11
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected] HABARI ZA NISHATI &MADINI Toleo No. 83 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Septemba 4 - 10, 2015 Bulletin News http://www.mem.go.tz TANESCO mwarobaini wa kuanguka nguzo huu hapa Tanzania kuwa ya kwanza kwa kuzalisha Graphite Soma habari Uk. 3 UK 2 >> Kuiga usimikaji wa nguzo wa Mongolia >> Kutanguliza chini nguzo ndogo ya zege

MEM 83 Online.pdf

Embed Size (px)

Citation preview

Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

Habari za nisHati &madini

Toleo No. 83 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Septemba 4 - 10, 2015

BulletinNews

Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

http://www.mem.go.tz

HABARI ZA NISHATI &MADINI

Toleo No. 51 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - 23-29 Januari , 2015

JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini Stephen Masele

Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga

Mkurugenzi Mtend-aji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dk. Lutengano Mwakahesya

Wabunge Soma habari Uk. 2

Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2

TANESCO mwarobaini wa kuanguka nguzo huu hapa

Tanzania kuwa ya kwanza kwa kuzalisha Graphite Soma

habari Uk. 3

UK2

>> Kuiga usimikaji wa nguzo wa Mongolia >> Kutanguliza chini nguzo ndogo ya zege

2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Na Mwandishi wetuMongolia

Kwa hakika miongoni mwa gharama kubwa ambazo Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limekuwa likitumia katika kuhakikisha

Watanzania na taifa kwa ujumla linakuwa na umeme wa uhakika na usiokatika ni ununuzi wa nguzo kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

Kwani hakuna asiyeelewa kwamba ili umeme ufike katika eneo lake au nyumba yake lazima nguzo zisimikwe halafu nyaya za umeme zipite juu yake na kufanya

nguzo kuwa kiungo muhimu sana katika sekta nzima ya nishati ya umeme.

Kwa sehemu kubwa ya nchi yetu ambayo imepata umeme nguzo ndiyo zilizotumika kupitisha waya wa umeme juu yake kwani kwa sasa bado sehemu ndogo na baadhi ya maeneo ndiyo ambayo nyaya za umeme zimepita chini ya ardhi (Underground cable) kupeleka umeme sehemu fulani.

Hivi karibuni Ujumbe wa maofisa waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini ulifanya ziara ya mafunzo nchini Mongolia kujifunza namna ambavyo walivyofanikiwa katika uchimbaji mdogo wa madini.

Pamoja na mafunzo hayo lakini katika pita pita za ujumbe huo miongoni mwa

mambo mengine ambayo walijifunza wakiwa katika mitaa mbalimbali ya mji wa Ulaanbataar, Mongolia ni namna walivyobuni usimikaji wa nguzo za umeme ili zisioze na kuanguka kutokana na kuoza kutokana na kuliwa na wadudu au maji na mvua.

Katika nchi ya Mongolia nguzo zilizosimikwa chini ya ardhi ni nguzo ndogo na fupi za zege halafu juu yake zimeunganishwa na nguzo za mbao ambazo kwa namna yoyote ile hazigusi maji au tope chini ya ardhi hali inayofanya nguzo hizo kudumu kwa kipindi kirefu.

Kwa hapa nchini Tanzania tumekuwa tukipata changamoto kubwa ya nguzo kuanguka kutokana na kuoza hasa katika kipindi cha mvua au katika maeneo yenye

tope mathalan maeneo ya Jangwani Dar es Salaam, Maswa - Simiyu na maeneo mengine mbalimbali.

Wataalam wa umeme wa Wizara ya Nishati na Madini, Idara ya ya Nishati pamoja na TANESCO wanaweza kujifunza kutoka Mongolia namna ya kutumia nguzo hizo ndogo na fupi kusimika chini ya ardhi na huku nguzo ya mbao kuunganishwa juu yake ili kuepuka usumbufu wa kubadilisha nguzo mara kwa mara zinapoanguka kutokana na sababu ya kuoza kutokana na kuliwa na wadudu pamoja maji halikadhalika kuepuka usumbufu kwa wateja kutokana na umeme kukatika kutokana na kuanguka kwa nguzo za umeme hasa katika kipindi cha mvua.

TANESCO mwarobaini wa kuanguka nguzo huu hapa

Maboresho makubwa kufanyika Idara ya madiniNa Mwandishi wetuMongolia

Wizara ya Nishati na Madini kupitia Idara ya Madini inatarajia kusaini Makubaliano ya Awali (Memorandum

of Understanding; MoU) kati yake na Wizara ya Madini ya nchini Mongolia ili kushirikiana kuboresha sekta ya madini hususan kwa wachimbaji wadogo.

Kamishna wa Madini Tanzania Mhandisi Paul Masanja alibainisha hayo alipokutana na Uongozi wa Wizara ya Madini ya Mongolia na kukubaliana kufanya kazi kwa pamoja ili Tanzania iweze kujifunza kutoka Mongolia kutokana na nchi hiyo kupiga hatua kubwa katika sekta ya madini hasa kwa wachimbaji wadogo ambao huchangia pato la taifa hilo.

