Upload
prof-handley-mpoki-mafwenga
View
97
Download
13
Embed Size (px)
Citation preview
MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUA
Mwananchi
Na Prof. Handley Mpoki Mafwenga Ph.D (finance -COU), MSc (finance -Strathclyde), MBA (Mg.Eco -ESAMI/MsM), LLM
(taxation- UDSM), LLB (Tudarco), PGD tax mgt (IFM), AD tax mgt (IFM)]
Ujenzi wa dhana potofu ndani ya akili na mioyo ya wana sheria ndicho chanzo cha kulaumu hadi
kufikia kutamka bayana kumshitaki Waziri Mkuu Mizengo Pinda juu ya Kauli yake aliyoitoa
Bungeni ikidaiwa kwenda kinyume na Haki za Binadamu. Lakini kabla wanasheria hao
hawajacheua kauli zao hizo ingekuwa vyema wangefanya tathmini ya Jeshi la Polisi Kimuundo na
Utendaji Kazi wake.
Jeshi la Polisi liliundwa kama moja ya njia za kujenga Ukoloni ambapo utawala wa Waingereza
uliendeleza Tarakibu ya Ireland (Royal Irish Constabulary Model) iliyokuwa tofauti na Tarakibu
ya Kiingereza (Metropolitan Model) lengo kubwa ilikuwa ni kusimamia Sheria za Kijeshi
(Paramilitary Law and Order) ingawa baadaye lilisimamia Usalama wa Raia lenye mamlaka ya
kulinda kutokea kwa makosa ya jinai kwa faida ya Jamii. Tarakibu ya Ireland ilihamia India na
kuboreshwa kisha kusambaa kwenye Makoloni mengine ikiwemo Afrika ya Mashariki. Hata
hivyo, kuwepo kwa jeshi la kitaalamu kulikuwa ni kulinda Ubepari kwa ajili ya kutafuta masoko
mapya na rasilimali mbalimbali.
Jeshi la Kikoloni liliwajibika kwa Watawala, kuifanya jamii iheshimu utawala uliokuwepo
likijengwa kwa utaratibu wa Amri kutoka vyeo vya juu hadi chini kiutawala (pecking order).
Ingawa wakati wa Tanganyika Jeshi lilikuwa likijengwa kwa kulinda sekta za mazao
yaliyomilikiwa na wageni, wakulima wazawa, na kutawala kupitia kwenye Utawala wa Asili chini
ya Machifu na kwa upande fulani chini ya Maafisa wa Kikoloni. Baadaye Jeshi hilo lilikuwa chini
ya utawala wa wilaya ambao ulifanya pia kazi ya Mahakama. Afisa wa Wilaya alikuwa ndiye
Kiongozi wa Polisi, Hakimu na Afisa Mkuu wa Magereza.
Kufuatia Muundo wa Vyama vya Wafanyakazi na Waafrika kuukataa utawala wa kikoloni, Jeshi la
Polisi lilifanyiwa mabadiliko na kuimarishwa kijeshi zaidi. Hata hivyo kufuatia kuundwa kwa
TANU Wakoloni waliacha kutumia Jeshi katika hadhi ya kijeshi isipokuwa pale tu migomo
inapotokea kwa kile kilichoitwa “Police Motorized Companies” kilichorithiwa baadaye na Kitengo
cha kutuliza ghasia (FFU). Kitengo hiki hapo awali kilitumika wakati wa migomo ya wafanyakazi
na wakati wa Operasheni Vijiji na kuwaondoa Wabarabaig kwenye eneo lililotolewa kwa NAFCO;
aidha lilitumika kwa wanafunzi wa chuo kikuu miaka ya sabini wakati wa migomo ya Akivaga na
wakati Fulani kutuliza ghasia za wafanyakazi wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Mwaka 1986.
Aidha, Jeshi hilo limetumika kutuliza ghasia kwenye Msikiti wa Mwembechai Magomeni Mwaka
1993, Uchaguzi wa Zanzibar Miaka ya 2000 na 2005 na maeneo mengi yakiwepo yale ya mjini
Arusha hivi karibuni.
Kwa Mujibu wa Sheria ya Polisi Sura ya 322 kifungu Na 5 neno “Force” kwa maana ya Jeshi la
Polisi kinabainisha kuwa “Jeshi la Polisi; litatumika ndani na mahala popote pa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa lengo la kulinda amani, kusimamia sheria na Kanuni, kuzuia na
kutafiti jinai, kulinda wahalifu, na kulinda mali na litatumika kwa ajili ya kazi zote zilizobainishwa
na watapaswa kuwa na silaha”.
