe hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niliombe Bunge lako Tukufuliweze kuzingatia yanayowasilishwa na tunayoyapitisha ndaniya Bunge lako Tukufu. Hiyo ilikuwa hoja ya kwanza ambayonilikuwa napenda kusema kuhusu mapato ya Serikali na jinsigani tunavyoyapeleka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambaloningependelea kulitolea maelezo hapa ni kuhusu Akaunti yaFedha ya Pamoja. Nakumbuka vizuri sana mwaka jana tulitoaahadi kama Serikali kwamba jambo hili l inaendeleakufanyiwa kazi. Tunafahamu, Serikali ina ngazi zake za kufanyamaamuzi, tayari watalaam wetu wameshamaliza kulifanyiakazi jambo hili na sasa tulipo kikao kilifanyika tarehe 9 Februari,2019 chini ya Mwenyekiti wa Kamati hii ambaye ni Makamuwetu wa Rais anafanya kazi nzuri sana mama yetu,Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Page 272: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

272

Mheshimiwa Mwenyekiti, kweli nimpongeze sanaMama Samia amesimama imara kuhakikisha Muungano wetuunakuwa imara na unaendelea kudumu tofauti nainavyowekwa hapa kwenye Bunge lako Tukufu kwambaChama cha Mapinduzi, tukumbuke ni Chama cha Mapinduzindicho kilichoasisi Muungano huu. Ni viongozi wa vyama hiviviwili kwa dhamira njema ya pande zote mbili za Muungano.Ndiyo maana nataka kumpongeza kwa dhati ya moyowangu Mheshimiwa Makamu wa Rais. Angekuwa na moyokama wa hao wanaotaka kupotosha Watanzania kwenyeBunge lako Tukufu tusingetoka. Serikali ina dhamira njemaya kuhakikisha jambo hili tunafika muafaka ambapotutakapoanza kuja kwenye migao halisi sasa ya fedha hizipande zote mbili za Muungano ziwe zimeridhika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimemsikiliza kaka yanguMheshimiwa Jaku anasema, Zanzibar wakati wanaunganawalikuwa wachache, hivyo Watanzania Bara wakatitunaungana tulikuwa milioni 55? Kwa hiyo tuangalie hoja hizi,base yetu ni nini ya kuleta hoja hizi. Kwa hiyo tunaposema4.5 ni ndogo umechukua kigezo gani kusema 4.5 ni ndogoinayopelekwa Zanzibar? Kwa hiyo tarehe 9 Februari, 2019,kikao kilichofanyika hapa Dodoma maamuzi yalifanyika.Kama tulivyokuwa tuna-report siku zote kwamba Serikaliinayafanyia kazi pale ambapo hatujaelewana na sasatumeelewana na unaandaliwa Waraka wa Baraza laMawaziri ili kwenda kufanya maamuzi ya mwisho na jambohili liweze kufika mwisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Komboamesema tutoe commitment, commitment ndiyo hiyo.Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kikao hili ameshaelekeza natayari waraka umeanza kuandaliwa, anataka commitmentnyingine ipi Mheshimiwa Kombo? Kwa hiyo Serikali ya Chamacha Mapinduzi imedhamiria kuona Muungano huuunaendelea kuwa imara, Muungano huu unaendelea kuwana faida na pande mbili zote za Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalolimeongelewa ni kuhusu kodi mara mbili. Nimekuwa mimi na

Page 273: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

273

naomba niwe shahidi ndani ya Bunge lako Tukufu, nimekuwanikisema siku zote hakuna kodi, hakuna bidhaa yoyoteinayotozwa mara mbili. Kinachotokea nimesema hapa najambo hili ni katika mambo ambayo yapo kwenye Warakaulioandaliwa wa Baraza la Mawaziri kwamba valuationsystem zetu kati ya Zanzibar na Tanzania Bara siyo moja.Watalaam wetu wamemaliza kuandaa taarifa yao yakitaalam, wameshaileta tayari inaingia kwenye Waraka huuunaoshughulikia kero za Muungano ili sasa tuweze kulitatua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuko kwenye dunia huruambayo tunafanya boiashara. Haiwezekani jirani yakoakaingiza bidhaa kutoka kwa jirani mwingine kwa bei ya chinihalafu bidhaa hiyo useme uilete nyumbani kwako ili uwezekufanya biashara. Hiyo haitowezekana, ni ngumu sana, kamakweli sisi ni Taifa moja, ni lazima tuwe na valuation systemmoja yenye manufaa mapana kwa Watanzania kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea kulikumbushaBunge lako Tukufu hakuna maendeleo bila kodi. Lazima kodiil ipwe na lazima il ipwe katika rate zi l izokubalika.Tunachikifanya Mamlaka ya Mapato Tanzania tuna-adoptinternational system…

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, tume-adopt international system ambayo…

MWENYEKITI: Mheshimiwa jaku kaa chini please.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, tume-adopt international system, tunainternational database sasa huwezi ukajifungia chumbaniukasema mimi siangalii kinachotokea duniani, mimi natakanilinde watu wangu, unalinda watu wako ukiwa na ninimkononi? Kwa hiyo ni lazima tukubaliane na duniainakwenda vipi, global business inakwenda vipi ili kwa pamojatuweze kuwaletea maendeleo Watanzania.

Page 274: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

274

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mgao wa Mashirikaya Umma; nilijulishe Bunge lako Tukufu kama ambavyowamesema Waheshimiwa Wabunge hapa, Benki Kuutunapeleka na tayari tarehe Mosi Februari, 2019 tumepelekazaidi ya shilingi bilioni 15 ambazo ulikuwa ni mgao kutokagawiwo la Benki Kuu. Kwa Mashirika mengine yaliyosaliatunaendelea kuyafanyia kazi na ni moja ya mamboyanayoshughulikiwa kwenye kero za Muungano ili kwapamoja Mashirika haya yaweze nayo gawiwo waliloanzakutoa, kwanza lazima, tukumbuke Mashirika haya yalikuwahayafanyi vizuri, Serikali imefanya jitihada kubwa Mashirikahaya yameanza kufanya vizuri kwa sasa tunalishughulikia ilikama linavyoingia gawiwo la Benki Kuu, moja kwa moja…

MWENYEKITI: Nakuongezea dakika moja malizia.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Kwa hiyo tunakwenda kumaliziana mashirika mengine likiingia tu gawiwo lile kwenye Mashirikahaya iende moja kwa moja asilimia 4.5 kwenda Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Benki yetu TPB; hiihuwa tunagawana kulingana na hisa ulizonazo kwenye Benkihii. Kwa hiyo hili halina changamoto yoyote, limekuwalikitendeka miaka yote ya Muungano na tangu TPB Bankilipoanza kutengeneza faida.

Mheshimiwa Mwenyekjiti, baada ya kusema haya,nirejee kuwapongeza Waheshimiwa Mawaziri Wizara hii nanaunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Naibu Waziri, Mazingira, ajiandae mtoahoja.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwakuwa ni mara yangu ya kwanza leo, naomba nichukue fursahii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu. Pia nimshukuru sanaMheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa

Page 275: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

275

kuniteua na kuendelea kuniamini kuwa Naibu Waziri, Ofisi yaMakamu wa Rais, (Muungano na Mazingira).

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nichukue fursa hiikumshukuru Makamu wa Rais, Mama yetu, Mama SamiaSuluhu kwa maelekezo na ushauri mzuri ambao amekuwaakiutoa kwenye Wizara na tumekuwa tukiufanyiakazi.Nichukue fursa hii pia kumshukuru Waziri Mkuu wa ushauriambao ameendelea kutupatia. Nimshukuru pia Waziri wanguMheshimiwa Januari, amekuwa ni mstari wa mbele sanakunipa mwongozo mzuri wa kuhakikisha natekelezamajukumu yangu, nimshukuru sana.

Mhshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru Katibu Mkuu,Naibu Katibu Mkuu pamoja na Watendaji wote katika Wizarayetu, tumefanya kazi kwa pamoja vizuri na hatimayetunaendelea vuzuri. Vile vile nimshukuru Mheshimiwa Spika,Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge wote, Mwenyekiti naWenyeviti wengine kwa kazi kubwa ambayo tumeendeleakuifanya kwa pamoja. Mwisho lakini siyo kwa umuhimu,niwashukuru pia wananchi wa Jimbo la Singida Mjini,wamekuwa wavumilivu kwa kipindi chote ambachonikitekeleza majukumu ya Serikali. Mwisho kabisa niwashukurupia Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira wametupaushirikiano mkubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwapongeze WaheshimiwaWabunge wote waliochangia na wengine wamechangiakwa maandishi, lakini nijikite kwenye maeneo machachehasa yahusuyo mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiangalia hotuba ya bajetiya Kambi Rasmi ya Upinzani ukurasa wa 10 wamegusia sualala Stiegler’s Gorge kwamba misitu inafyekwa sawa naukubwa wa Dar es Salaam nzima. Jambo hili likisemwa hivikwa Watanzania linaweza kuleta sura tofauti. Mtanzaniaanayeifahamu Dar es Salaam anaweza akaona eneo lilelinalokatwa miti litabaki kuwa jangwa, lakini ni wajibu wetusasa kufika mahali kueleza faida ya ule mradi wa Stiegler’sGorge ni nini.

Page 276: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

276

Mheshimiwa Mwenyekiti, pale Mbuga ya Selou inakilometa za mraba zaidi ya 50,000 lakini ni asilimia tatu tuambapo ule mradi unaotarajiwa kujengwa naumekwishaanza ndiyo zitatumika kwa ajili ya kuhakikishatunapata umeme wa megawatts 2,100.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile tunahitaji umemena tunahitaji umeme rafiki wa mazingira. Sisi ambao tukokwenye eneo hili la mazingira, huu umeme kwetu ndiyoumeme rafiki wa mazingira kuliko umeme wa mafuta. Kamaumewasikia Waheshimiwa Wabunge wengi wamekuwawakizungumza kwenye bajeti iliyopita ya TAMISEMI wanatakaumeme wa REA na mambo mengine yote, lakini umeme ulewanaouhitaji wanahitaji wapate umeme rafiki na hapanilitarajia na mimi kuona Waheshimiwa Wabunge kwanzawanampongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa na hatuakubwa ya ujasiri ya kuhakikisha kwanza tunapata umemerafiki wa mazingira ambao tunapata megawatts 2,100. Eneohili linahitaji ushirikiano wa pamoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini faida kubwa sanatunaipata. Unapozungumzia tu ile miti ambayo sisi hatukatiasilimia 3, ile miti ni kama 1.8 lakini faida ya ule umeme nikubwa kwa nchi nzima na duniani. Wamezungumzia habariya mabadiliko ya tabianchi kwamba tuwe na umeme rafikilakini leo wananchi wetu wanawekewa umeme ama umemeunaofika vijijini unahitaji kuwa wa gharama nafuu ambaponi lazima tuwe na umeme unaotokana na maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye eneo hili la umemekumekuwa na mambo mengi watu wanayaeleza lakiniwanaeleza kwenye eneo la kukata misitu lakini waeleze faidaya kile kinachopatikana pale. Mbali ya faida ya ule mradikwenye umeme pia kuna ajira, kilimo, ufugaji na mambomengi ambayo tunahitaji tushirikiane na wenzetu kwa ajili yakuhakikisha kwanza tunaweza kupata umeme huu ambaoutatusaidia kufikia malengo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yako maeneo menginewenzetu wamejaribu kuzungumzia lakini nieleze jambo moja

