17
P320/1. KISWAHILI (Nathari na Ushairi) Karatasi ya Kwanza AUGUST 2017 Saa 2 dakika 30 JINJA JOINT EXAMINATIONS BOARD Uganda Advanced Certificate of Education MOCK EXAMINATIONS AUGUST, 2017 KISWAHILI Karatasi ya Kwanza Muda: Saa mbili na nusu. MAAGIZO: Jibu maswali matatu kwa jumla; moja likitoka katika kila sehemu A, B, CH. @ 2017 Jinja Joint Examinations Board Pindua

P320/1 - Mukalele Rogers · Web viewJanet alijiunga na darasa la nane katika shule ya msingi ya Rematha. Shangaziye Janet aliyekuwa muuzaji wa ulevi uchwara wa shilingi kumi, alimwambia

  • Upload
    others

  • View
    0

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: P320/1 - Mukalele Rogers · Web viewJanet alijiunga na darasa la nane katika shule ya msingi ya Rematha. Shangaziye Janet aliyekuwa muuzaji wa ulevi uchwara wa shilingi kumi, alimwambia

P320/1.KISWAHILI (Nathari na Ushairi)Karatasi ya KwanzaAUGUST 2017Saa 2 dakika 30

JINJA JOINT EXAMINATIONS BOARD

Uganda Advanced Certificate of Education

MOCK EXAMINATIONS AUGUST, 2017�

KISWAHILI

Karatasi ya Kwanza

Muda: Saa mbili na nusu.

MAAGIZO:Jibu maswali matatu kwa jumla; moja likitoka katika kila sehemu A, B, CH.

@ 2017 Jinja Joint Examinations Board Pindua

Page 2: P320/1 - Mukalele Rogers · Web viewJanet alijiunga na darasa la nane katika shule ya msingi ya Rematha. Shangaziye Janet aliyekuwa muuzaji wa ulevi uchwara wa shilingi kumi, alimwambia

SEHEMU A: UFAHAMU

1. KATIBA MPYA YA SERIKALI

Kabla ya mambo aliyowambia mzee Shoka hayajatendwa, mwanadamu yaani

Jitu, alisimama akasema, "Ndugu zangu kabla mfalme Binti hajafa yatupasa

kumfundisha karama maalum ya kutawala watu kusudi baada ya kusikia katiba

mpya ya serikali aweze kujihukumu yeye mwenyewe.Aone kama alitenda haki

au hapana. Mimi, Bwana jitu, nawambia ya kuwa tangu leo mpaka mwisho wa

dunia watawala wote wa Utamaduni na serikali ambayo itafuata, kanuni tatu;

Kanuni ya kwanza: watu wote ni sawa. Hivyo hakuna ukoo kabla au taifa

lililo bora kuliko jingine. Kanuni ya pili: Serikali itakuwa serikali ile watu

waitakayo. Kanuni ya tatu: Mali ya nchi itagawanywa, kadri inavyowezekana ili

watu wote wanaichi waifaidi.

Nikijaribu kupanua hizi, mtaona ya kwamba kuna mambo mengi yanayozihusu.

Hebu tuchukue kanuni ya kwanza. Tangu leo nchi hii haitakuwa na machifu. Ebu

Kuchagua machifu kutoka ukoo mmoja ni sawasawa na kusema kwamba ukoo

huo ni bora kuliko koo nyingine. Lakini watu wote ni sawa.Kwa hiyo, mtu

yeyote, kutoka ukoo wowote, atachaguliwa na watu atawale, mradi tu watu

wawe wanampenda.

Kanuni ya pili inayoonyesha wazi ya kuwa serikali haitakuwa halali mpaka iwe

imechaguliwa na watu wenyewe. Kura itapigwa na raia watachagua wajumbe

wao watakaowakilisha maoni yao. Kutoka katika wajumbe hao, Serikali ya

kutawala nchi itaundwa. Mtu yule anayependwa na raia kuliko wote ndiye

ataunda serikali. Nawaachia watamaduni uhuru wa kuamua mtu kama huyo

atakuwa na sifa gani.

