3
MUHTASARI WA MAMBO YATAKAYOTEKELEZWA NDANI YA MIEZI SITA YA MWANZO KATIKA ASASI YA WAENDELEE-SINGIDA Ili asasi yoyote ya kijamii iweze kufanikiwa ni lazima kuwe na malengo ya aina mbili; Malengo ya mda mrefu na malengo ya mda mfupi. Malengo yote ya aina mbili ni lazima yawe na sifa zifuatazo: 1.Yanayotekelezeka 2. Yenye kipimo 3. Muda maalumu Yafutayo ni mapendekezo ya malengo ya mda mfupi (miezi sita ya mwanzo) kwa asasi ya ‘WAENDELEE/WIRWANA’ 1. Uhamasishaji Katika kuhakikisha kwamba jamii ya watu wa Singida kaskazini inatambua na kuipokea asasi ya WAENDELEE kwa mikono miwili na ushirikiano, ni lazima kuwe na uhamasishaji na kuitambulisha asasi katika jamii ili waitambue na kuzijua faida za asasi hiyo. Uhamasishaji huo ni utaambatana na kuanzisha vikundi mbalimbali vitakavyo jihusha na shughuli mbalimbali kama vile upandaji miti, kilimo, ufugaji wa nyuki n.k. Pia vikundi hivyo vitarahisisha uwezeshaji wa kiuchumi kama vile mikopo na maarifa. 2. Elimu Uhamasishaji ni lazima uambatane na elimu katika nyanja mbalimbali ili kuielimisha jamiii jinsi ya kutumia rasilimali zilizopo kwa ajili ya manufaa. Elimu hii naweza ikatolewa kwa

MUHTASARI-WIRWANA

Embed Size (px)

DESCRIPTION

MUHTASARI

Citation preview

Page 1: MUHTASARI-WIRWANA

MUHTASARI WA MAMBO YATAKAYOTEKELEZWA NDANI YA MIEZI SITA YA MWANZO KATIKA ASASI YA WAENDELEE-SINGIDA

Ili asasi yoyote ya kijamii iweze kufanikiwa ni lazima kuwe na malengo ya aina mbili; Malengo ya mda mrefu na malengo ya mda mfupi. Malengo yote ya aina mbili ni lazima yawe na sifa zifuatazo:

1.Yanayotekelezeka

2. Yenye kipimo

3. Muda maalumu

Yafutayo ni mapendekezo ya malengo ya mda mfupi (miezi sita ya mwanzo) kwa asasi ya ‘WAENDELEE/WIRWANA’

1. Uhamasishaji

Katika kuhakikisha kwamba jamii ya watu wa Singida kaskazini inatambua na kuipokea asasi ya WAENDELEE kwa mikono miwili na ushirikiano, ni lazima kuwe na uhamasishaji na kuitambulisha asasi katika jamii ili waitambue na kuzijua faida za asasi hiyo.

Uhamasishaji huo ni utaambatana na kuanzisha vikundi mbalimbali vitakavyo jihusha na shughuli mbalimbali kama vile upandaji miti, kilimo, ufugaji wa nyuki n.k. Pia vikundi hivyo vitarahisisha uwezeshaji wa kiuchumi kama vile mikopo na maarifa.

2. Elimu

Uhamasishaji ni lazima uambatane na elimu katika nyanja mbalimbali ili kuielimisha jamiii jinsi ya kutumia rasilimali zilizopo kwa ajili ya manufaa. Elimu hii naweza ikatolewa kwa vikundi ama kwa semin aka mile iliyofanyika tarehe 19-21 agosti, 2014 kwa ajili ya upandaji miti na ufugaji nyuki.

Elimu itakayotolewa itasaidia kuhakikisha jamii inaelewa na kutekeleza shughuli zote katika ubora unaohitajika.

Page 2: MUHTASARI-WIRWANA

3. Utambuaji wa rasilimali

Rasilimali zinazopatikana katika eneo husika ndiyo mtaji wa mafanikio wa asasi ya WAENDELEE. Hivyo kuzitambua rasilimali hizi ni hatua muhimu sana. Kwamfano kutakuwa na utambuzi wa rasilimali kama vile vyanzo vya maji na misitu ya asili ili kuweza kuona jinsi ya kuzitumia katika namna endelevu na salama kwa kizazi kilichopo na kijacho.

Kwa mfno kuna vyanzo vya maji (chemi chem.) na misitu ya asili ambayo imeanza kuharibiwa kutokana na kukosekana kwa mfumo mzuri wa matumizi ya vyanzo hivyo. Baada ya kubaini rasilimali hizo vitaundwa vikundi vya kuzisimamia kwa kutumia mbinu shirikishi kwa jamii ama zikasimamiw na asasi ya WAENDELEE kwa mikataba maalum na vijiji/mamlaka husika.

4. Uwezeshaji

Katika kuhakiksha utekelezaji wa malengo ya asasi unatimia kama ilivyokusudiwa ni lazima pawepo na uwezeshwaji wa kiuchumi na maarifa kikamilifu kwa vikundi, wananchi na watendaji wote wa asasi kwa ujumla. Kwa mfano kutakuwa na uwezeshwaji kwa kutumia mikopo kutoka katika mashirika ya ukopeshaji kama SIDO n.k. ili uetekelezaji wa malengo ya mda mrefu ikiwemo maendeleo na kunyanyua uchumi wa jamii nzima kwa ujumla uweze kutimia.