Upload
others
View
32
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
1
Toleo hili limetayarishwa na Mradi wa Mabadiliko ya Tabia Nchi, Kilimo na Kupunguza Umasikini Tanzania.
Juni 2014.
MAPENDEKEZO KWA WAWAKILISHI WALIOCHAGULIWA NA WANANCHI KUHUSIANA NA KULETA MABADILIKO KWA SERIKALI KATIKA KUSAIDIA KILIMO RAFIKI WA
MAZINGIRA KWA WAKULIMA WADOGO WADOGO
Tolea Kwa Lugha Rahisi Kwa Viongozi Wawakilishi wa Wananchi
2
1
Kuhusu Mradi wa Mabadiliko Ya Tabia Nchi na Kuondoa Umasikini Mradi unaojulikana kama “Mabadiliko ya Tabia Nchi, Kilimo na Kupunguza Umasikini: kuwafanya wakulima wadogo kuwa kiini cha sera na utendaji” ni mradi wa ubia unaotekelezwa na mashirika 5 ambayo ni: Mtandao wa Jumuiya za Uhifadhi Misitu Tanzania (MJUMITA), Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA), Asasi ya Uhifadhi wa Misitu Tanzania (TFCG), ActionAid Tanzania na Mtandao wa Kilimo Hai Tanzania (TOAM). Mradi huu unafadhiliwa kupitia Programu ya Uwajibikaji Tanzania (AcT). Mradi unatekelezwa katika ngazi ya taifa na katika ngazi ya chini kwenye vijiji 6 ndani ya wilaya 2 (vijiji 3 katika wilaya ya Kilosa na vijiji 3 katika wilaya ya Chamwino). Utayarishaji wa mradi huu unatokana na ukweli kwamba watu wengi nchini Tanzania ni wakulima wadogo na wanategemea kilimo katika maisha yao. Inapokuja katika suala la kutokutabirika kwa hali ya hewa, ni wakulima wadogo ndio wanaoathirika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi (CC). Imetambulika kwamba mabadiliko ya matumizi ya ardhi hasa ukataji wa misitu kutokana na kilimo cha kuhamahama, ndio chanzo kikubwa zaidi cha uzalishaji wa hewa ukaa nchini Tanzania. Uwekezaji katika kilimo na sera na taratibu za kilimo unatoa kipaumbele kwa mhamo kwenda kwenye kilimo kinachotegemea zaidi zana za kisasa zinazotumia mafuta na kilimo cha maeneo makubwa, kwa lengo la kuongeza tija na kufanya uzalishaji wa mkulima mdogo kuwa wa kibiashara. Wakati utaratibu huu unaweza kuongeza mavuno kwa kipindi kifupi, lakini unawaweka katika hatari hawa wakulima wadogo kuathirika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi. Tunaamini kwamba kuna njia mbadala katika matumizi ya ardhi na uzalishaji wa chakula ambazo zitataleta ‘mafanikio’ kwa vigezo vya kukabiliana na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi, lakini ukosefu wa ufahamu kwa upande wa wakulima wadogo na watunga sera kuhusu kukabiliana na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi, imekuwa ni tatizo.
Mradi huu unaonyesha kwa vitendo kilimo kinachoendeshwa na Wakulima Wadogo Wanaozingatia Mabadiliko ya Tabia Nchi (kilimo cha C3S) na usimamizi endelevu wa ardhi na maliasili katika kanda 2 za kilimo-ekolojia, kwa madhumuni ya kutoa mifano hai ya jinsi ambavyo wakulima wadogo wanaweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika njia ambazo zinaongeza kipato; kuongeza uhakika wa chakula na kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa. Mkakati huu unalenga katika kubadili tabia za wadau wawili muhimu: wakulima wadogo na maafisa watendaji wa wilaya. Wadau wengine muhimu ambao wanahusika na mkakati huu ni pamoja na: viongozi wa kuchaguliwa na wananchi kama Madiwani na Wabunge, wajumbe wa Kamati Elekezi ya Taifa ya Mabadiliko ya Tabia Nchi, na wanachama wa MJUMITA na MVIWATA.
Mradi unaweka msisitizo zaidi katika vipengele vya teknolojia vya kilimo cha C3S; muunganisho kati ya kilimo cha C3S na Programu ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi (Redd+) wilayani Kilosa; pia kutengeneza modeli ya jinsi maafisa wa Halmashauri za serikali za mitaa na viongozi waliochaguliwa wanaweza kuwasaidia wakulima wadogo kufanikisha hili. Hii ni pamoja na kufanya kazi na maafisa wa halmsashauri serikali za mitaa na viongozi waliochaguliwa wa wananchi katika kuhakikishwa kwamba kilimo rafiki wa mazingira (C3S) kinaingizwa katika Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (DADPs), na kushughulikia mapungufu ya kiutawala mahali pale kuhusiana na kilimo, usimamizi wa ardhi na maliasili.
Lengo la Mradi Umasikini umepungua miongoni mwa wakulima wadogo nchini Tanzania na uzalishaji wa hewa ukaa kutokana na kilimo umepungua kupitia matumizi ya kanuni za kilimo bora zinazohimili mabadiliko ya tabia nchi na uzalishaji mdogo wa hewa ukaa.
2
Kilimo Kinachozingatia Mabadiliko ya Tabia Nchi [CSA] kwa kifupi Mabadiliko ya Tabia Nchi yanaonekana dhahiri nchini Tanzania. Ukichukulia utegemezi wake wa asili katika hali ya hewa, uzalishaji wa kilimo unatishiwa na hali isiyotabirika inayosababishwa na kutotabirika kwa hali ya hewa na mabadiliko ya tabia nchi kutokana na matukio mabaya ya hali ya hewa kama vile mafuriko na ukame. Mabadiliko ya tabia nchi ni tishio kubwa zaidi la kimazingira kwa maisha hapa duniani, linaloathiri mazingira yetu, sio tu kimaumbile na kiuchumi, lakini pia kijamii na kitamaduni. Tanzania imekuwa ikikabiliwa na vipindi vya ukame vinavyotokea mara kwa mara ambavyo vimeathiri shughuli za kilimo, kusababisha uhaba wa chakula pia na kupungua kwa kiasi kikubwa cha uzalishaji wa umeme, na kusababisha madhara makubwa kwenye uchumi.
Lengo kuu la waraka huu Waraka huu unalenga katika kuonyesha kwa vitendo utaratibu jumuishi kuhusiana na kilimo kinachoendeshwa na Wakulima Wadogo Wanaozingatia Mabadiliko ya Tabia Nchi na Programu ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi. Huu ni muhtasari wa ripoti ya utafiti iliyotayarishwa Desemba 2013 kwa lengo la kutoa mapendekezo kwa wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kuhusiana na kuleta mabadiliko kwa serikali katika kuongeza msaada katika uwekezaji wa kilimo rafiki wa mazingira na kuwasaidi wakulima wadogo.
Waraka huu unatoa mapendekezo ya jinsi ambavyo serikali inaweza kusaidia kilimo cha wakulima wadogo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi, pia mapendekezo kuhusu elimu na utendaji bora katika kilimo cha wakulima wadogo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi kwa wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kuishawishi serikali katika kusaidia miradi inayozingatia mabadiliko ya tabia nchi.
