36
1 JAMHURI YA RWANDA WIZARA YA ELIMU TAASISI YA TAIFA YA UKUZAJI MITAALA S.L.P 608 KIGALI MUHTASARI WA SOMO LA KISWAHILI KIDATO CHA 4- 6 2010

MUHTASARI WA SOMO LA KISWAHILI KIDATO CHA 4- 6gssbsave.org/IMG/pdf/kiswahilialevel-3.pdf7 3. NGELI ZA MAJINA . Kuainisha ngeli za majina kwa njia ya kimofolojia Mwanafunzi aweze :

Embed Size (px)

Citation preview

1

JAMHURI YA RWANDA

WIZARA YA ELIMU TAASISI YA TAIFA YA UKUZAJI MITAALA

S.L.P 608 KIGALI

MUHTASARI WA SOMO LA KISWAHILI KIDATO CHA 4- 6

2010

2

UTANGULIZI Kiswahili ni lugha yenye asili ya kibantu ambayo hadi sasa imepiga hatua kimatumizi. Ki-sarufi , Ki-msamiati na yenye kutumiwa na jamii mbalimbali barani Afrika na ulimwengu kwa ujumla .Jamii ya Wanyarwanda imezungukwa na jamii nyingine zinazozungumza lugha ya Kiswahili, kwa hiyo inahitaji kufanya mawasiliano katika fani mbalimbali hususani Kisiasa , Kiuchumi na Kijamii.Mhutasari huu unawalenga wanafunzi wa mkondo wa lugha kwa miaka mitatu, yaani kidato nne, tano, na sita . Ili kumsaidia mwalimu kufundisha vizuri somo la Kiswahili, mhutasari huu umegawanyika Ki-vidato kwa kila kidato zimependekezwa mada zitakazofundishwa . Pia vitabu vya kiada kwa mwalimu na mwanafunzi vimeonyeshwa. Vilevle malengo mahsusi, njia za ufundishaji na kujifunzia , tathmini na vitabu vya rejea vimeonyeshwa . Jambo la kukumbukwa ni kwamba njia zilizowekwa katika mhutasari huu ni mapendekezo tu . Mwalimu anatazamiwa kutumia ujuzi wa ubunifu wake katika kutumia njia nyingine mbalimbali, vifaa pamoja na vitabu vya ziada.

3

MWONGOZO Lugha ya kiswahili kama tulivyosema katika utangulizi ni lugha iliyo na asili ya kibantu ambayo Kinyarwanda ni mojawapo ya lugha hizo.Kwa maana hiyo lugha hii tunatarajia haitakuwa ngumu au ngeni sana katika masikio ya Wanafunzi wetu wanaokusudia kujifunza lugha hiii , mathalani katika Kiswahili kuna maneno kama vile : mtu - umuntu mbwa - imbwa sahani - isahani Kwa hiyo kuna upatanisho wa ki-sarufi ambao hauko mbali sana na wa Kinyarwanda . Mwongozo huu pia umelenga kwenye matakwa na mahitaji ya nchi yetu katika kumjenga Mwanafunzi ili aweze kuisaidia jamii katika kukabiliana na matatizo mbalimbali, kwa mfano kujilinda na magonjwa yanayotokanayo na zinaa na ukimwi. Lugha hii ,itamsaidia mwanafunzi kupanua mawazo yake katika kuwasiliana na watu wengine kutoka jamii mbalimbali hivyo kuelewa maisha utamaduni na mambo mbalimbali yanayoweza kumsaidia yeye na jamii kwa ujumla , hivyo kumjengea tabia ya kuwa na heshima ,uvumilivu, upendo,amani, haki umoja na mshikamano pia demokrasia. Vilevile ataweza kujenga tabia ya kujiamini , kuwa huru katika kutoa mawazo yake hivyo kutambua kuwa ana wajibu wa kuheshimu haki za binadamu wengine na kuzingatia utu wa mtu. Mwanafunzi huyu pia anatarajiwa kuwa na mawazo ya kuondokana na ubaguzi wa aina yoyote,uwe wa Ki-kabila , Ki-dini, Ki-jinsia nk.