Page 277: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

277

kwenye eneo la taka ngumu na taka hatarishi, wakatinafanya ziara kwenye Mikoa sita ya Nyanda za Juu Kusinimoja ya hoja ilikuwa ni hiyo ya vyanzo vya maji lakini nyingineya taka. Vyanzo vya maji Mto Rufiji wenyewe unaunganishwaama unalishwa na mito mikuu mitatu: Mto Rwengu, MtoKilombero na Mto Ruaha Mkuu. Nimeenda kuangalia vyanzovya maji na namna vinavyohifadhiwa, nataka niwahakikishieWatanzania tunayo maji ya kutosha na Watanzania niwaadilifu wametunza vyanzo vya maji na tunahitajikuendelea kuwapa elimu waendelee kutunza vyanzo vyamaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nimeangalia eneo lataka ngumu na taka hatarishi, Kamati yangu imelizungumzavizuri, moja ya eneo ambalo linaleta changamoto ya taka,nimemsikia Mheshimiwa Hawa Mwaifunga pia amezungumzaeneo hili la taka, ni eneo ambalo ni vizuri kwa kwelitukashirikiana kwa pamoja. Nimeendelea kutoa elimukwenye mikoa yote ambayo nimepitia, nimetembeleamadampo na kuona namna ambavyo wanateketeza ziletaka zinapotoka majumbani na kupelekwa kwenyemadampo, eneo lile tumewaomba wenzetu wa Serikali zaMitaa walioko chini viongozi wale tunashirikiana kwa pamojajapo tunajaua kwenye Sheria yetu ya Mazingira ya mwaka2004, Ibara ya 6 kwamba jukumu la usafi ama la utunzaji wamazingira ni la kila Mtanzania ama ni la kila mwananchiambaye anaishi Tanzania. Eneo hili niwaombe WaheshimiwaWabunge tushirikiane pamoja, suala la uhifadhi wa mazingirasiyo la Wizara moja ama la Serikali peke yake ni suala la kilaMtanzania na kila kiongozi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Mheshimiwa Genzabukeamezungumza vizuri na niseme tu kwamba tumepokeaushauri wake juu ya kushirikiana na wenzetu hasa mashirikayale yanayo-deal na wakimbizi. Nimefika mpaka KageraNkanda nimeona uharibifu mkubwa wa miti na maeneomengine. Nimuahidi Mheshimiwa Genzabuke jambo hilitumelipokea na tutalifanyia kazi ipasavyo. (Makofi)

Page 278: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

278

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mtoleanikuahidi tu kwamba baada ya Bunge hil i nadhaninitakapokwenda Jimboni sasa niwasalimie wananchi wangu,nitakwenda kufanya ziara Dar es Salaam. Jambo kubwahapa siyo tu kutoza faini na hili tuliweke wazi, kwanzatunahitaji watu wale wapewe elimu. Kwa sababu kamaWatanzania kwenye gereji na maeneo menginehawajapewa elimu na tukakimbilia faini, hili kwa kwelihatutakubaliana nalo. Nikuahidi kwamba nitafika mwenyewenifanye ziara na pia tuwashirikishe wananchi ambaowameamua kuwa wajasiliamali kwenye maeneo haya.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wamezungumza suala laelimu, kwa kweli tunakubaliana nalo, suala la elimu halinamwisho hata kama tunaendelea kutoa inawezekana badoelimu inahitajika sana. Nimshukuru sana Mheshimiwa SaadaMkuya amesema elimu ya Muungano inayotakiwa sasa ianzieBungeni. Hili tunakuunga mkono, tutaanza nalo, najuaMheshimiwa Waziri ataeleza vizuri suala laMuungano.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini suala la elimu ni jambokubwa sana na siyo jambo la Wizara au Serikali peke yake,kila Mtanzania anayeelewa juu ya umuhimu wa utunzaji wamazingira anapaswa kuwaelimisha na wengine. Pia anayejuaumuhimu wa Muungano anapaswa kuwaelimisha nawengine. Sisi tutakuwa mstari wa mbele, tutaendelea namajukumu na mikakati yetu ya kuhakikisha kwamba elimu hiiinatolewa kadri inavyotakiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie kuendeleakuwaomba Waheshimiwa Wabunge kadri ambavyowametupongeza waendelee kutupa ushirikiano wa dhati nasisi kama ambavyo mnafahamu tunafikika na tuko tayarikufanya kazi wakati wote. Pale tunapobanwa mtuwie radhiinawezekana tusifike kwa wakati lakini tunaweza kushaurianana kusaidiana, majukumu haya yote ni yetu pamoja.

Page 279: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

279

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa, nichukuefursa hii kuishukuru sana familia yangu, mke wangu na watotoambao nao wamenivumilia kwa kipindi chote hikinimeendelea kutekeleza majukumu yangu vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya,naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Waziri mtoa hoja.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza, naomba nishukuru kwa fursa uliyonipa ya kujakuhitimisha hoja hii hapa siku ya leo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kuwashukuruwachangiaji wote, kwanza kwa Kamati zote mbili: Kamati yaViwanda, Biashara na Mazingira na Kamati ya Katiba naSheria kwa taarifa nzuri walizozitoa pamoja na ushauri, maonina mapendekezo ambayo wameyatoa katika taarifa zao.Pia napenda niwashukuru wachangiaji wote waliochangiakwa maandishi walikuwa 25, waliochangia kwa kuzungumzawalikuwa 9, jumla watu 34.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia napenda kuipongezaKambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa taarifa yao waliyosomana maneno yao walitueleza na yote tumeyapokea na yoteni ya kujenga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nimshukuru NaibuWaziri wa Fedha ambaye ametusaidia kuelezea baadhi yamambo na kujibu baadhi ya hoja. Pia namshukuru NaibuWaziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)Mheshimiwa Mwalimu Sima naye kwa mchango wake namajibu aliyoyatoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitajikita kwenye masualamachache ya jumla ambayo Waheshimiwa Wabungewaliyachangia. Kwanza suala la biashara kati ya Zanzibarna Bara ni jambo ambalo limejitokeza katika michango ya

Page 280: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

280

Waheshimiwa Wabunge wengi waliochangia masuala yaMuungano. Bahati nzuri Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedhaametusaidia kujibu kwamba changmoto za kikodi ndiyozilizokuwa zinakwamisha biashara kati ya Bara na Zanzibarzilitokana na mfumo tofauti wa ukadiriaji wa kodi kwa bidhaazinazoingia katika vituo vya forodha vilivyoko upande waZanzibar na vituo vya forodha vilivyoko upande wa Bara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hilo sasalinashughulikiwa kwa kuweka mfumo mmoja wa ukadiriaji wakodi kiasi kwamba bidhaa itakayoingia kwenye kituo chaforodha cha Zanzibar ikadiriwe kodi sawa na kituo chochoteambacho bidhaa hiyo imeingia kwa upande wa Bara. Imaniyetu ni kwamba hilo litapunguza malalamiko na maelezokwamba kunakutozwa kodi mara mbili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutambua haja yakushughulikia masuala ya fedha na biashara kwa wakatiwote, Kamati ya Pamoja ya kushughulikia changamoto zamasuala ya Muungano iliunda Kamati Ndogo ya Fedha,Biashara na Uchumi ya Mawaziri, Makatibu Wakuu nawataalam ambayo itakuwa inakutana mara mbili kwamwaka kushughulikia masuala ya fedha, uchumi na biasharayanayojitokeza mara kwa mara. Imani yetu ni kwambamfumo huu na Kamati hii sasa itasaidia kusukuma mambohaya kwa haraka zaidi na kutatua changamoto za biasharazinazojitokeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, imani yetu sisi tuliopo katikaOfisi ya Makamu wa Rais ni kwamba uchumi wa TanzaniaBara ni mkubwa kuliko uchumi wa Zanzibar na Zanzibar lazimaifikie soko la Bara na Bara vilevile lazima iwe na uwezo wakufikia soko la Zanzibar bila vikwazo vyovyote. Muungano huuni wa kisiasa, kijamii pia kiuchumi. Kwa hiyo, imani yetu nikwamba moja ya shabaha za Muungano ni kuleta ustawiwa watu wa pande zote na Muungano usionekane kikwazocha ustawi wa upande mmoja au mwingine. Sisi katika Ofisiya Makamu wa Rais, kwa maelekezo ya MheshimiwaMakamu wa Rais ni kwamba tufanye jithada zote ili fursa zauchumi, biashara na ustawi na zenyewe ziendelee.

Page 281: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

281

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wa Bara na Zanzibarwamekuwa wanafanya biashara hata kabla ya Muunganokwa miaka mingi, hata kabla ya Uhuru, hata kabla yaMapinduzi. Imani yetu ni kwamba kuwepo kwa Serikali kusiwekikwazo kwa biashara ya asili ambayo imekuwepo kwa miakamingi kati ya watu wa pande zote mbili. Hiyo ni dhamira yetukwamba ukubwa wa soko la Bara usaidie kujenga uchumiwa Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Tume ya Pamoja yaFedha, nadhani Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha amelijibulakini nitapenda niongezee machache. Ni kweli Tume yaPamoja ya Fedha imeundwa kwa mujibu wa Katiba na vilevileMfuko wa Pamoja na wenyewe umeundwa kwa mujibu waKatiba. Hili suala linajirudia mara kwa mara hapa Bungenikuhusu lini Mfuko huo utaanzishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtakumbuka kwamba kwamujibu wa Katiba, moja ya kazi za Tume ya Pamoja ya Fedhani kuchunguza kwa wakati wote mfumo wa shughuli za fedhawa Jamhuri ya Muungano na pia uhusiano katika mamboya kifedha kati ya Serikali mbili. Hiyo ni moja ya majukumumatatu ya Tume ya Pamoja. Tume hiyo ilifanya kazi kubwasana kuanzia miaka ya 90 na mwaka 2006 ikawasilisha ripotiSerikalini, nakumbuka ilikuwa tarehe 9 Oktoba, 2006 kwaWaziri wa Fedha wakati huo Mama Zakia Meghji na ripoti ileTume ilikuwa ni ya mapendekezo ya vigezo vya kuchangiana kugawana mapato ya Muungano. Ni ripoti iliyotokana nastudy ya muda mrefu kwenye nchi nyingi kuhusu mfumo sahihi,bora na na sawia (equitable) wa kugawana mapato nakuchangia mapato ya Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya ripoti i lekupokelewa, Serikali zote mbili ziliahidi kuifanyia kazi na kwelibaada ya pale ikapelekwa kwenye Baraza la Mawaziriwataalam wakaifanyia kazi, Baraza la Mawaziri la Jamhuriya Muungano wa Tanzania na mara kadhaa mapendekezoyale yalitengeneza cabinet paper ili yaweze kupitishwa natuwe na mfumo bora ikiwemo kuanzisha Akaunti ya Pamoja.

Page 282: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

282

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati mbaya hilohalikutokea kwa sababu moja au nyingine hadi tukaanzamchakato wa Katiba ambapo ndiyo ulionekana kwambautakuwa mfumo bora zaidi wa kushughulikia jambo hili. Kwahiyo, imani yetu ni kwamba mchakato wa Katibautakaendelea basi suala hili pia litaendelea kushughulikiwa.Tunashukuru kwamba pia Wizara ya Fedha inaendeleakulishughulikia suala hili. Kwa hiyo, Akaunti ya Pamoja ni takwala Kikatiba na lazima litekelezwe na lazima litatekelezwa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu vikao vya Kamati yaPamoja, tumesikia kwenye taarifa ya Kambi Rasmi ya Upinzaniikisema kwamba vikao hivi havina maana yoyote kwambavinakaa, hatuoni matunda na hakuna utekelezaji nakadhalika. Labda niseme tu kwamba mwaka 2006tulipoanzisha utaratibu mpya wa Kamati ya Pamoja ya Fedhakulikuwa na changamoto 15 za Muungano na kwa kutumiamfumo huu wa vikao zimetatuliwa changamoto 11 zimebakichangamoto tano (5).