Kamishna Masanja pamoja na ujumbe wake uliotembelea Mongolia, ulijifunza mambo mengi ambayo amekubaliana na watendaji wa Idara yake kuanza kutekeleza mara moja baadhi ya maeneo ikiwamo kuwashawishi na kuwaelimisha wachimbaji wadogo kuunda vikundi ambavyo vitafanya kazi kwa pamoja ya kuchimba madini badala ya kila mchimbaji kushiriki katika uchimbaji huo akiwa peke yake.

Alisema hiyo itawasaidia kuwa na mitaji ya kutosha na pia inakuwa rahisi kwa Serikali kuweza kuwapatia ruzuku na mikopo kama ambavyo hivi sasa Wizara iko katika hatua za mwisho za kuwakabidhi ruzuku wachimbaji hao wadogo ambao baadhi wako katika vikundi na wengine wanajishughulisha na biashara hiyo wakiwa peke yao.

Aidha, ujumbe huo wa Wizara ya

Nishati na Madini ulijifunza umuhimu wa kutembelea maeneo ya wachimbaji wadogo mara kwa mara ili kuweza kutoa elimu ya afya migodini na namna ya kuepuka ajali ndani ya migodi halikadhalika uchimbaji bora na wa kisasa wa madini.

Maeneo mengine ya kujifunza ambayo Mongolia imefanikiwa kwa kiasi kikubwa ni ushirikiano mkubwa na wa dhati katika Wizara ya tawala za mikoa na Serikali za Mitaa inayojumuisha Wakuu wa mikoa, Wilaya na Madiwani, Wizara ya Madini pamoja na wachimbaji wadogo kwa kuwatambua wachimbaji wadogo kama sekta halali na inayochangia pato la taifa.

Kutokana na ushirikiano huo Wizara ya Madini, Viongozi wa vitongoji na manispaa pamoja na wachimbaji wadogo wanashirikiana vizuri kila upande unatekeleza majukumu yake ipasavyo

kulingana na nafasi yake.Jambo kubwa ambalo ujumbe huo

ulivutiwa ni namna wachimbaji hao wadogo wanavyoheshimu na kufuata maelekezo ya Serikali na Manispaa bila hata ya kuwapo kwa sheria inayowaongoza kwani Serikali ikitoa amri hakuna anayepinga na wote wanaheshimu.

Miongoni mwa hatua ambazo Serikali ya nchi hiyo imefanikiwa katika sekta ya madini ni kuhakikisha kwamba hakuna madini yoyote yanauzwa na wachimbaji au madalali nje ya Mongolia kwani madini yote yanauzwa katika benki kuu ya nchi hiyo na si vinginevyo na mwenye mamlaka ya kuuza madini hayo nje ya nchi au kwa wanunuzi wengine wa nje.

Mongolia inafanya vizuri katika kuweka rekodi nzuri za Idadi ya Wachimbaji madini pamoja na watu wengine wanaojishughulisha na biashara nyingine mbali na madini wakiwamo wafugaji, wakulima na shughuli nyingine zinazochangia pato la taifa lao. Wizara ya Nishati na Madini inatakiwa kuiga Mongolia kwa kushirikiana na Ofisi ya taifa ya takwimu (National Bureau of Statistics) ili kufanya utafiti katika maeneo ya wachimbaji wadogo ili kupata rekodi ya idadi ya wachimbaji wadogo waliopo nchini.

Aidha, suala la utunzaji na uboreshaji wa mazingira limepewa kipaumbele kikubwa jambo linalofanya hata wananchi wenyewe kujali mazingira ya nchi ikiwamo wananchi wenyewe kushiriki katika kurekebisha (rehabilitation) maeneo yote yaliyokuwa yakitumika kuchimba madini na maeneo hayo kurudi katika mazingira ya uoto kama ilivyokuwa awali.

Mongolia ni taifa la mfano wa kuigwa katika mafanikio waliyoyapata katika sekta ya uchimbaji madini mdogo kwani wachimbaji wadogo wa nchi hiyo pia wamewekewa utaratibu mzuri wa kuwa wanachama wa mifuko ya jamii ambapo hupata bima mbalimbali ikiwamo za ajali kazini pamoja na afya kwa ujumla jambo ambalo hata Tanzania inatakiwa kuliangalia hilo kwa kina. Idara ya Madini imejifunza mengi katika ziara waliyoifanya na tunaamini kuona mabadiliko baada ya ziara hiyo hususan kwa wachimbaji wadogo.

MAFUNZO KUHUSU MAFUTA NA GESI

Washiriki kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi nyingine za Serikali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mafunzo kuhusu gesi na mafuta jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Kampuni ya ICF International.