Vipengele muhimu vya kuzingatia katika kuwasaidia Wakulima Wadogo Sehemu hii inalenga kuwasaidia viongozi waliochaguliwa kufahamu baadhi ya maeneo muhimu ambayo yatawasaidia kusukuma mbele ajenda ya kilimo rafiki wa mazingira ili ijumuishwe katika mipango ya maendeleo ya kilimo ya wilaya. Sehemu hii inaangalia mchakato wa Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya kwa kuzingatia miongozo ya serikali, sera zinazohusiana na kilimo na mazingira, na utendaji katika kilimo rafiki wa mazingira [vile vinavyohimizwa na serikali na vinavyofanyika kwa sasa]
Baadhi ya maeneo makuu ya taarifa katika mchakato wa Maendeleo wa Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (DADPs) Imefahamika wazi kutokana na miongozo ya Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya ya Desemba 2007 na toleo la marudio la Desemba 2011 kwamba, msisitizo umewekwa katika kushughulikia mahitaji na vipaumbele vya jamii katika hatua tofauti za mchakato wa maendeleo wa Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (DADP), (kijiji, kata na Wilaya). Lakini mambo yafuatayo yanahitaji kuzingatiwa:
Kwa desturi, ushiriki wa jamii unaonekana ni mdogo katika mchakato wa DADPs.
Mwongozo unatoa orodha ya aina ya wadau wa kilimo wa wilaya wanaostahili kuhusika katika mkutano wa wadau. Katika orodha hiyo kuna wawakilishi kutoka kwa wakulima (kundi vii la orodha). Hata hivyo, mwongozo hautaji idadi ya wakulima.
3
Idadi ya wawakilishi wa wakulima kwenye mkutano wa wadau haizingatii uwakilishi kutoka makundi maalumu na vipengele vingine kama jinsia, n.k.
Kwa vile mwongozo wa DADP hautaji idadi ya wawakilishi wa wakulima katika mkutano wa wadau wa kilimo katika wilaya na jinsi/vigezo vya kuwapata wawakilishi hao wa wakulima, kuna uwezekano mkubwa uwakilishi wa wakulima ukawa mdogo katika mikutano ya wadau na hivyo kuwa na uhakika mdogo wa kushughulikiwa kwa vipaumbele vya wakulima katika mipango ya DADP kutokana na muktadha wake.
Sauti za wakulima wadogo katika mkutano wa wadau huenda zisisikike kutokana na makundi ya watu walioko kwenye mkutano.
Maelezo muhimu ya kuzingatiwa kuhusu sera zinazohusiana na Kilimo Kinachozingatia Mabadiliko ya Tabia Nchi [CSA]. Utafiti kuhusu: Maandishi ya uzoefu na utendaji mzuri wa kilimo cha wakulima wadogo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi yameonyesha kwamba, sera za sekta mbalimbali nchini Tanzania ziko kimya inapokuja suala la Kilimo Kinachozingatia Mabadiliko ya Tabia Nchi. Hii pengine ni kwa sababu Kilimo Kinachozingatia Mabadiliko ya Tabia Nchi ni dhana mpya.
Utafiti kuhusu: Uchambuzi wa sera kuhusiana na kukabiliana na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi na Programu ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi (Redd+) yameonyesha mapungufu makubwa katika sera na utekelezaji wa sera ambao zinahusiana na:
Kutozingatiwa kwa hatari za mabadiliko ya tabia nchi katika sera ambayo pia inajionyesha katika mikakati na programu za utekelezaji.
Kukosekana kwa uelewano na uratibu wa masuala mtambuka hivyo kupelekea kwa juhudi kurudufiwa au kupinzana wakati wa utekelezaji.
Kutokuwepo kwa kuungwa mkono kwa taratibu za majaribio kwa ajili ya kushirikishana faida kati ya jamii, mamlaka za serikali za mitaa na serikali kuu kutokana na shughuli za kupunguza athari katika sekta za kilimo na misitu na
Kukosekana uhakika wa miliki ya ardhi miongoni mwa wakulima wadogo kunaweza kuharibu juhudi zozote za kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi na Programu ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi katika jamii (REDD+).
Aidha, utafiti wa kupata mapendekezo ya jinsi Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (DADP) zinavyoweza kushughulikia kukabiliana na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi kuhusiana na wakulima wadogo; kwa ujumla zinaonyesha kwamba:
Mabadiliko ya tabia nchi bado hayajajumuishwa katika utaratibu wa kawaida wa sera, programu na shughuli za baadhi ya sekta. Pia kwamba, hata pale ambapo mabadiliko ya tabia nchi yamejumuishwa katika utaratibu wa kawaida, usimamizi wake unatia mashaka na/au ni mdogo sana.
4
Kwa ukweli, kwa wastani kuna wataalamu wachache (kwa vigezo vya idadi na ujuzi) wanaoshughulika na ajenda ya kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi, na hii inaweza kuwa moja ya sababu zinazochangia kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi kutokupewa kipaumbele katika mipango ya DADPs kama ilivyoonekana katika mapitio ya mwongozo wa DADPs.
Utashi wa kisiasa mdogo au wa kutia mashaka wa kusukuma masuala ya mabadiliko ya tabia nchi katika programu na miradi ya maendeleo ya kitaifa na serikali za mitaa, hivyo kuachwa katika miradi mingi ya maendeleo.
Kukosekana kwa muunganisho rasmi baina ya kanuni za kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi na kazi za watafiti kwa ajili ya uthibitisho na baadaye kukuzwa na wafanyakazi wa ugani kwa ajili ya kusambazwa katika eneo kubwa na matumizi ya kanuni zilizofanikiwa za kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi.
5
Kanu
ni z
a ki
limo
bora
zin
azot
umiw
a na
wak
ulim
a w
adog
o Se
hem
u hi
i ina
leng
a ka
tika
kuw
awez
esha
vio
ngoz
i wal
ioch
agul
iwa
kuw
a na
uel
ewa
mzu
ri w
a ki
limo
kina
choz
inga
tia m
abad
iliko
ya
tabi
a nc
hi
(CSA
) pal
e w
alip
o. K
wa
kuzi
ngat
ia h
ilo, v
iong
ozi w
ataw
eza
kuch
agua
na
kush
auri
kanu
ni b
ora
zina
zow
eza
kutu
mik
a ka
tika
maz
ingi
ra y
ao h
ivyo
ku
wez
a ku
zite
tea.
Seh
emu
hii i
nato
a m
chan
gany
iko
wa
kanu
ni z
a CS
A k
atik
a ng
azi z
ote
[Kan
uni z
a en
eo h
usik
a au
za
wen
yeji
na z
ilizo
bore
shw
a au
kuk
ubal
ika
kim
atai
fa].
Kanu
ni z
a ki
limo
rafik
i w
a m
azin
gira
(CSA
) M
aele
zo m
afup
i ya
kanu
ni z
a CS
A
Was
ilish
o ka
tika
pic
ha
Faid
a/uw
ezo
Vikw
azo/
Chan
gam
oto/
ukom
o
Kupu
nguz
a ut
ifuaj
i wa
ardh
i [ku
tum
ia je
mbe
la
Mag
oye]
Utif
uaji
wa
ardh
i una
wez
a ku
fany
ika
kwa
kutu
mia
jem
be la
ku
tiful
ia a
mba
lo h
uvun
ja v
unja
m
abon
ge y
a ar
dhi k
atik
a m
ista
ri ya
kup
andi
a na
kua
cha
nafa
si
kati
ta m
ista
ri bi
la y
a ku
igus
a.
Eneo
lilil
otifu
liwa
huw
a ka
ma
eneo
dog
o la
kuk
usan
ya m
aji y
a m
vua
na k
uong
eza
upen
yaji
wa
maj
i. U
tifua
ji un
awez
a ku
fany
ika
kwa
kutu
mia
trek
ta a
u m
aksa
i.
