31
www.shepherdserve.org Unaruhusiwa kuchapa, kunakili, kugawa au kusambaza haya kwa njia yoyote ile, mradi tu usibadili chochote wala kukata chochote. Vile vile hairuhusiwi kuuza maelezo haya. © Haki zote zimehifadhiwa 2006 David Servant Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi David Servant Sura Ya Thelathini Hekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 1 Mada ya vita ya kiroho imezidi kupendwa sana katika kanisa la siku hizi. Kwa bahati mbaya sana, mengi yanayofundishwa kuhusu jambo hili yanapingana na Maandiko. Matokeo ni kwamba duniani kote, watumishi wengi wanafundisha na kutenda aina ya vita ya kiroho ambayo Biblia haisemi. Kwa kweli – kuna vita ya kiroho kimaandiko, na hiyo ndiyo itakiwayo kufanywa. Katika sura hii na inayofuata, tutatazama baadhi ya mawazo ya makosa ambayo yamezoeleka sana kuhusu Shetani na vita ya kiroho. Sura hizi ni ufupisho wa kitabu kizima kuhusu jambo hili, kiitwacho Mawazo Ya Kisasa Juu Ya Vita Ya Kiroho. Hekaya Ya Kwanza: “Katika milele iliyopita, Mungu na Shetani walipigana vita kubwa. Siku hizi, bado kuna mapambano kati yao.” Hekaya hii inakwenda kinyume na kweli moja thabiti na ya msingi sana kuhusu Mungu, inayofunuliwa katika Maandiko – kwamba Yeye ana nguvu zote. Yesu alituambia kwamba yote yanawezekana kwa Mungu (ona Mathayo 19:26). Yeremia alithibitisha kwamba hakuna kilicho kigumu kwa Mungu (ona Yeremia 32:17). Hakuna mtu wala nguvu viwezavyo kumzuia kufanya mapenzi Yake (ona 2Nyakati 20:6; Ayubu 41:10; 42:2). Mungu anauliza hivi kupitia kwa Yeremia, “Ni nani aliye kama Mimi … awezaye kusimama kinyume changu?” (Yeremia 50:44). Jibu ni kwamba, hakuna, hata Shetani hawezi. Kama Mungu kweli ana nguvu zote kama inavyosemekana katika Maandiko yote hapo juu, basi kusema kwamba Mungu na Shetani walikuwa katika vita au wako katika vita ni kudai kwamba hana nguvu zote. Kama Mungu aliwahi kushindwa hata mara moja, au alishindwa kidogo tu na Shetani, au kama ilimbidi kukabiliana naye na kupambana hata kwa muda mfupi, basi Yeye hana nguvu zote kama anavyojitangaza. Maelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia kuelewa nguvu alizo nazo, ukimlinganisha na Mungu wetu.

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

  • Upload
    others

  • View
    42

  • Download
    3

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

www.shepherdserve.orgUnaruhusiwa kuchapa, kunakili, kugawa au kusambaza hayakwa njia yoyote ile, mradi tu usibadili chochote wala kukatachochote. Vile vile hairuhusiwi kuuza maelezo haya. © Hakizote zimehifadhiwa 2006 David Servant

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziDavid Servant

Sura Ya ThelathiniHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 1

Mada ya vita ya kiroho imezidi kupendwa sana katika kanisa la siku hizi. Kwa bahatimbaya sana, mengi yanayofundishwa kuhusu jambo hili yanapingana na Maandiko.Matokeo ni kwamba duniani kote, watumishi wengi wanafundisha na kutenda aina yavita ya kiroho ambayo Biblia haisemi. Kwa kweli – kuna vita ya kiroho kimaandiko, nahiyo ndiyo itakiwayo kufanywa.

Katika sura hii na inayofuata, tutatazama baadhi ya mawazo ya makosa ambayoyamezoeleka sana kuhusu Shetani na vita ya kiroho. Sura hizi ni ufupisho wa kitabukizima kuhusu jambo hili, kiitwacho Mawazo Ya Kisasa Juu Ya Vita Ya Kiroho.

Hekaya Ya Kwanza: “Katika milele iliyopita, Mungu na Shetani walipigana vitakubwa. Siku hizi, bado kuna mapambano kati yao.”

Hekaya hii inakwenda kinyume na kweli moja thabiti na ya msingi sana kuhusuMungu, inayofunuliwa katika Maandiko – kwamba Yeye ana nguvu zote.

Yesu alituambia kwamba yote yanawezekana kwa Mungu (ona Mathayo 19:26).Yeremia alithibitisha kwamba hakuna kilicho kigumu kwa Mungu (ona Yeremia 32:17).Hakuna mtu wala nguvu viwezavyo kumzuia kufanya mapenzi Yake (ona 2Nyakati 20:6;Ayubu 41:10; 42:2). Mungu anauliza hivi kupitia kwa Yeremia, “Ni nani aliye kamaMimi … awezaye kusimama kinyume changu?” (Yeremia 50:44). Jibu ni kwamba,hakuna, hata Shetani hawezi.

Kama Mungu kweli ana nguvu zote kama inavyosemekana katika Maandiko yote hapojuu, basi kusema kwamba Mungu na Shetani walikuwa katika vita au wako katika vita nikudai kwamba hana nguvu zote. Kama Mungu aliwahi kushindwa hata mara moja, aualishindwa kidogo tu na Shetani, au kama ilimbidi kukabiliana naye na kupambana hatakwa muda mfupi, basi Yeye hana nguvu zote kama anavyojitangaza.

Maelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani

Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbingunikitakachotusaidia kuelewa nguvu alizo nazo, ukimlinganisha na Mungu wetu.

Page 2: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha wakisema, ‘Bwana! Hata pepowanatutii kwa jina lako.’ Akawaambia, ‘Nilimwona Shetani akiangukakutoka mbinguni kama umeme’ (Luka 10:17, 18).

Wakati Mungu mwenye nguvu zote alipoagiza Shetani afukuzwe mbinguni, Shetanihakuwa na uwezo wowote wa kupinga. Yesu alichagua lugha ya mfano ili kueleza jinsiShetani alivyoanguka haraka – kama umeme. Yaani, alianguka kutoka huko juu harakasana. Sekunde moja alikuwa mbinguni, na iliyofuata – PWAA! – amekwisha ondoka!

Kama Mungu anaweza kumfukuza Shetani mwenyewe haraka hivyo na kirahisi hivyo,haipaswi kuwa kitu cha ajabu kwamba watumishi Wake aliowapa agizo wanawezakuwafukuza mapepo haraka sana na kwa urahisi sana. Shida ni kwamba, kama wanafunziwa kwanza wa Kristo, wengi katika Wakristo wanaheshimu sana nguvu ya Shetani nabado hawajatambua kwamba nguvu za Mungu ni kubwa sana, sana, sana. Mungu ndiyeMwumbaji – Shetani ni kiumbe tu. Shetani hamwezi Mungu.

Vita Ambayo Haikuwepo

Ingawa itasikika kama kitu cha ajabu masikioni kwetu, tunahitaji kuelewa kwambaMungu na Shetani hawako katika vita, wala hawajawahi kuwepo, na hawatakuwa katikavita. Ni kweli kwamba wana makusudi na malengo tofauti, na ni kweli kusema kwambvawanapingana. Lakini, watu wawili wanapopingana, na mmoja awe na nguvu zaidi sanakuliko mwingine, upinzani wao hauwezi kuitwa vita. Je, mdudu anaweza kupigana natembo? Shetani – sawa na mdudu – alifanya juhudi za kinyonge sana kumpinga Yulemwenye nguvu sana sana. Upinzani wake ulishughulikiwa haraka sana, naye alifukuzwakutoka mbinguni “kama umeme”. Hapakuwa na vita hapo – ni mtu alifukuzwa.

Kama Mungu ana nguvu zote, Shetani hana nafasi hata ndogo tu ya kumzuia Mungukufanya anachotaka. Na kama Mungu anamruhusu Shetani kufanya kitu, mwisho wakekitu hicho ni kwa ajili ya kutimiza mapenzi Yake kama Mungu. Kweli hii itawekwa wazizaidi tunapoendelea kuchunguza Maandiko kuhusu mada hii.

Kufungwa Kwa Shetani Katika Siku Zijazo

Mamlaka makuu ya Mungu juu ya Shetani hayakuonyeshwa katika umilele uliopita tu,bali pia yataonyeshwa katika siku za baadaye. Tunasoma katika Ufunuo kwamba malaikammoja tu atamshika Shetani na kumfunga kwa miaka elfu moja (ona Ufunuo 20:1-3).Tukio hilo la wakati ujao haliwezi kusemekana ni vita kati ya Mungu na Shetani. Ona piakwamba Shetani hatakuwa na nguvu za kutoka gerezani humo, bali atafunguliwa wakatiMungu atakapotaka, na itakapokuwa sawa katika mapenzi Yake (ona Ufunuo 20:7-9).

Vipi Kuhusu “Vita Mbinguni” Ya Siku Zijazo?

Kama ni kweli kwamba Mungu na Shetani hawako vitani, na hawajawahi kuwepo, nahawatakuwa wakati wowote, mbona katika kitabu cha Ufunuo tunasoma kuhusu vitambinguni hapo baadaye, ambayo Shetani anahusika (ona Ufunuo 12:7-9)? Hilo ni swalizuri, na ni rahisi kulijibu.

Page 3: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

Ona kwamba vita hii itakuwa kati ya Mikaeli na malaika zake, na Shetani na malaikazake. Mungu hatajwi kuhusika katika vita hii. Kama angehusika, isingeitwa vita kwasababu, Mungu, akiwa na nguvu zote, angeweza kufinya upinzani wa aina yoyote kwamuda mfupi sana tu, kama alivyothibitisha tayari.

Malaika – pamoja na Mikaeli – hawana nguvu zote, na ndiyo sababu vita yao naShetani na malaika zake inaitwa vita kwa sababu kutakuwepo na mapambano kwa mudafulani. Lakini – kwa kuwa wao wana nguvu zaidi, watamshinda Shetani na majeshi yake.

Mbona Mungu asijihusishe na vita hii, na badala yake anawaachia malaika zake? Jibusi rahisi. Bila shaka, Mungu, akijua kila kitu, alijua kwamba malaika Zake wangeshindavita hiyo, na pengine ndiyo maana aliona hakuna haja Yeye ajihusishe.

Bila shaka Mungu angewamaliza wale Wakanaani waovu upesi na kwa urahisi kabisakatika siku za Yoshua, lakini aliamua kuwapa Waisraeli kazi hio. Kitu ambacho Munguangefanya bila shida yoyote kwa nukta chache, aliamua kuwaachia wafanye kwa mudamrefu, tena kwa juhudi nyingi sana. Pengine hilo lilikuwa linampendeza Mungu zaidikwa sababu lilidai imani kwa Waisraeli. Pengine ndiyo sababu hatahusika katika ile vitaya wakati ujao huko mbinguni. Labda. Ila, Biblia haisemi.

Sasa – kwa kuwa itakuwepo vita mbinguni huko baadaye kati ya Mikaeli na malaikazake na Shetani na malaika zake, hiyo isiwe sababu ya kudhani kwamba Mungu hananguvu zote – sawa tu na jinsi ambavyo vita za Israeli huko Kanaani zisiwe sababu yakutufanya kufikiri kwamba Mungu hana nguvu zote.

Je, Shetani Hakushindwa Na Yesu Pale Msalabani?

Mwisho – kwa habari ya hii mada ya kwanza kwamba Mungu na Shetani wanapiganavita, tuhitimishe kwa kutazama usemi huu uliozoeleka sana: Yesu alimshinda Shetanipale msalabani. Maandiko hayasemi kwamba Yesu alimshinda Shetani msalabani.

Tunaposema kwamba Yesu alimshinda Shetani, ni kana kwamba Shetani na Yesuwalikuwa katika vita, na hilo linaonyesha kwamba Mungu hana nguvu zote, na kwambaShetani hayuko chini ya mamlaka ya Mungu tayari. Kuna njia za KiBiblia za kuelezamambo yaliyompata Shetani wakati Yesu alipotoa maisha Yake pale Kalvari. Kwamfano: Maandiko yanatuambia kwamba kwa njia ya kifo Chake, Yesu “alimdhoofishayeye aliyekuwa na nguvu za mauti” (ona Waebrania 2:14, 15).

Je, Yesu alimdhoofisha Shetani kwa kiwango gani? Ni wazi kwamba Shetani ananguvu, vinginevyo mtume Yohana asingeandika hivi: “Dunia yote iko katika nguvu zayule mwovu” (1Yohana 5:19. Maneno mepesi kukazia). Kulingana na Waebrania 2:14,15, Shetani alidhoofishwa kwa habari ya “nguvu za mauti”. Nini maana yake?

Maandiko yanataja aina tatu za mauti: mauti ya kiroho, mauti ya mwili, na mauti yapili.

Kama tulivyokwisha jifunza mapema, mauti ya pili (au, kifo cha milele) inatajwakatika Ufunuo 2:22; 20:6, 14; 21:8, nayo huelezwa kwamba ni wakati ambapo waaminiwatatupwa katika ziwa la moto.

Mauti ya mwili hutokea wakati roho ya mtu inapotoka katika mwili wake, na mwiliwake unaacha kufanya kazi.

Mauti ya kiroho hueleza hali ya roho ya mwanadamu ambaye hajazaliwa mara ya pilikwa njia ya Roho Mtakatifu. Mtu aliyekufa kiroho ana roho ambayo imetengwa na

Page 4: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

Mungu, roho yenye asili ya dhambi, roho ambayo, kwa kiwango fulani, imeungana naShetani. Katika Waefeso 2:1-3 kuna picha kwa ajili yetu, ya mtu aliyekufa kiroho.

Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazomliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwakumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katikawana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katikatamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawakwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.

Paulo aliandika kwamba Wakristo wa Efeso walikuwa wafu katika makosa na dhambizao. Hakuwa anasema juu ya mauti ya mwili kwa sababu alikuwa anawaandikia watuwalio hai. Basi, alikuwa anasema kwamba wamekufa, kwa jinsi ya kiroho.

Nini kilichowaua kiroho? Ni “makosa na dhambi zao”. Kumbuka Mungu alikuwaamemwambia Adamukwamba siku atakayoacha kutii, angekufa (ona Mwanzo 2:17).Mungu hakuwa anasema juu ya kifo cha kimwili bali cha kiroho, kwa sababu Adamuhakufa kimwili siku alipokula lile tunda alilokatazwa. Ila, alikufa kiroho siku hiyo, nahakufa kimwili mpaka miaka mia nyingi baadaye.

Paulo akaendelea kusema kwamba Waefeso hao, kama wafu kiroho, walikuwawakienenda kulingana na makosa hayo na dhambi hizo, wakifuata “mtindo wa dunia”(yaani, wakifanya yote yaliyokuwa yanafanywa na kila mtu) na kumfuata “mfalme wauwezo wa anga”.

Huyo “mfalme wa uwezo wa anga” ni nani? Ni Shetani, anayetawala ufalme wake wagiza kama amiri jeshi mkuu anayesimamia majeshi ya pepo wabaya wanaokaa angani.Hizo pepo chafu zinaorodheshwa kulingana na vyeo katika sura mojawapo ya Waefeso(ona Waefeso 6:12).