3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

TahaririMEM

Na Badra Masoud

Five Pillars oF reForms

KWa HaBari PiGa simU KitenGo cHa maWasiliano

Bodi ya uhariri

Mhariri MkUU: Badra MasoudMSaNifU: Essy Ogunde

WaaNdiShi: Veronica Simba, asteria Muhozya, Greyson Mwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, rhoda James ,

Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

increase eFFiciencyQUality delivery

oF Goods/service

satisFaction oF tHe client

satisFaction oF BUsiness Partners

satisFaction oF sHareHolders

tel-2110490FaX-2110389

moB-0732999263

TANESCO nguzo za zege mwarobaini wa kukatika kwa umeme

tel-2110490FaX-2110389

moB-0732999263

Tanzania kuwa ya kwanza kwa kuzalisha madini ya Graphite

Na Zuena Msuya, Perth- Australia

Tanzania inatarajia kuwa mzalishaji namba moja duniani wa madini ya graphite y a n a y o t u m i w a

viwandani baada ya kiwango kikubwa cha madini hayo kugunduliwa nchini.

Akizungumza katika mkutano wa Africa Down Under (ADU) nchini Australia, Kamishina wa Madini Nchini, Mhandisi Paul Masanja alisema makampuni mengi yamejitokeza kutaka kuchimba madini hayo nchini Tanzania na endapo yataanza uzalishaji huo, Tanzania itakuwa ya kwanza duniani kwa uzalishaji.

Alisema kuwa, madini hayo tayari yameonekana kupata soko kubwa katika nchi zenye viwanda vingi kama vile China kwa kuwa yamekuwa yakitumika viwandani katika

kutengeneza vifaa vinavyotumia umeme kama vile vyombo vya Mawasiliano pamoja na betri.

“Takribani tani milioni 158 ya madini ya graphite yamegundulika nchini Tanzania hadi sasa kupitia watafiti kadhaa wanaoendesha utafiti wa madini hayo. Aidha, mashapo ya madini hayo yaliyogundulika huko Nachingwea, Epanko (Mahenge) na Mererani (Simanjiro) yameonekana kuwa na ubora wa hali ya juu,” alisema Masanja.

Aliongeza kuwa Kampuni ya Uranex imegundua graphite iliyo na ubora wa hali ya juu huko Kusini mwa Tanzania, hivyo kinachofanyika sasa ni kukamilisha taratibu za kuwapatia leseni ya kuchimba, pamoja na kusaini mkataba wa kuendeleza mradi huo (Mining Development Agreement) ili waanze uzalishaji.

Alisema hatua hiyo itaifanya Tanzania kuacha kutegemea

madini ya dhahabu zaidi katika kupata fedha za kigeni (export earnings) kupitia mauzo ya madini nje ya nchi.

Alisisitiza kuwa tayari Kampuni za Uranex, Peak Resources na Kibaran ambazo zote zinatoka Australia zipo kwenye hatua nzuri ya kuanzisha migodi ya kuzalisha madini ya graphite nchini Tanzania.

Kwa upande wa madini ya nickel, Mhandisi Masanja alisema Tanzania ina hazina kubwa ya madini hayo katika maeneo mbalimbali nchini na tayari baadhi ya makampuni yamefanya upembuzi yakinifu wa awali na kinachosubiriwa sasa ni kupanda kwa bei ya soko la dunia la madini hayo ili kampuni zilizowekeza zianze uzalishaji.

Alitaja kampuni hizo ni pamoja na Kabanga Nickel ya Canada, IMX Resources na Kibaran Resources ambazo ni za Australia.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limekuwa likitumia gharama kubwa katika manunuzi ya nguzo za umeme ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha kuwa Watanzania na Taifa kwa ujumla linakuwa na umeme wa uhakika na usiokatika.

Pamoja na Shirika hili kutumia gharama kubwa kwa ajili ya manunuzi ya nguzo, bado kumekuwepo na changamoto ya nguzo hizo za mbao kuanguka mara kwa mara hususan kipindi cha mvua hali inayopelekea kukatika kwa umeme na kusababisha hasara kubwa kwa Taifa kwa kuwa shughuli nyingi za kiuchumi zinasimama.

Ikumbukwe kuwa hakuna nchi yoyote duniani iliyopiga hatua katika maendeleo yake bila nishati ya umeme. Nishati ya umeme ni muhimu mno katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Hivi karibuni ujumbe wa Maofisa Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini ulifanya ziara katika nchi ya Mongolia lengo likiwa ni kujifunza namna ambavyo walivyofanikiwa katika uchimbaji mdogo wa madini.

Mbali na kujifunza kuhusu Sekta ya Madini, Maofisa Waandamizi wakiwa katika mitaa mbalimbali ya mji wa Ulaanbataar, Mongolia walipata fursa ya kujionea miundombinu ya umeme ambapo waliona namna Mongolia walivyobuni usimikaji wa nguzo za umeme ili zisioze na kuanguka kutokana na kuoza kutokana na kuliwa na wadudu au maji na mvua.

Katika nchi ya Mongolia nguzo zilizosimikwa chini ya ardhi ni nguzo ndogo na fupi za zege halafu juu yake zimeunganishwa na nguzo za mbao ambazo kwa namna yoyote ile hazigusi maji au tope chini ya ardhi hali inayofanya nguzo hizo kudumu kwa kipindi kirefu.

