26
www.shepherdserve.org Unaruhusiwa kuchapa, kunakili, kugawa au kusambaza haya kwa njia yoyote ile, mradi tu usibadili chochote wala kukata chochote. Vile vile hairuhusiwi kuuza maelezo haya. © Haki zote zimehifadhiwa 2006 David Servant Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi David Servant Sura Ya Ishirini Na Tisa Unyakuo Wa Kanisa Na Nyakati Za Mwisho Yesu alipotembea hapa duniani katika mwili wa mwanadamu, aliwaambia wanafunzi Wake waziwzi kabisa kwamba angeondoka kisha angerudi kuwachukua sikumoja. Wakati wa kurudi, angekwenda nao mbinguni. Kitu hiki siku hizi kinatiwa “Unyakuo.” Kwa mfano: Usiku ule kabla hajasulubiwa, Yesu aliwaambia hivi mitume Wake waaminifu kumi na moja: Msifadhaike mioyoni mwenu. Mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi. Kama sivyo, ningaliwaambia, maana naenda kuwaandalia mahali. Basi, mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. (Yohana 14:1-3. Maneno mepesi kukazia). Kilicho wazi katika maneno ya Yesu ni uwezekano wa kurudi Kwake wakati wale mitume wakiwa bado hai. Ukweli ni kwamba, baada ya kusikia maneno ya Yesu, wangeweza kudhani tu kwamba atarudi kuwachukua wakiwa bado hai. Tena, Yesu aliwaonya wanafunzi Wake mara nyingi sana kwamba wawe tayari kwa ajili ya kurudi Kwake. Hapo tena, uwezekano wa Yeye kurudi wakiwa hai ulikuwepo (ona mfano katika Mathayo 24:42-44). Kurudi Kwa Yesu Upesi Katika Nyaraka Mitume walioandika zile barua za Agano Jipya walithibitisha imani yao kwamba Yesu angeweza kurudi wakati wa maisha ya wasomaji wa barua zao. Kwa mfano: Yakobo aliandika hivi: Kwa hiyo ndugu, vumilieni hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani. Huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho. Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia (Yakobo 5:7, 8. Maneno mepesi kukazia).

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi...wangeweza kudhani tu kwamba atarudi kuwachukua wakiwa bado hai. Tena, Yesu aliwaonya wanafunzi Wake mara nyingi sana kwamba wawe tayari kwa

  • Upload
    others

  • View
    20

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

www.shepherdserve.orgUnaruhusiwa kuchapa, kunakili, kugawa au kusambaza hayakwa njia yoyote ile, mradi tu usibadili chochote wala kukatachochote. Vile vile hairuhusiwi kuuza maelezo haya. © Hakizote zimehifadhiwa 2006 David Servant

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziDavid Servant

Sura Ya Ishirini Na TisaUnyakuo Wa Kanisa Na Nyakati Za Mwisho

Yesu alipotembea hapa duniani katika mwili wa mwanadamu, aliwaambia wanafunziWake waziwzi kabisa kwamba angeondoka kisha angerudi kuwachukua sikumoja.Wakati wa kurudi, angekwenda nao mbinguni. Kitu hiki siku hizi kinatiwa “Unyakuo.”Kwa mfano: Usiku ule kabla hajasulubiwa, Yesu aliwaambia hivi mitume Wakewaaminifu kumi na moja:

Msifadhaike mioyoni mwenu. Mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi. Kama sivyo,ningaliwaambia, maana naenda kuwaandalia mahali. Basi, mimi nikienda nakuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi,nanyi mwepo. (Yohana 14:1-3. Maneno mepesi kukazia).

Kilicho wazi katika maneno ya Yesu ni uwezekano wa kurudi Kwake wakati walemitume wakiwa bado hai. Ukweli ni kwamba, baada ya kusikia maneno ya Yesu,wangeweza kudhani tu kwamba atarudi kuwachukua wakiwa bado hai.

Tena, Yesu aliwaonya wanafunzi Wake mara nyingi sana kwamba wawe tayari kwaajili ya kurudi Kwake. Hapo tena, uwezekano wa Yeye kurudi wakiwa hai ulikuwepo(ona mfano katika Mathayo 24:42-44).

Kurudi Kwa Yesu Upesi Katika Nyaraka

Mitume walioandika zile barua za Agano Jipya walithibitisha imani yao kwambaYesu angeweza kurudi wakati wa maisha ya wasomaji wa barua zao. Kwa mfano:Yakobo aliandika hivi:

Kwa hiyo ndugu, vumilieni hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulimahungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani. Huvumilia kwa ajili yake hatayatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho. Nanyi vumilieni, mthibitishemioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia (Yakobo 5:7, 8.Maneno mepesi kukazia).

Yakobo asingekuwa na haja ya kuwashauri wasomaji wake kuvumilia kuhusu kituambacho kisingetokea maishani mwao. Yeye aliamini kwamba kuja kwa Bwana“kunakaribia.” Kimantiki, Yakobo aliandika barua yake wakati kanisa lilipokuwalinapitia mateso makali (ona Yakobo 1:2-4), wakati ambapo waamini wangetamani sanakurudi kwa Bwana wao.

Paulo vile vile aliamini kwamba Yesu angeweza kurudi wakati wa maisha yawenzake. Anaandika hivi:

Lakini ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msijemkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana ikiwa twaaminiya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katikaYesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twaambieni haya kwaneno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kujakwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwasababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko,na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katikaKristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwapamoja nao katika mawingu ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwapamoja na Bwana milele. Basi farijianeni kwa maneno hayo (1Wathes.4:13-18. Maneno mepesi kukazia).1

Kutokana na hayo tunajifunza pia kwamba wakati Yesu atakaporudi kutokambinguni, miili ya waamini waliokufa itafufuliwa, kisha, pamoja na waamini walio haiwakati wa kuja Kwake, “kunyakuliwa ili kumlaki Bwana hewani” (Unyakuo). Kwa kuwaPaulo naye alitaja kwamba Yesu angewaleta wale waliokufa “ndani Yake” kutokambinguni, tunachoweza kusema ni kwamba wakati wa Unyakuo, roho za waaminiwalioko mbinguni zitaunganishwa na miili yao iliyofufuliwa punde tu.

Petro naye aliamini kwamba kuja kwa Kristo kulikuwa karibu sana, alipoandika baruayake ya kwanza kabisa.

Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwautimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo. …Lakinimwisho wa mambo yote umekaribia, basi iweni na akili, mkeshe katika sala.… Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katikaufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe (1Petro 1:13; 4:7, 13.Maneno mepesi kukazia).2

Na Yohana naye, alipoandika barua zake kwa makanisa, aliamini kwamba mwishoulikuwa karibu, na kwamba wasomaji wa siku zake wangeona kurudi kwa Yesu.

1 Maandiko mengine yenye kuonyesha imani ya Paulo kwamba Yesu angeweza kurudi katika wakati wauhai wake ni Wafilipi 3:20; 1Wathes. 3:13; 5:23; 2Wathes. 2:1-5; 1Timo. 6:14, 15; Tito 2:11-13;Waebrania 9:28.2 Maandiko mengine yenye kuonyesha imani ya Petro kwamba Yesu angeweza kurudi wakati wa uhaiwake ni 2Petro 1:15-19; 3:3-15.

Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpingaKristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwasababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. … Na sasa watotowadogo, kaeni ndani yake, ili kusudi atakapofunuliwa, mwe na ujasiri, walamsiaibike mbele zake katika kuja kwake. … Wapenzi, sasa tu wana waMungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwaatakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyomtakatifu (1Yohana 2:18, 28; 3:2, 3. Maneno mepesi kukazia).

Kukawia Kwake

Tukitazama nyuma miaka elfu mbili, tunatambua kwamba Yesu hakurudi mapemakama mitume Wake walivyotazamia. Hata katika siku zao, kuna waliokuwa wameanzakuwa na mashaka kama Yesu angerudi, kutokana na muda ulivyokuwa umepita tanguaondoke. Kwa mfano: Maisha ya Petro hapa duniani yalipokaribia kumalizika (ona2Petro 1:13, 14), Yesu alikuwa hajarudi bado. Basi, Petro aliwaandikia waliokuwa namawazo ya mashaka hivi, katika barua yake ya mwisho:

Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika sikuza mwisho watakuja nadhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe, nakusema, ‘Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babuzetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wakuumbwa.’ Maana hufumba macho yao wasione neno hili yakuwazilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia imefanyizwa kutoka katikamaji, na ndani ya maji kwa neno la Mungu. Kwa hayo dunia ile ya wakatiule ioligharikishwa na maji, ikaangamia. Lakini mbingu za sasa na nchizimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku yahukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu. Lakiniwapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kamamiaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja. Bwana hakawii kuitimizaahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumiliakwenu, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikilie toba. Lakinisiku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatowekakwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, nanchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea” (2Petro 3:3-10).

Petro anathibitisha kwamba kukawia kurudi kwa Yesu ni kwa sababu ya upendo narehema na huruma Zake – anataka kutoa nafasi zaidi watu watubu. Lakini anasema piakwamba hakuna mashaka yoyote – Yesu atarudi. Na atakaporudi, atakuja akiwa naghadhabu kubwa.

Vile vile Maandiko yako wazi kabisa – kama tutakavyo-ona – kwamba kurudi kwaKristo kwa ghadhabu kutatanguliwa na miaka ya dhiki isiyo na kifani ya dunia nzima, nakumwagwa kwa hasira ya Mungu juu ya waovu. Sehemu kubwa ya Kitabu cha Ufunuoinasema kuhusu kipindi hicho kinachokuja. Kama tutakavyoona baadaye katika mafunzoyetu, Maandiko yanaonyesha kwamba itakuwepo miaka saba ya dhiki, hapo baadaye.

Hakuna shaka yoyote kwamba Unyakuo wa kanisa utafanyika wakati fulani katika hiyomiaka saba, au karibu na hiyo miaka saba.

Je, Unyakuo Ni Lini Hasa?

Swali ambalo mara nyingi linawagawa Wakristo ni wakati hasa wa Unyakuo. Kunawanaosema kwamba Unyakuo utatokea kabla ya ile miaka saba ya dhiki. Kwa maanahiyo, unaweza kutokea wakati wowote. Wengine wanasema utatokea katikati ya ilemiaka saba ya dhiki. Na wengine tena wanasema utatokea punde tu baada ya dhiki yamiaka saba kufika katikati. Na kuna wengine nao wanaosema kwamba Unyakuo utatokeawakati wa Yesu kurudi na ghadhabu nyingi, mwishoni mwa kipindi cha Dhiki.

Hilo si swala la kugawanyikia, na makundi yote manne yanapaswa kukumbukakwamba yote yanakubali kwamba Unyakuo utatokea wakati fulani katika kipindi hichocha baadaye cha dhiki ya miaka saba, au karibu nacho. Hilo ni dirisha dogo sana katikaupana wa miaka maelfu ya historia. Hivyo, badala ya kugawanyika kutokana nakutokubaliana kwetu, ni afadhali tufurahie makubaliano yetu! Tena, si kitu tunaamini ninimaana haitabadilisha kitakachotokea.