Paulo akasema kwamba huyo mfalme wa giza ni “roho yule atendaye kazi sasa katikawana wa kuasi”. Maneno “wana wa kuasi” ni jina lingine tu la wasioamini wote, lenyekukazia kwamba asili yao ni ya dhambi. Baadaye Paulo anawataja kwamba “kwa tabia niwatoto wa hasira” (Waefeso 2:3. Maneno mepesi kukazia). Tena akaongezea na kusemakwamba Shetani alikuwa anafanya kazi ndani yao.

Shetani Kama Baba

Kama watu ambao hawajaokoka wanajua au hawajui, ni kwamba wao wanamfuataShetani, na ni watu wake katika ufalme wa giza. Wana asili yake ovu na ya kibinafsindani ya roho zao zilizokwisha kufa. Ukweli ni kwamba Shetani ni bwana wao kiroho, nababa yao. Ndiyo sababu wakati mmoja Yesu aliwaambia viongozi wa dini ambaohawajaokoka, hivi: “Ninyi ni wa baba yenu Ibilisi, ndiyo maana mnataka kufanyamapenzi yake” (Yohana 8:44).

Hiyo ndiyo picha mbaya ya mtu ambaye hajazaliwa mara ya pili! Anaishi akiwaamekufa kiroho, akiwa amejawa na asili ya Shetani, akiwa anakwenda kwenye mauti yamwili isiyoepukika anayoiogopa sana, na, atambue au asitambue, siku moja atapatikanana mauti mbaya zaidi sana – mauti ya milele – atakapotupwa katika ziwa la moto.

Ni muhimu sana tuelewe kwamba mauti ya kiroho, kimwili na milele ni madhihirishoya hasira ya Mungu juu ya mwanadamu mwenye dhambi, na kwamba Shetani anahusika

Page 5: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

katika kila moja. Shetani ameruhusiwa na Mungu atawale ufalme wa giza na wote wenye“kulipenda giza” (Yohana 3:19). Yaani, ni kama Mungu alimwambia Shetani hivi:“Wewe watawale kwa nguvu zako wale wote ambao hawaninyenyekei mimi.” Shetaniakawa chombo cha ghadhabu ya Mungu juu ya wanadamu waasi. Kwa kuwa wotewamefanya dhambi, wote wako chini ya nguvu za Shetani, wakijaa asili yake katika rohozao na kushikwa mateka ili kufanya mapenzi yake (ona 2Timo. 2:26).

Malipo Kwa Ajili Ya Kutekwa Kwetu

Lakini, tunaweza kumshukuru Mungu kwamba alikuwa na rehema juu ya binadamu,na kwa sababu ya huruma Zake, hakuna anayetakiwa kubaki katika hali hiyo mbaya.Kwa kuwa kifo cha Yesu badala yetu kilitosheleza madai ya haki ya Mungu, wale wotewanaomwamini Kristo wanaweza kuepukana na kifo cha kiroho na uteka wa Shetani kwasababu hawako tena chini ya hasira ya Mungu. Tunapomwamini Yesu Kristo, RohoMtakatifu huingia katika roho zetu na kufutilia mbali asili ya Shetani, na kuifanya rohozetu kuzaliwa mara ya pili (ona Yohana 3:1-16) na kuturuhusu kuwa washiriki wa asili yaMungu (ona 2Petro 1:4).

Turudie swali tuliloanza nalo. Wakati mwandishi wa Waebrania anaposema kwambaYesu, kwa njia ya kifo Chake, “alimdhoofisha yeye aliyekuwa na nguvu ya mauti, yaaniShetani” maana yake ni kwamba nguvu ya mauti ya kiroho, ambayo Shetani anayo juu yakila mtu asiyeokoka, imevunjwa kwa wote walio “katika Kristo”. Sisi tunahuishwakiroho kwa sababu ya Kristo; amekwisha lipa adhabu kwa ajili ya dhambi zetu.

Tena – kwa kuwa sisi hatujafa kiroho tena na hatuko tena chini ya utawala wa Shetani,hatuna haja ya kuogopa mauti ya mwili, kwa sababu tunajua kinachotungojea mbele –urithi wa utukufu mwingi, wa milele.

Mwisho – kwa sababu ya Yesu, tumekombolewa na mauti ya pili, yaani, kutupwakatika ziwa la moto.

Je, Yesu alimshinda Shetani pale msalabani? Hapana, kwa sababu hapakuwepo vitakati ya Yesu na Shetani. Ila, yesu alimdhoofisha Shetani kwa habari ya nguvu zake juu yamauti ya kiroho, ambayo kwa hiyo anawashikilia wasio-okoka katika utumwa wadhambi. Shetani bado ana nguvu za mauti ya kiroho juu ya watu ambao hawajaokoka, ilakwa habari ya wale walio katika Kristo, hana nguvu zozote juu yao!

Kuvuliwa Kwa Enzi Na Mamlaka

Hili pia linatusaidia kuelewa maana ya maneno ya Paulo, kwamba “enzi na mamlakazilivuliwa uwezo wake” katika Wakolosai 2:13-15.

Na ninyi mliokuwa mmekufa [kiroho] kwa sababu ya makosa yenu ….Aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote; akiishakuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwana uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani; akishakuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri,akizishangilia katika msalaba huo (maneno mepesi kukazia).

Page 6: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

Paulo anatumia lugha ya mfano, yenye kueleweka kirahisi, katika fungu hili. Katikasehemu ya kwanza, analinganisha hatia yetu na “hati ya madai”. Kile ambacho sisihatukuweza kulipa tulilipiwa na Kristo, aliyechukua deni letu la dhambi mpakamsalabani.

Katika sehemu ya pili, kama ambavyo wafalme wa kale walivyokuwa wanawavuasilaha wale waliokuwa wamewashinda vitani na kuwatembeza kwa ushindi katika mitaaya miji yao, kifo cha Kristo kilikuwa ushindi juu ya “falme, enzi na mamlaka,” yaani,majeshi ya mapepo wa ngazi za chini ambao hutawala wanadamu waasi, na kuwashikamateka.

Sasa – kutokana na fungu hili, hatuwezi kusema kwamba Kristo alimshinda Shetani?Labda, lakini kwa kuongeza maelezo. Inatupasa kukumbuka kwamba, katika fungu hili,Paulo alikuwa anaandika kwa lugha ya mfano. Na kila mfano una mahali ambapomlinganisho hubadilika na kupingana, kama tulivyojifunza katika sura juu ya kutafsirimaandiko.

Katika kutafsiri mifano ya Paulo katika Wakolosai 2:13-15, lazima tuwe makini. Niwazi kwamba hapakuwepo na “hati ya mashtaka” iliyokuwa imeandikwa dhambi zetuzote, iliyogongomewa pale msalabani. Ila, ni mfano wa yale ambayo Yesu alifanikisha.

Vivyo hivyo, mapepo waliotawala wanadamu ambao hawajaokokahawakunyang’anywa panga zao na ngao zao na kutembezwa na Yesu hadharanibarabarani. Lugha anayotumia Paulo ni ya mfano tu kuonyesha kile ambacho Yesualifanikisha kwa ajili yetu. Tulikuwa mateka wa pepo hizo. Lakini, kwa kufa kwa ajili yadhambi zetu, Yesu alitufungua kutoka uteka wetu. Si kwamba alipambana ana kwa anana hao pepo wabaya, wala hawakuwa vitani Naye. Wao, kwa kuruhusiwa na haki yaMungu, walikuwa ametutawala kwa nguvu zao maisha yetu yote. “Silaha” zao hazikuwazime-elekezwa kwa Kristo, bali kwetu. Lakini, Yesu “aliwanyang’anya silaha” zao.Hawana uwezo wa kutushika mateka tena.

Tusije tukafikiri kwamba kulikuwepo na vita ya miaka na miaka kati ya Yesu namapepo wa Shetani, na hatimaye Yesu akashinda vita hiyo pale msalabani. Tukisemakwamba Yesu alimshinda Shetani, ni vizuri tuelewe kwamba alimshind Shetani kwa ajiliyetu, si kwa ajili Yake Mwenyewe.

Wakati fulani nilifukuza mbwa mdogo aliyekuwa anamtishia binti yangu. Nawezakusema kwamba nilimshinda huyo mbwa, lakini usidhani kwamba huyo mbwa alikuwakitisho kwangu. Alikuwa anamtishia binti yangu. Ndivyo ilivyokuwa kwa Yesu naShetani. Yesu alimfukuza mbwa aliyekuwa anatutishia sisi, si Yeye.

Alimfukuzaje huyo Shetani mbwa? Alifanya hivyo kwa kuchukua adhabu za dhambizetu, na kwa njia hiyo kutuweka huru kutokana na hatia yetu mbele za Mungu. Kwakufanya hivyo, alituweka huru kutokana na hasira ya Mungu, na hivyo, wale pepowachafu ambao Mungu anawaruhusu kwa haki kabisa kuwatawala wanadamu waasihawakuwa na haki tena ya kututawala sisi. Mungu asifiwe kwa hilo!

Tunafikia mahali panapofaa, kutazama hekaya ya pili.

Page 7: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

Hekaya Ya Pili: “Zipo vita zinazoendelea katika ulimwengu wa roho, kati yamalaika wa Mungu na wa Shetani. Matokeo ya vita hizo hutegemeana na jinsi sisitunavyopigana vita kiroho.”

Tayari tumejifunza kutoka kitabu cha Ufunuo kwamba siku moja itakuwepo vitambinguni kati ya Mikaeli na malaika zake, na Shetani na malaika zake. Zaidi ya hapo,kuna vita nyingine moja kati ya malaika inayotajwa katika Maandiko, katika Danieli suraya kumi.1

Danieli anatuambia alikuwa akiomboleza kwa majuma matatu katika mwaka wa tatuwa utawala wake Koreshi, mfalme wa Uajemi. Mara malaika akamtokea kando ya MtoTigris. Kusudi la safari ya malaika lilikuwa kumpa yeye ufahamu juu ya wakati ujao wataifa la Israeli, na tayari tumetazama kwa kifupi yale ambayo Danieli aliambiwa kuhusuUnyakuo na Nyakati za Mwisho katika sura iliyotangulia. Katika mazungumzo yao,malaika huyo ambaye hatajwi jina alimwambia Danieli hivi:

Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyowako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yakoyalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako. Lakini mkuu waufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyoMikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; naminikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi (Danieli 10:12, 13.Maneno mepesi kukazia).

Danieli akajua kwamba maombi yake yalikwisha sikiwa majuma matatu kabla yakukutana na huyo malaika, lakini pia akajua kwamba malaika mwenyewe ametumiamajuma matatu kumfikia. Sababu ya kuchelewa kwa malaika ni kwamba, “mkuu waufalme wa Uajemi” alimpinga. Ila, alifanikiwa kupenya wakati Mikaeli, “mmoja wa haowakuu wa mbele” alipofika kumsaidia.

Alipokaribia kuondoka, malaika alimwambia Danieli hivi:

Na sasa nitarudi ili nipigane na mkuu wa Uajemi; nami nitakapotoka huku,tazama, mkuu wa Uyunani atakuja. Lakini nitakuambia yaliyoandikwakatika maandiko ya kweli; wala hapana anisaidiaye juu ya hao ila huyoMikaeli, mkuu wenu (Danieli 10:20, 21).

Zipo kweli kadhaa za kusisimua zipatikanazo katika fungu hili. Hapa tena tunaonakwamba malaika wa Mungu hawana nguvu zote, na wanaweza kuingia katika mapiganona malaika waovu. 1 Hoja mbili pinzani zinajibiwa hivi: (1) Yuda anataja mashindano kati ya Mikaeli na Shetani juu ya mwiliwa Musa, lakini hakuna vita inayotajwa. Tunachoambiwa na Yuda ni kwamba Mikaeli “hakuthubutu hatakumshtaki kwa kumlaumu [Shetani], bali alisema, ‘Bwana na akukemee’ “ (Yuda ms. 9). (2) Wakati Elishana mtumishi wake walipozungukwa na jeshi la Shamu katika mji wa Dothani, Elisha alimwomba Munguafungue macho ya mtumishi wake (2Wafalme 6:15-17). Basi, mtumishi wake akaona “farasi na magari yamoto” ambayo ni sawa tukisema yalikuwa yamepandwa na kuongozwa na jeshi la malaika katikaulimwengu wa roho. Lakini, huo si ushahidi kwamba walikuwa wamejiandaa kupambana na majeshi yapepo. Wakati mwingine malaika hutumiwa na Mungu kutekeleza hasira Yake dhidi ya binadamu waovu,kama ilivyoandikwa katika 2Wafalme 19:35, ambapo malaika mmoja tu aliua askari 185,000 wa Ashuri.

Page 8: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

Pili tunajifunza kwamba malaika wengine (kama vile Mikaeli) wana nguvu zaidikuliko wengine (kama huyo aliyezungumza na Danieli).

Maswali Tusiyokuwa Na Majibu Yake

Tunaweza kuuliza hivi: “Kwa nini Mungu hakumtuma Mikaeli kupeleka huo ujumbekwa Danieli moja kwa moja, ili kusiwe na kuchelewa kwa majuma matatu?” Ukweli nikwamba Biblia haituambii sababu za Mungu kumtuma malaika ambaye alijua kabisaasingeweza kumpita “mkuu wa ufalme wa Uajemi” bila kusaidiwa na Mikaeli. Ukweli nikwamba hatujui ni kwa nini Mungu atumie malaika yeyote ili kupeleka ujumbe kwa mtu!Mbona hakwenda Mwenyewe, au kusema na Danieli kwa sauti, au kumfikisha Danielimbinguni kwa muda tu ili amwambie? Hatujui!

Sasa je! Maandiko haya yanathibitisha kwamba kuna vita za mara kwa mara katikaulimwengu wa roho kati ya malaika wa Mungu na wa Shetani? Hapana. Maandiko hayayanathibitisha tu kwamba, miaka elfu kadhaa iliyopita, kulikuwa na mapambano yamajuma matatu kati ya malaika moja dhaifu wa Mungu, na malaika mmoja mwenyenguvu wa Shetani, aitwaye “mkuu wa ufalme wa Uajemi.” Vita hiyo, kama Munguangetaka, isingetokea kamwe. Vita nyingine ya malaika inayotajwa katika Biblia ni ile yawakati ujao huko mbinguni, iliyoandikwa katika Kitabu cha Ufunuo. Basi. Penginezimekuwepo vita zingine za malaika zilizotokea, lakini tukiamua hivyo tutakuwatunakisia tu – hatuna ushahidi.

Hekaya Iliyojengwa Juu Ya Hekaya

Je, hii habari ya Danieli na mkuu wa ufalme wa Uajemi inathibitisha kwamba vitayetu ya kiroho inaweza kuamua matokeo ya vita za malaika? Hapa tena, wazo hililinadhania (kutokana na maandiko machache sana) kwamba zipo vita mara kwa marakati ya malaika. Hebu tukisie tu na kukubali kwamba ndiyo, zipo vita za malaika marakwa mara. Je, habari hii kuhusu Danieli inathibitisha kwamba vita yetu ya kirohoinaweza kuamua matokeo ya vita za malaika ambazo pengine zinakuwepo?

