42
UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 1 UHAKIKI WA RIWAYA YA VUTA N’KUVUTE KITABU- VUTA N’KUVUTE MWANDISHI SHAFI ADAM SHAFI WACHAPISHAJI MKUKI NA NYOTA PUBLISHERS MWAKA 1999 Utangulizi Riwaya hii inazungumzia matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii yetu kwa sasa. Matatizo hayo ni kama vile matabaka, umaskini, ndoa za kulazimishwa, wivu katika ndoa, n.k Maudhui Dhamira kuu: Ukombozi Katika riwaya hii, mtunzi anajadili aina nne za ukombozi ambazo ni ukombozi wa kiutamaduni, ukombozi wa kisiasa, ukombozi wa kiuchumi na ukombozi wa kifikra. Ukombozi wa kiutamaduni Katika kujadili ukombozi wa kiutamaduni, mwandishi anaonesha kuwa baadhi ya mila na desturi zetu zinamkandamiza mwanamke. Baadhi ya mila hizo ni ile ya kumlazimisha mwanamke kuolewa na mtu asiyemtaka. Kama walivyofanya wazazi wa Yasmin kwa kumwozesha binti yao kwa nguvu kwa Bw. Raza. Yasmin hakumpenda Raza kwa sababu halikuwa chaguo lake. Hivyo, msanii anaonesha kuwa ili tujikomboe kiutamaduni lazima tuachane na mila hizo. Pili, kuna mila ya kumweka mwanamke utawani, kama alivyofanya Shihab baada ya kumuoa Yasmin. Shihab baada ya kumuoa Yasmin alimweka utawani. Jambo hili linazorotesha maendeleo ya mwanamke, kwani badala ya kushughulika na kazi za kimaendeleo hukaa ndani tu na kusubiri kuletewa kila kitu na mwanaume. Katika kupiga vita mila hii msanii anaonesha kuwa, Yasmin alitoroka kwa shihab kwa lengo la kuonesha kuwa mila kama hizi zimepitwa na wakati na jamii haina budi kuzitupilia mbali mila hizo. Hivyo, msanii anaishauri jamii kuwa, ili tuweze kujikomboa kiutamaduni hatuna budi kuachana na mila na desturi zilizopitwa na

Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

  • Upload
    others

  • View
    866

  • Download
    76

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 1

UHAKIKI WA RIWAYA YA VUTA N’KUVUTE

KITABU- VUTA N’KUVUTE

MWANDISHI – SHAFI ADAM SHAFI

WACHAPISHAJI – MKUKI NA NYOTA PUBLISHERS

MWAKA – 1999

Utangulizi Riwaya hii inazungumzia matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii yetu

kwa sasa. Matatizo hayo ni kama vile matabaka, umaskini, ndoa za

kulazimishwa, wivu katika ndoa, n.k

Maudhui

Dhamira kuu: Ukombozi Katika riwaya hii, mtunzi anajadili aina nne za ukombozi ambazo ni

ukombozi wa kiutamaduni, ukombozi wa kisiasa, ukombozi wa

kiuchumi na ukombozi wa kifikra.

Ukombozi wa kiutamaduni Katika kujadili ukombozi wa kiutamaduni, mwandishi anaonesha kuwa

baadhi ya mila na desturi zetu zinamkandamiza mwanamke. Baadhi ya

mila hizo ni ile ya kumlazimisha mwanamke kuolewa na mtu

asiyemtaka. Kama walivyofanya wazazi wa Yasmin kwa kumwozesha

binti yao kwa nguvu kwa Bw. Raza. Yasmin hakumpenda Raza kwa

sababu halikuwa chaguo lake. Hivyo, msanii anaonesha kuwa ili

tujikomboe kiutamaduni lazima tuachane na mila hizo.

Pili, kuna mila ya kumweka mwanamke utawani, kama alivyofanya

Shihab baada ya kumuoa Yasmin. Shihab baada ya kumuoa Yasmin

alimweka utawani. Jambo hili linazorotesha maendeleo ya mwanamke,

kwani badala ya kushughulika na kazi za kimaendeleo hukaa ndani tu na

kusubiri kuletewa kila kitu na mwanaume. Katika kupiga vita mila hii

msanii anaonesha kuwa, Yasmin alitoroka kwa shihab kwa lengo la

kuonesha kuwa mila kama hizi zimepitwa na wakati na jamii haina budi

kuzitupilia mbali mila hizo.

Hivyo, msanii anaishauri jamii kuwa, ili tuweze kujikomboa

kiutamaduni hatuna budi kuachana na mila na desturi zilizopitwa na

Page 2: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 2

wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha nyuma

maendeleo ya jamii nzima kwa ujumla.

Ukombozi wa kisiasa Hapa msanii anazungumzia harakati za wananchi wa Unguja na Pemba

za kujikomboa kutoka katika minyororo ya kunyonywa, kukandamizwa,

kunyanyaswa na kuonewa na wakoloni wa Kiingereza pamoja na

vijibwa vyao.

Katika kujadili hayo, msanii anaonesha wazi jinsi Denge na kundi lake

wanavyojishughulisha na harakati hizo kwa kutawanya vitabu vyenye

mawazo ya kijamaa, magazeti yanayopinga ukoloni na makaratasi

mengine ya uchochezi dhidi ya wakoloni. Wao waliamini kuwa kwa

kutumia vitabu, magazeti na makaratasi hayo, wananchi wa kawaida

wangeamka na kuzijua haki zao na hatimaye kuanza kupambana na

ukoloni huo.

Katika kujadili dhamira hii ya ukombozi wa kisiasa, msanii anaonesha

kuwa lazima tuwe na watu waliojitolea muhanga katika harakati hizo.

Denge na kundi lake walijitoa muhanga katika kuhakikisha kuwa nchi

yao inakombolewa kutoka katika mikono ya wakoloni kama asemavyo

Denge (uk. 145);

“Yasmin mimi najua unanipenda na mimi nakupenda vilevile, lakini

kuna kitu kimoja napenda uelewe, kuna mapenzi na wajibu wa mtu

katika jamii. Kila mtu ana wajibu fulani katika jamii na mimi wajibu

wangu mkubwa ni kufanya kila niwezalo kwa kushirikiana na wenzangu

ambao wengine unawajua na wengine huwajui ili kuona kwamba nchi

hii inakuwa huru. Hii ni kazi ngumu ina matatizo mengi na inahitaji

kujitoa muhanga na mimi ni miongoni mwa hao waliojitolea muhanga

kufa, kupona, potelea mbali. Tupo wengi tuliojitolea namna hiyo, tena

wengi sana, maelfu.”

Denge na kundi lake walifuatwa sana na askari, lakini hawakuacha

kueneleza harakati zao za kudai uhuru.

Vilevile msanii anaonesha kuwa ili tujikomboe kisiasa, lazima tuwe na

umoja na mshikamano, kwani umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

Denge na kundi lake walishirikiana sana katika harakati zao za

kupambana na wakoloni. Walishirikiana katika kutawanya vitabu,

Page 3: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 3

magazeti na makaratasi ya uchochezi dhidi ya ukoloni. Ingawaje mpaka

mwisho wa riaya hii ukombozi wa kisiasa ulikuwa bado haujapatikana,

lakini bado harakati hizo zilikuwa zinaendelea na kuna siku ukombozi

utapatikana.

Ukombozi wa kiuchumi Katika riwaya hii, msanii annaonesha harakati za watu wa Unguja na

Pemba za kujikomboa kiuchumi kutoka katika minyororo ya kunyonywa

na wakoloni wa Kiingereza. Uchumi wa Zanzibar kabla ya uhuru

ulikuwa mikononi mwa wazungu wachache ambao walikuwa

wanamiliki njia zote za uzalishaji mali.

Harakati za akina Denge na wenzake zililenga katika kuwakomboa

Waafrika kiuchumi kwa kuchukua njia kuu za kuzalisha mali toka kwa

wazungu wachache na kuziweka mikononi mwa Waafrika walio wengi.

Ukombozi wa kifikra Ukombozi wa kifikra ni ile hali ya kujua na kutambua matatizo

yanayoikabili jamii yako na wewe mwenyewe na kutafuta mbinu za

kujinasua kutoka katika matatizo hayo.

Kitendo cha Yasmin kuona kuwa baadhi ya mila na desturi

zinamnyanyasa mwanamke na kuamua kuachana nazo, inadhihirisha

wazi kuwa Yasmin alikuwa na uwezo wa kufikiri na kuona mbali. Mila

hizo ni kama vile mwanamke kulazimishwa kuolewa na mtu asiyemtaka

na kuwekwa utawani.

Pili, kitendo cha Denge na kundi lake kugundua kuwa wananyonywa,

wanaonewa na kukandamizwa na wakoloni ulikuwa ni ukombozi wa

kifikra na ndio maana walianzisha harakati za kudai haki zao za msingi.

Dhamira ndogondogo 1. Mapenzi na ndoa

Katika kujadili dhamira hii ya mapenzi, msanii ameainisha aina mbili za

mapenzi, mapenzi ya kweli na mapenzi ya pesa. Mapenzi ya kweli

tunayaona kati ya Mwajuma na Yasmin. Hawa walipendana hasa ndio

maana Yasmin baada ya kutoroka kwa mume wake, alikimbilia kwa

Mwajuma wakaishi pamoja. Katika kuonesha hayo msanii

anamwonesha Mwajuma kama mtu mwenye roho nzuri na mkarimu.

Page 4: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 4

Japokuwa alikuwa mtoto wa kimaskini lakini aliamua kumsaidia rafiki

yake Yasmin. Msanii anasema (uk. 22);

“Mwajuma ijapokuwa ni mtoto wa kimaskini alikuwa na roho nzuri ya

ajabu na roho nzuri yake ilichanganyikana na ukarimu usiokuwa na

mfano. Alikuwa yuko tayari kumkirimu mtu chochote kidogo alichokuwa

nacho. Alikuwa mwingi wa huruma na siku zote alikuwa tayari

kumsaidia yeyote aliyemweleza shida zake, pindi akiwa na uwezo wa

kumsaidia mtu huyo.”

Yasmin, baada ya kumtoroka mume wake, aliishi maisha yake yote kwa

Mwajuma mpaka alipoolewa na Shihab na baada ya kifo cha Shihab,

Yasmin aliendelea kuishi kwa Mwajuma mpaka alipokuja kuolewa na

Bukheti.

Mapenzi mengine ya kweli ni kati ya Bukheti kwa Yasmin. Bukheti

alimpenda sana Yasmin na ndiyo maana alifunga safari kutoka

Mombasa kuja Unguja kwa ajili ya kumtafuta Yasmin. Msanii

anaonesha hayo (uk. 41);

“Kwa Bukheti safari ya kutoka Mombasa mpaka Unguja ni safari ndefu

lakini safari hiyo ina urefu ulioje utakaomzuia yeye kukisaka kitu azizi

kama pendo la Yasmin.”

Bukheti licha ya kukataliwa na Yasmin hakukata tama, ndiyo maana

baada ya kifo cha mume wake Yasmin, Bukheti alifunga tena safari

kutoka Mombasa kwenda Zanzibar kubahatisha tena kwa Yasmin (uk.

230-231). Bukheti licha ya kupewa masharti; bado aliyatimiza na

hatimaye akamuoa Yasmin (uk. 274-277).

Mapenzi mengine ya kweli ni kati ya Denge na Yasmin. Hawa

walipendana hasa na wote wawili walikuwa na mapenzi ya kweli kwa

kila mmoja. Denge alimpenda sana Yasmin na Yasmin vilevile alikuwa

anampenda sana Denge katika shida na raha (uk. 115-127), (214-219).