Kwa hapa nchini TANESCO imekuwa ikipata changamoto kubwa ya nguzo kuanguka kutokana na kuoza hasa katika kipindi cha mvua au katika maeneo yenye tope mathalan maeneo ya Jangwani Dar es Salaam, Maswa- Simiyu na maeneo mengine mbalimbali.

Wataalam wa umeme kutoka Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO wanaweza kujifunza kutoka katika nchi ya Mongolia kwa kutumia nguzo zilizotengenezwa kwa zege chini na hivyo kuondokana na changamoto ya nguzo kuoza na kuanguka mara kwa mara na Serikali kuingia gharama ya kuagiza nguzo mpya mara kwa mara kutoka ndani na nje ya nchi.

Kamishna wa Madini Nchini, Mhandisi Paul Masanja akiwasilisha mada katika mkutano wa Africa Down Under 2015 (ADU), mjini Perth Australia.

4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

‘Africa Down Under 2015’ kuvutia wawekezaji zaidi TanzaniaNa Zuena Msuya, Perth- Australia

Serikali ya Tanzania imeendelea kutangaza fursa za uwekezaji katika sekta ya madini ili kuvutia mataifa mengi kuja kuwekeza nchini katika sekta

hiyo kutokana na kuwepo kwa madini mengi yanayoendelea kugunduliwa nchini kwa lengo la kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Hayo yameelezwa na Kamishna wa Madini Nchini, Mhandisi Paul Masanja

wakati wa Mkutano wa kumi na tatu wa Uwekezaji wa madini nchini Australia ujulikanao kama Africa Down Under 2015 (ADU) unaoandaliwa na chama cha wenye mitaji na waendelezaji miradi nchini Australia ambapo Tanzania inashiriki kwa mara ya tano.

Mhandisi Masanja alisema kuwa, kwa Tanzania kushiriki katika mkutano huo ni muhimu sana kwani inatoa fursa kwa wawekezaji makini duniani katika sekta ya madini kutambua fursa zilizopo Tanzania na hatua ambazo Serikali imekuwa ikizichukua ili kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini.

Akiwasilisha mada katika mkutano

huo, Mhandisi Masanja alielezea aina mbalimbali za madini yanayopatikana nchini, maendeleo ya sekta ya madini kwa miaka 15 iliyopita, miradi mipya ya madini iliyoibuliwa na wadau katika sekta, na hatua ambazo Serikali imezichukua hivi karibuni ili kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta ya madini.

Alitaja hatua hizo ni pamoja na kuanza kupokea maombi na malipo ya ada za leseni za madini kwa njia ya mtandao, kusainiwa kwa Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji Nchini (Tanzania Extractive Industries Transparency Initiatives Act of 2015), ujenzi wa miundombinu muhimu kwa ajili

ya miradi ya madini (umeme na barabara), na upatikanaji wa taarifa muhimu za kijiolojia chini ya utafiti uliofanywa na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST).

Kupitia taarifa hiyo, aliwataka wawekezaji makini kuelekeza mitaji yao na teknolojia nchini Tanzania kwani kuna uhakika mkubwa wa kufanikisha kurejesha fedha zao na kupata faida.

Mhandisi Masanja alisisitiza kwamba, Tanzania inayo mazingira yote wezeshi kwa wawekezaji katika sekta ya madini kuendesha shughuli zao kwa uhuru na uwazi bila kuingiliwa na Serikali, ili mradi tu wanaheshimu sheria zilizopo.

Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika mkutano wa Africa Down Under 2015 (ADU), uliofanyika mjini Perth nchini Australia.

5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

Mtwara kutoa leseni za madini ndani ya siku mojaNa Greyson Mwase, Mtwara

Ofisi ya Madini, Kanda ya Kusini yenye ofisi zake mjini Mtwara imeanza kutoa huduma za leseni za utafutaji na

uchimbaji wa madini ndani ya siku moja tofauti na ilivyokuwa awali.

Hayo yalisemwa na Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Aidan Mhando katika mafunzo kuhusu huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal; OMCTP) yaliyoshirikisha wachimbaji wa madini mkoani Mtwara.

Mhando alisema kuwa awali maombi yalikuwa yakichukua muda mrefu kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya mtandao na kuongeza kuwa ofisi yake imeboresha mtandao na kuanza kutoa leseni ndani ya siku moja.

Alisema ofisi yake ina uwezo wa kushughulikia ombi moja la leseni ndani ya nusu saa iwapo mwombaji atakuwa amekamilisha vigezo vyote vinavyotakiwa.

Alieleza kuwa tangu huduma ya mtandao iboreshwe ofisi ya madini imekuwa na uwezo wa kushughulikia maombi 20 kwa siku tofauti na awali ambapo ilikuwa inachukua muda mrefu.