Mara nyingi, watu wenye kusambaza mawazo haya huuliza swali hili: “Ingekuwajekama Danieli angekata tamaa baada ya siku moja?” Swali hilo halina jibu kutoka kwayeyote, maana Danieli hakuacha kumtafuta Mungu katika maombi mpaka huyo malaikaasiyejulikana alipofika. Ila, sababu ya kuliuliza ni kutushawishi tuamini kwamba,Danieli, kwa kuendelea katika vita ya kiroho, alikuwa funguo ya ushindi katika vita yahuyo malaika asiyetajwa jina. Kama Danieli angekata tamaa na kuacha kupambanakiroho, inadaiwa kwmaba huyo malaika asingempita yule mkuu wa ufalme wa Uajemi.Wanataka tuamini kwamba hata sisi, kama Danieli, lazima tudumu katika vita ya kiroho,la sivyo malaika fulani mwovu atawashinda malaika wema wa Mungu.

Sawa, lakini – Ni vizuri kwanza tujue kwamba Danieli hakuwa “kwenye vita yakiroho” – yeye alikuwa anamwomba Mungu. Hatusomi popote kwamba alisema kitukinyume cha mapepo, au kwamba aliwafunga, au kwamba “alipigana” nao. Ukweli nikwamba, Danieli hakujua kwamba kulikuwa na vita baina ya malaika mpaka baada yamajuma matatu kupita, na yule malaika asiyetajwa jina kumtokea. Yeye alitumia majumahayo matatu katika kufunga na kumtafuta Mungu.

Page 9: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

Basi tuliseme swali hilo kwa namna nyingine: Kama Danieli angeacha kuomba nakumtafuta Mungu baada ya siku moja au mbili, je, huyo malaika asiyetajwa jinaangeshindwa kumfikishia ujumbe wa Mungu? Hatujui, ila ni vizuri kusema kwamba yulemalaika asiyetajwa jina hakumwambia Danieli hivi: “Ni vizuri uliendelea kuomba maanakama si hivyo, nisingefanikiwa.” Hapana! Malaika alimsifu Mikaeli kwa kufanikiwakwake. Bila shaka Mungu ndiye aliyemtuma malaika huyo asiyetajwa jina, pamoja naMikaeli, Naye aliwatuma kama itikio la maombi ya Danieli kutaka kuelewa mamboambayo yangetokea katika siku zijazo za Israeli.

Ni mawazo tu kudhani kwamba kama Danieli angeacha kufunga au kumtafuta Mungu,Mungu angesema hivi: “Haya! Ninyi malaika wawili, Danieli ameacha kufunga nakuomba. Kwa hiyo, ingawa nilimtuma mmoja wenu kumpelekea ujumbe siku ile yakwanza alipoanza maombi, achaneni na huo ujumbe. Kitabu chake hakitakuwa na sura yakumi na moja wala ya kumi na mbili.”

Hakika Danieli alidumu katika maombi (si katika “vita ya kiroho”), na Mungualimwitikia kwa kutuma malaika. Sisi nasi tunapaswa kudumu katika kumwombaMungu, na kama Mungu atapenda, jibu letu linaweza kuja kwa njia ya malaika. Lakiniusisahau kwamba kuna mifano mingi sana ya malaika kupeleka jumbe muhimu sana kwawatu katika Biblia, ambapo hapataji hata sala moja ya mtu yeyote, licha ya kuombamajuma matatu.2 Tuwe na msimamo. Tena, kuna mifano mingi sana ya malaika kuwapawatu jumbe, na katika mifano hiyo hakuna kutajwa kwamba ilibidi wapambane namapepo walipokuwa wanatoka mbinguni. Labda hao malaika walipambana na mapepo ilikuweza kufikisha jumbe zao, lakini kama ilikuwa hivyo, hatuna habari, maana Bibliahaisemi.

Tunafikia kwenye hekaya ya tatu, inayoaminika sana.

Hekaya Ya Tatu: “Adamu Alipoanguka, Shetani Alipata Haki Ya AdamuKutawala Ulimwengu.”

Je, ni kitu gani kilichotokea kwa Shetani wakati binadamu walipoanguka?Kuna

wanaodhani kwamba Shetani alipata cheo kikubwa sana Adamu alipoanguka.Wanasema mwanzoni Adamu alikuwa ndiye “mungu wa dunia hii,” lakini alipoanguka,Shetani akapata cheo hicho na kuwa na haki ya kufanya chochote alichotaka hapaduniani. Hata Mungu hakuweza kumzuia kuanzia wakati huo na kuendelea, kwa sababuAdamu alikuwa na ”haki kisheria” kumpa Shetani cheo chake na nafasi yake, na Munguilibidi aheshimu makubaliano kati Yake na Adamu, ambayo sasa yalikuwa kwa Shetani.Inasemekana kwamba sasa hivi Shetani ndiye mwenye “hati miliki ya Adamu”, naMungu hawezi kumzuia kitu Shetani mpaka “hati miliki ya Adamu itakapofikia mwishowake”.

Tunauliza hivi: Je, nadharia hiyo ni kweli? Je, Shetani alipata “hati miliki ya Adamu”wakati binadamu walipoanguka? Jibu ni HAPANA KABISA! Shetani hakupata chochotewakati binadamu walipoanguka isipokuwa laana kutoka kwa Mungu, na ahadi kuhusukuangamizwa kwake kabisa.

Ukweli ni kwamba Biblia haisemi kwamba Adamu alikuwa ndiye “mungu wa duniahii”. Tena, Biblia haisemi kwamba Adamu alikuwa na haki kisheria ya kumpa mtu 2 Baadhi ya mifano hiyo ni Mathayo 1:20; 2:13, 19; 4:11; Luka 1:11-20, 26-38.

Page 10: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

mwingine mamlaka anayodhaniwa kuwa nayo juu ya dunia. Tena, Biblia haisemikwamba Adamu alikuwa na hati miliki ambayo siku moja ingefikia mwisho. Mawazohayo yote si ya KiBiblia.

Sasa basi: Adamu alikuwa na mamlaka gani? Tunasoma katika Mwanzo kwambaMungu alimwambia Adamu na Hawa hivi: “Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi nakuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenyeuhai kiendacho juu ya nchi” (Mwanzo 1:28. Maneno mepesi kukazia).

Mungu hakusema chochote kwa Adamu juu ya kuwa “mungu” duniani, au kwambaangeweza kutawala kila kitu, kama vile hali ya hewa na watu wote ambao wangezaliwabaadaye na kadhalika. Yeye alimpa Adamu na Hawa kama binadamu wa kwanza,utawala juu ya samaki, ndege na wanyama, na kuwaagiza waijaze dunia na kuitiisha.

Wakati Mungu alipotamka hukumu kwa mwanadamu, hakusema chochote kuhusuAdamu kupoteza inayodhaniwa kuwa nafasi yake kama “mungu wa dunia hii.” Tena,hakusema chochote kwa Adamu na Hawa kuhusu wao kutokuwa na mamlaka tena juu yasamaki, ndege na wanyama. Ni dhahiri kwamba bado binadamu wanatawala juu yasamaki na ndege na “kila kiendacho juu ya nchi”. Binadamu bado wanaijaza dunia nakuitiisha. Wakati wa kuanguka binadamu, Adamu hakupoteza mamlaka yake aliyopewana Mungu.

Je, Shetani Si “Mungu Wa Dunia Hii”?

Lakini, mbona Paulo anamtaja Shetani kuwa “mungu wa dunia hii,” na Yesu kumtajakuwa “mkuu wa dunia hii”? Ndiyo, lakini hakuna aliyesema kwamba Adamu aliwahikuwa “mungu wa dunia hii” au kwamba Shetani alipata cheo hicho kutoka kwa Adamu,alipoanguka.

Tena, jina hilo la Shetani kwamba ni “mungu wa dunia hii” halithibitishi kwambaShetani anaweza kufanya chochote atakacho hapa duniani, au kwamba Mungu hanauwezo wa kumzuia. Yesu alisema hivi: “Nimepwa mamlaka yote mbinguni na duniani”(Mathayo 28:18. Maneno mepesi kukazia). Kama Yesu ana mamlaka yote duniani, nikwamba Shetani anaweza kutenda kazi kwa ruhusa Yake tu.

Nani aliyempa Yesu mamlaka yote mbinguni na duniani? Bila shaka ni Mungu Baba,ambaye alikuwa nayo Mwenyewe, ili ampe Yesu. Ndiyo sababu Yesu alisema juu yaBaba yake kwamba ni “Bwana wa mbingu na dunia” (Mathayo 11:25; Luka 10:21.Maneno mepesi kukazia). Mungu amekuwa na mamlaka yote duniani tangu alipoiumba.Alitoa mamlaka kidogo kwa binadamu mwanzoni, na hawajawahi kupoteza kilealichokitoa Mungu.

Biblia inaposema juu ya Shetani kuwa mungu au mtawala au mkuu wa dunia hii,maana yake hasa ni kwamba watu wa dunia (yaani, ambao hawajazaliwa mara ya pili)wanamfuata Shetani. Yeye ndiye wanayemtumikia, wajue au wasijue. Yeye ni munguwao.

Je, Shetani Alifanya Toleo Lolote?

Nadharia hiyo ya Shetani kupata utawala imejengwa kwenye hadithi ya kujaribiwakwa Yesu huko nyikani na Shetani, kama ilivyoandikwa katika Mathayo na Luka. Hebutuchunguze maelezo atoayo Luka ili tuone tunachoweza kujifunza.

Page 11: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

[Shetani] Akampandisha juu, akamwonyesha miliko zote za ulimwengukwa dakika moja. Ibilisi akamwambia, ‘Nitakupa wewe enzi hii yote, nafahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa yeyote kamanipendavyo. Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako.’Yesu akajibu akamwambia, ‘Imeandikwa: Msujudie Bwana Mungu wako,umwabudu yeye peke yake’ (Luka 4:5-8).

Je, tukio hili linathibitisha kwamba Shetani ana mamlaka juu ya kila kitu duniani, aukwamba Adamu alimpa kila kitu, au kwamba Mungu hana uwezo wa kumzuia? Hapana,na sababu zinafuata.

Kwanza: Tuwe makini sana kuhusu kujenga itikadi juu ya tamko lililofanywa na mtuambaye Yesu anamwita “baba wa uongo” (Yohana 8:44). Wakati mwingine Shetanihusema ukweli, lakini kat ika swala hili, tunapaswa kuwa macho kwa sababu kilealichosema Shetani kinapingana na kitu ambacho kilikwisha semwa na Mungu.

Katika sura ya nne ya kitabu cha Danieli, tunapata hadithi ya kunyenyekezwa kwamfalme Nebukadneza. Huyu mfalme, akiwa amejaa kiburi juu ya cheo chake na nafasiyake na mafanikio yake, aliambiwa na nabii Danieli kwamba angepewa akili ya mnyamampaka atakapotambua kwamba “Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wawanadamu, naye humpa yeye amtakaye, awaye yote” (Danieli 4:25. Maneno mepesikukazia). Tamko hilo linatolewa mara nne katika habari hii, kutilia mkazo umuhimuwake (tazama 4:17, 25, 32; 5:21).

Ona kwamba Danieli alisema hivi: “Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wawanadamu.” Hiyo inaonyesha kwamba Mungu ana mamlaka kiasi fulani juu ya dunia,sivyo?

Ona vile vile kwamba anachosema Danieli ni kinyume kabisa na kile ambacho Shetanialimwambia Yesu. Danieli anasema “naye humpa yeye amtakaye, awaye yote”. Shetaniakasema, “nami humpa yeyote, kama nipendavyo” (Luka 4:6).

Sasa, wewe utamwamini nani? Mimi nimeamua kumwamini Danieli.Lakini – kuna uwezekano kwamba Shetani alikuwa anasema ukweli – tukitazama

alichosema kutoka upande mwingine.Shetani ni “mungu wa dunia hii” kama tulivyokwisha ona. Maana yake ni kwamba

anatawala ufalme wa giza, ambao ni pamoja na watu katika kila taifa waliomwasiMungu. Biblia inasema hivi: “Dunia yote pia hukaa katika yule mwovu” (1Yohana 5:19).Wakati Shetani alipodai kwamba angeweza kumpa yeyote apendaye mamlaka juu yafalme za dunia, yawezekana alikuwa anazungumza juu ya enzi yake mwenyewe, yaaniufalme wa giza, ambayo inaundwa na falme ndogo ndogo ambazo zinakubaliana kwasehemu na falme za duniani kijiografia. Tunajulishwa na Maandiko kwamba Shetani anangazi kadhaa za vyeo miongoni mwa pepo wake wabaya, ambazo kupitia hizo anatawalaufalme wake (ona Waefeso 6:12), na ni sawa tukikisia kwamba yeye ndiye mwenyekuwapandisha au kuwashusha vyeo hao pepo katika ngazi zao, maana ndiye mkuu. Kwahali hiyo, Shetani alikuwa anampa Yesu kihalali kabisa nafasi ya kuwa pepo msaidizi, iliamsaidie kutawala katika ufalme wake wa giza. Kitu alichopaswa kufanya Yesu nikumsujudia Shetani na kumwabudu. Shukuru kwa sababu Yesu hakukubaliana na nafasihiyo ya “kupanda cheo”!

Page 12: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

Nani Aliyempa Shetani Cheo Chake?

Sasa: Vipi kuhusu madai ya Shetani kwamba mamlaka juu ya falme hizo amepewayeye?

Hapa tena lazima tujue kuna uwezekano mkubwa tu kwamba alikuwa anadanganya.Lakini hebu tuseme alikuwa anasema ukweli, tuone.

Ona kwamba Shetani hakusema Adamu ndiye alimpa mamlaka hayo. Kamatulivyokwisha ona mapema, Adamu asingeweza kuwa alimpa Shetani kwa sababuhakuwa na kitu cha kutoa. Adamu alitawala samaki, ndege na wanyama, si falme.(Ukweli ni kwamba wakati Adamu anaanguka, hakukuwepo falme za watu za kutawala.)Tena, kama Shetani alikuwa anampa Yesu utawala juu ya ufalme wa giza, ambao nimapepo wote na watu ambao hawajaokoka, isingewezekana kabisa kwamba Adamundiye alimpa Shetani ufalme huo. Shetani alikuwa anatawala malaika walioanguka kablaAdamu hajaumbwa.

Yawezekana Shetani alimaanisha kwamba watu wote wa duniani walimpa yeyemamlaka juu yao, maana hawakujitolea kwa Mungu na kwa njia hiyo, kwa kujua aupasipo kujua, walikuwa wamejitolea kwake yeye.

Uwezekano bora zaidi ni kwamba Mungu ndiye alimpa mamlaka hayo. Inawezekanakabisa, kutokana na Maandiko, kwamba Mungu alimwambia Shetani, “Wewe na pepowako waovu mna ruhusa Yangu kutawala juu ya kila mtu ambaye hajajitolea kwangu.”Unaweza kushindwa kulipokea hilo, lakini baadaye utaona kwamba pengine hayo ndiyomaelezo bora zaidi ya madai aliyotoa Shetani. Kama kweli Mungu ni “mtawala juu yawanadamu wote” (Danieli 4:25), basi mamlaka yoyote ambayo Shetani anayo lazima awealipewa na Mungu.