Mapenzi mengine ya kweli ni kati ya Denge na kundi lake kama vile

Mambo, Chande, Sukutua, Mwajuma, Hussein, Pazi, Salehe, n.k. hawa

walipendana hasa na ndio maana walishirikiana katika shughuli

mbalimbali.

Kwa upande wa Mwajuma, naye alikuwa na mapenzi ya pesa.

Aliwapenda watu wenye pesa na ndiyo maana alimshauri Yasmin

Page 5: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 5

amwache Denge na kuolewa na Shihab ambaye alikuwa na pesa (uk.

169-179).

Kuhusu suala la mapenzi, msanii anaonesha kuwa uzuri na ubaya siyo

unaoamua mtu kupenda au kupendwa, kwani kuna wazuri wanaopendwa

na wasiopendwa. Pia kuna wazuri wasiojua kupenda wala kupendwa,

hali kadhalika kuna wabaya wanaopendwa na wasiopendwa au wabaya

wasiojua kupenda au kupendwa vilevile (uk. 88-89).

Msanii anaendelea kusisitiza kuwa, katika suala la mapenzi ni lazima

wale watu wanaohusika wapende wote, hayo ndiyo yatakuwa mapenzi

ya kweli. Kama mmoja anapenda zaidi ya mwenzake hapo kunakuwa na

walakini katika mapenzi hayo.

Katika suala la ndoa, msanii anaonesha ndoa za kulazimishana na

madhara yake kwa jamii. Yasmin alilazimishwa na wazazi wake

kuolewa na Raza lakini ndoa yao haikudumu. Kwa ujumla Yasmin

hakumpenda kabisa Raza, kwani alikuwa sawa na baba yake wa

kumzaa.

Vilevile katika suala hili, msanii anaonesha kuwa suala la ndoa lazima

waachiwe wale wanaopendana na siyo maamuzi ya wazee ndio

yatawale, kwani hayo ni mambo ya kizamani. Msanii anasema hivi (uk.

259);

“Hivyo! Humtaki huyo mchumba wako! Huyu Bashiri ana mambo ya

kizamani kwelikweli anataka akuchagulie mke yeye…..huyu ami yako

mpuuzi hayajui mambo leo. Bashiri. Hajui kama siku hizi vijana

wanatafutana wenyewe, kijana anatafuta wake. N‟do mnamwita vile siku

hizi geli-friend sijui au sivyo Bukheti.”

Hivyo anachosisitiza msanii ni uhuru katika suala zima la kuchagua

mchumba. Msanii anaeleza kuwa, suala hili lisiingiliwe na wazee.

Vilevile msanii amezungumzia suala la wivu katika ndoa. Shihab baada

ya kumwoa Yasmin kutokana na wivu aliokuwa nao, alimweka utawani

akafungwa kama wafungwa, msanii anayasema hayo (uk. 196-197);

“Wakati Denge amefungwa gerezani kumbe Yasmin naye amefungwa

kwa mumewe. Hakufungwa kama afungwavyo mahabusu ila yeye

alikuwa ametawishwa hana tofauti na mfungwa. Alikuwa hendi harudi

Page 6: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 6

yumo ndani tu kama kizuka; kwa sababu ya wivu aliokuwa nao

Shihab…..”

Msanii akijadili zaidi juu ya wivu katika ndoa vilevile ameonesha

madhara ya wivu. Wivu unapozidi katika ndoa kwanza ni rahisi ndoa

hiyo kuvunjika. Mfano, kutokana na wivu, Shihab aliwaacha wanawake

watatu na Yasmin alikuwa mke wake wan ne ambaye naye aliwekwa

utawani (uk. 197).

Pili, msanii anaonesha kuwa wivu ukizidi katika ndoa unamnyima uhuru

yule anayeonewa wivu. Katika ndoa yake na Shihab, Yasmin alikosa

uhuru kabisa, msanii anaonesha hayo (uk. 197) anasema;

„Alimpa kila starehe, ila uhuru wa kutoka na starehe zake zote ziliishia

ndani ya nyumba yake kubwa iliyokuwa na kila aina ya anasa ndani

yake, zote asizione kitu, kutwa akawa ananing‟inia madirishani

akiangalia wapiti njia na kuwahusudu jinsi walivyo huru. Alijiona kama

ndege aliyefungiwa tunduni akapewa kila kitu isipokuwa uhuru wake wa

kuruka hewani.”

Ni kutokana na wivu huo ndiyo maana Yasmin alimkimbia Shihab

akarudi tena Unguja kwa Denge ambaye hakuwa na wivu (uk. 207).

Vilevile kifo cha Shihab kinatokana na wivu huohuo. Kutokana na jinsi

alivyokuwa anampenda na wivu juu yake (uk. 211), na baada ya kuona

ajali ya ndege ile aliyoamini imemchukua mke wake naye alipofika

nyumbani kwake alikata roho kwa kihoro (215).

Hivyo, msanii anatahadharisha jamii kuwa wivu katika ndoa ni kitu

chenye madhara. Kwa hiyo, ni lazima tuwe waangalifu katika

kudumisha ndoa zetu.

2. Mivutano

Mvutano huu upo katika mgongano kati ya wazee na vijana. Huu

mgongano unadhihirisha mifumo miwili inayotofautiana kiuchumi,

kifalsafa na kimawazo kwa ujumla.

Uwezo wa mwanaume au mwanamke kutaka amchague mtu wa kuishi

naye ni jambo la kisasa ambalo miaka michache iliyopita, lilileta

matatizo makubwa huku kwetu.

Riwaya ya Vuta n‟kuvute inajadili mgongano wa namna hiyo, yaani

baina ya wazazi na watoto wa kisasa akina Yasmin na Bukheti na

Page 7: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 7

wazazi wao. Mgongano anaouonesha katika riwaya hii unatokana na

utamaduni wa kisasa na vile unavyopingana na utamaduni wa wakati

uliopita. Ni mvutano wa ukale na usasa.

Kwa hiyo, tunaziona taratibu mbalimbali za kijadi zilizochakaa. Kwa

mfano, wazazi wa Yasmin kumwoza binti yao kwa mzee Raza ambaye

ni sawa na baba yake wa kumzaa kwa nguvu, ni desturi za zamani

ambazo zinaendelea kupigwa kumbo na wakati. Yasmin na Raza

hawakulingana kabisa kiumri. Raza alikuwa mzee hasa kama

anavyosema msanii (uk.10);

“Alikuwa ni mume asiyelingana naye hata kidogo, si kwa umri wala

tabia kwani wakati Yasmin ni kigoli wa miaka kumi na tano tu, mumewe

Bwana Raza alikuwa zee la miaka hamsini na mbili. Wakati bwana Raza

kasha zeeka, Yasmin alikuwa mtoto mbichi asiyeelewa kitu chochote”

Yasmin alikubaliana na matakwa ya wazazi wake ili kuwaridhisha,

lakini yeye mwenyewe hakuona fahari yoyote kuolewa na mzee

anayeweza kumzaa (uk. 1) msanii anasema;

“Yasmin hakupenda hata kidogo kuolewa na mume yule kwani yeye

mwenyewe angelipendelea sana kupata mume kijana kama yeye

mwenyewe. Alipenda kumpata mume ambaye yeyote angelimuona

angelisema: “Kweli Yasmin kapata mume.” Alikuwa anatamani

kupenda lakini hakumpata wa kumpenda. Yeye alitaka kijana wa

makamu yake ambaye angelimuonesha pendo nay eye angelimmiminia

pendo lote alilokuwa nalo moyoni mwake.”

Kutokana na Yasmin kulazimishwa na wazazi wake, hakumpenda kabisa

huyo mume wake, hata akayachukia maisha yake mwenyewe. Alitamani

kufa kuliko kuendelea kuishi na bwana yule, msanii anasema (uk. 2);

“Kutokumpenda Bwana Raza pamoja na utumishi wa kutwa dukani pale

kulimfanya Yasmin ayachukie maisha ya unyumba na mumewe.

Alitamani kufa kuliko kujitolea mwili wake kwa bwana yule….”

Ni kutokana na hali hiyo, ndiyo maana Yasmin alikosa adabu kwa

mume wake na baadaye alimtoroka mume wake huko Mombasa na

kurudi Unguja kuanza maisha mapya.

Kitendo cha Yasmin kumwacha mume wake kilileta mvutano mkubwa

sana kati yake na wazazi wake. Kwanza mjomba wake alimfukuza

Page 8: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 8

(uk.18) hali kadhalika na mama yake alimfukuza na kumtenga kabisa

(uk.42-43).

Hivyo msanii anaonesha kuwa mara nyingi ndoa za kulazimishwa

hazidumu na pia zinaleta mfarakano wa kifamilia kama ilivyokuwa kwa

Yasmin ambaye alitukanwa matusi mengi sana na wazazi wake kama

vile mwanaharamu, mhuni, na matusi mengine mengi.

Katika riwaya hii msanii anawashauri wazee wasiwadharau watoto wao

wa kisasa, kwa kufikiri kuwa ati hawaelewi wafanyayo. Watoto hawa

yaani Yasmin amejitolea mhanga kuonesha kuwa katika dunia hii ya leo

desturi za kizamani hazifai tena. Mtoto asichaguliwe mchumba na wazee

wao bali mtoto mwenyewe. Mapenzi na mahaba ya kweli hayashindwi

lakini yatashinda kila kitu katika kujitekeleza na kujikamilisha. Kabila,

rangi, jadi, dini, ukoo – haya yote hayana nguvu za kutosha mbele ya

mapenzi ya dhati kama anavyosema Yasmin (uk. 98);

“……mimi Bwana Raza simtaki! Nimekubali kukosana na wazee wangu,

kuhasimiana na jamaa zangu, kubughudhiwa na wote wanaonijua! Yote

nimeyakubali kwa kumkataa bwana Raza. Jambo la uke na ume ni

jambo la hiari jamani….”

Kutokana na hilo, msanii anaitaka jamii kukubaliana na mabadiliko

yanayokuja katika jamii, kung’ang’ania mambo yaliyopitwa na wakati ni

kuleta migongano ya bure kati ya wazee na vijana wa kisasa ambao

wanautaka huo uhuru. Vijana wa sasa wanataka uhuru katika suala zima

la mapenzi. Sio wachaguliwe na wazazi wao tena. Vijana wa sasa

wanachojali ni pendo la dhati na mahaba ya kudumu, wala wao hawajali

asili zao. Haja kubwa ni tabia njema na ubinadamu usio na ubaguzi wa

mambo hayo. Msanii anasisitiza hayo (uk. 170) anasema;

“…..pendo jambo la hiari, hawawezi kunilazimisha kumpenda

nisiyemtaka.”

Anachosisitiza msanii katika dondoo hiyo ni kuwa, suala la mapenzi

waachiwe wale wanaopendana na sio mila au wazee ndio waamue.

Ndiyo maana baada ya Yasmin kumwacha Raza aliandamana na Denge,

akamwacha akaolewa na Shihab naye akamwacha akaenda tena kwa

Denge kisha akaenda kuolewa na Bukheti. Huo ndio uhuru alioutaka

Page 9: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 9

Yasmin navijana wenzake wa rika kama lake, uhuru wa kutoingiliwa

katika suala la mapenzi.

