112
Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania Mafunzo kwa Wakufunzi kuhusu Misingi ya Mbinu za Ufundishaji

Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

  • Upload
    others

  • View
    123

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania

Mafunzo kwa Wakufunzi kuhusu Misingi ya Mbinu za Ufundishaji

Page 2: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

www.foundations-of-teaching.org Kanusho: Waraka huu umefadhiliwa na Save the Children lakini haimaanishi kuwa maudhui yaliyomo lazima yanaakisi msimamo wake rasmi. Maudhui yanaweza kuwa yamerekebishwa ili kuendana na leseni ya Creative Commons. Save the Children haina udhibiti wa marekebisho na hivyo haliwezi kuwajibishwa kwa matumizi yanayoweza kutokea kuhusu taarifa zilizomo kwenye waraka huu. Hakimiliki Picha katika waraka huu © Save the Children 2017 na hairuhusiwi kunakiliwa bila ya ruhusa yake. Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya tovuti iliyoandikwa hapo juu. Shirika la Save the Children linaendesha shughuli zake katika nchi zaidi ya 120. Tunaokoa maisha ya watoto. Tunapigania haki zao.�Tunawasaidia kutimiza ndoto zao. EENET ni mtandao wa kusambaza taarifa unaokuza na kusaidia ujumuishaji wa wanafunzi wasio na fursa sawa katika elimu, hususani katika mazingira yenye uhaba wa vifaa.

Page 3: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Shukrani

Toleo la Tanzania Moduli hizi zimechukuliwa kutoka matoleo ya kimataifa ili kuzifanya zitumike kwa walimu wa Tanzania. Tunapenda kutambua mchango mkubwa kutoka kwa:

• Save the Children Timu ya Shinyanga • Wakufunzi wa walimu kutoka Chuo cha Ualimu Shinyanga • Maafisa Elimu wa Manispaa ya Shinyanga, Yesse Kanyuma na Nancy

Ng’winula Toleo hili limepitiwa na kuidhinishwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE).

Toleo la Kimataifa Kabrasha hili la Misingi ya Kuelekeza Ufundishaji liliandikwa kwa ajili ya Save the Children na washauri waliotoka Mtandao wa Uwezeshaji Elimu (EENET): Karen Chesterton Khayat, Sandra Graham, na Juliette Myers. Msaada wa Uhariri na jinsi ya kuendesha mradi ulitolewa na Ingrid Lewis. Wakati Alex Hauschild alitayarisha vifaa. Tunashukuru kwa dhati mchango maridhawa wa muda na kujitoa katika kutupatia mrejesho kuhusiana na vifaa kutoka vyuo mbalimbali ambapo kuna matawi ya Save the Children, ikiwa ni pamoja na Norway, Afghanistan, Tanzania, Uingereza, na Marekani, na kutoka kwa kundi la asasi ya Teachers in Crisis Contexts Working Group. Kazi hii iliongozwa na James Lawrie akiwa pamoja na Patrick Mroz-Dawes na Sebastian Blomli. Kazi hii sasa ni matokeo ya vifaa vya awali na yale yaliyoongezwa kutoka katika vyanzo vingine. Vyanzo hivyo vipo katika Kiambatisho cha 1.

Page 4: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Yaliyomo Utangulizi .................................................................................................................. 1

1. Andaa darasa lako kwa ajili ya mafunzo .............................................................. 5

2. Wafahamu na wahusishe wanafunzi wako wote ................................................ 15

3. Zifahamu familia na jamii za wanafunzi wako .................................................... 29

4. Udhibiti wa kuzuia wa darasa ............................................................................. 39

5. Udhibiti wa kiufumbuzi wa darasa ...................................................................... 53

6. Hakikisha wanafunzi wako wanalindwa: Sehemu ya 1 ...................................... 65

7. Hakikisha wanafunzi wako wanalindwa: Sehemu ya 2 ...................................... 79

8. Anza na hitimisha darasa kwa malengo ............................................................. 91

9. Elezea somo ..................................................................................................... 101

10. Tumia zana zingine ........................................................................................ 111

11. Tumia maswali na majibu ............................................................................... 127

12. Tumia jozi na vikundi ...................................................................................... 141

13. Tumia kazi za kufanya .................................................................................... 151

14. Tumia utofautishaji kwa ajili ya madarasa yenye wanafunzi wenye uwezo

mchanganyiko ................................................................................................ 163

15. Andaa na panga masomo kwa mtiririko ......................................................... 179

16. Wape wanafunzi mrejesho unaofaa ............................................................... 195

17. Upimaji wa ujifunzaji wa wanafunzi ................................................................ 207

18. Matumizi ya upimaji kuboresha ujifunzaji ....................................................... 221

Kiambatisho cha 1: Marejeleo .............................................................................. 231

Kiambatisho cha 2: Faharasa ya maneno yaliyotumika mara kwa mara ............. 234

Kiambatisho cha 3: Viunganisho kwa NTCF ........................................................ 235

Page 5: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

1

Utangulizi

Kuhusu Kozi hii ya Mafunzo Waraka huu ambao ni msingi wa stadi za ufundishaji umeandaliwa kuwafundisha wawezeshaji wa aina zote katika kuwasaidia walimu waweze kuwa na misingi muhimu na stadi wanazoweza kuzifundisha, mambo ambayo sasa yanakosekana. Kiwango duni cha ufundishaji kinadhihirisha mgogoro wa kidunia katika ujifunzaji wa mtoto. Walimu wenye kipato kidogo na walio katika sehemu zenye matatizo mara nyingi hutiwa moyo kuboresha kiwango cha ufundishaji katika madarasa yao kupitia mafunzo yanayotolewa na mashirika ya kiraia. Mafunzo haya hata hivyo, yanatokeza mabadiliko machache katika mafunzo kwa vitendo darasani. Nyenzo hii ya umilisi wa mafunzo ya msingi imeandaliwa kwa ajili ya wawezeshaji wa mafunzo wa aina zote ili kuwasaidia walimu kukuza stadi muhimu za mafunzo ya msingi na ujuzi unaohamishika ambao mara nyingi unakoseakana. Stadi za msingi zinazofafanuliwa hapa ni za muhimu kwa walimu wote. Walimu walijulikana kutokana na mapitio ya ushahidi wa kina. Moduli za kufundishia zilipagwa kwa kila stadi ya msingi. Kila moduli ilijumuisha malengo, vifaa, taarifa za kushirikishana za msingi, mafunzo kwa vitendo, viashiria vya mafanikio, mawazo kuhusu ujifunzaji wa kushirikiana na kujisomea, mawazo ya uelekezaji, na vipengele muhimu kuhusu jinsia na ushirikishwaji (hasa kuhusu ulemavu na kuwapo kwa wingi wa lugha). Moduli zote zimeandikwa kwa lugha ya wazi. Moduli zote zimeandikwa kwa lugha ya wazi. Istilahi yoyote ya kiufundi na kitaalamu imeelezwa katika kiambatisho namba 2. Moduli zote zimeandaliwa ili zifundiswe kwa upekee wake isipokuwa mada mbili ambazo kila moja itafundishwa kwa jozi ya moduli: Litawale darasa lako na hakikisha kuwa wanafunzi wanalindwa. Maelezo yametolewa pale ambapo kuna uhusiano wa wazi baina ya moduli.

Jinsi ya Kutumia Mwongozo Huu wa Mafunzo Vipindi vingi vya mafunzo vinatumia kama saa 2 hivi. Ingawa viongeza nguvu na vichocheo vya akili havijaorodheshwa katika mwongozo huu, inashauriwa kuwa wawezeshaji wavitumie pale vitakapohitajika. Wawezeshaji pia wanaweza kutaka kuanzisha mada kuhusu moduli fulani hata kabla ya kuanza moduli ya mafunzo. Jambo hili linaweza kufanyika kwa:

• Kuandika ubaoni sentensi/swali/nukuu; • Kusimulia hadithi;

Page 6: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

2

• Kuwajulisha kuhusu uzoefu binafsi; • Kutoa swali la kufikirisha; • Kuwataka washiriki wote kuandika sentensi kuhusu uzoefu wao wenyewe

kuhusiana na mada; • Kuwapatia picha yenye dokezo (k.v. picha, katuni [kibonzo]); • Kufanya kimchezo/kichocheo cha akili

Aidha, ni wazo zuri kutumia ‘vichocheo vya usikivu’ wakati wa moduli kuwaeleza wanafunzi ni wakati gani watoke katika kazi za makundi au jozi. Mapendekezo yanaweza kuwa ni pamoja na:

• Kuwapatia sauti/wimbo fulani; • Kushikilia kidokezo fulani (k.v. picha); • Kutamka neno fulani na wanafunzi wakaitikia; • Kutumia ishara ya mkono.

Ni jambo zuri kwa mwezeshaji kufanya tathmini mwishoni mwa kila moduli. Jambo hili litahusisha muhtasari na mwonekano wa jumla wa mawazo makuu yaliyoongelewa ili kupia uelewa wa wanafunzi. Toa muda mfupi wa ziada kwa jambo hili. Mwezeshaji anaweza kutumia maswali ya chemshabongo ili kupima ujifunzaji wa wahusika. Hii inaweza kuwa ni maswali mchanganyiko: yale yanayohitaji majibu ya moja kwa moja ambayo yatakuwa ama ni kweli au si kweli, na pia yale yanayoweza kuwa na majibu sahihi tofauti. Muundo wa maswali ya chemshabongo unaweza kuwa:

• Maswali ya kawaida ya chemshabongo yenye maswali na majibu ya msingi, yanayoulizwa kwa watu binafsi au kwa timu. Wanaweza kutoa majibu yaliyoandikwa ili yasahihishwe;

• Mtu wa kwanza kusema au kunyoosha mkono, ndiye anayepewa nafasi kujibu;

• Muundo wa michezo ya maswali ambapo washiriki wataoanisha maswali na majibu katika kadi;

• Majopo ya washindani wakijibu maswali mbele ya hadhira. Walio katika hadhira wanabeba kadi za kijani kukubali au kadi nyekundu kukataa majibu yaliyotolewa;

• Fanya maswali yako mwenyewe ambapo washiriki watatengeneza maswali na kuwataka washiriki wengine kuyajibu.

Kuzingatia Kiunzi cha Mafunzo ya Walimu ya MEST’s INSET Kozi hii imetoholewa itumike katika Mradi wa Save the Children wa Kuwezesha Walimu. Hata hivyo, tunatarajia kuwa MEST wataitumia kwa kozi zozote za maendeleo ya kiueledi ambapo wataona inafaa. Ikiendana na kiunzi cha mafunzo ya walimu cha MEST mwaka 2017 INSET, moduli hizi zinahusisha maendeleo ya

Page 7: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

3

kiueledi kutoka INSET inayoegemea mashuleni. Kila moduli inayo maoni ambayo yanaweza kutumika katika Jamii za Mafunzo (MEST 2017:3). Kozi hizi zimetengenezwa kwa msaada kutoka MEO. Moduli zinahusiana moja kwa moja na ule umilisi ambao MEST imeutaja kuwa ni muhimu kwa walimu wa Tanzania. Kila moduli inaanza kwa Malengo ya Mafunzo yanayohusiana na Kiunzi cha Kitaifa cha Umilisi wa Walimu - KKUW. Marejeleo ya KKUW yanatolewa baada ya kila Lengo la Ujifunzaji, na yameelezwa kwa kina katika Kiambatisho 3. Save the Children imetengeneza tathmini ya mahitaji ili kumsaidia mwalimu binafsi ili aweze kutambua uimara na udhaifu wake. Kila Mwalimu katika mradi wa Kuwezesha Walimu atapokea maelezo binafsi kuhusu Umilisi wa Mwalimu ili kumsaidia aweze kuangalia mwenendo wake katika maendeleo yake ya kitaalamu. Kila moduli inakuwa pamoja na mwongozo baada ya ujifunzaji kwa ajili ya walimu wenyewe (unajiongoza mwenyewe, na kwa rika-kwa-rika) na kwa wale wanaowaunga mkono walimu (viongozi waelekezaji, makocha). Vipengele vingine vya nyongeza vya ujifunzaji wa kitaalamu vinavyohusiana na kozi ni pamoja na:

• Kuelekezwa kutoka viongozi wa shule na wakufunzi wa Vyuo vya Ualimu; • Jumuiya za Mafunzo za Mwalimu katika shule; • Mafunzo ya kitaalamu, ikiwa ni pamoja na matumizi ya video; • Ujifunzaji binafsi; • Tathmini ya maendeleo.

Ujifunzaji wenye matokeo bora unawezekana kutokana na mchanganyiko wa mafunzo yanayoongozwa na mfundishaji, mafunzo binafsi, na yanye kuungwa mkono na wataalamu au wa rika la mjifunzaji. Walimu watajaribu yale waliyojifunza na kuyatafakari baadaye wakiwa na wenzao au wataalamu. Kozi hii imeundwa ili matokeo yake yawe mfano mzuri kwa ualimu kwa vitendo kwa wale wanaojifunza.

Kufundisha kwa kulenga somo mahususi Kozi hii inajihusisha na misingi ya ufundishaji na kwa hiyo si ya somo fulani mahususi. Kozi za ufundishaji walimu zinazolenga somo mahususi kama kusoma, kuhesabu na sayansi yanatarajiwa kuwa na athari kubwa wakati walimu washiriki wanapokuwa na misingi ya lazima ya stadi za kufundisha.

Page 8: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Andaa darasa lako kwa ajili ya kujifunza

4

1. Andaa Darasa Lako Ili Wanafunzi Wajifunze

¹ Jumla ya saa 2

Malengo ya Mafunzo Kufikia mwisho wa moduli hii, washiriki wataweza: • Kubainisha matendo yanayoandaa darasa kwa wanafunzi (NTCF 2.5) • Kuelewa umuhimu wa kuandaa darasa ili kukaribisha, kuthamini na kuheshimu wanafunzi wote (NTCF 2.5)

Vifaa vinavyohitajika • Chati za kuandikia • Peni

Page 9: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 1

5

Taarifa za kuwapa washiriki wakati wa moduli Wakati walimu wanapofundisha, wanakuwa katika mazingira ambapo mambo mengi yanakuwa nje ya mamlaka yao. Mwalimu anaweza kuwa hana uwezo wa kuamua ukubwa wa darasa, wanafunzi wawe kina nani, upatikanaji wa nafasi ya kujifunzia, au upatikanaji wa vifaa na nyenzo za kufundishia. Hata hivyo dhima ya mwalimu ni kuwa na uongozi wa darasa, kulipanga, kutumia rasilimali zilizopo, na kujiandaa kufundisha katika hali ambayo itawapa fursa za kujifunza wanafunzi wengi iwezekanavyo. Masomo yanaandaliwa na kufundishwa vizuri zaidi ikiwa mwalimu atapata muda wa kuyaandaa na kuliandaa darasa kwa ajili ya ujifunzaji. Mazingira ya kujifunza yanaandaliwa na walimu kutokana na namna wanavyowakaribisha wanafunzi na kuwatia moyo ili washiriki na kwa namna mazingira ya darasa yanavyoonekana. Darasa lililoandaliwa, lililopangiliwa, na linalotawaliwa vizuri humsaidia mwalimu kufundisha somo lile aliloliandaa, na kufikia malengo ya somo kwa wanafunzi wote darasani. Moduli hii inahusiana na moduli nyingine: Kutawala darasa lako (Sehemu 1 na 2), na ‘kuwajua na kuwajumuisha wanafunzi wako. Moduli hii inawapatia walimu maarifa na stadi stahiki juu ya kama msingi wa utoaji somo zuri. Ni kuhusiana na matendo wayachukuayo walimu na stadi wazitumiazo walimu ili kuleta mazingira chanya katika ujifunzaji.

Kazi za kufanya 1. Tafakuri ¹ Dakika 45

Nia ya shughuli hii ni kujenga picha ya darasa ambalo limetayarishwa vizuri kwa ajili ya ujifunzaji wa watoto wote. Fikiri – Kaa katika Jozi – Elezana Wagawe washiriki katika Jozi.

“Elezaneni kuhusu darasa ulilosoma ulipokuwa mwanafunzi na walimu waliokufundisha.

• Je mwalimu wako alikusaidia kujifunza vizuri? Ikiwa ndiyo, je mwalimu wako alifanya nini hasa

kilichokusaidia kujifunza? • Je mazingira ya darasani yalisaidia katika ujifunzaji wako? Ikiwa ndivyo, ni nini kilichosaidia? Ikiwa

sivyo, ni nini kingefanyika kufanya hali kuwa nzuri?” Baada ya muda wa majadiliano, waulize washiriki:

Sema

Sema

Page 10: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Andaa darasa lako kwa ajili ya kujifunza

6

“Kutoka katika Majadiliano yenu, bainisha ni nini ambacho kingeonyesha kuwa darasa fulani limeandaliwa vema ili kuwatia moyo, kuwaunga mkono na kuboresha usomaji wa watoto wote?”

Andika katika chati ya kujifunzia viashiria vya msingi vilivyotolewa na washiriki. Wagawe washiriki katika makundi 3 (au makundi zaidi ikiwa kuna washiriki wengi). Kila kundi lipe chati ya kujifunzia.

“Sasa tutachambua viashiria vya msingi tukivigawa katika makundi maalumu. Kundi A litakuwa na kichwa cha ‘Mpangilio wa Chumba cha Darasa’; Kundi B litakuwa na ‘Nyenzo na Vifaa vya darasa’; na Kundi C litaangalia ‘Matendo ya Mwalimu katika kuwaandaa Wanafunzi ili wajifunze’”.

Kundi A: Mpangilio wa Chumba cha Darasa

Kundi B: Nyenzo na Vifaa vya darasa

Kundi C: ‘Matendo ya Mwalimu kuwaandaa Wanafunzi ili wajifunze

Kutoka katika orodha, waeleze kila kundi kuweka viashiria katika kila kichwa. Wanaweza kuongeza ikiwa ni lazima.. Baada ya dakika 5, waombe kila kundi kupeleka chati yao kwa kundi jingine, ambalo litasoma na kuongeza chochote wanachodhani kinakosekana. Baada ya dakika 5 nyingine, makundi yabadilishane tena katarasi. Mwishoni mwa zoezi hili, kila kundi litakuwa limetoa mawazo katika kila moja ya vichwa 3. Weka chati hizi zote ubaoni. Wakiwa wote, waombe washiriki kuangalia ikiwa kuna kitu kilichorudiwa, uliza maswali na malizia kuandaa orodha ya ‘utayari wa darasa’. Gawa Kitini cha 1 kwa washiriki na waache walingalishe na yale yaliyomo katika chati yao waliyoiandaa. Waulize ikiwa watatakiwa kuongeza kwenye orodha yao, kiashiria kutoka katika Kitini cha 1.

2. Kujiandaa kwa kazi ya kushirikisha kikamilifu ¹ Dakika 30 Madhumuni ya shughuli hii ni ili kuelewa ni kwanini kila kiashiria ni muhimu nan i kwa vipi kina athari katika ushiriki na ujifunzaji wa wanafunzi. Kaa katika kundi lile lile.

Sema

Page 11: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 1

7

“Soma tena Kitini cha 1. Je kinawakilisha darasa lako mwenyewe na matendo unayofanya ili kuwakaribisha na kuwaandaa wanafunzi wako? Je kuna sehemu nyingine ambazo ungeweza kuziboresha?”

Andaa chati ya kujifunzia ikiwa na vichwa na orodha ya viashiria vifuatavyo (Taz. kwa mfano jedwali hapa chini). Watake makundi kufikiria NI KWANINI viashiria hivi ni muhimu katika maandalizi ya darasa.

“Angalia kifuatacho, na ukiwa na wanakikundi wenzako, jaza safu ya kulia.”

Kiashiria Kwanini viashiria hivi ni muhimu katika

maandalizi ya darasa kwa ajili ya ujifunzaji? Mwalimu anawakaribisha wanafunzi darasani, na kuwasaidia kutulia sehemu zao za kazi

Watoto wanajisikia kukaribishwa darasani. Wanajisikia kuthaminiwa. Kuna uwezekano wa watoto hawa kushiriki, kuwa watendaji na kujifunza. Inawajengea kujiamini na kujitambua.

Mwalimu huweka matarajio ya wazi Mwalimu hujua majina ya wanafunzi na watokako

Wanafunzi wote wanaweza kuona ubaoni

.

Kila mtoto ana kitabu au anaweza kukiona kwa urahisi

Wakati makundi yakiisha, wapatie Kitini cha 2 wakipitie pale wanapokutana. 3. Kuandaa Orodha Hakiki ¹ Dakika 30

Nia ya shughuli hii ni kutengeneza orodhahakiki ili kujua darasa limejitayarishaje. Orodhahakiki ni nyenzo ya kuwasaidia walimu ili kujua ikiwa wameliandaa darasa lao vizuri. Inaweza pia kutumia kutathmini utendaji wao. Kutumia viasharia kutasaidia walimu kuwa katika utaratibu wa kujiandaa vizuri na kuwasaidia kukuza stadi hizi. Kazi katika makundi yaleyale.

“Tumetambua baadhi ya njia ambapo darasa linaweza kuandaliwa kuunga mkono ujifunzaji. Sasa tunatambua sababu za kuwapo kwa vitendo mbalimbali. Sasa tutatumia majedwali ili kuwa na orodhahakiki ya mwisho ya Utayari wa Darasa. Hili

litakuwa ni jambo ambalo tutajisikia furaha kupimwa kwalo, na tunaweza kubadilishana na kutumia na darasa lolote lile katika shule yoyote. Tengeneza orodhahakiki ya mwisho ukitumia viasharia ulivyokwisha vitengeneza. Usitumie zaidi ya viashiria 10 katika orodhahakiki ya mwisho. Kwa mfano: Kiashiria Ndio Hapana

Sema

Sema

Sema

Page 12: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Andaa darasa lako kwa ajili ya kujifunza

8

1 Wanafunzi wote wamekaa wanapoweza kuona ubaoni 2 Darasa ni safi na limepangwa 3 Kila mtoto ana kitabu au anaweza kukiona kwa urahisi 4 Mwalimu anatabasamu na anawakaribisha wanafunzi 5 Mwalimu anaweka wazi matarajio yake

Waulize washiriki ikiwa wanaweza kutumia orodhahakiki hii kama mwongozo wa kutayarisha darasa lao kwa ajili ya ujifunzaji wa wanafunzi wote. Uliza ni namna gani orodhahakiki inaweza kuwa nyenzo inayofaa kuwasaidia waelekezaji au walimu wakuu katika kutoa mrejesho na kuunga mkono zaidi. Kwa mfano, hii inaweza kuwa yenye manufaa ikiwa shule moja ina mahitaji ya darasa machache kuliko nyingine, inaweza kuomba msaada zaidi. Ndani ya shule, orodhahakiki inaweza kumsaidia mwalimu mkuukuwatia moyo walimu wote kuwa na tabia njema wakati wakiandaa darasa. Waulize washiriki ikiwa wanafurahia chaguzi mbili za NDIYO (ikiwa kiashiria kimetimizwa) au HAPANA (ikiwa kiashiria hakijatimizwa). Au je wangelipendelea kipengele cha 3 cha uchaguzi kuhusiana na majibu ya swali, kwa mfano: Kila wakati Wakati mwingine Haikuwahi kutokea Imepatikana Imepatikana kiasi Haikupatikana kabisa. Amua, na kasha malizia Orodhahakiki ya Utayati wa Darasa katika Kujifunza. (Taz. Kitini cha 3 kwa Orodhahakiki ya kawaida). Huu ni mwisho wa moduli hii. Mwezeshaji apime iwapo malengo ya moduli hii yamefikiwa.

Viashiria vya mafanikio o Mwalimu ameweza kuelezea darasa ambalo limeandaliwa vizuri kuwasaidia

wanafunzi kufika, kushiriki na kujifunza. o Darasa la mwalimu limepangiliwa vizuri na liko katika hali inayowawezesha

wanafunzi kujifunza kama mazingira yanavyoruhusu. o Kupitia katika kujitayarisha, mwalimu ameweza kuweka msingi wa somo zuri na

lililoandaliwa vizuri.

Mawazo kwa ajili ya uelekezaji Mwalimu mkuu anaweza kufika darasani kabla ya kuanza kwa moduli (kabla wanafunzi hawajafika). Anaweza kujua matayarisho ya mwalimu na kuangalia

Page 13: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 1

9

dakika 10 za mwanzo za moduli zikoje. Mwalimu mkuu anaweza kutoa mrejesho unaoweza kumsaidia mwalimu (unapohitajika) kutegemea orodhahakiki.

Mawazo kwa ajili ya ujifunzaji wa pamoja/ binafsi • Walimu wanaweza kuandaa masomo yao, na madarasa yao kwa kutumia

orodhahakiki waliyoiandaa. Wanaweza pia kuandaa vipindi kwa pamoja. • Walimu wanaweza kutengeneza mfumo wa kusaidiana, wakizingatia na kutoa

mrejesho baina yao kutegemea viashiria.

Uzingatiaji wa masuala ya kijinsia na ujumuishi Wakati wa mafunzo na Uelekezaji, watake washiriki kufikiria ni kwa jinsi gani viashiria vinasaidia vizuri mpangilio wa darasa watakavyo, kuwapo kwa vifaa na kujiandaa kwa mwalimu kuhusiana na:

• Kuhakikisha wavulana na wasichana wanajisikia vizuri na wanashiriki ipasavyo;

• Kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu (kama vile, wasio zungumza lugha ya wengi, au waliojiandikisha kwa kuchelewa kwa miaka kadhaa);

• Kuwasaidia watoto wenye ulemavu. Kupitia mafunzo na uelekezaji, waombe walimu na walimu wakuu kupitia yafuatayo:

• Je darasa linaingilika kwa wanafunzi wote?

• Je kuna vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu, kwa mfano kwa wanafunzi wenye matatizo ya kuona au kusikia?

• Katika matayarisho yako, je umefikira athari za maandalizi yako kwa wasichana na wavulana?

• Je mwalimu anaweka mazingira yanayowapa heshima watoto wote? • Je kuna mabadiliko yoyote yanayohitajika kuhusu viashiria?