Shetani anatawala ufalme wa giza tu, ambao pia unaweza kuitwa “ufalme wa uasi.”Yeye alikuwa anatawala ufalme huo tangu siku ile alipofukuzwa mbinguni, kitukilichotokea kabla ya kuanguka kwa Adamu. Mpaka wakati Adamu alipoanguka, ufalmewa giza ulikuwa na malaika waasi tu. Lakini wakati Adamu alipotenda dhambi, yeyenaye akajiunga katika kundi la waasi, na ufalme wa Shetani tangu hapo ukawa nabinadamu waasi, pamoja na malaika waasi.

Shetani alikuwa anatawala juu ya ufalme wake wa giza kabla hata Adamu hajaumbwa.Basi, tusije tukafikiri kwamba Adamu alipoanguka, Shetani alipata kitu ambacho Adamualikuwa nacho. Hapana. Wakati Adamu alipotenda dhambi, alijiunga ufalme wa uasiambao ulikuwepo kwa muda mrefu tu – ufalme uliotawaliwa na Shetani.

Je, Mungu Alishtushwa Na Anguko?

Hitilafu nyingine katika nadharia kwamba “Shetani Alifaidika” ni kwamba, inamfanyaMungu aonekane mpumbavu, kana kwamba alishtukizwa na matukio ya anguko, na kwasababu hiyo, akajikuta katika hali ya kusikitisha. Je, Mungu hakujua kwamba Shetaniangewajaribu Adamu na Hawa na kwamba binadamu wangeanguka kwa sababu hiyo?Ikiwa Mungu anajua yote – na ni kweli anajua yote – basi alikuwa anajua yatakayotokea.Ndiyo sababu Biblia inatuambia kwamba alifanya mipango ya kukomboa wanadamu hatakabla ya kuwaumba (ona Mathayo 25:34; Matendo 2:2-23; 4:27, 28; 1Wakor. 2:7,8;Waefeso 3:8-11; 2Timo. 1:8-10; Ufunuo 13:8).

Page 13: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

Mungualimwumba Shetani akijua ataanguka, na alimwumba Adamu na Hawa akijuawataanguka. Hakuna jinsi ambavyo Shetani angeweza kumdanganya Mungu na kupatakitu ambacho Mungu hakutaka awe nacho.

Je, maana yake ni kwamba Mungu anataka Shetani awe “mungu wa dunia hii?”Ndiyo, kwa muda wote ambao itatimiza makusudi Yake. Kama Mungu asingemtaka

Shetani afanye kazi, angemzuia tu mara moja kama atakavyofanya wakati mmoja,katika Ufunuo 20:1, 2.

Lakini, si kwamba Mungu anataka yeyote abaki chini ya utawala wa Shetani. Munguanamtaka kila mmoja aokolewe na kuepukana na utawala wa Shetani (Matendo 26:18;Wakolosai 1:13; 1Timo. 2:3, 4; 2Petro 3:9). Lakini Mungu anamruhusu Shetani kutawalakila mtu anayependa giza (ona Yohana 3:19) – yaani, wale wote wanaoendelea kuwakinyume Chake.

Je, hakuna chochote tunachoweza kufanya ili kuwasaidia watu waepukane na ufalmewa Shetani wa giza? Kipo. Tunaweza kuwaombea na kuwaita watubu na kuiamini Injili(kama tulivyoagizwa na Yesu). Wakifanya hivyo, watawekwa huru kutoka mamlaka yaShetani. Lakini kudhani kwamba tunaweza “kuangusha” pepo wabaya wanaowashikiliawatu ni makosa. Kama watu wanataka kukaa gizani, Mungu atawaruhusu. Yesualiwaambia wanafunzi Wake kwamba kama watu katika miji fulani wasingepokeaujumbe wao, wakung’ute mavumbi ya miguu yao na kwenda mji mwingine (Mathayo10:14). Hakuwaambia wakae na kuangusha ngome juu ya mji huo ili watu wawezekupokea zaidi. Mungu huruhusu pepo wabaya kuwafunga watu wanaokataa kutubu nakumrudia Yeye.

Ushahidi Zaidi Kuhusu Mamlaka Ya Mungu Juu Ya Shetani

Yapo maandiko mengine mengi yenye kuthibitisha vizuri sana kwamba Munguhakupoteza mamlaka yoyote juu ya Shetani wakati mwanadamu alipoanguka. Bibliamara kwa mara inatuambia kwamba Mungu siku zote ana mamlaka juu ya Shetani, naatakuwa nayo. Shetani anaweza kufanya kile anachoruhusiwa kufanya na Mungu tu.Hebu tutazame kwanza mifano kadhaa kutoka Agano la Kale juu ya jambo hili.

Sura mbili za kwanza za kitabu cha Ayubu zinaeleza mfano wa mamlaka ya Mungujuu ya Shetani. Hapo tunasoma kuhusu Shetani mbele ya kiti cha enzi cha Mungu,akimshtaki Ayubu. Ayubu alikuwa mtiifu kwa Mungu kuliko mtu mwingine yeyoteduniani wakati huo. Basi, Shetani akamtafuta sana. Mungu alijua kwamba Shetani“ameweka moyo wake” juu ya Ayubu (1:8). Basi, alimsikiliza Shetani alipomshtaki kwakumtumikia Mungu tu kwa sababu ya baraka zote ambazo alikuwa anazifurahia (onaAyubu 1:9-12).

Shetani alisema Mungu alikuwa ameweka uzio kumzunguka Ayubu, na akamwombaaondoe baraka za Ayubu. Basi, Mungu alimruhusu Shetani kumtesa Ayubu kwa kiwangofulani. Mwanzoni, hakuruhusiwa kugusa mwili wa Ayubu, ila baadaye, Mungualimruhusu Shetani kuutesa mwili wake. Lakini alimkataza kumwua (Ayubu 2:5, 6).

Fungu hili moja la Maandiko hakika linathibitisha kwamba Shetani hawezi kufanyachochote anachotaka. Hakuweza kugusa mali za Ayubu mpaka Mungu alipomruhusu.Hakuweza kuiba afya ya Ayubu mpaka Mungu alipomruhusu. Na hakuweza kumwua

Page 14: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

Ayubu kwa sababu Mungu alimkataza.3 Ni hivi: Mungu anamtawala Shetani kikamilifu,hata tangu wakati wa anguko la Adamu.

Roho Mbaya Ya Sauli, “Kutoka Kwa Bwana”

Kuna mifano mingi ya Mungu akiwatumia pepo wabaya wa Shetani kama mawakalawa ghadhabu Yake katika Agano la Kale. Tunasoma hivi katika 1Samweli 16:14 – “Basiroho ya BWANA ilikuwa imemwacha Sauli, na roho mbaya kutoka kwa BWANAikamsumbua.” Hali hii bila shaka ilitokea kwa sababu ya adhabu ya Mungu juu ya Saulimfalme, aliyeacha kumtii Mungu.

Swali kubwa ni hili: Nini maana ya maneno yale, “roho mbaya kutoka kwaBWANA”? Je, maana yake ni kwamba Mungu alituma pepo anayekaa Naye hukombinguni, au maana yake ni kwamba Mungu aliruhusu pepo mmoja mwovu wa Shetanikumsumbua Sauli? Nadhani Wakristo wengi watakubaliana na maana ya pili, kutokanana mengine yanayofundishwa na Biblia. Sababu ya Maandiko kusema kwamba huyopepo alitoka “kwa BWANA” ni kutokana na ukweli kwamba kazi yake ya kumsumbuaSauli ilitokana na adhabu ya Mungu juu yake. Basi, tunaona kwamba hata pepo wakochini ya utawala wa enzi ya Mungu.

Tunasoma pia katika Waamuzi 9:23 hivi: “Kisha Mungu akapeleka roho mbaya katiya Abimeleki na watu wa Shekemu”, ili hukumu ya Mungu iwajie kwa sababu yamatendo yao maovu. Hapo tena, huyu pepo hakutoka mbinguni kwa Mungu bali katikaufalme wa Shetani, na aliruhusiwa na Mungu kutekeleza mambo maovu dhidi ya watufulani, waliostahili hayo. Pepo hawawezi kufanikiwa kutimiza mipango yao miovu dhidiya mtu awaye yote bila ya ruhusa ya Mungu. Kama si hivyo, basi Mungu hana nguvuzote. Kwa hiyo, tunaweza kuhitimisha kwa kusema kwamba, wakati Adamu alipoanguka,Shetani hakupata mamlaka yaliyozidi mipaka aliyoweka Mungu.

Mifano Ya Agano Jipya Kuhusu Nguvu Za Mungu Juu Ya Shetani

Agano Jipya linatoa ushahidi wa ziada wenye kupingana na hoja kwamba Shetanialifaidika kutokana na Anguko la Adamu.

Kwa mfano: Tunasoma katika Luka 9:1 kwamba Yesu aliwapa wanafunzi wake kumina mbili “mamlaka juu ya pepo wote”. Tena katika Luka 10:19, Yesu aliwaambia hivi:“Tazama, nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui,wala hakuna kitu chochote kitakachowadhuru” (maneno mepesi kukazia).

Kama Yesu aliwapa wao mamlaka juu ya nguvu zote za Shetani, ni kwamba Yeyealikuwa na hayo mamlaka. Shetani yuko chini ya mamlaka ya Mungu.

Baadaye katika Injili ya Luka tunasoma habari za Yesu akimwambia Petro hivi:“Simoni! Simoni! Tazama, Shetani ameomba ruhusa ili akupepete kama ngano” (Luka22:33, TLR). Maandiko yanaonyeshakwamba asingeweza kumpepeta Petro bila ya

3 Fungu hili zima pia ni ushahidi kwamba Ayubu “hakumfungulia Shetani mlango kwa sababu ya hofuyake,” kitu kinachoaminiwa na wengine. Mungu Mwenyewe alimwambia Shetani hivi kuhusu Ayubu,katika 2:3 – “Naye [Ayubu] hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ujapokuwa ulinichochea juu yake,ili nimwangamize pasipokuwa na sababu” (maneno mepesi kukazia).

Page 15: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

kupata ruhusa kutoka kwa Mungu kwanza. Hapo tena, Shetani anaonyesha kuwa chini yamamlaka ya Mungu.4

Kifungo Cha Shetani Cha Miaka Elfu Moja

Tunaposoma habari za kufungwa kwa Shetani na malaika mmoja tu katika Ufunuo 20,Adamu hatajwi hapo kwamba milki yake imefikia mwisho. Sababu itoleayo hapo nikwamba, “ili asiwadanganye tena mataifa” (Ufunuo 20:3).

Ajabu ni hii: Baada ya Shetani kufungwa miaka elfu moja, atafunguliwa, “nayeatatoka ili kuwadanganya mataifa, walio katika pembe nne za dunia” (Ufunuo 20:8).Hayo mataifa yatakayodanganywa yataandaa majeshi yao ili kushambulia Yerusalemu,mahali ambapo Yesu atakuwepo akitawala. Baada ya kuuzunguka mji, moto utatokambinguni na “kuwateketeza” (Ufunuo 20:9).

Je, kuna anayeweza kuwa mjinga kiasi cha kusema kwamba haki ya kumiliki yaAdamu ilihusu kipindi kifupi tu cha muda baada ya miaka elfu moja, na ndiyo maanaMungu ilibidi amwachie Shetani kwa sababu hiyo? Wazo kama hilo ni la kipuuzi!

Hapana! Tunachojifunza kwa mara nyingine tena kutoka fungu hili la Maandiko nikwamba Mungu ana mamlaka kamili juu ya Shetani, na humruhusu afanye udanganyifuwake ili kutimiza makusudi Yake tu.

Katika ule utawala wa Yesu hapo baadaye wa miaka elfu moja, Shetani hatakuwakatika utendaji – atashindwa kumdanganya mtu yeyote. Ila, watakuwepo watu dunianiwatakaokuwa watiifu kwa utawala wa Kristo kwa nje tu, ambao ndani watapendakumwona aking’olewa madarakani. Lakini hawatajaribu kufanya mapinduzi kwa sababuwanajua hawawezi kumpindua mtu “atakayetawala kwa fimbo ya chuma” (Ufunuo19:15).

Lakini Shetani atakapofunguliwa, ataweza kuwadanganya wale ambao wanamchukiaKristo mioyoni mwao, nao watajaribu kufanya yasiyowezekana, kwa sababu yaupumbavu. Naye Shetani atakaporuhusiwa kuwadanganya waasi waliojificha, hali halisiya mioyo yao itafunuliwa, ndipo Mungu kwa haki kabisa atakapowahukumu wale ambaohawastahili kuishi katika ufalme Wake.

Hiyo ndiyo sababu moja ya Mungu kumruhusu Shetani kuwadanganya watu siku hizi.Baadaye tutachunguza makusudi kamili ya Mungu kwa ajili ya Shetani, lakini kwa sasayatosha tu kusema kwamba Mungu hataki mtu yeyote abaki amedanganywa. Ila, anatakakujua kilichomo mioyoni mwa watu. Shetani hawezi kuwadanganya wale wanaojua nakuamini kweli. Lakini Mungu anamruhusu Shetani kuwadanganya wale ambao, kwasababu ya mioyo yao migumu, wanakataa ukweli.

Paulo anasema juu ya kipindi cha utawala wa mpingakristo, kama ifuatavyo:

Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwapumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapokwake; yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani,kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo; na katika madanganyo yoteya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipendaile kweli, wapate kuokolewa. Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya

4 Ona pia 1Wakorintho 10:13, mahali panapo-onyesha kwamba Mungu huweka mipaka ya kujaribiwakwetu. Hiyo inamaanisha kwamba humwekea mipaka mwenye kutujaribu pia!

Page 16: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

upotevu, wauamini uongo; ili wahukumiwe wote ambao hawakuiaminikweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu (2Wathes. 2:8-12.Maneno mepesi kukazia).

Ona kwamba anayetajwa kwamba atatuma “nguvu ya upotevu, wauamini uongo” niMungu. Lakini pia ona kwamba watu hao watakaodanganywa ni watu ambao“hawakuiamini kweli,” kuonyesha kwamba wao walipata nafasi, lakini bado walikataaInjili. Mungu atamruhusu Shetani kumtia nguvu mpingakristo kwa uwezo wa kufanyaishara za uongo na maajabu, ili wanaomkataa Kristo wadanganyike, na kusudi la Munguhatimaye ni kwamba “wote wahukumiwe.” Kwa sababu hiyo hiyo, Mungu anamruhusuShetani kuwadanganya watu siku hizi.