Huh
ifadh
i maj
i kw
a ku
pung
uza
mvu
kizo
kw
a ku
funi
ka
na m
atan
dazo
, hu
pung
uza
mm
omon
yoko
wa
ardh
i kw
a sa
babu
ud
ongo
wa
juu
umef
unik
wa,
hu
pung
uza
mga
ndam
izo
wa
udon
go, n
a ku
pung
uza
atha
ri za
m
vua
na u
pepo
.
Kam
a ha
ikuf
anyi
ka v
izur
i, m
agug
u ya
nash
inda
na
na z
ao k
uu, u
wez
ekan
o m
kubw
a w
a w
adud
u w
ahar
ibifu
na
mag
onjw
a ya
nayo
toka
na n
a m
abak
i ya
maz
ao, m
boji
hais
amba
zwi k
wa
usaw
a au
hul
undi
kana
kat
ika
udon
go w
a ju
u.
6
Maz
ao y
anay
ofun
ika
ardh
i H
aya
ni m
azao
am
bayo
kw
a ka
wai
da h
utam
baa
na
haya
shin
dani
i mw
anga
na
zao
kuu.
Hay
a ni
maz
ao a
mba
yo
hupa
ndw
a kw
a le
ngo
la
kufu
nika
udo
ngo
wak
ati n
a ba
ada
ya m
sim
u w
a ku
pand
a kw
a za
o ku
u ili
kup
ungu
za
mm
omon
yoko
wa
udon
go n
a ku
hifa
dhi u
nyev
u.
Huz
uia
mm
omon
yoko
w
a ud
ongo
un
aoto
kana
na
upep
o na
maj
i, hu
jeng
a m
boji
kwen
ye
udon
go (n
yasi
zi
nazo
funi
ka a
rdhi
), hu
inua
ubo
ra w
a m
aji,
huzu
ia m
agug
u, n
a hu
ambi
sha
nitr
ojen
i kw
a za
o lin
alof
uata
(z
ao la
mku
nde
linal
ofun
ika
udon
go).
Chan
gam
oto
za k
utum
ia
mim
ea in
ayof
unik
a ar
dhi
ni p
ale
maz
ao h
ayo
haya
wez
i kut
umik
a ka
ma
chak
ula
au k
ama
haya
na
mat
umiz
i men
gine
, hai
toi
mot
isha
wa
kuto
sha
wa
kuw
eza
kuya
tum
ia.
Pia
mis
imu
inaw
eza
kuw
a ni
cha
ngam
oto
hasa
ka
tika
mae
neo
amba
yo
yana
msi
mu
mm
oja
wa
mvu
a za
mud
a m
fupi
, m
azao
yan
ayof
unik
a ar
dhi y
anaw
eza
yasi
toe
king
a ya
udo
ngo
kwa
mw
aka
mzi
ma.
Kube
rega
na
kuch
oma
mab
aki y
a m
azao
H
ii ni
tekn
oloj
ia y
a as
ili
iliyo
enea
kat
ika
kand
a za
m
asha
riki n
a ka
ti.
Kuto
kuch
oma
mab
aki y
a m
imea
au
maz
ao k
unaw
eza
kuhi
fadh
i udo
ngo
na
unye
vu k
utok
ana
na
kwam
ba m
abak
i hay
o hu
funi
ka u
dong
o,
wak
ati k
utok
ucho
ma
hupu
nguz
a uz
alis
haji
wa
hew
a uk
aa
Inah
itaji
mab
adili
ko y
a fik
ra k
uhak
ikis
ha m
abak
i ha
yach
omw
i.
7
Mas
him
o ya
Cho
lolo
U
taal
amu
wa
asili
wa
kuvu
na
maj
i ya
mvu
a ul
iobu
niw
a na
ku
teke
lezw
a ka
tika
Man
ispa
a ya
Dod
oma,
hay
a ni
mas
him
o m
adog
o ye
nye
kipe
nyo
cha
sm 2
2 na
kin
a ch
a sm
30,
ya
liyoc
him
bwa
katik
a m
star
i wa
nafa
si y
a sm
60
kati
ya m
ashi
mo
na sm
90
kati
ya m
ista
ri ya
m
ashi
mo.
Mas
him
o ya
Cho
lolo
ya
mez
ungu
shiw
a ud
ongo
ku
zung
uka
mas
him
o ili
kus
aidi
a ku
hifa
dhi
maj
i ya
mvu
a,
mbo
lea
ya w
anya
ma
na m
boji,
na
mbe
gu 1
had
i 2 z
a m
ahin
di/
mta
ma/
uwel
e zi
naw
eza
kupa
ndw
a ka
tika
kila
shim
o.
Inak
uza
kupe
nyez
a kw
a m
aji y
a m
vua,
in
apun
guza
upo
tevu
w
a ud
ongo
, maj
i na
viru
tubi
sho
kuto
ka
sham
bani
, hup
ungu
za
kulu
ndik
ana
kwa
tope
na
ucha
fuzi
(wa
kem
ikal
i za
kilim
o)
mae
neo
ya c
hini
ya
mas
ham
ba.
Kuon
geze
ka k
wa
maj
i ard
hini
kw
ani
maj
i kw
enye
udo
ngo
hupo
tea
ardh
ini h
asa
kwen
ye u
dong
o w
a m
chan
ga .
Hup
ungu
za
mm
omon
yoko
kat
ika
sham
ba le
nye
udon
go
wen
ye m
boji
Maj
i kut
uam
a ku
naw
eza
kuto
kea
katik
a m
isim
u ya
m
vua
kubw
a
Eart
h Ba
sins
/bun
ds.
Ard
hi k
ufuk
uliw
a m
ithili
ya
bes
eni n
a nj
ia n
ying
ine
za k
uvun
a m
aji y
a m
vua
amba
yo in
awez
a ku
wa
katik
a um
bo la
dua
ra, n
usu
duar
a,
pem
be m
raba
au
mst
atili
, ik
izun
gush
iwa
vitu
ta v
ya
udon
go k
wa
mad
hum
uni y
a ku
vuna
maj
i ya
mvu
a kw
a aj
ili
ya m
atum
izi y
a m
mea
. Wak
ati
mw
ingi
ne v
ituta
vya
udo
ngo
hush
ikili
wa
na m
imea
(nya
si,
kund
e)
8
Hii
ni te
knol
ojia
inay
ofaa
kw
a w
akul
ima
wan
aopa
nda
maz
ao
yao
katik
a m
ipor
omok
o ya
vi
lima
.
Tekn
oloj
ia h
ii in
awez
a ku
chan
gia
katik
a on
geze
ko la
uza
lisha
ji w
a m
azao
pia
kuz
uia
mm
omon
yoko
wa
udon
go; k
ubor
esha
up
enya
ji w
a m
aji n
a m
lund
ikan
o w
a m
boji
Uta
yari
wa
wak
ulim
a ku
tum
ia te
knol
ojia
hii
na
kuac
hana
na
kilim
o ch
ao
cha
asili
Kute
ngen
eza
mbo
ji M
binu
muh
imu
na y
a gh
aram
a na
fuu
kwa
wak
ulim
a w
adog
o ya
ku
reje
leza
mab
aki y
a m
imea
na
wan
yam
a [m
agug
u, m
abak
i ya
maz
ao, m
abak
i yan
ayot
okan
a na
usi
ndik
aji w
a m
azao
, kin
yesi
ch
a m
ifugo
, mko
jo, n
.k.]