Akielezea mikakati ya ofisi yake katika utekelezaji wa mfumo mpya wa utoaji wa huduma za leseni kwa njia ya mtandao, Mhando alisema ofisi imejipanga kwa zoezi la kuhakikisha kuwa wateja wake wote wanaingizwa katika mfumo huo na kunufaika na huduma husika.

Aliongeza kuwa ili kuwafikia wachimbaji wa madini ya chumvi ambao idadi yako kubwa ni wazee, ofisi yake imeweka utaratibu wa kuwatembelea kwenye maeneo yao ya kazi, kuwapa elimu pamoja na kuwasajili kwenye mfumo huo.

Akielezea faida za mfumo mpya wa huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao, Mhando alisema kuwa mfumo utawawezesha wamiliki wa leseni za madini kupata taarifa za leseni zao wakati wowote pamoja na kufanya malipo ya leseni zao kwa njia ya mtandao yaani M-Pesa, Airtel Money na Tigo Pesa

“Mfumo huu utapunguza migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara kati ya wachimbaji na kuondoa dhana ya kwamba kuna upendeleo kwenye utoaji wa leseni za madini.” Alisema Mhando.

Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Aidan Mhando ( wa nne kutoka kushoto, waliokaa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Wizara ya Nishati na Madini na wachimbaji wa madini kutoka Lindi walioshiriki mafunzo ya huduma ya leseni za madini kwa njia ya mtandao yaliyofanyika mjini Lindi.

Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, kutoka kushoto ni Pendo Elisha, Charles Gombe na Aidan Mhando wakielezea hatua za Wizara katika kuboresha huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal; OMCTP) kwa wachimbaji wa madini (hawapo pichani) mjini Mtwara.

Baadhi ya wachimbaji wadogo wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa

6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

ZIARA YA MONGOLIA MENGI YA KUJIFUNZA NA KUIGA

Ujumbe wa Tanzania nchini Mongolia wakiangalia vifaa vinavyotakiwa kutumika ndani ya migodi ambapo Afisa wa Idara ya Usalama na Uokoaji Migodini wa nchi hiyo alipokuwa akiwaonesha.

Baadhi ya ujumbe wa Tanzania wakiangalia moja ya mgodi wa makaa ya mawe unaomilikiwa na mchimbaji mdogo. Wachimbaji wa makaa ya mawe nchini Mongolia baada ya kuchimba makaa hayo huyapeleka na kuuza katika kampuni ya umeme ya nchi hiyo ili kuzalisha umeme. Umeme wa Mongolia unazalishwa kutokana na makaa ya mawe

Ujumbe wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Ofisi ya Taifa ya takwimu walipokwenda kupewa maelezo ya namna Ofisi hiyo inavyofanya kazi ya kuhakikisha ina taarifa za kutosha za wachimbaji madini hususan wachimbaji wadogo

Ujumbe wa Tanzania ukipewa maelezo ya asili ya Taifa la Mongolia katika nyumba za asili zinazotumiwa na wafugaji wa nchi hiyo

7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

ZIARA YA MONGOLIA MENGI YA KUJIFUNZA NA KUIGA

Maofisa wa Wizara ya Nishati na Madini, Idara ya Madini walipokutana na Uongozi wa Jimbo mojawapo la Mongolia ambako ndiko kuna wachimbaji wadogo wengi na wamekuwa wakishirikiana kwa karibu na Serikali ya Jimbo hilo.

Kamishna wa Madini Nchini, Mhandisi Paul Masanja akipokea zawadi kutoka kwa mwenyeji wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini ya nchini Mongolia.

Maofisa Waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachimbaji wadogo wa Mongolia

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Kamishna wa Madini Nchini, Mhandisi Paul Masanja ulipokutana na uongozi wa Wizara ya Madini, Mongolia kujadiliana maeneo ya ushirikiano katika uboreshaji wa wachimbaji wadogo

8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Watumishi wapatiwa mafunzo ya Gesi na Mafuta

Rhoda James na Clinton Ndyetabula

Kampuni ya ICF kutoka Marekani kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini mwanzoni mwa wiki

wametoa mafunzo ya siku mbili ya Gesi na Mafuta kwa Watumishi wa Wizara pamoja na Taasisi za Serikali yaliyofanyika katika Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Taasisi hizo ni pamoja na Wakala wa Nishati Vijijini (REA); Shirika la Umeme Nchini (TANESCO); Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC); OSHA; Chuo Kikuu cha Dodoma na Chuo cha Madini Dodoma (MRI)

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Kamishna wa Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Hosea Mbise kwa niaba ya Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava alisema lengo la mafunzo hayo lilikuwa ni kuwajengea uelewa mpana kuhusu sekta ya gesi na mafuta watumishi wa Serikali na taasisi zake ili waweze kushiriki katika sekta hizo kikamilifu.

Alisema mbali na kutoa mafunzo kwa watumishi wa Serikali na taasisi zake, Wizara ya Nishati na Madini imekuwa ikitoa mafunzo kwa wananchi mbalimbali kwa kupitia vyombo vya habari na mafunzo kwenye maeneo yenye rasilimali ya gesi.