Marejeleo Vyanzo vifuatavyo vilitumika katika kuandaa moduli hii:

• “Discover Best Practices for Preparing Your Classroom for the New School Year.” Linapatikana: http://rethinkrethink.com/blog/2016/08/31/back-to-school-classroom-preparation/

• Dorrell, A. “Get Organized! Preparing Your Classroom for Learning”. Linapatikana: www.earlychildhoodnews.com/earlychildhood/article_view.aspx?ArticleID=572

Page 14: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Wafahamu na Wahusishe wanafunzi wako wote

10

Kitini cha 1 Darasa lilivyopangiliwa

Vifaa, nyenzo na zana za , darasani

Matendo ya Mwalimu kuwaandaa wanafunzi wote katika kujifunza

• Wanafunzi wote wanaona ubaoni

• Madawati na viti

vimepangwa ili kuwezesha majadiliano kwa vikundi

• Kuna mpango wa

ukaaji kwa watoto wote

• Darasa linaingilika

kwa wanafunzi wote (ikiwa haliingilikia 100%, kuna mpango kuwasaidia wanafunzi waweze kuingia, wawe huru kutoka na kuingia wakati wanapohitaji.)

• Mwalimu

anauwezo wa kuwaona wanafunzi wote

• Kuna vitabu vya kutosha kwa kila mwanafunzi

• Kuna chaki za kuandikia ubaoni

• Kila mwanafunzi ana

daftari la mazoezi na peni au penseli

• Kuna nyenzo za

kusaidia kujifunzia kwa wanafunzi anayehitaji

• Mwalimu anawakaribisha wanafunzi wote

• Mwalimu ameweka matarajio ya wazi kuhusu tabia na ujifunzaji

• Mwalimu anajua wanafunzi kwa

majina yao

• Mwalimu anawajua wanafunzi wake walivyo (watokako familia zao, lugha wanazoongea, uimara na udhaifu wao)

• Mwalimu anatengeneza mazingira ya

kuheshimiwa • Mwalimu anawahamasisha na

kuwashugulisha wanafunzi katika masomo yafundishwayo

• Mwalimu anaandaa mahali na

kutambulisha somo atakalofundisha pamoja na malengo yake

• Mwalimu anaweka kanuni au kurejea

kanuni zilizopo • Mwalimu anatoa nafasi kupata

maswali au mrejesho • Mwalimu anawashirikisha wavulana

na wasichana kwa usawa

Page 15: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 2

11

Kitini cha 2

Kiashiria Kwanini hili ni muhimu katika kuandaa darasa lako kwa ajili ya ujifunzaji?

Mwalimu anawakaribisha wanafunzi wote

ü Kuwatia moyo watoto kushiriki, kujifunza na kujishughulisha ipasavyo

ü Kujenga kujiamini na kujitambua ü Kukuza hali ya kujiona ni mwana shule na darasa fulani.

Mwalimu anafahamu majina ya wanafunzi

ü Hufanya wanafunzi kujiona wanakaribishwa na kuthaminiwa ü Husaidia kuwapo kwa uhusiano chanya baina ya wanafunzi

na walimu ü Husaidia kumfanya mwalimu aliongoze darasa na kutawala

tabia vizuri zaidi.

Mwalimu anawajua wanafunzi wake walivyo (watokako familia zao, lugha wanazoongea, uimara na udhaifu wao)

ü Humaanisha kuwa mwalimu anaweza kumfundisha kila mwanafunzi darasani na kuchochea kujishughulisha kunakotokana na tabia na mahitaji halisi ya mwanafunzi

ü Mwalimu anaweza kumsaidia mwanafunzi ikiwa anataarifa kuhusu maumivu makali ya nafsi

ü Mwalimu anaweza kuwa na mwitiko kuhusu mahitaji ya wanafunzi wenye ulemavu, mahitaji yao ya ujifunzaji, na tofauti zao za lugha na mila.

Mwalimu anatengeneza mazingira ya kuheshimiwa

ü Wanafunzi wanaweza kujishughulisha na ujifunzaji na kujifunza kutoka kwa wenzao.

Mwalimu anaweka mazingira ya wazi

ü Mwalimu anapokuwa wazi kuhusu kile kinachotarajiwa kutoka kwa wanafunzi kuhusiana na tabia zao, kazi na juhudi zao, na akalieleza wazi hili, hii huchangia kaika kuwapo kwa mazingira chanya ya ujifunzaji.

Mwalimu anaweka kanuni

ü Watoto wanatarajiwa kuendelea vizuri na sio rahisi kupotoka au kuwa na tabia mbaya katika mazingira ya ujifunzaji yenye mfumo wa wazi na ambao unaweza kubashirika.

ü Mifano ya mazoea ni pamoja na mwanzo wa darasa, mwisho wa darasa, kuwa na darasa safi, kuwa na wanafunzi katika makundi, kuwafanya wanafunzi wawe wasikivu, na kuwapo kwa muda wa shughuli mbalimbali.

Mwalimu anatumia mbinu chanya za kuweka nidhamu

ü Epuka matumizi ya adhabu zinazonyanyasa na kuumiza, ambazo hazisaidii mwanafunzi katika ujifunzaji, na badala yake weka namna mbadala ya kuwa na matokeo yaleyale.

Page 16: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Wafahamu na Wahusishe wanafunzi wako wote

12

Kitini cha 3 Kiashiria 1 Wanafunzi wamekaa mahali wanapoweza kuona ubao. 2 Darasa limepangwa na ni safi 3 Darasa linafikika kwa wanafunzi wote (wote wanaweza kuingia, kukaa

na kutoka kwa urahisi darasani). 4 Kila mwanafunzi ana daftari la mazoezi, peni na penseli 5 Ni rahisi kwa kila mwanafunzi kupata kitabu cha kiada (kila mtu kimoja

au kuchangiana) 6 Mwalimu anajua jina la kila mwanfunzi 7 Malimu anatabasamu na kuwakaribisha wanafunzi wote darasani 8 Mwalimu anaweka matarajio ya wazi kuhusu heshima na tabia ya kuwa

na usikivu darasani 9 Mwalimu anazunguka darasani kuwatuliza wanafunzi ili waanze moduli 10 Mwalimu anawasikiliza na kuwashughulisha wavulana kwa wasichana

kwa usawa mwanzoni mwa kila moduli 11 Zipo zana za kujifunzia ambazo zinafaa 12 Kuna maandalizi ya mbinu bora za kufundishia 13 Maandalizi ya shughuli za kufundishia na kujifunzia 14 Mwonekano wa mwalimu mbele ya wanafunzi

Page 17: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 2

13

2. Wafahamu na Wajumuishe

Wanafunzi Wako Wote

¹ Jumla ya saa 2 Malengo ya Mafunzo Kufikia mwisho wa moduli hii, washiriki wataweza: • Kuelewa umuhimu wa kuwahusisha

na kujua maana ya kuwahusisha wanafunzi wote (NTCF 2.4)

• Kueleza vikwazo wanavyokumbana navyo wanafunzi ambao hawakujumuishwa (NTCF 2.4)

• Kubuni stadi zitakazokusaidia kupunguza vikwazo katika ujifunzaji

na kutengeneza darasa jumuishi (NTCF 2.4)

Vifaa vinavyohitajika • Kuandaa chati ya kuandikia • Peni

Kadi za shughuli za Shule (zitolewe toka Kitini cha 2)

• Orodhahakiki za taarifa za Manafunzi • Kitini • Vidokezo vya Mwezeshaji

Page 18: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Wafahamu na Wahusishe wanafunzi wako wote

14

Taarifa za kuwapa washiriki wakati wa moduli Kuwahusisha wanafunzi wote katika elimu inamaanisha kuwa wanafunzi wote wapo shuleni na hakuna aliyeachwa. Inamaanisha kuwa watoto wote wanashiriki darasani na hakuna aliyeachwa. Na inamaanisha kuwa watoto wote wanapata kile ambacho wanauwezo nacho shuleni. Ni muhimu kutambua na kuelewa kuwa watoto hujifunza kwa njia tofauti na kwa kasi tofauti. Ikiwa walimu wataanzia hapa, mengi yatawezekana. Ushahidi unaonesha kuwa juhudi zinazofanywa kuwahusisha watu wote katika kusoma huwafaidisha wote. Elimu jumuishi inatambua kuwa watoto wote wanaweza kujifunza. Elimu jumuishi inatambua kuwa shule, walimu na mifumo ya shule ni lazima zibadilike na kuchukua wanafunzi wote wa aina mbalimbali, badala ya kulazimisha kubadilika kufuata mifumo ambayo haielewi wala kutimiza mahitaji yao. Elimu jumuishi: • Inatambua na kuheshimu tofauti zilizomo katika watoto: umri, jinsia, ukabila, lugha,

ulemavu na hadhi kiafya (kwa mfano HIV), Uwezo wa watoto (wenye vipawa, wanaojifunza taratibu), hadhi ya kiuchumi-jamii, yatima, watoto wa mitaani, wenyekutumia mabavu, umbali (toka nyumbani kwenda shuleni), n.k

• Inaruhusu miundo ya elimu, mifumo na mbinu za ufundishaji ili kupata mahitaji ya watoto wote;

• Ni mchakato ambao kila wakati unabadilika; • Hulenga kuwa na jamii jumuishi. Kuelewa kuwa watoto husoma na kukua kwa kasi tofauti ni jambo muhimu kwa walimu wanaotaka kuwa na wote wanaojifunza. Walimu wanahitaji stadi kusaidia tofauti hizi za wanafunzi. Stadi hasa huwa katika ufundishaji ulio wazi na unaopatikana lakini pia, katika kuwafahamu wanafunzi ili kuweza kuwasaidia katika mahitaji yao tofauti na katika uwezo wao na ukuaji tofauti. Mitazamo hasi ni kikwazo kikubwa katika kuwahusisha watoto. Walimu wanapaswa kuwa katika hali ya kuongea na kupinga ubaguzi ambao unaweza kuwa unasababishwa na mambo ya tamaduni, mila au sababu za kidini. Ubaguzi unaweza pia kuwa sababu ya imani kuhusu yale watoto fulani wanayoweza kufanya na yepi ambayo hawayawezi, au wanayotakia kufanya na ambayo hawatakiwi. Walimu pia wanapaswa kuwa na ufahamu na stadi za msingi ili kuweza kuwapatia watoto mahitaji muhimu ya kusoma darasani ambayo wanaweza kuyaendeleza wanapokwa kama walimu. Kuwajumuisha wanafunzi wote humaanisha kupunguza aina zote za vikwazo katika ujifunzaji wa watoto

Page 19: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 2

15

Kazi za kufanya 1. Tafakuri ¹ Dakika 30

Nia ya shughuli hii ni kusaidia kutafakari ni watoto wepi hutengwa mara kwa mara katika kupata elimu katika muktadha wetu na kile kinachosababisha haya. Wagawe washiriki katika makundi manne.

“Leo tutaangazia jamii zetu na shule zetu. Tutafikiria kuhusu watoto tunaowafahamu ambao hawapo shuleni au hawahudhurii kila siku, au wanaacha shule mapema, au

hawashiriki na kujifunza vizuri shuleni. Jadilianane katika makundi yenu hao watoto ni kina nani. Je ni wengi – unaweza kukadiria ni kama watoto wangangapi ambao hawapo shuleni katika jamii zenu?” Waulize makundi ni jinsi gani tunavyoweza kumtambua mtoto aliyeko darasani lakini hajifunzi. Sisi kama walimu tunaweza kumtambuaje? Mwombe mwakilishi katika kila kundi aeleze yaliyoonwa katika kundi lake.

“Angalia watoto mliowataja na jadili ni nini hicho ambacho: a) kinawafanya wasiwepo shuleni; b) kinawazuia wasijifunze wanapokuwa shuleni.

Andika majibu yako katika chati ya kuandikia.” Watake makundi kuangalia majibu yote. Katika kila jibu, sisitiza kuwa mtoto si tatizo. Waelekeze washiriki kutambua sababu zinazombagua mtoto.

“Ni tatizo katika mfumo wa elimu, shule na jamii, mawazo na tabia hasi, ambazo zinawabagua watoto.”

Toa baadhi ya mifano:

• Mtoto wa kike hawezi kwenda shuleni anapokuwa katika hedhi, kwani shuleni hakuna choo.. Kwahiyo mazingira ya shule ndilo tatizo.

• Mtoto anazungumza lugha tofauti kwa mwalimu na hawezi kuelewa somo. Hili ni tatizo la uwezo wa mwalimu (mwalimu hana stadi za kuweza kuwasiliana na mtoto).

• Wazazi wanadhani wanatakiwa kuwaacha nyumbani watoto wenye ulemavu. Hapa mila na desturi za jamii ndizo tatizo.

• Watoto huchelewa kufika shuleni kwani wanatakiwa kuombaomba au kuuza bidhaa ili kupata chakula cha siku: ufukara hapa ni tatizo.

Wapatie washiriki Kitini cha 1 na kipitie pamoja nao. 2. Jenga shule yako ili iwahusishe wote wanaojifunza ¹ Dakika 45

Sema

Sema

Sema

Page 20: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Wafahamu na Wahusishe wanafunzi wako wote

16

Nia ya shughuli hii ni ili washiriki: • Wafikirie kuhusu shule yenye uhalisia. • Wajizoeze kuamua ni mazingira gani yanaweza kuwapo ili kuweza

kuwachukua wanafunzi wote. • Wafahamu namna ya kufanya uamuzi na nini kipewe kipaumbele.

Wagawe washiriki katika makundi 4. Kila kundi lipe jozi ya kadi ya “tofali” kutoka Kitini cha 2. Weka humo kadi zisizo na maandishi.

“Hivi si vipengele vyote vya shule nzuri. Kuna vipengele ambavyo watu hudhani ndivyo hufanya shule kuwa nzuri, na vingine ambavyo watu hudhani havifanyi shule kuwa nzuri.

Chagua kadi tofali zitakazojenga shule yako uitakayo. Chomeka tofali hizo katika ukuta karibu nawe. Fikiria ni kwa nini unafanya maamuzi haya yote. Ikiwa kuna kipengele chochote muhimu kinachokosekana, unaweza kukiandika katika kadi zilizo wazi na kukiongeza katika ukuta wako. Ukimaliza, angalia upya uchaguzi wako. Weka alama katika tofali ambayo inawakilisha mambo ambayo unadhani ni magumu shuleni kuyapata katika muktadha wako. Eleza kwa nini.” Waambie makundi kuzunguka katika chumba kwa dakika 5 (kuzunguka ili kuangalia picha). Makundi yaangalie kwa kila moja ni ipi shule yenye uhalisia. Watake waangalie ni kwa namna gani kuna kufanana na kutofautiana. Liagize kundi MOJA kusimama mbele ya shule yao na kuonesha yafuatayo:

• Tabia kuu za shule yao ya mfano;

• Kwanini walichagua tabia hizi;

• Ni tofali gani ni rahisi kuliweka au kuliacha;

• Ni lipi lilikuwa gumu zaidi kuwekwa au kutolewa;

• Je mliamua kufuata nini ni lipi libakie na lipi litolewe? Mlitumia misingi ipi iliyowaongoza?

Acha makundi mengine yaongeze mawazo yao ikiwa wana jambo la kusema ambalo ni tofauti.

Shule zenye uhalisia huwa hazipo popote.

• Je ni kwanini inasaidia kufikiri kuhusu shule yenye uhalisia? • Inamaanisha nini kwamba makundi tofauti yamekuja na mawazo tofauti? • Ni kwa jinsi gani mambo tuliyoyachagua yanaunga mkono (yanasaidia) kuwahusisha watoto wote,

kwa maana ya wao kuwapo, kushiriki na katika mafanikio?

Sema

Sema

Page 21: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 2

17

• Je, kuna mambo yoyote tuliyoyachagua yanaweza kuwa magumu kwa wanafunzi kushiriki katika kupata elimu?

• Kwanini inasaidia kufikiria misingi ambayo kwayo uchaguzi mgumu unafikiwa? • Ni misingi gani ya kufanya maamuzi kuhusu kuboresha elimu ambayo inasaidia katika kujaribu

kuisaidia shule iwe yenye kupokea ? Kuweka kumbukmbu ya majadiliano haya katika chati 3. Suluhisho na Mikakati: Kuwajumuisha watoto wote darasani ¹ Dakika 45

Nia ya shughuli hii ni kukuza orodha ya msingi ya mikakati ya kiutendaji ambayo inaweza kutumiwa na walimu darasani na ambayo itawakusanya wanafunzi wote katika ujifunzaji. Tutaegemea katika hili kwenye mjadala wetu.

“Ni kazi ya mwalimu kumfahamu kila mwanafunzi akiwa mtu binafsi, ili wanafunzi waweze kutiwa moyo na kusaidiwa katika njia sahihi. Ikiwa tutafundisha somo lile lile kwa wote, basi huenda baadhi ya watoto au labda wengi wataachwa katika ujifunzaji.

Kuitika kwa kila mahitaji ya mtoto inaweza kuwa na changamoto zake, hasa pale ambapo darasa ni kubwa. Lakini hiyo haimaanishi kuwa walimu hawawezi kufanya jambo lolote lile”.

Wapatie washiriki Kitini cha 3. Eleza kuwa jedwali katika kitini lina vipengele maalumu ambavyo vinaweza kuathiri uwezo wa kujifunza wa mtoto. Waulize ikiwa wamepata kumwona mtu anayejifunza mwenye tabia au vipengele kama hivyo au kama wanataka kuongeza lolote. Wapatie mifano kutoka kwenye mwongozo wa mwezeshaji Wagawe washiriki katika makundi 4: • Waombe kila kundi kuchagua tabia 4 au zaidi kutoka katika jedwali. Wanapaswa

kuchagua angalau 3 zinazoweza kuwa changamoto katika ujifunzaji na ushiriki, na angalau 1 inayowezesha ujifunzaji.

• Jadili athari za kila tabia katika ujifunzaji na ushiriki (athari inaweza kuwa chanya au hasi; au yote mawili).

• Bainisha ni kwa namna gani walimu wanaweza kusaidia vizuri zaidi katika ujifunzaji na ushiriki wa mtoto mwenye tabia hizi. Sisitiza kuwa unahitaji mawazo yanayoweza kutendeka katika maeneo ambayo walimu wanafanya kazi, sio mapendekezo kwa mwalimu mwenye kila kitu.

Waombe kundi la 1 kuwasilisha kuhusu tabia 2 za changamoto na 1 inayowezesha ujifunzaji. Waombe kila kundi linalofuata kuwasilisha kuhusu tabia za ziada ambazo wamejadili. Ruhusu dakika 5 za maswali au maoni kila baada ya kundi kuwasilisha.

Sema

Page 22: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Wafahamu na Wahusishe wanafunzi wako wote

18

Andika kila wazo katika chati. Wakati huo huo, angalia yale wanayoyadhania washiriki. Kwa mfano, ikiwa mtoto anauwezo mkubwa wa kiakili, je inamaanisha kuwa atajifunza vema pia? Haitakuwa hivyo ikiwa amepoteza hamu ya kujifuza. Je, mwalimu anaweza kuutumia vipi uwezo wa mtoto huyo kiakili ili kuwasaidia wengine? Andika mawazo haya ya nyongeza. Waombe washiriki kunakili mikakati yote iliyoelezwa katia kundi kutoka katika chati kwenda katika vijitabu vyao vya mazoezi. Mwombe kila mshiriki kuchagua mkakati mmoja ambao atautumia katika kufundishia kutokea sasa. Wahamasishe kuchagua mikakati mingi inavyowezekana. Wapatie washiriki Kitini cha 4 ili warejelee. Kinaonesha thamani na umuhimu wa kutumia mikakati darasani ili kumjumuisha kila mtu. Pitia katika Kitini cha 5. Kinaonesha baadhi ya taarifa za awali ambazo walimu wanaweza kusikusanya kuhusiana na wanafunzi wao, kusaidia katika kuwafundisha wanafunzi wengine. Huu ni mwisho wa moduli hii. Mwezeshaji apime iwapo malengo ya moduli hii yamefikiwa.

Viashiria vya mafanikio Kufikia mwisho wa moduli hii, washiriki wataweza:

o Kubainisha ni mwanafunzi yupi anan’gan’gana kuwapo shuleni akijitahidi kuhudhuria shuleni na/au akijifunza darasani.

o Kueleza maana, misingi na umuhimu wa elimu jumuishi. o Kubuni mikakati kuwasaidia watoto wenye tabia na mazingira mbalimbali darasani.

Mawazo kwa ajili ya Uelekezaji Kuwahusisha wanafunzi wote ni mchakato unaobadilika na unaoendelea. Walimu wakuu na waelekezaji wanaweza kuwaleta walimu pamoja kila mara ili washirikishane uzoefu wao, changamoto na mafanikio yao katika kuwajumuisha wanafunzi wote kwa pamoja. Kubalianeni mpango huu na walimu wakuu au waelekezaji. Wakati wa mikutano hii walimu wanatakiwa kutiwa moyo ili kushirikishana namna walivyoweza kuwasaidia wanafunzi wenye matatizo, na kushauri namna watakavyofanya tofauti siku za usoni. Ikiwa walimu wanapata changamoto kutoka kwa mwanafunzi au kundi la wanafunzi, mwalimu mkuu au mwelekezaji anaweza kwenda kuliona darasa na kutoa mrejesho. Vinginevyo, wanaweza kuingia darasani kama walimu wenza, wakaliona tatizo na kusaidia kulitatua.

Page 23: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 2

19

Walimu wakuu wanaweza kupendekeza kutambuliwa kwa walimu wale walioonesha juhudi za kuwajumuisha wanafunzi wote. Wanaweza kuitwa ili waingine kwenye mashindano, wapewe tunzo, wapate barua za kutambua juhudi zao n.k.

Mawazo kwa ajili ya ujifunzaji wa pamoja/binafsi • Walimu hawana budi kukutana mara kwa mara, au kuwasiliana kwa kutumia

ujumbe (sms) kupigiana simu, kujadiiana na kupeana uzoefu, mafanikio na changamoto. Wanaweza pia kujifunza kuhusu mikakati ambayo wengine wameona ina mafanikio.

• Walimu wanaweza kuangalia vipindi vya walimu wenzao ili kuelewa vizuri zaidi na kuweza kutatua changamoto.

• Walimu wanaweza kukutana na kamati za shule ili kuomba wanajamii kusaidia ushiriki wa ujifunzaji wa wanafunzi hasa wenye matatizo.

• Kila wiki mbili au kila mwezi, walimu wanaweza kuchagua mkakati mmoja ili kuwasaidia watoto wenye matatizo katika kujifunza na kushiriki. Wanaweza kuweka kumbukumbu ya ni namna gani, na ni lini walipotumia mkakati, namna ilivyokuwa na jinsi inavyoweza kuboreshwa. Wanaweza kuwashirikisha maendeleo yao, walimu wakuu na au walimu wengine.

Marejeleo Vyanzo vifuatavyo vilitumika wakati wa kuandaa moduli hii:

• ESSPIN (2013) “Inclusive Education Approach Paper”, Education Sector Support Programme in Nigeria. Linapatikana: www.esspin.org

• TiCCWG (2016) “Training Pack for Primary School Teachers in Crisis Contexts” Module 2: Child Protection, Well Being and Inclusion. Teachers in Crisis Contexts Working Group. Linapatikana: www.ineesite.org/en/training-pack-for-primary-school-teachers-in-crisis-contexts

• TiCCWG (2016) “Training Pack for Primary School Teachers in Crisis Contexts” Module 3: Pedagogy. Teachers in Crisis Contexts Working Group. Linapatikana: www.ineesite.org/en/training-pack-for-primary-school-teachers-in-crisis-contexts

• Ministry of Education and Sports, Directorate of Education Standards, Uganda (2012) “Evaluating and Improving the Quality of Education”, Section 3, How Can we Improve our Teaching? Linapatikana: www.lcdinternational.org/improvement-guides

Page 24: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Wafahamu na Wahusishe wanafunzi wako wote

20

Mazingira jumuishi

ya Ujifunzaji

Kitini cha 1: Mazingira ya ujifunzaji shirikishi

Inajumuisha watoto WOTE: wasichana na wavulana; wanaotoka mila tofauti au lugha tofauti; wale wenye uwezo maalum au mahitaji ya ujifunzaji; wasichana wajawazito; walioathiriwa moja kwa moja kwa HIV na UKIMWI; nk.

Masuala nyeti kitamaduni, Huendeleza tofauti, na huchochea ujifunzaji kwa watoto WOTE

Salama; huwalinda watoto WOTE kutoka kuumizwa, ukatili, na unyanyasaji

Kukuza ushiriki, ushirikiano, na Kufanya kazi kwa pamoja

Kujifunza ni muhimu kwa maisha ya kila siku ya watoto; watoto huwajibika katika ujifunzaji wao

Kukuza fursa kwa walimu Kujifunza na kufaidika kutokana na ujifunzaji

Page 25: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 2

21

Kitini cha 2: Jenga kadi jumuishi za shule

Adhabu kali Walimu wanaotabasamu Njia za kulinda darasa dhidi ya mafuriko, wadudu, wanyama, matope

Walimu wanaoogopesha Hakuna ngazi, kila mtu anaweza kuzunguka kirahisi shuleni

Madirisha makubwa yaliyowazi ili watoto wenye uoni hafifu waweze kuona kwa urahisi

Vipo viti nusu ya waliopo shuleni Madirisha madogo, au yaliyofungwa ili kuzuia joto, vumbi na mvua

Vyoo tofauti, vilivyo salama kwa wasichana na wavulana

Viti vizuri kwa kila mmoja kukaa Vitabu vya msingi katika lugha zote ambazo watoto wanasiongea kama lugha zao za kwanza

Walimu wanaotumia Kiingereza tu ili watoto wapate kufahamu mengi kutokana nacho

Walimu waliofundishwa kutumia lugha ya alama kuwasiliana na watoto viziwi

Walimu waliofundishwa kumiliki darasa vema bila ya kutumia nguvu Darasa lenye kati ya watoto 30 na 40

Walimu ambao mara nyingi husoma kutoka kitabuni mbele ya darasa Walimu ambao hawawajibishi madarasa yao Darasa lenye wanafunzi hadi 200

Walimu ambao wanafurahia kutumia njia nyingi za kuchangamana na watoto na kuanzisha taarifa

Walimu ambao huwatia moyo watoto kusaidiana na wenzao

walimu ambao wanatuzwa kwa wanafunzi wao kupata alama za juu darasani

Walimu ambao wanatuzwa tu kwa darasa lao kupata alama za wastani au alama za juu

Shule na menejimenti ya shule ambayo hujaribu kutatua matatizo ambayo watoto huwa nayo kwa kuwapo na kuhudhuria shuleni

Shule ambayo hujaribu kuwatoa watoto ambao hupata alama za chini na hivyo kuathiri shule kupata alama za wastani

Page 26: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Wafahamu na Wahusishe wanafunzi wako wote

22

Kitini cha 3 Tabia

Hawezi kutembea Ana udhaifu katika kusikia/na au kuongea

Anaongea lugha tofauti na ile ya mwalimu/lugha ya shule Wavulana

Kabila la watu wachache Watoto wenye uwezo mzuri kimwili

Kutoka familia fukara Dhaifu au mgonjwa

Ana kipawa katika somo moja au zaidi

Ugumu wa kujifunza kwenye eneo moja au zaidi la kujifunza

Mwenye afya Tofauti za kidini kwa watoto walio wengi

Watoto wenye uwezo juu ya wastani

Kutoka katika familia yenye uhakika wa kipato

Wasichana Mama siyejua kusoma

Mtoto mwenye ualbino Hakuna mlezi mtu mzima

Hawezi kushika peni Ana tatizo la kuwa makini

Hawezi kuona Amekuwa mgonjwa wa kitu cha kuogofya

Page 27: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 2

23

Tabia Athari katika Ujifunzaji Wajibu wa Malimu

Page 28: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Wafahamu na Wahusishe wanafunzi wako wote

24

Kitini cha 4: Kuweka mikakati jumuishi

MIKAKATI KWA ELIMU JUMUISHI1. Bainisha watoto wenye mahitaji/ujifunzaji maalumu2. Tengenezashughulizadarasanizilizojumuishi3. Kuelewayaleyatakayofundishwa4. Husianishayanayofundishwanamazingirahalisi

Je, hii inawasaidiaje watoto kujifunza? 5. Inaonyesha heshima kwa wote huku mwalimu akiwa ndiye mfano.