Ina
sifa
ya
kuw
a m
bole
a ha
i am
bayo
hu
sisi
mua
viu
mbe
hai
kw
enye
udo
ngo
na
kubo
resh
a m
uund
o w
a ud
ongo
. Pia
ina
faid
a kw
a uw
ezo
wa
mim
ea k
uhim
ili
wad
udu
wah
arib
ifu n
a m
agon
jwa
Vikw
azo
vina
wez
a ku
jum
uish
a up
atik
anaj
i na
ubo
ra w
a m
ali g
hafi,
us
afiri,
ngu
vu k
azi n
a m
aji
9
Kuch
agua
maz
ao
yana
yow
eza
kuhi
mili
In
ahus
u m
atum
izi y
a ai
na
za m
azao
am
bazo
zin
awez
a ku
him
ili u
kam
e, m
agon
jwa
na
zina
zoko
maa
map
ema.
Inah
akik
isha
kiw
ango
fu
lani
cha
mav
uno
hata
kw
enye
mia
ka
mib
aya
Lich
a ya
uw
ezo
wao
, ch
anga
mot
o ku
bwa
inab
aki k
uwa
uzin
gatia
ji w
a ka
nuni
nyi
ngin
e za
ki
limo
ziliz
open
deke
zwa.
Chan
gam
oto
nyin
gine
ni
kwam
ba a
ina
za m
imea
ya
kie
nyej
i yen
ye u
wez
o zi
napo
tea
[Mm
omon
yoko
w
a ki
jene
tiki]
Kilim
o ch
a U
mw
agili
aji
Tekn
oloj
ia h
ii ni
muh
imu
kwa
kufid
ia u
nyev
u w
akat
i wa
upun
gufu
. Maj
i yan
awez
a ku
patik
ana
kuto
ka k
wen
ye
uvun
aji w
a m
aji y
a m
vua
na
maj
i yan
ayoi
ngia
kw
enye
hi
fadh
i ndo
go/m
abw
awa
yana
yohi
fadh
i maj
i kw
a aj
ili y
a um
wag
iliaj
i wak
ati w
a m
sim
u w
a m
vua
Mira
di m
idog
o ya
um
wag
iliaj
i na
mbi
nu
[pam
pu z
a ku
inua
, m
abw
awa
mad
ogo,
vi
sim
a vy
a ki
na k
ifupi
, m
atan
gi y
a ku
kusa
nya
maj
i ya
mvu
a n.
k.]
amba
zo w
akul
ima
wan
awez
a ku
mud
u hu
wez
a ku
fidia
up
otev
u w
a m
azao
ku
toka
na n
a uk
ame.
Skim
u ku
bwa
za
umw
agili
aji z
inah
itaji
uwez
o w
a uw
ekez
aji n
a us
imam
izi w
a ha
li ya
juu,
am
bazo
kw
a se
hem
u ku
bwa
zina
kose
kana
kw
a w
akul
ima
wad
ogo.
10
Kilim
o-m
isit
u Ki
limo-
mis
itu k
inah
usis
ha
kupa
nda
miti
ikiju
mui
sha
na
shug
huli
nyin
gine
za
kilim
o,
pam
oja
na m
ifugo
. Spi
shi
tofa
uti z
a m
iti z
inaw
eza
kupa
ndw
a na
ain
a m
balim
bali
za m
azao
kw
a ku
tum
ia m
iund
o m
balim
bali.
Zaid
i ya
kuto
a ch
akul
a ch
a m
ifugo
, kun
i, m
bao,
na
maz
ao
men
gine
miti
kat
ika
mifu
mo
ya k
ilim
o-m
isitu
pia
huk
uza
uhifa
dhi w
a ud
ongo
na
maj
i, hu
onge
za
rutu
ba y
a ud
ongo
, na
hufa
nya
kazi
kam
a ki
nga
ya u
pepo
kw
a m
azao
ya
karib
u.
Uha
ba w
a m
aarif
a kw
a w
akul
ima
katik
a ku
pand
a m
chan
gany
iko
mzu
ri w
a m
iti, m
azao
, mifu
go n
.k.
[kat
ika
uten
daji
halis
i]
Kuru
dish
ia m
isit
u kw
a Ku
pand
a m
iti
Hii
inah
usis
ha k
uhim
iza
jam
ii ku
anzi
sha
mas
ham
ba y
a m
iti a
mba
yo y
anaj
umui
sha
aina
mba
limba
li za
miti
kw
a m
atum
izi t
ofau
ti. V
ingi
nevy
o ja
mii
zina
ham
asis
hwa
kuhi
fadh
i m
isitu
Miti
ni m
uhim
u ka
tika
kuvu
na h
ewa
ya
kabo
ni d
ayok
said
i hi
vyo
inaw
eza
kuw
a nj
ia y
a ku
pung
uza
atha
ri; h
uhifa
dhi
maz
ingi
ra, c
hanz
o ch
a ki
pato
kup
itia
kuuz
a m
azao
yak
e na
ufu
gaji
wa
nyuk
i n.k
.
Kufa
ham
u au
kup
anda
ai
na z
enye
man
ufaa
ni
muh
imu
kwa
mat
umiz
i m
balim
bali
[kw
a m
ahal
i sa
hihi
na
wak
ati]
11
Mat
umiz
i ya
nish
ati
mba
dala
kam
a uz
alis
haji
wa
Biog
as
na m
atum
izi y
a m
ajik
o ya
nayo
okoa
nis
hati
Tekn
oloj
ia h
izi z
inal
enga
ka
tika
kupu
nguz
a ut
egem
ezi
mku
bwa
wa
miti
kam
a ch
anzo
ch
a ni
shat
i k.m
. Bio
gas k
wa
sehe
mu
kubw
a hu
tum
ia k
inye
si
cha
wan
yam
a ka
ma
mal
i gha
fi w
akat
i maj
iko
yana
yook
oa
nish
ati y
anah
itaji
kuni
cha
che
sana
kw
a w
akat
i mm
oja
Huz
alis
ha n
isha
ti kw
a aj
ili y
a ku
piki
a,
hudh
ibiti
kin
yesi
na
kupu
nguz
a u
zalis
haji
wa
hew
a uk
aa.
Mat
umiz
i ya
maj
iko
yana
yook
oa n
isha
ti ya
tapu
nguz
a uv
amiz
i w
a m
isitu
na
ukat
aji
miti
Biog
as w
akat
i mw
ingi
ne
ni g
hali
kwa
mku
lima
wa
kaw
aida
Mat
uta
yeny
e um
bo la
be
nchi
au
ngaz
i -
Hii
huw
eza
kufa
nyik
a kw
a ku
teng
enez
a ng
azi z
a m
awe,
ng
azi k
uwa
juu,
vis
horo
ba v
ya
mab
aki y
a m
azao
vin
avyo
kata
m
itere
mko
kup
ungu
za u
mba
li w
a m
aji y
anay
otiri
rika
na k
uzui
a ud
ongo
ulio
mom
onyo
ka
katik
a m
star
i wa
maw
e, m
atut
a ya
udo
ngo
au v
isho
roba
vya
m
abak
i ya
maz
ao, a
mba
yo
baad
a ya
mud
a hu
jeng
a m
atut
a m
ithili
ya
ngaz
i.
Kute
ngen
eza
mat
uta
ni
tekn
oloj
ia n
ying
ine
ya K
ilim
o ch
a M
abad
iliko
ya
Tabi
a N
chi
kwa
ajili
ya
kuhi
fadh
i udo
ngo
na m
aji a
mba
yo h
ufan
ya k
azi
vizu
ri ha
sa k
atik
a m
aene
o ye
nye
mte
rem
ko m
kali
Tekn
oloj
ia h
ii in
awez
a ku
chan
gia
onge
zeko
la
uza
lisha
ji pi
a ku
zuia
m
mom
onyo
ko w
a ud
ongo
; kub
ores
ha
upen
yaji
wa
maj
i ar
dhin
i na
mlu
ndik
ano
wa
mbo
ji
Kute
ngen
eza
mat
uta
ni k
azi n
gum
u ka
tika
hatu
a za
aw
ali,
laki
ni
baad
aye
mah
itaji
ya
nguv
ukaz
i yan
apun
gua
kwan
i ni m
aten
gene
zo
tu y
anay
ofan
yika
in
apoh
itajik
a.