“Wananchi wanapokuwa na elimu ya kutosha na kushirikishwa katika sekta ya gesi na mafuta,

inapunguza migogoro inayoweza kujitokeza na kuongeza imani kwa Serikali yao,” alisema.

Awali akielezea sekta ya gesi nchini Mhandisi Mbise alisema gesi iligunduliwa mwaka 1974 katika kisiwa cha Songo Songo na hadi sasa kiasi cha futi za ujazo trilioni 55 zimegunduliwa.

Aliongeza kuwa upatikanaji wa gesi kati ya mwaka 2010 hadi 2015 umeongeza matarajio makubwa kwa wananchi wa Tanzania na kwamba gesi itaanza kuwanufaisha wananchi.

Alisema kutokana na wananchi kuwa na matarajio makubwa katika uchumi wa gesi ipo haja ya kuendelea kuelimisha wananchi hasa wale ambao wamezingirwa na gesi hiyo na Watanzania kwa

ujumla kuhusiana na upatikanaji wake na faida zake.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa ICF, Sharon Paviling aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Kampuni yake katika kuelimisha Watumishi

hao na kusema ni matarajio yake kuwa watumishi hao watapata uelewa mpana wa sekta ya gesi na mafuta na hivyo kuchangia katika kuelimisha umma na ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

Washiriki kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi za Serikali wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika mafunzo hayo.

Kamishna wa Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Hosea Mbise akifungua mafunzo kuhusu gesi na mafuta yaliyoandaliwa na kampuni ya ICF International kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini yaliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Wawezeshaji katika mafunzo hayo. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa ICF International, Leonard Crook, Mkurugenzi wa Masuala ya Mashariki ya Kati na Afrika, Idara ya Nishati kutoka Marekani, Glen Sweetnam na Meneja wa ICF International Ananth P. Chikkatur.

9BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

Na Veronica Simba - Dodoma

Serikali imewataka wamiliki wa leseni za uchimbaji madini nchini kuisoma na kuifahamu vyema Sheria ya Madini ya mwaka 2010 ili kuepusha migogoro

inayojitokeza katika utendaji wao wa kazi. Rai hiyo imetolewa hivi karibuni

mjini Dodoma na Mhandisi Migodi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Nuru Shabani kwa wachimbaji madini wadogo, wakati akiwasilisha mada mbalimbali kuhusu mfumo mpya wa utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao katika semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini kupitia Kitengo cha Leseni.

“Napenda kusisitiza kuwa, kwa wale wamiliki wa leseni za madini, msiridhike na kumiliki leseni tu. Mnapaswa muisome na kuielewa vyema sheria ya madini ya mwaka 2010 ili kuepusha migogoro inayotokea kutokana na kukosa uelewa wa haki na taratibu mnazopaswa kuzingatia katika kazi yenu,” alisema.

Aidha, akielezea umuhimu wa mchimbaji mdogo wa madini kumiliki leseni husika, Mhandisi Shabani alisema Sheria ya Madini inatambua na kumpa mmiliki wa leseni halali huduma mbalimbali stahiki tofauti na baadhi ya watu wanavyodhani kuwa muhtasari unaotolewa na Kijiji ndiyo wenye kutambulika na kuthaminiwa zaidi.

Alisema kuwa muhtasari wa kijiji unatumika katika kusaidia kujenga mazingira rafiki, wezeshi na ya amani baina ya wananchi wa eneo husika na mmiliki wa leseni na mchimbaji wa madini katika eneo hilo lakini hautambuliki kisheria.

Hata hivyo, Mtaalamu huyo wa madini aliahidi kuyafikisha mahala stahiki mapendekezo yaliyotolewa na baadhi ya washiriki wa semina husika kuwa muhtasari wa kijiji upewe uzito unaostahili na kutambuliwa kisheria katika kushughulikia masuala mbalimbali yanayohusu kada hiyo kutokana na umuhimu wake.

Vilevile, Mhandisi Shabani, aliitaka jamii kufahamu kuwa hakuna sheria inayomlazimisha mmiliki yeyote wa leseni ya madini kutoa huduma kwa jamii kama vile kujenga shule au huduma nyinginezo kama kigezo cha kupewa ruhusa ya kuendelea na shughuli zake katika eneo husika.

“Mmiliki wa leseni anashauriwa kuzingatia umuhimu wa kujenga mahusiano mema na jamii inayomzunguka kwa kutoa huduma mbalimbali kwa jamii husika, lakini jamii kwa upande wake haipaswi kumlazimisha muhusika kutoa huduma kwao kama kigezo cha wao kumruhusu aendelee na shughuli zake,” alifafanua Mhandisi Shabani.

Wizara ya Nishati na Madini ilizindua mfumo wa kutoa huduma za leseni kwa njia ya mtandao mapema mwezi Juni mwaka huu mjini Dodoma ili kutoa huduma za haraka, kuongeza uwazi na kumuwezesha mteja kusimamia leseni zake mwenyewe.

