2
Wasaidizi wa misa Jumapili 20/01/ 2019 01.15 asubuhi: BLESSED IRENE STEFANI 3.00 asubuhi: YOUTH 05.30 asubuhi: ST. FRANCIS DE SALES 11.30 Jioni: Wahusika Masomo: 1. Is: 62: 1 –5 ; Zab: 96 2. 1 Wak: 12: 411; Injili: Yn: 2: 111 Wasimamizi wa PPC 20/01/ 2019 Cynthia Tororey Carolyne Ouko Alfred Kandara Elizabeth Litswa SHRINE OF MARY HELP OF CHRISTIANS - UPPER HILL Mandhari: ....“Kweli mimi nawabatiza kwa maji; lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto”. ..” Mungu Baba wa mbinguni, tunasadiki na kukiri kuwa utabaki Mungu uliye daima mwaminifu na kweli, unayerudisha na kuponya watu wako. Tunapoad- himisha Jubilei ya miaka ishirini na tano, ya kutabarukiwa kanisa la hija la Maria msaada wa wakristo, ambalo ni zawadi yako, tunakushukuru na kuku- sifu wewe. Ewe Bwana Yesu Kristo, uliyepakwa mafuta na kuteuliwa na Baba kuleta habari njema kwa maskini, kuwahubiri wafungwa kufunguliwa kwao, vipofu wapate kuona, waliogandamizwa wawe huru, na kutangaza mwaka wa Bwana kwa watu wake, uturejeshe katika neema. Uje Roho Mtakatifu na ukae katika jumuiya yetu, katika mwaka huu wa Jubi- lei. Tunakuomba uunde ndani yetu familia kwa ajili yako, na kwa ajili ya utu- kufu wa jina lako. Katika neema, upole na upendo wako, tuopoe kutoka yote yawezayo kututenganisha na ibada ya kweli. Ewe Utatu Mtakatifu, kwa maombezi yaWatakatifuYohane Bosko, Maria Domenika Mazzarello, Dominic Savio na watakatifu wote, katika familia ya Wasalesiani, na Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili, na aliye mlinzi na msaada wetu, tunaweka nia yetu kwako (............) Kwa njia ya Kristo Bwana wetu….. Amina. Nakala ya Jumapili UBATIZO WA BWANA 13 January, 2019 Mwaka C Sala ya Mwaka wa Jubilee Unaombwa kuzima simu yako Chukua nakala moja kwa kila familia. Ubatizo wa watoto wachanga 1. Chukua na kujaza fomu ya Ubatizo kabla ya mtoto kuingizwa kwenye orodha ya wanaobatizwa. 2. Mafundisho kwa wazazi na wasimamizi wa watoto wachanga wa Ubatizo ni Jumatano tarehe 13 Februari, 2019, kwenye Ukumbi wa mkutano. Saa 11.30 jioni 3. Ritriti kwa watakaobatiziwa watoto itaku- wa Jumamosi tarehe 16, Februari, 2019, saa 3.30 asubuhi. 4. Ubatizo wa watoto utakuwa tarehe 23 Februari, 2019 MATANGAZO 1. Sikukuu ya St. John Bosco huadhimishwa tarehe 31 Januari kila mwaka. Mwaka huu, tutaadhimisha sikukuu tarehe 27 Januari. Hii ni maadhimisho ya siku yetu kama familia kama parokia. Misa itakuwa moja siku hiyo, saa nne asubuhi. 2. Usajili wa Mafundisho ya Ubatizo kwa watoto wa zaidi ya miaka mitano unaendelea katika ofisi ya Shrine. 3. Mafundisho ya Katekesi (Watu wazima na wato- to) na Sunday school yatarejea tarehe 13 Januari, 2019. 4. Shajara zenye masomo ya Biblia mwaka huu zinzuzwa kwenye Bookshop; Kiingereza Ksh, 700, Swahili, Ksh. 600 /-. 5. Toleo la Kipindi Krisimasi la Shrine Digest linazwa hapo nje ya kanisa na katika bookshop. Tafadhali jichukulie nakala. 6. Shajara maalum za Mwaka wa Silver Jubilee ya Kanisa lute za 2019 zinapatikana kwa Ksh 700/-. Jipatie shajara yako kutoka Bookshop. 7. Kwa Wanaume wote, Chama cha Kitume CMA Don Bosco, kinaanzisha Batalion ya 24 ya Man Enough Jumamosi 19 Januari, 2019 saa 1 asubuhi. Jisajili kwenye hema nje ya kanisa baada ya Misa. 8. “Mothers of Sons” msimu wa 5 iliaanza tarehe 12 Januari, 2019 kwenye Conference Hall 1:30 asubuhi hadi 3:30 asubuhi. Jisajili kwa kutuma ujumbe mfupi kwa 0721469260. 9. Wiki ya Maombi kwa Umoja wa Wakristo itaanza Jan 18 hadi 25. Kutakuwa na sala maalum kwa lengo hili katika kila Misa. Salesians of Don Bosco, Upper Hill Road, P.O. Box 62322 00200,City Square, Nrb.Tel: 2714622, Office No: 0722 331 662, E-mail: [email protected] [email protected] Parish Priest/Shrine Director: 0716 876 680 Website www.donboscochurch.org, Mpesa Pay bill: 331 662 Shrine of Mary Help of Christians Je, umejiandikisha katika Parokia yoyote? Jiandikishe kwenye Parokia mojawapo. Wale wa- takaojiandikisha kama wanaparokia, wataanza kupata huduma kama wanaparokia miezi 3 baada ya kupata kadi. MISA ZA JUMUIYA 12.30 jioni Yatatolewa baadaye