3. Matabaka

Mtabaka ni dhamira nyingine inayojitokeza katika riwaya hii. Katika

kuonesha matabaka, msanii ameyagawa kwa kufuata rangi zao. Hapa

tuna Wazungu, Wahindi na Waafrika. Wazungu ni wale wakoloni wa

Kiingereza kama vile Inspekta Wright na wazungu wenzake. Wahindi

wanawakilishwa na akina Raza, Gulam na wengine, hawa walikuwa

wafanyabiashara. Waafrika wanawakilishwa na watu wa kawaida wote

kama vile Denge, Mwajuma, Mambo, Koplo Matata, Chande, Salehe,

Pazi, Huseni na wengine. Hawa walikuwa watu maskini, kula yao kwa

taabu, kulala kwao kwa taabu, n.k

Kuhusiana na aina tatu hizi za matabaka, kulikuwa na ubaguzi kati ya

matabaka haya. Ilikuwa si rahisi kwa Mzungu kuchanganyikana na

Mwafrika na vilevile ilikuwa si rahisi kwa Mhindi kuchanganyikana na

Mwafrika. Ndiyo maana baada ya Yasmin kukimbilia kwa Mwajuma,

Wahindi wenzake waliona amevunja mila na miiko ya Kihindi kama

asemavyo msanii (uk. 85);

“Kwa Wahindi Yasmin alikuwa asi, aliyevunja mila na miiko yao yote

kwa kuchanganyika na Waswahili.”

Kwa upande wa makazi, Waafrika waliishi ndani ya vibanda vidogo vya

uswahilini wakati Wazungu na Wahindi wanaishi kwenye marosheni na

majumba ya watukufu (uk. 98).

Vilevile kwa upande wa huduma zingine Waafrika walikwenda kwenye

maduka ya mchangani na darajani ambayo yaliuza bidhaa hafifu,

Wazungu na Wahindi waliingia ndani ya maduka ya Shangani na

Baghani ambayo yaliuza vitu kwa bei ghali na maduka hayo yalitoa

huduma za kila namna kwa hawa Wazungu na Wahindi (uk. 126).

Kwa upande wa starehe vilevile kulikuwa na ubaguzi kati ya Waafrika,

Wazungu na Wahindi. Wakati Wahindi wakistarehe Karimjee Club (uk.

130), Wazungu wao walistarehe English Club wakinywa bia za kila

aina, lakini Waafrika walikunywa gongo.

Page 10: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 10

Kwa ujumla, Wazungu na Wahindi walikuwa wanawanyonya,

wanawaonea na kuwanyanyasa Waafrika. Ni kutokana na hali hiyo,

ndiyo maana watu hawa walianzisha harakati za kutokomeza utawala

huo wa Kiingereza kwa kutawanya vitabu vyenye mawazo ya Marx na

wengine wenye msimamo kama wake huko Zanzibar.

Watu kama Denge waliamini kuwa, kwa kutumia vitabu hivyo pamoja

na magazeti yenye misimamo hiyohiyo, ndiyo itakayowaamsha

Waafrika ili waweze kupambana na ukoloni huo.

Mpaka mwisho wa kitabu, ukombozi wa Waafrika ulikuwa bado

haujapatikana na Waafrika wenyewe walikuwa bado hawajaelimishwa

vya kutosha. Vilevile watetezi wenyewe wamefungwa gerezani. Hapa

anachotaka kuonesha mtunzi ni kwamba, ukombozi si lelemama.

Unahitaji umoja na mshikamano, pamoja na kujitoa muhanga.

4. Dhana potofu na dharau

Hii ni dhamira ingine inayojitokeza katika riwaya hii. Kwa upande wa

dharau, tunaona Wazungu na Wahindi wakiwadharau Waafrika

kutokana na rangi yao nyeusi. Pamoja na umaskini wao. Msanii

anaonesha hayo (uk. 43) anasema;

“Sasa sina mwingine ila mimi na Waafrika, nd‟o ndugu zangu. Na

wanawadharau kwa sababu gani hasa? Wao si watu? Au kwa sababu

maskini? Ikiwa wao maskini na mimi nishakuwa maskini, nakula fadhila

zao, nakula fadhila za Mwajuma….”

Wakati wa ukoloni hali hii ya kumdharau Mwafrika ilikuwa imekithiri

sana katika bara hili la Afrika. Mwafrika aliwekwa katika daraja la tatu,

Mhindi la pili na Mzungu daraja la kwanza. Kwa upande wa huduma

Wazungu na Wahindi walipata huduma nzuri na Waafrika huduma duni.

Hali hii bado inaendelea hata baada ya uhuru, Wahindi na Wazungu

bado wanawadharau Waafrika.

Kutokana na dharau waliyonayo Wazungu kwa Waafrika, ilikuwa si

rahisi kwa Mwafrika kumwoa Mhindi au Mzungu. Hayo yanaoneshwa

(uk. 251). Msanii anasema;

“Hapana. Yeye mwenyeji wa Mombasa.”

“Mswahili?”

“Ndiyo”

Page 11: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 11

“Sasa Yasmin Bai unafikiri Gulam atakubali posa ya Mswahili”

“Uncle mimi n‟nachotaka ni stara. Nipate mume nistirike. Akiwa

Mswahili, akiwa Mhindi, akiwa Mzungu mimi kwangu ni sawasawa.

Wote hao ni watu.”

Yasmin alikuwa Mhindi lakini hakuwa na dharau kwa Waafrika. Aliona

nao ni watu kama watu wengine, hivyo nao wanahitaji kuheshimiwa

kama watu wengine. Katika (uk. 252) msanii anaonesha zaidi jinsi

isivyo rahisi kwa mhindi na Mwafrika (Mswahili) kuonana.

Kwa upande wa dhana potofu, kuna baadhi ya wahusika wana dhana

potofu hasa Wazungu na vibaraka wao. Koplo Matata na mabwana zake

wana dhana potofu juu ya mfumo wa kikomunisti na watu wake. Yeye

anaamini kuwa, ukomunisti ni mfumo ambao unakanusha kuwepo kwa

Mungu na dini. Vilevile kila kitu katika mfumo huu ni kugawana, msanii

anasema (uk. 100);

“Makoministi ni watu wasioamini Mungu wala dini, makafiri. Ni watu

wanaoamini kugawana kila kitu, kugawana wake zao, dada zao na hata

kugawana mama zao.”

Mawazo kama haya yanayotolewa na Koplo Matata, ambaye ni kijibwa

cha wakoloni, ni mawazo potofu. Wakoloni wanaupaka matope mfumo

huu kwani wanajua utawaamsha watawaliwa na kudai uhuru wao.

Mfumo huu unadai haki kwa kila mtu, usawa wa binadamu na mambo

mengine yanayotetea maslahi ya wengi.

Wakoloni kwa vile walitetea maslahi ya wachache waliwapiga vita sana

watu waliosomea Urusi na kuanza kuwapaka matope kuwa wanaleta

vurugu nchini. Katika kuhakikisha wananchi wa kawaida hawajihusishi

na harakati za kudai uhuru wao, wakoloni waliwaita wanaharakati hao

kama Komunisti ambao hawaamini Mungu hata dini, msanii anasema

(uk. 68);

“Sikiliza sista hawa wakoloni na vijibwa vyao ni watu wapumbavu

kabisa, kwao kila mtu ni Koministi; ukidai haki yako wewe Koministi,

ukisema kweli wewe Koministi. Ukipinga kutawaliwa wewe Koministi.

Lolote utakalolifanya madhali halina maslahi kwao basi wewe ni

Koministi. Maumau wa Kenya wameitwa makoministi. Wapigania uhuru

wa Algeria wameitwa Makoministi. Kila anayedai haki kwao ni

Page 12: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 12

Koministi, na sumu yao kubwa wanayoitumia ya kutaka kuwatenganisha

watu kama hao na wananchi wenzi wao ni kusema kwamba watu hao

wanaowaita Makoministi hawaamini Mungu.”

Haya ndiyo mawazo ya wakoloni na vijibwa vyao. Mawazo

yanayochochea chuki miongoni mwa wananchi wa kawaida dhidi ya

wapigania uhuru. Haya ni mawazo ambayo yamekusudiwa

kusambaratisha umoja na mshikamano miongoni mwa Waafrika. Ni

mawazo potofu, kwani yanamdumaza mtu kifikra na hivyo hawawezi

kujikomboa kutoka katika minyororo ya kugandamizwa, kunyonywa na

kuonewa na ukoloni huo.

5. Uvumilivu na ujasiri

Uvumilivuna ujasiri katika maisha ni dhamira mojawapo inayojadiliwa

katika riwaya hii. Kwanza, Yasmin alivumilia sana kuishi na Raza

mume wake wa kwanza ambaye alikuwa mzee sawa na mzee wake wa

kumzaa. Akiwa na Raza muda wote alishinda dukani, halafu kutokana

na kuwa aliozeshwa kwa nguvu na wazazi wake, hivyo hakumpenda

kabisa mume huyo. Uvumilivu wa jambo una kikomo chake, mwisho

Yasmin alishindwa na akaamua kuondoka na kumkimbia mume wake.

Vilevile Yasmin alimvumilia sana mume wake wa pili, Shihab. Shihab

baada ya kumwoa Yasmin alimuweka utawani kwa sababu ya wivu

wake. Yasmin aliyavumilia maisha hayo kama asemavyo msanii (uk.

198);

“Taratibu Yasmin aliyazoea maisha ya utawa, akawa mke wa nyumbani

aliyewekwa akakaa, akatulia na Shihab akawa anajisifu kwa rafiki zake

wote.”

Katika ndoa yake na Shihab, Yasmin muda wote alishinda ndani tu

kama mahabusu, hakuwa na ruhusa ya kwenda apendako. Yasmin

hakuwa na rafiki, shoga au jirani wa kuongea naye kama asemavyo

msanii (uk. 211);

“Nakuambia kaniweka ndani kama mwari, hata huyo mwari ana

afadhali sina shoga, sina jirani, sina jamaa, mimi na ndani na ndani na

mimi, siendi sirudi.”

Haya ndiyo maisha aliyoishi Yasmin na mume wake Shihab, maisha ya

utawa ambayo aliyavumilia. Waswahili husema mara nyingi mvumilivu

Page 13: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 13

hula mbivu lakini kwa Yasmin hakuona ukweli wowote, ndiyo maana

Yasmin aliomba ruhusa ya kwenda kuwaona wazazi wake na hakurudi

tena kwa Shihab kama Yasmin anavyosema (uk. 214);

“Sitorudi Abadan, sitorudi Abadan.”

Vilevile Yasmin aliyavumilia maisha aliyoishi kwa Mwajuma baada ya

kuachana na mume wake Raza na Shihab. Yalikuwa maisha magumu

sana kwake lakini aliyavumilia. Mwajuma na Yasmin waliishi maisha ya

dhiki na unyonge (uk. 21). Maisha yao yalitegemea rusuku kutoka kwa

marafiki na wahisani wa Mwajuma (uk. 33). Lakini Yasmin aliyavumilia

maisha haya yote.

Kwa upande wa tabaka la chini, waliishi maisha magumu sana, kula

kwao kulikuwa kwa tabu, kulala kwa tabu, lakini waliyavumilia maisha

haya. Kwa upande wa ujasiri tunaona kuwa kitendo cha Yasmin

kumkimbia mume wake wa kwanza ambaye vilevile hakumpenda,

kwani alilazimishwa na wazazi wake ni kitendo cha ujasiri. Yasmin

hakuona sababu kwanini aendelee kuishi na mume ambaye si chaguo

lake bali la wazazi wake.

Vilevile kitendo cha Yasmin kumkimbia Shihab, mume wake wa pili, ni

cha ujasiri kwani mume yule alikuwa na wivu mno na matokeo yake

ukamnyima uhuru Yasmin. Katika kutafuta uhuru huo, Yasmin

alimkimbia Shihab.

Kwa upande wa Denge na kundi lake walikuwa jasiri, ndiyo maana

waliendesha propaganda za kudai uhuru nchini Zanzibar kwa kutawanya

vitabu vya kijamaa na magazeti yanayopinga ukoloni. Walifuatwa sana

na wakoloni hao pamoja na vijibwa vyao lakini hawakuacha kudai haki

zao. Walifungwa gerezani lakini walipotoka msimamo wao ulikuwa

uleule wa kutaka wakoloni waondoke nchini mwao.