Ni kwa kuzingatia umuhimu wa matumizi ya mfumo huo mpya kwa wadau wa sekta ya madini nchini, Wizara kupitia Kitengo cha Usimamizi wa Leseni inaendesha zoezi nchi nzima kuwaelimisha wadau hao namna mfumo huo unavyofanya kazi.

Wamiliki wa leseni waaswa kuitumia sheria ya madini

Mjiolojia kutoka Ofisi ya Afisa Madini Mkazi – Dodoma, Affa Edward, akifungua mafunzo ya huduma za utoaji wa leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal – OMCTP). Mafunzo hayo yalifanyika hivi karibuni katika ukumbi wa ofisi hizo mjini Dodoma.

Mchimbaji madini mdogo kutoka Dodoma, Dominic Mwaria, akiuliza swali kwa Mwezeshaji wa Semina (hayupo pichani), kuhusu huduma za utoaji wa leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal – OMCTP). Mafunzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Madini mjini Dodoma.

Mhandisi Migodi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Nuru Shabani, akiwasilisha mada mbalimbali kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal – OMCTP) kwa Wachimbaji madini wadogo, wakati wa mafunzo yaliyofanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa Ofisi za Madini, mjini Dodoma.

MAFUNZO MASUALA YA JINSIA

Waratibu wa Masuala ya Jinsia (Gender Focal Point) kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Wawakilishi kutoka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na Wakala wa Usalama wa Afya Mahala pa Kazi (OSHA), katika picha ya pamoja katika mafunzo juu ya Uhusishaji wa masuala ya Jinsia katika usimamizi wa gesi asilia katika sekta za umma yanayoendelea nchini Swaziland.

10 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Na Greyson Mwase, Nachingwea

Imeelezwa kuwa dawa ya migogoro katika umiliki wa leseni za madini Kanda ya Kusini, itapatikana baada ya ofisi ya madini iliyopo Nachingwea kuanza kutumia

huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao.

Hayo yalisemwa na Afisa Madini Mkazi kutoka Nachingwea, Mayigi Makolobela alipokuwa akifungua mafunzo kuhusu huduma ya leseni za madini kwa njia ya mtandao yaliyoshirikisha wachimbaji wa madini katika wilaya za Ruangwa, Liwale na Nachingwea za Mkoani Lindi.

Makolobela alisema awali katika wilaya hizo kulikuwepo na migogoro ya umiliki wa leseni za madini iliyosababishwa na wamiliki wa leseni kuingiliana kwenye maeneo yao ya kazi huku kila mmoja akidai ni mmiliki halali wa eneo husika

Alisema wakati mwingine, maombi ya leseni yalikuwa yanagongana kutokana na wamiliki tofauti kuomba eneo moja ambapo inapotokea aliyewahi kutuma maombi akapatiwa leseni, mwombaji anayefuatia hudai kuwa kuna upendeleo umefanyika.

Alieleza kuwa katika mfumo huo mpya, mara baada ya maombi ya leseni kufanyiwa kazi kwa njia ya mtandao, mfumo hautaruhusu mwombaji mwingine kuomba leseni ya uchimbaji wa madini ya eneo husika.

Alisisitiza kuwa mbali na kuondoa

migogoro kwenye umiliki wa leseni za madini, mfumo huo utawezesha maombi mengi ya leseni za madini kufanyiwa kazi kwa haraka kwa kuwa maombi yote yatajazwa na waombaji wa leseni wenyewe.

Wakati huohuo Makolobela alisisitiza waombaji wa leseni kufuata sheria na kanuni za madini wakati wa maombi na usimamizi wa leseni za utafutaji na uchimbaji wa madini.

Na Zuena Msuya, Perth- Australia

Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera, Deodatus Kinawiro alisema atawapatia elimu zaidi ya madini wakuu wa wilaya

wengine wanaoongoza Wilaya zilizopo katika maeneo yenye madini.

Kinawiro alieleza hayo mjini Perth nchini Australia alipohudhuria mkutano wa kumi na tatu wa uwekezaji wa madini barani ‘Afrika - Africa Down Under 2015’ (ADU) unaoandaliwa na chama cha wenye mitaji na waendelezaji miradi nchini Australia ambapo Tanzania inashiriki kwa mara ya tano.

Alisema kuwa katika mkutano huo ambao mada mbalimbali ziliwasilishwa, zilimpatia fursa yeye binafsi ya kujifunza zaidi namna ambavyo maeneo ya uchimbaji wa madini yanavyoweza kuwa na maendeleo makubwa, hususani kwa Tanzania tofauti na ilivyo sasa.

“Nimeona nchi ya Australia katika Mji huu wa Perth ambao ni maarufu kwa uchimbaji wa madini umeendelea sana

tofauti na ilivyo katika maneo yetu kule Tanzania hivi sasa”.