4

Mwalimu anashauriwa kuchunguza yale ambayo yanafanana katika lugha mbili ili aweze kuyafundisha kwa urahisi Ni matumaini yetu kuwa haya yote yatazingatiwa katika mhutasari huu. MADHUMUNI KUFUNDISHA KISWAHILI KWA UJUMLA 1 Kumjengea Mwalimu msingi bora wa kutumia lugha hii na kuweza kuendelea na elimu ya

juu.kutumia lugha hii na kuendelea na elimu ya juu . 2. Kumpa mwanafunzi uwezo wa kutumia lugha ya kiswahili katika shughuli mbalimbali za

Kitaifa na Kimataifa . 3. Kumtayarisha mwanafunzi ili awe mjenzi bora wa lugha ya Kiswahili . 4. Kusaidia kukuza uwezo wa mwanafunzi katika kuongeea lugha hii na kuweza kuitumia

muda wote katika shughuli za ujenzi wa taifa . 5. Kukuza uwezo wa Mwanafunzi katika kujisomea na kuelewa mambo.mbalimbali yaliyomo

katika lugha ya kiswahili.

5

KIDATO CHA NNE

MADA KUU

MADA NDOGO

MADHUMUNI MAHSUSI

1. HISTORIA YA KISWAHILI

Asili ya Kiswahili Uhusiano wake na lugha za Kibantu na lugha za kigeni Lugha za kigeni Mfano : 1. Kiarabu Kiswahili Swalah Sala Khabar Habari 2 Kireno Kiswahili Mesa Meza 3. Kihindi Kiswahili Paisa pesa

Mwanafunzi aweze: Kueleza asili au chimbuko la Kiswahili na uhusiano wake na lugha za kigeni na kibantu akizingatia msamiati Lugha za kibantu Kinyarwanda Kiswahili Igiti Mti Umuntu Mtu Arandika Anaandika

6

4. Kijeruman i Kiswahili Schule shule 5.Kiingereza Kiswahil i Bicycle Baiskeli Kusaambaa na kuenea kwa lugha ya Kiswahili

Kusambaa na kuenea kwa Kiswahili Afrika ya Mashariki na kati.

2. FASIHI

Nadharia ya Fasihi - Fasihi Simulizi - Fasihi Andishi

Mwanafunzi aweze : Kufafanua - Nadharia ya Fasihi - Tanzu za Fasihi Simulizi na -Fasihi Andishi .

7

3. NGELI ZA MAJINA .

Kuainisha ngeli za majina kwa njia ya kimofolojia

Mwanafunzi aweze : Kutumia ngeli za majina kwa njia ya kimofolojia katika sentensi. Mfano 1) mu—mutoto = mtoto 2) aw-wa-toto = watoto 3) mu-mu-ti = mti 4) mi-mi-ti = miti 5) ji-ji—no = jino 6) kasha = kasha 7) m-ma-kasha = makasha 8) ki-ki-su = kisu 9) vi-vi-su = visu 10) n-guo = nguo 11)u-u-fa = ufa 12) ku-ku-imba = kuimba

4. USEMI ASILI NA

USEMI WA TAARIFA

Maana ya usemi wa asili

Mwanafunzi aweze : Kutaja usemi wa asili Mifano:

8

Usemi wa taarifa

`` Utanikuta nyumbani`` Ishimwe alimwambia rafiki yake.

Kutaja usemi wa taarifa Mfano : Ishimwe alimwambia

rafiki yake kuwa angelimkuta nyumbani

5. UTUNGAJI

Insha za wasifu Bendrea yetu, viongozi wetu

Mwanafunzi aweze : Kufafanua , kutunga insha za wasifu kulingana na jinsi atakavyoulizwa na mwalimu

6. AINA ZA MANENO

NOMINO VIWAKILISHI VIVUMISHI VITENZI VIELEZI VIUNGANISHI VIHISISHI

Mwanafunzi aweze: Kutambua na kutumia aina zote za maneno katika tungo mbalimbali .

9

KIDATO CHA TANO MADA KUU

MADA NDOGO

MADHUMUNI MAHSUSI

1. FASIHI

Fasihi Simulizi Fasihi Andishi Tofauti kati ya Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi

Mwanafunzi aweze kueleza : Tanzu za Fasihi simulizi na tanzu za fasihi andishi ambazo ni :

• Vitendawili • Hadithi • Methali • Nahau • Nyimbo • Tamathari za usemi • Hadithi fupi • N.K

2. TAMATHARI ZA

USEMI Tamathari za usemi na maana yake Tashibiha Sitiari

Mwanafunzi aweze: Kueleza tamathari za usemi zilizotumiwa katika kazi za fasihi

10

Kejeli Tasfida Dhihaka Takriri N.K

mbalimbali

3. MATUMIZI YA

LUGHA YA KISWAHILI

Rejesita mbalimbali

Mwanafunzi aweze: Kutaja na kueleza rejesita mbalimbali za Kiswahili zinazotumiwa katika mazingira mbalimbali kama , hotelini, mahakamani n.k

4. MNYAMBULIKO WA VITENZI

Kunyambua vitenzi

Mwanafunzi aweze : Kuonyesha viambishi vinavyounda kitenzi Mfano : analima-a-na-lim-a a =kiambishi kipatanishi au cha nafsi na=kiambishi awali cha wakati lim=mzizi a=kiambishi tamati