6. Inasisitiza uhusiano chanya na wa kiuaminifu.

7. Inakuza kujiamini na kujiheshimu.

8. Inawezesha usomaji na ushiriki makini: ikiboresha matokeo ya usomaji.

9. Inatokeza hali ya kujisikia kuwapo mahali, na wajibu.

10. Inasaidia mchakato wa ufuatiliaji wa usomaji wa mtu.

11. Mwalimu hujua ni lini atumie ukali na ni lini afundishe kwa kutia moyo.

12. Hali ya ustawi, mahitaji ya mtoto yanajulikana na kueleweka.

13. Kuzuia matatizo na masuala ya kitabia.

Page 29: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 2

25

Kitini cha 5: Maelezo ya Mafupi ya Mwanafunzi Mwalimu anaweza kuuliza maswali na kujaza fomu, au anaweza kuwaomba wanafunzi kujaza fomu wenyewe.

Jina la Mtoto: Darasa: Umri: Mwalimu: 1 Kuhusu Familia yangu

Mtoto anaishi na: • Wazazi • Familia pana

Ndugu: Kaka, dada (walio au ambao hawako shuleni)

2 Marafiki zangu

3 Mambo niyapendeleayo na yaniburudishayo

4 Shule yangu Niyapendayo kuhusu shule yangu: Nisiyoyapenda kuhusu shule yangu:

5 Uwezo na Stadi zangu shuleni Somo Nilipendalo/ Nisilolipenda Kile ninachokiweza Kile ninachotaka nipate msaada

6 Matarajio na niyatakayo Nitakapoondoka shuleni ningependa:

7 Mafanikio yangu (Michezoni, Ujifunzaji, mengine)

Page 30: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Wafahamu na Wahusishe wanafunzi wako wote

26

Muhtasari wa Mwelekezaji Mifano

Tabia Athari katika ujifunzaji Mwitiko wa Mwalimu

Mvulana mwenye ualbino hawezi kuona vizuri ubaoni

Hataweza kufuatilia malekezo au yale yanayotolewa kupitia ubaoni. Kuna uwezekano wa kuwa nyuma katika ujifunzaji na katika ushiriki wake

Mlete akae mbele darasani na uangalia ikiwa inasaidia au la. Mwangalie mvulana usoni mara kwa mara ili kuona sura yake ilivyo, kwani unaweza kuona ikiwa anashiriki au anajifunza. SZungumza na wazazi wa mtoto ili kujua zaidi atokako, changamoto na mafanikio yake.

Mvulana anaona hisabati ina changamoto

Kujifunza na kukumbuka dhana mpya kunahitaji muda na kurudia rudia

Mpatie usaidizi wa ziada wakati wa moduli ya hisabati. Panga masomo ya nyongeza, rudia, pitia na hakikisha uelewa. Mweke mvulana akae na yule ambaye anaona masomo ni rahisi.

Msichana anatarajiwa kufanya kazi za nyumbani kabla na baada ya shule

Anaweza kuchoka na hivyo kumwia vigumu Kumakinika. Anaweza kuchelewa shule na asifanye kazi za nyumbani au kuwasilisha kazi isiyobora.

Zungumza na PTA kuangalia masuala yanayomhusu msichana huyu. Jadiliana na wazazi wake; tafuteni kwa pamoja suluhisho zuri. Mpatie muda baada ya shule ili afanye kazi za shule, ajiunge na klabu za kimasomo/vipindi vya kupitia masomo.

Page 31: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli 3

27

3. Zifahamu Familia na Jamii za Wanafunzi Wako

¹ Jumla ya saa 2

Malengo ya Moduli Kufikia mwisho wa moduli hii, washiriki wataweza: • Kueleza umuhimu wa ubia wa pamoja

baina ya wazazi, walimu, shule na jamii kwa ajili ya ushiriki wa watoto na ujifunzaji wao (NTCF 3.4)

• Kubainisha uhusiano uliopo baina ya mashule, familia na jamii (NTCF 3.4)

• Kutumia mbinu mbalimbali za kuwashirikisha wazazi katika ujifunzaji wa watoto na kuunganisha shule na jamii (NTCF 3.4)

Vifaa vinavyohitajika • Chati • Peni • karatasi za kuandikia nukuu • Chati na peni za ziada kwa washiriki • Vitini

Page 32: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Elewa familia za wanafunzi wako na jamii zao

28

Taarifa muhimu za kushirikishana na washiriki wakati wa moduli hii Wazazi wanapounga mkono maendeleo ya watoto wao na ujifunzaji wao shuleni hili laweza kuwa na matokeo chanya katika elimu yao. Ufahamu wa walimu na namna wanavyozingatia hali za wanafunzi, uwezo wao na tabia zao nyingine vinaweza pia kuleta athari chanya. Matokeo yake ni kuwa na tabia, mahudhurio na mafanikio bora zaidi. Ushiriki wa wazazi wenye mafanikio kwa kawaida unamaanisha wanashiriki kikamilifu katika elimu ya watoto wao. Kwa mfano, wazazi wanaweza kusoma na watoto wao nyumbani, wanaweza kuwasaidia katika kazi zao za nyumbani, kuhudhuria mikutano ya wazazi, au kujitolea shuleni. Ushiriki wa wazazi na jamii unaweza pia kuchochea uwajibikaji mkubwa, ikiwa ni pamoja na mahudhurio mazuri ya walimu, kuwahi na utendaji bora darasani. Licha ya ushahidi chanya kuhusu kuhusika kwa wazazi, walimu hujisikia kuwa hawawezi kushirikiana na wazazi. Walimu wanaweza kufikiri kuwa familia hazitaki kushirikishwa, au walimu wanaweza kutokujiamini na kukosa stadi za kushirikiana na wazazi. Familia pia zinaweza zisijue namna ya kujihusisha na kuendelea kujihusisha. Wazazi wanaweza kuhisi hawana muda, au kuwa hawakaribishwi. Mawasiliano sahihi baina ya wazazi na walimu yanaweza kusaidia kuboresha utendaji wa wanafunzi. Shule ambazo zinakuza kushiriki kwa wazazi mara nyingi huunga mkono kuwa kufanikiwa kwa wanafunzi ni jambo linalohitaji ushirikiano kati ya shule, walimu na familia. Wazazi wanachukuliwa kuwa ni wabia muhimu katika usomaji, na matendo dhahiri yanachukuliwa kuunga mkono suala hili. Wanaonesha njia dhahiri ambazo kwazo ubiya unaweza kuanzishwa na kudumishwa. Ubia unahitaji kufanya kazi kwa pamoja kati ya walimu wakuu, walimu na wazazi. Kunaweza kuwepo changamoto, lakini ushahidi unaonesha kuwa faida inayopatikana ni kubwa kiasi cha kutokuweza kupuuzwa.

1. Tafakuri ¹ Dakika 45

Nia ya shughuli hii ni kuweza kutambua namna familia na wanajamii wanavyoweza kuwa na athari chanya kwa mahudhurio ya watoto, ushiriki wao na mafanikio shuleni.

“Fikiria kuhusu mtoto darasani kwako; hasa mtoto ambaye umekuwa ukimfundisha kwa muda. Je ni mvulana au msichana? Taja majina yao kimya kimya.”

Soma maelezo yote matatu katika Kitini cha kwanza katika kikao cha pamoja. Usichukue majibu yoyote kutoka kwa washiriki hadi maelezo yote matatu yawe yamesomwa. Acha washiriki watafakari wakati ukisoma.

Sema

Page 33: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli 3

29

Fikiri - Kaa katika Jozi - Elezana Washiriki wajadiliane na wenzao kuhusu maswali yafuatayo, kisha chukua nukuu ya majibu matatu mpaka manne katika kikao cha pamoja.

• Je, kulikuwa na swali lolote ambalo ulijisikia hujui kitu? Ni lipi?

• Kuna faida gani kwa mwalimu kumfahamu vizuri mwanafunzi? • Kuna faida gani kwa mwalimu kuifahamu na kushirikiana na familia ya

mwanafunzi?

• Kuna faida gani ya kufahamu na kuwasiliana na jamii atokako mtoto?

Shirikishana Kitini cha 2 na washiriki. Uliza: Je kitini hiki kinasisitiza nini? Kwa mfano, kinaonesha kuwa mtoto haishi peke yake, bali yupo ndani ya himaya ya wajibu na ulinzi. 2. Chukua muda kuwaunganisha: mwalimu-mzazi, shule-jamii ¹ Dakika 45

Madhumuni ya shughuli hii ni kuwasaidia walimu kukuza na kutumia mikakati ya kuimarisha mahusiano yao na wazazi na jamii pana.

“Katika shughuli ya awali, tulitafakari kuhusu jinsi ambavyo tayari tunashirikiana na wanafunzi wetu, na jinsi tunavyowafahamu vizuri wao, familia zao na jamii zao. Sasa

tutakusanya mikakati hii yote katika sehemu moja na tuongezee mingine mipya ambayo tunadhani itaongeza ufanisi”. Kazi za Kikundi Wapange washiriki katika makundi madogo ya watu 4 au 5. Kila kundi lipe vipande 3 vya chati. Wafanye yafuatayo:

• Katika Chati 1 – orodhesha mikakati ambayo tayari inatumika katika kuwashirikisha wazazi, na jamii, k.v kupitia katika kupanga mikutano ya wazazi shuleni, kuwaandikia wazazi kuhusu masuala yanayohusu watoto wao.

• Katika Chati 2 – andika changamoto walizonazo kwa kila mkakati, ikiwa zipo.

• Katika Chati 3 – andika suluhisho la kukabiliana na changamoto (kuhakikisha kuwa shughuli ya kujifunza ndiyo muhimu kwa watoto).

Mikakati Changamoto Suluhisho • • •

• • •

• • •

“Mkimaliza, acha orodha yako mezani na nenda katika chati ya kundi linalofuata (kundi 1 liende kuangalia chati ya kundi 2, kundi 2 liende kuangalia chati ya kundi 3, na

kadhalika).

Sema

Sema

Page 34: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Elewa familia za wanafunzi wako na jamii zao

30

Soma yale yaliyoandikwa na kundi jingine. Ikiwa mnaweza kufikiria masuluhisho mengine zaidi kwa changamoto, ziongeze kwa kutumia peni ya rangi nyingine.” Onesha Chati zote ubaoni kasha zungumzia yaliyomo katika chati hizo katika kikao cha pamoja.

“Je kuna mikakati mingine zaidi ambayo ungelipenda iongezwe”?

Makundi yajadili kwa kifupi na kuongeza mawazo mapya katika Chati zao. Toa muda kwa ajili ya maoni na maswali kuhusu mawazo mapya, katika kikao cha pamoja. 3. Orodha Hakiki kwa walimu: Kuhusiana na familia na jamii ¹ Dakika 30 Nia ya shughuli hii ni kwa walimu kufahamu na kutumia orodha hakiki ya mikakati ili kuwakutanisha familia pamoja na jamii katika maendeleo ya mtoto na ujifunzaji wake. Katika makundi yao, wape washiriki orodha hakiki katika Kitini cha 3.

“Kuna shughuli nyingi katika orodha hakiki ambazo walimu wanaweza kuzitumia ili kuwakutanisha walimu na jamii. Si lazima kuzitumia zote. Hii ni orodha hakiki ambayo

walimu wanaweza kutoa kinachohitajika kutegemea na muktadha.” Waombe washiriki kupitia orodha hakiki ili kulinganisha na orodha waliyonayo katika chati. Ikiwa kuna jambo lolote muhimu linakosekana, linaweza kuongezwa. Waombe makundi kuonesha mikakati ambayo wanadhani inaweza kufanyika vizuri kwao, kwa watoto darasani kwao n a kwa muktadha wao. Maliza kwa kuchukua maswali kadha katika kikao cha pamoja: ni mikakati gani wanadhani inaweza kufanyika vizuri na kwa nini?

Hii inahusiana na moduli ‘Wafahamu na wajumuishe wanafunzi wote’.

Huu ni mwisho wa moduli hii. Mwezeshaji apime iwapo malengo ya moduli hii yamefikiwa.

Viashiria vya mafanikio o Mwalimu anaweza kufafanua umuhimu wa kuwashirikisha wazazi, familia na jamii

ili kusaidia maendeleo ya watoto na mafanikio yao shuleni. o Mwalimu anaweza kubainisha uimara na udhaifu wa mikakati ambayo tayari

inatumika.

Sema

Sema

Page 35: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli 3

31

o Mwalimu anaweza kuangalia na kutumia mikakati mbalimbali kushirikisha familia na jamii katika ujifunzaji wa watoto.

Mawazo kwa ajili ya uelekezaji Walimu wakuu na waelekezaji wanaweza kusaidia walimu kuitohoa na kutumia mikakati toka katika orodha hakiki. Ikiwa mwalimu atamwalika mzazi shuleni ili kujadili maendeleo ya mtoto au suala la tabia, mwalimu mkuu au mwelekezaji anaweza kuwapo ili kutoa usaidizi na mrejesho kuhusu namna mwalimu alivyoushughulikia mkutano. Mwalimu mkuu anaweza kutoa msaada endelevu wa jitihada za walimu za kuwashirikisha wazazi katika ujifunzaji.

Mawazo kwa ajili ya ujifunzaji wa pamoja/ binafsi • Walimu wanaweza kupitia orodha hakiki pamoja na walimu wengine shuleni na

kupanga jinsi ya kutohoa na kutumia mikakati. • Walimu wanaweza kushirikiana na kamati ya menejimenti ya Shule na PTA (ikiwa

zipo) ili kuelewa majukumu na wajibu wao vizuri zaidi. Waulize ni nini wanachoweza kukifanya zaidi kinachoweza kuwa na athari katika mafanikio ya mwanafunzi.

Uzingatiaji wa masuala ya kijinsia na ujumuishi • Wakati ukiwauliza washiriki wanachokijua kuhusu familia na jamii, chunguza

ikiwa wanajua kuhusu ubaguzi wa kijinsia au upendeleo unaoegemea katika mila au dini.

• Wakati ukiwauliza washiriki wanachokijua kuhusu familia na jamii, chunguza ikiwa wanajua kuhusu ulemavu wowote au ubaguzi wa kikabila au upendeleo unaoegemea katika mila au dini.

• Wakati unaandaa mikakati ya kushirikisha wazazi na jamii, hakikisha kuwa kuna msimamo kuhusu kupunguza ubaguzi. Fikiria jinsi uhusiano baina ya mzazi-mwalimu-jamii unavyoweza kupunguza ubaguzi ambao ni kikwazo kwa watoto kupata elimu, kushiriki na kujifunza.

Marejeleo Vyanzo vifuatavyo vilitumika katika kutayarisha moduli hii:

• Child Trends (2013) “Parental Involvement in Schools”. Linapatikana: www.childtrends.org/indicators/parental-involvement-in-schools/

• Goodall, J na Vorhaus, J (2011) “Review of Best Practice in Parental Engagement”, Department for Education, UK. Linapatikana:

Page 36: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Elewa familia za wanafunzi wako na jamii zao

32

www.gov.uk/government/uploads/system/uploads/attachment_data/file/182508/DFE-RR156.pdf

• Ministry of Education and Sports, Directorate of Education Standards, Uganda (2012) “Evaluating and Improving the Quality of Education”, Section 3, How Can we Improve our Teaching? Linapatikana: www.lcdinternational.org/improvement-guides

• Education World “Parent Involvement in Schools”. Linapatikana: www.educationworld.com/a_special/parent_involvement.shtm

• Save the Children and ESSPIN (2012) “Community Voice for Better Schools. School-based management committees improving schools in Nigeria. Summary of a qualitative research study”. Linapatikana: www.esspin.org

• TiCCWG (2016) “Training Pack for Primary School Teachers in Crisis Contexts” Module 2: Child Protection, Well Being and Inclusion. Teachers in Crisis Contexts Working Group. Linapatikana: www.ineesite.org/en/training-pack-for-primary-school-teachers-in-crisis-contexts

• UNESCO (2006) “Embracing Diversity: Toolkit for creating inclusive learning-friendly environments”. Specialized Booklet 2: Practical tips for teaching large classes. Bangkok, Thailand. Linapatikana: www.unescobkk.org/education/inclusive-education/resources/ilfe-toolkit/

Page 37: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli 3

33

Kitini cha 1: Maswali ya tafakuri 1. Tafakari juu ya kile ukijuacho kuhusu mtoto kutokana na kile ukionacho shuleni. Uliza: • Je, mtoto anatabia nzuri darasani? • Je, mtoto hufanya vizuri katika masomo yake? • Ni masomo gani ni changamoto kwa mtoto? • Je, mtoto anashiriki vema katika shughuli? • Je, mtoto anauhusiano mzuri na wanafunzi wenzake darasani na kwako kama

mwalimu? • Je, mtoto huja shuleni mara kwa mara? • Je, hufika kwa wakati? • Je, mtoto anatatizo lolote maalumu katika ujifunzaji, au katika kufika na

kuondoka shuleni? 2. Tafakari yale uyajuayo kuhusu maisha ya mtoto mbali na yale ya shuleni Uliza: • Je, ukifikiria watu au miundo ya kifamilia inayomzunguka mtoto ni kipi kati ya

hivyo vipo karibu na mtoto? (wazazi/walezi, kaka, dada, shangazi/wajomba, babu/bibi, binamu, marafiki)

• Je, unamfahamu yeyote kati yao? • Je, wanasaidia elimu ya mtoto wao? • Msaada wao ni sawa kwa wasichana na wavulana? • Wanasaia vipi? • Wanakutembelea kujua maendeleo ya mtoto wao? • Je, unaungana nao katika maendeleo ya mtoto wao? • Je, wanasaidia kazi za nyumbani za mtoto wao? • Je, wanajihusisha na juhudi za jamii kuboresha shule? • Je, wanaweza kuchua hatua kama mtoto wao akiwa na matatizo au kutokua na

nidhamu? 3. Mbali na mtoto na familia, Tafakari juu ya jamii anayoishi mtoto

Uliza: • Unaifahamu jamii hiyo? • Unajua chochote kuhusu utamaduni na jadi? • Unajua imani ya kidini ya watu? • Unajua kama ni jamii maskini sana au yenye unafuu? • Unajua kama ni jamii yenye amani au kama kuna migogoro kati yao au katika

jamii hiyo ni tatizo? • Unawajua viongozi wa kijadi au kidini? • Kama wakikuongelesha lugha tofauti, unamjua mtu anaeweza kukutafsiria

ukikutana nao? • Wanaunga mkono shule na elimu kwa wavulana? Na kwa? • Je, ni kawaida kuwa na ndoa za mapema? • Je, shule inashirikiana na jamii kuboresha kujifunza?

Page 38: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Elewa familia za wanafunzi wako na jamii zao

34

• Je, kuna kamati hai ya menejimenti ya shule inayofanya kazi vizuri? Kitini cha 2

MashirikayaKitaifanaKimataifa

Jamii

Shule

FamilianaMarafiki

Page 39: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 4

35

Kitini cha 3: Orodha hakiki. Fahamuwanafunzi wako, wazazi, na jamii

Walimu Wanaweza

Walimu wanaweza kushirikiana na wazazi

Kupanga mikutano ya waalimu na wazazi katika muda ambao wazazi wanaweza kuhudhuria Kuhamasisha wazazi kuhusu majukumu yao katika kusaidia maendeleo ya kujifunza kwa wavulana na wasichana Kujenga mazingira ya kukaribisha uwazi ili kuhamasisha wazazi kama wabia Kuwakaribisha wazazi kusaidia ujifunzaji shuleni Kushirikisha wazazi kwenye ratiba za kazi za nyumbani na kuwahimiza wawasaidie watoto wao Kupanga ‘siku za wazazi’ ambazo wazazi wanaweza wakatembelea shule na kutazama watoto wao darasani Kutumia barua au simu kuwasiliana na wazazi kwa ajili ya taarifa au kama kuna wasiwasi wowote Kukaribisha wazazi shuleni kwa ajili ya mikutano ya maendeleo ya mmoja kwa mmoja, au kama kuna wasiwasi juu ya ustawi wa ulinzi wa mtoto Kushirikisha taarifa na mafanikio kwenye mbao za matangazo Kuweka viwango vya ujifunzaji, na kuwataarifu wazazi ili washiriki kusaidia kufikiwa kwa viwango hivyo Kupanga ‘sherehe za tuzo’ kwa ajili ya watoto na wazazi wao Kupatikana mwisho wa kazi za siku za shule wakati wazazi wanachukua watoto wao shuleni Kukaribisha wazazi ili kusaidia klabu za baada ya shule, ikiwemo klabu za michezo Kuungana na wazazi kupitia Kamati ya Bodi ya Menejimenti ya Shule (BMS) Kukaribisha wazazi waliobobea katika mambo maalumu ili kuendesha mafunzo au kuzungumza kweye mikutano Kuwa mbunifu: panga ‘siku ya Leta mzazi wako shuleni’

Walimu wanaweza kushirikiana na jamii

Kuhudhuria mikutano ya Kamati za Shule – Jielekeze katika ujifunzaji wa watoto Kukaribisha viongozi wa kijadi na kidini na viongozi wa kijiji kweye mafunzo/mikutano Kutoa taarifa juu ya mafanikioya mwananfunzi kwa jamii kupitia kamati za shuleBMS au UWW Kutoa taarifa juu ya changamoto ya mahudhurio, ujifunzaji na mahitaji ya mwanafunzi kupitia Kamati za shule na BMS Kuhakikisha Kamati za shule BMS na wanajua, wanashiriki na kufuatilia viwango vya ujifunzaji Kukaribisha na kushirikisha jamii na mashirika yanayoweza kusaidia watoto au shule m.f. Vyama vya wanawake, mitandao ya wanafunzi wa zamani

Page 40: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Udhibiti wa kuzuia wa darasa

36

Kukaribisha wanajamii kwenye sherehe za tuzo au kwenye michezo ya shule/ufanisi Kupanga ‘siku za jamii-shule’ na ipe jamii changamoto ili kusaidia shule/ujifunzaji

4. Mikakati ya Awali ya Udhibiti wa Darasa

Page 41: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 4

37

¹ 1 hour 45 in total

Malengo ya moduli Kufikia mwisho wa moduli hii, washiriki wataweza:

• Kuunda jamii ya darasa kwa kutumia mbinu madhubuti za udhibiti wa darasa (NTCF 2.5)

• Kutumia mbinu na shughuli za kila siku za uratibu zinazochochea ujifunzaji wa wanafunzi (NTCF 2.5)

Vifaa vinavyohitajika • Chati

Kalamu/peni • Chati zilizoanaliwa • Vitini

Page 42: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Udhibiti wa kuzuia wa darasa

38

Taarifa muhimu za kuwashirikisha washiriki kwenye moduli hii Siku hizi udhibiti wa darasa umekuwa sio tu kusimamia na kuangalia nidhamu, bali humaanisha stadi na mbinu mbalimbali ambazo walimu huzitumia kuweka mazingira mazuri ya kujifunzia. Udhibiti wa darasa huwafanya wanafunzi wawe wanaofuata taratibu, huwa wasikivu, makini (wanaweka umakini katika kujifunza), na wenye tija. Udhibiti wa darasa hujumuisha kila kitu ambacho walimu hufanya ili kusaidia na kuboresha ujifunzaji wa wanafunzi. Kuna pande mbili za udhibiti wa darasa:

• Mikakati ya awali ya udhibiti wa wa darasa;

• Mbinu za kiufumbuzi za udhibiti wa darasa.

Katika moduli ya 4 , tutaweka umakini katika kuangalia mikakati ya awali ya udhibiti wa darasa na umuhimu wa mtazamo chanya kwa ufundishaji, kuweka matarajio, na kuanzisha shughuli za kila siku. Katika moduli ya 5 , tutaangalia kwa kina mbinu za kiufumbuzi za udhibiti wa darasa: kwa kutumia njia za usimamizi chanya wa nidhamu kama vile ubadilishaji wa tabia mbaya. Moduli hizi zitazingatia maarifa na stadi zilizopatikana katika moduli zingine za: ‘Andaa darasa lako kwa ajili ya ujifunzaji na ‘Wafahamu na wajumuishe wanafunzi wako wote’.