Kama Mungu hakuwa na sababu ya kumruhusu Shetani kufanya kazi hapa duniani,angekwisha mfukuza aende mahali pengine, wakati alipoanguka. Tunaambiwa katika2Petro 2:4 kwamba kuna malaika fulani waliotenda dhambi ambao tayari Munguamekwisha watupa kuzimu, na kuwafunga katika “vifungo vya giza, wakisubirihukumu.” Mungu wetu mwenye nguvu zote angeweza kufanya hivyo hivyo kwa Shetanina kwa yeyote katika malaika zake kama ingefaa mapenzi Yake makamilifu. Lakini, kwamuda kidogo zaidi, Mungu ana sababu nzuri tu za kumruhusu Shetani na malaika zakekufanya kazi hapa duniani.

Hofu Ya Mapepo Kuteswa

Tunapomalizia mafunzo yetu kuhusu hekaya hii, tutazame mfano mmoja kutokaMaandiko, unaohusu watu wawili kutoka Gerasi, waliokuwa na pepo.

Naye [Yesu] alipofika ng’ambo katika nchi ya Wagerasi, watu wawiliwenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtuasiweze kuipitia njia ile. Na tazama, wakapiga kelele wakisema, ‘Tunanini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhulawetu?’ (Mathayo 8:28, 29. Maneno mepesi kukazia).

Mara nyingi habari hii hutumiwa na wale wenye kufundisha kwamba ShetaniAlifaidika ili kuunga mkono mawazo yao. Wanasema hivi: “Unaona! Pepo walimwombaYesu awatendee haki. Walijua hakuwa na haki ya kuwatesa kabla ya wakati wakumalizika kwa haki ya umiliki nchi aliyokuwa nayo Adamu, yaani, wakati ambapo waona Shetani wangetupwa katika ziwa la moto ili wateswe humo mchana na usiku hatamilele.”

Ukweli ni tofauti kabisa. Wao walijua kwamba Yesu alikuwa na uwezo na haki zotekuwatesa wakati wowote aliotaka. Ndiyo sababu walimwomba awahurumie. Waliogopasan asana kwamba Mwana wa Mungu angewatuma wakateswe mapema zaidi. Lukaanatuambia kwamba walimsihi “asiwaagize waende shimoni” (Luka 8:31). Kama Yesuhakuwa na haki hiyo kwa sababu ya haki fulani ambayo Shetani anadaiwa alikuwa nayo,wasingejali hata kidogo.

Hao pepo walitambua kwamba walikuwa wakitegemea rehema zsa Yesu kabisa, kamainavyo-onekana kwa wao kumwomba asiwatume nje ya nchi (Marko 5:10), nakumwomba awaruhusu kuwaingia kundi la nguruwe lililokuwepo (Marko 5:12), wao

Page 17: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

kumsihi wasitupwe “shimoni” (Luka 8:31), na kumwomba Kristo wasiteswe “kabla yawakati”.

Tutazame hekaya nyingine inayoaminiwa sana, kuhusu Shetani.

Hekaya Ya Nne: “Shetani Kama ‘mungu wa dunia hii’ Anatawala Kila KituDuniani – Serikali Za Wanadamu, Majanga, Na Hali Ya Hewa.”

Katika Maandiko, Shetani anatajwa na mtume Paulo kwamba ni “mungu wadunia hii” (2Wakor. 4:4) na kuitwa na Yesu “mkuu wa dunia hii” (Yohana 12:31;

14:30; 16:11). Kutokana na majina haya ya Shetani, wengi wamedhani kwambaanatawala kikamilifu kabisa dunia. Japo tumekwisha tazama maandiko ya kutoshakuweka wazi kosa la hekaya hii, itatusaidia kujifunza zaidi ili tuwe na ufahamu kamilikuhusu jinsi ambavyo nguvu za Shetani zilivyo na mipaka. Ni lazima tuwe makinikwamba ufahamu wetu kuhusu Shetani usiwe umejengwa kwenye maandiko manne tuyenye kumtaja kwamba ni mungu, au mkuu wa dunia hii.

Tunapochunguza Biblia zaidi tunaona kwamba zaidi ya Yesu kumtaja Shetanikwamba ni “mkuu wa dunia hii” alimtaja Baba Yake wa mbinguni kwamba ni “Bwanawa mbingu na nchi” (Mathayo 11:25; Luka 10:21. Maneno mepesi kukazia). Tena,mtume Paulo hakumwita Shetani kuwa ni “mungu wa dunia hii” tu, bali pia aliongeza,kama Yesu, akamtaja Mungu kuwa ni “Bwana wa mbingu na nchi” (Matendo 17:24.Maneno mepesi kukazia). Hii hututhibitishia sisi kwamba Yesu wala Paulo hawatakitudhani kwamba Shetani ana mamlaka kamili juu ya nchi. Lazima mamlaka ya Shetaniyawe na mipaka.

Tofauti muhimu sana kati ya maandiko hayo yanayotofautiana inapatikana katikamaneno mawili: dunia na nchi. Japo tunayatumia kwa pamoja, katika Kiyunani hayomawili hayafanani. Tukiisha elewa jinsi yanavyotofautiana, ufahamu wetu kuhusumamlaka ya Mungu na ya Shetani hapa duniani yanaongezeka sana.

Yesu alimwita Mungu Baba kuwa ni Bwana wa nchi. Neno la Kiyunani linalotafsiriwanchi ni ge. Hili linamaanisha sayari hii tunayoishi, na neno la Kiingereza geography (au,jiografia) limetokana nalo.

Kinyume chake, Yesu alisema kwamba Shetani ni mtawala wa dunia hii. Neno laKiyunani linalotafsiriwa dunia ni kosmos, ambalo kikawaida husema juu ya mpango auutaratibu. Linazungumzia watu badala ya sayari yenyewe. Ndiyo sababu Wakristo maranyingi wanasema juu ya Shetani kama “mungu anayetawala taratibu za dunia hii.”

Kwa sasa hivi, Mungu hana mamlaka yote juu ya dunia kwa sababu hajawatawalawatu wote wa dunia. Sababu yake ni kwamba, amewapa watu wote uchaguzi kuhusu naniawe bwana katika maisha yao, na wengi wamechagua kumpa Shetani nafasi hiyo.Tusisahau kwamba hiari ya mwanadamu ni sehemu ya mpango wa Mungu.

Paulo alitumia neno tofuati la Kiyunani kusema juu ya dunia, alipoandika juu yamungu wa dunia hii. Ni neno aion, ambalo mara nyingi hutafsiriwa kama kipindi, majira,nyakati, yaani, wakati maalum uliopangwa au kuwekwa. Shetani ni mungu wa kipindi auwakati huu wa sasa.

Nini basi maana ya yote hayo? Nchi ni sayari tunayokaa. Dunia ni watu ambaowanakaa kwa sasa duniani, n asana sana wale ambao hawamfuati Yesu. Waowanamfuata Shetani, na wamenaswa katika utaratibu wake uliopotoka, wa dhambi. Sisikama Wakristo tunasemekana “tupo duniani” lakini si “wa dunia” (Yohana 17:11, 14).

Page 18: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

Tunakaa miongoni mwa raia wa ufalme wa giza, lakini ukweli ni kwamba tuko katikaufalme wa nuru – ufalme wa Mungu.

Basi, sasa tunalo jibu. Kwa ufupi tu ni hivi: Mungu anatawala dunia nzimakimamlaka. Ila, kwa ruhusa ya Mungu, Shetani anatawala “taratibu za dunia” tu, yaani,anawatawala wale raia wa ufalme wake wa giza. Kwa sababu hii, mtume Yohanaaliandika kwamba “dunia nzima (sio nchi nzima) iko katika nguvu za yule mwovu”(1Yohana 5:19).

Hii haimaanishi kwamba Mungu hana mamlaka juu ya dunia au mipangilio ya dunia,au watu katika dunia hii. Kama Danieli alivyosema, Yeye ni “anatawala katika falme zawanadamu, naye humpa yule amtakaye” (Danieli 4:25). Bado anaweza kumwinua aukumshusha mtu yeyote amtakaye. Ila, kama “mtawala” mkuu “juu ya falme zawanadamu” amemruhusu Shetani kuwatawala wanadamu wote walio kinyume Chake,yaani, waasi.

Tutazame Toleo La Shetani

Hii tofauti kati ya dunia na nchi itatusaidia pia kuelewa jaribu la Yesu pale nyikani.Huko, Shetani alimwonyesha Yesu “falme zote za dunia kwa dakika moja.” Shetaniasingempa Yesu nafasi ya kisiasa juu ya serikali za wanadamu duniani – yaani, kitutunachoita urais au uwaziri mkuu. Si Shetani anayewainua na kuwashusha wanadamuwakuu wa dunia – ni Mungu.

Badala yake – Shetani bila shaka alimwonyesha Yesu falme zote ndogo ndogo katikaufalme wake wa giza duniani kote. Alimwonyesha Yesu mpangilio wa utawala wakipepo, ambao, katika maeneo yao, wanatawala juu ya ufalme wa giza, pamoja na walebinadamu waasi ambao ni raia wao. Shetani akampa Yesu mamlaka juu ya utawala wake– kama Yesu angejiunga na uasi wa Shetani dhidi ya Mungu. Hapo, Yesu angekuwamakamu wake katika ufalme wa giza.

Utawala Wa Mungu Juu Ya Serikali Za Binadamu, Duniani

Hebu tuonyeshe vizuri zaidi mipaka ya mamlaka ya Shetani kwa kutazama maandikokwanza, yenye kuthibitisha mamlaka ya Mungu juu ya serikali za duniani za wanadamu.Shetani anayo mamlaka kiasi katika serikali za duniani za wanadamu kwa sababu anamamlaka juu ya watu ambao hawajaokoka, na serikali mara nyingi hutawaliwa na watuambao hawajaokoka. Lakini, Mungu ndiye mwenye mamlaka yote juu ya serikali zawanadamu, na Shetani anaweza kuzitumia kwa kiwango ambacho Mungu ataruhusu tu.

Tayari tumekwisha tazama maneno ya Danieli kwa mfalme Nebukadneza, lakini kwasababu ni kitu kinachosaidia, hebu tuyatazame tena.

Mfalme mkuu Nebukadneza alikuwa ameinuka sana kwa kiburi kutokana na uwezowake na mafanikio yake makubwa. Basi, Mungu akatangaza kwamba atashushwa mpakachini kabisa ili aweze kujifunza kwamba “Aliye Juu anatawala katika falme zawanadamu, naye humpa yeyote amtakaye” (Danieli 4:17). Ni dhahiri kwamba Mungundiye anahusika na kupanda kwa Nebukadneza kufikia ukuu kisiasa. Ndivyo ilivyo kwakila kiongozi wa kidunia. Mtume Paulo, akisema juu ya watawala wa duniani, alitangazakwamba “kila mamlaka hutoka kwa Mungu, na zilizoko zimewekwa na Mungu”(Warumi 13:1).

Page 19: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

Mungu ndiye mamlaka kuu katika ulimwengu wote. Kama kuna mwenye mamlakamwingine, ni kwa sababu Mungu amempa kidogo, au amemruhusu mwingine kuwa nayokidogo.

Vipi basi kuhusu watawala waovu? Je, Paulo anamaanisha kwamba hata waowanawekwa na Mungu? Ndiyo. Mapema kidogo katika barua hiyo hiyo, Paulo aliandikahivi: “Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao ya kwamba, ‘Nilikusimamisha kwakusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, Jina langu likatangazwe katika nchi yote’.”(Warumi 9:17). Mungu alimwinua Farao – mwenye moyo mgumu – kwa kusudi lakujitukuza Mwenyewe. Mungu angeonyesha nguvu Zake kuu kupitia miujiza Yake yaukombozi – nafasi iliyopatikana kwa kuwepo mtu jeuri ambaye Yeye Mwenyewealimwinua.

Kwani, jambo hili haliko wazi katika mazungumzo ya Yesu na Pilato? Pilato,akishangazwa na jinsi ambavyo Yesu hakumjibu maswali yake, alisema hivi: “Mbonahuzungumzi nami? Hujui kwamba nina mamlaka ya kukuachia huru, na mamlaka yakukusulubisha?” (Yohana 19:10).

Yesu akamjibu hivi: “Wewe usingekuwa na mamlaka juu Yangu, kama usingepewakutoka juu” (Yohana 19:11. Maneno mepesi kukazia). Akijua tabia ya Pilato ya uoga,Mungu alimwinua ili mpango Wake kwa Yesu kufa msalabani uweze kufanikiwa.

Ukisoma vitabu vya historia katika Agano la Kale kwa haraka haraka, utaona kwambawakati mwingine Mungu huwatumia watawala wanadamu ambao ni waovu kamamawakala wa hasira Yake juu ya watu wanaostahili hukumu. Nebukadneza alitumiwa naMungu kuleta hukumu Yake juu ya mataifa mengi katika Agano la Kale.

Ipo mifano mingi sana ya watawala ambao Mungu aliwainua au kuwashusha katikaBiblia. Kwa mfano: Katika Agano Jipya tunasoma juu ya Herode ambaye hakumpaMungu utukufu wakati baadhi ya raia wake walipopiga kelele mbele zake na kusema,“Hiyo ni sauti ya mungu, si ya mwanadamu!” (Matendo 12:22).

Ikawaje? “Mara, malaika wa Bwana akampiga … naye akaliwa na funza, akafa”(Matendo 12:23).

Kumbuka hivi: Herode alikuwa raia katika ufalme wa Shetani, lakini hakuwa nje yamamlaka ya Mungu. Basi, Mungu anaweza kumwangusha kiongozi yeyote wa dunianihata sasa, kama akitaka.5

Ushuhuda Binafsi Wa Mungu

Kwa kumalizia, hebu tusome kile ambacho Mungu Mwenyewe aliwahi kusemakupitia nabii Yeremia, kwa habari ya enzi na ukuu Wake juu ya falme za wanadamu,hapa duniani.

5 Je, maana yake ni kwamba tusiwaombee viongozi wa kiserikali, au tusipige kura kwa kuwa tunajuaMungu humwinua yeyote amtakaye kuwa juu yetu? Hapana. Katika demokrasia, hasira ya Mungu ikondani kwa ndani. Tunampata tunayemchagua, na watu waovu kwa kawaida huchagua waovu wenzao. Kwasababu hii, wenye haki wanapaswa kupiga kura. Tena, katika Agano la Kale na Jipya, tunashauriwakuwaombea viongozi wetu wa kiserikali (Yeremia 29:7; 1Timo. 2:1-4). Maana yake ni kwamba tunawezakumshawishi Mungu anapofanya maamuzi Yake juu ya nani atawale. Kwa kuwa hukumu ya Mungu wakatimwingine huja kwa kupitia viongozi waovu wa serikali, na kwa sababu mataifa mengi yanastahili hukumuhata hivyo, tunaweza kuomba na kupata reheme Zake, ili nchi yetu isipatikane na kila kitu inachostahilikupata.

Page 20: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

Ee nyumba ya Israeli, je! Siwezi mimi kuwatendea ninyi vile vile kamamfinyanzi huyu alivyotenda? Asema Bwana. Angalieni, kama udongoulvyo katika mkono wa mfinyanzi, ndivyo mlivyo ninyi katika mkonowangu, Ee nyumba ya Israeli. Wakati wowote nitakapotoa habari za taifa,na habari za ufalme, kuung’oa, na kuuvunja, na kuuangamiza; ikiwa taifalile nililolitaja litageuka, na kuacha maovu yake, nitaghairi, nisitendemabaya yale niliyoazimia kuwatenda. Na wakati wowote nitakapotoahabari za taifa na habari za ufalme, kuujenga na kuupanda, ikiwa watatendamaovu mbele za macho yangu, wasiitii sauti yangu, basi nitaghairi,nisitende mema yale niliyoazimia kuwatendea (Yeremia 18:6-10).