11

5. UHAKIKI 6. UFUPISHO

Maana na aina za uhakiki Umuhimu wa uhakiki Jinsi ya kufanya uhakiki Sifa za uhakiki Matatizo ya uhakiki Kufupisha kazi ya Fasihi

Mwanafunzi aweze: Kueleza maana ya uhakiki Kutaja aina za uhakiki Kuhakiki kazi mbalimbali za Fasihi Kutaja sifa , umuhimu na matatizo ya uhakiki Mwanafunzi aweze: Kueleza maana ya ufupisho Kufupisha kazi alizopewa

7. HOTUBA Maana ya hotuba Sifa za hotuba Aina za hotuba Muundo wa hotuba

Mwanafunzi aweze : Kutaja na kueleza maana ya hotuba ,aina za hotuba , muundo wa hotuba na kutunga hotuba za aina mbalimbali akifuata muundo uliokubalika.

12

8. AINA ZA TUNGO

Kuainisha tungo za Kiswahili

Mwanafunzi aweze: Kutaja , kueleza na kutunga aina mbalimbali za tungo Mfano : Tungo Sahili Tungo tegemezi Tungo amabatano Tungo changamano Tungo nyofu Tungo tata n.k

9. SARUFI MIUNDO

Kupambanua /Kuchanganua tungo

Mwanafunzi aweze: Kupambanua /Kuchanganua tungo kwa njia zifuatazo: Njia ya maneno Njia ya visanduku Njia ya matawi

10. UTUNGAJI • Utungaji wa barua mbalmbali

• Barua za kikazi, biashara, mwaliko, gazetini

Mwanafunzi aweze: Kutunga aina mbalimbali za barua Mfano Barua za kikazi,biashara mwaliko, gazetini

13

KIDATO CHA SITA

1. FASIHI

Riwaya Tamthiliya Majigambo Ushairi

Mwanafunzi aweze : Kuchambua kazi mbalimbali za Fasihi andishi akizingatia fani na maudhui

2. FASIHI SIMULIZI

Ngonjera Tenzi Majigambo Hadithi

Mwanafunzi aweze: Kuchambua kazi mbalimbali za Fasihi Simulizi akizingatia fani na maudhui

3. MNYAMBULIKO WA VITENZI

1. Dhana ya kitenzi 2. Aina za kitenzi - Halisi - Kishirikishi 3. Viambishi awali vya kitenzi

-Viambishi vya kukanusha -Viambishi vya hali

Mwanafunzi aweze : Kutaja aina za vitenzi Kutaja aina mbalimbali za viambishi Kutofautisha viambishi katika vitenzi Mfano Kitenzi halisi Anaimba Alikuwa anaimba Kitenzi kishirikishi

14

-Viambishi vya masharti -Viambishi vipatanishi -Viambishi rejeshi -Viambishi yambwa

4. Viambishi tamati vya kitenzi Huwekwa baada ya mzizi katika kitenzi Viambishi vya kauli Viambishi vya vimalizio vya kitenzi Viambishi viulizi

Dalili ya mvua ni mawingu Amekwenda kuitwa Viambishi vya kukanusha Siimbi Asiandike Hatumwoni Viambishi vya wakati na-li-ta Ninaandika Uliandika Ataandika Viambishi vya hali Hali ya kuendelea Anaandika Hali timilifu Nimeandika Hali ya mazoea Yeye hupenda masomo Hali ya mfululizo

15

Nilikwenda sokoni nikanunua ndizi Alikuwa aki ja hapa kila jioni Viambishi vya mashariti Ungemwona ungempenda Viambishi vipatanishi Analima Mti umeanguka Viambishi rejeshi Kikulacho ki nguoni mwako Wanaolima sana wamezawadiwa Viambishi vya yambwa Yambwa tendwa Anakupenda Yambwa tendewa Ali niandikia Viambishi vya kauli

16

-an- wanapendana wa-na-pend-ana --ish-a-anaimbisha a-na-imbisha --am Zimwi limefichama li-me-fi-cha-ma mlango umefungika u-me-fu-ngi-ka Viambishi vimalizio vya kitenzi -a- kujenga ku-je-ng-a anaandika –a-na-andika i-hatuandiki ha-tu-andik-i e-usiandike –u-si-andik-e eni-/ni twendeni –tu-ende-ni njooni njoo-ni Kiambishi cha uelezi Je ? ulifikaje u-li-fika-je