Mikakati ya awali ya Udhibiti wa darasa Ni muhimu kuanzisha uhusiano chanya na kujenga uelewa juu ya jamii ya wanafunzi katika darasa. Kujua wanafunzi kwa majina, chimbuko lao na vikwazo vyovyote wanavyoweza kukutana navyo katika kujifunza husaidia kuimarisha udhibiti wa darasa (Kama ilivyojadiliwa katika moduli ya 1, 2 na 3). Walimu wanapaswa watafute njia za kuwahamasisha wanafunzi ili wawe makini na wenye hamasa ya kujifunza au kufanya kazi wanazopewa. Kuanzisha utaratibu wa kila siku ili wanafunzi wajue cha kufanya na matarajio, na lini humsaidia pia mwalimu kudhibiti darasa. Ni muhimu kuhimiza na kudumisha tabia njema. Kuna njia mbalimbali za kufikia hili, kama vile kusifia kwa mdomo, chati za zawadi, au kutoa vyeti vya kila juma/mwezi vinavyotambua tabia njema. Washiriki wajaribu kufikiria njia zingine za kubainisha tabia njema. Kanuni ‘kuu 5’ za udhibiti wa darasa ni:

1. Kuweka matarajio bayana kuhusu tabia darasani; 2. Kuanzisha utaratibu wa kila siku unaochochea ujifunzanji. Utaratibu wa kila siku

hutupatia muundo wa siku na hisia za umadhubuti (kama vile kuanza/kumaliza darasa, kuita majina kwa ajili ya mahudhurio, kutumia muda wa mzunguko,

Page 43: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 4

39

kuandaa kazi za jozi/vikundi, pamoja na mrejesho, kugawana na kurejesha karatasi na vifaa);

3. Kuwashirikisha wanafunzi kwa kujua majina yao, kuufanya mtaala uhusiane na maisha yao ya kila siku, kuandaa maandalio ya somo yanayohimiza kufanya kazi pamoja, kutambua historia za wanafunzi;

4. Kutambua na kusifia tabia njema, kuwahimiza wanafunzi kujenga tabia ya kufanya kazi pamoja, na kuonesha kazi darasani. Haya yote hujulikana kama uhamasishaji chanya;

5. Usimamizi chanya wa nidhamu kwa kuanzisha na kukubaliana kuhusu matarajio na kurekebisha tabia mbaya, kuwatendea wanafunzi wote kwa haki.

Kanuni hizi zinaweka msingi imara wa udhibiti wa darasa, huwasaidia walimu kuzuia utovu wa nidhamu, na kuweka mazingira mazuri ya kujifunza. Angalia Kitini cha 1 na cha 4 kwa maelezo na mawazo zaidi. Udhibiti wa darasa unaozingatia usawa wa kijinsia Wakati wote hakikisha wasichana na wavulana wanapewa nafasi sawa ya kushiriki katika kazi na shughuli za kila siku. Jaribu kuepuka kuendeleza mitazamo hasi ya kijinsia (kama vile wasichana kufanya usafi, wavulana kunyanyua vitu vizito). Fikiria mambo yanayoweza kuwafanya wasishirikiane na ondoa vikwazo vyote. ‘Kikwazo’ kinaweza kuwa mtazamo wa kijamii unaozuia wavulana na wasichana kufanya kazi pamoja. Jaribu kuweka mazingira ambayo kazi za pamoja kati ya wavulana na wasichana (au watoto wenye historia tofauti) zinaweza kufanyika kikamilifu.

Kazi za kufanya

1. Mwalimu ninayempenda zaidi ¹ Dakika 30 Lengo la kazi hii ni kutafakari kuhusu walimu ambao wamekuwa na mchango mkubwa kwa elimu yako. Itakusaidia pia kutafakari aina ya mwalimu unayetaka uwe. Walimu wenye mtazamo chanya mara nyingi hudhibiti madarasa yao vizuri. Gawa Kitini cha 2.

“Ninataka utafakari kuhusu mwalimu wako wa zamani. Chati kuhusu Kitini cha 2 kina safu-wima 4: vitendo vya mwalimu, vitendo vya mwanafunzi, mazingira ya darasa, na hisia. Mazingira ya darasa ni miundombinu halisi na mpangilio wa darasa na matumizi ya zana za kufundishia zinazoonekana. Hisia ni jinsi unavyoweza kujisikia katika mazingira husika. Sasa nitakuuliza maswali kadhaa, na kisha tutajadili majibu yetu katika kikundi. Kwanza, ninataka umfikirie mwalimu anayempenda zaidi. Ulikuwa unajisikiaje kuwa darasani mwake? Jaza katika chati – chini ya vitendo vya mwalimu, unaweza kuandika vitu alivyovifanya mwalimu wako ambavyo ulivipenda au vilivyofanya darasa lake liwe nzuri. Zingatia aina ya hisia ambazo mwalimu unayempenda zaidi aliziweka darasani”.

Sema

Page 44: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Udhibiti wa kuzuia wa darasa

40

Baada ya dakika 5, jadili majibu katika majopo. Mwite mmoja wa washiriki aje aandike majibu katika chati.

“Sasa ninataka ufikiri kuhusu walimu wako ambao huwapendi kabisa. Walikuwaje? Walikufundishaje? Madarasa yao yalikuwa na mazingira gani na ulijisikiaje kuhusu mazingira hayo? Jaza mstari wa pili katika chati katika kitini na tutajadili tena kama kikundi”.

Baada ya dakika 5, jadili majibu katika majopo. Mwite mshiriki mwingine aje aandike majibu katika chati (hakikisha kuna usawa wa kijinsia hapa). Tafakari kuhusu tofauti miongoni mwa majibu yaliyotolewa. Waulize washiriki nini wangependa wabadili.

“Mwisho, ninataka utafakari kuhusu darasa zuri kwako wewe kama mwalimu. Darasa hilo litakuwaje? Ni maneno gani utatumia kulielezea?”

Waagize washiriki wajaze safu-mlalo ya tatu katika Kitini cha 2. Baada ya dakika 5, jadili majibu katika majopo. Uliza: • Je, mambo haya yanatueleza nini kuhusu walimu wazuri na mitazamo yao? • Je, haya yanahusianaje na udhibiti wa darasa? Kwa njia zipi? Majibu yanaweza kuhusu: jinsi shughuli na mbinu zinavyoweza kuwahamasisha wanafunzi kujifunza na kuwashughulisha darasani; na jinsi vitendo vya walimu vinavyoweza kutengeneza mitazamo chanya. Zingatia: Kama heshima inajitokeza kama changamoto, jadili maana yake. Sisitiza umuhimu wa ulinzi wa mtoto na uwekaji wa mazingira salama ya shule. Eleza kuwa tutaangalia suala hili kwa kina katika moduli inayoitwa ‘Hakikisha wanafunzi wako wanalindwa’, sehemu ya 1 na 2.

Kwa maelezo zaidi, rejea moduli ya ‘Hakikisha wanafunzi wako wanalindwa’.

“Katika moduli hii, tutajifunza mbinu za kutusaidia kuwa walimu tunaotaka kuwa”.

Sema

Sema

Sema

Page 45: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 4

41

2. Kuweka bayana matarajio na kanuni ¹ Dakika 20

Lengo la kazi hii ni kuelewa jinsi matarajio na kanuni bayana za darasa zilivyo sehemu muhimu ya udhibiti wa darasa. Matarajio

“Kama tulivyoona katika kazi iliyopita, mara nyingi huwa tuna matarajio ya walimu ‘wazuri’. Ni muhimu pia kwamba tuna matarajio kwa wanafunzi na tunayabainisha waziwazi. Hii ni kanuni muhimu ya udhibiti wa darasa. Husaidia kuweka mazingira mazuri ya kujifunzia”.

Rejea Kitini cha 1, ‘Kanuni kuu 5 za udhibiti wa darasa’. Hebu tuangalie matarajio hayo ni yapi. Fikiri - Kaa katika Jozi - Elezana Waagize washiriki watafakari kuhusu (kwa sekunde 30):

1. Wanafunzi wanatarajia nini kutoka kwako? 2. Unatarajia nini kutoka kwa wanafunzi wako?

Waagize washiriki wakiwa na wenza wao wajadili mawazo yao (kwa dakika 1). Kisha, waagize washiriki kadhaa wawasilishe mrejesho kuhusu mawazo yao kwa darasa zima (dakika chache). Andika katika chati matarajio yetu kuhusu wanafunzi. Sampuli ya majibu ni kama: mwalimu anaandaa kazi za kufurahisha, mwalimu anapima uelewa, mwalimu anatoa maelekezo/maagizo yanayoeleweka, mwalimu anawagawa wanafunzi katika vikundi/jozi, wanafunzi wanaweka umakini katika kazi, wanafunzi wanaonesha mikono juu wanapotaka kuzungumza, wanafunzi wanaheshimu mazingira yao, wanafunzi wanashiriki kazi kikamilifu, wanafunzi wanatii maelekezo/maagizo. Uliza: Ni kwa jinsi gani matarajio haya husaidia kuweka mazingira mazuri ya kujifunzia? Sisitiza wazo kwamba kuweka matarajio ni muhimu kwa udhibiti wa darasa.

“Ndiyo kwanza tumetoka kutumia mbinu ya Fikiri-Weka katika Jozi-Elezana – hapa ndipo mwalimu humpa mwanafunzi muda wa kutafakari peke yake, kisha waagize wakae kwenye jozi ili wajadili, na kisha walieleze darasa zima. Hii ni mbinu inayofaa kwa madarasa yako. Huhakikisha kuwa wanafunzi wote wanashirikishwa, na wanapewa muda wa kutafakari kuhusu majibu na kuchambua mawazo”.

Sema

Sema

Page 46: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Udhibiti wa kuzuia wa darasa

42

Kanuni

“Kuwa bayana kuhusu aina ya tabia tunazozitaka madarasani mwetu huhusu uwekaji wa mazingira ya ushirikiano ambapo walimu na wanafunzi wanajua na kuelewa kinachotarajiwa kutoka kwa kila mmoja. Sehemu muhimu ya usimamizi chanya wa nidhamu ni kuwashirikisha wanafunzi katika udhibiti wa darasa. Njia mojawapo ya kufanikisha hili ni kuanzisha kanuni za pamoja za darasa kwa ajili ya wanafunzi wetu kujifunza. Kanuni huwasaidia wanafunzi kuelewa vizuri madhara na hivyo kuwa na ulazima mdogo wa kuchukua hatua za kinidhamu. Andika kanuni zako kwa lugha inayoeleweka kirahisi kwa wanafunzi na bandika kwenye ukuta wa darasa. Unaweza kuwa na kanuni 10-15 katika darasa lako, lakini hapa tutaweka umakini katika kutunga kanuni 3 ili kuokoa muda”.

Waagize washiriki waangalie katika chati mahali walipoandika matarajio yao kwa wanafunzi. Waagize washiriki wote waje kwenye chati na waweke alama ya vema matarajio matatu ambayo ni muhimu zaidi kwao. Chukua matarajio matatu yenye alama nyingi zaidi – hizi ndizo kanuni kuu tatu. Uliza: Kwanini kanuni hizi ni muhimu? Kwanini tunafuata kanuni? Kumbuka kwamba kunaweza kukawa na marudio kutoka sehemu iliyotangulia, hivyo, fupisha majadiliano haya. Andika kwenye chati mawazo ya washiriki.

“Hili ni zoezi zuri kulifanya pamoja na wanafunzi wako. Ni muhimu sana kwa wanafunzi ili waelewe kwa nini wanafuata kanuni. Ni muhimu kwa wanafunzi kujua kwamba kanuni zipo kwa manufaa yao, si kwa kwa manufaa ya walimu. Hivyo, wewe na wanafunzi wako mnapotunga kanuni za darasa, hakikisha kila mmoja anaelewa jambo hili.”

3. Shughuli za kila siku ¹ Dakika 30

Lengo la kazi hii ni kuelewa jinsi shughuli za kila siku zinavyotumika kama mbinu ya udhibiti wa darasa. Gawa darasa katika makundi mawili yenye ukubwa sawa na wape Kitini cha 3. Kipe kila kikundi kisa kimoja. Baada ya dakika chache, viagize vikundi kupendekeza mshiriki mmoja atakayewasilisha majibu yao na kuyajadili (Zingatia: majibu ya Kisa cha 1 yanaweza kuwa yote isipokuwa A (epuka kazi za vikundi), majibu ya Kisa cha 2 yanaweza kuwa yote isipokuwa A).

“Shughuli za kila siku za darasa ni mambo yanayojirudia mara kwa mara. Ni sehemu ya shughuli za shule za siku na husaidia mambo kwenda kama yalivyopangwa. Shughuli za kila siku husaidia kuunda jamii ya darasa na huweza kuweka muundo, kuwa sehemu ya darasa, na umadhubuti kwa wanafunzi”.

Waulize washiriki aina ya shughuli za kila siku zilizopo katika madarasa yao. Majibu yanaweza kuwa ni pamoja na: kunyoosha mkono unapotaka kuzungumza; kufanya

Sema

Sema

Sema

Page 47: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 4

43

usafi kwa kutumia nyimbo; wanafunzi walioteuliwa kugawa na kurudisha karatasi na vifaa kwa kutumia; kupata usikivu wa wanafunzi kwa kutumia ishara za mwili au alama; kuwagawa wanafunzi kwenye vikundi kwa kuhesabu namba au kutumia rangi/maumbo; kuwapa wanafunzi kazi za darasani ili kuweka mazingira ya umiliki (kama vile kazi za nyumbani au kukusanya daftari la mahudhurio); kukaa pamoja; kusikiliza na kuzungumza kwa zamu. Zingatia kwamba baada ya shughuli za kila siku kuwa zimeanzishwa, ni muhimu zifahamike na zidumishwe. Gawa Kitini cha 4. Waagize washiriki wafanye kazi kwa kujitegemea na waangalie sehemu ya ‘Shughuli za kila siku’ katika jedwali. Wanapaswa kuweka alama ya vema katika safu-wima ili kuonesha mambo ambayo tayari wanayajua, mambo wanayopenda kuyafanya, na mambo ambayo wasingependa kuyafanya. 4. Uwezo na Changamoto zangu ¹ Dakika 25

Lengo la kazi hii ni kubainisha umadhubuti na udhaibu wako kuhusu udhibiti wa darasa.

“Tumeshaona jinsi ambavyo udhibiti wa darasa si usimamiz wa nidhamu pekee. Unahusu stadi na uwezo mbalimbali (matendo, mitazamo, maarifa) ambao walimu hutumia kusaidia na kuimarisha ujifunzaji wa mwanafunzi”.

Waagize washiriki watafakari kuhusu uzoefu wao binafsi kuhusu ufundishaji – upi ni umadhubuti wako katika kudhibiti darasa? Nini unaona ni changamoto na kwa nini? Waagize washiriki waandike haya kwenye chati katika madaftari yao. Baada ya dakika 10, mwagize kila mshiriki aeleze moja ya uwezoi wake. Kisha, muagize kila mshiriki abainishe changamoto 3.

“Tutarejea kwenye changamoto hizi na kuunda mbinu za kukabiliana nazo katika moduli inayofuata, ‘Dhibiti darasa lako, sehemu ya 2’.”

Huu ni mwisho wa moduli hii. Mwezeshaji apime iwapo malengo ya moduli hii yamefikiwa.

Viashiria vya mafanikio o Mwalimu anaweza kueleza kwa kifupi mbinu za udhibiti wa darasa ili

kutengeneza mazingira mazuri ya kujifunzia. o Mwalimu anaweza kueleza waziwazi matarajio yake ya kitabia kutoka kwa

wanafunzi. o Mwalimu ameanzisha shughuli za kila siku zinazochochea ujifunzaji na tabia

njema.

Sema

Sema

Page 48: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Udhibiti wa kuzuia wa darasa

44

Mawazo kwa ajili ya usimamizi Mwelekezaji au mwalimu mkuu:

• Amfuatilie mwalimu akiwa darasani ili kubainisha matarajio na kanuni alizoziweka.

• Achunguze masuala yanayofanyika vizuri na yasiyofanyika vizuri

• Achunguze matumizi ndani ya darasa ya shughuli za kila siku zilizoanzishwa ndani ya darasa

• Atoe mrejesho wa jinsi masuala haya yanavyoweza kurekebishwa na kuboreshwa.

Mawazo kwa ajili ya ujifunzaji wa pamoja/binafsi • Walimu wanaweza kurudia kusoma ‘Kanuni kuu 5 za udhibiti wa darasa’ (Kitini

cha 1). • Wanaweza kuhifadhi kumbukumbu za kanuni na shughuli za kila siku za darasa

ambazo wamezijaribu. Ni mbinu zipi zilifanikiwa zaidi na kwa nini. Walimu wanaweza kutumia Kitini cha 4 ili kupata mawazo ya jinsi ya kuanza.

• Walimu wanaweza kuhimizwa kuchunguza maelezo yao katika Kitini cha 2: Je, kuna lolote wanaloweza kufanya kuendeleza utendaji wao ili kuwa mwalimu/darasa ‘bora’ walilolibainisha?

• Kitini cha 4 kinaonesha njia kadhaa za kufanikisha Kanuni kuu 5 za udhibiti wa darasa. Walimu wanaweza mara kwa mara kujikumbusha kuhusu njia hizi.

• Weka malengo: Walimu wanaweza kuchagua mbinu moja kila baada ya majuma mawili au mwezi mmoja ambao wangependa kujiimarisha. Wanaweza kutunza shajara ya jinsi na lini walitumia mbinu husika, jinsi ilivyofanya shughuli, na jinsi ambavyo wangeweza kuboresha zaidi.

Marejeleo Vyanzo vifuatavyo vimetumika kuandaa moduli hii:

• TiCCWG (2016) “Training Pack for Primary School Teachers in Crisis Contexts” Module 3 - Pedagogy. Teachers in Crisis Contexts Working Group. Linapatikana: www.ineesite.org/en/training-pack-for-primary-school-teachers-in-crisis-contexts

Page 49: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 4

45

Kitini cha 1: Kanuni 5 za udhibiti wa darasa

Kanunizakulimududarasa

NidhamuNjema:Kurekebisatabiambayanakuweka

utaratibuwaadhabu

KuanziashaUtaratibuwakilasikuunaoeleweka

Kuwekabayanamatarajio yatabia

zilizonjema

Ushirikishwaji haiwawanafunziiliwahamasikekujifunza

Motishachanyahuwafanya

wajisikiewaposalamana

wanasaidiwa

Page 50: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Udhibiti wa kuzuia wa darasa

46

Kitini cha 2: Mitazamo kuhusu ufundishaji

Swali Vitendo vya mwalimu

Vitendo vya wanafunzi

Mazingira ya darasa Hisia

1.

2.

3.

Page 51: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 4

47

Kitini cha 3: Shughuli za kila siku Kisa cha 1: Ndiyo kwanza wanafunzi wameagizwa wafanye kazi za vikundi. Wanafunzi wanachukua muda mrefu kujikusanya kwenye vikundi vyao kwa sababu wanazungumza miongoni mwao. Baadhi ya wanafunzi wanaonekana hawajui cha kufanya na wanaonekana kuchanganyikiwa. Je, mwalimu angeweza kufanya nini kuzuia utovu wa nidhamu?

A. Kuepuka kazi za vikundi B. Kuweka matarajio bayana kuhusu tabia njema za kazi za vikundi C. Kuweka kanuni za darasa kuhusu kazi za vikundi D. Kuwarejesha vikundini wanafunzi wenye utovu wa nidhamu na kisha kuwafuatilia

kwa karibu. Toa sababu zako kwa majibu uliyochagua. Kisa cha 2: Umempa vitini mwanafunzi mmoja aliyeketi mbele ya darasa achukue kimoja kisha asogeze vingine kwenye meza inayofuata. Wanafunzi wanaongea miongoni mwao na wanaanzisha fujo. Unagundua kuwa vitini havijasambaa zaidi ya meza mbili za mwanzo. Je, mwalimu angeweza kufanya nini kuzuia hali hii kutokea?

A. Kuepuka kugawa vitini. B. Kuanzisha shughuli za kila siku kuhusu ugawaji wa vitini kwa utaratibu. C. Kumkumbusha mwanafunzi aliyeacha kusogeza vitini avisambaze. D. Kuweka matarajio bayana kuhusu ushirikiano wa wanafunzi wakati wa kugawana

vitini. Toa sababu zako kwa majibu uliyochagua.

Page 52: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Udhibiti wa kuzuia wa darasa

48

Kitini cha 4: Shughuli za kila siku ili kufanikisha kanuni kuu 5 za udhibiti wa darasa

Kanuni Kuu 5 Njia za kuhimiza tabia njema

Tayari ninafanya

Ningependa kufanya

Nisingependa kufanya

Matarajio bayana

• Shirikiana na wanafunzi kuandaa orodha ya kanuni za darasa

• Toa maelekezo yanayoeleweka kabla ya kila kazi inayojumuisha maelekezo rahisi ya shughuli husika, lengo lake, muda wa kufanya kazi, na vifaa vinavyohitajika

• Eleza lengo la sababu ya kuwa na matarajio husika

• Kabla ya kuanza kazi husika, chunguza kiwango cha uelewa wa wanafunzi kuhusu maelekezo

Shughuli ya kila siku

Anzisha shughuli ya kila siku ili kuwasaidia wanafunzi kuzoea kufanya mambo kwa mpangilio na mazingira yanayoeleweka. Usibadilishebadilishe na yafanye yanayotabirika. Mifano ya shughuli za kila siku: • Kufanya usafi • Paredi • Kuanza darasa • Mapumziko • Kurudi darasani • Pumziko fupi

Page 53: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 4

49

• Kurudi darasani • Michezo na

burudani • Mkusanyiko wa

jioni • Kumaliza darasa

Ushirikishaji • Wataje wanafunzi wako kwa majina unapozungumza nao

• Andaa andalio la somo linalohusisha mtaala na uwezo na mambo ambayo wanafunzi wanayapenda.

• Zingatia: - Historia za

wanafunzi (hususani iwapo kama wamewahi kupata maumivu ya nafsi) na jinsi hali hiyo inavyoweza kuathiri tabia zao darasani.

- Ulemavu wa viungo wa wanafunzi na mahitaji maalumu ya kujifunzia.

- Elewa tofauti za kitamaduni na kilugha za wanafunzi.

• Andaa andalio la somo linalowapa wanafunzi fursa ya kufanya kazi pamoja.

• Lenga kutumia burudani, shughuli na kazi za ujifunzaji hai.

Kichocheo chanya

• Weka mazingira ya wanafunzi kujisikia

Page 54: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Udhibiti wa kuzuia wa darasa

50

salama kuelezana fikra na mawazo yao.

• Wasaidie wanafunzi kujenga uhusiano mwema miongoni mwao.

• Wape wanafunzi mrejesho endelevu na chanya kuhusu shughuli na ushiriki wao darasani.

• Kaa na wanafunzi ili kuzungumzia masuala mbalimbali.

• Hakikisha kuwa wanafunzi wanajisikia vizuri na wanafanya kazi vizuri wanapokaa karibu na wenzao.

• Wahimize wanafunzi kubandika kazi zao nzuri, kutengeneza mbao za kuoneshea shughuli zao, na kuondoa darasani vifaa/zana za kufundishia mwishoni mwa kila somo.

Uadabishaji chanya

• Kuwa na utaratibu unaoeleweka wa kusimamia matarajio yako: pongeza tabia njema, badilisha tabia mbaya, na watendee wanafunzi wote kwa usawa.

• Zunguka darasani kila mara wakati wa somo ili kufuatilia tabia za wanafunzi.

Ungependa kufanya nini zaidi?

Page 55: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 5

51

5. Udhibiti wa Kiufumbuzi wa Darasa

¹ Jumla ya saa 2

Malengo ya moduli Kufikia mwisho wa moduli, washiriki wataweza: 1. Kutengeneza jamii bora ya

darasa kwa kutumia mbinu bora za udhibiti wa darasa (NTCF 3.5)

2. Kutumia usimamizi bora wa nidhamu kushughulikia tabia mbaya (NTCF 3.5)

Vifaa vinavyohitajika • Karatasi za chati

Peni • Chati iliyokwishaandaliwa • Vitini

Page 56: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Ulinzi wa Watoto: Sehemu ya 1

52

Taarifa za kuwapa washiriki wakati wa moduli Katika moduli hii, tutaendelea kujifunza kuhusu udhibiti sababishi wa darasa wakati huohuo tukiangalia udhibiti wa kiufumbuzi wa darasa. Hatua hii itatumia maarifa na stadi tulizojifunza katika moduli iliyotangulia ya ‘Dhibiti darasa lako’ sehemu ya 1. Tafadhali zingatia kuwa ‘Dhibiti darasa lako’ sehemu ya 1 na 2 zimebuniwa zitumike pamoja. Angalia ‘Taarifa za kuwapa washiriki katika moduli hii’ kutoka katika moduli ya ‘Dhibiti darasa lako’, sehemu ya 1 na rejea Kitini cha 1 na 4 kutoka katika moduli ya ‘Kanuni kuu 5’ za udhibiti wa darasa. Kanuni hizi zinatoa msingi madhubuti wa udhibiti wa darasa, kwa kuwasaidia walimu kuzuia utovu wa nidhamu na kutengeneza mazingira mazuri ya kujifunzia. Udhibiti wa kiufumbuzi wa darasa

Udhibiti wa kiufumbuzi wa darasa ni jinsi unavyoshughulikia tabia mbaya za wanafunzi. Mara nyingi hujulikana kama usimamizi wa nidhamu. Utovu wa nidhamu unapotokea, ni muhimu kutafakari kwa makini jinsi ya kushughulikia. Kwanza, tulia kisha tafakari kuhusu kitendo anachofanya mwanafunzi. Unadhani kwanini mwanafunzi anafanya afanyavyo? Kubadilisha tabia kunasaidia kushughulikia tabia mbaya kabla hali haijawa mbaya. Inampa mwalimu fursa ya kumwongoza mwanafunzi ili awe mtiifu. Hii inaweza kufanyika kwa kutumia mbinu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na: kueleza bayana kuhusu tabia njema inayotarajiwa (mfano, unaweza kuomba kuzungumza kwa kunyoosha mkono wako juu /au kuuliza vizuri); kunyamaza ghafla ili kurejesha usikivu wa wanafunzi na kunyamazisha kelele; kutumia ‘masimulizi chanya’ yanayosifia wanafunzi wenye tabia njema na kuwasifia wanafunzi pale wanapobadili tabia mbaya na kuwa watiifu zaidi. Kama mwanafunzi ataendelea kuwa mtovu wa nidhamu, utapaswa kumweleza madhara ya tabia yake mbaya. Ikiwezekana, mweleze hili sehemu ya falagha na ana kwa ana badala ya mbele ya wanafunzi wengine (mfano, koridoni nje ya darasa). Ni muhimu kumpa mwanafunzi fursa ya kutafakari na kueleza kwanini tabia zao ni mbaya. Hali hii inawasaidia kuelewa kwanini wanakaripiwa. Karipio linapaswa kuendana na tabia mbaya husika. Karipio halipaswi kuwa la mabavu au la kudhalilisha. Kama mwanafunzi hawezi kueleza kwanini tabia yake ni mbaya, mwalimu amweleze kwa upole na kwa dhati. Udhibiti wa darasa unaozingatia usawa wa kijinsia na ambao ni jumuishi

Tumia njia chanya kuhimiza ushirikiano miongoni mwa wanafunzi, lakini hakikisha kuwa adhabu/karipio lolote dhidi ya tabia mbaya halikiuki misingi ya kitamduni na kijamii. Usiwaadhibu wanafunzi wa jinsi moja tu na kuwaacha wa jinsi nyingine.