Serikali hiyo itakayochaguliwa na watu itatawala kwa muda ambao nyinyi

mtajichagulia. Baada ya muda huo, uchaguzi wa watu wote utafanywa kuchagua

serikali mpya. Nyinyi mkiona serikali iliyotawala haifai na imetenda mambo

mabaya basi msiichague. Chagueni serikali nyingine. Lakini mkiona serikali

© 2017 Jinja Joint Examinations Board Pindua

2

Page 3: P320/1 - Mukalele Rogers · Web viewJanet alijiunga na darasa la nane katika shule ya msingi ya Rematha. Shangaziye Janet aliyekuwa muuzaji wa ulevi uchwara wa shilingi kumi, alimwambia

mliyoichagua kwanza imetumia haki na imefanya maendeleo ya kutosha

hakuna sababu msiendelee kuichagua. Serikali hiyo itakayotawala isidhulumu

raia kama binta alivyo fanya; iepukane na damu. Kila mara ifanye kazi yake

ikikumbuka kuwa bila watu hakuna serikali.

Serikali hiyo iwape watu uhuru wa kusema na kutoa maoni yao kwa njia

yoyote ile itakayogunduliwa siku zijazo; lazima iwape watu uhuru wa

kufuata dhamila zao wanapowatumikia miungu wao; lazima iwape watu

uhuru wa kutetea haki zao.

Pamoja na hayo, ni vizuri serikali kuhimiza kusahihishwa. Mfalme Binta

aliangalia kusahihishwa kama dhambi; lakini serikali mpya ya watamaduni

iangalie kusahihishwa kama dawa, langalie kusahihishwa kama dawa ya

kutibu. Serikali hufanywa na watu.Watu wanaweza kukosa. Kwa hiyo serikali

isiwe kichwa ngumu ikakataa kusikiliza maoni ya raia. Kila mtu katika

serikali hii mpya anapaswa kuwa na jambo la kusema kwa sababu serikali ni

yake. Hivyo, anapaswa kusikiliza kadri iwezekanavyo. Lakini masahihisho

yasifanywe kwa ajili ya masahihisho. Masahihisho yanayohitajiwa ni

masahihisho yanayojenga nchi na wala si yale yanayobomoa. Upinzani wa

kuiangamiza nchi, upinzani wa kuleta hatari nchini ni upinzani wa kuifanya

serikali isitende kazi.

Kanuni ya tatu ni kanuni inayowahimiza watawala wagawe mali ya nchi

kwa usawa. Hii ina maana ya kuwainua watu wote hasa wakulima na

wafanyakazi. Hii ina maana kwamba, kwa kufuata hali ilivyo, serikali ifanye

juu chini kuziba pengo kati ya watu masikini na matajiri.

Kwa kifupi, kanuni za katiba ya serikali ni hizo. Kwa kufuata kanuni hizo�

mtaweza kujenga serikali ya haki."

Baada ya Bwana Jitu kumaliza hotuba yake, watu walipiga vigelegele�

vilivyopasua hewa. Vigelegele viliendelea kwa muda wa dakika tano huku

watu wakiruruka na kusema, Hiyo ndiyo � serikali! Hiyo ndiyo serikali!"

© 2017 Jinja Joint Examinations Board Pindua

3

Page 4: P320/1 - Mukalele Rogers · Web viewJanet alijiunga na darasa la nane katika shule ya msingi ya Rematha. Shangaziye Janet aliyekuwa muuzaji wa ulevi uchwara wa shilingi kumi, alimwambia

MASWALI:

i. Bwana Jitu amependekeza kuwa tangu wakati wake hadi mwisho wa dunia kufanywe nini? (Alama 03)

ii. Bwana Jitu ana mawazo gani juu ya mtawala Binta? (Alama 04)iii. Kutokana na mawazo na maelezo ya Bwana Jitu, mtawala Binta ana

sifa zipi? Thibitisha. (Alama 05)iv. Tambua maudhui sita yanayozungumziwa katika makala hapo juu.