Baada ya kusema hayo, sina budi kusema kwamba, kwa miaka ishirini na mitano yakwanza katika maisha yangu ya Kikristo, niliamini kwamba Unyakuo utatokea kabla yaDhiki ile ya miaka saba. Niliamini hivyo kwa sababu ndivyo nilivyofundishwa, na piakwa sababu sikutaka kupitia mambo ninayosoma habari zake katika Kitabu cha Ufunuo!Ila, nilipoendelea kujifunza Maandiko, nilianza kupata mtazamo tofauti. Hebu kwapamoja tutazame Biblia inavyosema, na tuone tutafikia maamuzi gani. Hata kamasitafanikiwa kukushawishi ujiunge na upande wangu, hebu tuendelee kupendana!

Mafundisho Pale Mlima Wa Mizeituni

Hebu tuanze kwa kutazama sura ya 24 ya Injili ya Mathayo, sehemu ya Maandikoambayo ni ya msingi sana kwa habari ya matukio ya nyakati za mwisho na kurudi kwaYesu. Pamoja na sura ya 25, sehemu hiyo huitwa Mafundisho Pale Mlima Wa Mizeituni,kwa sababu sura hizo mbili ni taarifa ya mahubiri ambayo Yesu alitoa kwa baadhi yawanafunzi Wake wa karibu sana3 hapo mlimani. Tunaposoma mafundisho hayo,tutajifunza kuhusu matukio mengi ya nyakati za mwisho, nasi tutaona uwezekano wawanafunzi wa Yesu kufikiri muda wa Unyakuo ni upi, waliposikia mafundisho yenyewe.

Yesu akaenda zake, akatoka hekaluni. Wanafunzi wake wakamwendea ilikumwonyesha majengo ya hekalu. Naye akajibu akawaambia, ‘Hamyaonihaya yote? Amin nawaambieni, halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalohalitabomoshwa.’Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni,wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha wakisema, ‘Tuambie! Mambohayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wadunia?’ (Mathayo 24:1-3).

3 Katika Marko 13:3 wanatajwa wale wanne waliokuwepo: Petro, Yakobo, Yohana na Andrea. Mafundishoya pale Mlima wa Mizeituni yanapatikanapia katika Marko 13:1-37 na Luka 21:5-36. Utapata habari kamahizo katika Luka 17:22-37 pia.

Wanafunzi wa Yesu walitaka kujua habari za wakati ujao. Sana sana walitaka kujuamajengo ya hekalu yangebomolewa lini (kama Yesu alivyokuwa ametabiri) na isharagani ingeonyesha wakati wa kurudi Kwake na mwisho wa wakati.

Ukilitazama hivyo, tunajua kwamba majengo ya hekalu yalibomolewa kabisa mwakawa 70 B.K. na jemadari Tito, akiongoza majeshi ya Kirumi. Pia tunajua kwamba Yesubado hajarudi kujichukulia kanisa Lake, kwa hiyo, hayo matukio mawili hayafuatani,wala hayatokei wakati mmoja.

Yesu Ajibu Maswali Yao

Inaonekana kwamba Mathayo hakuandika jibu la Yesu ka swali la kwanza, kuhusukuharibiwa kwa majengo ya hekalu baadaye. Ila, Luka alifanya hivyo katika Injili yake(ona Luka 21:12-24). Katika Injili ya Mathayo, Yesu alianza moja kwa mojakuzungumza kuhusu ishara ambazo zingetangulia kurudi Kwake mwisho wa wakati.

Yesu akajibu akawaambia, ‘Angalieni mtu asiwadanganye [ninyi]. Kwasababu wengi watakuja kwa jina langu wakisema, Mimi ni Kristo; naowatadanganya wengi. Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita;angalieni [ninyi] msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ulemwisho bado. Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifal na ufalmekupigana na ufalme; kutakuwa na njaa na matetemeko ya nchi mahalimahali. Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu.’ (Mathayo 24:4-8. Manenomepesi kukazia).

Kutokana na jinsi mahubiri hayo yalivyoanza, ni dhahiri kwamba Yesu aliaminikwamba hao wanafunzi Wake wa karne ya kwanza wangekuwa hai wakati ishara hizozinazotangulia kurudi Kwake zinapotendeka. Ona anasema nao moja kwa moja,kibinafsi. Katika sura hii ya 24, Yesu anasema na wanafunzi Wkae moja kw amoja zaidiya mara ishirini. Basi, wasikilizaji Wake wote wangeamini kwamba wataishi na kuonahayo yote ambayo Yesu ametabiri.

Lakini ni kweli kwamba wanafunzi wote waliomsikiliza Yesu siku hiyo wamekufasiku nyingi sana. Ila, tusidhani kwamba Yesu alikuwa anawadanganya. Yeye Mwenyewehakujua wakati atakaporudi (ona Mathayo 24:36). Kweli ilikuwa inawezekana kwa walewaliosikiliza mafundisho Yake pale Mlima wa Mizeituni kuwa hai wakati wa kurudiKwake.

Kilichokuwa cha msingi kabisa kwa Yesu ni kwamba wanafunzi Wakewasidanganywe na makristo wa uongo, kama itakavyokuwa katika siku za mwisho.Tunajua kwamba Mpinga Kristo mwenyewe atakuwa kristo wa uongo, na atadanganyadunia kwa sehemu kubwa. Watuw atamhesabu kuwa mwokozi mzuri sana.

Yesu alisema zitakuwepo vita, njaa na matetemeko, lakini pia alionyesha kwambahayo matukio si ishara za kurudi Kwake bali ni “mwanzo wa utungu” tu. Ni salamakusema kwamba matukio hayo yamekuwepo kwa miaka zaidi ya elfu mbili iliyopita. Ila,anachosema Yesu baada ya hapo ni kitu ambacho hakijatokea.

Dhiki Inaaza Katika Dunia Nzima

Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwawatu wa kuchukuwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu. Ndipo wengiwatakapojikwaa, nao watasalitiana na kuchukiana. Na manabii wengi wauongo watatokea, na kudanganya wengi. Na kwa sababu ya kuongezekamaasi, upendo wa wengi utapoa. Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho,ndiye atakayeokoka. Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katikaulimwengu wote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwishoutakapokuja (Mathayo 24:9-14. Maneno mepesi kukazia).

Hapa tena – kama ungewauliza wale waliomsikiliza Yesu siku hiyo swali hili: “Je,mnatazamia kuwa hai ili kuona kutimia kwa mambo hayo?” bila shaka wangejibu ndiyokwa uhakika sana, maana Yesu alisema nao moja kwa moja.

Kama tulivyosoma – mara tu baada ya “utungu” kuna tukio ambalo kweli halijatokea,la wakati wa Wakristo duniani kote kuteswa. Tutachukiwa na “mataifa yote”. Yesualikuwa anazungumza juu ya wakati fulani ambapo hayo yangetokea – si kipindi chajumla cha miaka mia nyingi, maana alisema hivi baada ya hayo, “Ndipo wengiwatakapojikwaa,nao watasalitiana na kuchukiana.”

Bila shaka anachosema hapo kinahusu kurudi nyuma kwa waamini Wakristo ambaobaada ya hapo watawachukia waamini wengine, maana wasioamini hawawezi“kuanguka,” tena, wanachukiana tayari. Basi, mateso ya dunia nzima yatakapoanza,kutakuwa na kurudi nyuma kwa watu wengi wanaodai kwamba ni wafuasi wa Kristo.Kama ni wakweli au ni waamini bandia – yaani kondoo au mbuzi – wengi sanawataanguka, nao watafichua majina ya waamini wengine kwa watesaji, wakiwachukiawale waliodai kuwapenda. Matokeo ni kwamba kanisa duniani kote litasafishwa.

Halafu tena kutakuwa na ongezeko la manabii wa uongo, na mmoja anatajwa sanakatika kitabu cha Ufunuo kuwa mwenzake mpinga Kristo (ona Ufunuo 13:11-18; 19:20;20:10). Maasi yataongezeka na kufikia mahali pa kumaliza kabisa upendo kidogoutakaokuwa umesalia mioyoni mwa watu, na wenye dhambi watakuwa wabaya kukithiri.

Wafia Dini Na Watakaosalia

Ingawa Yesu alitabiri kwamba waamini watapoteza maisha yao (ktk 24:9), si wote,maana aliahidi kwamba wale watakaovumilia mpaka mwisho wataokolewa (ona 24:13).Yaani, kama hawataruhusu wadanganywe na wale makristo wa uongo au manabii wauongo, na kama watashinda jaribu la kuacha imani yao na kuanguka, wao wataokolewana Kristo wakati anaporudi ili kuwakusanya mawinguni. Huu wakati wa dhiki baadayepamoja na ukombozi wake ulifunuliwa kidogo kwa nabii Danieli pia. Yeye aliambiwahivi

Na kutakuwa wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanzakuwapo taifa hata wakati uo huo; na watu wako wataokolewa; kila mmojaatakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. Tena, wengi wa haowalalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wamilele, wengine aibu na kudharauliwa milele (Danieli 12:1, 2).

Wokovu bado utatolewa kwa neema hata katika siku hizo, maana Yesu aliahidikwamba Injili itahubiriwa kwa mataifa yote, kutoa nafasi moja ya mwisho ya kutubu,ndipo mwisho utakapokuja.4 Tunasoma kitu katika Kitabu cha Ufunuo ambachokinaweza kuwa kutimizwa kwa ahadi ya Yesu.

Kisha nikaona malaika mwingine akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injliya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila nalugha na jamaa. Akasema kwa sauti kuu, ‘Mcheni Mungu na kumtukuza,kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanyambingu na nchi na bahari na chemchemi za maji’. (Ufunuo 14:6, 7. Manenomepesi kukazia).

Kuna wanaodhani kwamba sababu ya malaika kuhubiri Injili wakati huo ni kwamba,kufikia hapo katika kipindi cha dhiki ya miaka saba, Unyakuo utakuwa umetokea nawaamini wote watakuwa wameondoka. Lakini, hayo ni mawazo tu.

Mpinga Kristo

Nabii Danieli alifunua kwamba mpingakristo atakuwa na nafasi katika hekalu laYerusalemu litakalojengwa upya, katikati ya ile miaka saba ya dhiki, na kujitangazakwamba ni Mungu (ona Danieli 9:27 – tutajifunza baadaye). Tukio hili ndilo Yesuanazungumzia alipoendelea kufundisha pale Mlima wa Mizeituni, kama ifuatavyo:

Basi, hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabiiDanieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu), ndipo waliokatika Uyahudi na wakimbilie milimani; naye aliye juu ya dari asishukekuvichukua vitu vilivyomo nyumbani mwake; wala aliye shambani asirudinyuma kuchukua nguo yake. Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao sikuhizo! Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku yasabato. Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokeanamna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapokamwe.5 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu yeyote;lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo (Mathayo 24:15-22).