MATANGAZO SHRINE OF MARY HELP OF CHRISTIANS UPPER …donboscoshrine.org/donbosco/bulletins/UBATIZO_WA_BWANA_Mwaka_C.pdf · Tunakuomba uunde ndani yetu familia kwa ajili yako, na kwa

  • Upload
    others

  • View
    7

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MATANGAZO SHRINE OF MARY HELP OF CHRISTIANS UPPER …donboscoshrine.org/donbosco/bulletins/UBATIZO_WA_BWANA_Mwaka_C.pdf · Tunakuomba uunde ndani yetu familia kwa ajili yako, na kwa

Wasaidizi wa misa Jumapili 20/01/ 2019

01.15 asubuhi: BLESSED IRENE STEFANI

3.00 asubuhi: YOUTH

05.30 asubuhi: ST. FRANCIS DE SALES

11.30 Jioni: Wahusika

Masomo: 1. Is: 62: 1 –5 ; Zab: 96

2. 1 Wak: 12: 4—11; Injili: Yn: 2: 1—11

Wasimamizi wa PPC 20/01/ 2019

Cynthia Tororey

Carolyne Ouko

Alfred Kandara

Elizabeth Litswa

SHRINE OF MARY HELP OF CHRISTIANS - UPPER HILL

Mandhari: ....“Kweli mimi nawabatiza kwa

maji; lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho

Mtakatifu na kwa moto”. ..”

Mungu Baba wa mbinguni, tunasadiki na kukiri kuwa utabaki Mungu uliye

daima mwaminifu na kweli, unayerudisha na kuponya watu wako. Tunapoad-

himisha Jubilei ya miaka ishirini na tano, ya kutabarukiwa kanisa la hija la

Maria msaada wa wakristo, ambalo ni zawadi yako, tunakushukuru na kuku-

sifu wewe.

Ewe Bwana Yesu Kristo, uliyepakwa mafuta na kuteuliwa na Baba kuleta

habari njema kwa maskini, kuwahubiri wafungwa kufunguliwa kwao, vipofu

wapate kuona, waliogandamizwa wawe huru, na kutangaza mwaka wa Bwana

kwa watu wake, uturejeshe katika neema.

Uje Roho Mtakatifu na ukae katika jumuiya yetu, katika mwaka huu wa Jubi-

lei. Tunakuomba uunde ndani yetu familia kwa ajili yako, na kwa ajili ya utu-

kufu wa jina lako. Katika neema, upole na upendo wako, tuopoe kutoka yote

yawezayo kututenganisha na ibada ya kweli.

Ewe Utatu Mtakatifu, kwa maombezi yaWatakatifuYohane Bosko, Maria

Domenika Mazzarello, Dominic Savio na watakatifu wote, katika familia ya

Wasalesiani, na Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili, na aliye mlinzi na

msaada wetu, tunaweka nia yetu kwako (............) Kwa njia ya Kristo Bwana wetu…..

Amina.

Nakala ya Jumapili

UBATIZO WA BWANA

13 January, 2019

Mwaka C

Sala ya Mwaka wa Jubilee

Unaombwa kuzima simu yako

Chukua nakala moja kwa kila familia.