Page 57: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 5

53

Kazi za Kufanya 1. Mikakati ya awali ya udhibiti wa darasa ¹ Dakika 45

Lengo la kazi hii ni kubainisha kanuni tano za udhibiti bora wa darasa na jinsi kanuni hizi zinazvyoweza kutumika kivitendo.

“Mikakati ya awali ya udhibiti wa darasa unatumia mbinu nyingi muhimu kutengeneza mazingira madhubuti ya kujifunzia. Tumejifunza baadhi ya mbinu hizi katika Moduli ya 4. Je, unakumbuka baadhi ya mawazo makuu tuliyojifunza kuhusu mbinu husika?”

Rejea Kanuni Kuu 5 kwenye chati na mjadiliane. Kwa kifupi, andaa muhtasari wa mawazo mliyoyajadili (matarajio, shughuli za kila siku). Wagawe washiriki katika vikundi. Waagize wazingatie kisa cha kwanza katika Kitini cha 1 na waibue njia za kushughulikia changamoto husika. Kama ni muhimu, wakumbushe Kanuni Kuu 5. Baada ya dakika 10, waagize kila kikundi kitoe mrejesho wa majadiliano yao. Taja mbinu zozote ambazo hawakuzieleza, kama vile kuwasikiliza kwa makini wanafunzi watiifu, kutumia ukimya wa ghafla ili kurejesha usikivu wakati wa somo (Kitini cha 2 kina baadhi ya mapendekezo ya jinsi ya kurekebisha tabia). Waagize washiriki kufanyia kazi visa vilivyosalia. Tenga dakika 5 kwa kila kisa. Wakati wa kutoa mrejesho, hakikisha kuna usawa wa kijinsia kwa waliojitolea kuzungumza kwa niaba ya vikundi. 2. Udhibiti wa kiufumbuzi wa darasa ¹ Dakika 45

Lengo la shughuli hii ni kujifunza jinsi ya kubadili tabia mbaya kwa namna bora na zisizo za mabavu.

“Wakati unaweza kutengeneza mazingira mazuri, si wakati wote watoto watakuwa watiifu kama unavyotaka wawe. Unahitaji mbinu za kushughulikia tabia hasi kwa namna bora”.

Waagize washiriki waibue njia ambazo wanafunzi “huonesha utovu wa nidhamu” madarasani mwao. Kabla hawajajigawa katika vikundi, uliza iwapo washiriki wanaweza kubainisha kwanini tabia hii huweza kutokea. Fikiri– Kaa katika Jozi – Elezana Waagize washiriki wakae kwenye jozi na wajadili uzoefu wao. Kwa pamoja, wanahitaji kufanya kazi kwa kutumia mti wa maamuzi uliomo kwenye Kitini cha 2, ili kuwasaidia kuamua namna bora ya kushughulikia tabia hii. Iagize jozi isome sehemu ya ‘kurekebisha tabia mbaya’.

“Sasa tutafakari kuhusu madhara ya tabia mbaya, na ambayo ni sugu”.

Sema

Sema

Sema

Page 58: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Ulinzi wa Watoto: Sehemu ya 1

54

Waagize washiriki wajadili na majirani zao kwa dakila 2 jinsi walimu walivyoshughulikia utovu wa nidhamu alipokuwa shuleni. Je, kuna mwalimu aliyewaadhibu kwa mabavu au kwa kuwaonea? Je, walijisikiaje kuhusu shule na kuhusu mwalimu husika? Pokea maelezo kadhaa kutoka kwa kikundi. Kama mshiriki atasema alipigwa shuleni na waliona ni sawa tu, sisitiza kuwa adhabu za mabavu au zinazodhalilisha zinaweza kusitisha tabia mbaya kwa muda tu, lakini mara nyingi zina madhara ya muda mrefu. Uliza kikundi mifano ya madhara ya tabia mbaya. Kwa mfano, mtoto anaweza kuwa na hofu au hasira, jambo linaloweza kusababisha matatizo ya ukosefu wa umakini au utoro. Uliza jinsi ya kuepuka kuwadhalilisha au kuwaumiza kimwili watoto. Wakumbushe washiriki kuwa kumtoa mtoto nje ya darasa na kuzungumza naye kwa upole, kwa dhati, na kumweleza madhara ya tabia mbaya ni adhabu isiyodhalilisha kuliko kumwadhibu mbele ya wanafunzi wenzake. Uliza: Tumejadili mbinu gani leo ambazo ni mbadala mzuri wa adhabu za kudhalilisha/viboko? Andika majibu ya washiriki katika chati na omba mapendekezo ya ziada. Wachochee kwa kuwauliza jinsi walimu wanavyoweza kuwafanya walimu wakuu wachukue hatua za ziada za usimamizi wa nidhamu (pia zisizo za mabavu/isiyo ya udhalilishaji). Andika mapendekezo haya katika chati. Zingatia pia kwamba tutajadili kwa kina suala hili katika ‘Hakikisha wanafunzi wako wanalindwa’, sehemu ya 1 na 2. Waombe kikundi pendekezo moja au mawili kuhusu jinsi ya kuwa mfano bora kwa walimu wengine katika kuhamaisha mbinu/njia zisizo za mabavu na siziso za udhalilishaji.

Nenda: ‘Hakikisha wanafunzi wako wanalindwa’, sehemu ya 1 na 2 kwa maelezo na taarifa zaidi kuhusu ulinzi wa watoto.

3. Kurekebisha tabia na madhara ya tabia mbaya ¹ Dakika 20

Lengo la shughuli hii ni kufanya mazoezi ya kurekebisha tabia mbaya na kuelewa vizuri na kushughulikia changamoto mbalimbali. Waagize washiriki wafanye kazi katika vikundi vya watu 5 wakiigiza kisa fulani. Waagize washiriki wanne waoneshe utovu wa nidhamu. Mshiriki mmoja wa kujitolea aigize anaongea na wanafunzi wengine darasani; 2. Aigize anaweka miguu juu ya dawati na anachungulia nje ya dirisha; 3. Aigize anachezea mdoli au simu; 4. Aigize anasukuma kichwa cha mwanafunzi mwingine. Muagize mshiriki mwingine ajitolee kuigiza nafasi ya mwalimu. Mwalimu anajaribu kutumia mbinu za kiufumbuzi za udhibiti wa darasa (tumia mifano ya kwenye Kitini cha 2).

Page 59: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 5

55

Nafasi ya mwalimu itazunguka kwa zamu miongoni mwa washiriki waliosalia – kila mshiriki atapata fursa ya kuigiza nafasi ya mwalimu kwa dakika 3 kila mara. Mwalimu atapaswa kudhibiti muda na ataonesha ishara dakika 3 zitakapoisha. Baada ya dakika 15, omba mrejesho. Uliza:

• Ni jambo gani lilifanikiwa?

• Ni jambo gani lingeweza kufanywa tofauti?

• Je, kuna mbinu zozote ungependa kuzijaribu?

• Ni madhara gani ya tabia ungependa kupendekeza kwa ajili ya tabia hii mbaya? Hakikisha kuwa maoni ni chanya na yanayojenga. Gawa Kitini cha 3. Pendekeza kuwa kitini hiki kinatumika kwa ajili ya ujifunzaji wa kujitegemeana/au kufanya kazi na wenzake katika kuigiza visa vinavyowezekana. Hii itasaidia kuchochea ujifunzaji katika moduli hii. 4. Ibua ufumbuzi wa changamoto ¹ Dakika 10

Lengo la shughuli hii ni kutumia uliyojifunza katika moduli hii kushughulikia changamoto ulizozibainisha mwishoni mwa ‘Mikakati ya awali ya udhibiti darasa’, sehemu ya 1. Rejea changamoto ambazo walimu waliziorodhesha mwishoni mwa moduli iliyopita katika ‘Dhibiti darasa lako’, sehemu ya 1. Waombe washiriki wafikirie stadi na mbinu za kushughulikia changamoto hizi. Kwa mfano: kurekebisha tabia mbaya, kuanzisha shughuli za kila siku darasani, kuandaa kanuni pamoja na wanafunzi, kutumia kazi za vikundi au jozi. Kushughulikia masuala na maswali yoyote yaliyosalia. Uandaaji wa somo na udhibiti wa darasa

Wakati wa kuandaa somo, tenga muda kwa ajili ya shughuli za kila siku. Hakikisha unatumia mchanganyiko wa shughuli ili kuwashughulisha wanafunzi.

Huu ni mwisho wa moduli hii. Mwezeshaji apime iwapo malengo ya moduli hii yamefikiwa.

Page 60: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Ulinzi wa Watoto: Sehemu ya 1

56

Viashiria vya mafanikio o Walimu wanaweza kudhibiti kiutulivu shughuli za ujifunzaji. o Walimu wanaweza kuwafanya wanafunzi kuweka umakini kwenye kazi. o Walimu wanaweza kutumia mbinu mseto za udhibiti wa tabia wa kuzuia na wa

kurekebisha. o Walimu wanatumia masimulizi chanya ili kuchochea tabia njema. o Walimu wanashughulikia tabia korofi au tabia zisizofaa kwa kutumia mbinu za

kurekebisha tabia. o Walimu wanafanya ufuatiliaji wa tabia kwa kutumia madhara yasiyo ya mabavu, kama

ni muhimu, kwa tabia mbaya ambazo ni sugu.

Mawazo kwa ajili ya uelekezaji Mwelekezaji au mwalimu mkuu anaweza kumfuatilia mwalimu kuhusu mbinu mbalimbali za usimamizi wa darasa, ikiwa ni pamoja na mbinu zote zilizoorodheshwa katika ‘Mikakati ya Awali ya kudhibiti darasa lako’, sehemu ya 1, Kitini cha 4. Wanaweza:

• Kuangalia matumizi ya mbinu za kulimudu darasa

• Kuhimiza maendeleo endelevu na matumizi ya mbinu mpya ndani ya muda uliokubaliwa

• Kutoa mrejesho wa mara kwa mara na mapendekezo ya jinsi ya kuboresha

• Kuweka umakini mahususi katika taratibu za usimamizi wa nidhamu zinazozingatia masuala ya jinsia na zisizo za kiudhalilishaji.

Mawazo kwa ajili ya ujifunzaji wa pamoja/binafsi • Walimu wanaweza kusoma Kitini cha 1 kuhusu ujifunzaji wa kujitegemea (‘Kanuni tano

kuu za udhibiti wa darasa) kutoka ‘Mudu darasa lako’, sehemu ya 1. Kitini cha 4 kutoka katika moduli hiyohiyo kinaonesha njia kadhaa za kufanikisha ‘Kanuni kuu 5’.

• Walimu wanaweza kujikumbusha visa katika Kitini cha 1 cha moduli hii. Wanaweza kujiuliza: je, kuna visa unavyoweza kuongeza kutokana na uzoefu wako binafsi? Je, kuna kitu chochote ambacho ungefanya tofauti?

• Walimu wanaweza kujikumbusha kuhusu Kitini cha 2 kuhusu usimamizi chanya wa nidhamu.

• Wanaweza kutumia Kitini cha 3 kwa ajili ya ujifunzaji wa kujitegemea au ujifunzaji wa pamoja na wenzao. Wanaweza kuigiza visa husika na kuvijadili.

• Walimu wanaweza kuweka kumbukumbu za mbinu za udhibiti wa darasa walizozitumia. Hizi ni kumbukumbu za mbinu zilizofanikiwa, zile ambazo hakufanikiwa, na kwa nini. Walimu wanaweza kutumia Kitini cha 4 kutoka katika ‘Dhibiti darasa lako’, sehemu ya 1 na Kitini cha 2 kutoka katika moduli hii ili kupata mawazo.

• Weka malengo: Walimu wanaweza kuchagua mbinu moja kwa kila majuma mawili au kwa kila mwezi wanaotaka kuboresha. Wanaweza kuwa na shajara ya jinsi na lini

Page 61: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 5

57

walitumia mbinu husika, jinsi mbinu ilivyofanikiwa, na jinsi ambavyo wangeweza kuboresha zaidi.

Marejeleo Vyanzo vifuatavyo vilitumika katika kuandaa moduli hii:

• TiCCWG (2016) “Training Pack for Primary School Teachers in Crisis Contexts” Module 3 - Pedagogy. Teachers in Crisis Contexts Working Group. Linapatikana: www.ineesite.org/en/training-pack-for-primary-school-teachers-in-crisis-contexts

Page 62: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Ulinzi wa Watoto: Sehemu ya 1

58

Kitini cha 1: Kuzuia tabia mbaya/kurekebisha tabia 1. Ndiyo kwanza umewaachia wanafunzi wafanye shughuli fulani wao wenyewe.

Mwanafunzi aliyekaa nyuma ya darasa anageukageuka na kuzungumza na wanafunzi wengine. Unapomuuliza anachokifanya, hajui cha kusema.

• Tafakari kwanini mwanafunzi husika anafanya hivyo.

• Je, mwalimu anaweza kufanya nini ili kuzuia hali kuwa mbaya zaidi? 2. Wanafunzi ndiyo kwanza wamewasili ili kuanza siku. Wamehamasika na wana nguvu

na wote wanazungumza wenyewe kwa wenyewe. Kiwango cha sauti darasani kinaongezeka. Unataka kuanza somo na unahitaji usikivu wa wanafunzi.

• Je, mwalimu anaweza kufanya nini kurejesha usikivu wa wanafunzi na kuwa tayari

kuanza somo? 3. Umeandaa kazi ya kufanya, na unadhani itafanikiwa sana. Unaelezea kuhusu kazi

husika, lakini kazi inapoanza unagundua kuwa haiendi kama ulivyopanga. Wanafunzi hawafanyi vizuri kazi husika na hawaelewi jambo lenyewe.

• Tafakari kwanini wanafunzi wanafanya hivyo.

• Je, mwalimu anaweza kufanya nini ili kuzuia hali kuwa mbaya zaidi? 4. Umekuwa ukitoa mhadhara kwa dakika 20. Wakati unaandika ubaoni, wanafunzi

wananong’ona na wanarushiana vitu.

• Je, mwalimu anaweza kufanya nini kuzuia hali hii?

Page 63: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 5

59

Kitini cha 2: Usimamizi chanya wa nidhamu Tulia kisha tafakari

Vitendo vya wanafunzi vinapokuvurugia utaratibu, jiulize maswali yafuatayo kabla hujachukua hatua:

Page 64: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Ulinzi wa Watoto: Sehemu ya 1

60

Kurekebisha tabia mbaya

• Rudia kuelezea matarajio. • Masimulizi chanya: Mwalimu anataja tabia njema ili kuwakumbusha wanafunzi wote

mambo wanayopaswa kuyafanya. • Ukaribu: Mwalimu anapaswa wakati wote kuzunguka darasani anapofundisha. Hali hii

hudhibiti tabia mbaya. Mwalimu anapomkaribia mwanafunzi ambaye hafanyi kazi aliyoagizwa, kwa kawaida mwanafunzi husika ataacha tabia mbaya na atakuwa msikivu tena.

• Ukimya wa ghafla: Mwalimu anaacha kuzungumza na anasubiri tabia mbaya kukoma kabla hajaendelea na somo.

• Toni au kiwango cha sauti: Mwalimu anaweza kubadili toni au kiwango cha sauti ili kurejesha usikivu darasani. Wakati mara kwa mara sauti ya mwalimu huwa ya juu, mwalimu kamwe hapaswi kupoteza udhibiti. Mwalimu hapaswi kuwapayukia wanafunzi.

• Ishara za kimwili: Mwalimu anaweza kutumia ishara mbalimbali za kimwili ili kurejesha usikivu wa wanafunzi (mfano, ishara za mikono, kugonganisha vidole, kupiga makofi, kuonesha vidole, na kugonganisha viganja). Walimu watapaswa kutumia ishara hizi kila mara (Tazama: ‘Dhibiti darasa lako’, sehemu ya 1).

• Iwapo wanafunzi wataendelea kuonesha utovu wa nidhamu baada ya kuwa umeshajaribu kurekebisha tabia, nenda hatua inayofuata.

Kubainisha madhara ya utovu wa nidhamu • Tekeleza hili sehemu ya falagha kadri iwezekanavyo.

• Waagize wanafunzi watafakari kwanini tabia zao hazikubaliki.

• Bainisha madhara ya utovu wa nidhamu. Hakikisha madhara yanaendana na utovu wa nidhamu. Kwa mfano, wanafunzi wapelekwe kwa mwalimu mkuu kwa makossa sugu/au tabia za hatarishi darasani.

• Mwanafunzi akibisha, msikilize kwa heshima na kuwa tayari kukubali kwamba unaweza kuwa hukufahamu jambo fulani darasani.

Page 65: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 5

61

Kitini cha 3: Igizo na kadi za wahusika. Tabia na madhara Badili aina za tabia mbaya ili kuakisi masuala ya kawaida katika mazingira yako. Igizo la 1 – Wahusika Mwalimu – Anza kuwafundisha wanafunzi wako somo la kawaida kuhusu mada yoyote uliyoichagua. Unaweza kutumia kitabu cha kiada kama nyenzo ya kukusaidia. Wanafunzi wataanza kuonesha utovu wa nidhamu. Fanya maamuzi ya jinsi ya kukabiliana na tabia hiyo mbaya. Mwanafunzi wa 1 – Utaonesha utovu wa nidhamu wakati wa somo. Kila wakati utakuwa ukizungumza na mwenzako aliyekaa karibu nawe. Mwanafunzi wa 2 – Utaonesha utovu wa nidhamu wakati wa somo. Hutakuwa msikivu na utakuwa ukichezea nywele zako. Mwanafunzi wa 3 – Utaonesha utovu wa nidhamu wakati wa somo. Utakataa kufanya kazi, hata pale mwalimu anapokuagiza. Baada ya dakika chache, unatoka nje ya darasa kwa fujo tena bila ruhusa. Wanafunzi wengine – Mtakuwa wanafunzi watiifu. Mnatii maagizo ya mwalimu na mnafanya mlizopangiwa. Igizo la 2 – Wahusika Mwalimu – Darasa lako linafanya mtihani. Umetunga mtihani na unasimamia wanafunzi wanapoufanya. Wanafunzi wataanza kuonesha utovu wa nidhamu. Fanya maamuzi ya jinsi ya kukabiliana na tabia hiyo mbaya. Mwanafunzi wa 1 – Utaonesha utovu wa nidhamu wakati wa somo. Utaibia waziwazi kwenye kazi ya mwanafunzi mwingine. Mwanafunzi wa 2 – Utaonesha utovu wa nidhamu wakati wa somo. Utawapa wenzio vikaratasi vyenye majibu na utapiga miluzi. Wanafunzi wengine – Mtakuwa wanafunzi watiifu. Mnatii maagizo ya mwalimu na mnafanya kazi mlizopangiwa.

Page 66: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Ulinzi wa Watoto: Sehemu ya 1

62

6. Hakikisha Wanafunzi Wako Wanalindwa: Sehemu ya 1

¹ Jumla ya Saa 2 Malengo ya Moduli Kufikia mwisho wa moduli hii, wasiriki wataweza:

• Kueleza mahitaji ya kimwili, kiakili, kijamii, na kihisia ya watoto (NTCF 5.4)

• Kueleza haki za watoto na jinsi zinavyohusiana na mahitaji (NTCF 5.3)

• Kufafanua majukumu na wajibu wa walimu katika kulinda haki na ustawi wa watoto (NTCF 5.5)

• Kuanza kutumia maarifa haya darasani na shuleni (NTCF 5)

Vifaa vinavyohitajika • Chati zinazoonesha michoro ya

mahitaji ya watoto • Vitini

Page 67: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 5

63

Taarifa za kuwapa washiriki wakati wa moduli Ni muhimu walimu wajue mahitaji na haki za watoto. Walimu watumie darasani uelewa wao wa mahitaji na haki za watoto ili waweze kuongeza ushiriki na ujifunzaji wa watoto wote. Bila uwepo wa kanuni za msingi – kama vile usalama, adabu/heshima, umadhubuti/uimara, kuafikiana/kukubaliana, ustawi, na kuthaminiwa – kuna uwezekano mkubwa watoto wasistawi/wasifanikiwe. Wanaweza kuacha kuja shule, au kama bado wataendelea kuwapo darasani, wanaweza wasiwe wanajifunza kwa kiwango kinachofikia uwezo wao. Wewe ukiwa mtu mzima na mwalimu, una wajibu wa kulinda haki za watoto. Hii ina maana kwamba unawajibika kwa watoto. Pia, ina maana kuwa una jukumu muhimu la kutekeleza la kuweka mazingira salama, yenye ulinzi, yasiyo na vurugu, na yenye kuheshimika. Hali hii huwasaidia watoto kujifunza na kukua. Hii ina maana kuwa siku zote unapaswa ufanye mambo kwa maslahi ya watoto unaowatunza. Watoto wana mahitaji mengi, na mahitaji haya hutofautiana kulingana na umri au iwapo ni wasichana au wavulana. Ustawi wa mtoto unategemea kupatikana kwa mahitaji haya. Kwakuwa watoto hawawezi kupata mahitaji yao yote wao wenyewe, watu wazima katika jamii na shuleni wana wajibu wa kuhakikisha kuwa mahitaji ya watoto yanapatikana. Hali hii ni bayana zaidi panapokuwa na shida (mgogoro au majanga ya asili). Ni muhimu kujua kuhusu ulinzi wa watoto na kuchukua hatua katika hali za shida au majanga/dharura. Haki za Watoto Haki za watoto zinahusu jinsi tunavyochangamana nao na jinsi tunavyowaheshimu watoto wote. Haki za watoto ni masuala tunayoamini kuwa ni ya haki kwa kila mtoto ulimwenguni kote. Haki zinawahusu watoto wote bila kujali jinsi, kabila, uwezo, au dini zao. Hii ina maana kwamba haki ni za wote. Haki zimebainishwa katika sheria za kimataifa katika Mkataba wa Haki za Watoto. Mkataba huu unaainisha kuwa mtoto ni mtu mwenye umri wa miaka 0 hadi miaka 18. Serikali ambazo zimeridhia mkataba huu zinawajibika kuhakikisha kuwa watoto wote wanalindwa, bila kujali asili au hali zao. Walimu wanapaswa kutekeleza wajibu wao wa kuwalinda watoto wawapo madarasani na shuleni, na pia kutoa taarifa kuhusu hali au matukio yanayoashiria unyanyasaji au kudhuru watoto.

Page 68: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Ulinzi wa Watoto: Sehemu ya 2

64

Kazi za Kufanya 1. Mahitaji na Haki za Watoto Lengo la kazi hii ni kukuza maarifa na uelewa wa mwalimu kuhusu mahitaji na haki za watoto, na kuwasaidia walimu husika waweze kutumia maarifa na uelewa huu darasani na shuleni. 1a. Mahitaji ya Watoto ¹ Dakika 30

“Watoto wana mahitaji tofauti na ya watu wazima. Kupata mahitaji haya kunachangia ustawi wa jumla wa mtoto. Shida zinafanya iwe ngumu zaidi kuhakikisha kuwa mahitaji ya watoto yanafikiwa. Kwa kuanza moduli hii,

tutatafakari mahitaji ya watoto katika jamii yetu.” Wagawe washiriki katika vikundi vya watu 4 au 5.

“Zingatia Kitini cha 1. Tutafanya kazi katika vikundi ili kuibua mahitaji ya watoto. Angalia mchoro wa mtoto. Jadili na andika majibu yako ya maswali yafuatayo

katika chati: • Kichwa: Mtoto anahitaji nini kiakili? • Moyo: Mtoto anahitaji nini kihisia? • Mikono: Mtoto anahitaji nini kimwili? • Miguu: Mtoto anahitaji nini kijamii?”

Mfano Kichwa: mtoto anahitaji kichocheo na fursa ili awe mbunifu. Mikono: mtoto anahitaji chakula ili awe na afya njema. Wajibu wa Kijinsia

Viagize vikundi vifanye mapitio ya majibu yao na viongeze mahitaji yoyote yanayoweza kuwa muhimu kutegemeana na ama ni msichana au mvulana. • Je, wasichana na wavulana wana mahitaji tofauti? • Kwanini ni mhimu kwa mwalimu kuzingatia tofauti hizi? • Je, msichana mlemavu ana mahitaji gani darasani? • Je, mvulana anayezungumza lugha tofauti na ni wa kabila tofauti ana

mahitaji gani darasani? Waulize iwapo watoto wanaweza kutimiza mahitaji haya yote wao wenyewe. Ndiyo/Hapana/Kwanini? Muombe mshiriki mmoja ajitolee kuandika majibu ya Kikundi cha 1 kwenye mchoro ulio kwenye chati. Ongeza majibu kutoka kwenye vikundi vingine iwapo yanatofautiana na ya kikundi cha 1. Tumia Kitini cha 2 kuongeza

Sema

Sema

Page 69: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 5

65

mahitaji yoyote muhimu yanayokosekana, ambayo ni muhimu kwa washiriki kuyafahamu. Uliza jinsi shida/dharura zinavyoweza kutatiza kuhakikisha kuwa mahitaji ya watoto yanafikiwa. Changamoto hizi zinatatuliwaje? Kwa mfano, shule zinawezaje kuhakikisha kuwa watoto wanalindwa kikamilifu iwapo kutatokea majanga? 1b. Haki za Watoto ¹ Dakika 30

“Binadamu, bila kujali umri, mahali wanapoishi, utamaduni wao au hali zao za kijamii na kiuchumi, wana mahitaji ya msingi sawa. Mahitaji haya ni pamoja na chakula, huduma za afya, malazi, elimu, na ulinzi. Kila mtu ana haki ya

kupata mahitaji haya. Mkataba wa KImataifa wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Watoto wa Mwaka 1989 unasisitiza haki hizi za watoto. Mkataba huu umeridhiwa na nchi zote isipokuwa Somalia na Marekani”. “Nitawapa kila kikundi kadi (Kitini cha 3), zenye kauli kutoka katika Mktaba wa Kimataifa wa Haki za Watoto. Kama kikundi, someni kadi husika na oanisha haki zilizoandikwa na moja ya mahitaji uliyobandika kwenye mchoro wa mtoto uliopo kwenye chati. Kwa mfano, Ibara ya 31 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watoto inasema kuwa watoto wana haki ya kucheza, na haki hii inalinda hitaji la kitendo cha kimwili, hivyo, kadi inapaswa kuwekwa katika mkono wa mtoto”. Baada ya kauli za haki zote kuwa zimebandikwa:

“Haki hazikusudiwi kuwaruhusu watoto kufanya chochote watakacho. Haki zipo ili kufanikisha mahitaji ya watoto wote na kuimarisha ulinzi na ustawi wao”.