Je, unaona sasa kwamba hakuna jinsi ambayo Shetani angeweza kumpa Yesu utawalahalali juu ya falme za duniani za wanadamu za kisiasa, wakati alipokuwa anamjaribu palenyikani? Kama alikuwa anamwambia kweli (kama ambavyo anafanya wakati mwingine),basi alichokuwa anampa Yesu ni utawala juu ya ufalme wake wa giza.

Lakini je, Shetani ana ushawishi katika serikali za wanadamu? Ndiyo, lakini ni kwasababu yeye ndiye bwana wa kiroho juu ya watu ambao hawajaokoka, na watu ambaohawajaokoka wamo katika serikali za wanadamu. Ila, ana mamlaka kiasi cha ruhusaanayopewa na Mungu kuwa nayo, na Mungu anaweza kuvuruga mipango ya Shetaniwakati wowote anaotaka. Mtume Yohana aliandika juu ya Yesu kwamba ni “mtawala wawafalme wa dunia” (Ufunuo 1:5).

Je, Shetani Huleta Majanga Na Hali Mbaya Ya Hewa?

Kwa kuwa Shetani ni “mungu wa dunia hii,” wengi wamedhani kwambaanatawala hali ya hewa, na ndiye mwenye kuleta majanga yote kama vile ukame,

mafuriko, vimbunga, matetemeko, na kadhalika. Lakini je, hivyo ndivyo Maandikoyanavyotufundisha? Hapa tena inabidi tuwe makini kutokujenga itikadi yetu kuhusuShetani kutokana na andiko moja tu linalosema hivi: “Mwivi haji isipokuwa aibe, kuuana kuharibu” (Yohana 10:10). Mara nyingi sana watu wametumia mstari huu kuthibitishakwamba kila kitu kinachoiba, kuua au kuharibu hutoka kwa Shetani. Lakini, tukitazamaBiblia zaidi tunajifunza kwamba Mungu Mwenyewe wakati mwingine huua na kuharibu.Hebu tazama mafungu haya matatu, kutoka katika mifano mingi tu iliyopo.

Mtoa sheria na mwenye kuhukumu ni mmoja tu, ndiye awezaye kuokoana kuangamiza (Yakobo 4:12. Maneno mepesi kukazia).

Lakini nitawaonya mtakayemwogopa; mwogopeni yule ambaye akiishakumwua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanum; naam, nawaambia,Mwogopeni huyo! (Luka 12:5. Maneno mepesi kukazia).

Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeniyule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum (Mathayo10:28. Maneno mepesi kukazia).

Page 21: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

Tukisema kwamba kila kitu kinachohusisha kuua au kuharibu ni kazi ya Shetani,tunakosea. Kuna mifano mingi sana ya Mungu kuua na kuharibu katika Biblia.

Tujiulize hivi: Wakati Mungu aliposema juu ya mwizi anayekuja kuua, kuiba nakuharibu, alikuwa anasema juu ya Shetani, au mwingine? Hapo tena, tunachohitaji nikusoma maneno Yake katika mantiki yake. Mstari mmoja kabla hajasema aliyosema juuya mwizi kuja kuiba, kuua na kuharibu, Yesu alisema hivi: “Wote walionitangulia ni wezina wanyang’anyi, na kondoo hawakuwasikia” (Yohana 10:8). Tunaposoma maelezo yoteya Yesu katika Yohana 10:1-15 akisema Yeye ni Mchungaji mwema, inakuwa wazi zaidikwamba maneno aliyotumia – mwizi na wezi – yanawahusu waalimu wa uongo naviongozi bandia wa dini.

Maoni Mbalimbali Kuhusu Hali Mbaya Ya Hewa Na Majanga

Kimbunga au tetemeko linapotokea, swali la kitheolojia hutokea katika akili za watuwanaomwamini Mungu. Ni hili: “Nani amesababisha hili?” Kwa Wakristo wanaoaminiBiblia, ni mawili: Aidha ni Mungu, au ni Shetani.

Wengine wanaweza kupinga hivi: “Hapana! Mungu hahusiki! Watu ndiyowanahusika. Mungu anawahukumu kwa ajili ya dhambi zao.”

Kama Mungu analeta kimbunga na matetemeko kwa sababu ya hukumu Yake juu yadhambi, basi kweli tunaweza kuwalaumu binadamu waasi badala ya Mungu, lakini hatahivyo, Mungu bado anawajibika, kwa sababu majanga kama hayo yasingetokea bila yaagizo Lake.

Au kama ni kweli kwamba Mungu humruhusu Shetani kutuma vimbunga namatetemeko ili kuleta hukumu Yake juu ya wenye dhambi, basi tunaweza kusema niShetani anayesababisha, lakini bado Mungu anawajibika. Sababu ni kwamba, Yeye ndiyealiyemruhusu Shetani kusababisha uharibifu huo, na ni kwa sababu majanga hayoyanatokea kama itikio Lake kwa dhambi.

Kuna wanaosema si Mungu wala Shetani wanaohusika katika vimbunga namatetemeko, bali ni “matukio ya kawaida ya kiasili katika dunia yetu ya dhambi.” Hatahao wanajaribu kwa mbali kuweka lawama juu ya binadamu kwa majanga ya kiasili,lakini nao wanapotea. Maelezo hayo hayamwondoi Mungu katika picha. Kama vimbungani “tukio la kawaida kiasili katika dunia yetu ya dhambi”, nani aliyeamua iwe hivyo? Nidhahiri kwamba vimbunga havitengenezwi na mwanadamu. Yaani, havitokei kwa sababukiasi fulani cha uongo kimejaa katika anga. Matetemeko hayatokei wakati kiasi fulanicha watu wanapozini.

Hapana. Ni hivi: Kama kuna mahusiano kati ya kimbunga na dhambi, basi Munguanahusika, kwa sababu vimbunga ni madhihirisho ya hukumu Yake juu ya dhambi. Hatakama vinatokea bila mpangilio, ni lazima iwe kwa amri ya Mungu, na kwa hali hiyo,anahusika.

Hata kama hakuna mahusiano yoyote kati ya dhambi na majanga, na iwe kwambaMungu alikosa alipoitengeneza dunia na kusababisha udhaifu katika umbo la duniampaka kuna nyakati linasogea, na iwe kwamba taratibu za hali ya hewa mara kwa marahuondoka kwenye mpango, bado Mungu angebeba wajibu kwa ajili ya matetemeko navimbunga, kwa sababu Yeye ndiye Mwumbaji, na makosa Yake yanawadhuru watu.

Page 22: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

Hakuna Kitu Kinachoitwa “Asili Mama”

Basi, tuna majibu mawili yanayoweza kutolewa kuhusu swala la majanga. AidhaMungu au Shetani wanahusika. Kabla hatujatazama Maandiko fulani ili kuamua jibusahihi, hebu tufikiri zaidi majibu hayo mawili.

Kama Shetani ndiye mwenye kuleta majanga, basi Mungu anaweza au hawezikumzuia. Kama Mungu anaweza kumzuia Shetani asilete majanga na hamzuii, basi hapotena anawajibika. Janga lisingetokea bila ruhusa Yake.

Twende upande wa pili. Hebu tudhani kwamba Mungu hawezi kumzuia Shetani,lakini angetaka. Je, kitu kama hicho kipo?

Ikiwa Mungu hawezi kumzuia Shetani asilete janga, basi ni kwamba Shetani ananguvu zaidi ya Mungu, au Shetani ni mjanja kuliko Mungu. Kimsingi, hicho ndichokinachosemwa na wale wanaosema kwamba “Shetani alipata utawala wa dunia wakatiAdamu alipoanguka.” Wanadai kwamba Shetani ana haki kisheria kufanya chochoteanachotaka hapa duniani kwa sababu yeye aliiba hati miliki ya Adamu. Sasa – tusemekwamba Mungu angependa kumzuia Shetani lakini hawezi kwa sababu inabidi aheshimuhati miliki ya Adamu ambaye sasa iko mikononi mwa Shetani. Maana yake ni kwamba,Mungu alikuwa mjinga kiasi cha kutoweza kuona mambo ambayo yangetokea wakati waanguko la mwanadamu, lakini Shetani, kwa sababu ana akili kuliko Mungu, sasa amepatazile nguvu ambazo Mungu alitaka asiwe nazo. Haiwezekani kuwa hivyo. Shetani hanaakili kuliko Mungu!

Kama nadharia kwamba “Shetani Alifaidika” ni ya kweli, tungetaka kujua ni kwa niniShetani hasababishi matetemeko na vimbunga zaidi kuliko vlivyoko sasa, na kwa ninihalengi idadi kubwa ya Wakristo. (Ukisema “ni kwa sababu Mungu ha tamruhusu alengeidadi kubwa ya Wakristo”, tayari umekubali kwamba Shetani hawezi kutenda chochotebila ruhusa ya Mungu.)

Tukifupisha mambo, majibu mawili tu yanayowezekana ni haya: Aidha (1) Munguhusababisha matetemeko na vimbunga, au (2) Shetani hufanya hivyo kwa ruhusa yaMungu.

Ona hapo kwamba bila ya kujali jibu gani ni sahihi, Mungu bado ndiye mwenyekuwajibika? Watu wanaposema, “Mungu hakutuma kimbunga hicho – ni Shetanialiyefanya kwa ruhusa ya Mungu,” hawamwondolei Mungu wajibu kama wanavyodhani.Kama Mungu angeweza kumzuia Shetani asisababishe kimbunga, bila ya kujali kamaalitaka au hakutaka, bado anawajibika. Binadamu waasi wanaweza kuwa wa kulaumiwakwa sababu ya dhambi zao (ikiwa kimbunga kilitumwa na Mungu au kuruhusiwa naMungu kama hukumu), lakini bado itakuwa upuuzi kusema Mungu hahusiki kwa njiayoyote ile, au hawajibiki.

Ushuhuda wa Maandiko

Je, Maandiko yanasema nini hasa kuhusu “majanga”? Je, Biblia inasema kwambayanaletwa na Mungu au na Shetani? Tuanze kwa kutazama matetemeko kwa sababuBiblia inataja mengi.

Kulingana na Maandiko, matetemeko yanaweza kutokea kama hukumu ya Mungu juuya wenye dhambi wanaostahili. Tunasoma hivi katika Yeremia: “Mbele ya ghadhabu

Page 23: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

yake [Mungu] nchi yatetemeka, wala mataifa hawawezi kustahimili hasira yake”(Yeremia 10:10. Maneno mepesi kukazia).

Isaya anatoa onyo lifuatalo:

Naye atajiliwa na BWANA wa majeshi kwa ngurumo, na tetemeko lanchi, na sauti kuu, na chamchela, na tufani, na mwali wa moto uteketezao(Isaya 29:6. Maneno mepesi kukazia).

Utakumbuka bila shaka katika siku za Musa kwamba nchi ilifunuka na kuwamezaakina Kora na wafuasi wake waasi (ona Hesabu 16:23-34). Hili lilikuwa tendo la hukumuya Mungu kabisa. Mifano mingine ya hukumu ya Mungu kwa matetemeko inapatkanakatika Ezekieli 38:19; Zaburi 18:7; 77:18; Hagai 2:6; Luka 21:11; Ufunuo 6:12; 8:5;11:13; 16:18.

Matetemeko mengine yanayotajwa katika Maandiko si matendo ya hukumu yaMungu, ila yalisababishwa na Mungu. Kwa mfano: Kulingana na injili ya Mathayo,kulikuwa na tetemeko wakati Yesu alipokufa (Mathayo 27:51, 54) na lingine wakatialipofufuka (Mathayo 28:2). Je, Shetani alisababisha hayo?

Wakati Paulo na Sila walipokuwa wanaimba sifa kwa Mungu usiku wa manane katikagereza huko Filipi, “mara kukatokea tetemeko kubwa la nchi, misingi ya gerezaikatikiswa, na mara ile ile milango yote ikafunguliwa, na minyororo ya kila mmojaikalegezwa” (Matendo 16:26. Maneno mepesi kukazia). Je, Shetani ndiye alisababishatetemeko hilo? Hapana. Hata mkuu wa gereza aliokoka baada ya kuona nguvu za Mungu.Na hilo si tetemeko la pekee lililosababishwa na Mungu katika kitabu cha Matendo (onaMatendo 4:31).

Hivi karibuni nilisikia kuhusu Mkristo mwenye nia njema tu, ambaye, baada yakusikia juu ya uwezekano wa kutokea kwa tetemeko katika sehemu fulani, alisafiri hadihapo kwenda kufanya “vita ya kiroho” dhidi ya Shetani. Unaona kosa katika dhana hiyo?Ingekuwa sawa kimaandiko kwake kumwomba Mungu awarehemu hao watu walioishikatika eneo hilo. Na kama angefanya hivyo, asingekuwa na haja ya kupoteza muda wakena fedha kwenda kwenye eneo lenyewe – Mungu angeombwa pale pale nyumbanikwake. Ila, kufanya vita na Shetani ili kuzuia tetemeko si kitu kinachoungwa mkono namaandiko.

Vipi Kuhusu Vimbunga?

Neno kimbunga halipo katika Maandiko, lakini tunaweza kupata mifano ya upepomkali. Kwa mfano:

Washukao baharini katika merikebu, wafanyao kazi yao katika majimengi, hao huziona kazi za BWANA, na maajabu yake vilindini. Maanahusema, akavumisha upepo wa dhoruba, ukayainua juu mawimbi yake(Zaburi 107:23-25. Maneno mepesi kukazia).

Lakini BWANA alituma upepo mkuu baharini, ikawa tufani kubwabaharini, hata merikebu ikawa karibu na kuvunjika (Yona 1:4. Manenomepesi kukazia).

Page 24: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne zanchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu yabahari, wala juu ya mti wowote (Ufunuo 7:1).

Ni dhahiri kwamba Mungu anaweza kuanzisha dhoruba za upepo mkali, na kuzizuia.6

Katika Biblia nzima, kuna mstari mmoja tu unaotaja kwamba Shetani alituma upepo.Ni katika majaribu ya Ayubu. Mjumbe alimletea taarifa hivi: “Upepo mkali ulikujakutoka nyikani, ukaipiga nyumba pande zote, nayo ikawaangukia vijana, nao wamekufa”(Ayubu 1:19).

Kutokana na kusoma sura ya kwanza ya kitabu cha Ayubu tunajua kwmaba Shetanindiye aliyesababisha matatizo kwa Ayubu. Lakini, tusisahau kwamba asingewezakufanya chochote kumdhuru Ayubu au watoto wake bila ya ruhusa ya Mungu. Basi, hapotena tunaona kwamba Mungu anatawala upepo.