4. UAMBISHAJI WA VITENZI

Viambishi awali na viambishi tamati vya

Mwanafuni aweze : Kuongeza viambishi mbalimbali

17

kitenzi kwenye mizizi ya vitenzi ili kuvipa maana mpya Mfano : Tend Anatenda Inatendeka Wanatendana

5. UAMBISHAJI WA MANENO YA KISWAHILI

Uundaji wa maneno ya kiswahili

Mwanafunzi aweze : Kueleza maana ya uambishaji Kuunda na kunyambua maneno fulani kutoka maneno mengine Mfano : Dhana ya udogo Mtoto –kitoto,—mto-kijito,kitanda-kijitanda Dhana ya ukubwa Kikapu –kapu,mtu-jitu,jamvi-jamvi Dhana ya dhahania

18

Mtoto –utoto ,mjane-ujane Uambishaji wa majina toka vivumishi baya-ubaya-,uerevu-mwerevu Uambishaji wa vitenzi kutoka majina : Kucheza-mchezaji,kulipa-malipo Kusema-usemi, kula-mlo Kutulia –utulivu, adabu – kuadibika Kuumba-kiumbe Uambishaji wa vitenzi kutoka vivumishi: bora-kuboresha refu-kurefusha nene-kunenepa Uambishaji wa vitenzi kutoka vielezi zaidi---kuzidi karibu---kukaribisha

19

sawa—kusawazisha haraka----kuharakisha Uambishaji wa vielezi kutoka majina: Mzungu---kizungu(amevaa kizungu) Mtoto----kitoto (anacheza kitoto) Uambishaji wa vielezi kutoka vivumishi zuri----vizuri ema---vema kali---vikali

6.UTUNGAJI

Risala

Mwanafunzi aweze: Kueleza yafuatayo : • Maana ya risala • Aina za risala • Muundo /uumbo la risala • Anayepaswa kusoma risala • Sehemu na mahali inakopaswa

kusomwa • Kutunga risala Mwanafunzi aweze :

20

Hotuba Kueleza Maana ya hotuba Sifa za hotuba nzuri Aina za hotuba Ushirikiano na hadhira Muundo / umbo la hotuba Kutunga hotuba Anayepaswa kusoma hotuba Fundisho muhimu wakati wa kutoa hotuba Umuhimu wa kusema ukweli Kujali hadhira Mahali na hali ya hewa Hotuba husomwa na nani au husemwa . na nani? Fundisho muhimu wakati wa kutoa hotuba Umuhimu wa kusema ukweli. Kujali hadhira Mahali na hali ya hewa

21

NJIA ZA UFUNDISHAJI Kiswahili ni lugha yenye asili ya lugha za kibantu, hivyo ni lugha ambayo inaweza kueleweka upesi ikifundishwa vizuri kwa vile wanafunzi wamezoea kuisikia ingawaje hawaielewi.Ni lugha iliyo na upatanisho wa kisarufi ulio karibu na lugha ya Kinyarwanda Mfano : Kiswahili Kinyarwanda Shati ishati Mtoto analia umwana ararira Njia za ufundishaji wa somo hili ni nyingi sana kulingana na fani inayofundishwa lakini kuna njia ambayo inaweza kujumuisha fani zote (Structro Global Methods ).,Kwa mfano mwalimu akiwa anafundisha ufahamu wakati huo anaweza kufundisha MSAMIATI,METHALI,NAHAU n.k . Hata hivyo kuna njia ambazo Mwalimu anaweza kutumia anapofundisha nyanja tofauti za lugha , hususani sarufi ambazo ndizo nyanja kuu za lugha yoyote ile. Ili kurahisishia Mwalimu na kumwonyesha jinsi anavyoweza kulikabili na kulifanikisha somo lake .hapa tumeonyesha mbinu mbalimbali za ufundishaji wa lugha hii.

22

MAZUMGUMZO Zoezi la mazungumzo linalenga kumpa uwezo mwanafunzi kutumia lugha ya Kiswahili kwa ufasaha katika somo lake. Mwalimu hana budi kuzingatia kufundisha kuanzia mambo mepesi wanayoelewa kuelekea wasiyoyajua. Mazungumzo yatakayotolewa darasani yawe yale yenye manufaa kwao, mfano maamkizi,kucheza mpira, usafi n.k Inampasa Mwalimu awe mdadisi kwa kushirikisha na wanafunzi wote darasani akitumia mbinu ya majibizano ya wanafunzi wao kwa wao. Mwalimu akosoe makosa yanayojitokeza kila mara mathalani matamshi, lafudhi,shadda, au kiimbo. Mwalimu awaelekeze namna ya kutambua na kupanga mawazo makuu ya habari aliyoisoma au kusimulia . Mwalimu awaonyeshe mbinu za kujibu maswali yatokanayo na ufahamu. MSAMIATI Katika ufundishaji wa msamiati,mwalimu aeleze maana ya maneno kwa kutumia vitu halisi, picha , maigizo, maswali na majibu na mifano mbalimbali. Wanafunzi washirikishwe kikamilifu kwa kutoa mifano yao wenyewe .