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto hizizimetatuliwa katika vikao na siyo kwa njia nyingine na sikuzote mambo yote yanamalizwa kupitia vikao. Kwa hiyo, sisihatuamini kabisa kwamba vikao hivi havina maana kwasababu tumeona matunda yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu wanapokuwa namambo wanayamaliza kupitia vikao. Kwa hiyo, ingependezakama wenzetu Waheshimiwa wangetueleza zaidi ya vikaoni ipi namna bora zaidi ya kuzungumza mambo yaMuungano. Sisi tunaamini vikao ni namna bora zaidi. Bahatinzuri katika kikao cha tarehe 9 Februari, 2019, hapa Dodomacha Kamati ya Pamoja tuliamua kurasimisha na kuimarishamfumo wa vikao hivi ili tuweze kufuatilia maelekezo namaagizo yake na kuhakikisha kwamba yanayoamuliwayanatekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, imezungumzwa kwambavikao vinakaa na changamoto za Muungano haziiishi.

Page 283: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

283

Naomba niseme hapa kwamba changamoto za Muunganohazitakuja kuisha hata siku moja na dhana kwamba kwasababu kuna changamoto basi Muungano haufai ni potofukabisa. Siku ya kwanza Muungano umepitishwa, siku ya pilikulitokea changamoto ya namna ya kuunganisha majeshi,mfumo wa fedha na masuala ya ushirikiano wa kimataifa namambo mengine, siku ya pili tu ya Muungano. Nakumbukawakati ule tulikubaliana kwamba masuala ya fedhayatakuwa ya pamoja lakini kukawa na mkanganyiko kuhusunafasi ya Peoples Bank of Zanzibar na BoT lakini mambo hayayalimalizwa kwa vikao na leo changamoto ile hakuna.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika miaka ya 55 yaMuungano changamoto ambazo leo hatuzizungumzii kwasababu zimemalizwa ni nyingi. Kwa hiyo, sisi tunaaminikwamba Muungano huu kikubwa ni mfumo na utaratibuambao tutauweka wa kumaliza changamoto na hilo ndioambalo tunalifanya sasa. Kudhani kwamba hakutakuwa nachangamoto ni ndoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, imeongelewa kuhusumainstreaming ya masuala ya Muungano, utaona ni hojailiyotolewa na Mheshimiwa Saada Mkuya. Sisi tunadhanikwamba ni hoja muhimu na ya msingi. Wewe unafahamu naWaheshimiwa Wabunge wanafahamu kwamba kwenye kilabajeti ya kila Wizara iwe ni ya Maji, Miundombinu au Maliasilikuna mambo huwa hayakosi UKIMWI na rushwa siku zote hatakama hayahusu sekta hizo lakini yamo kwenye bajeti zote zaWizara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tunaamini kwamba tufikemahali kwamba kwenye kila bajeti ya kila Wizara iwe yaMuungano isiwe na Muungano basi suala la Muungano nalenyewe liwepo kama ripoti ambayo inatolewa. Hil itunalizungumza Serikalini kwa sababu kwa Wizara zaMuungano kuna ulazima wa kushirikiana na mambo yakutekeleza lakini kwenye Wizara ambazo siyo za Muunganotunahamasisha ushirikiano. Kwa hiyo, itapendeza hapakwenye hotuba za bajeti kila Wizara ikasema imeshirikianavipi na upande wa pili. (Makofi)

Page 284: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

284

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile napenda nawenzetu wa Zanzibar kama tutazungumza na kukubalianapia katika bajeti zao na wenyewe waseme katika mwakauliopita wa fedha kama ambavyo kwenye masuala yarushwa na UKIMWI wanaripoti basi vilevile kwenye masualaya Muungano kuwa na ripoti. Tunaamini hatua hii itasaidiakuimarisha Muungano na italazimisha wenzetu na wenginewaripoti kuhusu masuala ya muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda niseme tu kwambawatu wengi hawajui lakini hakuna Wizara isiyo ya Muunganokwenye Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iweni Wizara ya Maji ambayo siyo jambo la Muungano au Wizaraya Utalii ambayo siyo jambo la Muungano, Wizara zote ni zaMuungano. Mheshimiwa Dkt. Kibwangalla anaitwa Waziri waMaliasili na Utalii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwasababu hakuna Wizara ya Bara, Wizara zote ni za Muungano.Kwa hiyo, kila Wizara ina wajibu wa kuchukua hatua zakuhakikisha kwamba angalau tunashirikiana na upande wapili kuhusu masuala ya Muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, imetoka hapa hoja kwambaSerikali ya CCM haina nia na Muungano huu. Mimi huwasipendi kuingia kwenye mambo ya kushambuliana kwenyevyama na mambo ya siasa za aina hiyo, lakini kauli hii lazimaijibiwe. Katika mambo ambayo yanapaswa kuwa nje ya siasani masuala ya Muungano. Kwenye nchi zote kuna baadhi yamambo ambayo siasa haipaswi kuingizwa. Kwenye nchi zawenzetu kuna mambo ambayo yamemalizwa siyo tenamjadala na kwenye nchi yetu mimi imani yangu ni kwambaMuungano ni jambo ambalo tunapaswa kuwa tumelimazahalipaswi kuwa na u-CCM, u-CUF, u-ACT wala namnanyingine yoyote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa mfano wa nchi yaMarekani, wao ni Muungano wa Kifederali na ule Muunganouliletwa kwa vita, kuna nchi zilikuwa hazitaki kuwa sehemuya Muungano na vita ikapiganwa na wale ambaohawakutaka kuwa sehemu ya Muungano wakaingizwakwenye Muungano kwa kushindwa kwenye vita hasa

Page 285: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

285

Majimbo ya Kusini. Tangu wakati ule leo United States ofAmerica, aidha, iwepo au isiwepo siyo tena hoja ya siasawala kampeni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nadhanitunapaswa kufika hapo kwamba wakati wa uchaguzihaipaswi Muungano wetu kuwa kwenye referendum. Kwasababu kilichopo sasa hivi ni kila uchaguzi unapofanyikaMuungano ni kama vile upo kwenye kura ya maoni. Kwa hiyo,kama nchi tunapaswa kuondoka huko. Wenzetu ambaowameungana kila mahali, hata Marekani Muungano waouna miaka zaidi ya 200, lakini kila siku wana kauli yaowanasema, to strive for a more perfect union. Kwamba,Muungano wao wa miaka 200 bado hauko perfect. kwa hiyo,nasi leo tukija hapa Bungeni tukataka leo miaka 55 tuwe naa perfect union tutakuwa tunaomba mambo ambayohayako tayari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Muungano huukazi yetu ni kuendelea kuujenga na namna ya kuujenga siyokuusimanga na kuchukulia changamoto ndogo na kuupakamatope na kuupa jina baya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, asilimia zaidi ya 94 yaWatanzania wamezaliwa ndani ya Muungano, hawajuiTanganyika, wanajua wamezaliwa ndani ya Muungano nahawana pengine pa kwenda na utambulisho wao ni waMuungano. Kwa hiyo, nawaomba na kuwasihi WaheshimiwaWabunge ambao huwa tunarushiana vijembe na manenona wale wanasiasa ambao wanatumaini changamoto zaMuungano zitasaidia kuwabeba, basi tuache hivyo, wotetufanye kazi pamoja kuuimarisha Muungano wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniimezungumzia kuhusu muundo wa Muungano na kwambandiyo chanzo cha changamoto na kwamba haufai na ndiyoumetuletea matatizo mengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nisingependa kwendakwenye mjadala huu kwa sababu ni mrefu na wote tunajua

Page 286: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

286

mjadala huu tuliufanya wakati tunafanya mchakato waKatiba. Ambacho naweza kusema ni kwamba, Waasisi waMuungano, Mwalimu Nyerere na Mzee Karume, kablahawajaamua Muungano wa aina tuliyonayo leo, walitafakarimiundo yote ya kila aina, wakatazama dunia nzima,wakatazama mazingira yetu, wakatazama haiba ya watuwetu, wakatazama ukubwa wa pande zote mbili nawakaamua kuwa na Muungano wa kipekee duniani ambaondiyo tulionao leo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiniuliza mimi sababu yakudumu kwa Muungano huu, tofauti na Muungano waSenegal na Gambia, tofauti na Muungano wa Misri, Syria nakwingineko ni kwa sababu ya muundo wake. Tunatofautiana;wengine wanadhani Muungano wetu una shida kwa sababuya muundo wake, lakini sisi tunaamini Muungano wetuumedumu kwa sababu ya muundo wake. Kwa hiyo, kikubwani kuendelea kuimarisha mifumo na taratibu za kushughulikiamasuala yanayojitokeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tuna bahati kwambaMuungano wetu una bahati ya kuundwa katika misingi yakijamii, kwa sababu mahusiano ya kijamii ya watu wa pandezote yamekuwepo kabla ya mapinduzi, yamekuwepo kablaya uhuru na yamekuwepo kabla ya Muungano. Kikubwa tuni sisi kuendelea kuimarisha masuala ya kitaasisi na kisheriana kiutaratibu ili tuendelee kuwatendea haki watu ambaoni ndugu wa pande zote mbili za Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, limezungumziwa hapa sualala vyombo vya moto, kwamba haipendezi ikawa kuna ugumuwa kuingia na gari lako kutoka upande wa pili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana kabisakwamba ni jambo linalokera, linaloudhi kwamba gari kutokaZambia au Malawi, linavinjari kwa urahisi katika nchi yetu,lakini gari kutoka Zanzibar linapata bughudha. Hilo jambohalikubaliki kabisa. (Makofi)

Page 287: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

287

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati nzuri sasa Serikaliimeanza kulishughulikia jambo hilo na Mwanasheria Mkuu waSerikalin anafahamu kwamba kulikuwa tayari namapendekezo ya mabadiliko ya Sheria ya Usajili wa Magarina Sheria nadhani ya Polisi na ilishafika kwenye Mkutano waKamati ya Baraza la Mawaziri ya Katiba na Bunge ilimabadiliko yafanyike kuhakikisha kwamba jambo hilolinakwisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati mbaya tukashauriwakwamba ili utaratibu huo udumu na uwe imara, tuhakikishekwamba zinawekwa taratibu ili wale watu ambao wanawezakutumia mwanya kuingiza magari na badaye kuyauza kwaupande mwingine, basi wasifanikiwe. Sasa study hiyoiliyofanywa na TRA na wengine imekamilika, nasi tunaaminikwamba wachache ambao wanaweza kutumia fursa hiyovibaya wasiwaharibie watu wengi wema ambao wanatakakusafiri na vyombo vyao vya moto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, utaratibu huoutawekwa na ni imani yangu kwamba mabadiliko hayo yasheria yatafywa mapema kupitia kwa wenzetu ili jambo hilotulimalize. Ni kero kubwa na ni aibu kusema kweli. Kwa hiyo,imani yetu ni kwamba litakwisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, limezungumzwa suala lamifuko ya plastic. Naomba niseme, tumezungumza kwa kirefukwenye hotuba yetu, lakini naomba niseme tu kwambadhamira hii ni njema. Kwenye hili tumejipanga vizuri kwasababu tumeshirikisha wadau mapema zaidi. Tunaaminikwamba suala hili ili tufanikiwe ni lazima twende hatua kwahatua. Kwa sasa hatuwezi kupiga marufuku kila kitu; kunabaadhi ya vifungashio vinavyotumia plastick ambavyo nilazima vitumie plastick, kwa mfano, mikate, maziwa, madawana vinginevyo. Imani yetu ni kwamba, kwa sasa vitaruhusiwaili tusilete bughudha na mtikisiko kwenye uchumi na kuongezabei za bidhaa kwa watu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaanza namifuko hii ambayo ni kero, hata hivyo kwa vifungashio