Tufani Ya Galilaya

Vipi kuhusu ile “tufani kali” iliyowavamia Yesu na wanafunzi Wake wakati fulaniwalipokuwa wanavuka Bahari ya Galilaya? Bila shaka ilisababishwa na Shetani, maanaMungu asingeweza kutuma upepo ambao ungepindua mtumbwi wenye Mwana Wake!“Ufalme ukifitinika juu yake wenyewe utaanguka.” Basi, kwa nini Mungu atume upepoambao ungeweza kumdhuru Yesu na wanafunzi Wake kumi na wawili?

Hizo ni hoja nzuri, lakini hebu tufikiri kidogo. Kama Mungu hakutuma upepo, na iweni Shetani, basi lazima tukubali bado kwamba Mungu alimruhusu Shetani autume.Hivyo, swali lile lile bado linahitaji kujibiwa: Kwa nini Mungu amruhusu Shetani kutumatufani ambayo ingeweza kumdhuru Yesu na wale kumi na wawili?

Je, kuna jibu? Pengine Mungu alikuwa anawafundisha wanafunzi kuhusu imani.Pengine alikuwa anawapima. Pengine alikuwa anampima Yesu, ambaye ilibidi “ajaribiwekatika mambo yote kama sisi, ila yeye hakutenda dhambi” (Waebrania 4:15). Ili awezekujaribiwa kikamilifu, Yesu ilibidi apitie katika tukio la kumfanya ahofu. Pengine Mungualitaka kumtukuza Yesu. Pengine alitaka kufanya hayo yote yaliyotajwa hapo juu.

Mungu aliwaongoza wana wa Israeli ukingoni mwa Bahari ya Shamu akijua kabisakwamba walikuwa wamenaswa na jeshi la Farao lililowafuatia. Lakini je, hakuwaanawakomboa Waisraeli? Kama ndivyo, mbona alikuwa anajipinga kwa kuwaongozakwenye sehemu ambapo wangeuawa kabisa? Je, huo si mfano wa “ufalme kufitinika juuyake wenyewe”?

Hapana kwa sababu, Mungu hakukusudia kuwaachia Waisraeli waangamizwe. Nayehakukusudia kuwaacha Yesu na wanafunzi Wake kuzama, wakati alipotuma aualipomruhusu Shetani kusababisha tufani katika Bahari ya Galilaya.

Pamoja na hayo – Biblia haisemi kwamba Shetani alituma tufani hiyo katika Bahari yaGalilaya, wala haisemi Mungu ndiye alituma. Kuna wanaosema kwamba ni Shetani kwasababu Yesu aliikemea ikatulia. Sawa, lakini si hoja yenye nguvu. Yesu hakumkemea

6 Maandiko mengine yenye kuthibitisha kwamba Mungu anatawala upepo ni haya: Mwanzo 8:11; Kutoka10:13, 19; 14:21; 15:10; Hesabu 11:31; Zaburi 48:7; 78:76; 135:7; 147:18; 148:8; Isaya 11:15; 27:8;Yeremia 10:13; 51:16; Ezekieli 13:11, 13; Amosi 4:9, 13; Yona 4:8; Hagai 2:17. Katika hiyo mifano mingi,Mungu alitumia upepo kama kifaa cha kuhukumu.

Page 25: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

Mungu – Yeye alikemea upepo. Mungu Baba angeweza kufanya vivyo hivyo. Yaani,angeweza kusababisha tufani kwa neno, kisha akautuliza kwa kuukemea. Kwa kuwaYesu alikemea tufani si uthibitisho kwamba Shetani ndiye aliyeileta.

Hapa tena tusijenge theolojia yetu juu ya mstari mmoja ambao hauthibitishi kituchochote. Tayari tumetaja maandiko mengi yenye kuthibitisha kwamba Mungu ndiyeanayetawala upepo, na mara nyingi inasemekana kwamba Yeye ndiye aliyeutuma. Hojani kwamba, Shetani, hata ingawa ndiye “mungu wa dunia hii,” hana mamlaka huru juu yaupepo, wala hana haki ya kusababisha tufani au kimbunga wakati wowote au mahalipopote anapotaka.

Basi – wakati vimbunga vinapotokea, tusione kana kwamba ni kitu ambacho kiko njeya uwezo wa Mungu – kitu ambacho angependa kukizuia lakini hawezi. Yesualipokemea ule upepo na tufani katika Bahari ya Galilaya ni ushahidi tosha kwambaMungu anaweza kusimamisha tufani akitaka.

Na kama Mungu anatuma (au anaruhusu) tufani, basi lazima awe na sababu fulani, najibu linalofaa zaidi kwa habari ya kutuma au kuruhusu tufani yenye kuleta uharibifumkubwa kabisa ni kwamba, anawaonya na kuwahukumu watu wasiotii.

“Lakini, Wakati Mwingine Vimbunga Hudhuru Wakristo”

Ila sasa – vipi kuhusu Wakristo ambao wanaathiriwa na majanga ya kawaida?Kimbunga kinapopiga mahali, hakibomoi nyumba za wasiokuwa Wakristo tu. Je,Wakristo hawaepushwi na ghadhabu ya Mungu kutokana na kifo cha Yesu kama dhabihukwa ajili yao? Tunawezanje basi kusema kwamba Mungu ndiye anayehusika na majanga,wakati yanaweza kuwadhuru watoto Wake Mwenyewe?

Kwa kweli hayo ni maswali magumu. Ila, tunapaswa kutambua kwamba majibu yakehayatakuwa rahisi kama tutayajenga kwenye dhana potofu kwamba Shetani husababishamajanga. Kama Shetani anasababisha majanga yote, inakuwaje Mungu amruhusukufanya mambo yatakayodhuru watoto wa Mungu Mwenyewe? Bado tatizo ni lile lile.

Lakini Biblia inasema wazi kabisa kwamba walio katika Kristo “si watoto waghadhabu” (1Wathes. 5:9). Pia, inasema kwamba “ghadhabu ya Mungu inawakalia” walewasiomtii Yesu (Yohana 3:36). Sasa – ghadhabu ya Mungu inawezaje kukaa juu yawasiookoka bila ya kuwaathiri walio-okoka, na huku wote wanaishi pamoja? Jibu nikwamba, wakati mwingine haiwezekani, na huo ndiyo ukweli.

Siku zile za Waisraeli kutoka Misri, Waisraeli wote walikuwa wanakaa mahalipamoja, na mapigo ambayo Mungu alituma juu ya Wamisri kama hukumu hayakuwa-athiri (ona Kutoka 8:22, 23; 9:3-7; 24-26; 12:23). Lakini kwa habari yetu, tunaishi nakufanya kazi pamoja na “Wamisri”. Kama Mungu atawahukumu kwa njia ya janga,tutaepukaje?

Kuepuka ndiyo neno muhimu hapa, katika kuelewa jibu la swali letu. Ingawa Nuhualiepuka ghadhabu ya Mungu wakati gharika ilipofunika dunia, bado aliathirika, maanailimbidi afanye kazi kujenga safina, kisha alikaa mwaka mzima na wanyama wengi tukatika safina. (Tusisahau: Agano la Kale pamoja na Agano Jipya humtaja Mungu kuwandiye aliyeleta gharika ya Nuhu, si Shetani. Ona Mwanzo 6:17; 2Petro 2:5).

Lutu pia aliponya maisha yake wakati hukumu ya Mungu ilipokuja juu ya Sodoma naGomora, lakini alipoteza kila kitu katika moto ulioshuka. Hukumu ya Mungu juu yawaovu ilimwathiri mtu mwenye haki.

Page 26: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

Miaka ya baadaye tunaona Yesu akiwaonya waamini waliokuwa Yerusalemu kwambawakimbie watakapoona mji wao umezungukwa na majeshi, maana hizo zitakuwa siku“za ghadhabu” (Luka 21:22, 23) – kuonyesha wazi kabisa makusudi ya ghadhabu yaMungu kwa kuruhusu Warumi kuuzingira Yerusalemu mwaka wa 70 B.K. Sifa kwaMungu kwa Wakristo waliojali maonyo ya Kristo, maana waliponya maisha yao, lakinibado walipoteza kila kitu walichotakiwa kuacha Yerusalemu.

Katika hiyo mifano yote mitato, tunaona kwamba watu wa Mungu wanaweza kutesekakiasi fulani, wakati hukumu ya Mungu inaposhuka juu ya waovu. Basi, hatuwezi kuamuatu kwamba kwa kuwa wakati mwingine Wakristo huathirika na majanga, Mungu hahusikikuyaleta.

Sasa – Tufanye Nini?

Tunaishi katika dunia iliyolaaniwa na Mungu – ambayo inakumbwa na ghadhabu yaMungu wakati wote. Paulo aliandika hivi: “Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa [ sio“itadhihirishwa”] kutoka mbinguni dhidi ya uovu wote na uasi wa wanadamu” (Warumi1:18). Kama wanaoishi katika dunia ovu, iliyolaaniwa na Mungu, hatuwezi kuepukakabisa matokeo ya ghadhabu ya Mungu juu yake, hata ingawa hiyo ghadhabuhaielekezwi kwetu.

Tukijua hayo, tufanyeje? Kwanza: Tumwamini Mungu. Yeremia anaandika hivi:

Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, ambaye BWANA nitumaini lake. Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji,uenezao mizizi yake karibu na mto; hautaona hofu wakati wa hari ujapo,bali jani lake litakuwa bishi; wala hautahangaika mwaka wa uchache wamvua, wala hautaaacha kuzaa matunda (Yeremia 17:7, 8).

Angalia – Yeremia hakusema kwamba mtu anayemtegemea Bwana hatakabiliwa nahari. Hapana. Wakati hari na mwaka wa uchache wa mvua vinapokuja, yule mtuanayemtegemea Bwana ni sawa na mti wenye kueneza mizizi yake pembeni ya kijito.Yeye anakuwa na mahali pengine pa kupatia, wakati dunia inayomzunguka inahangaika.Habari za Eliya kulishwa na kunguru wakati wa njaa huko Israeli ni mfano mmoja (ona1Wafalme 17:1-6). Daudi aliandika hivi kuhusu wenye haki: “Katika siku za njaawatajazwa na vingi” (Zaburi 37:19).

Lakini – njaa haziletwi na Shetani? Hapana – Maandiko hayasemi hivyo. Kwenyehilo, Mungu anawajibika, na njaa mara nyingi husemwa kwamba ni matokeo yaghadhabu Yake kwa watu wanaostahili. Kwa mfano:

Kwa sababu hiyo BWANA wa majeshi asema hivi, ‘Tazama,nitawaadhibu watu hawa; vijana watakufa kwa upanga; wana wao nabinti zao watakufa kwa njaa’ (Yeremia 11:22. Maneno mepesi kukazia).

BWANA wa majeshi asema hivi, ‘Tazama, nitaleta juu yao upanga, nanjaa, na tauni, nami nitawafanya kuwa kama tini mbovu zisizowezakuliwa, kwa kuwa ni mbovu’ (Yeremia 29:17).

Page 27: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

Mwanadamu! Nchi itakapofanya dhambi na kuniasi kwa kukosa,nikaunyosha mkono wangu juu yake na kulivunja tegemeo la chakulachake, na kuipelekea njaa, na kukatilia mbali mwanadamu na mnyama …(Ezekieli 14:13. Maneno mepesi kukazia).

Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache; tena mlipovileta nyumbaninikavipeperusha. Ni kwa sababu gani? Asema BWANA wa majeshi. Nikwa sababu ya nyumba yangu inayokaa hali ya kuharibika, wakati ambaponinyi mnakimbilia kila mtu nyumbani kwake. Basi, kwa ajili yenu mbinguzimezuiliwa zisitoe umande, nayo nchi imezuiliwa isitoe matunda yake.Nami nikaita wakati wa joto uje juu ya nchi, na juu ya milima, na juu yanafaka, na juu ya divai mpya, na juu ya mafuta, na juu ya kila kitu itoachonchi, na juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya kazi zote zamikono (Hagai 1:9-11. Maneno mepesi kukazia).

Katika mfano huu wa mwisho, tunasoma kwamba Waisraeli walilaumiwa kwa sababuya ukame uliotokana na dhambi yao, lakini bado, Mungu anasema Yeye ndiyeameutuma.7

Mungu anapotuma njaa kwa watu waovu, nasi tuwe tunakaa katikati yao,tunachopaswa kufanya ni kuamini kwamba atatupa mahitaji yetu. Paulo alithibitishakwamba njaa haiwezi kututenga na upendo wa Kristo! “Ni nani atakayetutenga naupendo wa Kristo? Je, ni dhiki, au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?”(Warumi 8:35. Maneno mepesi kukazia). Ona kwamba Paulo hakusema Wakristohawatakabiliwa na njaa kamwe. Anaonyesha kwamba wanaweza, japo yeye, kamamwanafunzi wa Maandiko, alijua kwmaba njaa inaweza kutumwa na Mungukuwahukumu waovu.

Utii Na Hekima

Pili – Tunapaswa kuwa watii na kutumia hekima ya Mungu kuepuka kunaswa katikatukio lolote la ghadhabu ya Mungu linalolengwa duniani. Nuhu alijenga safina yake, Lutualielekea vilimani, Wakristo wa Yerusalemu walitoroka mji wao; wote hao ilibidi kumtiiMungu ili kuepuka kunaswa katika hukumu Yake juu ya waovu.

Kama ningekuwa naishi katika eneo linalokumbwa na vimbunga, ningejenga nyumbayenye nguvu ambayo haiwezi kubomolewa, au nyumba ya bei rahisi ambayo ni rahisikuijenga tena! Kisha, ningeomba. Kila Mkristo anapaswa kuomba na kuwa msikivu kwaYule ambaye Yesu aliahidi kwamba “atawajulisha mambo yatakayokuja” (Yohana16:13), ili aweze kuepuka ghadhabu ya Mungu juu ya dunia.

Tunasoma katika Matendo 11 kuhusu nabii Agabo ambaye alionya juu ya njaa kubwaambayo ingewaathiri Wakristo waliokaa Uyahudi. Matokeo ni kwamba Paulo na Barnabawalianza kukusanya sadaka ili kuwasaidia (ona Matendo 11:28-30).

7 Ukitaka kusoma zaidi kuhusu Mungu kuleta njaa, angalia Kumbu. 32:23, 24; 2Samweli 21:1; 24:12, 13;2Wafalme 8:1; Zaburi 105:16; Isaya 14:30; Yeremia 14:12, 15, 15; 16:3, 4; 24:10; 27:8; 34:17; 42:17;44:12, 13; Ezekieli 5:12, 16, 17; 6:12; 12:16; 14:21; 36:29; Ufunuo 6:8; 18:8). Yesu Mwenyewe alisemakwamba Mungu “hunyesha mvua juu ya wenye haki na waovu” (Mathayo 5:45). Mungu anatawala mvua!

Page 28: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

Je, mambo kama hayo yanaweza kutokea leo? Hakika, maana Roho Mtakatifuhajabadilika, wala upendo wa Mungu haujapungua. Ila, ni bahati mbaya sana kwambabaadhi ya watu katika mwili wa Kristo siku hizi hawako wazi kwa karama namadhihirisho ya aina hiyo ya Roho Mtakatifu, na kwa sababu hiyo, “wanamzimishaRoho” (1Wathes. 5:19) na kukosa mambo bora ya Mungu.