23

UTUNGAJI Utungaji unaweza kuzingatia fani mbili yaani mazungumzo na kuandika . Mazungumzo yawe juu ya jambo lenye maarifa na manufaa . Mfano; Umoja na mshikamano wa wanyarwanda , amani,maendeleo ya nchi na magonjwa kama ukimwi n,k

a) yawepo matayarisho juu ya jambo litakalozungumzwa ili wakati usipotee bure.Lengo lijulikane wazi tangu mwanzo wa somo.

b) Mwalimu atilie mkazo uchaguzi wa maneno bora na matokeo yake kwenye matumizi. c) Wanafunzi wapewe mazoezi wakitunga hotuba fupu fupi.Hii inaweza kukuza vipaji vya

kujieleza na kujiamini. d) Mazungumzo na mijadala itumiwe kama chanzo au utangulizi wa kuandika utungaji.

Utungaji wa kuandika unalenga kumwezesha mwanafunzi kutumia lugha hii katika fani na njia mbalimbali katika fani hii kwa ufasaha.Utungaji uanzie kwenye mambo mepesi wanafunzi wanayoyafahamu, mfano insha fupi fupi kuhusu taratibu za kila siku kama :michezo ya kuigiza n.k Mwalimu awaelekeze namna ya kupangilia mawazo kwa utaratibu unaostahili mmoja au kwa makundi. Mazungumzo yanaweza kuambatana na mijadala ambayo yaweza kufanyika aidha ndani au nje ya darasa kulingana na mada inayozungumziwa . Wakati wote mwalimu azingatie

24

kiimbo(lafudhi,shada), mpango wa mawazo,matumizi ya semi, nahau na ufasaha wa lugha , ukweli,usawa na uhakika wa mambo. Wanafunzi wakishapata msamiati wa kutosha Mwalimu hana budi awape nafasi ya kujieleza mbele ya darasa katika kikundi, hivyo matayarisho kamili yafanyike na lengo lake liwe wazi.Kazi zinaweza kufanyika katika somo hili ni kama vile hotuba fupi michezo mifupi ya kuigiza,hadithi fupi za fasihi simulizi, nyimbo mashairi mepesi , mdahalo n.k. KUANDIKA Taaluma ya kuandika haina budi itolewe kwa wanafunzi kuanzia mambo wanayoyafahamu .Hapa mwalimu inampasa kufuatilia hati ya kila mwanafunzi kuumba neno, sentensi na vifungu vya habari.Mwalimu hana budi kufuatilia matumizi na alama na vituo katika hati ya mwanafunzi.Mwanafunzi atoe mazoezi mengi yaliyo na vipashio visivyopatikana katika lugha ya Kinyarwanda , mfano dhalimu,thamani , aghalabu n.k KUSOMA NA UFAHAMU Kusoma kwa kutafakari ndilo lengo kuu katika fani hii.Taratibu za kusoma kifungi cha habari zifuatwe,mathalani kusoma kimya kimya , kwa sauti na kwa haraka . mwalimu anaweza kumtumia mwanafunzi mmoja kusoma huku wengine wakifuatilia vitabuni mwao.

25

KUSIKILIZA Mwalimu atumie vipengele mbalimbali katika kuzoeza usikivu wa wanafunzi wake,katika mazungumzo,hadithi, nyimbo na ushairi. Vitu hivyo vinaweza kuwa ni moja kwa moja au vilivyonaswa kwenye kanda za sauti, kama baada ya kupewa kichwa cha habari ya kuzungumzia ,kikundi kimoja cha wanafunzi kinaweza kupewa fursa ya kuzungumza .Wanafunzi wengine watasikiliza na baadaye kutoa mhutasari wa yaliyozungumziwa au kutoa yanayohusu mazungumzo hayo . Hali kadhalika vifungu vya habari , hadithi nyimbo na mashairi vinaweza kutumika katika kupima matamshi ambayo labda bado yanaathiri uzungumzaji wa wanafunzi. Wakati mwingine itambidi Mwalimu apange zoezi maalum kama kusoma au kuimba kifungu cha maandishi chenye kukazia sauti fulani inayokosewa na wanafunzi. N.B stadi ya usikivu hufundishwa pamoja na stadi nyingine ili kupumzisha mara kwa mara akili ya mwanafumzi , kama kuimba , kutoa mhutasari wa yaliyosikilizwa , chemsha bongo n.k