12
Mat
anda
zo
Hii
kwa
kaw
aida
ni t
abak
a do
go k
atik
a m
akut
ano
ya
udon
go n
a he
wa.
Mat
umiz
i ya
mat
anda
zo y
anaw
eza
kuch
ukua
na
fasi
ya
mat
ayar
isho
ya
vita
lu
vya
mbe
gu k
atik
a m
ifum
o ya
ki
limo
amba
po h
akun
a ut
ifuaj
i w
a ar
dhi.
Mat
anda
zo y
a as
ili
amba
yo h
utum
ika
sehe
mu
nyin
gi y
anaj
umui
sha:
taba
ka
la m
ajan
i mak
avu,
mab
aki
ya m
azao
[mab
ua, m
ajan
i, n.
k.],
maj
ani m
abic
hi k
utok
a kw
enye
miti
, mim
ea h
ai [m
azao
ya
nayo
funi
ka a
rdhi
, mbo
lea
ya
kija
ni n
.k.]
Zaid
i ya
kupu
nguz
a ku
chip
ua n
a ku
kua
kwa
mbe
gu z
a m
agug
u, m
atan
dazo
ya
naw
eza
kubo
resh
a ku
kua
na u
shin
dani
w
a m
azao
yal
iyol
imw
a kw
a ku
hifa
dhi u
nyev
u w
a ud
ongo
na
kure
kebi
sha
hali
ya
joto
la u
dong
o
Katik
a ba
adhi
ya
maz
ingi
ra, m
atam
dazo
ya
naw
eza
kuzi
dish
a m
atat
izo
ya m
agug
u.
Mat
anda
zo y
anay
otok
ana
na v
ium
be h
ai k
wa
mfa
no
maj
ani y
aliy
osin
dikw
a (h
ei) k
utok
a vy
anzo
vi
ngin
e vi
sivy
okuw
a vy
a sh
amba
, yan
awez
a ku
beba
mbe
gu z
a sp
ishi
mpy
a ya
mag
ugu
sham
bani
.
Maz
ao a
nuw
ai
Kuju
mui
sha
maz
ao
mch
anga
nyik
o am
bayo
hay
ana
ushi
ndan
i kat
ika
sham
ba m
oja.
Ka
tika
mae
neo
ya m
ilim
ani,
kuan
zish
wa
kwa
maz
ao y
a ku
funi
ka a
rdhi
mw
isho
wa
msi
mu
wa
kupa
nda
ili k
ulin
da
udon
go w
akat
i wa
kian
gazi
in
awez
a ku
fany
ika
kwa
kufa
idik
a na
uny
evu
ulio
baki
.
Kuzu
ia m
mom
onyo
ko
wa
udon
go k
utok
ana
na u
pepo
na
maj
i, ku
onge
za m
boji
ardh
ini (
nyas
i kam
a za
o la
kuf
unik
a ud
ongo
), ku
inua
ub
ora
wa
maj
i, ku
zuia
m
agug
u ya
siot
e n.
k.
Pia
huha
kiki
sha
huko
si
kabi
sa m
azao
Jinsi
ya
kupa
ta n
a ku
pand
a m
chan
gany
iko
mzu
ri w
a m
azao
has
a ka
tika
maz
ingi
ra y
a w
akul
ima
wad
ogo
13
Ufu
gaji
nyuk
i ka
tika
seh
emu
ziliz
ohifa
dhiw
a
Idad
i na
aina
tofa
uti z
a m
izin
ga
huni
ng’in
izw
a ka
tika
msi
tu a
u sh
amba
la m
iti [
iliyo
pand
wa
na
bina
dam
u au
la a
sili]
U
nahi
fadh
i bi
oanu
wai
Kwa
njia
isiy
o ra
smi
huzu
ia u
vam
izi w
a m
isitu
.
Vyan
zo v
ya k
ipat
o ku
toka
na n
a as
ali
na m
azao
yak
e
Ute
kele
zaji
mdo
go
wa
sher
ia n
dogo
za
maz
ingi
ra k
atik
a ng
azi
ya k
ijiji
Kuvu
na m
aji y
a m
vua
Ni m
uhim
u ka
tika
mae
neo
yeny
e uh
aba
wa
maj
i na
ni m
uhim
u za
idi k
atik
a za
ma
hizi
za
mab
adili
ko y
a ta
bia
nchi
. Kuv
una
maj
i ya
mvu
a ni
uku
sany
aji w
a m
aji
yana
yotir
irish
wa
na m
vua
kwa
mad
hum
uni m
balim
bali.
M
aji y
a m
vua
yaliy
okus
anyw
a ya
naw
eza
kuhi
fadh
iwa
kwen
ye
udon
go a
u ku
kusa
nyw
a kw
enye
hifa
dhi
Muh
imu
katik
a ku
onge
za u
nyev
u w
akat
i wa
kian
gazi
[k
upiti
a m
binu
za
umw
agili
aji w
a m
aton
e] n
a ni
cha
nzo
cha
maj
i kw
a m
ifugo
Kute
gem
ea u
kubw
a w
a en
eo la
kuv
una
maj
i, ni
ka
zi n
gum
u ku
anzi
sha
katik
a ha
tua
za a
wal
i.
Maa
rifa
ya k
iasi
fula
ni
yana
hita
jika
ili k
uanz
isha
m
wel
ekeo
sahi
hi n
a vi
wan
go
Kuan
zish
wa
kwa
mir
adi m
idog
o m
bada
la y
a uz
alis
haji
mal
i kam
a vi
le u
fuga
ji w
a m
buzi
na
kuku
Hiz
i ni a
ina
za sh
ughu
li m
bada
la
za u
zalis
haji
mal
i am
bazo
zi
naw
eza
kufid
ia h
atar
i na
atha
ri zi
nazo
toka
na n
a ha
li ya
hew
a ku
toku
tabi
rika
k.m
. Ufu
gaji
wa
kuku
, ufu
gaji
nyuk
i, m
buzi
, ng
uruw
e n.
k.
Hut
awan
ya h
atar
i ya
kuko
sa k
ipat
o na
ni
uhak
ika
wa
chak
ula
katik
a m
iaka
mib
aya
Baad
hi y
ao z
imek
uwa
chan
zo c
ha
kutu
mai
niw
a ch
a ki
pato
na
lishe
Kufu
ga w
anya
ma
wad
ogo
kuna
hita
ji m
aarif
a na
uj
uzi w
a ku
tosh
a ili
mira
di
hiyo
iwe
na m
anuf
aa.
14
Ute
ndaj
i mw
ingi
ne w
a w
akul
ima
wad
ogo
Ute
ndaj
iM
aele
zoFa
ida
Mbo
lea
vund
e ai
na y
a M
apam
bano
– Ko
ndoa
D
odom
a
Ch
imba
shim
o le
nye
kina
cha
mita
3 n
a up
ana
wa
mita
2.5
m.
W
eka
taba
ka la
maj
ivu
la u
nene
wa
inch
i 1
chin
i kab
isa
na p
akaz
a kw
enye
kut
a za
pe
mbe
ni h
adi n
usu
futi
kuto
ka c
hini
Ong
eza
taba
ka la
nya
si k
ama
nusu
futi
kuto
ka c
hini
Ende
lea
na o
ngez
a m
abak
i ya
vium
be h
ai
hadi
shim
o lim
ejaa
takr
iban
i nus
u m
ita
kuto
ka u
saw
a w
a ar
dhi.