Hayo ni maelezo yaliyo dhahiri zaidi kuhusu dhiki ambayo Yesu alizungumziamapema (ktk 24:9). Wakati mpingakristo atakapotangaza kwamba yeye ni Mungu kutokahekalu la Yerusalemu, mateso yasiyofikirika yatatokea dhidi ya wanaomwamini Yesu.Kwa kujitangaza kwamba yeye ni Mungu, mpingakristo atatazamia kilamtu kutambuauungu wake. Basi, wafuasi wote wa kweli wa Kristo watakuwa maadui wa taifa, watu wa

4 Mara nyingi ahadi hii huondolewa mahali pake. Watu husema mara kwa mara kwamba kabla Yesuhajarudi, imetupasa kukamilisha kazi ya kuufikia ulimwengu kwa Injili. Lakini, katika mantiki hii, ahadi hiiinazungumzia kutangazwa kwa mwisho wa Injili duniani kote kabla ya mwisho wa dunia.5 Kama Unyakuo wa kanisa unatokea wakati huo katika ile Dhiki ya miaka saba kama wenginewanavyosema, maagizo ya Yesu kamba waamini wakimbie kuokoa maisha yao yasingekuwa na maanakwa sababu si watanyakuliwa wote?

kusakwa na kuuawa. Ndiyo sababu Yesu aliwaambia waamini wa Uyahudi wakimbiliemilimani bila kukawia, wakiomba kwamba kutoroka kwao kusizuiwe na sababu yoyoteile.

Wazo langu ni kwamba ingekuwa vizuri kwa waamini wote duniani kukimbiliamaeneo yaliyofichika wakati huo, maana tukio hilo litatangazwa duniani kote kwa njia yatelevisheni. Maandiko yanatuambia kwamba dunia nzima itadanganywa na mpingakristona kudhani yeye ndiye Kristo wao, nao watampa mamlaka na heshima zote.Atakapojitangaza kwamba ni Mungu, watamwamini na kumwabudu. Atakaponenamakufuru dhidi ya Mungu wa kweli – Mungu wa Wakristo – atashawishi dunia yoteiliyodanganyika ili kuwachukia wale wanaokataa kumwabudu (ona Ufunuo 13:1-8).

Yesu aliahidi ukombozi kwa ajili ya watu Wake mwenyewe kwa “kukatisha” hizosiku za dhiki, vinginevyo, “asingeokoka mtu yeyote” (24:22). Huko “kukatizwa” sikuhizo Naye “kwa ajili ya wateule” bila shaka ni kitu kinachohusu Yeye kuwakomboawakati atakapoonekana na kuwakusanya mawinguni. Yesu hata hivyo hatuambii hapakwamba ukombozi huo utatokea muda gani baada ya mpingakristo kujitangazia uungu.

Vyovyote vile – tunarudia kusema hapa tena kwamba Yesu aliwaacha wasikilizajiWake siku hiyo wakiwa wanajua kwamba wangeishi na kumwona mpingakristoakitangaza uungu wake, na kupigana vita na Wakristo. Hili linapingana kabisa na wazo lawale wanaosemakwamba waamini watanyakuliwa kabla ya tukio hilo. Kamaungemwuliza Petro, Yakobo au hata Yohana kwamba Yesu angerudi kuwaokoa kabla yatamko la mpingakristo kwamba ni Mungu, wangekujibu, “Si hivyo”.

Vita Dhidi Ya Watakatifu

Katika sehemu zingine, Maandiko yanatabiri juu ya mateso ya mpingakristo kwawaamini. Kwa mfano: Yohana alifunuliwa, naye akaandika hivi katika kitabu chaUfunuo:

Naye [mpingakristo] akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, yamakufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, namaskani yake, nao wakaao mbinguni. Tena akapewa kufanya vita nawatakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa nalugha na taifa (Ufunuo 13:5-7. Maneno mepesi kukazia).

Ona hapo kwamba mpingakristo atapewa “uwezo wa kufanya kazi yake” kwa mieziarobaini na mbili, au, miaka mitatu na nusu kamili. Huu ndiyo wakati unaoitwa nusu yawakati wa kipindi cha Dhiki ya miaka saba. Ni sawa kabisa kufikiri kwamba ni ile mieziarobaini na mbili ya mwisho ya Dhiki, ndipo mpingakristo atakapopewa “uwezo wakufanya kazi yake,” kwa sababu mamlaka yake yataondolewa kabisa wakati Kristoatakaporudi kufanya vita naye na majeshi yake wakati wa kumalizika kwa Dhiki.

Ni dhahiri kwamba “uwezo wak ufanya kzi yake” kwa miezi arobaini na mbili maanayake ni mamlaka maalum, maana mpingakristo atapewa mamlaka kiasi fulani na Mungukatika wakati wake wa kumiliki. Haya “mamlaka maalum ya kufanya kazi” yanawezakuwa ni muda atakaopewa wa kuwashinda watakatifu, maana, tunasoma hivi katikakitabu cha Danieli:

Nikatazama, na pembe iyo hiyo [mpingakristo] ilifanya vita na watakatifu,ikawashinda; hata akaja huyo mzee wa siku [Mungu], nao watakatifu wakeAliye Juu wakapewa hukumu; na majira yakawadia watakatifu waumilikiufalme. … Naye [mpingakristo] atanena maneno kinyume chake Aliye Juu,naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye Juu; naye ataazimu kubadilimajira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakatimbili, na nusu wakati (Danieli 7:21, 22; 25. Maneno mepesi kukazia).

Danieli alitabiri kwamba watakatifu wangetiwa mikononi mwa mpingakristo kwa“wakati, nyakati, na nusu wakati.” Maneno hayo yaeleweke kwamba ni miaka mitatu nanusu, kama utafananisha na Ufunuo 12:6 na 14. Tunaambiwa katika Ufunuo 12:6kwamba mwanamke fulani ambaye ni mfano, atapewa mahali pa kujificha nyikani ili“atunzwe na kulishwa” huko kwa muda wa siku 1,260, ambazo ni sawa na miaka mitatuna nusu kwa mwaka wenye siku 360. Kisha, mistari nane baadaye, anatajwa tena, nawakati huo inasemekana atapewa mahali nyikani ili “atunzwe na kulishwa” kwa “wakati,nyakati, na nusu ya wakati.” Basi, “wakati, nyakati, na nusu ya wakati” ni sawa na zilesiku 1,260, au miaka mitatu na nusu.

Kumbe katika mantiki hii, neno “wakati” maana yake mwaka, na “nyakati” maanayake miaka miwili, na “nusu ya wakati” maana yake nusu mwaka. Lugha hii ya ajabuinayopatikana katika Ufunuo 12:14 bila shaka ina maana kama katika Danieli 7:21. Basi,sasa tunajua kamba watakatifu watatiwa mikononi mwa mpingakristo kwa miaka mitatuna nusu, ambao ndiyo muwa ule ule tunaoambiwa katika Ufunuo 13:5 kwambampingakristo atapewa “uwezo wa kufanya kazi yake.”

Mimi nadhani vipindi hivyo viwili vya miezi arobaini na mbili vinafanana. Kamavitaanza wakati wa mpingakristo kujitangaza kwamba ni Mungu katikati ya ile Dhiki yamiaka saba, basi ni kwamba watakatifu watatiwa mikononi mwake kwa miaka mitatu nanusu inayofuata, na Yesu atawakomboa atakapotokea mawinguni na kuwakusanyawaende Naye wakati huo, au karibu na mwisho wa hiyo Dhiki. Lakini, kama hiyo mieziarobaini na mbili inaanza wakati mwingine katika kipindi cha Dhiki ya miaka saba, basiinatubidi tukubali kwamba Unyakuo utatokea wakati fulani kabla ya mwisho wa Dhiki yamiaka saba.

Tatizo la hoja hiyo ya mwisho ni kwamba inabidi watakatifu watiwe mikononi mwampingakristo kabla ya kuingia hatarini na kuhitaji kukimbilia milimani wakatianapojitangaza kuwa Mungu. Hilo ni gumu.

Tatizo la hoja ile ya kwanza ni kwamba watakatifu watakuwepo duniani bado wakatiMungu atakapokuwa anamimina hukumu duniani, tunazosoma katika kitabu cha Ufunuo.Tutatazama ugumu huo baadaye. Tuendelee na Mafundisho ya Mlima wa Mizeituni.

Masiya Wa Uongo

Ndipo Yesu akafafanua zaidi kwa wanafunzi Wake umuhimu wa kutodanganywa nahabari kuhusu maKristo wa uongo.

Wakati huo mtu akiwaambia, ‘Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kulemsisadiki. Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo,

nao watatoa ishara kubwa na maajabu, wapate kuwapoteza, kama yamkini,hata walio wateule. Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. Basiwakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki. Kwamaana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi,hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa kuwapopote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai (Mathayo 24:23-28).

Ona tena hapa jinsi Yesu anavyosema na wanafunzi moja kwa moja. WasikilizajiWake pale Mlima wa Mizeituni wangetazamia kuishi mpaka waone kutokea kwamakristo wa uongo na manabii wa uongo ambao wangetenda miujiza mikubwa. Na bilashaka wangetazamia kumwona Yesu akirudi mawinguni kama umeme.

Hatari ya kurudi nyuma wakati huo itakuwa kubwa sana, maana mateso dhidi yawaamini yatakuwa makali mno na makristo wa uongo na manabii wa uongowatashawishi watu sana kutokana na miujiza yao. Hii ndiyo sababu Yesu anarudia tenana tena kuwaonya wanafunzi Wake kuhusu yatakayotokea muda mfupi tu kabla ya kurudiKwake. Hakutaka wao wapotoshwe kama itakavyokuwa kwa wengi. Waamini wa kwelina walio thabiti watamngoja Yesu arudi mawinguni kama umeme, ambapo walewasiokuwa wafuasi Wake kweli watavutwa kwa makristo hao wa uongo kama taiwanavyovutiwa na mzoga nyikani.

Ishara Mawinguni

Yesu akaendelea hivi:

Lakini mara baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoamwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbingunizitatikisika, ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni;ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwonaMwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu nautukufu mwingi. Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu yaparapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwishohuu wa mbingu mpaka mwisho huu (Mathayo 24:29-31).

Mifano au picha katika sehemu hii ya mafundisho ya Yesu pale Mlima wa Mizeitunibila shaka ingekuwa inafahamika na Wayahudi wa siku Zake, maana inatoka katika Isayana Yoeli, na inazungumzia hukumu ya mwisho ya Mungu, mwisho wa dunia. Maranyingi huitwa “siku ya Bwana”, wakati jua na mwzi vitatiwa giza (ona Isaya 13:10, 11;Yoeli 2:31). Ndipo wakazi wote wa dunia watakapomwona Yesu akirudi mawingunikatika utukufu Wake, nao wataomboleza. Kisha malaika wa Yesu “watawakusanyawateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu,”kuonyesha kwamba waamini watanyakuliwa na kukusanywa ili kumlaki Yesumawinguni, na hayo yote yatatokea baada ya mlio wa “baragumu”.