Uliza iwapo kuna maswali kuhusu mahitaji na haki za watoto. Waombe washiriki watoe mifano ya jinsi wanavyoweza kutumia maarifa haya katika madarasa yao. Ruhusu mifano 4-5. 3. Dhima na wajibu wa mwalimu kama mtu mwenye wajibu

¹ Dakika 60 Lengo la kazi hii ni kwa walimu kuelewa maana ya kuwa ‘mwenye-wajibu’ na kuweza kuchukua hatua stahiki kuhusu ulinzi wa watoto. Pitia mifano iliyotolewa na washiriki mwishoni mwa kazi 1b kuhusu jinsi walimu wanavyoweza kuanza kutumia maarifa ya mahitaji na haki za watoto. Sisitiza mifano inayoonesha wajibu wa mwalimu wa kuchukua hatua ya kulinda mahitaji na haki za watoto. Sisitiza kwamba watu wazima wote ni watu wenye-wajibu.

Sema

Sema

Page 70: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Ulinzi wa Watoto: Sehemu ya 2

66

Uliza iwapo wanakubaliana na kauli kwamba: “Kama mwalimu, nitashughulikia kwa namna bora kusaidia ustawi na ujifunzaji wa mtoto. Kama mwalimu, ninawajibika. Iwapo haki za mtoto zinakiukwa darasani mwangu au shuleni, nina wajibu wa kuchukua hatua stahiki”. Elezea kuwa jukumu kuu la walimu mara nyingi ni kuwafahamisha watu wazima wengine matatizo ya watoto. Hivyo, ni sawa iwapo mwalimu atashindwa kutatua tatizo husika yeye peke yake. Kuwaomba msaada wa wengine ni suala muhimu katika kulinda haki za watoto. Toa mifano, kama hii ifuatayo: Iwapo mtoto anakuja darasani akiwa na njaa, mahitaji yake yanakuwa hayajatimizwa na itamwia vigumu kuwa makini na kujifunza. Mwalimu anaweza kwenda kwa mwalimu mkuu au kamati ya shule ili kuiomba jamii a) imnunulie mtoto chakula; b) imshawishi mzazi wa mtoto anunue chakula. Iwapo msichana amekasirika au ametoroka shule, mwalimu anaweza kumuuliza msichana mwenyewe au rafiki zake sababu ya hali hiyo. Inagundulika kuwa msichana anataka kuondolewa shuleni ili aolewe mapema. Mwalimu anaweza kuongea na mwalimu mkuu na kamati ya shule ili kupata msaada wa kuwashawishi wazazi waachane na mipango ya ndoa, na/au kumwacha msichana aendelee na shule.

Uliza: “Je, kuna watoto walio katika hatari zaidi za kunyanyaswa, kuonewa, na kupuuzwa kuliko wengine? Kama ndiyo, hawa ni watoto gani, na ni nini kinawafanya wawe katika hatari zaidi?”

“Tutafanya kazi kwenye vikundi vilevile na kila kikundi kitasoma kisa mahususi (Kitini cha 4) Kila mtu katika kikundi chako anapaswa kusoma hadithi na kisha kwa pamoja wajibu maswali yafuatayo:

• Mahitaji ya mtoto katika hadithi hii ni yapi? • Ni haki zipi zimekiukwa? • Ni hatua gani zingeweza kuchukuliwa na walimu shuleni ili kumlinda mtoto?”

Majibu ya Mfano • Kisa cha 1: Mwalimu anaibua kisa kwa mwalimu mkuu na/au kamati ya

shule. Familia zinaarifiwa ili zishughulikie jinsi wasichana wanavyoweza kuja shuleni kwa usalama, mfano kwa kutembea kwa makundi.

• Kisa cha 2: Mwalimu anaweza kuongea na mvulana au kuwapigia simu wazazi wake ili kubainisha tatizo. Baada ya tatizo linalomkabili mvulana kufahamika, linaweza kutatuliwa. Mwalimu hatumii adhabu.

Sema

Page 71: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 5

67

• Kisa cha 3: Mwalimu anaweza kuieleza kamati ya shule kuwa watoto wanafahamu vizuri zaidi mambo yanayowafanya yajisikie salama au si salama ndani na nje ya shule, na kwamba wanapaswa kuulizwa wao wenyewe.

• Kisa cha 4: Mwalimu anaweza kuzungumza na wafanyakazi wengine wa shule ili kubainisha kwamba mvulana napaswa kuwa shuleni kama watoto wengine na kuwashauri wabadili mitazamo yao.

“Kama mwalimu, jukumu letu ni kufuatilia na pia kuchukua hatua ili kulinda haki za mtoto na kuhakikisha ustawi wa mtoto. Je, kuna yeyote mwenye hadithi au mifano inayotokana na uzoefu wa kushughulikia masuala ya ulinzi

wa watoto darasani au shuleni?” Huu ni mwisho wa moduli hii. Mwezeshaji apime iwapo malengo ya moduli hii yamefikiwa. Viashiria vya mafanikio o Mwalimu ameonekana akitengeneza mazingira ya adabu/heshima na

mazingira ya kujifunzia yaliyo salama, ambayo yanadhihirishwa na kiwango kikubwa cha ushiriki wa wanafunzi wakati wa somo.

o Mwalimu anahimiza mahusiano chanya kati yake na wanafunzi na miongoni mwa wanafunzi wenyewe kwa wenyewe.

o Mwalimu anawajibika kwa mahitaji, tabia, na haki za watoto. o Mwalimu anatoa taarifa zinazohusiana na masuala ya ulinzi wa wmtoto

iwapo zitaibuka. Stadi za kwenda nazo darasani • Utawasikiliza watoto na kuelewa vema changamoto wanazokabiliana nazo. • Utaweza kutambua na kukabiliana ipasavyo mahitaji ya watoto shuleni.

• Utaweza kuwalinda ipasavyo watoto dhidi ya madhara mbalimbali.

• Utazungumza na watoto panapokuwa na matatizo na kitabia au kama watoto watagombana/pigana, badala ya kutoa adhabu.

• Utachukua hatua ili kuwasaidia na kuwalinda watoto kwa kuzingatia uelewa wa jukumu na wajibu wako kama mwalimu.

Ujumuishaji

Shida huwaathiri watoto kwa namna mbalimbali. Ni muhimu kwa walimu kuzingatia athari kwa wavulana, kwa wasichana, kwa watoto wanaotoka katika jamii duni, na watoto wenye ulemavu. Hii itawasaidia walimu kuwapa msaada na kuwalinda ipasavyo watoto wote.

Sema

Page 72: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Ulinzi wa Watoto: Sehemu ya 2

68

Mawazo kwa ajili ya ujifunzaji wa pamoja/ binafsi • Walimu wanaweza kupanga kukutana na walimu wengine, wanaume na

wanawake, ili kujadiliana na kukubaliana jinsi ya kuimarisha ulinzi na kutoa msaada kwa watoto wote madarasani.

• Walimu wanaweza kujadiliana na watoto jinsi ya shule zinavyoweza kuwa salama na zenye ulinzi zaidi. Hii inaweza kujumuisha kubuni sheria ndogondogo za darasani ambazo ni rafiki kwa watoto.

• Walimu wanaweza kukubaliana na mwalimu mkuu, kamati ya shule, na walimu wengine kuhusu nini kifanyike ili kuwasaidia watoto waweze kujilinda wawapo shuleni, nyumbani, na njiani kwenda na kurudi shuleni.

• Walimu wanaweza kujifunza zaidi kuhusu Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watoto na jinsi unavyotumika katika sehemu zao za kazi.

• Wanaweza pia kujifunza zaidi kuhusu kanuni za kazi kwa walimu shuleni/nchini mwao, kama zipo.

Marejeleo Vyanzo vifuatavyo vilitumika kuandaa moduli hii:

• ESSPIN “Child Protection Training Materials” (hazipo mtandaoni)

• ESSPIN (2013) “Mentoring and Training Pack for Supporting School Based Management Committees in Nigeria”. Linapatikana: www.esspin.org

• International Rescue Committee (IRC). (2006). Creating healing classrooms: Tools for teachers and teacher educators. United States: International Rescue Committee, Children and Youth Protection Development Unit. Linapatikana: http://toolkit.ineesite.org/toolkit/INEEcms/uploads/1088/Creating_Healing_Classrooms_Tools.pdf

• OECD (2014). “What does it take to become a teacher? Education at a Glance 2014: OECD Indicators”. Indicator D6. OECD Publishing. Linapatikana: www.oecd-ilibrary.org/education/education-at-a-glance-2014/indicator-d6-what-does-it-take-to-become-a-teacher_eag-2014-34-en

• Save the Children Sweden (hakuna tarehe) “Positive Discipline, What is it and How to Do It: A manual for facilitators, educators and trainers”. Linapatikana: http://resourcecentre.savethechildren.se/sites/default/files/documents/4871.pdf

• Save the Children UK (hakuna tarehe) “What is Child Protection? Training Module 1”. Linapatikana: http://resourcecentre.savethechildren.se/sites/default/files/documents/5403.pdf

Page 73: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 5

69

• TiCCWG (2016) “Training Pack for Primary School Teachers in Crisis Contexts” Module 2: Child Protection, Well Being and Inclusion. Teachers in Crisis Contexts Working Group. Linapatikana: www.ineesite.org/en/training-pack-for-primary-school-teachers-in-crisis-contexts

itini cha 1

Page 74: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Ulinzi wa Watoto: Sehemu ya 2

70

Kitini cha 2

Page 75: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 5

71

Kitini cha 3

Page 76: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Ulinzi wa Watoto: Sehemu ya 2

72

Page 77: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 5

73

Page 78: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Ulinzi wa Watoto: Sehemu ya 2

74

Page 79: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 5

75

Kitini cha 4: Visa kuhusu Ulinzi wa Watoto Kisa cha 1 Watoto wengi kutoka maeneo fulani ya jamii wameacha kuja shule tangu tukio lilipotokea. Hali hii inatokea pamoja na juhudi zilizofanywa na jamii na shule ili kuhakikisha elimu inaendelea kutolewa. Katika moja ya matukio, mtoto mmoja kutoka katika eneo husika alikabiliwa na fisi ingawa alifanikiwa kukimbia, lakini watoto wengine na familia zao sasa zinaogopa kupita njia hii kwenda shule na badala yake wanakaa tu nyumbani. Kisa cha 2 Uwezo wa kitaaluma wa mvulana shuleni umeshuka mno tangu kutokea kwa janga. Anaonekana kutopenda, ana hofu, na woga darasani na mahudhurio yake hayatabiriki. Wakati mwingine anaonesha utovu wa nidhamu na hana adabu kwa walimu wake na wanafunzi wenzake. Kisa cha 3 Kamati ya Shule imepanga kuifanya shule kuwa salama na mazingira tulivu ya kujifunzia kwa watoto. Watoto wenyewe wanataka waulizwe kuhusu masuala yanayopaswa kuboreshwa, Kamati ya Shule inawafukuza na kuwaambia kuwa wao ni watoto tu, na kwamba wawaachie watu wazima washughulikie mambo haya. Kisa cha 4 Mvulana wa miaka nane katika jamii ana ulemavu. Angependa kuwa katika darasa la kawaida pamoja na watoto wenzake, lakini watumishi maofisa wa shule na walimu wanadhani itafaa zaidi iwapo mtoto atakaa nyumbani. Mtoto na wazazi wake wanataka abaki shuleni. Maswali ya Tafakuri • Mahitaji ya watoto katika visa hivi ni yapi? • Ni haki zipi za mtoto zimekiukwa?

• Ni hatua gani zingeweza kuchukuliwa na walimu shuleni kushughulikia visa hivi?

Page 80: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Ulinzi wa Watoto: Sehemu ya 2

76 Content Missing

7. Hakikisha Wanafunzi Wako Wanalindwa: Sehemu ya 2

¹ Jumla ya saa 2

Page 81: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 7

77

Taarifa muhimu za kushirikishana na washiriki katika moduli hii Kuelewa mahitaji na haki za watoto ni hatua muhimu katika kuyafanya madarasa sehemu salama ambako watoto wote wanaweza kujifunza, kucheza, kukua. Walimu wana jukumu muhimu katika kufikia na kulinda ustawi wa watoto. Hatua zinazofuata ni kutumia uelewa huu: kukuza stadi za kutambua wakati watoto wanapokuwa na matatizo; kutambua vihatarishi wanavyoweza kuvipata watoto wawapo darasani na shuleni; kubuni hatua za kusaidia kuzuia utokeaji wa masuala ambayo ni hatarishi kwa watoto, na hatua za kushughulikia vihatarishi hivyo pale vinapotokea. Kanuni au taratibu rasmi na zisizo rasmi na mifumo ya udhibiti kwa ajili ya tabia za walimu na wanafunzi huweza kusaidia kuweka mazingira salama zaidi. Hii ni pamoja na miongozo ya kanuni za kazi na msaada wa kitaalamu kuhusu tabia za kimaadili ya walimu. Kama zana hizi hazipo, zinaweza kuandaliwa na kukubaliwa katika eneo husika. Wanafunzi washirikishwe pia katika uandaaji wa kanuni za darasa na shule (zingatia moduli inayoitwa ‘Simamia darasa lako’, sehemu ya 1). Hatua hii inaweza kusaidia kuweka mazingira salama kwa wote. ‘Mikataba’, miongozo, au orodha hakiki ya masuala ya ulinzi wa watoto inaweza kubuniwa madarasani na shuleni kwa kushirikiana na walimu na wanafunzi, wazazi, na jamii. Tayari kunaweza kukawa na njia rasmi za kuripoti matukio ya unyanyasaji au ukatili dhidi ya watoto unaotokea mazingira ya shule. Ni muhimu, hususani wakati wa matatizo, kwa walimu na wanafunzi kuzifahamu njia hizi. Pale ambapo njia hizi hazipo, hatua zinaweza kuchukuliwa kuwasaidia walimu na wanafunzi kufahamu hatua za kuchukua. Moduli hii itatoa maarifa na stadi za nyongeza kuwasaidia walimu kuweka mazingira salama kwa watoto wote na kuchukua hatua stahiki matatizo yanapotokea.

Rejea moduli ya 5 na 6 (udhibiti wa kiufumbuzi na hai wa darasa) kwa maelezo zaidi kuhusu udhibiti wa nidhamu.

Page 82: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Ulinzi wa Watoto: Sehemu ya 2

78

Kazi za kufanya 1. Kutambua masuala ya ulinzi wa mtoto ¹ Dakika 20 Pale ambapo watoto hawajisikii salama au wanaolindwa, wanaweza kuonesha dalili za unyonge. Lengo la kazi ya 1 na 2 katika moduli hii ni kuwasaidia washiriki kutambua dalili za unyonge kwa watoto, na kuona vihatarishi vinavyoweza kutokea darasani na shuleni.

“Walimu wana nafasi nzuri ya kufuatilia mabadiliko ya tabia za watoto kwa sababu ya muda mwingi ambao watoto huwa chini ya uangalizi wao. Walimu wana jukumu la kupunguza vihatarishi kwa watoto madarasani mwao na kuweka mazingira ya ulinzi ambayo yatawafanya watoto waweze kujifunza.

Moja ya majukumu ya mwalimu ni kufuatilia maendeleo ya watoto darasani. Walimu lazima washughulikie kila dalili za unyonge au chuki zinazoweza kuathiri ustawi wa watoto, ushiriki, na kujifunzaji”. Uliza: Tutajuaje kuwa mtoto alikuwa anakabiliwa na tatizo au alikuwa mnyonge darasani mwako? Ni tabia zipi zinaweza kudokeza hali ya unyonge? Kusanya mrejesho kutoka kwa washiriki na andika kwenye chati. Mifano ya mrejesho ni: kulia, hasira, kupigana, kuchelewa shule/darasani, kujitenga, utoro, usikivu finyu, uchafu, kuumwa, majeraha/alama mwilini, kutomaliza kazi za darasani, na ukimya uliopitiliza. Uliza: Kwanini mtoto anaweza kuchelewa shule kila mara au kuwa na mahudhurio yasiyoeleweka? Kwanini mtoto hawezi kuwa na usikivu darasani? Kusanya tena majibu kutoka kwenye majopo. Mfano wa majibu ni: huenda anapaswa kufanya kazi za nyumbani; huenda anapaswa kuuza au kutembeza bidhaa mitaani kabla hajaja shuleni; huenda anaonewa na watoto wenzake au mwalimu fulani; labda ni mgonjwa; labda ametelekezwa chumbani. Sisitiza umuhimu wa kuzungumza na kila mwanafunzi ili kufahamu kwanini anachelewa au ana mahudhurio yasiyoeleweka shuleni, au kwanini ana usikivu duni darasani. Hali inaweza kuwa nje ya uwezo wa mtoto, hivyo hapaswi kuadhibiwa. Mwalimu anaweza kuwasiliana na wazazi pia ili kupata uelewa sahihi wa hali husika, na ili kupata msaada wa jinis ya kutatua tatizo husika.

Sema

Page 83: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 7

79

2. Kubainisha masuala hatarishi katika mazingira ya shule ¹ Dakika 40

Wagawe washiriki katika jozi.

“Shirikiana na mwenzi wako. Chagua shule ambayo mmoja wenu anafundisha (au kama hujaanza kufundisha, chagua shule ambayo mmoja wenu alisoma). Chora ramani ya shule husika na mazingira yake.”

Mfano

“Ukishakamilisha kuchora ramani, iangalieni pamoja ili mkubaliane kuhusu mambo yanayoweza kuifanya shule isiwe mahali salama kwa watoto. Fikiria sehemu katika eneo la shule ambayo yanayoweza yakawa na usalama mdogo kwa watoto. Yaoneshe mambo haya kwenye ramani kwa kutumia rangi tofauti”.

Mifano: eneo la choo kama lipo mbali na majengo makuu ya shule, au iwapo choo kimeharibika; vyoo vichafu; wavulana na wasichana kutumia choo kimoja; uwiano wa wanafunzi na matundu ya vyoo; maeneo ya vichaka; maeneo ambayo wachuuzi/waendesha bodaboda hukusanyika; njia za nyaya za umeme; barabara yenye magari mengi; mito (watoto wanaweza kushindwa kuvuka); “Fikiria mazingira halisi ya shule, lakini pia fikiria watu waliopo shuleni ikiwa ni pamoja na wanafunzi na walimu. Fikiria jinsi tabia zao zinavyoweza kuwasababishia watoto wasijisikie salama au wenye furaha” Mifano: wanafunzi wadogo kiumri kuwaonewa na wanafunzi wakubwa; vitisho au vipigo kutoka kwa walimu; lugha kali ya walimu.

Sema

Sema

Page 84: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Ulinzi wa Watoto: Sehemu ya 2

80

Jozi zikishamaliza kutafakari, ning’iniza ukutani ramani zao za shule na washiriki wazunguke kuziangalia. Katika jopo, orodhesha kwenye chati sababu kuu hatarishi zilizobainishwa na jozi. Uzingatiaji wa usawa wa kijinsia na ujumuishi

Uliza: Je, kuna masuala hatarishi zozote ambazo zinahusishwa zaidi na wasicha kuliko wavulana, au kinyume chake?

Uliza: Je, kuna masuala hatarishi zozote mahususi kwa wanafunzi wenye ulemavu?

Zingatia tofauti hizi.

Fanyia mapitio orodha ya masuala hatarishi. Sisitiza zile ambazo zinahusishwa na tabia na matendo ya walimu au wanafunzi. Iwapo hazikutajwa, ongeza adhabu ya viboko, ubabe, na udhalilishaji wa kingono na kijinsia. Lengo ni kuhakikisha kuwa kundi limebainisha vihatarishi vikubwa kabisa kwa watoto katika maeneo ya shule. Walimu wote wanapaswa wavifahamu vihatarishi hivi. 3. Masuala hatarishi yanayohusishwa na tabia za walimu na

wanafunzi ¹ Dakika 30

Lengo la kazi hii ni kubainisha vihatarishi kwa ulinzi wa wanafunzi vinavyoweza kutokea darasani na shuleni kutokana na vitendo vya walimu na wanafunzi wengine. Lengo ni kutusaidia kuzuia na kushughulikia vihatarishi hivi.

“Kama walimu, lazima tuhakikishe kuwa hatuzuii kufikiwa kwa mahitaji ya watoto, kukiuka haki za watoto, au kutumia mamlaka yetu kuwakandamiza watoto. Pia, tunapaswa kuweza kutambua na kukabiliana ipasavyo pale tunaposhuhudia watu wazima wengine wakiwadhuru watoto, na kuhakikisha kuwa wanafunzi hawadhuriani”.

Wagawe washiriki katika vikundi vinne. Kipangie kila kikundi moja ya mada zifuatazo za ulinzi wa mtoto: 1. Adhabu ya viboko 2. Ubabe 3. Unyanyasaji wa kingono na kijinsia 4. Adhabu zinazodhalilisha

Sema

Page 85: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 7

81

Kila kikundi lazima kijibu maswali yanayohusiana na mada yake. Kikundi kifanye kazi kwa dakika 10.

Kikundi cha 1 Kikundi cha 2 Kikundi cha 3 Kkundi cha 4 Adhabu ya

viboko Ubabe Unyanyasaji wa

kingono na kijinsia

Adhabu zinazodhalilisha

Maswali ambayo vikundi vitajibu:

• Je, tutafasilije mada hii? • Je, mada hii inaathirije ustawi na ujifunzaji wa watoto? • Sisi kama walimu, tunaweza kufanya nini kuzuia jambo hili kutokea

darasani mwetu? • Sisi kama walimu, tunaweza kufanya nini kushughulikia suala hili

likitokea?

Mwagize msemaji wa kila kikundi atumie dakika 2 kuwasilisha majibu ya kikundi chake kwa maswali manne. Toa muda kwa ajili ya maoni au nyongeza yoyote baada ya vikundi vyote kuwa vimewasilisha majibu yao. Tumia Kitini cha 1 kuongezea fasili au majibu yoyote ambayo washiriki hawakuyasema.

“Mifano hii ni baadhi ya njia hatari zaidi ambazo wanafunzi wanaweza kudhurika wawapo shuleni. Zinazoweza kuwa na madhara ya muda mrefu kwa ustawi na ujifunzaji wa watoto”.

Eleza kuwa njia mbadala mahususi ambazo ni chanya za kudumisha nidhamu madarasani zinaweza kupatikana kwenye moduli zinazoitwa ‘Dhibiti darsa lako’, sehemu ya 1 na 2. 4. Darasa langu lenye ulinzi na usalama ¹ Dakika 30

Lengo la kazi hii ni kuwasaidia walimu kuchukua hatua pale masuala ya ulinzi wa watoto yanapotokea.

“Kwa kuzingatia kazi iliyotangulia, tutaunda orodha 2 za kufanyia uhakiki. Orodha hizi zinaweza kutumiwa na walimu wote, mwalimu mkuu, na wanafunzi wote, kama ‘viwango vya msingi’ kwa ajili ya madarasa salama na yanayolindwa. Orodha moja ya uhakiki italenga kuzuia, na nyingine itahusu hatua za kushughulikia masuala ya ulinzi wa mtoto yanapotokea”.

Chora kwenye karatasi ya chati mchoro wa duara la ulinzi kutoka katika Kitini cha 2. Shirikiana na washiriki katika makundi kuandika vitendo vya ulinzi katika duara. Jaribu kuibua masuala muhimu 7 tu. Zingatia kuwa kitini tayari kimeshajazwa, lakini kazi hii inaweza kuibua masuala mengine/zaidi.

Sema

Sema

Page 86: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Ulinzi wa Watoto: Sehemu ya 2

82

Andika jedwali katika karatasi cha chati la ‘hatua za kushughulikia masuala ya ulinzi wa mtoto darasani na shuleni’. Shirikiana na washiriki kwenye jopo ili kuibua masuala matano. Zingatia kuwa kitini tayari kimeshajazwa mapendekezo lakini kazi hii inaweza kuibua mengine/zaidi. Huu ni mwisho wa moduli hii. Mwezeshaji apime ili kujua iwapo malengo ya moduli yamefikiwa.

Viashiria vya mafanikio o Mwalimu anaweza kufahamu masuala ya ulinzi wa mtoto miongoni mwa

wanafunzi na walimu. o Mwalimu anaweza kubainisha vihatarishi vya ulinzi wa mtoto na kuchukua

hatua za kuzuia na/au kuvishughulikia. o Mwalimu anachukua hatua mara moja kushughulikia migogoro, ubabe, na

tabia za kibaguzi na ukosevu wa adabu. Mawazo kwa ajili ya uelekezaji Mwalimu mkuu au mwelekezaji anaweza kutumia orodha za kufanyia tathmini zilizoandaliwa na washiriki ili kutolea mrejesho wa jinsi walimu walivyofanikiwa kutengeneza mazingira yenye ulinzi na usalama madarasani mwao. Pale ambapo kuna kanuni za kazi za walimu au hatua za kikatiba za ulinzi wa mtoto, walimu wakuu au wakufunzi wanaweza kuongezea mafunzo zaidi au msisitizo.

Mawazo ya ujifunzaji wa pamoja/ binafsi • Walimu wakuu wanaweza kuandaa vikao/majukwa ya mara kwa mara ya

kuwakutanisha walimu ili kupeana hoja zozote kuhusiana na tabia za watoto, mahudhurio, kuwahi shuleni, ushiriki, na ujifunzaji. Wanaweza kujadiliana, kushauriana, na kuchukua hatua zaidi kadri iwezekanavyo.

• Pale ambapo kuna kanuni za kazi za kikatiba au hatua za ulinzi kwa walimu, walimu wazisome na wazijadili pamoja.

• Majukwaa ya kupeana uzoefu yanaweza kujumuisha jinsi walimu walivyofanikiwa kushughulikia visa/matukio mbalimbali (mathalani, kushughulikia ubabe darasani), au jinsi walivyotumia njia chanya za kudhibiti nidhamu ili kupata matokeo mazuri kwa watoto.