Katika kitabu kuhusu maisha yake, Marehemu Demos Shakarian, mkuu namwanzilishi wa huduma ya Full Gospel Businessmen, anaeleza jinsi ambavyo Mungualizungumza na Wakristo waliokaa nchi ya Armenia mwishoni mwa miaka ya 1800, kwakupitia nabii mvulana aliyekuwa hajui kusoma wala kuandika. Aliwaonya juu ya mauajimakubwa yanayokuja, na matokeo ni kwamba, Wakristo Wapentekoste ambao waliaminimambo ya namna hiyo walikimbia nchi, pamoja na babu zake Shakarian. Muda mfupibaadaye, Waturuki walivamia Armenia, na WaArmenia zaidi ya milioni moja waliuawa,ikiwa ni pamoja na wale Wakristo waliokataa kusikia maonyo ya Mungu.

Tutakuwa na busara sana tukidumu kuwa wasikivu kwa Roho Mtakatifu na kumtiiMungu, la sivyo tutajikuta tunapitia katika ghadhabu ya Mungu ambayo Yeye hakutakatuipitie. Kuna wakati Elisha alimwambia mwanamke mmoja hivi: “Ondoka, ukaendewewe na jamaa yako, ukae hali ya kigeni utakakoweza kukaa; kwa sababu BWANAameiita njaa; nayo itakuja juu ya nchi hii muda wa miaka saba” (2Wafalme 8:1).Ingekuwaje kama huyo mwanamke angepuuzia ushauri wa nabii?

Tunasoma katika kitabu cha Ufunuo onyo la ajabu sana kwa watu wa Mungu, kwambawatoke “Babeli” wasije wakanaswa katika hukumu ya Mungu juu yake.

Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema, ‘Tokeni kwake[Babeli] enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigoyake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Munguamekumbuka maovu yake … Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakujakatika siku moja, mauti na huzuni na njaa, naye atateketezwa kabisa kwamoto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu(Ufunuo 18:4, 5, 8. Maneno mepesi kukazia).

Tunapohitimisha, tuseme hivi: Mungu ni mwenyezi – anatawala hali ya hewa namajanga. Amejithibitisha Mwenyewe kama Bwana juu ya nguvu za asili katika Biblia –kuanzia kusababisha mvua siku arobaini wakati wa Nuhu, hadi aliponyesha mvua yamawe pamoja na kutuma mapigo mengine juu ya adui za Israeli, hadi kusababisha kwakeupepo mkali dhidi ya merikebu ya Yona, hadi kukemea Kwake ile tufani katika Bahari yaGalilaya. Kama Yesu alivyosema, Yeye ni “Bwana wa mbingu na nchi” (Mat hayo11:25). Ukitaka ushahidi zaidi wa Maandiko kuhusu mamlaka na ukuu wa Mungu juu yanguvu za asili, angalia katika Yoshua 10:11; Ayubu 38:22-38; Yeremia 5:24; 10:13;31:35; Zaburi 78:45-49; 105:16; 107:33-37; 135:6, 7; 147:7, 8, 15-18; Mathayo 5:45;Matendo 14:17.

Majibu Kwa Maswali Machache

Kama Mungu anawahukumu watu kwa njia ya njaa, gharika na matetemeko, je, nimakosa kwetu sisi kama wawakilishi wa Mungu, kusaidia na kupunguza makali yamateso ya wale watu ambao Mungu anawahukumu?

Page 29: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

Hapana, kamwe. Tunapaswa kutambua kwamba Mungu anampenda kila mtu, pamojana wale watu anaowahukumu. Japo litashangaza masikio yetu, hukumu Yake kwa njia yamajanga ni onyesho la upendo Wake. Inawezekanaje? Ni hivi: Kupitia matatizo namagumu ambayo yanaletwa na majanga, Mungu anawaonya watu anaowapenda kwambaYeye ni mtakatifu na mwenye kuhukumu, na kwamba kuna malipo kwa ajili ya dhambi.Mungu anaruhusu mateso ya muda ili kuweza kuwasaidia watu waamke na kuona hitajilao la Mwokozi – ili waepuke ziwa la moto. Huo ni upendo!

Muda wote ambapo watu wanapumua, Mungu bado anawaonyesha rehemawasiyostahili, na unakuwepo bado wakati wao kutubu. Kupitia huruma yetu na msaada,tunaweza kuonyesha upendo wa Mungu kwa watu wanaopitia ghadhabu Yake ya muda,lakini ambao wanaweza kuokoka na ghadhabu Yake ya milele. Majanga ni nafasi nzuri tuza kuwafikia watu wa dunia ambao Yesu aliwafia.

Je! Kitu muhimu kuliko vyote maishani si kuwafikishia watu ujumbe wa Injili?Tunapokuwa na mtazamo wa milele, mateso ya wale walionaswa katika majanga si kituukilinganisha na mateso ya wale watakaotupwa katika ziwa la moto.

Ni kweli pia kwamba watu huwa wasikivu kwa Injili wanapokuwa katika mateso.Kuna mifano mingi sana katika Biblia kuhusu ajabu hii, kuanzia toba ya Israeli wakati wamateso kutoka kwa mataifa jirani, mpaka habari ya Yesu kuhusu mwana mpotevu.Wakristo wanapaswa kutazama majanga kama nyakati ambapo mavuno yamekwishakuiva, tayari kuvunwa.

Hebu Tuseme Ukweli

Sasa – ujumbe wetu uweje, kwa watu wanaojaribu kurejelea hali ya kawaida kimaishabaada ya kimbunga au tetemeko? Tutawajibuje kama watataka jibu la kitheolojia kuhusuyaliyowapata? Hebu tuseme kweli inayofundishwa na Biblia, na kuwaambia watukwamba Mungu ni mtakatifu na kwamba dhambi yao ina malipo. Tuwaambie kwambaile kelele kubwa sana ya kimbunga ni mfano mdogo tu wa nguvu ambazo MwenyeziMungu anazo, na hofu waliyosikia wakati nyumba yao ilipotikiswa si kitu ukilinganishana hofu itakayowashika watakapotupwa jehanamu. Na, tuwaambie kwamba, ingawa sisisote tunastahili kutupwa jehanamu, Mungu anaturehemu na kutupa sisi muda wa kutubuna kumwamini Yesu, ambaye kwa njia Yake tutaokolewa na ghadhabu ya Mungu.

Wengine watasema, “Tusiwatishe watu kuhusu Mungu.” Jibu linatoka katikaMaandiko, hivi: “Kumcha Bwana ni mwanzo wa maarifa” (Mithali 1:7). Watuwasipomcha (au kumwogopa, kumheshimu) Mungu, hawajui kitu chochote.

Itakuwaje Kama Watu Watamkasirikia Mungu?

Je, watu hawatamkasirikia Mungu kwa sababu ya mateso yao? Labda, lakini tunahitajikuwasaidia waone kiburi chao, kwa upole. Hakuna mwenye haki ya kumlalamikiaMungu kwa mambo anayomtendea, kwa sababu sote tunastahili kutupwa katika ziwa lamoto tangu zamani. Badala ya kumlaani Mungu kwa yanayowapata, watu wanatakiwakumsifu kwa kuwapenda kiasi hicho, cha kuwaonya. Mungu ana kila haki ya kumpuuzakila mtu, na kuwaacha wote wafuate njia zao wenyewe kuelekea jehanamu. LakiniMungu anawapenda watu, Naye anawaita kila siku. Anawaita kimya kimya kwa mauayanayochanua kwenye miti ya matunda, kwa nyimbo za ndege, kwa ukuu wa milima, na

Page 30: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

kwa kung’aa kwa nyota nyingi kila siku. Anawaita kupitia dhamiri zao, kupitia mwiliWake yaani Kanisa, na kwa njia ya Roho Mtakatifu. Lakini, wanapuuza mwito Wake.

Kwa hakika si mapenzi ya Mungu kwa watu kuteseka, lakini wanapoendeleakumpuuza, anawapenda kiasi cha kutosha kutumia njia zingine kali zaidi ili kuwafanyawamsikilize. Vimbunga, matetemeko, gharika, na njaa ni baadhi ya njia zingine kali.Mungu hutazamia kwamba majanga kama hayo yatashusha viburi vya watu nakuwafikisha mahali pa kuwa na akili ya kuelewa.

Je, Mungu Anakuwa Hajatenda Haki?

Tunapomtazama Mungu na dunia yetu kwa mtazamo wa KiBiblia, hapo ndipotunapokuwa tukifanya sahihi. Mtazamo wa KiBiblia ni kwamba kila mtu anastahilighadhabu ya Mungu, ila, Yeye ni mwenye rehema. Wakati watu wanaotesekawanaposema kwamba wanatazamia kutendewa vizuri zaidi na Mungu kuliko inavyokuwawakati huo, Mungu hujisikia vibaya. Ni kwamba kila mtu anapokea rehema nyingi zaidisana kuliko anavyostahili.

Katika kufafanua zaidi jambo hili, Yesu wakati mmoja alisema kitu kuhusu majangamawili yaliyotokea katika siku Zake. Tunasoma hivi katika Injili ya Luka:-

Na wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha habari ya Wagalilayawale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao. Akawajibuakawaambia, ‘Je! Mwadhani ya kwamba Wagalilaya hao walikuwa wenyedhambi kuliko Wagalilaya wote, hata wakapatwa na mambo hayo?Nawaambia, Sivyo. Lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyohivyo. Au wale kumi na wanane, walioangukiwa na mnara huko Siloamu,ukawaua, mwadhani ya kwamba wao walikuwa wakosaji kuliko watuwote waliokaa Yerusalemu? Nawaambia, Sivyo. Lakini msipotubu, ninyinyote mtaangamia vivyo hivyo’ (Luka 13:1-5).

Ni hivi: Wagalilaya waliokufa kwa mkono wa Pilato wasingeweza kusema, “Munguhajatutendea haki, maana hajatuokoa na Pilato!” Hapana. Wao walikuwa wenye dhambiwaliostahili kufa. Tena, kulingana na Yesu, wale Wagalilaya waliopona wangekosea sanakama wangefikia uamuzi kwamba wao hawana dhambi nyingi sana kama jirani zaowaliouawa. Hawakuwa wamefanya kazi ili kupata upendeleo mkubwa kutoka kwaMungu – ni kwamba walipewa rehema zaidi.

Ujumbe wa Kristo ulikuwa wazi kabisa: “Ninyi nyote ni wenye dhambi. Dhambi inamatokeo yake. Kwa sasa, mnaishi kutokana na rehema za Mungu. Basi, tubuni kablamuda haujawaishia na ninyi.”

Akamalizia maelezo Yake kuhusu majanga hayo kwa kutoa mfano juu ya rehema zaMungu, kama ifuatavyo:

Akanena mfano huu: Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katikashamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate.Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, ‘Tazama, miaka mitatuhii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu. Uukate, mbonahata nchi unaiharibu?’ Akajibu akamwambia, ‘Bwana, uuache mwaka huu

Page 31: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileMaelezo Ya Kristo Kuhusu Nguvu Za Shetani Wakati mmoja Yesu alisema kitu kuhusu kuanguka kwa Shetani kutoka mbinguni kitakachotusaidia

nao, hata niupalilie, niutilie samadi; nao ukizaa matunda baadaye, vema!La usipozaa, ndipo uukate’ (Luka 13:6-9).

Hapa, haki na rehema za Mungu vinaonekana. Haki ya Mungu inasema, “Ukate mtiusio na faida!” Lakini rehema Zake zinasema, “Hapana! Upe muda zaidi wa kuzaamatunda.” Kila mtu asiye na Kristo ni kama mti huo.

Je, Tunaweza Kukemea Vimbunga Na Gharika?

Swali moja la mwisho kuhusu majanga. Hivi, tukiwa na imani ya kutosha, hatuwezikukemea na kuzuia majanga kutokea?

Kuna na imani maana yake kuamini mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa. Basi, imanilazima ijengwe juu ya Neno la Mungu. Bila hivyo inakuwa si imani, bali ni tumaini autarajio tu. Katika Biblia, hatupati mahali penye kutuahudi kwamba tunaweza kukemea nakutuliza vimbunga. Basi, hakuna jinsi mtu anavyoweza kuwa na imani ya kufanya hivyo(isipokuwa kama Mungu atampa imani hiyo kwa enzi Yake na mamlaka Yake).

Tufafanue zaidi. Njia ya pekee ya mtu kuwa na imani ya kukemea kimbunga ni kamaana uhakika kwamba Mungu hatai kimbunga hicho kipige eneo fulani. Kamatulivyojifunza katika Maandiko, Mungu ndiye mwenye kutawala upepo, Naye anahusikakabisa na vimbunga. Basi, ni kitu kisichowezekana kwa mtu kuwa na imani thabitikwamba anaweza kuzuia kimbunga wakati Mungu Mwenyewe ameagiza kiwepo. Labdatofauti kwa hilo ni kama Mungu angebadilisha mpango Wake juu ya kimbunga hicho,ambayo inawezekana kama itikio Lake kuhusu maombi ya mtu kwamba awe na rehema,au itikio Lake kwa t oba ya watu wale ambao alikuwa anataka kuwahukumu (habari zaNinawi katika siku za Yona ni mfano rahisi). Lakini, hata kama Mungu angebadilishamawzo Yake, bado si rahisi mtu awe na imani ya kukemea na kutuliza kimbunga bila mtuhuyo kujua kwamba Mungu kabadilisha mawazo Yake na pia kwamba Mungu alitakayeye akemee na kuzuia kimbunga hicho.

Mtu pekee aliyekemea na kuzuia upepo mkali alikuwa Yesu. Njia ya pekee kwetu sisikufanya hivyo ni kama Mungu angetupa “karama ya imani” (au karama ya “imanimaalum” kama inavyoitwa wakati mwingine), ambayo ni mojawapo katika zile karamatisa za Roho zinazotajwa katika 1Wakorintho 12:7-11. Sawa na karama zingine zote zakiroho, karama ya imani hutenda kazi kama Roho apendavyo, si kama sisi tupendavyo(ona 1Wakor. 12:11). Basi, Mungu asipokupa wewe imani maalum ya kukemeakimbunga kinachokuja, usisimame katika njia yake, ukijifanya kwamba unatenda hivyokwa imani. Ondoka njiani – kipishe kabisa! Pia, omba ulinzi wa Mungu na umwombeawe na rehema kwa watu wale wanaohukumiwa, ukimwomba aponye maisha yao iliwapate muda zaidi wa kutubu.

Tazama: Wakati Paulo alipokuwa amefungwa kwenye merikebu kuelekea Rumi, namerikebu hiyo ikasukumwa na tufani kali baharini kwa majuma mawili, hakukemea ilibahari itulie (Matendo 27:14-44). Ni kwa sababu asingeweza. Ona pia kwamba Mungualiwahurumia watu wote waliokuwa merikebuni, maana wote 276 waliokoka baada yamerikebu kuvunjika (ona Matendo 27:24, 34, 44). Ni dhahiri kwamba Mungualiwahurumia kwa sababu Paulo alimwomba awahurumie.