Hivyo, msanii anaonesha kuwa uvumilivu na ujasiri katika maisha ni

chachu ya maendeleo katika jamii. Na watu wasipokuwa wavumilivu

hukata tama haraka. Wasipokuwa jasiri huwa waoga. Matokeo yake ni

kurudisha nyuma maendeleo ya jamii husika.

6. Umoja na mshikamano

Page 14: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 14

Umoja na mshikamano ni dhamira ingine inayojadiliwa katika riwaya

hii. Msanii anaonesha kuwa, katika harakati zozote za kudai uhuru,

umoja na mshikamano ni kitu muhimu sana.

Denge na kundi lake yaani Mambo, Chande, Zanga, Salehe, Pazi,

Huseni na wengine walishirikiana sana katika harakati za kuutishia

utawala wa kikoloni nchini Zanzibar, walishirikiana kwa kugawa vitabu

vya akina Marx, magazeti pamoja na makaratasi mengine yaliyochapwa

maalumu kwa kupinga ukoloni Zanzibar.

Vilevile tunaona wafanyakazi wa Unguja walivyoonesha mshikamano

na umoja wao katika maandamano yaliyofanyika tarehe mosi Mei.

Katika maandamano hayo, wafanyakazi walikuwa wengi sana na

walibeba mabango na vitambaa vilivyoandikwa maneno ya kuhimiza

kuungana kwa wafanyakazi na kuulaani ukoloni (uk. 139).

Katika kuhakikisha kuwa Denge anatolewa gerezani, Mambo, Yasmin,

Mwajuma na Bukheti walishirikiana sana pamoja na Sukutua. Kutokana

na ushirikiano huo waliweza kumtorosha Denge kutoka Unguja na

kumpeleka Kenya ili kukwepa mkono wa serikali ya wakoloni (uk. 272-

274).

Vilevile Mwajuma na Yasmin walikuwa na umoja na mshikamano wa

hali ya juu sana katika maisha yao yote. Yasmin baada ya kwenda kuishi

kwa Mwajuma walishirikiana katika taabu na raha bila ubaguzi wowote

kati yao.

7. Usaliti

Usaliti ni dhamira nyingine inayojadiliwa na mwandishi katika riwaya

hii. Katika kujadili dhamira hii, msanii ameonesha jinsi Yasmin

alivyowasaliti wazazi wake kwa kumwacha mume wake Raza, na

matokeo yake ni kutengwa na jamaa zake. Yasmin hakumpenda kabisa

Raza kwa sababu hakuwa chaguo lake, bali alilazimishwa na wazazi

wake kuolewa naye na hatimaye akamwacha. Huu ni usaliti mzuri kwani

hapa msanii anaitahadharisha jamii kuwa si vizuri kumlazimisha mtoto

wako kuolewa na mtu asiyemtaka.

Usaliti mwingine ni ule wa Yasmin kwa Koplo Matata na wakubwa

wake (Wazungu). Koplo Matata alimweka Yasmin amchunguze Denge

pamoja na mienendo yake yote na alitakiwa kutoa taarifa zake polisi

Page 15: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 15

lakini badala ya kufanya kazi hiyo kwa siri alimwambia yote Denge (uk.

145-148). Kwa hiyo taarifa zote alizozipeleka Yasmin polisi zilipikwa

na Denge makusudi. Kama hiyo baada ya Yasmi kupewa karatasi za

kwenda kupeleka kwa Denge kwa siri ili ziwe kidhibiti cha kumtia

hatiani Yasmin alimkabidhi Denge karatasi hizo kama asemavyo

(uk.154);

“Waliingia ndani na baada ya kuingia tu, Yasmin alimkabidhi Denge

yale makaratasi. “Koplo Matata kanambia niyalete kwako, lakini wewe

usijue kama nimeyaleta.”

Usaliti wa Yasmin kwa Koplo Matata ni usaliti mzuri kwani

aliwaonesha wakoloni na vijibwa vyao kuwa hakuna hata mtu mmoja

katika nchi ile anayekubaliana na matendo yao. Vilevile aliwajulisha

kuwa katika harakati hizo Denge hayupo peke yake bali kuna wengine

pia, hivyo huo ni usaliti mzuri. Ni kutokana na usaliti huo ndio maana

Koplo Matata akafukuzwa kazi (uk. 161).

Usaliti mwingine ni wa Askari jela aliyewasaidia kina Mambo na

Yasmin kumtorosha Denge jela (uk. 143). Askari yule alikiuka maadili

ya kazi yake kwa kuwasaliti wakoloni na vibaraka wao na kuanza

kushirikiana na wapigania uhuru ambao walikuwa wakisakwa kila kona

ya nchi (uk. 245);

“Unamjua Yasmin?” aliuliza yule askari. Denge alinyamaza kimya,

hakumjibu kitu, usiwe na wasiwasi mimi mwenzako, najua mnataka

nini.”

Kwa upande wa wakoloni, huu ni usaliti mbaya lakini kwa wapigania

uhuru huu ni usaliti mzuri, kwani inaonesha kuwa hata walinzi wa

utawala huo wa kikoloni nao wamechoka kutawaliwa na kunyanyaswa

na ukoloni huo, ndiyo maana wanamua kuwasaidia wapigania uhuru.

Kama alivyofanya askari huyu kwa kusaidia kumtorosha Denge

gerezani.

Kwa upande mwingine, watu kama Koplo Matata na askari wengine wa

kiafrika waliomtumikia mkoloni. Hawa ni wasaliti wa Waafrika wenzao,

kwani walisaidiana na wakoloni katika kuwakandamiza na kuwaonea

wananchi wa kawaida. Hawa walikuwa vijibwa vya wakoloni na

walitumiwa na wakoloni kwa lengo la kutimiza malengo yao, ambayo ni

Page 16: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 16

kinyume kabisa na mahitaji ya wananchi wa kawaida. Akina Koplo

Matata walikuwa vibaraka wa wakoloni hao kwani walikuwa wanalipwa

kutokana na kazi zao hizo. Hivyo msanii anaitahadharisha jamii kuwa

suala la ukombozi si lelemama, lazima tuwe macho na wasaliti.

8. Nafasi ya mwanamke

Katika riwaya hii, mwanamke amechorwa katika nafasi mbalimbali.

Kwanza mwanamke amechorwa kama kiumbe duni asiye na maamuzi

yoyote katika jamii. Mfano mzuri ni pale Yasmin anapolazimishwa na

wazazi wake kuolewa na mtu asiyemtaka (uk. 1). Hili linaonesha kuwa

mwanamke ni kiumbe duni ambaye hana maamuzi yoyote katika jamii.

Vilevile Yasmin kuwekwa utawani na Shihab inaonesha uduni wa

mwanamke katika jamii. Shihab baada ya kumuoa Yasmin alimuweka

utawani, kila wakati akawa anafungwa ndani na hivyo kukosa uhuru

aliotakiwa kuupata (uk. 197).

Pili, mwanamke amechorwa kama mwanamapinduzi ambaye hataki

kung’ang’ania mila na desturi zilizopitwa na wakati. Mfano ni Yasmin

kwenda kutafuta uhuru wake baada ya kumkimbia Raza. Vilevile

tunamuona Yasmin akimwacha Shihab ambaye alimuweka utawani

baada ya kumuoa na kwenda kwa Denge na kuishi naye. Huu wote ni

uwanamapinduzi alioonesha Yasmin katika riwaya hii.

Tatu, mwanamke anaoneshwa kama mtu mpole na mwenye huruma.

Mfano mzuri ni Mwajuma ambaye alimsaidia sana Yasmin baada ya

kumuacha mume wake Raza. Mwajuma alimchukua Yasmin na akaanza

kuishi naye katika hali yake ya umaskini, wakasaidiana katika shida na

raha.

Nne, mwanamke anaoneshwa kama chombo cha starehe. Mfano ni

Mwajuma na Yasmin. Yasmin alikuwa akimstarehesha Denge na

Mwajuma kwa Mambo.

Ujumbe 1. Suala la mapenzi waachiwe wale wanaopendana na sio wazazi

kuwalazimisha watoto na uhuru huo lazima uwe na mipaka yake.

2. Mila na desturi zilizopitwa na wakati katika jamii hazina budi

kutupiliwa mbali katika jamii

Page 17: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 17

3. Uvumilivu, ujasiri, umoja na mshikamano ni mbinu muhimu za

kujikomboa

4. Ubaguzi wa rangi katika jamii ni kikwazo cha ujenzi wa jamii

5. Ushauri ni kitu muhimu, lakini lazima kuwe na mipaka yake

6. Ukweli humuweka mtu huru

Migogoro a) Yasmin v/s wazazi wake

b) Yasmin v/s Raza

c) Yasmin v/s Denge

d) Denge v/s serikali

e) Yasmin v/s Mwajuma

f) Yasmin v/s Koplo Matata

Msimamo Mwandishi anaonesha msimamo wa kimapinduzi kwani ameonesha

wazi kuwa jamii yetu ina baadhi ya mila na desturi zilizopitwa na

wakati, hivyo jamii lazima izifutilie mbali.

Falsafa

Mtunzi anaelekea kuamini kuwa mapenzi ya kweli yatapatikana katika

jamii ikiwa kutakuwa na uhuru wa kuchagua yule unayemtaka, badala

ya kulazimishwa na wazazi.

Fani

Muundo Mwandishi ametumia muundo wa moja kwa moja. Anaanza masimulizi

yake kwa kuelezea ndoa ya Raza na Yasmin, Yasmin kumwacha Raza,

Yasmin kwa Mwajuma, Yasmin kuolewa na Shihab na mwisho ndoa ya

Yasmin na Bukheti.

Mtindo Mwandishi ametumia mtindo wa monolojia (masimulizi) kwa kiasi

kikubwa ingawa pia kumejitokeza dayalojia. Katika kuukamilisha

mtindo wake msanii pia ametumia barua (uk. 168), nyimbo (uk. 85-86).

Pia nafsi zote tatu zimetumika.

Matumizi ya lugha

Page 18: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 18

Mwandishi ametumia lugha rahisi inayoeleweka hata kwa msomaji wa

kawaida, pamoja na misema, methali,tamathali za semi na mbinu

nyingine za kisanaa.

Misemo/Nahau a) Kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa (uk. 205)

b) Hujui kama mkono wa serikali ni mrefu (uk.71)

c) Wacha kutia chumvi (uk. 54)

d) Hana mbele wala nyuma (43)

e) Alipiga moyo konde (uk. 42)

f) Kuna dansa la kukata na shoka (uk.35)

g) Maji yamezidi unga (uk. 15)

Methali a) Asiyekubali kushindwa si mshindani (uk. 271)

b) Mwangaza mbili moja humponyoka (uk. 230)

c) Mzoea punda hapandi farasi (uk. 207)

d) Heri nusu shari kuliko shari kamili (uk.42)

Tamathali za semi

Tashibiha

1. Bwana Raza amekaa juu ya kiti amevimba kama kiboko (uk. 9)

2. Kijana yule aliyekuwa na macho makali kama kurunzi (uk. 13)

3. Ametoa macho kama chui (uk. 31)

4. Yeye na ndani na ndani nay eye kama mwari (uk. 33)

5. Mweupe kama mgonjwa wa safura (uk. 82)

Tashihisi 1. Chumbani mle watu wakaanza, hawaonani na mbu wakaanza

kujiandaa kwa karamu yao (uk. 194)

2. Nuru ya jua iliingia kwa hamaki chumbani mle na ilikashifu uchafu

wote wa chumba kile (uk. 49)

Tabaini 1. Mabinti waliolelewa wakaleleka, waliofunzwa wakafunzika,

waliotunzwa wakajitunza (uk. 85)

2. Hatua si hatua, mseto si mseto, ugali si ugali (193)

3. Sina shoga, sina jirani, sina jamaa, mimi na ndani na ndani na mimi,

sirudi sirudi (uk. 211)

Page 19: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 19

Mbinu nyingine za kisanaa

Takriri 1. Yeye hakuona isipokuwa Yasmin, Yasmin, Yasmin gani naye? (uk.