Page 87: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 7

83

Marejeleo Vyanzo vifuatavyo vimetumika kuandaa moduli hii:

• ESSPIN “Child Protection Training Materials” (halipatikani mtandaoni)

• ESSPIN (2013) “Mentoring and Training Pack for Supporting School Based Management Committees in Nigeria”. Linapatikana: www.esspin.org

• International Rescue Committee (IRC). (2006). Creating healing classrooms: Tools for teachers and teacher educators. United States: International Rescue Committee, Children and Youth Protection Development Unit. Linapatikana: http://toolkit.ineesite.org/toolkit/INEEcms/uploads/1088/Creating_Healing_Classrooms_Tools.pdf

• OECD (2014). “What does it take to become a teacher? Education at a Glance 2014: OECD Indicators”. Indicator D6. OECD Publishing. Linapatikana: www.oecd-ilibrary.org/education/education-at-a-glance-2014/indicator-d6-what-does-it-take-to-become-a-teacher_eag-2014-34-en

• Save the Children Sweden (hakuna tarehe) “Positive Discipline, What is it and How to Do It: A manual for facilitators, educators and trainers”. Linapatikana: http://resourcecentre.savethechildren.se/sites/default/files/documents/4871.pdf

• Save the Children UK (hakuna tarehe) “What is Child Protection? Training Module 1”. Linapatikana: http://resourcecentre.savethechildren.se/sites/default/files/documents/5403.pdf

• TiCCWG (2016) “Training Pack for Primary School Teachers in Crisis Contexts” Module 2: Child Protection, Well Being and Inclusion. Teachers in Crisis Contexts Working Group. Linapatikana: www.ineesite.org/en/training-pack-for-primary-school-teachers-in-crisis-contexts

Page 88: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Ulinzi wa Watoto: Sehemu ya 2

84

Kitini cha 1 Kikundi cha 1 Kikundi cha 2 Kikundi cha 3 Kikundi cha 4

Adhabu ya viboko Ubabe Unyanyasaji wa kingono na kijinsia Adhabu zinazodhalilisha

Tunawezaje kufafanua mada hii?

Mateso ya kimwili dhidi ya mtoto ni yale yanayosababisha madhara halisi au yanayoweza kuwa halisi ya kimwili yanayofanywa na mtu mwenye wajibu, mamlaka, au anayeaminiwa.

Ubabe ni tabia mbaya na ya kichokozi inayohusisha kukosekana kwa usawa wa madaraka/nguvu. Tabia hii hurudiwarudiwa au kuna uwezekano wa kurudiwa kwa muda fulani.

Unyanyasaji wa kijinsia ni dhana jumuishi inayohusu kitendo chochote cha kudhuru kinachofanywa kinyume na ridhaa ya mtu, na kinachofanywa kwa kuzingatia jinsia ya mtu. Inafahamika kuwa, wakati ni kweli kuwa wanawake na wasichana ndiyo waathirika wakuu, wanaume na wavulana nao huathiriwa pia na vitendo hivi.

Adhabu ambazo humuaibisha na kumdhalilisha mtoto hadharani, inayomwondolea heshima, fahari, na utu wake. Huweza kuambatana na adhabu za kimwili au kauli za mdomo pekee.

Je, mada hii inaathirije ustawi na ujifunzaji wa watoto?

Ushahidi unaonesha kuwa adhabu hii ina athari mbaya kwa ujifunzaji na makuzi ya mtoto na kwamba inaweza kumfunza mtoto kwamba mabavu ni njia sahihi ya kutatua matatizo.

Ubabe unaweza kuwa na athari mbaya sana kwa maisha ya watoto kwa ujumla, na kwa ushiriki na ujifunzaji wao iwapo utatokea shuleni. Watoto wanaweza kuogopa kwenda shuleni au wanaweza kukosa furaha darasani.

Kama ilivyo kwa aina zingine zozote za unyanyasaji shuleni, inaweza kuwa na madhara mabaya sana kwa ushiriki na ujifunzaji wa mtoto. Kwakuwa kwa ujumla wasichana na wanawake ndiyo walioathirika zaidi, unyanyasaji wa kingono na kijisnia unaweza kuwa na athari mbaya sana, hususani katika mazingira ambamo elimu kwa

Athari zake ni hasi kwa makuzi, ushiriki, na ujifunzaji wa mtoto. Inaweza kuwa na madhara hasi zaidi ya adhabu za kimwili.

Page 89: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 7

85

wasichana tayari ni changamoto.

Sisi kama walimu, tunaweza kufanya nini kuzuia jambo hili kutokea darasani mwetu?

Jifunze njia zingine za udhibiti wa darasa: tumia njia chanya za kudumisha nidhamu, sifia tabia njema, shughuli za kila siku, ujifunzaji hai, nk..

Jenga utamaduni wa kuheshimiana, kukubaliana, na kuvumiliana darasani. Tumia vikao vya wafanyakazi, mikutano ya wanafunzi, vikao vya walimu na wanafunzi kujenga mazingira mazuri shuleni. Imarisha mwingiliano na ujumuishi chanya wa kijamii.

Jenga mazingira ya darasa ya kuhehimiana, ambapo wasichana na wavulana wanatendewa kwa usawa. Wakati wa kupanga na kutekeleza shughuli mbalimbali, zingatia athari zake kwa wasichana na wavulana, na kwa wavulana na wasichana wenye ulemavu.

Jenga mazingira ya darasa ya kuheshimiana, ambapo watoto wote watajihisi kuthaminiwa. Kama mtoto ataonesha utovu wa nidhamu, shughulikia tabia mahususi bila kudhamiria kumdhalilisha mtoto husika.

Sisi kama walimu, tunaweza kufanya nini kushughulikia suala hili likitokea?

Tukiwaona walimu wengine wakitoa adhabu ya viboko, tunapaswa kuchukua hatua. Tunaweza kuzungumza na mwalimu kuhusu umuhimu wa kutumia adhabu mbadala, kutoa taarifa kwa mwalimu mkuu, na kuchukua hatua kumsaidia mtoto amejeruhiwa.

Ingilia kati ili kusitisha ubabe na toa msaada kama ni lazima (kwa mfano, kama zimetumika silaha). Onesha mfano wa tabia ya kuheshimiana.

Toa taarifa za matukio ya unyanyasaji wa kingono na kijinsia shuleni kwa mwalimu mkuu au mtumishi mahususi anayeshughulikia masuala hayo. Chukua hatua kuhakikisha usalama wa mwathirika, na mpatie huduma za matibabu haraka iwezeknavyo.

Toa taarifa za uwepo wa adhabu zozote za kudhalilisha shuleni zinazotolewa na ama na walimu au na watoto wengine kwa mwalimu mkuu au mtumishi mahususi anayeshughulikia masuala hayo. Chukua hatua kupunguza athari za tukio kwa mtoto husika.

Page 90: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Ulinzi wa Watoto: Sehemu ya 2

86

Kitini cha 2: Kuweka mazingira ya ujifunzaji salama na yenye ulinzi

KUZUIA

Sisitizauhusianowakuheshimianadarasani

Fuatiliatabianaushirikiwawatoto

Kuwekakanuninavitendovyadarasavitakavyochukuliwa

kwawalewatakaokiukakanuni

Himizakuheshimu

nakufurahiatofautiShughulikia

harakadalilizaunyonge

Tumianjiachanya

kudumishanidhamu

Wekawazimatarajiokwaajiliyatabianjema

Wahamasishewatotokuripoti

matukio

Page 91: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Module 7

87

Hatua za kushughulikia masuala ya ulinzi wa mtoto darasani na shuleni

1 Toa taarifa za matukio ya ulinzi kwa mwalimu mkuu au mtumishi anayeshughulikia masuala ya ulinzi wa mtoto ili yafikishwe ngazi za juu, iwapo kuna utaratibu na kama ni lazima.

2 Ingilia kati ili kukomesha visa/matukio yanayohusiana na ulinzi wa mtoto (kwa mfano, ubabe na unyanyasaji wa kingono na kijinsia) ukishuhudiwa. Omba msaada kama silaha zimehusika au kama kuna vihatarishi vya usalama wako.

3 Hakikisha kuwa mwathirika anapata huduma na msaada, na kama ni lazima, huduma za afya (huduma za afya zinahitajika katika matukio ya ubakaji/unyanyasaji wa kingono).

4 Toa taarifa za tukio kwa wazazi au walezi wa mtoto, na waite shuleni ili mjadiliane/kutafuta msaada.

5

Kama mtoto atatoa taarifa ya tukio Fulani au atakuja shuleni akiwa amechukia/ameumia kutokana na tukio husika, msikilize na weka kumbukumbu. Mweleze kuwa unapaswa kutoa taarifa kwenye ngazi za juu, kutegemeana na ukubwa wa tukio lenyewe.

6

Walimu wanaweza kuwa wa kwanza shuleni kugundua watoto wanapoonesha dalili za kupuuzwa/kutelekezwa, kuadhibiwa, au kudhalilishwa majumbani kwao. Toa taarifa kwa mwalimu mkuu au mtumishi mwenye dhamana kuhusu hali hizi. Itisha huduma ya afya kama ni lazima. Yafahamu mashirika au asasi zingine za kijamii zinazojishughulisha na masuala ya ulinzi na usalama wa mtoto ili kupata msaada nje ya shule.

Page 92: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Anza na hitimisha masomo kwa madhumuni

88

8. Anza na Hitimisha Moduli kwa Malengo

¹ Jumla ya saa 2 Malengo ya moduli Kufikia mwisho wa moduli, washiriki wataweza:

• Kuanza somo kwa madhumuni, na malengo bayana ya mafunzo (NTCF 3.1)

• Kueleza kwanini masomo yanapaswa kuwa na maana na yanayohusiana na maisha ya wanafunzi (NTCF 3.1)

• Kuhusisha masomo/mafunzo ya awali na ya sasa (NTCF 3.1)

• Kumaliza vipindi kwa kufanya mapitio ona kuhitimisha (NTCF 3.1)

Vifaa vinavyohitajika • Karatasi za chati • Peni/kalamu • Vikaratasi vyenye gundi • Chati na Peni/kalamu za ziada kwa

ajili ya washirikis • Vitini

Page 93: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 8

89

Taarifa muhimu za kushirikishana na washiriki katika moduli hii Mwanzo wa moduli Moja ya nyakati muhimu ambazo mwalimu huwasiliana na wanafunzi ni mwanzo kabisa wa somo. Huu ni wakati ambao walimu hubainisha madhumuni ya somo, na ni wakati wanaotumia kuweka malengo ya ujifunzaji. Tafiti zinaonesha kuwa kuweka madhumuni na malengo bayana na yanayoendana na somo kwa wanafunzi huboresha matokeo ya ujifunzajina kuwahamasisha wanafunzi kujifunza. Sehemu nyingine muhimu ya mwanzo wa somo ni kuhusianisha somo lililopita na somo lililopo na uzoefu; na pia kuhusianisha somo jipya na mazingira ya wanafunzi. Hatua hii hufanya ujifunzaji uwe wa malengo na wenye thamani. Bila haya, kuna uwezekano mdogo wa wanafunzi kuhifadhi maarifa na stadi zilizofundishwa darasani. Ujifunzaji hufanyika vema wanafunzi wanapojiamini, wanapokuwa na mtazama chanya, na wanapokuwa wamehamasika. Hili ni jambo muhimu sana. Walimu wanapowasilisha somo kwa wanafunzi, wanatuma ujumbe wa hamasa (kwa njia ya maneno, kazi, jinsi masomo yanavyofundishwa). Wanafunzi husikiliza na kuamua kiasi cha muda, juhudi, na uvumilivu wanaotaka kuweka katika mafunzo yao. Kwa maneno rahisi, wanafunzi (rahisi kwenda magumu), huamua jinsi masomo yanavyovutia na kufurahisha. Walimu mahiri ni wale ambao wanaotambua vizuri hamasa na hisia za wanafunzi wao. Walimu wa namna hii hufahamu dhima yao katika kuwahamasisha wanafunzi kwa kutumia mtaala ili uendane na mazingira ya wanafunzi, ufurahishe, na uwe shirikishi. Hii huweza kuwafanya manafunzi wawe na hamasa na wenye mtazamo chanya. Hisia hasi kama vile kukata tamaa—huweza kuingilia kati mchakato wa ujifunzaji.

Mwisho wa moduli Walimu wanaweza kutumia hatua za mwisho za somo kufanya mapitio ya mada na kupima uelewa, na hatimaye kutengeneza muhtasari. Hii hurejesha usikivu/umakini wa wanafunzi kwenye malengo makuu na matokeo ya somo husika. Muhtasari humwezesha mwalimu fursa ya kurudia uhusiano kati ya mada ya somo la sasa na lililopita, maarifa, uzoefu, au masuala wanayoyapenda. Hii huchochea mchakato muhimu wa kitambuzi unaosaidia kupandikiza ujifunzaji miongoni mwa wanafunzi na kuwaacha wakijisikia vizuri baada ya darasa. Mwisho wa somo ni fursa pia ya kupima mafanikio ya somo lililopo na kuhusisha ujifunzaji na malengo na maudhui ya somo linalofuata. Hii huwasaidia wanafunzi kujiandaa na kuwa tayari kupokea maudhui ya somo linalofuata.

Page 94: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Anza na hitimisha masomo kwa madhumuni

90

Kazi za kufanya

1. Kuhusianisha somo lililopita ¹ Dakika 20

Lengo la kazi hii ni kujifunza jinsi kuhusianisha somo lililopita kunavyofanya masomo kuwa ya malengo nay a thamani.

“Tuanze moduli hii kwa kufikiria jinsi tunavyoweza kutumia maarifa/ujuzi tulionao katika kuyafanya masomo yetu yajielekeze zaidi katika kuwashirikisha kikamilifu wanafunzi wetu”.

Wagawie washiriki vikaratasi vyenye gundi au karatasi tupu. Waagize waandike mambo waliyojifunza kuhusu wanafunzi wao katika moduli ‘Wafahamu na wajumuishe wanafunzi wako wote’ na/au ‘Dhibiti darasa lako’, sehemu ya 1 na 2.

Waeleze watumie kikaratasi kimoja chenye gundi kwa wazo moja. Waite wabandike ukutani vikaratasi vyao vyeye mawazo.

Tembea kuzunguka darasa ili kuangalia vikaratasi vilivyobandikwa. Wahimize washiriki kuelezana majibu. “Hii ni mbinu ya ‘andika haraka’ inayoweza kukusaidia kupima masuala ambayo wanafunzi wako tayari wanayafahamu kuhusu mada iliyopo. Je, kuna njia zingine tunazoweza kutumia kupata maarifa kutoka kwa wanafunzi? [Zinaweza kujumuisha chemshabongo na michezo]. Je, maelezo haya changamani yanatueleza nini kuhusu wanafunzi wetu?” Sampuli ya majibu inaweza kujumuisha: historia zao, jamii zao, vikwazo wanavyokabiliana navyo, shughuli za kila siku na kazi wanazotumia darasani kuwashughulisha. Uliza: Kwanini ni muhimu kufahamu hili? Kama haijatajwa, wakumbushe washiriki kuwa baadhi ya wanafunzi huenda hawazungumzi lugha kuu ya shule wawapo nyumbani. Hivyo, wanaweza wakawa wanapata shida kuelewa masomo.

“Katika kazi inayofuata, tutatumia mambo ambayo tayari tunayafahamu kuhusu wanafunzi wetu”

2. Ni mambo gani wanafunzi wangu huyapendelea? ¹ Dakika 30

Lengo la kazi hii ni kujifunza jinsi ya kuyafanya masomo kuwa yenye maana kwa wanafunzi.

“Sasa tutatafakari zaidi jinsi tunavyoweza kuyafanya masomo kuwa yenye maana na yenye uhusiano kwa mwanafunzi”. Eleza kwanini hii ni muhimu. Wagawe washiriki katika vikundi vidogovidogo.

Sema

Sema

Sema

Sema

Page 95: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 8

91

Waagize vikundi kujadili masuala yaliyowafurahisha na kuwahamasisha sana wanafunzi wao wakati wa ufundishaji (Kwa mfano, wimbo, mchezo, au tukio). Fanya hivi kwa dakika, na kisha pokea mrejesho kutoka kwenye vikundi. Uliza: Mtajumuishaje mambo haya kwenye masomo yenu? Je, mnaweza kutumia masuala haya kuanza au kuhitimisha somo ili kuwashirikisha kikamilifu wanafunzi wenu? Kwa mfano, kama wanafunzi wanapenda michezo, unaweza kutumia matokeo ya mechi za soka kuwasaidia kuelewa hisabati? Je, kuna wimbo unaoweza kuwa na ujumbe muhimu? Je, kuna jambo lolote lililotokea kwenye vyombo vya habari ambalo linaweza kulifanya somo lako la historia lenye maana zaidi?

Wape vikundi dakika 5 za kujadili na kisha pata mrejesho kutoka katika vikundi kadhaa. Uliza: Je, kazi hii ilikua ni rahisi au ngumu? Kwanini unadhani ni wazo zuri kujumuisha mambo haya kwenye somo? Elezea manufaa ya kufanya ujifunzaji unaofurahisha, unaohusisha mazingira ya wanafunzi, na unaoibua mtazamo chanya kuhusu ujifunzaji.

Uzingatiaji wa masuala ya kijinsia Unapofikiria namna nzuri ya kuwashirikisha na kuwahamasisha wanafunzi, kwa mfano, mwanzoni mwa somo, jaribu kuchagua kitu fulani chenye mvuto kwa wavulana na wasichana, na watoto wenye historia tofauti. Hakikisha kuwa linakuwa jambo fulani, ambalo wanafunzi wote watajisikia vizuri kujadili.

Uliza: Ni mambo gani huathiri uwezo wa wanafunzi kushiriki katika masomo? (Kwa mfano, kuzungumza lugha tofauti nyumbani; kutoona vizuri; kutosikia vizuri; kutoweza kuzungumza hadharani kutokana na mila na desturi za kijinsia) fanya zoezi hili kwa dakika 5 kisha waeleze vikundi watoe mrejesho wa mijadala yao. Uliza: Je, utajumuishaje mambo haya kwenye masomo yako? Utafanya nini kuwasaidia wanafunzi kuelewa kwa urahisi zaidi lugha inayotumika darasani? Utafanya nini kuwasaidia wanafunzi wasioona au wasiosikia vizuri kushiriki kikamilifu katika masomo darasani?

Wape vikundi dakika 5 za kujadili hili na kisha kupata mrejesho kutoka kwa vikundi kadhaa. Ongeza mapendekezo kama vile: kuweka malengo ya somo ili kuwasaidia wanafunzi kujifunza na kufanya mazoezi ya lugha mpya (angalia moduli inayoitwa ‘Andaa somo kwa mtiririko sahihi’); kutumia lugha ya viungo vya mwili ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa; kuwahimiza baadhi ya wanafunzi kuwatafsiria wengine; kuwahimiza wanafunzi wenye ulemavu wa macho kugusa zana za kufundishia au vitu vingine; kuwahimiza wanafunzi wasiosikia kuchora au kutengeneza vitu vinavyoonekana vinavyosaidia kumbukumbu; kuomba kupewa mafunzo ya lugha ya alama; kuhakikisha kuwa huzibi kinywa au hugeuki wakati wa kuzungumza.

3. Kuweka bayanamalengo ya somo ¹ Dakika 30

Page 96: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Anza na hitimisha masomo kwa madhumuni

92

Lengo la kazi hii ni kuonesha thamani ya kuwabainishia wanafunzi malengo ya ujifunzaji. Fikiri – Kaa katika Jozi – Elezana Uliza: Lengo la mafunzo ni nini? Waagize washiriki wapeane majibu na wenza wao. Kisha ita jozi moja au mbili zieleze majibu katika jopo.

“Lengo la mafunzo ni kauli bayana na fupi kuhusu jambo ambalo wanafunzi wataweza kufanya kufikia mwisho wa mwaka wa shule/kozi/mradi/darasa. Tutajifunza kwanini kuwawekea wanafunzi malengo bayana mwanzoni mwa somo kunaweza kuboresha na kuhamasisha mafunzo”.

Wagawe washiriki katika vikundi vya washiriki wannewanne. Mshiriki mmoja katika kila kikundi anakuwa mwalimu. Walimu waje mbele ili wapokee maelekezo, karatasi ya chati, na kalamu zao. Mpe kila mwalimu maelekezo yaliyoandikwa kwenye kikaratasi kilichokatwa kutoka kwenye Kitini cha 1 na waagize waanze ‘darasa’ lao. Wape kila kikundi dakika kumi za kukamilisha kazi husika. Waeleze washiriki kuwa kila kikundi kimepewa maelekezo tofauti; hivyo wasitazamiane. Zingatia kuwa lengo la mafunzo ni kujifunza orodha ya maneno ya mazingira ya shule. Baada ya dakika 10, uliza: • Timu yako ilijisikiaje wakati wa kazi? Hamasika, sisimka, changanyikiwa? Kwanini?

• Kwanini kazi ilikuwa nzuri zaidi kwa Timu ya 4 kuliko kwa Timu ya 1?

• Kwanini ni muhimu kufikiria malengo ya somo lako kabla ya kuandaa na kuanza somo husika?

Mifano ya majibu: Lengo la mafunzo halikuwa bayana kwa Timu ya 1, 2 na 3. Timu ya 4 ilipewa taarifa kamili zaidi. Lengo la Timu ya 4 liliandikwa kwa kuzingatia jinsi wanafunzi watakavyotathminiwa. Kujua lengo kunawasaidia wanafunzi kufanya kazi na kuridhika wanapoikamilisha.

“Sehemu muhimu ya kuanza somo lako kwa malengo kuwabainishia wanafunzi matokeo ya mwisho ya kazi mnayoifanya nyote. Hii husaidia kuwashirikisha na kuwahamasisha wanafunzi na hivyo kuboresha matokeo ya mafunzo”.

Rejea moduli inayoitwa ‘Andaa somo kwa mtiririko sahihi’ ili kujifunza zaidi jinsi ya kutumia malengo ya mafunzo katika uandaaji wa somo.

4. Hitimisha masomo kwa malengo ¹ Dakika 30

Lengo la kazi hii ni kujifunza jinsi na sababu ya kuhitimisha masomo kwa malengo.

“Hebu tutafakari jinsi tunavyoweza kuhitimisha masomo yetu kwa malengo. Mengi ya mawazo yaleyale tuliyoyaona katika jinsi ya kuanza somo yanafanana na ya kuhitimisha somo. Fikiria kuhusu tuliyojifunza katika moduli hii. Utatumiaje stadi hizi katika masomo yako

Sema

Sema

Sema

Page 97: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 8

93

yajayo? Utaandaa jinsi utakavyoanza na kuhitimisha masomo hayo kwa malengo, na jinsi utakavyowasilisha malengo ya mafunzo”.

Wagawie washiriki Kitini cha 2. Waagize wajibu maswali. Baada ya dakika 15, waagize washirikishane mawazo yao kwa dakika 5. Ita jozi kadhaa zielezane mifano yao kwa darasa zima. Waagize washiriki wafanye mapitio ya kumbukumbu zao za masomo ya awali kuhusu mambo ambayo wanafunzi wanayapendelea (kutoka katika kazi ya 2). Waagize vikundi kuibua mawazo zaidi kuhusu jinsi watakavyotumia mafunzo yao. Jadili kwa dakika 5, kisha waagize washiriki kupeana mawazo. Waagize washiriki wachague moja ya mawazo kutoka kwenye mjadala wa kikundi (kazi ya 2) ili walijaribishe katika ufundishaji wao wiki ijayo.

“Je, kuna yeyote anayeweza kunieleza ni stadi ipi tumeijaribisha katika moduli hii?”

Pokea majibu kadhaa, ukihakikisha kuwa washiriki wanaongelea juu ya kuhitimisha somo, kufanya mapitio na kufanya majumuisho ya somo. Eleza kuwa tumefanya majaribio ya utendaji mzuri. Tumia sehemu ‘Taarifa’ mwanzoni mwa muduli hii, kueleza kwanini ni muhimu suala hili ni muhimu kwa ufundishaji mzuri. Wagawie washiriki Kitini cha 3. Kitini hiki kinatoa muhtasari wa mawazo makuu. Pendekeza washiriki watumie Kitini cha 3 kwa ajili ya ujifunzaji binafsi. Huu ni mwisho wa moduli hii. Mwezeshaji apime iwapo malengo ya moduli hii yamefikiwa.

Sema

Page 98: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Anza na hitimisha masomo kwa madhumuni

94

Viashiria vya mafanikio o Mwalimu anaweza kuanza somo kwa malengo, akiwa na madhumuni bayana ya somo

lililopo.

o Mwalimu anaweza kuandaa na kuwasilisha somo linalowashirikisha kikamilifu wanafunzi kwa sababu linaloendana na mazingira ya mwanafunzi na lina maana kwao.

o Mwalimu anahusisha somo lililopo na lililotangulia.

o Mwalimu anahitimisha somo kwa malengo kwa kufanya mapitio, kutoa muhtasari na kuhusisha somo lililopo na lijalo.

Mawazo kwa ajili ya uelekezaji Walimu wakuu na wakufunzi wanaweza kushudia madarasa ili kupima iwapo maarifa na ujuzi unatumiwa na walimu. Itafaa pia kuzungumza na wanafunzi kuhusu uzoefu wao kuhusu mwalimu husika, kupima iwapo wanafunzi wanafahamu malengo ya mafunzo, na iwapo wamehamasika kujifunza. Hili linaweza kufanyika kwa kutumia majadiliano ya vikundi-lengwa, na mwalimu husika anaweza kujumuishwa. Kisha, mwalimu mkuu au mwelekezaji anaweza kuzungumza na mwalimu na kumweleza mambo yaliyofanikiwa na kujadiliana masuala yanayohitaji maboresho zaidi.

Mawazo kwa ajili ya ujifunzaji wa pamoja/ binafsi • Walimu wanaweza kufanya mapitio ya maandalio ya somo na kuchunguza maeneo

yanayohitaji mabadiliko ili kuanza na kuhitimisha somo kwa malengo. • Katika ushuhudiaji wa kitaaluma, washuhudiaji wazingatie jinsi walimu wengine

wanavyoanza na kuhitimisha masomo. Walimu wanapaswa wajiulize: je, ninaweza kuiga au kutumia mbinu hizi katika masomo yangu?

• Walimu wanaweza kufanya mapitio ya Kitini cha 3 na kujikumbusha mawazo makuu. Kisha, wanaweza kuchagua stadi au mbinu moja wanayotaka kuifanyia kazi wiki ijayo.