Hapa tena, kama ungemwuliza Petro, Yakobo au Yohana ikiwa Yesu angewarudiakabla au baada ya wakati wa mpingakristo na dhiki kuu, bila shaka wangesema, “Baada.”

Kurudi Kwake, Na Unyakuo

Hii sehemu ya Mafundisho ya pale Mlima wa Mizeituni inaeleweka sana, kulinganana tukio ambalo Paulo aliandika juu yake, ambalo bila shaka ni Unyakuo wa kanisa,ingawa waandishi wengi wa vitabu vya kufafanua Biblia wanasema linatokea kabla yakipindi cha Dhiki kuanza. Hebu tazama andiko lifuatalo, tulilotazama mwanzoni mwasura hii.

Lakini ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msijemkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwatwaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolalakatika yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni hayakwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kujakwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwasababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko,nasauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katikaKristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tuli hai, tuliosalia, tutanyakuliwapamoja nao katika mawingu ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwapamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo. Lakini ndugu,kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie. Maana ninyiwenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwiviajavyo usiku. Wakati wasemapo, Kuna amani n salama, ndipo uharibifuuwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, walahakika hawataokolewa (1Wathes. 4:13 – 5:3. Maneno mepesi kukazia).

Paulo aliandika juu ya Yesu kuja kutoka mbinguni kwa parapanda ya Mungu nakwamba waamini watanyakuliwa “mawinguni ili kumlaki Bwana hewani.” Ni sawakabisa na yale Yesu aliyokuwa akieleza katika Mathayo 24:30, 31 – yanayotokea baadaya kutokea kwa mpingakristo na dhiki.

Tena, Paulo alipoendelea kuandika kuhusu kurudi kwa Kristo, anataja kwambaingetokea lini – “majira na nyakati” – na kuwakumbusha wasomaji wake kwambawalikuwa wanafahamu vizuri sana kwmaba “siku ya Bwana ingekuja kama mwivianavyokuja usiku.” Paulo aliamini kwamba kurudi kwa Kristo na Unyakuo wa waaminioungetokea “siku ya Bwana,” siku ambapo hasira kali na maangamizi vingewapata walewaliokuwa wanatazamia “amani na salama.” Kristo anaporudi kulinyakua kanisa Lake,hasira Yake itashuka juu ya dunia.

Hili linakubaliana vizuri sana na kile ambacho Paulo aliandika katika barua kwaWathesalonike baadaye, kuhusu kurudi kwa Kristo na hasira Yake.

Kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi;na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa kufunuliwakwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wakekatika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu,nawao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu; watakaoadhibiwa kwa maagamiziya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake; yeyeatakapokuja ili kutukuzwa katika watakaifu wake, na kustaajabiwa katika

wote waliosadiki katika siku ile, (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwakwenu). (2Wathes. 1:6-10. Maneno mepesi kukazia)

Paulo alisema kwamba wakati ambao Yesu angerudi kuwapa nafuu Wathesalonikewaliokuwa wanateswa (ona 1Wathes. 1:4, 5), angetokea “pamoja na malaika wake katikamwali wa moto” ili kuwaadhibu wale waliokuwa wanawatesa wao, kutoa hukumu yahaki, inayostahili. Hii haifanani na kile kinachosemwa na wengi, kwamba Unyakuoutatokea kabla ya dhiki, na kanisa kunyakuliwa na Kristo kabla ya kile kipindi cha dhikicha miaka saba kuanza. Hii pia huitwa kuja kwa siri kwa Yesu ili kunyakua kanisa Lake.Hapana kabisa! Maelezo haya yanafanana na kile ambacho Yesu alieleza katika Mathayo24:30, 31 – kurudi Kwake karibu au mwishoni mwa kipindi cha dhiki kuu –anapowanyakua waaminio na kumimina hasira Yake juu ya wasoiamini.

Siku Ya Bwana

Baadaye, katika barua hiyo hiyo, Paulo aliandika hivi:

Basi ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu YesuKristo, na kukusanyika kwetu mbele zake, kwamba msifadhaishwe upesihata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, walakwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwanaimekwisha kuwapo (2Wathes. 2:1, 2).

Kwanza: Ona kwamba mada ya Paulo ni kurudi kwa Kristo na Unyakuo. Aliandikakuhusu “kukusanyika kwetu mbele zake,” akitumia maneno yale yale ambayo Yesualitumia katika Mathayo 24:31, alipozungumza juu ya malaika ambao “wangekusanya”wateule Wake “kutoka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho ule.”

Pili: Ona kwamba Paulo anayaita matukio hayo kuwa ni “siku ya Bwana,” sawa naalivyofanya katika 1Wathesalonike 4:13 hadi 5:2. Hilo liko wazi kabisa.

Kisha anaendelea hivi:

Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yoyote; maana haiji, usipokujakwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wauharibifu; yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwachoMungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu laMungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu (2Wathes.2:3, 4. Maneno mepesi kukazia).

Wakristo Wathesalonike walikuwa wanadanganywa kwa namna fulani kwamba sikuya bwana – ambayo kulingana na Paulo lazima ianze kwa Unyakuo na kurudi kwa Kristo– ilikuwa imekwisha fika. Akatamka wazi wazi kwamba haiji mpaka baada ya uleukengeufu (labda ndiyo kule kurudi nyuma ambako Yesu alizungumzia katika Mathayo24:10) na baada ya mpingakristo kujitangaza kwamba ni Mungu kutoka hekalu laYerusalemu. Basi, Paulo anawaambia waamini Wathesalonike wazi wazi kwamba

wasitazamie kurudi kwa Kristo – au Unyakuo – wala siku ya Bwana, mpaka baada yatamko la mpingakristo kwamba ni Mungu.6

Kisha, Paulo anaelezea kuhusu kurudi kwa Kristo na jinsi anavyomwangamiza kabisampingakristo.

Je, hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambienihayo? Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa,hata atakapoondolewa. Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambayeBwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwaufunuo wa kuwapo kwake; yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wakutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo; nakatika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababuhawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa (2Wathes. 2:5-10).

Paulo alitamka kwamba mpingakristo atakomeshwa “kwa ufunuo wa kuja Kwake”Kristo. Kama “ufunuo” Wake ni sawa na ule unaotajwa wakati wa Unyakuo – kiasi chamistari tisa nyuma (ktk 2:1), basi mpingakristo atauawa wakati huo huo ambapo Kanisalitakusanywa ili kumlaki Bwana hewani. Hii inalingana na taarifa itolewayo katikaUfunuo sura ya 19 na 20. Hapo tunasoma juu ya kurudi kwa Kristo (ona Ufunuo 19:11-16), kuangamizwa kwa mpingakristo na majeshi yake (ona 19:17-21), kufungwa kwaShetani (ona 20:1-3) na “ufufuo wa kwanza” (ona 20:4-6), ambapo waamini waliouawakatika kipindi cha Dhiki yamiaka saba watafufuliwa. Kama huu ndiyo ufufuo wa kwanzakweli kweli kwa maana ya jumla kwamba ni kwa ajili ya wenye haki, basi hakunamashaka kwamba Unyakuo na kurudi kwa Kristo katika hasira Yake kunatokea wakatihuo huo ambapo mpingakristo anaharibiwa, maana, Maandiko yanatuambia wazi kabisakwamba wote waliokufa katika Kristo watafufuliwa wakati wa Unyakuo (ona 1Wathes.4:15-17).7

Kuwa Tayari

Hebu turudi tena kwenye Mafundisho pale Mlima wa Mizeituni.

Basi kwa mtini jifunzeni mfano. Tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanuamajani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu. Nanyi kadhalika,myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni. Aminnawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia.8 Mbingu

6 Hii inapinga hoja kwamba maneno ya Yesu katika Mafundisho pale Mlima wa Mizeituni yanawahusuwaamini wa Kiyahudi tu ambao wataokolewa wakati wa Dhiki, maana wengine wote walio-okoka kabla yaDhiki watakuwa wamekwisha nyakuliwa. Paulo anawaambia waamini Wathesalonike – mataifa – kwambaUnyakuo wao na kurudi kwa Kristo visingetokea mpaka baada ya mpingakristo kujitangaza kwamba niMungu, kitu kinachotokea katikati ya Dhiki ya miaka saba.7 Kuna wanaosema kwamba huu ufufuo unaotajwa katika Ufunuo 20:4-6 ni sehemu ya pili ya ufufuo wakwanza, ufufuo uliotokea wakati wa kurudi mara ya kwanza kwa Kristo wakati wa Unyakuo. Nini sababuya tafsiri hiyo? Kama ufufuo wa Ufunuo 20:4-6 ni wa pili, mbona usiitwe “ufufuo wa pili”?8 Ingawa waliomsikia Yesu siku hiyo wanaweza kuwa walidhani kwamba kizazi chao ndicho kingeyaonahayo yote, tunajua sivyo. Basi, lazima tutafsiri maneno ya Yesu katika 24:34 kumaanisha kwamba mambo

na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe (Mathayo 24:32-35).

Yesu hakutaka wanafunzi Wake wanaswe bila kufahamu – na hilo ndilo jambo lamsingi katika Mafundisho ya pale Mlima wa Mizeituni. Wangejua kwamba “yukomalangoni” baada ya kuona “mambo hayo yote” – dhiki duniani kote, kurudi nyuma kwawatu, kutokea kwa manabii na makristo wa uongo, tangazo la mpingakristo kwamba niMungu, na kutiwa giza jua na mwezi pamoja na kuanguka kwa nyota, wakati karibu nakurudi Kwake.

Ila, baada tu ya kuwaambia kuhusu ishara zitakazotangulia kuja Kwake kwa miakamichache, au miezi au siku, aliwaambia sasa wakati hasa wa kurudi Kwake ungebakiakuwa siri.

Walakini kwa habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaikawalio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake (Mathayo 24:36).

Mara nyingi andiko hili linatajwa kinyume cha mantiki yake! Kwa kawaida linatajwaili kuunga mkono dhana kwamba hatuna habari Yesu atarudi lini, kwa sababu anawezakurudi wakati wowote na kunyakua kanisa. Lakini katika mantiki yake, Yesuhakumaanisha hicho. Alikuwa ndiyo kamaliza kuhakikisha kwamba wanafunzi Wakewangekuwa tayari kwa ajili ya kurudi Kwake kwa kuwaambia ishara nyingi ambazozingetokea muda mfupi tu kabla ya kurudi Kwake. Sasa anachowaambia ni kwamba, sikuhasa na saa havitafunuliwa kwao. Tena, Yesu hasemi juu ya kuja Kwake mara ya kwanzakabla ya kipindi cha Dhiki ya miaka saba kuanza, wakati ambapo kanisa lingenyakuliwa,bali kuhusu kurudi Kwake wakati wa mwisho au karibia mwisho wa Dhiki. Hilo halinamatatizo ukitazama mantiki vizuri.

Je, Kurudi Kwake Hakujulikani Kabisa?