Zaid
i ya
mab
aki y
a vi
umbe
hai
yal
iyow
ekw
a kw
enye
shim
o,
mte
ngen
ezaj
i ana
onge
za p
ia m
aji m
acha
fu
yana
yoto
kana
na
shug
huli
za n
yum
bani
na
mko
jo w
a w
anya
ma.
Li
napo
jaa,
mch
anga
nyik
o hu
u w
a m
abak
i ya
vium
be h
ai h
ufun
ikw
a na
ta
baka
la m
ajiv
u na
kuf
uatiw
a na
taba
ka
dogo
la n
yasi
za
mal
isho
. Maj
i mac
hafu
ya
nayo
toka
na n
a sh
ughu
li za
nyu
mba
ni
yana
ende
lea
kuon
gezw
a ili
kuf
anya
liw
e na
un
yevu
Baad
a ya
mie
zi 5
had
i 6, m
bole
avun
de
iko
taya
ri ku
tum
ika.
Mat
okeo
yak
e ni
m
chan
gany
iko
wa
udon
go w
enye
rang
i ya
kaha
wia
iliy
opau
ka h
adi k
ijivu
.
Wak
ati w
a m
sim
u w
a ku
pand
a,
mbo
leav
unde
hut
umik
a kw
a ki
pim
o ch
a ¼
ha
di ½
lita
kw
a ki
la sh
imo
la k
upan
dia.
Ku
onge
zeka
kw
a m
avun
o ya
mah
indi
had
i gu
nia
20 k
wa
eka
Ku
onge
zeka
kw
a ki
pato
ch
a pe
sa
Ka
ya z
ina
uhak
ika
wa
chak
ula
15
Kuba
dili
mto
w
a m
chan
ga
kuw
a ar
dhi y
a ki
limo–
Kon
doa
Dod
oma
Ki
tu c
ha k
wan
za n
i kuc
him
ba m
ashi
mo
yeny
e um
bo la
mst
atiri
.
Baad
a ya
kufi
kia
udon
go w
a ka
wai
da,
onge
za m
bole
avun
de k
uong
eza
rutu
ba
ya u
dong
o kw
ani b
aadh
i ya
viru
tubi
sho
vim
echu
kuliw
a na
maj
i yan
ayot
iririk
a
Funi
ka m
bole
avun
de n
a ud
ongo
wa
kaw
aida
na
pand
a m
begu
. Baa
da
ya m
begu
kuc
hipu
a na
kad
ri m
iche
in
avyo
staw
i, ru
dish
ia m
chan
ga k
ujaz
a m
ashi
mo
hadi
usa
wa
wa
mch
anga
au
hadi
m
mea
una
poto
a m
aua.
Katik
a ha
tua
hii,
iliyo
baki
ni k
uvun
a kw
ani
mm
ea h
auhi
taji
kum
wag
iliw
a m
aji a
u ku
palil
ia. W
akat
i mw
ingi
ne v
iuad
udu
vina
hita
jika
kutu
mik
a
Ku
wez
a ku
badi
li m
to w
a m
chan
ga k
uwa
ardh
i ya
kilim
o
Ku
onge
zeka
kw
a uz
alis
haji
na k
ipat
o ch
a pe
sa k
wa
kila
kip
ande
cha
en
eo
Mbi
nu z
a U
mw
agili
aji w
a as
ili il
i kuo
ngez
a U
zalis
haji
wa
Maz
ao –
M
ufind
i Iri
nga
Jum
la y
a m
ianz
i 50
hadi
60
hula
zwa
kwen
ye
mife
reji
na k
ufuk
iwa.
Mab
omba
hay
a hu
wez
esha
mtir
iriko
wa
maj
i kufi
ka sh
amba
ni.
Wak
ati w
a um
wag
iliaj
i hal
isi,
vipa
nde
vya
bom
ba z
a pl
astik
i huf
ungw
a kw
enye
mau
ngio
ka
ti ya
mab
omba
ya
mia
nzi n
a uw
azi i
li ku
rahi
sish
a um
wag
iliaj
i
Ubu
nifu
huu
um
ewez
esha
ku
mw
agili
a m
boga
na
maz
ao m
engi
ne k
wa
maf
anik
io k
atik
a sh
amba
la
eka
3 kw
a m
wak
a m
zim
a.
16
Mapendekezo kwa vyombo vya serikali katika kusaidia Kilimo Kinachozingatia Mabadiliko ya Tabia Nchi:
Mapendekezo kuhusu “mchakato” wa kutayarisha mipango ya maendeleo inayohusiana na Kilimo Kwa kufanya utafiti kutoka kwenye tafiti mbalimbali, viongozi wa kuchaguliwa wanaweza kukumbana na mapendekezo yafuatayo kuhusiana na kuboresha mchakato wa kutayarisha mipango ya kilimo hususani Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (DADP) inayozingatia Kilimo Kinachozingatia Mabadiliko ya Tabia Nchi.
Kwa kujua kwamba dhana ya Kilimo Kinachozingatia Mabadiliko ya Tabia Nchi haifahamiki vyema kwa wadau wengi katika ngazi ya wilaya, viongozi wa kuchaguliwa watahitaji kutoa ushauri/kufanya mapitio ya Timu ya Uwezeswhaji ya Wilaya. Huu ushauri/mapitio unaweza kulazimisha kupendekeza kigezo cha uwakilishi pamoja na mambo mengine, kuwa na ujuzi na uzoefu wa kutosha katika masuala yanayohusiana na mabadiliko ya tabia nchi. Wazo lililopo hapa ni kuhakikisha kunakuwepo kwa jumuisho la kitaalamu linalotoa matokeo ya kukabiliana na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi na Programu ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi katika jamii (REDD+) katika mipango mingi ya DADPs,
Viongozi wanashauriwa kutetea uwepo wa rasilimali za kutosha kwa ajili ya kujenga uwezo wa miradi ya Kilimo Kinachozingatia Mabadiliko ya Tabia Nchi (k.m. kutoa mafunzo ya vitendo, kuunda vikundi/vilabu vya jamii vya mazingira na kukutana nao mara kwa mara, kutembelea jamii nyumbani/eneo la mradi na miradi ya kuamsha ufahamu katika ngazi ya vijiji na vitongoji katika masuala yanayohusiana na mabadiliko ya tabia nchi na kukabiliana nayo na kupunguza athari katika Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Kijiji (VADP) ambayo hutumika kutengeneza DADPs
Mchakato wa sasa wa kutayarisha DADPs unazingatia idadi ndogo ya sera zinazohusiana na kilimo. Ushauri unaotolewa hapa ni kwamba mipango hiyo hiyo ipanuliwe ili kujumuisha sera na programu mtambuka kama vipengele muhimu katika kutayarisha mipango inayogusa Kilimo Kinachozingatia Mabadiliko ya Tabia Nchi, kama vile Sera ya Mazingira, Sera ya Maji, Misitu, Sera ya Ardhi na sheria zinazohusika ambazo hazizungumziwi vya kutosha katika mipango ya DADPs.
Viongozi wa kuchaguliwa waone kwamba, uwakilishi makini wa wakulima wadogo katika majukwaa ya wadau wa wilaya unakuwepo [rejea sehemu 2.1 ya mwongozo wa maendeleo ya DADPs– 2011]. Mwongozo hautamki idadi wala vigezo vya kuwapata wawakilishi wa wakulima, ukizingatia ukubwa wa vijiji, kata katika kila moja ya wilaya zinazolengwa.