Page 288: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

288

tutaweka standards ili viweze kukusanywa na kurejelezwa.Hiyo, tunaamini tutafanikiwa. Hata wale wenye chupa zaplastick vile vile imani na mpango wetu ni kuweka ulazimawa wao kushiriki kwenye mipango ya recycling, kwambahuwezi kuwa unazalisha chupa za Kilimanjaro halafu hunahabari hiyo chupa inaishia wapi? Lazima ushiriki kwenyeutaratibu wa kuirejesha na kuirejeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kanuni mpya piazitatoa mahitaji hayo. Naomba Waheshimiwa Wabungetusaidiane, kwa sababu tutakapofanikiwa jambo hilitutakuwa tumefanya jambo la kihistoria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna shaka kuhusu mbadalakwamba, je, mbadala upo na unatosha? Naombaniwaambie kwamba wenzetu Wakenya ambao wamepigamarufuku mifuko ya plastic, mifuko yao ya karatasi wanaitoaTanzania. Wenzetu Warwanda, ukienda kule Mufindi PaperMills, malighafi yote ya mifuko ya karatasi ya Rwanda inatokaMufindi na Rwanda inasifika, Kigali, kama mji safi kabisa hapaAfrika, sababu ni nini? Sababu ni sisi ndio tunawapa karatasi,wanapata mifuko ya karatasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa wale wametuhakikishiakwamba uwezo wa ku-supply mifuko ya karatasi hapa nchiniwanao na kwamba, changamoto yetu kubwa kwa sasa nikuhakikisha wanaongeza production na usambazaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kanuni tunazotoa zitatoaadhabu kwa wanaouza mifuko, wanaoweka na kwawanaoingiza ndani ya nchi. Kunaweza kukatokea mtikisikona malalamiko kidogo kwenye zoezi hil i, naombaWaheshimiwa Wabunge muiunge mkono Serikali kuhakikishakwamba, jambo hili linafanikiwa. Kwa sababu, siku zotehakuwezi kukosa malalamiko kwenye masuala makubwa yamabadiliko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu matumizi ya mkaana ukataji wa miti, hii ni changamoto kubwa sana sana. Kiladadika moja inayoenda hapa nchini, misitu inayofyekwa ni

Page 289: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

289

sawa na kiwanja cha mpira. Tangu niongee hapa nadhanini dakika 15, misitu iliyofyekwa ni sawa na viwanja vya mipira15. Tena hizi ni takwimu za chini na sehemu kubwa ni ukatajiwa mkaa, kilimo kisicho endelevu, uzururaji wa mifugo, nakadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wataalam wa mazingirahapa, akina Mheshimiwa Dkt. Sware wanafahamu kwambamisitu ina thamani katika mifumo ya kiikolojia na utajiri wanchi unapimwa kwenye mambo mengi; kuna utajiri wa watuwenyewe, utajiri wa vitu na utajiri wa maliasili. Katika nchizinazoongoza duniani kwa utajiri wa maliasili, wanaita NaturalResources Wealth Per Capita. Tanzania ni moja kati ya nchizinazoongoza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika miaka 20 iliyopitautajiri wa Tanzania kwa maliasili kwa maana thamani ya mito,maziwa, misitu, na kadhalika, thamani yake per capitainashuka kwa asilimia 35 kwa miaka 20 iliyopita, ingawa GDPper capita inapanda, lakini natural resources per capitainashuka chini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, dalili pekee ya kwambamaendeleo siyo sustainable ni pale utajiri wenu wa maliasiliunaposhuka wakati utajiri mwingine unaenda juu. Kunawakati hata ule unaenda utashuka utakutana na ule wachini. Kwa hiyo, tuna wajibu mkubwa kuhakikisha kwambamaendeleo tunayoyatafuta ili yawe endelevu, hatuna budikulinda maliasili zetu kwa nguvu zetu zote kwa sababu, ndiyoutajiri tulionao. Kwa hiyo, sisi ndani ya Serikali tunazungumzana wenzetu wa Wizara ya Maliasili na Wizara nyingine husikaili kuwa na makubaliano kuhusu mwenendo wa kulindarasilimali za nchi zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, hili jambotunazungumza na wenzetu kwamba sisi tunaamini msituuliosimama na miti iliyosimama ina thamani hata kwenyekilimo kwa sababu hata mahindi ili yazae lazima kuwe nawale wadudu na nyuki wanaofanya polination naowanatoka kwenye misitu. Ukipewa shamba sasa hivi lenye

Page 290: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

290

msitu, usipokata msitu unanyang’anywa kwa sababuhujaliendeleza, ehee! Nasi tunaamini kwamba msitu vilevileunaposimama na wenyewe una thamani yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hili tunalizungumzakwamba kuna mwenzetu mmoja akiona mti umesimamaanauona ni gogo na lenyewe ni chanzo cha mapato. Kwaupande mwingine ule mti pia unaweza kuuweka nyuki nakuzalisha. Kwa hiyo, ni mambo ambayo tunazungumza ndaniya Serikali ili kuhakikisha kwamba tunatunza nchi yetu; namaelekezo ya viongozi wetu, mmemsikia Mheshimiwa Raisalipokuwa Njombe alisema tulinde misitu yetu kwa nguvu zetuzote na mapori yetu yote. Imani yangu ni kwambatutaendelea kufanya hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabungetumewasikia kilio chenu kuhusu kasi ya ukataji wa miti na kasiya nchi yetu kuwa jangwa. Ukombozi haupo kwenyekupanda miti, ukombozi upo kwenye kutunza miti iliyopoisikatwe, kwa sababu miti iliyopandwa haifiki asilimia naneya miti yote iliyopo nchini. Tusipokata miti ni bora zaidi kulikokuhangaika kupanda miti mingine. Kwa hiyo, huko ndiyoambako jitihada zitaelekezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, imezungumzwa kuhusuutendaji wa NEMC na nilizungumza asubuhi kuhusu reformsambazo tunafanya. Tumepokea kabisa malalamiko kuhusuutendaji wa NEMC na malalamiko hayo ni ya kweli kwasababu, kulikuwa na changamoto kubwa za ucheleweshajiwa vibali, gharama za vibali na mambo mengineyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeeleza kwa kirefuasubuhi hatua tunazochukua. Bahati nzuri tumepata uongozimzuri, tunaye Mwenyekiti wa Bodi ya NEMC ambaye tukonaye hapa, Profesa Asnath Chagu, tuna Mkurugenzi Mkuumpya, anapanga safu yake vizuri. Tumesikia changamoto yawatumishi wachache wa NEMC, bahati nzuri wenzetu waUtumishi wametusaidia, wametupa kibali cha kuajiri watu 30mwaka huu, lakini zaidi ya hapo tumewaelekeza watu waNEMC kwamba, kuna vijana wengi sana wamesoma

Page 291: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

291

mazingira na jiografia kwenye vyuo vikuu na hawana kazi nani vijana wazuri na wasomi. Tumesema kwa sababu kazi zaNEMC ni nyingi, wawachukue kwa mkataba kama internsna kuwatumia kwenye kazi za kwenda kufuatilia, kusimamia,na kadhalika, wapate posho na uzoefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, sasa hivi tunao 40na miezi michache tutaongeza 100 na mwaka ujaotutaongeza 100 wengine kuhakikisha kwamba footprints yaNEMC nchi nzima inakuwa kubwa. Tunafungua Ofisi za Kandaili kuhaklikisha kwamba NEMC inatoa huduma kote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, NEMC sasa hiviinabadilisha mtazamo wake kutoka taasisi ya kipolisi na kuwataasisi ya huduma zaidi kwa wawekezaji na kwa wananchi.Nimewaambia watu wa NEMC, nyie mkionekana mnafungaviwanda, mnatoza fine, mnakusanya pesa, sawa ni kazi zenu,lakini ukisoma sheria mna kazi kubwa na muhimu zaidiikiwemo utafiti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, sheria inasemaNEMC inapaswa kuweka orodha ya milima na vilima vyotenchini. Sheria ilisema, ndani ya miaka mitano baada ya sheriakuundwa kuwe na orodha iliyochapishwa kwenye Gazeti laSerikali kuhusu milima na vilima vyote nchini na hatari yamazingira kwa vilima hivyo. Hiyo ni kazi ya NEMC. NEMCinaruhusiwa kumiliki maeneo yaliyolindwa kwa Sheria yaMazingira. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tutabadilishamwelekeo wa NEMC ionekane ni taasisi kubwa na yenyeheshima na yenye hadhi, siyo ya kufukuzana na watu nakuchelewesha vibali, na kadhalika. Kwa hiyo, mtaiona NEMCtofauti na tutaendelea kutoa huduma kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda niseme kwamba,tunataka uwekezaji na uwekezaji ni muhimu, lakini tunaaminiuwekezaji lazima uende sambamba na hifadhi ya mazingira.Sasa nataka kusema, mtu yeyote ambayeanacheleweshewa kibali na NEMC au anaamini NEMC

Page 292: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

292

inamcheleweshea kibali, aje kwetu sisi moja kwa mojatutamsaidia papo hapo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho limezungumzwasuala la UNHCR Kigoma na madhara ya wakimbizi kwenyeuharibifu wa mazingira. Tumeongea na wenzetu wa Shirikala Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi kuhakikisha kwambakwanza makambi yetu yanafanyiwa Tathmini ya Athari kwaMazingira (EIA) na hali ya mazingira inarejeshwa na kwambawananchi pia wanapata manufaa na huduma ambazowakimbizi wanazipata ikiwemo maji, na kadhalika. Kwa hiyo,Waheshimiwa Wabunge wa Kigoma hili tunalishughulikia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la mfumo mzimawa usimamizi wa mazingira. Sheria ya mazingiraimetengeneza architecture, mfumo wa usimamizi wamazingira. Sheria ya Mazingira imetoa maelekezo kwa Wizarana Taasisi nyingine za Umma na binafsi, lakini hususan naSerikali za Mitaa kuhusu mambo ya kufanya. Kwa hiyo,Maafisa wa Mazingira wanaajiriwa na Halmashauri na kamatizinapaswa kuundwa kwenye ngazi ya Halmashauri. Kwa hiyo,kikubwa tunachofanya sisi ni kushirikiana na TAMISEMIkuhakikisha kwamba ule mfumo wa usimamizi wa mazingiraambao unahusu Wizara zote unasimamiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Mazingira inasemakila Wizara iwe na mratibu wa mazingira na kila Halmashauriiwe na Afisa Mazingira na kila Sekretarieti ya Mkoa iwe naMratibu wa Mazingira. Kila kijiji kiwe na Kamati ya Mazingira,kila Kitongoji, kila Mtaa, kila Kata, kila Wilaya. Hapo ndipomfumo mzima wa usimamizi wa mazingira utakuwaumekamilika na kwamba NEMC peke yake haiwezi kuwakwenye kila Mtaa, kila Kijiji na kila Kitongoji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi kubwa tumeifanyakatika mwaka uliopita kuhakikisha kwamba mfumo huuunakuwepo, kuna baadhi ya mikoa imefanya kazi nzuri sanaya kuhakikisha kwamba Mitaa yote, Vijiji vyote vina Kamatiya Mazingira na matunda tunayaona katika usimamizi wamazingira.