26

UFUNDISHAJI METHALI NA VITENDAWILI Methali hutuma lugha ya mkato yenye kubeba shehena kubwa ya maudhui na ujumbe , katika methali kuna mafunzo, maonyo na marekebisho mbalimbali ya maisha ya jamii.Aghalabu methali hutumia lugha ya mafumbo ambayo huhitaji kufumbuliwa ili kuweza kunufaika na maadili yaliyofichwa ndani ya methali inayohusika . Walimu wanaofundisha kiswahili wanapaswa kufundisha methali kama wanavyofundisha uchambuzi wa mandishi mengine ya Fasihi. Watachambua maudhui yaliyomo katika kila methali, maana yake, mafundisho , ujumbe uliomo katika methali , mafundisho yaliyoma katika methali na matumizi ya methali hiyo mfano :`` MVUMILIVU HULA MBIVU ``Maana ya methalihi ni kwamba asiwe mtu mwenye kukata tamaa upesi , maudhui yanayojitokeza katika methali hii ni kwamba kila kitu kizuri hupatikana kwa shida na ili mtu akipate hupaswa kupambana na matatizo mengi . Ujumbe tunaoupata katika methali hiyo ni kwamba ili mtu afanikiwe katika jambo fulani hana budi kukabiliana na matatizo yote bila kakata tamaa. Mwalimu wa kiswahili anapaswa kufundisha methali kwa kueleza maana ya methali yenyewe , maudhui yaliyomo katika methali , ujumbe na matumizi ya methali hiyo. Vitendawili pia vina maudhui , maadili na ujumbe ndani yake .Vitendawili ni semi fupi fupi zilizo fumbwa ambazo mtu anapaswa kuzifumbua ili kupata manufaa yaliyomo katika kitendawili hicho.

27

NJIA ZA KUFUNDISHA MASHAIRI , TENZI NA NGONJERA Mashairi , Tenzi na Ngonjera ni fani mojawapo maarufu katika fasihi iliyobeba shehena kubwa ya maadili na ujumbe ndani yake .Wakati wa kufundisha mashairi , Ngonjera na Tenzi mwalimu hana budi kusoma kwa uangalifu ubeti hadi ubeti ili kupata maudhui , maadili na ujumbe uliotolewa na wasanii katika sanaa waziandikazo. Mfano:katika kuchambua mashairi, njia zifuatazo zinaweza kutumika : Kwanza ni kuchunguza maudhui yaliyomo katika shairi kama yanavyozungumzia maswala ya kisiasa ,kiuchumi, kiutamaduni au yale ya kijamii. Pili ni kuchambua ubeti kwa ubeti kwa kila mstari au utenzi ili kupata dhana iliyomo katika kila ubeti . Tatu ni kuchunguza maudhui ,maadili na ujumbe uliomo katika kila shairi.Mwalimu akifanya hivyo atawezesha wanafunzi kupata maadili na ujumbe katika mashairi wayasomayo, na hii itawasaidia wanafunzi kuona migogoro na matatizo yaliyomo katika jamii na jinsi ya kutatua migogoro hiyo. Vile vile katika ufundishaji wa vipengele hivyo , fani na maudhui vionyeshwe wazi kwa wanafunzi , na kuambiwa kuwa ni vitu muhimu ambavyo haviachani .

28

Katika ufundishaji wa fani mwalimu hana budi kuangalia mbinu na taratibu za utungaji wa mashairi . Mfano : Mashairi ya kimapokeo : Mwalimu awaeleze wanafunzi miundo mbalimbali iliyotumika hasa Mashairi upande wa fani.

- Yafanyike majadiliano kuhusu mahusiano kati ya hadithi na hali halisi ya maisha - Yachunguzwe maadili/ mafunzo yaliyomo. - Falsafa ya mwandishi/ msimamo wa hadithi. - Hadithi inamhusu nani ? jamii ipi kwa vipi ?

Mwalimu yampasa kupitia kipengele cha mtazamo wa fikira. Mtazamo wa fikra huonyesha jinsi anavyotazama kitu au kufafanua kile kinachomgusa au kinachomchomachoma moyoni mwake . Katika ushairi viungo vya mwili vinaweza kupewa utu , nafsi na uhuru wa kuishi kama viumbe vyenye nafsi za pekee vinavyoweza kufikiri na kuamua vyenyewe . Katika ulimwengu wa ushairi miti, wanyama , jua mwezi na vitu vyote vionekanavyo juu ya uso wa dunia vyaweza kupewa uhai na utu vikaishi kama binadamu . Jina la kitabu lijadiliwe na kulinganishwa na maudhui yake .Udhaifu na usanifu ujadiliwe . Mwanafunzi apewe fursa ya kutoa maoni juu ya ufundi uliotumika katika andiko / hadithi na pawepo mijadala ya wanafunzi kuhusiana na migogoro iliyomo na usuluhishi wake.