(Alama 06)

v. Kutokana na Bwana Jitu masahihisho yanayohitajika ni yale yanayojenga na si yale yanayobomoa. Kauli yake hii inamaanisha nini? (Alama 05)

vi. Eleza mbinu za lugha zozote tano ambazo zinajitokeza katika matini.(Alama 10)

SEHEMU B: NATHARI2. KAA MASAA

Kwa mara nyingine tena wakazi wa kijiji cha kutana walikusaanyika na

kuomboleza na kutoa heshima zao za mwisho kwa mmoja wao aliyewaacha

mkono. Hawakujua ni nani ambaye angefuata baada ya mamake Janet. Imepita

wiki moja tu, tangu wamzike babake Janet. Wazazi wake walipofariki Janet

hakuwa na yeyote wa kumtegemea. Alilazimika shingo upande kwenda kuishi

kwa shangaziye katika mtu wa mabanda wa Rematha jijini. Janet alijiunga na

darasa la nane katika shule ya msingi ya Rematha. Shangaziye Janet aliyekuwa

muuzaji wa ulevi uchwara wa shilingi kumi, alimwambia janet alipowasili hapo

kibandani kwake, Lazima ulete pesa za chakula ukirudi hapa jioni. Ushasikia?� � Akasema huku akimkazia Janet macho, Lazima ufanye maarifa ya kujipatia�

chakula. Janet hakujua amjibuje shangaziye. Alikuwa mbumbumbu.� �Maisha katika mtaa wa mabanda wa Rematha yalikuwa tofauti kabisa na maisha

ya kijijini alikozaliwa Janet. Alishangaa kuwaona wasichana wa darasa la nne tu,

wakitor oka shule. Wasichana hawa wa umri wa miaka kumi waliondoka

nyumbani wakivalia sare za shule, lakini bila wazazi wao kujua, walivalia nguo

za nyumbani ndani. Wazazi wa watoto hawa walishtukia watoto wao

© 2017 Jinja Joint Examinations Board Pindua

4

Page 5: P320/1 - Mukalele Rogers · Web viewJanet alijiunga na darasa la nane katika shule ya msingi ya Rematha. Shangaziye Janet aliyekuwa muuzaji wa ulevi uchwara wa shilingi kumi, alimwambia

wameambukizwa magonjwa ya ngono! Wengine walilala nje siku tatu bila

wazazi wao kujua waliko. Janet alikuwa akistaajabu ya Musa, lakini punde

angeyaona ya firauni. Baadhi ya wanafunzi wenzake walikuja shuleni wakiwa

walevi chakari! Wengine walitumia dawa za kulevya na kunusa gundi. Visa vya

ubakaji na mauaji vilipotoka, wenyeji walisikika, Hiyo ni bahati mbaya.� �Ukifika roma, fanya yale yanayofanywa na warumi. Jeni aliyekuwa, darasa moja� �

na janet alisikika akimshauri, kasa akaongezea. Hapa ni taooo sio ushaagoo.�

Lazima ukae masaa ama sivyo uta-dead juu ya ubao. Janet alishawishika kufuata�

mashauri ya Jeni. Aliyakumbuka maneno ya marehemu mamake pale alipovunja

ungo. Janet sasa umekuwa mtu mzima. Vilinde viungo vyako vya uzazi kwa�

wivu-usimkubalie mtu yeyote akuchezee. Usikubali zawadi ama mapendeleo

yoyote kutoka kwa mtu usiyemfahamu.. Janet alihiari kufa njaa badala ya kujitia�� �

katika vitendo vya kujidunisha vilivyoweza kuhatarisha maisha yake na hatimaye

kumwangamiza. Alikula yamini kuwa hangefuata asilani maagizo ya shangaziye, � Kufanya maarifa ya kujipatia chakula. Leo ya tatu, Janet hajatia riziki tumboni.� � Janet alizirai darasani mwalimu alipogundua kuwa huduma ya kwanza aliyopewa

Janet na wanaskauti haikumsaidia alikimbia hima kwenye kioski.