Hoja ambayo mara nyingi hutumika dhidi ya Unyakuo kutokea karibu au wakati wamwisho wa Dhiki ni kwamba kurudi kwa namna hiyo kusingekuwa kitu kisichojulikanakama Yesu alivyodaiwa kusema, kwa sababu kurudi kwa namna hiyo kungetazamiwakwa matukio ya Dhiki. Lazima kuwe na Unyakuo kabla ya dhiki, la sivyo waaminiwasingehitaji kuwa tayari na kukaa macho kama Maandiko yasemavyo wanapaswakuwa, maana watajua ni miaka saba au zaidi kabla ya Yesu kurudi.

Ila, hoja hii inapingwa na ukweli kwamba lengo kuu la Mafundisho ya Yesu paleMlima wa Mizeituni lilikuwa ni kuhakikisha kwamba wanafunzi Wake wawe tayari kwaajili ya kurudi Kwake wakati au karibu na mwisho wa Dhiki, naye aliwafunulia isharanyingi tu ambazo zingetangulia kuja Kwake. Mbona Mafundisho ya Mlimani yamejaamashauri mengi sana kwamba watu wawe tayari na kuwa macho, ingawa Yesu alijuakwamba kurudi Kwake kuko mbele miaka mingi sana baada ya kusema maneno hayo?Bila shaka ni kwa sababu Yesu aliamini kwamba Wakristo wanahitaji kuwa tayari nakuwa macho hata ingawa kurudi Kwake bado kuko miaka mingi mbele. Mitume ambao

hayo yote yatafanyika katika kizazi kimoja, au pengine kwamba taifa la Wakristo (au Wayahudi basi)lisingepita mpaka mambo hayo yote yatimie.

katika barua zao waliwashauri waamini kuwa macho na kuwa tayari kwa ajili ya kurudikwa Yesu walikuwa wanamwiga Yesu Mwenyewe.

Tena, wale wanaoamini kwamba Unyakuo kabla ya dhiki ndiyo wenye kuhalalishamashauri yoyote ya kuwa tayari, wana tatizo lingine. Kulingana na mawazo yao, kurudikwa Yesu mara ya kwanza hutangulia dhiki kwa miaka saba. Kwa hiyo, kurudi kwa Yesumara ya kwanza kulingana na hoja zao hakuwezi kutokea wakati wowote – lazimaitakuwa ni miaka saba kabla ya Dhiki kuanza. Basi, hakuna haja ya kutazamia kwambaYesu atarudi mpaka matukio duniani yakamilike na kuwa tayari kuanza miaka saba yaDhiki. Matukio hayo yanaweza kutazamiwa na kuhakikishwa kabisa.

Wengi wenye kuamini Unyakuo kabla ya dhiki – kama ni wakweli – watasemakwamba wanajua Yesu hatarudi leo wala kesho kwa sababu ya hali ya kisiasa duniani.Bado yapo matukio yaliyotabiriwa ambayo hayana budi kutimizwa kabla ya ile miakasaba ya Dhiki kuanza. Kwa mfano: Kama tutakavyoona katika kitabu cha Danieli,mpingakristo atafanya agano na Israeli kwa miaka saba, na huo utakuwa ndiyo mwanzowa kipindi cha Dhiki. Hivyo basi, kama Unyakuo unatokea miaka saba kabla ya dhikikuanza, lazima utokee wakati mpingakristo atakapofanya agano lake la miaka saba naIsraeli. Basi, hakuna haja ya wale wanaoshikilia kwamba Unyakuo utafanyika kabla yaDhiki kutazamia Yesu atarudi kabla ya kuona kitu katika siasa kinachofanya hayoyawezekane.

Zaidi ya hayo – kwa wale wanaoamini kwamba Unyakuo utatokea kabla ya dhiki, nakuamini kwamba Yesu atarudi mwishoni mwa Dhiki pia, maana yake ni kwamba sikukamili ya kurudi kwa Yesu mara ya pili inaweza kujulikana kimahesabu. Mara tuUnyakuo utokeapo, mtu yeyote angeweza kukadiria na kujua kile ambacho Yesu alisemani Baba tu akijuacho. Unachofanya ni kuhesabu mbele miaka saba tu.

Tuseme tena hivi – Kutokana na yale ambayo Yesu alisema, Yeye hakutaka kurudiKwake kuwe kitu cha kuwashtua watu. Ukweli ni kwamba alitaka kurudi Kwakekutazamiwe, na hivyo akataja matukio kadhaa ya Dhiki. Yesu hakutaka wanafunzi Wakewakutwe hawako tayari, kama ambavyo dunia itakutwa. Basi anaendelea kusema hivikatika Mafundisho Yake pale Mlima wa Mizeituni:

Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kujakwake Mwana wa Adamu. Kwa kuwa kama vile siku zile ziliozkuwa kablaya gharika watu walivyokuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, hatasiku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hata Gharika ikaja,ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmojaaachwa. Wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmojaaachwa.9 Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwanawenu. Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamumwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa.Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saamsiyodhani Mwana wa Adamu yuaja (Mathayo 24:37-44).

9 Hakuna tofauti yoyote ikiwa mwenye kupatikana na hukumu katika mifano hii ni mwenye kutwaliwa aumwenye kubaki, kama ambavyo watu wengi hubishana. Hoja ni kwamba, kuna watakaokuwa tayari kwaajili ya kurudi kwa Kristo, na kuna ambao hawatakuwa tayari. Utayari wao utaamua umilele wao.

Hapa tena, kitu ambacho Yesu anajali ni kwamba wanafunzi Wake wawe tayari kwaajili ya kurudi Kwake. Hicho ndicho kilisababisha yote aliyosema kabla ya hapa na baadaya hapa, katika mafundisho Yake. Maonyo Yake mwengi kwamba wawe tayari nawakeshe si kwamba ni kwa kuwa kurudi Kwake kutakuwa kwa kushtukiza, bali ni isharaya jinsi ambavyo itakuwa vigumu kwa sababu ya upinzani wa wakati wenyewe,kuendelea kuwa macho na kuwa tayari. Basi, wale wanaotarajia Unyakuo kabla ya Dhiki,wakati wowote, wanaodhani kwamba wako tayari kuliko Wakristo wengine, wanawezawasiwe tayari kwa uhalisi kabisa, kwa kile kinachokuja. Kama hawatazamii dhiki yoyotena wajikute katikati ya mateso ya dunia nzima, wakati wa utawala wa mpingakristo,jaribu la kuanguka linaweza kuwazidi nguvu. Afadhali kuwa tayari kwa kilekinachofundishwa na Maandiko kwamba kitatokea.

Halafu tena – kama ungemwuliza Petro, Yakobo au Yohana kwamba walitazamiakumwona lini Yesu akirudi, wangekwambia kuhusu ishara hizo zote ambzo Yesualiwaambia zingetokea, kabla ya kurudi Kwake. Wasingetazamia kumwona kabla yakipindi cha dhiki, au kutokea kwa mpingakristo.

Mwivi Usiku

Ona kwamba hata mfano wa Yesu wa “mwivi usiku” uko katika mantiki ya Yeyekudhihirisha ishara nyingi ambazo zingewasaidia wanafunzi Wake wasinaswe ghafulakwa kurudi Kwake. Basi, mfano huo hauwezi kutumiwa kisahihi kuonyesha kwambahakuna mtu anayeweza kuwa na wazo lolote kuhusu Yesu anarudi lini.

Paulo na Petro walitumia mfano wa Yesu wa “mwivi usiku” walipokuwa wanaandikakuhusu “siku ya Bwana” (ona 1Wathes. 5:2-4; 2Petro 3:10). Waliamini huo mfanoulikuwa na maana kwa habari ya Yesu kurudi kwa ghadhabu wakati wa au mwisho waDhiki ya miaka saba. Ila, Paulo aliwaambia hivi wasomaji wake: “Bali ninyi, ndugu,hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi” (1Wathes. 5:4). Yeye alitafsiri kwausahihi mfano wa Yesu, akitambua kwamba wale walio macho na makini kuona zileishara, na wenye kumfuata Yesu kwa utiifu, hawakuwa gizani mpaka kuja kwa Kristokuwapate kwa ghafula. Kwa watu namna hiyo, Yesu asingekuja kama mwivi usiku. Niwale walio gizani tu ndiyo wangeshtushwa – na ndivyo Yesu alivyofundisha. (Ona vilevile matumizi ya Yesu ya maneno “mwivi usiku” katika Ufunuo 3:3 na 16:15. Hapoanatumia maneno hayo kusema juu ya kuja Kwake kwenye vita ya Har-magedoni.)

Kuanzia hapa na kuendelea katika Mafundisho Yake ya pale Mlima wa Mizeituni,Yesu alirudia kuwaonya wanafunzi Wake kuwa tayari kwa ajili ya kurudi Kwake. Hapohapo akawaambia pia jinsi ya kuwa tayari, aliposema mifano kuhusu mtumwa asiyekuwamwaminifu, kuhusu wanawali kumi, na kuhusu talanta, na baadaye akatabiri hukumu yakondoo na mbuzi (yote inafaa kusomwa). Katika hiyo mifano yote, aliwaonya kwambajehanamu ilikuwa inawasubiri wale wote wasiokuwa tayari kwa ajili ya kurudi Kwake(ona Mathayo 24:50, 51; 25:30, 41-46). Njia ya kuwa tayari ni kupatikana ukifanyamapenzi ya Mungu, wakati Yesu atakaporudi.10

10 Ni dhahiri kwamba uwezekano wa wanafunzi wa Yesu kutokuwa tayari wakati wa kurudi Kwakeulikuwepo, maana aliwaonya sana kuhusu hilo. Kama aliwaambia kwamba adhabu ni hukumu ya milelekwa kutokuwa tayari kwa sababu ya dhambi, basi ilikuwa inawezekana kwao kupoteza wokovu kwasababu ya dhambi. Hili linapaswa kutupa angalizo juu ya umuhimu wa utakatifu, na tutambue kwamba ni

Hoja Nyingine

Kuna wanaopinga Unyakuo unaotokea karibu na, au mwisho wa Dhiki kwa msingikwamba, kulingana na Biblia, wenye haki hawaadhibiwi pamoja na wasio haki. Ushahidini mifano ya watu kama Nuhu, Lutu na Waisraeli kule Misri.

Kweli, tunazo sababu nzuri tu za kuamini kwamba wenye haki hawatakutwa naghadhabu ya Mungu wakati wa dhiki ya miaka saba, maana hilo litakuwa kinyume naahadi nyingi na mifano mingi ya Biblia. (Ona mfano: 1Wathes. 1:9, 10; 5:8).

Lakini, Yesu alitabiri juu ya dhiki kuu ambayo ndani yake wenye haki watateseka.Mateso hayo hayatatoka mikononi mwa Mungu, bali mikononi mwa wasioamini.Wakristo hawaepushwi na mateso – wameahidiwa mateso. Katika kipindi cha Dhiki yamiaka saba, waamini wengi watapoteza maisha yao (ona Mathayo 24:9; Ufunuo 6:9-11;13:15; 16:5-6; 17:6; 18:24; 19:2). Wengi watakatwa vichwa (ona Ufunuo 20:4).