“Nitatumia mbinu walizotumia wenzetu huku Australia ili angalau tuweze kubadili taswira ya Miji yetu yenye shughuli nyingi za uchimbaji madini kama Mwanza, Shinyanga, Arusha, nk. Ni muhimu miji yetu pia iwe na maendeleo kama wenzetu walivyofanikiwa. Hili nitawashirikisha Wakuu wa Wilaya wenzangu,” alisema Kinawiro.

Aliongeza kuwa maeneo kama vile Geita, Tarime, Karagwe, Chunya, Manyoni, Simanjiro na Babati yangetakiwa kuwa na uchumi mkubwa kutokana na kupatikana kwa madini mengi kama nchi nyingine kama Ghana na Mali.

Kwa upande wake, mmoja wa watanzania walioshiriki katika maonesho hayo ambaye ni mshauri kutoka Kampuni ya Kibaran Resources, Sauda Simba alisema kuwa maonesho hayo yanatoa fursa ya kuitangaza Tanzania kuhusu aina ya madini yaliyopo na namna ambavyo wawekezaji wanaweza kuwekeza.

Simba aliipongeza Wizara kwa kuwa na Banda kwenye Maonesho hayo ambalo limekuwa kivutio kwa wawekezaji wengi wa madini nchini Australia.

Maonesho ya Africa Down Under 2015 yameshirikisha mataifa 30 kutoka Afrika na zaidi ya wawekezaji 500 kutoka Australia

huku Mataifa 15 ya Afrika yakiwasilisha mada mbalimbali ikiwemo Tanzania.

Mkutano wa ‘Africa Down Under 2015’ kuwanufaisha ma DC

Suluhisho la migogoro ya leseni za madini Kanda ya Kusini kupatikana

Mkuu wa wilaya ya Karagwe Deodatus Kinawiro akisaini kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Nishati na Madini mjini Perth Australia.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo kuhusu huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini (hawapo pichani)

Afisa Madini Mkazi kutoka Nachingwea Mayigi Makolobela, akielezea hali ya maombi ya leseni za madini katika wilaya ya Nachingwea katika mafunzo hayo. Kutoka kulia ni Charles Gombe na Upendo Elisha ambao ni wawezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Wizara ya Nishati na Madini.

Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Erick Mkoma akielezea mikakati ya Serikali katika ukusanyaji wa kodi za madini kwa kutumia mfumo wa huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal; (OMCTP)

11BulletinNewshttp://www.mem.go.tz Habari za nisHati/madini

Kwa wadau wa sekta za Nishati na Madini, tembelea kurasa mpya za Wizara kwenye Mitandao ya Kijamii ya Twitter na Facebook kwa anuani ya ‘Nishati na Madini’ Karibu tuhabarishane na

tujadili kuhusu sekta za Nishati na Madini kwa maendeleo ya Watanzania wote.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Ujumbe wa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini w a n a t a r a j i a

kuondoka wiki ijayo kuelekea mjini Bangkok, Thailand kuhudhuria maonyesho ya 56 ya vito na usonara.

Lengo la ziara hiyo nchini Thailand ni kutangaza madini ya vito mbalimbali yaliyopo nchini ikiwamo Tanzanite ambayo inapatikana Tanzania pekee katika eneo la Mererani wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara.

Aidha, ziara hiyo ni fursa kubwa kwa taifa la Tanzania

hususan katika sekta ya Madini kuvutia wanunuzi mbalimbali duniani wanaokwenda kuwavutia kuja Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya vito yanayofanyika kila mwaka mkoani Arusha kununua madini ya vito na kuufanya mji wa Arusha kuwa kituo kikubwa cha madini ya vito katika bara la Afrika.

Ni dhahiri kwamba maonesho hayo ya vito Bangkok ni jitihada za Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini hususan Idara ya Madini kuwatafutia masoko wachimbaji na wafanyabiashara wa madini hasa wale wadogo.

Katika maonesho hayo wachimbaji na wafanyabiashara wa madini hasa

ya vito watapata mawasiliano kwa wanunuzi mbalimbali wa kimataifa badala ya kuwatumia madalali ili kuweza kuuza madini yao kwa wanunuzi walengwa na kuuza madini kwa bei nzuri na hatimaye kupata faida maradufu.

Maonesho hayo ya vito yanatoa fursa pia kwa sekta

nyingine kujitangaza pamoja na kuitangaza Tanzania duniani mathalan sekta ya utalii ambapo madini ya vito yanakwenda pia na ujumbe wa vivutio vya utalii vilivyopo nchini ikiwamo mbuga za wanyama pamoja na mlima wa Kilimanjaro.

Wachimbaji, Wafanyabiashara madini kuhudhuria maonesho ya vito Bangkok

 

Extractive Inter-stakeholders Forum (EISF) in Collaboration with the Ministry of Energy and Minerals

(MEM) Invites You to participate and exhibit    

The TANZANIA OIL, GAS AND MINERALS BUSINESS AND SUPPLY CHAIN

Creating awareness on the Extractive Industry Value Chains, Financing, Marketing and Business Opportunities

The event will be held on 24-25 March 2016 at Hyatt Regency Dar es Salaam - The Kilimanjaro