Ubatizo wa watoto wachanga

1. Chukua na kujaza fomu ya Ubatizo kabla ya mtoto kuingizwa kwenye orodha ya wanaobatizwa. 2. Mafundisho kwa wazazi na wasimamizi wa watoto wachanga wa Ubatizo ni Jumatano tarehe 13 Februari, 2019, kwenye Ukumbi wa mkutano. Saa 11.30 jioni 3. Ritriti kwa watakaobatiziwa watoto itaku-wa Jumamosi tarehe 16, Februari, 2019, saa 3.30 asubuhi. 4. Ubatizo wa watoto utakuwa tarehe 23 Februari, 2019

MATANGAZO

1. Sikukuu ya St. John Bosco huadhimishwa tarehe 31 Januari kila mwaka. Mwaka huu, tutaadhimisha sikukuu tarehe 27 Januari. Hii ni maadhimisho ya siku yetu kama familia kama parokia. Misa itakuwa moja siku hiyo, saa nne

asubuhi.

2. Usajili wa Mafundisho ya Ubatizo kwa watoto wa zaidi ya miaka mitano unaendelea katika ofisi ya

Shrine.

3. Mafundisho ya Katekesi (Watu wazima na wato-to) na Sunday school yatarejea tarehe 13 Januari,

2019.

4. Shajara zenye masomo ya Biblia mwaka huu zinzuzwa kwenye Bookshop; Kiingereza Ksh, 700,

Swahili, Ksh. 600 /-.

5. Toleo la Kipindi Krisimasi la Shrine Digest linazwa hapo nje ya kanisa na katika bookshop.

Tafadhali jichukulie nakala.

6. Shajara maalum za Mwaka wa Silver Jubilee ya Kanisa lute za 2019 zinapatikana kwa Ksh 700/-.

Jipatie shajara yako kutoka Bookshop.

7. Kwa Wanaume wote, Chama cha Kitume CMA Don Bosco, kinaanzisha Batalion ya 24 ya Man Enough Jumamosi 19 Januari, 2019 saa 1 asubuhi. Jisajili kwenye hema nje ya kanisa baada

ya Misa.

8. “Mothers of Sons” msimu wa 5 iliaanza tarehe 12 Januari, 2019 kwenye Conference Hall 1:30 asubuhi hadi 3:30 asubuhi. Jisajili kwa kutuma

ujumbe mfupi kwa 0721469260.

9. Wiki ya Maombi kwa Umoja wa Wakristo itaanza Jan 18 hadi 25. Kutakuwa na sala maalum kwa

lengo hili katika kila Misa.

Salesians of Don Bosco, Upper Hill Road, P.O. Box 62322

00200,City Square, Nrb.Tel: 2714622,

Office No: 0722 331 662, E-mail:

[email protected]

[email protected]

Parish Priest/Shrine Director: 0716 876 680

Website www.donboscochurch.org,

Mpesa Pay bill: 331 662

Shrine of Mary Help of Christians

Je, umejiandikisha katika Parokia yoyote?

Jiandikishe kwenye Parokia mojawapo. Wale wa-

takaojiandikisha kama wanaparokia, wataanza

kupata huduma kama wanaparokia miezi 3 baada

ya kupata kadi.

MISA ZA JUMUIYA 12.30 jioni

Yatatolewa baadaye

Page 2: MATANGAZO SHRINE OF MARY HELP OF CHRISTIANS UPPER …donboscoshrine.org/donbosco/bulletins/UBATIZO_WA_BWANA_Mwaka_C.pdf · Tunakuomba uunde ndani yetu familia kwa ajili yako, na kwa

SOMO LA KWANZA Isa. 40: 1-5, 9-11

Somo katika kitabu cha Nabii Isaya.

Watulizeni, wapeni tulizo watu wangu, asema

Mungu wenu. Semeni na moyo wa Yerusa-

lem, utangazieni ya kwamba; Huduma yake

ngumu imekwisha, dhambi yake imeondole-

wa, Maana kwa mkono wa BWANA amepokea

adhabu maradufu kwa maovu yake yote.

Mtu analia: Tengenezeni jangwani njia ya

BWANA! Nyosheni nyikani barabara kwa Mun-

gu wetu! Kila bonde lifukiwe, kila mlima na

kilima kishushwe, Njia zenye kupotoka

zinyoshwe, na njia zenye mashimo zisawa-

zishwe. Hapo utukufu wa BWANA utafunuliwa,

na watu wote watauona mara; maana kinywa

cha BWANA kimenena haya. Panda juu ya mli-

ma mrefu, uutangaziye Sioni habari njema!