84)

2. Haweshi, ingia toka na kila wakija Denge, Denge na umewakosea nini

hasa? (uk. 86)

3. Haya tunywe, tunywe kwa afya ya mgeni wetu (uk. 26)

Mjalizo 1. Raha ya kuwa karibu naye wakaongea, wakacheka, wakafurahi (uk.

14)

2. Kula mkate wa ufuta, mkate wa maji, mkate wa mayai (uk. 80)

Mdokezo 1. Naona siku hizi…….(uk. 15)

2. Unani…..(uk. 16)

3. Mbona unaogopa dada, unafikiri si……(uk. 25)

4. Halafu kanigaia shilingi ishirini na ……..(uk. 67)

Tanakali sauti (Onomatopea) 1. Oooooh, Yasmin alijilaza kitandani akapumua kwa machofu ya safari

aliyokwenda (uk. 44)

2. Ngo, ngo, ngo, aligonga mlango (uk. 8)

Matumizi ya Kiingereza 1. Passing showa (uk. 17)

2. Brother, you fool (uk. 31)

3. Come on (uk. 32)

Wahusika

Yasmin Huyu ndiye mhusika mkuu katika riwaya hii. Yasmin alikuwa na kijuso

kidogo, macho makubwa, pua ndogo na nyembamba, alikuwa na nywele

nyingi. Vilevile alikuwa si mrefi lakini hakuwa mfupi.

Kwa tabia Yasmin alikuwa mwanamke aliyekuwa akipenda mabadiliko

ndiyo maana aliamua kumkikimbia mume wake wa kwanza

aliyelazimishwa na wazazi wake kuolewa naye.

Vilevile Yasmin alikuwa anapenda uhuru wa kuchagua mchumba wake

yeye mwenyewe na hakupenda wivu ndiyo maana alimkimbia Shihab

Page 20: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 20

kutokana na wivu wake. Yasmin alikuwa mvumilivu na mtu jasiri sana.

Aliyavumilia maisha magumu aliyoishi kwa Mwajuma, pamoja na

vituko vyote alivyokumbana navyo.

Wahusika wadogo

Mwajuma Alikuwa na uso mwembamba uliochongoka sawasawa na macho

remburembu. Alikuwa mrefu wa wastani. Mwajuma alikuwa mpole,

mkarimu na mwenye roho nzuri, na alikuwa tayari kumsaidia mtu

chochote kidogo alichokuwa nacho. Vilevile alikuwa na huruma sana

kwa Yasmin.

Kadhalika alikuwa ni msichana asiyependa kujikera nafsi yake na

aliutumia uhuru wake wa maisha kama alivyopenda. Alikuwa tayari

kufanya lolote lile ambalo alihisi litamletea furaha bila ya kujali

wengine watasema nini. Vilevile alikuwa mwanachama wa chama cha

“Cheusi dawa”, kikundi cha taarabu. Kutokana na huruma, upole na

ukarimu wake Mwajuma anafaa kuigwa na jamii.

Denge Alikuwa mrefu wa futi sita, mwembamba na mkakamavu. Umbile lake

ni la rangi ya maji ya kunde, pua yake ilikuwa ya wastani. Denge

alikuwa mwanaharakati wa kupinga utawala wa Mwingereza kisiwani

Unguja na Pemba. Katika harakati zake alisambaza vitabu vya Karl

Marx, magazeti yanayopinga ukoloni, pamoja na makaratasi ya

uchochezi dhidi ya ukoloni.

Denge ni mfano mzuri wa vijana ambao wako mstari wa mbele katika

harakati za kupambana na ukoloni hapa nchini, hivyo ni mfano mzuri wa

kuigwa.

Wahusika wengine katika riwaya hii ni Koplo Matata, Chande, Sukutua,

Raza, Salehe, Inspekta Wright, Shihab, Bukheti, n.k

Mandhari Riwaya hii imetumia mandhari halisi ya visiwa vya Unguja, maeneo ya

Tanga na Mombasa –Kenya. Lakini matukio mengi yamefanyika

Unguja. Vilevile kuna mandhari ya dukani, gerezani, baharini,

nyumbani, mtaani, baa, klabuni, n.k

Jina la kitabu

Page 21: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 21

Jina la kitabu linasadifu vizuri yaliyomo ndani ya kitabu hiki. Msanii

anaonesha mivutano mbalimbali katika kitabu hiki.

Kwanza kuna mvutano kati ya Yasmin na wazazi wake. Huu unatokana

na Yasmin kumwacha mume wake Raza ambaye wazazi wake

walimlazimisha aolewe naye.

Pili, kuna mvutano kati ya Yasmin na Raza. Yasmin hakumpenda kabisa

Raza, kwani kiumri Raza alikuwa ni sawa na baba yake wa kumzaa.

Hivyo katika maisha yake ya ndoa na Raza wakawa na mivutano ya kila

siku.

Tatu, kuna mvutano kati ya wakoloni na vijibwa vyao na wananchi wa

kawaida wakiwakilishwa na Denge, Chande, Sukutua, Mambo na

wengine. Hawa wanataka uhuru wa kujiamulia mambo yao wenyewe,

wanataka uhuru wa kumiliki njia kuu za uchumi badala ya wakoloni.

Nne, kuna mvutano kati ya Yasmin na Shihab. Huu unatokana na wivu

wa kimapenzi. Shihab alikuwa na wivu sana kwa mke wake, matokeo

yake akamnyima uhuru kwa kumweka utawani hatimaye Yasmin

akamkimbia.

Mwisho, kuna mivutano ya kinafsia ambayo iliwahusu wahusika

wenyewe. Hawa walikuwa na migongano ya kimawazo katika vichwa

vyao. Mfano ni Yasmin, Bukheti, Denge, n.k

Kufaulu kwa mwandishi - Mwandishi amefaulu sana kwa kuonesha mvutano wa vijana na

wazee.

- Kifani amefaulu sana hasa katika uteuzi mzuri wa lugha na ujenzi wa

wahusika. Lugha ni rahisi na inayoeleweka kwa kila mtu.

Kutofaulu kwa mwandishi - Suluhisho la mgogoro kati ya wakoloni na wananchi halijaoneshwa,

kwani tunaona tu wapigania uhuru wanawekwa ndani na wengine

wanatoroka kwenda nje ya nchi. Je, hawa watu watatumia mbinu gani

katika kujikomboa? Msanii hajaonesha.

- Matumizi ya lugha ya Kiingereza ni udhaifu mwingine wa msanii,

kwani mtu asiyefahamu lugha hiyo hataweza kuelewa ujumbe uliomo

kwa urahisi.

Page 22: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 22

- Msanii hajaonesha mipaka ya uhuru unaotakiwa kwa watoto wetu.

Kwa mfano, Yasmin ametumia uhuru wake wa kumchagua Shihab

lakini naye ndoa yao haikudumu. Au uhuru wa Yasmin wa kuolewa na

kuachika ndio uhuru unaotakiwa? Msanii hajaonesha vizuri.

UHAKIKI WA RIWA YA MFADHILI

KIDATO CHA 5 NA 6

KITABU – MFADHILI

MWANDISHI – HUSSEIN TUWA

WACHAPAJI – MACMILAN

MWAKA – 2007

UTANGULIZI

Mfadhili ni riwaya inayoongelea suala la mapenzi na ndoa, ikonesha

matatizo mbalimbali yanayotokana na mapenzi na ndoa na athari zake

kwa wanaohusika. Ni riwaya inayoongelea juu ya penzi zito baina ya

Gaddi Bullah na Dania Theobald, na jinsi penzi hilo lilivyoingiliwa na

mitihani na majaribu makubwa. Ni riwaya ambayo kwa mapana yake

inajadili kwa kiasi kikubwa suala la mapenzi na ndoa na athari zake kwa

jamii.

MAUDHUI

Dhamira

Mwandishi katika riwaya hii licha ya kujadili dhamira ya mapenzi na

ndoa, vilevile amejadili dhamira mbalimbali kama vile usaliti, umuhimu

wa uongozi bora, wizi wa mali ya umma, chuki, uzembe kazini, dharau,

uongo na ulaghai, n.k

Page 23: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 23

Dhamira kuu: Fadhila

Katika kujadili suala hili mwandishi anaonesha jinsi suala la

kufadhiliana lilivyomuhimu katika jamii bila ya kujali unayemfadhili

alikutendea mema au mabaya huko nyuma. Mfano mzuri katika suala

hili ni fadhila za Gaddi kwa Dania, ambapo mwandishi anaonesha jinsi

Gaddi alivyogeuka mfadhili wa ini kwa Dania na kuokoa maisha ya

Dania licha ya kutendwa unyama usiosemeka katika mahusiano yao.

Ukweli huu unadhihirishwa na Dkt. Viran alipokuwa akimshawishi

Dania juu ya kwenda kumuona Gaddi na hatimaye akamtobolea siri

kuwa Gaddi ndiye mfadhili wa ini lake.

Dhamira ndogondogo

1. Mapenzi na ndoa

Katika kujadili dhamira hii msanii ameainisha aina kuu mbili za

mapenzi na ndoa; mapenzi ya kweli na mapenzi ya uongo, ndoa ya kweli

na ya uongo.

Tukianza na mapenzi ya kweli, haya yanaoneshwa kati ya Gaddi

Bullah na dada yake Bi. Hanuna. Hawa walipendana kwelikweli na ndio

maana mmoja akiwa na tatizo linakuwa ni tatizo la wote wawili. Mtu

akimwudhi Gaddi amemwudhi na dada yake Bi. Hanuna, na

walisaidiana katika shida zao zote.

Mapenzi mengine ya kweli ni kati ya Gaddi na Dania. Mwanzoni

walipendana hasa; mchana walikuwa wakienda kula chakula pamoja na

hata walifikia hatua ya kutembeleana. Gaddi katika kuonesha mapenzi

kwa Dania, alimsaidia kwa kila hali hata wakati war aha na shida (uk.

101-106). Hata baada ya Dania, kumsaliti Gaddi, bado alimpenda na

hata akamfadhili baada ya kusalitiwa na Jerry kwa mara ya pili (uk. 137-

139).

Page 24: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 24

Pia kuna mapenzi ya kweli kati ya Gaddi na Junior, mtoto wa Dania.

Pamoja na kwamba Junior hakuwa mtoto wake, Gaddi alimpenda sana

na ndio maana baada ya Junior kuumia mkono aliyempeleka hospitalini

ni Gaddi na wala si Baba yake Jerry (uk. 118). Vilevile, Junior aliposikia

taarifa za ugonjwa wa Gaddi alilia na wakati wa kifo cha Gaddi wosia

pekee alioutoa kwa Dania ni kumtunza vizuri Junior, anasema (uk. 146);

“Gaddi akimgeukia Dania. “Junior Dania……..Junior mtunze vizuri

Junior! Umepata bahati ya kue…ndelea kuishi ili umtunze

mwan…na….o!” Gaddi aliyasema yote hayo kutokana na mapenzi

aliyokuwa nayo kwa Junior.

Mapenzi mengine ya kweli ni ya Mama Mlole (Bi. Fausta) kwa

wafanyakazi wa chini yake kama Gaddi na Dania. Pamoja na Gaddi

kuharibu kazi, mama Mlole alimtetea sana asifukuzwe kazi bali

aangaliwe upya (uk. 69-71). Vilevile alimtetea sana Dania asifutwe kazi

kipindi anaumwa. Mama Mlole ni mfano wa viongozi wenye mapenzi

ya kweli kwa wale anaowaongoza.