Page 293: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

293

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala limezungumzwala kutotosha fedha. Labda niseme tu kwamba fedha siku zotehazitoshi na hasa kwenye nchi kama yetu. Sasa ambachonataka kusema ni kwamba kuna Bajeti ya Ofisi ya Makamuwa Rais ya Mazingira, pia kuna fedha za mazingira zinazokujanchini katika ujumla wake. Ukiangalia Bajeti ya Ofisi yaMakamu wa Rais na ukaichukulia kwamba ndiyo fedha zamazingira hapa nchini utakuwa umefanya makosa. Nitatoamfano kwamba, sisi Ofisi ya Makamu wa Rais tumewatafutiaWizara ya Maji fedha kwenye Mfuko wa Kimataifa waMabadiliko ya Tabia-Nchi (Green Climate Fund).Tumehakikisha wamezipata. Fedha zile ni shilingi bilioni 250ambazo zinaenda kuleta maji Simiyu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa zingekuwa kwenyebajeti yetu, si ajabu kusingekuwa na maneno. Kuna fedhazimepitia kwetu lakini ziko Wizara ya Kilimo; kuna fedhazimepitia kwetu, lakini ziko Wizara ya Mifugo. Kwa hiyo,inawezekana fedha zikaonekana hapa kidogo, sisi kazi yetuwakati mwingine ni kuwatafutia wengine fedha kupitiamikataba ya Kimataifa ambayo sisi ni wanachama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tutaendeleakufanya hivyo. Tunaamini kwamba ni kweli rasil imalizinahitajika zaidi na tunaamini pale Mfuko wa Mazingirautakapokuwa umeanza kazi, basi na wenyewe utachangiakatika kuhakikisha kwamba fedha zaidi zinapatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna masuala mengineyamezungumziwa ya GMO, Mheshimiwa Chiza; masuala yamatumizi ya maji kwenye umwagiliaji, masuala ya matumiziya gesi na Mheshimiwa Ruth Mollel, ameongea kuhusu sualala nafuu ya kodi kwenye mitungi ya gesi ili kuokoa misitu. Hilotutazungumza na wenzetu wa Wizara ya Fedha kuhakikishakwamba linafanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu ambacho ni kikubwa nacha msingi ni kwamba tunaona na tunafarijika sana nakupanuka kwa nishati mbadala ya mkaa. Kiwango cha gesiya mitungi kinachotumika mwaka huu ni kikubwa mara mbili

Page 294: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

294

ya kilichotumika mwaka jana 2018 na tunaamini kadiri miakainavyoenda na tunaona uwekezaji katika eneo hilo, imaniyetu ni kwamba tutafanikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mita 60nilizungumzia asubuhi kwamba tunaweka kanuni na utaratibuwa kuweza kuhakikisha kwamba tunafanikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani mambo yalemakubwa na ya msingi, suala la elimu ya Muungano ni kwelilazima nikiri kwamba hatujafanya vizuri, wakati mwinginetunafanya mambo makubwa lakini hatuyazungumzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na hoja kwambavikao vya Muungano ni vya sir i kwamba hakunatransparency, hiyo siyo kweli. Udhaifu wetu ni kwamba labdabaada ya kikao tulipaswa kuitisha press conference ili watuwajue. Kwa hiyo, tumechukua maoni na ushauri kuhusunamna ya kuelezea wananchi kuhusu nini kinafanyika na ofisizetu hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa nirudi tenakwenye suala la Muungano kwa kifupi kwamba, kuna kazinyingi sana kwenye Muungano zinafanyika hasa kupitia kwaviongozi wakubwa, hasa kupitia kwa wataalam, miradi,uhusiano na ushirikiano uliopo lakini mjadala wetu kuhusuMuungano umejikita kwenye changamoto. Sisi tunadhanikwamba tunayo kazi ya kuonyesha kwamba definition yaMuungano sio vikao vya changamoto bali ni mambomengine mengi yanayofanyika ambayo hayaonekani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,naomba nitoe ahadi kwa Waheshimiwa Wabunge kwambawale ambao hoja zao sijazigusa na hata wale ambaonimezigusa basi tutaziandika vizuri, tutatoa majibu vizuri natutawapatia kabla Bunge la bajeti hii halijakwisha ili wawezekusoma majibu yao kwa sababu muda wa kujibu hapawakati mwingine hautoshi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.

Page 295: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

295

MWENYEKITI: Toa hoja.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwaheshima na taadhima kubwa, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WAKIMATAIFA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.

MWENYEKITI: Katibu.

NDG. JOSHUA CHAMWELA – KATIBU MEZANI:

KAMATI YA MATUMIZI

MATUMIZI YA KAWAIDA

Fungu 31 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano naMazingira

Kif. 1001 – Administration and HR Management Division….................................….Sh. 2, 973,514,560/=

MWENYEKITI: Haya orodha tayari ipo hapa yawachangiaji katika mshahara wa Waziri, MheshimiwaKubenea.

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia. Kwa mujibuwa sheria mbalimbali za Jamhuri ya Muungano, mambo yamikopo na misaada kutoka nje ambayo Serikali ya MapinduziZanzibar inataka kukopa kutoka nje ni lazima ipate kibali chaSerikali ya Muungano. Sasa nataka commitment ya Serikalikwamba ni lini italeta Bungeni Muswada wa Mabadiliko yaSheria ambao utairuhusu Zanzibar kukopa kutoka nje bilakutegemea idhini ya Serikali ya Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili ni muhimu kwasababu kuna miradi mikubwa ambayo ipo Zanzibarimeshindwa kutekelezwa kwa sababu ya ukosefu wa fedha.

Page 296: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

296

Kwa mfano, upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifacha Abeid Aman Karume, Bandari ya Zanzibar na sasa hivimiradi kama ya gesi inaweza ikakwama ikiwa Serikali yaZanzibar haikupewa mamlaka ya kukopa yenyewe kutokanje ya nchi. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wakatimwingine inatekeleza miradi yake ambayo iko nje ya ilemiradi ambayo sio kipaumbele cha Zanzibar. Kwa mfano,ujenzi wa reli ya kati hata pengine Daraja la Salenda. Kwahiyo, naomba Serikali itoe commitment ya kuleta mabadilikoya sheria na iwapo kama sikuridhika na majibu hayo nitatoashilingi ili tuweze kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru sana kuhusu hoja ambayo ameiletaMheshimiwa Kubenea, ameuliza ni lini Serikali italetaMuswada, lakini kama ambavyo nimeeleza wakatinachangia hoja hii; yapo mambo mengi ambayo yapokwenye mchakato wa majadiliano katika ngazi ya wataalamambayo sasa tumesema yamekamilika kwenye ngazi yawataalam, sasa tunaandika Waraka wa Baraza la Mawaziriili mambo hayo yaweze kupatiwa ufumbuzi na kupata tibaya kudumu. Kwa hiyo, moja ya jambo hilo ambalo lipo kwenyewaraka huo ni jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwombe MheshimiwaKubenea avute subira na niliombe Bunge lako Tukufu wavutesubira, Serikali ina dhamira njema sana ya kuhakikisha kerozote za Muungano zinaondoka. Kuwekwa kwa mfumo huujinsi ulivyo upo kisheria, kwa hiyo, hilo nimwombe sana avutesubira ili Serikali imalize mchakato huu na Bunge ni hili hilitutakuja kutoa majibu hapa hapa. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa AG.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, pamoja na majibu aliyoyazungumza

Page 297: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

297

Mheshimiwa Naibu Waziri ambayo yanazungumzia mchakatowa kisheria, lakini ni vyema tukakumbushwa kwamba sualala mikopo ni suala la Muungano kwa mujibu wa Katiba yetuna kwa hiyo, tutakapokuwa tukizungumzia mchakato huowa kisheria lakini tukumbuke kwamba lipo katika Katiba yetuna ni lazima pia tuwe tumelifanyia kazi kwenye katibavinginevyo pia huo mchakato unaweza usifike mbali.

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nafahamu kwamba kwa mujibu wa Ibara ya (iv)kumeorodheshwa mambo ya Muungano, lakini hili ni mojaya kero ya Muungano ya muda mrefu sana. Sasaninavyotaka waseme lini huo mchakato wa kubadilishaKatiba na sheria yake unaletwa Bngeni. Sasa hapa Wazirianasema tutaleta, tupo kwenye majadiliano, tupo kwenyeBaraza la Mawaziri; ni mambo yale yale ya miaka nenda,rudi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, natoa hoja iliwenzangu waweze kuniunga mkono tuweze kulijadili jambohili kwa mapana zaidi na kwa maslahi makubwa ya Taifaletu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.(Makofi)

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naafiki.

MWENYEKITI: Hoja imeungwa mkono. WachangiajiMheshimiwa Mwigulu, Mheshimiwa Simbachawene,Mheshimiwa Maftaha, Mheshimiwa Zitto, Mheshimiwa Jaku,Mheshimiwa Komu, Mheshimiwa Almas, Mheshimiwa Rehanina Mheshimiwa Ashatu.

Tunaanza na Mheshimiwa Komu.

MHE. ANTHONY C. KOMU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Naomba niunge mkono hoja aliyotoaMheshimiwa Kubenea kwa sababu tunavyozungumza nianjema ya Muungano hapa ndipo tunapoanzia.

Page 298: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

298

Inavyochukua takribani miaka 55, mambo hayayanazungumzwa na tuaahidiwa kwamba yataletwa, halafuhayaletwi, sasa hii inakwenda kutishia huu Muungano ambaokimsingi tunajivunia na hii nia njema haionekani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo kubwa hapa ni kwanini tunafikiri kwamba sasa Zanzibar inapaswa ipewe fursatena haraka sana ya kuweza kujisimamia na kukopa kwakadri inavyoona ni kwa sababu vipaumbele vya TanzaniaBara au kwa maana ya Serikali ya Muungano sio vipaumbelevya Zanzibar na Zanzibar ina mambo yake ambayo ni yamsingi sana. Wakati Mheshimiwa Jaku anachangiaaliorodhesha mambo kibao ambayo Zanzibar inawajibikakufanya kwa ajili ya ustawi wa watu wake, lakini kwa sababuya vikwazo kama hivi, sababu ya kero kama hizi mambo hayohayawezi kufanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Kubeneaamerejea hapa upanuzi wa Bandari ya Zanzibar na upanuziwa uwanja wa ndege Zanzibar, sasa haiwezi kufanyika kwasababu tu ya hiki kikwazo ambacho kipo kwenye Katiba. Kwahiyo, nafikiri ili huu Muungano wetu uweze kuwa endelevuna uweze kuwa ni Muungano ambao kweli utaendeleakuwepo, ni lazima jambo hili lifanyiwe kazi sasa hivi. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Zitto.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naminaunga mkono hoja ya Mheshimiwa Kubenea kwambaSerikali itoe commitment ya lini italeta Muswada wa Sheriaya Kufanya Mabadiliko ya Katiba ili kuweza kuiruhusu Zanzibariweze kuingia mikataba ya mikopo na misaada ya Kimataifamoja kwa moja bila kutegemea dhamana (guarantee) aukuruhusiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Maelezo ambayo Serikali inayatoa kuhusiana na michakatoni maelezo ambayo hayaaminiki na hayaaminiki kwa mifanodhahiri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 1977, Katiba Ibaraya 134 ilianzisha Tume ya Pamoja ya Fedha, ilichukua mpaka

Page 299: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

299

mwaka 1996, Serikali ya Chama cha Mapinduzi kuletaMuswada wa Tume hiyo ya Pamoja ya Fedha. Ilichukua tenampaka mwaka 2003 Serikali ya Chama cha Mapinduzi kuletaKanuni za kuitekeleza hiyo Sheria ya Tume ya Pamoja yaFedha, yaani ililetwa sheria na tume kuundwa na mpaka sasatume haijaanza kufanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, zaidi ya yote, uchambuziuliofanywa na Tume ya Pamoja ya Fedha unaoneshakwamba mapato ya Muungano ambayo yanapaswakugawanywa pande zote mbili za Muungano yanatumiwana Tanzania Bara na Zanzibar haipati hata senti tano, kiasikwamba kwa makusanyo ya sasa hivi, kama Tume ya Pamojaingekuwa inafanya kazi na mapato ya idara na wizara zaMuungano yakagawanywa sawasawa, wala Zanzibarisingehitaji misaada kwa sababu bajeti yake nzima ingewezakuendeshwa na wizara na mapato ya fedha za Muungano.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama jambo hili lakikatiba halitekelezwi… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Almas.