Polisi wanapambana na kazi ngumu na ya hatari ambayo ni lazima udhibiti wa fujo ufanyike, na
hivyo kazi zao lazima ziwe na upinzani kutoka kwa jamii kwa vile kuna baadhi ya watu hawaridhii
kukamatwa, hivyo nguvu shurti itumike. Ukosekanaji wa nguvu umesababisha Polisi kuuwawa,
kuumia na kukosa heshima kwa wananchi na hivyo kuacha kundi la wanaofanyiwa uharifu kukosa
kinga na haki zao. Hata hivyo, nguvu inatakiwa kuwa ndogo (minimum force) katika kufikia
malengo yaliyopo; Kabla ya kutumia nguvu polisi wanapaswa kushawishi, kutumia nguvu bila
silaha, kutumia nguvu na silaha zisizo za hatari, nguvu kwa kutumia silaha zenye madhara, na
mwisho huwa ni nguvu iliyokithiri. Hata hivyo zipo silaha zilizobainishwa kutegemeana na
matukio ya uhalifu kama vile fimbo za polisi, minyororo, pingu, mbwa, bunduki, mabomu ya
machozi nk. Aidha, Polisi hawapaswi kutumia nguvu iliyokithiri hadi kufikia kuua au kuumiza
wahalifu na yapo maeneo maalum ya mwili ambayo polisi anapaswa kupiga bila kuathiri afya ya
mharifu hata angekuwa Jambazi, ingawa ipo pia nafasi kwa Polisi kujilinda (self-defence) dhidi ya
hali inayohatarisha maisha yake na hivyo kulazimika kuua bila kukusudia. Pengine hapa watu wa
haki za Binadamu wamechelewa kwani walipaswa kuhangaikia matukio ya watanzania ambao
Polisi wamekuwa wakienda kinyume na taratibu (kama yapo) na mchakato wa kutumia
nguvu(kama upo) kuliko kushupalia kauli ya Waziri Mkuu iliyojikita kwenye taratibu za kutumia
nguvu kisheria (minimum force procedure).
Polisi wanayo haki ya kutumia nguvu kwa dhana ya kuzuia uhalifu na chini ya Utawala wa Sheria
ni Nguvu ile tu muhimu inayohitajika (necessary force); na inapotumika kwa mtu ni ile ambayo ni
stahiki na muhimu kutegemeana na mazingira (reasonable and necessary force). Sheria ya Kutumia
Nguvu (Use of Force Doctrine) inatumiwa na Jeshi la Polisi ili kuweka hali ya usalama na
kuioanisha na mahitaji ya maadili kwa ajili ya kulinda haki na maisha ya wanaohatarisha amani na
wanaohisiwa kufanya hivyo. Na iwapo jamii inaumia itaashiria kuwa Polisi alikuwa akijilinda na
mtu akifa katika tukio inahalalishwa kuwa ni mauaji halali (justifiable homicide). Moja ya Kazi
kubwa ya Dola ni kulinda raia wake dhidi ya hatari za ndani na nje ya nchi ili wananchi wajisikie
wako salama wakati wote. Hii ndiyo inayowafanya wananchi wawe na imani na nchi yao. Ukosefu
wa Nchi kushindwa kulinda Sheria na Kanuni na kutokuwepo kwa usalama wa maisha na mali ya
raia unaweza kusababisha fujo.
Kauli ya Mhe Waziri Mkuu ni ya Ujumla zaidi haikubainisha ni kipigo au nguvu ipi itumike kwani
Sheria zipo zinazobainisha nguvu gani itumike. Wakuu wa Jeshi la Polisi tokea enzi za ukoloni
hadi sasa ndiyo wenye dhamana ya kutoa amri ya kutumia Nguvu; kwa upande wa Waziri Mkuu
inabaki kuwa Ushauri au Agizo na siyo Amri. 1Ni kazi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi kupokea agizo
na kulitolea Amri kwa Mujibu wa Sheria ya Jeshi la Polisi Sura ya 322 Kifungu Na 7(1)(2)
ikisomwa pamoja na Kifungu Na 8 (1) na Kanuni zake (Code of Conducts) na huwa na sura
1Viongozi Wa Polisi Wakati wa Ukoloni Hadi Uhuru na Orodha ya IJP toka Uhuru, Wakati Wa Muungano
hadi sasa
(1916 – 1920 Major S.T. Davis). (1920 – 1929 E.F. Brown) (1929 – 1933 G.H. Kiram) (1933 – 1942F.A.B. Nicholl) (1942 – 1949E.B. Birthray) (1949 – 1951W.A. Muller) (1951 – 1958 R.E. Fouler) (1958 – 1962 G.S. Wilson) ( 1962 – 1964 E.N. Shaidi) (1964 – 1970 Elangwa N. Shaidi) (1970 – 1973 Hamza Azizi) (7/8/1973 –Aug 1975 Samweli H. Pundugu) (8/8/1975 – Nov 1980 Philemon N. Mgaya) (2/11/1980 – 30/11/1984 Solomoni Liani)(1/12/1984 – 3/5/1996 Harun G. Mahundi)( 4/5/1996 – 2/3/2006 Omar I. Mahita) (3/3/2006 Hadi sasa Saidi A. Mwema)
iliyotofauti katika utekelezaji wake. Kwa Waziri Mkuu huwa ni “Ideological Order” na kwa IGP
huwa ni “Coercive Force Order”.