Mwalimu alipondoka, Jeni alipaaza sauti na kusema Huyu mshamba kutoka�

ushaagoo nikimwambia akae masaa kama supuu wa mtaa, ananiona zuzu

mpungufu wa akili. Maneno ya Jeni yalikatiziwa na mwalimu aliyerejea na�

pakiti ya maziwa na nusu ya mkate. Baada ya kusikiliza masaibu ya Janet,

mwalimu alikata kauli kumkaribisha akae kwake baada ya kushauriana na mkewe

ambaye pia alikuwa mwalimu. Wahisani hawa walimkaribisha Janet nyumbani

kwao akawa kama mmoja wa watoto wao wawili waliosoma katika shule za

bweni. Matokeo ya mtihani yalipotangazwa, Janet alikuwa miongoni mwa

wanafunzi hamsini bora kote nchini. Walisani hawa walijifunga vibwe bwe

kumsomesha Janet katika shule ya taifa alikopata nafasi, ingawa walikuwa

wamelemewa na mzigo wa karo za watoto wao wenyewe.

Ama Kweli chanda huvikwa pete.

© 2017 Jinja Joint Examinations Board Pindua

5

Page 6: P320/1 - Mukalele Rogers · Web viewJanet alijiunga na darasa la nane katika shule ya msingi ya Rematha. Shangaziye Janet aliyekuwa muuzaji wa ulevi uchwara wa shilingi kumi, alimwambia

Janet aliendelea kukaa kwa wahisani wake wakati wa likizo. Alipokuwa likizoni,

alikwenda kumtembelea Jeni alipopashwa habari kwamba ni mgonjwa; mguu

mmoja kaburini na mwingine duniani. Alionekana si mtu wa ulimwengu huu

tena. Dalili zote zilindhihirisha kuwa jua la feni lilikuwa limekucha. Hata

hivyo, Jeni alijikaza kisabuni na kumwambia Janet kwa sauti dhaifa. Afa afadha��� ���..li we-we u-li-ye-ka-ta-a ku-sha-wi-shi-wa. Kwa za-wa-di n-na pe-e-sa n- ma-ko-��nda na ma-dee wa. Ma-three.. alimaliza huku pumzi zikimwenda mbio. Haya� ��� � �

ndiyo matokeo ya kukaa masaa? Janet alijiuliza kimoyomoyo.

MASWALI:1. Kwa nini ni muhimu kila mtu kujua hali yake kuhusiana na ukimwi (Alama 3)

2. Ni hatua gani jamii inafaa kuchukua ili kushughulikia maslahi ya watu kama Jeni? (Alama 6)

3. Toa maana ya methali zifuatazo kama zilivyotumika katika hadithi (Alama 4)

(a) Akistaajabu ya Musa anayaona ya firauni.�(b) Chanda chema huvikwa pete

4. Eleza maana ya Nahau hizi. (Alama 10)

(a) Aliyewaacha mkono

(b) Shingo upande.

(c) Alipovunja ungo

(d) Hiari

(e) Kula yamini

(f) Kata kauli

(g) Funga vibwebwe

(h) Jua lilikuwa limekuchwa.

(i) Mguu mmoja kaburini, mwingine duniani

(j) Jikaza kisabuni

5. Ni mafunzo yapi unayojifunza kutokana na hadithi hii? (Alama 6)

6. Ipe hadithi hii kichwa kingine kifaacho (Alama 4)

SEHEMU CH: USHAIRI

© 2017 Jinja Joint Examinations Board Pindua

6

Page 7: P320/1 - Mukalele Rogers · Web viewJanet alijiunga na darasa la nane katika shule ya msingi ya Rematha. Shangaziye Janet aliyekuwa muuzaji wa ulevi uchwara wa shilingi kumi, alimwambia

ABDILATIF ABDALLA : Sauti ya Dhiki3. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

Ama Kwa Heri

Nakuaga ndugu yangu, kwa heri ya kuonana

Naondoka nenda zangu, hiwa na simanzi sana

Simanzi moyoni mwangu, kwa tulivyozoweyana

La kutenda ndilo sina, ela kwenenda nendako

Nawe kaa kwa salama, salama wa salimini

Nakutakiya uzima, na furaha ya moyoni

Siku moja ni lazima, tutakutana wendani

Kwa hili nina yakini, bora sote tuwe hai

Siwa kukukumbuka, popote nitapokuwa

Na ngawa naondoka, mimi mbali nawe kuwa

Daima utanitoka, ndani ya change kifuwa

Hakuna cha kukutowa, nendapo takwenda nawe

Ndu yangu Israel, mambo huwenda yakija

Kwamba tutakuwa mbali, si hoja hiyo si hoja

Mbali ni yetu miili, bali nyoyo zi pamoja

Moja na moja si moja, lakini kwetu ni yiyo

Beti tano namaliza, mbele hakusongeleki

Ningetaka kuongeza, lakini mbele sifiki

Mingine nayabakiza, yote hayaelezeki

Kwa heri ndugu rafiki, kwa heri ya kuonana

MASWALI:

(a) Shairi hili ni la aina gani? (Alama 6)

(b) Toa ujumbe unaopitishwa kwa msomaji katika shairi hili. (Alama 12)

(c) Kwa kutumia mifano mbalimbali kutoka shairi hili, toa maana ya

© 2017 Jinja Joint Examinations Board Pindua

7

Page 8: P320/1 - Mukalele Rogers · Web viewJanet alijiunga na darasa la nane katika shule ya msingi ya Rematha. Shangaziye Janet aliyekuwa muuzaji wa ulevi uchwara wa shilingi kumi, alimwambia

(i) Dhamira.

(ii) Mizani

(iii) Utao

(iv) Ukwapi

(v) Urari wa mizani (Alama 15)Au

4. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

Wasafiri Tuamkeni

Bado safari ni ndefu, wasafiri tusichoke

Natusiwe madhaifu, twendeni hadi tufike

Tusafiri bila hofu, wenye nazo ziwatoke

Huu ndio mwanzo wake, siwo mwisho wa safari

Twendeni tusonge mbele, twendeni tusianguke

Mwaona mlima ule? Pale ndipo mwisho wake

Tupande chake kilele, bendera tuitundike

Huu ndio mwanzo wake, siwo mwisho wa safari

Twendeni tukifahamu, kila mtu akumbuke

Safari yetu ni ngumu, si rahisi ndiya yake

Kuna miba yenye sumu, tunzani tusidungike

Huu ndio mwanzo wake, siwo mwisho wa safari

Ni ndiya yenye msitu, na mirefu miti yake

Imejaa nyama mwitu, kila mmoja na pake

Na wakionapo kitu, ni lazima wakishike

Huu ndio mwanzo wake, siwo mwisho wa safari

Na kuna bahari pana, na kirefu kina chake

Mawimbi makubwa sana, ni ajabu nguvu zake

Hiyo hatuna namna, ni lazima tuivuke

Huu ndio mwanzo wake, siwo mwisho wa safari

© 2017 Jinja Joint Examinations Board Pindua

8

Page 9: P320/1 - Mukalele Rogers · Web viewJanet alijiunga na darasa la nane katika shule ya msingi ya Rematha. Shangaziye Janet aliyekuwa muuzaji wa ulevi uchwara wa shilingi kumi, alimwambia

Kusafiri ni lazima, tukitaka tusitake

Wale waliyo wazima, maguu nayanyosheke

Na aliye na kilema, naabebwe na mwenzake

Huu ndio mwanzo wake, siwo mwisho wa safari

Na mshikaji bendera, kwa vizuri naishike

Daima nawe imara, wala asilainike

Ay'ongoze barabara, huko twendako tufike

Huu ndio mwanzo wake, siwo mwisho wa safari

MASWALI:

(a) Shairi hili lina muwala ukilisoma. Nini maana ya muwala katika shairi?

(Alama 04)

(b) Kulingana na shairi hili, wewe kama mtahiniwa, kibwagizo cha shairi

kinakupa ujumbe upi? (Alama 04)

(c) Shairi hili linatuamsha kama wasafiri duniani mbali na safari za

kutembea hadi mahali fulani je, tuna safari zipi tunazoshughulikia

maishani? Eleza kwa kutoa angalau hoja sita. (Alama 12)

(d) Chambua muundo wa nje wa shairi hili ukizingatia angalau vipengele saba. (Alama 14)

MWINYI HATIBU MOHAMED: Malenga wa Mrima

Ama

5. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali

MUZUIA MUMBU

Leo nawambia hembu nipatieni kalio.� �Ninene naye mbumbumbu, wa kutojua upeo.