Vilevile kuna mapenzi ya kweli kati ya Nunu na Dania. Nunu alikuwa

bega kwa bega na Dania wakati wa maandalizi ya harusi ya Dania na

Jerry. Nunu alimsaidia sana Dania. Vilevile alimshauri sana Dania

asirudiane na Jerry kwa vile alimsaliti mara ya kwanza (uk. 113-115).

Pia alimsaidia sana kumlea mtoto wake Junior wakati Dania yuko kituo

cha kuponya walevi (uk. 115). Kama hiyo haitoshi, Nunu alikuwa bega

kwa bega na wazazi wa Dania wakati wa ugonjwa wake na hata

akamsaidia kumtafuta Gaddi na Bi. Hanuna ili awaombe msamaha kwa

yote aliyowatendea.

Kuna mapenzi ya kweli kati ya Nunu na Boaz. Hawa walipendana kwa

dhati na ndiyo maana shida ya Nunu ilikuwa shida ya Boaz pia. Ni

kutokana na mapenzi ya dhati waliyokuwa nayo ndiyo maana

Page 25: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 25

walisaidiana kwa hali na mali, kwa heri na shari katika kumtafuta Gaddi

aliyekuwa anatakiwa na rafiki yake Dania. Hata wakafikia hatua ya

kuhatarisha maisha yao kwa kumteka nyara Bi. Hanuna kwa lengo la

kumsaidia Dania (uk. 36-56).

Mapenzi mengine ya kweli ni kati ya Dakta Viran na Gaddi. Hawa

walipendana hasa, na ndiyo maana Viran alimsaidia Gaddi katika

matatizo mbalimbali. Kwa mfano, kumtibu mpenzi wake Dania,

kumtibu yeye mwenyewe alipopata shinikizo la moyo, baada ya

kuachwa na Dania na mwisho Viran anakuwa mpatanishi kati ya Gaddi

na Dania na Nunu kutokana na ugomvi wa kuachwa kwa Gaddi na

mpenzi wake Dania. Vilevile tunamwona Dakta Viran anavyohangaika

kuokoa maisha ya Gaddi kutokana na ugonjwa aliokuwa anaumwa

ingawa hakufanikiwa. Haya yote aliyafanya kwa sababu alimpenda

Gaddi kwa dhati na Gaddi vilevile alimpenda Viran.

Vilevile kuna mapenzi ya dhati kati ya wazazi wa Dania kwa mtoto wao

Dania. Wazazi wake Dania walimpenda sana mtoto wao, ndiyo maana

wakati wa shida za Dania walimsaidia kwa hali na mali hadi

wakampeleka Afrika Kusini kutibiwa ugonjwa wake wa ulevi. Wakati

wa ugonjwa wake wa ini, wazazi wake walimsaidia sana mpaka hatua

ya kuweka matangazo redioni ili kumsaidia mtoto wao kwa mtu ambaye

angejitolea ini. Gharama zote walikuwa tayari kumlipa mtu yeyote

ambaye angejitokeza kufanya hivyo. Hayo ni mapenzi ya dhati ya

wazazi kwa binti yao.

Mapenzi mengine ya dhati ni kati ya Nunu na Gaddi. Nunu alimpenda

Gaddi kwa dhati, ndiyo maana alimshauri sana Dania asimwache Gaddi

na kurudiana na Jerry. Nunu alimkatalia Dania asirudiane na Jerry si

kwa sababu alimsaliti, bali awe na Gaddi aliyemsaidia wakati wa shida

Page 26: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 26

(uk. 114-115). Vilevile Gaddi alimpenda Nunu kama rafiki mzuri

anasema (uk. 146);

“………Nunu”… “A…Abee! Nunu aliitikia kwa upole huku akitiririkwa

na machozi “wewe…..ni rafiki…mzuri….. “Gaddi alimwambia……”

Baada ya kifo cha Gaddi, Nunu pamoja na wengine wote walilia sana

kuonesha mapenzi yao kwa Gaddi.

Mapenzi ya uongo

Mapenzi ya uongo ni kati ya Jerry kwa Dania. Jerry inaonesha

hakumpenda kwa dhati Dania na ndiyo maana alimsaliti wakati wa

harusi yao. Jerry alipenda zaidi masomo kuliko kufunga ndoa na Dania.

Aliona maandalizi ya harusi lakini akaondoka kwenda Marekani kusoma

kwa ahadi ya kurudi siku ya harusi. Lakini siku ilipofika Jerry

hakuonekana na hivyo ndoa ikashindikana kufungwa.

Vilevile kitendo cha Jerry kumtoroka Dania akiwa hospitalini pindi

ambapo msaada wake ulitakiwa ni usaliti unaothibitisha kuwa hakuwa

na mapenzi ya dhati kwa Dania. Jerry alitakiwa kumfadhili Dania ini ili

kuokoa maisha yake, lakini siku ilipofika hakufika hospitalini na

hawakumwona tena (uk. 133-135)

Mapenzi mengine ya uongo ni kati ya rafiki yake Gaddi kwa Gaddi.

Huyu hakuwa rafiki wa kweli kwani alimshauri vibaya Gaddi (uk. 64).

Kana kwamba hiyo haikutosha, alimtorosha mke wa Gaddi na

kumuweka kinyumba (uk. 64-67). Kuhusu suala la ndoa, nazo zipo za

aina mbili ambazo ni ndoa za kweli na ndoa za uongo. Ndoa ya kweli ni

kati ya Gaddi kwa Nyambuja. Gaddi alimpenda sana mkewe na alimjali

kwa kila kitu. Lakini mke wake hakuwa na mapenzi ya dhati katika ndoa

yao. Baada ya mwaka mmoja tu wa ndoa yao, Nyambuja alianza

kumsaliti mumewe kwa kuchelewa kurudi nyumbani, kusafiri bila

Page 27: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 27

taarifa kwa mume wake na mwisho akamwacha na kwenda kuolewa na

rafiki wa mumewe (uk. 60-67).

2. Usaliti

Usaliti ni dhamira ingine ambayo imejadiliwa sana katika riwaya hii

ya Mfadhili. Katika kujadili dhamira hii, msanii anaonesha jinsi watu

mbalimbali wanavyosaliti wenzao na athari za usaliti huo kwa wahusika.

Kwanza tunaoneshwa jinsi Nyambuja alivyomsaliti mume wake na

kwenda kuolewa na rafiki wa mumewe. Kwa upande mwingine rafiki

wa Gaddi alimsaliti Gaddi na kumchukua mke wa rafiki yake. Usaliti

huu ulisababisha Gaddi kupoteza umakini kazini kutokana na msongo

wa mawazo na kuishia kupewa barua ya onyo kwa kuidhinisha malipo

hewa ya matengenezo ya magari ya kampuni (uk. 62-63).

Usaliti mwingine ni ule wa Afisa usafirishaji kwa kumsaliti Gaddi

kazini. Huyu aliandaa vocha ya malipo hewa na kuipeleka kwa Gaddi

ikasainiwe. Matokeo ya usaliti huo ni Gaddi kushushwa cheo na

kuhamishwa chake cha kazi (uk. 71-72)

Usaliti mwingine ni wa Dania kwa Gaddi. Kwanza Dania alimsaliti

Gaddi kwa kutoandaa ripoti aliyotakiwa kuiandaa kwa ajili ya kusomwa

kwenye kikao cha wakuu wa vitengo. Dania hakuandaa ripoti hiyo, na

siku ya kikao hakuonekana kazini hadi muda wa kikao ulipoanza saa

mbili na nusu Asubuhi (uk. 77-79). Matokeo yake Gaddi alimlima barua

ya onyo na kumtaka ajieleze. Lakini kwa busara za Mama Mlole

alisuluhisha mgogoro huu.

Pili, Dania alimsaliti Gaddi kwa kumwacha wakiwa katika mapenzi

mazito na wakati huohuo wanajiandaa kufunga ndoa. Dania alimwacha

Gaddi na kurudiana na Jerry ambaye alimsaliti siku ya harusi yake.

Page 28: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 28

Matokeo ya usaliti huo ni Gaddi kupata ugonjwa wa shinikizo la moyo,

kupigana na Jerry, na dada yake Bi. Hanuna kuwekwa ndani (polisi).

Usaliti wa Jerry kwa Dania. Kwanza alimsaliti Dania wakati wa harusi

yao. Jerry hakuhudhuria harusi hiyo, alikuwa Marekani na wakati

huohuo aliahidi kuwa angehudhuria (uk. 83-85). Ni kutokana na usaliti

huo, harusi ilishindikana na kumfanya Dania aingie kwenye matatizo

makubwa ya ulevi wa pombe kali (uk. 87). Kutokana na ulevi huo Dania

alipata ugonjwa wa ini.

Pia Jerry alimsaliti Dania akiwa mgonjwa mahututi hospitalini kwa

kuahidi kutoa ini baada ya vipimo kuonesha inawezekana, lakini

hakufanya hivyo. Kwanza, hakumsaidia kwa kumpa ini. Pili akamtoroka

akiwa kitandani hospitalini (uk. 133-134). Katika kuokoa maisha ya

Dania, pamoja na kwamba alimsaliti, Gaddi alijitokeza kuwa mfadhili

wa ini kwa Dania.

Katika riwaya hii mtunzi anaonesha kuwa wasaliti katika jamii wapo,

anaweza kuwa mkeo (Nyambuja), mpenzi wako (Dania), mfanyakazi

mwenzako (Afisa usafirishaji), mumeo (Jerry) au rafiki yako wa karibu

(rafiki wa Gaddi), hivyo tuwe macho na wasaliti, kwani wanaharibu

mapenzi ya watu na kazi zao.

3. Umuhimu wa uongozi mzuri

Mwandishi amejadili dhamira hii katika riwaya yake ya Mfadhili. Katika

kujadili dhamira hii, msanii anamtumia mhusika Mama Mlole. Mama

Mlole alikuwa kiongozi mzuri ambaye aliwajali wale aliowasimamia,

jambo ambalo linasaidia kuongeza ufanisi katika kazi yake.

Gaddi Bullah alipopata matatizo kazini yaliyotokana na athari za

kuachwa na mke wake, Mama Mlole alimtetea sana asifukuzwe kazi

baada ya kumweleza matatizo yake (uk. 70). Na ni Mama Mlole

Page 29: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 29

huyohuyo aliyependekeza Gaddi ahamishiwe Dar es Salaam ili

aangaliwe zaidi badala ya kufukuzwa kazi. Mama Mlole alifanya hivyo

kutokana na utendaji mzuri wa kazi aliokuwa nao Gaddi mwanzoni

kabla ya kukumbwa na matatizo yaliyomsibu.

Vilevile ni Mama Mlole aliyemtetea Dania asifukuzwe kazi baada ya

kuachwa na Jerry. Baada ya kuvunjika kwa ndoa yake na Jerry, utendaji

wake wa kazi uliathirika sana. Alifikia hatua ya kuja ofisini akiwa

amelewa (uk. 88) na hatua aliyofikia ilikuwa aachishwe kazi. Lakini

Mama Mlole kama Afisa utumishi wa kampuni alimtetea sana na

akapendekeza apewe likizo bila malipo kwa muda wote atakaokuwa

kwenye matibabu ya ulevi wake (uk. 88)

Kiongozi mzuri daima hupendwa na watu anaowaongoza na mara nyingi

ufanisi wake kazini vilevile huwa mzuri. Hapa msanii anachotaka

kuifundisha jamii ni kuwa cheo ni dhamana lazima kukitumia kwa faida

ya watu wote na sio kunyanyasa wengine.

4. Bidii katika kazi

Bidii katika kazi ni dhamira ingine inayojitokeza katika riwaya hii

ya Mfadhili. Katika kujadili dhamira hii, mwandishi anaonesha kuwa ili

kuleta maendeleo katika jamii lazima kuwa na bidii katika kazi.