Basi, kama kila mwamini katika taifa fulani atauawa, hakutakuwa na chochote chakuzuia ghadhabu ya Mungu isimwangukie kila mmoja katika taifa hilo. Na kwa hakika –kama kuna waamini katika taifa, Mungu aweza kuwalinda kutokana na huku Zakezitakapokuwa zinawaangukia waovu. Wakati wa hukumu Zake kule Misri katika siku zaMusa, alithibitisha hilo. Mungu alizuia hata mbwa asibweke kinyume cha Mwisraeli,huku hukumu baada ya nyingine kushuka juu ya Wamisri jirani (ona Kutoka 11:7). Vivyohivyo tunasoma katika kitabu cha Ufunuo kuhusu nzige wenye kuuma watu,watakaoachiliwa ili kuwatesa waovu wa dunia kwa miezi mitano, lakini wanaambiwa nahawaruhusiwi kuwatesa Wayahudi mia na arobaini na nne elfu (144,000) watakaokuwawametiwa muhuru maalum kwenye vipaji vya nyuso zao (ona Ufunuo 9:1-11).

Unyakuo Katika Kitabu Cha Ufunuo

Hakuna popote katika Kitabu cha Ufunuo tunaposoma juu ya Unyakuo wa kanisa,wala hatusomi juu ya kutokea kwa Kristo kwingine, isipokuwa katika Ufunuo 19,anapokuja ili kumwua mpingakristo na majeshi yake katika vita ya Har-magedoni.Hakuna lolote linalosemwa kuhusu Unyakuo kutokea hata hapo. Ila, ufufuo wa wafia diniwa Dhiki unatajwa kutokea wakati huo (ona 20:4). Kwa kuwa Paulo aliandika kwambawafu katika Kristo watafufuliwa wakati wa kurudi kwa Kristo, ambapo pia kanisalitanyakuliwa, mstari huu pamoja na mingine tuliyokwisha tazama, hutuongoza kuaminikwamba Unyakuo hautatokea mpaka mwisho wa Dhiki ya miaka saba, kamainavyoonekana katika Ufunuo 19 na 20. Lakini, yapo mawazo mengine tofauti.

Kuna wanaopata Unyakuo katika Ufunuo sura ya 6 na 7. Katika Ufunuo 6:12 na 13,tunasoma juu ya jua kuwa “jeusi kama gunia la singa” na nyota kuanguka kutokambinguni – ishara mbili ambazo Yesu alisema zingetokea muda mfupi tu kabla yakuonekana Kwake na kuwakusanya wateule (ona Mathayo 24:29-31). Kisha baadayekatika sura ya 7, tunasoma juu ya kundi kubwa la watu wakiwa mbinguni, kutoka kilataifa, kabila na lugha, ambao “wametoka katika dhiki ile kuu” (7:14). Hawatajwi kwambani wafia dini kama wanavyotajwa wengine katika sura iliyotangulia (ona 6:9-11), na hilo

upuuzi kusema kwamba waamini hawawezi kupoteza wokovu wao, kama wengine wanavyosema nakufundisha.

linatufanya tuseme kwamba wamenyakuliwa, hawajauawa – ni waaminiowaliokombolewa kutoka katika dhiki ile kuu.

Ni sahihi kudhani kwamba Unyakuo utatokea wakati fulani mara tu baada ya matukiohayo ya mbinguni yanayotajwa katika Ufunuo 6:12 na 13, kwa sababu yanafanana nayale aliyosema Yesu katika Mathayo 24:29-31. Ila, hatuna ishara iliyo dhahiri kuhusuwakati wa kutokea hayo mambo yanayotajwa katika Ufunuo 6:12 na 13, katika kipindicha dhiki ya miaka saba. Kama matukio yanayotajwa katika Ufunuo 6:1-13 yanafuatana,na kama Unyakuo unatokea mara tu baada ya 6:13, hilo linatuongoza kuamini kwambaUnyakuo hautatokea mpaka baada ya kufunuliwa kwa mpingakristo (ona 6:1, 2), na vitaya dunia nzima (ona 6:3-4), njaa (ona 6:5, 6), kufa kwa robo ya watu wa duniani kwavita, njaa, magonjwa na wanyama wakali (ona Ufunuo 6:7-8), na wafia dini wengikupatikana (ona Ufunuo 6:9-11). Hakika matukio hayo yote yanayotajwa yanawezakutokea kabla ya kumalizika kipindi cha Dhiki cha miaka saba, lakini pia yanaweza kuwandiyo yatakayotokea katika kipindi chote cha miaka saba cha dhiki, na Unyakuo kuwamwisho kabisa.

Wazo la Unyakuo kutokea kabla ya mwisho wa miaka saba ya dhiki linaongezewauzito na kweli kwamba Kitabu cha Ufunuo kinaeleza juu ya makundi mawili ya hukumusaba, baada ya Ufunuo sura ya 8, kama ifuatavyo: “hukumu za baragumu” na “hukumuza vitasa”. Hizi za vitasa zinasemekana ndiyo mwisho wa ghadhabu ya Mungu (ona15:1). Lakini, kabla ya hukumu hizo za vitasa kuanza, Yohana anawaona “wale wenyekushinda, watokao kwa yule mnyama na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake,wamesimama kandokando ya hiyo bahari ya kioo” (15:2). Hawa watakatifu washindiyawezekana walinyakuliwa. Lakini tena, yawezekana walifia imani yao. Maandikohayaelezi. Tena, hatujui kama mambo ya 15:2 yana uhusiano wowote na maelezo yamambo yanayotajwa hapo.

Kweli nyingine inayopatikana katika Ufunuo, yenye kuweza kuongezea uzito kwenyewazo la Unyakuo kutokea kabla ya mwisho wa miaka saba, ni hili: Wakati wa “hukumuya baragumu” ya tano katika Ufunuo 9:1-12, tunaambiwa kwamba nzige wenye kuumawataruhusiwa kuwadhuru wale tu “wasiokuwa na muhuri ya Mungu kwenye vipaji vyanyuso zao” (9:4). Watu pekee tunaoambiwa watakuwa na muhuri ni Waisraeli mia naarobaini na nne elfu (144,000) tu (ona Ufunuo 7:3-8). Basi inaonekana kwamba waaminiwengine wote itabidi wanyakuliwe kabla ya baragumu hiyo ya tano ya hukumu;vinginevyo, hawataepuka nguvu za hao nzige waumao. Tena, kwa sababu nzige haowatawaumiza watu kwa miezi mitano (9:5, 10), inadhaniwa kwamba ni lazima Unyakuoutokee miezi mitano kabla ya kumalizika kwa miaka ile saba ya Dhiki.

Kuna jinsi ya kufafanua hoja hizo. Pengine kuna wengine waliotiwa muhuru ambaohawatajwi katika kitabu cha Ufunuo. Vyovyote vile, kama hili linathibitisha kwambaUnyakuo utatokea kabla ya hukumu yabaragumu ya tano, pia linaonyesha kwamba kunakundi moja la waamini ambao hawatanyakuliwa kabla ya kuachiwa kwa hao nzigewaumao – wale Waisraeli mia na arobaini na nne elfu (144,000) waliotiwa muhuri. Ila,watakuwa na alama ya kuwalinda wasipatikane na ghadhabu ya Mungu, itakayokuwainatolewa kwa njia ya nzige hao waumao.

Tuhitimishe. Cha kusema ni kwamba bila shaka Unyakuo utatokea karibu na mwishoau mwishoni kabisa mwa ile miaka saba ya Dhiki. Waamini wasihofu kuhusu ghadhabuya Mungu, lakini pia wawe tayari kwa ajili ya mateso makali na hata kufa kwa ajili yaimani yao.

Kipindi Cha Dhiki

Hebu tutazame kwa karibu zaidi kile ambacho Maandiko yanafundisha kuhusu ilemiaka saba ya Dhiki. Tunapataje saba kwamba ndiyo urefu wa Dhiki? Ni lazimatujifunze kitabu cha Danieli, ambacho kinatoa ufunuo mpana zaidi kuhusu nyakati zamwisho, pamoja na kitabu cha Ufunuo.

Katika sura ya tisa ya kitabu chake, tunagundua kwamba Danieli ni mtumwa hukoBabeli, na Wayahudi wenzake. Akiwa katika kujifunza kitabu cha Yeremia, Danielialigundua kwamba muda wa utumwa wa Wayahudi huko Babeli ungekuwa miaka sabini(ona Danieli 9:2; Yeremia 25:11, 12). Baada ya kutambua kwamba kipindi cha miaka ilesabini kinakaribia kumaliziika, alianza kuomba, akitubu dhambi za watu wake nakuomba rehema. Malaika Gabrieli alimtokea kama jibu la maombi yake, na kumfunuliawakati ujao wa taifa la Israeli, mpaka wakati wa Dhiki na kurudi kwa Kristo. Unabii uliokatika Danieli 9:24-27 ni wa kushangaza sana katika Maandiko. Unabii wenyewe nikama ifuatavyo, pamoja na maelezo zaidi katika mabano.

Muda wa majuma sabini [bila shaka ni majuma yanayowakilisha miakakama tutakavyoona – jumla ya miaka 490] umeamriwa juu ya watu wako[Israeli], na juu ya mji wako mtakatifu [Yerusalemu], ili kukomesha makosa[labda maana yake ni tendo kuu la dhambi kwa Israeli – kumsulubishaMasiya wao], na kuishiliza dhambi [pengine maana yake ni kazi yaukombozi ya Kristo pale msalabani], na kufanya upatanisho kwa ajili yauovu [maana yake ni ile kazi ya Kristo ya ukombozi pale msalabani], nakuleta haki ya milele [mwanzo wa utawala wa Yesu duniani], na kutiamuhuri maono na unabii [pengine kuonyesha mwisho wa kuandikwa kwaMaandiko Matakatifu, au kutimizwa kwa unabii wote unaohusiana nautawala wa Miaka elfu], na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu [penginekusimamishwa kwa hekalu la kipindi cha utawala wa Kristo miaka elfumoja hapa duniani]. Basi ujue na kufahamu ya kuwa tangu kuwekwa amriya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu [amri hii ilitolewa na MfalmeArtashasta mwaka wa 445 K.K.] hata zamani zake masihi aliye mkuu[Bwana Yesu Kristo]; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini namawili [yaani, jumla ya majuma 69 au miaka 483] utajengwa tena pamojana njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu [hii inahusukujengwa upya kwa Yerusalemu, uliokuwa umeharibiwa na WaBabeli]. Nabaada ya yale majuma sitini na mawili [yaani, miaka 483 baada ya amri yamwaka wa 445 K.K.], masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu[Yesu angesulubiwa mwaka wa 32B.K., tukihesabu mwaka kulingana nakalenda ya Kiyahudi yenye siku 360 kwa mwaka]; na watu [Warumi] wamkuu atakayekuja [mpingakristo] watauangamiza mji na patakatifu[maelezo kuhusu kuharibiwa kwa Yerusalemu mwaka wa 70 B.K. namajeshi ya Kirumi chini ya uongozi wa Tito]; na mwisho wake utakuwapamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwishakukusudiwa. Naye [huyo ‘mkuu atakayekuja’ – mpingakristo] atafanyaagano thabiti na watu wengi [Israeli] kwa muda wa juma moja [au miaka

saba – hiki ni kipindi cha Dhiki]; na kwa nusu ya juma hiyo [yaani, miakamitatu na nusu] ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimamachukizo la uharibifu [wakati mpingakristo atakapojisimamisha mwenyewekatika hekalu la Kiyahudi huko Yerusalemu na kujiita Mungu – ona2Wathes. 2:1-4]; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwaimemwagwa juu yake mwenye kuharibu [Yesu atakuja, na kumshindampingakristo] (Danieli 9:24-27. Maneno mepesi kukazia).