MHE. ALMAS A. MAIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana na nichangie hoja hii, lakini siungi mkonohoja ya Mheshimiwa Kubenea. Serikali ya Mapinduzi Zanzibarinapotaka kukopa nje inatoa taarifa tu kwa Serikali yaMuungano, haijakataliwa hata siku moja. Serikali yaMapinduzi Zanzibar narudia, inapotaka kukopa nje, inatoataarifa kwa Serikali ya Muungano na sababu ni moja kubwasuala la fedha ni la Muungano. Vilevile, wanaokopeshaZanzibar wanataka dhamana ya Serikali ya Muungano,hawataki Serikali ya Zanzibar peke yake… (Makofi)

MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

Page 300: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

300

MHE. ALMAS A. MAIGE: Na hiyo inafanya Serikali yaMuungano iweze kusajili madeni yanayokopeshwa Zanzibarndio sababu kubwa. Kwa hiyo, siungi mkono suala laMheshimiwa Kubenea. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Jaku.

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti,nikushukuru. Kwanza mtoa mada ndugu yangu sasa hiviuliyechangia, Mwanasheria alisema hili suala lipo Katiba yaJamhuri ya Muungano, sasa nashukuru anasema Zanzibartunakopa, tutapata wapi fursa hiyo na hili suala lipo kwenyeKatiba ya Jamhuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekuwa nikisema siku zotehumu tena kwa lugha nyepesi kabisa na kwa uchungu,Zanzibar uchumi wake ni mdogo inategemea zao la karafuuna competitor wake mkubwa ni Indonesia na wa pili ni utalii.Sasa Zanzibar inataka kukua kuendelea mbele inalia naupanuzi wa uwanja wa ndege na bandari iliyopo pale.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni suala la msingi,nawashangaa viongozi commitment semeni tu mwakammoja, miezi sita; suala la VAT limechukua muda gani? Kituchepesi (simple) kabisa hiki mpaka tuvutane? Haileti suranzuri; nataka commitment ni lini miezi sita/mwaka mmojatunazidi kuumia sisi Zanzibar, hali hairidhishi jamani. Hata mtumzima akilia kuna jambo wazee, tufikirieni jamani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiunga mkono hoja yaMheshimiwa Kubenea asilimia 95 niwe mkweli. Nitakuwamasuuli kwa sababu Mwenyezi Mungu ataenda kuniuliza,nimetoka upande wa Zanzibar mimi, kama sikutetea maslahiya Zanzibar nitakuwa mnafiki, sio uzuri wala uungwana.Mungu ataenda kuniuliza mie, baada ya siasa kuna…(Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

Page 301: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

301

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Maftah hukuombaeeh? Sorry, Mheshimiwa Simbachawene, Mheshimiwa Mattarsorry, nimesema Mheshimiwa Mattar, umeomba wewe?

MHE. MATTAR ALI SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Niunge mkono hoja ya Mheshimiwa Waziri. Lazimanikatae hoja ya Mheshimiwa Kubenea kwa sababu zifuatazo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa MheshimiwaWaziri ametoa commitment, mchakato unaanza kufanyiwakazi na unaendelea kufanyiwa kazi na utaletwa kwenyeBunge hili, sijaona sababu ya kuweka msisitizo nini tufanyehili suala liishe. Mheshimiwa Waziri amezungumza vizuri, badotuna nafasi ya kukopa sisi kama Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,tuna nafasi nzuri na tunapata mikopo mizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwombe MheshimiwaKubenea, hiyo shilingi amrejeshee Mheshimiwa Wazirituendelee kufanyia kazi, hali ya mikopo ya Zanzibar kupatatunapata kwa wakati ambao tunataka. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Simbachawene, jiandaeMheshimiwa Rehani.

MHE. GEORGE B. SIMBACHAWENE: MheshimiwaMwenyekiti, niseme tu kwamba yapo mambo na miradimikubwa ambayo imefanyika katika nchi hii kwa mashirikianoya Serikali zote mbili na yanafanyika Zanzibar na TanzaniaBara. Kusema kuna tatizo kubwa la mikopo ambalo sasalinahitaji urgency mimi naweza nikasema sawa, lakini yapomambo makubwa hapa yamefanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mimi niseme tutakwa na sheria inayoombwa na Mheshimiwa Kubenea yakusema ije sheria hapa si jambo dogo, ni mabadiliko ya Katibamaana Nyongeza ya Kwanza ile namba 8, mikopo nabiashara za nje ni mambo ya Muungano. Sasa siyo jambodogo na ndiyo maana wenzetu hata Uingerezawanazungumzia Brexit hawatoki haraka haraka, badowanakwenda nalo taratibu, mambo yanayohusu stability ya

Page 302: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

302

nchi hatuwezi kukurupuka hivi. Serikali inatoa commitmentkwamba tunalijadili jambo hili l itafika levels zote nalitamalizika, siyo jambo jepesi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia ushauriunaotolewa unatolewa na nani? Hawa wasioupendaMuungano ndiyo wanaotupa ushauri juu ya Muungano sisi?Lazima tuwe makini na aina ya ushauri na nani anayetoaushauri. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Rehani ajiandaeMheshimiwa Mwigulu.

MHE. SALUM MWINYI REHANI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kupata fursa hii. Nami nataka kuchangia katikajambo hili, kinachotakiwa hapa ni commitment, siyo jambolingine lolote, kwa sababu hili jambo kweli linakwaza Zanzibar,lazima tuseme ukweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe mfano mmoja,Zanzibar imetoa proposal ya kujenga Bandari ya Mpigaduri,sasa hivi ni mwaka wa nane…

MBUNGE FULANI: Hamna kitu.

MHE. SALUM MWINYI REHANI: Imekwama na ilipatasupport au mkopo kupitia EU lakini bado suala hili ni laKikatiba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nakubali kwamba niprocess lakini tunataka tuone progress, miaka nane imepitabado hatujaona progress. Kwa hiyo, Waziri atuambie hapani muda gani hili suala tutakuwa na mwelekeo. Au tupewealternative nyingine ya kuhakikisha kwamba hii miradimikubwa kama hii ya kimkakati basi inaweza kupataufumbuzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwigulu.

Page 303: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

303

MHE. MWIGULU L. NCHEMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,hili jambo tunaloliongelea ni jambo la Kikatiba lakini pia ni lakiuchumi. Upande mmoja wa Kikatiba Mwanasheria Mkuuwa Serikali ameshaelezea vizuri kwamba marekebisho yakeyanahitaji kwanza kushughulikiwa Kikatiba. Kwa maana hiyopale tu kwenye sehemu ya Kikatiba ni lazima jambo hililichukue muda kwa maana linatakiwa lifanyiwe kazi kwauangalifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ukirudi kwenye upandewa kiuchumi, niwaombe wote wanaochangia hapawaelewe kitu kimoja kwamba hili jambo la kukopa liliwekwasehemu moja kwa sababu ulipaji nao unafanyika sehemumoja. Kwa maana hiyo, huwezi ukafungulia ukopaji halafumlipaji akawa mwingine, lazima anayelipa aangalie spaceya ulipaji na makusanyo yake kama yanaruhusu kuwezakukopa mkopo ambao unafanyika katika Taifa husika.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maana hiyo taratibu zakisasa za ku-assess kama Taifa linaruhusiwa kukopa unatakiwauangalie kwanza kama kuna fedha zinabaki baada yakufanya malipo ya lazima ndipo uweze ku-assess kwambaunaweza ukaruhusu kukopa mradi A, B, C, D. Kwa maanahiyo, katika mazingira haya tuliyonayo sisi tukishaangaliasehemu ile ya Kikatiba, ni vyema Waheshimiwa Wabungetukazingatia upande wa uwezo wa kulipa. Hata kama spaceile ingeruhusiwa, hata kama Zanzibar ingepewa nafasi yakukopa bado kuna jambo lazima lifanyiwe analysis kwambaulipaji wake utafanyika kwa namna gani. Hata sisiWabunge…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. MWIGULU L. NCHEMBA: Tumewekewa ukomo wakukopa kufuatana na jinsi ambavyo tunaweza tukalipa.(Makofi)

Page 304: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

304

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Ashatu.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, kama nilivyoanza mwanzo, nimwombe sanaMheshimiwa Kubenea aiachie shilingi ya Mheshimiwa Wazirikwa sababu ya maelezo mazuri ambayo ameanza kuyatoaMheshimiwa Mwigulu. Dhamira ya Serikali ni njema sana,kama ambavyo Waheshimiwa Wabunge wamesemakuhakikisha miradi yote mikubwa inatekelezwa pande zotembili za Muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, amesema MwanasheriaMkuu wa Serikali hili ni jambo la Kikatiba, ndiyo maana miminilianza kusema mchakato wake umeanza, yapo mamboambayo tunajadiliana na moja kubwa ambalo ameliongeaMheshimiwa Mwigulu ni kwamba tunapoomba Zanzibariruhusiwe kukopa moja kwa moja, je, nani wa kulipa mkopohuo? Turudi tu kwenye hoja hiyo ya msingi kwambatunapomruhusu yeye akope ni nani wa kulipa? Hili ni jambola Muungano lazima hilo liwekwe mezani ndiyo maananimesema Serikali mbili zinajadiliana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, umetolewa mfano waTerminal II, ndiyo maana mambo haya yanachukua mudamrefu aliye-default wala siyo upande wa Muungano, walio-default ni wasimamizi wa mradi wenyewe. Kwa hiyo, hayamambo ni sensitive ndiyo maana tunaomba tuyachukuliehivyo ili tuweze kwenda salama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, umeongelewa mfano hapawa mkopo wa kujenga Bandari ya Mpigadori, tukumbukeMheshimiwa Waziri wa Fedha aliwahi kusimama kwenyeBunge lako Tukufu akasema mkopo huu unapoombwa,amesema Mheshimiwa Almas Maige dhamana inayowekwani ya Tanzania Bara lakini wanataka kitu gani? Hichowanachokitaka ili watoe mkopo huo kwa ajili ya ujenzi waBandari ya Mpigaduri ni kuweka dhamana Benki Kuu yaTanzania, hivi tuko tayari kuuza utu wetu Watanzania?(Makofi)

Page 305: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

305

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, yapo mambo ya kuangalia. Kamati yetu yaMadeni ya Taifa inayashughulikia moja baada ya lingine natumeuanza mchakato, nimwombe Mheshimiwa Kubeneaarudishe shilingi ili kwa dhamira njema tuweze kumaliza sualahili. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa AG una chakuongeza?

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, sina.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Chenge.

MHE. ANDREW J. CHENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba tuweke record sawa. Nadhani Mheshimiwa NaibuWaziri wa Fedha na Mipango ameteleza tu ulimi. Guaranteeau dhamana inayotolewa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuriya Muungano na kwa mujibu wa Sheria ya Mikopo, Dhamanana Misaada, sheria ya mwaka 1974 ambayo majuzi tutuliifanyia marekebisho hapa, dhamana hiyo inatolewa naJamhuri ya Muungano wa Tanzania, hatuna Serikali ya Bara.Nimeona tulinyooshe hilo kwa sababu ni suala la msingi sana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Kubenea, baadaya aliyosema Mheshimiwa Mtemi Chenge bado una hoja?

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninayo hoja na hoja yangu ni kwamba Wazirianapozungumza juu ya dhamana inatolewa na Benki Kuu,Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ina share katika Benki Kuu ya

Page 306: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

306

Tanzania. Ndiyo maana inapata gawio kila mwaka paleambapo Benki Kuu inapata faida. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, MheshimiwaSimbachawene anazungumza juu ya jambo hili kubwa likokwenye Katiba. Yeye alikuja na hoja hapa ya mchuzi wazabibu ambao ulikuwa tayari umepitishwa kwenye bajeti yanchi na tukabadilisha, mapato ya nchi yakaondolewa, kwanini tunataka Zanzibar iwe koloni la Tanganyika? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nilitegemea Serikali ijehapa iseme baada ya miezi mitatu au minne kwa sababuSerikali imeshasema haina kipaumbele katika mchakato waKatiba mpya. Kwa hiyo, tunataka mabadiliko katika Katibatuliyonayo na marekebisho ya sheria ili Serikali ya MapinduziZanzibar kama nchi iweze kukopa nje bila hisani ya Serikaliya Jamhuri ya Muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba Bungehili lihojiwe ili record ikae sawasawa. Wangapi wanaungamkono hoja yangu na wangapi wanataka Zanzibar iendeleekuwa koloni la Tanganyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kubenea, futa hilo nenokoloni.