Baadhi ya fursa ambazo viongozi wa kuchaguliwa wanaweza kutumia katika kunadi na kuunga mkono ajenda yao ya Kilimo Kinachozingatia Mabadiliko ya Tabia Nchi inaweza kujumuisha yafuatayo:
Asili ya ugatuzi wa shughuli za programu ambayo inaweza kuwezesha au kuruhusu jamii kujumuisha masuala ya Kilimo Kinachozingatia Mabadiliko ya Tabia Nchi na Programu ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi katika jamii (REDD+) kwenye shughuli zao za kipaumbele kama watakuwa na ufahamu huo.
Mikakati na programu za maendeleo zihimize ubia wa sekta binafsi ambao unaweza kutoa fursa kwa uwekezaji wa ubia na kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi hasa kwenye Programu ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi katika jamii (REDD+) iwapo jamii itakuwa imewezeshwa vyema.
17
Kujenga uwezo na kutaasisisha ambako kutatoa miundo katika ngazi ya kijiji kwa ajili kukuza uwekezaji katika Kilimo Kinachozingatia Mabadiliko ya Tabia Nchi na Programu ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi katika jamii (REDD+).
Kuna uwezekano wa kuongeza uzalishaji wa chakula, uhakika wa chakula na kipato cha kaya za wakulima wadogo iwapo watajumuishwa katika programu ya SAGCOT ya AGG. Hii itapunguza shinikizo la kupanua kilimo hivyo kuepuka ukataji wa misitu na uzalishaji wa hewa ukaa.
Fursa za faida na kipato kwa jamii kwa kuwekeza katika kilimo-hifadhi na hifadhi za maliasili.
Mapendekezo ya sera Sehemu hii inatoa baadhi ya mapendekezo ambayo viongozi wa kuchaguliwa wanaweza kuyatumia kutetea hoja zao, kwa madhumuni ya kuboresha mazingira ya sera ambazo zinajumuisha dhana na utendaji unaohusiana na Kilimo Kinachozingatia Mabadiliko ya Tabia Nchi. Baadhi ya mapendekezo haya ni pamoja na mambo yafuatayo [ijapokuwa yanaweza kuwa zaidi ya haya]:
Viongozi wa kuchaguliwa wanaweza kuwezesha mapitio na kurasimishwa kwa ubunifu unaohusiana na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kuwa sera ambazo zitafanya kazi kama kichocheo chenye nguvu kwa wakulima kushiriki. Hapa, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yana wajibu muhimu katika kujenga ufahamu na kuwapatia wakulima teknolojia stahiki.
Kama sehemu ya maamuzi ya sera mbalimbali, viongozi wa kuchaguliwa wanaweza kuhakikisha kwamba mipango ya DADPs [iliyounganishwa na sekta zinazohusiana], inatumika kuwezesha utayarishaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Kijiji (VLUPs) ambayo inaweka mipaka iliyo wazi katika maeneo ya makazi, ardhi ya mifugo, ardhi ya kilimo na ardhi ya akiba. Hii itapunguza na kudhibiti baadhi ya tabia mbaya ambazo si rafiki kwa hali ya hewa/ekolojia kwa mfano kuchoma moto vichaka, kilimo cha kuhamahama, kukata miti n.k. Hii pia itahimiza kuanzishwa na kuhifadhiwa kwa misitu ya kijiji na hivyo kusaidia miradi ya Mabadiliko ya Tabia Nchi (REDD).
Viongozi wa kuchaguliwa watekeleze au wanapaswa kutekeleza wajibu muhimu wa kusimamia sheria husika ambazo moja kwa moja au kwa njia nyingine zinahusiana na Kilimo Kinachozingatia Mabadiliko ya Tabia Nchi.
Baadhi ya mbinu za kujumuisha kukabiliana na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi katika sera, programu na mipango ya kisekta zinaweza kuwa na mambo yafuatayo:
Viongozi wa kuchaguliwa wanaweza kuchukua jukumu la kuratibu na kuhakikisha kwamba ni sharti kwa wizara, idara na wakala wa sekta za mabadiliko ya tabia nchi, wafadhili na wadau muhimu katika ngazi ya sekta kuchukua hatua za kuhakikisha kwamba kukabiliana na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi na vipaumbele vya mpango wa REDD+ vilivyoanzishwa katika ngazi ya taifa, zinarasimishwa katika sera, mikakati, programu na mipango husika ikiwemo mipango ya DADPs.
Kuongeza motisha na vichocheo miongoni mwa wadau wa mabadiliko ya tabia nchi kushirikishana na kuchangia uzoefu wao katika mchakato wa kutayarisha mipango ya DADPs. Hii inaweza kufanikishwa kupitia mambo yafuatayo:
18
Kutayarisha sera makini au mazingira ya uwezeshaji ambayo yanalenga katika kukuza utendaji katika mbinu zenye mafanikio za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika ngazi ya shamba, kuwezesha kushirikishana habari na uzoefu, na njia za kutekeleza utendaji wa kukabiliana na mabadiliko katika njia ambayo wakulima wanamudu. Sera, Sheria na Taratibu katika ngazi za taifa na wilaya zinahitaji kutambua ubunifu unaofanywa na wakulima vijijini na kuukuza.
Kuboresha matumizi ya mitandao ya mawasiliano na vyombo vya habari vinavyoibukia vyenye maslahi katika mabadiliko ya tabia nchi ili kuinua ufahamu na kuongeza madai ya ndani kwa shughuli za mabadiliko ya tabia nchi.
Mapendekezo kuhusu utendaji katika Kilimo Kinachozingatia Mabadiliko ya Tabia Nchi (C3S) Wakiwa wawakilishi na/au watetezi wa jamii wanazowakilisha, viongozi waliochaguliwa wanaweza kufanya kampeni, kushawishi na ikiwezekana kutumia nguvu zao za kisiasa kushawishi sio mbinu zote za kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi, bali zile ambazo wakulima wanamudu na zinazofaa kutumika katika maeneo husika. Baadhi ya mbinu hizo za kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi ambazo zinaweza kutumika na ambazo wakulima wadogo wanaweza kumudu kwa kuzingatia nguvu, uwezo na faida zilizoainishwa katika matriki hapo juu, zinaweza kujumuisha mambo yafuatayo [ijapokuwa yanaweza kuwa zaidi ya haya]:
i. Kanuni za usimamizi wa udongo na virutubisho: Kutengeneza mboji na matumizi yake: Kuboresha utunzaji na kuinua ubora wa mbolea ya
wanyama. Mbolea ya wanyama inatakiwa ihifadhiwe chini ya kivuli, ikingwe dhidi ya mwanga wa jua wa moja kwa moja na mvua ili kupunguza uzalishaji wa hewa ya Naitrojeni. Mbolea ihifadhiwe na kuiacha ioze na kupunguza joto kabla ya kutumika shambani ili kupata manufaa makubwa zaidi. Inapotumika shambani ifunikwe na udongo au ichanganywe na udongo ili kupunguza uzalishaji wa gesi ukaa na upotevu wa Naitrojeni.