Katika kujadili hili mtunzi anamtumia Gaddi Bullah ambaye alionesha

kuwa kijana mdogo lakini mchapakazi mzuri. Alipendwa sana na

wafanyakazi wote waliokuwa chini yake na hata wakuu wake wa kazi

huko makao makuu (uk. 59).

Pili tuna Dania, mwanzoni alikuwa mmoja kati ya wafanyakazi wenye

nidhamu, bidii na ushirikiano mkubwa hapo makao makuu. Dania akiwa

anatoka kwenye familia ya kitajiri. Aliwaheshimu wafanyakazi wote na

wala hakuruhusu utajiri wa wazazi wake umpe kichwa. Kutokana na

Page 30: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 30

utendaji wake mzuri wa kazi, ndiyo maana alipewa wadhifa wa

kuongoza kitengo muhimu cha kukusanya madeni cha kampuni na

kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.

Katika kujadili zaidi dhamira hii, msanii anaonesha kuwa matatizo ya

mtu binafsi au hata ya kifamilia yanaweza kupunguza bidii na ufanisi wa

mtu katika kazi anayoifanya. Kama ilivyokuwa kwa Gaddi na Dania.

Gaddi alipoachwa na mke wake alichanganyikiwa na kupoteza umakini

katika kazi hata akasaini na kuidhinisha cheki hewa (uk. 63) ambayo

ilimletea matatizo makubwa kazini kwake.

Vilevile Dania baada ya kuachwa na Jerry, ufanisi wake wa kazi

ulipingua na kufanya kazi hovyo. Kwanza, utendaji wake uliathirika

vibaya sana. Alifika ofisini akiwa amelewa. Kutokana na kitendo hicho,

wazazi wake ilibidi wampeleke kwenye kituo maalumu cha kutibu watu

wenye tatizo la ulevi wa kupindukia huko Afrika Kusini (uk. 88).

Kwa ufupi msanii anaonesha kuwa bidii katika kazi ni kichocheo cha

maendeleo ya jamii. Pindi mtu anapokumbwa na matatizo, mara nyingi

ufanisi wake wa kazi hupungua na hupata matatizo. Matatizo hayo

yanaweza kuwa ya kufukuzwa kazi au kushushwa cheo kama

ilivyokuwa kwa Gaddi. Vilevile matatizo yanaweza kumfanya mtu

achanganyikiwe, aache kazi na kuuza kila kitu kama alivyofanya Gaddi

baada ya kuachwa na Dania. Kwa hiyo, mwandishi anaitahadharisha

jamii kuepukana na matatizo.

5. Chuki

Chuki ni dhamira ingine inayojadiliwa katika riwaya ya Mfadhili. Katika

kujadili dhamira hii, msanii anaonesha wahusika mbalimbali na chuki

zao binafsi zinazosababishwa na mambo mbalimbali.

Page 31: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 31

Kwanza, Bi. Hanuna alikuwa na chuki na Nunu kwa sababu ya Dania.

Kitendo cha Dania kumuacha kaka yake, Gaddi wakati wako katika

mapenzi ya raha na furaha. Kitendo hiki kilimuudhi sana Bi. Hanuna.

Hata Nunu alipokwenda kwake kuomba msaada wa kumpata Gaddi

alikataa katakata. Pia shida yao alikataa hata kuisikiliza kutokana na

chuki aliyokuwa nayo, Bi. Hanuna anasema (uk. 25);

“Shida?” Aliguna kwa kebehi”. Eti shida! Mnaijua shida ninyi? Hebu

niondokee hapa sasa hivi mwana asiye haya we! Shida niulize mimi

mliyenisweka gerezani….”

Hata Nunu anapojitetea kuwa ya zamani wayaache wagange yaliyopo,

Bi. Hanuna anamkatalia Nunu (uk. 24);

Bi. Hanuna vilevile alikuwa na chuki na Dania. Hii ilikuwa baada ya

kumwacha kaka yake, Gaddi na kumweka ndani (gerezani) Bi. Hanuna.

Hapo ndipo chuki ya Bi. Hanuna ilipoanza kwa Dania kama anavyosema

(uk. 125);

“Na ni hapo ndipo chuki ya Bi. Hanuna dhidi ya Dania Theobald

ilipodhihiri moyoni mwake. Wakati akimtazama ndugu yake akisema

maneno yake na jinsi sura yake ilivyokuwa na uchungu na kukata tama,

Bi. Hanuna alijua kuwa Dania Theobald atakuwa adui yake milele!!”

Msanii anaendelea kuonesha kuwa, jinsi Bi. Hanuna alivyokuwa

anamwona mdogo wake akiteseka ndivyo alivyozidi kumchukia Dania,

msanii anasema (uk. 126):

Bi. Hanuna alimueleza. Na kadiri alivyokuwa anamweleza kisa kile

ndivyo ghadhabu dhidi ya Dania ilivyozidi kumpanda”

Page 32: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 32

Ni kutokana na chuki hiyo ndiyo maana Bi. Hanuna alikwenda kwa

Dania na kumtukana matusi mengi ambayo yalisababisha vurugu kubwa.

Msanii anaonesha chuki ya Bi. Hanuna kwa Dania hivi (uk. 126-127)

Wewe ni Malaya usiye na haya baradhuli na hayawani! Hukumstahili

mdogo wangu hata kidogo! Bi. Hanuna alimwambia kwa hamasa na

muda huo Jerry alitoka ndani na kuanza kumfukuza huku akimtukana”

Kutokana na tukio hilo, Bi. Hanuna alikamatwa na polisi na kuwekwa

rumande kwa kosa la shambulizi. Bi. Hanuna akalala rumande siku ile.

Wakati mdogo wake amelala hospitalini yeye alikuwa amelala rumande

na aliumia sana na akazidisha chuki yake kwa Dania kama anavyosema

msanii (uk. 127);

“Kwa hakika chuki yake kwa Dania iliongezeka maradufu, na aliapa

kumchukia kwa uhai wake wote uliobakia.”

Ni kutokana na chuki hiyo kwa Dania ndiyo maana alikataa kuwaeleza

Nunu na Boaz, Gaddi alipo. Vilevile alikataa hata kupeleka barua kwa

Gaddi iliyotoka kwa Dania ya kuomba msamaha (uk. 24) mpaka

alipomuona kweli Dania akiwa katika hali ya kukatisha tama ya kuishi

(uk. 56).

Mhusika mwingine aliyeonesha chuki waziwazi kwa wahusika wengine

ni Dania. Dania alikuwa na chuki na Gaddi Bullah kwa kumwona kama

mtu aliyemnyang’anya cheo chake, msanii anasema (uk. 75);

“Chuki kubwa ilijengeka moyoni mwa Dania dhidi ya Gaddi Bullah.

Kwake, Gaddi alikuwa ni mtu aliyemchukulia wadhifa wake na

kumdhalilisha kama mwanamke, na alimwona ni mmoja tu kati ya

wanaume wengi ambao kwake walikuwa wanyama na wahalifu.”

Page 33: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 33

Dania anamwona Gaddi kama mnyama au mhalifu kutokana na chuki.

Matokeo yake alijikuta akizidi kumchukia zaidi na zaidi. Chuki

haikuishia ofisini tu bali hata kwenye sehemu za starehe hakutaka hata

kukaa naye, mpaka alifikia hatua ya kumfukuza kwenye meza

aliyokuwa amekaa na mtoto wake Junior kwenye baa, msanii anasema

(uk. 76);

“Naomba utupishe….hapa ni mahali petu! Dania alimjibu kifedhuli”

Kutokana na chuki aliyokuwa nayo Dania kwa Gaddi, anafikia hatua ya

kumharibia kazi ili aonekane hafai (uk. 77-79). Matokeo yake Dania

akaandikiwa barua kali na Gaddi ya onyo na kumtaka ajieleze ni

kwanini asifukuzwe kazi (uk. 79).

Dania vilevile alikuwa na chuki na Jerry hasa baada ya kumwacha

wakati maandalizi yote ya harusi yao yamekamilika. Kitendo cha Jerry

kushindwa kuja kwenye harusi kama alivyoahidi kilimwudhi sana

Dania. Dania alilia sana. Hata Jerry aliporudi kutoka Marekani

alimfukuza kama mmbwa nyumbani kwake, msanii anasema (uk. 107);

“Toka! Dania alimfokea kwa ukali huku akimwonyesha sehemu ulipo

mlango wa kutokea kwa kidole chake….Nasema ondoka Jerry na sitaki

uje tena kunifuata hapa, wala popote pale niwapo! Ondoka!”

Nunu naye alikuwa na chuki na Jerry kwa sababu ya kumwacha rafiki

yake Dania. Hata Jerry alipokwenda kwake kuomba msaada wa

kumshawishi Dania alimfukuza na kumtaka asirudi tena nyumbani

kwake (uk. 109);

Wazazi wa Dania nao walikuwa na chuki na Jerry kwa sababu ya

kumsaliti mtoto wao. Jerry alipokwenda kwao kuwaomba msamaha

walikuwa wakali zaidi ya mbogo na walimfukuza nyumbani kwao (uk.

109-110).

Page 34: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 34

Msanii katika kujadili dhamira hii ya chuki, anaonesha kuwa wenye

chuki kuna wakati watasameheana. Bi. Hanuna anamsamehe Dania,

Gaddi vilevile anamsamehe Dania, Bi. Hanuna anamsamehe Nunu,

halafu Dania anamsamehe Jerry ingawa msamaha huo ulileta matatizo

mengine kwa Gaddi na Bi. Hanuna. Hivyo, msanii anaonesha kuwa

umsamehe mtu aliyekufanyia makosa ili uishi kwa amani na utulivu.

6. Dharau

Dharau ni dhamira inayojitokeza katika riwaya hii ya Mfadhili. Katika

kujadili dhamira hii, msanii anamtumia Nyambuja kama mtu mwenye

dharau kwa mumewe. Nyambuja hakuwa na upendo wowote kwa mume

wake na ndio maana alikuwa anamdharau. Hata akiulizwa swali na

mumewe majibu aliyokuwa anayatoa yalikuwa yamejaa dharau tupu (uk.

60). Vilevile kitendo cha Nyambuja kusafiri safari za ghafla na

kumtaarifu mumewe kwa simu ni sehemu ya dharau. Gaddi kama mume

wake alistahili kuagwa kwa kufuata taratibu za mume na mke zilivyo,

lakini Nyambuja hakujua hilo ila dharau ilitawala (uk. 61).

Kitendo cha Nyambuja kufanya mapenzi na rafiki yake Gaddi na

kumwacha nayo ni dharau ya hali ya juu. Hata barua aliyomwandikia

Gaddi (uk. 65) ni barua iliyojaa dharau ya Nyambuja kwa Gaddi. Mara

nyingi mwanamke mwenye dharau ndani ya nyumba kwa mume wake

husababisha kuvunjika kwa ndoa na ndivyo ilivyotokea kwa Gaddi na

Nyambuja.

Mhusika mwingine anayeonesha kuwa na dharau ni Dania. Kwanza

alimdharau Gaddi siku ya kwanza tu alipomkuta ofisini kwake. Kitendo

cha Dania kumwita Gaddi kwamba wewe ni “Gaidi Bullah” (uk. 73) ni

sehemu ya dharau aliyoionesha kwa Gaddi. Vilevile kitendo cha Dania

kumfukuza Gaddi kwenye meza aliyokuwa amekaa na mtoto wake

Junior kwenye baa ni sehemu ya dharau. Dania alimfukuza Gaddi

Page 35: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 35

kwenye meza kama mbwa mwizi; ambapo katika hali ya kawaida

asingefanya hivyo, au angemwomba kwa upole awapishe na sio kwa

kumkaripia kama mtoto mdogo, hii yote ni dharau.