29

NJIA ZA KUFUNDISHA FASIHI Ziko njia nyingi ambazo mwalimu wa somo la fasihi anaweza kuzitumia ili kufanikisha somo lake na kuwafanya wanafunzi kulipenda somo lake la fasihi lakini hapa zimependekezwa njia zifuatazo: Njia ya kwanza ni njia ya majadiliano ya darasa zima. Njia hii huweza kuwasaidia wanafunzi kujenga stadi ya kuzugumza Huwazoeza wanafunzi kusema na kujadili mambo mbalimbali mbele ya hadhara bila woga .Njia hii si kwamba inawazoeza kuzungumza hadharani tu bali inawafunza namna ya kujadili mambo yenye mantiki. Pia hupevuka kimawazo na kujadili mambo kwa undani zaidi. Njia ya pili ni ile ya vikundi vya majadiliano wanafunzi hugawanywa katika vikundi vidogo vidogo vyenye washiriki watano hadi saba.Baada ya kuligawa darasa katika vikundi, Mwalimu hutoa swali moja kwa kila kikundi , ili kila kikundi kijadili swali lake kwa uwezo wake .Njia hii huwapa nafasi wanafunzi wengi katika kikundi kutoa mawazo mbele ya kikundi bila haya .

30

Njia ya tatu Mwalimu anaweza kutumia njia ya mazoezi. Kawaida katika njia hii Mwalimu hutoa maswali kadhaa kufuatia njia iliyokwisha fundishwa . Maswali yaweza kufanyiwa humo darasani katika kipindi cha somo la fasihi . Mwisho Mwalimu awaelekeze wanafunzi katika kufuata fani na maudhui katika kuchambua au kuhakiki vitabu mbalimbali vya fasihi. NJIA ZA KUFUNDISHA HADITHI Mwalimu afundishe somo hili kwa kutumia vipengele vifuatavyo:

1. Wanafunzi wasome na kuelewa yaliyomo katika hadithi na kisha majadiliano na mazungumzo yafuatwe.

2. Maoni juu ya hadithi hiyo yatolewe kuhusu aina au lengo lake pamoja na mazingira yaliyotumiwa katika hadithi .

3. Mwalimu aonyeshe muundo , mawazo hadi mwisho wa hadithi , mtiririko wa visa , mahali palipo na upeo wa hadithi, aonyeshe jinsi muundo unavyosaidia katika kuelewa hadithi na mtiririko wa masimulizi.

4. Mwalimu afundishe dhamira , wazo au ujumbe ulioko katika hadithi ,baada ya kusikiliza mchango wa wanafunzi kuhusiana na hoja hiyo .

5. Wahusika wajadiliwe na uhusika wao .Mjadala ufanyike kuhusiana na vipengele vya maswali.

31

Mfano : - Nani mhusika mkuu . - Wahusika wanahusiana je wao kwa wao ? - Zipi nafasi zao katika hadithi - Wamepevuka vipi lengo na dhamira ya mwandishi. Kipengele cha mtindo katika ufundishaji wa hadithi kielezwe kwa kujadili maswali Mfano :

- Nani anasimulia ? na kwa nini ? - Mwandishi ametumia mbinu gani katika kuwasilisha mawazo yake ? - Matumizi ya picha , lugha na vipengele vyake.

TATHMINI Kwa kila kazi yoyote inayotolewa darasani haina budi kufanyiwa tathmini ili kujua uelewa wa wanafunzi. Hii humsaidia Mwalimu kuelewa pamoja na kumwezesha kuendelea na somo anaporudia somo hilo.Mwalimu inambidi ajue sababu za kutofanikiwa kwa somo lake na ikibidi aweze akabadili njia za ufundishaji. Katika kutathmini mwalimu anashauriwa yafuatayo : Kutoa zoezi kila baada ya somo na masahihisho yafanywe kabla ya kuendelea na somo jingine. Mwalimu anashauriwa kutumia maswali ya mdomo akiwashirisha wanafunzi ili wajenge tabia ya kujieleza na kujiamini. Mazoezi yatakayotolewa yazingatie sauti za kusoma , kuandika na kuzungumza .