Eti azuia mumbu, yaoleni makulio.

Yaoleni makulio, eti azuia mumbu.

Yundani ya kiminyano, mikono ni yake ngao.

Kasiga hana usono, kwa majasho na kupuo.

Haetuki kwa hilino, yu katika angamio.

© 2017 Jinja Joint Examinations Board Pindua

9

Page 10: P320/1 - Mukalele Rogers · Web viewJanet alijiunga na darasa la nane katika shule ya msingi ya Rematha. Shangaziye Janet aliyekuwa muuzaji wa ulevi uchwara wa shilingi kumi, alimwambia

Yaoleni makulio, eti azuia mumbu.

Mumbu hasinua miti, yenye vimo na matao.

Si mno kupitwa kati, madharae ni kilio.

Uwe maji ya magoti, sisi hatunyeti nao.

Yaoleni makulio, eti azuia mumbu.

Huko juu ushukapo, ni yowe na makamio.

Pili kila kilichopo si masiki si mabao.

Hakiachwi ila hapo, hufanya maandamio.

Yaoleni makulio, eti azuia mumbu.

Ni vipi huyu mwenzetu, akatekwa na kileo.

Ajivika hana matu, kwa wingi wa bambalio.

Atakula mtukutu, asambe ni mwendeleo.

Yaoleni makulio, eti azuia mumbu.

Jinsi alivyotuna, katika hili tukio.

Lau kwamba tamnena, jawabule ni mkao.

Heri njia kugawana. Kila mtu ende kwao.

Yaoleni makulio, eti azuia mumbu.

MASWALI

(a) Andika ubeti wa pili katika lugha nathari. (Alama 5)

(b) Onyesha namna mshairi alivyotumia uhuru wa shairi MZUIA �MUMBU.� (Alama 10)

(c) Msomaji wa shairi hili anapata hisia zipi? (Alama 8)

(d) Eleza mafunzo msomaji wa shairi anayopata. (Alama 10)

Au

6. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali

KUSEMA

Ungamuona kuhani, anena hamezi mate.

Angaka na kujighani, malumbi ashinda wote.�

© 2017 Jinja Joint Examinations Board Pindua

10

Page 11: P320/1 - Mukalele Rogers · Web viewJanet alijiunga na darasa la nane katika shule ya msingi ya Rematha. Shangaziye Janet aliyekuwa muuzaji wa ulevi uchwara wa shilingi kumi, alimwambia

Jitulize kwa makini, akili asikuchote.

Kusema ni kwetu sote, mawazo ni kwa wachache.

Urembo wa binadamu, na uzawa pande zote.

Usikutiye hamumu, ukamba hanayo tete.

Twa kidogo sehemu, mwengine mwache agute.

Kusema ni kwetu sote, mawazo ni kwa wachache.

Hata vitisho na nguvu, kichwani mwako yafute.

Maguvu si saidivu, yapishe njia yapite.

Ukaechi kwa utuvu, na moyo usikutute.

Kusema ni kwetu sote, mawazo ni kwa wachache.

Mathali mtu tajiri, kajaaza kote kote.

Iwa ni mwenye nadhari, wenende kisha usite.

Kwenda anayo dosari, dhibiti asikuvute.

Kusema ni kwetu sote, mawazo ni kwa wachache.

Uaminifu na vyeo, tumbo yasikerekete.

Wangapi wachafuo, na hadhi wazifumbate.

Malumbanaji ni chuo, pekee tulikamate.

Kusema ni kwetu sote, mawazo ni kwa wachache.

MASWALI

(a) Eleza maana ya kibwagizo cha shairi hili. (Alama 5)

(b) Shairi hili linawalenga akina nani? Eleza. (Alama 10)

(c) Tambua na ueleze maudhui matatu yanayopatikana katika shairi hili.

(Alama 10)

(d) Kwa kurejelea shairi, eleza matumizi ya mbinu zifuatazo:

(i) Inkisari,

(ii) Mazda. (Alama 8)

© 2017 Jinja Joint Examinations Board Pindua

11