Paza sauti kwa nguvu, uutangaziye Yerusal-

emu habari njema! Paza sauti, usiogope!

Sema kwa miji ya Yuda: Tazama, Mungu

wenu! Yupo hapa BWANA Mungu: anakuja

kwa uwezo, na mkono wake unatawala; Tuzo

la ushindi wake linamsindikiza, mateka yake

yanamtangulia. Kama mchungaji, ana-

chunga kundi lake; mkononi mwake anawa-

kusanya wanakondoo, Anawachukua kifuani

mwake, anawaongoza kondoo wenye kun-

yonyesha.

Neno la Bwana

SOMO LA PILI Tit. 2:11—14; 3:4—7

Somo katika waraka wa kwanza wa Paulo

kwa Tito.

Maana neema ya Mungu imetoka kwa ku-

waokoa watu wote. Nayo inatuongoza

kuzuia yasiyo ya Mungu, na kupinga tama za

kidunia, tupate kuishi duniani hapa kwa kiasi,

kwa haki na kwa uchaji wa Mungu tukingoja

heri tunayoitazamia na ufunuo wa utukufu wa

Maungu mkuu na wa Mwokozi wetu Yesu

Kristo. Yeye amejitoa mwenyewe kwa ajili

yetu, ili atukomboe katika uovu wote, na

ajitakasie watu walio mali yake ya pekee na

wenye bidii kutenda mema. Lakini wema wa

Mwokozi wetu Mungu na hisani yake kwa

Wanadamu zilipotokea, ametuokoa, lakini si

kwa sababu ya matendo maadilifu tuliyoten-

da sis, isipokuwa kwa Huruma yake akitu-

osha tupate kuzaliwa tena na kutengenezwa

upya na Roho Mtakatifu. Mungu

amemweneza huyo ndani yetu kwa wingi

kwa ajili ya Yesu Kristo, Mwaokozi wetu, tu-

pate kuthibitishwa kwa neema yake na hivyo

kufanywa warithi wa uzima wa milele tunao-

tumaini.

Neno la Bwana

Wimbo Wa Katikati

Zab. 104

K) Umsifu BWANA, ee roho yangu!

Ee BWANA, Mungu wangu u mkuu sana!

1. Ee Bwana Mungu wangu u mkuu sana,

Umejivika fahari na adhama; Umejivika

mwanga kama vazi; Umetandaza anga kama

hema. (K)

2. Umeweka nguzo za ghorofa zake juu ya

maji. Umefanya mawingu kuwa gari lako;

Umekwenda juu ya mbawa za upepo Ume-

fanya pepo kuwa wajumbe wako; Na ndimi za

moto, kuwa watumishi wako. (K)

3. Ee BWANA, jinsi gani zilivyo nyingi kazi

zako! Zote umezifanya kwa hekima; Dunia

imejaa viumbe vyako Bahari iko kule, kubwa

na pana sana, Ndimo mlimo viendavyo bila

idadi, Viumbe hai vidogo na vikubwa. (K)

4. Hao wote hukutazamia wewe, Uwape

chakula chao kwa wakati wake Wewe hu-

wapa, nao wanakiokota; Wewe unakunjua

mkono wako, nao wanashiba mema (K)

5. Ukiuficha uso wako, wanafadhaika,

kiondoa pumzi yao, wanakufa Na kuyarudia

mavumbi yao Ukiipeleka roho yako wanaumb-

wa, Na unafanya upya uso wa nchi. (K)

SHANGILIO

Aleluya, aleluya,

mbingu zilifunguka na sauti ya Bwana

ikasikilika, “Huyu ni Mwanangu, mpendwa

wangu, msikieni yeye.”

Aleluya.

INJILI Lk. 3: 15-16, 21-22

Somo katika Injili ilivyoandikwa na Luka.

Siku ile: watu walipokuwa wakingoja yataka-

yotokea, wote wakiwaza-waza mioyoni

mwao habari za Yohane, kama labda yeye

ndiye Kristo, Yohane alijibu akawaambia

wote, “Kweli mimi nawabatiza kwa maji;

lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi,

ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya

viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho

Mtakatifu na kwa moto”. Ikawa, watu wote

walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye

amebatizwa, naye anaomba, mbingu zili-

funuka; Roho Mtakatifu akashuka juu yake

kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti

ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu,

mpendwa wangu; nimependezwa nawe.

Injili ya Bwana