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,wangapi ambao wanataka Zanzibar bado iendeleekutegemea Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

MWENYEKITI: Hapana, hiyo sio hoja yako, hoja yako nikubadilisha sheria.

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,sawa. Nataka Bunge lihojiwe lini Serikali italeta sheria hapaBungeni ya kubadilisha Katiba na hiyo sheria ili Zanzibar iwezekukopa, naomba Wabunge wahojiwe.

Page 307: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

307

MWENYEKITI: Hapana, Mheshimiwa Kubenea, mimindiyo nitakayehoji na hiyo sio hoja ya Bunge.

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,sawa. Yale ambayo sio hoja yangu nimeyaondoa, nilete hojayangu.

MWENYEKITI: Umefuta?

MHE. SAED A. KUBENEA: Nimeonda yale ambayo siyohoja yangu yamebaki yale ambayo ni hoja yangu.

MWENYEKITI: Sawa, sasa nitawahoji kuhusu hoja yaMheshimiwa Kubenea kwa yale aliyoyasema mwanzo.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kukataliwa)

MHE. MWIGULU L. NCHEMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti.

MWENYEKITI: Mheshimwa Mwigulu.

MHE. MWIGULU L. NCHEMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,samahani sana, siwarejeshi nyuma…

MWENYEKITI: Tumeshafunga hoja.

MHE. MWIGULU L. NCHEMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,wala haiathiri.

MWENYEKITI: Tumeshafunga hoja, samahani sana.Mheshimiwa Kiteto Zawadi.

MHE. KITETO Z. KOSHUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwenendo wa upatikanajifedha katika masuala ya mazingira ni hafifu, hili liko wazikabisa. Upo Mfuko ambao ulianzishwa kisheria mwaka 2007ili kusimamia na kuyalinda mazingira. Kwa bahati mbaya sana

Page 308: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

308

Mfuko huu umekuwa haupati fedha kutoka Serikalini walakatika chanzo chochote kile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nisipopata maelezoya kutosha nitashika shilingi. Nachoomba Serikali inipemaelezo ni msimamo gani iliyonao kuanzisha tozo maalumambazo zitaweza kuchangia katika Mfuko huu wa Mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, tozo ya mazingira.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweliSerikali ilianzisha Mfuko wa Mazingira kupitia Sheria yaMazingira na ulikuwa haujaanza kazi kitambo lakini mwakajuzi Mheshimiwa Rais akateua Mwenyekiti na Wajumbe waBodi. Tulifanya utafiti wa aina ya vyanzo ambavyo vinawezakutumiwa na mfuko huu na kuongeza uwezo wa nchikusimamia mazingira. Vyanzo hivi vilihusisha tozo za shughulizinazohusu mazingira ikiwemo mikaa, magogo na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Kamati ya Serikaliinayohusu kodi na tozo na jambo hilo lipo huko ili tukubalianendani ya Serikali na wenzetu kuhusu zipi ambazo zinawezakupitishwa kwa sababu hizi zinahusu sekta nyingine, hatuwezisisi peke yetu tukaamua kutoza kila mtu ili fedha ziendekwenye mazingira. Ni muhimu tukubaliane na wenzetu nahasa Wizara ya Fedha ili kuhakikisha kwamba tozo tunazotoahaziongezi gharama za maisha, kufanya biashara lakinivilevile zinatupatia fedha kwa ajili ya hifadhi na usimamizi wamazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, namshukuru sanaMheshimiwa Kiteto kwamba yeye ni Mjumbe wa Kamati yaMazingira, anaelewa na anaumia kuhusu mazingira nakuhusu mfuko huu kutokuwa na fedha. Kwa hiyo, tutaendeleakufanya kazi, hasa na Wizara ya Fedha, ili mapendekezo yaleya vyanzo yaweze kupita na mabadiliko madogo ya sheriakuhusu mfuko ule yaje hapa Bungeni ili tuweze kuyapitisha

Page 309: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

309

na vyanzo vipitishwe basi mfuko huu na wenyewe uwezekufanya kazi yake.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kiteto.

MHE. KITETO Z. KOSHUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana kwa maelezo ya Mheshimiwa Waziri na hasaalipozungumzia marekebisho ya Sheria hii ya Mazingira.Nachoomba Serikali itoe tu commitment kwamba ni linimabadiliko ya Sheria hii ya Mazingira yataletwa hapaBungeni. Hiyo yote ni kuipatia Wizara hii ya Mazingira nguvuza kuweza kusimamia vile vyanzo vya mapato ili viwezekusaidia katika mfuko huu. Sina haja ya kuondoka na shilingiya Waziri lakini naomba tu commitment ya Serikali.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, commitment,mchakato unaendelea?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Mwanasheria Mkuu wa Serikali alituandikia barua Mawaziriwote ambao wana sheria ambazo wangependa zibadilishweili mambo yao yaende vizuri na sisi tulimjibu kwa kumuandikiakuhusu vifungu muhimu kikiwemo hiki ambacho tunatakakibadilishwe. Bahati nzuri alitujibu na akatualika tukajadilianena watu wake kuhusu lugha ambayo inaweza kutumikakwenye haya mabadiliko. Kwa hiyo, suala hili analoMwanasheria Mkuu na limefika pazuri, wakati wowoteMuswada wa Sheria wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbaliutakapokuja Bunge imani yetu ni kwamba mabadiliko hayoyatakuwepo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kiteto umeridhika?

MHE. KITETO Z. KOSHUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ndiyo.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Bobali.

Page 310: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

310

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Hoja yangu mimi ni mabadiliko ya tabianchilakini nItazungumzia zaidi kwenye suala la kuongezeka kwakina cha bahari na hatua zinazochukuliwa na Serikali kuzuiabahari isiendelee kula ama kuchukua sehemu ya miji yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma maandiko yawaandishi mbalimbali yanathibitishi kwamba ifikapo mwaka2050 ujazo wa bahari utaongezeka katika eneo la Tanzaniakwa futi 0.5 mpaka futi 1.4. Hiki ni kiwango kikubwa na kamaSerikali haitachukua hatua madhubuti kuna hatari Miji yaLindi, Bagamoyo, Mikindani, Pangani na mingineyo ikapotea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nipongeze hatua Serikaliiliyochukua la Barack Obama Drive, wamefanya kazi nzuri.Kwa nini Serikali isitenge fedha zoezi lile likafanywa nchi nzimakuzuia maji katika Miji ya Tanga, Pangani, Bagamoyo, Dar esSalaam, Lindi na Kilwa? Pale Kilwa Kisiwani kuna Msikiti wazamani wa enzi hizo sasa hivi unazama na Mheshimiwa Wazirianajua kwa sababu bahari inaendelea kusogea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba commitment yaSerikali, nimesoma kwenye vitabu sioni fedha zilizotengwakwa ajili ya jambo hili. Mheshimiwa Kiteto kazungumza hapa,hii National Environmental Program ambayo ilikuwa adoptedmwaka 2007 haipati fedha na kama haipati fedha maanayake inashindwa kukabiliana na mambo makubwa kamahaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba commitment yaSerikali, nimeona mmetenga fedha za maendeleo shilingibilioni 19, shilingi bilioni 1 ya ndani na shilingi bilioni 18 za nje,fedha ambazo hatuna uhakika wa kuzipata. Ni lini Serikaliitaweka mkakati madhubuti kuhakikisha kwamba wanalindamaeneo haya ya miji ya pwani isije ikachukuliwa na bahari?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nisiporidhika, nitatoa shilingiili Bunge liweze kupata fursa ya kujadili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.

Page 311: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

311

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Mheshimiwa Bobali yuko sahihi kabisa kwa kweli. Nchi yetusisi ina ufukwe wa kilometa 1,400 kutoka kule juu Moa (Tanga)mpaka Msimbati (Mtwara) na karibu kila eneo kwenyeufukwe limeathirika sana na mabadiliko ya tabianchi na bahrikula ardhi. Kuna baadhi ya maeneo walikuwa wanalimampunga na mazao mengine, siyo tu kwamba bahari imelikahata yale maeneo hawawezi tena kulima. Kuna baadhi yavisima vilikuwa vinatoa maji ya baridi sasa hivi vinatoa majiya chumvi kwa sababu ya bahari kusogea. Kwa hiyo, athariza mabadiliko ya tabianchi zinaathiri sana maisha ya watuna Mheshimiwa Bobali yuko sahihi kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna vitu viwili ambavyo sisitunadhani ni muhimu kuvifanya. Kwanza, nchi yetu ni sehemuya Mkataba wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi natunalipa fee na una fursa mbalimbali. Moja ya fursa niAdaptation Fund, Mfuko wa Kuhimili Athari za Mabadiliko yaTabianchi. Ili upate fedha na hata huu mradi wa Barabaraya Barack Obama, Kigamboni, Pangani, Mikoko - Rufiji,tulizipata baada ya kutengeneza andiko ili tuweze kufikia hizofedha za Adaptation Fund.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba ndugu yangu,Mheshimiwa Bobali tukae pamoja na tuangalie kwakeanaposema na hata Wabunge wengine kwenye maeneokama hayo, kikubwa ni kuandika mradi, fedha kwa ajili yakuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi hazitolewi kwajumla, zinatolewa kwa specific project. Kwa mfano, watu waSimiyu walijenga hoja kwamba kuna ukame sana, hakunamaji kwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi, wamepatashilingi bilioni 250 kutoka kwenye GCF.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ndugu yanguMheshimiwa Bobali, ni vizuri umelisema hapa lakini ili tulifanyiekazi tutatuma wataalam waangalie tuone kama tunawezakuandika mradi kwa ajili ya eneo mahsusi ambalo umelisema

Page 312: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

312

halafu tutaona kama ni Adaptation Fund au ni GCF au nikwingine ili tuone kama ni kupanda mikoko au kujenga ukutaifanyike. Tuko tayari kushirikana nawe na Wabunge katikamaeneo ya pwani ambao wameathirika na athari za baharikula ardhi. Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Bobali maneno mazitohayo ya Waziri.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza namshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kukubali uhalisiana ameona ukubwa wa tatizo. Naomba sasa kilealichokisema kwamba Wabunge wanaotoka kwenyemaeneo hayo waweze kumwona ili kumpa taarifa, isiwe sasani jambo la sisi kumtafuta. Naomba Mheshimiwa Waziriaandae kikao maalum, atuite twende tukampe uhalisia, kwasababu jambo hili lina National interest, tuweze kuokoamaeneo haya ya nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namrudishia shilingi yake.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Saada Mkuya.

MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Nashukuru kwa kupata nafasi hii. Sina nia yakushika shilingi ya Mheshimiwa Waziri isipokuwa natakacommitment yake. Maelezo yangu ni kwamba kuna hajakubwa sana ya kutoa elimu inayohusu Muungano.Nilimwambia Mheshimiwa Waziri katika mchango wetukwamba kwa sababu focus ilikuwa kwa wanafunzi pamojana jamii nyingine ambayo siyo katika Bunge letu, lakini kwamaelezo haya yaliyotoka katika mjadala huu, kuna urgentkubwa sana ya kuwanza na masomo haya yanayohusuMuungano, process zake na sheria zake kuanzia katika Bungeletu hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka commitmentya Mheshimiwa Waziri haya mafunzo yanaanza lini? Maanayake siyo kwamba mtafanya au hamfanyi, hoja hapa

Page 313: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

313

imeonekana dhahiri hata wale ambao wana authorityhawajui exactly hili jambo linaendaje? Tunahitaji MheshimiwaWaziri atupe commitment lini tunaanza mafunzo yanayohusuMuungano katika Bunge letu hili la Jamhuri ya Muunganowa Tanzania?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAISMUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakubaliana na hasa baada ya kushuhudia na kusikiamaneno yaliyokuwa yanatoka kwenye mjadala uliopita.Kweli elimu ya Muungano inabidi ianzie Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tuko tayari kufanyamafunzo hayo hata kabla ya Bunge hili la bajeti halijaishawakati wowote ule. Imani yetu ni kwamba hakutahitajikamalipo kwa ajili ya kuja kushiriki hayo mafunzo, kwa sababuutakaposema kwamba ulipwe ili kupata elimu ya Muunganondipo tutakapoanza changamoto. Kwa sababu Mheshimiwaameyadai, sisi tuyafanya lakini yatakuwa hayana posho. Kwahiyo, sisi tuko tayari hata kabla ya Bunge kwisha.

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Saada, una lolotela kuongeza?

MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti,sina la kuongeza, namshukuru Mheshimiwa Waziri. NaaminiWabunge wote tutakuwa pamoja kusikiliza, kwa sababumaneno mengine yanayotoka ni maneno ambayo wewemwenyewe unahisi unataka kutetemeka, yaani sijui una-feelvipi. Sasa watu wanaotusikiliza wanachukua haya manenona ni maneno ya hatari sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, sote tuna wajibu,lazima tupate semina kuhusu Muungano tukubalini bilamalipo. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Jaku HashimAyoub.

Page 314: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

314

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Narudia tena, sina nia ya kuzuia shilingi yandugu yangu Mheshimiwa January. Katika mchango wangunilisema kuna baadhi ya mashirika na taasisi ikiwemo NBC,NMB, POSTA BANK, TTCL, TCRA, TCA, Zanzibar hayapatimchango. Ni l ini atafuatil ia angalau Zanzibar ipatekujikwamua kutokana na hali hii? Ni hilo tu. (Makofi)

MWENYEKITI: Waziri wa Fedha.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kwa fursa hii na kwa hoja hii yaMheshimiwa Jaku. Kama nilivyosema wakati nachangia hojahii ya Mheshimiwa Waziri kwamba jambo hili ni katika mamboambayo tunakamilisha muundo wake wa jinsi gani ambavyogawio hili ambalo mashirika haya yatakuwa yanatoa,utakwenda moja kwa moja kama ambavyo tumefanya kwaBenki Kuu ya Tanzania na kama ambavyo TPV Benki piainatoa gawio lake kulingana na shares ambazo Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar inayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, namwombaMheshimiwa Jaku, Mashirika yetu yameanza kutoa gawio,mwaka 2018 ndiyo tumeona mashirika mengi na sasa Ofisiya Msajili wa Hazina na Ofisi ya Mlipaji Mkuu wa Serikaliwanakamilisha mjadala huu na wenzetu wa Zanzibarkuhakikisha kwamba gawio lile linakwenda kama lilivyo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Jaku, maneno mazito hayo.

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti,maneno nakubali kweli mazito, lakini mdomo unasema, lakinivitendo ndiyo kazi.

MWENYEKITI: Vitendo vinakuja. Kwa hiyo, nakushukuru,ahsante. Mheshimiwa Dkt. Sware. (Makofi)

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi hii. Sera yetu yaMazingira ya 1997 iliyozaa Sheria yetu ya Mazingira ya 2004

Page 315: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

315

imeweka bayana majukumu ya wadau mbalimbali ambaowanatakiwa watekeleze sheria hii ya kusimamia mazingiraikianzia ngazi za Serikali za Mitaa mpaka ngazi ya Taifa.Nikisema hivi, kuanzia Serikali ya Mitaa ina maana nahusishaWizara ya TAMISEMI na wengine wanakuwa wanasimamiwaplus TAMISEMI na Wizara ya Muungano na Mazingira.Usimamizi na utekelezaji huu wa Sheria yetu ya Mazingirainakuwa reflected kwenye bajeti ambayo inatakiwa isomekekwenye kitabu chetu hiki cha bajeti kupitia mafungu au votembalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimepitia mbalimbali kutokaWizara 22, ni Wizara tano tu ambazo zimeweka kifungumahususi ambacho kinagusa masuala ya Mazingira. Hii nikatika ngazi ya Serikali Kuu. Pia katika ngazi ya Mabaraza yaMazingira au Vikao au Kamati za Mazingira ngazi ya Serikaliza Mitaa, huku pia haijawa reflected. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa pia Mfuko wetuwa Mazingira sasa kwa ukubwa wake hauna fedha, Wizarahusika ambazo zinatakiwa zisimamie mazingira hazijawekafedha. Cha kushangaza, kuna Wizara; kama Wizara ya Ardhi,Wizara ya Maji, Wizara ya Viwanda na Biashara ambaoKamati ya Bunge inasimamia Viwanda Biashara na Mazingira,hazina fungu au vote ambayo inahusia mazingira. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kupata ufafanuziau mikakati ya Waziri kusima kwamba suala hili linafanyiwajekazi ili kwamba sasa mazingira yawe kipaumbele cha kweliambayo ipo reflected kwenye bajeti yetu iweze kufanyiwakazi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama sitaridhika na maelezoya Mheshimiwa Waziri, basi nakusudia kushika shilingi yake.Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, hata mambo yakitaalam unataka kushinda shilingi?

Page 316: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

316

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwelisheria ya Mazingira ina sehemu kabisa, tena ina vifungu vingi;kuanzia kifungu cha 34 mpaka kifungu cha 42, vifungu vyotevinazungumzia wajibu wa Local Goverment katika usimamiziwa mazingira. Vile vile, nyuma yake inaelezea Wizara zaKisekta kuanzia Kifungu cha 30 mpaka 33 na moja ya mahitajini kwamba kila Wizara ya Kisekta lazima iwe na Mratibu waMazingira; iwe Wizara ya Afya, Maji, Miundombinu nakadhalika. Ni kweli kwamba katika Wizara zote 22, ni Wizarasita tu ndiyo zina Waratibu wa Kisekta. Kwa hiyo,tumewasiliana na wenzetu na ni imani yetu kwambawatatujibu kwamba kila Wizara itakuwa na Mratibu waMazingira. Hilo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, Mheshimiwa Makamuwa Rais ameelekeza kwa kuwaandikia Viongozi wa Mikoawahakikishe kwamba wajibu wa Serikali za Mitaa kwenyeMazingira unazingatiwa ikiwemo kila halmashauri iajiri AfisaMazingira kila Kijiji, Kata, Mtaa, Kitongoji kiwe na Kamati yaMazingira kama Sheria inavyoitaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo wetu Wizarawanaweza kulizungumzia na nyuma li l ikuwepo; naMheshimiwa Ruth Mollel atakuwa shahidi kwamba katika kilabajeti ya kila Wizara na Mamlaka ya Serikali za Mitaa kulikuwana budget code ya Mazingira, kama ambavyo kuna budgetcode ya UKIMWI hata kama Wizara haihusiki na UKIMWI, lakinivilevile kulikuwa na budget code ya Mazingira ili fedhazitengwe kidogo na shughuli za mazingira zifanyike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tumezungumza nawenzetu Wizara ya fedha ili ile budget code irudi ili kwenyevitabu vyote hivi tunavyopitisha angalau kuwe na shughuliambayo kila Wizara na Mamlaka ya Serikali za Mitaazinafanya kuhusu mazingira. Bahati nzuri mazungumzoyamefika pazuri, ni imani yetu kwamba katika mwaka ujaowa fedha itakuwa siyo huu tunaoujadili sasa, ni huo unaokuja,tutakuwa na budget code ya Mazingira ili taasisi zote naWizara zote ziweze kuwa na programme za mazingira,

Page 317: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

317

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimhakikishieMheshimiwa Dkt. Sware kamba maelekezo kwa Wizara zaKisekta na Mamlaka Serikali za Mitaa kuhusu wajibu waokwenye Sheria za Mazingira wameshaelekezwa na viongoziwetu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Sware.

MHE. DKT. IMMACULATA S. SEMESI: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi. Nimepokea maelezo yaMheshimiwa Waziri, kwa hiyo, sikusudii tena kutoa shilingi,nimeridhika. Kwa mantiki hiyo sasa tunategemea kitabu hikikwa bajeti inayokuja ya mwaka 2020/2021 basi hivyo vifunguvitasomeka viwe vina vitengo mahususi ambavyo vitakuwavinashughulikia masuala ya mazingira. Nashukuru. (Makofi)

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 1002 – Finance and Accouts Unit.............Sh. 265,805,000/=Kif. 1003 – Policy and Planning Division..........Sh. 639,200,000/=Kif. 1004 – Government Communication

Unit....................................................Sh.184,718,000/=Kif. 1005 – Internal Audit Unit...........................Sh. 200,718,000/=Kif. 1006 – Procurment Management Unit.....Sh. 127,344,000/=Kif. 1007 – Information and Communication

Technology Unit...............................Sh.163,934,000/=Kif. 1008 - Legal Services Unit...........................Sh. 193,354,000/=Kif. 2001 – Union Secretariat........................... Sh. 608,988,000/=Kif. 5001 – Environment.................................Sh. 4,489,798,440/=

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 26 - Ofisi Binafsi ya Makamu wa Rais

Kif. 1001 – Admin. & Human Resources Mgt..............................Sh.7,855,093,000/=

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Page 318: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

318

MIPANGO YA MAENDELEO

Fungu 31 – Ofisi ya Makamu wa Rais

Kif. 1001 – Administration and Human Resource division..........................Sh.1,000,000,000/=

Kif. 5001 – Environment ..............................Sh. 18,218,915,442/=

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

(Bunge lilirudia)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Mtoahoja.

T A A R I F A

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwamujibu wa kanuni za kudumu za Bunge toleo la Januari 2016kanuni ya 104 (3)(a)na (b) kwamba Bunge lako lililokaa kamaKamati ya Matumizi, limekamilisha kazi yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwamba taarifaya Kamati ya Matumizi ikubaliwe na Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO:Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.

MWENYEKITI: Hoja imeungwa mkono. Sasa nitawahoji.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ofisi ya Makumu wa Rais

Muungano na Mazingira yalipitishwa na Bunge)

Page 319: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

319

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, hongera sana natimu yako nawashukuru Wabunge wote kwa kazi nzurimliyoifanya. Wale wote ambao mliona umuhimu wa majibuya Mheshimiwa Waziri na kurudisha shilingi yake mmeonyeshauungawana sana na majibu mazuri yametoka. Hongera sanaMheshimiwa Waziri. Very professional answers.

Baada ya maneno hayo, naaharisha shughuli zaBunge mpaka kesho, saa 3.00 asubuhi.

(Saa 1.15 Usiku Bunge liliahirishwa hadi siku ya Jumatano, Tarehe 17 Aprili, 2019 Saa Tatu Asubuhi)

Page 320: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

320

(Footnotes)1Romanus C. Ishengoma - Faculty of Forestry and NatureConservation Sokoine University of AgricultureMorogoro -National trends in Biomas Energy in Tanzania- Presentation on 26– 27 February, 2015 Dar es Salaam.

3Intended Nationally Determined Contributions(INDCs) were prepared in consistence with decision1/CP.20, and will be implemented by 2030.

Page 321: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

321

Page 322: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

322

Page 323: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

323

Page 324: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

324

Page 325: MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA TANO · 2019-05-06 · wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015, Mifuko inaweza kutoa mikopo kwa SACCOS hadi asilimia 10 ya rasilimali za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

325