32

Katika kufanya tathmini Mwalimu anashauriwa kutumia aina mbalimbali za utunzi wa maswali. Mfano :

i) Maswali kujibu kweli au si kweli ii) Kutaja iii) Kuoanisha iv) Kujaza nafasi zilizo wazi v) Maswali kujieleza, kujadili n.k

Mwalimu atoe mazoezi ya kufanyia nyumbani na masahihisho yafanyike kabla ya kuendelea na somo linalofuata . Kila baada ya kumaliza mada mwalimu anashauriwa kutoa jaribio kwa wanafunzi ili kupima uelewa wao , ieleweke pia kuwa majaribio baada ya mada haimzuii mwalimu kutoa majaribio ya dharura ili kuona iwapo wanafunzi hufuata somo hili . Mtihani ni lazima utolewe kila baada ya kumaliza muhula .Maswali yatokane na mada zote zilizofundishwa katika kipindi hicho , lakini hii haimzuii Mwalimu kutumia baadhi ya maswali kutoka vidato vilivyotangulia ili kupima kumbukumbu ya wanafunzi. Tathmini itolewe kila baada ya muhula wa mwisho.Mtihani ni lazima uhusishe mada zote zilizofundiswa kwa mwaka mzima Vile vile hii haimzuii Mwalimu kutoa maswali yanayotokana na ujuzi wa jumla bila kuangalia ya kwamba mwanafunzi alifundishwa au la .

33

MAPENDEKEZO

Ili kufanikisha madhumuni ya mhutasari huu , mambo yafuatayo yamependekezwa : i) Walimu watakaofundisha somo hili wapewe semina za kutosha kuhusiana na ufundishaji

wa mada zilizo katika somo hili. ii) Ili kuendeleza lugha hii nchini Rwanda , wizara haina budi kuwa na ushirikiano na Taasisi

za ukuzaji wa lugha ya Kiswahili zilizoko katika nchi jirani zenye uzoefu na taaluma ya kutosha katika ufundishaji na utaratibu wa lugha hii ya Kiswahili. Mfano BAKITA ( Tanzania ), vile vile Kenya na idara za ukuzaji wa lugha za Kiafrika na Ulimwengu.

iii) Katika uimarishaji wa Kiswahili , inapendekezwa kuundwe chombo maalum cha kitaifa kitakachoshughulikia lugha hii yaani uratibu na uenezaji wa lugha hii ,

iv) Walimu wapewe motisha kila inapowezekana ili kuleta hamasa katika utendaji wao wa kazi.

v) Washirikishwe wataalamu wachache waliopo katika kutunga vitabu , majarida na vitini vitakavyosaidia katika ufundishaji wa somo hili .

vi) Vitabu , majarida yanayoeleza kuhusu matatizo yanayoikumba jamii vitungwe au kuandikwa hasa vile vinavyohusu na kujilinda na magonjwa ya hatari kama vile ukimwi yaani (sida)

vii) Kuwepo ukaguzi wa mara kwa mara katika shule ili kuona jinsi gani somo la kiswahili linavyofundishwa .

viii) Vitabu visivyopungua viwili kwa kila fani ya Fasihi Riwaya , Tamthilya, na Ushairi vifundishwe .

34

VITABU VYA MAREJEO

1) Vitabu vyote vilivyoorodheshwa kidato cha kwanza na kidato cha tatu. 2) KAPINGA C

Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu 1983 TUKI DSM 3) Wizara ya mafunzo ya Msingi na Sekondari

Kitabu cha Kiswahili IV-V Kitabu cha Mwanafunzi Nov 1987

4) SHIHABUDDIN CHIRAGUDDINI Mathias na Mnyampala Histotria ya Kiswahili DSM 1977

5) Wizara ya mafunzo ya msingi na sekondari Kitabu cha kiswahili IV B Kitabu cha mwanafunzi

6) Wizaraya Mafunzo ya Msingi na Sekondari Kitabu cha kiswahili IV-VA Kitabu cha mwanafunzi nov 1987

7) Wizara ya Mafunzo ya Msingi na Sekondari Kitabu cha Kiswahili Agosti 1987

35

WALIOSHIRIKI KATIKA KUTUNGA MHUTASARI HUU

Gatera Augustin : Mkurugenzi Idara ya Lugha na Sayansi jamii ( Msimamizi) Rubaya Anthony : Mkuzaji mitaala Idara ya Kiswahili ( Mkuu wa idara ya kiswahili) Liyetona Ernest Andrew : Mkaguzi wa Elimu idara ya Kiswahili Habiyakare Poponi: Idara ya Kswahili Baraza la mitihani Neema Vestine : Shule ya Sekondari Apred –Ndera (GS –AAPRED – Ndera) Mutemberezi Francois : Shule ya Sekondari APPEC – Remera –Rukoma ( College Appec-Remera-Rukoma)

WACHAPISHAJI Taasisimya Taifa ya Ukuzaji mitaala ( NCDC)

36