Miaka 490 Maalum

Baada ya amri ya mwaka wa 445 K.K. iliyotolewa na Mfalme Artashasta kwambaYerusalemu ujengwe tena, Mungu alitoa miaka 490 maalum sana katika historia yawakati ujao. Lakini hiyo miaka haikuwa yenye kufuatana – iligawanywa katika sehemumbili – moja yenye miaka 483 na nyingine yenye miaka saba. Wakati ile miaka 483 yakwanza ilipokamilika (mwaka ule Yesu aliposulubiwa), saa ilisimama. Danieliasingeweza kudhani kwamba saa ingesimama kwa muda unaozidi miaka elfu mbili!Wakati fulani huko baadaye, saa itaanza tena kutembea, na itatembea kwa miaka saba yamwisho. Hiyo miaka saba ya mwisho haiitwi tu “Dhiki”, bali pia inajulikana kama “jumala sabini la Danieli.”

Hiyo miaka saba imegawanywa katika vipindi viwili vya miaka mitatu na nusu.Kama tulivyojifunza katika unabii wa Danieli, itakapofikia katikati, mpingakristoatavunja agano lake na Israeli na “kukomesha sadaka na dhabihu.” Kisha, kamaalivyotuambia Paulo, ataketi katika hekalu la Yerusalemu na kujitangaza kuwa niMungu.11 Hilo ndilo “chukizo la uharibifu” alilotaja Yesu (ona Mathayo 24:15). Ndiyosababu waamini wa Uyahudi wanapaswa “kukimbilia milimani” (Mathayo 24:16), maanahuo ndiyo mwanzo wa dhiki mbaya zaidi iliyowahi kuowepo duniani (ona Mathayo24:21).

Yawezekana “kukimbia kwa Wayahudi” kulionekana na Yohana kwa jinsi ya mfanokatika maono yake, katika sura ya 12 ya kitabu cha Ufunuo. Kama ndivyo, waamini waKiyahudi watakuta mahali maalum pa usalama pameandaliwa kwa ajili yao huko nyikani,watakapo”tunzwa na kulishwa” kwa miaka mitatu na nusu, ambao ndiyo mudautakaokuwa umebaki wa kipindi cha Dhiki ya miaka saba (ona Ufunuo 12:6, 13-17).Yohana aliona Shtani akikasirishwa na kutoroka kwao, na vita iliyofuata aliyoifanya kwawale wengine “wazishikao amri za Mungu na ushuhuda wa Yesu” (Ufunuo 12:17).Ndiyo sababu ni vizuri waamini duniani kote wakimbilie usalama katika maeneoyaliyofichika, wakati mpingakristo atakapotangaza ‘uungu’ wake huko Yerusalemu.

Ufunuo Wa Mwisho Wa Danieli

Fungu lingine la maandiko lenye kuvutia kutoka Danieli ambalo hatujalitazama, ni ilemistari 13 ya mwisho ya kitabu chake cha kushangaza sana. Ni maneno yaliyotamkwa namalaika. Yanafuata sasa, pamoja na maelezo zaidi katika mabano.

11 Hii inatuonyesha kwamba lazima hekalu la Yerusalemu lijengwe tena maana kwa sasa hakuna hekalulolote huko Yerusalemu (mwaka 2005 kitabu hiki kinapoandaliwa).

Wakati huo Mikaeli [malaika] atasimama, jemadari mkuu asimamayeupande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfanowake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo [bilashaka hii ni ile dhiki ambayo Yesu alisema juu yake katika Mathayo 24:21];na wakati huo watu wako wataokolewa [pengine ndiyo kule kukimbia kwaWayahudi, au kuokolewa kwa waamini wakati wa Unyakuo]; kila mmojaatakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. Tena, wengi wa haowalalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wamilele, wengine aibu na kudharauliwa milele [huu ni ufufuo wa wenye hakina waovu]. Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; nahao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele.[Baada ya ufufuo wao, wenye hai watapokea miili mipya itakayong’aa kwautukufu wa Mungu.] Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya,ukakitie muhuri kitabu hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio hukona huko, na maarifa yataongezeka. [Maendeleo ya kushangaza sana katikausafirishaji na maarifa katika karne iliyopita yanaonekana kutimiza unabiihuu.]

Ndipo mimi, Danieli, nikatazama, na kumbe, wamesimama wengine wawili,mmoja ukingoni mwa mto upande huu, na mmoja ukingoni mwa mtoupande wa pili. Na mmoja akamwuliza yule mtu aliyevikwa nguo za kitani,aliyekuwa juu ya maji ya mto; ‘Je! Itakuwa muda wa miaka mingapi hatamwisho wa mambo haya ya ajabu?’ Nami nikamsikia yule mtu aliyevikwanguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji yam to, hapo alipoinua mkono wakewa kuume na mkono wake wa kushoto kueloekea mbinguni; akaapa kwayeye aliye hai milele na milele, ya kwamba itakuwa wakati, na nyakatimbili, na nusu wakati [sawa na miaka mitatu na nusu, kulingana na ufunuowenye kufumbua katika Ufunuo 12:6 na 12:14); tena watakapokuwawamekwisha kuvunja nguvu za hao watu watakatifu, ndipo mambo hayoyote yatakapotimizwa. [Sawa tu na jinsi Danieli 7:25 ilivyotueleza kwambawatakatifu watatiwa mikononi mwa mpingakristo kwa miaka mitatu nanusu. Inaonekana dhahiri kwamba ni ile miaka mitatu na nusu ya mwishokatika ile miaka saba ya Dhiki. Mwisho wa matukio hayo yote yaliyotajwana malaika utakuja wakati “nguvu za watakatifu” zitakapokwisha“kuvunjwa.”] Nami nikasikia, lakini sikuelewa; ndipo nikasema, ‘Ee Bwanawangu, mwisho wa mambo haya utakuwaje?’ Akasema, ‘Enenda zako,Danieli; maana maneno haya yamefungwa na kutiwa muhuri, hata wakatiwa mwisho. Wengi watajitakasa, na kujifanya weupe, na kusafika [kwa njiaya dhiki bila shaka]; bali wabaya watatenda mabaya; wala hataelewa mtumbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndiyo watakaoelewa. Natangu wakati ule ambapo sadaka ya kuteketezwa ya daima itaondolewa, nahilo chukizo la uharibifu litakaposimamishwa, itapata siku elfu na mia mbilina tisini. [Hizo siku zisitafsiriwe kumaanisha muda utakaopita katikati yahayo matukio mawili, kwa sababu yote yanatokea katikati ya ile miaka saba.Inatakiwa kueleweka hivi: tangu wakati wa matukio hayo mawili, siku1,290 zitapita mpaka kitu kingine kikubwa kitakapotokea mwishoni. Siku

1290 ni zaidi ya miaka mitatu na nusu kwa siku 30, kwa hesabu ya miakayenye siku 360. Muda huu hutajwa mara kwa mara katika maandiko yakinabii ya Danieli na Ufunuo. Sababu ya kuongezwa hizo siku thelathinihaitajwi na haijulikani. Tena, malaika akamwambia Danieli hivi:] Heriangojaye, na kuzifikilia siku hizo elfu na mia tatu na thelathini na tano.[Sasa tena tuna siku zingine arobaini na tano zisizojulikana ni za nini.]Lakini enenda zako hata utakapokuwa mwisho ule; maana wewe utastarehe,nawe utasimama [kufufuka kwa Danieli mwenyewe] katika kura yakomwisho wa siku hizo. (Danieli 12:1-13).

Ni dhahiri kwamba kitu kizuri sana kitatokea mwisho wa hizo siku 75 za ziada!Itabidi tusubiri ili tuone.

Kutokana na kusoma sura za mwisho za kitabu cha Ufunuo, tunajua kuna matukiomengi ambayo yatakuwepo mara tu baada ya Kristo kurudi – moja likiwa Karamu yaArusi ya Mwana Kondoo. Malaika alimwambia Yohana hivi juu ya jambo hilo, “Heriwalioalikwa kwenye karamu ya arusi ya Mwanakondoo” (Ufunuo 19:9). Pengine hiindiyo baraka hiyo hiyo inayotajwa na malaika aliyesema na Danieli. Kama ni hivyo,karamu hiyo ya utukufu mwingi itatokea kama miezi miwilina nusu hivi baada ya kurudikwa Yesu.

Labda zile siku sabini na tano zimejaa vitu vingine ambavyo tunajua vitatokea,kulingana na ilivyoandikwa katika sura za mwisho za kitabu cha Ufunuo, kama vilekutupwa kwa mpingakristo na nabii wa uongo katika ziwa la moto; kufungwa kwaShetani; na kuanzishwa kwa utawala wa ufalme wa Kristo duniani kote (ona Ufunuo19:20 hadi 20:4).

Kipindi Cha Miaka Elfu

Utawala wa Miaka Elfu ni jina linaloeleza wakati ambapo Yesu Mwenyeweatatawala dunia nzima kwa kipindi cha miaka elfu moja (ona Ufunuo 20:3, 5, 7). Hiiinatokea baada ya ile Dhiki ya miaka saba. Isaya aliona utawala wa Kristo juu ya dunia,miaka elfu tatu na zaidi iliyopita. Anaeleza hivi:

Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume; nauweza wa kifalme utakuwa begani mwake; naye ataitwa … Mfalme waamani. Maongeo ya enzi yake na amani hayatakuwa na mwisho kamwe,katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake, kuuthibitisha nakuutegemeza kwa hukumu na kwa haki, tangu sasa na hata milele (Isaya9:6, 7. Maneno mepesi kukazia).

Vivyo hivyo, malaika Gabrieli alimtangazia Mariamu kwamba Mtoto wakeangetawala ufalme usio na mwisho. Alimwambia hivi:

Malaika akamwambia, ‘Usiogope Mariamu, kwa maana umepata neemakwa Mungu. Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; najina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliyejuu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki

nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho’(Luka 1:30-33. Maneno mepesi kukazia).12

Wakati wa Miaka Elfu, Yesu binafsi atatawala kutoka Yerusalemu, pale MlimaSayuni, na mlima huo utainuliwa na kuwa mrefu kuliko sasa. Utaala Wake utakuwa wahaki kabisa kwa mataifa yote, na itakuwepo amani kamili na halisi duniani kote.

Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya BWANAutawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifayote watauendea makundi makundi. Na mataifa mengi watakwenda nakusema, ‘Njoni, twende juu mlimani kwa BWANA, nyumbani kwa Munguwa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapitoyake. Maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la BWANA katikaYerusalemu. Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemeawatu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikukiyao iwe miundu; taifa halitainua upana juu ya taifa lingine, walahawatajifunza vita tena kamwe (Isaya 2:2-4).

Hata Zekaria naye alitabiri hayo hayo, kama ifuatavyo:

BWANA wa majeshi asema hivi, ‘Mimi nina wivu kwa ajili ya Sayuni,wivu mkuu, nami nina wivu kwa ajili yake kwa ghadhabu kuu.’ BWANAasema hivi, ‘Mimi nimerudi Sayuni, nami nitakaa katikati ya Yerusalemu;na Yerusalemu utaitwa, Mji wa kweli; na Mlima wa BWANA wa majeshiutaitwa, Mlima Mtakatifu.’ … BWANA wa majeshi asema hivi, ‘Itatokeahalafu ya kwamba watakuja mataifa na wenyeji wa miji mingi; wenyeji wamji huu watauendea mji huu, wakisema, ‘Haya! Twendeni zetu kwa harakatuombe fadhili za BWANA, na kumtafuta BWANA wa majeshi; mimi naminitakwenda.’ Naam, watu wa kabila nyingi na mataifa hodari watakujaYerusalemu kumtafuta BWANA wa majeshi, na kuomba fadhili zaBWANA. BWANA wa majeshi asema hivi, ‘Siku hizo watu kumi, wa lughazote za mataifa, wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi;naama, wataushika wakisema, Tutakwenda pamoja nanyi, kwa maanatumesikia kwamba Mungu yu pamoja nanyi’. (Zekaria 8:2-3; 20-23).

Biblia inafundisha kwamba waamini watatawala pamoja na Kristo katika kipindihicho cha miaka elfu moja. Viwango vya majukumu na wajibu zao katika ufalme Wakevitategemeana na uaminifu wao kwa sasa (ona Danieli 7:27; Luka 19:12-27; 1Wakor.6:1-3; Ufunuo 2:26, 27; 5:9, 10 na 22:3-5).

12 Andiko hili linaonyesha jinsi ilivyo rahisi kukosea kuhusu matukio ya kinabii kwa kusoma isivyo.Mariamu angeweza kudhani kihalali kabisa kwamba Mtoto wake maalum sana angekalia kiti cha enzi chaDaudi baada ya miaka kadhaa. Gabrieli alimwambia angezaa mwana ambaye angetawala juu ya nyumba yaYakobo, kana kwamba kuzaliwa kwa Yesu na kutawala vingekuwa vitu vinavyofuatana. Mariamuasingeweza kudhani kwamba kuna zaidi ya miaka elfu mbili kati ya kuzaliwa na kutawala. Sisi piatunapaswa kuwa makini – tusije tukatafsiri unabii vibaya.

Tutakuwa katika miili yetu ya ufufuo, lakini watakuwepo watu wengine wakiishikatika miili yao ya kawaida tu duniani. Tena, inaonekana urefu wa maisha utarudishwa,na wanyama wakali watakoma kuwa hivyo.

Nami nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe watu wangu; sauti yakulia haitasikiwa ndani yake tena, wala sauti ya kuomboleza. Hatakuwapotena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maanamtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi mwenyeumri wa miaka mia atalaaniwa. … Mbwa-mwitu na mwana-kondoowatalisha pamoja, na simba atakula majani kama ng’ombe; na mavumbiyatakuwa chakula cha nyoka. Hawatadhuru wala kuharibu katika mlimawangu mtakatifu wote, asema BWANA (Isaya 65:19, 20, 25. Ona pia Isaya11:6-9).

Biblia imetaja sana habari za Miaka Elfu inayokuja – hasa katika Agano la Kale.Ukitaka kujifunza zaidi, soma Isaya 11:6-16; 25:1-12; 35:1-10; Yeremia 23:1-5; Yoeli2:30 hadi 3:21; Amosi 9:11-15; Mika 4:1-7; Sefania 3:14-20; Zekaria 14:9-21 na Ufunuo20:1-6.

Vile vile, Zaburi nyingi za kinabii zinahusiana na kipindi cha Miaka Elfu. Kwamfano: Soma fungu hili katika Zaburi ya 48.

Bwana ndiye aliye mkuu, na mwenye kusifiwa sana. Katika mji wa Munguwetu, katika mlima wake mtakatifu. Kuinuka kwake ni mzuri sana, ni furahaya dunia yote. Mlima Sayuni pande za kaskazini, Mji wa Mfalme mkuu.Mungu katika majumba yake amejijulisha kuwa ngome. Maana, tazama,wafalme walikusanyika; walipita wote pamoja. Waliona, marawakashangaa; wakafadhaika na kukimbia. Papo hapo tetemeko liliwashika,utungu kama wa mwanamke azaaye (Zaburi 48:1-6. Maneno mepesikukazia).

Wakati Yesu atakaposimamisha utawala Wake huko Yerusalemu wakati wa kuanzakwa kipindi cha Miaka Elfu Moja, inaonekana kwamba watawala wengi wa duniawatakaopona Dhiki watapata taarifa ya utawala wa Yesu na kusafiri kwenda huko ilikujionea wenyewe! Watakachokiona kitawashangaza.13

Ukitaka Zaburi zingine zenye kusimulia habari za utawala wa Kristo katika MiakaElfu, angalia Zaburi 2:1-12; 24:1-10; 47:1-9; 66:1-7; 68:15-17; 99:1-9 na 100:1-5.

Umilele

Mwisho wa kipindi cha Miaka Elfu ni mwanzo wa kitu kinachoita na wasomi waBiblia “umilele”, muda unaoanza kwa mbingu mpya na nchi mpya. Kisha, Yesuatamrudishia Baba kila kitu, kulingana na 1Wakorintho 15:24-28.

13 Kutokana na maandiko mengine, inaonekana kwamba kipindi cha Miaka Elfu kitaanza kwa wasioaminikujaza dunia, si waamini tu. (Ona Isaya 2:1-5; 60:1-5; Danieli 7:13, 14).

Hapo ndipo mwisho, [Yesu] atakapompa Mungu Baba ufalme wake;atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. Maana shartiamiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. Aduiwa mwisho atakayebatilishwa ni mauti. Kwa kuwa, ‘Alivitiisha vitu vyotechini ya miguu yake’ [Zaburi 8:6]. Lakini atakaposema, ‘Vyotevimetiishwa,’ ni dhahiri ya kuwa yeye [Baba] aliyemtiishia vitu vyotehayumo. Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake [Baba], ndipoMwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote,ili kwamba Mungu awe yote katika wote.

Shetani ambaye atakuwa amefungwa kwa kipindi chote hicho cha miaka elfu,atafunguliwa mwisho wake. Ndipo atawadanganya wale ambao ndani yao wanamwasiYesu, waliokuwa wanajifanya kumtii wakati wa kipindi hicho chote (ona Zaburi 66:3).

Mungu atamruhusu Shetani kuwadanganya ili kudhihirisha hali halisi yamiyo yao,waweze kuhukumiwa kihalali. Katika kudanganywa kwao, watajikusanya ilikuushambulia mji mtakatifu – Yerusalemu – lengo lao likiwa kuipindua serikali ya Yesu.Vita haitadumu sana kwa sababu moto utashuka kutoka mbinguni na kuteketeza majeshiyaliyouzunguka mji, na Shetani atatupwa milele katika ziwa la moto na kiberiti (onaUfunuo 20:7-10).

Kujikusanya huko kwa ajili ya vita kunatabiriwa katika Zaburi ya 2, kama ifuatavyo:

Mbona mataifa wanafanya ghasia, na makabila wanatafakari ubatili?Wafalme wa dunia wanajipanga, na wakuu wanafanya shauri pamoja, juu yaBWANA, na juu ya masihi wake [Kristo], ‘Na tuvipasue vifungo vyao, nakuzitupia mbali nasi kamba zao!’ Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwanaanawafanyia dhihaka. Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake, nakuwafadhaisha kwa ghadhabu yake. ‘Nami nimemweka mfalme wangu juuya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.’ [Yesu sasa anazungumza na kusemahivi:] ‘Nitaihubiri amri. BWANA aliniambia, Ndiwe mwanangu, mimi leonimekuzaa. Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, na miishoya dunia kuwa milki yako. Utawaponda kwa fimbo ya chuma, na kuwavunjakama chombo cha mfinyanzi.’ Na sasa, enyi wafalme, fanyeni akili, enyiwaamuzi wa dunia, mwadibiwe. Mtumikieni BWANA kwa kicho,shangilieni kwa kutetemeka. Shikeni yaliyo bora, asije akafanya hasirananyi mkapotea njiani, kwa kuwa hasira yake itawaka upesi. Heri wotewanaomkimbilia!

Hukumu Ya Mwisho

Kabla ya kuanza Umilele, hukumu moja itatolewa. Wasio haki wote wa nyakati zotewatafufuliwa kutoka wafu ili wasimame mbele ya kiti cha enzi cha Mungu nakuhukumiwa kulingana na matendo yao (ona Ufunuo 20:5; 11-15). Kila mtu ambaye kwasasa yuko Hades (kuzimu) atafikishwa hukumuni hapo. Hukumu hii inajulikana kama“Hukumu ya Kiti Kikubwa cha Enzi, Cheupe”. Kisha, atatupwa Jehanamu – katika ziwala moto. Hiyo inaitwa “mauti ya pili” (Ufunuo 20:14).

Umilele unaanza kwa kupita kwa mbingu na nchi za kwanza, na hivyo kutimiza ahadiya Yesu ya zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita: “Mbingu na nchi zitapita, bali manenoyangu hayatapita kamwe” (Mathayo 24:35).

Kisha, Mungu ataumba mbingu na nchi mpya, sawa na Petro alivyotabiri katika baruayake ya pili, hivi:

Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi. Katika siku hiyo mbinguzitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, nakufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea. Basi, kwakuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu watabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, mkitazamia hata ije sikuile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwazikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? Lakini, kama ilivyoahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaandani yake (2Petro 3:10-14. Ona pia Isaya 65:17, 18).

Hatimaye – Yerusalemu mpya utashuka kutoka mbinguni mpaka chini duniani (onaUfunuo 21:1, 2). Mawazo yetu hayawezi hata kuanza kuelewa utukufu wa mji huo,wenye eneo kubwa sana – karibu nusu ya bara la Afrika (ona Ufunuo 21:16), au maajabuya miaka hiyo isiyo na mwisho. Tutaishi katika jamii kamilifu milele, chini ya utawalawa Mungu, kwa utukufu wa Yesu Kristo!