Vilevile Dania alionesha dharau ya hali ya juu baada ya kumwacha na

kurudi kwa Jerry. Majibu aliyokuwa anamjibu Gaddi yalikuwa majibu

ya kijeuri na dharau tupu (120-123). Lakini msanii anaitahadharisha

jamii kuwa makini juu ya suala la dharau kwani unayemdharau leo

huwezi kujua baadaye anaweza kukufaa. Dania alimwacha Gaddi,

alimdharau, lakini baadaye akawa mfadhili wa ini lake baada ya

kutelekezwa na Jerry kwa mara ya pili akiwa mgonjwa mahututi

hospitalini. Hivyo, tuepuke dharau kwani hazina maana yoyote.

7. Nafasi ya mwanamke katika jamii

Katika riwaya hii, mwanamke amechorwa katika nafasi mbbalimbali.

Kwanza amechorwa kama kiumbe asiye na msimamo katika kufanya

maamuzi. Hapa tunamuona Dania akiwa na maamuzi yasiyofaa, kwa

kutokuwa na msimamo na kuamua tena kumrudia Jerry ambaye

alimuumiza mwanzoni.

Pili, mwanamke amechorwa kama mtu mwenye huruma na mshauri

mzuri. Mfano mzuri ni Nunu alivyomhurumia rafiki yake, Dania na

kumhangaikia kwa hali na mali. Vilevile tunaoneshwa jinsi alivyokuwa

mshauri mzuri wa Dania.

Tatu, mwanamke amechorwa kama mtu katili na msaliti. Hapa

tunamuona Nyambuja na Dania walivyomtenda vibaya Gaddi na

hatimaye kumsaliti na kwenda kwa wanaume wengine.

Nne, mwanamke amechorwa kama mtu jasiri. Hapa tunamuona Nunu

ambaye alifanya kazi kubwa sana ya kumpatanisha Dania na Gaddi hata

Page 36: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 36

akafikia hatua ya kumteka kwa nguvu dada yke Gaddi, Bi. Hanuna, ili

aweze kuwasaidia kumpata Gaddi.

Tano, mwanamke amechorwa kama mtu mwenye upendo, moyo wa

huruma na wa kusaidia. Hapa tunamuona Bi. Hanuna alivyokuwa na

upendo kwa kaka yake Gaddi, halafu pia tunamuona Mama Mlole

alivyokuwa na upendo kwa wafanyakazi wa chini yake.

Ujumbe

1. Rafiki wa kweli ni yule anayekusaidia au kukujali wakati wa shida.

2. Si kila king’aacho ni dhahabu

3. Mtu anapotenda kosa, lazima akubali kutubu kosa

4. Ni vigumu kumpata mtu mwenye mapenzi ya kweli au

atakayekupenda kama unavyompenda wewe

5. Bidii na ufanisi katika kazi ni chanzo cha maendeleo katika jamii

6. Matatizo, majaribu, chuki na dharau ni vitu vya kutegemewa

kwenye mapenzi na ndoa.

7. Kipenda roho hula nyama mbichi

Falsafa

Msanii anaamini kuwa katika suala la mapenzi kuna kupenda na

kutopendwa, kuna kuoa na kuachwa. Hivyo, ni vigumu kupata mtu

mwenye mapenzi ya dhati.

Msimamo

Msimamo wa mwandishi ni wa kimapinduzi, kwani anaonesha wazi

kuwa katika suala la mapenzi na ndoa kuna changamoto zake. Watu

Page 37: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 37

lazima tukubali kusameheana kwani hujui ni yupi atakayekusaidia

wakati wa shida.

Mtazamo

Mwandishi anaonekana kuwa na mtazamo wa kiyakinifu, kwani

ameyaweka mambo wazi kwa kuonesha kuwa mapenzi ya dhati yapo

kwa akupendaye asiyekupenda usimtegemee anaweza kukuumiza.

Migogoro

1. Mgogoro kati ya Gaddi na Nyambuja

2. Mgogoro kati ya Gaddi na Dania

3. Mgogoro kati ya Gaddi na Jerry

4. Mgogoro kati ya Nunu, Boaz na Bi. Hanuna

5. Mgogoro kati ya Dania na Jerry

6. Mgogoro kati ya Jerry na wazazi wa Dania

7. Mgogoro kati ya Nunu na Jerry

8. Mgogoro kati ya Gaddi na rafiki yake

FANI

Muundo

Msanii ametumia muundo changamano, amechanganya muundo rejea na

moja kwa moja. Sura ya kwanza ametumia muundo wa rejea na kuanzia

sura ya pili na kuendelea ametumia muundo wa moja kwa moja mpaka

mwisho wa riwaya.

Mtindo

Page 38: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 38

Msanii ametumia kwa kiasi kikubwa mtindo wa masimulizi na kiasi

kidogo mtindo wa dayalojia, nafsi zote tatu zimetumika. Vilevile kuna

matumizi ya barua (uk. 65).

Matumizi ya lugha

Lugha aliyotumia ni lugha rahisi iliyojaa misemo, methali, tamathali za

semi na mbinu nyingine za kisanaa.

Misemo/Nahau

Jibu lile lilimkata maini (uk. 36)

Methali

a Ukiyastaajabu ya Musa utayaona ya Firauni (uk. 27)

b Hakuna marefu yasiyo nan cha (uk. 117)

c Ni bora nusu shari kuliko shari kamili (uk. 127)

d Mkaidi hafaidi mpaka siku ya Iddi (uk. 135)

Tamathali za semi

Tashibiha

a Paa lake lililokuwa limejengwa kwa mithili yam domo wa

lile dege aina ya Concord (uk. 11)

b Gari iliruka mbele kama jiwe na kutimua vumbi (uk. 41)

c Kamfukuza kama mbwa kutoka kwenye nyumba ya

marehemu mumewe (uk. 60)

Mbinu nyingine za kisanaa

Tanakali sauti (Onomatopea)

Page 39: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 39

a Vilitilia mkazo uharaka wa binti yule kwa kutoa sauti za Ko! Ko!

Ko! (uk. 1)

b Aaakh! Ni – niache! Uuuuuwwiiiii !! Yallaaaah (uk. 37)

Takriri

a Toka hapa ! Ondoka! Na usirudi tena! (uk. 32)

b Nimesema sitaki! Sitaki! Sitaki! (uk. 35)

c Sikubali! Sikubali! Nawaambia nitawashitaki kwa hili ! (uk. 43)

Mdokezo

a Oh! Mungu wangu, sasa itakuwaje jamani….(uk. 13)

b Ah! Ni kweli Anti….lakini…..(uk. 12)

Wahusika

Gaddi Bullah

1. Huyu ndiye mhusika mkuu wa riwaya hii. Huyu alikuwa meneja

wa kampuni

2. Kijana mchangamfu na mwenye huruma

3. Mkarimu na mchapakazi

4. Alikuwa na upendo wa dhati

5. Ni msamehefu na mwenye kuzitawala hasira zake

6. Mume wa kwanza wa Nyambuja na mpenzi wa Dania

7. Gaddi anafaa kuigwa na jamii kutokana na tabia na matendo yake

mazuri

Page 40: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 40

Dania

1. Huyu ni mwanamke ambaye alizaliwa katika familia ya kitajiri

2. Ni mwenye hasira anapokuwa amechukizwa na mwenye chuki

3. Hana msimamo na hudanganyika kirahisi

4. Ni mfanyakazi mwenye nidhamu, bidii na ushirikiano

5. Alikuwa mlevi wa kutupwa baada ya kuachwa na Jerry

6. Dania ni mwanamke ambaye anafaa kuigwa kwa baadhi ya mambo

na hafai kuigwa kwa baadhi ya mambo

Bi. Hanuna

1. Huyu alikuwa dada wa Gaddi Bullah, alimpenda sana mdogo wake

kiasi cha kukataa kumsaliti

2. Alikuwa na chuki na mtu yeyote aliyemuudhi mdogo wake

3. Bi. Hanuna anafaa kuigwa na jamii kutokana na mapenzi

aliyokuwa nayo kwa mdogo wake

Jerry

1. Huyu alikuwa mpenzi wa Dania na alikuwa mtaalamu wa

kompyuta

2. Jerry alikuwa mcheshi, mtanashati na mwenye mvuto mkubwa

kwa akina dada

3. Jerry alikuwa katili na msaliti mkubwa kwani alimsaliti Dania

mara mbili

Page 41: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 41

4. Jerry hakuwa na mapenzi ya kweli ndio maana alikuwa muongo na

laghai wa mapenzi

5. Jerry kutokana na tabia zake hafai kuigwa na jamii

Nunu

1. Huyu alikuwa rafiki wa Dania

2. Alikuwa na mapenzi ya kweli kwa watu na aliwasaidia sana watu,

maana aliwasaidia sana wakati wa shida. Hivyo, anafaa kuigwa na

jamii

Wahusika wengine wanaojitokeza katika riwaya hii ni Boaz, Mama

Mlole, Mary, Aisha, Agnes, Junior na wengineo.

Mandhari

Mandhari ya riwaya hii ni halisi, inatalii maeneo kama vile Arusha, Dar

es Salaam na Pemba. Katika sehemu hizo zote kuna mandhari ya ofisini,

nyumbani, baa, barabarani, hospitalini, n.k

Jina la kitabu

Kwa kiasi kikubwa jina la kitabu linasadifu yale yaliyomo katika kitabu.

Mfadhili ni mtu anayemdhamini mtu katika kugharimia kitu fulani.

Hivyo katika riwaya hii msanii anaonesha ufadhili wa aina mbalimbali

kama ifuatavyo:

Kwanza tunaona ufadhili wa Mama Mlole kwa Gaddi baada ya

kukumbwa na kashfa ofisini kwake asifukuzwe kazi. Mama Mlole ndiye

aliyemtetea Gaddi hata kumhamishia Dar es Salaam kwa uangalizi zaidi.

Pili, Mama Mlole alimfadhili Dania asifukuzwe kazi kutokana na kuwa

mlevi sugu baada ya kuachwa na mpenzi wake Jerry.

Page 42: Mwalimu Wa Kiswahili - KITABU- VUTA N’KUVUTE ......UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019 MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 Uk 2 wakati zinazomnyanyasa mwanamke, kwani zinarudisha

UHAKIKI WA VUTA N’KUVUTE & MFADHILI 2019

MWALIMU WA KISWAHILI 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.com Uk 42

Tatu, Mama Mlole alimfadhili Gaddi na Dania kwa kuwapatanisha

kutokana na uhasama baina yao ambao ungeathiri utendaji kazi.

Gaddi vilevile alimfadhili Dania baada ya kuachwa na Jerry hata kuwa

mlevi wa kupindukia. Pili, Gaddi alimfadhili Dania kwa kumpa ini lake

moja wakati anaumwa baada ya kusalitiwa mara ya pili na Jerry. Tatu,

Gaddi alimfadhili Junior kwa kumpeleka hospitali baada ya kuumia

mkono. Isingekuwa Gaddi pengine Junior angepata matatizo makubwa

zaidi.

KUFAULU NA KUTOFAULU KWA MWANDISHI

KUFAULU

1. Kimaudhui, msanii amefaulu kuonesha matatizo mbalimbali

yaliyoko katika jamii yetu hasa katika suala la mapenzi na ndoa na

kuonesha suluhisho la matatizo hayo.

2. Kifani, amefaulu kutumia lugha rahisi na inayoeleweka na ujenzi

mzuri wa wahusika wake.

KUTOFAULU

1. Kutumia viswahili badala ya Kiswahili sanifu (uk. 15-16)

2. Matumizi ya Kiingereza, kwa mtu asiyejua Kiingereza atashindwa

kupata ujumbe.