Matumizi ya mbolea: Katika kilimo cha asili cha wakulima wadogo, hii inamaanisha matumizi
ya kinyesi cha wanyama kwa ajili ya kuboresha mboji na muundo na sifa za udongo – pointi muhimu hapa mi kwamba, ni mbinu ya asili ambayo wakulima wanaimudu na inayotumika sehemu nyingi
Kujumuisha mbolea ya kilimo hai na za kiwandani kwa ajili ya uzalishaji wa mazao, matumizi ya mbolea hizi katika wakati na kipimo kinachofaa kulingana na mahitaji ya zao husika ni muhimu. Mbolea zinazotokana na wanyama zinaweza kutumika kwa kuchanganywa na mbolea za kiwandani za fosfeti wakati wa kupanda na mbolea zenye Naitrojeni zinaweza kutumika kwa kiwango kidogo wakati wa kutifua ardhi.
ii. Kanuni za kusimamia mmomonyoko wa udongo na hifadhi ya maji Kutengeneza matuta: ni teknolojia ya Kilimo-Hifadhi kwa ajili ya kuhifadhi udongo na
maji ambayo hufanya kazi vizuri katika maeneo yenye mteremko mkali. Matuta hujengwa kwa kutengeneza visharoba vya mawe na udongo vyenye mifereji au pasipo mifereji ili kutengeneza maeneo ya ardhi yanayofanana na ngazi.
Mtaro kwenye kontua: ni njia nyingine ya kuvuna maji ya mvua shambani, ambapo mitaro na matuta hutengenezwa kukata mteremko (sambamba na kontua) mtaro ukiwa juu ya
19
mteremko na tuta likiwachini ya mteremko pakiwa na nafasi ya takribani mita 1.5. Mitaro hii inatumika kuzuia maji ya mvua na hutumika kuzuia maji yasitoke nje ya mitaro. Mitaro kwenye kontua inafaa katika kilimo mseto hasa nafaka na maharage.
Mfumo wa mashimo ya Ngoro/Matengo: Mashimo ya Ngoro/Matengo ni nija za wenyeji za kuhifadhi maji kwenye udongo ambayo huboresha rutuba ya udongo na mavuno ya mazao, mfumo huu hupatikana katika milima yenye miteremko mikali ya Wilaya ya Mbinga, Kusini Magharibi mwa Tanzania. Nyasi zilizofukiwa katika shimo la Ngoro, zinapooza huongeza rutuba ya udongo, shimo huvuna maji ya mvua na kupunguza mmomonyoko.
Mashimo ya Chololo. Chololo ni njia nyingine ya wenyeji kuvuna maji ya mvua shambani, iliyotayarishwa na kutumika katika wilaya ya Dodoma Vijijini, njia hii inajumuisha mashimo madogo yenye kipenyo cha sm. 22 na kina cha sm 30, yaliyochimbwa kufuata mstari wa nafasi ya sm 60 kati ya shimo na shimo na sm 90 kati ya mistari ya mashimo.
Kuweka matandazo: huu ni utaratibu muhimu kwa ajili ya kuboresha hali ya hewa ya udongo; kukuza maisha ya udongo, muundo na rutuba. Zaidi ya faida hizi, huhifadhi unyevu wa udongo; kupunguza kukua kwa magugu, kupunguza uharibifu kutokana na athari za mionzi ya jua na mvua [kudhibiti mmomonyoko] na kupunguza haja ya utifuaji wa ndani zaidi wa udongo.
Mikakati ya kudhibiti mmomonyoko: kupunguza mtiririko wa maji kwa kutumia vishoroba vya mabaki ya mimea, kuelekeza maji yanayotiririka kuelekea eneo la hifadhi, kuzuia maji yasipotee kwa kupanda nyasi sambamba na barabara za vijijini, njia za miguu na njia za uchungaji, kupunguza na kuzuia makorongo kwenye milima.
Kuvuna maji ya mvua na hifadhi ya maji katika maeneo ya hifadhi: hutoa maji kwa ajili ya umwagiliaji wakati wa kipindi kirefu cha ukame na kwa ajili ya uzalishaji wa mazao yenye thamani kubwa kama vile mboga.
Kupanda mazao kwenye vishoroba: huu ni utaratibu ambapo wakulima wanapaswa kupanda mazao yao kwenye miteremko. Mazao hupandwa katika mistari mwembamba kukata kontoua kwenye kilima. Vishoroba vya ardhi kati ya mistari huachwa bila ya kutifuliwa na nyasi za asili, hii hupunguza kasi ya mtiririko wa maji ya mvua kuelekea chini ya mteremko na huzuia yasiondoe udongo wa juu. Maji mengi zaidi hupenya kwenye udongo na kuleta unyevu kwa mazao.
iii. Kanuni za kudhibiti wadudu waharibifu na magonjwa Kilimo mseto: kilimo hiki huhusisha kupanda mazao mawili au zaidi kwa wakati mmoja
kwenye shamba hilo hilo. Kilimo hiki ni shadidi kwa vigezo vya muda na nafasi. Utafiti umeonyesha kwamba kilimo mseto kina athari chanya kwa kigezo cha kudhibiti kutokea kwa wadudu, magonjwa na magugu.
Kubadilisha mazao: Utaratibu wa kupanda mazao tofauti katika kipande hicho hicho cha ardhi katika utaratibu wa kurudiarudia mazao hayo. Ina maana utaratibu uliopangwa wa mazao mahususi yanayopandwa katika shamba hilo hilo. Kubadilisha mazao kunapendekezwa ili kupata uanuwai wa mazao, kupunguza matukio ya wadudu waharibifu na magonjwa ya zao mahususi
20
Anuwai ya mazao: Kilimo cha zao moja tu kuna hasara nyingi kama vile kuongeza matukio ya wadudu waharibifu na magonjwa, mfumo wa mizizi unaofanana hupelekea katika muundo dhaifu wa udongo na hatimaye uzalishaji wa chini. Ili kufanya uzalishaji wa mazao kuwa endelevu, kilimo cha mazao anuwai kinapendekezwa katika maeneo ya milimani.
iv. Matumizi ya mbegu bora zinazoweza kutumika katika kanda maalumu za kilimo kiekolojia [Mazao na aina zinazohimili hali ngumu]: Kuchagua mazao na aina za mazao ni jambo la msingi sana katika uzalishaji wowote wa mazao. Ukichukulia athari za mabadiliko ya tabia nchi, mazao yanayokomaa kwa muda mfupi/aina zinazokomaa mapema yana uwezekano mkubwa wa kuhimili mabadiliko ya tabia nchi na kupunguza hatari ya mazao kushindwa kukua kutokana na kukosa unyevu. Kwa ujumla, aina bora za mimea ambazo zinahimili magonjwa na wadudu waharibifu zinapaswa kupandwa katika maeneo haya.
v. Kuchagua, Kuhifadhi na Kuboresha rasilimali za Kijenetiki Bila ya kuhatarisha miradi na juhudi za watafiti, kuimarisha uwezo wa jamii kusimamia rasilimali
za kijenetiki [upatikanaji na kuhifadhi aina na mbegu za kienyeji, kutunza na kuhifadhi mbegu] ni muhimu kadri utendaji wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi unavyohusika. Iwapo wana sayansi, mawakala wa serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yatashirikiana na wakulima katika kujaribu kuboresha uchaguzi, uhifadhi na usambazaji wa rasilimali za kijenetiki, usimamizi wa vitu hivi unaweza kuleta manufaa na kuwa hai.
vi. Mifumo ya kilimo jumuishi Kilimo jumuishi cha mimea – mifugo – samaki Kilimo – misitu katika maeneo/misitu iliyohifadhiwa
Vii. Nishati mbadala: Kufunga mitambo/vitengo vya Biogas Kufunga vifaa vya nishati ya jua Matumizi ya majiko yanayookoa nishati [kutumia kuni kidogo kwa kila shughuli ya kupika].
Kwa Mawasiliano zaidi, wasiliana Na
Actionaid TanzaniaPlot No. 115,Ngorongoro streetMikocheni B AreaP.O.BOX 21496,Dar es salaam, TanzaniaEmail: [email protected]: www.actionaid.org/tanzania
21
22