Marejeleo Mwanzo vifuatavyo vimetumika kuandaa moduli hii:

• TiCCWG (2016) “Training Pack for Primary School Teachers in Crisis Contexts” Module 4 – Curriculum and planning. Teachers in Crisis Contexts Working Group. Linapatikana: www.ineesite.org/en/training-pack-for-primary-school-teachers-in-crisis-contexts

Page 99: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 8

95

Kitini cha 1: Kubainisha malengo ya mafunzo Maelekezo haya yanapaswa yaandikwe kwenye vipande vidogo va karatasi kabla kazi haijaanza.

Timu ya 1: Wanafunzi wataweza kuchora shule. Timu ya 2: Wanafunzi wataweza kuchora shule yenye uwanja wa michezo. Timu ya 3: Wanafunzi wataweza kuchora shule yenye wanafunzi wakicheza mpira wa miguu uwanjani. Timu ya 4: Wanafunzi wataweza kuchora shule yenye wanafunzi wakicheza mpira wa miguu uwanjani siku ya jua kali. Wanafunzi wataweza kubainisha mambo muhimu ya shule husika.

Page 100: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Anza na hitimisha masomo kwa madhumuni

96

Kitini cha 2: Kufanya ujifunzaji uwe wenye maana na unaohusianisha mazingira ya wanafunzi 1. Fikiria masomo matatu ukayofundisha wiki ijayo. 2. Kwa kila somo, fikiria mbinu mbili zitakayoyafanya masomo hayo yaanze na

kuhitimishwa vizuri na yawe shirikishi kwa wanafunzi wako.

3. Kama wanafunzi wako wanazungumza lugha tofauti, wana ulemavu, au wana mahitaji maalumu, ni mbinu gani zingine unazozifikiria ambazo zitasaidia kuwashirikisha?

4. Kwa kila somo, fikiria kuhusu jinsi utakavyowasilisha kwa wanafunzi wako wote malengo na madhumuni ya mafunzo.

5. Baada ya dakika 10, mshirikishe mwenzako mawazo yako.

6. Mweleze mwenzako mambo chanya mawili kuhusu mbinu zao. Waeleze jambo moja ambalo wanaweza kuliboresha zaidi.

Page 101: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 8

97

Kitini cha 3: Muhtasari wa vipengele vya mafunzo ya ujifunzaji binafsi Mwanzo wa somo Moja ya nyakati muhimu ambazo mwalimu huwasiliana na wanafunzi ni mwanzo kabisa wa somo. Huu ni wakati unaotumika kubainisha madhumuni ya somo, na pia ni wakati wa kuweka bayana malengo ya mafunzo. Tafiti zinaonesha kuwa kubainisha madhumuni na malengo ya somo na namna yanavyohushisha mazingira ya wanafunzi kunaboresha matokeo ya ujifunzaji kwa kuwahamaisha wanafunzi kujifunza. Kuhusisha mafunzo ya awali Sehemu nyingine muhimu ya mwanzo wa somo ni kuhusisha ujifunzaji na uzoefu wa ufundishaji wa awali, jambo linalofanya ujifunzaji kuwa wenye malengo na wa thamani. Bila hatua hii, kuna uwezekano finyu kwa wanafunzi kuhifadhi maarifa na ujuzi uliotokana na somo husika.

Kuwahamasisha wanafunzi Ujifunzaji hufanyika kikamilifu wanafunzi wanapojiamini, wanapokuwa na mtazamo chanya, na wanapohamasika. Japokuwa inaonekana ni jambo dhahiri, umuhimu wa kuweka mazingira kama haya hauwezi kupuuzwa. Walimu wanapowasilisha masomo kwa wanafunzi, huwasilisha pia ujumbe wa hamasa (kwa njia maneno, kazi, na jinsi somo linavyofundishwa). Wanafunzi husikiliza na kutumia muda, juhudi, na uvumilivu wanaopaswa kuweka katika mchakato wao wa ujifunzaji. Kwa kifupi, wanafunzi hupendelea kujifunza kikamilifu kutokana na somo linavyovutia na kusisimua. Walimu mahiri ni wale wanaotambua hamasa na hisia za wanafunzi wao. Hutambua wajibu wao wa kuwahamasisha kwa kuendana mtaala ili uvutie, uwe shirikishi, na unaohusika, na kwa kuwahamasisha wanafunzi. Hisia hasi – kama vile kukata tamaa – hukatisha mchakato wa ujifunzaji, jambo ambalo huweza kuzuia moja kwa moja ujifunzaji kufanyika.

Kuhitimisha somo Walimu wanaweza kutumia mwisho wa somo kufanya mapitio ya maudhui na uelewa wa wanafunzi na hatimaye kutoa muhtasari somo. Hatua hii huelekeza usikivu kwenye madhumuni makuu na matokeo ya somo kufikiwa. Muhtasari pia humpa mwalimu fursa ya kurudia uhusiano kati ya maudhui ya somo lililopo na maarifa mengine na uzoefu wa awali. Hatua hii huwezesha mchakato muhimu wa kifikra unaosaidia kuwezesha ujifunzaji wa wanafunzi na hivyo kuwaacha wanafunzi wakiwa na fikra chanya baada ya somo.

Page 102: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Fafanua somo

98

9. Elezea Somo

¹ Jumla ya saa 2

Malengo ya Moduli hii Kufikia mwisho wa moduli hii, washiriki wataweza:

• Kutumia maelezo kueleza maudhui ya somo ili kuongeza ushiriki na ujifunzaji wa wanafunzi (Eneo la 3 la NTCF)

Vifaa vinavyohitajika • Karatasi za chati • Peni • Ubao wenye maelekezo • Ubao wa chaki/mweupe

na Peni/chaki, kifutio • Vitini

Page 103: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 9

99

Taarifa za kuwapa washiriki katika moduli hii Namna maudhui ya somo yanavyoelezwa kwa wanafunzi ina athari kubwa kwa uelewa na uwezo wao wa kujifunza ujuzi. Wanafunzi hunufaishwa na maelezo rahisi na mafupi. Maelezo hayo ni matokeo ya mwalimu kutafakari na kuanda jinsi ya kuwasilisha ujumbe madhubuti. Maelezo yaliyoandaliwa vizuri na yanayotumia mifano, vifaa na/au maonesho hufanikisha sana ujifunzaji. Maneno yoyote mapya katika somo yanahitaji maelezo yanayoeleweka. Maelezo mazuri ya mwalimu yanategemea mambo yafuatayo: • Matumizi ya lugha inayoeleweka ambayo tayari wanafunzi wanaifahamu.

Wakati mwingine utahitaji kufafanua wazo kwa kutumia lugha-mama ya mwanafunzi na pia kuelezea kwa Kiswahili. Hatua hii itarahisishia sana wanafunzi kuelewa. Wataweza pia kukuza zaidi stadi zao za Kiswahili;

• Kumudu maudhui ya somo;

• Maudhui ya somo yaliyotolewa kwa hatua zilizopangika badala ya maudhui yote kwa mkupuo;

• Uelewa wa mambo ambayo wanafunzi wako tayari wanayafahamu kuhusu mada (rejea pia moduli inayoitwa ‘Anza na hitimisha masomo kwa malengo’).

• Matumizi ya mifano au maonesho yanayokumbukika na yanayohusiana na mada;

• Kuendelea kuuliza maswali ili kupima uelewa wa wanafunzi;

• Kuwashirikisha kikamilifu wanafunzi wote.

Watoto hujifunza kwa namna tofautitofauti na wanambinu mbalimbali za kujifunza. Baadhi ya watoto hujifunza vizuri zaidi kwa kutumia zana zinazoonekana kama vile vielelezo, maneno kwenye ukurasa, au kutazama picha. Wengine hujifunza vizuri zaidi kwa kusikiliza. Mara nyingi watoto hujifunza vizuri zaidi kwa ‘kutenda’, kama kazi zimeelezwa na kutekelezwa vizuri. Walimu wanaweza kutumia maelezo ili kuendana na mbinu hizi mbalimbali. Aidha, wanaweza kutumia njia mchanganyiko ili kuwasilisha masomo. Kuna uwezekano mkubwa kwa hatua hizi kuboresha uzoefu wa kielimu na ujifunzaji wa wanafunzi wote darasani. Ni muhimu kwa mwalimu kufuatilia iwapo wanafunzi wanaelewa maelekezo, maagizo, ufafanuzi, na maelezo. Hili linaweza kufanywa kwa namna mbalimbali na itamsaidia mwalimu kuboresha jinsi ya kuelezea dhana, maarifa, ujuzi tofautitofauti, na kutoa maelekezo.

Kazi za kufanya 1. Maelezo yanahitaji vielelezo ¹ Dakika 50

Lengo la kazi hii ni kuonesha jinsi maelezo yanavyoweza kutolewa vizuri zaidi kwa wanafunzi wote darasani. Waagize washiriki kufanya kazi katika jozi.

Page 104: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Fafanua somo

100

“Leo tutajifunza jinsi ya kufunga aina mahususi ya kifundo kwa kutumia vipande vya uzi. Nitawaelezeeni jinsi ya kufunga na kisha kila jozi itajaribu kufunga kifundo chake”. Mwalimu anaweza kutumia zana za kufundishia ili kuwaonesha wanafunzi jinsi ya kufanya.

Kwanza, shika kipande cha uzi na kizungushe kwenye nguzo iliyosimama wima (kama vile mguu wa kiti au meza). Upande wa kulia wa uzi uwe na kitanzi. Kisha, shika kipande sehemu ambayo uzi unapishana katika kitanzi kati ya dolegumba na kidole cha shahada. Kisha shika kitanzi kiubapa. Baada ya hapo, chukua chukua kipande cha upande wa kulia na kipitishe juu kwenye kitanzi. Kisha, kipitishe kipande hichohicho chini ya kipande nyoofu karibu na kitanzi na kisha katikati ya kitanzi. Mwisho, shika vipande vyote viwili kwa mkono mmoja na sukuma kifundo kuelekea juu ya nguzo iliyosimama wima (au mguu wa meza au kiti – kama ndiyo unaotumia). Sasa utakuwa umefanikiwa kufunga kifundo”. Toa maelekezo kwa mdomo tu. Usioneshe kwa kutumia zana. Gawa vipande vya Kamba/uzi na waagize washiriki wafunge kifungo. Usirudie maelekezo au kusaidia. Waache wajaribu kwa dakika kadhaa na kisha waulize:

• Je, kazi hii ni rahisi au ngumu?

• Kwanini?

Sampuli ya majibu Ilikuwa ngumu kwa sababu: • Haikuwezekana kukumbuka orodha ndefu ya maelekezo. • Hatukushuhudia wakati kifundo kikifungwa. • Hatukuwa na uzi wa kujaribia wakati mwalimu akielezea. • Maelekezo magumu yalitolewa kama ‘mhadhara’ bila kuonesha vitendo..

Uliza: • Je, mwalimu alitumia lugha inayoeleweka? Ndiyo/Hapana • Kama mwalimu angetumia lugha tofauti kuelezea, je, tungeelewa (mathalani,

kwa kutumia lugha ya viungo vya mwili)? Ndiyo/Hapana • Je, mwalimu alikuwa na maarifa ya kutosha ya somo? Ndiyo/Hapana

• Je, mwalimu alielezea hatua kwa hatua jinsi ya kufunga kifundo? Ndiyo/ Hapana

• Je, mwalimu alipima ili kujua iwapo tayari mlikuwa mnajua jinsi ya kufunga kifundo? Ndiyo/Hapana

• Je, mwalimu alionesha kwa vitendo jinsi ya kufunga kifundo? Ndiyo/Hapana • Je, mwalimu alipima ili kujua iwapo mlikuwa mnaelewa au la? Ndiyo/Hapana • Je, mwalimu aliwashirikisha kwa vitendo katika kujifunza jinsi ya kufunga

kifundo? Ndiyo/Hapana

Sema

Page 105: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 9

101

Uliza: Kwa kazi hii, ni mambo gani yangeleta tofauti kubwa kwa ujifunzaji wa wanafunzi? Yaorodheshe kwenye chati. Mapendekezo Kwa mafunzo madhubuti, mwalimu angeweza: • Kuanzisha mada na kisha kuwaagiza wanafunzi wasikilize na waangalie; • Kutumia lugha inayoeleweka na rahisi kuelezea jinsi ya kufunga kifundo; • Kuandika ubaoni maelekezo ya jinsi ya kufunga kifundo; • Kuonesha jinsi ya kufunga kifundo wakati akielezea; • Kuelezea hatua ya kwanza kwa kuonesha, na kisha kuwaacha wanafunzi wafanye

mazoezi; • Kuelezea hatua ya pili kwa kuonesha, na kisha kuwaacha wanafunzi wafanye

mazoezi; • Kusisitiza/kurudia vipengele ambavyo mwalimu aliona wanafunzi walikabiliana na

ugumu; • Kuwaruhusu wanafunzi wafanye mazoezi ya kufunga kifundo katika vikundi; • Kutembelea vikundi ili kuona maendeleo na kutoa msaada pale inapolazimu.

Wagawie washiriki Kitini cha 1 na kipitie kwa pamoja.

2. Njia bora za kuboresha maelezo yetu ¹ Dakika 70

Lengo la kazi hii ni kumwezesha mwalimu kuwa na namna bora ya kutoa maelezo. Uliza: Iwapo mwalimu amekuwa akieleza kwanini mgogoro au vita ilizuka katika nchi jirani, ikiwa ni sehemu ya historia ya somo; ni vipengele gani vya orodha hakiki ya Ndiyo/Hapana vilivyotumika katika kazi ya awali vinaweza kuwa muhimu zaidi? Je, kuna chochote unachoweza kuongeza (mfano, matumizi ya picha au michoro, vielelezo, mfululizo wa matukio, hadithi binafsi ya shujaa fulani)?

“Kujifunza jinsi ya kufanya jambo au kujifunza ujuzi maalumu kunategemea uoneshaji mzuri. Uoneshaji mzuri unagawa ujuzi katika hatua mbalimbali. Mwalimu hupima ili kufahamu iwapo wanafunzi wamemudu kila hatua kabla ya kuendelea na hatua inayofuata. Maudhui ya somo yanakuwa na maana kutegemeana na njia uliyochagua kuyaelezea”.

Wagawe washiriki katika vikundi na kipe kila kikundi maswali kama ifuatavyo:

Kikundi cha 1

Kama mwalimu aliuliza na baadhi ya wanafunzi wakajibu kuwa tayari wanajua jinsi ya kufunga kifundo, mwalimu afanye nini?

Waagize wanafunzi husika watulie wkati ukielezea na kuonesha. Kisha, watumie wanafunzi hawa wakishirikiana na wanafunzi wengine kuonesha na kuwasaidia kufanya mazoezi.

Sema

Page 106: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Fafanua somo

102

Kikundi cha 2

Mwalimu anaweza kufanya au kusema nini ili kuendelea kupima iwapo wanafunzi wanafuatilia somo au la?

Waagize wanafunzi kurudia maelekezo. Uliza iwapo kila mmoja anaelewa. Wahakikishie kuwa wanaweza kuuliza maswali iwapo hawaelewi au wamechanganyikiwa.

Kikundi cha 3

Je, mwalimu anawezaje kuwashirikisha zaidi wanafunzi ili kusaidia ufafanuzi?

Tumia onesho na waruhusu wanafunzi kufanya mazoezi iwapo ujuzi/stadi zinafundishwa. Wagawe wanafunzi kwenye jozi na mwagize mmoja wao aeleze/arudie kazi husika mbele ya wengine. Tumia ujuzi wa mwalimu kuhusu mitindo/mbinu za ujifunzaji za wanafunzi kuchagulia njia husika.

Kikundi cha 4

Mwalimu anaweza kufanya nini kuifanya lugha inayotumika darasani ieleweke?

Fundisha kwanza maneno yoyote mapya kwa lugha-mama ya wanafunzi. Fanya mazoezi na kisha anza na tumia maneno mapya katika lugha yoyote ya pili, ambayo ni muhimu kwa shule. Kama inafaa, katika lugha-mama na lugha ya pili, tumia maneno yaleyale kote katika somo ili kuepusha kuwachanganya wanafunzi. Rahisisha na fupisha.

Vikundi vijipange (kwa dakika 10) kisha vifanye mazoezi (dakika 10) ya kuelezea jinsi ya kufunga kifundo kwa kutumia marifa waliyojifunza katika moduli hii. Kila kikundi kipange pamoja, na kisha mshiriki mmoja awe mwalimu. Kikundi cha 1 kiwafundishe Kikundi cha 2 (Kikundi cha 3 na 4 kishuhudie na kijaze katika Orodha hakiki ya Ndiyo/Hapana). Kikundi cha 3 kiwafundishe Kikundi cha 4 (Kikundi cha 1 na 2 washuhudie na wajaze kwenye orodha hakiki). Kama kuna muda wa kutosha, kiagize pia Kikundi cha 2 kiwafundishe Kikundi cha 1, na Kikundi cha 4 kiwafundishe Kikundi cha 3. Kikundi kinachoshuhudia kitumie Orodha hakiki ya Ndiyo/Hapana (Kitini cha 2) kitoe mrejesho kwa kuzingatia sehemu ya maoni katika orodha hakiki.

“Kutumia matendo mablimbali, kama yale yaliyooneshwa katika moduli hii, kunaweza kuwasaidia walimu kuelezea vizuri masomo. Si lazima kutumia matendo yote haya kila wakati. Chagua matendo yatakayosaidia zaidi kuwasilisha ujumbe”.

Sema

Page 107: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Moduli ya 9

103

Hii ni kwa sababu: • Watoto hujifunza kwa namna tofautitofauti; • Mitindo/mbinu mbalimbali humwezesha kila mwanafunzi kujifunza kwa namna

ambayo inayofaa zaidi kwake; • Ujifunzaji hai ni njia muhimu ili watu waweze kujifunza na kutumia ujuzi mpya; • Maelezo ya mdomo peke yake hayatoshi. Yanapaswa yasaidiwe na mbinu

zingine; • Huepusha somo kuchosha na badala yake huleta ‘kasi’ darasani.

Rejea: moduli inayoitwa ‘Tumia kazi ili kufahamu zaidi kuhusu kazi za kusaidia ujifunzaji; moduli inayoitwa ‘Tumia jozi au vikundi’ kufahamu zaidi kuhusu kufanya kazi katika jozi na vikundi.

Huu ni mwisho wa moduli hii. Mwezeshaji apime ili kujua iwapo malengo ya moduli yamefikiwa.

Viashiria vya mafanikio o Mwalimu anaweza kueleza kwanini ni muhimu kutumia mbinu mbalimbali za

kufafanua jambo.

o Mwalimu anaweza kuonesha jinsi ufafanuzi unavyoweza kusaidiwa ili kuwa na ufundishaji na ujifunzaji madhubuti.

o Mwalimu anaweza kutumia mbinu mbalimbali ili kusaidia ufafanuzi wa maelekezo na maudhui ya somo.

Mawazo kwa ajili ya uelekezaji Mwalimu mkuu au mwelekezaji anaweza kutekeleza usimamizi wa ufuatiliaji ili kuwasaidia walimu kukamilisha ufafanuzi wao wa masomo kwa kutumia orodha hakiki. Wanaweza kushuhudia somo na kisha kutoa mrejesho kwa kutumia orodha hakiki.

Mawazo kwa ajili ya ujifunzaji wa pamoja/ binafsi • Walimu wanaweza kushuhudia mafunzo rika, ili wazoee kutumia njia hizi na

kuzifahamu baada ya muda fulani.

• Walimu wakuu au wakufunzi wanaweza kuwapa walimu fursa ya kujadili changamoto na mafanikio ili kuwasaidia kukuza stadi/ujuzi ili waziongeze kupitia majaribio, makosa, na ujifunzaji.

• Walimu wanaweza kutafakari kuhusu mazoezi yao na kisha kuchukua maelezo ya matendo ili kuufanya ufafanuzi uwe wa kueleweka zaidi.

Uzingatiaji wa masuala ya jinsia Chunguza ili kufahamu iwapo wavulana na wasichana wanafuatilia somo na kwamba wote wanashiriki. Kama ni lazima, vipange upya vikundi au kazi ili

Page 108: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Fafanua somo

104

kuongeza ushiriki. Hakikisha kuwa maonesho na mifano inawahusu na inawavutia wanafunzi wote darasani.

Marejeleo • Schleicher, A. (mhariri) (2012) “Preparing teachers and developing school leaders

for the 21st century: Lessons from around the world”, OECD Publishing. Linapatikana: http://www.oecd.org/site/eduistp2012/49850576.pdf

• TiCCWG (2016) “Training Pack for Primary School Teachers in Crisis Contexts” Module 3: Pedagogy. Teachers in Crisis Contexts Working Group. Linapatikana: www.ineesite.org/en/training-pack-for-primary-school-teachers-in-crisis-contexts

Page 109: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Module 9

105

Kitini cha 1

Njia ya Ufafanuzi Manufaa Hasara

Mwalimu huelezea tu jinsi ya kufunga kifundo (jinsi ya kufanya jambo

(hufafanua, hutoa mhadhara)

• Huhitaji maandalizi na muda mfupi. • Huwezi kuwa mbadala salama zaidi kwa

mwalimu iwapo hana uhakika na nyenzo za kufundishia.

• Hakuna njia ya kufahamu iwapo wanafunzi wote wameelewa au wanasikiliza.

• Hakuna fursa kwa wanafunzi kufanyia mazoezi au kujifunza haswa maarifa husika.

• Hakuna hatua ya taarifa itakayokuwa rahisi kuielewa.

• Wanafunzi wasiozungumza vizuri lugha inayotumika hawataelewa.

• Wanafunzi wanaweza kuona somo halivutii.

Mwalimu huonesha kwa kutumia kipande cha uzi wakati akielezea.

• Huchangamsha mada, husaidia wanafunzi kuelewa taarifa mpya.

• Husaidia watoto wasiozungumza lugha moja kuelewa vizuri zaidi.

• Hufanya mada iwe na maana na shirikishi.

• Wanafunzi watahitaji muda wa kujaribu bila kunakili kutoka kwa mwalimu ili kuhakikisha kuwa wanaweza kutumia ujuzi wao wenyewe.

Mwalimu huandika maelezo ubaoni na kisha anawaacha wanafunzi wajaribu kufunga kifundo.

• Hutoa fursa ya wanafunzi kujifunza kwa kujaribu, njia ambayo inayoweza kusaidia wapate maarifa.

• Wanafunzi wanashirikishwa kwenye ujifunzaji wao

• Inaweza kuwa ngumu kwa baadhi ya wanafunzi bila msaada wa ziada kama vile kuonesha vitu dhahiri.

• Wanafunzi wengine wanaweza wasielewe maudhui, na hivyo kuachwa nyuma katika ujifunzaji.

Mwalimu huwagawa washiriki katika vikundi au jozi.

• Huwezesha wanafunzi kutatua matatizo wakishirikiana na wenzao na hivyo kukuza stadi za kijamii/mawasiliano. Wanafuni wanweza wasiwe na hofu ya kukosea

• Huweza kuwa na kelele na ngumu kudhibiti tabia.

• Wanafunzi wasioelewa wanaweza wasionekane kwa sababu ya kikundi kinachowazunguka.

Page 110: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Fafanua somo

106

na hivyo kuweza kufanya vizuri kwenye kikundi. Wanafunzi ambao hawazungumzi lugha anayozungumza mwalimu, wanaweza kuzungumza lugha yao ili kupata ufumbuzi wa tatizo husika.

• Ujifunzaji hai

• Wanafunzi wengine wanaweza kufanya kazi kubwa zaidi ya wengine.

1. Mwalimu huonesha kwa vitendo, kisha hurudia tena huku akitumia lugha-mama ya wanafunzi. Kama kuna mwanafunzi mwenye ulemavu wa macho, mwalimu anahakikisha kuwa anagusa uzi katika kila hatua. Kama kuna mwanafunzi mwenye

ulemavu wa kusikia, mwalimu awaagize wanafunzi wengine wamwandikie jambo linalosemwa.

2. Mwalimu amwagize mwanafunzi aoneshe, na kisha aliagize darasa zima lijadili umadhubuti na udhaifu kuhusu jambo lililooneshwa na mwanafunzi.

3. Mwalimu aandike maelekezo na michoro ubaoni. Kama kuna maneno mapya ya lugha-mama au lugha ya pili ya wanafunzi, mwalimu ayatambulishe na yafanyiwe mazoezi.

4. Mwalimu aziagize jozi au vikundi vya wanafunzi kufanya kazi kwa kufuata maelekezo.

• Wanafunzi wenye mitindo/mbinu na historia tofauti za ujifunzaji wanashirikishwa na wanapata fursa nyingi za kujenga na kufanyia mazoezi ujuzi na maarifa yanayohitajika.

• Huchukua muda mwingi – lakini wanafunzi wengi watapata maarifa yanayotakiwa, ikiwa na maana kwamba hutumia muda mchache ili kuelewa au kufanya marudio wakati ujao.

Page 111: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Module 9

107

Kitini cha 2: Orodha hakiki Vigezo Ndiyo Hapana Maoni

Kila inapowezekana, mwalimu anatumia lugha inayoeleweka na

ambayo wanafunzi tayari wanaifahamu.

Maelezo si marefu sana, bali ni mafupi na yanayoeleweka

Mwalimu anaonesha ujuziwa somo husika

Mwalimu anaelezea somo kwa hatua, badala ya kuelezea

maarifa yote kwa wakati mmoja

Mwalimu hupima maarifa ambayo wanafunzi tayari wanayo

Mwalimu anazingatia mbinu/mitindo tofautitofauti ya ujifunzaji na mahitaji mbalimbali ya wanafunzi

Mwalimu anatumia maonesho wakati wa kufundisha

Mwalimu anatumia zana zinazoonekana na zinazoshikika kuongezea ufafanuzi

Mwalimu hupima ili kujua iwapo wanafunzi wanafuatilia mafunzo

au la

Mwalimu huwashirikisha wanafunzi kikamilifu

Mwalimu huchagua mbinu mbinu zinazofaa zaidi kwa ajili ya

maudhui husika

Mwalimu huanzisha na kufanyia mazoezi lugha ya mama na ya

pili inayohusiana na maudhui

Page 112: Misingi ya Ufundishaji Nchini Tanzania - static.miraheze.org · Matini hii imechukuliwa kutoka zana za Creative Commons, The Foundations of Teaching, Linapatikana katika anuani ya

Fafanua somo

108